fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 17, 18

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 17, 18

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

MAWINGU ANGAVU YALETA MVUA MWANANA

KIKOMO CHA SANAMU ZA KIBINADAMU NA WANAOZIABUDU

                                    

1

WAZO LA KUTAFAKARI NA OMBI

Nitasoma kutoka “ Mount of Blessings,” kuanzia aya ya kwanza kwenye ukurasa wa 170. Ukurasa huu ume-gemea andiko, “Usitutie majaribuni, bali tuokoe kwa yule Mwovu” {1TG17 2.1}

M.B., uk. 170- “ Jaribu ni ushawishi wa kutenda dhambi, na hili halitoki kwa Mungu, bali kwa Shetani, na kutokana na uovu wa mioyo yetu wenyewe. “Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, Na Yeye Mwenyewe hamjari-bu mtu yeyote.” – {1TG17 2.2}

Shetani anatafuta kutuweka katika majaribu ili uovu wa tabia zetu zionekane mbele ya watu Na malaika, ili adai sisi ni wake… Adui anatuelekeza katika dhambi kisha anatushtaki mbele ya ulimwengu wa mbingu kuwa sisi hatufai upendo wa Mungu….”- {1TG17 2.3}

Kila jaribu linalokataliwa, kila jaribio linalovumiliwa, hutupa uzoefu mpya katika ujenzi wa tabia. Nafsi ina-yopinga jaribu kwa uwezo wa Mbingu huonyesha dunia Na ulimwengu ufanisi wa neema ya Kristo. {1TG17: 2.4}

Hapa panaonekana kuwa Shetani ni mjaribu mkuu wa nafsi zetu, kuwa anajaribu daima kutuangusha. Lakini hawezi kutufanyia chochote iwapo mioyo yetu iko sawasawa na Mungu, Na ikiwa tutakaa ndani ya uzio ambao amejenga kutuzunguka atafaulu tu iwapo sisi wenyewe tutamfanikisha. Ikiwa tutajiachia kwa dhambi kwa hiari, kwa hivyo tutakuwa tumejisalimisha kwa Shetani kwa hiari. Tusisahau kuwa hakuna atakayeendelea kwa njia yake Na vile vile kuomba sala ya Bwana bila kuwa mwongo. Lakini wale wanaofuata kile Bwana Amesema Na kumruhusu Bwana kuelekeza hatua zake, hatawahi kukosea. Tuombe tuwe miongoni mwa kundi hili la mwisho. {1TG17: 2.4}

2

MAWINGU ANGAVU YALETA MVUA MWANANA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MHUDUMU WA KIDAUDI WA WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 30, 1946

KANISA LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutasoma sura ya kumi ya Zekaria. Ili kupata wakati wa utimilifu wa unabii wake pamoja na ahadi ulio nazo, hatuhitaji kuona zaidi ya aya ya kwanza ya sura ya kwanza. {1TG17 3.2}

Zekaria 10 :1 “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.”

Semi hizi unajua, hazijatumiwa Na Uvuvio kiholela, neno “Mvua ya masika” lazima liwe na maana yake maalum na halisi. Uvuvio ulichagua kutumia neno “mvua” kwa sababu mvua hufanya vitu kumea Na kuleta mavuno tele. Neno “masika” huashiria Mvua kabla ya mavuno, mvua inayokamilisha ukuaji na inayoivisha nafa-ka. {1TG17 3.2}

Kwa hivyo, Mvua ya masika ya Kweli, ni ile ya mwisho kabisa, ile itakayokuza watu wa Mungu kwa ajili ya mavuno, wakati ambao Mungu Atatenganisha ngano toka kwa magugu(Mat. 13:30), wanawali wenye busara kutoka kwa wapumbavu(Mat. 25:1-12), samaki wazuri kutoka kwa wabaya(Mat. 13:47, 48), Na Kondoo kutoka kwenye mbuzi(Mat. 25:32, 33). Kwa ufupi, mavuno ni siku ya utakaso, siku ya hukumu ni

