fbpx

Trakti Namba 01

Trakti Namba 01

Ya-Ziada Kabla ya “Saa ya Kumi na Moja”

FUMBO LA MAFUMBO LIMEWEKWA WAZI!

1 (Jalada)

Hati miliki, 1933,1940, 1941

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

Kwa nia ya kufikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inataka kuepuka njia inayoongoza hadi kwa uharibifu wa mwili na roho, kijitabu hiki kitasambazwa bila malipo kadri toleo hili litakapoendelea kuwapo.

1

Toleo la Tatu Lililosahihishwa

Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu

Mlima Karmeli

Waco, Texas

Kimechapishwa Marekani

2

DIBAJI

MWENYEWE KUTAZAMIA KILA MSHALE WA NURU.

Mtu anayemtegemea mwingine kuchunguza ujumbe kutoka kwa Bwana, anaufanya mwili kuwa kinga yake, na hivyo anatenda kwa upumbavu kama asiye na akili zake mwenyewe. Na “mawazo yanayotegemea hukumu ya wengine ni hakika, upesi au baadaye, kupotoshwa.” — Elimu, uk. 231. {TN1: 3.1}

Vile vile, mtu ambaye anaruhusu chuki kumzuia kutoufanya uchunguzi wa lolote jipya, linalokuja katika jina la Bwana, ni mkafiri bila kujua. {TN1: 3.2}

Vivyo hivyo yeye ambaye ameridhika na mafanikio yake ya sasa katika Neno la Mungu, anasema kwa kweli: “Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, na sihitaji kitu.” {TN1: 3.3}

Haya yote, kwa kutenda mbali mbali sehemu ambayo yalisababisha kemeo lililoandikwa dhidi ya Walaodekia, na hivyo kutimiza unabii ambao hawagepaswa kutimiza, wanajiandaa kutapikwa (Ufu. 3:14-18). Na iwapo wanaendelea katika hali yao ya kutosheka kwa ubinafsi ya kwamba wana ukweli wote, na hivyo hawana haja ya kitu zaidi, watakataa kwa dharau kila dai jipya kwa ukweli na kutupa ujumbe ndani ya jaa kwa sababu unakuja kupitia njia isiyoyotarajiwa. Kwa hakika, basi, kijitabu hiki kisingalikuwa kufunuliwa kwa unabii, ukweli si wa

3

kuepukwa kwamba wakati ufunuo ulipokuja, wangeutendea kwa namna hiyo, na hivyo kuutupailia mbali wokovu wao! {TN1: 3.4}

Katika vizazi vyote, wote ambao huweka matumaini yao kwa watu wanaoitwa eti wenye busara, na Wakristo wakuu wa siku, wote wanaodhaniwa kuwa wanamcha Mungu, wamenyang’anywa taji ya uzima wa milele, kama walivyokuwa walei wa Kiyahudi katika siku za Kristo kwa sababu yao kushindwa kuchukua jukumu kamili kwa wokovu wao wenyewe. Kwa ushupavu wakiamini hekima ya wanaoitwa eti “watu wakuu,” walikataa kuamini maneno ya Kristo: “Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.” Mat. 11:25 “Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? … Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?” 1 Kor. 1:20. {TN1: 4.1}

“… iwapo ujumbe unakuja ambao huelewi, vumilia uweze kusikia sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa, ukilinganisha andiko kwa andiko, ili uweze kujua kama lina au halina msingi wa neno la Mungu.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65. {TN1: 4.2}

Hautakoma, basi, Ndugu, Dada, kuiga makosa ya wengine? Je! Hautafaidika kwayo? Ikiwa unataka, unawajibika kutumia akili yako mwenyewe ili kuufikia wokovu, usije ukakosa kuelewa ukweli unaookoa katika ufichuzi muhimu,

4

Ya ziada Kabla Ya “Saa Kumi Na Moja” Viunganishi Vya Biblia. {TN1: 4.3}

Mwito wa Ezekieli kwa ofisi ya unabii ni mojawapo wa uzoefu wa kuvutia zaidi wa manabii wa kale, na ufunuo wa yale aliyoyaona kwenye mto Kebari huenda ni wa umuhimu mkubwa zaidi kwa mbingu na dunia wakati huu kuliko maono mengine kwenye kumbukumbu takatifu, sababu kwa njia ya ajabu unafunua Hicho Kinachounganisha Mbingu na Dunia, kama vile mlango wa bahari unavyounganisha bahari mbili muhimu. Hivyo uchambuzi huu wa maono ya Ezekieli ambayo huleta kwa nuru dunia ikijiliwa na Mfalme wa Ulimwengu, yanaweza kuitwa vizuri, “Viunganishi vya Biblia.” {TN1: 5.1}

Msomaji ambaye angeweza kufahamu vyema huu unaonekana kuwa mfano wa kukanganya na kutatanisha wa mifano ya Biblia, atafuata mchoro kwa ukurasa wa jalada, pamoja na

Ufafanuzi Wa Nabii Wa Mafumbo Yaliyoelezwa Hapa. {TN1: 5.2}

“Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo. {TN1: 5.3}

“Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. Na kila mmoja

5

alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. {TN1: 5.4}

“Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia….. {TN1: 6.1}

“Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote. Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa Bwana. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja aliyenena.” Ezek. 1:4-10, 27, 28. {TN1: 6.2}

“Ikawa, hapo alipomwagiza huyo mtu aliyevaa bafta, akisema, Twaa moto kutoka katikati ya magurudumu yazungukayo katikati ya hao makerubi,

6

akaingia, akasimama karibu na gurudumu moja.” Ezek. 10:6. {TN1: 6.3}

Katika tukio hili la ajabu ambalo Ezekieli aliona kando ya mto katika nchi ya Wakaldayo, umakini wetu wote sasa unahitajika. Likiwa “kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa Bwana,” ni dhahiri, basi, alikuwa

Bwana kwa Kimoja cha Viti Vyake vya Enzi. {TN1: 7.1}

Mbali na uwepo huu wa Mungu ambao Ezekieli aliona (Ezek. 1:28), Biblia hufafanua Mungu akiwa ameketi kwenye nyakati zingine tatu — mara moja jinsi Isaya alivyoona, na mara mbili kama alivyoona Yohana Waufunuo; yaani: {TN1: 7.2}

(1) “… Nalimwona Bwana ameketi kwenye kiti cha enzi, kilichoinuliwa na juu sana, na msafara Wake ukalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu Wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.” Isa. 6:1-4. {TN1: 7.3}

(2) “Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;… Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao

7

walikuwa na taji za dhahabu…. Na taa saba za moto zilikuwa zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.” Ufu. 4:2, 4-6. {TN1: 7.4}

(3) “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo.” Ufu. 22: 1. {TN1: 8.1}

Kwa sababu kiti cha enzi alichokiona Isaya kilikuwa “treni” (msafara), na kwa vile uliingia hekaluni, “mihimili ya mlango ilisonga kwa sauti ya huyo aliyelia, na nyumba ikajaa moshi” (Isa. 6:1, 4), kwa hivyo ni kiti cha enzi cha kusafiri, ilhali cha Ufunuo 4, kilicho na “bahari ya kioo” mbele yake, na kile cha Ufunuo 22, kilicho na “mto…wa uzima” mbele yake, ni viti vya enzi vilivyotuama. {TN1: 8.2}

Ingawa kile alichokiona Ezekieli ni sawa na kile ambacho Isaya alionyeshwa, hata hivyo ni viti vya enzi mbalimbali na tofauti, maana kila mmoja wa “maserafi” wa maono ya Isaya anayo mabawa sita, ilhali kila mmoja wa “makerubi” wa maono ya Ezekieli anayo manne tu. Katika cha mwisho, isitoshe, makerubi walisimama chini ya kiti cha enzi, ilhali kwa cha kwanza, walisimama juu yake. Kwa kumbukumbu, kwa hivyo, vipo viti vya enzi vinne — viwili vilivyotuama, na viwili vinavyosafiri. {TN1: 8.3}

8

Ili kubainisha eneo la kiti cha enzi cha Ufunuo 4, na kile cha Ufunuo 22, twaona tuanze na cha mwisho, kile ambacho “mto…wa uzima” hutokea, ni, anasema Waufunuo, “kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo” — ambacho Kristo aliketi juu yake mkono wa kulia wa Mungu baada ya kufufuka Kwake. Cha kwanza, kilicho na bahari ya kioo mbele yake, ni (pia kulingana na mtazamo wa Yohana) katika patakatifu mno pa hekalu la mbinguni, maana Yohana aliona mbele yake “taa saba za moto” (Ufu. 4:5) — kiambatanisho cha hekalu. “Vile katika maono mtume Yohana alipewa kuona hekalu la Mungu mbinguni aliona pale ‘taa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi.’” — Pambano Kuu, uk. 414. {TN1: 9.1}

Kisha, kuwahusu Baba na Mwana wakihama kutoka kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo — kile ambacho mto wa uzima upo — hadi kwenye kiti cha enzi ambapo bahari ya kioo ipo, tunasoma: “Nalimuona Baba akiinuka kutoka kwa kiti cha enzi, na kwa gari la moto aliingia patakatifu pa patakatifu ndani ya pazia, na kuketi. Kisha Yesu akainuka kutoka kwenye kiti cha enzi,… Kisha kwa gari la mawingu, na magurudumu kama mwako wa moto, likizungukwa na malaika, likaja alipokuwa Yesu. Aliingia ndani ya gari na akapelekwa patakatifu mno, pale Baba aliketi” — Maandishi ya Awali, uk. 55. {TN1: 9.2}

