fbpx

MISINGI YA IMANI YA WADAUDI WAADVENTISTA WASABATO

Ukijitokeza mwaka wa 1930 kutoka ndani ya dhehebu la Waadventista Wasabato (“kanisa la Walaodekia”), Ushirika wa Wanadaudi Waadventista wa Sabato umekabidhiwa kazi ya kiunabii (ilivyotabiriwa katika Isaya 52: 1) ya kuliandaa kanisa la Laodekia, la mwisho na “magugu” kati ya “ngano,” kwa ajili ya kutangaza injili “duniani kote.” Mat. 24:14.

Ushirika huu, kwa pamoja na dhehebu la Waadventista wa Sabato, una ‘imani fulani za msingi, sifa kuu am-bazo, pamoja na marejeleo ya Maandiko ambayo juu yake imejengwa,’ mwanzoni imefanywa muhtasari kama ifuatavyo:
  1. Kwamba Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Jipya yalitolewa kwa uvuvio wa Mungu, yanasheheni ufunuo wa kutosha wa mapenzi Yake kwa wanadamu, na ni kanuni isiokosea ya imani na desturi. 2 Tim. 3:15-17.
  2. Kwamba Uungu, au Utatu, huhusisha Baba wa Milele, wa pekee, Kiumbe cha kiroho, Mwenye nguvu, Aliye Mahali Pote, Anayejua yote, asiye na kikomo kwa hekima na upendo, Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Baba wa Milele, ambaye kwa Yeye vitu vyote viliumbwa na kupitia Kwake wokovu wa majeshi ya waliokombolewa utatimizwa; Roho Mtakatifu, kiumbe cha tatu cha Uungu, nguvu kuu ya urejesho katika kazi ya ukombozi. Mat. 28:19.
  3. Kwamba Yesu Kristo ni Mungu hasa, akiwa wa maumbile sawa na asili kama Baba wa Milele. Alipokuwa aki-hifadhi asili yake ya Uungu Alijitwalia asili ya familia ya kibinadamu, aliishi duniani kama mwanadamu, alionye-sha katika maisha Yake kama Mfano wetu kanuni za haki, zilithibitisha uhusiano Wake na Mungu kwa miujiza mingi ya nguvu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu msalabani, akafufuliwa kutoka kwa wafu, na akapaa kwa Baba anakoishi milele ili kutuombea. Yoh. 1: 1, 14; Ebr. 2: 9-18; 8: 1, 2, 4: 14-16; 7:25.
  1. Kwamba kila mtu ili kuupata wokovu lazima apitie uzoefu wa kuzaliwa upya, kwamba huu unajumuisha mabadiliko yote ya maisha na tabia kwa nguvu ya kuumba upya ya Mungu kupitia imani katika Bwana Yesu Kris-to Yohana 3:16, Mathayo 18: 3; Matendo 2: 37-39.
  2. Kwamba ubatizo ni ibada ya kanisa la Kikristo na unapaswa kufuata toba na msamaha wa dhambi. Katika maadhimi-sho yake imani inaonyeshwa katika kifo, mazishi, na ufufuo wa Kristo. Kwamba mtindo sahihi wa ubatizo ni kwa kuzamishwa. Warumi 6: 1-6; Matendo 16: 30-33.
  3. Kwamba mapenzi ya Mungu jinsi yanavyohusiana na mienendo ya maadili yanaelezwa katika sheria Yake ya amri kumi, kwamba hizi ni kanuni zisizobadilika, kuu za maadili, zinazowaunganisha wanadamu wote, katika kila kizazi. Kutoka 20: 1-17.
  4. Kwamba amri ya nne ya sheria hii isiyobadilika huhitaji kuadhimisha Sabato ya siku ya saba. Hii taasisi ta-katifu wakati huo huo ni ukumbusho wa uumbaji na ishara ya utakaso, ishara ya pumziko la anayeamini kutoka kwa kazi zake za dhambi , na kuingia kwake ndani ya pumziko la nafsi ambalo Yesu huahidi kwa wale wanaokuja Kwake (Mwa. 2: 1-3; 1, Kut. 20: 8-11, 31: 12-17; Ebr. 4: 1- 10.
