15 Jun Trakti Namba 12
1 (Jalada)
Hati miliki 1941
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. Houteff
Katika nia ya kufikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inatumaini kuiepuka njia inayoongoza kwenye uharibifu wa mwili na roho, trakti hii inasambazwa bila malipo kadiri toleo hili linadumu.
TRAKTI NAMBA 12
KIMECHAPISHWA TENA 1946
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Imechapishwa Marekani
2
YALIYOMO
MUNGU PEKEE ANAJUA YA BAADAYE 5
YAMETABIRIWA KATIKA HALI TUMIZI YA PICHA 6
SIMBA, DUBU, CHUI, NA MNYAMA DUBWANA 7
MNYAMA KAMA CHUI 19
Kuanguka Kwa Uprotestanti Na Kinuka Kwa Udikteta 24
MNYAMA WA PEMBE MBILI 25
Mfano Wa “Sanamu Ya Mnyama” 28
MNYAMA MWEKUNDU SANA AKIENDESHWA NA BABELI MKUU 30
Je, Babeli Anamwakilisha Nani? 36
AWAMU YA MWISHO YA WANYAMA 38
“Bahari” Huonyesha Eneo La Wanyama Watano 39
“Nchi” Huonyesha Kikoa Cha Mnyama Wa Pembe Mbili 39
“Nyika” Huonyesha Kikoa Cha Mnyama Mwekundu Sana 40
MWANAMKE ALIYEVIKWA TAJI YA NYOTA KUMI NA MBILI NA MASALIA WAKE 42
Katika Ufalme Wa Babeli Kuingia Katika Nchi Yao 46
Ugavi Mpya Wa Ardhi 48
WATU WA MATAIFA WATAFUKUZWA KUTOKA KATIKA NCHI TAKATIFU 49
Gogu Ni Nani? 50
BWANA ATAYAHARIBU NA KUYAHUKUMU MATAIFA 51
MATUKIO YA SASA AMBAYO YANAWEZA KUTIMIZA UNABII 53
3
DANIELI KUMI NA MOJA — MUHTASARI
“Kile Ambacho Kimenakiliwa Katika Maandiko” 57
Matendo Yanayomtambulisha Mfalme Wa Kaskazini 59
Idadi Za Tawala 61
Ufunguo 63
Kaskazini Yashinda Kusini — Yachukua Misri Na Palestina 65
Katika Utukufu Wa Ufalme 66
Agharikishwa Na Mafuriko — Anapoteza Misri Na Palestina 67
Tena Wainuka Kwa Utawala 67
Rekodi Ya Historia Ya Kujipendekeza Na Ukristo Wa Kulazimishwa 69
Historia Hueleza Ugavi Wake Wa Ardhi Kwa Faida 72
Utawala Wa Pili Wa Kusini; Waushinda Utawala Wa Nne Wa Kaskazini 73
Wote Walinena Uongo 77
Dhidi Ya Agano Takatifu 79
Analitia Unajisi Hekalu Anaiondoa Ya Kila Siku 81
Anampuuza mungu Na Hamu Ya Wanawake 82
Utawala Wa Tano Wa Kaskazini Unashinda Utawala Wa Pili Wa Kusini 83
Mapitio 86
Anatangaza Vita – Ila Si Dhidi Ya Mfalme Wa Kusini
Tendo Lake La Mwisho 89
Hitimisho 91
KUUWEKA MOYONI NA WANUFAIKE 91
4
DUNIA JANA, LEO, KESHO
JE, UJERUMANI AU UINGEREZA ITASHINDA?
Kwa sababu tunaishi katika wakati ambapo tunaweza kutarajia chochote, lakini kuwa na uhakika wa sifuri, kwa hivyo wote wanaojumuisha watawala, wana-diplomasia, na wanajeshi, bila shaka watashangaa kwa kile hasa kitatokea kwa mgogoro wa sasa wa Ulaya. {TN12: 5.1}
Kwa wakati huu (1941) vikosi vya kutisha vya Hitler vinaendelea bila kuzuilika ufurushaji wao kwa “Bi mkubwa wa Bahari,” wa dunia na hadi sasa hakuna chochote kimeweza kukabiliana na ghadhabu ya mauaji yao, na matokeo yake kwamba Ulaya imesimama katika mshangao wa hofu, na ulimwengu wote kushtuka kwa kustaajabia kile kilicho mbele, tayari kama Nebukadnezza alivyokuwa katika siku yake, kutoa karibu kila kitu ili ajue, lakini
Mungu Pekee Anajua Ya Baadaye. {TN12: 5.2}
Wenye hekima wa leo hawawezi kutabiri ya baadaye kuliko ambavyo wangaliweza wenye busara wa wakati wa nabii Danieli (Dan. 2). Ikiwa unafikiri kwamba taarifa hii ni ya kupotosha basi kabiliana na changa-moto: “Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo. Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani,
5
tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au watuonyeshe yatakayotokea baadaye. Tujulisheni yata-kayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja.” Isa. 41:21-23. {TN12: 5.3}
Yule Ambaye alitabiri kuinuka na kuanguka kwa Babeli na mataifa yalioufuata, ndiye pekee anayejua ni nini kitakachokuwa tokeo la “dhiki ya mataifa” ya sasa. Luka 21:25. Kwa nuru, basi, juu ya swali hili mu-himu sasa la maanani kwanza katika kila akili timamu, tunamgeukia Mungu wa manabii, Ambaye hutuhimiza tuyachunguze maandiko ya waonaji Wake wa zamani. Humo, matukio yote ya ulimwengu ya-nayowahusu “wana” Wake (Isa. 45:11),
Yametabiriwa Katika Hali Tumizi Ya Picha. {TN12: 6.1}
Historia ya ulimwengu katika unabii imeandikwa kwanza, kwa maneno halisi; pili, kwa maneno ya kielele-zo; tatu, kwa maneno ya mifano; na nne, kwa maneno ya picha. Kwa ajili ya ufupisho, na kwa maslahi ya kuuwezesha ufahamu, kuzuia uwezekano wa kupotoshwa, mjumbe huyu mnyamavu anauwasilisha ujumbe wake katika hali tumizi ya picha. {TN12: 6.2}
Falme ambazo zimeanguka, falme ambazo bado zingalipo, na falme ambazo zitakuja baadaye, ambazo sheria zake huhusisha watu wa Mungu, zimenakiliwa kwa hali tumizi ya picha na wote Danieli na Yohana Wa-ufunuo. {TN12: 6.3}
6
Sasa ili kwamba hata dhamira ya mkafiri sana na asiyeamini iweze kushawishiwa, mada ya trakti hii inajul-ishwa kwa nembo ambazo umuhimu wake wa unabii umekuwa tayari historia:
Simba, Dubu, Chui, Na Mnyama Dubwana. {TN12: 7.1}
“Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. {TN12: 7.2}
“Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele. {TN12: 7.3}
“Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. {TN12: 7.4}
“Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwan-za, naye alikuwa na pembe kumi. Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.” Dan. 7:2-8. {TN12: 7.5}
7
[Picha ya Wanyama Wanne Wakubwa]
8
Wanyama hao wawili, alisema malaika, “ni wafalme wanne, watakaotokea duniani.” Dan. 7:17. {TN12: 9.1}
Kabla maono ya Danieli ya wanyama hawa, Nebukadnezza, mfalme wa Babeli ya kale wakati akiwa na utata mkubwa kuhusu kipindi cha ufalme wake, alionyeshwa katika ndoto sanamu kubwa iliyojumuisha vyuma vinne. Kichwa chake kilikuwa cha “dhahabu”; kifua chake na mikono ilikuwa ya “fedha”; mapaja yake, ya “shaba”; miguu yake, ya “chuma”; na nyayo zake, za “chuma iliyochanganywa na udongo.” Akiyafafanua maono Danieli akamwambia mfalme: {TN12: 9.2}
“Wewe u kichwa kile cha dhahabu. Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma. . . Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. {TN12: 9.3}
“Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo. {TN12: 9.4}
“Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:38-44. {TN12: 9.5}
9
[Picha ya Sanamu Kubwa]
10
Dhahiri, vyuma vinne vya ile sanamu kubwa ni nembo ya, kama wale wanyama wanne, wafalme wanne wanaofuatana katika vipindi vyao mwafaka. Nyayo (kulia na kushoto) za chuma na udongo huwakilisha wazi migawanyiko miwili ya wafalme (mirengo ya kulia na kushoto) katika kipindi cha tano — wakati am-bapo Mungu wa Mbinguni “atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele.” vidole vya nyayo, huashiria, bila shaka, wingi wa wafalme katika pande zote mbili, mirengo ya kulia na ya kushoto. {TN11: 11.1}
Katika mfano mwingine, kondoo mume na beberu wa awamu tatu, Danieli aliona kwamba beberu katika awamu yake ya kwanza (ile ya “pembe kubwa” — mfalme wa “Uyunani”), alimkanyagia chini kondoo mume (“Wamedi na Waajemi”), na baada ya pembe kubwa kuvunjika (Alexander alipokufa), pembe nne zikazuka badala yake (ufalme ukagawanyika katika sehemu nne), na kwamba hatimaye kutoka kwa moja ya hizo nne, akaja wa tano, “pembe kubwa zaidi” (Rumi). (Angalia Danieli 8:9, 20, 21-23.) {TN12: 11.2}
Wengine hufikiri “pembe kubwa zaidi” — ya tano — huwakilisha Antiochus, ambaye alitawala moja ya mi-gawanyiko hiyo minne, lakini hili haliwezi kuwa, kwa sababu pembe kubwa zaidi kutokea ndani ya moja ya nne, huashiria ufalme wa tano si mmoja kati ya nne kupanuliwa. Zaidi ya hayo, neno, “kubwa zaidi,” kinyume na neno, “kubwa,” huashiria ufalme mkubwa zaidi kuliko wa Alexander. Na kama ufalme wa An-tiochus katika ukuu wake
11
haukuwa hata nusu ya wa Alexander, dhana hii inadunishwa. {TN12: 11.3}
Ufalme wa Kirumi ndio uliokuwa mkubwa zaidi kuliko wa Alexander, na kwa hivyo
12
ndio wa pekee unaoitikia ile nembo. Katika kwenda kusini, kisha mashariki, kisha kuelekea nchi ya uzuri, magharibi (Palestina), ni lazima ilienda katika pembe nne za dira, ndivyo ambavyo Rumi ulifanya. {TN12: 12.1}
Danieli 8: 9 husema kwamba “pembe kubwa zaidi” ilitokea kwenye moja ya pembe nne za beberu, lakini hasemi ni kutoka kwa ipi. Danieli 11:5, hata hivyo, hulezea kwamba “mmoja wa wakuu” wa ufalme wa kusini angekuwa na utawala mkubwa. Mkuu huyu, kwa hivyo huwakilishwa na pembe kubwa sana, na huonyesha kwamba ilitoka kwenye pembe ambayo iliwakilisha mfano wa utawala wa Ptolemi — mgawanyiko wa kusini. Hapa limeonyeshwa lile historia hushindwa kuandika kuhusu chimbuko la Rumi ya Upagani. {TN12: 13.1}
Sasa tunaona kwamba ingawa katika Danieli 2 na 7 majina ya wafalme hayajafanywa yajulikane, yamefichuliwa katika Danieli 8. Na kwa sababu Danieli 2 na 8 huthibitisha Danieli 7, inafuata kwamba vyuma vinne vya ile sanamu kubwa, na wanyama wanne wakubwa, ni nembo za tawala nne za kale: Babeli, Wamedi na Waajemi, na Rumi ya Upagani, mtawalia. {TN12: 13.2}
Ramani zifuatazo nne huonyesha kwamba historia huthibitisha unabii. {TN12: 13.3}
13
14
15
16
Nyayo na vidole vya ile sanamu (Dan. 2), vikiwa mchanganyiko wa chuma na udongo, hutabiri utawala ambao hauwezi kushikamana pamoja, udongo ukiisababisha kuvunjika vipande vipande — katika falme zilizogawanyi-ka: baadhi kubwa, baadhi ndogo, “sehemu zenye nguvu, na sehemu zilizovunjika.” {TN12: 17.1}
17
Ni dhahiri maandiko haya huelezea jamii ya wafalme wa sasa katika hali yao ya waliooana (iliyochanganywa “na mbegu ya wanadamu”). Ikija kama tokeo la kuvunjika kwa Rumi ya Upagani, wao hufanya ufalme wa tano na uliogawanyika tofauti-tofauti. Hivi picha hii ya unabii hubashiri waziwazi kwamba watawala wa leo, ha-wawezi kushikamana mmoja kwa mwingine (Dan. 2:42, 43), wamepotea kwa milipuko ya siku zote na uhasa-ma kati yao wenyewe. {TN12: 18.1}
Ramani ya 5 huonyesha migawanyiko mamboleo, kabla ya Vita Kuu vya 2, vya ulimwengu wa kale. {TN12: 18.2}
18
Inavyokubalika kote kote, awamu mbili za mnyama wa nne — moja na pembe kumi, nyingine na pembe saba pamoja na “pembe ndogo” (Dan. 7:7, 8) — huwakilisha, kwanza, Rumi ya Upagani, na pili, Rumi ya Upapa , na “pembe ndogo” (kichwa cha pembe), dola ambayo ilitawala, ilikuwa ya kidini na kisiasa. {TN12: 19.1}
Wanyama hawa wanne ni sanjari za “dhahabu,” “fedha,” “shaba,” na “chuma” ya “sanamu kubwa.” {TN12: 19.2}
Katika nembo hii ya kinabii ya wanyama wanne, pamoja na utimizo wake wa kihistoria, tunaona matukio ya kisiasa yanayopita na matokeo yanayobadilika ya hali ya kisiasa ya ulimwengu tangu wakati wa Babeli ya kale mpaka wakati wa Rumi iliyofanywa ya Ukristo. Sanamu kubwa, hata hivyo, hutuleta hadi sasa, wakati ambapo tunajikuta tunatawaliwa na wafalme wake wa vidole. Lakini jinsi mfululizo wa Danieli wa wanyama una-vyoonyesha ila tu sehemu ya historia ya dunia, mfululizo mwingine ni lazima kuukamilisha. Mfululizo mwingine tu u katika Ufunuo, nembo ya kwanza ambayo ni
MNYAMA KAMA CHUI. {TN12: 19.3}
“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi,
19
na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. {TN12: 19.4}
“Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti lika-pona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnya-ma uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? {TN12: 20.1}
“Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina Lake, na maskani Yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila am-baye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. {TN12: 20.2}
“Mtu akiwa na sikio na asikie. Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.” Ufu. 13:1-10. {TN12: 20.3}
20
Mseto wa kiwiliwili cha mnyama huyu — kinywa cha simba, miguu ya dubu, mwili wa chui, na pembe kumi — ni ushahidi mwaminifu kwamba yeye ni mzawa wa Babeli (simba), Wamedi na Waajemi (dubu), Uyunani (chui), na Rumi ya Upagani (pembe kumi). Kwa hivyo mnyama huyu ni chungu cha kuyeyusha cha falme nne za zamani za dunia, na lazima, pamoja na vichwa vyake saba na pembe kumi za vilemba, ndio sifa ya dunia ya leo. {TN12: 21.1}
Cha mnyama kipindi cha miezi arobaini na miwili, huangukia wakati wa Rumi ya Upapa — ufalme baada ya Rumi ya Upagani; ilhali
21
