fbpx

Trakti Namba 09

“TAZAMA NAVIYAFANYA VITU VYOTE KUWA VIPYA”

Katika maneno ya kinabii, “Tazama, nayafanya yote kuwa upya” (Ufu. 21:5), Mungu huonya kwamba “vitu vyote” vitachakaa. Ili kuelewa kwa usahihi unabii huu, ni lazima tukumbuke ukweli kwamba ili kitu cha zamani kufanywa kipya, ni lazima kwanza kisambaratishwe, — kipunguzwe kuwa hali ya sehemu zake za asili au vipande ambavyo vilikuwa kabla ya kuunganishwa mseto wa jumla, — kisha kifanyiwe ukarabati, kutengenezwa, na kuunganishwa tena. Wakati ambapo mchakato huo, isitoshe, unapoendelea, kitu kile ambacho kinakarabatiwa hakiwezi, bila shaka, mpaka kimalizike, kirejelee tena shughuli yake. Wakati wa kipindi cha kufanywa upya, kiko nje ya kazi na nje ya matumizi. {TN9: 3.1}

Katika suala hili, kuchakaa kwa “vitu vyote” ni, wanavyoelewa vyema wanafunzi wote wa Biblia, matokeo yake, si ya uchakavu wa kawaida ambao unaambatana na ukongwe, ila wa laana ya dhambi iliyoletwa na Shetani kuwadanganya mataifa. Kwa hivyo, wakati “vitu vyote” vya duniani viko katika mchakato wa kufanywa upya, na hivyo nje ya shughuli na nje ya matumizi, dunia, baada ya kuwa si kitu ila rundo, lazima kabisa iwe naam shimo la kuzimu. {TN9: 3.2}

Basi, andiko, “Tazama, nafanya vitu vyote kuwa upya,” huashiria kipindi cha kusambaratisha na ukarabati wa

3

vitu vyote — wakati ambapo Shetani anafungwa kama ilivyotabiriwa katika unabii mintarafu

MILLENIA. {TN9: 3.3}

Kwa sababu fundisho la millenia huwasilisha maswali kadhaa ya kusumbua na yaliyoondolewa uhitaji mu-himu kwa wokovu wa kila mwanadamu, na kwa kuwa ukweli pekee yake utaiweka nafsi huru kutoka kwa udanganyifu na dhambi, na kuutakasa moyo, hitaji ni muhimu, kwa hivyo, kwamba tugundue jibu sahihi kwa kila swali kama hilo. {TN9: 4.1}

Katika maono yake ya ufunguo, ya kukumbatia millenia, Yohana “nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. {TN9: 4.2}

“Kisha nikaona,” anaendelea, “ viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wa-siomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wa-la katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na

4

Kristo miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja Naye hiyo miaka elfu. {TN9: 4.3}

“Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka ku-wadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya wa-takatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye ku-wadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. {TN9: 5.1}

“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na Yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zika-kimbia uso Wake, na mahali pao hapakuonekana. {TN9: 5.2}

“Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafungu-liwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa

5

wafu waliokuwamo ndani yake; na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Waka-hukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. {TN9: 5.3}

“Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.” Ufu. 20:1-15; 21:1. {TN9: 6.1}

Hapa, kwa ushuhuda wa Bwana, Mwenyewe, ni kweli ambazo “imetupasa kuziangalia zaidi” (Ebr. 2:1) ili kufikia ukweli halisi na wote — hitimisho la kawaida kwa yote maandishi ya Biblia kuhusu millenia na masomo yanayohusiana; kweli ambazo pia, zinazusha swali: Je! dunia wakati wa millenia ni

Ukiwa Au Inayokaliwa? {TN9: 6.2}

Kwa kutazama maandiko kadhaa yanayohusiana na suala hili na kwa masuala yanayohusiana katika swali hilo, tunapaswa kuzingatia mahitimisho yetu tu kwa uzito wa ushahidi, ili kwamba tusiweze tu kuujua ukweli wote, lakini pia tusifundishe chochote ila ukweli — lengo maradufu ambalo linaweza kuafikiwa tu kwa kutoa uhuru wa kigezo kwa yote maandishi ya manabii na yale ya Waufunuo. Na kwa kuwa Ufunuo ni kukunjua kwa unabii, busara hutuhimiza kuendelea kutoka kwa

6

unabii hadi kwa ufunuo. Katika munganiko huu, kwa hivyo, tunayashughulikia kwanza maneno ya Yere-mia: {TN9: 6.3}

“Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele ya Bwana, na mbele ya hasira Yake kali. Maana Bwana asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini Sitaikomesha kabisa. Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu Mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala Sikujuta wala Mimi sitarudi nyuma niyaache.” Yer. 4:23-28. {TN9: 7.1}

Tendo hapa lililoonyeshwa dhidi ya zilizosimuliwa hukumu za Mungu zilizokuja kwa nchi ya Israeli ya kale, kwa sababu ya uasi wao, haliwezekani, kwa sababu haswa ya mambo, liwekewe mipaka tu kwa nchi hiyo. Haiwezekani, kwa maneno mengine, kufanywa finyu, kama wengine wanavyofikiri linaweza, ku-maanisha kwamba nchi ya watu wa Mungu tu imefanywa au itafanywa “ukiwa” na kuachwa “ukiwa” na “utupu,” — bila nuru na bila ndege au mnyama au mwenyeji, — na wengine duniani kuachwa ili kufurahia baraka hizi zote. Maandiko lazima, kinyume chake, yachukuliwe jinsi yanavyosomwa, kuonyesha kwamba dunia yote

7

itaathirika kila sehemu. Kwa mtazamo wa ukweli huu, kwa hivyo, neno nchi bila shaka haliwezi kufasiriwa, kama ilivyofanywa na baadhi, kumaanisha ile “nchi” — Palestina tu. {TN9: 7.2}

Wakati Israeli ya zamani, zaidi ya hayo, ilichukuliwa na mataifa, milima na vilima haikufanywa kutetemeka na “kusogea huko na huko”; miji haikubomolewa kabisa na kuachwa bila mkaazi; ndege hawakulazimish-wa kuruka mbali kutoka kwa nchi; na nchi haikuachwa gizani. Kwa hivyo, dhahiri, kutawanywa kwa Wayahudi hakukuweza kutimiza unabii wa Yeremia 4:23-28. Nchi, kwa hivyo, lazima tena itakuwa, kama siku ya kwanza ya uumbaji, “ukiwa, na utupu.” Mwa. 1:2. Na kama ilivyokuwa wakati huo “giza. . . juu ya uso wa vilindi vya maji,” itakuwa hivyo tena. {TN9: 8.1}

Kutoka kwa aya ambazo zimetangulia, tunaona kwamba wakati aya za kwanza ishirini na mbili za Yeremia 4 hunena dhidi ya uovu wa Israeli ya kale, aya ya ishirini na tatu hadi ya ishirini na saba ni aya zilizoingizwa kati, na hutangaza uharibifu wa dunia na uharibifu wa waovu wote popote watakapo kuwa. Kwa kuziacha aya zilizoingizwa kati, uendelevu wa wazo unaunganishwa: {TN9: 8.2}

“Kwa maana watu Wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa. . . Kwa ajili

8

ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu Mimi nimeyanena haya, na kuya-kusudia, wala Sikujuta wala Mimi sitarudi nyuma niyaache.” Yer. 4:22, 28. {TN9: 8.3}

Na wazo likiwa limeunganishwa hivyo, ukweli unatokea kwamba katika aya ya ishirini na nane, “Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi,” kiwakilishi-nomino hayo hupata chimbuko lake la kutangulia, “uovu,” katika aya kabla ya wazo la aya zilizoingizwa katikati. Yer. 4:23-27, kwa hivyo, zimeingizwa katikati kuonyesha kwamba kama vile Mungu hakuwachilia watu Wake wa kale kwa uovu wao, vivyo hivyo Yeye hawezi kuuwachilia ulimwengu leo kwa uovu wake, ila Yeye atazishughulikia sawa dhambi zote iwe ni zinafanyika kanisani au duniani. Kwa ufupi Mungu ananena kwa watu Wake, Israeli: kwa uovu kama wako “nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi.” Je Mimi, mnadhani nitawachilia ninyi? {TN9: 9.1}

Ilhali, hata hivyo, katika Yeremia 4, Bwana ananena dhidi ya Israeli, ingawa anamaanisha kwa uharibifu wa dunia, katika Isaya Yeye ananena dhidi ya dunia na kuipendelea nchi ya Israeli, akisema: “Bali kwa haki Yeye atawahukumu maskini, Naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; Naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa Chake, na kwa pumzi ya midomo Yake atawaua wabaya.” Isa. 11:4. Iwapo upo uwezekano wowote wa kuelewa Yeremia 4 kuihusu tu nchi ya Israeli, hapo

9

hakika hakuna chochote cha kukanusha andiko hili kutoka katika Isaya 11. {TN9: 9.2}

“Muda nchi idumupo,” zaidi ya hayo, anaahidi Bwana, “majira ya kupanda na mavuno, wakati wa baridi na wa hari, wakati wa kaskazi, na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.” Mwa. 8:22. Maneno, “muda nchi idumupo,” huonyesha dhahiri kizuio cha muda, humaanisha kwamba ingawa dunia haitadu-mu daima, hata hivyo idumupo, hali zilizotajwa zitatawala. {TN9: 10.1}

Pia: “. . . Bwana akasema moyoni Mwake, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala Sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.” Mwa. 8:21. Na kuongezea azimio hili, Yeye anaahidi: “Hii ndio ishara ya agano Nifanyalo kati Yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde Wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi. Hata itakuwa Nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, Nami nitalikumbuka agano Langu, lililoko kati Yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; Nami nitauangalia nipate kulik-umbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai chenye mwili kilichoko katika nchi. {TN9: 10.2}

10

“Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndio ishara ya agano nililoliweka kati Yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.” Mwa. 9:12-17. {TN9: 11.1}

Ingawa katika maandiko haya Bwana ameapa kamwe hataharibu kwa mafuriko tena kila kiumbe hai, Hapeani ahadi ya kutowaangamiza waovu kwa njia nyingine. Kwa maneno mengine, uhakikisho pekee unaotolewa katika maandiko yaliyotajwa hapo juu ni kwamba hakutakuwa na mafuriko mengine kwa ulimwengu wote. Zaidi ya hili, hata hivyo, haitadumu. Kutoka kwa yote maingilio ya maadili na ya busara pamoja na ya Maandiko, cha mwisho na kikomo kabisa cha miili yote itakayoangamizwa, ni hitaji kamili

Wakati Wa Kuja Kwa Kristo. {TN9: 11.2}

Kusema waziwazi kwamba miji hiyo itabomolewa “mbele ya Bwana, na kwa hasira Yake kali” (Yer 4:23-26), na si kwa mafuriko au kwa mamlaka ya mataifa, Biblia hufunga kabisa mlango kwa jaribio lolote la kupotosha unabii huu kwa namna ya kufanya uwezekano wa utimizo wake kuwa wakati mwingine isipokuwa ule wa kuonekana kwa Bwana. Kisha Yeye “Mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza,” pia “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa Chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo Kwake.” 1 Thes. 4:16; 2 Thes. 2:8. {TN9: 11.3}

11

Kwa sababu, zaidi ya hayo, mapigo saba ya mwisho (Ufu. 16) ni, inavyoeleweka sana, yataanguka kwa wale ambao hawakutubu baada ya kufungwa kwa muda wa rehema na kabla ya kuonekana kwa Bwana, na kwa sababu kukusanywa kwa watu wa Mungu kutatangulia mapigo (maana sauti kutoka mbinguni ilisema, “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” — Ufu. 18:4), lazima, tu kabla mapigo kumiminwa, na kabla Kristo kuonekana mara ya pili, wenye haki wote walio hai, kwa usalama wao, watatenganishwa na dhambi na wadhambi, ili wasije wakaangamizwa pia. {TN9: 12.1}

