fbpx

IMANI ONGEZO ZA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

Kwa sababu ya pepo nyingi za Mafundisho yanayovuma katika Kanisa la Saa ya Kumi na Moja ni muhimu kwetu kutaarifu hapa imani yetu ziada, ambayo ni uthibitisho tu wa imani yetu katika Ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji. Kwa mujibu wa Bakuli la Dhahabu tunaamini kama ifuatavyo:

Funza Tu Kile Ambacho Kimechapishwa

 1. Kwamba Vitabu vyote vya Fimbo ya Mchungaji vilichapishwa kabla ya kifo cha nabii katika Magombo, Trakti na Msimbo wa Nembo. Mahubiri yaliyochapishwa katika vitabu vitano vinavyojulikana zaidi kama Msimbo mpya, ni nyongeza ambayo haikuvuviwa kwa Ujumbe na havipaswi kusomwa au kufundisha kutoka kwavyo. Tunaelewa agizo “Fundisha tu lile ambalo limechapishwa,” humaanisha yale yaliyochapishwa na marehemu Ndugu V. T. Houteff. Kwa mujibu wa 8SC1-12: 20.2.4ABN5: 55.1- 56.1.

Ghala, Makao Makuu na Eneo

 1. Kwamba Mungu hajawahi kuwa na vuguvugu zaidi ya moja kwa wakati mmoja na haiwezi kuwa vinginevyo sasa. Kanisa la Mungu limetambuliwa vizuri katika kila kizazi kwa kutii ukweli wa sasa. Kwa mujibu wa SR2: 125.1SR2: 93.2SR2: 257.41TG51: 10.4;1SC13: 11.4 .
 1. Kwamba Mungu analo ghala moja tu kwa wakati mmoja na pale ni popote pale ambamo hutolewa ukweli wa sasa; na ukweli wa sasa kwa wakati huu ni utakaso katika Kanisa la saa ya Kumi na Moja, kanisa la Wadaudi Waadventista wa Sabato. Kwa mujibu wa 1SC5: 9.12TG30: 18.2.
 1. Kwamba upo Mlima Karmeli akisi mmoja tu na upo katika eneo la Waco, Texas na haujawekewa mipaka kwa Njia ya 2500 Mlima Karmeli ila badala yake kwa ekari zote 375 zilizonunuliwa na nabii wa Mungu. 1SC16: 1.12SC5,6: 3.1.22SC10: 2.1.1.
 1. Kwamba Ezekieli 47 haihusiani kwa vyovyote na harakati za makundi mbalimbali ya Wadaudi iwe ni kuelekea mashariki, magharibi, kusini au kaskazini lakini inahusiana moja kwa moja na hekalu akisi litakalojengwa na kanisa lililotakaswa na mgao mpya wa ardhi katika Ufalme. Kwa mujibu wa 1TG13: 5.26.2, 6.3 and 2TG42: 38.1.

Kanisa Ndani Ya Kanisa

 1. Kwamba Dhehebu la Waadventista wa Sabato, Israeli mamboleo (kabila kumi na mbili), lina makanisa mawili; Kanisa la saa ya tisa (Kanisa la S. D. A.) na Kanisa la saa ya kumi na moja (Kanisa la D. S. D. A.); sanjari kwa Israeli ya zamani baada ya kifo cha Mfalme Sulemani, yaani Yuda na Israeli. Kwa hivyo, Kanisa la D. S. D. A. ni kanisa ndani ya kanisa au “vuguvugu ndani ya vuguvugu”, kile ambacho ndicho vuguvugu, ndivyo lilivyo vuguvugu ndani ya vuguvugu. Kwa mujibu wa Math 20:6; SR2: 93.2TN4: 57.466.3WHR: 33.22TG34: 24.1-25.2
church within church.

Utakaso Katika Sehemu Mbili

 1. Kwamba utakaso wa Dhehebu la Waadventista wa Sabato, malimbuko ya mavuno, u katika sehemu mbili, utakaso wa kwanza utakuwa katika Kanisa la Saa ya Kumi na moja na wale watu sita wa Ezekieli sura ya tisa, ambao una muda wa kuingilia kati baina ya kutiwa muhuri na mchinjo, wa pili u katika Kanisa la saa ya Tisa na wale watu watano wa Ezekieli sura ya tisa, wakati yule mtu aliye na kidau cha wino angali anatia alama – katika maangamizo ya waovu kwa ujumla – ambamo hakuna muda wa kuingilia kati baina ya kutiwa muhuri na mchinjo. Kwa mujibu wa Ezek. 9:2; TN3: 71.1-2SR2: 185.3TN3: 76.178.1LDSDA: 3.2JL6: 2.1SR1: 37.2TN1: 38.21TG52.