Akinakili tukio lilo hilo kama alivyoliona, Danieli anasema: “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi;

9

mavazi Yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa Chake kama sufu safi; kiti Chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Danieli 7:9, 10. {TN1: 9.3}

Nia yetu kubwa, hata hivyo, kwa hatua hii, ni kujua eneo na kazi ya kiti cha enzi ambacho Ezekieli aliona, na kukihusu anasema: “… Nikaona, na tazama, upepo wa kisulisuli ulitoka upande wa kaskazini” Ezek. 1:4. Ukweli kwamba “upepo wa kisulisuli,” uliokifunika kiti cha enzi, “ulikuja,” asema Ezekieli, unaonyesha kwamba kiti hiki cha enzi, kama kile cha Isaya 6, ni cha kusafiri, na ya kwamba kilikuja kwenye kingo za mto Kebari. {TN1: 10.1}

“Huyu ndiye kiumbe hai,” Ezekieli anaendelea kusema, niliyemwona chini ya Mungu wa Israeli [Ambaye yuko “ juu ya makerubi] karibu na mto Kebari; nikajua kwamba wao ni makerubi.” “Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu.” Ezek. 10:20, 19. {TN1: 10.2}

Gari lilipokuwa likipanda “kutoka kwa nchi” linaonyesha kwamba katika haswa kiti hiki cha enzi, Mungu huizuru dunia na kisha, wakati kazi Yake imekamilika, hurudi mbinguni, kwa kawaida, tumaini letu kuu ni kujua jibu kwa swali,

10

Lini Maono Haya Ya Unabii Yatatimizwa? {TN1: 10.3}

Kwa mujibu wa Ezekieli 2:3; 3:1, 4, 5, 7, nabii alipaswa kuutangaza ujumbe wake kwa “nyumba ya Israeli” yote (neno “nyumba ya Israeli,” linamaanisha kabila kumi na mbili au kabila kumi tu jinsi jambo linavyoweza kuwa). Bado hakuelewa maana ya maono. Angeelewa, angaliweza kuyafafanua, badala ya kutangaza: “Ndipo nikawafikia watu waliohamishwa, huko Tel-abibu, waliokuwa wakikaa karibu na mto Kebari, nikakaa huko walikokuwa wakikaa; nikaishi huko kati yao muda wa siku saba, katika hali ya mshangao mwingi.” Ezek. 3:15. {TN1: 11.1}

Kwa sababu kwa wakati wa maono, nyumba ya Yuda, ufalme wa kabila mbili, ulikuwa mateka katika nchi ya Wakaldayo, na nyumba ya Israeli, ufalme wa kabila kumi, ulikuwa umefurushwa kati ya mataifa ambako walikuwa wamepelekwa na kutawanywa miaka kadhaa kabla (2 Wafalme 17:6), haukuwapo uwezekano wa Ezekieli kuwapelekea ujumbe. Na kwa vile ni wa nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda (Ezek. 9: 9), — kabila kumi na mbili, — kwa hivyo ulikuwa unabii katika wakati wa Ezekieli. {TN1: 11.2}

Taifa la Wayahudi, isitoshe, hadi wakati wa Kristo, hawakuwa na nuru kwa unabii huu, na ulionekana kuwa mgumu kueleweka, na hata usiokuwa salama kwa akili ya kawaida kuusoma. “Sura hii yote ilionekana haungefafanuliwa na uliojaa mafumbo, kwa Waebrania wa kale, kwamba, tunavyojifunza

11

kutoka kwa Mtakatifu Jerome (Ep. ad Paulin.,) hawakumruhusu yeyote kusoma kabla ya kuwa na umri wa miaka thelathini. “Toleo la Douay, tini wayo kwa Ezekieli 1:5. Na pasipo kuona nuru katika maandiko haya mpaka sasa, Kanisa la Kikristo limefanya jaribio dogo au hakuna kuufafanua. {TN1: 11.3}

Na hatimaye kwa sababu hakuna mchinjo kama huo ulioelezwa katika Ezekieli 9 umewahi kutukia, utimizo wake ni wazi wa baadaye. {TN1: 12.1}

Wazi kabisa, kwa hivyo, maono yalikuwa unabii wakati wa Ezekieli, na yamekuwa unabii tangu wakati huo. Na iwapo yatawahi kutimizwa, na kutosalia maandishi yasiyofaa na yasiyofaidi, — kitu ambacho Mungu hajaumba, — basi siri yake lazima, bila shaka, sasa ifunuliwe, na hatua yake itekelezwe hivi karibuni. {TN1: 12.2}

Katika nuru safi ya ukweli huu, sura ya tisa inaonekana kushikilia kilele cha mandhari ya maono. Akielezea kazi ya kutisha ambayo Bwana atafanya ambapo, pamoja na makerubi, Anaizuru nchi, inaonyesha matokeo ya kuogofya kwa wale wanaoukataa ujumbe Wake: kuzikosa baraka Zake, kuupoteza ufalme! Mauti, uzoefu wa kutisha, utakuwa ni hatima ya wote wanaokataa sasa kuamka na kujua kuihusu, lakini ambao wanachagua afadhali wabaki katika hali ya kutoujua ukweli Wake, na

Kusudi la Bwana kuja Katika Kiti Chake cha Enzi. {TN1: 12.3}

Wakati nabii alipokuwa akitazama upande wa kaskazini, aliona “wingu kubwa” linakuja kama

12

“kisulisuli” kwa dunia. Akiangalia kwa kupendezwa sana kujongea kwake karibu na karibu, hatimaye aliona “viumbe hai,” “magurudumu,” na vingine vyote, — “umbo la mfano wa utukufu wa Bwana.” Ndipo, “nikaanguka” anasema, “juu ya uso wangu, na nikasikia sauti ya yule aliyesema [bila shaka Bwana Mwenyewe alipokuja kumpa Ezekieli ujumbe].” {TN1: 12.4}

“ … Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi Mimi; wao na baba zao wamekosa juu Yangu, naam, hata hivi leo. Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao. Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.” Ezek. 1:28; 2:3-6. {TN1: 13.1}

“Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno Yangu. Maana wewe hukutumwa kwa watu wa maneno mageni, ama wa lugha ngumu,….ambao maneno yao huwezi kuelewa.” Ezek. 3:4-6. {TN1: 13.2}

13

Maneno haya ya amri (yenye maana nzito kwa wote) hufunua kwamba ujumbe ambao nabii alipokea ni kwa ajili ya watu wa Mungu tu, na kwa hivyo, kwa upanuzi wa busara, maono yote, ambapo haya ni sehemu, yanapata kutimizwa kwa wakati mmoja ambao Bwana anatuma onyo kwamba kwa sababu kanisa Lake liko katika hali ya chini sana kiroho, — “wakaidi na wenye vipaji vigumu” na “nyumba ya kuasi,” — Yeye atafanya ndani yake kazi ya kutia alama na kuchinja. Na katika Biblia yote itapatikana katika kanisa moja hali na tabia, chanzo, wakati, na tokeo kujibu lile la unabii, na hilo ni katika

Kanisa la Laodekia. {TN1: 14.1}

Kemeo la Ufu. 3:14-18 dhidi ya Walaodekia, na kemeo la Ezek. 2:1-7 na 3:4-7 dhidi ya “nyumba ya Israeli,” zikiwa ni sawa, kila moja kwa sababu hii ni kitimizo cha kingine: kimoja ni Ufunuo wa kile kingine ambacho ni unabii. {TN1: 14.2}

Zote hutetea onyo la Roho ya Unabii kwamba hakuna “udanganyifu mkubwa ulioje unaoweza kuja juu ya akili za wanadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, wakati ambapo wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha [badala ya hali bora], hata sasa ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ambapo wale wanaohutubiwa hujidanganya

14

kwamba wako katika hali ya juu ya kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umasikini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayesema, na ushuhuda wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {TN1: 14.3}

Kwa sababu Bwana husema kwamba “maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi. (Ezek 3:7), basi, hakika, kila mmoja anayetaka kuokolewa, “aazimie kujua” ubaya “wa” kesi “yake (Shuhuda , Gombo la 1, uk. 163), na

Wakati wa Hali ya Chini Kiroho ya Kanisa. {TN1: 15.1}

Watu wa Mungu wangeendelea kuwa waliojidanganya, “wakaidi na wenye mioyo migumu,” na hali ya kiroho ya kanisa iendelee kudidimia, basi pamoja na kanisa kama hilo Bwana hangeweza kumaliza kazi Yake duniani, na muda wa rehema lazima mwishowe ufungwe kwa ulimwengu katika giza nene, bila kuwa na watakatifu walio hai wa kuhamishwa bila kufa wakati kwa kuonekana kwa Kristo. {TN1: 15.2}

“Bwana hatendi kazi sasa,” inasema Roho ya Unabii, “kuzileta nafsi nyingi katika ukweli, kwa sababu ya washiriki wa kanisa ambao hawajawahi kuongoka, na wale waliokuwa wameongoka lakini wakakengeuka. Ni mvuto gani hawa washiriki wasiomcha mungu watakuwa nao

