fbpx

Fimbo Ya Mchungaji Gombo La 1

Fimbo Ya Mchungaji Gombo La 1

ISA. 58:1

“Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama

Tarumbeta, uwahubiri watu wangu kosa lao,

na nyumba ya Yakobo dhambi zao.”

Watu 144,000 wa Ufunuo 7–

Mwito wa Matengenezo

Na

V.T. Houteff

Gombo la Kwanza

Limechapishwa nchini Marekani.

3

Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1

Hakimiliki 1930

Na V.T. Houteff

Mchoro wa Kiufundi Umefanywa Na

Martin S. Ramstat

4

FIMBO YA MCHUNGAJI

Kitabu, Gombo la 1

5

UTANGULIZI

Ni nia ya kitabu hiki kufunua ukweli wa watu 144,000 waliotajwa katika Ufunuo 7 lakini lengo kuu la chapisho hili ni kuleta matengenezo kati ya watu wa Mungu. Ukweli uliosheheni hapa ndani umegawanywa katika sehemu saba, ukitoa uthibitisho kutokea kwa pembe saba mbali mbali, kuzuia shaka yoyote au mkanganyiko. Mada hii imefanywa kuwa wazi kwa matumizi ya Biblia na maandishi yaliyotolewa na Roho ya Unabii. {SR1: 5.1}

Ukweli uliofunuliwa hapa una umuhimu mkubwa kwa kanisa sasa hivi kwa sababu ya hatari iliyotabiriwa ambayo watu wa Mungu watakutana nayo hivi karibuni. Unaitisha hatua yenye uamuzi kwa upande wa waamini kujitenga na walimwengu wote na dunia; watie nanga kwa Mwamba Imara kwa kutii ukweli wote unaojulikana kwa dhehebu hili, iwapo lazima tuepuke maangamizi makubwa. “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina lako: Isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.” Mika 6:9. {SR1: 5.2}

— MWANDISHI.

6

YALIYOMO

 

Utangulizi.

Faharisi ya Mada.

Utangulizi Wa Yaliyomo

 

Sehemu ya 1. Watu Mia na Arobaini Na Nne Elfu.

Sehemu ya 2. Madaraja Manne Ya Waliokombolewa.

Sehemu ya 3. Esau Na Yakobo.

Sehemu ya 4. Israeli Ni Nani Kwa Ile Ahadi?

Sehemu ya 5. Unabii Wa Ezekieli Nne.

Sehemu ya 6. Muhtasari Wa Sura Za Isaya.

Sehemu ya 7. Nini Maana Ya Sura Ya Nne Ya Mika?

Muhtasari Wa Masomo Ya Matengenezo — Je! Ni Nini Hufanya Makafiri?

Muhtasari Wa Watu 144,000.

Chati Ya Muhtasari Ya Masomo Yote Mawili.

Jinsi Ya Kuchunguza Habari Zilizowasilishwa, Iwapo Ni Sahihi.

Mika Sita Na Saba — Unabii Wa Kitabu Hicho, Wakati Unaofaa Kwa

Uchapishaji.

Wajibu — Yeye Anayeupokea Ukweli.

Pingamizi Zinazoweza Kuibuka.

7

FAHARISI YA MADA

Utangulizi wa Yaliyomo.

Utangulizi.

Sehemu Ya 1.

WATU MIA NA AROBAINI NA NNE ELFU …………………………13

Haijalishi, Maadamu Mtu Anafanya Haki ………….…………………….14

Maana Ya Miaka Saba Ya Wingi

Na Miaka Saba Ya Njaa ……………………………………………….15

Miaka Saba Ya Wingi, Na Miaka Saba Ya Njaa ……………………….19

Watu 144,000 Ni Kina Nani? …………………………………………..20

Je! Watu 144,000 Watawahi Kufa? ……………………………………..22

Je! Dada White Atakuwa Pamoja Na Watu 144,000 ……………………24

Watu 144,000 Pekee Wanaingia Hekaluni ………………………………25

Ni Muhuri Wa Aina Gani? ………………………………………………26

Mihuri Miwili ……………………………………………………………27

Ezekieli 9 Si Muhuri Wa Sabato ………………………………………..29

Kutiwa Muhuri Kunaanza — Kanisa Liko Chini Kiroho ………………….30

Kisababishi Cha Kuugua Na Kulia ……………………………………..33

Sehemu Ya Orodha Ya Machukizo Kanisani …………………………..34

Je! Huku Kutiwa Muhuri Kutaendelea Hadi Kwa

Kufungwa Muda Wa Rehema? …………………………………………….35

Watu Watano Wamfuata Yule Mmoja ……………………………………….37

Tofauti Kati Ya Watu 144,000 Na Watakatifu Wengine ………………..38

Sehemu Ya 2.

MAKUNDI MANNE YA WALIOKOMBOLEWA ……………………41

Kundi la 1 ……………………………………………………………….41

Kundi la 2 ……………………………………………………………….42

Kundi la 3 ……………………………………………………………….42

Kundi la 4 ……………………………………………………………….42

Mifano Na Uakisi ……………………………………………………….43

Ufafanuzi Wa Maandishi Ya Awali, Ukurasa Wa 15 …………………..45

Eliya Huwakilisha Watu 144,000 ………………………………………46

Musa — Mfano Wa Ufufuo Wa Wenye Haki ……………………………47

Mfano Wa Ufufuo Maalum ……………………………………………..47

Mfano Wa Ufufuo Wa Pili ………………………………………………48

Mfano Wa Mauti Ya Pili ………………………………………………..48

Gwaride Ya Waliokombolewa ………………………………………….49

Elezo La Kidau Cha

Wino Wa Mwandishi Cha Maandishi ya Awali, ukurasa 279 ……….51

Sehemu Ya 3.

ESAU NA YAKOBO ……………………………………………………52

Nembo Ya Kushindana …….……………………………………………54

Wakati Na Kanisa ………………………………………………………54

Makundi Mawili Ya Watu .……………………………………………..55

Nembo Ya Haki Ya Kuzaliwa ………………………………………….55

8

Nembo Ya Nywele ……………………………………………………..55

Nembo Ya Kisigino Cha Esau …………………………………………56

Nembo Ya Kuwa Mwekundu ………………………………………….56

Nembo Ya Tabia Ya Esau …………………………………………………….56

Baraka Ya Esau ……………………………………………………………57

Nembo Ya Mchuzi Wa Dengu …………………………………………58

Edomu — Mfano ………………………………………………………..59

Badiliko La Majina ……………………………………………………..60

Kupoteza Na Kufaidika …………………………………………………60

Ndoto Ya Yakobo ………………………………………………………61

Kina Mama Za Israeli …………………………………………………..61

Yakobo Kurudi Nyumbani: Wakati Wa Taabu …………………………62

Mfano Wa Nchi Ya Ahadi — Israeli Katika Nyumba Ya Baba …………62

Sehemu Ya 4.

ISRAELI NI NANI KWA ILE AHADI? ………………………………..64

Miaka Ya Wingi — Na Ya Njaa ………………………………………..68

Yusufu Mfano Wa Kristo ………………………………………………68

Farao, Mfano Wa — …………………………………………………….69

Mwanzo Wa Njaa ………………………………………………………70

Wamisri, Mfano Wa Mataifa …………………………………………..70

Wamisri Walijiuza Wenyewe Kwa Farao ………………………………71

Yusufu Awaondoa Watu Kotekote Misri ………………………………72

Watu 70, Mfano Wa Shirika ……………………………………………73

Yakobo Mfano Wa “James” ……………………………………………75

Nchi Ya Gosheni ……………………………………………………….76

Yusufu Alilisha Israeli …………………………………………………76

Wachungaji …………………………………………………………….77

Farao Mwingine Akainuka …………………………………………….77

Mabwana-kazi / Wasimamizi ………………………………………….77

Msiwape Nyasi Tena …………………………………………………..81

Wakunga ……………………………………………………………….86

Watoto Wanaume Katika Mto Nile …………………………………….87

Watoto Wanaume Wa Dhehebu — Jinsi Walivyozamishwa …………..88

Binti-Mfalme Apata Musa …….………………………………………89

Chaguo la Musa ……………………………………………………….90

Dhana Ya Musa …………………………………………………………….90

Matumizi Ya Huo Mfano ………………………………………………91

Musa Nyikani ………………………………………………………….93

Matumizi Ya Funzo ……………………………………………………94

Fimbo Ya Mchungaji ………………………………………………….95

Kifo Cha Mzaliwa Wa Kwanza ……………………………………….96

9

Mwana-kondoo Wa Pasaka ……………………………………………97

Bahari Ya Shamu / Nyekundu …………………………………………99

Mlima Sinai …………………………………………………………..100

Kanisa Limepewa Jina Jipya …………………………………………100

Idadi Ya Israeli Ni Ngapi? …………………………………………….101

Ni Nini Kinachojumuisha Masalia? ………………………………….102

Wingu Mchana — Moto Usiku ……………………………………….104

Yusufu, Mfano Wa Kristo ……………………………………………105

Farao, Mfano Wa Viongozi …………………………………………..106

Miaka 430 Ya Kukaa Pamoja Na Mateso ……………………………108

Chati Ya Sanjari …………………………………………………112-113

Sehemu Ya 5.

UNABII WA EZEKIELI NNE,

Yanayotukia Ndani Ya Siku 390 …………………………………….114

Ngano, Nembo Ya Imani …………………………………………….118

Shayiri, Nembo Ya Roho …………………………………………….118

Kunde, Nembo Ya Neema ………………………………………………118

Dengu, Mfano Wa Fundisho La Ubatizo Kwa Kuzamishwa ………..119

Mtama, Nembo Ya Siku 2300 ……………………………………….119

Kusemethi, Nembo Ya Sabato Katika Uhusiano Na

Patakatifu ………………………………………………………….120

Zote Ndani Ya Chombo Kimoja …………………………………….120

Mkate Wa Shayiri ……………………………………………………122

“Nitakutia Pingu” …………………………………………………….122

“Utakunywa Maji Pia” ……………………………………………….122

Chakula Kwa Kipimo — Maji Kwa Kipimo .…………………………123

Elezo La Ezekieli 4:12, 14, 15 ……………………………………….123

Siku Arobaini, Na Yale Yanayotukia Ndani Yazo …………………..125

Saba — Namba Kamilifu ……………………………………………..126

Ukauhusuru / Ukauzingire ……………………………………………128

Utengo Katika Kanuni ……………………………………………….129

Wakati Wa Njaa Ya Kiroho ………………………………………….130

Sehemu Ya 6.

MUHTASARI WA ISAYA, SURA YA 54-56 Kwa jumla ……………135

Isaya 54 — Mwanzo wa Barua — “Mungu Wa Faraja” ……………….135

Isaya 55 — Mungu Aita Turudi — Neno Ambalo Hubadilisha ……….140

Divai ………………………………………………………………….141

Maziwa ……………………………………………………………….142

Kwa Nini Kutoa Fedha Kwa Kitu Ambacho Si Chakula? ……………144

Isaya 56 — Baraka Kwa Myahudi Na Mtu

Wa Mataifa — Walinzi Vipofu ………………………………………145

Isaya 57 — Mwenye Haki Na Mwovu

Katika Siku Ya Taabu ……………………………………………….146

Isaya 58 — Saumu Ya Kweli — Sabato Imerejeshwa …………………147

10

Isaya 59 — Mkombozi Aahidiwa Kwa Watu Wanaotubu ……………150

Isaya 60 — Ushindi Wa Mwisho Wa Wenye Haki ……………………152

Isaya 61 — Wajenzi Wa Mahali Pa Kale Palipoharibiwa …………….153

Isaya 62 — Watu Watakatifu — Waliokombolewa Wa Bwana ……….154

Isaya 63 — Aliteswa Kwa Ajili Ya Watu Wake ………………………156

Waliokombolewa Wake ………………………………………………157

Isaya 65 — Watu Walioandaliwa Kwa

Ajili Ya Mbingu Mpya Na Nchi Mpya ……………………………..160

Isaya 66 — Kukusanywa Ndani Kutoka Kwa

Mataifa: Ibada Katika Nchi Mpya …………………………………..165

Sehemu Ya 7.

Nini Maana Ya SURA YA NNE YA

MIKA? ………………………………………………………………173

MUHTASARI WA MAFUNZO YA MATENGENEZO — Nini

Hufanza Makafiri ……………………………………………………182

Mungu Huwafunulia Manabii Wake Siri ..…………………………..196

Sheria Ya Mungu — Imevunjwa Vipi? …….…………………………198

Je! Kanisa Liko Katika Hali Bora? …………………………………..198

Nini Kimepatikana Katika Kipindi Cha

Miaka Minne Iliyopita ………………………………………………201

Jibu Kwa Hoja Ya Mhindi Ya Ukurasa Wa 182-183 …………………204

Je! Wakristo Wanawezaje Kwenda Mbinguni

Iwapo Umbali Ni Mkubwa Hivyo? …………………………………205

MUHTASARI WA WATU 144,000–

Jeraha La Mauti Limepona …………………………………………..205

Mnyama Kama Chui — Ufu. 13:1-10 ………………………………..210

Chati — Jeraha Lake La Mauti Limepona ……………………………221

.

CHATI YA MUHTASARI–Ufafanuzi Wa Mifano …………………..223

Agano la Kale (Sehemu Ya Pili) ……………………………………..223

Chati Ya Muhtasari Wa Mifano ………………………………………224

Agano la Kale (Sehemu Ya Tatu) ……………………………………225

Agano Jipya (Sehemu Ya Kwanza) …………………………………..227

Agano jipya (Sehemu Ya Pili) ………………………………………….227

Agano Jipya (Sehemu Ya Tatu) ………………………………………228

Agano la Kale (Sehemu Ya Kwanza) –Melkizedeki,

Mfalme Wa Salemu …………………………………………………229

Jinsi Ya Kuchunguza Habari Zilizowasilishwa. (Iwapo Ni Sahihi) …231

Mika Sita Na Saba — Unabii Wa Kitabu Hicho,

Wakati Unaofaa Kwa Uchapishaji …………………………………236

Wajibu — Yeye Anayeupokea Ukweli ………………………………..245

Pingamizi Zinazoweza Kuzuka ……………………………………….252

MWITO WA MAMA …………………………………………………252

CHATI

Sanjari …………………………………………………………..112, 113

Ezekieli Nne (Miaka 430) ………………………………………133, 134

Mnyama Kama Chui Wa Ufu. 13:1-10 ………………………………210

Jeraha Lake La Mauti Limepona ……………………………………..221

Chati Ya Muhtasari Ya Mifano ……………………………………..224

11

UTANGULIZI

Chapisho HILI husheheni mada moja kuu pekee yenye funzo maradufu; yaani, watu 144,000, na mwito wa matengenezo. Lengo katika mtazamo ni kuwaandaa watu wa Mungu kwa maangamizi yanayokaribia ya unabii wa Ezekieli, sura ya 9. Hakuna fundisho jipya lililofundishwa, wala halishtumu yale tunayo. Nuru ya ajabu kati ya kurasa zake huangaza juu ya idadi kubwa ya maandiko ambayo hatukuwa na ufahamu kwayo hapo awali. Ufasiri wa maandiko haya huungwa mkono kabisa na maandishi ya Dada E.G. White, ambayo huitwa Roho ya Unabii. {SR1: 11.1}

Chapisho hili halitetei Vuguvugu jipya, na hupinga kabisa hatua kama hizo. Huleta uthibitisho mzuri ambao hauwezi kupingwa kwamba kanisa la Waadventista wa Sabato lilikuwa limetumiwa na Mungu kuendeleza kazi Yake tangu mwaka 1844. {SR1: 11.2}

Ifuatayo Ni Sehemu Ya Orodha Ya Sura Za Biblia: {SR1: 11.3}

Ufunuo 7; 13:1-3. Isaya 4, Na Sura Ya 54 Hadi 66 kwa jumla. {SR1: 11.4}

Ezekieli 4 Na 9. Mika 4 Hadi 7 kwa jumla. {SR1: 11.5}

Vuguvugu La Kutoka. {SR1: 11.6}

Mifano Ya Wazee Wa Imani. {SR1: 11.7}

“Kilio Kikuu.” {SR1: 11.8}

Maelezo Kamili Ya Watu 144,000. {SR1: 11.9}

Maana ya Esau Na Yakobo. {SR1: 11.10}

Tendo La Martin Luther Katika Unabii. {SR1: 11.11}

Vipindi Vya Mfano Na Vya Uakisi. {SR1: 11.12}

12

Mungu wa Waebrania amekutana nasi: Twakuomba, tupe ruhusa, twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu Bwana Mungu wetu; asije Akatupiga kwa tauni, au kwa upanga. Kut. 5:3.

13

SEHEMU YA 1

WATU MIA NA AROBAINI NA NNE ELFU

Mada hii ya Ufunuo 7 bila shaka ni mada ya Biblia inayojadiliwa mara kwa mara na Waadventista wa Sabato na wanafunzi wengine wa Biblia, kuliko ukweli wowote mwingine wa Biblia. Nadharia nyingi zimeendelezwa na dhehebu, lakini hakuna hata moja iliyoshinda mtihani bila mkinzano. Watu wakuu wa maarifa ya Kibiblia na ya kilimwengu wamechunguza Biblia kwa bidii na hawajathibitisha lolote kuhusu kundi hili ni kina nani. {SR1: 13.1}

Tunasoma katika Pambano Kuu, ukurasa wa 397: “Roho ya dhambi itatuongoza kutoka kwa kweli, na Roho wa Mungu atatuongoza katika kweli. Lakini, wewe wasema, mtu anaweza kuwa makosani, na akafikiri ana Ukweli. Nini basi? Tunajibu, Roho na neno hupatana. Iwapo mtu anajihukumu mwenyewe kwa neno la Mungu, na kupata uwiano kamili katika neno lote, basi lazima aamini ana ukweli; lakini ikiwa anapata roho ambayo yeye huongozwa nayo haipatani na kiini kizima cha sheria au kitabu cha Mungu, basi na aenende kwa uangalifu, asije akanaswa katika mtego wa ibilisi. “ {SR1: 13.2}

Dada E.G. White bila shaka alikuwa anafahamu sana mada hii kuliko mtu yeyote anayeishi wakati huu, kwa maana aliandika mengi juu yao na alikuwa na maono kuwahusu. Hakuna shaka kwamba yeye, pia, alitumia muda mwingi kuchunguza katika Bibilia na maandishi yake mwenyewe, lakini ameshindwa kuonyesha kundi halisi kwa kuyakusanya marejezo pamoja, na kuifumbua siri hiyo. Swali ni: Mbona watu hawa wanaomcha Mungu waliouchunguza ukweli kwa dhati wameshindwa kutoa ushahidi wowote kuhusu kundi hili la ajabu ni kina nani haswa? Jibu tunalotoa ni: Kwa sababu haukuwa ukweli wa sasa katika wakati wao. {SR1: 13.3}

Dada White angeweza kutoa nadharia ya aina fulani inayofaa na sahihi zaidi kuliko nadharia nyingine yoyote ambayo imewahi kuendelezwa. Alitumia hekima na uamuzi mzuri kwa kuyaacha maoni yake mwenyewe. Mungu atayaonyesha mambo haya kwa wakati mwafaka tu. Watu wanaweza

14

kufanywa waamini jambo kwa muda, lakini lisipokuwa kweli, haliwezi kudumu. Kwa hivyo haitakuwa busara na kupoteza muda kwa mtu kujaribu kubainisha watu 144,000 ni kina nani, mpaka baada ya chuo kukunjua na ukweli mmoja kuufunua mwingine. Iwapo somo hili litaifichua siri hiyo na kuipatanisha kwa Maandiko na Roho ya Unabii, basi lazima tuhitimishe kwamba wakati mwafaka wa Mungu kwa ajili ya mada hii umekuja. {SR1: 13.4}

Dada White alikuwa amepokea uvuvio kwa mada hii, lakini, kama Danieli, hakuruhusiwa kujua ni kina nani, vipi, na lini wangefanzwa, hadi wakati uliowekwa na Mungu. Ifuatayo ni dondoo iliyoandaliwa naye kwa ajili ya Mzee E.E. Andross: “Najihisi mwenye imani Mzee Andross, kwamba ndugu huko Kusini mwa California watapata baraka kwa kupitia mafundisho ya Maandiko mintarafu watu 144,000 na kuleta uzito juu ya mafundisho haya nuru yoyote inayoweza kuwa katika maandishi yaliyochapishwa ya Roho ya Unabii, na kwa kulifikiria jambo hili kwa njia ya sala katika mahusiano yake yote, Naamini kwamba Mungu ataufanya ukweli uwe wazi kabisa ili kuwezesha kuepuka maswali yasiyohitajika na yasiyofaidi ambayo sio muhimu kwa wokovu wa roho za thamani.” {SR1: 14.1}

Siku fulani somo hili lazima lieleweke, kwa maana Uvuvio huwa haufanyi taarifa zozote zisizokuwa na maana, na haziwezi kuwa katika Biblia kama pambo. Lazima ieleweke kabla ya namba hiyo (144,000) kufanzwa au haitakuwa na thamani yoyote. Itakapoeleweka, itaongoza miguu ya watu 144,000 katika njia nyoofu jinsi jumbe za malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu zimeongoza maelfu ya nafsi kwa Kristo. {SR1: 14.2}

Haijalishi, Maadamu Mtu Anafanya Haki?

Imenenwa na wengine kwamba haijalishi iwapo mtu anaelewa mada ya watu 144,000 au la, maadamu anafanya haki. Hakika hii ni kweli ikiwa TUNAFANYA HAKI, lakini tunawezaje kujua iwapo tuntenda haki au la, isipokuwa tuyaelewe mafundisho ya Biblia? Tunawezaje kujua ikiwa tunatunza Sabato iliyo sahihi, au tuko katika kanisa sahihi, isipokuwa tulielewe fundisho hilo? Kwa nini ni muhimu kuelewa Danieli 7, mnyama na sanamu yake, na unabii mwingi wa Biblia? Iwapo hatuelewi mada ya watu 144,000, tunaweza kukosa kutiwa muhuri, kwa sababu itakuwa haina maana kuielewa

15

baada ya kutiwa muhuri, jinsi itakuwa haina thamani kuelewa mnyama na sanamu yake baada ya kumaliza kazi yake duniani. {SR1: 14.3}

Ujumbe wa malaika huyu wa Ufunuo 7 — malaika anayepanda kutoka mashariki — ni muhimu kama jumbe za malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu wa Ufu. 14:6-11. Lazima ueleweke na kupeanwa kwa watu kwa wakati unaofaa, pia kama wa malaika mwenye nguvu wa Ufu. 18:1. Kilio kikuu lazima kije katika wakati fulani. Malaika huyu wa Ufunuo 7, hawezi kuwa malaika wa tatu, kwa maana maelezo ya Yohana kuwahusu hutofautiana. Malaika watatu wa Ufunuo 14 wanaruka katikati ya mbingu, au mahali jua husimama adhuhuri, lakini yule wa Ufunuo 7, anapanda kutoka mashariki, au kuchomoza kwa jua. Ujumbe wa malaika huyu haujawahi kueleweka kwa wakati wowote, wala kutangazwa na dhehebu hili au watu wengine wowote, na nadharia tu ndizo zimeendelezwa. Ni dhahiri kwamba ukweli huu, kama kweli zingine, lazima uje kwa wakati mwafaka. {SR1: 15.1}

Maana Ya Miaka Saba Ya Wingi Na Miaka Saba Ya Njaa Hupatikana Tu Kwa Njia Moja

Wakati somo la kutatanisha linapofanywa kuwa wazi, basi lazima tuamini kwamba wakati umekuja, lakini hili kama vile ukweli wote wa Biblia, hupatikana tu kwa njia moja, na katika mahali pamoja; yaani, ghala (Biblia). Kumbuka kwamba jinsi Yusufu wa siku za kale alivyodhibiti ghala, vivyo hivyo Kristo hudhibiti Maandiko na nyakati. Watu wengi waliomcha Mungu hapo zamani walikwenda kwa Kristo (Yusufu) na wakapata ukweli wote wa sasa (nafaka) kwa wakati huo haswa ili waweze kutumia. Wakati Yeye (Kristo) ni mkarimu, Yeye pia ni mwangalifu, na kwa hivyo hana chochote cha kupoteza. Wakati Yusufu alikusanya nafaka huko Misri na kuihifadhi katika maghala, hakuyafanya ili ajitajirishe, bali ili kudumisha uhai katika miaka saba ijayo ya njaa. Nafaka hiyo ilikuwa nembo ya Neno la Kristo jinsi tutakavyojitahidi kuthibitisha. {SR1: 15.2}

Sababu za kuamini kwamba miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa katika siku za Yusufu katika Misri ya kale huwakilisha historia ya ulimwengu katika sehemu mbili za wakati ni kama ifuatavyo: {SR1: 15.3}

Katika Gombo la 3, ukurasa wa 369, tunasoma, “Isaka alikuwa mfano wa Mwana wa Mungu, ambaye alitolewa kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.” Tena

16

tunasoma katika Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa wa 112, “Na katika kondoo mume aliyetolewa na Mungu badala ya Isaka, Abrahamu aliona nembo ya Yeye ambaye angekufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu.” Kwa hivyo Isaka na kondoo mume ni nembo za kujinyenyekeza kwa Kristo, kifo, na dhabihu. {SR1: 15.4}

Kumhusu Yona, tunasoma katika Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa wa 406, “Jinsi Yona alikuwa siku tatu mchana na usiku ndani ya tumbo la nyangumi, Kristo alipaswa kuwa muda uo huo ‘katika moyo wa nchi.’ Na kama mahubiri ya Yona yalikuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo mahubiri ya Kristo yalivyokuwa ishara kwa kizazi Chake.” Tazama pia Manabii na Wafalme, ukurasa wa 274. {SR1: 16.1}

Elisha alikuwa nembo ya Kristo. Manabii na Wafalme, ukurasa wa 240: “Kama Mwokozi wa wanadamu, ambaye Elisha alikuwa mfano Wake, katika utumishi wake kati ya wanadamu aliunganisha kazi ya uponyaji na ile ya kufundisha.” Hizi ndizo sababu Isaka, Yona, na Elisha ni mifano ya Kristo, wakiwakilisha awamu na umuhimu tofauti wa kazi ya Kristo. {SR1: 16.2}

Kumhusu Yusufu tunasoma katika Wazee na Manabii, ukurasa wa 369: “Yusufu alikuwa mwakilishi wa Kristo. Katika mfadhili wao ambaye kwake Wamisri wote walimwelekea kwa shukrani na sifa, watu hao wapagani walipaswa kuuona upendo wa Muumba na Mkombozi wao.” Misri lilikuwa taifa lililoabudu sanamu, na ni nembo ya ulimwengu katika dhambi. Yusufu alikuwa mfano wa Kristo, mtawala wa ulimwengu. Jinsi Yusufu alivyotumwa Misri ili kuhifadhi uzima; vivyo hivyo Kristo alitumwa ulimwenguni (Misri) kuhifadhi uzima. Tukinukuu kutoka kwa Wazee na Manabii, ukurasa wa 231, tunasoma: “Mungu alinituma kabla yenu kuwahifadhi ninyi kuwa uzao katika dunia, na kuokoa maisha yenu kwa ukombozi mkuu.” Kwa hivyo imeandikwa kwamba ukombozi huu ulikuwa funzo la mfano la baraka ya kiroho. Lakini Yusufu aliubariki vipi ulimwengu wa kale? Je! Haikuwa kwa nafaka aliyohifadhi katika miaka saba ya wingi? Isingekuwa kwa maghala makubwa yaliyojaa kawi inayotoa uhai, Yusufu angekuwa baraka gani kwa ulimwengu wa zamani kama isingekuwa kwa hekima yake aliyopewa na Mungu kukusanya nafaka ambayo kwayo angeulisha ulimwengu kwa wakati wa hitaji lake kuu? Nafaka ambayo Yusufu alihifadhi ni baraka kama ilivyoandikwa, ile nafaka huwakilisha baraka ya kiroho (Neno la Mungu). Neno la Mungu ni mkate wa kiroho na watu wameishi kwa huo. {SR1: 16.3}

17

“Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.” Ezek. 3:1. “Maneno yako yalionekana, nami nikayala na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu na shangwe ya moyo wangu: Maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana Mungu wa majeshi.” Yer. 15:16. “Akawanyeshea mana ili wale, akawapa nafaka ya mbinguni.” Zab. 78:24. “ Baba zetu waliila mana jangwani; kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula [nafaka] cha mbinguni ili wale. Yesu akawaambia, Amin, amin, Nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba Yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni.” Yohana 6:31, 32. “Yeye ashindaye Nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa.” Ufu. 2:17. “Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu: Na nilipokwisha kukila, tumbo langu likatiwa uchungu.” Ufu. 10:10. {SR1: 17.1}

Unabii wa mwisho umetumika kwa William Miller baada ya kukichambua kitabu cha Danieli na kupokea fundisho lake. Kusema ki-mfano, alikula hicho kitabu kidogo, ambacho kilikua sehemu yake na watendakazi wenzake. Hili lisingekuwa kweli, asingekuwa aliutangaza ujumbe huo kwa uchangamfu kama huo alivyofanya. Jinsi tukio lililotarajiwa liliposhindwa kutukia katika mwaka 1844, kwao ulikuwa uzoefu mchungu, na hivyo kutimiza Maandiko kwamba watu wamekula Neno la Mungu. {SR1: 17.2}

Iwapo ile nafaka haiwakilishi Neno jinsi ilivyo katika Biblia, basi swali linaweza kuulizwa, Yusufu ni mfano wa nini? Isaka, Yona, na Elisha kila mmoja huwakilisha awamu fulani ya kazi ya Kristo, na ikiwa Yusufu humwakilisha Kristo; chakula kilichokusanywa, — Neno; ghala, — Biblia, basi miaka saba ya wingi, katika wakati ambao chakula kilikusanywa lazima uwe nembo, vinginevyo picha haiwezi kuwa kamilifu; na iwapo miaka ya wingi ni mfano, basi miaka ya njaa lazima izingatiwe. Kila moja ya sehemu hizi mbili za wakati hubeba namba “saba,” ikimaanisha “ukamilifu”, ujazi wa wakati (wote, au wakati wote). {SR1: 17.3}

Nembo hiyo inaweza kuwakilisha kitu kimoja pekee, nacho ni historia ya ulimwengu katika sehemu mbili kubwa za wakati; yaani K.K. na B.K. na

18

msalaba (Kristo), ukiwa ndio mstari wa kugawanya. “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.” Ni kwa sababu hii Yesu alifanya taarifa hiyo kwa maana hatuna mwingine hadi sasa. Miaka ya wingi ni K.K. katika wakati ambamo Mungu alitoa mengi kutosheleza hitaji la ulimwengu kwa miaka ya njaa (wakati wa Agano Jipya, B.K.). Jinsi Yusufu alivyokusanya nafaka maghalani na watumishi wake, — Wamisri, vivyo hivyo Kristo alilikusanya Neno la Mungu (chakula cha kiroho) katika Biblia (ghala) na wajoli Wake, manabii. “Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi Amesema nasi katika Mwanawe, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa Yeye aliufanya ulimwengu.” Ebr. 1:1, 2. Isingekuwa kwa kusudi hili basi tunauliza, ingeweza kuwa kwa nini? Mungu aliyehusika na tukio hilo hakutenda hivyo ili kuleta mateso kwa raia Wake, au kuufisha ulimwengu kwa njaa, kwa sababu njaa haikuwepo Misri tu, maana tunasoma, “Na njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi.” Mwa. 41:56. Kama hii haikuwa nembo, kwa nini Mungu alileta njaa juu ya dunia yote? Watu wengine wanaweza kuwa na ugumu wa kusadikishwa, na wengine hawawezi kushawishika kamwe, lakini upatano wa somo hauwezi kutiliwa shaka. {SR1: 17.4}

Iwapo miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa si mfano wa historia ya ulimwengu; Maghala makubwa ya Yusufu sio mfano wa Biblia; nafaka iliyokusanywa katika miaka saba ya wingi si mfano wa Neno katika Biblia; kulisha ulimwengu sio mfano wa wakati wa Agano Jipya unaotumia Maandiko yaliyokusanywa katika wakati wa Agano la Kale; basi tunauliza, I wapi mifano ya matukio haya yote? Je! Mungu hajatoa injili katika mifano na vile vile katika unabii? “Kristo alikuwa msingi wa uchumi wa Kiyahudi. Mfumo wote wa mifano na nembo ulikuwa unabii ulioshindiliwa wa injili, utoaji ambao ulikuwa umefungiwa ahadi za ukombozi.” Matendo ya Mitume, ukurasa wa 14. Iwapo miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa haikuwakilisha historia ya ulimwengu, sanjari vile vile zitajitahidi kutokeza yale ambayo hayangewezekana bila kukusudia. Yesu alisema, “Yakusanye masazo

19

ya vipande viliyobaki kisipotee chochote.” Lilikuwa Neno Lake ambalo lilizidisha mikate na samaki; makombo haya huwakilisha maneno yale yale Aliyoyanena. {SR1: 18.1}

Tunasoma yafuatayo katika Gombo la 2, ukurasa wa 606: “Nimeagizwa kutoka kwa Mungu kukwaambia kwamba hakuna mshale mwingine wa nuru kupitia Shuhuda utaangaza kwenye njia yako, mpaka utakapoweka kwa matumizi ya vitendo nuru ambayo umepewa tayari.” Lakini sasa lazima tuwe na nafaka la sivyo tutakufa. Kama watu tumejivunia sana kwamba tuna ukweli wote, lakini taarifa kama hiyo haiwezi kupatikana kati ya kurasa za Roho ya Unabii. “Hakuna mshale mwingine wa nuru utaangaza kwenye njia yako, mpaka utakapoweka kwa matumizi ya vitendo nuru ambayo umepewa tayari.” Maneno haya hupendekeza kwamba iko nuru zaidi itakayoangaza, na nuru ni ukweli. Tena, kunukuu kutoka Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 107: “Hakuna mtu anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ilioko kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia hili, amesema, ‘Nimeweka mbele yako mlango wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.’ Hata kama viongozi wetu wote wanaweza kukataa nuru na kweli, mlango huo utakuwa bado wazi. Bwana atawainua watu watakaowakabidhi watu ujumbe wa wakati huu.” {SR1: 19.1}

Miaka Saba Ya Wingi, Na Miaka Saba Ya Njaa

Miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa katika siku za Yusufu kule Misri ya kale huwakilisha historia ya ulimwengu katika sehemu mbili za wakati jinsi ilivyoelezwa hapo awali; yaani K.K. na B.K. Kila moja ya sehemu hizi hubeba namba ya Kibiblia “saba” (ikimaanisha ukamilifu). Miaka saba ya wingi ni K.K. Ingawa mtu anaweza kutilia shaka matumizi uliofanywa hapa, funzo tunalopata kutoka kwayo ni kweli. Katika wakati wa Agano la Kale, Mungu alitoa mengi kupitia kwa manabii Wake, na Kristo (Yusufu) aliyahifadhi ghalani (Biblia), lakini kwa kuwa hatuna kumbukumbu kwamba kulikuwa na nafaka yoyote iliyobaki wakati miaka saba ya njaa ilipokuwa imepita, wala hapakuwa na upungufu wowote. Kwa hivyo ni wazi, kwamba Maandiko yote yanapaswa kueleweka (kutumiwa) kabla ya kuja kwa Kristo mara ya pili. {SR1: 19.2}

Ndoto ya Farao iliyoandikwa katika Mwa. 41:17-20, husomeka kama ifuatavyo: “Katika ndoto yangu, tazama, nalikuwa nikisimama ukingoni mwa mto:

20

Na, tazama, ng’ombe saba wanatoka mtoni, wanono wazuri; wakajilisha manyasini: Kisha, tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda baada yao, dhaifu wabaya sana wamekonda, katika nchi yote ya Misri sijaona kama hao kwa udhaifu: Na hao ng’ombe waliokonda wabaya wakawala wale ng’ombe saba wa kwanza wale wanono.” Kumbuka kwamba ng’ombe saba waliokonda na wabaya waliwala wale ng’ombe walionona. Kwa kusoma Mwanzo 41:21, tunaona wale ng’ombe saba waliokonda hawakunona baada ya kuwala ng’ombe saba wanono, jambo ambalo huashiria kwamba hakutakuwa na maandiko katika akiba, lakini yote yatafunuliwa. Wazo ni kwamba ile miaka saba (B.K.) itatumia nafaka yote (Neno) katika ile miaka saba (K.K.) kama inavyowakilishwa pia na masuke ya ngano katika Mwa. 41:22-24. Je! hili sio wazi kwamba maandishi yote katika Agano la Kale yatatimizwa na kueleweka kabla ya mwisho wa B.K. (kuja mara ya pili kwa Kristo)? Lakini si ni kweli kwamba sehemu kubwa au sehemu bado haijaeleweka? Je! mtu anawezaje kusema kwamba ana ukweli wote na hana na hawezi kuelezea sehemu kubwa ya Biblia? Je! Tumwombe Mungu ayafumbue macho yetu ili tuweze kuona na kuinuka kutoka kwa utepetevu huu wa Ulaodekia ambao tumetumbukia ndani? {SR1: 19.3}

Watu 144,000 Ni Kina Nani?

Mada ni, “Je! Watu 144,000 ni kina nani?” Mtajo wa mara ya kwanza kwa namba hii katika Biblia ni katika Ufu. 7:4: “Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri: watu mia na arobaini na nne elfu kutoka makabila yote ya wana wa Israeli.” Ufu. 7:2. “Nami nikamwona malaika mwingine akipanda kutoka mashariki, akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai: Akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne, waliopewa kuidhuru nchi na bahari.” Kumbuka kwamba malaika huyu anapanda na hashuki. Kinyume na hili, Ufu. 18:1 husema, “Baada ya mambo hayo nalimwona malaika mwingine ameshuka kutoka mbinguni, mwenye uwezo mkuu, na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.” Malaika huyu mwenye nguvu hapandi, hashuki, wala haji, lakini “ameshuka.” Iwapo malaika alisafiri kutoka mbinguni kuja duniani chini ya dakika 15 kujibu ombi (Dan. 9:4-23), wakati ambapo huchukua mwangaza mamilioni ya miaka kusafiri sehemu ya umbali huo,

21

tunaweza kuelewa kwa urahisi mbona usemi “amekuja” umetumika, ukimaanisha kutokea ghafla bila onyo. Malaika huyu ni malaika wa Kilio Kikuu, nyongeza kwa malaika wa tatu na ujumbe wa anguko la Babeli kama ulivyotolewa na malaika wa pili unarudiwa, jinsi ulivyotabiriwa katika sura ya 18 ya Ufunuo. Hivyo watu wa Mungu wanaandaliwa kusimama katika saa ya kujaribiwa, ambayo watakutana nayo hivi karibuni. {SR1: 20.1}

Maandishi ya Awali, ukurasa 277: “Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake. Uwezo mkuu na utukufu alipewa yule malaika, na aliposhuka, nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Nuru iliyoambatana na malaika huyu ilipenyeza kila mahali, huku akipiga kelele kwa nguvu, kwa sauti kuu, ‘Umeanguka, umeanguka Babeli, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’ Ujumbe wa anguko la Babeli, jinsi ulivyopeanwa na malaika wa pili, unarudiwa, pamoja na kutajwa zaidi kwa ufisadi ambao umekuwa ukiingia makanisani tangu mwaka 1844. Kazi ya malaika huyu inaingia kwa wakati mwafaka kujiunga na kazi kubwa ya mwisho ya ujumbe wa malaika watatu, unapoumuka kuingia katika kilio kikuu. Na hivyo watu wa Mungu wanaandaliwa kusimama katika saa ya kujaribiwa, ambayo watakutana nayo hivi karibuni. Naliona nuru kuu ikitua juu yao, na waliungana kwa ujasiri kuutangaza ujumbe wa malaika wa watatu… Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao jinsi kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga kwa ujumbe wa malaika wa pili mwaka 1844.” {SR1: 21.1}

Kuhusu malaika watatu wa Ufu. 14:6-11, Yohana anaandika: “Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu,… na mwingine malaika wa tatu akawafuata.” Malaika hawa, wakiwa wanafuatana, walionekana wakiruka katikati ya mbingu ambapo jua lingekuwa katikati wakati wa adhuhuri, kwa uwezo wake kamili. Iko tofauti kati ya malaika hawa na wale walio katika Ufunuo 7 na 18:1. Malaika hawa “hawapandi” wala “hawajashuka,” bali huendelea “kuruka katikati ya mbingu.” Maana ni kwamba jumbe za malaika hawa hazina nguvu kama ule wa Ufu. 18:1, kwa maana Yohana husema alimwona malaika “ameshuka,” yaani, amesimama juu ya nchi. Malaika aliyetajwa hapa yu karibu, lakini wale malaika wengine

22

watatu wako mbali. Nembo hii huonyesha kwamba hawawezi kuwa na nguvu kama yule aliye karibu, lakini malaika hawa watatu wanaruka na huendelea kuruka. Maana ni kwamba wakati hawana nguvu kama yule, wanaendelea kwa muda mrefu hadi malaika huyu mwingine wa Ufu. 18:1 ajiunge nao, jinsi ambavyo umekuwa ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu hadi sasa. {SR1: 21.2}

Tunarejea kwa malaika wa Ufunuo 7, yule ambaye tunavutiwa sana wakati huu. Malaika huyu akipanda kutoka mashariki. “Kupanda” hapa hakuwezi kumaanisha kuondoka au kupaa kwenda mbali, bali kuja tu, au kujongea. Kwa mfano, asubuhi jua linapochomoza au linapopanda, halijoto huongezeka wakati linapokaribia adhuhuri, ndivyo ilivyo na malaika huyu ambaye atawatia muhuri watu 144,000. Malaika huyo alionekana akija, lakini anachukua muda. Kutia muhuri hakuwezi kuanza hadi baada ya kuwasili kwake, maana muhuri wa Mungu aliye hai u mkononi mwake. Iwapo tunaweza kutambua wakati atakapofika tunaweza kujua mwanzo wa wakati wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000. Je! Tulijua wakati ambapo ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu ulianza? Jibu letu ni: Naam. {SR1: 22.1}

Hamna sababu ya kutojua wakati maalum malaika huyu wa Ufunuo 7 atakapowasili. Iwapo hatungejua wakati, hatungekuwa na ujumbe wowote, na ikiwa Shetani anaweza kutuhadaa kutoka kwa ukweli wa sasa, ameshinda kwa nguvu zake za udanganyifu. Unabii wa Yohana katika Ufunuo 7, kumhusu malaika huyu anayepanda ulikuwa tu maono ya kitu ambacho kingekuja, na utimizo wa unabii huu uligunduliwa wakati Dada White alipewa njozi yake ya kwanza katika mwaka 1844, ambayo ilikuwa njozi ya watu 144,000. Soma Maandishi ya Awali, ukurasa wa 13-20. Yohana alitabiri juu ya vuguvugu hili na eneo la malaika akipanda mashariki (maono ya Yohana) likawa uhalisi katika mwaka 1844, lakini malaika yuko mashariki, na lazima tusubiri kuwasili kwake, kwa maana atakapowasili, kutiwa muhuri kunaanza. {SR1: 22.2}

Je! Watu 144,000 Watawahi Kufa?

“Watakatifu walio hai, 144,000 kwa idadi;” hatupaswi kuhitimisha kwamba ni sehemu tu ya sehemu nzima inayoweza kujumuisha hiyo namba na bado uwe ukweli, kwa maana taarifa iliyofanywa na Uvuvio haiwezi kupingana kwa sababu

23

husomeka “144,000 kwa idadi.” Wakati kundi hili linatajwa, ni wakati uo huo ambapo Mungu anajulisha siku na saa ya kuja kwa Yesu. Iwapo tunaweza kubainisha ni kwa wakati gani wa historia ya ulimwengu Mungu atatamka siku na saa ya kuja kwa Yesu, basi tunaweza kujua mengi zaidi kulihusu kundi hili. Kunukuu Maandishi ya Awali, ukurasa wa 285: “Lakini palikuwa na sehemu moja wazi yenye utukufu uliotulia, ambayo sauti ya Mungu ilitokea kama maji mengi, ikitetemesha mbingu na nchi. Palikuwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi. Makaburi yalifunuliwa, na wale ambao walikuwa wamekufa kwa imani chini ya ujumbe wa malaika wa tatu, wakitunza Sabato, walitokea… Na Mungu alivyotamka siku na saa ya kuja kwa Yesu, na kukabidhi agano la milele kwa watu Wake.” {SR1: 22.3}

Mtu anaweza hapa kudhani kwamba waliofufuka na walio hai hujumuisha hiyo namba, lakini hatuamini kwamba Roho ya Unabii ingeyaita makundi yote mawili (walio hai na waliofufuliwa) watakatifu walio hai. Watu 144,000 ni watakatifu walio hai; wale wengine, waliofufuliwa watunza Sabato. Ili kufanya liwe bayana, dondoo nyingine imetolewa, inayopatikana katika Pambano Kuu, ukurasa wa 637: “ Mvua ya mawe kubwa sana, kila moja ‘kama uzani wa talanta [kilo hamsini], inafanya kazi yake ya uharibifu. Miji yenye kiburi zaidi ya dunia imetandazwa chini… Makaburi yamefunuliwa, na “wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi … wataamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine aibu na kudharauliwa milele.” Wote ambao wamekufa katika imani ya ujumbe wa malaika wa tatu wanatoka kaburini wamepewa utukufu, kulisikia agano la Mungu la amani na wale ambao wameitunza sheria Yake.” Hili linafanya kuwa wazi wazi kwamba watunza Sabato waliofufuliwa watatokea katika ufufuo maalum wa Danieli 12. Huu ni wakati ambapo Mvua ya mawe kubwa sana inafanya kazi yake ya uharibifu (pigo la 7). “Na huyo malaika wa saba akamimina kitasa chake juu ya anga; … Na mvua ya mawe kubwa sana ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu, kila jiwe kama uzani wa talanta moja [kilo hamsini]: Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.” Ufu. 16:17, 21. Watunza Sabato waliofufuliwa hawakuishi katika wakati wa mapigo, kwa maana walifufuliwa wakati wa pigo la saba, ili kwamba walisikie tangazo la siku na saa ya kuja kwa Yesu. {SR1: 23.1}

24

Iwapo ushahidi unaweza kuletwa kwa mtazamo kwamba watu 144,000 (kwa idadi) waliishi kabla ya pigo la saba, basi tuna uthibitisho bayana kwamba watu 144,000 hawakufa kamwe. Pambano Kuu, ukurasa wa 649: “Nao wauimba ‘wimbo mpya’ mbele ya kile kiti cha enzi, wimbo ambao hapana mtu anayeweza kujifunza ila wale watu 144,000. Ni wimbo wa Musa na Mwana-Kondoo, — wimbo wa ukombozi. Hapana mtu ila watu 144,000 wanaweza kujifunza wimbo huo; kwa maana ni wimbo wa uzoefu wao, — uzoefu ambao hakuna kundi lingine lolote limewahi kuwa nao… Wameiona dunia ikiharibiwa kwa njaa na tauni, jua likiwa na nguvu ya kuwaunguza wanadamu kwa joto kali, na wao wenyewe wamevumilia mateso, njaa, na kiu.” Hapa ipo taarifa wazi wazi kwamba watu 144,000 waliishi katika wakati wa pigo la nne, jua likiwa na nguvu ya kuwaunguza watu kwa joto kali. “Na malaika wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua; nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.” Ufu. 16:8. Hili ni pigo la nne. Je! Wangewezaje (144,000) kupitia pigo la nne iwapo ufufuo maalum wa watunza Sabato (wale waliokufa chini ya ujumbe wa malaika wa tatu) haukutukia hadi karibu mwisho wa pigo la saba? Iwapo “wameona dunia ikiharibiwa kwa njaa na tauni na wao wenyewe wamevumilia njaa na kiu,” lazima wawe wameishi wakayapitia hayo mapigo yote. {SR1: 24.1}

Tena, “Wauimba wimbo mpya” … ambao hapana mtu anayeweza kujifunza ila wale watu 144,000 … kwa maana ni wimbo wa uzoefu wao, — uzoefu ambao hakuna kundi lingine lolote limewahi kuwa nao.” Inawezekana vipi kwa wote kuuimba wimbo huo iwapo ni wimbo wa uzoefu wao isipokuwa wote wana uzoefu sawa? Wale ambao walikuwa kaburini wamekuwa na uzoefu wa mauti, kaburi, ufufuo, na kupokea mwili mpya. Lakini wale ambao kamwe hawakufa wameona utimizo wa Ezekieli 9; Isaya 63; Isaya 60; kufungwa kwa ujumbe wa malaika wa tatu, (kilio kikuu, kufungwa kwa muda wa rehema), mapigo yote saba ya mwisho, nao wauimba wimbo huu (wa uzoefu na ukombozi wao) “ambao hapana mtu anayeweza kujifunza ila wale watu 144,000.” {SR1: 24.2}

Je! Dada White Atakuwa Pamoja Na Watu 144,000

Dada White alipelekwa katika maono kwa mojawapo wa sayari nyingi ambayo ilikuwa na

25

miezi saba, ambako alikutana na Henoko mzee mwema. Mahali hapo palikuwa pazuri sana na tumaini lake kubwa la kupendezwa hivi kwamba akamsihi malaika amwache akae huko. “Kisha malaika akasema, ‘Lazima urudi duniani na ikiwa u mwaminifu, wewe, pamoja na watu 144,000 mtakuwa na upendeleo wa kuzuru dunia zote na kutazama kazi za mikono ya Mungu.’” Tazama Maandishi ya Awali, ukurasa wa 40. Hakuna mkanganyo katika taarifa hii, kwa maaana malaika alimwambia kwamba yeye, pamoja na watu 144,000, kumaanisha yeye ni mmoja pamoja nao lakini si mmoja wao. Bila shaka atakuwa pamoja nao kwa sababu anaweza kuitwa mama yao (akiwa mjumbe na mwasisi wa vuguvugu hili), na hatuwezi kuwaza watauimba wimbo wa Musa na yeye (Musa) asikuwe pale. Kwa sababu wao ni watu 144,000, kundi maalum lililo na uzoefu maalum, sio sababu kwa nini wengine wasisafiri pamoja nao, kwa maana bila shaka Abrahamu, Isaka, na Yakobo watakuwa pamoja nao, wakiwa kina baba katika mfano. Je! Ni pingamizi gani inaweza kutolewa iwapo wengine wangesafiri nao? Tunaweza kukisi kwamba Yesu atawapatia waliokombolewa wote angalau safari moja kwenda kwa dunia zingine. {SR1: 24.3}

Watu 144,000 Pekee Wanaingia Hekaluni

“Na tulipokuwa tunakaribia kuingia ndani ya hekalu takatifu, Yesu alipaza sauti Yake nzuri na akasema, ‘Watu 144,000 pekee ingia mahali hapa,’ na tukapiga kelele, ‘Aleluya.’ Hekalu hili lilitegemezwa na nguzo saba za dhahabu safi, lilisimamishwa na lulu za utukufu zaidi. Mambo ya ajabu niliyoyaona hapo, siwezi kuelezea … Naliona hapo meza za mawe ambazo majina ya watu 144,000 yaliandikwa kwa herufi za dhahabu. Baada ya kuuona utukufu wa hekalu, tulitoka ndani.” Maandishi ya Awali, ukurasa wa 19. Ni wazi kwamba hakuna wengine wangeingia ndani ya hekalu takatifu isipokuwa watu 144,000, na tena ni wazi kwamba aliingia ndani, kwa maana asema, “Mambo ya ajabu niliyoyaona hapo, siwezi kuelezea,” na “baada ya kuuona utukufu wa hekalu, tulitoka ndani.” Hangeweza kuona mambo ndani ya hekalu isipokuwa alikuwa ameingia ndani, na asingeweza kutoka ndani iwapo kamwe hakuwa ameingia ndani. {SR1: 25.1}

Wengine wanaweza kufikiri kwamba Dada White ni mmoja wa watu 144,000 kwa sababu aliingia ndani ya hekalu hili, na sasa kwa sababu amekufa sehemu hiyo ya watu

26

144,000 itafufuliwa. Hakuna sababu ya kuchanganyikiwa hapa. Angeweza kuingia hekaluni kabla, au baadaye, au angeingia moja kwa moja nao, na bado hilo halingebadilisha hilo wazo. Lazima tukumbuke hii ni njozi tu na sio watu halisi 144,000. Hawakuwa wamefanzwa kwa wakati huo, wala yeye hakuwa hapo katika mwili. Njozi hii ilipeanwa kwake atoe ripoti na kuufunua ukweli fulani. Kwa maneno mengine, alikuwa mwandishi wa habari. Je! Ni aina gani ya ripoti ambayo ingetolewa iwapo hangeingia hekaluni? Amri, “watu 144,000 pekee ingia mahali hapa, haikuwa na mtajo kwake iwapo alipaswa kukaa nje au kuingia. Yeye ni mmoja pamoja nao, lakini si mmoja wao. {SR1: 25.2}

Ni Muhuri Wa Aina Gani?

Rejeleo limefanywa katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 445. Mada ni juu ya kutiwa muhuri kwa Ufunuo 7, watu 144,000. Tunanukuu: “Huku kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu ni sawa na kule alionyeshwa Ezekieli katika maono.” Sasa iwapo kutiwa muhuri kwa watu 144,000 wa Ufunuo 7, ni sawa na Ezekieli 9, ili kupata aina gani ya huu muhuri, na wakati wa kuanza kwake, lazima tuchambue Ezekieli 9:1-9: “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja aliye na kifaa chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na, tazama, watu sita wakaja wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kifaa chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni: wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu Yake, mpaka kizingiti cha nyumba. Akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni; Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na kwa hao wengine Aliwaambia nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige: jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma: Waueni kabisa mzee

27

na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake: lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Akawaambia, Itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa: haya enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikaachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? Ndipo Akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana.” Ni bayana kwamba kutiwa muhuri kwa watu 144,000 ni Ezekieli 9, — utengo (upepeto kanisani — wamchao Mungu kutoka kwa wasiomcha). Gombo la 1, ukurasa wa 181: “Naliuliza maana ya upepeto nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi wa kweli kwa Walaodekia.” Soma ukurasa wote. Kumbuka upepeto unaanza baada ya ushuhuda usiopinda wa “Shahidi wa Kweli” kuja. {SR1: 26.1}

Mihuri Miwili

Je! Sabato ndio muhuri wa watu 144,000? Kwanza kabisa itagundulika kwamba ufafanuzi wa “muhuri” ni: Chombo ambacho hutumiwa kutia muhuri, kubana, au kufungasha kwa usalama; kuhakiki au kuamua pasipo shaka; kuonyesha na kubainisha; mteule. Juhudi itafanywa kuleta wazi ushuhuda wa kutosha wa Biblia kumridhisha yeyote anayeamini Maandiko kwamba wote waliookolewa katika vizazi vilivyopita na vile vile wale ambao wataokolewa sasa lazima wawe na muhuri wa Mungu. Paulo, katika barua yake kwa Waefeso alisema kwamba walipaswa kutiwa muhuri. “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” Efe. 4:30. Neema ya utakaso iliyofanywa ndani ya nafsi na Roho Mtakatifu ndiyo muhuri na uhakikisho wa ukombozi ujao wa mtu, wa ufufuo wa furaha. Matumizi na mwisho wa muhuri huu ni utakatifu na usalama wa kitu kilichotiwa muhuri kutoka kwa macho ya udadisi na mikono ya vurugu, ambayo vinginevyo ingetumiwa vibaya na wageni na maadui; hivyo watoto wa Mungu wamepita lawama

28

za dunia ya uovu. Wamehifadhiwa kama vitu vya thamani kwa matumizi ya Mungu mwenyewe, kuwa Naye mbinguni. Kunukuu 2 Tim. 2:19, iliyoandikwa kwa Wakorintho: “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio Wake.” “Naye ndiye aliyetutia muhuri, akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.” 2 Kor. 1:22. {SR1: 27.1}

Tunasoma katika Ufunuo 8 na 9, kuwahusu malaika saba wenye baragumu saba. Baragumu hizi saba huonyesha matukio makuu ya kisiasa na ya ki-vita ambayo yalipaswa kutukia katika wakati wa kanisa la injili. Kutiwa muhuri kwa watu 144,000 ni kwa wakati wa baragumu ya sita. Kuanzia Ufu. 9:1, tunasoma kuhusu yule malaika na baragumu ya tano. Aya ya 4 ya sura hii tunanukuu: “Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote; ila wale watu wasio na muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.” Hapa tunaona kwamba miaka mingi kabla ya ujumbe wa malaika wa tatu kuanza kuhubiriwa, watakatifu wa Mungu walitiwa muhuri na muhuri wa Mungu, kama wale walio chini ya ujumbe wa malaika wa tatu watakavyotiwa muhuri. Kwa mujibu wa maandiko haya ambayo yameelezwa wazi wazi, lazima tuhitimishe kwamba watakatifu wa Mungu wametiwa muhuri kwa ukweli wa sasa katika vizazi vyote, na uwao wote ule ukweli wa sasa, huo ndio muhuri. Ukweli wa sasa chini ya ujumbe wa malaika wa tatu ni ukweli wa Sabato, kwa hivyo, Sabato ni muhuri unaowatia muhuri watu ambao ni watiifu kwayo. Kunukuu Pambano Kuu, ukurasa wa 452: “Muhuri wa sheria ya Mungu unapatikana katika amri ya nne … Sabato ilipobadilishwa na utawala wa upapa, huo muhuri uliondolewa katika sheria.” Maandishi ya Awali, ukurasa wa 58: “Wakati wa kutiwa muhuri ni mfupi sana, na hivi karibuni utakwisha.” {SR1: 28.1}

Wale waliokufa chini ya ujumbe wa malaika wa tatu, wakitunza Sabato, wametiwa muhuri kwa ukweli wa Sabato, lakini watu 144,000 hawafi kamwe. Wakati wanapaswa kutunza Sabato na kuupokea muhuri huo, lazima waugue na kulia kwa sababu ya machukizo ambayo yanafanyika ndani ya kanisa, kwa maana vinginevyo hawawezi kupokea alama ya malaika aliye na kidau cha wino wa mwandishi wa Ezekieli 9, ambao ni muhuri kwa mujibu wa Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 445; Gombo la 5, ukurasa wa 210-16; Gombo la 3, kurasa

29

266-7. Kutiwa muhuri kwa watu 144,000 ni utengo wa waaminifu kutoka kwa wasio waaminifu; kutakaswa kwa kanisa. Wale ambao hawatii ukweli, na kujiingiza katika dhambi na machukizo, ambao hujaribu kuyafunika maovu yaliyopo, wataanguka chini ya mfano wa watu watano walio na silaha za kuchinjia za Ezekieli 9. {SR1: 28.2}

Sabato imekuwa ukweli wa sasa tangu mwaka 1845, na ikiwa ndio muhuri wa sheria ya Mungu imekuwa ikitia muhuri sheria kati ya watu wa Mungu tangu mwaka huo. Isa. 8:16 “Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.” Hii imekuwa kazi ya malaika wa tatu, na kwa sababu hii malaika wa tatu hana muhuri, kwa maana muhuri u katika sheria, lakini yule malaika wa Ufunuo 7, ana muhuri mkononi mwake. Ezekieli humwita mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi ambaye ataweka alama kwa watu wanaougua na kulia dhidi ya machukizo yote yanayofanyika kati yake (kanisa). Huu ndio muhuri wa watu 144,000, lakini wote waliookolewa chini ya malaika wa tatu wametiwa muhuri wa Sabato. Watu 144,000 wakiwa na muhuri huu pia wametiwa alama (wametiwa muhuri) na malaika wa Ufunuo 7, ambao ni sawa na ule wa Ezekieli 9. Kwa maneno mengine, unaweza kuitwa muhuri maradufu. {SR1: 29.1}

Ezekieli 9 Si Muhuri Wa Sabato

Muhuri huu wa watu 144,000 si muhuri wa Sabato. Walakini, wale wanaotiwa muhuri lazima wawe watunza Sabato. Ni muhuri, au alama, inayoyatenganisha makundi mawili ndani ya kanisa, na wale ambao wametiwa muhuri, au kutiwa alama hawajatiwa alama kwa sababu hutunza Sabato tu, bali kwa sababu wanaugua na kulia kwa sababu ya machukizo yote ambayo yanafanywa kanisani. Kwa hivyo kutiwa muhuri na mchinjo u ndani ya kanisa la Mungu, na sio Babeli, au ulimwenguni. Ni katika Yerusalemu, na Yuda pekee, nyumba ya Israeli (kanisa). “Yuda” katika Ezek. 9:9 huwataja wale walio madarakani, kwa sababu Yuda ilichukua ofisi ya Walawi baada ya kabila la Lawi kuchukuliwa mateka. Hakuna wazo kuhusu ulimwengu au wasiomcha Mungu. Wakati kutiwa alama (kutiwa muhuri) kumekwisha, wale watu watano walio na silaha za kuchinjia wanaanzia kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba, kumaanisha walezi wa kiroho

30

wa maslahi ya watu. Tazama Gombo la 3, ukurasa wa 266, 267, na Gombo la 5, ukurasa wa 210-212. {SR1: 29.2}

Tunanukuu Gombo la 5, ukurasa wa 211: “Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao. Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu Wake kwa hukumu.” Gombo la 3, ukurasa wa 265: “Lakini iwapo dhambi za watu zinaachiliwa na wale walio katika nafasi za uwajibikaji, kununa Kwake kutakuwa juu yao, na watu wa Mungu, kama mwili, watawajibishwa dhambi hizo.” {SR1: 30.1}

Wale ambao wametiwa muhuri (wamewekwa alama) na kuokoka hayo maangamizo ni wale ambao watajumuisha namba ambayo unabii hutangaza kuwa ni watu 144,000. Dhehebu letu lina idadi ya karibu watu 300,000. Hili humaanisha dhehebu litagawanywa nusu na hudokeza wanawali kumi, watano kati yao walikuwa wenye busara na watano walikuwa wapumbavu. Kwa maneno mengine, nusu kwa nusu. Mungu awasaidie watu Wake, na atupatie maono ya kujua dhambi ni nini ili tuweze kuondoa uovu wa kuleta msiba ulioko kanisani (nyumba ya Mungu). Maono kama haya yatasababisha tuugue na kulia kwa sababu ya machukizo ambayo yanafanywa kati yake. Yeye anayeelewa laana ya dhambi hataufunika uovu ulioko ili apate upendeleo wa yeyote. Mungu atuinue kutoka kwa kiwango cha chini kiroho ambacho tumeanguka, na atuokoe kutoka kwa hali hii ya Ulaodekia, ya uvuguvugu. Tuweze, kama Ninawi wenye hekima wa zamani, tuushinde unabii, ili mbingu iweze kufurahi. {SR1: 30.2}

Kutiwa Muhuri Kunaanza — Kanisa Liko Chini Kiroho

Ni dhahiri kwamba iwapo kutia muhuri na mchinjo u katika nyumba ya Mungu, kanisa (watu Wake), na ikiwa zaidi ya nusu ya watu lazima waangamie kwa dhambi zao isipokuwa watubu, na iwapo chini ya nusu moja ya washirika wa sasa wangekuwa 144,000, hakika hakungekuwa kumeanza miaka mingi iliyopita; na sembuse

31

mwanzo wa ujumbe wa malaika wa tatu, kwa maana hapakuwapo kanisa wakati huo ila watu wachache tu. Kusingeweza kuanza wakati kanisa lilikuwa katika hali nzuri, ya kiroho. Lazima kuwe kulianza wakati kanisa liko katika kiwango chake cha chini kabisa, na kutiwa unajisi kwa dhambi. Wale ambao wataupokea muhuri na kuokoka huo mchinjo lazima waugue na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Gombo la 8, ukurasa wa 250, husema, “Isipokuwa kanisa, ambalo sasa linachachishwa na kurudi nyuma kwake, litubu na kuongoka, litakula tunda la matendo yake, hata litajichukia lenyewe.” {SR1: 30.3}

Akinena kuhusu watu 144,000, Gombo la 5, ukurasa wa 210-11, husema, “Hawa waliougua, na kulia walikuwa wakishikilia maneno ya uzima; [ujumbe] walikuwa wamekemea, wameshauri, na kusihi. Wengine waliokuwa wakimvunjia Mungu heshima, walitubu na kunyenyekeza mioyo yao mbele Yake. Lakini utukufu wa Bwana ulikuwa umeondoka Israeli; ingawa wengi bado walikuwa wakiendelea na namna za dini, uwezo na uwepo Wake ulikosekana. Katika wakati ambapo ghadhabu Yake itatokea kwa hukumu, hawa wanyenyekevu, wafuasi waliojitolea wa Kristo watatofautishwa kutoka kwa wengine wote wa ulimwengu kwa uchungu wa roho yao, ambao unaonyeshwa kwa kuugua na kulia, makemeo na maonyo. Ilhali wengine hujaribu kufunika vazi juu ya uovu uliopo, na kuruhusu uovu mkubwa ulioenea kila mahali, wale walio na bidii kwa heshima ya Mungu na upendo kwa watu, hawatanyamaza ili wapate fadhili za yeyote… Huomboleza na kuitesa mioyo yao kwa sababu kiburi, tamaa, ubinafsi, na udanganyifu wa karibu kila aina u kanisani… Daraja ambalo halihisi kuhuzunishwa juu ya kuchakaa kwao kiroho, wala kuomboleza juu ya dhambi za wengine, litaachwa bila muhuri wa Mungu… Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walisimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameisaliti imani yao.”{SR1: 31.1}

Gombo la 5, ukurasa wa 82: “Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, Angaliwaheshimu

32

kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi. Lakini walijitenga kutoka kwa Mungu, wakaridhia mvuto wa ulimwengu, na Bwana akawakataa.”{SR1: 31.2}

Gombo la 5, ukurasa wa 211-12: “Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaza sauti zao tena kamwe kama tarumbeta kuonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa bubu, ambao hawakuweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja. Machukizo ambayo waaminifu walikuwa wakiugulia na kulilia yalikuwa yote yaliyoweza kutambuliwa kwa macho ya wanadamu, hata hivyo dhambi mbaya kabisa, zile ambazo zilichochea wivu wa Mungu msafi na mtakatifu, hazikufichuliwa… Mwenendo wetu wenyewe wa utendaji utaamua iwapo tutapokea muhuri wa Mungu aliye hai, au kuangamizwa na silaha za kuchinjia.” Iwapo tungemaki wakati halisi wa kuanza kwa kutiwa muhuri huu, tungesema kulianza wakati fulani katika mwaka 1929. Nafasi haitaturuhusu hapa kutoa sababu zetu za kuamini hivi, lakini katika uchambuzi mwingine hili litashughulikiwa. {SR1: 32.1}

Ili kupata ufahamu sahihi wa ujumbe wa malaika wa tatu tutaugawanya katika vipindi vitatu: (1) Mwanzo wa kutangazwa kwa Sabato ya kweli, Ufu. 14:6-11; (2) Matengenezo, na kutiwa muhuri kwa watu 144,000, Ufu. 7:1-8; (3) Kilio Kikuu, Ufu. 18:1. Ukweli wa kutiwa muhuri (144,000) ukishafanywa ujulikane, ni dhahiri kwamba tuko katika kipindi cha pili. Iwapo hatungekuwa tumejua kuanza kwa ujumbe wa malaika wa tatu mwanzoni mwake, hatungekuwa na ujumbe wowote. Kwa hivyo, lazima tujue wakati wa vipindi viwili vya mwisho vilipokuja, vikiwa si vya umuhimu mdogo. {SR1: 32.2}

33

Sababu Ya Kuugua Na Kulia

Gombo la 5, kurasa 210, 211: “Katika wakati ambapo ghadhabu Yake itatokea kwa hukumu, hawa wanyenyekevu, wafuasi waliojitolea wa Kristo watatofautishwa kutoka kwa wengine wote wa ulimwengu kwa uchungu wa roho yao, ambao unaonyeshwa kwa kuugua na kulia, makemeo na maonyo. Ilhali wengine hujaribu kufunika vazi juu ya uovu uliopo, na kuruhusu uovu mkubwa ulioenea kila mahali, wale walio na bidii kwa heshima ya Mungu na upendo kwa watu, hawatanyamaza ili wapate fadhili za yeyote. Nafsi zao zenye haki zinaudhiwa siku baada ya siku kwa matendo na mazungumzo yasiyo matakatifu ya waovu. Hawana uwezo wa kuuzuia mkondo wa bubujiko la uovu, na hivyo wamejawa na huzuni na kamsa. Huugua mbele ya Mungu kuona dini imedharauliwa katika nyumba haswa za wale ambao wamepata nuru kubwa. Huomboleza na kuitesa mioyo yao kwa sababu kiburi, tamaa, ubinafsi, na udanganyifu wa karibu kila aina u kanisani.” Roho wa Mungu, ambaye huchochea kemeo, anakanyagiwa chini ya miguu, ilhali watumwa wa Shetani hushinda. Mungu amevunjiwa heshima, ukweli kufanywa usiokuwa na maana… Machukizo ambayo waaminifu walikuwa wakiugulia na kulilia yalikuwa yote yaliyoweza kutambuliwa kwa macho ya wanadamu, hata hivyo dhambi mbaya kabisa, zile ambazo zilichochea wivu wa Mungu msafi na mtakatifu, hazikufichuliwa.” {SR1: 33.1}

Gombo la 1, ukurasa 471, 472: “Kosa kubwa limefanywa na baadhi ya watu wanaokiri ukweli wa sasa, kwa kuingiza biashara katika mkondo wa mfululizo wa mikutano, na kwa ulanguzi wao kukengeusha mawazo kutoka kwa kusudi la mikutano… ‘Imeandikwa, Nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala, lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wezi.’ Wafanyabiashara hawa wangeweza kusihi kama udhuru ya kwamba bidhaa walizoshikilia kuuza zilikuwa kwa ajili ya sadaka za dhabihu. Lakini kusudi lao lilikuwa kupata faida, kupata raslimali, kujilimbikizia… Wachungaji wamesimama katika mimbari na kutoa mahubiri ya utakatifu, na kisha kwa kuingiza biashara, na kutenda sehemu ya muuzaji, hata katika nyumba ya Mungu, wamezikengeusha dhamira za wasikilizaji wao kutoka kwa mashauri yaliyopokelewa, na kuharibu matunda ya kazi yao… Wakati

34

na nguvu zao zinapaswa kuhifadhiwa, ili juhudi zao ziweze kuwa za uangalifu katika mfululizo wa mikutano. Wakati na nguvu zao hazipaswi kutumika kuuza vitabu vyetu wakati vinaweza kuletwa mbele ya umma na wale ambao hawana mzigo wa kulihubiri neno.”{SR1: 33.2}

Gombo la 8, ukurasa wa 250: “Ni nani anaweza kusema kwa kweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto; mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimwona Mwalimu wetu akiyaonyesha mavazi ya kile kinachoitwa eti utakatifu. Aliyararua, Akaufunua wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha akanambia: ‘Je, huoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia?’ Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba?” Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu zinakosekana.” Kwa hivyo wakati na hali ya kanisa mwanzoni mwa kutiwa muhuri kwa watu 144,000 imeonyeshwa vizuri kwa Biblia na Roho ya Unabii. Ni ukweli ulioungamwa kati ya Waadventista wa Wasabato kwamba kanisa limekuwa likiporomoka kwa miaka kadhaa, lakini halijawahi kuwa katika hali ya chini kiroho kama lilivyo sasa. Sasa hakuna tofauti hata ndogo kati ya kanisa na dunia. {SR1: 34.1}

Sehemu Ya Orodha Ya Machukizo Kanisani

1. Ukosefu wa kicho katika nyumba ya Mungu: Isa. 56:7; Gombo la 5, ukurasa wa 492-500. {SR1: 34.2}

2. Kufuata mitindo ya ulimwengu: Isa. 3:16; Gombo la 1, ukurasa wa 269, 270; Gombo la 4, ukurasa 632; Gombo la 3, ukurasa 379; Gombo la 5, ukurasa 78; Gombo la 1, ukurasa 189-191; Gombo la 1, ukurasa 135, 136; Gombo la 4, ukurasa 631. {SR1: 34.3}

3. Kutumia fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula (matengenezo ya afya): Isa. 55:2; Gombo la 5, ukurasa wa 197; Isa. 56:12. (dondo nyingi zinaweza kutolewa kutoka katka shuhuda juu ya mada hii, lakini nafasi haitaziruhusu hapa). {SR1: 34.4}

4. Matumizi ya zaka — walimu wa shule (wale wanaofunza Maandiko)

35

hawalipwi na zaka kama ilivyostahili kuwa: Gombo la 6, ukurasa wa 215. {SR1: 34.5}

5. Nyumba ya Mungu imefanywa kuwa nyumba ya biashara kwa kununua na kuuza machapisho kila aina ya dhehebu: Isa. 58:3; Isa. 56:7; Gombo 1, ukurasa 471, 472; Gombo la 8, ukurasa 250. {SR1: 35.1}

6. Bei ghali katika taasisi zetu wakati zinapaswa kuwa chini ya gharama za sasa: Gombo la 8, ukurasa wa 142; Isa. 56:12; Isa. 58. {SR1: 35.2}

7. Kutoamini katika Roho ya Unabii: Iwapo hakuungamwi kwa maneno, kunatambulika kwa matendo. {SR1: 35.2}

8. Kushindwa kuwajulisha washiriki wa kanisa kuhusu ujumbe wa Eliya: Mal. 4:5; Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 475; Gombo la 4, ukurasa wa 402, 403. {SR1: 35.4}

9. Abrahamu alimtii Mungu katika yote aliyomwamuru, na alikuwa mwangalifu hata kwa jambo ndogo kabisa; kwahivyo ikahesabiwa kwake kuwa haki, lakini sisi hatujatenda hivyo. Tazama Mwa. 26:5; Mwa. 15:6. {SR1: 35.5}

10. Ahadi ya nchi (Kanaani ya mbinguni) ni kwa uzao wa Abrahamu. Yesu alisema, “Kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu. [Iwapo ninyi si watoto wa Abrahamu] Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda.” Tazama Yohana 8:39-44. (Kwa kuzitenda kazi za Abrahamu), “Basi mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawasawa na ahadi.” Gal. 3:29. {SR1: 35.6}

11. Kusisitiza kwamba tuna ukweli wote na hatuna haja ya kitu. {SR1: 35.7}

12. Kukataa madai ya Kimaandiko bila uchunguzi kuhusu nuru yake. Gombo la 5 ukurasa wa 211: “Machukizo ambayo waaminifu walikuwa wakiugulia na kulilia yalikuwa yote yaliyoweza kutambuliwa kwa macho ya wanadamu, hata hivyo dhambi mbaya kabisa, zile ambazo zilichochea wivu wa Mungu msafi na mtakatifu, hazikufichuliwa.” {SR1: 35.8}

Je! Huku Kutiwa Muhuri

Kutaendelea Hadi Kwa Kufungwa Muda Wa Rehema?