Kufuatia kumiminwa kwa pigo la saba, “miji ya mataifa ilianguka,” unasema Ufunuo, “na kila kisiwa kika-kimbia, wala milima haikuonekana tena” (Ufu. 16:19 20), kuonyesha tena kwamba wakati wa kuonekana kwa Kristo dunia itafanywa kuwa utupu na ukiwa; ya kwamba wale watakaoishi na kutawala pamoja Naye itawapasa kuokolewa na kukingwa kabla ya kuonekana Kwake; na kwamba baada ya hapo hakutakuwa na muda wa rehema tena. Kisha watafufuka waliokufa ndani ya Kristo: “Kwa sababu Bwana Mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” 1 Thes. 4:16, 17. {TN9: 12.2}

12

Kizazi cha millenia cha amani ni hivyo, waziwazi, kitatumika, si kwa dunia, ila katika “majumba” huko juu, kwa maana ahadi ya Bwana ni: “Nyumbani mwa Baba Yangu mna makao mengi; kama sivyo, Ninga-liwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi Mimi nikienda na kuwaandalia mahali, Nitakuja tena niwakaribishe Kwangu; ili nilipo Mimi, nanyi mwepo.” Yoh. 14:2, 3. {TN9: 13.1}

Hivyo, wakati wa Kristo kuonekana mara ya pili, wote wenye haki na waovu wote wanapokea mishahara yao: watakatifu waliokufa wanafufuliwa kwa uzima wa milele, na watakatifu walio hai wanabadilishwa kuwa wa kutokufa kwa kufumba na kufumbua jicho, na kisha pamoja na waliofufuliwa kupelekwa mbinguni (1 Kor. 15:52, 53, 1 Thes. 4:15-17) ilhali waovu walio hai wanaingia ndani ya makaburi yao (2 Thes. 2: 8; Isa. 11:4; Ebr. 10:27; Luka 19:27). Na kwa sababu tangu ufufuo wa watakatifu wote hadi ufufuo wa waovu wote (Ufu. 20:5), inanyooka miaka elfu (millenia), kipindi hiki, dhahiri, basi, hakiwezi kuwa wakati wa kupokea thawabu, ila badala yake lazima kiwe wakati ambao wenye haki wanafurahia mbinguni tuzo walizopokea tayari, na ambacho waovu wanapumzika katika makaburi yao. {TN9: 13.2}

Kati ya wale ambao wataangamia wakati wa kuonekana kwa Bwana, Isaya husema: “. . . watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.” Isa. 24:22. Wakiwa gerezani “siku nyingi,” hawa waovu dhahiri ni ambao ha-wakuwa hai “tena

13

hata itimie ile miaka elfu” (“siku nyingi”) “zimetimia” (Ufu. 20:5), wakati “watajiliwa” — kuitwa kutoka makaburini mwao kupokea tu, baada ya kukaa muda mchache, mauti ya pili, yakisababishwa na “moto” ukishuka “kutoka kwa Mungu mbinguni.” (Angalia Ufunuo 20:9, 14.) {TN9: 13.3}

“Mauti ya pili” ni mwisho na kikomo kabisa cha waovu. Kwa wenye haki, hata hivyo “haina nguvu,” na wanatawala milele baada ya hapo katika nchi iliyoumbwa upya (Ufu. 20:6; Dan. 7:27). Wao ni waliokom-bolewa wa vizazi vyote, — umati mkubwa wa watakatifu, — na hata hivyo watakuwa kama wachache tu kwa kulinganisha na mkusanyiko wa vikosi vingi vya watu waovu tangu wakati wa Kaini hadi kufungwa kwa muda wa rehema, wasioweza kuhesabika “kama mchanga wa bahari.” Ufu. 20:8. {TN9: 14.1}

Kwa hivyo ni dhahiri kwamba ingawa wakati wa kuonekana Kwake, Bwana “ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa Chake, na kwa pumzi ya midomo Yake atawaua wabaya.” (Isa. 11:4), iwe ni washiriki wa kanisa au la, Yeye atawahifadhi na kuwaacha wenye haki. Kwa hivyo,

Wenye Haki Ndiyo “Walioachwa.” {TN9: 14.2}

Kutoa unabii, alivyofanya Yeremia, wa kuharibiwa kwa dunia, Isaya husema: “Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake. . . Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa

14

dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndio sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndio sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu. . . Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana. Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.” Isa. 24:1, 4-6, 19, 20. {TN9: 14.3}

Aya hizi, zinabeba uendelezaji wa wazo, huelezea kile Bwana atafanya kwa dunia ilhali zile zilizoachwa (Isa. 24:2, 3, na 7 hadi 18 pamoja), jinsi zilivyoonyeshwa na alama za kuruka, husheheni mawazo yaliyoingizwa kati zikielezea namna Yeye atakavyofanya, na kutangaza kwamba Atawapa daraja moja la watu baraka zote, na kuleta kwa daraja lingine laana zote. Aya ya 2 na ya 3 hufunua dunia ikifanywa utupu wa wakazi wake wote, bila kujali nafasi ya mtu yeyote, iwe ni ya heshima au ya aibu — kutoka kwa kuhani wa kicho mpaka mtumwa wa chini. Na aya ya 4 hadi ya 12 hufichua kwamba furaha yote itaondolewa kwa watu; ya kwamba maafa makubwa yatawasonga kabla ya dunia kufanywa tupu; na ya kwamba “Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.” Isa. 24:13. Kwa ufupi, aya hizi huonyesha kwamba kabla tu kuifanya utupu nchi, kutakuwa na upepeto mkuu kati ya

15

watu, na matokeo kwamba wote ambao hawapatikani imara katika Kristo, — Njia, Kweli, na Uzima (Yoh. 14:6), — wataanguka; ilhali wale wanaopatikana kuwa imara, watakuwa “walioachwa,” na hivyo kuwa

Waliotakaswa — Watasimama Milele. {TN9: 15.1}

“Hawa watapaza sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga kelele toka baha-rini.” Isa. 24:14. “Basi,” anashauri nabii kwa mtazamo wa matumaini haya, “mtukuzeni Bwana katika mashariki, litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.” Isa. 24:15. {TN9: 16.1}

Kwa kumshangilia Bwana wakati wanapitia “moto” (majaribio — 1 Pet. 4:12), waaminifu “watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan. 12:10. {TN9: 16.2}

“Lakini ni nani,” anauliza nabii Malaki, akinena kwa wakati huu na tukio hilo, “atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa,

16

Naye atawatakasa wana wa Lawi, Atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3:2, 3. {TN9: 16.3}

Kundi hili lililotakaswa ambalo litasimama imara wakati wa upepeto katika nchi (kanisa — Isa 19:24), pia linaletwa kwa mtazamo katika unabii wa Isaya, sura ya 24, aya ya 14: “. . . wataimba kwa utukufu wa Bwa-na”; ilhali katika aya ya 16 linaonyeshwa kundi andamo lililotakaswa ambalo limekusanywa “kutoka pande za mwisho wa dunia,” na kutoka kwao “wataimba, hata utukufu kwa wenye haki.” Upepeto, kwa maneno mengine, unawaleta ndani malimbuko na mavuno ya pili ya watakatifu — moja kutoka kanisani, “kati ya nchi,” na lingine kutoka ulimwenguni, “pande za mwisho wa dunia.” Na wakati wale kutoka ndani ya ka-nisa “wanaimba utukufu kwa Bwana,” wale wa kutoka ulimwenguni wanaimba “utukufu kwa wenye haki.” {TN9: 17.1}

Hivyo tunaona dhahiri kwamba waliokombolewa kutoka ndani ya kanisa — watumwa wa Mungu (malimbuko, au mzaliwa wa kwanza — neno la Kibiblia kwa ajili ya ukuhani au ukasisi) — wanasimama imara wakati wa upepeto “kati ya nchi,” na matokeo ya kwamba wao wanaupeleka ukweli kwa mataifa yote wakati wa “upepeto” ulimwenguni, na hivyo kuupeleka wokovu kwa wengi. Makundi haya mawili ya walio hai ni lazima, kwa hivyo, ni waliokombolewa pekee ambao wanasalia baada ya upepeto. Wao wamehifadhi-wa, “wameokolewa,” kutoangamizwa, kwa sababu majina yao

17

“yanapatikana yameandikwa katika kitabu.” Dan. 12:1. Na ya kwamba “hawajaachwa” kwa nchi wakati imeachwa katika hali yote ikiwa imevunjika, ukiwa, na tupu, ila badala yake “wameachwa” kutoangamizwa, Isaya, mwenyewe, anaweka wazi wakati anaposema “ndio sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.” Isa. 24:6. Maneno haya hayamaanishi hata kwamba waliokombolewa wanasalia duniani wakati wa uharibifu wake, lakini “wameachwa,” wamesazwa, kutoka kwa uangamizi. {TN9: 17.2}

Kuziunganisha kweli zilizo mbele yetu, tunapata kwamba millenia inakaribishwa na msururu wa matukio ya mara sita yakitukia kwa utaratibu ambao yametajwa: (1) Mungu kuwaangamiza wanafiki ndani ya kani-sa; (2) kuwaita Walio Wake kutoka katika mataifa, na kisha kuwaingiza ndani ya kanisa lililotakaswa — Ufalme; (3) kufunga muda wa rehema; (4) kuwaangamiza waovu; (5) kuwafufua wafu wenye haki na ku-wahamisha bila kufa wenye haki walio hai; (6) na mwisho, kuifanya dunia ukiwa. {TN9: 18.1}

Pamoja na kilele cha matukio haya sita ya mwisho, ambayo Biblia huyaita mwisho wa dunia, pazia kuteremshwa milele kwenye sarakasi ya vizazi virefu ya dhambi na ukombozi. Kabla yake, hata hivyo, “ha-bari njema ya ufalme [ishara za mwisho (Mat. 24)],” alisema Kristo, “itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote [sasa]; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mat. 24:14), na itatimia, kama ilivyoandikwa: “. . . Mbingu zikaondolewa kama ukurasa

18

unavyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.” Ufu. 6:14. “Maana Bwana asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa” kuongeza hata hivyo: “lakini Sitaikomesha kabisa.” (Yer. 4:27) — akiacha ahadi ya

Dunia Kufanywa Upya. {TN9: 18.2}

Akitazama mbele hadi kwa kuvunjika kwa dunia, Mtume Petro anasema: “. . . Lakini, kama ilivyo ahadi Yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.” 2 Pet. 3:13. {TN9: 19.1}

Na Yohana Wa-ufunuo, aliruhusiwa katika maono ya unabii kuona baada na kabla ya millenia, anaandika: “. . . Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zime-kwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye atafanya maskani Yake pamoja nao, [ilhali wakati wa miaka elfu, watakaa pamoja Naye (Ufu. 20:4)] nao watakuwa watu Wake. Naye Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. {TN9: 19.2}

19

“Na Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, Nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Ome-ga, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa Mwanangu. Bali waoga, na wasi-oamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, se-hemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” Ufu. 21:1-8. {TN9: 20.1}

Kwa sababu manabii na Wa-ufunuo, pia, waliona nchi ya kwanza na mbingu ya kwanza zikitoweka na mpya zikichukua nafasi, mtu yeyote angekuwa kama mpumbavu iwapo angeweza kutokuwa mwaminifu kwa kuukataa na kuupinga ukweli huu wazi, na hivyo kujidanganya na kuwakanganya wengine. Hivyo hitaji ni la haraka sana kwamba wote wazingatie kwa uangalifu zinazotokea

Sababu Zaidi. {TN9: 20.2}

Kama dunia isingeharibiwa mwanzoni mwa millenia, hitaji gani lingekuwapo la kufanya “vitu vyote upya”? Ufu. 21:5. Iwapo, zaidi ya hayo, wakati wa kizazi cha millenia watakatifu hawangepaswa kukaa mbinguni, basi halingekuwapo hitaji la kuwa na “Yerusalemu mpya” (Ufu. 21:2, 10) huko. Na iwapo, isitoshe,