15

kwa waongofu wapya? Je, hawataufanya usiokuwa na maana ujumbe aliopeana Mungu ambao watu Wake watatangaza?” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 371. {TN1: 15.3}

Kufikia hadi wakati huu Yeye amekuwa akijizuia kwa sababu ya washiriki ambao hawajaongoka na waliorudi nyuma katika kanisa, Yeye atafanya nini sasa wakati, jinsi Anavyosema, “nyumba yote ya Israeli ni wakaidi na wenye vipaji vigumu”? Ukweli hasa kwamba Yeye anajizuia, ni ushahidi wa kutisha kwamba lazima Yeye afanye kazi maalum kwa kanisa kabla limalize kazi Yake duniani. {TN1: 16.1}

Uso kwa uso uhakika huu mzito, kila mmoja, kwa hivyo, ambaye anatafuta “urithi wa huko juu,” atadumisha uadilifu kamili na uwazi wa akili anapojifunza kuihusu kazi maalum inayohusika, asije kwa maradhi yake ya Ulaodekia, asipate

Tiba: {TN1: 16.2}

“…Wakati hukumu ya upelelezi inaendelea mbinguni,…itakuwapo kazi maalum ya utakaso, ya kuondoa dhambi, miongoni mwa watu wa Mungu duniani… Kisha kanisa ambalo Bwana wetu wakati wa kuja Kwake kulipokea Mwenyewe litakuwa ‘kanisa tukufu, lisilo na waa, au kunyanzi, au kitu kingine chochote.’ Kisha litaonekana kama asubuhi, zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango.” “Likiwa limefunikwa katika silaha za haki ya Kristo, kanisa linaingia kwenye pambano lake la mwisho …. litakwenda mbele katika

16

dunia yote, likishinda na kushinda.” — Pambano Kuu, uk. 425; Manabii na Wafalme, uk. 725. {TN1: 16.3}

Tia alama maneno yaliyo kwa italiki : “lisilo na waa,” “pambano lake la mwisho,” “linakwenda katika dunia yote, likishinda na kushinda.” Maneno haya yanasisitiza kanisa safi na la kushinda vita, lililo kamilifu kwa “kazi maalum ya utakaso” ambayo lazima ifanyike kabla kazi ya injili ikamilike katika sehemu yoyote ya dunia. {TN1: 17.1}

Kuonyesha uhodari wa kanisa kwa kazi kubwa ambayo limekabidhiwa, Uvuvio unendelea: “Miujiza mikubwa ilifanywa wagonjwa waliponywa, na ishara na maajabu yaliwafuata waminio.” — Maandishi ya Awali, uk. 278. {TN1: 17.2}

Kwa kuwa kazi hizi za nguvu zinafanyika wakati wa “Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu,” utakaso, kwa hivyo, bila kupingwa unatukia mwanzoni mwa “Kilio Kikuu.” Na kutokana na hili unafuata kama umuhimu wa busara kwamba unabii wa Ezekieli wa kutia alama na kuchinja lazima uwe na tangazo la utakaso wa kanisa. {TN1: 17.3}

Akiendelea kuona katika maono makerubi na utukufu wa kiti cha enzi cha Mungu, nabii alimwona Bwana akija penye kizingiti cha nyumba (kanisa), na jinsi Alivyomwagiza malaika Wake aliyekuwa “amevaa kitani” na “ambaye alikuwa na kidatu cha wino wa mwandishi kiunoni mwake,” Ezekieli alimsikia akimwamuru mtu huyo: “Pita kati ya mji,

17

kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. {TN1: 17.4}

“Na hao wengine Aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. {TN1: 18.1}

“Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu Yako juu ya Yerusalemu? Ndipo Akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni.” Ezek. 9:3-9. {TN1: 18.2}

Akifunua utengo kamili wa waovu kutoka miongoni mwa wenye haki, aya hizi, kwa hivyo, kiunabii zinaonya kimbele juu ya utakaso ulio karibu wa kanisa — wokovu wake wa pekee. Na ukifanyika katika “mji,” “Yerusalemu,” “Israeli,” na “Yuda,”

18

— majina ambayo hapana kitu kwa ulimwengu ambacho kinaweza kuitwa maana yanawahusu watu wa Mungu kanisa, — kazi hii ya mtengo ni, vivyo hivyo, yenye mipaka kwa kanisa. {TN1: 18.3}

Ukweli, zaidi ya hayo, kwamba waovu wanaondolewa miongoni mwa wenye haki, pia inaonyesha kwamba utengo huo hauwezi kuwa ulimwenguni. Kama ungalikuwa, ungefanyika kwa njia tofauti — wenye haki kuondolewa miongoni mwa waovu. {TN1: 19.1}

Kumbuka kwamba Bwana alimwambia Ezekieli: “Mwanadamu, Nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa taifa asi, walioniasi Mimi; wao na baba zao wamekosa juu Yangu, naam, hata hivi leo.” “Maana wewe hukutumwa kwa watu wa maneno mageni, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli.” (Ezek 2: 3; 3: 5) — utume ambao utasababisha

Kutiwa Muhuri Watu 144,000 — Malimbuko. {TN1: 19.2}

“Malaika huyu mwenye nguvu,” inasema Roho ya Unabii, “ana mkononi mwake muhuri wa Mungu aliye hai, au wa Yeye pekee anayeweza kupeana uzima, ambaye anaweza kutia kwenye vipaji alama….” {TN1: 19.3}

“Huku kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu ni sawa na kule alionyeshwa Ezekieli katika maono. Yohana pia alikuwa shahidi wa ufunuo huu wa kushangaza sana.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 444, 445. {TN1: 19.4}

Kutiwa muhuri (Ufu. 7) ni sawa na kutiwa alama (Ezek. 9), — “utakaso,”

19

— sisi hivi tunapewa mitazamo miwili ya “kazi ya kufunga kwa kanisa,…wakati wa kutiwa muhuri kwa watu mia na arobaini na nne elfu ambao watasimama bila mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu…. Wao huhisi kwa undani makosa ya watu wanaojidai kuwa ni wa Mungu. Hili kwa mkazo limesisitizwa na mfano wa nabii kwa kazi ya mwisho chini ya kielelezo cha watu kila mmoja aliye na silaha ya kufisha mkononi mwake. Mtu mmoja kati yao alikuwa amevaa kitani, akiwa na kidatu cha mwandishi kiunoni mwake.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266. {TN1: 19.5}

Kwa sababu utakaso, au kutiwa muhuri, kulikuja mwanzoni mwa “Kilio Kikuu,” jinsi tumekwisha ona tayari, watu 144,000 basi ni “malimbuko” — wa kwanza kutiwa muhuri; ambapo wale wametiwa muhuri baada ya utakaso wa kanisa, ni mavuno ya pili, ambao Yohana (baada ya kuwaona 144,000 waliotiwa muhuri) anasema: “Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7:9. {TN1: 20.1}

Kwa hivyo ukweli kwamba upo ukusanywaji ndani mavuno mawili, kunaonyesha kwamba kutiwa alama au kutiwa muhuri ni katika sehemu mbili — vipindi viwili — na ya kwamba ziko

Ripoti Mbili za Kutiwa Muhuri. {TN1: 20.2}

“Na tazama,” asema Ezekieli, “mtu aliyevaa kitani, ambaye alikuwa na kidau cha wino

20

kiunoni mwake, aliripoti kazi hiyo [akiwa bado duniani] akisema, Nimefanya jinsi Ulivyoniamuru.” Ezek. 9:11. Hapa ipo ripoti ya kwanza, iliyotolewa alipokamilisha kutia muhuri kanisani — kuwatia muhuri malimbuko, watu 144,000. {TN1: 20.3}

“Naliona,” anasema mtumishi wa Bwana, “…malaika mwenye kidatu cha mwandishi kiunoni mwake akarudi kutoka duniani, na akaripoti kwa Yesu kwamba kazi yake alikuwa ameikamilisha, na watakatifu walikuwa wamehesabiwa na kutiwa muhuri.” — Maandishi ya Awali, uk. 279. Hapa ni ripoti yake ya pili, aliyoitoa alipokamilisha kutia muhuri duniani — kuwatia muhuri mavuno ya pili, umati mkubwa. {TN1: 21.1}

Kulinganisha ripoti zote mbili, kila moja inaonekana kuwa wa tukio tofauti: Katika ripoti ya kwanza, Bwana alikuwa juu ya “kizingiti cha nyumba” duniani (Ezek. 9:3); kwa ya pili, Alikuwa katika hekalu la mbinguni. {TN1: 21.2}

Baada ya malaika kufanya ripoti yake ya kwanza, Bwana akamwamuru: “Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi, ukayamwage juu ya mji. Akaingia ndani mbele ya macho yangu.” Ezek. 10:2. {TN1: 21.3}

Lakini baada ya ripoti yake ya pili, “….jeshi lote la malaika waliweka taji zao wakati Yesu alipofanya tamko zito, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki;

21

na mtakatifu na azidi kutakaswa.” — Maandishi ya Awali, uk. 279, 280. {TN1: 21.4}

Iwapomuda wa rehema ungefungwa wakati wa ripoti ya kwanza (Ezek. 9:11), Bwana lazima, kwa mujibu wa taarifa iliyotangulia, angekuwa mbinguni, kisha ashuke duniani ili kuwapokea watakatifu Wake, badala ya kuwa tayari duniani, kisha kupanda hadi katika kiti Chake cha enzi, jinsi ambavyo Yeye hufanya, bila watakatifu Wake (Ezek. 10:19). {TN1: 22.1}

