15 Jul Trakti Namba 15
TRAKTI NAMBA 15
KWA MAKANISA SABA
KUZIFUNGUA LAKIRI SABA
Jalada
Hati miliki 1947
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. Houteff
***
Katika nia ya kufikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inatumaini kuiepuka njia inayoongoza kwenye uharibifu wa mwili na roho, trakti hii husambazwa bila malipo kadri toleo hili linadumu.
“Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.” Yohana 12:31.
YALIYOMO
Ishara Za Nyakati | 5 |
Danieli 7 | 16 |
Kuvunjwa kwa Lakiri Saba | 35 |
Nembo Ya Lakiri Ya Kwanza | 38 |
Nembo Ya Lakiri Ya Pili | 41 |
Nembo Ya Lakiri Ya Tatu | 44 |
Nembo Ya Lakiri Ya Nne | 49 |
Nembo Ya Lakiri Ya Tano | 51 |
Nembo Ya Lakiri Ya Sita | 53 |
Nembo Ya Lakiri Ya Saba | 63 |
Kanisa Hai Daima Na Adui Wake | 68 |
Mwongozo Kwa Ufasiri Sahihi Wa Nembo Za Pembe Na Vichwa | 72 |
Faharisi ya Maandiko | 91 |
TRAKTI 15
HII HUMAANISHA NINI KWAKO?
Ni mafanikio gani tungeweza kupata katika kuvipigia debe vitabu vyetu, na ni wema gani vingeweza kufanya ikiwa wanaotazamiwa kuvinunua na wasomaji wangeweza kwanza kutafuta ushauri kutoka kwa wachungaji wa madhehebu yao na kutii ushauri wao? Sisi sote tunajua jibu — Hakuna vitabu vingeuzwa na hakuna vitabu vingesomwa. {TN15: 1.1}
Na iwapo tungaliutafuta ushauri kutoka kwa wachungaji wa madhehebu yetu ya awali na kupokea mashauri yao, wangapi kati yetu wangekuja kuwa Waadventista wa Sabato? Jibu la jumla ni, “hapana hata mmoja wetu.” Hivi ndivyo imekuwa hatima ya wote ambao wamefuata maamuzi ya watu ambao hawakuvuviwa dhidi ya watu wa Mungu waliovuviwa. Watu wa kidini, watu waliokita mizizi katika dini yao, kama walivyokuwa makuhani na walimu katika siku za Kristo, wamekuwa na mafanikio sana kuzuilia mbali nuru ya Mungu kutoka kwa watu. Huu ni ukweli kwamba mtu awaye yote kamwe asiweze kusahau au kupuuza kuzingatia. {TN15: 1.2}
Zaidi ya hayo, kwa kuwa haki zetu za kibinafsi za kuzichunguza kweli zinazodaiwa kutumwa kutoka kwa Mungu, bila kuingiliwa na wachungaji wetu wa awali, zilitutoa ndani ya makanisa
1
ambayo huzingatia tu kweli za zamani, na kutuleta katika ukweli wa sasa wa Ujio miaka kadhaa iliyopita, Je, tunapaswa sasa kuzisalimisha haki hizi na kuwategemea wengine kiroho kutuambia ni nini Ukweli na ni nini uongo? Kwa nini tujihukumu nafsi zetu kuwa walemavu kiroho badala yake kuwa Wakristo wazima? Na kwa nini kulipokea neno la mchungaji sasa dhidi ya Ukweli mpya wa sasa unaodaiwa kuvuviwa, iwapo hatua hiyo tuliyochukua awali ilikuwa hatari, ingekuwa ilituhadaa kuupokea Ukweli wa Ujio? Je, si ukweli kwamba ikiwa tungewaruhusu watu wengine wafikiri kwa niaba yetu, tungedanganywa vibaya sana kama vile watu wa kawaida wa Uyahudi waliohadaiwa na makuhani na walimu katika siku za Kristo? {TN15: 1.3}
Kwa mtazamo wa uzoefu wa wale ambao wamekwisha enenda mbele yetu, tunajihisi kuamini kwamba utakipokea kijizuu hiki kinachotumwa kwako, na ambacho kina maana sana kwetu na kwa maelfu ya Waadventista wa Sabato wengine duniani kote. Je, utakichunguza mwenyewe kama walivyofanya Waberoya waungwana (Mdo. 17:10, 11), bila kutegemea ushawishi au kuchukia bila sababu kwa watu wengine? Sala tu na kujifunza
2
kutakuzuia dhidi ya uovu na kukuongoza kwenye nuru ya ajabu ya Mungu — {TN15: 2.1}
“…Lakini jihadhari kukataa lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106. {TN15: 3.1}
“Bado upo ukweli wa thamani sana ambao utafunuliwa kwa watu katika wakati huu wa hatari na giza, lakini ni kusudi la Shetani aliloazimia kuzuia nuru ya kweli isiangaze ndani ya mioyo ya wanadamu. Iwapo tungetaka kuwa na nuru ambayo imeandaliwa kwa ajili yetu, tunapaswa kuonyesha tumaini letu kwa ajili yake kwa kulichunguza kwa bidii neno la Mungu. Kweli za thamani ambazo zimekuwa hazijulikani kwa muda mrefu zitafunuliwa kwa nuru ambayo itadhihirisha thamani yake takatifu; kwa maana Mungu atalitukuza neno lake, kwamba
3
liweze kuonekana katika nuru ambayo hatujawahi kuiona awali. Ila wale wanaodai kuupenda ukweli lazima waweze kutanua uwezo wao, ili waweze kuelewa mambo ya kina ya neno, ili Mungu atukuzwe na watu Wake waweze kubarikiwa na kuelimishwa. Kwa mioyo ya unyenyekevu, iliyojishusha kwa neema ya Mungu, mnapaswa kuja kwa jukumu la kuyapekua Maandiko, tayari kuupokea kila mwali wa nuru takatifu, na kutembea katika njia ya utakatifu.” — Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 25 {TN15: 3.2}
4
LAKIRI SABA
— Ishara za Nyakati —
“Ufunuo wa Yesu Kristo, Aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa Wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; Naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa Wake Yohana; aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufu. 1:1-3. {TN15: 5.1}
Yesu Kristo alitoa Ufunuo kuwaonyesha watumwa Wake “mambo” ambayo hayana budi kuwako upesi (Ufu. 1:1). Kuandaa njia ya maono ya yale “mambo,” Sauti ilitambulisha hiyo mada na ujumbe maalum kwa kila mmoja wa malaika saba (uongozi) ambao ulikuwa ni usimamizi wa vinara saba vya taa (makanisa) mtawalia. Jumbe hizi zimeandikwa katika sura ya 2 na ya 3. {TN15: 5.2}
Ijayo Yohana alielekezwa kuona taratibu takatifu za mahakama kwa mfululizo wa matukio: {TN15: 5.3}
“Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, Nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti.
“Na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua
5
PICHA
ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa
6
mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. {TN15: 5.5}
YALE AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO UPESI
[Picha: UFUNUO SURA YA NNE NA YA TANO]
“Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikuwa zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.” {TN15: 7.1}
“Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
“Na hao wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.” {TN15: 7.3}
“Na hao wenye uhai wanapompa Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye Aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele Yake Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia Yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, {TN15: 7.4}
“Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa Wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi Yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.” {TN15: 7.5}
“Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba. {TN15: 7.6}
“Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja mihuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu
7
astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.” {TN15: 7.7}
“Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, Yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile mihuri zake saba. {TN15: 8.1}
“Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. {TN15: 8.2}
“Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata Alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.” {TN15: 8.3}
“Nao waimba wimbo mpya wakisema, wastahili Wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa Ulichinjwa, Ukamnunulia Mungu kwa damu Yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” {TN15: 8.4}
“Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
“Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na vile ambavyo viko ndani ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na
8
uweza una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na Yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. {TN15: 8.6}
“Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.” Ufunuo 4, 5. {TN15: 9.1}
Utimilifu halisi wa haya “mambo” ulikuwa ni hauna budi kuwako — baada ya maono ya Yohana; yaani, katika wakati wa Yohana huu utaratibu mtakatifu wa mahakama ulikuwa bado haujatukia, ila ungetukia, wakati fulani baada ya maono yale, baada ya karne ya kwanza. Hasa ambavyo ingekuwa punde au muda mrefu baada ya hapo, hata hivyo, hayakufunuliwa kwa Yohana. {TN15: 9.2}
Yeye alichukuliwa katika maono ili kuona na kuandika “mambo” hayo yenye matukio ambayo yangetukia mwanzoni mwa wakati wa jopo la ki-mahakama la Ufunuo 4, 5 lingeketi hakika. Kuhusu “mambo,” yale mengine, mambo ambayo yanafuata kama matokeo ya tukio hilo, alihakikisha Yeye Aliye na “funguo za kuzimu na za kifo,” baadhi yalikuwa na mengine yangekuwa (Ufu. 1:19); yaani, wakati jopo hili la Mungu linaketi, basi baadhi ya “mambo” ambayo yanaletwa kwa mtazamo yakiwa ni matokeo ya tukio hilo, tayari ni historia, ilhali baadhi ya hayo bado ni unabii — baadhi huonyesha nyuma na baadhi huonyesha mbele. {TN15: 9.3}
Jambo la kwanza na muhimu zaidi linalofanyika katika kikao hiki kitakatifu, ni kukifungua kitabu. Ikumbukwe, pia, kwamba kitabu kimefungwa na
9
lakiri saba (Ufu. 5:1). Kwa kuwa ni sehemu saba, kila sehemu moja moja imetiwa lakiri , lakiri saba kwa ujumla yote inafunguliwa mtawalia, ikiruhusu kila sehemu kuyakunjua yaliyomo yake yenyewe: Lakiri ya kwanza, au sehemu ya kitabu, hufichua mambo ya Ufunuo 6:2; ya pili, mambo ya aya ya 4; ya tatu, mambo ya aya ya 5 na 6; ya nne, mambo ya aya ya 8; ya tano, mambo ya aya ya 9 hadi 11; ya sita, mambo ya aya ya 12 hadi 17 na sura ya 7; ya saba, mambo ya sura ya 8 hadi 22. Kwamba lakiri ya saba husheheni sura ya 8 hadi ya 22 huonekana upesi kwa ukweli kwamba kila sura inaunganishwa na kiunganishi “na.” Kwa maneno mengine, Ufunuo, isipokuwa kwa sura tano za kwanza, ni uzalisho wa mambo yaliyokuwa kwenye kumbukumbu ndani ya hizo lakiri, na ambayo kwa matokeo ya kufungua hizo lakiri yalionyeshwa kwa picha mbele ya macho ya Yohana. {TN15: 9.4}
Sasa Ukweli huonyesha waziwazi kwamba Ufunuo haukubuniwa na kitu ambacho kiliasisiwa kwa maono ya Yohana, ila kwamba hujumuisha mambo ambayo kitabu kilichotiwa lakiri kilisheheni na ambayo yalifanywa yajulikane wakati huo. Kwa sababu maandishi ya Yohana yalinakili mambo ambayo kitabu kilichofunikwa kwa lakiri kilifichua hatua kwa hatua lakiri zake zilipofunguliwa, Uvuvio ulikipatia jina la
10
heshima “Ufunuo” — mambo yaliyofunikwa yakafunuliwa, mambo ya siri yakafichuliwa. {TN15: 10.1}
Mambo ya msingi katika sura ya 4 na ya 5, sura zilizotajwa hapo awali, ni haya: {TN15: 11.1}
(1) Kwamba mlango ulifunguliwa, si duniani, bali mbinguni; {TN15: 11.2}
(2) Kwamba Yohana alivyotazama ndani, aliona “Mmoja” ameketi kwa kiti cha enzi; {TN15: 11.3}
(3) Kwamba kitabu kilichofunikwa na lakiri saba kilikuwa katika mkono Wake wa kuume; {TN15: 11.4}
(4) Kwamba kitabu hicho hatimaye kilifunuliwa, na matokeo yake kama filamu Yohana alionyeshwa yaliyokuwa ndani yake, na ya kwamba yeye alipoyaandika akatupatia Ufunuo; {TN15: 11.5}
(5) Kwamba vilikuwapo pia vitabu vingine (Ufu. 20:12), na ya kwamba ingawa havikufungwa lakiri, Yohana hakuelekezwa kuona yale yalichokuwa yameandikwa humo; {TN15: 11.6}
(6) Wazee ishirini na wanne walikuwa wameketi kukizunguka kiti cha enzi; {TN15: 11.7}
(7) Kwamba Mwana-Kondoo (pia huitwa Simba) na elfu elfu mara kumi elfu, na maelfu ya maelfu ya malaika walikizunguka kiti cha enzi; {TN15: 11.8}
(8) Kwamba walikuwapo wanyama wanne, taa saba za moto (vinara vya taa), na bahari ya kioo; {TN15: 11.9}
(9) Kwamba Sauti hasa kwa mkazo ilimjulisha Yohana kwamba alikuwa akipewa taswira fupi tu tukio la unabii ambalo lingetukia tarehe
11
ya baadaye — “hayana budi kuwako upesi” kutoka kwa wakati wake, wakati fulani baada ya karne ya kwanza. {TN15: 11.10}
