fbpx

Trakti Namba 06

Trakti Namba 6

Kwa Nini Uangamie?

Hati miliki 1936, 1941, 1942

na V.T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, trakti hii inatumwa bila malipo. Inaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote upesi na kushikilia lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunganisha.

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitakazotumwa kwetu zitathaminiwa.

TRAKTI NAMBA 6

Toleo la Tatu Lililosahihishwa

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Kimechapishwa Marekani.

2

 

YALIYOMO

 

Hukumu Mwenyewe …………………………………………….…3

Kazi Ovu Ya Mshindani Wake …………………………………..3

Kusihi Kwa Roho Mtakatifu ……………………………………..4

“Alitabiri Mpaka Kwa Yohana” …………………………………5

Sala ya Kristo …………………………………………………………..11

Kusudi la Shetani Ililopagwa Kimbele ………………………11

Yajitafutie Kitu Bora ………………………………………………..13

Kutoka Kwa Kalamu Ya “Mwana Makala” ……………….13

Karama Zaa Roho ……………………………………………………14

“Roho Ya Unabii” Imekataliwa Kabisa ……………………..15

Maandiko Hufundisha Ukweli Katika Njia Kadhaa …..16

Hali-Tumizi Ya Mfano Wa Ufafanuzi Uliovuviwa.

Zek. 4 ……………………………………………………………………..17

Uvuvio Unafafanua Mfano …………………………….……….19

Muhtasari Wa Zekaria Nne …………………………..…….….24

Dawa Maalum Ya Mbinguni ……………………………………25

Duka la Maziwa La Ulimwengu Linawawezesha

Wateja Kukataa Uovu Na Kuchagua Wema …………….27

Siagi Na Asali …………………………………………………………..28

Ni Mifano Ya Nini? ……………………………………………..…..28

Ng’ombe Mke Mchanga Na Kondoo Wawili …………….29

Asali ………………………………………………………………………..30

Dunia Ya Maziwa Yanayozalisha Siagi …………………..…31

Nchi Kufurika “Maziwa na Asali” ………………………………32

Shamba Lake La Mizabibu Ukiwa ……………………..…….33

Eneo La Kuwatupa Nje Watakatifu …………….……………35

Hadi Shamba La Mizabibu Lirejeshwe Kikamilifu …….38

Kama Mbegu Ya Haradali ……………………………………….39

“Ng’ombe Wadogo Kukanyaga” ………………..…………..40

YALIYOMO (Yaendelezwa.)

Utukufu Wa Wakati Ujao …………………..……………………41

Utanusurika Kupitia “Siagi na Asali” …..……………………42

“Mtu Atawalisha” ……………………………………………………44

Roho Ya Unabii Na Miigo Yake ……………………………..…..45

Tafakari Zinazotupwa Juu Ya Tabia Za Mtu

Haziuathiri Ukweli ………………………………………………..47

Kukanusha Kwa Uongo ……………………………………………49

Jibu la Mshtakiwa ……………………………………………………50

Je, Ni Lini Mlango Ulifunguliwa? Je, Ni Lini

Viti Vya Enzi Viliwekwa? ……………………………………….53

Lengo La Kuweka Kiti cha Enzi ………………………………..…54

Viti Vya Enzi Viwili – Kimoja Cha Utawala

Na Kimoja Cha Hukumu …………………………………….……57

Likipiga Vita Uweli Kwa Ujinga ………………………..…….…59

Zekaria, Sura Ya Kwanza ……………………………….…………60

Kwa Wengi Lakini Si Kwa Wote ……………………….….……65

Kabla Injili Kwenda Kwa Mataifa Yote, Mchinjo

Mkubwa Unatukia …………………………………………………..67

Rai Ya Mwisho Ya Bwana …………………………….………….70

Vipi Juu Ya Fundisho La Wanawake? ………………….……75

Hitimisho …………………………………………………..……….…..79

KWA NINI UANGAMIE?

Duka La Maziwa La Ulimwengu Litakulisha

Hukumu Mwenyewe

Kusudi la trakti hii likiwa kujulisha na kufikisha bila malipo kwa kila nafsi aminifu, hata kwa fukara zaidi na kwa mkaazi wa dunia aliye mbali zaidi, wingi wa bidhaa isiyokuwa ya kawaida kwa ubora ya Duka Kuu La Maziwa La Ulimwengu, kwa hivyo ni muhimu kuondoa mbele ya wateja wake

Kazi Ya Uovu Ya Mshindani Wake. {TN6: 3.1}

Ya mengi ya mashambulizi siku hizi yanayofanywa na huyu adui dhidi ya jeshi la wateja wa duka la maziwa, hayajakuwa bila shaka makali kama yale dhidi ya Dhehebu la Waadventista wa Sabato, mtumiaji mkuu wa bidhaa za duka la maziwa, na hasa dhidi ya kazi ya mwasisi wa dhehebu, Bi, E.G. White, ambaye maandishi yake yanafahamika na jumuiya kuwa Roho ya Unabii (Ufu. 12:17; 19:10). {TN6: 3.2}