hali yake iliyojeruhiwa (Ufu. 13:3), humwonyesha katika kipindi cha Uprotestanti. Tena, mnyama huyu hu-wakilisha vipindi vitatu — (1) kipindi kabla ya hali yake iliyojeruhiwa; (2) kipindi wakati wa jeraha lake; na (3) kipindi ambacho jeraha lake limepona. {TN12: 21.2}
Isitoshe, nembo hii huonyesha kwamba Uvuvio huuhesabu ulimwengu wa Uprotestanti kuwa bado ni ulim-wengu wa Kirumi. Hili tunajua kutoka kwenye pembe kadhaa, ya kwanza ambayo ni ukweli kwamba cha mnyama kipindi cha miezi arobaini na miwili kinalingana na kile cha “wakati” wa pembe ndogo (miezi 12), “nyakati” (miezi 24), “na nusu wakati” (miezi 6). Kazi dhidi ya Mungu na watu Wake katika kumbukumbu zote mbili ni muda wa miezi arobaini na miwili. {TN12: 22.1}
Pembe za mnyama dubwana zikiwa bila vilemba, na pembe za mnyama kama chui zikiwa na vilemba, hu-onyesha kwamba wa mwisho ni nembo ya dunia baada ya pembe zisizokuwa na vilemba (wafalme ambao wangeinuka — Dan. 7:24) za mnyama wa awali zilikuwa na vilemba. {TN12: 22.2}
Sasa, ambavyo tumeona, ni wazi kuwa Rumi ya Upapa (awamu ya pili ya mnyama dubwana) ilikuwa muungano wa utawala wa kanisa na serikali (pembe yenye kichwa, ikiwa na “macho ya mwanadamu, na kin-ywa kinachonena mambo makuu” — Dan. 7:8), na ya kwamba matengenezo ya Uprotestanti yalisababisha utengo wa hizo mbili. Hivyo, wakati Rumi ya Upapa iliinuka na kutawala ilifananishwa kimbele na pembe yenye kichwa ya mnyama dubwana, anguko lake limeonyeshwa na kichwa
22
cha kawaida kilichojeruhiwa cha mnyama kama chui — sehemu ya pembe (nguvu za serikali) ikiwa imeon-dolewa. Kanisa likiwa limevuliwa nguvu kuu ambayo serikali ilikuwa imelivika, na matokeo yake kwamba serikali sasa ziko huru kwa kanisa, na kanisa liko chini ya utiisho kwa serikali. {TN12: 22.3}
Hilo likiwa ukweli kwamba kichwa kilichojeruhiwa huashiria mwili wa kidini, na ya kwamba hakuna utofauti wa sura kati ya kichwa kilichojeruhiwa na vichwa sita ambavyo havikujeruhiwa, basi ukweli wa msingi ni kwamba vyote ni mifano ya miili ya dini. Zaidi ya hayo, jinsi unabii huu wa mifano unavyohusika na Ustaarabu wa Magharibi, nyumbani kwa Ukristo, vichwa bila shaka hufanya madhehebu ya Ukristo, kama “makanisa sa-ba ya Asia” (Ufu. 2, 3), tofauti moja ikiwa kwamba makanisa ya Asia labda yalienea kipindi cha muda mrefu zaidi kuliko vichwa. {TN12: 23.1}
Isitoshe, wakati mnyama huyo akipokea jeraha la mauti hufananisha Rumi ya Ukristo ikiwa imedhalilishwa hadi kifo (imenyang’anywa mamlaka yake ya kiserikali), kupona kwa jeraha lake humwonyesha akiwa amein-uliwa kwa uhai tena (baada ya kupata tena nguvu zake za kiserikali). Na kwa sabau jeraha lilisababishwa na mkono wa Matengenezo halingeweza kupona kamwe iwapo mkono huo ungeyaendeleza ukitumia dhidi yake upanga wenye makali kuwili. Kupona, kwa hivyo, huonyesha wazi
23
Kuanguka Kwa Uprotestanti Na Kuinuka Kwa Udikteta. {TN12: 23.2}
Ingawa upo ufasiri mmoja sahihi wa kila fundisho la Biblia, bado umati mkubwa wa fasiri zinazopingana ziko katika ulimwengu wa Ukristo leo, na matokeo yake kwamba umegawanyika katika madhehebu mengi na mitengano (vichwa), bila mawili kuamini sawa. Ndani yake upo ushahidi wa maamuzi kwamba makanisa haya yamemvua Roho Mtakatifu, na yanakimbia kwenda mbele katika giza. Kwa sababu yanadai kufundisha Ukweli, lakini badala yake mafundisho na amri za wanadamu, yanakemewa kwa kuwa na “jina la makufuru” lililoan-dikwa kwa vichwa vyao (Ufu. 13:1). {TN12: 24.1}
Hata sasa, katika masaa ya kukifunga kipindi cha injili, kanisa linasema: “Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu”, — ukweli wala manabii, — ingawa kwa kweli ni “wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” (Ufu. 3:16, 17), na karibu kutapikwa iwapo linashindwa sasa kuyapaka macho yake mafuta haya safi, ya ziada. Na kwa sababu ni sahaulifu kwa hali yake ya unyonge, sasa liko tayari sio tu kuukataa ujumbe wa mwisho unaokuja kwalo na maonyo na makaripio kabla ya siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana (Mal. 4:5), lakini pia kumsulubisha tena Mwokozi Angekuja katika mwili kulikemea, na hivyo kuurudia uasi wake wa zamani, kama ilivyoonyeshwa na Musa.
24
kuupiga “mwamba” mara mbili (Hes. 20:11). {TN12: 24.2}
Undani kwa undani, hadi hapa tumewezeshwa kuona kwamba kupona kwa jeraha ni ishara sio tu ya kanisa kushindwa kuyaendeleza matengenezo ya Uprotestanti hadi yakamilike, lakini pia ya serikali za dunia ‘haraka kurejea kwa kanuni za udikteta wa Zama za Giza — kwa utawala wa utendaji kabla ya jeraha kupasishwa. Marudio haya ya zamani yataletwa na
MNYAMA WA PEMBE MBILI. {TN12: 25.1}
“Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizope-wa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
“Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na ku-wafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
“Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo;
25
maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufu. 13: 11-18. {TN12: 25.2}
Utawala ambao unawakilishwa na mnyama wa pembe mbili utajitambulisha na “nabii wa uongo,” maana kwa pamoja “walitupwa wangali hai ndani ya ziwa la moto.” Ufu. 19:20. Kutokana na hili ni wazi kuona kwamba ishara ambazo mnyama hufanya mbele ya watu, na ambazo kwazo huwapotosha “wanaokaa juu ya nchi” (Ufu. 13:13, 14), zinafan-ywa na nabii wa uongo (Ufu. 19:20) “mbele ya huyo mnyama.” Ufu. 13:14. Dhahiri, basi mamlaka ya serikali ya mnyama, pamoja na nguvu ya nabii isiyokuwa ya kawaida, huonyesha kwa muungano wa mnyama na nabii — uhusi-ano wa wawakilishi wa serikali na wa kanisa. {TN12: 26.1}
Akiwa na pembe mbili tu, sio kumi, mnyama huyo kwa hivyo huonyesha serikali ya ndani nchi, sio ya ulimwengu, serikali. Hata hivyo, ataushawishi Ukristo wote “kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi”; yaani, atabuni kuanzishwa kwa serikali ya dunia yote, akizitawaza upya kanuni za
26
utawala wa serikali na kanisa wa Rumi ya Upapa. Akiwa mrejeshaji wa kanuni hizi, yeye, pamoja na nabii, watakuwa dikteta mkuu wa dunia, na sio tu kufinyanga sera za kisiasa na za kidini za serikali, lakini pia biashara ya dunia. Ataamuru “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufu. 13:17. {TN12: 26.2}
Mnyama huyu humwakilisha mtu ambaye anasimama akiwa kiongozi wa taifa, na ambaye ushawishi wake unakwenda mbali na kote miongoni mwa wafalme wa dunia. Anajulikana zaidi kwa tarakimu — namba ya siri “mia sita sitini na sita.” Ufu. 13:18. {TN12: 27.1}
Imani iliyopo kwamba namba “666” ni tarakimu ya kitambulisho cha utawala mwingine, ni yai la Mfalme wa Gi-za, na imekusudiwa kukificha ikiwezekana kitambulisho cha utawala huu wa pembe mbili. Uvuvio huiweka ile ta-rakimu kwa mnyama wa pembe mbili, na pale tunapaswa kuiacha. Wakati namba mwishowe imebuniwa, watumwa wa Mungu watakuwa na uwezo wa kuwashawishi “wenye hekima” wote kuwa ni nani ambaye mnyama huyo hu-wakilisha. Sasa tunaona, hata hivyo, kwamba hakuna yeyote anayejifunza Neno la Mungu, adanganywe wakati utawala huu utakapojitokeza kwenye ukumbi wa utendaji. Hata hivyo, licha ya onyo la Mungu dhidi ya kumsujudia mnyama, ulimwengu unashindwa kutii, na matokeo yake kwamba hata baada ya namba yake kubuniwa, “Naye awafanya wote,
27
wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 13:16. {TN12: 27.2}
Kifungu hiki, “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,” huashiria kwamba wote ambao, baada ya kuusikia ukweli, wanaendelea kusujudia, aidha kidini au kidunia, sanamu, “yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira Yake.” Ufu. 14:9, 10. {TN12: 28.1}
Ugunduzi kamili wa thawabu ya utukufu ambayo inawasubiri wanadamu hata sasa itawashurutisha watu kupiga kelele kwa furaha! Na vile vile ugunduzi wa adhabu ya kutisha ambayo inawasubiri wote ambao hawawezi kumfanya Mungu kuwa kimbilio lao, utawafanya hata sasa kulia na kusaga meno yao. Ili wote kwa uhalisi waweze kuona matarajio haya mbadala, na kuhimizwa hivyo basi kutubu, Bwana amekuwa na maumivu makuu sio tu kunakili kimchoro maelezo ya uovu ambayo, kupitia chombo cha mnyama Shetani amekusudia kwa ulimwengu wote, lakini pia kabla kuufanya uovu kama huo, mkamilifu
Mfano Wa “Sanamu Ya Mnyama.” {TN12: 28.2}
Mfano ulianza wakati — {TN12: 28.3}
“Nebukadnezza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Ndipo Nebukadnezza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali,
28
na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wa-kati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadnezza aliyoisimamisha. . . {TN12: 28.4}
“Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadnezza aliyoi-simamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.” Dan. 3:1-6. {TN12: 29.1}
Katika utekelezaji wa amri hii kali na ya uovu, vipo vipengele vitatu mashuhuri: Cha kwanza kwa onyo huaonyesha jinsi ambavyo mnyama atayashurutisha mataifa yote na watu chini ya utawala wake kumwabudu yeye na sanamu ambayo atabuni; cha pili kudumisha ahadi kwamba kama ilivyokuwa katika siku ya Nebukad-nezza, Mikaeli aliwaokoa na kuwakweza wale waliokataa kuiabudu sanamu ya dhahabu (Dan. 3:12-30), hivyo leo Yeye atawaokoa na kuwakweza wote wanaokataa kumwabudu mnyama na sanamu yake ; na cha tatu kwa utukufu kinafunua kwamba kama vile wote walivyosimama hapo kwa uaminifu, waliuongoza umati wa wote wa juu na wa chini kumtambua Yeye kuwa ni Mungu Aliye Juu sana, hivyo leo wote watakaotii onyo la kutomwabudu mnyama au sanamu yake, “watang’aa kama mwangaza wa anga; nao watawaongoza wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Dan. 12:1-3. {TN12: 29.2}
29
Smbamba na historia, “neno la unabii lililo imara,” likiwa limetuongoza mfano kwa mfano kutelemka kuzipitia falme likianza na Babeli ya kale, na kutelemka hadi kwa ulimwengu wa sasa unaotawaliwa na serikali za mafarakano, hakika litatuongoza hadi mwisho wa wakati. Kwa hivyo tunakabiliwa na hitaji la mantiki kwa nembo nyingine ya mnyama, moja unayotabiri ulimwengu wa kidini na kisiasa wa kesho. Bila nembo ya kutupeleka zaidi ya ulimwengu wa leo, Neno la Mungu la unabii litakuwa pungufu. Hivyo, kwa ajili ya kufu-atanisha mawazo, mwendelezo, na ukamilifu, mfululizo huu wa nembo za wanyama lazima uhusishe mnyama mwingine, ambaye haswa atafichua Ulimwengu wa Kesho. Nembo ya pekee iliyosalia ni
MNYAMA MWEKUNDU SANA AKIENDESHWA NA BABELI MKUU. {TN12: 30.1}
“Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. {TN12: 30.2}
“Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU,
30
MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.” {TN12: 30.3}
“Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnya-ma huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi. {TN12: 31.1}
“Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzi-ma tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba aliku-wako, naye hayuko, naye atakuwako. {TN12: 31.2}
“Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu. Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. {TN12: 31.3}
“Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa mabwana, na Mfalme wa wafalme, na hao walio pamoja Naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu. {TN12: 31.4}
“Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watam-fanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri Lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe. Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa,
31
wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Ufu. 17:1-18. {TN12: 31.5}
Sasa kutoka kwa udhahiri wa kufanana kati ya mnyama kama chui na mnyama mwekundu sana, mtu anapaswa kutambua kwamba wa mwisho ni sanamu ya wa awali, jeraha lake la mauti likiwa limepona na pembe zake zisizoku-wa na taji. Pembe zisizokuwa na taji za wa mwisho huonyesha kwamba anaiwakilisha dunia katika wakati ambapo hakuna wafalme waliotawazwa, ila badala yake dunia inatawaliwa na kiongozi wa kidini — mwanamke anayemwendesha mnyama. {TN12: 32.1}
32