Kutiwa muhuri kwa watu 144,000 hakuwezi kuendelea hadi mwisho wa muda wa rehema, kwa maana lazima watiwe muhuri muda mrefu kabla ya wakati huo, na lazima kufungwe kabla ya kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Maandishi ya Awali, ukurasa wa 277 husema: “Naliona malaika wakiharakisha wakiingia na kutoka mbinguni,

36

wakishuka duniani, na tena wakipaa mbinguni, wakifanya tayari kutimizwa kwa tukio lingine muhimu. Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake. Uwezo mkuu na utukufu alipewa yule malaika, na aliposhuka, nchi ikaangazwa kwa utukufu wake… Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu.” Inaonekana katika usemi, “malaika wakiharakisha wakiingia na kutoka,” mwandishi anarejelea kutimizwa kwa Ezekieli 9; kisha anafuata malaika mwenye nguvu wa kilio kikuu cha Ufu 18:1. {SR1: 35.9}

Ezekieli 9, haiwezi kufikia utimizo wake wakati Kristo atakapokuja katika mawingu, kwa sababu huo mchinjo u kanisani. Kanisa la Kristo lazima liwe takatifu na safi, lisilokuwa na doa lolote kabla ya Yesu kuja. Ikiwa hatuko katika hali hii safi, hatuwezi kutumaini kusimama katika wakati wa taabu, wala hatuwezi kuepuka athari za mapigo. Kanisa litashindwa kusimama bila mwombezi baada ya muda wa rehema kufungwa au kabla, iwapo kuna kitu kimoja kichafu katika kambi ya Israeli. “Kwa maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli: huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.” Yoshua 7:13. {SR1: 36.1}

Kama kielezo na ulinganisho wa uaminifu na umoja wa watu wakati wa taabu mapigo yanapoanguka, tunanukuu Maandishi ya Awali, ukurasa wa 282-3: “Naliona watakatifu, wakihama mijini na vijijini, na wakiungana pamoja katika makundi, na kuishi katika maeneo ya faragha zaidi. Malaika waliwapatia chakula na maji, ilhali waovu walikuwa wanateseka kwa njaa na kiu. Kisha naliwaona watu wakuu wa dunia wakishauriana, na Shetani na malaika zake wakijishughulisha kuwazunguka. Nikaiona hati, ambayo nakala zake zilitawanywa katika sehemu mbali mbali za nchi, zikitoa amri kwamba isipokuwa watakatifu waisalimishe imani yao ya kipekee, waiache Sabato, na kuiadhimisha siku ya kwanza ya juma, watu walikuwa huru baada ya muda fulani, kuwaua… lakini malaika katika umbo la watu wa vita waliwapigania. Shetani alitamani kuwa na fursa ya kuwaangamiza watakatifu wa Aliye Juu;

37

lakini Yesu aliwaagiza malaika Zake kuwalinda… Kisha ukaja umati wa waovu wenye hasira, na tena umati wa malaika waovu, wakiwaharakisha waovu wawaue watakatifu. Lakini kabla waweze kuwafikia watu wa Mungu, waovu lazima kwanza walipite kundi hili la malaika watakatifu, wenye nguvu. Hili lilikuwa haliwezekani. Malaika wa Mungu walikuwa wakiwafanya warudi nyuma, na pia kusababisha malaika waovu waliokuwa wakiwasonga kuanguka nyuma.” Ni dhahiri hapa kwamba watu wa Mungu wamejitenga wako peke yao, bila waovu kati yao. Malaika watakatifu hawangeweza kuwalinda watu waovu kutoka kwa umati wa waovu. Hapa tunaona watu wa Mungu wametengwa na uovu wote. Kwa hivyo hili laonyesha kwamba wako katika umoja mkamilifu wakati wanaondoka vijijini. {SR1: 36.2}

Basi utakaso huu wa kanisa ulikuwa lini? Ezekieli 8, hutuambia kuhusu machukizo yanayofanywa kati ya Yerusalemu (kanisa); Ezekieli 9, hufunua matokeo kwa wale wasiougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote. “Mdhambi mmoja anaweza kueneza giza ambalo litaitenga nuru ya Mungu kutoka kwa mkutano wote.” Gombo la 3, ukurasa 265. {SR1: 37.1}

Watu Watano Wamfuata Yule Mmoja

Watu walio na silaha za kuchinjia lazima wamfuate mara moja yule aliye na kidau cha wino wa mwandishi. Mungu lazima awatenganishe watu Wake iwapo kuwatia muhuri kutakuwa na thamani yoyote na isipokuwa utengo ufanyike, kumiminwa kwa Roho Mtakatifu hakuwezi kushuka kwa ukamilifu juu ya watu wa Mungu. “Naliuliza maana ya upepeto nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi wa kweli kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu usiopinda. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu… Naliuliza kilichokuwa kimefanya badiliko hili kubwa. Malaika akajibu, ‘Ni mvua ya masika, burudiko kutoka kwa uwepo wa Bwana, kilio kikuu cha malaika wa tatu.” Maandishi ya Awali, ukurasa wa 270, 271. Ni

38

wazi kwamba upepeto lazima utukie kabla ya “Kilio Kikuu.” Watu walio na silaha za kuchinjia walikuwa tayari wanachinja kabla ya yule mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi kurudi kuripoti jambo kwamba alikuwa amefanya kama alivyoamriwa. Tazama Ezekieli 9:8, 11. {SR1: 37.2}

Tofauti Kati Ya Watu 144,000 Na Watakatifu Wengine

Akimaanisha Israeli (baada ya mwili) ambayo ni mfano wa Israeli wa kweli; yaani, watu 144,000, Mungu alisema, “Israeli ni mzaliwa Wangu wa kwanza.” Ukuhani katika Israeli ya zamani ulitakiwa kuundwa na mzaliwa wa kwanza wa kila familia, kwa hivyo ukuhani huitwa mzaliwa wa kwanza. Iwapo Israeli wangemtii Mungu katika maagizo Yake yote, mpango huu ungetekelezwa, lakini walipofika Mlima Sinai walitengeneza ndama wa dhahabu na kumwabudu. {SR1: 38.1}

Musa aliposhuka kutoka mlimani, alichukua rekodi ya wote ambao walikuwa wameabudu ndama. “Akiwa amesimama katika lango la marago, Musa aliwaita watu, ‘Ni nani aliye upande wa Bwana? Na aje kwangu.’ Wale ambao hawakujiunga na uasi walipaswa kuchukua msimamo wao upande wa kulia wa Musa; wale ambao walikuwa na hatia lakini walitubu, upande wa kushoto. Amri hiyo ilifuatwa. Ilibainika kwamba kabila la Lawi halikuwa limeshiriki katika ibada hiyo ya sanamu” Wazee na Manabii, ukurasa wa 324. Kwa sababu hii Mungu aliliheshimu kabila la Lawi. Tunasoma kwa ukurasa wa 277: “Baada ya kuanzishwa kwa utumishi wa hema, Bwana alijichachagulia kabila la Lawi kwa kazi ya patakatifu, badala ya mzaliwa wa kwanza wa watu.” {SR1: 38.2}

Lakini Mungu alisema, “Israeli ni mzaliwa Wangu wa kwanza”, — Israeli wa kweli — watu 144,000. Ahadi hiyo, basi, itaweza kutimizwa hapa. Juu yao tunasoma “kuwa alimbuko kwa Mungu na Mwana-Kondoo.” Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, basi watu 144,000 watakuwa makuhani na Walawi. Isaya 61, haingeweza kulirejelea kundi lingine isipokuwa Israeli wa ahadi watu 144,000, na kwa watu wa Mataifa ambao watakaokuja kwa Bwana kupitia kwa kazi zao. Tunasoma katika Isa. 66:19, 20, “Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa… Nao watawaleta ndugu zenu kutoka mataifa yote kuwa sadaka kwa Bwana.” Hawa (144,000) ambao wataokoka maangamizo

39

ya Ezekieli 9, na Isaya 63, ambayo Isa. 66:16, 17, hutaja, watatumwa kwa kazi kubwa ya umishonari katika wakati wa kilio kikuu. {SR1: 38.3}

Tunasoma katika Isa. 61:5, 6, “Na wageni [Mataifa, au wale ambao sio wa watu 144,000] watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila watakuwa wakulima wenu na watunzaji wa mizabibu yenu. Bali ninyi mtaitwa Makuhani wa Bwana: watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu: Mtakula utajiri wa Mataifa, na kwa utukufu wao mtajisifu.” Wengine kuliko wao wenyewe (144,000) watalisha mifugo yao na kuitunza mizabibu yao (kuwafanyia ukulima) kwa namna ile ile kama ilivyokuwa kwa kabila la Lawi, kwa sababu hawakuwa na ardhi. Ingawa Walawi hawakuwa na urithi wa ardhi, walipokea karibu asili mia 25 ya ongezeko katika zaka na sadaka, kwa hivyo wengine badala yao wenyewe walifanya kazi yao. Ndivyo ilivyo na watu 144,000, ambao watakuwa makuhani katika nchi mpya. Wazo hapa sio kwamba zaka na sadaka kutoka kwa watu zitakuwa udhamini wao katika nchi mpya. Maandiko haya yametolewa tu kuonyesha nafasi ambayo wanamiliki. {SR1: 39.1}

Isa. 61:7 inasema: “Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wao watafurahi katika sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu: Furaha yao itakuwa ya milele.” Yakiwa na viwakilishi-nafsi viwili, “yenu” na “wao,” kiwakilishi-nafsi “yenu” hupokea maradufu kwa aibu yao, lakini kiwakilishi-nafsi “wao” wataimiliki nchi. “Yenu” ni kiwakilishi-nafsi cha mtu wa pili ambaye Mungu anazungumza naye, na katika hali hii kinahusu Israeli (ambao ni watu 144,000), lakini kiwakilishi-nafsi “wao” hurejelea watu wa Mataifa ambao hawakuhesabiwa kati ya makabila kumi na mbili na kwa hivyo hawajajumuishwa katika watu 144,000, lakini wameokolewa kwa maana “wao” watafurahi katika sehemu yao. {SR1: 39.2}

Katika Gombo la 5, ukurasa wa 475-6, ukinena kuhusu watu 144,000, tunasoma: “Watakuwa wafalme na makuhani kwa Mungu… ‘Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako’.” Kwa hivyo, watu 144,000 ni makuhani, na Kristo Kuhani Mkuu, (na Mfalme). Inaweza kusemwa kwamba wakati muda wa rehema unapofunga Kristo anayavua mavazi Yake ya kikuhani, na sio Kuhani tena, lakini hakuna haja ya kuwa na mkanganyiko katika hili, kwa maana tunasoma katika Isa. 66:22, 23: “Kama vile mbingu mpya na

40

nchi mpya, Nitakazofanya, zitakavyokaa mbele Yangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele Yangu asema Bwana.” Kwa hivyo tunaona kwamba utakuwapo mfumo wa ibada katika mbingu na nchi mpya ambao utahitaji Makuhani na Walawi. {SR1: 39.3}

41

SEHEMU YA 2

MAKUNDI MANNE YA WALIOKOMBOLEWA

Uchambuzi unaofuata umetolewa ili kuthibitisha kwamba umati mkubwa wa Ufu. 7:9, ni watakatifu walio hai, ambao, pamoja na watu 144,000, watahamishwa bila kuonja mauti kwa ujio wa pili wa Kristo. Wote waliookolewa katika historia ya ulimwengu, kutoka kwa Abeli mwenye haki hadi kwa kufungwa kwa muda wa rehema, wamegawanywa katika makundi manne makuu, tofauti, na mbali mbali, kama ifuatavyo: {SR1: 41.1}

Kundi la 1: Watu 144,000 wa Ufu. 7; yaani, makabila kumi na mbili ya Israeli wa ahadi; kundi maalum na uzoefu maalum. {SR1: 41.2}

Kundi la 2: Waliohamishwa bila kuonja mauti wakati wa kuja kwa Kristo katika mawingu (umati mkubwa wa Ufu. 7:9). {SR1: 41.3}

Kundi la 3: Mamilioni wa vizazi vyote ambao waliuawa kwa ajili ya imani yao. {SR1: 41.4}

Kundi la 4: “Wale ambao hapo awali walikuwa wenye bidii kwa kazi ya Shetani, lakini walinyakuliwa, kama kinga kutoka motoni, wamemfuata Mwokozi wao kwa ibada ya ndani, na kujitolea sana.” Pambano Kuu, ukurasa wa 665. {SR1: 41.5}

Mataifa na serikali za dunia hujitukuza kwa mpangilio wa kifahari wa majeshi yao, na sare zao hutengenezwa kulingana na vyeo, ili kwamba kwa sare, mtu atambue cheo cha askari, na ni wa kitengo au kikosi kipi. Hatupaswi kudhani kwamba Mungu mkuu ana utaratibu mdogo kwa watu Wake waliokombolewa kuliko mataifa ya dunia kwa majeshi yao. Tunajua Mungu ana utaratibu bora zaidi kuliko ule serikali yoyote ya dunia inaweza kubuni. Juhudi itafanywa kuthibitisha kwamba kila mojawapo wa makundi manne yaliyotajwa hapo juu yana sare zao ambazo kwazo yanaweza kutambuliwa na kupangwa. {SR1: 41.6}

Kundi la 1

Katika Maandishi ya Awali, ukurasa wa 16, 17, tunasoma: “Hapa juu ya bahari ya kioo watu 144,000 walisimama katika mraba kamili. Baadhi yao walikuwa na taji za kung’aa sana, wengine zisizo za kung’aa sana. Taji zingine zilionekana kuwa nzito kwa nyota, ilhali zingine zilikuwa na chache tu. Wote waliridhika kabisa na taji zao. Na wote walikuwa wamevikwa joho jeupe

42

la utukufu kutoka mabegani hadi miguuni mwao.” Watu 144,000 wanasifiwa kuwa na “joho jeupe la utukufu” kama sehemu ya mavazi yao. {SR1: 41.7}

Kundi la 2

Kundi la 2, ni wale waliohamishwa bila kuonja mauti (mbali na watu 144,000). Ufu. 7:9, husema, “Baada ya hayo [watu 144,000] nikaona, na tazama, umati mkubwa sana, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Itaonekana kwamba kundi hili wana mitende mikononi mwao. {SR1: 42.1}

Kundi la 3

Maandishi ya Awali, ukurasa wa 18, 19: “Tulipokuwa tukisafiri, tulikutana na wenzi ambao pia walikuwa wakitazama utukufu wa mahali hapo. Naliona rangi nyekundu kama upindo kwa mavazi yao; taji zao zilikuwa angavu; mavazi yao yalikuwa masafi meupe. Tulipowasalimu, nalimuuliza Yesu walikuwa kina nani. Alisema walikuwa ni wafia-imani waliouawa kwa ajili Yake. Pamoja nao walikuwapo jamii isiyohesabika ya watoto wadogo; wao pia walikuwa na upindo wa rangi nyekundu kwa mavazi yao. “ Kwa hivyo kundi la 3, (wafia-imani) wanasifiwa kuwa na rangi “nyekundu kwa mavazi yao.” {SR1: 42.2}

Kundi la 4

Wadhambi wakubwa walinyakuliwa kama kinga kutoka motoni, lakini walikufa kifo cha kawaida. {SR1: 42.3}

Hawa hawana joho mabegani mwao, mitende mikononi mwao, wala rangi nyekundu kama upindo kuzunguka mavazi yao, lakini wanazo taji za dhahabu. Taji zao hutofautiana na taji za watu 144,000, wa mwisho wakiwa na “nyota” katika taji zao, kama ilivyoelezwa chini ya kichwa “Kundi la 1.” Kwa hivyo tunayo maelezo ya makundi haya manne, na nembo za mavazi yao, na yanaweza kufupishwa kama ifuatavyo: {SR1: 42.4}

Kundi la 1 — Watu 144,000 wana joho jeupe la utukufu, na nyota katika taji zao. {SR1: 42.5}

43

Kundi la 2 — Umati mkubwa wa Ufu. 7: 9, wanayo mitende mikononi mwao. {SR1: 43.1}

Kundi la 3 — Mamilioni ya vizazi vyote ambao waliuawa kwa ajili ya imani, wana rangi nyekundu kuzunguka upindo wa mavazi yao. {SR1: 43.2}

Kundi la 4 — Wadhambi wakuu walionyakuliwa kama kinga kutoka motoni, lakini walikufa kifo cha kawaida, wenye mavazi meupe, na taji za dhahabu, lakini hawana nyota kwa taji zao. Sawa na wale wa Ufu. 4:4. {SR1: 43.3}

Lazima iwepo sababu dhahiri ya kuelezea sare maalum ambayo imekuwa lazima kwa kusudi la kuufunua ukweli huu. {SR1: 43.4}

Mifano Na Uakisi

Roho ya Unabii husema Eliya huwakilisha wale watakaokuwa hai wakati Kristo atakapokuja, na kubadilishwa kwa kufumba na kufumbua jicho, na kuhamishwa bila kuonja mauti. Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa wa 421: “Eliya, ambaye alikuwa amehamishwa bila kuonja mauti hadi mbinguni, aliwakilisha wale watakaokuwa hai duniani wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili, na ambao watabadilishwa kwa nukta moja, katika kufumba na kufumbua jicho, kwa tarumbeta ya mwisho.” {SR1: 43.5}

Mtajo umefanywa kwa Henoko katika Wazee na Manabii, ukurasa wa 88, 89: “Tabia ya kiungu ya nabii huyu huwakilisha hali ya utakatifu ambayo inapaswa kuafikiwa na wale ambao watakuwa ‘waliokombolewa kutoka duniani’ wakati wa ujio wa pili wa Kristo… Lakini kama Henoko, watu wa Mungu watatafuta usafi wa moyo, na kufuata mapenzi Yake, mpaka watakapoakisi chapa ya Kristo. Kama Henoko watauonya ulimwengu kuhusu ujio wa pili wa Bwana, na kuhusu hukumu ambazo zitajiliwa juu ya uasi, na kwa mazungumzo yao matakatifu na mfano wao watazihukumu dhambi za wasiomcha Mungu. Jinsi Henoko alivyohamishiwa bila kuonja mauti hadi mbinguni kabla ya uharibifu wa ulimwengu kwa maji vivyo hivyo wenye haki walio hai watahamishwa bila kuonja mauti kutoka duniani kabla ya uharibifu wake kwa moto.” {SR1: 43.6}

Ingawa Eliya huwakilisha wale ambao watahamishwa bila kuonja mauti katika ujio wa pili wa Kristo, Henoko, pia, huwawakilisha. Watu hao wote walihamishwa bila kuonja mauti. Swali ni, Mbona mifano miwili? Kwa sababu yapo makundi mawili ya watu watakaohamishwa bila kuonja mauti; watu 144,000,

44

na umati mkubwa wa Ufu. 7:9. Watu 144,000, ni Waisraeli; umati mkubwa sio. Henoko si Mwisraeli, kwa hivyo hawezi kuwakilisha Israeli, watu 144,000. (Jina “Israeli” halikuwepo hadi kwa wakati wa Yakobo, ambao ulikuwa karne nyingi baada ya Henoko kuhamishwa. Ufafanuzi wazi zaidi kwa hiyo mada utapeanwa katika sehemu nyingine). Tutabainisha ni kundi gani Henoko huwakilisha kwa sare anayojivika. Maandishi ya Awali, ukurasa wa 40, husema: “Huko nalimwona Henoko mzee mwema, ambaye alikuwa amehamishwa bila kuonja mauti. Katika mkono wake wa kulia alikuwa na mtende wenye utukufu, na kwa kila jani liliandikwa ‘Ushindi.’” Hapa tunamwona Henoko, pia, ana “mtende” mkononi mwake, sawa na umati mkubwa, kundi namba 2. {SR1: 43.7}

Henoko husemekana kuwa ni wa saba kutoka kwa Adamu. “Saba” humaanisha kukamilika, kumaliza; na hivyo kuwa mfano mkamilifu wa kundi lililowakilishwa naye katika Ufu. 7:9 (umati mkubwa). Tutajitahidi kuleta uthibitisho mwingine kwamba umati mkubwa wenye “mitende mikononi mwao” umehamishwa bila kuonja mauti pamoja na watu 144,000. Katika Pambano Kuu, ukurasa wa 665 tunasoma kuhusu kundi la 2, 3, na la 4. Sehemu inayorejelea kundi la 4, husomeka kama ifuatavyo: “Karibu na kiti cha enzi ni wale ambao hapo awali walikuwa wenye bidii kwa kazi ya Shetani, lakini walinyakuliwa, kama kinga kutoka motoni, wamemfuata Mwokozi wao kwa ibada ya ndani, na kujitolea sana. Kisha ni wale waliokamilika kwa tabia ya Kikristo katikati ya uongo na ukafiri, wale ambao waliiheshimu sheria ya Mungu wakati ulimwengu wa ukristo uliitangaza kuwa ni bure.” Hapa imetiwa ndani kila dhambi inayowezekana kwa mdhambi katika vizazi vyote (ambao wamechukua msimamo kwa upande wa Mungu). {SR1: 44.1}

Lakini kwa kundi la 2 (umati mkubwa), hakuna dondoo iliyotolewa kuhusu wao ni aina gani ya watenda dhambi. Kundi la 1 (watu 144,000), wanaitwa Israeli, kundi spesheli lililo na uzoefu maalum. {SR1: 44.2}

Baada ya kujuulisha kila dhambi inayowezekana kwa mdhambi katika Kundi la 4 (wale ambao watafufuliwa), na wafia-imani katika kundi la 3, Uvuvio husema, “Na nyuma ya hao ni ‘umati mkubwa’… wamevaa mavazi meupe, na mitende mikononi mwao.” Kwa hivyo, kundi hili halingeweza kuorodheshwa na yale mengine mawili, au na watu 144,000. Iwapo Kundi la 2 (umati mkubwa), wangekuwa waliookolewa na kufufuliwa kutoka katika vizazi vyote, basi wote waliookolewa lazima wawe na mitende mikononi mwao, lakini kwa vile ni wazi

45

sio wote wana mitende, basi hawa sio wote waliookolewa katika vizazi vyote, bali ni waliohamishwa bila kuonja mauti tu, mbali na watu 144,000. Mtende ni nembo ya ushindi kwa kifo na kaburi; yaani, kamwe hawakufa. {SR1: 44.3}

Tena, kuzungumzia kundi lilo hilo, tunasoma katika Ufu. 7:14, sehemu ya mwisho: “Akaniambia, Hao ndio waliotoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” Kwa hivyo kundi hili lilipitia dhiki ya Danieli 12, ambayo iko katika wakati wa mapigo saba ya mwisho. Ufu. 7:16, sehemu ya mwisho: “wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.” Wanapitia katika pigo la nne, kwa hivyo ni wazi kwamba kundi hili linaishi katika wakati wa mwisho, katika ujio wa pili wa Kristo, — watahamishwa bila kuonja mauti. {SR1: 45.1}

Ufafanuzi Wa Maandishi Ya Awali, Ukurasa Wa 15

Akizungumzia tangazo lililotolewa kuhusu kuja kwa Kristo (siku na saa), ambayo ni kabla ya ufufuo wa jumla, na kwa wakati wa ufufuo maalum, tunasoma: “Punde tulisikia sauti ya Mungu kama maji mengi, ambayo ilitangaza siku na saa ya kuja kwa Yesu. Watakatifu walio hai, 144,000 kwa idadi, walijua na kuelewa hiyo sauti, ilhali waovu walifikiri ni ngurumo ya radi na mtetemeko wa nchi. Wakati Mungu alipoitangaza hiyo saa, Alimimina juu yetu Roho Mtakatifu, na nyuso zetu zilianza kuangaza na kung’aa kwa utukufu wa Mungu, kama Musa aliposhuka kutoka juu ya Mlima Sinai. Watu 144,000 wote walikuwa wametiwa muhuri na kuwa kwa umoja mkamilifu. Kwa vipaji vya nyuso zao viliandikwa, Mungu, Yerusalemu Mpya, na Nyota ya utukufu yenye jina jipya la Yesu. Kwa hali yetu ya furaha, takatifu waovu walikasirishwa, na wangekimbia kwa nguvu kutushika na kututupa gerezani, wakati tungenyosha mkono kwa jina la Bwana, nao wangeanguka chini wakiwa wadhaifu.” {SR1: 45.2}

Hatupaswi kuelewa kwamba wote waliokuwepo wakati huo na kusikia tangazo lililofanywa kuhusu “siku na saa” walikuwa watu 144,000 pekee. Lugha iliyotumika hudhihirisha wazi kwamba walikuwapo zaidi, kwa maana viwakilishi-jina “yetu”, “zetu”, “zao”, na “yetu” hutumika. Katika kuwaonyesha watu 144,000, kifungu dhahiri “zao” kimetumika. Yeye

46

hajiweki kama mmoja wa watu 144,000, lakini, badala yake, kiwakilishi-jina “yetu” kimetumika; kwa hivyo, lazima liwepo kundi lingine la walio hai mbali na watu 144,000. {SR1: 45.3}

Eliya Huwakilisha Watu 144,000

Iwapo Henoko huwakilisha umati mkubwa wa Ufu. 7:9, basi Eliya huwakilisha watu 144,000, kwa maana ni wawili tu katika historia ya ulimwengu waliohamishwa bila kuonja mauti. Uthibitisho zaidi si lazima; hata hivyo, sababu zingine zitatolewa mbona Eliya aliwakilisha watu 144,000. Eliya aliona ukame na njaa katika Israeli; ndivyo itakavyokuwa kwa watu 144,000, kwa maana tunasoma katika Pambano Kuu, ukurasa wa 649: “Wameiona nchi ikiharibiwa kwa njaa na tauni, jua likiwa na nguvu ya kuwaunguza watu kwa joto kali.” Eliya alikuwa na joho juu ya mabega yake (2 Wafalme 2:8) vivyo hivyo watu 144,000 wana joho. “Na wote walikuwa wamevikwa joho jeupe la utukufu kutoka mabegani hadi miguuni mwao.” Maandishi ya Awali, ukurasa wa 17. {SR1: 46.1}

Kunukuu kutoka katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 475: “Unabii lazima utimizwe. Bwana anasema: ‘Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni mwenye bidii sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.” Dada White hamaanishi kusema kwamba yeye ndiye yule nabii Eliya, lakini husema waziwazi kwamba nabii lazima aje, na husemekana kuwa ni nabii aliye na ile ile “roho na nguvu ya Eliya.” Nabii huyu lazima aje kabla ya Ezekieli 9 kutimizwa, kwa maana unabii wa Ezekieli ni sawa na uzoefu wa Eliya na Israeli katika siku za Ahabu. Kazi ya Eliya katika siku za Ahabu, mfalme wa Israeli, ilikuwa kuwathibitishia Waisraeli kwamba walikuwa wameasi imani, na baada ya kufanya hivyo, aliwashika makuhani, au manabii, na kukata vichwa vyao, na kuvitupa katika kijito. Hiyo ndiyo ilikuwa roho na nguvu ya Eliya. {SR1: 46.2}

Tunasoma katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 445: “Huku kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu [watu 144,000: Ufu. 7] ni sawa na kule ilioonyeshwa Ezekieli katika maono.” Basi kuiwa muhuri kwa watu

47

144,000 ni sawa na Ezekieli 9, na kule kutia alama kwa mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi ni muhuri. Mara tu kutiwa muhuri kunapomalizika, “watu watano walio na silaha za kuchinjia wanafuata baada yake na kuwaua wazee na vijana, wasichana na watoto wadogo, na wanawake. Wakaanzia kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” {SR1: 46.3}

Ni kwa wakati huu watu 144,000 wamewekwa alama, au kutiwa muhuri. Ezekieli 9 inafaa uzoefu wa Eliya kwa sababu hii: Nabii, au ujumbe huitwa, Eliya, “kwa roho na nguvu ya Eliya.” Nabii Eliya alifikiri Israeli wote walikuwa wameasi imani, na ya kwamba yeye pekee ndiye aliyekuwa amesalia, lakini Bwana alisema alikuwa na watu 7,000 ambao hawakuwa wamemsujudia Baali. “Saba” huashiria namba kamili au kamilifu, ambayo husimama kama nembo, katika tukio hili ikimaanisha idadi kamili ya maelfu. Idadi kamili ya wateule ni 144,000. Kwa hivyo sisi pia, kama Eliya, hufikiri kanisa lote limeelea kuingia duniani (limemsujudia Baali). Hivyo Eliya husimama kama mfano wa watakatifu 144,000 walio hai, waliohamishwa bila kuonja mauti. {SR1: 47.1}

Musa — Mfano Wa Ufufuo Wa Wenye Haki

“Musa kwa mlima wa baraka alikuwa shahidi wa ushindi wa Kristo juu ya dhambi na mauti. Aliwakilisha wale watakaotoka kaburini wakati wa ufufuo wa wenye haki.” Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa wa 421. Musa huwakilisha ufufuo wa kwanza, au wa jumla wa Ufu. 20:6. {SR1: 47.2}

Mfano Wa Ufufuo Maalum

Iwapo Musa huwakilisha ufufuo wa jumla, ni nani, basi, ambaye angewakilisha ule wa mseto, ufufuo maalum wa Dan. 12:2? Tuna ule wa Mat. 27:52, 53. “Na makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala, nao wakiisha kutoka makaburini mwao baada ya kufufuka Kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.” Watakatifu walioshiriki katika ufufuo huu walikusanywa kutoka katika vizazi vyote. Baadhi ambao, labda, walikuwa wameishi wakati ule ule Kristo alikuwa akihubiri, na walikuwa wamefahamiana Naye na

48

kazi Yake, walikuwa mashahidi wa ufufuo Wake. Soma Maandishi ya Awali, ukurasa wa 184; Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa 786. {SR1: 47.3}

Bado ipo sababu nyingine kwa nini Mat. 27:52, ni mfano wa ufufuo huu mseto. Wale ambao walifufuliwa pamoja na Kristo walishuhudia uungu wa Kristo kwa wale waliomsulubisha. Akinena juu ya ufufuo huu mseto, Danieli asema: “Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine aibu na kudharauliwa milele.” Wakati huo watakuwapo wenye haki watakaojumuishwa ambao waliishi na kushuhudia kusulubishwa; pia wale waliomsulubisha, na waliomchoma, kwa maana, (Ufu. 1:7) “Tazama, Yuaja na mawingu: na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma.” Kwa hivyo, ufufuo ambao ulishuhudia uweza wa Mungu kwa hawa wauaji wa Mwanawe, ulikuwa mfano wa wenye haki ambao watafufuliwa katika ufufuo mseto (maalum). {SR1: 48.1}

Mfano Wa Ufufuo Wa Pili

Waovu watakaokuja katika ufufuo mseto wa Dan. 12:2, na ambao ni lazima wafe mauti ya pili wakati wa kuja kwa Kristo, ni mfano wa wale watakaofufuka mwishoni mwa millenia, unaoitwa ufufuo wa waovu. Soma Pambano Kuu, ukurasa wa 661, 662; Maandishi ya Awali, ukurasa wa 52, 53. {SR1: 48.2}

Mfano Wa Mauti Ya Pili

Limekuwa swali linalotatanisha iwapo waovu wanaotokea katika ufufuo maalum wa Dan. 12:2, wataendelea kuishi, au kufa na waovu walio hai wakati wa ujio wa pili wa Kristo, na kufufuliwa mwishoni mwa miaka 1,000. Kwa sababu Mungu haachi lolote pasipo kufanywa, Yeye ametabiri kila jambo katika unabii, na katika mifano pia. Iwapo tuna mfano wa kila kila tukio lingine, lazima tuwe na mfano wa hili. Waovu wanaofufuliwa, lazima wafe pamoja na waovu wengine wakati wa kuja kwa Kristo katika mawingu ili kuwa mfano wa mauti ya pili mwishoni mwa millenia. {SR1: 48.3}

Sasa swali ni, Je! Watafufuka tena katika ufufuo wa pili pamoja na waovu? Kujibu swali hili, Maandishi

49

ya Awali, ukurasa wa 292 husema: “Kwa ufufuo wa kwanza wote watokea katika uzuri wa kutokufa; lakini kwa wa pili alama za laana zinaonekana kwa wote. Wafalme na wakuu wa dunia watu wa hali ya chini, wasomi na wasio na elimu, watokea pamoja. Wote wanamwona Mwana wa Adamu; na wale watu waliomdharau na kumdhihaki, walioiweka taji ya miiba kwa nyusi Zake takatifu, na kumpiga kwa mwanzi, wanamtazama Yeye katika utukufu Wake wa kifalme. Wale waliomtemea mate katika saa ya kuhukumiwa Kwake sasa wanageuka kutoka kwa Mkazo unaopenyeza wa macho Yake na kutoka kwa utukufu wa uso Wake. Wale waliochoma mkuki ubavuni Mwake wanatazama alama za ukatili wao kwa mwili Wake.” Kwa hili tunaelewa kwamba watu wale wale wako tena katika ufufuo wa pili. Kwa hivyo walifufuliwa mara ya pili mwishoni mwa miaka 1,000, wafe katika mauti ya pili, ambayo wao wenyewe walikuwa mfano wake, (kwa kufa mauti ya pili pamoja na waovu walio hai wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili mawinguni). Kwa hivyo tuna unabii na mfano kwa kila tukio ambalo limetukia, au litakalotukia katika ulimwengu huu wetu mwovu. {SR1: 48.4}

Wazo La Ukamilifu:

1. Ufufuo wa Musa.

2. Ufufuo wakati Yesu alipofufuka.

3. Ufufuo maalum wa Danieli 12:2.

4. Ufufuo wa kwanza wa Ufu. 20:6.

5. Kuhamishwa bila kuonja mauti kwa Henoko.

6. Kuhamishwa bila kuonja mauti kwa Eliya.

7. Kuhamishwa bila kuonja mauti kwa jumla wakati wa kuja kwa Kristo. {SR1: 49.1}

Hivyo, tunayo tena namba “saba”, ishara ya ukamilifu, wote, au kwisha. Ufufuo mara nne na kuhamishwa bila kuonja mauti mara tatu hujumuisha watakatifu wote waliofufuliwa na kuhamishwa bila kuonja mauti, ambayo yote hufanya jumla ya saba, au mwisho. {SR1: 49.2}

Gwaride Ya Waliokombolewa

Itakuwa gwaride ya ajabu ilioje wakati waliokombolewa wa

50

vizazi vyote wakienda taratibu wakipitia barabara za dhahabu katika maeneo ya mbinguni kati ya walio safi na wenye heri. {SR1: 49.3}

1. Kuusindikiza msafara mkubwa tunaona mamilioni ya malaika waliowahudumia waliokombolewa katika vizazi vyote. {SR1: 50.1}

2. Musa, mfano wa waliofufuliwa, na mtu wa kwanza kuandika katika Biblia, tunamwona akitembea aste aste mbele kama kiongozi wa wale waliofufuliwa, amevikwa vazi jeupe na taji ya dhahabu inayong’aa kichwani mwake. Wale waliofufuliwa anaowaakilisha ni Kundi la 4, wamevikwa mavazi meupe na wanazo taji za dhahabu. {SR1: 50.2}

3. Kisha tunamwona Abeli mwema, asiye na hatia, akiwakilisha walioifia imani na vazi jeupe tukufu na rangi nyekundu kwenye vazi lake kama upindo, akiwaongoza mamilioni ya walioifia imani wa vizazi vyote (Kundi la 3), ambao mavazi yao ni kama yale ambayo yamevaliwa na kiongozi wao, Abeli. {SR1: 50.3}

4. Sasa tunamwona Henoko mzee mwema, akiwa na shada nyeupe inayong’aa kuzunguka kichwa chake: Juu yake taji nzuri inayong’aa kuliko jua na katika mkono wake wa kulia mtende wa utukufu. Ni kupitia kwake umati mkubwa uliohamishwa bila kuonja mauti unaongozwa na kuwakilishwa, wote wakiwa wamevaa mavazi meupe masafi, mitende mikononi mwao, na taji za dhahabu vichwani mwao. {SR1: 50.4}

5. Mwisho wa wote waliokombolewa, Eliya jasiri, mwenye joho jeupe la utukufu kutoka mabegani mwake hadi kwa nyayo: Mfano na kiongozi wa kundi la ajabu zaidi, ijapokuwa ni dogo kwa idadi. Likiwa kundi maalum, na uzoefu maalum wa ukuhani wa kifalme, watu 144,000, katika joho la utukufu, safi na jeupe kutoka mabegani mwao hadi kwa nyayo zao, na nyota kwenye taji zao. Ufu. 14:5, “Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo; kwa maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.” {SR1: 50.5}

6. Iwapo wana wa Mungu (kina Adamu) kutoka katika dunia zingine walijiwasilisha wenyewe mbele ya Bwana kwa mujibu wa Ayubu 1:6, katika mkutano wa baraza, basi hakika wana wa Mungu (kina Adamu) kutoka katika dunia zingine zote hawatatengwa kwa gwaride ya ajabu, na ya pekee katika upeo wa Umilele usio na mwisho. {SR1: 50.6}

7. Mwisho wa yote, Yesu wenye utukufu, umati wa mbinguni wa elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu elfu ya malaika. Hilo litakuwa kusanyiko la ajabu ilioje! Je! Tunaweza kupata jambo lolote lenye uwiano zaidi kuliko hili katika Biblia yote? Itaonekana

51

tena tunayo namba kamili ya Kibiblia “saba,” na haiwezi kufanywa izidi au ipungue, na bado ijumuishe wote. Je! Hili halipasi kuamsha upendo na bidii yetu wakati tunapoliona tukio la utukufu lililohifadhiwa kwa ajili ya watu waaminifu wa Mungu? {SR1: 50.7}

Elezo La Kidau Cha Wino Wa Mwandishi Cha Maandishi ya Awali, Ukurasa 279

Mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi wa Ezekieli 9, ndiye anayetekeleza kuwatia muhuri watu 144,000 muda mrefu kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema. Wengine wanaweza kuelewa vibaya taarifa iliyofanywa katika Maandishi ya Awali, na hivyo kuchanganyikiwa. Kwa manufaa ya mtu kama huyo tunafanya ufafanuzi huu. Tukinukuu taarifa hiyo inayopatikana katika Maandishi ya Awali, ukurasa wa 279, tunasoma: “Naliwaona malaika wakikimbia huko na huko mbinguni. Malaika aliye na kidau cha wino wa mwandishi kiunoni akarudi kutoka duniani, na kuripoti kwa Yesu kwamba kazi yake ilikuwa imefanywa, watakatifu walikuwa wamehesabiwa na kutiwa muhuri. Ndipo nikamwona Yesu, ambaye alikuwa akihudumu mbele ya sanduku lililokuwa na amri kumi, akakitupa chini chetezo. Akainua mikono Yake, na kwa sauti kuu akasema, ‘IMEKWISHA.’” {SR1: 51.1}

Bila shaka ni wazi kwamba alikuwa malaika mwenye kidau cha wino wa mwandishi, na ya kwamba kazi yake ilikuwa imefanywa; pia ya kwamba kazi ya Yesu ilikuwa imekwisha katika Patakatifu pa mbinguni (muda wa rehema ulifungwa). Kwa sababu malaika huyu anacho kidau cha wino wa mwandishi kiunoni mwake sawa na yule mtu katika Ezekieli 9, ni uthibitisho kwamba ni malaika yule yule, kwa maana inaweza kudhaniwa kwamba wapo malaika zaidi ya mmoja walio na chombo kama hicho. Hata hivyo, anaweza kuwa malaika yule yule wa kutia muhuri katika matukio yote mawili, lakini wazo ni kwamba, wakati yule mtu wa Ezekieli 9, anapowatia muhuri watu 144,000, kazi yake inaendelea katika wakati wote wa mavuno. {SR1: 51.2}

Watakatifu lazima wahesabiwe na kutiwa muhuri katika kizazi hiki sawa na wale waliotiwa muhuri katika vizazi vilivyopita. Ni dhahiri kazi yake imekuwa ikiendelea tangu dhambi ilipoingia katika familia ya wanadamu, labda kuanzia kwa Abeli, na itaendelea hadi mwisho wa muda wa rehema, wakati ambapo kazi yake itakuwa imefanyika. {SR1: 51.3}

52

SEHEMU YA 3

ESAU NA YAKOBO

“Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa: Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Watoto wakapambana tumboni mwake; naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. Bwana akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako; kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili; na mkubwa atamtumikia mdogo. Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama, mapacha walikuwamo tumboni mwake. Wa kwanza akatoka naye alikuwa mwekundu, mwili wote kama vazi la nywele; wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino; Akaitwa jina lake Yakobo.” Mwa. 25:21-26. {SR1: 52.1}

Uvuvio husema kwamba Rebeka hakuwa na watoto na Isaka alimwomba Bwana na Bwana akamsikia na Bwana akampa mapacha. Iwapo hivi ndivvo ilivyo hakika haikuwa bahati mbaya. Bwana alikuwa ndani yake. Lakini ikiwa aliomba mtoto tu, mbona Yeye alimpa mapacha? Hatudhani kwamba Bwana alimpa mapacha ili kusababisha taabu nyingi katika familia kama ilivyofanya. Mbona walishindana ndani ya mama? Kwa nini moja mwekundu na nywele kote mwilini, na yule mwingine mweupe na laini? Na mbona mmoja ashike kisigino cha mwenzake? Maswali haya yote huja akilini mwetu. Kwa sababu iwayo yote, ilikuwa imebuniwa na Mungu, kwa sababu Yeye alimpa watoto. Hakika hakuna mtu angefikiri Mungu alifanya hivi bila kusudi kwa mtazamo. Mungu mwenyewe alimwambia yule mama kwamba ni funzo la maana, kwa sababu alimwambia “Kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili.” Ni kweli kwamba tokeo lilikuwa mataifa mawili kwenye jukwaa la utendaji; Edomu na Israeli, lakini funzo liko wapi? {SR1: 52.2}

Funzo liwaalo lote, lazima liwe kwa watu wa Mungu. Haliwezi kuwa la wakati wa Agano la Kale, kwa maana hawakuwahi kunufaika nalo kwa njia yoyote.

53

Tunasoma katika Gal. 4:22-25, kwamba Isaka alikuwa mfano wa kanisa la Agano Jipya, na Ishmaeli wa la Kale. “Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Abrahamu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili; bali yule wa mwungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano: kwa maana hawa ndio maagano mawili; moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Uarabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa, kwa kuwa u utumwani pamoja na watoto wake.” {SR1: 52.3}

Paulo anaandika hapa kwamba Ishmaeli huwakilisha Israeli wa kimwili. Hajiri huwakilisha kanisa ambalo lilipangiliwa hapo Mlima Sinai wakati Musa alipowachagua wazee sabini. Tazama Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 382. Sanhedrini iliundwa na watu sabini, kwa hivyo, namba “70” huwakilisha shirika la kanisa. Kwa hivyo Paulo husema, “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai [mwanamke — nembo ya kanisa] ulioko Uarabuni.” Shirika lilo hilo, baada ya kutangatanga kwa miaka arobaini jangwani, lilivuka Yordani na kujisimamisha huko Yerusalemu. “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Uarabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa, kwa kuwa u utumwani pamoja na watoto wake.” Hajiri, wakati huo, alikuwa nembo ya kanisa kabla ya msalaba; Yerusalemu, wa zamani. {SR1: 53.1}

Tena tunasoma tukianzia aya ya 26: “Bali Yerusalemu wa juu [Yerusalemu mpya ulioko mbinguni sasa. Ufu. 21] ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi sote. Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa usiyezaa [Sara]; paza sauti ulie, wewe usiye na utungu: Maana wtoto wake aliyeachwa pekee ni wengi [aliyeachwa — kwa maana Sara alisogea kando na kumpa Hajiri mumewe] kuliko wa huyo aliye na mume [Hajiri]. Basi, ndugu zangu kama Isaka, sisi tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile aliyezaliwa kwa mwili [Ishmaeli] alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho [Isaka], ndivyo ilivyo sasa.” Gal. 4:26-29. (Kwa maana Israeli wa zamani katika siku za mitume waliwatesa Wakristo.) Hapa Uvuvio husema Sara huwakilisha Yerusalemu ulio juu, mbinguni sasa (Ufu. 21), na ndiye mama wetu sisi sote. Paulo, kwa kuliandikia kanisa la Agano Jipya

54

(Mataifa) husema, “Basi, ndugu zangu kama Isaka, sisi tu watoto wa ahadi.” Paulo humaanisha kwamba Isaka huwakilisha watoto wa Agano Jipya, na Sara ni nembo ya kanisa. {SR1: 53.2}

Tukirejea kwa mada yetu, “Esau na Yakobo,” liwalo lote funzo la hawa mapacha, haliwezi kutumika kwa kanisa la Agano la Kale, kwa sababu ikiwa Isaka ndiye baba yao, na huliwakilisha kanisa la Agano Jipya, basi funzo lazima linahusu kanisa linalowakilishwa naye. Iwapo baba alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walizaliwa, funzo haliwezi kuwa kwa sehemu ya kwanza ya hilo kanisa. Nembo hiyo lazima iwe ya kipindi cha mwisho. {SR1: 54.1}

Nembo Ya Kushindana

Watoto walishindana kabla ya kuzaliwa. Katika hili, pia, lazima liwepo funzo. Limekusudiwa kuonyesha wazi wakati ambapo matumizi yanafanywa. Limefafanuliwa na umri wa baba kwamba funzo ni la kipindi kingine. Pambano la hao watoto lilikuwa kabla yao kuzaliwa; funzo, basi, ni kwa watu wa Mungu kabla tu wao kuokolewa. {SR1: 54.2}

Wakati Na Kanisa

Funzo haliwezi kuwa katika makanisa mawili. Mbona? Kwa sababu wamezaliwa kutoka kwa mama mmoja. Lazima waje chini ya ujumbe uleule mmoja. Kwa nini? Kwa sababu ni wazawa wa baba yule yule. Iwapo hiki ni kizazi kitakachoshuhudia mwisho, na kanisa ambalo litaokolewa na kuhamishwa bila kuonja mauti, basi lazima huu uwe ni wakati ambao funzo hili linauhusu. Sasa swali ni, je! katika kanisa gani litapata utimizo wake? Linaweza tu kutimizwa katika kanisa la kweli la Mungu. Ikiwa makanisa ya Kiprotestanti yameanguka na kuitwa Babeli, basi hayana sehemu wala fungu katika fungu hili. Iwapo kanisa la Waadventista wa Sabato ni Israeli wa kweli, na lina ujumbe ambao hakuna shirika lingine hufundisha; na ikiwa ujumbe tunaoutangaza ni, ujio wa Kristo na mwisho wa dunia katika kizazi hiki, basi hili ndilo lile kanisa. {SR1: 54.3}

55

Makundi Mawili Ya Watu

Biblia husema hao pacha huwakilisha tabaka mbili za watu. Iwapo hili ni kweli, basi yapo makundi mawili ya watu ndani ya kanisa. Kundi moja linawakilishwa na Esau, na lile lingine na Yakobo. Tukirejelea Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 46, tunasoma: “Kuna mivuto miwili hasimu inayoendelea kuvutana juu ya washiriki wa kanisa. Mvuto mmoja unafanya kazi kwa ajili ya utakaso wa kanisa, na mwingine kwa ajili ya kuwapotosha watu wa Mungu.” Mmoja wa hao pacha alikuwa mwekundu na mwenye nywele mwili wote, na yule mwingine alikuwa laini na mweupe. Watu wote wawili ni wadhambi. Kwa nini? Kwa sababu Esau alikuwa mwekundu, ambayo ni rangi nyekundu sana, nembo ya dhambi. Yakobo alikuwa mweupe, lakini jina humsaliti, kwa maana jina “Yakobo” humaanisha “mdanganyifu.” {SR1: 55.1}

Nembo Ya Haki Ya Kuzaliwa

Esau ndiye aliyezaliwa kwanza. Chochote kilichopaswa kurithiwa na haki ya mzaliwa wa kwanza kilikuwa cha Esau. Sheria ya Biblia ni kwamba mzaliwa wa kwanza alikuwa na haki ya ukuhani. Kwa sababu hii, Yakobo alitamani haki ya mzaliwa wa kwanza ya Esau. Esau, basi, huwakilisha tabaka la ukuhani. {SR1: 55.2}

Nembo Ya Nywele

Jinsi alivyozaliwa mwenye nywele mwili wote, mwili wake lazima ulifunikwa na kanzu nzito ya nywele, kwa maana wakati Yakobo alitaka kumdanganya baba yake ili kupata hiyo baraka, Rebeka mama yake, alifunikwa shingo na mikono yake kwa ngozi za wana-kondoo. Tuhuma ya Isaka iwapo ni Esau au Yakobo aliyenena, ilimlazimisha kuukagua mwili wa mwanawe. Mwa. 27:22, 23, “Basi Yakobo akamkaribia Isaka babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau. Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa na nywele, kama mikono ya nduguye Esau: basi akambariki.” Kanzu nzito ya nywele juu ya mwili wa Esau haikuwa ya asili, na sababu pekee kwa nini Mungu alikuwa amemuumba hivyo ilikuwa kuwakilisha tabia ya tabaka analowakilisha. {SR1: 55.3}

56

Nywele hizo zilikuwa ishara ya mamlaka, heshima, utukufu, na talanta (zawadi ambazo Mungu hutoa), kumwezesha kutekeleza majukumu ya ofisi yake kama kuhani wa familia. Sababu zifuatazo zimetolewa kwa kuamini hivyo: Mungu, hapo mwanzo alimuumba mwanamume na mwanamke. Alimfanya mwanamme huyo awe mfalme na mtawala juu ya uumbaji Wake wote, na Akamvika taji ya heshima, utukufu, na mamlaka — talanta muhimu kwa utendaji wa ofisi yake. Kwa huyo mwanamme alimpa ndevu, na sio kwa mwanamke. Nywele za Samsoni zilikuwa nembo ya uwezo wake. Katika 1 Kor. 11:15, tunasoma: “Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake.” {SR1: 56.1}

Nembo Ya Kisigino Cha Esau

Wakati wa kuzaliwa kwa hao pacha, Esau alitokea kwanza, na Yakobo alikishika kisigino cha Esau, kwa hivyo mdogo aliongozwa na mkubwa. Hilo halingeweza “kutokea” tu, kwa maana unaonekana kuwa ni muujiza. Huu ndio wakati pekee ambao umakini wetu unaitwa kwa tukio la aina hii, kwa hivyo, lazima Mungu alikuwa amekusudia hivyo, na iwapo Yeye alikusudia, lazima liwepo funzo ndani yake. Haitakuwa vigumu kwa mtu kuona funzo lililofundishwa hapa kwa huo muujiza. Yakobo aliongozwa kutoka na kisigino cha Esau, kwa hivyo, Esau lazima awakilishe tabaka la viongozi. {SR1: 56.2}

Nembo Ya Kuwa Mwekundu

Esau alizaliwa mwekundu, lakini Yakobo alikuwa mweupe na laini. Kama sheria, mapacha huzaliwa wakifanana, lakini katika kisa hiki ilikuwa kinyume. Hakuna kufanana kati ya Esau na Yakobo kama ndugu mapacha, katika tabia, mwonekano, rangi, au sitara. Kwa hivyo, tuna muujiza mwingine. Nembo hii ni rahisi kuielewa. Nyekundu ni sawa na nyekundu sana. Biblia hutumia nyekundu sana kama nembo ya dhambi, ilivyo katika Isa. 1:18; Ufu. 17:3; Ufu. 12:3. Esau huwakilisha tabaka la watu wadhambi, na vile vile Yakobo. Lakini tabaka ambalo Esau huwakilisha wamepewa haki na fursa kubwa za kutenda mema. {SR1: 56.3}

Nembo Ya Tabia Ya Esau

Tabia ya uanaume wa Esau hufunua tabia ya

57

ukuhani ambao yeye huwakilisha. Esau alikuwa mwindaji hodari, mtu wa porini. Maslahi yake yote yalikuwa katika mchezo na tumbo lake, lakini hakuvutiwa na nafasi yake kama kuhani wa familia. Tabaka linalowakilishwa naye huvutiwa zaidi na anasa, kupata faida, na mambo ya dunia kuliko walivyo katika haki walizopewa na Mungu. Esau alishindwa kudhibiti hamu yake ya kula. Alifikiria zaidi tumbo lake kuliko alivyofikiria nafasi yake (ofisi ya ukuhani). Yeye huwakilisha tabaka la watu ambao mungu wao ni tumbo lao. Wangependelea kukidhi uchu wao wa kula kuliko kutekeleza wajibu wao na kushika ukweli wa Mungu. {SR1: 56.4}

Baraka Ya Esau

Esau alikuwa na baraka ya thamani karibu naye: Urithi wa uzima wa milele. Ilikuwa haki yake kuzaa (kurithi) wana 12 (makabila) ya Israeli. Kutokea kwa Esau wangekuja manabii, wafalme, na wakuu. Kupitia kwa mbari ya Esau Mfalme wa wafalme, Kristo mbarikiwa angekujia. Baraka hizi zote za ajabu zilingalikuwa zake. {SR1: 57.1}

Wapo wengi ambao ni kama Esau. Yeye huwakilisha tabaka ambalo lina baraka maalum karibu nao. Baraka hiyo ni nini? Ni urithi — makabila 12 ya Israeli wa kweli, 144,000, ambao watakuwa kama makuhani na wafalme. Soma Gombo la 5, ukurasa wa 475, 476. Daraja hili lina haki ya kuleta ujio wa pili wa Kristo, na kuliongoza kanisa lipite mipaka ya Kanaani ya mbinguni, na katika utukufu wa Mungu. Jinsi ambavyo mbari ya Esau ilikuwa na fursa ya kuleta ujio wa kwanza wa Kristo, na kwa sababu Esau alishindwa kwa upande wake, hivyo, tabaka hili linalowakilishwa na Esau liko katika hatari ya kushindwa kwa upande wao. Fikiri kuhusu kukosa urithi wa milele, maisha ambayo ni ya kudumu kama maisha ya Mungu, Muumba wa dunia zote; furaha isiyo na kipimo, na uzito wa milele wa utukufu. {SR1: 57.2}

Lakini Esau alitamani mlo kipenzi na kujinyima haki yake ya mzaliwa wa kwanza ili kutosheleza uchu wa kula na akapokea tu chakula kidogo, — bakuli lake la mchuzi mwekundu. Yeye huwakilisha tabaka hili ambalo limepewa nuru kubwa na haki ya kutenda wema, lakini hushindwa kufanya hivyo. Daraja hili litajinyima uzito wa utukufu wa milele ambao hakuna midomo ya mwanadamu inaweza kusimulia. Esau alijidanganya kwamba angeweza kuiuza haki yake ya kuzaliwa apendavyo, na

58

ainunue tena apendavyo, lakini alipotaka kuinunua tena, hata kwa dhabihu kubwa sana kwa upande wake, hakuweza kufanya hivyo. Alitubu kwa uangalifu na kwa machozi, lakini yote yalikuwa bure. Wazo la kutisha kama nini kujinyima ukweli ili kupata faida ya ulimwengu na hasara ya uzima wa milele. Soma Gombo la 2, ukurasa wa 38, 39. Nukuu ifuatayo imetolewa katika Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 182: “Jinsi Esau alipozinduka kuona upumbavu wake wa kubadilisha bila kufikiri alipokuwa amechelewa sana kurudisha alichokuwa amepoteza, ndivyo itakavyokuwa siku ya Mungu kwa wale ambao wameuza urithi wao wa kwenda mbinguni kwa ajili ya kutosheleza tamaa.” {SR1: 57.3}

Kwa sababu ya kutojali kwake baraka na matakwa ya matakatifu, Esau huitwa katika Maandiko, “mtu najisi.” Yeye huwakilisha wale ambao huchukulia kirahisi ukombozi ulionunuliwa kwa ajili yao na Kristo, na wako tayari kujinyima urithi wao kwenda mbinguni kwa mambo yanayoharibika ya dunia. Umati wa watu unaishi kwa ajili ya sasa bila kufikiri au kujali siku zijazo. Kama Esau, wao hupiga kelele, “Tule na tunywe, kwa maana kesho tutakufa.” Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 181. {SR1: 58.1}

Nembo Ya Mchuzi Wa Dengu

Yakobo alikuwa mtu wa uwandani aliishi katika mahema, ilhali Esau aliwinda nyikani. “Yakobo akapika mchuzi,” uliotayarishwa kwa kutumia kusemethi, tena mwekundu. Hatujui aina ya kikolezi cha rangi ambacho Yakobo alitumia kupata rangi ya kuvuta macho ya mlo huo wa kuwaziwa; ni dhahiri yeye pekee ndiye aliyeijua siri hiyo. {SR1: 58.2}

“Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake ‘Edomu.’ Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya mzaliwa wa kwanza? Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza; naye akamwapia: Akamuuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau chakula na mchuzi wa dengu; naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake; hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.” Mwa. 25:29-34. {SR1: 58.3}

Esau alikuja kutoka nyikani siku hiyo bila windo lolote. Alipoingia ndani ya nyumba, alimwona Yakobo akipamba chakula hicho cha kupendeza.

59

Mara Esau akapaza sauti akasema: “Tafadhali unipe hicho chakula chekundu nile; kwa kuwa ninazimia mimi.” Esau hakuzimia kwa sababu ya njaa kali, bali, alipoona aina mpya ya chakula, hakuweza kuudhibiti uchu wake wa hamu ya kula. Jibu la Yakobo lilikuwa, “Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza,” ikiwa lazima upate chembe ya chakula hiki. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa: itanifaa nini haki hii ya mzaliwa wa kwanza? Esau hakuwa kwa hatua ya kufa kwa sababu ya njaa au ugonjwa wa mwili, kwa maana mtu mgonjwa hawezi kula kama alivyofanya. Wala haikuwa kwa sababu ya ukosefu wa chakula, kwa sababu alikuwa katika nyumba ya baba yake, na Isaka alikuwa mkwasi. Ilikuwa kwa sababu ya tamaa yake ya huo mlo wa kusemethi, kwa maana “Kwa sababu ya kutojali kwake baraka na matakwa ya matakatifu, Esau huitwa katika Maandiko, ‘mtu najisi.’ Yeye huwakilisha wale ambao huchukulia kirahisi ukombozi ulionunuliwa kwa ajili yao na Kristo, na wako tayari kujinyima urithi wao kwenda mbinguni kwa mambo yanayoharibika ya dunia. Umati wa watu unaishi kwa ajili ya sasa bila kufikiri au kujali siku zijazo. Kama Esau, wao hupiga kelele, ‘Tule na tunywe, kwa maana kesho tutakufa.’” — Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 181. {SR1: 58.4}

“Jinsi Esau alivyoamka kuona upumbavu wa ubadilishaji wake bila kufikiri wakati alipokuwa amechelewa sana kufidia hasara yake, ndivyo itakavyokuwa katika siku ya Mungu kwa wale ambao wameuza urithi wao wa mbinguni kwa kuziridhisha tamaa zao za ubinafsi.” Kimenukuliwa, ukurasa wa 182. Lazima tufanye uchaguzi wetu wakati tunapewa uhuru wa kuchagua aidha mchuzi wa kusemethi au haki ya kuzaliwa. {SR1: 59.1}

Edomu — Mfano

Ubadilishaji huo ulifanywa. “Naye akaiuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo.” Wakati huo jina lake likabadilishwa, kwa hivyo, jina lake akaitwa “Edomu.” Kwa hivyo, “Esau aliidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.” Jina “Edomu” humaanisha “nyekundu” au nyekundu sana, nembo ya dhambi. Esau alizaliwa akiwa mwekundu lakini hakuitwa jina hilo (Edomu) mwanzoni. Tabaka ambalo Esau huwakilisha liko katika hatari ya kupoteza kwa sababu ya uchu wa kuridhisha tamaa za ubinafsi (kupuuza matengenezo ya kiafya), kwa hivyo wanaitwa “Edomu.”

60

Hili ndilo daraja ambalo nabii Isaya amelitaja katika Isa. 63:1. {SR1: 59.2}

Badiliko La Majina

Wote Esau na Yakobo huwakilisha tabaka mbili za wadhambi: Esau, kwa rangi ya ngozi yake, na Yakobo, kwa jina lake. Majina ya wote wawili yalibadilishwa: Yakobo, kwa sababu alitamani kitu cha thamani; Esau, kwa sababu ya tamaa. Jina la Yakobo lilimaanisha “mdanganyifu”; jina “Esau” (kwa Kiebrania: Nywele nyingi, ambalo kwa mfano “angeheshimiwa,” kama ilivyoelezwa hapo awali) humaanisha “anayemaliza.” Kumbuka maana ya kushangaza ya hilo jina, ikimaanisha tabaka lililopewa fursa ya kumaliza kazi. Katika Ufu. 3:14-16, tunasoma: “Na kwa malaika wa kanisa la Laodekia andika; …. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu.” Gombo la 5, ukurasa wa 82: “Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, angaliwaheshimu kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi. Lakini walijitenga kutoka kwa Mungu wakajitiisha kwa mvuto wa dunia, na Bwana akawakataa.” {SR1: 60.1}

Kupoteza Na Kufaidika

Yakobo, pacha mdogo, au yule aliyekuja mwisho, kwa kukishikilia kisigino cha Esau, huwakilisha tabaka ambalo lilikuja katika ujumbe wa malaika wa tatu kupitia kwa uongozi wa daraja lililowakilishwa na Esau. Yakobo alikuwa na tumaini la dhati na juhudi kubwa kwa nafasi ambayo kaka yake alishikilia. Ingawa alikuwa maskini wa sifa ambazo Esau alikuwa nazo za kutekeleza majukumu ya ofisi hii, ambayo alitamani na kununua, lakini, kwa bidii yake kubwa na azimio, alifanya vyema. Bei aliyolipa ilikuwa chakula — hakikufaa kitu; lakini kile alichopokea kilikuwa cha thamani kubwa. Bila kujali ni kiasi gani cha mafunzo au talanta ambayo mtu anayo katika kazi fulani, kamwe hawezi kufanikiwa isipokuwa anayo bidii kubwa na kupendezwa katika safu hiyo. {SR1: 60.2}

61

Esau alikuwa na makubwa ya kupoteza, lakini hasara yake ilikuwa faida ya Yakobo. Kile ambacho Yakobo alitoa kama malipo ya mali ya Esau kilikuwa cha thamani ndogo, kwa hivyo, kile ambacho Esau alipata kilikuwa kidogo kuliko kitu chochote. Haukupita muda mrefu baada ya Yakobo kuhifadhi baraka kutoka kwa baba yake, Isaka, ya kwamba Esau, akiwa amejawa na majuto, alitishia maisha ya Yakobo. Makundi yote mawili yanayowakilishwa na Esau na Yakobo yanaweza kuwa na shida: Moja, kwa sababu ya utambuzi wa hasara yao; lile lingine, kwa sababu ya chuki iliyodhihirishwa dhidi yao. {SR1: 61.1}

Ndoto Ya Yakobo

Yakobo, kwa ushauri wa wazazi wake, aliondoka nyumbani na kwenda Padan-Aramu, na akiwa safarini, usiku wa kwanza kabisa, Mungu alimtokea katika ndoto, “Na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi na ncha yake yafika mbinguni: tena tazama malaika wa Mungu wanapanda na kushuka juu yake.” Mwa. 28:12. Ngazi hiyo humwakilisha Kristo; Mungu, Baba alisimama juu yake; Yakobo chini yake. (Mwa. 28:13). Ndoto hii ilimpa Yakobo ujasiri mkubwa, naye akaweka nadhiri kwa Mungu. {SR1: 61.2}

Yakobo alikuwa sasa awe baba ya Israeli (makabila 12) ambaye kupitia kwake mataifa mengi yatabarikiwa; mfano wa Israeli kwa ahadi, makabila 12, watu 144,000. Ndoto ambayo aliota usiku ilikuwa tu maono na uwakilishi wa tukio fulani la baadaye. Maana ya hiyo ndoto inaweza kuwa jambo moja tu. Iwapo ngazi humwakilisha Kristo, malaika kama wajumbe, Mungu Baba kwenye ncha, na Yakobo chini yake, humaanisha muunganisho kamili kwa mbingu na Israeli wa kweli, — mvua ya masika, kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Tazama Ufu. 18:1. {SR1: 61.3}

Kina Mama Za Israeli

Lakini kumbuka kwamba Yakobo alikwenda Padan-Aramu, kwa nyumba ya Bethweli, baba ya mama yake, huko alioa Lea na Raheli, binti za Labani. Zilpa na Bilha, wajakazi wa Lea na Raheli, pia wakawa wake zake. Hawa ni kina mama ambao makabila kumi na mawili yalitokea, lakini wao ni kina mama tu katika mfano wa makabila ya kweli — watu 144,000. Lea alikuwa mke halali pekee kwa Yakobo; Raheli

62

alikuwa dada yake. Zilpa na Bilha walikuwa wajakazi. {SR1: 61.4}

Acha Lea awakilishe kanisa la kweli la Kristo (Waadventista wa Sabato); Raheli, kanisa dada, lakini sio la kweli (Waprotestanti); Zilpa na Bilha, ulimwengu (wa kidini na wasio na dini). Hawa ni kina mama wa watu 144,000, na namna wao (144,000) wamekusanywa. Lakini wakati makabila kumi na mawili yalitoka kwa kina mama wengi, walizaliwa kwa baba mmoja. Ndivyo ilivyo na wa kweli — watu 144,000. Wakati wamekusanywa kutoka kwa makanisa yote na ulimwengu, lazima waletwe katika kanisa moja, katika kipindi kile kile cha historia ya kanisa, na ujumbe ule ule (ujumbe wa malaika wa tatu). {SR1: 62.1}

Yakobo Kurudi Nyumbani: Wakati Wa Taabu

Mwishoni mwa miaka ishirini Yakobo alikuwa akirudi nyumbani kwa nchi ya ahadi na nyumba ya baba yake akiwa na mali nyingi. Wakati alipofika nyumbani kwa baba yake alikuwa na wanawe kumi na wawili (wakuu wa makabila kumi na mawili). Kabla Yakobo hajaingia nyumbani mwa baba yake alipitia pambano la kutisha na akashindana na malaika mpaka alfajiri. Mwanzo 32:24-29. {SR1: 62.2}

Kushindana kwa Yakobo na malaika huashiria wakati wa “taabu ya Yakobo” (kwa kanisa). Tunasoma katika Maandishi ya Awali, ukurasa wa 36, 37: “Amri ilitangazwa kuwaua watakatifu, iliyowasababisha kulia mchana na usiku kwa ajili ya ukombozi. Huu ulikuwa ni wakati wa taabu ya Yakobo.” Tazama pia Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 202-203. {SR1: 62.3}

Mfano Wa Nchi Ya Ahadi — Israeli Katika Nyumba Ya Baba

Iwapo nchi ya ahadi Kanaani ni mfano wa Kanaani ya mbinguni ya ahadi, basi nyumba ya baba ya Yakobo ni mfano wa nyumba ya Baba yetu. Vivyo hivyo, wakati Israeli (wa kweli) wataingia katika nyumba ya Baba yetu ndani ya Kanaani ya mbinguni itakuwa na makabila kumi na mawili, watu 144,000. Swali linazuka, Je! Hao ndio wote watakaookolewa katika ujumbe wa malaika wa tatu? Kumbuka kwamba Yakobo alipoingia nyumbani mwa baba yake na wanawe kumi na wawili alikuwa na watumwa wengi, wa kiume na wa kike, ambao walizidi kabila zake (wana) mara nyingi. Ndivyo ilivyo kwa Israeli (wa kweli), ambao pamoja nao utakuwa “umati mkubwa

63

ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu.” Ufu. 7:9. (Umati huo mkubwa ulikuja kwa juhudi za yale makabila baada ya kutimizwa kwa Ezekieli 9). {SR1: 62.4}

Uchambuzi huu hauwezi kufaa kisa kingine wala kanisa lingine lolote katika historia yote ya dunia. Waadventista wa Sabato ndio watu na kanisa la pekee ambalo limewahi kuitwa Israeli, walio na ukweli wa matengenezo ya afya, na ya kwamba wanaweza kuwa katika hatari ya kuuza haki yao ya kuzaliwa kwa bakuli la mchuzi wa kusemethi. Kwa ukweli huu pekee, ilhali zipo zingine nyingi, tunaweza kujua kwamba kanisa la Waadventista wa Sabato ni kanisa la Mungu. {SR1: 63.1}

64

SEHEMU YA 4

ISRAELI NI NANI KWA ILE AHADI?