Tena: nabii akiwa ameachwa nyuma wakati Bwana alipokwenda juu, kimfano huonyesha kwamba katika huku kushuka na kupanda maalum, watakatifu hawapelekwi mbinguni, ila tu kuwekwa huru kutoka kwa dhambi na wadhambi — kufanywa wafae kwa kazi ya mwisho. {TN1: 22.2}

Kwa ripoti ya pili ya malaika, hata hivyo, Yesu akiwa mbinguni, “aliondoka patakatifu mno” (Maandishi ya awali, uk. 280) kushuka duniani. {TN1: 22.3}

Ulinganifu huu mfupi unaleta katika mtazamo wa msingi ukweli maradufu kwamba wakati wa ripoti ya kwanza, Yesu aliingia hekaluni, wakati wa ripoti ya pili, Aliondoka humo. {TN1: 22.4}

Zaidi ya malaika kutoa taarifa ya kutia muhuri na kuchinja kanisani Ezekieli hakuonyeshwa. Bali Isaya alionyeshwa. Aliwaona

Waliookoka Wanakwenda Kwa Mataifa Yote. {TN1: 22.5}

“Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili,” asema

22

nabii wa injili, “kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi…. Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa,….visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote….mpaka mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:16, 19, 20. {TN1: 22.6}

Kwa sababu “wale waliookoka” mchinjo (watu 144,000) “watawaleta ndugu zenu wote [wote watakaookolewa katika ‘Kilio Kikuu’]…ndani ya nyumba ya Bwana,” kisha inafuata kwamba wale waliookoka ndio wanaomaliza kazi — kwa sababu wanaitwa “watumwa wa Mungu.” Ufu. 7:3. {TN1: 23.1}

Ujumbe, zaidi ya hayo, kwa kuwa umewapata kanisani, si katika ulimwengu, kwa hivyo ni “bikira;” yaani, “hawajatiwa unajisi na wanawake” (Ufu. 14:4) — makanisa ya ulimwengu. Na hawana uongo vinywani mwao, wakiwa wameviweka mbali na

Kulaumu na Kutafuta Makosa. {TN1: 23.2}

“Watahoji na kulaumu kila kitu” inasema Roho ya Unabii ikionya kuhusu utakaso, “ambacho huinuka ukweli unapokunjua, kulaumu kazi na msimamo wa wengine, kulaumu

23

kila tawi la kazi ambalo hawana sehemu. Watajilisha makosa na mapungufu ya wengine, ‘mpaka,’ akasema yule malaika, ‘Bwana Yesu atainuka kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, na kujivika mavazi ya kisasi, na kuwashangaza katika karamu yao isiyotakatifu; na watajikuta hawajajiandaa kwa ajili ya karamu ya jioni ya Mwana-Kondoo.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690. {TN1: 23.3}

Maneno haya ya mazito, kila mmoja ayaweke vyema moyoni, na yeyote asiache adui kumdanganya “kwa maneno na hotuba nzuri” kuhusu swala hili la uhai na kifo. Kaza akilini mwako ukweli kwamba kuinuka kwa Kristo “kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho” hakuwezi kuwa baada ya muda wa rehema kufungwa, maana, kumbuka kwa uangalifu, “ Atainuka” wakati ambapo “ukweli unafunuliwa.” {TN1: 24.1}

Kila mmoja achukue tahadhari kwamba asianguke kwa kuhukumu ujumbe au wajumbe, bali afadhali “augue na kulia,” jinsi Bwana anavyoamuru, “dhidi ya machukizo yote yanayofanyika kati yake [kanisa],” asije akapatikana akiwa upande mbaya akitembea na watenda maovu, na hivyo kuangamizwa kwa kuanguka chini ya silaha za kuchinja za malaika. {TN1: 24.2}

“Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu Wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. Chukua msimamo, Ndugu, Dada, upande wa kulia, na hakikisha, “baada ya kufanya yote,

24

kusimama, “kwa kuwa, hakuna kuukwepa ukweli, Bwana ameukaza mkono Wake kuwatenga “waovu kutoka kati ya wenye haki” kama inavyoonekana zaidi

Katika Nuru ya Mifano. {TN1: 24.3}

“Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi…. Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 22:11, 13. {TN1: 25.1}

Huku kupeleleza na kutupa nje kutafanyika kabla ya kufungwa kwa kipindi cha rehema, kwa sababu sherehe ya ndoa ilikuwa haijafanyika wakati “mfalme aliingia ndani ili kuwaona wageni.” {TN1: 25.2}

“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 13:47-50. {TN1: 25.3}

Katika maandiko haya, pia, unaonekana utakaso wa kanisa, maana wabaya wanaondolewa kati ya wazuri, na si wazuri kutoka kati ya wabaya, yaani,

25

wabaya walio katika juya (kanisa) wanatupwa nje, na wazuri kuhifadhiwa. {TN1: 25.4}

Juya hili huwakilisha kazi ya injili hadi wakati wa utakaso wa kanisa, kwa maana baada ya kanisa kutakaswa, wa namna hii tu ambao “wanapaswa kuokolewa” watapewa ushirika: “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Isa. 52:1. {TN1: 26.1}

Kamsa hii ya kuamsha lazima ivume kabla kufungwa kwa muda wa rehema, kwa maana haitatenda kwa manufaa baadaye, hakika itakuwa tu dhihaka. Wala haitafaa wakati wa “Kilio Kikuu,” kwa maana wakati huo kanisa halitakuwa linalala na bila “mavazi ya uzuri:” “Ni wale tu,” inathibitisha Roho ya Unabii, “ambao wameshindana na kuyashinda majaribu kwa uwezo Wake Mwenye Nguvu wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza ujumbe huu wakati utakapokuwa umeumuka katika Kilio Kikuu. “ — Mapitio na Kutangaza, Nov. 19, 1908. “Na katika siku hiyo hapatakuwa na Mkanaani tena katika nyumba ya Bwana wa majeshi.” Zek. 14:21. {TN1: 26.2}

“Mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.” Isa. 62:2. “Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku;

26

Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.” Isaya 60:11. {TN1: 26.3}

Katika utakaso wa kanisa, “malaika … watawatenga waovu kutoka kwa wenye haki” (Mat. 13:49), ila katika wakati wa “Kilio Kikuu,” watawakusanya wenye haki kutoka kati ya waovu. Hivyo imeandikwa: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake…. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18:1, 4. {TN1: 27.1}

Mitengo hii miwili tofauti, kila mmoja kwa wakati tofauti, inatukia wakati (kwa kujumlisha ukweli hasa), katika muda wa malimbuko, waovu wanaondolewa kati ya wenye haki kanisani (juya), na katika wakati wa, mavuno ya pili, wenye haki wanachukuliwa kutoka kati ya waovu Babeli. Na kanisa la namna hii — safi kabisa — hudokeza kimbele kabisa

Ujumbe Safi. {TN1: 27.2}

Unabii wa Ezekieli ukijifunua wenyewe kuwa ni ujumbe kwa kanisa leo, nabii, mwenyewe, lazima kwa hitaji, hatimaye, awawakilishe wajumbe watakaoupeleka ujumbe kwa kanisa kwa wakati uliowekwa. Na kwa kuitikia amri ya Bwana, “usiwe

27

wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.” (Ezek. 2:8; 3:3), inaonyesha kwamba wajumbe humtii Bwana na hulipenda Neno Lake zaidi ya kila kitu. {TN1: 27.3}

“Nami,” alisema Bwana “nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu,.. Lakini hapo Nitakaposema nawe, Nitafumbua kinywa chako, nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. Yeye asikiaye na asikie; naye akataaye na akatae; maana wao ni nyumba yenye kuasi.” Ezek. 3:26, 27. {TN1: 28.1}

Tangazo hili zuri la Bwana, Mwenyewe, linaonyesha kwamba ujumbe usitiwe unajisi — ukweli safi, ushahidi kamili dhidi ya uchafuzi wa maneno ya mtu. Wajumbe, wakiwa wamefanywa bubu, wanaweza kusema tu wakati Anapofungua vinywa vyao, na lile Analoweka tu katika vinywa vyao — “Bwana MUNGU asema hivi.” Pasipo kujitwalia sifa njema, wao

Watauinua Uvuvio. {TN1: 28.2}

“Mtu akijiona,” asema Mtume Paulo, “kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.” 1 Kor. 14:37. {TN1: 28.3}

Mungu anapoongea kupitia kwa mtu, mtu huyo, kama kipaza sauti Chake, lazima akiri ukweli, asije akapatwa na hatima sawa na

28

iliyompata Herode, ambaye, “Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.” Mdo. 12:21-23. {TN1: 28.4}

Kutoka kwa uzoefu huu wa kutisha, ulioandikwa kuwa onyo kwetu, na kutoka kwa ukweli mwingine mzito ulioletwa mbele humu, tunaona wazi kwamba ili Bwana awatayarishe watumwa Wake kwaajili ya muhuri Yeye anaweka mbele kila somo muhimu, hata somo lililo katika

Namna Ujumbe Unavyotolewa. {TN1: 29.1}

Msomaji atatambua kwamba, ingawa nabii aliagizwa kwenda kuwaambia watu wake, lakini badala ya kuambiwa la kusema, aliamriwa: “funua kinywa chako, ule Nikupacho. Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake…. Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, Naye akanilisha lile gombo.” Ezek. 2:8, 9; 3:1, 2. {TN1: 29.2}

