fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 51, 52

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 51, 52

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

JE, DINI NI KITU KILICHO HAI NA KINACHOKUA? AU JE, NI KITU KILICHOKUFA NA KINACHODIDIMIA?

WATU WATANO WACHINJA BAADA YA MMOJA KUTIA ALAMA

                                    

1

WAZO LA SALA

Msisumbukie Ya Kesho

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” kuanzia ukurasa wa 18. {1TG51: 2.1}

“Kristo alitafuta kuondoa kile kilichouficha ukweli …. Maneno Yake yaliweka mafundisho ya maumbile na ya Bibilia katika sehemu mpya, na kuyafanya kuwa ufunuo mpya …. Alitoa somo, ‘Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo [kwa unyenyekevu wa uzuri wa asili]; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.’’ Kisha ukafuatia uhakikisho mtamu na somo muhimu, ‘Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?” Katika mahubiri ya mlimani maneno haya … yalinenwa kwa Umati wa watu, kati yao walikuwapo wanaume na wanawake waliokuwa wamejaa wasiwasi na mahangaiko, na waliotoneshwa kwa kukata tamaa na huzuni. Yesu akaendelea: “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? au, Tunywe nini? au, Tuvae nini? (kwa maana haya yote Mataifa huyatafuta;) kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kwamba mnahitaji hayo yote.” {1TG51: 2.2}

Tuombe sasa kwamba kama watumwa wa Kristo, tufanye yote tuwezayo kuondoa yale ambayo yanauficha Ukweli wa leo; ya kwamba tuipate nuru kupitia maumbile na Bibilia; kwamba tugundue ya kuwa Bwana anatujali zaidi kuliko ambavyo Yeye hujali maua; kwamba tujifunze Kumtegemea na kuyatenda maagizo Yake, na kutokuwa tena kama Mataifa ambao husumbukia mambo ya ulimwengu huu; kwamba tujue Yeye ataona ya kuwa tunapata mahitaji yetu yote ikiwa shughuli yetu kuu ni kuuendeleza Ufalme Wake. {1TG51: 2.3}

2

JE, DINI NI KITU KILICHO HAI NA KINACHOKUA? AU JE, NI KITU KILICHOKUFA NA KINACHODIDIMIA?

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JULAI 26, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Je! Dini ni kitu ambacho hukua na kupanuka, au ni kitu ambacho husimama tuli? Siku ile nyingine tu tulisikia kwenye redio mchungaji fulani akijisifu kwamba dhehebu lake halijaongeza au kutupilia mbali fundisho tangu lianzishwe. Je! Hiki ni kitu cha kujivunia? au ni kitu cha kusikitikia? Hili ni swali ambalo sasa tunatamani kupata jibu. {1TG51: 3.1}

Ikiwa ulimwengu hausimami tuli, iwapo huendelea jinsi ambavyo hufanya, basi kwa nini kanisa lisimame tuli? Je! Kwanini kanisa lisimjue Mungu zaidi na Bibilia zaidi leo kuliko lilivyojua jana? Je! Kwa nini Ukristo ujivunie kutoongeza mafundisho ya Bibilia? Je! Ulimwengu huu ungalikuwaje iwapo kila kitu kisingalikuwa kikisonga mbele jinsi ilivyo! {1TG51: 3.2}

Iwapo tungelinganisha maarifa na mafanikio ya ulimwengu katika miaka 50 au 100 iliyopita na maarifa na mafanikio ya Kanisa yaliyoongezeka katika kipindi sawa cha wakati, tunaweza kuona kwamba hakuna ulingani-fu kwa vyovyote. {1TG51: 3.3}

Angalia ustawi ambao ulimwengu umefanya, na tazama upumbavu ambao Kanisa linakuza. Naam, nasema lina-kuza, kwa sababu inaonekana kuwa badala ya kusikitikia

3

ukweli wa kutokuwa limeongeza au kuacha fundisho, na badala ya kuwahimiza watu kuwa macho kwa ujilio wa Mungu, wanafanya kuwa shughuli yao kuwazuia walei wasikutane na wajumbe wa Mungu na Ukweli Wake unaoendelea, na “ chakula kwa wakati wake,” na ujumbe wa Mungu wa leo. Chochote kisichokuwa na chimbu-ko katika mabaraza yao wenyewe, walei wanaambiwa wasiwe na la kufanya kwacho. Hili hulifanya kwa sababu wao wenyewe hawazipokei Kweli ambazo Mungu hutuma; na kwa sababu ikiwa yupo yeyote wa ushirika wao akutane nao na Kuupokea, wao kwa kawaida watalazimika kujiunga na Ukweli popote Ukweli upo. Kwa hivyo ni shughuli yao kuu kuwaweka washiriki gizani na kwa kuhofia kwamba mtu fulani atawadanganya iwapo wa-tajiweka wazi kwa chochote ambacho wachungaji wao hawakiidhinishi. {1TG51: 3.4}

