fbpx

Fimbo Ya Mchungaji Gombo La 2

Fimbo Ya Mchungaji Gombo La 2

3

FIMBO YA MCHUNGAJI

Gombo la 2

Na V. T. HOUTEFF

“Kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.” Mat. 13:52

4

FIMBO YA MCHUNGAJI

Kitabu, Gombo La 2

Hakimiliki, 1932

Na V.T. HOUTEFF

5

 

ORODHA YA CHATI

 

SIKU TATU MCHANA NA USIKU KATIKA MOYO

WA NCHI ……………………………………………………………………22

SANAMU YA DANIELI 2 ………………………………………………29

WANYAMA WANNE WA DANIELI 7 ………………………………..31

SIMBA WA DANIEL 7 …………………………………………………35

DUBU WA DANIELI 7 …………………………………………………37

CHUI WA DANIELI 7 …………………………………………………..39

MABAWA YA SIMBA YAKAKWANYULIWA, NAYE

AKAPEWA MOYO WA KIBINADAMU …………………………………44

BEBERU NA KONDOO MUME WA DANIELI 7 ……………………..51

MNYAMA DUBWANA KATIKA HATUA YAKE YA

KWANZA DANIEL 7:7 …………………………………………………57

MNYAMA DUBWANA KATIKA HATUA YAKE YA

PILI. DANIEL 7:8 …………………………………………………………..59

MWANAMKE NA JOKA LA UFUNUO 12 ……………………………64

MWANAMKE NA MABAWA YA TAI WA UFUNUO 12 ……………74

WANYAMA WA DANIELI NA UFUNUO …………………………….84

HISTORIA YA DUNIA KATIKA NEMBO ZA

BEBERU NA KONDOO DUME ……………………………………….128

KUANGAMIZWA KWA WANYAMA,

MAVUNO, NA MAPIGO ………………………………………………150

MIHURI SABA NA MAVUNO …………………………………………204

HISTORIA YA INJILI, MWITO WA SAA YA KUMI NA MOJA,

MATHAYO 20. HISTORIA YA INJILI …..………………………………224

GHARIKA — MFANO NA UAKISI ……………………………………250

MAHEKALU MAWILI KATIKA MFANO NA UAKISI ………………270

MTO MKUBWA WA EZEKIELI 47 ……………………………………294

6

FAHARISI YA SOMO

UTANGULIZI ……………………………………………………………..9

NI KWA JINSI GANI MAANDIKO YALITOLEWA? ………………….12

Dhambi Dhidi Ya Roho Mtakatifu Ni Nini? …..……………………….13

KUMTAMBULISHA KRISTO MWOKOZI WETU.

Siku Tatu Mchana Na Usiku Ndani Ya Moyo Wa Dunia………………..17

Maandalio Ya Pasaka ……………………………………………………20

Ratiba Kutoka Kwa Pasaka Hadi Kwa Ufufuo ………………………….23

UNABII WA DANIELI NA UFUNUO WA YOHANA

HUSHEHENI HISTORIA YA DUNIA ……………………………………..27

Nembo Ya Mabawa Na Mbavu ………………………………………….33

“Inuka Ule Nyama Tele” …………………………………………………42

Mabawa Ya Simba Yakakwanyuliwa …………………………………..42

Naye Akapewa Moyo Wa Kibinadamu …………………………………45

DUBU NA CHUI …………………………………………………………50

Beberu Na Kondoo Mume ………………………………………………53

Ufalme Wa Shaba Watawala Dunia …………………………………….53

MNYAMA DUBWANA. DAN. 7 ……………………………………….56

Juhudi Za Kusimamisha Serikali Za Kidini ……………………………56

JOKA JEKUNDU. Ufu. 12 ………………………………………………65

Vita Mbinguni …………………………………………………………..66

Wakati Lilipotupwa Nje …………………………………………………66

Pembe Na Vichwa Vya Joka ……………………………………………68

Vilemba Vya Joka ……………………………………………………….69

Mshitaki Wa Ndugu …………………………………………………….69

KANISA LA MUNGU KATIKA NEMBO YA

MWANAMKE. Ufu. 12 …………………………………………………….71

TAJI YENYE NYOTA KUMI NA MBILI KATIKA KIPINDI

CHA AGANO JIPYA ……………………………………………………….76

MNYAMA KAMA CHUI. Ufu. 13:1-10 …………………………………85

Vilemba Na Pembe ……………………………………………………87

Pembe Na Vichwa Vyote Vipo ………………………………………..88

Nembo Ya Vichwa ……….…………………………………………….88

Kichwa Kimoja Kikatiwa Jeraha La Mauti ……………………………96

Jeraha Lake La Mauti Likapona …………………………………………………..97

Dunia Yote Ikamstaajabia Mnyama Yule ………………………………98

Jina La Makufuru ………………………………………………………98

Kutenganisha Magugu Kutoka Kwa Ngano ………………………….101

Imani Ndani Ya Wanadamu Ni Mtego Hakika Wa Shetani ………….103

Muhtasari Mfupi Wa Mnyama Kama Chui …………………………..106

MNYAMA MWENYE PEMBE MBILI. Ufu. 13:11-18 ………………108

MNYAMA MWEKUNDU SANA. Ufu. 17 ……………………………111

MWANAMKE ALIYEKETI KWA “MNYAMA,”

KWA “VICHWA” NA KWA “MAJI MENGI.” Ufu. 17 …………………121

Ni Nani Mwanamke Aketiye Juu Ya Mnyama? ………………………121

Ni Kwa Muda Gani Mwanamke Amekuwapo? ………………………123

7

FAHARISI YA SOMO

PEMBE KUBWA SANA YA DAN. 8:9 ………………………………126

Mamlaka Ya Rumi Si Yake Wenyewe; Afahamuye Mafumbo ……….127

Pembe Hufichua Yale Ambayo Mnyama Hushindwa Kufichua ………129

Ikaliangusha Chini Jeshi Na Nyota ……………………………..129

Ya Kila Siku Na Patakatifu Pakaangushwa Chini ……………………..130

Kanisa Lilifanywa Vipi Kuwa La Upagani? ……………………..134

Jinsi Ibada Ya Sanamu Ilipenyeza Kanisani ……………………………136

MUHTASARI — Ile Pembe “Yatawala Dunia Yote” ………………….139

Sabato “Ilikanyagwa” Mara Moja Tu ………………………………….141

Ibada Maradufu Katika Vizazi Vyote ………………………………….142

MNYAMA (666), NABII WA UONGO, MAMA WA

MAKAHABA, MTU WA KUASI, WAO NI NANI? ……………………148

Kuangamizwa Kwa Yule Mnyama Na Nabii Wa Uongo ………………152

Kuangamizwa Kwa “Mtu Wa Kuasi” ………………………………….153

Mama Wa Makahaba Si Mnyama ………………………………………153

Wakati Wa Mwanamke Kuangamizwa …………………………………154

Nabii Wa Uongo Ni Nani? ……………………………………………..157

Mwanamke Ameketi Juu Ya Vichwa ……………………………………157

Mwanamke Ameketi Juu Ya Mnyama …………………………………158

Kikombe, Vito Vya Thamani, Na Rangi Za Kutazamisha ……………..159

MUHTASARI ………………………………………………………….160

WATU MIA NA AROBAINI NA NNE ELFU. Ufu. 7 Na 14 …………163

Watu 144,000 Watiwa Muhuri Wakiwa Ndani Ya Kanisa ……………163

Watumwa Wa Mungu Katika Wakati Wa Mavuno ……………………166

Je! Watu 144,000 Ni Wa Jinsia Zote? …………………………………167

MWISHONI MWA MLANGO WA REHEMA,

MAKABURI YANAKOMA — 14 NA 15 …………………………………170

SURA YA ISHIRINI NA NNE YA MATHAYO, NA

ISHARA ZA KUJA KWA KRISTO ………………………………………174

Zilikabidhiwa Kwa Dhehebu La S.D.A. ………………………………178

Wanawali Kumi–Mathayo 25 …………………………………………180

Muhtasari Wa Wanawali Kumi ………………………………………..185

MIHURI SABA NA HEKALU ………………………………………….187

Mpango Wa Ukombozi Ulitangulia Anguko ………………………….188

Je! Hekalu Ni Mahali Pa Milele Pa Kiti Cha Enzi Cha Mungu? ………188

Ki Wapi Kiti Cha Enzi Alichokiona Yohana? …………………………189

Hukumu Na Mihuri–Ufunuo Sura Ya 4 ……………………………….194

Bahari Ya Kioo …………………………………………………………198

Kukifungua Kile Kitabu ………………………………………………..200

Mihuri Kwa Vipindi–Ufunuo Sura Ya Sita ……………………………201

Maana Ya Farasi Na Wapanda Farasi ………………………………….202

Muhuri Wa Kwanza–Farasi Mweupe ………………………………….205

Mpanda Farasi Wa Kwanza …………………………………………….205

Muhuri Wa Pili–Farasi Mwekundu ……………………………………206

Mpanda Farasi Kwa Farasi Mwekundu …………………………………207

Muhuri Wa Tatu–Farasi Mweusi ………………………………………208

Mizani Mkononi Mwa Mpanda Farasi …………………………………209

Usiyadhuru Mafuta Wala Divai ………………………………………..210

Muhuri Wa Nne ………………………………………………………..211

Muhuri Wa Tano ……………………………………………………….212

Muhuri Wa Sita …………………………………………………………213

Muhuri Wa Saba, Ufunuo 8:1-5 ……………………………………….214

Matengenezo Kwa Mtazamo …………………………………………..219

Muhtasari Wa Mwanzo Na Mwisho Wa Mihuri …..…………………..221

8

NGANO NA SHAYIRI KILA MOJA KWA DINARI ………………….222

Majira Ya Saa Za Kale …………………………………………………225

Mwito Wa Mapema Asubuhi …………………………………………..226

Mwito Wa Pili Kwa Saa Ya Tatu ………………………………………227

Mwito Wa Saa Ya Sita Na Ya Tisa …………………………………….227

Mwito Wa Saa Ya Kumi Na Moja ……………………………………..229

Mbona Mmesimama Hapa Bila Kazi? …………………………………231

Wa Mwisho Watakuwa Wa Kwanza Na Wa Kwanza

Watakuwa Wa Mwisho …………………………………………………….233

Wape Ujira Wao ……………………………………………………….235

Mbona Mapema Asubuhi? …………………………………………….236

Mavuguvugu Saba Ya Dunia Yote ……………………………………236

Sababu Mbona Masaa Matatu Kwa Kila Vuguvugu …………………..237

MBONA KOSA LA MILLER; GHARIKA NI NINI KWETU? ……….240

Gharika Mfano Wa Maangamizo Ya Waovu ………………………….246

Gharika Hulingana Na Pasaka Na Kusulubishwa ……………………..254

Maana Ya Mwezi Wa Kwanza Na Wa Pili ……………………………256

Kaini Na Abeli …………………………………………………………257

HEKALU LA KWANZA NA LA PILI–MFANO

NA UAKISI ………………………………………………………………..259

Hekalu La Pili ………………………………………………………….259

Tofauti Sisisi Na Ya Kiroho Kati Ya Hayo Mahekalu Mawili ………..261

Hekalu La Kwanza Kihalisi Kubwa, Bali Kiroho Ni La Pili ………….262

Wakati Wa Kulijenga Hekalu La Uakisi (Kanisa) …………………….266

Amri Tatu Zilitolewa Kabla Ya Hekalu Kujengwa ……………………273

Shutuma Za Uongo Na Visingizio …………………………………….273

Pingamizi Dhidi Ya Ile Njia Mungu Anaweza Kutumia ………………275

Amri Ya Pili Ya Kulijenga “Hekalu” ………………………………….276

Amri Ya Tatu Ya Kulijenga “Hekalu” …………………………………278

Wakati Wa Kulisimamisha Kanisa La Kweli …………………………279

Nguvu Ya Watu Wa Mungu Kuijenga Nyumba Yake ………………..280

Tokeo La Utiifu Kwa Neno La Mungu ……………………………….281

ZEKARIA 4 …………………………………………………………….283

Mabomba Mawili Ya Dhahabu …………………………………………285

Taa Saba ………………………………………………………………285

Mirija Saba Ya Dhahabu ………………………………………………285

Ni Nini Kilichovuviwa Na Ambacho Hakijavuviwa? …………………287

MTO WA MAONO YA EZEKIELI ……………………………………290

Ezekieli 47 …………………………………………………………….291

KUHESABIWA HAKI KWA IMANI; NI NINI? ……………………..299

9

UTANGULIZI

Kitabu hiki hakijachapishwa kufafanua, au kutoa maelezo kwa kweli ambazo zilifunuliwa awali, na kupokelewa hivyo, bali kitafichua hali halisi ambazo Mungu amehifadhi kwa vizazi vingi, si tu ili zisije zikatoweka, bali pia kuzuia maana yake isigunduliwe na watu wa hekima. Hivyo basi, Yule ambaye huyadhibiti Maandiko ana uwezo wa kufunua ukweli wa sasa kwa watu Wake katika wakati ambao unahitajika. Kwa hivyo, ingawa kweli kama hizo mwanzoni ni za kinabii, zinakuwa mpya, na husimama kama barua ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu kwa watu katika wakati zinapofunuliwa. “Mungu Bwana anena… Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, Nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.” (Isa. 42:5,9.) Hivyo, zitathibitisha yaliyomo katika chapisho hili kuwa mapya, ya kupendeza, ya kuelimisha, ya kuvuvia, na ya kuongoa. Ujumbe ambao linabeba ukifundishwa kwa nembo na mifano iliyoelezwa kwa njia ya chati, inakuwa rahisi, na wote ambao wanautafuta ukweli wakiwa na nia ya kuwa wanaofaa kwa ghala la mbinguni, wanaweza kuuelewa kwa urahisi. {SR2: 9.1}

Kitabu cha “Ufunuo” husemekana kwamba ni kitabu ambacho kimefungwa kilichojawa na nembo za ajabu, zisizoeleweka kwa wanadamu. Hili ni kweli kwa vitabu vyote vya kinabii. Yule ambaye hukiri ukweli huu kwa kitabu cha “Ufunuo,” moja kwa moja hukiri kwamba haelewi Biblia, kwa maana vitabu vyote vya Maandiko Matakatifu hukutana na kuhitimika katika “Ufunuo.” Hivyo basi, kukielewa kitabu hicho ni kuielewa Biblia. “Yule ambaye huzifunua hizo siri kwa Yohana atampa mchunguzi wa ukweli mwenye bidii mwonjo wa kimbele wa mambo ya Mbinguni. Wale ambao mioyo yao i wazi kwa kuupokea ukweli watawezeshwa kuelewa mafundisho yake, na watapewa baraka iliyoahidiwa kwa wale ‘wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo.’” — “Matendo ya Mitume.” uk. 584,585. Hivyo, Ufunuo ukieleweka, utafunua Ghala kuu na kuleta nuruni siri zote za kinabii zilizohifadhiwa mle ndani. {SR2: 9.2}

Ujumbe katika gombo hili uliratibiwa kinabii utimizwe kwa mfano wa “Mwenye nyumba” aliyewaajiri watumwa katika shamba Lake la “mizabibu.” (Mat. 20:1-16). Kuthibitisha kwamba ni “mwito” wa “saa ya 11,” — wa mwisho, na kwa wakati mwafaka. Uhakika kwamba ufunuo huu wa ajabu wa Maandiko hauwezi kupingwa, huthibitisha huo ujumbe kuwa sahihi, na uvuvio wake kuwa wa kweli. Mwito huu wa kinabii umejikita kwa unabii wa Danieli, na maelezo yake yanafanywa wazi

10

na kitabu cha Ufunuo. Hivyo, unafafanuliwa kwa njia ya mifano. Nembo hizi za kinabii za wanyama, mabawa, pembe, vichwa, n.k., huthibitisha kwamba ni nembo kamilifu sana katika kufunua ukweli unaowakilishwa nazo na zinapotumika kwa usahihi ni hakika kwamba maana yazo haiwezi kupotoshwa. {SR2: 9.3}

Jinsi ambavyo mchafuko wa sasa na kutoyaelewa Maandiko miongoni mwa Wakristo unathibitishwa na kuzidishwa kwa madhehebu, ni dhahiri kwamba makanisa yako katika hali ya Ulaodekia: “Nyonge, na yenye mashaka, na maskini, na ya upofu, na uchi.” Na kwa kukana shtaka la taarifa hii iliyo wazi huthibitisha maneno ya “Shahidi wa Kweli” kuwa sahihi, “nawe hujui.” Wakifikiri wako sawa, “Shahidi wa Kweli” anatangaza: “Umekosea kabisa.” Ni udanganyifu mkubwa ulioje kuliko huu? (Soma Ufu. 3:14-18). Kwa sababu Biblia husema wazi kwamba ni “kweli” ambayo itatuweka “huru,” hatuwezi kujichunguza kwa ukaribu na yale mambo tunayoyaamini, kwa maana iwapo hamna makundi mawili kati ya madhehebu mengi ya Ukristo yanaamini sawa, ni dhahiri kwamba mengi, ikiwa si yote, ni yenye upofu. Na kwa sababu Biblia i sawa katika maneno: “Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili,” hivyo basi itakuwa bure kupinga ukweli — dunia yaelekea “shimoni.” Je, taarifa hii isiyopingika haitaweza kuwaamsha wanaodai kuwa ni watu wa Mungu waache kusinzia na kulala kwao? Uzoefu wa zamani huthibitisha kwamba wengi watasema, “Si mimi.” Akifahamu kwamba udanganyifu huu ungeinuka katika siku za mwisho, Mungu amebuni uwakilishi huu wa ukweli kwa njia ya picha, ambao kwa huo Yeye anaweza kulielimisha kanisa Lake na kuwaita watu Wake. {SR2: 10.1}

Wakati adui amefanikiwa katika kulipotosha Neno lililoandikwa, Mungu anaiang’aza nchi kwa utukufu wake kutumia mafunuo haya ya nembo; na kwayo Yeye hufichua ukweli wote na kuweka wazi mitego ya ibilisi! Hivyo kupitia kwa mifano na nembo Yeye huwafanya wanyenyekevu kuwa wenye hekima na kuwaaibisha wenye akili kwa kuonyesha kwamba pale ambapo hakuna mfano hapawezi kuwapo ukweli. {SR2: 10.2}

Gombo hili linasheheni ufunuo mkamilifu wa nembo za historia yote ya ulimwengu, ya serikali za kiraia na ya kidini. Sababu ambayo maajabu haya yalichorwa kwa njia ya nembo ni sawa na ile ambayo ilisababisha Kristo kufundisha kwa mifano. “Wakaja wanafunzi, wakamwambia [Kristo], Kwa nini wasema nao kwa mifano? Akajibu, akawaambia, kwa maana ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.” (Mat. 13:10, 11). “Bali waovu watatenda maovu: wala hataelewa mtu mwovu awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” (Dan. 12:10.) “Sababu kuu ya kufunza kwa mifano ni ili ukweli uweze kufunuliwa kwa wana wa Mungu na wakati uo huo ufichwe kutoka kwa adui zake… Kwa sababu ii hii unabii ambao ulielezea zile tawala

11

kuu dhidi ya wakristo na kazi yao mpaka mwisho wa wakati ulipaswa uvikwe katika lugha ya nembo na mifano ili kukinga uhifadhi wake.” Lesoni ya Shule ya Sabato Robo Mwaka,” uk. 33, robo ya pili, 1932. “Kristo alikuwa msingi wa uchumi wa Kiyahudi. Mfumo wote wa mifano na nembo ulikuwa unabii ulioshindiliwa wa injili, utoaji ambao ulikuwa umefungiwa ahadi za ukombozi.” — “Matendo ya Mitume, “ uk. 14. {SR2: 10.3}

Kila moja ya mada hizi zinaweza kufafanuliwa pakubwa, ila tungalifanya hivyo, gombo hili lingekuwa kubwa sana, pia lisilokuwa la kina. Hivyo tumeacha maelezo mengi. {SR2: 11.1}

(Herufi Nzito Zote Ni Zetu.)

MWANDISHI

12

NI KWA JINSI GANI MAANDIKO YALITOLEWA?

JINSI MUNGU HUNENA NASI

“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, siku hizi za mwisho amenena na sisi katika Mwana wake.” (Ebr. 1:1.) Bwana akamwita Abrahamu kwa sauti Yake. Pia Alizungumza naye kupitia kwa malaika, ndoto. (Mwanzo 12:1; 15:12,13; 17:1-6; 18:1-22). Yakobo alikuwa na uzoefu sawa. (Tazama Mwanzo 28:12; 32:1, 2). Aliye mkuu MIMI NIKO alinena na mtumwa wake Musa kutoka kwa kichaka kilichokuwa kinawaka moto. (Kut. 3:1-10). Israeli walisikia sauti ya Mungu kutoka kwenye wingu juu ya mlima Sinai. (Kut. 20:18,19.) Amri kumi “ziliandikwa kwa chanda cha Mungu.” (Kut. 31:18.) Farao mfalme wa Misri na Nebukadnezza mfalme wa Babeli welipewa ndoto, lakini Roho wa Mungu, kupitia kwa Yusufu na Danieli walifunua siri hizo. (Mwa. 41:28-36; Dan. 2:19). Daudi na Suleimani waliandika Zaburi na Mithali, si kwa njozi, ndoto au malaika, bali kwa sauti nyamavu ya Roho wa Mungu iliyopigwa chapa akilini mwa watumwa Wake. Mungu alinena kwa Esta na Ruthu kwa uzoefu kupitia kwa maongozi ya uungu. Yohana alipokea “Ufunuo” kwa njozi. Mungu hunena nasi pia kwa mifano na uakisi — kupitia katika sheria za sherehe, kupitia kwa wazee wa imani na kwa uzoefu wa Israeli ya zamani. (Tazama Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, uk. 223-235.) {SR2: 12.1}

Mungu alitumia wafu na walio hai, wanyama wa kondeni, ndege wa angani, samaki wa baharini, ardhi na maji, jua, mwezi, na nyota, kufunua mpango Wake wa uungu na kuwadumisha watumwa wake, n.k. (Tazama Mwa. 16:7, 9; 1 Sam. 6:7-15; Hes. 22:30; 1 Wafalme 17:4-6; Yona 2:10; Mat. 17:27; Hes. 16:32; Mat. 24:29.) Mungu anazo njia elfu ambazo anaweza kutumia kutoa msaada kwa nukta. Kwa kweli, ni lipi zaidi ambalo upendo wa Mungu ungefanya kwa wanadamu walioanguka? {SR2: 12.2}

Maandiko Hufunuliwa Vipi, Na Kufasiriwa Vyema?

Uchanganuzi wa historia ya zamani na ya sasa, zote takatifu na ya kidunia, huthibitisha kwamba ukweli uliotiwa muhuri, au ukweli wa kinabii haujawahi kufunuliwa kupitia kwa mfumo wa elimu ya dunia, au kwa hekima ya mwanadamu, ila tu kwa uwezo wa Mungu. Iwapo kitu chochote ni kweli, ni kitu hiki kimoja. Kasema Yesu: “Wakati Yeye, Roho wa Kweli, Atakapokuja, Atawaongoza awatie kwenye kweli yote.” (Yohana 16:13). Kristo wazi wazi hutangaza, kwamba tunaongozwa katika kweli, si kwa hekima ya mwanadamu bali kwa Roho wa Mungu. Si katika sehemu ya ukweli, ila katika kweli

13

yote. Wakati Mungu anafunua ukweli, Anaweza kuwaongoza watumwa Wake katika kweli yote, hawezi kuruhusu vyombo kama hivyo kuchanganya ukweli Wake na uongo. Ingawa wanaweza kuwa wasielewe yote, bado ujumbe ambao wanaubeba ni ukweli na si kitu bali ukweli. Hivyo basi, kweli hizo kiasili hufunuliwa na uvuvio pekee. Wakati ambao umeteuliwa na Mungu kutimika, wakati huo Mungu huwaita watumwa Anaohiari, na kwa Roho wa Kweli hufunua sehemu ya Neno Lake kwao. Kwa kawaida kwa njia ya ujumbe ambao lazima kwanza waupeleke kanisani. {SR2: 12.3}

Kwa uwezo sawa Mungu aliwavuvia watumwa Wake wengi, manabii, kila mmoja akiandika sehemu ya Biblia, na zilipounganishwa zikafanya kitabu kamili, kinachoshughulikia mada moja kuu — wokovu ndani ya Kristo. Ingawa baadhi ya waandishi hawa waliishi wakitengana mamia ya miaka kati yao, bado kila sehemu ya Maandiko huwiana kwa ukamilifu, — moja ikitupa nuru kwa nyingine. Hivyo huthibitisha kwamba Mungu ndiye alikuwa msimamizi wa Maandiko na kwa ustadi aliwaongoza watumwa Wake katika kweli yote. {SR2: 13.1}

Dhambi Dhidi Ya Roho Mtakatifu, Ni Nini?

Kwa sababu Biblia haina makosa, vivyo hivyo ufasiri wake chini ya Roho yuleyule wa Uvuvio lazima pia uwe sahihi. Kwa hivyo, ufasiri wa Biblia ni kweli, wakati tu umefunuliwa kupitia mkondo wa uvuvio. Hamna njia nyingine ambayo Mungu anaweza kuwaongoza watu Wake katika kweli yote. Chochote kipungufu kwa hili hakiwezi kufunua kweli ya Biblia, ijapokuwa ilivyo rahisi. Akasema Malaika kwa Danieli, “Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika Maandiko ya kweli: wala hapana anisaidiaye juu ya mambo haya, ila Mikaeli, mkuu wenu.” (Dan. 10:21.) Mojawapo wa vipawa kwa kanisa katika Kipindi cha Ukristo, ni “manabii.” “Naye alitoa wengine kuwa, mitume; na wengine manabii.” (Efe. 4:11.) {SR2: 13.2}

Paulo, tena hutangaza kuhusu Maandiko katika wakati wake na baadaye: “Hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine, kama walivyofunuliwa Mitume Wake watakatifu na Manabii zamani hizi katika Roho.” (Efe. 3:5). Wakati ukweli wa Maandiko umewasilishwa na watumwa wa Mungu, “barua” inaweza kueleweka kwa wote wanaoichambua; Lakini Roho yuleyule huhitajika ili kutia muhuri, kubadili moyo, na kuziongoza hatua katika upya wa maisha. Uwezo huu wa kubadilisha unapeanwa tu wakati mpokeaji wa ukweli kwa unyenyekevu hutubu kutoka dhambini, anaukana ulimwengu na kumpokea Kristo. Wakati ujumbe kama huo umewasilishwa, wale ambao humpinga mjumbe na kupinga ukweli, humkataa Roho, na kutenda dhambi dhidi Yake. Roho ndani ya ujumbe ndiyo njia pekee ya kuamsha dhamiri. Anapotendewa uasi, mdhambi hujikata kutika kwa mkondo ambao Mungu hutumia kufanya mawasiliano. “Kwa sababu hiyo

14

Nawaambia, kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu: ila kwa kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa. Na mtu ye yote atakayenena neno dhidi ya Mwana wa Adamu, atasamehewa; bali yeye atakayenena neno dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” (Matt. 12:31, 32.) {SR2: 13.3}

Ulimwengu wa kabla ya gharika ulitenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuamini katika ujumbe wa kweli uliotumwa kuwaokoa kutoka kwa gharika ya kutisha. Kwa hivyo, waliangamia katika dhambi ambayo kamwe hawatasamehewa. Lilo hilo ni kweli wakati mtu anaasi dhidi ya ujumbe wa Mungu katika kizazi chochote. Watu hawahukumiwi kwa sababu wametenda dhambi, bali wanahukumiwa wakati ambapo wanatia sikio nta kwa mwito wa Mungu ambao ungewaokoa kutoka kwa dhambi zao. {SR2: 14.1}

Kwa sababu kweli zote za kinabii hufunuliwa kwa wakati mwafaka, ni dhahiri kwamba hakuwezi kuwapo lolote linaloweza kufunuliwa kwa hekima ya mwanadamu, haijalishi ni rahisi kama nini. Wakati Mungu anafunua sehemu ya neno Lake takatifu kupitia kimojawapo cha vyombo Vyake viteule, uchanganuzi wa historia huthibitisha kwamba wao kamwe hawapotoki kulingana na ujumbe ambao wanautoa. Pia ni kweli kwamba wale ambao walikosea katika ujumbe wao uliodhaniwa kuwa wa kweli, hawakuwa na ukweli. Basi Mtume mkuu asema: “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho Wake: Maana Roho huchunguza yote, naam, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu, ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea, roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho Mtakatifu; tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu: maana kwake huyo ni upuzi: wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” (1 Kor. 2:10-14). Kwa hivyo, wakati ujumbe unatangazwa, aidha ni ukweli mtupu au hakuna ukweli ndani yake, isipokuwa nukuu za manabii.{SR2: 14.2}

“Bado ukweli kwamba Mungu ameyafunua mapenzi Yake kwa wanadamu kupitia kwa Neno Lake, hajafanya kusiwe na hitaji la uwepo na uongozi endelevu wa ROHO MTAKATIFU. Kinyume na hilo, Roho aliahidiwa na Mwokozi wetu, kuwafunulia watumwa Wake Neno, kuangaza na kuyatekeleza mafunzo yake. Na kwa sababu alikuwa Roho wa Mungu ambaye alivuvia Biblia, haiwezekani kwamba mafunzo ya yule Roho kamwe yanaweza kuwa kinyume na yale ya Neno” — “Pambano Kuu,” uk. VII. {SR2: 14.3}

15

Wale ambao wana mwelekeo wa kutilia shaka uwezo wa Mungu kumwongoza mtu katika kweli yote, hawakani tu pasi na ufahamu uaminifu wa Neno Lake, bali pia hupunguza nguvu zake kwa tendo lao, na hivyo “Wamemwekea mpaka Mtakatifu wa Israeli.” (Zab. 78:41). {SR2: 15.1}

“Roho wa Mungu hakutolewa – wala kamwe hawezi kupeanwa – kuchukua nafasi ya Biblia; kwa maana Maandiko hutaja wazi wazi kwamba Neno la Mungu ndilo kipimo ambacho kwacho mafundisho yote na uzoefu wote lazima upimwe. Asema mtume Yohana, ‘Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu: kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.’ (1 Yohana 4:1). Na Isaya atangaza, ‘Na waende kwa sheria na ushuhuda, ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.’ (Isa. 8:20).” — “Pambano Kuu,” uk. VII. {SR2: 15.2}

“Jina ‘nabii’ jinsi linavyotumika katika Biblia… hufanya kazi kuwataja wanaume na wanawake wanaohusika katika utumishi mpana kuhusiana na kazi ya Mungu. Baadhi yao kamwe hawakutamka unabii jinsi jina hilo linavyoeleweka kwa kawaida … Baadhi walitumika tu kwa tukio maalum, wengine kwa mfululizo mrefu wa miaka. Baadhi waliandika ujumbe ambao Mungu aliwafunulia, na wwengine waliutoa kwa njia ya kunena. Kwa wengine, kama katika kisa cha Danieli na wengine, walikabidhiwa unabii uliofika katika upeo wa siku za baadaye, sehemu ambazo bado hazijatimizwa.

“Wengine walikuwa wajumbe wa Mungu walioinuliwa katika vipindi vya hatari kuu, kuonya kanisa na ulimwengu kuhusu hukumu za kutisha, na kuwaita watu warudi kuwa watiifu kwa Mungu. Kama hao walikuwa Samweli, Eliya, Yohana Mbatizaji, na wengine. Yohana alikataa dai la jina la kinabii, akadai badala yake kwamba alikuwa sauti au mjumbe wa Mungu, aliyetumwa kuitayarisha njia ya Bwana katika kuwaita Israeli kwa toba. Lakini kama mjoli wa Mungu alitangazwa na Yesu kuwa nabii, na ‘hata zaidi ya nabii.’ Luka 7:26. ‘Hakika Bwana hatafanya neno lo lote, bali Yeye huwafunulia watumishi Wake manabii siri Zake.’ Amosi 3:7.” — “Ukweli wa Sasa,” Gombo la 5, Na. 72. {SR2: 15.3,4}

“Katika maana ya upeo nabii ni yule aliyenena katika uvuvio wa moja kwa moja, akiwasilisha kwa watu jumbe ambazo alikuwa amepokea kutoka kwa Mungu. Lakini pia jina hilo lilipeanwa kwa wale ambao, ingawa hawakuwa wamevuviwa hivyo moja kwa moja, walikuwa wameitwa na Mungu kuwaelimisha watu katika kazi na njia za Mungu.” — “Elimu,” uk. 46. {SR2: 15.5}

Hawa wajumbe wa mbingu kwa kawaida ni wanaume na wanawake wenye tabia ya unyenyekevu; wengine hata hawangeweza kusoma wala kuandika. Ingawa hawakuwa na manufaa ambayo watu wakuu huwa nayo, hivi vyombo mikononi mwa Mwenye uwezo wote, vilisababisha maarifa ya kibinadamu na ukuu wa ulimwengu kuzama usiwe na maana. Hivyo

16

Mungu alitafuta kwa mbinu hizi kudhiririsha uwezo Wake unaobadilisha katika mtambo wa mwanadamu katika akili na tabia. Kuasi dhidi ya vyombo viteule vya Mungu ni kukana uwezo Wake na kupendelea ule wa mwanadamu, kumweka mfaji juu ya wa milele, ambaye anaweza kusambaza maarifa zaidi kwa sekunde moja, kuliko mwanadamu anavyoweza kufanya katika maisha yake yote. {SR2: 15.6}

Ijapokuwa kweli zinafunuliwa kupitia mikondo iliyovuviwa, chombo cha uovu mara kwa mara kimezichanganya na uongo. Watendakazi wa uovu kama hao mara nyingi hukimbilia kutumia sehemu za ufunuo wa Mungu, kuzitumia kwa njia isiyo halali kama kabari ya kuingilia ili kupitisha upotovu na hivyo kuwadanganya wasio dhabiti. Yeyote asije akajidanganya kwamba anaweza kukwepa utumwa wa ibilisi kwa jitihada za kujifunza za mwingine. Kila mmoja lazima ajifunze mwenyewe kuelewa msimamo wake mwenyewe, na kwa akili za uelekevu awe tayari kuwasikiza wote na roho inayoweza kufunzwa ya mtoto. “Amin, Nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.” (Marko 10:15.) Chuki, imewalaghai wengi na kuharibu nafsi nyingi zaidi ya mtego wowote ule ambao umebuniwa na yule mdanganyifu mkuu. Yule ambaye hukataa kusikia sababu ambazo zinapeanwa na mwingine, ndiye mjinga zaidi. Mtu kama huyo kwa kawaida huchukizwa kwa sababu hoja iliyowasilishwa hukinzana na mtazamo wake wa mada hiyo, au inaweza kuwa kwamba hujiona kuwa msomi zaidi au mwenye hadhi ya juu zaidi cha kijamii. Wengine hawatausikia ukweli kwa maana huumiza dhamiri zao za dhambi na kwa kuogopa kwamba lazima wajitenge kutoka kwa tamaa fulani ya ubinafsi. Kikundi hiki ki chini ya nguvu ya ibilisi, na njiani kwenda maangamizo ya milele — kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. Wale ambao ni waaminifu katika makosa yao ndio wale haswa ambao hupatikana chini kabisa ya mkoba wa ibilisi wa utekaji nyara. Kundi hili ndilo gumu Zaidi kushawishi kwamba wamo njiani kwenda jahanamu. {SR2: 16.1}

17

KUMTAMBULISHA KRISTO MWOKOZI WETU

SIKU TATU MCHANA NA USIKU NDANI YA MOYO WA NCHI

Swali kwamba ni kwa muda upi Kristo alisalia kaburini, na siku ambayo Alizikwa na kufufuka, limejadiliwa kwa mapana kama vile tu mada nyingine yoyote ya Biblia. Idadi ya nadharia zimeendelezwa na bila shaka muda wenye thamani kubwa umebadhiriwa, lakini, mkanganyiko juu ya mada hii haujapungua, lakini badala yake umeongezeka. {SR2: 17.1}

Mtu fulani ameuliza, “Je hilo lina nini kuhusu wokovu wetu?” Inawezekani lisiwe na uzito kwa wokovu wa baadhi, ila yaonekana kwamba kwa wengine lina kiasi kikubwa kuuhusu. Dada fulani alisema: “Naamini yote ambayo Dhehebu la S—- hufundisha, lakini siwezi kukubaliana na msimamo ambao dada W—- hushikilia kuhusu mada ya kuzikwa na kufufuka kwa Kristo. Najua kwamba Kristo alikuwa siku tatu mchana na usiku ndani ya kaburi, ila dada W—- hushikilia Alizikwa Ijumaa jioni na akafufuka Jumapili asubuhi. Kwa hivyo, siwezi kuamini katika maandiko yake yote, na kwa sababu hii sijakuwa, na sitakuwa, mshiriki wa kanisa lako.” {SR2: 17.2}

Kutolielewa swali hili kumemzuia huyu dada kutojiunga na kanisa. Sasa, ikiwa kanisa hilo hasa lina ukweli kwa ulimwengu katika wakati huu, na kutoelewa kwa huyu dada kumemzuia asije akaikubali, basi lazima tukubali kwamba mada hii ambayo imejadiliwa kwa mapana ina jambo fulani kuhusu wokovu wa watu fulani, kusema machache kabisa. {SR2: 17.3}

Kristo alisema: “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa: kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye hupata; naye abishaye atafunguliwa.” {SR2: 17.4}

Pasingekuwapo kitu kinachompendeza Mungu zaidi kuliko mmoja wa watoto Wake kuomba kwa imani njia ya kweli. Iwapo ipo nguvu katika maneno ya Kristo, basi hakika yeye anayetamani kujua ukweli na anayetaka kuutii, ingawa unaweza kudai kwamba auze na kuwapa maskini, aukane ulimwengu na vishawishi vyake vyote, haitawezekana kwa nafsi hiyo kusalia gizani. Hebu mtafuta kweli afanye kiapo kama hicho kwa Mungu na hivyo ajaribu uwezo na ahadi Zake zisizoshindwa kamwe

18

kupitia kwa maneno ya Mwana Wake. Ila ingawa inawezekana kuwadanganya wanadamu, kamwe hatuwezi kumshurutisha Mungu. Yeye anajua kilicho moyoni. {SR2: 17.5}

Mojawapo ya sababu kuu za kuzuka mchafuko kati ya wanafunzi wa Biblia ni kwa sababu hawaamini kabisa katika usemi wa yale maneno ya Biblia. Wao hufikiri ni wenye hekima kuliko manabii ambao walivuviwa na Roho wa Mungu, na hivyo hutamani kusahihisha maneno na maana ya Biblia Takatifu! Hivyo wafaji wamejaribu kumrekebisha na kumkosoa Asiye na Mwisho, ambaye hekima Yake, uwezo, na maono hayatafitiki! Hata kama wanajua ufasiri wao wa andiko hauwiani hasa na maudhui yote ya kile kitabu na sheria, hawaoni maafa, na hawamchi Mungu. Na ukweli unapofunuliwa wao hukataa kubadili uongo kwa ukweli kwa maana hukinzana na thiolojia yao potovu. Tunaalika uangalifu wenye makini wa msomi kwa mada hii na ya kwamba azingatie uwiano wa ajabu wa Maandiko na hekima kuu iliyotumika ndani yake. {SR2: 18.1}

Yule dada aliulizwa: “Ushahidi wako u wapi kwamba Kristo alikuwa siku tatu mchana na usiku kaburini?” “Jibu langu ni,” alisema, “katika Mathayo 12:40, ‘Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.’” Tena aliulizwa, “Ni siku gani unadhani Kristo alikufa?” Akasema, “Yohana 19:31 lina jibu: ‘Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya Sabato, (maana Sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe.’” Hapa alieleza kwamba haikuwa siku ya maandalio kwa ajili ya Sabato ya siku ya saba, kwa maana Sabato hiyo ilikuwa siku “Kubwa,” kwa hivyo ilikuwa maandalio ya pasaka — Jumatano. Kisha akaanza kuhesabu, “Alhamisi (1), Ijumaa (2), Jumamosi (3); Jumatano usiku (1), Alhamisi usiku (2), Ijumaa usiku (3). Hivyo kuna siku tatu mchana na usiku.” {SR2: 18.2}

Kwa mujibu wa kuwaza kwa yule dada anadhani maelezo yake yako sawa pasi na tashwishi yoyote. Lakini zingatia kwamba Kristo alikufa saa ya tisa, masaa matatu tu kabla ya mwisho wa siku (Mat. 27:46-50) na alizikwa machweo — saa kumi na mbili (Luka 23:52-56). {SR2: 18.3}

Iwapo Alizikwa Jumatano, Angekuwa siku tatu kamili na usiku nne kamili kaburini, kwa maana Biblia husema wazi wazi: “Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka [maawio] siku ya kwanza ya juma, [Jumapili asubuhi] wakaja Mariamu Magdalaene na Mariamu yule mwingine kulitazama kaburi.” (Mat. 28:1.) Tena tunanukuu kutoka Marko 16:9, “Naye

19

Yesu alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene.” {SR2: 18.4}

Hebu na tuchunguze nadharia hii kutoka kwa mtazamo mwingine. Yesu alisema: “Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe.” (Mat 26:2). “Kisha [baada ya siku hizo mbili] wakakusanyika pamoja wakuu wa makuhani … wakafanyanya shauri pamoja ili wamkamate Yesu kwa hila, na kumwua.” (Mat. 26:3,4.) Wakati Kristo alisema maneno: “Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka,” haingekuwa baada ya mwanzo wa Jumanne, iwapo Pasaka ingekuwa Alhamisi. Basi yote ambayo yalijiri kuhusiana na hukumu Yake, kusulubishwa, kufa, na kuzikwa, yalikuwa yatimizwe kutoka Jumanne asubuhi [karibu adhuhuri] mpaka machweo Jumatano, ambayo hayangewezekana kulingana na ratiba ya Biblia jinsi ambavyo tutajitahidi kuweka wazi. {SR2: 19.1}

Zingatia Maandiko haya: “Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu wanafunzi Wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?” Hii ilikuwa siku ya maandalio ya Pasaka. “Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira Yangu ni karibu; kwako Nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi Wangu. Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka. Basi kulipokuwa jioni, aliketi chakulani pamoja na wale Thenashara. Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” (Mat. 26:17-22). Karamu ya Pasaka inaweza kusherehekewa tu baada ya machweo mwanzoni mwa siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu: “Mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni ni pasaka ya Bwana.” (Law. 23:5.) Hii ndiyo siku ya mwisho ya maandalio kwa ajili ya pasaka. Kwa hivyo, Yesu bado hakuwa mikononi mwa makuhani wakati wa maandalio kwa ajili ya sherehe ya pasaka, na hata mbali zaidi kusulubishwa. Aidha, Mathayo yu wazi kabisa kwa hii mada na haachi nafasi ya ubishi: “Nao walipokuwa wakila [pasaka], alisema, Amin Nawaambia, mmoja wenu atanisaliti” (Mat. 26:21.) Yesu angelikulaje pasaka na wale thenashara ikiwa alikuwa amekwishasulubishwa na kuzikwa? Tuko tayari kukubali ukweli, bali wakati ambapo nadharia inapingwa na Maandiko, basi tusije tukanyenyekea kwa mahitimisho yaliyo na makosa, kwa maana, yeye aaminiye uongo ni chukizo kwa Mungu. {SR2: 19.2}

Turuhusu tuweze kutatua utata kwa kweli ambazo zaweza kuhimili mtihani. Hebu msomaji azingatie kwamba pasaka ni shughuli ya siku saba, au kile kinachoitwa “juma la pasaka.” Tunanukuu Law. 23:4-8: “Sikukuu za Bwana ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake.

20

Mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni ni Pasaka ya Bwana. Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu: mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu: msifanye kazi yo yote ya utumishi. Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku saba: siku ya saba ni kusanyiko takatifu: msifanye kazi yo yote ya utumishi.” {SR2: 19.3}

Sasa zingatia, Sabato ya siku ya saba huthibitiwa na mzunguko wa kila juma, na pasaka kwa kalenda ya kila mwezi. Hivyo, katika kila juma la pasaka lina Sabato ya siku ya saba na inaweza kuangukia siku yoyote kati ya siku zile saba za pasaka. Tena, zingatia kwamba siku ya kumi na nne huitwa siku ya “Pasaka,” lakini ya kumi na tano “Sherehe” ya Pasaka. (Tazama Hes. 28:17; Yos. 5:11.) Sabato ya siku ya saba huitwa, “Sabato.” Sadaka ya mganda ilikuwa ni malimbuko ya mavuno na ilitolewa mbele ya Bwana keshoye baada ya Sabato, yaani, siku ya kwanza ya juma, kwa kawaida inayoitwa Jumapili. (Tazama Law. 23:11). Sadaka ya mganda ilikuwa mfano wa ufufuo — malimbuko. Mitume alisema: “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala” — wale ambao Aliwafufua. 1 Kor. 15:20; pia Mat. 27:52,53). {SR2: 20.1}

Hivyo Kristo “aliwaongoza watekwa mateka” siku ile ile ambayo mfano ulionyesha. {SR2: 20.2}

Maandalio Ya Pasaka

Pasaka ni sherehe ya siku saba; kwa hivyo, maandalio kwa juma hilo yalihitaji muda zaidi ya siku moja. Kunukuu Kut. 12:3, 6, “Siku ya kumi ya mwezi huu [wa kwanza] kila mtu atatwaa mwana-kondoo… Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule.” Watu waliagizwa mriwa kuanza maandalio siku ya kumi ya mwezi. Siku ya kumi na nne, kabla ya machweo, chachu yote ilipaswa kuondolewa katika nyumba zao. Kisha siku ya kumi na tano ikawadia, ikiwa ndiyo siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu, na juma la pasaka likaanza kwa kumchinja mwana-kondoo wa pasaka. “Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa.” (Kut. 12:15.) Hivyo basi, siku ya kumi na nne ilikuwa siku ya mwisho ya maandalio, na ya kumi na tano, au ya kwanza ya sherehe, ilikuwa kusanyiko takatifu, na hawastahili kufanya kazi ya utumishi katika siku hiyo. Mathayo 26:17, ina rejeleo kwa siku ile ambayo Yesu alikula pasaka na wale thenashara. (Tazama Mathayo 26:20, 21.) {SR2: 20.3}

Siku pekee ambazo zinawezekana kuwa za juma la pasaka zilikuwa jinsi

21

[Ukurasa Mtupu]

22

 [Chati ya Pasaka: Siku Tatu Mchana Na Usiku Ndani Ya Moyo Wa Nchi]

23

ifuatavyo: Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza katika mwaka huo ilikuwa Jumatano, na siku ikakoma machweo (jioni). Siku ya kwanza ya sherehe ya pasaka (siku ya 15 ya mwezi) ikaja Alhamisi, ya pili, Ijumaa; ya tatu; Jumamosi (Sabato); ya nne, Jumapili; ya tano, Jumatatu; ya sita, Jumanne; ya saba na ya mwisho ya sherehe hiyo ikaja Jumatano siku ya 21 ya mwezi huo. (Fuatilia chati iliyo kwa uk. 22). {SR2: 20.4}

Ratiba Kutoka Kwa Pasaka Hadi Kwa Ufufuo

Mwana-kondoo hangeweza kuchinjwa kabla ya siku ya kumi na nne jioni na aitwe “Mwanakondoo wa Pasaka” kulingana na agizo lililopeanwa katika Maandiko yafuatayo: “Na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja (mwana-kondoo) jioni.” (Kut. 12:6.) Tuseme kila kitu kilikuwa tayari na mwana-kondoo alichinjwa mara tu jua lilipotua. Ungalichukua takribani dakika kumi na tano mpaka afe; kisha ngozi lazima iondolewe. Mbali na hilo kila sehemu yake ilihitajika kuandaliwa, ioshwe, na kurejeshwa ndani katika sadaka na mwanya ushonwe pamoja, kwa maana hapakuwa na sehemu yake yoyote itupwe, isipokuwa taka. Kwa hivyo, matayarisho kwa ajili ya kuchoma ile sadaka ingehitaji muda usiopungua saa moja. Hivyo tunasoma: “Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani.” (Kut. 12:9). {SR2: 23.1}

Mbinu ya kale ya kuoka ilihitaji muda zaidi ya mbinu yetu ya kisasa. Fimbo ilipenyezwa katika ile sadaka, kisha ikatiwa kwa makaa ya moto, na ikawa inageuzwa kila wakati kwa kutumia ile fimbo. Mbinu hii ya kuoka ingehitaji takribani masaa manne. Kula pasaka huweka rasmi meza ya Bwana, na agizo la unyenyekevu, kisha kuimba wimbo, kungeongeza saa moja na nusu zaidi. Kisha wakaenda kwenye mlima wa Mizeituni. (Tazama Marko 14:26). Mlima ule ni takribani nusu maili mashariki mwa ukuta wa tatu wa mji. Kwa hivyo, ulikuwa umbali kiasi kutoka mahali ambapo pasaka ilisherehekewa. Hivyo ingaliwachukua karibu nusu saa kufika kule kwa miguu; ambapo baada ya hayo Yesu aliwachukua wale watatu mpaka bustani ya Gethsemane. {SR2: 23.2}

Haukuwa chini ya muda wa saa moja na nusu uliotumika wakiwa mlimani na katika bustani Yesu alipokuwa anaomba; ambapo baadaye mitume waliambiwa wapumzike kwa kulala, kwa maana Yesu alienda kuomba mara tatu, na Aliporudi, mara mbili akawapata wamelala, “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja Nami hata Saa Moja?” (Mat. 26:40.) Tunaweza kudhani kwamba

24

walitumia angalau saa moja wakiwa wamelala, lau maneno ya Bwana wakati wa kurudi Kwake mara ya tatu: “Laleni sasa” (Math. 26:45), yangenenwa bure. Baada ya matukio haya Yuda akawasili pamoja na umati na kukawa na muda kidogo uliotumika kumtwaa yesu; na wakati ambapo walimwongoza hadi kwa makuhani lazima ulikuwa umetumika muda usiopungua masaa mawili. Kulingana na hesabu hii ya wakati, jumla ya saa zilizotumika kutoka machweo Jumatano jioni (mwanzo wa pasaka kwa kumchinja mwana-kondoo) hadi wakati ambapo Yesu alielekezwa kwa kuhani mkuu hazingalichukua chini ya masaa kumi na mawili. {SR2: 23.3}

Uchanganuzi wa ratiba iliyotangulia, huthibitisha kwamba wakati ambapo Yesu aliongozwa kwa Kayafa, kuhani mkuu, ilikuwa karibu saa ya kumi na mbili, au muda mfupi kabla ya maawio Alhamisi asubuhi; na baada ya kuhukumiwa Kwake mbele ya kuhani mkuu, “Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio [ukumbi wa hukumu]: nayo ilikuwa alfajiri.” (Yohana 18:28). “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita: naye [Pilato] akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme Wenu!” (Yohana 19:14). Kwa sababu Yohana husema kwamba ilikuwa alfajiri walipomwondoa kwa Kayafa na kumwongoza hadi katika ukumbi wa hukumu, na pia kwa maana husema ya kwamba ilikuwa takribani saa ya sita (aidha usiku wa manane, au adhuhuri kulingana na majira ya kale), basi lazima ilikuwa muda mfupi baada ya usiku wa manane (takribani saa ya sita) wakati Pilato aliwaambia Wayahudi, “Tazama Mfalme Wenu,” maana Yohana hangeita adhuhuri, alfajiri. Hivyo basi, baada ya Yeye kuhukumiwa na Sanhedrini wakamwita Pilato, kisha wakaenda katika ukumbi wa hukumu. Hili lilifanywa asubuhi ya siku iliyofuata, baada ya kumtwaa Yesu kutoka ndani ya Bustani — mapena Ijumaa asubuhi. {SR2: 24.1}

Yohana asema, “Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka.” Tumekwisha elezea hapo awali kwamba matayarisho ya mwana-kondoo wa pasaka hayakuwa siku moja, bali jambo la siku nne. {SR2: 24.2}

Isitoshe, Mathayo husema wazi wazi: “Wakaiandaa Pasaka. Basi kulipokuwa jioni [Kristo] aliketi chakulani pamoja na wale Thenashara. Nao … wakala. (Mat. 26:19-21). Kwa hivyo, maandalio ya pasaka yaliyotajwa na Yohana, hayawezi kuwa maandalio ya mwana-kondoo wa pasaka, bali badala yake maandalio kwa ajili ya Sabato ya pasaka (siku ya saba), yanayoitwa maandalio ya pasaka, kwa sababu yalikuwa katika juma la pasaka, jinsi ilivyokuwa ikitukia mara moja tu kwa mwaka. Hivyo basi, hiyo Ijumaa hiyo inaitwa “maandalio ya pasaka.” Hivyo, Sabato ya siku ya saba katika juma la pasaka iliitwa “Siku Kuu,” kwa maana ilikuwa Sabato ndani ya Sabato — siku kuu zaidi katika mwaka. {SR2: 24.3}

Kulingana na kadirio la saa, viongozi wa Kiyahudi walimhukumu Yesu kutoka saa sita Alhamisi asubuhi, hadi takribani saa kumi na mbili kamili Ijumaa asubuhi (saa za kale). Saa tisa baadaye — saa ya tatu (Ijumaa), Yesu alisulubishwa. (Tazama Marko 15::25.) Baada

25

ya kuwa msalabani kwa masaa matatu jua likatiwa giza (saa sita — adhuhuri. Tazama Marko 15:33). Masaa matatu baadaye Yesu alikata roho na jua likatoa tena nuru. (Tazama Mat. 27:45-50). Katika masaa matatu yaliyosalia mpaka machweo, maandalizi ya haraka sana yalifanya na Mwokozi akawekwa katika kaburi jipya la Yusufu kabla tu ya Sabato ya siku ya saba kuingia. Tunanukuu Luka 23:53-56: “Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake. Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na Sabato ikaanza kuingia. Na wale wanawake, waliokuja Naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili Wake ulivyowekwa. Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu; na siku ya Sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.” Hivyo Yesu alisalia ndani ya kaburi kutoka saa kumi na mbili kamili Ijumaa jioni mpaka takribani saa kumi na mbili kamili Jumapili asubuhi. Hili pia huthibitishwa na Marko 16:9, “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma.” Kwa hivyo, jumla ya takribani masaa thelathini na sita ndani ya kaburi; na jumla kuu ya masaa themanini na nne kutoka mwanzoni mwa pasaka mpaka kufufuka. {SR2: 24.4}

Sasa zingatia, kwamba kutoka wakati mabapo Wayahudi walimshika Kristo (Alhamisi saa ya kumi na mbili) hadi kufufuka Kwake (Jumapili saa ya kumi na mbili), kulikuwa na masaa sabini na mbili kamili au siku tatu mchana na usiku. Hivyo kutimiza maneno ya Yesu: “Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.” (Mat. 12:40). Dhana kwamba katika “moyo wa nchi ina maana ya katika kaburi, ni dhana ya mwanadamu pasi ma msingi wa Biblia. Iwapo Mwokozi katika mawazo Yake alikuwa alikuwa na uzoefu Wake kaburini, Angalisema hivyo. Iwapo kaburi Lake lilikuwa katikati ya nchi — takribani maili 4,000 chini ya uso wake (moyo wa nchi) basi mtu anaweza akasema kwamba Alimaanisha moyo wa nchi. Yesu alitumia usemi huo kuashiria kwamba Alipaswa kuwa siku tatu mchana na usiku mikononi mwa wadhambi, na kaburini. Mbona wadhambi huitwa “moyo wa nchi”? Kwa sababu mwanadamu aliumbwa kutoka kwayo kwa mujibu wa Mwanzo 3:19, “Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.” {SR2: 25.1}

Kwa hatua hii twavuta umakini wa msomaji katika ile chati kwa ukurasa 22. Zingatia jinsi ambavyo hekima ya milele imetumika kubuni mchoro wa kafara kuu (Msalaba) kwa ajili ya wanadamu, ambayo ni ushahidi ya upendo wa Mungu usio na mpaka. Zingatia kwanza, kwamba mkono wa saa kwa kidude cha saa ulizunguka mara tatu. Zingatia kwamba kila tukio lilikuwa masaa matatu kwa kila sehemu (3 X 9 na 6 X 12), kufanyiza msalaba. {SR2: 25.2}

Sasa tazama kwamba nafasi ya msalaba jinsi ulivyo kwa kidude cha saa, hapaonyeshi uwiano sahihi. Lakini iwapo msomaji ata-

26

geuza ule mchoro juu chini kwa mfano, ambao utaonyesha jinsi ambavyo saa za kale zilipima wakati — ukiwa unarekebishwa na machweo saa kumi na mbili kamili, kisha msalaba unaonekaka katika lake kamili; hivyo tunao mtazamo mwingine wa ukamilifu wa Mungu. {SR2: 25.3}

Mstari unaopita katikati ya kidude cha saa kati ya saa ya nne na ya tano, kumi na kumi na moja — ulionyesha ncha ya kaskazini na ya kusini, hutoa nafasi kamili ya dunia jinsi inavyokwenda katika mzunguko wake wa kila mwaka. Sasa tazama upande wa juu kulia kwa jua jinsi lilivyokuwa wakati huo katika uhusiano wake sahihi kwa nchi, wakati ambapo lilitiwa giza kutoka saa ya sita mpaka saa ya tisa na tunaona jua lilisimama katika nafasi halisi kwa saa zilizosalia gizani! Je, picha hii si kamilifu — pasipo shaka? Iwapo ni hivyo, ingewezekana mwanadamu mwenye maarifa kuwaza kwamba hili lote lilifanyika kiajali? Je, hili halionyeshi ushahidi usio na tashwishi kwamba Mungu alikuwa ameliagiza rasmi mbeleni hili lote, na ya kwamba kwa uwezo Wake mkuu limekuja kutimilika kuwafunza wana Wake mpango Wake, na wokovu ambao umepeanwa kwao? Alisema Paulo, “Matendo yalikamilishwa tangu kutiwa msingi kwa ulimwengu.” (Ebr. 4:3.) Yohana pia hutangaza kwamba mwana-kondoo alichinjwa tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. (Tazama Ufu. 13:8). Mdhambi, “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” {SR2: 26.1}

Ingawa mwana-kondoo wa pasaka alikuwa mfano wa kusulubishwa kwa Kristo, haikukusudiwa kwamba Yeye aweze kutolewa siku ile ile mwana-kondoo alichinjwa. Ukweli huu unajidhihirisha wenyewe, kwa maana mwana-kondoo alichinjwa jioni na Kristo alisulubishwa asubuhi — masaa matatu baada ya maawio, — na akafa masaa matatu kabla ya jioni. {SR2: 26.2}

27

UNABII WA DANIELI NA UFUNUO WA YOHANA HUSHEHENI HISTORIA YA DUNIA

“Heri asomaye, na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo: kwa maana wakati u karibu.” (Ufu. 1:3) {SR2: 27.1}

“Mtu awaye yote asifikiri, kwa sababu hawawezi kufafanua maana ya kila nembo katika Ufunuo, kwamba ni bure wao kukitafiti hiki kitabu kwa juhudi kujua maana ya ukweli uliomo. Yeye ambaye alizifichua hizi siri kwa Yohana atampa mchunguzi wa kweli mwenye bidii mwonjo wa mambo ya mbinguni. Wale ambao mioyo yao i wazi kwa kuupokea ukweli watawezeshwa kuelewa mafundisho yake na watapewa baraka iliyoahidiwa kwa wale ‘wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo.’” — “Matendo ya Mitume,” uk. 584. {SR2: 27.2}

“Katika Ufunuo vitabu vyote vya Biblia hukutana na kwishia. Hapa ni kikamilisho cha kitabu cha Danieli. Kimoja ni unabii; na kile kingine ufunuo. Kitabu kilichofungwa si Ufunuo, bali ile sehemu ya unabii wa Danieli unaohusiana na siku za mwisho. Yule malaika aliamuru, ‘Lakini wewe,Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hadi wakati wakati wa mwisho.’” — Kimenukuliwa, uk. 585. {SR2: 27.3}

“Namba saba huonyesha ukamilifu…ilhali zile nembo zilizotumika hufichua hali ya kanisa katika vipindi tofauti katika historia ya dunia.” — Kimenukuliwa, uk. 585 {SR2: 27.4}

“Wanadamu wafaji wanapaswa kujichunga dhidi ya kuwadhibiti wanadamu wenzao, wakichukua nafasi iliyopewa Roho Mtakatifu. Watu wasijihisi kwamba ni haki yao kuupatia ulimwengu lile wanalodhani kwamba ni ukweli, na kukataa kwamba lolote lisipeanwe kinyume cha mawazo yao. Hii si kazi yao. Mambo mengi yataonekana wazi wazi kama ukweli, ambayo hayatakubalika kwa wale ambao hufikiri kwamba ufasiri wao wa Maandiko siku zote ni sawa. Mabadiliko mengi ya uamuzi yatahitajika kufanywa kuhusiana na mawazo ambayo wengine wameyapokea kama yasiokuwa na makosa.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 76. {SR2: 27.5}

Sehemu kubwa ya himaya ya Ukristo hukubali kwamba tunaishi katika siku za mwisho za historia ya hii dunia. Wakati ambapo Kristo aliulizwa na wanafunzi Wake kuhusu ishara za kurudi Kwake tena duniani, na za mwisho wa dunia, mojawapo wa ishara nyingi Alizopeana ilikuwa; “Basi, mtakapoliona chukizo la uharibifu, lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu, (asomaye

28

na afahamu:).” (Mathayo 24:15). Ni dhahiri kutoka kwa maneno ya Bwana kwamba kitabu cha Danieli husheheni habari kuhusu ishara za nyakati na za mwisho wa dunia. Unabii wa Danieli ulikuwa wa thamani ndogo kwa wanafunzi na kanisa la Kikristo la kwanza, kwa maana Danieli husema kitabu kilitiwa muhuri hadi wakati wa mwisho. (Dan. 12:4). Na kwa sababu kitabu hicho sasa ki wazi ni Dhahiri kwamba tunaishi katika nyakati za mwisho. Ufu. 22:6-10). Lakini kitabu hicho kilikuwa kifunguliwe kwa kundi moja la watu na kifungwe kwa kundi lingine, kwa maana aliongeza, “Wengi watatakaswa, na kufanywa weupe, na kusafika; bali waovu watatenda maovu: wala hataelewa mtu mwovu awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” (Dan. 12:10). Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuweze kujitenga na uovu wote na tuwe watiifu kwa matakwa ya Mungu, ikiwa tutakielewa na kupokea Baraka zilizo mle kitabuni. {SR2: 27.6}

Nia ya chapisho hili si kufafanua nembo ambazo hapo awali zimeelezwa kwa ukamilifu katika machapisho mbalimbali na kuthibitishwa kuwa sahihi katika muhtasari wa kijumla mpaka sasa, bali nia yetu ni kutatua vipengele fulani ambavyo vimefichwa na Roho wa Mungu kwa muda. Nembo mashuhuri ambazo zimeeleweka sana na wanafunzi wa Biblia, zitaangaziwa kwa ufupi, kutosha tu ili kuunganisha wazo na nembo ambazo zitafafanuliwa. Tutajitahidi kuthibitisha kwamba nembo za kitabu cha Danieli na Ufunuo husheheni historia yote ya ulimwengu, ya kiraia na ya kidini, kutoka kwa uumbaji hadi kwa ukombozi. {SR2: 28.1}

Katika sura ya pili ya Danieli, kuanza na ufalme wa kwanza wa dunia yote (Babeli) baada ya gharika, tunayo historia ya ulimwengu kutoka wakati huo mpaka kwa ujio wa Kristo mara ya pili, au hadi mwisho wa dunia ya sasa, ikiwakilishwa katika mfano mmoja mkuu wa chuma. “Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama sanamu kubwa sana. Sanamu hii iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi, kifua chake na mikono yake ni ya fedha, tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba, miguu yake ni ya chuma, na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande… Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele:wala watu wengine hawataachiwa enzi yake, bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba, na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu: basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa

29

[Kielezo: Sanamu ya Danieli 2]

30

baadaye: na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.” (Dan. 2:31-34, 44, 45). {SR2: 28.2}

Ile dhahabu, fedha, shaba, na chuma zimefasiriwa kuwakilisha Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani na Rumi. Mchanganyiko wa chuma na udongo — nyayo na vidole — falme za sasa zinazofuatia anguko la Rumi. Unabii wa ajabu huu, rahisi sana na kweli kabisa. Ila mfano huu mkuu hufunua tu mfumo, jinsi ulivyo, wa historia ya ulimwengu wetu. {SR2: 30.1}

Katika sura ya saba ya Danieli tunao mpangilio sawa wa matukio yanayofuatana katika nembo za wanyama mbali mbali. Sababu ya urudufu pacha ni kuonyesha kwa kina matukio ya kihistoria ambayo yalikuwa yatukie ndani ya huo mfumo wa mfano mkuu. “Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku, na, tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai: Nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa kibinadamu. Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake: wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele. Kisha nikatazama, na kumbe! mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. Baadaye nikaona katika njozi za usiku, na tazama mnyama wa nne, mwenye kutisha mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi; naye alikuwa na meno ya chuma makubwa sana: alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake: na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza; naye alikuwa na pembe kumi. Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yazo nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa: na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.” (Dan. 7:2-8). {SR2: 30.2}

Simba, dubu, chui na myama dubwana huwakilisha falme zile zile kama dhahabu, fedha, shaba na chuma. Nembo hizi zisizo za kawaida na maalum zilizounganishwa na hao wanyama, yaani, mabawa, mbavu, pembe, na vichwa, zina uwezo wa kufichua siri za matukio ya kihistoria ambayo yalipaswa yatimie ndani ya vipindi hivi vikuu vya kihistoria. Jambo la ajabu zaidi kuhusu nembo hizi za kinabii ni kwamba zina uwezo mkamilifu wa kufichua ukweli, na zikikwisha kueleweka vyema, haziwezi zikahitilafiana. Ufasiri wowote wa nembo za kinabii ambao hauafikiani kwa ukamilifu na maelezo yaliyotolewa kamwe sio wa kutegemewa. Ufasiri wa nembo kama hizo si kwamba unapaswa uwe

31

[Kielezo: Wanyama Wanne Wa Danieli 7]

32

[Ukurasa Mtupu]

33

tu na uwiano na maudhui yote ya kitabu na sheria ya Mungu, ila sharti pia uonyeshe funzo fulani muhimu kwa watu wa Mungu; na wakati ambapo maelezo kama hayo, yanarejelewa, yanatolewa kwa Maandiko, wakati huo tu ndipo tunao ukweli. {SR2: 30.3}

Wakati ambapo kichwa cha dhahabu kwa ile sanamu kubwa kiliwakilisha ufalme wa Babeli kwa upeo wa utukufu wake, yule simba hutanda kipindi kikubwa zaidi kwa mujibu wa Mwanzo 10:8-10: “Kushi akamzaa Nimrodi: akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele ya Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi hodari wa kuwinda wanyama mbele ya Bwana. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.” Mwanzo wa ufalme wa Nimrodi ulikuwa “Babeli,” au jinsi ilivyo katika Kiyunani, “Babiloni.” Mamlaka yake yalienea zaidi ya miji minne ya bondeni; yaani, Babiloni, Ereku, Akadi na Kalne. Ikiwa msomaji atafungua Mwanzo 10:1-8 na kuhesabu kwa makini watu waliozaliwa kutoka kwa familia ya Nuhu baada yao kutoka ndani ya safina ya gharika mpaka kuzaliwa kwa Nimrodi, itanabainika kwamba Nimrodi ni wa 26 kuzaliwa baada ya gharika. Mahali ambapo mji huo ulikuwa palikuwa katika nchi ya Shinari, kama ulivyo katika Mwanzo 11:2: “Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.” {SR2: 33.1}

Jina Babeli (Babiloni katika Kiyunani) lilianza wakati mnara wa Babeli ulikuwa unajengwa, Ambapo baadaye Mungu aliuvuruga huo umati kwa lugha mbalimbali. Kwa mujibu wa Danieli, mji mkuu wa Babiloni ulisimama katika bonde lilo hilo: “Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake [Mfalme wa Babiloni],… naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari.” (Dan. 1:2). Kwa hivyo Babiloni ulianzishwa mara tu baada ya gharika, pengine wakati fulani kati ya mwaka 2,400 na 2,300 K.K., na ukawa umefika upeo wake kama ufalme wa dunia nzima kati ya mwaka 400 au 500 K.K. Babeli, katika ustawi wake, ulikuwa umechukua kipindi cha takribani miaka 1,800 au zaidi. Hakika hamna yeyote atakayewaza kwamba Babeli ulifanya kasi kubwa sana kuuteka ulimwengu wa zamani. {SR2: 33.2}

Nembo Ya Mabawa Na Mbavu

Tunaweza sasa kuuliza maana ya mabawa kwa mgongo wa simba na chui; pia mbavu kinywani mwa dubu. Mabawa kwa mgongo wa simba hakika hayawezi kuwakilisha kasi, jinsi wengine wamekwisha kufunza. Iwapo mabawa yalikuwa yawakilishe wepesi yangalikuwa kwa dubu, kwa maana Koreshi na Dario waliuteka Babeli wa zamani kwa usiku mmoja. Aidha, ikiwa mabawa husimamia kasi kwa mnyama mmoja, sharti vivyo hivyo yasiwakilishe lilo hilo kwa mwingine. Je! Yanaweza kuwakilisha kasi kwa chui mwenye vichwa vine? Hakika la. Tathmini ya kina ya hizo nembo

34

huonyesha kwamba yule mnyama chui hakuwa na uhusiano wowote na Aleksanda alipouteka Umedi na Uajemi. Yule chui huwakilisha huo ufalme baada ya ushindi kutimilika. Hivyo vichwa vinne ni ile migawanyiko minne ya Uyunani baada ya kifo cha Aleksanda; yaani, “Kassanda, Lysimakus, Ptolemi, na Selukasi.” {SR2: 33.3}

Vita na ushindi baina ya Umedi na Uajemi na Uyunani vimeletwa kwa umakini wetu katika Danieli 8:5-7: “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi: na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili: na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake, bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga: wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake.” {SR2: 34.1}

Katika Danieli 8:20,21, Danieli aliambiwa na malaika kwamba beberu “ni Uyunani,” kondoo mume, “Umedi na Uajemi,” na pembe kuu kati ya macho yake, ni “mfalme wa kwanza.” Kwa hivyo, ushindi wa wepesi wa Aleksanda unawakilishwa na “beberu” ambaye hakugusa nchi. Iwapo mabawa yangelikuwa yanawakilisha kasi yangalikuwa kwa mgongo wa “beberu” na si kwa chui. Kwa sababu ukweli wa yale ambayo yamesemwa hauwezi kukanwa, na kwa vile wazo ambalo limetumbuizwa na baadhi linapingana na zile nembo, lazima tutazame kwingine kwa utumizi wa “mabawa.” Tunawaza ni salamba zaidi na kuwa na busara na pia kuwa uelekevu zaidi kwa mtu kukubali makosa yake–maana sisi binadamu tunaweza kuyafanya mengi–badala ya kuhusika katika mafafanuzi ya Neno la Mungu yanayopingana. {SR2: 34.2}

Kwanza, lazima tuelewe kwamba Uvuvio unanakili kwa kutumia nembo hizi historia ya dunia yote. Tusije tukasahau kwamba ulikuwapo ulimwengu kabla ya gharika. Ikiwa mmoja wetu angejaribu kazi hii ya ajabu ya usanifu-majengo kubuni mwongozo, au chati, ya historia ya ulimwengu huu, kwa hakika tutazingatia kwa ukamilifu simulizi la sehemu zake zote. Mungu akiwa asiye na mwisho katika hekima, pia katika uwezo, kwa hakika hangesahau au pasi na kuwazia apuuze katika chati Yake kuu ya matukio ya kihistoria kuzingatia ulimwengu Wake kabla ya gharika. {SR2: 34.3}

Rekodi ya ukaguzi mtakatifu wa historia ya dunia hii kutoka uumbaji hadi kwa ukombozi itakuwa wa maana kuu katika wakati huu wa sasa. Katika kizazi cha ukafiri, kumkana Mungu, na unafiki, watu ambao hudai kuwa wenye busara katika mambo ya kidunia na hata ya kidini, wamepoteza mtazamo wa chanzo cha hekima na maarifa ya kweli. “Kwa maana kwamba, kwa sababu walipomjua Mungu, hawakumtukuza Yeye kama ndiye Mungu wala

35

[Kielezo: Simba wa Danieli 7:2,4]

36

[Ukurasa Mtupu]

37

[Kielezo: Dubu wa Danieli 7:5]

38

[Ukurasa Mtupu]

39

[Kielezo: Chui wa Danieli 7:6]

40

[Ukurasa Mtupu]

41

kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima, walipumbazika.” (Rumi. 1:21, 22). Hata wale ambao hudai kuwa walimu wa haki, wameipoteza imani yao katika hesabu ya Biblia ya uumbaji. Mungu akiwa na ufahamu wa ukanaji wenye udanganyifu wa sasa wa Neno Lake, amebuni ramani ya kinabii katika nembo za wanyama, mabawa, mbavu, pembe, vichwa, vilemba, n.k., ambazo kwazo Yeye huonyesha wazi katika picha hizi za kinabii zinazopitishwa moja baada ya nyingine, zile kweli, kwa nguvu ambayo inapasa kuwaaibisa wanadamu na kuwaonyesha ujinga wao mkubwa na ukosefu wa hekima. {SR2: 34.4}

Kulingana na hesabu ya Biblia, gharika ilikuja zaidi ya miaka 1,600 baada ya uumbaji. Mungu alianzisha jamii ya wanadamu kupitia kwa Adamu na Eva. Kwa hivyo, watu wamoja, jamii moja, lugha moja na taifa kuanzia kwa uumbaji hadi kwa gharika. Utawala aliopewa Adamu tunauita ufalme wa kwanza wa dunia yote wa Kiadamu. Babeli ulikuwa wa pili; Umedi na Uajemi ni wa tatu, Uyunani wa nne, Rumi wa tano, hali iliyovunjika ya Rumi (iliyowakilishwa na nyayo na vidole vya ile sanamu kubwa ya Danieli 2, ambayo ni ustaarabu usio dhabiti wa sasa) ni wa sita, na kutoka kufunga kwa millenia baada ya ufufuo wa waovu hadi kwa mauti yao ya pili, ni wa saba na wa mwisho. Hivyo namba ya Biblia saba, kama siku zote, huashiria, ukamilifu. Kwa hivyo, falme hizo saba za ulimwengu wote, zikifunua historia kamili ya dunia, humaanisha mwisho wa dhambi na ufalme wake. {SR2: 41.1}

Ikiwa sisi wanadamu tungebuni chati kama hiyo kwa nembo za wanyama, ni hakika tungeweza kuwa na maarifa ya kutosha kuhesabu kila mnyama kwa utaratibu wake wa kawaida. Hatuwezi kudhani kwamba Mungu ana upungufu wa kufikiri katika ukamilifu Wake wa ajabu. Kwa hivyo, Amehesabu kila mnyama. Tunapaswa kwanza kuhesabu wale waliowakilisha wakati wa Agano la Kale, na ile sanamu kubwa ya madini; yaani, dhahabu — Babeli; fedha — Umedi na Uajemi; shaba — Uyunani. Dhahabu ndiyo kuu kwa madini ambayo ingeweza kusimama kama namba moja; fedha ni ya pili kwa dhahabu, kwa hivyo namba mbili; shaba ni ya tatu kwa dhahabu, kumaanisha namba tatu. Simba, chui na dubu, wanahesabiwa kwa namna hiyo. Simba ni mfalme au mkuu wa wanyama, kwa hiyo namba moja, inayolingana na dhahabu. Dubu ni wa pili kwa simba, kwa hivyo namba mbili, inayolingana na fedha. Chui ni wa tatu kwa simba, hivyo namba tatu, inayolingana na shaba. Hizi ni jozi ya kwanza ya namba, lakini bado ipo jozi nyingine ambayo tunapaswa kunena. {SR2: 41.2}

Haya yangeturejesha kwa mada yetu ya ni nini maana ya mabawa kwa simba na pia kwa chui, na mbavu kinywani mwa dubu. Mungu kwa hakika hangeitoa ramani ya historia ya ulimwengu, kuanzia wakati wa gharika mpaka mwisho, na

42

ashindwe kutilia maanani sehemu zake zote. Lazima kiwepo kitu fulani katika chati hii ya matukio ya kihistoria kuashiria kwamba Alikuwa na uongozi wa ulimwengu wote kabla ya gharika, jinsi imekwisha elezwa hapo awali. Ufalme huo ukiwa wa kwanza, kwa kawaida husimama kama namba moja; Babeli, namba mbili; Umedi na Uajemi, namba tatu; na Uyunani, namba nne. Iwapo dai hili ni sahihi, lazima tuipate jozi hii ya namba kwa simba, dubu, na chui. {SR2: 41.3}

Mabawa kwa simba humaanisha ufalme namba mbili. Simba kwa kawaida ni wa kwanza — kwanza kutoka wakati wa gharika bali (asiye wa kawaida) na mabawa mawili, wa pili tangu uumbaji. Mbavu kinywani mwa dubu huashiria ufalme namba tatu. Dubu kwa kawaida ni wa pili kutoka wakati wa gharika, bali (asiye wa kawaida), kwa mbavu tatu ni wa tatu tangu uumbaji; mbavu zinatumika, kwa maana mabawa huwa mawili mawili. Mabawa manne kwa chui humaanisha kwamba Uyunani ni ufalme wa nne wa ulimwengu wote. Chui kwa kawaida ni wa tatu tangu wakati wa gharika, bali (asiye wa kawaida), kwa mabawa, wa nne tangu uumbaji. Historia huruka, hivyo mabawa hufanya nembo kamilifu. {SR2: 42.1}

“Inuka Ule Nyama Tele”

“Inuka, ule nyama tele,” mbavu zilisema kwa dubu. (Dan. 7:5.) Umedi na Ujemi ulifungua njia kwa vita vya kifalme, kwa hivyo: “Inuka, ule nyama tele.” Kwa hivyo ufalme baada ya ufalme uliingia katika vita vya umwagaji wa damu. Mbavu kinywani mwa yule dubu haziwezi kuashiria mataifa, jinsi ambavyo wengi wamekwisha fundisha, kwa maana mataifa huwakilishwa na pembe, wala sio na mbavu. Wala haziwezi kumaanisha majimbo fulani ambayo Umedi na Uajemi haungeweza kuyateka, kwa maana anazo kinywani mwake, na itakuwa haipatani kudhani kwamba Waajemi wangeyakandamiza mataifa fulani zaidi ya mengine. Ingalikuwa hivyo, dubu angaliwakanyagia chini kama alivyofanya mnyama dubwana. (Dan. 7:7.) Nembo hiyo i kinyume na dhana kama hizo, na hamna ithibati wala funzo linaloweza kutokana na nadharia kama hiyo. {SR2: 42.2}

Mabawa Ya Simba Yakakwanyuliwa

Tukirejea kwa simba, nembo ya Babeli, Danieli asema: “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai: nikatazama hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa kibinadamu.” (Dan. 7:4). “Mabawa yake yakafutuka manyoya.” Nembo hii humaanisha sawa na kung’olewa kwa pembe tatu kutoka kwa myama dubwana. (Dan. 7:8). Ikiwa kung’olewa kabisa pembe humaanisha ufalme wao ulichukuliwa kutoka kwao, basi kukwanyuliwa mabawa huashiria kwamba Babeli, kama ufalme namba mbili ulikuwa utoweke, kutimiza tafsiri ya Danieli ya

43

[Ukurasa Mtupu]

44

[Kielezo: Mabawa Ya Simba Yakakwanyuliwa, Naye Akapewa Moyo Wa Kibinadamu]

45

mwandiko ukutani: “Na tafsiri ya maneno haya ni hii: Mene; Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.” (Dan. 5:26.) Kwa hivyo, Babeli ukaanguka katika mikono ya wafalme wa Umedi na Uajemi. Hivyo mabawa yake “yalifutuka manyoya,” na ufalme wa Umedi na Uajemi, namba tatu, ukafuata simba, namba mbili. {SR2: 44.3}

Naye Akapewa Moyo Wa Kibinadamu

Baada ya mabawa ya simba kukwanyuliwa, asema Danieli: “Akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Chochote kile ambacho kinamaanishwa na nafasi ya yule mnyama na kubadilishwa kwa moyo, matumizi yake ni baada ya Babeli kuanguka chini ya utawala wa Umedi na Uajemi, maana alisimama kama mwanadamu baada ya mabawa “kukwanyuliwa.” Ikiwa tutapata uelewa wa hiyo nembo, lazima kwanza tuzingatie kazi ya moyo, kwa maana nembo yenyewe lazima iwe kamilifu, la sivyo ukweli hauwezi kubainishwa. {SR2: 45.1}

Kazi ya moyo ni kudumisha kawi ya uhai ndani ya mwili. Acha moyo usifanye kazi na yote yanapotea. Hiki kiungo muhimu sana ndicho mtawala wa mwili. Jinsi ambavyo ufalme hujumuisha watu wengi, na mahitaji yao, hivyo ndivyo mwili ulio hai unavyojumuishwa na umati wa chembechembe za seli zenye uhai, na manufaa yake. Jinsi wajibu wa mfalme ni kudumisha nguvu ya uhai ndani ya ufalme wake, pia kuadhibu au kun’goa uovu na kusimamia wema, hivyo ndivyo moyo hufanya. Kwa kubana na kupanuka hudhibiti na kutoa mtiririko, wa kawi hai katika umbo la damu safi. Ushahidi uliokusanywa hadi hapa Huthibitisha kwa moyo ni nembo inayofaa ya mfalme. Lakini lazima tubainishe tofauti kati ya moyo wa mwanadamu na wa mnyama. Danieli 4:16, akizungumza juu ya adhabu ambayo ingemwangukia mfalme kabla afukuzwe kutoka kwa kiti chake cha enzi hadi kondeni pamoja na wanyama, asema: “Moyo wake ubadilike usiwe moyo wa binadamu na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.” Baada ya moyo wa mfalme kubadilishwa, akapoteza fahamu yake, kimaumbile akawa sawa na ng’ombe maksai. “Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa likampata Nebukadnezza: alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.” (Dan. 4:33). {SR2: 45.2}

Akili ya kibinadamu haijumuishi umbo la nje la wanadamu, lakini badala yake huishi katika moyo wa mwanadamu. Wazo hili husisitizwa kwa dhati na maandiko: “Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.” Kwa hivyo, mfano (moyo wa mtu) unaweza kumaanisha akili. Walakini, huo mfano hauwezi kukata kauli ya maono ya mwanadamu, lakini badala yake

46

uelewa sahihi wa Mungu, maana Biblia husema: “Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu.” (Zab. 53:1.) Kupata maono wazi ya uweza usio na mwisho wa Yule wa Milele ndio Mungu huuita elimu ya kweli. Jumla ya mfano ni kwamba, Babeli ililazimishwa kukiri uwepo wa Aliye Juu kwa kumwondoa mfalme mmoja (moyo wa mnyama) na kumsimamisha mwingine (moyo wa mtu). {SR2: 45.3}

Baada ya kuweka wazi lile mfano unaonekana kuashiria, lazima tufanye uchunguzi mfupi wa mfalme wa zamani ili kuona iwapo ufasiri huu unaweza kuungwa mkono kabisa na huo mfano wa moyo. Kama mfano wa milele uliowekwa na gharika kwa vizazi vya baadaye ulikuwa umeshindwa kuwafunza watawala wa Wakaldayo nguvu za Mungu na uwepo Wake, Muumba wa wanadamu kwa rehema Zake, subira na uvumilivu mwingi, bila kunia kwamba mtu yeyote asipotee, Alijitahidi sana kuliokoa taifa hilo. “Bwana hakawii kuitimiza ahadi Yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana Hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” (2 Petro 3:9.) {SR2: 46.1}

Wakati ndoto ya sanamu kubwa ilipotolewa kwa Nebukadnezza kumbukumbu yake ya kitu hicho ilifutwa, lakini hisia ilioachwa akilini mwake iliongezeka sana. Baada ya shinikizo la dharura kwa wenye hekima kushindwa kuifunua ndoto ya mfalme, Danieli, kwa ufunuo wa Mungu, alilifichua jambo hilo la kushangaza kwa kuifasiri hiyo ndoto. Muujiza huu wa ajabu ungalikuwa umemwongoa Mfalme na watu wote wenye hekima wa Babeli kwa ibada ya Waebrania, maana kwa nguvu ya Mungu wa Danieli walikuwa wameokoka hukumu ya kifo; lakini halikuwapo badiliko kwa wema. Ingawa mfalme alimtukuza Mungu kwa kinywa chake, moyo wake ulitanga mbali kutoka Kwake. Mfalme hakuharibu sanamu katika nchi, lakini kwa upofu wake aliendelea kuzisimamisha kubwa zaidi; maana kwa muda mfupi baada ya kufasiriwa ndoto hiyo aliwashurutisha watu wake wote kuisujudia “sanamu ya dhahabu” ambayo alikuwa ameisimamisha katika uwanda wa Dura. (Soma sura ya tatu ya Danieli.) {SR2: 46.2}

Waebrania watatu kukataa kuisujudia sanamu hiyo, na kwa muujiza ambao waliokolewa nao kutoka ndani ya tanuru la moto, ulikuwa umeathiri sana akili za watawala, lakini huo pia, haukuweza kuubadili moyo wa mfalme. Tena alimtukuza Mungu wa miungu kwa kinywa chake lakini si kwa matendo yake. Matendo maovu ya mfalme yalifanya iwe lazima adhabu ya Mungu. Kwa hivyo juhudi kubwa ya kumleta kwa utambuzi wa tegemeo lake kwa Muumba ilikuwa lazima. Ndoto aliyopewa (katika Danieli nne), ya mti mkubwa — nembo yake mwenyewe — na ufasiri wayo na Danieli, ulikuwa amemshawishi mfalme huyo mwenye moyo mgumu kwa ukweli wake, na hukumu ambayo ingemwangukia, isipokuwa angetubu. Danieli alisema: “Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki,

47

ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha .… Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli …. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadnezza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.” (Dan. 4:27, 29, 33.) {SR2: 46.3}

Mwisho wa uzoefu huo mchungu, mfalme alisema: “Basi mimi, Nebukadnezza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo Yake yote ni kweli, na njia Zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, Yeye aweza kuwadhili; (Dan. 4:37.) Ingawa alikiri nguvu za Yule wa Milele, akamwabudu Yeye, na akatamka maneno ya sifa kwa usemi mtukufu, mfalme alishindwa kuusalimisha moyo wake wa kipagani na kuachana na mfumo wa ibada ya kipagani. Alishindwa kukumbatia umuhimu mkubwa wa kuupatia maarifa ya Yehova uzao wake kwa ajili ya utulivu na kudumu kwa ufalme wake. {SR2: 47.1}

Uzoefu huu wa ajabu ulikuwa ni funzo la mfano kwa wafalme wa siku zijazo. Muda mfupi baada ya utizo wa ndoto hiyo, mjukuu wa wafalme alikuwa amekikalia kiti cha enzi. Kwa mazoea yake ya kishenzi alijasiri kumwasi Mungu wa miungu, na Mfalme wa wafalme, ambaye anaweza kuwafanya ng’ombe kuwa wafalme na wafalme kuwa ng’ombe, na watawala kutoka kwa watumwa. “Maana siko mashariki wala magharibi, wala nyikani itokako heshima. Bali Mungu ndiye ahukumuye; humdhili huyu na kumwinua huyu.” (Zab. 75:6, 7.) {SR2: 47.2}

Vyombo vitakatifu awali havikuwa vimewahi kutiwa unajisi na mfalme yeyote kama katika karamu ya ulevi ya Belshaza. Mungu atavumilia hadi mwanadamu atakapovuka mpaka. Hilo Belshaza alitenda kwa kuleta vyombo vitakatifu mbele ya mabwana wake, na masuria, na miungu ya kipagani. Kwa kuonekana mwandiko wa mkono ukutani dhamiri yake yenye hatia ilimsumbua; viuno vyake vikalegea, na magoti yake yakagongana moja dhidi ya lingine. Belshaza, kama baba yake, alimdharau Danieli na kuwaita wenye hekima wa Babeli wafasiri maandishi hayo; ingawa angefaa kuwa alijua wao hawakuwa na uwezo wa kufunua siri. Mwishowe Danieli aliitwa na alipoonekana akasema: “Na tafsiri ya maneno haya ni hii: Mene, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. Tekeli, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. Peresi, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.” (Dan. 5:26-28.) Uzoefu wenye thamani wa baba yake ambao ulikuwapo kwake yeye kuufikia ungekuwa baraka za milele, lakini kwa kupuuza uwezo wa Mungu Mfalme alibatilisha manufaa ya baraka kuwa laana, na kuleta kikomo kabisa cha ufalme wake. Kila raslimali kumfanya simba (Babeli) asimame kama mwanadamu chini ya utawala wa wafalme wa Wakaldayo ilikuwa imeisha, na kila juhudi kushindwa.