  5. Kwamba sheria ya amri kumi huonyesha wazi dhambi, ambayo adhabu yake ni kifo. Sheria haiwezi kum-wokoa mkosaji kutoka kwa dhambi yake, wala kumpa uwezo wa kumzuia kutenda dhambi. Kwa upendo wa milele na rehema, Mungu hutoa njia ambapo hili linaweza kufanywa. Yeye hutoa mbadala, hata Kristo Mwenye Haki, kufa kwa niaba ya mwanadamu, na ‘Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.’ 2 Kor. 5:21. Kwamba mmoja huhesabiwa haki, sio kwa utiifu wa sheria, ila kwa neema iliyo katika Kristo Yesu. Kwa kumkubali Kristo, mwanadamu anapatanishwa na Mungu, ana-hesabiwa haki kwa damu Yake kwa ajili ya dhambi za zamani, na kuokolewa kutoka kwa nguvu za dhambi kwa maisha yake ya ndani. Hivi injili inakuwa ‘nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila aaminiye.’ Uzoefu huu unafanywa na uwakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humhakikishia habari ya dhambi na kumwongoza hadi kwa Mbeba-Dhambi, kumshawishi aaminiye kuingia agano jipya la uhusiano, ambapo sheria ya Mungu inaandikwa moyoni mwake, na kupitia uwezo unaomwezesha wa Kristo anayekaa ndani, maisha yake yanaletwa kufanana kabisa na maagizo ya Mungu. Heshima na sifa za mabadiliko haya ya ajabu zote ni zake Kristo. 1 Yoh. 3: 4; Rum. 7: 7; Rum. 3:20; Efe. 2: 8-10; 1 Yoh. 2: 1, 2; Rum. 5: 8-10; Gal. 2:20; Efe. 3:17; Ebr. 8: 8-12.
  1. Kwamba Mungu ‘pekee ana hali ya kutokufa.’ 1 Tim. 6:15. Mwanadamu wa uvumbi humiliki asili aliyoridhi ya dhambi na ya kufa. Uzima wa milele ni zawadi ya Mungu kwa njia ya imani ndani ya Kristo. Rum. 6:23. “Yeye aliye na Mwana anao uzima.” 1 Yoh. 5:12. Hali ya kutokufa watapewa waadilifu wakati wa ujio wa pili wa Kristo, wakati watakatifu waliokufa wanafufuliwa kutoka makaburini na wenye haki walio hai wanahamishwa kumlaki Bwana. Kisha inakuwa kwamba wale waliohesabiwa kuwa waaminifu ‘wanavaa kutokufa.’ 1 Kor. 15: 51-55.
  2. Kwamba hali ya mtu katika kifo ni ile ya kukosa fahamu. Kwamba watu wote, wema na wabaya sare, wanasalia kaburini tangu kifo hadi kwa ufufuo. Mhu. 9: 5, 6; Zab. 146: 3, 4; Yoh. 5:28, 29.
  3. Kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote waadilifu na waovu. Ufufuo wa waadilifu utafanyika wakati wa ujio wa pili wa Kristo; ufufuo wa waovu utafanyika miaka elfu baadaye, mwishoni mwa milenia. Yoh. 5:28, 29; 1 Thes. 4: 13-18; Ufu. 20: 5-10.
  4. Kwamba mwishowe wadhambi wasiotubu, Shetani akiwamo, mwasisi wa dhambi, atapunguzwa, kwa moto wa siku ya mwisho hadi kwa hali ya kutokuwa hai na kuwa kana kwamba hakuwa, na hivyo kuusafisha ulimwen-gu wa dhambi na wadhambi. Rum. 6:23, Mal. 4: 1-3, Ufu. 20: 9, 10; Obadia 16.
  5. Kwamba hakuna kipindi cha unabii [kumaanisha kuweka muda wa kiunabii wa tarehe kamili ya kuja kwa Kristo] kimepeanwa katika Biblia kufikia ujio wa pili, ila kwamba kile kirefu zaidi siku 2300 za Dan. 8:14, kilikoma mwaka wa 1844, na kutuleta kwa tukio linaloitwa ku-patakasa patakatifu.