Isitoshe, taarifa, “pembe kumi . . . ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.” (Ufu. 17:12), hakika huagiza kwamba falme zilizotawazwa za leo, ambazo zilizuka kutoka kwa Rumi iliyoanguka, na ambazo huwakilishwa na pembe zilizo na vilemba za mnyama kama chui, zitavuliwa taji, zitang’olewa mamlakani. {TN12: 33.1}
Pembe zisizokuwa na taji za mnyama mwekundu sana, zaidi ya hayo, “wana shauri moja” na “wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao” (Aya ya 13) wakati ambapo mwanamke “anatawala juu ya wafalme wa dunia.” Aya ya 18. {TN12: 33.2}
Kukaa kwake vichwani (Aya ya 9), huashiria kwamba yeye atayadhibiti makanisa; na kumwendesha huyo mnyama huashiria kwamba atakuwa mkuu wa ulimwengu. Mfumo huu wa ibada na utawala si jambo jipya chini ya jua, kwa maana “Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.” Ufu. 18:24. Yeye ni, kwa hivyo, anaitwa kwa usahihi Babeli, jina la wa kale zaidi, wa kwanza, ufalme wa ulimwengu — mfano. {TN12: 33.3}
Babeli hii ya uakisi, ambayo wakati huu watu wa Mungu wataitwa watoke ndani yake, hata itadhibiti biashara ya dunia, jinsi inavyofichuliwa wazi katika utabiri kwamba wakati utawala wake utakwisha, basi — {TN12: 33.4}
“. . . wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na
33
lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marima-ri; na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu. . . Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu; kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali; wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa! Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.” Ufu. 18:11-13, 15-19. {TN12: 33.5}
Hivyo, muda mfupi baada ya kusimamishwa, shirikisho hili la kanisa na serikali litatoweka kabisa, kama “jiwe la kusagia” kubwa ambalo linatupwa katika bahari (Aya ya 21). Na kilio cha waombolezaji wake kitakuwa: “kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa.” Ufu. 17:12; 18:10, 17. Hii saa ambayo inaleta maumivu ya kifo cha Babeli, haiwezi kuwa nyingine isipokuwa ile ambayo, kulingana na mfano wa Yesu (Mat. 20:11-16), ni ya mwisho kwa saa ya mfano (kipindi) cha kutwa (muda wa rehema); yaani, kutoka kwa mwito wa watumwa wa saa ya kumi na moja (ujumbe
34
wa mwisho kwa ulimwengu — Mal. 4:5), hadi saa ya kumi na mbili (jua likitua saa za kale), mwisho wa siku — kufungwa kwa kipindi cha injili (Mat. 24:14), mwisho wa mavuno (Yer. 8:20), kufungwa kwa muda wa rehema (Ufu. 22:11). {TN12: 34.1}
Zile “Pembe kumi” za mnyama mwekundu sana (watawala ambao yeye anatawala kwa saa moja) hatimaye “watam-fanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.” Ufu. 17:16. Hivyo hatimaye watampindua milele, na mfumo ambao anawakilisha, “sanamu ya mnyama,” utavunjwa. Kwa mwangwi huu wa an-guko la Babeli, “na hao wafalme wa nchi. . . watalia na kumwombolezea. . . wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.” Ufu. 18:9, 10. {TN12: 35.1}
Maombolezo ya “wafalme” huonyesha kwamba wanamhurumia, wakati ambapo pembe humchukia. “Wafalme,” kwa hivyo, hawawezi kuwa wale ambao huwakilishwa na pembe za mnyama zisizokuwa na taji, ila badala yake wale ambao wanawakilishwa na pembe zenye taji za mnyama kama chui. Wao ni wafalme waliotawazwa ambao waliinuka baada ya kuanguka kwa Rumi ya upagani, na ambao sasa wanaharakisha kwenda uhamishoni. {TN12: 35.2}
Utambulisho wa Babeli ukiwa mada iliyojadiliwa sana miongoni mwa wanafunzi wa Ufunuo, linazuka, kwa hivyo, hitaji la kuhakiki:
35
Je, Babeli Amwakilisha Nani? {TN12: 35.3}
Sasa ya kwamba nuru imefukuza kabisa giza ambalo kwa muda mrefu limeizonga mada hii, mwanafunzi wa unabii anaweza kuona wazi kutoka kwa nembo kwamba katika nafasi ya kwanza Babeli huuwakilisha mfumo unaokuja wa kidini, kisiasa na kiuchumi wa mataifa, wala sio taasisi au shirika fulani; pili, kwamba mnyama anayemwendesha ni mfano wa ufalme wake; na tatu, kwamba u karibu kupita kutoka kwa unabii kuingia historia — hakika, umeanza tayari kuzuka nje ya ukungu kama ilivyokuwa mwambao wa Amerika kwa Christopher Columbus na wenzake wakati walipokaribia Bara kubwa la Magharibi. {TN12: 36.1}
Mnyama huyo akiwa anaendeshwa na mwanamke, Babeli hufichua dhahiri kweli tatu muhimu: ya kwanza, kwamba mwito wa watu wa Mungu watoke Babeli (Ufu. 18:4), ni mwito kwa ajili yao watoke kati ya mataifa ambayo yana-wakilishwa na mnyama ambaye anamwendesha (kutawala); ya pili, kwamba walioitwa watatoka katika ufalme wake uliojaa dhambi kwa sababu utaharibiwa kwa mapigo; na ya tatu, wao kutoka kwake kunalazimisha kwenda kuingia mahali ambako dhambi haipo na ambapo hakuna hatari ya mapigo kuanguka. Kwa hivyo, wao kutoka kwa ufalme wake lazima wawe wanakwenda kwenye ufalme wa Mungu. {TN12: 36.2}
Basi onyo dhidi ya kuipokea alama (Ufu. 14:9-11), pamoja na mwito wa kutoka kwake utarudiwa kwa kilio
36
kikuu zaidi kote kote katika ufalme wa Babeli. {TN12: 36.3}
Wote wanaojikuta katika ufalme wake, na wale wanaojikuta nje yake, lazima wakati huo haraka waamue kuupokea muhuri wa Mungu badala ya alama ya mnyama iwapo wanataka kuokoka ghadhabu ya Mungu. Kwa kufanya hivyo, kundi la kwanza lazima litoke kwake, na kundi la mwisho lazima likae nje yake. Licha ya adhabu ya kifo kwa kuchukua msimamo kama huo (Ufu. 13:15), hawapaswi kusita au kushindwa kufanya maamuzi kwa sehemu ya upande wowote. {TN12: 37.1}
Wale walio ndani ya Babeli lazima watii sauti ambayo inasema: “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18:4. Na wale walio nje, lazima kwa makini watii onyo: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira Yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele ya Mwa-na-Kondoo.” Ufu. 14:9, 10. {TN12: 37.2}
Nuru kwa mada hii itaenea kama moto kwenye mabua makavu hadi mwishowe iangaze nchi yote (Ufu. 18:1), na wote wanaotembea katika mwako wake majina yao yatawekwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Wa-tapata ukombozi kutoka kwa juhudi za mwisho alizoazimu Adui kuutumbukiza ulimwengu
37
kuzimu kwa uangamizi wa milele. Kwa ajili yao, malaika akasema, “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako. . . na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12:1. {TN12: 37.3}
Nembo hiyo sasa inatuongoza kwa
AWAMU YA MWISHO YA WANYAMA. {TN12: 38.1}
Wanyama wa Danieli 7 na mnyama kama chui wa Ufunuo 13, walitoka
38
baharini, lakini mnyama wa pembe mbili aliinuka katika nchi (Aya ya 11), na mnyama mwekundu sana alisimama nyikani (Ufu. 17:3). Ili kupata eneo la kijiografia la serikali ya kila mnyama, ni muhimu kwanza kuhakiki maana ya nembo “bahari,” “nchi,” na “nyikani.” {TN12: 38.2}
“Bahari” Huonyesha Eneo La Wanyama Watano
Kwa sababu katika ufalme wa maumbile, bahari ni ghala (nyumba) ya maji, kwa hivyo katika ufalme wa nembo, “bahari” lazima iwe mahali ambapo mataifa yalizaliwa — Nchi ya Kale. Wanyama watano ‘(simba, Dubu, Chui, na mnyama dubwana, pamoja na mnyama kama chui) wakitoka baharini, huashiria kwamba huwakilisha falme ambazo zimeinuka katika Nchi ya Kale, jinsi historia inavyothibitisha. {TN12: 39.1}
Kwa sababu bahari huonyesha eneo la wanyama hawa, bila shaka, basi,
“Nchi” Huonyesha Kikoa Cha Mnyama Wa Pembe Mbili. {TN12: 39.2}
Kwa sababu mahali mataifa yalikozaliwa huwakilishwa na bahari, basi “nchi,” kinyume kwa “bahari,” huonyesha kikoa cha mnyama wa pembe mbili mbali kutoka kwa Nchi ya Kale. Lakini kupata hasa ni ipi kati ya serikali za Kikoa Kipya huwakilisha,
39
tunapaswa kuziangalia sifa za mnyama mwenyewe. {TN12: 39.3}
Pembe zake mbili ambazo hazina vilemba huonyesha watawala wawili wasiokuwa wa ki-falme, ilhali umbo lake la uchanga kama mwana-kondoo hutabiri ujana usiokuwa na hatia. Na akiwa na uwezo wa kulazimisha yule anayeweza kununua na ambaye hawezi, inaonyesha kwamba anawakilisha taifa linaloongoza katika kudhibiti utajiri wa dunia na sekta ya viwanda. {TN12: 40.1}
Umoja wa Majimbo ya Amerika ni serikali ya pekee katika ulimwengu ambayo inaitikia kauli hizi zote. Ilichimbuka katika ulimwengu mpya (“nchi”), sio katika maeneo ya ulimwengu wa kale (“baharini”). Ni serikali ya pekee ambayo ni kama mwana-kondoo — changa na ya Kikristo, iliyoasisiwa kwa kanuni zisizo za hatia za amani na uhuru, na ikiwa na vyama viwili visivyokuwa vya kifalme ambavyo hutawala (pembe zisizokuwa na taji), cha Jamhuri na cha Kidemokrasia. {TN12: 40.2}
Maadamu nembo za “baharini” na “nchi,” pamoja na sifa za wanyama, kikamilifu huonyesha makao ya kila mnyama, vivyo hivyo
“Nyika” Huonyesha Kikoa Cha Mnyama Mwekundu Sana. {TN12: 40.3}
Kwa kutofautisha, nyika ni kinyume cha shamba la mizabibu. Na kwa vile shamba la mizabibu ni mfano wa nyumba ya watu wa Mungu (Isa. 5:7), nyika inaweza tu kuwakilisha
40
nyumbani kwa watu wa Mataifa. Mnyama huyo akiwa nyikani huashiria kwamba wakati atakapotokea, litakuwako shamba la mizabibu. Bila shaka, utakuwa upuzi kutaja “nyikani” ikiwa ulimwengu wote ni nyika. {TN12: 40.4}
(Kwa maelezo kamili mintarafu wanyama hawa wa nembo, soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2.) {TN12: 41.1}
Uhakika kwamba vyote shamba la mizabibu na nyika vipo kwa wakati mmoja, huonyesha, kwanza, kwamba Babeli, akimwendesha (akitawala) mnyama, anatawala tu kwa nyika (ulimwengu wa Mataifa); na pili, kwamba kutoka kwake watu wa Mungu wanaitwa waingie katika shamba la mizabibu (ufalme uliorejeshwa), pale ambapo hakuna dhambi, na pale ambapo hakuna hofu ya kupokea mapigo. Kuuhusu huu ufalme wa usalama nabii Danieli aliandika: {TN12: 41.2}
“Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:44. {TN12: 41.3}
Mada ya shamba la mizabibu, sasa, inalazimisha uchanganuzi wa
41
MWANAMKE ALIYEVIKWA TAJI YA NYOTA KUMI NA MBILI NA MASALIA WAKE. {TN12: 41.4}
Ni kujithibitisha mwenyewe kwamba mwanamke, Babeli, ni bandia wa “mwanamke” aliyemzaa Mwana wa Mungu (Ufu. 12:1), ambaye kumhusu Maandiko husema: {TN12: 42.1}
“Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke
42
yule aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.” Ufu. 12:13, 14. {TN12: 42.2}
Kuanzia, tunaona kutoka kwenye andiko hili kwamba mwanamke aliondoka katika shamba lake la miza-bibu (nchini kwao — Palestina) na akaenda katika ulimwengu wa Mataifa baada ya mtoto wake kuzaliwa; yaani, katika kipindi chake cha Ukristo, wakati joka alimtesa kupitia chombo cha Wayahudi (Mdo. 8:1, 13:46, 50, 51). Halafu tunaona kwamba baada ya kuwa huko kwa muda fulani, hali zilikuwa kama kumzuia kujilisha mwenyewe, na kwa hivyo ikawa muhimu kwamba apate kulishwa na mtu fulani “kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” {TN12: 43.1}
Miaka mitatu na nusu baada ya kufufuka kwa Kristo, kanisa liliondoka Palestina (shamba la mizabibu), na wakati lilipokuwa katika ulimwengu wa Mataifa (nyikani), “Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke [aliwalazimisha wapagani kubatizwa kuingia katika Ukristo, na kujiunga na kanisa], maji kama mafuriko, amfanye kuchukuliwa [kujazwa washenzi] na mto ule.” Aya ya 15. Akiwa amefurika hivyo, alipaswa kulishwa (kudumishwa) na Bwana, kwa sababu wengi wa wafuasi wake walikuwa wame-fanywa washenzi, na karibu wote ambao hawakuwa, waliuawa na “mafuriko.” Kwa hivyo Yeye asingekuwa amemlisha (kumhifadhi akiwa hai) kwa muujiza, Kanisa lingeangamia wakati wa hizo
43
zama za giza la dini. Kweli, limeweza kujilisha tangu yale Matengenezo, lakini wasio waongofu (mafuriko) bado yapo kati yake. Anayo, hata hivyo, ahadi hii ya uokozi: {TN12: 43.2}
“Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.” Aya ya 16. [TN12: 44.1}
Au, kueleza kwa uandishi, wale wasio waongofu ambao sasa wako kati ya kanisa, watachinjwa na kuzikwa. Waongofu wakati huo watapelekwa katika ufalme. Kisha joka “akamkasirikia yule mwanamke . . . afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Aya ya 17. {TN12: 44.2}