“Uzoefu huu wa Waisraeli [walipoondoka Misri] uliandikwa kwa ajili ya mafundisho ya wale ambao wataishi katika siku za mwisho. Kabla ya pigo lifurikalo kuja juu ya wakazi wa dunia, Bwana anawaita wote ambao ni Waisraeli kweli kweli wajiandae kwa tukio hilo.” Gombo la 6, ukurasa wa 195. Makabila kumi na mbili ya Israeli wa kimwili ni mfano tu wa Israeli wa ahadi (watu 144,000). Jinsi walivyokuwapo watu wa mataifa kati ya Israeli (wa mfano), watakuwapo watu wa mataifa katika Israeli wa kweli. {SR1: 64.1}

Sehemu ya mwanzo ya kanisa la Kikristo (wakati wa mitume) haingeweza kuitwa Israeli, kwa maana historia ya kanisa wakati huo ilifananishwa na Isaka, kwa mujibu wa Gal. 4:22-31, na jinsi ilivyofafanuliwa kwa ukurasa wa 53, 54. Isaka hakuitwa Israeli, kwa maana alikuwa baba ya Yakobo, na Yakobo ndiye aliyeitwa Israeli, kwa hivyo, Israeli, iwayo sehemu yoyote ya kanisa ni lazima ije wakati fulani wa baadaye katika historia ya kanisa. Yakobo alikuwa baba ya kabila kumi na mbili za Israeli, na ikiwa Israeli wa kimwili ni mfano wa Israeli wa ahadi (wa kweli), basi hebu tujifunze mwanzo wa Israeli wa kimwili, iwapo tutatambua, au kujua Israeli wa ahadi, — watu 144,000. {SR1: 64.2}

Safari ya Israeli kuingia Misri haikuwa bila kusudi. Sababu iwayo yote kwayo, Mungu alikuwa ndani yake. Yusufu aliwaambia ndugu zake (Mwa. 45:5): “Basi sasa msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku: maana Mungu alinituma mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.” Yusufu anatangaza kwamba Mungu ndiye aliyesababisha yeye kwenda Misri. Mungu alikuwa pia amemwambia Abrahamu kwamba yeye, na uzao wake wangekaa na kuteswa katika nchi ya kigeni miaka 430. Lakini kwa nini Mungu aliwatuma kwenda Misri? Mbona Yusufu aliuzwa akiwa na umri wa miaka 17, kijana mdogo tu, mikononi mwa Waishmaeli wakatili, na kupelekwa nchi ya kigeni kuuzwa tena kama mtumwa? Sisi bila shaka hatutafanya

65

makosa kwa kufikiri kwamba Yusufu alizimia moyoni akiwa safarini. Hakika lazima ilikuwapo sababu ya kutendewa vibaya hivyo. {SR1: 64.3}

Huko Misri, Yusufu aliuzwa kutumika kama mtumwa, na baadaye akatupwa gerezani kwa miaka kadhaa. Kwa nini Mungu aliongoza Israeli katika nchi ile ya kigeni ambapo ibada ya sanamu ilitawala kila mahali? Hakika Mungu alijua kwamba katika nchi hiyo wangekuwa watumwa baada ya muda mfupi tu. Mbona mbingu iliruhusu watu wa Mungu wateule kuwa watumwa wa taifa ambalo sanamu zao zilikuwa miungu yao? Kwa nini Mungu aliruhusu mijeledi ya mabwana-kazi wa Misri kucharazwa migongoni mwa watu Wake? Mbona upendo wa Mungu uliruhusu watoto wa Abrahamu (rafiki wa Mungu) wakiwa bado wachanga, kuzamishwa ndani ya mto Nile? Ni nani anayeweza kusema Mungu wetu mkuu alikuwa hajui mambo haya yote yaliyotokea, au ya kwamba Yeye alifanya makosa? Jibu pekee linaloweza kutolewa ni kwamba yote yalibuniwa na mbingu. Lakini hayo yote yalikuwa ya nini? Mungu lazima alikuwa na sababu maalum na kusudi mahsusi liwe funzo la mfano ili lifundishwe kwa wakati fulani. Mtu anaweza kusema, Mungu alifanya hayo yote kuonyesha uwezo Wake, lakini, je! Mungu mwenye hekima na mkuu, aliyajaa upendo na rehema, awaangamize watoto Wake ili kuonyesha uwezo Wake? Hata baba wa duniani, mfaji, binadamu hawezi kuthubutu kuwaangamiza watoto wake ili kuonyesha uwezo wake. Nani atathubutu kusema wanadamu wana upendo mkuu au hukumu bora kuliko Mungu mkuu, ambaye rehema Zake haziwezi kupimiwa, ambaye upendo Wake hujaza dunia zote, ambaye hekima Yake haiwezi kuchunguzwa, ambaye hukumu Yake ni haki? {SR1: 65.1}

Sio tu wateule Wake waliteseka kwa utumwa na ukatili, lakini Wamisri pia. Mwanzoni mwa vuguvugu la Kutoka, Waisraeli walipoondoka, mapigo yalikuja juu ya Misri yote, na taifa hilo karibu liangamizwe. Usiku wa Pasaka, palikuwa na kifo katika kila nyumba ambayo haikuwa na damu mwimo wa mlango, na ndani ya kila zizi la wanyama. {SR1: 65.2}

“Na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.” Kut. 11:5. {SR1: 65.3}

66

Israeli wakasafiri hadi kwa Bahari ya Shamu, na Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari, na maji yakagawanyika. Israeli waliingia baharini, na wakatembea wakavuka juu ya ardhi kavu. Wamisri wakawafuata mpaka katikati ya bahari, na Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari, maji yakarudi, na kuyafunika magari, na wapanda farasi, na jeshi lote la Farao lililokuja baharini nyuma yao; “hakusalia hata mmoja wao.” {SR1: 66.1}

Israeli wakaja nyikani ambako walitangatanga kwa miaka 40. Maelfu yao waliangamia kwa sababu ya kutokuamini. Mwishoni mwa safari ya nyikani, watu walivuka Yordani. Wakati Israeli walipokuwa mbali na Kanaani, nchi hiyo ilikaliwa kwa wingi na mataifa ya kipagani. Israeli walilazimika kuwaangamiza kwa upanga ili waimiliki hiyo nchi. Fikiri juu ya kupoteza uhai, huzuni, na mateso: Yote kwa sababu Mungu aliwapeleka Israeli Misri, na kuwarejesha tena. Mungu hakika hangewaangamiza raia Wake: “ili kuonyesha uwezo Wake tu.” {SR1: 66.2}

Katika 1 Kor. 10:11, 12, akinena juu ya uzoefu wa wana wa Israeli, tunasoma: “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano: yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya dunia. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” Iwapo sisi ni watu ambao miisho ya dunia inakaribia kuja, basi mifano yao imeandikwa ili kutuonya sisi. Hii ndio sababu Mungu aliwaongoza wana wa Israeli kuingia Misri na kurejea tena. Fikiri ilivyo kubwa gharama ya kuifanyiza hiyo picha. Mafunzo yanayotokana na mifano hii mikuu ni makubwa zaidi kuliko jinsi ambavyo tumewahi kutambua. Wengi maelfu walipoteza maisha yao ili kuzalisha picha hiyo, kwa azma ya kwamba maelfu wengi zaidi waweze kuokolewa kuliko wale walioangamia. Hebu basi tuyachunguze kwa uangalifu mafunzo ambayo yalikusudiwa kwa masomo na maonyo yetu. {SR1: 66.3}

“Farao akaota ndoto: Na, tazama, alisimama kando ya mto. Na, tazama, ng’ombe saba wazuri wanono walipanda kutoka mtoni; wakajilisha manyasini. Na, tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya wamekonda;

67

wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto, Kisha hao ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri wanono. Basi Farao akaamka… Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko: Farao akawahadithia ndoto yake; wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo… Ndipo Farao akapeleka watu akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani… Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria: nami nimesikia habari zako, ya kwamba usikiapo ndoto waweza kuifasiri… Naye Farao” akamwambia Yusufu ile ndoto. “Yusufu akamwambia Farao… Mungu amemwonyesha Farao yale Yu karibu kufanya. Wale ng’ombe saba wema ni miaka saba;… Na wale ng’ombe saba dhaifu wabaya waliopanda baada yao ni miaka saba… Tazama, miaka saba ya shibe inakuja katika nchi yote ya Misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri… Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana… Ikawa katika miaka ile saba ya shibe nchi ikazaa kwa wingi. Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba, kilichokuwa katika nchi ya Misri, akaweka chakula katika miji: Chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake. Yusufu akakusanya nafaka kama mchanga wa bahari, nyingi mno, hata akaacha kuhesabu; maana ilikuwa haina hesabu.” Mwa. 41:1-49. {SR1: 66.4}

Tutajitahidi kuleta ushahidi wa kutosha katika uchambuzi huu ili kuonyesha kwamba uzoefu wa Israeli huko Misri ni picha ya Israeli wa kweli (watu 144,000) katika kanisa la Waadventista wa Sabato. “Wakati vuguvugu la kutoka lilikuwa vuguvugu kubwa, vuguvugu la ujio wa pili litakuwa kubwa zaidi. Mungu atawatoa watu, sio katika taifa moja tu, bali kutoka katika kila taifa chini ya mbingu, na Yeye atawaongoza waingie Kanaani ya mbinguni. Vuguvugu hili la ujio, ambalo vuguvugu la kutoka lilikuwa mfano, tunaamini lilitabiriwa katika unabii katika lugha ya mchocheo ifuatayo: ‘Na itakuwa katika

68

siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili ili kuwaokoa watu Wake, waliosalia. Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake;… kama vile ilivyokuwako kwa Israeli katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.’” Mapitio na Kutangaza, Oktoba 10, 1929, ukurasa wa 4, 5. “Vuguvugu la Kutoka kwa namna fulani ni mfano [picha] ya kufungwa kwa kazi ya Mungu chini ya Vuguvugu la Ujio.” “Kila vuguvugu huinuka kutimiza unabii wa wakati mwafaka.” Uhakika wa Vuguvugu la Ujio, na W.A. Spicer. Ukweli kwamba Israeli wa kimwili ni mfano (picha), uzoefu wao lazima urudufishwe na wa kweli, vinginevyo hapawezi kuwapo mfano. {SR1: 67.1}

Miaka Ya Wingi — Na Ya Njaa

Mungu aliruhusu wingi, na vile vile njaa. Kila mmoja hubeba namba “saba,” kumaanisha “kamilifu,” au “kamilika.” Sehemu hizi mbili za wakati zinaweza kumaanisha jambo moja ambalo sio lingine isipokuwa dunia hii katika historia, katika migawo miwili mikubwa; yaani K.K. na B.K., na msalaba kama mstari wa kugawanya. Miaka saba ya wingi huwakilisha kipindi cha Agano la Kale wakati ambao Mungu alitoa mengi, kwa maana kupitia kwa manabii Wake watakatifu Alihifadhi katika ghala kubwa, ambalo leo tunaita Biblia. Katika Mat. 11:13, tunasoma: “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.” Ni kwa sababu hii kwamba Yesu alitoa taarifa hiyo hapo juu, kwa sababu hatuna mwingine hadi sasa. {SR1: 68.1}

Katika miaka saba ya wingi (K.K.) Mungu alilihifadhi neno Lake katika Biblia kulisha ulimwengu (Misri) katika miaka saba ijayo ya njaa (B.K.). “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi Amesema nasi katika Mwana, Aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa Yeye aliufanya ulimwengu.” Ebr. 1:1, 2. Agano Jipya ni utimizo wa la kale. {SR1: 68.2}

Yusufu Mfano Wa Kristo

Yusufu alikuwa mfano wa Kristo. Tazama Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 239, 240. Mungu wetu katika wakati wa Agano la Kale (miaka saba ya wingi) alisema na watu Wake kwa njia nyingi na manabii Wake, na

69

akaamuru mambo haya yaandikwe, kwa azma ya kunena na watu Wake katika siku hizi za mwisho (wakati wa Agano Jipya, au miaka saba ya njaa) kwa kila mmoja wetu mmoja mmoja kwa sauti ya Neno Lake jinsi linavyopatika (lilivyohifadhiwa) katika Biblia. {SR1: 68.3}

“Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa: Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu, akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake; Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo, na watu wakapiga kelele mbele yake, pigeni magoti: hivyo akamweka mtawala juu ya nchi yote ya Misri. Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.” Mwa. 41:40-44. Hakuna upendeleo au heshima kubwa zaidi ambayo Farao angemwonyesha Yusufu; na Wamisri wote wakamsujudia. Tunapoendelea katika uchambuzi huu tutathibitisha bila shaka kwamba Yusufu ni mfano mkamilifu wa Kristo. {SR1: 69.1}

Farao, Mfano Wa —

Iwapo Yusufu alikuwa mfano wa Kristo, na Farao alimheshimu Yusufu kuliko mtu yeyote aliyewahi kuheshimiwa na mfalme yeyote, na Yusufu — na Farao wanafanya kazi bega kwa bega, basi Farao lazima asimamie kiwakilishi fulani, au mfano. Haitakuwa vigumu kutambua ni nini ambacho Farao huwakilisha. Kile ambacho kilimheshimu Kristo zaidi ya kila kitu ambacho chaweza kuheshimiwa duniani, ndicho Farao huwakilisha. {SR1: 69.2}

Kanisa la mitume lilimheshimu Kristo zaidi ya kila kitu kinachoweza kuheshimiwa, kiasi kwamba, wote waliyatoa maisha yao. Hakuna heshima kubwa zaidi ambayo Kristo amepokea duniani na sehemu nyingine yoyote katika historia ya kanisa Lake. Kwa hili tunaelewa kwamba Farao huwakilisha kanisa la mitume, au shirika. Matumizi yaliyofanywa hapa yatathibitisha kuwa ni sahihi tunapoendelea katika uchambuzi huu. (Maelezo zaidi juu ya mada hii yametolewa kwa ukurasa wa mwisho wa sehemu hii.) {SR1: 69.3}

70

Mwanzo Wa Njaa

Mstari wa kugawanya kati ya miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa ni msalaba. “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.” Mat. 11:13. Pale ambapo miaka saba ya wingi hukomea, miaka saba ya njaa huanzia. Mwaka wa kwanza wa njaa ni mwanzo wa kanisa la Kristo wakati wa mitume. Mtu anaweza kuhoji, Kwa nini njaa mwanzoni mwa kanisa la Kikristo? Je! Hawakupata nafaka ya kutosha (ukweli)? Naam, lakini waliipata kutoka kwa ghala kubwa (Biblia) kwa njia ile ile jinsi Wamisri walivyoipokea nafaka yao katika miaka ya njaa, — kutoka kwa ghala kubwa mkononi mwa Yusufu. Tazama ukurasa wa 15-18. {SR1: 70.1}

Wamisri, Mfano Wa Mataifa

Miaka saba ya njaa ilianza wakati Wamisri walipomjia Farao wapate chakula na Farao aliwaambia Wamisri wote, “Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni… na Yusufu akazifungua ghala zote, na kuwauzia Wamisri.” Mwa. 41:55, 56. “Yusufu akakusanya fedha zote zilizoonekana katika nchi ya Misri, na katika nchi ya Kanaani, kwa nafaka waliyoinunua: Yusufu akazileta zile fedha nyumbani mwa Farao. Fedha zote zilipokwisha katika nchi ya Misri, na katika nchi ya Kanaani, Wamisri wote walimjia Yusufu, wakisema, Tupe sisi chakula: kwa nini tufe mbele ya macho yako? Maana fedha zetu zimekwisha… Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu: Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng’ombe, na badala ya punda: naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule. Na mwaka ule ulipokwisha, wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu, ya kwamba fedha zetu zimekwisha; na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu; hakikusalia kitu mbele ya bwana wetu, ila miili yetu na ardhi zetu: Kwa nini tufe mbele ya macho yako, sisi na ardhi yetu? Utununue sisi na ardhi yetu kwa chakula, na sisi na ardhi yetu tutakuwa watumwa wa Farao:… Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote

71

ya Misri; maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake… Wakasema, Umetulinda hai: na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.” Mwa. 47:14-25. {SR1: 70.2}

Mwanzoni mwa njaa, Wamisri walikwenda kwa Farao ili wapate nafaka, badala ya kwenda kwa Yusufu. Walimfahamu sana Yusufu, kwa maana alikuwa liwali wa Misri kwa miaka minane au zaidi. Yusufu alizuru nchi yote ya Misri, na kila Mmisri alimsujudia. Wakati wa miaka ya wingi, alikuwa Yusufu ambaye alinunua mahindi kutoka kwa Wamisri, na inaonekana kushangaza kwamba walikwenda kwa Farao. Lazima ilikuwa ni kwa majaliwa ya Mungu ya kwamba walikwenda kwake. {SR1: 71.1}

Imefafanuliwa kwamba Farao aliwakilisha shirika la kanisa au uongozi. Wamisri hawawezi kuwakilisha kitu kingine chochote isipokuwa watu wa Mataifa katika siku za mitume. Mataifa walikuja kanisani (Farao) ambapo waliambiwa waende kwa Yusufu (Kristo). “Atakavyowaambia, fanyeni.” Yaani, kanisa katika utakatifu wake bila kitu kigeni kati yao, liliwaelekeza watu wa Mataifa kwa Kristo kama mpaji wao wa uhai, jinsi Farao alivyowaelekeza Wamisri kwa Yusufu. {SR1: 71.2}

Wamisri Walijiuza Wenyewe Kwa Farao

“Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri, maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa imewazidi sana: nchi ikawa mali yake Farao.” Mwanzo 47:20. Katika aya zilizotangulia za hiyo sura tulisoma Wamisri walitumia fedha zao zote kwa nafaka; na fedha zilipokwisha, walipeana wanyama kwa kubadilishana; na wanyama walipokwisha, wakatoa ardhi; na ile ardhi ilipokwisha kuuzwa, wakajiuza, wakawa watumwa wa Farao. Huu ndio mfano, lakini kwa utimilifu wa mfano huu, tunasoma katika maandiko yafuatayo: “Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: Wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi: na neema nyingi ikawa

72

juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji: kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume:… Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba,… Mlawi,… Alikuwa na shamba, akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.” Matendo 4:32-37. Hivyo Myahudi na mtu wa Mataifa waliuza nyumba na ardhi zote na kuleta thamani zake na kuziweka miguuni pa mitume, na kuwa watumishi wa kanisa (Farao). {SR1: 71.3}

Tena tunasoma Matendo 5:1-10, “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume. Lakini Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?… Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa.” Kwa hivyo yeyote ambaye alijifanya kuuza, na kuzuia sehemu ya thamani iliyopokelewa, katika siku za mitume, alikufa kama wale ambao hawakumuuzia Farao vyote huko Misri. Yesu alisema “Viuze ulivyonavyo vyote kisha Unifuate.” Kwa hivyo mfano ulikutana na uakisi. {SR1: 72.1}

Yusufu Awaondoa Watu Kotekote Misri

“Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri;… Na hao watu, akawahamisha akawaweka katika miji tangu upande huu wa mipaka ya Misri hata upande huu.” Mwa. 47, sehemu ya aya ya 20, 21. Huu ndio mfano, ufuatao ni utimizo wa mfano huo: Matendo 8:1, “Naye Sauli alikuwa akiidhinisha kifo chake [Stefano]. Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.” {SR1: 72.2}

Itaonekana kwamba mitume walikuwa nyumbani (Yerusalemu), na hakuna kumbukumbu ambapo mitume waliuza ardhi yao. Sasa tunanukuu mfano wa mitume: Mwanzo 47:22, “Ila ardhi za makuhani hakuzinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao:

73

Kwa hiyo hawakuuza ardhi zao.” Inashangaza kuona jinsi hili linavyolingana hata kwa mambo madogo zaidi. {SR1: 72.3}

Watu 70, Mfano Wa Shirika

Israeli walifika Misri katika mwaka wa pili wa njaa. Mwa. 45:10, 11, “Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng’ombe zako, na yote uliyo nayo: Nami nitakulisha huko; maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo.” Kuwasili kwa Israeli huko Misri huwakilisha nembo fulani ambayo ndani yake lazima iwe na funzo. Kumbuka kwamba funzo hili haliwezi kuwa kabla ya sehemu ya kwanza ya kanisa la Kikristo, kwa maana Israeli walikuja katika mwaka wa pili wa njaa. Funzo, basi, lililokusudiwa hapa, ni kwa kipindi cha mwisho katika historia ya kanisa. Ikiwa tungependa kujua ukweli wa tukio hilo, na funzo linalokusudiwa kupatikana kutoka kwalo, rejeleo lazima lifanywe hapa kwa idadi ya nafsi hai zilizoingia Misri. “Na wana wa Yusufu, waliozaliwa huko Misri, walikuwa wawili; watu wote wa nyumba ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini.” Mwa. 46:27. {SR1: 73.1}

Biblia husema watu wote walioingia Misri walikuwa sabini kwa idadi. Iwapo tunaweza kwa njia fulani kupata maana ya hiyo namba, basi tutalielewa funzo. Musa, pamoja na wana wa Israeli, walipofika Sinai, alilipanga kanisa huko, na kwa kulipanga, aliwateua wazee sabini. Shirika lilo hilo, miaka mingi baadaye, lilivuka Yordani na kuingia katika nchi ya ahadi. Huko walikuwa na Sanhedrini ambayo ilijumuisha watu sabini. Kwa hivyo, namba “sabini” ni nembo ya shirika la kanisa. Maana, basi, ni kwamba litakuwapo shirika la kanisa, wakati fulani katika historia ya B.K. Iwapo hii ni kweli, basi kanisa ambalo Kristo, na mitume walilipanga lazima lisambaratike, na kwa lazima lipangwe tena. Hii ni kweli, kwa sababu kanisa la Kikristo lilisambaratishwa katika vizazi vya giza katika wakati wa mwanzo wa utawala wa upapa. Wakati litakapopangwa tena, litatimiza kwa sehemu Yoeli 2:32, “Na katika

74

mabaki hao Bwana atakaowaita.” Siku au miaka, 2300, ya unabii wa Danieli katika sura ya nane hutupatia ukweli wote wa historia ya kanisa mpaka mwaka 1844, hadi wakati huo hapakuwa na mwito wa kupangwa upya. Iwapo ungekuwako, au ikiwa mwito huu wa kupangwa upya ungetimizwa kabla ya mwaka 1844, basi unabii wa Danieli ungekuwa umeutaja. Kwa sababu unabii huo u kimya, na hajakuwapo nabii wa Mungu aliyeinuka tangu kanisa lilipoanguka katika utawala wa upapa karibu mwaka 538 B.K. hadi mwaka 1844, basi ukweli wa nembo hiyo bado ulikuwa katika siku zijazo. {SR1: 73.2}

Wakati kipindi cha kinabii kilipomalizika mwaka 1844, mahali “Patakatifu Mno” katika Hekalu la mbinguni palifunguliwa, ambamo Kristo aliingia. Iwapo tukio hili lilitia alama mwanzo wa upatanisho, haungekuwapo wakati bora, au mwafaka zaidi kwa mwito kutoka mbinguni kuliko mwishoni mwa kipindi hicho kikubwa cha unabii; siku ya upatanisho ikiwa wakati muhimu zaidi kwa kanisa. Waadventista wa Sabato waliitwa kwa mkono wa nabii, na kivitendo ni watu pekee ambao huamini katika siku 2300. Sisi ni watu wa pekee ambao tumezitangaza tangu mwaka 1844, na sasa wako katika upatanisho, au wakati wa hukumu. Andiko la hilo limenukuliwa hapa: “Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja: msujudieni yeye aliyezifanya mbingu, na nchi, na bahari, na chemchemi za maji.” Ufu. 14:6, 7. Waadventista wa Sabato pekee wanaweza kutimiza mfano huo, maana kwa wakati huu waliitwa na nabii wa Mungu, kujipanga kama dhehebu, na kutangaza habari njema: “Injili hii kwa ulimwengu wote katika kizazi hiki.” Kwa hivyo nembo “sabini” ilikutana na utimizo wake kwa wakati huo. {SR1: 74.1}

Wazo lingine juu ya uzoefu wa Israeli:– Wakati nduguze Yusufu walifika Misri, walikwenda moja kwa moja kwake kupata nafaka. “Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.” Mwa. 42:6. Wana wa Yakobo walikuwa wageni katika nchi na hawakumjua ndugu yao ambaye alikuwa liwali. Kwa majaliwa ya Mungu hawakuja kwa Farao,

75

jinsi Wamisri walivyofanya, ili kupata nafaka, lakini moja kwa moja kwa mtu aliyefaa, — Yusufu. Kinyume na hili, Wamisri ambao wangepaswa kujua vyema, wakiwa wamejua utawala wa nchi yao, walikwenda kwa Farao kupata nafaka, lakini mfalme wao aliwaambia “Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.” Wamisri lazima walimjua Yusufu, akiwa liwali wao kwa zaidi ya miaka minane wakati huo. Katika miaka saba ya wingi, ni Yusufu ambaye walimuuzia chakula ambacho alihifadhi kwa ajili ya wakati wa njaa. Yusufu aliendeshwa katika gari la Farao juu ya nchi yote ya Misri, na Wamisri wote wakamsujudia, kwa hivyo isingewezekana kwa wao kutomjua. Hii ikiwa ni nembo, inaweza tu kupata utimizo wake katika simulizi linalofuata: {SR1: 74.2}

Wamisri (watu wa Mataifa) walikwenda kwa Farao (uongozi wa kanisa la mitume) ili wapate nafaka. Mitume waliwaelekeza watu wa Mataifa (waongofu) kwa Kristo kama Farao alivyowaelekeza Wamisri kwa Yusufu, akisema, “Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni.” Iwapo hii ndio maana tunayoipata kutoka kwa Wamisri kwenda kwa Farao, basi maana ya wana wa Yakobo kwenda moja kwa moja kwa Yusufu humaanisha kwamba wakati kanisa hilo litapangwa tena, watu wataweza kwenda moja kwa moja kwa Kristo (Yusufu). Funzo lililokusudiwa ni, kwamba mwanzoni mwa kanisa katika mwaka 1845, ambalo halikuwa na uongozi wa kweli (Farao) wa kwenda kwake, wao kwa lazima walikwenda moja kwa moja kwa Kristo (jinsi wana wa Yakobo walivyokwenda kwa Yusufu). {SR1: 75.1}

Yakobo Mfano Wa “James”

Kanisa la Waadventista wa Sabato ambalo lilikuja kuwapo mwaka 1845 likawa Israeli (vuguvugu ambalo Israeli wa kweli, watu 144,000 wanafanzwa). Itagundulika kwamba majina ya baba zao wa kimwili, na wa ile ahadi hufanana. Jina la baba wa Israeli wa kimwili lilikuwa “Yakobo.” Ndivyo lilivyo jina la baba wa Israeli wa ile ahadi (vuguvugu la Waadventista wa Sabato). Lakini mtu anaweza kusema, alikuwa Yakobo katika la zamani, na James White katika la mwisho. Ni kweli, lakini majina “Yakobo” na “James” ni sawa. Tena, njozi ya kwanza kabisa ambayo Dada White aliona ilikuwa juu ya watu 144,000, na lengo la dhehebu hili limekuwa kufanza idadi hiyo. {SR1: 75.2}

76

Nchi Ya Gosheni

Mwanzo wa dhehebu hili ulifananishwa na kuingia kwa Israeli Misri jinsi kulivyoelezwa hapo awali. Sasa tutazingatia ukweli wa nchi ya Gosheni. Yusufu aliwaleta Israeli ndani ya Misri na akawapatia sehemu ya hiyo nchi wakae ndani ambayo ilikuwa ardhi bora katika nchi ya Misri, na huko Yusufu akawalisha, kondoo zao, mifugo yao na ng’ombe, na kila kitu walichokuwa nacho. Tazama Mwanzo 45:10. {SR1: 76.1}

Ardhi ya Gosheni husimama kama nembo ya Madola Yaliyoungana ya Marekani ambayo ndani yake kanisa lilikuja kuwapo. Wakati nchi yetu huzaa kama ardhi ya Gosheni, tajiri zaidi ulimwenguni, na taifa la Uprotestanti, ndiyo bora kwa kazi ya umishonari, kwa maana imefanyizwa na mataifa yote, na kwa hivyo kama ardhi ya Gosheni, yenye kuzaa zaidi ndani ya Misri (ulimwengu). {SR1: 76.2}

Yusufu Alilisha Israeli

Mwanzoni mwa miaka saba ya njaa Wamisri waliuza kila kitu na wakawa watumwa kwa Farao, ambao wana rejelea kanisa la mitume na watu wa Mataifa wakati huo, ambao waliuza nyumba zao, na mashamba yao, na waliokuwa na vitu vyote shirika, jinsi ilivyofafanuliwa hapo awali. Lakini Israeli hawakuuza mali yao yoyote, wala hawakulipa chakula ambacho Yusufu aliwalisha. Israeli, basi, huliwakilisha kanisa sasa. Mwanzoni mwa kanisa katika mwaka 1845, Kristo (Yusufu) alilifungua ghala na kutupatia ukweli wote (nafaka) ambao tunaweza kuchanganua. Je! Sio ukweli kwamba hakuna watu wengine wakati wowote katika historia ya kanisa ambao wamepokea ukweli mwingi kama ule ambao Mungu ametupatia katika wakati wetu? Kanuni juu ya kanuni, amri juu ya amri, maagizo juu ya maagizo, tumepewa, ili sisi, kama watu, tuweze kujua na kuelewa njia za Bwana, tutii sauti Yake, tushike agizo Lake, amri, maagizo, na sheria; na hivyo kuwa “watoto wa Abrahamu, na warithi sawa sawa na ile ahadi.” Hili linapogunduliwa katika mioyo ya wanadamu ndipo watakapotimiza agizo alilopewa Petro. Petro akasema, “Wewe wajua Nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo Zangu.” {SR1: 76.3}

77

Wachungaji

“Farao akawauliza hao nduguze [Yusufu], Kazi yenu ni nini? Wakamwambia Farao, Watumwa wako tu wachunga wanyama, sisi, na baba zetu pia.” Mwa. 47:3. Israeli walikuwa wachungaji ambayo ni nembo ya wamishonari kama wale walishao wana-kondoo wa Mungu. Katika sehemu ya mwanzo ya kanisa, usemi ulikuwa, “Kila Mwadventista wa Sabato ni mmishonari, na kila mmishonari mhubiri.” Unapaswa kuwa hivyo sasa. “Vita kuu haijakuwa kati ya dini na hakuna dini; ni kati ya dini ya Mungu na dini ya mwanadamu.” — Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. {SR1: 77.1}

Farao Mwingine Akainuka

“Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, ambaye hakumjua Yusufu.” Kut. 1:8. Iwapo Farao wa kwanza, aliyemwinua Yusufu (Kristo), aliwakilisha uongozi katika siku za mitume, basi Farao huyu mpya lazima awakilishe uongozi wa vuguvugu hili la sasa wakati mada hii ilijulikana. Kumbuka, huyu Farao mpya hakumjua Yusufu (Kristo). Maana ni kwamba uongozi wa shirika hili umeacha kumfuata Bwana wao, — “Kristo.” Gombo la 5, ukurasa wa 217: “Dhambi za kuudhi na za kiburi zimekaa kati yetu. Hata hivyo maoni ya jumla ni kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho upo katika mipaka yake yote. Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani.” Ufafanuzi zaidi wa Mafarao kuwa mfano, umetolewa kwa ukurasa wa mwisho wa sehemu hii. {SR1: 77.2}

Mabwana-kazi / Wasimamizi

Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, ambaye hakumjua

78

Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi:… Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Raamsesi. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa, ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea… Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali:… Nao wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu, kazi ya chokaa, na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba.” Kut. 1:8-13. {SR1: 77.3}

“Wana wa Israeli,” Farao alisema, “ ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Hebu tushughulike kwa busara na tupunguze nguvu zao.” Kwa hivyo wao (Waisraeli) walivutwa kutoka kwa mazizi ya kondoo hadi kwenye yadi za matofali, na mashambani, lakini hili halikupunguza nguvu zao. Farao akasema, “Basi tuwawekee wasimamizi juu yao ili wawatese.” Kumbuka matumizi. Farao ndiye mfalme, anayetawala. Wasimamizi katika kisa hiki hawawezi kuwa wengine isipokuwa tabaka la wachungaji waliotajwa katika Gombo la 5, ukurasa wa 217: “Kutilia shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani.” {SR1: 78.1}

Hakuna tena usemi wa Waadventista wa Sabato, “kila Mwadventista wa Sabato ni mmishonari, na kila mmishonari mhubiri.” kama ilivyokuwa zamani. Lakini, ni kiasi gani kwa kila mtu? au, umefanya bajeti yako? badala ya, Je! umeleta nafsi yoyote kwa Kristo? Je! Washiriki wa kanisa lako wako karibu Naye? Haumaanishi hapa kwamba Wakristo hawapaswi kutoa kwa ajili ya kazi hiyo. Tunapaswa kutoa, na kutoa kwa ukarimu zaidi ya tulivyotoa zamani, lakini zawadi zetu zinapaswa kutoka kwa moyo wa radhi, na sio kwa tokeo la mijeledi. Watu wanapaswa kulishwa chakula cha kiroho ili waweze kuhisi hitaji la kutoa bila kukandamizwa kwa mada hiyo. {SR1: 78.2}

Musa alipokaribia kujenga patakatifu nyikani, Mungu alimwamuru, akisema: “Waambie wana wa Israeli, kwamba waniletee sadaka. Kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka Yangu.” Musa aliamriwa

79

kuchukua sadaka kutoka kwa wale tu ambao walitoa kwa hiari kutoka moyoni mwao. Tumeambiwa na Roho ya Unabii kwamba wachungaji hawapaswi kuweka juhudi na wakati wao wote kwa kanisa. Washiriki hawapaswi kutarajia mahubiri kila Sabato. Wachungaji wanapaswa badala yake wajihusishe kufanya kazi kwa watu wa nje. Soma Gombo la 9, ukurasa wa 140. Je! Tumezingatia agizo hili? Kwa mfano, tuna wachungaji wengi huko Los Angeles na maeneo ya karibu, lakini tunazo juhudi ngapi za umma? Imetangazwa muda mfupi tu uliopita kwamba zilikuwapo mbili tu. Hivyo ndivyo imekuwa kwa miaka kadhaa. Je! Hawa wachungaji hufanya nini siku baada ya siku, na juma baada ya juma? Inaonekana hawafanyi kitu isipokuwa kuandaa matini katika siku sita za juma ili wahubiri siku ya Sabato, na kisha ni aidha kitu cha kuuza, au makadirio fulani ya kukusanya. {SR1: 78.3}

Je! Tunasoma mahubiri mangapi katika Biblia yakisisitiza watu watoe fedha, au wanunue kitu fulani ili kutegemeza kazi? Hakuna hata moja. Tumeitia unajisi nyumba ya Mungu kufanya biashara hata asubuhi ya Sabato, saa ambayo imetengwa kama siku ya kupumzika ili kumwabudu Mungu. Gombo la 1, ukurasa 471, 472: “Kosa kubwa limefanywa na baadhi ya watu wanaokiri ukweli wa sasa, kwa kuingiza biashara katika mkondo wa mfululizo wa mikutano, na kwa ulanguzi wao kukengeusha mawazo kutoka kwa kusudi la mikutano. Laiti Kristo angalikuwa sasa duniani, angewafukuza hawa wachuuzi na walanguzi, iwapo ni wachungaji au watu, kwa mijeledi ya kamba ndogo, kama alipoingia hekaluni zamani.… Wachungaji wamesimama katika mimbari na kutoa mahubiri ya utakatifu, na kisha kwa kuingiza biashara, na kutenda sehemu ya muuzaji, hata katika nyumba ya Mungu, wamezikengeusha dhamira za wasikilizaji wao kutoka kwa mashauri yaliyopokelewa, na kuharibu matunda ya kazi yao…. Wakati na nguvu zao zinapaswa kuhifadhiwa, ili juhudi zao ziweze kuwa za uangalifu katika mfululizo wa mikutano. Wakati na nguvu zao hazipaswi kutumika kuuza vitabu vyetu wakati vinaweza kuletwa mbele ya umma na wale ambao hawana mzigo wa kulihubiri neno [wainjilisti]. {SR1: 79.1}

“‘Imeandikwa, Nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala, lakini

80

ninyi mmeifanya kuwa pango la wezi.’ Wafanyabiashara hawa wangeweza kusihi kama udhuru ya kwamba bidhaa walizoshikilia kuuza zilikuwa kwa ajili ya sadaka za dhabihu. Lakini kusudi lao lilikuwa kupata faida, kupata raslimali, kujilimbikizia.” Gombo la 1, ukurasa wa 472. {SR1: 79.2}

Baraza letu la eneo linajua kuhusu agizo lililotolewa hapa, na uovu unaofanywa makanisani. Kwenye Kongamano la Vuli lililofanyika Milwaukee, Wisconsin, mwaka 1923, swali la uuzaji wa vitabu siku ya Sabato lililetwa kwa uhusiano na maswala mengine, na azimio lifuatalo lilipitishwa na kuchapishwa: “Kwamba kampeni zote za kutangaza majarida au uuzaji wa vitabu siku ya Sabato ziondolewe, na ya kwamba wale wanaohusika na kuendeleza kampeni hizi waelekezwe kwa mbinu ya ubembe wa nyumba kwa nyumba kwa kuzuru kamati katika uhusiano na kampeni za uuzaji wa vitabu: {SR1: 80.1}

“Kwamba tunaalika nyumba zetu za uchapishaji kuchukua tahadhari kuwatumia watu wetu kwa niaba ya miradi ya nyumba za uchapishaji, na kujizuia kutuma kwa maafisa wa kanisa maswala yatakayowasilishwa siku ya Sabato, na kufanya mipango kwanza na mabaraza ya Mitaa, Muungano, na Baraza Kuu.” — Milwaukee Kongamano la Vuli, Oktoba 9-17, 1923. Mapitio na Kutangaza ya Novemba 22, 1923. Soma Gombo la 9, ukurasa 260. {SR1: 80.2}

Tunasoma katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 477: “Jambo la kigeni, limeingia katika makanisa yetu. Watu ambao wamewekwa katika nafasi za majukumu kwamba waweze kuwa wasaidizi wa busara kwa watenda kazi wenzao, wamedhani kwamba wamewekwa kuwa wafalme na watawala katika makanisa kumwambia ndugu mmoja, Fanya hili; kwa mwingine, Fanya Lile; na kwa mwingine, Hakikisha kufanya kazi kwa njia hii na hii.” Kwa hivyo Farao amewakokota watu kutoka zizi la kondoo hadi kwa yadi zamatofali, au shambani. Mabwana-kazi, wakiwa wameamriwa kusimamia kazi hiyo, husisitiza matofali (bajeti), na kuwachosha watu. Dhambi zilizopo kanisani hupitishwa na hakuna anayejali. Wale ambao hukemea makosa hujiletea hasira yao. Katika Gombo la 3, ukurasa wa 266, akinena kuhusu hali ndani ya kanisa kwa wakati wa kutiwa muhuri (alama) kwa watu 144,000, na mchinjo ndani ya kanisa, tunasoma: {SR1: 80.3}

81

“Wale ambao wameruhusu haya makosa wamedhaniwa na watu kuwa ni wapole sana na wenye tabia ya upendo, kwa sababu tu walijiepusha kutekeleza wajibu wazi wa Maandiko. Kazi hiyo haikukubalika kwa hisia zao, kwa hivyo, waliiepuka.” {SR1: 81.1}

Msiwape Nyasi Tena

“Na siku ile ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema, Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu awali. Na waende wakatafute majani wenyewe. Hao wasimamizi wa watu na wanyapara wao wakatoka, wakasema na watu, wakanena, Farao asema hivi, Mimi siwapi majani. Enendeni wenyewe, jipatieni majani hapo mtakapoyaona: Kwa maana kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.” Kut. 5:6, 7, 10, 11. {SR1: 81.2}

Farao hatatoa majani: Yaani, hatatoa msaada wowote, lakini watu lazima wazalishe idadi sawa ya matofali. Mwanzoni mwa shirika hili (Waadventista wa Sabato), taasisi za dhehebu, zahanati, na hospitali zilijengwa kwa kusudi la kuwatunza watu wetu (washirika wa kanisa). Baada ya kutambua tatizo la mgonjwa, na chanzo kujulikana, pamoja na maagizo, usaidizi au matibabu yalitolewa. Usaidizi huu ulipaswa kutolewa iwapo waliweza kulipia, sehemu ndogo, au sufuri. Kama hiyo ndiyo kazi ya Msamaria mwema. {SR1: 81.3}

“Katika namba za zamani za Shuhuda kwa Kanisa nimezungumza juu ya umuhimu wa Waadventista wa Sabato kuanzisha taasisi kwa manufaa ya wagonjwa, haswa kwa wanaoteseka na wagonjwa kati yetu. Nimesema juu ya uwezo wa watu wetu wenyewe, kwa suala la fedha, kutenda hili; na tumehimiza kwamba, kwa kuzingatia umuhimu wa tawi hili la kazi kubwa ya maandalio ya kukutana na Bwana… {SR1: 81.4}

“Nilipowaona wale waliosimamia na kuelekeza, wakiingia ndani ya hatari nilizoonyeshwa, ambazo nalikuwa nimewaonya hadharani, na pia katika mazungumzo ya faragha na kwa barua, mzigo wa kutisha ulikuja juu yangu. Yale ambayo nalikuwa nimeonyeshwa kama mahali ambapo wagonjwa wanaoteseka kati yetu wangeweza kusaidiwa, palikuwa mahali ambapo kujinyima, ukarimu, imani

82

na kumcha Mungu kulipaswa kuwa kanuni zinazotawala. Lakini wakati wito usiostahili ulifanywa kwa ajili ya fedha nyingi, na taarifa kwamba hisa zilizochukuliwa zitalipa asilimia kubwa; ilhali ndugu ambao walishikilia nafasi katika taasisi hiyo walionekana kuwa tayari kuchukua mishahara mikubwa kuliko wale walioridhika na ambao walijaza nafasi zingine na muhimu katika kazi kuu ya ukweli na matengenezo; wakati nilipojua, kwa uchungu, kwamba, ili kuifanya taasisi hiyo ipendwe na wale wasio wa imani yetu, na kupata ufadhili wao, roho ya maelewano ilikuwa ikikita mizizi upesi sana katika ile Taasisi, iliyodhihirishwa kwa matumizi ya Bwa., Binti, na Bi, badala ya Ndugu na Dada, na katika tafrija maarufu, ambazo wote waliweza kushiriki katika namna zilizolinganishwa kwa mzaha wa kitoto; — nilipoyaona mambo haya, nikasema, Haya sio yale nalionyeshwa kama taasisi ya wagonjwa, ambayo ingeshiriki baraka ya ishara ya Mungu. Hiki ni kitu kingine. Na bado hesabu za majengo makubwa zaidi zilifanywa, na wito wa pesa nyingi ulihimizwa. Jinsi ilivyosimamiwa wakati huo, ningeweza kuiona Taasisi hiyo, kwa ujumla, kama laana… {SR1: 81.5}

“Baadhi ya waliokuja Battle Creek wakiwa Wakristo wanyenyekevu, waliojitolea, wenye imani, walikwenda zao wakiwa karibu makafiri. Mvuto wa jumla wa mambo haya ulikuwa unajenga chuki dhidi ya matengenezo ya afya ndani ya wengi wanyenyekevu mno, waliojitolea zaidi, na walio bora wa ndugu zetu, na ulikuwa ukiharibu imani katika Shuhuda zangu na katika ukweli wa sasa… {SR1: 82.1}

“Ndugu ambao wamesimama kwa uongozi wa hii kazi wametoa kwa watu wetu wito wa fedha kwa msingi kwamba matengenezo ya afya ni sehemu ya kazi kuu iliyounganishwa kwa ujumbe wa malaika wa tatu. Katika hili wamekuwa wakweli. Ni tawi la kazi kuu ya Mungu, ya uhisani, ya ukarimu, ya kujitolea, na ya fadhili. Basi kwa nini hawa ndugu waseme, ‘Hisa katika Taasisi ya Afya italipa asilimia kubwa,’ ‘ni uwekezaji mzuri,’ ‘kitu cha faida’? Mbona wasizungumzie vile vile hisa katika Shirika la Uchapishaji italipa asilimia kubwa? Iwapo haya ni matawi mawili ya kazi iyo hiyo kuu ya kufunga ya maandalio kwa ujio wa Mwana wa Adamu, kwa nini yasiweze kuwa? Au mbona yote yasifanywe kuwa maswala ya ukarimu? Kalamu na sauti

83

ambayo iliwasihi marafiki wa kazi hiyo kwa niaba ya mfuko wa uchapishaji, haikufanya uhamasisho kama huo.” Gombo la 1, ukurasa wa 633-636. {SR1: 82.2}

Je! Taasisi zetu sasa zinajipimaje kwa ushuhuda huu usiopinda? Je! Tunaweza kusema kwamba ni za hisani, za ukarimu, zinazojitolea, za fadhili? Sikiza faida kubwa wanazopata. Uwasilishaji umefanywa wa ripoti ya kila mwaka ya Zahanati ya Mtakatifu Helena, kama ilivyoonekana katika Kinasa Maandishi cha Umoja wa Pasifiki cha Aprili 25, 1929. “Noti zilizolipwa mwishoni mwa mwaka1925, zilikuwa $ 60,044 (senti hazijatolewa hapa. Katika mwaka 1926, zilikuwa zimepunguzwa hadi $ 49,031; katika mwaka 1927, hadi $ 36,321; na mwishoni mwa mwaka 1928, zilikuwa chini hadi $ 26,415. Katika miaka mitatu zilipunguzwa kutoka $ 60,000 hadi $ 33,629. Rasilimali, zilizowekwa na za sasa, mwishoni mwa mwaka 1928 , $ 371,105. Madeni ni $ 45,809. Kuna kupungua kwa madeni karibu $ 5,000. Fedha mkononi mwishoni mwa mwaka 1928, $ 10,749. Thamani ya sasa, $ 325,296 …. Mapato ya jumla, $ 456,258. Faida, $ 437,284. Wastani wa mahudhurio ya kila siku ya wagonjwa yalikuwa 85 na zaidi, na mapato kutoka kwa wagonjwa moja kwa moja, $ 261,363. Pato la faida $ 10,439.39.” {SR1: 83.1}

Inawezekanaje kwa taasisi kufanya kazi yoyote ya uhisani hata ndogo, na bado ipate $ 111,988 juu ya thamani yake ya sasa kwa mwaka mmoja? Kumbuka: Thamani ya sasa, $ 325,296. Mapato ya faida, $ 437,284 katika mwaka 1928. Lakini hii sio mbaya zaidi. Ndugu zetu wamepofuka sana hivi kwamba hufikiri faida hizi kubwa zinawapatia sifa nzuri kwa usimamizi wao wa busara, na kujisifu juu yake, na kusema kwamba zahanati inanawiri. Kweli Mungu wetu alijua kile Alichokuwa akinena aliposema Walaodekia ni vipofu, wanyonge, wenye mashaka, na maskini, na uchi, ingawa wao hufikiri ni matajiri na wamejitajirisha, na hawana haja ya kitu. Tazama tofauti ya kujisifu kati ya Walaodekia, na taasisi zingine ambazo wengine hufikiri ibilisi ni kiongozi wazo. Ifuatayo ni ripoti ya kila mwaka ya misheni huko Los Angeles kwa mwaka uo huo wa 1928: Bidhaa hizi hupeanwa bila malipo kwa wahitaji. “Ripoti ya kila mwaka ya mwaka unaoishia Desemba 31, 1928, inaonyesha milo 527,481 iliandaliwa; mahali pa kulala 137,287 palifanywa tayari; huduma za kufua, vyombo 53,334; huduma za kinyozi,

84

20,394; bafu, 12,339; mavazi yaliyosambazwa, 32,541; Viatu vilivyorekebishwa 1791; ajira iliyopatikana kwa watu 9,204; misaada ya matibabu aliyotolewa 3,117; wakati ripoti ya kanisa huonyesha kwamba katika mwaka watu 15,340 walikiri wokovu katika mikutano ya kila siku ambayo ni endelevu kutoka saa 05 asubuhi hadi saa 11 Jioni, na huendeshwa na vikundi kutoka katika makanisa ya madhehebu yote.” (Imenakiliwa kutoka kwa gazeti la Los Angeles.) {SR1: 83.2}

Je! Shetani amekuwa mhisani kuliko Kristo? Kwa nini tumeenda kulala? Je! Ni dola na senti ambazo Bwana hutaka? Je! Mambo haya hayaharibu imani ya umma kwa watu wa Mungu? Je! Mambo haya yanaongeza au yanapunguza matunda ya kazi yetu? Je! Tunamwakilisha Mungu na kuupeleka ujumbe wa malaika wa tatu kwa ulimwengu unaokufa? Je! Kristo ndiye kielelezo na mfano wetu? Kwa nini tumemruhusu shetani atudanganye? Je! Huu sio mwito wa kuwaamsha watu wa Mungu kwa utumishi kama wa Kristo? Tutaendelea kulala hadi lini? Ni vibaya kabisa kwa watu wa Mungu kumnyima yule ambaye hayuko katika imani kupokea manufaa ya Mungu mikononi mwa watu Wake, lakini ni vibaya mara elfu zaidi kumnyima mmoja wa Israeli, ambaye angejitoa muhanga na kutupa kura yake pamoja na watu wa Mungu, mwaminifu katika kutoa zaka na sadaka jinsi ambavyo Bwana amemwezesha. Iwapo Mungu angeruhusu umaskini kumshinda mtu kama huyo kwa ugonjwa au ukongwe, tuwafanyeje? Je! Tuwaache waende zao na kuwaambia, Mungu akubariki? Je! Hospitali ya nchi ni ya watu wa Mungu, na hospitali za Mungu ni za kutengeneza fedha? Je! Shamba la kaunti ni la watu wa Mungu, huko na watu wasiomcha Mungu, na kwa wale najisi mezani pao jinsi tunavyoamini kutoka kwa mtazamo wa kidini, kati ya unajisi, nguruwe, na tumbaku? Je! Hapa ni aina ya mahali pa mtoto wa Mungu, na hekalu la Roho Mtakatifu kwa mujibu wa imani yetu? Je! Tutatoa jibu gani tutakalompa Yeye wakati Atakapokuja? Je! Tutasikia maneno, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu,” jinsi tunavyosoma katika Mat. 25:35, 36? “Kwa maana Nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; Nalikuwa na kiu, mkaninywesha; Nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; Nalikuwa uchi, mkanivika; Nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; Nalikuwa kifungoni, mkanijia.” Je! Usemi huu utakuwa wetu, au tutajipata

85

katika mkono wa kushoto na laana mbaya jinsi ilivyo katika Mat. 25:41-43, 46: “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake: Kwa maana Nalikuwa na njaa, msinipe chakula; Nalikuwa na kiu, msininyweshe: Nalikuwa mgeni, msinikaribishe; Nalikuwa uchi, msinivike; Nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele, bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” {SR1: 84.1}

Kunukuu Gombo la 1, ukurasa 639: “Mapema mwanzoni mwa mwaka 1850 ndugu huyu alikuwa mtunza Sabato, na kuanzia tarehe hiyo alichangia kwa ukarimu mashirika kadhaa ambayo yameanzishwa kuendeleza kazi ya injili, mpaka akawa maskini. Lakini wakati mwito, wa haraka, usio na idhini ulikuja kwa Taasisi, akachukua hisa jumla ya dola mia moja. Katika mkutano huko ——- alijulisha tatizo la mkewe, ambaye ni mdhaifu sana, na anafaa kusaidiwa, lakini lazima asaidiwe haraka, wakati wowote. Pia alisimulia hali zake, na akasema kwamba ikiwa angeweza kuamuru hizo dola mia moja wakati huo katika ile Taasisi, angeweza kumpeleka mkewe huko kutibiwa, lakini kama ilivyokuwa, hakuweza. Tulimjibu kwamba kamwe asingekuwa amewekeza dola katika Taasisi hiyo, na ya kwamba lilikuwapo kosa katika jambo ambalo hatungeweza kusaidia; na hapo suala hilo likaachwa. Siwezi kusita kusema kwamba dada huyu anapaswa kutibiwa, majuma machache angalau, katika Taasisi hiyo bila malipo. Mumewe anaweza kufanya lakini sio zaidi ya kulipa nauli yake kwenda na kutoka Battle Creek.” Je! Tunayo matatizo kama haya kwa wakati huu? Je! Tunashughulika na watu hawa kama mkulima mwingine anavyoshughulika na farasi wake? Humtunza farasi vyema wakati ni mchanga na anafanya kazi yake, lakini wakati yule mnyama anazeeka na kuwa mdhaifu, basi humfukuza nje katika uwanja wa wazi wakati wa majira ya baridi, wakati haswa huyo farasi maskini anahitaji huduma bora. Je! Hatufanani na mkulima huyu mwenye moyo mgumu ambaye hampi farasi wake chakula katika majira ya baridi, na baridi kali mgongoni mwa yule mnyama aliyechoka, ili kuhifadhi vifurushi kadhaa vya majani? Ukatili, sivyo? Ameachiwa msomaji kulijibu swali hilo. {SR1: 85.1}

86

Wakunga

“Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa, ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli…. Mfalme wa Misri akasema na wakunga wa Waebrania. Akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania…. ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni: bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.” Kut. 1:12, 15, 16. “Wakunga” huwakilisha walimu wa shule ya kanisa, ambao huwalea watoto katika mfumo wa elimu. Unaweza kuhoji, Je! Inawezekana kwamba shetani angejaribu kuwadanganya walimu, na kutia sumu katika akili za watoto? Ibilisi haachi kamba moja legevu. Kumbukumbu hapa imetolewa kwa Jarida la Nyumbani na Shule la Elimu ya Kikristo, la Desemba, 1929, lililochapishwa na Baraza Kuu la Waadventista wa Sabato, Washington, D.C., na kila mwalimu katika dhehebu anapaswa kuwa mchangiaji wa jarida hili. Suala lililotajwa hapo juu limejaa hadithi za Krismasi, utunzaji wa Krismasi, na mipango ya Krismasi na zawadi, ambayo walimu wanapaswa kuwapokeza watoto. Kwa sababu itakakuwa ndefu sana kunukuu yote, sentensi ya mwisho kabisa, na maneno ya kufunga chini ya aya “Kile Krismasi Inaweza Kumaanisha Siku Zote” imenukuliwa hapa: “Na, kwa ujumla, ubatizo wa ukweli, unyenyekevu, na ukweli katika maadhimisho ya siku kuu ya kuzaliwa ya ulimwengu.” Fikiria maneno haya, msomaji mpendwa. Jarida la Waadventista wa Sabato, lililochapishwa na Baraza Kuu, kuiinua siku kuu ya ulimwengu ya ibada ya sanamu kuwa siku ya kuzaliwa ya Kristo, na kuikabidhi walimu wa dhehebu. {SR1: 86.1}

“Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale watoto wanaume.” Kut. 1:17. Hapa tuna nembo moja nzuri, na tuseme, Amina kwa walimu “Walimwogopa Mungu.” Tunakusihi uwapeleke watoto wako katika shule ya dhehebu, kwani ndio mahali pazuri zaidi kwao. “Mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua.” Kut. 1:15. Maana ya majina haya ni: “Uzuri” na “fahari.” Hakika hiyo. Ilikuwa haiwezekani kwa wakunga wawili kuhudumia

87

umati huo mkubwa wa wanawake, lakini ukweli ni, kwamba walikuwa wawili tu. Sababu ya hili ni kuifanya hiyo nembo iwe kamilifu, kumaanisha tabaka zote mbili za walimu, wa kiume na wa kike, “uzuri” na “fahari.” {SR1: 86.2}

Watoto Wanaume Katika Mto Nile

“Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha: na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.” Kut. 1:20, 22. Lengo kuu la mpango wa Farao halikuwa kupunguza idadi ya watu. Laiti hili lilikuwa ndilo lengo lake, angemwua yule wa kike, kwa maana siku hizo walioa wake wengi. Kama angekuwa ameamuru kuwatupa watoto wa kike katika mto, na kuwaokoa wanaume, angeweza kutimiza kusudi lake, na pia kuongeza watumwa wake kwa maana ni wanaume ambao walitengeneza matofali. Tunasoma katika Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 242: “Shetani ndiye alikuwa mtoa hoja katika jambo hili. Alijua kwamba mkombozi alipaswa kuinuliwa kati ya Waisraeli; na katika kumwongoza mfalme kuwaangamiza watoto wao alitarajia kulishinda kusudi la Mungu.” Hii ndilo lilikuwa kusudi la hiyo shughuli nzima. Kwa sababu hii ni nembo, matumizi sasa yatafanywa. {SR1: 87.1}

Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 475, chini ya sura yenye kichwa “Ruhusu Mbingu Iongoze”, tunasoma: “Unabii lazima utimizwe. Bwana asema: ‘Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni mwenye bidii sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.” Hakuna taarifa iliyo wazi zaidi ingeweza kutolewa kuliko hii, kwamba lazima tumtarajie nabii, au ujumbe katika siku za hivi karibuni. Iwapo hii ni taarifa iliyovuviwa, basi inaonekana litakuwa jukumu la walinzi kwenye kuta za Zayuni kuwaelimisha na kuwaelekeza watu kwamba yupo nabii, au ujumbe wa kutazamia. Lakini tuna nini? Kinyume chake, maoni ya jumla ya dhehebu lote ni, “hakuna

88

nabii anayekuja, wala hakuna ujumbe wowote unaotarajiwa. Tuna ukweli wote, na hatuhitaji hata mmoja, “ni kelele kutoka kwa kambi ya Israeli. Hivyo tunaona jinsi adui wa zamani amefanya kichinichini nakala ya udanganyifu wake na kanisa wakati huu. Jinsi Farao alivyokuwa bila fahamu ya lengo kuu la amri yake, vivyo hivyo kwa viongozi kukosa fahamu, mdanganyifu mjanja amejaribu kumzamisha nabii, au ujumbe wa matengenezo kwa wakati huu. Hivyo inathibitisha katika kila tukio kwamba uzoefu wa Israeli huko Misri ni picha ya Israeli, wa kweli. Iwapo nabii, au hata ujumbe uweze kuja, kanisa haliko tayari kupokea lolote kati ya hayo. Tokeo lake laweza kuwa sawa na ilivyokuwa kwa taifa la Kiyahudi na kuja kwa Kristo. Ni wazo la kutisha kama nini. “Ijapokuwa ilionekana kwa Wamisri kuwa masilahi ya ufalme yalikuwa kuwashikilia watu hawa utumwani, kusudi la kweli nyuma ya hayo yote lilikuwa azimio la Shetani, nguvu ya joka (Isa. 51:9), kuwashikilia watu wa Israeli katika utumwa wa dhambi, na kuzuia kazi ya matengenezo ambayo kwayo Mungu alikuwa ameunyosha mkono Wake kadiri wakati wa unabii huo ulipokuja.” Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. {SR1: 87.2}

Watoto Wanaume Wa Dhehebu — Jinsi Walivyozamishwa

Je! Shetani amemzamisha mtoto yeyote wa kiume katika mto Nile wakati huu? Wako wapi wanaume katika dhehebu hili? Lazima wawe ndani ya mto Nile, kwa maana ni nembo ya dhambi ulimwenguni, na huko ndiko kwa kawaida tunawapata wanaume; na wanawake kanisani. Swali linaweza kuulizwa, Ni nini kilichowachekecha nje wanaume hao? Roho ya Unabii hufundisha kwamba tunapaswa kuhakikisha kuwa ajira inatolewa kwa waongofu wapya ndani ya ukweli, ili kuwawezesha kuitunza Sabato. Pia kuwatunza maskini na wagonjwa kati yetu. Agizo hili lote limepuuzwa kabisa, na tokeo lake ni kwamba wanaume wamechujwa nje ya kanisa. Wanaume hupenda ukweli kama wanawake, lakini mara tu wanapousikia ukweli, wanaanza kuhoji kuhusu mambo. Mara ugumu unatokea, na swali linaulizwa, Nawezaje kutunza Sabato, na bado nishikilie nafasi yangu? Iwapo naweza kuiacha nafasi yangu, je! Naweza kupata nyingine? Je! Kanisa

89

laweza kunisaidia kupata kitu cha kufanya? Je! Kanisa laweza kutoa msaada ikiwa lipo hitaji kubwa, kama vile ukosefu wa chakula, mavazi, au katika tatizo la ugonjwa? Maswali haya yote yanajibiwa mara moja na, LA. Tokeo lake ni kwamba, uamuzi hufanywa na ukweli hukataliwa. {SR1: 88.1}

Laiti kanisa lingeweka kitia moyo kwa safu hizi, msimamo huu usingechukuliwa na wahusika wapya wenye nia, na tokeo lingekuwa kwamba wanaume na wanawake wangekuwa ndani ya kanisa. Wanaume wakiwa wachuma mshahara, ongezeko la zaka na sadaka, haziwezi kukadiriwa, na matumizi madogo katika misaada yatakuwa kipande kidogo tu kwa kulinganisha. Shirika la ajira lingekuwa taaluma nzuri kwa dhehebu. Sio tu ajira ingeweza kupatikana kutoka kwa watu nje ya shirika, lakini kazi kati ya Waadventista ingehifadhiwa na Waadventista. Kwa hivyo wanaume “wametupwa” ulimwenguni (“Nile”), lakini wanawake wameachwa (“wakiwa hai”) kanisani. {SR1: 89.1}

Binti-Mfalme Ampata Musa

Kunukuu Kut. 2:2, 3: “Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mwana: Na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami akamtia mtoto ndani yake; akakiweka katika majani kando ya mto.” Majaliwa ya Mungu yanamwongoza binti mfalme wa Misri mtoni ili aoge, na baada ya kukiona hicho kisafina, alimtuma mjakazi wake kukichukua. Aliona kwamba mtoto analia, akamwonea huruma. Dadake yule mtoto akamkaribia binti Farao, akasema, “Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako akunyonyeshe mtoto huyu?” Baada ya kuwasili kwa mama ya mtoto, binti Farao akamwambia, “Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee.” Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao akiwa na miaka 12, na binti mfalme akamwita “Musa.” Funzo hapa ni kwamba, pamoja na mipango yote ya Shetani, haitawezekana kushinda kusudi la Mungu. {SR1: 89.2}

90

Chaguo la Musa

Jinsi Musa (mfano) alipokea elimu ya juu zaidi ambayo nyua za Farao zingeweza kuzalisha, baada ya kubaleghe alilazimika kuchagua mojawapo ya mambo mawili: ama kiti cha enzi cha Misri, au kuteseka pamoja na wana wa Israeli. Vivyo hivyo, Musa mamboleo (wa uakisi) hupokea elimu ya juu kabisa ambayo dhehebu linaweza kutoa (amebaleghe) akiwa amekamilisha elimu, “profesa.” {SR1: 90.1}

Musa mamboleo vile vile analazimika kuchagua mojawapo ya mambo mawili: Ama profesa duniani (Misri) na kipato kikubwa, umaarufu, na anasa za dhambi kwa kwa kitambo kidogo au kufanya kazi kwa dhehebu na mshahara mdogo, na kupata mateso na kanisa (wana wa Israeli). Jinsi Musa (mfano) alivyochagua wa mwisho, ndivyo Musa wa uakisi anajifurahisha kukaa na dhehebu, “Akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwa Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri.” Takwimu za vuguvugu kwa hivyo tunaambiwa, zinaonyesha kwamba 90% ya watoto ambao husoma katika shule za dhehebu husalia wakweli kwa ujumbe. Hii linathibitisha somo linalofundishwa hapa ni sahihi. {SR1: 90.2}

Dhana Ya Musa

“Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake,… akamwona Mmisri anampiga Mwebrania… akamuua yule Mmisri, akamficha ndani ya mchanga. Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana: Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, “Mbona unampiga mwenzako?” Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi, kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa… Lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani.” Kut. 2:11-15. {SR1: 90.3}

Musa alidhani angewakomboa wana wa Israeli kwa nguvu au kwa silaha, kwa hivyo akavingirisha mikono yake na kuanza jukumu lake. Dhana potofu ya Musa kuhusu mbinu ambayo ingetumika katika ukombozi wa Israeli haikuwa tu jambo baya kwa mtu huyo. Iwapo hiyo ndio njia aliyoelewa Israeli wangepata uhuru wao, alishindwa kutekeleza mpango huo. Taabu yake haikuwa kwa sababu ya ukosefu wa elimu, au mafunzo kama jemadari wa majeshi, kwamba alishindwa kuutekeleza

91

mpango wake, lakini kwa sababu alikuwa mwoga sana na alimwogopa Farao. Iwapo hii haikuwa sababu ya kushindwa kwake, mbona basi alimuua Mmisri mmoja tu, akamzika mchangani, na baada ya kujulikana, akimbie na kuacha Israeli iangamie utumwani? Ikiwa nia yake, au ufahamu, ulikuwa kuongoza Israeli dhidi ya majeshi ya Misri, hakupaswa kumficha Mmisri mchangani, bali angemwacha juu ya ardhi kuwa mfano, na kisha kuwasaka wengine. Kwa kukosa kuutekeleza mpango wake ulioupendekeza, Musa alifanya kosa maradufu. {SR1: 90.4}

Musa huyu wa kale ni nembo ya Musa mamboleo (uongozi wa sasa). Kwa sababu kufeli kwa Musa hakukuwa kwa sababu ya ukosefu wa mafunzo, lakini kwa sababu ya wazo potofu la mbinu ambayo ingetumika, ndivyo ilivyo na uongozi wa sasa. Jinsi Musa alivyoshindwa mwenyewe kutimiza mpango wake wa kimakosa (kile alichodhani ni uamuzi wa busara), vivyo hivyo uongozi sasa umeshindwa kwa upande wao. Lengo limekuwa kumaliza kazi katika kizazi hiki ambacho kwa uhalisia kimepita, na kwa kiwango cha mwendo kazi inaenda sasa, haiwezi kukamilishwa kwa miaka mingine 100. “Tuko katika hatari ya kuamini mbinu, uongozi, na utumishi wa mibano mingi, ambao ukichukuliwa pekee yake, mwishowe unaweza kusababisha mchafuko tu, kutoridhika, na kushindwa.” Mapitio na Kutangaza, Februari 20, 1930. {SR1: 91.1}

Matumizi Ya Huo Mfano

Iwapo Farao ndiye mfalme, (uongozi) anayewatawala watu, basi kanisa ni “malkia”, kisha “binti-mfalme” ni shule ya kanisa. Misri ni nembo ya ulimwengu na Mto Nile nembo ya dhambi za ulimwengu. Kwa msaada wa mama mcha Mungu, Musa (mfano) hakutupwa ndani ya mto Nile. Ndivyo ilivyo kwa Musa mamboleo, ambaye, kwa msaada wa mama yake Mkristo ameokolewa kutoka kwa mto Nile (dhambi ulimwenguni), lakini wakati hawezi kumficha tena, na lazima ampeleke kwenye shule za nchi ambako dhambi hutawala, shule ya kanisa (“binti-mfalme”) anampata. Jinsi Musa (mfano) alivyopokea elimu yake kwa msaada wa binti-mfalme, vivyo hivyo Musa mamboleo hupokea elimu yake kwa msaada wa shule ya kanisa. {SR1: 91.2}

92

Sisi, kama Musa, tumefikiri kwamba tunapaswa kuwakomboa Israeli kwa nguvu za silaha (msaada wa wanadamu). Kama Musa, sisi ni waoga sana kutimiza lolote. Imenenwa na mchungaji mwema wa Mungu, “Hili ni kosa kanisani, na lile sio sawa, na linapaswa kurekebishwa, lakini hatuwezi kulitenda.” Mbona? Kwa sababu anaogopa atapoteza kazi yake. Lakini tufanye nini? Fanya kazi kwa ajili ya Mungu na kumtumaini Yeye, au fanya kazi kwa ajili ya Farao na uamini katika kazi hiyo? {SR1: 92.1}

Akinukuu Gombo la 5, ukurasa wa 80-82: “Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika upepeto mkuu utakaotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha ya kwamba pepeto Lake li mkononi Mwake, Naye atausafisha uwanda Wake kabisa…. Wale ambao wameamini katika akili, ustadi, au talanta, hawatasimama wakati huo kuwa viongozi wa askari. Hawakufululiza mwendo na nuru. Wale ambao wamethibitsha wenyewe kwamba si waaminifu wakati huo hawatakabidhiwa kundi. Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na Yeye hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa kupepetwa, wa kupimwa watafunuliwa waonekane. Wako sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu. Lakini, inaweza kuwa chini ya hali ngumu isiyopendeza ya nje ambapo waangavu wa tabia halisi ya Kikristo utafunuliwa…. Katika wakati huu, dhahabu itatenganishwa kutoka kwa takataka kanisani…. Wengi kama nyota ambao tumewatamani kwa mng’ao wake, watajitokeza nje gizani…. Wale dhaifu sana na wenye kusitasita kanisani watakuwa kama Daudi — tayari kutenda na kujasiri…. Wakati huo kanisa la Kristo litaonekana ‘zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango’…. Mungu atafanya kazi katika siku zetu ambayo ni wachache huitazamia. Atawaamsha na kuwainua miongoni mwetu wale ambao wamefundishwa na kupakwa mafuta ya Roho Wake, badala ya kwa mafunzo ya nje ya taasisi za kisayansi. Taasisi hizi hazipaswi kudharauliwa au kushutumiwa; zimewekwa na Mungu, lakini zinaweza kupamba tu sifa za nje. Mungu

93

atadhihirisha kwamba Yeye hawategemei wanadamu wasomi, wa kujikweza.”{SR1: 92.2}

Musa Nyikani

“Lakini Musa akakimbia kutoka kwa uso wa Farao, akakaa katika nchi ya Midiani … Basi kuhani wa Midiani …. akampa Musa binti yake Zipora awe mkewe …. Basi huyo Musa alikuwa akichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani: Naye akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika kwenye mlima wa Mungu … [Horebu], … na kumbe, kichaka kiliwaka moto, na kichaka hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kichaka haki hakiteketei …. Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kichaka, akasema, Musa, Musa. Akasema, Mimi hapa …. Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, … Nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri,… Haya basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli katika Misri. Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani hata niende kwa Farao, … Musa akamwambia Bwana, Ee Bwana wangu, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako: Maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito. “Mimi ni wa midomo isiyotahiriwa, na Farao atanisikilizaje?” Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu, au kiziwi, au mwenye kuona, au kipofu? Si mimi Bwana? Basi sasa enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena…. Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, ni Fimbo. Akamwambia, Itupe chini. Akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia kutoka mbele yake. Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia. Akaunyosha mkono wake, akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake …. Akasema, Ee Bwana, nakusihi, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma. Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa.” Soma Kut. 2:15 hadi 4:13. {SR1: 93.1}

94

Matumizi Ya Funzo

Musa huyu wa mwisho ni Musa aliyebatili elimu isiyo sahihi. Kumbuka, yeye si mwepesi wa kusema, hana ufasaha, ulimi wake ni mzito, na “ wa midomo isiyotahiriwa “ (ambayo haijafunzwa). Hajui jinsi ya kumkaribia Farao. Yeye huogopa kwa wazo la kusimama mbele ya mfalme mkuu, jinsi zebaki husinyaa kutoka kwa upepo wa kaskazini, lakini ingawa Musa huyu ni mlemavu, ana ujasiri; yeye si mwoga. Anahatarisha maisha yake, kwa maana aliulizwa mara moja tu kumshika yule nyoka wa ajabu kwa mkia, na akafanya hivyo. Musa huyu sio mkuu wa taji, bali mchungaji wa kawaida tu. Mchungaji Musa ni mfano wa watu ambao wataleta matengenezo na kutumiwa wakati wa Kilio Kikuu”, kinacholetwa kwa mtazamo katika nukuu zifuatazo. Kunukuu Picha za Maisha, ukurasa wa 245: “Mungu anatwika mabega yasiyo na uzoefu mizigo. Anawafanya wafae kuwa waangalizi, kujasiri, na kujihatarisha pia.” Gombo la 5, ukurasa wa 82: “ Atawaamsha na kuwainua miongoni mwetu wale ambao wamefundishwa na kupakwa mafuta ya Roho Wake, badala ya kwa mafunzo ya nje ya taasisi za kisayansi.” {SR1: 94.1}

Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 300: “Isipokuwa wale ambao wanaweza kusaidia katika ______ waamshwe kwa hisia ya wajibu wao, hawataitambua kazi ya Mungu wakati kilio kikuu cha malaika wa tatu kitakaposikika. Wakati nuru inakwenda kuiangaza nchi, badala ya kuja kwa msaada wa Bwana, watataka kuifunga kazi Yake ili iafikiane na mawazo yao finyu. Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna itakayokuwa kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa wanadamu. Watakuwapo wale kati yetu siku zote watakaotaka kuthibiti kazi ya Mungu, kulazimisha hata hatua gani zitafanyika wakati kazi inasonga mbele chini ya uongozi wa yule malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua hatamu mikononi Mwake. Watendakazi watashangazwa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kuileta na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki.” Wale ambao wanahesabiwa kuwa watendakazi wazuri watahitaji kusogea karibu na Mungu, watahitaji mguso wa kiungu.” Pia soma Isaya 3. “Sio

95

watu wenye vipaji vikuu na vyeo ambao wanahitajika sana kuliko watu ambao ni wakuu katika imani, utakatifu, kujitoa wakfu, na upendo. Watu ambao ni wakuu kwa ajili ya Mungu na wakuu katika unyenyekevu, uaminifu, na kujikana nafsi, — juu ya hayo kuueneza ujumbe wa Mungu, maisha, na baraka kwa wanadamu, na kwa kuuendeleza ufalme Wake katika dunia yote.” Mapitio na Kutangaza, Feb. 20, 1930. {SR1: 94.2}

Fimbo Ya Mchungaji

Roho ya Unabii husema katika Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa 251, kwamba fimbo ya Musa ilikuwa nembo ya uwezo wa Mungu. Fimbo ya mchungaji: Nguvu ya Mungu; kondoo: watu wa Mungu; fimbo ya mchungaji ni kifaa ambacho hutumiwa kuwanasa kondoo. Fimbo katika hili ni kifaa ambacho hutumiwa kuwanasa watu. Inaweza kuwa nini? Haiwezi kuwa kitu kingine chochote ila ukweli fulani wa Biblia, wa ajabu, ulio wazi, na unaokata wenye makali kuwili ambao hauwezi kupingwa. Utakapofunuliwa, utazalisha nyoka (watu), au waongofu, kupitia kwa matengenezo. Lakini Wamisri walifanya lilo hilo pia, kwa sababu kila mtu alitupa chini fimbo yake, na zikawa nyoka, na labda zaidi kwa idadi, kwa sababu kila mtu alitupa chini fimbo yake, lakini walikuwa bandia. Nembo za unafiki (Wakristo bandia); bali fimbo ya Musa ilizimeza fimbo za Wamisri. Nembo ya ushindi kwa Israeli wa kweli. Tokeo lake ni upinzani, lakini Israeli wa kweli anashinda mwishowe. {SR1: 95.1}

Katika Gombo la 5, ukurasa wa 696 tunasoma: “Hawakusababisha kwa uhalisi fimbo zao kuwa nyoka, ila kwa uchawi, wakisaidiwa na mdanganyifu mkuu, aliyezifanya zionekane kama nyoka, kuigiza kazi ya Mungu.” Nembo ya taswira ya nje ya Ukristo kwa Waadventista wa Sabato. Lakini mtu anaweza kusema, Nini? Watu wa Mungu kufananishwa na nyoka? Mbona si kwa kondoo? Iwapo Kristo mpole na mnyenyekevu alifananishwa na nyoka wa shaba jangwani ambaye Musa alimwinua ili wana wa Israeli wamtazame, na kuponywa kutokana na kuumwa na nyoka wakali, basi watu wa Mungu wangefananishwa na nyoka pia. Ikiwa fimbo ingegeuzwa kuwa kondoo ingeharibu hiyo nembo, kwa maana watu 144,000 hawatakuwa kondoo katika zizi la kondoo na kutunzwa na mchungaji wa kidunia, bali ni kinyume chake.