20

watakatifu wakati huo waishi duniani, Sauti ya Unabii haingalisema waliishi “pamoja na Kristo,” ila badala yake Kristo aliishi pamoja nao. Na hatimaye, iwapo watatawala pamoja Naye kwa nchi, pale ambapo wa-taishi milele, unabii haungesema kwamba “walitawala pamoja na Kristo miaka elfu,” ila badala yake kuta-wala pamoja Naye milele. {TN9: 20.3}

Alisema Yohana, alipotazama mbele kwa wakati ambao Kristo ataishi na kutawala pamoja nao duniani: “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo Wake, Naye atamiliki hata milele na milele.” Ufu. 11:15. “Na ufalme na mamlaka,” asema Danieli, kuhusu watakatifu “kutawala pamoja Naye,” na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu Wake Aliye juu; ufalme Wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.” Dan. 7:27. {TN9: 21.1}

Mbinguni waliokombolewa watatawala pamoja na Kristo miaka elfu tu, ilhali duniani Yeye atatawala pamoja nao milele na milele; maana “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.” Zab. 115:16. “Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; Ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; Ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.” Isa. 45:18. {TN9: 21.2}

21

Kuona kwamba Maandiko husema mengi juu ya “mbingu,” pia kuhusu “mbingu ni mbingu za Bwana,” alifanya jukumu jipya, kwa hivyo, la kuhakiki tofauti kati ya mbinguni na mbingu ni mbingu za Bwana hutua kwa kila mtu anayetafuta ukweli. Kwa mujibu wa mwisho wa umbali huu, tunapaswa kuzingatia kwanza

Mbingu Hapo Mwanzo. {TN9: 22.1}

“Na liwe anga katikati ya maji,” akasema Bwana, hapo akiumba dunia, “likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu.” Mwa. 1:6-8. {TN9: 22.2}

Hapo mwanzo, “Bwana Mungu alikuwa hajainyeshea,” hebu tukumbuke, “nchi mvua” (Mwa. 2:5), na maji yalikuwa “juu ya anga” na “chini ya anga”; na anga, Aliliita “Mbingu.” Mwa. 1:7, 8. Maji haya yaliyoga-wanyika hayawezi kuwa maji katika mawingu, ambayo sasa hutumika kuinyunyiza ardhi, kwa kuwa maji ya juu hayakuwa katikati ya anga, kama yalivyo mawingu, ila juu yake. Hivyo kama vile dunia ilikuwa imezungukwa na anga, vivyo hivyo pia anga lilizungukwa na maji. Dunia ilikuwa, kwa maneno mengine, iliyozongwa maradufu, jinsi ilivyoonyeshwa katika kielelezo, — kwanza kwa anga; kisha kwa maji. {TN9: 22.3}

22

Kwa sababu zote anga na maji zilikuwa maanga, na maji yaliunda tu blanketi nyembamba kulizunguka anga, mionzi ya jua iliangaza juu ya nchi kwa uangavu tu kama vile inavyofanya sasa. Na kwa sababu, pia, mionzi ya jua wakati huo ilipasha

23

moto maji kabla ya kupoa na kupita kwenye bamba nzito la anga, ilikuwa moto wakati ilifikia maji juu ya anga kuli-ko ilivyo sasa chini ya anga wakati inapofika kwa nchi. Ikiwa kwanza imeenezwa na maji, mionzi iliyafanya moto; nayo, kwa kusambazwa kwa lile anga, maji ya moto yalifanya ujotojoto kwa dunia sawasawa kila mahali — kwenye ncha na pia kwenye ikweta. Tofauti tu katika joto ilikuwa tukio la uwepo wa mwanga (mchana) na kutokuwepo kwa mwanga (usiku). Kwa hivyo, basi, kama sasa, usiku ulikuwa navuguvugu kuliko mchana. Lakini kwa vile hali hii hai-po tena, ni dhahiri kwa wakati fulani janga lilisababisha

Kuvunjika Kwa Mfumo-Joto Wa Dunia. {TN9: 23.1}

Hapo mwanzo, kanda zenye barafu za sasa za ncha zilinawiri kwa mimea na kujaa wanyama ambao wanajiolojia sasa hupata wamehifadhiwa katika barafu. Ni nani, basi, angeweza kuwa na shaka kwamba maji “juu ya anga” yaliku-wa mfumo wa dunia wa kusawazisha joto? Lakini mara tu maji, kwa utimizo wa utabiri wa Nuhu, yalianza kushuka, — kwa kweli, hata kabla ya kupata nafasi yoyote ya kushuka kwenye maeneo ya chini ya dunia, — mfumo huu asili wa kisawazisha joto ulivunjika haraka, na mvua, ilipokuwa ikianguka juu ya nchi, ikaganda kwa ghafla katika kanda za ncha ambazo wanyama waliokuwa wangali hai wakaganda nayo: hakika hawakuwa na wakati hata wa kumeza

24

chakula chao, kama inavyothibitishwa na ufukuaji wa wanajiolojia tofauti tofauti. {TN9: 24.1}

Dunia, sasa ikiwa bila mfumo wake wa kusawazisha joto, inaathiriwa na joto kali wakati jua lipo katika nafasi ka-ma ile ya kupitisha mionzi yake kwa bamba nyembamba la anga ilivyo adhuhuri, wakati jua linaangaza moja kwa mo-ja chini badala ya juu ya mshazari; na hata kwa joto kali wakati kuna uwiano wa angahewa, kama ule unaosababishwa na unyevu na kimo cha chini; ilhali hali kinyume na hizi, huleta kinyume chake kabisa. Kubadilika-badilika, kwa an-gahewa ya kinyume chake kabisa iliyoletwa na gharika, ni moja nyingine tu ya matokeo ya laana ambazo ziliandama kutokuamini kwa mwanadamu katika maonyo na makemeo ya Mungu, na kutozitii amri za Mungu. {TN9: 25.1}

Hiki chenye shida kilichovunjika kisawazisha joto cha Asili, pamoja na matokeo ya hali mbaya kwa dunia, yote ambayo hulilia si tu kwa ajili ya nchi mpya, ila pia kwa mbingu mpya, yanageuza umakini wetu kwa

Mfumo Wa Jua Na Sayari Zake. {TN9: 25.2}

Uvuvio hutangaza kwamba jua liliumbwa siku ya nne ya juma la uumbaji, na sayansi ya unajimu imegundua kwamba katika mfumo wetu wa jua zipo nje ya Dunia sayari zingine nane zinazotegemea jua kwa nuru, nishati ya jo-to, na kawi ya uhai . (Uwezekano ni kwamba sayari zingine tatu

25

zitagunduliwa, maana kwa mujibu wa Mwanzo 37:9 na kweli zingine, lazima unahitajika kuwa na sayari kuu kumi na mbili katika mfumo wetu wa jua.) Katika juma la uumbaji, kwa hivyo, Mungu lazima hakuumba si tu dunia bali pia mfumo wote wa jua. Vinginevyo, sayari zilizopo bila faida ya ushawishi wa kuendeleza maisha wa jua, zingekuwa lazima zimeathirika kuwa ukiwa na kwa ujumla kuwapo bila maana kabisa. Uvuvio, zaidi ya hayo, husema pia kwamba katika juma la uumbaji, Mungu aliumba dunia, jua, mwezi, na “nyota pia.” Mwa. 1:16. {TN9: 25.3}

Bila jua, mfumo wetu wa jua ungekuwa tu rundo la sayari bila kitengo cha kuzithibiti, ulioachwa kuwayawaya na kugongana dafrao angani, kudumu tu, kwa ghafla isiyokuwa na huruma ya hali ya bahati nasibu, mfululizo usiokuwa na mwisho wa migongano ya kiajali. Zimeumbwa na kuwekwa kwa mwendo pamoja, ingawa, kwa Mkono ambao huzidumisha, sayari zote kwa usalama hufuata jua linapoangaza katika anga kwa kasi kubwa ya maili 400,000,000 kwa mwaka. {TN9: 26.1}

Mbingu yetu na dunia, kwa hivyo, zikiwa sehemu katika mfumo wa jua, basi zote kutoweka na kufanywa upya lazima kuuhusisha mfumo wote. Si tu mbingu yetu, kwa hivyo, lakini pia

Hitaji La Mbingu Ni Mbingu Za Bwana Kufanywa Upya. {TN9: 26.2}

Kila mojawapo wa sayari katika mfumo wetu wa jua zikiwa zimezungukwa na anga lake au mbingu,

26

zipo, kwa hivyo, mbingu nyingi (anga) kama zilivyo sayari katika huo mfumo. Kwa “mbingu” hizi za sayari hutumika kwa maandiko yafuatayo: {TN9: 26.3}

“Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi.” Yer. 4:28. “Na jeshi lote la mbinguni litafumu-liwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.” Isa. 34:4. {TN9: 27.1}

“Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.” 2 Pet. 3:10. {TN9: 27.2}

“Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zote zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, nazo zitabadilika.” Zab. 102:26. {TN9: 27.3}

“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele Yangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.” Isa. 66:22. {TN9: 27.4}

Kama tokeo la dhambi kwa dunia, ambalo husababisha viumbe vyote kuugua (Rum. 8:22), jamii yote ya jua imeteseka. Maandiko yaliyotangulia huonyesha kwamba si tu dunia, bali pia mbingu za Bwana, zimechakaa

27

chini ya laana ya dhambi; ya kwamba dhambi ni ugonjwa wa kuambukiza ulio na matokeo makubwa; kwamba “Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.” (1 Kor. 12:26); ya kwamba Mungu ataiondoa dhambi kabisa na hivyo kwamba Yeye atafanya ukiwa si tu dunia, bali pia mfumo wote wa jua; na kwamba wakati anaiumba dunia mpya, Yeye ataufanya upya mfumo wa jua pia! {TN9: 27.5}

“Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.” Nah. 1:9. “Akaniambia, andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.” Ufu. 21: 5. {TN9: 28.1}

“Angalieni,” Yeye anasema zaidi, akinena kwa mtazamo wa siku ambayo Yeye atatekeleza “atakomesha kabisa,” “Nitawatumia Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.” Mal. 4:5. Kwa hivyo maneno ya Yesu: “ Kweli Eliya yuaja kwanza, naye”

“Atarejesha Vitu Vyote.” Mat. 17:11. {TN9: 28.2}

Ingawa vilipotea kupitia dhambi, vyote vilivyoumbwa hapo mwanzo vitarejeshwa katika “nyakati za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii Wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.” Mdo. 3:21. Akiwa ameumba bahari kabla ya mwanzo wa dhambi, basi kuiondolea mbali baada ya kuangamizwa kwa dhambi, kama wengine wanavyofundisha

28

kwamba Yeye atafanya, hakika hakutakuwa Kwake kurejesha “vitu vyote,” ila badala yake Yeye kuviondolea mbali, na kumaanisha kwamba hapo mwanzo Yeye alifanya makosa kuumba bahari hivyo kinyume cha tangazo Lake “kuwa ni vyema.” Mwa. 1:10. Maadamu, zaidi ya hayo, nyoka, si bahari, alimsababisha Adamu na Hawa kutenda dhambi (Mwa. 3:1-7), na kwa sababu nyoka atakuwa katika ufalme uliorejeshwa (Isa. 65:25), kwa nini, basi Mungu aiondolee mbali bahari? {TN9: 28.3}

“Bwana ni Mungu mwenye wivu,” atangaza nabii Nahumu katika maono yake ya wakati wa mwisho “Naye hu-jilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, Naye ni mwingi wa hasira; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui Zake, huwawekea adui Zake akiba ya hasira. Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia Yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu Yake. Yeye huike-mea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; hulegea nalo ua la Lebanoni. Milima hutetema mbele Yake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele ya uso Wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake. Ni nani awezaye kusimama mbele ya ghadhabu Yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira Yake? Hasira Yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na Yeye. Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; Naye huwajua hao wamkimbiliao. Lakini kwa gharika ifurikayo

29

Atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui Zake hata gizani. Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakome-sha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.” Nah. 1:2-9. {TN9: 29.1}