48

Kwa hivyo, wakati ulikuwa umekuja wa Bwana kutumia dawa ya mwisho kwa ufalme wa simba. {SR2: 47.3}

Koreshi, ambaye habari zake Mungu alikuwa amezinena kupitia kwa nabii Wake miaka mingi mbeleni, alipewa kuingia katika mji mkuu wa mfalme wa Wakaldayo. (Angalia Isa. 45:1.) Babeli kama ufalme namba mbili ulitoweka, na nembo ya mabawa “yaliyokwanyuliwa” ikatimizwa. “Usiku huo Belshaza mfalme wa Wakaldayo aliuawa.” Moyo wa simba ni mfano wa mfalme wa kishenzi — Belshaza ambaye aliuawa — na hivyo moyo wa mnyama uliondolewa. Mwanadamu hupendekeza, lakini mara nyingi uwezo mwingine ambao yeye hana udhibiti, hukata shauri. {SR2: 48.1}

Danieli alifanywa kuwa rais wa kwanza juu ya wakuu 120 kwa sababu “roho bora ikuwa ndani yake.” Koreshi na Dario wote waliongoka kwa ibada ya Mungu wa kweli. Kwa hivyo, mkono wa milele ambao huingilia kati katika maswala ya wanadamu, ulimsimamisha mfalme wa chaguo Lake mwenyewe. {SR2: 48.2}

Kwa namna hii mifano hiyo ilitimizwa na simba “akainuliwa juu ya nchi, akasimamishwa kwa miguu kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa kibinadamu.” {SR2: 48.3}

Moyo ni nembo inayofaa ya mtawala wa taifa. Tofauti kati ya mfalme wa kiungu na mwovu ni tofauti sana kati ya moyo wa mwanadamu na wa kihayawani. Moyo ni nguvu inayotoa uhai kwa mwili wa mwanadamu, kama vile mfalme ndiye kichwa cha taifa. {SR2: 48.4}

Baada ya uhuru kupeanwa kwa Wayahudi, Koreshi, katika tangazo lake alisema: “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi, Bwana Mungu wa mbinguni amenipa falme zote za dunia; Yeye ameniamuru nimjengee nyumba kule Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi ni nani kati yenu nyote mlio watu Wake, Bwana, Mungu wake na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (Yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.” (Ezra 1:2, 3.) Ushawishi huu wa kiungu wa wafalme wa Wamedi na Waajemi haukukoma hadi miaka kadhaa baadaye. Amri iliyotolewa na Koreshi iliandikwa katika hati na kuwekwa huko Achmetha, katika jumba la kifalme ambalo liko katika mkoa wa Wamedi. Miaka kadhaa baadaye hati iliyopatikana na Dario, amri hiyo ilitekelezwa mara moja. Koreshi alikuwa ameamuru kwamba wote wanapaswa kutoa sadaka ya hiari, na mfalme mwenyewe alichangia bila kikomo. Alisema: “Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng’ambo ya mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe.” (Ezra 6:8.) Aliamuru zaidi kwamba mahitaji yote ya kudumisha huduma za dhabihu “wapewe kila siku bila kukosa.” Kisha akaongeza “wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka

49

zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na ya wanawe.” (Ezra 6:10) Nebkadnezza alikiri kuongoka baada ya uzoefu wake wa ajabu na Mungu wa mbinguni, na kutangaza: “Na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu: Naye hufanya kama atakavyo katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani: wala hapana awezaye kuuzuia mkono Wake, wala kumwuliza, unafanya nini Wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia; na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia, na mawaziri wangu na madiwani wangu wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadnezza namhimidi na kumtukuza na kumheshimu Mfalme wa mbinguni, maana matendo Yake yote ni kweli, na njia Zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.” {SR2: 48.5}

Ingawa maneno matukufu yaliyonenwa na mfalme wa Wakaldayo yanaonekana kuonyesha badiliko la moyo, matendo yake yalionyesha kushindwa yale ambayo kinywa chake kilitangaza. Ni utofauti ilioje kati ya mfalme wa Babeli, na wafalme wa Wamedi na Waajemi! Nebukadnezza alikataa kuwaweka huru watu wa Mungu, alikataa kurejesha chombo kitakatifu kwa Mfalme wa mbinguni; hakutoa amri ya kuijenga tena nyumba ya Mungu; hakutoa zawadi ya aina yoyote kwa Mfalme wa wafalme; hakufundisha maarifa ya Yehova kwa watu wake; aliwaacha watoto wake na nyumba yake waabudu miungu ya mataifa ya kuni na mawe; hakufanya juhudi kumpa Mungu utukufu, isipokuwa kwa kinywa chake. {SR2: 49.1}

Ijapokuwa tunayo mifano hii hai mbele yetu, lakini ni mara ngapi tunakiri kwa vinywa vyetu yale yaliyo sawa na kweli, na hatufanyi harakati za kuufikia Mkono ulionyooshwa wa upendo wa Mungu. Umati wa watu unaiga kiwango kilichowekwa na yule mfalme wa kale. “Watu hawa hunikaribia kwa midomo yao, na huniheshimu kwa midomo yao; lakini mioyo yao iko mbali Nami.” (Mat. 15:8.) {SR2: 49.2}

Ingawa Nebukadnezza alishindwa katika mambo haya matakatifu, Mungu, kwa rehema Zake kuu alimwokoa Mfalme. Mungu alimvumilia kwa muda mrefu mfalme wa Babeli, lakini “mfalme aliyejivuna alikuwa amekuwa mtoto mnyenyekevu wa Mungu; mtawala mkatili, mwenye kiburi, alikuwa mwenye hekima na huruma. Yeye ambaye alikuwa amemtukana na kumkufuru Mungu wa mbinguni, sasa aliutambua uwezo wa Aliye Juu zaidi, na alijitahidi kukuza kicho cha Yehova na furaha ya raia wake. Chini ya kemeo lake Yeye ambaye ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, Nebukadnezza alikuwa amejifunza mwishowe somo ambalo watawala wote wanahitaji kujifunza.” — “Manabii na Wafalme,” uk. 521. {SR2: 49.3}

50

DUBU NA CHUI

Kielelezo kilichofanyizwa na wafalme wa Babeli kinapaswa kuwa na funzo la mfano kwa wafalme wote wanaofuata. Ushawishi wa kiungu wa Koreshi pia ungeweza kuhifadhiwa, lakini wafalme wa Umedi na Uajemi, kama Wakaldayo, walikuwa wakitazamia utukufu wa kilimwengu bila kumcha Yeye anayeweza kuzisimamisha Falme, na kuwauzulu wafalme. {SR2: 50.1}

Funzo la thamani kubwa lililofundishwa kwa adhabu ya wafalme wa Wakaldayo, lingekuwa baraka kwao, lakini kwa fikira zao za ubatili waliacha chanzo cha hekima ya kweli na kutoka kwa nguvu ambayo haishindwi kamwe. Kwa hivyo lile ambalo lilikusudiwa kama baraka likawa hukumu. Kwa hivyo, wafalme wa Umedi na Uajemi waliendelea kuwa wabaya kuliko wafalme wa Uyunani ambao sanamu zao zilikuwa miungu yao, na tamaa yao iliyopotoka kama sheria yao pekee ya maisha. Kwa hivyo tena wakati ulikuwa umekuja wa mbavu katika kinywa cha dubu kunena, “Inuka ule nyama tele.” Kwa hivyo, mkono wa Mweza Yote uliondolewa kwa mfalme wa Uajemi, na Aleksanda, kwa wepesi wa tai kwa mwendo wa askari akapanda juu ya mawindo yake. Kwa hivyo, Umedi na Uajemi ulifungua lango la vita vya umwagaji damu katika historia ya ulimwengu wetu. Kwa njia hii maneno, “Inuka, ule nyama tele,” yakapata kutimizwa. {SR2: 50.2}

Danieli anasema: “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake…. Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.” (Dan. 8:5-7, 20, 21.) Kwa hivyo, Aleksanda, ambaye upendo wake kwa ushindi wa vita hakujua mipaka, alikuwa wa kwanza kuongoza kwa mafanikio magharibi dhidi ya mashariki. {SR2: 50.3}

Lakini punde tu baada ya Aleksanda kushinda ufalme, yeye alijihusisha na ulevi kupindukia na kufariki akiwa bado katika ujana wake. Kwa hivyo pembe ya “beberu” ilivunjika kati ya macho yake, “Na badala yake zikasimama pembe nne mashuhuri kuelekea

51

[Kielezo: Kondoo Mume na Beberu]

52

Ukurasa Mtupu

53

pepo nne za mbinguni.” Aleksanda bila kuwa na mrithi wa kukirithi kiti cha enzi, ufalme uligawanywa kati ya majemadari wake wanne, yaani, Kassanda, Lisimakas, Ptolemi, na Selukasi. Kwa hivyo wakati na majaliwa yalimleta mnyama kama chui mwenye vichwa vinne. {SR2: 50.4}

Kondoo Mume na Beberu

Mapigano yote kati ya mataifa yamefananishwa na kondoo mume na beberu, na pembe mbalimbali zikiinuka na kuvunjika. Kwa nini kondoo mume na beberu? Mbona si aina zingine za wanyama? Yesu anatoa jibu: “Na mataifa yote watakusanyika mbele Yake; Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto.” (Mat. 25:32, 33.) {SR2: 53.1}

Kupitia kwa wanyama hawa wanaofugwa nyumbani uvuvio huwasilisha wazo kwamba wakazi wa dunia ni kondoo na mbuzi tu — dini ya kweli na ya uongo. Pia huashiria kwamba vita ni mapambano kati ya wema na uovu. Lakini mbona Umedi na Uajemi kwa kondoo mume, na Uyunani kwa beberu? Kwa nini si kinyume? Wafalme wa himaya ya Wamedi na Waajemi walikuja kuwa waamini katika Mungu wa kweli kama ilivyofafanuliwa hapo awali; kwa hivyo walikuwa na kanuni kinyume na wale wa Uyunani. Kwa sababu hiyo Umedi na Uajemi uliwakilishwa kwa kondoo mume na Uyunani kwa beberu. La ajabu ni kutambua jinsi ilivyo kamilifu hekima na uangalifu na utunzi wa Yule Aishiye milele, alivyotekeleza kubuni nembo hizi. Mweza Yote tu ndiye anayeweza kuvumbua kama hii sanaa kamilifu ya kinabii, kutabiri matukio ya kihistoria. {SR2: 53.2}

Ufalme Wa Shaba Watawala Dunia

Imeelezwa hapo awali kwamba wanyama simba, dubu, na chui wamehesabiwa na Mungu. Chui akiwa ufalme wa nne kutoka kwa uumbaji, na kadiri namba kwa mtindo huo zinavyokomea kwake, kwa kawaida swali lingeibuka: Kwa nini usiendelee utaratibu wa namba kwa wanyama waliomfuata chui? Zipo sababu kadhaa kwa mabadiliko na yule mnyama haswa. Wakati Rumi ulikuwa ukiinuka polepole kutokea ndani ya ufalme wa Uyunani mwishowe ulifyonza mgawanyo wa mwisho wa Uyunani na nasaba ya Ptolemi ikawa mkoa wa jimbo la Kirumi karibu mwaka 27 K.K. Kwa hivyo Agano la Kale lilifungwa na Uyunani na Jipya likaanza na Rumi. Kwa hivyo, kati ya Uyunani na Rumi upo mpaka wa kugawanya. Pia imegunduliwa kwamba wanyama wanaowakilisha Agano la Kale hawana pembe, lakini wale walio katika Jipya wanazo pembe. Wanyama wote ambao huashiria kufunga kwa kipindi cha mfano na kuanza kwa kipindi cha uakisi. {SR2: 53.3}

54

Namba za Biblia ni kama nyufa za madini mengi ya chuma chini ya uso wa dunia. Maelfu hutembea juu ya hazina hizi ambazo hazijulikani mpaka nguvu fulani isiyoonekana izilete zionekane. Tunajua kwamba Utatu huonyeshwa vyema kwa matumizi ya maneno, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo sisi huonyesha sifa za Mungu kwa maneno matatu, ambayo ni, aliye mahali pote, mwenye kujua yote, na mweza yote. Kipengele hiki chaweza kupanuliwa zaidi. {SR2: 54.1}

Iwapo tatu ni nembo ya Utatu wa Yehova, nne lazima imaanishe kile ambacho hutoka Kwake, jinsi ilivyoonyeshwa katika uumbaji. Makerubi hujumuisha viumbe hai wanne, kila mmoja akiwa na uso wa simba, wa ndama, wa mwanadamu na wa tai, mtawalia. Kuna kanda nne za dunia: Mashariki, Kaskazini, Kusini na Magharibi, ambazo huashiria ukamilifu wa mwelekeo; vivyo hivyo: majira ya baridi, masika, majira ya joto na vuli hutanda mzunguko kamili wa misimu. Tumeona tayari kwamba zilikuwapo falme nne za ulimwengu wote katika historia ya dunia kutoka kwa uumbaji hadi kwa kusulubishwa. Tunaweza pia kutambua ukweli unaohusiana na mada hii kwamba upo mchanganyiko wa mara tatu pamoja na wa mara nne kama unavyoonekana wazi katika kazi ya uumbaji ambayo siku nne za kwanza zilitumika katika kuumba tufe, na tatu zilizosalia katika uumbaji wa viumbe hai na kwishia katika pumziko la Sabato. Siku ya nne iliona vitu vionekanavyo vya uumbaji vimekamilika, na siku ya tano na ya sita, zilikuwa za kuijaza dunia wanyama na watu. Katika kitabu cha Ufunuo chini ya mada ya mihuri saba, tunaona kwamba mihuri minne ya kwanza ilitenganishwa wazi kutoka kwa mitatu ya mwisho kwa nembo za farasi wanne. Kwa hivyo huonekana kwamba kipimo cha mara nne katika kila tukio hutangulia kile cha mara tatu, kama vile katika utaratibu wa uumbaji: kila mgawanyo ukifikia kikomo katika saba ya ukamilifu. Kwa sababu hii zipo sehemu nne katika sanamu kubwa ya Danieli Mbili, wanyama wanne katika njozi ya Danieli, mabawa manne na vichwa vinne kwa chui ambaye tarakimu katika mtindo huo zilikomea. Kwa hivyo ni dhahiri kwamba Agano la Kale lilifungwa kwa namba ya mfano — nne (mnyama chui). Kuonyesha kwamba mahitaji yote muhimu ya wokovu wa familia ya binadamu yalikamilishwa chini ya kipindi cha namba hii mashuhuri, “nne,” kama ilivyokoma karibu na wakati wa kusulubishwa. Kwa hivyo namba hii hutumika kuhusiana na matukio ya kumaanisha duniani kote. {SR2: 54.2}

55

Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Pigeni na kelele katika mlima Wangu mtakatifu; wenyeji wote wa nchi na watetemeke; kwa maana siku ya Bwana inakuja, kwa sababu inakaribia. (Yoeli 2:1.)

56

MNYAMA DUBWANA.

DANIELI 7:7

Kumfuata chui mwenye vichwa vinne huja mnyama dubwana wa Danieli 7:7, anayewakilisha ufalme wa nne wa dunia yote kutoka kwa gharika, lakini wa tano kutoka kwa uumbaji. Rumi huwakilishwa na nembo ya kutisha sana kuliko falme zilizopita kabla yake. Lazima iwepo sababu maalum kwa nini ufalme wa Rumi unawakilishwa na mnyama dubwana. Nembo hiyo hufichua kwamba mfumo wa serikali ya Rumi ulikuwa mpangilio ambao haungeweza kufafanuliwa. Njia ya karibu kwa jina sahihi ni neno — dubwana. {SR2: 56.1}

Sasa tutaangalia usimamizi wake wa serikali. — Kusulubishwa kwa Kristo na mauaji ya wafia-imani ya Wakristo hutoa ushahidi kwamba mamlaka makuu ya Warumi yalijengwa kwa upagani, ambao ulikuwa vitani na Ukristo. Kwa sababu hawa Wakristo waliuawa kwa kukataa kuabudu miungu ya watu, ni dhahiri kwamba Wayahudi walitumia mkono wa serikali ya kiraia ya Rumi kujaribu na kulazimisha itikadi zao za kidini; Yesu akiwa mfano, kwa maana Yeye alisulubishwa kama tokeo la pambano la kidini. Rumi katika karne ya kwanza uliwatesa Wakristo, lakini baada ya kuchukua Ukristo, uliwatesa wapagani kwa ukatili; kuwalazimisha kujiunga na kanisa linaloitwa eti la Ukristo. Kutoka kwa ushahidi uliokusanywa, ni wazi kuona kwamba ufalme wa Warumi ulikuwa chombo aidha cha Myahudi Mpagani, au Mkristo; kikibadilika-badilika kumpendelea mmoja, na kisha mwingine. Kwa kuwa tabia ya mamlaka ya Ufalme wa Kirumi haungeweza kufafanuliwa kama wa Kipagani, Kiyahudi, au wa Kikristo, “dubwana” ndiyo nembo pekee inayofaa. Inasemekana kuhusu Konstantino wakati wa kifo chake kwamba raia wake hawakujua ni aina gani ya mazishi wangemfanyia, kwa sababu alidai kuwa Mkristo, lakini moyoni alikuwa Mpagani. Labda mataifa mengi na vile vile wengine wanaodai kuwa Wakristo kwa wakati huu wa sasa ni dubwana kama Warumi, kwa maana mtume amefafanua hali yao hivi: “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 Tim. 4:3, 4.) {SR2: 56.2}

Juhudi Za Kusimamisha Serikali Za Kidini

Swali laweza kuchipuka: Ni nini kilichomzuia Shetani kuanzisha ufalme wa kidini kabla ya kufunga kipindi cha Agano la Kale? Jibu la pekee ambalo laweza kutolewa, ni, taifa la Wayahudi lilimruhusu yeye kuyafumba macho yao. Waliambiwa wasifanye muungano na ulimwengu, lakini, bila kukumbuka agizo hilo walifanya muungano na Warumi, na hilo ndilo lililomsaidia Shetani kufanikisha mpango wake. {SR2: 56.3}

57

[Kielezo: Mnyama Dubwana Katika Awamu Yake Ya Kwanza. Dan. 7:7]

58

[Ukurasa Mtupu]

59

[Kielezo: Mnyama Dubwana Katika Awamu Yake Ya Pili. Dan. 7:8]

60

[Ukurasa Mtupu]

61

Yafuatayo yataonyesha kwamba adui huyu mkuu wa wanadamu alijaribu mchakato kama huu katika siku za Babeli: “Nebukadnezza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha … lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadnezza aliyoisimamisha: Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao …. mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu ya dhahabu.” (Dan. 3:1, 4-7.) Lakini walikuwapo Waebrania watatu waliopatikana wameasi amri ya mfalme na wakakataa kuisujudia hiyo sanamu. “Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadnezza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; Naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha … Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto …. Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Ndipo Nebukadnezza … akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa Mwana wa Mungu. Kisha Nebukadnezza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku.” (Dan. 3:16-18, 20, 22-26.) {SR2: 61.1}

Ndipo watu hawa wakatoka bila madhara. Ni ya ajabu ambayo Mungu alifanikisha tu na watumwa watatu dhidi ya ufalme wa ulimwengu. Watu hao watatu, wakiwa na imani ndani ya Mungu, walivunja mpango wa Shetani, wakakomesha kuanzishwa kwa serikali ya kidini na kuifanya amri ya mfalme kuwa sufuri. {SR2: 61.2}

Shetani alifanya njama kama hiyo katika serikali ya Umedi na Uajemi na mipango ilitekelezwa kwa fitina

62

na mfalme bila kujua. Ingawa Danieli alitupwa ndani ya tundu la simba, yeye pia, alitoka bila madhara, lakini maadui zake waliangamia kama wale waliowatupa Waebrania wale watatu katika tanuru la moto. Hivyo nguvu za Shetani zilivunjwa katika falme hizi mbili za zamani. Laiti kungekuwa na watu kama hawa Waebrania katika siku za kuanzishwa kwa ufalme cha Rumi, au wakati wa kufunga historia ya Agano la Kale na wakati wa kuanza kwa Agano Jipya, hali zingalikuwa tofauti kabisa. Ulimwengu u katika hitaji la dharura wakati huu la watu kama wale Waebrania watatu, ambao wangependa kuyatoa mhanga maisha haya ya sasa kuliko kumkosea Mungu wao — watu kama Danieli, ambaye alimtazamia Bwana kwa imani thabiti na hakuwa na kosa katika majukumu yake ya kidini na ya kawaida. Kupitia kwa watu kama hawa ulimwengu umebarikiwa kwa manufaa ya milele na thawabu ambazo vinywa vya wanadamu haviwezi kuelezea. {SR2: 61.3}

“Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu yake aletaye habari njema, yeye aitangazaye amani, aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu, auambiaye Zayuni, Mungu wako anamiliki! Sauti ya walinzi wako! watapaza sauti zao, wataimba pamoja; maana wataona jicho kwa jicho, jinsi Bwana atakavyourejesha tena Zayuni.” (Isa. 52:7, 8.) {SR2: 62.1}

63

[Ukurasa Mtupu]

64

[Kielezo: Mwanamke Na Joka Wa Ufunuo 12]

65

JOKA JEKUNDU

Ufu. 12:3

“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake ulikokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake … Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” (Ufu. 12:1-4, 9.) Joka lilionekana mbinguni na kwa kuwa “lilitupwa nje,” ni dhahiri kwamba nembo hiyo asili yake ni mbinguni. Kulihusu inasemekana: “Huyo nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi, na Shetani.” Kumbuka kwamba joka ni mfano wa Shetani, kama vile Mwana-Kondoo aliye na “pembe saba na macho saba” ni nembo ya Kristo. (Ufu. 5:6.) {SR2: 65.1}

Kwa sababu wanyama wengi hufanyiza mnyororo usiokatika wa falme za dunia, joka haliwezi kupenyeza kati ya viunganishi kama nembo ya mfumo tofauti wa kidunia; kwa hivyo huwakilisha yale Maandiko husema: “Ibilisi, na Shetani.” Kielezo kimetolewa kuufichua mpango wa Shetani kwa wakati fulani katika historia ya ulimwengu wetu. {SR2: 65.2}

“Mwanamke aliyevikwa jua” anaeleweka kuwa kanisa la Mungu. Mtoto aliyemzaa alikuwa Kristo. Nyota kumi na mbili ambazo hujumuisha taji ya mwanamke mwanzoni zilikuwa nembo za wazee wa imani kumi na wawili. Hili litafanywa wazi katika somo lingine. Kwa hivyo, tutajitahidi kuweka wazi wakati wa joka na kazi yake. Itakumbukwa kwamba joka lilisimama tayari kummeza mtoto (Kristo) mara tu Yeye alipozaliwa. Ni dhahiri, kwamba yule nyoka wa zamani alijihami kwa vichwa saba na pembe kumi kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. {SR2: 65.3}

“Na mkia wake ulikokota theluthi ya nyota za Mbinguni.” Maandiko yanajielezea yenyewe kuhusi ni kina nani nyota za mfano, kwa maana Uvuvio husema: “Akatupwa hata nchi, na Malaika zake wakatupwa pamoja naye.” {SR2: 65.4}

Kwa hivyo, “theluthi ya nyota” huwakilisha wale malaika ambao walidanganywa na pambano la Shetani. Kunukuu “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 3, uk. 115: “Shetani, katika uasi wake,

66

alichukua theluthi ya malaika. Walimwacha Baba na Mwana Wake, na kuungana na kidudumtu cha uasi.” Swali laweza kuchipuka: Je! mbona aliwakokota na mkia wake na sio kwa njia nyingine yoyote? Nembo hiyo ina uwezo mkamilifu wa kuonyesha namna Shetani alivyowakokota hadi kwa nchi. Laiti ungalikuwa umefanywa kwa makucha, ungemaanisha kwamba Shetani alimshinda Mikaeli (Kristo), na kwa mabavu akawaburuta nje theluthi ya malaika. Lakini kwa sababu aliwakokota kwa mkia wake, maana ni kwamba theluthi ya malaika walijiunga naye katika uasi dhidi ya Mikaeli. Kwa maana wakati joka hilo lilipotupwa nje kwa kawaida lilikuwa likija kwanzia kichwa, lilipokuwa likiwakokota kwa mkia wake, huonyesha kwamba walimfuata kwa hiari. Hivyo Kristo hangeweza kufanya lolote kwa ajili yao. {SR2 : 65.5}

Vita Mbinguni

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika Zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. “ (Ufu. 12:7, 8.) Pambano hilo lilikuwa mbinguni. Jina “Mikaeli” humaanisha aliye kama Mungu; kwa hivyo ni mojawapo wa majina mengi ya Kristo. Danieli humwita Yeye “Mikaeli Jemadari Mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako.” (Dan. 12:1.) Kristo anayo majina mengi, kila moja likibeba ufafanuzi wa awamu fulani, au tabia ya kazi Yake. Malaika akamwambia Yusufu, “nawe utamwita jina Lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu Wake kutoka kwa dhambi zao.” Yeye anaitwa pia “Immanueli,” kumaanisha, “Mungu pamoja nasi.” n.k. {SR2: 66.1}

Wakati Lilipotupwa Nje

Shetani asingalitupwa kutoka mbinguni mara tu baada ya kutenda dhambi, au wakati alipomdanganya Adamu na Eva, kwa maana katika Ayubu 1:6, 7, tunasoma: “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele ya Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huko humo.” “Wana wa Mungu” ni wawakilishi wa dunia ambazo hazikuanguka dhambini sawa na Adamu kabla ya kutenda dhambi, walioumbwa kwa mkono wa Mungu, na wawakilishi katika kiwango sawa na Adamu kama asingalikuwa ameanguka dhambini kutoka kwenye kiti chake cha enzi. Kunukuu kutoka katika Roho ya Unabii: “Makamanda wa majeshi ya malaika, wana wa Mungu wawakilishi wa dunia ambazo hazikuanguka dhambini, wamekusanyika. Baraza la mbinguni ambalo hapo mbeleni Lusifa alimshtaki Mungu na Mwana Wake, wawakilishi wa hizo milki zisizo na dhambi ambazo

67

kwazo Shetani alifikiri kuanzisha ufalme wake.” — “Tumaini La Vizazi Vyote,” uk. 834. {SR2: 66.2}

Shetani bado alikuwa na uwezo wa kwenda mbinguni katika wakati wa Ayubu. Kwa hivyo, lazima alitupwa nje baadaye. Asema Yohana: “Na yule joka alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.” (Ufu. 12:13.) Hatua muhimu inayofuata ni kupata wakati joka lilimtesa “mwanamke” (Kanisa la Kikristo); basi tutakuwa na ukweli wa wakati ambapo Shetani alitupwa nje. Wakati huo wa mateso umeandikwa katika Matendo 8:1, “Na Sauli alikuwa anaridhia kifo chake [Stefano]. Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.” Kwa hivyo mateso makuu dhidi ya kanisa yalikuwa karibu mwaka 34 B.K. Ni kweli kwamba Shetani alimtesa Kristo kabla ya wakati huo, lakini Kristo si yule “mwanamke.” Yeye ndiye “Mtoto” ambaye Shetani alitamani “kummeza.” Kwa hivyo, Shetani alitupwa nje mara tu baada ya Kristo kupaa Mbinguni. Roho ya Unabii ikinena juu ya tukio hilo inasema: {SR2: 67.1}

“Wote wapo kumkaribisha Mwokozi wao. Wana hamu ya kusherehekea ushindi Wake na kumtukuza Mfalme wao … Anawasilisha kwa Mungu mganda wa kutikiswa, wale waliofufuliwa pamoja Naye kama wawakilishi wa umati ule mkubwa ambao utatoka kaburini wakati wa ujio Wake mara ya pili … Sauti ya Mungu imesikika ikitangaza kwamba haki imeridhika. Shetani ameshindwa. Wanaotaabika, wanaojitahidi wa Kristo juu ya nchi ‘wanakubaliwa katika Wapendwa.’ Mbele ya malaika wa mbinguni na wawakilishi wa dunia ambazo hazijaanguka, wanatangazwa kuwa wenye haki. {SR2: 67.2}

“Shetani aliona kwamba maficho yake yalikuwa yameng’olewa. Serikali yake ilitandazwa wazi mbele ya malaika ambao hawakuanguka na mbele ya ulimwengu wa mbinguni. Alijionyesha kama mwuaji. Kwa kuimwaga damu ya Mwana wa Mungu, alijing’oa kutoka kwa huruma za viumbe wa mbinguni. Tangu hapo kazi yake ilizuiwa. Wowote ule mwenendo angeweza kunuia, hangeweza tena kuwangojea malaika wakija kutoka katika makao ya mbinguni, na mbele yao kuwashtaki ndugu za Kristo ya kuwa wamevaa nguo za weusi na unajisi wa dhambi. Kiungo cha mwisho cha huruma kati ya Shetani na ulimwengu wa mbinguni kilikatwa.” — “Tumaini La Vizazi Vyote,” uk. 833, 834, 761. {SR2: 67.3}

Wakati alipokokota theluthi ya nyota (malaika) kutoka mbinguni, na wakati wa vita mbinguni, yalikuwa matukio mawili tofauti. Aliwakokota malaika wakati walimfuata kutoka mbinguni hadi kwa dunia na kutafuta kummeza Kristo. “Na yule joka alipoona ya kuwa ametupwa kwa nchi;” yaani, baada ya Kristo kusulubishwa, Shetani kwa kurudi kwake mbinguni alikatazwa

68

kuingia. Kwa hivyo “aliona” — akaelewa kwamba alikuwa ametupwa nje. Wakati huo akalitesa kanisa. {SR2: 67.4}

Pembe Na Vichwa Vya Joka

Wakati pekee unaowezekana kwa matumizi ya pembe, vichwa, na taji za mfano yatakuwa kwa mfungo wa kipindi cha zamani, na mwanzoni mwa Kipya. Kwa maana joka lilionekana katika umbo hilo wakati Kristo alipaswa kuzaliwa. Pembe huwakilisha sawa kama zinavyofanya kwa mnyama yeyote wa mfano. Zikiwa ni kumi kwa idadi hiyo nembo humaanisha kwamba athari za mpango wake zilihisiwa duniani kote. Humaanisha pia kwamba Shetani alikuwa amepata udhibiti kamili wa mataifa ambayo yalikuwa yakiwakilishwa na zile pembe kumi za yule mnyama dubwana wa Danieli 7; na kwa hivyo akamwongoza Herode kuwaua watoto wakati wa kuzaliwa kwa Kristo akiwa na tumaini la kumwangamiza Mwokozi — kummeza “Mtoto.” {SR2: 68.1}

Tusipuuze ukweli kwamba vyote pembe, vichwa na taji, vilikuwepo wakati yeye alisimama tayari “kummeza Mtoto wake.” Kwa hivyo, iwayo yote maana ya nembo hizi, zote lazima ziwepo kwa wakati mmoja. Kama hili lisingekuwa hivyo, nembo za vichwa na pembe zingeonyeshwa zikija moja baada ya nyingine kama wanyama, na pia kama pembe za kondoo mume na beberu wa Danieli 8. Lilo hilo ni kweli na yule mnyama dubwana wa Danieli 7:7, ambaye kwake pembe tatu kati ya kumi “ziling’olewa kabisa.” Ambapo mifumo na serikali hazipo zote kwa wakati mmoja, hizo nembo huonekana moja baada ya nyingine kwa mpangilio wazo sahihi. Kwa hivyo tunaona kwamba Uvuvio ni mkamilifu kwa kila hali, na bila makosa katika kufunua ukweli uliokusudiwa. Kwa hivyo, itakuwa haipatani kwa mtu kuhitimisha kwamba “pembe” na vile vile “vichwa” vinaweza kuwakilisha mpangilio unaofuatana wa mifumo almuradi vyote vinaonekana katika kundi, na kwa umoja na mnyama ambaye huvibeba. {SR2: 68.2}

Haiwezekani pia kwamba pembe na vichwa vyote vinaweza kuwakilisha serikali za kiraia, au wafalme. Iwapo pembe huwakilisha mifumo ya kisiasa, basi vichwa haviwezi. Ikiwa kichwa kilichotiwa jeraha kwa mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1-3 huwakilisha shirika la kidini, basi vichwa vyote lazima viwakilishe mifumo ya kidini. Walakini, liko jambo tofauti na chui mwenye vichwa vinne wa Danieli 7:6, kwa maana yeye hana pembe na vichwa vyake vimethibitishwa kuwa vya kiraia kwa pembe nne za beberu. Ni ukweli usiopingika kwamba nembo hizo zimekusudiwa kufunua sehemu za kiraia na za kidini katika kipindi kilichowakilishwa na yule mnyama dubwana katika awamu zake zote mbili — Rumi ya kifalme na ya upapa. {SR2: 68.3}

Kama taji huwakilisha mamlaka ya kiraia na kwa sababu zinavyoonekana kwa vichwa badala ya kwa pembe, ni dhahiri kwamba kanisa ndani

69

kipindi hicho lilikuwa likitumia nguvu ya udikteta ya kiraia kueneza mafundisho yake. Kwa hivyo masomo yaliyo katika nembo hizi ni makubwa zaidi kuliko tunavyoweza kuelewa katika muda mfupi. Kwa sababu kweli zilivyoletwa kuhusu maumbile ya nembo haziwezi kupingwa, tuna msingi mzuri wa matumizi yazo. {SR2: 68.4}

Joka na vichwa vyake saba na pembe kumi, pamoja na taji vichwani, lilionekana wakati wa kuzaliwa kwa Kristo kama ilivyoelezwa hapo awali, na huchukua kipindi sambamba na yule mnyama dubwana. Vichwa huwakilishwa na namba “saba” ya Biblia, kumaanisha “ukamilifu,” na hukumbatia kila mfumo wa kidini katika siku za Kristo. Maadamu joka huwakilisha shetani anayedhibiti vichwa, nembo hiyo bila kukosea humaanisha uasi kamili. Haijakusudiwa kufichua kwamba mfumo wa ibada ya kipagani uliongozwa na shetani, kwa maana haujawahi kamwe kuwa vinginevyo. Ni kanisa la Kiyahudi ambalo lilikuwa limeasi-imani, na hilo ndilo liliifanya namba ya Biblia iwe “vichwa saba.” Uasi-imani kama huo ulikuwa umeunasa ulimwengu katika siku za Nuhu, na uovu wake ulifanya isiwezekane dunia kuendelea. Kwa hivyo, hitaji, kwa manufaa ya wanadamu, lilileta gharika. Uasi-imani wa kutisha wa Wayahudi ulipelekea lisiepukwe janga lingine linalofanana na gharika ya kuogofya. Kwa sababu Mungu hangetaka kuupindua ulimwengu kwa gharika mara ya pili, na bado adumishe ahadi Yake isiyoshindwa kwa mtumwa wake mwaminifu Nuhu, alimtuma Mwanawe afe badala ya ulimwengu. Kwa hivyo, ulimwengu haukuangamia kwa sababu ya dhabihu kuu zaidi ya Mwana wa Mungu; na ulimwengu upo leo kwa sababu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. {SR2: 69.1}

Vilemba Vya Joka

Ijayo tunadokeza vilemba na maana yavyo. Imefafanuliwa kwamba vilemba huwakilisha mamlaka ya kiraia. Vichwa vikiwa vimevikwa vilemba, hufichua kwamba makanisa ya wakati huo yaliajiri mkono wa serikali ya kiraia. Lau hili lisingekuwa kweli, Wayahudi hawangemsulubisha Bwana wa utukufu; wala wasingalimpiga Stefano kwa mawe, au kuwakata vichwa na kuwaua wengine. Ulikuwa mkono wa serikali ya kiraia ya Rumi, ilioongozwa na joka, ambayo kupitia kwayo Wayahudi walifanya uhalifu huu wa kutisha; uliosababisha uharibifu wao wenyewe. {SR2: 69.2}

Mshitaki Wa Ndugu

Baada ya joka kutupwa chini kutoka mbinguni kwa mujibu wa maono asema Yohana: “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo Wake: kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashtakiye mbele ya Mungu wetu, mchana na usiku.” (Ufu. 12:10.) “Mashtaka ya Shetani dhidi ya wale ambao

70

humtafuta Bwana hayaongozwi na yeye kutopendezwa na dhambi zao. Yeye hushangilia katika mapungufu ya tabia zao; kwa maana anajua kwamba ni kwa sababu ya kuasi sheria ya Mungu tu anaweza kupata nguvu juu yao.” — Manabii na Wafalme, uk. 585, 586. Wakati Roho wa Mungu anahimiza kemeo, Atafunua dhambi na kumkemea mdhambi. Lakini Shetani, humtia moyo mtenda dhambi ajitolee bila kufahamu ajiingize mwenyewe kutenda uasi, kisha anamshtaki mbele ya Hakimu mkuu Mbinguni, kama “amevikwa mavazi meusi na unajisi wa dhambi,” ili kuhifadhi hukumu yake. Watu wa Mungu lazima wajifunze kugundua sauti ya Roho wa Kristo, na vile vile roho ya Shetani. Wakati hizo mbili zinapopambana, Moja itajitahidi kwa utii wa Neno la Mungu, lakini ile nyingine itaruhusu dhambi na kuchukuana na mdhambi. Kwa njia hii Shetani anapata uwanja, kwa sababu mtenda dhambi huipenda dhambi yake. {SR2: 69.3}

71

KANISA LA MUNGU KATIKA NEMBO YA MWANAMKE.

UFUNUO 12

“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, Yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti Chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.” (Ufu. 12:1-6.) {SR2: 71.1}

Kumbuka kwamba vitu vilivyoonyeshwa katika maono vilikuwa mbinguni, si kwa nchi. Kwa hivyo, chochote nembo hizi zinaweza kumaanisha, lazima kiwe cha asili ya mbinguni. Tena kumbuka kwamba vazi lake pekee ni jua, na ya kwamba taji yake ilijumuisha “nyota kumi na mbili” tu. Angalia kwamba yeye hajasimama juu ya “mwezi,” kwa maana Waufunuo anasema, “mwezi ulikuwa chini ya miguu yake.” Lazima tujifunze kwa umakini sifa za nembo hizi, kwa maana ndivyo tu tunaweza kujua maana yazo. Pia maki kwamba alikuwa tayari kumzaa mtoto mwanamume, na ya kwamba huyo “akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti Chake cha enzi.” {SR2: 71.2}

Ni ukweli uliokubalika kwamba mtoto huyo alikuwa Kristo, aliyepaa juu baada ya kufufuka Kwake. (Marko 16:19.) Hiyo nembo ikiwa ya asili ya mbinguni, “mwanamke” hawezi kumwakilisha Mariamu, mama ya Kristo, lakini yeye huwakilisha kanisa (“mwanamke”) ambalo lilikuwa tayari kumzaa, au ambalo Kristo angezaliwa ndani yake. Kwa hivyo Yohana katika maono alikuwa akitazama nyuma zaidi mbele ya kuzaliwa kwa Kristo. {SR2: 71.3}

Imefundishwa na wengine kwamba yule “mwanamke” ni nembo ya kanisa la Kikristo, na ya kwamba mwezi uliokuwa chini ya miguu yake huwakilisha kipindi cha sheria za Musa au mfumo wa sherehe za kafara ambao ulikuwa umepita, na akiwa amevikwa jua, kumaanisha utukufu wa injili katika kipindi kipya. Kwa mujibu wa yafuatayo, madai haya yanathibitika kuwa si sahihi. {SR2: 71.4}

72

Iwapo “mwanamke” huwakilisha kanisa la Kikristo, ni vipi kanisa lilo hilo (mwanamke) lingeweza kuwa na utungu wa kumzaa Kristo, ambaye kupitia Kwake kanisa hilo lilianzishwa miaka thelathini baadaye? Ikiwa tunasema kwamba mwanamke huliwakilisha kanisa la Kiyahudi, lingewezaje kukimbilia nyikani na kukaa huko kutoka mwaka 538 hadi 1798, katika kipindi cha Ukristo? Iwapo “mwezi” chini ya miguu yake huashiria mwisho wa mfumo wa kafara za sheria za Musa, mbona haukukoma kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, kwa sababu mwezi ulikuwa chini ya miguu yake kabla Yeye kuzaliwa. Ikiwa ulikuwa umekoma kwa wakati huo, ungewezaje kuwa nembo ya kifo cha Kristo? Iwapo vazi lake la mwangaza wa jua ni nembo ya injili katika kipindi cha Ukristo, ni vipi kanisa hilo (mwanamke) liliweza kuvikwa nayo miaka kabla ya kipindi cha injili kuanza, likiwa limevikwa nayo kabla yule mtoto kuzaliwa? Je! Ni lipi kati ya makanisa hayo mawili, la Kiyahudi au la Kikristo, lililomzaa Kristo? Iwapo lilikuwa kanisa la Kiyahudi, basi ni vipi nuru lililokuwa limevikwa nayo liweze kutumika kwa kanisa la Kikristo? Iwapo maswali haya hayawezi kujibiwa, basi tunalazimika kwenda kwa undani zaidi katika somo. {SR2: 72.1}

Dhana iliyoendelezwa kwamba “mwanamke” ni nembo ya kanisa la Kikristo pekee, na “mwezi” ya mfumo wa sherehe za Kiyahudi, huthibitika kuwa si sahihi. Kanisa la Kikristo lilianzishwa karibu mwaka wa 31 B.K., au si mapema kuliko mwaka wa 27, wakati ambapo Kristo alianza kuhubiri; akiwa karibu na umri wa miaka thelathini. Kwa hivyo nembo hiyo huonyesha nyuma miaka thelathini na moja kabla ya mwanzo wa kanisa la Kikristo, kwa maana “mwanamke” huyo (kanisa) “alikuwa akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa” {SR2: 72.2}

Kwa hivyo lilikuwa kanisa la Kiyahudi ambalo “lilimzaa” Mwana wa Mungu na sio la Kikristo. Kwa hivyo, “yeye [kanisa la Kiyahudi] alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa”; yaani, ahadi ilitolewa kwa Israeli kwamba Masihi angezaliwa kupitia kwa taifa hilo na kanisa hilo (“mwanamke”). Joka la zamani, likijua njia ambayo “mtoto” huyo angekujia, kwa ukaribu lilitazama likiwa na nia ya kumwangamiza Yule aliyeahidiwa mara tu Yeye atakapozaliwa. Ulikuwa wakati huo, ambapo joka kwa mkono wa Herode, “aliwaua watoto wote waliokuwa Bethlemu na viungani mwake mwote,” akitazamia kumwangamiza Mfalme aliyekuwa akija. (Tazama Mat. 2:16.) {SR2: 72.3}

Ushahidi huthibitisha kwamba nembo ya “mwanamke” hutwaa vipindi vyote viwili, K.K. na B.K. Hivyo, kwa sababu mwezi ulikuwa chini ya miguu yake kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, lazima uwe nembo ya kipindi cha wakati ambacho kilikuwa kimetangulia kanisa la Kiyahudi. Kwa vile “mwanamke” alikuwa “amevikwa jua” kabla ya kumzaa “Mtoto,” ni dhahiri kwamba hiyo nembo, “kuvikwa jua,” ilitimizwa kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Iwapo mwezi ni mfano, basi, nembo ya “jua” lazima iwe kitu kikuu, kwa maana, “mwezi” hutegemea jua kwa mwangaza, na huyo “mwanamke” alikuwa amevikwa nao. Kwa hivyo, “jua” na “mwezi” lazima izingatiwe. Katika Mwanzo 1:16, tunaambiwa kwamba mianga ya jua na mwezi itawale mchana na usiku. “Jua” kwa hivyo lazima liashirie kipindi ambacho kanisa la Mungu limepewa nuru kubwa, na “mwezi” lazima uwe mfano wa kipindi kilichotangulia. Nuru kubwa haiwezi kuwa injili ya Kristo katika Agano Jipya. Wala “mwezi” hauwezi kuwakilisha mfumo wa sherehe chini ya uchumi wa Wayahudi, kwa maana “mwanamke” huyo alikuwa amevikwa “jua,” na “mwezi ulikuwa chini ya miguu yake” wakati mfumo wa sherehe ulikuwa bado upo, kwa maana mtoto alizaliwa baada ya “mwanamke” kuvikwa “jua.” Kristo Mwenyewe, kwa kuila Pasaka kabla ya kusulubishwa Kwake, alithibitisha ukweli kwamba sheria za sherehe zilikuwa bado zipo miaka 34 baada ya kuzaliwa Kwake. (Tazama Mat. 26:18-21.) {SR2: 72.4}

73

[Ukurasa Mtupu]

74

[Kielezo: Mwanamke Mwenye Mabawa Ya Tai Mkubwa Wa Ufunuo 12]

75

Iwapo taarifa ya hapo juu ni sahihi, basi lazima tuvitafute vipindi viwili kama hivyo ambavyo vinaweza kufaa kikamilifu hizo nembo. Cha kwanza ni kile kabla ya Biblia kutokea, na cha pili ni kile kilicho na Biblia — “kilichovikwa Nuru” — Neno la Mungu lililoandikwa. Hivyo ki-mfano, kipindi cha kwanza chaweza kuitwa, usiku, kilichotawaliwa na “mwezi,” na cha pili, mchana, kinachotawaliwa na “jua.” Kwa hivyo, “mwanamke aliyevikwa jua,” na “hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa,” ni kipindi baada ya Israeli kutoka Misri, na kwa wakati huo kipindi bila Biblia, “mwezi” kilikuwa kinatoweka. {SR2: 75.1}

Tutaleta uthibitisho mwingine kutokea pembe tofauti, kufanya maradufu uhakika wa wazo kwamba “mwanamke” huviwakilisha vipindi vyote viwili — kabla na baada ya Kristo. Ufunuo 12:14 husema: “Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.” Kumbuka kwamba alipewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa. Iwapo mabawa hayakuwa ya mfano, ni nini kusudi lake? Kwa sababu mabawa ya simba na chui mwenye vichwa vinne wa Danieli 7 yaliwakilisha vipindi, kama ilivyofafanuliwa hapo awali kwenye ukurasa wa 33-34, basi mabawa mawili makubwa lazima yaashirie vipindi viwili vikuu vya historia ya kanisa. Tai akiwa mfalme wa nyuni, na kama inavyosisitizwa kwamba yalikuwa ya “tai yule mkubwa,” ni dhahiri kwamba hiyo nembo lazima ishikilie kila kipindi tangu mwanzo wake. Kwa hivyo bawa moja hutwaa historia yote ya kanisa kutoka anguko la Adamu hadi kusulubishwa kwa Kristo, na lingine kutoka kwa kusulubishwa Kwake hadi mwisho wa dunia hii ya leo (ujio Wake wa pili). Kwa hivyo huthibitisha kwamba lipo kanisa moja la kweli katika vizazi vyote. {SR2: 75.2}

Taji yake ya nyota kumi na mbili hapo awali iliwakilisha wazee wa imani kumi na wawili

76

na baadaye kabila kumi na mbili baada ya kutoka Misri, kwa wakati ambao nuru ya ajabu ilikuwa iking’aa kutoka kwa Neno la Mungu (Biblia), ililivika kanisa (mwanamke) wakati lilipokuwa utungu wa kumzaa “mtoto” (ahadi ya Masihi). Lakini taji ya nyota kumi na mbili katika kipindi cha Agano Jipya huwakilisha mitume kumi na wawili. Namba kumi na mbili ni nembo ya serikali. Yesu aliwaambia, “Ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.” (Mat. 19:28.) Ukweli huu huthibitishwa na mfano (kabila kumi na mbili). Itagundulika kwamba katika kufanya hesabu ya makabila ya Israeli ya Kiroho (watu 144,000) kwa kutumia mfano (Israeli asili) kama ilivyo katika Ufunuo 7:5-8, kabila la Dani limekosekana, na badala yake kabila la Manase, mzaliwa wa kwanza wa Yusufu amehesabiwa. Mfano huo hulingana kikamilifu na uakisi, kwa maana Yuda Iskariote alikuwa mmoja wa “mitume kumi na wawili,” alitupwa kando, ambaye Dani ni kivuli. Na badala yake Paulo wa Tarso akaongezwa, ambaye Manase ni kivuli chake. Kwa hivyo, tunaona uwiano kamili katika mfano na uakisi. Funzo katika mfano huu kwa nembo hizi zisizokosea, hufundisha kwamba Mungu amekuwa na kanisa moja tu, ukweli mmoja, na njia moja ya wokovu kwa vizazi vyote. Lilo hilo limeonyeshwa katika maneno ya Paulo: “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu; Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja Naye ni Baba wa wote, Aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.” (Efe. 4:4-6.) {SR2: 75.3}

Kanisa la Mungu limefananishwa pia na vitu vya duniani; tunazungumza juu ya nembo za wanawake; yaani, Hajiri, na Sara. Wa kwanza ni nembo ya Kiyahudi, na wa mwisho Kanisa la Kikristo. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 136.) Nembo hizi za kidunia huonyesha kanisa la Mungu katika sehemu na hali tofauti. Lakini “mwanamke aliyevikwa jua” na mabawa yake ya “tai” akiwa wa asili ya mbinguni, huwakilisha kanisa la kweli la Mungu (ukweli) katika mstari mmoja unaoendelea, na Mtoto wake, Mwokozi na Mkombozi wetu wa pekee katika vipindi vyote viwili — kabla na baada ya Kristo. {SR2: 76.1}

TAJI YENYE NYOTA KUMI NA MBILI KATIKA KIPINDI CHA AGANO JIPYA

Maono ya Yohana katika Ufunuo sura ya kumi na mbili, hushughulika na mada kuu mbili; yaani, “mwanamke aliyevikwa jua,” na “joka jekundu.” Ya mwisho imefafanuliwa. (Tazama ukurasa wa 65-69.) Nembo ya “mwanamke” katika wakati wa Agano Jipya hutanda kwa migawanyo mitatu: wa 1, kipindi cha mitume; wa 2, kutokuwepo kwake kutoka kwa ustaarabu (nyikani) kwa siku 1260 (miaka ya mateso ya upapa, Ufu 12:6, 14); wa 3, kipindi cha mwisho cha kanisa wakati linapambana na joka. (Ufu. 12:15-17.) Kipindi cha kwanza na cha pili kitafafanuliwa kuhusiana

77

na somo lingine. Maelezo ya kipindi cha tatu hupatikana katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 151, 152. {SR2: 76.2}

Kwa hivyo, azma yetu katika sura hii ni kusimulia kwa ufupi somo lililofundishwa na yake “taji yenye nyota kumi na mbili.” Tunauliza swali: Je! Ni nani aliyeziteua mamlaka hizi zinazojiita eti za kitume za siku ya leo? Inasemekana kwamba baada ya mitume kulala, jozi nyingine ya namba iyo hiyo inayo haki ya kuwa mitume. Tuseme hilo dai ni kweli; yapo mamia ya makanisa, na iwapo kila mojawapo la hayo lilikuwa na mitume kumi na wawili, kungekuwa na kuzidisha kwa maelfu yao kwa wakati mmoja, na ikiwa tendo hilo lingekuwa limerudiwa katika kila kizazi, ungekuwapo umati usiohesabika wa mitume wakati Kristo atakapoonekana. Iwapo wamekuwapo maelfu ya mitume, ni dhahiri kwa Andiko lifuatalo kwamba hawataingia kamwe katika mji wa Mungu kama mitume, kwa maana Uvuvio unasema: “Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na wawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.” (Ufu. 21:14.) {SR2: 77.1}

Iko tofauti gani kati ya mtume na mchungaji wa injili? Iwapo hakuna tofauti basi wanapaswa kuwapo zaidi ya mitume kumi na wawili katika kanisa la kwanza, kwa maana walikuwapo zaidi ya kumi na wawili waliohusika katika ukasisi huo. Kristo alikuwa amewateua kumi na wawili, lakini Yudasi hakuhesabiwa wakasalia kumi na mmoja tu. Baada ya Kristo kupaa juu, wale kumi na mmoja walikubaliana kumteua mtu mwingine mahali pa Yudasi: “Kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na hao mitume kumi na mmoja.” (Matendo 1:26.) Kwa hivyo, walijaza idadi hiyo. Sasa iwapo Mathiya alichukua nafasi ya Yudasi, basi lazima wakuwepo watu kama hao kumi na watatu kwa mujibu wa Warumi 1:1, “Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa Mtume, na kutengwa aihubiri injili ya Mungu.” {SR2: 77.2}

Tia alama kwa uangalifu kwamba taji ya “mwanamke” inazo “nyota kumi na mbili” tu na katika msingi wa mji yapo tu majina ya mitume kumi na wawili. Ni yupi kati ya hao wawili, Mathiya au Paulo, ambaye hajatambuliwa Naye, aliyeuweka msingi wenye thamani wa Mji Mtakatifu? Ikiwa tunasema Paulo, tunamfanya kuwa muongo. Iwapo tunasema Mathiya, basi kuwekewa kwake mikono na wale kumi na mmoja hakukuwa na matokeo yoyote katika kumteua mtume. Nini basi? Katika Matendo 1:26, ni mwanzo na mwisho tunasikia kumhusu Mathiya, lakini sivyo kwa Paulo. Ikiwa Mathiya ndiye mtume, basi hakika yeye hastahili kama Paulo. Je! Ni kupi kati ya kuwekewa mikono ambako kwafaa kuheshimiwa zaidi? Je! Ni kwa Paulo na Kristo Mwenyewe alipokutana naye njiani kuelekea Dameski, au Mathiya, kwa mikono ya mitume? {SR2: 77.3}

Swali liko wazi. Hakuna mikono ya mwanadamu inayostahili kumteua mtume, bila kujali nafasi yake ya juu katika uhusiano na injili. Mikono mitakatifu ya Kristo na uwepo Wake wa kibinafsi tu unaweza kumteua mtu kwa ofisi kama hiyo. Huu ni ushahidi

78

usioweza kupingwa, kwa maana “mwanamke” anayo taji yenye “nyota kumi na mbili” tu. Kwa hivyo, ni nani aliye na nguvu ya kumwekea mwingine mikono na hivyo kuzidisha “nyota”? {SR2: 77.4}

Je! Mtume ni nini? Jibu. — Yule ambaye “ametengwa kuihubiri injili ya Mungu.” Lakini iwapo hii ndio maana ya hilo jina, basi wote ambao wanahusika katika kutangaza injili, wakiwa wametengwa lazima wawe mitume. Kwa hivyo, neno, “mtume,” lazima liwe na umuhimu maalum na maana ya undani kuliko kutengwa kuihubiri injili ya Mungu tu. Mtume Paulo aliitwa kuwa mtume kwa watu wa Mataifa. Kwa hivyo yeye, na wale kumi na mmoja wakawa waasisi wa duniani wa kanisa la watu wa Mataifa, na Kristo akiwa kiongozi mtakatifu. Kuzungumzia karama kanisani, mitume ndio wa kwanza, kwa maana bila mwasisi haliwezi kuwapo jumuiya, na hivyo karama zingine hufuata. (Tazama 1 Kor. 12:28.) {SR2: 78.1}

Taji ni utukufu wake, na zile nyota (mitume kumi na wawili) ndiyo mamlaka yake pekee ya duniani. Hapa upo ushahidi wa kushangaza kwamba eti mitume wa siku hizi wameitwa hivyo kwa uongo. Nabii anaweza kudai mamlaka kama nabii lakini kamwe si kama mtume. Hata hivyo, kuna tofauti kati ya manabii wa Agano la Kale na wale wa Jipya; wa la mwisho wakiwa chini ya mamlaka ya wa la kale; kwa maneno mengine, anaweza kuwa mfasiri au mfichuzi wa Biblia: “Kwa maana manabii wote na torati [ya sherehe — katika mifano] walitabiri mpaka wakati wa Yohana.” (Mat. 11:13.) Ufasiri ni sahihi tu wakati umevuviwa na Roho yule yule, kwa hivyo maneno mwafaka yanafunuliwa. Sio tu kwamba kumbukumbu za kihistoria huthibitisha hili, lakini Biblia hulitilia mkazo sana jambo hilo, kwa maana husema wazi kwamba sisi, “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Yesu Kristo Mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” (Efe. 2:20.) Tena tunasoma: “Lakini Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, Atawaongoza awatie kwenye kweli yote: kwa maana Hatanena kwa shauri Lake mwenyewe, lakini yote Atakayoyasikia Atayanena; na mambo yajayo atawapasha habari yake.” (Yohana 16:13.) Je! Liko wapi hitaji la mitume kama hao? Je! Maneno ya mitume hayamo ndani ya Biblia? Ikiwa tunapaswa kuteua jozi ya watu kama hao, hatutakuwa tunamweka kando huyo “mwanamke” na yake “taji yenye nyota kumi na mbili”? Iwapo tutaweka kando hiyo “taji” kwa hiari ya kuwateua mitume, tutafanya nini na injili iliyokabidhiwa kanisa na mitume waliowekewa mikono na Kristo? Sikia mamlaka ya taji yenye nyota: “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote nyingine isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote nyingine isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.” (Gal. 1:8, 9.) “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila,

79

wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.” (2 Kor. 11:13.) Ulimwengu umejazwa na wanaoitwa eti mitume na madhehebu ya kila aina, je! sivyo? Ni wakati wa watu wa Mungu kuanguka kwa magoti mbele ya Muumba wao, na wayachunguze Maandiko wenyewe, ili wapate kujua ukweli ni nini? Kwa nini mtu aupokee uamuzi wa mwingine? Kwa kufanya hivyo tunaporwa uzoefu wetu wenyewe. Iwapo ni hivyo, hatuwezi kuuliza swali, Je! Taswira ya baadaye ya ulimwengu ni nini? Hakuna mtu anayeokolewa kwa sababu anaweza kukiri ushahidi wa ukweli, au kwa sababu anaweza kuwa wa kanisa, au imani yake sahihi. Ni kwa uzoefu wake mwenyewe pekee, uliojengwa kwa msingi wa ushahidi wa ukweli. uliopokelewa moyoni, ambao unaweza kuhuisha akili, na kuifanya upya nafsi, ili aweze kutembea katika upya wa maisha. Haiwezekani kabisa kuingia katika ufalme wa Kristo bila mguso wa kibinafsi wa utukufu wa Mungu. Yesu alisema: “Amin, amin, Nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” (Yohana 3:3.) Maandiko yafuatayo yana ushahidi ule ule. “Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu; wala tohara, siyo ile ya nje tu katika mwili: bali yeye ni Myahudi, aliye Myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.” (Rom. 2:28, 29.) {SR2: 78.2}

“Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwa si kitu, bali kuzihifadhi Amri za Mungu.” (1 Kor. 7:19.) “Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana Yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, Naye hughairi mabaya.” (Yoeli 2:13.) “Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.” (Rumi. 16:18.) {SR2: 79.1}

Kulirejelea wazo letu la asili: wale kumi na mmoja waliruhusiwa utekelezaji wa kumwekea mikono Mathiya ili kuwa funzo kwa siku hii ya leo na dini yake ya mtindo mpya, likionyesha kwamba Mungu hajamkabidhi mtu yeyote mamlaka ya utume — isipokuwa kwa wale kumi na wawili. Agizo kwa ukasisi ni: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu: na kuwafundisha kuyashika yote Niliyowaamuru ninyi: na tazama, Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (Mat. 28:19,20.) “Basi wewe, mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani Mwangu, ukawape maonyo Yangu. Nimwambiapo mtu mwovu, Ewe mtu mwovu, hakika utakufa; nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu huyo mwovu atakufa katika uovu wake; lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako.” (Ezek. 33:7, 8.) {SR2: 79.2}

Kwa uhalisia “nyota” kumi na mbili kwenye “taji ya mwanamke” mwanzoni

80

ziliwakilisha wazee wa imani kumi na wawili; baadaye kabila kumi na mbili za Israeli wa asili, baada ya hapo mitume kumi na wawili, na mwisho makabila kumi na mawili ya Israeli wa Kiroho (watu 144,000). Kwa hivyo tena inathibitika namba nne “kuwa namba muhimu, na ya kwamba kupitia kwa yule “mwanamke” hivi vipindi vinne vimewakilishwa. {SR2: 79.3}

Mungu ambaye aliona mbeleni ubinafsi wa wanadamu! Alimwamuru nabii aandike yafuatayo: “Mnawala walionona, Mnajivika manyoya, Mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama-mwitu, walipokuwa wametawanyika. Kondoo Zangu walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu: naam, kondoo Zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta. Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; Kama Mimi niishivyo, asema Bwana Mungu; kwa sababu kondoo Zangu walikuwa mateka, kondoo Zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji Wangu hawakutafuta kondoo Zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo Zangu; kwa sababu hiyo, Enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; Bwana Mungu asema hivi: Tazama, Mimi ni juu ya wachungaji, Nami nitawataka kondoo Zangu mikononi mwao, Nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; wala wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; Nami nitawaokoa kondoo Zangu kutoka vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. Maana, Bwana Mungu asema hivi; Tazama, Mimi mwenyewe, naam, Mimi, nitawatafuta kondoo Zangu, na kuwaulizia.” (Ezek. 34:3-11.) {SR2: 80.1}

Kwa ulinganisho Roho wa Mungu alichora picha halisi kutoka kwa kundi la kondoo na wachungaji; watu wa Mungu kama kundi; na ukasisi kama wachungaji. Watu wakweli wa Mungu wataiga kondoo, na walinzi Wake wataiga mchungaji mwema anayejali kondoo wake. Chochote kipungufu kwa hili ni chukizo machoni pa Mungu. Iwapo tutaweza kujifunza somo lililokusudiwa lazima kwanza tupate ufahamu wazi wa kivuli (wachungaji na kondoo), kwa maana, uakisi (wachungaji na washiriki wa kanisa) wanaombwa kuiga kielelezo. {SR2: 80.2}

Taswira imechukuliwa kutoka kwa mbinu ya zamani ya kuchunga kundi. Malisho yaliyo wazi ya milimani na vilimani yalihitaji daima utunzi wa mchungaji kwa kondoo. Bara kubwa iliwavuta kondoo na wachungaji umbali mkubwa kutoka nyumbani, na kuendelea kuhama kwenye mandhari kulifanya isiwezekane kupata makazi ya kudumu ya aina yoyote kwa ajili ya kondoo, au

81

wachungaji. Kwa hivyo, msaada mwingine ulihitajika. Kila mchungaji alikuwa na idadi fulani ya mbwa, kulingana na kipimo cha kundi, kwa usalama wa kondoo kutoka kwa mwanadamu na mnyama. Kwa sababu kitu kimoja kilitegemeza kingine, punda alitumika kubeba mahitaji muhimu kwa ajili ya kondoo, mbwa na wachungaji. Haya yalijumuisha mavazi, vifaa vya kujifunika usiku, vyakula vya wachungaji na pia vya mbwa, dawa, bendeji, nk. Mnyama mwaminifu alibeba huo mzigo mgongoni mwake kila siku ya mwaka. Mwisho wa siku mchungaji alihesabu kondoo wake. Iwapo mmoja alikosekana, alienda kumtafuta mara moja, kwa sababu haikuwa salama kwa mmoja kutanga mbali na kundi. {SR2: 80.3}

Hali bora ya kondoo ilikuwa thibitisho la uaminifu wa mchungaji na ustahiki wa kuajiriwa kwake. Yeye hakuwa tu atafute malisho mazuri, bali pia ahudumu kama tabibu wa mifugo pia. Mara nyingi kondoo angevunjika mguu wake na lilikuwa jukumu la mchungaji kukirejesha kwa ustadi, kipande na kulifunga jeraha bendeji. Katika kusafiri juu ya uso unaoparuza wa nchi, ambapo kulikuwa na miamba na misuguo, ajali zilikuwa za mara kwa mara. Wakati mwingine mwiba ungeudunga mwili, au jeraha lingine dogo litukie, ambalo labda halikusababisha maumivu, na halikuweza kugunduliwa na mchungaji, bado nzi anaweza kuwa alitaga mayai yake kwenye kidonda kilicho wazi, na mabuu punde yakaweza kukua na kupenyeza chini ya ngozi na hadi kwa mfupa; hili lilikuwa tukio la kawaida. Kwa wakati kama huo umakini wa mchungaji unaelekezwa kwa maradhi ya kondoo na wakati huo lazima atoe utunzi wa pekee na kukifunga kidonda bendeji. {SR2: 81.1}

Mwana-kondoo, au hata kondoo alipokuwa mgonjwa na mdhaifu sana kulifuata kundi lilikuwa jukumu la mchungaji kumtunza na kumbeba. Ikiwa inampasa kumchukua mwana-kondoo mikononi mwake, kondoo mama daima huwa kando yake akimwangalia, na kunena naye. Viumbe hawa waungwana hujali, hulisha, na kuwahifadhi wana-kondoo wao wakiwa wasafi bila mawaa. Je! Ninyi kina mama mnafanya kama hayo kwa watoto wenu? Je! Ninyi wachungaji (makasisi) wa kundi la Mungu mnatenda yale kila mchungaji wa zamani aliwafanyia kondoo wake? Au, huwa mnajilisha na kujitunza wenyewe zaidi kuliko jinsi mnavyolitunza kundi la Mungu? Je! Mnastahili ujira wenu? {SR2: 81.2}

Mchungaji wa zamani alilazimika kutoa hesabu kamili ya kundi, hata kwa kila jambo dogo kabisa. Je! Mnafikiri Mungu atahitaji machache kwenu? Je! kondoo Wake sio wa thamani kubwa zaidi? Daudi alihatarisha maisha yake kwa ajili ya mwana-kondoo, lakini Mungu alimwokoa kutoka kwa simba na dubu. Daudi, kwa heshima ya Mungu, na kwa usalama wa watu wake, alihatarisha maisha yake, alilikabili Jitu Goliati, lakini Mungu alimtia Mfilisti huyo mikononi mwa Daudi, na kumfanya Daudi kuwa mfalme juu ya taifa Lake. Je! Unafikiri atatenda machache kwako, iwapo wewe, pia, utamwiga Mchungaji Mwema? {SR2: 81.3}

Yesu alisema: “Mimi ndimi mchungaji mwema: Mchungaji mwema

82

huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara, wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi, kama vile Baba anijuavyo, Nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. “(Yohana 10:11-15.) {SR2: 81.4}

Nabii Isaya alipotazama mbele kwa hali za siku hizi husema: “Naam, mbwa hao wana choyo sana hawashibi kamwe, na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno: wote pia wamegeuka upande wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka kwa makao yake.” (Isa. 56:11.) {SR2: 82.1}

83

[Ukurasa Mtupu]

84

[Kielezo:Wanyama Wa Danieli Na Ufunuo]

85

MNYAMA KAMA CHUI

UFU. 13:1-10

Mnyama dubwana wa Danieli 7, anayewakilisha Rumi katika awamu yake ya kwanza, huonyesha kinabii kwa pembe zake kumi kwamba walikuwapo wafalme kumi ambao wangeinuka kutoka Rumi. Katika awamu yake ya pili huonyeshwa kwamba upapa ungeinuka, uwaangushe wafalme watatu, na kuwadhoofisha watakatifu wake Aliye juu kwa kipindi cha miaka 1260. Lakini hasemi kuhusu anguko la ufalme wa Rumi au upapa. Yu kimya juu ya matengenezo ambayo yalikuja kabla au baada ya 1798 B.K. Kwa hivyo, ukosefu wa habari kwa nembo za mnyama huyu, lazima ipatikane mahali pengine fulani katika Neno la kinabii la Mungu. Hii lazima ilitafutwe katika kitabu cha Ufunuo, kwa sababu ni kikamilisho cha unabii wa Danieli. {SR2: 85.1}

Mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1-10 ni unabii pekee wa mifano unaosimulia kuhusu anguko la ufalme wa Rumi, kuvikwa vilemba kwa wafalme kumi, jeraha la upapa, matengenezo na kuinuka kwa Uprotestanti, na kukamatwa kwa papa. {SR2: 85.2}

“Nami nikasimama juu ya mchanga wa bahari, kisha nikaona mnyama akitoka baharini, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na kwenye pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.” (Ufu. 13:1.) Kumbuka mnyama huyu anayo idadi sawa ya pembe kama yule “dubwana” katika awamu yake ya kwanza (Rumi ya kifalme). Danieli husema, pembe kumi kwa yule mnyama anayewakilisha Rumi “ni wafalme kumi watakaotokea.” (Dan. 7:24.) Pembe zinazoashiria ulimwengu wa Warumi katika hadhi yake ya kifalme, pia zilionyesha mbele kwa wakati ambapo ufalme huo ungegawanyika katika sehemu, au falme kumi. Kwa maneno mengine, wakati pembe kimsingi ziliwakilisha ulimwengu wa Warumi katika mfumo wake wa kifalme, baadaye huwakilisha ulimwengu wa sasa katika hali yake iliogawanyika tangu anguko la Rumi — sawa na vidole kumi kwa sanamu kubwa ya Danieli 2. {SR2: 85.3}

Mnyama dubwana katika hatua yake ya kwanza anazo pembe kumi. Kwa sababu katika hatua yake ya pili pembe ndogo ilizuka, na tatu kati ya kumi ziling’olewa kabisa, humaanisha kwamba haziwezi kamwe kurejeshwa kama wafalme. Pembe zikiwa zimepunguzwa hadi kwa namba saba ya Biblia, iliashiria kwamba upapa ungekuwa na utawala kamili kwa ulimwengu wote kama linavyohusika kanisa la Kikristo. Kwa hivyo, pembe kumi kwa mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1, haziwezi kuashiria kwamba zile tatu zilizong’olewa zimechukua mamlaka yao mara ya pili. {SR2: 85.4}

Kwa sababu idadi ile ile ya pembe zinaonekana kwa kila mnyama anayefuata; yaani, dubwana (Dan. 7:7); mnyama kama chui

86

(Ufu. 13:1); na mnyama mwekundu sana (Ufu. 17:3); wanaowakilisha kipindi chote cha Agano Jipya, ni dhahiri kwa kweli zilizokusanywa kwamba namba ya hizo pembe imekusudiwa kuashiria ulimwengu wote. Kwa vile hazipo kwa mnyama wa Ufunuo 13:11-18, zinathibitisha ukweli kwamba mnyama huyo mwenye pembe mbili huwakilisha mfumo wa ndani. Kwa hivyo, ni wazi bila shaka kwamba idadi isiyobadilika ya pembe (kumi) imebuniwa kuwakilisha ulimwengu wa watu na serikali. (Fuata kielezo kwa ukurasa wa 84.) {SR2: 85.5}

Kwa sababu simba, dubu, chui mwenye vichwa vinne, na mnyama dubwana (nembo za Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani na Rumi) umeunganishwa kwa kila mmoja, mnyororo usiovunjika wa wanyama kufanya kuwa isiwezekane kwa mnyama mwingine wa ulimwengu wote (mfumo) kukingama mpangilio wao wa mfululizo. Kwa hivyo, mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1-9, lazima amfuate yule mnyama dubwana (Rumi). {SR2: 86.1}

Ufu. 13:2, 3: “Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Mseto wa yule mnyama hufunua ukweli kwamba yeye ni mzawa wa wanyama wanne waliokuwepo kabla yake. Kinywa cha simba miguu ya dubu, mwili wa chui, na idadi ya pembe, zote hudokeza tabia zake za urithi kama zinavyoshuka kutoka Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. Ukweli huu usioweza kupingwa huthibitisha kwamba yeye ndiye mnyama wa tano wa ulimwengu wote. {SR2: 86.2}

Mnyama kama chui alitokea baharini kwa namna moja kama wanyama wanne kabla yake. (Danieli 7:3.) Kwa hivyo, mnyama wa Ufunuo 13:1-9 ameumbwa kutoka kwa tokeo la vita na ghasia kati ya mataifa, vivyo hivyo kama Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. Kwa sababu ushahidi uliofunuliwa kwa nembo hauwezi kupingwa, mnyama kama chui huchukua kipindi baada ya anguko la Rumi ya kifalme, sambamba na nyayo na vidole — chuma na udongo wa sanamu kubwa katika Danieli 2. Kwa maneno mengine, mnyama kama chui huwasili na mwisho wa kipindi kinachowakilishwa na awamu ya kwanza ya mnyama dubwana, ilhali awamu ya pili ya mnyama dubwana (Rumi ya upapa) huendelea hadi 1798. Kwa hivyo, mchakato unaokunjua wa mmoja, hulaliana na mwanguko wa yule mwingine. Kwa Yohana mnyama kama chui hakuonyeshwa katika mchakato wake unaokunjua, badala yake kwa tendo lake la kufunga anasema, “Na pigo lake la mauti likapona.” Aliona katika maono yule mnyama baada ya jeraha la mauti kupona, maana yeye hutumia kitenzi cha zamani, “likapona.” Lakini katika maono ya Danieli kazi yote ya yule mnyama dubwana ilikuwa katika

87

siku za baadaye. Akasema Nabii: “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria: nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” (Dan. 7:25.) Danieli katika maono alitazama historia iliyowakilishwa na wale wanyama, mbele; ilhali Yohana alitazama nyuma; au kwa maneno mengine, Danieli aliona lile mnyama angefanya, ilhali Yohana alionyeshwa lile mnyama huyo alikuwa amefanya. {SR2: 86.3}

Vilemba Na Pembe

Kumhusu mnyama “mwenye pembe kumi na vichwa saba, na kwenye pembe zake ana vilemba kumi,” Yohana anasema, “nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” Kichwa kilichojeruhiwa huwakilisha upapa, uliojeruhiwa na Martin Luther ambao mwanzoni uliwakilishwa na pembe yenye kichwa ya yule mnyama dubwana kuonyesha tu utawala na mamlaka ya upapa. Lakini “mnyama kama chui” huuonyesha upapa katika hali yake iliyojeruhiwa, na papa kuwekwa kifungoni. Kwa hivyo, wanyama hao wawili (dubwana na kama chui) hulaliana kila mmoja, kutoka kwa anguko la Rumi ya kifalme hadi mwaka 1798. Kwa hivyo, wakati mnyama dubwana katika hatua yake ya pili huwakilisha upapa, huo huelezewa na “yule kama chui.” Mmoja hufunua mamlaka ya udhalimu, na mwingine huelezea anguko lake. Kwa maana pembe ndogo ilikuwa na nguvu na ikawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu kwa miaka 1260 (Dan. 7:25.) Lakini mnyama kama chui pia “akafunua kinywa chake kwa makufuru”, na akapewa nguvu kuendelea miezi arobaini na miwili.” (Ufu. 13:6, 5.) Namba ya miezi ni sawa na “wakati na nyakati mbili na nusu wakati” — siku 1260 (miaka), hesabu ya siku 30 kwa mwezi. {SR2: 87.1}

Kwa kifungo cha Papa Pius wa 6, na kifo chake mnamo Agosti 19, 1799, shughuli fulani ilifanyika kati ya mnyama dubwana na mnyama kama chui. Kichwa na pembe ziliondolewa kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine, kwa mfano. Katika kufanya mabadiliko pembe ndogo “ikiwa na macho ya mwanadamu na kinywa kilichonena maneno makuu,” ilibadilishwa kutoka kwa pembe yenye kichwa hadi kwa kichwa cha kawaida kilichotiwa jeraha, kuonyesha upapa ulikuwa umepoteza mamlaka yake ya kidini, na haukuwakilishwa tena na pembe yenye kichwa (mseto wa kanisa na serikali ya kiraia). {SR2: 87.2}

Kwa sababu tukio hilo lilikomesha kipindi cha unabii cha miaka 1260 ya Danieli 7:25 na Ufunuo 13:5, lilizivika pembe za mnyama kama chui vilemba kabisa, likimaanisha kwamba serikali ya kiraia sasa iko huru kwa kanisa. Vilemba kwenye pembe zake huashiria anguko la ufalme wa Rumi, likionyesha kwamba wafalme kumi ambao walifananishwa na zile pembe kumi za yule mnyama dubwana, wamepokea ufalme wao. {SR2: 87.3}

88

Pembe Na Vichwa Vyote Vipo

“Mimi Yohana nalimwona yule mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kwenye pembe zake ana vilemba kumi.” Tusiupuuze ukweli kwamba pembe, vilemba, na vichwa vyote viko kwa mnyama. Kwa hivyo, maana yoyote inayotolewa kwa ile nembo, vyote lazima viwepo kwa wakati huo pigo lake la mauti lilipona. Kama isingekuwa hivyo, nembo za vichwa na pembe zingekuja moja baada ya nyingine kama ilivyokuwa kwa pembe ndogo na zile zingine tatu ambazo “ziling’olewa kabisa” kutoka kwa mnyama dubwana wa Danieli 7:7. Mbinu kama hiyo imefuatwa na “beberu.” Baada ya pembe mashuhuri (Aleksanda) kuvunjika, nne zilizuka kuchukua nafasi yake (migawanyo minne ya Uyunani), na baada ya hizi ikaja pembe kubwa sana ambayo kimsingi iliwakilisha Rumi. (Dan. 8:8, 9.) {SR2: 88.1}

Pale ambapo mifumo na serikali hazipo kwa wakati mmoja, nembo huonyesha mpangilio unaofuatana. Jambo lingine la kukumbukwa kwamba kila nembo ya mwandamano wote wa wanyama huonyesha kweli ambazo zingetukia katika kipindi kilichowakilishwa na kila mnyama, na hakuna hata mmoja kati yao hurejelea jambo lolote la wakati uliopita, isipokuwa tabia za urithi za mababu. {SR2: 88.2}

Kwa hivyo, vichwa au pembe hazina kumbukumbu kwa chochote kabla au baada ya kipindi kilichowakilishwa na mnyama. Pia sio kawaida kwa vichwa (viungo vya mnyama) kuishi kabla au baada ya mnyama mwenyewe. Kwa hivyo, itakuwa haipatani kuhitimisha kwamba pembe vile vile na vichwa vyaweza kuwakilisha mpangilio unaofuatana wa mifumo almuradi vyote vinaonekana kwa wakati wa tendo la kufunga la yule mnyama. Mnyama kama chui katika hali yake iliyojeruhiwa lazima amekusudiwa kuonyesha kinabii hali iliyopo pamoja na ustarabu wa sasa. {SR2: 88.3}

Nembo Za Vichwa

Haiwezekani kwamba pembe na vichwa vyote vyaweza kuwakilisha serikali za kiraia au wafalme. Iwapo pembe huwakilisha upande wa kisiasa, basi vichwa haviwezi. Yohana husema kumhusu yule mnyama kama chui, “Niliona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” Kwa sababu “kichwa” ambacho “kilitiwa jeraha” huwakilisha mfumo wa kidini, basi vyote saba lazima viwakilishe mashirika ya kidini, kwa maana vichwa vyote vinafanana, isipokuwa jeraha. Kwa hivyo ni ukweli dhahiri kwamba nembo hizo zimekusudiwa kufunua pande za kiraia na za kidini kwa ulimwengu wa sasa. {SR2: 88.4}

Vilemba huwakilisha mamlaka ya kiraia kama ilivyoelezwa hapo awali. Kama vingekuwa kwa vichwa jinsi vilivyo kwenye joka la Ufunuo 12:3, vingemaanisha kwamba makanisa yanatumia mkono wa kiraia wa serikali

89

kueneza mafundisho yao kama ilivyokuwa katika siku za Rumi ya kifalme na ya upapa, iliyowakilishwa na joka. Lakini kwa vile vilemba viko kwa pembe, na serikali ni huru kutoka kwa kanisa huthibitisha nembo za vilemba kuwa sahihi. Maadamu kweli zilizotolewa kuhusu maumbile ya hizo nembo haziwezi kupingwa, ni dhahiri kwamba tuna msingi thabiti wa matumizi yazo. {SR2: 88.5}

Mnyama kama chui ni mzawa wa falme nne za kale. Kwa hivyo, yeye huwakilisha ulimwengu, lakini haswa ustaarabu mzima wa magharibi, pamoja na mifumo yake ya kiraia na ya kidini. Vivyo hivyo vichwa huwakilisha Ukristo pekee. Yohana anasema: “Mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba, na kwa pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.” Ukweli kwamba lipo jina la makufuru kwa vichwa ni thibitisho la ziada kwamba vyaweza kuwakilisha tu mashirika ya kidini, kwa maana kukufuru ni sawa na unafiki, na unafiki humaanisha jaribio la kuchanganya takatifu na la kawaida. Lakini Bwana husema: “Najua makufuru ya hao wasemao kuwa ni Wayahudi [Wakristo], na sio, lakini ni sinagogi la Shetani.” (Ufu. 2:9.) “Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.” (1 Tim. 1:20.) “Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana Mungu asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili kwa kuwa wamekosa kosa juu yangu.” (Ezek. 20:27.) “Maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima: basi, kwa ajili ya hayo Nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.” (Isa. 65:7.) Kuasi Neno la Mungu ni kukufuru. {SR2: 89.1}

Kwa kawaida swali linatokea, madhehebu haya ya makufuru yanaweza kuwa yapi? Kwa kweli yanaweza kuwa mengi; zingatia kuzidishwa kwa madhehebu. Neno la Mungu la kinabii, likinena juu ya wakati huu wa sasa linasema: “Mkijua kwanza neno hili, kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe.” (2 Pet. 3:3.) “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima, ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 Tim. 4:3, 4.) {SR2: 89.2}

Je! Ni nini kimeleta mkanganyiko wa siku ya sasa? Kwa sababu wameacha ukweli wa Biblia ndilo jibu pekee ambalo laweza kutolewa. Je! inawezekana kwamba yote yanaweza kuwa sawa wakati hakuna mawili yanayoamini sawa, yakiwa na biblia moja, injili moja, Bwana mmoja, kuzimu kumoja kwa kuepuka na mbingu moja kupata? Yesu alisema: “Na kondoo wengine

90

Ninao, ambao si wa zizi hili: na hao nao Imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja, na mchungaji mmoja.”(Yohana 10:16.) {SR2: 89.3}

Kama haya machafuko ya Shetani kwa wakati huu yalikuwa karibu kutokea katika siku za Paulo. Alipojazwa na roho wa Mungu, alitamka maneno haya kwa kemeo kali: “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja wala pasiwe kwenu faraka; bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana ndugu zangu, nimearifiwa, habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kati yenu. Basi maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na Mimi ni wa Apolo; na Mimi ni wa Kefa, na Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibishwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?” (1 Kor. 1:10-13.) Ni tofauti kubwa ilioje kati ya msimamo uliochukuliwa na mtumwa wa Mungu aliyejazwa Roho, na wanaojidai kuwa mitume wa leo. {SR2: 90.1}

Yesu alisema, “na hayo watawatendea kwa sababu hawajamjua Baba wala mimi.” (Yohana 16:3.) Laiti wanaoitwa eti viongozi wa Kikristo wangalikuwa wakiongozwa na Roho wa Mungu wangeiga mfano uliowekwa na manabii na mitume; basi hapangekuwapo mgawanyiko katika ukweli wa Biblia. Hali ya siku ya leo hakika ni makufuru na inatimiza maneno ya Mwalimu: “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Mat. 24:24.) {SR2: 90.2}

Kwa mtazamo wa mkanganyiko huu mkubwa unaonekana upo ugumu wa kuamua mara moja ni nani aliye sahihi na ni nani aliyekosea. Yesu alisema: “Tena Nawaambia ya kwamba, wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.” (Mat. 18:19.) Haliwezi kuwapo jambo la kumpendeza Mungu kuliko mmoja wa watoto Wake kuomba kwa uaminifu njia ya kweli; kwa hivyo, mtu kama huyo hataachwa gizani: “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” (Mat. 7:7.) {SR2: 90.3}

Iwapo watu wanajali kuupata ukweli, unaweza kufanywa kwa urahisi. Lakini ukweli wa jambo ni kwamba hawajali. Watu wangeridhia kudanganywa kuliko kumuuliza Mungu awaonyeshe ukweli Wake. Naam, wao huomba, lakini sala zao hazisikizwi, kwa maana: “Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo.” (Mit. 28:9.) Wanaoitwa eti Wakristo wa siku ya leo, husema, “Andiko hilo liko katika Agano la Kale na kwa

91

Wayahudi pekee.” Tunafungua Agano Jipya kwa nuru juu ya mada hii: “Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” (Mat. 5:19.) Waaminifu moyoni, kwa mshangao, husikia neno kutoka kwa wenye kudhihaki makafiri wa siku ya leo: “Hiyo haimaanishi sheria ya Mungu; ni amri ya Yesu: Mpende jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.” Kweli, lakini ni ipi kati ya amri hizo kumi ambazo unaweza kuvunja na bado utimize amri za Yesu? Na iwapo unampenda jirani yako, utamkosea heshima Mungu wako? Je! nne za kwanza hazitunzwi kuonyeshwa heshima kwa Mungu; na sita za mwisho kupima upendo wetu kwa wanadamu? {SR2: 90.4}

Yesu alisema: “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.” (Mat. 22:40.) Je! Mwana pekee wa Mungu anafanya kazi kinyume na Baba Yake? “Ufunuo wa Yesu Kristo, Aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi, naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana.” (Ufu. 1:1.) “Hapa ndipo penye subira ya Watakatifu: hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” (Ufu. 14:12.) Je! Yesu hajasema kwamba watakatifu Wake huzishika amri za Mungu? Tena nia ya mwili huzusha pingamizi, “Wanazishika amri za Mungu, na sio sheria.” Lakini Roho anatangaza: “Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi, na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji. Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.” (Yak. 2:9-12.) “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa malango yake.” (Ufu. 22:14.) {SR2: 91.1}

Utunzaji wa amri Zake ni cheti cha kwenda mbinguni. “Na waenende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” (Isa. 8:20.) “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu: kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” (Rumi. 8:7.) “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri Zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.” (1 Yohana 2:4.) Baada ya kupoteza mwanya mmoja wa kishetani, nia ya mwili hushikilia mwingine, ikiwa imeazimia kumtumikia ibilisi na kujidanganya na kwa pua lake hewani yeye hutamka maneno, “Hatupaswi kutunza sheria kulingana na neno ila kulingana na Roho,

92

‘Kwa maana neno huua lakini Roho hupeana uhai.’” Mtazamo wake potovu kuhusu ukweli ulivyo, humwongoza kuamini kwamba kushika Sheria kulingana na Roho lazima apuuze Neno la Mungu lililoandikwa, na kuishika Sheria Takatifu kulingana na njia zake mwenyewe, na katika kupatana na nia yake ya mwili, ikilifanya bure andiko la Yehova mwenyewe (angalia Kut. 31:18), na hivyo kumwinua mfaji juu ya Aishiye milele! Je! ni kukufuru kulioje mtu anaweza kufanya? Tunatoa hapa maelezo mafupi ya mada hiyo. {SR2: 91.2}

Kutunza sheria kulingana na neno ni kujenga ukuta kuizunguka walivyofanya Mafarisayo wenye kiburi. Tunanukuu 1 Yohana 3:15, “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji.” Kwa hivyo, ingawa hatufanyi mauaji na bado tunamchukia ndugu yetu tumeshika sheria bila lawama kulingana na neno, lakini sio kulingana na Roho. Kuzitunza sheria kulingana na Roho kuna maana pana kuliko nia ya mwili inavyoweza kufikiri. Iwapo ni lazima niishike sheria yote, lazima nilishike Neno lote la Mungu katika kila jambo, vinginevyo, nitamdharau Yeye, na nitakuwa muasi wa sheria kama mwana asiyemheshimu baba yake wa duniani, na kuwa na hatia ya amri ya tano katika sheria. {SR2: 92.1}

“Je! Tunaokolewa kwa sheria?” La, hasha! Tunahukumiwa kwa sheria. Kwa hivyo, iwapo kwa makusudi hatulitii Neno la Mungu, tunaanguka chini ya hukumu ya sheria. “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi.” (Ebr. 10:26.) Lakini ikiwa tunapenda haki ya Mungu kama ilivyoonyeshwa katika sheria Yake, na kuamua kulitii Neno Lake Takatifu ambalo linapatikana popote (Biblia au Roho ya Unabii) kulingana na ufunuo wa Roho Wake, basi tunapokea nguvu ambayo inatuwezesha kulitimiza kusudi takatifu, na hivyo dhambi zetu zinafutwa kwa damu ya Kristo, na hivyo tunafanywa huru kutoka kwa sheria na hukumu yake — tunawekwa chini ya neema ya Mungu. {SR2: 92.2}

Ni kweli kwamba watu hupenda kudanganywa, wakijihadaa kwamba wako njiani kwenda mbinguni, ilhali Shetani hupepesa jicho kwa ujinga wao. Neno la Mungu husema: “Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya ukweli itatukanwa …. Lakini hao, kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika upotovu wao. (2 Petro 2:2, 12.) Hili huthibitisha jinsi madhehebu yalivyoanza kuchipuka. {SR2: 92.3}

Jinsi ambavyo imethibitishwa, na kukubalika kwa ujumla kwamba “makanisa saba” ya Ufunuo, sura ya pili na ya tatu, yaliwakilisha historia ya kanisa katika enzi ya Ukristo, ni dhahiri kwamba kanisa hilo liligawanyika katika sehemu saba. Laodekia likiwa la mwisho, nalo pia liko katika hatari ya kuanguka kwa mujibu wa ushuhuda

93

wa Shahidi wa kweli: “Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu.” (Ufu. 3:16.) Mungu ametuma ujumbe baada ya ujumbe kutia nuru kwa Neno Lake lililoandikwa. Zilikusudiwa kusahihisha makosa, kukemea dhambi, na kumrudi mdhambi; lakini viongozi wa kila sehemu walizitupa nje jumbe hizo, na wachache waliokuwa tayari kutoa dhabihu vyote kwa ajili ya ukweli walilazimika kuachana na yale makanisa na kukaza mwendo na nuru. Laiti viongozi wangekuwa tayari kurekebisha makosa yao na kulitakasa kanisa, ingekuwapo tu sehemu moja. Kwa kuukataa ukweli kila sehemu ilijikata yenyewe kabisa kutoka kwa mkono wa nguvu wa Mungu. Kwa hivyo, hakuna hata mojawapo wa makanisa haya limekuwa na nuru ya nyongeza kwa Maandiko isipokuwa ile ambayo ilipeanwa kwao na waasisi wa kila vuguvugu. Ukweli huu hulithibitisha Neno la Mungu la kinabii kuwa sawa, na kadiri sehemu husika ikiwa kongwe hukumu inakuwa kubwa zaidi. Kwa hivyo, makanisa haya yanawakilishwa na “vichwa”; “makufuru” juu yavyo, humaanisha anguko la hivyo vichwa. Iwapo yatakataa mwito huu wa mwisho pia basi ufunuo wa kweli hizi utakuwa dhidi ya hayo makanisa, na utaleta uharibifu wayo wa mwisho. {SR2: 92.4}

Ujumbe kuwahusu watu 144,000, na mwito wa matengenezo yaliyowasilishwa kwa kanisa la Waadventista wa Sabato mwaka 1930 vile vile ulikataliwa. Kwa hivyo, kadiri uongozi wa makanisa hayo kamwe haujawahi kuupokea ujumbe kwa wakati wowote, hakika unatimiza unabii ufuatao: “Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa: tazama, wamelikataa neno la Bwana; wana hekima gani ndani yao? …. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa Bwana: basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.” (Yer. 8:9; 10:21.) {SR2: 93.1}

“Vichwa saba” vya “mnyama kama chui” huwakilisha siri hii ya uovu na unafiki, vikionyesha jinsi kila moja lilianguka katika mtego lilipoufikia. Kwa hivyo, tangu wakati wa Luther na kuendelea, Mungu aliruhusu kwamba mafuriko ya Shetani (wasio waongofu) yawatupe nje watu Wake. Kwa hivyo, Yeye amekuwa akiliita kanisa Lake kutoka kwa vuguvugu moja kwenda kwa lingine. {SR2: 93.2}

Kwa hivyo, wale ambao hushusha kiwango, na kukataa kufanya matengenezo wakati kupiga tarumbeta inapovuma, ndio hasa wale husababisha mgawanyiko katika kanisa la Mungu! “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.” (Rumi. 16:17, 18.)