Kwamba maono ya Yohana ni utabiri wa tukio sawa na lile lililofunuliwa kwa Danieli (sura ya 7), huonekana kwa haraka kutoka kwa ulinganifu mfupi ufuatao: {TN15: 12.1}
MAONO YA DANIELI: (Danieli 7) | MAONO YA YOHANA: (Ufunuo) |
1.”Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa.” Dan. 7:9 | 1. “Kisha nikaona viti vya enzi.” Ufu. 20:4 {TN15: 12.2} |
2. “Na mmoja aliye Mzee wa siku ameketi.” Dan. 7:9 | 2. “Na Mmoja ameketi juu ya kile kiti.” Ufu. 4:2. {TN15: 12.3} |
3. “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake.” Dan. 7:10. | 3. “Nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto.” Ufu. 15:2 {TN15: 12.4} |
4. “Mmoja kama Mwana wa Adamu akaja … akamkaribia huyo Mzee wa siku, wakamleta karibu mbele Yake.” Dan. 7:13 | 4. “Katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne … Mwana-Kondoo amesimama. Ufu. 5:6” {TN15: 12.5} |
5. “Vitabu vikafunuliwa.” Dan. 7:10 | 5. “Na vitabu vikafunguliwa.” Ufu. 20:12 {TN15: 12.6} |
6. “Maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake.” Dan. 7:10 | 6. “Nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi… na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu.” Ufu. 5:11 {TN15: 12.7} |
12 | |
7. “Hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Dan. 7:10 | 7. “Saa ya hukumu Yake imekuja.” Ufu. 14:7. “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufu. 20:12 {TN15: 13.1} |
Waonaji wote wawili waziwazi hutangaza kwamba tukio waliloliona lilikuwa “Hukumu.” Tofauti kati ya picha hizo mbili ni kwamba Danieli aliongozwa kutazama ndani ya Hekalu wakati maandalio yalikuwa yakifanyika kwa Hukumu kukutana; ilhali Yohana aliongozwa kutazama ndani ya Hekalu baada ya hukumu kuanzishwa; hakika, Yohana hakuona tu Hukumu ikiendelea, ila aliona matukio yote tangu mwanzo hadi mwisho. {TN15: 13.2}
Kwa mfano, Danieli aliona mambo wakati viti vya enzi vilikuwa “vikiwekwa,” na wakati Mzee wa siku alikuwa akihama kutoka Kiti cha enzi cha Utawala (kiti ambacho juu yake Kristo aliketi kwa mkono wa kuume wa Baba — Ufu. 22:1) hadi kwa kiti cha enzi cha Hukumu (kiti cha enzi ndani ya hekalu). Kisha ilikuwa kwamba “Mmoja kama Mwana wa
13
Adamu alikuja, “na wakamleta karibu mbele ya” Mzee wa Siku (Dan. 7:13), si kwa mkono Wake wa kulia.” Lakini wale ambao wangeketi juu ya “viti vya enzi” vingine, ambavyo wakati huo “viliwekwa,” vikiwa vimepangwa, walikuwa bado hawajafika. Wakati Yohana alipotazama ndani hata hivyo, aliwaona wazee ishirini na wanne wameketi tayari kwenye viti vya enzi. {TN15: 13.3}
Danieli aliona “Mmoja kama Mwana wa Adamu” wakati Alipokuwa akiletwa karibu mbele ya Mzee wa Siku. Lakini Yohana alimwona Yeye baada ya kuletwa hapo. {TN15: 14.1}
Kwa Yohana kuonekana Kwake Alikuwa kama “mwana-kondoo,” na mmoja wa wazee akamwita “simba wa kabila la Yuda.” (hakika Yeye ni “Mwana wa Adamu,” Mwokozi, Mfalme wa Israeli — Kristo, Bwana.) Mbali na hayo, Yohana pia aliwaona wenye uhai wanne humo, kinara cha taa, na kitabu wakati kilipokuwa kinafunuliwa. Kurejelea, Danieli aliona tu sehemu ya maandalio, ilhali Yohana aliona ufunguzi wa Hukumu, na vikao vyote baadaye. {TN15: 14.2}
Jopo la Mahakama, Uvuvio hujulisha, hujumuisha mwamuzi — Mzee wa Siku; mashahidi — malaika; wakili — Mwana-kondoo; jopo la majaji — wazee; watuhumiwa — wenye uhai; na mtawala wao — “Simba wa kabila la Yuda.” (Kwamba wenye uhai wanne ni nembo ya uwakilishi ya watakatifu, kama wanyama wa Danieli 7 ni mfano wa mataifa, huwekwa wazi kwa taarifa ya mwenye uhai mwenyewe: “… kwa kuwa ulichinjwa,
14
ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa.” Ufu. 5:9.) {TN15: 14.3}
Mwanafunzi wa Ukweli unaoendela atamaki pia kwamba Danieli hurejelea kikao kimoja cha mahakama, ingawa hutaja hukumu mara mbili, — kwanza katika aya ya 10 ya sura ya 7, na pili katika aya ya 22. Hii itaonekana katika aya nane zifuatazo: {TN15: 15.1}
Katika aya kumi na nne za kwanza, Danieli huelezea yote aliyoyaona katika maono. Na katika Dan. 7:15 huelezea jinsi alivyokuwa na huzuni na fadhaa baada ya kuiangalia kazi ya uharibifu ambayo mnyama wa nne alifanya. Kisha, katika Dan. 7:16, husema kwamba alimkaribia malaika aliyekuwa amesimama karibu, na akamwomba ufasiri wa mambo aliyokuwa ameona. Kwa kuzingatia ombi hili, malaika akajibu: {TN15: 15.2}
“Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. Lakini watakatifu Wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.” Dan. 7:17, 18. {TN15: 15.3}
Ufafanuzi huu mfupi sana haukumridhisha Danieli. Na akiwa na nia hasa ya kujua kwa undani mambo yaliyotajwa katika Dan. 7:7-14 — ukweli kuhusu Hukumu, vile vile kuhusu mnyama wa nne na pembe yake ndogo ambayo ilikuwa na macho ya mwanadamu na kinywa cha kunena mambo makuu — Danieli aliomba
15
ufafanuzi zaidi, tena kwa hitaji akitaja Hukumu. Basi, malaika huyo alielezea kwa upesi, akizuilia kikamilifu ufafanuzi wake kwa nembo ya mnyama wa nne na kwa Hukumu. {TN15: 15.4}
Picha: DANIEL 7
“Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.” {TN15: 16.1}
“Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” {TN15: 16.2}
“Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu Wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na
16
sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. {TN15: 16.3}
“Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele. Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu Wake Aliye juu; ufalme Wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.” Dan. 7:23-27. {TN15: 17.1}
Dhahiri, basi, Danieli aliona tu kikao kimoja cha jopo la mahakama, lakini akakitaja mara mbili — kwanza kuhusiana na kuelezea aliyoyaona katika maono, na pili kuhusiana na upatikanaji wa ufafanuzi wa malaika kwa maono. {TN15: 17.2}
Hukumu itafanyika, malaika alimfafanulia Danieli, baada ya pembe ndogo kuinuka, na kabla ya watakatifu kuumiliki ufalme. (Angalia Dan. 7:8, 9, 22.) {TN15: 17.3}
Ila Yohana, baada ya kuonyeshwa matukio yote ya mahakama, huelezea Hukumu katika sehemu tatu, katika vikao vitatu tofauti: kimoja kabla ya kimya cha nusu saa (Ufu. 8:1), kimoja baada yake, na kimoja cha tatu wakati wa miaka elfu ( Ufu. 20:11, 12). Ukweli huu huonekana kutoka kwa mambo yafuatayo: {TN15: 17.4}
Wakati wa kipindi cha mihuri sita, wakati kikao cha kwanza cha Hukumu kinaendelea, wenye uhai wanne hawapumziki usiku na mchana, wakisema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwa, na yuko, na atakayekuja.” Ufu. 4:8. Lakini wakati lakiri ya saba inafunguliwa,
17
kimya kinakuwa mbinguni (wenye uhai wananyamaza, pia “umeme,” “ngurumo,” na “sauti” zinakoma — Ufu. 4:5) “kama muda wa nusu saa.” Ufu. 8:1. Kimya hufichua wazi kwamba kikao cha kwanza cha matukio ya Jopo la mahakama kimefungwa, na ya kwamba kikao cha pili kinaanza baada ya kimya kukamilika. {TN15: 17.5}
Kikao cha tatu, kile cha wakati wa miaka elfu, ki penye “Kiti cha Enzi Kikuu Cheupe” (Ufu. 20:11, 12), kiti cha enzi chake Yeye ambaye kutoka kwa uso Wake dunia na mbingu zinatoweka. Penye kiti hiki cha enzi cha mwisho hakuna “bahari ya kioo,” hakuna “wenye uhai,” hakuna “Simba,” hakuna “Mwana-Kondoo,” na ingawa vipo “viti vya enzi” vidogo (Ufu. 20:4), Uvuvio hausemi katakata ni nani wanakaa juu yavyo. {TN15: 18.1}
Sasa mazingira ya Hukumu katika kila mojawapo ya vikao vitatu vya jopo la mahakama na wakati halisi vinapofanyika kwa uhalisi yataonekana katika uchanganuzi wa ukaguzi ufuatao: {TN15: 18.2}
Ingawa matukio ya vikao viwili vya kwanza ni tofauti kidogo, viko sawa katika masuala mengine yote. Cha tatu, hata hivyo, ni tofauti kabisa kwa viwili vya kwanza. Tofauti zinaonekana kwa sababu kabla ya kimya cha nusu saa kutukia, ipo penye kiti cha enzi “bahari ya kioo kama bilauri” (Ufu. 4:6), na hakuna yeyote anayesimama juu yake; lakini baada ya kimya cha nusu saa kupita, taswira inabadilika: “bahari ya kioo” na “iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na
18
sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.” Ufu. 15:2. {TN15: 18.3}
Kwa maneno mengine, katika kikao cha kwanza cha Hukumu hakuna yeyote anayesimama juu ya bahari ya kioo, na bahari yenyewe ni “kama bilauri;” ilhali kwa kikao cha pili bahari inaonekana kama mto wa moto, na watakatifu wanasimama kwayo. {TN15: 19.1}
Ukweli kwamba vikao viwili vya kwanza vinafanyika kabla ya dunia kutoweka, kabla ya hali ya sasa ya ulimwengu kufika kikomo; pia ukweli kwamba kikao cha pili kinafunga pamoja na watakatifu wanaoishi hasa wakati wa mwisho, wakati wa sanamu ya mnyama, wakati tu kabla ya dunia kutoweka; — haya yote hutoa ushahidi usioweza kupingwa kwamba vikao viwili vya kwanza, vya kabla ya millenia vinaleta dunia ya sasa mwisho; ya kwamba Hukumu sio kitu zaidi au kisichozidi utengo wa “magugu” kutoka kwa “ngano,” wote kati ya wafu na miongoni mwa walio hai; kwamba ni kuwapeleza wageni wote kwa jicho pevu kuamua ni nani waliojivika, na ambao hawajajivika, “vazi la harusi” — jambo ambalo linaamua ni nani atakayeachwa na ni nani atakayeangamizwa dunia inapotoweka. {TN15: 19.2}
Kwamba wafu wanahukumiwa katika kikao cha kwanza, na walio hai katika kikao cha pili, inaonekana kutoka kwa mfano wenyewe: Kama ilivyoelezwa hapo awali, wakati wa kikao cha kwanza hakuna
19
yeyote aliyesimama juu ya bahari ya kioo, na bahari yenyewe ni “safi kama bilauri.” Lakini katika kikao cha pili, watakatifu wanasimama kwa bahari, na imechangamana na moto (nembo ya uzima). {TN15: 19.3}
Kisha, pia, katika vikao viwili vya kwanza, Mwokozi anawakilishwa kama mwana-kondoo aliyechinjwa (Ufu. 5:6), akiweka kwa uthabiti matukio katika wakati wa kipindi cha rehema — ambapo damu ya Mwana-Kondoo inapatikana ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu. Na tamko la Danieli kwamba “watakatifu Wake Aliye juu wakapewa hukumu,” baada ya hapo “na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.” (Dan. 7:22), kidete huweka wakati wa Hukumu mbele ya wakati watakatifu wanaupokea Ufalme. Kwa hivyo, uzito wa ushahidi tena na tena unasimama kuonyesha kwamba Hukumu sio kitu kisichozidi au zaidi ya ukaguzi wa “wageni” ambao wamekuja kwenye karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo, ambao wamejiunga na kanisa. Wale hatimaye wanapatikana hawajajivika vazi la harusi, wanatupwa nje. {TN15: 20.1}
Pia, ukweli kwamba mwishowe Hekalu limefunguliwa, kwamba malaika saba na wenye uhai wanatoka ndani yake, kisha wakati huo linajazwa moshi kutoka kwa utukufu wa Mungu ili kwamba mtu awaye yote asiweze kuingia ndani yake “hadi mapigo saba ya malaika saba yatimizwe” (Ufu. 15:5-8), hadi miji ya mataifa ianguke, hadi kila kisiwa kikikimbie, na milima kutoweka (Ufu. 16:19, 20),
20
— haya yote huonyesha dhahiri kwamba pamoja na kipindi cha pili jopo la Mahakama linafungwa, Mlango wa rehema unafungwa kwa wote, mapigo yanamiminwa, na dunia inatoweka. Kisha inaanza, penye Kiti Kikuu cha enzi Cheupe, Hukumu kuu ya wafu, ya wale ambao hawataamka katika ufufuo wa kwanza, na wale ambao, badala ya kuhamishwa bila kuonja mauti, wanauawa kwa mwangaza wa kuja Kwake. {TN15: 20.2}
Kutangulia matukio haya ya mwisho “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. {TN15: 21.1}
“Na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake Yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa Chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.” Ufu. 19:20, 21. Kisha inakuwa kwamba malaika anamfunga Ibilisi, mwasi wa mwisho, na dunia inatoweka. {TN15: 21.2}