96

Kwa sababu hii nyoka hutumiwa kama nembo, ikimaanisha hekima; hawezi kutishwa (isingekimbia kwa kuhofia chochote: Kinyume cha kondoo). Watajazwa na Roho Mtakatifu, watangaze ujumbe na washinde kwa ushujaa. “Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi, yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu. Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya Mataifa kati ya kabila nyingi mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo: Ambaye, akiwa anapita katikati hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.” Mika 5:7, 8. {SR1: 95.2}

Kifo Cha Mzaliwa Wa Kwanza

“Musa akasema, Bwana asema hivi, Kama usiku wa manane Mimi nitatoka nipite kati ya Misri: na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.” Kut. 11:4, 5. “Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa gerezani; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama….pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.” Kut. 12:29, 30. {SR1: 96.1}

Mzaliwa wa kwanza, nembo ya tabaka la ukuhani, uwakilishi wa Ezek. 9:6, sehemu ya mwisho “Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” “Tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa gerezani,” nembo ya Ezek. 9:6: “Waueni kabisa mzee na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake:… Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Nembo ya “mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe” nembo ya Isa. 63:18 na Isa. 64:1; Hesabu. 26:10. {SR1: 96.2}

“Katika kisa cha dhambi ya Akani, Mungu alimwambia Yoshua, ‘Sitakuwa tena nawe, isipokuwa uharibu kile kilichotiwa wakfu kati yako.’ Je! Tukio hili linalingana vipi na mwenendo unaofuatiliwa na wale ambao hawatapaza sauti yao dhidi ya dhambi na makosa, lakini ambao

97

huruma zao siku zote huelekezwa kwa wale wanaoitaabisha kambi ya Israeli na dhambi zao? Mungu akamwambia Yoshua, “Huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata utakapoondoa kile kitu kilichotiwa wakfu kati yako.” Alitangaza adhabu ambayo ingefuata uasi wa agano hili…. Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye wakamtwaa Akani mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo; wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema Mbona umetutaabisha hivi? Bwana atakutaabisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto baada ya kuwapiga kwa mawe.” Gombo la 3, ukurasa wa 267-8. {SR1: 96.3}

“Bwana akasema na Musa, akamwambia, Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.” Kut. 13:1, 2. Nembo ya ukuhani mpya, na mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe anayewakilisha mfumo wa msaada, au utunzi. “Laiti kesi kama ya Akani ingekuwa kati yetu, wapo wengi ambao wangewashtaki wale ambao wangeweza kutenda sehemu ya Yoshua kusaka makosa, kwamba wanayo roho ya uovu, ya kutafuta makosa. Mungu hapaswi kuchezewa shere, na maonyo Yake kupuuzwa na kudhihakiwa na watu wapotovu.” Gombo la 3, ukurasa 270. {SR1: 97.1}

Mwana-kondoo Wa Pasaka

“Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja:… nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule: na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla…. Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka: ni pasaka ya Bwana…. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo: Nami nitakapoiona ile damu,

98

Nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, Nitakapoipiga nchi ya Misri.” Kut. 12:3-13. {SR1: 97.2}

“Sherehe zote za sikukuu zilikuwa mifano ya kazi ya Kristo. Uokozi wa Israeli kutoka Misri ulikuwa funzo la kielezo au ukombozi, ambao Pasaka ilikusudiwa kuwekwa katika kumbukizi. Mwana-kondoo aliyechinjwa, mkate usiotiwa chachu, mganda wa malimbuko, ilimwakilisha Mwokozi.” Tumaini la Vizazi Vyote, ukurasa wa 77. {SR1: 98.1}

Mwana-kondoo humwakilisha Kristo. Isa. 53:7. {SR1: 98.2}

Mwana-kondoo ayechomwa juu ya moto, Roho wa Mungu. Mwa. 15:17; Matendo 2: 3; Law. 9:24. {SR1: 98.3}

Ulaji wa ile nyama: Kristo ndiye maisha yetu, kwa maana “ndani Yake tunaishi, na twatembea, na kuwa kwetu.” Yohana 6:53. {SR1: 98.4}

Viuno vilivyofungwa: Ukweli wa Mungu, Neno. Efe. 6:14. {SR1: 98.5}

Viatu miguuni: Utayari wa injili. Efe. 6:15. {SR1: 98.6}

Fimbo mkononi: Upanga wa Roho. Efe. 6:17. {SR1: 98.7}

Mtamla kwa haraka. Msisite; Jitayarishe; upelekaji wa haraka. Kut. 12:11. {SR1: 98.8}

Kut. 12:34, “Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.” {SR1: 98.9}

Chombo cha kukandia ni Biblia. Efe. 6:13. {SR1: 98.10}

Unga ni neno la Mungu lililo ndani yake [Biblia]. Ezek. 44:30 (mfano). {SR1: 98.11}

Usiotiwa chachu: Neno la Mungu ambalo halijachakachuliwa, na lazima lihifadhiwe hivyo. Ufu. 22:18. {SR1: 98.12}

Vyombo vya kukandia mabegani mwao: Humaanisha hakikisha unalo na Neno lote la Mungu siku zote pamoja nawe. Hivi ndivyo mtakavyotoka Misri. Efe. 6:13. “Utumwa huko Misri huwakilisha utumwa wa dhambi. Ahadi za ukombozi ni ahadi za injili. Nguvu iliyofunuliwa katika hukumu juu ya miungu ya Misri huashiria kipimo cha nguvu iliyotolewa kwa ukombozi kutoka kwa utumishi mgumu wa ‘mungu wa ulimwengu huu.’” Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. {SR1: 98.13}

Damu kwenye miimo ya mlango ni nembo ya “muhuri”, Ufunuo 7;

99

“alama,” Ezekieli 9 (Ufu. 7 na Ezek. 9, ni alama iyo hiyo au muhuri). Tazama Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 445. {SR1: 98.14}

Damu inayopakwa kwenye kizingiti cha juu ya mlango ni kiashirio kwamba muhuri, au alama ambayo watu 144,000 watatiwa muhuri kwayo, itaonekana. {SR1: 99.1}

“Mwimo wa mlango” na “kipaji cha uso” vyote vina maana sawa. Hatumaanishi kusema kwamba ni chapa fulani inayoonekana, au alama kwenye vipaji vya nyuso zao, bali “muhuri” wa tabia, kanuni, au sheria; kiwango kikiwa Neno safi la Mungu. Kwa hivyo wanapaka damu kwenye miimo ya mlango, na ndugu zao kanisani wanaweza kufahamu mabadiliko. {SR1: 99.2}

Wale tu ambao wanaweza kuwa na muhuri ni wale wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo (dhambi) yote ambayo hufanywa ndani ya kanisa. Lakini ikiwa yeyote atashiriki na kujaribu kuufunika uovu uliopo kanisani, basi wanaachwa bila muhuri. Soma Gombo la 5, ukurasa wa 207-12; Gombo la 3, ukurasa 266. {SR1: 99.3}

Bahari Ya Shamu /Nyekundu

Bahari ya Shamu huwakilisha Isaya 63. Edomu humaanisha “nyekundu.” “Edomu” ni Esau, ndugu pacha wa Yakobo. Jina lake lilibadilishwa kuwa Edomu kwa sababu aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa bakuli la “mchuzi mwekundu wa kusemethi”, na Esau mwenyewe alikuwa mwekundu, kwa hivyo, tunayo Bahari Nyekundu, mtu mwekundu, mchuzi mwekundu. Soma Esau na Yakobo, Sehemu ya 3. {SR1: 99.4}

“Bahari,” nembo ya “watu.” Ufu. 17:15. {SR1: 99.5}

Farao na jeshi lake: Wachochezi wakuu dhidi ya matengenezo. “Misri ilikuwa imestawisha shirika tata la kidini. Ilijivunia taasisi zake za kidini; iliwadharau watu hawa Israeli ambao hawakuabudu kulingana na dini maarufu, na ambao sasa, chini ya ujumbe wa matengenezo uliohubiriwa na Musa, walikuwa bado wanachukua msimamo wao kikamilifu kuwakilisha ukweli na sheria ya BWANA.” Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. {SR1: 99.6}

Bozra: zizi la kondoo (kanisa). Mika 2:12; Isa. 34:6. {SR1: 99.7}

Waedomi: Wale ambao waliuza haki yao ya kuzaliwa ili kuridhisha uchu wa kula. Wao hufanya tumbo zao kuwa mungu wao; wakiukaji wa matengenezo ya afya. Kwa maelezo zaidi tazama ukurasa 156, chini ya kichwa “Aliteswa kwa Ajili ya

100

Watu Wake.” “Utumwa huko Misri huwakilisha utumwa wa dhambi. Ahadi za ukombozi ni ahadi za injili. Nguvu iliyofunuliwa katika hukumu juu ya miungu ya Misri huashiria kipimo cha nguvu iliyotolewa kwa ukombozi kutoka kwa utumishi mgumu wa “mungu wa ulimwengu huu.” Ushindi mtukufu katika Bahari ya Shamu hutabiri ushindi ambao umehakikishwa kwa kila mtoto wa Mungu anayeamini.” Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. {SR1: 99.8}

Mlima Sinai

“Mwezi wa tatu, baada ya Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, siku iyo hiyo wakafika jangwa la Sinai.”… “Mungu akanena maneno haya yote, akisema, Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila Mimi.” Kut. 19:1; Kut. 20:1-3. Hapa ndipo ile miaka 430 ilikoma, kuanzia kwa Abramu alipoondoka Uru. Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 760. Hapa ndipo pale Musa alipangilia kanisa, wakati alipowateua wazee sabini, na pale Mungu alizungumza na watu Mwenyewe. Uzoefu pale Sinai ni nembo ya kupangiliwa upya kwa kanisa, — Mungu Mwenyewe analisimamia kundi. Tunasoma katika Gombo la 5, ukurasa wa 80: “Tumekuwa na mwelekeo wa kufikiri kwamba pale ambapo hakuna wachungaji waaminifu, hawawezi kuwapo Wakristo wakweli; lakini hii sivyo. Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji si waaminifu Yeye atachukua usimamizi wa kundi mwenyewe. Mungu hajawahi kamwe kulifanya kundi livitegemee kabisa vyombo vya kibinadamu. Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika upepeto mkuu utakaotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli.” {SR1: 100.1}

Kanisa Limepewa Jina Jipya

“Kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika;… Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu.” Ufu. 3:14-

101

16. Kumbuka kwamba uwepo wa jina la sasa — “Waadventista wa Sabato” ni la muda tu, vinginevyo jina hilo litatapikwa kutoka kinywani Mwake. “Na Mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya litakalotajwa na kinywa cha Bwana.” Isa. 62:2. “Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu [watu 144,000]: Kwa maana Bwana Mungu atakuua, naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine.” Isa. 65:15. Soma Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 300. {SR1: 100.2}

Hapa ndipo unabii wa Isaya katika sura ya 52:1 utakapotimizwa: “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu: Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Soma pia Isaya 4. Zef. 3:13 “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” {SR1: 101.1}

“Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu.” Unabii huu hata sasa haujawahi kukutana na utimizo wake katika historia ya kanisa, kwa maana wamekuwapo walio najisi siku zote kati yake; lakini tumshukuru Mungu kwa ahadi hii ya ukarimu. Chuo kinapiga kona. Je! Tumwombe Mungu kwamba tusianguke njiani wa kinapokata kona? “Likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ ‘litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 725. {SR1: 101.2}

Idadi Ya Israeli Ni Ngapi?

Imewekwa wazi kwamba Israeli ya kimwili ni picha ya Israeli ya ahadi. Katika vuguvugu la kutoka, makabila yote yalitoka Misri. Iwapo hii ni picha ya Israeli ya ahadi, basi makabila yote kumi na mawili lazima yatoke sasa pia. Makabila kumi na mawili lazima yaokoke maangamizo ya Ezekieli 9 (kifo cha mzaliwa wa kwanza), na Isaya 63 (Bahari Nyekundu). Idadi yao inasemekana kuwa 12,000 kutoka katika kila kabila, na kufanya jumla ya 144,000. Kwa sababu kwamba

102

wamepitia uzoefu wa aina hiyo kama Israeli ya zamani, wao (watu 144,000) wanauimba wimbo mpya wa Musa na Mwana-Kondoo. “Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia ndani yake Roho wake Mtakatifu? Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akamstarehesha: Ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.” Isa. 63:11-14. Maandiko haya hayawezi kutajwa kwa kundi lingine kuliko lile tunalozungumzia. {SR1: 101.3}

Ni Nini Kinachojumuisha Masalia?

Ufafanuzi wa “mabaki” ni: Kilichosalia baada ya utengo, kuondolewa, au kuharibiwa kwa sehemu. (Kamusi Sanifu). Mwanzo wa kanisa la Kristo katika siku za mitume haukuwapo “skrubu” kubwa tu iliyoanza kubingiriza, ikipungua na kupungua kwa karne zote, na sasa, tukiwa mwishoni mwa historia ya kanisa imekuwa sehemu ndogo zaidi, au iliyosalia. Lakini, kinyume chake, kanisa wakati huo lilikuwa limeanza tu kubingiriza, na lilikuwa na mwanzo mdogo tu. Limekuwa likibingiriza na kubingiriza, na likiingiza ndani wote katika kila kizazi, na mwishoni kabisa mwa historia ya kanisa kwa hakika ni mabaki. “Mabaki” humaanisha sehemu ndogo sana, kigae, au chembe. Bwana alisema mavuno ni mwishoni mwa dunia; malaika ndio wavunaji. Kisha yapo mavuno ya kuvunwa. “Mavuno” maana yake ni mkusanyiko wa mazao; kukusanya, kuhifadhi, au kuingizwa ndani. Kwa mujibu wa hili mavuno hakika humaanisha mabaki, lakini tu kinyume chake, kwa maana wakati wa mavuno tunakusanya ndani mengi. {SR1: 102.1}

Mabaki ya Israeli lazima wawe kitu kingine kuliko kile ambacho tumefikiri kuwa “mabaki” ni sehemu ndogo, au sehemu ambayo imesalia baada ya uharibifu. Uharibifu ni upepeto wenye nguvu, wakati wa kuchujwa ambao ni utengo wa matabaka mawili ndani ya kanisa (kutiwa muhuri kwa watu 144,000) kama ilivyotabiriwa katika Ezekieli 9, na Isaya 63. Wale wanaookoka ndiyo “mabaki.” Biblia haitoi ufafanuzi

103

mwingine wa “mabaki” kuliko ule uliopeanwa hapa. Tazama Law. 5:13; 2 Wafalme 19:4; Isa. 37:4; Ezra 9:8; Isa. 1:9; Isa. 11:11; Isa. 16:14; Yer. 44:28; Ezek. 6:8; Yoeli 2:32; Rum. 11:5; Ufu. 11:13. {SR1: 102.2}

Katika sura ya kumi na moja ya Isaya, limeandikwa tukio lilo hilo ambalo tumejaribu kuelezea hapa. Katika aya ya kumi na moja tunasoma kuhusu mabaki ambayo tunazungumza juu yake: “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena mara ya pili ili ajipatie watu wake waliosalia.” Isa. 11:11. Maandishi ya Awali, ukurasa wa 270: “Naliuliza maana ya upepeto nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi wa kweli kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu usiopinda. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” {SR1: 103.1}

Isa. 11:12, sehemu ya kwanza: “Naye atawatwekea mataifa bendera.” Tena tunasoma katika Isa. 66:19, “Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa.” Sura ya 63 ina kumbukumbu sawa na Isaya 59, sehemu ya aya ya 19, imenukuliwa hapa: “Basi wataliogopa jina la Bwana toka magharibi na utukufu wake toka maawio ya jua.” “Ishara” ni pana kutoka mashariki hadi magharibi, na ina maana kwa ulimwengu wote. “Uharibifu” ni “ishara” na mfano kwa mataifa, na “mabaki” ni wale waliosalia (watu 144,000). Kufuatia hili tunacho “Kilio Kikuu” (mavuno): “Wale ambao hupanda juu kwa kila hatua, na kustahimili kila jaribu, na kushinda, iwe kwa gharama iwayo yote wameutii ushauri wa Shahidi wa Kweli, na watapokea mvua ya vuli, na kwa hivyo kufanywa wafae kuhamishwa bila kuonja mauti.” Gombo la 1, ukurasa wa 187. “Akasema, La; msije mkayang’oa magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno: Na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu na myafunge matita matita ili mkayachome: Bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.” Mat. 13:29, 30. {SR1: 103.2}

Wazo lilo hilo pia linaungwa mkono katika Wazee wa Imani na Manabii,

104

ukurasa wa 541: “Sikukuu ya Vibanda haikuwa tu ya ukumbusho, bali ya mfano. Haikuonyesha tu nyuma kwa safari ya nyikani, bali, kama sherehe ya mavuno, ilisherehekewa kwa ukusanywaji wa mavuno ya nchi, na ilionyesha mbele kwa siku kuu ya kukusanya ya mwisho, wakati Bwana wa mavuno atawatuma wavunaji Wake kuyakusanya magugu pamoja katika matita kwa moto, na kuikusanya ngano ndani ya ghala Lake. Kwa wakati huo, waovu wote wataangamizwa.” (Wale walio nje ya kanisa.) {SR1: 103.3}

Kumbuka kwamba utengo unatukia mwanzoni tu mwanzoni mwa mavuno; pia ya kwamba magugu yanakusanywa kwanza. Utengo huo unatia alama mwanzo wa mavuno. Mavuno ni kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. (Ufu. 18:1). Katika wakati huu wa mavuno umati mkubwa (wa Ufu. 7:9) na mitende mikononi mwao unakusanywa. Wakati umati huu mkubwa unaundwa na kukusanywa ndani ya ghala Lake, wavunaji wanawafunga waovu kwa matita matita (wanatengwa, au kuwekwa kando kutoka kwa kanisa) kwa ghadhabu ya Mungu. Tazama Ufu. 14:19. {SR1: 104.1}

Wingu Mchana — Moto Usiku

“Bwana naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo ili awaongoze njiani, na usiku ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku; ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu. [Hakuwa Musa aliyewaongoza Israeli kutoka Misri, bali nguzo ya wingu iliyotangulia mbele za watu.] “Bwana naye akawatangulia…awaongoze njiani…wapate kusafiri mchana na usiku. Wala ile nguzo ya moto haikuondoka… mbele ya hao watu.” Kut. 13:21, 22. Kwa mujibu wa 1 Kor. 10:4, katika nguzo hii ya wingu mchana na nguzo ya moto usiku alikuwa Kristo mwenyewe: “Wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa Kristo.” Kwa hivyo tunaona kwamba Bwana Mwenyewe aliwaongoza Israeli watoke, na sio Musa. Watu pamoja na Musa walilifuata wingu. Yote aliyofanya Musa ni kuwafikishia watu maneno na maagizo aliyopokea kutoka kwa Bwana. {SR1: 104.2}

105

Huu ndio uzoefu wa Israeli wa kimwili, ambao tunauita picha ya Israeli wa ahadi. Iwapo hii ni kweli, basi watu 144,000 lazima wapate uzoefu uo huo wa kutoka kwa walimwengu (Misri). Gombo la 5, ukurasa wa 80: “Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji sio wa kweli atalisimamia kundi Mwenyewe.” Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 283: “Katika moja ya vifungu vya ajabu sana na vyenye faraja vya unabii wa Isaya mtajo umefanywa kwa nguzo ya wingu na moto kuwakilisha utunzi wa Mungu kwa watu Wake katika pambano kuu la mwisho na nguvu za uovu: ‘Bwana ataumba juu ya makao yote ya Mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku, kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia, na kujificha wakati wa tufani na mvua.’” Kwa hivyo, wazo la Israeli kuwa picha linaungwa mkono na Biblia na Roho ya Unabii. {SR1: 105.1}

Yusufu, Mfano Wa Kristo

Yusufu husimama kama mfano mkamilifu wa Kristo. Kwanza kabisa, jina “Yusufu” humaanisha “ yeye ataongeza.” Kwa hivyo Kristo aliongezea familia ya wanadamu kwa ya mbinguni. Iwapo dhambi yoyote ingeandikwa dhidi ya Yusufu, ingeharibu mfano huo, kwa sababu Kristo si mdhambi. Yusufu alipendwa na babaye kuliko ndugu zake wote. Kumhusu Kristo tunasoma katika Ebr. 1:9, “Umependa haki, umechukia maasi; kwa hivyo Mungu, naam, Mungu wako, amekutia mafuta na mafuta ya shangwe kupita wenzio.” {SR1: 105.2}

Yusufu alitumwa kwenda Misri kuhifadhi maisha ya ndugu zake katika miaka saba ya njaa. Vivyo hivyo, Kristo alishuka kuhifadhi maisha ya ndugu Zake katika ulimwengu huu wa dhambi, katika B.K. {SR1: 105.3}

Yusufu aliuzwa kwa Waishmaeli ambao walikuwa wana wa Ishmaeli, uzao wa Abrahamu wa kimwili. Vivyo hivyo, Kristo aliuzwa kwa makuhani, uzao wa Abrahamu, (Israeli wa kimwili). {SR1: 105.4}

Yusufu alikuwa liwali, na hakuna mtu aliyeweza kuinua mkono au mguu, katika nchi yote ya Misri, bila ufahamu wa Yusufu. Vivyo hivyo,

106

Kristo ni liwali juu ya ulimwengu (Misri), na hakuna mtu awezaye kuinua mkono au mguu bila ufahamu wa Kristo. {SR1: 105.5}

Jinsi alivyolikuwa mmoja tu juu ya Yusufu, yaani Farao, vivyo hivyo, yuko mmoja tu juu ya Kristo: Mungu, Baba. {SR1: 106.1}

Yusufu alikuwa na umri wa miaka 30 alipoanza kuwa liwali; Kristo alikuwa na umri wa miaka 30 alipotiwa mafuta. {SR1: 106.2}

Jinsi Yusufu alivyomwoa binti ya kuhani mwabudu sanamu, vivyo hivyo, Kristo anaoa kanisa Lake ambalo linaundwa na mataifa yaabuduo sanamu. {SR1: 106.3}

Jinsi Yusufu alivyokusanya nafaka katika miaka saba ya wingi katika maghala ili kulisha ulimwengu katika miaka saba ya njaa, vivyo hivyo, Kristo alilikusanya Neno la Mungu katika wakati wa Agano la Kale ndani ya ghala kubwa (Biblia) kulisha ulimwengu katika wakati wa Agano Jipya. Mtu anaweza kusema, Agano Jipya lilikuja katika B.K. Kweli, lakini Agano Jipya ni utimizo tu wa Agano la Kale. {SR1: 106.4}

Kama Yusufu asingekuwa liwali wa Misri kabla ya mwanzo wa miaka saba ya wingi, ingeharibu maana yake, na mfano huo basi usingekuwa umeonyesha kwamba Kristo alitawala kabla ya historia ya ulimwengu kuanza. Kwa hivyo tunaona Yusufu ni mfano mkamilifu wa Kristo. {SR1: 106.5}

Farao, Mfano Wa Viongozi

Yule Farao ambaye alimheshimu Yusufu ni mfano kamili wa kiongozi wa duniani wa kanisa la mitume. Kama Farao asingekuwa Mmisri angeharibu mfano huo. Misri, nembo ya ulimwengu, huashiria uongozi wa duniani uliochukuliwa kutoka ulimwenguni. Isingekuwa kwamba Farao alimheshimu Yusufu kuliko kila mtu huko Misri, au iwapo hangekuwa amewaamuru Wamisri kwenda kwa Yusufu ili wapate nafaka, ingekuwa imeharibu nembo ya uongozi wa kanisa katika siku za mitume, kwa maana walimtukuza na kumheshimu Kristo juu ya kila mtu katika ulimwengu wote, pia walimpendekeza Kristo kwa watu wa Mataifa kama mtoaji wa maisha yao. {SR1: 106.6}

Iwapo Farao wa kwanza hufanza mfano kamili wa uongozi wa kanisa katika siku za mitume basi lazima tumpokee Farao wa mwisho ambaye hamjui Yusufu, kama mfano kamili wa uongozi wa kanisa ambao umeacha kumfuata Kristo, Kiongozi wao. Gombo la 5, ukurasa

107

217: “Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri.” Kwa hivyo Israeli wa kweli (watu 144,000) walifanywa kuwa watumwa chini ya utumwa wa Wamisri (dhambi duniani). “Utumwa ndani ya Misri huwakilisha utumwa wa dhambi.” Mapitio na Kutangaza, Januari 23, 1930. “Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, vyote viko katika karamu zao: Lakini hawaiangalii kazi ya Bwana, wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao wanaona kiu sana. “ Isa. 5:12, 13. {SR1: 106.7}

Israeli ikiwa ni mfano wa vuguvugu hili la Ujio sio wazo jipya linalofikiriwa tu katika somo hili. Dhehebu lote huamini hivyo, kwa maana tunasoma katika Mapitio na Kutangaza ya Oktoba 10, 1929, taarifa zifuatazo: “Wakati vuguvugu la kutoka lilikuwa vuguvugu kubwa, vuguvugu la ujio wa pili litakuwa kubwa zaidi. Mungu atawatoa watu, sio katika taifa moja tu, bali kutoka katika kila taifa chini ya mbingu, na Yeye atawaongoza waingie Kanaani ya mbinguni. Vuguvugu hili la ujio, ambalo vuguvugu la kutoka lilikuwa mfano, tunaamini lilitabiriwa katika unabii katika lugha ya mchocheo ifuatayo: ‘Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili ili kuwaokoa watu Wake, waliosalia,’ ‘Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake;… kama vile ilivyokuwako kwa Israeli katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.’ Isaya 11:16.” {SR1: 107.1}

Neno “mfano” humaanisha sawa na neno “picha”. Kipiga-picha cha kwanza kabisa kubuniwa kiliitwa “mfano wa bati.” Kwa hivyo tunayo idhini ya dhehebu kwamba “Israeli wa kimwili” ni picha ya Israeli wa ahadi (watu 144,000). Jinsi Mungu alivyowaita Israeli kutoka Misri zamani, ndivyo ilivyo sasa, Mungu anaita kanisa Lake kutoka kwa walimwengu na ulimwengu, liweze kuwa watu waliotengwa, wa kipekee kwa heshima na utukufu Wake. Hili halimaanishi vuguvugu lingine, bali linamaanisha kwamba Mungu atashughulika na mwili mzima, na wale watakaookoka ni Israeli, watu 144,000. {SR1: 107.2}

Kunukuu Mapitio na Kutangaza, Mei 1, 1930: “Kila jambo ovu

108

lazima litikiswe kutoka kwa vuguvugu. Ndivyo ilivyokuwa katika vuguvugu la kutoka. Wakati dhambi ilikuwa kati ya watu, Bwana hakuliacha vuguvugu hilo ambao Alikuwa amelitoa Misri na kulianzisha lingine. Yeye hakuwaita waamini watoke ndani yake, lakini alitikisa kutokuamini hadi nje ya hilo vuguvugu [kwa maangamizo yaliyosababisha kifo chao]. Aliitakasa kwa kuweka kando kila kitu ambacho hakikuwa cha hilo vuguvugu ambalo Yeye alikuwa akiongoza kulingana na ahadi Yake. Kwa kisingizio kimoja au kingine, kutokuamini na mchafuko yaliondoka, ilhali vuguvugu lenyewe lilisonga mbele.” {SR1: 107.3}

Iwapo vuguvugu la kutoka ni picha ya lile la kweli, basi kipindi cha miaka 430 kilichounganishwa na Israeli ya kale lazima kizingatiwe na ile ya sasa. {SR1: 108.1}

Miaka 430 Ya Kukaa Pamoja Na Mateso

Kipindi cha miaka 430 cha kukaa ugenini pamoja na mateso na Abrahamu, Isaka, na Israeli, ambacho kilianza na Abrahamu alipoondoka Uru, hulingana na wakati wetu kutoka kwa Matengenezo na Luther, hadi kwa kutiwa muhuri Israeli ya ahadi (watu 144,000). Kunukuu Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 760: “Wakati halisi uliotumika Misri unaweza kuwa karibu miaka 215 tu. Biblia husema kwamba ‘kukaa ugenini kwa wana wa Israeli’ kulikuwa miaka 430. Abrahamu, Isaka, na Yakobo, mababu wa Waisraeli walikuwa wageni ndani ya Kanaani. Kipindi cha miaka 430 kilianzia kwa ahadi aliyopewa Abrahamu alipoamriwa kuondoka Uru ya Wakaldayo. Miaka 400 ya Mwa. 15:13 inaanzia kipindi cha baadaye. Kumbuka kwamba kipindi cha Miaka 400 sio tu wakati wa kukaa ugenini, bali cha mateso. Hiki, kulingana na Maandiko, lazima kihesabiwe kutoka kwa miaka thelathini baadaye, karibu wakati ambapo Ishmaeli, ‘aliyezaliwa kwa mwili, alivyomtesa yule [Isaka] aliyezaliwa kwa Roho.’ Gal. 4:29.” {SR1: 108.2}

Paulo, katika Gal. 3:15-17, husema kwamba tangu kufanywa kwa agano na Abrahamu hadi kwa kupeanwa sheria huko Sinai ilikuwa miaka 430. Kutoka kwa Maandiko haya basi, hatupaswi kuelewa kwamba Waisraeli walikuwa Misri miaka 400. Tazama Kut. 12:40. Kwa mujibu wa hii miaka 430 ilianzia kwa Abrahamu alipoondoka Uru, na kwishia

109

Mlima Sinai. Kwa hivyo inabidi tuzingatie kipindi hiki chote, tukianza na Abrahamu, ambacho kiko na wakati dhahiri wa hali fulani zilizopo. Mwanzoni mwa miaka 430, ibada ya sanamu ilitawala kila mahali: Abrahamu pekee ndiye aliyeitwa atoke. Hiyo ndio hali ya kiroho iliyotia alama mwanzo wa kipindi cha kinabii katika mfano wake. Vivyo hivyo mwanzo wa wakati wa nakala pacha au uakisi lazima kitiwe alama na wakati wa hali ya chini ya kiroho. Katika wakati wa Martin Luther tunao uzalishaji halisi wa uzoefu wa Abrahamu, kwa maana katika wakati wa Luther giza la kiroho na ibada ya sanamu ilitawala kila mahali. Abrahamu ni mfano unaofaa wa Luther. {SR1: 108.3}

Abrahamu aliitwa na Mungu kwa neno lililonenwa, Luther kwa lililoandikwa. Abrahamu ni baba wa imani; hali kadhalika Luther. Fundisho alilofunza Luther lilikuwa “mwenye haki ataishi kwa imani.” Ikiwa hii ni kweli, basi miaka 430 katika wakati wetu ilianza na Luther. Karibu mwaka 1500 B.K. Luther aligundua katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Urfurt, Biblia ya Kilatini, na akafurahi sana kwamba ilisheheni zaidi ya vifungu vilivyotumika kwa kawaida. Hivyo Mungu kwa neno Lake, alimwita Luther kutoka katika Rumi ya Upapa. {SR1: 109.1}

Tunacho kwanza, kipindi cha miaka 400 na kisha kikaongezwa hadi miaka 430. Kwa hivyo, tuna kipindi cha miaka 30 cha kushughulikia kwanza. Imeelezwa kwamba miaka 30 ilikoma wakati ambapo Ishmaeli alimtesa Isaka. Kwa mujibu wa hili, karibu mwaka 1530 B.K., jambo fulani lazima liwe lilitukia. Ni nini kilichotukia katika mwaka 1530? Maungamo ya Augsburg: Hati iliyotayarishwa na Luther ambayo iliwasilishwa na Waprotestanti kwa Mkutano wa Augsburg kwa Mfalme Charles wa 5, na Kongamano hilo, na kusainiwa na mataifa ya waprotestanti ilipitishwa kama imani yao, na walimpinga papa. Hili hufanana na Sara aliyeteta dhidi ya Hajiri na Ishmaeli walipoondoka katika nyumba ya Abrahamu, na uhakikisho wa agano la Ahadi ambalo lilifanywa na Isaka. Jinsi Sarah alivyoteta dhidi ya Hajiri na Ishmaeli, ndivyo Waprotestanti walivyoupinga utawala wa upapa. Hii ndilo haswa lililopaswa kutukia mwaka 1530 B.K. ili kufaa hilo tukio la unabii. {SR1: 109.2}

Wakati huo Isaka aliteswa na Ishmaeli, yeye (Isaka)

110

alikuwa na umri wa miaka mitano, na wakati Yakobo alipozaliwa, Isaka alikuwa na miaka 60; kwa hivyo, tunaongeza miaka 55 kwa 1530 ambayo inatuleta mwaka 1585 B.K. Ufafanuzi wa kipindi hiki utatolewa baadaye. Kutoka kwa kuzaliwa kwa Yakobo hadi wakati Israeli walipokwenda Misri ilikuwa miaka 130. Ukiongeza namba hii kwa 1585 inatupatia 1715 B.K. Ufafanuzi wa kipindi hiki pia utatolewa baadaye. Tangu wakati Israeli walikwenda Misri hadi kuzaliwa kwa Musa ilikuwa miaka 135. Kuongeza hii kwa 1715 inaleta jumla kwa 1850 B.K. Kipindi hiki kinatiwa alama na kuzaliwa kwa Musa, ambaye alikuwa tumaini, mkombozi, kwa ajili ya Israeli. {SR1: 109.3}

Ni nini kilichotukia mwaka 1850? Ushuhuda wa kwanza uliandikiwa kanisa na kupewa kichwa “Kwa Wale Wanaoupokea Muhuri Wa Mungu Aliye Hai.” Umesainiwa, E. G. White. Kwa hivyo kuzaliwa kwa Musa, tumaini la Israeli wa kimwili, hufanana na kuzaliwa kwa ushuhuda wa kwanza kwa kanisa, tumaini la Israeli wa ahadi, watu 144,000. Kwa hivyo tunaona uwiano mkamilifu katika mfano na uakisi. Tazama Chimbuko na Ustawi wa Waadventista wa Sabato, ukurasa wa 749. {SR1: 110.1}

Musa akiwa na umri wa miaka 40 alijaribu kuwakomboa Israeli, na akashindwa. Kuongeza miaka 40 kwa 1850, tunapata 1890 B.K. Je! Ni nini kilitokea kwa wakati huu? Taarifa ifuatayo ilifanywa na Dada White mwaka 1892: “Iwapo watu wa Mungu wangekuwa wameenda kufanya kazi kama walivyopaswa kuifanya mara baada ya mkutano wa Minneapolis katika mwaka 1888, dunia ingalikuwa imeonywa kwa miaka miwili na Bwana angalikuwa amekuja.” — Matangazo ya Baraza Kuu, 1892. (Dondoo hii ilitolewa na mchungaji wa Waadventista wa Sabato wa Los Angeles, Calif.) Karibu wakati uo huo (1890) Uhuru wa Kidini wa Kitaifa ulianzishwa na dhehebu. Hivyo jaribio na kutofaulu kwa uzoefu wa Musa kuwaweka huru Israeli kutoka katika utumwa wa Misri kunalingana na kuanzisha uhuru wa kidini, na watu wa Mungu walishindwa kutekeleza wajibu wao. “Jumuiya ya Uhuru wa Dini wa Kitaifa lilianzishwa Julai 21, 1889.” Chimbuko na Ustawi wa S.D.A., ukurasa 752. {SR1: 110.2}

Miaka arobaini baadaye Musa aliitwa na kutumwa tena Misri na akawaweka Israeli huru kutoka katika utumwa wa Misri. Kuongeza 40 kwa 1890 kunaleta jumla kwa 1930. Kipindi hiki kinapaswa kuwekwa alama na matengenezo na utakaso wa kanisa, kutimiza Malaki 3, na

111

Ezekieli 9. “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono Wake tena mara ya pili kuwaokoa mabaki ya watu Wake, waliosalia.” Isa. 11:11. {SR1: 110.3}

Vipindi viwili, 1585 na 1715, vitafafanuliwa sasa. 1585 huafikiana na kuzaliwa kwa Yakobo, na 1715 huafikiana na Israeli kuingia Misri. Kule kuingia Misri na watu sabini kulikuwa mfano wa kuzaliwa kwa Waadventista wa Sabato jinsi kulivyoelezwa kwa ukurasa wa 73-74, lakini Uadventista wa Sabato haukuzaliwa hadi mwaka 1845. Ili kupata ukweli wa vipindi hivi viwili lazima tuhesabu kurudi nyuma hadi kuzaliwa kwa Yakobo, kwa maana ni kuzaliwa tunakoshughulikia. Tunayo miaka 130 tangu kuingia Misri hadi kuzaliwa kwa Yakobo, na miaka 85 tangu kuzaliwa kwa Yakobo hadi kutoka kwa Abrahamu Uru. Kwa hivyo, lazima turudi nyuma na kuondoa kipindi cha miaka 85 ya kwanza (kutoka kuondoka Uru hadi kuzaliwa kwa Yakobo) kutoka 1930 na tunapata 1845. Kwa hivyo, tunapata mwaka wa kuzaliwa kwa Waadventista. Binti Ellen Harmon wakati huo alipata njozi yake ya kwanza na ilikuwa juu ya watu 144,000 (Israeli wa ahadi), na mswada wa kwanza uliochapishwa wakati huo juu ya ukweli wa Sabato uliitwa “Tumaini la Israeli.” Tazama Chimbuko na Ustawi wa Waadventista wa Sabato, ukurasa wa 749. {SR1: 111.1}

Sasa ondoa kipindi cha miaka 130 (tangu kuzaliwa kwa Yakobo hadi kuingia Misri) kutoka 1845 na tunapata 1715 B.K., mwaka ambao uliwekwa alama na Israeli kuingia Misri. Kwa hivyo, 1715, unakuwa mstari wa kugawanya kati ya Kanaani na Misri, jinsi Kristo alivyokuwa mstari wa kugawanya kati ya K.K. na B.K. Ona jinsi inavyofanana kwa chati. Iwapo hizi sanjari zilibuniwa na Mungu, basi mwanzo na mwisho wa unabii kama ulivyo kwa chati ifuatayo, utakuwa sahihi. {SR1: 111.2}

112

[Chati Ya Sanjari]

113

Hii ndio sababu tuna 1500 B.K. kama mwanzo wa unabii huu, na iwapo sanjari hizi zilibuniwa na Mungu, basi mwanzo na mwisho wa unabii kama ulivyo kwa chati hii, utakuwa sahihi. Tazama chati kwa unabii wa Ezekieli kwa ukurasa wa 133. {SR1: 113.1}

114

SEHEMU YA 5

UNABII WA EZEKIELI NNE,

(Yanayotukia Ndani Ya Siku 390)

“Maana nimekuagizia miaka ya uovu wao iwe kwako hesabu ya siku, yaani siku mia tatu na tisini: Ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli. Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda siku arobaini: siku moja kwa mwaka mmoja nimekuagizia.” Ezek. 4:5, 6. Unabii wa sura ya nne ya Ezekieli unapata utimizo wake katika siku zetu. Unabii huu hauwezekani kurejelea Israeli wa kimwili, ingawa inashughulikia kipindi cha miaka 430 kwa namna ile ile jinsi unabii uliotolewa kwa Abrahamu. “Akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yao, watawatumikia watu wale; nao watateswa muda wa miaka mia nne.” Mwa. 15:13. Lakini Kut. 12:40 husema, “Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini.” Kwa hivyo unabii kwa Abrahamu ulifanywa katika sehemu mbili, ya kwanza ikiwa miaka 400, na kisha hadi miaka 430. Unabii wa Ezekieli umefanywa haswa kwa namna ile ile, katika sehemu mbili, lakini sio kwa idadi sawa ya miaka katika kila sehemu. Badala ya miaka 400, tuna miaka 390, na badala ya miaka 30, tuna 40, ikifanya jumla sawa ya 430 katika kila kisa Iwapo unabii huu unarejelea unabii uliotolewa kwa Abrahamu, ingekuwapo idadi sawa ya miaka katika kila sehemu, lakini kwa vile haifanani, lazima kiwe kipindi kingine cha wakati. {SR1: 114.1}

Tena, unabii wa Israeli wa kimwili ni kwamba wangekaa ugenini na kuteswa miaka 430, lakini unabii huu wa Ezekieli husema katika aya ya 13, “Bwana akasema Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao hali kimetiwa unajisi kati ya mataifa Nitakakowafukuza.” Kwa hivyo ni dhahiri kwamba unabii huu unarejelea Kipindi kingine cha wakati, na uzoefu, kuliko kile cha uzoefu wa Israeli huko Misri. Unabii uliotolewa kwa Abrahamu wa miaka 430 ulikoma

115

wakati ambapo wana wa Israeli walitoka Misri, ambapo ni kwa mujibu wa tarehe ya Biblia (Toleo la Mfalme James) mwaka 1491 K.K. Kulingana na mpangilio uo huo wa wakati, kipindi cha miaka 430 ya wana wa Israeli kilikuwa kimemalizika miaka 896 kabla ya hata Ezekieli kupewa maono ya unabii wake, na aliuweka unabii huo katika siku za baadaye, kwa maana hutumia wakati ujao. “Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao hali kimetiwa unajisi.” Kwa hivyo haiwezekani kabisa kwa mtu kufanyiza hitimisho kwamba nabii hizi mbili zinashughulikia kipindi na uzoefu sawa wa Israeli kule Misri. {SR1: 114.2}

Kipindi hiki (na Ezekieli) hakikuwa kinarejelea Israeli ya kimwili katika wakati wa Ezekieli, kwa sababu Bwana alisema (Ezek. 4:5), “Maana Nimekuagizia miaka ya uovu wao, iwe kwako hesabu ya siku, yaani siku mia tatu na tisini: Ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli.” Katika aya hii Bwana alisema siku (au miaka) 390 ni kwa ajili ya uovu wa nyumba ya Israeli, lakini katika aya ijayo kipindi cha miaka 40 kinarejelea Yuda. “Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda siku arobaini.” Kwa hivyo, Israeli na Yuda wanatajwa. {SR1: 115.1}

Ufalme wa makabila kumi na mawili ya Israeli uligawanyika sehemu mbili katika miaka yao ya mapema; yaani, Israeli na Yuda. Lakini wakati Ezekieli alikuwa na maono haya palikuwa na mgawanyiko mmoja tu, kwa maana makabila kumi yalikuwa yametekwa na kupelekwa uhamishoni mwaka 721 K.K., miaka 126 kabla ya unabii huu kufanywa, kulingana na mpangilio uo huo. Ukiwa katika siku zijazo, unabii huo, basi, haungeweza kurejelea Israeli ya kimwili. Kipindi hiki cha miaka 430 hakijawahi kutumika kwa wakati wowote, au kwa watu, zamani, na kwa hivyo, haijawahi kufafanuliwa, sawa tu na nabii nyingi ambazo hazikueleweka hadi zilipokutana na utimizo wazo. Iwapo wakati wa utimizo wake umekuja, basi ndipo tu tutaweza kuelewa utabiri huu. {SR1: 115.2}

Tunaanza na aya ya nne na kuendelea (baadaye tutachukua tatu za kwanza, na aya mbili za mwisho). Israeli ya kimwili ilikuwa mfano wa Israeli ya ahadi (144,000), kama ilivyofafanuliwa kwenye ukurasa wa 64-113. Uzoefu wa wana wa Israeli huko Misri ulikuwa picha ya

116

dhehebu letu, kwa hivyo uzoefu wao unazalishwa tena katika kila jambo na watu hawa, na iwapo kuna miaka 430 iliyounganishwa na Israeli ya kimwili, basi kipindi hicho hicho cha wakati lazima kiunganishwe na ya kweli. Kipindi cha miaka 430 (na Arahamu) hakikuhusiana tu na Israeli ya zamani, bali na Abrahamu, Isaka, na Yakobo pia. Unabii kwa Abrahamu wa miaka 430 ulianza na mwito wa kutoka Uru, na ukakwishia Mlima Sinai; lakini hii miaka 430 iliyokwishia Mlima Sinai ilikuwa mfano jinsi ilivyoelezwa kwa ukurasa 108-109. {SR1: 115.3}

Miaka 430 ya mfano iliyotabiriwa kwa Abrahamu ilianza katika ya kweli (wakati wetu) na Martin Luther, kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 108-111, kwa hivyo nabii zote mbili — ule wa Abrahamu na ule wa Ezekieli — hurejelea kipindi hicho hicho katika wakati wetu. Ule wa Abrahamu husimama kama mfano, bali ule mwingine ni unabii wa moja kwa moja, na zote mbili zinaenda sambamba katika wakati wetu. Tunaweza kuwazia kwamba kipindi cha miaka 390 kilianza karibu mwaka 1500 B.K., (wakati Luther alipata Biblia), na kukoma katika mwaka 1890 B.K., pale ambapo kipindi cha miaka 40 kilianzia, ambacho kingekoma katika mwaka 1930. Hata hivyo, hatuwezi kuelezea siku au mwezi halisi, au hata mwaka, kwa sababu (1) hatujui siku halisi ya mwito wa Luther; (2) unabii hushughulika na mwaka wa Kiyahudi, au labda wa Kiebrania, kwa hivyo, ni suala la miezi ambayo hatuwezi kubainisha. Unaweza kwenda hadi mwaka 1931, au hata baadaye, iwapo zile sanjari jinsi zilivyoelezwa kwa chati, ukurasa wa 112, 113, hazikubuniwa na Mungu kuonyesha ukweli huu. Swali linaweza kuulizwa, Kwa nini Mungu atengeneze unabii maradufu kwa jambo lile lile? — kwa sababu unabii wa zamani (mfano) hutoa tu maelezo kutoka mwanzo wa ujumbe wa malaika wa tatu hadi kwa utimizo wa Ezekieli 9. Unabii wa Ezekieli hutoa habari hiyo kwa mapana na marefu tangu mwanzoni mwa matengenezo ya Luther hadi kwa Ezekieli 9, kutiwa alama watu 144,000, na kukikunjua chuo. (“Yote yanayohusiana na jambo hili bado hayajaeleweka, wala hayataeleweka mpaka chuo kikunjuliwe.” Gombo la 6, ukurasa wa 17.) {SR1: 116.1}

Kinaweka wazi kwamba kuna kipindi cha miaka 430 kuanzia kwa matengenezo ya Luther hadi kwa utakaso wa kanisa, kama tutakavyojitahidi kuthibitisha kwa unabii wa Ezekieli ambao tunanukuu hapa. “Tena wewe lala ubavu wako wa kushoto, ukauweke uovu wa nyumba ya Israeli

117

juu yake: kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala juu yake kwa kadiri hiyo utauchukua uovu wao. Maana nimekuagizia miaka ya uovu wao iwe kwako hesabu ya siku, yaani siku mia tatu na tisini: Ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli. Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda siku arobaini: siku moja kwa mwaka mmoja Nimekuagizia …. Pia ujipatie ngano, na shayiri, na maharagwe, na dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa nafaka hizo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako, yaani siku mia tatu na tisini utaula. Na chakula chako utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku moja: utakila kwa wakati wake. Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya sita ya hini: Utayanywa kwa wakati wake.” Ezek. 4:4-6, 9-11. {SR1: 116.2}

Ezekieli aliamriwa aulalie upande wake wa kushoto kwa siku 390 wakati ambao alipaswa kula na kunywa. Baada ya siku 390 kumalizika, lazima ageuke upande wake wa kulia na aulalie kwa siku arobaini, lakini katika wakati huu lazima asile. Siku 390 ni miaka halisi 390 kwa mujibu wa sehemu ya mwisho ya Ezek. 4:6. Jinsi ambavyo tumefanya matumizi, miaka 390 ilianza na Luther na kukoma katika mwaka 1890. Katika kipindi hiki cha wakati Ezekieli aliambiwa ale na kunywa akiwa ameulalia upande wake wa kushoto. Aliambiwa ale nini? — aina sita za chakula; yaani, ngano, shayiri, maharagwe, dengu, mtama, na kusemethi (pambizo). Hatupaswi kuelewa aina hizi sita kuwa ni chakula cha nyenzo ili kudumisha uhai wa mwili, lakini kama nembo za chakula cha kiroho (mafundisho) ya aina sita ili kudumisha maisha ya kiroho. Kama hizi hazingekuwa nembo za ukweli, Bwana asingemuuliza Ezekieli kupata idadi spesheli ya nafaka, na ya kwamba azitie katika chombo kimoja, na kuzioka ziwe keki fulani, na kula kwa wakati maalum, katika namna fulani, na kipimo cha maji kilichowekwa. Mafundisho haya sita yanaweza kuwakilishwa na hatua sita kwenda juu (Matengenezo; juhudi ya kulileta kanisa katika hali yake ya usafi). {SR1: 117.1}

118

Ngano, Nembo Ya Imani

Sehemu ya kwanza ya chakula cha kiroho au ukweli ambao tulipaswa kupokea, uliowakilishwa na ngano, ulikuwa “imani”, jinsi ulivyofundishwa na Luther, kwa maana fundisho lake lilikuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Ngano, iliyokuwa nembo ya fundisho ambalo Luther alitupatia lazima liwe kamilifu ndani yake lenyewe ili kufanya nembo kamili ya fundisho hilo. Ona ukweli wa ngano: Imekuwa ikitumika katika vizazi vyote, na kila mtu huitumia na ni vigumu kuishi bila hiyo. Vivyo hivyo, wote lazima wawe na fundisho la “imani.” “Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Yeye” ndivyo Biblia husema. Si Wakristo pekee, bali dini zingine lazima ziwe na imani na vile vile wao lazima watumie ngano. Hata mkafiri, na mkana Mungu lazima adhihirishe imani katika chochote anachoweza kuamini. Tunaweza kuona kwamba uvuvio ulitumia aina sahihi ya nembo kuliwakilisha fundisho la “imani.” {SR1: 118.1}

Shayiri, Nembo Ya Roho

Sehemu ya pili ya chakula, au ukweli ambao tulipaswa kupata uliwakilishwa na shayiri. John Knox alikuwa mtu aliyefuata ambaye alifanya hatua ya pili kwa kufundisha fundisho lililowakilishwa na shayiri ambalo lilikuwa ukweli wa “Roho Mtakatifu.” Shayiri haitumiwi kwa kawaida au sana kama ngano. Kwa kweli, watu wachache wangeitumia, na kwa hiyo, ni nadra sana. Watu wengi hawajui shayiri ni nini; ndivyo ilivyo na fundisho la “Roho Mtakatifu.” Wakati fundisho la Roho Mtakatifu linaaminiwa na baadhi ya Wakristo, haliaminiwi na wengine. Wengine hawaelewi ukweli wa Roho ni nini, kama vile wengine hawajui shayiri ni nini; kwa hivyo nembo inayowakilisha fundisho la pili ni kamilifu, kama ile ya kwanza. Uzoefu wa Gideoni na ndoto ya Wamidiani ya mkate wa shayiri ulioipindua hema huthibitisha vivyo hivyo. Soma Waamuzi 7:13, 14. {SR1: 118.2}

Kunde, Nembo Ya Neema

Kunde hutumika sana na kwa kawaida na watu wote na katika vizazi vyote sawia na ngano John Wesley, mtu wa tatu

119

Kwa jukwaa la utendaji kama mwana-matengenezo mkuu, alifanza hatua ya tatu kwenda juu kwa kufundisha fundisho la “Neema”, ambalo liliwakilishwa na kunde. Wote huamini katika neema. Kiasi kwamba watu hawamchi Mungu tena, na wameitangaza sheria Yake kuwa bure. Yeye ni mwenye neema sana, na ni mwingi wa rehema, wao husema, na kwa vile tuko chini ya neema, Mungu hatafanya mema wala mabaya. Hivyo, Wakristo siku hizi wamepotosha maana yake ya kweli, pia wote wanavyopenda kunde, na wamepotosha jina sahihi kwa kuyaita “nyama ya nguruwe na maharagwe.” Je! Ni nembo gani inayofaa zaidi ambayo ingechaguliwa kuwakilisha fundisho la neema kuliko ile ambayo Mungu amechagua? {SR1: 118.3}

Dengu, Mfano Wa Fundisho La Ubatizo Kwa Kuzamishwa

Dengu hutumika kuwakilisha sehemu ya nne ya ukweli. Alexander Campbell husifiwa kwa kuifanza hatua ya nne kwenda juu kwa kufundisha fundisho la ubatizo kwa kuzamishwa, lililowakilishwa na dengu. Aina za (dengu) zinazowakilisha fundisho la nne (ubatizo wa kuzamisha) hazijulikani au kutumika kama shayiri: ndivyo ilivyo kwa ukweli wa kuzamishwa. Ubatizo kwa kuzamishwa katika namna ya zamani haufanyiki kwa ujumla, pia kama dengu zisivyotumiwa kwa ujumla. Tena Mungu ametumia aina sahihi ya nembo kuwakilisha sehemu hii ya ukweli. {SR1: 119.1}

Mtama, Nembo Ya Siku 2300

Sehemu ya tano ya ukweli imewakilishwa na mtama, na mwana-matengenezo wa tano alikuwa William Miller. Alifundisha unabii wa Danieli 8:14, ambao ulikuwa fundisho la siku 2300. Mtama haujulikani sana, na wale wanaoujua husema ni wa thamani ndogo, nyasi za mwituni tu ambazo hazina thamani yoyote ya kilimo, na sisizotamanika na mtu yeyote. Walakini ni nafaka nzuri. Ndivyo ilivyo na fundisho lililofundishwa na Miller. Hakuna aliye na matumizi yoyote kwa hilo na Waadventista wa Sabato ndio watu pekee wanaolifundisha. Wale ambao hawalipokei fundisho hili husema kwamba halifai kitu, na humushtumu Miller kama nabii wa uongo. Ingawa ni unabii wa ajabu na hufunua ukweli mkuu, lakini watu hawaupokei. “Haufai kitu,

120

bila thamani ya kiroho, na hatuuhitaji”, ndicho kilio. Tena swali linaulizwa, Je! nembo iliyo bora kuliko mtama haikupatikana kuliwakilisha fundisho la siku 2300? {SR1: 119.2}

Kusemethi, Nembo Ya

Sabato Katika Uhusiano Na Patakatifu

Nafaka ya mwisho iliyotajwa katika unabii wa Ezekieli ni kusemethi, inayowakilisha ukweli wa sita au fundisho ambalo ni ukweli wa Sabato katika nuru jinsi ilivyotolewa na Dada E.G. White, katika uhusiano na Patakatifu pa mbinguni. Ufafanuzi wa “kusemethi” (ulivyo kwenye pambizo) kwa mujibu wa Kamusi Sanifu ni kama ifuatavyo: “Nafaka iliyo kati ya ngano na shayiri … Ilikuwa nafaka kuu ya Misri ya kale, ikiwa ni ngano nyekundu ya wakati wa Musa, lakini inakuzwa sasa haswa Uswisi, kusini mwa Ujerumani, na kaskazini mwa Uhispania.” {SR1: 120.1}

Kusemethi ni nafaka ya zamani, iliyotumika ndani ya Misri ya kale katika siku za Musa, na ilikuwa ngano nyekundu katika siku za Yusufu. Vivyo hivyo Sabato ni ukweli wa zamani ambao ulianzia katika Bustani ya Edeni, na ilikuwa tendo la mwisho la Uumbaji. Ilikuwa ukweli katika siku za Musa, mtu wa kwanza ndani ya Biblia ambaye alianzisha utunzaji wa Sabato. Kusemethi inajulikana kushinda mtama, na inayo thamani fulani ya kilimo, lakini katika sehemu fulani tu za dunia, pia jinsi Sabato inavyojulikana kuliko siku 2300. Je! Mtu yeyote atathubutu kusema hizi si nembo kamilifu, au ya kwamba ni ufasiri tu wa mtu fulani, na ni ajali tu, au imetokea tu, na bado zinafaana kikamilifu? Lakini hadi hapa ni awamu moja tu imefafanuliwa. {SR1: 120.2}

Zote Ndani Ya Chombo Kimoja

Bwana alimwambia nabii Ezekieli, “Ukazitie zote katika chombo kimoja” (Ezek. 4:9). Sasa itaangaliwa iwapo kweli aliyatia mafundisho haya yote katika chombo kimoja. Luther aliliamini fundisho alilofundisha, lakini adui mkuu aligharikisha kanisa kwa udanganyifu. Sio kwa kubishana na ukweli. La, hapana. Bali kupendekeza kwa watu kwamba sasa wanayo kweli yote, na ya kwamba kwa hakika walikuwa sawa,

121

na hivyo kufanya mioyo yao kuwa migumu dhidi ya nuru zaidi. Punde ukweli wa ziada ulikuja, lakini Shetani alikuwa tayari ameligharikisha kanisa na mawakala wake, na chuki iliamshwa dhidi ya nuru mpya. Tokeo lake lilikuwa kwamba wengi waliukataa ukweli. Wachache waliiona hiyo nuru na kama ilivyo kawaida, kanisa lilipiga kura kuwaondoa kanisani. Hitaji lilizalisha vuguvugu jipya, au dhehebu. Kama huo ndio umekuwa uzoefu na kanisa katika kila ukweli unaosonga mbele ukipanda juu hadi kwa wakati wetu. {SR1: 120.3}

Vivyo hivyo, ukweli uliowakilishwa na shayiri (Roho) ulikataliwa na wale waliokuwa wamelipokea fundisho lililowakilishwa na ngano (imani). Knox aliamini ukweli wote aliokuwa nao na pia ukweli wote ambao Luther alifundisha. Kwa hivyo ngano na shayiri zilikuwa katika chombo kimoja na kupelekwa kwa hatua ya pili. {SR1: 121.1}

Kisha sisi tuna ukweli unaofananishwa na kunde (neema) na iliowasilishwa na Wesley, ambaye aliamini pia kweli zilizofundishwa hapo awali na Luther na Knox, ambazo ziliwakilishwa na ngano na shayiri. Hatua ya tatu ilifanzwa, na ngano, shayiri, na kunde/maharagwe zilikuwa katika chombo kimoja. Ukweli wa nne uliwakilishwa na dengu (kubatizwa kwa kuzamishwa) na kufundishwa na Campbell, ambaye aliamini mafundisho ya Luther, Knox, na Wesley. Kwa hivyo ngano, shayiri, kunde na dengu zilipelekwa kwa hatua ya nne, na katika chombo kimoja. Ukweli wa tano (siku 2300) uliwakilishwa na mtama, na hatua hii kwenda juu ilifanywa na William Miller ambaye aliamini kweli zote zilizowakilishwa na ngano, shayiri, kunde, na dengu. Hatua ya tano ilifanzwa na aina tano za chakula cha ukweli zilibebwa katika chombo kimoja. {SR1: 121.2}

Sasa tunakuja kwa aina ya mwisho ya nafaka: “kusemethi” (Sabato), ikihusiana na hukumu. Je! Si ukweli kwamba dhehebu la Waadventista wa Sabato huziamini kweli hizi zote: Ngano (imani); shayiri (Roho Mtakatifu); kunde/maharagwe (neema); dengu (ubatizo wa kuzamishwa); mtama (siku 2300); kusemethi (Sabato, na ukweli wa patakatifu)? Itaonekana Bwana alisema, “Ukazitie zote katika chombo kimoja.” Hakusema katika vyombo viwili, au zaidi, ila katika kimoja. Hakuna watu wengine isipokuwa Waadventista wa Sabato ambao huamini katika siku 2300 (utakaso wa Patakatifu), na ni hili dhehebu (chombo)

122

ambalo hufundisha mafundisho hayo yote sita jinsi yanavyowakilishwa na hizo aina sita za vyakula. Hivyo unabii huu unapata utimizo wake katika siku zetu, na tunashangazwa na ugumu wa kuelewa hekima kuu ya Bwana Mungu wetu. {SR1: 121.3}

Mkate Wa Shayiri

Bwana alimwambia Ezekieli, “Nawe utakila kama mkate wa shayiri.” Ezek. 4:12. Kwa nini ngano, kunde/maharagwe, mtama, na kusemethi zilitengenezwa kama mkate wa shayiri? Kwa nini sio kama keki ya ngano, au keki ya nafaka zingine? Ukweli wa Roho Mtakatifu uliwakilishwa na shayiri; kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 118. Kwa sababu hii Ezekieli aliambiwa azioke ziwe mkate wa shayiri, kumaanisha ukweli ulikuja kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na sio kwa msaada wa wanadamu. {SR1: 122.1}

“Nitakutia Pingu”

Kunukuu Ezek. 4:8, tunasoma: “Na tazama, nitakutia pingu, wala hautageuka toka upande mmoja hata upande wa pili, hata utakapozitimiza siku za mazingiwa yako.” Nabii alipaswa kulalia upande wake wa kushoto siku 390. Katika wakati huu alipaswa kula aina hizo mbali mbali za chakula. Lakini mbona upande wa kushoto? Kwa nini si kulia? Kwa sababu nembo hiyo isingekuwa kamilifu iwapo angeulalia upande wake wa kulia ilhali akila. Tumbo la mwanadamu lina umbo la kitu kama hilali [mwezi mwandamo], na shingo nyembamba upande wa kulia kama mlango. Iwapo mtu analalia upande wake wa kushoto, mlango uko juu, dhidi ya nguvu za uvutano, na kwa hivyo itakuwa vigumu kumimina wenyewe, ambapo itasababisha chakula kubaki ndani yake. Zisingekuwa pingu ambazo Bwana alimfungia Ezekieli, angeweza kugeuka upande wake wa kulia, na hivyo kuharibu hiyo nembo. Maana yake ni kwamba ingawa adui mkuu alijaribu kutupa nje kwa lazima kila ukweli kwa kutumia chuki na visingizio, na kuwatupa nje ya kanisa wale waliokuwa wakifundisha kweli hizi mpya jinsi ilivyokuwa katika kila tukio hapo zamani, lakini Mungu alihakikisha kwamba kila ukweli ungesalia hadi Yeye atakapoziweka katika chombo kimoja, na ndivyo ilivyo. {SR1: 122.2}

“Utakunywa Maji Pia”

“Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya sita ya

123

hini: Utayanywa kwa wakati wake.” Ezek. 4:11. Maji, yanaponywewa hupeana uhai; bila hayo, haiwezekani kuwa na uhai. Kristo, akinena na mwanamke kisimani, alisema: “Bali yale maji nitakayompa ytakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujikia uzima wa milele.” Yohana 4:14. Kristo alitaja “maji” kama nembo ya uzima wa milele. Maana ya nembo ya kunywa maji na kula mikate ya shayiri ni kwamba roho ni kwamba nafsi hai zilipaswa kuokolewa kwa kila ukweli mpya (Roho wa uzima). {SR1: 122.3}

Chakula Kwa Kipimo — Maji Kwa Kipimo

Ezek. 4:10, 11 — “Na chakula chako utakachokula kitapimwa…. Utakunywa kwa kuyapima.” “Kipimo” na “uzito” ni nembo zinazoashiria kwamba Mungu angetoa ukweli kwa kipimo tu, kidogo kwa wakati. Jinsi unabii unavyosomeka, “utakula na kunywa kwa wakati wake”, na hivyo ndivyo Mungu amepeana nuru ndogo kwa wakati kadiri tuwezavyo kuelewa. Imekuja kwa mpangilio kamili wa Kibiblia: Imani, Roho, neema, ubatizo, wakati wa mwisho, na Sabato (Pumziko). {SR1: 123.1}

Abrahamu, baba wa waaminifu, ni nembo ya imani; Isaka, nembo ya Roho wa ukweli (jinsi ambavyo Biblia husema alizaliwa kwa njia ya Roho); Yakobo nembo ya neema, (maana jinsi alivyokuwa mtu mdhambi, lau isingekuwa neema ya Mungu, hangeweza kushinda). Vuguvugu la Kutoka ni nembo ya ubatizo, maana tunasoma katika 1 Kor. 10:2, “Wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari.” Maisha ya nyikani ni nembo ya swala la patakatifu mwishoni mwa siku 2300; ilikuwa nyikani ambapo patakatifu pa mbinguni palifafanuliwa na pa duniani. “Nchi ya ahadi” ni nembo ya pumziko la Sabato. Katika nchi ya ahadi walipaswa kupumzika iwapo wangaliwafukuza wapagani lakini kwa sababu ya kiburi cha kitaifa na kutokuamini, walishindwa kupata raha iliyoahidiwa. Uasi wa Israeli katika nchi ya ahadi ni nembo ya kushindwa kwetu kumtii Mungu kwa wakati huu wa sasa. {SR1: 123,2}

Elezo la Ezekieli 4:12, 14, 15

Unabii wa ajabu jinsi ulivyo, sehemu ya kusikitisha zaidi sasa inapaswa kusimuliwa.

124

Andiko ambalo karibu linanukuliwa labda halijawahi kusomwa hadharani au kurudufishwa tena katika fasihi, lakini ikiwa halingechambuliwa kamwe, kusomwa hadharani, au kuchapishwa, lakini kama halingechunguzwa, kusomwa hadharani, au kuchapishwa, Mungu hangeliweka katika Biblia. Walakini, liko humo, bila shaka kwa kusudi, na lazima lizingatiwe. Dondoo hiyo jinsi inavyopatikana katika Ezek. 4:12, 14, 15, husomeka ifuatavyo: — “Nawe utakioka mbele ya macho yao, juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu …. Ndipo nikasema, Ee Bwana Mungu! Tazama, roho yangu haikutiwa unajisi: Maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu au iliyoraruliwa na hayawani, wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu. Ndipo akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ng’ombe badala ya mashonde ya mwanadamu, nawe utauoka mkate wako juu ya hayo.” {SR1: 123.3}

Nabii aliambiwa kwamba hangeweza kutumia kuni, au makaa ya mawe kuoka mikate juu yake, lakini kwamba atumie “mashonde yatokayo katika mwanadamu.” Kwa Ezekieli ilikuwa yenye kuchukiza sana, na aliomba udhuru. Bwana alitoa idhini, sio kwa kulazimishwa, ila kwa ajili ya Ezekieli tu, kwa kumwambia Ezekieli auoke kwa “mashonde ya ng’ombe.” Aya ya 13 hutoa elezo la hiyo nembo kama ifuatavyo: “Bwana akasema,” ‘Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula mkate wao hali umetiwa unajisi kati ya Mataifa.’” Nembo hiyo ni: Kila sehemu ya ukweli ambao umekuja kufikia sasa, umetiwa unajisi, pamoja na ule wa mwisho (Sabato), bila kujali maagizo yote tuliyopewa, kanuni juu ya kanuni, na amri juu ya amri. Picha hiyo hutoa simulizi; nembo hazidanganyi. Badala ya kukerwa kwa sababu tunaambiwa makosa yetu, tunapaswa kumsifu Mungu tu kwamba kwa rehema Yake ametoa mwito wa matengenezo, ili tusiachwe tuangamie katika dhambi zetu, bali tumepewa nafasi ya kuchagua yule tutakayemtumikia. {SR1: 124.1}

Swali linaweza kuulizwa, Je! Tumeutiaje unajisi ukweli wa Mungu? Dondoo moja tu kati ya nyingi itanukuliwa hapa. Gombo la 1, ukurasa 471, 472: “Kosa kubwa limefanywa na baadhi ya watu wanaokiri ukweli wa sasa, kwa kuingiza biashara katika mkondo wa mfululizo wa mikutano,… Wachungaji wamesimama katika mimbari na kutoa mahubiri ya utakatifu, na kisha kwa kuingiza biashara, na kutenda sehemu ya muuzaji, hata katika nyumba ya Mungu….

125

mzigo wa kuuza machapisho yetu haupaswi kuwa juu ya wachungaji wanaotenda kazi katika neno na mafundisho.” Gombo la 8, ukurasa wa 250: “Nalimwona Mwalimu wetu [Kristo] akiyaonyesha mavazi ya kile kinachoitwa eti utakatifu. Aliyararua, Akaufunua wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha akanambia: ‘Je, huoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia? “Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba? Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu zinakosekana.’” Kwa hivyo tunao ushahidi kwamba kila ukweli hadi sasa umetiwa unajisi, ukiwemo wa Sabato. {SR1: 124.2}

Siku Arobaini, Na Yale Yanayotukia Ndani Yazo

Hadi hapa, miaka 390 imefafanuliwa, na sasa tutazingatia siku 40, — au miaka. Baada ya Ezekieli kumaliza siku 390, aliambiwa ageuke sasa upande wake wa kulia na aulalie siku 40. Tofauti na siku 390, hatakiwi kula chochote, bali afunge saumu siku zote arobaini, na katika kipindi hiki cha wakati lazima aulalie upande wake wa kulia. Jinsi tulivyoelezea hapo awali, iwapo mtu ataulalia upande wake wa kushoto tumbo haliwezi kumimina lenyewe; lakini sasa lazima aulalie upande wake wa kulia. Nafasi hii ingelipatia tumbo lake fursa ya kumimina lenyewe. Kwa kawaida, iwapo tumbo lingemimina na lisiweze kuchukua chakula kingine, angekuwa na njaa (nembo ya njaa ya kiroho). {SR1: 125.1}

Nembo hiyo ni kwamba, kanisa limekuwa likididimia kiroho kwa miaka arobaini, na halijakuwa na chakula kipya cha kiroho cha kujilisha. Wengine wanaweza kusema, “Tunayo Biblia na Shuhuda na hujilisha kwazo.” Ni kweli tumekuwa nazo, lakini zimefunikwa kwetu, kwa sababu hatukutumia ipasavyo ukweli tumewahi kupata, na ni ukweli kwamba kanisa halijapata nuru mpya kwa maandiko ambayo hayakueleweka miaka arobaini iliyopita. {SR1: 125.2}

Kipindi cha miaka arobaini kilianza mwaka 1890, kwa mujibu wa chati kwa ukurasa wa 112-113, ambapo wakati huo miaka 390 ilikoma. Wakati karibu umepita, na sasa lazima tupate chakula la sivyo tutakufa, na Mungu kwa rehema

126

Yake amewakumbuka watu Wake na anawatumia mwaliko wa kusogea karibu kwa karamu nyingine nzuri. {SR1: 125.3}

Je! Ninyi, ndugu mwaweza kusogea karibu kwa karamu kuu? Au mtatoa udhuru? Je! Mtasema, “Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame: tafadhali unisamehe.” Au jibu lako litakuwa, “Nimenunua ng’ombe jozi tano ninakwenda kuwajaribu.” Au litakuwa kwamba “nimeoa mke na kwa hivyo siwezi kuja.” Kumbuka kwamba “maskini, na vilema, na viwete, na vipofu”: Kutoka “katika njia kuu na vichochoro vya mji” hawatasita-sita; nyumba itajaa. “Kwa maana nawaambia, kwa hakuna hata mmoja kwa wale walioalikwa atakayeionja karamu yangu.” Tazama Luka 14:16-24. {SR1: 126.1}

Saba — Namba Kamilifu

Katika unabii huu tunapata mafungu sehemu sita pekee, na hatua sita tu zimefanywa. Luther, Knox, Wesley, Campbell, Miller na White. Namba “sita” sio namba kamilifu. Ni dhahiri basi, kwamba bado ipo sehemu nyingine itakayofuata, na hatua ya kupanda. “Saba” ni namba kamilifu, ya Kibiblia. Swali ni, Kwa nini sehemu ya saba haikujumuishwa katika unabii huu? Kwa sababu zile sita zilichafuliwa; zilitiwa unajisi kwa maandalizi ya mwanadamu, mawazo, na mipango ya mwanadamu imeingizwa na kufuatwa, ambayo, machoni pa Mungu ni kama “mashonde.” Haitakuwa hivyo kwa ile ya saba, kwa maana ndiyo ya mwisho; lazima iwe safi. Sehemu hii ya mwisho, safi na isiyo na unajisi, inawakilishwa na malaika wa Ufu. 18:1, “Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa na utukufu wake.” Ni kwa wakati huu ambapo unabii wa Isaya utatimizwa. Isa. 52:1, 2: “Amka, amka: jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, Mji Mtakatifu: Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; inuka, uketi, Ee Yerusalemu: Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa [kanisa safi la Mungu].” {SR1: 126.2}

Kumbuka sehemu ya mwisho ya aya ya kwanza: “Kwa maana tokea sasa hataingia

127

ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Wamekuwapo siku zote ndani ya kanisa watu wasiotahiriwa, na walio najisi, na wasio waongofu, katika historia yake yote, lakini hapa nabii anatangaza hawatakuwapo “tena.” Tumpe Mungu wetu shukrani kwa ahadi hii ya thamani, na kwa ufunuo wa Neno Lake. Zefania pia anatangaza, “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo, wala ulimi wa hadaa hautaonekana vinywani mwao; kwa maana watakula na kulala wala hapana mtu atakayewaogofya.” Katika Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa 725, tunasoma: “Likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” {SR1: 126.3}

Inaweza kufafanuliwa kwamba hii inatuleta kwa ufunguzi wa muhuri wa saba wa Ufu. 8:1. Kanisa kwa hatua ya saba, chini ya muhuri wa saba, na katika baragumu ya saba. Kwa hili tunajua kwamba tuko kwenye mipaka ya Umilele. Je! vinywa vya yeyote kati yetu vingeweza kutamka maneno haya, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, na sisi hatukuokoka?” Lakini tutaufikiaje ukamilifu huu? Haitakuwa rahisi. Isipokuwa tujitahidi kamwe hatutaifikia hatua hiyo, maana yule adui halegezi ukamba mmoja. Ameleta hitilafu kwenye njia yote, katika kila hatua, na kila sehemu ya ukweli, na mipango yake imeimarika sasa kuliko hapo awali. Walakini, unabii umetangaza kwamba watu 144,000 hawajamsujudia Baali, “na katika vinywa vyao haukuonekana uongo: Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.” Kwa wakati huu dhehebu linaajiri watenda kazi wa injili wapatao 10,000, lakini itakuwaje wakati 144,000 bila uongo, doa au kunyanzi, au kitu chochote kama hicho, wakiwa wamejazwa Roho wa Mungu, watazunguka ulimwengu? Huo ndio mwanzo wa hatua ya saba. Si ajabu nabii alitangaza, “tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” “Nami nitamfanya kuwa taifa lenye nguvu.” Mika 4:7. {SR1: 127.1}

Wakati unabii wa miaka 430 unapata mwanzo wake kwa Matengenezo na Luther, na wengine, funzo ni kwa wakati huu, na

128

watu katika kizazi hiki. Kamwe hapo kabla unabii huu haujawahi kueleweka, na mpaka sasa hakuna mtu aliyewahi kupokea mengi kutoka kwa huo, lakini wakati unapotimia, Mungu anaufanya ufahamike. Hivi ndivyo Amewaongoza watu Wake siku zote. Aya ambazo hazijafafanuliwa zitazingatiwa sasa. {SR1: 127.2}

Ukauhusuru/Ukauzingire

“Wewe nawe, mwanadamu, jipatie tofali, uliweke mbele yako, kisha chora juu yake mfano wa mji, yaani Yerusalemu.” Ezek. 4:1. Tafsiri ya Kiebrania husomeka: “Chora” juu yake mji; yaani “Yerusalemu,” (mji: Nembo ya ushirika wa kanisa). Ezekieli aliambiwa achore mji, na kuuita Yerusalemu, na lazima uchorwe kwa tofali. Karatasi au ngozi haingeweza, kwa maana isingekuwa ya kudumu kama tofali. Ukiwa umechorwa kwa tofali hauwezi kufutwa. Wazo ni kwamba unabii huo hakika utatimia, na baada ya hapo utakuwa historia, mtu hawezi kufuta vitu vilivyoonyeshwa; viko hapo kudumu kwa vizazi vyote. (Tofali lililotajwa hapa halijatengenezwa. Ni tofali asili la mwangaza, na huchimbwa kwa mabamba makubwa, ambayo katika sehemu fulani za nchi hiyo hupatikana kwa wingi. Hutumika kwa kiasi kikubwa au hasa kwa kuezekea na kutengeneza sakafu). {SR1: 128.1}

Ezek. 4:2: “Ukauhusuru, ukajenge ngome dhidi yake, na kufanya boma dhidi yake, ukaweke makambi pia juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa dhidi yake pande zote.” “Ukauhusuru”: Yaani, uuvamie mji (kanisa) na jeshi kuulazimisha ujisalimishe; jitahidi kupata umiliki wa mji, — kanisa. “Ukajenge ngome dhidi yake”: Ngome inayouzunguka mji huufanya uwe salama, kwa hivyo “ukajenge ngome dhidi yake” humaanisha kuhakikisha kwamba hakuna anayeponyoka. “Na kufanya boma dhidi yake”: neno “boma” katika tafsiri ya Kiyunani limetafsiriwa (Proho’mata), kumaanisha “migongo iliyoinika/milima”, ambayo ni tuta linaloizunguka ngome, na hivyo kufanya kila juhudi na tahadhari ili kuulinda mji. “Ukaweke makambi pia juu yake”: Yaani, fanya makao ya muda. Wazo ni, — fanya maandalizi ya kukaa hapo mpaka utakapouteka mji. “Na uweke magogo ya kuubomoa dhidi yake pande zote”: Au, kama ilivyo katika pambizo, “viongozi wakuu”: kumaanisha kifaa

129

cha kutumia kugonga au kuponda. “Ram” ni kondoo dume, ambaye hutumiwa kama nembo ya watu wa Mungu, nao watashambulia pande zote mpaka mji utakapotekwa. Kifaa ambacho wanatumia kushambulia ni Ukweli wa Biblia ulio wazi, unaokata na kusadikisha. {SR1: 128.2}

“Mji” (Yerusalemu) ni kanisa la Mungu; yaani, Waadventista wa Sabato (Israeli). Mungu Mwenyewe alilianzisha kanisa hili na nabii, na ipo tofauti kubwa kati ya kanisa hili, na makanisa katika wakati wa Matengenezo kuanzia wakati wa Luther na kuendelea. Mungu aliruhusu watu Wake wapigiwe kura kuondolewa kanisani na wengi katika nyakati zilizopita, na walilazimika kuanzisha vuguvugu lingine hadi kwa hatua inayofuata ambayo wangefanya, na kuendelea. Katika hali hii, Mungu atashughulikia mwili mzima. Wale wanaougua na kulia dhidi ya machukizo ambayo hufanywa kanisani watatiwa muhuri na yule mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi. Wale ambao wameamua kutenda uovu, yaani, kutenda kinyume na sheria zilizowekwa na Roho wa Mungu kupitia Shuhuda kwa kanisa wataangamizwa na watu watano walio na silaha za kuchinjia za Ezekieli 9. Hakuna anayeweza kuponyoka, kwa maana mji umezingirwa na kujengewa boma, na kulindwa. Ni ukweli, kwamba katika kila kizazi ambapo Mungu alionyesha ukweli na kusudi Lake katika maneno yaliyo wazi, baada ya kukataliwa, watu hao waliathirika kwa kisasi cha Mungu mwenye nguvu na mkuu. Kwa mfano, walioishi kabla ya gharika, miji ya Sodoma, Misri, Wakanaani, Babeli, na Yerusalemu wa zamani. {SR1: 129.1}

Utengo Katika Kanuni

“Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati yako na mji huo: ukaelekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.” Ezek. 4:3. “Ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati yako na mji huo [kanisa]”: Nembo ya utengo usioweza kupenyezwa kati ya makundi hayo mawili. Hili halimaanishi kwamba hawaoni, au hawasemi mmoja kwa mwingine, bali utengo katika kanuni, sheria, au mwongozo. “Ukaelekeze uso wako juu yake”: Jinsi jemadari wa majeshi anavyouelekeza uso wake dhidi ya taifa lingine, kwa nia ya kushinda. “Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli”: Ishara

130

ni kwa wale ambao wametiwa alama au muhuri; yaani, watu 144,000, kwa maana wao ni Israeli, wa Kweli. {SR1: 129.2}

Wakati Wa Njaa Ya Kiroho

“Tena Akaniambia, Mwanadamu, tazama, Nitalivunja tegemeo la chakula katika Yerusalemu: nao watakula mkate kwa kuupima, na kwa kuutunza sana; nao watakunywa maji kwa kuyapima, na kwa kushangaa; wapate kupungukiwa na mkate na maji, na kustaajabiana, na kukonda kwa sababu ya uovu wao.” Ezek. 4:16, 17. Aya ya 13 inauhusu wakati wa miaka 390; Ezek. 4:16, 17, hadi kwa wakati wa miaka arobaini. Mwanzo wa aya ya 16 huonyesha kwamba upo mkatizo katika unabii, kwa maana tunasoma: “Tena Akaniambia”, yaani, vile vile, au zaidi ya hayo. “Nitalivunja tegemeo la chakula katika Yerusalemu” (Nitakatiza, au nitapunguza). “Nao watakula mkate kwa kuupima na kwa kuutunza sana, nao watakunywa maji kwa kuyapima na kwa kushangaa”: Yaani, kiasi kidogo, mpaka chakula chao kitakapokwisha, na watapata njaa. “Kustaajabiana” (mshangao): Yaani, tunaweza kusema kwamba tunao ukweli, au ni watu wa Mungu, lakini hatuelewi mbona hivi na vile; nguvu imekosekana, na kuna kitu kibaya. {SR1: 130.1}

Aya ya 17 ni utimizo wa unabii ulio katika Ezek. 4:16. Toleo la Douay linaonekana kuifanya uwe wazi zaidi ambapo Ezek. 4:17, imenukuliwa hapa: “Ili kwamba chakula na maji yatakapokosekana kila mtu aanguke dhidi ya ndugu yake, na wadhoofike kwa uovu wao.” Mwanzo wa aya hiyo kwa Kiyunani, na Kibulgaria ni sawa isipokuwa neno “watu” limetumika badala ya “ndugu”. Tafsiri ya Kiebrania husema hivi: “Ili waweze kukosa chakula na maji, na kufadhaika kila mmoja na mwingine na kudhoofika kwa sababu ya uovu wao.” “Ili kwamba chakula na maji yatakapokosekana kila mtu aanguke” (Douay): Yaani, katika wakati wa kipindi cha miaka arobaini, watamaliza chakula chao, na maji (kiroho) na kuwa na njaa kweli kweli ili waweze kugundua makosa yao. Kunukuu Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 419: “Mungu anahitaji mambo fulani kwa watu Wake;

131

iwapo watasema, sitautoa moyo wangu uache kutenda jambo hili, Bwana huwaacha waendelee na uamuzi wao wa unaodhaniwa kuwa wa busara bila hekima ya mbinguni, mpaka andiko hili (Isa. 28:13) litimie. Usiseme, nitafuata mwongozo wa Bwana hadi kwa hatua fulani ambayo inalingana na uamuzi wangu, na kisha ushikilie maoni yako mwenyewe, ukikataa kufinyangwa katika mfano wa Bwana. Hebu swali liulizwe, Je! Haya ni mapenzi ya Bwana? Sio, Je! Haya ni maoni au uamuzi wa ________?” “Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo, na kule kidogo; ili waende, na kuanguka nyuma, na kuvunjika, na kunaswa, na kuchukuliwa.” Isa. 28:13. {SR1: 130.2}

Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 105-107: “Hatupaswi kufikiri, kama walivyofanya Wayahudi, kwamba maandishi na maoni yetu hayana makosa; sio na mapapa, kwamba watu fulani ndio walezi pekee wa ukweli na maarifa, ya kwamba watu hawana haki ya kuyachunguza Maandiko kwa ajili yao wenyewe, lakini lazima wapokee maelezo yaliyotolewa na Mababa wa kanisa …. Wale wanaoruhusu chuki izuie nia dhidi ya kuupokea ukweli hawawezi kupokea mnururisho mtakatifu. Hata sasa, wakati wazo la Maandiko linapowasilishwa, wengi hawahoji, Je! Ni kweli, — kwa upatano na neno la Mungu? ila, Ni nani anayeliunga mkono? na lisipokuja kupitia njia ambayo haswa huwafurahisha, hawalikubali. Wakiwa wameridhika kabisa na maoni yao wenyewe, kwamba hawatachunguza ushahidi wa Maandiko, na shauku ya kujifunza, bali hukataa kupendezwa, kwa sababu tu ya chuki zao. {SR1: 131.1}

“Bwana mara kwa mara hufanya kazi pale ambapo kamwe hatumtaraji Yeye; Yeye hutushangaza kwa kuzifunua nguvu Zake kupitia vyombo vya chaguo Lake mwenyewe, ilhali Yeye hupita kwa watu ambao tumewatazamia kuwa wale ambao nuru inapaswa kupitia ndani yao. Mungu hutaka tuupokee ukweli kwa sifa yake wenyewe, — kwa sababu ni ukweli…. Lakini jihadhari kukataa lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi

132

wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali. {SR1: 131.2}

“Hakuna mtu anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ilioko kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia hili, Yeye amesema, ‘Nimeweka mbele yako mlango ulio wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.’ Hata kama viongozi wetu wote wanaweza kukataa nuru na kweli, mlango huo utakuwa bado wazi. Bwana atawainua watu watakaowakabidhi watu ujumbe kwa wakati huu…. Tuseme ndugu alishikilia mtazamo ambao ulikuwa tofauti na wako, na aweze kuja kwako, akipendekeza kwamba uketi pamoja naye na mfanye uchunguzi wa jambo hilo katika Maandiko; je! utainuka, ukiwa umejaa chuki, na kushutumu maoni yake, ilhali ukikataa kumsikiliza bila ubaguzi? Njia pekee sahihi ingekuwa kuketi chini kama Wakristo, na kuchunguza msimamo uliowasilishwa, katika nuru ya neno la Mungu, ambalo litaufunua ukweli na kufichua makosa. Kudhihaki maoni yake hakutadhoofisha msimamo wake hata kidogo ukiwa ni wa uongo, au kutia nguvu msimamo wako iwapo ulikuwa wa kweli. Iwapo nguzo za imani yetu hazitasimama kwenye kipimo cha uchunguzi, ni wakati upasao tuweze kujua. Lazima isikuwepo roho ya Ufarisayo inayokuzwa kati yetu.” Ijapokuwa mtu anaweza kupinga kwa ukaidi matumizi ya moja kwa moja ya maandiko yaliyonukuliwa hapa, hakika hakuna atakayehoji somo lililofundishwa katika chapisho hili na bado adai kuwa kwa upatano na vuguvugu hilo. {SR1: 132.1}

133

[Chati ya Ezekieli Nne (Miaka 430)]

134

135

SEHEMU YA 6.