Kwa sababu historia ya kanisa ni hivyo, na sehemu ya mwisho

94

(Walaodekia) iko katika hali mbaya zaidi, na chini ya hukumu kubwa kuliko yoyote iliyotangulia, na kwa sababu hakuna wakati uliobaki wa kuliita vuguvugu jipya, basi ujumbe wa nuru ya kushangaza na kemeo kali kupitia Neno la Mungu, na udhihirisho wa Hukumu za Mungu, ndio tiba ya pekee ambayo inaweza kuleta uongofu na matengenezo ya kweli. Hivyo kuliandaa kanisa kusimama “bila doa, kunyanzi au kitu kama hicho,” ambalo laweza kunenewa: “Joka akamkasirikia yule mwanamke [kanisa kama mwili] akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” (Ufu. 12:17.) Ni usafi wa kanisa ambao huchochea hasira ya lile joka. {SR2: 93.3}

Haya “Makanisa saba” pia yalifananishwa na “vinara saba vya taa,” na uongozi wa makanisa yayo hayo, kwa “malaika saba.” Kwa hivyo tunasoma: “Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba: na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.” (Ufu. 1:20.) “Na kwa Malaika wa kanisa la Laodekia andika.” (Ufu. 3:14.) Kumbuka kwamba ujumbe umeelekezwa kwa yule Malaika (uongozi), na sio kwa kinara cha taa (kanisa kama mwili.) Kwa hivyo, hukumu ile si kwa kinara cha taa, lakini kwa malaika. “Kwa kuwa wewe wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” (Ufu. 3:17.) Ndugu zangu, hili sio dhidi yenu, kwa maana ni Kristo anayenena aliyewafilia, lakini itakuwa hivyo, ikiwa hamtabadilisha mwenendo wenu wa kutenda. {SR2: 94.1}

Iwapo Kristo kwa kuyakusanya makanisa haya saba katika kundi la vinara saba vya taa na kutoa rekodi chafu kabisa kwa lile la mwisho, Yeye hawaiti Walaodekia Babeli, basi wala ufasiri wa “vichwa” haufanyi hivyo. Si kwa sababu Walaodekia ni bora hivi kwamba hawajaitwa Babeli, kwa sababu rekodi yao ni mbaya zaidi, lakini ni kuonyesha kwamba kwa mujibu wa nuru yao iliyoongezeka, Yeye atashughulika nao kwa njia tofauti. Ni ya kudhihirisha kwamba iwapo “malaika” (uongozi) wa kanisa la Walaodekia ataukataa ujumbe wa “Shahidi wa Kweli,” Yeye hawezi kuwaita watu 144,000 kutoka kati yao kuingia katika vuguvugu lingine kwa mwito wa Ufunuo 18. “Tokeni kwake enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake,” (Ufu. 18:4), lakini badala yake kwa ujumbe wa Ufunuo 7 na Ezekieli 9. Hivyo kuwafungua watu Wake, na kwa haraka “kuimaliza kazi, na kuifupisha katika haki: kwa maana kazi fupi Bwana ataifanya katika nchi.” (Rumi. 9:28.) {SR2: 94.2}

Kutotii Neno la Mungu ni kukufuru, na kukufuru

95

ni unafiki; Hivyo ni kusema, wao si kile wanadai kuwa. Unafiki huficha dhambi zinazopiga kelele chini ya uso wa wema. Dhambi hii ya unafiki ni ngumu kuponywa kwa sababu haigunduliwi kwa urahisi na wanadamu. Hatuwezi kufahamu mioyo ya wengine au kupambanua kati ya vazi la unafiki na maisha ya utakatifu. Udanganyifu wa kiroho una mwanzo wake kutoka kwa kiumbe kingine tofauti na mwanadamu. Kwa hivyo, mpango huo ni wa ujanja sana hivi kwamba hauwezi kutambuliwa kwa uchunguzi wa mwanadamu. Aina hii ya udanganyifu unaweza tu kutambuliwa chini ya uchunguzi wa karibu wa Neno takatifu la Mungu na kwa msaada wa Roho Wake. {SR2: 94.3}

“Njia mwafaka ya kutibu mpango kama huo wa udanganyifu ni imani thabiti kwamba lipo jicho la Mungu anayetazama yote; ambaye huona dhambi popote ilipo, na ataileta hukumuni. Mnafiki anaweza kuficha dhambi yake kwa macho ya wengine na wakati mwingine kwa dhamiri yake mwenyewe lakini kamwe hawezi kuilazimisha kwa Mungu.” Paulo, akitazamia mbele kwa wakati kama huu, asema: “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. (2 Tim. 4:3, 4.) “Basi wewe umfundishaye mwingine, je! hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?” (Rumi. 2:21-23.) Kwa asiyejali na asiye na mwelekeo, Ayubu anatoa maelezo kama ifuatavyo: “Utakula nguvu za mwili wake: naam mzaliwa wa kwanza wa mauti atazila nguvu zake.” (Ayubu 18:13.) {SR2: 95.1}

Hivyo vichwa saba ki-mfano vitaonyesha wazi hayo “maeneo ya juu” yanayotawaliwa na viongozi wasiotakaswa ambao wamejaribu kuchanganya yaliyo matakatifu na ya kawaida, na kukataa kulisikia Neno la Bwana. Namba ya Biblia “saba,” inayomaanisha ukamilifu, kwa kawaida itajumuisha Wakristo wote kwa wakati ule ukweli wa kinabii utafanywa ujulikane. Uasi imani kama huo si jambo la kushangaza katika historia ya watu wa Mungu, kwa wakati na mara kwa mara kanisa limeanguka chini ya mafuriko ya kishetani. Katika siku za Luther hali zilikuwa mbaya kama wakati ambapo kanisa lilimsulubisha Kristo. Iwapo kizazi hiki ni kiovu zaidi kuliko chochote kabla yake, ni nini kinachoweza kulipatia kanisa chanjo kutoka kwa uasi huo? Inakubalika na wanafunzi wengi wa Biblia kwamba lengo la unabii wa aina hii hueleweka tu wakati lengo la kinabii linalotazamiwa limedhihirika kikamilifu. Kwa hivyo, huu ni wakati ambao hizo nembo huzungumza. Walakini, upo upande mwingine kwa hili, ambao kwa huo tutathibitisha kwamba kauli zilizowasilishwa ni kweli. {SR2: 95.2}

96

Kichwa Kimoja Kikatiwa Jeraha La Mauti

Yohana asema: “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” Kwa sababu kichwa kilichojeruhiwa humaanisha pigo la Luther kwa upapa, kuchukuliwa mateka kwa papa katika mwaka 1798 ilikuwa ishara ya ukamilifu wa lile jeraha na ya kwamba kipindi cha kinabii kilikuwa kimeisha. Kwa hivyo kutimiza maneno: “Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka.” (Ufu. 13:10.) Kama upapa ungalikuwa haukupokea jeraha la mauti kutoka kwa Luther, papa asingetupwa gerezani na jemadari wa Ufaransa kwa maana kabla mamlaka ya upapa kupokea upanga wa Luther, papa alitawala kwa nguvu zaidi. Lakini hilo pigo lilidhoofisha nguvu zake, na tokeo lake lilikuwa kwamba Uprotestanti ulikuja kwenye jukwaa la utendaji. Maumivu ya daima yalianza kukikereketa “kichwa,” hadi mwishowe papa akatua gerezani. Udhia uliendelea hadi mwaka 1870, wakati nguvu ya muda ya papa iliondolewa. Hilo likuwa pekecho la mwisho la “kichwa,” lilionyesha kwamba kilikuwa kimeachwa ili “jeraha lake la mauti” lipone. {SR2: 96.1}

Kunukuu maneno ya Luther akielezea jinsi upapa ulivyotiwa jeraha: “Naliweka mbele neno la Mungu; Nilihubiri na kuandika — hayo ndio yote nilifanya. Na bado nilipokuwa nimelala,… neno ambalo nilikuwa nimehubiri liliupindua upapa, ili kwamba hakuna mkuu wala mfalme ameutenda madhara makubwa hivyo. Na bado sikufanya chochote; Neno peke ndilo lililoyafanya hayo yote.” — “Pambano Kuu,” ukurasa wa 190. “Nalianza kazi hii kwa jina la Mungu,” Luther alisema, “itakamilika bila mimi, na kwa uwezo Wake.” — Kimenukuliwa. uk. 142. Mtu awaye yote asiielewe vibaya taarifa ifuatayo maana mwandishi yule yule ameziandika zote mbili. Kwa hivyo itakuwa si haki kupotosha taarifa moja, maana kwa kufanya hivyo tutaitupa nje ya uwiano na ile nyingine. Ikinena kuhusu miaka 1260 tunasoma: “Kipindi hiki, kama kilivyoelezewa katika sura zilizotangulia, kilianza na ukuu wa upapa, mwaka 538 B.K, na kikakoma mwaka 1798. Kwa wakati huo, papa alichukuliwa mateka na jeshi la Ufaransa, na utawala wa upapa ukapokea jeraha lake la mauti, na utabiri ulitimizwa. “Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka!” — Kimenukuliwa, uk. 439. Kumbuka kwamba lengo la mwandishi katika taarifa hii si kusema ni vipi jeraha lilivyopokelewa, lakini ni kuonyesha kwamba kipindi cha kinabii kilikoma na papa kufungwa gerezani, ambacho hakikutimiza maneno, “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti” (Ufu. 13:3), lakini badala yake Maandiko yalinukuu “‘Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka.’” (Ufu. 13:10.) Je! Tutampuuza Mungu na Roho Wake, na kumpa Berthier sifa hiyo, na hivyo kuhalalisha upumbavu? {SR2: 96.2}

Jeraha Lake La Mauti Likapona

“Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote

97

ikamstaajabia mnyama yule.” (Ufu. 13:3.) William Miller alitangaza kipindi cha kinabii cha siku 2300 kabla tu ya mwaka 1844. Unabii huo wa kushangaza ulipelekwa kwa Jumuiya ya Wakristo kwa uwezo mkubwa na Roho wa Mungu. Ingawa viongozi wa makanisa ya jina tu hawakuweza kuupinga ukweli uliotolewa na Miller, waliligeuza sikio wasilisikie fundisho alilofundisha yeye. {SR2: 96.3}

Lakini kwa sababu kuvunjika moyo kulivyokuja mwaka wa 1844 kupitia kutokuelewa kile ambacho kingetukia mwishoni mwa kipindi cha kinabii, vuguvugu lililoundwa na Miller lilifikia mwisho wake. Ujumbe wa malaika wa pili wa Ufunuo 14:8, ulikuwa umetangaza kwamba Babeli (makanisa kabla tu ya mwaka 1844) yalikuwa yameanguka. Yaani ni kusema kwamba Mungu hataruhusu nuru iangaze kwa neno Lake kupitia makanisa haya yaliyoanguka. Laiti Mungu asingekuwa ameliita mbele vuguvugu lingine la Uprotestanti jeraha la mauti lingekuwa limepona kwa wakati huo. {SR2: 97.1}

Kwa vuguvugu lililoitwa na Mungu, na kusaidiwa na maandishi ya “Roho ya Unabii,” kusudi la Mungu lilikuwa kuendelea kulidumisha “jeraha la mauti” kwa “kichwa.” Lakini Neno la Mungu la kinabii husema: “Jeraha lake la mauti lilipona.” Kwa kuwa Neno Takatifu la Mungu hutangaza kwamba jeraha lilipona, na kwa sababu unabii huo hauwezi kuvunjika, ni kweli kwamba jeraha “lilipona.” {SR2: 97.2}

Lakini iwapo Uprotestanti, kwa utiifu wa Neno la Mungu, ndio ulilolitia lile jeraha, basi Uprotestanti wa kweli pekee unaweza kukidumisha kile kidonda kichungu kichwani. Iwapo hilo jeraha limepona, basi ni dhahiri kwamba wale ambao Mungu alikuwa amewapatia ujumbe kwa ajili ya ulimwengu unaopotea wameshindwa kwa njia ile ile jinsi kila vuguvugu limeshindwa tangu ulimwengu ulipoanza. Ni jambo la kushangaza sana kuona jinsi adui wa zamani amefanikiwa kulitia unajisi kanisa katika kila kizazi kupitia uongozi wake. Akili za juu zaidi za mwanadamu zimekuwa daima zikiongozwa makosani na kwa hivyo zimemtumikia Shetani kwa anguko lao wenyewe. Je! Watu wa Mungu hawatafaidika kamwe kwa kweli hizi za kihistoria na za kibiblia? Je! Haya mambo hayajaandikwa ili kutuonya sisi ambao tumefikiwa na miisho ya ulimwengu? Mungu, kwa Neno Lake Takatifu, huamuru: “Mwacheni mwanadamu, ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua lake: kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” (Isa. 2:22.) {SR2: 97.3}

Jinsi ambavyo imekubalika kwamba kutekwa kwa papa mwaka wa 1798 ilikuwa ishara kwamba hilo pigo lilikuwa limekamilishwa, basi kwa vile amepata nguvu yake ya muda inathibitisha zaidi kwamba jeraha la mauti limepona. Kweli hizi haziwezi kukanushwa, kwa maana imekubalika kwamba tukio la mwaka 1798 ni kweli; kwa hivyo lile la mwaka 1929 haliwezi kupingwa. Kwa kuwa hivyo, huu ndio wakati ambao hiyo nembo ya kinabii huzungumza, “jeraha lake la mauti lilipona.” Soma “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, kwa maana hilo gombo lote hushughulikia mada hiyo. {SR2: 97.4}

98

Dunia Yote Ikamstaajabia Mnyama Yule

“Jeraha lake la mauti limepona,” Yohana asema, “na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Kumbuka kwamba dunia ilimstaajabia mnyama na sio kichwa. Kwa hivyo, haliwezi kumaanisha kwamba dunia ingelazimika kujisajili katika ushirika wa mfumo uliowakilishwa na kichwa. Maana yake ni kwamba ulimwengu wote umeshiriki ile roho ya yule mnyama — udunia. Ulimwengu kwa ujumla haujawahi kuwa vinginevyo. Haingewezekana kusema kwamba “dunia yote ikamstaajabia mnyama yule” ikiwa watu ambao Mungu amewakabidhi injili wako huru kutoka kwa roho ya yule mnyama. Lakini lazima iwe kwamba wameisaliti imani yao, na wameshiriki roho yake. I wapi tofauti kati ya kanisa na dunia! {SR2: 98.1}

Jina La Makufuru

“Na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.” Yaani, upinzani kwa ukweli unaojulikana, usemi wa kijeuri usio na kicho na kutomheshimu Mungu, au vitu ambavyo vinachukuliwa kuwa vitakatifu — kudhihaki nafsi na mamlaka ya Mungu. Nabii Isaya, akitazama mbele kwa wakati huu wa udanganyifu wa ujumla, unaoongozwa na wanaoitwa eti waongozi wa kiroho, asema: “Na katika siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja, wakisema tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe: lakini tuitwe tu kwa jina lako, utuondolee aibu yetu.” (Isa. 4:1.) {SR2: 98.2}

Ni ukweli uliokubalika kati ya wanafunzi wa Biblia kwamba makanisa huwakilishwa na “wanawake.” Mwanamke safi — kanisa safi, kama ilivyo katika Yeremia 6:2, Ufunuo 12:1; mwanamke kahaba — kanisa la upotovu, kama ilivyo katika Ufunuo 17:4, 5. Isaya husema, wapo “wanawake” saba. Namba hiyo hujumuisha makanisa yaya haya. Yanasema, “Tutakula chakula chetu wenyewe.” Yaani, wanataka kufuata njia yao wenyewe; hawajali njia ya Mungu (Neno). “Tutavaa nguo zetu wenyewe,” yaani, wanapendelea mipango yao wenyewe badala ya mipango ya Mungu au haki Yake. Kwa hivyo, walijivika mavazi ya haki yao wenyewe. Kusudi lao ni waitwe kwa jina la mtu mume mmoja; Yaani, kwa jina la Kristo (Wakristo) kuondoa aibu yao. Watu wamekuja kudhani wanaweza kufanya jambo lolote chini ya kisingizio cha Ukristo na kutoweka nalo. Mungu atawaacha waendelee na mwenendo wao hadi wao, kama Belshaza, wamevuka mpaka wa neema ya Mungu, na wakati huo Yeye atawaita watoe hesabu. {SR2: 98.3}

“Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake: nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” (Ufu. 13:4.) Swali laweza kuulizwa, Je! Watu wanaodai kuwa eti Wakristo wanawezaje

99

kuliabudu joka? Jibu ni rahisi, na kuliabudu joka kwaweza kuonekana wazi. Mfumo wa sasa wa ibada na taasisi zinazoitwa eti za Kikristo bila shaka ni za kipagani. Kuadhimisha Jumapili, Krismasi, na Pasaka, n.k., kulianzia Babeli ya zamani, kutoka kwa dini ya zamani ya kipagani kwa heshima ya kimungu jua. Wakristo, katika nyakati za kisasa, hudhani wanamheshimu Mungu Aliye Juu zaidi kwa mila za kipagani wakiziita “Mafundisho ya Kikristo.” Uprotestanti umezishika sherehe hizi za kipagani kama mruba kwenye mwili wa mwanadamu. Jinsi konokono hufyonza damu bila kujua kwamba kushiba kwake kutamletea uharibifu, ndivyo ilivyo na waprotestanti na maadhimisho yao ya kipagani, hata wakithubutu kuziita kwa jina la Kristo. Kukufuru kweli kweli! Kila mwanafunzi wa historia ya kale anajua hili kuwa ni kweli; vivyo hivyo kila mwanafunzi wa Biblia anajua sherehe hizi zinazoitwa eti za Kikristo si za kibiblia na vile vile si za kikristo. Iwapo taasisi hizi zilikuwa za Kikristo, au za Kibiblia, bila shaka zingalikuwa zimenenwa katika Biblia. Lakini kwa sababu hazipatikani katika Neno la Mungu, Wakristo ingalikuwa bora waachane nazo wasije wakapatikana wanaliabudu joka. {SR2: 98.4}

Yeremia, akitazama mbele kwa wakati huu wa uasi, asema: “Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo. Maana desturi za watu hao ni ubatili: maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi, na shoka. Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike.” (Yer. 10:2-4.) Ingawa Neno hutangaza, “Msijifunze njia za mataifa,” wanaodai eti ni wachungaji wa injili wataukata mti kutoka mwituni na kuupamba kwa fedha na dhahabu, kisha watathubutu kuiita jina la Kristo — Mti wa Krismasi. Je! Ni kukufuru gani kukubwa ambako mtu anaweza kufanya? Je! Wachungaji na walimu wa dini hawajui mambo haya? Yesu alisema, “Mungu ni Roho: Na wamwabuduo Yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” {SR2: 99.1}

Yohana aliwasikia watu wakimdharau Mungu, wakisema, “Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” Yaani, ni nani anayeweza kuukomesha mfumo huu wa ibada ya kipagani; yuko mmoja? Wanapinga mamlaka ya Mungu. Yawezekana usitamkwe kwa maneno, lakini hudhihirishwa wazi kabisa kwa tendo. Utambuzi wa watu umefishwa na dhambi, na wakati jaribio linafanywa la kushirikisha lililo takatifu na la kawaida au la kipagani, hawaoni uovu. Ingawa Neno la Mungu hutangaza: “Bali katika kila neno tujipatie sifa njema kama watumishi wa Mungu, katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida, katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio na unafiki,

100

katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto, kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema: kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa, kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote. Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa …. Msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa: kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao na kati yao nitatembea; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha, Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” (2 Kor. 6:4-11, 14-18.) {SR2: 99.2}

Ni uasi kwa lililo wazi “Bwana asema hivi” ambao umeleta machafuko na fedheha katika ulimwengu wa Kikristo kwa wakati huu. Kweli wana-matengenezo hawakuyaona makosa haya yote, na hawakuwa na jukumu, kwa maana hawakuwa na nuru kuyahusu. Kwa kadiri Mungu amepeana nuru kwa Neno Lake, kwa viwango, na kufanya iwezekane kufahamu ukweli, Yeye anatarajia tuupokee, na hivyo kutuongoza kwenye ushindi. {SR2: 100.1}

Lakini mtu anaweza kusema, iwapo Mungu anaweza kuwaokoa wengine kwa nuru ndogo, mbona Yeye atupatie zaidi? Kati ya sababu nyingi tutatoa maelezo kwa mbili tu. Kupitia nuru iliyoongezeka kwa Neno, Mungu anaweza kuuokoa umati badala ya wachache. Sababu ya pili ni, kwa sababu sehemu ya mwisho ya kanisa itahamishwa bila mauti badala ya kufufuliwa, tunahitaji nuru ya kutosha kutuandaa kukutana na Mungu na viumbe viishivyo milele. {SR2: 100.2}

Ujinga kama huo kwa Neno la Mungu katika siku za Nuhu uliileta dunia kwa uharibifu wake kwa maji. Hali ya uovu kama hiyo iliipunguza kuwa majivu miji ya Sodoma na Gomora. Iwapo katika siku za Kristo, unafiki kama huo, chini ya taswira ya wema, uliuhitaji uhai wa Mwana wa Mungu ili Uuhifadhi ulimwengu usiangamizwe, matokeo yatakuwaje wakati huu wa sasa? Mungu hawezi kuuangamiza ulimwengu, kwa sababu Yeye ana umati wa kuokoa. Yeye hana Mwana mwingine kuwa zawadi kwa kanisa, kwa maana Kristo ndiye Mwana “pekee” wa Mungu. Ikiwa wazo timilifu la Mungu ni kuibariki dunia kupitia kwa kanisa Lake duniani, na kwa wale ambao wamekabidhiwa injili kwa

101

ajili ya ulimwengu wamewaacha kondoo na wanamtumikia shetani, katika nafsi zao wenyewe, liko wapi tumaini la ulimwengu? Jibu la pekee ambalo laweza kutolewa ni, ole wao wadhambi walioko Zayuni. Mungu atawakusanya kondoo Wake. Atakuwa na kanisa; lakini itakuwa nini thawabu ya wale ambao waliagizwa kuwalisha wana-kondoo nao wanajilisha wenyewe? Kristo, anayeuona mwisho tokea mwanzo, na kwa jicho Lake linaloyaona yote linakazia umakini kwa hali za siku ya leo, amesema: “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, Nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mwovu akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki [pamoja na vichwa vya wanyama]; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” (Mat. 24:45-51.) {SR2: 100.3}

Kutenganisha Magugu Kutoka Kwa Ngano

Petro aliuona wakati ambapo Mungu atalihukumu kanisa: “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” (1 Pet. 4:17.) Je! Utakuwaje mwisho wa yule ambaye haingii katika safina ya usalama, lakini huthubutu kuzuia njia ya wengine? Kwa sababu nabii alipoona siku ya kulipiza kisasi kwa mdhambi ndani ya Zayuni, na Bwana akirejea kutoka kwa mchinjo, aliuliza: “Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Mimi ambaye hunena katika haki, hodari kuokoa .… Maana siku ya kisasi i moyoni mwangu, na mwaka wao niliowakomboa umewadia. Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia, Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza: basi mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu; ghadhabu yangu, ndiyo iliyonitegemeza. Nitawakanyaga watu kwa hasira yangu, na kuwalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nitaiangusha nguvu yao chini.” (Isa. 63:1, 4-6.) {SR2: 101.1}

Ya kuogofya ni siku ambayo hivi karibuni itamwangukia mlinzi juu ya kuta za Zayuni, kwa maana wenye haki pekee watahifadhiwa. “Wale ambao wangeridhia kufa kuliko kufanya tendo baya ndio pekee watakaopatikana waaminifu.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 53. Mtengo wa walio safi kutoka kwa walio najisi umefafanuliwa vyema na Ezekieli. Wale ambao wanastahili

102

kuokoka ule uharibifu watatiwa alama na mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi, baada ya hapo watu watano walio na silaha za kuchinja watalipiga kundi ambalo litaachwa bila alama. Akasema Bwana, “Waueni kabisa mzee na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake: lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Akawaambia, Itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa: haya enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji.” (Ezek. 9:6, 7.) Kwa wakati huu magugu yametengwa kutoka kwa ngano kwa mujibu wa maneno ya Kristo: “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno Nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome: bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.” (Mat. 13:30.) {SR2: 101.2}

Utakaso wa kanisa la Mungu hutia alama mavuno au “Kilio Kikuu” cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu, kwa maana Bwana wa mavuno atangaza, “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno” Ngano iliyokusanywa mwanzoni mwa mavuno na kwa mtengo wa magugu ndani ya kanisa, inaitwa malimbuko ya mavuno. Yohana alipoliangalia kundi hilo alisikia wimbo wa furaha, usioweza kuelezewa kwa vinywa vya wanadamu: “Nao wakauimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee: wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule ila watu mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake; kwa maana ni mabikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, wakiwa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” (Ufu. 14:3, 4.) “Wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule.” Uzoefu tu unaweza kusimulia furaha iliyo ndani ya moyo kwa wakati ambapo umeokolewa kutoka kwa uharibifu wa milele, na kupewa uzima wa milele bila kuonja mauti — kujumuishwa katika vizazi visivyokoma vya milele! — maisha ambayo hupimwa kwa maisha ya Mungu. {SR2: 102.1}

Imani Ndani Ya Wanadamu Ni Mtego Hakika Wa Shetani

Tunaweza kuchunguza nyuma sana kama tunavyotaka na ni hakika kwamba tutagundua kwa mshangao wetu na huzuni, kwamba uongozi wa kanisa umedanganywa sana hivi kwamba katika kila kipindi ulishindwa kutambua ukunjuzi wa chuo; na kadiri umati wa watu uliopofushwa ulijiunga upande wa viongozi waliopotoka dhidi ya ukweli uliofunuliwa, waliligawanya kanisa la Mungu katika sehemu nyingi. Hivyo kwa kuwashinda wakuu wa mbele, Shetani ameweza kuwashughulisha wamfanyie kazi, na kwa hivyo kulipindua kanisa kama kundi. Ili kuhakiki usahihi wa taarifa mbayo imetangulia haitakuwa

103

muhimu kutoa maelezo juu ya kweli zaidi ya ujio wa kwanza wa Kristo. Kwa hivyo, uchunguzi mfupi wa enzi ya Ukristo itazingatiwa hapa. {SR2: 102.2}

Shetani alikuwa ameyapaka kwa “brashi chafu” macho ya akili zenye werevu zaidi za wanadamu mwishoni mwa kipindi cha Agano la Kale. Macho yao ya kiroho yalifungwa plasta kwa ustadi kiasi kwamba hawakuweza kuona mfyatuko wa umeme mwangavu kama jua, katika usiku wa giza nene. Utimizo wa unabii, miujiza iliyozunguka kuzaliwa kwa Kristo, tabia Yake isiyo na doa, kazi Yake isiyo ya ubinafsi na maajabu katika kila hatua, mguso, kutazama na kutenda, kuliyajaza mazingira hayo na upendo wa Mungu. Wanadamu waliokuwa wamekosa hisia za kuona tangu kuzaliwa kwao, walihisi nguvu ya uponyaji ya Yule Asiye na mwisho. Vipofu walimwona Bwana wa utukufu na wakamsifu Mungu, lakini walimu wa dini ya Israeli hawakuathiriwa kwa uwezo uliosogeza hata vitu visivyo hai. Dunia ilitetemeka; na jua likafunika uso wake; miamba ilipasuka na makaburi yakafunuliwa; wafu walifufuka na kumwona Mwana wa Mungu. Lakini Mafarisayo, makuhani, na marabi wenye kiburi, walioheshimiwa kwamba hawakosei kamwe, hawakuweza kuhisi, kuona, wala kusikia. Hakuna ajabu zaidi kuliko ile iliyoandikwa kwa vitendo vya viongozi vipofu wa wakati huo. Yohana, akinena kuhusu uzoefu huo, asema: “Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani: wala giza halikuiweza.” (Yohana 1:4, 5.) {SR2: 103.1}

Yamkini kila mshale wa nuru ilioonyesha kuja kwa “Mwana-Kondoo wa Mungu” ilikuwa imepeanwa kwa watu waliokuwa wamechaguliwa; lakini haikuwafaidi. Yesu alisema: “Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, si giza kubwa hilo!” Laiti uzoefu huu ungeweza kuwaamsha viongozi na watu kwa wakati huu wa sasa kutoka kwa kujiamini nafsi na usalama bandia hadi kwa uchunguzi wa bidii wa ukweli halisi wa Biblia. {SR2: 103.2}

Kanisa la Kikristo la kwanza vivyo hivyo lilivutwa katika vizazi vya giza. Mara tu mitume walipolala Shetani aliwapanga maajenti wake, watu mashuhuri, kuingia ndani ya kanisa. Viongozi waliokuwa tayari wamepofushwa macho waliwekea mikono yao juu ya watu, sio kutoka kwa mtazamo wa uwakfu, lakini wa ukuu, na hivyo kuwafanya wachungaji wa kundi. Katika saa ya giza totoro la kanisa la Kikristo Mungu, kwa mkono wa Luther, aliuita umati wa watu kuwa makini kwa udanganyifu huo wa kutisha, lakini ni wachache ambao walikuwa tayari kumsikiliza mtawa wa kiume mnyenyekevu. Mtu angefikiria kwamba wasomi sana wangekuwa wa kwanza kuiona nuru katika yaliyo wazi “Bwana asema hivi.” Luther, akiwa na mapambano makubwa, na kuhatarisha maisha yake, aliasisi dhehebu la Walutheri. Lakini alipolala, vuguvugu hilo vivyo hivyo lilipotoka na likaganda dhidi ya nuru mpya kwa Neno la Mungu. {SR2: 103.3}

104

Hivyo John Knox alikuja na ukweli wa ziada, viongozi wa kanisa hilo walikataa kupendezwa, kwa hivyo hitaji lilizalisha dhehebu la Kiprestiberi. Uzoefu huu umerudiwa na Wesley, Campbell, Miller, na White. (Angalia “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 32-114.) “Tunayo mengi ya kuhofia kutoka ndani kuliko kutoka nje. Vikwazo kwa nguvu na mafanikio ni vikubwa zaidi kutoka ndani ya kanisa lenyewe kuliko kutoka ulimwenguni.” — Mapitio na Kutangaza, Machi 22, 1887. Iwapo hatari dhidi ya kanisa imekuwa kutokea ndani, kupitia ujasiri katika uongozi uliodanganyika katika kila kizazi, ni nini kitakachobadilisha mambo kwa wakati huu? {SR2: 104.1}

Kweli hizi mintarafu mitego hakika ya Shetani, huvuma na kuvuma tena kwa maombolezo makuu kumwamsha anayelala haswa wakati huu. Sikia sauti ya baragumu: “Jikung’ute mavumbi; amka, uketi, Ee Yerusalemu: jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa.” (Isa. 52:2.) Kuchukia bila sababu, na kuwategemea wanadamu, katika imani ya kuwa na ukweli wote na ya kwamba hakuna hitaji la wowote, imezimeza nafsi nyingi kuliko mtego wowote uliowahi kubuniwa na adui wa wanadamu. Daraja ambalo hupokea maamuzi ya wengine bila kufanya uchunguzi wenyewe, na kukataa kupendezwa kusikia na kuhojiana na Maandiko, wamedanganywa kuhusu ukweli wa sasa katika kila kizazi. “Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima, ya kwamba ni ya ubatili.” (1 Kor. 3:19, 20.) {SR2: 104.2}

Watu ambao huheshimiwa kuwa ni wakuu na ulimwengu, Mungu ni nadra kuwatumia. Kwa jumla, waelimishaji wakuu wa kizazi hiki wana nia ya mwili, kwa hivyo zalisho kutoka kwa shule za wanadamu ni uadui dhidi ya Mungu. “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu: kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” (Rumi. 8:7.) Iwapo Mungu angewatumia, lazima kwanza, pamoja na mtume mkuu, wajikane nafsi. Paulo alisema: “Kuhubiri habari njema: wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa.” (1 Kor. 1:17, 19.) “Basi, ndugu zangu, Mimi nilipokuja kwenu, Sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, Yeye aliyesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu, na hofu, na matetemeko mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu.” (1 Kor. 2:1-4.) {SR2: 104.3}

Mungu alimpeleka Musa jangwani na huko chini ya usimamizi Wake

105

Alimfundisha kwa miaka arobaini — wakati Musa aliacha yote ambayo alikuwa amejifunza katika shule za Misri, wakati huo tu Mungu aliweza kumtumia kuwa chombo cha mkono Wake hodari. Wakati Musa alijihisi kuwa na uwezo wa kuwakomboa Israeli kutoka utumwa wa Wamisri alishindwa; lakini alipojiona mwenyewe asiyejiweza, wakati huo alikuwa na nguvu. Iwapo Mungu apaswa kumpa nuru kubwa mtu aliyejihisi anafaa sana, na kuheshimiwa hivyo na ulimwengu, mwanadamu angejitukuza na kumnyang’anya Mungu utukufu. “Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Ee Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya Uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.” (Mat. 11:25.) Mungu hujifunua Mwenyewe kupitia vyombo na njia ambazo hufikiriwa haba na wanadamu. Kwa hivyo Yeye hufanya muujiza wa kufanya yasiyowezekana yawezekane, akifunua uweza Wake na kumwamsha anayelala kwa nuru na sauti takatifu. Watu wenye ukuu imekuwa nadra kuipokea nuru yoyote kwa Neno la Mungu eti kwa sababu ya thamani ya ukweli wake; daraja hili kwa jumla huupokea ukweli wa Biblia baada ya kuwa maarufu na unapohubiriwa na watu wenye sifa kubwa kuliko wao. {SR2: 104.4}

Akasema Nabii, “Mwacheni mwanadamu, ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua lake: kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” (Isa. 2:22.) “Ni kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wanadamu.” (Zab. 118:8.) Nabii Mika, akitazama mbele kwa wakati huu wa kuufanya mwili kuwa kinga, anasema, “Msimwamini rafiki msimwekee kiongozi tumaini.” (Mika 7:5.) Watu wa Mungu lazima wajifunze kumtegemea Yeye tu, kulingana na “Bwana asema hivi.” Yeye anaweza kutumia chombo cha kibinadamu kueneza nuru, lakini itaangaza kwa Neno la Mungu lisilokosea kamwe. Nuru kama hiyo itaondoa dhambi na kumkemea mdhambi, imwinue Kristo, imtukuze Mungu, na iwashushe watu. “Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana pekee yake, atatukuzwa siku hiyo. Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yeyote aliyeinuka; naye atashushwa chini.” (Isa. 2:11, 12.) {SR2: 105.1}

Shetani anajua jinsi ya kudanganya ili usiweze kugunduliwa kwa urahisi. Yeye hujifunza mwelekeo wa watu, na kitu kinachovutia zaidi yeye hukiweka kuwa mtego. Kwa sababu kizazi hiki kinaamini akili ya kibinadamu na ki tayari kwamba wengine wafikiri kwa ajili yao, Ibilisi atawasilisha kwa daraja hili nafsi ya kustaajabisha zaidi ambayo ulimwengu haujawahi kutazama. Akasema mtume: “Wala si ajabu; maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.” (2 Kor. 11:14.) {SR2: 105.2}

Vyombo vya Mungu vya kuwasilisha nuru juu ya Neno Lake vitakuwa tofauti na vile vya Shetani. Yesu akasema, “Nakushukuru, Ee Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya Uliwaficha wenye hekima na akili,

106

ukawafunulia watoto wachanga.” (Mat. 11:25.) Kwa nabii Isaya, ilifunuliwa kwamba Mungu atawatumia watu wanyenyekevu kuwashusha wenye kiburi: “Kwa maana tazama, Bwana Bwana wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo, tegemeo lote la chakula, na tegemeo lote la maji. Mtu hodari, na mtu wa vita, mwamuzi, na nabii, mpiga ramli, na mzee, jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na msemaji hodari. Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala. Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake: Mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.” (Isa. 3:1-5.) Alisema Yesu. “Basi ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu mdogo, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu anipokea mimi.” (Mat. 18:4, 5.) {SR2: 105.3}

Muhtasari Mfupi Wa Mnyama Kama Chui

Imethibitishwa hapo awali kwamba mnyama kama chui kwa vichwa vyake saba, na pembe kumi ni kiwakilishi cha mfumo wa ulimwengu wote. Wanyama wanne wa Danieli 7; ambao ni simba, dubu, chui, na dubwana walionyeshwa katika maono kama falme nne za ulimwengu wote zikiinuka mmoja baada ya mwingine. Hivyo, unabii na vile vile historia huthibitisha kwamba Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani na Rumi zilichukua nafasi mmoja baada ya mwingine. Mnyororo huu usiovunjika wa miunganisho minne hufanya isiwezekane kupenyeza kati ya yeyote wa wanyama wanne kwa mfumo wa ulimwengu wote. Kwa hivyo, mnyama kama chui lazima aje katika mstari baada ya mnyama wa nne. Kama “pembe kumi” za yule mnyama dubwana ziliwakilisha “wafalme kumi” ambao wangetokea katika ufalme wa Rumi, “vilemba kwa hizo pembe” huthibitisha kwamba mnyama kama chui huwakilisha kipindi baada ya kuanguka kwa ufalme wa Rumi, kwa wakati ambao “wafalme kumi” walipokea ufalme wao. Kwa sababu yeye pia “alitokea Baharini,” ni dhahiri kwamba yeye pia angeumbwa kutoka kwa tokeo la vita. Kwa hivyo kuanguka kwa ufalme wa Rumi kulimzaa mnyama wa tano. Kinywa chake cha simba, miguu ya dubu, mwili wa chui, na pembe kumi, huonyesha kwamba yeye ni mzawa wa Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. {SR2: 106.1}

Alipokifunua kinywa chake kukufuru kwa miezi arobaini na mbili, au miaka 1260, haiwezekani kukataliwa kwamba yeye huwakilisha kipindi cha upapa kutoka mwaka 538 B.K. hadi 1798 B.K. — wakati ambapo kichwa cha upapa kilipokea jeraha lake la mauti. Lakini kama jeraha lake lilikuwa lipone wakati fulani baada ya mwaka 1798, ni dhahiri kwamba yeye pia huwakilisha historia ya ulimwengu huu baada ya kufungwa kwa Papai Pius wa 6 hadi kwa wakati “jeraha lake la mauti lilipona;” hivi vipindi vilizalisha Ukatoliki na Uprotestanti. {SR2: 106.2}

107

Lingekuwa jambo lisilo la busara, na lisilofaa kubuni mnyama huyu wa kinabii iwapo hizo nembo zitashindwa kufunua Uprotestanti jinsi zinavyofanya Ukatoliki. Kabla miaka 1260 kumalizika mwaka 1798, madhehebu manne ya Kiprotestanti yalikuwapo tayari; yaani la Kilutheri, la Prestiberi, la Methodisti, na la Baptisti. Lakini baada ya mwaka 1798 likaja la Waadventista wa Siku ya Kwanza; na la Waadventista wa Sabato kutoka mwaka 1844 hadi 1929 yalikamilisha vichwa vyake saba. Kwa sababu Uprotestanti ulianguka kwa kutangazwa Ujumbe wa Malaika wa Pili baada ya 1844, na jinsi nembo ya Ufunuo 13 mwaka 1930 ilifunua kwamba Waadventista wa Sabato “walimstaajabia mnyama yule” (ulimwengu), matukio haya mawili yaliliponya lile jeraha, na kuandika kukufuru juu ya vichwa vyote saba. Kwa hivyo, utimilifu kamili wa unabii huu wa nembo ulifunua ukweli wa yule mnyama. Kwa vile vijidhehebu vingine vyote ni vichipuko kutoka kwa madhehebu haya saba vichwa vilijumuisha himaya yote ya Ukristo hadi mwaka 1930. Kwa sababu neno la Mungu la kinabii husema, “Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule” (udunia), na sio kukistaajabia kichwa (upapa), humaamisha kwamba wametanga kuufuata ulimwengu na sio kuufuata Ukatoliki. Kutoka katika uasi huu mkuu ujumbe wa Ufunuo 7:1-8, utawatia muhuri na kuwaokoa watakatifu 144,000, kutoka ndani ya kanisa la S.D.A. ambao hawataonja mauti. Lakini ujumbe unaowakilishwa na malaika wa Ufunuo 18, ambaye kwa utukufu wake nchi itaangazwa, atatoa mwito wa kutoka katika ulimwengu “umati mkubwa” wa Ufunuo 7:9. {SR2: 107.1}

Mungu, ambaye ni mwangalifu haswa kwa manufaa ya kanisa Lake kwa kuufunua ukweli Wake kwa watu Wake, amewasilisha kwetu picha zinazoshangaza za matukio ya kihistoria; ambazo ni ushahidi wa upendo wa milele kwa Israeli wateule Wake — malimbuko ya mavuno Yake. Kwa hivyo “Mungu wa Yakobo,” maelfu ya miaka mbeleni, alikuwa ameweka mipango Yake ya kuwasilisha kwa watu Wake kazi ya sanaa ya kinabii yenye mguso mtakatifu. {SR2: 107.2}

108

MNYAMA MWENYE PEMBE MBILI.

UFU. 13:11-18

Yohana alipoyaona maono hayo kwa shauku kubwa, mawazo yake yakaelekezwa kwa kitu kingine cha kushangaza: “Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.” (Ufu. 13:11.) Karibu tu wakati wa hatua ya pili na ya mwisho ya yule mnyama dubwana ulikuwa ukome, utawala mwingine wa kidunia ulikuwa uje juu ya jukwaa la utendaji, kwa mujibu wa yale maono. Ni ajabu kuona jinsi hizo nembo ni sahihi hata kwa wakati wake mwafaka na mpangilio. Mnyama aliye na pembe kama mwana-kondoo (ahadi ya ukuaji) ni nembo dhahiri ya taifa “polepole liliinuka kama kutoka kwa mpango mdogo hadi kwa ufalme wenye nguvu.” “Kama mwana-kondoo,” ni kitambulishi cha serikali iliyoinuka mwaka 1776 B.K. (Tazama “Pambano Kuu,” uk. 439-441.) {SR2: 108.1}

Mnyama huyu amekubalika kama nembo ya Muungano wa Madola ya Amerika. Kwa hivyo, nia yetu si kuleta ukweli unaohusu matumizi yake. Kusudi letu ni, jinsi lilivyoelezwa awali, kwa ufupi kumuunganisha mnyama mmoja na mwingine kwa kutoa nuru juu ya nembo ambazo hazijaeleweka. {SR2: 108.2}

Itakumbukwa kwamba kila mnyama anayewakilisha wakati wa Agano Jipya anazo pembe kumi isipokuwa huyu. Tunasisitiza kwamba pembe kumi husimama kama nembo ya mifumo ya ulimwengu wote. Ukweli huu huthibitisha kwamba yule mnyama mwenye pembe mbili huwakilisha serikali ya mtaa. Kwa sababu tawala za kiraia au serikali hufananishwa na pembe, mnyama huyu haswa akiwa nazo mbili, ni dhahiri kwamba taifa linalowakilishwa kwa nembo hii, litakuwa na muundo maradufu wa serikali. Kama asemavyo Yohana, “Yule mnyama akanena kama joka,” hufichua wazi kwamba itakataa kabisa katiba yake, na uhuru wa raia wake waliopewa na Mungu utatupiliwa mbali. Kwa mujibu wa Ufu. 13:12, utawala huu utaiga mnyama “wa kwanza mbele yake” (sheria ya upapa): “Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake, naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” Iwapo taifa hili kubwa litajitwalia daraka la dhamiri ya raia wake kwa kutunga sheria, jinsi wanavyoweza, au wasivyoweza kuabudu, itakuwa kinyume na vipengele katika katiba yake — kunena kama joka. Kunukuu katiba ya Muungano wa Madola ya Amerika, marekebisho ya kwanza kuhusu maswala ya kidini, husema: “Bunge halitafanya sheria yoyote kuheshimu kuanzishwa dini, au kupiga marufuku zoezi lake la uhuru.” Iwapo nchi hii itatekeleza kabisa marekebisho haya, itaafikiana kabisa na vipimo vya hiyo nembo. {SR2: 108.3}

109

Aya ifuatayo hufichua ukweli kwamba lile joka la zamani litatumia nguvu yake kuwadanganya watu wengi iwezekanavyo: “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga, naye akaishi.” (Ufu. 13:13, 14.) Kwa hivyo atatumia nguvu za mateso na kufanya miujiza. {SR2: 109.1}

Kwa sababu Neno hufunua wazi udanganyifu huu mkubwa, mtu angefikiri kwamba ulimwengu ungefumbua macho yake na kukataa kulogwa na maajabu hayo ya Kishetani. Lakini Shetani anajua kwamba watu ni wasahaulifu kwa Neno la Mungu, na ya kwamba hisia zao husisimka kwa urahisi kwa maajabu yasiyo ya kawaida na unenaji kwa ufasaha wa wanadamu. Kwa hivyo, ataufanya mkamilifu huo udanganyifu na wengi watatumbukia ndani bila kujali maonyo. Akili ya mwanadamu haiwezi kuelewa hiyo nguvu ya ajabu na isiyozuilika ambayo hivi karibuni itaeneza kivuli chake cha kutisha juu ya wakazi wa dunia. Hakuna mwanadamu anayeweza kusimama dhidi ya mfumo huo usio wa kawaida, wa kiraia na kidini. Wale ambao ni wanafunzi wa Neno, wakimtegemea Mungu kwa ukamilifu, na hivyo kwa kujazwa na Roho Mtakatifu, watauepuka mtego huo kuogofya. {SR2: 109.2}

“Wale ambao wangeridhia kufa kuliko kufanya tendo baya ndio pekee watakaopatikana waaminifu.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 53. Usalama wao pekee utakuwa,” Bwana asema hivi.” Lazima wamtazame Mungu kama mkombozi wao wa pekee, jinsi walivyofanya Waebrania watatu katika Babeli ya zamani na kama Danieli katika tundu la simba. Acha matokeo yake yawe yanavyoweza kuwa, watu wa Mungu wanaweza kukingwa tu kwa kuchukua msimamo wa Shadraka, Meshaki na Abednego, kama wakati walipomjibu mfalme: “Ee, Nebukadnezza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto, Naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.” (Dan. 3:16-18.) {SR2: 109.3}

Watu wa Mungu, pamoja na Danieli, wataweza kusema kwa wakati wa kuokolewa kwao: “Mungu wangu amemtuma malaika Wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru: kwa kuwa mbele Yake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena pia mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. (Dan. 6:22.) Katika wakati huo wa majaribu itaonekana wazi ni nani atakayemtumikia Mungu na ni nani ambaye hatamtumikia. Wakati huo wa taabu utawagawanya wakazi wa dunia katika matabaka mawili tofauti, kama kondoo na mbuzi. {SR2: 109.4}

110

“Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” (Ufu. 13:15-17.) {SR2: 110.1}

Amri hii kali ya yule mnyama mwenye pembe mbili itatumiwa na mataifa ya ulimwengu, na sanamu ya yule mnyama, ambayo itadai utiifu kwa muundo wa ibada ya kidini, itasimamishwa kimataifa. Alama ya mnyama ni utunzaji wa Jumapili. Chini ya kisingizio kimoja au kingine, wasiojali na wasio na mwelekeo wataiabudu sanamu ya mnyama, na kuipokea ile chapa. Wale tu ambao wamejiimarisha kwa imani ndani ya Mungu, maarifa ya Neno Lake, na utiifu kwa maagizo matakatifu kupitia utakaso wa moyo kwa nguvu za Roho Mtakatifu, wataweza kuokoka mikongojo ya shetani. Wakati watu wa Mungu wamezuiliwa kununua na kuuza, chanzo chao tu cha riziki kitakuwa kupitia kwa majaliwa ya Mungu. Njia moja au nyingine, kwa muda huo mfupi, Mungu atawaruzuku na kuwatunza watu Wake. Lakini inaweza kuwa katika hali sawia na iliyokuwa katika safari ya nyikani. {SR2: 110.2}

“Wakati umekaribia sana, ambapo, kama wanafunzi wa kwanza, tutalazimika kutafuta kimbilio katika sehemu zenye ukiwa na faragha. Kama kuhusuriwa kwa Yerusalemu na vikosi vya Warumi ilikuwa ishara ya kukimbia kwa Wakristo wa Yudea, hivyo kutwaa mamlaka kwa upande wa taifa letu, katika kutekeleza amri ya Sabato ya upapa, itakuwa onyo kwetu. Basi utakuwa ni wakati wa kuihama miji mikubwa kwa maandalizi ya kuihama ile midogo hadi kwa makao yaliyojificha kati ya maeneo ya milima.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 464, 465. Aya ya 18 ya Ufunuo 13, itafafanuliwa katika somo lingine. {SR2: 110.3}

111

MNYAMA MWEKUNDU SANA.

UFU. 17

“Akanichukua katika Roho hata nyikani: nikaona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.” (Ufu. 17:3.) Mnyama huyu haswa hawezi kuwa nembo ya Rumi kama wengine walivyodhani. Sababu ya kwanza ni, kwamba mnyama dubwana wa Danieli 7, kama ilivyofafanuliwa hapo awali, ni nembo ya Rumi, na alionekana akipanda kutoka baharini; lakini yule mnyama mwekundu sana, Yohana asema, alikuwa jangwani. Kwa hivyo, vikosi ambavyo vilimleta yule mnyama mwekundu sana kwenye jukwaa la utendaji ni kinyume cha vile ambayo vilimleta yule dubwana. {SR2: 111.1}

Sababu ya pili ni, malaika alipokuwa karibu kumwonyesha Yohana maono, alimwambia, “Njoo huku; Nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi.” (Ufu. 17:1.) Kisha Yohana akachukuliwa hadi nyikani na huko akamwona yule mwanamke amempanda mnyama. Sababu ambayo yale maono yametolewa ni kumwonyesha hukumu ya yule mwanamke. Lakini hakuhukumiwa katika siku za Rumi; hukumu yake bado i katika siku zijazo, na itatekelezwa chini ya malaika wa “Kilio Kikuu” wa Ufunuo 18. (Tazama aya ya 8, na 10.) Kumpanda mnyama ndilo tendo lake la mwisho; kwa hivyo, yule mnyama lazima awakilishe kipindi atakachohukumiwa ndani yake. Ipo sababu ya tatu kwa nini yule mnyama hawezi kuwa nembo ya Rumi. Kitabu cha Danieli, na kitabu cha Ufunuo viliandikwa haswa kwa kizazi kinachoishi wakati wa mwisho, na sio sana kwa ulimwengu wa Warumi. (Angalia Dan. 12:4.) Hawakuwa na ufahamu wa maandishi ambayo yalikuwa yanahusu siku za mwisho, na kwa hivyo hayangeweza kuwafaidi. Kwa hivyo, ingekuwa haifai na upumbavu kwa upande wa Mungu kufanya matumizi ya wanyama wote kwa Rumi, na kuacha kipindi ambacho vitabu hivyo vinatumika bila uwakilishi wa nembo. {SR2: 111.2}

Tunaamini kwamba lazima iwepo habari zaidi kamili ya nembo kwa kizazi hiki cha sasa kuliko chochote cha zamani. Kwa hivyo, hazipatani sana na hazina maana kwa wale ambao wamemtumia mnyama “kama chui” wa Ufunuo 13, na “mwekundu sana” wa Ufunuo 17, kwa kuongezea “mnyama dubwana” wa Danieli 7, kama nembo za Rumi. Je! Mbona nembo nyingi za Rumi na sufuri kwa kipindi ambacho vitabu hivyo viliandikiwa? Isitoshe, hakuna kweli za kuunga mkono madai kama hayo. Kemeo kubwa zaidi kwa madai kama hayo asili yake ni somo moja kutoka kwa mnyama mmoja jinsi wao hufanya kutoka kwa mwingine. Iwapo hakuna

112

somo maalum kwa kila mmoja wao, kwa nini wamepeanwa? Kutumia vichwa, wanavyozifanya pembe kuwa alama za serikali, huonyesha kwamba hawakuwa na nuru kutoka kwa Mungu aliye mkuu na mwenye hekima yote. Iwapo kila neno humaanisha serikali, mbona Uvuvio ulitumia nembo zote za pembe na vichwa? {SR2: 111.3}

Kumbuka jinsi ulivyo ukosefu wa akili kutumia mwanamke aliyempanda mnyama, au aliyeketi juu ya vichwa kwa Ukatoliki katika wakati wa Agano Jipya, na vichwa kwa miundo saba mfululizo ya serikali katika kipindi cha Agano la Kale. Malaika akasema: “Vile vichwa saba ni milima saba, anayokalia mwanamke huyo.” (Ufu. 17:9.) Iwapo kanisa la upapa lilikuja kuwapo mwaka 508 B.K., lingewezaje “kukalia” serikali yoyote karne nyingi kabla? Tena, iwapo vichwa vilichukua nafasi ya kila kimoja, uthibitisho u wapi? Je! vyote havipo hapo kwa mnyama na yule mwanamke amevikalia? Kama vile mnyama mwekundu sana kwa pembe zake kumi na vichwa saba huthibitisha kuwa ni wa ulimwengu wote, mnyororo unaofuatana wa wanyama (simba, dubu, chui mwenye vichwa vinne, dubwana, na kama chui) hufanya isiwezekane kwa mnyama mwingine wa ulimwengu wote kupenyeza mnyororo wao usiovunjika wa viunganishi vitano. Tendo kama hilo litakuwa jaribio la kuupindua unabii, na historia. Kwa hivyo, kipindi pekee ambacho chawezekana awakilishe kitakuwa ni baada ya “jeraha la mauti” la mnyama kama chui kupona — kuwa mnyama wa sita wa ulimwengu wote. {SR2: 112.1}

Kwa sababu “mwekundu sana” ni wa mwisho katika mwandamano wa nembo za wanyama, lazima amiliki tabia zote za wazazi wake wa kale. Pembe kumi za mnyama dubwana, vichwa saba vya mnyama kama chui, na vichwa vyake ambavyo havijajeruhiwa, huonyesha kwamba anakuja kwenye jukwaa la utendaji baada ya jeraha la mauti kupona. Rangi yake nyekundu sana humaanisha laana, kama inavyofanya kwa joka (shetani), katika Ufunuo 12:3, na maneno, “aenenda kwenye uharibifu,” (Ufu. 17:11), hufichua kwamba atauleta ulimwengu huu mwisho kwa laana ambayo itasababisha “uharibifu kabisa; maangamizi kabisa; taabu za baadaye au mauti ya milele.” — “Kamusi Wastani.” {SR2: 112.2}

Kwa hivyo, ikiwa mnyama huyu huwakilisha ulimwengu wetu kwa wakati huu, halingekuwa jambo la upumbavu kwa Mungu, kama Yeye angekuwa amepuuza kuona kimbele kuzidishwa kwa vijidhehebu vya siku ya leo, na machafuko makubwa kati ya Jumuiya ya Wakristo, iwapo nembo kwa huyu mnyama zinashindwa kuonyesha hali halisi ya makanisa? Kwa sababu mnyama dubwana huelezea anguko la kanisa katika kipindi anachowakilisha lazima pia yule mwekundu sana. Kwa kweli, hii ndio sababu kuu ya kwa nini wanyama hawa wa kinabii wamewasilishwa. {SR2: 112.3}

Mnyama mwekundu sana ndiye mnyama wa mwisho wa mfano katika mnyororo mwendelevu wa matukio ya kihistoria. Mnyama huyu hapandi kutoka baharini kama wanyama kabla yake, lakini alionekana nyikani. Kwa hivyo, mnyama mwekundu sana ameumbwa kwa

113

tukio la kihistoria tofauti na wanyama kabla yake. Nembo hiyo humaanisha kwamba sio mizozo na vita kati ya mataifa ambavyo humleta mnyama huyu kwenye jukwaa la utendaji, lakini badala yake ni kanuni iliyo kinyume kwa ile nembo — bahari iliyochafuka. {SR2: 112.4}

Anazo pembe kumi na vichwa saba, sawa na yule mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1-3. Tofauti pekee kati ya vichwa vya wanyama hao wawili ni jeraha la mauti kwa yule kama chui. Kwa sababu “jeraha lake lilipona,” ni dhahiri kwamba yule “mwekundu sana” ni endelezo la yule “kama chui” Asema Yohana, “Na jeraha lake la mauti lilipona.” {SR2: 113.1}

Kwa hivyo yule mnyama mwekundu sana ana vichwa saba bila jeraha. Vichwa saba huwakilisha jumuiya ya Wakristo jinsi vinavyofanya kwa mnyama kama chui, lakini ni katika nembo ya yule mwekundu sana, ya kwamba vimeitwa Babeli. Kwa vile yeye amejaa majina na makufuru, huthibitisha ukweli kwamba yeye huwakilisha kipindi cha dhambi iliyozidi. “Mwenye kujaa majina,” humaanisha kipindi cha uzidisho mkubwa wa yanaoitwa eti madhehebu ya Kikristo; “na kukufuru,” kwa sababu ya kukataa ukweli wa sasa, (kukataa kurekebishwa) na bado huthubutu kujiita kwa jina la Kristo (Wakristo). {SR2: 113.2}

Pembe “kumi” humaanisha sawia na kwa wanyama walio mbele yake, kumaanisha mfumo wa ulimwengu wote. Iwapo vichwa vya mnyama kama chui huwakilisha mashirika ya kidini, basi yule (mwekundu sana) hukumbatia ustaarabu wote wa sasa, wa kiraia na wa kidini (pembe na vichwa). Kumbuka kwamba joka la Ufunuo 12:3, lina vilemba kwa vichwa vyake, sio kwa pembe zake. Imefafanuliwa awali kwamba wakati vilemba vinaonekana kwa vichwa, humaanisha mfumo wa kisiasa na kidini. Lakini ikiwa vitaonekana kwa pembe huonyesha kwamba serikali hiyo ni huru kwa kanisa. {SR2: 113.3}

Itagundulika kwamba yule mnyama mwekundu sana hana vilemba, kama yule dubwana wa Danieli 7:7, 8. Zile pembe kumi katika hatua ya kwanza ya yule mnyama dubwana, ziliwakilisha Rumi ya kifalme, hazikuwa na vilemba kwa sababu zilikuwa bado hazijapokea ufalme. Lakini katika hatua yake ya pili (baada ya kuanguka kwa Rumi ya kifalme) kwa uhalisia zilipaswa kuwa zimevikwa vilemba, “pembe ndogo” ikiwa na “macho ya mwanadamu na kinywa kilichonena makuu” (mseto wa pembe yenye kichwa — muungano wa kanisa na serikali — upapa) ukiwa mkuu, pembe hazingeweza kuwa na vilemba, kuonyesha upapa ungetawala juu ya wafalme. Mnyama mwekundu sana pia anadhibitiwa na mwanamke aliyeketi juu ya mgongo wake (kanisa na serikali). Kwa hivyo humaanisha kwamba yeye ndiye mamlaka, au kilemba, kwa sababu anamtawala mnyama. Hii ni mojawapo wa sababu ambazo taji hazipo kwa mnyama huyu. La mwisho ni sanamu ya wa kwanza kuthibitisha ukweli kwamba yule mnyama mwekundu sana huwakilisha kipindi cha “sanamu ya mnyama,” akitimiza Ufunuo 13:12,15: “Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake, naye aifanya

114

dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Akapewa uwezo kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. “ Tofauti kati ya hiyo mifumo miwili mikali hufunuliwa kwa zile nembo mbili (pembe yenye kichwa kwa mmoja, na mwanamke aliyempanda yule mwingine). {SR2: 113.3}

Mnyama dubwana anayo “pembe yenye kichwa” moja tu — nembo ya mfumo wa dhehebu moja kwa muungano wa utawala wa kiraia na imani ya kidini. Lakini yule mnyama mwekundu sana anavyo vichwa saba, ambavyo humaanisha mseto wa madhehebu chini ya mamlaka makuu ya kidini na kisiasa (mwanamke). Yeye huiwakilisha dunia yetu mwishoni mwake, na mamlaka yake makuu na nadharia ya theolojia chini ya ufalme wa “mwanamke”. {SR2: 114.1}

Kipindi kilichowakilishwa na yule mnyama mwekundu sana kilianza mwaka 1929, kwa wakati ambapo jeraha la mauti lilipona. Lakini kazi yake haijastawi kikamilifu hadi yule “mwanamke” atakapoketi mgongoni mwake. {SR2: 114.2}

Mwanzo wa tendo hilo utatiwa alama wakati utabiri unaofuata utakapotimizwa kabisa: “Wakati Uprotestanti utanyoosha mkono wake kuvuka ghuba ili kuufumbata mkono wa nguvu za Kirumi, wakati utakapofika juu ya kuzimu kufumbata mikono na Mizimu, wakati ikiwa chini ya ushawishi wa muungano huu mara tatu, nchi yetu itakataa kabisa kila kanuni ya katiba yake kama serikali ya Uprotestanti na Wana-jamhuri, na itaanzisha njia kwa uenezi wa udanganyifu na upotovu wa upapa, basi tutaweza kujua kwamba wakati umekuja wa Shetani kufanya kazi ya kustaajabisha, na ya kwamba mwisho umekaribia.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 451. {SR2: 114.3}

Ufunuo 17:8, “Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko; na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye yuko.” “Mnyama yule uliyemwona” (mwekundu sana), akasema malaika, “alikuwako naye hayuko.” Kama ilivyofafanuliwa hapo awali, yule mnyama alianza kuonekana kwa jukwaa la historia mwaka 1929. Kwa hivyo, neno, “alikuwako,” huwakilisha kipindi kutoka tarehe iliyotajwa hapo juu hadi wakati ambapo atakuwa, “hayuko.” {SR2: 114.4}

Kipindi kinachowakilishwa na neno “hayuko,” ni miaka elfu ya kufungwa kwa Shetani — millenia: “Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu moja, akamtupa katika shimo la kuzimu, akamfungia humo, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu

115

itimie: na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.” (Ufu 20:2, 3.) {SR2: 114.5}

Kipindi hiki kinaanza na ujio wa pili wa Kristo na mwisho wa dunia hii ya sasa. Wakati huo Andiko la Ufunuo 20:6, litatimizwa: “Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza: juu ya hao mauti ya pili haina nguvu, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.” Wakati wafu wenye haki wanafufuliwa na kuunganishwa na walio hai, basi unabii wa Yeremia utaeleweka kabisa: “Nikaangalia, na, tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele ya Bwana, na mbele ya hasira Yake kali. Maana Bwana asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini Sitaikomesha kabisa.” (Yer. 4:26, 27.) {SR2: 115.1}

Wakati miji imevunjika na nchi kuwa ukiwa, basi tumaini la waliokombolewa litatimilika: “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: Kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani: na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Thes. 4:16, 17.) Kwa wakati huo mtakatifu ambapo watakatifu wataondoka, dunia itaachwa gizani kama ilivyoelezewa na Yeremia: “Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi: kwa sababu Mimi nimeyanena haya, na Nimeyakusudia, wala sitajuta, wala Mimi sitarudi nyuma niyaache. Mji mzima utakimbia kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi na wenye pinde; wataingia vichakani na kupanda juu ya majabali: kila mji utaachwa, hapana hata mtu mmoja atakayekaa ndani yake.” (Yer. 4:28, 29.) {SR2: 115.2}

Wakati huo, ambapo watakatifu wanaingia kupitia malango ya lulu maono ya Yohana yatatimizwa: “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu: nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya Neno la Mungu, na hao ambao hawakumsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao, nao wakaishi wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.” (Ufu. 20:4.) Wenye haki watatumia miaka elfu kuwahukumu waovu waliokufa. Kwa uchunguzi zaidi wa millenia tazama “Wazee na Manabii,” uk. 103; “Pambano Kuu,” uk. 321, 662. {SR2: 115.3}

“Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza…. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vikafunguliwa: na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima: na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa

116

katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” (Ufu. 20:5, 12.) Vitabu husheheni kumbukumbu za waovu; kitabu cha uzima kimefunguliwa na kukaguliwa na watakatifu, na ndani yake huona tu majina ya wenye haki. Majina ya wengine walionekana ndani yake yalifutwa, ilhali majina ya wengine hayakuingizwa kamwe kati ya kurasa zake. {SR2: 115.4}

Tukirejea kwenye mada yetu: “Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.” Kufikia hapa, tumeelezea sehemu ya kwanza ya Andiko lililonukuliwa (aliwako naye hayuko). Sasa tunaangalia maneno, “Naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.” Katika kipindi cha millenia waovu watahukumiwa; na mwisho wake, Kristo na watakatifu watarudi duniani. Yohana anashuhudia hili: “Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” (Ufu. 21:2.) Wakati Kristo na watakatifu na mji unaposhuka, wakati huo, Andiko lifuatalo litatimizwa: “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake: wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” (Ufu. 20:13.) Kumbuka kitenzi, “wakahukumiwa,” kikiwa wakati uliopita, chaonyesha kwamba walihukumiwa kabla ya ufufuo wao. Kwa ufufuo wa waovu, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake kwa “muda mchache.” (Angalia Ufu. 20:3.) Kwa jinsi hii yule mnyama (ulimwengu) “atapanda kutoka kuzimu.” {SR2: 116.1}

Lakini malaika pia alisema, yule mnyama “yuaenda kwenye uharibifu”; yaani, baada ya kupaa. Shetani anafunguliwa kwa muda mchache tu. Yeye na waovu wanaishi miaka mia moja baada ya ufufuo. (“Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, kurasa 164, 165.) Biblia husema kwamba mwishoni mwa miaka mia moja “Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufu. 20:14,15.) Mauti ya pili ya waovu ni kifo cha milele, “nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.” (Obadiah 16.) Akizungumzia maangamizi ya Shetani, asema nabii: “Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia: umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.” (Ezek. 28:19.) {SR2: 116.2}

“Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, naam, wote watendao uovu, watakuwa makapi: na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi, hata haitawaachia shina wala tawi.” (Mal. 4:1.) Kwa jinsi hii yule mnyama atakwenda kwenye uharibifu. (Ufafanuzi wa Webster kwa neno uharibifu ni: “kuangamizwa kabisa; kupoteza nafsi kabisa au furaha katika hali ya wakati ujao.”) {SR2: 116.3}

Imefupishwa kama ifuatavyo: Mnyama “alikuwako” ni

117

kipindi kabla ya millenia; na, “naye hayuko,” ni wakati wa millenia; na “naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu,” ni kipindi baada ya millenia, wakati ambapo waovu wote watafufuliwa na kwenda kwenye uharibifu; yaani, mwishoni mwa miaka mia moja, waovu, Shetani na malaika wake wataangamizwa kwa moto. {SR2: 116.4}

“Na hao wakaao juu ya nchi watastaajabu, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye yuko.” (Ufu. 17:8.) Utakuwa mshangao ulioje kwa waovu watakaposhuhudia umati mkubwa kama mchanga wa bahari kwa idadi, ghafla ukiwa hai. Litakuwa jambo ambalo halijawahi kuingia katika mawazo yao. Kumbuka kirai, “Tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Neno hili hujumuisha waovu wote tangu ulimwengu ulipoanza na huthibitisha hakika kwamba ufasiri huu ni sahihi. {SR2: 117.1}

Ufu. 17:9, “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba, anayokalia mwanamke huyo.” Vichwa vyote kwa wakati mmoja vikiwa vipo kwa mnyama, na huyo mwanamke akiwa amevikalia, huthibitisha kwamba “milima” yote saba lazima iwepo wakati uo huo. Haiwezi kuwa inakuja mmoja baada ya mwingine kwa maana mwanamke anavikalia vyote, kumaanisha muungano mmoja mkubwa kwa ushenga wa yule mwanamke. Huitwa “milima,” jinsi dhehebu la Mungu linavyoitwa “mlima,” katika Isaya 2:2, na Mika 4:1. “Mlima” (umoja) ni dhehebu la Mungu, lakini “milima” (kwa wingi kwa wote wawili Isaya na Mika) hurejelea madhehebu yale yale yaliyowakilishwa na vichwa kwa yule mnyama. Kwa hivyo “vichwa saba ni milima saba.” {SR2: 117.2}

Ufu. 17:10, “Na wako wafalme saba: watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yuko, na mwingine hajaja bado; naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.” Kumbuka kwamba halisemi “nao ni,” lakini “wako.” Kwa hivyo hivyo “vichwa” haviwezi kuwa nembo za wafalme. Wafalme hutawala kwa mpangilio wa kurithi, kwa maana, watano wameanguka, na mmoja yuko, na mwingine hajaja bado. Kumbuka namba ya Biblia “saba,” humaanisha ukamilifu. Kwa sababu yule mnyama pia huwakilisha waovu ambao watafufuka kutoka kwa wafu upande wa pili wa millenia, na ikiwa wote ambao waliishi kutoka kwa Kaini hadi mwisho wa kizazi hiki cha sasa watafufuliwa, basi wafalme saba kuhusiana na yule mnyama lazima watumike kwa historia nzima ya ulimwengu tangu kwa uumbaji hadi mwisho. “Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza, na wa mwisho, Mimi Ndiye.” (Isa. 41:4.) {SR2: 117.3}

Kwa sababu ufafanuzi wa unabii wa nembo unavyoeleweka kwa mara ya kwanza wakati huu, na maadamu unabii kama huo hufunuliwa tu kwa wakati mwafaka, na somo linalopatikana linahusu kizazi hiki cha sasa,

118

basi utabiri huo ni ukweli wa sasa. Kwa hivyo, lazima tuzingatie matumizi ya kitenzi cha Biblia wakati wa zamani na wa sasa. Sheria hii ya sarufi hufuatwa katika Maandiko, na ni njia moja ya kutambua ukweli wa sasa. Usimruhusu adui akukoseshe kwa jambo hili akitumia falsafa au theolojia ya ubatili. Maandiko ni makamilifu ndani yake yenyewe. Tafsiri ya Mfalme Yakobo hutegemewa kama tafsiri yoyote “nzuri.” Uwe mwangalifu kwa maelezo ya tafsiri ambazo wewe mwenyewe hauelewi. Usimwamini mtu. {SR2: 117.4}

“Na wako wafalme saba: watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yuko, na mwingine hajaja bado; naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.” (Ufu. 17:10.) “Mfalme,” ambaye “yuko” lazima aweze kuwa yule aliyepo kwa wakati huu, na yule ambaye “hajaja bado,” lazima awe katika siku zijazo. Kwa hivyo watano ambao “wameanguka,” lazima wawe zamani. Hii itakuwa nafasi ya haki kwa mtu kuchukua bila kulidhuru Neno takatifu la Mungu. Kama inavyorejelea historia yote ya ulimwengu chini ya dhambi, lazima tuzingatie idadi ya falme za ulimwengu wote, au vipindi, tangu ulimwengu ulipoanza. Upo mmoja kabla ya gharika, kama ulivyoelezewa hapo awali; wa pili ni Babeli; wa tatu, Umedi na Uajemi; wa nne, Uyunani; na wa tano ufalme wa Rumi. Hawa watano wameanguka. Yule ambaye “yuko,” ni ustaarabu wa sasa tangu kuanguka kwa Rumi chini ya nembo ya” mnyama kama chui an yule “mnyama mwekundu sana,” hadi mwanzoni mwa millenia, kipindi ambacho huitwa Rumi katika hali yake iliyovunjika iliyowakilishwa kwa nyayo na vidole vya sanamu kubwa ya Danieli 2. Hawa ndio wafalme sita. “Watano wameanguka” na mmoja “yuko.” Yule mwingine ambaye “hajaja bado,” lazima aweze kuwa kipindi baada ya millenia, sambamba na mnyama ambaye atapanda kutoka kuzimu. {SR2: 118.1}

Ni ajabu kuona jinsi Mungu ameionyesha historia ya ulimwengu wetu kwa nembo kamilifu kama hizo, kwa kutumia namba ya ukamilifu katika kila tukio. Kwa hivyo mpango Wake wa kiungu, utawala, na mwongozo kwa watu Wake, umefunuliwa kutoka kizazi hata kizazi. Akizungumzia mfalme wa saba, yule wa baada ya millenia, andiko lasema, “Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache,” sambamba na yule wa Ufunuo 20:3, “Na baada ya hayo yapasa [Shetani] afunguliwe muda mchache.” {SR2: 118.2}

Ufunuo 17:11, “Na yule mnyama aliyekuwako, naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.” Kufunua siri inavyoonekana, yote yaliyo muhimu, ni kuwahesabu wanyama wa kinabii wanaowakilisha vipindi na mataifa. Kuanzia yule mnyama wa kwanza na tunapofunga na wa mwisho, lazima awe “wa nane” na “ni mmoja wa wale saba.” Simba (Babeli) ndiye wa kwanza, dubu (Umedi na Uajemi) ni wa pili; chui mwenye vichwa vinne (Uyunani) ni wa tatu; dubwana (Rumi)

119

ni wa nne; mnyama kama chui (kutoka anguko la Rumi hadi mwaka 1929) ni wa tano; yule aliye na pembe kama ya mwana-kondoo (Madola ya Amerika) ni wa sita; mwekundu sana (kutoka mwaka 1929 hadi mwisho wa dunia hii ya sasa) ni wa saba; yuleyule “mwekundu sana” atakayepanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu (kutoka kwa ufufuo wa waovu hadi kwa mauti yao ya pili), ni wa nane: “Na yule mnyama aliyekuwako, naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.” Yeye ni wa nane, lakini ni “mmoja wa wale saba,” kwa sababu “Yeye alikuwako naye hayuko, naye yuko.” Yaani, yule mnyama mwekundu sana anaonekana kwenye jukwaa la utendaji mara ya pili (kwanza, kabla ya millenia na pili, baada ya millenia, na ufufuo wa pili). Kwa hivyo, yeye ni wa nane, lakini ni mmoja wa wale saba: “Naye aenenda kwenye uharibifu” (mauti ya pili ya waovu.) Rahisi kama ilivyo, hata sasa ni kamilifu zaidi, husimulia ukweli na kurekebisha makosa. Hapa tunaona jozi nyingine ya namba ikijumuisha mnyororo mzima wa wanyama. Joka jekundu katika Ufunuo 12:3, haliwezi kuhesabiwa na hao wanyama wengi kwa sababu hilo si nembo ya taifa au serikali fulani. Hilo humwakilisha Shetani na njama zake kwa wakati fulani, kwa maana huitwa “Ibilisi, na Shetani.” (Ufu. 12:9.) {SR2: 118.3}

Ufu. 17:12, “Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado; lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.” Zile pembe kumi humaanisha sawa sawa na zilizo kwa mnyama dubwana. Kwa vile ustaarabu wa sasa ulijumuishwa katika yule mnyama (ufalme wa Rumi) na kuwakilishwa na zile pembe, ndivyo pia umati wa waovu kwa upande wa pili wa millenia umejumuishwa ndani ya mnyama mwekundu sana hufananishwa na pembe. Kwa hivyo “hawajapokea ufalme bado.” Lakini “wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.” Kirai hiki cha mwisho (saa moja pamoja na mnyama) kitafafanuliwa kikamilifu kuhusiana na somo lingine. {SR2: 119.1}

Ufu. 17:13, “Hawa wana shauri moja, nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.” Wafalme ambao walizaliwa kutoka kwa kifalme wa Rumi wamekuwa kwenye mapigano yasiyokoma na yatakuwa hivyo hadi mwisho. Alisema nabii: “Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu: lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.” (Dan. 2:43.) Lakini kwa kundi lisilohesabika upande wa pili wa millenia haitakuwa hivyo: “Hawa wana shauri moja, nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.” (Ufu. 17:13.) {SR2: 119.2}

Ufu. 17:14: “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana-Kondoo atawashinda: kwa maana Yeye ni Bwana wa mabwana, na Mfalme wa wafalme: na hao walio pamoja Naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.” Shetani ataukusanya umati mkubwa na kuwadanganya

120

mara nyingine tena. Atayakusanya majeshi ya mataifa mwishoni mwa miaka mia moja dhidi ya mji mtakatifu — Yerusalemu mpya, na hivyo kufanya vita na Mwana-Kondoo: “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake, naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu kuwakusanya kwa vita: ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa: Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao wakateswa mchana na usiku hata milele na milele.” (Ufu. 20:7-10.) {SR2: 119.3}

“Wakateswa mchana na usiku hata milele na milele.” Kumbuka kwamba halisemi watateswa, lakini “wakateswa”; Yaani, wanaadhibiwa mara moja milele. “Mchana na usiku,” humaanisha kwamba wataadhibiwa na kuangamizwa kwa njia ile ile kama walioishi kabla ya gharika — kwa kunyesha mvua, “mchana na usiku,” — maji kwa maangamizi ya zamani, na kwa moto ya mwisho. {SR2: 120.1}

Rangi ya yule mnyama (nyekundu sana) hufichua kwamba watu wa Mungu watakuwa wameitwa na ujumbe wa “kilio kikuu,” na kwa hivyo mbali na tofauti kutoka kwa ulimwengu. Kwa hivyo, kumwacha yule mnyama akiwa “mwekundu sana” (ameondolewa wazuri — ametengwa), ishara ya kuwa chini ya hukumu, kuachwa bila udhuru — tayari kuangamia. “Aliyejaa majina na makufuru,” humaanisha kuzidisha madhehebu na unafiki. Slio la sura hiyo litafafanuliwa katika somo lingine. {SR2: 120.2}

121

MWANAMKE ALIYEKETI KWA “MNYAMA,” KWA “VICHWA” NA KWA “MAJI MENGI.”

UFUNUO 17

“Akaja mmoja wa wale malaika saba wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku; Nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi.” (Ufu. 17:1.) Malaika aliyekuwa akiongea na Yohana ni mmoja wa wale saba ambao walikuwa na vitasa saba vya mapigo saba ya mwisho. (Angalia Ufu. 15:7; 16:1.) Itagundulika kwamba alikuwa tayari na kitasa cha pigo, lakini lilikuwa halijamiminwa wakati huo alipomwambia Yohana, “Njoo huku; Nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu.” Kwa habari iliyotolewa, ni hakika kwamba tukio lililotabiriwa kwa hiyo nembo, mwanamke aketiye juu ya yule mnyama, ni la muda mfupi tu kabla ya mapigo kumiminwa na katika wakati ambapo yule “mwanamke” atahukumiwa. {SR2: 121.1}

Ni Nani Mwanamke Aketiye Juu Ya Mnyama?

Sababu ya Yohana kuonyeshwa maono hayo, imefanywa wazi kwa maneno ya malaika: “Njoo huku; Nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba aketiye juu ya maji mengi.” Ufasiri wa malaika kwa yale “maji mengi” umetolewa katika Ufunuo 17:15 “Jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha.” Mwanamke aliyeketi juu yake huashiria kwamba wakazi (maji) walikuwa wameanguka katika mtego wake wa udanganyifu (ameketi juu yao). {SR2: 121.2}

“Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu, naye alikuwa na kikombe kama cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo na machafu ya uasherati wake.” (Ufu. 17:4.) Mwanamke ni nembo ya mfumo wa dini bandia. Kutoka katika kikombe chake hutoa mafundisho ya uongo. Kwa kuwa ni kama cha dhahabu, kina taswira ya utukufu — chavutia. Mavazi yake ya thamani yenye rangi za kuvutia na vito vya thamani hudhihirisha wazi fahari ya huyu mwanamke mwovu zaidi na majivuno yake ya kifalme, na kiburi. Kwa nguvu ya kuvutia kwake, kusikozuilika kwa jicho la mwanadamu, amewashinda watu wenye akili zenye nguvu zaidi — “Ambaye wafalme wa nchi wamezini naye.” Mamilioni wenye nguvu za kiakili, watu ambao huonekana kama majitu miongoni mwa wakazi wa dunia, wameanguka waathirika wasiojiweza katika mtego wake.

122

Wafalme wa dunia wanayo hatia ya ukahaba wa kiroho na yule “mwanamke” (wamelewa kwa mafundisho ya uongo), na hivyo kunaswa katika mitego yake ya kimahaba. {SR2: 121.3}

Shirika lolote linaloitwa eti la Kikristo linalotoa mafundisho ya uongo chini ya mandhari ya wema, kwa udhahiri linathibitiwa kwa nguvu ya yule “mwanamke.” Asili ya mafundisho yote haya ya uongo yanaweza kufuatiliwa nyuma ndani ya kile kikombe kama cha dhahabu. Malaika akasema: “Vile vichwa saba ni milima saba, anayokalia mwanamke huyo.” Imefafanuliwa hapo awali kwamba vichwa ni nembo za yanayojiita eti madhehebu ya Wakristo, na kwa sababu yeye huketi juu yavyo vyote, humaanisha ni muungano wa makanisa chini ya kiongozi mmoja — yule “mwanamke.” Namba ya Kibiblia “saba” hujumuisha mashirika yote kama haya. {SR2: 122.1}

Iwapo makanisa yote kwa wakati huu wa sasa yangeongozwa na Roho Mtakatifu, hayangekuwapo machafuko kati ya yale yanayoitwa eti madhehebu ya Kikristo. Kwa sababu haiwezekani kwa yote kuwa sawa wakati hakuna mawili yanaamini mamoja, ni halali kusema kwamba wale wanaokunywa mvinyo kutoka katika “kikombe cha uasherati wake,” si wachache, kwa maana Uvuvio husema: “Nao wakazi wa nchi wamelevywa kwa mvinyo wa uasherati wake.” (Ufu. 17:2, sehemu ya mwisho.) {SR2: 122.2}

Kumbuka kwamba yule “mwanamke” huketi juu ya “maji mengi,” pia juu ya “vichwa,” na juu ya yule mnyama.” (Angalia Ufu. 17:1, 3, 9.) Kwa sababu haiwezekani kwa mtu mmoja kuketi juu ya vitu vyote vitatu kwa wakati mmoja, nembo za kinabii zaonyesha ulaghai wa kiroho katika vipindi vitatu tofauti. Kwa hivyo Yohana anatangaza: “Nilimwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu sana.” Sio juu ya “maji mengi”, wala kwa “vichwa”. Kabla kumwona, malaika alisema, Mwanamke “aketiye juu ya maji mengi.” Ni yule malaika aliyeongeza, “Vile vichwa saba ni milima saba, anayokalia mwanamke huyo.” (Angalia Ufunuo 17:1, 9) Kwa hivyo, Yohana aliuona unyonyaji wake wa mwisho tu (kuketi juu ya mnyama). Kwa hivyo, hiyo nembo, aketiye juu ya “maji mengi” ni tendo lake la kwanza, kwa mujibu wa hayo maono. {SR2: 122.3}

Kwa hivyo, mafanikio yake ya kwanza (aketiye juu ya maji mengi”), lazima yalikuwa zamani kwa wakati nembo ya kinabii imefunuliwa. Hivyo, kuketi juu ya vichwa yanakuwa mafanikio yake ya pili, na kuketi juu ya Mnyama ndio ya mwisho; kwa wakati ambao anahukumiwa. {SR2: 122.4}

Maadamu makanisa ya Kiprotestanti yanawakilishwa na hivyo vichwa, asingeweza kukaa juu yavyo kabla ya matengenezo, kwa maana vilikuwa bado havijakuwapo. Kwa sababu vichwa ambavyo yule “mwanamke anakalia” havijajeruhiwa, ni dhahiri kwamba nembo ya kinabii itakutana na utimizo wake wakati fulani baada ya jeraha la mauti la mnyama kama chui wa Ufunuo 13:3, limepona. Hiyo

123

nembo, kuketi juu ya vichwa, humaanisha muungano wa makanisa, kwa maana yeye huvikalia. {SR2: 122.5}

Kwa hivyo, wakati Ukatoliki, Uprotestanti, na Imani za Mizimu zinafumbata mikono ya kila mmoja kwa ushenga wa muungano, wakati huo yatanenwa, “mwanamke amekalia vichwa.” {SR2: 123.1}

Nembo ya “mwanamke ameketi juu ya mnyama,” itakutana na utimizo wake wakati hilo shirikisho la kidini ltafanya muungano na tawala za ulimwengu. Tendo kama hilo litaweza kumpa yule mwanamke uthibiti kamili wa mnyama mzima, pembe na vichwa — ulimwengu. Wakati huo Maandishi yafuatayo yatapata utimilifu wake: “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule.” (Ufu. 13:16, 17.) {SR2: 123.2}

Kwa hivyo nembo ya “mwanamke” aketiye juu ya “maji mengi,” huwakilisha kipindi kabla ya matengenezo. Hii ilikuwa kweli wakati wa ubabe wa upapa, maana kwa wakati huo upapa ulitawala ulimwengu wa Warumi — “jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha.” Kwa hivyo yule “mwanamke” aliketi juu ya “maji mengi” wakati wa miaka 1260 ya unabii ya Danieli 7:25, lakini bado atavikalia “vichwa,” na juu ya “mnyama” huyo. Laiti angalikuwa alimkalia yule mnyama dubwana badala ya “maji mengi,” ingekuwa nembo kwa njia isiyo sawa, kwa maana, yule “mwanamke,” kwa chombo cha Ukatoliki, hakuutawala ulimwengu wote (mnyama), lakini juu ya “jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha” (maji mengi). Kwa hivyo, ile nembo, “kukaa juu ya mnyama mwekundu sana,” humaanisha mfumo wa kimataifa wa kidini na kisiasa. {SR2: 123.3}

Ni Kwa Muda Gani Mwanamke Amekuwapo?

Swali hili linaweza kujibiwa kwa Maandiko yafuatayo: “Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona, nikastaajabu ajabu kuu.” (Ufu. 17:6.) Kwa kweli hili laweza kusemwa kulihusu kanisa la Rumi, kwa sababu, liliwatesa Wakristo na kuwaua. Kwa hivyo, yeye “amelewa” kwa damu yao. Ukweli, kanisa la Rumi limekuwa na uhusiano usio halali na yule “mwanamke”; lilikuwa na limelewa kwa mvinyo wa uasherati wake. {SR2: 123.4}

Huyo “Mwanamke” hakuanzishwa na kanisa la Rumi, lakini badala yake alilizalisha kanisa hilo. Kwa hivyo, lazima tutafute kurudi nyuma uwepo wake zaidi ya mwanzo wa upapa. Ufunuo 18:24, huangaza nuru kwa mada hii: “Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.” Neno takatifu la Mungu hutangaza kwamba yule “mwanamke”

124

ana hatia ya damu ya wafia-imani katika vizazi vyote. Kwa hivyo, yule “mwanamke” amelewa kwa damu ya Abeli, na kwa hivyo damu ya wafia-imani “wote” hupatikana ndani yake; akithibitisha kwamba Kaini alikuwa mteja wake wa kwanza kwa kutoa kafara bandia (fundisho la uongo), na kwa kumuua kaka yake. {SR2: 123.5}

Wako wengi sana wanaojiita eti Wakristo, ambao kama Kaini, husema, “Hakuna tofauti yoyote; kitu kimoja ni kizuri na kingine.” Lakini Mungu hapokei mbadala na si dini ya mwanadamu. Hiyo ambayo hekima ya mwanadamu imebuni, ni haki ya mwanadamu, na si haki ya Kristo. Kwa hivyo, ni chukizo machoni pa Mungu. Uzi wa mwanadamu wa utiifu kwa mahitaji ya Mungu ukiwa umedhoofishwa, na maelekeo ya dhambi kuimarishwa kutoka kizazi hadi kizazi, maumbile ya mwanadamu hayawezi kuwa bora wakati huu wa sasa kuliko wakati wanafunzi walipomuuliza Yesu: “Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?” Watajiitao eti Wakristo, kama Mafarisayo, huchukizwa wanapoambiwa makosa yao, na kukemewa dhambi zao. “Akajibu akasema, kila pando asilolipanda Baba Yangu wa mbinguni litang’olewa. Waacheni: hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.” (Mat. 15:12-14.) {SR2: 124.1}

“Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la Siri, Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba na Machukizo ya Nchi.” (Ufu. 17:5.) Mwanamke aliyempanda mnyama ndiye mama. Vichwa saba kwa yule mnyama ni nembo za binti zake (makahaba). Ukatoliki ni binti yake wa kwanza katika nembo hii, na kama Uprotestanti ulivyoibuka kutoka kwa Ukatoliki, basi, Uprotestanti uasi-imani kwa kuzidishwa madhehebu, ni binti zake pia. Au inaweza kusemwa, yule mwanamke “ndiye mama wa Ukatoliki, na Ukatoliki ndiye mama wa Uprotestanti. Asema Wa-ufunuo: “Nikaona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru.” (Ufu. 17:3) Kwa hivyo idadi ya “vichwa,” na “kujaa majina,” hujumuisha vichipuko vyote kutoka kwa Uprotestanti na Ukatoliki. Kama hakungalifanywa mtajo wa “kujaa majina,” zaidi ya saba, na “mwekundu sana,” rangi ambayo humaanisha kwamba watu wa Mungu wameitwa kutoka kwake, kwa hivyo, “mwekundu sana” — ameondolewa wazuri — chini ya laana tayari kuangamia, namba ya Kibiblia “vichwa saba,” ingejumuisha pamoja na wale ambao wanapeleka ujumbe wa Mungu ilivyokuwa katika kipindi cha mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1, kwa wakati jeraha lake la mauti lilipona. Kwa hivyo, isingalikuwa imeruhusu kanisa ambalo “huzishika amri za Mungu, na kuwa na Imani ya Yesu,” na kwa hivyo ingekuwa inapingana na Andiko lifuatalo: “Joka akamkasirikia yule mwanamke [kanisa la Mungu], akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake

125

waliosalia [Israeli wa kweli — watu 144,000], wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.” (Ufu. 12:17.) {SR2: 124.2}

Mungu hajawahi kuwa na vuguvugu zaidi ya moja kwa wakati mmoja na haiwezi kuwa vinginevyo sasa, kwa maana Kristo hawezi kugawanyika. (Angalia 1 Kor. 1:13.) Kanisa la Mungu limetiwa alama vyema katika kila kizazi kwa utiifu ili kuwasilisha ukweli. Jambo lenyewe hulithibitisha dai hilo kuwa kweli kwa sababu liko kanisa moja pekee katika kipindi cha yule mnyama ambalo lina “Roho ya Unabii” na amri zote kama zilivyoandikwa na kidole cha Mungu. Alisema Yesu: “Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” (Mat. 5:19.) Ni kanuni hii takatifu ambayo itaugawanya ulimwengu katika madaraja mawili — amri za Mungu na mila za wanadamu. “Na mataifa yote watakusanyika mbele Yake; Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi: Atawaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto.” (Mat. 25:32, 33.) {SR2: 125.1}

126

PEMBE KUBWA SANA YA DANIELI 8:9

“Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume mwenye pembe mbili: na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu ilizuka mwisho. Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake. Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi. Na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbil: na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake, bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga: wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake. Na yule beberu akajitukuza sana: na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni. Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.” (Danieli 8:3-9.) {SR2: 126.1}

Malaika akimpa Danieli ufasiri anasema: “Yule kondoo mume uliyemwona mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Na yule beberu mwenye manyoya mengi ni mfalme wa Uyunani: na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake. Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.” (Danieli 8:20-23.) {SR2: 126.2}

“Na wakati wa mwisho wa ufalme wao [migawanyiko minne ya Uyunani], mfalme wa uso mkali … atasimama.” Andiko hili hutumika kwa ufalme wa Rumi, kwa maana mfalme huyu lazima asimame mwisho wa utawala wa wafalme wa Uyunani. Wa Ptolemi ulikuwa wa mwisho wa ile migawanyiko minne ya Uyunani kuanguka chini ya ubabe wa ufalme wa Rumi. Pamoja na kushindwa kwa Antonio, na kifo cha Kleopatra karibu mwaka 27 K.K., utawala iliojulikana wa Ptolemi ulifika kikomo, na Misri ikawa mkoa wa

127

taifa la Rumi. Yeye alipaswa kusimama “wakati wakosao watakapotimia.” Wayunani hawajawahi kuwa chochote ila wakosao; kwa hivyo, hiyo nukuu yaweza kutumika kwa taifa la Kiyahudi pekee, kwa wakati ambao watu waliopewa neema ya Mungu wangekuwa wamezidi kumbukumbu yoyote ya hapo awali ya ufisadi wa maadili na wa Kiroho. Taifa la Wayahudi lilifikia hali hiyo wakati wa ubabe wa Rumi, na ujio wa kwanza wa Kristo. Kwa hivyo, mfalme huyu wa “uso mkali” ni ufalme wa Rumi, baada ya “wakosao” (Wayahudi) kufikia “ukamilifu” wao. {SR2: 126.3}

Mamlaka Ya Rumi Si Yake Wenyewe; Afahamuye Mafumbo

“Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe: naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo, naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu. Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama: naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu, lakini atavunjika bila kazi ya mikono.” (Danieli 8:24, 25.) {SR2: 127.1}

“Afahamuye mafumbo,” na “nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe.” Ustawi wake unafanikishwa kwa amani; basi, ikiwa ni kwa amani, Andiko haliwezi kuwa na marejeleo ya tamaa ya kushambulia maeneo. Uwezo wake ulipaswa kuelekezwa dhidi ya watu watakatifu (Wakristo). “Naye atasimama pia dhidi ya Mkuu wa wakuu” (Kristo). {SR2: 127.2}

Ili mwanadamu apate kufahamu mafumbo, lazima atumie nguvu zisizo za kawaida, na nguvu hizo haziwezi kuwa zake mwenyewe. Swali lajitokeza ni wapi alipata nguvu zake nyingi. Iwapo shambulio lake litakuwa dhidi ya Kristo na watu Wake, haitakuwa vigumu kutambua aina ya nguvu ambayo atatumia. Walakini, Yohana anatupa chanzo cha nguvu hii ya ajabu. {SR2: 127.3}

“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili: naye alikuwa ana mimba akilia, hali ana utungu, na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake ulikokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi: na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo limle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma: na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti Chake cha enzi.” (Ufu. 12:1-5.) {SR2: 127.4}

128

[Kielezo: Historia ya Dunia katika Nembo za Kondoo Mume na Beberu]

129

Mwanamke ni nembo ya kanisa la Mungu; taji ya nyota kumi na mbili ni mamlaka au serikali yake (mitume kumi na wawili), na mtoto ni Kristo. Katika aya ya tisa tunaambiwa kwamba joka ni “Ibilisi, na Shetani.” Ilikuwa chini ya umbo la Herode kwamba joka lilisimama mbele ya yule mwanamke tayari kummeza mtoto wake mara tu azaapo. {SR2: 129.1}

“Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto mchanga na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata Nikuambie neno: kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.” (Mat. 2:13.) {SR2: 129.2}

Kwa hivyo, nguvu ambayo Rumi ilitumia katika ukatili wake dhidi ya “watu watakatifu na Mkuu wa wakuu” ilikuwa nguvu ya joka la zamani, na kwa hivyo wafalme wa Rumi “hufahamu mafumbo” ambayo kupitia kwayo, ibilisi, alikuwa ameazimia kumwangamiza Kristo na wafuasi Wake. (Fuata chati kwa ukurasa wa 128). {SR2: 129.3}

Pembe Hufichua Yale Ambayo Mnyama Hushindwa Kufichua

Kwa sababu Umedi-Uajemi na Uyunani kila mmoja huwakilishwa na nembo mbili — Umedi-Uajemi kwanza na kondoo mume, na pili na dubu; na Uyunani kwanza na mbuzi na pili na mnyama kama chui mwenye vichwa vinne, kwa hivyo Rumi iliwakilishwa kwanza na pembe kubwa sana kwa beberu, na ya pili na mnyama dubwana. Hatua ya kwanza ya yule mnyama wa nne huwakilisha Rumi ya kifalme, lakini hatua ya pili, baada ya pembe zake tatu kung’olewa kabisa, hufafanua Rumi ya upapa. (Tazama kurasa 56-59). Mnyama anayewakilisha Rumi ya kifalme hatoi habari nyingi kuhusu muundo wa serikali ya Rumi, lakini lile ambalo halijafunuliwa na huyo mnyama linawekwa wazi na ile pembe kubwa sana ya beberu. Kwa hivyo, lazima tuangalie nguvu na mwenendo wa ile pembe kubwa sana. {SR2: 129.4}

Ikaliangusha Chini Jeshi Na Nyota

Asema Danieli: “Na yule beberu akajitukuza sana: na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni. Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile na ya nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu yake Aliye Mkuu wa jeshi hilo.” (Dan. 8:8, 10.) {SR2: 129.5}

“Jeshi la mbinguni” haliwezi kumaanisha taifa la Wayahudi wakati huo kwa sababu Wayahudi walikuwa wamewaua manabii, na walikuwa wameukataa ujumbe ambao Mungu alikuwa ametuma kupitia kwa watumwa Wake wanyenyekevu, hata kusiwe na kuponya. Kwa hivyo walikuwa bila nabii tangu wakati wa Malaki. Laiti wangalitii sauti ya Mungu kupitia wajumbe

130

Wake, Yeye asingaliwaacha waanguke chini ya nira ya Rumi. {SR2: 129.6}

Wayahudi walifikiri jinsi ambavyo Wakristo wengi hufanya kwa wakati huu. Walichukua msimamo kwamba walikuwa wenye hekima na walipendelewa na Mungu, hata ingawa walikuwa wamekataa kila mshale wa nuru, na walidharau kabisa kusihi na rehema za Yehova. Mtazamo wao mpotovu kwa ukweli wa Mungu, na chuki dhidi ya nuru kwa neno la Mungu, iliwapora hekima na maarifa ya Aliye juu hadi mwishowe wakaongozwa kwa dhambi ya kutisha na hukumu. Walipokataa ujumbe waliopewa na mitume kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, walitenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, na hapo wakafunga njia pekee ambayo kwayo Mungu angeweza kusema nao. {SR2: 130.1}

Kwa hivyo, Wayahudi, chini ya laana kama hiyo, hawangeweza kuitwa “jeshi la mbinguni,” na sio “nyota” hata kidogo. “Naam ikajitukuza hata juu yake Aliye Mkuu wa jeshi hilo.” (Dan. 8:11.) “Mkuu” ni Kristo, na “jeshi” ni Wakristo. Haya ni matumizi pekee sahihi ambayo yanaweza kufanywa kwa huo usemi. {SR2: 130.2}

“Nyota” sio wengine isipokuwa mitume, kwa sababu waliwakilishwa na taji ya mwanamke wa Ufunuo 12:1. Kwa hivyo, “nyota” zilizoangushwa chini zinalenga mitume, na “jeshi,” kwa Wakristo baada ya kusulubishwa kwa Kristo, wakati Rumi, pamoja na Wayahudi, waliwatesa na kuwaua kwa sababu ya imani (“kuangushwa chini”). “Naam ikajitukuza hata juu yake Aliye Mkuu wa jeshi hilo”; yaani, utawala wa Rumi ulijiinua dhidi ya Kristo — Mkuu wa Wakristo. {SR2: 130.3}

Ya Kila Siku Na Patakatifu Pakaangushwa Chini

“Ikamwondolea sadaka ya kila siku, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake dhidi ya sadaka ya kila siku kwa sababu ya makosa, nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda na kufanikiwa.” (Dan. 8:11, 12.) {SR2: 130.4}

Roho ya Unabii, ikitoa maelezo kwa andiko hilo, husema: “Basi nikaona kuhusiana na ya ‘kila siku’, Danieli 8:12, kwamba neno ‘dhabihu’ liliongezwa kwa hekima ya mwanadamu, na ni bayana si sehemu ya maandiko hayo.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 74. Hili likiwa ni kweli, lazima tulipuuze lile neno “dhabihu,” lakini tulishikilie la “kila siku,” ingawa neno “dhabihu” limeandikwa kwa mlazo, kuonyesha kwamba liliongezwa, maono yalitolewa kuhusiana na hayo maandishi, na kufanya dhahiri kwamba ukweli muhimu umehusishwa katika maneno ya “kila siku,” na “patakatifu.” Lolote liwalo ya “kila siku,” iliondolewa na “Pembe Kubwa Sana.” {SR2: 130.5}

Katika Danieli 11:31, kumbukumbu imefanywa kwa tukio lilo hilo:

131

“Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu ndiyo ngome, nao wataondoa dhabihu ya kila siku, …watalisimamisha chukizo la uharibifu.” {SR2: 130.6}

Hiyo aya ambayo imenukuliwa inaweka wazi wazo kwamba ya “kila siku” na “patakatifu” lazima yawe ni sehemu ya ukweli wa Mungu. Wazo hili haliwezi kupotoshwa bila kuyadhuru Maandiko. Kumbuka lugha iliyotumiwa: “Nao watapatia unajisi mahali patakatifu ndiyo ngome, nao wataondoa ya “kila siku.” Baada ya kupatia unajisi “patakatifu” na kuiondoa ya “kila siku,” kisha linasema: “Watalisimamisha chukizo la uharibifu” Yaani ni kusema: “Patakatifu” na ya “kila siku” vilibadilishwa na lile chukizo. Chukizo lazima liwe taasisi fulani ya kidini ya Wapagani, na ya kwamba fundisho la kipagani (“chukizo”) lilipaswa lifanye ukiwa. Yaani ni kusema, liliharibu “patakatifu,” ya “kila siku,” na “ukweli”; au kama ilivyoonyeshwa katika Danieli 8:13, “Kukanyagia chini ya miguu.” “Na ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.” (Dan. 8:12.) {SR2: 131.1}

Yesu, akizungumzia tukio hilo hilo, husema: “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye, na afahamu.”) (Mat. 24:15 .) {SR2: 131.2}

Yesu huita ya “kila siku” na “patakatifu,” “mahali patakatifu.” Hakuna hekalu la Kipagani ambalo Bwana angeita “mahali patakatifu,” wala haliwezi kutiwa unajisi, kwa maana siku zote limekuwa najisi. Hakuna ya kila siku ya kipagani inayoweza kuwa takatifu. Kwa hivyo, ya “kila siku” na “patakatifu” lazima vishikilie ukweli muhimu kwa kanisa la Kikristo, na nabii alitangaza kwamba lilikuwa “likanyagiwe chini ya miguu.” Neno “dhabihu” kuhusiana na ya “kila siku” lilionyeshwa kuwa liliongezwa kwa hekima ya mwanadamu, kama lilivyoelezewa hapo awali. Ilionyeshwa pia kwamba neno ya “kila siku” ni sahihi. Kwa hivyo, haliwezi kuongezewa neno lingine; lazima libaki jinsi lilivyo. {SR2: 131.3}

Wakati Danieli alikuwa akiangalia kwa uangalifu tukio hilo katika maono, husema: “Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya ya kila siku, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini kukanyagisha patakatifu na jeshi? Naye akanambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Dan. 8:13, 14.) {SR2: 131.4}

Kipindi cha kinabii cha siku 2300 (miaka), ukweli unaojulikana vyema wa Biblia, ulifundishwa kwanza na William Miller kabla tu ya mwaka 1844. Kwa hivyo, hatutatoa ufafanuzi wake hapa. Inatosha kusema kwamba kipindi kirefu cha kinabii kilimalizika mwaka 1844. Swali liliulizwa na mtakatifu mmoja, Je! Haya maono katika habari ya

132

ya kila siku, patakatifu na jeshi? Kisha linajibiwa na mtakatifu mwingine, “Hadi siku elfu mbili na mia tatu.” Ni lazima tu kubainisha ni kweli gani mbili muhimu zilizoletwa kwenye nuru katika mwaka 1844, na tutakuwa na ukweli wa kile kinachomaanisha ya “kila siku” na “patakatifu.” Hujielezea zenyewe katika maneno na wakati — ukweli wa Sabato na Patakatifu, jinsi zilivyofundishwa kwa pamoja katika mwaka 1844 B.K. {SR2: 131.5}

Fundisho la Sabato ndio ukweli pekee wa Biblia katika kipindi cha Ukristo ambao unahusiana na siku halisi, kwa hivyo, huitwa ya “kila siku.” Neno “kila siku,” katika Kiebrania na Isaka Leeser hutafsiriwa “daima.” Kwa hivyo linathibitisha wazi kwamba Sabato (fundisho la ya kila siku) ni ukweli wa daima na wa milele. {SR2: 132.1}

Kwa sababu Sabato (ya kila siku) ilipoondolewa, na “chukizo kusimamishwa,” basi hicho ambacho kilichukua nafasi ya Sabato Takatifu, na ukweli wa Patakatifu, kinaitwa “chukizo.” Kwa hivyo utunzaji wa Jumapili na ukuhani bandia ndio vitu pekee ambavyo neno “chukizo” laweza kutumika, kwa maana siku ya saba ilibatilishwa na siku ya kwanza ya juma, Jumapili — “chukizo linalofanya ukiwa.” Yaani, Sabato ilisahaulika, au “kutupwa chini,” hadi mwaka 1844, pamoja na ukweli wa patakatifu. Maadamu ukweli mintarafu ibada ya patakatifu “ulivyotupwa chini,” (ukweli wa ukuhani wa Kristo katika hekalu la mbinguni), ukuhani wa Upagani, au Upapa, jinsi unavyoitwa sasa, ulisimamishwa, na hivyo kuondoa kutoka katika kanisa kazi ya kweli ya upatanisho ya Kristo. Ukweli wa patakatifu, pamoja na Sabato, uliletwa nuruni mwaka 1844, wakati ambapo hukumu (kuondoa dhambi) ilianza katika hekalu la mbinguni, ikitimiza unabii ufuatao: {SR2: 132.2}

“Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye Mzee wa siku ameketi, mavazi Yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa Chake kama sufu safi: kiti Chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu Zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake: maelfu elfu wakamtumikia Yeye, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” (Danieli 7:9, 10.) {SR2: 132.3}

Kwa utimilifu wa unabii huu, ujumbe wa malaika wa kwanza ulitangazwa: “Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja.” (Ufu. 14:6, 7.) Huu ni ukweli mwingine unaojulikana wa Biblia. (Soma “Pambano Kuu,” uk. 352-356.) {SR2: 132.4}

133

Kweli za patakatifu na Sabato zilirejeshwa mahali pazo sahihi mwaka 1844. Lakini swali kuhusu ni wakati gani mafundisho haya mawili matakatifu “yaliangushwa chini,” au “kukanyagishwa chini ya miguu,” bado lapaswa kujibiwa. Malaika, akizungumza na Danieli mintarafu wakati huo, akasema: “Na tangu wakati ule ambapo dhabihu ya kila siku itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini. Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.” (Dan. 12:11, 12.) {SR2: 133.1}

Itagundulika kwamba hakuna baraka iliyotamkwa wakati wa kikomo cha siku (miaka) za kinabii 1290, lakini kuna baraka maalum iliyoahidiwa kwa wale watakaosubiri hadi siku (miaka) 1335 zitimie. Kwa hivyo, mwisho wa miaka 1335 ya “kila siku” (Sabato) ilipaswa kurejeshwa, na baraka ni kwa wale ambao wataishi kuanzia wakati huo, iwapo wataelewa na kuupokea ukweli wake. {SR2: 133.2}

Ili kubainisha wakati wa kinabii ambapo Sabato ya siku ya Saba (ya “kila siku”), na “kweli” (“patakatifu”) ilikanyagishwa chini ya miguu, na utunzaji wa Jumapili na ukuhani wake wa Upagani ulisimamishwa badala yake, itakuwa lazima kuondoa miaka 1335 kutoka 1844, ambayo itaelekeza nyuma kwa mwaka 508 B.K., (kwa mujibu wa kalenda ya Kiebrania). Katika mwaka huo Kweli za ya “Kila Siku” (Sabato) na “Patakatifu” “ziliangushwa chini,” na “Chukizo” (Jumapili) “kusimamishwa.” {SR2: 133.3}

Ili kuelewa ukweli wa miaka (“siku”) 1290, ongeza takwimu hii kwa 508, ambayo inaelekeza mbele kwa mwaka 1798 B.K. kwa wakati ambapo siku za kinabii 1260 za Danieli 7:25 zilikoma na kuwekwa gerezani Papa Pius wa 6. Kwa hivyo, “jeshi” kukanyagishwa chini ya miguu kinabii kulikoma mwaka 1798, lakini kweli za “patakatifu” na ya “kila siku” hazikurejeshwa na kuwekwa kanisani hadi baada ya kutimizwa kwa siku (miaka) 1335 mwaka 1844. Ushuhuda huu usio na shaka huthibitisha kwamba vuguvugu ambalo lilitokea mwaka 1844 ni kanisa la kweli la Mungu, na lililotabiriwa na Mungu. Kwa hivyo husuluhisha machafuko yaliyoenea katika Jumuiya ya Wakristo, kuhusu ni dhehebu gani ambalo lina ukweli kwa wakati huu; pia huyang’oa mengine yote kuwa ni ya uongo, kwa maana ndilo vuguvugu pekee ambalo lina ukweli wa patakatifu. {SR2: 133.4}

Kwa sababu kweli za mafundisho hayo mawili yasiyoweza kutenganishwa yaliangushwa chini mwaka 508 B.K., kwa maandalizi ya kusimamishwa upapa, vivyo hivyo papa kufungwa gerezani mwaka 1798 yalikuwa ni maandalizi ya kurejeshwa kwa ukweli wa Biblia uliofundishwa kwa pamoja, Sabato na Patakatifu. Uwajibikaji unaotua kwa upapa sio utunzaji wa siku, lakini badala yake, tamaa ya kubadilisha sheria ya Mungu, kama inavyoonyeshwa katika Danieli 7:25: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria.” Upapa ulifikiria kufuta kabisa Sabato ya siku ya Saba

134

kutoka kwa sheria ya milele, na kuandika siku ya kwanza ya juma mahali pake. {SR2: 133.5}

Kanisa Lilifanywa Vipi Kuwa La Upagani?