“. . . Nikaona” asema Yohana Wa-ufunuo, pia baada ya kutazama kuharibiwa kwa dunia,”mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.” Ufu. 21:1. {TN9: 30.1}

Ni lini hapakuwa na bahari tena? — Wakati ambapo mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza ilitoweka. Maandiko hayasemi kwamba haitakuwapo bahari tena katika nchi mpya. Husema tu kwamba “wala hapana bahari tena” wakati ambapo mbingu na dunia zilikuwa katika hali ya kuondolewa — “zimetoweka.” Kwa maneno mengine, sehemu ya kwanza ya aya huonyesha “mbingu mpya na nchi mpya,” ilhali sehemu ya mwisho hutabiri juu ya kutokuwepo bahari tena kabla ya “mbingu mpya” na “nchi mpya” kufanywa. {TN9: 30.2}

Hivyo kwa mwisho kabisa wa Neno Lake Mwenyewe Bwana atavileta vitu vyote kwa kikomo, hata kukausha mito na bahari wakati ambapo Yeye anaiondoa kabisa dhambi. {TN9: 30.3}

Maana pamoja na mbingu na nchi yetu, kwa hivyo, mfumo wetu wote wa jua utapita, si tu watakatifu kutoka du-niani, wakati huo, lakini pamoja nao pia wana wa Mungu

30

kutoka kwa mfumo wote, wataishi na kutawala pamoja na Kristo Mbingu za mbingu kwa miaka elfu moja! O, ni fadhili ya ilioje! Ni fursa ya namna gani! Ni mkusanyiko ulioje utakaokuwa! {TN9: 30.4}

“Nimeona upendo mwororo ambao Mungu anao kwa watu Wake, na ni mkuu sana. . . Mbinguni ni mahali paz-uri. Natamani kuwa huko, na kumtazama mpendwa wangu Yesu, ambaye aliutoa uhai Wake kwa ajili yangu, na ni-badilishwe kuwa chapa ya utukufu Wake. O, kwa lugha ya kusimulia utukufu wa ulimwengu mwangavu ujao! Nina kiu kwa mito iliyo hai inayoufanya furaha mji wa Mungu wetu.” — Maandishi ya Awali, uk. 39. {TN9: 31.1}

Tuzo hii yenye utukufu sana humchochea mmoja kujifunza zaidi kuujua ukweli. Kwa Ufunuo, kukunjua kwa unabii, kwa hivyo, mmoja ameelekezwa kwa uchunguzi muhimu wa

MATUKIO YA MILLENIA. {TN9: 31.2}

Hebu tuangalie kwa makini maandiko ambayo hunakili mambo ambayo yatatukia kabla tu ya miaka elfu kuanza — mambo ambayo yatasababisha kizazi cha millenia ya amani, jinsi yalivyofunuliwa kwa Yohana: {TN9: 31.3}

“. . . Nalitazama . . . farasi mweupe, na Yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wakweli . . . Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina Lake aitwa, Neno la Mungu . . . Naye ana jina limeandikwa katika vazi Lake na paja Lake,

31

“MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.” Ufu. 19:11, 13, 16. {TN9: 31.4}

Hapa Kristo anajifunua Mwenyewe, si kama kuhani au kama mwana-kondoo, bali kama Mfalme wa wafalme, akikanyaga “shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.” Ufu. 19:15. Hii ni Yake

Kuwachinja Waovu Wote. {TN9: 32.1}

“Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua…akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na Yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi Yake. {TN9: 32.2}

“Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, am-bazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule

32

farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.” (Ufu. 19:17-21) — kazi ya mwisho ambao inaonekana kwa urahisi kwamba waovu

Wanachinjwa tu kabla ya Millenia. {TN9: 32.3}

Kwa sababu baada ya millenia, waovu hawatauawa na nyama yao haitaliwa na ndege, ila badala yake kuangamizwa kwa moto (Ufu. 20:9), Ufunuo 19:17-21 inaonekana kutaja uangamizaji wa kabla ya millenia. {TN9: 33.1}

Kwa uamuzi, kwa hivyo, Mfalme wa wafalme atawachinja, kabla tu ya millenia, wote isipokuwa wenye haki — isipokuwa wale wanaopata “kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake.” Ufu. 15:2. Kisha watakatifu waliokufa watafufuliwa, ilhali waovu waliokufa watakabaki makaburini mwao, pamoja na waovu watakaokuwa hai, ambao wote watauawa na Bwana, hawataishi “hata miaka elfu” “imetimia.” Ufu. 20:5. {TN9: 33.2}

Kwa sababu, zaidi ya hayo, mwanzoni mwa millenia, wakati waovu wanauawa, mbingu na nchi zinatoweka, kisha, kama tokeo,

Watakatifu Wanahamia Eneo Lingine. {TN9: 33.3}

Jinsi ambavyo Ufunuo husema kwamba “waliishi na kutawala pamoja na Kristo miaka elfu” (Ufu. 20:4), Kristo kwa hivyo haishi,

33

nao duniani, lakini badala yake wanaishi Naye “mahali” ambapo Yeye aliwaandalia, na ambapo Yohana anasema (baada ya kuona “mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimetoweka” na kubadilishwa na “mbingu mpya na nchi mpya” — Ufu. 21:1). “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwi-sha kupita, wala hapana bahari tena.” Ufu. 21:2. {TN9: 33.4}

Waovu wakiwa wamefichwa katika makaburi yao, na wenye haki wakiwa wameenda kuishi na Kristo, kwa hivyo

Shetani Anaachwa Pekee Yake. {TN9: 34.1}

Akitangatanga duniani hadi ufufuo wa waovu (Ufu. 20:13), Shetani amefungwa kwa miaka elfu ya upweke! Akiwa amefungwa na msururu huu wa hali, hawezi “kuwadanganya mataifa” (Ufu. 20:3), hadi wafu ambao “hawakuishi tena hata miaka elfu itimie,” waishi tena, baada ya

Hukumu Wakati Wa Milenia. {TN9: 34.2}

Iwapo hakimu wa kidunia hawezi kumtia hatiani na kumhukumu mhalifu bila manufaa ya kesi na jopo la majaji, hakika, basi, mwenye haki yote Mungu wa Mbinguni hawezi. Hawezi kupitisha hukumu ya mwisho kwa waovu, kuwathibitishia dhambi na kuwahukumu kufa “mauti ya pili” (Ufu. 20:14), hata baada ya kuwapa watakatifu (jopo la majaji) fursa ya kushuhudia wenyewe hukumu ya waovu — waume, wake, watoto, jamaa,

34

marafiki, na wanaowafahamu wakati huo wasiokuwa kwenye majumba ya juu — na kuzikagua kumbukumbu zao zi-nazoonyesha kwa nini hawako pale, ila badala yake wanaoza ndani ya makaburi yao chini. {TN9: 34.3}

Kwamba hakuna sababu iachwe kwa mtu yeyote kwa ajili ya ujinga au kosa kwa ukweli huu, Yohana hakuonye-shwa tu kiti kikuu cha enzi cheupe ambacho huketi Jaji wa Milele, “ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso Wake,” (Ufu. 20:11) , ila pia viti vya enzi vingine, au viti, ambavyo bila shaka hukaa jopo la majaji. Na badala ya “elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,” (Ufu. 5:11) wa malaika kama mashahidi, aliona wakiwapo katika tukio hilo pia “roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu . . . Huo ndio ufufuo wa kwanza.” Ufu. 20:4, 5. {TN9: 35.1}

Ukweli, hata hivyo, kwamba “hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.” (Ufu. 20:5), hu-onyesha kwamba wale waliokuwa mbele ya kiti cha enzi walifufuliwa. {TN9: 35.2}

Lakini waliokufa, “wadogo kwa wakubwa,” ambao hawataamka katika ufufuo wa kwanza (Ufu. 20:6), Yohana aliona ki-mfano “wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguli-wa, ambacho ni

35

cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufu. 20:12. Pamoja na kufunga kwa kazi hii, yaja matukio

Baada ya Hukumu. {TN9: 35.3}

Wakati hukumu ilikuwa imekwisha na miaka elfu imepita, “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Ufu. 20:13. {TN9: 36.1}

“Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye atafanya maskani Yake pamoja nao, nao wa-takuwa watu Wake. Naye Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” Ufu. 21:2-4. {TN9: 36.2}

Baada ya kushuka pamoja na watakatifu, ambao watatawala milele pamoja Naye katika nchi iliyofanywa upya, Kristo anawaita waovu waliokufa kutoka makaburini mwao, ambapo sambamba “sauti kubwa kutoka mbinguni” inasikika, “ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye

36

atafanya maskani Yake pamoja nao” (Ufu. 21:3), ilhali wakati wa miaka elfu, “wameishi” pamoja Naye (Ufu. 20: 4). Halafu,

Shetani Anafunguliwa Kwa Muda Mchache. {TN9: 36.3}

Kwa ufufuo wa waovu waliokufa, “. . . Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.” Ufu. 20:7, 8. {TN9: 37.1}

Mintarafu “muda mchache” ambamo Shetani ataruhusiwa kuwadanganya mataifa, nabii Isaya alimsikia Bwana akinena: {TN9: 37.2}

“Maana, tazama, Mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala haya-taingia moyoni. Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi Niviumbavyo; maana, tazama, Naumba Ye-rusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Nami nitaufurahia Yerusalemu, Nitawaonea shangwe watu Wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.” Isa. 65:17-20. {TN9: 37.3}

Msomaji ataona kwamba wakati Bwana anaumba mbingu mpya na nchi

37

mpya basi, tangu wakati ambao waovu wanaamka kutoka makaburini mwao hadi wakati watakapoangamizwa milele kwa mauti ya pili, — “muda mchache,” — “hatakuwapo tena [miongoni mwao] mtoto wa siku chache [hakuna kuzaa tena], wala mzee asiyetimia siku zake [tena hakuna kifo kabla ya siku za mtu kutimia]; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.” Wote wazee na wachanga (yaani, wale ambao wanabaki katika makaburi yao wakati wa millenia) baadaye watatokea pamoja, kila mmoja kuishi “miaka mia moja” — “muda mchache” ambao Shetani atawadanganya tena. Hakutakuwa na kifo wala kuzaa, ila wote waovu baadaye watalaniwa milele kwa

Mauti Ya Pili. {TN9: 37.4}

Sehemu hiyo ya nchi mpya ambayo miguu ya waovu itakuwa imekanyaga na kuitia unajisi wakati wa “muda mchache,” itatakaswa na moto utakaokuja “ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu” na kuwachoma na kazi zao, il-hali wale ambao wataimiliki nchi mpya milele, watakingwa ndani na nje kuuzunguka “mji mtakatifu.” Ufu. 21:2. {TN9: 38.1}

“Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi,

38

mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele . . . Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” Ufu. 20:9, 10, 14, 15. {TN9: 38.2}

Kwa sababu si Shetani pekee, bali pia “mtu ye yote ambaye hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto,” moto katika ziwa unaendeleza tu uharibifu unaofanywa na moto utakaokuja “ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.” Ufu. 20:9. Baada ya miaka elfu, kwa maneno mengine, moto unaokuja “ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu,” utababisha “ziwa la moto” (Ufu. 20:10) na kuwaangamiza milele wad-hambi wote. Kuhusu uharibifu huu wa mwisho, onyesho la kabla ya millenia linapeanwa wakati mnyama na nabii wa uongo wanatupwa ndani ya “ziwa la moto” — kaburi lao kwa miaka elfu. Na kwa vile moto hauendelei, bila shaka, kuwaka wakati wa miaka elfu, maneno, “ibilisi. . . akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na nabii wa uongo “ (Ufu. 20:10), yanaonyesha kwa hivyo kwamba yapo yote maangamizi ya mfano na ya uakisi; ziwa la moto kabla ya millenia, likiwa mfano wa lile baada ya millenia. {TN9: 39.1}

“Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo,” anasema mtume,

39

“Imewapasa Ninyi Kuwa Watu Wa Tabia Gani?” {TN9: 39.2}

Maandiko yanahimiza kwamba wale walio katika Kweli wawe “katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitaza-mia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi Yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hivyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele Yake.” (2 Pet. 3:11-14), na zaidi sasa ambapo Yeye