Akiwa amechochewa kwa hasira kuhusu utakaso wake, joka atafanya vita “juu ya wazao wake waliosa-lia.” Dhidi ya mwanamke binafsi, hata hivyo, hatapigana naye, kwa sababu washirika wake, watu 144,000 (malimbuko — Ufu. 7:3-8 ; 14:4), wale wa kwanza kuingia katika ufalme, wanasimama pamoja na Mwa-na-Kondoo, Mfalme, juu ya Mlima Zayuni (Ufu. 14:1). Uwanja wa kasri Lake. Hivyo wakiwa watawala wa makabila, wanawakilishwa na mwanamke aliyevikwa taji. Na wakiwa katika nchi yao, wanalindwa kutoka kwa joka ambalo kwa sababu hiyo linawatesa tu “masalia,” wale walioachwa nyuma, ambao bado wako Babeli lakini hatimaye wanaitwa watoke kwake (Ufu. 18:4). {TN12: 44.3}
44
(Kwa maelezo kamili juu ya Ufunuo 12, soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 64-82.) {TN12: 45.1}
Malimbuko ya ufalme yaja kama tokeo la upepeto, utengo kanisani, kama ulivyoonyeshwa na mifano ya juya na shamba: Samaki wazuri wanaondolewa ndani ya juya (kanisa), na kuwekwa ndani vyombo (ufalme — Mat. 13:48), na ngano inachukuliwa kutoka kati ya magugu, na kuwekwa ndani ya ghala (ufalme — Aya ya 30). Kama samaki wabaya, wanatupwa mbali; kama magugu, yanachomwa moto. (Kwa ajili ya uchanganuzi wa kina wa mavuno, soma Trakti Namba 3, Hukumu na Mavuno.) {TN12: 45.2}
Mavuno ya pili, hata hivyo, wale ambao bado wako Babeli baada ya utakaso, wanachukuliwa kutoka kati ya waovu (Ufu. 18:4), badala ya kwamba wabaya kuondolewa kati ya wema (Mat. 13:49). {TN12: 45.3}
Joka kufanya nao vita kunasababishwa na wao kuwa na Ushuhuda wa Yesu, Roho ya Unabii (Ufu. 19:10), kwa kuwa watunza amri badala ya waabudu wa mnyama na sanamu yake. Lengo la joka ni kuwazuia wasitoke Babeli na hivyo kuingia katika Ufalme unaokua kwa haraka. Kisha inakuwa, hata hivyo, kwamba ulimwengu utawaona watu wote wa Mungu wakitoka
45
Katika Ufalme Wa Babeli Kuingia Katika Nchi Yao. {TN12: 45.4}
Ukweli sasa ukiwa umewekwa wazi kwamba mnyama mwekundu sana ni nembo ya utawala ambao juu yake anatawala “Babeli mkuu, mama wa makahaba,” inafuata kwamba mipaka yake itapanuka kwa umbali zaidi ya mipaka ya mataifa yanayosujudu kwa mamlaka yake. Kwa hiyo, mwito, “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” (Ufu. 18:4), ni mwito kwa ajili yao watoke katika utawala wake, kwamba wasishiriki dhambi zake, wala wasiyapokee mapigo yake. Wale wanaoitikia rai za Bwana, lazima, bila shaka, wawe na mahali palipo huru kwa dhambi pa kwenda, ambapo wataweza ‘kukaa salama,’ ingawa yawezekana hakuna “makomeo wala milango” karibu hapo (Ezek. 38:11). Katika kimbilio hili “watakusanywa kutoka kwa mataifa, nao watakaa salama wote.” Ezek. 38:8. Kwa hivyo, “Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.” Isa. 54:13. {TN12: 46.1}
Watu wa Mungu wakati huo hawataweza kumtumikia Bwana huko “Babeli” na “Misri” kuliko wasinga-liweza kufanya hivyo katika siku za Ezra au Musa, kwa sababu wakati mapigo yanamiminwa juu ya Babeli, kama “moto na kiberiti” ulivyomiminwa juu ya Sodoma na Gomora, basi ikiwa watakaa miongoni mwa walio hai wa kidunia, hawataweza tena kuepuka uharibifu wa mapigo kuliko Lutu angeweza kuokoka
46
moto, iwapo angeendelea kukaa Sodoma. Hivyo wote wanaotaka kuepuka uharibifu uliotabiriwa amin lazima watoke Babeli, kama Lutu na familia yake walivyotoka Sodoma. {TN12: 46.2}
“Na itakuwa,” kwa hivyo, “katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, Atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Isa. 2:2-4. (Soma pia Isaya 11:11, 12, 15, 16.) {TN12: 47.1}
“. . . Bwana Mungu asema hivi; tazama, Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, Nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; Nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele.
47
Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mo-jawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, Nami nitawatakasa; basi watakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wao. {TN12: 47.2}
“Na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu Zangu, na kuzishika amri Zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi Nili-yompa Yakobo, mtumishi Wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi Wangu, atakuwa mkuu wao milele. {TN12: 48.1}
“Tena Nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; Nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu Pangu Nitapaweka katikati yao milele. Tena maskani Yangu itakuwa pamoja nao; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Na mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, Mimi niwatakasaye Israeli, patakatifu Pangu patakapokuwa katikati yao milele.” Ezek. 37:21-28. {TN12: 48.2}
Katika uthibitisho wa ukweli kwamba watu wa Mungu watakuwa tena ufalme, Ezekieli anatabiri
Ugavi Mpya Wa Ardhi. {TN12: 48.3}
Nabii huwasilisha ugavi wa ardhi tofauti kabisa na ule wa
48
wakati wa Yoshua (Yos. 17): Utakuwa katika kanda kutoka mashariki hadi magharibi. Dani atapata sehemu ya kwanza kaskazini, na Gadi, sehemu ya mwisho kusini. Kati ya mipaka ya hawa wawili zitakuwa sehemu za makabila yote yaliosalia. Hekalu litakuwa katikati ya nchi, na karibu nalo utakuwa mji. (Tazama Ezekieli 48). {TN12: 48.4}
Ukweli kwamba ugavi kama huu wa nchi ya ahadi haujawahi kamwe kufanywa, huonyesha kwamba bado ni wa wakati ujao. Pia ukweli kwamba hekalu litakuwa pale, ilhali halitakuwa katika nchi mpya (Ufu. 21:22), bila shaka huthibitisha kwamba mpangilio huu wa kipekee ni wa kabla ya millenia. Zaidi ya hayo, ukweli maradufu kwamba jina la mji ni “Bwana yupo Hapa,” na kwamba eneo lake, kulingana na ugavi wa nchi, lazima liwe tofauti na lile la Yerusalemu ya kale, linaonyesha kwamba Yerusalemu sio mji huo . {TN12: 49.1}
Zaidi ya hayo, Maandiko huonyesha wazi wazi kwamba
WATU WA MATAIFA WATAFUKUZWA KUTOKA KATIKA NCHI TAKATIFU. {TN12: 49.2}
“Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika ali-yesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu. Kisha Bwana akanionyesha maseremala wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya ni-ni? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha
49
pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.” Zek. 1:18-21. {TN12: 49.3}
Hapa tunaona, kwanza, kwamba tawala za mataifa katika kuwatawanya watu wa kale wa Mungu, hu-wakilishwa kama pembe nne, na baadaye, katika kuwatupa nje Mataifa, huwakilishwa kama maseremala wanne. Hivyo pia imetabiriwa ki-mchoro kwamba “wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.” Luka 21:24. {TN12: 50.1}
(Soma Ezekieli 36 na 37; Yeremia 30 na 31.) {TN12: 50.2}
Ingawa swali letu la kwanza linapaswa kuwa, “Tutafanya nini ili kuepuka kuwatii maadui wa Mungu, ili tupatikane tunastahili sehemu katika ufalme Wake wakati uovu huu utakapokuja?” Hata sasa wengi wanatunga swali lao la kwanza,
Gogu Ni Nani? {TN12: 50.3}
Mtu kujaribu kwa raslimali zake mwenyewe kuelezea ni nani Gogu, ni kwake yeye kujaribu kutenda lisilowezekana — mradi ambao unaweza kutokeza kukata tamaa tu. Hili linaonekana katika ukweli kwamba ingawa Biblia husema waziwazi kwamba mahali pa vijiji visivyokuwa na maboma katika milima ya Israeli, — nchi ya Israeli yenyewe (Palestina), ambako baba za taifa la Waisraeli waliishi, — lakini watu wamejaribu kutuambia kwamba iko Amerika! {TN12: 50.4}
Hivyo ni kwamba katika udanganyifu wao wenyewe
50
BWANA ATAYAHARIBU NA KUYAHUKUMU MATAIFA. {TN12: 50.5}
“Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba; hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kunyang’anya vitu vya watu walionyang’anya vitu vyao, asema Bwana Mungu. {TN12: 51.1}
“Tena, itakuwa katika siku hiyo, Nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wa-taliita, Bonde la Hamon-Gogu. Na kwa muda wa miezi saba nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi. Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile Nitakapotukuzwa, asema Bwana Mungu. {TN12: 51.2}
“Kwa sababu hiyo, Bwana Mungu asema hivi, sasa Nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, Nita-wahurumia nyumba yote ya Israeli; Nami nitalionea wivu jina Langu takatifu. Nao watachukua aibu yao, na makosa yao yote waliyoniasi, watakapokaa salama katika nchi yao wenyewe, wala hapana mtu ataka-yewatia hofu; Nitakapokuwa nimewaleta tena kutoka kabila za watu, na kuwakusanya kwa kuwatoa katika nchi za adui zao, na kutakaswa kati yao mbele ya macho ya mataifa mengi. Nao watajua ya kuwa Mimi Ndimi Bwana, Mungu wao, kwa kuwa Naliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na Mimi ni-kawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala Sitawaacha tena huko kamwe, hata mmoja-wapo; wala Sitawaficha uso Wangu tena; kwa maana Nimemwaga Roho Yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana Mungu.” Ezek. 39:9-13, 25-29. {TN12: 51.3}
51
“Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, Nitakusanya mataifa yote, Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko Nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi Yangu. {TN12: 52.1}
“Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana. Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Ye-hoshafati; maana huko ndiko Nitakakoketi Niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.” Yoeli 3:1, 2, 9-12. {TN12: 52.2}
“Na mataifa yote watakusanyika mbele Yake; Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; Atawaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto. Kisha Mfalme Atawaambia wale walioko mkono Wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu.” Mat. 25:32-34. {TN12: 52.3}
Lakini kwa wale walio upande Wake wa kushoto Yeye atasema: “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Mat. 25:46. {TN12: 52.4}
(Kwa uchanganuzi kamili wa ufalme, soma Trakti Namba 8, Mlima Zayuni Saa ya Kumi na Moja, na Trakti Namba 9, Tazama Navifanya Vyote Kuwa Vipya, uk. 40-64.) {TN12: 52.5}
Haya ni baadhi ya matukio ya baadaye ambayo yatafuata hivi karibuni kwa mfululizo wa haraka katika kuukaribisha ufalme. Kisha linafuata
52
kufungwa kwa muda wa rehema, na kumiminwa kwa mapigo saba ya mwisho, ambayo yataanguka kwa wale ki-mfano wanasimama kwa mkono Wake wa kushoto — wale walio nje ya Palestina. Basi wakati mapigo yanamiminwa, vita kuu zaidi vitapiganwa, “ vita vya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi”, — uliotarajiwa kwa muda mrefu mwisho wa ulimwengu, — Har-Magedoni (Ufu. 16:12-16). {TN12: 52.6}
Kurejea sasa kwa mgogoro uliopo wa ulimwengu wetu, kwa sababu, kama ilivyoelezwa awali, wafalme wali-otawazwa wa leo (Ufu. 13) tayari wamepungua kuwa wachache, na kwa sababu makanisa, katika kilio chao cha amani na usalama, yanajitahidi kufumbata mikono moja kwa lingine, tunapaswa kutenda kwa hekima sasa kuuliza katika
MATUKIO YA SASA AMBAYO YANAWEZA KUTIMIZA UNABII. {TN12: 53.1}
Kwa sababu kibishanio kati ya mataifa yenye hasira ya leo ni masoko ya dunia, na kwa sababu makanisa yanatishwa na serikali za kikatili, na kwa hivyo yanashauriwa kujishinikiza pamoja ili kuudumisha Ukristo, ukweli hivyo unathibitishwa kwamba wakati umekaribia kwa uhuisho wa ufalme uliotabiriwa wa dunia nzima wa kidini, kisiasa na kibiashara, dawa inayodhaniwa kuyatibu magonjwa ya dunia. {TN12: 53.2}
Sasa inaonekana kwamba unabii wa Ufunuo 17 na 18, picha ya mwisho katika mchezo wa kuigiza unao-chezwa na mataifa, karibu unaidhinishwa. {TN12: 53.3}
53
Mataifa yanayoshindana tayari yamegawanyika katika makambi mawili tofauti ya itikadi: Kwa upande mmoja ni serikali za kidemokrasia, ilhali upande mwingine ni za kiimla. Iwapo za mwisho zinaendelea kufanikiwa kupeleka sheriani ushindi wao usiokoma wa kuutawala ulimwengu na enzi, njia pekee ya kujinasua kwa mataifa ya Kikristo, jinsi wanavyoyaona matatizo yao kibinadamu, itakuwa kuyasalimisha mamlaka yao kwa kanisa. Kwa maana, kuona Mkatoliki anakabiliana na Mkatoliki, na Mprotestanti dhidi ya Mprotestanti, katika pambano la kufa, watavuviwa katika kitisho cha hofu kumwekea matandiko mnyama, na kulianzisha tena kanisa kama dereva wake ili kujiweka huru kutokana na pingu za kiimla, ili kuulinda Ukristo. Wataona ushindi katika mbinu hii, ikiwa watanyimwa katika vita, hasa kwa sababu dha-hiri kwamba wengi wa mamilioni ya washiriki wa makanisa haya, katika kila jeshi la mataifa ya kiimla yaliyoungana katika vita, watayaheshimu maagizo ya kanisa, juu ya yale ya serikali zao. {TN12: 54.1}