Walikuwa wafalme wa Rumi ambao waliolifanya kanisa liwe la upagani, na kwa sababu wapagani waliadhimisha Jumapili siku zote, Sabato iliwekwa kando kama ilivyohusika mamlaka ya kanisa, mapadre na wafalme. Wapagani hawakujali chochote kuhusu Sabato. Hawakufunzwa utakatifu wake, na Wakristo wachache ambao walijaribu kuitunza siku takatifu walipotelea katika umati. Muda mfupi baadaye ibada za Sabato zilikuwa jambo lililopitwa na wakati. Hili lilifanikishwa katika mwaka 508 B.K. Tendo hili la kishetani liliandaaa njia na upapa ulianzishwa mwaka 538. Papa aliwekwa kuwa mtawala kamili, mfalme wa wafalme, na mrekebishaji wa wazushi kwa yake yanayoitwa eti mamlaka matakatifu. Mpango huo ulikuwa wa kuendeleza mafundisho ya uongo, na kuuweka ukweli chini milele. Ni jambo la ajabu sana, jinsi adui wa zamani wa wanadamu amefanikiwa kuzidanganya akili zenye nguvu zaidi. Yeye huwateka nyara kwa uharibifu wao wenyewe. Ndivyo ambavyo imekuwa katika kila kizazi. {SR2: 134.1}

Kama ilivyoelezewa hapo awali, mwanzoni Rumi uliwatesa Wakristo. Lakini joka la zamani lilipoona kwamba mateso hayangaliweza kuipindua imani yao, likabadilisha mpango wake, na likabuni mpango wa kishetani wa hila zaidi kuliharibu kanisa. Lilifanya kazi, kama siku zote, kupitia moyo wa kimwili, akitumia chombo cha mwanadamu kutekeleza udanganyifu usioonekana kwa jicho la kibinadamu. {SR2: 134.2}

“Rumi ya Gibbon,” Gombo la 2, uk. 273, 274, husema: “Kwa amri za uvumilivu, yeye [Konstantino] aliondoa uzuizi wa muda ambao ulikuwa hadi hapo umekwamisha maendeleo ya Ukristo; na wachungaji wake wamilifu wengi walipata idhini ya bure, faraja ya uhuru, kuidhinisha kweli zenye manufaa za ufunuo kwa kila hoja ambayo ingeweza kuathiri kufikiri au kicho cha wanadamu. Uwiano halisi wa dini mbili [Ukristo na Upagani] uliendelea ila kwa muda …. Miji iliyosainia bidii ya kuendeleza uharibifu wa hiari wa mahekalu yao [ya Wapagani] ilitofautishwa kwa fursa za manispaa, na kutuzwa kwa michango maarufu …. Wokovu wa watu wa kawaida ulinunuliwa kwa kiwango cha chini, iwapo ni kweli kwamba, kwa mwaka mmoja, watu kumi na mbili elfu walibatizwa huko Roma, mbali na vipimo vya idadi ya wanawake na watoto, na kwamba vazi jeupe na vipande ishirini vya dhahabu, vilikuwa vimeahidiwa na mfalme kwa kila mwongofu. Hii ilikuwa sheria ya Konstantino, ambayo iliwapa uhuru watumwa wote ambao wangeukumbatia Ukristo.” {SR2: 134.3}

Kwa njia hii, Rumi ililifanya kanisa kuwa la kipagani, na kile ambacho mateso yalishindwa kufanya, michango na mapendeleo yalifanikisha. Kwa kadiri

135

Wakristo washindi walikuwa wakisonga mbele dhidi ya ukuta wa mateso usioweza kupenywa ambao uliungwa mkono na shetani alirudi nyuma ghafla, na kuuruhusu kubomoka. Kwa hivyo, wakati mateso yalipokoma, yalisababisha ubomoke kwa mfano, kwa nguvu zao wenyewe. Kwa hivyo kile ambacho utawala wa kishetani ulishindwa kufanya kwa mateso, alifanikisha kwa kurudi nyuma ghafla. Joka la zamani lilipoona kwamba halingeweza kuipindua nyumba hiyo ya kiroho kwa mateso, lilibadilisha mpango huo na kutumia nguvu yake kudhoofisha msingi wa mitume kwa hongo na vishawishi mbalimbali kwa upendeleo wa wapagani dhidi ya Wakristo. Kadiri wapagani walikimbilia kujiunga na kanisa, upepo wa uasi-imani uligeuka dhidi ya Wakristo. Badala ya kanisa kuufanyiza ulimwengu kuwa wa Ukristo, ulimwengu ulilifanya kanisa kuwa la upagani. Kwa njia hii Wakristo walianguka chini ya nguvu ya “joka” na kwa hivyo vichwa vyake vikawameza (wakafanywa wapagani). Lakini kwa sababu Shetani alikusudia kuulinda kikamilifu mpango wake aligeuza mateso kwa wapagani, akiogopa kwamba roho ya kweli ya Kikristo ingehuishwa iwapo hayo madhehebu mawili, la Kikristo na la Upagani, yangekuwa hai. {SR2: 134.4}

Gibbon anasema: “Chini ya utawala wake [Athanasi], Ukristo ulipata ushindi rahisi na wa kudumu; na mara tu tabasamu la udhamini wa kifalme ulipoondolewa, ubunifu wa Upagani, ambao ulikuwa umeinuliwa kwa shangwe na kukuzwa kwa sanaa ya Yulio ulizama kabisa mavumbini.” — “Rumi ya Gibbon,” Gombo la 2, uk. 521. {SR2: 135.1}

“Agizo maalum alipewa Cynegius, mkuu wa mkoa wa mashariki wa Preatori, na baadaye kwa Counts Jovius na Gaudentia, maafisa wawili wa safu mashuhuri katika nchi za Magharibi; ambao walielekezwa kufunga mahekalu, kunasa au kuharibu vyombo vya ibada ya sanamu, kuondoa marupurupu ya mapadre, na kutaifisha mali iliyowekwa wakfu kwa manufaa ya mfalme, ya kanisa, au ya jeshi …. Mengi ya mahekalu hayo yalikuwa na minara ya kifahari na mizuri sana ya ujenzi wa Uyunani; na mfalme mwenyewe alikuwa amependezwa kutouharibu utukufu wa miji yake mwenyewe, au kupunguza thamani ya mali zake … Nchini Shamu, aliyekuwa bora na wa kiungu Marcello, jinsi alivyoitwa kimtindo na Theodoret, askofu aliyehuishwa na moto wa mitume, aliazimu kuyatandaza kwa ardhi hayo mahekalu ya kifahari …. Lakini wakati hukumu ya uharibifu dhidi ya sanamu za Alexandria ilitangazwa, Wakristo walianzisha kelele za shangwe na kutukuza ilhali Wapagani kwa huzuni, ambao ghadhabu yao ilikuwa imesababisha hofu kuu, waliondoka kwa hatua za kimya …. Theofilo alisonga mbele kulibomoa hekalu la Serapis, … na kujiridhisha kwa kulipunguza jengo lenyewe kuwa rundo la takataka, ambalo sehemu yake muda mfupi baadaye iliondolewa, ili kutoa nafasi kwa kanisa, lililojengwa kwa heshima ya wafia-imani wa Kikristo.” — “Rumi ya Gibbon,” Gombo la 3, uk. 140-146. {SR2: 135.2}

136

Kwa njia hiyo Wapagani walijiunga na kanisa la Kikristo kwa kulazimishwa na hongo badala ya kushawishika kuwa ni wadhambi, na hapo Ukristo ukatoa nafasi kwa ibada ya sanamu. Asema Gibbon: “Dini zote mbili kwa kupokezana zilikuwa zimefedheheshwa kwa kulikoonekana kupatikana kwa waongofu wasio na thamani, wa wapiga kura wa watawala wa rangi ya zambarau, ambao wangeweza kupita, bila sababu, bila kuona aibu, kutoka kanisani hadi hekaluni, na kutoka kwa madhabahu za Mshitarii/Jupita hadi kwenye meza takatifu ya Wakristo.” — Kimenukuliwa, Gombo la 2, uk. 522. {SR2: 136.1}

Kanisa katika usafi wake, lililojazwa na roho wa Yesu mpole na mnyenyekevu, lilipigana dhidi ya kukandamizwa na kuteswa. Waliwaombea wale ambao wangeweza kuwaua, wakisema, “Bwana, wasamehe, kwa maana hawajui wanalolitenda.” Wao, kama Stefano, walipiga magoti chini ya mvua ya mawe, wakisihi, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Lakini Wakristo ambao hapo zamani walikuwa na bidii kwa kiwango safi cha kanisa, walichukua kilemba cha mamlaka ya serikali ya kiraia, na wakawalazimisha Wapagani kujiunga katika safu zao. {SR2: 136.2}

Wakati Wapagani na Wakristo walipokuwa wamoja, joka lilitumia nguvu na mamlaka yake kuu ndani ya upapa. Kwa ufalme huu imara wa ukasisi likafuta Sabato ya siku ya Saba kutoka katika sheria ya Mungu, na badala yake likaingiza Jumapili ya kipagani. Katika hatua hii lilielekeza nguvu yake dhidi ya kukosa uaminifu kwa madai ya upapa. Mamlaka haya ya kipapa yaliendelea kuwaangamiza watakatifu wa Aliye Juu, kama ilivyo katika Danieli 7:25. Jinsi Shadraki, Meshaki, na Abednego huko Babeli, na Danieli huko Umedi na Uajemi, walizuia kuanzishwa kwa serikali ya kidini, na kuifanya sufuri amri ya mfalme, ndivyo Luther alivyouondoa ufalme wa upapa, na kukomesha mamlaka ya upapa. Kwa sababu pigo la Luther lilidhoofisha nguvu yake na Uprotestanti daima ulilichubua jeraha lake, papa, kwa mkono wa Berthier, akawekwa nyuma ya vifungo vya gereza. {SR2: 136.3}

Jinsi Ibada Ya Sanamu Ilipenyeza Kanisani

Mistari michache tu kutoka kwa kalamu ya Gibbons ikielezea jinsi ibada ya sanamu na watakatifu ilipenyeza katika kanisa la Kikristo: “Miili ya Mtakatifu Andrea, Mtakatifu Luka, na Mtakatifu Timotheo, ilikuwa imepumzika karibu miaka mia tatu kwenye makaburi yaliyofunikwa. Kutoka huko ilisafirishwa, kwa heshima kubwa hadi kwa kanisa la mitume, ambalo ukuu wa Konstantino ulikuwa umejenga ukingoni mwa *Milango-Bahari ya Wathrake. Karibu miaka hamsini baadaye, milango-bahari hiyo iliheshimiwa kwa uwepo wa Samweli, mwamuzi na nabii wa watu wa Israeli. Majivu yake, yaliyowekwa kwenye chombo cha dhahabu, na kufunikwa kwa barakoa ya hariri, yalipelekwa na maaskofu mikononi mwa kila mmoja wao…. Katika kipindi kirefu cha miaka elfu moja na mia mbili, ambayo ilipita kati ya utawala

137

wa Konstantino na matengenezo ya Luther, kuwaabudu watakatifu na mabaki ya vitu vya kidini kulivuruga usafi na unyenyekevu kamili wa mfano wa Kikristo: na baadhi ya dalili za kuzorota zinaweza kutazamwa hata katika vizazi vya kwanza ambavyo vilichukua na kukuza uvumbuzi huu wa madhara…. Wakristo walizuru kila mara kwenye makaburi ya wafia-imani, kwa tumaini la kupata, kutoka kwa maombezi yao yeye nguvu, kila aina ya baraka za kiroho, lakini zaidi, za kidunia. Waliomba uhifadhi wa afya zao, au tiba ya udhaifu wao; uzao wa wake zao wagumba, au usalama na furaha ya watoto wao.” — Kimenukuliwa; Gombo la 3, uk. 156, 157, 162. {SR2: 136.4}

* Melezo: Karibu na Istambul, Uturuki. Kati ya Bahari Nyeusi na Bahari Aegea.

Makundi yote mawili yalihimizwa kwa njia isiyo halali, Wakristo wasahau roho ya injili, na Wapagani kuchukua umbo la roho ya kanisa. Theolojia tukufu na rahisi ya Wakristo wa kwanza ilivurugwa polepole. Nguvu za ushetani zilirudishwa nyuma. Ingawa hakuweza kushinda shughuli za wahandisi wa Kikristo kwa mateso, alifanikiwa kwa udanganyifu. {SR2: 137.1}

Wakati mateso yasiyokuwa ya haki dhidi ya Wakristo yalikuwa yamekoma, kanisa lilichukua hatua ya kuanguka. Ijapokuwa wachache waliheshimu utakatifu wa Sabato, hawakusumbuliwa hadi baada ya ufalme wa kidini kuanzishwa mwaka wa 538. Joka lilikuwa limeazimia kwa umakini kuendeleza mseto wa dini na taifa, Ukristo kwa jina lakini Upagani kwa matendo. Shetani alikusudia kuusimamisha upapa, na “kuwaangamiza watakatifu wa Aliye Juu.” Mateso, kwanza dhidi ya kanisa la Kikristo la kwanza, na pili, dhidi ya upagani kwa kupendelea Ukristo, yalibadilishwa chini ya utawala wa upapa. Wakristo wachache ambao waliheshimu Sabato ya siku ya Saba, kwa njia zingine waliwindwa kama sungura, na walitakiwa kutii kikamilifu dini halali ya mapapa lakini isiyo ya ukristo. {SR2: 137.2}

Kurudi kwa mada yetu, — “Pembe kubwa sana.” Rumi katika hali yake iliyogawanyika iliangusha kweli na kuikanyagia chini. Lakini haikutekeleza kwa ghafla au kwa nanma ya kudhulumu. Utunzaji wa Jumapili polepole ulipenyeza ndani ya kanisa la Kikristo. Mwanzoni masaa ya asubuhi yalizingatiwa kuwa angalau matakatifu, kwa sababu Bwana alikuwa amefufuka mapema siku hiyo. Baada ya kuwa rasmi, utakatifu zaidi uliambatanishwa kwayo, na masaa yakaongezwa hadi adhuhuri. Mwishowe siku nzima ilitengwa kama siku ya ibada. {SR2: 137.3}

Wakati Jumapili ilizidi kukua zaidi na zaidi takatifu, Sabato ya siku ya Saba ilikuwa ikiporomoka, na kupungua utakatifu kidogo kidogo. Hapa tunaona mfano ambao unapaswa kutiwa alama kwa uangalifu na Wakristo wote. Kuongeza kitu chochote kwa dini ya Kristo, ingawa chaweza kuonekana kizuri kwa nje, husababisha uchungu wa mauti kutokea chini yake. Mungu wetu amebuni dini inyotosha

138

kuliokoa kanisa, ikiwa itafuatwa kwa uangalifu. Yeye hahitaji usaidizi wa mwanadamu, wala Yeye hawezi kukubali vyombo vilivyoundwa na mwanadamu. {SR2: 137.4}

“Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki: Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” (Ufu. 22:18, 19.) {SR2: 138.1}

Kanisa la Rumi lilibadilisha usafi wa ukweli kwa hekima ya kibinadamu na mila za mwanadamu. Au, jinsi Danieli anavyosema: “Na jeshi [mafuriko ya Upagani] likatolewa kwake pamoja na dhabihu ya kila siku kwa sababu ya makosa, nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda na kufanikiwa.” (Dan. 8:12.) “Jeshi” dhidi ya ya “kila siku” walikuwa Wapagani ambao hawakuongoka walioletwa ndani ya kanisa; kwa hivyo, “kwa sababu ya makosa.” Tofauti ilioje na njia iliyotumiwa na Yohana Mbatizaji! “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba.” (Mat. 3:7, 8.) {SR2: 138.2}

Inaweza kuwa faida kuuliza: je! kanisa kwa wakati huu linaiga Yohana au Warumi? Je! Washiriki wake ni Wakristo au Wapagani? Bwana alimwagiza mtumwa Wake kuonya Israeli ya zamani dhidi ya mazoea hatari kama hayo. Yeye akasema: “Nawe utawaambia waasi, yaani nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi; Enyi nyumba ya Israeli, katika machukizo yenu yote na yawatoshe, kuwa mmewaingiza katika patakatifu Pangu wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu Pangu, wapatie unajisi, naam nyumba Yangu.” (Ezek. 44:6, 7.) {SR2: 138.3}

Kwa kweli, je! watu wanamfanyia Mungu kazi au wanajifanyia wenyewe? Malaika, katika kutoa maagizo kwa Danieli, huita Sabato na ukweli wa patakatifu, “Kweli.” (Angalia Danieli 8:12.) Hakika, huo ni ukweli. Kwa kutunza Sabato tunamheshimu Mungu kwa kutambua ukumbusho mtakatifu wa uumbaji wa Kristo. {SR2: 138.4}

“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi Amesema nasi katika Mwana, Aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa Yeye aliziumba dunia.” (Ebr. 1:1, 2.) {SR2: 138.5}

Kwa sababu dhambi iliingia katika familia ya mwanadamu, Bwana alianzisha ukweli wa patakatifu, ambao kwa kivuli huonyesha dhabihu Yake, kifo na ufufuo — ufunuo wa ukombozi wetu. Kwa hivyo katika kutunza Sabato na ukweli wa patakatifu, tunakiri waziwazi kwamba

139

Kristo ni Muumba na Mkombozi. “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia.” (Marko 2:28.) {SR2: 138.6}

Biblia ni ufunuo wa uumbaji na ukombozi katika Kristo — Muumbaji na Mkombozi. Kwa hivyo, Sabato na Patakatifu hujumuisha “Kweli.” (Angalia Waebrania 9:10, 4:4-10.) Kwa hivyo mafundisho haya mawili yameunganishwa pamoja, hayawezi kutenganishwa, na hubeba ukweli wote. {SR2: 139.1}

Je! Tunatunzaje ukweli wa Patakatifu? Hutunzwa, si katika mfano, bali katika uakisi. Kwa imani tunaamini kwamba Kristo, Kuhani wetu Mkuu, katika patakatifu pa mbinguni anahudumu kwa niaba yetu, kama ilivyofundishwa kwa mfano na patakatifu pa duniani, palipojengwa na Musa. Jinsi Israeli ilivyozingatia mahitaji ya utumishi wake katika mfano, ndivyo tunavyolazimika katika uakisi. Kwa hivyo “tunatangaza kweli [Sabato na Patakatifu] kikamilifu zaidi.” {SR2: 139.2}

MUHTASARI

Ile Pembe “Yatawala Dunia Yote”

Ili kuelewa kikamilifu kile kinachofundishwa katika sura hii, tunaita umakini tena kwenye chati iliyo kwa ukurasa wa 128. Sasa hebu tufuate chati hiyo pamoja na kusoma. Katika utafiti uliotangulia imethibitishwa kwamba ile “pembe kubwa sana” ya “beberu” haiwakilishi Rumi ya kifalme tu, bali pia Rumi ya upapa, na ulimwengu wa sasa vile vile; kwa maana ile “pembe” ilimtesa Kristo kwanza na wafuasi Wake chini ya utawala wa ufalme wa Rumi. Ukweli ulioonyeshwa na ya “Kila siku” na “Patakatifu” ulikanyagiwa chini “kwa sababu ya makosa” katika kipindi cha hali iliyovunjika ya Rumi hadi mwaka 508 B.K.; kwa maana serikali ya kifalme ilifikia kikomo katika mwaka 476. Isitoshe, utawala wa upapa “ulikanyagia” ukweli wa Mungu chini hadi kwa kikomo cha miaka 1260 ya kinabii, na kumalizikia kwa kifungo cha papa mwaka 1798. Lakini “Patakatifu” na ya “Kila siku” zilizuiliwa ardhini na “Pembe Kubwa Sana” hadi mwaka 1844. Wakati huo ilipoteza kuzidhibiti, na nguvu ya “JUMBE ZA MALAIKA WATATU” ikauinua ukweli kutoka ardhini, au kutoka “chini ya miguu” na kuuweka ndani ya kanisa. Kwa hivyo, ile “Pembe Kubwa Sana” ni nembo ya kipindi chote cha Agano Jipya hadi kwa ujio wa Kristo mara ya pili — sambamba na miguu ya chuma, na nyayo na vidole vya sanamu kubwa ya Daniel 2. {SR2: 139.3}

Hizi ni kweli ambazo hazwezi kukanushwa. Walakini, upo uthibitisho mwingine ambao unabeba ushahidi ulio sawa. Nabii akasema: “Na baada ya zamani zako [mfalme wa Babeli] utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe, na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.” (Danieli 2:39.) {SR2: 139.4}

Ufalme “wa shaba” unakubaliwa kuwakilisha Uyunani, lakini

140

ukweli ni kwamba Uyunani haukuwahi kutawala dunia yote. Ncha ya mbali zaidi ya dira iliofikiwa na Aleksanda Mkuu ilikuwa sehemu ya India. Wala Rumi ya kifalme haikuweza kutawala juu ya dunia yote. Nini basi? Je! Danieli ana makosa katika kuifasiri ile ndoto? Iwapo yapo makosa yoyote, Danieli hawezi kuwa na kosa. Wajibu kwa kawaida utamwangukia Mungu ambaye alikuwa mwangalizi wa maandishi yote, na ufasiri wa Maandiko. Iwapo Danieli alikuwa amekosea lilikuwa jukumu la Mungu kumfanya arekebishe. Lakini kwa sababu Mungu ni mkamilifu katika kazi Yake yote, Hawezi kuruhusu kosa katika Neno Lake Takatifu. Danieli yu sawa katika ufasiri wake na ufalme “wa shaba” lazima utawale juu ya dunia yote, kwa maana mengine yote yanaweza kushindwa, lakini Neno la Mungu litasimama milele. {SR2: 139.5}

Wakati ile pembe mashuhuri ya yule beberu kati ya macho yake (Aleksanda) ilipovunjika, zingine nne zilizuka badala yake (migawanyiko minne ya Uyunani). Baada ya hizi pembe nyingine ndogo ilitokea katika moja ya hizo nne, “iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa mashariki, na upande wa nchi ya uzuri.” (Danieli 8:9.) Kumbuka kwamba pembe hii ilikua sana. Yaani ni kusema, ilikuwa kubwa kuliko ile iliyokuwa “kati ya macho yake” (Aleksanda). Hiyo pembe kubwa sana ilielekea upande wa kusini, na upande wa mashariki, na kuelekea upande wa nchi ya uzuri (Yerusalemu) kama ilivyo katika Zaburi 106:24 na Zekaria 7:14. Kijiografia, Babeli, ambako Danieli alikuwa na maono, uko mashariki mwa Yerusalemu. Kwa hivyo, katika maono yule “beberu” alisimama Babeli. Ili kufanya mduara, pembe iliekea kwa ncha nne za dira, au, jinsi Danieli husema, “kuelekea upande wa kusini, na upande wa mashariki, na upande wa nchi ya uzuri.” Nembo hiyo humaanisha kwamba ile pembe kubwa sana ingepanua ufalme wake juu ya dunia yote — ncha nne za dira. Ukweli ni, ile pembe huwakilisha Rumi katika migawanyiko yake mitatu — ya Kifalme, ya Upapa, na ulimwengu wa sasa unaoyumba-yumba. {SR2: 140.1}

Biblia i sawa katika kutoa taarifa kuhusu ufalme wa shaba, “utakaoitawala dunia yote,” kwa maana shaba humwakilisha “beberu.” Kwa hivyo nabii alisema: “Beberu akatoka upande wa magharibi juu ya uso wa dunia nzima.” (Danieli 8:5.) {SR2: 140.2}

Laiti Danieli angalisema kumhusu mnyama dubwana, kuwa nembo ya Rumi ya kifalme na ya upapa, ya kwamba ingetawala ulimwengu wote, dai hilo lingethibitika kuwa si sahihi. Mnyama dubwana, katika hatua yake ya kwanza, huwakilisha Rumi ya kifalme, na katika hatua yake ya pili, Rumi ya upapa hadi mwaka 1798, wakati ambapo huyo mnyama alifikia mwisho wake kwa kifungo cha papa Pius wa 6, na kutoa nafasi kwa “mnyama kama chui” wa Ufunuo 13:1-3. {SR2: 140.3}

141

Kumbuka usahihi wa uvuvio. Je! Nabii amesema, “ufalme wa chuma utatawala ulimwengu wote,” ingekuwa kweli kwa habari ya chuma kutawala, lakini uthibitisho kama huo ungekuwa umelipuuza somo hili la ajabu lililofundishwa na beberu wa nembo. Lililo kweli kuhusu chuma na udongo, ni kweli kuhusu beberu; na moja hulingana na lingine. {SR2: 141.1}

Pembe hiyo huenea zaidi ya mwaka 1798, na hadi kwa ujio wa pili wa Kristo, sambamba na chuma (miguu, nyayo na vidole) ya sanamu kubwa katika Danieli 2. Kuihusu “pembe” tunasoma, “atavunjika bila kazi ya mikono.” (Danieli 8:25.) Maneno yale yale ya usemi hutumika kwa nyayo na vidole vya sanamu kubwa katika Danieli 2:45. “Na katika siku za wafalme hao,” asema Danieli, “Mungu wa Mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele.” (Danieli 2:44.) Kwa hivyo, ustaarabu wa sasa ni zao la beberu, au ufalme wa shaba. Uvuvio ungalikuwa umesema ufalme wa chuma utatawala juu ya dunia yote, ungeiharibu picha hiyo, kwa maana dhahabu, fedha na shaba (wakati wa Agano la Kale), husimama kwa miguu ya chuma (wakati wa Agano Jipya). Kwa hivyo ile nembo huthibitisha kwamba kipindi cha Agano la Kale husimama kwa kipindi cha Ukristo (Kristo); na kipindi cha Agano Jipya hujilisha kwa kipindi cha Agano la Kale. {SR2: 141.2}

Kiwiliwili cha sanamu kubwa, kikiwakilisha kiumbe hai kilicho na viungo vyote vilivyo hai, hulingana na Biblia, kwa maana Agano la Kale ni ghala kubwa la Neno la Mungu, na Jipya hujilisha kutoka kwa la Kale. Katika kipindi cha Kale, Bwana alilikusanya Neno la Mungu katika Biblia ili kuulisha ulimwengu katika kipindi cha Jipya. Agano Jipya ni utimilifu wa la Kale. Neno la Mungu huelezea ukamilifu katika kila njia. {SR2: 141.3}

Sabato “Ilikanyagwa” Mara Moja Tu

Tunaitisha tena umakini wako kwa “mwanamke” (kanisa) wa Ufunuo 12, ambamo tunaambiwa alipewa “mabawa Mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke aende zake nyikani… ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.” (Ufu. 12:14, 6.) Kwa sababu mabawa ya simba (Babeli) na chui mwenye vichwa vinne (migawanyiko minne ya Uyunani, Dan. 7:4, 6) huwakilisha vipindi vya historia ya ulimwengu, (angalia ukurasa wa 33-42 ), hivyo mabawa ya yule mwanamke pia lazima yamaanishe vipindi viwili vikuu vya historia ya kanisa. Tai akiwa mfalme wa nyuni, mabawa yake lazima yawakilishe mkuu, kiongozi au wa kwanza. Kwa hivyo, kila bawa lazima liwe nembo ya mojawapo wa hivi vipindi viwili vikuu tangu mwanzoni kabisa. {SR2: 141.4}

Uvuvio usingalikuwa umesisitiza ukweli kwamba mabawa yalikuwa ya tai yule mkubwa tungeweza kuhitimisha kwamba moja linaweza kuwakilisha kipindi cha Agano la Kale, na lingine kwa enzi ya

142

Ukristo. Lakini neno, mkubwa, haliruhusu mahitimisho kama hayo. Kwa hivyo, mojawapo la yale mabawa lazima lishikilie historia ya kanisa kutoka kwa uumbaji hadi kusulubishwa kwa Kristo, na lile lingine kutoka kwa ufufuo hadi mwisho wa dunia hii ya sasa. Hapa pia, itawezekana sisi kuhitimisha kwamba bawa moja laweza kuwakilisha kipindi kabla ya Biblia kuja, na lile lingine kwa kipindi cha Biblia baada ya kutoka (Misri). Lakini maneno ya Wa-ufunuo yanalipindua wazo hilo, kwa maana asema: “Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke aende zake nyikani, hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati mbili, na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.” (Ufu. 12:14.) Kwa hivyo, alipewa mabawa aruke hadi nyikani katika wakati wa Agano Jipya. {SR2: 141.5}

Nembo hiyo huonyesha kwamba Mungu amekuwa na kanisa moja (kweli) katika vizazi vyote, na ya kwamba msalaba wa Kristo ndio kitovu pekee cha kivutio. Somo hilo hufundisha kwamba kanisa la Mungu lilikimbilia nyikani mara moja tu katika historia yake yote, na hilo tukio lilikuwa kuanzia mwaka 538 hadi 1798 B.K. Katika wakati huu kweli za Sabato na Patakatifu “ziliangushwa chini,” au “kukanyagiwa chini.” Kwa hivyo, mwendelezo wa kweli hizi haujawahi kabla ya mwaka 538 kukatizwa na uongozi wa kanisa. Ingawa kweli hizi takatifu zinaweza kuwa hazikuheshimiwa siku zote na washiriki au viongozi kanisani, zilikuwepo pale kwa wale waliozihitaji. Kwa hivyo, ukweli wa milele wa Mungu ungekuwa umetunzwa na watu Wake, wazi wazi, katika vizazi vyote isipokuwa kwa kipindi chini ya utawala wa upapa. {SR2: 142.1}

Tena kumbuka, kwamba kweli iliangushwa chini, na “mwanamke” (kanisa) alikuwa amekimbilia nyikani. Uvuvio husema: “Ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko.” (Ufu. 12:6, 14.) Kwa hivyo, wakati kweli “iliangushwa chini” na uongozi wa kanisa katika wakati huo, na “chukizo likasimamishwa,” Mungu alikuwa na wengine waliokuwa wamejificha ambao waliitunza Sabato Yake na walikuwa na ufahamu wa ukweli wa Patakatifu katika miaka yote 1260 ya safari ya nyikani. Hivyo alitunzwa (kulishwa), kuonyesha kwamba angerejea. {SR2: 142.2}

Ibada Maradufu Katika Vizazi Vyote

Kwa kuitazama chati, historia ya utunzaji wa Sabato na Jumapili, au ibada ya kweli na ya uongo, itaonekana wazi. Hapo mwanzo Bwana aliwaumba Adamu na Hawa, na akaweka wanandoa hao watakatifu katika bustani ya Mungu, lakini wazazi wetu wa kwanza walikosa shauri la yule Aliye Juu, na dhambi ikaingia nyumbani Edeni. Ili kuhifadhi mpango Wake wa asili kwa familia ya wanadamu, Yeye alilazimika kuwaondoa wazazi wetu kutoka kwa makao yao ya Edeni. Kwao walizaliwa wana na mabinti; tazama Mwanzo 5:4. Wana wao wawili wa kwanza wanaletwa kwa umakini wetu na Maandiko

143

kwa ulinganisho ambao ni wa kushangaza sana, na ambao unapaswa kufikiriwa kwa uangalifu na kila anayejidai kuwa wa dini. {SR2: 142.3}

Dhabihu na ibada ya kidini ya wazawa wa kwanza katika familia ya wanadamu, hufichua kwamba Mwokozi wa ulimwengu alikuwa amefanya ujulikane mpango wa wokovu kwa familia ya Adamu. Mfumo wao wa ibada uliobuniwa na Muumba Mwenyewe, ulikuwa mkamilifu, na ulio na uwezo kumwokoa mdhambi kutoka kwa dhambi yake. Ya Abeli ibada ya kidini yenye uangalifu, kulingana na maagizo ya Mungu aliyemwabudu, huonyesha kwamba ibada kama hiyo pekee, heshima na sifa, inaweza kukubalika kwa Mungu. Kaini hakuzingatia ile amri, na kwa hivyo kwa kuwasilisha kile ambacho Mungu hakuhitaji akaanzisha dini yake mwenyewe. Kwa sababu baadaye mara moja alimuua ndugu yake linapaswa kuwa funzo la mfano kwa wote: kwamba ibada kulingana na mielekeo ya wanadamu, hata iwe nzuri na isiyo na hatia, haiwezi kumtakasa na kumwokoa yule mwabudu. Lakini badala yake humzamisha dhambini zaidi, na uharibifu wa mwisho. Walio na mwelekeo wa kuwatesa wale ambao hawaabudu kama wao, wanasujudu na Kaini chini ya madhabahu yaliyojengwa kwa matofali. Madhabahu kama hayo ni zalisho la mwanadamu kwa kubadilisha aina ya yaliyo halisi; na hata ingawa yawe yanaonekana ya kuvutia zaidi kuliko madhabahu ya mawe, hakuna nguvu ya kutakasa ndani yake, na ibada zake ni za sumu ya kufisha. Ushahidi hauwezi kukataliwa kwamba aina zote mbili za ibada (ya kweli na ya uongo) zilianzishwa karibu kwa wakati mmoja, na huendeshwa kando na kando. Zote zilionekana zisizo na hatia na ziliendeshwa karibu kwa usawa na tofauti kwamba moja inauwiana na kitabu na sheria ya Mungu, na nyingine hapana. {SR2: 143.1}

Njia mbili kwa chati, kando ya Abeli, huwakilisha ukweli wa milele wa Mungu, Sabato na Patakatifu. Sabato ilianzia katika bustani ya Mungu. “Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi Yake yote Aliyoifanya; Akastarehe siku ya saba, Akaacha kufanya kazi Yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, Akaitakasa: kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe akaacha kufanya kazi Yake yote Aliyoiumba na kuifanya.” (Mwanzo 2:2, 3.) {SR2: 143.2}

Kwa sababu ya dhambi, ukweli wa patakatifu uliongezwa baada ya anguko la Adamu. Kweli zote ni muhimu sana. Sabato tunaitunza ili kuepuka kutenda dhambi, lakini ukweli wa Patakatifu ni wa kutuokoa baada ya kutenda dhambi. Mmoja ni wa kutuzuia tusianguke, na ule mwingine ni tiba ikiwa tutaanguka! Iwapo, baada ya kupokea maarifa ya kweli, tunavunja Sabato, tumetenda dhambi na tumemkataa Muumbaji, ambayo ni mbaya zaidi kuliko dhambi ya Adamu. Kwa kutoutii ukweli wa Patakatifu, tunaukataa mpango huo (au tiba), na tunamkataa Mwokozi wa Wokovu wetu. Soma “Tumaini la Vizazi Vyote,” ukurasa wa 165. Sabato ni sehemu ya Sheria ya Amri

144

Kumi. (Kutoka 20:1-17.) Ukweli wa Patakatifu ni sheria ya wokovu wetu, baada ya kutenda dhambi. Adamu alitenda dhambi kwa kula tunda alilokatazwa. Lusifa alitenda dhambi kwa kujisimamisha kama mungu. Alisema, “Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu: Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini: Nitapaa kupita vimo vya mawingu; Nitakuwa kama aliye Juu.” (Isaya 14:13, 14.) {SR2: 143.3}

Kwa kula tunda alilokatazwa, Adamu alivunja sheria ya afya (chakula), na kwa kufanya hivyo yeye pia, isivyo moja kwa moja, alivunja Sheria ya Amri Kumi; maana kwa kuasi Neno la Mungu alimdharau Yeye jinsi mtoto angemdharau baba yake wa duniani kwa kutotii, na hapo kuvunja amri ya tano. (Kutoka 20:12.) Kwa hivyo, Adamu ana hatia ya kukiuka sheria mbili, ilhali Lusifa alivunja moja tu, Sheria ya Amri Kumi, kwa maana hakula chochote ambacho Mungu alikuwa amekataza. {SR2: 144.1}

Dhambi ya Adamu ilimleta kaburini (mavumbini), kwa maana, baada ya kula tunda alilokatazwa lilifanya mageuzi mwilini mwake, na kwa hivyo uovu ulipasishwa kutoka kwa baba hadi kwa mwana. Lakini kwa sababu Lusifa hakuasi sheria ya afya, kifo cha kawaida hakikuwa na nguvu juu yake. Adamu, kwa kutii mpango uliofanywa kwa ajili ya ukombozi wake — kukubali tiba — atafanywa hai kwa ufufuo. Kwa Lusifa, kwa kuikataa haki iyo hiyo na kuidanganya familia ya mwanadamu, Mungu alisema: “Utashushwa mpaka kuzimu, mpaka pande za mwisho za shimo.” (Isaya 14:15.) “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako …. Nitakuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto … Kwa wingi wa maovu yako katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nitatokeza moto kutoka ndani yako, nao utakuteketeza, nami nitakufanya kuwa majivu juu ya nchi machoni pa watu wote wakutazamao. Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia: umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.” (Ezek. 28:15, 16, 18, 19. ) {SR2: 144.2}

Liko funzo hapa ambalo linafaa tulichunguze. Hebu mwenye dhambi aweke kidole chake kwa dhambi yake. Kwa kutotii neno la Mungu kwa namna yoyote ile, unavunja moja au zaidi kwa sheria Zake za milele. Hii ni fursa yako ya mwisho ama kuupokea au kuukataa wokovu. Rehema inabisha mlangoni kwa mara ya mwisho. Je! Wewe kaka, wewe dada, utausalimisha moyo wako kwa Mungu? {SR2: 144.3}

Umakini wa msomaji unaitishwa tena kwenye chati. Njia mbili zinazopita kando ya Abeli na kuuzunguka msalaba, huonyesha kwamba kweli za Sabato na Patakatifu ni za milele na takatifu, na ya kwamba utambuzi wa utakatifu wazo haujawahi kutupwa

145

nje ya kanisa la Mungu hadi baada ya mwaka 508 B.K.; kwa wakati ambapo “beberu” na pembe yake kubwa sana “aliangusha kweli chini.” Lakini katika mwaka 1844, ukweli wa Mungu kwa nguvu ya “Ujumbe wa Malaika Watatu,” ulifunuliwa tena. Ni dhahiri kwamba Sabato na Patakatifu, (sheria na injili) haziwezi kutenganishwa. Iwapo hujakuwa ukilitii neno la Mungu kwa namna yoyote, je! sasa, kwa mwito wa mwisho, utasema, “Bwana, Niko hapa. Utwae moyo wangu wa kijiwe na unipe moyo wa nyama?” Je! Utasihi kwamba Aiandike sheria Yake moyoni mwako? Malaika anasubiri kukutia alama kwa muhuri wa Mungu. Je! Utachagua giza badala ya nuru? Wakati malaika anaiangaza nchi kwa utukufu wake, je! utamruhusu auangaze moyo wako? Bado kitambo kidogo na ukweli wa Mungu utashinda, mbona ubaki nyuma? Je! Utaabudu kwa ukaidi, kama Kaini, na dini ambayo haiwezi kuokoa? Je! Utamdharau Mwokozi aliyekufia, na kumheshimu mshindani na adui wa roho yako? Kwa nini upotee katika muda mchache tu, katika millenia ya giza? (Fuata chati.) Je! Utakuwa tayari wakati Yesu atakuja kuwachukua watakatifu Wake hadi kwenye majumba juu? Kumbuka kwamba kuutunza ukweli ndiyo mafunzo ya kwenda kwa mji wa Mungu. “Hii ndiyo jumla ya maneno yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri Zake: maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.” (Mhu. 12:13.) {SR2: 144.4}

“Siku” (miaka) 1290 na 1335, kuhusiana na ya “kila siku” na “patakatifu” za Danieli 12:11, 12, sasa zinaeleweka kwa mara ya kwanza. Huu ukiwa ni wakati ambapo zimefunuliwa, ni dhahiri kwamba tunashughulika na ukweli wa sasa. Kwa hivyo, Maandiko hayo lazima yananena moja kwa moja kwetu wakati wa sasa. Kwa hivyo, laana na baraka za sura hii zinahusu kizazi hiki, na tumepewa fursa ya kuchagua aidha moja au ile nyingine. {SR2: 145.1}

Ni muhimukwamba tutoe maelezo kwanza kwa aya ya 10 ya Danieli 12, kwa sababu inaleta ukweli kwamba kwa wakati Maandiko haya yamefunuliwa, “Wengi watatakaswa na kufanywa weupe, na kusafika; bali waovu watatenda maovu wala hataelewa mtu mwovu awaye yote, bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Kwa hivyo, inahitajika kwamba tutubu dhambi zote na kujitenga na kila njia ya uongo, na hivyo kuwa na maono yetu safi, ili tuweze kuelewa. {SR2: 145.2}

“Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako: na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo: na wakati huo watu wako wataokolewa, kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” (Danieli 12:1.) Jina “Mikaeli” humaanisha “aliye kama Mungu.” “Kristo ndiye chapa ya mng’ao wa Baba,” na Jemadari mkuu wa watu Wake.

146

Kwa hivyo hilo jina humaanisha Kristo. Kwa wakati huu, Kristo (Mikaeli) atasimama kwa ajili ya watu Wake, na kila mtu ataokolewa ambaye anaonekana ameandikwa katika kile “Kitabu.” Kwa hivyo watu wa Mungu hawahitaji kuogopa katika wakati wa taabu. {SR2: 145.3}

“Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” (Danieli 12:2.) Itagunduliwa kwamba ufufuo uliotabiriwa katika Andiko hili ni wa mseto — baadhi ni wenye haki , ilhali wengine ni waovu. Kwa hivyo, huu ni ufufuo maalum, na ulio huru kwa ule iliotajwa katika 1 Wathesalonike 4:16, 17, kwa maana lasema wazi: “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: Kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani: na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” {SR2: 146.1}

Yohana pia anaweka wazi kwamba wenye haki pekee wameitwa wakati wa kuja kwa Bwana, kwa maana husema: “Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza: juu ya hao mauti ya pili haina nguvu.” (Ufu. 20:6.) Kwa hivyo, ufufuo mseto lazima utangulie ule wa kuja kwa Kristo katika mawingu. Wale ambao wataamka “na kudharauliwa milele” lazima wawe ni wale waliomchoma Kristo, na hivyo kutimiza Andiko lifuatalo: “Tazama, Yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona Yeye, na hao waliomchoma Yeye.” (Ufu. 1:7.) {SR2: 146.2}

“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” (Danieli 12:3.) Wale ambao ni “walio na hekima” ndio “watakaoelewa,” na wao watawaongoza wengi kwa haki; kwa hivyo watang’aa kama nyota “milele na milele.” Hawa sio wale ambao walifufuliwa katika ufufuo maalum, kwa maana utakuwa baada ya kufungwa kwa rehema, na karibu mwishoni mwa pigo la saba, muda mfupi tu kabla ya kuja kwa Bwana. Kwa hivyo wale waliofufuliwa hawatakuwa na nafasi ya kumwongoza yeyote kutenda haki. Kwa hivyo, wale ambao watang’aa kama nyota ni watu 144,000, na wote watakaoshiriki katika kazi ya kufunga injili. Fikiri juu ya ile ahadi tukufu! Je! Kuna kitu kama hicho katika ulimwengu wote? Je! Unaweza kulinganisha nini na raha ya mbinguni mbele ya Mungu? Uzima wa milele, bila maumivu au machozi! Tazama Ufunuo 7:17, na Isaya 11:6, 7; 65:25. {SR2: 146.3}

“Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho: wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.” (Danieli 12:4.) Je! Ni uthibitisho gani dhahiri tunaweza kuuliza kutushawishi kwamba huu ni wakati wa

147

mwisho? Je! Maarifa yameongezeka? Je! Wengi wanakimbia huko na huko? Wakati Danieli hasimulii jinsi kukimbia kunavyotekelezwa Nahum husimulia: “Magari yametameta kama mwako wa mienge katika siku ya kujitengeza kwake … Magari [ya mitambo] yanafanya mshindo njiani, yanasongana-songana katika njia kuu: kuonekana kwake ni kama mienge, yanakwenda upesi kama umeme.” (Nahumu 2:3, 4.) Unabii ukiwa unaeleweka, ni dhahiri kwamba hiki “kitabu” kimefunuliwa, na ya kwamba wakati wa mwisho umefika. {SR2: 146.4}

“Ndipo mimi Danieli nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili, mmoja ukingoni mwa mto upande huu, na mmoja ukingoni mwa mto upande wa pili. Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu? Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, akaapa kwa Yeye aliye hai milele na milele ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati; tena atakapokuwa amekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.” (Danieli 12:5-7.) {SR2: 147.1}

Swali liliulizwa, “Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu?” Jibu, ni kwamba, “itakuwa wakati [mwaka mmoja], nyakati mbili [miaka miwili] na nusu wakati [nusu ya mwaka].” Siku thelathini kwa mwezi, miezi kumi na mbili kwa mwaka, ni sawa na siku (miaka) za unabii 1260 . {SR2: 147.2}

Kipindi cha kinabii huonyesha nyuma kwa ubabe wa upapa, na mateso ya watu wa Mungu kutoka mwaka 538 hadi 1798 B.K. (Angalia Dan. 7:25, na Ufu. 12:6, 14; 13:5.) Mwisho wa kipindi kirefu cha unabii ambacho ndani yake upapa ulitawanya nguvu ya watu watakatifu, u katika wakati zamani miaka mia na thelathini. Malaika akatangaza, katika wakati huu “ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.” Je! Haya yote hayathibitishi kwamba tuko kwenye ukingo wa umilele? {SR2: 147.3}

Je! Wewe ndugu, Wewe dada, utajivika haki ya Kristo? Au utaendelea kusubiri muda kidogo, hadi baada ya mavuno kupita? Mtu fulani atatamka maneno yafuatayo kwa kutamaushwa sana: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” (Yeremia 8:20.) Je! Utakuwa Wewe, au nitakuwa Mimi? {SR2: 147.4}

“Nami nikasikia, lakini sikuelewa: ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje? Akasema, Enenda zako, Danieli: maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri hata wakati wa mwisho.” (Danieli 12:8, 9.) Je! yamefungwa sasa? Iwapo sivyo, basi huu sio wakati ambao nabii huzungumzia? “Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.” (Danieli 12:12.) {SR2: 147.5}

148

MNYAMA (666), NABII WA UONGO, MAMA WA MAKAHABA, MTU WA KUASI, WAO NI NANI?

Namba ya siri “666” ya yule mnyama katika Ufunuo 13:18 jinsi inavyotumika kwa upapa, huthibitisha kwamba si kwa mujibu wa maandiko na vile vile ukosefu wa akili. Wakati namba za herufi za jina la papa hubeba namba 666, yapo majina mengine mengi, pamoja na majina ya watu binafsi, ambayo hubeba namba ile ile. Kwa kuhesabu tu thamani ya idadi ya namba kwa cheo, au jina, tunapata huwafaa wengi, kwa hivyo lazima tutafute uthibitisho wa Kibiblia kuifanyia matumizi. Isipokuwa tuthibitishe hivyo wazo hilo itakuwa si sahihi na lisivyo haki kuitumia nembo hiyo kwa mtu awaye yote. {SR2: 148.1}

Wazo mintarafu matumizi ya nembo ya nabii wa uongo wa Ufunuo 19:20, yule mwanamke kwa mnyama mwekundu sana wa Ufunuo 17, yule mnyama kaman chui wa Ufunuo 13, mnyama mwekundu sana wa Ufunuo 17, na yule mnyama dubwana wa Danieli 7, kama nembo za upapa, sio ya kibiblia na pia halina busara. {SR2: 148.2}

“Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama; akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu namba ya mnyama huyo: maana ni hesabu ya kibinadamu; na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.” (Ufu. 13:11-18.) {SR2: 148.3}

“Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo

149

[Ukurasa mtupu]

150

[Kielezo: Kuangamizwa kwa Wanyama, Mavuno na Mapigo]

151

mnyama. “(Ufu. 13:14.) Mnyama aliyetajwa hapa ndiye mwenye pembe kama za mwana-kondoo. Lakini mtu mwingine fulani ametambulishwa na kiwakilishi “yeye” ambaye “alikuwa na nguvu kufanya miujiza mbele ya huyo mnyama” (kama mwana-kondoo). Andiko linalofuata litaonyesha wazi kuwa ni nani anayefanya miujiza: “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, [mbele ya yule mnyama mwenye pembe mbili] ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake. Hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.” (Ufu. 19:20.) Kwa hivyo, miujiza inafanywa na nabii wa uongo mbele ya yule mnyama mwenye pembe mbili. {SR2: 148.4}

Wako wanyama wengi waliozungumziwa katika Biblia, lakini mnyama huyu mwenye pembe mbili ndiye tu anayeweza kuitwa “binadamu.” Itakumbukwa kwamba kutoka aya ya 11 kuendelea, ya sura ya 13 ya Ufunuo Maandiko hunena kumhusu yule mnyama mwenye pembe mbili na hufunga kwa maneno haya: “Maana ni hesabu ya kibinadamu; na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.” Kwa hivyo, namba ya siri “666,” ni ya mnyama mwenye pembe mbili wala si mwingine. Walakini, hatuwezi kuhitimisha kwamba hakuna mtu kabla yake ambaye hawezi kuwa na namba kama hiyo. {SR2: 151.1}

Wazo kwamba upapa huitwa mnyama ni kosa kabisa. Upapa umewakilishwa na nembo kwa wanyama wawili tofauti. Kwanza, kwa yule “dubwana” wa Danieli 7, na “pembe ndogo yenye macho ya mtu, na kinywa kilichonena maneno makuu;” pili, kwa “mnyama kama chui” wa Ufunuo 13, na kichwa “kilichotiwa jeraha la mauti.” Wanyama hawa ni wa ulimwengu wote, wakiwakilisha dunia yote kwa wakati wao, ya kiraia na ya kidini. Kwa hivyo, haingesemwa kwa mnyama yeyote yule, “ni … ya kibinadamu.” Upapa ukiwa ni sehemu tu ya hao wanyama wote wawili (pembe yenye kichwa kwa mmoja, na kichwa kilichotiwa jeraha kwa mwingine) hauwezi kuitwa “mnyama.” Mnyama mwenye pembe mbili ndiye wa pekee anayewakilisha ya mtaa serikali ya kidini na ya kiraia. Kwa hivyo, kwake pekee inaweza kusemwa, ni ya “kibinadamu.” Kwa hivyo ye yote atakayesimama kwa uongozi wa dola ile ya utesi jinsi ilivyofafanuliwa katika sura hii, na kuwakilishwa na yule mnyama, ndiye atakayebeba namba ya siri 666. Roho ya Unabii pia hueleza kwamba “Mfalme wa Kaskazini” anayeletwa kwa mtazamo katika Danieli 11:45, na mnyama mwenye pembe mbili wa Ufunuo 13, ni dola ile ile na ya kwamba itabeba namba hii ya siri 666. Tunanukuu: “Dola hii ndiyo ya mwisho itakayolikanyagia chini kanisa la kweli la Mungu: na kwa sababu kanisa la kweli bado linakanyagiwa chini, na kutupwa nje na Jumuiya yote ya Wakristo, inafuatia kwamba utawala wa mwisho wa kukandamiza haujafika ‘mwisho wake’; na Mikaeli hajasimama. Dola hii ya mwisho inayowakanyagia chini watakatifu inaletwa kwa mtazamo katika Ufu. 13:11-18.

152

Namba yake ni 666.” — “Neno kwa Kundi Dogo,” uk. 8, 9. Tumethibitisha ukweli wa ile namba kwa njia moja, sasa tutauthibitisha kwa njia nyingine. {SR2: 151.2}

Kuangamizwa Kwa Mnyama Na Nabii Wa Uongo

Kuangamizwa kwa “nabii wa uongo” na “mnyama” kumetabiriwa wazi wazi: “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake… hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto… Na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga uliotoka katika kinywa chake: na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.” (Ufu. 19:20, 21.) Mwisho wao kabisa unafanikishwa kwa kutupwa wakiwa hai katika ziwa la moto. Lakini waliosalia wote wa ulimwengu (“masalia”) wote waliuawa kwa “upanga uliotoka katika kinywa Chake: na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.” {SR2: 152.1}

Ziwa la moto ambalo wanyama na yule nabii wa uongo walitupwa ndani, haliwezi kuwa kwa wakati wa kuja kwa Kristo katika mawingu, kwa sababu waovu hawataangamizwa kwa moto wakati huo, lakini “Kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo Kwake.” (2 Thes. 2:8.) Mnyama na nabii wa uongo watatupwa katika ziwa la moto baada ya pigo la sita na kabla ya mwisho wa dunia. Uangamizaji huu wa “masalia,” wale walioachwa baada ya kuangamizwa yule mnyama na nabii, sio baada ya millenia, kwa maana waovu wakati huo hawataangamizwa kwa upanga ambao “ulitoka kinywani Mwake,” lakini kwa moto ambao “ulishuka kutoka mbinguni ukawala.” (Ufu. 20:9.) Baada ya millenia na kuangamizwa kwa waovu hakuna kiumbe hai kitakachokula kingine. (Tazama Isaya 11:6-9.) Kwa hivyo, yule mnyama na nabii wa uongo walitupwa katika ziwa la moto kabla ya millenia; na ziwa hilo la moto linakuwa mfano wa kuangamizwa kwa waovu upande wa pili wa millenia — mauti ya pili — kwa uharibifu wa mwisho wa umati wote umeelezewa kwa maneno yafuatayo: “Mauti na kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili yaani hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufu. 20:14,15.) Kwa namna hiyo ulimwengu utapewa mfano kabla ya millenia, wa uharibifu baada ya miaka elfu kumalizika. Mfano wa yule mnyama na nabii wa uongo ni wa kuonyesha kwamba waovu wote watatupwa wakiwa hai katika ziwa la moto, na hiyo ndiyo mauti ya pili. Kunena kuhusu kuangamizwa milele kwa Ibilisi, Neno husema: “Na yule Ibilisi mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo.” (Ufu. 20:10.) Yaani, mnyama na nabii wa uongo hawaamki

153

katika ufufuo wa pili, kuonyesha kwamba hakuna ufufuo kutoka kwa mauti ya pili. Tena, tunaona upo mfano kwa kila tukio, na mtu awaye yote asidharau mifano, kwa maana pale ambapo hakuna mfano, hakuna ukweli. Namba 666 imethibitishwa zaidi na

Kuangamizwa Kwa “Mtu Wa Kuasi” {SR2: 152.2}

Weka alama kwa uangalifu, kwa mujibu wa ushuhuda ufuatao, kuangamizwa kwa upapa ni wakati mwingine na kwa mchakato mwingine. “Paulo husimulia wazi kwamba mtu wa kuasi ataendelea hadi ujio wa pili. Hadi mwisho kabisa wa wakati ataiendeleza kazi yake ya udanganyifu.” — “Pambano Kuu,” uk. 579. Kwa hivyo upapa utasalia hadi kwa ujio wa pili wa Kristo, wakati ambapo waovu wataangamizwa kwa mwangaza wa kuja Kwake. Kwa hivyo, upapa ni kitu kimoja, na nabii wa uongo ni kingine, na yule mnyama bado ni kingine. Mnyama “666” na nabii wa uongo, ambao watatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto, ndio wanaoitengeneza sanamu ya yule mnyama — mfano wa ibada katika kipindi cha miaka 1260. {SR2: 153.1}

Wakati wa udanganyifu huo wa jumla umekaribia. Utachukua zaidi ya maarifa makubwa ya theolojia kuuepuka mtego wa nguvu zaidi ambao ukuu wake Shetani haujawahi kubuni. Miujiza ya ajabu itakuwa ya kushawishi na itakayoonekana kuwa ni roho ya kweli ya ibada italeta usadikisho wa ndani kwa wale ambao watapotoshwa. Kwa sababu watu wakuu wa dunia watatangaza ibada yake kuwa ya kweli, makutano ya watu watayapokea maamuzi yao bila uchunguzi wa kibinafsi. Ongeza kwa haya yote tangazo lifuatalo la mamlaka ya umma: “Wote watakaokataa kuisujudia sanamu ya mnyama wanapaswa kuuawa,” na tunayo nguvu kubwa ambayo uwezo wa mwanadamu hauwezi kupinga kwa nukta. Ni kwa ufahamu wa kinabii wa ukweli pekee, na imani katika “Bwana asema hivi,” na katika nguvu ya Roho Wake, mtu anaweza kuiepuka mitego yenye hila ya shetani. {SR2: 153.2}

Mama Wa Makahaba Si Mnyama

Imefafanuliwa kwamba upapa ungesalia hadi mwisho. Iwapo yule mwanamke aliye juu ya mnyama mwekundu sana (Babeli Mkuu) atafikia mwisho wake kwa wakati mwingine na kwa njia nyingine, yeye hawezi kuwa nembo ya upapa jinsi wengine wamedhani. Ufunuo 17:16, ikizungumza kuhusu huyo mwanamke na pembe za yule mnyama mwekundu sana, inasema: “Na zile pembe kumi ulizoziona kwa huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.” {SR2: 153.3}

154

Kumbuka, hakutupwa katika ziwa la moto kama yule mnyama na yule nabii wa uongo, lakini nao (hizo pembe) “watamfanya kuwa mkiwa na uchi na watamla nyama yake.” Kwa hivyo kuangamizwa kwa yule mwanamke ni kwa wakati tofauti, na kwa njia nyingine tofauti na ile ya upapa, nabii wa uongo, na mnyama. Kwa sababu yale ambayo yamesemwa hayawezi kupingwa, ni dhahiri “mnyama” ni kitu kimoja, “nabii wa uongo” kingine, na upapa kingine, na “mwanamke” bado ni kingine. Ni ya umuhimu mkubwa kwamba mambo haya yaeleweke kwa usahihi, maana kwa maarifa ya kweli pekee, Mungu anaweza kuwaongoza watu Wake hadi kwa ushindi. {SR2: 154.1}

Wakati Wa Mwanamke Kuangamizwa

Kubainisha wakati wa kuangamizwa kwa Babeli (mwanamke), itakuwa lazima kurejelea Danieli 7:11,12, “Nikatazama wakati huo kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe: nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao: walakini maisha yao yalidumishwa kwa msimu na wakati.” Kwa habari za wale wanyama wengine — simba, dubu, na chui, walinyan’anywa mamlaka yao, lakini walisalia hai, wakati yule mnyama dubwana alifikia mwisho wake. Wanyama ambao hudumu wakiwa hai, huwakilisha wazawa wa falme tatu za kale. Wakiwa wamenyang’anywa ufalme wao, wakazi (wanyama) wako hapa kwa wakati huu wa sasa. Mwisho wa wanyama hawa ungemaanisha mwisho wa dunia. {SR2: 154.2}

Mnyama dubwana sio mnyama wa mwisho wa historia ya dunia hii, kwa maana anafuatwa na mnyama kama chui wa Ufunuo 13:1, na mnyama mwekundu sana wa Ufunuo 17:3. Yule wa mwisho ni nembo ya mwisho ya matukio ya kihistoria, ambayo kwayo ulimwengu huu wa sasa na ule wa baada ya millenia utaletwa kwa kikomo, kama ilivyoelezewa hapo awali. Kwa hivyo, kuangamizwa kwa mnyama dubwana ni kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Ikiwa maisha ya wanyama wale watatu kabla yake “yalidumishwa,” wakati wao hauwezi kupanuliwa zaidi ya ujio wa pili wa Kristo. Danieli anasema: “Maisha yao yalidumishwa kwa msimu na wakati.” Kwa hivyo, tangu wakati mwili wa mnyama dubwana utaangamizwa, kutakuwa na “msimu na wakati,” hadi mwisho wa dunia hii ya sasa. {SR2: 154.3}

Iwapo Danieli humaanisha mwaka kwa “wakati,” na nusu ya mwaka kwa “kuugawanya wakati,” katika aya ya 25 ya sura iyo hiyo, basi lazima amaanishe vivyo hivyo katika aya ya 12. Iwapo ufasiri unaaminika katika aya moja lazima uaminike katika nyingine. Kwa hivyo, “wakati” utakuwa mwaka mmoja, na “msimu” sehemu ya nne ya mwaka, na hivyo kufanya jumla ya mwaka mmoja na miezi mitatu. Hata hivyo, kipindi katika

155

aya ya 25 kina jina la kinabii la siku (miaka) 1260, lakini “wakati” katika aya ya kumi na mbili hauwezi kuwa wa kinabii, kwa maana wakati huo ungemaanisha miaka 450 halisi. Ni dhahiri kwamba kutoka kwa wakati yule mnyama atakapoangamizwa, hadi mwisho, itakuwa miezi kumi na tano halisi. {SR2: 154.4}

Itakumbukwa kwamba kuangamizwa kwa yule “mnyama” ni unabii wa kuangamizwa kwa yule “mwanamke.” Tunanukuu maandiko yanayowarejelea wote mawili: “Nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.” (Danieli 7:11.) “Na zile pembe kumi ulizoziona kwa huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.” (Ufu. 17:16.) Maangamizo ya wote ni sawa (mnyama na mwanamke). Isitoshe, ni kile kipindi chini ya nembo ya mwanamke aliyempanda mnyama ambacho hufanya sanamu ya mnyama kama chui katika hatua yake ya kwanza (kabla kutiwa jeraha) au ya mnyama dubwana katika hatua yake ya pili; kwa maana, kipindi cha miaka 1260 kiliwakilishwa na wanyama wote wawili. Sanamu hiyo ni dini ya uongo iliyoanzishwa kimataifa. Kwa hivyo, mmoja ni mfano wa yule mwingine. Kwa hivyo kuangamizwa kwa mnyama wa awali (dubwana) ni unabii wa kuangamizwa kwa “mwanamke,” na maangamizo ya mmoja, ni maangamizo ya yule mwingine. Humaanisha kinabii kwamba ile “sanamu” (mwanamke aliyempanda mnyama — muungano wa mfumo huo wa kidini na kisiasa), utaangamia miezi kumi na tano (“msimu na wakati”) kabla ya “masalia” (ulimwengu wote uliobaki). Ikumbukwe kwamba maono ya Danieli ni unabii, na maono ya Yohana ni ufunuo. Kwa hivyo, kuangamizwa kwa mnyama dubwana ni unabii, na kuangamizwa kwa mwanamke ni utimizo wa unabii. {SR2: 155.1}

Andiko lifuatalo likirejelea wakati huyo “mwanamke” aliangamizwa, lasema: “Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu, na utukufu, na nguvu zina Bwana Mungu wetu: Kwa kuwa hukumu Zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahaba mkuu, aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa Wake mkononi mwake. Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake ukapaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa Wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.” (Ufu. 19.1-5.) {SR2: 155.2}

Mwanamke huyo akaangamizwa na moshi wake ukapanda juu “milele na milele,” ilhali “wazee” na “wenye uhai” walikuwa mbele ya kiti cha enzi. Hili huthibitisha kwamba hukumu katika Patakatifu Mno ilikuwa haijakoma, au angalau jopo lilikuwa bado

156

halijaondoka mahali pa hukumu, (lilielezewa katika sura nyingine) kwa maana baada ya watakatifu kuhesabiwa na kutiwa muhuri, dhambi zao zikiwa zimefutwa katika hukumu iliyotajwa, rehema itafungwa, na patakatifu ambapo hukumu inafanyika pataachwa na wazee, na wanyama, vile vile na “Mwana-Kondoo,” na jeshi lote la malaika. Baada ya hapo “hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba…” (Angalia Ufu. 15:5-8.) Basi ni dhahiri kwamba huyo mwanamke aliangamizwa kabla ya mapigo saba ya mwisho kumiminwa. {SR2: 155.3}

Kunukuu Ufunuo 19:6, “Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya: kwa kuwa Bwana Mungu wetu Mwenyezi amemiliki.” Wakati Kristo yu ndani ya hekalu na hukumu inaendelea, Yeye hamiliki, bali ni Kuhani na Wakili, akizifuta dhambi za wenye haki. Lakini Atakapomaliza hukumu ya upelelezi, basi atavikwa taji ya Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. (Tazama Ufu. 19:16.) {SR2: 156.1}

Baada ya “moshi wake kupaa juu hata milele na milele,” jeshi la mbinguni likapiga kelele, “Haleluya: kwa kuwa Bwana Mungu wetu Mwenyezi amemiliki.” Kwa hivyo, watakatifu wote walihukumiwa mara tu kabla ya kuangamizwa kwa huyo “mwanamke,” na baada ya kuteketezwa kwa moto, Kristo anavikwa taji kuwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana; wakati huo watatoka hekaluni na mapigo saba ya mwisho kumiminwa. {SR2: 156.2}

Maandiko yafuatayo hubeba ushahidi zaidi. Likasema jeshi la mbinguni: “Na tufurahi tukashangilie, tukampe utukufu wake: kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’aayo na safi: kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo.” Aliendelea Malaika, “Njoo huku, Nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo… akanionyesha ule mji mkubwa, Yerusalemu mtakatifu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.” (Ufu. 19:7-9; 21:9, 10.) Kwa hivyo, mke wa Mwana-Kondoo ni Mji Mtakatifu na si kanisa, na wale walioalikwa kwenye karamu ya harusi (watakatifu) ndio wageni. (Tazama “Pambano Kuu ,” ukurasa 427.) Wale ambao walikuwa mbele ya kiti cha enzi, walisema kuhusu Yerusalemu Mpya: “Mkewe amejiweka tayari. Na kwake akapewa [kwa mji] kuvikwa kitani nzuri, ing’aayo na safi…kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.” (Ufu. 19:7, 8.) Kwa hivyo, mke wa Mwana-Kondoo atakuwa tayari rehema itakapofungwa watakatifu watakapohesabiwa, kwa maana wao ni “kitani” yake. Kwa ule wakati yule mwanamke (Babeli) aliteketezwa, watakatifu (kitani) walikuwa tayari. Maangamizi yake yatakuwa ishara kwamba rehema imefungwa. Wakati huo wengine watapata

157

fahamu na ku sema, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” (Yer. 8:20.) Wengine “watatanga-tanga toka bahari hata bahari, na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki, watapiga mbio wakienda huko na huko kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” (Amosi 8:12.) Wakati watu wa Mungu watakuwa wameacha kazi waliyopewa na Mungu, jibu lao litakuwa: “Hatuna chochote kwa ajili yenu, mavuno yamepita, wokovu umekoma, mmechelewa sana.” {SR2: 156.3}

Nabii Wa Uongo Ni Nani?

Kama ilivyofafanuliwa hapo awali nabii wa uongo si upapa au yule mnyama mwenye pembe mbili, na yeye si Ibilisi, kwa maana tunasoma: “Na yule Ibilisi mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo.” (Ufu. 20:10.) Kwa hivyo, nabii wa uongo ndiye atatangulia udhihirisho wa Shetani mwenyewe. Akasema mtume, “Wala si ajabu; maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.” (2 Kor. 11:14.) {SR2: 157.1}

Kwa sababu mafundisho ya nabii wa uongo hayawezi kuungwa mkono kabisa na Maandiko, miujiza inafanywa ili kuhifadhi imani ya watu. Kwa vile watu wakuu na viongozi wa dini watatangaza kwa umma kwamba kinachoitwa eti dini ya kweli ni ukweli wa Kristo, na ya kwamba yule nabii wa uongo ni mtumwa Wake, umati wa watu utatumbukia katika mtego wa Shetani. Utabiri wake wa uongo wa kuja kwa Bwana, utatimizwa na Shetani mwenyewe atakapotokea kama malaika wa nuru. Kiwi cha mwangaza wake, na utimizo wa utabiri wa nabii wa uongo, pamoja na udanganyifu mwingi uliopo tayari, utanasa umati mkubwa kuliko wa kwanza. “Atakapokuwa akionekana kwa watoto wa watu kama tabibu mkuu anayeweza kuponya magonjwa yao yote, ataleta magonjwa na maafa, hadi miji maarufu itapunguzwa kuwa maganjo na ukiwa.” — “Pambano Kuu,” uk. 589. {SR2: 157.2}

Mwanamke Ameketi Juu Ya Vichwa

Malaika akasema: “Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.” (Ufu. 17:9.) Imefafanuliwa hapo awali kwamba vichwa huwakilisha Jumuiya ya Ukristo ya sasa iliyoasi imani, (angalia ukurasa wa 88-96). Vinaitwa “milima” (madhehebu), saba kwa idadi, kumaanisha yote. Kama kahaba anaketi kwa vyote saba, nembo iliyo na ushahidi usiokosea inaonyesha kwamba kinachoitwa eti Jumuiya ya Ukristo itajisalimisha yenyewe itawaliwe na kiongozi mmoja, ambaye mwanamke huyo ni nembo. (Tazama “Pambano Kuu,” ukurasa 588.) {SR2: 157.3}

158

Utangulizi kwa hiyo nguvu ya kufanya miujiza, Uprotestanti, Ukatoliki na Umizimu watakuwa wamefumbata mkono wa kila mmoja kupitia shirikisho la kanisa. Tofauti za maoni katika maswala ya mafundisho zitaangaliwa kuwa zisizo na umuhimu wowote kwa wokovu. Wataona katika umoja huo utakaoonekana hauna hatia vuguvugu kuu la utatuzi wa tofauti na pia la uongofu wa ulimwengu. Katika kutokea kwa nabii wa uongo, na kwa Shetani mwenyewe, matarajio yao yatatimia, na kuukaribisha wakati wa millenia ya amani iliyotarajiwa kwa muda mrefu utatangazwa kuwa umekaribia. Kwa hivyo kijuu-juu utatoa ushahidi kwamba migogoro ya ulimwengu inakaribia kukoma. Lakini kwa sababu watu wa Mungu wameonywa kuhusu hayo yote, watakataa kuabudu sanamu ya yule mnyama, ambayo ni dini ya uongo ya kimataifa, na watashtakiwa kuwa waasi, wasumbufu wa amani, na wanaosababisha taabu. Hili litaleta mateso makubwa ya Ufunuo 12:17. {SR2: 158.1}

Nao wataambiwa: “Je! Wewe ndiye mtaabishaji wa Israeli?” Hapo watakatifu watawajibu kwa namna ile ya nabii Eliya: “La bali … kwa kuwa umeziacha amri za Bwana, nawe umemfuata Baali,” itawakasirisha waovu na kuwasababisha wagadhabike dhidi ya wasio na hatia. {SR2: 158.2}

Mwanamke Ameketi Juu Ya Mnyama

Pindi Wa-ufunuo uliona katika maono yule mnyama ambaye hubeba namba 666, na nabii wa uongo akishinikiza utiifu kwa dini ya uongo kwa sheria na miujiza ndani ya mipaka ya serikali inayowakilishwa na yule mnyama mwenye pembe mbili, alionyeshwa taswira nyingine ya kushangaza: “Nikaona,” anasema, “mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu, naye alikuwa na kikombe kama cha dhahabu mkononi mwake kilichojawa na machukizo na machafu ya uasherati wake.” (Ufu. 17:3, 4.) Nembo hii hufichua kwamba baada ya yule mwanamke kuketi juu ya “vichwa” (akaunganisha makanisa) pia alifanikiwa kuketi juu ya yule mnyama. Mnyama ni nembo ya dunia yote ya sasa — serikali za kiraia (pembe kumi) na dini (vichwa saba). Maadamu mwanamke aliyeketi juu ya vichwa humaanisha muungano wa makanisa, vivyo hivyo, kuketi juu ya mnyama huwakilisha kimataifa kanisa na serikali zinazotawaliwa na kiongozi yule yule (mwanamke). Kwa hivyo, ni mfumo wa kimataifa wa dini na mseto wa kanisa na serikali. Katika mfumo kama huo watu wakuu wa dunia wataona maono ya kutatua taabu za ulimwengu, na kuwafanya watu na mataifa kuwa undugu wa dunia yote, kutimizwa kwa ushenga wa dini, 1 Thes. 5:3,

159

“Wakati wasemapo, kuna amani na salama; ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, …wala hakika hawataokolewa.” Ingawa nia yao ni kupunguza uhalifu na vile vile vita, tumaini lao litakuwa bure. {SR2: 158.3}

Kikombe, Vito Vya Thamani, Na Rangi Za Kutazamisha

Kikombe mkononi mwa mwanamke kikiwa cha chuma chenye thamani zaidi, na kwa vile amepambwa kwa dhahabu na vito vya thamani, huashiria jaribu kubwa zaidi — litakalotambulika kikamilifu katika nguvu ya kufanya miujiza na yule nabii wa uongo na Shetani mwenyewe. Kikombe chake (vitabu) husheheni mafundisho ya uongo, na kikiwa kama cha “dhahabu,” huonyesha kwamba wamepakwa Ukristo kwa nje. Kwa hivyo maneno yafuatayo ya kinabii yatapata utimizo wake: “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” (Ufu. 13:15-17.) {SR2: 159.1}

“Kama huo utakuwa uzoefu wa watu wa Mungu katika mapambano yao ya mwisho na nguvu za uovu … Shetani huwaongoza watu wengi kuamini kwamba Mungu atafumbia macho hali yao ya kutokuwa waminifu katika mambo madogo ya maisha; lakini Bwana huonyesha katika kushughulika Kwake na Yakobo kwamba Yeye hawezi kabisa kuidhinisha au kuvumilia uovu. Wote wanaojaribu kutafuta kisingizio au kuficha dhambi zao, na kuziruhusu zibaki katika vitabu vya mbinguni bila kuungamwa na kusamehewa, watashindwa na Shetani.” — “Wazee na Manabii,” uk. 202. “Wale ambao hawana ulinzi wa Mungu hawatapata usalama katika sehemu yoyote au nafasi.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 8, uk. 50. Kwa habari ya wakati huo wa taabu alisema Kristo: “Mwenye kuiona nafsi yake” ili apate kibali cha wanadamu “ataipoteza: naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili Yangu, ataiona.” (Mat. 10:39.) Wakati huo utaonyesha yule anayemtumikia Mungu na asiyemtumikia. Wakati huo, ulimwengu utagawanywa katika makundi mawili makubwa — “Kondoo mkono Wake wa kuume na mbuzi mkono Wake wa kushoto.” (Mat. 25:33.) Dhahiri itaonekana kwamba watu wa Mungu lazima aidha waangamie au wajisalimishe kwa matakwa ya waovu, lakini malaika hodari walio na nguvu watabadilisha mkondo wa maangamizi. {SR2: 159.2}

“Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa. Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala

160

fundi, awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa: maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi; kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.” (Ufu. 18:21-23.) {SR2: 159.3}

Wakati umati wa watu unatumbukia katika mtego wa ibilisi, na wakati anajaribu kuliondoa kabisa kanisa, “Ujumbe wa Malaika wa Tatu” unavunja vizuizi kwa uwezo mkubwa na “kilio kikuu,” ukisema, “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” (Ufunuo 18:4.) Na wakati “Kilio” cha yule malaika (mjumbe) kinavuma katika nchi umati mkubwa wa mataifa yote unaacha mfumo wa uongo, lakini maarufu wa ibada, na dhidi ya upendeleo wote wa kidunia wanachukua msimamo wao na watakatifu chini ya ulinzi wa nguvu za Mungu. Hili litachochea hasira ya joka. {SR2: 160.1}

MUHTASARI

(Fuata Chati Kwenye Ukurasa Wa 150)

Hesabu ya matukio katika sura hii huonyesha kikamilifu matukio makuu ya unabii ambayo yanapaswa kutokea kwa mfuatano wa kasi kama ulivyoonyeshwa kwa ramani. Muungano wa makanisa unaowakilishwa na “mwanamke” aliyeketi juu ya “vichwa” lazima ufanyike kabla ya utawala mseto wa huyo “mnyama” na “nabii wa uongo” utimizwe kabisa. Zile nembo (“nabii wa uongo” na “mnyama”) hufichua kwamba utakuwapo muungano wa kitaifa wa kanisa na serikali. Lakini mwanamke aliyempanda mnyama, humaanisha mfumo wa kimataifa wa kanisa na serikali, unaotekelezwa na sheria za serikali ya kiraia, na nguvu ya miujiza. Mwishoni mwa muda wa rehema, muungano unaowakilishwa na nembo ya “mnyama mwekundu sana,” utavunjwa kwa maangamizi ya “mwanamke” au kiongozi wa shirikisho hilo kama ilivyoonyeshwa kwenye kona ya chati. Dunia kwa wakati huo, kama inavyowakilishwa na pembe za yule mnyama, “watamchukia” yule kahaba, watampindua, na “kumteketeza kwa moto;” ambacho si kitu kingine isipokuwa mapinduzi dhidi ya kiongozi wa mfumo huo wa kidini na kisiasa. Wakati huo unabii wa Ufunuo 16:19, utatimizwa: “Na mji ule mkuu [Babeli] ukagawanyika mafungu matatu.” Yaani, umoja wa Uprotestanti, Ukatholiki, na Umizimu ulivunjwa. Kumbuka kitenzi, “ulivunjwa,” kikiwa katika wakati uliopita, huonyesha kwamba mji mkuu Babeli uligawanywa kabla ya mapigo saba kumiminwa; yaani, mwishoni mwa

161

muda wa rehema, wakati mwanamke alipinduliwa. “Na miji ya mataifa ikaanguka: na Babeli ule mkuu [katika hali yake iliyogawanyika] ukakumbukwa mbele ya Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira Yake.” (Ufu. 16:19, sehemu ya mwisho.) Ukali wa ghadhabu ya Mungu utamiminwa juu ya Babeli katika hali yake iliyogawanyika katika wakati wa pigo la saba. {SR2: 160.2}

Kichwa cha mnyama dubwana wa Danieli saba, katika moto unaoteketeza na “mwanamke” kama wanavyoonyeshwa kwenye ramani, huwakilisha tukio lilo hilo. Yule “mnyama” ni unabii, na “mwanamke” ni ufunuo wa unabii huo. Kisha malaika wanne wa Ufunuo saba, ambao walikuwa “wanazishikilia pepo nne za dunia [mataifa yakiwa yamedhibitiwa], kwamba pepo zisivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote,” wataziachilia hizo pepo “zivume;” na hakuna chochote kitakachobaki kuyaunganisha mataifa na watu pamoja na kuzuia uhasama, mizozo ndani na nje, itasababisha vita vya mwisho vya “Armagedoni.” (Ufu. 16:14,16.) Kutoka kwa hatua hiyo ya ramani (kufungwa kwa muda wa rehema) hadi kwa ujio wa pili wa Kristo na mwanzo wa millenia, itakuwa miezi kumi na tano — “msimu na wakati.” (Dan. 7:11, 12.) {SR2: 161.1}

Karibu na wakati wa pigo la saba yule mnyama na nabii wa uongo watatupwa ndani ya ziwa la moto. Utimizo halisi, na wao watakuwa mfano wa maangamizi ya mwisho ya waovu baada ya millenia, ambayo ni mauti ya pili. Maangamizi ya mwanamke aliyempanda mnyama mwekundu sana, na yule nabii wa uongo pamoja na yule mnyama mwenye pembe mbili wakiwa wametupwa wangali hai katika ziwa la moto, humaanisha kwamba mfumo huu wa kidini na kisiasa utavunjwa kimataifa. {SR2: 161.2}

Bwana atakapotokea, watakatifu watakusanywa (Mat. 24:30), na waovu wataangamizwa. (2 Thes. 2:8.) Mataifa yanawakilishwa na “wanyama,” “mtu wa kuasi” na ile “pembe ndogo yenye macho ya mtu na kinywa kilichonena mambo makuu.” (Danieli 7:25.) {SR2: 161.3}

Sanamu kubwa ya Danieli mbili, hulingana na wanyama wa Danieli saba. Wanyama hawa pia huwakilishwa na mnyama kama chui wa Ufunuo kumi na tatu — kinywa cha simba, miguu ya dubu, mwili wa chui, na pembe kumi. Mnyama mwekundu sana wa Ufunuo kumi na saba ni mwendelezo wa mnyama kama chui baada ya jeraha lake la mauti kupona. Anaonyeshwa hivyo kwa chati kumaanisha kwamba anazo tabia za wanyama wote waliomtangulia. Kwa hivyo, maangamizi ya hao wanyama wa Danieli saba, pia ni maangamizi ya wanyama ambao walionyeshwa kwa Yohana katika maono; na mwisho wa wanyama wote, humaanisha mwisho wa dunia. {SR2: 161.4}

Jiwe kubwa la Danieli mbili, lililoipiga sanamu

162

kwa nyayo ni nembo ya kuja kwa Kristo; na kuvunjika-vunjika kwa sanamu hiyo humaanisha kuvunjika-vunjika kwa mataifa. Kwa sababu yule mnyama mwekundu sana huileta dunia hii ya sasa kwa kikomo, yeye pia huiwakilisha dunia hii upande wa pili wa millenia, baada ya ufufuo wa pili. {SR2: 161.5}

Moto ulioshuka kutoka mbinguni juu ya yule mnyama, humaanisha mauti ya pili ya waovu, miaka mia moja baada ya ufufuo wa pili. Wakati huo unabii wa Henoko utatimizwa: “Angalia, Bwana anakuja, … ili afanye hukumu juu ya “wote,” na kuwaadhibisha wote walio waovu … kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu Yake.” (Yuda 14, 15.) Wakati aya ya 14 ya Yuda inahusu ujio wa Kristo kwa Patakatifu Mno katika hekalu la mbinguni, na aya ya 15 kwa ujio Wake wa pili, ukamilifu wa hayo maneno utatimizwa baada ya millenia, maana kwa wakati huo pekee Yeye atatekeleza “hukumu” ya mwisho juu ya wote wasiomcha Mungu, kutoka kwa Kaini hadi mwisho wa dunia hii ya sasa. {SR2: 162.1}

Sehemu ya kwanza ya ramani, iliyoandikwa tarehe 1929, hadi kwa tao, iliyotiwa alama Ezekieli 9, ni kipindi ambacho ndani yake watu 144,000 wanatiwa muhuri — utengo wa magugu kutoka kwa ngano — utakaso wa kanisa. Kwa sababu watu 144,000 ni “malimbuko,” utimizo wa Ezekieli 9 na kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu (watu 144,000), ni alama ya kuanza kwa mavuno ya mwisho, au kama vile pia huitwa, “Kilio Kikuu.” Wakati huo umati mkubwa wa Ufunuo 7:9, utakusanywa ndani ya kanisa na watumwa wa Mungu (watu 144,000). (Tazama Isaya 66:19, 20.) {SR2: 162.2}

Kesi za wote ambao wametiwa muhuri kutoka mwaka 1929 hadi muda wa rehema kufungwa kabisa zitachunguzwa mbele ya kiti cha enzi katika hekalu la mbinguni wakati bado wako hai. Uchunguzi utaanza baada ya kutimizwa Ezekieli 9. Wale ambao wametiwa muhuri kutoka mwaka 1929 hadi kwa utimizo wa Ezekieli 9 (kufungwa muda wa rehema kwa kanisa), ni watakatifu walio hai, watu 144,000 kwa idadi, ambao hawatakufa kamwe — watahamishwa bila kuonja mauti. Kundi ambalo lilipuuza fursa yao liliachwa bila muhuri kuangamia chini ya maangamizi ya Ezekieli 9; Isaya 63; na Isaya 66:15-17. Mfano huu wa uharibifu wa wadhambi kanisani ni mfano wa maangamizi ya wadhambi ulimwenguni baada ya kufungwa kwa muda wa rehema kwa dunia. Umati mkubwa wa Ufunuo 7:9, unaoishi wakati wa kufungwa kwa muda wa rehema kwa ulimwengu, pia hawatakufa, ambao kwa ajili yao watu 144,000 walikuwa mfano. Lakini waovu wote wakiwa wameachwa bila muhuri, wataangamia. “Hii ndiyo jumla ya maneno; Mche Mungu [sio mwanadamu] nawe uzishike amri Zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.” (Mhu. 12:13.) {SR2: 162.3}

163

WATU MIA NA AROBAINI NA NNE ELFU.