ANAUSIMAMISHA UFALME WAKE. {TN9: 40.1}

“Katika siku hiyo” (wakati ambapo Bwana anakaribia kuifanya dunia ukiwa), “atapeleka mkono Wake mara ya pi-li,” asema nabii Isaya, “ili ajipatie watu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawat-wekea mataifa bendera, Atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, Atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.” Isa. 11:11, 12. {TN9: 40.2}

Kazi ya kuwakusanya iliyowekwa katika maandiko haya, huonyesha kwamba kabla ya kufufuliwa kwa wenye haki (1 Thes. 4:16) na kabla ya kuangamizwa kwa mataifa kabla ya

40

millenia, Bwana atauanzisha kwanza ufalme Wake wa watakatifu walio hai pekee, kama unavyoonekana kutoka kwa unabii wa Danieli 2: “jiwe” likiwa “limechongwa” mlimani (Dan. 2:45), na likiwa mfano wa ufalme wa Kristo katika mwanzo wake. (Dan.2:44), basi mlima ambao limechongwa, lazima hapana shaka uwakilishe kanisa ambalo kutoka ndani yake malimbuko ya ufalme, watu 144,000, wanakusanywa. Na kama jiwe linakua na kuwa “mlima mkubwa” (Dan. 2:35) baada ya “kuchongwa,” ni dhahiri mwanzoni linawakilisha ufalme ukiwa uchanga — “malimbuko” pekee. Ukweli pia, kwamba jiwe linakua na kuijaza “dunia yote,” ni ushahidi mwingine katika uthibitisho kwamba baada ya ufalme huu uliotarajiwa kwa muda mrefu “umesimamishwa,” umati mkubwa utajiunga nao. Isingekuwa hivi, basi jiwe hilo halingekuwa “mlima mkubwa.” Kuwa kwake, isitoshe, mwanzoni sehemu ndogo sana ya mlima, huonyesha kwamba ufalme una mwanzo mdogo sana, kama anavyosema Bwana: “Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali,. . . nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote.” Mat. 13:31, 32. {TN9: 40.3}

“Mlima,” ufalme wa Mungu, dhahiri, basi, unaanzishwa na malimbuko ya walio hai (watu 144,000) na wakifu-atiwa na mavuno ya pili ya walio hai (umati mkubwa – Ufu. 7:9), na unakamilika kwa malimbuko na mavuno ya pili ya wafu — watu 120 (wale waliopokea

41

Roho siku ya Pentekoste), pamoja na wale waliofufuka na Kristo (Mat. 27:52, 53), na umati mkubwa ambao wal-impokea Yeye baada ya Pentekoste (Mdo. 5:14), na wote watakaoamka kwa uzima wa milele katika ufufuo wa Danie-li 12:2, na waliokufa wa vizazi vyote, ambao watafufuka kwa siku kuu ya ufufuo (Ufu. 20:6), pia wale wa Ezek. 37:1-14. {TN9: 41.1}

Kurejelea kwenye unabii wa Danieli, humo tunapata

Siku Ambazo Ufalme Utasimamishwa. {TN9: 42.1}

“Na katika siku za wafalme hao [si baada ya, ila , siku za wafalme ambao ni mfano wa nyayo na vidole vya sanamu kubwa] Mungu wa mbinguni,” anasema Danieli, akiitisha umakini kwa ufalme wakati wa mwanzo wake “atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali [ufalme] utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:44. Hivyo tunaona kwamba wakati mataifa ya kizazi chetu (mfano wa nyayo na vidole vya sanamu kubwa ya Danieli 2:41, 42) bado ya-po, Bwana atauanzisha ufalme ambao Yeye atatumia kuyapindua. Kisha itasemwa: “Ufalme wa dunia umekwisha ku-wa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo Wake, Naye atamiliki hata milele na milele.” Ufu. 11:15. {TN9: 42.2}

42

Akitangaza adhabu ya Israeli ya kale, nabii Hosea aliandika maandishi mazito: “. . . wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago” Hos. 3:4. Kwa wakati uo huo, hata hivyo, ahadi ilitolewa kwamba “baada ya hayo [baada ya siku nyingi] wana wa Israeli watarejea, na kumtafu-ta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema Wake kwa kicho siku za mwi-sho.” Hos. 3:5. {TN9: 43.1}

Kwa sababu Daudi wa zamani yu kaburini mwake, mfalme aliyeahidiwa hapa lazima aweze kuwa ni Daudi wa uakisi, kama vile Eliya wa Malaki 4:5 lazima aweze kuwa Eliya wa uakisi. Vinginevyo, ili kutimiza huu unabii, Daudi wa kale lazima bila shaka afufuke kutoka kwa kaburi lake, na Eliya wa kale ashuke kutoka Mbinguni. {TN9: 43.2}

Tangazo la Danieli (uk. wa 42) kwamba kwa ufalme huu wa uakisi, Bwana atayavunja-vunja mataifa, na tangazo la Yeremia (katika aya inayofuata) kwamba ni shoka Lake la vita, yanaonyesha dhahiri

Ya Ufalme Kazi Ya Kulipiza Kisasi {TN9: 43.3}

“Wewe u shoka Langu na silaha Zangu za vita,” asema Bwana kwa Israeli mamboleo (wale ambao wataujumuisha ufalme mchanga), “kwa wewe Nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe Nitaharibu falme; . . . na kwa wewe Nita-wavunja-vunja

43

mwanamume na mwanamke; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe Nitawavunja-vunja ki-jana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe Nitawavunja-vunja maliwali na maakida.” Yer. 51:20-23. {TN9: 43.4}

Andiko hili haliwezi kutumika kwa Israeli ya siku ya Yeremia, kwa maana ilikuwa ikipoteza badala ya kushinda, na tangu siku hiyo hadi leo, haijakuwa na ufalme wake. Ni dhahiri kwa hivyo Israeli wa siku hizi za mwisho ufalme, kupitia kwao ambao ni chombo chake Mungu atauleta ulimwengu huu kwa kikomo. {TN9: 44.1}

Ufalme huu unaokuja hivi karibuni usiokuwa kama ufalme wa kidunia, ila kama wa mbinguni, mipaka yake itakuwa mahali pa

Amani Kamili Na Usalama Kamili. {TN9: 44.2}

Akisifia yote mfalme na ufalme utakaoanzishwa baada ya “siku nyingi,” nabii Isaya anatangaza: “. . . bali kwa haki Atawahukumu maskini, Naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; Naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kin-ywa Chake, na kwa pumzi ya midomo Yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno Vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. {TN9: 44.3}

44

“Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwa-na-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima Wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.” Isa. 11:4-9. {TN9: 45.1}

Enzi hii iliyotabiriwa ya haki kamili, amani, na maarifa ya Mungu (katika ufalme) chini ya utawala wa “fimbo” (Daudi) na “Tawi” (Kristo), lazima ianze

Kabla Ya Kufungwa Kwa Muda Wa Rehema. {TN9: 45.2}

Maandiko huonyesha kwamba ufalme unasimamishwa kabla, badala ya, mwanzoni mwa millenia, maana “katika siku hiyo [katika siku ambayo ufalme umeanzishwa na amani inatawala] . . . shina la Yesse [fimbo na Tawi] . . . li-simamalo kuwa ishara kwa kabila za watu [wa ufalme],” anasema Isaya, na “hiyo ndiyo ambayo mataifa wataitafuta.” Isa. 11:10. Na kama baada ya kufungwa kwa muda wa rehema, milango ya ufalme itakuwa imefungwa kwa wote, ishara lazima kwa hivyo isimamishwe kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema: wakati wa pekee ambao Mataifa wa-tapata fursa ya

45

kuongoka kwa Bwana na kwa ufalme Wake, — hitimisho la kawaida kwa maandiko yafuatayo: {TN9: 45.3}

“Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo Nitakapowarudisha wafungwa wa watu Wangu.” Hos. 6:11. {TN9: 46.1}

Hivyo itakuwa “katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” Isa. 2:2, 3. {TN9: 46.2}

“Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili Yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadha-bu Yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo Wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wa-taharibiwa kabisa.” {TN9: 46.3}

46

“Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; ili kupapamba mahali Pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu Yangu. Na wana wa watu wale waliokutesa watakuja kwako na ku-kuinamia; nao wote waliokudharau watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; nao watakuita, mji wa Bwana, Zayuni wa Mtakatifu wa Israeli. Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi.” (Isa. 60:9-15) katika nchi

Ambapo Ufalme Unasimama; Hapo Dhambi Haipo. {TN9: 47.1}

“Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, Nitakapowarejeza watu Wangu wa Israeli na Yuda walio-fungwa, asema Bwana; Nami nitawarudisha hata nchi Niliyowapa baba zao, nao wataimiliki . . . Maana Nitakurud-ishia afya, Nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, ni Zayuni, ambao hapana mtu autakaye. {TN9: 47.2}

“Bwana asema hivi, Tazama, Nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. {TN9: 47.3}

47

“Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; Nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena Nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.” Yer. 30:3, 17-19. {TN9: 48.1}

“Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya [kazi ambayo inaweza kufanyika tu katika muda wa rehema], Nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda.” Ezek. 36:24-27. {TN9: 48.2}

Kwa wakati huu unaokaribia, ambapo watu wa Bwana waliotawanyika watakusanywa “kutoka kati ya mataifa,” na kurudishwa katika “nchi yao wenyewe,” mioyo yao itabadilishwa; kisha kwa tendo hilo itasemwa: “Kila mtu ali-yezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani Yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” 1 Yoh. 3:9. Wakati huo sheria ya dhambi, ambayo sasa hutawala katika moyo wa asili, haipo hai tena. Hivyo ukiwa huru kutoka kwa udikteta wa dhambi, “moyo wa jiwe”

48

utabadilishwa na “moyo wa nyama” na sheria ya Mungu kuandikwa juu yake milele. {TN9: 48.3}

Ukweli hasa kwamba Mungu sasa ataurejesha ufalme wa Israeli, unaibua swali kama Yeye hataweza kufanya hivyo kupitia shughuli za sasa za

Wayahudi Kurejea Yerusalemu. {TN9: 49.1}

Kuhusiana na shughuli za sasa katika Yerusalemu ya zamani, na za kurejea kwa Wayahudi katika nchi yao, kama ni kutimiza ahadi zilizofanywa kwa uzao wa Yakobo, hatupaswi kupoteza taswira ya ukweli kwamba ahadi hazitapata utimizo wake kwa kurudi katika nchi ya ahadi, kwa aidha Wayahudi waliomkana na kumsulubisha Bwana wao au uzao wao ambao kwa karibu miaka elfu mbili wameshindwa kumpokea Yeye kama Mwokozi wao, ila badala yake Mungu kwa kuwaleta hapo Wayahudi ambao ni Wayahudi si kwa ukoo tu ila pia kwa imani. {TN9: 49.2}

Ahadi, kwa hivyo, bila shaka ni kwa wale wa mwisho na kwa uzao wao ambao walijumuisha kanisa la Kikristo lilipokuwa likianza, na ambao walikuwa tayari kufa, badala ya kumkana, Bwana wao. Ahadi si, katika maneno men-gine, kwa wasio waongofu (wakiwakilishwa kwanza na Ishmaeli, na pili Esau); badala yake ni kwa ndugu zao wadogo — Wayahudi walioongoka (wakiwakilishwa kwanza na Isaka, na pili Yakobo). Kwa hivyo ni wale ambao wamemru-husu Bwana kuyabadilisha majina yao kutoka kwa “Wayahudi” (Israeli wa kimwili) kuwa

49

“Wakristo” (Israeli wa kiroho), jinsi Yakobo baba yao, alimruhusu Mungu kubadilisha jina lake kutoka Yakobo hadi Israeli. Hivyo kwa kuzaliwa kiasili uzao wa Yakobo, na kwa kuzaliwa kiroho, uzao wa Kristo (Kweli), wote ni wana wa Yakobo na wana wa Mungu, na hivyo Wayahudi kamili, Waisraeli kweli kweli. {TN9: 49.3}