Je, si yasiyopatana kwamba wakati mwingi, nguvu, na fedha hutumiwa na watu na madhehebu mbalimbali kutoa utangazaji mbaya kwa mwandishi yeyote wa vitabu vya kidini, ilhali yanayoufunika ulimwengu ni mamia ya itikadi za Kikristo na waandishi, kila mmoja akijaribu kutetea mtazamo wa kidini tofauti kutoka kwa wengine? Kwa vile upo Ukweli mmoja tu, na kwa vile hakuna

3

makundi mawili yanayopatana kikamilifu kuhusu kile ambacho ni ukweli kwa kawaida si yote yanaweza kuwa sahihi, ila yote isipokuwa moja lazima yamekosea. Kwa nini, basi, mafundisho ya Bi. White yanaletwa ndani kwa upinzani zaidi kulingana na ukubwa wa wafuasi kuliko mojawapo wa mengine yote? {TN6: 3.3}

Kwa sababu kila mjumbe aliyetumwa na mbingu kutoka siku ya Adamu hadi leo, amepigwa vita vikali na watu wanaodai kwamba wanaongozwa na Mungu, basi ukweli tu wa upinzani dhidi ya maandishi ya Bi. White hautaweza kuthibitisha kuwa ana makosa. Na kwa vile yeye amekuwa lengo kuu la upinzani leo, ilivyokuwa kwa manabii katika siku yao, basi kujua iwapo maandishi yake ni hatari na ya uharibifu au salama na sahihi, tunapaswa kuugeuza umakini wetu kwa mafunuo ya Mungu, ambayo hufunua yaliyopita, ya sasa, na ya baadaye. Humo kazi yake, sahihi au ya makosa, lazima ipatikane. Kwa unabii tu, tunaweza kuthibitisha au kupinga, kujua kile tunachoamini na kuamini kile tunachokijua, na kwa usalama kupokea au kukataa ujumbe wowote. Vinginevyo imani yetu inaweza kuwa imejengwa tu kwa kukosa uhakika, — kwa msingi wa mchanga, — ambao mwishowe itatuletea kukata tamaa upande wa “mkono wa kushoto” wa Mwalimu. Ili kuhakikisha kusimama mkono Wake wa kuume, hatupaswi kushindwa kutii kwa umakini

Kushihi Kwa Roho Mtakatifu: {TN6: 4.1}

“Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye

4

giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.” 2 Pet 1:19, 20. {TN6: 4.2}

Lakini kelele na kilio cha upinzani ni, Ondolea mbali unabii kwa wakati huu Kwa maana manabii wote na torati

“Walitabiri Mpaka Wakati Wa Yohana.” Matt. 11:13. {TN6: 5.1}

Iwapo Maandiko yaliyonukuliwa hapo juu humaanisha kwamba hawangekuwepo manabii tena baada ya Yohana, basi asingalikuwepo hata mmoja tangu wakati huo. Na kama hii ingekuwa ndio maana yake, basi Maandiko yangekuwa yanakinzana yenyewe, kwa maana hutoa ushahidi kwamba wakati Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, Yeye pia alikuwa “nabii.” Luka 24:19. Na ingawa Yohana Mbatizaji hakuandika neno moja la kinabii, bado alikadiriwa na Kristo kuwa mkuu wa manabii (Luka 7:28). Pia Mathayo, Marko, na Luka, chini ya Roho ya Uvuvio, waliandika juu ya Kristo na kazi Yake. Vivyo hivyo, Yohana, Petro, na Paulo, na wengine walioishi pamoja nao wakati huo, walitabiri kwa haki yao kuhusu mambo mengi ambayo yangekuja. Yote haya Kimaandiko yamepewa jina la hadhi “nabii.” {TN6: 5.2}

Yesu Mwenyewe hushuhudia kwamba kitabu cha Ufunuo ni unabii, kwa maana malaika “aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani,

5

mambo yote alioyaona” anasema: “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufu. 1:2, 3. “Kwa maana Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.” Ufu. 22:18. {TN6: 5.3}

Sasa ukweli kwamba unabii huu uliandikwa karibu karne moja baada ya Yohana Mbatizaji kukatwa kichwa, ni stakabadhi ya kihistoria kwamba manabii hawakukoma pamoja naye. Kwa hivyo, kukosa kuelewa maana ya Mathayo 11:13 ili kumfanya Yohana kuwa nabii wa mwisho, upinzani unajaribu kubadilisha nafasi ya karama ya unabii katika enzi ya Kikristo, fasiri za “apendavyo mtu tu” (zisizovuviwa) za Maandiko. Na kwa kufanya hili, wanaongozwa ama kupuuza au kujaribu kufafanua visivyo maneno yasiyoweza kupingwa ya Paulo: “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.” (1 Kor. 12:28) — ushahidi kamili kwamba ya pili kwa karama nane kwa kanisa katika enzi ya Kikristo, ni manabii. {TN6: 6.1}

Ingawa nyingi za hizi karama, hasa kunena kwa lugha na maongozi, hutafutwa kwa bidii na makanisa ya Kikristo, moja — “manabii” — ambayo ilidharauliwa na Wayahudi, imekataliwa kabisa na karibu himaya yote ya

6

Kikristo! Hivi roho ambayo ilichochea mauaji ya manabii wa kale kwa mkono wa viongozi wa Kiyahudi, leo hii inafanya kwa kweli kila aina ya kazi ile ile ya uharibifu kutumia upinzani uliopangwa. {TN6: 6.2}