UFUNUO SABA NA KUMI NA NNE

Msingi wa somo hili muhimu zaidi umeshughulikiwa sana katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1. Kwa hivyo, tunakusudia kuleta tu awamu ambayo haionekani katika gombo la kwanza. Maswali yafuatayo yatajibiwa katika sura hii: Je! Kwa wakati ambao Bwana anamwamuru malaika awatie muhuri (watu 144,000) wanapatwa na ujumbe huo ulimwenguni au kanisani? Je! Watatiwa muhuri kwa wakati gani? Kwa nini wao ni “mabikira”? Mbona hakuna “uongo” vinywani mwao? Je! Wao ni wanaume pekee au ni wa jinsia zote mbili? Kwa nini wanaitwa “watumwa wa Mungu”? Mbona wao ni Israeli? {SR2: 163.1}

Tunanukuu kutoka katika maandishi ya “Roho ya Unabii”: “Huu ulikuwa wakati wa taabu ya Yakobo. Kisha watakatifu wote wakalia kwa uchungu wa roho, na wakaokolewa kwa sauti ya Mungu. Watu mia moja na arobaini na nne elfu walishinda. Nyuso zao ziliangaza kwa utukufu wa Mungu.” — “Picha za Maisha,” ukurasa 117. Kumbuka kwamba watu 144,000 kwa idadi walikuwepo katika “wakati wa taabu ya Yakobo.” Kwa mujibu wa nukuu inayofuata, wakati huo wa taabu utaanza mara tu baada ya kufungwa kwa muda wa rehema: “Wakati Kristo atakomesha kazi Yake kama mpatanishi kwa niaba ya mwanadamu, wakati huo huu wakati wa taabu utaanza.” — “Wazee na Manabii,” ukurasa 201. Wakati huo wa taabu ni kabla ya yeyote kati ya watakatifu wanaolala kufufuliwa, kwa hivyo watu 144,000 hawafufuliwi, ila ni watakatifu walio hai ambao hawajawahi kuonja mauti na watahamishwa kwa ujio wa pili wa Kristo. {SR2: 163.2}

Watu 144,000 Watiwa Muhuri Wakiwa Ndani Ya Kanisa

Ili kuweka hili wazi lazima tutoe maelezo kuhusu ya mfano siku ya upatanisho. Siku hiyo mashuhuri katika mfumo wa sherehe ilikuwa siku ya utakaso, hukumu na kukingwa. Amri ilitolewa kwamba katika mwezi wa saba na katika siku ya kumi ya mwezi huo (siku ya upatanisho) kila Mwisraeli alipaswa kuitesa nafsi yake, aungame dhambi yake, na kuleta dhabihu. Yeye ambaye alishindwa kuitikia mwito wa Mungu alikatiliwa mbali (aliangamia) kutoka kati ya watu wa Mungu. Kwa hivyo, ilikuwa siku ya hukumu na utakaso wa kambi ya Israeli. Wakati ambapo mdhambi aliangamia, wacha Mungu walihifadhiwa. Mfano huo ulio hai uliwekwa kwa manufaa yetu wakati huu wa sasa, ambao juu yetu siku ya upatanisho ya uakisi imekuja. Picha hii katika hekalu la duniani imekusudiwa kuonyesha kazi ya lile la mbinguni. {SR2: 163.3}

164

Wakati hukumu ilifunguliwa mwaka 1844, kama ilivyoelezewa hapo awali, uchunguzi ulianzia kwa wafu, na wakati sehemu hiyo ya kazi itakamilika, basi itaanza hukumu ya walio hai. Wakati uchunguzi wa kongamano la wafu ukiwa unaendelea, hauwezi kuwapo mtengo kati ya kongamano la walio hai. Lakini wakati Kuhani wetu Mkuu ataanza upatanisho kwa ajili ya walio hai, lazima uwepo ujumbe wa ukweli wa sasa — ukipiga tarumbeta — ukimhimiza kila mtu kumshikilia Mwana-Kondoo wa Mungu (Kristo) ambaye tu, ki-mfano, anaweza kuja katika hekalu, aungame dhambi yake na kuuhifadhi uhai wake. Isipokuwa kufungwa kwa hukumu ya wafu na kuanza kwa ya walio hai kufanywe tujue, hatutakuwa na ukweli wa sasa wakati hukumu ya walio hai i kwenye kikao. Wala hukumu kama hiyo haitakuwa halali au ya haki. Yeye anayeshindwa kuitikia mwito wa mbinguni, ataachwa bila muhuri au ulinzi wa Mungu, na kwa hivyo lazima atakatiliwe mbali kati ya watu Wake, kama ilivyofananishwa na huduma katika ya mfano siku ya upatanisho. {SR2: 164.1}

Mtume anasema: “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu.” (1 Petro 4:17.) Ukweli kwamba kwa kanisa la “Waadventista wa Sabato” pekee umekuja ujumbe kama huo uliotajwa, uliowasilishwa kwao katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, ni thibitisho la ziada kwamba kanisa hili haswa ni nyumba ya Mungu. Wakati huu wa hukumu pia huitwa “wakati wa mavuno.” “Viacheni vyote vikue hadi wakati wa mavuno,” Kristo alisema, “na wakati wa mavuno Nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome: bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.” (Mat. 13:30.) Maneno ya Bwana wetu yanapatana kabisa na ya mfano siku ya upatanisho, yakitabiri kwamba ni siku ya kutenganisha magugu na ngano, au kuwakatilia mbali wadhambi wasiotubu kutoka kati ya watu wa Mungu ( utakaso wa kanisa). Kwa hivyo, mavuno yanaanza na kazi ya kufunga kwa kanisa. Kristo alisema: “Viacheni vyote vikue hadi wakati wa mavuno.” Katika Ufunuo 14:4, kwa habari ya watu 144,000 tunasoma, “Ni malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba katika utakaso au mtengo wa magugu kutoka kwa ngano katika kanisa la Mungu, watakuwapo watu 144,000 ambao wameungama dhambi zao; na kwa hivyo kufanywa weupe na wasafi kwa damu ya Kristo yenye thamani, kwa maana wao ni “malimbuko.” Hili pia limethibitishwa na “Roho ya Unabii,” kwa maana tunasoma: “Huku kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu ni sawa na kule alionyeshwa Ezekieli katika maono.” — “Shuhuda Kwa Wachungaji,” ukurasa wa 445. Tunanukuu kutoka katika “Shuhuda Kwa Kanisa,” Gombo la 3, uk. 266: “Watu wa kweli wa Mungu, walio na roho ya kazi ya Bwana, na wokovu wa watu moyoni, daima wataitazama dhambi katika tabia yake halisi, ya uovu.

165

Siku zote watakuwa kwenye pande za kushughulikia kwa uaminifu na uwazi dhambi ambazo huwazonga kwa urahisi watu wa Mungu. Hasa katika kazi ya kufunga kwa ajili ya kanisa, katika wakati wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000.” {SR2: 164.2}

Tena kwa ukurasa wa 267: “Maki jambo hili kwa uangalifu: Wale wanaoipokea alama safi ya ukweli, iliyowekwa ndani yao kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, iliyowakilishwa na alama ya mtu aliyevaa kitani, ni wale ‘wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika’ kanisani… Soma sura ya tisa ya Ezekieli. Lakini mchinjo wa jumla kwa wale wote ambao hawaoni hivyo tofauti kubwa kati ya dhambi na haki, na hawajihisi kama wale wanaosimama katika shauri la Mungu na kuipokea alama, umeelezewa kwa amri kwa wale watu watano walio na silaha za kuchinjia: ‘Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa mzee na kijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu.” {SR2: 165.1}

Ufafanuzi wa “jumla” ni: “mkubwa lakini sio wa ulimwengu wote.” Kwa hivyo haumaanishi maangamizi ya dunia atakapotokea Bwana; lakini unahusianishwa na waovu kanisani. Mchinjo huu ni halisi, utawatenga na kuwaweka huru watu wa Mungu kutoka kwa dhambi na wadhambi, vinginevyo kutia alama hakungekuwa na maana. Mada iyo hiyo tena inaletwa kwa mtazamo katika “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, ukurasa wa 211: “Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu.” Ghadhabu ya Mungu haiwezi, na haijawahi kuwa ya kiroho. Tunakumbushwa tena kwamba watu 144,000 ni masalia: “Sasa hakika wao ni masalia watu walio ishara” … ‘Katika siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka. Tena itakuwa ya kwamba, yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu, yaani kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu.’” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, ukurasa wa 476. Kwa hivyo watu 144,000 ni wale ambao wametiwa muhuri katika hukumu kwa kanisa, na pamoja nao hukumu kwa walio hai ilianzia. Kwa hivyo, wao ni malimbuko. {SR2: 165.2}

Wakati namba hii imetiwa muhuri, muda wa rehema utafunga kwa kanisa, na hukumu kwa wale walio ulimwenguni itaanza. “Magugu” yanapoangamia kwa ule wakati muda wa rehema unafunga kwa kanisa, vivyo hivyo mwishoni mwa hukumu kwa ulimwengu wadhambi watafikia kikomo chao; mmoja ni mfano wa mwingine. Kwa habari ya watu 144,000: “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira.” (Ufu. 14:4.) “Wanawake” waliotajwa katika Maandiko haya ni nembo za makanisa

166

najisi. “Wanawake” hawa wanaletwa kwa mtazamo katika Ufunuo 17, chini ya mfano wa mwanamke aliyeketi juu ya yule mnyama mwekundu sana. Tunanukuu Ufunuo 17:5: “Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli mkuu, mama wa makahaba na machukizo ya nchi.” Mama huyu na binti zake ni wale “wanawake” ambao watu 144,000 hawajatiwa unajisi nao, kwa sababu ujumbe wa kutiwa muhuri uliwapata ndani ya kanisa. Kwa hivyo wakiwa katika kanisa la Mungu wakati wametiwa muhuri, ni “mabikira” — “hawajatiwa unajisi na wanawake” (na makanisa yaliyoanguka). {SR2: 165.2}

Watumwa Wa Mungu Katika Wakati Wa Mavuno

Katika Ufunuo 7:3, watu 144,000 huitwa “Watumwa wa Mungu wetu.” Iwapo ni watumwa, basi lazima wawe na majukumu ya kutekeleza. Wanaletwa tena kwa mtazamo na nabii Isaya kuhusiana na utakaso wa kanisa na kuangamizwa kwa waovu: “Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka (watu 144,000) kwa mataifa …. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka kwa mataifa kuwa sadaka kwa Bwana, … katika chombo safi hadi katika nyumba ya Bwana” — kanisa. (Isa. 66:19,20.) “Na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.” (Isa. 4:2.) Kwa hivyo, watu 144,000 huitwa “watumwa.” (Kwa uchunguzi zaidi wa Isa. 66, angalia “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 165-172.) {SR2: 166.1}

Husemwa pia kulihusu kundi hili la ajabu: “Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo.” (Ufu. 14:5.) Andiko hili huweka wazi kwamba injili wanayoitangaza ni Neno la kweli la Mungu. Kwa hivyo, ujumbe wanaouwasilisha kwa ulimwengu hauwezi kutiliwa shaka kuhusu usafi wake. Nabii wa Patmo baada ya kunena kuhusu kutiwa muhuri kwa watu 144,000 anasema: “Baada ya hayo nikaona, na, tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” (Ufu. 7:9.) Kwa hivyo, umati huu mkubwa unakusanywa kutoka kwa mataifa yote, baada ya kazi ya kufunga kwa kanisa, na katika wakati wa mavuno makubwa. Mitende mikononi mwao humaanisha ushindi dhidi ya yule mnyama na sanamu yake, kifo na kaburi. Mmoja wa wazee walio mbele ya kiti cha enzi alisema kuwahusu: “Hao ndio waliotoka katika dhiki ile iliyo kuu” (wakati wa taabu ya Yakobo). (Ufu. 7:14.) Mtumwa wa Bwana pia hushuhudia katika nukuu zifuatazo: “Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa; na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika mapango na chini ya miamba ya milima; wakiiambia milima na miamba,

167

Tuangukieni, tusitirini mbele ya uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu ya hasira Yake imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu. 6:14-17. {SR2: 166.2}

“‘Baada ya hayo nikaona, na, tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu, wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo…. Hao ndio waliotoka katika dhiki ile iliyo kuu nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo’… Ufu. 7:9, 14. {SR2: 167.1}

“Katika Maandiko haya makundi mawili yanaletwa kwa mtazamo. Kundi moja wenyewe waliruhusu kudanganywa, na kuungana na wale ambao Bwana ana vita nao.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, uk. 267, 268. Maadamu Roho ya Unabii huonyesha wazi haya makundi mawili (wale ambao waliililia miamba, na wale walio na mitende) wote waliishi katika wakati wa ile dhiki kuu na ghadhabu ya Mungu, ni dhahiri kwamba umati mkubwa ulio na mitende mikononi mwao ni watakatifu walio hai waliovutwa kwa injili katika wakati wa mavuno kwa kazi ya watu 144,000. {SR2: 167.2}

Je! Watu 144,000 Ni Wa Jinsia Zote?

Amri ya kulitia alama kundi hili ili lisianguke chini ya silaha za kunjia kwa mfano watu watano, inasomeka kama ifuatavyo: “Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso za watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.” (Ezekieli 9:4.) Kwa sababu Neno husema: “Ukatie alama katika vipaji vya nyuso za watu,” kwa hivyo wengine wameshikilia msimamo kwamba hilo kundi lote linajumuisha wanaume pekee. Sababu ya pili iliyotolewa kwa wazo hili baya ni kwamba watakuwa wafalme na makuhani na kwa hivyo lazima wawe wanaume. Wazo lililochukuliwa na vifungu hivi haliwezi kuthibitishwa na sehemu zingine za Maandiko. Kwa hivyo tunalazimika kuchunguza zaidi kwa undani katika hiyo mada. {SR2: 167.3}

Wakati Ezekieli huwaita “watu,” Yohana husema wao ni “mabikira.” (Ufu. 14:4.) Sasa, ikiwa tunapaswa kuchukua msimamo kwamba Ezekieli humaanisha wanaume pekee, basi tunaweza vile vile kusema, Yohana humaanisha wanawake pekee. Inawezekana kwamba mwandishi mmoja anapingana na mwingine? Hapana hakika. Tunahitimisha kwa Maandiko yafuatayo kwamba watu 144,000 ni wa jinsia zote: “Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, kwamba watu wote wapate kuamini kwa Yeye.” (Yohana 1:7.) “Watu wote,” lazima wajumuishe wanaume na wanawake, vinginevyo wokovu ungekuwa kwa wanaume tu. “Nami, Nikiinuliwa

168

juu ya nchi, Nitawavuta watu wote Kwangu.” (Yohana 12:32.) Ikiwa neno watu wote katika andiko hili halijumulishi jinsia zote mbili, basi wanawake wamepotea. “Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama haoni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.” (Matendo 17:30.) Tena, iwapo “watu wote” hayajumuishi wanaume na wanawake, basi wanawake hawajaamriwa kutubu. Ni dhahiri kwamba nomino, watu, ni jina la mkusanyo la Kibiblia la wote wanaume na wanawake. Hilo ni kweli kwa uumbaji, maana, Mungu alimuumba mwanamke kutoka kwa mwanamume. Kwa hivyo, yeye ni mwenzi-wa-mume. Tena katika Wagalatia 3:28, tunasoma: “Hapana mtu mume wala mtu mke: maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.”{SR2: 167.4}

Kwa kuwa hakuna tofauti kati ya jinsia katika Kristo, basi tunaona kwamba wanawake na wanaume wanaweza kuwa wafalme na makuhani. Wazo lilo hilo laweza kuchukuliwa kwa uzoefu wa taifa la Wayahudi: “Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule …. Wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.” (Waamuzi 4:4, 5.) Mwanamke huyu alimiliki nafasi ya mwanamume, kuwa mwamuzi wa watu wa Mungu, ambayo ni sawa na mfalme. Sio mfalme tu, bali yeye pia alikuwa ni nabii wa kike. Tena tunasoma katika Luka 2:36, 37, “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri: na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake; naye alikuwa mjane wa miaka themanini na minne, hakuondoka katika hekalu, ila aliabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Pia mke wa Shalumu akiwa nabii mke alifundisha Israeli na kukisimamia chuo hicho. (Angalia 2 Wafalme 22:14-16.) Filipo mwinjilisti alikuwa na binti wanne ambao pia walitabiri. (Tazama Matendo 21:8, 9.) {SR2: 168.1}

Kutoka kwa taarifa ya Paulo katika 1 Timotheo 2:12, “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu,” utatambua maana hapa ni kwamba, mwanamke anapaswa kuwa chini ya utiifu kwa mwanamume jinsi Mungu alivyoamuru, na sio kwamba yeye amekatazwa kushikilia ofisi ya mwalimu. Tena tunanukuu, “Wanawake na wanyamaze ndani ya makanisa: maana hawana ruhusa kunena; bali wameamriwa kuwa chini ya utiifu, kama vile inenavyo torati nayo.” (1 Kor. 14:34.) Soma sura hiyo na utaona kwamba Paulo anataka kuanzisha utaratibu katika makanisa, kwa sababu kulikuwa na machafuko makubwa katika kunena kwa lugha zisizojulikana. Kwa hivyo, ili kuzima machafuko, anasema: “Wanawake na wanyamaze katika kanisa.” Yeye hawakatazi kunena ikiwa wanalo jukumu la kutekeleza. Iwapo funzo hili lingalikuwa limepewa utiifu ingalikuwapo tofauti kubwa iliyoboreshwa katika nyumba ya Mungu. {SR2: 168.2}

Hapo mwanzo Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke sawa, kama mfalme na malkia. “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia,

169

Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha: mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” (Mwa. (1:28.) Kumbuka kwamba walipewa ufalme wote wawili. Walakini, baada ya kutenda dhambi badiliko lilifanywa: “Akamwambia mwanamke, … na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, Naye atakutawala.” (Mwa. 3:16.) Kwa hivyo, baada ya mwanamke kufanya dhambi alianguka chini ya serikali ya mwanadamu. Lakini kile ambacho Hawa alipoteza kwa udanganyifu, kitarejeshwa kwa ukombozi. Hivyo tena usawa wa wote utasimamishwa kama wafalme na malkia. Kwa hivyo, “Hakuna mwanamume wala mwanamke ndani ya Kristo Yesu.” Kristo mwenyewe huthibitisha wazo hilo katika usemi ufuatao: “Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi, wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walio mbinguni.”{SR2: 168.3}

Kwa hivyo nomino “watu” iliyotumika na Ezekieli, na nomino “bikira” iliyotumika na Yohana ni neno la mkusanyo la Kibiblia linalowashughulisha wote. Zaidi ya hayo, dhehebu lina idadi zaidi kidogo ya 300,000 kwa wakati huu. Karibu theluthi yake moja ni wanaume. Iwapo kila mwanamume alitiwa muhuri na kuhesabiwa kama mmoja wa watu 144,000, bado tungekuwa na upungufu sana kufikia idadi hiyo. Tena tunakumbuka wakati wa pasaka huko Misri damu kwa mwimo wa mlango ilikuwa mfano wa kutiwa alama au muhuri. (“Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 96-98.) {SR2: 169.1}

Katika usiku huo popote damu ilionekana kwenye mwimo wa mlango, mzaliwa wa kwanza akiwa ni mwanamume au mwanamke, hakufa, itakuwa hivyo sasa, wale wanaopokea muhuri, wameipaka damu kwa mwimo wa mlango (kipaji cha uso), na kwa sababu mzaliwa wa kwanza wa makundi yote mawili, wale waliokufa na wale ambao hawakufa, walikuwa mfano wa ukuhani wa sasa (ukasisi), kwa udhahiri, ule mfano huashiria ukasisi katika uakisi unaojumuisha jinsia zote mbili — mzaliwa wa kwanza aliyekufa huwakilisha daraja ambalo litaanguka chini ya silaha za kuchinjia za watu hao watano, na mzaliwa wa kwanza ambaye aliokoka kifo, huwakilisha kundi ambalo litapokea alama ya mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi na kupita kutoka kwa kifo hadi uzimani. Kwa hivyo mzaliwa wa kwanza aliyeishi na kupita katika bahari ya shamu, ni mfano wa watu 144,000. Malimbuko ya mavuno, ni watumwa wa Mungu katika wakati wa “kilio kikuu” cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu. {SR2: 169.2}

Baada ya utakaso wa kanisa na kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu, wakati huo ujumbe katika sura ya 18 ya Ufunuo utafikia kilele katika “kilio kikuu.” “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” (Ufu. 18:4.) Watakatifu wanapoisikia sauti ya Mchungaji mwema katika ujumbe wa injili, wanajitenga kwa ulimwengu na kujiunga na watu 144,000. Wakati mchakato huu wa kupepeta katika makanisa yaliyoanguka unaendelea, mtu aliye na

170

kidau cha wino wa mwandishi anawatia muhuri wale wanaotoka kwake. Watakatifu wote watakapotoka Babeli na kuingia kanisani, basi kazi ya mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi itakoma na muda wa rehema utafungwa. (Tazama “Maandishi ya Awali,” uk. 279.) Kwa hivyo, shughuli ya watu watano walio na silaha za kuchinjia itaendelea na kazi yao itakoma wakati Kristo atakapokuja kuwachukua watakatifu Wake kwa maana wao ni wasimamizi wa mji — kanisa. (Tazama Ezek. 9:1; “Pambano Kuu,” uk. 656.) Wakati huo dunia ya sasa itafika mwisho na millenia ya ukiwa itaanza; wakati ambapo watakatifu watawahukumu waovu. {SR2: 169.3}

Watu 144,000 wanaitwa Israeli kwa sababu uzoefu wao ni nakala pacha ya Israeli wa Kale wakitoka Misri kwenda kumiliki nchi ya ahadi. Misri ya kale ni nembo ya dunia. Utumwa wa Misri ni nembo ya utumwa wa dhambi. Vuguvugu la Kutoka ni mfano wa kanisa linalojitenga na dhambi na wadhambi. Maangamizi ya mzaliwa wa kwanza huko Misri na kuzamishwa katika bahari ya shamu, huashiria kuangamizwa kwa waovu katika kuwatenga watakatifu. Nyikani ni nembo ya kanisa likiwa mbali na ulimwengu. Kuangamizwa kwa wasiotii nyikani, ni kielezo cha kulidumisha kanisa likiwa safi baada ya kutakaswa. Kuimiliki nchi ya ahadi ni mfano wa Israeli (watakatifu) kuimiliki dunia. Vita dhidi ya wapagani katika nchi ya ahadi huashiria kuangamizwa kwa waovu ulimwenguni. Tunapitia njia iyo hiyo mara nyingine tena, na kwa kufanya hivyo, lazima tuepuke makosa ambayo yalifanywa katika uzoefu wa zamani. {SR2: 170.1}

MWISHONI MWA MLANGO WA REHEMA, MAKABURI YANAKOMA —

Ufunuo 14 NA 15

Ufu. 14:1, “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Zayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja Naye, wenye jina Lake na jina la Baba Yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.” “Mwana-kondoo” huashiria Kristo, kumaanisha nafasi Anayoshikilia kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema, wakati bado akiwaombea watu Wake; kwa hivyo, idadi maalum ya watakatifu itasimama pamoja Naye kwa nchi wakati Yeye bado yu mahali Patakatifu Mno. Mlima Zayuni katika Yerusalemu wa zamani palikuwa eneo la zamani la mji huo, na mahali pa makao ya kifalme ya Daudi na warithi wake. Kwa hivyo, kutoka kwa mtazamo huo lazima tuwasilishe maana ya “Mwana-Kondoo” ambaye alisimama juu ya Mlima Zayuni. Tunaambiwa kwa Maandiko yafuatayo Bwana alikuwa ametoa ahadi kwamba nyumba ya Daudi (Mlima Zayuni) ilikuwa nuru kwake na kwa wanawe milele. “Lakini Bwana

171

hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama Alivyomwahidi kuwa atampa nuru yeye na wazao wake milele.” (2 Nya. 21:7.) Ahadi hiyo haikuwa kwa Mlima Zayuni (nyumba ya Daudi) katika Yerusalemu wa zamani, kwa maana uwepo wa taifa la Wayahudi ulikuwa na masharti. {SR2: 170.2}

“Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi; bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani Kristo.” — “mwana wa Daudi.” (Gal. 3:16.) Kwa hivyo, Mlima Zayuni, kama ulivyo katika Ufunuo 14:1, ndio mahali pakuu pa kifalme katika Yerusalemu wa mbinguni, jinsi Daudi mwenyewe anavyosema; “Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya mbari ya Daudi.” (Zab. 122:5.) Daudi alitazamia wakati ambapo hukumu mbinguni ingeanzishwa: “Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.” (Zekaria 13:1.) {SR2: 171.1}

Kwa hivyo, maono ya Yohana ya watu 144,000 walipokuwa wamesimama kwa Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo, ni tukio baada ya kundi hili maalum la watakatifu kutiwa muhuri, wakati fulani kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema. Kutiwa muhuri kwa watu 144,000 ni mwishoni mwa hukumu ya wafu, na mwanzoni mwa hukumu ya walio hai. Kwa hivyo, wanalo jukumu kubwa la kutekeleza juu ya dunia kuhusiana na hukumu. Utumishi wao ulionyeshwa kwa mfano na Israeli ya kale wakati walipaswa kuimiliki Nchi ya Ahadi. Nabii Zekaria amefafanua vyema wakati huo: “Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, na kama malaika wa Bwana mbele yao. Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba Nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu [kanisa]. Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba: nao watanitazama Mimi ambaye walimchoma, [kwa sababu Yeye alikufa kwa dhambi zao] nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee, nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.” (Zek. 12:8-11.) Utakuwa uzoefu wa ajabu ilioje tunapoelewa kikamilifu upendo wa Mungu na bei iliyolipwa kwa ajili ya ukombozi wetu! {SR2: 171.2}

Nabii Mika huwaita watu 144,000, “mabaki ya Yakobo.” (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 102.) “Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake: ndivyo atakavyotukomboa kutoka kwa Ashuru, yeye huja katika nchi yetu, na wakati anaingia ndani ya mipaka yetu. “Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi, yasiyomngojea mtu,

172

wala kuwakawilia wanadamu. Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa kati ya kabila nyingi mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo: ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa. Mkono wako utainuliwa juu ya adui zako, na adui zako wote watauliwa mbali …. Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa, wasiosikiliza.” (Mika 5:6-9, 15.) {SR2: 171.3}

“Yeye Fungu la Yakobo siye kama hawa; maana Ndiye aliyeviumba vitu vyote: Na Israeli ni fimbo ya urithi Wake: Bwana wa majeshi ndilo jina Lake. Wewe u shoka Langu na silaha Zangu za vita [144,000]: kwa wewe Nitawavunja-vunja mataifa, na kwa wewe Nitaharibu falme; na kwa wewe Nitamvunja-vunja farasi na yeye ampandaye; na kwa wewe Nitalivunja-vunja gari la vita na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe Nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe, na kwa wewe Nitawavunja-vunja maliwali na maakida.” (Yer. 51:19-23.) Kwa hivyo, katika kutimizwa kwa maono ya Yohana, watu 144,000 “Watasimama juu ya Mlima Zayuni,” sio kwa mwili, lakini katika maana ya nafasi wanayomiliki. Vivyo hivyo na wanawali watano walioingia pamoja Naye katika harusi. (Tazama “Pambano Kuu,” uk. 427.) Jinsi Israeli ya zamani ilikuwa tisho kwa mataifa katika nchi ya ahadi, vivyo hivyo tu Israeli ya Mungu kwa wakati huu itakuwa tisho kwa mdhambi ulimwenguni, na jinsi Israeli ya zamani ilibidi ipigane ikitumia upanga ili kuimiliki nchi, vivyo hivyo Israeli ya sasa lazima ipigane ikitumia “upanga wa Roho” ili imiliki ulimwengu (nchi ya ahadi). {SR2: 172.1}

“Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu: na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakivipiga vinubi vyao: na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee: wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila watu mia na arobaini na nne elfu, waliokombolewa katika nchi.” (Ufu. 14:2, 3.) {SR2: 172.2}

Wimbo huo uliimbwa mbinguni na viumbe vya mbinguni mbele ya kiti cha enzi, na mbele ya wanyama, na wazee. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba hukumu ilikuwa inaendelea. (Maelezo zaidi yatafuata.) Kumbuka kwamba watu 144,000 hawakuuimba, lakini wangeweza tu kujifunza huo “wimbo” jinsi ulivyoimbwa mbinguni; Yaani, wao pekee yao walielewa ukweli wa mbinguni haswa kwa wakati huo na nafasi yao kuhusiana na ujumbe ambao lazima wautangaze. {SR2: 172.3}

“Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika,

173

Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa: Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya kazi zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.” (Ufu. 14:13.) “Wafu wafao katika Bwana tangu sasa,” yaani, kutoka mwanzoni mwa “kilio kikuu.” Kwa hivyo neno latangaza kwamba baadhi ya watakatifu watalazwa ndani ya kaburi hata katika wakati wa mavuno (kilio kikuu). Tunanukuu kutoka “Mashauri kwa Afya,” uk. 375 “Wengi watazikwa walale kabla ya mateso makali ya wakati wa taabu kuja juu ya ulimwengu.” {SR2: 172.4}

Ambapo baadhi ya watakatifu watazikwa walale katika wakati wa “kilio kikuu,” hilo limewekwa wazi na Ufunuo 15:1, 2, ya kwamba wote walio hai baada ya muda wa rehema kufungwa na kabla ya kuanza kumiminwa mapigo watahamishwa bila kuonja mauti: “Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia. Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto: na wale waliokuwa wamemshinda yule mnyama, na sanamu yake, na hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo wakiwa na vinubi vya Mungu.” “Bahari ya kioo” ni nembo ya uzima wa milele. (Imefafanuliwa katika sura nyingine.) Kwa kadiri wote waliokuwa wamepata ushindi walisimama kando-kando ya bahari, huashiria kwamba wamepita kutoka kwa kifo kwenda uzimani, na kituo chao sasa ni “Mungu, Yerusalemu mpya.” {SR2: 173.1}

Ufu. 15:5-8: “Na baada ya hayo nikaona, na, tazama, hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa: Na wale malaika saba wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi na meupe, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu. Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba vitasa saba vya dhahabu vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele. Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu, na uweza Wake; wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.” Baada ya upelelezi kukamilika na kila kesi kuamuliwa, hekalu la ushuhuda litafunguka kama wakati lile la mfano lilivyofunguka mwishoni mwa mfumo wa kafara: “pazia ambalo liligawanya vyumba viwili lilipasuka vipande viwili toka juu hata chini.” (Tazama Mat. 27:51.) {SR2: 173.2}

Mlango ambao utafunguliwa baada ya kufungwa kwa rehema ni mlango wa kuingia patakatifu ambao ulifungwa mwaka 1844. Baada ya kufungwa kwa muda wa rehema hekalu litajazwa na nguvu na utukufu wa Mungu ili mtu awaye yote asiweze kuingia ndani hata baada ya mapigo saba yametimizwa. Kuonyesha kwamba watu wote wa Mungu walisimama juu ya bahari ya kioo (uzima wa milele) kisha mlango wa rehema ukafungwa. Kwa hivyo baada ya Yesu kuondoka mahali patakatifu mno, watumwa wa Mungu hawatakuwa na matini ya kuhubiri kwa mazishi na injili kwa wadhambi. {SR2: 173.3}

174

SURA YA ISHIRINI NA NNE YA MATHAYO, NA ISHARA ZA KUJA KWA KRISTO

“Hata alipokuwa Ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja Kwako, na ya mwisho wa dunia? Yesu akajibu akawaambia, Angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina Langu, wakisema, Mimi ni Kristo, nao watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita: angalieni msitishwe: maana hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme: kutakuwa na njaa, na tauni, na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua: nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina Langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Mat. 24:3-14.) {SR2: 174.1}

Swali la moja kwa moja lililowekwa kwa Kristo na jibu Lake kuhusu uhakikisho wa kuja Kwake kwa mara ya pili, na mwisho wa dunia hii ya sasa, ni wazi sana na hujieleza lenyewe bila kuacha nafasi ya kutilia shaka. Yeye hakusema kwamba mwisho wa dunia ya sasa ya dhambi hautakuja, lakini Alisema wazi kwamba utakuja. Walakini Alisema kabla ya mwisho kuja, “Injili hii ya ufalme [ishara za ujio Wake wa pili kama zilivyotabiriwa katika sura hii] itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote [sio kwamba mataifa yote yataongoka, ila kuwa ushuhuda] hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Wale wanaofundisha kinyume cha maelezo haya wazi ya Bwana, ni wale ambao Yeye hunena kuwahusu: “Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.” Isitoshe, Bwana husema: “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki, ukaonekana hata magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja Kwake Mwana wa Adamu.” (Mat. 24:27.) {SR2: 174.2}

Wakati baadhi ya manabii hawa wa uongo hukana kabisa kuja Kwake, wengine huthubutu kusema, “Yeye amekwisha kuja.” Bado wengine hudai kwamba hakuna mtu atakayemwona Atakapokuja, lakini, Atauanzisha ufalme Wake kwa dunia, na ulimwengu huu hautafika mwisho

175

kamwe, n.k. Tunauliza swali: Je! Kristo anasimulia hadithi isiyo ya kweli, au je! manabii hawa wa uongo wanatimiza utabiri Wake kwa kujaribu kuwadanganya watakatifu mintarafu kuja Kwake, na kuipindua imani yao katika Neno la Bwana, na hivyo kuwapunja taji ya uzima? Iwapo hawa si waongo ambao Yeye huwanena, basi ni kina nani? {SR2: 174.3}

Iwapo watendakazi wa maovu kama hao huthubutu kujaribu kupotosha usemi Wake wazi kama ilivyo katika tukio hili, je! isiweze kutarajiwa kwamba watajaribu kuupindua ukweli wote wa Biblia? {SR2: 175.1}

Kristo atakapokuja “kama vile umeme utokavyo mashariki, ukaonekana hata magharibi,” manabii hao wa uongo watatahayarika. Wa-ufunuo pia anatangaza: “Tazama, Yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona Yeye, na hao waliomchoma Yeye: [yaani, wale waliomchoma watafufuliwa kabla ya kuja Kwake. Tazama Dan. 12:2] na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili Yake. Naam. Amina. (Ufu. 1:7.) Naam, Kristo wetu atakuja na tutamwona Yeye jinsi Alivyo, “Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu: Ndiye tuliyemngoja Atuokoe; Huyu ndiye Bwana; tuliyemngoja, na tushangilie na kuufurahia wokovu Wake.” (Isa. 25:9.) {SR2: 175.2}

Ingawa manabii hawa wa uongo na wadhambi hawataki kumuona Yeye akija, lazima watamwona: “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika mapango na chini ya miamba ya milima; wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini mbele ya uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu ya hasira Yake imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” (Ufu. 6:15-17.) Na hivyo ndivyo mwisho utakavyokuja kwa wadhambi, lakini si kwa watu wa Mungu: “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: Kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Thes. 4:16, 17.) {SR2: 175.3}

Kwa wadhambi siku hiyo itakuwa siku ya kuogofya, na kwa hao Yeye atakuja “kama mwivi usiku,” lakini sivyo kwa wale wanaomngojea Yeye. Maana, akizungumzia juu ya mateso makuu ambayo yaliwapata watu Wake katika vizazi vya giza wakati wa miaka 1260 ya Danieli 7:25, Asema: “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika: ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya

176

mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika Zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule Wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” (Mat. 24:29-31.) {SR2: 175.4}

Bwana akitazama mbele kwa kizazi hiki, asema, “kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota.” (Luka 21:25.) Kwa hivyo, “mara tu baada ya ile dhiki” (mateso makubwa) jua lilipaswa kuwa giza. Tarehe 19 Mei, 1780, unabii huu ulitimizwa. Kunukuu “Pambano Kuu”: “‘Karibu ikiwa sivyo kwa jumla pekee yake, kama ishara ya kushangaza na ya aina yake ambayo haijaelezeka … husimama siku ya giza ya Mei 19, 1780 — giza la kigeni kabisa lililozifunika mbingu zilizoonekana na anga huko New England.” Aliyeshuhudia kwa macho mwenyeji wa Massachusetts hulielezea tukio hilo kama ifuatavyo: {SR2: 176.1}

“Asubuhi jua lilichomoza kwa uzuri, lakini mara likafunikwa. Mawingu yakashuka chini, na kutoka kwayo, yalikuwa meusi na ya kutisha, yalivyoonekana upesi baada ya hapo, umeme ukawakawaka, radi ikanguruma, na mvua kidogo ikanyesha. Kuelekea saa tatu, mawingu yakawa mepesi, na yakaonekana kama rangi ya shaba, na ardhi, miamba, miti, majengo, maji, na watu wakabadilishwa kwa nuru hii ya ajabu, isiyo ya kawaida. Dakika chache baadaye, wingu zito jeusi likatanda juu ya anga lote isipokuwa mzingo mwembamba kwenye upeo wa macho, na kulikuwa na giza kama ambavyo huwa saa tatu jioni ya majira ya joto …. {SR2: 176.2}

Hofu, wasiwasi, na mshangao pole pole ukajaza akili za watu. Wanawake walisimama mlangoni, wakitazama mandhari ya giza; watu walirudi kutoka kwa kazi zao mashambani; seremala aliacha zana zake; mhunzi nyumba yake ya kufua chuma, mfanyabiashara aliacha meza yake. Shule zilifungwa, na kwa kutetemeka watoto walikimbia kuelekea nyumbani. Wasafiri wakawekwa kwa nyumba ya mashambani iliokuwa karibu. “Nini kinachokuja?” kiliuliza kila kinywa na moyo. Inaonekana kana kwamba kimbunga kilikuwa karibu kupiga hadi upande mwingine wa nchi, au kana kwamba ilikuwa siku ya kukomeshwa kwa vitu vyote …. {SR2: 176.3}

‘Kiwango cha giza hili kilikuwa cha kustaajabisha. Lilitazamwa hadi mbali mashariki kama Falmouth. Kuelekea upande wa magharibi lilifikia sehemu ya mbali zaidi ya Connecticut, na hadi Albany. Kulelekea upande wa kusini, lilitazamwa kando-kando pwani ya bahari; na kaskazini hadi umbali kama ambavyo makazi ya Amerika hutanda. {SR2: 176.4}

“Giza kubwa la siku lilifuatwa, saa moja au mbili kabla ya jioni, na sehemu ya anga iliyokuwa wazi, na jua likatokea, ingawa bado lilikuwa limefunikwa katika ukungu mweusi, mzito. ‘Baada ya jua kutua, wingu likaja tena juu, na likakuwa giza upesi sana.’ ‘Wala giza la usiku halikuwa lisilo la kawaida na la kutisha kuliko lile la mchana; Ingawaje ulikuwapo mwezi mpevu, hakuna kitu kilichoonekana lakini kwa msaada wa

177

nuru nyingine bandia, ambayo, wakati ilionekana kutoka kwa nyumba za jirani na maeneo mengine kwa mbali, ilionekana kupitia aina ya giza la Wamisri ambalo lilionekana kuwa lisiloweza kupenyezwa kwa mionzi. Alisema aliyeshuhudia tukio hilo: ‘Sikuweza kufikiri kwa wakati huo, kwamba iwapo kila sayari yenye mwanga katika ulimwengu wote ilikuwa imefunikwa kwa vivuli visivyoweza kupenyezwa, au kuondolewa zisiwepo giza halingeweza kuwa kamili.’ Ingawa saa tatu usiku huo mwezi kamili ulichomoza, ‘haukuwa na athari hata ndogo kufukuza kabisa vivuli kama mauti.’ Baada ya usiku wa manane giza likatoweka, na mwezi, ulipoonekana kwanza, ulikuwa unaonekana kama damu. {SR2: 176.5}

“Mei 19, 1780, husimama katika historia kama ‘Siku ya Giza.’ Tangu wakati wa Musa, hakuna kipindi cha giza la uzito sawa, eneo, na muda, ambao limewahi kurekodiwa. Maelezo ya tukio hili, kama yalivyotolewa na walioshuhudia kwa macho, ni mwangwi tu wa maneno ya Bwana, yaliyoandikwa na nabii Yoeli miaka elfu mbili ishirini na tano iliyopita kabla kutimia kwalo: “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.” {SR2: 177.1}

“Mnamo 1833, miaka miwili baada ya Miller kuanza kuwasilisha kwa umma ushahidi wa Kristo kuja hivi punde, ishara ya mwisho ilionekana kati ya hizo ambazo ziliahidiwa na Mwokozi kama dalili za ujio Wake wa pili. Yesu alisema, “Nyota zitaanguka kutoka mbinguni.’ Na Yohana katika Ufunuo alitangaza, alipotazama katika maono matukio ambayo yangetangaza siku ya Mungu. ‘Nyota za mbinguni zikaanguka juu ya nchi, kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.’ Utabiri huu ulipokea utimizo wa kuvutia na wa kushangaza katika manyunyu makuu ya nyota Novemba 13, 1833. Hilo lilikuwa onyesho kubwa sana na la ajabu la nyota zinazoanguka ambalo halijawahi kuandikwa; “Anga yote, juu ya Marekani yote, wakati huo, kwa masaa mengi, katika mfyatuko wa moto! Hakuna ishara ya kimbingu iliyowahi kutukia katika nchi hii, tangu mwanzo wa kutulia kwake, ambayo ilitazamwa kwa kuvutiwa sana na kundi moja katika jamii, au kwa hofu kubwa na kamsa na lingine.’ “Utukufu wake na uzuri wa kutisha bado huendelea kukaa katika mawazo ya wengi. …. Kamwe mvua haikunyesha nzito kuliko vimondo vilivyoanguka kwa nchi; mashariki, magharibi kaskazini, na kusini, ilikuwa sawa. Kwa ufupi, mbingu zote zilionekana kuwa kwa mwendo…. Onyesho hilo, jinsi lilivyoelezwa katika jarida la Profesa Silliman, lilionekana kote Amerika Kaskazini … Kuanzia saa nane hadi mchana mkamilifu, anga likiwa kamilifu na bila wingu, mchezo usiokoma wa mianga miangavu inayong’aa uliendelea kufuliza katika mbingu zote. {SR2: 177.2}

“Hakuna lugha, kwa kweli, inayoweza kusimulia fahari ya onyesho hilo kubwa; … hakuna mtu ambaye hakulishuhudia anaweza kutunga

178

wazo la kutosha la ufahamu wa utukufu wake. Ilionekana kana kwamba mbingu zote zenye nyota zilikuwa zimekusanyika kwa kituo kimoja karibu na upeo, na zilikuwa zikichomoza kwa wakati mmoja, kwa kasimwelekeo ya umeme, hadi kwa kila sehemu ya upeo wa macho; na bado hazikuisha — maelfu zilifuata upesi mikondo ya maelfu, kana kwamba ziliumbwa kwa ajili ya hafla hiyo.’ {SR2: 177.3}

“Katika Jarida la Biashara la New York la Novemba 14, 1833, ilionekana makala ndefu kuhusu ishara hii ya ajabu, lilikuwa na taarifa hii: ‘Hakuna mwanafalsafa au msomi aliyesimulia au kunakili tukio, nadhani, kama lile la jana asubuhi. Nabii miaka elfu na mia nane iliyopita alilitabiri sawasawa, iwapo tutakuwa katika taabu ya kuelewa nyota zitaanguka kumaanisha nyota zinazoanguka… katika maana pekee ambayo inawezekana kuwa kweli kihalisi.’ {SR2: 178.1}

“Hivyo ndivyo ishara ya mwisho kati ya hizo ishara za kuja Kwake ambazo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuzihusu, ‘Nanyi kadhalika myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.’ Baada ya mambo haya, Yohana aliona, kama tukio kubwa litakalokuja, mbingu zikikunjwa kama karatasi, wakati dunia ilitetemeka, milima na visiwa vikaondolewa kutoka mahali pake, na waovu kwa hofu wakatafuta kukimbia kutoka kwa uwepo wa Mwana wa Adamu.” Pambano Kuu, uk. 306-308, 333, 334. {SR2: 178.2}

Kristo alikuwa amewaagiza watu Wake watazame ishara za ujio Wake, na washangilie kama wangeziona dalili za Mfalme wao anayekuja. “Basi mambo hayo yaanzapo kutokea,” Alisema “changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu; kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.” (Luka 21:28.) Aliwaonyesha wafuasi Wake miti ya msimu wa kuchipua iliyokuwa ikichipuza, na kusema: “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu: Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.” (Mat. 24:32, 33.) Wakati Mwokozi ameelezea waziwazi ukaribu wa kuja Kwake kwa kizazi ambacho kitashuhudia ishara hizi zote, Yeye hajatuacha gizani kuhusu ni muda gani tangu wakati wa utimilifu wa ishara hizi hadi kwa tukio hilo kubwa na tukufu, kwa maana Yeye aliongezea: “Kizazi hiki [ambacho kimeziona ishara hizo] hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.” (Mat. 24:34.) Kwa sababu kizazi kilichonenwa na Bwana chakaribia kupita, na ufalme wa uzima wa milele kukaribishwa, mchunguzi wa ukweli hapaswi kupuuza fursa yake kwa kuruhusu mambo yasiyo na umuhimu kushughulisha akili, au wakati wake. {SR2: 178.3}

Zilikabidhiwa Kwa Dhehebu La S.D.A.

Injili ya kuja kwa Kristo katika kizazi hiki, na ishara za nyakati zilivyo katika Mathayo 24, zilikabidhiwa

179

Dhehebu la Waadventista wa Sabato tangu mwaka 1844. Hakuna kundi lingine la watu ambalo limekuwa na mzigo wa ujumbe ambao hufundishwa katika sura hii (hizo ishara na mwisho wa dunia), na uharaka wa kuutangaza kwa upesi katika kizazi hiki. Kwa hivyo, pongezi, au hukumu yoyote ambayo imeandikwa kwa “mtumwa” katika Mathayo 24, haiwezi kuwahusu watu wengine. Isitoshe, kwa maana sehemu ya Ukristo iliyosalia ilikuwa imeanguka mwaka 1844 kwa sababu walizikataa jumbe ambazo zilitumwa kwao na kwa hivyo Mungu hangeruhusu nuru iangaze kupitia kwao tangu wakati huo, ni dhahiri kwamba injili ya sura ya 24 ya Mathayo haingeweza kutangazwa na watu wengine wowote. Kwa hivyo, taarifa kumhusu yule mtumwa katika aya ifuatayo inalihusu tu dhehebu lililotajwa hapo juu. {SR2: 178.4}

“Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba Yake, awape watu [ulimwengu] chakula kwa wakati wake” — ukweli wa sasa? (Mat. 24:45.) Kumbuka, kwamba liko swali mtumwa huyu mwaminifu anaweza kuwa nani. Iwapo wale watu ambao kimsingi injili hii ilikabidhiwa kwao wangalikuwa waaminifu, basi ahadi ifuatayo ingekuwa yao: “Heri mtumwa yule, ambaye Bwana wake Ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin Nawaambieni, atamweka juu ya vitu Vyake vyote.” (Mat. 24:46, 47.) Maana ya “vitu Vyake vyote” ni kuikamilisha injili, kuleta haki ya milele, na kuukaribisha ufalme wa Kristo! Ahadi ya ajabu kama nini! Lakini tazama hatari ya kupoteza utukufu huu wa milele: “Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja Kwake; akaanza kuwapiga wajoli wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi.” (Mat. 24:48, 49.) “Mtumwa” (kwa umoja) ambaye “ataanza kuwapiga wajoli wenzake” (kwa wingi) humaanisha uongozi — “malaika” wa kanisa la Walaodekia — wale walio wasimamizi wa “nyumba.” Lakini “watumwa” (kwa wingi) wanahusu ukasisi chini ya uongozi huo. Kwa kutokuwa na uaminifu “mtumwa huyo,” injili imekawilishwa; kizazi kinakaribia kupita, na kazi i miaka mingi nyuma. Tokeo lake ni, kwamba kucheleweshwa hakujadhihirishwa kwa vitendo pekee, lakini pia husemwa kwa maneno, “Bwana wangu anakawia kuja Kwake.” Na kadri dhambi moja inavyoelekeza kwa nyingine, fundisho la “Matengenezo ya Afya,” ulaji wa vyakula ambavyo vimebadilishwa kwa uvumbuzi wa kisasa “vitoweo” vya Babeli, nk. — kujiingiza katika tamaa za mwili, yamepuuzwa sana, na hivyo kutimiza maneno, “kula na kunywa pamoja na walevi.” {SR2: 179.1}

Fundisho la matengenezo ya afya husemekana kuwa “mkono wa kulia wa Ujumbe wa Malaika wa Tatu,” na ya kwamba kazi ya matibabu ni “mkono wa kulia wa ujumbe.” Wazo la mageuzi ya afya ni jambo lililopitwa na wakati kadiri kanisa kama kundi linavyohusika,

180

na uongozi haujali. Lakini hilo sio baya zaidi, mtumwa huyu wa Mungu asiye mwaminifu hata amethubutu kuunyoosha mkono wake juu ya ghuba kuunda muungano haramu wa taasisi za matibabu za dhehebu na zile za ulimwengu ambazo hupingana vikali na wazo la matengenezo ya afya — mkono wa kulia wa “Ujumbe wa Malaika wa Tatu.” Njia haswa ambayo ilianzishwa ili kudumisha na kuendesha sehemu hiyo ya kazi, inafungwa kamba kwa muungano na sasa ili kuudumisha muungano huu limelazimishwa kutoa kafara kanuni ile ambayo kwayo ilianzishwa. Hapo shirika la Mungu la kutibu wagonjwa na kuzuia magonjwa kwa kuishi kiafya na uponyaji wa kiungu kupitia utiifu kwa ukweli, limebadilishwa na dawa za kulevya. {SR2: 179.2}

Kwa hivyo shetani ameukata kabisa mkono wa kulia wa “Ujumbe wa Malaika wa Tatu,” na kwa kifaa hiki cha ujanja amelipora kanisa la Mungu taasisi zake za matibabu! Ni janga lililoje! Ni hasara ilioje! Je! Watu waaminifu wa Mungu kwa wakati kama huu wasingekuja kwa msaada wa Bwana dhidi ya wenye nguvu? Ni vipi kundi la watu wenye nuru kubwa wanaweza kuwa vipofu sana ni zaidi ya uelewa wa mwanadamu; ni siri! {SR2: 180.1}

Laiti wao (wale waliokabidhiwa jukumu hili kubwa) wangalikuwa waaminifu kwa amana waliokabidhiwa, baraka za milele zinazopatikana katika aya ifuatayo zingekuwa zao: “Atamweka juu ya vitu vyake vyote.” Lakini kwake yule anayeupuuza utume wa Bwana wake: “Bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyomtazamia Yeye, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” (Mat. 24:50, 51.) Laiti wangekuwa wameutii ujumbe wa mwisho uliotumwa kwao, ukiitisha mageuzi ya uamuzi katika mambo haya, sura ifuatayo (Mathayo 25) ingalikuwa tofauti kinabii. {SR2: 180.2}

Wanawali Kumi–Mathayo 25

“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wenye busara, na watano wapumbavu. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao: Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, Haya, bwana arusi yuaja; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi: afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda

181

kununua, bwana arusi akaja; nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin Nawaambia, Siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa ambayo Mwana wa Adamu atakuja.” (Mat. 25:1-13.) {SR2: 180.3}

Angalia kwamba sura ya 25 ni endelezo la ya 24. Weka alama kwa neno, “ndipo,” likimaanisha wakati walitimiza maneno ya kinabii yaliyo katika Mat. 24:48-51. Wanawali ni mfano wa kanisa. Namba “kumi,” ina maana ya nembo inayomaanisha ulimwengu (kanisa kama kundi). Kumbuka kwamba wote ni “mabikira.” Watu 144,000 hutajwa kwa neno lilo hilo. (Angalia Ufu. 14:4.) Neno “mabikira,” humaanisha kwamba daraja linalowakilishwa nao (kumi), sio wale ambao wameitwa watoke Babeli (makanisa yaliyoanguka) kwa wakati “kilio” kinafanywa. Kwa maana, iwapo wangetoka Babeli kwa mwito “Tokeni kwake, enyi watu wangu” (Ufu. 18:4), wangekuwa wametiwa unajisi na “wanawake” (makanisa yaliyoanguka), na kwa hivyo, hawangeweza kuitwa “mabikira.” Kwa hivyo, ujumbe wa “Kilio cha Usiku wa Manane” lazima uwapate ndani ya nyumba ya Mungu — mabikira. {SR2: 181.1}

“Kilio cha Usiku wa Manane” kilitangazwa mara ya kwanza kabla ya mwaka 1844, na kuja kwa “Bwana-arusi” kulikuwa ni ujio wa Kristo hadi patakatifu mno katika hekalu la mbinguni kwa hukumu ya upelelezi ya watakatifu. Upelelezi ukiwa katika sehemu mbili; ya kwanza, hukumu kwa wafu, na ya pili kwa walio hai, “kilio” lazima kirudiwe, vinginevyo hatungekuwa na ukweli wa sasa kwa wakati wa hukumu ya walio hai. “Kilio” cha walio hai kikiwa ni cha umuhimu mkubwa kwa dunia kuliko kile cha wafu, na kwa sababu “mabikira” ni mfano wa kanisa lililo hai, huo mfano lazima uwe na matumizi ya moja kwa moja kwa kanisa wakati huu wa sasa, — ujio wa bwana-arusi kwa hukumu ya walio hai. Lakini isivyo moja kwa moja huonyesha nyuma hadi mwanzoni mwa “Kilio cha Usiku wa Manane” (ujumbe wa malaika wa kwanza — hukumu ya wafu). Jumbe hizo zikiwa za tukio lile lile, hukumu, zote (kwa walio hai na kwa wafu) huitwa “kilio cha usiku wa manane.” Lilo hilo huthibitishwa na mfano wenyewe. {SR2: 181.2}

“Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, Haya, bwana arusi yuaja; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.” Kumbuka kwamba “walisinzia na kulala” kabla ya kilio kufanywa. Katika msimu wa joto wa mwaka 1844, kati ya wakati ambapo ilifikiriwa kwanza kwamba siku 2300 zingemalizika (Machi 21), na tarehe ya pili (Oktoba 22 ya mwaka uo huo), kipindi hiki walikihusisha kama “wakati wa kukawia.” Lakini maki kwamba “kilio” kilikuwa kikiendelea kwa miaka

182

kadhaa (ujumbe wa Miller), na wakati wa kukawia ukatumika mwishoni mwake baada ya kugundua kosa lao, ambalo ni kinyume na matumizi sahihi ya mfano huo; maana kwa mujibu wa mfano huo walikawia kabla ya kilio kufanywa. Kwa hivyo, wakati wa kukawia lazima uwe hukumu kwa wafu, kabla ya bwana-harusi kuja kwa upelezi wa walio hai, ambao ni ndani ya wakati “mabikira kumi” walipevuka. Kwa hivyo, huo ni wakati ambao wote walisinzia na kulala. Matumizi haya pia yanapatana kikamilifu na ujumbe kwa Walaodekia. (Tazama Ufu. 3:14-19; Isa. 52:1, 2.) {SR2: 181.3}

Iwapo matumizi yaliyotajwa hapo juu ni sahihi, basi mwishoni mwa kipindi cha kukawia, au kabla tu ya kuanza kwa hukumu ya walio hai, lazima uwepo ujumbe — “kilio”; na ikiwa “mabikira” ni mfano wa kanisa kama kundi katika wakati wa “kilio,” basi, ujumbe lazima uwe wa kanisa pekee. Hili pia limethibitishwa katika “Pambano Kuu,” ukurasa wa 425. Maadamu kipo “kilio” kama hicho kilichowasilishwa katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, hakionyeshi tu kwamba matumizi ya mfano huo ni sahihi, lakini pia huthibitisha kanisa hilo kuwa ni “Nyumba ya Mungu.” {SR2: 182.1}

“Wote walisinzia na kulala.” Taarifa hii ya Bwana huthibitisha kwamba kanisa kama kundi limekuwa linalala — ikiwa katika upatano kamili na ufafanuzi wa awali wa sura ya 24 ya Mathayo. Watano walikuwa wapumbavu na watano wenye busara. Namba “kumi” ikiwa ni nembo ya kanisa kama kundi, idadi ya tano kwa tano, yamaanisha nusu kwa nusu. Idadi ya dhehebu kwa wakati huu ni izidio kidogo 300,000; nusu ya idadi hii itakuwa karibu 150,000. Iwapo tunapaswa kuondoa waliokufa (waliokengeuka, lakini bado wako kwenye kumbukumbu ya kanisa), namba inayopatikana baada ya mapunguzo kama hayo itakuwa karibu 144,000. Hivyo tena inathibitisha kwamba watu 144,000 ni mabikira watano wenye busara; na wapumbavu ndio wale watakaoanguka chini ya silaha za kuangamiza mikononi mwa wale “watu watano.” {SR2: 182.2}

“Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.” “Mafuta” ni nembo ya Roho wa Mungu katika umbo la ujumbe (ukweli); kwa maana, ni kitu kinachotoa nuru (Neno la Mungu la unabii). Taa lazima iwe nembo ya moyo ambao ndani yake Neno (mafuta) huhifadhiwa. Kuzitengeneza taa zao, ni “kutayarisha” mioyo yao; yaani, dhamiri zao zikiwa zimeamshwa walianza kuonyesha nia. Lakini ni watano tu kati yao ambao walikuwa na ugavi wa ziada wa mafuta katika vyombo vyao. Walipoondoka kumlaki bwana-arusi, taa za wale wapumbavu zikazimika; na walipojikuta ndani ya giza, lilifanya kwendelea kwao kusiwezekane. Sasa, swali linatokea: Ni nini kilifanya taa zao zizimike, na mbona waliweza kurudi nyuma, lakini hawakwenda mbele? Maadamu ujumbe wa hukumu kwa wafu ulikuwa

183

ukweli wa sasa tangu mwaka 1844, mwanzoni mwa hukumu kwa walio hai (wakati ambapo kilio kilifanywa), haukwendelea kuwa ukweli tena. Kwa sababu hiyo taa zao zilizimika. Hawangeweza kusonga mbele kwa sababu walikuwa wapumbavu; yaani, hawakuipokea ile nuru — hukumu kwa walio hai. Je! “mafuta” yalikuwa mbali na mfikio wao? Maneno katika mfano huo huthibitisha kwamba wote walisikia kilio, “wakaamka, wakazitengeneza taa zao.” Watano kati yao walishindwa kupata usambazaji wa mafuta kwa sababu walikuwa “wapumbavu,” — hawakujifunza wenyewe. Waliwaruhusu wengine kufikiri kwa niaba yao; walichagua upande rahisi, maarufu, na kuyapokea maamuzi ya viongozi, waliiga makosa ya wengine na kwa hivyo wakaachwa bila kusambaziwa mafuta, — waliporwa ukweli, wakalaghaiwa kuhusu utukufu, na kuachwa gizani! {SR2: 182.3}

“Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.” Mwishowe mabikira wapumbavu walijiona wako gizani. Kisha wakaenda kwa wenye busara na kuomba mafuta kama zawadi; “Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi: afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.” Mafuta haya huuzwa na lazima kiwepo kitu fulani kilichopeanwa kwa kubadilishana kupata usambazaji. Bei ambayo walipaswa kulipa ilikuwa “kuugua na kulia kwa sababu ya machukizo yaliyofanywa kati yake,” kuacha dhambi na kutii ukweli. Risiti yao kwa thamani ya kubadilishana ingekuwa muhuri wa Mungu aliye hai katika vipaji vya nyuso zao. {SR2: 183.1}

“Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin Nawaambia, Siwajui ninyi.” Wakati mabikira wapumbavu mwishowe walipokuja mlangoni, ni dhahiri kwamba waliyapata mafuta (walipata habari ya ujumbe) lakini kulikuwa na ukawio — mlango ulikuwa umefungwa, na wakaachwa nje. Sasa, mbona hawakujali mwanzoni, na kuwa na bidii mwishowe? Uzoefu katika tukio hili ni karibu sawa na ule wa gharika. Wakati Nuhu alitangaza kuja kwa gharika, ulimwengu ulipuuza ujumbe huo; lakini wale walioamini, waliingia ndani ya safina kwa wakati mwafaka na mlango ukafungwa. Lakini si muda mrefu baadaye, ishara za utabiri wa Nuhu zilionekana; na matone ya mvua yalipoanza kunyesha watu wengi waovu walishtuka na kukimbilia safina, lakini mlango ulikuwa umefungwa na waliachwa nje. Mlango ambao “ulikuwa umefungwa,” ni nembo inayoonyesha kwamba mlango wa rehema kwa kanisa ulikuwa umefungwa muda mfupi tu baada ya mabikira wapumbavu kushtuka. Mwishowe walikuwa tayari kulipa bei na kuyanunua mafuta; lakini halikuwa badiliko la moyo, hofu tu ya kupoteza. Mwenendo wao wa kutenda ulikuwa umewaacha bila muhuri — “mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi”

184

alikuwa amewapita. Ni kosa baya kama nini! Kuvunjika moyo kulioje! Karibu waokolewe, lakini wakapotea kabisa. {SR2: 183.2}

“Ujio wa Kristo kama kuhani wetu mkuu mahali patakatifu mno, kwa utakaso wa patakatifu, uliofunuliwa katika Danieli 8:14; ujio wa Mwana wa Adamu kwa Mzee wa siku, jinsi ulivyoonyeshwa katika Danieli 7:13; na ujio wa Bwana kwa hekalu Lake, uliotabiriwa na Malaki, ni maelezo ya tukio lile lile; na hili pia huwakilishwa na ujio wa bwana-arusi kwa arusi, ulivyoelezwa na Kristo, katika mfano wa wanawali kumi, wa Mathayo 25.” — “Pambano Kuu,” uk. 426. {SR2: 184.1}

Maelezo ya Danieli yanahusu mwanzo wa hukumu kwa wafu; lakini yale ya Malaki 3:1-3, yanahusu hukumu kwa walio hai — yote ni ya tukio hilo moja — siku ya upatanisho — utakaso wa patakatifu. {SR2: 184.2}

“Ujio wa bwana-arusi, ulioonyeshwa hapa, utafanyika kabla ya arusi. Arusi huwakilisha Kristo kuupokea ufalme Wake. Mji mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ambao ni mji mkuu na mwakilishi wa ufalme, huitwa ‘bibi-arusi, mke wa mwana-kondoo.’ Malaika akamwambia Yohana, Njoo huku, nitakuonyesha bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. ‘Alinichukua katika roho,’ Asema nabii, ‘akanionyeshea mji huo mkubwa, Yerusalemu mtakatifu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.’ Dhahiri, basi, bibi-arusi huwakilisha mji mtakatifu, na wanawali ambao hutoka kwenda kumlaki bwana-arusi ni nembo ya kanisa. Katika Ufunuo watu wa Mungu husemekana kuwa wageni kwenye karamu ya arusi. Iwapo ni wageni, hawawezi kuwakilishwa pia kama bibi-arusi. Kristo, jinsi alivyoeleza nabii Danieli, atapokea kutoka kwa Mzee wa siku mbinguni; ‘enzi, na utukufu na ufalme;’ Ataupokea Yerusalemu Mpya, mji mkuu wa ufalme Wake, ‘ulioandaliwa kama bibi-arusi aliyepambwa kwa mumewe.’ Baada ya kuupokea ufalme, Atakuja katika utukufu Wake, kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, kwa ukombozi wa watu Wake, ambao wataketi ‘pamoja na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo,’ kwenye meza Yake katika ufalme Wake, kushiriki karamu ya jioni ya arusi ya Mwana-Kondoo.” — “Pambano Kuu,” uk. 426, 427. {SR2: 184.3}

Wanawali waliitwa wamlaki Yeye, na hivyo kwa imani huingia ndani pamoja Naye ili kuonekana mbele ya Baba — Jaji Mkuu. Muhuri ni kibali; huweka majina yao katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo na kwa hivyo huwapa haki ya kuonekana mbele ya Baba katika hukumu; sio kwa uhalisi, bali kwa mfano; na kwa hivyo dhambi zao kufutwa. Mathayo 24:36, 50, ni maelezo ya tukio lilo hilo. “Basi, kesheni, kwa maana hamwijui siku wala saa ambayo Mwana wa Adamu atakuja.” (Mat. 25:13.) Hili linarejelea wakati wa hukumu, na si kuja Kwake duniani; kwa maana, watakatifu wataijua siku na saa

185

ya kuja kwa Kristo katika mawingu kuwapokea waliokombolewa, jinsi itakavyotangazwa na Baba muda mfupi kabla ya kuja Kwake. (Tazama “Pambano Kuu,” uk. 640.) {SR2: 184.4}

Muhtasari Wa Wanawali Kumi

Namba, “kumi,” ikiwa ni nembo ya ulimwengu wote, huliwakilisha kanisa kama kundi kabla ya kuanza kwa hukumu ya walio hai — katika kipindi cha kutiwa muhuri watu 144,000, na kabla ya “Kilio Kikuu” cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu; kikiwa kipindi cha malimbuko ya mavuno. Wanawali watano wenye busara ni wale waliomwamini Mungu na neno Lake pekee; bila kumtegemea mwanadamu, na walikuwa na njaa ya kweli, wakitafuta nuru, na kuipokea kwa furaha ilipokuja. Hivyo waliupokea muhuri ulioidhinishwa na Mungu, dhambi zao zikafutwa, na maisha yao yakahakikishwa — walipita kutoka kwa hukumu na kifo hadi kwa utukufu na uzima wa milele. Ni watumwa, wafalme na makuhani wa Mungu — 144,000 kwa idadi. {SR2: 185.1}

Wanawali watano wapumbavu ni wale waliowategemea wanadamu; walikuwa tayari kwamba wengine wafikiri na kusoma kwa niaba yao. Upendo wao kwa ulimwengu huu na mambo yake, ulizidi upendo wao kwa Kristo na ulimwengu ujao. Hawakuwa na hisia ya kweli kwa matokeo ya kutisha ya dhambi. Bidii yao kwa ajili ya ubinafsi, ilizamisha bidii yao kwa ajili ya nyumba ya Mungu na heshima Yake. Waliridhika na taa zao zilizokuwa zikiwaka na mafuta kidogo ndani yazo. Hawakuona hitaji la nuru zaidi — manabii, ukweli au ujumbe. Walisema mioyoni mwao, sisi ni tajiri na tumejitajirisha wala hatuna haja ya kitu. Walikuwa na chuki dhidi ya nuru kwa neno la Mungu, na hawakuupokea ukweli kwa sababu njia ambayo ulikujia haikuwa ya chaguo lao. {SR2: 185.2}

Maarifa ya ukweli wa sasa, ambayo wanawali watano wapumbavu walikuwa nayo tangu mwaka 1844 ni hukumu ya wafu, na ndiyo yalikuwa mafuta pekee ndani ya taa zao. Hukumu ya walio hai ilipoanza, na “kilio kikafanywa,” walipatikana bila mafuta haya ya ziada katika vyombo vyao; walikuwa wamepuuza amri ya Bwana wao: “Basi, kesheni, kwa maana hamwijui siku wala saa ambayo Mwana wa Adamu atakuja.” Kwa hivyo wale wenye hekima walipoondoka kwenda kumlaki bwana-arusi taa za wapumbavu zikazimika, kwa maana, hukumu ya wafu ilikuwa imepita. Kwa hivyo, haikuwa ukweli wa sasa tena, na hivyo wakaachwa gizani. Mwanzoni mwa hukumu za Mungu waliona kosa lao na wakakimbilia kwa safina ya usalama, lakini ilikuwa mbali na ufikio wao kwa maana hawakujua lolote kuhusu ujumbe huo, na wakati walipokuwa wameupata (walizijaza taa zao mafuta), hapo palikuwa na ukawio, malaika alikuwa amepita “kati ya mji, kati ya Yerusalemu,”

186

kanisa — kutiwa muhuri kulikuwa kumekwisha, na mlango wa rehema kwa kanisa ulikuwa umefungwa — mlango ukafungwa. Kwa hivyo waliachwa nje. Kisha wakaja na maneno haya: “Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin Nawaambia, Siwajui ninyi.” “Mwekee fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Kutakuwa kuvunjika moyo kulioje! {SR2: 185.3}

Itagunduliwa kwamba ufungwaji wa mlango wa rehema kwa kanisa na ule wa ulimwengu ni matukio mawili tofauti. La awali ni uwakilishi mdogo wa la mwisho. Andiko la kwa lililotangulia linapatikana katika Mathayo 25:11, 12; lakini kwa la mwisho tunasoma: “Mwenye kudhulumu, na azidi kudhulumu: na mwenye uchafu, na azidi kuwa mchafu: na mwenye haki na azidi kufanya haki: na mtakatifu, na azidi kuwa mtakatifu. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” (Ufu. 22:11, 12.) Wakati huu wale ambao walikuwa kama wanawali watano wapumbavu, watasema, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” (Yer. 8:20.) “Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari, na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki, watapiga mbio wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” (Amosi 8:12.) {SR2: 186.1}

187

MIHURI SABA NA HEKALU

Ili kufanya matumizi yafaayo ya mihuri saba, lazima tuwe na ufahamu bora wa utumishi wa hekalu la mbinguni, chanzo chake, na lengo la uwepo wake kama lilivyofundishwa na hekalu la duniani lililojengwa na Musa. (Ebr. 8:5.) {SR2: 187.1}

Katika ujenzi wa hekalu na utumishi, umefunuliwa mpango wa wokovu. Chumba cha kwanza, kiliitwa patakatifu, ambamo kuhani mkuu alihudumu kila siku kwa dhabihu na namna tofauti za zawadi na kutawadha, palikuwa mahali pa kuungama dhambi. Hayo yote yalikuwa kivuli cha mambo ya mbinguni kufunua wazi mpango wa wokovu. Chumba cha pili, ndani ya pazia, kiliitwa “patakatifu mno,” au “patakatifu pa patakatifu,” kilifunguliwa tu katika mwezi wa saba, na siku ya kumi ya mwezi huo, kila mwaka; humo ukombozi kutoka kwa hukumu ya sheria ulihakikishiwa. (Law. 23:27-30, 16:34.) Iliitwa siku ya upatanisho, hukumu, au utakaso wa Patakatifu. (Law. 16:33, Dan. 7:10; 8:14.) Hii ilikuwa siku ya kufuta dhambi zilizorundana katika mwaka, na ilikuwa nembo ya siku kuu ya upatanisho; si kwa mfano, bali kwa uhalisi. (Tazama Law. 16:19. Pia “Pambano Kuu,” ukurasa wa 485.) Kiti kilichofunikwa na makerubi kikiwa kinaitwa kiti cha rehema, huthibitisha kwamba ni kiti cha enzi cha rehema, na kwa hivyo kiti cha enzi cha hukumu, ambapo wadhambi wanaweza kupata rehema. {SR2: 187.2}

Mfumo wote — kuhani, dhabihu, na utumishi — ulikuwa mfano wa Kristo na utumishi Wake katika hekalu la mbinguni, ambalo Bwana aliliweka na si mwanadamu. (Angalia Ebr. 8:2, na “Matendo ya Mitume,” ukurasa wa 14.) Mahali patakatifu palikuwa pa kuungama dhambi, bali patakatifu mno pa kuzifuta dhambi. {SR2: 187.3}

Wakati utumishi katika hekalu la duniani ulikuwa ukifanya kazi, haungeweza kuwapo utumishi katika lile la mbinguni hadi baada ya Kristo kupaa na kuwa Kuhani wetu Mkuu. (Angalia Waebrania 8.) Kwa hivyo, wakati utumishi wa mbinguni ulianza, huduma katika la duniani zilikoma. Waabudu wa kweli ndani ya la duniani, ambao kwa imani walitazama mbele kwa utumishi wa la mbinguni, walihesabiwa katika vitabu vya mbinguni kama wanaostahili uzima wa milele. Kumbukumbu zao zilipaswa kuchunguzwa wakati Kristo Kuhani wetu Mkuu alipoingia ndani ya pazia hadi patakatifu mno kuzifuta dhambi. (Angalia Dan. 7:10.) {SR2: 187.4}

Roho wa Mungu husema: Haiwezekani kwamba dhambi za wanadamu zinapaswa kufutwa hadi baada ya hukumu kwa wakati ambao

188

kesi zao zitachunguzwa.” — “Pambano Kuu,” ukurasa wa 485. Wakati huduma katika patakatifu pa duniani zilikuwa zinatekelezwa, la mbinguni lilitumika kama hifadhi ya dhambi zilizoungamwa. Vivyo hivyo ni kweli hata chini ya utumishi wa Kristo wakati alipokuwa patakatifu, hadi Alipoingia patakatifu mno. {SR2: 187.5}

Mpango Wa Ukombozi Ulitangulia Anguko

Hekalu la mbinguni likiwa kwa ajili ya kuungamwa na kufutwa kwa dhambi, halingeweza kuwapo kabla ya dhambi kuingia na kuleta hitaji la jengo kama hilo. Ingawa ibada ya patakatifu ilianzishwa baada ya Adamu kutenda dhambi, mpango wa wokovu ulikuwapo siku zote, na ulifunuliwa ndani, na kwa, utumishi wa patakatifu. Kwa hivyo mpango ambao ulitangulia anguko hupatikana katika Kristo, ambaye ndani yake ilikuwapo na ipo nguvu ya kuwakomboa wote. {SR2: 188.1}

Je! Hekalu Ni Mahali Pa Milele Pa Kiti Cha Enzi Cha Mungu?

Hekalu la duniani lilipokuwapo Mungu alikutana na watu Wake katika patakatifu mno ambapo uwepo Wake ulidhihirishwa kati ya makerubi kwa kiti cha rehema. Kwa hivyo, wengine wamechukua msimamo kwamba mahali pa milele pa kiti cha enzi cha Mungu ni katika “patakatifu mno” pa hekalu la mbinguni, lakini wazo kama hilo ni kinyume kwa mfano na uakisi. Sababu ya kwanza ni, kwamba hekalu halikuwapo siku zote, jinsi ilivyofafanuliwa hapo awali; pili, patakatifu mno palifungwa wakati Kristo alikuwa akihudumu katika patakatifu. Paulo asema: “Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni.” (Ebr. 8:1.) Iwapo kiti cha enzi cha Mungu kilikuwa “patakatifu mno” wakati Kristo alipaa juu, wakati huo Yeye lazima angalikuwa aliingia papo hapo “patakatifu mno,” badala ya “patakatifu.” Msimamo kama huo ni kinyume kwa Maandiko na utumishi. Mungu alikutana na watu Wake wa zamani katika patakatifu mno, ambapo, kwa mfano, dhambi zao zilifutwa. Kwa hivyo, kuonyesha kwa njia ya mfano, kwamba Yeye hawezi kukutana uso kwa uso na watakatifu Wake hadi baada ya kukutana nao katika “patakatifu mno” — amezifuta dhambi zao, sio kwa mfano, lakini kwa uhalisi — katika siku ya upatanisho ya uakisi. Tutalithibitisha hili tena kutokea kwa pembe nyingine. {SR2: 188.2}

Wa-ufunuo, katika maono karibu mwaka 96 B.K., aliruhusiwa kutazama ndani ya vyumba vyote viwili. Sauti kutoka mbinguni ikanena naye, “Panda hata huku, nami Nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.” Kisha akaona kiti cha enzi kimewekwa, na mmoja ameketi juu ya kile kiti cha enzi, na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na bahari ya kioo kama bilauri. (Angalia Ufu. 4:1-6.) Sauti ilimwambia kwamba mambo ambayo aliona yangetukia “baada ya hapo,” yaani, siku za usoni kutoka kwa wakati wa maono. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba hapakuwa na kiti cha enzi hapo kwa wakati huo — karibu miaka 62 baada ya Kristo kupaa hadi kwa

189

Baba. Kwa hivyo, Kristo aliketi mkono wa kuume wa Mungu, lakini si kwa kiti cha enzi katika hekalu. Nini, basi? Je! Mungu anavyo viti vya enzi zaidi ya kimoja? “Kiti cha Enzi” ni kikalio, na popote Mungu hukaa, hapo ndipo kiti Chake cha Enzi kilipo. Kumbuka kwamba “karibu na mbele ya kiti cha enzi” ndani ya hekalu, iko “bahari ya kioo.” {SR2: 188.3}

Sasa tunasoma kuhusu kiti cha enzi kingine: “Kisha akanionyesha mto safi wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo.” (Ufu. 22:1.) Tena, kumbuka kwamba kutoka kwa mojawapo wa viti vya enzi hutoka “mto wa uzima,” lakini kutoka kwa kingine, “bahari ya kioo.” Kwa hivyo, vipo viti vya enzi viwili. Kristo aliketi mkono wa kuume wa Mungu kwa kiti cha enzi ambacho hutoka “mto wa uzima,” kwa maana hiki ndicho huitwa “kiti cha enzi cha Mungu na cha mwana-kondoo.” Hapa ni pahali pa milele pa makao ya Mungu; lakini kile ndani ya hekalu kiliwekwa kwa wakati uliopo, (Angalia Dan. 7:9, 10), wakati wa utumishi wa Kristo katika patakatifu mno, ambacho ni kiti cha enzi cha hukumu — cha kuzifuta dhambi na kupeana thawabu. Kile ambacho hutoka mto wa uzima ni kiti cha enzi cha uzima na cha milele. {SR2: 189.1}

Ki Wapi Kiti Cha Enzi Alichokiona Yohana?

Ufunuo 4:1, 2, 4-6: “Baada ya hayo Naliona, na, tazama, mlango ukafunguka mbinguni: na sauti ile ya kwanza Niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami; ikisema, Panda hata huku, nami Nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara Nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mmoja ameketi juu ya kile kiti …. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi: na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo, na sauti: na taa saba za moto zilikuwa zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo roho saba za Mungu. Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo kama bilauri: na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne wamejaa macho mbele na nyuma.” {SR2: 189.2}

Maelezo ya mahali pale huthibitisha ya kwamba ni katika hekalu la mbinguni. Hilo huungwa mkono na Roho ya Unabii: “Katika maono mtume Yohana alipewa taswira ya Hekalu la Mungu mbinguni, aliona humo ‘taa saba za moto zikiwaka mbele ya kiti cha enzi.’ Alimwona malaika ‘aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, na akapewa uvumba mwingi, ili auvukize na sala za watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu yaliyokuwa mbele ya kiti cha enzi.’ Hapa nabii aliruhusiwa kuona chumba cha kwanza cha hekalu mbinguni; na akaona humo ‘taa saba za moto’ na ‘madhahabu

190

ya dhahabu’ yaliyowakilishwa na kinara cha taa cha dhahabu na madhabahu ya uvumba katika hekalu la duniani. Tena, ‘Hekalu la Mungu lilifunguliwa,’ na akatazama katika pazia la ndani, ndani ya patakatifu pa patakatifu. Hapa aliona ‘sanduku la agano Lake,’ lililowakilishwa na kasha takatifu lililotengenezwa na Musa ili lihifadhi sheria ya Mungu.” — “Wazee na Manabii,” ukurasa wa 356. {SR2: 189.3}

Katika hekalu la duniani, kuhani mkuu pekee aliruhusiwa kuhudumu katika chumba cha pili, ndani ya pazia, na ilikuwa imeeleweka na wengine kwamba kiti cha enzi alichokiona Yohana hakikuwa katika patakatifu mno, kwa sababu wazee ishirini na nne wako mbele ya kiti cha enzi. Wazo hilo si sahihi, kwa maana litakuwa jambo lisilo la kiakili kuchukua msimamo kwamba Mungu angehamisha kiti Chake cha enzi kutoka katika “patakatifu mno,” hadi “mahali patakatifu,” badala ya wazee kuingia katika patakatifu mno mbele ya kiti cha enzi. Isitoshe, ni kiti cha enzi cha Yule wa Milele ambacho hufanya chumba cha pili kuwa patakatifu mno. Kwa hivyo, ikiwa tutachukua msimamo hivyo, iwapo wazee na wale wanyama, au viumbe havikuruhusiwa katika chumba cha pili mbele ya kiti cha enzi, wala hawataruhusiwa katika chumba cha kwanza mbele ya kiti cha enzi. Kuchukua msimamo mwingine wowote zaidi ya huu ungemaanisha kwamba chumba ni kitakatifu kuliko Muumba na kiti Chake cha enzi. {SR2: 190.1}

Kulingana na Paulo, huduma zilizokuwa katika pazia ya hekalu la duniani haziwezi kuweka wazi yote yanayofanyika katika la mbinguni. Alisema: “Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu mno ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.” (Ebr. 9:8.) Kwa hivyo, lazima tupate ukweli wa utumishi katika hekalu la mbinguni kutokea kwa pembe nyingine. Tunanukuu Danieli 7:9, 10: “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye Mzee wa siku akaketi, mavazi Yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa Chake kama sufu safi: kiti Chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake: maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake: hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” {SR2: 190.2}

Nabii alionyeshwa mwanzo wa hukumu (upatanisho), au ambavyo huitwa pia, kupatakasa patakatifu, ambayo hufanyika katika chumba cha patakatifu mno; kwa maana yeye husema, “hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Sasa kumbuka kwamba, “Maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake.” Kwa hivyo tunaona kwamba Paulo yuko sawa kwamba utumishi wa la mbinguni haikudhihirishwa kikamilifu kwa utumishi wa la duniani. Ingawa kuhani mkuu

191

pekee aliruhusiwa kuingia mahali patakatifu mno ndani ya la duniani, kundi lisilohesabika liliingia ndani ya la mbinguni. Kwa hivyo u wapi ushahidi kwamba wazee hawawezi kuwa katika patakatifu mno? Haiwezekani kutumia utimizo wa siku 2300 za kinabii — miaka — ya maono ya Danieli katika sura ya 8, aya ya 14, kwa wakati mwingine wowote kuliko hukumu katika mwaka 1844. {SR2: 190.3}

Kipindi hiki cha kinabii kilianzia kwa kutolewa amri ya kuurejesha na kuujenga Yerusalemu. (Dan. 9:25.) Amri iliyotolewa na mfalme wa Uajemi ilitekelezwa mwaka 457 K.K. (Angalia Ezra 7.) Kwa hivyo kilimalizika mwaka 1844; kwa wakati ambapo Kristo alipita kutoka “patakatifu” hadi mahali “patakatifu mno.” Kwa kujifunza zaidi, tazama “Pambano Kuu,” ukurasa wa 486. {SR2: 191.1}

Tutajitahidi kuthibitisha kwamba maono ya Danieli ni ya tukio moja na yale ya Yohana. Danieli hunena kuhusu viti vya enzi (wingi), kisha hufanya tofauti ya kiti cha enzi cha Mungu (Mzee wa siku) kwa “mto kama moto” ukitokea mbele Yake. Kitabu cha Danieli ni unabii, lakini maono ya Yohana ni ufunuo. Danieli husema aliona “viti vya enzi,” lakini Yohana hutupatia idadi yavyo — ishirini na vitano kwa jumla. (Ufu. 4:2, 4.) Danieli husema, “mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele yake;” Yohana hutuambia ule mto ni nini: “Bahari ya kioo iliyochangamana na moto.” (Ufu. 4:6; 15: 2.) Danieli husema: “Maelfu elfu … na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele yake.” Yohana hutuambia hao ni nani: “Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi na za wale wenye uhai na za wale wazee: na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu mara maelfu.” (Ufu. 5:11.) Danieli husema, “hukumu ikawekwa na vitabu vikafunuliwa.” Yohana huongeza kwamba kimojawapo cha vitabu kilikuwa katika mkono wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi na kilikuwa kimetiwa mihuri saba. (Ufu. 5:1.) Kwa hivyo Yohana hutupatia ufunuo wazi zaidi wa tukio lile lile. {SR2: 191.2}

Mlango alioona “wazi” ni pazia kati ya “patakatifu” na “patakatifu mno,” kwa maana hakuna mwingine ambao ulikuwa umefungwa. Kwa hivyo, neno “baada ya hayo” katika Ufunuo 4, aya ya 1, humaanisha kutoka kwa wakati wa maono — kuonyesha mbele hadi kwa mwaka 1844. {SR2: 191.3}

Ingawa kuhani wa hekalu la duniani aliingia mahali “patakatifu mno” mara moja tu kwa mwaka, kwa mujibu wa Paulo, Kristo aliingia mahali patakatifu mara moja milele. (Angalia Ebr. 9:12.) Na kuhusu wakati huo mtume asema, Yeye “aonekane sasa mbele ya Mungu kwa ajili yetu,” katika “patakatifu mno.” (Ebr. 9:24.) Kwa hivyo, Kristo hakuweza kuingia katika chumba cha kwanza kama kuhani kabla ya kufufuka Kwake kutoka kwa wafu, kwa wakati ambapo Alianza kuwa Kuhani wetu Mkuu; wala hangeweza kuingia katika patakatifu mno katika hadhi hiyo kabla ya siku ya hukumu, kwa maana Paulo husema, Yeye “aliingia mara moja tu.” Basi unabii wa Danieli na ufunuo wa Yohana, hauwezi kuwa wa

192

tukio lingine isipokuwa kuanza hukumu katika tarehe iliyoelezewa (1844). {SR2: 191.4}

Ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo ndio huletwa mbele ya uwepo wa Mungu — katika mahali “patakatifu mno.” Mtume asema: “Basi ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu mno kwa damu ya Yesu.” (Ebr. 10:19.) Kadiri maono yayo hayo yanavyoendelea, tunapita hadi kwa sura ya tano na ya sita ya Ufunuo. {SR2: 192.1}

Kunukuu Ufu 5:1, 3, 5-7; 6:1, “Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba… Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama… Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie: tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. Nikaona, na, kumbe, katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi… Kisha nikaona hapo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile mihuri saba.” {SR2: 192.2}

Kitabu kilichotiwa na mihuri saba, katika mkono wa kuume wa Jaji Mkuu, lazima kisheheni majina ya wale ambao dhambi zao zinapaswa kufutwa. Kwa kuwa hiki ni kitabu pekee ambacho “hakuna mtu mbinguni au duniani… aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama,” isipokuwa Mwana-Kondoo aliyekuwa mbele ya kiti cha enzi (Angalia sura ya 5:1-9), ni wazi bila shaka kwamba kitabu kilicho na mihuri saba ni kile kinachoitwa “Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.” Na kwa hicho hukumu ilifunguliwa. Hilo limekaririwa katika Ufunuo 20:12, “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima: na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” (Tazama “Pambano Kuu,” ukurasa wa 480.) Kwa sababu hili haliwezi kupingwa, ni dhahiri kwamba msingi wa matumizi ya mihuri umesimamishwa. {SR2: 192.3}

Tunanukuu Maandiko ya mihuri minne ya kwanza: “Nikaona, na tazama farasi mweup: na yeye aliyempanda ana uta; akapewa taji: naye akatoka, ali akishinda, tena apate kushinda. Na alipoufungua muhuri wa pili, Nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo uone. Akatoka farasi mwingine mwekundu sana: na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane: naye akapewa upanga mkubwa.