  6. Kwamba hekalu la kweli, ambalo hema ya duniani ilikuwa mfano, ni hekalu la Mungu lililo Mbinguni, am-balo Paulo hulizungumzia katika Waebrania 8 na kuendelea, na ambalo Bwana Yesu kama kuhani wetu mkuu, ni mtumishi; na kazi ya ukuhani ya Bwana wetu ni uakisi wa kazi ya Kuhani wa Kiyahudi wa enzi ya awali; kwamba hili hekalu la mbinguni ndilo la kutakaswa mwishoni mwa siku 2300 za Dan. 8:14; kutakaswa kwalo kukiwa, ka-ma katika mfano, kazi ya hukumu, ikianza na kuingia Kristo kwa awamu ya hukumu ya huduma Yake katika hekalu la mbinguni kivuli chake katika huduma ya la duniani ya kulitakasa hekalu kwa siku ya upatanisho. Kazi hii ya hukumu katika hekalu la mbinguni ilianza maka wa 1844. Kukamilika kwake kutafunga rehema kwa mwa-nadamu.
  1. Kwamba Mungu, katika wakati wa hukumu na kulingana na kujishughulisha Kwake kwa usawa na jamii ya wanadamu kuwaonya juu ya matukio yanayokuja ya umuhimu yanayoathiri hatima yao (Amosi 3: 6, 7), hutuma umbele utangazaji wa unavyojongea ujio wa pili wa Kristo; kwamba kazi hii inawakilishwa na malaika watatu wa Ufunuo 14, na kwamba ujumbe wao mara tatu huleta kwa mtazamo kazi ya matengenezo ya kuwaandaa watu ku-kutana Naye wakati wa kuja Kwake.
  2. Kwamba wakati wa kupatakasa patakatifu, unaambatana na kipindi cha kuutangaza ujumbe wa Ufunuo 14, ni wakati wa hukumu ya upelelezi, kwanza kuhusu wafu, na pili, kuhusu walio hai. Hukumu hii ya upelelezi inaamua ni nani kati ya makumi ya maelfu wanaolala katika mavumbi ya dunia wanastahili sehemu katika ufufuo wa kwanza, na ni nani wake walio hai wanastahili kuhamishwa bila kuonja mauti. 1 Pet. 4:17, 18; Dan. 7:9, 10, Ufunuo 14: 6, 7, Luka 20:35.
  3. Kwamba wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa watu wakumcha Mungu, wasioiga misemo ya uovu na maa-dili yasiyo ya kawaida wala wasiambatane na njia zisizo za haki za dunia, wasiopenda anasa zake za dhambi wala kuupokea upuuzi wake. Kwamba aaminiye anapaswa kuutambua mwili wake kama hekalu la Roho Mtakatifu, na kwamba kwa hivyo anapaswa kuufunika mwili huo kwa mavazi safi, nadhifu na ya heshima. Zaidi ya hayo, kwamba katika kula na kunywa na katika mkondo wake wote wa mazoea anapaswa kuyageuza maisha yake kama inavyotakiwa kuwa mfuasi wa Mwalimu mpole na mnyenyekevu. Hivi aaminiye ataongozwa kujiepusha na viny-waji vyote vya sumu, tumbaku, na dawa zingine za kulevya, na kujizuia kila tabia na mazoea ya kuutia unajisi mwili na roho. 1 Kor. 3:16, 17; 9:25; 10:31: 1 Tim. 2: 9, 10; 1 Yohana 2: 6.
  4. Kwamba kanuni takatifu ya zaka na sadaka kwa ajili ya kuunga mkono injili ni kuutambua umiliki wa Mungu katika maisha yetu, na kwamba sisi ni wasimamizi ambao wanapaswa kumpa hesabu juu ya yote Ameweka kwa umiliki wetu. Law. 27:30; Mal 3: 8-12; Mat. 23:23; 1 Kor. 9: 9-14, 2 Kor 9: 6-15.
  5. Kwamba Mungu ameweka ndani ya kanisa lake karama za Roho Mtakatifu, kama zilivyoorodheshwa katika 1 Wakorintho 12 na Waefeso 4. Kwamba karama hizi hufanya kazi kwa uwiano na kanuni za Mungu za Biblia, na zimetolewa kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu , kazi ya ukasisi, na kuujenga mwili wa Kristo. Ufu. 12:17, 19:10; 1 Kor 1: 5.