Wakati wanatoa sifa na heshima kwa manabii waliokufa ambao waliuawa na mababu zao, Wayahudi waliwakataa manabii waliokuwa hai, na hivyo wakajiletea tangazo la maombolezo la Bwana: {TN6: 7.1}

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.” Mat. 23:29, 30. {TN6: 7.2}

Wakristo wa sasa ambao hudharau karama ya unabii katika kizazi hiki, na pia ambao hukana kwamba Maandiko ya Agano la Kale hayana maana yoyote katika kipindi cha injili, hivyo basi huwakataa manabii wote, na wakati uo huo huwatambua kwamba walikuwa watumwa wa Mungu . Hivyo washirika wa namna hii wa kanisa huendelea kuyajenga na kuyapamba makaburi ya manabii kama walivyofanya Wayahudi ambao walidai kumwamini Musa lakini, walipopimwa, walionekana kuwa waongo. Kwa namna hiyo Wakristo wengi leo hujidai kuamini Biblia yote, lakini hufundisha kwamba sheria zote na taratibu, maonyo yote na hukumu, huwahusu tu Wayahudi wa kale, ilhali neema zote kwa shauku nyingi huziweka kifuani ndani ya kanisa la Kikristo! {TN6: 7.3}

7

Ya siku ya sasa inayoitwa eti karama ya aina za lugha ni upuuzi mwingi, na si tena karama ya Kibiblia kuliko isivyo Jumapili siku ya “Sabato” iliyotakaswa; na karama ya maongozi imegeuzwa vibaya kuwa taasisi ya mamlaka ya watu wa daraja moja, desturi, viwango, na vitu kama hivyo, ambavyo, katika hali zake duni, si chochote ila mashirika ambayo kwa madhara yake hufanya vita dhidi ya Ukweli na kutangua uchaji wa kanisa kwa Mungu. Katika hali hii ya mambo, je, hawa wanaojidai kuwa Wakristo wa leo wanadhani ni bora zaidi ya Wayahudi wote wabaya wa jana? {TN6: 8.1}

“Amka, amka,” hulia Neno, “jifungulie mwenyewe kutoka kwa” vifungo vilivyofanyizwa na binadamu “vya shingo lako, Ee binti Zayuni uliyefungwa.” Isa 52:2. “Msimzimishe Roho,” Ee kanisa la Mungu! “Msitweze unabii, jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna.” 1 Thes. 5:19-21. {TN6: 8.2}

Usiendelee kuupuuza tena ukweli kwamba karama ya manabii ni ya pili kwa mpangilio, na karama za maongozi na aina za lugha ni za mwisho. Kwa hivyo, tia alama, kwa hivyo kwamba wale wanaoidharau karama ya unabii lakini huziinua karama za maongozi na aina za lugha, ni dhahiri wanalivuta gari kutoka upande wake wa nyuma, na wanakwenda kwa uelekeo usiofaa. Kwa wao Kristo anasema: “nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Ufu. 3:17. {TN6: 8.3}

Wale ambao kwa upande mmoja hubishana kwamba hawangepaswa kuwapo manabii baada ya

8

Yohana Mbatizaji, na ambao kwa upande mwingine hujidai kuamini katika Maandiko ya Agano Jipya yaliyoandikwa baada ya kifo cha Yohana, wao wenyewe wamo gizani, na wako, kwa fasiri zao za wapendavyo tu (zisizovuviwa) za Maandiko wanaeneza wingu la giza popote waendako. Mungu awarehemu wote. {TN6: 8.4}

Katika nuru ya kweli hizi taarifa ya Yesu kwamba “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana,” bila shaka yana maana tofauti kabisa kutoka kwa kile kimefundishwa na watu ambao hawakuvuviwa. Iwapo yanaangazwa na Roho Yule yule Ambaye aliyaandikisha, tokeo la ufasiri ni suluhisho lisilo na utata, likifunua kwamba Kristo aliwatenga manabii katika makundi mawili — wale mpaka kwa Yohana na wale baada yake. {TN6: 9.1}

Historia takatifu huonyesha kwamba manabii katika kundi la kwanza walipokea Neno moja kwa moja kutoka kwa Mungu kwa njia ya Roho Wake. Hawakulazimika kuthibitisha sehemu yoyote ya unabii wao kwa maandiko ya manabii waliowatangulia. Ingawa manabii katika mgawanyo wa pili wameteuliwa na kutiwa mafuta na Roho kuyafasiri Maandiko ya manabii wa mgawanyo wa kwanza. {TN6: 9.2}

Tofauti hii muhimu na utengo huonyesha kwamba Maandiko ya Agano la Kale yanasheheni nuru ya wokovu wetu kwa vipindi vyote — cha Wayahudi na cha Wakristo. Na mtu anapofikiri kwamba kipindi cha awali

9

kinaitwa enzi ya “mfano,” na cha mwisho “uakisi,” basi ushahidi juu ya ushahidi unagongomea msumari hitimisho kwamba injili ya Agano Jipya inategemea Injili ya Agano la Kale ikiwa imefunuliwa. {TN6: 9.3}