193

Na alipoufungua muhuri wa tatu, Nikamsikia mwenye uhai wa tatu akisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi mweusi, na yeye aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake… Na alipoufungua muhuri wa nne, Nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi wa rangi ya kijivujivu: na yeye aliyempanda jina lake lilikuwa Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.” (Ufu. 6:2-5, 7, 8.) {SR2: 192.4}

Wengine wametumia mihuri saba ya sura ya sita ya Ufunuo kwa kanisa wakati wa Agano Jipya, lakini hizo nembo ni kinyume na matumizi hayo. Katika wakati wa Agano la Kale na Jipya, kanisa la Mungu limewakilishwa na nembo ya mwanamke msafi. (Angalia Yeremia 6:2; Ufu. 12:1.) Uvuvio haufanyi mabadiliko katika kanuni ya nembo ya kanisa najisi, kwa maana katika Ufunuo 17:1, 4, 5, kahaba hutumika kuonyesha kanisa, au makanisa, ambayo yameanguka au ya uongo. Badiliko la kanuni hii (kutoka “mwanamke” hadi “mwanaume” au “farasi”) haliwezi kupatikana mahali popote katika Biblia. {SR2: 193.1}

Sio Kimaandiko tu kutumia wanaume na farasi kama nembo za kanisa, lakini pia hazifai kwa ujumla. Wala hakuna uthibitisho wowote unaoweza kutolewa kuonyesha kwamba mihuri hutumika kwa wakati wa Agano Jipya pekee. Kwa hivyo, matumizi ya hizo nembo lazima yatafutwe mahali pengine. Kwa hivyo tunakabiliwa na hitaji la kuchunguza kwa kina kuhusu mada hiyo. Kwa mujibu wa ushauri wa mtumwa wa Bwana, tumeagizwa kujifunza hili, kwa sababu hushikilia ukweli muhimu kwa wale watakaoshiriki katika kufunga kazi ya injili. Kunukuu “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, ukurasa wa 267: “Sura ya tano ya Ufunuo inahitaji kuchunguzwa kwa ukaribu. Ni ya umuhimu mkubwa kwa wale ambao watashiriki katika kazi ya Mungu kwa siku hizi za mwisho.” {SR2: 193.2}

Laiti sura hiyo ingalikuwa imeeleweka vyema, kufafanuliwa, na kuchapishwa kabla ya ushuhuda ulio hapo juu kuandikwa, lisingalikuwapo hitaji la udharura huu. Isitoshe, iwapo ingalikuwa imefafanuliwa hapo zamani, liko wapi somo lenye umuhimu mkubwa kama huu, na ni nani anayebeba jukumu la kulipeleka kwa ulimwengu? Lakini sura ya tano, iliyotengwa kwa ya nne na ya sita haiwezi kueleweka, kwa sababu sura hizi husheheni mada moja; inayoitwa mihuri saba. Sura ya tano imetajwa kwa sababu ni moyo na ufunguo wa hiyo mada. {SR2: 193.3}

Haitawezekana kulielewa vyema somo la mihuri katika sura ya sita, isipokuwa tulijue jambo fulani kuhusu “wazee,” “kitabu” na “wanyama” wa sura ya nne, ambamo maono huanzia. Tunapopata maarifa fulani ya majukumu yao mbele ya kiti cha enzi, na madhumuni ya hilo kongamano,

194

na hiyo hafla, basi tu tunaweza kufanya matumizi sahihi ambayo yanaweza kuthibitishwa kuwa ni kweli. {SR2: 193.4}

Isipokuwa maana ya kila nembo imefafanuliwa inavyofaa ili zisiweze kuhitilafiana, na funzo la ukweli wa sasa na maana maalum inayotokana na ufasiri haiwezi kutegemewa na hauwezi kuwapo ukweli ndani yake. Mungu huwa hafanyi marudio ya bure, wala Yeye hataupoteza wakati wa watumwa Wake kuyaandika. Kwa hivyo, kila nembo ndogo ina maana yake, na hufichua ukweli mkubwa. {SR2: 194.1}

Hukumu Na Mihuri–Ufunuo Sura Ya 4

Ufu. 4:1: “Baada ya hayo Naliona, na, tazama, mlango ukafunguka mbinguni: na sauti ile ya kwanza Niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami; ikisema, Panda hata huku, nami Nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo” Mlango ambao ulifunguliwa hauwezi kuwa mwingine isipokuwa ule unaovitenganisha vyumba viwili; yaani, patakatifu kutoka kwa patakatifu mno, katika hekalu la mbinguni, kama vilivyoonyeshwa na hekalu la duniani lililojengwa na Musa. Chumba hicho kilipaswa kufunguliwa mwanzoni mwa hukumu, iliyoonyeshwa kwa mfano na siku ya upatanisho jinsi ilivyoelezewa hapo awali. Basi hatufanyi kosa kwa kuhitimisha kwamba mandhari hayo ni hukumu katika kikao, na kama vile ile sauti ilinena kwa Yohana, “Nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo,” ni dhahiri kwamba alitazama mbele katika maono hadi kwa ufunguzi wa hukumu katika mwaka 1844. {SR2: 194.2}

Iwapo mahitimisho haya ni sawa, na yale maono huelezea hukumu ikiendelea, basi iyo hiyo lazima ithibitishwe na mambo yaliyoonekana katika maono. Hukumu katika kikao huhitaji jaji, wakili, jopo la majaji, na wawakilishi wa wale ambao watahukumiwa, kwa sababu hawawezi kuwa hapo (mbinguni) kibinafsi. Lazima viwepo vitabu vilivyosheheni majina, na kumbukumbu za matendo, ya wale watakaohukumiwa; pia wakati wa hukumu, na thawabu. Tunanukuu andiko linaloelezea Jaji Mkuu: “Na mara Nalikuwa katika roho: na, tazama, kiti cha enzi kiliwekwa mbinguni na mmoja akaketi juu ya kile kiti. Na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki: na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.” (Ufu. 4:2 na 3.) {SR2: 194.3}

Utukufu wa Mungu huwakilishwa na mfano wa mawe ya thamani. Upinde wa mvua hufunua ahadi ya Mungu isiyoshindwa kamwe na rehema kuu. Mungu akanena kwa Nuhu: “Hii ndiyo ishara ya agano Nifanyalo kati Yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele: Mimi nauweka upinde Wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi.” (Mwa. 9:12, 13.) {SR2: 194.4}

Aya ifuatayo huonyesha jopo la majaji: “Na viti ishirini

195

na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi: na juu ya vile viti Naliona wazee ishirini na wanne wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.” (Ufunuo 4:4.) Taji za dhahabu huashiria mamlaka yao ya kifalme kuchukua hatua juu ya kesi hiyo. Mavazi meupe huonyesha kwamba wao ni wanadamu kutoka duniani, waliokombolewa (Ufunuo 4:6.) “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua mihuri zake: kwa kuwa ulichinjwa, umetukomboa kwa Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila, na lugha, na jamaa na taifa.” (Ufunuo 5:8, 9.) Kumbuka wote wanyama na wazee waliimba, wakisema: “Kwa kuwa umetukomboa watu wa kila kabila, na lugha, na jamaa na taifa.” Kwa hivyo, wanyama, na vile vile wazee, wamekombolewa kutoka duniani. {SR2: 194.5}

Tena, kumbuka kwamba wanyama na wazee walifanya idadi ya ishirini na nane. Haingewezekana kwa watu ishirini na wanane kukombolewa kutoka kwa kila kabila, na lugha, na jamaa na taifa: kwa maana iwapo angalikombolewa mtu mmoja tu kutoka kwa kila taifa, idadi hiyo ingefika maelfu, badala ya ishirini na wanane. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba “wanyama wanne” ni nembo ambazo huwakilisha makundi manne ya watakatifu waliokusanywa kutoka katika vizazi vyote, na kutoka kwa kila kabila, na lugha, na jamaa na taifa. Vivyo hivyo falme za ulimwengu baada ya gharika huwakilishwa na wanyama kwa njia ya nembo. Hivyo kwa njia ya wanyama huwakilishwa wale ambao watahukumiwa. {SR2: 195.1}

“Na hawa wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na mbele na nyuma na ndani wamejaa macho: wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.” (Ufunuo 4:8.) “Wamejaa macho.” Macho hutoa nuru kwa mwili. Kwa hivyo, husimama kama nembo, kuashiria kwamba watu wa Mungu wamekuwa na nuru ya kutosha katika kila kizazi. “Mbele na nyuma” humaanisha nuru ya kinabii, ikiwafunulia ya zamani, ya sasa na ya siku za baadaye; hili likiwa limewezeshwa kwa Roho wa Mungu na malaika watakatifu. Namba “nne” huonyesha kwamba yapo makundi manne ya watakatifu yatakayozingatiwa katika hukumu. Mawili kati ya makundi haya yatafufuliwa; yaani, wale waliokufa kawaida, na wale waliouawa kwa sababu ya imani. Mengine mawili ni wale watakaohamishwa bila kufa wakati wa kuja kwa Kristo; yaani, watu 144,000 wa Ufunuo 7:1-8, na umati mkubwa ukiwa na mitende mikononi mwao, kama unavyoonyeshwa katika Ufunuo 7:9. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, ukurasa wa 41-51.) Kwa sababu mabawa ya simba, na pia ya mnyama kama chui mwenye vichwa vinne (Babeli na Uyunani) huwakilisha

196

namba ya vipindi jinsi ilivyoelezewa hapo awali (kwa ukurasa wa 33-42), lazima yawakilishe vipindi kwa wanyama hawa. Yataonyesha wazi muhuri ambao chini yake hukumu ilianzia — muhuri wa sita — kwa hivyo mabawa sita. “Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.” Yaani, Mungu kabla ya hukumu, katika wakati wa hukumu, na baada ya hukumu. {SR2: 195.2}

Ufu 4:7: “Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama, na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu, na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.” Wanyama hao kwa maumbile pia huwakilisha vipindi vinne vya kanisa. Mnyama wa kwanza ni kama simba. “Simba” ndiye mfalme wa wanyama, na amekusudiwa kuonyesha kipindi cha kwanza cha kanisa kabla ya sehemu ya sherehe, ambayo kwayo hukumu ilianzia. (Tazama chati katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 224.) Mnyama wa pili akiwa “kama ndama,” ni dhahiri kwamba huwakilisha sehemu ya dhabihu, au ya mfano. Kwa hivyo yule mnyama aliye na “uso wa mwanadamu” lazima awakilishe kipindi cha uakisi baada ya kusulubishwa. Na mnyama wa nne alikuwa kama “tai arukaye.” Yeye huwakilisha kipindi katika wakati wa mavuno. Kipindi cha mwisho kimewakilishwa na tai arukaye kuashiria kanisa ambalo litatahamishwa bila kuonja mauti. “Tai arukaye” ni mfalme wa nyuni, jinsi simba alivyo mfalme wa wanyama, ambayo ni ishara ya ushindi, na hivyo kufanyiza nembo kamili. Kwa vile hukumu ya wafu ilianza na mnyama kama simba, — mfalme wa wanyama, — vivyo hivyo hukumu ya walio hai inaanza na mnyama kama tai, — mfalme wa nyuni. Ukweli wote wa hawa “wanyama wanne” haujafunuliwa bado. {SR2: 196.1}

Kwa sababu wanyama na wazee humsifu na kumwabudu Mungu, ni ushuhuda wa kutosha kwamba uumbaji umeridhika kwamba Yeye ni mwenye haki, na kweli, na Muumba wa vyote. Wale ambao majina yao yameandikwa ndani ya kitabu cha “mihuri saba” ndio ambao dhambi zao zinafutwa kwa damu ya thamani ya Kristo. Basi sifa, na heshima, na utukufu ni kwa Mungu wetu milele na milele. {SR2: 196.2}

“Mimi, naam Mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili Yangu mwenyewe, wala Sitazikumbuka dhambi zako.” (Isa. 43:25.) “Nitaivumilia ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa nimemwasi, hata Atakaponitetea teto langu, na kunifanyia hukumu: Atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki Yake. Atarejea, na kutuhurumia, atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.” (Mika 7:9,19.) Je! Sisi pamoja na mtume mkuu tutasema: “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote, hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu, ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu?” (Warumi 8:38, 39.) {SR2: 196.3}

197

Hadi sasa umakini wetu umeitwa kwa Jaji Mkuu, jopo la majaji wazee ishirini na nne, wanyama wanne wanaowakilisha wale watakaohukumiwa, na kitabu kilichosheheni majina — kilichofungwa kwa mihuri saba. Sasa umakini wetu unaelekezwa kwa wakili. {SR2: 197.1}

“Nikaona, na, kumbe, katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.” (Ufu. 5:6-8.) {SR2: 197.2}

“Mwana-kondoo” ni nembo ya Kristo, mtetezi wetu. Yohana alisema: “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya, ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.” (1 Yohana 2:1.) {SR2: 197.3}

Pembe saba kwa Mwana-Kondoo humaanisha ukamilifu wa nguvu na mamlaka, ikithibitisha maneno yaliyonenwa na Kristo: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” (Mat. 28:18.) Nguvu hii isiyo na kifani ni kwa ajili ya manufaa yetu, na imemetolewa bure. Yesu alisema: “Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” (Mat. 17:20.) Mpenzi rafiki, maneno haya ni aidha kweli au si kweli. Hapawezi kuwapo katikati. Maadamu Kristo hawezi kusema uongo, je! Utalijaribu neno Lake lisiloshindwa kamwe, na kumruhusu Yeye atimize ahadi Yake? {SR2: 197.4}

Macho saba ya Mwana-Kondoo huashiria ukamilifu wa maono, ushahidi kwamba hakuna kitu kilichofichwa kutoka kwa Wakili wetu, na ya kwamba mambo yote yako wazi na uchi Kwake; vivyo hivyo na Mungu Baba. Mtunga Zaburi hufafanua nguvu ya Mungu katika maono kwa maneno yafuatayo: “Niende wapi nijiepushe na Roho Yako? Niende wapi niukimbie uso Wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko: Ningefanya kuzimu kitanda changu, tazama, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono Wako utaniongoza, na mkono Wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika; hata usiku utakuwa nuru inizungukayo; Naam, giza nalo halikufichi kitu; bali usiku huangaza kama mchana: giza na mwanga kwako ni sawasawa.” (Zab. 139:7-12.) {SR2: 197.5}

Wa-ufunuo husema pembe na macho ya Mwana-Kondoo “ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.” Uwezo huu wote, kwa nguvu na maono, umejumuishwa na kuonyeshwa na Roho wa Mungu. Yesu alisema, “Yawafaa ninyi Mimi niondoke: kwa maana Mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja

198

kwenu; bali Mimi nikienda Zangu, Nitamtuma kwenu.” (Yohana 16:7.) “Lakini huyo Msaidizi, ambaye ni Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina Langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha, yote Niliyowaambia.” (Yohana 14:26.) {SR2: 197.6}

“Taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.” (Ufu. 4:5.) Taa za moto, saba kwa idadi, zilizo mbele ya kiti cha enzi, huwakilisha ukamilifu wa ukweli wa Mungu — ukweli wa sasa uliofunuliwa kwa kila kizazi tangu mwanzo wa ulimwengu — na ambao kwa huo tunahukumiwa. Wale ambao ni watiifu kwa nuru na ukweli wote waliopewa, wameyafikia mahitaji — wanatiwa muhuri, na wanaodolewa kwa hukumu ya sheria ya Mungu. {SR2: 198.1}

“Taa saba … ndizo Roho saba za Mungu.” (Ufu. 4:5.) Andiko hili huthibitisha ukweli kwamba nuru na ukweli hufunuliwa na Roho wa Mungu pekee. “Lakini huyo Msaidizi, ambaye ni Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina Langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha, yote Niliyowaambia.” (Yohana 14:26.) Kukataa nuru na ukweli wa sasa ni dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. “Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa: bali yeye atakayenena neno dhidi ya Roho Mtakatifu [ukweli wa sasa] hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.” (Mat. 12:32.) Mwenendo wetu kwa ukweli wa sasa aidha “utaufanya mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya: kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.” (Mat. 12:33.) Kwa hivyo, ukweli wa sasa una uwezo wa kumbadilisha mtu na kumwezesha kufaa kwa uzima wa milele, ambao ni muhuri wa Mungu aliye hai. Yesu alisema: “Amin, amin, Nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” (Yohana 3:5.) {SR2: 198.2}

Bahari Ya Kioo

“Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo kama bilauri: na katikati ya kile kiti cha enzi na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne wamejaa macho mbele na nyuma.” (Ufu. 4:6.) Kwa mujibu wa semi katika aya ambayo imenukuliwa hapo juu, inamaanisha kwamba wanyama wako kati ya kiti cha enzi na kukizunguka kiti cha enzi. Ingekuwa haiwezekani wao kuwa katikati, na pia kukizunguka kiti cha enzi — kiti cha rehema. Iwapo walikuwa katikati ya kiti cha enzi, wangekuwa wanachukua nafasi ya Mungu, Jaji, na Mwanawe, Mwana-Kondoo. Kwa hivyo, tunahitimisha kwamba ibara ya kwanza ya aya hiyo imepotoshwa. Kwa kuacha nukta pacha hilo Andiko lingesoma kama ifuatavyo: “Na

199

mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo kama bilauri na katikati ya kile kiti cha enzi.” Kwa hivyo, ni bahari ya kioo iliyo katikati, na mbele ya kiti cha enzi; na sio wanyama. “Bahari ya kioo” hutokea kwa kiti cha enzi, na ni nembo ya uzima wa milele kwa namna ile ile jinsi “Mwana-Kondoo” alivyo nembo ya Kristo, Wakili wetu. {SR2: 198.3}

Bahari ni kitu kipana sana juu ya dunia; kwa hivyo hutumika kuwakilisha umilele. “Safi kama bilauri” huashiria ukamilifu, uhuru kutoka kwa dhambi na kasoro. Katika Ufunuo 15:2, tunasoma: “Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto.” Moto ungekuwa nembo pekee kamilifu ambayo ingetumika kuwakilisha uhai. Kwa hivyo, bahari ya kioo hutokea kwenye kiti cha enzi cha Mungu, na huwakilisha uzima wa milele, ambao ni thawabu ya wale ambao majina yao yako katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, ndani ya hiyo mihuri saba. “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo, au uongo: bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” (Ufu. 21:27.) Katika hukumu watakatifu “wale waliopata ushindi dhidi ya yule mnyama, na dhidi ya sanamu yake, na dhidi ya hesabu ya jina lake,” wamepewa kusimama juu ya bahari ya kioo — uzima wa milele. (Ufu. 15:2.) {SR2: 199.1}

Mpangilio na eneo la tukio, kama ilivyoelezwa na Yohana, huthibitisha kwamba ni hukumu iliyo katika kikao kwa sababu inafanyika katika “Patakatifu pa Patakatifu” — palipoonyeshwa kwa mfano na hekalu la duniani na utumishi wake, ambamo Haruni kuhani mkuu, alihudumu katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi huo. Iliitwa siku ya upatanisho — hukumu, kupatakasa patakatifu au utakaso wa kanisa — utengo wa magugu na ngano. Hapo tunaona Jaji Mkuu (Mungu Baba), Wakili (Mwana-Kondoo — Yesu Kristo mwenye haki), jopo la majaji (wazee ishirini na wanne — waliojivika mavazi ya haki ya Kristo — mavazi meupe); uwakilishi wa wale ambao watahukumiwa (wanyama wanne) nuru na ukweli ambao wametunza (taa saba), thawabu ambayo watapewa wale watakaohukumiwa (bahari ya kioo), na kitabu kinachosheheni majina ya wenye haki wote kuanzia kwa Adamu na kuendelea hadi mwisho wa kufungwa kwa muda wa rehema — mwisho wa injili (mihuri saba). “Kisha nikaona katika mkono wa kuume Wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba.” (Ufu. 5:1.) Kwa sababu kitabu hicho husheheni majina ya wote waliotiwa muhuri kwa muhuri wa Mungu (kweli Yake) kinaitwa kitabu cha mihuri, pia kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. {SR2: 199.2}

Katika andiko lifuatalo tunauona ulimwengu wote ukitazama kwa shauku kubwa maswala ya familia ya wanadamu wakati chuo kinapokunjua, kuwafunulia siri ya Mungu: “Na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu,

200

aliyeviumba vitu vyote kupitia kwa Yesu Kristo.” (Efe. 3:9.) Kunukuu Ufunuo 5:11-14, “Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi na za wale wenye uhai na za wale wazee: na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu mara maelfu; Wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza, na utajiri, na hekima, na nguvu, na heshima, na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni, na juu ya nchi, na chini ya nchi, na katika bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia vikisema, Baraka, na heshima, na utukufu, na uweza una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka, wakasujudu na kumwabudu Yeye aliye hai hata milele na milele.” Maandiko yaliyonukuliwa yanathibitisha kwamba ulimwengu wote umeridhika na upendo wa Mungu, na haki ya Kristo. Tunarejelea Ufu. 5:13: “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni, na juu ya nchi, na chini ya nchi, na katika bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia vikisema, Baraka, na heshima, na utukufu, na uweza una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo hata milele na milele.” {SR2: 199.3}

Kukifungua Kile Kitabu

“Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja mihuri zake? Hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana, kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua na kukisoma hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie: tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na kuzivunja zile mihuri zake saba. Na nikaona, na, kumbe, katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume Wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.” (Ufu. 5:2-8.) {SR2: 200.1}

Andiko hili hufichua kwamba hakuna mwingine katika ulimwengu wote mkubwa wa Mungu ambaye anastahili, au anayeweza kukifungua kile kitabu, kwa maana “Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, ameshinda.” Kristo alijipata jina la heshima lililo hapo juu kwa kuzaliwa Kwake, na kwa ushindi Wake msalabani kwa wale ambao wangemwamini kama Mwokozi wa

201

Dunia. Ameshinda kwa kumwaga damu Yake pale Kalvari; kwa hivyo hakuna mwingine anayeweza kukifungua kile kitabu kwa maana Yeye pekee aliyekufa kwa ajili ya jamii ya wanadamu. “Kitabu” hiki kina majina ya watakatifu, na “mihuri saba” hujumuisha, kinabii, historia ya ulimwengu, katika wakati ambao watakatifu wanatiwa muhuri. Vipindi hivi saba vya historia ambayo haijatimizwa vilifunga kitabu hicho, na mmoja pekee ambaye angeweza kukifungua — kutazama wakati ujao — alikuwa “Mwana-Kondoo.” Kitabu “kiliandikwa ndani na nyuma” — “kiliandikwa ndani” ni neno la kinabii la Mungu; “na nyuma,” ni utimizo wa kihistoria wa unabii. “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.” (Ufu. 13:8.) “Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, Aviitaye vizazi tangu mwanzo?” (Isa. 41:4.) {SR2: 200.2}

Ni Kristo ambaye ameandaa njia ya utaratibu huu wa mahakama kuwatetea watu Wake, na kuzifuta dhambi zao. “Katika utumishi wa mfano, ni wale tu ambao walikuja mbele ya Mungu kwa maungamo na toba, na ambao dhambi zao, kupitia damu ya sadaka ya dhambi, zilihamishwa hadi patakatifu, walikuwa na sehemu katika ibada siku ya upatanisho. Kwa hivyo katika siku kuu ya upatanisho wa mwisho na hukumu ya upelelezi, kesi pekee zinazozingatiwa ni zile za watu wanaodai kumwamini Mungu. Hukumu ya waovu ni kazi tofauti na iliyotengwa, na itafanyika baadaye. ‘Hukumu lazima ianzie katika nyumba ya Mungu: na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasiotii injili utakuwa nini?’ Vitabu vya kumbukumbu vinapofunguliwa katika hukumu, maisha ya wote ambao wamemwamini Yesu yanakuja kwa uchunguzi mbele ya Mungu. Kuanzia kwa wale wa kwanza walioishi juu ya dunia, Wakili wetu huwasilisha kesi za kila kizazi mtawalia, na kufunga na cha walio hai.” — “Pambano Kuu,” uk. 480, 483. {SR2: 201.1}

Mbali na kitabu kilicho mkononi mwa jaji, vipo vitabu vingine, lakini hiki ambacho hapana mtu mwingine aliye mbinguni wala duniani aliyestahili kukifungua, isipokuwa “Mwana-Kondoo,” ndicho kinachoitwa “Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.” Na Wa-ufunuo husema kwamba wale tu watakaoingia katika mji wa Mungu ni ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. “‘Kitabu cha ukumbusho’ kikaandikwa mbele ya Mungu, ambamo yameandikwa matendo mema ya wale ‘waliomcha Bwana, na kulitafakari jina Lake.’” — Kimenukuliwa, uk. 481. {SR2: 201.2}

Mihuri Kwa Vipindi–Ufunuo Sura Ya Sita

Kwa sababu ushahidi ulioletwa hauwezi kupingwa ya kwamba pamoja na kitabu cha mihuri hukumu ilifunguliwa, na kama ilivyoanzia kwa wenye haki waliokuwa wa kwanza kuishi juu ya dunia, na kwishia na wa mwisho, ni hakika kwamba mihuri saba hutanda juu ya historia yote

202

ya ulimwengu. Kwa hivyo, hujumuisha kila mtakatifu tangu mwanzo wa ulimwengu. Ile namba “saba” hubeba ushahidi uo huo. {SR2: 201.3}

Maadamu iko mihuri saba kwa utaratibu mfululizo, ni wazi kwamba historia ya ulimwengu wetu imegawanywa katika vipindi saba tofauti. Hukumu huanza na cha kwanza na kwishia na cha mwisho. Ni dhahiri mihuri sita ya kwanza hukamilisha kesi za wale ambao walikuwa wamekufa kabla ya hukumu, na wakati iko kwenye kikao; lakini kipindi cha saba cha muhuri, kikiwa cha mwisho, lazima kiwahusu walio hai. {SR2: 202.1}

Upo ushahidi wa kutosha wa maandiko kwamba waliookolewa wote katika vizazi vyote wametiwa muhuri na muhuri wa Mungu; kwa sababu hii vipindi saba vinaitwa “mihuri saba,” na majina ya wale waliotiwa muhuri yameandikwa katika kitabu kile; kwa sababu hiyo, kitabu kile kimefunikwa mihuri saba. (Tazama Yohana 6:27; Efe. 4:30; 1:13; 2 Tim. 2:19; 2 Kor. 1:22; Ufu. 9:4.) {SR2: 202.2}

Maana Ya Farasi Na Wapanda Farasi

Ufunuo 6:1-8, “Kisha nikaona hapo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile mihuri saba, nikasikia, mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi mweupe: na yeye aliyempanda ana uta; akapewa taji: naye akatoka ali akishinda, tena apate kushinda. Na alipoufungua muhuri wa pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo uone. Akatoka farasi mwingine mwekundu: na yeye aliyempanda alipewa uwezo kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane: naye akapewa upanga mkubwa. Na alipoufungua muhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi mweusi; na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa dinari, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari, wala usiyadhuru mafuta wala divai. Na alipoufungua muhuri wa nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne ikisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi wa rangi ya kijivujivu: na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.” {SR2: 202.3}

Wale farasi ni nembo za dunia, zikifunua mabadiliko manne makubwa tangu mwanzo wa ulimwengu, na wapanda farasi huonyesha familia ya wanadamu chini ya mageuzi haya manne makuu; hivyo kufanya nembo kamili, kwa maana tunaiendesha dunia jinsi tungeweza kumwendesha farasi. Laiti dhambi haingeingia ndani ya familia ya wanadamu angalikuwapo farasi mmoja tu. Lakini maadamu dhambi ilipoingia na kuharibu mpango wa Mungu kwa watoto Wake, nchi ililaaniwa, na kwa hivyo badiliko

203

[Ukurasa Mtupu]

204

[Kielezo: Mihuri Saba Na Hukumu]

205

kubwa likaja; na kadiri dhambi ilivyozidishwa laana baada ya laana ikaongezwa. Kwa hivyo, farasi mweupe alifuatwa na mwekundu, na mwekundu na mweusi, na mweusi na wa rangi ya kijivujivu. {SR2: 202.4}

Mpanda farasi kwa farasi mweupe alipewa taji, lakini baada ya dhambi kuingia alipoteza taji yake ya ufalme na utukufu. Kwa hivyo, mpanda farasi kwa farasi mwekundu, badala ya kuwa na taji, ana upanga mkubwa; na kwa ule upanga aliongezewa mizani, na kwa mizani hiyo, mauti. {SR2: 205.1}

Muhuri Wa Kwanza–Farasi Mweupe

Ufunuo 6:2, “Nikaona, na tazama farasi mweupe: na yeye aliyempanda ana uta; akapewa taji: naye akatoka ali akishinda.” “Nyeupe” ikiwa nembo ya usafi, humaanisha kwamba farasi mweupe huwakilisha mwanzo wa ulimwengu wetu — usio na dhambi, jinsi dunia ilivyokuwa katika vazi lake la uzuri na ukamilifu, pamoja na maajabu yote juu ya ardhi na baharini. {SR2: 205.2}

“’Bwana Mungu akapanda bustani mashariki mwa Edeni;’ … Kila kitu ambacho Mungu alikuwa amekifanya kilikuwa ukamilifu wa uzuri, na hakuna kitu kilichoonekana kipungufu … Katika bustani hii ilikuwapo miti mikubwa ya namna-namna, mingi kwayo ilikuwa imejaa matunda yenye harufu nzuri na matamu sana. Ilikuwapo mizabibu ya kupendeza … ilionyesha mandhari mazuri zaidi, matawi yake yalikuwa yameinamisha chini kwa uzito wayo matunda ya kuvutia, ya rangi za kupendeza na za namna-namna.” — “Wazee wa Imani na Manabii,” uk. 46, 47. {SR2: 205.3}

Dunia na maua yake maridadi na zulia la kijani kibichi hai, ambalo juu yake mbingu za samawati zilitanda kama kuba yake, zilionyesha maandhari asilia ya uzuri na umaridadi ambao hakuna lugha inaweza kuelezea. Bwana Msanii mkuu pekee ndiye anayeweza kuzalisha ajabu kama hiyo bila kasoro. {SR2: 205.4}

Mpanda Farasi Wa Kwanza

Maadamu farasi mweupe huwakilisha mwanzo wa dunia yetu katika hali yake isiyokuwa ya dhambi, mpanda farasi hawezi kuwa mwingine yeyote isipokuwa Adamu mwenyewe, ambaye hukumu ilianzia kwake. Taji ni nembo ya mamlaka ya kifalme. “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” (Mwa. 1:26.) Lilo hilo limeonyeshwa kwa maneno, “Akapewa taji.” Kwa hivyo, Bwana aliianzisha dunia kamilifu, na mfalme aliyeumbwa na mkono wa Mungu, na sisi ni wana wa Kifalme. {SR2: 205.5}

“Tazama farasi mweupe: na yeye aliyempanda … akatoka ali akishinda, tena apate kushinda.” Maneno hayo ya mfano ni utimizo

206

wa maneno yaliyonenwa na kinywa cha Muumba: “Na Mungu akawabarikia (Adamu na Hawa), Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha.” (Mwa. 1:28.) Ulikuwa mpango wa Mungu kuzidisha familia ya wanadamu, na kuwawezesha kuitiisha nchi. Kwa hivyo, Adamu akatoka ali akishinda tena apate kushinda. Ingawa dhambi iliingia, na mauti yakadai familia ya wanadamu, mpango wa Mungu umetekelezwa, na dunia inakaliwa. Kwa hivyo “akatoka ali akishinda tena apate kushinda.” {SR2: 205.6}

“Nami nikaona, na tazama, farasi mweupe: na yeye aliyempanda ana uta.” Upinde ni zana iliyotumika kushinda (kujaza). Kwa hivyo, Adamu alipewa upinde (Hawa) kulingana na maneno: “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake; Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala: kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake: na ule ubavu, alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu, akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu: basi ataitwa Mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika Mwanamume. (Mwa. 2:18, 21-23.) “Naye Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa: kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.” (Mwa. 3:20.) Kwa hivyo taasisi hii takatifu ilianzishwa na Muumba wa ulimwengu wote. “‘Ndoa na iheshimiwe’; ilikuwa mojawapo wa zawadi za kwanza za Mungu kwa mwanadamu, na ni mojawapo wa taasisi mbili ambazo, baada ya anguko, Adamu alitoka nazo nje ya malango ya Paradiso.” — “Wazee wa Imani na Manabii,” uk. 46. Kwa hivyo Adamu alishinda (akaikalia dunia) pamoja na upinde (Hawa). {SR2: 206.1}

Muhuri Wa Pili–Farasi Mwekundu

“Na alipoufungua muhuri wa pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo uone. Akatoka farasi mwingine mwekundu: na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane: naye akapewa upanga mkubwa.” “Akatoka farasi mwingine mwekundu.” Iwapo farasi mweupe huwakilisha kipindi cha kwanza, basi farasi mwekundu lazima asimamie kile kilichofuata. “Nyekundu” ni sawa na nyekundu sana, ambayo ni nembo ya dhambi na hukumu. {SR2: 206.2}

Baada ya Adamu kutenda dhambi, dunia ililaaniwa, na uzuri wake mkamilifu ukaharibika. Kwa hivyo farasi mweupe alitoweka, na mwekundu akachukua nafasi yake. Akasema Mungu, “Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.” Lakini nembo hii hutumika moja kwa moja baada ya gharika, kwa maana uso wote wa dunia ulibadilishwa kwa ile gharika. Laana ya tatu ya kutisha

207

ikatua juu yake kama tokeo la dhambi. Maji yalipoanza kupungua, vilima na milima ilikuwa imezungukwa na bahari kubwa, yenye takataka…. Dunia ilionyesha mandhari ya mchafuko na uharibifu ambao hauwezekani kuelezewa. Milima, iliyokuwa maridadi sana katika ulinganifu wayo kamili, ilikuwa imevunjika na isiyo ya kawaida. Mawe, kingo za miamba, na miamba inayoparuza ilikuwa sasa imetapakaa juu ya uso wa dunia. Katika maeneo mengi, vilima na milima ilikuwa imetoweka, bila kuacha alama mahali ilipokuwa imesimama; na nyanda zilikuwa zimetoa nafasi kwa safu za milima. Mabadiliko haya yalionekana zaidi katika baadhi ya sehemu kuliko zingine. Pale ambapo hapo zamani zilikuwapo hazina tajiri duniani za dhahabu, fedha, na vito vya thamani, zilionekana alama kubwa zaidi za laana. Na kwa nchi ambazo hazikuwa zimekaliwa, na zile ambazo zilikuwa na uhalifu mchache, laana ilitua kidogo zaidi.” — “Wazee na Manabii,” ukurasa wa 108. Kwa hivyo farasi mwekundu huwakilisha kipindi cha baada ya gharika. {SR2 : 206.3}

Mpanda Farasi Kwa Farasi Mwekundu

“Na yeye aliyempanda alipewa uwezo kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane: naye akapewa upanga mkubwa.” Mara tu dhambi ilipoingia katika familia ya wanadamu, iliongezeka haraka, kama mti uzaao matunda. Ni tofauti kubwa ilioje kati ya yule mpanda farasi wa kwanza na wa pili. Hana tena taji kichwani mwake, lakini badala yake, upanga mkubwa mkononi mwake. Mwenye haki Abeli alikuwa wa kwanza kuanguka chini ya makali yake. Lakini kwa sababu ile nembo ina matumizi ya moja kwa moja baada ya gharika, hupata utimizo wake kamili katika mnara wa Babeli. {SR2: 207.1}

Wakati wakazi wa dunia walipoanza kuongezeka baada ya gharika, dhambi iliongezeka vivyo hivyo, na ingawa ilibidi waamini utabiri wa Nuhu wa gharika, wakatilia shaka utabiri wake baada ya gharika. “Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi… Nami nitalithibitisha agano Langu nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika, wala hakutakuwa tena gharika baada ya hayo kuiharibu nchi. Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano Nifanyalo kati Yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde Wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi.” (Mwa. 9:1, 11, 13.) {SR2: 207.2}

Kutoamini kwao katika neno la Mungu lililonenwa na Nuhu, kuliwachochea, kwa kumkaidi Mungu, kushiriki katika kujenga mnara wa Babeli kama ngome dhidi ya gharika ya pili. (Tazama Mwa. 11:3, 4.) Mungu kwa kutopendezwa juu ya wao kutozijua nguvu Zake, na kutoliamini neno Lake, kulimfanya Yeye auharibu ule mnara na kuichafua lugha yao. “Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende

208

usoni pa nchi yote… Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.” (Mwa. 11:8, 9.) Machafuko kwa mnara wa Babeli yalizalisha jamaa na lugha. Wakati walipogawanyika katika makabila yaliyojitenga, yale jirani yalianza kugombana moja kwa lingine. Wakati yalipokua mataifa, ugomvi wao uligeuka kuwa vita. {SR2: 207.3}

Kwa hivyo kipindi chini ya “farasi mwekundu” kilizaa machafuko yaliyopo kati ya mataifa. Kwa hivyo, alipewa uwezo “kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane: naye akapewa upanga mkubwa.” Kwa hivyo ushahidi huthibitisha kwamba farasi mwekundu hukiwakilisha kipindi baada ya gharika; na mpanda farasi, wakazi wake, sambamba na “simba” (Babeli), na baadaye na “dubu” (Umedi na Uajemi). Mwanzoni mwa serikali ya Uajemi, ugomvi wa hapo awali ulizuka katika vita vya umwagaji damu, kwa hivyo maneno kwa mbavu kinywani mwa dubu, “Inuka, ule nyama tele” (Dan. 7:5) yalitimizwa kikamilifu. Kwa hivyo, amani iliondolewa katika nchi kwa upanga mkubwa mkononi mwa mpanda farasi kwa farasi mwekundu. {SR2: 208.1}

Muhuri Wa Tatu–Farasi Mweusi

Ufunuo 6:5, “Na alipoufungua muhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi mweusi; na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.” Farasi mweupe ni nembo ya usafi, akiwa amezamishwa na mwekundu ambaye ni nembo ya dhambi, na nafasi ya mwekundu ikiwa imechukuliwa na “mweusi” huashiria giza la kiroho, au upofu wa kiakili. Kwa hivyo, rangi (nyeusi), humaanisha imani potovu kuhusu utu wa Mungu. {SR2: 208.2}

Wakati mwanadamu aliingia dhambini, nguvu zake za maadili na kiroho zilidhoofishwa kwa kiwango ambacho maono yake ya uwepo wa Mungu asiyeonekana yalifutwa. Ufisadi wa kiroho wa mdhambi na mielekeo ya uasherati ilimtaka mungu anayeonekana kumkomboa kutoka kwa uharibifu wa milele. Kwa hivyo ibada ya Yule asiyeonekana na aliye kila mahali iliachwa, na ibada ya sanamu ikachukua nafasi Yake. Hali hii ya giza la kiroho ilikuwa imewalemea wakazi wa ulimwengu wetu katika siku za Abramu, karibu miaka mia tatu tu baada ya gharika. {SR2: 208.3}

Kwa vile hakuna kumbukumbu ya ibada ya sanamu kabla ya wakati huo, farasi mweusi lazima awakilishe kipindi kutoka tarehe hiyo hadi kwa enzi ya Ukristo. Ni dhahiri Israeli wa mwili huja chini ya kipindi cha farasi mweusi. Katika kila tukio, wakati ulimwengu ulifikia kilele cha udanganyifu wa Shetani, Mungu, kwa rehema Yake na

209

upendo kwa wadhambi, alilazimika kufanya hatua fulani kuhifadhi muda wa rehema kwa wanadamu. Wakati huo Yeye hangeweza kuwaangamiza wadhambi watoke kwa uso wa dunia na bado aitimize ahadi Yake kwa Nuhu. Kuhakikisha kulihifadhi hilo agano Yeye alimwita Abramu kutoka kwa ibada ya sanamu hadi kwa ibada ya Mungu wa kweli, akilianzisha taifa tofauti kwa familia moja sawa na ile ya Adamu na Nuhu; na tokeo lake likawa kwamba Wazee kumi na wawili wa Israeli walitokea, ambao kwa wao Mungu alifanza taifa moja kubwa. {SR2: 208.4}

Mizani Mkononi Mwa Mpanda Farasi

Ufu. 6:5, sehemu ya mwisho, “Nikaona, na tazama farasi mweusi; na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.” Kwa sababu taji na uta wa mpanda farasi mweupe hutaja haki zake, na upanga mkubwa mkononi mwa mpanda farasi mwekundu huonyesha haki yake, kwa hivyo mizani iliyo mkononi mwa mpanda farasi mweusi lazima iwe inataja watu na tabia zao, katika kipindi hicho. {SR2: 209.1}

Mizani hutumika kwa madhumuni ya kibiashara. Kwa hivyo, ile nembo huashiria utangulizi wa wazo la kibiashara. Kabla ya, au karibu wakati wa Abramu, biashara ya uuzaji kati ya mataifa haikujulikana. Lakini katika kipindi kilichowakilishwa na farasi mweusi wazo hili lilizaliwa. Jamii za Wafoinike na Wasemiti [Waebrania, Waaramu, Waarabu, na Wakushi] zinajulikana kwa ugunduzi unaozidi kuongezeka, na Sidoni na Tiro kama vituo vyao vikuu vya biashara. “Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?” (Isa. 23:8.) {SR2: 209.2}

“Lazima tuwataje watu wengine ‘Wadogo’ wa jamii hii ya Wasemiti [Waebrania, Waaramu, Waarabu, na Wakushi] ambao ushawishi wao juu ya ulimwengu umekuwa na nguvu zaidi kuliko ule wa Misri, au Babeli — Wafoinike. Jimbo lao pia lilikuwa dogo sana moja wapo wa ya zamani kabisa… Miji yao mikuu ilikuwa Sidoni, na, kwa umbali mfupi, malkia wa miji ya Wafoinike, Tiro. Lakini katika wakati wangeweza kueneza makoloni yao ya kibiashara katika nchi zote za Mediterrenia, na katika nchi zingine, siku zote wakisaka maeneo mapya ya Uuzaji na vituo vya kibiashara. Walikuwa nyuki wa ulimwengu wa kale wakibeba mbelewele ya utamaduni huo popote walipokwenda. Mahitaji ya uuzaji na biashara yaliwasukuma kuifanya kamilifu alfabeti, na kutoka kwao ulimwengu wa magharibi uliipata. Kwa namna fulani walikuwa wa kipekee katika ulimwengu wa kale, na utofauti huu walizikwa pamoja nao. Kwa maana hawakuwa na hamu ya vita, isipokuwa biashara; hawakujali kulipa kodi kwa mamlaka ya kijeshi, almuradi mamlaka hayo hayangehitilafiana na haki zao za uuzaji. Walikuwa na uwezo kama wa Wayunani wa kuishi wenyewe hata wawe Misri, Babeli, Ashuru, Uajemi au awamu nyingine yoyote ya ustaarabu

210

iliyotolewa; lakini kipaji chao kikuu kilikuwa katika uvumbuzi, ujuzi wa kiufundi, shughuli za biashara, na katika viwanda. Katika kazi za vyuma, dhahabu, pembe za ndovu, vioo, na rangi za zambarau walisimama katika ulimwengu wa kale bila kifani. {SR2: 209.3}

“Tunakumbuka kutoka katika Agano la Kale kisa cha azma ya Daudi ya kujenga hekalu linalostahili kuabudiwa Mungu wa Israeli. Anaambiwa kwamba kazi hiyo ingefaa iachwe kwa mwanawe Sulemani. Kwa hivyo tunaona Sulemani akifanya mkataba na Hiramu, Mfalme wa Tiro. Hiramu alitakiwa kutoa mbao za mierezi na miberoshi, pamoja na maseremala na waashi kwa ajili ya jengo hilo, na kusafirisha vifaa kwa mashua hadi Yuda. Wingi wa fahari ya nje ya utawala wa kustaajabisha na kujivunia wa Sulemani unapaswa kupewa sifa kwa ustadi wa kiufundi wa hawa mafundi stadi wa Wafoinike. Kupitia miji yao ilitiririka biashara yenye faida sana ya Uarabuni na Mashariki: na watengeneza bidhaa wao walidumishwa wakijishughulisha kufanza bidhaa zao za vyuma, vioo, na zambarau. Baharini na ardhini walisafiri kila mahali — wamishonari wa biashara — wafanya biashara stadi wa Ulimwengu wa Kale. Wakati wa Homer Wafoinike walisifiwa kuwa maharamia — wanyang’anyi — na wafanya biashara kwa sababu ya hitaji tu. Huenda si kitu kuliko hekaya, lakini tunaambiwa walileta mapambo yao ya shanga, na mikufu ya bei nafuu, ambayo waliuza kwa bei ghali na waliteka nyara wavulana na wasichana ili kuwauza katika masoko ya mashariki kama biashara ya ziada.” — “Maarifa Muhimu, — Wafoinike,” Gombo la 1, uk. 69, 70. {SR2: 210.1}

Usiyadhuru Mafuta Wala Divai

Ufu. 6:6, “Nikasikia sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, … angalia usiyadhuru mafuta wala divai.” Kwa mujibu wa Ufunuo 4:6, wale wenye uhai wanne wamekizunguka kiti cha enzi. Kwa hivyo, kiti cha enzi kiko katikati ya wanyama. Asema Yohana: “Nikasikia sauti katikati ya hao wenye uhai wanne.” Mojawapo wa mambo aliyosikia ni, “Angalia usiyadhuru mafuta wala divai.” Kwa hivyo, iwayo yote maana ya ile nembo, si ya wanadamu, bali ni ya Mungu, kwa maana Ndiye aliyeamuru, “Angalia usiyadhuru mafuta wala divai.” {SR2: 210.2}

Ni ukweli unaokubalika na karibu wanafunzi wote wa Biblia kwamba “mafuta” hutumika na Maandiko kama nembo ya Roho Mtakatifu, ilivyo katika Zaburi 45:7; Isaya 61:1-3; Zekaria 4:12. “Divai” hutumika kama nembo ya damu ya Kristo, na jinsi “uhai ulivyo katika damu,” divai huashiria uzima wa milele, unaopatikana tu ndani ya “Mwana-Kondoo wa Mungu aiondoaye dhambi ya ulimwengu.” Yesu alisema, “Maneno hayo ninayowaambia ni roho tena ni uzima” — “mafuta” na “divai.” Maneno katika Biblia ni “Roho” na “Uzima.” Kwa hivyo, ile amri, “usidhuru mafuta na

211

divai,” humaanisha Biblia — Roho na Uzima. Lakini mbona amri hiyo alipeanwa haswa kwa mpanda farasi huyu? Mbona si kwa mmojawapo wa wale wengine? Jibu pekee linaloweza kutolewa ni kwamba kile kipindi chini ya farasi mweusi na mpanda farasi wake kilizalisha Biblia. Amri hiyo ilifuatwa na Biblia ikaja. Katika wakati wa ibada ya sanamu na giza nene la kiroho, Mungu, kwa upendo Wake ambao haushindwi kamwe, aliibariki familia ya wanadamu kwa zawadi ya Neno Lake lililoandikwa kuwa Nuru kwa ulimwengu. Sauti kutoka kwa kiti cha enzi “Usiyadhuru mafuta wala divai,” ni sauti katika Biblia na maneno ya Yehova. Sehemu iliyosalia ya aya ya sita itafafanuliwa katika somo lingine. {SR2: 210.3}

Muhuri Wa Nne

Ufu. 6:7 na 8: “Na alipoufungua muhuri wa nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne ikisema, Njoo uone. Nikaona, na tazama farasi wa rangi ya kijivujivu: na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.” {SR2: 211.1}

Kwa sababu wakati wa Agano la Kale hufunga na muhuri wa tatu, Jipya huanza na ufunguzi wa muhuri wa nne. Kwa hivyo, farasi wa rangi ya kijivujivu na mnyama dubwana wa Danieli 7:7, 8, humiliki kipindi kile kile. Ni dhahiri mnyama mmoja lazima afanane na yule mwingine au nembo hiyo haitakuwa kamilifu. Rumi iliwakilishwa na mnyama dubwana kwa sababu serikali yake ilikuwa mseto wa sheria za kiraia na za kidini, na mafundisho ya Kipagani na ya Kikristo. Kwa hivyo, ilikuwa isiyoweza kuelezeka kama ilivyofafanuliwa hapo awali. Farasi wa rangi ya kijivujivu ana maana ile ile, kwa sababu rangi yake ni hafifu, yenye upungufu, isiyokuwa na rangi maalum au dhahiri. Kijivujivu — isiyoelezeka [dubwana]. {SR2: 211.2}

Mpanda farasi huwakilisha wanaotawala viongozi wa serikali. Jina lake ni Mauti. “Mauti na Kuzimu [hadesi au kaburi kama ilivyo katika toleo lililorekebishwa] akafuatana naye.” Haya ni maelezo makamilifu ya dola isiyo ya haki, inayotesa ya Kirumi, inayolingana na mnyama jinsi Danieli alivyomwona: “Alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake.” Katika ufunguzi wa muhuri wa nne, Rumi, chini ya nembo ya mnyama dubwana katika hatua zake zote (ya kifalme na ya upapa) uliwatesa raia wake kwa imani yao ya kidini, na mamilioni walipoteza maisha yao. Kwa hivyo, “Mauti na Kuzimu [kaburi] akafuatana naye.” {SR2: 211.3}

“Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi: waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.” Hapa umetolewa wakati halisi ambao Rumi ya kifalme na ya upapa ingetawala dunia,

212

ingewaua wafuasi wa Kristo kwa njia hizi tofauti tofauti za ukatili. Tena, angalia ukamilifu wa Maandiko yakitumia kitenzi jina “nao,” yakimaanisha zote Rumi ya kifalme na ya upapa, pia mamlaka ya serikali ya kiraia na kidini. Kumbuka sehemu ya kwanza ya sentensi. “Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi.” Ulimwengu huu wa sasa, tangu uumbaji hadi mwisho wake au mwanzoni mwa millenia, utakuwa miaka 6,000. Mpanda farasi wa kijivujivu alipaswa kuwa na mamlaka juu ya robo ya dunia. Tunagawanya 6,000 katika sehemu nne sawa, na tunapata miaka 1500. Kwa hivyo, mateso ya kikatili na yasiyo ya haki ya Rumi yalikuwa yapoteze nguvu zake mwishoni mwa miaka 1500 au robo. Hilo ndilo lililotukia haswa. Wakati huo Martin Luther aliinuka dhidi ya upapa na kuutia jeraha la mauti, kwa chombo cha ukweli — “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Na tokeo lilikuwa kwamba Uprotestanti ulikuja kwenye jukwaa la utendaji dhidi ya upapa. Hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tano upapa ulitawala kwa ukuu kama mfalme wa wafalme, kwa mkono wa chuma wa serikali katika vazi la kile kilichoitwa eti mamlaka ya kiroho; lakini wakati huo mamlaka yake yalivunjwa. {SR2: 211.4}

Kuanzia kusulubishwa kwa Kristo hadi kwa “Maungamo ya Augsburg,” hati iliyoandaliwa na Luther, ilijumuisha kipindi cha miaka 1500. Hati hii ilisainiwa na mataifa ya waprotestanti na kupitishwa kama imani yao, na ilikuwa mateto dhidi ya papa. Hivyo kwa wakati uliowekwa, mamlaka yao ya Kipagani na ya Upapa, yalivunjwa. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 209-222.) Kwa hivyo kutimiza kikamilifu unabii wa ki-mfano kwamba “wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi.” Hapa upo ukweli ambao unapindua wazo kwamba dunia imekuwapo kwa zaidi ya miaka 6,000. Pia huthibitisha matumizi ya mihuri kuwa sahihi kabisa. {SR2: 212.1}

Farasi wanne tu wanajulishwa badala ya saba, au, farasi kwa muhuri. Nne ni namba nyingine ya Kibiblia inayoashiria kwamba uwakilishi wa farasi ni wa ulimwenguni kote (ncha nne za dira). (Tazama ukurasa wa 54). Wakati idadi ya farasi huwakilisha athari za laana ya dhambi kwa ulimwengu wote idadi ya mihuri huashiria ukamilifu wa injili na watakatifu kutiwa muhuri. {SR2: 212.2}

Muhuri Wa Tano

Ufu. 6:9-11: “Na alipoufungua muhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao: Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu nyeupe;

213

wakaambiwa, wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao, itakapotimizwa.” {SR2: 212.3}

Kufungwa kwa muhuri mmoja na kufunguliwa kwa mwingine kulitumia kipindi cha miaka thelathini. Kwa hivyo muhuri wa nne ulifungwa mwaka 1530 B.K., hadi kwa wakati ambao mpanda farasi aliye wa rangi ya kijivujivu alikuwa na mamlaka. Kwa hivyo, matengenezo kupitia kwa Luther yanaanguka chini ya muhuri wa tano; na baada ya kufunuliwa Yohana alionyeshwa, “roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu,” chini ya muhuri wa nne. “Wakaambiwa [wale waliouawa], wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao, itakapotimizwa.” Maneno hayo huonyesha kwamba ingawa udikteta ulikuwa umepoteza nguvu zake, mateso hayakuwa yamekoma kabisa, kwa maana wajoli wenzao na ndugu zao walikuwa bado hawajauawa chini ya muhuri wa tano. Asema Yohana: “Na alipoufungua muhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu.” Kwa hivyo, ni Wakristo waliouawa. {SR2: 213.1}

Madhabahu ni nembo pia, kwa hivyo pia lazima izingatiwe. Madhabahu hutumika kwa ibada; na kama roho za wale waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu zilikuwa chini yake, tunajua kwamba ilikuwa madhabahu ya ibada ya kweli — matengenezo ya Luther. {SR2: 213.2}

Muhuri Wa Sita

Ufu. 6:12,13: “Nami nikaona alipoufungua muhuri wa sita, na, tazama, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota za mbinguni zikaanguka juu ya nchi, kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.” {SR2: 213.3}

Muhuri wa sita unafunguliwa na tetemeko la ardhi la Lisbon la Novemba 1, 1755. Kufuatia tetemeko la ardhi jua likatiwa giza, Mei 19, 1780, na mwezi ulionekana kama damu usiku uliofuata. “Kuanguka kwa nyota,” kunarejelea mvua kubwa ya vimondo ya Novemba 13, 1833. Yesu, akitazama mbele kwa utimizo wa ishara hizi, alisema: “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika.” (Mat. 24:29.) Kwa hivyo, chini ya muhuri wa sita zilikuja ishara za wakati wa mwisho — tetemeko kubwa la ardhi mwaka 1755, siku ya giza katika mwaka 1780 nyota zilizoanguka katika mwaka 1833, na mwanzo wa hukumu katika mwaka 1844. {SR2: 213.4}

Kwa Ufu. 6:14-17, maelezo yanapatikana katika “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, uk. 267, 268: “‘Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa wakati umevingirishwa pamoja; na kila mlima na kisiwa

214

kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima; wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini mbele za uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo: Kwa maana siku iliyo kuu ya hasira Yake imekuja; naye ni nani awezaye kusimama? (Ufu. 6:12-17.) Baada ya hayo nikaona, na, tazama, umati mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu, wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo… Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.’ … Ufunuo 7:9-17.” {SR2: 213.5}

Kwa mujibu wa ushuhuda ufuatao, Ufunuo 6:12-17, una matumizi maradufu, na ni wazi kwamba aya hizi pia hurejelea kwa wakati wa utakaso wa kanisa la Mungu, kwa maana mtumwa wa Bwana husema, “Katika maandiko haya makundi mawili yanaletwa kwa mtazamo. Kundi moja waliruhusu wenyewe kudanganywa, na kuungana na wale ambao Bwana ana vita nao. Walifasiri visivyo ujumbe uliotumwa kwao, na kujivika mavazi ya haki ya ubinafsi. Dhambi haikuwa dhambi machoni mwao. Walifundisha udanganyifu kama ukweli, na kupitia kwao nafsi nyingi zilipotoshwa.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, ukurasa 268. Imeamuliwa, kutoka kwa ushuhuda ambao umenukuliwa hapo juu, kwamba wamefundisha uongo. Tunamwomba msomaji azingatie lile ambalo limefundishwa kwa njia ya nembo zinazopatikana katika vitabu vya Danieli na Ufunuo. Kwa mfano, fikiria ukweli ulioletwa kwa mtazamo hapa, ukilinganishwa na yale ambayo yamefundishwa kwa miaka kadhaa. {SR2: 214.1}

Muhuri wa Saba, Ufunuo 8:1-5

Ufu. 8:1, 3-5: “Hata alipoufungua muhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu; akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba, ukapanda mbele ya Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi: kukawa na sauti, na radi, na umeme na tetemeko la nchi.” {SR2: 214.2}

215

Tumeacha aya ya pili, kwa maana inarejelea baragumu saba. Kimya mbinguni kama muda wa nusu saa hakiwezi kuwa ujio wa pili wa Kristo, jinsi ambavyo wengine wamefikiri, kwa sababu baadaye malaika mwenye chetezo cha dhahabu na uvumba, alitoa maombi ya watakatifu kutoka kwa madhabahu ya dhahabu. Madhabahu yako katika mahali patakatifu, mkabala tu na kiti cha enzi kilicho katika patakatifu mno. Hivyo vyumba viwili vilitenganishwa na pazia. Katika siku ya upatanisho, pazia au mlango wa hekalu la duniani ulifunguliwa na kuhani mkuu aliingia ndani. Lakini ikumbukwe kwamba mlango (pazia) uliachwa wazi wakati kuhani mkuu alikuwa akihudumu. Kwa hivyo vyumba viwili vikawa kimoja. Kwa sababu hii mkutano haukuruhusiwa mahali patakatifu siku hiyo, jinsi walivyokuwa kwa nyakati zingine, kwa maana pazia ilipoinuliwa, patakatifu pia palikuwa patakatifu mno. Kwa hivyo wakati mlango wa patakatifu mno ulipokuwa wazi, mlango wa patakatifu ulifungwa. Kwa hivyo, kuhani mkuu pekee alivitumia vyumba hivyo vyote kwa siku ya upatanisho. (Tazama Law. 16:17.) Kwa hivyo madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi, ambayo juu yake malaika alitoa maombi ya watakatifu, yalitumika, na hutumika katika vipindi vyote viwili — kabla, na katika wakati wa hukumu. Maadamu jopo lote la mahakama (Jaji, Wakili, Wazee, n.k.) walikuwa hekaluni baada ya muhuri wa saba kufunuliwa, ni dhahiri kwamba hukumu ilikuwa ikiendelea, na muda wa rehema haukuwa umefungwa wakati wa “kimya.” Kwa maana baada ya hukumu kukoma na muda wa rehema kufungwa, hakuna mtu anayeweza kuingia katika hekalu. (Tazama Ufu. 15:8.) {SR2: 215.1}

Iwapo “kimya” cha “nusu saa” kingeonyesha ujio wa Kristo, wakati ambapo Yeye angewachukua watakatifu Wake pamoja Naye, hapangekuwa na hitaji kwa malaika kutoa maombi yao. Isitoshe, ingekuwa bure “kuutupa” moto, ambao ni Roho wa Mungu, kutoka kwa madhabahu ya dhahabu hadi duniani. Tena, ikiwa kufunuliwa kwa muhuri wa saba kwamaanisha kuja kwa Kristo, basi wale tu walio chini ya mihuri sita ndio wangezingatiwa katika hukumu, na haungekuwapo muhuri wa saba, ambao ungeonyesha ukosefu wa ukamilifu na ukamilisho wa hukumu, na wa injili. Ingekuwa pia kinyume na idadi ya mihuri kwa kile kitabu. Kwa sababu mihuri sita hurejelea vipindi sita ambavyo watakatifu walitiwa muhuri, lazima ule wa saba pia utumike kwa kipindi cha kutia muhuri; vinginevyo hauwezi kuitwa, “muhuri” wa saba. {SR2: 215.2}

Sasa hebu tuangalie ukweli kama ulivyofundishwa na muhuri wa mwisho. Kumbuka kwa uangalifu mpangilio wa kila tendo. Muhuri unafunuliwa, na kimya kinafuata, kwa maana linasema: “Hata alipoufungua muhuri wa saba, kukawa kimya.” Tafsiri Iliyosahihishwa, Weymouth, Biblia za Kiyunani, na Kibulgaria husomwa vivyo hivyo. Hicho kimya kilifuatwa na ujio wa malaika kwa madhabahu na chetezo, baada ya kutoa maombi ya watakatifu. Na kisha

216

akakijaza chetezo moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi: kukawa na sauti, na radi, na umeme na tetemeko la nchi. Huu ndio utaratibu halisi wa kila tukio. {SR2: 215.3}

Ni nini kilichosababisha kimya? Hukumu ilipoanza, Yohana anasema: “Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo;” na wale wenye uhai wanne “hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi.” (Ufu. 4:5, 8.) Sauti huwa endelevu mchana na usiku wakati hukumu inaendelea. Lakini wakati fulani baada ya muhuri wa saba kufunuliwa sauti hizi zilikuwa kimya kwa karibu nusu saa. Baada ya malaika kutoa maombi ya watakatifu, na kuutupa moto juu ya nchi, sauti zilianza tena. “Kukawa na sauti, na radi, na umeme na tetemeko la nchi.” Kwa udhahiri hukumu hiyo, kwa sababu fulani, ilikuwa imekoma, na nusu saa baadaye ikaanza tena. Haiwezi kuwa vinginevyo, kwa maana, iwapo hukumu ilikuwa ikiendelea, na wenye uhai na wazee wakiwa wamenyamaza, ingeonyesha kwamba palikuwa na kitu fulani kibaya — kitu ambacho hawangeweza kusema “amina” na kumsifu Mungu. Kwa hivyo, hitimisho pekee sahihi ni, kwamba kwa sababu fulani hukumu ilipumzika kwa nusu saa. {SR2: 216.1}

Ni nini kilifanyiza huo mkatizo na kuleta hilo badiliko? Hebu sasa tubainishe kwanza urefu wa nusu saa ya kinabii. Siku katika wakati wa kinabii huwakilisha mwaka. (Ezek. 4:6.) Saa moja ni sehemu ya ishirini na nne ya mwaka wa kinabii, na kuhesabu siku thelathini kwa mwezi, yangekuwa kama majuma mawili. Nusu saa itakuwa nusu ya majuma mawili; kwa hivyo, siku saba halisi. Siku saba zilitumika kwa utakaso. (Tazama Kut. 29:35, 37; Law. 12:2; 13:4, 5; 1, 9, 11, 12, 14, 15, 21, n.k.) Kutoka kwa dondoo hizi tunahitimisha kwamba “nusu saa” au siku saba huwakilisha utakaso wa kanisa, ukionyesha mbele utimizo wa Malaki 3:1-6. Lakini tuna uthibitisho dhahiri zaidi, ambao utaondoa mashaka yote. {SR2: 216.2}

Katika maadhimisho ya Pasaka, Bwana aliwaamuru Israeli kusherehekea hafla hiyo siku saba. (Tazama Law. 23:5-8.) Hakika hakuna mtu atakayesema kwamba Mungu aliwaamuru watu Wake kuadhimisha hafla hiyo siku saba bila lengo. Israeli wa kimwili kuingia Misri, kisha kutoka Misri kwenda hadi Mlima Sinai, pasaka huko Misri usiku wakati malaika wa mauti alipompiga mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na mnyama wakati wa kuondoka kwa Israeli, ni mifano kwa kanisa wakati huu — kanisa linalotoka Misri — udunia, utakaso wa kanisa, utengo wa magugu kutoka kwa ngano — utimizo wa Ezekieli 9. (Ufafanuzi kamili wa mada hiyo umetolewa katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 64-113; tazama pia chati kwenye ukurasa wa 224.) Roho ya Unabii hushuhudia hili kwa taarifa ifuatayo: “Pasaka ilipaswa kuwa ya ukumbusho na

217

ya mfano, sio tu kuonyesha nyuma kwa ukombozi kutoka Misri, lakini mbele kwa ukombozi mkubwa ambao Kristo alipaswa aufanikishe katika kuwaweka huru watu Wake kutoka kwa utumwa wa dhambi.” — “Wazee na Manabii,” uk. 277. {SR2: 216.3}

Kwa hivyo kimya cha nusu saa huelekeza mbele kwa tukio hili kubwa kwa ajili ya kanisa la Mungu. Utimizo wake utatuleta kwa wakati wa mavuno, au kama unavyoitwa, Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu wa Ufunuo 18 — ujumbe wa mwisho kwa dunia. Kwa hivyo, wakati watu watano walio na silaha za kuchinjia wanawaondolea mbali wale wanaowakilishwa na magugu ndani ya kanisa, kutakuwa na kimya mbinguni kama muda wa nusu saa (siku saba), baada ya hapo hukumu itaanza tena kwa wale watakaotiwa muhuri wakati wa mavuno makubwa, ambayo ni mwisho wa dunia. Yesu alisema: “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno: na katika wakati wa mavuno Nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome: bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.” — kanisa. (Mat. 13:30.) {SR2: 217.1}

Wale ambao watatiwa muhuri kwa wakati huo walionekana na Yohana kama umati mkubwa walio na matawi ya mitende mikononi mwao. (Tazama Ufu. 7:9.) Kwa hivyo chuo kimegeuza mkondo, na kutiwa muhuri kwa wale ambao watahukumiwa wakiwa hai, kumeanza. Kama tulivyosema hapo awali, usiku wa pasaka huko Misri ni mfano wa utakaso wa kanisa, utengo wa magugu kutoka kati ya ngano. Waisraeli kuivuka ile Bahari ya Shamu kulielekeza mbele kutimizwa kwa Isaya 63. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 96-103.) {SR2: 217.2}

Kwa hivyo, nabii hutangaza maneno ya Bwana: “Maana siku ya kisasi i moyoni Mwangu, na mwaka wao Niliowakomboa umewadia.” (Isa. 63:4.) Tunanukuu aya ya 1-3, pia 17, 18: “Ni nani huyu atokaye Edomu, mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Mimi ninenaye katika haki, mwenye uwezo kuokoa. Kwa nini mavazi yako yamekuwa mekundu, na mavazi yako kama ya mtu akanyagaye zabibu? Nimelikanyaga shinikizo peke Yangu; wala katika watu hakuwapo mtu pamoja Nami: naam, Nitawakanyaga kwa hasira Yangu, Nitawaponda kwa ghadhabu Yangu; na mavazi Yangu yatatiwa madoa kwa damu yao… Ee Bwana, mbona umetukosesha njia Zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi Wako. Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu: adui zetu wamepakanyaga patakatifu Pako.” {SR2: 217.3}

Nabii alimwona Kristo mwenyewe akirudi kutoka kwa mchinjo wa Waedomu — daraja ambalo lilikuwa likiwadanganya watu wa Mungu kanisani, magugu, au maadui waliokuwa wamepakanyagia

218

chini patakatifu. “Bozra” humaanisha “zizi la kondoo” — kanisa. Aliona mavazi Yake yametiwa madoadoa kwa damu ya magugu, katika kuwaokoa watu Wake kutoka mikononi mwao. Nabii aliuliza: “Kwa nini mavazi yako yamekuwa mekundu, na mavazi yako kama ya mtu akanyagaye zabibu?” Utakaso wa kanisa hufanya iwe lazima kwa Kristo kuondoka mahali pa hukumu na kushuka chini ili kuwakoa watu Wake waliokombolewa (watu 144,000), na hili ndilo linalosababisha hukumu kukoma, na sauti kuwa kimya kwa karibu nusu saa — siku saba. Roho ya Unabii hushuhudia vivyo hivyo. “Bwana Yesu atainuka kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, na kujivika mavazi ya kisasi, na kuwashangaza katika karamu yao isiyo takatifu; na watajikuta hawajajiandaa kwa ajili ya karamu ya jioni ya Mwana-Kondoo.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 690. Petro, akitazama mbele kwa utakaso wa kanisa la Mungu, na kuanza kwa hukumu ya walio hai, asema: “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu: na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? (1 Petro 4:17.) {SR2: 217.4}

Laiti kanisa kama kundi, au angalau viongozi wa dhehebu la Waadventista wa Sabato wangeupokea ujumbe wa matengenezo jinsi ulivyowasilishwa kwao katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, hapangekuwa na ulazima wa daraja hilo kuanguka kwa mfano wa watu watano wenye silaha za kuchinjia. Ni kuupokea au kuukataa ujumbe ambao utakata kauli ya hatima ya madaraja mawili jinsi ilivyoelezewa katika ushuhuda ufuatao: “Naliuliza maana ya upepeto nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi wa kweli kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu usiopinda. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 270. {SR2: 218.1}

Katika patakatifu pa duniani, kuhani mkuu aliingia katika chumba kitakatifu mno mara moja kwa mwaka, na haswa kwa siku hiyo kila Mwisraeli alipaswa kuungama dhambi yake. Yeye ambaye alipuuza kutii matakwa ya Mungu alikatiliwa mbali kutoka kwa watu wake. (Tazama Law. 23:29, 30.) Kwa hivyo siku ya upatanisho ya uakisi, hukumu, au utakaso wa patakatifu, kama ulivyowekwa katika Danieli 8:14, ni siku ya utakaso kwa kambi ya Israeli, kanisa — kuondolea mbali dhambi na wadhambi. Hekalu la duniani lilikuwa mfano wa lile la mbinguni. (Tazama Ebr. 9:23, 24.) Lilianzishwa pamoja na mfumo wake wa sherehe kuelekeza mbele kwa kazi ya Kristo, Kuhani wetu Mkuu ndani ya hekalu la mbinguni katika kipindi cha

219

uakisi — wakati wa Agano Jipya. Kwa sababu hekalu na utumishi wake wote, lilikuwa mfano wa lile la kweli, la mbinguni, chini ya utumishi wa Kristo, kwa hivyo siku ya mfano ya upatanisho lazima ionyeshe ukweli katika kipindi cha uakisi — wakati wetu. {SR2: 218.2}

Wakati hukumu kwa walio hai inaendelea, kila dhambi lazima iungamwe na kuachwa. Yeye ambaye ataipuuza fursa hii kuu, atapata amejihusisha katika uharibifu wa milele — amekatiliwa mbali kutoka kwa watu Wake. Kuipuuza mada hii muhimu sana hakutatufaidi hata kidogo. {SR2: 219.1}

Matengenezo Katika Mtazamo

Matengenezo makubwa katika mtazamo, yaliyowakilishwa wazi wazi na malaika kwa madhabahu ya dhahabu na maombi ya watakatifu, na kutupwa kwa moto kutoka madhabahuni hadi kwa dunia, kumetabiriwa pia, katika ushuhuda ufuatao: “Katika maono ya usiku viwakilishi vilipita mbele yangu vya vuguvugu kubwa la matengenezo kati ya watu wa Mungu. Wengi walikuwa wakimsifu Mungu. Wagonjwa waliponywa, na miujiza mingine ilifanywa. Roho ya maombezi ilionekana; hata jinsi ilivyodhihirishwa kabla ya siku kuu ya Pentekoste. Mamia na maelfu walionekana wakizuru familia, na kufunua mbele yao neno la Mungu. Mioyo ilisadikishwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, na roho ya uongofu wa kweli ilidhihirika. Kwa kila upande milango ilifunguliwa wazi kwa utangazwaji wa ukweli. Ulimwengu ulionekana kuangazwa na mvuto wa kimbingu. Baraka kubwa zilipokelewa na watu wa kweli na wanyenyekevu wa Mungu.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, uk. 126. {SR2: 219.2}

Ndugu zangu, Bwana anazungumza nasi. Je! Hatutaitii sauti Yake? Je! Hatutazitengeneza taa zetu na kutenda kama watu ambao wanamtarajia Bwana wao aje? “Wakati ni ule unaoitisha kuiangaza nuru, na kuchukua hatua.” Amka, nakusihi, kutoka katika usingizi wa mauti. Usiiruhusu siku ya mwisho ikupate hoi wa hazina ya mbinguni. {SR2: 219.3}

Je! Wote walio hai watahukumiwa na kutiwa muhuri chini ya muhuri wa saba? Au wengine wameshughulikiwa kabla ya huo muhuri kufunuliwa? Kujibu swali hili tunanukuu Ufunuo 8:3, “Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu; akapewa uvumba mwingi, ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.” Kumbuka, maombi yanatolewa kwa ajili ya watakatifu wote. Hakuna mtu, anayejua ukweli wa Mungu, angethubutu kuwaombea wafu, kwa sababu ni chukizo mbele ya Mungu; sembuse malaika angefanya dhambi kama hiyo. {SR2: 219.4}

Mtunga Zaburi hutangaza kwamba maombi kwa ajili ya wafu ni ubunifu wa mataifa, “Wakajiambatiza na Baal-Peori,

220

wakazila dhabihu za wafu. Wakamkasirisha kwa matendo yao: na tauni ikawashambulia.” (Zab. 106:28, 29.) “Sio wafu wamsifuo Bwana, wala wo wote washukao kwenye kimya.” (Zab. 115:17.) Iwapo wafu hawamsifu Mungu, malaika anawezaje kuwasilisha ombi kwa ajili yao mbele ya Mungu? {SR2: 219.5}

Kirai, “watakatifu wote,” kinarejelea walio hai wote ambao watahukumiwa. Ni dhahiri hili linafanywa chini ya muhuri wa saba. Iwapo “wote,” basi ni dhahiri kwamba watakatifu wote walio hai wanahesabiwa chini ya muhuri wa saba. Hivyo, kwa ufunguzi wa muhuri wa mwisho, unaanzisha hukumu kwa watakatifu wote walio hai. Usiruhusu chochote kikukanganye kwa jambo hili. Ikiwa tunasema maombi ya watakatifu wote yalikuwa na uhusiano fulani na wafu, basi yangepaswa kutolewa mwanzoni mwa hukumu — kufunuliwa kwa muhuri wa kwanza, kwa sababu baada ya hukumu maombi hayawezi kuwafaidisha. {SR2: 220.1}

Kumbuka maneno wakati wa ufunguzi wa hukumu kwa wafu mwaka 1844: “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.” (Ufu. 5:8.) Tia alama kwamba hakuna malaika aliyetoa maombi, lakini sala za watakatifu ziliwasilishwa na wanyama na wazee kupitia sifa na vinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, yaani, hapakuwa na maombi yaliyotolewa kwa ajili ya wafu, lakini maombi yao ambayo walikuwa wameomba, yalirekodiwa wakiwa bado hai, yaliwasilishwa mbele ya kiti cha enzi. Watu 144,000 wanatiwa muhuri kabla ya kimya “cha nusu saa,” au wakati wa kufunuliwa kwa muhuri, lakini wanahukumiwa katika kipindi cha muhuri wa saba, kwa maana maombi yalikuwa kwa ajili ya watakatifu “wote” — walio hai. {SR2: 220.2}

Je! Ipo njia yoyote ambayo tunaweza kubainisha wakati wa kufunuliwa kwa muhuri, na mwanzo wa hukumu kwa walio hai? Iwapo Mungu kwa uaminifu alifunua kwa walio hai ilipoanza hukumu kwa wafu, haiwezekani kwamba Yeye atauweka sirini wakati wa hukumu kwa walio hai. Iwapo Yeye angefanya hivyo, hatungekuwa na ukweli wa sasa katika wakati wa muhuri wa mwisho; wala haiwezi kuwapo haki katika usiri kama huo, wala hukumu kama hiyo haiwezi kuwa ya halali. Kwa hivyo, ufunuo wa hukumu kwa walio hai, ni wa umuhimu sana kama ufunuo wa injili yenyewe. Kwa maana hukumu (kuzifuta dhambi) ni tendo la kuweka taji katika injili ya Kristo. Kwa hivyo tunahitimisha kwamba wakati muhuri unafunuliwa, na hukumu kwa walio hai kuanza, lazima tujue. Siku ya upatanisho katika mfano wake huthibitisha lilo hilo, kwa maana Waisraeli walijuzwa vyema juu ya tukio hilo, wajibu wao, na matokeo yake. {SR2: 220.3}

Tarehe ya tukio hilo tukufu zaidi kwa wenye haki, lakini lenye uzito mkubwa kwa waovu, itajulikana kwa utimizo

221

wa aya ifuatayo: “Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu akautupa juu ya nchi: kukawa na sauti, na radi, na umeme na tetemeko la nchi.” (Ufu. 8:5.) Kuutupa moto kutoka kwa madhabahu hadi kwa nchi ni kumiminwa kwa Roho wa Mungu. Tumesema hapo awali kwamba kitabu cha Ufunuo ni kuufunua unabii, na si unabii wake wenyewe. Kwa hivyo, tunapata utabiri wa tukio hili tukufu katika Yoeli 2:28, 29. “Sauti, na radi, na umeme,” huashiria ufunguzi wa hukumu kwa walio hai, jinsi vile vile zinavyoashiria ufunguzi wa hukumu kwa ajili ya wafu. (Tazama Ufu. 4:5.) Tetemeko la ardhi litakuwa ishara ya tukio hilo. {SR2: 220.4}

Muhtasari Wa Mwanzo Na Mwisho Wa Mihuri

Muhuri wa kwanza hufunika kipindi chote kutoka kwa Adamu hadi kwa gharika; wa pili, kutoka kwa gharika hadi kwa Abrahamu; wa tatu, kutoka kwa Abrahamu hadi kwa Kristo; wa nne, kutoka kwa Kristo hadi mwaka 1500 B.K.; wa tano, kutoka mwaka 1500 B.K. hadi mwaka 1755 B.K.; wa sita, kutoka mwaka 1755 B.K. hadi kwa utimizo wa Ezekieli 9; wa saba, hadi kufungwa kwa muda wa rehema. {SR2: 221.1}

Walakini, mihuri, kwa maana moja ya neno, haifungi. Huendelea na kulaliana. Kwa mfano, wakazi wa dunia bado wanazidishana (Adamu — “akishinda tena apate kushinda”); vita kati ya mataifa daima vinaendelea kuongezeka, na amani imetoweka kwa nchi. Kwa hivyo, “upanga” bado u mkononi mwa mpanda farasi. Biashara bado inakua daima (“mizani”), na mateso hayajakoma bali yataamka, na kuleta taabu mfano wake haujawahi kuwapo, jinsi ilivyoelezewa na nabii Danieli. (Dan. 12:1.) Ishara za nyakati zilizo chini ya kufungwa kwa muhuri wa sita zinanena kwa sauti kuu zaidi na zaidi. Lakini muda mfupi baada ya kufungwa kwa muhuri wa saba, kila kitu duniani kitakoma kwa miaka elfu moja. {SR2: 221.2}

222

NGANO NA SHAYIRI KILA MOJA KWA DINARI

Katika somo letu la “Mihuri Saba” tulihifadhi kwa ufafanuzi wa baadaye andiko lifuatalo: “Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne ikisema, Kibaba cha ngano kwa dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja.” (Ufu. 6:6.) Tena tunageuza umakini wa msomaji kwa ukweli kwamba sauti ilitokea kwenye kiti cha enzi. (Tazama sura ya 5, aya ya 11.) Kwa hivyo, bei ya hizo nafaka imewekwa na Jaji Mkuu. {SR2: 222.1}

Lazima kiwepo kitu cha umuhimu mkubwa katika nembo hizi, kwa kuwa Yehova Mkuu Mwenyewe anazungumza. Chaweza kuwa nini? Tafsiri ya Weymouth husomeka kama ifuatavyo: “Ujira wa kutwa nzima kwa mkate, ujira wa kutwa nzima kwa mikate mitatu ya shayiri.” Weymouth hufasiri dinari kama mshahara wa siku. Tunaamini maneno ya Yesu huthibitisha hili: “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.” (Mat. 20:1, 2.) Dinari ni mshahara wa kutwa uliowekwa na mwenye nyumba wa shamba la mizabibu. {SR2: 222.2}

Kumbuka kwamba shayiri ni theluthi moja tu ya bei ya ngano; kwa maneno mengine, mmoja anaingia shambani na kukusanya kipimo kimoja tu cha ngano na kupokea malipo ya kutwa nzima, lakini yule mwingine ambaye yuafanya kazi kutwa nzima hukusanya vipimo vitatu vya shayiri, na hapokei zaidi ya ujira wa kutwa moja — “dinari moja.” Nembo hizi zina uhusiano wa karibu sana na mfano uliotolewa na Kristo. Kwa hivyo, hebu msomaji aizingatie mada hii, kwa maana hapa upo ukweli unaostahili umakini wetu. {SR2: 222.3}

“Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi, na hao nao akawaambia; Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki Nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu; na chochote kilicho sawa, ndicho mtakachopokea.” (Mat. 20:3-7.) {SR2: 222.4}

“Mwenye nyumba” katika mfano hurejelea Mungu Baba, kwa maana mfano huo utaufunua ufalme wa mbinguni.

223

[Ukurasa Mtupu]

PICHA

[Chati ya Saa za Mfano katika Kutwa]

225

Kwa hivyo, shamba la mizabibu ni ulimwengu na wale waliotumwa kufanya kazi ndani yake ni kanisa. Mfano huo hauwezi kurejelea kutwa moja halisi ya masaa kumi na mbili, ambayo Mungu ametoa wito mara tano kwa wafanyakazi katika shamba la mizabibu (ulimwengu); kwa maana hakuna kumbukumbu ambapo Mungu aliinua mashirika matano ya kanisa kwa siku moja, na kuyafanya yote yatende kazi kwa wakati mmoja. Kwa hivyo, wito katika mfano lazima utande juu ya kipindi cha historia ya dunia kuhusiana na kanisa, na kipindi hicho Yesu hukilinganisha kwa mfano wa kutwa ya saa kumi na mbili ambamo Yeye aliajiri wafanyakazi katika hafla tano tofauti. Iwapo tunaweza kutambua wakati ambao kila moja ya wito huu hutaja, basi tutaelewa kikamilifu somo hilo na wakati tunamoishi. Tutajitahidi kuthibitisha kwamba mfano huo unarejelea “ngano na shayiri,” kila moja kwa “dinari.” {SR2: 222.5}

Kumbuka kwamba mwenye nyumba alipatana bei tu na wale wa kwanza kuajiriwa. Pia, kumbuka kwamba walienda kazini asubuhi. Aliajiri wafanyakazi kwa awamu tano. Nne kati yazo zilikuwa masaa matatu mbalimbali; lakini mwito wa tano na wa mwisho ulikuwa masaa mawili tu baada ya wa nne ambao ulikuwa mwanzoni mwa saa ya kumi na moja — saa moja tu kabla ya jua kutua. {SR2: 225.1}

Majira Ya Saa Za Kale

Kuogopa kwamba wengine hawataweza kuelewa saa za kale, tunahisi ufafanuzi mfupi unaweza kuwa muhimu. Ili kuufanya uwe wa kina zaidi tunaita umakini wa msomaji kwa chati, ukurasa wa 22. Katika siku za Kristo, na hata sasa katika baadhi ya nchi, wakati hurekebishwa machweo saa kumi na mbili kamili. Karibu na ikweta, ambapo mchana na usiku ni sawa daima, jua hutua saa kumi na mbili kamili na kuchomoza saa kumi na mbili kamili. Kwa hivyo, saa sita kamili itakuwa adhuhuri katika sehemu ya nuru, kwa mujibu wa chati, na saa sita kamili katika sehemu ya giza, itakuwa usiku wa manane. Hii ndiyo aina ya saa ambayo Yesu alitumia katika mfano huo. {SR2: 225.2}

Kwa hivyo, mwito wa kwanza kwa wale ambao mwenye nyumba alipatana nao bei dinari moja kwa kutwa, ingekuwa saa kumi na mbili asubuhi — maawio. Mwito wa pili, kwa “saa ya tatu,” ni masaa matatu tu baada ya jua kuchomoza. Mwito wa tatu kwa “saa ya sita,” itakuwa adhuhuri. Awamu ya nne, kwa “saa ya tisa,” itakuwa masaa matatu baada ya saa ya adhuhuri, au saa tisa kwa saa za kisasa. Mwito wa tano, masaa mawili baadaye, kwa “saa ya kumi na moja,” itakuwa saa kumi na moja kulingana na wakati wa sasa, na saa moja tu kabla ya jua kutua. {SR2: 225.3}

Kwa maelezo ya awali ya Ufunuo 6:6, (“Kibaba cha ngano kwa dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa

226

dinari moja”), tutajitahidi kuthibitisha kwamba nembo hizo huonyesha kwa mfano wa mwenye nyumba, na Yesu kwa njia ya mfano alitazama mbele kwa maono ya Yohana. Ikiwa maelezo hayo yanafaa kikamilifu ule mfano na yale maono, kwa uwiano na kitabu cha Mungu na sheria, na somo la ukweli wa sasa litokeze kwayo, basi ni lazima tu tuupokee kama ukweli. {SR2: 225.4}

Mwito Wa Mapema Asubuhi

Mat. 20:1, 2, “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.” Yesu hangeweza kuwataja watu wengine wowote isipokuwa Israeli wa kimwili, kwa maana ndio wale ambao Mungu alipatana bei nao na kuwatuma katika shamba Lake la mizabibu — ulimwengu. Kazi yao ilijumuisha kumwakilisha Muumba au mwenye nyumba, na kutupatia Biblia. Mwandishi wa Zaburi ameifanza kumbukumbu ifuatayo ya mapatano: “Analikumbuka agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. Agano Alilofanya na Abrahamu, na uapo Wake kwa Isaka, Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, na Israeli liwe agano la milele.” (Zaburi 105:8-10.) {SR2: 226.1}

Agano hilo lilifanywa na Abrahamu, ambalo lilikuwa tu ahadi kwake na kwa uzao wake, lakini Abrahamu hakupata ahadi hiyo. “Uapo Wake kwa Isaka;” Yaani kusema, Mungu alitangaza kwa dhati kwamba Yeye atalitekeleza agano Lake. Lakini Isaka, kama baba yake, “hakupata ahadi hiyo.” Yeye “alilomthibitishia” lilo hilo “Yakobo”; yaani, Aliliamuru, akalifanya kuwa thabiti, au kulisimamisha. Agano lililofanywa na ABrahamu lilitambuliwa na Yakobo kama sheria. Lakini “kwa Israeli, liwe agano la milele.” Kwa hivyo, Israeli aliipokea ahadi hiyo. Kwa hivyo, ni Israeli ambao walioenda kufanya kazi katika shamba la mizabibu baada ya kutoka Misri. “Kama neno lile Nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri, na roho yangu inakaa kati yenu: msiogope.” (Hagai 2:5.) Isaya hunena juu ya shamba la mizabibu ambalo ndani yake lenyewe lilikuwa nembo ya ulimwengu. (Isa. 5.) Kwa hivyo, mwito wa mapema asubuhi wa mwenye nyumba kuwaita wafanyakazi katika shamba Lake la mizabibu, unahusu mwito wa Israeli kutoka Misri. Kwa nini huaitwa “mapema asubuhi?” Kwa wakati huo Musa alikuwa akiandika Biblia, ambayo ni nuru ya ulimwengu. Kwa hivyo, “mapema” alfajiri, kwa maana Maandiko yalikuwa yameanza kuandikwa. Kwa hivyo kipindi tangu Biblia ilipokuja huitwa kutwa, kwa mujibu wa mfano huo. Ambao huashiria kwamba neno la Mungu lililoandikwa ni nuru ya ulimwengu. {SR2: 226.2}

227

Mwito Wa Pili Kwa Saa Ya Tatu

“Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.” (Mat. 20:2.) Mshahara uliokubaliwa kati ya pande zote, ni ahadi ya Mungu kwa Israeli. “Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi, na hao nao akawaambia; Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki Nitawapa. Wakaenda.” (Mat. 20:3, 4) Baada ya kuuthibitisha mwito wa kwanza haitakuwa vigumu kubainisha wa pili. Kumbuka kwamba hawa hawakuwa wa kundi moja, bali “wengine,” waliokuwa hawana kazi. Iwapo sio Israeli, basi wanaweza kuwa ni Mitume na watu wa Mataifa mwanzoni mwa enzi ya Ukristo, kama ilivyoandikwa katika Matendo 13:46: “Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa, wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.” {SR2: 227.1}

Kumbuka kwamba halikuwapo agano na kundi la pili. Walienda, wakiwa na imani na “Mtu mwema” kwamba watapokea chochote kilicho sawa. Mwito wa Mataifa haukutegemea agano lolote maalum. Waliitikia, wakitumaini ahadi ya ukarimu wa Mungu kwa Israeli, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Kwa hivyo, mwito wa Mitume, na Mataifa, huwakilishwa na “mwito wa saa ya tatu.” {SR2: 227.2}

Wito Wa Saa Ya Sita Na Ya Tisa

“Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.” (Mat. 20:5.) Kila mojawapo wa wito ukiwa katika awamu, ukiendelea kwa kutwa nzima, ni dhahiri kwamba lazima uje mmoja baada ya mwingine kwa vipindi tofauti. Kwa kila tukio lazima uwepo mwito — ujumbe. Ikiwa ni hivyo, hauwezi kuwa tu mwito wa matengenezo — utiifu kwa ujumbe wa zamani. Kwa hivyo, matengenezo kupitia kwa Luther hayangezingatiwa hapa, kwa sababu yalikuwa tu uamsho kwa ujumbe uliotolewa kabla ya wakati wake. Alisema Luther “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Knox, Wesley, na Campbell hawakuweza kuingia katika huo mfano, kwa maana wao pia walikuwa na wito tu wa matengenezo (utiifu) kwa ujumbe (mafundisho) uliopelekwa kwa Mataifa — kanisa la kwanza la Kikristo. Fundisho la Roho Mtakatifu na Knox, Neema na Wesley, na Ubatizo kwa kuzamishwa na Campbell yalifundishwa na mitume. Tutawasilisha uthibitisho zaidi kutoka kwa pembe nyingine kuonyesha kwamba wana-matengenezo waliotajwa hapo juu hawajajumuishwa katika mfano huo. {SR2: 227.3}

Maadamu Israeli na Mataifa katika mwito wa kwanza na wa pili walijumuisha kanisa la Mungu katika shamba la mizabibu kisha mwito wa tatu, wa nne, na wa tano lazima iwakilishe kanisa katika shamba la mizabibu pia.