Mwenendo kama huo unaweza kuzuia maendeleo kwa miaka, lakini hauwezi kufanikiwa kamwe, — la, sio zaidi ya wapinzani wa Galileo walifanya dunia iwe tambarare kwa kumlazimisha akane msimamo wake kwamba dunia ni duara, na sio zaidi kuliko Rumi ilifanikiwa dhidi ya Matengenezo ya Uprotestanti au makuhani na ma-rabi dhidi ya Ukristo. Ni, kwa hivyo, wakati ufaao kugundua kwamba watu ambao lazima washikiliwe katika kutolijua jambo fulani ili wadumishwe kuwa waaminifu kwa Kanisa, hakika haifai kuwa nao; na kwamba njia pekee ya kuwawezesha kuwa waaminifu hakika, na kufanywa imara katika Ukweli, na kuokolewa katika Ufal-me, ni kufundisha Ukweli na kisha kuwapatia uhuru wa kuchagua ili kwamba wao wenyewe waweze kujua Ukweli ni nini na uongo ni nini. Kuwaweka gizani kuhusu yale wadanganyifu hufundisha (iwapo ni wadanganyifu), ni kuwadumisha wasikijue kilicho angani. Ni kuifunga milele njia ya Mbingu ya mawasiliano, na kuwafanya watu wawe wanyonge wa kiroho na kana kwamba ni mitambo tu. Lazima watu wenyewe wajue Ukweli ni nini, na wenyewe lazima waamue ni nini watakachofanya Nao ikiwa watapewa

4

usajili kwa Ufalme. Wote ambao lazima wazuiliwe ndani ya ugo, au kuongozwa kwa kamba au kusukumwa kwa rungu kwa mfano katika Ufalme, watapata mlango umefungwa, na watamsikia Bwana akisema, “Ondokeni Kwangu; Sikuwajua ninyi.” Wachungaji hawajaitwa kuwa mabwana wa kazi, au kuwa dhamiri ya wengine. Wameitwa kuwa waalimu wa Ukweli. {1TG51: 4.1}

Ikiwa Kanisa halistawi pamoja na Ukweli, iwapo kwa kila kipindi haliongezi maarifa kwa maarifa yasiyotiliwa shaka, basi, ninao uhakika, halina kitu cha kujivunia. Sio amilifu, njia yake ya mawasiliano na Mbingu imekatika, limeachwa na Mungu, limekufa. Haliwezi kamwe kwaandalia washiriki wake “chakula kwa msimu unaofaa” kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu. {1TG51: 5.1}

Hebu kwa mfano tuichukue dini kama ilivyo katika Bibilia leo. Haikuja yote mara moja. Badala yake, ilichukua kitu kama miaka elfu nne kujikusanya, na karibu miaka elfu mbili zaidi kuelewa kwa kadri ambavyo Kanisa limeelewa kufikia sasa. {1TG51: 5.2}

Iwapo tunaweza kulinganisha maarifa ya Abeli kuhusu dini na maarifa ya Mkristo kuihusu, hapana shaka tuta-gundua kwamba hakuna ulinganifu, kwamba Abeli alijua kwa kulinganisha kanuni ya kwanza tu ya imani ya Mkristo. Ikiwa dini, kwa hivyo, sio kitu kilicho hai, kinachokua, na kinachoendelea, basi ni nini? {1TG51: 5.3}

Dini ya Abeli ya miaka elfu sita iliyopita imestawi na kupanuka kukidhi mahitaji ya watu wa leo. Hili Uvuvio kuongeza juu yake, na Wenyewe kuifunua. Iwapo Kanisa halikui kulingana na kuongezeka na kupanuka, basi linawezaje kuwa Kanisa hai? Na linawezaje kuambatana

5

na ishara za nyakati, na maendeleo katika hekalu juu? {1TG51: 5.4}

Hebu tusome: {1TG51: 6.1}

Efe. 4: 11-14 — “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wain-jilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

Uvuvio unaweka wazi kwamba mpango wa Mungu ni kuwa Kanisa linastahili kukua katika maarifa na ukamilifu hata sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. {1TG51: 6.2}

Kwa sababu Kanisa halijafikia kiwango kilichowekwa katika aya hii ya Maandiko, ni dhahiri kwamba linahitaji kuwa na maarifa zaidi kuihusu dini ya Bibilia kuliko lilivyo nayo kwa wakati huu. {1TG51: 6.3}

Likiwa bado mbali kuufikia umoja kama huu wa imani, maarifa, na ukamilifu, tunaliona hitaji liko wazi kama kioo: Sisi Wakristo tunahitaji kuanza kukua, vinginevyo msimu wa ukuaji kama huo utapita na tutabaki mbilikimo, ambao hatutakuwa tumestawi

6

vya kutosha ili kustahiki kuwa na maskani katika Ufalme. Ndipo itakapotukia kwamba Wakristo wote kama hao ambao hawajakomaa watalia kwa uchungu, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatu-kuokoka.” Yer. 8:20 {1TG51: 6.4}

Maarifa ya Bibilia unaona, ni njia ya Mbingu kwa wokovu na umilele, lakini njia ya mchungaji mamboleo ni ku-waweka watu wasijue kile kinachofundishwa nje ya duara zao, ili waweze kuwa na wanadamu chini ya udhibiti wao. {1TG51: 7.1}

Kwamba Ukweli unakua, na ya kwamba tuambatane pamoja Nao, sasa tutasoma: {1TG51: 7.2}

Ufu. 14: 6-10 — “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Hapa upo uwakilishi wa jumbe tatu, mmoja ukifuata mwingine. Isipokuwa tuambatane na kila mmoja wazo hatua kwa hatua, tutajikuta tukifuata nyuma ya wakati, kama Wayahudi hadi leo. {1TG51: 7.3}