Hivyo ndivyo millenia inavyoanza, na hivyo malaika anamtupa Ibilisi kuzimu — mahali ambapo haiwezekani kwa mtu mwingine yeyote kusimama — anamfungia humo, na kutia lakiri juu yake, “asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie [mpaka ufufuo wa pili]: na
21
baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakakapewa Hukumu” wakati wa miaka elfu. {TN15: 21.3}
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso Wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufu. 20:1-5, 11, 12. {TN15: 22.1}
Yohana aliona kwamba baada ya mambo hayo kutukia, “bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake: na wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” Ufu. 20:13-15. (Tazama pia Pambano Kuu, uk. 480.) {TN15: 22.2}
Ni Kibiblia hakika kwamba mwanzoni mwa millenia waovu wote “waliuawa kwa upanga wake Yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa Chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.” (Ufu. 19:21), na kwamba waliohukumiwa penye Kiti Kikuu cha enzi Cheupe ni wafu, na pia ya kwamba mtawalia
22
waliohukumiwa wote wanafufuliwa mwishoni mwa miaka elfu; yaani, jinsi Yohana anavyosema, basi “bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.” Ukweli huu huthibitisha kwa maneno ya hakika kwamba hakuna walio hai duniani wakati wa “miaka elfu,” na kwamba wale wanaokuja katika ufufuo wa pili, wote ni waovu — wote ambao hawatakuja katika “ufufuo wa kwanza “ (Ufu. 20:6), wote watakaowajibishwa mauti ya pili (Ufu. 20:14). {TN15: 22.3}
Isitoshe , kwa sababu kipo kikao kimoja tu cha Mahakama kilichoketi wakati wa millenia, “viti vya enzi” vya Ufu. 20:4 lazima viwepo katika kikao pamoja na Kiti Kikuu cha enzi Cheupe. Zaidi ya hayo, hakuna uwezekano kwamba “Kiti Kikuu cha enzi Cheupe” kingekuwa katika kikao chenyewe. {TN15: 23.1}
Na, pia, kuona kwamba ufufuo wa kwanza, ufufuo wa mwanzoni mwa millenia, unawaleta watakatifu wote, wenye haki, na hakuna wengine, inafuata kwamba ufufuo wa pili, ufufuo mwishoni mwa millenia, unawaleta waovu wote, na hakuna mtakatifu miongoni mwao. {TN15: 23.2}
Matukio haya yote ya mwisho katika masaa ya kufunga ya injili, huthibitisha tena na tena kwamba hakuna mmoja wa waovu atakuwa hai wakati wa miaka elfu, miaka baada ya dunia kutoweka na kabla yake
23
kuumbwa upya, na vile vile wakati wote huo hakuna yeyote atakayeokolewa, na hakuna yeyote atakayepotea. {TN15: 23.3}
Kama ilivyoonyeshwa awali, waovu wote watakufa mwanzoni mwa millenia; kwanza mnyama na nabii wa uongo, kisha masalia, wengine wa dunia. (Tazama Ufunuo 19:20, 21). Watakatifu, hata hivyo, walio hai na wale ambao watafufuliwa wakati wa mwanzo wa millenia wote wataishi na kutawala miaka elfu na Kristo, sio Kristo pamoja nao. Hao wafu waliosalia, dunia yote, hawatakuwa hai hata itimie ile miaka elfu (Ufu. 20:4, 5). {TN15: 24.1}
“Naenda” alisema Yesu, “kuwaandalia mahali. Basi Mimi nikienda na kuwaandalia mahali, Nitakuja tena Niwakaribishe Kwangu; ili nilipo Mimi, nanyi mwepo.” Yoh. 14:2, 3. Dhahiri, wale wanaoishi wakati wa millenia, wanaishi na Kristo katika majumba ya juu. Kisha, baada ya miaka elfu, anafichua Yohana, “bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; nao [walikuwa] wamehukumiwa kila mtu kadiri ya matendo yake.” Ufu. 20:13. {TN15: 24.2}
Hivyo, waovu watafufuliwa kutoka kwa wafu wakati miaka elfu ikimalizika, na matokeo yake Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake, na ataweza kuwadanganya wale ambao majina yao hayakupatikana katika kitabu cha uzima, “ Gogu na Magogu,
24
kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.” {TN15: 24.3}
“Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.” Ufu. 20:7-10, 14. Tukio hili la mwisho katika sarakasi ya mwisho ya dhambi, linaleta umilele usiokuwa na dhambi kwa dunia. {TN15: 25.1}
Bado zaidi, kama wote watakatifu walio hai na waliofufuka wanachukuliwa “kuishi na kutawala na Kristo,” na kama wote wale wanaohukumiwa penye Kiti Kikuu cha enzi Cheupe, wanahukumiwa wakiwa kwa wafu, ukweli unasimama wazi zaidi na zaidi kwamba hakuna waovu walio hai wakati wa miaka elfu. Hakika hakuna, kwa maana nchi na mbingu kwa wakati huo zitakuwa zimetoweka, zimeondolewa kwa matabaka yao ya awali, kuwa ukiwa kwa maisha na utupu (Isa. 24:1-6; Yer. 4:23-26), “kuzimu” (Ufu. 20:1) ambamo hakuna mtu anayeweza kusimama. Lazima, watakatifu, wale waliosazwa, wanaishi na kutawala miaka elfu pamoja na Kristo katika mbingu za mbingu, palipo na “majumba mengi.” Wakati miaka elfu inafika kikomo, Mji Mtakatifu utashuka, majumba,
25
Yerusalemu Mpya, na watakatifu pamoja nao (Ufu. 21:2). Kuanzia wakati huo kuendelea watakatifu hawaishi pamoja na Kristo ila Yeye anaishi pamoja nao (Ufu. 21:3). {TN15: 25.2}
Kama ilivyoelezwa hapo awali, kwa Yohana wakati wa kuanzishwa kwa Hukumu ilinenwa bila mkazo kwamba “haina budi kuwako upesi” kutoka kwa wakati wake lakini kwa Danieli ilionyeshwa dhahiri ingeanza wakati fulani baada ya “pembe ndogo” kuinuka, na kabla ya watakatifu kuumiliki Ufalme (Dan. 7:8-11). Tarehe halisi, ingawa, imebainishwa na Danieli 8:14 — “Akamwambia, hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa,” magugu yataondolewa ndani yake. Wakati huo, ambapo utakaso unaendelea, kanisa linatangaza: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja. Msujudieni Yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufu. 14:7. (Kwa ufafanuzi kamili wa Danieli 8:14, soma Trakti Namba 3, Hukumu Na Mavuno.) {TN15: 26.1}
Kwa sababu kitabu kilichofungwa na lakiri saba, kitabu cha pekee ambacho “hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi … aliyestahili kukifungua … wala kukitazama,” isipokuwa Simba wa kabila la Yuda, bila shaka ni Kitabu ambacho matendo ya wanadamu hunakiliwa, kwa kadiri lakiri zenyewe zinavyofunua. {TN15: 26.2}
Ukweli huuUvuvio pia huthibitisha: “Hivyo viongozi wa Wayahudi walifanya uchaguzi wao. Uamuzi wao uliandikwa katika kitabu ambacho Yohana alikiona mkononi mwa Yeye aliyeketi juu ya kiti cha enzi, kitabu
26
ambacho hakuna mtu aliyeweza kustahili kukifungua. Katika ulipizi kisasi wake wote uamuzi huu utatokea mbele yao katika siku ambayo kitabu hiki kitafunguliwa na Simba wa kabila la Yuda.” — Mafunzo ya Yesu kwa Mifano, uk. 294. {TN15: 26.3}
Kile ambacho kitabu hiki kinasheheni, sasa kinakuwa dhahiri kabisa: Kinasheheni historia ya dunia na matendo ya watu wote. Na, bila shaka, busara huamua kwamba kwa ufunguzi wa kitabu, upelelezi wa jopo la Mahakama kwa matendo ya watu waliojidai kuwa wa Mungu unapaswa kuanza, kama vile Ufunuo wenyewe unavyofichua. Zaidi ya hayo, kwa sababu maneno na nembo ya Ufunuo hufasiri wowote kuliko ule uliofanywa hapa, ukweli wa mambo haya sasa unasimama imara na hakika. {TN15: 27.1}
Hekalu (kanisa), chombo ambacho huwahifadhi watu wa Mungu, basi ndilo litakalotakaswa. Hatimaye, hata hivyo, kama ilivyoelezwa awali, wanadamu wote, hata wapagani wanapaswa kuja mbele ya kizimba cha jopo la Hukumu ya Mungu, mbele ya “Kiti Kikuu cha Enzi Cheupe.” {TN15: 27.2}
Hivyo, tukio hilo lilikuwa “halina budi kuwako upesi” tangu wakati wa Yohana, wakati ambapo yangepelelezwa mambo ambayo yalitukia kabla ya wakati wa Yohana, na mambo yaliyotukia baada ya wakati wake (Ufu. 1:19) — matendo ya watu wote tangu mwanzo hadi mwisho. {TN15: 27.3}
Kinabii, Hukumu iliwekwa na vitabu vikafunguliwa, lakini hakuna mtu yeyote katika ulimwengu wote wa Mungu alistahili
27
kukifungua kitabu kilichofunikwa, au hata kutazama ndani yake, isipokuwa Mwana-Kondoo — Mwokozi wa ulimwengu, Mfalme wa wafalme, Simba wa kabila la Yuda, Mfalme wetu na Mtetezi, wa Uumbaji Alpha na Omega, Mwanzo na Mwisho. Hivyo ni kwamba, kama Mtetezi wetu wa pekee, Yeye Ambaye ameishi miongoni mwetu, Ni Yeye pekee anayeweza kupitia uzoefu wa kibinafsi kuelewa na kwa huruma kuzifungua siri za zamani, za sasa, na za baadaye — mmoja tu anayestahili kukifungua kitabu na kuwatetea wanadamu walioanguka. {TN15: 27.4}
Mlango uliofunguka mwanzoni mwa maono ya Yohana, huonyesha nyuma kwa siku ya Upatanisho, Kivuli, siku ya pekee kwa mwaka mzima ambayo mlango kati ya Patakatifu na Patakatifu Mno ulifunguliwa, na vyumba viwili kufanywa kuwa kimoja, na wakati huo huo mlango wa nje kufungwa. Kwa hivyo, alionyeshwa kuanza kwa Upatanisho wa uakisi, Yohana aliona mlango wa ndani ukifunguka, vyumba viwili vikafanywa kuwa kimoja. {TN15: 28.1}
Katika Upatanisho wa kivuli hatima ya kila mtu miongoni mwa waliojidai kuwa watu wa Mungu, iliwekwa isitanguke milele — wale waliozingatia matakwa ya sheria waliachwa waishi, na wale ambao hawakuzingatia, “walikatwa kabisa” kutoka miongoni mwa watu. Hivyo ni lazima pia iwe katika Upatanisho wa uakisi. {TN15: 28.2}
“Katika huduma ya kivuli, wale tu waliokuwa wamekuja mbele ya Mungu kwa kuungama na kutubu, na ambao dhambi zao, kupitia
28
kwa damu ya kafara ya dhambi, zilihamishwa hadi katika hekalu, walikuwa na sehemu katika huduma ya siku ya upatanisho. Kwa hivyo katika siku kuu ya upatanisho wa mwisho na hukumu ya upelelezi [Hukumu ya vikao viwili vya kwanza, wakati wa kutenga magugu kutoka kwa ngano, samaki wabaya kutoka kwa wema, kutoka miongoni mwa wote wafu na walio hai — mavuno] , kesi tu zinazoshughuliwa ni za watu waliojidai kuwa wa Mungu” (Pambano Kuu, uk. 480), wale ambao kwa wakati mmoja au mwingine walikubali mwito na wanayo haki ya kuvikwa “vazi la harusi.” Hivyo swali: Iwapo hukumu “ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Pet.4:17. {TN15: 28.3}
Kadiri vitabu vya rekodi vinapofunguliwa katika Hukumu, maisha ya wote ambao “juya” (kanisa) la wokovu limewahi kuwanasa, wema na wabaya pamoja, yanakuja kwa mapitio mbele ya Mungu, ili kutenganishwa. Humo kuhitimu kwa kila mmoja kunachunguzwa na kuamuliwa. Hakika, Hukumu ni mavuno. Naam, magugu yoyote kung’olewa kabisa na kuwekwa kando kuharibiwa, na ngano yoyote kuwekwa “ghalani” (ufalme) kwa ajili ya matumizi ya Mwalimu, wanatenganishwa katika siku ya Upatanisho ya uakisi. Kuanzia kwa wale waliokuwa wa kwanza kuishi kwa nchi, Mtetezi wetu huwasilisha kesi za kila kizazi mtawalia, na kufunga Hukumu ya kabla ya millenia na washiriki walio hai wa kanisa. {TN15: 29.1}
29
Utukufu wa Mungu huwakilishwa na mfano wa mawe ya thamani. Na upinde wa mvua juu ya Kiti Chake cha enzi cha Hukumu hufunua ahadi Yake isiyoshindwa kamwe na rehema kuu. Hili Yeye alimjulisha Nuhu wakati alipotangaza: {TN15: 30.1}
“Hii ndio ishara ya agano Nifanyalo kati Yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde Wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi…. Nami nitalikumbuka agano Langu, lililoko kati Yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.” Mwa. 9:12, 13, 15. {TN15: 30.2}
Uwepo wa Mwana-Kondoo mbele ya kiti cha enzi hutuhakikishia kwamba “Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.” 1 Yoh. 2:1. {TN15: 30.3}
Pembe saba za Mwana-Kondoo huashiria ukamilifu wa nguvu na mamlaka, katika uhakikisho ambao Kristo alisema: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” Mat. 28:18. Nguvu Yake isiyokuwa na kikomo kwa manufaa yetu, na kwa matumizi yetu. Yeye hutangaza: “Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” Mat. 17:20. {TN15: 30.4}
Macho saba ya Mwana-Kondoo huashiria kwamba mambo yote ni wazi na uchi Kwake.