“. . . Najua,” alisema malaika, “na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.” Ufu. 2:9. {TN9: 50.1}

Ingawa kanisa la awali la Kikristo lilijumuishwa na Wayahudi asilia, hata hivyo walipoanza kuitwa “Wakristo” (dini mpya ya Wayahudi) kinyume cha Wayahudi (dini ya zamani ya Wayahudi), wao hatua kwa hatua walipoteza utam-bulisho wao wa kijamii, mpaka mwishowe wao wote wakaacha kuitwa Wayahudi; ilhali kote katika karne nyingi Wayahudi wasiokuwa Wakristo wamehifadhi kikamilifu utambulisho wao wa kijamii. {TN9: 50.2}

“Kwa maana imeandikwa,” anaandika Paulo, ki-mfano akitambulisha safu hizi mbili, “Abrahamu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa

50

anatumika pamoja na watoto. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana ime-andikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume. {TN9: 50.3}

“Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.” Gal. 4:22-31. {TN9: 51.1}

Basi, kwa sababu watu 144,000 kwa udhahiri hawawezi kujumuishwa na Wayahudi ambao hawajaongoka kwa Kristo, tunaona kwamba tunapaswa kuchimba kwa kina

Kuwatambua Watu 144,000. {TN9: 51.2}

1. Wao ni “malimbuko.” Ufu. 14:4.

2. Wanatiwa muhuri katika wakati wa amani ambapo malaika wanne “wanazishikilia pepo nne.” Ufu. 7:1-3.

3. Hawajatiwa “Unajisi pamoja na wanawake.” Ufu. 14:4.

51

4. Vinywani mwao “haukuonekana uongo.” Ufu. 14:5

5. Wanasimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni, na, ndio wamfuatao Yeye “popote aendako.” Ufu. 14:1, 4.

6. Wanalo “jina la Baba Yake lililoandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 14:1.

7. Kufuatia wao kutiwa muhuri, umati mkubwa “watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha,” anasema Wa-ufunuo, “wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7:1-9. Katika nuru ya kweli hizi saba, kitambulisho na utume wa watu 144,000 unakuwa hakika. {TN9: 52.1}

Ukweli mtupu ndani yake kwamba wao ni malimbuko, hautupatii haki ya kuhitimisha kwamba walitiwa muhuri wakati wa sehemu ya mwanzo ya historia ya wanadamu. Hakika, wao kuwa ni Waisraeli, wazawa wa Yakobo, bila shaka hupinga kwamba wao wametiwa muhuri wakati wa Adamu hadi wa Nuhu au wa Nuhu hadi wa Yakobo — ka-bla ya Israeli kuzaliwa. Wala hawangeweza kuwa wametiwa muhuri wakati wa miaka mitatu na nusu ya ukasisi binafsi wa Kristo duniani, iwapo huo inajionyesha kama wakati bora: kwa sababu Kristo, Mwenyewe, na wafuasi Wake wote wakati huo waliteswa, na wengi wao waliuawa; ilhali wakati wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000, “pepo nne,” mfa-no wa mataifa yote yaliyotapakaa kwenye pembe nne za dunia,

52

hazijaachiliwa kuvuma — kudhuru chochote (Ufu. 7:1). {TN9: 52.2}

Na kwa sababu katika wakati wa kipindi cha kutiwa muhuri, mataifa yanazuiliwa kuzuia kutiwa muhuri kwa wenye haki, na “malaika wanne” (Ufu. 7:2) wameamriwa kutowadhuru waovu, tunaona kwamba watu 144,000 wanatiwa muhuri katika wakati wa amani — sio, hata hivyo, wakati wa amani miongoni mwa mataifa yenyewe, ila badala yake kwa wakati ambao mataifa hayajaruhusiwa kulitesa kanisa (wale ambao wanatiwa muhuri) wala malaika kuruhusiwa kuwadhuru waovu. Hali hii, hata hivyo, ikiwa ni kinyume na ile ambayo ilikuwapo katika siku za mi-tume, wakati Warumi na Wayahudi waliwatesa Wakristo, na wakati Mungu aliutwaa uhai wa Anania na Safira, na ku-leta uharibifu juu ya Yerusalemu, hakuna yeyote, kwa hivyo, anaweza kuhitimisha kwa uaminifu kwamba watu 144,000 walitiwa muhuri wakati huo. {TN9: 53.1}

Wala hawakuweza kuwa, kama wengine wanavyofikiri, wale walioamka katika makaburi yao wakati Kristo “alikata roho” (Mat. 27:50, 52, 53), maana, zaidi ya sababu zilizotolewa tayari, malaika alikuja “kutoka mashariki “ si kuwaita watoke makaburini mwao ila kuwatia muhuri kwenye vipaji vya nyuso zao (Ufu. 7:3, 4). {TN9: 53.2}

Wa-ufunuo, zaidi ya hayo, aliambiwa kuhusu mambo ambayo angeandika, yangekuwa “hayana budi kuwako upesi” (Ufu. 4:1) — baada ya 96 B.K., alipoyaona maono. Na

53

zaidi ya hayo, kutiwa muhuri kwa watu 144,000 kunatukia wakati wa “muhuri wa sita” kabla ya kufunguliwa kwa muhuri wa “wa saba” (Ufu. 6:12-17; 7:1-17; 8:1), muda mfupi kabla ya mwisho wa mambo yote. {TN9: 53.3}

Na bado zaidi, badala ya kuitwa wazaliwa wa kwanza, wanaitwa “malimbuko” — jina ambalo linaonyesha kwamba wao ni wa

Mazao Ya Kwanza Ya Mavuno. {TN9: 54.1}

Kwa sababu vitabu vyote vya Biblia hukutana na kwishia katika Ufunuo, kutiwa muhuri kwa watu 144,000 lazi-ma kama tokeo kupate kikamilisho chake katika maandiko ya manabii. Na kwa sababu hakuna popote ila katika Eze-kieli 9 linapatikana tukio linalofanana na lile la Ufunuo 7, inafuata kwamba kutia alama na kutia muhuri ni sawa, yote mawili yatawatenga waovu kutoka kati ya wenye haki: malaika katika la awali, wakiwapiga wote ambao hawana ala-ma; malaika katika la mwisho, wakiwadhuru wote ambao hawana muhuri. (Angalia Ezekieli 9:4-6; Ufunuo 7:2, 3; 9:15.) {TN9: 54.2}

Ukweli, kwa hivyo, ya kwamba hakuna wakati wowote katika historia ya kanisa, isipokuwa katika siku ya Nuhu, Mungu amewahi kuwaangamiza waovu wote na kuwahifadhi tu watakatifu, ni ushahidi wa hitimisho kuthibitisha kwamba kutia alama, au kutiwa muhuri, kwa watu 144,000 bado hakujakamilika. Dhahiri, basi, kati ya watu wa Mungu wale ambao hawawezi kupokea muhuri, wanawakilishwa, katika kielelezo cha mfano, na “magugu,” na kuangamizwa, ambapo wale wanaopokea muhuri na kuokoka

54

kuangamizwa, wanawakilishwa na “ngano,” na kuwekwa ghalani — ufalme (Mat. 13:30). {TN9: 54.3}

Kwa sababu “magugu” na ngano vitakua pamoja hadi kwa mavuno, na kwa sababu mavuno ni mwisho wa dunia (Mat. 13:30, 39), ni wazi kwamba watu 144,000 wanaitwa malimbuko kwa sababu ni kundi la watakatifu (ngano) la kwanza kutenganishwa kutoka kwa magugu. Wao ni, zaidi ya hayo,

Kundi Ambalo Halijatiwa Unajisi Na Wanawake. {TN9: 55.1}

Kwa mujibu wa Ufunuo 7, watu 144,000 ni wa kabila kumi na mbili, Israeli na Yuda, sio wa watu wa Mataifa; pia, kutia alama na mchinjo, kwa mujibu wa Ezekieli 9, yote yatatukia katika Israeli na Yuda, kanisa, ambamo mavu-no, hukumu, inaanzia. Na, iwapo hukumu, anauliza mtume, “ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Pet. 4:17. {TN9: 55.2}

Katika nuru iliyojikusanya inayolenga suala hili, watu 144,000, “malimbuko,” wanasimama wazi kama Wayahudi Wakristo ambao watapatikana kanisani mwanzoni mwa mavuno. Katika hadhi hii hawajanajisiwa na wanawake. Wamekuwa, kwa maneno mengine, tangu kuzaliwa kwao watu wa Mungu (Wayahudi) — hawajanajisiwa na ibada ya kipagani. “Wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako,” na matokeo yake kwamba wakati Yeye anasimama juu ya Mlima Zayuni, wao, pia, wanasimama hapo. {TN9: 55.3}

55

Na zaidi, kweli kwamba “hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira,” na ya kwamba ni “watumwa wa Mungu wetu,” zinadokeza dhahiri kwamba

Watalikusanya Kundi Lililotiwa Unajisi Na Wanawake, Mavuno Ya Pili. {TN9: 56.1}

Kundi hili la watakatifu lazima wawe wale ambao wamewahi kuolewa kwa bibi fulani asiyekuwa Mkristo, kanisa la kipagani, na ambao kwa hivyo si wazawa wa Yakobo au kanisa la Kikristo. Kwa hivyo yatakuwa mavuno mawili — moja kutoka kwa kanisa na moja kutoka ulimwenguni: rekodi ya la awali, huiwataja tu Waisraeli, watu 144,000, wale wasiotiwa unajisi na wanawake, ingawa haisemi kwamba haitawezekana kuwapo na wengine; ilhali rekodi ya la mwi-sho, hata hivyo, dhahiri hukumbatia “umati mkubwa” kutoka kwa mataifa yote ambao bila shaka lazima wawe wote wasiotiwa unajisi na waliotiwa unajisi — Wayahudi na wa Mataifa. {TN9: 56.2}

Hivyo, basi baada ya kutiwa muhuri kwa watu 144,000, malimbuko, unakuja umati mkubwa kutoka kwa mataifa yote, wa mwisho wanaweza, kwa kufaa, kuitwa tu mavuno ya pili. Vinginevyo watu 144,000 hawawezi kuitwa malimbuko: maana pale ambapo hakuna ya pili, hapawezi kuwa na ya kwanza. Na malimbuko watu 144,000, wakiwa watakatifu walio hai, basi pia, kwa hivyo, yalivyo mavuno ya pili umati mkubwa. Malimbuko, zaidi ya hayo wakiwa sawa na wazaliwa wa kwanza, wao kwa hivyo ni

56

wachungaji, “watumwa wa Mungu” — wale ambao watawaleta ndani mavuno ya pili. {TN9: 56.3}

Akitabiri kuhusu utengo kwa moja, na kukusanywa ndani kwa lingine, Isaya anatangaza: “Kwa maana Bwana ata-teta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. . . Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu ambao hawajaisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:16, 19, 20. {TN9: 57.1}

Kumbuka kwamba wale wanaonusurika mchinjo wa Bwana wanatumwa kutangaza sifa Zake na kuonyesha utu-kufu Wake kati ya Mataifa. “Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote.” Kwa maneno mengine, wa-tahubiri “habari njema ya ufalme. . . katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Mat. 24:14. Kazi hii kubwa, ambayo hakuna wengine wameweza kufanikisha, hawa waliookoka wataweza, kwa sababu

57

Katika Vinywa Vyao Haukuonekana Uongo. {TN9: 57.2}

Ukweli kwamba watu 144,000 hawana uongo katika vinywa vyao huonyesha kwamba, kama watumwa wa Mungu, wanao ujumbe wa kutangaza, na ya kwamba watapatikana bila hatia kwa kuutangaza: wakinena ukweli na sio chochote ila ukweli, watafanikiwa kotekote waendako na ujumbe, ingawa wanatumwa nao