Mchanganyiko kama huu wa hali utasababisha mwigo wa utawala wa kimataifa wa kanisa na serikali wa Vizazi vya Katikati, na utasafirisha kwenye rundo la takataka chombo bora zaidi duniani cha uhuru wa kibinadamu — Katiba iliyovuviwa na Mungu ya Umoja wa Majimbo ya Amerika. Kwa kuwa maendeleo haya yatafanya matatizo ya dunia kuwa mabaya zaidi, itakuwa ishara ya kwamba malaika wanne
54
wameziachilia pepo, na ya kwamba watu 144,000 Waisraeli wametiwa muhuri (Ufu. 7:3-8). {TN12: 54.2}
Na ni nini zaidi, mfumo ambao, kwa machungu ya kifo kwa kutoukubali, mfumo kamili wa ibada kinyume cha dhamiri, si chochote ila Demokrasia na Ukristo. Dini ya kulazimishwa si pungufu ya kushika miguu ya raia, badala ya amri ya wafuasi wa hiari. {TN12: 55.1}
Kuanguka kasi kwa wafalme wa mataifa (yanayowakilishwa na pembe zenye taji za mnyama kama chui) kinyume na wanaoinuka watawala wasiokuwa na taji wa mataifa (wanaowakilishwa na pembe zisizokuwa na taji za mnyama mwekundu sana), kunaonyesha kwamba ulimwengu unapita kutoka kwa kipindi cha serikali za kifalme, na kuingia katika kipindi cha serikali zisizo za kifalme. {TN12: 55.2}
Mapinduzi ya kiimla kwa udemokrasia yatahatarisha uendelevu wa Ukristo wa kitaifa. Ili kukabiliana na dhoruba hii, serikali za Kikristo zitakuwa tayari zimemketisha mwanamke kwa mnyama huyo malkia wa dunia aliyetabiriwa — Babeli Mkuu. Kisha atasema moyoni mwake: “Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.” Ufu. 18:7. {TN12: 55.3}
Muungano huu wa kanisa na serikali utaleta “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo.” Dan. 12:1. Hata hivyo, “mtu atakaye kuiokoa [kuyalinda] nafsi yake” kwa kutotii ukweli, “ataipoteza,” anasema Kristo, “na mtu atakayepoteza [hatarisha] nafsi yake kwa ajili Yangu” kwa kusimama
55
kidete kwa ukweli, “ataiona.” Mat. 16:25. Na nabii anatangaza kwamba “wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. . . Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan. 12:1, 10. {TN12: 55.4}
Bila Kristo hakuna mfumo unaoweza kuufumua msokotano wa ulimwengu, ila unaweza tu kulifanya fundo kuwa baya zaidi. Babeli mkuu, kwa hivyo, anaweza kudumu lakini kwa muda mfupi — “saa” moja ya mfano — na kisha atafagiliwa mbali na pembe zisizokuwa na taji (Ufu. 17:16), tokeo la wakati wa taabu hatimaye unafikia kufungwa kwa muda wa rehema, na kwa ushindi na kutawazwa kwa “MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA BWANA” (Ufu. 19:16), Ambaye haki Yake ni kutawala. {TN12: 56.1}
Kwa hivyo ni kwamba “na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, am-bao hautaangamizwa:” ila “utasimama milele.” Dan. 2:44. “Amin, Nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.” Mat. 24:34. Kisha, na si hadi wakati huo, dunia itaweza kutarajia amani. {TN12: 56.2}
56
Kwa hiyo “neno la unabii lililo imara zaidi,” ambalo halishindwi kamwe kusema ukweli, linatangaza kwamba wala Uingereza au Ujerumani, ila badala yake Babeli Mkuu (sanamu ya mnyama) mwishowe, kwa muda mchache, atafaidika kwa vita. Siku zote, hata hivyo, hakuna isipokuwa watu wa Mungu watafaidika. Watawekwa huru kwa kuwa “ufalme, ambao hautaangamizwa milele” au “watu wengine hawataachiwa enzi yake.” Dan. 2:44. {TN12: 57.1}
Ni ulioje umuhimu, basi, kwamba tuihifadhi nuru ambayo hadi hapa imeangaza katika mawazo yetu kwa Neno la Unabii lisiloshindwa kamwe, na utimilifu wake wa kihistoria, ili kwamba sio tu tuweze kuiacha njia inayoongoza kwenye maangamizi, ila pia tuweze kutembea katika njia ya usalama wa milele. Kufikia mwisho huu, hebu tuangalie sura ya Biblia ambayo sikuzote imewakanganya wanafunzi wa unabii, lakini ambayo sasa, katika nuru ya Ukweli wa Sasa, imekuwa ni mojawapo ya unabii wa Biblia rahisi sana na una-oeleweka: {TN12: 57.2}
DANIELI KUMI NA MOJA — MUHTASARI,
“Kile Ambacho Kimenakiliwa Katika Maandiko.”
“Nami sasa Nitakuonyesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Uyunani. Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa mamlaka kubwa, na kutenda apendavyo. Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo;
57
kwa maana ufalme wake utang’olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao.” Aya ya 2-4. {TN12: 57.3}
Dhahiri ilivyo, kutoka kwa aya hizi, kwamba Ufalme wa Wamedi na Waajemi ulipaswa kuangushwa na “mfalme mwenye nguvu” wa Uyunani (Alexander
58
Mkuu), na halafu kugawanywa katika sehemu nne (ya kusini, kaskazini, upande wa mashariki na magharibi), “utang’olewa, hata kwa ajili ya wengine.” Hivyo ilikuwa kwamba baada ya kifo cha Alexander, ufalme uligawanyika, “na kila sehemu moja ikapeanwa kwa kila mmoja wa majemadari wanne waliofanya shirikisho. Wa kwanza, Ptolemi alishika mamlaka ya kifalme huko Misri; wa pili, Selukasi, Syria na Asia ya Juu; wa tatu, Lisimakus, Thrake na Asia Ndogo hadi Tauro; na wa nne, Kassanda alichukua kama mgao wake Makedonia.” — Historia ya Ulimwengu, uk. 100. {TN12: 58.1}
Ni vyema kukumbuka kwamba mbali na kutaja maeneo ya kijiografia ya migawanyiko minne ya Uyunani, kumbu kumbu ya kinabii ya mnyororo mzima wa matukio yote umeshirikisha mfalme wa kusini na mfalme wa kaskazini. Matendo ya mfalme wa kaskazini, hata hivyo, yanasisitizwa hasa kuonyesha kwamba akaunti yote ya kinabii impean-wa hasa kufichua kujiingiza kwake kwa mambo matakatifu. Kwa hivyo inafuata orodha ya baadhi ya
Matendo Yanayomtambulisha Mfalme Wa Kaskazini. {TN12: 59.1}
(1) Anamshinda mfalme wa kusini, na kuuteka ufalme wake (aya za 15, 16), baada ya hapo anasimama katika “nchi ya uzuri” (aya ya 16) — Palestina. {TN12: 59.2}
(2) Katika utukufu wa ufalme huo, mwenye kutoza ushuru atasimama (aya ya 20). {TN12: 59.3}
59
(3) Ufalme wake “unagharikishwa” na silaha za mafuriko kutoka mbele yake (aya ya 22), na anapoteza Misri na Palestina. {TN12: 60.1}
(4) Baadaye atatenda kwa hila, naye atakuwa hodari pamoja na watu wadogo (aya ya 23). {TN12: 60.2}
(5) Anawapotosha waovu kwa maneno ya kujipendekeza (aya ya 32). {TN12: 60.3}
(6) Ataigawa nchi kwa rushwa (aya ya 39). {TN12: 60.4}
(7) Anakuwa na nguvu mara ya pili, lakini anashindwa na mfalme wa kusini (aya za 25, 29, 30). {TN12: 60.5}
(8) Wafalme wote wawili wanasema uongo walipo pamoja mezani (aya ya 27). {TN12: 60.6}
(9) Baada ya kuwa na nguvu mara ya pili, na akiwa amejihusisha na vita ambavyo hakufanikiwa na mfalme wa kusini, moyo wake anauweka kinyume cha agano takatifu (aya ya 28). {TN12: 60.7}
(10) Anapatia unajisi patakatifu pa ngome, na kuiondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku (aya ya 31). {TN12: 60.8}
(11) Anaiacha miungu ya baba zake (aya ya 37), anamtambua mungu mgeni (aya ya 39), na kuipuuza hamu ya wanawake (aya ya 37). {TN12: 60.9}
(12) Katika wakati wa mwisho, anamshinda tena mfalme wa kusini, ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati (aya ya 40); tena ataingia katika nchi hiyo ya uzuri. Baada ya hayo, Edomu na Moabu na wakuu wa watu wa Amoni, wanaokoka kutoka mkono mwake (aya ya 41); na
60
Walibia, pia Wakushi, watafuata nyayo zake (aya ya 43). {TN12: 60.10}
(13) Habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha. Kwa hivyo, atatoka kwa ghadhabu nyingi, kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi (aya ya 44). {TN12: 61.1}
(14) Naye atapanda hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri, lakini atafikilia mwisho wake, wala hakuna atakayemsaidia (aya ya 45). {TN12: 61.2}
Kuanza na Ufalme wa kale wa Wamedi na Waajemi (aya ya 2, 3), mnyororo wa matukio ya unabii huu unafikia wa-kati ambapo “mfalme wa kaskazini” atapanda “hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri” (aya ya 45), na mwisho wake, jinsi malaika alivyofafanua, na matukio ya Danieli 12: “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake hauku-wapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja ataka-yeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12:1. {TN12: 61.3}
Ukifunika kipindi hicho cha muda mrefu, karne nyingi, utawala wa wafalme ambao historia yake imeandikwa katika unabii huu, bila shaka umepita chini ya
Idadi Za Tawala. {TN12: 61.4}
Kuona kwamba hakuna mwanadamu ambaye ameishi siku zote katika karne hizi, ni
61
dhahiri kwamba majina, “mfalme wa kusini” na “mfalme wa kaskazini,” inahusu mistari miwili ya watawala. Kuona pia kwamba hakuna serikali au ufalme umesimama thabiti katika vizazi vingi, ni dhahiri vivyo hivyo kwamba mistari hii miwili imepitia vipindi
62
mahsusi vya wenye enzi — tawala nyingi. Kwa sababu hii, Biblia huwatofautisha kwa majina yao ya nasaba ya kijiografia. {TN12: 61.5}
Sasa ni wazi kutoka kwa Maandiko kwamba jimbo la Uyunani kusini mwa Mediterrania, la Ptolemi, ndilo la kwanza kupata jina, “mfalme wa kusini,” ilhali jimbo la kaskazini mwa Mediterrania, la Lisimakus, ndilo la kwanza kupata jina “mfalme wa kaskazini.” Kuhusiana na mipaka ya mistari hii miwili ya watawala, Mediter-rania, kwa hivyo, inakuwa ncha ya dira ambayo kutoka kwayo lazima itegemewe kuwahesabu. {TN12: 63.1}
Katika mwaka 281 K.K, Lisimakus aliongeza kwa ufalme wake ule wa Kassanda; kisha katika mwaka 279 K.K, Selukasi alimshinda Lisimakus na kuutwaa ufalme wake, kisha majimbo ya mashariki, kaskazini, na magharibi yakawa moja, ilhali Ptolemi alishikilia lake mwenyewe, jimbo la kusini. Nasaba ya Selukasi, kwa hivyo, iliingia katika utawala wa pili wa kaskazini, ilhali nasaba ya Ptolemi iliendelea kuwa utawala wa kwanza wa kusini. {TN12: 63.2}
Kufikia hapa, maono ya kinabii yamekuwa wazi kwa wote, lakini kutoka hapa kuendelea, yamesalia kufungwa ingawa wengi wamejaribu kuyafunua. Kuufungua, bila ufunguo, mlango uliofungwa, ni, bila shaka, kuuvunja mlango. Lakini, kwa sababu hauwezi kuvunjwa, mlango uliofungwa wa Unabii hauwezekani kufunguliwa bila
Ufunguo. {TN12: 63.3}
Njia rahisi na nzuri ya kutokosa kukiona kitambulisho cha wafalme hawa wawili, ni
63
kuiruhusu kalamu ya Unabii kufuatilia kwenye ramani ya historia, watawala mtawalia wa Misri na Palestina. Kwa maana majina ya wafalme ambao waliozitwaa na kuzipoteza nchi hizi za kale, yameandikwa katika sura hii ya kinabii ili kuhifadhi utambulisho na kufunua maazimio maovu ya wote mfalme wa kusini na mfalme wa kaskazini. {TN12: 63.4}
Kumbuka sasa, kwa kuanza, mfalme wa kusini anaitawala “nchi ya uzuri,” Palestina, pamoja na Misri, na mfalme wa kaskazini anaitwaa nchi ya uzuri mara mbili (aya za 16, 41). Iwapo anaitwaa mara mbili, basi lazima aweze kuwa ameipoteza mara moja. Kwa hiyo, wafalme wote wawili waliitawala mara mbili, na kui-poteza mara mbili. Lakini mfalme wa kaskazini, wa mwisho kuitawala anaimiliki “ katika wakati wa mwisho,” wakati ambapo wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka (Dan. 12:4) — wakati wetu. Maki hili kwa uangalifu, kwa maana shughuli hizi za ardhi zinatoa ufunguo wa kitambulisho cha wafalme hawa tangu wakati wa kifo cha Alexander hadi wakati wetu. {TN12: 64.1}
Malaika alisema kwa mkazo kwamba wafalme wa kutawala Palestina, pamoja na Misri, walikuwa kama ifu-atavyo: Kwanza, mfalme wa kusini (Ptolemi); pili, mfalme wa kaskazini (Roma ya Upagani); tatu, mfalme wa kusini (Uturuki); na nne mfalme wa kaskazini (Uingereza). Hapa, katika kurasa ishirini na tano zifuatazo, ni maelezo ya unabii unaohusiana na historia. {TN12: 64.2}
Kwa kuzingatia kweli hizi za msingi zilizotangulia, tunapaswa sasa kutathmini
64
sawa sawa kukunjua kwa gombo, na kwa busara kuulinganisha ukurasa wa unabii na ukurasa wa historia tun-apopita kutoka kwa wakati wa utawala wa kwanza wa kaskazini, ule wa Lisimakus, kuendelea mbele ya wakati wa utawala wa pili wa kaskazini, ule wa Selukasi shujaa, ambaye aliuteka utawala wa Lisimakus, na kuendelea hadi wakati wa utawala wa kaskazini wa tatu, ule wa Rumi, dola ambayo iliupindua ufalme wa Selukasi. Na kwa sababu simulizi la kinabii lilitolewa kuifichua kazi ya mfalme wa kaskazini wakati wa utawala wa tatu, basi tunaongozwa kulichunguza kundi la matendo ya kinabii yaliyotajwa awali, kama yalivyoelezwa kwenye ukurasa wa 59-61. {TN12: 64.3}
(1)
Kaskazini Yashinda Kusini — Yachukua Misri na Palestina.