30
“Niende” anasema mtunzi wa Zaburi, “wapi nijiepushe na roho Yako? Niende wapi niukimbie uso Wako? Kama ningepanda mbinguni,” anatangaza, “Wewe uko; ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, na kukaa pande za mwisho za bahari; huko nako mkono wako utaniongoza, na mkono Wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; giza na mwanga Kwako ni sawasawa.” Zab. 139:7-12. {TN15: 30.5}
Naam, nembo za “pembe saba,” “macho saba,” na “taa za moto saba,” hakika ni “roho saba za Mungu,” kazi ya Roho katika awamu zote, akitumwa ulimwenguni kote, kuwapatia nguvu watakatifu dhidi ya majeshi ya uovu, pia nuru kwa Injili ya Kristo, maono ya hali yao ya sasa na ya utukufu wao wa baadaye, na kadhalika. Kwa hivyo uhakikisho wa Mwokozi, “yawafaa ninyi Mimi niondoke, kwa maana Mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali Mimi nikienda Zangu, Nitampeleka kwenu.” Yoh. 16:7. “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina Langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote Niliyowaambia.” Yoh. 14:26. Kwa udhahiri, basi, mambo yoyote ambayo Uvuvio Wenyewe
31
haufundishi na kufasiri, hayafai kukumbukwa, kufundisha, au hata kuyasikiliza. {TN15: 31.1}
Taa za moto zikiwa saba kwa idadi, hizo, naam, zinaweza kuwakilisha kanisa lililo hai (Ufu. 1:20) lililovikwa nuru ya Ukweli wote wa Mungu — likifundisha ukweli wa sasa kwa kila kizazi mtawalia tangu ulimwengu kuanza, ukweli ambao kazi za kila mmoja hupelelezwa na kuhukumiwa, haki ya kila mmoja kupimwa kwenye mizani. {TN15: 32.1}
Basi mtu kuzikataa aidha nguvu za Roho, maono, nuru, ni hakika kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, na “hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” Mat. 12:32. Katika hukumu mtu wa namna hii hakika atapatikana amepungukiwa. {TN15: 32.2}
Kuihusu bahari ya kioo, katika maneno ya Danieli ni “mto wa moto,” ilhali katika maneno ya Yohana ni “bahari ya kioo iliyochangamana na moto.” Mto huu wa moto unaotoka penye kiti cha enzi kisichodumu cha mahakama, na Mto wa Uzima unaotoka penye kiti cha enzi cha utawala (Ufu. 22:1), lazima kwa namna fulani uwakilishe kitu ambacho ni cha kawaida kwa viti vya enzi vyote viwili. Na chaweza kuwa nini? — Iwapo mto, pamoja na Mti wa Uzima, ni uwakilishi wa kiini kinachoendeleza uhai, basi bahari ni uwakilishi wa uzima wa milele, kwa sababu “bahari” ni ghala, chanzo cha maji yote — hudumisha mitiririko ya mito. {TN15: 32.3}
32
“Moto” ni nembo inayofaa ya uzima, na “bahari” nembo inayofaa ya umilele, kuonyesha kwamba hizi mbili, uzima na umilele, hutoka kwa kiti cha Mungu pekee. {TN15: 33.1}
“Safi kama kioo,” bila shaka, huashiria ni huru kutoka kwa kasoro zote. Vipawa hivi, ambavyo vikikosa kuwapo vingine vyote hupotea, hutolewa bure kwa wote ambao dhambi zao zimeoshwa katika damu ya thamani ya Mwana-Kondoo, Mwokozi, Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. {TN15: 33.2}
“Na ndani yake [mji] hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Ufu. 21:27. {TN15: 33.3}
Bila shaka, wote wanaopata ushindi “juu ya mnyama, na juu ya sanamu yake, na juu ya alama yake, na juu ya taridadi ya jina lake,” wanapokea tuzo yao — “kusimama juu ya bahari ya kioo.” {TN15: 33.4}
Kuzifungua mtawalia lakiri saba na maudhui yake ya kibinafsi, kwa mtiririko huo hufunua kwamba historia ya wanadamu imegawanywa katika vipindi saba tofauti. {TN15: 33.5}
Sasa Ukweli hufichua kwamba kwa kuifungua lakiri ya kwanza — na ufunguzi wa sehemu ya kwanza ya kitabu — Hukumu inaanza. Pia ni udhahiri wenyewe kwamba penye kiti cha enzi cha Hukumu cha Mungu, katika vikao Vyake vitatu, nembo za Maangamizi huonyesha mataifa na watu, watakatifu na wadhambi, makanisa na makasisi, Shetani na malaika zake, — zamani, sasa, na siku zijazo. Hivyo “vitabu vyote vya Biblia
33
hukutana na kwishia ndani ya Ufunuo.” — Matendo ya Mitume, uk. 585. {TN15: 33.6}
Na sasa kuendelea na uchambuzi au mada, itakuwa vyema kukumbuka kwamba ufasiri wowote wa maandiko ambao hushindwa kwa ulinganifu kujenga jengo lisiloweza kuharibiwa la ukweli na kuleta somo la umuhimu maalum kwa wakati uliopo sasa, ni la uongo, lisilovuviwa na roho wa Kweli — kitu cha ubatili. {TN15: 34.1}
Isitoshe, kwa sababu habari iliyo wazi katika kurasa hizi na ufafanuzi mzuri wa maandiko yanayoshughulikiwa hauwezi kupuuzwa na yeyote ambaye ni mwaminifu kwake mwenyewe, basi ni lazima iwe kwamba kwa kuridhika kwao msingi wa matumizi ya “mambo” aliyoyaona Yohana, umesimamishwa imara. {TN15: 34.2}
Maandiko, anavyojua kila mwanafunzi wa Biblia yamekusudiwa kuwa ukweli wa sasa kwa wakati fulani — “chakula kwa wakati wake,” hususan mwafaka ili kukidhi mahitaji ya watu.” Sasa mambo haya yote yaliwajia kwa mifano; na yameandikwa kwa ajili ya mawaidha yetu, ambao mwisho wa ulimwengu umekuja.” 1 Kor. 10:11. Kwa maneno mengine, Maandiko ni sawa na hati za muda mrefu, au noti za benki, ambazo huwa halali kwa wakati fulani. Kwa hivyo, basi, wakati uliokusudiwa na Uvuvio ni wakati ambao mtu lazima azibadilishe kwa fedha, kwa mfano. {TN15: 34.3}
Hii ni kweli haswa kwa Ufunuo na kwa sababu tumefikia wakati wenyewe hasa kwa kusudi
34
Kiliandikwa, tunaweza sasa kwa ujuzi wa moyo wote na bila kushuku kukariri: “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufu. 1:3. {TN15: 34.4}
Tukiwa sasa tumepitia haya matayarisho mwanafunzi wa Ukweli endelevu anapaswa kuwa tayari kwa uelewa kujifunza Ufunuo wa mambo ambayo yataiandaa njia na kumwezesha kwa moyo wote kujua kwamba sasa wakati umekaribia, kwamba maarifa ya Ufunuo yatamwezesha kusimama katika “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana.” Anapaswa kuona kwamba sasa ndio wakati wa kujipatia maarifa ya “mambo” ambayo hayangeweza kufanywa yajulikane kabla ya
KUVUNJWA KWA LAKIRI SABA. {TN15: 35.1}
“Kisha nikaona hapo Mwana-Kondoo Alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda. {TN15: 35.2}
“Na Alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa. {TN15: 35.3}
“Na Alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi,
35
na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai. {TN15: 35.4}
“Na Alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.” Ufu. 6:1-8. {TN15: 36.1}
Kwa mtazamo wa ukweli kwamba lakiri husheheni historia ya dunia, rangi tofauti za farasi wanne — nyeupe, nyekundu, nyeusi, na kijivujivu — dhahiri huonyesha hali nne tofauti, moja baada ya nyingine. {TN15: 36.2}
Kisha, pia, taji ya aliyempanda wa kwanza, na upanga wa aliyempanda wa pili, pia mizani ya wa tatu, na jina la kifo kwa wa nne, — wote wanne namna rahisi jinsi nembo za Mungu zinavyoweza kuonyesha, zinafichua kwamba kwa matendo ya mwanadamu dunia imeenda kutoka kwa mema hadi kwa mabaya, kisha kutoka kwa mabaya hadi kwa mabaya zaidi na ya kwamba mwanadamu anahitaji kusaidiwa kutoka kwa ukatili wake, anahitaji kuelimishwa tena kwa mapenzi ya Muumba wake. Ufunuo wa mapenzi ya Mungu, hata hivyo, unakuwa wazi tu kwa kiasi cha utayari wa mtu kuziacha dhana zake na nia ya ubinafsi. {TN15: 36.3}
Musa, alipata ilikuwa rahisi mara elfu moja kuwaongoza watu kutoka Misri, kuliko kuiongoza Misri kutoka ndani mwao. Kufaidika kwa vikwazo vyao, kutupilia mbali
36
kila nadharia na nia ya ubinafsi mara moja, pasipo kuchukua miaka arobaini au hata siku arobaini, Kalebu na Yoshua wa leo bila sura ya shaka wanaona kwamba kwa farasi kinaonyeshwa kitu ambacho kimeumbwa na Mungu, lakini hutawaliwa (huendeshwa) na mwanadamu. Na ni kipi kingine isipokuwa dunia, ambayo mtu alipewa haki ya kuitawala? {TN15: 36.4}
[Picha ya Lakiri Nne za Kwanza]
37
Ni dhahiri, basi, chochote kingine (farasi na wapanda farasi), wanaweza kuwakilisha, iwapo kwa hakika hufichua kwamba kukengeuka kwa mwanadamu kutoka kwa haki kumeidunisha tabia yake, kumesababisha apoteze taji yake aliyopewa na Mungu pamoja na farasi wake mweupe serikali yake ya amani; yaani, kile kilichokuwa safi, “mweupe,” bila kasoro, mwanadamu amekisababisha kuwa najisi, cha udhalimu na ugomvi, cha udikteta, wenye nguvu na mauaji. {TN15: 38.1}
Kadiri dhambi ilipozidi, laana baada ya laana iliongezeka, na hivyo farasi mweupe aliandamwa na mwekundu, mwekundu na mweusi, mweusi na kijivujivu. {TN15: 38.2}
Sasa kufumbua ukweli wa yaliyomo katika kila lakiri, mambo ambayo kitabu kilichofungwa huleta kwa umakini wa jopo la Mahakama linalokizunguka kiti cha enzi cha Mzee wa Siku, na kwetu sisi ambao huyasoma kwa dhamiri ya uelekevu katika kuutafuta ukweli unaookoa, tunaanza na
NEMBO YA LAKIRI YA KWANZA. {TN15: 38.3}
“Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!
38
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.” Ufu. 6:1, 2. {TN15: 38.4}
[Picha ya Lakiri ya Kwanza]
Kwa kawaida, lakiri ya kwanza, ambayo Hukumu inafunguliwa kwayo, lazima isheheni mambo ya wakati haswa mwanzo wa jamii ya wanadamu. Kimantiki, basi, farasi mweupe, wa kwanza katika nembo hutambulisha hali iliyokuwapo kwanza ya ulimwengu — safi na isiyokuwa na dhambi na mtawala wa taji ya Mungu (aliyempanda farasi), ambaye mwanzoni hakuwa na lengo ila kuitiisha nchi na kuijaza na viumbe vya milele kama Mungu. Dunia yenyewe ilikuwa imefunikwa kwa vazi la uzuri na usafi, na maajabu yote juu ya nchi na baharini. Hakuna kilichopungukiwa. {TN15: 39.1}
39
Katika bustani ya Edeni “ilikuwa na miti ya kila aina, mingi ilikuwa ya matunda yenye harufu nzuri na matamu sana. Ilikuwapo mizabibu ya kupendeza … ikiwasilisha mandhari ya neema sana, na matawi yake yakining’inia chini kwa mzigo wa matunda yakutamanisha, yenye ladha nzuri na rangi mbalimbali.” — Mababu na Manabii, uk. 47. {TN15: 40.1}
Dunia katika ujana wake, ikiwa imejazwa na maua yenye maridadi na kufunikwa na zulia la kijani hai, iliyofanyizwa kwa mbingu za samawi, ilionyesha uzuri wa asili na fahari jinsi ambavyo hakuna lugha inayoweza kuelezea. Ajabu iliyo hai bila makosa, ambayo tu Msanii Mkuu Mwalimu angeweza kuileta. {TN15: 40.2}
Mpanda farasi na farasi wake mweupe (mfalme aliyevikwa taji na Mungu, Adamu, na serikali yake ya amani, farasi wake mweupe), ni, kwa hivyo, wa kwanza kupimwa kwa mizani, wa kwanza kuja kwa mapitio mbele ya Kiti cha enzi cha Mahakama. Kwa hivyo, tunakumbushwa tena kwamba tukio hili la kupeleleza tabia, Hukumu, ni jambo lile hasa ambalo lingetukia “hayana budi kuwako upesi” kutoka wakati wa Yohana, miaka baada ya karne ya kwanza ya enzi ya Ukristo. {TN15: 40.3}
Kilemba cha mpanda farasi na uta wake hukumbusha ofisi ambayo mwanadamu mwanzo aliijaza papo hapo Mungu aliposema, “Na Tumfanye mtu kwa mfano Wetu, kwa sura Yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
40
Mwa. 1:26. Na Mungu akawabariki Adamu na Hawa, na Mungu akawaambia, “zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha.” Mwa. 1:28. {TN15: 40.4}
Ni dhahiri kwamba penye Kiti cha Enzi cha Hukumu, farasi mweupe, mpanda-farasi, na taji yake, ki- mfano humtambulisha Adamu, mfalme aliyeumbwa na Mungu, na ufalme wake. Na ikiwa kitu cha pekee ambacho aliamriwa kushinda kilikuwa dunia, kwa kuijaza na kuisimamia, basi ni nini kingine chochote katika uwanja wa mfano kinaweza kuwa “upinde,” chombo cha kutumia kushinda kwa busara kisimwakilishe Hawa? {TN15: 41.1}
Kizazi kinachofuata kuitwa kutoa hesabu kwa ajili ya imani yake na uaminifu, kinaletwa nuruni katika
NEMBO YA LAKIRI YA PILI. {TN15: 41.2}
“Na Alipoufungua muhuri wa pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.” Ufu. 6:3, 4. {TN15: 41.3}
Kwa sababu farasi mweupe na aliyempanda amevikwa taji huwakilisha kipindi cha kwanza cha wanadamu, basi farasi mwekundu na aliyempanda muuaji anayeharibu amani, lazima awakilishe kipindi kinachofuata, kipindi ambacho mauaji na vita kwa mara ya kwanza vilizuka. {TN15: 41.4}
Abeli, bila shaka, alikuwa mhanga wa kwanza. Na kama tokeo, dunia yote ya Nuhu
41
iliangamizwa kwa gharika, na “laana ya tatu ya kutisha ikatua juu yake ikiwa ni matokeo ya dhambi.” — Mababu na Manabii, uk. 107. {TN15: 41.5}
[Picha ya Lakiri ya Pili]