3

siku akisi ya upatanisho, siku ambayo wenye dhambi wanakataliwa mbali. Kwa hivyo mvua hii ya kiroho ita-fanyia kanisa kama vile mvua ya kawaida inavyofanyia konde. Pasipo mvua ya masika, watakatifu wasingeweza kukomaa kwa ajili ya ghala la mbinguni, wala magugu kwa ajili ya moto. Kwa hivyo basi, kwa “mvua ya masika” inaashiriwa mvua ya rasharasha ya Kweli ya mwisho. Na pia, hii sehemu ya Kweli lazima ije bure kwa kila mshiriki wa kanisa ambaye anaishi tu kabla ya wakati wa mavuno namna mvua inavyokujia kila nyasi kondeni. Pindi tu huu mguso wa ukomavu utakapokamilishwa, mundu utawekwa kwenye nafaka azizi ya dhahabu. Lakini tukumbuke kuwa hazitaachwa kondeni kuoza, zitawekwa katika “ghala,” (Ufalme) huku magugu ya-kichomwa, hivyo asema Bwana(Mat. 13:30). “Mvua ya masika” inaashiria nini? Je, ni Kweli ifanyayo muujiza, au ni Uwezo ufanyao muujiza? Nabii Yoeli anaelezea kuwa Uwezo wa kufanya miujiza kutakuja baada ya “mvua ya awali na ya masika. “ Anasema: {1TG17 3.3}

“Hata itakuwa, baada ya hayo[baada ya mvua ya vuli na ya masika – Yoeli 2:23], ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.” Yoeli 2 :28, 29 {1TG17 4.2}

Waziwazi basi, “mvua ya masika” ni Kweli ifanyayo muujiza unaowafanya watakatifu wakomae kwa ajili ya mavuno ambao 144,000 ni mamalimbuko(Uf. 14:4). Basi ili kukusanya mazao ya pili, Mungu amwaga Roho wake juu ya kila mtakatifu katika malumbuko, (juu ya “kila nyasi kondeni”) mkongwe ama mdogo, mvulana ama msichana si juu ya mmoja hapa na juu ya mwengine pale. {1TG17 4.3}

Dhahiri “mawingu angavu” husimamia vyombo vinavyopeleka Kweli ambavyo huitawanya kotekote katika

4

shamba la Bwana, kwa kila mshiriki wa kanisa – “kila nyasi,” ngano au gugu. {1TG17 4.4}

Kuzungumza waziwazi, mawingu meusi yanadokeza mvua nzito sana na haribifu ambayo hutisha wanaotazama. Kinyume, mawingu angavu yanadokeza mvua mwanana, ya aina inayoshuka kwa namna ambayo ardhi inaweza kunyonya yote. Haijiharibu. {1TG17 5.1}

Kwa hivyo, tunapozungumza kiroho, mawingu meusi yanasimamia chimbuko la mambo hatari ya kusoma na yaliyo makuu kwa mtu kukaribisha au kufahamu. Lakini mawingu angavu yanasimamia chimbuko la machapisho madogo yaliyosheheni Kweli ambayo inaekeweka upesi yenye “chakuka cha wakati wake,” Kweli inayokuja kwa vipimo vilivyo rahisi kula, rahisi kusiliki yote, na hivyo kukomaza anayeipokea kwa ajili ya matumizi ya “Bwana” Na kwa ajili ya huduma yake. {1TG17 5.2}

Wakati huo, pia, “mvua ya masika” kiroho lazima ianguke kwa huru na bila gharama kwa wapokezi kama il-ivyo mvua ya kawaida. Kwa hivyo dunia haijawahi shuhudia kamwe maandishi mengi sana yakitawanywa kama maandishi haya. Mamilioni! Hivyo ndivyo machapisho haya madogo yanayoeleweka, mawingu meusi, yali-yosheheni Kweli ya sasa, yanavyotawanywa kama majani ya demani kila mahali katika Laodekia kwa kila mshiriki wa kanisa, “kwa kila nyasi” katika shamba la Bwana. Matokeo ya mwisho? “Zaidi ya elfu moja,” yasema Uvuvio Unahakikisha, “hivi karibuni wataokoka kwa siku moja, wengi wao watafuatilia mivuto yao ya kwanza ulitokana na kusoma machapisho yetu.”-”Review and Herald,” Nov. 10, 1885. Alimradi, pamoja na mawingu meusi ya dunia ambayo sasa yanaangama juu ya wale wasio na matumaini kwa ahadi za Mungu, kuna mawingu haya haya angavu yanayoangama juu ya watoto wa Mungu waaminifu wenye imani na wenye matu-maini. {1TG17 5.3}