7

Wale ambao hushindwa kuambatana na Ukweli maadamu Uvuvio Unapoufunua, kamwe hawawezi kuufikia “umoja wa imani,” na “kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” Hivi watakuwa “ watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuli-wa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu,…” Efe. 4:13, 14. {1TG51: 8.1}

Kwa udhahiri, basi, dini yenyewe ni kitu hai na kinachokunjua, lakini janga ni kwamba sio wote wanaambatana nayo. {1TG51: 8.2}

Wacha tuchunguze ndani ya somo hili muhimu hata kwa uthabiti zaidi. Ukweli, unajua, uliendelea kukunjua na kukua hata baada ya kifo cha Musa. Wayahudi, hata hivyo, waliwauwa manabii na hawakuendelea mbele zaidi ya pale ambapo Musa aliwaacha. Kwa kweli, waliporomoka daima. Na hivyo wapo pale walipo leo kwa sababu walishindwa kuubadilisha mwenendo wao hata ingawa nabii baada ya nabii alitumwa ili kuwazuia kuanguka shimoni ambamo walikuwa wanatumbukia upesi. Hata Kristo Mwenyewe alishindwa kuwaamsha kwa kitisho cha hali yao. Wachache tu ambao kwa ulinganifu waliiona taa nyekundu, hatari, na kumrudia Bwana. {1TG51: 8.3}

Huku kusitasita na kukengeuka kamwe hakukukoma. kumeendelea na kuendelea hadi leo hii. Hata kanisa la kwanza la Kikristo lenyewe hatimaye lililala, na likaleta Vizazi vya giza la dini. Zaidi ya hayo, ingawa Uvuvio uliweka nuru angavu ya Ukweli mikononi mwa Matengenezo wakati wa giza kuu la siku hiyo, bado Kanisa kwa ujumla lilishindwa kuiona nuru, lilishindwa kuona hitaji la matengenezo. Badala ya kuja kwenye nuru, kanisa lilitenda yote lililoweza kuizima. Wateule, hata hivyo, walitoka gizani na kuingia

8

nuruni. Kwa hivyo ilikuwa kwamba dhehebu lingine, dhehebu la Kilutheri, lilianzishwa. {1TG51: 8.4}

Lakini huu ulikuwa mwanzo wa Matengenezo. Kwa sababu Ukweli mmoja baada ya mwingine ulianza kuji-funua, na kila mmoja ulilazimisha kuanzishwa kwa dhehebu jipya kwa sababu kila mmoja wa binti wakubwa (madhehebu), yakifuata nyayo za mama, mwenyewe, alikataa kuambatana na jumbe. Kwa kweli, dhehebu la Ki-lutheri lenyewe, kama mengine yote kabla au baada yake, liliridhika kubaki pale ambapo Luther aliliacha. Na hivyo kwa ajili ya hitaji lingine, dhehebu la Kiprestiberi, likazaliwa. Hivyo chini ya mkondo wa wakati dhehebu moja baada ya jingine limetenda vivyo hivyo. {1TG51: 9.1}

Hivi ndivyo ambavyo imekuwa katika karne zote. Hii ndio sababu hakuna kanisa moja ambalo limepanda juu zaidi kuliko pale wasisi waliopoyaacha. Na hii ndio sababu Wakristo, badala ya kukua katika umoja wa imani, kila siku inapopita, wanazidi kutoungana katika imani na kuwa mahasimu kwa imani ya kila mmoja. {1TG51: 9.2}

Kujisifu, kwa hivyo, kwamba dhehebu la mmoja halijawahi kuongeza fundisho au kuacha moja, ni kukubali kwamba kanisa lake linasimama tuli, karibu kusema, “Sisi ni matajiri tumejitajirisha, wala hatuna haja ya kitu,” ilhali kwa kweli wao ni “wanyonge, wenye mashaka, maskini, vipofu, na uchi,” lakini hawajui. {1TG51: 9.3}

Ni wazi kabisa, dini ni kitu ambacho hukua na hukunjua, lakini watu wake kama shirika hawajawahi kuambatana nayo. {1TG51: 9.4}

Sehemu yake ya kushangaza zaidi ni kwamba wale ambao wameyaongoza madhehebu baada ya kifo cha waasisi wayo, badala ya kuwafundisha walei kutazamia na

9

kusubiri Ukweli zaidi uliofunuliwa, badala yake wanafundisha kwamba kanisa lao lina Ukweli wote na kwamba hakuna hitaji la ukweli zaidi. {1TG51: 9.5}

Hapa tunaona kwamba “kanisa la wanamgambo” kwa uhalisi ni kanisa ambalo linafanya vita dhidi ya Ukweli unaoendelea, na kwamba “kanisa la washindi” ni kanisa ambalo linaenenda na ustawi wa Ukweli. {1TG51: 10.1}

Ukweli huu ulionekana katika hatua ya kwanza kabisa kuelekea ustawi katika dini: Kaini na Abeli walikuwa wakijaribu kutembea katika njia kuu ya maendeleo kila mmoja kwa kutoa kafara. Abeli aliabudu kulingana na hekima ya Mungu, ilhali Kaini aliabudu kulingana na hekima ya mwanadamu. Sadaka ya Kaini ilikuwa tu ghushi kwa ya Abeli. Hapa tunaona kwamba palipo Ukweli, hapo pia upo wa bandia. Wakati yapo madhehebu ambayo yalianzishwa juu ya Ukweli, yapo pia ya bandia, na hilo ndilo jambo muhimu la kuzidishwa kukubwa kwa madhehebu na vijidhehebu. {1TG51: 10.2}