Wakati Ambapo Pepo Zimeachiliwa Na Kuvuma. {TN9: 58.1}

Malaika wale ‘wakizuia pepo kwenye pembe nne za nchi humaanisha kwamba wanazuia taabu fulani ya ulimwengu wote ambayo, ikianza wakati kanisa liko katika hali yake ya Ulaodekia, itazuia kutiwa muhuri. Na kutoka kwa ukweli huu, inafuata kwamba haraka baada ya watu 144,000 kutiwa muhuri, taabu itaanza, ikimaanisha malaika wame-ziachilia pepo. Katika taabu hii “mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo” (Dan. 12:1), umati mkubwa utaletwa uso kwa uso wakati ambapo watakuwa wakiitwa kutoka Babeli (Ufu. 18:4) hadi katika ufalme. {TN9: 58.2}

Wakati huu wa taabu unaonyeshwa kimbele na taabu ya sasa ambayo kanisa linasababisha kwa malimbuko, wale ambao wanatiwa muhuri, kutiwa alama, kati yake, watakaohamishwa hadi kwa ufalme — ghalani (Mat. 13:30), vyombo (Mat. 13:48). {TN9: 58.3}

Kwa hivyo, kama kuifanya sanamu ya mnyama (Ufu. 13: 11-18) ku, katika

58

unabii, tukio la pekee la ulimwengu wote la aina hii, na kama umati mkubwa ukiwa na mitende mikononi mwao un-atoka katika dhiki kuu, hitimisho la pekee la busara ni kwamba baada ya watu 144,000 kutiwa muhuri, na wakati pepo zinavuma, mavuno ya pili yatakusanywa na kazi ya injili kufungwa. {TN9: 58.4}

Taabu italipuka kwa sababu mnyama wa Pembe mbili atatoa amri “kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufu. 13:17 . Hivyo joka “akamkasirikia mwanamke” na “akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 12:17. Na wakati uo huo malaika wataruhusiwa kuwadhuru wote wanaolitaabisha kanisa la Mungu, na wanaojaribu kujiunga nalo kwa namna sawa yanavyofanya magugu sasa. Kwa kuwadhuru waovu hivyo, malaika wanatekeleza “hasira ya Mwana-Kondoo.” Kwa mtazamo wa hili, Bwana anauliza, “nani awezaye kusimama?” Ufu. 6:17. Ni “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana” (Mal 4:5), na “wenye dhambi walio katika Zayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wanafiki.” Kwa hivyo maswali: “Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?” — Ni wale tu ambao wanajiona wanahitaji kila kitu. Na hawa ni

59

Wale Watakaomwona Mfalme. {TN9: 59.1}

“Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu. Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. {TN9: 60.1}

“Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri Wake, yataona nchi iliyoenea sana. Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara? Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo. Angalia Zayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika. Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo. Kwa maana Bwana Ndiye mwamuzi wetu; Bwana Ndiye mfanya sheria wetu; Bwana Ndiye mfalme wetu; Ndiye atakayetuokoa.” Isa. 33:14-22. {TN9: 60.2}

“Mikaeli,” “Jemedari Mkuu,” wakati huo “atasimama” na kumwokoa “kila mmoja

60

atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12:1. {TN9: 60.3}

Kwa sababu siku hiyo Bwana atawachunga waaminifu na kuwaadhibu wasio waaminifu, ujumbe unaotangaza hii “siku iliyo kuu na ya kutisha” (Mal 4:5), unaitwa, Fimbo ya Mchungaji. “Sauti ya Bwana,” kwa hivyo, “inaulilia mji,. . .

“Isikieni Hiyo Fimbo Na Yeye Aliyeiagiza.” Mika 6: 9. {TN9: 61.1}

Likiwa limezama katika kusinzia na kulala kwa Ulaodekia, “mji,” kanisa, katika juhudi za huruma ya Mungu kuliandaa dhidi ya siku hii ya taabu, litashtuliwa kwa uhai kwa kilio Chake cha dharura: {TN9: 61.2}

“Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Isa. 52:1. {TN9: 61.3}

“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu Wake utaoneka-na juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.” Isa. 60:1-3. {TN9: 61.4}

Kanisa la Walaodekia, likiwa la mwisho kwa makanisa saba, ni sehemu ya mwisho

61

ya kanisa la Kikristo ambamo ngano na magugu yamechangamana. Washindi, waliotiwa alama, kutoka kwalo, wale ambao huisikia Fimbo, wanaanzisha sehemu ya nane ya kanisa — ile inayowakilishwa na “ghala” (Mat. 13:30) na “vyombo” (Mat. 13:48), pia kwa “kinara cha taa za dhahabu” cha Zekaria 4. Kulihusu Bwana anasema: “. . . Na ma-taifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.” Isa. 62:2, 3. {TN9: 61.5}

Miongoni mwa Walaodekia, hata hivyo, wale wanaokataa kuamka na kuishughulikia hali hiyo, ambao hawata “ugua na. . . kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika katikati yake” (Ezek. 9:4) wataachwa bila alama, na hivyo wataanguka chini ya silaha za kuchinja za malaika (Ezek. 9), ilhali wale wanaopokea alama wataziepuka na kukingwa kutokana na taabu, kinga ikiwakilishwa na ghala na vyombo (Mat. 13:30, 48). {TN9: 62.1}

Huu uhifadhi wa ngano kwa upande mmoja, na kuyachinja magugu kwa upande mwingine, kati ya malimbuko, — wale walio kanisani, — hodokeza utabiri wa kuwahifadhi wema na kuwaangamiza wabaya kati ya mavuno ya pili, wale walio Babeli (Ufu. 18:4). Hivyo

62

Kazi Katika Laodekia Huashiria Ile Katika Babeli. {TN9: 62.2}

Wakati Bwana sasa anawamaki malimbuko wa ufalme Wake, walio katika Laodekia “wazee” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211), wakidhani kwamba wanatenda maagizo Yake kwa kuwalazimisha walei wasiwasikilize wajumbe wa Bwa-na na wasisome ujumbe Wake katika Fimbo ya Mchungaji, wanajaribu kuwazuia wasiipokee alama Yake, ambayo ita-wahifadhi wasiangamie. Na kama unabii unavyoonyesha, pambano hili, linapomalizika Laodekia, litasambaa hadi Babeli wakati Bwana anaanza kuyamaki mavuno ya pili ya ufalme Wake, na kwa sababu mnyama, akidhani (kama wanavyofanya wazee sasa) kwamba anatenda maagizo ya Bwana, anaamuru kwamba “wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao” (Ufu. 13:16), wanapokea alama yake badala ya Bwana, ambayo itawahifadhi, pia, wasiangamie. {TN9: 63.1}

Huku kutiwa alama kuwili (kwa mnyama na kwa Bwana) ndani yake zenyewe huonyesha muda wa kutenganisha raia wa mbinguni kutoka kwa raia wa dunia. Na kwa sababu hii ni kazi ambayo haijawahi kuwapo, inaleta wakati wa taabu mfano wake haujawahi kuwapo — “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana.” Taabu ya sasa ndani ya Laodekia kwa hivyo itasambaa hadi katika Babeli na kupevuka kuwa wakati wa taabu mfano wake haujawahi kuwapo, endeleo ambalo linaonyesha kwamba utawala sawa wa kishetani ambao sasa unafanya kazi ndani ya Laodekia, hivi karibuni utajionyesha kabisa, kwa kuungana

63

na mnyama, ndani ya makanisa ya Babeli, huko kupinga kutiwa alama kwa matunda ya pili kama ilivyo sasa katika Laodekia ukipinga kutiwa alama kwa malimbuko. {TN9: 63.2}

Na isitoshe, kama sehemu ya nane ya kanisa, kanisa la milele ni la sehemu ya saba, kanisa la muda vivyo hivyo mnyama wa nane, dunia baada ya millenia, ni ya mnyama wa saba (Ufu. 17:11), dunia kabla ya millenia. {TN9: 64.1}

Huu ulinganifu usioweza kuepukwa kati ya kazi ya Mungu na kazi ya Shetani, ambayo Uvuvio huleta hivyo kwa haraka na waziwazi kwa mtazamo, hujinenea kwamba tunaingia katika “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana” — ukweli ambao unapaswa kuchochea mioyo yetu kuliko chochote kimewahi kufanya. {TN9: 64.2}

Na kwa sababu “tokea sasa” tangu wakati ambapo watu 144,000 wametiwa alama na wadhambi kuondolewa mbali kati yao, hapana tena waovu kuchangamana na watakatifu, — tokea wakati huo hadi milele, kwa hivyo,

Kanisa La Ufalme, La Nane, Linasalia Safi. {TN9: 64.3}

Kinabii akitazama mbele kwa hali ya kanisa lililotakaswa, nabii Zekaria aliona kwamba “kila chombo katika Ye-rusalemu, na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa Bwana wa majeshi; nao wote watoao dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo

64

hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya nyumba ya Bwana wa majeshi.” Zek. 14:21. {TN9: 64.4}

“Bali agano hili ndilo Nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria Yangu ndani yao, na katika mioyo yao Nitaiandika; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Wala ha-watamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana Watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana Nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” Yer. 31:33, 34. {TN9: 65.1}

Kisha litatokea Neno la Bwana: “Sikieni, ninyi mlio mbali, Niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza Wangu.” Isa. 33:13. {TN9: 65.2}

Wote ambao wametambua na kunufaika kwa nguvu Zake zamani, pamoja na wote ambao watatambua na kufaidika kwa nguvu Zake katika siku zijazo, watapatikana katika

Makundi Matano Ndani Ya Ufalme. {TN9: 65.3}

Makundi haya ni (1) watu 144,000, Waisraeli malimbuko ya walio hai, ambao “mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe,” naye “mwenye kutawala atakuwa mtu wa jamaa yao” (Yer 30:21); watarejea Yerusalemu, na kusimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo; (2) wale ambao Yohana aliona, baada ya kutiwa muhuri watu 144,000, wali-okusanywa kutoka “kila taifa, na kabila, na

65

jamaa, na lugha,” wakati wa “dhiki kuu,” “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo” — umati mkubwa ambao utakwenda Yerusalemu kabla ya ufufuo; (3) wale watakaofufuka kwa uzima wa milele katika ufufuo wa Danieli 12:2; (4) wale Waisraeli ambao watatokea katika ufufuo wa Ezekieli 37:1-14; (5) wote wanaokuja katika ufufuo wa Ufunuo 20:6; — kwa pamoja, hawa ni Waisraeli na watu wa Mataifa ambao watarudi Yerusalemu, kuimiliki nchi ya ahadi, na kisha dunia yote. {TN9: 65.4}

Inashangaza, ni kazi bure, kwa hivyo (kwa mtazamo wa yale tumeona katika kurasa hizi), lengo linaloimarika la kuujenga tena Yerusalemu, jinsi vuguvugu moja linavyojaribu kufanya kwa kuitikia unabii wa ufalme, kwa kuwapele-ka huko Wayahudi wasiokuwa Wakristo; na jinsi vuguvugu lingine linavyojitahidi kufanya hivyo kwa kuitikia unabii ule ule, kwa kuupeleka huko ulimwengu unaozungumza Kiingereza. {TN9: 66.1}

Ufalme wa wote waamini na wasioamini hautakuwa bora kuliko falme za leo. Utakuwa, hakika, si kitu zaidi ya Babeli, si kitu zaidi ya “ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.” Ufu. 18:2. Kufanya kazi kwa tumaini la aina hiyo ni kuchukua hatua ndefu ya kuuleta ndani “upotovu wenye nguvu” wa Shetani, ukimuiga Kristo katika ufalme bandia. {TN9: 66.2}

66

Hivyo ni kwamba “wale tu ambao wamekuwa wanafunzi wa bidii wa Maandiko, na walioupokea upendo wa kweli, watakingwa kutoka kwa upotovu wenye nguvu ambao utauteka nyara ulimwengu. Kwa ushuhuda wa Biblia hawa watamgundua mdanganyifu katika maficho yake. . . Je! watu wa Mungu sasa wamekita mizizi imara kwa neno Lake ya kwamba hawatajisalimisha kwa ushahidi wa hisia zao? Je! wao, katika mgogoro huo, watashikamana na Biblia, na Biblia tu?” Pambano Kuu, uk. 625. {TN9: 67.1}