5

6

Kwa hivyo Kaka na Dada, huitaji kusikiliza sauti zinazokushawishi kujizuia kunyeshewa na mvua hii laini, au kujibari chini ya mwavuli wa mtu. Toka nje na ujitaamamu rasharasha hii inayohitajika sana. Kimetumwa kukupa ukomavu unaouhitaji, na kukuwezesha kuishi katika siku kuu na ya kutusha ya Bwana, hukumu ya walio hai. Usiwie zaidi, toka uende kwenye uwazi na uruhusu rasharasha hili ya thamani kukuangukia, acha likuroweze kwa kupenya na kupenya ili malaika wasikupate kuwa hufai kwa ajili ya “ghala” na kukutupa kwenye moto pamoja na magugu. Uvuvio unaweka wazi iwezekanavyo kuwa hakuna nafsi yeyote(hakuna kengee moja la nyasi), itafaa ufalme(“ghala”) ikiwa itakosa kunyonya mvua hii ya Kweli. {1TG17 7.1}

Ni muhimu aje basi kuwa mjitaamamu kwa ajili ya mvua hii. Hapa, huwezi waya kusimama mkavu chini ya miavuli ya wachukia-Kweli. Toka chini ya miavuli yao ya kishetani ili usipotee milele, ili usilie bila matumaini kuwa, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, Na hatujaokoka.” Yer. 8:20 {1TG17 7.2}

Zekaria 10:2 “Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hap-ana mchungaji.”

Hapa panaelezwa wazo kuwa ujenzi huu wa tabia na hekima na “mvua” nyepesi inayoleta nuru, inayomfanya mtu afae kwa ajili ya jamii ya Mbinguni, itawapata wanaosubiri wakisikiliza sanamu zikinena “ubatili” na wale waaguzi wakielezea ndoto za uongo wakijaribu kufariji bila mafanikio. Huwezi kuitikia Sauti ya Uvuvio na ku-geuka kutoka kusikiliza sanamu? {1TG17 7.3}

Hao ni kina nani ikiwa si wajumbe wapeketevu wanaochukia Kweli na wanaojiona bora

7

wanaosujudiwa na washiriki, wahubiri waongo wanaojaribu kufariji kwa kuhubiri uongo. {1TG17 7.4}

Kwa hivyo, uhuisho na matengenezo lazima yafanye kazi zao miongoni mwa wahudumu na washiriki pamo-ja. Kwa kweli kondoo wanataabika kwa kuwa hakuna mchungaji halisi popote, wote wameenda njia zao. {1TG17 8.1}

Zekaria 10:3 “Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.”

Fungu hili linafunua kuwa Bwana ametembelea watu Wake na Kweli iliyofunuliwa kabla ya kutenganisha mbuzi toka kwa kondoo ambapo atatunuku kondoo na kuadhibu mbuzi, kazi ya Hukumu ya walio hai. Ziara Yake inawafanya watumishi wake kama farasi mzuri katika shamba lake. {1TG17 8.2}

Zekaria 10:4 “Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila mtawala pamoja.”

Bwana Mwenyewe anachagua kutoka Yuda jiwe la “pembeni” (mwanzilishi), “msumari” (mtengenezaji), “upinde” (Kweli, au kifaa ambacho kwacho twapata ushindi dhidi ya Adui), na kila “mdhalimu” (mtawala). Kwa hivi, Anajenga nyumba ya Yuda. {1TG17 8.3}

Zekaria 10:5 “Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watap-iga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.”

Ushindi utakuwa mkamilifu sana kiasi kwamba hata

8

mapepo yanayowaongoza maadui wetu katika vita, yatachanganyikiwa yenyewe. {1TG17 8.4}

Zekaria 10:6 “Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia.”