Kwa sababu maneno ambayo Ezekieli alipaswa kuwaambia watu wake yalipatikana katika kitabu alichokula, kile “kitabu” hakiwezi kuwa kingine isipokuwa

29

Biblia, ambamo hutoka ujumbe unaofikia upeo wa

Furaha, Kuomboleza, na Ole. {TN1: 29.3}

“Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake. Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!” (Ezek. 2:9, 10) — hali ya kuogofya ya andiko linaloonyesha mchinjo katika Ezekieli 9, na ole zilizotangazwa katika mifano ya Mwalimu: “bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” “Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 24:50, 51; 22:13. {TN1: 30.1}

Na zamani kupitia mtumishi Wake Musa, aliwaambia watu Wake: “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo Yake yote na amri Zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.” Kumb. 28:15. “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako.” Kumb. 30:19. {TN1: 30.2}

30

“Kitabu” ambacho Ezekieli alikula kilikuwa “kimeandikwa ndani na nje” (Ezek. 2:10), andiko “ndani,” kwa hivyo, linaweza kuwa Neno la Mungu la kinabii, likitangaza laana na baraka zilizoandikwa katika Biblia; ilhali andiko “nje,” haliwezi kuwa kitu chochote ila kumbukumbu imara ya utimilifu wa hayo ya ndani– ile kumbu kumbu, kwa ufupi, ya unabii kuwa historia; kuonyesha hivyo kwamba Mungu amelisema na atalitekeleza. {TN1: 31.1}

Andiko “ndani na nje,” isitoshe, huashiria pia kwamba ujumbe utakuwa katika mfano na uakisi. {TN1: 31.2}

Ezekieli alipokila kile “kitabu,” kilikuwa, jinsi pia itakavyofahamika, kinywani mwake “kama asali kwa utamu,” wala si “kichungu” katika “tumbo” lake, kama vile Yohana alivyokula (Ufu. 10:10). Ingawa, kwa hivyo, jinsi Neno linavyoonyesha, hakutakuwapo kuvunjika moyo na ujumbe huu, jinsi ilivyokuwa kwa ule wa mwaka wa 1844 B.K., bado, kwa huzuni, unatangaza kwamba kwa onyo lake, watu ambao onyo umetumwa kwao

Wataziba Masikio Yao na Kufunga Milango Yao. {TN1: 31.3}

“Bali nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe; kwa kuwa hawanisikilizi Mimi; maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi.” Ezek. 3:7. “Lakini wewe, mwanadamu, tazama, watakutia pingu, nao watakufunga kwazo, wala hutakwenda nje kati yao:….

31

kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi.” Ezek.3:25, 26. {TN1: 31.4}

“Katika kazi ya mwisho ya uchaji,” inatabiri Roho ya Unabii kwa mtazamo sawa, “watu wakuu wachache watahusishwa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. “…hawataitambua kazi ya Mungu wakati kilio kikuu cha malaika wa tatu kitakaposikika. Wakati nuru itakapotokea kuangaza nchi, badala ya kuja kwa msaada wa Bwana, watataka kuifunga-funga kazi Yake ili kukidhi mawazo yao finyu…. Watakuwapo miongoni mwetu wale ambao siku zote watataka kuithibiti kazi ya Mungu, hata kuamuru ni harakati gani zitafanywa wakati kazi inaendelea mbele chini ya uongozi wa malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. Kwa hivyo swali:

Ujumbe Huo Utawafikiaje Watu? {TN1: 32.1}

Kwa sababu ya wao kukataa kusikia, “Mungu atatumia njia na mbinu,” inajibu Roho ya Unabii, “ambayo itaonekana kwamba Anachukua mamlaka mikononi Mwake. Watendakazi watashangaa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kutimiza na kukamilisha kazi Yake ya haki.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {TN1: 32.2}

“Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji si waaminifu Yeye atalichunga kundi Mwenyewe…. Katika wakati huu, dhahabu itatenganishwa kutoka kwa takataka

32

kanisani. Uungu wa kweli utabainishwa wazi kutoka kwa mfano wa kumetameta kwake. Wengi kama nyota ambao tumewatamani kwa mng’ao wake, watajitokeza nje ya giza…. Wale ambao wamekuwa waoga na wasiojiamini, watajitangaza wazi kwa ajili ya Kristo na ukweli Wake. Wale dhaifu sana na wenye kusitasita kanisani watakuwa kama Daudi — tayari kutenda na kuthubutu” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, 81) — kweli ambazo, pamoja na zile zinazofuata, zinaonyesha kwamba

Hakuna Kinachoweza Kumzuia Bwana. {TN1: 32.3}

Kutupia jicho picha ya jalada msomaji ataona kwamba “mabawa mawili ya kila mmoja” wa viumbe hai “yaliunganishwa moja kwa lingine.” Ezek. 1:11. Wote na magurudumu kwa hivyo, kila mmoja aliunda mraba: “gurudumu moja na kerubi mmoja, na gurudumu lingine na kerubi mwingine.” Ezek. 10:9. {TN1: 33.1}

Jinsi Ezekieli alivyoona wale viumbe wakijongea, aliona kwamba walikuwa na “uso wa mwanadamu” mbele, “uso wa tai” nyuma, “uso wa simba upande wa kuume,” na “uso” wa ng’ombe upande wa kushoto” (Ezek. 1:10) kwa maana wote wanne walikuwa na “pande nne” (Ezek. 1:8); pia ya kwamba walikuwa na mabawa, “mawili…upande huu, na…mawili…upande ule” (Ezek. 1:23). Aliyaona magurudumu hai, zaidi ya hayo yalipangwa hivi kwamba “walienda kwa pande zao nne.” Ezek. 1:17. (Tazama ukurasa wa jalada.) {TN1: 33.2}

Njozi ya pande nne za viumbe hai pamoja na mizunguko minne

33

ya magurudumu, inawezesha kwenda pembe nne — mbele au nyuma, kulia au kushoto: viumbe hai “hawakugeuka walipokuwa wakienda.” Ezek. 10:11. {TN1: 33.3}

“Na miguu yao” ilivyokuwa “ya kunyooka” (Ezek. 1:7), iliwawezesha kwenda kwa uhuru uelekeo wowote bila kugeuka, ili kwamba “waende na kurudi kwa kasi kama kunavyoonekana kumulika kwa umeme” (Ezek. 1:14). “Na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao” (Ezek. 10:19), “na mfano wa mikono ya mwanadamu ulikuwa chini ya mabawa yao.” Ezek. 10:21. {TN1: 34.1}

Kwa sababu haya magurudumu, yalivyofanya mraba “kwenda na kurudi kwa kasi,” na maadamu “juu yao,” Mungu alikuwa ameketi juu ya kiti Chake cha enzi, ni dhahiri kwamba huu mtambo hai wa ajabu ni gari la Mungu — gari Lake ambalo Yeye ametumia kuja kuuleta ujumbe kuwatenganisha “waovu kutoka kati ya wenye haki.” Hivyo umefanywa hai uadhimisho kwamba kwa maana “vita ni vya Bwana,” hakika “Atalichunga kundi Mwenyewe.” {TN1: 34.2}

“Kwa sababu mizunguko yenye kukanganya ya magurudumu ilikuwa chini ya uongozi wa mkono uliokuwa chini ya mabawa ya makerubi, hivyo michezo ya kutatanisha ya matukio ya kibinadamu i chini ya uthibiti wa Mungu. Katikati ya ushindani na machafuko ya mataifa, Yeye aliyeketi juu ya makerubi bado huelekeza mambo ya dunia hii. {TN1: 34.3}

“Historia ya mataifa hutuzungumzia leo. Kwa kila taifa na kwa kila mtu

34

Mungu amegawa nafasi katika mpango Wake mkuu. Leo watu na mataifa yanapimwa kwa timazi iliyo mkononi Mwake Yeye ambaye daima hafanyi kosa. Wote ni kwa uchaguzi wao wenyewe wanaamua hatima yao, na Mungu huyatangua yote kwa ajili ya kuyafanikisha makusudi Yake.” — Manabii na Wafalme, uk. 536. {TN1: 34.4}

“Katika maono ya Ezekieli, Mungu mkono Wake ulikuwa chini ya mabawa ya makerubi. Hili ni la kuwafundisha watumwa Wake kwamba ni uwezo wa Mungu unaowapatia mafanikio. Yeye atafanya kazi nao iwapo watauweka mbali uovu, na kuwa wasafi katika mioyo na maisha. {TN1: 35.1}

“Nuru yenye kung’aa ambayo hupita kati ya viumbe hai kwa kasi ya umeme huwakilisha kasi ambayo kazi hii hatimaye itaendelea mbele hadi kukamilika” kwa niaba ya watu Wake wakati wa saa ya Hukumu (Shuhuda, Gombo la 5 uk. 754): maana nyuso za viumbe hai ni

Mfano wa Watakatifu katika Wakati wa Hukumu. {TN1: 35.2}

Nyuso za makerubi zilivyo sawa na zile za wanyama wa Ufunuo, zote lazima zina maana muhimu ya kutimiza kwa kidokezi ambacho Yohana anatoa: “Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili Wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa Ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu Yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa.” Ufu. 5:9. {TN1: 35.3}