“Basi mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima, na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga. Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri [Palestina], na uharibifu utakuwa mkononi mwake.” Aya ya 15, 16. {TN12: 65.1}
Andiko hili hutuleta hakika kwa wakati wa utawala wa tatu katika ufalme wa kaskazini, ule wa Rumi ya Upagani, ambao ulipindua kabisa utawala wa kwanza wa ufalme wa kusini, ule wa nasaba ya Ptolemi. Misri na Palestina kisha zikapita
65
kutoka mikononi mwa mfalme wa kusini (Ptolemi) kuingia katika mikono ya mfalme wa kaskazini (Rumi): “Katika mwaka wa 63 K.K. jemedari wa Kirumi Pompey. . . alipambana dhidi ya Yerusalemu. . . Syria. . . ikawa kitu cha Kirumi.” — Uwanja wa Vita, na Helaire Belloc. Na katika mwaka wa 31 K.K. “Misri ikawa Mkoa wa Rumi.” — Kitabu Kipya cha Marejeleo ya Mwanafunzi. {TN12: 65.2}
Kwa sababu dola iliyoupindua utawala wa Ptolemi na kuchukua Misri na Palestina, hutambulishwa na malaika kama mfalme wa kaskazini, na maadamu Rumi ya Upagani ilikuwa ndio dola hiyo, inafuata kwamba jina, “mfalme wa kaskazini,” baada ya kupita kutoka kwa Lisimakus (ambaye utawala wake ulikuwa ufalme wa kwanza wa kaskazini), kwa Selukasi (ambaye utawala wake ulikuwa ufalme wa pili wa kaskazini), ukaanguka kwa wafalme wa Kirumi (ambao utawala wao ulikuwa ufalme wa tatu wa kaskazini). Tazama Ramani ya 4, uk. 17. {TN12: 66.1}
Pamoja na hivi vipindi mahsusi vya tawala, tunaletwa chini hadi mwaka wa 31 K.K., ambapo kwa wakati huo Rumi haikutawala tu falme za Lisimakus, Selukas, na Ptolemi, bali pia Ufalme wa Kassanda — Ufalme wote wa Alexander. {TN12: 66.2}
(2)
Katika Utukufu Wa Ufalme
“Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake.” Aya ya 20. {TN12: 66.3}
Kaisari Augusto, mfalme wa Kirumi, ndiye aliyeutoza ulimwengu kodi: {TN12: 66.4}
66
“Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwen-gu. (Na kodi hii ilifanywa mara ya kwanza Sirenio alipokuwa liwali wa Shamu). Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, (kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi).” Luka 2:1-4. {TN12: 67.1}
Kwa sababu huyu mtoza kodi angeinuka wakati ufalme ungekuwa katika utukufu wake, taarifa hiyo humaan-isha kwamba utukufu wake ungefifia. {TN12: 67.2}
(3)
Agharikishwa Na Mafuriko — Anapoteza Misri na Palestina
“Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia.” Aya ya 22. {TN12: 67.3}
Hapa kunaonyeshwa kuvunjika kwa Ufalme wa Kirumi mikononi mwa majeshi ya Wabaribari ambayo yali-fagilia chini na, kama mafuriko, yakafurika sana. Tazama ramani ya 8. {TN12: 67.4}
(4)
Tena Wainuka Kwa Utawala
“Na baada ya maagano atatenda kwa hila; maana atapanda, naye atakuwa hodari pamoja na watu wachache.” Aya ya 23. [TN12: 67.5}
Kutoka kwa taarifa hii ya kinabii, tunaona kwamba Rumi ungeinuka kutoka kwa uharibifu wake na
67
fedheha, na kuwa thabiti tena, lakini wakati huu kwa udanganyifu, pamoja na “watu wachache.” Katika mnyororo huu wa unabii, basi, Rumi huonyeshwa katika awamu mbili tofauti, Upagani na Upapa, kama vile ilivyo-
onyeshwa kwa mnyama wa nne wa mfano wa Danieli 7. Kwa hivyo ilikuwa kwamba baada ya Rumi ya Upagani kujiona imeshambuliwa na kunyenyekezwa hata kwa ardhi, chini na nje, kwa mfano, ilitunga udanganyifu ambao ingeweza kuutumia kujirudisha mamlakani tena. Mpango huo ulisababisha kanuni za sheria za kidini, utekelezwaji wake ambao uliendeshwa na “watu wachache” — wanaojiita eti Wakristo. {TN12: 67.6}
68
Haukuitisha mapinduzi kwa wafalme, ila badala yake kuwafanya kuwa Wakristo. Hivyo kwa amani mfalme wa kaskazini alifanikiwa kuuinua juu mpango wake wa kutawala kama mfalme wa wafalme wa kiroho kwa jina la Mungu wa Mkristo. Kwanza ilitawala kwa mataifa, pili kwa wafalme wa mataifa. {TN12: 69.1}
Kweli hizi za kihistoria na za Kibiblia huonyesha kwamba mataifa yaliyofanywa kuwa ya Kikristo, chini ya kichwa kimoja cha kiroho, hujumuisha awamu ya pili ya Rumi, na Uvuvio uliupatia jina “mfalme wa kaskazini.” Kwenye kiti chake cha enzi, wafalme sawa na wakulima, ndani ya milki yake iliyosambaa sana ya Rumi iliyofanywa kuwa ya Kikristo, walisujudu kwa utiifu kamili na ibada. Hivyo kwa njia ya hila, alikuwa thabiti tena, jinsi aya zifuatazo za historia zinavyohakikisha. {TN12: 69.2}
(5)
Rekodi Ya Historia Ya Kujipendekeza Na Ukristo Wa Kulazimishwa.
“Maaskofu, au waangalizi wa makanisa ya Kikristo, mwanzo hawakujishushia heshima
69
katika roho ya upole ya mwasisi wa dini yao. Lakini kwa muda mrefu walitafuta mamlaka yasiyodumu, na manufaa ya kidunia. Maaskofu wa miji mikubwa walishika mamlaka juu ya yale ya mashambani yaliyoizunguka; na Rumi, Konstantinopo, Alexandria, Antiokia, na Yerusalemu ikawa viti vya mamlaka ya kidini; na maaskofu wao wangesemekana kujumuisha wachache katika kanisa. . . Rumi ikawa, katika zama za giza, mfalme wa wafalme; hakuna zaidi — alidai kuwa mahali pa Mungu.” — Historia ya Ulimwengu, uk. 198, 199. {TN12: 69.3}
“Wakati wa kutawazwa kwa Charlemagne, Papa Leo wa 3, baada ya kuweka taji juu ya kichwa chake, alimsifu kwa jina la mfalme wa Warumi. Alikuwa ameyazima mataifa ya washenzi ya Ulaya, isipokuwa Waskandinavia, au Wadenmak, na ufalme wake ulijumuisha Ufaransa, Ujerumani, Italia, na kaskazini mwa Hispania. Kutoka mashariki Irene, malkia wa Konstantinopo, alitafuta urafiki kwake, na hata khalifa wa Bagdadi, wa kifalme Haruna al-Ras al-Raschid, aliingia katika mawasiliano naye, na kumpelekea funguo za kaburi takatifu la Yerusalemu. Charlemagne, ingawa mshenzi ambaye kwa mara ya kwanza hangeweza kuandika jina lake, lakini ‘alisaini mikataba yake kwa kipini cha upanga wake, na kuitekeleza kwa ncha yake,’ bado alikuwa na huruma kubwa kwa watu wasomi. . .” — Ki-menukuliwa Tayari, uk. 203. {TN12: 70.1}
“. . . WITIKIND, hodari zaidi na maarufu wa wakuu wao, kwa muda mrefu waliukumbatia
70
Ukristo, na kujiuzulu silaha zake. Charlemagne hatimaye aliwaajibisha watu wa Uingereza ya kale, chini ya adhabu ya kifo, kuupokea ubatizo. Aliwavamia na kuwashinda Wahunni na Waskandinevia.” — Kimenukuliwa Tayari, uk. 202. {TN12: 70.2}
“. . . Charles, kutoweza kuwazuia wavamizi, akawaachia wilaya ya Nuestria, baadaye ikaitwa Normandy, na akampa binti yake Rollo katika ndoa. Lakini mkuu wa Norman alikuwa, hata hivyo, kwa kumtukuza Charles, aka-piga magoti na kumbusu kidole cha kifalme. . .” — Kimenukuliwa Tayari, uk. 202. {TN12: 71.1}
“Alfredi [mfalme wa Uingereza] aliwapa Wadenmak kibali cha kukaa huko Northumberland na Mashariki ya An-glia, kwa sharti la wao kutawaliwa na sheria zake, na kuukumbatia Ukristo. Walipaswa kubatizwa; na mfalme mwenyewe alisimama kama bwana-mkubwa kwa GUTHRUM mkuu wao. . . “ — Kimenukuliwa Tayari, uk. 209. {TN12: 71.2}
“Alipata kisingizio cha kuuvamia ufalme wa Lombardi, katika uadui wa DESIDERIO dhidi ya papa. Charlemagne aliivuka iliyo kubwa Mtakatifu Bernard kutoka Geneva, na akafanikiwa kuitwaa Pavia na Verona. Lombardi kwa mu-da mfupi ilitiishwa chini, na mfalme kufanywa mateka. Charlemagne kisha alizuru Rumi, ambako alipokelewa na pa-pa Adrian 1, na kila onyesho la furaha, na kumsifu kama mkombozi wa kanisa. Alijisababisha atawazwe kuwa mfalme wa Lombardi.” — Kimenukuliwa Tayari, uk. 201. {TN12: 71.3}
Katika njia hii ya udanganyifu alikuja mfalme wa kaskazini, na kupata “ufalme kwa
71
kujipendekeza” (Aya ya 21) na kwa kuheshimu “mungu wa ngome “ kama ilivyotabiriwa katika aya za 24, 38, 39. {TN12: 71.4}
(6)
Historia Hueleza Ugavi Wake Wa Ardhi Kwa Faida
“MFUMO WA UKABAILA ni neno linalotumiwa kueleza namna ambayo wakuu, walioshinda kwa msaada wa majeshi yao, na kukaa katika nchi walizoziteka, waligawanya ardhi kati ya wafuasi wao; na madeni na manufaa yali-yoongezeka kutokana na ugavi huu. Wakati mkuu, au mfalme, alipoona eneo lote ambalo halijagawanywa kwa upande mmoja, na kundi la wafuasi wake waliotaka kulikalia kwa upande mwingine, swali kwa kawaida lilizuka, ataligawanya vipi? Hali isiyotulia ya ulimwengu ilipaswa kuzingatiwa. Ikiwa aliligawanya miongoni mwa watu wake, bila kuuhifadhi mwelekeo wa ki-vita, wangekuwa nyara za baadhi ya magenge yaliyojihami, yaliyosaka makao. Kiongozi, kwa hivyo, baada ya kuhifadhi aliyochagua, alitoa sehemu kubwa ya ardhi kwa majemedari wa wakuu wake, — kwa sharti la wao kumtukuza, wakilipa kiasi fulani cha fedha, na kuonekana shambani na idadi fulani ya wafuasi, wakati wowote alipoitisha msaada wao. Maofisa wakuu hawa, baada ya kuhifadhi kile walichotaka kwa ajili ya ma-tumizi yao, waligawa salio la ardhi waliyogawiwa, kwa waliowapenda;
72
ambao wangetoa fedha na askari kwa ajili yao, kama ilivyokuwa wao kwa mfalme. Wenyeji waliotekwa waliosalia wakawa watumwa, na walihamishwa pamoja na mashamba. Hawa wafalme waliinuka kwa ushujaa wao wenyewe; lakini kwa suluhu na taifa lao, mfalme kwa ujumla alikuwa kwanza achaguliwe katika familia zao, kisha wa kurithi-wa.” — Historia ya Ulimwengu, uk. 200. {TN12: 72.1}
(7)
Utawala Wa Pili Wa Kusini; Waushinda Utawala Wa Nne Wa Kaskazini
“Naye atachochea nguvu zake na ushujaa wake juu ya huyo mfalme wa kusini kwa jeshi kubwa; na mfalme wa kusini atafanya vita kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi; lakini hatasimama; maana wa-tatunga hila juu yake. Naam, walao sehemu ya chakula chake watamwangamiza, na jeshi lake litaghari-kishwa; na wengi wataanguka wameuawa. . . Ndipo atakaporudi mpaka nchi yake mwenye utajiri mwingi; na moyo wake utakuwa kinyume cha hilo agano takatifu; naye atafanya kama apendavyo, na kurudi mpaka nchi yake. Kwa wakati ulioamriwa atarudi, na kuingia upande wa kusini; lakini wakati wa mwisho mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa wakati wa kwanza. {TN12: 73.1}
“Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighad-hibikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.” Aya ya 25, 26, 28-30. {TN12: 73.2}
Tumeona tayari kutoka kwa unabii, pia kutoka kwa historia, kwamba utawala wa kwanza wa kusini (wa Ptolemi) ulipinduliwa na utawala wa tatu wa kaskazini (ule wa
73
Rumi ya Upagani). Na kwa sababu Rumi ya Upagani kamwe haikupigana vita dhidi ya dola nyingine yoyote ya kusini, pointi mbili husimama wazi: Kwanza, kuufuata utawala wa Ptolemi, mfalme mwingine wa kusini lazima awe ameinuka; na pili, vita dhidi ya mfalme huyu wa kusini vilipiganwa na utawala uliofuata Rumi ya Upagani, ule wa Rumi iliyofanywa kuwa ya Kikristo, utawala wa nne wa kaskazini. Ulichochea “nguvu zake na ushujaa wake dhidi ya mfalme wa kusini.” {TN12: 73.3}