228

Tunageuza umakini wa msomaji kwa “mwanamke” mwenye taji ya nyota kumi na mbili wa Ufunuo 12:1, 6, 14. Yeye akiwa nembo ya kanisa, alipewa mabawa ya tai aruke hadi nyikani kwa siku — miaka 1260. Kwa hivyo, wakati alikuwa nyikani halingekuwapo kanisa katika shamba la mizabibu. Kipindi kirefu cha kinabii kimewekwa na kukubaliwa kuwa kipindi kuanzia mwaka 538 B.K. hadi 1798 B.K. Kwa hivyo, wakati wa safari ndefu ya “mwanamke” nyikani, hauwezi kuwapo mwito kwa wafanyakazi katika “shamba la mizabibu.” Hivyo, wito tatu wa mwisho katika mfano lazima uwe ulipata utimizo baada ya mwaka 1798, kwa wakati ambao “mwanamke” alipaswa arejee kutoka “nyikani.” Kwa hivyo swali lifuatalo linaulizwa: Iwapo kanisa (“mwanamke”) lilikuwa nyikani kati ya mwaka 538 na 1798, katika kipindi ambacho wana-matengenezo waliotajwa hapo juu walifanya kazi yao ya ajabu kuleta matengenezo kwa kutii Maandiko, je! hawakuitwa na kutumwa na Mungu? Jibu. — Hakika waliitwa na kutumwa. Hakuna shaka kwa hilo. Kazi, tabia, na kujitolea kwao hujibu lile swali. Fikiri juu ya Luther, baba wa Uprotestanti, ambaye alihatarisha maisha yake kama wale watumwa wakuu wa Mungu wa hapo zamani. Mungu, kwa mkono wa Luther, alivunja milango ya giza, akakomesha mateso ya kutisha na umwagaji damu wa watakatifu wa Aliye Juu, na kusababisha nuru katika neno Lake lililoandikwa kuangaza ndani ya mioyo ya watu. Isingekuwa kwa juhudi na bidii ya hawa wana-matengenezo wa kiungu, mwanamke (kanisa) lingekuwa nyikani hadi leo, na haungekuwapo Uprotestanti. Kwa hivyo, utumishi wao usio na ubinafsi ulivunja nguvu ya udikteta na kwa Papa kutiwa gerezani kulikikamilisha hicho kipindi kirefu cha unabii. Kwa hivyo, Mungu, kupitia utumishi wa watu hawa alikuwa amlete “mwanamke” (kanisa) kutoka nyikani na kuandaa njia ya mwito wa tatu, saa ya sita. {SR2: 227.4}

Wito katika saa ya sita, ya tisa, na ya kumi na moja, lazima ifanane na ile iliyotangulia — iliyofanzwa na ujumbe maalum, uliohubiriwa kwa mara ya kwanza — ambao ungeifanya iwe muhimu kwa kila tukio kwa ajili ya kundi lingine — “wafanyakazi.” Maumbile ya jumbe hizi pia lazima zimekuwa ulimwenguni kote, kwa maana zilitumwa katika Lake “shamba la mizabibu” — ulimwengu. Mwito wa tatu kwa hivyo, uliowakilishwa na saa ya sita, lazima ulikuja wakati fulani baada ya mwaka 1798 B.K., kwa wakati ambao yule “mwanamke” alitakiwa kurejea. Ujumbe kama huo uliwasilishwa kwa ulimwengu baada ya mwaka 1798 B.K. na kabla ya mwaka 1844 B.K. katika mahubiri na William Miller ya siku 2300 za Danieli 8:14. Kwa hivyo, ujumbe kupitia kwa Miller uliwakilishwa na kundi lililoajiriwa kwa “saa ya sita.” {SR2: 228.1}

Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya

229

vile vile.” (Mat. 20:5.) Kumbuka kwamba maneno haya yanahusa kwa karibu wito wa “saa ya sita na ya kenda,” ilhali zile wito zingine zimetenganishwa. Maana ni kwamba hizi jumbe mbili zinazowakilishwa na “saa ya sita na ya kenda,” ni za kuunganishwa kwa karibu. Kwa hivyo, mwito wa saa tisa lazima uje baada ya kazi ya Miller kufikia kikomo. Ulikuwa ukweli wa Patakatifu, na hukumu ya upelelezi iliyohubiriwa tangu mwaka 1844, ikiwa imefungashwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu wa Ufunuo 14:6-11. Kwa hivyo, Jumbe za Malaika Watatu ziliujumuisha mwito huo mwaka 1844. {SR2: 228.2}

Mwito Wa Saa Ya Kumi Na Moja

Mwito wa saa ya kumi na moja ni wa mwisho kwa kumbukumbu, na saa moja tu kabla ya jua kutua — millenia. Wakati wa kuupeleka kwa ulimwengu ni mfupi kuliko ujumbe wowote wa ulimwengu wote uliowahi kutolewa. Ingawa wakati ni mfupi sana eneo lake juu ya uso wa dunia ni pana zaidi kuliko kwa wowote. Uwasilishaji wake kwa upesi ni wa umuhimu wa hali ya juu, maana kwa huo dunia itahukumiwa. {SR2: 229.1}

Watumwa wa Mungu hawatakuwa na wakati au tumaini la masumbuko ya ulimwengu huu, kwa maana upo mji ulioandaliwa kwa ajili yao ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Kwa kuwa tuna muda wa kutosha kujiandaa kuhamishwa bila kuonja mauti, lazima tusimruhusu adui auibe wakati wetu wa thamani. Kwa sababu kazi ni kubwa, upana wake ni mkubwa sana, na umuhimu wake ni mkuu sana, Mungu amevuvia sayansi ya kisasa kubuni, na kutengeneza vifaa vya kasi ili kumaliza kazi Yake upesi. “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho: wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Wengi watatakaswa, na kufanywa weupe, na kusafika, na kujaribiwa, bali waovu watatenda maovu; wala hataelewa mtu mwovu awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” (Dan. 12:4, 10.) {SR2: 229.2}

Ushahidi katika mfano wa Kristo hufichua wazi wazi mwito mwingine wa wafanyakazi kwa shamba la mizabibu kati ya ule wa mwaka 1844, na millenia, unaoitwa, kwa saa ya kumi na moja. Hili likiwa ni kweli, mbona, kwamba lile vuguvugu lililoitwa saa ya tisa (mwaka 1844) halijaonya kanisa kimbele kwamba upo ukweli zaidi utakaofuata na ujumbe mwingine, “mwito,” utakaokuja? Je! Mungu amepuuza kutoa onyo na kuwaacha watu Wake gizani? Tunajibu swali hilo kwa kunukuu shuhuda zifuatazo: “Kwa mtazamo wa siku hiyo kuu, Neno la Mungu kwa lugha tukufu na ya kuvutia anawaita watu Wake waamke kutoka kwa uzembe wao wa kiroho, na kuutafuta uso Wake kwa toba na unyenyekevu: “Pigeni tarumbeta katika Zayuni, pigeni na kelele katika mlima Wangu mtakatifu.” — “Pambano Kuu,” uk. 311. {SR2: 229.3}

“Kisha nikamuona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana

230

nguvu na uwezo kwa ujumbe wake…. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao jinsi kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga kwa ujumbe wa malaika wa pili mwaka 1844.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 277. Tena tunasoma, “Uwe na hakika kwamba zipo jumbe zitakazokuja kutoka kwa vinywa vya wanadamu, chini ya uvuvio wa Roho Mtakatifu. “Piga kelele, usiiache … uwaonyeshe watu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 296. “Ujumbe mwingine wa onyo na maagizo ulipaswa kupeanwa kwa kanisa.” — “Pambano Kuu,” uk. 425. {SR2: 229.4}

“Unabii lazima utimizwe.” Asema Bwana: Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni hodari sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 475. “Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.” (Mal. 4:5.) Je! Mungu, kupitia “Roho ya Unabii,” na pia kwa Maandiko, hajawaonya kimbele wazi wazi watu Wake kwamba wanapaswa kuutarajia ujumbe wakati wowote? “Kuliko hapo awali, tusiombe tu kwamba watumwa waweze kutumwa katika shamba kubwa la mavuno, ila kwamba tuweze kuwa na ufahamu safi wa ukweli, ili kwamba wajumbe wa kweli watakapokuja, tuweze kuupokea ujumbe na kumheshimu mjumbe.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 6, uk. 420. {SR2: 230.1}

Iwapo onyo limetolewa, kwa nini watu kutokea kwa mimbari wamefumba macho yao kwa Neno la Aliye Juu, na kufunua vinywa vyao kunena hadithi kwa kongamano lao, kwa kutangaza kwamba wana ukweli wote na hawahitaji ujumbe wala nabii? Je! Uongo na unafiki huu haujafungulia njia udanganyifu wa jumla kanisani kwa kuimarisha imani yao kwamba hawana haja ya kitu na wako njiani kwenda mbinguni? Fikiria kuchukia bila sababu na usalama wa uongo ambao ujumbe utalazimika kupitia. Fikiria kule kupoteza maisha iwapo watu wataupokea uamuzi wa viongozi. Je! Mtego wa kutisha sana kama huo wa udanganyifu haujawanasa watu wa Mungu katika kila vuguvugu lililoitwa? Imani ndani ya viongozi, na kuyapokea maamuzi yao bila uchunguzi imewadanganya watu katika kila kizazi. Ni nini kitakachogeuza mkondo sasa? Wazo la kutisha kama nini na jukumu kubwa lililoje! Mungu awasaidie watu Wake watafute nuru na ukweli kwa ajili yao wenyewe, na juhudi yao iweze kudai maelezo na hesabu ya mambo haya. {SR2: 230.2}

Ujumbe ni upi? Ujumbe wa saa ya kumi na moja sio

231

mwimgine isipokuwa Ufunuo 18 — kilio kikuu cha Malaika wa Tatu. Kunukuu “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 59: “Ujumbe uu huu [Malaika wa Tatu] utatangazwa mara ya pili. ‘Na baada ya mambo hayo nalimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye nguvu kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.’ Ujumbe huu ni wa mwisho ambao utawahi kupeanwa kwa ulimwengu, na utatimiza kazi yake.” — “Pambano Kuu,” uk. 390. {SR2: 230.3}

“Kwa hivyo ujumbe wa malaika wa tatu utatangazwa. Kadiri wakati unapokuja ili utolewe kwa nguvu kubwa, Bwana atafanya kazi kupitia vyombo vya unyenyekevu, akiongoza nia za wale wanaojitoa wakfu kwa utumishi Wake. Wafanyakazi watawezeshwa kuhitimu badala yake kwa kutiwa mafuta na Roho Wake, kuliko kwa mafunzo ya nje ya taasisi za uandishi [vitabu]. Watu wa imani na maombi watahimizwa kusonga mbele kwa bidii takatifu, wakitangaza maneno ambayo Mungu huwapatia. Dhambi za Babeli zitawekwa wazi. Matokeo ya kutisha ya kutekeleza sheria za maadhimisho ya kanisa kwa mamlaka ya serikali, kupenyezwa kwa Umizimu, maendeleo ya siri lakini ya haraka ya nguvu ya papa, — yote yatafunuliwa wazi. Kwa maonyo haya mazito watu watachochewa. Maelfu kwa maelfu watasikiza ambao hawajawahi kusikia maneno kama haya. Kwa mshangao wanasikia ushuhuda kwamba Babeli ni kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu ya kukataa ukweli uliotumwa kwalo kutoka mbinguni. Kadiri watu wanawaendea walimu wao wa zamani na swali la kutaka kujua, Je! mambo haya ni kweli? Wachungaji wanawasilisha hadithi, wanatabiri mambo laini, ili kutuliza hofu yao, na kutuliza dhamiri iliyoamshwa. Lakini kwa kuwa wengi wanakataa kuridhishwa na mamlaka matupu ya wanadamu, na kudai bayana ‘Bwana asema hivi,’ ule ukasisi maarufu, kama Mafarisayo wa zamani, waliojazwa hasira kadiri mamlaka yao yanapohojiwa, wataukemea ujumbe huo kama wa Shetani, na kuchochea umati wa watu wanaopenda dhambi kuwatukana na kuwatesa wale wanaoutangaza.” — Kimenukuliwa, uk. 606, 607. {SR2: 231.1}

Mwito wa saa ya kumi na moja, kwa uhalisi, ni sawa na ule wa saa ya tisa. Mwito wa saa ya tisa unarudiwa na nyongeza ya kutajwa ufisadi makanisani; pia unaongezewa nuru na nguvu. {SR2: 231.2}

Mbona Mmesimama Hapa Bila Kazi?

Wafanyakazi waliajiriwa kutoka “sokoni.” Soko lazima limaanishe kanisa ambalo Mungu huwaita wafanyakazi Wake kwa utumishi. Kumbuka wale walioajiriwa katika kila tukio walikuwa bila kazi. Maana yake ni kwamba kila ujumbe ambao umewahi kuja ulimwenguni mwetu, haukuja kupitia kwa wale walio katika nyadhifa za juu kanisani. Ulipelekwa na watu wanyenyekevu, ambao huduma zao uongozi wa kanisa

232

ulifikiri haukuzihitaji. Katika kila kisa ujumbe umekataliwa na wakuu katika kanisa. Maki swali lililoulizwa na mwenye nyumba, “Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?” Maana ni kwamba walipaswa kuwa kazini. Wakamwambia “Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri.” Wakati uongozi wa kanisa umepotoka, kazi inadhibitiwa na daraja fulani, na kizuizi cha marufuku kuwekwa kwa wengine wote. Kwa hivyo, wale haswa ambao Mungu hutaka kuwatumia husukumwa kando na kusalia bila kazi. {SR2: 231.3}.

Wafanyakazi walioajiriwa na uongozi kama huo huchaguliwa kutoka kwa mtazamo wa elimu ya kiufundi kama mtihani wa kufuzu, badala ya maarifa ya Kibiblia, kujitoa wakfu, na utiifu kamili kwa ukweli wote. Mazoea kama hayo ni kinyume na agizo la Biblia. Tunanukuu: “Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, chonjo, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mvumilivu, asiyegombana, asiye mchoyo, mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (Yaani mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)” (1 Timotheo 3:2-5.) Mitume katika kuwachagua watu kwa ofisi takatifu, walisema: “Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho Mtakatifu na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili.” (Matendo 6:3.) {SR2: 232.1}

Musa alitumia miaka arobaini katika shule ya Kristo. Alipokuwa akichunga kondoo alibadilisha mafunzo yake ya Misri kwa maarifa na hekima ya Mkuu Mimi Niko. Kwa hivyo alifanywa afae kuwaongoza watu Wake kutoka Misri. Paulo alionyeshwa kwamba hekima yake ya kidunia inayopatikana katika shule ya wanadamu ilikuwa ya kudhuru, na isiyofaa katika kazi ya Kristo, kwa hivyo huyo mtume alitangaza: “Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu, ila Yesu Kristo, Aliyesulubiwa. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu.” (1 Kor. 2:1, 2, 4.) Paulo alimaanisha kwamba alikuwa ameamua kuhubiri Biblia na Biblia pekee, ambayo humfunua Kristo na Yeye aliyesulubiwa. Alihubiri kwa nguvu ya Roho wa Mungu, na sio kwa hekima ya wanadamu. Kwa hivyo, mtume msomi alijiinamisha hadi kwa kiwango cha wavuvi wasiojua katika maarifa ya kibinadamu, wakati uo huo akipanda juu na wale kumi na mmoja kwa hekima ya Mungu, ambayo kwa kulinganisha heshima ya kidunia na ukuu wa kibinadamu huzama katika uduni. Kwa hivyo, lilio takatifu haliwezi kuchanganywa na la kawaida. {SR2: 232.2}

Mwenye nyumba akasema, “Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu; na

233

iliyo haki, ndiyo mtakayopokea.” Mungu huwaomba wanaume na wanawake wainuke na kwenda kufanya kazi katika shamba la mizabibu, wakitumaini katika thamani ya Neno Lake. “Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu, wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo: maana mtenda kazi astahili posho lake. Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka.” (Mat. 10:9-11.) “Akawauliza, Je! Hapo Nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!” (Luka 22:35.) {SR2: 232.3}

Maki hoja ifuatayo kwa uangalifu: Kuanzia saa ya tisa mwaka 1844, hadi kwa saa ya kumi na mbili, au kufungwa kwa muda wa rehema, yapo masaa matatu kamili tu. Idadi ya masaa huashiria kwa nembo kwamba upo wakati wa kutosha wa muda wa rehema kutoka mwaka 1844 hadi mwisho, kwa vuguvugu moja — masaa matatu. Andiko la Ufunuo 10:6 hutumika hapa: “Hapatakuwa na wakati.” Kila vuguvugu ambalo Mungu amelianzisha tangu mwanzo wa ulimwengu, lilikwenda kwa umbali huo, na Alipotuma ujumbe, au nuru mpya juu ya Neno Lake, viongozi waliikataa, na hitaji lilizalisha vuguvugu jipya. {SR2: 233.1}

Iwapo viongozi katika kanisa la Mungu kwa wakati wa sasa wataweza kuupokea mwito wa saa ya kumi na moja, litakuwa jambo lisilo la kawaida. Lakini wakiukataa, Mungu hawezi kuanzisha vuguvugu jipya, kwa maana “hapatakuwa na wakati.” Mavuguvugu mapya kwa kawaida huanza na watu wachache na huhitaji miaka kuendeleza, na baada ya muda ufisadi huingia. Kwa hivyo, Yeye hataweza kumaliza kazi Yake hapa duniani kwa mpango kama huo. Maneno ya Bwana yatangaza kwa mfano kwamba uongozi katika vuguvugu lililoitwa mwaka 1844 utaukataa ujumbe wa saa ya kumi na moja, kwa maana Yeye husema wale ambao walikuwa karibu kuajiriwa, walikuwa “wamesimama bila kazi”; yaani, hawakuwa wale waliokuwa kazini ambao aliajiri. {SR2: 233.2}

Ikiwa hakuna wakati wa vuguvugu jipya, basi lipo suluhisho moja tu la shida yenye utata, nalo ni kutenganisha “ngano” kutoka kati ya “magugu” kwa kulipiga daraja ambalo linadhibiti kazi na kuwaweka watu wa Mungu katika kifungo cha dhambi. Kwa hivyo, maadui wa Mungu wanaondolewa njiani na watu watano wa Ezekieli 9. Mada hii imewekwa wazi katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1. {SR2: 233.3}

Wa Mwisho Watakuwa Wa Kwanza Na Wa Kwanza Watakuwa Wa Mwisho

Tukirejea kwa andiko letu: “Kibaba cha ngano kwa dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja.” (Ufu. 6:6.) Kwa nini ngano imetajwa kwanza, na shayiri mwisho? Mbona isiwe

234

kinyume? Kwa nini shayiri vibaba vitatu zaidi kwa dinari moja dhidi ya kibaba kimoja cha ngano? Au mbona isiwe kinyume? Maandiko ni makamilifu na hakuna kasoro inayoweza kupatikana ndani yake. Kwa hivyo, lazima iwepo sababu ya utaratibu huu wa mpangilio, na pia kiasi cha kila nafaka. Shayiri hukomaa mapema zaidi kuliko ngano. Kwa hivyo, wale walioajiriwa kwanza lazima wawakilishwe na shayiri, vinginevyo nembo hiyo haiwezi kuwa kamilifu. Shayiri, basi, huwakilisha taifa la Kiyahudi, kwa waliajiriwa kwanza. Kwa kawaida ngano lazima iwakilishe wale walioitwa saa ya kumi na moja. Ni ajabu jinsi Maandiko yalivyo makamilifu. {SR2: 233.4}

Mbona ni aina mbili tu za nafaka zilizoletwa kwa mtazamo? Kwa nini sio tano? Nafaka mbili hizo zinatosha kutoa kielezi cha lile wazo na kulitatua somo. Lakini sababu kuu ya nafaka mbili pekee ni kuvuta umakini kwa mwito wa kwanza na wa mwisho, kwa sababu mtajo umefanywa wa Israeli wawili tu; yaani, Israeli wa kimwili (uzao wa Abrahamu), na Israeli wa kiroho (watu 144,000). Lakini kusudi la somo ni kwa wale wa mwisho, ambao waliajiriwa saa ya kumi na moja, kwa maana ukweli wa mfano huo haujawahi kueleweka kwa kundi lingine lolote. {SR2: 234.1}

Kumbuka kwamba wale wa kwanza kuajiriwa walifanya kazi kutwa nzima, bali wale walioajiriwa mwisho walifanya kazi saa moja tu. Kwa sababu hiyo sauti ilisema, “vibaba vitatu vya shayiri” dhidi ya “kibaba kimoja cha ngano” kwa dinari — ujira wa siku moja. Muda kati ya kila mwito ulikuwa masaa matatu. “vibaba” huashiria masaa ya mfano yanayotumika kazini. Vipindi vya masaa matatu kati ya kila mwito ni nembo ya muda kamili wa wakati ulioruhusiwa kwa kila vuguvugu, au ujumbe, bila maana maalum kuhusu idadi ya miaka. Wale walioitwa mwisho, walifanya kazi kwa saa moja tu, lakini pia walipokea sawa sawa. Ukarimu wa yule Mtu Mwema humaanisha kwamba watumwa wote wa Mungu wanapewa thawabu sawa, sio kwa kadiri ya matendo yao, bali kulingana na ukarimu wa mwenye nyumba. {SR2: 234.2}

Sasa swali mbona sauti kutokea kwa kiti cha enzi ilisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa dinari moja,” kwanza, na “vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja,” mwisho, litajibiwa. Kunena kibinadamu ilipaswa kuwa kinyume, maana kwa ngano umewakilishwa ujumbe wa mwisho (saa ya kumi na moja) na kwa shayiri wa kwanza (mapema asubuhi — Israeli wakitoka Misri). Laiti sauti ingaligeuza hesabu ya hizo nafaka, lingekuwa kosa, kwa sababu Yesu alisema: “Kulipokuchwa, yule Bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea

235

kila mtu dinari. Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mtu mwema mwenye nyumba, wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. Naye akamjibu mmoja wao akamwambia Rafiki, Sikudhulumu: hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako uende zako: Napenda kumpa huyu wa mwisho, sawa na wewe. Si halali Yangu kutumia vilivyo vyangu kama Nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu, kwa sababu ya Mimi kuwa mwema? Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho: kwa maanawengi wameitwa, bali wateule ni wachache.” (Mat. 20:8-16.) Kwa hivyo kibaba cha ngano kwa dinari moja, kwanza, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari, mwisho. Wale walionung’unika huwakilisha sehemu hiyo ya taifa la Kiyahudi ambao hawakustahili, na kirai, “Rafiki, Sikudhulumu …. Chukua iliyo yako uende zako,” humaanisha kukataliwa kwa hilo taifa. {SR2: 234.3}

Wape Ujira Wao

Kumbuka kwamba wale walioajiriwa mwisho walilipwa kwanza, na wa kwanza, walilipwa mwisho. Kwa sababu wote walizingatiwa sawa, wale walioajiriwa kwanza walinung’unika, ingawa walilipwa ujira wote. Tendo lao la dharau humaanisha kwamba taifa la Kiyahudi halikustahili ujira wao, na yule Mtu Mwema akawaambia, “Chukua iliyo yako uende zako.” Maadamu Israeli wa kale huwakilishwa na mwito wa kwanza, kama ilivyoelezewa hapo awali, kwa wao maneno hayo yanawahusu, na kwa sababu wao ndio waliolalamika, huthibitisha mfano huo kuwa sahihi. {SR2: 235.1}

Mbona wa kwanza walilipwa mwisho, na wa mwisho walilipwa kwanza? Jibu. — Ujira ambao watumwa wa Mungu hupokea ni uzima wa milele, na huwakilishwa na dinari. Kwa hivyo, wale ambao wamepewa hakikisho la kuishi milele, ni wale walioajiriwa mwisho, na kwa mujibu wa huo mfano, lilikuwa kundi liloitwa saa kumi na moja. Ni wale ambao wametiwa alama au kutiwa muhuri na yule mtu aliye na kidau cha wino wa mwandishi wa Ezekieli 9, au kama Yohana anavyomwita, malaika aliye na muhuri wa Mungu; naye akatia muhuri, au kuwatia alama, watu 144,000. (Tazama Ufu. 7.) Kundi hili tukufu ndilo la kwanza ambalo linapewa hakikisho la kutokuonja mauti kamwe. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 22-24.) Kwa hivyo wanalipwa kwanza lakini wale ambao waliitwa mapema asubuhi (Israeli wa kimwili) watafufuliwa (wenye haki) Kristo atakapokuja katika mawingu, kwa wakati ambao watapewa kutokufa. “Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.” Kwa sababu hii, wale waliotiwa muhuri na kuokolewa na Ujumbe wa Malaika wa Tatu tangu mwaka 1844, wanafufuliwa katika ufufuo maalum kabla ya Kristo kuja. (Tazama Dan. 12:2; “Maandishi ya Awali,” uk. 285.) {SR2: 235.2}

236

Mbona Mapema Asubuhi?

Ushahidi ulioletwa unaonyesha kwamba wito (jumbe) kabla Israeli kutoka Misri hazikujumuishwa katika mfano huo, na ya kwamba mwito wa Israeli ulikuwa “mapema asubuhi.” Yesu amegawanya historia ya kanisa katika mfano huu kwa sehemu mbili sawa za masaa kumi na mbili kila moja. Katika huo Yeye hutaja tu sehemu inayoitwa mchana, — kipindi cha Biblia. “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.” (Yohana 11:9.) Kwa hivyo, kipindi kabla ya Biblia kuja huitwa usiku. Si kwamba watu wa Mungu waliachwa gizani mintarafu neno Lake, lakini kwamba lilipokezwa kwa njia ya kinywa kutoka kwa baba hadi kwa mwana, ilhali neno lililoandikwa ni ufunuo wa moja kwa moja — nuru. Kwa hivyo Ameionyesha historia ya kanisa Lake kwa saa 24 za kidude cha saa. Tunaweza kuelewa vyema uchambuzi huu kwa muhtasari mfupi tunapofuata chati kwa ukurasa wa 224. {SR2: 236.1}

Kuna wito mara tano pekee katika mfano ule; wa Kwanza, wale walioitwa mapema — Israeli kutoka Misri; wa Pili, wale ambao walikwenda kufanya kazi katika shamba la mizabibu saa ya tatu — kanisa la kwanza la Kikristo; wa Tatu, mwito wa saa ya sita — William Miller na wafanyakazi wenzake; wa Nne, mwito wa saa ya tisa — malaika wa Tatu katika kilio chake cha kwanza baada ya mwaka 1844; wa Tano, mwito wa saa ya kumi na moja — Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu. Kwa sababu namba “saba” hutumika katika kila mojawapo wa matendo ya Mungu yaliyokamilika kumaanisha ukamilifu, lazima ilikuwapo wito mara mbili kama hiyo kabla ya wakati wa Israeli, vinginevyo mfano huo ungeonyesha kutokamilika katika kutangaza injili. “Na Henoko pia, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana yuaja na makumi maelfu ya watakatifu Wake.” (Yuda 14.) Kwa kuwa Henoko alikuwa na ujumbe wa ulimwengu wote wa kuja kwa Bwana, ujumbe wake ndio mwito wa kwanza. Mwito wa Nuhu ni wa pili kutoka kwa uumbaji. Kwa hivyo, “saba” kwa jumla, kumaanisha ukamilifu, kumaliza, mwisho wa injili. {SR2: 236.2}

Mavuguvugu Saba Ya Dunia Yote

Hadi hapa tumekuwa tukirejelea wito pekee, lakini sasa tunaelekeza umakini wetu kwa mavuguvugu. Mwanzo wa vuguvugu la Kwanza ni kutoka kwa wakati Adamu alitenda dhambi hadi kwa ujumbe wa Henoko, la Pili, kutoka kwa Henoko hadi kwa Nuhu; la Tatu, kutoka kwa Nuhu hadi kwa Musa; la Nne, kutoka kwa Musa hadi kwa mitume, la tano, kutoka kwa mitume hadi kwa Miller; la Sita, kutoka kwa Miller hadi kwa E.G. White; la Saba, kutoka kwa E.G. White hadi mwisho. Kutoka kwa mwito wa mwisho hadi kikomo, ikiwa ni saa moja tu, huthibitisha kwamba hakuna wakati wa vuguvugu jipya. Na

237

vuguvugu jipya lingeitupa namba saba nje ya maana yake. Kwa hivyo, vuguvugu la zamani lazima litakaswe na kusonga mbele. {SR2: 236.3}

Wakati unaoruhusiwa kwa kila vuguvugu umewekwa alama kwa kidude cha saa ya Mungu kama masaa matatu. Saa tatu za kwanza kwenye kidude huonyesha kutoka kwa uumbaji hadi kwa anguko la Adamu; kwa hivyo huacha masaa ishirini na moja tu ya kimfano kwa muda wa rehema kwa wanadamu. Nyakati saba mara tatu sawa na ishirini na moja, kwa hivyo, tunayo sababu nyingine kwa nini malaika alisema, “Hapatakuwa na wakati.” {SR2: 237.1}

Sababu Mbona Masaa Matatu Kwa Kila Vuguvugu

Ukweli ufuatao unathibitisha zaidi kwamba historia ya kanisa katika mfano huu inawakilishwa na kidude cha saa ishirini na nne. Iwapo mwito ulikuja kwa Israeli mapema asubuhi, saa ya kumi na mbili, na siku ikafungwa saa ya kumi na mbili ifuatayo, inayoitwa mchana, kwa sababu neno la Mungu lililoandikwa lilikuwa hai kutoa nuru kwa kanisa, basi kipindi kilichotangulia Biblia kimfano huitwa usiku. {SR2: 237.2}

Wengine wanaweza kuhoji ushahidi wa kuruhusu masaa matatu kwa kila tukio — tangu uumbaji hadi anguko la Adamu, na tena hadi kwa Henoko na Nuhu. Iwapo Mungu alifanya kazi kwa ratiba ya masaa matatu na kusulubishwa kwa Yesu (angalia chati kwa ukurasa wa 22), na sheria iyo hiyo ilifuatwa katika kipindi kinachoitwa “mchana,” basi hakika Yeye hangefuata kanuni nyingine katika kipindi kinachoitwa “usiku.” Sababu ya Yeye kufuata kanuni hiyo ni kuwasilisha kwa kanisa Lake wakati halisi wa historia yake kwa vipindi. {SR2: 237.3}

Hebu tuchunguze ushahidi kutokea kona nyingine. Mtu wa kwanza aliyetenda dhambi anaitwa Adamu wa kwanza. Sasa kitazame kidude cha saa; kutoka saa ya tatu katika sehemu ya giza (anguko la Adamu) mkabala na saa ya tatu katika sehemu ya nuru, na tunamwona Adamu wa pili (Kristo aliyesulubishwa). Tena, angalia saa ya sita katika sehemu ya giza ya kidude cha saa (Henoko akitabiri kuhusu kuja kwa Kristo) mkabala na saa ya sita ya sehemu ya nuru, na hapo tunamwona Miller pia akitabiri juu ya tukio lilo hilo (kuja kwa Kristo). Hii ni mojawapo wa sababu mbona Mungu alimruhusu Miller kutangaza kuja kwa Kristo mwaka 1844. Sasa itazame saa ya kenda, Nuhu akitabiri mwisho wa dunia katika kizazi chake, mkabala na saa ya tisa katika sehemu ya nuru, tunamwona E.G. White akitabiri juu ya mwisho wa dunia katika kizazi hiki. (Na hapo ndipo kizazi hiki kilianzia.) Na kwa saa ya kumi na mbili (Israeli wa kimwili wakitoka Misri) mkabala na saa ya kumi na mbili (machweo), tunaona Israeli wa Kiroho (bidhaa iliyokamilika) wakitoka duniani (Misri.) Kwa hivyo, hakuna swali ila anguko la Adamu, unabii wa Henoko, na Nuhu, matukio hayo yalikuja kwa hizo saa kama yanavyoonyeshwa kwa chati. {SR2: 237.4}

238

Hapa tunaona mfano mwingine. Ukweli wa Mungu kwa dunia kabla ya Biblia kuja, unafanana na ukweli Wake katika wakati wa Biblia, kuonyesha kwamba Mungu ana ukweli mmoja tu, Kristo mmoja, na injili moja katika vizazi vyote. Kwa hivyo, ile dhana iliyofundishwa na wanaojidai eti ni wachungaji wa injili kwamba Mungu alikuwa na njia moja ya kuwaokoa watu kabla ya Biblia kuwapo, nyingine wakati wa Agano la Kale na wazawa wa Abrahamu, na nyingine kwa Agano Jipya na kwa Mataifa, n.k., ni udanganyifu wa Ibilisi na hakuna ukweli ndani yake. Sio tu mambo yaliyoandikwa huuthibitisha ukweli na kufichua makosa lakini hata kufikiri kwa kawaida hutuambia haiwezi kuwapo haki katika njia kama hiyo inayobadilika-badilika ya wokovu — “Kwa kuwa mimi ni Bwana, sina kigeugeu.” {SR2: 238.1}

Saa ya kumi na mbili kwa kidude cha saa, upande wa kushoto, huwakilisha maawio na wa kulia, machweo; saa ya sita katika sehemu ya nuru, adhuhuri, na sita sehemu ya giza, usiku wa manane. Ujumbe kwa saa ya sita na Miller unaitwa kilio cha usiku wa manane (tazama “Maandishi ya Awali, uk. 277.) kwa sababu inalingana na ile ya Henoko. Yesu alisema: “Lakini usiku wa manane, pakawa na kilio, Angalia, bwana arusi yuaja: tokeni mwende kumlaki.” (Mat. 25:6.) Saa ya sita katika sehemu ya nuru husimama pia kama adhuhuri wakati jua likiwa katika nguvu zake kamili. Biblia ilianza kuchomoza kwa saa ya kumi na mbili na wakati ujumbe kupitia kwa Miller ulipohubiriwa, uliowakilishwa na mwito wa saa ya sita, yote Agano la Kale na Jipya yalikuwa yamekusanywa na kuchapishwa; hivyo pia humaanisha adhuhuri. {SR2: 238.2}

Ujumbe uliotangazwa na Henoko ulikuwa unabii ukitazama mbele hadi kwa mwaka 1844 wakati Yesu aliingia patakatifu mno pamoja na watakatifu Wake kwa hukumu ya upelelezi. Kwa hivyo, mahubiri ya Miller yalikuwa utimilifu wa unabii wa Henoko. Kwa hivyo unaitwa Kilio cha Usiku wa Manane. Kwa sababu mada ya hukumu haikueleweka hadi baada ya kikao chake kuanza, haikuwezekana Miller kufanya matumizi sahihi kwa lile tukio lililotarajiwa wakati huo. Kumbuka usemi wa kisarufi ambao Kristo alitumia: “Pakawa na kilio.” Yeye hutumia wakati uliopita, kuthibitisha ukweli kwamba maana halisi ya ujumbe wa Miller ingeeleweka baada ya mwito huo kufanywa. “Palikuwa,” Yeye alisema, badala ya patakuwa na “kilio.” {SR2: 238.3}

Ushahidi katika uchambuzi huu huthibitisha uungu wa Kristo, na nguvu Yake katika maono hata katika maelezo madogo kabisa, ya zamani, ya sasa na ya baadaye. Ikiwa ukweli kama huu, ulio wazi na rahisi, thabiti kabisa na hakika katika kufunua maajabu ya Maandiko hauwezi kuubadilisha moyo wa msomaji basi tunahitimisha kwamba hakuna kitu kikubwa zaidi kitakachokuwa cha thamani yoyote. Iwapo wafu watafufuka kutoka kaburini, au hata ikiwa malaika atashuka kutoka mbinguni, kundi hilo lingesema nguvu hiyo ni ya Ibilisi. Mtunga Zaburi huelezea Ukuu wa Neno la Mungu kwa lugha ifuatayo:

239

“Nitasujudu nikilikabili hekalu Lako takatifu na nitalishukuru jina Lako kwa ajili ya fadhili Zako na ukweli Wako: kwa maana Umelikuza neno Lako kuliko jina Lako lote.” (Zab. 138:2.) Yesu alisema: “Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa, hata mtu akifufuka katika wafu.” (Luka 16:31.) {SR2: 238.4}

Saa moja ya Ufunuo 17:12, ambayo ndani ya wakati wake zile pembe za mnyama mwekundu sana zilipokea mamlaka kama Wafalme, ni kipindi kutoka kwa mwito wa saa ya kumi na moja hadi mwisho wa historia ya dunia — kutoka kwa saa ya kumi na moja hadi saa ya kumi na mbili ya mfano. {SR2: 239.1}

240

MBONA KOSA LA MILLER; GHARIKA NI NINI KWETU?

Alisema Henoko: “Angalia, Bwana yuaja na kumi maelfu ya Watakatifu Wake.” (Yuda 14.) Unabii huu wa Henoko sio kuja mara ya pili kwa Kristo mawinguni, kwa maana Yeye atakapotokea katika utukufu Haji “pamoja na watakatifu Wake,” ila badala yake kuwachukua watakatifu wake. Wala hakutakuwa kuja Kwake pamoja na watakatifu Wake upande wa pili wa millenia, kwa maana katika hali kama hiyo haungeweza kuwa ujumbe kwa dunia kabla ya gharika. Ingekuwa isivyofaa na bila lengo, au funzo kwa watu hao, iwapo Henoko angalihubiria ulimwengu kuja kwa Kristo mara ya tatu kabla ya kuhubiri kuja Kwake mara ya pili kwa watakatifu Wake. Nini basi? {SR2: 240.1}

Henoko alitabiri kuhusu ujio wa Bwana kwa hekalu Lake mahali patakatifu mno patakatifu katika hekalu la mbinguni pamoja na watakatifu Wake kwa mfano (sio kimwili) kwa hukumu ya upelelezi ili kuzifuta dhambi zao, ni tukio ambalo nabii Malaki hurejelea: “Angalieni, Nitamtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu: Naye Bwana Mnayemtafuta, atalijilia hekalu Lake ghafula, naam yule mjumbe wa agano, Mnayemfurahia: angalieni Atakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo: Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa: Naye atawatakasa wana wa Lawi, Atawasafisha kama dhahabu na fedha, nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” (Mal. 3:1-3.) “Angalieni, Nitamtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu, naam yule mjumbe wa agano.” Mjumbe sio Bwana Mwenyewe, lakini kumbuka kwamba yeye ndiye atakayemtengenezea Bwana njia. Anaitwa “yule mjumbe wa agano” (makubaliano au ahadi). Kwa sababu Maandiko hayo ni ya siku za mwisho, huyu mjumbe wa ahadi hawezi kuwa mwingine isipokuwa yule ambaye Bwana ameahidi: “Angalieni, Nitawatumia Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.” (Mal. 4:5.) {SR2: 240.2}

Bwana alikuja kwa hekalu Lake patakatifu mno mwaka 1844 kwa hukumu ya wafu, ambayo ilikuwa utimizo wa Danieli 7:9, 10. Malaki huzungumzia hukumu kwa walio hai, ambayo ni ya matukio yale yale (hukumu). Kwa maana nabii husema: “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama

241

atakapoonekana Yeye? Kwa maana … ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa: Naye atawatakasa wana wa Lawi, Atawasafisha kama dhahabu na fedha, nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” (Mal. 3:2, 3.) Kwa sababu wafu hawawezi kutakaswa, au kutoa sadaka, ni dhahiri kwamba ni utakaso wa kanisa, kwa maana “Atawatakasa wana wa Lawi” — makuhani — watu 144,000. Isitoshe Bwana husema: “Nitamtuma mjumbe Wangu,” na kwa sababu hakuna mjumbe anayeweza kutumwa kwa wafu, lazima uwe ujumbe kwa walio hai. {SR2: 240.3}

Tukirejea kwa unabii wa Henoko: “Angalia, Bwana yuaja na kumi maelfu ya Watakatifu Wake.” Neno “maelfu” likiwa katika wingi, halionyeshi idadi ya watakatifu wanaokuja pamoja Naye. Lakini ikiwa neno “kumi maelfu,” halina ufafanuzi wa namba wa aina yoyote, basi neno “kumi,” lingekuwa marudio ya bure na ya kigeni kwa Maandiko. Kwa hivyo, lazima tutafute ufafanuzi wa nembo ya neno hilo. Namba “kumi,” ina maana sawa na “wanawali kumi” wa Mathayo 25, kumaanisha ulimwengu wote (kanisa kama kundi). Kwa hivyo kimfano huwafunga watakatifu kwa pamoja — wote waliookolewa kutoka kwa Adamu hadi mwisho. Kwa hivyo, unabii wa Henoko ulianza kutimizwa mwaka 1844, wakati huo “Bwana alikuja na majina na kumbukumbu za wale ambao wamelala kaburini, na wakati upelelezi wa wafu unapokamilika, kisha Anakuja na majina ya watakatifu walio hai. Mwanzo na watu 144,000, na baadaye “umati mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha.” (Ufu. 7:9.) Kwa hivyo, utimizo kamili wa maneno ya kinabii, “Angalia, Bwana yuaja na kumi maelfu ya Watakatifu Wake,” yatatimizwa mwishoni mwa muda wa rehema utakapofungwa. Kuhusu ujio huu wa Bwana (kwa ajili ya wafu) William Miller alikuwa mjumbe, na ujumbe wa Eliya nabii — mjumbe wa agano — ndiye mtangulizi wa kuja Kwake pamoja na watakatifu walio hai, wote wa tukio lilo hilo — hukumu. {SR2: 241.1}

Katika “Pambano Kuu,” uk. 426, ikitaja ujio wa pili wa Kristo, sehemu ya Yuda 14 imenukuliwa na ya Yuda 15, kukamilisha sentensi kwa neno “yuaja;” sehemu ile ya aya “na kumi maelfu ya watakatifu Wake,” hutumika kwa ujio Wake hekaluni mbele ya “Mzee wa siku.” Neno “yuaja” kutoka Yuda 14, na Yuda 15, hutumika kwa ujio Wake wa pili, sawa na Zekaria 13:6. Aya ya (6) hutumika kwa ujio wa pili wa Kristo na aya ya (7) kwa kusulubishwa Kwake. Pia kumbuka kwamba yale maelezo ni kwa Yuda 15, kuhusiana na hukumu juu ya waovu na si kwa watakatifu. {SR2: 241.2}

Kweli, Henoko alitabiri juu ya siku ya upatanisho ya uakisi (wakati wetu), lakini ikiwa ujumbe wake haukuwa na maana kwa dunia

242

kabla ya gharika, basi kuhubiri kwake kungekuwa kwa wonyesho tu. Kwa hivyo, lililo la kweli kwa ujumbe wake sasa, pia lilikuwa la kweli kwa walioishi kabla ya gharika; na iwapo taarifa hii ni sahihi, lazima uwepo ulinganifu mkamilifu wa dunia wakati huo, na dunia sasa. Kuhubiri kwa Henoko kulifuatwa na kuhubiri kwa Nuhu. Wakati dunia ya zamani haikuwa na ufahamu kamili kuhusu kuja kwa Mwokozi, wao pia, kama kizazi cha sasa, walikuwa wakimtafuta na kumngojea Yeye ambaye atawakomboa kutoka kwa dhambi na mauti, na kuwarejesha katika bustani ya Edeni. Kwa midomo yao walikiri hamu kuu kwa ajili Yake Ambaye walitarajia kumwona katika utukufu Wake, lakini mwenendo wao dhidi ya habari njema katika ujumbe kupitia kwa Henoko: “Angalia Bwana yuaja,” ulifichua wazi lililokuwa mioyoni mwao. Kama ilivyotarajiwa kwa ujumla kwamba Bwana angekuja wakati huo, na ya kwamba Henoko hakuwa amepewa nuru kuhusu namna ya kuja Kwake, aliutangaza ujumbe wake kwa upatano Kamili na mtazamo maarufu wa kizazi hicho. Sasa swali ni, je! nini kiliwafanya waukatae ujumbe almradi utangazwaji wake ulikuwa unapatana na matarajio yao na hawangeweza kuupinga ukweli wake? Swali hili linaweza kujibiwa kwa uzoefu wa Yohana Mbatizaji. {SR2: 241.3}

“Yohana hakuelewa kabisa asili ya ufalme wa Masihi. Alitazamia Israeli kukombolewa kutoka kwa maadui zake wa kitaifa; lakini ule ujio wa Mfalme katika haki, na kusimamisha Israeli kama taifa takatifu, lilikuwa lengo kuu la tumaini lake.” — “Tumaini la Vizazi Vyote,” uk. 103. {SR2: 242.1}

Lingalikuwa jambo lisilo la busara na dhuluma kwa watu wateule wa Mungu iwapo Angewaacha gizani kuhusu wakati wa tukio muhimu zaidi katika historia yote ya kanisa — ujio wa Kristo. Sehemu hiyo ya kipindi kirefu cha unabii cha siku (miaka) 2300 ya Danieli 8:14, ambayo ilikuwa inalihusu taifa la Kiyahudi; yaani, majuma sabini, au miaka 490, walielewa vyema, kwa maana: “Ilijulikana sana kwamba majuma sabini ya unabii wa Danieli, yaliyofunika ujio wa Masihi, yalikuwa karibu kumalizika; na wote walikuwa na hamu ya kushiriki katika enzi hiyo ya utukufu wa kitaifa ambayo ilitarajiwa wakati huo.” — “Tumaini la Vizazi Vyote,” uk. 133. {SR2: 242.2}

Nuru ilikuwa ikiangaza kwa taifa la Kiyahudi, na walikuwa wamejuzwa vyema habari Zake (ambaye walikuwa wametumia mamilioni ya dola kwa dhabihu, na mamia ya miaka katika huduma za sherehe), wakati ambao Angekuja, na asili ya ufalme Wake. Kwa sababu watawala wa taifa walikuwa wameanguka chini ya dhambi walidharau ukosoaji wa manabii. Kwa hivyo sifa ya ufalme uliotarajiwa wakati huo ilifasiriwa vibaya, lakini wakati waliuelewa vyema na kukubalika kitaifa. Kama vile Yohana hakuwa amepewa nuru kuhusu lile lingetukia baada ya Mtiwa Mafuta

243

kuja, aliutangaza huo ujumbe kwa upatano kamili na wazo maarufu la ule wakati wa kinabii, na wa ufalme uliokuwa ukija. Sasa, kwa sababu haukuwapo utata kati ya mafundisho ya Yohana Mbatizaji na watawala wa Israeli, ni nini kilichowafanya waukatae ujumbe wake? {SR2: 242.3}

“Kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, mtoto wa Zekaria angepaswa kuelimishwa kwa ajili ya ukuhani. Lakini mafunzo ya shule za marabi yangemfanya asifae kwa kazi yake. Mungu hakumtuma kwa walimu wa theolojia kujifunza jinsi ya kufasiri Maandiko. Alimwita jangwani, ili apate kujifunza juu ya maumbile, na Mungu wa maumbile. {SR2: 243.1}

“Lilikuwa eneo lenye upweke ambako alipata makao yake, katikati ya vilima vyenye ukame, mabonde ya mwituni, na mapango yenye miamba. Lakini lilikuwa chaguo lake kuacha starehe na anasa za maisha kwa ajili ya nidhamu yenye makali nyikani.” — “Tumaini la Vizazi,” uk. 101. {SR2: 243.2}

Kwa sababu Waandishi na Mafarisayo walisema kumhusu Kristo na mitume: Hatuwataki watu hawa wajinga kututawala, walimimina shutuma zile zile dhidi ya Yohana, na hili lilikuwa udhoofishaji wa maslahi yao ya milele. Kikwazo chao cha pili kilikuja wakati “kutokea kwa kipekee kwa Yohana kuliyarejesha nyuma mawazo ya wasikilizaji wake kwa waonaji wa zamani. Katika tabia na mavazi yake alifanana na nabii Eliya. Akiwa na roho na nguvu ya Eliya alishutumu ufisadi wa kitaifa, na kukemea dhambi zilizokithiri… Kama nembo ya kutakasa kutoka kwa dhambi, aliwabatiza katika maji mengi ya Yordani. Hivyo kwa funzo muhimu lenye maana alitangaza kwamba wale waliodai kuwa watu wateule wa Mungu walikuwa wametiwa unajisi kwa dhambi, na ya kwamba bila utakaso wa moyo na maisha hawangeweza kushiriki katika ufalme wa Masihi… Yohana aliwatangazia walimu wa Israeli kwamba kiburi, ubinafsi, na ukatili wao uliwadhihirisha kuwa ni kizazi cha nyoka, laana ya kufisha kwa watu, badala ya wana wa mwenye haki na mtiifu Abrahamu.” — “Tumaini la Vizazi Vyote,” uk. 104-106. {SR2: 243.3}

Hivyo ndivyo mtangulizi wa Kristo alivyofanya, kwa maana aliwaona watu wake wamedanganywa, wenye kinaya, na wakiwa wamelala katika dhambi zao. Alitamani sana kuwaamsha kwa maisha matakatifu. Mungu huwa hatumi wajumbe kumbembeleza mdhambi. Yeye huwa hatumi ujumbe wowote wa amani ili kuwaliwaza wale ambao hawajatakaswa katika usalama wa kusababisha kifo. Kwa sababu Yohana aliwaonya watu wake kuhusu hatari na maangamizi ya taifa lake, walimchukia zaidi. {SR2: 243.4}

Sasa, ni nini kiliufanya ulimwengu wa kabla ya gharika kuukataa ujumbe wa Henoko? Ujumbe wa Henoko kwa Dunia ya Zamani ulikuwa vivyo hivyo katika upatano mkamilifu na pokeo maarufu la “kuja kwa Bwana,” lakini kwa sababu kazi yake ilibeba karipio sawa na lile la Yohana Mbatizaji, pia alijiletea kukasirikiwa na watu wake. Kwa kuuwacha ujumbe wa wokovu ambao ungezifuta

244

dhambi zao (unabii wa Henoko juu ya hukumu), wenyewe walijiweka chini ya hukumu kubwa zaidi. Kwa kukataa njia pekee ya wokovu wao, walijikata kabisa kutoka kwa Nguvu inayovishikilia vitu vyote, na kwa hivyo wakaialika gharika ya kutisha. {SR2: 243.5}

Mungu, hakutaka mtu yeyote apotee, alimwamuru Nuhu atangaze ile hatari kimbele, na kutoa njia na vifaa kwa wale ambao wangependa kuokoka ule uharibifu. Lakini walipoukataa ujumbe kupitia kwa Henoko walifanya vivyo hivyo na ujumbe kupitia kwa Nuhu. Kwa kuwa jumbe hizi zilivuviwa na Roho Mtakatifu, walitenda dhambi dhidi Yake; kwa hivyo, hawatasamehewa milele. {SR2: 244.1}

Kwa hivyo ujumbe kupitia kwa William Miller ulikuwa utimilifu wa unabii wa Henoko — pia ukiwa nakala. Iwapo hili ni sahihi, lazima uwepo ulinganisho kamili wa mmoja kwa ule mwingine. Kwa sababu Henoko hakuelewa kabisa namna ya “kuja kwa Bwana,” na Yohana Mbatizaji sifa ya Ufalme ambao ungesimamishwa, vivyo hivyo Miller alifasiri visivyo “utakaso wa patakatifu,” na akatangaza kuja kwa Bwana duniani badala ya kuingia mahali Patakatifu Mno. Iwapo wengine watamshtaki Miller kuwa nabii wa uongo, wanaweza vivyo hivyo kumshtaki Henoko na Yohana. Mahitimisho kama hayo ya upofu na ya haraka ni jaribio la kuipindua Biblia yote. {SR2: 244.2}

Sasa swali linazuka, Kwa nini Mungu aliwaruhusu watumwa Wake kusalia gizani kuhusu lile ambalo lingetukia mwishoni mwa ujumbe wao? Zipo sababu kadhaa. Jumbe za Henoko na Miller zilikuwa sawa kwa yule mtangulizi wa ujio wa kwanza wa Kristo. Ujumbe wa Yohana ulikuwa wa kuiandaa njia ya kuja kwa Bwana, wala sio kufafanua namna ya ufalme Wake. Ndivyo ilivyokuwa kwa Miller na Henoko. Sababu ya pili. — Laiti Yohana angalipewa nuru kwamba ufalme wa Kristo haukuwa wa ulimwengu huu, ingeleta mzozo mkali wa ndani na taifa lake. Kwa hivyo, swali la kujadiliwa kama hilo lingekuwa limepindua kazi yake na kuufanya ujumbe wake kuwa bure kwa watu Wake. Lakini kwa sababu hapakuwa na ubishi kuhusu lile alilowafunza wasikilizaji wake liliwaacha viongozi wa Israeli waliopofushwa na dhambi bila udhuru. Laiti wangeupokea ujumbe wake, na kutubu dhambi zao, hilo lingeyafumbua macho yao ya kiroho, na kuwasili kwa Yule Mtiwa Mafuta kungewaangazia sehemu yote ya safari iliyokuwa imesalia. {SR2: 244.3}

Katika wakati wa Miller Jumuiya ya Wakristo haikukosa kujua kuhusu swali la patakatifu kuliko taifa la Kiyahudi lilivyokuwa kuhusu ufalme wa Kristo. Kwa hivyo, laiti Miller angalipewa nuru juu ya mahali ambapo Kristo angekuja mwisho wa siku 2300; yaani, kuja Patakatifu Mno kwa hukumu ya watakatifu, ujumbe wake ungeleta hoja nyingi na majadiliano

245

matupu. Kwa hivyo wakati na utangazwaji wa kile kipindi cha kinabii ungepuuzwa, na juhudi zake kuvurugwa. Lakini katika namna alivyoutangaza ujumbe wake hakuwapa nafasi ya kupinga, na kwa sababu maadui wa Mungu hawangeweza kupotosha ufafanuzi wake wa Maandiko, na kukataa kupendezwa na yale aliyofundisha, uliwaacha bila udhuru. {SR2: 244.4}

Hivyo ujumbe wa malaika wa pili wa Ufunuo 14:8, ulitangazwa mara tu baada ya kuvunjika moyo, Ukisema, “Babeli umeanguka, umeanguka.” Yaani, ulimwengu katika mwaka 1844 ulianguka kwa njia sawa na ile kabla ya ule wa gharika. Ulimwengu wa sasa huitwa Babeli, kwa sababu ufalme wa Babeli ndio wa kwanza baada ya gharika. Kwa hivyo Babeli ukawa mama wa mataifa. {SR2: 245.1}

Dunia yetu inasimama wakati huu wa sasa katika mahali pale kama ile kabla ya gharika. Ulimwengu wa Zamani ulihukumiwa kwa kuukataa ujumbe huo katika kivuli chake, na Mpya katika uakisi. Tia alama jinsi ulivyo ulinganifu wa matukio hayo ya kushangaza: Baada ya utangazwaji wa hiyo habari njema (kuja kwa Bwana kupitia kwa Henoko) ulipuuzwa kabisa na Ulimwengu wa Zamani na maandalio yakapuuzwa, Nuhu alitangaza mwisho wa dunia katika kizazi chake. Ujumbe wa Miller ulifuatwa na tangazo sawa na lile la Nuhu, kama lilivyotangazwa baada ya mwaka 1844, “Mwisho wa dunia katika kizazi hiki.” {SR2: 245.2}

Kama ilivyofahamika kwamba Kristo angekuja duniani katika tarehe iliyotarajiwa, na hilo fundisho lilidumu bila kupingwa kwamba kurejea kwa Mwana wa Mungu aliyetarajiwa kwa muda mrefu kulikuwa kumekaribia, kungepaswa kuwa kwa kuwavutia sana wale waliolikiri jina la Kristo kama Mwokozi na Mkombozi wao wa pekee. Laiti sifa walizotangaza kwa midomo yao pia zingekuwa mioyoni mwao, wangeipokea hiyo habari njema kwa furaha na kufanya maandalizi yote iwezekanavyo kwa tukio hilo tukufu zaidi katika historia yote. Lakini kadiri walipokataa kupendezwa, walidhihaki, na kukataa katakata — wakionyesha tabia yao ya kweli na hivyo kujitia alama wenyewe kama mbuzi. Kwa sababu habari zilizoinuliwa zaidi na za kutia moyo za utukufu wa mbinguni zilikataliwa, na mjumbe kutothaminiwa katika visa vyote viwili (Ulimwengu wa Kale na wa Kisasa), ni kweli kwamba kweli iwayo yote inayowasilishwa, bila kujali ukubwa wake wa utukufu, hawa wadhihaki wa leo hawataiamini, na hivyo wataileta hukumu juu yao wenyewe. {SR2: 245.3}

Kwa sababu Mungu alitangaza hatari kwa Ulimwengu wa Zamani kupitia mahubiri ya Nuhu katika kizazi kimoja, ndivyo Yeye kimbele alivyouonya ulimwengu kuhusu mwisho wake katika kizazi hiki. Jinsi matayarisho yalivyotolewa kabla ya gharika kwa wale ambao walitaka kuokoka huo uharibifu, vivyo hivyo Yeye ametoa njia na vifaa kwa wote wanaotaka kukwepa adhabu inayoikabili dunia yetu. Si kuingia ndani ya safina

246

iliyojengwa kwa kutumia mikono ya mwanadamu, La, hapana, huo ulikuwa mfano tu; bali kuingia ndani ya “majumba mengi” yaliyotayarishwa na Bwana mwenyewe; sio ndani ya safina inayoelea juu ya maji mengi yenye kichaa; ila ndani ya majumba yaliyotulia juu ya misingi ya mawe ya thamani. Gharika ile ya kutisha ni mfano wa millenia ya giza. Jinsi watu waaminifu wa Mungu walivyookolewa wakati huo, ndivyo pia watavyookolewa sasa; lakini mdhambi sasa, ataangamia kama mdhambi wakati huo. {SR2: 245.4}

Gharika Mfano Wa Maangamizo Ya Waovu

Iwapo gharika ni mfano wa millenia, na kizazi kilichoangamia wakati huo ni mfano wa kizazi kinachoishi sasa, basi idadi ya siku zilizotumika katika uharibifu wa Ulimwengu wa Zamani lazima izingatiwe kwa uharibifu wa ulimwengu huu wa sasa. {SR2: 246.1}

“Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana Nimekuona wewe u mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki. Kwa maana baada ya siku saba Nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usik, na kila kilicho hai Nilichokifanya juu ya uso wa nchi Nitakifutilia mbali. Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. Nuhu akaingia katika safina, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye, kwa sababu ya maji ya gharika. Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka. Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini mchana na usiku. Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini, nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi. Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.” (Mwa. 7:1, 4, 5, 7, 10-12, 17, 24.) {SR2: 246.2}

“Maji yakadumu kuondoka katika nchi: na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka. Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi: mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana. Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina alilolifanya: Akatuma kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. Kisha akatuma njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote: naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza

247

mle safinani. Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, Njiwa akamjia jioni; na, tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake ambalo amelitunda: basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa, naye asimrudie tena kamwe. Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi: Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. Mungu akamwambia Nuhu, akisema, Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe.” (Mwa. 8:3, 5-13, 15, 16.) {SR2: 246.3}

Baada ya Nuhu mwaminifu kutoa onyo kwa kizazi chake na kumaliza ujenzi wa safina, Mungu alimwamuru mtumwa Wake aingie ndani yake siku saba kabla ya mvua kuanza. Kama yeye, na wale wote ambao walipaswa kuingia ndani ya safina waliingia katika mashua hiyo ya ajabu iliyotulia juu ya nchi kavu bila ushahidi ulioonekana kwamba ingewahi kupata nafasi ya kuelea, Bwana aliufunga mlango. {SR2: 247.1}

Siku sita zilipita bila ishara yoyote dhahiri ya gharika, lakini mwisho wa siku ya saba, mvua iliyomiminwa kutoka juu na chemchemi zilizobubujika kutoka chini ziligongana, na utabiri wa Nuhu ulianza utimizo wake wa kutisha katika uharibifu wa nchi. Kadiri maji kutoka juu na chemchemi kutoka chini ziliufunikiza uso wa dunia dhiraa kumi na tano kwenda juu, na kuharibu kila kitu kilichokuwa hai mwishoni mwa siku arobaini mchana na usiku, ghafla zilikoma kutoka kwa kitisho hadi kwa utulivu, kutoka kwa ghadhabu hadi kwa amani, kana kwamba ziliridhishwa kwa mafanikio ya ushindi juu ya uasi dhidi ya ukweli na haki. Kwa siku mia moja na kumi hayakuongezeka wala kupungua, lakini yalishikilia usawa wake kwa muujiza. Wakati jumla ya siku mia na hamsini na saba zilipotimia tangu siku Nuhu alipoingia ndani ya safina, yalianza kupungua; yaani, chemchemi za vilindi zilifunua vinywa vyake ili kuyameza ndani ya vina vya nchi. {SR2: 247.2}

Sasa tunarudi kutatua utata unaoonekana wa Maandiko katika kunakili muda wa gharika na kufungika katika safina. “Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.” (Mwa. 7:11.) Mwezi wa pili na siku ya kumi na saba ya mwezi huo ilikuwa tarehe ya mwaka wa jua kulingana na kalenda ya walioishi kabla ya gharika wakati gharika ya ghadhabu ilipoanza hujuma zake kali dhidi ya kila chenye uhai duniani. Hasira iyo hiyo ya maumbile iliendelea vikali siku arobaini, na ilipofikia kilele chake na kuwaangamiza wakazi

248

ghafla ikatulia. Kuongeza siku arobaini kwa tarehe iliyotangulia kutaonyesha kwamba mvua ilikoma siku ya ishirini na saba ya mwezi wa tatu. “Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua [ikatulia] juu ya milima ya Ararati.” (Mwanzo 8:4.) {SR2: 247.3}

Kwa hivyo, tangu siku mvua ilipoanza hadi ile safina ilipotulia, (sio ardhini lakini kutokuelea) ilikuwa miezi mitano kamili. Lilo hilo limeandikwa katika Mwa. 8:3, “Maji yakadumu kutoondoka katika nchi: na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka.” Ukweli huu huthibitisha kwamba kalenda ya kila mwezi ya dunia kabla ya gharika ilikuwa na siku thelathini kwa mwezi (5 x 30 = 150). {SR2: 248.1}

“Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi: mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.” (Mwa. 8:5.) Yaani, tangu siku maji yalipopungua hadi siku ile milima ilipoonekana, ilikuwa siku sabini na nne. Siku (13) kukamilisha mwezi wa saba, siku (30) katika mwezi wa nane, siku (30) katika mwezi wa tisa, na siku (1) kutoka kwa mwezi wa kumi = siku 74 kwa jumla. {SR2: 248.2}

“Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi.” (Mwa. 8:13.) Yaani, tangu siku ile vilele vya milima vilipoonekana hadi siku ile maji yaliporudi mahali pake, zilikuwa siku tisini — siku (29) kukamilisha mwezi wa kumi, siku (30) katika mwezi wa kumi na moja, siku (30) katika mwezi wa kumi na mbili, na siku (1) kutoka kwa mwezi wa kwanza wa kuanza mwaka mpya, kufanya jumla ya siku tisini. {SR2: 248.3}

Rekodi ifuatayo itatupatia idadi ya siku za kukausha uso wa dunia na kuwa mgumu kutokana na athari za maji: “Na katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.” (Mwa. 8:14.) Kwa hivyo, dunia ilikuwa imekauka katika muda wa siku hamsini na sita tangu siku ile maji yalipoondolewa — siku (29) za kukamilisha mwezi wa kwanza, na siku (27) kutoka kwa mwezi wa pili, kufanya jumla ya siku (56). {SR2: 248.4}

Ufuatao ni muhtasari na jumla ya siku: siku (40) wakati wa mvua, siku 110 hadi wakati yalipoanza kupungua, siku 164 kwa maji kupungua ndani ya vina ya nchi, na siku (56) kwa nchi kukauka, kufanya jumla ya siku 370; na saba kabla ya gharika kuanza, kufikia jumla kuu ya siku 377 — miezi kumi na mbili na siku kumi na saba kwa jumla (siku 30 kwa mwezi). {SR2: 248.5}

Hakika hakuna mtu angeweza kudhani kwamba mpangilio wa gharika na idadi iliyowekwa ya siku kwa kila tendo zilibuniwa bila kufikiri na Mungu mwenye haki na hekima yote. Kwa nini Nuhu na familia yake pamoja na viumbe hai vyote vilivyoingia ndani ya safina

249

Ukurasa Mtupu

250

PICHA

[Chati ya Gharika — Mfano na Uakisi]

251

vilifungiwa humo kwa siku saba kabla ya mvua kuanza? Ingekuwa si busara na ukatili kwa upande wa Mungu, pia gharama ghali kwa Nuhu, na mzigo mkubwa kwa viumbe vyote vilivyokuwa safinani katika kuongeza muda wa uhifadhi wao iwapo haungekuwa na funzo la maana kwa vizazi vya baadaye. Kwa nini Atumie siku arobaini kuigharikisha dunia wakati Angeweza kufanya hivyo kwa muda mfupi sana? Kwa nini aurefushe uhifadhi wa viumbe Vyake ndani ya safina, kwa kuvizuilia uhuru wa maji katika mwenendo wake wa kushuka, na kuyalazimisha kudumisha mwinuko [kutoongezeka wala kupungua] wake dhiraa kumi na tano kwenda juu kwa siku 110? Au mbona isiwe zaidi au kidogo? Kwa nini Yeye asababishe maji kupanda juu katika siku arobaini, na atumie siku 164 (zaidi ya mara nne) kupungua? Je! Si kinyume na maumbile? {SR2: 248.6}

Dunia ilikuwa chini ya maji kwa zaidi ya miezi kumi, na wakati mabubujiko ya kasi yaliyofyatuka kutoka chini yalikuwa yamegeuza umbo la dunia kwa nguvu ya mwendo wayo wa kwenda juu, umbo lilikuwa tonge la ute wa tope. Lakini baada ya maji kushuka hadi katika nyanda za chini, na katika vina vya nchi, Yeye aliifanya nchi ikauke kwa muda wa siku hamsini na sita tu. Kila kitu Mungu alifanya kuhusiana na gharika kilikuwa kinyume na maumbile na kwa uamuzi au kufikiri kwa mwanadamu. Bila shaka, ilibuniwa hivyo kuwa funzo halisi kwa wale ambao mwisho wa dunia umekuja. {SR2: 251.1}

Yafuatayo hayatathibitisha tu kwamba yale ambayo yamesemwa ni sahihi, bali pia yataonyesha kwamba kufungwa kwa mlango wa safina siku saba kabla ya uharibifu wa gharika kuanza, ni mfano unaowakilisha ule wakati kutoka mwisho wa muda wa rehema hadi mwanzoni mwa mapigo. Yatathibitisha zaidi kwamba ile mvua ya siku arobaini usiku na mchana ni mfano wa maangamizo ya waovu katika mapigo. Siku zile 110 (baada ya mvua kukoma na kabla ya maji kupungua) ni mfano wa wakati wa waovu, wote wakati wa millenia na kwa miaka mia moja baadaye. Pia kwamba kuisafisha nchi kwa maji ni mfano wa maangamizo ya waovu kwa moto (mauti ya pili) baada ya millenia, na siku hamsini na sita ambazo nchi ilikauka ni mfano wa kupoa kwa nchi baada ya utakaso wake kutoka kwa dhambi na wadhambi. {SR2: 251.2}

Kwa sababu mifano iliyotajwa hapo juu ni nembo za matukio sita tofauti ya vipindi vinavyoshughulika na siku, miezi na miaka, kutegemea tukio husika, maana yake halisi haiwezi kufafanuliwa kwa kuyalinganisha, wala njia kama hiyo haitathibitisha lolote katika swala hili, wala hata kuonyesha Mwenye Uwezo wote katika kuubuni mfano. Kwa hivyo, maana yake halisi itapatikana kwa kuzidisha na namba za Kibiblia za maana maalum kufaa tukio hilo na kuupanua mtazamo. Pia lile funzo linalotoka kwa njia kama hizo lazima lithibitishe usahihi na uwiano kamili kutokea kila pembe ambayo mtu anaweza kufikiri; kwa hivyo jambo moja hulithibitisha lingine. {SR2: 251.3}

252

Kwa hivyo, kwanza tutazingatia siku saba (kutoka wakati Nuhu alipoingia safinani hadi mwanzoni mwa gharika) ambazo tulieleza kuwa ni mfano wa wakati kati ya kufungwa kwa muda wa rehema na kuanza kwa mapigo. Mbinu itakayotumika kufunua urefu wa muda katika kipindi hicho pia itaonyesha kwamba muda wa rehema kwa wanadamu, na ukamilifu wa utangazwaji wa injili umefungwa. Namba pekee inayofaa ya Kibiblia ambayo inaweza kutumika kuelezea matukio kama hayo na pia kufunua idadi ya siku kutoka kwa tukio moja hadi kwa lingine, itakuwa namba saba. Kwa hivyo, lazima tuzidishe mfano huo na namba ya Kibiblia ya ukamilifu. Kwa hivyo, 7 x 7 = siku 49 kuanzia kufungwa kwa muda wa rehema hadi mwanzoni mwa mapigo. Kwa hivyo, kuanguka kwa mapigo kunapaswa kuwa ishara kwa waovu kwamba wamepotea! O, ni kuvunjika moyo kulioje kwao, ambao, kama walioishi kabla ya gharika hutarajia kuokolewa, lakini hujikuta wamepotea wenyewe. {SR2: 252.1}

Kuhesabu kwa njia kama hiyo kulitumika kubainisha mwaka wa yubile. Bwana akasema: “Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, miaka saba mara saba na muda wa sabato saba za miaka zitakuwa kwenu, miaka arobaini na kenda.” (Law. 25:8.) Mwaka wa hamsini wakati ardhi ilipumzika ikiwa pia ni mfano wa millenia (kuonyesha kwamba ardhi itatunza pumziko la Sabato), vivyo hivyo hesabu kama hiyo imetumika. Kwa hivyo, mwanzoni mwa miaka elfu ndio mwanzo wa yubile katika uakisi wake. Na jinsi ardhi ilirudishwa kwa wamiliki halali katika mwaka wa yubile wa mfano, ndivyo itakavyokuwa katika uakisi — itarejeshwa kwa watakatifu. “Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, nao watairithi nchi milele, tawi la upanzi wangu, kazi ya mikono yangu, ili Nitukuzwe.” (Isa. 60:21.) {SR2: 252.2}

Namba ijayo na tukio la kushughulikia ni siku arobaini mchana na usiku halisi wakati ilinyesha, zikilinganishwa na zile za uakisi (kuangamizwa kwa waovu katika wakati wa mapigo na hadi kuja kwa Kristo mara ya pili). Maangamizo ya waovu duniani kote lazima tuzidishe huo mfano na namba inayoashiria ulimwengu wote, ili kuthibitisha kwamba uharibifu utajumuisha ncha nne za dira. Imethibitishwa hapo awali kwamba kumi ndiyo namba pekee inayofaa; kwa hivyo, 40 x 10 = 400, na hivyo kuleta jumla ya siku 449, au mwaka mmoja na robo (miezi 15) kutoka kwa mfungo wa muda wa rehema hadi kuja kwa Kristo kuwachukua watakatifu Wake. Ukweli huu utathibitishwa kutokea kwa pembe nyingine kuhusiana na uchambuzi mwingine. {SR2: 252.3}

Kwa sababu sehemu mbili za gharika (7 x 7 = siku 49 na 10 x 40 = siku 400) zinatuleta hadi mwisho wa dunia, kisha sehemu ya tatu (siku 110 wakati maji yalidumisha mwinuko

253

[kutoongezeka wala kupungua] wake dhiraa kumi na tano kwenda juu au tangu wakati mvua ilipokoma hadi wakati maji yalipungua) lazima zitumike kwa millenia. Nayo pia ikiwa ni ya ulimwengu wote, tunalazimika tena kuzidisha namba kumi na huo mfano, 110 x 10 = 1100. Millenia ikiwa na urefu wa miaka 1000, na miaka 100 ng’ambo yake (baada ya ufufuo wa waovu hadi kwa uharibifu wao wa mwisho, angalia “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 164), zikifanza jumla ya miaka 1100. Hili huthibitisha kwamba siku 1100 zilizotokana na kuzidisha kwetu ni za kinabii (siku kwa mwaka). Kwa hivyo zile siku halisi zinazosalia za mkaragazo wakati maji yalikuwa yakipungua na dunia ilikuwa ikijisafisha kutoka kwa gharika, lazima zitumike kwa maangamizo ya mwisho ya waovu na utakaso wa dunia kwa moto. {SR2: 252.4}

Kwa hivyo, idadi ya siku za mfano zinatumika kihalisi jinsi gharika ilivyokuwa, na kama ifuatavyo: Tangu siku ambayo maji yalipungua hadi wakati vilele vya milima vilipoonekana, zilikuwa siku sabini na nne, na tisini zaidi hadi yote yalipotoweka, zikifanya jumla ya siku 164; katika wakati ambamo waovu na matendo yao yanachomwa moto kuwa majivu. (Mal. 4:1.) {SR2: 253.1}

Siku hamsini na sita zilizobaki (wakati nchi ilikuwa ikikauka) hutumika kwa wakati dunia ilikuwa inapoa, na kwa sababu Nuhu alitoka safinani, vivyo hivyo watakatifu watatoka nje ya Mji Mtakatifu na kuimiliki nchi milele na milele. “Na ufalme na mamlaka, na ukuu wa ufalme chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu, ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii Yeye. Huu ndio mwisho wa jambo lile.” (Dan. 7:27, 28.) {SR2: 253.2}

Ni hakika kwamba hakuna kitu kinachoweza kutoshea kikamilifu kabisa kiajali. Lakini fikiri kuhusu utambuzi wa ajabu kama huo katika kubuni ajabu ya namna hii ambayo inaweza kufunua kwa picha hai siku za baadaye kwa maelfu ya miaka! Je! Ushahidi kama huu si ishara ya upendo wa Mungu kwa viumbe walioanguka! Shukrani huumuka kutoka mioyoni mwetu, twakosa maneno, tunaweza tu kupaaza sauti na Mwandishi wa Zaburi: “Neno Lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. Nimeapa nami Nitaifikiliza, kwamba nitazishika hukumu za haki yako.” (Zab. 119:105, 106.) {SR2: 253.3}

Si ajabu tu kuunda taa inayotoa nuru kwa kawi ya mshumaa kama hiyo ya kushangaza lakini pia inashangaza jinsi Mungu wetu anavyoweza kuficha maajabu Yake machoni pa watu wenye hekima na busara. Kisha kwa wakati Wake mwafaka Huwaweka juu ya vilima virefu ambavyo kwavyo Anaweza kuangazia njia ya mtafuta kweli, na kwa nguvu yake inayoangaza Awafumbe macho waovu. “Kwa hivyo watu wasiofahamu wataangamia.” (Hosea 4:14.) “Nuru imemzukia mwenye haki, na furaha wanyofu wa moyo.” (Zab. 97:11.) {SR2: 253.4}

254

Mungu wetu angeweza kunena nasi moja kwa moja kupitia kwa manabii kama nyakati za zamani, lakini haingewezekana kuisambaza nuru nyingi kwa kizazi kimoja. Wala hatungeweza kuelewa maana yake jinsi tunavyoweza kwa mifano hii au nembo hizi. Pia akijua udanganyifu mkubwa, kutokuamini na kutilia shaka kwa watu wenye kujitakia makuu ambao wangeinuka, Yeye ameyaweka maajabu haya ndani ya Biblia kufunua wazi makosa na kuufichua ukweli, na hivyo kumpindua adui wa wanadamu; pia kuwaacha wanafiki na wasio amini bila udhuru. {SR2: 254.1}

Jinsi kila kitu kilichokuwa hai nje ya safina wakati wa gharika kiliangamia, vivyo hivyo katika millenia ya giza kila kitu kitakachokuwa hai kitarudi mavumbini, isipokuwa shetani na malaika zake. Ingawa wanadamu wanafundisha kuhusu millenia ya amani, fundisho lao litakuwa bure, nao watalala kwa huzuni isipokuwa watubu. {SR2: 254.2}

Gharika Hulingana Na Pasaka Na Kusulubishwa

Mungu wetu alimwamuru Nuhu na familia yake, wanyama, ndege na vitu vitambaavyo kuingia ndani ya safina siku ya maandalio — Ijumaa. “Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina… kama vile alivyomwamuru Mungu: Bwana akamfungia.” Sabato ilipokuwa ikiingia, ikiwa siku ya kumi ya mwezi wa pili. (Mwa. 7:13, 16.) Siku saba baadaye, au mwanzoni mwa Sabato iliyofuata, siku ya kumi na saba ya mwezi, “chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka” ikanyesha juu ya nchi siku arobaini mchana na usiku. Mvua ilikoma siku ya ishirini na saba ya mwezi wa tatu, na siku ya nne ya juma — Jumatano machweo. Upo ulinganifu wa ajabu kati ya gharika na juma la pasaka; pia kuhusiana na kusulubishwa, kufufuka, na kupaa kwa Kristo. Kwa hivyo, majaliwa haya ya Mungu yanastahili kuzingatiwa kwa bidii. Waisraeli waliamriwa kumtenga mwana-kondoo wa pasaka na kundi siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, na walipaswa kumchinja siku ya kumi na nne ya mwezi huo jioni. (Kut. 12:3, 6.) {SR2: 254.3}

Wakati Kristo alisulubishwa, akazikwa, na kufufuka ndani ya juma la pasaka, mzunguko wa kila juma na kalenda ya kila mwezi hulingana kama ifuatavyo: Siku ya kumi ambayo mwana-kondoo alipaswa kutengwa kutoka kwa kundi, iliangukia Sabato ya siku ya saba mwaka huo; ambayo ilikuwa sanjari na siku ya juma na mwezi wa siku ya kwanza ya Nuhu kufungiwa safinani. Mwishoni mwa siku ya kumi na nne ya mwezi baada ya Kristo kuadhimisha sikukuu [karamu] ya mwana-kondoo wa pasaka, Alipelekwa mbele ya makuhani; akafa Ijumaa siku ya kumi na sita ya mwezi, akazikwa mwanzoni

255

mwa siku ya kumi na saba (Sabato), ambayo hulingana na kuanza kwa gharika, na akafufuka siku ya kumi na nane — Jumapili. Alipopaa juu siku arobaini baadaye, iliangukia Alhamisi siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili; ikiwa siku iyo hiyo ya juma, kama ile iliyofuatia siku arobaini za mvua. Maelezo yetu ya hapo awali yalionyesha kwamba ile siku iliyofuatia zile siku arobaini za mvua, ilionyesha kwa mfano, mwisho wa dunia, ukifuatiwa na kuondoka kwa watakatifu duniani. {SR2: 254.4}

Hatuwezi kudhani kwamba Mungu alikuwa ameleta sanjari hizi bila lengo kwa mtazamo. Kwa sababu kukoma kwa mvua ni mfano wa mwisho wa dunia hii, kwa hivyo kupaa kwa Kristo na wale waliofufuliwa pamoja Naye, ni mfano wa kupaa kwa watakatifu katika ujio wa Bwana. Pia hufunua kwamba kuja Kwake kutakuwa siku ya Jumatano, na msafara wa utukufu utang’oa nanga kwenda Mbingu za mbingu siku ya Alhamisi. Tena tunaambiwa kwamba itawachukua watakatifu siku saba kupaa hadi kwa kiti cha enzi cha Mungu, na ya kwamba tutapumzika Sabato katika mojawapo wa sayari tukiwa safarini. Kutokana na hili ni dhahiri kwamba Kristo atakuja katikati ya juma. Kwa hivyo tena tunaona kwamba jambo moja hulithibitisha lingine. Hesabu za karibu kama hizo za ratiba ya matukio ambayo yatatukia hivi karibuni, huweka wazi kwamba mwisho wa mambo yote umekaribia, vinginevyo habari hiyo ingekuwa bado haijawasilishwa. {SR2: 255.1}

Nuru hii ikiwa inasambazwa kwa njia ya maajabu ya matukio ya mifano, ni udhihirisho wazi kwamba upo mfano wa kila tukio la masilahi muhimu kwa kanisa la Mungu, ambayo ni vithibitisho hakika na maelezo wazi ya majaliwa ya Mungu. Kwa maana hakuna mfano wa lile la uongo, walimu wa nadharia bila uwakilishi wa mfano kwa madai yao ya kinachoitwa eti kweli za Biblia, na wale ambao huziamini, ni kama kipofu akimwongoza kipofu. Mifano hutekelezwa ili kufunua wazi kosa na kufichua ukweli. Walio waaminifu watampinga shetani kwa kuzikumbatia kweli, na kwa kutembea katika nuru. {SR2: 255.2}

Mwana-kondoo wa pasaka akiwa alitengwa kutoka kwa kundi siku ya kumi, huwa sanjari na utengo wa wenye haki kutoka kwa waovu duniani kabla ya gharika. Siku ya mazishi ya Kristo hulingana na siku ya kuanza gharika, na pia kuanza kwa mapigo; na kupaa Kwake siku iliyofuata baada ya mvua kukoma, pia na mwisho wa dunia na uhamisho bila mauti wa watakatifu. Sanjari hizi ni kamilifu na siku ya juma na ya mwezi, lakini moja ni mwezi mapema katika msimu kuliko nyingine; pasaka ikiwa katika mwezi wa kwanza, na gharika katika mwezi wa pili. Imefafanuliwa tayari kwamba pasaka ni mfano wa kufungwa kwa muda wa rehema kwa

256

kanisa, (tazama ukurasa wa 216-218) na kufungwa kwa safina ni mfano wa kufungwa kwa muda wa rehema kwa ulimwengu. Kwa hivyo, ziko siku thelathini za mfano kati ya kufungwa kwa muda wa rehema mmoja na ule mwingine. Laiti tungepewa nuru jinsi ya kufafanua siku hizi za mfano (30) zingeonyesha idadi halisi ya miaka tangu kutimizwa kwa Ezekieli tisa (Pasaka), hadi kwa mfungo wa mwisho wa muda wa rehema. Ukweli huu labda hautafanywa ujulikane hadi baada ya kazi ya injili kufungwa. Kwa muhtasari wa gharika katika mfano na uakisi, tunavuta umakini wa msomaji kwenye chati iliyo kwa ukurasa wa 250. {SR2: 255.3}

Maana Ya Mwezi Wa Kwanza Na Wa Pili

Kazi ya kufunga kwa kanisa huonyeshwa na mwezi “wa kwanza,” na mavuno ya ulimwengu na mwezi wa “pili.” Kwa sababu ukweli mmoja huufunua mwingine, umakini wetu umeelekezwa kwa Yoeli 2:23, 28, 29: “Furahini basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana Mungu wenu: kwa kuwa Yeye amewapa ninyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki, Naye atawanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, katika mwezi wa kwanza, Hata itakuwa baada ya hayo, ya kwamba Nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume kwa wake watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono: tena juu ya watumishi wenu wanaume kwa wanawake katika siku zile Nitamimina roho yangu.” Kumbuka kwamba “mvua” inakuja kwanza na kumiminwa kwa roho Wake baadaye. Kwa hivyo, mvua ni kitu kimoja, na kumiminwa kwa roho ni ni kitu kingine. {SR2: 256.1}

Kwa ile “mvua” huwakilishwa nuru kubwa kwa Neno la Mungu ambayo ni ya kukomaza mavuno na kuiangaza nchi kwa utukufu wake — malaika wa Ufunuo 18:1. Kumiminwa kwa Roho ni nguvu ambayo inapaswa kuwashukia watumwa wa Mungu ili kuiendeleza kazi inayowakilishwa na mvua ya masika na ya vuli. “Juu ya wote wenye mwili” ni Roho ambaye atawasadikisha walio waaminifu moyoni kuhusu ukweli na kuwaleta ndani ya kanisa, ambapo Pentekoste ilikuwa mfano. “Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta.” — huwakilisha mavuno makubwa ya nafsi ambayo yatakusanywa ndani na matokeo ya “mvua” na “Roho.” (Yoeli 2:24.) {SR2: 256.2}

“Mvua” hunyesha katika “mwezi wa kwanza,” yaani, mwezi ambao kazi ya kufunga kwa ajili ya kanisa huwakilishwa — wakati wa kutiwa muhuri watu 144,000. Kwa hivyo, katika kipindi hicho cha wakati (kabla ya Ezekieli Tisa) nuru kubwa itafunuliwa. Inashangaza kuona mpangilio mkamilifu wa kisarufi wa maneno kwa wakati wa utimizo wake, ukigawanya wazi Neno la kweli kana kwamba liliandikwa tu wakati maneno ya unabii yanafunuliwa.

257

“Kwa kuwa Yeye amewapa ninyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki” ni nuru ya ukweli ambayo inasifiwa na mvua ya masika ambayo lazima ilinyesha kabla ya wakati wa mvua ya vuli. Kwa hivyo, mvua ya masika si nyingine isipokuwa maandishi ya “Roho ya Unabii.” Uthibitisho zaidi wa hili utatolewa katika sura nyingine. {SR2: 256.3}

Lakini kumbuka kwamba kunyesha kwa mvua ya masika kunarudiwa na mvua ya vuli: “Naye atawanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, katika mwezi wa kwanza.” Kwa hivyo mvua ya masika (Roho ya Unabii) inanyesha mara ya pili — inafunuliwa kikamilifu zaidi katika wakati wa “mvua ya vuli” — mara ya kwanza huru kwa mvua ya vuli, na mara ya pili ikihusishwa na mvua ya vuli katika “mwezi wa kwanza” (kabla ya Ezekieli Tisa). Maana yake ni, ukweli uliorekodiwa katika maandishi ya “Roho ya Unabii” haukueleweka kikamilifu hadi kwa wakati wa mvua ya vuli. Kwa hivyo mvua ya masika huja tena na mvua ya vuli, na hili ndilo linasababisha “Kilio Kikuu.” {SR2: 257.1}

Kaini Na Abeli

Ukweli mwingine wa ajabu unavyoonekana kwenye chati ni uhalifu uliofanywa na Kaini kumuua kaka yake Abeli. Hawa wakiwa ndugu wawili wa kwanza na ugomvi wa kwanza juu ya dini, pia mauaji ya kwanza katika familia ya wanadamu, hakika lazima yashikilie funzo la umuhimu mkubwa. {SR2: 257.2}

Kwa mujibu wa sheria ya Biblia ukuhani ulipaswa kufanzwa kutoka kwa mzaliwa wa kwanza wa kila familia. Hivyo, kwa haki za sheria, Kaini alikuwa kuhani. Bwana mwenyewe aliusema ukweli huu Aliponena na Kaini kusema: “Na mapenzi yake yatakuwa kwako [pambizo, mtiifu], nawe utamtawala.” (Mwa. 4:7.) Kwa hivyo, wanaume hawa wawili huwakilisha makundi mawili ya watu. Kwa sababu ukweli huu hauwezi kukanushwa, Kaini lazima awakilishe daraja la uongozi (makuhani), na Abeli ushirika wa kweli wa kanisa. Kaini ndiye alimwasi Mungu kwa kutoa dhabihu ya uongo, na kwa sababu Abeli alitii na kuabudu kwa njia iliyoagizwa na Muumba, alisababisha kukasirikiwa na kaka yake mkubwa. {SR2: 257.3}

Iwapo taarifa kwamba Kaini na Abeli huwakilisha madaraja mawili ya watu ni sahihi, basi iyo hiyo lazima ithibitishwe na kweli za kihistoria. Tulieleza kwamba Kaini ambaye alikuwa mfano wa uongozi alimtesa yeye ambaye ni mfano wa ushirika wa kweli. Kwa njia hiyo kila sehemu ya kanisa la Mungu imeasi imani kupitia uongozi usiojitolea kwa Mungu, na kila ujumbe ulioitisha matengenezo vivyo hivyo, wao, waliutupa nje ya kanisa. Katika upofu wao walikuwa wameamua kuwafanya watu wasiijue kweli

258

na hivyo waliwatesa wajumbe na wale walioupokea ujumbe na kutii ukweli. Kwa hivyo, hitaji liliita vuguvugu moja baada ya lingine. Ni wazo la kutisha lililoje kwa wale wanaobeba jukumu hili kubwa! Na ni hatari ilioje kwa kundi linaloruhusu wengine kufikiria na kutenda kwa niaba yao! Tabaka ambalo huyapokea maamuzi ya wengine, iwe ni kwa ajili au dhidi ya ukweli, wamedanganyika na kuporwa uzima wa milele, kwa maana hawawezi kuwa na uzoefu wao wenyewe, hakuna uongofu wa kweli, wala badiliko la moyo. Ndugu zangu: maneno haya si dhidi yenu, kwa sababu ni Mungu anayenena kupitia katika neno Lake la kweli kuwaokoa kutoka kwa shimo la kuzimu. Je! Hamtamruhusu Afanye kazi kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu Wake? Je! Hamtakuwa kondoo Zake? {SR2: 257.4}

259

HEKALU LA KWANZA NA LA PILI–MFANO NA UAKISI

Mtume Paulo akinena kwa kulinganisha hekalu la Sulemani na kanisa, huelekeza kidole kwa Kristo kama “jiwe kuu la pembeni; katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema” anasema “kuwa maskani ya Mungu katika Roho.” (Efe. 2:20-22.) Daudi, akitazama mbele kinabii kwa ujenzi wa hekalu la kwanza na mwanawe, na pia kuhusu matumizi yake kwa kanisa la Kristo asema: “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa Bwana; nalo ni ajabu machoni petu.” (Zab. 118: 22, 23.) {SR2: 259.1}

Yakinena juu ya hekalu la kale Maandiko husema: “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni: wala nyundo wala shoka wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.” (1 Wafalme 6:7.) Jiwe la kipekee ambalo lilikuwa limekwisha kuchongwa kufaa pembe kuu ya hekalu, lilikataliwa; na ingawa wajenzi walilikataa “jiwe kuu” la nyumba hiyo, Mtunga Zaburi husema: “Neno hili limetoka kwa Bwana; nalo ni ajabu machoni petu.” Kukataliwa kwa lile “jiwe,” Bwana aliufanza mfano, na hivyo kutabiri, kukataliwa kwa Kristo na taifa la Kiyahudi. (Tazama Matendo 4:10, 11.) Kwa maana Yesu husema: “Jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa [jiwe] kuu la pembeni.” (Mat. 21:42.) Kwa hivyo limekuwa kuu la pembeni, basi ni dhahiri kwamba hekalu la kwanza lilikuwa kiwakilishi cha nyumba ya Kiroho, na mfano wa kanisa la Kikristo, Kristo mwenyewe aliwakilishwa na jiwe kuu la pembeni “walilolikataa waashi,” akiwa mkuu na mwasisi wa kanisa la Kikristo. {SR2: 259.2}

Hekalu La Pili

Katika kulijenga hekalu la pili, Haggai na Zekaria walitabiri na kuimarisha mikono ya watu kwa Neno la Mungu. Maandishi ya hao manabii wawili hubeba uthibitisho katika kila mstari, kwamba utimizo kamili wa unabii wao utafahamika katika siku za mwisho za historia ya dunia hii. Kwa sababu

260

wamefunganisha utabiri huu na ujenzi wa hekalu la pili, ni dhahiri kwamba muundo halisi wa jengo hilo la kifahari una maana ya kiroho kwa kanisa katika kazi ya kufunga injili. Zekaria, akitazamia mbele kwa wakati wa hekalu la kiroho (sehemu ya mwisho ya kanisa) na ujenzi wake, anasema: “Tazama mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni chipukizi naye atakua katika mahali Pake, naye atalijenga hekalu la Bwana: Naam yeye atalijenga hekalu la Bwana, naye atauchukua huo utukufu, ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; naye atakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi: na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili. Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.” (Zek. 6:12, 13, 15.) {SR2: 259.3}

“Naye atauchukua huo utukufu.” Kwa Kristo utukufu wa ukombozi kwa jamii iliyoanguka ni Wake. “Yeye atupendaye, na kutuosha dhambi zetu katika damu Yake…. utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele.” (Ufu. 1:5, 6.) Yeye “ataketi akimiliki katika kiti Chake cha enzi, Naye atakuwa Kuhani katika kiti Chake cha enzi.” (Zek. 6:13.) “Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na Mkuu wa wafalme wa dunia.” (Ufu. 1:5.) “Naye atakuwa Kuhani katika kiti Chake cha enzi.” Ni dhahiri kwamba wakati uliotabiriwa ni wakati fulani baada ya kusulubishwa na kabla ya muda wa rehema kufungwa; kwa maana Yeye ni “kuhani.” Kristo, “chipukizi,” “atakua katika mahali Pake”; yaani, Angechipuza kutokea kwa taifa la Kiyahudi, “naam yeye atalijenga hekalu la Bwana.” Kwa hivyo, hekalu ambalo “Yeye atajenga” halikuwa hekalu halisi katika Yerusalemu ya kale, kwa maana lilikuwa hekalu ambalo Yeye atajenga baada ya kuzaliwa Kwake. “ Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana.” Kwa kuwa hii haikuwa kweli na hekalu halisi, maneno hayo lazima yatumike kwa lile la uakisi. Wakati huo nabii anasema: “Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku hiyo, nao watakuwa watu Wangu.” (Zek. 2:11.) “Katika siku hiyo;” yaani, katika wakati wa “Kilio Kikuu,” umati mkubwa utaongoka kwa kanisa. Katika Zekaria 13:8, imesemekana kwamba theluthi moja ya wakazi “watakuja,” na ndio ambao “watajenga katika hekalu la Bwana,” ambalo lile halisi lilikuwa mfano. {SR2: 260.1}

Zekaria kisha aliona tawala ambazo “zilitawanya Yuda, Israeli, na Yerusalemu” (mfano, pia uakisi), zikiwakilishwa na “pembe nne.” Mara tu baadaye aliziona pembe zile zile na maseremala wanne (soma Zek. 1:18-21), wakiwakilisha vyombo vilivyotumiwa na Bwana kuwarejesha watu Wake na nyumba ya ibada Yake, katika mfano na uakisi; yaani, Mataifa waliolitawanya kanisa pia watakuja na kulijenga lilo hilo. {SR2: 260.2}

261

Tofauti Sisisi Na Ya Kiroho Kati Ya Hayo Mahekalu Mawili

Huduma za kidini katika mahekalu yote mawili zilitekelezwa kwa namna ile ile, lakini kwa fahari ya muundo, wa ndani na wa nje, hekalu la Sulemani kwa usemi wa kulinganisha, lilikuwa bora zaidi. Lakini Bwana kwa kinywa cha nabii Haggai aliwauliza wale ambao wakati huo walikuwa wakifanya ujenzi wa nyumba ya Mungu: “Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii [hekalu la Sulemani] katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu siyo kama si kitu? Utukufu wa nyumba hii ya mwisho utakuwa mkuu kuliko utukufu wa ile ya kwanza, asema Bwana wa majeshi: na katika mahali hapa Nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.” (Haggai 2:3, 9.) {SR2: 261.1}

Utukufu halisi wa hekalu la pili ukilinganishwa na wa la kwanza ulikuwa “kama si kitu,” lakini Neno husema: “Utukufu wa nyumba hii ya mwisho utakuwa mkuu kuliko utukufu wa ile ya kwanza.” Kwa uhalisi hii haikuwa kweli. Kwa hivyo, utukufu wa mahekalu haya mawili kwa kuyalinganisha, haumo katika maumbo halisi, yanayoonekana, ila badala yake katika kusimama kwayo kiroho. Kwa hivyo, mahekalu yote hayawezi kuwa mfano wa kipindi kimoja cha enzi ya Ukristo, kwa sababu moja hutofautiana kabisa na lile lingine. Kwa kuwa hii ni kweli, basi mfano huo huonyesha kwamba kanisa la Kikristo katika mfano huu limegawanywa katika sehemu mbili. Hivyo basi, katika mfano, hekalu la pili humaanisha kwamba sehemu ya mwisho ya kanisa itakuwa kuu zaidi, ambayo ikilinganishwa na ile ya kwanza husimama kama si kitu. {SR2: 261.2}

Sehemu hizi mbili za historia ya kanisa pia zilionyeshwa katika maono ya Patmo. Kwa Yohana alionyeshwa Kanisa la kweli la Mungu la Kiroho katika vizazi vyote, katika nembo ya mwanamke. Alipewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa ili aruke hadi nyikani kwa siku (miaka) 1260. Nyikani huwakilisha vizazi vya giza, ndani ya wakati ambao alikuwa nje ya ustaarabu (kutoka mwaka 538 B.K hadi 1798 B.K.) Kwa hivyo, kipindi hiki cha miaka 1260 ya kinabii, kiligawanya kanisa la kweli katika sehemu mbili; yaani, kutoka kwa kusulubishwa hadi mwaka 538 B.K. na kutoka mwaka 1798 B.K. hadi mwisho wa wakati. Kwa hivyo sehemu ya kwanza, au inavyoitwa, kanisa la mitume, lilifananishwa na hekalu la kwanza; na sehemu ya mwisho na lile hekalu la pili. Hili halisemi kwamba Mungu hakuwa na watu wa kweli kati ya mwaka 538 B.K. na mwaka 1798 B.K. kwa maana Neno lasema, “Hapo alishwapo kwa wakati na nyakati mbili na nusu ya wakati.” (Ufu. 12:14.) Somo lililofundishwa hapa ni kwamba, sehemu ya kwanza ya kanisa katika karne chache za kwanza ilijaliwa Sabato ya kweli — “ya kila siku” — na ukweli wa patakatifu; lakini kabla ya mwaka 538 B.K. ukweli ulikuwa “umeangushwa chini.” (Dan. 8:12, 13.) Sehemu ya pili baada ya kutimizwa kwa kipindi cha miaka 1260 huashiria kwamba lilikuwa tena limejaliwa ukweli ambao “uliangushwa

262

chini,” na matengenezo kati ya sehemu hizi mbili (kutoka mwaka 538 B.K. hadi mwaka 1798 B.K.) ya kanisa, au “mwanamke,” yalikuwa yatayarishe njia ya kurejea kwake, au kwa urejesho wa ukweli. Kwa maana mahekalu yote mawili, ambayo sehemu hizi mbili zilifananishwa, huwakilisha ibada pamoja na kweli za Sabato na patakatifu. {SR2: 261.3}