Kauli, “Nami nitaitia nguvu,” badala ya kuokoa, “nyumba ya Yuda,” na “nami nitaokoa” badala ya kutia nguvu “nyumba ya Yusufu,” inamaanisha kuwa nyumba ya Yuda itaokolewa kabla ya nyumba ya Yusufu, na ili kuokoa nyumba ya Yusufu Atatia nguvu nyumba ya Yuda. Mazao ya pili yanahitaji kuokolewa, ilhali malimbu-ko yanahitaji kufanywa kufaa kwa kazi. Pamoja wanakusanywa kwenye sehemu moja, (“ghala,” Ufalme). Bwa-na anazidisha hisani hii kwa nyumba zote mbili kwa kuwa ana huruma juu yao na atawatendea kama kwamba hawakumfanya Yeye kuwatupilia nje. {1TG17 9.1}

Zekaria 10:7 “Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa di-vai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana.”

Kina baba watafurahi na watoto wataiona. Kwa hivyo “atageuza moyo wa kina baba kuelekea watoto, na moyo wa watoto kuelekea kina baba zao…” {1TG17 9.2}

Zekaria 10:8 “Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka.”

Wataongezeka, hivyo ni, mazao ya pili

9

yataongezewa “malimbuko.” (Ufu. 7:4, 9). – {1TG17 9.3}

Zekaria 10:9 “Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi.”

Zekaria 10:10 “Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; nami nita-waingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana.”

Wateule watakusanywa kutoka kila mahali, na watasambaa mbali hata nchi ya Gileadi na Lebanoni. Sehemu itakuwa ndogo sana kwao hata wakati ule. {1TG17 10.1}

Zekaria 10:11, 12- “Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka. Nami nita-watia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina lake, asema Bwana.”

Hivyo ni kusema kuwa ukusanyaji wa watu hautazuiwa. Kizuizi chochote kitatolewa. Utawala wa dhambi utakomeshwa. Mataifa ambayo yametumikisha watu wa Mungu yatanyenyekezwa, na fimbo zao(viti vya enzi) hazitakuwa tena. {1TG17 10.5}

Kuwa imara katika Bwana, tembea juu na chini ukifurahi na bila woga, Asema Bwana. {1TG17 10.6}

Kazi ambayo Mungu Ameanza katika moyo wa binadamu kwa nuru na hekima ya mbingu, lazima iendelee mbele daima. “… Kila mmoja atambue hitaji

10

lake. Lazima kila unajisi utupwe kutoka moyoni, na kusafishwa ili Roho aishi mle. Ilikuwa kwa maungamo na kuacha dhambi, kwa maombi ya bidii na kujiweka wakfu kwa Mungu, ndivyo wafuasi wa awali walivyoji-andaa kwa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Kazi sawa na hiyo japo kwa kiwango kikubwa, lazima ifanyike sasa. Wakati huo chombo binadamu alikuwa aulizie tu baraka, na kumsubiri Bwana kukamikisha kazi inayomhusu. Ni Mungu ndiye aliyeanza kazi, na Atamaliza kazi Yake, akifanya binadamu ku-wa kamilifu katika Yesu Kristo. Lakini kusiwe na kupuuza nehema inayosimamiwa na mvua ya vuli. {1TG17 10.7}

“Ni wale tu wanaoishi kulingana na nuru wanayo, watapokea nuru zaidi. Iwapo hatuendelei kila siku kwa kielelezo cha maadili tendi ya Kikristo, hatutatambua ishara za Roho Mtakatifu wakati ya mvua ya masika. Inaweza kuwa ikiangukia mioyo kote karibu nasi, lakini hatutatambua au kuipokea.” Testimonies to Ministers,” p. 507. {1TG17 11.1}

Kwa kuwa Kweli hii ni nyeti mno, usiruhusu adui yeyote wa Kweli iliyofunuliwa kukuchanganya. Akijaribu kukushawishi dhidi ya Kweli hii, umshughulishe, umfanye atoe tafsiri zaidi ya maandiko haya ya Biblia. Ikiwa hatakupa kitu bora au kizuri, basi mwambie ajishulishe na kazi zake na wewe utajali zako. {1TG17 10.2}

11

KITO JOHARI CHA KUTAFAKARI NA KUOMBA

Nitasoma kutoka “Mount of Blessing,” ukurasa 171, kuanzia katika aya ya pili. Somo hili ni endelezo la somo letu la Sabato iliyopita, linalotokana na sala ya Bwana. {1TG18: 12.1}