Kaini kumuua Abeli kwa kufanya lile ambalo Bwana alimtaka afanye, ni mfano wa ibada ya uongo, wa upinzani na wa mateso. Hivi ndivyo ilivyokuwa zamani, na bado ilivyo: Wote ambao wako katika uongo daima hupatika-na maadui dhidi ya Ukweli na huwatesa wale wanaotenda Kweli. {1TG51: 10.3}

Sasa tuseme kwamba Abeli alikuwa ameishi hadi siku yetu na alikuwa ameufuata ustawi wa Ukweli kupitia kila kizazi, ingalikuwaje uzoefu wake katika dini? – Yeye angaliweza kuwa alijiunga na mavuguvugu ya Henoko; la Nuhu; la Abrahamu; la Yakobo; la Musa; na manabii wote; la Yohana Mbatizaji; la Mitume; kisha na Walutheri; na Waprestiberi; na Wamethodisti; la Waadventista wa Siku ya Kwanza; na la Waadventista wa

10

Siku ya Saba; na mwishowe angalijiunga na Wadaudi Waadventista wa Siku ya Saba. Ili yeye aendelee kuam-batana na Ukweli unaoendelea, Abeli angelazimika kuliacha vuguvugu moja na kujiunga na lingine mwanzoni mwa kila ufunuo mpya wa Ukweli, vinginevyo angalisalia kama asiyejua katika maendeleo ya dini kama walivyo Wayahudi. {1TG51: 10.4}

Sasa tunaona waziwazi jinsi ukweli unavyoweza kufanya, kwamba katika vizazi vyote, Kanisa linaloshinda lilikuwa na bado linajumuisha washiriki wa Kanisa ambao bila kukoma waliendelea kupanda ngazi ya Ukweli siku zote hadi siku ya leo. {1TG51: 11.1}

Ezekieli 36:23, 24 — “Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.”

Hapa ukweli tena umesisitizwa: Wale ambao wameazimia kukaa chini kwenye safu ya kwanza ya ngazi ya Ukweli, wataachwa hapo ili wakae milele. Lakini wale wanaoshikamana na Ukweli watarudishwa katika nchi yao, hawataendelea kukaa kwenye viti na Walaodekia na kutoendelea kuzikanyaga ardhi za Mataifa. {1TG51: 11.2}

Aya ya 25 — “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.”

Utakaso huu kamili na wa mwisho, unaona, unapatikana tu baada ya Kanisa linaloshinda kuingia

11

Nchi ya Ahadi. Wale ambao wanashindwa kushikamana na Ukweli na ambao huchagua kukaa na sanamu zao, hawataweza kuziendeleza tamaa zao za kibinafsi, kwa maana “nao watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele ya utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.” Isa. 2:19 {1TG51: 11.3}

Aya ya 26 — “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”

Wakati utakaso huu utakapofanyika, kisha inakuwa kwamba moyo mpya na roho mpya zitapeanwa kwa wote ambao sasa wanajitahidi kukua katika maarifa ya Mungu, na ambao kwa wakati huo wanapatikana katika Ufal-me. Baada ya upasuaji huu wa moyo kutukia, kuyafanya mapenzi ya Mungu kitakuwa kitu cha kawaida: Hakutakuwapo tena kushindana dhidi ya moyo wa mwili. {1TG51: 12.1}

Aya ya 27-29 — “Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mta-zishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote; nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena.”

Dan. 12: 1 — “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”

12

Lo, dunia tayari imeelekea kwa wakati wa taabu. Na inapofikiwa, kimbilio litapatikana tu kwenye Ukweli wa sasa, Ukweli unaoliweka jina la mmoja katika kitabu cha Mikaeli cha Mbinguni. {1TG51: 13.1}

Aya ya 10 — “Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wa-la hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.”

Ni nani wenye busara: — Lazima wawe ni wale ambao wanayatafuta “mafuta ya dhahabu,” wale walio na vyombo vilivyojaa (Mat. 25: 1-13). Wale ambao wameingizwa kupitia mlangoni ni wale ambao wamepata na kuifuata ramani ya Ukweli wa sasa. {1TG51: 13.2}

Dini, Ndugu, Dada, sio kitu kilichokufa na kinachodidimia. Ni kitu kinachoishi na kinachokua, na watu wa Mungu hukua pamoja nayo. {1TG51: 13.3}

Na sasa kwa kuhitimisha natamani kukuachia swali hili ili utafakari na ujijibu mwenyewe: Je, Uzoefu huu — uzoefu wa kustawi na Ukweli — uzoefu wako? Iwapo sivyo, basi kwa nini sivyo? naam, kwa nini? Je, Sio wa thamani kwa kila kitu — pesa, nyumba, ardhi, marafiki, mama, baba, waume au wake? Je, Sio wa thamani zaidi ya haya yote ili kuyafanya maradufu? (Tazama Isaya 61: 6, 7; Marko 10: 28-31.) {1TG51: 13.4}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG51: 13.5}

13

ANDIKO LA SALA

Kuzileta Kweli Mpya

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Katika Mifano,” ukurasa wa ishirini, kuanzia aya ya pili. {1TG52: 14.1}