Hekalu La Kwanza Kihalisi Kubwa, Bali Kiroho Ni La Pili

Palikuwa na kitu kitukufu kwa hayo mahekalu yote mawili; na ukuu wa moja ulikuwa kama “si kitu” kulinganishwa na lile lingine. La kwanza kwa kuonekana lilizidi la pili, na la pili kiroho lilizidi la kwanza; lakini zawadi ya tukufu kwa yote mawili ilikuwa bila kifani. Kwa sababu moja liliwakilisha kanisa la kwanza la Kikristo, na lile lingine sehemu ya mwisho ya kanisa lilo hilo, ni dhahiri kwamba sehemu zote mbili zilijaliwa utukufu mkubwa; lakini utukufu wa kanisa la kwanza ulikuwa halisi, na la mwisho wa kiroho, kwa mujibu wa ile mifano. {SR2: 262.1}

Kanisa la kwanza la Kikristo lilikuwa kihalisi kubwa, kwa sababu Kristo, “Jiwe kuu la pembeni,” alionekana wakati huo katika umbo Lake la kibinadamu. Kwa hivyo utukufu halisi wa hekalu la Sulemani ulikuwa nembo kamili! Lakini mfano huo huonyesha kwamba utukufu wa kanisa la kwanza ulikuwa si kitu ukilinganishwa na sehemu ya mwisho ya kanisa lilo hilo. Kwa hivyo, uwepo unaoonekana wa Kristo (katika umbo Lake la kibinadamu) katika kanisa la kwanza, ulikuwa si kitu ukilinganishwa na uwepo Wake usioonekana katika kazi ya kufunga ya kanisa la injili! {SR2: 262.2}

Tunafikiri kuhusu miujiza ya ajabu — kutoa mapepo, uponyaji wa wagonjwa, na kuwafufua wafu! Tunashangaa tunapofikiri kuhusu ufufuo Wake, kupaa Kwake juu, na maonyesho ya utukufu siku ya Pentekoste! Lakini maajabu haya yote hayatakuwa kitu yakilinganishwa na udhihirisho mtakatifu wa utukufu zaidi katika wakati wa mavuno! {SR2: 262.3}

Tusifikiri kwamba wakati Kristo atakapotokea mawinguni udhaifu wa watakatifu utaondolewa. Kazi hii lazima ifanyike kabla ya wakati huo, baada ya hapo ndipo kutokufa kutapeanwa. “Yeye aniaminiye, kazi nizifanyazo Mimi,” alisema Yesu, “yeye naye atazifanya; naam na kubwa kuliko hizo atafanya.” (Yohana 14:12.) Utimizo mkamilifu wa maneno haya bado uko mbele na lazima utimizwe kabla ya ujio Wake wa pili. “Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.” (1 Kor. 15:53, 54.) {SR2: 262.4}

263

Kwa hivyo, katika wakati wa “Kilio Kikuu,” miujiza itafanyika — wagonjwa wataponywa, macho ya vipofu yatafunguliwa, viziwi watasikia, ndimi za bubu zitalegezwa, na vilema wataruka-ruka kwa furaha! Taswira ya utukufu ilioje! Wale ambao hawajawahi kuona nuru, watautazama utukufu wa Bwana! Wale ambao hawajawahi kusikia sauti, sasa wanasikiliza nyimbo tukufu za vinubi vya malaika, na uimbaji wa watakatifu! Msisimuko ulioje! Furaha ilioje! “Naye Mungu atafuta kila chozi katika macho yao; wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena: kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” (Ufu. 21:4.) {SR2: 263.1}

“Angalieni, nawaambia ninyi siri; Hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilishwa. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa … Hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.” (I Kor. 15:51-54.) {SR2: 263.2}

Watakatifu walio hai wanaposhuhudia wafu wa vizazi vyote wakiinuka kutoka kwa vitanda vyao vya mavumbini, wataleta furaha isiyoelezeka. Wakati huo kuona marafiki na wapendwa wakikutana, wakiwa wamevikwa miili yenye utukufu isiyoweza kuharibika, wakitembea angani kupitia sayari zisizo na dhambi, na mwishowe kuingia katika Mbingu za mbingu! Msafara mtukufu ulioje wa viumbe visivyo kufa — watakatifu na malaika, na Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, “Baba wa milele, na Mfalme wa Amani,” kati yao! Wakiruka kwa kasi kutoka kwa dunia iliyolaaniwa kwa dhambi kwenda Kitovu cha vituo katika siku “saba” tu, ilhali itachukua “nuru” mamilioni ya miaka kufanya safari ya umbali usiowazika kama huo! Je! Unaweza kutambua chombo kinachokwenda kwa kasi sana kama hiki! Mungu akataza kwamba tusijinyang’anye utukufu kama huu. Kuishi muda wa saa moja mbinguni, bila dhambi, maumivu au machozi, hofu au kifo, ni wa thamani zaidi ya miaka elfu moja katika maskani za uovu. {SR2: 263.3}

Ndugu zangu, kutii Neno la Mungu, na kuwa waaminifu kwa agizo kwa manufaa yenu wenyewe, si kudai mengi sana kutoka kwenu. Je! Mtaruhusu ubinafsi na dhambi iwanyang’anye taji ya uzima? Hekima yenu ya kibinadamu na maarifa ya kidunia yatathibitika kuwa meusi kama giza lenyewe, iwapo mtamruhusu adui mjanja awapore furaha ya mbinguni ambayo inapaswa kuwa yenu katika vizazi vyote vya milele. {SR2: 263.4}

Ingawa kanisa la kwanza la Kikristo liliathiriwa kwa mateso ya kutisha, lilifanikiwa jinsi ya ajabu. Watu elfu tatu walioongoka siku ya Pentekoste “kwa wale waliokuwa wakiokolewa,” ilikuwa ajabu kuona. Lakini ukuaji haraka wa sehemu ya kwanza ya kanisa, ikilinganishwa na sehemu ya pili na ya mwisho itakuwa kama

264

si kitu, kwa mujibu wa ule mfano. Kwa hivyo, lilo hilo linathibitishwa na Neno la Mungu la kinabii kupitia nabii Zekaria, na jinsi utabiri huo uliunganishwa na ujenzi wa hekalu la pili, au na mfano wa sehemu ya pili ya kanisa, ambayo tunazungumzia haswa kwa wakati huu, matumizi ya Maandiko yafuatayo lazima yawe sahihi: {SR2: 263.5}

“Imba ufurahi, Ee binti Zayuni: maana, tazama, Ninakuja, Nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku hiyo, nao watakuwa watu Wangu; nami Nitakaa kati yako.” (Zek. 2:10, 11.) “Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu [kanisa bila kutaja eneo] kumtafuta Bwana wa majeshi na kuomba fadhili za Bwana.” (Zek. 8:22.) “Malango yako nayo yatakuwa wazi daima: hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri [pambizo, mapato] wa Mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.” (Isa. 60:11.) “Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote, asema Bwana, mafungu mawili ndani yake yatakatiliwa mbali nao watakufa; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami Nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami Nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo: wataliitia jina Langu, nami Nitawasikia: Mimi nitasema, watu hawa ndio Wangu: nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.” (Zek. 13:8, 9.) {SR2: 264.1}

Je! Ni kitu gani waongofu elfu tatu kwa siku moja kulinganisha na theluthi moja ya watu waliookolewa wa kizazi hiki cha sasa! Waliokusanywa ndani wakati wa masaa ya mwisho ya muda wa rehema! Kwa kweli wakati huo, itasemwa, utukufu wa hekalu la kwanza, au sehemu ya kwanza ya kanisa, ulikuwa kama si kitu ukilinganishwa na ule wa ya pili. Sehemu ya mwisho ya kanisa katika wakati wa “kilio kikuu” kwa kweli ni wakati wa mavuno na mwisho wa dunia. {SR2: 264.2}

Kanisa la kwanza la Kikristo lilikuwa kanisa lililoongoka la haki; hata hivyo magugu na ngano yalipaswa kukua pamoja “hadi wakati wa mavuno.” (Mat. 13:30.) Maneno haya, “hadi wakati wa mavuno,” hayawezi kuwa makosa; kwa hivyo, mwanzoni mwa mavuno mtengo utafanyika. Kwa hivyo kanisa katika wakati wa “kilio kikuu” litakuwa kanisa safi na takatifu, lisilo na doa, wala kunyanzi, au kitu chochote kama hicho: kanisa bila uongo. Iwapo taarifa iliyotangulia ni sahihi basi iyo hiyo lazima ipatikane katika Neno la Mungu la unabii. {SR2: 264.3}

Ndugu zangu ninawasihi msikie sauti ya Mchungaji Mwema: “Amka, amka; jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu: kwa maana tokea sasa [tangu sasa na kuendelea] hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; uondoke, uketi, Ee Yerusalemu: jifungulie vifungo

265

vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa.” (Isa. 52:1, 2; A.R.V.) Kwa sababu maneno haya ni wazi kabisa, tunawezaje kuyatilia shaka, au kupotosha maana yake? — Lazima iwe kwamba kanisa la Mungu limelala mavumbini! Mungu wako anakuita, Ee Zayuni. Kanisa la Mungu, “ndicho chombo pekee juu ya nchi ambacho Yeye huweka heshima Yake kuu” liko utumwani; limefungwa na “shingo” lake kwa “watu wa maneno laini na hotuba nzuri. “Sikia Maneno ya Mungu wako, Ee Zayuni, inuka na uketi juu ya kiti chako cha enzi kwa maana utawahukumu mataifa. Kwa nini uufanye mwili kuwa kinga yako? Je! Mungu wako hawezi kukuokoa? Je! “Neno la Mungu wako si hai, tena lina nguvu, tena lina makali kuliko upanga ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo?” “Kwa ajili ya Zayuni Sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu Sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.” Ndugu zangu, “Piteni, piteni katika malango; itengenezeni njia ya watu; tutieni, tutieni barabara kuu; toeni mawe yake; twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.” (Isa. 62:1, 10.) {SR2: 264.4}

“Mabaki ya Israeli [watu 144,000] hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao: kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” (Zef. 3:13.) “Siku hiyo katika njuga za farasi [wale wanaopeleka injili] yataandikwa maneno haya watakatifu kwa Bwana; navyo vyombo [wanaomiliki kweli] vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu [safi na visivyo na unajisi]. Naam, kila chombo katika Yerusalemu [kanisa] na katika Yuda [sehemu inayoongoza ya kanisa] kitakuwa kitakatifu kwa Bwana wa majeshi, nao wote watoao dhabihu [sadaka] watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake [wale wanaohudumu katika mambo matakatifu], wala katika siku hiyo hatakuwamo tena Mkanaani [asiye mwongofu] ndani ya nyumba ya Bwana wa majeshi.” (Zek. 14:20, 21.) Hili ndilo kanisa ambalo huwakilishwa katika Ufunuo 12:17, “Wanaoshika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.” Yule “mwanamke” huwakilisha kanisa kama mwili. “Mabaki ya uzao wake” ni watu 144,000 ambao joka anafanya vita dhidi yao. Vita vinafanywa dhidi yao, kwa sababu wao ni viongozi wa duniani na waasisi wa vuguvugu hilo. “Wa uzao wake” huashiria kwamba wao ni sehemu ya “mwanamke,” au kwa maneno mengine, watu 144,000, na umati mkubwa, ni vuguvugu moja tu — familia moja. {SR2: 265.1}

Kwa watakatifu wa kanisa hili takatifu baraka hutangazwa: “Heri wazitendao amri Zake, wawe na haki kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” (Ufu. 22:14.) {SR2: 265.2}

266

Yakobo, baba wa Israeli wa kweli katika mfano, aliota ndoto njiani akienda Padan-Aramu, “Na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni: tena tazama malaika wa Mungu wanapanda na kushuka juu yake. Naye akaogopa, akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.” (Mwa. 28:12, 17.) Ndoto ya Yakobo ilikuwa ya kinabii wa wakati ambapo kutakuwa na uhusiano kamili na mawasiliano ya daima kati ya mbingu na dunia — “kilio kikuu” cha ujumbe wa malaika wa tatu — wakati wa mavuno. Kwa kanisa hilo tukufu maneno haya hutumika: “Hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.” Ni kwa utangazwaji wa injili kupitia hiyo nyumba ya Kiroho tu ndipo Mungu anaweza kuwaokoa watu Wake. Litakuwapo zizi Moja, Mchungaji Mmoja, Bwana Mmoja, Ukweli Mmoja wa kukumbatia, wokovu Mmoja wa kupokea, njia Moja ya kusafiri, lango Moja la kupitia, msafara Mmoja wa kuchukua, na wakati Mmoja wa kuondoka, Mbingu Moja ya kuingia, watu Wamoja, na familia Moja takatifu. Haiwezi kuwapo njia nyingine! {SR2: 266.1}

“Haiwezekani kutoa wazo lolote la uzoefu wa watu wa Mungu ambao watakuwa hai duniani wakati utukufu wa mbinguni na marudio ya mateso ya zamani yamechangamana. Watatembea katika nuru inayotoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Kwa njia ya malaika kutakuwa na mawasiliano ya daima kati ya mbingu na nchi.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 9, uk. 16. {SR2: 266.2}

Wakati Wa Kulijenga Hekalu La Uakisi (Kanisa)

Tulielezea kwa sehemu kwamba yale mahekalu mawili halisi, yaliyojengwa mtawalia katika Yerusalemu wa zamani, yalikuwa mifano ya sehemu mbili za kanisa la Kikristo. Tofauti kubwa halisi na ya kiroho ya majengo haya miwili ya mfano ilifafanuliwa kwa kulinganisha kwa mifano na uakisi. Ingawa tungeweza kuipanua sana mada hii, tumeondoa maandiko mengi kwa kuelezea kweli kwa ufupi, tukijaribu kuchora kwa kalamu picha kamili ya somo hili muhimu kwa Jumuiya ya Wakristo. {SR2: 266.3}

Swali lililo mbele yetu ni, lini uakisi utakutana na utimizo wake kamili? Katika aya zilizotangulia ilifafanuliwa kwamba sehemu ya kwanza ya kanisa la Kikristo ilikoma mwaka 538 B.K.; na ya pili lazima ianze baada ya mwaka 1798 B.K., wakati huo yule “mwanamke” alipaswa kurejea kutoka nyikani. {SR2: 266.4}

Uchunguzi wa karibu wa mfano huo ndio njia pekee inayowezekana kuweka wazi ukweli, sio tu wa swali lililotangulia, lakini pia wa yanayofuata: Iwapo yule “mwanamke” angerejea kutoka nyikani hadi katika shamba la mizabibu (ustaarabu) baada ya kukoma kipindi cha kinabii cha miaka 1260, nini kilichotokea mwaka 1798 kuthibitisha kwamba “yeye” alirejea

267

katika mwaka huo? Maadamu kufungwa gerezani na kifo cha papa hujibu upande mmoja wa hilo swali na kutatua mwisho wa hicho kipindi cha kinabii, ishara i wapi kuonyesha kwamba yule “mwanamke” alirejea kutoka nyikani? Iwapo ufasiri uliokubalika wa yule “mwanamke” ni nembo ya kanisa, na ikiwa alikuwa “nyikani “ kutoka mwaka 538 B.K. hadi mwaka 1798 B.K., vipi kuhusu yale madhehebu manne makuu ambayo yaliinuliwa kabla ya wakati huo; yaani, Walutheri, Wapresbiteri, Wamethodisti, na Wabaptisti? Je! Hawakuwa yule “mwanamke” (kanisa)? Wanafunzi wa Biblia wameshindwa kutatua fumbo hili kwa sababu ya wao kukosa nuru kwa Neno la Mungu. Kurunzi kuu ya upekuzi kwa uwezo wa Roho inayoangaza kupitia kwa hiyo mifano, ndiyo njia pekee inayoweza kuondoa kizuizi na kuisafisha njia kufahamu siri hizi na zingine nyingi ambazo zinafikiriwa hazieleweki na ambazo zinakanganya akili za mwanadamu. Kwa hivyo, lile hekalu la mfano wa kanisa (mwanamke) ndiyo njia pekee ambayo kwayo maswali haya yanaweza kujibiwa. {SR2: 266.5}

Yale “mahekalu” na yule “mwanamke” huwakilisha kanisa kama mwili; au kwa maneno mengine, nembo ya yule mwanamke ni ufunuo wa ile mifano (mahekalu), na yale mahekalu ni unabii wa nembo ya yule “mwanamke” — kanisa. Itatambulika kwamba washiriki mbali mbali wa kanisa hilo huwakilishwa na mseto wa vitu vya yale mahekalu: “Ninyi nanyi kama mawe yaliyo hai mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.” (1 Petro 2:5.) “Vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.” (Rum. 12:5.) “Katika Yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.” (Efe. 2:21.) Kwa hivyo, haya mahekalu mawili huwakilisha — kanisa, na Kristo. Kristo Kuhani wetu Mkuu, hufananishwa na “jiwe kuu la pembeni,” na utumishi Wake wa ukuhani kwa utumishi wa sherehe au patakatifu pa haya mahekalu mawili sisisi. {SR2: 267.1}

Utumishi wa hekalu la duniani kwa ajili ya wokovu wa jamii ya wanadamu, katika mifano na nembo, hufunua utumishi wa Kristo ndani ya lile la mbinguni. Ambao uliundwa kwa sheria mbili; yaani, “amri kumi” na “sheria za sherehe.” Mbao zile za amri kumi ziliwekwa ndani ya hilo sanduku la agano, na zile za sherehe au sheria ya Musa ziliwekwa kando ya sanduku la agano. (Tazama Kumb. 10:2; 31:26.) Mbona sheria mbili? Sheria ya maadili huonyesha wazi dhambi, “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” (Rum. 3:20.) “Kwa maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” (Rum. 4:15.) Lakini sheria ya sherehe “Iliongezwa kwa sababu ya makosa hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi” (Gal. 3:19.) Ambayo ilikuwa dawa ya kumponya mdhambi na kumweka huru kutoka kwa hukumu ya sheria ya maadili. Kristo

268

(huyo mzao) alipokuja, Aliichukua sheria hii ya maagizo (sheria ya Musa) “akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.” (Kol. 2:14.) Utumishi wa duniani wa sheria ya maagizo haukuweza kutoa uhai wenyewe, kwa sababu ulikuwa tu kivuli cha ule wa kweli. Kwa hivyo, wakati wa kusulubishwa kwa Kristo ulikoma na ule wa mbinguni, ambao wa duniani ulikuwa kivuli chake, ukaanza. Utumishi wa mahekalu yote mawili halisi ulifanana. {SR2: 267.2}

Kwa hivyo, mahekalu haya mawili ni mifano ya sehemu mbili za kanisa la Kikristo na utumishi wa hekalu la uakisi uliundwa kwa sheria hizi mbili — maadili na sherehe. Sehemu ya kwanza ya kanisa la Kikristo, tangu kusulubishwa hadi mwaka 538 B.K., walijaliwa hekalu kama hilo; yaani, walikuwa na maarifa kamili ya kazi katika lile la mbinguni hadi wakati huo na imani yao ilipatana na huduma yake. Lakini katika mwaka 538 B.K. imani ya utumishi huu mtakatifu ilitupwa nje ya kanisa, au jinsi Danieli anavyosema, “ilikanyagiwa chini ya miguu” (Dan. 8:13), na kubadilishwa na ukuhani wa upagani, pamoja na sheria za sherehe za upagani, na za maadili, au utumishi wa upapa, na ibada ya Jumapili. Kwa hivyo, jinsi hekalu la kwanza lilivyoashiria sehemu ya kwanza ya kanisa la kwanza la Kikristo na imani katika utumishi wa kweli ya patakatifu, vivyo hivyo, hekalu la pili limefananishwa na sehemu ya mwisho ya kanisa lilo hilo na imani katika utumishi wa patakatifu ambao utafanana na ule wa kwanza. {SR2: 268.1}

Ufafanuzi uliotangulia unajibu mojawapo wa maswali yetu. Makanisa ya Kiprotestanti yaliyoinuliwa kabla ya yule “mwanamke” kurejea kutoka nyikani yalikuwa katika giza kuu mintarafu utumishi wa patakatifu. Kwa hivyo, hayajawakilishwa na yule “mwanamke,” au na lile “hekalu,” kwa maana, jinsi tulivyoeleza awali, yale mahekalu ya mfano huwakilisha sehemu zote mbili za kanisa na sheria mbili takatifu; yaani, za maadili na za sherehe. Kwa hivyo yule “mwanamke” huwakilisha kanisa linalozishika “amri za Mungu — sheria ya maadili, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo” — sheria ya sherehe au mpango wa wokovu uliofunuliwa katika nuru ya “Roho ya Unabii.” (Ufu. 12:17.) Wana-matengenezo, kabla yule “mwanamke” kurejea kutoka nyikani, waliitwa na Mungu kama hatua ya matayarisho ya kumrudisha katika “shamba la mizabibu”; yaani, kuusimamisha utumishi wa kweli wa hekalu la uakisi — ibada ya kweli ya kanisa. {SR2: 268.2}

Hekalu la Sulemani lilipoporwa vyombo vitakatifu na kuharibiwa na Nebukadnezza mfalme wa Babeli, Babeli ya kale ikawa mfano; na lau isingekuwa hivyo, haingekuwapo Babeli mamboleo — ya uakisi. (Ufu. 18:2.) Kwa sababu hakuna ubishi juu ya Babeli hizi ni nani, si vigumu kufichua siri hiyo; na uthibitisho wa moja pia utaiweka wazi ile nyingine. Iwapo hilo dai katika uchambuzi huu ni sahihi kwamba hekalu la Sulemani

269

Ukurasa Mtupu

270

[Chati: Yale Mahekalu Mawili Katika Mfano Na Uakisi]

271

lilikuwa mfano wa sehemu ya kwanza ya kanisa la Kikristo, basi lazima uwepo ulinganisho kamili kwa mfano na uakisi. {SR2: 268.3}

Jinsi mfano ulivyoangamiza mfano, kwa hivyo uakisi lazima umeangamiza uakisi; yaani, Babeli ya zamani (mfano wa upapa) ililipora na kuliharibu hekalu la Sulemani (mfano wa kanisa la kwanza la Kikristo) na kupeleka Israeli utumwani. Unabii huu wa mfano ulikutana na utimizo wake kamili mwaka 538 B.K. wakati upapa ulipotokea na kuliharibu kanisa (la Kikristo), ukawanyanganya ukweli, na kuwaongoza wafuasi wa Kristo utumwani (chini ya utawala wa upapa). Jinsi ibada ya kweli ya patakatifu iliondolewa na Babeli ya zamani wakati Israeli ilitekwa nyara, pamoja na uharibifu wa hekalu, hivyo ndivyo upapa ulivyouondoa ukweli na kimkakati ukabadilisha hapa duniani, maana ya kazi ya upatanisho ya Kristo katika hekalu la mbinguni, ambayo mfumo wa sherehe za hekalu la kwanza ulikuwa mfano katika kipindi kabla ya hukumu kuanza. Hivyo hekalu la pili huwakilisha ule wakati hukumu ilikuwa ikiendelea. Na jinsi vyombo vitakatifu vilibebwa kutoka ndani ya na kuwekwa katika hekalu la kipagani katika nchi ya wapagani, hivyo ndivyo upapa ulikanyagia chini chini “ukweli” na kusimamisha ukuhani wa kipagani katika kinachoitwa eti kanisa la Kikristo katika vizazi vya giza, wakati yule “mwanamke” alikuwa nyikani, ambayo nchi ya kipagani — Babeli ilikuwa mfano wake. {SR2: 271.1}

Sanjari yetu ya pili ni anguko la ufalme wa Babeli kwa ushindi wa wafalme wa Umedi na Uajemi. Ikumbukwe kwamba katika usiku wa karamu ya ulevi wa Belshaza, Koreshi na Dario waliuteka huo ufalme na kumwua mfalme. Utimizo wa huo mfano katika uakisi, ambao hulinganishwa na Papa kufungwa jela mwaka 1798 B.K., na kufuatwa na mauti yake. Kwa hivyo kifo cha Belshaza ambaye alimkaidi Mungu wa mbingu na nchi, ni mfano wa papa ambaye alikufuru kwa “wakati, nyakati mbili na nusu wakati,” akitimiza Danieli 7:25 na Ufunuo 13:10. Wakati huo miaka 1260 ya kinabii ya safari ya yule “mwanamke” nyikani ilikoma. {SR2: 271.2}

Tena tunarejelea mfano huo. Kwa kifo cha Belshaza utekwaji wa watu wa Mungu ulikoma na wakawekwa huru; hili hulingana na kikomo cha miaka 1260 ya mateso dhidi ya watu wa Mungu na upapa — kanisa na serikali. Anguko la ufalme wa Babeli halikuwa kitu kilichojenga hekalu huko Yerusalemu, bali lilikuwa hatua ya matayarisho ya ujenzi wake. Jinsi kifo cha Belshaza kilikuwa hatua ya matayarisho kuelekea kuanzishwa kwa ibada ya kweli hekaluni, vivyo hivyo kifo cha papa kilikuwa hatua ya maandalizi kuelekea kuanzishwa kwa ibada ya kweli ya kanisa. Iwapo ni hivyo, basi mfano huo huonyesha wazi kwamba hakuna kitu ambacho kingekuwa kimetukia kwa kanisa mwaka 1798 B.K. kuashiria

272

kwamba yule “mwanamke” alikuwa amerejea kutoka nyikani. Hili linatuleta kwa sanjari ya tatu. {SR2: 271.3}

Koreshi alikuwa mwabudu wa kipagani wakati alipouteka Babeli; lakini mawazo yake yakaelekezwa kwa utimizo wa Maandiko, na akaonyeshwa kwamba jina lake liliandikwa katika lile gombo takatifu miaka mingi kabla ya kuzaliwa kwake, na ya kwamba alikuwa ameyatimiza maneno ya nabii Isaya: “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi Wake, ambaye Nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake; Nami nitalegeza viuno vya wafalme, ili kufungua malango mbele yake; hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza: Nitavunja vipande vipande malango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma: Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa Mimi, Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam Mungu wa Israeli… Nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua.” (Isa. 45:1-4.) “Nimwambiaye Koreshi, yeye ni mchungaji Wangu, naye atayatenda mapenzi Yangu: hata ataunena Yerusalemu, utajengwa; na hilo hekalu, msingi Wako utawekwa.” (Isa. 44:28.) {SR2: 272.1}

Kwa hivyo moyo wake wa upagani ulibadilishwa, na kwa shukrani aliandika maneno haya: “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi, Bwana Mungu wa mbinguni amenipa falme zote za dunia; Naye ameniamuru nimjengee nyumba huko Yerusalemu uliyoko katika Yuda.” (Ezra 1:2.) Baada ya kuongoka kwake alitambua kwamba ibada ya kipagani huko Babeli ilikuwa ya uongo. Kwa hiyo, akatangaza katika eneo lote la Babeli: “Bwana Mungu wa Israeli, Ndiye Mungu, aliye Yerusalemu…Tena Koreshi mfalme alivitoa vyombo vya nyumba ya Bwana, alivyokuwa amevileta Nebukadnezza toka Yerusalemu, na kuvitia katika nyumba ya miungu yake; Naam vyombo vile ndivyo alivyovitoa Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, naye akavihesabu mbele ya Sheshbaza, mkuu wa Yuda.” (Ezra 1:3, 7, 8.) Kwa hivyo ibada ya kipagani ya Babeli ilitangazwa kuwa ya uongo muda fulani baada ya kifo cha Belshazza na anguko la milki yake. Kwa hiyo, Koreshi alitoa amri ya kujenga nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mambo mengi hivyo kwa huo mfano, sasa umakini wetu unageuzwa kwa utimizo wake katika uakisi. {SR2: 272.2}

Kulingana na mfano huo, ni lazima tutafute tangazo wakati fulani baada ya mwaka 1798 B.K. ambalo litapiga chapa yanayoitwa eti makanisa ya Kikristo kama Babeli na ibada yao ya uongo. Hivi ndivyo ilivyotokea. Mara tu baada ya mwaka 1844 B.K. ujumbe wa malaika wa pili wa Ufunuo 14:8 ulitangazwa, ukisema: “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Kwa hiyo,

273

ni dhahiri kwamba nuru inayoangaza kupitia hiyo mifano ndio njia pekee inayoweza kufafanua haya mafumbo ya kinabii katika Neno la Mungu. Pamoja na tangazo la anguko la Babeli, ilitangazwa kwamba zile zinazoitwa eti sherehe za Kikristo, kama utunzaji wa Jumapili, Krismasi, na Pasaka, pia ubatizo wa kunyunyizia maji, na mafundisho mengine ya uongo hayakuwa ya kibiblia na yalikuwa asili ya kipagani. Lakini jinsi Babeli ya zamani ilivyoshindwa kuachana na mfumo wa kipagani wa kuabudu, na kuchukua ibada ya Mungu pekee wa kweli, vivyo hivyo, Ukristo mamboleo umekataa kufanya matengenezo au kuacha mazoea haya. Kazi ya kweli ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, pamoja na Sabato ya siku ya Saba jinsi ilivyofundishwa wakati huo, pia haijazingatiwa! {SR2: 272.3}

Amri Tatu Zilitolewa Kabla Ya Hekalu Kujengwa

Ingawa Koreshi alitoa kwa hiari rasilimali zake kufadhili ujenzi wa nyumba ya Mungu na utumishi wake mtakatifu, na kwa mamlaka akaamuru kwamba lazima ijengwe, Wasamaria, au Wayahudi wa kutia fitina, walivuruga maendeleo ya msingi na wakazuia kukamilishwa kwake. Kwa hivyo, ingawa ujumbe (amri) mwaka 1844 ulitangazwa kuijenga nyumba ya Mungu na kurejesha ibada ya kweli kulingana na sheria na manabii, huo mfano huonyesha kwamba maendeleo yamevurugwa, na kukamilishwa kwake kumezuiliwa na Wayahudi wenye fitina — Waadventista Wasabato wasio wa kweli. Ukweli huu umesemwa wazi wazi katika “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 217: {SR2: 273.1}

“Nimejaa huzuni wakati ninapowaza hali yetu kama watu. Bwana hajaifunga Mbingu kwetu, lakini mwenendo wetu wa kuendelea kurudi nyuma umetutenga na Mungu. Kiburi, tamaa, na kuipenda dunia vimeiishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kuhukumiwa… Kanisa limegeuka nyuma na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na aste aste linarudi kuelekea Misri. Hata sasa wachache wameshtuka au kushangazwa kwa ukosefu wao wa nguvu za kiroho.” {SR2: 273.2}

Shutuma Za Uongo Na Visingizio

Hawa Wasabato ambao hawajaongoka wanapoambiwa kweli hizi, kutozilaumu au kutozitafutia makosa, bali kuwaamsha kutoka kwa udanganyifu wa kupumbaza wa kutisha na usalama bandia, wanaanza kutoa visingizio kwa namna ifuatayo: “Sisi ni watu wa Mungu.” “Hili ni kanisa la Mungu.” “Hakuna vuguvugu lingine la kufuata. “ Ni uovu kulitia hatiani kanisa lililo vitani.” “Unaweka wakati.” “Haupaswi kubomoa bali ujenge.” “Waepuke wale wanaofanya migawanyiko.” “Hawatakuwapo manabii zaidi.” “Tuna ukweli wote na hatuna haja ya zaidi.” {SR2: 273.3}

274

Ndugu zangu, jinsi ambavyo mmezitunza taa zenu, je! hamtajipatia “mafuta ya ziada” (ukweli), na kutenda kama watu wanaomtazamia Bwana wao aje? Hakuna mtu anayekana ukweli kwamba ninyi ni watu wa Mungu, lakini mkumbuke kwamba Wayahudi pia wakati mmoja walikuwa watu Wake. Hakuna anayetaka kuthibitisha kuwa hili si kanisa la Mungu, lakini je! huu ndio wakati pekee ambao Yeye amewahi kuwa na kanisa? Hatudai kwamba lipo vuguvugu lingine la kufuata. Lakini je! Neno la “Shahidi wa Kweli” halisemi, “Nitakutapika utoke katika kinywa Changu?” Iwapo kuliita kanisa lililo vitani katika matengenezo ili wayapake macho yao dawa ya macho waweze kuona, ili aibu ya uchi wao isionekane, ni uovu jinsi mnavyosema, basi mwanena dhidi ya nani? Na ni njia gani zingine Yeye anaweza kutumia kuiita hali hii “mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu” ya Ulaodekia, itubu? “Nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi?” {SR2: 274.1}

Je! Ni yule anayeitisha utiifu kwa ukweli kulingana na Neno la Mungu anayebomoa au ni wale ambao wamevunja kila kanuni ya ukweli wa ujumbe tunaotangaza? Nani amesababisha migawanyiko? Je! Ni yeye anayeitisha utiifu kwa Neno, au yule anayekataa kusikia mwito kutoka Mbinguni? Je! Mnakumbuka kwamba kanisa la Kikristo liligawanyika katika sehemu saba za matengenezo kwa sababu jumbe zilikataliwa? Je! Ni nani anayepaswa “kuepukwa?” Je! Ni yeye anayeupokea ukweli bila kujali unakuja kutokea wapi, au yule anayeruhusu chuki bila sababu kuzuia akili zake zisiupokee ukweli? Huwa mnadai ya kwamba mna ukweli wote, na ya kwamba hakuna hitaji la wowote, ni kukana kila neno lililoandikiwa kanisa. Ni kukataa mapema kila ujumbe wa ukweli au nuru ambayo Mungu anaweza kuchagua kutuma. Ni kumfungia Mungu nje, na kulikata kanisa kabisa kutoka kwa mkono Wake ulionyooshwa. Ni hatua ya matayarisho kuelekea kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. Madai yenu kwamba hakutakuwa na manabii tena, ni kutupilia mbali mapema mvua ya masika na “kilio kikuu!” Ni kukataa Neno katika umbo lake la kinabii, kwa maana tunasoma: “Hata itakuwa baada ya hayo, ya kwamba Nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume kwa wake watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.” (Yoeli 2:28.) {SR2: 274.2}

Ndugu zangu kuna kitu cha kuogofya kama tabia hii isiyo ya kiungu inayotendwa na watu ambao wanapaswa kuwa walinzi kwenye kuta za Zayuni? Iwapo mnajihesabu kuwa hamstahili ufalme wa milele, je! hamtaiondoa mikono yenu katika kanisa la Mungu? Je! Hamtatoa uhuru wa kidini kwa kondoo na mwaache wafanye uamuzi wao wenyewe? Mbona msitende kama mtakavyo wengine wawatendeeni? Ni vigumu kwenu kuwa

275

wakaidi. Je! Hamtasema, Bwana unataka tufanye nini? Je! Mwajua kwamba damu ya kondoo waliopotea itatakikana mikononi mwenu? {SR2: 274.3}

Shutuma zenu dhidi ya kuweka wakati ni kama mtu anayezungumza akiwa hana fahamu. Ni wakati gani halisi umewekwa? Je! Mnamaanisha Ezekieli, sura ya nne? Iwapo ndivyo hamtaichunguza mada hiyo kwa ukaribu kidogo kuliko ambavyo mmefanya na mwone inasema nini? Je! Hamwoni kwamba hicho kipindi cha unabii kilikuwa tayari kimekoma wakati taarifa hiyo ilipofanywa? Au mnamaanisha kusema kwamba Mungu hajui urefu wa muda kutoka kwa tukio moja hadi kwa lingine, na ya kwamba Yeye lazima asiuweke katika Biblia? Je! Hamwoni kwamba sanjari zilizorekodiwa katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 112, 113, huthibitisha ufasiri wa Ezekieli nne kuwa sahihi, au ukweli usingekuwa umekuja? {SR2: 275.1}

Pia mtaona kwa ukurasa wa 222, kwamba miaka 430 ya kinabii iliyotumika mwanzoni kwa Abrahamu na uzao wake, hulaliana na ile 430 ya Ezekieli 4. Miaka 430 ya Ezekieli inapaswa kukoma katika mwaka 1929, au 1930 lakini utimilifu kamili wa kipindi cha unabii cha Abrahamu katika uakisi wake bado kiko mbele (kutoka Misri). Chati iliyo kwa ukurasa wa 112, 113, huonyesha kikomo chake katika mwaka 1930, kwa maana jinsi tulivyosema hapo awali, kimeorodheshwa na hizo sanjari ambazo zinafaa kabisa unabii wa Ezekieli. Kwa vile haiwezekani kufanza chati ya wakati bila tarehe yoyote kupita, tumetumia sanjari hizi, na imetajwa waziwazi kwamba tarehe hiyo sio dhahiri. (Tazama chati kwa ukurasa wa 133.) Unabii wa Ezekieli umekusudiwa kuonyesha mbele hadi kwa tangazo la matengenezo yaliyotabiriwa, na ule kupitia Abrahamu, hadi kwa kikamilisho chake (Ezekieli tisa). {SR2: 275.2}

“Na hao waonaji watatahayarika, na wenye kubashiri watafadhaika: naam hao wote watajifunika midomo yao; kwa maana hapana jawabu la Mungu. Bali mimi hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana, nimejaa hukumu, na uwezo, nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Wanaijenga Zayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha. Ila hata hivyo watamtegemea Bwana, na kusema, Je! Hayupo Bwana katikati yetu? Hapana neno ovu lolote litakalotufikia. Basi kwa ajili yenu Zayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.” (Mika 3:7-12.) {SR2: 275.3}

Pingamizi Dhidi Ya Ile Njia Mungu Anaweza Kutumia

Historia huthibitisha kwamba wengi wameinuka dhidi ya njia ambayo Mungu ametumia kufunua Neno Lake Takatifu. Ndivyo ilivyo sasa. Wengine husema:

276

“Iwapo Mungu atanena kwa watu wake, Anaweza kufanya hivyo kupitia kwa mmoja wa watu wetu viongozi.” Hilo laweza kuwa hivyo, lakini ushahidi u wapi kwamba Yeye hawezi kukiita chombo kinyenyekevu zaidi kutoka kwa kundi la kondoo Wake? Kweli za kihistoria huthibitisha kwamba Yeye ni nadra kujifunua kupitia kwa watu wakuu. Mbona Yeye abadilishe njia Yake sasa? Wengine huwaza dhidi ya watumwa wa Mungu kwa sababu ya kuonekana kwao kwa nje, asili ya kuzaliwa kwao, au lahaja za asili ya lugha, n.k. Ndugu zangu, je! mtamwekea mpaka Baba na Muumba wa jamii ya wanadamu kwa vizuizi vyenu vya taifa, mtu au nchi, kwa mawazo yenu finyu na hekima yenye majivuno ya ubinafsi? Moyo ambao huwaza theolojia kama hizo zisizo za akili kwa kujiona bora, ni kama yule mfarisayo mwenye kiburi kwa ulinganisho na mtoza ushuru aliyetubu. Hawa wana-itikadi werevu na wa kujisifu ndio wasiojua kabisa, maana kwa kufanya hivyo, wao humruhusu baba wa kujiinua nafsi kuwapora uzima, na umilele. Wakati watu kama hao wamepofushwa kwa uharibifu wao wenyewe, ni wakala werevu na wa umuhimu kwa adui wa roho. Maana kwa kuporwa kwao huendeleza ushawishi usiokoma kama “kijiwe kilichotupwa ziwani; wimbi hufanyizwa, na lingine na lingine tena, na kadiri yanavyoongezeka, mduara hupanuka, hadi ufike ufuoni kabisa.” {SR2: 275.4}

Je! “Maneno yako ya uzima” yatakuwa na mvuto gani kwa wengine iwapo unafikiri heshima yako ni kubwa sana, na ya kwamba yao ni duni sana? Matendo yako yanazungumza zaidi kuliko maneno yako, yakiwaambia wanyonge wa kundi: Mtutazame sisi, na mujitazame kama si kitu. Ikiwa kitendo kibaya kimefanywa dhidi ya kondoo mmoja kwa kutoa ukweli usiopinda, wengine watatendewa vivyo hivyo. Kwa wachungaji kama hao maneno yafuatayo yamenenwa: {SR2: 276.1}

“Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona: lakini hamwalishi kondoo. Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.” (Eze. 34:3, 4.) {SR2: 276.2}

Amri Ya Pili Ya Kulijenga “Hekalu”

Kwa kukandamiza wapinzani wa Mungu walisitisha kazi ya amri ya kwanza. Lakini kwa wakati ufaao amri ya Koreshi iliofanywa upya na mfalme Dario, na “Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu: na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu wakiwasaidia.” (Ezra 5:2.) {SR2: 276.3}

Lakini ingawa amri hii ya pili ilikuwa na nguvu zaidi dhidi ya maadui wa hekalu, walifanya Wayahudi wasiendelee kwa uwezo wa

277

silaha. Ule mfano kwa amri ya pili bila kukosea hufichua kwamba kungekuwa na ujumbe mwingine baada ya mwaka 1844, ambao pamoja na mtajo wa ziada ungepaswa kutangaza — songa mbele kwa imani, jitahidi kulisimamisha kanisa safi na ibada ya kweli kwa kutii Neno la Mungu (haki kwa imani). Mfano huo pia hufichua kwamba ujumbe huu wa pili ungeshindwa na kazi kuvurugwa. Sasa angalia jinsi mfano huo hulingana, hufunua ukweli, na kuweka wazi mipango ya shetani. Katika mwaka 1888 ujumbe kama huo (amri) ulitoka, lakini viongozi wakati huo waliukataa jinsi ushuhuda ufuatao unavyothibitisha: “Bwana kwa huruma Yake kuu alituma ujumbe wa thamani sana kwa watu Wake. Ujumbe huu ulikuwa wa kuleta waziwazi kwa ulimwengu Mwokozi aliyeinuliwa, dhabihu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Uliwasilisha haki kwa njia ya imani katika Dhamana; uliwaalika watu waipokee haki ya Kristo, ambayo hudhihirishwa kwa kutii amri zote za Mungu. Wengi walikuwa wamemsahau Yesu.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 91. {SR2: 276.4}

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa uwezo wa Roho asema mjumbe: “Kamwe sitawahi, nafikiri, kuitwa tena kusimama chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu kama nilivyosimama Minneapolis. Uwepo wa Yesu ulikuwa pamoja nami. Wote waliokongamana katika mkutano huo walikuwa na fursa ya kujiweka upande wa ukweli kwa kumpokea Roho Mtakatifu, ambaye alitumwa na Mungu katika wimbi la utajiri wa upendo na rehema. Lakini ndani ya vyumba vilivyomilikiwa na baadhi ya watu wetu zilisikika dharau, kulaumu, kudhihaki, kufanya mzaha, kucheka. Udhihirisho wa Roho Mtakatifu ulidaiwa kuwa eti ushupavu wa kidini… Matukio yaliyofanyika kwa mkutano huo yalimfanya Mungu wa mbinguni aaibike kuwaita wale walioyashiriki ndugu Zake. Yote haya Mlinzi wa mbinguni aliyaona, na yakaandikwa katika kitabu cha Mungu cha ukumbusho.” — “Ushuhuda Maalum kwa Ofisi ya Mapitio na Kutangaza,” uk. 16, 17, ulioandikwa katika mwaka 1896. {SR2: 277.1}

“Waliianza kazi hii ya kishetani Minneapolis. Baadaye, walipoona na kuhisi wonyesho wa Roho Mtakatifu, akishuhudia kwamba ujumbe huo ulikuwa wa Mungu, waliuchukia zaidi, kwa sababu ulikuwa ni ushuhuda dhidi yao… Bado watu hawa wamekuwa wakishikilia nyadhifa za amana, na wamekuwa wakiielekeza kazi hiyo kulingana na mfano wao wenyewe, kadiri wawezavyo.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 80. {SR2: 277.2}

“Lakini iwapo … wanakuza roho ile ile iliyoutambulisha mwenendo wao kabla na baada ya mkutano wa Minneapolis, watajaza kikamilifu matendo ya wale ambao Kristo aliwashtumu Alipokuwa juu ya nchi. Hatari za siku za mwisho zimetujia. Soma Mathayo 25:14.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 79. Pia tunawasilisha ushuhuda ulioandikwa kutoka kwa shahidi aliyeona kwa macho: “Ujumbe

278

wa 1888 uliungwa mkono na Dada White kama ujumbe wa sasa… wachache kati ya viongozi waliutambua kuwa hivyo. Karibu wote kama kikosi waliasi, hata kudai kwamba watu hao walikuwa wamemshawishi isivyofaa Dada White kuwapendelea kwa uwezo fulani isioonekana, kwa hivyo walikataa Roho ya Unabii… Hawa watu wawili (Wazee Jones na Wagoner) na Dada White… walinyimwa kutumia hekalu kubwa… Kwa hivyo unaona sio tu (90%) lakini karibu (95%) ya viongozi wetu waliasi.”{SR2: 277.3}

Amri Ya Tatu Ya Kulijenga “Hekalu”

Kwa sababu amri ya kwanza na ya pili ya wafalme wa Umedi na Uajemi zilishindwa kukamilisha ujenzi wa hekalu na kurejesha utumishi mtakatifu wa mfano, amri ya tatu iliwekwa, kisha mfalme akaongeza: “Pia nimetoa amri, kwamba mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe, na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili. Na Mungu huyu aliyelifanya jina lake likae pale na aangamize wafalme wote na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili na kuiharibu nyumba hii ya Mungu iliyoko Yerusalemu. Mimi Dario nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi… Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa kwa msaada wa kuhubiri kwao Haggai nabii na Zekaria mwana wa Iddo. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi. Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario.” (Ezra 6:11-15.) {SR2: 278.1}

Itagunduliwa kwamba amri ya tatu ilitishia maisha ya watu na mataifa yasiokuwa aminifu: “Mtu awaye yote atakayelibadili neno hili,” alisema mfalme, “nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.” Mengi sana kwa huo mfano. Sasa tunakuja kwa uakisi. Mfano huo huonyesha kwamba ujumbe wa 1844 na 1888 unapaswa kufuatwa na ule wa tatu. Lakini kulingana na huo mfano, ujumbe wa tatu unapaswa kuwa mkali. Ujumbe ambao utadai utiifu na kutekelezwa hukumu kuu juu ya wale ambao watapinga amri yake. Na kwa mujibu wa mfano huo, ni ujumbe wa tatu ambao utatimiza utume wake. {SR2: 278.2}

Katika mwaka 1929 ujumbe kama huo ulikuja kwa kanisa la Waadventista wa Sabato, na uliandikwa na kuchapishwa mwaka 1930, kwa jina la heshima “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1. Na kwa sababu huo ujumbe ulikwenda kwa udada wote wa makanisa (mbali iwezekanavyo) kote duniani, yule mtu aliyevaa kitani, ambaye alikuwa na kidau cha wino wa mwandishi kiunoni, aliambiwa: “Pita kati ya

279

mji, kati ya Yerusalemu [kanisa], ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake [kanisani]. Na kwa hao wengine aliwaambia nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige: jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma: Waueni kabisa mzee na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake: lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu [Baraza]. Basi wakaanza kwa wazee [Wazee wa kanisa] waliokuwa mbele ya nyumba.” (Ezek. 9:4-6.) {SR2: 278.3}

Juu ya andiko hili ulijengwa msingi wa ujumbe, ukitangaza kinabii, kwamba watu 144,000 watatiwa alama, na waliosalia sasa kanisani lazima wakione cha mtema kuni isipokuwa watubu na kusonga mbele na ukweli wa Mungu. Lakini ingawa hakuna mmoja awaye yote wa dhehebu lote ameweza kupinga ukweli wa watu 144,000 kwa ujumla, au hata kwa sehemu, wala hawajathubutu kukanusha mashtaka juu ya machukizo yaliyokuzwa kati yao, wameinuka dhidi ya ujumbe na wanapendelea kushikilia machukizo yao jinsi maadui wa Mungu walivyopinga ujenzi wa hekalu hadi mwisho kabisa. Jinsi amri ya mfalme wa Umedi na Uajemi ilivyotangaza kwa maadui wa nyumba ya Mungu ikisema: “Mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.” Vivyo hivyo Neno la Mungu limetangaza sasa, “waueni kabisa mzee na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake.” Iwapo ujumbe kama huu hauwezi kuwashawishi watu wa Mungu kutenda vyema, basi ni nini kinachoweza kufanya hivyo? Walakini, jinsi kusudi la Mungu lilivyotekelezwa katika mfano huo, hivyo ndivyo itakavyokuwa katika uakisi. Inashangaza kutambua jinsi uakisi hulingana na mfano. {SR2: 279.1}

Hakukuwa na mabadiliko yaliyofanywa katika amri za Koreshi na kwa sababu zilikuwa urudiaji wa mara kwa mara ndivyo imekuwa kwa uakisi. Kwa hivyo hapawezi kuwapo mabadiliko yoyote kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu, bali nuru kubwa na uwezo utaongezwa kwake. “Ya kutisha ni kazi yake. Utume wake ni wa kuogofya. Yeye ndiye malaika atakayeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kufunga, ngano kwa ghala la mbinguni.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 118. {SR2: 279.2}

Wakati Wa Kulisimamisha Kanisa La Kweli

Katika Hagai 2:23, akinena juu ya ujenzi wa “mfano” (hekalu la pili) lakini akitazama mbele kinabii kwa utimizo wa uakisi (kanisa katika usafi wake), Neno la Mungu kupitia kwa nabii lilimjia Zerubabeli ambaye aliweka msingi wa ule mfano (hekalu), na ambaye Neno husema ni pete yenye muhuri

280

au ishara ya uakisi. Tunasoma kuhusu lile Mungu atafanya kwa wakati huo: {SR2: 279.3}

“Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi; Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, Nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; Nami nitatikisa mataifa yote, na tumaini la mataifa yote litakuja: Nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. Fedha ni mali Yangu, na dhahabu ni mali Yangu, asema Bwana wa majeshi. Utukufu wa nyumba hii ya mwisho utakuwa mkuu kuliko utukufu wa ile ya kwanza, asema Bwana wa majeshi: na katika mahali hapa Nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.” (Haggai 2:6-9.) {SR2: 280.1}

“Nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, Nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; Nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini, kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.” (Hag. 2:22.) {SR2: 280.2}

Ni dhahiri kwa Andiko hili kwamba kanisa hili tukufu litaanzishwa mwanzoni mwa mwisho wa historia ya ulimwengu huu wakati falme za dunia zitakapofikia kikomo. Akifasiri maono ya Zekaria, malaika alinena kumhusu Zerubabeli, akisema: “Mikono yake Zerubabeli imeuweka msingi wa nyumba hii; na mikono yake ndiyo itakayoimaliza.” (Zek. 4:9). Yaani, waasisi wa lile la uakisi ambao Zerubabeli alikuwa mfano wao, waliuweka msingi katika mwaka 1844. Zerubabeli akiwa ni “ishara” kwa uakisi (kwa kuuweka msingi na kuikamilisha ile nyumba), humaanisha kwamba kukamilishwa kwa nyumba ya kiroho (kukamilishwa kwa kanisa la Mungu — kuwahesabu watakatifu) kutatekelezwa katika kizazi kimoja (katika siku za maisha ya mwanadamu, kuanzia mwaka 1844.) {SR2: 280.3}

Nguvu Ya Watu Wa Mungu Kuijenga Nyumba Yake

“Bwana wa majeshi asema hivi; kama ukienda katika njia Zangu, na kama ukishika maagizo Yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba Yangu, nawe utazilinda nyua Zangu, Nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu. Sikiliza sasa, Ee Yoshua kuhani mkuu, wewe, na wenzako waketio mbele yako: maana hao ni watu walio ishara: kwa maana tazama, Ninamleta mtumishi Wangu aitwaye chipukizi.” (Zek. 3:7, 8.) “Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani: nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao, na hao wapandao farasi watafadhaishwa.” (Zek. 10:5.) {SR2: 280.4}

“Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Pigeni na kelele katika mlima Wangu mtakatifu. Wenyeji wote wa nchi na watetemeke: kwa maana siku ya Bwana inakuja. kwa sababu inakaribia; Siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu, kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima: hao ni wakuu tena wenye nguvu;

281

mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi. Moto unakula mbele yao: na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao limekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao. Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi, ndivyo wanavyopiga mbio. Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. Mbele yao watu wanahangaika: nyuso zote zimegeuka kuwa nyeusi kwa hofu. Watapiga mbio kama mashujaa; watapanda ukuta kama watu wa vita; nao wataendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawatazipotosha safu zao: Wala hapana mmoja atakayemsukuma mwenzake; wataendelea mbele kila mmoja katika njia yake: na watakapouangukia upanga, hawatajeruhiwa. Watakimbia huko na huko katika mji; watapiga mbio juu ya ukuta, watapanda na kuingia ndani ya nyumba; wataingilia madirishani kama aingiavyo mwivi. Nchi itatetemeka mbele yao; mbingu zitatetemeka: jua na mwezi utatiwa giza, na nyota kuacha kuangaza.” (Yoeli 2:1-10.) “Nchi,” “jua,” “mwezi,” na “nyota” hazina uhusiano wowote na Mat. 24:29. Ishara za kinabii za hizo sayari zilizotajwa zitapata utimizo wake kamili kabla ya kuanza kwa millenia. {SR2: 280.5}

Tokeo La Utiifu Kwa Neno La Mungu

“Bwana wa majeshi asema hivi; itatokea halafu ya, kwamba watakuja watu na wenyeji wa miji mingi: Na wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe mbele ya Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi: Mimi nami nitakwenda. Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba mbele ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi; Katika siku hizo itakuwa, ya kwamba watu kumi wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi, wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi: kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.” (Zek. 8:20-23.) {SR2: 281.1}

Maana ya “watu kumi” ni sawa na “wanawali kumi” wa Mathayo 25:1. Wanawali kumi huashiria kanisa kama mwili; na wale “watu” ki-mfano humaanisha wale ambao watafanywa waongofu kwa kanisa, na ya kwamba watatoka katika lugha, na mataifa yote. “Wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi;” yaani, yule ambaye ni Myahudi humwakilisha Kristo katika umbo la watakatifu Wake (watu 144,000), “nguo Yake”

282

huwakilisha ukweli au kanisa kwa ujumla, ambao watu 144,000 wamevikwa ki-mfano. {SR2: 281.2}

“Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote,asema Bwana, mafungu mawili yatakatiliwa mbali nao watakufa; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, Nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, Nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo: wataliitia jina Langu, nami Nitawasikia: Mimi nitasema, watu hawa ndio Wangu: nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.” (Zek. 13:8, 9.) {SR2: 282.1}

“Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa Mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.” (Isa. 60:11.) {SR2: 282.2}

283

ZEKARIA 4

Nembo za uakisi za hekalu la pili (mfano), zilionyeshwa kwa Zekaria katika maono na zikaandikwa katika sura ya nne ya unabii wake kama ifuatavyo: {SR2: 283.1}

“Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta kwa taa zote saba zilizo juu yake: Na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa lile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini? Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa Majeshi … Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yake? Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.” (Zek. 4:1-6, 12-14.) {SR2: 283.2}

Hivi neno la Mungu linawakilishwa na nembo hizi. Kwa hivyo, ufasiri wazo utafichua namna ya kuliwasilisha Neno la Mungu kwa Zerubabeli. Sio kwa Zerubabeli ambaye alihusika katika ujenzi wa hekalu la mfano, kwa maana alipewa maelekezo kwa njia ya mdomo na manabii Zekaria na Haggai. Kwa hivyo, kwa sababu maana ya nembo hizi za kinabii hawakuzielewa, lazima zitumike kwa wale ambao watashiriki katika kulijenga lile la uakisi, au hekalu la kiroho (kanisa), jinsi ilivyofafanuliwa hapo awali. {SR2: 283.3}

Kila mojawapo wa nembo hizi lazima zifasiriwe kwa ushahidi usiokinzana, na maana yazo lazima ifanyize mbinu ambayo Mungu ataliwasilisha Neno Lake kwa watumwa Wake. Imesemwa hapo awali kwamba vitabu vyote vya Biblia hukutana, na kwishia katika kitabu cha Ufunuo. Kwa hivyo, ufunuo wa unabii wa Zekaria lazima upatikane humo pia. {SR2: 283.4}

Tunanukuu: “Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa

284

saba: na vile vinara saba ni makanisa saba.” (Ufu. 1:20.) Itafahamika kwamba hizo jumbe kwa makanisa hayo saba hazijaelekezwa kwa vinara vya taa (kanisa kama mwili), bali kwa wale malaika, zikisema, “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika.” (Ufu. 3:14.) Malaika huyu si malaika wa mbinguni, kwa maana ana makosa — yu chini ya hukumu na karibu kutapikwa nje, isipokuwa atubu. Ndiye malaika anayekisimamia kile kinara cha taa (kanisa). Kwa hivyo, wale malaika saba humaanisha uongozi wa yale makanisa saba, na hivyo vinara vya taa ni nembo ya yale makanisa saba. Kwa hivyo, makanisa katika mfano huu huwakilishwa na vinara vya taa. Kwa hivyo, kile kinara cha taa katika maono ya Zekaria humaanisha kanisa kama mwili. {SR2: 283.5}

Ufunuo wa miti ya mizeituni hupatikana katika sura ya kumi na moja na kwa aya ya nne: “Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Bwana wa nchi.” Mizeituni na vinara vya taa ni mashahidi hao wawili. (Tazama Ufu. 11:3.) Zekaria pia husema kwamba “Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.” (Zek. 4:14.) Kwa hivyo, miti hii miwili ya mizeituni, na vinara viwili vya taa haviwezi kutenganishwa, kwa sababu vyote “vinasimama karibu na Bwana wa dunia yote.” Hivyo vinara viwili katika mfano huu huwakilisha kanisa la Mungu katika sehemu mbili, na kila moja ina mti wa mzeituni. Malaika alimfasiria Zekaria kwamba ni Neno la Mungu kwa Zerubabeli. Kwa hivyo, hivyo vinara viwili huwakilisha makanisa ya Agano la Kale na Jipya (la Kiyahudi na la Kikristo). Na hiyo miti miwili ya mizeituni ni nembo za Biblia ya Agano la Kale na Jipya (Neno la Mungu kwa Zerubabeli). Mashahidi hawa wawili “nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini (kutoka mwaka 538 B.K. hadi mwaka 1798 B.K.) hali wamevikwa magunia.” (Ufu. 11:3.) “Mashahidi hao wawili huwakilisha Maandiko ya Agano la Kale na Jipya.” — “Pambano Kuu,” uk. 267. {SR2: 284.1}

Kwa hivyo tuna kinara cha taa kwa kila moja ya sehemu mbili za kanisa la Mungu wakati Maandiko yalikuwa yanaandikwa. Kinara kimoja cha taa na mzeituni mmoja kwa lile la Kiyahudi, na kinara kimoja na mti mmoja wa mzeituni kwa lile la mitume, na saba kwa historia iliyobaki ya kanisa hadi wakati wa mtengo wa magugu kutoka kwa ngano, au hadi mwanzoni mwa mavuno. Kwa hivyo kile kinara cha taa (kanisa) katika maono ya Zekaria ni cha kumi, kumaanisha ni kanisa la ulimwengu wote; kuonyesha kanisa lililo hai ambalo litaungana na watakatifu wote tangu mwanzo wa ulimwengu — ambalo litajiunga na kanisa la dunia zote za Mungu! Kinara hiki katika maono ya Zekaria ni kile cha utukufu, ambacho kwa kulinganisha, vingine vyote husimama kama “si kitu” — kwa uwiano kamili na hekalu la pili, ambalo kwa kulinganisha la kwanza lilisimama kama “si kitu.” {SR2: 284.2}

285

Mabomba Mawili Ya Dhahabu

Ukweli basi, kinara cha taa huwakilisha kanisa, na miti miwili ya mizeituni Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Sasa, “Je! Haya mabomba mawili ya dhahabu ni nini,” ambayo “yenyewe hupitisha mafuta ya dhahabu?” Tunanukuu kutoka kwa “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 7, uk. 249: “Taa ya ndani lazima isambaziwe mafuta ambayo hutiririka kutoka kwa wajumbe wa mbinguni kupitia mabomba ya dhahabu hadi kwa bakuli la dhahabu. Mawasiliano ya Bwana hayaji kwa mwanadamu bure.” Kwa hivyo, yale mabomba mawili ya dhahabu ambayo hupitisha mafuta ya dhahabu hadi ndani ya bakuli la dhahabu ni wajumbe wa Mungu wa uvuvio ambao kupitia ndani yao ukweli wa sasa hufunuliwa, na wafasiri pekee wa kweli wa Maandiko. Mafuta huwakilisha Neno la Mungu lililofunuliwa kutoka kwa Biblia jinsi linavyofafanuliwa kupitia kwa watumwa Wake aliowateua, na bakuli husimulia machapisho ambayo mafunuo haya yamekusanywa. Huu ndio “Ushuhuda wa Yesu” — “Roho ya Unabii.” (Ufu. 12:17; 19:10.) Ufunuo ambao Yohana alipokea unaitwa “Ushuhuda wa Yesu.” (Tazama Ufu. 1:9.) Kwa hivyo, ushuhuda wa Yesu pia ni Roho ya Unabii, kwa sababu ushuhuda Wake umefunuliwa tu na Roho Mtakatifu kupitia njia ya kibinadamu. Kwa hivyo Maandiko yaliyofasiriwa na Uvuvio, ndio ushuhuda pekee ambao unaweza kuwa, “ushuhuda wa Yesu” — ukweli bila makosa. {SR2: 285.1}

Taa Saba

Iwapo kinara cha taa huwakilisha kanisa kama mwili, basi zile taa saba juu yake lazima zimaanishe udada wa makanisa yaliyotawanyika ndani ya dhehebu hilo. Namba ya Kibiblia ya ukamilifu hulitia ndani vuguvugu lote kwa ujumla. Ukweli huu pia umethibitishwa na nukuu ifuatayo: “Wakati watiwa-mafuta wanapomimina wenyewe mafuta yao katika mabomba ya dhahabu, mafuta hutiririka kutoka ndani yao hadi kwa bakuli la dhahabu, ili yatiririke hadi ndani ya taa, makanisa.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 337. {SR2: 285.2}

Mirija Saba Ya Dhahabu

Ikiwa “bakuli la dhahabu” ndilo husheheni ufasiri wa Maandiko yaliyovuviwa au maandishi ya Roho ya Unabii, na taa au makanisa yanasambaziwa mafuta kutoka ndani ya lile bakuli kupitia mirija saba ya dhahabu, basi ukasisi huwakilishwa na ile mirija, ambayo jukumu lake ni kulisha kanisa lote kwa Neno la Mungu lililovuviwa tu. Ukweli huu pia umethibitishwa na “Roho ya Unabii,” jinsi tunavyosoma: “Mafuta ya dhahabu huwakilisha Roho Mtakatifu. Mafuta haya wachungaji wa Mungu wanapaswa kusambaziwa daima, ili wao pia, waweze kuyawasilisha kwa kanisa.” — Kimenukuliwa,

286

uk. 188. Kumbuka, mirija saba (Ukasisi) huchota mafuta kutoka ndani ya bakuli la dhahabu, sio moja kwa moja kutoka kwa miti ya mizeituni (Maandiko). {SR2: 285.3}

Funzo hili la mfano mtakatifu ni wazi sana kwamba haliwezi kueleweka vibaya, au maana yake kupotoshwa. Njia pekee salama ambayo kwayo watumwa wa Mungu na kanisa Lake wanaweza kuwa huru kwa makosa, wakiwa wamejaa imani bila uongo vinywani mwao (wote wakinena jambo moja), ni mwongozi asiyekosea kamwe — “Roho ya Unabii.” Kupokea kile kinachoitwa eti ukweli, bila uvuvio, ni mtego wa ibilisi wa udanganyifu, na wale wanaotetea mafundisho kama hayo ya uongo ndio wagumu zaidi na wasiowezekana kabisa kuokoa kutoka kwa shimo la kuzimu la Shetani; kwa maana yeye huwafanya waamini kwamba kukiri makosa yao kutawafanya wasifae kuwa walimu, na kufedhehesha hadhi yao ya juu. {SR2: 286.1}

Yeye anayekana ufasiri uliovuviwa wa Maandiko anaikana ofisi ya Roho Mtakatifu, na anatenda dhambi dhidi Yake — akitenda dhambi ambayo hawezi kusamehewa! {SR2: 286.2}

Kinara hiki cha dhahabu ni nembo ya kushangaza zaidi katika Biblia inayolihusu kanisa la Mungu. Mpangilio wake na namba kamili ya taa, bakuli, mabomba, na mirija, yote ya dhahabu, na miti yake miwili ya mizeituni ikimimina yenyewe mafuta ya dhahabu hadi ndani ya bakuli la dhahabu, hufichua kwamba sehemu ya mwisho ya kanisa la Mungu, itakuwa kanisa la utukufu zaidi katika vizazi vyote. Haya “mawasiliano ya daima” kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa kanisa, yanayowakilishwa na matawi ya mizeituni yanayomimina “Mafuta ya Dhahabu kutoka kwayo yenyewe” hadi ndani ya bakuli moja la Dhahabu, na jozi yake kamili ya Mirija ya Ugavi kutoka ndani ya bakuli hadi katika taa zake zote, yataleta kila sehemu ya mwili mzima kwa uwiano kamili; kanisa bila hila. {SR2: 286.3}

Nembo hii ya kinabii bila kukosea huonyesha mbele kwa shirika la mbinguni linalofyonza udhaifu na upungufu wa binadamu kuwa utukufu wa milele. “Kanisa tukufu, lisilo na doa, wala kunyanzi, wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” (Efe. 5:27.) Kanisa linaloshika “amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.” “Likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — “Manabii na Wafalme,” uk. 725. (Wimbo. 6:10.) Kwa hiki “kinara cha taa” ni ahadi: “Tazama, Nitakufanya kuwa chombo cha makali kipya cha kupuria chenye meno: utaifikicha milima, na kuisaga, nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.” (Isa. 41:15.) {SR2: 286.4}

Lile “jiwe moja” — kanisa — litakuwa na maono kamili ya utukufu wa mbinguni: “Maana litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya

287

Yoshua; katika jiwe moja yako macho saba: tazama, Nitachora machoro yake, asema Bwana wa majeshi, Nami nitauondoa uovu wa nchi ile katika siku moja. Katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu na chini ya mtini.” (Zek. 3:9, 10.) Kwa watumwa wa Mungu (kanisa) wamepewa kumiliki nchi, na kurejesha ardhi kwa watakatifu ambao waliimiliki hapo mwanzoni. Kwa hivyo, “Wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu: kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimenena hayo.” (Mika 4:4.) {SR2: 286.5}

“Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani: nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao, na hao wapandao farasi watafadhaishwa.” (Zek. 10:5.) “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu asema Bwana wa majeshi.” (Zek. 4:6.) {SR2: 287.1}

“Na katika siku hiyo Nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote: wote watakaojitwika jiwe hilo watakatwa vipande-vipande, ingawa watu wote wa dunia watakusanyika pamoja dhidi yake… Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao katika siku hiyo atakuwa kama Daudi; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” (Zek. 12:3, 8.) “Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote, mafungu mawili yatakatiliwa mbali nao watakufa asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo: wataliitia jina Langu, nami Nitawasikia: Mimi nitasema, watu hawa ndio Wangu: nao watasema Bwana ndiye Mungu wangu.” (Zek. 13:8, 9.) {SR2: 287.2}

“Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.” (Zab. 87:3.) “Paza sauti na mpige kelele, enyi wenyeji wa Zayuni: maana Aliye Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.” (Isa. 12:6.) “Imba na ufurahi, Ee binti Zayuni: maana, tazama, Ninakuja, nami Nitakaa kati yako, asema Bwana.” (Zek. 2:10.) {SR2: 287.3}

Ni Nini Kilichovuviwa Na Ambacho Hakijavuviwa?

Watu wajanja chini ya nguvu ya mdanganyifu mkuu, kwa maneno mazuri na hotuba laini wametafuta kupindua imani ya watakatifu katika neno la Mungu kwa karibu tafsiri zisizohesabika za Maandiko, na wingi wa madhehebu; kufanya karibu isiwezekane kwa mmoja kupata njia ya kutoka kwa huo mchafuko, na hivyo kumfanya asijue ukweli. Mungu, akijua mapema kuhusu mbinu hizi za hila, kinabii Ameonyesha ukweli kwa kukitumia kinara hiki cha taa katika kusanyiko la

288

sehemu zake, zikionyesha kwa mfano kwamba ukweli wa Biblia hufunuliwa na Uvuvio pekee. Maneno yaliyoandikwa yanaweza kupotoshwa, lakini nembo hapana. Hivyo kufanya iwezekane kwa wote wasomi, na wasiojua kusoma, kupambanua mara moja tofauti kati ya ukweli na uongo. {SR2: 287.4}

Swali laweza kuzushwa na baadhi, Je! Nawezaje kubainisha lile ambalo limevuviwa, na lile ambalo halijavuviwa? Neno la kinabii la Mungu lina uwezo wa kujibu hilo swali na kuondoa mkanganyiko, likigawanya moja kutoka kwa lingine kama ngano inavyotenganishwa na makapi. Kwanza, “kwa sheria na ushuhuda: ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” (bila uvuvio). (Isa. 8:20.) Pili, makanisa ambayo yalikuwepo mara kabla ya mwaka 1844, yalianguka kwa kutangazwa ujumbe wa malaika wa pili (Ufu. 14:8), kuonyesha kwamba Mungu hangeendelea kujifunua Mwenyewe kupitia njia hiyo. Kwa hivyo, kila nadharia, na kichipuko au kidhehebu ambacho kimechipuza kutoka kwa madhehebu yaliyokuwepo wakati huo, ni ya uongo bila nuru ndani yake. Hili pia limethibitishwa na ukweli kwamba karibu waandishi au waasisi wote wa nadharia hizo na mavuguvugu haya hawafanyi madai ya uvuvio. {SR2: 288.1}

Unabii wa Ezekieli, sura ya nne (uliofafanuliwa katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 115-133), huthibitisha kwamba Luther, Knox, Wesley, Campbell, Miller, na E.G. White waliitwa na Mungu. Umethibitishwa pia kwa mfano wa Mathayo 20 kwamba Luther, Knox, Wesley, na Campbell hawakupewa nuru kuhusu ukweli wa kinabii, lakini walivuviwa kuitisha matengenezo kwa kweli fulani ambazo zilifunuliwa kabla ya wakati wao, na “kukanyagiwa chini ya miguu.” Umethibitishwa zaidi kwa mfano uo huo kwamba kupitia kwa Miller na White, kweli za kinabii zilifunuliwa ambazo hazikuwa zimewahi kufundishwa hapo awali. (Tazama kurasa 227, 228). Umeonyeshwa pia kwa unabii wa Ezekieli kwamba nuru na ukweli kwa Maandiko ungeendelea kwa miaka 390, yaani, kutoka mwaka 1500 B.K. hadi mwaka l890 B.K.; na wakati huo ungekoma kwa miaka arobaini. (Tazama “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 114-133.) {SR2: 288.2}

Kwa hivyo, wakati vuguvugu la mwaka 1844 lilitangaza kwamba nuru ilikuwa imekoma kufunuliwa kupitia madhehebu yale mengine yote, linaonyeshwa kwa unabii wa Ezekieli kwamba nuru ingeendelea na lile la mwisho, hadi mwaka 1890. Ukweli huu pia unajidhihirisha wenyewe, maana Dhehebu la Waadventista wa Sabato halijakuwa na nuru zaidi kwa Maandiko katika hiyo miaka arobaini iliyotajwa. Kwa hivyo, nadharia yoyote, au kinachoitwa eti ukweli, ambao unaweza kuwa umeendelezwa na baadhi ndani ya dhehebu hili (S.D.A.) ambao haukuwa umefunuliwa kabla ya mwaka 1890, pia ni ya uongo; ingawa mambo mengine yaliandikwa katika Roho ya Unabii, hayakupaswa kueleweka hadi mwaka 1929. Kweli zilizofunuliwa kabla ya mwaka 1844, hadi mwaka

289

1929, zinapatikana katika maandishi ya “Roho ya Unabii,” na lile ambalo halijaandikwa hapo, halina thamani yoyote. Sio hadi akili zetu zitakapokuwa zimeondolewa kwa nadharia hizi zote za uongo ndipo tunaweza kuelewa ukweli. Kwa maneno mengine Walaodekia lazima wakiri kwamba lile shtaka dhidi yao ni la kweli — “wanyonge, wenye mashaka, maskini, vipofu, na uchi;” na kwa kuupokea ukweli wapake macho yao “dawa ya macho;” kwa maana ni “shahidi wa kweli anayenena, na Neno Lake lazima liwe sahihi.” Pata mafafanuzi yako “katika Bakuli,” na hautakuwa na taabu kujua ukweli, au kuepuka mtego ulio tayari wa udanganyifu. Kwa hivyo ugumu wa kujua tofauti kati ya ukweli na uongo umeondolewa. {SR2: 288.3}

290

MTO WA MAONO YA EZEKIELI

Hapo awali ilifafanuliwa kwamba unabii wa Zekaria unahusu kanisa katika wakati wa “Kilio Kikuu.” Hivyo unakuwa ukweli wa sasa. Tunanukuu kutoka Zekaria 12:8. “Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” — mbele ya umati mkubwa wa Ufunuo 7:9. {SR2: 290.1}

Kanisa katika usafi wake huitwa kwa Maandiko haya, “Nyumba ya Daudi.” Kwa hivyo, neno hili linakuwa mojawapo wa majina ya kanisa katika wakati wa “Kilio Kikuu.” Kwa hivyo lile kanisa chini ya jina hili litakuwa kama Mungu mbele ya watu. Maana yake ni sawa na Kutoka 7:1, “Bwana akamwambia Musa Angalia, Nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao: na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako” (mtumwa). Yaani, “Wewe utaiwakilisha nafsi Yangu, na kutenda kama Mungu kwa kutaka utiifu kwa maagizo yako, na kwa kuadhibu kutotii na adhabu ambayo hakuna mtu yeyote isipokuwa Mungu anaweza kusababisha; kwa sababu hiyo utapata usaidizi Wangu wa nguvu zote.” Huu ndio utume kwa kanisa katika wakati wa mavuno. Mtume Petro alipewa nguvu kama hizo za kiungu aliposema: “Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania, aliposikia maneno haya, akaanguka akafa… Hata muda wa saa tatu baadaye, mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Ndipo Petro akamwambia… angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake, akafa: wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.” (Matendo 5:4, 5, 7, 9, 10.) {SR2: 290.2}

“Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.” (Zek. 13:1.) Kumbuka kwamba chemchemi hii inaweza kuosha vitu viwili; kwanza dhambi, na pili unajisi. Je! Ni tofauti gani kati ya kimoja na kingine? “Dhambi ni uasi wa sheria.” (1 Yohana 3:4.) Na tokeo la dhambi ni kuoza mwili. “Haya semeni na wana wa Israeli mkawaambie, mtu ye yote atakapokuwa na kisonono kimtokacho mwilini mwake, atakuwa najisi kwa ajili ya kisonono chake.” (Law. 15:2.) Neno la kibiblia la ugonjwa ni, “Unajisi.” Pia, kuingiza

291

ndani ya mwili katika umbo la chakula kile kilichokatazwa na Neno la Mungu, ni uasi wa sheria, na uharibifu wa mwili (unajisi). {SR2: 290.3}

“Kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu; nami Nitawakaribisha.” (2 Kor. 6:17.) “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati, wala mchafu, wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana: kwa kuwa kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. Basi msishirikiane nao. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru… Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee.” (Efe. 5:5-8, 11) Mungu anaweza kuponya roho na mwili; lakini hatauponya mwili kabla ya kuiponya roho — “dhambi” kwanza, kisha “unajisi.” “Nami Nitawaokoeni kutoka kwa uchafu wenu wote; Nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena.” (Ezek. 36:29.) Nguvu inayoweza kuosha uchafu wa mtu yeyote, “imefunguliwa kwa nyumba ya Daudi na kwa wakazi wa Yerusalemu” na imewakilishwa na ile “chemchemi” ya unabii wa Zekaria. {SR2: 291.1}

Asema Ezekieli: “Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu,” na “katika mwaka wa kumi na nne baada ya kupigwa mji, siku iyo hiyo mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, akanileta huko.” (Ezek. 40:1.) Kama ilivyoandikwa katika sura ya arobaini na saba, Ezekieli alionyeshwa katika maono habari fulani za ujenzi wa hekalu miaka kadhaa kabla ya Waisraeli kuachiliwa huru kutoka uhamisho wa Babeli. Imeelezwa hapo awali kwamba lile Hekalu lililojengwa baada ya kutekwa kwao lilikuwa mfano wa kanisa hili hasa katika wakati wa “kilio kikuu” — “nyumba ya Daudi.” Kwa hivyo, mto unaotoka kwenye hekalu kwa mujibu wa maono ya Ezekieli unatumika wakati huu, na ni upanuzi wa “chemchemi” hii ambayo inapaswa kuwa katika “nyumba ya Daudi” kanisa. “Kutoka kwa chemchemi hii hutiririka mto mkubwa ulioonekana katika maono ya Ezekieli.” — Mashauri kwa Afya,” uk. 210. Hadi hapa tumefafanua matumizi ya “chemchemi” hii, mahali na wakati, na pia kwamba ule mto mkubwa ulioonekana katika maono ya Ezekieli hutiririka kutoka kwayo. Sasa tutachambua maana ya mto huu mkubwa. {SR2: 291.2}

Ezekieli 47

Aya ya 1: “Baadaye akanileta tena mpaka lango la nyumba; na, tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba kwa njia ya mashariki: maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea

292

upande wa mashariki, nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kuume wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu.” Maji yalikuja kutokea upande wa kusini wa madhabahu, na kisha kuelekea mashariki, huonyesha wazi kwamba yalitoka kaskazini, ambako ki-mfano humaanisha kwamba iwayo yote maana ya yale “maji,” yanatoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu, kwa sababu kiko “katika pande za kaskazini.” (Isa. 14:14; Zab. 48:2; 75:6.) {SR2: 291.3}

Wakati umakini wa Ezekieli uligeuzwa hadi ndani ambamo mara ya kwanza aliona maji, asema: “Ndipo akanileta nje kwa njia ya lango upande wa kaskazini, akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje kwa njia yake iliyoelekea mashariki; na, tazama, maji yalitoka upande wa kuume. Na alipotoka mtu yule mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake kwenda masharikini, akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka viweko vya miguu. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha; maji yakafika mpaka viuno. Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka: maana maji yalikuwa yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika. Akaniambia, Mwanadamu, je! Umeona haya? Kisha akanichukua, akanirudisha mpaka ukingo wa mto. Basi nikiisha kurudi, tazama kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana upande huu na upande huu. Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba [jangwani], na kuingia katika bahari: Maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka. Tena itakuwa, kila kiumbe hai, kisongamanacho, kila mahali utakapofika mto huo, kitaishi: kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yatafika huko; maana maji yale yataponyeka; na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo. Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana. Bali mahali penye matope na maziwa yake hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi. Na karibu na mto juu ya ukingo wake, upande huu na upande ule, utamea kila mti wa chakula ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe: utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu: na matunda yake yatakuwa ni chakula, na majani yake yatakuwa ni dawa.” (Ezekieli 47:2-12.) {SR2: 292.1}

Itagundulika kwamba jinsi Ezekieli alivyoyaona kwanza maji kando ya madhabahu, yalikuwa na umuhimu kidogo kulinganisha

293

Ukurasa Mtupu

294

PICHA

[Chati ya Mto wa Ezekieli]

295

na kile alichokiona nje ya lango. Wakati kijito kidogo mara moja kinaumuka kuwa mto mkubwa, huwakilisha kitu cha ukuaji wa haraka sana. Maji haya yana maana sawa na maji katika Ufunuo 17:15, “Watu, na umati, na mataifa, na lugha.” Kwa maana malaika alimwambia Ezekieli: “Maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka.” (Ezek. 47:8.) Kwa hivyo, maji haya huwakilisha umati mkubwa “ambao hakuna mtu anayeweza kuhesabu” ambao utaponywa kutoka kwa dhambi na ugonjwa, utakaookolewa katika wakati wa “kilio kikuu” kupitia kwa ukasisi wa “nyumba ya Daudi” (kanisa). Jinsi Ezekieli hakuweza kuogelea mto huu, nembo hiyo inapatana kikamilifu na Ufunuo 7:9, “Umati mkubwa, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha … wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” {SR2: 292.2}

Kumbuka kuwa sababu ya maji yale yataponyeka, ni kwamba “yataingia baharini.” Ikiwa ule mto mkubwa unawakilisha watakatifu kutoka duniani, basi ile bahari lazima iwe nembo ya dunia zisizo na dhambi (wakazi) katika ulimwengu wote wa Mungu. Jinsi ule mto unavyoingia baharini, humaanisha kwamba watakatifu watakutana na mataifa ya milele ambayo hayajui dhambi, na tukiwa “tumetokezwa,” lazima “tuponywe” kabla hatujakutana! Kweli za nembo hii zinathibitisha kwamba hii ni sehemu ya mwisho ya kanisa la Mungu — kanisa ambalo litatahamishwa bila kuonja mauti! Jitayarishe, jitayarishe, jitayarishe, sasa tunasimama juu ya pepo za milele — maisha ambayo hayatakoma kamwe. {SR2: 295.1}

Maji yanayofanyiza mto huu mkubwa huwakilisha umati wa watakatifu waliopewa nguvu ya uponyaji kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu; kwa maana Neno husema, “Na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.” (Ezek. 47:9, sehemu ya mwisho.) Uponyaji huu si wa usio na kipimo, bali ni wa kudumu; kwa maana tunasoma: “Tena itakuwa, kila kiumbe hai, kisongamanacho, kila mahali utakapofika mto huo, kitaishi” (milele). {SR2: 295.2}

Baada ya malaika kupima dhiraa elfu mara tatu, asema Ezekieli: “Akaniambia, Mwanadamu, je! umeona haya? Kisha akanichukua, akanirudisha mpaka ukingo wa mto. Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana, upande huu na upande ule. Na karibu na mto juu ya ukingo wake,” malaika alisema, “upande huu na upande ule, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe: utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu: na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.” (Ezek. 47:6, 7, 12.) {SR2: 295.3}

296

Thamani ya majani na matunda ya miti hii ni sawa na mti wa uzima kwa mujibu wa Ufunuo 22:2, “Na upande huu na upande ule wa huo mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.” Maana yake ni kwamba kanisa la Mungu (nyumba ya Daudi) limepewa nguvu kutoka kwa kiti cha enzi kutoa uzima wa milele bila mwonjo wa mauti kwa wale wanaopokea ukweli, na wako tayari kuwa sehemu ya mto huu mkubwa. Kwa sababu hii ndiyo sehemu pekee ya kanisa la Mungu ambayo imepewa injili yenye mamlaka ya uponyaji wa kudumu na uzima wa milele Neno latangaza: “Yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” (Zek. 12:8.) {SR2: 296.1}

“Kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko… Tena itakuwa kwamba wavuvi watasimama karibu nao toka Engedi mpaka En-eglaimu… samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.” (Ezek. 47:9, 10.) Samaki huwakilisha wale ambao watafanywa kuwa waongofu kwa kanisa — “mto.” “Na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.” (Ezek. 47:9.) Ukasisi unafananishwa kama wavuvi. “Yesu akawaambia, Nifuateni, nami Nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” (Marko 1:17.) Mitume wakati mmoja waliliacha juya la injili na wakaacha kuwa wavuvi wa watu, walipokwenda kuvua samaki kwa faida, “ila usiku ule hawakupata kitu. Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni… basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna chakula? Wakamjibu, La. Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.” (Yohana 21:3-6.) Mafanikio hayashindwi kamwe wakati amri ya Bwana inapewa utiifu. Laiti ukasisi ungekuwa daima ukimuuliza Yesu ni wapi na jinsi ya kulitupa juya, kungekuwa na wingi wa “samaki” — waongofu — na kamwe bila ukosefu wa “chakula” — rasilimali. {SR2: 296.2}

“Upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki.” (Ezek. 47:1.) Kusimama kwa nyumba hiyo huthibitisha kwamba huwakilisha ibada ya kweli, kwa maana hivyo ndivyo watu wateule wa Mungu walivyoamriwa kujenga mahekalu yao. Israeli walimwabudu Mungu migongo yao ikielekea mashariki ili kuwakumbusha kwamba hawakupaswa kuheshimu ibada ya jua na ibada ya sanamu. {SR2: 296.3}

“Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba [jangwani], na kuingia katika bahari.” (Ezek. 47:8.) Inashangaza kuona jinsi nembo hizi zilivyo kamilifu

297

katika kila tukio. Uelekeo huu wa dira humaanisha kwamba ujumbe wa “kilio kikuu” utaanza kuelekea mashariki wakati utakapofunuliwa mara ya kwanza. Washirika wa kanisa kwa wingi wakiwa mashariki mwa California na ng’ambo ya Atlantiki, kwa kawaida ujumbe lazima uanze kuelekea mashariki. Unabii huu wa ki-mfano hufichua kwamba ujumbe wa “kilio kikuu” utaanzia California. Kwa hivyo kutimiza maneno ya kinabii ya “Roho ya Unabii” katika barua kwa Mzee E.E. Andross: “Najihisi mwenye imani Mzee Andross, kwamba ndugu huko Kusini mwa California watapata baraka kwa kupitia mafundisho ya Maandiko mintarafu watu 144,000 na kuleta uzito juu ya mafundisho haya nuru yoyote inayoweza kuwa katika maandishi yaliyochapishwa ya Roho ya Unabii, na kwa kulifikiria jambo hili kwa njia ya sala katika mahusiano yake yote, Naamini kwamba Mungu ataufanya ukweli uwe wazi kabisa ili kuwezesha kuepuka maswali yasiyohitajika na yasiyofaidi ambayo sio muhimu kwa wokovu wa roho za thamani.” {SR2: 296.4}

Mashariki ikiwa mwelekeo wa Kibiblia wa kuabudu sanamu, pia huashiria kwamba huo ujumbe umeelekezwa kuwaongoa wadhambi na kuharibu ibada ya sanamu. “Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena: pia Nitawafukuza manabii na roho za uchafu watoke katika nchi.” (Zek. 13:2.) {SR2: 297.1}

Malaika alipima dhiraa elfu mara nne kuelekea mashariki (elfu — “kumi” mara mia moja). Mbona efu mara nne? Kwa nini isiwe zaidi au inayopungua? Imeelezwa hapo awali kwamba namba “kumi” ni nembo ya ulimwengu wote, na namba nne ukamilifu wa dunia au ncha nne za dira. Kwa hivyo humaanisha ki-mfano kwamba ujumbe huo ni wa ulimwengu wote; na wakati unaanza kuelekea mashariki, unaenea kutoka ncha hadi ncha, na kuizunguka dunia kabisa (10 x 100 = 1,000 — mara nne.) Kwa uwiano kamili na maneno ya Kristo: “Na hii injili ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; na hapo ndipo mwisho utakapokuja. “ (Mat. 24:14.) {SR2: 297.2}

“Bali mahali penye matope na maziwa yake hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi.” (Ezek. 47:11.) “Maziwa (mabwawa)” na “mahali penye matope” huwakilisha madhehebu na vidhehebu vilivyojitenga na huo “mto mkubwa,” na ya kwamba hawataokolewa, au kuponywa. “Yataachwa yawe chumvi,” humaanisha kupotea milele, kama mke wa Lutu. “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku Zake Mwana wa Adamu… Na kadhalika kama ilivyokuwa katika siku za Lutu… Mkumbukeni mke wa Lutu.” (Luka 17:26, 28, 32.) {SR2: 297.3}

“Tena itakuwa, wavuvi watasimama

298

karibu nao toka Engedi mpaka En-eglaimu; [miji hiyo miwili] patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu.” (Ezek. 47:10.) Miji hii miwili huonyesha kwamba samaki wananaswa katika sehemu mbili, En-gedi (kanisa la S.D.A.) ambamo kutoka ndani watu 144,000 wanakusanywa — malimbuko. En-eglaim (Babeli au ulimwengu) ambamo kutoka ndani yake umati mkubwa wa Ufunuo 7:9 unakusanywa. Mchoro kwa chati, ukurasa wa 294, huwakilisha kanisa la S.D.A. (En-gedi) linapokuwa “Nyumba ya Daudi,” na mahali pa mto (En-eglaim) humaanisha ulimwengu. Kijito kutoka kwa chemchemi ambapo huanzia hadi kwa lango la mashariki, huwakilisha watu 144,000, na mto huwakilisha umati mkubwa. “Kuna mto, vijito vyake vitaufurahisha mji wa Mungu, patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake, hautatetemeshwa: Mungu atausaidia, asubuhi na mapema.” (Zab. 46:4, 5.) {SR2: 297.4}

KUHESABIWA HAKI KWA IMANI; NI NINI?

Baraka zote zilizoandikwa katika sura zilizotangulia zimefungwa katika zifuatazo:

Ingawa somo hili muhimu zaidi ni rahisi sana kuliko kweli zote za Biblia, limekanganywa sana, na kwa kiasi kikubwa halieleweki. Mfano wa uzoefu wa mtu mmoja katika mambo ya Mungu na kwake kuhesabiwa haki kwa imani, kunapaswa kuondoa mkanganyiko ulioenea kote, na kuondoa pazia ambalo limekinga macho ya waaminifu. “Ila kwa wale wa imani ya Abrahamu; aliye baba yetu sisi sote; (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi), mbele Yake Yeye aliyemwamini, yaani Mungu, Mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.” (Rum. 4:16, 17.) {SR2: 298.1}

Wakati mbinu iliyofuatiliwa na Abrahamu inafuatwa, basi, wakati huo tu, yeyote kati yetu anaweza kuhesabiwa haki, hakuna njia nyingine. “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawasawa na ahadi.” (Gal. 3:29.) “Kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu.” (Yohana 8:39.) Hebu tuangalie imani ya Abrahamu, uzoefu na kuhesabiwa haki. “Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki, ninyi mnaomtafuta Bwana: uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa. Mwangalieni Abrahamu baba yenu.” (Isa. 51:1,2.) {SR2: 298.2}

299

Katika yafuatayo itagundulika kwamba Abrahamu aliitika bila kusita kwa yote Mungu alimwamuru afanye: “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi Nitakuonyesha… Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru… Bwana akamtokea Abramu, akasema Uzao wako Nitawapa nchi hii: naye huko akamjengea madhabahu Bwana, aliyemtokea.” (Mwa. 12:1, 4, 7.) “Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo upande wa kaskazini, na wa kusini, na wa mashariki, na wa magharibi: maana nchi hii yote uionayo, Nitakupa wewe, na uzao wako hata milele. Na uzao wako Nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi: hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake na marefu yake; maana Nitakupa wewe nchi hiyo. Basi Abramu akajongeza hema yake, akaja akakaa kwenye uwanda tambarare wa Mamre, nao uliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.” (Mwa. 13:14-18.) {SR2: 299.1}

“Mungu akamwambia Abrahamu, Nawe ulishike agano Langu, wewe, na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano Langu utakalolishika, kati ya Mimi na wewe na uzao wako baada yako; Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa … Abrahamu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake wanaume wote wa watu wa nyumba ya Abrahamu; akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, jinsi Mungu alivyomwambia.” (Mwa. 17:9, 10, 23.) {SR2: 299.2}

“Mungu akamwambia Abrahamu, Neno hili lisiwe baya machoni pako kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako; kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake; kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akatwaa mkate, na kiriba cha maji, akampa Hajiri, akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu.” (Mwa. 21:12, 14.) “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu: naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee Isaka, umpendaye, ukaende zako mpaka nchi ya Moria; ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo Nitakaokuambia. Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akawachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda akafika mahali pale alipoambiwa na Mungu… Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka

300

mwanawe, akamweka juu ya madhabahu juu ya zile kuni. Abrahamu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu, Abrahamu: naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno: kwa maana sasa najua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee… Malaika wa Bwana akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, Akasema, Nimeapa kwa nafsi Yangu, asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee: Katika kubariki Nitakubariki, na katika kuzidisha Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; Na katika uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa; kwa sababu umetii sauti Yangu.” (Mwa. 22:1-3, 9-12, 15-18.) {SR2: 299.3}

“Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki: naye aliitwa rafiki wa Mungu.” (Yakobo 2:23.) Kwa kufanya mambo ambayo Mungu alimwuliza alipata rekodi hii: “Kwa sababu Abrahamu alisikia sauti Yangu, akayahifadhi maagizo Yangu, na amri Zangu, na hukumu Zangu, na sheria Zangu.” “Katika uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.” (Mwa. 26:5, 4.) Kuwa na imani kama ya mtoto katika Neno, na kufanya yote ambayo Mungu amesema, ndio utakaso na haki pekee ambayo ni ya Kristo. Kama hao ndio wana wa Abrahamu, na ile ahadi ni yao. Wao hutangaza waziwazi kwamba damu ya Kristo ina uwezo wa kuwaokoa kutoka kwa utumwa wa dhambi, na kutoka kwa hukumu ya sheria. Watairithi nchi milele na milele. Hawa ndio Israeli wa Mungu. Hakuna wengine, na hii pekee ndiyo haki na utakaso kwa imani. {SR2: 300.1}

301 – 304 (Faharisi ya Maandiko haijajumuishwa)

>