Kwa sababu Maandiko hufafanua kwamba kanisa katika vizazi vyote limeongozwa kwenye ukweli tu kwa njia ya karama ya unabii, Mkristo hana chaguo ila kuhitimisha kwamba mapenzi ya Mungu na mpango kwa wakati huu ni kama ulivyokuwa nyakati zilizopita; yaani, kwamba maarifa ya wokovu yatolewe kwa njia ya maandiko ya manabii wa Agano la Kale, jinsi yanavyofafanuliwa na wale ambao juu yao, kadiri chuo kinapokunjua, Yeye huwajazi Roho yule yule ambaye Yeye aliwaongoza “watakatifu wa Mungu” “zamani.” 2 Pet. 1:21. “Kwa kuwa Mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.” Mal. 3:6. {TN6: 10.1}

Mungu angalikuwa ameiweka katika umoja himaya ya Ukristo kwa njia ya Uvuvio, ukweli uliofunuliwa, lakini watu ambao hawakuvuviwa hawakujinyenyekeza na wakatanguliza ufasiri wao wapendavyo tu, na matokeo mabaya ambayo wameleta machafuko sasa ya aibu ya madhehebu. {TN6: 10.2}

Mchafuko huo wa maoni kwa Maandiko yaliyopo si tu kati ya dhehebu moja na lingine, lakini pia ndani ya safu za kila dhehebu lenyewe, yanaweka wazi kwamba hayaongozwi na Roho Ambaye Kristo alituma “kuongoza … katika kweli yote” ili wamini wote ndani Yake wawe na umoja.

10

Umoja huu kwa njia ya Roho, unafundishwa kwa dhati katika

Sala Ya Kristo. {TN6: 10.3}

“Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani Yangu, Nami ndani Yako; hao nao wawe ndani Yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba Wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa Nimewapa wao; ili wawe na umoja kama Sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani Yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa Ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda Mimi.” Yohana 17:21-23. {TN6: 11.1}

Dhana zisizokoma za kitheolojia kwa Maandiko, pamoja na matokeo ya aina tofauti na hadithi za kufurahisha zilizotungwa kwa werevu na wanadamu, daima zinazidisha machafuko, uhasama, migawanyiko ambayo husababisha migogoro ya kanuni za imani na madhehebu. Ilhali Wakristo wangekuwa hawafanyi chochote ila kuuthibitishia ulimwengu kwa umoja mkamilifu kwamba Baba amemtuma Mwana. {TN6: 11.2}

Kuonyesha kwamba Yeye hulitambua dhehebu moja tu, Kristo alisema: “Na kondoo wengine Ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao Imenipasa kuwaleta; na sauti Yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.” Yohana 10:16. Ukosefu wa umoja uliopo kati ya Wakristo wa leo, kwa hivyo, hautimizi la Mungu, ila

Kusudi La Shetani Lililopangwa Kimbele. {TN6: 11.3}

Unaoitwa eti ulimwengu wa Wakristo wa leo

11

kwa umbali huu umeyaacha maadili ya Mungu kwa kanisa Lake kama kuifikia hatua ambapo hata sala yake Kristo hushindwa kuwakatisha tamaa, na kuwaleta kutambua kwamba imani zao tofauti za kuwa sahihi ni hakika zote zina makosa. Wale ambao hawana uhusiano na kanisa lolote, na kwa wale uongofu wao makanisa hudai kwamba yanajitahidi kutumia raslimali zao na wakati wao, hutazama kwa dharau na kicheko katika upotovu huu na unafiki. Wakristo wa aina hii wanampendeza Shetani tu na wanajidanganya wenyewe na wale ambao huwatazama. {TN6: 11.4}

Shetani anaviongoza vikosi hivi vinavyofanana na Ukristo kujionyesha kama wapumbavu mbele ya ulimwengu, ili kwamba kwa njia ya upumbavu wao usiokuwa na ufahamu anaweza kumtukana Kristo, na wakati uo huo aweze kuufanya ulimwengu uamini kwamba Baba hakumtuma Mwana. Isipokuwa haya majeshi yasiokuwa na umoja yawe macho kwa hatma yao, Shetani atawatumbukiza hivi karibuni kwenye uharibifu wa milele. Janga hili la milele litawajibishwa tu kwa wao kuidharau karama ya Roho ya Unabii macho ya kanisa (1 Sam. 9:9, Isa. 29:10) ambayo tu yanaweza kuona na kuwavuta katika hali ya umoja, umoja usioweza kuvunjika. {TN6: 12.1}

Wachungaji wa makanisa, kwa kujaribu kuyafasiri Maandiko “wapendavyo tu” (bila Roho Mtakatifu), wameandaa makapi mbele ya kondoo, na matokeo yake makundi yameachwa