35

Ukweli haswa kwamba wanyama hawa wamekombolewa kwa damu ya Kristo na watatawala kwa dunia, unaonyesha kwamba wao ni mfano wa watakatifu, jinsi wanyama wa Danieli ni mifano ya mataifa. Kwa hivyo, lazima nyuso za makerubi, kama ilivyo kwa nyuso za wanyama wanaosimama mbele ya kiti cha enzi cha Hukumu, ni mfano wa watakatifu katika wakati wa Hukumu. {TN1: 36.1}

Bwana akiwa “juu yao [makerubi] juu,” ni ishara kwamba hili ni gari lililo hai ambalo Yeye, Mwokozi wao, baadaye atatumia kuwahamisha bila kufa watakatifu. {TN1: 36.2}

Na “kwa kila upande wa lile gari la mawingu,” inaunga mkono Roho ya Unabii, “kulikuwa na mabawa, na chini yake yalikuwa magurudumu hai; na vile gari lilifingirisha kwenda juu, magurudumu yalilia, ‘Mtakatifu,’ na mabawa, yalivyosogeza, yalilia, ‘Mtakatifu,’ na msafara wa malaika watakatifu kulizunguka lile wingu, wakalia, ‘Mtakatifu mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mwenyezi Mungu!’ na watakatifu katika wingu wakalia ‘Utukufu! Alleluya!’” — Maandishi ya Awali, uk. 287. {TN1: 36.3}

Ya kwamba saa ya furaha kwa wote inajongea tutakapopanda katika gari hili la utukufu sana, hivyo inachochea mioyo yetu kama kutufanya kwa haki kupiga mayowe kuuliza:

Je, Gari Hili Litawasili Lini? Je, Litakaa Kwa Muda Gani? {TN1: 36.4}

Yanapochunguzwa katika nuru ya kweli nne kuu zilizo thabiti, maswali haya kwa kweli yanajijibu: (1)

36

Bwana huja juu ya nchi katika gari hili; (2) kutoka ndani yake Anamwamuru Ezekieli aende anene kwa watu Wake; (3) Ezekieli hakupeana ujumbe kwa watu wa siku yake; (4) ataupeleka kwa watu mwanzoni mwa “Kilio Kikuu.” {TN1: 36.5}

Hivi inaonekana kwamba wakati ukiwadia kwamba kanisa limefikia hali iliyoelezwa na Bwana (Ezek. 3-9), siri ya maono litafunuliwa, na ujumbe kupelekwa kwa kanisa. Na ya kwamba kanisa tayari limefikia wakati huu na hali imethibitishwa kikamilifu katika kweli-tatu kwamba sehemu ya kwanza ya “ufunuo huu wa kushangaza sana” (uliopanuliwa humu ndani), ulichapishwa Desemba 1930, katika kitabu cha kurasa 255 kinachoitwa Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1; kwamba sehemu ya pili ilichapishwa mwezi wa Septemba 1932, katika kitabu cha kurasa 304 kinachoitwa Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2; na kwamba sehemu ya tatu — mfululizo wa trakti (ambapo hii ni ya kwanza) ambazo tangu mwaka wa 1933 kwa jumla ni kurasa 898 — zinajumuisha Gombo la 3. {TN1: 37.1}

Ukweli, kwa hivyo, kwamba kutoka kwa lile gari, Bwana humwamuru nabii kwenda kunena, kupeleka ujumbe, kwa watu Wake, na ya kwamba jumla ya ujumbe ni zaidi ya kurasa 1250 za nyaraka zilizochapishwa tangu mwaka wa 1930, zikifunua ukweli wake kutoka kwa pembe tofauti, hufunua kwa uzito kwamba lile gari, ingawa halionekani kwa wanadamu (kama vile kwa “yule kijana” kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto — 2 Wafalme 6:17), tayari limewasili. {TN1: 37.2}

37

Na kwa sababu tayari liko hapa, ni lazima liwe ni chombo cha Mungu atakachotumia kama namna ya kituo cha kazi, ambacho Bwana anatoa maagizo na kuielekeza kazi Yake, na kwa kupitia kwacho atafanya hivyo hadi “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote,…. kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Mat. 24:14. “Mwisho” — ajabu! Kwa wale ambao wanasema “Iko wapi ahadi ile ya kuja Kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.” (2 Pet. 3:4); lakini kwa wale ambao wameutarajia kwa muda mrefu, watasema, “Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie” (Isa. 25:9). — mwisho, wa kuogofya kutisha! unapaswa kuwaelekeza wote ili kuhakiki

Kusudi la Ujumbe. {TN1: 38.1}

“Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana…. Nami, jicho Langu halitaachilia, wala Sitaona huruma.” Ezek. 9:8-10. {TN1: 38.2}

Baada ya wanaougua na kulia kutiwa alama (ambapo isieleweke kwamba inakamilishwa katika ukamilifu wake kote ulimwenguni kabla ya kuchinja kufuata popote), mchinjo kukamilishwa, na swala hilo

38

kuripotiwa, Bwana “Naye akamwambia mtu yule aliyevaa bafta, akasema, Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi, ukayamwage juu ya mji.” Ezek. 10: 2. {TN1: 38.3}

Kumiminwa “makaa ya moto…juu ya mji” huwakilisha utakaso kamili wa moyo (Watendakazi wa Injili, uk. 23) matokeo ya kumiminwa kwa Roho Mtakatifu kwa wale wanaoipokea ile “alama” — wale wanaookoka ule “mchinjo.” {TN1: 39.1}

Baada ya kukamilika “mchinjo,” na kabla ya kutawanywa kwa “makaa ya moto” “juu ya mji,” “Basi, makerubi walisimama upande wa kuume wa nyumba….nalo wingu likaujaza ua wa ndani.” Ezek. 10:2, 3. Baadaye, “wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika nchi machoni pangu,” asema nabii. Ezek. 10:19. Kisha baadaye akawaona tena “wakiinua mabawa yao” (Ezek. 11:22, 23), kuonyesha kwamba ingawa walikuwa wameondoka baada ya utengo kutekelezwa (Ezek. 10:3, 19), walirudi baadaye, na sasa walikuwa sasa wanaondoka mara ya pili. {TN1: 39.2}

Mji ukiwa umetakaswa hivyo dhambi na wadhambi, na hakuna ila “masalia,” watakatifu, kubaki, “Kwa maana Mimi, asema Bwana, Nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, Nami nitakuwa huo utukufu ndani yake…. Imba, ufurahi, Ee binti Zayuni; maana, tazama, Ninakuja, Nami nitakaa kati yako, asema Bwana.

39

Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu Wangu; Nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako.” Zek. 2:5, 10, 11. (Kwa ufafanuzi zaidi wa aya hizi, angalia Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 259-282.) {TN1: 39.3}

Maki kwamba wakati Yeye anapokaa kati ya watu Wake, “mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile,” na ya kwamba Yeye atakuwa “ukuta wa moto kuzunguka pande zote.” Hapa tumeonyeshwa na kuhakikishiwa tena kwamba “siku hiyo,” katika siku ambayo Bwana atachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe na kuja kukaa kati ya mji, Uwepo Wake, gari Lake la ajabu, litakuwa ulinzi kuwazunguka watu Wake! {TN1: 40.1}

Kwa hivyo inaonekana kwamba Bwana amekuja kuwatakasa watu Wake kwa kuwaondoa waovu kati yao, “kulichunga “ kundi Lake safi, na pamoja nao kumaliza kazi Yake. Katika hili tunaona kwamba kanisa limefikia upeo wa hatari yake. Yeye aliye na utungu “lazima azae.” Na “Maana Zayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.” Isa. 66:8. {TN1: 40.2}

Kisha gari, likishawekwa wakfu kwa watakatifu, na kujazwa kwa nafasi, litapaa mbali kwa bandari ya utukufu — “nchi ambayo i mbali sana.” “…na vile gari lilifingirisha kwenda juu, magurudumu yalilia, ‘Mtakatifu,’ na msafara wa malaika watakatifu kulizunguka wingu, wakalia, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu , Bwana Mwenyezi Mungu,

40

Mwenye nguvu! Na watakatifu katika wingu wakalia, Utukufu! Alleluya! ‘Na gari lilifingirisha kwenda juu kuelekea mji mtakatifu.” — Maandishi ya Awali, uk. 287, 288. {TN1: 40.3}

Katika mtazamo wa tarajio hili la utukufu, pamoja na kusimamia ukubwa na enzi ya utukufu wa kazi mbele iliyo yetu, na wakati mfupi sana ambamo inapaswa kutekelezwa, kila mmoja aharakishe kushiriki

Jukumu la Wale Wanaoupeleka Ujumbe. {TN1: 41.1}

Kwa sababu Ezekieli huwakilisha wale ambao ujumbe umeifikia mioyo yao, basi Bwana ananena kwao anaposema: “Mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa Changu, ukawape maonyo haya yatokayo Kwangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.” {TN1: 41.2}

“Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, Nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala

41

matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako. Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako.” Ezek. 3:17-21. {TN1: 41.3}