MUHTASARI WA ISAYA, SURA YA 54-56 KWA JUMLA

Mwito huu wa matengenezo kama ulivyoonyeshwa hapa ni tokeo la moja kwa moja la kusoma sura kumi na tatu katika kitabu cha Isaya, jinsi yalivyobuniwa na dhehebu la Waadventista wa Sabato na kuwasilishwa kwa makanisa katika dhehebu lote ulimwenguni. Masomo haya yalifundishwa katika idara ya Shule ya Sabato wakati wa Januari, Februari, na Machi ya mwaka 1929, na kuanzia sura ya 54, ilikoma na ya 66. Tunaamini mkono wa Mungu ulikuwa ukiongoza, na ya kwamba masomo haya yalikuja kwa wakati mwafaka kupitia maongozi ya Mungu, kwa nia ya kuwaamsha watu Wake kuchukua hatua kutoka kwa hali ya uvuguvugu ya Ulaodekia, na udhaifu wa kiroho. {SR1: 135.1}

Katika Gombo la 3, ukurasa wa 492, tunasoma: “Baraza Kuu, ambalo ni mamlaka ya juu kabisa ambayo Mungu anayo duniani.” (“Baraza Kuu” linalozungumziwa hapa sio maoni ya mtu mmoja, bali Kongamano Kuu la ndugu waliokusanyika kutoka sehemu zote za dunia, kama ilivyofafanuliwa katika Watendakazi wa Injili, ukurasa wa 489: “Lakini ikiwa, katika Baraza Kuu, uamuzi wa ndugu waliokongamana kutoka sehemu zote za dunia unatumiwa. Uhuru wa kibinafsi na uamuzi wa kibinafsi haupaswi kudumishwa kwa ukaidi lakini usalimishwe”). Kwa sababu hii, Mungu aliliheshimu Baraza Kuu, na akatuma masomo kupitia mkondo huo, kwa nia ya kuleta matengenezo ndani ya dhehebu lote katika robo moja ya masomo ya Shule ya Sabato. {SR1: 135.2}

Sura hizi kumi na tatu za Isaya ni barua moja endelevu iliyoandikwa kwa kanisa. Ingawa zimekuwa katika Biblia kwa karne nyingi, zilikusudiwa kwa ajili yetu wakati huu wa sasa, na husimama kama waraka wa moja kwa moja kwa kanisa sasa. Sura ya 54 ndio mwanzo wa barua, na hukoma na ya 66. Sababu zifuatazo zimetolewa kwa kuamini hivi. {SR1: 135.3}

Mwanzo wa Barua — “Mungu Wa Faraja” — Isaya 54

“Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako

136

kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu: Maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake aliyeolewa, asema Bwana.” Isa. 54:1. Sura ya nne ya Wagalatia husema mwanamke anayetajwa hapa, yule “tasa,” “yeye asiyekuwa na utungu,” “aliyeachwa,” ni Sara. Yule mwingine, aliyeitwa aliyeolewa, ni Hajiri. Sara ni aliyeachwa, kwa sababu alisogea kando na kumpa Hajiri mmewe kwa hivyo Hajiri ndiye aliyeolewa. Sara alikuwa tasa, hakuwa na mtoto, ilhali Hajiri alikuwa na Ishmaeli. {SR1: 135.4}

“Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa usiyezaa; paza sauti, ulie wewe usiye na utungu; maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume.” Gal. 4:27. Gal. 4:25, husema Hajiri huwakilisha kanisa la Agano la Kale au Yerusalemu huko Palestina. “Maana Hajiri huyu ni kama Mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa, na uko utumwani pamoja na watoto wake.” “Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi sote. Ndiposa, ndugu, sisi si watoto wa mjakazi bali tu watoto wa yule aliye mwungwana.” Gal. 4:26, 31. Kwa hivyo Sara (mwungwana) ni nembo ya Yerusalemu wa juu, au kanisa la Agano Jipya. {SR1: 136.1}

Ishmaeli huwakilisha watoto wa kanisa la Agano la Kale, bali Isaka, watoto wa kanisa la Agano Jipya (la Kikristo). “Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.” Gal. 4:28, 29. Kama vile Abrahamu alivyomfukuza mjakazi (Hajiri) na mtoto wake (Ishmaeli), ndivyo Mungu alivyolitupa nje kanisa la Agano la Kale, au Yerusalemu wa sasa. Gal. 4:30: “Lakini lasemaje Andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe; kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.” Andiko hilo linafanya mada hii kuwa wazi kabisa isieleweke vibaya. Sara ni nembo ya kanisa la Kikristo, na Hajiri, ya kanisa la Kiyahudi. {SR1: 136.2}

Tukifungua sura ya 54 ya Isaya, itagunduliwa kwamba sura hii imeelekezwa kwa mwanamke tasa, asiye na mtoto, na aliyeachwa, — Sara, ambaye ni nembo ya kanisa la Kikristo. Roho ya Unabii,

137

ikitoa maelezo juu ya sura hii, husema unabii huo ni wa kanisa la injili kwa wakati huu. Tunasoma katika Manabii na Wafalme, ukurasa wa 374, 375: “Akitazama mbali zaidi katika vizazi vingi, nabii aliona utimizo halisi wa ahadi hizi tukufu. Aliwaona wanaotangaza habari njema ya wokovu wakienda miisho ya dunia, kwa kila jamaa na watu. Alisikia Bwana akisema kulihusu kanisa la injili, ‘Tazama, Nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa Mataifa kama kijito kifurikacho;’ akasikia agizo: ‘Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako: usiwakataze, ongezea urefu wa kamba zako, vikaze vigingi vya hema yako, kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki Mataifa.’ Yehova alimwambia nabii huyo kwamba atatuma mashahidi Wake ‘kwa mataifa, Tarshishi, Puli, Ludi,…Tubali, na Yavani, visiwa vilivyo mbali.’ Nabii huyo alisikia sauti ya Mungu ikiliita kanisa Lake kwa kazi yake teule, ili njia iweze kutayarishwa kwa ajili ya kuukaribisha ufalme Wake wa milele.” {SR1: 136.3}

Unabii huu haungeweza kuwa kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya kanisa la Kikristo, kwa maana tunasoma katika Isa. 54:17 “Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.” “Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa”: Iwapo andiko hili lingerejelea sehemu ya kwanza ya kanisa, au kabla ya vizazi vya giza, basi Mungu angekuwa alishindwa kutekeleza ahadi Yake. Kumbuka kwamba tangu mwanzo wa kanisa la Kikristo mawe, panga, misalaba, kamba, moto, na zana zingine nyingi za kikatili ambazo ziliundwa dhidi ya kanisa zilifanikiwa, na zikaendelea kufanikiwa hadi karibu katikati ya karne ya 18, kwa hivyo Nabii hakuweza kutaja sehemu ya kwanza ya kanisa. Nukuu ifuatayo itathibitisha wakati ambao andiko hilo linatumika: “Watu wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako…. ‘Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa; na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu

138

utauhukumu kuwa mkosa.’… Likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’… Saa ya giza kuu ya pambano la kanisa na nguvu za uovu, ni ile inayotangulia mara siku ya ukombozi wake wa mwisho. Lakini anayemwamini Mungu hahitaji kuogopa; kwa maana ‘wakati mlipuko wa wale wa kutisha ni kama dhoruba dhidi ya ukuta,’ Mungu atakuwa kwa kanisa Lake ‘kimbilio kutoka kwa tufani.” Manabii na Wafalme, ukurasa wa 725. {SR1: 137.1}

Tena tunasoma katika Maandishi ya Awali, ukurasa wa 284, 285: “Watakatifu walipokuwa wakiondoka mijini na vijijini, walikimbizwa na waovu, ambao walitaka kuwaua. Lakini panga zilizoinuliwa kuwaua watu wa Mungu zilivunjika na kuanguka kwa udhaifu kama nyasi. Malaika wa Mungu waliwakinga watakatifu. Walipokuwa wakilia mchana na usiku ili kuokolewa, kilio chao kilikuja mbele ya Bwana.” Kwa hivyo tuna uthibitisho kwamba sura hiyo iliandikwa kwa ajili ya watu wa Mungu ambao wataishi wakati wa mwisho. Kusudi katika makala hii sio kufafanua yote yaliyomo katika sura hiyo, bali kuonyesha wakati ilipokusudiwa, na maelezo machache ya maagizo. Katika uchambuzi mwingine tutaweza kuchukua sura hizi zote kila moja peke yake, aya kwa aya. {SR1: 138.1}

Katika Isa. 54:14, 15, kuna faraja kubwa kwa ajili ya watu wa Mungu, na inapaswa kuimarisha imani yetu. “Utathibitika katika haki: Utakuwa mbali na kuonewa; kwa maana … yamkini watakusanyana, lakini si kwa shauri langu: Watu wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.” Wakati wa kutimizwa kwa aya hizi umeonyeshwa vyema katika Maandishi ya Awali, ukurasa wa 282, 283: “Naliona watakatifu, wakihama mijini na vijijini, na wakiungana pamoja katika makundi, na kuishi katika maeneo ya faragha zaidi. Malaika waliwapatia chakula na maji, ilhali waovu walikuwa wanateseka kwa njaa na kiu. Kisha naliwaona watu wakuu wa dunia wakishauriana, na Shetani na malaika zake wakijishughulisha kuwazunguka. Nikaiona hati, ambayo nakala zake zilitawanywa katika sehemu mbali mbali za nchi, zikitoa amri kwamba isipokuwa watakatifu waisalimishe imani yao ya kipekee, waiache Sabato, na kuiadhimisha siku ya kwanza ya juma, watu walikuwa huru baada ya muda fulani,

139

kuwaua. …lakini malaika katika umbo la watu wa vita waliwapigania. Shetani alitamani kuwa na fursa ya kuwaangamiza watakatifu wa Aliye Juu; lakini Yesu aliwaagiza malaika Zake kuwalinda… Kisha ukaja umati wa waovu wenye hasira, na tena umati wa malaika waovu, wakiwaharakisha waovu wawaue watakatifu. Lakini kabla waweze kuwafikia watu wa Mungu, waovu lazima kwanza walipite kundi hili la malaika watakatifu, wenye nguvu. Hili lilikuwa haliwezekani. Malaika wa Mungu walikuwa wakiwafanya warudi nyuma, na pia kusababisha malaika waovu waliokuwa wakiwasonga kuanguka nyuma.”{SR1: 138.2}

Isa. 54:11, 12, zinayo ahadi nyingine nzuri, na huonyesha usafi na utakatifu wa watu wa Mungu. “Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi. Nami nitafanya madirisha yako akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.” Maandiko haya hayawezi hata kidogo kutaja Yerusalemu Mpya, — Mji Mtakatifu, kwa maana hakuna dondoo iliofanywa kuhusu kuta za mji huo kwamba ziko na madirisha, wala hapawezi kuwa na hitaji lolote kwa ajili yake, maana ni malango kumi na mbili tu yametajwa. Isitoshe, malango yametengenezwa kwa lulu moja kubwa, na sio kwa almasi. (“Na yale malango kumi na mawili ni lulu kumi na mbili: Kila lango ni Lulu moja.” Ufu. 21:21.) Aya zinazozingatiwa wakati huu zinahusu nyumba ya kiroho ambayo hekalu la Sulemani lilikuwa nenbo yake. Nyumba hii ya kiroho inatajwa na Paulo katika Efe. 2:20-22 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema, na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.” {SR1: 139.1}

Kumbuka kwamba nyumba hii ya kiroho ina misingi, madirisha, malango, na mipaka (kuta). Misingi hurejelea mitume, Yesu Kristo Mwenyewe akiwa jiwe kuu la pembeni. Tazama Efe. 2:20. Madirisha ya nyumba hutumiwa kutoa mwangaza. Hili linarejelea manabii ambao hutabiri mambo kimbele na kutoa nuru juu ya mada jinsi ilivyo katika 1 Sam. 9:9, (“Hapo zamani katika Israeli, mtu

140

alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya, twende kwa mwonaji: Maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa mwonaji.”) “Malango” ya nyumba hutumika kwa kusudi la kuwaingiza wale ambao wana haki, na kuwazuilia nje wengine wote. Hili halingekuwa na maana nyingine isipokuwa walinzi kwenye kuta za Zayuni (ukasisi). “Mipaka” (kuta) humaanisha washiriki wa kanisa “mawe yaliyo hai.” 1 Pet. 2:5, “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.” {SR1: 139.2}

Kumbuka aina na ubora wa nyenzo zilizotumika hapa katika nyumba hii ya kiroho. Ni za thamani zaidi ya zinazojulikana kwa wanadamu — “Nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri” (Isa. 54:11). Misingi ya yakuti samawi, madirisha ya akiki nyekundu, malango ya alumasi, na mipaka ya mawe yapendezayo. Mfikirie Yesu kama jiwe kuu la pembeni lenye thamani; mitume, waliotoa dhabihu maisha yao, kama misingi ya ajabu; manabii (ambao wengi wao waliuawa kwa ukatili, hata kufikia kiwango cha kukatwa kwa msumeno kati ya magogo mawili), kama madirisha ya kutia nuru nyumba hii nzuri; na wale ndani ya kanisa katika wakati wa vizazi vya giza, walioathirika na kuteswa na watesi wakatili, kupamba kuta za nyumba hii ya utukufu zaidi, ya kiroho. {SR1: 140.1}

Kila mtu na ajiulize, Je! Nimefaa kutumika katika jengo hili la kiroho ambalo mawe yake yana rangi nzuri? Je! Niko tayari kumtumaini Mungu, na kuteseka kwa ajili Yake, lolote Atakaloruhusu kwa manufaa yangu? Au nautaka ulimwengu, na mbingu, pia? Je! Tunaweza kumtumikia Mungu na Mali? Je! Kwa njia yoyote tunaweza kupuuza maagizo tuliyopewa na Roho wa Mungu, na tutarajie kustahili kufaa kati ya wale ambao wangeridhia kufa, kuliko kutotii hata amri Zake ndogo kabisa? Ni wazo la kutissha kama nini. Je! Kanisa linaweza kubadilisha maagizo ya Mungu kwa mipango ya busara ya wanadamu? {SR1: 140.2}

Mungu Aita Turudi — Neno Ambalo Hubadilisha — Isaya 55

“Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; naam, njoni, nunueni divai

141

na maziwa bila fedha na bila thamani. Kwa nini kutoa fedha kwa kitu ambacho si chakula? na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.” Isa. 55:1, 2. Neno “Haya” humaanisha “kila mtu,” au “yeyote atakayesikia.” Haikuwa hivyo katika wakati wa Agano la Kale, kwa maana Myahudi wakati huo alifikiri Biblia ilikuwa ya uzao wa Abrahamu pekee. {SR1: 140.3}

“Njoni majini, naye asiye na fedha.” Maji ni kitu muhimu zaidi cha kudumisha uhai; kwa wanadamu, mnyama, na mimea. Ni kitu kipatikanacho kwa wingi zaidi, na bila hicho uhai hauwezi kuwapo. Katika aya hii yana maana ya kuwakilisha uhai wa kiroho, ambao umefungashwa na Umilele. Yesu, akinena kwa yule mwanamke kisimani, alisema, “Yeyote atakayekunywa maji Nitakayompa hataona kiu milele; bali maji Nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujikia uzima wa milele.” Yohana 4:14. {SR1: 141.1}

Maji hufanyizwa na vitu viwili; yaani oksijeni na haidrojeni. Bila haidrojeni uhai hauwezi kuwapo, na bila oksijeni, uhai ungekoma chini ya dakika kumi na tano. Maji hayauzwi kamwe; ni ya bure. Thamani tunayolipa mijini sio ya maji, bali ya huduma inayotolewa katika kuleta hitaji hili kwetu kwa matumizi ya kila siku. Wala hayauzwi katika Maandiko, lakini hutolewa bure. Hakuna thamani inayoweza kuwekwa kwa ajili ya uzima wa milele. Laiti ungaliuzwa, hakuna mtu angeweza kuununua, kwa hivyo nembo iliyotumika hapa ni kamilifu. Haingewezekana kutumia mbadala vitu vingine vya duniani kuwakilisha uhai wa kiroho. {SR1: 141.2}

Divai

“Naam, njoni, nunueni divai na maziwa bila fedha na bila thamani.” Ingawa maji ni bure, divai na maziwa huuzwa, lakini hakuna thamani iliyowekwa, wala ubadilishaji haufanywi kwa fedha. Kitu fulani lazima kitolewe katika biashara ili kufanya shughuli hiyo. Je! Chaweza kuwa nini? Jibu linapatikana katika aya ya saba, kama ifuatavyo: “Mtu mwovu na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, naye atamwonea rehema; atasamehe sana.” Sisi

142

lazima tuziache njia zetu na mawazo yetu, na badala yake, tuchukue mawazo ya Mungu na kufuata njia Zake. Isa. 55:8: “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu sio njia zangu, asema Bwana.” Sio mpaka baada ya shughuli hii kufanywa ndipo yeyote anaweza kumpendeza, kumtumikia, au kumwelewa Mungu, wala kuingia mbinguni. Wakati shughuli hii imefanywa, mawazo, njia, matumaini, matendo, na mwanadamu mzima kuwa amebadilishwa. Je! Tunapataje mawazo ya Mungu? Ni kwa njia moja tu yanaweza kupatikana. Mawazo na njia za Mungu hupatikana katika Neno Lake (Biblia). Mtu ambaye atafuata maagizo kamili kwa njia ya Roho wa Mungu yuko katika angahewa ya mbinguni, na hutembea na Mungu kama Henoko wa zamani. {SR1: 141.3}

Je! Divai na maziwa ni nini? Kwanza tutazungumza juu ya divai. Wakati maji yana oksijeni nyingi, divai ina madini mengi ya chuma. Kwa ukosefu wa chuma mwilini, oksijeni, haitakuwa na umuhimu wowote kwa mwili wa mwanadamu, maana chuma ndio treni ambamo oksijeni husafirishiwa katika mwili wote wa mwanadamu. Mara tu oksijeni inapoingia katika mapafu, chombo cha chuma huchukua elementi hiyo na kuisafirisha katika mwili mzima. Kwa hivyo, chochote kile divai huwakilisha, bila hiyo, maji (uhai) hayatakuwa na umuhimu wowote, na vile vile maji bila divai (kama nembo) hayatakuwa na umuhimu kabisa. Divai huwakilisha damu ya Kristo. Kwa hivyo, divai hutumika kwa uhusiano na meza ya Bwana; nembo ya damu iliyomwagika ya Kristo. Iwapo lazima uwe na uzima wa milele (maji), lazima pia uwe na damu ya Kristo (divai) kwa maana moja haitakuwa na thamani bila ile nyingine. Tena tunaona kwamba hakuna kibainishi kingine chochote cha duniani, kitu, au elementi inayoweza kutumika kuwakilisha damu ya Kristo. {SR1: 142.1}

Maziwa

Nembo inayofuata iliyotajwa ni maziwa, nayo pia, lazima iwe kamilifu ndani yake yenyewe ili kuonyesha ukweli uliokusudiwa na Roho wa Mungu. Mwili wa mwanadamu umeumbwa na elementi kumi na sita tofauti. Iwapo tutamaliza usambaziwaji kwetu wa moja ya vitu hivi, na maisha yasikome mara moja (kulingana na elementi inayokosekana), taabu itaweza kuwapo mahali fulani ndani ya mwili wa mwanadamu. Iwapo maziwa yangesheheni

143

elementi zote zinazohitajika kuudumisha mwili wa mwanadamu, maana ya nembo hiyo ingeonyesha kwamba nembo mbili za kwanza, au mafundisho hayana umuhimu wowote mkubwa. Kwa sababu maziwa hayana madini yote muhimu, huashiria kwamba fundisho linalowakilishwa na maziwa pekee halitoshi. (Madini ya chuma hayamo ndani ya maziwa. Ingawa chembe ya chuma hupatikana ndani ya maziwa, ni ndogo sana hivi kwamba inaweza kuelezwa kwa lugha ifuatayo: “Kiasi au madini ya chuma yanayopatikana katika galoni kumi [lita 40] za maziwa yanaweza kuwekwa ndani ya ukando wa jicho la mtu”). Yale ambayo hayapatikani ndani ya maziwa hutolewa na divai. Kwa hivyo mafundisho matatu yaliyofundishwa hapa hayawezi kutenganishwa moja kutoka kwa lingine. {SR1: 142.2}

Je! Ni fundisho gani lililofundishwa na maziwa? Nembo hii ni rahisi kuelewa. Maziwa huwakilisha Neno la Mungu linalopatikana katika Biblia. 1 Pet. 2:2, “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini ya akili maziwa ya neno, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu.” Neno la Mungu ni kamilifu na litatoa mafundisho (elementi) yote yanayohitajika kwa ajili ya moyo wa mwanadamu kutuwezesha tuwe wakamilifu, lakini bila umwagaji wa damu ya Kristo, hayatatunufaisha hata kidogo. Wala Neno na damu havingetusaidia sana iwapo hayakuwapo maisha ndani ya Mwana wa Mungu. Kwa hivyo, maji, divai, na maziwa vimechanganywa, na haviwezi kutenganishwa kimoja kutoka kwa kingine na bado vidumishe uzima wa milele. Nembo zilizo kamilifu sivyo? {SR1: 143.1}

Tuseme uweze kuongeza kitu ndani ya maziwa, hayatakuwa ya kigeni? Na iwapo ni ya kigeni kwa maziwa, hayatakuwa ya kigeni kwa mwili wa kibinadamu? Ikiwa hii ni kweli, lazima tuhitimishe yatakuwa sumu kwa mwili wa mwanadamu. “Lakini,” unasema, “tuseme nikiongeza elementi ya chuma, basi haitakuwa sumu.” Kwa kuongeza elementi nyingine, itaharibu maziwa, na hayatakuwa maziwa tena. Haiwezekani kwa hekima ya kibinadamu kuboresha kazi ya Mungu. Vivyo hivyo, haiwezekani kwetu kupuuza mojawapo wa maneno ya Mungu na bado tudumishe maisha ya kiroho, wala hatuwezi kuongeza, ingawa jambo hilo laweza kuwa nzuri, jinsi tunavyoliona. Litaharibu Neno, na halitakuwa Neno la Mungu tena, jinsi ambavyo maziwa hayatakuwa maziwa tena. Neno la Mungu lazima lihifadhiwe ndani ya moyo wa

144

mwanadamu, likiwa safi na bila kutiwa unajisi, iwapo lazima tuishi kwalo. “Vazi hili, lililofumwa katika kitanda cha mfumi wa mbinguni hakina ndani yake uzi mmoja wa ubunifu wa kibinadamu.” — Mafunzo ya Yesu kwa Mifano, ukurasa wa 311. {SR1: 143.2}

(Mtu anaweza kusema, iwapo maziwa sio lishe kamili, vipi mtoto mchanga anaweza kukuzwa kwa maziwa na bado awe na afya kamilifu? Mungu, ambaye alitengeneza maziwa, alijua kile mtoto huhitaji kwa ukuaji wake, na kile maziwa yanaweza kutoa, kwa hivyo Yeye amefanya uandalizi kabla mtoto hajazaliwa. Kati ya tumbo na utumbo mdogo, katika sehemu hiyo ya matumbo hupatikana “kidonge” kikubwa. “Kidonge” hiki huwekwa hapo kutoa madini ya chuma. Mlango wa kuingia utumbo mdogo, vile vile kwa tumbo, ni mdogo sana kwa hicho “kidonge” kupita ndani. Kwa hivyo kinalazimika kusalia hapo. Kila wakati lishe inapopita, hufyonza sehemu ya chuma; kwa hivyo elementi hiyo husambazwa, na mtoto hawezi kuwa na upungufu. Kadiri mtoto anavyozidi kukua, hicho “kidonge” hupungua polepole kwa kipimo. Kama ilivyo kwa mtoto wa mwanadamu, ndivyo ilivyo pia kwa uhai wa wanyama). Kwa kweli Mungu wetu hawezi kukosea na ni nani anayeweza kufahamu hekima Yake? {SR1: 144.1}

Kwa Nini Kutoa Fedha Kwa Kitu Ambacho Si Chakula?

“Kwa nini kutoa fedha kwa kitu ambacho si chakula? na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.” Isa. 55:2. Tunapotumia pesa zetu kwa chakula ambacho hakina madini yote yanayohitajika, au ikiwa ni cha uwiano usio sawa, basi sio jinsi Muumba alivyokitengeneza. Katika hali kama hiyo tumetumia fedha zetu kwa kile ambacho si “chakula.” {SR1: 144,2}

Wakati tunanunua chakula lazima tuwe waangalifu sana katika uteuzi wetu na tuhakikishe kwamba hakijatiwa unajisi, au Michakato ya utengenezaji, kutenganisha na kusaga. Katika vyakula kama hivyo madini yanayohitajika kudumisha afya ya mwili hayapatikani. Itakuwa tu ni kupoteza pesa kununua vyakula kama hivyo. Madhara mabaya yanayofanywa kwa utumiaji wa bidhaa hizi mbovu sio kwa pochi tu, bali kwa afya yake katika kupunguza nguvu zake za mwili. Utunzi wa mwili wa mwanadamu hutegemea usambazaji wa chakula tunachoupatia. {SR1: 144.3}

145

Baraka Kwa Myahudi NaMtu Wa Mataifa — Walinzi Vipofu — Isaya 56

Mwanzoni mwa sura hii Mungu anawauliza watu Wake, “shikeni hukumu mkatende haki.” Sababu iliyotolewa ni kwamba wokovu Wake u karibu kuja, na haki Yake kufunuliwa. Wazo ni kwamba chuo hivi karibuni kitapiga kona, na utaratibu wa sasa wa mambo lazima ubadilike. Iwapo walinzi ambao Mungu anazungumza nao hawataanza kuisafisha nyumba kwa ujumla, Mungu atalazimika kujipatia walinzi ambao watapaza sauti zao kama tarumbeta na kuwaonyesha watu Wake “makosa yao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Mungu, katika sura hii, anawauliza watu Wake utunzaji mwangalifu wa Sabato, bila kujali wao ni nani, bila ubaguzi wa tabaka, jamii, au watu. Kwa njia hiyo watapata ahadi ya agano Lake, na sadaka zao, na dhabihu zitakubaliwa juu ya madhabahu Yake. {SR1: 145.1}

Yapo mashtaka makali dhidi ya walinzi Wake kuhusu kushindwa kwao kushughulikia dhambi ndani ya kanisa na tokeo lake ni kwamba watu Wake wanaangamizwa na adui. “Walinzi Wake ni vipofu: Wote pia hawana maarifa, wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kubweka.” Isa. 56:10. Kirai “mbwa walio bubu” sio kuwadhalilisha, bali kimetumika hapa kama nembo. Kati ya wanyama wote mbwa ni rafiki bora wa mwanadamu, na ni shughuli ya mbwa kumlinda bwana wake, au kumwonya kuhusu hatari kwa sauti ya kubweka kwake. Lakini iwapo mbwa huyo atakuwa bubu na ashindwe kutoa sauti, basi hatakuwa tu asiye na maana kwa bwana wake ila ni hatari, maana hawezi kutegemewa. Kwa hivyo, “mbwa” ni nembo kamilifu ya mlinzi juu ya watu wa Mungu. {SR1: 145.2}

Mchungaji mzuri mwaminifu ni rafiki bora wa mwanadamu kwa kumwonya juu ya hatari inayohusika na dhambi, lakini iwapo huyo mchungaji hatapiga kamsa na kutoa onyo, basi amekuwa kama “mbwa aliye bubu.” Sio tu asiye na maana bali hatari, maana hivyo ndivyo kondoo wanaangamizwa na adui. Walinzi hawajashtakiwa tu kwa kutozishughulikia vyema dhambi zilizo ndani ya kanisa, lakini pia ni wenye tamaa. “Husema, njoni, nitaleta divai, na tunywe sana kileo.” Isa. 56:12. Hili hurejelea walinzi wale wale au watumishi walivyo katika Mat. 24:48-50, ambao ni walafi, hupuuza

146

matengenezo ya afya, na hawaioni hatari. Soma “Isaya Nabii wa Injili,” ukurasa wa 25, aya ya kwanza. Walinzi waliotajwa na nabii sio wale walioko Babeli (makanisa maarufu), bali “walinzi Wake” katika kanisa Lake la kweli. Kwa mujibu wa Shuhuda Wachungaji, ukurasa wa 445, Ezekieli 9 ni kutiwa muhuri kwa watu 144,000. Masimulizi juu ya unabii wa Ezekieli katika Gombo la 5, ukurasa wa 211, tunasoma: “Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao. Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu Wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaza sauti zao kamwe kama tarumbeta kuonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa walio bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” {SR1: 145.3}

Mwenye Haki Na Mwovu Katika Siku Ya Taabu — Isaya 57

Sura nzima ya 57 hushughulikia ibada ya sanamu ndani ya kanisa la Mungu. Watu wa Mungu waliitwa kutoka Babeli. Sababu mbona tumeitwa tutoke ni kwamba tunapaswa kuachana na mila za Babeli. Sura hii huufunua ukweli. Ingawa tulitoka huko, tulileta mila na ibada za sanamu ndani ya nyumba ya Mungu. Uovu unaozungumziwa katika sura hii ni utunzaji wa Krismasi na zawadi za Krismasi mmoja kwa mwenziwe. Aya y 9 husema, tumemheshimu mfalme (ibilisi) kwa kutenda hivi, na “kujishusha” wenyewe “hata kuzimu.” Hakika hii ni kweli. Sisi kama watu hutumia fedha za Bwana kuwaambia umma kwamba Krismasi sio siku ya kuzaliwa ya Kristo, na kisha hugeuka na kufanya jambo lile lile ambalo ulimwengu unafanya. Kwa njia kama hizi tunahusishwa katika unafiki wa hali ya juu. {SR1: 146.1}

Isa. 57:4, 5, na 6, huelezea kuhusu matendo maovu ya Israeli ya zamani, na

147

yameandikwa katika sura hii kufanya ulinganisho na watu sasa, kana kwamba kusema tunafanya sawa na wao huko nyuma, na sisi sio bora. Kunukuu Gombo la 1, ukurasa wa 129: “Naliona kwamba wengi wanaodai kuamini ukweli kwa siku hizi za mwisho, hufikiri ni ajabu kwamba wana wa Israeli walinung’unika walipokuwa wakisafiri; kwamba baada ya matendo ya ajabu ya Mungu pamoja nao, waweze kuwa wasio na shukrani hata kusahau Aliyokuwa amewafanyia. Malaika akasema, ‘Ninyi mmetenda vibaya sana kuliko wao.’” Ili kuifafanua sura nzima, lazima ichukuliwe aya kwa aya, lakini kwa kuwa ni refu sana, haiwezi kushughulikiwa kwa wakati huu wa sasa. {SR1: 146.2}

Saumu Ya Kweli — Sabato Imerejeshwa — Isaya 58

Isa. 58:1 — “Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Mungu huwauliza walinzi Wake kupiga kelele na wasiache jambo moja bila kufanywa; kupaza sauti zao kama tarumbeta, na wasiogope ni umbali gani sauti inaweza kufika; waonyeshe makosa na dhambi kwa watu Wake, kwa kuisafisha nyumba kwa ujumla, “kwa maana wokovu Wake u karibu kuja, na haki Yake kufunuliwa.” Kunukuu Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 427, tunasoma: “Isafishe kambi uharibifu huu wa maadili, hata ikiwaondoa watu katika nyadhifa za juu kabisa. Mungu hawezi kuchezewa-chezewa.” {SR1: 147.1}

Aya ya pili huelezea watu ambao Yeye anataka kunena nao. Sehemu ya kwanza ya aya ya tatu huelezea kuhusu malalamishi ambayo watu Wake wanafanya. “Tumefunga,” “na tumejitaabisha nafsi zetu, lakini sala zetu hazisikizwi.” Yeye haangalii, ndicho kilio chao. Sehemu ya mwisho ya aya hiyo inasimulia tatizo liko wapi: “Fahamuni, katika siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.” Mfungo huu hauwezi kuwa saumu ya chakula, kwa maana mtu anapofunga kwa chakula anaruhusiwa kupata raha, na kuzitenda kazi zake zote. Kwa kweli, mtu lazima ayatekeleze majukumu yake ya kila siku kama kawaida, ili asionyeshe taswira ya nje ya kufunga. Mwokozi wetu huhitaji kwamba jukumu hili lifanyike kwa uaminifu, na si kwa unafiki, kwa utukufu wa Mungu, na sio kwa kuwavutia na kujionyesha kwa watu.

148

Yesu alisema, “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki, wenye uso wa kukunjamana: Maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe, ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso, Ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; Mat. 6:16-18. {SR1: 147.2}

Tunaporudi kwa Isaya 58, aya ya 13, husimulia huu ni mfungo wa aina gani. “Kama ukigeuza mguu wako usihalifu Sabato, usifanye anasa yako katika siku ya utakatifu wangu; na ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana, yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutozifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe.” Kwa hivyo, saumu iliyotajwa hapa sio mfungo wa chakula, bali wa anasa, kazi na njia zetu na mawazo yetu, na ya kwamba lazima tumheshimu Mungu na kuitunza Sabato Yake takatifu. Shtaka ni kwamba, tunatenda kazi zetu zote siku ya Sabato. Kama watu tumesahau maana ya kweli ya kutunza Sabato. Tumekuja kudhani kwamba chochote kinachohusu dini kwa wingi au uchache charuhusiwa katika siku takatifu ya Mungu. Husemekana, Ni kazi ya Bwana. Lakini Mungu hajawahi kusema popote katika Maandiko kwamba watu Wake wako huru kufanya namna zote za kazi (zinazohusu dini) siku ya Sabato. Kazi ambayo inaweza kufanywa kwa siku nyingine isipokuwa Sabato si kazi ya Sabato. “Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote.” {SR1: 148.1}

Kumbuka jinsi ambavyo hiyo amri inavyosema: “Kazi yoyote.” Mungu hamaanishi kwamba tunaweza kufanya kazi zetu kwa siku sita, na Yake siku ya Sabato. Anasema ni siku ya kupumzika: Si pumziko la kimwili, bali ya kiroho. Kwa mfano, litakuwa kosa mmoja kuuza vitabu vizuri vya kidini siku ya Sabato, hata ikiwa atayaelekeza mapato yote kwa kanisa. Litakuwa kosa kwa daktari wa upasuaji kufanya upasuaji kwa wagonjwa siku ya Sabato ikiwa unaweza kufanywa wakati mwingine. Litakuwa kosa kwa muuguzi kupeana matibabu kwa wagonjwa siku ya Sabato iwapo haikuwa lazima kabisa. Soma Gombo la 7, ukurasa

149

106. Litakuwa kosa kwa baraza la kanisa kukutana siku ya Sabato na kujadili shughuli za kanisa, au kupanga mipango ya aina yoyote. Litakuwa kosa kwa mtunza Sabato kujitwika mzigo wa matangazo ya ki-injili kwa mfululizo wa mikutano, na kuyasambaza nyumba kwa nyumba siku ya Sabato. Aina hizi zote za kazi zinaweza kufanywa kwa siku nyingine isipokuwa Sabato. {SR1: 148.2}

Tunapofanya kazi ya namna hii siku ya Sabato, tunaifanya kujiokolea saa moja au zaidi ya siku kwa siku inayofuata, kwa hivyo tunamnyang’anya Mungu wakati Wake na kuuongeza kwa anasa zetu za kidunia. Ikiwa ni kosa kwa mtu kwenda kuuza vitabu vizuri vya kidini siku ya Sabato, ingawa ayaelekeze mapato yote kwa Kanisa, itakuwa ni kosa maradufu kuuza kitabu hicho hicho katika nyumba ya Mungu siku ya Sabato, bila kujali kitakachofanywa na mapato yake. Iwapo haya yote ni ya kweli, basi litakuwa ni kosa kwenda nje na karatasi za Ukusanyaji wa Mavuno na kupokea michango ya kupeleka ujumbe siku ya Sabato. Ni wakati mwafaka wa Mungu kuita umakini wetu kwa mambo haya. {SR1: 149.1}

Kunukuu Wazee wa Imani na Manabii, ukurasa wa 313, 314: “’Basi mtaishika hiyo Sabato, kwa kuwa ni takatifu kwenu…. Kwa kuwa kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.’ Maelekezo yalikuwa yametolewa punde, kwa ujenzi bila kukawia wa hema ya ibada kwa huduma ya Mungu; na sasa watu wanaweza kuhitimisha, kwa sababu lengo lililokuwa kwa mtazamo lilikuwa utukufu wa Mungu, na pia kwa sababu ya hitaji lao kubwa la mahali pa ibada, kwamba wangehalalishwa kufanya kazi kwenye jengo hilo siku ya Sabato. Ili kuwalinda kutokana na kosa hili, onyo lilitolewa. Hata utakatifu na uharaka wa kazi hiyo maalum kwa ajili ya Mungu si lazima iwaongoze kuihalifu siku Yake takatifu ya kupumzika” {SR1: 149.2}

Salio la sura ya 58, hufundisha kwamba lazima tuwatunze maskini na wagonjwa wa watu wetu, badala ya kuwapeleka kwa makao, au hospitali ya jimbo, iwapo tunataka kujifurahisha katika Bwana. Yapo mafunzo mengi ambayo tunaweza kupata kutoka kwa utumishi wa Israeli ya kale. Mungu aliwapa Sabato ya siku ya saba kama siku ya kupumzika kwa sifa na shukrani. Ingawa dhabihu ilikuwa takatifu, huduma ya kidini, iliyohitaji kazi nyingi, hawakuruhusiwa kuitekeleza katika Sabato ya siku ya saba.

150

Kwa sababu hii Mungu aliwapa Sabato za kila mwezi ambazo kwazo walipaswa kufanya kazi hiyo takatifu. Iwapo Mungu hakuruhusu kila namna ya huduma ya kidini kufanywa katika Sabato ya siku ya saba wakati huo, je! Yeye ataruhusu sasa? “Mimi Bwana si kigeugeu.” Soma Law. 23. {SR1: 149.3}

Mkombozi Aahidiwa Kwa Watu Wanaotubu — Isaya 59

Isa. 59:2-8, husimulia jinsi dhambi zetu ni mbaya na za kusikitisha mbele ya Mungu. Aya ya kwanza ina ahadi ya ajabu: “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia.” Ikiwa tutatubu dhambi zetu na kumurudia Yeye kwa kufunga na kuomba, Ataturehemu, na atayasikia maombi yetu. Ingawa dhambi zetu ni nyingi sisizoelezeka, Isa. 59:9-13, ni ya ripoti nzuri. Baadhi ya watu wanao ufahamu na wanatubu kutoka kwa dhambi zao. Katika Isa. 59:16-19, ni unabii wa kusikitisha sana kutaja. Unawahusu wale ambao walikuwa wametwikwa jukumu la kuleta matengenezo kwa kuwasilisha hayo masomo kwa kanisa katika nuru yake ya kweli, wakita kila dhambi kwa jina lake sahihi badala ya kuyahusisha kwa watu wengine na nyakati zingine, na hivyo kugeuza maagizo yaliyokusudiwa kwa kanisa. Mashauri katika Maandiko yalipuuzwa na hayakuzingatiwa, na lile ambalo Mungu alitarajia kwa watu Wake katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 1929, halikutimizwa, kwa sababu tu wale walio katika nyadhifa za uwajibikaji walishindwa kutekeleza wajibu wao. {SR1: 150.1}

Isa. 59:16, sehemu ya kwanza “Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi.” Mungu “alistaajabu.” Musa na Haruni “walisimama kati ya wafu na walio hai.” Hesabu. 16:48. Mungu alimtumia Eliya juu ya Mlima Karmeli. 1 Wafalme 18. Katika tatizo lililoletwa hapa, Mungu hapati mtu yeyote (Ezek. 22:30), kwa hivyo Yeye Mwenyewe anaingilia kati. {SR1: 150.2}

Isa. 59:16-18 “Basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia. Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake; akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho. Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao

151

wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.” Mungu hujivika sifa Zake Mwenyewe, na husonga mbele kurekebisha mambo. Laiti angekuwapo mtu, Mungu angemwachia mtu huyo aifanye hiyo kazi, lakini kwa sababu hakukuwapo mtu, Yuaifanya Mwenyewe. Hili huonyesha mojawapo ya kanuni za Mungu za kufanya kazi. Atatumia mtu mmoja, au taifa, kusaidia kurekebisha au kuadhibu lingine. Wakati hilo linaposhindwa kufanywa, Mungu huingilia kati. Wakati Mungu atakuja na kisasi kwa wengine, Yeye huja na wokovu kwa wengine. Isa. 59:20: “Na Mkombozi atakuja Zayuni.” Hili halimaanishi kuja kwa Kristo mara ya pili mawinguni, kwa maana litatukia kabla ya muda wa rehema kufungwa. Yeye haji na kisasi kwa wasiomcha Mungu katika ulimwengu, bali yuaja ndani ya kanisa. Na Yeye atakapokuja, Ataitenda kazi iliyotajwa katika Mal. 3:1-3. {SR1: 150.3}

Isa. 59:19: “Basi wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua.” Mungu ataufanya ujio huu kuwa mfano kwa mataifa, kama vile Alivyofanya na Sodoma na Gomora. Isa. 59:19, sehemu ya mwisho: “Wakati adui atakapokuja kama gharika, Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake.” Yohana katika Ufu. 12:15, huzungumzia tukio hili. “Nyoka akatoa katika kinywa chake nyuma ya huyo mwanamke, mafuriko amfanye kuchukuliwa na mto ule.” Mwanamke anayetajwa hapa ni kanisa la Mungu (Waadventista wa Sabato) “ambao huzishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.” “Mafuriko” sio sheria ya Jumapili, au mateso yoyote hapo zamani. Sheria ya jumapili ina mpangilio tofauti, na imefafanuliwa katika Ufunuo 13, kama utawala wa utesi utakaotekeleza alama ya mnyama. {SR1: 151.1}

“Mafuriko” ni sawa na “maji”, ambayo humaanisha watu (ndani ya kanisa) wasio waongofu, ambao Shetani huwatumia kusababisha kanisa lichukuliwe kwa namna ya utulivu, ili mtu yeyote asiushuku huo udanganyifu mkubwa. Kwa njia hii anajaribu kuwadanganya yamkini wateule (144,000) kama ingewezekana. Kwa vile haiwezekani, Kristo Mwenyewe anaingilia kati na kuwaokoa watu Wake (wale wanaougua na kulia dhidi ya machukizo yote kanisani) na wakati huo kuwafanya kuwa mfano wa wengine.

152

Ufu. 12:16, “Nchi ikamsaidia huyo mwanamke, nchi ikafunua kinywa chake, na kuyameza mafuriko yale aliyoyatoa yule joka katika kinywa chake.” Maana ni kwamba wanakufa, kwa kuzikwa ardhini, jinsi ilivyo katika Hes. 16:32, “Nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao, na wote walioshikamana na Kora na vyombo vyao vyote.” Kwa hivyo, “Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake.” Isa. 59:19, sehemu ya mwisho. Hili litatimiza Mat. 13:29, 30: “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno.” Utengo huo utatia alama mwanzo wa mavuno, ambayo ni Kilio Kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Ufu. 18:1. Roho wa Mungu anamiminwa juu ya watu Wake (wale wanao okoka mangamizo), na ahadi ni, kwamba haitaondoka kamwe. Isa. 59:21, “Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema Bwana; Roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema Bwana, tangu sasa na hata milele.” Soma “Isaya Nabii wa Injili,” Gombo la 3, ukurasa wa 43-49. {SR1: 151.2}

Mara tu utengo unapomalizika, na Shetani kupoteza na mpango wake wa udanganyifu, kanisa linajikuta katika pambano kubwa na adui. Ufu. 12:17, “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia [wale walioachwa], wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.” (Vita dhidi ya huyo mwanamke ni sheria ya jumapili). {SR1: 152.1}

Ushindi Wa Mwisho Wa Wenye Haki — Isaya 60

Sura hii huanza na maneno “Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia.” Mvua ya Vuli, Roho wa Mungu, na utukufu wa uweza Wake. Sura hiyo husimulia juu ya kukusanya wakati wa mavuno. Umati mkubwa unaojumuishwa na mataifa yote, na madaraja ya watu, matajiri na maskini pia, kutoka kila matabaka ya maisha; wafalme na watawala kati yao, na pia utajiri wa watu wa Mataifa utakuja kanisani. Taifa na

153

ufalme ambao hautawatumikia (kanisa) utaangamia. Umati uliokusanywa hapa ni wale walio na mitende mikononi mwao. Ufu. 7:9. {SR1: 152.2}

Isa. 60:19, 20, husimulia usafi wa kanisa la Mungu na utunzi Wake juu ya watu Wake. Isa. 60:21, husema, “Watu wako nao watakuwa wenye haki wote.” Wachafu na wasio waongofu hawataruhusiwa kanisani. “Amka amka; jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu mji mtakatifu: Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Isa. 52:1. “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; Wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao: Kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” Zeph. 3:13. Aya ya 22, ya Isaya 60: hutaja mafanikio yao katika kuziongoa roho kwa Kristo. {SR1: 153.1}

Wajenzi Wa Mahali Pa Kale Palipoharibiwa — Isaya 61

Aya ya kwanza na sehemu ya aya ya pili inamhusu Kristo Mwenyewe mwanzoni mwa ukasisi Wake. Roho ya Unabii husema utajirudia wenyewe na watu wa Mungu. Hili litatimia katika wakati wa mavuno, na watu 144,000 (wale ambao wataokoka maangamizo ya Isaya 59, na 63), ambao kwa juhudi zao umati mkubwa wa Ufu. 7:9, unafanzwa. {SR1: 153.2}

Isa. 61:2, “Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu.” Mwaka unaokubaliwa hauwezi kuwa wakati wa kinabii, maana ungemaanisha miaka 365. Lazima uwe mwaka halisi wa miezi kumi na mbili. Ipo sababu nzuri ya kuamini kwamba huu lazima uwe mwaka ambao yale masomo yalikuja, na ukweli ndani yake kufanywa ujulikane. Huu usingekuwa mwaka wa kinabii, mwito haungekuwa umekuja, maana Mungu hutunza wakati sahihi. Kwa Ninawi, Mungu alitoa siku arobaini kutubu. Sasa kwa watu Wake Anawapa mwaka mmoja kufanya mema, la sivyo Atalazimika kuwatapika kutoka katika kinywa Chake, na hili linawahusu wale ambao jukumu liko juu yao. “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika;… Nayajua matendo

154

yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto: Ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa changu.” Ufu. 3:14-16. “Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, angaliwaheshimu kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi. Lakini walijitenga kutoka kwa Mungu wakajitiisha kwa mvuto wa dunia, na Bwana akawakataa.” Gombo la 5, ukurasa wa 82. {SR1: 153.3}

Siku ya kisasi katika Isa. 61:2, inafuata mwaka. Siku hiyo inaweza kuwa ya kinabii, ambayo kwa hali hiyo, inamaanisha mwaka halisi. Kwa hivyo, inamaanisha mwaka katika kila kisa. Mwaka huu wa kisasi si mapigo saba ya mwisho, wala si kuangamizwa kwa waovu katika ujio wa pili wa Kristo. Unatukia kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema, maana katika Isa. 61:4 tunasoma: “Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.” Maana ya aya hii ni kuurejesha ukweli wa Mungu ambao umekanyagiwa chini ya miguu kwa vizazi vingi. Watu 144,000 — Israeli wa kweli wa Mungu — ndio wajenzi. Kwa hivyo, tunaona kwamba baada ya siku ya kisasi, ukweli wa Mungu utarejeshwa na kufunuliwa kwa watu. Kwa hivyo, lazima uwe kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema. Salio la sura hiyo huthibitisha wazo lilo hilo. {SR1: 154.1}

“Siku ya kisasi” ni sawa na katika Ezekieli 9; Isaya 63; na Isaya 61; kama ilivyoelezwa hapo awali. Isa. 61:6, ikimaanisha watu 144,000, husema wao ni makuhani, kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 37, 38. {SR1: 154.2}

Watu Watakatifu — Waliokombolewa Wa Bwana — Isaya 62

Katika Gombo la 3, ukurasa wa 65, wa “Isaya Nabii wa Injili,” tunasoma: “Sitanyamaza.” Mungu ananena. Ameazimia kwamba haki ya watu Wake itaonekana, na Yeye hatanyamaza hata itimizwe. Maneno hayaonyeshi uamuzi tu, bali pia kwamba umekuwapo ukawiaji, kwamba sasa tatizo limefika,

155

na ya kwamba Mungu yuko katika bidii kubwa kuona kazi imekamilishwa. Mungu amekusudia kuwafanya onyesho watu Wake ulimwenguni. Anataka kuonyesha kinachoweza kufanywa katika mwili wa mwanadamu; na Hatatulia ameridhika mpaka watu Wake waiakisi sura Yake kikamilifu. Wakati hilo limetimizwa, nchi itaangazwa kwa utukufu wa Mungu. Ufu. 18:1.” {SR1: 154.3}

Isa. 62:2: “Jina jipya.” Dalili ya uzoefu mpya ambao wamepitia, ambao ni utengo, au upepeto, kama ulivyofafanuliwa. Mungu Mwenyewe kwa kinywa Chake mwenyewe anapeana jina ili lisiweze kughushiwa. Wakati ambapo jina linapokelewa ni mwishoni mwa kipindi cha miaka 430 jinsi ilivyofafanuliwa kwenye chati kwa ukurasa wa 112-113. Kwa hivyo, kanisa limepangwa upya chini ya jina jipya. Jina la zamani, likiwa limetiwa unajisi, halingeweza kudumishwa tena. Hakuna mtu anayejiita kwa jina la zamani, maana wale ambao hawakustahili kuwa na jina jipya waliangamia chini ya mfano wa watu watano walio na silaha za kuchinjia za Ezekieli 9. Jina hilo linabaki tu kuwa laana. Katika Isa. 65:15, tunasoma: “Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule Wangu: Kwa maana Bwana Mungu atakuua, Naye atawaita watumishi Wake kwa jina lingine.” Utaratibu wa zamani wa mambo ukiwa umebadilishwa. Walinzi ambao hawakuwa waaminifu wameangamia. {SR1: 155.1}

“Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu, hawatanyamaza kamwe mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya.” Isa. 62:6. (Hawa ndio walinzi chini ya jina jipya.) Isa. 62:8 na 9, hufunua utunzi na ulinzi wa Mungu juu ya kanisa Lake. Katika aya ya 10 ni agizo la Mungu kwa watu Wake: “Piteni, piteni katika malango; itengenezeni njia ya watu; tutieni, tutieni barabara kuu; toeni mawe yake, twekeni bendera kwa ajili ya watu.” Katika aya ya 11 Mungu husema Ametangaza kwa watu watakaoishi mwishoni mwa ulumwengu: “Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Zayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu Yake i pamoja Naye, na kazi Yake i mbele Yake.” {SR1: 155.2}

156

Aliteswa Kwa Ajili Ya Watu Wake — Isaya 63

Isa. 63:1-3, “Ni nani huyu atokaye kutoka Edomu, na mavazi ya kutiwa damu kutoka Bozra? Huyu aliye mtukufu katika mavazi yake, anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Mimi ninenaye katika haki, hodari wa kuokoa. Kwa nini mavazi yako kuwa mekundu, na nguo zako kama za mtu akanyagaye shinikizo la zabibu? Nimelikanyaga shinikizo peke yangu, wala katika watu hakuwapo mtu pamoja Nami: Naam Nitawakanyaga kwa hasira yangu, na kuwaponda kwa ghadhabu Yangu; na mavazi Yangu yatatiwa madoa kwa damu yao, Nami Nitazichafua nguo Zangu zote.” {SR1: 156.1}

Sehemu ya mwisho ya sura iliyotangulia huzungumzia “watu watakatifu, waliokombolewa na Bwana.” Sehemu ya kwanza ya sura hii ni mintarafu wale ambao wamemkataa Bwana (wale ambao wataliacha jina kuwa laana). Kwao wao siku ya kulipiza kisasi imekuja. Picha hiyo si ya kupendeza kuitazama, lakini ni ya kweli. Ni “kazi ya ajabu” ya Mungu. Edomu ni jina lingine la Esau. Tazama Mwanzo 25:30. Esau alibadilishwa jina lake kwa sababu aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa bakuli la mchuzi wa dengu. Daraja lililo hapa linaitwa Edomu kwa sababu wameuza haki yao ya kuzaliwa kwa kujitosheleza nafsi ili kuridhisha tamaa, mungu wa hamu ya kula (kuyapuuza matengenezo ya afya), kama ilivyofafanuliwa kwa ukurasa wa 59, 60. “Bozra” ni jina la mji. Jina hilo humaanisha “zizi la kondoo,” nembo ya kanisa. {SR1: 156.2}

Isa. 63:4: “Maana siku ya kisasi i moyoni Mwangu, na mwaka wa waliokombolewa Wangu umekuja.” Kumbuka, “siku ya kisasi” Bwana asema i ndani ya “moyo” Wake, lakini “ mwaka wa waliokombolewa Wangu umekuja.” Kumbuka kitenzi “umekuja” kiko katika wakati wa sasa, kama vile Ufu. 14:7, “Akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja.” Sisi, kama watu, hushikilia kwamba kitenzi “imekuja” kiliandikwa katika wakati wa sasa kwa sababu hukumu mbinguni ilifanyika (mwishoni mwa siku 2300 za unabii wa Danieli) mwaka 1844, lakini haikueleweka hadi baada ya kipindi cha Kinabii kilipokuwa kimepita, kwa hivyo Mungu hakukusudia kufanya hukumu ijulikane

157

hadi baada ya saa hiyo kuja. Kwa sababu hii Uvuvio uliandika tukio hilo katika wakati wa sasa, “imekuja,” ili kiweze kuwa sahihi kisarufi. Kwa hivyo William Miller alifanya makosa ya tukio hilo kutimia mwishoni mwa siku 2300; yaani, ukweli wa patakatifu, Yesu alipokuwa akiingia Patakatifu Mno, na kuanza hukumu. {SR1: 156.3}

Iwapo andiko lililotangulia ni hakika, basi lile katika Isa. 63:4, ni la kutegemewa kama liwalo lolote. Sura hii, au tukio lililoandikwa ndani yake, kamwe halijawahi kueleweka, kwa hivyo lazima Mungu alikuwa ameuhifadhi unabii huo kwa muda fulani. Sasa unabii umeeleweka na ukiwa katika wakati wa sasa, lazima tuamini, basi, kwamba “mwaka wa waliokombolewa Wake umekuja.” Ikiwa mtu hatauamini ufasiri iliotolewa, basi anamaanisha kusema Mungu amekosea kuandika kitenzi hicho katika wakati wa sasa. Hili laweza kusemwa iwapo si kwa maneno, basi kwa tendo. {SR1: 157.1}

Waliokombolewa Wake

Nini maana ya “waliokombolewa Wake?” “Maana siku ya kisasi i moyoni Mwangu, na mwaka wa waliokombolewa Wangu umekuja.” Isa. 63:4. Hapa umerejezwa kwa Kut. 15:13, ambao ni wimbo Musa na wana wa Israeli waliimba baada ya kuokolewa kutoka Misri na kwa Bahari ya Shamu. “Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa; kwa uweza wako Uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.” Kut. 15:13. Uvuvio hutumia neno lile lile “waliokombolewa” katika wimbo wa ukombozi. Uzoefu wa Israeli ukiwa mfano wa Israeli, wa kweli, (watu 144,000), na nakala ya kanisa sasa, kama ilivyoelezwa katika Sehemu ya 4 sisi pia, lazima tukombolewe kama wao. Kwa sababu hii, nabii alitumia kifungu “mwaka wa waliokombolewa wangu umekuja.” Kulingana na maandiko, huu lazima uwe mwaka (ambao masomo hayo yalikuja — 1929), wakati Mungu alianza kuwakomboa watu Wake kutoka kwa ufisadi ndani ya kanisa. Hii ndio sababu wanaimba wimbo wa Musa na Mwana-Kondoo. Huu usingekuwa mwaka wa kinabii mwito haungekuja, kwa maana Mungu hutunza wakati kwa usahihi. {SR1: 157.2}

Kunukuu Kut. 15:14-16, “Kabila za watu watasikia, watatetemeka; wakaao Palestina utungu utawashika. Ndipo wakuu

158

wa Edomu watashangaa; mashujaa wa Moabu tetemeko litawapata; watu wote wakaao Kanaani watayeyuka. Hofu na woga utawaangukia; kwa uweza wa mkono wako watakaa kimya kama jiwe; hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, hata watakapovuka watu wako, uliowanunua.” Nchi ya Kanaani huwakilisha nchi ambayo kanisa wakati huu wa sasa lilikujia kuwapo; yaani, Majimbo Yaliyoungana ya Amerika. Jina ‘Palestina “humaanisha” ardhi ya wageni.” Majimbo ya Amerika hujumuishwa na wageni; watu kutoka katika mataifa mengi, na jamii. “Wakuu wa Edomu” hurejelea daraja moja na wale waliotajwa katika Isa. 63:1, kama ilivyoelezwa hapo awali. Jina “Moabu” humaanisha “projeni,” au mababu. {SR1: 157.3}

Kunukuu Isa. 63:5, “Nikatazama, wala hakuwapo wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuwapo mwenye kutegemeza; basi mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu; ghadhabu yangu, ndiyo iliyonitegemeza.” Sehemu hii ya unabii hakika imepata utimizo wake. Masomo hayo yalikuja kwa kanisa kupitia kwa mkondo sahihi, na yakawasilishwa na idara ya Shule ya Sabato, lakini yakapitiwa kijuu-juu. Dhambi zilizotajwa zilihusishwa kwa watu wengine, hakuna marekebisho ya aina yoyote yaliyofanywa, na funzo lililokusudiwa likapotea. Jambo hilo lote limesahaulika na hakuna anayejali, kwa hivyo, “hakuwapo wa kusaidia.” Mungu “alishangaa hakuwapo mwenye kutegemeza.” Tunashangaa pia. Andiko hilo liko wazi, na kwa maelezo ya somo hilo yalikiri kwamba mchinjo u ndani ya kanisa kabla ya kuja kwa Kristo mara ya pili mawinguni. Soma “Isaya Nabii wa Injili,” ukurasa wa 49, 70-73; pia Lesoni ya Robo Mwaka ya somo lilo hilo. Iwapo ujumbe kama huu hautawaamsha watu, basi swali laweza kuulizwa, Ni nini kingine kingefanya hivyo? Kwa hivyo mbingu “ilishangaa.” Hakika, watu wamesema mioyoni mwao, “Bwana ameiacha nchi, na Bwana haoni; Hatatenda mema wala mabaya.” {SR1: 158.1}

Isa. 63:6: “Nitazikanyaga kabila za watu kwa hasira Yangu, Nitawalevya kwa ghadhabu Yangu, Nami nitaimwaga damu yao chini.” A.R.V., “nitamwaga damu yao ya uhai.” Isa. 63:7-9, husimulia wema, rehema, na wingi wa fadhili zenye upendo za Bwana. {SR1: 158.2}

159

“Katika mateso yao yote Yeye aliteswa.” Aya hizi huleta kwa mtazamo wazo la ajabu na lenye baraka la Mungu kuteswa na watu Wake. Isa. 63:10, hutoa ulinganisho kwamba tunapomwasi Mungu, Yeye hugeuka kuwa adui yetu. Kuanzia aya ya 11 na kuendelea, pamoja na sura ya 64, ni sala ya mtu fulani wa watoto wa Mungu. Kwa kuona uovu unajongea, amemimina nafsi yake kwa Mungu katika maombi, ili awaokoe watu Wake Akikumbuka matendo ya Mungu kwa watu Wake wateule na uokozi wa ajabu wa Israeli kutoka Misri, yule ambaye anatoa sala hiyo bila shaka anaielewa hali hiyo. {SR1: 159.1}

Uzoefu wa Israeli huko Misri ni nakala, na ombi hilo ni kwa mtu kama Musa. Isa. 63:11-13: “Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha kutoka baharini pamoja na mchungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia ndani yake Roho wake Mtakatifu? Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu kwa mkono wa kuume wa Musa, aliyetenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae?” {SR1: 159.2}

Isa. 63:16 “Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri: wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu. Jina lako ni la milele.” Lugha iliyotumiwa katika aya hii inathibitisha bila shaka kwamba mtu huyo si Mwisraeli (Myahudi) wa kimwili. Watu walio katika tatizo hapa hawatoki kwa uzao wa Abrahamu, “ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri.” Isingewezekana kwa nabii Isaya, au mtu mwingine yeyote wa taifa lake kutamka maneno hayo wakati walijisifu juu ya ukweli kwamba walikuwa wa Israeli, uzao wa Abrahamu, ambalo kwa wao ilikuwa heshima kubwa. {SR1: 159.3}

Isa. 63:17: “Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.” Aya hii hufunua sababu ya Mungu kukasirishwa na watu Wake: Kosa; wenye moiyo migumu, wasiomcha Mungu. “Mbona umetukosesha njia zako?” Hili si shtaka dhidi ya Mungu kwamba amewafanya watende dhambi, lakini badala yake wanatani kwamba Mungu angetumia adhabu kali hata zaidi kuwarudisha katika fahamu zao. {SR1: 159.4}

160

Isa. 63:18: “Watu wako watakatifu waliumiliki kwa muda mfupi tu: Adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.” “Adui zetu”: Isa. 59:18 husimulia kwamba adui zao ni adu za Bwana. Wamepakanyaga patakatifu kwa wingi wa uchuuzi, kicheko, kunong’ona, mazungumzo ya kawaida, kutengeneza kujipodoa, na aina zingine za ibada ya sanamu kumvunjia Mungu heshima mbele za uso Wake (ndani ya kanisa Lake). Isa. 63:19: “Sisi ni wako. Wewe hauwamiliki kamwe; hawakuitwa kwa jina lako.” Hawajafuata maagizo ya Mungu. Ingawa wao hujitambulisha kati ya watu wa Mungu katika nyumba Yake ya sala, kwa kweli hawajaitwa kwa jina Lake. {SR1: 160.1}

“Isaya Nabii wa Injili”, ukurasa wa 73 (Masomo ya Leo) akitoa maelezo kwa “Aya ya 1-6,” inasema, “Aya hizi zinapaswa kuleta mawazo mazito kwa kila mtu. Hakuna picha ya kutisha zaidi katika Biblia yote kuliko sehemu hii inavyowasilisha. Ule mfano wa Mungu kupiga hatua mbele kukanyaga shinikizo la ghadhabu Yake ni wa kutisha. Lakini ni kweli. Esau alikuwa na fursa yote ambayo mtu yeyote angeweza kuwa nayo kujua kati ya mema na mabaya. Yeye kwa makusudi aliamua vibaya, na akawa mtesi wa watu wa kweli wa Mungu. Tunawazia kwamba hakuna yeyote ambaye hasira ya Mungu itamjilia kikamilifu kabisa kuliko wale ambao wameujua ukweli, ambao wanahusiano nao kwa karibu, kwa mfano, na bado wanauacha na kuwa watesi wa wale ambao hutenda mema. Hata jinsi lilivyo jambo la heri kuupokea ukweli, vivyo hivyo ni jambo la kutisha kuukataa. Na kukataa hakuhitaji kujumuisha ukweli wote. Kukataa sehemu inaweza kuwa hatari kama kuukataa wote. Kwa hivyo wote wanapaswa kujihadhari.” Soma Gombo la 5, ukurasa wa 492; Gombo la 8, ukurasa wa 248-250; Gombo la 1, ukurasa wa 190; Gombo la 1, ukurasa wa 471-472; Gombo la 5, ukurasa wa 207-216; Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 380; Gombo la 2, ukurasa wa 708; Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 206, 407, 408. {SR1: 160.2}

Watu Walioandaliwa Kwa Ajili Ya Mbingu Mpya Na Nchi Mpya — Isaya 65

Isa. 65:1, “Nalitafutwa na hao ambao hawakuuliza habari zangu; Nalionekana kwa hao ambao hawakunitafuta; Nikasema, Nitazameni, nitazameni,

161

kwa taifa ambalo halikuitwa kwa jina langu.” Lugha iliyotumika katika aya hii i katika wakati uliopita. Hata hivyo, ipo nafasi ya mabishano iwapo i katika wakati uliopita au wa sasa, kama ilivyotafsiriwa katika Toleo la Mfalme James. Kijacho, ambacho kwa jumla kiko katika wakati uliopita, kimenukuliwa kutoka kwa tafsiri ya Kiebrania na Isaac Lesser. “Naliruhusu mwenyewe kutafutwa na wale ambao hawakuuliza habari zangu; Naliruhusu mwenyewe nionekane kwa hao ambao hawakunitafuta: Nikasema, hapa niko kwa taifa ambalo halikujiita kwa jina langu.” Toleo la Kiyunani, pia la Kibulgaria yote yako katika wakati uliopita, lakini hebu tunukuu aya iyo hiyo ambayo ilinukuliwa na Paulo kwa Warumi, kama ilivyo katika toleo la Mfalme James. Rumi. 10:20, “Na Isaya anao ujasiri mwingi sana, asema, Nalionekana kwa hao ambao hawakunitafuta; Nalidhihirika kwa hao ambao hawakuniulizia.”{SR1: 160.3}

Hakika hakuna mtu anayeweza kupinga lugha aliyotumia Paulo, maana alikuwa ameelimishwa vyema lugha za Kiebrania na Kilatini. Isitoshe, Paulo alifanya tafsiri hiyo chini ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, kwa hivyo lazima tuamini andiko hili jinsi lilivyotafsiriwa naye — kutoka kwa Kiebrania hadi kwa Kiyunani, — katika wakati uliopita. Tutazungumza juu ya Isa. 65:2, kisha turejee na wazo. “Nimewanyooshea mikono yangu mchana kutwa watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe.” Kumbuka kwamba wakati aya ya kwanza iko katika wakati Uliopita, ya pili iko katika wa sasa. Paulo hutumia aya ya kwanza kwa watu wa Mataifa katika wakati wake, lakini ya pili kwa Israeli, — ya kimwili. Hapa ipo fursa ya kuyashughulisha mawazo kwa mada hii. Paulo anatumia andiko hilo katika wakati uliopita kwa wakati wa sasa katika siku yake, lakini andiko lile katika kitenzi cha wakati wa sasa hulitumia kwa watu wa zamani. Njia ile ambayo matumizi hayo yalifanywa hakika hayaonekani kuwa sawa na sahihi kisarufi, lakini hatuwezi kusema Paulo alifanya makosa. Matumizi na tafsiri lazima iwe sahihi, na vile vile sawa kisarufi. {SR1: 161.1}

Hekima iliyotumika katika andiko hili ni ya kushangaza, na inapasa kutufanya tumtukuze Mungu wetu. Paulo, chini ya Roho wa Uvuvio alifanya hayo matumizi, ili kuliondolea andiko hilo mkanganyiko unaoonekana. Sura hiyo haikuandikwa kwa ajili ya Israeli, wala kwa Mataifa katika siku za Paulo, bali moja kwa moja kwa ajili ya kanisa

162

wakati huu wa sasa. Ikiwa hili laweza kuthibitishwa, lazima tulipokee kama ukweli wa sasa moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Andiko hilo likiwa si sahihi kisarufi kuhusu matumizi yake huthibitisha kwamba wakati wa sura hii ulikuwa haujafika bado, sawa na maandiko na nabii zingine. Halingeweza kueleweka, wala kutumika kwa usahihi hadi wakati uliowekwa. Kisha Mungu hulifunua Neno Lake kwa watu Wake kwa njia Atakayoichagua, lakini linaweza kuja kwa njia isiyotarajiwa. {SR1: 161.2}

Aya ya kwanza kwa usahihi inawahusu Mataifa, ya pili ilitumika kwa Israeli ya kimwili, ambayo ni mfano wa Israeli ya ahadi (144,000, kanisa kwa wakati huu wa sasa, yaani, Waadventista wa Sabato). Kwa sababu hii, Paulo ilibidi atumie andiko hilo kwa ile ya mfano, maana ile ya kweli bado haikuwapo. Sasa, wakati ukiwa umewadia, andiko hilo ni sahihi kisarufi, aya ya kwanza katika wakati uliopita kwa Mataifa katika wakati wa Paulo, ya pili kwa kanisa kwa wakati huu wa sasa, katika wakati wa sasa. Kwa hivyo tunao uthibitisho mzuri wa matumizi na wakati ambao andiko hili linahusu. Hili lapasa kuielekeza mioyo yetu kwa Mungu, na kutufanya tuchunguze kwa bidii unabii ulio katika sura hii. {SR1: 162.1}

Nafasi haitaruhusu kuwasilisha hapa yote ambayo sura hii husheheni. Muhtasari tu wa baadhi ya mambo utatolewa. Shtaka dhidi ya kanisa si la kupendeza, lakini halipaswi kumvunja moyo yeyote kati yetu, kwa maana Mungu wetu ni mwenye huruma na yu tayari kutusamehe dhambi zetu ikiwa tutakiri hatia yetu. Isingekuwa hivyo, Asingekuwa ametuma ujumbe. Sehemu ya mwisho ya Isa. 65:3, imenukuliwa hapa: “Wakitoa dhabihu katika bustani zao na kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya matofali.” Lazima tuelewe kwamba hizi ni nembo lakini si vigumu kuzifafanua. Zingalikuwa haziwezekani kuzielewa, hakuna mtu angeweza kufaidika nazo, kwa hivyo nembo hizo hazingetumika katika sura hiyo. “Bustani” hutumika kwa maonyesho. “Dhabihu” ni sawa na zawadi. “Uvumba,” kwa mujibu wa Ufu. 8:3, 4, ndio njia ambayo maombi hutumwa kwa Mungu. Hakuna popote katika Biblia tunaweza kusoma juu ya watu wowote wa Mungu wakijenga madhabahu za matofali. Madhabahu kwa ajili ya Mungu siku zote yalijengwa kwa mawe. {SR1: 162.2}

Tofauti kati ya tofali na jiwe sasa itazingatiwa.