Licha ya adhabu hii na somo lake, mara tu wakazi wa dunia walipoongezeka baada ya gharika, dhambi pia iliongezeka. Na ingawa watu wangeweza tu kutoa sifa kwa utabiri sahihi wa Nuhu kwa mafuriko, walikosa kumwamini katika utabiri wake ujao: utabiri kwamba haingekuwepo tena “gharika ya kuiangamiza dunia.” Mwa. 9:11. Hata
42
upinde wa mvua mawinguni, ishara ya Bwana Mwenyewe ya agano Lake la kutoigharikisha dunia mara ya pili, ulishindwa kuwashawishi. {TN15: 42.1}
Ni fumbo lililoje dhambi ilivyo hakika! Kwanza hawakuamini hata uwezekano wa gharika, na ijayo hawakuamini katika kutowezekana nyingine! Kweli, hukumu ya asiyeamini ni ya upumbavu kama hukumu ya mwanamke wa mashambani ambaye, alipoona kwa mara ya kwanza treni ikiwa kwenye reli, alitangaza kwa dhati, “haitaanza kwenda kamwe!” Kisha baada ya kuona ikianza kwenda, tena akatangaza, kwa mkazo kama hapo awali, “haitasimama kamwe!” Hivyo wakati roho ya kutoamini katika Neno siku zote imefisha ganzi akili na kutiisha mwili kutenda dhambi na kuoza, hata katika siku ambayo wanadamu walikuwa na nguvu na kuishi kwa muda mrefu, roho ile ile bado ina mashiko zaidi kwa wanadamu leo. {TN15: 43.1}
Badala ya kuwaweka huru kutoka kwa hofu, Neno la Mungu lililonenwa kupitia kwa Nuhu liliwachochea walioishi baada ya gharika kujihisi kwamba kulikuwa na hitaji lisiloepukwa kuujenga mnara wa Babeli kama kinga dhidi ya gharika ya pili. Kutofurahishwa na kutoamini kwao na kamsa ya uongo, hata hivyo, Bwana alionyesha ghadhabu Yake kwa kuhitilafiana na mradi wao wa uovu na wa upumbavu: Yeye aliharibu mnara wao na kuvuruga lugha yao. Hivyo ilikuwa kwamba mchafuko hapo Babeli (Mwa. 11:8, 9) ulizalisha jamaa na lugha zilizopo. {TN15: 43.2}
43
Hatimaye, jinsi wajenzi waliochanganyikiwa walipotengana katika vikundi, waliokuwa majirani wakaanza kugombana mmoja kwa mwingine. Na baada ya muda kuendelea kuwa mataifa, ugomvi wao ukakuwa vita. Kwa hivyo, ukweli wa kihistoria kwamba vita kwa mara ya kwanza vilizuka baada ya kuvurugwa kwa lugha, huonyesha kwamba farasi mwekundu na, hasa, aliyempanda, huonyesha kipindi ambacho mnara wa Babeli uliangamizwa kabisa, na ambao amani yake ilipisha vita. {TN15: 44.1}
Isitoshe, nanga nyingine ya uthibitisho, ni kirai, “kuiondoa amani katika nchi,” kwa maana chaonyesha wazi kwamba amani ilikuwapo kabla ya wakati huo. {TN15: 44.2}
Matokeo ya dhambi ya Adamu, ingawa, hayakukoma kwa tendo la kuharibu maisha na mali kama ilivyo vita. Yaliwaongoza wazawa wake kwa kuzorota kukubwa, hata ibada ya sanamu, kuziangamiza nafsi kwa njia ya dini, ambayo, katika tamasha ya dhambi, imefunuliwa katika
NEMBO YA LAKIRI YA TATU. {TN15: 44.3}
“Na alipoufungua muhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.” Ufu. 6:5, 6. {TN15: 44.4}
Kama ambavyo tumeona, farasi mweupe huwakilisha serikali ya mwanadamu kwa dunia wakati bado ilikuwa ni safi na tupu. Na sasa, kwa vile nyeusi
44
ni kinyume cha nyeupe, farasi mweusi lazima awakilishe serikali ya mwanadamu katika giza la kiroho na utekwani — hali ya kinyume na ile iliyowakilishwa na farasi mweupe. {TN15: 44.5}
[Picha ya Lakiri ya Tatu]
Hili limethibitishwa na historia: Hata kurudi nyuma hadi wakati wa Abrahamu, miaka mia tatu tu baada ya gharika, ibada ya sanamu ilikuwa imewalemea wenyeji wa dunia. Ulikuwa wakati huo ya kwamba Abrahamu aliondoka Harani, katika nyumba ya baba yake na nchi (Mwa. 11:31; 12:1). Wazawa wake, Israeli, kwa muda mrefu wakawa watumwa wa Farao, na baadaye kwa Nebukadnezza, Mfalme wa Babeli. {TN15: 45.1}
45
Jozi ya mizani mkononi mwa mpanda farasi lazima iweze kuonyesha wazi wazi zaidi kipindi ambacho farasi mweusi na aliyempanda hutanda, na wanachowakilisha. Kama tulivyoona upinde wa mpanda farasi wa kwanza huwakilisha njia ambazo Adamu aliitiisha nchi (kwa maana jamii yote ya wanadamu walikuja kupitia kwake); na upanga wa mpanda farasi wa pili, njia ambayo wazawa wa Adamu waliiondoa amani katika nchi. Kwa namna ile ile, mizani ya mpanda farasi wa tatu lazima kwa mwelekeo huu iwakilishe kile ambacho wanadamu baadaye walikianzisha. Na ni nini zaidi ya aina ya biashara ambayo nembo hiyo ingeweza kuonyesha? Mtu yeyote kwa utayari anaweza kutambua kwa urahisi kwamba mtu mwenye jozi ya mizani lazima awe na kitu cha kufanya kinachohusu kununua na kuuza. {TN15: 46.1}
Katika wakati wa Abramu, ujuzi wa kibiashara kati ya mataifa haukujulikana. Lakini wakati uliofuata, kipindi kilichowakilishwa na farasi mweusi, wazo hilo lilizaliwa. Wakati huo Sidoni na Tiro vikawa vituo vikuu vya kibiashara. Na Uvuvio huuliza swali: “Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?” Isa. 23:8. {TN15: 46.2}
Tiro, malkia wa Wafoinike ulikuwa mbali mfupi tu kutoka Sidoni. “Katika wakati wangeweza kueneza makoloni yao ya kibiashara katika nchi zote za Mediterrenia, na
46
katika nchi zingine, siku zote wakisaka maeneo mapya ya Uuzaji na vituo vya kibiashara. Walikuwa nyuki wa ulimwengu wa kale wakibeba mbelewele ya utamaduni huo popote walipokwenda. Mahitaji ya uuzaji na biashara yaliwasukuma kuifanya kamilifu alfabeti, na kutoka kwao ulimwengu wa magharibi uliipata. Kwa namna fulani walikuwa wa kipekee katika ulimwengu wa kale, na utofauti huu walizikwa pamoja nao. Kwa maana hawakuwa na hamu ya vita, isipokuwa biashara; hawakujali kulipa kodi kwa mamlaka ya kijeshi, almuradi mamlaka hayo hayangehitilafiana na haki zao za uuzaji. Walikuwa na uwezo kama wa Wayunani wa kuishi wenyewe hata wawe Misri, Babeli, Ashuru, Uajemi au awamu nyingine yoyote ya ustaarabu iliyotolewa; lakini kipaji chao kikuu kilikuwa katika uvumbuzi, ujuzi wa kiufundi, shughuli za biashara, na katika viwanda. Katika kazi za vyuma, dhahabu, pembe za ndovu, vioo, na rangi za zambarau walisimama katika ulimwengu wa kale bila kifani. {TN15: 46.3}
“…Kupitia miji yao ilinoga biashara ya faida sana ya Arabia na Mashariki: na wazalishaji wao waliendelea kubadilisha bidhaa zao za madini ya chuma, vioo na zambarau. Baharini na ardhini walisafiri kila mahali — wamishonari wa biashara — walimu wa mapatano wakuu wa Dunia ya Kale.” — Maarifa Muhimu, Wafoinike, Gombo la 1, uk. 69, 70. {TN15: 47.1}
Amri ile, “usiyadhuru mafuta wala divai,” ilitoka katikati ya kiti cha enzi, kutoka kwa Mzee wa Siku, si
47
kutoka kwa mpanda farasi. Kwa hivyo, zile bidhaa mbili, mafuta na divai, haziwakilishi tu kitu ambacho Mungu pekee anaweza kuumba lakini pia kile ambacho Yeye huazimia kukihifadhi wakati watu waovu wangetaka kukiharibu; hivyo hitaji la Yeye kuamuru dhidi ya mtu yeyote kuyadhuru. Na ni bidhaa gani zingine za kiroho ambazo mafuta na divai haswa wakati huo — wakati wa farasi mweusi — zingewakilisha ila bidhaa ambazo Biblia ilitoa? Zaidi ya hayo, ni ukweli uliokubaliwa na karibu wanafunzi wote wa Biblia, kwamba “mafuta” huakilisha ukweli wa kinabii, ukweli ambao humulika nuru kwa wakati ujao, ambao huangaza njia ya msafiri (Zab. 45:7, Zek. 4:12); na kwamba divai huwakilisha sehemu ya ukweli ambao humfanya mpokeaji kuwa na furaha, kumfanya atende tofauti kuliko awali (Isa. 61:1-3). {TN15: 47.2}
Kwa muhtasari, ni dhahiri kwamba amri hiyo, “usiyadhuru mafuta wala divai,” ilizuia kuhitilafiana na maandishi ya Maandiko, tena kuonyesha kwamba kule kuifungua lakiri ya tatu hufichua kipindi ambacho alfabeti ilibuniwa na ambacho biashara ilichimbuka; kipindi ambacho Biblia ilikuwa inaandikwa, na ambacho taifa moja lilitawala lingine; kipindi ambacho kilizaa Falme. {TN15: 48.1}
Hivyo, wakati wa Agano la Kale linafungwa na muhuri wa tatu, mwanzo wa Jipya unafunuliwa katika
48
NEMBO YA LAKIRI YA NNE. {TN15: 48.2}
[Picha ya Lakiri ya Nne]
“Na alipoufungua muhuri wa nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.” Ufu. 6:7, 8.
Kwa sababu farasi wa rangi ya kijivujivu huangukia kipindi sawa kama yule mnyama dubwana wa Danieli 7:7, 8 (tazama uk. 16, 17), kipindi kilichofuata lakiri ya tatu, wote hivyo hufanana. Kwa hakika, rangi yake kwa sababu ni hafifu, iliyo pungufu, isiyokuwa ya rangi maalum
49
au halisi, farasi katika ukaguzi wa mwisho ni dubwana, pia. Ni dhahiri kabisa ya kwamba mpanda farasi wa rangi ya kijivujivu ni kisawe na yule aliyenena kinyume chake Aliye Juu, pamoja naye ambaye angewadhoofisha watakatifu, “na kuazimu kubadili majira na sheria.” Dan. 7:25. Huonekana kuwakilisha kilele cha ibada ya sanamu. Serikali ya kale ya Kirumi huwakilishwa barabara na mnyama dubwana, kwa kweli uongozi wake ulikuwa mchanganyiko wa sheria za kiraia na za kidini, za mafundisho ya Upagani na ya Ukristo. Hakuna mtu angaliweza kueleza iwapo serikali ya Kirumi ilikuwa ya Upagani au ya Ukristo, ya Kiyahudi au ya Mataifa. {TN15: 49.2}
Jina la yule mpanda farasi, “kifo,” pia linafaa barabara roho ya wakati huo ya utesi na ukatili wa wote Wayahudi na Warumi. Historia na unabii vilevile huthibitisha kwamba utawala wa uchochezi wa Kirumi “ulikula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake.” Dan. 7:19. {TN15: 50.1}
Ukweli kuhusu “robo ya nchi,” ambayo juu yake walipewa uwezo “kuua kwa upanga, na kwa njaa, na kwa kifo, na kwa wanyama wa nchi,” hugunduliwa kwa urahisi: Kugawanya 6,000, miaka kutoka uumbaji hadi mwanzo wa millenia, katika sehemu nne sawa, inatoa miaka 1500 (“sehemu ya nne”), mwishoni mwa muda ambao huo utawala ungefifia. Tena, kwa sababu ni ukweli kwamba mauaji ya watakatifu yalianza kwa Kristo kusulubishwa, hii “robo ya
50
nchi” kwa hivyo ilianza wakati huo na kumalizika kwa “Maungamo ya Augsburg,” hati iliyoandaliwa na Luther na kuwasilishwa katika Mkutano wa Augsburg kwa Mfalme, Charles 5, mwaka 1530, — miaka 1500 kamili baada ya kufufuka kwa Kristo (kwa kuzingatia kwamba enzi ya Ukristo ni miaka 3 1/2 tarehe ya umbele), wakati ambapo utawala wa Kirumi ulidhoofika. {TN15: 50.2}
Mapungufu haya hayawezi kutuhumiwa zaidi kwa sababu katika nuru ya ukweli wa kihistoria kwamba mapambano ya Kiprotestanti dhidi ya udikteta, hatimaye yalisababisha mateso kukoma. Hivyo ni kwamba sehemu hii ya maandiko inayojadiliwa, ilitimizwa mwaka 1530 kwa kudhoofishwa kwa tawala za Wayahudi-Wapagani na tawala za Wakristo-Wapagani za kuua kwa upanga, njaa, kifo, na wanyama. {TN15: 51.1}
(Sehemu hii ya unabii, kwa kutukia, hupindua dhana potovu kwamba dunia imekuwapo kwa muda mrefu zaidi ya miaka 6,000.) {TN15: 51.2}
Katika hatua hii ni vyema kumaki kwamba wakati idadi ya farasi, wanne, huwakilisha pembe nne za dira, idadi ya lakiri, saba, huwakilisha ukamilifu wa injili, kutiwa lakiri kwa watakatifu. {TN15: 51.3}
Baada ya kuona ukweli wa lakiri nne za kwanza zilizofunuliwa, sasa tunapaswa kuchunguza
NEMBO YA LAKIRI YA TANO. {TN15: 51.4}
“Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu,
51
wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.” Ufu. 6: 9-11. {TN15: 51.5}
[Picha ya Lakiri ya Tano]
Uhakika kwamba roho zililia kutoka chini ya madhabahu, mahali ambapo ukweli wa Mungu hutolewa, huonyesha dhahiri kwamba waliuawa kwa uthabiti wao katika Neno la Mungu, na kwamba kwa uaminifu wao walipewa mavazi meupe — walihesabiwa kuustahili umilele. Kwamba walikuwa wafia imani wa kipindi kilichopita, kipindi cha muhuri wa nne, ni
52
wazi kutoka kwa ukweli kwamba walikuwa tayari wamekufa wakati muhuri wa tano ulifunguliwa. {TN15: 52.1}
Aidha, madhabahu huashiria upya wa imani, matengenezo. Hiyo ndio ilikuwa maana yake kwa Nuhu, Abrahamu, Isaka, na Yakobo katika matukio waliyojenga madhabahu yao (Mwa. 8:20; 12: 8; 26:25; 35:14). Roho ‘kuwa chini ya madhabahu, zinaonyesha kwamba waliyatoa kafara maisha yao kwa ajili ya utume sawa na utume wa wafia imani wakati wa Matengenezo ya Kiprotestanti. Na swali, “Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu?” pia jibu, “wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao,” kwa uhakika huthibitisha kwamba mateso na mauaji ya muhuri wa nne yalipaswa kuingiliana na muhuri wa tano, na kwamba Hukumu ya wafu (wafia imani) haingeanza hadi baada ya mateso kuwa yamekoma, lakini kwamba hakika ingeanza. {TN15: 53.1}
Mlolongo huu wa matukio ya kihistoria sasa unatuleta wakati wa matukio yajayo, yale yanayofunuliwa katika
NEMBO YA MUHURI WA SITA. {TN15: 53.2}
“Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.” Ufu. 6:12, 13.