  1. Kwamba ujio wa pili wa Kristo ni tumaini kubwa la kanisa, kilele kikuu cha injili na mpango wa wokovu. Kuja kwake kutakuwa halisi, binafsi, na dhahiri. Matukio mengi muhimu yatahusishwa na kurudi Kwake, kama vile ufufuo wa wafu, kuangamizwa kwa waovu, utakaso wa dunia, tuzo ya wenye haki, kuanzishwa kwa ufalme wake wa milele. Utimilifu karibu wote wa safu mbalimbali za unabii hasa ule uliyomo katika vitabu vya Danieli na Ufunuo, na hali zilizopo katika ulimwengu wa kimwili, kijamii, kiviwanda, kisiasa na kidini, zinaonyesha kwamba kuja kwa Kristo ‘kumekaribia, hata kwenye malangoni. ‘Wakati kamili wa tukio hilo haujatabiriwa. Waumini wanahimizwa kuwa tayari, kwa maana ‘katika saa ile msiyodhani, Mwana wa Adamu’ atafunuliwa. Luka 21: 25-27; 17: 26-30; Yoh. 14: 1-3; Mdo. 1: 9-11; Ufu. 1: 7; Ebr. 9:28; Yak. 5: 1-8; Yoeli 3: 9-16; 2 Tim. 3: 1-5; Dan. 7:27; Mat. 24:36, 44.
  2. Kwamba utawala wa Kristo wa milenia hufunika kipindi kati kati ya ufufuo wa kwanza na wa pili, wakati ambapo watakatifu wa vizazi vyote watakaa pamoja na Mwokozi wao Mbarikiwa Mbinguni. Mwishoni mwa mile-nia, Mji Mtakatifu na watakatifu wote watashuka kwa dunia. Waovu, waliofufuliwa katika ufufuo wa pili, watae-nea juu ya uso wa dunia na Shetani kiongozi wao ili kuizingira kambi ya watakatifu, wakati moto utashuka kutoka kwa Mungu Mbinguni na kuwateketeza. Katika moto mkubwa ambao unamwangamiza Shetani na jeshi lake, dunia yenyewe itaumbwa upya na kutakaswa kutokana na madhara ya laana. Hivi ulimwengu wa Mungu utatakaswa kutoka kwa uchafu wa doa la dhambi. Ufu. 20; Zek. 14: 1-4; 2 Petro 3: 7- 10.
  3. Kwamba Mungu ataumba vitu vyote upya. Dunia, kurejeshwa kwa uzuri wake wa awali, itakuwa milele makao ya watakatifu wa Bwana. Ahadi kwa Abrahamu, kwamba kwa njia ya Kristo yeye na uzao wake wataimili-ki dunia katika vizazi visivyokoma vya milele, itatimizwa. Ufalme na utawala na ukuu wa ufalme chini ya mbingu zote utapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu ambaye ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zote zitamtumikia na kumtii Yeye. Kristo, Bwana, atatawala kwa ukuu na kila kiumbe kilicho mbinguni na duniani na chini ya nchi, na vile vilivyo baharini vitatoa baraka na heshima na utukufu na nguvu kwa Yeye anayeketi juu ya kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo milele na milele (Mwa. 13: 14-17, Rum. 4:13, Ebr. 11: 8-16, Mat. 5: 5, Isa. 35, Ufu. 21: 1-7; Dan. 7 : 27; Ufu. 5:13.) “Kitabu cha Mwaka cha Dhehebu la Waadventista wa Sabato, Toleo la 1947, kur. 4-6.
KWA KUONGEZEA kwa misingi hii ya imani inayoshikiliwa sawa na Waadventista wa Sabato, Ushirika wa Wadaudi unashikilia:
  1. Kwamba karama ya unabii katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (kupitia chombo ambacho kanisa lilian-zishwa mwaka wa 1844 na kukuzwa na kudumishwa kwa miongo saba) kilikoma udhihirisho wake mwaka wa 1915 na hakikudhihirishwa tena hadi mwaka wa 1930, na kwamba kikomo hiki na udhihirisho huu ni sambamba na kukoma karama ya unabii katika Agano la Kale na udhihirisho wake katika Agano Jipya.
  2. Kwamba ulidhihirisho wa sasa ulipangwa kulingana na unabii wa miaka 430 wa Ezekieli 4, na ya kwamba ndiyo “Nyongeza” iliyotarajiwa katika Maandishi ya Awali, uk. 277.