M.B., p. 171 — “Si salama kwetu sisi kusita kutafakari manufaa yatakayovunwa kutokana na kujitoka kwa mapendekezo ya Shetani. Dhambi yamaanisha fedheha na janga kwa kila nafsi ambayo inajiingiza ndani yake; ila ni ya kupofusha na kudanganya katika hali yake, na itatusawishi kwa mawasilishaji ya kuvutia. Ikiwa tutajitosa katika sehemu ya Shetani, hatuna hakikisho la ulinzi kutoka kwa nguvu zake. Kadiri ya uwezo wetu, tunapaswa kufunga kila mwanya ambao mjaribu anaweza kuutumia kutupata. {1TG18: 12.2}

“Ombi, ‘Usitutie majaribuni,’ lenyewe ni ahadi. Ikiwa tutajikabidhi kwa Mungu, tuna hakikisho, ‘Hatakubali mjaribiwe juu ya uwezo wenyu; ila atafanya pamoja na jaribu hilo pia njia ya kutoroka, ili muweze kulistahimili.’ ” {1TG18: 12.3}

Sasa tutapiga magoti na kuomba ili tuweze kutambua kwamba dhambi inapofusha na kudanganya katika hali yake; kwamba inaelekeza katika fedheha na janga; na kwamba ili tuwe katika upande salama, sharti hata kutafakari tu tusitafakari kujitoa kwa mapendekezo ya Shetani, kwa maana punde tu tukijitosa katika sehemu yake hatuwezi kutarajia ulinzi wa Mungu. Hebu pia na tumshukuru Bwana kwa hakikisho la kufariji kwamba ikiwa tutajikabidhi kikamilifu kwake, Yeye hatakubali tujaribiwe juu ya uwezo wetu. {1TG18: 12.4}

12

KIKOMO CHA SANAMU ZA KIBINADAMU NA WANAOZIABUDU

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, DESEMBA 7, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutajifunza Zekaria, sura ya 13. Hebu tuanze na aya ya kwanza. {1TG18: 13.1}

Zek. 13: 1 — “Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.”

Kirai “katika siku hiyo” kinaonyesha nyuma matukio yaliyotangulia, nyuma katika sura ya kumi na mbili. Humo tunaona kwamba tukio hilo ni maombolezo makubwa huko Yerusalemu (sura ya 12, aya ya 12-14). Hivyo “kati-ka siku hiyo,” katika siku ya maombolezo makubwa, chemchemi hii itafunguliwa. {1TG18: 13.2}

Ili kupata wakati ambapo maombolezo yatatukia, ni muhimu kwamba turudi yuma zaidi katika sura ya kumi na mbili. Bora zaidi, tunapaswa kuipitia sura hiyo kutoka kwa aya ya kwanza kuendelea, kwa sababu yanaletwa kwa mtazamo makundi saba ya matukio mbalimbali na tofauti, moja likifuata lingine. {1TG18: 13.3}

Matukio mashuhuri ya kila kikundi ni haya: (1) Yerusalemu utafanywa “kikombe cha kuyumba-yumba” na ma-taifa ya dunia “yatauhusuru Yuda na pia Yerusalemu.” (2) “Katika siku hiyo” mataifa yote yatakusanyika pamoja dhidi yake. (3) “Katika siku hiyo” Bwana “atampiga kila farasi kwa ushangao, na yeye ampandaye kwa wazi-mu,” na pia Yeye atayafumbua “macho Yake juu ya nyumba ya Yuda.” Maliwali wa Yuda wakati huo watasema mioyoni mwao, “Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu katika Bwana wa majeshi Mungu wao.” (4) “Katika siku hiyo” Yerusalemu utakaliwa

13

tena. (5) “Katika siku hiyo yeye aliye dhaifu kati yao” atakuwa kama Daudi; na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu. (6) “Katika siku hiyo” Bwana atatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana dhidi ya Ye-rusalemu. Naye ataimimina juu ya nyumba ya Daudi, na juu ya wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na ya kuomba. (7) “Katika siku hiyo” kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu. {1TG18: 13.4}

Hivyo tukio moja litategemea juu ya lingine, moja likifuata lingine, mwisho wake ni maombolezo makuu huko Yerusalemu. Katika siku ya tukio hili la maombolezo, kwa hivyo, chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi itafun-guliwa. Hebu sasa tuunganishe Zekaria 13: 1 na aya ya 2. {1TG18: 14.1}

Zek. 13: 1, 2 — “Katika siku hiyo [katika siku maombolezo makuu yanatukia] watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi. Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.”