53
Ni mojawapo ya imani misingi ya Dhehebu kwamba unabii wa muhuri wa sita ulianza kutimizwa kwa lile tetemeko kubwa la ardhi la Lisbon mnamo Novemba 1, 1755. Kufuatia tetemeko lile la ardhi, Mei 19, 1780, jua lilikuwa giza, na mwezi ulionekana kama damu usiku uliofuata. Kisha “kuanguka kwa nyota,” marasharasha makuu ya vimondo ya Novemba 13, 1833 (Pambano Kuu, kr. 304-309, 333, 334). {TN15: 54.1}
Akitazama mbele kwa maonyesho ya kimbingu (ishara za nyakati), Yesu alionya kimbele kwamba zingeonekana “mara moja
54
baada ya dhiki” kukoma (Mat. 24:29). Kwa hiyo, wakati amani, vita, biashara, alfabeti, na mateso ni ishara za nyakati na utambuzi wa mihuri mitano ya kwanza, kama vile tetemeko la ardhi, siku ya giza, na marasharasha ya vimondo ni ishara za nyakati na ni kitambulisho cha muhuri wa sita. {TN15: 54.2}
Misukosuko hii ya kimataifa na maonyesho ya kimbingu kati ya miaka 1755 na 1833, kwayo yenyewe, hata hivyo, inaonekana kuwa utabiri wa mambo ambayo yatatukia wakati wa siku kuu na ya kutisha ya Bwana. “Ikiwa hii ni kweli, basi tetemeko la ardhi kimbele ni kivuli cha mtikiso, upepeto unaokuja, kati ya mataifa, kama ilivyotabiriwa na manabii: {TN15: 55.1}
“ “Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto ulao; na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu. Na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.” Isa. 30:27, 28; Nah. 2: 3. {TN15: 55.2}
Jua kuwa giza kungeweza kuashiria kufungwa kwa injili, mwisho wa wakati wa muda wa rehema, wakati ambapo “watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” Maana, tazama, giza litafunika dunia, na
55
giza kuu litazifunika kabila za watu.” Amosi 8:12; Isaya 60: 2. {TN15: 55.3}
Mwezi, unaohusishwa na jua, hufanya nembo inayofaa ya kanisa, chombo ambacho Neno la Mungu, huakisi, nuru ya ulimwengu. Mwezi kuwa kama damu mara baada ya jua kuwa giza, ukikataa kuakisi nuru, itakuwa ni dalili muafaka ya kanisa likiwa limekamilisha kazi yake ya wokovu, kutoendelea kuhitaji kuiakisi Nuru ya Injili. Na kanisa lenyewe, naam, kwa wakati huo, limepewa uzima wa milele, limeokolewa kutoka kwa uharibifu kama ilivyokuwa mzaliwa wa kwanza katika makao ambamo miimo ya milango ilikuwa imepakwa damu ya kafara jioni ya Pasaka katika nchi ya Misri. {TN15: 56.1}
Nyota zinazoanguka ni kidokezi cha siku kuu na ya kutisha ya Bwana — siku ambayo “mbingu … zitatoweka” (2 Petro 3:10), siku ambayo jeshi lake litafumuliwa, na ambayo Ibilisi na jeshi lake, pia waovu ndani ya kanisa na duniani, “watanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.” Isa. 34: 4. {TN15: 56.2}
Ishara hizi zote zinasimama kama mashahidi waaminifu kwamba muhuri wa sita, kipindi cha wakati cha sita, kinaleta siku kuu ya Mungu, hasira ya Mwana-kondoo. {TN15: 56.3}
“Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na
56
kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu. 6: 14-17. {TN15: 56.4}
Katika aya hizi ni taswira ya hatima, hofu, na dhamiri zilizosononeka za wote ambao hawawezi kusimama siku ya Hukumu ya walio hai, siku kuu na ya kutisha ya Bwana — hasira ya Mwana-Kondoo katika mkuu “wakati wa taabu mfano wake haukuwapo” (Dan. 12: 1), siku inayofuata kuonekana kwa wa uakisi “nabii Eliya” (Mal. 4: 5) — naam, siku ambayo wale hawajajivika vazi la harusi, wanatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno (Mathayo 22: 11-13). {TN15: 57.1}
Pia katika maandiko haya (Ufu. 6: 14-17), anadai Roho wa Kweli, “vyama viwili vinaletwa kwa mtazamo. Chama kimoja walijiruhusu kudanganywa, na kusimama upande pamoja na wale ambao Bwana ana vita nao. Walizifafanua visivyo jumbe zilizotumwa kwao, na wakajivika mavazi ya haki ya ubinafsi.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 268. {TN15: 57.2}
Hivyo ni kwamba wakati mihuri minne ya kwanza inatupitisha vipindi vya siku ambayo kazi za mwanadamu zinawekwa dhahiri,
57
mihuri mitatu ya mwisho inatupitisha katika siku ya Mungu, siku ambayo Ukweli Wake na matendo Yake yanawekwa dhahiri. {TN15: 57.3}
Kwamba kuwepo na kilele cha aina fulani katika kazi ya jopo la Mahakama katika hatua hii ya Maandiko (Ufu. 6: 14-17), sio siri. Kinapigwa stempu na matukio ambayo yanakamilisha utawala wa dhambi, na hili linang’amuliwa hata na wadhambi wenyewe, ni dalili nzuri sana kwamba katika muhuri wa sita Hukumu ya wafu inafungwa, na maandalizi ya Hukumu ya walio hai yanaanza. Ni “siku ya kutisha” kwa waovu. {TN15: 58.1}
Zaidi ya hayo, kama vile awamu ya kwanza ya Hukumu inapita na sura ya sita ya Ufunuo, awamu ya pili inaanza na sura ya saba; yaani, inaanza kwa kuwatia muhuri watakatifu walio hai, malimbuko. Ni “siku kuu” kwa wenye haki. {TN15: 58.2}
“Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.” {TN15: 58.3}
“Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.” Ufu. 7: 1-4. {TN15: 58.4}
58
Kutokana na kidokezi kwamba “pepo nne” zitavuma na malaika wanne
59
watadhuru mara tu watumishi wa Mungu wanatiwa muhuri kinaonekana kukaribia “wakati wa taabu” mfano wake haukuwapo (Dan 12: 1). {TN15: 59.1}
Kujongea kutoka pembe nne za dira, pepo lazima ziwakilishe msukosuko kote duniani wa aina fulani. Ni dhahiri sana pia, kwamba kuvuma kwazo na kudhuru kwa malaika, kunawakilisha majeshi mawili katika vita. Kuvuma kwa pepo ni, bila shaka, hasira ya mataifa dhidi ya watakatifu; na kudhuru kwa malaika ni bila shaka hukumu ya Bwana ikiwaangukia adui Zake. Kwa maneno mengine, kudhuru kwa malaika na pepo kuvuma pamoja huwakilisha taabu kati ya Mungu na mataifa inayowahusisha wote watakatifu na wadhambi. Hakika, ni siku kuu na ya kutisha ya Bwana. {TN15: 60.1}
Tofauti kati ya “dhiki kuu, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu” (Mat. 24:21), na “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa” (Dan. 12: 1). ), ni wakati wa “dhiki kuu” watakatifu waliuawa (Mat. 24:21, 22), wakati wa “taabu” wanaokolewa (Dan. 12: 1). {TN15: 60.2}
Kwamba malaika ‘wanaoshikilia pepo haimaanishi wao wanayazuia mataifa kupigana kati yao wenyewe, inawekwa wazi kwa ukweli kwamba pepo hazikushikiliwa zisigongane pepo dhidi ya pepo (taifa dhidi ya taifa), ila badala yake kuidhuru nchi, bahari, na miti. Aidha, kwamba mataifa kutoka kaskazini na
60
kutoka kusini, kutoka mashariki na kutoka magharibi yalihusika katika Vita Kuu ya I ya Dunia, na pia katika Vita Kuu ya II, ingawa 144,000 bado hata sasa hawajatiwa muhuri, ni ushahidi mwingine usiopingwa kwamba taabu ambayo inatabiriwa na upepo kuvuma na malaika kdhuru, bado ni ya baadaye. Kwamba ni msukosuko wa kimataifa, unaonekana tena katika ukweli kwamba pepo kwa upande mmoja, na malaika kwa upande mwingine, utaitaabisha dunia na bahari. {TN15: 60.3}
Kwa kuwa ni hitimisho la awali kwamba Shetani yu dhidi ya watakatifu, na kwamba Bwana yu dhidi ya wanaouchukia ukweli na umati wa watenda uovu, somo linakuwa wazi kama kioo: Wakati zinaachiliwa, pepo zitavuma dhidi ya waaminifu “masalia”, dhidi ya wale walioachwa baada ya nchi kukifunua kinywa chake na kuyameza “mafuriko,” “magugu” (Ufu. 12:16, 17); lakini malaika waliowekwa kudhuru, watawapiga wale watakaofanya vita dhidi ya masalia. Wale ambao majina yao yanapatikana katika kitabu, “wanaokolewa.” Dan. 12: 1. Kuona kwamba wale 144,000, wajoli wa Mungu, bado hawajatiwa muhuri (bado hawajafunikwa, hawajalindwa, na hawajakuwa tayari kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni, ila bado wamechangamana na magugu) malaika wameamriwa kusitisha mgongano. {TN15: 61.1}
Kwa hiyo, wakati kazi hii ya kutiwa muhuri imekamilika, basi malaika ambao wanashikilia pepo, wataziachilia pepo kuvuma, na malaika
61
ambao wataidhuru nchi, bahari, na miti, wataianza kazi yao. Kusema vinginevyo, kuziachilia pepo kuvuma, ni kumruhusu mnyama wa pembe mbili kuamuru “hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” (Ufu. 13:15); na kuruhusu malaika kudhuru, ni kuruhusu amri ya Bwana kuchukua mkondo wake: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.” Ufu. 14: 9, 10. Onyo hili linafuatwa na utabiri: {TN15: 61.2}
“Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.” Ufu. 9:15. {TN15: 62.1}
Amri zote mbili zitatekelezwa baada ya watu 144,000 kutiwa muhuri. {TN15: 62.2}
Hapa inaonekana kwamba kutoka miongoni mwa malimbuko ya mavuno, wanakuja watu 144,000, wajoli wa Mungu kwa kazi ya kufunga ya mavuno makubwa. Hawa ndio watakatifu wa kwanza ambao watawahi kuondolewa “magugu” miongoni mwao. Jitayarishe, Ndugu, Dada, kwa maana wakati umekaribia. {TN15: 62.3}
Tumeona sasa kwamba mihuri sita ya kwanza hufunua awamu ya ukweli unaofunika historia ya dunia tangu wakati wa Adamu kuendelea
62
hadi wakati wetu. Awamu hii ya ukweli inafunua kutiwa muhuri kwa malimbuko na mavuno ya pili: Kutoka miongoni mwa malimbuko wanakuja watu 144,000 — elfu 12,000 kutoka kati ya kila kabila kumi na mbili za wana wa Israeli. Kushuka kupitia karne nyingi, wao wamezawa kwanza kama Wayakobo na kisha Wakristo. Baada ya hao, wanakuja mavuno ya pili, umati mkubwa kutoka “kwa mataifa yote.” Ufu. 7: 9-17. {TN15: 62.4}
(Ile dhana kwamba watakatifu walio hai wakati wa ujio wa Bwana ni 144,000 tu kwa idadi, imekashifiwa kwa maana haiachi nafasi ya hata mtu mmoja kuokolewa kutoka kwa taifa isipokuwa wazawa wa Yakobo, sio hata kutoka kwa wazawa wa Abrahamu, isipokuwa kupitia kwa Yakobo mwenyewe. Halafu, ile dhana hulifanya neno “malimbuko” kuwa kitu bure kwa sababu haitetei mavuno ya pili.) {TN15: 63.1}
Salio ya Ufunuo, imefungashwa ndani ya
NEMBO YA MUHURI WA SABA. {TN15: 63.2}
“Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. (TN15: 63.3)
“Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. {TN15: 63.4}
63
“Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi. Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.” Ufu. 8: 1-6. {TN15: 64.1}
Baada ya muda vithibitisho vya jopo la Mahakama — sauti “zikisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenye Nguvu,” ngurumo za radi na umeme, — vinakoma kwa muda wa nusu saa, dhahiri kabisa kuonyesha kwamba jopo la mahakama kwa Kikao cha kwanza cha Hukumu kinafungwa. {TN15: 64.2}
Kufuatia hili, malaika saba wanapewa baragumu saba. Wakati uo huo, malaika ambaye amesimama kwenye madhabahu, anatoa maombi ya watakatifu wote, anachukua chetezo, anakijaza moto wa madhabahu, kuutupa juu ya nchi. Halafu inakuwa kwamba moto uliotoka mbinguni, “ngurumo za radi, na umeme, na sauti,” ambazo kikao cha kwanza cha Hukumu kilifunguliwa katika hekalu la mbinguni (Ufu. 4: 5), zinashuka juu ya nchi kwa mpango wa kinyume (sauti , radi, umeme – Ufu. 8: 5), na nyongeza ya tetemeko la ardhi. {TN15: 64.3}
Kisha baragumu saba zinavuma, moja baada ya nyingine. Kwa sauti ya baragumu ya saba (sio kwa kufuniliwa muhuri wa saba) pakawa “sauti kuu,” zikisema, “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.” Ufu. 11:15. {TN15: 64.4}
64
Kimya cha nusu saa mbinguni kinazileta sauti chini kwa nchi, na wakati wa kuvuma kwa baragumu ya saba siri ya Mungu inatimizwa (Ufu. 10: 7). Kisha inakuwa kwamba “falme za dunia hii zinakuwa falme za Bwana wetu.” Je, yote haya yanamaanisha nini? — Hili tu: {TN15: 65.1}
Jinsi ambavyo tumeoona, kimya hugawanya vikao viwili vya jopo la Mahakama kabla ya milenia, kimoja kwa ajili ya wafu na kingine kwa ajili ya walio hai, na moto kutoka kwa madhabahu ya mbinguni, sauti, umeme na ngurumo za radi, zinashuka juu ya nchi. Kweli hizi, pamoja na maandiko kadhaa juu ya somo hili, mbali na salio la Ufunuo, sura zote baada ya kuufungua muhuri wa saba, huthibitisha kwamba Hukumu ya walio hai, kutakaswa kwa hekalu la duniani, ni kitu kinachotukia juu ya nchi, sio mbinguni tu! {TN15: 65.2}
“Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula, … Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.” Mal. 3: 1, 2. {TN15: 65.3}
Naam, kazi ya kikao cha pili cha jopo la Mahakama inajumuisha hekalu la duniani, kanisa. Wakati huo “moto” wa Bwana u “ katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu.” Isa. 31: 9. {TN15: 65.4}
65
“Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. {TN15: 66.1}
Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.” Mika. 4: 2-4. {TN15: 66.2}
“… ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu … {TN15: 66.3}
“Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.” Mat. 25: 31-34, 41. {TN15: 66.4}
66
“Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. Huu ndio mwisho wa jambo lile …. “ Dan. 7:27, 28. {TN15: 67.1}
Mambo haya yote yanaashiria dhahiri katika wakati ambao “kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu,” jambo ambalo hasa linasababisha kuanguka kwa “Ashuru,” mamlaka ambayo inatawala Yerusalemu wakati Mungu atawakomboa Watu wake (Isa 31: 7, 8). {TN15: 67.2}
Ukweli kwa hiyo hauna tatizo: Kati ya Hukumu ya wafu na Hukumu ya walio hai kinasimama kimya cha muda wa nusu saa, wakati unaoshughulishwa kukifunga kikao cha kwanza cha jopo la Mahakama na kujiandaa kwa kikao cha pili. {TN15: 67.3}
Aya zilizosalia za sura ya 8, pia sura ya 9-11, zinatoa maelezo ya baragumu saba, makala kamili ambayo yanapatikana katika Trakti Namba 5, “Onyo la Mwisho.” {TN15: 67.4}
Sasa tunaletwa kwa sura ya 12 ya Ufunuo, ambayo inahusika na somo la
67
KANISA LILILO HAI DAIMA NA ADUI WAKE. {TN15: 67.5}