“Katika sehemu ya mwanzo ya huduma Yake, Kristo alikuwa amenena na watu kwa maneno wazi ili kwamba wasikilizaji Wake wote wangaliweza kuwa wamezifahamu kweli ambazo zingaliwafanya kuwa wenye hekima kwa wokovu. Lakini mioyoni mwa wengi kweli hazikuwa zimeota mizizi, na zilikuwa zimenyakuliwa upesi. ‘Kwa hivyo nasema nao kwa mifano,’ Alisema; ‘Kwa kuwa wakitazama hawaoni; na wakisikia hawasikii, wala kuelewa …. Yesu alitumaini kuamsha uchunguzi. Alitafuta kumzindua asiyejali, na kupiga chapa ya ukweli juu ya moyo ….” {1TG52: 14.2}

Katika siku ya Kristo ilikuwa vigumu sana kuzileta kweli mpya kwa watu kama ilivyo leo. Yesu alitumia kila njia iliyowezekana kuwavutia watu katika Ukweli wa sasa wa siku Yake, lakini unajua mafanikio machache Ali-yokuwa nayo — wachache tu wa watu wa kawaida. Walioitwa eti watu wasomi wa siku walimpinga Yeye vikali na kutumia wakati wao na raslimali Kumshtaki kwa uongo kwa jambo moja, kisha kwa lingine. Katika aina ya ulimwengu tunamoishi hatuwezi kutarajia watu wawe tofauti leo kuliko vile walivyokuwa katika siku Yake. Hebu kwa hivyo tuombe kwamba tuweze daima kuwa macho, kwamba tuendelee kutoridhika zaidi na mafani-kio yetu kadri siku zinavyopita tusije, pia, kupatikana tumepungukiwa — tumerudi katika Ulaodekia. Tuombe kwamba mioyo yetu iwe wazi daima kwa Ukweli Wake unaokunjua, na kwamba tusipoteze hamu yetu kwa “chakula kwa msimu unaofaa.” {1TG52: 14.3}

14

WATU WATANO WACHINJA BAADA YA MMOJA KUTIA ALAMA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 2, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada ya somo letu alasiri hii inapatikana katika sura ya tisa ya Ezekieli. Tutaanza na {1TG52: 15.1}

Ezekieli. 9: 1-6 — “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka ki-zingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione hu-ruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msim-karibie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee

15

waliokuwa mbele ya nyumba.”

Kumbuka kwamba kwa amri ya Bwana, malaika wasimamizi watawachinja wadhambi ndani ya Yerusalemu (kanisani), sio ulimwenguni. Ni wale tu wanaoyachukia machukizo, wale wanaopokea alama kwa kuugua na kulia dhidi ya maovu ndio watakaoachwa. {1TG52: 16.1}

Siku ambayo Ezekieli alipata maono haya huko Babeli, Yerusalemu tayari ulikuwa uhamishoni na kuwa utupu wa watu wake kwa miaka. Tazama Ezekieli 1: 1; 8: 7. Hakuna kusafishwa au utakaso kama huu ulivyoonyeshwa hapa uliwahi kutukia katika siku ya Ezekieli au kwenye historia ya kanisa tangu siku yake. Ni, kwa hivyo, hakika kwamba unabii huo bado haujatimizwa. {1TG52: 16.2}

Uvuvio katika siku zetu, zaidi ya hayo, unaweka utakaso huu uliotabiriwa bado katika siku zijazo na hufanya maelezo haya: {1TG52: 16.3}

“Daraja ambao hawahisi kuhuzunishwa juu ya kuchakaa kwao kiroho, wala kuomboleza juu ya dhambi za wengine, wataachwa bila muhuri wa Mungu. Bwana huwaamuru malaika zake, watu walio na silaha za kuchinjia mikononi mwao: Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na ki-jana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’ {1TG52: 16.4}

“Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu,” anasema Roho wa Mungu, “walikuwa

16

wameusaliti uaminifu wao.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 211. {1TG52: 16.5}

Maadui wa Mungu, unakumbuka, wamechukua umiliki wa makanisa, lakini hivi karibuni meza zitapinduliwa, na watumwa wa Ibilisi hawatakuwapo tena; wataanguka na hawatapatikana. {1TG52: 17.1}

Watu, unakumbuka, wanadanganywa na wazee ambao wameisaliti imani yao. Unajua vyema kwamba manabii, mitume, Yesu Kristo, na wana matengenezo, wote katika nyakati zao walitukanwa na kudhihakiwa kama “Vi-chipuko,” lakini tunamshukuru Mungu kwamba “vichipuko” na Ukweli, sio kilele kilichokufa, vilishinda. {1TG52: 17.2}

“… Wao [wazee] walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu za Mungu kama vile siku za awali.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 211. {1TG52: 17.3}

Je, huu sio sasa msimamo wa wazee? Je, sasa wao hawapigi kelele amani na usalama? Je, sasa hawahubiri kwamba Ezekieli tisa hautatukia na kwamba hautafanyika kanisani, kwamba ujumbe huu ni kamsa ya uongo? Tufanye nini ili kumwamsha mtu anayelala akiota? Wanaota ndoto kwamba- {1TG52: 17.4}

“… Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wanasema, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.” “Mungu hatawachinja watu Wake,” “Kanisa ni chombo Chake cha thamani zaidi duni-ani,” wao husema. {1TG52: 17.5}

Kwa kweli kanisa ni chombo Chake cha thamani zaidi duniani, na hiyo hasa ndio sababu Yeye atalitakasa, ndio sababu Yeye atawachinja waovu kati kati yake

17

na kuwatia muhuri (kuwahifadhi) waliotubu ili Ajipatie kanisa safi, “lisilo na waa, wala kunyanzi, wala kitu chochote kama hicho.” — Efe. 5:27. {1TG52: 17.6}

“… Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaza sauti zao tena kama tarumbeta kuonye-sha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na wa-toto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 211. Kuendelea zaidi, Roho wa Mun-gu huuliza: {1TG52: 18.1}

“Ni nani wanaosimama katika shauri la Mungu kwa wakati huu? Je, ni wale ambao kwa kweli husamehe makosa miongoni mwa wanaodai kuwa watu wa Mungu, na ambao hunung’unika mioyoni mwao, ikiwa sio wazi, dhidi ya wale ambao wangekemea dhambi? Je, ni wale ambao huchukua msimamo wao dhidi yao, na kuwaonea hu-ruma wale wanaofanya makosa? La, hasha! Isipokuwa watubu, na kuaicha kazi ya Shetani katika ku-wakandamiza wale walio na mzigo wa kazi, na kuiinua mikono ya wadhambi ndani ya Zayuni, hawatapokea alama ya idhini ya kutiwa muhuri wa Mungu. Wataanguka katika maangamizi ya waovu ya jumla, yalio-wakilishwa kwa kazi ya watu watano wenye silaha za kuchinjia. Maki jambo hili kwa uangalifu: Wale wanaoipokea alama safi ya ukweli, iliyowekwa ndani yao kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, iliyowakilishwa na alama ya mtu aliyevaa kitani, ni wale ‘wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika’ kani-sani. Upendo wao kwa usafi na heshima na utukufu wa Mungu ni hivyo, na wanayo picha ilio wazi sana ya uovu uliokithiri wa dhambi kwamba wanawakilishwa kama wako katika uchungu, hata kuugua na kulia. Soma sura ya tisa ya Ezekieli.” Basi Roho anasema: {1TG52: 18.2}

“Lakini mchinjo kwa ujumla wa wale wote ambao hawaoni

18

hivyo tofauti kubwa kati ya dhambi na haki, na hawajihisi kama wale wanaosimama katika shauri la Mungu na kuipokea alama, umeelezewa kwa amri kwa wale watu watano walio na silaha za kuchinjia: ‘Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika pa-takatifu pangu.’” — “Shuhuda,” Gombo la 3, uk. 267. {1TG52: 18.3}

Hapa yanaonyeshwa madaraja mawili kanisani — waaminifu na wasio waaminifu — wale ambao huiona dhambi kama dhambi na wale wanaoitazama kama burudani. Pia umeonekana kwamba kanisa lina kazi ya kufunga, kazi ambayo lazima ifanywe hasa kwa ajili yake, sio kwa ajili ya ulimwengu. Kwa kuongezea, unafunua kwamba kazi ya kufunga kwa ajili ya kanisa ni kutiwa muhuri kwa watu 144,000, kwamba wao, kwa hivyo, ndio wale wa-takaohisi kwa undani maovu kati ya watu wanaomkiri Mungu. {1TG52: 19.1}

Aya ya 7-11 — “Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikaachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wa-kati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwa-na ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni. Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; lakini nita-leta njia yao juu ya vichwa vyao. Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.”

19

Je, Utengo huu wa waovu kutoka kati ya wenye haki utatukia lini? Yesu huuweka katika mwisho wa dunia. Yeye husema: {1TG52: 20.1}

“Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.” Mat. 13:30, 47, 48. {1TG52: 20.2}

Kama magugu wanachomwa; kama samaki wabaya, wanatupwa nje. Hii ndio njia ambayo Ufalme unakujia, asema Bwana. Na mavuno ni nini iwapo sio Hukumu ya Walio Hai? — kazi ambayo inamtenganisha mmoja kutoka kwa mwingine. {1TG52: 20.3}

“Watu wa kweli wa Mungu,” unasema Uvuvio, “walio na roho ya kazi ya Bwana, na wokovu wa watu moyoni, daima wataitazama dhambi katika tabia yake halisi, ya uovu. Siku zote watakuwa kwenye pande za kushughulikia kwa uaminifu na uwazi dhambi ambazo huwazonga kwa urahisi watu wa Mungu. Hasa katika kazi ya kufunga kwa ajili ya kanisa, katika wakati wa kutiwa muhuri kwa watu mia na arobaini na nne elfu am-bao watasimama bila mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, watahisi sana makosa ya watu wanaomkiri Mungu. Hii imewekwa kwa nguvu na mfano wa nabii wa kazi ya mwisho chini ya onyesho la watu kila mmoja akiwa na silaha ya kuchinjia mkononi mwake.” — “Shuhuda,” Gombo la 3, uk. 266. Unasimama upande gani? {1TG52: 20.4}

Sasa mada ya watu 144,000 inasimama kwa uangavu kuliko hapo awali. Sasa unaweza kuona wazi kwamba wale