Kwa sababu ya walinzi wa zamani kutokuwa waaminifu, Bwana anamfanya Ezekieli wa uakisi — yeye-mme na yeye-mke ambao “huomboleza na kulia kwa machukizo yanayofanyika kati yake” (kanisa) — “mlinzi” (Ezek. 3:17) badala yao. Uwe mwangalifu, kwa hivyo, Ndugu, Dada, msije mkausaliti uaminifu wenu na kujipata mmetupwa nje. “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” 1 Kor. 10:12. Wale tu ambao wanajinyenyekeza hivi sasa, Bwana atawakweza wakati upasao wawe

Walinzi Wake Waaminifu Kusimama Mbele ya Wasio Waaminifu. {TN1: 42.1}

“Wale ambao wameamini kwa akili, ubunifu, au kipaji, hawatasimama hatimaye mbele ya askari. Hawakuambatana na nuru. Wale ambao wamejidhihirisha kuwa wasio waaminifu wakati huo hawatakabidhiwa kundi. Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na Yeye hawezi kuwatumia” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {TN1: 42.2}

“Watumwa wa Bwana wataitwa wazushi. Wachungaji watawaonya watu

42

wasiwasikilize. Nuhu alitendewa vivyo hivyo wakati Roho wa Mungu alikuwa akimsihi kupeana ujumbe ….” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 233. {TN1: 42.3}

Ukweli kwamba mabaraza yetu hupeana vibali vya uchungaji tu kwa watu waliofundishwa chuoni, ni thibitisho kwamba wanaamini “akili, ubunifu, na kipaji.” “Walinzi wa Mungu hawatapiga kelele, ‘Amani, amani,’ wakati Mungu hajasema amani. Sauti ya walinzi waaminifu itasikika: ‘Enendeni kutoka hapa, msikiguse kilicho najisi… Iweni wasafi mnaovibeba vyombo vya Bwana.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 83. {TN1: 43.1}

Pokea maagizo na ujifunze kutii neno la Bwana, kwa kufanya hivyo Yeye atakuwezesha kufanya mambo makuu kwa jina Lake. Elekeza sikio lako na usikie hakikisho la kutia moyo la Bwana: “Tazama, Nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso vyao. Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi….maneno Yangu yote Nitakayokuambia, yapokee moyoni mwako, na kuyasikia kwa masikio yako. Haya! Enenda uwafikilie….ukaseme nao, na kuwaambia, Bwana MUNGU asema hivi; kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia.” Ezek. 3:8-11. {TN1: 43.2}

Zaidi ya hilo, mwendo wa lile gari unaothibitiwa na Roho huonyesha kwamba Roho atakuwa nguvu inayothibiti yote: maana “Kila mahali

43

ambako roho hiyo ilitaka kwenda, [viumbe hai] walikwenda; walikuwa na roho ya kwenda huko nayo magurudumu yaliinuliwa juu karibu nao; kwa maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu.” Ezek. 1:20. {TN1: 43.3}

“Kuliko hapo awali, tusiombe tu kwamba watumwa waweze kutumwa katika shamba kubwa la mavuno, ila tuwe na ufahamu safi wa ukweli, ili wajumbe wa kweli watakapokuja, tuweze kuupokea ujumbe na kumheshimu mjumbe.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 420. Basi, kwa hivyo, mtakaseni Bwana wa majeshi Mwenyewe, na

Waacheni Wanadamu. {TN1: 44.1}

Unapojipata chini ya majaribio makali ikiwa utatii masadikisho yako ya ndani na kushikilia ukweli, lazima basi umruhusu Bwana pekee awe mwongozi wako, na Uvuvio mwalimu wako wa pekee. Usithamini wokovu wako kuwa duni kwa kuiamini busara ya mwingine. Uwe mwenye hekima: utii neno la Bwana, uchunguze mwenyewe, wala usikawie, kwa maana hujui muda mwembamba ulio kati yako na mbingu! “Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.” Mika. 7:5. {TN1: 44.2}

Watawala wa Israeli ya zamani — makuhani, waandishi na mafarisayo — waliwanyima watu haki yao waliyopewa na Mungu kuyachunguza wenyewe mafundisho ya Kristo,

44

waliangamia pamoja na waathirika wao chini ya hukumu ya sheria ambazo zilipaswa kuwaokoa. {TN1: 44.3}

“Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.” Luka 11:52. {TN1: 45.1}

Kosa hili la mauti lilirudiwa wakati wa Matengenezo, pia katika kuhubiri jumbe za Malaika wa Kwanza, wa Pili, na wa Tatu. Kwa hivyo kila mmoja aliyeupokea ukweli endelevu na kuwa mshiriki wa dhehebu la Waadventista wa Sabato, alifanya hivyo tu kwa kuufanya uchunguzi mwenyewe na kuamua bila kumtegemea kuhani au mwandishi au mfarisayo. Na iwapo mbinu hiyo ya uchunguzi ilikuwa ya akili timamu na salama awali, ni ya hakika hata sasa tunapolielewa Neno la Mungu bora zaidi kuliko tulipoamini kwanza! Na ingawa kwa kuifuata kwa utiifu njia ambayo Mungu huamuru, walinzi wasiokuwa waaminifu wa leo “wanakutupa nje,” na kuliondoa jina lako kutoka kwenye vitabu vya kanisa, unapaswa kufurahi (Isa. 66:5, Luka 6:22 23), na kwa furaha ustahimili jaribio la imani yako ukijua kwamba “lakufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.” (2 Kor. 4:17); ya kwamba, hakika, kupokea kwako ukweli na kuutii ni jambo la pekee ambalo milele litauhakikisha ushirika wako na waliokombolewa, katika kanisa la milele, na ya kwamba kitabu cha pekee ambacho kinastahili kuwa na jina lako ni “Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.” {TN1: 45.2}

45

“Watu huyapokea mafafanuzi ya wachungaji wao kwa Maandiko, wala hawayachunguzi wenyewe. Hivyo kwa kufanya kazi kupitia kwa wachungaji,” husema Shetani, “naweza kuwathibiti watu kulingana na mapenzi yangu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 473. Hivyo kwa sababu ya “wale….walio na imani ndani ya watu wanaoongoza, na kuyapokea maamuzi yao;….wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu wanaoongoza watazikataa.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106,107. “….iwapo wanaendeleza upinzani wao kufikia kulipinga lile ambalo hawajakuwa na uzoefu kwalo,….kanisa laweza kujua kwamba hawako sawa.” — Shuhuda, Gombo la 5 uk. 668, 669. {TN1: 46.1}

“Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.” 1 Sam. 15:22. {TN1: 46.2}

“Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.” Zef. 1:12. {TN1: 46.3}

“Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3:3. {TN1: 46.4}

Yeye “Ambaye pepeto lake li mkononi Mwake,… atausafisha sana uwanda Wake; na kuikusanya

46

ngano Yake ghalani, bali makapi Atayateketeza kwa moto usiozimika.” Mat. 3:12. {TN1: 46.5}

“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Dan. 12:3. {TN1: 47.1}

“Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu Wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. {TN1: 47.2}

“Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. {TN1: 47.3}

“…Bwana wa majeshi anapanga jeshi kwa vita.” Isa. 13:4. {TN1: 47.4}

“Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na Yeye aliyeiagiza.” Mika. 6:9. {TN1: 47.5}

“Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno Langu, litokalo katika kinywa Changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi Yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale Niliyolituma.” Isa. 55:10, 11. {TN1: 47.6}

47

“Lakini jihadharini na kukataa lile ambalo ni kweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kinga yao.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106. {TN1: 48.1}

“Kwa ajili ya Zayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.” Isa. 62:1. {TN1: 48.2}

O ndugu zangu wachungaji, ingawa mmeifanya migumu mioyo yenu dhidi ya ujumbe na kwa uthabiti mmekataa “kuusikiliza,” hata sasa Mungu bado anawasihi kujisalimisha kabla kuchelewa sana. Hivyo hii

Mwito wa Pili Na Sala. {TN1: 48.3}

Ingawa mmepuuza isivyo haki mwito ulioandikwa wa Bwana uliowekwa mikononi mwenu kwenye kongamano la Baraza Kuu mwaka wa 1930, na kwa ushupavu mmeyageuza macho yenu na hatua zenu mbali na nuru ya ziada ya “Ujumbe wa Malaika Watatu,” bado hata isivyo haki zaidi mlitangaza (kabla ya kukutana nasi na “kamati ya uchunguzi ya Baraza,” Februari 19, 1934, pale Los Angeles, California) katika dhehebu lote ripoti ya uongo kwamba mlitusikiza. Lakini licha ya masingizio haya yasiyofaa, bado Mungu anawapenda, na tunawapenda, na Yeye atawasamehe na kutoshikilia lolote dhidi yenu ikiwa mtamwomba Yeye kwa toba. {TN1: 48.4}

48

(Kabla ya toleo la kwanza la nakala hii kuchapishwa, wote hawakuwa wametusikiza. Ila tangu wakati huo wametusikiza. Lakini ulikuwa mbaya zaidi kuliko usingalikuwapo hata mmoja, unaonekana kutoka kwa ripoti amini katika Trakti yetu Namba 7 Hesabu Ushahidi Pande Zote Mbili Kabla Kufyatua kwa ajili au Dhidi ya.) {TN1: 49.1}

Maneno yangu kwa kwaida yanapotoshwa, na kubeba inavyoonekana uzito mdogo tu na baadhi, sala yangu, kwa hivyo, itakuwa kutoka katika Maandiko, na mwito wangu kutoka katika Roho ya Unabii. Hakika, ndugu zangu, mtazingatia maneno ya Mungu: {TN1: 49.2}