Mambo mawili yanadhihirika wazi katika aya hizi: (1) kwamba nyumba ya Daudi lazima iwepo kabla ya chem-chemi ya utakaso kufunguliwa; (2) kwamba utakaso unaanza na kuyakatilia mbali majina ya sanamu, na kuwatu-pa nje ya nchi manabii wa uongo na roho chafu. {1TG18: 14.2}

Katika somo letu lililopita la sura ya kumi ya Zekaria, tulijifunza kwamba hizi sanamu ni za aina inayonena; kwamba ni watu. Hakuna shaka, kwa hivyo, kwamba hawa ni ndugu wachungaji ambao huhubiri juu yao wenyewe badala ya Kristo, na ambao waumini huwaabudu. Kama matokeo, waumini wanawafuata kwa upofu, na maamuzi yoyote ambayo “sanamu” zao huyafanya kuhusu ni nini ukweli na ni nini uongo, ni nini dhambi na ni nini haki, hayo ndiyo maamuzi ambayo washiriki huyatekeleza. Hizi “sanamu,” kwa hivyo zinatengeneza hali sawa na ile ambayo makuhani, waandishi, na

14

Mafarisayo walitengeneza katika siku za ujio wa kwanza wa Kristo. Kwa hivyo, waabudu sanamu hawaji-taabishi wenyewe kibinafsi kuzichunguza jumbe mpya, na kwa hivyo wao kwa upumbavu huwafuata wanadamu badala ya Kristo na Ukweli wake endelevu. Hawa, pamoja na manabii na roho chafu, wataondolewa katika nchi. {1TG18: 15.1}

Aya ya 3-5 — “Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii. Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii, kila mmoja wao, atayaonea haya maono yake atoapo unabii; wala hawatavaa joho ya nywele ili kudanganya watu; bali atasema, Mimi si nabii kamwe; mimi ni mkulima wa nchi; kwa maana nalifanywa mtumwa tokea ujana wangu.”

Majina ya sanamu (majina ya kujisifu ya vyeo vya wanadamu) yatasahauliwa milele: Katika siku hiyo, baadaye, wala nabii wa uongo au roho mchafu hatavumiliwa katika nchi. Kwa kweli, sio hata baba au mama wakati huo hawatamvumilia mwana wao kujifanya kuwa hivyo, ila watampeleka kwa wafishaji. Itakuwa kwamba watu am-bao hata sasa wanajikweza, na kuhubiri bila “kutumwa,” wataaibika wakati macho yao yanapofumbuka wazi wanapopatikana katika udanganyifu wao — katika utabiri wa uongo, na ufasiri wa apendavyo mtu wa Maandi-ko. Hawatajivika tena mavazi ya udanganyifu. Badala yake, watasema, “Mimi sio nabii, sio hata mchungaji, mi-mi ni mchungaji tu, mkulima wa kawaida.” {1TG18: 15.2}

Nabii Ezekieli pia alipewa taswira ya hali hii: “Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lo lote! Ee Israeli, manabii wako wamekuwa kama mbweha, mahali palipo ukiwa.

15

Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa, wala hamkuitengenezea nyumba ya Israeli boma, wapate kusimama vitani katika siku ya Bwana. Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, Bwana asema; lakini Bwana hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa. Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena mabashiri ya uongo? Nanyi mwasema, Bwana asema; ila mimi sikusema neno. Basi tazama, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu mmenena ubatili, na kuona uongo, basi, kwa sababu hiyo, mimi ni juu yenu, asema Bwana MUNGU. Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo; hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU. {1TG18: 16.1}

“Kwa sababu hiyo, kwa sababu wameshawishi watu wangu, wakisema, Amani; wala hapana amani; na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorogwa vema;