20

watakaokoka mchinjo uliotabiriwa katika Ezekieli tisa, ni watu 144,000 ambao ni watumwa wa Mungu wa siku zijazo, malimbuko ya mavuno, tokeo la utakaso wa patakatifu (kanisa), kazi ya hukumu ya upelelezi kwa walio hai. Kazi hii na Ukweli huu, kwa hivyo, ndio wa muhimu zaidi kwa ajili ya siku, na unapaswa kuzingatiwa kwa moyo wote ikiwa mmoja anatarajia kuipokea alama na muhuri na kuepuka mchinjo, kuishi siku kuu na ya kutisha ya Bwana. Kupuuza kwetu kuugua na kulia kwa sababu ya machukizo kanisani kutamaanisha kupotea kwetu milele. Tusidhubutu kuruhusu chochote kupotosha umakini wetu kutoka kwa kazi hii kuu na tukufu kwa ajili ya watakatifu, na ya kutisha sana na isiyo tukufu kwa wadhambi. Kazi hii lazima “ishughulishe mawazo yote, umakini wote.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 118. Chochote kisiruhusiwe kuhitilafiana na maslahi yako ya milele. La, sio kwa sekunde, maana siku imekaribia kwisha! Nini? — marafiki, jamaa, waume, wake, ni lazima uwapoteze na wewe mwenyewe iwapo Ukweli huu utashindwa kukushawishi wewe na wao? Ila ahadi kwa waaminifu ni: “Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.” Isa. 61: 7. {1TG52: 20.5}

Je, Wewe, Ndugu, Dada, kweli unaelewa, kweli unang’amua, hatari kama ilivyotajwa wazi wazi hapa? Je, Unaona utabiri kwamba ujumbe wa kutiwa muhuri utapingwa na wale wanaoyaendeleza machukizo? Je, U pamoja nao? Natumai la. Je, lipo basi swali lolote kwamba iwapo ndugu wataachwa pasipo kuijua kazi hii ya utakaso ambayo Mungu anakaribia kuitenda kati ya watu Wake, nasema, ikiwa wataachwa bila kuijua, ha-wataanguka katika maangamizi ya jumla kwa waovu, yaliyowakilishwa na kazi ya watu watano wenye silaha za kuchinjia? {1TG52: 21.1}

Ni wazi kwamba wadhambi wote kanisani wataangamia

21

katika mchinjo huu wa waovu, wawe wanaume, wanawake, au watoto. Wazazi ambao wanaendelea kumtumikia Ibilisi watakuwa pamoja na watoto wao wachanga kuzimu; na wazazi wanaoachana na machukizo watakuwa pamoja na watoto wao wachanga kwenye Ufalme. Unasimama wapi? Je, wewe u pamoja na wale ambao wana mzigo wa kazi hii, au u dhidi yao? Hii unaona ni saa ya uamuzi kwa ajili yako, kwa ajili yangu. {1TG52: 21.2}

“…Maki jambo hili kwa uangalifu,” anashauri Roho wa Mungu. “Wale wanaoipokea alama safi ya ukweli, ili-yowekwa ndani yao kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, iliyowakilishwa na alama ya mtu aliyevaa kitani, ni wale ‘wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika’ kanisani. Upendo wao kwa usafi na heshima na utukufu wa Mungu ni hivyo, na wanayo picha ilio wazi sana ya uovu uliokithiri wa dhambi kwamba wanawakilishwa kama wako katika uchungu, hata kuugua na kulia. Soma sura ya tisa ya Ezekieli.” — “Shuhuda,” Gombo la 3, uk. 267. {1TG52: 22.1}

Je, Ni nani Waadventista wa Sabato wa kweli kwa wakati huu muhimu? — Wale wanaoipinga kazi ya kufunga kwa ajili ya kanisa? au wale wanaoweka moyo na roho yao ndani yake? Hebu tukabiliane na hali hiyo kwa uaminifu na kwa dhati. Hebu tupake macho yetu haya mafuta ya Mbinguni ili tuweze kuona na kujua Ukweli ni nini. Wale tu wanaotubu na kuukuza ujumbe wa saa hii badala ya kupigana dhidi yake watasimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. {1TG52: 22.2}

Ruhusu nisome tena: {1TG52: 22.3}

“Katika wakati ambapo ghadhabu yake itatokea kwa hukumu, hawa wanyenyekevu, wafuasi waliojitolea wa Kristo watatofautishwa kutoka kwa wengine wote wa ulimwengu kwa uchungu wa roho yao, ambao unaonye-shwa kwa kuugua na

22

kulia, makemeo na maonyo. Ilhali wengine hujaribu kufunika vazi juu ya uovu uliopo, na kuruhusu uovu mkubwa ulioenea kila mahali, wale walio na bidii kwa heshima ya Mungu na upendo kwa watu, hawatanyamaza ili wapate fadhili za yeyote. Nafsi zao zenye haki zinaudhiwa siku baada ya siku kwa matendo na mazungumzo yasiyo matakatifu ya waovu. Hawana uwezo wa kuuzuia mkondo wa bubujiko la uovu, na hivyo wamejawa na huzuni na kamsa. Wanaugua mbele ya Mungu kuona dini imedharauliwa katika nyumba hasa za wale ambao wamepata nuru kubwa. Huomboleza na kuzitesa nafsi zao kwa sababu kiburi, tamaa, ubinafsi, na udanganyifu wa karibu kila aina u kanisani. Roho wa Mungu, ambaye huchochea kemeo, anakanyagiwa chini ya miguu, ilhali watumwa wa Shetani hushinda ….” — “Shuhuda,” Gombo la 5, Uk. 210, 211. {1TG52: 22.4}