“Bwana, nimependa makao ya nyumba Yako, Na mahali pa maskani ya utukufu Wako.” Zab. 26:8. Na “… Maana wivu wa nyumba Yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.” “Kwa maana aliyetukana si adui; … Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu,… Tulipeana shauri tamu; na kutembea pamoja Nyumbani mwa Mungu.” Zab. 69:9; 55:12, 13, 14. Kwa hivyo “Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina Lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa Zako.” 1 Nya. 16:35. {TN1: 49.3}

“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Isa. 1:18. “Na dawa ya macho

49

ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Ufu. 3:18. {TN1: 49.4}

Mwenendo wenu, ndugu zangu, dhidi ya nuru ya utukufu sasa inayoangaza juu ya “Ujumbe wa Malaika Watatu,” ni utimizo wa unabii: “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu,” — ukweli au manabii, — mnakataa kuwa na nia ya kuchunguza kilio cha Malaika ambaye utukufu wake “utaangaza nchi.” {TN1: 50.1}

“Nuru ambayo itaangaza nchi kwa utukufu wake itaitwa nuru ya uongo, na wale wanaokataa kutembea katika utukufu wake unaoendelea.” — Mapitio na Kutangaza, Mei 27, 1890. {TN1: 50.2}

“Nabii anatangaza, ‘Baada ya hayo, naliona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na uwezo mwingi; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.’ Waangavu, utukufu, na nguvu zitaunganishwa na ujumbe wa malaika wa tatu, na kusadikisha kutafuata popote unapohubiriwa katika wonyesho wa Roho. Atawezaje yeyote kati ya ndugu zetu kujua wakati nuru itakapokuja kwa watu wa Mungu?” — Mapitio na Kutangaza, Aprili 1, 1890. {TN1: 50.3}

Mnajua nyote vyema kwamba Ukweli, ambao tumekuwa tukiufurahia sana tangu mwaka wa 1844, umekuja kupitia mtumwa aliyeteuliwa na Mungu ambaye maandishi yake tunayaita “Roho ya Unabii.” Sauti hiyo sasa inazungumza nanyi, upya, katika mwito huu wa dharura: {TN1: 50.4}

50

“Mtu yeyote asifikie hitimisho kwamba hakuna ukweli zaidi utakaofunuliwa.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 53. Hakuna mtu atakayeamua “kwamba ukweli wote umefunuliwa, na ya kwamba Yeye wa Milele hana nuru zaidi kwa watu Wake.” — Kimenukuliwa, uk. 60. {TN1: 51.1}

“Filipo akamwona Nathanieli, akamwambia,” Tumemwona ambaye Musa katika sheria, na manabii waliandika, Yesu Mnazareti, Mwana wa Yusufu. “Na Nathanaeli akamwambia:” Je! kitu chema chaweza kutoka Nazareti? Chuki na kutoamini kulichipuka ndani ya moyo wa Nathanieli, lakini Filipo hakujaribu kuupiga vita. Alisema, ‘Njoo uone.’” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 63. {TN1: 51.2}

“…iwapo ujumbe unakuja usiouelewa, vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa,…kwa maana msimamo wako hautatikiswa kwa kukutana na makosa. Hakuna wema au ushujaa kuendeleza vita daima gizani, Kuyafumba macho yako usije ukaona, kufunga masikio yako usije ukasikia, kuufanya mgumu moyo wako kwa ujinga na kutoamini usije ukajinyenyekeza na kukubali kwamba umepokea nuru kwa mambo fulani ya ukweli.” {TN1: 51.3}

“Kujitenga mbali na uchunguzi wa ukweli si njia ya kutekeleza agizo la Mwokozi ‘kuyachunguza Maandiko.’ Je, ni kuchimba hazina

51

zilizofichwa kuyaita matokeo ya kazi ya mtu fulani rundo la takataka, na kutofanya uchunguzi wa kina ili kuona iwapo vipo vito vya thamani katika kusanyiko la wazo ambalo unahukumu?… Hivyo ndivyo kwamba Wayahudi walifanya katika siku za Kristo, na tumeonywa kutotenda walivyofanya na kuongozwa kuchagua giza badala ya nuru… Hakuna hata mmoja kati ya wale wanaofikiri kwamba wanajua yote ni mkongwe sana au wenye akili sana kujifunza kutoka kwa wanyenyekevu wa wajumbe wa Mungu aliye hai.” — Kimenukuliwa awali, uk. 65, 66. {TN1: 51.4}

“Nuru ya thamani itaangaza kutoka kwa Neno la Mungu, na mtu yeyote asithubutu kulazimisha nini kitakacholetwa au kisichostahili kuletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangaza Atakazotuma, na kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yote ile nafasi yake ya mamlaka, hakuna yeyote aliye na haki ya kufungia mbali nuru kutoka kwa watu. Wakati ujumbe unapokuja kwa jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu ataweza kujipatia udhuru wa kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kumudu kusimama nyuma katika mtazamo wa kutojali na kujiamini, na kusema: ‘Najua ni nini ukweli. Nimeridhika na msimamo wangu. Nimeweka vigingi vyangu, na Sitaondolewa mbali na nafasi yangu, liwalo liwe. Sitausikiza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli. Ilikuwa kwa kufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndio sababu ujumbe

52

wa mbinguni haujawafikia.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65. {TN1: 52.1}

O, Wandugu, udhuru gani mtakaokuwa nao iwapo mnakataa kusikiza rai hii pia? Je! utatetea hekima yenu na kuokoa nafsi zenu iwapo mtajikuta upande mbaya? Ikiwa ndivyo, hakika basi mtataka kufanya yote. Lakini iwapo sivyo, basi fanyeni hima kuwa upande wa kuume, hata ingawa kutawashusha hadi mavumbini kuja kwenye Nuru. Msiweze kusema tena: “Amezichukua Shuhuda kutoka kwa mkutadha wake.” Mweze kukoma kujaribu kuizuia njia, ili kwamba ujumbe usiwafikie watu, hata mmeonywa: “mtu yeyote asithubutu kulazimisha nini kitakacholetwa au kisichostahili kuletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangaza Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu.” Mungu hukataza! {TN1: 53.1}

(italiki zote ni zetu)

Ingawa mada ya somo la hii trakti lingepanuliwa sana, kwa ajili ya uzito, limefupishwa hivi, likibeba kauli muhimu tu kufunua ujumbe unaosihi penye milango ya kanisa pendwa la Mungu. Yeyote kwa hivyo, ambaye amesoma hadi hapa, asiruhusu kikwazo chochote kimuzuie kutuma ombi la vyote

53

VITABU BILA MALIPO {TN1: 53.2}

Mfululizo wa vitabu vya Ukweli wa Sasa unaonyesha kwamba “Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.” (Ezek. 12:23); yaani, maono ya unabii yaliyoonekana kuwa yamejaa siri, sasa yamekuwa ukweli dhahiri. {TN1: 54.1}

Trakti kumi na tatu, hadi sasa (1941) karibu kurasa 900, zitatumwa bila malipo kwa mtu yeyote anayetuma ombi. {TN1: 54.2}

Tuma maombi yote kwa Shirika Uchapishaji la Ulimwengu kwenye anwani iliyo ndani ya ukurasa wa jalada. {TN1: 54.3}

“…Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Yohana 16:13. {TN1: 54.4}

KIELEZO CHA ROHO YA UNABII

54

KIELEZO CHA MAANDIKO MATAKATIFU

55

KIELEZO CHA MASOMO

Mwenyewe Kutazamia Kila Mshale wa Nuru 3,4

Ya-ziada Kabla ya Saa Kumi na Moja! Dadaneli za Biblia 5

Ufafanuzi wa Nabii wa Mafumbo Yaliyoelezwa hapa 5-7

Bwana Kwa Kimoja cha Viti Vyake vya Enzi 7-10

Lini Maono Haya ya Unabii Yatatimizwa? 11,12

Kusudi la Bwana Kuja Katika Kiti Chake cha Enzi 12-14

Kanisa la Laodekia 14,15

Wakati wa Hali ya Chini ya Kiroho ya Kanisa 15,16

Dawa 16-19

Kutiwa Muhuri watu 144,000 — Malimbuko 19,20

Ripoti Mbili za Kutia Muhuri 20-22

Waliookoka Wanaenda Kwa Mataifa Yote 22,23

Kulaumu na Kutafuta Makosa 23-25

Katika Nuru ya Mifano 25-27

Ujumbe Safi 27,28

Uinua Uvuvio 28,29

Namna Ujumbe Unavyopokewa 29,30

Wa Furaha, Kuomboleza, na Msiba 30,31

Wataziba Masikio Yao na Kufunga Milango Yao 31,32

Ujumbe Huo Utawafikiaje Watu? 32,33

Hakuna Kinachoweza kumzuia Bwana 33-35

Mfano wa Watakatifu katika Wakati wa Hukumu 35,36

Je, Gari Hili Litawasili Lini? Je, Litakaa Kwa Muda Gani? 36-38

Kusudi la Ujumbe 38-41

Wajibu wa Wale Wanaobeba Ujumbe 41,42

Walinzi Wake Waaminifu Kusimama Mbele ya Wasio Waaminifu 42-44

Mwacheni Mwanadamu 44-48

Rufaa ya Pili na Sala 48-53

56

>