163

Tofali ni zalisho la mwanadamu, lakini jiwe ni kazi ya Mungu. Hebu sasa tuchunguze somo lililokusudiwa hapa. “Bustani,” onyesho; “Dhabihu,” zawadi; “Uvumba,” sala; “Matofali,” pendekezo lililoundwa na mwanadamu. Shtaka ni kwamba, tunatoa dhabihu kwa onyesho tunapotoa sala zetu kwa Mungu (juu ya madhabahu ya matofali); tunamfuata mwanadamu badala ya neno safi la Mungu, jinsi lilivyopeanwa kwa kanisa. {SR1: 162.3}

Isa. 65:4: “Waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pa sanamu za ukumbusho, walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vichukizavyo u katika vyombo vyao.” “Kati ya makaburi;” “katika mahali pa sanamu za ukumbusho,” kumaanisha vifaa vilivyotengenezwa na wanadamu ambavyo hakuna ufufuo. “Nyama ya nguruwe,” “mchuzi wa vitu vya kuchukiza:” Humaanisha kupuuza matengenezo ya afya; mtu hula chochote uchu wa hamu yake hutamani. {SR1: 163.1}

Isa. 65:5: “Watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi; kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe.” Wakati daraja hili si watendaji wa ukweli, lakini wao hufikiri ni bora kuliko wengine, na wakiwa hivyo ni wenye kujitakia makuu, kwa tendo lao husema, “sisi ni watakatifu kuliko wewe.” Katika aya ya 6, Mungu asema, “Nitalipa ujira wao vifuani mwao.” Kwa habari iliyotolewa tayari, msomaji anaweza kuamua maana ya aya ya saba. {SR1: 163.2}

Isa. 65:8: “Bwana asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu; kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo Nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, Nisiwaharibu wote.” “Kichala” hujumuishwa na zabibu nyingi na ni nembo ya kanisa kama mwili. Bwana asema Yeye hatawaangamiza wote. “Divai” katika kichala huwakilisha damu ya Kristo, na kwa sababu hii, wote hawaangamizwi. Aya ya kumi husimulia ahadi hiyo kwa wale watakaookoka. Aya ya 11 na 12 husimulia tabaka ambalo litaangamia. Mchinjo hapa ni sawa na ule wa Ezekieli 9. Kunukuu Isa. 65:12, — “Kwa hivyo Nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu Nilipoita, hamkuitika; Niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni Pangu, mlichagua mambo Nisiyoyafurahia.” {SR1: 163.3}

Isa. 65:13 na 14, huonyesha utunzi wa Mungu kwa watu wake na mateso ya daraja lile lingine. Isa. 65:15: “Nanyi mtaliacha jina lenu

164

kwa laana kwa wateule Wangu: Maana Bwana Mungu atakuua, naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine.” Aya hii imefafanuliwa hapo awali kuhusiana na sura ya 62, ukurasa wa 155. Daraja lililotajwa hapa ni sawa na lile katika Gombo la 5, ukurasa wa 82: “Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, angaliwaheshimu kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi. Lakini walijitenga kutoka kwa Mungu wakajitiisha kwa mvuto wa dunia, na Bwana akawakataa.” {SR1: 163.4}

Isa. 65:16: “Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani ataapa kwa Mungu wa kweli; kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni Pangu.” “Atajibariki kwa Mungu wa kweli: Watu wengi watajibariki wenyewe, lakini si kwa Mungu wa kweli. Yaani, wanajipatia utajiri, au baraka nyingiulani lakini si kwa uaminifu. Wengine “wataapa,” lakini si kwa Mungu wa kweli. Yaani watasema uongo, lakini baada ya Mungu kulitakasa kanisa Lake mambo haya yote yatatoweka,na kusahaulika. {SR1: 164.1}

Isa. 65:17-19, husimulia juu ya nchi mpya. Isa. 65:20, hapa imenukuliwa kutoka kwa tafsiri ya Kiebrania na Isaac Lesser. “Humo hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimiza siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi atalaaniwa yeye (atakayekufa) akiwa na umri wa miaka mia.” Inaonekana tafsiri hii inafanya maana ya aya iwe wazi zaidi kuliko ya Mfalme James. Maandiko huzungumza juu ya wakati mwishoni mwa miaka 1000 (millenia) baada ya ufufuo wa waovu. Wakati huo hakutakuwapo kuzaliwa kwa watoto wachanga. “Humo hatakuwapo tena mtoto wa siku chache.” Kwa hivyo somo sio gumu sana kwa mtu kuelewa. Waovu wote wanaitwa katika ufufuo wa pili, wawe wazee au watoto wachanga (wakati walipokufa). Wote wanafufuka kwa wakati mmoja. Hii saa inakuwa kuzaliwa kwa waovu wote katika uhai wa pili. Hakitakuwapo kifo cha kawaida, au kisicho cha kawaida, kwa maana wote lazima waishi hadi kwa wakati wa mauti ya pili, ambayo ni kwa “moto ukashuka kutoka kwa Mungu mbinguni ukawala.”

165

Soma Ufu. 20:7-10. “Bali mtenda dhambi atalaaniwa yeye (atakayekufa) akiwa na umri wa miaka mia.” Andiko hili linatabiri urefu wa maisha ya waovu baada ya kufufuliwa kuwa ni miaka 100. “Humo hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimiza siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi atalaaniwa yeye (atakayekufa) akiwa na umri wa miaka mia.” Katika kipindi hiki cha miaka 100, waovu wanafanya maandalizi yao ya kuushambulia mji mtakatifu. Soma Ufu. 20:8, 9. {SR1: 164.2}

Isa. 65:21-25, husimulia watakatifu katika nchi mpya. Hapa upo ushahidi mwingine kwamba sura hiyo imekusudiwa kwa ajili ya watu kwa wakati wa mwisho, kwa maana aya zinazoifunga zinazungumza juu ya nchi mpya. {SR1: 165.1}

Kukusanywa Ndani Kutoka Kwa Mataifa: Ibada Katika Nchi Mpya — Isaya 66

Isa. 66:1: “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?” Nyumba iliyotajwa hapa ni nyumba ya kiroho jinsi ilivyo katika Efe. 2:20-22, ambayo hekalu la Sulemani lilikuwa nembo yake. Nukuu ifuatayo inapatikana katika Manabii na Wafalme, ukurasa wa 35, 36: “Kwa hivyo kadiri hilo jengo juu ya Mlima Moria liliinuliwa kimyakimya na ‘mawe lililotayarishwa kabla halijafikishwa hapo: Ili kwamba sauti ya nyundo wala shoka wala chombo chochote cha chuma haikusikika ndani ya nyumba, ilipokuwa ikijengwa’, mapambo yalikamilishwa kulingana na vigezo ambavyo Daudi alivikabidhi kwa mwanawe. {SR1: 165.2}

Funzo lililokusudiwa hapa ni kwamba mawe ya kiroho (washiriki wa kanisa) wanapaswa kutayarishwa kabla ya kuletwa humo. Kwa nini, basi, wanafunzi hupewa ubatizo na ushirika kanisani bila kupewa maagizo katika ukweli wote wa ujio? Inashangaza kujua idadi kubwa ya wale wanaoitwa eti Waadventista wa Sabato hawaamini maandiko ya Roho ya Unabii, na hawajui kabisa ukweli juu ya matengenezo ya afya. Je! Hizi si kanuni za kimsingi katika kanisa? Je! Matengenezo ya afya si mkono wa kuume wa ujumbe wa malaika

166

wa tatu? Je! Uendelezaji wa zoezi hili haujalipeperusha kanisa kuingia duniani? {SR1: 165.3}

Hekalu zuri huonyesha mapenzi ya Mungu kwa kanisa Lake. Kwa sababu hii, Mungu alimwaga utajiri mwingi sana kwa jengo hili la kifalme juu ya Mlima Moria. Kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa katika jarida la kila mwezi la Jumuiya ya Wasanifu-ujenzi ya Illinois, ulifikia jumla kubwa sana ya zaidi ya dola bilioni themanini na saba. Makadirio kadhaa huonyesha jumla ya gharama kuwa $ 87,212,210,840. Jumla hii huwakilisha utajiri wa taifa. Swali ni, Je! Israeli ilipataje kukusanya fedha nyingi sana ili kumimina kwa jengo mmoja tu? Mungu kamwe hatuulizi tufanye lolote isipokuwa Yeye Mwenyewe afanye liwezekane. {SR1: 166.1}

Kiasi kikubwa cha utajiri uliotumika kwa hekalu hili kubwa lenye fahari huwakilisha utunzi na upendo wa Mungu kwa watu Wake, na pia utukufu wa kanisa. Sulemani alitambua kwamba hekalu hili lilikuwa tu nembo ya hekalu ambalo hangeweza kujenga. Katika 2 Nya. 2:6, tunasoma: “Lakini ni nani awezaye kumjengea Yeye nyumba, ikiwa mbingu na mbingu za mbingu hazimtoshi? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele yake?” Mungu anawauliza watu Wake wakati huu wa sasa, “Mtanijengea nyumba ya namna gani?” (Isa. 66:1). Toleo la Douay husomeka: “Ambayi ninyi mtanijengea?” Tafsiri ya Kiebrania husomeka: “Nyumba ambayo mwaweza kunijengea?” {SR1: 166.2}

“Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.” Andiko hili huonyesha kutowezekana kwa mwanadamu mfaji kumfanyia Mungu chochote, isipokuwa akifanye kupitia ndani yake. Lazima ni kero lililoje kwa mbingu tunaposema tunapaswa kuimaliza kazi ya Mungu katika kizazi hiki, au kujaribu kumjengea Yeye nyumba kwa mipango ya wanadamu. Tumesema hilo, na tumetenda hivyo, lakini tumeshindwa. Sasa Mungu anatuuliza “Mtanijengea nyumba ya namna gani?” Mtu anaweza kusema, Tazama dhehebu hili kubwa ambalo tumejenga. Iwapo kuna ukuu wowote kulihusu, si kwa sifa ya mwanadamu. Ingawa tumejisifu kwa juhudi zetu nyingi, Mungu hutuacha tuendelee kulingana na uamuzi wetu tunaodhani kuwa ni wa busara hadi tuanguke na kugundua kosa letu. Ukweli, ni dhehebu

167

kubwa, lakini Mungu halioni jinsi tunavyoliona. Kwa kiwango tunachokwenda itatuchukua mamia ya miaka kuimaliza kazi hiyo, na ukweli wa jambo hilo ni kwamba, hatuwezi kamwe. Isitoshe, jinsi lilivyo dhehebu kubwa, haliko tayari kuhamishwa bila kuonja mauti kwa hivyo tunaweza kujiuliza, Nyumba ambayo tumeijenga iko wapi? Sura ya kumi na tatu ya Ezekieli imeandikwa kwa ajili ya kanisa wakati huu wa sasa ambapo tunanukuu Ezek. 13:5: “Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa wala hamkuitengenezea nyumba ya Israeli boma wapate kusimama vitani katika siku ya Bwana.” {SR1: 166.3}

“Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?” Huwa tunajiita watunza Sabato na hujivunia sana kutii amri za Mungu, lakini hapa tunaulizwa “na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?” Tumeitia unajisi siku takatifu ya Mungu, na kuichafua Sabato kwa biashara, kama ilivyoelezwa hapo awali kwa Ukurasa 147-148. Tazama pia ukurasa wa 124. Mchungaji mzuri wa Mungu, baada ya kuulizwa kuhusu mamlaka ya kuuza machapisho yetu siku ya Sabato katika nyumba ya Mungu, alisema, “Ni swali tu kuhusu kiasi gani cha machapisho yetu kinapaswa kuuzwa Sabato.” Mgongano katika mawazo ya mchungaji huyu ulijibiwa kwa maneno matatu mafupi: “Hakuna hata moja.” Lakini jibu hili halikumridhisha mtu huyo katika nafasi hiyo takatifu, na akaongeza, “Israeli ya kale walimchinja mwana-kondoo na kumtoa sadaka siku ya Sabato. Kwa hivyo, tunaweza kuuza vitabu vyetu.” Jibu lililopeanwa kwa hili lilikuwa, “Ikiwa Israeli walimtoa kafara mwana-kondoo kwa Sabato ya siku ya saba waliambiwa wafanye hivyo, lakini wewe umeambiwa usifanye hivyo, na hiyo ndiyo tofauti.” Ukweli wa jambo hilo ni kwamba Mungu hakuwapa Israeli ya kale Sabato ya siku ya saba kwa ajili ya kutoa dhabihu, bali kwa siku ya kupumzika. Sabato za kila mwezi ziliongezwa kwa ajili ya hizo dhabihu. Soma Law. 23. {SR1: 167.1}

Katika aya ya pili ya Isaya 66, Mungu hutuambia kwamba mambo haya yote tunayojivunia, Yeye ameviumba hivi vyote na vikapata kutokea, “lakini mtu huyu ndiye Nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge mwenye roho [mwungamaji] iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. “ Isa. 66:3: “Yeye achinjaye ng’ombe ni kama amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo, ni kama yeye akataye shingo ya mbwa; yeye atoaye dhabihu, ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba, kama yeye abarikiye sanamu. Naam, wamezichagua

168

njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.” Andiko hilo ni dhahiri bila kukosea kwamba dhabihu, sadaka, sala zetu, na namna yoyote ya dini tunayoweza kuwa nayo, sio tu chukizo Kwake, bali ni yeye kuudhi zaidi. “ Naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.” {SR1: 167.2}

Isa. 66:4: “Mimi nami Nitachagua madanganyo yao, nami Nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu Nilipoita, hawakuitika; na Niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua Nisiyoyafurahia.” Mungu aliita katika masomo haya yalipokuja kanisani kupitia idara ya Shule ya Sabato, lakini yalikuja na yakaenda, na yamesahaulika. Hivyo basi, kwa sababu wamezichagua njia zao wenyewe, na kufanya uovu mbele ya Mungu, na hawakufurahia kufuata maagizo yaliyopeanwa kwa kanisa, sasa, Anasema Atachagua madanganyo yao, na Ataleta hofu zao juu yao. Ni jambo la kuogofya kuziba sikio kwa sauti ya Mungu. Wakati aya hii inazungumza juu ya daraja ambalo limeamua kufuata chaguo lao badala ya njia ya Mungu, aya inayofuata huzungumzia daraja ambalo humcha Mungu na kuthubutu kumtumikia Yeye. Kwa hivyo, ni wazi bila kukosea kwamba yapo matabaka mawili ya watu kanisani. {SR1: 168.1}

Isa. 66:5: “Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu waliowachukia, waliowatupa nje kwa ajili ya jina langu, wamesema, na atukuzwe Bwana: Bali Yeye ataonekana kwa furaha yenu, lakini watatahayarika.” Aya hii huonyesha kwamba ingawa mwito katika hayo masomo ulikataliwa na wale walio katika nafasi za uwajibikaji, Neno la Mungu halirudi Kwake bure, kwa maana daraja katika aya hii humcha Mungu, na watetemekao kwa sababu ya Neno Lake, na tokeo lake ni kwamba upo mgawanyiko kanisani. Tabaka ambalo linampinga Mungu ni kubwa kwa wingi, au, wale walio na ushawishi mkubwa juu ya washirika wa kanisa, maana aya hiyo inasema wanawatupa nje ndugu zao (tabaka la wamchao Mungu) kwa ajili ya jina Lake. Daraja ambalo linawatupa nje watu wa Mungu wanadhani wanafanya utumishi Wake, kwa maana andiko linasomeka: [wao] “Wamesema, na atukuzwe Bwana.” {SR1: 168.2}

Ni vibaya kwa mtu kulikataa Neno la Mungu, lakini ni

169

vibaya zaidi wakati mtu kama huyo amepofushwa sana, hivi kwamba kwa kuukataa mwito wa mbinguni, hufikiri anafanya utumishi wa Mungu. Aya hiyo ina ahadi ya kutia moyo kwa wale wanaomcha Mungu, maana husema, “Yeye ataonekana kwa furaha yenu,” na wakati Bwana ataitimiza ahadi Yake, watesi wa Mungu “watatahayarika.” Umekuwa mmojwapo wa ujanja wa Shetani katika historia yote ya kanisa kuligharikisha na maajenti wake, na wasio waongofu, ili kwamba ukweli ukija kanisani, mara tu watu wa Mungu watakapouitikia mwito huo, yeye husimama tayari kupiga kura kupitia ndani ya wengi wa wafuasi wake. Tokeo lake ni kwamba ulazima ulizalisha vuguvugu au dhehebu jipya, bali, kwa mujibu wa Isa. 66:4 na 6, Mungu atashughulika tofauti kabisa katika hali hii. Sababu ikiwa, maana Mungu alilipanga dhehebu hili Mwenyewe kwa mkono wa nabii, na Ametupatia nuru maalum ya ukweli wa sasa. Kwa hivyo, hutuacha bila udhuru na Mungu atashughulika ipasavyo na watu. {SR1: 168.3}

Kunukuu Gombo la 3, ukurasa wa 265: “ Lakini iwapo dhambi za watu zinaachiliwa na wale walio katika nafasi za uwajibikaji, kununa Kwake kutakuwa juu yao, na watu wa Mungu, kama mwili, watawajibishwa dhambi hizo. Katika kushughulika na watu Wake hapo zamani, Bwana huonyesha ulazima wa kulitakasa kanisa kutokana na makosa.” Ile “Sauti ya fujo,” aya ya sita, inahusu daraja ambalo limechagua njia yao wenyewe badala ya njia ya Bwana, ambaye Yeye huwaita adui Zake. {SR1: 169.1}

Isa. 66:7 na 8: “Kabla hajaona utungu, alizaa; kabla maumivu yake hayajampata, alizaa mtoto mwanamume. Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? au taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Zayuni mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” Katika aya hizi mbili ulinganisho umefanywa kwa kanisa wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo (la Kiyahudi), na kanisa kabla tu ya kuja Kwake mara ya pili. “Kabla hajaona utungu, … kabla maumivu yake hayajampata.” Hili hurejelea kanisa wakati Kristo alipokuja. Halikumtarajia Yeye (halikuona utungu), wala halikuhisi, au kujua alipokuja Yeye. Ingawa halikustahili, “lilimzaa mtoto mwanamume.” {SR1: 169.2}

Kanisa linalotajwa katika aya ya nane ni kinyume cha

170

lile lililo katika aya ya saba. Wakati umefika kwa vuguvugu kuu, ambalo maelfu wataongoka katika siku moja. Hili ndilo kanisa katika wakati wa mvua ya vuli, kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Kanisa limekuwa likitaka kwa bidii sana. Mara tu kunapokuwa na utungu halisi kwa ajili ya usafi wa wadhambi, kazi itakamilika, karibu mara moja. “Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? au taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Zayuni mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” {SR1: 169.3}

Aya ya tisa huonyesha kwamba Mungu ndiye anayefanya kazi hiyo. Aya ya kumi husema wale wanaompenda (kanisa) na wanaomwombolezea sasa, watafurahi na kushangilia. Aya ya kumi na moja huonyesha ni kwa nini watafurahi na kushangilia: Kwa sababu ya ukweli na nuru katika Neno la Mungu linalowakilishwa na maziwa ambalo litakuja kwa kanisa. “Mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake; mpate kukama na kufurahiwa na wingi wa utukufu wake.” Isa. 66:11. Isa. 66:12-14, husimulia utunzi wa Mungu kwa watu Wake, na upendo wa kanisa kwa washiriki wake, neema ya Bwana kwa watumwa Wake, na ghadhabu kwa adui Zake. {SR1: 170.1}

Isa. 66:15-17: “Kwa maana, tazama, Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli, ili atoe malipo kwa ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili kwa moto na kwa upanga wake: Nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani nyuma ya mti ulio katikati, wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya, watakoma pamoja asema Bwana.” Kuja kwa Bwana “kwa moto… ili atoe malipo kwa ghadhabu Yake,” sio kuja kwa Kristo mawinguni kuwapokea watu Wake. Ni kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema, na katika wakati wa utakaso wa kanisa. Tazama Mal. 3:1-3. Anakuja na kisasi kwa wale wanaolikiri jina Lake, lakini wanaomfuata mwanadamu badala ya Kristo, na tokeo lake ni kwamba hawatii ukweli Wake. (Tabaka ambalo hawafanyi uchunguzi wenyewe lakini huyapokea maamuzi ya wengine wanaomfuata mwanadamu, na wamenaswa katika makucha ya shetani.) {SR1: 170.2}

“Nyuma ya mti mmoja”: Pambizo husomeka, “mmoja baada ya mwingine.”

171

andiko hapa linathibitisha hiyo tafsiri: “Kufuata kiongozi.” Yaani, watu wamependelea kumfuata mtu aliye katika nafasi ya juu badala ya kutafuta wenyewe katika Neno na kudai “Bwana asema hivi.” “Katika bustani nyuma ya mti mmoja”: Kirai hiki pia hupendekeza “mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” Kula tunda lililokatazwa katika bustani ya Edeni kulileta dhambi ikuwepo. Shtaka hapa ni sawa, baya zaidi. Wanadamu wamechagua chakula chao kuwa vitu ambavyo Mungu amekataza, na “kutumia fedha kwa kile ambacho si chakula.” “Kwa upanga wake Bwana atateta na wote wenye mwili.” Hili haliwahusu wale walio nje ya kanisa, kwa maana tunasoma katika Isa. 66:19, “Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa.” Sehemu ya mwisho: “Nao watahubiri utukufu wangu katika Mataifa.” Ni wazi hapa kwamba wale ambao wataokoka maangamizo, Mungu atawatuma kwa mataifa yote, na kutangaza utukufu Wake kwa Mataifa. Kwa hivyo, lazima liwe ndani ya kanisa tu, na kwa muda mrefu kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema. “Mataifa” yaliyotajwa katika aya ya 19 ni kuonyesha tu eneo kubwa lililoshughulikiwa na watumwa Wake (katika mataifa yote). {SR1: 170.3}

Maangamizo yaliyotajwa katika Isa. 66:15-17, na Isaya 63, ni sawa. Kwa hivyo, Mungu anawafanya kuwa mfano, au ishara kwa mataifa yote, kwa maana tunasoma katika sehemu ya mwisho ya aya ya kumi na nane, na sehemu ya kwanza ya kumi na tisa: “Wakati unakuja, Nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja na watauona utukufu wangu. Nami nitaweka ishara kati yao.” {SR1: 171.1}

Isa. 66:20: “Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote kuwa sadaka kwa Bwana juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana, kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi. Aya hii huonyesha ukusanywaji wa Mataifa hadi kwa kanisa na watumwa Wake (watu 144,000). “Mlima wake mtakatifu” humaanisha dhehebu Lake; “Yerusalemu” humaanisha sehemu inayoongoza. {SR1: 171.2}

Isa. 66:21: “Na baadhi yao Nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema Bwana.” Tumeelezea hapo awali kwamba

172

watu 144,000 watakuwa makuhani na Walawi, lakini katika aya hii Bwana asema atawachukua pia watu wa Mataifa “kuwa makuhani na Walawi.” Sababu yake imetolewa katika aya mbili zifuatazo. Isa. 66:23: “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele yangu, asema Bwana.” Utakuwako mfumo wa ibada, kwa hivyo hitaji la makuhani na Walawi. {SR1: 171.3}

Isa. 66:24: “Nao watatoka nje, na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” “Maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika:” Mwili wa mtu huliwa na funza na maana ni kwamba funza hawa hawatakufa hadi mwili utakapofanywa kuwa mavumbi. Wala moto hautazimika mpaka “mizoga” ipunguzwe kuwa majivu. Sababu mbona funza na moto umetajwa hapa imenenwa katika aya ya kumi na sita: “Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili kwa moto na kwa upanga wake.” Maangamizo yanatimizwa na vyote viwili, na pale ambapo upanga unatumiwa, hapo ndipo funza atafanya kazi yake. “Funza hawatakufa …. moto wao hautazimika”, humaanisha kwamba unabii huo ni wa hakika, na maangamizo yaliyotabiriwa yatatimizwa. {SR1: 172.1}

173

SEHEMU YA 7

NINI MAANA YA SURA YA NNE YA MIKA?

“Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima, na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.” Mika 4:1. Andiko hilo liko wazi bila kukosea; kwamba lilikusudiwa kwa siku za mwisho, kwa maana husomeka: “Lakini itakuwa katika siku za mwisho.” Ni wazi pia kwamba andiko hili litatimizwa, maana husema: “itakuwa.” {SR1: 173.1}

Ni ukweli unaokubalika kwamba karibu wanafunzi wote wa Biblia hukubali kwamba “mlima” unaozungumziwa katika sura hii ni nembo ya kanisa la Mungu (dhehebu), ambalo hekalu lililojengwa kwa Mlima Moria lilikuwa mfano. Nabii hutangaza kwamba kanisa la Mungu lingesimamishwa juu ya milima (madhehebu), na kuinuliwa juu ya vilima (vidhehebu, au mashirika). Kuinuliwa, si na ulimwengu, bali na Roho wa Mungu kwa uwezo, ukweli, na haki, na watu watamiminika ndani yake. Mungu amenena hilo kupitia kwa nabii Wake mtakatifu, kwa hivyo utakuwa upumbavu, na udanganyifu mtu kubishana, au kujaribu kupuuza maana ya neno takatifu. {SR1: 173.2}

Unabii uu huu pia umeelezewa katika sura ya pili ya Isaya ambayo tunanukuu. “Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana yeye peke yake atatukuzwa siku hiyo.” Isa. 2:11. Iwapo kila kitu ambacho ni cha kibinadamu kitashushwa na kuinamishwa chini, na Bwana peke yake atainuliwa katika siku hiyo, mtu anaweza kuona wazi kwamba unabii huo utatimimizwa, kwa maana Bwana ameinuliwa duniani na kanisa Lake kama ilivyoonyeshwa na nabii Isaya. “Nawe utakuwa taji ya utukufu katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena Aliyeachwa; wala nchi yako haitaitwa tena Ukiwa. Bali utaitwa Hefziba, na nchi yako Beula: Kwa kuwa Bwana anakufurahia.” Isa. 62:3,4.

174

Wakati mlima wa Bwana “umewekwa imara juu ya milima, na kuinuliwa juu ya vilima,” basi bila shaka “watu watamiminika ndani.” {SR1: 173.3}

Wakati huu wa utukufu ulionenwa na nabii, Mika, si mwingine bali ni kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Sura ya 60 ya Isaya ni unabii wa kanisa wakati wa “mvua ya vuli,” ambao tunanukuu kutoka kwayo: “Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litafunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu: Bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wamekusanyana, wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali, na binti zako watabebwa nyongani.” Isa. 60:1-4. {SR1: 174.1}

“Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.” Ufu. 18:1. “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; Wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; Kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” Zeph. 3:13. “Maana, tazama, giza litafunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu: Bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu Wake utaonekana juu yako.” Isa. 60:2. Wakati wa utukufu kama huo uko mbele ya kanisa la Mungu. {SR1: 174.2}

Mika 4:2, sehemu ya kwanza: “Na mataifa mengi yatakuja, na kusema, Njoni, twende juu kwa mlima wa Bwana, na kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake; nasi tutatembea katika mapito yake.” Maneno ambayo yamenukuliwa yananenwa na mataifa. Wakati kanisa la Mungu limetakaswa na kujazwa na Roho Mtakatifu, “likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” Manabii na Wafalme, ukurasa wa 725. {SR1: 174.3}

Kwa kweli, watu wataulizana na kualikana, wakisema, “ Njoni, twende juu kwa mlima wa Bwana, na kwa

175

nyumba ya Mungu wa Yakobo.” “Kwa hiyo, malango yako yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea vikosi (pambizo, utajiri) wa Mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao…. Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. Wana wa watu waliokutesa watakuja kwako na kukuinamia; nao wote waliokudharau watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; nao watakuita; Mji wa Bwana, Zayuni wa Mtakatifu wa Israeli.” Isa. 60:11, 13, 14. Hakika, huu ni wakati wa mavuno ulionenwa na manabii, na mavuno makubwa kutoka kwa mataifa yote. “Nyumba ya Mungu wa Yakobo” ikimaanisha kanisa ambalo watu 144,000 wametiwa muhuri kuingia, — Israeli wa kweli. {SR1: 174.4}

Mika 4:2, sehemu ya mwisho: “Kwa maana sheria itatoka Zayuni, na neno la Bwana kutoka Yerusalemu.” Wakati sheria ya Bwana inapotangazwa na kanisa Lake, unaweza kuona wazi nini kinachomaanishwa na kanisa la haki: Watu wenye haki ambao watatii sauti ya Bwana. Zefania, akiangalia tangu zamani katika vizazi vingi kwa jicho la kinabii, aliliona kimbele kanisa hili tukufu. “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; Kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” Zeph. 3:13. Hakuna anayehitaji kutolielewa andiko hili. Litatimizwa jinsi lilivyoandikwa. Ingawa wengine wanaweza kudhani unabii huu ni maneno matupu kwa sababu watu wanasema, “twende juu kwa mlima wa Bwana.” {SR1: 175.1}

Tunasoma katika Ushauri kwa Walimu: “‘Bali agano hili ndilo Nitakalolifanya na nyumba ya Israeli; baada ya siku zile, asema Bwana, Nitatia sheria Yangu ndani yao na kuiandika katika mioyo yao; Nami Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; Kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana: Maana Nitawasamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena. Yer. 31:33, 34.’” {SR1: 175.2}

“‘Na mataifa mengi yatakuja, na kusema, Njoni, twende juu kwa mlima wa Bwana, na kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; 176

Naye naye atatufundisha njia zake; nasi tutatembea katika mapito yake; Kwa maana sheria itatoka Zayuni, na neno la Bwana kutoka Yerusalemu.’ Mika 4:2.” Ushauri kwa Walimu, ukurasa wa 454, 455. Kumbuka kwamba Roho ya Unabii hufanya matumizi kwa Mika 4:2 kama unabii wa kweli ambao utatukia na kupata utimizo wake na watu wa Mungu, kwa kuhusisha aya hiyo na Isa. 54:11-14; Yer. 31:33, 34; ambayo ni maandiko yatakayotimizwa wakati wa “Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu.” {SR1: 175.3}

Mika 4:3, “Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naya atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali, nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; Taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” “Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naya atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali.” Katika Isa. 60:10, 12, tunayo maelezo ya maandishi hayo. “Na wageni watajenga kuta zako, na wafalme wao watakuhudumia:… Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.” {SR1: 176.1}

“Nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; Taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Aya hii husomeka kinyume kabisa cha Yoeli 3:10, “Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki: Aliye dhaifu na aseme Mimi ni hodari.” {SR1: 176.2}

Maandiko haya hufunua tabaka mbili za watu. Daraja moja litamiminika kanisani katika makundi makundi makubwa: Wafalme, na viongozi wakuu wa majeshi ambao wamekuwa wakiunda silaha za kuangamiza na kujiandaa kwa vita. Sasa injili imewashinda. Wakati wanapojiunga na kanisa hukusanya zana zao za vita, na kuzifua kuwa majembe ya miundu. “Ghasia hazitasikiwa tena katika nchi yako, ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; bali utaziita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.” Isa. 60:18. Daraja lile lingine, nje ya kanisa, hujiandaa kwa vita, likiyafua majembe yao yawe panga, na miundu yao iwe mikuki. Kundi moja la watu wanajiandaa kuhamishwa bila kuonja mauti, ilhali lile lingine linajiandaa kwa kuteka nyara. Kwa hivyo maandiko yote mawili yanakwenda sambamba na yatatimizwa katika

177

wakati uo huo. Kwa hivyo ulimwengu utagawanyika katika tabaka kubwa mbili yaliyotengana na tofauti: Kutenganisha ngano kutoka kati ya makapi, mbuzi kutoka kati ya kondoo. {SR1: 176.3}

Mika 4:4, “Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake, wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.” Maana ya aya hiyo ni kwamba kanisa la Mungu liko katika usalama kabisa, na hakuna anayehitaji kuogopa. Kumbuka kwamba watu 144,000 wametiwa muhuri kabla ya wakati huu, na maisha yao ni hakika; hakuna anayeweza kuwadhuru wala kugusa maisha yao ya sasa, au maisha yajayo, kwa maana wao ni watakatifu walio hai, wanaopaswa kuhamishwa bila kuonja mauti. Wakiwa na uhakikisho huu, hakuna anayeweza kuwaogofya, na watashinda kwa ushujaa. Kunukuu Isaya 60:17, sehemu ya mwisho, na 18: “Nitawafanya wasimamizi wako wawe amani, na hao wakutozao fedha kuwa haki. Ghasia hazitasikiwa tena katika nchi yako, ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; bali utaziita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.” {SR1: 177.1}

Mika 4:5, “Kwa maana wote watakwenda kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana Mungu wetu milele na milele.” Aya hiyo i wazi bila kukosea kwamba ulimwengu utagawanywa katika matabaka mawili makubwa, na tofauti. Watu wa Mungu hawatahusiana hata kidogo na waovu, na watasema, “ wote watakwenda kila moja kwa jina la mungu wake.” Lakini “sisi tutakwenda kwa jina la Bwana Mungu wetu milele na milele.” {SR1: 177.2}

Mika 4:6, “Katika siku hiyo, asema Bwana, Nitamkusanya yeye achechemeaye, Nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye Niliyemtesa,” kumaanisha kanisa sasa, katika hali hii ya sasa. “Nitalifanya liwe mabaki:” Yaani, baada ya utengo, (utakaso), wale walioachwa, — watu 144,000, wakiwa masalia. Yale mateso ni wakati wa utakaso. {SR1: 177.3}

Mika 4:7, “Nami Nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu; Na Bwana atawamiliki katika mlima Zayuni tangu sasa hata milele.” “Yeye aliyetupwa mbali,” — kanisa wakati huu wa sasa “lilitupwa mbali,” au jinsi inavyosomeka katika Ufu. 3:16, “Nitakutapika utoke katika kinywa changu,” — kumaanisha hali ya sasa ya Ulaodekia. Bali kwa rehema Yake Yeye

178

atawakusanya mabaki (wale waliosalia) na kulifanya kanisa kuwa “taifa lenye nguvu” kwa kuwakusanya n watu wa Mataifa katika ujumbe. Jeshi kubwa la watu 144,000, waliojazwa na Roho Mtakatifu watatangaza ujumbe bila woga ulimwenguni kote, wakisonga mbele wakishinda na kushinda. “Mdogo atakuwa elfu, na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi Bwana Nitayahimiza hayo kwa wakati wake.” Isa. 60:22. “Na Bwana atawamiliki tangu sasa hata milele:” Kristo Mwenyewe analisimamia kundi mara moja na milele. “Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji sio wa kweli atalisimamia kundi mwenyewe.” Gombo la 5, ukurasa wa 80. {SR1: 177.4}

Mika 4:8, “Na wewe, Ee mnara wa kundi, ngome ya binti Zayuni, utajiliwa, naam mamlaka ya kwanza yatakuja; ufalme wa binti Yerusalemu.” Aya hii inajulikana kwa wote. Unabii wa Kristo, — “Ee mnara wa kundi …. utajiliwa, naam mamlaka ya kwanza yatakuja.” “Mamlaka ya kwanza” ni utawala ambao Adamu alipoteza. Ahadi ni kwamba Kristo ataurejesha wote, na kisha kwa urithi, utakuja kwa kanisa (watu Wake). “Ufalme utamjia binti ya Yerusalemu.” {SR1: 178.1}

Mika 4:9, “Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako? Mshauri wako ameangamia? Hata umeshikwa na utungu kama mwanamke wakati wa kuzaa.” Wakati huu wa kulia na maumivu hauwezi kuwa mwingine ila wakati ulio mbele yetu, wakati wa utakaso. “Angalieni, Nitamtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; Naye Bwana, mnayemtafuta atalijia hekalu lake ghafla, naam yule mjumbe wa agano, mnayemfurahia; angalieni, atakuja; asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.” Mal. 3:1, 2. {SR1: 178.2}

Mchakato huu wa utakaso hautakuwa jambo rahisi kwa upande wa watenda dhambi, maana “moto wa mtu asafishaye fedha na sabuni ya mtu afuaye nguo” inatumiwa, na wakati Mungu atakamilisha mchakato huu wa kusafisha, atakuwa na watu watakatifu na safi. Kisha kutakuwa na wakati mtukufu wenye furaha na shangwe katika Bwana, kama ilivyo kwa mwanamke aliye katika utungu, lakini wakati

179

mwana amezaliwa inakuwapo furaha kubwa. Lakini swali linaulizwa, “ Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako? Mshauri wako ameangamia?” Ingawa inaweza kuonekana kuwa uchungu lakini hakuna anayehitaji kuogopa, kwa kuwa kanisa la Mungu lina Mfalme na mshauri ambaye hasinzii wala kulala.” Tanuru huangaliwa kwa karibu. Mtenda dhambi ataangamia, lakini wamchao Mungu watahifadhiwa. {SR1: 178.3}

Mika 4:10, “Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Zayuni, kama mwanamke mwenye utungu; Maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba, utafika hata Babeli, huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa kutoka kwa mikono ya adui zako.” Aya hii huonyesha kwamba baada ya utakaso, kanisa halihamishwi mara moja kwenda Yerusalemu Mpya mbinguni, lakini linaachwa kufanya kazi yake teule hapa duniani. “Maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba, utafika hata Babeli, huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa kutoka kwa mikono ya adui zako.” {SR1: 179.1}

“Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Zayuni, kama mwanamke mwenye utungu.” Ufafanuzi wa andiko hili unapatikana katika Isa. 66:7, 8. Tunanukuu aya ya 7: “Kabla hajaona utungu, alizaa; kabla maumivu yake hayajampata, alizaa mtoto mwanamume.” Mwanamke huyu “alizaa kabla ya hajaona utungu, kabla maumivu yake hayajampata, alizaa mtoto mwanamume.” Mwanamke huyo ni kanisa la Agano la Kale katika siku za Kristo. Kristo ndiye mtoto mwanamume lililomzaa, lakini halikuona utungu, wala halikupata maumivu yake. Yaani, halikumjua Yeye; halikuhisi maumivu ya uokozi. Jinsi ambavyo ungekuwa muujiza kwa mwanamke kuzaa mtoto kwa njia hii, kwa hivyo ulikuwa muujiza kwamba Kristo alizaliwa kwa mama huyo asiyestahili (kanisa la Kiyahudi: Kwa sababu alikuwa amekengeuka). Kunukuu Isa. 66:8: “Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Zayuni mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” Wakati ulikuwa muujiza kwa kanisa la Kiyahudi kumzaa Kristo; bado upo muujiza mkubwa zaidi kwa kanisa lililotajwa

180

katika aya hii, maana wakati ambapo lile la pili liliona utungu lilizaa watoto wake. Itakuwa ajabu kwa jambo kama hilo, maana haiwezekani nchi kuzaa kwa siku moja, au taifa kuzaliwa mara moja. Walakini litafanyika, “maana Zayuni mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” {SR1: 179.2}

Kunena kibinadamu, kuikamilisha kazi ya injili katika kizazi hiki (kizazi hiki kikiwa karibu kimepita) itakuwa kazi isiyowezekana; lakini unabii hutangaza kwamba yasiyowezekana yatatimizwa. Kanisa lililopata utungu na kuzaa watoto wake ni kanisa katika wakati wa kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu. Upo ukusanywaji mkubwa wa kutimizwa katika muda mfupi tu. “Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.” Ufu. 18:1. “Na mataifa mengi yatakuja, na kusema, Njoni, twende juu kwa mlima wa Bwana, na kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo.” {SR1: 180.1}

Mika 4:11, “Na sasa mataifa mengi wamekusanyika juu yako, wasemao, Na atiwe unajisi, macho yetu na yaone shari ya Zayuni.” Mara tu kanisa la Mungu kama mwili (sio kama mtu mmoja mmoja) linaokoka kunaswa na ibilisi (maana walio najisi hawataingia ndani), na kuwa lenye bidii, likiwa limejazwa na Roho wa Mungu, ghadhabu ya adui wa zamani itaamshwa, na italeta utimizo wa Ufu. 12:17. “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” {SR1: 180.2}

Wakati huu wa taabu pia umeelezwa na Roho ya Unabii. Maandishi ya Awali, ukurasa wa 33, 34: “Na mwanzoni mwa wakati wa taabu, tulijazwa Roho Mtakatifu tulipokwenda mbele na kutangaza Sabato kikamilifu zaidi… Waovu walifikiri kwamba tumeleta hukumu juu yao, na wakainuka na kushauriana kutuangamiza kutoka kwa nchi, walifikiri kwamba wakati huo uovu utakomeshwa. Katika wakati wa taabu sisi sote tulikimbia kutoka mijini na vijijini, lakini tukafuatwa na waovu, walioingia katika nyumba za watakatifu na upanga.” Pia ukurasa wa 282, 283. “Naliona watakatifu, wakihama

181

mijini na vijijini, na wakiungana pamoja katika makundi, na kuishi katika maeneo ya faragha zaidi. Malaika waliwapatia chakula na maji, ilhali waovu walikuwa wanateseka kwa njaa na kiu. Kisha naliwaona watu wakuu wa dunia wakishauriana, na Shetani na malaika zake wakijishughulisha kuwazunguka. Nikaiona hati, ambayo nakala zake zilitawanywa katika sehemu mbali mbali za nchi, zikitoa amri kwamba isipokuwa watakatifu waisalimishe imani yao ya kipekee, waiache Sabato, na kuiadhimisha siku ya kwanza ya juma, watu walikuwa huru baada ya muda fulani, kuwaua.” Yeremia pia huelezea wakati huu wa taabu. “Wachungaji na makundi yao ya kondoo watamjilia; watapiga hema zao karibu naye pande zote; watalisha kila mmoja mahali pake.” Yer. 6:3. {SR1: 180.3}

Mika 4:12, “Lakini wao hawajui mawazo ya Bwana, wala hawafahamu shauri lake; Kwa maana atawakusanya kama miganda sakafuni.” Waovu hawawezi kumfahamu Mungu. Wakati wanatafuta kuwaangamiza watu Wake badala yake wao wanausimamisha mti wa kuwanyongea wenyewe. Jinsi Hamani mwovu aliandaa mti wa kutoa uhai wa Mordekai, Myahudi, alifanikiwa tu kutundika mwenyewe shingo yake juu yake, vivyo hivyo waovu watachanganyikiwa katika siku ya Mungu, maana hawayafahamu mawazo ya Bwana. {SR1: 181.1}

Mika 4:13, “Haya simama upure, Ee binti Zayuni: Kwa maana Nitafanya pembe yako kuwa chuma nami Nitazifanya kwato zako kuwa za shaba. Nawe utaponda-ponda mataifa mengi; na faida yao utaiweka wakfu kwa Bwana, na mali zao kwa Bwana wa dunia yote.” Kanisa la Mungu litapura livune, lifunge matita, lichome na kuharibu. Waovu wataangamia na kuwa kana kwamba hawahi kuwapo. “Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu ambao wasiotaka kukutumikia wataangamia; naam, mataifa hayo yataangamizwa kabisa.” Isa. 60:12. {SR1: 181.2}

182

MUHTASARI WA MAFUNZO YA MATENGENEZO 

Nini Hufanza Makafiri

Swali limeulizwa Je! Ni nini huwafanza makafiri? Kwanza kabisa, tutalifafanua neno. “Kafiri,” — “mtu ambaye hana imani ya kidini.” Kamusi Sanifu. Iwapo hii ni kweli, basi aliye na dini, iwe ya aina yoyote, si kafiri. Ni ukweli unaokubalika kwamba wale walio kwa pembe fulani ya dunia gizani, mbali na ustaarabu, au Ukristo, si watu wasio wanadini. Yaani, kama sheria wao huamini katika aina fulani ya kiumbe kikuu, au nguvu isiyo ya kawaida. Hili likiwa hivyo, lazima tukiri kwamba himaya ya wapagani haichangii uzorotaji huu unaofagilia kwa kasi sana katika mataifa. Ukafiri una chanzo chake katika nchi zilizostaarabika. Jitihada itafanywa hapa kutaja ni nani anayehusika moja kwa moja na uovu huu ulioenea, ambao, kama saratani unakula na kuondoa maadili ya mataifa. {SR1: 182.1}

Hoja ifuatayo iliwasilishwa kwa hadhira katika jiji kuu fulani hivi karibuni na mtu ambaye alikuwa amevalia mavazi ya Kihindi, na ambaye alidai kuwa Chotara. Mtu huyu alisema, “Dunia yetu hii huzunguka kwenye mhimili wake mara moja kwa kila masaa ishirini na nne. Wakati wa mchana tunasimama juu ya dunia na jua likiwa juu ya kichwa, lakini usiku tunasimama chini ya dunia, tukining’inia kwa miguu yetu mwezi na nyota zikiwa chini yetu angani. Ukikutana na Mkristo wakati wa mchana, “aliendelea Mhindi huyo,” na umwulize anaenda wapi, atakuambia anaenda mbinguni. Ukimuuliza, Mbingu iko wapi? anaelekeza juu kwa jua, na kusema, ‘Huko ni mbinguni.’ Lakini ukutane naye saa kumi na mbili baadaye, usiku wa manane, wakati yuko chini ya dunia, na umwulize basi mbingu iko wapi. Wakati huu anaelekeza juu kwenye nyota, akifikiri yuaelekeza katika mwelekeo ule ule kama alivyofanya wakati wa mchana, na kusema, ‘Huko ni mbinguni.’” {SR1: 182.2}

Halafu akaongeza, “Wakristo hawajui mbingu iko wapi, wala hawajui ni njia ipi wanaenda. Haijalishi ni wakati wa mchana au usiku, siku zote huelekeza wima juu. Isitoshe,

183

wanajimu wamekuwa wakipiga picha za jua na sayari kwa miaka mingi. Baadhi ya hizi jua ziko mbali sana angani ingechukua mamilioni ya miaka ya nuru kufika huko, lakini bado hawajawahi kupiga picha mbinguni [kiliko kiti cha enzi cha Mungu], kwa hivyo iwapo iko mbingu yoyote, lazima iwe mbali sana hivi kwamba ikiwa Wakristo hawa wangesafiri kwa kasi sana kama mwangaza (maili 186,000 kwa sekunde), ingewagharimu mamilioni kwa mamilioni ya miaka kufika huko. Hili halingewezekana kwa kipindi cha maisha ya mwanadamu umewekewa kikomo kwa miaka michache tu.” {SR1: 182.3}

Lile ambalo Mhindi huyu amesema ni kweli, kadiri pingamizi lake linavyohusika, na kuhusu kutowezekana mtu kufika mbinguni, yaani kunena kibinadamu. Itachukua muda angalau mwanafunzi mzuri wa Biblia kutoa jibu la kumridhisha kafiri wa aina hii lakini wazo lililokusudiwa hapa, ni kwamba kukutana kwa Mkristo na yule Mhindi kulimfanya (Mhindi) kuwa kafiri badala ya Mkristo. Uovu haukukoma hapo, maana kwa upande wake, yule Mhindi sasa anafanza mamia na maelfu ya watu makafiri kwa kutumia kinachoitwa eti nuru aliyopokea kutoka kwa yule anayeitwa eti Mkristo. Uzoefu wa Mhindi huyu hufundisha kwamba mtu yeyote anayekiri jina la Kristo, mwenendo wake wa kutenda na mazungumzo anapokutana na ulimwengu, ana mvuto wa maamuzi kwa heri au uovu, na kwa zamu, kama mawimbi ya bahari, wimbi moja hubeba lingine, na lingine tena lingine. “Tupa kijiwe ndani ya ziwa, na wimbi hufanyizwa, na lingine, na lingine tena, na kadiri yanavyoongezeka mduara hupanuka hadi ufike ufuoni kabisa. Hivyo kwa mvuto wetu; zaidi ya ufahamu au udhibiti wetu husimulia wengine katika baraka au katika laana.” Mafunzo ya Yesu kwa Mifano, ukurasa wa, 343, 344. {SR1: 183.1}

Ni dhahiri yapo makundi mawili ya Wakristo. Kundi moja hufanya wanafunzi kwa Kristo, ilhali kundi lingine huchangia makafiri dhidi ya Kristo. Tunaweza kujiuliza, Je! Mimi ni wa kundi gani? 2 Kor. 13:5, “Jichunguzeni wenyewe, kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu, isipokuwa mmekataliwa?” Kunukuu 2 Tim. 2:15, “Jitahidi kujionyesha umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la ukweli.” Amri hii ni nzuri kama amri yoyote ya Biblia. Angalau inapaswa

184

kuwa nzuri kama amri ya tano ya sheria. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” Kut. 20:12. {SR1: 183.2}

Iwapo baba amwamuru mwanawe afanye jambo fulani na mwana huyo akatae kutii, amekosa kumheshimu baba yake wa hapa duniani, na amekuwa muasi wa amri ya tano. Lakini ikiwa mtu anaulizwa kufanya jambo fulani na Baba yake wa mbinguni na akatae kuitikia mwito huo, mtu kama huyo amekosa kumheshimu Baba yake wa mbinguni, na amekuwa muasi kwa amri ya kwanza, “Usiwe na miungu mingine ila Mimi.” Kwa kweli, anavunja amri nne za kwanza ambazo ni heshima kwa Mungu, ilhali sita za mwisho ni upendo kwa mwanadamu. “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yak. 2:10. {SR1: 184.1}

Kunukuu sehemu ya kwanza ya 1 Pet. 3:15, “Bali mtakaseni Bwana Mungu mioyoni mwenu.” Maana yake ni kwamba Mungu peke yake anapaswa kukaa moyoni na hakuna kitu kingine kinachopaswa kuingilia kati. Inawezekana kwa mtu kutii amri katika 2 Tim. 2:15, kama ilivyonukuliwa hapo awali, lakini bila utakaso wa moyo wake kwa Bwana Mungu, ikiwa atatumia muda wa maisha kusoma, itakuwa bure kuhusiana na mambo ya kiroho, ambayo tunazungumzia. Kwa upande mwingine, iwapo mtu atatii amri hizi mbili (1 Pet. 3:15 na 2 Tim. 2:15), basi lazima awe na uwezo wa kutimiza sehemu ya mwisho ya aya hiyo, “mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu.” 1 Pet. 3:15. Aina ya jibu tunalompa kila mtu huthibitisha ikiwa tunashika amri za Mungu au la. Iwapo jibu letu ni kama la Mkristo aliyetajwa hapo juu, basi sisi pia hatujui mbingu iko wapi, wala hatujui tunakokwenda. Mvuto wetu utakuwa kama ule wa kufanza makafiri dhidi ya Kristo badala ya kuwa wanafunzi wa Kristo. Mkristo ambaye amemtakasa Bwana Mungu moyoni mwake anaweza kutoa jibu bora kwa Mhindi aliyetajwa hapo juu kuliko yule anayeitwa eti Mkristo. {SR1: 184.2}

Kunukuu Isa. 14:13, “Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; nami Nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za

185

mwisho za kaskazini.” Lusifa alitaka kupanda mpaka pande za kaskazini kwa sababu huko ndiko kiliko kiti cha enzi cha Mungu, na mahali kilipo kiti cha enzi cha Mungu, huko ndiko iliko mbingu pia. Iwapo Mkristo huyu angekuwa ameonyesha kuelekea kaskazini saa sita adhuhuri sawa sawa na dira, na katika mwelekeo uo huo usiku wa manane, au kwa wakati wowote, miisho ya mistari yote iliyo mbali ingekutana mahali pale pale. Jibu hili lingekuwa sahihi na la kufundisha pia. Mjeledi dhidi ya mbingu pamoja na mchafuko ungeepukwa, na jumla ya mema yanayotokana na jibu la hekima hayangeweza kukadiriwa. Jibu kwa Mhindi huyu, na maelekezo ya mbinguni yametolewa mwishoni mwa sura hii. {SR1: 184.3}

Lusifa alisema atapanda mpaka pande za kaskazini. Angeweza kupanda iwapo angalikuwa ametii amri ya Bwana. Lakini hapana, Lusifa alifikiri alijua vyema kuliko Mungu wake, na alitaka kufanya uboreshaji mbinguni. Akiwa mwaminifu katika udanganyifu wake, alijaribu kazi isiyowezekana. Katika Isa. 14:15, tunasoma: “Lakini utashushwa mpaka kuzimu, mpaka pande za mwisho za shimo.” Tokeo lake badala ya kupanda pande za kaskazini ambako alitaka kwenda, alishuka chini katika pande za shimo (kwa upande ulio kinyume). Vivyo hivyo, Wakristo wengi sasa, kama Lusifa, hufikiri wanaenda kupanda juu pande za kaskazini (Mbingu) lakini katika njia yao wenyewe, wakitaka kuboresha hekima ya Mungu aliye Hai. Wanavutiwa sana kwenda mbinguni kuliko wanavyostahili kujifunza na kutii maagizo dhahiri waliyopewa katika Neno la Mungu. Ingawa ni waaminifu katika dhana yao potofu ya mwelekeo wa mbinguni, watajikuta chini katika pande za shimo (kuzimu). Kuvunjika moyo kwa mtu kama huyo kutakuwa kukubwa kuliko tunavyofikiria. Uzoefu tu unaweza kusimulia huzuni na sikitiko kwa wakati kama huo. Kundi hili la Wakristo sio tu kwamba wanajidhuru wenyewe, bali ni wa kuwadhuru wengine, na ndio wale ambao Bwana wetu alisema, “Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya.” Yohana 8:44. {SR1: 185.1}

Kunukuu 2 Kor. 13:5, “Jichunguzeni wenyewe, kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu, isipokuwa mmekataliwa?” Sisi, kama Waadventista wa Sabato, hatungefanya kosa lo lote kwa mbingu wala dhuluma

186

kwetu wenyewe iwapo tungechukua hesabu ya uzoefu wetu wa Kikristo ili tuweze kujua tunakoelekea. Sisi, kama watu, tumeheshimiwa na mbingu na ujumbe maalum kwa ulimwengu katika kizazi hiki. Huuita ujumbe huu “Ujumbe wa Malaika wa Tatu” ambao ni mseto wa ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu wa Ufu. 14:6-12. Kiini cha ujumbe tunaoutangaza unaweza kupangwa katika masomo matano: (1) wakati wa mwisho; (2) hukumu (siku ya upatanisho, tangu mwaka 1844); (3) kuja mara ya pili kwa Kristo katika kizazi hiki; (4) urejesho wa Sabato ya kweli; (5) kuwaita watu wa Mungu kutoka Babeli (ibada ya sanamu) ambayo tunafafanua kuwa ni Jumapili, Pasaka, na maadhimisho ya Krismasi, n.k. Kwa sababu wamekataa kukiri na kuacha utamaduni wa hizi zinazoitwa eti taasisi au sherehe za Kikristo ndio sababu kuu ya anguko la Babeli. Mwito ni wayaache mazoea haya ya kipagani hadi kwa ibada ya kweli ya Yehova. {SR1: 185.2}

Tunafundisha kutoa zaka kwa kutegemeza injili. Huwa tanadai kwamba sisi ni watu ambao huzishika amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu, ya mwisho ikiwa ni karama ya Roho wa Unabii; pia mafundisho ya matengenezo ya afya, matengenezo ya mavazi, n.k. Kusudi kuu na la pekee la mafundisho haya likiwa ni kuandaa watu wa pekee kwa utukufu na heshima ya Mungu mwenyewe; watu watakaomlaki Bwana bila kuonja mauti, au, kuamka katika ufufuo maalum wa Danieli 12. “Bali ninyi ni mzao mteule, Ukuhani wa kifalme, na taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu; mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.” 1 Pet. 2:9. {SR1: 186.1}

Ujumbe huu utapenyeza katika sehemu za miisho za dunia, maana kwa huo ulimwengu utahukumiwa. Watakaokataa watahukumiwa kifo, ni ujumbe wa kuogofya sana kuliko tunavyoweza hata kutambua. Hiki ndicho kiini na lengo la ujumbe tunaoutangaza kwa kila jamaa, lugha, na watu, na uwasilishaji wake mbele ya umma katika maajabu yake yote unayo athari kubwa. Watu husikiliza kwa upendezo mwingi sana na kukazia fikira, wakiwa na bidii ya kuelewa kila wazo linaloelezwa. Wakipendezwa katika ukweli, wanaanza kuchunguza kwa

187

undani zaidi katika Neno. Wanajipatia vitabu vya Roho ya Unabii, na kwa hamu kubwa wanaanza kuchunguza katika hizo kurasa takatifu. {SR1: 186.2}

Kwa kuamini jinsi ambavyo wamefunzwa kwamba hii ni siku ya hukumu, wao hutarajia kuona watu wa Mungu wakijiondoa katika dhambi zote kwa kutii Neno Lake takatifu, na haswa maagizo yaliyokabidhiwa kanisa na mjumbe Wake katika kizazi hiki. Wanapochunguza katika maandishi ya Roho ya Unabii, kwa kawaida huja kwa vifungu vifuatavyo: Mashauri kwa Afya, ukurasa wa 277: “Mawazo yetu ya kujenga na kupamba taasisi zetu yanapaswa kufinyangwa na kufanyizwa kulingana na ujuzi wa kweli, na maarifa ya kinachomaanisha kutembea kwa unyenyekevu na Mungu. Kamwe haipaswi kufikiriwa kwamba ni muhimu kutoa taswira ya utajiri. Kamwe taswira haipaswi kutegemewa kama njia ya kufanikiwa. Huu ni udanganyifu. Tamaa ya kufanya taswira ambayo sio kwa kila njia inayofaa kazi ambayo Mungu ametupatia kufanya, taswira ambayo inaweza kudumishwa tu kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha, ni udhalimu usiokuwa na huruma. Ni kama donda-ndugu ambalo daima hula ndani ya utumbo. {SR1: 187.1}

“Watu wanaotumia akili huthamini utulivu kuliko madaha na maonyesho. Ni makosa kudhani kwamba kwa kuendeleza wonyesho, wagonjwa zaidi, na kwa hivyo fedha zaidi, zitapatikana. Lakini hata kama mwenendo huu utaleta ongezeko la udhamini, sisi “hatutaidhinisha kuruhusu hospitali zetu kupambwa kulingana na maoni ya anasa ya kizazi hiki.” {SR1: 187.2}

Gombo la 5, ukurasa wa 188, ukimzungumzia Abrahamu, Isaka na Yakobo: “Waliishi tu kwa utukufu wa Mungu, na walitangaza wazi wazi kwamba wao ni wageni na wasafiri duniani wakiitafuta nchi iliyo bora, ambayo ni ya mbinguni. Mwenendo wao ulitangaza imani yao… Lakini leo watu wanaokiri kuwa wa Mungu wanadumishaje heshima ya jina Lake? Je! Ulimwengu unawezaje kuelewa kwamba wao ni watu wa kipekee? Je! Wanatoa ushahidi gani wa uraia wa Mbinguni?… Kadiri mwenendo wenu ulipokuwa ukiwasilishwa mbele yangu nalielekezwa kwenye makazi yaliyojengwa hivi karibuni na watu wetu katika mji huo. Majengo haya ni minara mingi sana ya kutokuamini kwenu mafundisho ambayo mnadai

188

kushikilia. Yanatangaza mahubiri kwa ufanisi zaidi kuliko yoyote yanayowasilishwa kutokea kwenye mimbari. Naliona walimwengu wakiyaelekezea kidole kwa mzaha na dhihaka, kumaanisha kuikataa imani yetu. Yanatangaza yale ambayo wamiliki wamekuwa wakinena mioyoni mwao, — ‘Bwana wangu anakawia.’” {SR1: 187.3}

Gombo la 7, ukurasa wa 59, 91, 92: “Bwana ameniamuru niwaonye wale ambao katika siku za baadaye wataanzisha vituo vya hospitali katika maeneo mapya, waanzishe kazi yao kwa unyenyekevu, wauweke wakfu uwezo wao kwa utumishi Wake. Majengo yatakayojengwa hayapaswi kuwa makubwa au ya gharama ya juu. Hospitali ndogo za mitaa lazima zianzishwe kuhusiana na shule zetu za mafunzo”…”Lazima pia tukumbuke kwamba kazi yetu ipatane na imani yetu. Tunaamini kwamba Bwana atakuja hivi karibuni, na imani yetu haipaswi kuwakilishwa katika majengo tunayojenga? Je! tutaweka fedha nyingi katika jengo ambalo litateketezwa hivi karibuni katika moto mkubwa? Fedha zetu humaanisha roho, na zinapaswa kutumika kuleta maarifa ya ukweli kwa wale ambao, kwa sababu ya dhambi, wako chini ya hukumu ya Mungu.” {SR1: 188.1}

Gombo la 9, ukurasa wa 71: “Mungu hukusudia kwamba tutajifunza mafunzo kutoka kwa kushindwa kwa zamani. Haimpendezi kuwa na madeni kuzilemea taasisi Zake. Tumefikia wakati ambapo lazima tuipatie kazi Yake sifa kwa kukataa kujenga majengo makubwa na ya gharama ya juu. Tusiige makosa ya zamani, na kujihusisha zaidi katika deni.” {SR1: 188.2}

Ni fursa ya msomaji kuuliza kutoka kwa watu wa Mungu kwa nini maagizo yaliyotolewa na yule ambaye tunaamini kuwa nabii wa Mungu kwa wakati huu wa sasa hayajatekelezwa. Sasa tunakabiliwa uso kwa uso na andiko letu, “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu.” 1 Pet. 3:15. Je! Ni jibu gani tunaweza kutoa ambalo lingeonyesha upole na hofu ndani ya mioyo ya watu wa Mungu? Je! Jibu letu lingetoa sifa kwa kazi ya Mungu na watu Wake? Je! Jibu hilo linaweza kuisimamisha imani ya huyo mdadisi katika ujumbe na watu wanaolibeba jukumu hili kubwa? Tutasema nini? Iwe ni kwa neno au kimya, hilo

189

jibu linaweza kuwa tu, “Naam, hilo ndilo nabii husema, lakini sio tunalotenda.” Je! Jibu kama hilo litamvutia mtu kwamba tunaamini kwamba hii ni siku ya upatanisho, na ya kwamba kila mtu lazima aungame dhambi yake? Je! Mtu huyo sasa aweza kuupokea ukweli na kuwa Mkristo? Au je! Yeye, na yule Mhindi aliyetajwa hapo awali awe kafiri? Uwezekano mkubwa angekubali wa mwisho, na ukweli kukakataliwa. Lakini hapa sio mahali ambapo uovu hukomea. {SR1: 188.3}

Mwingine yuaja na swali lifuatalo: “Ninyi huhutubu kwamba Krismasi si siku ya kuzaliwa ya kweli ya Kristo; kwamba ni siku ya kuzaliwa kwa mlaghai, siku ya taasisi ya kipagani, na ibada ya sanamu. Mmetuambia kwamba Wakristo hawapaswi kushiriki ndani yake, na kwa sababu hii tunatakiwa tutoke ndani ya Babeli iliyoanguka. Mbona basi ninyi hufanya sawa na wale walioko Babeli? Mnatoa zawadi na kupokea zawadi, mnatuma na kupokea salamu za Krismasi kama wale ambao hawajui tofauti.” Je! Tutampa jibu gani mdadisi huyu wa pili ambalo litasimamisha imani yake katika kile tunachokiamini? {SR1: 189.1}

Iwapo tunajibu hilo swali au la, matendo yetu yametangaza, “Naam, hivyo ndivyo tunavyohubiri, lakini sivyo tunavyotenda.” Je! Huu si unafiki wa namna ya juu kabisa? Je! Jibu letu sasa limeilazimisha nafsi hii maskini kupokea au kukataa ukweli? Uwezekano mkubwa ataukataa ukweli na kujiunga na safu ya ukafiri sasa ikiwa hajawahi hapo awali. Lililo kweli kuhusu Krismasi, liko vivyo hivyo kuhusu Pasaka, n.k., lakini upepo haukomi hapa. {SR1: 189.2}

Mtu wa tatu kwenye mstari anakuja na vifungu vifuatavyo: Gombo la 6, ukurasa wa 215, 216, “Mabaraza yetu huangalia katika shule wafanyakazi waliosoma na kufunzwa vyema, na yanapaswa kuzipatia shule hizo udhamini wenye moyo na akili. Nuru imepeanwa wazi kwamba wale wanaohudumu katika shule zetu, wakifundisha neno la Mungu wakiyafafanua Maandiko, wakiwafundisha wanafunzi katika mambo ya Mungu, wanapaswa kudhaminiwa kwa fedha za zaka… Kanuni zile zile ambazo, iwapo zitafuatwa, zitaleta mafanikio na baraka kwa shule zetu za mafunzo na vyuo, zinapaswa kudhibiti mipango yetu na kazi kwa shule za kanisa.” Nabii huyu ambaye ninyi husema ni nabii wa Mungu sema hivi

190

na vile. Mbona basi hamwalipi walimu wetu wa shule kwa zaka jinsi ambavyo Mungu ameamuru? Mbona mnaitia Sabato unajisi kwa kuchanga mshahara wa walimu katika saa ya ibada? Iwapo huyu ni nabii wa Mungu, kwa nini mmedharau maagizo mliopewa? Je! Humumchi Mungu? Sasa mtu huyu aweza kuambiwa nini? Yawezekana tusiseme lolote. Lakini hilo halitaficha uovu huo maana matendo yetu yamefunua siri ifuatayo, “Naam, hilo ndilo Mungu amesema kupitia kwa nabii Wake, lakini sivyo tunavyofanya.” {SR1: 189.3}

Kiasi gani cha zaka mnachofikiri mtu huyu atalipa baada ya kujua kwamba tumeitumia vibaya? Je! Mazoea kama hayo yataimarisha imani yake kwa ujumbe na kwa watu? Je! Sasa atajinyima siku moja kwa juma na sehemu moja kwa kumi ya mapato yake na labda nafasi [kazi] yake? Nafsi yake iko hatarini, na itahitajika kwa kichwa cha nani? Hilo laogofya, sivyo? {SR1: 190.1}

Wa nne anawasili na Gombo la 1, ukurasa 471, 472: “Kosa kubwa limefanywa na baadhi ya watu wanaokiri ukweli wa sasa, kwa kuingiza biashara katika mkondo wa mfululizo wa mikutano, na kwa ulanguzi wao kukengeusha mawazo kutoka kwa kusudi la mikutano. Laiti Kristo angalikuwa sasa duniani, angewafukuza hawa wachuuzi na walanguzi, iwapo ni wachungaji au watu, kwa mijeledi ya kamba ndogo, kama alipoingia hekaluni zamani…’ Akawaambia, Imeandikwa, nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala, lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wezi.’ Wafanyabiashara hawa wangeweza kusihi kama udhuru ya kwamba bidhaa walizoshikilia kuuza zilikuwa kwa ajili ya sadaka za dhabihu. Lakini kusudi lao lilikuwa kupata faida, kupata raslimali, kujilimbikizia… Wachungaji wamesimama katika mimbari na kutoa mahubiri ya utakatifu, na kisha kwa kuingiza biashara, na kutenda sehemu ya muuzaji, hata katika nyumba ya Mungu, wamezikengeusha dhamira za wasikilizaji wao kutoka kwa mashauri yaliyopokelewa, na kuharibu matunda ya kazi yao… Wakati na nguvu zao zinapaswa kuhifadhiwa, ili juhudi zao ziweze kuwa za uangalifu katika mfululizo wa mikutano. Wakati na nguvu zao hazipaswi kutumika kuuza vitabu vyetu wakati vinaweza kuletwa mbele ya umma na wale ambao hawana mzigo wa kulihubiri neno.” {SR1: 190.2}

191

Mtu huyu mgeni aliyependezwa anauliza swali, “Mbona ninyi huuza machapisho yenu kanisani? Kwa nini mnaitia Sabato unajisi kwa bidhaa zenu? Je! Saa za Sabato asubuhi sio takatifu na za ibada pekee? Mmenambia huu alikuwa nabii wa Mungu kwa kizazi hiki. Kwa nini mmedharau lile onyo? Je! kitabu hiki hakijaandikwa na nabii huyo ambaye mnadai kumwamini?” Tutamwambia nini mtu huyu? Je! Lipo lolote tunaweza kusema ambalo litaweza kutuondolea hatia? Ikiwa tunajibu kwa neno, au kwa ukimya, matendo yetu yameonyesha tendo lifuatalo, “Naam, hivyo ndivyo nabii wa Mungu amesema, lakini sivyo tunavyotenda.” Tumeimba wimbo wetu, lakini vipi kuhusu roho ya mtu huyu? {SR1: 191.1}

Mtu anayefuata yuaja na Gombo la 8, ukurasa wa 141, 142: “Wale ambao ni imara kwa ukweli hawapaswi kutengwa kwa kuwapendelea walimwengu. Bei hazipaswi kuwekwa juu sana ili kukidhi gharama za sasa hivi kwamba maskini, kwa kiasi kikubwa, watatengwa na manufaa ya Hospitali.” {SR1: 191.2}

“Kitabu hiki kinachodaiwa kuwa ni neno la Mungu lililovuviwa, na ambacho husemekana kuwa kinasheheni maagizo yote kwa kanisa kwa wakati huu wa sasa husema taasisi za dhehebu hazipaswi kuweka bei zao juu kukidhi matumizi (ya kuziendesha) ya sasa. Ripoti ya hivi punde na Bulletin kwa mujibu wa Baraza Kuu mwaka 1930 ni: Dhehebu limepokea mapato ya jumla ya $ 116,000,000 kwa miaka minne kutoka kwa taasisi hizi. Iwapo nabii huyu wa Mungu amesema, “Hampaswi kuweka bei zenu juu kukidhi matumizi ya sasa,” vipi basi mlitengeneza mamilioni haya ya dola kwa miaka minne mifupi tu? Kwa nini hamjafuata maagizo? Je! Mungu wenu huwa hamaanishi yale Asemayo?” {SR1: 191.3}

Jibu letu litakuwa nini wakati huu? Je! Tutasema ni bora kutoa dhabihu kuliko kutii? Je! Hili ndilo huwa tunafundisha? Au tutasema Mungu amekuwa kigeugeu na hajali hata kidogo iwapo neno Lake linaheshimiwa au la? Je! Tutasikia “umetenda vyema” kwa kumpoteza kondoo na kuleta madola? Je! Yeye yuatafuta dhahabu kuliko kondoo? Tutasema nini? Je! Tutasema taasisi zetu zinastawi

192

na maamuzi yetu ni bora kuliko ya Mungu? Hatuwezi kunena haya kwa maneno, lakini matendo yetu yamefunua yale yaliyo mioyoni mwetu. Lakini vipi kuhusu roho hii maskini? Je! Atapiga kura yake pamoja na watu wa Mungu, au kwa nafasi ya ukafiri? Lo! ni nani atakayelipa thamani ya damu yake? {SR1: 191.4}

Mstari bado haujafikia mwisho wake, kwa maana mwingine mdadisi yuaja na idadi kubwa ya marejezo, yote kutoka katika Biblia na Roho ya Unabii, akitaka kuuliza juu ya maagizo ya kanisa kuheshimu matengenezo ya afya. Vitabu hivi, ambavyo hudaiwa vimeandikwa kwa ajili ya watu wa Mungu kwa kizazi hiki cha mwisho hufundisha uzingatifu wamatengenezo ya afya. Nabii huyu ameliagiza kanisa kuanzisha taasisi za afya kila mahali, zikijumuisha Maduka ya utengenezaji vyakula vya afya, migahawa ya afya, shule na walimu kwa sanaa ya upishi; pia kwamba washiriki wa kanisa lazima wajiepushe na vyakula ambavyo huhesabiwa na mamlaka ya afya kuwa havifai kiafya. {SR1: 192.1}

Matengenezo ya afya yanastahili kuchochewa kila mahali, na inaonekana nabii huyu yu sawa katika suala hilo. Nabii huyo pia hudai kwamba wale ambao hupuuza kanuni za afya hawawezi kuingia ndani kupitia malango ya lulu ya Mji Mtakatifu, kwa mujibu wa taarifa ifuatayo kutoka katika Gombo la 5, ukurasa wa 197: “Badala ya kukaa mezani ambapo chakula bora kimeandaliwa, atapendelea kula katika migahawa, kwa sababu huko anaweza kuridhisha ulafi bila kujizuia… Mtu huyo anaabudu katika kihekalu cha hamu potovu. Yeye ni mwabudu sanamu. Nguvu ambazo, zikitakaswa na kuadilishwa, zinaweza kutumika kumheshimu Mungu, zinadhoofishwa na kufanywa kuwa za utumishi kidogo. Kukasirika ovyoovyo, ubongo uliochanganyikiwa, na mishipa iliyolegea ni miongoni mwa matokeo ya kupuuza sheria za maumbile. Yeye ni dhaifu kiutendaji, asiyetegemewa… Hivyo Mungu wa Israeli anavunjiwa heshima, ilhali uwezo wa Shetani unaheshimiwa na kuinuliwa.” {SR1: 192.2}

Gombo la 2, ukurasa wa 69: “Mwenendo mbaya wa kula au kunywa huharibu afya, na pamoja nao utamu wa maisha… Maelfu wameshindwa kuzuia tamaa zao potovu za kula, wamekula chakula kizuri, jinsi walivyokiita, na kama tokeo, wamejiletea homa, au maradhi

193

mengine makali, na kifo hakika. Hiyo ilikuwa raha iliyonunuliwa kwa gharama kubwa. Hata sasa wengi wamefanya hivi, na hawa wanaojiua kimakusudi wamesifiwa sana na marafiki zao na mchungaji, na kupelekwa moja kwa moja Mbinguni wakati wa mauti yao. Wazo lililoje! Walafi Mbinguni! La, hapana; kama hao hawataingia kamwe kwenye malango ya lulu ya mji wa dhahabu wa Mungu.” {SR1: 192.3}

“Iwapo mambo haya yameandikwa na nabii wa Mungu, kama inavyodaiwa, kwa nini mmechukulia kwa wepesi shauri la Bwana? Mbona watu wenu wengi hula vyakula vya nyama? Nabii aliandika kwamba watu wa Mungu lazima waache chakula cha nyama. Iwapo mambo haya ni hivyo, basi mnatarajiaje kuingia kupitia malango ya lulu? Je! Mungu wenu hamaanishi Analosema?” Je! Matendo yetu hayajatoa jibu lifuatalo kwa nafsi hii yenye bidii? “Naam, nabii husema hivyo, lakini sivyo tunavyotenda.” Mtu anaweza kusema, Ni jukumu la ukasisi kuwafunza watu kanisani, na lile ambalo sijui siwezi kuwajibika. Kwa manufaa ya mtu kama huyo tunanukuu andiko lifuatalo: “Basi wewe, Mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hilo kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mwovu, Ewe mtu muovu, hakika utakufa; nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo aiache njia yake, mtu mwovu huyo atakufa kwa uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.” Ezekieli 33:7, 8. {SR1: 193.1}

Wa saba, yuaja kwenye msitari na idadi kubwa ya marejezo kutoka katika Biblia na Shuhuda, anataka kuuliza kuhusu mambo kadhaa ambayo ni swali akilini mwake. “Je! Marejezo haya hayafundishi wazi wazi kwamba watu wa Mungu hawawezi na hawapaswi kufuata mitindo ya dunia, na ya kwamba mapambo yasitumiwe na washiriki wa kanisa? Gombo la 1, ukurasa 270: “Unabii wa Isaya 3, uliwasilishwa mbele yangu, kama unazihusu siku hizi za mwisho; na maonyo yanapeanwa kwa binti za Sayuni ambao wamefikiria tu kuonekana na kujionyesha. Soma aya ya 25: ‘Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.’ Nalionyeshwa kwamba andiko hili litatimizwa kabisa. Vijana wanaume na wanawake

194

wanaokiri kuwa Wakristo lakini hawana uzoefu wowote wa Kikristo, na ambao hawajabeba mizigo yoyote na hawajahisi wajibu wa kibinafsi, wanapaswa wathibitike. Watashushwa chini mavumbini, na watatamani uzoefu katika mambo ya Mungu, ambao wameshindwa kujipatia.” {SR1: 193.2}

Isa. 3:16-24, “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Zayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyooshwa na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao; basi kwa hivyo Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao. Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao, na pete za masikio, na vikuku, na taji zao, na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu, na pete, na azama, na mavazi ya sikukuu, na debwani, na shali, na vifuko, na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji. Hata itakuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa na uvundo, na badala ya mishipi kamba, na badala ya nywele zilizosukwa vizuri upaa, na badala ya kisibau mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.” {SR1: 194.1}

“Mbona basi washiriki wa dhehebu lenu wanavaa vitu hivi, na wanaruhusiwa kushiriki sehemu ya uamilifu katika kanisa hata kufikia kiwango cha kuhudumu ofisini, pia wakiwa wanabaraza la kanisa lenu? Maagizo ya nabii wenu ni, kwamba washiriki wa kanisa katika kuwavika watoto wao wanapaswa kuwasitiri sawasawa kwa mavazi, yakifunika sehemu zote muhimu za mwili.” Nabii huyu hudai kwamba maagizo haya lazima yafuatwe kwa karibu ili kulinda afya na ukomavu wa watoto wenu. Ninyi hudai huyu ni nabii wa Mungu na magombo haya husheheni maagizo kwa ajili ya kanisa kwa kizazi hiki. Kwa nini mmedharau ushauri wa nabii wenu? Je! Hamwamini maandishi haya, au mnafikiri maagizo haya si mazuri? Ikiwa hamjali maslahi ya watoto wenu, je! hamwogopi Mungu wenu?” {SR1: 194.2}

Maswali mengi yameulizwa, lakini wacha tuyajibu kwa

195

yafuatayo: Wakati Mungu wenu atatokea kulipiza kisasi juu ya waovu, na iwapo atawauliza maswali yote yaliyotangulia, Mtamjibu nini? Mat. 22:12-14 itanukuliwa hapa: “Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni, mkamtupe katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.” {SR1: 194.3}

Bado mwingine anataka kupata ukweli na anawasilisha swali lake kwa bidii wakati huu kutoka katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 475: “Unabii lazima utimizwe asema Bwana: ‘Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni hodari sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.’” “Nabii huyu mnayesema ni nabii wa Mungu hudai kwamba nabii mwingine, au ujumbe, utakuja kanisani, lakini mnasema kwamba mna ukweli wote na ya kwamba hamhitaji ukweli zaidi au manabii. Kwa nini hamjawaelimisha watu wenu kutarajia ujumbe kabla mwisho? Je! hamwogopi kwamba tokeo lake sasa laweza kuwa sawa na wakati wa Kristo na Wayahudi?” Swali hili litajibiwa na andiko lifuatalo. Tunamnukuu Kristo, akinena kwa Wayahudi, “Hivi mwajishuhudia wenyewe ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.” Mat. 23:31, 32. {SR1: 195.1}

Baada ya maswali haya yote kuulizwa bila kupata majibu sahihi, je! tumetii andiko, “mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu”? Hatupaswi kushangaa iwapo mdadisi anatoa maoni yake ya kibinafsi kwa njia ifuatayo: “Ninyi watu hufundisha jambo moja lakini mwatenda lingine. Mmeondoka kwa misingi ya fundisho lenu. Mafundisho yenu kama yalivyoandikwa katika vitabu vyenu ni mazuri na hupatana na sheria na

196

shuhuda, lakini ushuhuda wenu wa kibinafsi na mazoea yenu ni kinyume na lolote lililochapishwa katika vitabu vyenu.” Bila shaka hizi ni baadhi ya sababu mbona kati ya watu 104,000 waliobatizwa katika miaka minne iliyopita, maelfu fulani hamsini na mbili waliacha ukweli, na maelfu fulani tu arobaini na nane walibaki kanisani. Kumbuka kwamba idadi kubwa zaidi yao ilitoka kuliko wale waliokaa ndani. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo ni rahisi kuwafanza makafiri. {SR1: 195.2}

Mungu Huwafunulia Manabii Wake Siri

Iwapo Shuhuda kwa kanisa ziko na uhusiano wowote na Roho wa Mungu, na ikiwa mambo haya yaliyoandikwa katika makala hii ni kweli, basi lazima tuamini kwamba Mungu amefanya jambo hilo lijulikane kwa mtumwa Wake nabii, (mwasisi wa dhehebu hili). Njozi ifuatayo imenukuliwa kutoka Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 469: “Wakati Roho wa Bwana aliposhuka juu yangu, nalionekana kuwa katika mojawapo wa makongamano yenu. Mwanabaraza wenu mmoja alisimama, mwenendo wake ulikuwa wa uamuzi kabisa na wenye bidii alipokuwa ameshikilia mswada mbele yenu. Naliweza kusoma wazi wazi kichwa cha mswada huo; kilikuwa Mlinzi wa Marekani. Ukosoaji ulifanywa kwa huo mswada na mwandiko wa vipengee ndani yake kuchapishwa. Waliokuwa barazani walionyesha vifungu fulani, wakatangaza kwamba hiki lazima kiondolewe, na hicho lazima kibadilishwe. Maneno mazito yalitamkwa kukosoa mbinu za huo mswada, na roho yenye nguvu isiyokuwa ya Kristo ikashinda. Sauti zilikuwa zimeamua na kukaidi. Mwongozi wangu alinipa maneno ya kuonya na kukaripia niyaseme kwa wale walioshiriki katika mkutano huu, waliokuwa wepesi kutamka shutuma zao na kulaani. Kwa msingi hili ndilo karipio lililotolewa: Bwana hajaongoza katika kongamano hili, na ipo roho ya ugomvi kati ya washauri. Akili na mioyo ya watu hawa haiko chini ya mvuto wa udhibiti wa Roho wa Mungu.” {SR1: 196.1}

Mlinzi wa Marekani lilikuwa mojawapo wa majarida ya dhehebu katika siku za mwanzo za vuguvugu hili. Mabadiliko ambayo yalipendekezwa kufanywa hayamaanishi kwamba mambo yaliyokuwa haswa katika mswada huo yangebadilishwa au kuondolewa. Lazima tukumbuke kwamba ni njozi tu, na inaweza kumaanisha jarida lolote la dhehebu

197

lililo na ukweli wa Mungu. Tulisoma katika sehemu ya juu ya ukurasa uu huu ambayo njozi hii imenukuliwa: “Msifikiri kwamba mtapatikana kama vyombo vya heshima katika wakati wa mvua ya vuli, ili kupokea utukufu wa Mungu, iwapo mnaziinua nafsi zenu kwa ubatili, mkinena mambo ya upotovu, sirini mkikuza mizizi ya uchungu.” Kutokana na hili ni wazi kwamba njozi hiyo inagusa wakati punde tu kabla ya mvua ya vuli. {SR1: 196.2}

Unabii katika maono haya ulikuwa umetimizwa, na ni nani atakayethubutu kutilia shaka uthibitisho wa Roho wa Mungu? Nani angethubutu kuunga mkono ukiukaji wa wazi wa mambo matakatifu dhidi ya kujidhuru mwenyewe? Mungu ameunyosha mkono Wake ili awakomboe watu Wake. Farao na jeshi lake hawawezi kumshinda Mungu mwenye nguvu zote. “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataunyosha tena mkono wake mara ya pili ili awaokoe watu wake, watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari… Na Bwana ataungamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri, na kwa upepo wake mkali atatikisa mkono wake juu ya mto, naye ataupiga uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu. Na kutakuwa na njia kuu kwa mabaki ya watu wake, waliobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11:11, 15, 16. {SR1: 197.1}

Mungu bado atakuwa na watu wasafi na kanisa safi, na malango ya kuzimu haiwezi kulishinda. “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu: Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Isa. 52:1. “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; Wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; Kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” Zef. 3:13. {SR1: 197.2}

Sheria Ya Mungu — Imevunjwa Vipi?