Usiendelee kumtumikia Shetani. Usiendelee kuupiga vita Ukweli wa Mungu dhidi ya masilahi yako. Roho ya Unabii katika mistari hii imefanya iwe wazi kama inavyoweza kufanywa, kwamba wakati ambapo ujumbe wa kutiwa muhuri unapoletwa kwa usikivu wa watu, watumwa wa Ibilisi watashinda kwa muda, wakati ambapo watumwa wa Mungu na Ukweli Wake kwa muda watakanyagiwa chini ya miguu na wale wanaoyadhibiti makanisa. Kazi hii ya uovu, mnajua nyote, tayari inaendelea: Ndugu wachungaji tayari wanaupiga vita ujumbe badala ya kuufundisha. Mimbari inamilikiwa na watu ambao Sabato baada ya Sabato huifanya kuwa jukwaa la shutuma baada ya shutuma dhidi ya Ukweli huu, Ukweli wa Hukumu kwa Walio Hai. {1TG52: 23.1}

Kwa sababu nabii wa injili katika sura ya sitini na sita pia alipewa nuru juu ya mada hii, tutaifungua. {1TG52: 23.2}

Isa. 66: 15-17, 19 — “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya

23

moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao wa-takaouawa na Bwana watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani [katika maeneo ya ibada], nyuma ya mti mmoja [wakimfuata kiongozi], wakila nyama ya nguruwe, na ma-chukizo, na panya, watakoma pamoja, asema Bwana…. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa.”

Hapa imesisitizwa kwamba mchinjo utatukia kanisani miongoni mwa wale ambao wanayajua vyema mambo ya Mungu, hivi kwamba wale wanao okoka wanatumwa kutangaza utukufu Wake, na umaarufu Wake kati ya Ma-taifa. Zaidi ya hayo, ukweli hasa kwamba Mataifa hawajachinjwa lakini wanapaswa kufundishwa na Mungu baada ya mchinjo kutendeka, hakika inadhihirisha kwamba mchinjo huo unatukia kanisani tu, na kabla ya rehe-ma kufungwa kwa Mataifa. Kurudia, wale wanao okoka ule mchinjo wanatumwa kuhubiri wokovu kwa Ma-taifa. {1TG52: 24.1}

Aya ya 20 — “Nao [waliokoka, lasema andiko] watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.”

Kwa sababu watu 144,000 ni malimbuko, na pia watumwa wa Mungu, na wote ni wa nyumba ya uakisi ya Yuda na Israeli, lazima wawe waliokoka na

24

waliotumwa. Wale ambao wanawaleta nyumbani kwa Bwana kutoka katika mataifa yote (Ufu. 7:9) lazima, kwa hivyo, wawe mavuno ya pili. Wa awali ni mavuno kutoka kwa kanisa, na wa mwisho mavuno kutoka kwa Ma-taifa (Angalia Ufunuo 7: 2-9). {1TG52: 24.2}

Ili kuuzima Ukweli, wazee katika uovu wao na ujinga sasa hufundisha walei kwamba mada ya watu 144,000 ni swali lisilo hakika badala ya Ukweli uliofunuliwa! Ibilisi angalitaka iwe hivyo ili watu waweze kuanguka chini ya silaha za kuchinja za malaika. Upuzi kama nini! Na, je, Ibilisi amewanasa kama nini watu wanaoyatawala makanisa! Je, wao hawawadanganyi yamkini hata wateule, watu 144,000? Huu hakika ni wakati kwa ajili yako wa “kuja kwa msaada wa Bwana dhidi ya walio hodari,” iwapo utaipokea alama ya kibali cha Mungu, na ikiwa utaokoka silaha za mchinjo za malaika — iwapo “utasazwa,” ikiwa utakuwa wa masalia. {1TG52: 25.1}

Haijawahi kufanywa jitihada kubwa sana ya kuwaamsha watu wowote katika kizazi chochote, kama juhudi ya leo. Mamia na maelfu, naam, mamilioni, ya trakti zimesambazwa kote kote katika Dhehebu. Hizi zimekuwa zikiendelea kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Kwa kweli inaweza hata kunenwa kwa kanisa: {1TG52: 25.2}

“Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodo-ma, ungalikuwapo mji huo hata leo. Walakini

25

nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.” Mat. 11: 21-24. {1TG52: 25.3}

Ibilisi leo, unaona, ana watu walio ndani kabisa shimoni kuliko alivyokuwa nao katika siku za Kristo au katika siku za Luther. Ushindi wa Bwana, naam, na ushindi wa wale ambao wanaokoka kutoka shimoni, utakuwa wa utukufu zaidi. “Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.” Isa. 62:12. {1TG52: 26.1}

“Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. {1TG52: 26.2}

Waovu kanisani, unakumbuka, mwishowe wamefikia kikomo chao. Unasimama na kundi gani? Pamoja na wale ambao hufumba macho yao kwa Ukweli huu? au na wale ambao hujaribu Kuuleta mbele? Wewe hukumu kesi yako mwenyewe. {1TG52: 26.3}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo bada-la ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {1TG52: 26.4}

26

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG52: 27.1}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 51, 52

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>