Ufalme pekee ambao umeinuka kutoka kusini tangu utawala wa Ptolemi kuanguka, na ambao umetawala Misri na Palestina, ni ule wa Waarabu: “Waislamu, wanaozungumza Kiarabu jamii ya uzao mseto, wakifanyiza sehemu ya idadi ya Wabaribari, na kupata jina lao kutoka kwa Mauri, wenyeji wa kale wa Mauretamia, am-bao uzao wao halisi ni, hata hivyo, Waamazirkhi, tawi la Waarabu. Waarabu mamboleo wamechipuka kutoka kwa muungano wa wenyeji wa kale wa eneo hili na Waarabu waliowashinda, walionekana katika karne ya 7. Kwa sababu Waislamu waliowashinda Wavisigothi huko Uhispania (mwaka 711-713) walitoka Afrika Kaskazini, jina la Waarabu pia walihusishwa nalo na waandishi wa Kihispania, na katika uhusiano huo ni visawe kwa Waarabu na Wasarakeni. Waarabu hawa walisukuma kuelekea kaskazini hadi Ufaransa, mpaka wakarudishwa nyuma na Charles Martel katika vita kuu ya Tours mwaka 732, baada ya hapo walijizuilia kivitendo
74
kwa Uhispania kusini mwa Ebro na Sierra Guadarrama. . . Waarabu waliofukuzwa, walikaa kaskazini mwa Afrika, walianzisha miji ambayo kutoka kwayo walivizia pwani za Uhispania, na hatimaye wakakua nchi za uharamia za Ub-aribari, ambazo unyang’anyi ulikuwa chanzo cha kuzikereketa tawala za Kikristo zilizostarabika hadi hata karne ya sasa.” — Kamusi Elezo ya Karne ya Ishirini, Gombo la 6, uk. 24. {TN12: 74.1}
Mapambano kati ya kusini na kaskazini kufuatia vita vya Wayunani na Warumi, vilikuwa kati ya Waislamu na Wakristo. Wakati huo, kwa hivyo, wakati jina, “mfalme wa kaskazini,” hutumika kwa watawala wa Rumi iliyofanywa kuwa ya Kikristo, jina “mfalme wa kusini,” hutumika kwa watawala wa Waislamu. {TN12: 75.1}
(Alimradi Wasarakeni, Waarabu, na Waturuki — Waislamu — ni warithi wa Ufalme wa Mohammed katika tawala tofauti, sisi hapa, kwa sababu ya ufupi, tunatumia jina “Waislamu” kwa wote, kana kwamba ni ufalme mmoja.) {TN12: 75.2}
Haya matukio ya kinabii na ya kihistoria yaliyoandikwa yanafanya isiwezekane kutumiwa vibaya majina hayo, au kuzikanganya hizo tawala. {TN12: 75.3}
Zaidi ya hayo, aya (25, 26, 28-30) ambazo sasa tunazingatia, husifia ushindi kwa mfalme wa kusini, na historia huonyesha kwamba, kwa wakati halisi ambao maandiko yanaonyesha, Waislamu waliinuka kutoka Afrika, na pia waliyavamia
75
Mataifa ya Kikristo kaskazini mwa Mediterrania. Kisha ilikuwa kwamba Rumi ilipoteza Misri na Palestina. {TN12: 75.4}
Katika aya hizi, viwakilishi-nafsi vya wapinzani wawili “mfalme wa kusini” na “mfalme wa kaskazini,” haviwezi kufuatiliwa na sheria ya sarufi, lakini kwa mantiki ya matukio: {TN12: 76.1}
“Naye [mfalme wa kaskazini] atachochea nguvu zake na ushujaa wake juu ya huyo mfalme wa kusini kwa jeshi kubwa; na mfalme wa kusini atafanya vita kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi; lakini [mfalme wa kaskazini] hatasimama: maana watatunga hila juu yake. Naam, walao sehemu ya chakula chake [chakula cha mfalme wa kaskazini] watamwangamiza [mfalme wa kaskazini], na jeshi lake [mfalme wa kusini] litagharikisha; na wengi wataanguka wameuawa. . . Ndipo [akiwa ameshindwa] atakaporudi [mfalme wa kaskazini] mpaka nchi yake mwenye utajiri mwingi; na moyo wake utakuwa kinyume cha hilo agano takatifu; naye [mfalme wa kaskazini] atafanya kama apendavyo, na kurudi mpaka nchi yake. Kwa wakati ulioamriwa atarudi, na kuingia upande wa kusini; lakini wakati wa mwisho mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa wakati wa kwanza.” Aya za 25, 26, 28, 29. {TN12: 76.2}
Ijapokuwa “yeye” wa aya ya 28 anarudi mpaka “nchi yake mwenye utajiri mwingi,” hakuzichukua kama nyara kutoka kwa mfalme wa kusini, ambaye jeshi lake lilimgharikisha na kusababisha wengi “kuanguka wameuawa,” ha-wakusimama (aya ya 26), ila lazima awe ameupokea kutoka kwa waongofu wa dini yake. Wale waliokula sehemu ya chakula chake (aya ya 26), watumwa wake, na ambao baadaye watamwangamiza, walikuwa, mwanzoni, Waprotes-tanti. {TN12: 76.3}
76
Kama “yeye” wa aya ya 29 anarudi kwa wakati ulioamriwa na anakuja upande wa kusini, “yeye” basi ndiye mfalme wa kaskazini amekwenda chini kwa vita vingine. Haya ndio maelezo ambayo historia huthibitisha, na hivyo huoneka-na kwamba kitambulisho kwenye mabano cha viwakilishi-nafsi ni sahihi. {TN12: 77.1}
Shambulio la magharibi kwa Waislamu lilianza “mwaka 639 B.K.,” wakati “waliivamia nchi, na Misri ikawa wila-ya ya Waislamu.” — Kitabu Kipya cha Marejeo ya Mwanafunzi. {TN12: 77.2}
Kwa hivyo, kufuata wa Ptolemi, Waislamu, ambao utawala wao ulikuwa wa pili wa kusini, waliingia katika jina, “mfalme wa kusini.” {TN12: 77.3}
Mnamo 814 B.K., Rumi (mfalme wa kaskazini) alikuwa tayari amewaachia Waislamu Misri na Palestina Waislamu (mfalme wa kusini). {TN12: 77.4}
Ukristo unaotawala dhamiri kutoka kaskazini, na Uislamu unaotawala dhamiri kutoka kusini, umekuwa siku zote tangu zamani katika migogoro ya maeneo na ya kidini. Na yeyote akichukua kipande cha ufalme wa mwingine, ali-walazimisha, kwa adhabu ya kifo kutoridhia, imani yake ya kidini kwa mateka wake. {TN12: 77.5}
(8)
Wote Walinena Uongo
“Na katika habari za wafalme hao wawili, mioyo yao watanuia kutenda madhara, nao watasema uongo walipo pamoja mezani;
77
lakini hilo halitafanikiwa; maana mwisho utatokea wakati ulioamriwa.” Aya ya 27. {TN12: 77.6}
Ile meza moja ambapo wafalme wote husema uongo, ni, bila shaka, mfano; yaani, Rumi ya Upapa ilitangaza kwa wafungwa wao kwamba dini ya Kirumi ilitangulia kuonyeshwa kwa tangazo la malaika Gabrieli kwa Mariamu kwamba angemzaa mwana Mwokozi wa ulimwengu; vile vile Uislamu ijayo ulitangaza kwa watu wale wale (kwenye meza moja), walipokuwa mateka wao, kwamba malaika Gabrieli alimtokea Mohammed na kumpa dini ambayo watu wote wa dunia wanapaswa kuwa nayo. {TN12: 78.1}
Ijapokuwa tangazo la Rumi kulihusu lile Gabrieli alimwambia Mariamu, limethibitishwa hakika, dini halisi ya Rumi, ikiwa tu imepakwa Ukristo, haikuwa dini ya Yule Ambaye Gabrieli alimnena kimbele. Iwapo Mohammed alipokea dini yake kutoka kwa Gabrieli, hakuwahi kamwe. Kwa hivyo, Mapasha wote waliofanywa kuwa Waislamu na mabwana-wakubwa waliofanywa kuwa Wakristo, walikuwa wakisema uongo kwenye meza moja — watu. Lakini hawa “hawatafanikiwa,” alitangaza malaika, “maana mwisho utatokea wakati ulioamriwa”; yaani, dini zao za uongo zitakoma kwa wakati ulioamriwa: hazitadumu milele. {TN12: 78.2}
Ramani ya 9 huonyesha matokeo ya mwisho — mataifa ambayo yalifanywa kuwa ya Kikristo daima, na mataifa yaliyofanywa kuwa ya Uislamu daima. {TN12: 78.3}
78
(9)
Dhidi ya Agano Takatifu
Kuona hitaji la kupatana na washenzi ili kuwafanya mawindo rahisi, mfalme wa kaskazini akaweka moyo wake dhidi ya “agano takatifu”
79
(aya ya 28, 30, 32) yaani, aliangusha kutoka kwa imani ya Kikristo Sabato ya uumbaji (Kut. 20:8-11), ambayo Bwana “alibariki na kuitakasa” kama ukumbusho wa kazi Yake, “agano la milele” Kut. 31:16, 17. {TN12: 79.1}
Mfalme wa kaskazini akiwa na werevu na wale tu ambao “waliliacha agano takatifu,” hutatua pointi mbili: kwanza ya kwamba wote hawakuiacha Sabato; pili ya kwamba watu wachache ambao alitumia kupata nguvu, hawakuwa wa-fuasi wa Kristo waaminifu, ila wakafiri. {TN12: 80.1}
“Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.” Aya ya 32. {TN12: 80.2}
Aya hii hufichua tabia ya kila daraja: kwanza, la wakafiri; na pili, la waaminifu. Kuhusu hatima ya waaminifu, tunasoma: {TN12: 80.3}
“Na hao walio wenye hekima katika watu watafundisha wengi; hata hivyo wataanguka kwa upanga, na kwa moto, na kwa kufungwa, na kwa kutekwa nyara, siku nyingi. Basi watakapoanguka, watasaidiwa kwa msaada kidogo; lakini wengi wataambatana nao kwa maneno ya kujipendekeza.” Aya za 33, 34. {TN12: 80.4}
Aya hizi, mbali na kutabiri mauaji ya wafuasi waaminifu wa Kristo, hubashiri Matengenezo, “msaada mdogo,” na kutabiri kwamba hali yake ya sasa iliyoanguka imesababishwa na “kujipendekeza.” {TN12: 80.5}
80
(10)
Analitia Unajisi Hekalu Anaiondoa Ya Kila Siku
“Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wa-taondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.” Aya ya 31. {TN12: 81.1}
Kwamba hii miunganisho mitatu ya Ukweli (kulitia unajisi hekalu, kuondolewa ya kila siku, na kulisimamisha chukizo) katika mnyororo wa matukio ya kinabii, hutuleta karne kadhaa katika enzi ya Ukristo, huthibitishwa kika-milifu na Kristo akiwarejelea wao kama wakati ujao kutoka kwa wakati alipotamka ile amri: {TN12: 81.2}
“Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika pata-katifu (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani.” Mat. 24:15, 16. {TN12: 81.3}
Hekalu la washenzi tayari ni najisi, na kwa hivyo haliwezi kutiwa unajisi. Dhahiri, basi, hekalu la ngome (sio la washenzi) lilitiwa unajisi kwa kuingizwa ndani yake ukuhani wa upagani na washenzi kuongozwa
81
wasiokuwa waongofu. “Hekalu” ni kanisa la Kikristo, maana katika kipindi uchafuzi ulifanyika halikuwapo hekalu huko Yerusalemu. (Mintarafu “ya kila siku,” soma Trakti Namba 3, Hukumu na Mavuno, uk. 38, 39.) {TN12: 81.4}
(11)
Haijali miungu Na Hamu Ya Wanawake
“Wala hataijali miungu ya baba zake; wala yeye ataipuuza hamu ya wanawake; wala hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya wote. . . Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataiga-wa nchi kwa rushwa.” Aya ya 37, 39. {TN12: 82.1}
Hakuna taifa ila Rumi iliyofanywa kuwa ya Kikristo hutimiza unabii huu, kwa maana ndiye pekee aliyemkataa mungu wa baba zake (mungu wa Wapagani), na kumtambua mungu mgeni (Mungu wa Wakristo). {TN12: 82.2}
Na ingawa alidai kuwa amempokea Mungu wa Wakristo kwa moyo wote, andiko hili hufunua udanganyifu wa dai lake. {TN12: 82.3}
“Wala. . . ataipuuza hamu ya wanawake.” Aya ya 37. {TN12: 82.4}
82
Hamu ya mwanamke ni nyumba (Mwa. 3:16) — hamu ambayo Bwana aliweka ndani ya moyo wake. Taasisi ya Kirumi ya watawa wa kike na waume, kwa hivyo, si kwa agizo la Mungu. {TN12: 82.5}
(12)
Utawala wa Tano wa Kaskazini Unashinda Utawala wa Pili wa Kusini
“Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atamshambulia. . . mfalme wa kaskazini.” Aya ya 40. {TN12: 83.1}
Malaika aliyeandikisha maandishi ya Danieli, anaelezea kwamba katika wakati wa mwisho unabii huu ungefunu-liwa, na ya kwamba kwa wakati huo “wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.” Dan. 12:4. {TN12: 83.2}
Uvumbuzi wa kisasa, hasa katika milki ya kusafiri na mawasiliano, hutambulika kama utimizo wa lililotabiriwa ongezeko la maarifa. Ukuaji wa sasa wa maarifa, kwa hivyo, huonyesha kwamba sasa tunaishi katika wakati wa mwi-sho. Penye mwanzo wake, ulitangaza Uvuvio, (katika karne ya kumi na nane) mfalme wa kusini “atamshambulia” mfalme wa kaskazini — katika wakati ambapo mfalme wa kaskazini — {TN12: 83.3}
“. . . atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita,
83
na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati. Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokoka mkononi mwake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa wana wa Amoni. Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.” Aya za 40-43. {TN12: 83.4}