Mfano wa Awamu Ya Yuda Na Israeli

 1. Kwamba sisi ni Yuda mamboleo, wazawa wa wale Wayahudi waliojumuisha Kanisa la Kwanza la Kikristo, ilhali, Walaodekia au “mama” kama anavyoitwa mara nyingi na Wadaudi wengi, ni Israeli mamboleo, wazawa wa kabila kumi waliotawanywa na Ashuru ya zamani. Kwa mujibu wa LDSDA: 3.21TG37: 11.22TG6: 15.3.

Wengine Kando na Wale 144,000

 1. Kwamba Waisraeli 144,000 pekee ndio watakaookolewa katika mavuno ya malimbuko ya walio hai, bali watakuwamo “idadi kubwa kutoka katika nchi za Mataifa,” ambao watakuwa pamoja na watu 144,000, watakookolewa katika mavuno yaliyotajwa. Kwa mujibu wa TN3: 98.2ABN4: 35.1.

Ufufuo Maalum

 1. Kwamba wale wanaoamka katika ufufuo maalum hawapelekwi katika ufalme kwa wakati mmoja kama malimbuko ya walio hai, wale 144,000 na walio pamoja ma wao, ila badala yake, wanapelekwa katika ardhi zilizoko nje tu ya Ufalme, ardhi ambazo punde tu baadaye zitaongezewa ndani ya mipaka ya Ufalme (nchi hizi hazitakuwa sehemu ya Babeli kama tulivyoamini hapo awali), pale wajaribiwe na kupewa fursa ya kukubali Ukweli wa Wakati kwa wakati huo, ambao kwao watawageuza wengi hadi kwenye haki. Kwa mujibu wa TN12: 37.12TG7: 11.215.1.
 1. Kwamba wa’S.D.A. wote waliokufa chini ya ujumbe wa Malaika wa Tatu wakitunza ukweli wa Sabato watatokea katika ufufuo maalum ambao unajumuisha, lakini haujawekewa mipaka kwa Dada E. G. White na Ndugu V. T. Houteff. Hakuna ufufuo maalum maalum kabla ya ufufuo maalum wa Danieli 12. Kwa mujibu wa DAN. 12:2; 2TG7: 11-12TN9: 41.1.

Usitie Tena Msingi wa Toba

 1. Kwamba sisi, Wadaudi, sharti tujiokoe kwanza kabla ya kuweza kuwaokoa ndugu zetu katika kanisa la saa ya Tisa. Kwa mujibu wa 9SC1-12: 7.2.7.
 1. Kwamba lazima kwanza tulie kwa machukizo yaliyo katikati yetu kabla ya kulia kwa machukizo yaliyo katikati ya Walaodekia. Kwa mujibu wa EZEK. 9:4.
jl6_6_hunt_them (1)

Kampeni Za Kuzingira

 1. Kwamba kampeni za sasa za kuzingira ambazo zinaendeshwa na Wadaudi zinazojumuisha ila hazijawekewa mipaka kwa usambazaji wa vitabu kwa wale ambao hatujawafanya kuwa marafiki, mbele ya makanisa ya SDA, mikutano ya makambi, vikao vya Baraza Kuu, ni chukizo na fedheha kwa Ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji. Kampeni hizi zilianzishwa na Florence Houteff, kwa mujibu wa barua kutoka kwa Kamati Kuu ya DSDA hadi kwa Baraza Kuu la kanisa la SDA yenye tarehe ya Februari 17, 1959 iliyochapishwa katika Gombo la 14 la Msimbo wa Nembo Namba 6.
 1. TKwamba tunapaswa kuendesha kampeni ya “kukusanya majina” ili tuweze kuwavua na vitabu kisha tuwawinde kwenye “malango yao iwe wako jijini au vijijini.” 7SC1-6: 2.1.1-47SC7-12: 17.2.7-18.1.38SC1-12: 24.1.6-24.2.49SC1-12: 18.2.5-7JL6: 5.3.