Iwapo baba wa duniani angemwuliza mwanawe afanye jambo fulani, na huyo mwana akatae kufanya jambo hilo, amevunja sheria ya

198

amri ya tano, na huyo mwana, kwa kutotii kwake mwito huo, amekosa kumheshimu baba yake. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” Kut. 20:12. Lakini ikiwa Baba yetu wa Mbinguni ametuuliza tufanye jambo fulani, na tukatae kutii, tumekosa kumheshimu, na tumekuwa waasi wa amri ya kwanza. Kwa kweli, tutakuwa tumevunja amri nne za kwanza, ambazo ni za heshima kwa Mungu. Walio watiifu kwa maagizo haya ni wale wanaompenda Mungu na kuzishika amri Zake. “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kut. 20:3. “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi Nisemayo?” Luka 6:46. “Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mat. 7:21. {SR1: 197.3}

Je! Kanisa Liko Katika Hali Bora?

Katika Matangazo ya Baraza Kuu Namba 2, ya 1930, taarifa imefanywa kwamba tuko katika hali bora. Ongezeko katika washiriki na fedha linatolewa kama sababu ya kuunga mkono taarifa hiyo. Walakini, yule ambaye ataliamini dai hilo anasema moyoni mwake nukuu zifuatazo ni za uongo. Gombo la 3, ukurasa wa 252-257, 260: “Ujumbe kwa kanisa la Walaodekia ni wa kushtua na wa kuleta mashtaka, na unawahusu watu wa Mungu kwa wakati huu wa sasa…Watu wa Mungu wamewakilishwa katika ujumbe kwa Walaodekia kama katika nafasi ya usalama wa kimwili. Wako shwari, wanajiamini kuwa katika hali ya upeo wa mafanikio ya Kiroho. ‘Kwa sababu unasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu chochote; wala haujui ya kwamba wewe ni mwenye mashaka, na mnyonge, na maskini, na kipofu, na uchi.’ {SR1: 198.1}

“Ni udanganyifu mkubwa ulioje unaoweza kuja kwa akili za binadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wao wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli unawapata wa Mungu katika udanganyifu

199

wa kusikitisha, na hata sasa ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni ya kusikitisha machoni pa Mungu. Ilhali wale walengwa wanajidanganya kwamba wako kwenye hali ya juu ya kiroho, Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umaskini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayenena, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi. {SR1: 198.2}

“Ni vigumu kwa wale ambao wanajihisi salama katika ufanisi wao, na ambao hujiamini kwamba ni matajiri katika maarifa ya kiroho, kuupokea ujumbe ambao hutangaza kwamba wamedanganywa na wanahitaji kila neema ya kiroho. Moyo ambao haujatakaswa ni ‘mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha nani awezaye kuujua.’ Nalionyeshwa kwamba wengi wanajidanganya kwamba wao ni Wakristo wema ambao hawana mshale wa nuru kutoka kwa Yesu. Hawana uzoefu ulio hai kwa ajili yao wenyewe katika maisha ya utauwa. Wanahitaji uzoefu wa kina na wa kujishusha nafsi mbele ya Mungu, kabla wahisi hitaji lao la kweli la juhudi ya bidii, ya uvumilivu kuihifadhi neema yenye thamani ya Roho… Wanafikiri ushuhuda wa Roho wa Mungu katika makaripio haujahitajika, au ya kwamba haumaanishi wao. Kama hao wako katika hitaji kuu la neema ya Mungu na utambuzi wa kiroho, ili wapate kugundua upungufu wao katika maarifa ya kiroho… Lakini ujumbe wa Shahidi wa Kweli hufunua ukweli kwamba udanganyifu wa kutisha uko juu ya watu wetu, ambao hufanya kuwa lazima uje kwao kwa maonyo, iili kukatiza kusinzia kwao kwa kiroho, na kuwazindua kuchukua hatua ya uamuzi… Kutoamini kunawafumba macho, ili wasijue hali yao ya kweli. Shahidi wa Kweli anaelezea upofu wao: ‘wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.’ {SR1: 199.1}

“Imani katikaa kuja kwa Kristo hivi karibuni inadidimia. ‘Bwana wangu anakawia’ hayasemwi tu moyoni, bali huonyeshwa kwa maneno, na kwa uamuzi zaidi katika matendo. Ujinga katika wakati huu wa kukesha unaziba hisia za watu wa Mungu kuhusiana na ishara za nyakati. Uovu wa kutisha ambao umekuwa mwingi huitisha bidii kubwa

200

na ushuhuda ulio hai, kuzuilia dhambi nje ya kanisa… Wale wanaolidharau onyo hilo wataachwa katika upofu ili wajidanganye. Bali wale wanaolitii, na kwa bidii watekeleze kazi ya kujitenga kutoka kwa dhambi zao ili wapate neema zinazohitajika, watakuwa wanafungua mlango wa mioyo yao ili Mwokozi mpendwa aingie ndani na kukaa nao. Kundi hili utalipata daima likiwa katika upatano kamili na ushuhuda wa Roho wa Mungu. Wachungaji wanaohubiri Ukweli wa Sasa hawapaswi wasiupuuze ujumbe mtakatifu kwa Walaodekia… Shahidi wa Kweli hutangaza kwamba unapodhani u katika hali nzuri ya ustawi, u mhitaji wa kila kitu. {SR1: 199.2}

“Watu wa Mungu lazima waone makosa yao, na waamke kwa toba yenye bidii, na kuziondoa hizo dhambi ambazo zimewaweka katika hali ya kusikitisha ya umasikini, upofu, unyonge, na udanganyifu wa kutisha.” {SR1: 200.1}

Ukweli kwamba ndugu zetu hufikiri kwamba tuko katika hali bora huthibitisha kwamba Uvuvio husema ukweli. Huwa tunafikiri tuko sawa ilhali sote tumekosea. Kunukuu Gombo la 3, ukurasa wa 270, 271: “Wale wanaofanya kazi katika kicho cha Mungu kuondoa katika kanisa vizuizi, na kurekebisha makosa ya kuhuzunisha, ili watu wa Mungu waone umuhimu wa kuchukia dhambi, na kufanikiwa katika usafi, na ya kwamba jina la Mungu liweze kutukuzwa, watakumbana daima na vishawishi vya upinzani kutoka kwa wale ambao hawajajitoa wakfu. Zefania anaelezea hivyo hali halisi ya kundi hili, na hukumu za kutisha ambazo zitakuja juu yao.” “Huu ndio mji ule wa furaha, uliokaa pasipo kufikiri, uliosema moyoni mwake, Mimi niko, wala hapana mwingine ila mimi; umekuwaje ukiwa, mahali pa kulala pa wanyama wa bara? Kila mtu apitaye karibu atazomea, na kutikisa mkono wake.” Zef. 2:15. {SR1: 200.2}

“Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! Hakuitii sauti, hakukubali kurudiwa; hakumtumaini Bwana; hakumkaribia Mungu wake. Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; waamuzi wake ni mbwa mwitu wa jioni, hawasazi kitu chochote hata siku ya pili. Manabii wake ni watu hafifu na wadanganyifu.

201

Makuhani wake wamepatia unajisi patakatifu, wameifanya sheria udhalimu. Bwana kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.” Zef. 3:1-5. {SR1: 200.3}

Nini Kimepatikana Katika Kipindi Cha Miaka Minne Iliyopita

Katika Kongamano Kuu la mwaka 1930, lililofanyika San Francisco, Calif., Takwimu zifuatazo zimeripotiwa kwa msisimuko mkubwa na kujiinua kwa sifa bora za dhehebu kubwa. Ushirika wote ulimwenguni kote miaka minne iliyopita ulikuwa 250,988. Ripoti za hivi punde zilizopatikana mwaka 1930, kwenye kikao cha Kongamano la San Francisco zasema washiriki wameongezeka hadi 299,555. Ongezeko katika kipindi cha miaka minne tangu Kongamano Kuu la mwisho lililofanyika Milwaukee, Wisconsin, ni 48,567. Mapitio na Kutangaza, Juni 1, 1930, ukurasa wa 39-41. Ndugu wale hufikiri hili ni ongezeko kubwa la washiriki, na kwa hivyo, tuko katika hali bora, ndizo kelele. {SR1: 201.1}

Kisa cha msichana mdogo wa mkulima fulani kimesimuliwa jinsi alivyouza pauni chache za cheri kwa mgeni kwa dinari chache. Alifikiri itakuwa busara kuweka bangili yake ya dhahabu ndani ya mkoba wa cheri ili ziweze kumpa uzito zaidi, na kupokea fedha zaidi kwa kufanya hivyo. Mtoto huyo alisisimka ajabu kwa shughuli yake aliyodhani kuwa ya hekima, akakimbia ndani ya nyumba, na kwa furaha akapaza sauti kwa mamaye kwamba alikuwa amepokea fedha nyingi kuliko zile za kawaida kwa cheri zake kwa kutupa ndani ya hizo cheri bangili ya dhahabu. Kwa upande wa mtoto, lilikuwa ongezeko kubwa, na uamuzi wa hekima, lakini kwa ufahamu wa mama kuhusu kito cha thamani kubwa kilichopeanwa kwa uhalisi kilikuwa kivunja moyo kikuu. {SR1: 201.2}

Kujisifu kwa dhehebu kuhusu kinachoitwa eti ongezeko kubwa la washiriki ni kweli kama lililodhaniwa kuwa ongezeko kubwa la thamani ya cheri zilizouzwa na huyo msichana mdogo. Hebu tuchukue hesabu ya gharama ambayo tumelipa kwa faida ndogo ya washiriki. Tutajaribu kuthibitisha kwamba watoto waliozaliwa ndani ya dhehebu hili katika miaka minne iliyopita (iwapo waliokolewa kanisani), ongezeko la washiriki juu kidogo kwa 48,000 lingekuwa zaidi ya maradufu, hata ingawa hangekuwamo mmoja aliyeongezwa kutoka nje ya kanisa. Iwapo hii ni kweli,

202

basi zaidi ya nusu ya watoto waliozaliwa kwa dhehebu wamepotelea duniani, hata iwapo ziada yote ya washiriki wapya walikuwa watoto wa kanisa. Lakini ikiwa ongezeko hili halitoki kabisa ndani ya kanisa, basi watoto wengi wa dhehebu wamepotea, na hilo litamaanisha tumebadilisha vito (watoto) vyetu kwa waongofu wachache kutoka katika nchi za kipagani, jinsi yule msichana mdogo alivyobadilisha bangili yake ya dhahabu kwa uzani wa cheri. {SR1: 201.3}

Wazo la kutisha kama nini kuwapoteza watoto wako kwa idadi ya zaidi ya 97,000, na matumizi ya karibu $ 165,000,000, zote kwa muda wa miaka minne kuleta tu watoto wachache kutoka ulimwenguni. Iwapo unatambuliwa kwa kweli msiba ni mzito kuliko mtu anavyoweza kustahimili. Fikiri juu ya upotezaji mkubwa wa maisha, kujinyima, na kazi ndani ya hiyo miaka minne. Lakini sehemu mbaya zaidi ni kwamba tunajisifu badala ya kuomboleza, na kwa hivyo liko tumaini dogo tu la kuponya jeraha kubwa. Je! Si kweli kwamba Walaodekia ni vipofu na wamelala ilhali wanadhani wao ni matajiri na wamejitajirisha kwa mema? Sasa tutaleta ushahidi kwamba shtaka lililofanywa hapa ni la kweli. {SR1: 202.1}

Ongezeko la washiriki katika miaka minne iliyopita ni juu kidogo ya 19% tu. Hili lingemaanisha kwamba kanisa lenye washiriki 200 linapaswa kuzalisha watoto wasiopungua kumi kwa mwaka, au karibu 39 kila baada ya miaka minne. Makadirio haya ni ya chini sana, kutoka kwa kanisa ambalo linalofanyizwa aghalabu na wanawake jinsi la Waadventista wa Sabato lilivyo. Kwa mfano, tutazingatia kanisa la Exposition Park huko Los Angeles, Cal. Washirika wa sasa wa kanisa hili ni takribani 230. Karibu 30 wa washiriki hawa wametengwa na ni nadra kuhudhuria ibada za kanisa siku ya Sabato, kwa hivyo tutazingatia washiriki 200 tu ambao huhudhuria ibada za Sabato. {SR1: 202.2}

Ongezeko la washiriki kwa dhehebu katika miaka minne iliyopita likiwa juu kidogo ya 19%, kwa hivyo kanisa la kima kilichotajwa hapo juu linapaswa kuzalisha watoto wapatao 39 katika miaka minne au kuwa na watoto wapatao 39 kati ya miaka miwili hadi sita ili kukidhi ongezeko tumefanya. Chekechea katika Shule ya Sabato ya kanisa lililotajwa huchukua watoto kuanzia miaka miwili hadi saba. Mpito wa wakati ni miaka mitano badala ya minne. {SR1: 202.3}

203

Takwimu za kufikia ongezeko katika washiriki ni chini ya kumi kila mwaka kwa umri uliowekwa, kwa hivyo katika kipindi cha miaka mitano idadi ya watoto wa umri huo haingezidi 49 katika chekechea ya Shule ya Sabato iwapo kila mtoto wa umri huo alihudhuria idara iliyotajwa ya taasisi hii. Katika kanisa hili haswa, ni nusu tu ya washirika wa kanisa huhudhuria Shule ya Sabato, lakini nusu nyingine inaweza kuwapo tu kwa ibada ya kuhubiri, na pale ambapo wazazi hawako, watoto pia hawako. Kwa hivyo lazima iwepo chini ya nusu ya watoto kuanzia miaka miwili hadi saba walio katika idara ya chekechea ya Shule ya Sabato. Nusu ya watoto wa umri wa chekechea inapaswa kuwa chini ya ishirini na tano kufikia asilimia iliyoongezeka ya washiriki katika miaka minne. Idadi ya watoto katika taasisi iliyotajwa wanaohudhuria idara ya chekechea ya Shule ya Sabato ni karibu 35. Idadi inayohitajika kufikia madai hayo ni chini ya 25; kwa hivyo tuna 10 juu ya idadi iliyokadiriwa. Takwimu hizi huthibitisha asilimia ya watoto wanaozaliwa kila miaka minne kwa dhehebu hili kuwa si chini ya 35% ya washirika. Kwa hivyo, iwapo watoto wote wa dhehebu waliozaliwa kila baada ya miaka minne wangeokolewa kanisani, bila juhudi yoyote ya kueneza injili kwa waongofu wa nje, ongezeko kwa miaka minne iliyopita lingekuwa 35% badala ya 19%. Lakini ukweli ni, kwamba asilimia ya watoto kuzaliwa Marekani ni ndogo sana kuliko ile ya nchi za kigeni. Pale ambapo yuko mtoto mmoja katika nyumba ya Mwamerika, wapo wengine watatu zaidi katika nyumba ya nchi fulani ya kigeni, kwa hivyo watoto waliozaliwa kwa dhehebu hili kila baada ya miaka minne ni zaidi ya mara mbili ya ongezeko la washiriki kwa kipindi hicho hicho cha wakati. {SR1: 203.1}

Pale ambapo tumepata washiriki wapya 48,567, watoto waliozaliwa katika dhehebu hili wangekuwa wamezidi juu ya 97,000, na ya kwamba kwa takwimu hii wangeshughulikia wale ambao wamekufa, na wengine kuwanusuru. (Imekadiriwa wale waliokufa katika miaka iyo hiyo minne kuwa ni karibu 3500). Kwa hivyo tunao ushahidi kwamba “Kondoo” ambao Mungu amewapa hawa watu kuwalea kwa ajili Yake wamepotelea duniani (wameliwa na adui), na hakuna mtu

204

anayejali. Hakuna huzuni wala majonzi katika kambi ya Israeli, lakini badala yake, iko karamu na furaha na kujisifu na upofu. {SR1: 203.2}

“Liko wapi kundi lako ulilopewa, kundi lile zuri? Utasema nini wewe wakati atakuadhibu? Kwa kuwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako, na kuwa wakuu juu yako: Je! Huzuni haitakushika, kama utungu wa mwanamke aliye katika kuzaa?” Yer. 13:20, 21. “Aliye hai, naam aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; baba atawajulisha watoto kweli yako.” Isa. 38:19. “Ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa; wasimame na na kuwaambia wana wao.” Zab. 78:6. “Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula; na hao waliokuwa na njaa wamepata raha: Naam huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba; na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.” 1 Sam. 2:5. Mungu awasaidie watu Wake katika siku hii kuu ya udanganyifu ambapo adui mjanja anajaribu kuwadanganya yamkini hata walio wateule. {SR1: 204.1}

Jibu Kwa Hoja Ya Mhindi Ya Ukurasa Wa 182-183

“Jitahidi kujionyesha umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la ukweli.” 2 Tim. 2:15. “ Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa hofu.” 1 Pet. 3:15. Amri hiyo katika Biblia ni kwamba Mkristo lazima ajifunze, na ya kwamba lazima pia amjibu kila mtu. Mhindi huyu akiwa mmoja wa “kila mtu,” kwa mujibu wa Maandiko lazima iwepo njia, na ni jukumu la Mkristo kumjibu kwa upole na kwa hofu. {SR1: 204.2}

“Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande zamwisho za kaskazini.” Isa. 14:13. Lusifa alitaka kupanda mpaka pande za kaskazini kwa sababu huko ndiko kiliko kiti cha enzi cha Mungu. Akasema Mtunga Zaburi, “Kuinuka kwake ni mzuri sana, furaha

205

ya dunia yote, ni mlima Zayuni, pande za kaskazini, mji wa Mfalme mkuu.” Zab. 48:2. {SR1: 204.3}

Kiti cha enzi cha Mungu kiko kaskazini. Mtu anaweza kuonyesha kaskazini wakati wowote kutoka sehemu yoyote ya dunia, na miisho ya mistari yote iliyo mbali ingekutana mahali pale pale. Laiti yule aliyeitwa eti Mkristo angeonyesha upande wa kaskazini, jibu lingekuwa sahihi na lenye kupatana na Biblia; kwa hivyo huo mchafuko na mjeledi vyote vingeepukwa. Kuonyesha pande za kaskazini hakumaanishi kwamba mbingu iko mahali fulani katika pembe ya kaskazini ya anga pana la mbingu yenye nyota, maana tunaelewa kwamba kiti cha enzi cha Mungu kiko katikati ya dunia zote. {SR1: 205.1}

Mhimili wa dunia huinama katika mwelekeo wa msharazi kuhusiana na mzuguko wake. Ikiwa tutaelekeza upande mwingine isipokuwa kaskazini au kusini wakati wowote utakuwa aidha mashariki au magharibi. Katika wakati wa mchana, kuelekeza upande wowote (isipokuwa na mhimili wa dunia) tunaelekeza upande wa mashariki (jua), na usiku magharibi, bila mwelekeo wowote maalum angani. Mwelekezo kwa jua hujumuisha mashariki; mwelekeo kinyume na jua ni magharibi kushughulika na mfumo wetu wa jua pekee, lakini mwelekeo wa kaskazini hushughulika na katikati ya dunia zote. {SR1: 205.2}

Hakuna kitu kama juu na chini angani. Kitu pekee ambacho kingejumuisha juu ni kitovu cha mvuto (kiti cha enzi cha Mungu): Chini (au kusini) iko katika mwelekeo mkabala na kiti cha enzi cha Mungu, (anga kubwa la mbinguni). Kituo cha mvuto kimezungukwa na kisiwa cha dunia nyingi. Mhimili katika kila kisiwacha dunia nyingi (au sayari nyingi za jua, sayari nyingi, na dunia nyingi) zote huelekeza kwa kituo kimoja cha mvuto (kiti cha enzi cha Mungu). Kituo hiki chenye enzi kubwa na kikuu kabisa husimama kama kilele cha juu kabisa juu ya mlima mkubwa ambao uumbaji wote hukizunguka, kila moja huning’inia kwa uwezo usioonekana (mnyororo) uliyounganishwa kwa mhimili wake wa kaskazini sawa na timazi inayoning’inia kutoka kwa saa kubwa. {SR1: 205.3}

Je! Wakristo Wanawezaje Kwenda Mbinguni Iwapo Umbali Ni Mkubwa Hivyo?

Kasi ya upesi zaidi duniani inayojulikana na sayansi ya kisasa kwa wakati huu wa sasa ni nuru ambayo kukwenda kwa kiwango cha maili 186,284 kwa

206

sekunde. Iwapo mtu angepaa kwa mabawa ya nuru kwenda kwa nebula kubwa Orioni, kungemchukua miaka 600 kufikia umbali huo wa maajabu ya mbinguni ambayo yamevutia sana umakini wenye bidii kwa sayansi mamboleo. Tukinukuu kutoka Maandishi ya Awali, ukurasa wa 41, tunasoma: “Anga liligawanyika na kuvingirika nyuma; kisha tukaweza kutazama juu kupitia nafasi ya wazi katika Orioni, ilikotokea sauti ya Mungu. Mji mtakatifu utashuka chini kupitia katika nafasi hiyo iliyo wazi.” Iwapo mji mtakatifu utakuja kupitia katika nafasi hiyo tunaweza kuwaza vyema kwamba nafasi hiyo tukufu ya Orioni ndilo lango la hiyo njia kuu refu inayoendelea hadi mbinguni (kiti cha enzi cha Mungu). Lakini fikiri kuhusu umbali mrefu hadi kwa lango hili la kushangaza zaidi. Ikiwa itachukua miaka 600 ya nuru kulifikia lango la hiyo njia kuu iliyo mbali sana, basi tunajiuliza, Je! Itachukua miaka mingapi ya nuru kufikia mwisho wa pili wa njia kuu ya mbinguni hadi kwa mji wa Mfalme mkuu pande za kaskazini? {SR1: 205.4}

Sisi wanadamu hatuwezi kutoa jibu la moja kwa moja kwa swali hili kubwa ila kusema tu kwamba umbali kutoka kwa dunia hadi kwa kitovu cha dunia zote (kiti cha enzi cha Mungu) ni mkubwa sana hivi kwamba sisi viumbe wafaji twaduwazwa tu. Tunashangazwa na ugumu wa kuhesabu umbali, au hata miaka ya nuru. Lakini iwapo umbali huo ni mkubwa kupita uelewa wa wanadamu, basi sisi, kama yule Mhindi aliyetajwa hapo awali, tunauliza swali, Je! Wakristo watafikaje mbinguni? Waza kwamba ajabu kubwa (treni/msafara) ambayo itawachukua waliokombolewa itakwenda kwa kasi sana ya nuru, ikisafiri maili 186,000 kwa sekunde, itachukua sehemu kubwa sana ya umilele kufika mji wa Mfalme Mkuu (mbinguni). {SR1: 206.1}

Hapa tutaona kile tunachotazama kama mfyatuko wa kasi. Mbingu hukadiria kuwa ni ya kujikokota sana. Kwa mfano, tutazingatia kumhusu Yesu baada ya ufufuo. Mariamu alikuwa wa kwanza kukutana Naye. Alipomfikia Bwana wake, Yesu akamwambia, “Mariamu, usinishike; kwa maana Sijapaa kwenda kwa Baba Yangu.” Yohana 20:17. Siku nane baadaye Yesu aliwatokea tena wanafunzi Wake. “Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, … na uutie ubavuni Mwangu; wala usiwe usiyeamani, bali aaminiye.” Yohana 20:27. Iwapo Yesu hakumruhusu Mariamu amguse kwa sababu Alikuwa bado Hajaenda kwa Baba Yake baada

207

ya kufufuka Kwake, hatuwezi kuwaza Alimruhusu Tomaso atie kidole chake ubavuni Mwake isipokuwa Alikuwa ameenda mbinguni kwa Baba Yake. Yesu, kwa juma moja au chini yake, alifanya safari ya kwenda mbinguni na kurudi duniani. {SR1: 206.2}

Tuseme huyu Mhindi alitaka kwenda mbinguni, na akachagua kupaa juu ya mabawa ya nuru. Kuanzia siku iyo hiyo Kristo alifufuka kutoka kaburini, akipitia angani kwa kiwango cha maili 186,000 kwa sekunde, bado angekuwa safarini. Zaidi ya hayo, nebula, — ambayo sisi ni sehemu yake ni kipenyo cha miaka ya nuru 300,000. Kwa hivyo, bado angekuwa ndani ya mipaka ya mji ya nebula yetu. Mwandishi fulani, akiongea juu ya kitovu cha dunia zote (kiti cha enzi cha Mungu), amefafanua umbali huo kwa maneno yafuatayo: “Lakini suluhisho la siri ya umbali hadi kwa kitovu cha vituo — kwa sehemu hiyo ya mbali katika anga ambayo ni kitovu cha mvuto kwa makumi ya maelfu ya galaksi — kitalazimika kungoja kukamilisha kwa utafiti wetu wa nebula ambao utachukua kutoka miaka kumi hadi kumi na tano au zaidi; na yawezekana isitatuliwe kamwe.” {SR1: 207.1}

Kasi ya nuru ni ya kujikokota sana kwa kasimwelekeo ya vyiumbe vya kimbingu kuzunguka ulimwengu wote mkubwa wa Mungu. Danieli alihisi hitaji na kuomba kwa Mungu wake ombi ambalo limeandikwa katika Dan. 9:4-19. Sala hii fupi ya aya kumi na tano tu inaweza kusomwa kwa chini ya dakika tano, lakini tunaweza kuwaza alikuwa mwangalifu sana katika sala yake na akachukua muda wake: Labda dakika kumi au hata ishirini. Kunukuu rekodi ya Danieli mwenyewe: “Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba…. Gabrieli niliyemwona katika njozi…akirushwa upesi, alinigusa…akasema, Ee Danieli… mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, Nami nimekuja kukupasha habari.” Dan. 9:20-23. Hapa iko rekodi ya kiwango cha kasi ambayo ni zaidi ya ufahamu wa mwanadamu. Maombi kwenda mbinguni na malaika kuja duniani yalifanikishwa chini ya dakika ishirini. Mbingu pekee inajua jinsi malaika anavyoweza kuruka umbali huo mkubwa, usioweza kunenwa kwa dakika chache tu. Hakutakuwa na shida,

208

ugumu, au kawio lolote katika safari hiyo tukufu baada ya Wakristo kuanza. Lakini hakika sisi hukawia sana kuanza, na hilo ndilo tatizo letu pekee ambalo lazima tusuluhishe kuhusiana na umbali huo, na safari kutoka duniani hadi mbinguni. {SR1: 207.2}

209

MUHTASARI WA WATU 144,000–

Jeraha La Mauti Limepona

“Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti; na pigo lake la mauti likapona; Na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Ufu. 13:3. Hueleweka kwa ujumla kati ya Waadventista wa Sabato kwamba kwa sababu serikali ya Italia ilimpa papa nguvu za utawala wa kiraia siku ya 11 ya Februari, 1929, kuwa tukio la utimizo wa kinabii, tutatoa kwamba ufasiri huo ni sahihi, na “jeraha la mauti” limepona. Kumbuka vitenzi “lika” na “pona” vyote viko katika wakati uliopita. Kwa kuwa hili ni hivyo, ni dhahiri kwamba unabii huu maalum unapaswa kueleweka kabisa baada ya kutimizwa kwake (kuhusu lini na jinsi ulivyotimizwa). {SR1: 209.1}

Iwapo tukio la tarehe iliyotajwa hapo juu lilitimiza unabii huo, basi hatutafanya kosa iwapo tutawaza kwamba sehemu ya mwisho ya aya hiyo pia imepata utimizo wake. “Na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Kunukuu kutoka katika Gombo la 6, ukurasa wa 14: “Unabii wa Ufunuo unatimizwa, ya kwamba ‘dunia yote ilimataajabia mnyama yule.’ Ufu. 13:3. “Dunia ikiwa sasa kwa wakati huu wa sasa haina hali bora ya kiroho, lakini mbaya zaidi, tunaweza kuhitimisha kwamba Andiko hilo limepata utimizo wake kikamilifu. Jeraha hilo “limepona” vile vile dunia “imemstaajabia mnyama yule.” {SR1: 209.2}

Hatuhitaji kudhani kwamba dunia italazimika kujiandikisha katika ushirika wa kundi hilo la watu ili kutimiza huo unabii. Kumbuka dunia haikukistaajabia kichwa kilichotiwa jiraha bali yule mnyama. Maandiko hushughulikia katika maana ya mambo ya kiroho. Tena, kunukuu kutoka katika Gombo la 6, ukurasa wa 15: “Ibada hii ya kishetani ilifunuliwa kwake [Yohana], na ilionekana kwake kana kwamba dunia yote ilikuwa imesimama ukingoni mwa uharibifu.” Dunia imeshiriki roho ya yule mnyama, na hivyo kutimiza utabiri wa Mungu. {SR1: 209.3}

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake

210

211

ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake jina la kukufuru.” Ufu. 13:1. Kumbuka mnyama huyu ana vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Ili kupata ufahamu kamili wa huu unabii lazima tuanze kutoka shinani hadi kileleni. (Maana mara ya kwanza wafalme hawa kumi (pembe) wanaletwa kwa umakini wetu na Maandiko, yanayopatikana katika Dan. 2:41, 42, wanaowakilishwa na vidole kumi vya sanamu kubwa katika ndoto ya Nebukadnezza. Baada ya kumfunulia mfalme kikomo cha ufalme wake wa dhahabu, uliowakilishwa na kichwa cha dhahabu, na chini kupitia katika mkondo wa wakati hadi kwa ujio wa Kristo mara ya pili, Danieli husema, “Na katika siku za wafalme hawa Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele.” Dan. 2:44. {SR1: 209.4}

Katika Danieli 7, unabii uu huu wa historia ya dunia umerudiwa kwa nembo za wanyama. Wafalme wanaowakilishwa na vidole vya sanamu kubwa wakati huu wanawakilishwa na pembe kumi za mnyama “wa nne” na “dubwana” katika aya ya 7. Sababu ya kurudufishwa hivyo ni kuleta ukweli wa ile pembe ndogo (utawala wa upapa, aya ya 8). Zile pembe kumi (wafalme) zinarudiwa tena katika Ufu. 13:1, ili kuonyesha wakati wa huo unabii jinsi ulivyoelezwa na Danieli, — “na katika siku za wafalme hawa Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme.” {SR1: 211.1}

Kumbuka kwamba mnyama huyu (chui) wa Ufu. 13:1-3, alitokea baharini, kama vile wanyama wanne wa Danieli 7, kwa hivyo, mchakato unaomleta mnyama huyu kwa jukwaa la utendaji ni sawa zile zinazowakilisha Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. Iwapo pembe kumi za mnyama huyu huwakilisha wafalme walioko kwa wakati ambapo “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme” (kunukuu maneno ya Danieli), basi mnyama mwenyewe huwakilisha kipindi kinachofuata Rumi, kwa maana kuvunjika kwa ufalme wa Rumi kulileta uwepo wa wafalme hawa. Pia huitwa “Rumi katika hali yake iliyovunjika” inayowakilishwa na sanamu kubwa ya Dan. 2:42, ambayo miguu na vidole vyake vimejumuisha chuma na udongo. Chuma ni madini ya chuma ambayo huwakilisha Rumi; udongo, sehemu iliyovunjika. {SR1: 211.2}

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake jina la kukufuru.” Ufu. 13:1.

212

Nembo zilizotolewa na Uvuvio zina uwezo kamili wa kufunua ukweli pasipo shaka yoyote. Ufasiri wowote wa unabii ambao hauafikiani kabisa na vipimo vya nembo hizo si aina ambayo inaweza kutegemewa, na punde au baadaye italipuka. {SR1: 211.3}

Imekubalika kwamba zile pembe kumi huwakilisha falme kumi ambazo Rumi iligawanyika. Ufasiri huu ni wa kweli, kwa maana utaona hizo pembe kumi ni pembe zilizo na vilemba. Vilemba huashiria wafalme hawa wamepokea ufalme wao, lakini angalia kwa uangalifu vichwa havina vilemba, kwa hivyo vichwa hivyo saba haviwezi kuwakilisha falme au serikali za kiraia. Kwa hivyo itakuwa kukosa hekima na kuwa mdanganyifu hata kufikiri kwamba vichwa vyaweza kuwakilisha tawala za kiraia hapo zamani au baadaye. {SR1: 212.1}

Vichwa vyote saba hufanana bila tofauti ya kimoja kutoka kwa kingine. Iwapo kichwa kilichotiwa jeraha huwakilisha mfumo wa kidini, basi lazima tuhitimishe kwamba vile sita huwakilisha miili ya kidini. Idadi yavyo ikiwa namba ya Kibiblia “saba,” humaanisha “vyote,” au kamili.” {SR1: 212.2}

Laiti vichwa vingekuja kimoja baada ya kingine kama wanyama wa Danieli 7 na pembe ndogo baada ya zile tatu “kung’olewa,” vingemaanisha aina za mifumo inayofuatana. Kwa maana vyote saba vilikuwepo kwa wakati mmoja, nembo hiyo huonyesha kwamba mifumo yote saba lazima itawale wakati ule ule mmoja. {SR1: 212.3}

Hivi vichwa saba haviwezi kuwakilisha kitu chochote wakati wowote kabla ya kuanguka kwa ufalme wa Rumi maana kile kinachowakilisha lile liliofanyika kabla ya anguko la Rumi huonyeshwa katika mseto wa yule mnyama, bila vichwa saba na pembe kumi (jinsi alivyoonyeshwa katika aya ya pili). Sehemu ya chui huwakilisha Uyunani (Dan. 7:6); miguu ya dubu, Umedi na Uajemi (Dan. 7:5); na kinywa cha simba huwakilisha Babeli (Dan. 7:4). Mseto wa yule mnyama katika Ufu. 13:1, 2, katika muundo wake, ni ushahidi kwamba anakuja kwa jukwaa la utendaji baada ya falme kuu nne za ulimwengu; yaani, Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. Kwa hivyo, anakuwa mnyama wa tano, akiwakilisha kipindi ambacho kilifuata anguko la Rumi. Pembe kumi

213

za wanyama wote wawili, Dan. 7:7, na Ufu. 13:1, hali kadhalika na vidole kumi vya Dan. 2:42, huwakilisha falme zile zile kumi ambazo Rumi iligawanyika kwazo. Wafalme hawa kumi huonyesha ustaarabu katika kipindi cha tano, au kile kilichofuata Rumi hadi kwa wakati wetu, na kwendelea hadi kurudi kwa Kristo mara ya pili, kwa mujibu wa Dan. 2:44. “Na katika siku za wafalme hawa Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele.” {SR1: 212.4}

Isitoshe, kumbuka kwamba zile pembe kumi kwa mnyama dubwana wa Dan. 7:7, haziko na vilemba, lakini zile zilizo kwa mnyama kama chui wa Ufu. 13:1, ziko na vilemba. Nembo hiyo huonyesha kwamba pembe zilizo kwa hao wanyama wote huwakilisha wafalme wale wale: Sisizo na vilemba kwa mnyama wa kwanza kwa sababu wafalme hao (pembe) hawakuwa na ufalme hata kabla ya kuanguka kwa Rumi. Ukweli kwamba mnyama kama chui anazo pembe zilizo na vilemba ni kwamba anakuja kwa jukwa la utendaji baada ya anguko la Rumi, kwa wakati ambapo wafalme hawa walipokea falme zao. {SR1: 213.1}

Pembe ndogo kwa mnyama wa Dan. 7:8, ambayo ilizuka baadaye kati ya zile kumi, na mahali ambapo tatu zilianguka imefasiriwa kuwa kichwa cha upapa, kutoka mwaka 538 B.K hadi 1798, na ambacho kilitiwa jeraha katika karne ya kumi na tano. Jeraha hilo la mauti lilileta mgawanyiko na kuzidisha vichwa jinsi vinavyoonyeshwa katika Ufu. 13:1. Vichwa sita huwakilisha Uprotestanti, na kile kilichojeruhiwa, Ukatoliki. Waprotestanti sita, na kichwa kimoja Katoliki hufanza namba ya Kibiblia “saba,” ikimaanisha “kamili” (vyote). Pembe kumi hizo huwakilisha ustaarabu huu wa sasa chini ya utawala wa kiraia; vichwa ni nembo za jumuiya yote ya Ukristo. {SR1: 213.2}

Unabii huu huonyesha ustaarabu wote ambao ulitokea kupitia kwa falme nne za ulimwengu wote na anguko la Rumi. Lakini hauwezi kujumuisha mataifa na watu wengine, maana maumbile ya yule mnyama hujumuishwa tu na Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi, kama ilivyoelezwa hapo awali. Iwapo idadi ya hizo pembe ilikuwa “saba,” lazima ziweze kuwa na maana ya Kibiblia (yote), lakini kwa sababu namba “kumi” imetumika, zingine zote zimetengwa. {SR1: 213.3}

Hata hivyo, mataifa na watu ambao wametengwa na nembo “kumi,” na pia kwa maumbile ya yule mnyama hayajaachwa

214

nje kabisa, maana anguko la zile pembe tatu kwa mnyama wa Dan. 7:8, liliacha salio la namba ya Kibiblia “saba.” Kwa hivyo kuanguka kwa hao wafalme watatu; ambao ni, Heruli, Ostrogothi, na Vandal walitoa ishara kwa umoja wa sasa wa karibu na ulimwengu wote na uvumbuzi wa kisasa. Kwa hivyo, ushawishi wa ustaarabu wa magharibi, wa kiraia na wa kidini (uliowakilishwa na hizo nembo, — pembe na vichwa), ulihusisha ustaarabu wote wa sasa. Kwa hivyo unabii huo wa mfano umetimizwa. {SR1: 213.4}

Unabii wa Ufu. 13:3, “Na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule,” unaonyesha uasi mkubwa. Nambari ya kibiblia “saba” hujumuisha kila kitu kinachowakilishwa na hivyo vichwa (kuendeshwa kwa yule mnyama na akiongozwa na shetani). Kumbuka jina la kukufuru liko kwa vichwa vyote saba — nembo za viongozi wasio waaminifu wa dini, wakidhihaki utu au mamlaka ya Mungu, chini ya vazi la Ukristo. Kusudi la mpango kamili wa kishetani ni kudanganya dunia yote. Kauli iliyotolewa na Kristo ni ya kweli, kwamba yeye (Shetani) atajaribu “kuwadanganya kama yamkini hata hao wateule [watu 144,000].” Roho ya Unabii, ikiongea kulihusu andiko hili, husema: “Ibada hii ya kishetani ilifunuliwa kwake [Yohana], na ilionekana kwake kana kwamba ulimwengu wote ulikuwa umesimama ukingoni mwa uharibifu. Lakini alipoangalia kwa upendezi mkubwa, aliliona kundi la watu wa Mungu wanaoshika amri.” Gombo la 6, ukurasa wa 15. {SR1: 214.1}

Hatupaswi kushangaa iwapo tutaona kwamba hapo awali hatukuelewa kabisa maana ya kweli ya mchakato wa kupona. Huwa tunarudia ufafanuzi wa hivyo vitenzi, vikiwa katika wakati uliopita: “kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti; na pigo lake la mauti likapona: na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Ni dhahiri kwamba Uvuvio uliona kimbele kwamba kupona hakungeeleweka wazi mpaka utabiri wa Mungu utimizwe. Roho ya Unabii hulishuhudia jambo hili, kwa kusema, “Alama ya mnyama ni haswa ilivyotangazwa kuwa ilivyo. Sio yote kulihusu jambo hili hata sasa yanaeleweka, wala hayataeleweka mpaka chuo kitakapokunjuka.” Gombo la 6, ukurasa wa 17. Iwapo chuo kimepiga kona, wakati huo tu tunaweza kutarajia ukweli wa kulifunua andiko hilo. {SR1: 214.2}

215

Uhamisho wa Papa Pius wa 6, mwaka 1798, na kifo chake huko Valence, Ufaransa, Agosti 19, 1799, si kutiwa jeraha, si zaidi ya kifo cha papa yeyote kabla au baada yake. Kilitimiza tu Ufu. Rev. 13:10, — “Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka.” Pia kipindi kikuu cha kinabii cha miaka 1260 ya Dan. 7:25. Wala uchaguzi wa papa mwingine haukuliponya lile jeraha. Ilikuwa tu ishara ya pigo la mauti kutekelezwa. Vivyo hivyo kwa kurejeshwa utawala wa kiraia kwa papa mwaka 1929, sio kitu kilicholiponya lile jeraha, bali ni ishara tu kwamba limepona. {SR1: 215.1}

Kumbuka kwa makini kwamba jeraha la mauti halikupasishwa na moja ya zile pembe kumi (kama ile pembe ndogo ya Dan. 7:8, ambapo baadaye tatu zikaanguka). Iwapo yoyote kati ya hizo pembe ilikuwa imepasisha hilo jeraha, ingeonyesha kwamba lilipaswa kupasishwa na utawala wa kiraia (kwa hivyo Berthier angepewa sifa ya kutoa hilo pigo). Lakini kwa sababu pembe hizo hazikuwa na uhusiano wowote na kichwa, ni dhahiri kwamba upasishwaji ulitokea ndani ya kichwa hicho kwa hivyo Luther ndiye pekee ambaye anaweza kupewa sifa ya kutoa hilo pigo. {SR1: 215.2}

Uhamisho wa papa mwaka 1798, ulikuwa ishara tu ya upande wa kimwili ilioonyesha kwamba pigo lilikuwa limetolewa, lakini upande wa kiroho wa ukweli umepuuzwa kabisa. Laiti kichwa kisingekuwa kilipokea jeraha la mauti na Martin Luther, papa hangewekwa gerezani na Berthier, au na jemadari mwingine yeyote, maana kabla ya upanga kutolewa, papa alitawala kwa ukuu. Lakini pigo la Luther lilidhoofisha uwezo wake, kwa hivyo kudhuru kwa uendelevu kulianza kukitonesha hicho “kichwa.” Utoneshaji huu uliendelea hadi mwaka 1870, wakati mwishowe utawala wa muda wa papa ilipoondolewa. Huo ukiwa utoneshaji wa mwisho “kichwani,” huonyesha kwamba kiliachwa kipone “jeraha lake la mauti”. Wazo lililoanzishwa na Uriah Smith katika “Danieli na Ufunuo” ni sahihi kwa kadiri sehemu ya kimwili inavyohusika. {SR1: 215.3}

Uchaguzi wa papa mpya (kimwili) ulitoa ishara kwamba jeraha la mauti lingepona. Tunachopendezwa zaidi kujua ni sehemu ya kiroho ya hiyo mada, ambayo tutajitahidi kwa muda mfupi kuleta kwa wakati huu. Sababu ya unabii huu kuletwa kwa

216

umakini wetu katika sura hii ni kufunua ukweli wa kichwa ambacho kilipata pigo la mauti. Kumbuka kwamba mnyama huyo ana vichwa “saba”; kile “kimmoja” kilijeruhiwa lakini “sita” hapana. Kichwa kilichopokea jeraha hufasiriwa kuwa kichwa cha upapa, kilichotiwa jeraha na “Martin Luther.” Pigo hilo likiwa lilitolewa na fundisho la kweli la Kibiblia lililofundishwa na Luther, tokeo lake lilikuwa kwamba Uprotestanti ulikuja kwa jukwaa la utendaji kwa kukipinga hicho “kichwa.” Hili ndilo lililofanyiza lile “jeraha.” Kauli hiyo ikiwa ni ya kweli, basi maadamu Uprotestanti unadumu kuwa mwaminifu kwa kanuni za Biblia, na kichwa kuwapo, jeraha (kidonda) hilo litasalia kuwa wazi. Lakini iwapo Uprotestanti utaacha ahadi yao “Biblia, na Biblia tu,” au kukataa nuru mpya jeraha hilo litapona, na dunia itamstaajabia mnyama yule (uasi). {SR1: 215.4}

Kichwa kilichotiwa jeraha hakikutaabishwa sana kwa sababu papa alikuwa ameanguka chini ya udongo, wala hakitataabishwa kamwe almuradi mtu mwingine anaweza kujaza nafasi yake. Jambo pekee ambalo limekitaabisha hicho kichwa na kumkasirisha yule mnyama ni Uprotestanti wa kweli. Ibilisi anajua hilo na hicho kichwa chalijua, lakini watu wa Mungu wameliruhusu joka la zamani kuyafunika macho yao kwa sufu. Amka, ndugu! Amka, dada! Usimruhusu adui mjanja akudanganye ukose taji ya uzima kwa saa ya kumi na moja! {SR1: 216.1}

Je! Kifo cha papa ni muhimu zaidi kuliko kuzaliwa kwa Uprotestanti? Je! Uhamisho wa papa ni heshima kubwa kuliko kutengwa katika Jumba la Wartburg? Je! Berthier ni shujaa mkuu kwa kufunga malango ya gereza kuliko yule mtawa mnyenyekevu aliyeyafungua wazi ili atupwe ndani papa aliyewahi kutukuka? Je! si uthabiti wa tabia, na uthabiti wa kusudi, na imani kwa Mungu, katika mjumbe wa kimbingu ametenda haya yote yawezekane? Iwapo Luther ndiye mkuu zaidi, na tendo lake tukufu zaidi, kwa nini Uvuvio uandike unabii kwa uhamisho na kifo cha papa, badala ya tendo la Luther? {SR1: 216.2}

Mbona Uvuvio utambue kuondolewa au kurudishwa utawala wa muda wa papa, badala ya kurejeshwa kwa Biblia, na kulifukuzia mbali giza? Je! Si Mungu, kwa mkono wa Luther, ameyagawanya malango ya giza, na kusababisha nuru iangaze

217

kwa Neno Lake lililoandikwa? Je! Imani na bidii ya mjumbe huyu wa mbinguni haijamaliza mateso ya kutisha na umwagaji damu wa watakatifu wake Aliye Juu? Jibu pekee slenye haki kwa maswali haya mengi ni: Pigo la Luther lilipasisha jeraha kichwani, na ni Uprotestanti wa kweli pekee ndio unaoweza kuliweka jeraha hilo wazi. {SR1: 216.3}

Katika mwaka 1844, wakati tangazo lilipotolewa kuhusu anguko la Babeli mamboleo kwa kuhubiriwa ujumbe wa malaika wa pili wa Ufu. 14:8, jeraha lingekuwa limepona, kwa maana Babeli ulikuwa umeanguka, na ungekuwa umeleta utimizo wa, — “na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Lakini “Waadventista wa Sabato” walikuja kwenye jukwaa la utendaji, na hivyo kuudumisha mwiba ndani ya jeraha hilo kwa kutangazwa kwamba ndio Waprotestanti wa kweli tangu wakati huo. Hili likiwa hivyo, basi almuradi Waadventista wa Sabato (kama mwili) wadumu kuwa wakweli kwa kanuni na mafundisho ambayo yamelijenga vuguvugu hili kuu, hilo jeraha haliwezi kupona, wala haiwezi kunenwa “dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” {SR1: 217.1}

Kwa sababu tumetoka kwa misingi, — utiifu kamili kwa Neno la Mungu, ambalo kwalo twaweza tu kuzishika amri Zake kama Waadventista wa kweli, — basi tumeuacha msingi wa kiungu, na kumstaajabia yule mnyama. Iwapo jeraha limepona, basi sisi, kama watu, tumeishiriki roho ya yule mnyama (dunia). Jinsi uhamisho wa papa ulikuwa ishara ya kukamilishwa kwa kupasishwa lile jeraha, kwa hivyo kurudishwa kwa utawala wa kiraia kwa upapa katika mwaka 1929, ni ishara kwamba Uprotestanti wa kweli umepoteza nguvu zake, kwa hivyo dunia ikamstaajabia mnyama yule. {SR1: 217.2}

Uasi huu wa jumla unaoongozwa na viongozi wa dini waliodanganyika hauwezi kuwa wa kuhimiza utakaso wa kanisa la Mungu, maana wakati huo ni wakati wa mavuno ambamo wakati huo Mataifa wa Isaya 60, wataongoka kwa kanisa. Akinena juu ya wakati mtukufu wa mavuno, nabii asema: “Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa: Naye Bwana yeye peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo.” Isa. 2:17. Kanisa la Mungu litainuliwa kama ilivyotabiriwa na Isaya 2, na Mika 4; soma ukurasa wa 173-81. Kwa hivyo, wakati wa mavuno hauwezi kuwa wakati wa uasi kwa kanisa la Mungu. Laiti lingekuwa hivyo, Mungu asingekuwa na kanisa. {SR1: 217.3}

218

Nabii Isaya, akiutaja wakati huu wa giza la kiroho, asema: “Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja, wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa mavazi yetu wenyewe; lakini tuitwe tu kwa jina lako, utuondolee aibu yetu.” Ni ukweli uliokubaliwa kwamba wanawake wanaozungumziwa hapa huwakilisha makanisa. Namba ya kibiblia “saba” imetumika kama nembo, ikimaanisha “yote,” kwa hivyo nembo hiyo hailiondoi lolote, bali humaanisha “yote.” Roho ya Unabii hushuhudia hili kwa kusema namba “saba” humaanisha ukamilifu. Matendo ya Mitume, ukurasa wa 585. Kwa kawaida itawajumuisha Waadventista wa Sabato pia, vinginevyo yasingekuwa “yote.” Wakati wanawake hawa wanakataa maagizo ya Kristo kupitia katika Neno Lake na haki Yake, inayowakilishwa na chakula na mavazi, walitamani kuitwa kwa jina Lake (Wakristo), lakini wakati dunia iko ukingoni mwa uharibifu Mungu mara moja anaanza kufanya kazi, na kurekebisha mambo, kama ilivyotabiriwa katika aya ya pili. {SR1: 218.1}

“Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana na kupendeza kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.” Isa. 4:2. Kumbuka kwamba ahadi hii tukufu ni kwa wale watakaookoka (Israeli — watu 144,000). Hili haliwataji watu walioko duniani, ila kwa wale walio ndani ya kanisa la Mungu, kwa maana aya ya tatu husema, “yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu.” Aya ya nne hutupatia wakati dhahiri kabisa kwamba ni wakati wa kutakaswa kwa kanisa Lake, kwani inasema: “Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni, na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake kwa roho ya hukumu, na kwa roho ya kuteketeza.” {SR1: 218.2}

Wakati dunia imemstaajabia mnyama yule, Mungu anao watu 144,000 ambao “hawajamsujudia Baali.” Ingawa wanaonekana wamepotea bila mchungaji, mkono wa Nguvu zote unawaangalia. Katika taarifa iliyonukuliwa hapo awali kutoka katika Gombo la 6, ukurasa wa 15, ikizungumzia uasi wa kutisha kila mahali ulioenea wakati huu, (kwa maana kwamba dunia imemstaajabia mnyama yule) inasema, “Lakini alipoangalia [Yohana] kwa upendezi mkubwa, aliliona kundi la

219

watu wa Mungu wanaoshika amri [watu 144,000]. Kwenye vipaji vya nyuso zao walikuwa na muhuri wa Mungu aliye hai, na imani ya Yesu… Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa.” Kumbuka kwamba baada ya kutiwa muhuri kwa watu 144,000 kutakuwa na wengine ambao watakufa katika Bwana (kuokolewa), kwa maana hilo andiko husomeka “tangu sasa,” likimaanisha kutoka kwa wakati kundi hili lilipotiwa muhuri. {SR1: 218.3}

Watu 144,000 ni watakatifu walio hai, watakaohamishwa bila kuonja mauti. “Bwana amewafungia ndani. Mahali waendako kumeandikwa — MUNGU, YERUSALEMA MPYA.” Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 446. Kwa hivyo, wale wafao “katika Bwana” lazima wawe kati ya wale ambao wameokolewa, baada ya utengo (wakati wa mavuno) wakati ambapo Isa. 52:1 na Zef. 3:13, yanatimizwa. Wale wafao wakati huo labda ni wale ambao hawawezi kuvumilia taabu wakati hukumu za Mungu zinaanguka juu ya nchi katika wakati wa mapigo. Wakati Mungu anaisafisha njia kwa ajili ya mapigo saba ya mwisho kwa kuwalaza baadhi ya watu Wake walale kaburini, Yeye amefanya vivyo hivyo kwa tukio litakalofanyika mwaka 1931 (iwapo tarehe hiyo ni sahihi). Kwa maana tunasoma katika Isa. 57:1, “Mwenye haki huangamia wala hakuna atiaye hayo moyoni. Na watu wataua huondolewa, wala hakuna afikiriye kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na uovu utakaokuja.” {SR1: 219.1}

Tena, tunaita umakini wako katika wakati uliopita na wakati ujao wa hilo andiko; ilhali Ufu. 14:13, liko katika wakati ujao, Isa. 57:1, liko katika cha zamani. Huu ukiwa ukweli wa sasa, ni rahisi kuona kwamba sisi, kwa wakati huu wa sasa, tunasimama kati ya maandiko haya mawili. Tukio lililotabiriwa la utakaso wa kanisa la Mungu katu si dogo kabisa. Wale ambao hawawezi kustahimili hukumu hiyo wamelazwa makaburini mwao, ilhali 144,000 wanasalia na wataokoka, lakini salio lingine ndani ya kanisa (sasa) wataangamia katika huo uharibifu. Mungu awasaidie watu Wake. {SR1: 219.2}

Kwa nabii Isaya, uasi huu mkuu, unaoendelezwa na waongozi vipofu wa kiroho, ulifunuliwa, ambao yeye anauelezea katika maandiko yafuatayo: “Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi. Basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu na haki yake, ndio iliyomsaidia.” Isa. 59:16. “Nikatazama,

220

wala hakuna wa kusaidia; nikashangaa kwa kuwa hakuna wa kutegemeza: Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, ghadhabu yangu, ndiyo iliyonitegemeza.” Isa. 63:5. Mika, akitazama mbele kwa udanganyifu huu wa jumla, asema:” Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini.” Mika 7:5. {SR1: 219.3}

Haijawahi kupeanwa nuru nyingi juu ya tukio moja lolote la kinabii tangu mwanzo wa dunia, jinsi ambavyo Bwana ametoa juu ya mada hii ambayo imewekwa katika chapisho hili (kutiwa muhuri kwa watu 144,000, na mchinjo ndani ya kanisa kuhusiana na mavuno, ingawa haijachapishwa yote). Kwa hivyo, itawaacha watu bila udhuru. Yeye atakayepuuza kufanya maandalizi yanayohitajika kwa tukio hili adhimu atakuwa anatenda dhambi isiyosameheka. Kwa mtu kama huyo, siku hiyo ni ya kutisha. “Basi Nitakutenda hivi, Ee Israeli: Na kwa sababu Nitakutenda hivi, ujiweke tayari kukutana na Mungu wako, Ee Israeli.” Amosi 4:12. {SR1: 220.1}

“Amka, amka; jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu…Jikung’ute kutoka mavumbi; inuka, ukae chini…jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa.” Isa. 52:1, 2. {SR1: 220.2}

Itakuwa ya kupendeza kutambua jinsi Mungu ameuonyesha ulimwengu wetu kwa nembo. Wakati vichwa sita vya Waprotestanti na kimoja cha Katoliki hufanza namba ya Kibiblia “saba,” kumaanisha Jumuiya yote ya Wakristo, Mungu ameuthibitisha unabii uo huo na nabii Ezekieli, na ukatekelezwa na wana-matengenezo tangu wakati wa Luther; yaani, Luther, Knox, Wesley, Campbell, Miller, na Dada White: Hawa watu wacha Mungu walijinyima yote kwa juhudi za kuliongoza kanisa la Mungu kurudi kwa kiwango chake cha usafi. Lakini jinsi adui mjanja alifanikiwa kulibomoa la kwanza, aliendelea kutumia mbinu iyo hiyo hadi la mwisho. Wanamageuzi hawa sita wakuu kwa upande wa Kiprotestanti walianzisha madhehebu sita makuu yaliyowakilishwa na hivyo vichwa sita, na kanisa Katoliki (mama wa Uprotestanti), la saba, na hivyo kujumuisha Jumuiya yote ya Wakristo katika hali yake iliyotiwa unajisi. Kwa sababu hii Uvuvio ulipeana namba ya Kibiblia “saba.” (Tazama unabii wa Ezekieli kwa ukurasa wa 114-32.) Pia tunayo makanisa “saba” ya Ufunuo 2, na 3,

221

222

kuanza na kanisa la Efeso, na kuendelea katika vizazi vyote hadi kwa wakati wetu (Walaodekia). Namba hii ya kibiblia “saba” hujumuisha historia yote ya kanisa katika kipindi cha uakisi hadi kwa wakati wa utengo wa magugu kutoka kwa ngano, kama ilivyotabiriwa na Kristo katika Mat. 13:30. Namba “saba” hutumika kumaanisha yote, au hadi kikomo cha magugu. Tazama chati, ukurasa wa 224. {SR1: 220.3}

Ingawa uasi huo mkubwa na kukufuru kumenasa ulimwengu, kanisa la Mungu 144,000 kwa idadi, wakiwa wametawanyika kwa upana na urefu wa nchi bila mchungaji, hawajamsujudia Baali. Wakati Walaodekia wanapepetwa na kuchujwa (wanatapikwa nje) kwa maangamizo, Mungu analisimamia kundi Mwenyewe. Hivyo, kanisa na ujumbe utashinda kwa shangwe. Tazama Gombo la 6, ukurasa 427, Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 300. {SR1: 222.1}

Wakati kipindi cha miaka 430 ambacho kilihusiana na Israeli huko Misri, na miaka 430 ya Ezekieli 4:5, 6, inakwenda sambamba katika wakati wetu, chati hii (Jeraha Lake La Mauti Limepona) huonyesha kwamba kimoja hulialia kingine. Maana, siku (miaka) arobaini, katika wakati ambao Ezekieli alipaswa kufunga akiwa amelalia upande wake wa kulia humaanisha njaa ya kiroho (kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 125, na chati kwa ukurasa wa 133) ilianza katika mwaka 1890, na ikakoma katika mwaka 1929. Matumizi hayo huthibitisha kuwa ni ya kweli na tukio lililofanyika Februari 11, 1929 (kupona kwa lile jeraha), ikiwa ni ishara kwamba kipindi hicho cha kinabii kilikuwa kimekoma. Inathibitishwa pia na ukweli uliokuja, kwa maana mwishoni mwa hizo siku arobaini Ezekieli alipaswa kuinuka, ale na kuwa huru. Iwapo hiyo miaka arobaini ya kinabii haingekuwa imemalizika, hatungeweza tumeupokea ukweli uliochapishwa katika kitabu hiki, lakini uhakika ni kwamba ukweli umekuja. Kwa hivyo, kwa 1930, ondoa miaka arobaini ya kinabii na unapata 1890, wakati ambapo kanisa lilianza kudidimia. Tazama chati kwa ukurasa wa 221. {SR1: 222.2}

223

CHATI YA MUHTASARI–

Ufafanuzi Wa Mifano

Nia na kusudi la chati hii (kwenye ukurasa ufuatao) ni kujumlisha masomo yote mawili (matengenezo, na watu 144,000). Kupitia chati hii tunaona uwiano kamili wa yale ambayo yamefundishwa katika chapisho hili. Pia inatuwezesha kuangalia ndani ya somo hili muhimu zaidi. Mungu, ambaye mwangalifu haswa kwa manufaa ya kanisa Lake kwa kuufunua ukweli Wake kwa watu Wake, amewasilisha kwetu picha zinazoshangaza za matukio ya kihistoria; ambazo ni ushahidi wa upendo wa milele kwa Israeli wateule Wake — malimbuko ya mavuno Yake. Kwa hivyo “Mungu wa Yakobo,” maelfu ya miaka mbeleni, alikuwa ameweka mipango Yake ya kuwasilisha kwa watu Wake kazi ya sanaa ya kinabii yenye mguso mtakatifu. {SR1: 223.1}

Mtunga Zaburi alisema, “Mungu aliye hodari, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi toka maawio ya jua hata machweo yake. Tokea Zayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu amemulika. Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele Yake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. Ataziita mbingu zilizo juu na nchi pia, awahukumu watu wake. Nikusanyieni watakatifu Wangu; waliofanya agano Nami kwa dhabihu. Na mbingu zitatangaza haki Yake: Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu. Selah. Sikieni, Enyi watu wangu, nami Nitashuhudia dhidi yako: Mimi ndimi niliye Mungu, naam Mungu wenu. “ Zaburi 50:1-7. {SR1: 223.2}

Agano la Kale (Sehemu Ya Pili)

Kuzungumzia sehemu ya pili kwenye chati ya muhtasari, inayoitwa “Mifano ya Wazee wa Imani” ni sehemu ambayo ilizalisha wazee wa imani (kwa sababu hii tumeipatia jina hilo), ambao Mungu aliwachagua kimbele kuwa kama minara, na kama vibao vya ishara kwa mfano, na mifano kwa kanisa Lake katika wakati wake mwafaka, ili kutimiza kusudi takatifu. Minara? Naam; zaidi ya minara. Sauti zao hunguruma kwa miangwi, na kurudia miangwi tena, zikiendelea katika vizazi vingi, na katika wakati wetu zinasikika kwa sauti kubwa mno. {SR1: 223.3}

224

225

Sehemu namba tatu, inayoitwa “Mifano ya Sherehe” ni sehemu ambayo, kwa utumishi wa Hekalu kuhusiana na Patakatifu, imetupatia nembo za masomo yasiyokosea, yenye thamani kubwa. Ingawa asili yake ni karne nyingi zilizopita, nyimbo zake tamu za wokovu kutoka kwa upendo wa Baba, kuendelea mbele kupitia katika njia ya jamii ya wanadamu, zimefika kwa wakati wetu bila kupoteza hata sauti moja. Nembo hizi zilizoteuliwa na Mungu zilipaswa kumfunua Mwasisi wa upendo kwa familia ya wanadamu katika vizazi vyote. {SR1: 225.1}

Hakika, tumefikia kizazi cha maarifa makubwa, lakini yanaonekana kuwa ni ya umuhimu mdogo tu, na ni kidogo sana katika maarifa ya kumjua Yeye ambaye Kwake baraka zote hutoka: Katika hekima, maarifa, afya, na nguvu kutimiza mambo makuu. Laiti watu wa Mungu wasingeanguka katika uchawi wa kusinzia, kulala usingizi, wingi wa nembo hizi na mifano ya kale, pamoja na maana ya kweli ya umuhimu mkubwa kwa kanisa la Mungu, zingekuwa zimefunuliwa zamani sana. Mengi mema yangetimizwa na baraka ambazo zingepatikana kutoka kwa maarifa kama hayo haziwezi kukadiriwa. Wakati ulimwengu unafanya maendeleo ya haraka katika hekima ya kibinadamu na vyombo vya uovu, watu wa Mungu hawajafanya maendeleo yoyote bora katika safu yoyote. Kwa miaka mingi tumekuwa tukijiondoa kwake Yeye ambaye ndiye Chanzo cha hekima yote ya kweli. {SR1: 225.2}

Agano la Kale (Sehemu Ya Tatu)

Mifano iliyoagizwa rasmi katika sehemu ya pili ilianza mara moja kutimizwa kwa uakisi wayo punde tu vuguvugu la kutoka lilipopisha sehemu ya tatu. Usiku wa pasaka ulizalisha sehemu hii (ya mifano ya sherehe). Hajiri (mfano) alikutana na uakisi ambao ulisherehekewa na kuwekwa wakfu kwa maonyesho, ishara, na maajabu makuu. Alisema Paulo, katika Gal. 4:25, “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Uarabuni.” Hivyo, Hajiri alikuwa mama wa mfano wa kanisa hilo, na Abrahamu, baba wa kimwili, na Ishmaeli, nembo ya watoto kutoka kwa uzao wa Abrahamu. Mama, baba, na mwana huyo ni mfano wa Israeli ya kimwili nembo kamilifu, sivyo?). Kwa hivyo, nembo tatu kutoka katika sehemu namba mbili zilipata utimizo wazo kwa uakisi katika sehemu ya tatu. {SR1: 225.3}