  3. Kwamba kilidhihirishwa upya katika kazi ya kufunga kwa kanisa ili kutekeleza kutiwa muhuri watumwa 144,000 wa Mungu (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na kupeana nguvu na msukumo (Maandishi ya Awali, uk. 277) kwa Ujumbe wa Malaika Watatu (Ufu. 14: 6-11) ili kwamba watumwa 144,000 wajazwe nguvu waweze kukamilisha kazi ya kufunga kwa dunia, na kuwakusanya ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote (Isaya 66:19, 20; 18: 4).
  1. Kwamba kuangamizwa kwa magugu kutoka miongoni mwa malimbuko ya walio hai (Mat. 13:30, 48, 49; Ezek. 9: 6, 7) ni tokeo la utakaso wa kanisa.
  2. Kwamba hapo hapo baada ya hayo, malaika wataziachilia pepo nne (Ufu. 7: 1-3), ambapo utaanza wakati wa taabu na Mikaeli kusimama kuwaokoa kutoka kwayo, wote ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo (Dan. 12: 1).
  3. Kwamba malaika ‘kuziachilia pepo nne kuvuma pembe nne za dunia (Ufu. 7: 1), sio tarajio la vita vya dunia ila badala yake sheria ya kutekelezwa dunia nzima katika Babeli na sanamu ya mnyama, na ya kwamba mtu yeyote asiweze kununua au kuuza isipokuwa yeye anayeiabudu “sanamu.” Ufu. 13: 15-17.
Rev-7
  1. Kwamba halafu, wakati wa taabu ya Yakobo (Yer. 30: 7) kwa wale 144,000, wana wa Yakobo, kwa mantiki inatokeza wakiwa safarini kurudi nyumbani (Mwa. 32: 1, 24) kwa nchi ya baba zao (Ezek. 36:28; 37:21, 25).
  2. Kwamba tukio la kihistoria ambalo limetajwa hapo juu litasababisha watu 144,000 kupata majina yao yanaba-dilishwa kama baba yao, Yakobo (Mwa. 32:28), na kama kundi kupokea jina jipya ambalo kinywa cha Bwana kitanena (Isa. 62 : 2).
  3. Kwamba haya matukio yatafikia upeo katika kuanzishwa kwa Ufalme (Dan. 2:44; Isa. 2: 1-4; Mika 4; Ezek. 37), ambamo wale 144,000, wamfuatao Mwana-Kondoo “kila aendako” (Ufu. 14: 4), watasimama pamoja naye juu ya Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1), na hapo “kuupokea utajiri wa watu wa mataifa.” Isa. 60: 5, 11.
  4. Kwamba pamoja na mfululizo huu wa matukio utahakiki Kilio Kikuu cha Malaika anayeiangaza nchi kwa utu-kufu wake (Ufu. 18: 1), wakati Sauti nyingine inapiga kelele, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4.
  5. Kwamba katika kuitikia mwito huu, mataifa mengi yatasema: “Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika 4: 2.
  6. Kwamba Sauti itaacha kupiga kelele wakati watakatifu wote watakakuwa wamekusanywa kutoka katika mataifa yote. Kisha itakuwa “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” Amosi 8:11, 12.
  1. Kwamba basi kutafuatia kutenguka kwa muungano wa dunia nzima wa sanamu ya mnyama (Ufu. 19: 1-3), kufungwa kwa hukumu ya upelelezi ya walio hai (Ufu. 15: 5-8), mwisho wa muda wa rehema (Ufu. 22:11), na kumiminwa kwa mapigo saba ya mwisho juu ya waovu (Ufu. 16).
  2. Kwamba chini ya pigo la saba, majeshi yaliyojipanga kwa pambano la Har-Magedoni yatapigana na, na yataangamizwa na, majeshi ya Mbinguni (Shuhuda, Gombo la 6, uk. 406), na kwamba Kristo atatokea katika utu-kufu Wake wote, kuwaangamiza waovu waliosalia, kuwafufua watakatifu waliokufa (1 Thess. 4:15-17), na kui-karibisha milenia (Ufu. 20: 5).
  3. Kwamba kwa muda mchache (Ufu. 20: 3), miaka mia moja (Isaya 65:20), baada ya milenia, waovu wataishi tena na hatimaye wataangamizwa kwa moto (Ufu. 20: 9), ambapo vitu vyote vitarejeshwa, na mpango halisi wa Mungu utaendelea kufikia utimilifu mkamilifu katika umilele usiokatizwa wa furaha ya mbinguni (Ufu. 21: 4).
>