Kwa mtazamo huu wa dharura kulilinda tumaini la Mkristo linalotia taji, ufalme, ni muhimu, kwa hivyo, kuzikusanya pointi kuu hadi hapa zilizothibitishwa katika kukusanywa. Hivyo

Muhtasari Wa Malimbuko Na Mavuno Ya Pili. {TN9: 67.2}

1. Wakati ambapo “magugu” “wana wa yule mwovu” (Mat. 13:38), umetimia kamili, kisha yataanza “mavuno,” na yatautaleta “mwisho wa ulimwengu huu.” Mat. 13:30, 40. Ukitukia katika mwisho wa dunia, uhitaji wake ni ku-wakusanywa watu kupitia kwa ujumbe wa Eliya, wa mwisho uliotumwa kutoka Mbinguni wa kutangaza injili, ambao unahubiriwa kwanza kwa kanisa kabla ya siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana (Mal. 4:5), na kisha kote ulimwengu-ni katika siku hiyo iliyotarajiwa kwa muda mrefu. {TN9: 67.3}

67

Ujumbe unapata juya limejaa hapo unapowasili na kisha kusababisha mgawanyiko kati ya wale wanaoupokea na wale wanaoukataa, unawawezesha malaika kuchagua wabaya kutoka kati ya wazuri (Mat. 13:48). Hawa “wazuri” ni malimbuko ya waliokombolewa. Kisha unafuata utengo katika mwito mkamilifu: “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18:4. Hawa walioitwa watoke ni mavuno ya pili. {TN9: 68.1}

Katika tukio la kwanza, wabaya wanatupwa nje kutoka kati ya wazuri walionaswa katika juya (ujumbe unaotulia ndani ya kanisa); ilhali katika tukio la pili, waaminifu kwa Mungu pekee wanaitwa kutoka miongoni mwa wadhambi huko Babeli, bila kuwa na magugu kati yao. {TN9: 68.2}

Magugu na ngano zilikuwa zimechangamana katika tukio la kwanza kwa sababu “watu walipolala,” asema Bwana, “akaja adui akapanda magugu katikati ya ngano”; Ilhali ngano imewekwa huru kutoka kwa magugu katika tukio la mwisho kwa sababu, asema Bwana: “Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya.” Isa. 62:6. {TN9: 68.3}

Ufalme wa Babeli ukiwa umewakilishwa na mnyama wa rangi nyekundu, mnyama ambaye juu yake ameketi mwanamke (Ufu. 17), nembo hiyo kwa hivyo ni mwakilishi wa mfumo wa kidini na

68

kisiasa. Kipengele cha kidini kinawakilishwa na mwanamke; kipengele cha kiraia, kwa pembe za mnyama: pamoja, utabiri ki-mfano wa mfumo wa kimataifa wa muungano wa kanisa na dola. Mnyama peke yake, bila pembe, hu-wakilisha, kama wanyama wa Danieli 7, umati wa dunia — raia wa Babeli ya uakisi ambao kutoka miongoni mwao watu wa Mungu wanaitwa. Kusanyiko hili linajumisha utengo wa mavuno ya pili. {TN9: 68.4}

Kutoka kwa hili, ukweli unaonekana tena kwamba malimbuko na mavuno ya pili ya walio hai (yale yali-yokusanywa kutoka ndani ya kanisa mwanzoni mwa “siku iliyo kuu na ya kutisha,” na mengine yaliyokusanywa kutoka Babeli katika siku hiyo) yanajumuisha ufalme ukianza na kabla ya ufufuo wa wafu. {TN9: 69.1}

Kweli, zaidi ya hayo, kwamba wazuri tu kutoka kwenye juya walihifadhiwa, na ya kwamba watu wa Mungu pekee waliitwa watoke Babeli, wanashangilia ufalme kama nyumba ya watakatifu pekee. {TN9: 69.2}

“Bali agano hili ndilo,”anatangaza Bwana, mintarafu ukweli huu mtukufu wa ufalme, “Nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria Yangu ndani yao, na katika mioyo yao Nitaiandika; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana;

69

kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana Nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao Sitaikumbuka tena.” Yer. 31:33, 34. {TN9: 69.3}

“Nao watawaita,” anasifu Isaya, “Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana.” Isa. 62:12. Anahakikisha, “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.” Isa. 35:8. {TN9: 70.1}

2. Wakati “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote” (Mat. 24:14), kazi ya Injili itakamilika, na muda wa rehema utafungwa kwa kila mwanadamu. {TN9: 70.2}

3. Wakati Wayahudi na watu wa Mataifa ambao wameitikia mwito wamekusanywa kutoka pembe nne za dunia, basi mavuno yatakoma: wakati huo mwisho wa muda wa rehema uliokuwa ukikawia umetoweka milele: kisha mwi-sho utakuwa umekuja, na kutoka kwa “kiti kikuu cha enzi cheupe” itakuwa imetokea amri isiyoweza kubadilika: “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Ufu. 22:11. {TN9: 70.3}

Wakitambua kwa hofu yao, kwa kupita kwa muda wa rehema, ya kwamba wamepotea

70

milele, wenye kupuuza watalia kwa uchungu: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” Yer. 8:20. {TN9: 70.4}

“Tazama, Naja upesi,” anatangaza Kristo, likifuata tamko Lake la kufunga kwa muda wa rehema (Ufu. 22:11), “na ujira Wangu u pamoja Nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Ufu. 22:12. Hapa ni ushahidi ulio tia nanga kwamba muda wa rehema unafungwa kabla ya kurejea Bwana akionekana. {TN9: 71.1}

4. Penye mwisho wa pigo la saba, Bwana, Mwenyewe, akionekana kwa kila jicho (Ufu. 1:7), “Atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo wa-tafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana he-wani; na hivyo tutakuwa

“Pamoja Na Bwana Milele.” 1 Thes. 4:16, 17. {TN9: 71.2}

“Pamoja na watakatifu waliokufa wa vizazi vyote wakiwa wamefufuliwa na kuunganishwa na watakatifu walio hai, ufalme umekamilika kabisa — watakatifu wakishawekwa upande Wake wa kuume (ufalme), na waovu, upande Wake wa kushoto (Babeli). Kisha, wakati Mfalme anawafukuza wale walio upande Wake wa kushoto “kuingia adhabu ya milele,” Yeye anawaambia wale walio upande Wake wa kulia “Njoni, mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu.” Mat. 25:46, 34. Kufuata hili linatambulika la muda mrefu

71

tokeo lililotazamiwa la matumaini yenye utukufu lililozalishwa na ahadi ya Kristo: “Nyumbani mwa Baba Yangu mna makao mengi; kama sivyo, Ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi Mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe Kwangu; ili nilipo Mimi, nanyi mwepo.” Yoh. 14:2, 3. {TN9: 71.3}

Tumaini hili lenye mchocheo la kila Mkristo limetabiriwa kwa uzuri sana katika kuhamishwa bila kufa kwa Henoko (Mwa. 5:24), kwa Eliya (2 Fal. 2:11), na ufufuo wa umati ambao Kristo aliuongoza kwenda juu (Mat. 27:52, 53, Efe. 4:8) — mfano wa mara tatu katika umoja wa mara tatu na sheria ya Mungu ya mifano kwamba pale palipo na mfano, lazima pia pakuwepo uakisi. {TN9: 72.1}

Usingekuwapo, hakika, katika uhusiano huu uakisi (kupaa kwa watakatifu wote), basi hapangekuwapo mfano (kuhamishwa bila kufa kwa Henoko na Eliya, na kupaa kwa umati). Mfano ungekuwa bila msingi, usiokuwa na len-go, na wa kupotosha. Si tu watakatifu, kwa hivyo, bali pia

Mbingu Zitatoweka. Waovu Wataililia Milima Iwaangukie. {TN9: 72.2}

Pamoja na mwisho wa pigo la saba utakuja ukamilifu wa mwisho, ambao, anasema Wa-ufunuo: “. . . mbingu [anga ya dunia yetu — Mwa. 1:8]

72

zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na watu wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,” wakiiambia “milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele ya uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira Yake, ime-kuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu. 6:14-17. {TN9: 72.3}

Ukweli kwamba matukio haya yote pamoja na kurudi mara ya pili kwa Kristo, pia na kweli kwamba unabii hu-tangaza dhahiri ya kuwa Mungu atawakusanya watu Wake wote kutoka kati ya mataifa, na kuwaita walio Wake Mwenyewe kutoka makaburini mwao, kuwanyakua wote waliokombolewa — wote walio hai na waliofufuliwa — ku-kutana Naye angani na kwenda pamoja Naye kwenye majumba ambayo Amekuwa akiwaandalia tangu kupaa Kwake, kuwaangamiza waovu wote, kuiacha dunia tupu bila uhai au nuru, kisha Aifanye utupu na ukiwa, na mwishowe, ku-towaacha wafu waishi tena hadi miaka elfu imekwisha, — kweli hizi zote huonyesha wazi kwamba dunia itakuwa kati-ka hali ya machafuko maadamu watakatifu “wanaishi na kutawala” pamoja na Kristo mbinguni wakati wa miaka elfu moja. {TN9: 73.1}

Kwa njia hii, Shetani anafungwa kwa msururu wa hali ambazo zinamfanya asiweze tena

73

kuwadanganya mataifa hata miaka elfu imetimia, na mpaka Bwana atakaporudi tena pamoja na watakatifu, awaite waovu waliokufa kutoka makaburini mwao, na kuwaruhusu waishi kwa muda mchache — muda ambao

Shetani Anawadanganya Tena. {TN9: 73.2}

Akitazama mbele hadi kwa ufufuo baada ya millenia, Wa-ufunuo aliona kwamba waovu “Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. . . Hii ndiyo mauti ya pili.” Ufu. 20:9, 10, 14. {TN9: 74.1}

Kisha “ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu Wake Aliye juu; ufalme Wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. Huu ndio mwisho wa jambo lile.” Dan. 7:27, 28. {TN9: 74.2}

Kuona kwamba mambo haya yote hayana budi kutukia upesi, “Simameni katika njia kuu,” asema Bwana, “mka-one, mkaulize habari za

“Mapito Ya Zamani.” Yer. 6:16. {TN9: 74.3}

“Wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo,

74

ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.” 1 Tim. 1:4. “Wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli.” Tito 1:14. “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” 2 Tim. 4:3, 4. {TN9: 74.4}

“. . . Neno langu na kuhubiri kwangu,” Mtume Paulo anasema, “hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.” 1 Kor. 2:4, 5. {TN9: 75.1}

Hebu ushauri huu uwaonye watu wa Mungu wayaache mazoea hatari ya kuning’iniza mafundisho yao na imani yao kwa ndoano zilizonakshiwa dhahabu za mafafanuzi yaliyopotoshwa na utoaji kutoka kwa lugha wasizozijua (Kie-brania, Kigiriki, na hii, hiyo, au nyingine) na fasiri zilizofasiriwa ambazo hutia nguvu na kutumikia maslahi ya maoni yasiyofaa ya kitheolojia na upendeleo bora kuliko linavyofanya toleo lililoidhinishwa — toleo ambalo Mungu, katika majaaliwa Yake na katika kujua Kwake kimbele kwa kumaliza kazi Yake akitumia ulimwengu wa kunena Kiingereza, amepeana kwa watu Wake kuwaongoza katika ufalme Wake. Jihadharini, kwa hivyo, kwa unafiki wa

75

ulaghai wa udhamini, ambao hudhaniwa kuwa kutegemewa zaidi kuliko ule ambao Mungu, Mwenyewe, amechagua na kufanya kwa urahisi. {TN9: 75.2}

“Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno Yangu hayatapita kamwe.” Mat. 24:35. {TN9: 76.1}

-O-O-O-

(Italiki Ni Zetu)

76

FAHARISI YA MAANDIKO

77

>