12

Yajitafutie Kitu Bora. {TN6: 12.2}

Wakristo waliolishwa makapi, wakiwa na utapia mlo, hawawezi kuhukumu vyema. Baadhi yao, kwa hivyo, wana matumaini ya kupata “kitu bora” kutoka kwa wale ambao huwaona kuwa waaminifu zaidi; wengine hutarajia kupokea kutoka kwa wale wanaoangaliwa kuwa ni Madakta wa Uungu; ilhali wengine bado hufikiri kukipata katika hili au dhehebu lile tu kwa sababu Baba au Mama au mtu mwingine wa ushawishi au jamaa fulani ni wa dhehebu hilo. Kwa chaguzi hizi za upumbavu ambazo hazihitaji juhudi za akili au uzoefu wa kibinafsi, ni za kushangaza, zikiongoza tena kwa makapi. Na ulimwengu usiokuwa wa Wakristo, daima hutazama kwa undani, hugeuka kwa uchukizo kutokana na mienendo hii na mingine ya kipumbavu na inayotofautiana katika eneo la Wakristo. Hivi waumini, badala ya kuwaongoa wasioamini kwa Ukristo, wanawafukuza tu mbali zaidi kutoka kwa huo! {TN6: 13.1}

Kwamba wengine, pia, wanafahamu hatari hii kama ya kondoo, kujihisi salama kufuata kengele, huonyeshwa kwa mkazo katika kesi ya kubuni ya familia inayoonekana katika kejeli ya kibonzo

Kutoka Kwa Kalamu Ya “Mwana Makala.” {TN6: 13.2}

“Maria huenda kwa kanisa la Wabaptisti ingawa yeye ni mshiriki wa kanisa la Prestiberi (baada ya kufanywa ajiunge na kanisa akiwa na umri mdogo wa miaka 10, kabla hajajua ni nani Bwana au Ibilisi ni nani), lakini huhudhuria kanisa la Wabaptisti kwa

13

sababu dada yake wa kambo ni wa kanisa hilo. Yohana huenda kanisa la Katoliki, kwa sababu wateja wake wengi huenda huko. Jack huenda kanisa la Kampeli kwa sababu mchumba wake huenda huko … Patricia huenda kanisa la Walutheri kwa sababu mwalimu wake wa shule hufundisha darasa la shule ya Jumapili pale. Betty huenda kanisa la Wabaptisti na mama yake, kwa sababu yeye hajakuwa mtu mzima wa kutosha hata kujua zaidi.” — Habari Za Dallas Asubuhi, Desemba 28, 1940. {TN6: 13.3}

Wale ambao kwa uaminifu wanautafuta wokovu kwa njia ya Kristo, lazima “wajiunge” Naye kwa uongofu kwa ajili ya Ukweli; na njia ya pekee ya yeyote kuweza kufanya hivyo, ni kwa furaha kuzikaribisha zote

Karama Za Roho. {TN6: 14.1}

“Naye,” anasema Paulo Mmoja Ambaye pekee yake, kwa njia ya Karama Zake zote, aweza kuliunganisha kanisa Lake, “alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” Efe. 4:11-13. “ Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.” Ufu. 3:22. {TN6: 14.2}

14

Ingawa Roho wa Mungu amenena katika haya maneno hakika, bado mmoja hupata, baada ya kura ya maoni ya jumla kati ya Wakristo, kwamba

“Roho ya Unabii” Imekataliwa Kabisa. {TN6: 15.1}

Kundi kubwa la wanaojidai kuwa Wakristo wanasema hakika katika mioyo yao: Ili mradi tunaamini kwamba Mungu yupo na pia Kristo, tu wa kanisa, tunaishi maisha ya uaminifu, na kufanya tendo zuri mara kwa mara kadiri tunavyopata fursa, tuko njiani kuelekea Mji Mtakatifu. Na la kusikitisha kusema, hili tumaini legevu na hatari linalopotosha liko hata katika dhehebu la Waadventista wa Sabato. {TN6: 15.2}

Inasikitisha, pia, ingawa dhehebu liliasisiwa kwa karama ya unabii, waumini wake wa siku hizi — wachungaji na walei pia — wanaendelea kutofautiana siku zote miongoni mwao juu ya karama ya unabii, kama vile walivyo kwa maswala mengine katika Maandiko. Na miongoni mwa wale wanaozingatia kwamba maandishi ya Bi. White yamevuviwa, wengi wao hawayajui na hawayatii, kama walivyo wale ambao huwa hawakiri imani kwayo kabisa. {TN6: 15.3}

“Kanisa,” husema, kuhusiana na hali hii, “limegeuka nyuma na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na aste aste linarudi

15

kuelekea Misri. Hata sasa wachache wameshtuka au kushangazwa kwa ukosefu wao wa nguvu za kiroho. Kutilia shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {TN6: 15.4}

Hata sasa makundi yote mawili kanisani husisitiza kwamba wao ni Waadventista wa Sabato wema! O ni kinaya mno kilioje kwamba tofauti ya kutisha kama hii katika maswala matakatifu imezifunika akili za viumbe vyenye uwezo wa kupambanua! Naam, ni msiba ulioje! hasa wakati hali haikustahili kuwa ilivyo: maana kwa ulinzi wa kutosha dhidi yake,

Maandiko Hufundisha Ukweli katika Njia Kadhaa. {TN6: 16.1}

Mbali na kufundishwa na shuhuda halisi za manabii, injili hufundishwa pia kwa unabii wa mifano. Katika linalotuhusu sasa hivi, kwa hivyo, pamoja na mafundisho ya Roho jinsi ambavyo Mungu hulifunua kwa wanadamu Neno Lake lililoandikwa, tunapaswa kuangalia si tu kwa la halisi bali pia kwa shuhuda za mifano za manabii. Na kwa sababu sura ya nne ya Zekaria ni ufichuzi wa picha ya njia ambayo Mungu hulifunua Neno Lake, tunaelekezwa humo kwa ajili ya ufafanuzi wa

16

Hali-Tumizi Ya Mfano Wa Ufafanuzi Uliovuviwa.