La kwanza la haya kuja kwa mapitio penye Kiti cha Enzi cha Hukumu, ni kanisa lililo hai daima. {TN15: 68.1}
“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili:” {TN15: 68.2}
“Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.” {TN15: 68.3}
“Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.” {TN15: 68.4}
“Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.” {TN15: 68.5}
“Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.” {TN15: 68.6}
“Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.” Ufu. 12: 1-6. {TN15: 68.7}
Ni wazi kuona kwamba huyu “mwanamke” alikuwa amevikwa jua na akashambuliwa na joka hata kabla ya mtoto wake, Kristo, kuzaliwa; naam, miaka kabla ya kanisa la Kikristo na Injili kuwapo. Kusema, basi, kwamba anawakilisha kanisa la Agano Jipya lililovikwa injili ya Kristo, hakika halina msingi na la uelewa finyu dhana kama vile kusema kwamba kifaranga
68
huanguliwa kabla ya yai kutagwa. {TN15: 68.8}
“Amevikwa jua,” mwanamke ni, bila shaka, kanisa la Mungu lililo hai daima, lililovikwa Nuru kutoka Mbinguni, Biblia. “Neno lako,” anasema mtunzi wa Zaburi, “ni… mwanga wa njia yangu.” Zab. 119: 105. {TN15: 69.1}
Mwezi, jinsi tunavyojua, ni chombo ambacho huakisi nuru ya jua na
69
usiku kuangazwa. Kwa kuwa u chini ya miguu ya mwanamke, ni nembo inayofaa sana ya kipindi kabla ya Biblia kuwapo, kipindi kutoka kwa uumbaji hadi kwa Musa. Awamu hii ya mfano inaonyesha wazi hakika kwamba mwanamke alikuwa anaibuka kutoka katika kipindi ambacho Neno la Mungu, “jua,” lilionyeshwa sio moja kwa moja, lilipokezwa kutoka kwa baba hadi kwa mwana, na kwamba alikuwa akiingia katika kipindi ambacho ndani yake alikuwa amevikwa Nuru ya Mungu, Biblia. {TN15: 69.2}
Zaidi ya hayo, alikuwa na mtoto wakati alipokuwa amevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake. Hili ndani yake lenyewe linaonyesha kwa hakika kwamba mwanzoni anawakilisha kanisa baada ya kupokea ahadi ya kumleta Mwokozi wa ulimwengu, “mtoto mwanamme, Ambaye angeyatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma.” Yeye “alinyakuliwa hadi kwa Mungu na kwa kiti Chake cha enzi.” Yeye, bila shaka, ni Kristo, Bwana. {TN15: 70.1}
Nyota kumi na mbili zinazojumuisha taji ya mwanamke, bila shaka zinaonyesha serikali ya Mungu duniani, mamlaka ya jumla ya kanisa — yale ya mababu kumi na wawili, ya kabila kumi na mbili za mitume kumi na wawili, na ya 12,000 kutoka kati ya kila kabila kumi na mbili za Israeli (watu 144,000). {TN15: 70.2}
Pia itaonekana kwamba anaonyesha kanisa lililo hai daima la Mungu likiwa bado katika vita na adui. {TN15: 70.3}
“Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake
70
vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.” Ufu. 12: 3, 4. {TN15: 70.4}
Iwapo mwanafunzi wa Ukweli uliovuviwa na Mbingu atahitaji kujua somo ambalo linafundishwa kwa nembo hii, sasa anapaswa kutambua kwa uangalifu maana ambayo pembe zisizo na taji za joka na vichwa vyake ambavyo vina taji hubeba. Pia, iwapo mwanafunzi wa Ukweli atafaidika na kile Maandiko hufundisha, ataweza kutambua barabara kwamba Maandiko yaliyotangulia na vigezo vinavyopatana na akili vinapaswa kuzingatiwa. {TN15: 71.1}
Cha kuanzia, kwa vile pembe za joka ni kikundi cha kumi, ni lazima ziwakilishe wafalme au falme zote ambazo zipo kwa wakati huo, kama vile vidole kumi vya sanamu kubwa ya Danieli, sura ya 2, na pia pembe kumi za mnyama wa sura 7, huwakilisha wafalme au falme zilizopo ulimwenguni pote katika vipindi vyao. {TN15: 71.2}
Wala haupaswi kupuuzwa ukweli kwamba pembe zote, vichwa, na taji, zilikuwa kundi la pamoja wakati ambapo joka lilisimama tayari “kumla Mtoto wake.” Hasa jinsi nembo inavyoonyesha, zinawakilisha mungano wa vyama viwili mbali mbali na tofauti (pembe na vichwa), vyote vikiwa hai wakati uo huo, sio kimoja baada ya kingine. Ni vyema kukumbuka, pia, kwamba ingawa pembe hukua na kung’oka, vichwa havifanyi hivyo kamwe. {TN15: 71.3}
71
MWONGOZO KWA UFASIRI SAHIHI WA NEMBO ZA PEMBE NA VICHWA
Pembe za joka zikiwa bila taji, lazima zionyeshe taswira ya mfano wa watawala sawa na wale walioonyeshwa na pembe zisizokuwa na taji za mnyama wa nne wa Danieli, za beberu na kondoo-mume wake, na za mnyama mwekundu sana wa Yohana na mnyama wa pembe mbili; yaani, pembe zisizo na taji za joka zinaonyesha mamlaka za aina fulani zisizokuwa na taji, kama vile pembe zisizokuwa na taji za mnyama yeyote wa mfano. Kwa mfano, pembe kumi zisizokuwa na taji za mnyama wa nne wa Danieli, malaika alifafanua, zinawakilisha wafalme ambao wangeinuka katika Dola ya Kirumi, walikuwa bado kuzichukua taji zao. Baadaye, hata hivyo, pembe yenye kichwa baada ya kuwa imepoteza mamalaka yake na wafalme waliotarajiwa walipokuwa wamezipokea falme zao, baada ya hapo wamewakilishwa na pembe zilizo na taji, kwa pembe za mnyama-kama chui (Ufu. 13), nembo ya dunia baada ya kuanguka kwa Roma. {TN15: 72.1}
Tena, pembe kumi zisizo na taji za mnyama mwekundu sana (Ufu. 17), mnyama ambaye baada ya muda mrefu anamridhi yule wa mfano kama chui, anaonyesha wafalme ambao “hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.” Ufu. 17:12. Kwa maneno mengine, kwa kuwa hawana ufalme wao wenyewe wakati wote ambapo Babeli amempanda (anamtawala) mnyama kwa “saa,” pembe hizo kiasili hazina taji. {TN15: 72.2}
Kwa kuwa pembe hizi kumi zilikuja kuwapo kama kikundi, kwa hiyo zinawakilisha watawala waliopo wakati wa mnyama. Wakati ambapo pembe zinawakilisha
72
mamlaka ambazo zipo moja ikiandama nyingine, Uvuvio haushindwi kudokeza hivyo kwa kuonyesha pembe fulani kuzuka na zingine kuanguka. Kwa mfano, tatu
73
DANIELi 8
kati ya pembe za mnyama wa nne wa Danieli “ziling’olewa kabisa,” na badala yake pembe mashuhuri yenye kichwa ilizuka. Kwa namna hiyo, wakati pembe ile kubwa
74
ya beberu ilipovunjika, nne zilizuka kuchukua nafasi yake, na ile ya tano, pembe kubwa sana iliyofuatia baadaye (Dan. 7 na 8). Kisha pia, hata wanyama, wenyewe, kwamba katika vipindi vyao wanawakilisha ulimwengu, walitoka katika bahari mmoja akimfuata mwingine. Kwa hiyo mifano yote ya Mungu huonyesha mamlaka kwa usahihi kadri wakati na matukio huzisababisha ziweze kutokea au kutoweka, kama vile hali itakavyokuwa. {TN15: 72.3}
Kwa maneno mengine, wakati utawala mmoja unatofautiana na mwingine, na wakati zinapokuwa mamlakani au kutokuwa kwa wakati sawa, Uvuvio kamwe hausahau kuweka utofauti. Iwapo Ulisahau kufanya hivyo, basi fikiria jinsi yangekuwa yasivyopatana na akili, yasiyotegemewa, yanayopingana na yasiyoeleweka mafundisho Yake hakika, na ingekuwaje kazi bure mtu yeyote hata kujaribu kuujua ukweli halisi! Hekima ya kibinadamu tayari imeonyesha kutokuwa na uwezo wa kuelewa siri za Neno la Mungu, hata ingawa zimepangwa kikamilifu kama vile Mungu Mwenyewe anavyoweza kuzipanga. Kwa kweli, kadri mtu katika jitihada ajaribu kuelezea siri za Mungu, ni mbali zaidi na ukweli atatangatanga. {TN15: 75.1}
Zaidi ya hayo, haiwezekani kwamba Uvuvio ungekuwa usio wa maana kama kuweka katika kundi vipengele viwili tofauti (vile vinavyowakilishwa na pembe na vile vinavyowakilishwa na vichwa) kuwakilisha aina moja ya serikali. Wala haiwezekani kuwaza kwamba Ungeweka katika kundi pembe na vichwa pamoja iwapo vyote havingekuwapo
75
halisi kwa wakati mmoja. La, Uvuvio haungeweza kuchanganya hivyo maneno yake, na bado utarajie sisi kuelewa mafundisho Yake, tujue namna ya kufasiri nembo Zake na ni lini kutarajia matukio halisi kufanyika. Na ingekuwaje jambo linalopatana na akili iwapo mamlaka yanayowakilishwa na pembe na mamlaka yanayowakilishwa na vichwa hayangetofautiana kitabia kama vile zilivyo pembe na vichwa halisi? {TN15: 75.2}
Kuhusiana na maana ya vichwa, Uvuvio Wenyewe kwa kuwa ndicho chanzo pekee cha habari, tunaenda tena kwa unabii wa Danieli 7. Hapo inaonekana kwamba pembe ndogo ya mnyama wa nne, ikiwa na macho na kinywa cha “mwanadamu,” hakika ilikuwa pembe ya kichwa — mwunganisho wa vipengele viwili tofauti. Na ikiwa ni nembo ya serikali ya Kanisa na Nchi (mwunganisho wa mamlaka za kiraia na za kidini wakati wa Vizazi vya Kati), inatatua bila shaka kwamba wakati ambapo sehemu ya pembe inasimama kwa awamu ya kiraia, sehemu ya kichwa inasimama kwa awamu ya dini — kwa njia inayoeleweka, pia, kwa sababu dini inapaswa kuwa ubongo wa serikali yoyote. Aidha, serikali za kiraia zilianzishwa awali juu ya serikali za kanisa. Nembo hivyo inamaanisha wazi kwamba serikali ya Mkana Mungu ni karibu nzuri kama ilivyo pembe yoyote mbali na kichwa chake. Ya namna hii inaweza kulinganishwa na kuku ambaye kichwa chake kimekatwa: Katika shida yake, kuku asiye na kichwa huruka kwa nguvu kubwa, lakini hajui wapi anakoenda, na anakuwa hai ila kwa dakika chache. {TN15: 76.1}
76
Zaidi ya hayo, serikali iliyofuata baada ya mamlaka ya kiraia kuondolewa mbali kwa muundo wa kidini na kisiasa wa Vizazi vya Kati, inaletwa kwa mtazamo katika nembo ya mnyama kama chui (yule ambaye mtawalia anafuata katika safu ya nembo za wanyama ). Ndani yake serikali za kidini na kisiasa zikisha kuwa zimevunjwa zinaonyeshwa na kichwa cha kawaida kilichojeruhiwa, mfumo wa kidini bila mamlaka ya kiraia, kile kinachougua kutokana na pigo la mauti — dhahiri kutokana na pigo ambalo liliondolea mbali mamlaka yake ya kiraia. {TN15: 77.1}
Kutoka kwa vigezo hivi ni dhahiri hasa kwamba katika matukio yote ambapo nembo ya wanyama iliyo na pembe na vichwa pamoja, vichwa katika kila tukio vinaashiria makundi ya kidini, makundi ambayo yana la kufanya na mambo matakatifu ya Mungu, ambayo yana uwezekano kuchanganya mambo matakatifu ya Mungu na mambo ya kawaida ya dunia. Jina la makufuru juu ya vichwa vya mnyama kama chui, huvifunua kwamba vimefanya dhambi hiyo. {TN15: 77.2}
Na sasa, kuendelea na somo la joka, inaweza kuonekana wazi kwamba ili upatano udumishwe, ufafanuzi wa Kibiblia wa vichwa vya joka na pembe lazima iwe kwamba vya awali ni makundi ya kidini, na vya mwisho, serikali za kiraia. Na ni ngapi kati yake ambazo pembe na vichwa vya joka vinawakilisha? — Serikali zote za kiraia na makundi yote ya kidini hasa wakati huo. Tunajuaje hili? — Kwa sababu zipo pembe kumi
77
na vichwa saba ambavyo vina taji, na kwa sababu tarakimu ya namba ya Kibiblia “kumi” inaashiria ulimwengu wote, na namba “saba” inaashiria ukamilifu. (Angalia Trakti Namba 3, Hukumu na Mavuno, uk. 94, toleo la 1942.) {TN15: 77.3}
Kutoka kwa mifano ambayo imetangulia kutajwa, tunaona tayari kwamba wakati umekuja kwa wanafunzi wote waaminifu wa Biblia, wanafunzi wanaouandama Ukweli unaookoa, kutambua kwamba Uvuvio kamwe haufanyi chochote bure au kiholela. Kazi yake daima hujengwa kwa usahihi, daima ya kutegemewa kwa thamani ya kuchunguza, na bayana zaidi ya kurekebisha. {TN15: 78.1}
Ni ukweli unaotambulika pia, kwamba taji daima husimama kwa mamlaka ya kifalme. Na vile ambavyo zinavyoonekana kwenye vichwa vya joka, sio kwenye pembe zake, inadhihirika hasa kwamba wakati ambapo joka alitawala dunia zote za kiraia na za kidini, hata hivyo aliweka taji kwa za kidini. {TN15: 78.2}
Kwa maneno mengine, kanisa lilishikilia fimbo ya mamlaka; Kanisa liliketi juu ya kiti cha enzi cha joka. Na ukweli kwamba idadi ya pembe za joka inawakilisha ulimwengu na idadi ya vichwa vyake ambavyo vina taji, ukamilifu, pamoja na ukweli kwamba kanisa la Wayahudi na la Warumi yote yalimtesa Bwana, unaonyesha kwamba joka kwa ujumla anawakilisha ulimwengu kamili wa Kishetani na kidini, ya kwamba Shetani alikuwa ameuchukua ulimwengu mateka. Kama aliyeushinda na aliyejihami kwa pembe na vichwa, alimsukuma Herode kuwaua watoto wachanga mara tu alipojua kuzaliwa kwa Kristo. Hii alilifanya na
78
tumaini la kumwangamiza Mwokozi, kummeza mtoto na hivyo kuuendeleza ufalme wake mwenyewe. Hiyo ndiyo ilikuwa hali ya ulimwengu katika Ujio wa kwanza wa Kristo, na hivyo kanisa likawezeshwa kumsulubisha Bwana, kumpiga Stefano kwa mawe, na kuwakata vichwa wengine, na bado likiziepuka adhabu za mamlaka ya kiraia. {TN15: 78.3}
Kwa sababu hii hasa Mwana wa Adamu, Mkombozi wa ulimwengu, alikuja tu kwa wakati Alivyofanya. Joka, hata hivyo, ili kuilinda dola yake ya Kishetani, alingojea kwa subira na kwa uangalifu kuwasili kwa Mwokozi wa dunia aliyeahidiwa. Kwa hiyo ilikuwa kwamba wakati kanisa la Mungu lililo hai daima lilipokuwa na mtoto, na likilia kumzaa, joka na vichwa vyake saba vya taji na pembe kumi, alisimama tayari kumwangamiza mtoto mara tu Anapozaliwa. {TN15: 78.4}
Uasi kama huu ulikuwa umeshika ulimwengu katika siku za Nuhu, pia, na ukafanya kuwa ni hitaji kwa Bwana kufanya kitu kuuokoa ulimwengu. Kwa ajili ya wanadamu, Muumba alituma gharika ili kukomesha uovu. Kwa namna hiyo uasi wa kutisha wa Wayahudi katika siku za ujio wa kwanza wa Kristo, ulidai janga lingine la kuangamiza kabisa kama gharika ya kutisha ili kuondoa uovu tena. Lakini, isipokuwa kwa sababu nyingine yoyote kuliko kuihifadhi ahadi Yake isiyoshindwa kamwe kwa mtumishi wake mwaminifu Nuhu, Mungu hangeweza kuupindua ulimwengu kwa mara ya pili. Na hivyo alimtuma Mwanawe afe
79
badala ya ulimwengu. Katika nuru hii, unasimamaje mbele uangavu zaidi kuliko awali utume wa Mkombozi! Kwa kifo chake Yeye hakika aliiokoa dunia dhidi ya uharibifu wakati huo, na kwa ufufuo Wake Alifanya uwezekano wake ikuwepo leo. {TN15: 78.5}
“Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake….