16

basi waambie hao wanaoupaka ukuta chokaa isiyokorogwa vema, ya kwamba utaanguka; kutakuwa mvua ya kufurika; nanyi, enyi mvua ya mawe makubwa ya barafu, mtaanguka; na upepo wa dhoruba utaupasua. Na huo ukuta utakapoanguka, je! Hamtaambiwa, Ku wapi kupaka kwenu mlikoupaka? Basi Bwana MUNGU asema hivi; Nitaupasua kwa upepo wa dhoruba, katika ghadhabu yangu; tena kutakuwa mvua ya barafu ya kufurika katika hasira yangu; na mawe makubwa ya barafu katika hasira ya kuukomesha. Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ndivyo nitakavyotimiza ghadha-bu yangu juu ya ukuta ule, na juu yao walioupaka chokaa isiyokorogwa vema; nami nitawaambieni, Ukuta huo hauko sasa, wala wao walioupaka hawako.” Ezek. 13: 3-15. {1TG18: 16.2}

Ni kama nini jukumu la kutisha ambalo linakaa juu ya wale ambao hushughulikia bila kujali Neno la Mungu, wanaojifanya kama waangalizi wa roho kwa watu lakini ambao kwa kweli wanalinda kwamba hakuna nafsi itaokoka kutua katika Jehanamu. Wote wao na machukizo yao watatumbukia shimoni. Hakika, iwapo maten-genezo yoyote yanahitajika katika Ukristo, kwa hakika yanahitajika zaidi katika safu hii moja. {1TG18: 17.1}

Kwa kuwa sasa tumejifunza vyema, hebu tusiendelee tena kuzitengeneza sanamu za wanadamu; hebu tusipeane nafasi ndani yetu kwaa roho chafu. Hebu badala yake tupeane kwa Roho wa Mungu nafasi ya kutuongoza kati-ka Kweli yake endelevu daima na ufahamu wa kibinafsi. {1TG18: 17.2}

Hebu tuwe wafuasi wa Kristo, sio kamwe tena wa Paulo, wa Apolo, wa Kefa, au wa mwingine fulani. {1TG18: 17.3}

Aya ya 6, 7 — “Na mtu atamwambia, Je! Jeraha hizi ulizo nazo kati ya mikono yako ni nini?

17

Naye atajibu, Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu. Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema Bwana wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo wa-tatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.”

Sina maelezo maalum kwa aya ya 6 na 7, isipokuwa yale yanayojulikana miongoni mwa Wakristo. {1TG18: 18.1}

Aya ya 8 — “Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao wa-takufa, asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo.”

Katika utengo huu, kwa mujibu wa aya ya 8, watu wamegawanywa katika mafungu matatu: Kwa udhahiri wapo watakatifu, wanafiki, na wapagani. Mafungu mawili ya mwisho yatakatiliwa mbali (yatatengwa kwa watakati-fu), nao watakufa. Kuhusu siku zijazo za la awali kwa matatu, hebu tusome–

Aya ya 9 — “Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.”

Katika uhusiano huu, nabii wa injili aliagizwa kuandika: “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na makundi nyota hazitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu

18

kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali; nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. {1TG18: 18.2}

“Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali. Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe. Kila mtu atakayeonekana atachomwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.” Isa. 13: 9-15. {1TG18: 19.1}

Juu ya onyo hili nabii Zefania anaongezea hivi: “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake. Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! {1TG18: 19.2}

“Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. Fedha yao wala

19

dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.” Zef. 1: 12-18. {1TG18: 19.3}

Maandiko haya yanajifafanua yenyewe, na yanalifanya somo letu liwe wazi kama kioo: Mara tu nyumba ya Daudi inapoanzishwa, mara tu malimbuko yanafika Mlima Zayuni na huko kusimama na Mwana-Kondoo, chemchemi ya utakaso itafunguliwa. Kisha inakuwa kwamba mavuno makubwa yataanza wakati ambapo kila punje ya “ngano” itawekwa “ghalani,” lakini kila punje isiyofaa inachomwa (Mat. 13:30). Halafu inakuwa kwamba kila “samaki” mzuri atawekwa katika vyombo, wakati kila mbaya atatupwa nje (Mat. 13:48). Kisha ina-kuwa kwamba kila aliyejivika “vazi la harusi” ataandaliwa chajio cha harusi, ila kila mtu ambaye hajajivika vazi atatupwa katika giza la nje (Mat. 22: 11-13). {1TG18: 20.1}