226

Wakati mwana-kondoo wa pasaka alipompisha Hajiri, (nembo ya kanisa chini ya uchumi wa Kiyahudi), pia aliadhimisha kuanzishwa kwa mfumo wa sherehe, kwa hivyo sehemu namba tatu ikawa mama wa mifano ya sherehe. Mifano yenyewe sio kitu halisi, sio zaidi ya picha ilivyo, bali ni uwakilishi ambao huonyesha ushahidi usiokosea, kitu amba kiko kwa mtazamo. Mwana-kondoo wa pasaka ni mfano kamili wa “Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” (Yohana 1:29). {SR1: 226.1}

Kwa sababu sehemu ya sherehe (namba tatu) ilikaribishwa na kondoo halisi wa pasaka, pia ilifungwa na yule wa uakisi. Jinsi mfano ulivyokutana na uakisi, alisema mtume, “kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka kwa ajili yetu” (1 Kor. 5:7), kwa hivyo, utawala wa Hajiri kama nembo ya kanisa la mfano (Israeli ya kimwili) ulikoma kwenye msalaba wa Kalvari. Kule kuliweka mbali kanisa la Agano la Kale na watoto wake, pia kumefananishwa vile vile katika sehemu namba mbili. Kunukuu Gal. 4:29-31, “Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa yule aliye mwungwana.” {SR1: 226.2}

Ni dhahiri kwamba Wokovu unahubiriwa katika mifano na vile vile katika neno. Upo mfano kwa kila tukio na shughuli ya kanisa kuhusiana na injili ya Kristo. Kikomo cha hii mifano kulifunga kipinda cha mifano, na kukaribisha cha uakisi ambacho chini yake kila mfano lazima utimizwe kwa uakisi wake. {SR1: 226.3}

Wakati uzazi wa kanisa la Agano la Kale ni “wa kimwili,” wa Jipya ni wa Kiroho, kwa hivyo Sara akawa nembo ya kipindi chote cha uakisi. Paulo, akiliandikia kanisa hili alisema, “Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa usiyezaa, paza sauti ulie, wewe usiye na utungu; maana watoto wake aliye pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume.” Abrahamu ndiye mume, na baba wa kiroho duniani badala ya wa kimwili. Kwa vile ziko sehemu tatu za mfano kabla ya Kristo, pia ziko tatu baada ya

227

Kristo. Watoto wa Abrahamu na Sara (Isaka na Yakobo), waliozaliwa kwa ahadi, ni nembo zinazofaa kwa kanisa la Agano Jipya. {SR1: 226.4}

Agano Jipya (Sehemu Ya Kwanza)

Kwa vile Isaka alikuwa mzaliwa wa kwanza “wa kiroho,” kwa kawaida lazima awakilishe sehemu ya kwanza, kuanzia kwa msalaba wa Kristo. Kunukuu maneno ya Paulo, yeye asema, “Basi, ndugu zangu, kama Isaka, sisi tu watoto wa ahadi.” Gal. 4:28. Isaka, basi, huwakilisha hiyo sehemu kutoka msalabani hadi mwaka 1844, maana haujakuwapo mwito mwingine hapo kabla. Mwanzo wa kila sehemu iliyopita na pia mwisho wa hizo sehemu ulitiwa alama na tukio muhimu; vivyo hivyo na kikomo cha sehemu inayowakilishwa na Isaka. Mwaka 1844, ni wakati pekee unaofaa kwa sehemu hiyo kupita na kukaribisha ya pili, wakati ambapo hukumu katika Hekalu la mbinguni ilianza. Bila shaka chuo ilibidi kiweze kupiga kona, na tena mfano ulikutana na uakisi. {SR1: 227.1}

Agano jipya (Sehemu Ya Pili)

Yakobo, akiwa mwana wa Isaka, kwa kawaida anafuata katika mstari. Yakobo, basi, ni nembo ya sehemu ya pili baada ya Kristo (kama ilivyoonyeshwa kwenye chati) kuanzia mwaka 1844. Lengo la kanisa tangu wakati huo limekuwa kuwafanza watu 144,000. Kama vile Yakobo alikuwa baba wa kabila kumi na mbili za Israeli, — mfano; kwa hivyo yeye ndiye baba katika mfano wa uakisi (watu 144,000, — wa kweli). Sehemu inayowakilishwa na Yakobo ndiyo kipindi pekee cha nembo inayofaa kuwazaa watu 144,000. Punde tu namba hii imefanyizwa na kutiwa muhuri, sehemu hii itapita na kuikaribisha nyingine. {SR1: 227.2}

Kwa sababu lilikuwapo tukio muhimu na kila sehemu iliyofuata (mwishoni mwa moja, na mwanzoni mwa ile nyingine), lazima kiwepo jambo lisilokuwa na matokeo madogo ambayo yangefanya mabadiliko ya sehemu hii ambayo tumejitambulisha nayo. Tukio hilo muhimu si lingine isipokuwa kutakaswa kwa kanisa la Mungu, na utengo wa magugu kutoka kati ya ngano. Yesu alisema, “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno.” Huo utengo utaanzisha mavuno. Kumbuka kitenzi “hata,” kinachomaanisha “hadi.” Wakati huu mzito sana

228

kwa kundi moja (magugu), na wa utukufu kwa lingine (watu 144,000), hutupa nje sehemu inayowakilishwa na Yakobo, na kuelekeza mbele nyingine. {SR1: 227.3}

Agano Jipya (Sehemu Ya Tatu)

Yesu alisema, “na katika wakati wa mavuno Nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, na myafunge matita matita mkayachome.” Magugu, kwa hivyo yanakusanywa punde tu kabla ya mavuno, na kuchomwa katika wakati wa mavuno (maana kumbuka kiambishi awali “katika”). “Bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.” Mat. 13:30. Ngano huwakilisha watu 144,000; lile “ghala” ni nembo ya usalama. Kundi hili tukufu limeokolewa na kulindwa. Shetani hawezi kuwadhuru. Watahamishwa bila kuonja mauti. Yohana hufafanua wao kama “malimbuko [ya mavuno] kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” {SR1: 228.1}

Magugu yanaodolewa na watu watano wenye silaha za kuchinjia wa maono ya Ezekieli. Hili ndilo tukio linalofanya badiliko, na kulileta kanisa la Mungu, katika sehemu ya mwisho ya muda wa rehema (Israeli), kama ilivyoonyeshwa kwenye chati. {SR1: 228.2}

Alikuwa Yakobo, baba wa kabila kumi na mbili, ambaye jina lake lilibadilishwa kuwa Israeli. Jina jipya la Yakobo ni nembo inayofaa ya sehemu inayoitwa “Israeli.” Hivyo tena mfano utakutana na uakisi. {SR1: 228.3}

Alikuwa Yakobo, ambaye, usiku, akiwa njiani kwenda Padan-Aramu aliota ndoto ya ngazi kubwa ambayo ilifika mbinguni kutoka duniani, na “malaika wa Mungu walipanda na kushuka juu yake.” Maono haya yalikuwa uwakilishi wa “Mvua ya Vuli,” na “Kilio Kikuu” cha ujumbe wa malaika wa tatu katika wakati wa mavuno. Ngazi, ikimwakilisha Kristo; malaika, wajumbe; Mungu Baba kwa ncha moja, na Yakobo kwa ncha nyingine, ikimaanisha uhusiano mkamili wa mbingu na dunia. {SR1: 228.4}

Ijapokuwa muda wa sehemu hii ya mwisho ya wakati wa rehema (inayoitwa Israeli), ni mfupi kuliko chochote cha vipindi vilivyokitangulia, kitakuwa wakati mtukufu sana wa kanisa la Mungu. Nabii Isaya, akitazama mbele hadi kwa wakati huu, anasema, “Amka, amka, jivike nguvu

229

zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; kwa maana tokea sasa hataingia tena ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Asilani kabla ya wakati huu kwa mtazamo, kanisa la Mungu halijajidumisha huru kabisa bila wasiojitakasa na waso waongofu (magugu: asiyetahiriwa na aliye najisi) kati yake, lakini sasa wakati umekuja ambapo Yeye lazima alitakase kanisa Lake na kulidumisha likiwa hivyo.” Zefania, akiuataja wakati huu, husema, “Mabaki ya Usraeli hawatatenda uovu, wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao.” Zefania 3:13. {SR1: 228.5}

Katika wakati huu wa “mavuno” (Kilio Kikuu), ujumbe wa malaika wa tatu utapenyeza hadi sehemu za mbali sana za dunia hii iliyolaaniwa na dhambi. Yohana, akionesha mbele kwa mavuno haya matukufu ya kukusanywa, asema, “Nikaona, na tazama, umati mkubwa sana, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele Mwana-Kondoo, wamevaa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7:9. Mungu “Atakamilisha kazi na kuifupisha kwa haki.” Rumi. 9:28. Hivyo ndivyo kanisa la Mungu litafanywa tayari kukutana na Bwana wake. Isaya, akitazama mbele kwa kanisa hili linalomwakisi “aliye Mtakatifu”, asema, “Nawe utakuwa taji ya utukufu katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.” Isa. 62:3. Tukufu ni kanisa la Mungu katika siku ya Bwana. {SR1: 229.1}

Yohana, baada ya kuona katika njozi kanisa kumaliza kazi, kufungwa kwa muda wa rehema, na hukumu za Mungu katika mapigo saba ya mwisho, asema, “Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yeye aketiye juu yake, ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.” Ufu. 20:11. {SR1: 229.2}

Agano la Kale (Sehemu ya Kwanza) —

Melkizedeki, Mfalme Wa Salemu

Sehemu kuu ya kwanza katika chati inayoitwa “Melkizedeki” tumeihifadhi kwa ufafanuzi mpaka sasa. Kumbuka sehemu kuu mbili zifuatazo zenye kichwa “Hajiri” na “Sara” ni sehemu za historia ya kanisa na wazazi wa duniani, ya kwanza ikiwa “ya kimwili,” na ya pili “ya Kiroho,” kwa hivyo, Hajiri na Sara

230

ni nembo zinazofaa kwa sehemu hizi kuu mbili, na Abrahamu kama baba. Sehemu hizi mbili (“Hajiri” na “Sara”) ni tofauti na ile ya kwanza (“Melkizedeki, Mfalme wa Salemu”) ambayo haina hata mojawapo wa majina haya ya nembo. Ni sehemu ya historia ya kanisa bila uzazi wa duniani wenye nembo. {SR1: 229.3}

Ili kuafiki kiwango kitakatifu cha ukamilifu, kwa nembo na pia kwa takwimu, katika historia yote ya kanisa la Mungu, lazima Yeye atoe nembo inayofaa haswa kwa sehemu hii jinsi ambavyo Ametoa kwa sehemu mbili zilizotangulia. Iwayo yote nembo hiyo, lazima iwe ni aina ya kuonyesha historia ya kanisa bila uzazi wa duniani. {SR1: 230.1}

Paulo hutupatia habari ya nembo inayofaa kwa sehemu hii katika Ebr. 7:1-3, — “Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu Aliye juu, aliyekutana na Abrahamu alipokuwa akirudi katika kuwachinja hao wafalme, akambariki; ambaye Abrahamu alimpa sehemu ya kumi ya vitu vyote; tafsiri ya jina lake kwanza ni Mfalme wa haki, tena Mfalme wa Salemu, maana yake, Mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana nasaba, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu; huyo adumu kuhani.” Ingawa sisi wanadamu hatuwezi kuelewa uwepo wa mtu huyu “Melkizedeki, Mfalme wa Salemu,” lazima iwe kweli kwamba “hana baba, hana mama, hana nasaba, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake,” hivyo kufanya nembo inayofaa kamilifu kabisa ya sehemu hiyo ya kanisa la Mungu. Tena tunaona ukamilifu wa Mungu katika nembo kamilifu kwa historia yote ya kanisa Lake. {SR1: 230.2}

Mara tu dhambi ilipoingia mwanzoni kwa wazazi wa familia ya wanadamu, na kabla ya kufukuzwa watoke kwa maskani yao ya Edeni, mipango iliyokuwa imebuniwa tayari ya kurudi kwa maskani yao asili ya makao ya milele ilijulishwa kwao na pia kwa yule nyoka. Mipango hii ya Mungu iliyowekwa mapema hueleweka vyema kwa kuzichunguza shughuli Zake za ajabu takatifu kwa familia ya wanadamu zinazoendelea katika vizazi vyote jinsi zinavyoonyeshwa kwenye chati hii. {SR1: 230.3}

Mungu wetu ametimiza mipango Yake iliyoamriwa kimbele bila mabadiliko hata kwa maelezo madogo kabisa. Yesu alisema, “Hayo ndiyo

231

maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe mambo yote, yaliyoandikwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi kunihusu Mimi.” Luka 24:44. Roho wa Mungu alimwongoza Mwandishi wa Zaburi ayaandike maneno haya, “Bwana atainyosha toka Zayuni fimbo ya nguvu zako: Uwe na enzi kati ya adui zako … Bwana ameapa, wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.” Zaburi 110:2, 4. {SR1: 230.4}

Ingawa hatuwezi kuelewa hekima kama hiyo ya milele, hutupatia ufahamu bora wa upendo wa Mungu kwa wadhambi, na dhana yetu potofu ya kile kinachoitwa eti maarifa ya mambo ya kibinadamu. Kwa yule “MIMI NIKO,” wa milele, anayeumiliki umilele, mbele yake giza ni nuru, na mipaka ya mbali sana angani ni mahali pa kuweka miguu Yake, ambaye huuona mwisho tangu mwanzo, na ambaye kwake yeye miaka elfu ni kama jana tu, mambo yote yako wazi na uchi Kwake. {SR1: 231.1}

Mtunga Zaburi alisema, “niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso Wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko. Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe, uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, na kukaa pande za mwisho za bahari; huko nako mkono Wako utaniongoza, na mkono Wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo ingekuwa usiku, giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangaza kama mchana: Giza na mwanga Kwako ni sawasawa… Maarifa hayo ni ya ajabu; yanishinda mimi, hayadirikiki siwezi kuyafikia.” Zaburi 139:7-12, 6. Hekima na maarifa ya asiye na mwisho ni zaidi ya ufahamu kwa wafaji. Maajabu tunayoyaona na matukio ambayo hufanyiza historia ya ulimwengu wetu ni urudufishwaji wa ramani za mbinguni. {SR1: 231.2}

Jinsi Ya Kuchunguza Habari Zilizowasilishwa. Iwapo Ni Sahihi

“Maana ni nani katika ninyi kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza, na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza, baada ya kuuweka msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki.” Luka 14:28, 29.

232

Funzo ambalo linatoka kwa andiko hili ni kwamba yule ambaye haichunguzi mipango na takwimu zake si mtu mwenye hekima, kwa hivyo, halitakuwa kosa kwetu kuwaza kwamba Yesu hutaka tuzichunguze kweli za Biblia kabla ya kuzipokea kuwa ni hivyo. {SR1: 231.3}

Kwa sababu Mungu hawezi kukosea, matendo Yake yote husimulia “ukamilifu” hata kwa “nukta moja au kistari kimoja.” Taarifa hiyo ikiwa ni ya kweli, Yeye angekuwa ameandaa njia ambayo kwayo tunaweza kukagua na kuuhakiki ukweli Wake. Chati hii (ukurasa 224), ikiwa ni muhtasari wa ujumbe ambao chapisho hili husheheni, inapaswa kueleza iwapo inauthibitisha kwamba ni sahihi au la. Iwapo yaliyomo huthibitisha kwamba 100% ni kweli, lazima tuupokee kama ukweli wa Mungu. Kwa wanafunzi wote wa Biblia, namba “tatu” na “saba” hukubalika kuwa ni namba za Kibiblia ili kuzihakiki kweli za Maandiko. Roho ya Unabii hushuhudia hili pamoja na Biblia. “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu: Na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, na maji, na damu: Na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” 1 Yohana 5:7, 8. {SR1: 232.1}

“Katika ufunuo aliopewa lilifunuliwa tukio baada ya tukio la msisimuko wa kupendeza katika uzoefu wa watu wa Mungu, na historia ya kanisa ilitabiriwa hadi mwishoni kabisa mwa wakati. Katika mifano na nembo, mada zenye umuhimu mkubwa ziliwasilishwa kwa Yohana, ambazo alipaswa kuziandika, ili watu wa Mungu wanaoishi katika kizazi chake na katika vizazi vya baadaye waweze kuwa na akili za ufahamu wa hatari na mapambano yaliyo mbele yao.” Matendo ya Mitume, ukurasa 583. Hili likiwa hivyo, tutayapima yaliyo ndani ya kitabu hiki, kama yalivyoonyeshwa kwenye chati. {SR1: 232.2}

Kumbuka kwamba ziko sehemu kuu “tatu” katika chati ya muhtasari: yaani, (1) Melkizedeki, kuhani wa Mungu Aliye Juu Zaidi; (2) Hajiri; (3) Sara. (I) Melkizedeki kuhani wa Mungu Aliye Juu, (II) ukuhani wa Walawi (III) ukuhani kwa mfano wa Melkizedeki. Kwa hivyo, ukuhani mmoja huunganishwa na mwingine. Sasa hesabu sehemu ndogo za wakati wa rehema katika zote mbili kabla na baada ya msalaba. Katika kila mgawo tuna sehemu ndogo “tatu.” Tena, hesabu sehemu zote katika kabla na baada ya msalaba,

233

pamoja na mapigo, na tunapata namba “saba,” ikimaanisha mwisho wa dunia. {SR1: 232.3}

Turuhusu tuitishe umakini wako mara hii ya tatu kwa mifano. I Mifano ya wazazi; yaani, Abrahamu (baba); Hajiri na Sara (kina mama) ikifanza namba “3.” II. Watoto:– Ishmaeli, Isaka, na Yakobo, wakifanza namba kuwa “3.” III. Jina la Yakobo lilibadilishwa kuwa Israeli, Hajiri na Ishmaeli walifukuzwa na kufanza tena naba “3.” Upo mstari wa nne wa takwimu kwa uchunguzi wako wa makini. Jina “Abraham” lina herufi “saba”, likimaanisha kamili, au baba kwa historia yote ya baadaye ya kanisa. Ishmael pia lina herufi “7”; kwisha, au kumaliza; kumaanisha amemaliza; hakuna hata mmoja wa uzao wake alimfuata. {SR1: 233.1}

Jina la Abrahamu wakati aliitwa kutoka Ur (kabla Mungu hajaongeza herufi mbili za ziada — H na A) liliandikwa kwa herufi tano: (Abram). Mwanawe, Isaka, na wake zake wote wanayo namba ile ile ya herufi katika majina yao. Kwa kawaida swali huzuka, kwa nini tano? Mbona si tatu au saba? Kama majina yao yangekuwa na upungufu au zaidi ya herufi “5”, picha hiyo ingeharibiwa. Kwa nini? Kwa sababu herufi “7” za Abrahamu na “5” za Hajiri hufanza “12” kwa ujumla, — nembo ya makabila kumi na mbili ya Israeli ya kimwili. Sara na Abrahamu pia ni “12,” ikimaanisha makabila kumi na mbili ya Israeli ya Kiroho. Vivyo hivyo kwa habari ya Isaka na Yakobo, pia ikimaanisha mfululizo (mmoja atamfuata mwingine). {SR1: 233.2}

Israeli hutamkwa kwa herufi sita. Iwapo jina hili lingekuwa na zaidi au na upungufu lingeharibu hiyo picha. Kwa nini? Kwa sababu herufi sita huonyesha sehemu ya sita. Israeli ya kweli (watu 144,000) wametiwa muhuri mwishoni mwa sehemu ya tano. Laiti jina hilo lingekuwa la herufi saba, lingemaanisha “kufungwa kwa wakati wa rehema,” badala ya “mwanzo wa mavuno.” Israeli, katika wakati wa mavuno, watapokea jina jipya litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Soma Isa. 62:2. Liwalo lote jina hilo linavyoweza kuwa, tuna uhakika litakuwa kamilifu, kukamilisha picha ya wakati wa rehema, na vile vile kuonyesha kikomo cha wote waliokombolewa, au kufungwa kwa wakati wa rehema. Ole wake yule ambaye anaweza kufikiri ubunifu huu wote wa ajabu katika uzuri

234

wa ukamilifu ni bahati nasibu tu, au ajali. Mtu kama huyo anamkana Fundi Mkuu wa uumbaji wote. Anasujudia mageuzi ya uwepo wa mwanadamu (kutukia tu). Tazama chati kwenye ukurasa wa 224. {SR1: 233.3}

Mfumo wa pili wa kuhakiki ukweli umetolewa na Isaya, nabii. “Na waenende kwa sheria na ushuhuda: Ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa. 8:20. Yaliyomo katika chapisho hili hayapatani tu na andiko hilo, bali “huiinua” sheria na ushuhuda na vile vile maandiko yote ya Roho ya Unabii. {SR1: 234.1}

Tatu:– Ujumbe uliowasilishwa hapa hauleti mafundisho yoyote mapya, au kupinga yale tuliyonayo, bali huyakuza kwa kuonyesha ukubwa na umuhimu wake wa kweli. Wala hayaitishi vuguvugu jipya bali huthibitisha kwamba vuguvugu lili hili litaibuka kuwa kubwa zaidi. {SR1: 234.2}

Kwa sababu Mungu aliona kimbele mavuguvugu yote ambayo yangeinuka dhidi, au kwa ajili ya kanisa Lake, Angekuwa ameonyesha ujumbe huu aidha kuwa wa uongo, au wa kweli. Yeye aliona kimbele vuguvugu fulani lingeinuka na kudai kwamba kanisa ni “Babeli,” kwa hivyo Alitupatia onyo kwamba ni la uongo. Soma Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 49, 53. Tena, Mungu aliona kimbele kwamba wengine watakuja na kuuita ukasisi “ukuhani wa uongo,” na Akatuonya kwamba hawakutumwa kutoka Kwake. Soma Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 51. Pia Aliona kimbele kwamba wengine watatangaza “siku na saa ya kuja mara ya pili kwa Kristo,” nk. Kwa hivyo, Mungu amelionya kanisa siku zote. Hakuna mahali tunapata unabii wowote ukipingana dhidi ya ujumbe uliowasilishwa katika kitabu hiki. Haiwezekani kupata upinzani, kuona kwamba ujumbe wote umetolewa katika Biblia na Shuhuda, na kutabiriwa na vyote viwili. {SR1: 234.3}

Iwapo yeyote atafikiri ujumbe huu wa matengenezo ni wa uongo, ilhali hawezi kupata unabii dhidi yake, atakuwa akisema, Mungu amepuuza hatari hiyo na Ameshindwa kufichua njama hiyo. Kwa hivyo, mtu kama huyo anamaanisha kusema kwamba Mungu anajua tu machache katika kutabiri siku za baadaye. Lakini ukweli wa swala hilo ni kwamba Mungu anajua yote tokea

235

mwanzo hadi mwisho. Kwa hivyo, Yeye ameweza kuwasilisha ujumbe wa onyo kama huu kwa watu Wake ulioandikwa mapema kwa maelfu ya miaka. {SR1: 234.4}

236

Mika Sita Na Saba –Unabii Wa Kitabu Hicho, Wakati Unaofaa Kwa Uchapishaji

Masomo ambayo hujumuisha hili gombo yalichapishwa kwanza kuwa kitabu katika hati ya mswada, ambaoo uliitwa “Fimbo ya Mchungaji” Nakala kama hizo thelathini na tatu zilipeanwa kwa waliokuwa viongozi (jumuiya ya wachungaji) ya dhehebu la Waadventista wa Sabato, — ndugu wa uzoefu, wachungaji na marais wa mabaraza. Hili lilifanywa hivyo ili kufuata maagizo yaliyokabidhiwa kanisa na Roho wa Mungu. Tunanukuu kutoka Gombo la 5, ukurasa wa 293: “Yapo majaribu elfu mafichoni yalioandaliwa kwa wale walio na nuru ya ukweli: na usalama pekee kwa kila mmoja wetu ni katika kutopokea fundisho jipya, wala Maandiko mapya, kabla kwanza kuyawasilisha kwa ndugu wenye ujuzi. Weka mbele yao kwa roho ya unyenyekevu na yenye kufunzwa, kwa sala ya bidii; na iwapo hawaoni nuru ndani yake, ukubaliane na hukumu yao, kwa maana ‘katika wingi wa washauri upo usalama.’” {SR1: 236.1}

Ingawa yaliyomo katika kitabu hiki hayaingizi mafundisho mapya au ufasiri mpya wa maandiko ambayo yamekubaliwa na dhehebu na kuidhinishwa na Mungu, tuliwaza ni bora kuiwasilisha nuru hii kwa ukasisi kwanza. {SR1: 236.2}

Masomo haya yaliwasilishwa katika hati ya mswada kwa viongozi wa vuguvugu hili kubwa kwa upekuzi wao wakati walipokuwa wamekongamana katika kikao cha Baraza Kuu cha 1930 huko San Francisco, Calif. Yaliwasilishwa kwa ombi la dhati na mwandishi wa hati hiyo. Kuwasihi ndugu zetu wapendwa wayapekue yaliyomo katika nakala hiyo katika uchunguzi wa makini, sala ya dhati, na imani kwake Yeye ambaye ni mwenye rehema na anayetaka sana kwamba tuujue ukweli wa wokovu wetu kuliko tulivyo sisi wenyewe; ambaye angelifunua neno Lake kwa watoto Wake wote na kuweka wazi makosa kwa wema wa pande zote mbili. {SR1: 236.3}

Mwito huu ulifanywa kwa watumishi wa Mungu kwa ombi kwamba wanapaswa kuihakiki nuru mpya kwa kitabu cha Mungu cha ukweli wote, na lolote watakalogundua au kusudi lao kwa makala hiyo, watuandikie katika

237

njia ya undugu kama watafuta nuru. Hili waliahidi kulitekeleza mapema iwezekanavyo, tukiwa tumewahakikishia kwamba ukweli au makosa yoyote wanayoweza kuthibitisha, kwa Bibilia, au kwa Roho ya Unabii, tuko tayari kukubali. Tulihisi hakika kwamba wao, kama wachungaji wa kundi, wangekuwa wenye bidii kutenda haki katika kicho cha Bwana. Iwapo walifikiri tulikuwa tumeongozwa makosani, tulitarajia wao kama walezi wa urithi wa Mungu watusaidie kwa Neno la Mungu. {SR1: 236.4}

Kwa vile hati hiyo iliwekwa mikononi mwao, na wakati chapisho hili linakwenda kwa matbaa, zaidi ya miezi mitano imepita. Tunahisi sasa wamekuwa na wakati wa kutosha angalau kuandika na kutupatia habari kuhusu mswada huo na nia yao. Mpito wa wakati ni ushahidi kwamba ndugu zetu wameshindwa kutekeleza ahadi yao na pia wajibu wao. Kwa udhahiri hawa wachungaji wa Mungu na viongozi wa dhehebu hili kubwa lazima wamepuuza maagizo yanayoheshimu maswala ya aina hii jinsi walivyopewa na Roho ya Unabii. “Iwapo ndugu anafundisha makosa, wale walio katika nafasi za uwajibikaji wanapaswa kujua; na iwapo anafundisha ukweli, wanapaswa kusimama upande wake. Sote tunapaswa kujua lile linalofundishwa kati yetu; maana likiwa ni ukweli, tunahitaji kuujua.” Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa 110. {SR1: 237.1}

Ikiwa wamezingatia takwa lililonukuliwa hapo juu, kwa kuchunguza kwa unyoofu katika ile hati waliyopewa, na kupata makosa, wajibu wao ni, kama wawakilishi wake Yeye aliyewaacha wale tisini na tisa na kwenda kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea, kumwita mwandishi aidha mwenyewe, au kwa barua kutafuta kufanya upatanisho na yule anayekosea. Kunukuu Gombo la 6, ukurasa wa 21, 22: “Nafsi moja ina thamani zaidi mbinguni kuliko ulimwengu wote wa mali, nyumba, ardhi, fedha.” {SR1: 237.2}

Kwa upande mwingine, iwapo hawakupata kosa, na bado wanakataa kufanya nia yao ijulikane, hata baada ya kufanya mwito wa pili na wa tatu kwa baraza letu la mtaa basi labda wanataka kutimiza unabii ufuatao jinsi unavyopatikana katika Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 106, 107. “Lakini jihadhari kukataa

238

lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali. {SR1: 237.3}

“Hakuna mtu anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ilioko kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia hili, Yeye amesema, ‘Nimeweka mbele yako mlango ulio wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.’ Hata kama viongozi wetu wote wanaweza kukataa nuru na kweli, mlango huo utakuwa bado wazi. Bwana atawainua watu watakaowakabidhi watu ujumbe kwa wakati huu…. {SR1: 238.1}

“Tuseme ndugu alishikilia mtazamo ambao ulikuwa tofauti na wako, na aweze kuja kwako, akipendekeza kwamba uketi pamoja naye na mfanye uchunguzi wa jambo hilo katika Maandiko; je! utainuka, ukiwa umejaa chuki, na kushutumu maoni yake, ilhali ukikataa kumsikiliza bila ubaguzi? Njia pekee sahihi ingekuwa kuketi chini kama Wakristo, na kuchunguza msimamo uliowasilishwa, katika nuru ya neno la Mungu, ambalo litaufunua ukweli na kufichua makosa. Kudhihaki maoni yake hakutadhoofisha msimamo wake hata kidogo ukiwa ni wa uongo, au kutia nguvu msimamo wako iwapo ulikuwa wa kweli. Iwapo nguzo za imani yetu hazitasimama kwenye kipimo cha uchunguzi, ni wakati upasao tuweze kujua. Lazima isikuwepo roho ya Ufarisayo inayokuzwa kati yetu.” {SR1: 238.2}

Tunasikitika sana kwamba tunapaswa kuweka wazi kwa umma upuuzaji huu mkubwa kwa upande wa ndugu zetu, na kutopendezwa kwao katika mambo ya Mungu. Kama jambo la wajibu kwa upande wetu, na upendo kwa ndugu zetu, na kwa kanisa la Mungu, hatukupata suluhu la kuzuia kuyatangaza mambo yaliyoandikwa katika sura hii, na bado tujilinde dhidi ya mtazamo wetu kueleweka vibaya kwa kupeana kitabu hicho. Si kwamba tunataka kuepusha shutuma dhidi yetu, bali kwa usalama wa kanisa la Mungu tukitaka kuwakinga wale ambao wanaweza kushambuliwa kwa urahisi na walio wepesi kushutumu. Tena tunanukuu kutoka kwa Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300: {SR1: 238.3}

“Isipokuwa wale ambao wanaweza kusaidia katika ______ waamshwe kwa hisia ya

239

wajibu wao, hawataitambua kazi ya Mungu wakati kilio kikuu cha malaika wa tatu kitakaposikika. Wakati nuru inakwenda kuiangaza nchi, badala ya kuja kwa msaada wa Bwana, watataka kuifunga kazi Yake ili iafikiane na mawazo yao finyu. Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda kazi katika kazi hii ya mwisho kwa namna itakayokuwa kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa mwanadamu. Watakuwapo wale kati yetu siku zote watakaotaka kuthibiti kazi ya Mungu, kulazimisha hata hatua gani zitafanyika wakati kazi inasonga mbele chini ya uongozi wa yule malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua hatamu mikononi Mwake. Watendakazi watashangazwa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kuileta na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki. Wale ambao wanahesabiwa kuwa watendakazi wazuri watahitaji kusogea karibu na Mungu, watahitaji mguso wa kiungu.” {SR1: 238.4}

Kwa kuona hatari inayojongea jinsi ilivyofunuliwa katika “Fimbo ya Mchungaji,” tumesubiri kwa hamu miezi hii yote kwa hofu kwamba tunaweza kusubiri kwa muda mrefu zaidi, na hivyo tushindwe kupiga kamsa na kuendelea pia kusonga mbele na sauti ya tarumbeta kabla tusikie kutoka kwa ndugu zetu. Wakati tulipokuwa tunasubiri na kuomba, andiko fulani lilifunuliwa kwetu, linalopatikana katika Mika 6, ambalo sasa tunalileta kuthibitisha kwamba Mungu amenena na watu Wake kupitia kwa neno lililoandikwa, akitupatia agizo la kusonga mbele bila kuchelewa na kupaza sauti hakika ya tarumbeta. {SR1: 239.1}

Ingawa kitabu cha nabii huyu mdogo kiliandikwa karne nyingi zilizopita, kilikusudiwa kanisa kwa sasa, wakati huu hasa. Kiliwekwa ndani ya Biblia (chuo) katika siku za Israeli ya kale, kiliandikwa kwa njia ambayo wao, pia, wangeweza kupata manufaa fulani kwacho sawa sawa na sehemu zingine za maandiko ambazo ziliandikwa moja kwa moja kwa taifa hilo la zamani na kuwekwa ndani ya chuo hicho ili sisi tujifunze na kutuonya jinsi ilivyoonyeshwa katika 1 Kor. 10:11, na mtume mkuu kwa Mataifa. Lakini ingawa sehemu fulani za Maandiko hayo ziliandikwa kama

240

waraka kwa Israeli ya zamani, nayo pia yangeturejelea sisi kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kwa vile shirika hili la ujio ni nakala ya vuguvugu hilo la zamani. Hata hivyo, kitabu cha Mika kimeandikwa moja kwa moja kwa kanisa la wakati huu wa sasa. {SR1: 239.2}

Kunukuu Mika 6:1: “Basi sasa sikieni asemayo Bwana; Simama, ushindane mbele ya milima, na vilima navyo visikie sauti yako.” Ni ukweli kwamba unabii wa sura hii kamwe haujawahi kueleweka kwa wakati wowote, na hakuna yeyote aliyewahi kufaidika sana kutokana nao, somo lolote tu kutoka kwa kifungu fulani linaweza kuwa limetolewa kwa uhusiano na uchambuzi mwingine. Swali laweza kuulizwa, Kwa nini haujaeleweka? Je! Ni kwamba hakuna mtu aliyejaribu kuichambua sehemu hii ya Maandiko? Bila shaka wanafunzi wengi wacha Mungu, wenye bidii wametumia wakati mwingi wa thamani bila matokeo yoyote kuufunua ukweli wa sura hiyo. {SR1: 240.1}

Sababu ya kushindwa kwao kufunua wazi unabii huo ni kwa maana u katika wakati wa sasa. “Basi sasa sikieni asemayo Bwana; Simama, ushindane mbele ya milima, na vilima navyo visikie sauti yako.” Kutokana na ukweli huu, tunajua kwamba uvuvio kamwe haukutarajia kwamba uweze kufunuliwa kabla ya wakati uliokusudiwa, vinginevyo ungekuwa si sawa kisarufi. Kwa namna ile ile kama Ufu. 14:7, “Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” Laiti andiko hili lingekuwa katika wakati ujao, William Miller asingekuwa alifanya makosa kuhusu tukio ambalo lingetokea katika mwaka 1844. Yeye anayedhibiti Maandiko dhahiri hakukusudia kuufunua ukweli huo hadi baada ya saa ya hukumu kuanza katika mwaka 1844. Sheria iyo hiyo inapaswa kuzingatiwa katika kweli zote za Biblia ili kuhakiki kimamlaka wakati fulani wa kinabii. {SR1: 240.2}

Tulisema hapo awali kwamba ukweli huu ulikuja kupitia idara ya Shule ya Sabato katika mwaka 1929, katika masomo ya robo ya kwanza ya mwaka huo, kuanzia Isaya 54 hadi sura ya 66 kwa ujumla. Ya 54 ilikuwa ya kwanza kufunua kwamba sura hizi ziliandikwa moja kwa moja kwa kanisa haswa kwa wakati huu kama ilivyoelezwa kwenye ukurasa wa 136-40. Katika Isa. 58:1 tulijifunza kwamba Mungu atazifichua dhambi zilizo ndani ya

241

kanisa, na kwa hivyo kufanya mwito wa matengenezo. Tunanukuu aya hiyo: “Piga kelele usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” {SR1: 240.3}

Andiko hili sasa limepata utimizo wake. Baada ya dhambi hizi zilizopo kufunuliwa, masomo haya yakaandikwa, hati hiyo ikiwa na kichwa “Fimbo ya Mchungaji,” na kuwekwa mikononi mwa viongozi wa vuguvugu hili. Kwa hivyo “Kelele” kama “tarumbeta” inavuma. Ushahidi wa dhambi zilizopo zikiwa zimefanywa zijulikane (zimeonyeshwa) kwa watu wa Mungu na kwa nyumba ya Yakobo, pia ukionyesha kwamba Walaodekia wamepuuza mialiko ya Shahidi wa Kweli, kwa hivyo, aibu ya uchi wetu imeonekana. “Nakupa shauri ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka, upate kuona.” Ufu. 3:18. {SR1: 241.1}

Sasa tunanukuu Isa. 60:1, “Ondoka uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia.” Kumbuka kitenzi “imekuja” kiko katika wakati wa sasa. “Nuru” ni ukweli. Andiko hili pia lilitimizwa. Fikiri kuhusu nuru ya ajabu ambayo imekuja kupitia masomo hayo jinsi yalivyokusanywa katika chapisho hili. Kumbuka kwamba haipingi ukweli ambao kanisa liko nao tayari, bali hufunua ukuu wa kweli na umuhimu wa ujumbe wake. Lakini hii ni sehemu tu ya nuru ambayo imekuja kupitia katika zile sura za thamani. Nuru zaidi itafuata hivi karibuni katika chapisho lingine. {SR1: 241.2}

Mwito ni, “Inuka, uangaze.” … kwa maana “utukufu wa Bwana umekuzukia.” Ameachwa msomaji aruhusu uzoefu huu mtukufu uingie kwanza katika maisha yake mwenyewe, na kwa bidii ainuke na kuangaza awe tayari kuukabili upinzani kutoka ndani na nje. “Ghadhabu ya Mungu i juu ya watu wake, na Yeye hatadhihirisha uwezo wake kati yao wakati dhambi ziko kati yao, na zinakuzwa na walio katika nafasi za uwajibikaji. Wale wanaofanya kazi kwa kicho cha Mungu kuliondolea kanisa vizuizi, na kurekebisha makosa mabaya, ili watu wa Mungu waone umuhimu wa kuchukia dhambi, na wafanikiwe katika

242

usafi, na ya kwamba jina la Mungu liweze kutukuzwa, watakutana siku zote na vishawishi vya upinzani kutoka kwa wale ambao hawajajitoa wakfu.” Gombo la 3, ukurasa wa 270, 271. {SR1: 241.3}

Tukirejea kwa Mika 6:1, “Basi sasa sikieni asemayo Bwana.” Kumbuka kitenzi “sikieni” kiko katika wakati wa sasa, kwa hivyo ni ukweli wa sasa. Lakini tunapaswa kusikia nini? “ Simama, ushindane mbele ya milima, na vilima navyo visikie sauti yako.” “Milima” humaanisha kama vile katika Mika 4:1, sehemu ya kwanza. Tofauti pekee kati ya aya hizi mbili ni kwamba ya mwisho ni umoja, lakini ya kwanza ni wingi. “Mlima” katika sura ya 4, humaanisha kanisa la Mungu (dhehebu) kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 173, lakini “milima na vilima” kama vile katika sura ya 4:1 (sehemu ya mwisho) na 6:1, ikiwa katika wingi itamaanisha makanisa na mashirika. Kwa maana hii haingeweza kurejelea kanisa la Mungu, kwa sababu Yeye hulitambua kanisa moja pekee kama Lake. Pia “vilima” vikiwa kwa wingi vitamaanisha vidhehebu, au mavuguvugu madogo madogo, nk. {SR1: 242.1}

“Navyo visikie sauti yako.” Wazo linaloweza kutolewa ni hili: Viongozi wetu wanachukua aidha muda mrefu sana, au labda kamwe hawana nia ya kufanya lolote na nuru mpya iliyowasilishwa kwao katika “Fimbo ya Mchungaji,” kwa hivyo, usisubiri tena, “Simama, ushindane mbele ya milima, na vilima navyo visikie sauti yako.” (ifanye wazi kwa umma). Hili likiwa hivyo, tulilazimika kuchapisha kitabu hicho na kukitoa bila kukawia. {SR1: 242.2}

Lakini milima inapaswa kusikia nini? Je! Atashindana na nini? Jibu limetolewa katika aya ya pili. “Sikieni, Enyi milima, mateto ya Bwana, na ninyi enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana Bwana ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli.” Kumbuka watasikia kwamba Bwana anateta na watu Wake, Naye atahojiana na Israeli (watu 144,000, Israeli wa kweli). Lakini watasikiaje? Je! Ni ipi mbinu ya kuipeleka hiyo sauti kwenye milima na vilima? Jibu kwa hili linapatikana katika aya ya tisa. {SR1: 242.3}

“Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina lako: Isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiteua.” Mika 6:9. Kumbuka ni sauti ya Bwana. Sauti inalia ndani ya

243

“mji.” (Mji, au Yerusalemu ni nembo za kanisa la Mungu sawa na “mlima,” tofauti kati ya nembo hizo ni kwamba “mlima” humaanisha dhehebu lote, bali “mji” humaanisha sehemu inayoongoza ya mwili huo). Je! Ni kupitia mbinu gani sauti ya Bwana inalia ndani ya mji (kanisa)? Sehemu ya mwisho ya hiyo aya inalijibu swali: “Isikieni hiyo fimbo.” Ili kuisikia fimbo, lazima iwe ni ya namna ambayo huzungumza. {SR1: 242.4}

Fimbo pekee ambayo watu wa Mungu wamewahi kuulizwa kuisikia ni hii “Fimbo ya Mchungaji.” Wakati ule tulipokipatia kitabu hiki jina, hatukujua lolote kuhusu unabii katika kitabu cha Mika, wala hatukujua kifungu hiki kilikuwa humo. Tunamaanisha kusema si maarifa yetu yoyote katika andiko hili ambayo yalitulazimisha kukipatia kitabu hicho jina hilo, bali tunahisi ilifanywa kwa majaliwa yale yale ya Mungu ambayo yaliufunua ukweli wote, ili kutimiza andiko hilo. Tazama pia maelezo kwa ukurasa wa 95, chini ya kichwa “Fimbo ya Mchungaji.” {SR1: 243.1}

Tena, kumbuka “Mtu mwenye hekima ataliona jina lako.” Hekima iliyotajwa si ile ambayo ulimwengu unaweza kutoa, bali ya mbinguni. Toleo la Douay linasoma kama ifuatavyo: “Na wokovu [hekima] utakuwa kwa hao wanaolicha [wanaoliona] jina lako: sikieni, Enyi makabila.” Wazo lilo hilo limeletwa katika sura ya saba, aya ya 14. “Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao mwituni, katikati ya Karmeli. Na walishe katika Bashani na Gileadi, kama katika siku za zamani.” “Walishe watu wako kwa fimbo yako:” Kitenzi “walishe” kinapaswa kueleweka kama chakula cha kiroho, na chakula hicho (ukweli) hupatikana ndani ya “Fimbo,” kwa hivyo tumepewa amri ya kutoa kitabu (“Kulisha watu wako [wa Mungu]).” Karmeli, Bashani, na Gileadi hutumika kama nembo za malisho mazuri ya kiroho. Maeneo haya ndiko Israeli walipata ushindi wao. Mlima Karmeli ni mahali ambapo Eliya alipata uzoefu na Israeli iliyokengeuka katika siku za Ahabu. Ilikuwa huko Karmeli ambapo yeye (Eliya) aliushusha moto kutoka mbinguni ulioteketeza dhabihu juu ya madhabahu, baadaye hapo aliwachinja manabii wa Baali. {SR1: 243.2}

Tunanukuu Mika 7:15: “Kama katika siku zile za kutoka kwako

244

katika nchi ya Misri Nitamwonyesha mambo ya ajabu.” Kumbuka kwamba Mika na vile vile Isaya, hutangaza kwamba watu wa Mungu (Israeli ya kiroho) watapata uzoefu sawa na ule wa vuguvugu la Kutoka, kama lilivyoelezwa katika Sehemu ya 4. Tena, kumbuka katika kuliendesha vuguvugu la Kutoka, Mungu alimwambia Musa, “Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo utazifanya zile ishara … na Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.” Kut. 4:17, 20. Ilikuwa kwa uwezo ndani ya hiyo “fimbo ya Mungu” ya kwamba Israeli alitoka Misri. Vuguvugu hili la ujio likiwa ni nakala ya lile ndani ya Misri, na la Kutoka, tunayo tena “fimbo ya Mungu.” {SR1: 243.3}

Inashangaza kuona uvuvio wa Maandiko. Ni makamilifu wakati wake mwafaka ukiwa umekuja. Katika tukio kama hilo pekee Maandiko ni sahihi kisarufi. Hatuwezi kuzichambua hizo sura zote kwa wakati huu wa sasa, lakini kwa habari iliyotolewa tayari, mtu anaweza kuonyesha maana ya kila aya kwa juhudi kidogo ya kusoma kwa upande wake. Soma sura ya sita na ya saba na utambue kwamba wakati uliopita, wa sasa, na wa baadaye u katika mpangilio mkamilifu wa kisarufi wakati matukio hayo yanaeleweka vyema. Zingatia kanuni ile ile katika Mika sura ya nne kama ilivyoelezwa kwa ukurasa wa 173-81. Hii ni mojawapo wa sheria za kugundua ukweli wa sasa. Haingewezekana sisi kuchapisha ndani ya gombo hili nuru yote ambayo imekuja kwetu kupitia masomo haya, bali tunatarajia kwamba nayo hivi karibuni ndani ya gombo lingine. {SR1: 244.1}

245

Wajibu — Yeye Anayeupokea Ukweli

NI dhahiri kwamba ujumbe uliowasilishwa katika chapisho hili si ujumbe wa kubuni vuguvugu jipya, bali ujumbe wa badiliko kwa utauwa wa kweli. Kuwaita watu wa Mungu warejee kwa maagizo, amri, na kanuni Zake kwa kutii kabisa Neno Lake lituandae kukutana na Mungu wetu na kuokoka maangamizo. {SR1: 245.1}

Katika siku za Israeli ya kale, watu wa Mungu walikengeuka mara kadhaa kutoka kwa mpango Wake mtakatifu, ambapo ukengeufu huo ulifanya lazima Yeye atume jumbe za onyo kupitia kwa watumwa Wake, manabii. Maonyo hayo mazito hayakuzingatiwa hata kidogo na taifa hilo la zamani. Hata hivyo wale watumwa waaminifu wa Mungu walitekeleza wajibu wao kwa uangalifu mkubwa. Ingawa uhai wao ulikuwa hatarini, ujumbe wao wa upendo haukuthaminiwa, walinyanyaswa kikatili na watu waliokuwa wateule hapo awali. Watumwa hao waaminifu wa Mungu hawakuthubutu kuanzisha vuguvugu lao wenyewe. Jukumu lao lilikuwa kuwasilisha ujumbe, na kuyaacha matokeo kwake Yeye anayeweza kushughulikia hali hiyo. Ndivyo itakavyokuwa sasa. “Utakuwapo mfululizo wa matukio ya kufichua kwamba Mungu ndiye Bwana wa hali hiyo.” Gombo la 9, ukurasa wa 96. {SR1: 245.2}

Wale wanaoupokea ujumbe huu wanatakiwa kuamka watoke katika udhaifu wao wa kiroho hadi kwa toba ya kweli ya kiungu. Wanapaswa kuamka kimya kimya, lakini wazi wazi, ili wauwasilishe ukweli kwa ndugu na dada zao ndani ya kanisa, kwa bidii na kwa moyo katika kicho cha Bwana bila kutilia shaka lolote, wakimwachia Mungu matokeo. {SR1: 245.3}

“Ninapomwambia mtu mwovu, Ee mtu mwovu, hakika utakufa; nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo aiache njia yake, mtu mwovu huyo atakufa katika uovu wake; lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mwovu kwa sababu ya njia yake kusudi aiache, wala yeye asiiache njia yake, atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako. Na, wewe mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli ninyi mwasema hivi, kwamba, makosa yetu na dhambi zetu ni juu yetu, nasi tumedhoofika katika dhambi hizo, basi tungewezaje kuwa hai? Ezek. 33:8-10. {SR1: 245.4}

246

Roho ya Unabii, ikinena kwa kuzingatia matukio yaliyotabiriwa katika chapisho hili inasema, “Wale wanaotembea katika nuru wataziona ishara za hatari inayojongea; lakini hawapaswi kukaa kimya, bila kujali matarajio ya maangamizo, wakijifariji kwa imani kwamba Mungu atawakinga watu Wake katika siku ya kujiliwa. Pishia hilo mbali. Wanapaswa kutambua kwamba ni jukumu lao kufanya kazi kwa bidii kuwaokoa wengine, wakimtazamia Mungu katika imani thabiti awasaidie.” Gombo la 5, ukurasa 209. {SR1: 246.1}

“Piga kele usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. {SR1: 246.2}

Pingamizi Zinazoweza Kuzuka

Kwa sababu wote waliokuwa na ujumbe wa ukweli waliathirika kwa mateso katika vizazi vilivyopita, ni lazima itarajiwe hivyo sasa. Adui wa haki yote, kwa zana ya kibinadamu katika vazi la dini, amepinga ukweli wa Mungu katika kila hatua. Kifo cha Abeli kwa mikono katili ya kaka yake, Kaini, ilikuwa ishara kwa wafuasi wote wa ukweli kwamba mateso yangezuka dhidi yao kwa ndugu zao kanisani. Ndivyo, imekuwa hadi kwa siku yetu wenyewe. {SR1: 246.3}

Adui mjanja ana busara mno kutoupinga ukweli na mafundisho ambayo tayari yamekubaliwa kuwa ni ya kweli, lakini atawaongoza watu kupuuza kanuni ambazo ukweli huo ulijengwa juu yake, na hatua kwa hatua hujaza upungufu kwa hekima ya kibinadamu, na hivyo kuliongoza kanisa kuingia katika giza la kiroho. Wachungaji walio katika hali hii ya kiroho hawawezi kutambua umuhimu wa utiifu kamili kwa Neno la Mungu. Kundi lao hufanywa kuhisi kwamba uzoefu wao wa Kikristo ni bora, na watu wanaongozwa kuiamini hekima ya kibinadamu (kukubali uamuzi wao), badala ya kutafuta ukweli wao wenyewe, na imani kwa Mungu. “Bwana asema hivi; Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana.” Yer. 17:5. {SR1: 246.4}

Ushirika hupeanwa kwa wengi wote ambao hutaka kujiunga na kanisa lakini bila uchunguzi kuhusu imani yao na kupokea kwao kweli yote. Kwa njia hiyo, wasiojitoa wakfu hujipenyeza kanisani

247

na kwa ushawishi wao huwaongoza wengine kutenda dhambi. Mazoea haya endelevu huongeza haraka idadi ya wasio waaminifu, ilhali wafuasi wa Kristo waliojitolea hupungua na kupungua. Wakati nuru ya ukweli inakuja, na mwito wa matengenezo, viongozi, wakiwa wamepofushwa na giza la kiroho, huinuka dhidi ya mwito wa mbinguni. Wakitangaza kwamba wana ukweli wote, na hawahitaji wowote, ingawa ndani mioyoni mwao wanajua ni ukweli wa Mungu, wao hushutumu ujumbe na mjumbe kama Israeli ya zamani, kwa sababu hukemea matendo yao yasiyo ya kiungu. Wale ambao hawajatakaswa moyoni hawajali kufanya uchunguzi wenyewe, lakini huyakubali maamuzi ya viongozi. Tokeo lake ni kwamba waaminifu wachache hutupwa nje kwa njia ya kura nyingi, ilhali shetani mkongwe kwa shangwe hushinda. Hili ni kweli haswa katika wakati wetu, kuanzia kwa kanisa la Kilutheri, hadi juu ya mstari. William Miller na Binti Harmon walitendewa vivyo hivyo. Mungu aliruhusu zoezi hili la kuendelea kuwanyang’anya watu wa Mungu mali zao za kanisa, na kuwalazimisha kuanzisha vuguvugu jipya, lakini Yeye hatairuhusu hilo sasa. {SR1: 246.5}

Ikizungumza juu ya upinzani Luther alilazimika kuukabili, Roho ya Unabii husema, “Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu alipiga kelele dhidi ya dhambi zilizopo za viongozi wa kanisa; na alipokutana na dhoruba ya upinzani kutoka kwa makasisi, ujasiri wake haukukoma, kwa maana alitegemea mkono wenye nguvu wa Mungu, na kumtumaini Yeye kwa ushindi.” Maandishi ya Awali, ukurasa wa 223. “Kadiri upinzani unapozidi kuongezeka, watumwa wa Mungu wanafadhaika tena; maana wao wanaonekana kwamba ndio wameleta taabu. Lakini dhamiri na Neno la Mungu linawahakikishia kwamba mwenendo wao ni sawa ; na ijapokuwa mateso yanaendelea, wanaimarishwa kuyastahimili.” Pambano Kuu, ukurasa wa 610. Yesu alisema, “Heri ninyi, watakapowashutumu, na kuwatesa, na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili Yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni: kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.” Mat. 5:11, 12. Kumbuka:– Manabii waliteswa, na sio makuhani. {SR1: 247.1}

Ukweli unaposemwa katika manaeno wazi utafichua dhambi na kuihukumu

248

dhamiri ya mdhambi yenye hatia. Ingawa mjumbe, akiwa hatarini kwa mateso na dhihaka, hata kuhatarisha maisha yake, anautangaza ukweli kwa upendo wa kuokoa, mdhambi mara nyingi atainuka dhidi ya rafiki wa roho yake. Alisema nabii “Walakini, ukimwonya mtu mwovu kwa sababu ya njia yake kusudi aiache; wala yeye asiiache, atakufa huyo katika uovu wake; lakini wewe umejiokoa roho yako.” Ezek. 33:9. {SR1: 247.2}

Mashtaka yafuatayo yanaweza kuibuliwa na yanatarajiwa kukabiliwa. Wengine wanaweza kusema, Unanena mabaya, ukitafuta makosa, na unaleta lawama. Lakini hali ya mambo ni kwamba yule anayeupeleka ujumbe kutoka mbinguni hadi kwa mdhambi mwenye hatia hawezi kushtakiwa kwa lolote kati ya mashtaka yaliyotajwa hapo juu. Wajibu si wake yule anayeupeleka ujumbe, bali wa Mungu, anayeutuma ujumbe huo. Yeye anayesema maovu dhidi ya mjumbe ananena maovu dhidi ya Mungu kwa madhara yake mwenyewe. {SR1: 248.1}

Wengine wanaweza kusema, Haujateuliwa kwa ukasisi, na si kazi yako, lakini Yule aliye na ujumbe si lazima ateuliwe na kutiwa mikono ya watu ndiposa aupeleke ujumbe kuliko alivyofanya Amosi. Yeye ambaye hutuma ujumbe ni mkuu kuliko yule aliyeteuliwa na kuwekewa mikono ya wanadamu. Amosi alikuwa mchungaji tu, lakini Mungu alipomwita, na kumpa ujumbe wa kuwasilisha kwa wafalme na makuhani wa Israeli ya zamani, hakukataa bali alitii sauti ya Mungu na kuuwasilisha ujumbe. (Amosi 1:1). Je! Mungu amefungwa kwa kamba za wanadamu? Yeremia pia alikuwa mtoto tu wakati Mungu alimwita. Ingawa alijiona hakuwa na uwezo wa kulibeba hilo jukumu Bwana alisema, “Usiseme, mimi ni mtoto. Maana utakwenda kwa kila mtu Nitakayekutuma kwake nawe utasema kila neno Nitakalokuamuru.” Yer. 1:7. {SR1: 248.2}

Watu ambao hudhani kwamba ofisi yao huwaweka katika nafasi ya Musa na Haruni wanafanya kosa kubwa sana. Watu kama hao hawawezi kuwa aidha mmoja wao. Hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Musa kwa sababu hajafa wala kuwa bubu. Biblia ni Musa. Yesu alisema, “Wasipowasikia Musa na manabii.” Haruni ni mfano wa Kristo, kwa hivyo, yeye ambaye anafikiri yuko katika nafasi ya viongozi hao wakuu wawili anatupa kando mamlaka ya Biblia, na Kristo Kuhani. Yeye ambaye angeweza

249

kudai mamlaka kama hayo anajiweka mwenyewe katika nafasi ya Kora. Tazama Hesabu 16; na 26:10. Na kikomo chake kitakuwa mwisho mchungu. {SR1: 248.3}

Wapenzi Ndugu na dada:– Tunawasihi katika jina la Kristo Mwokozi wenu, mwe wakweli kwa Mungu kama watu Wake wakuu katika vizazi vilivyopita. Tunaitisha umakini wenu kwa Danieli, Shadraka, Meshaki, na Abednego. Fikiri jinsi watu hawa walivyosimamia kwa kanuni za kweli za kidini kumpendeza Mungu. Walihatarisha maisha yao, lakini wakakataa kuabudu sanamu. Jinsi Mungu alivyowapa thawabu kwa imani yao, Yeye atawathawabisha maisha ambayo yatakuwa sawa na maisha ya Mungu. Kataeni kujikwaa juu ya vikwazo vya wengine. Tunawarejeza kwa uzoefu wa Wakristo wa jina tu mwanzoni mwa vuguvugu la ujio, kama ulivyoandikwa katika maandishi na Roho ya Unabii. Tunanukuu kutoka katika Pambano Kuu, ukurasa wa 380: {SR1: 249.1}

“Lakini makanisa kwa ujumla hawakulipokea onyo hilo. Wachungaji wao, ambao kama ‘walinzi kwa nyumba ya Israeli,’ wangekuwa wa kwanza kutambua ishara za kuja kwa Yesu, walikuwa wameshindwa kujifunza ukweli, ama kutoka kwa ushuhuda wa manabii au kutoka kwa ishara za nyakati. Kadiri matumaini na matarajio ya ulimwengu yalivyoijaza mioyo, upendo kwa Mungu na imani katika neno Lake ilikuwa imepoa; na fundisho la ujio lilipowasilishwa, liliamsha tu chuki yao na kutoamini. Ukweli kwamba ujumbe huo, kwa kiwango kikubwa, ulitangazwa na walei, ulisisitizwa kama hoja dhidi yake. Kama zamani, ushuhuda wazi wa neno la Mungu ulikabiliwa na kuhoji, ‘Je! Yupo yeyote kati ya watawala au Mafarisayo aliyeamini?’ Na kwa kupata jinsi kazi ilivyokuwa ngumu ya kupinga hoja zilizotolewa kwa vipindi vya unabii, wengi walipinga kuuchambua unabii huo, wakifundisha kwamba vitabu vya unabii vilitiwa muhuri, na havingeweza kueleweka. Makutano, wakiwaamini kabisa wachungaji wao walikataa kulisikiliza onyo; na wengine, ingawa waliuamini ukweli, hawakuthubutu kukiri, wasije wakatupwa nje ya sinagogi.’ Ujumbe ambao Mungu alikuwa ametuma kwa ajili ya kulipima kanisa na kulitakasa, ulifunua kwa hakika umati jinsi ulivyokuwa mkubwa ambao ulikuwa umeweka upendo wao kwa ulimwengu huu badala ya Kristo.

250

Kamba ambazo ziliwafunga duniani zilikuwa na nguvu kuliko vivutio vya kwenda mbinguni. Walichagua kusikiliza sauti ya hekima ya kidunia, na wakakengeuka kwa ujumbe wa kujihoji wa kweli.” {SR1: 249.2}

Yesu alisema, “mkumbuke mke wa Lutu.” Kimbia kwa ajili ya maisha yako kwa sababu elementi zilizotumika Sodoma zitatumika katika ulimwengu huu mwovu wakati huu wa sasa. Linganisha ujumbe huu kwa Biblia na Shuhuda. Usikubali maamuzi ya wengine, bali jifunze mwenyewe. “Wakati ujumbe unawasilishwa kwa watu wa Mungu, hawapaswi kuinuka kwa upinzani dhidi yake; wanapaswa kwenda katika Biblia, wakiulinganisha kwa sheria na ushuhuda, na iwapo hautahimili kipimo hiki, si ukweli.” Shuhuda kwa Wachungaji, ukurasa wa 119. {SR1: 250.1}

Hakuna mtu anayepaswa kuogopa au kurudi nyuma kuutangaza ujumbe huu kuanzia kwenye mimbari ya Waadventista wa Sabato, maana ni fundisho safi la Waadventista wa Sabato, linalowaita watu wa Mungu warudi kwa kanuni ambazo dhehebu hili kubwa lilisimamishwa juu yake. Baadhi watalipinga na kujaribu kulizuia ilhali hawawezi kuyafafanua hayo Maandiko kwa njia nyingine. Lakini yule ambaye huuchukua mzigo wa kuupeleka ujumbe, lazima asisitize na kuwa mwaminifu kuendesha masomo yake. {SR1: 250.2}

Katika siku za Kristo wanafunzi Wake walisimama kidete kwa haki yao na kumtangaza Mwokozi aliyefufuka hekaluni. Waongozi waliopofushwa kiroho waliwaamuru watoke nje, lakini walirudi tena, na tena hili lilirudiwa, hata Mafarisayo makafiri walipowatupa gerezani. Kwa muujiza walitolewa nje na mara wakarudi hekaluni, na tena wakahubiri fundisho lililodhaniwa kuwa la kigeni licha ya upinzani. Uvumilivu kama huu wa kuwaokoa ndugu na dada zao kutoka kwa maangamizo yanayokaribia huitwa na maadui wa Kristo “uasi,” hata wakitumia Maandiko kuthibitisha shutuma zao kuwa za kweli. Lakini jambo la hakika ni kwamba, yule ambaye ni mvumilivu kutekeleza wajibu wake kwa Mungu wake, kwa wema wa ndugu zake, si ambaye anayo hatia. Yeye ambaye atachukia ujumbe kutoka mbinguni ni muasi mbele ya Mungu mkuu. Ofisi au cheo cha mtu kama huyo hakitamsafisha zaidi kuliko kilivyomsafisha yule Mfarisayo mwenye kiburi katika vazi la kirabi. Ingawa baadhi wanaweza kuonyesha kwa ofisi yake ya mamlaka haitampa udhuru, wala haitamhukumu mjumbe wa Mungu. Udhuru

251

mwingi na mashtaka mengine yatawasilishwa, lakini yule anayefanya utumishi wa Aliye juu hapaswi kukengeushwa kwa njia yoyote, bali asonge mbele katika jukumu lake na imani kwa Mungu ili awaokoe ndugu zake kutoka kwa adhabu inayokaribia. Roho ya Unabii, kwa mtazamo wa ujumbe huu husema: “Laiti kesi kama ya Akani ingekuwa kati yetu, wapo wengi ambao wangewashtaki wale ambao wangeweza kutenda sehemu ya Yoshua kusaka makosa, kwamba wanayo roho ya uovu, ya kutafuta makosa.” Gombo la 3, uk. 270. {SR1: 250.3}

Endapo jina la mtu fulani litaondolewa katika vitabu vya kanisa kwa ajili ya kuendeleza ujumbe, usivunjike moyo kwa njia yoyote ila songa mbele kana kwamba hakuna jambo lililotukia. Lipa zaka yako ya uaminifu na sadaka kwa kanisa lako, na ujihisi kama “NDIYO” nyumba ya Baba yako. Endelea na kazi yako ya matengenezo na wengi unaoweza kuwavutia. Ushirika wako kwa vitabu vya kanisa ni kumbukumbu tu ya kanisa na hasara au uharibifu pekee ambao mtu anaweza kupata kutokana na kutokuwepo kwa jina lake kwa rekodi hiyo ni kwamba hawezi kutumika kama afisa, au kusema lolote katika maswala ya shughuli ya kanisa. Wale ambao wanatazamia kuja kwa Kristo hivi karibuni hawataki kuhudumu ofisini, iwapo huduma yao haitakikani kwa kanisa. Wale ambao hujisukuma mbele kupata nafasi kama hiyo wao huonyesha nia yao kuwa mbaya, na ya kwamba mioyo yao sio sawa na Mungu. Kulihifadhi jina lako ndani ya kitabu cha kanisa kwa hasara ya kiwango cha Biblia hakutakupeleka mbinguni, wala kukosekana kwalo kwa kumbukumbu kama hiyo hakutakuzuia usiingie katika Mji Mtakatifu. {SR1: 251.1}

“Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu y alake aletaye habari njema, yeye aitangazaye amani; aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu; auambiaye Zayuni, Mungu wako anamiliki!” Isa. 52:7. {SR1: 251.2}

“Wengi wamejaribiwa kuhusiana na kazi yetu, na wanaitilia shaka. Wengine katika hali yao ya kujaribiwa wamezilaumu shuhuda za kukaripia ambazo tumewapa kwa matata na mafadhaiko ya watu wa Mungu. Wao hufikiri shida i kwa wale ambao huutangaza ujumbe wa onyo, ambao huonyesha dhambi za watu na kurekebisha makosa yao. Wengi wamedanganywa na adui wa

252

nafsi… Wao hudhani kwamba watu wa Mungu hawahitaji kushughulikiwa kwa uwazi na kukaripiwa, lakini ya kwamba Mungu yu pamoja nao… Je! Ni mtazamo gani hawa watafanya kwa ujumbe wa Shahidi wa Kweli kwa Walaodekia? Hapawezi kuwa na udanganyifu hapa. Ujumbe huu lazima utangazwe kwa kanisa la uvuguvugu na watumwa wa Mungu. Lazima uwaamshe watu Wake kutoka kwa usalama wao na udanganyifu hatari kuhusu wanavyosimama kwa uhalisi mbele ya Mungu. Ushuhuda huu ukipokelewa, utawaamsha kwa utendaji, na utaongoza kwa kujishusha nafsi na kuungama dhambi… {SR1: 251.3}

“Watu wa Mungu lazima waone makosa yao, na waamke kwa toba yenye bidii, na kuziondoa hizo dhambi ambazo zimewaweka katika hali ya kusikitisha ya umasikini, upofu, unyonge, na udanganyifu wa kutisha. Nalionyeshwa kwamba ushuhuda usiopinda lazima uwe hai kanisani. Hili pekee ndilo litajibu ujumbe kwa Walaodekia. Makosa lazima yakaripiwe, dhambi lazima iitwe dhambi, na uovu lazima ukabiliwe mara moja na kwa uamuzi, na uwekwe mbali kutoka kwetu kama watu.” Gombo la 3, ukurasa wa 258-260. {SR1: 252.1}

“Ondoka, uangaze;

Kwa kuwa nuru yako imekuja,

Na utukufu wa Bwana

Umekuzukia.

Isa 60:1.”

__________________

MWITO WA MAMA

Na Bi E. Hermanson.

“Lakini mtumwa yule mwovu akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyoijua, na atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki. Mat. 24:48-51. {SR1: 252.2}

Kama Waadventista, tunafundishwa kwa andiko lililo hapo juu kwamba halimaanishi tu kulewa divai, bali pia na ulafi. Tunaweza pia kulewa kwa masumbuko ya maisha haya. Tazama Luka 21:34. Andiko hili la mwisho hutuambia pia kwamba lazima tuwe wangalifu tusije wakati wowote

253

mioyo yetu ikalemewa na ulafi, na hivyo kuwa “yule mtumwa mwovu ambaye atasema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia.” {SR1: 252.3}

Nikiwa mshiriki wa dhehebu la Waadventista wa Sabato, na mama wa watoto watatu, nia yangu imekuwa ni kuwafundisha watoto hawa ambao Mungu amenipa katika njia ambayo wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu na kwa ukweli Wake. Ni mtihani mkubwa kuwazuia kushiriki kile kinachoitwa eti anasa za dunia, na kwa hivyo kutoka kwa roho ya ulimwengu, ili wasipotoshwe katika wazo lao la kile Mungu hutaka sisi tufanye kama watoto Wake waaminifu. Kazi sio rahisi, na jukumu sio la chini. Halijapunguzwa kwa vyovyote vile kwa kushiriki na wale wa ulimwengu. {SR1: 253.1}

Kwa mtazamo wa onyo tulilopewa katika Maandiko, haionekani kuwa sawa kwamba ratiba kama zifuatazo zinapaswa kufadhiliwa na kitivo iwapo tutawavutia watoto wetu na vijana katika mafundisho wazi, yasiyopinda ya Mwokozi wetu. Akili changa kwa kawaida hazifahamu upande mzito wa maisha, na kwa miadi na hafla nyingi ambazo huwekwa mbele yao daima kwa njia hii, hufanya kuwa vigumu kwao kupendezwa kujitahidi “kuingia kupitia mlango ulio mwembamba.” Luka 13:24; Mat. 7:13. {SR1: 253.2}

Zifuatazo ni baadhi ya hafla zilizonakiliwa kutoka “Matangazo ya kila Juma” chini ya tarehe 14 Novemba, na Novemba 21, 1930, na kutolewa na mojawapo wa taasisi zetu zinazoongoza huko Los Angeles. {SR1: 253.3}

Habari za Chama

Kitivo cha Kati ya wa Elimu ya Juu–Waliohitimu Awali Kukutana Kuogelea: … Jambo kuu la kutazamwa jioni lilikuwa maonyesho ya kupiga mbizi na Georgia Coleman, bingwa wa kitaifa kwa wanawake wa kupiga mbizi…. {SR1: 253.4}

Chama cha Karamu ya jioni Novemba: Hiki chaahidi lishe ya aina yake. Watatu-pamoja na msomaji kutoka chama cha Wanawake cha Glee cha U.S.C. atakuwa kivutio kikuu. Bill Hunter, Mkurugenzi wa Wanariadha wa U.S.C. atatusimulia machache juu ya michezo. Pata tiketi zako mapema. {SR1: 253.5}

Matukio Yajayo

Nov. 24: Chama cha Karamu ya jioni.{SR1: 253.6}

Nov. 25: Wadogo dhidi ya Wafanyakazi Mchezo wa Besiboli. {SR1: 253.7}

254

Nov. 28: Mashindano ya michezo ya Golfu Mechi itakuwa kwenye Montebello Park. {SR1: 254.1}

Desemba 2: Kitivo dhidi ya Watumishi Mchezo wa Besiboli. {SR1: 254.2}

Desemba 9: Kitivo dhidi ya Wadogo Mchezo wa Besiboli, saa 1:00. Wafanyakazi timu ya 1 dhidi ya Wafanyakazi timu ya 2, saa 11:00. {SR1: 254.3}

Desemba 16: Wakubwa dhidi ya Wadogo Mchezo wa Besiboli. {SR1: 254.4}

Desemba 21-26: Karamu ya Likizo ya kijumba melini, Ziwa la Dubu Mkubwa. {SR1: 254.5}

Hotuba ya Afya, Y.M.C.A., Ijumaa, saa 2:00 usiku. {SR1: 254.6}

Kitivo-Wenye elimu ya Juu Mechi Mchezo Golfu: Ijumaa asubuhi Novemba 28…. {SR1: 254.7}

Kitivo-wazima mchezo wa Besiboli Jumanne iliyopita ulisababisha alama 3-13. Hii, hata hivyo, haifai kwa hakika kuwakilisha u karibu wa shindano ikilinganishwa na makabiliano yaliyopita. Michezo michache zaidi na kitivo watakuwa wakishikilia yao wenyewe, hata hivyo, H____ S____ na W___ (hawatakawia mbio nyingi za nyumbani. H____ inashikilia rekodi hadi sasa …. {SR1: 254.8}

Roho ya Unabii, ikitoa maelezo juu ya besiboli, n.k. husema, “Naliambiwa na Mwelekezi wangu: ‘Angalia, na tazama ibada ya sanamu ya watu Wangu, ambao nimekuwa nikisema, na kuamka mapema, na kuwaonyesha hatari zao. Nikaona kwamba wangezaa matunda.’ Walikuwapo baadhi waliokuwa wakijitahidi kufanya kwa ustadi, kila mmoja akijaribu kumshinda mwingine kukimbia kwa kasi ya baiskeli zao. Palikuwa na roho ya ugomvi na ushindani kati yao kuhusu ni nani aliyepaswa kuwa mkuu zaidi. Roho ilikuwa sawa na ile iliyodhihirishwa katika michezo ya besiboli kwenye uwanja wa chuo. Akasema Mwongozi wangu: ‘Mambo haya ni makosa kwa Mungu. Kote karibu na mbali watu wanaangamia kwa ajili ya mkate wa uzima na maji ya wokovu.’” Gombo la 8, ukurasa 52. {SR1: 254.9}

Kwa nini kuwapeleka vijana kwa Y.M.C.A.? Je, haingewezekana hotuba ya afya ifanywe katika kanisa letu au kumbi za shule? Kwa nini mashindano ya Klabu ya Golfu asubuhi ya Ijumaa? Je! Hatukuambiwa katika Maandiko kuwa Ijumaa ni siku ya maandalio ya Sabato, si siku ya anasa? Kama sheria, iwapo mtu anafanya maandalizi mazuri, hakuna wakati mwingi wa kupoteza katika kucheza kitu chochote. {SR1: 254.10}

Hatuwezi kuwa na pingamizi kwa uogeleaji, lakini ni athari gani ya onyesho la ujuzi wa michezo ya ubingwa na majadiliano ya namna hii kuhusu “Michezo”

255

kwa vijana? Je, yatajenga ari kubwa ndani yao kumtumikia Kristo? {SR1: 254.11}

Tunawezaje kama kina mama kuwatunza watoto wetu mbali na ulimwengu iwapo kitivo cha shule kinawapeleka kwenye taasisi za kidunia ambamo wao hutupwa ndani ya mahusiano na machafuko mseto? Je, tunaishi kulingana na kanuni ambazo Dhehebu letu la Waadventista wa Sabato lilianzishwa? “Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba Nitakaa ndani yao, na kati yao Nitatembea; nami Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana.” 2 Kor. 6:16, 17. {SR1: 255.1}

Kwa mtazamo wa bubujiko hili la maji ya uasi likiongozwa na waelekezi wa kiroho waliopotoka, kwa tathmini yangu, mnyama kama chui wa Ufu. 13:1-3, amepata utimizo wa kushangaza zaidi wa unabii wa ile nembo — “dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Dunia kwa ujumla imekuwa ikimfuata mnyama yule. Kwa sababu hii ulimwengu unahitaji injili, lakini Mungu anapoitoa hiyo taarifa “dunia YOTE ikamstaajabia mnyama yule,” basi lazima iwe kwamba wale ambao Mungu amewapa nuru kubwa wameshiriki roho ya dunia, hivyo kuutimiza unabii huo. {SR1: 255.2}

Kuukumbuka wajibu wetu kwa ulimwengu na ujumbe wa malaika wa tatu hakika mzigo juu ya moyo wangu kwa ajili ya watoto na vijana ni mzito. Ninatoa mwito kwa kila Mwadventista wa Sabato mwaminifu aamke kwa sala na kufunga dhidi ya hizi zinazoitwa eti anasa za kizazi hiki, kuwaokoa watoto wetu wakati shetani anatafuta kuwadanganya yamkini hata walio wateule. {SR1: 255.3}

256

>