Kupita zaidi ya tangazo la kinabii la ushindi wa Waislamu, na kuja kwa “wakati wa mwisho,” katika karne ya kumi na nane, tunapata kwamba mfalme aliyefanywa kuwa wa Kikristo wa kaskazini katika utawala wake wa tano (tawala za Kikristo zilizo huru kwa kanisa) mwanzoni zitamvamia mfalme wa kusini (Ufalme wa Waislamu), na hatimaye kui-teka tena Misri na Palestina kutoka kwake na nchi zingine nyingi zaidi ya zile ambazo zilijumuisha ufalme wa Waislamu. {TN12: 84.1
Ramani ya 10 hutilia mkazo Ufalme wa Uturuki kwa ukuu wake, na pia hutoa tarehe ambazo mikoa mbalimbali ilianguka. Kwa mujibu wa ramani, kuporomoka kwa Ufalme kulianza mwaka 1699 (mwanzoni mwa wakati wa mwisho — Dan. 12:4). {TN12: 84.2}
84
Hadi mwaka wa 1915, wakati Uingereza ilitangaza nchi lindwa ya Uturuki mwishoni na kuanzisha himaya yake, Misri ilikuwa jina la utegemezi wa Uturuki. Lakini tangu 1883,
85
kufuatia uasi wa Arabi Pasha, Misri ilikuwa imetawaliwa kwa uhalisia na Uingereza Kuu chini ya balozi jeme-dari.” — Kitabu Kipya cha Marejeleo ya Mwanafunzi. {TN12: 85.1
“Palestina [nchi ya uzuri], kwa miaka mingi nyumbani kwa nasaba ya Waebrania, ilikuwa chini ya udhibiti wa Rumi wakati wa Kristo. Katika karne ya saba ilipita chini ya utawala wa Kiislamu, na kutoka mwaka 1516 hadi 1919 ilikuwa mikononi mwa Waturuki na sehemu ya Ufalme wa Uturuki.” — Kitabu cha Ulimwengu. {TN12: 86.1
Edomu, Moabu, na wakuu wa wana wa Amoni (wale wa Ng’ambo ya Yordani) kisha wakaja chini ya mamlaka ya Uingereza Kuu. (Tazama Ramani ya 5, ukurasa wa 18.) Neno, hata hivyo, husema “zitaokoka mkononi mwake,” likionyesha kwamba ingawa sasa anawamiliki, atawapoteza. {TN12: 86.2
Na “Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake”; labda watamfuata — kuwa wake. {TN12: 86.3
Ili kukaza ukweli katika akili zetu kabla ya kupita kutoka kwa unabii uliotimizwa hadi kwa unabii ambao haujatimizwa, ni muhimu kushughulikia yafuatayo
Mapitio: {TN12: 86.4}
Baada ya kugawanywa kwa ufalme wa Alexander, Misri na Palestina zilikuwa, kama ilivyoonekana hapo awali, zilitawaliwa kwanza, na Ptolemi; pili, na Rumi ya Upagani (aya za 15, 16); tatu, na Waislamu mwanzoni mwa anguko la Rumi iliyofanywa kuwa ya Kikristo (aya ya 22);
86
na nne, tena na Wakristo — hasa Uingereza Kuu (aya ya 41). {TN12: 86.5}
Hivi ndivyo vipindi maalum tu vya kihistoria na kinabii ambavyo vimeandikwa kushirikisha nchi za kale za Misri na Palestina. Usalimishaji wa nchi hizi, na mfalme mmoja wa kinabii hadi kwa mwingine, bila kukosea hum-tambulisha “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini” tangu wakati wa kugawanywa ufalme wa Alexander hadi wakati wa sasa, na hauachi nafasi ya shaka au mabishano. {TN12: 87.1}
Rumi (mfalme wa kaskazini) kuingia mara ya pili katika “nchi ya uzuri” (aya ya 41), huonyesha kwamba inga-wa, kama ilivyoelezwa hapo awali, iliitwaa nchi kutoka kwa wa Ptolemi (aya ya 16) baadaye, mwaka 633 B.K., ikaipoteza kwa Uturuki, na mwaka 1919 — “katika wakati wa mwisho” akaitwaa yote tena. {TN12: 87.2}
Hapa ni thibitisho rahisi kwamba katika nyakati za kisasa watawala wa Kiislamu wamo katika unabii uitwao “mfalme wa kusini,” ilhali wafalme wa Uingereza, pamoja na familia iliyovurugika ya wafalme wa Kikristo ambao unabii husema haitashikamana moja kwa nyingine (Dan. 2:43) ), huitwa “mfalme wa kaskazini.” {TN12: 87.3}
Katika kipindi chake cha Upagani, Rumi huwakilishwa kwa miguu miwili ya chuma, na katika kipindi chake ilipofanywa ya Kikristo, kwa nyayo zake na vidole vya chuma vilivyochanganywa na udongo. {TN12: 87.4}
Kwamba “mfalme wa kaskazini” (Dan. 11:7) na utawala wa pembe ndogo yenye kichwa (iliyo na macho ya mtu na kinywa kilichonena
87
maneno kinyume chake Aliye juu — Dan. 7:25) ni mmoja na utawala sawa, ameonyeshwa tena na ukweli kwamba “wakati, nyakati, na nusu wakati,” ni muda uliotolewa katika matukio yote mawili. Angalia Danieli 12:7. (Sura ya kumi na mbili ni endelezo la ya kumi na moja.) {TN12: 87.5}
Sasa inaonekana wazi kwamba kupita kwa Misri na Palestina kutoka kwa aina ya mikono ya watu wamoja hadi nyingine, ni ufunguo ambao umelifumbua fumbo la Danieli 11. Na ukweli, unaoangaza kwa mng’ao wa jinsi hii, hufanya wazi kabisa kwamba mafundisho maarufu eti Uturuki ni “mfalme wa kaskazini,” na kwamba Uin-gereza ni ufalme uliojitokeza wa Israeli, yamekusudiwa na roho ya ukosaji ili kuwafanya watu wa Mungu ku-kosa kabisa kuuona ukweli, na kuuweka msimamo wao, pale wasipopajua. {TN12: 88.1}
(13)
Anatangaza Vita — Ila Si Dhidi Ya Mfalme Wa Kusini
Hadi hapa katika mnyororo huu wa matukio, kila kiunganishi kimekuwa unabii uliotimizwa, lakini aya ambazo tutazingatia ijayo, husheheni viunganishi vya unabii ambao haujatimizwa. Kupitia jicho la imani, kwa hivyo sasa tuna-paswa kutazama katika siku za baadaye: {TN12: 88.2}
“Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuha-ribu, na kuwaondolea mbali watu wengi.” Aya ya 44. {TN12: 88.3}
Taabu ya mwisho ya mfalme haitainuka kutoka kwa mfalme wa kusini akimshambulia
88
ila kwa “habari zitokazo mashariki na kaskazini,” ikionyesha kwamba anavutwa katika pambano hili la mwisho kwa ajili ya ubabe, si kwa mtu yeyote kutangaza vita dhidi yake, ila yeye kutangaza vita dhidi ya wengi kwa sababu “habari zitokazo mashariki na kaskazini” zimemtaabisha. {TN12: 88.4}
Iwapo shughuli za mashambulizi za Ujerumani kaskazini ya Mediterrania, na Wajapani upande wa mashariki, ni habari ambazo zimesababisha Uingereza kuingia vitani dhidi ya wengi, na hamna shaka kwa hilo, basi hivi vita vya pili vya dunia vitaelekeza kwa utimilifu wa sura nzima inayozingatiwa. {TN12: 89.1}
(14)
Tendo Lake La Mwisho
“Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.” Aya ya 45. {TN12: 89.2}
Unajithibitisha wenyewe kwamba kuweka “hema zake za kifalme” hakuwezi maanisha kuweka makao yake ma-kuu. Hema zake, kwa hivyo, zinaweza kuashiria tawi la kasri lake. Na chaguo lake kuliweka “katika mlima mtakatifu wa uzuri,” huashiria kwamba mahali pale pamekusudiwa kuambatanishwa na hema zake utakatifu wa Mungu wa Mkristo. Kuwekeza hema zake za kifalme na utakatifu kama huo, kunaweza kumaanisha kwamba itakuwa nyumba ya makao makuu ya inayokuja hivi karibuni serikali ya kidini ya ulimwengu, ambayo tayari tumeangalia. {TN12: 89.3}
89
Lakini eneo moja, labda Mlima Sinai, liko “kati ya bahari” — Bahari ya Shamu na Mediterrania. Yeye kulichagua ba-dala ya Yerusalemu, humaanisha kwamba ni kwa sababu Palestina, kama Edomu, Moabu na Amoni, “wataokoka mkononi mwake.” {TN12: 90.1}
Taarifa, “ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia,” huonyesha kwamba hapo awali alisaidiwa na utawala fulani mwingine, na ya kwamba hawezi kuendelea muda mrefu baada ya hapo, na inawezekana ina maana kwamba dini yake itaangamizwa na pembe za yule mnyama mwekundu sana (Ufu. 17:16). {TN12: 90.2}
Sasa ni inaonekana kwamba “hema zake za kifalme” zinakusudiwa kuwakilisha utakatifu, na kwamba mwanamke anayemwendesha mnyama (Ufu. 17:3), anatatua matatizo ya ulimwengu ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini, ukw-eli ni bayana kwamba serikali za sasa za Kikristo zitapangwa upya, na kutawaliwa na kiongozi wa kidini — sio na Hit-ler. {TN12: 90.3}
Sala yetu, kwa hivyo, ni ya kwamba wote wahakikishe kwamba majina yao yamo katika Kitabu cha Uzima cha Mikaeli, kwa maana wale ambao majina yao hayamo, wataachwa kwenda chini katika maangamizo ya milele. {TN12: 90.4}
Kama uhakikisho wa kuagana kwamba sasa tunaishi katika wakati wa mwisho, na kwa sababu wakati huo unakari-bia kupita kuingia katika umilele, tunanukuu maneno mazito ya malaika: {TN12: 90.5}
“Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa
90
wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” Dan. 12: 1, 2. {TN12: 90.6}
Hitimisho
Kwa sababu unabii ulioshughulikiwa hapa ndani, huunganisha pamoja karne nyingi za historia, tumewezeshwa, katika upeo wa trakti hii kushughulikia ila kwa ufupi historia inayohusika, kutoa uzingativu maalum kwa sehemu ambayo Bwana ataongoza nyayo za kila mmoja ambaye anayo hamu ya kuubeba msalaba na kumfuata Yeye kwa usalama kupita juu ya shimo la kuzimu, ambamo wote wanaoishi watatumbukia ndani hivi karibuni. Ukweli hapa ulioletwa mwangani, ukiangaza jinsi unavyofanya, unapaswa kuwashawishi na kuwaongoa waaminifu wote wanaotaka kuokoka maangamizi yanayokuja. Kwa hivyo wote waweze
KUUWEKA MOYONI NA WANUFAIKE. {TN12: 91.1}
Kama safu ya maisha ili kuwahifadhi wafuasi waaminifu wa Kristo wasifagiliwe na dini ya ufalme aidha mmojawapo, Mungu ameufanyiza mnyororo wa matukio ya kinabii yaliyoletwa kwenye mtazamo hapa ndani. {TN12: 91.2}
Wale ambao hutarajia kuongozwa na kuokolewa na Neno la Kweli, pia kuokolewa kutoka kwa wakati wa taabu,
91
Mikaeli atakaposimama (Dan. 12:1), taabu ambayo shida ya sasa ya mataifa inakaribia kuisababisha, hapaswi kusitasita sasa kuuchukua msimamo upande wa haki na ukweli. Kwa sababu hii, Ndugu, Dada, nuru sasa inaangaza njiani mwako. {TN12: 91.3}
Kwa wale wanaoliweka moyoni onyo la Bwana na ambao husimama upande Wake, imefanywa ahadi: “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Dan. 12: 3. {TN12: 92.1}
“Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan. 12:10. {TN12: 92.2}
Na sasa baada ya “jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri Zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.” Mhu. 12:13. Sasa inuka na uangaze, ifanye sifa ya mtunga Zaburi kuwa yako; sema, “Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; nimekuwa nikitangaza miujiza Yako hata leo.” “Ee Bwana, Wewe u Mungu wangu; nitakutukuza na kulihimidi jina Lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.” Zab. 71:17; Isa. 25:1. {TN12: 92.3}
92
RAMANI
Namba 1-4, 6 na 7 zimetolewa kati ya ramani katika Falme za Biblia, na A.T. Jones. {TN12: 93.1}
Namba 5 imetolewa kati ya ramani zilizoonekana katika Habari za Asubuhi za Dallas katika mwaka 1941. {TN12: 93.2}
Namba 8 imetolewa kwa mojawapo ya mfululizo wa ramani katika Historia ya Kale ya Myers, Toleo lililosa-hihishwa. {TN12: 93.3}
Namba 9 na 10 zimetokezwa tena kutoka kati ya ramani za Matatizo ya Dunia Mpya katika Jiografia ya Siasa. {TN12: 93.4}
VIELELEZO
Vielelezo vya Jalada: Cha juu na Knott katika Habari za Asubuhi za Dallas; cha chini na Sakren. {TN12: 93.5}
AINA ZOTE ZA ITALIKI NI ZETU.
93
“Basi uwaambie, Bwana Mungu asema hivi, . . . Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote. Kwa maana hayatakuwapo tena maono yo yote ya ubatili, wala ubashiri wa kujipendekeza, katika nyumba ya Israeli. Maana Mimi ni Bwana; Mimi nitanena, na neno lile Nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, Nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana Mungu.” Ezek. 12:23-25. {TN12: 94.1}
94