Katika maneno ya mifano haya yote yanaweza kufupishwa kama ifuatavyo: Wale ambao kwa mafanikio hud-hamiria kusazwa kama “ngano,” kama “samaki” wazuri, na kujivika vazi la harusi, ni wale ambao wamepata shamba la hazina kubwa na lulu ya thamani kubwa na wamefanya yote kuvinunua. {1TG18: 20.2}

“Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 13:49, 50. {1TG18: 20.3}

Tumefikia nyakati za uchaji, Ndugu na Dada. Sasa ni wakati wa kujivika vazi jeupe. Sasa ni wakati wa kununua shamba lenye hazina kubwa, na

20

lulu ya thamani kubwa. “Je, wewe? Je, mie” Ndilo swali kuu ambalo tunapaswa haraka kujibu bila ushawishi au kuhitilafiwa na watu wengine. {1TG18: 20.4}

Tunapaswa sasa kuweza kuona jinsi kazi ya Injili inavyokamilika, na kwamba wazo ambalo tumekuwa nalo juu yake ni la ubunifu tu wa mwanadamu. Sasa inaonekana wazi namna watenda dhambi wavyofanywa watakatifu, jinsi chemchemi kubwa ya Mungu inaweza kututakasa sisi sote, ya kutufanya kuwa weupe kama theluji ikiwa tunamruhusu Yeye. Kwa hivyo haijalishi tulikuwa nini jana, jambo muhimu ni nini tutakachofanya leo, na nini tunachohitajika kuwa kuanzia sasa kuendelea. {1TG18: 21.1}

Hapa inaonekana kwamba iwapo hatuufikii ujuzi wa Kweli, na ikiwa hatuuruhusu kuifanya kazi Yake ili-yokusudiwa ndani yetu, tunawezaje kufanywa wanaofaa kuishi mbele ya uwepo wa Mungu mtakatifu? Unaona, kuamini au kutoamini katika ukweli kama huu, hakika kunamaanisha kitu. Lakini kubishana, kama ambavyo wengine hufanya, juu ya suala kama “siku tatu mchana na usiku” (Mat. 12:40) bila kufanya chochote kulihusu hata kama hoja hiyo watashinda, ni vibaya zaidi kuliko Ufarisayo. Ibilisi anaweza kutufanya tujishughulishe na mambo yasiyo muhimu na vitu ambavyo hatuelewi. {1TG18: 21.2}

Katika mwaka wa 1931, baada ya “Fimbo ya Mchungaji”, Gombo la 1, kutoka kwenye matbaa, tulichapisha ma-kala ya kurasa mbili ambamo tulisema kwamba kile ambacho Mungu ametuongoza ndani yake ni ama ukweli wote au hakuna ukweli. Tangu wakati huo tumechapisha kitabu kingine na zaidi ya trakti ishirini za mfululizo wa “Salamu Mwafaka”, zote zikisheheni mada za mafundisho. Machapisho haya yameenezwa kote kote katika Dhehebu, lakini hadi leo leo Dhehebu halijajaribu rasmi hata mara moja kukanusha suala lolote kwa ujumla wake. Wao daima hujaribu kuondoa yale tuliyo nayo kwa maandiko haya, lakini kamwe

21

hawatupatii kitu bora zaidi. Yote tumekwisha sikia au kuona ni upotovu, au baadhi ya taratibu kama hiyo ina-vyofuatwa na watunza siku za kwanza wakiwa wanajadiliana na watunza Sabato. {1TG18: 21.3}

Usiwaruhusu maadui wa Kweli iliyofunuliwa waendelee na upotovu wao, lakini wakemee kwa Biblia. Najua kwamba sio Mbulgaria kutoka Milima ya Rhodope ambaye amewafanya Wamarekani wasomi kukuna vichwa vyao. Haiwezekani kwamba mtu huyu ameweza kulitikisa Dhehebu kutoka katikati hadi kwenye mzingo. Iwapo hujui ni Nani kwa kweli, basi ungalitafuta kujua bila kukawia. {1TG18: 22.1}

* * *

Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. Iki-wa unataka kupeana yoyote kwa marafiki au jamaa zako Waadventista, unaweza kuagiza nakala za ziada au ku-tuma majina na anwani zao kwa orodha yetu ya watumiwa. {1TG18: 22.2}

22

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 17, 18

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>