Zekaria 4. {TN6: 16.2}

“Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa lile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini? Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu, asema Bwana wa majeshi…. {TN6: 17.1}

“Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.” Zek. 4:1-6, 12-14. {TN6: 17.2}

17

[Chati: Zekaria Sura ya 4]

18

Kuthibitisha wakati ambao unabii huu wa mfano unazungumzia, Bwana, akinena kupitia kwa nabii Hagai, aliyetabiri wakati uo huo kama nabii Zekaria, anasema: {TN6: 19.1}

“Nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, Nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; Nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake. Katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi Wangu, mwana wa Shealtieli, asema Bwana, Nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi.” Hag. 2:22, 23. {TN6: 19.2}

Unakutana na utimilifu wake mwishoni mwa dunia wakati Mungu atakapovipindua viti vya enzi na kuziangamiza falme za dunia, unabii wa Haggai huonyesha kwamba Zerubabeli, mtumishi wa Bwana ni mfano wa watumishi Wake leo, ambao ni lazima, hata hivyo, ndio “chapa” ya uakisi. Na kwa vile maono ya Zekaria, zaidi ya hayo, hayajawahi kueleweka hadi sasa, yanaweza kuwa yananena moja kwa moja tu kwetu kwa wakati huu. Maadamu, kwa hivyo, kielezi chake cha “Neno la Bwana kwa Zerubabeli” kitapata utimilifu wake leo, tunapaswa basi kutoa usikivu wetu wenye bidii

Uvuvio Unapoufafanua Mfano. {TN6: 19.3}

“Hili ndilo Neno la Bwana kwa Zerubabeli.” Zek. 4:6. Hali-tumizi ambayo

19

Mungu atatumia sasa, katika wakati wa mwisho, anapowasiliana na Zerubabeli — maliwali au wachungaji wa watu Wake — imewekwa chini katika mfano. Kwa hivyo hebu tuufafanue kwa uangalifu kipengele kwa kipengele cha mfano. Tunapoelewa maana ya “miti ya mizeituni,” “kinara cha taa,” “bakuli la dhahabu,” na “mirija,” basi mfano wenyewe bila utata utaeleza jinsi ambavyo Maandiko, ambayo Mungu hutumia kuwasiliana na watumwa Wake, yatafafanuliwa. {TN6: 19.4}

Kwa sababu vitabu vyote vya Biblia hukutana na kwishia katika Ufunuo, ambao ni ufichuzi wa unabii, tunaita usikivu wa msomaji kwenye kifungu ndani yake, ambacho Yohana hurekodi ofisi ya miti hii ya mizeituni: {TN6: 20.1}

“Nami nitawaruhusu mashahidi Wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Bwana wa dunia yote.” Ufu. 11:3, 4. {TN6: 20.2}

Mizeituni hii inaitwa “mashahidi,” “watiwa-mafuta,” “manabii.” Ilipaswa kutoa unabii hali imevikwa magunia kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Hiki ni kipindi sawa na kile katika Danieli 7:25 na Ufunuo 12:14; yaani, kwa “wakati na nyakati mbili na nusu wakati”: “wakati” — mwaka mmoja; “nyakati mbili” — miaka miwili — “nusu wakati” — nusu ya mwaka; — miezi arobaini na miwili kwa ujumla. Ni

20

sawa pia kwa hicho cha Ufunuo 13:5, “miezi arobaini na miwili”; na kwa hicho katika Ufunuo 12:6, “siku elfu moja na mia mbili na sitini.” Katika kila tukio, muda, kuhesabiwa kwa kanuni ya Biblia ya siku thelathini kwa mwezi, zinakuwa siku 1260. {TN6: 20.3}

Zinapohesabiwa kwa wakati halisi, kulingana na Ezekieli 4:6, hizi siku 1260 za muda wa unabii ni sawa na miaka 1260. Kuendelea na ukweli uliowekwa imara (tazama Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 126-139) kwamba kipindi hiki cha muda ni unabii wa miaka 1260 kutoka 538 B.K. hadi 1798, tunaletwa kwa hitimisho linalofuata kwamba yeyote au chochote kilichotoa unabii hali kimevikwa “magunia” katika kipindi hiki, ndicho kile kinachoashiriwa na hii “mizeituni miwili.” {TN6: 21.1}

Ukweli kwamba hakuna chochote ila Biblia Yenyewe ilitoa unabii kwa muda wa kipindi cha miaka 1260, — dini ya Zama za Giza, — unaonyesha moja kwa moja kwamba miti miwili ya “mizeituni”, ambayo malaika alisema ni Neno la Mungu (Zek. 4:6), ni mfano wa Maandiko ya Agano la Kale na Jipya yakitoa “unabii hali yamevikwa magunia.” Kwa maneno mengine, yalijiruhusu kudhalalishwa na kufunikwa kuachwa bila kusomwa, ingawa yalikuwa na uwezo wa kuwaangamiza “adui zao,” na hata “kuifunga mbingu, mvua isinyeshe.” {TN6: 21.2}