Kipindi Cha Kulima Kwa Ng’ombe

 1. Kwamba uamsho na matengenezo makuu yaliyotabiriwa katika Shuhuda kwa Kanisa Gombo la 9, ukurasa wa 126, na UFU. 8:5 yatatukia katika kanisa la saa ya Tisa baada ya utakaso katika kanisa la saa ya Kumi na Moja na kabla ya kusimamishwa ufalme wa amani wa Mungu katika Nchi ya Ahadi. Kwa mujibu wa LDSDA: 5.112.2SR2: 219.21TG17: 5.3.
 1. Kwamba awamu ya jembe la ng’ombe ya ujumbe wa kutiwa muhuri bado i mbele na itaanza baada ya kuangamizwa kwa ng’ombe hafifu, wanawali wapumbavu, Kora, Dathani na Abiramu, wapelelezi kumi na kina Akani, katika Vuguvugu la Wadaudi Waadventista wa Sabato, kanisa la saa ya Kumi na Moja. Kwa mujibu wa TN6: 40.1ABN2: 55.25SC1-5: 9.1.4.

Ushirika

 1. Kwamba upo muungano mmoja tu nao ni muungano wa kanisa na serikali wa Isaya sura ya 8 ambao huanzia katika Ashuru mamboleo na kuendelea hadi katika Babeli mamboleo na tunaambiwa na Isaya kwamba tusiseme lolote kwa wale ambao wameambiwa waungane, badala yake tunapaswa kumtakasa Bwana Mungu wetu. Kwa mujibu wa Isa 8:11-22; 2TG41: 18.3-21.31TG27: 8.2-9.1.

Wakati wa Dhiki Ya Yakobo

 1. Kwamba ipo dhiki moja tu, DAN. 12: 2; UFU. 13:15-17; ambayo ni alama ya mnyama, na inapoanza itapiga kwanza masalia ya mafuriko, UFU. 12:16. Yeremia aliandika kuhusu dhiki iyo hiyo, YER. 30:7, ambayo inawahusu tu wale 144,000, ilhali Yohana na Danieli walinena juu ya hiyo dhiki kama inavyowahusu wale 144,000 na umati mkubwa. Kwa mujibu wa TN15: 61.1TN5: 118.1TN9:58.2; 2TG10: 29.3-4TN8:22.1 and 2SC2:4.8-10.
 1. Kwamba wakati wa dhiki ya Yakobo utatukia baada ya utakaso wa kanisa la saa ya Tisa. Kwa mujibu wa FB: 12.3.

Propaganda Ya Pigo La Mtoano

 1. Kwamba hakuna pigo la mtoano lililotekelezwa kwa ujumbe huu katika mwaka 1959 na kamwe halitatekelezwa. Pigo la mtoano humdokeza mpokeaji wa pigo akiwa amepoteza pambano. Kwa vile Kristo ni Jenerali ambaye hajawahi kushindwa vita hakungekuwapo na pigo la mtoano lililotekelezwa kwa ujumbe huu ambao umeamuliwa kimbele kushinda. Lilikuwapo jaribio la kutekeleza pigo la mtoano katika mwaka wa 1959 kama ilivyoonya Fimbo, hata hivyo, baada ya jaribio hilo, vuguvugu lilijipanga upya katika mwaka wa 1961 muda mfupi kabla ya Dada Houteff na baraza kuu lake kuivunja jumuiya na vuguvugu hilo linaendelea hadi leo. Kwa mujibu wa WHR 33.2;ABN1: 67.1 and 68.1.

Daudi Akisi

 1. Kwamba Daudi Aakisi siye Ndugu V. T. Houteff wala ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, bali ni mtu ambaye Kristo atamtuma awatawale kwa niaba Yake kabla ya kurudi Kwake kufanya hesabu na watumishi Wake, Wadaudi. Kwa mujibu wa TN9: 43.2TN8: 71.1,22TG2: 14.317.2.

Utatu

 1. Kwamba Utatu unaashiria Wale watatu wa Uungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kwa mujibu wa SR2: 54.17SC1-6: 13.2.4-13.2.6TN3: 91.4FB: 3.42TG10: 21.4 AND 2TG19: 16.2.
>