“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
“Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
“Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.” Ufu. 12: 4, 7-9, 13. {TN15: 80.1}
Hapa kunaelezewa “kutupwa nje” mara mbili tofauti. Maki kwamba katika tukio la kwanza, joka aliwakokota malaika kwa mkia wake. Lakini, unashangaa, kwa nini si kwa makucha yake? — Kwa sababu rahisi hivi ingeonyesha kwa uongo kwamba Shetani alimshinda Bwana na kwa hiyo akawaburuta kutoka mbinguni theluthi ya malaika. Lakini kwa vile aliwakokota kwa mkia wake, maana ya kweli ni wazi — kwamba theluthi ya malaika ilimfuata kwa hiari. Walishikilia mkia wake, hivyo kusema, wakati alipokuwa anaongoza. “Waligeuka
80
kutoka kwa Baba na Mwana wake, na kuungana na kidudumtu wa uasi.” – Shuhuda, Gombo la 3, uk. 115. Joka aliwashawishi malaika na wakamfuata kutoka mbinguni hadi kwa dunia ambapo alijaribu kumwangamiza Kristo. {TN15: 80.2}
Tukio hili la Ufu. 12: 4, joka kuziangusha chini nyota, lilitangulia tukio la Ufu. 12: 9, Bwana kulitupa chini joka. La awali lilitukia kabla ya Bwana kuzaliwa na la mwisho baada ya kufufuka Kwake. Hili linafanywa wazi katika aya zifuatazo: {TN15: 81.1}
Katika siku za Ayubu Shetani alikuwa bado na ufikivu wa mbinguni, kwa maana tunaambiwa kwamba “… Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.” Ayubu 1: 6, 7. {TN15: 81.2}
Shetani, wakati huo, hakufukuzwa kutoka mbinguni mara baada ya kuasi au hata wakati aliwafanya Adamu na Hawa kutenda dhambi. Badala yake, lazima ilikuwa ni baada ya wakati wa Ayubu. Lakini kubainisha ni wakati gani, tutasoma Ufu. 12:13: “ Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.” Kwa hiyo alitupwa nje kabla ya kwenda kulitesa kanisa. Hili alilifanya wakati “siku ile kukatukia adha kuu
81
ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.” Mdo 8: 1. Ukweli huu pia umewekwa wazi na Roho ya Unabii: {TN15: 81.3}
Kwa ushindi Bwana alichukuliwa hadi kwa Mungu na kwa kiti Chake cha enzi. “… wote wapo kumkaribisha Mwokozi wao. Wana hamu ya kusherehekea ushindi Wake na kumtukuza Mfalme wao … Anawasilisha kwa Mungu mganda wa kutikiswa, wale waliofufuliwa pamoja Naye kama wawakilishi wa umati ule mkubwa ambao utatoka kaburini wakati wa ujio Wake mara ya pili …. Sauti ya Mungu imesikika ikitangaza kwamba haki imeridhika. Shetani ameshindwa. Wanaotaabika, wanaojitahidi wa Kristo juu ya nchi ‘wanakubaliwa katika Wapendwa.’ Mbele ya malaika wa mbinguni na wawakilishi wa dunia ambazo hazijaanguka, wanatangazwa kuwa wenye haki. {TN15: 82.1}
“Shetani aliona kwamba maficho yake yalikuwa yameng’olewa. Serikali yake ilitandazwa wazi mbele ya malaika ambao hawakuanguka na mbele ya ulimwengu wa mbinguni. Alijionyesha kama mwuaji. Kwa kuimwaga damu ya Mwana wa Mungu, alijing’oa kutoka kwa huruma za viumbe wa mbinguni. Tangu hapo kazi yake ilizuiwa. Wowote ule mwenendo angeweza kunuia, hangeweza tena kuwangojea malaika wakija kutoka katika makao ya mbinguni, na mbele yao kuwashtaki ndugu za Kristo ya kuwa wamevaa nguo za weusi na
82
unajisi wa dhambi. Kiungo cha mwisho cha huruma kati ya Shetani na ulimwengu wa mbinguni kilikatwa.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 833, 834, 761. {TN15: 82.2}
Hakika, akijua kwamba alikuwa amekwisha kujiletea kikomo cha kutoingia tena mbinguni kuwashtaki ndugu, na akijua kwamba hata kukaa kwake duniani kungekuwa muda mchache tu,
SHETANI ALITUPWA CHINI MWENYE GADHABU NYINGI. {TN15: 83.1}
Baada ya joka kutupwa chini, Yohana alisikia sauti kuu ikisema mbinguni: {TN15: 83.2}
“Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.” Ufu. 12: 10-12. {TN15: 83.3}
“Madai ya Shetani dhidi ya wale wanaomtafuta Bwana hayasababishwi na kutopendezwa kwake kwa dhambi zao. Hujiinua katika mapungufu yao ya tabia, kwa maana anajua kwamba kwa njia ya uasi wao kwa sheria ya Mungu anaweza kupata nguvu juu yao.” — Manabii na Wafalme, uk. 585, 586. {TN15: 83.4}
Shetani, tunaona, humhimiza mtenda dhambi bila kutambua kufanya dhambi, na hivyo kuifanya thabiti hukumu yake, sio hapa duniani, ila mbinguni. Mbele ya Jaji wa haki, Shetani humshtaki
83
mvunja sheria wa “kuwa amevaa mavazi ya weusi na unajisi wa dhambi.” Lakini wakati Roho wa Mungu anaposhawishi kwa kemeo, Huifichua dhambi na kumkemea mtenda dhambi kupitia kanisa Lake. {TN15: 83.5}
Watu wa Mungu daima wanapaswa kuwa macho kwa sauti ya Roho wa Kristo, na pia kuwa chonjo kutambua roho ya Shetani. Wakati hizi mbili zinagongana, moja hujitahidi kulitii Neno la Mungu, wakati nyingine huruhusu dhambi na kumuunga mkono mdhambi. Katika mbinu hii ya mwisho ya hila Shetani mara nyingi hupata msingi na kumshinda mdhambi kuingia safu zake, kwa kuwa mdhambi huipenda dhambi yake. Waaminifu, hata hivyo, humshinda “kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao.” Hawapendi “maisha yao hata kufa.” Ufu. 12:11. {TN15: 84.1}
“Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.” Ufu. 12:14. {TN15: 84.2}
Kwa kuwa nyika ni kinyume cha shamba la mizabibu, taarifa “ ili aruke nyikani” kwa mkazo inasisitiza kwamba lazima awe ameondoka katika shamba la mizabibu. Na hivyo ndivyo alivyofanya hasa: Muda mfupi baada ya kufufuka, kanisa (mwanamke) liliondoka katika nchi takatifu (shamba la mizabibu) na likaenda katika nchi ya watu wa Mataifa (nyikani). {TN15: 84.3}
Mbali na kweli hizi za kihistoria, pia tunayo maana ya Biblia ya shamba la mizabibu: “Kwa maana
84
shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza.” Isaya 5: 7. {TN15: 84.4}
Bila shaka, kwa hivyo, nyikani, ambako mwanamke alikuwa akilishwa kwa wakati huo, ni nchi ya watu wa Mataifa. Na ya kuwa mwanamke alihitaji kukimbia
85
Kutoka kwa uso wa nyoka katika nchi yake, inaonyesha kwamba joka alikuwa ameifanya nchi takatifu kuwa makao yake makuu. Pasipo kuridhika na hili, hata hivyo, akamfuata hata nyikani. {TN15: 85.1}
“Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.” Ufu. 12:15. {TN15: 86.1}
Katika tumaini la kumwangamiza mwanamke, nyoka mwanzoni alimtesa. Aliposhindwa, hata hivyo, kufikia lengo lake, ghafla alibadili mbinu zake. Aliacha mateso na badala yake akaanza kumfanya rafiki. Lakini gharama gani kwa mwanamke! Kwa hila akatoa maji kama mafuriko nyuma yake, akionekana kuweka juhudi kubwa ya kumburudisha, wakati kwa uhalisi ilikuwa juhudi kubwa ya kumwangamiza. {TN15: 86.2}
Maneno ya ki-mfano ya Uvuvio yanaelezea kwamba kuwalazimisha watu wa Mataifa kuwa Wakristo na kuwamimina katika kanisa wakati wa karne ya nne ya enzi ya Kikristo, hakikuwa kweli kitendo cha urafiki. Badala yake kilikuwa kama mto wa kuathiri unaofurika ili kuuzamisha uwezo wa kuokoa wa Ukristo. Kwa maneno mengine, Uvuvio ulitabiri kipindi ambamo joka aliwavika wanasiasa wa Kipagani vazi la Ukristo na kisha akawaongoza kuwalazimisha wapagani wasiokuwa Wakristo kujiunga na kanisa, ili waweze kwa namna hiyo kulifanya la upagani badala yake kuwafanya kuwa Wakristo. {TN15: 86.3}
Katika uthibitisho, tunanukuu sehemu ya maelezo kutoka kwa kazi ya Bwana Gibbon: “Kwa amri za uvumilivu, yeye [Konstantino]
86
aliondoa uzuizi wa muda ambao ulikuwa hadi hapo umekwamisha maendeleo ya Ukristo; na wachungaji wake wamilifu wengi walipata idhini ya bure, faraja ya uhuru, kuidhinisha kweli zenye manufaa za ufunuo kwa kila hoja ambayo ingeweza kuathiri fikira au kicho cha wanadamu. Uwiano halisi wa dini mbili [Ukristo na Upagani] uliendelea ila kwa muda …. Miji iliyosainia bidii ya kuendeleza uharibifu wa hiari wa mahekalu yao [ya Wapagani] ilitofautishwa kwa fursa za manispaa, na kutuzwa kwa michango maarufu … Wokovu wa watu wa kawaida ulinunuliwa kwa kiwango cha chini, iwapo ni kweli kwamba, kwa mwaka mmoja, watu kumi na mbili elfu walibatizwa huko Roma, mbali na vipimo vya idadi ya wanawake na watoto, na kwamba vazi jeupe na vipande ishirini vya dhahabu, vilikuwa vimeahidiwa na mfalme kwa kila mwongofu.” Hii ilikuwa “sheria ya Konstantino, ambayo iliwapa uhuru watumwa wote ambao wangeukumbatia Ukristo.” — Rumi ya Gibbon, Gombo la 2, uk. 273, 274 {TN15: 86.4}
“Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.” Ufu. 12:16. {TN15: 87.1}
“Nchi,” silaha ya Mungu yenye nguvu, hatimaye itamsaidia mwanamke. Itayameza “mafuriko”; yaani, mbinu ile ile ya Mwenyezi Mungu ambayo, kulingana na mfano, inayaondolea mbali magugu na kuyachoma, pia inawaondolea mbali wote ambao wamejiunga na
87
kanisa lakini ambao bado ni wapagani moyoni. Na ni nini kinachotokea hatimaye? — Maandiko yanatoa jibu: {TN15: 87.2}
“Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.” Ufu. 12:17. {TN15: 88.1}
Neno la heshima “masalia” linafichua kwamba uzao wake umegawanywa katika sehemu mbili: mmoja unachukuliwa, na mwingine unaachwa. Nehemia, kwa mfano, anaelezea: “waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu.” Neh. 1: 3. “Masalia” daima inawakilisha sehemu moja ya yote, ama kubwa au ndogo. {TN15: 88.2}
Na tambua kwamba joka anafanya vita, sio dhidi ya masalia wa “mafuriko,” bali dhidi ya masalia wa uzao wake. Kristo akiwa mtoto wa pekee wa mwanamke, wazao wake ni Wakristo, wale waliozaliwa katika kanisa kupitia kwa Roho wa Kristo. Kwa hivyo, tendo la kuwapeleka malimbuko hadi Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1) linaleta hali ambayo inawafanya masalia wa wale ambao bado wameachwa miongoni mwa Mataifa. Katika tukio hili, kwa hiyo, wao, mavuno ya pili, ni masalia. {TN15: 88.3}
Hebu ikumbukwe kwamba ni baada ya nchi kuyameza mafuriko kwamba joka atamkasirikia mwanamke, na “ kufanya vita juu ya wazao wake [sio pamoja na mwanamke mwenyewe], wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. “ Ufu. 12:16 17. Dhahiri, basi, hakuna kuliepuka hitimisho
88
kwamba kuondolea mbali mafuriko ya Shetani bila shaka ni kulitakasa kanisa, kuwaangamiza wale ambao wamejiunga na kanisa kupitia msaada wa nyoka. Utakaso huu ni jambo ambalo hasa linaloliwezesha kanisa kama mwili kuzishika amri za Mungu na pia kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo, Roho wa Unabii aliye hai (Ufu. 19:10), katikati yake. Hii ndilo tumaini lake pekee, nguvu yake pekee, ukombozi wake pekee. Katika nuru hii, Uvuvio sasa unaweka uhai mpya ndani ya maneno — {TN15: 88.4}
“Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Isa. 52: 1. {TN15: 89.1}
Utakaso wa kanisa, kwa hiyo, hautaleta wakati wa milenia ya amani. Hakika sivyo ila utaleta mwisho wa waovu kanisani, na kwa hiyo ghadhabu kubwa ya Shetani dhidi ya masalia, dhidi ya wale ambao, bado wangali miongoni mwa Mataifa, wanathubutu baada ya hapo kusimama upande wa Bwana. Hata hivyo, wataokolewa ikiwa, kama itakavyokuwa kuhatarisha maisha yao — iwapo wanasimama upande wa Bwana na hivyo kuweka majina yao katika “kitabu.” Dan. 12: 1. {TN15: 89.2}
Joka hawezi kufanya vita na mwanamke, kanisa ambalo lina washiriki malimbuko, kwa sababu kwa wakati huo liko pamoja na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1), pale ambapo joka hawezi kufika. {TN15: 89.3}
89
Kwa ajili ya kujifunza zaidi Ufunuo 12, soma Trakti Namba 12, Dunia, Jana, Leo, na Kesho, toleo la 1946, kr. 45-48. (Ingawa mada ya somo la Ufunuo imeshughulikiwa kwa sehemu humu, nafasi ndogo katika trakti hii hainiruhusu kuendelea). {TN15: 90.1}
90