Na kutoka katika miti hii miwili (Maagano), jinsi Zekaria alivyoona, mafuta ya dhahabu hutiririka

21

kwa njia ya “mabomba mawili ya dhahabu,” ambayo humimina ndani ya “bakuli la dhahabu.” Kisha kutoka ndani ya bakuli, “mifereji saba,” au “mirija,” nayo hukisambazia kinara cha taa cha dhahabu “mafuta ya dhahabu.” {TN6: 21.3}

Kwa sababu mizeituni miwili husimamia Maandiko ya Agano la Kale na Jipya, kwa kawaida mafuta ya dhahabu yanayotiririka kutoka kwayo huwakilisha “Neno la Bwana” katika kipindi cha Kikristo, si kama vile linavyokuja moja kwa moja kutoka mbinguni, ila linavyokuja kutoka katika Biblia. {TN6: 22.1}

Kufunua ijayo maana ya kinara cha taa, Kristo (akiifunua siri Aliyomwonyesha Yohana), anasema: “Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.” Ufu. 1:20. {TN6: 22.2}

Katika taarifa hii fupi ya maelezo, Kristo hutuambia kwamba makanisa saba yamewakilishwa na vinara saba vya taa, hivyo kuweka ukweli kwamba kinara cha taa ni nembo ya kanisa — nuru ya ulimwengu (Mat. 5:14). {TN6: 22.3}

Sehemu ya kwanza ya Ufunuo 1:20, kama ilivyonukuliwa tayari, inaweka wazi kwamba yuko malaika anayetunza kila kinara cha taa, na ya kwamba Yohana aliagizwa kuandika, si kwa vinara vya taa, bali kwa malaika wasimamizi juu ya vinara. Kwa hivyo maneno, “na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika” (Ufu. 3:14), hufanya wazi kwamba

22

ni malaika ambaye ni “mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” {TN6: 22.4}

Kemeo hili mwisho huonyesha wazi kwamba yule malaika si kiumbe cha mbinguni, ila ni mfano tu wa waangalizi wa duniani ambao wamepewa usimamizi kwa kanisa (kinara cha taa). Wajibu wao, unavyofunua mfano, ni kukisambazia kinara cha taa mafuta, na kukitunza na kukiwezesha kuwaka — kuangaza. Vivyo hivyo, kinara cha taa chenyewe ni mfano wa walei pekee bila uongozi. {TN6: 23.1}

Katika maono ya Zekaria, hata hivyo, wachungaji wamewakilishwa, si na malaika saba, ila kwa mifereji “saba.” Wanapokea mafuta kutoka kwenye bakuli, na kukilisha kinara cha taa. {TN6: 23.2}

Wazi wazi, basi, bakuli ambamo mafuta ya dhahabu huhifadhiwa, linaashiria ghala la Ukweli wa Sasa — Neno lililofasiriwa. “Ghala” la pekee ambalo linasheheni maelezo yaliyovuviwa kwa Maagano yote ni vitabu vya Roho ya Unabii. Vitabu hivyo, kwa hivyo ni “bakuli la dhahabu.” Mfano huu dhahiri unaonyesha kwamba kutoka kwa hivyo vitabu wachungaji wanapaswa kuupata ukweli unaotoa nuru ambayo wataisambaza kwa kanisa, ili liweze kung’aa kwa uangavu katika dunia hii ya giza, kuwavuta kwenye nuru “watu wote” ambao huchukia giza. {TN6: 23.3}

Mabomba mawili ambayo mafuta hupitia hadi ndani ya bakuli, yanaweza kuwakilisha tu njia (manabii) ambao kupitia kwa wao

23

mafuta hupelekwa kutoka kwenye Biblia hadi ndani ya bakuli, katika kipindi ambacho miti ya mizeituni yote miwili (Agano la Kale na Jipya) i hai — Enzi ya Kikristo. {TN6: 23.4}

Hebu msomaji angalie kwa upekuzi onyesho la mfano katika ukurasa wa 18, na ataona kwamba haiwezekani kabisa kwa kinara cha taa (washirika wa kanisa) na kwa mifereji (wachungaji) wenyewe kufyonza mafuta moja kwa moja kutoka kwa miti ya mizeituni. Ufasiri wa Maandiko, kwa hivyo, ikiwa imekabidhiwa mabomba mawili (manabii) katika enzi ya Kikristo, unaonyesha kwamba “hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu,” bali ni wa uvuvio tu. {TN6: 24.1}

Sasa, ili kubana milele katika mawazo yetu ukweli kwa mada hii ya umuhimu wote, hebu tupige darubini katika

Muhtasari Wa Zekaria Nne. {TN6: 24.2}

Kitengo hiki cha mfano, kikiwa kimeonyesha kwamba Biblia inaweza kufasiriwa hakika tu na Roho Aliyeiandikisha, kinaonyesha kwamba kanisa linaweza kuongozwa katika Kweli tu kwa hali-tumizi hii inayothibitiwa na Roho: kupitia kwa wafasiri (mabomba mawili ya dhahabu), ambao pekee yao wanahitimu na kuwezeshwa kuzalisha chakula kwa majira yake (mafuta ya dhahabu) kutoka kwa Maandiko (miti ya mizeituni) hadi ndani ya ghala (bakuli la dhahabu) la Ukweli wa Sasa; na kupitia kwa wachungaji (mifereji saba), ambao pekee yao wanapaswa kuyapitisha kutoka kwa bakuli yale mafuta hadi kwa kanisa

24

(kinara cha taa), ili kiweze kumulika nuru ya uzima kwa hii dunia ya giza na inayokufa. {TN6: 24.3}

Hapa katika somo la mchoro Mungu bila kukosea anafundisha kwamba Yeye huyathibiti Maandiko na kwamba Yeye Huyafunua hitaji linapotokea, jinsi Yusufu alivyoweza kuthibiti nafaka zote katika maghala ya Misri ya kale, ili kuzitoa wakati wa njaa. Na kwa kupitia kwake tu Waisraeli, pamoja na Wamisri, wangepata nafaka wakati wa hitaji, na vivyo hivyo tu kutoka kwa Kristo, Mfalme, kupitia kwa vyombo Vyake Vilivyojazwa Roho — akina Yusufu (Wafasiri Wake maalum aliowateua wa ndoto na maono ambayo Biblia husheheni, iwapo ni ya kukemea na kuliangazia kanisa au kuwaonya kimbele Mataifa) — twaweza kuyapata “mafuta” ambayo Mungu ameyaweka ndani ya Biblia. {TN6: 25.1}

Katika kufichua kupitia mfano wa Zekaria mbinu iliyovuviwa ya kufasiri Maandiko, Mungu kwa uchoraji amependekeza, kwa ajili ya magonjwa mbali mbali ya kidini ya siku hizi,

Dawa Mahsusi Ya Mbinguni. {TN6: 25.2}

Magonjwa mengi sugu ya kiroho ambayo sasa yanalisumbua kanisa la Kikristo, husababishwa kwa sehemu kubwa na Wakristo bila kujua kuyapinda, kuyavuruga, na kuyapotosha Maandiko. Mazoea haya, Ibilisi ameyatumia kutaga mayai na kuyalea ili kuupinga Ukweli wa Sasa, kuharibu imani katika Maandiko,

25

kudanganya nafsi, na kuongeza ukufuru, akitumaini kwa kufanya hivyo kulikata kabisa taifa la watu kutoka kwa maarifa ya Mungu wa kweli na wa pekee aliye hai, na hivyo hatimaye kutoka kwa uso wa dunia. {TN6: 25.3}

Ndugu, Dada, kwa kila mmoja wetu moja kwa moja linatua jukumu muhimu la kuamua iwapo tutachagua kuwafuata manabii wa Mungu katika vipindi vya Agano la Kale na Jipya, au kujiunga na maadui wa Mungu ambao wanatetea fasiri zisizovuviwa za Maandiko, na ambao pamoja na wanaowaunga mkono, iwapo wanaendelea katika mwenendo wao wa uovu, watakuwa na hatia, pamoja na Wayahudi, kwa damu iliyomwagwa ya manabii. {TN6: 26.1}

Vigezo hivi vizito vitawahimiza wote walio waaminifu kwa wao wenyewe na kwa Mungu, kutenda kwa mujibu wa ukweli wa uchaji kwamba Yeye huufunua ukweli jinsi ambavyo huchagua. Yatakuongoza kuchukua njia ya Mungu kwa ajili ya kimbilio lako, na hivyo kuikimbia tufani inayojikusanya upesi ambayo inakaribia kulipuka kwa hasira yake yote ya kutisha kwa dhambi na mdhambi. {TN6: 26.2}

Kuona kimbele hali ya giza yenye kukanganya ambayo watu leo wanatupa kwa Biblia, na kuiacha njia iliyo wazi ya Maandiko, kama matokeo ya kutokujali kwao kabisa karama ya unabii, Mungu kwa hivyo amelazimika kwa uadilifu kuweka katika Neno Lake lililoandikwa aina fulani ya tangazo la kinabii la uovu huu mkuu na matokeo yake, jinsi alivyofanya kuhusu

26

hatma ya hatari iliyowangukia watu Wake wa kale, na juu ya hatma yao iliyofuata. {TN6: 26.3}

Ili kuonyesha hili, hebu sasa, na kumbukumbu maalum kwa karama ya unabii (ofisi yake, na uhusiano wake kwa wachungaji na pia kwa walei katika kipindi cha Agano Jipya), tutazama namna

Duka La Maziwa La Ulimwengu Huwawezesha Wateja Kukataa Uovu Na Kuchagua Wema. {TN6: 27.1}

“Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.” Isa. 7:14, 15. {TN6: 27.2}

Inakubaliwa kwamba mtoto anayezungumziwa hapa kinabii, ni Kristo. Na kwa mujibu wa aya hizi, Aliagizwa lishe maalum, kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji (Luka 1:15, Mat. 3:4). Hata hivyo hakuna rekodi inayoonyesha kwamba mlo wa Kristo ulikuwa wa “siagi na asali” halisi. Ipo kumbukumbu, hata hivyo, kwamba Yeye alikula vyakula vyote vilivyotakaswa vilivyoliwa kwa kawaida na Wayahudi wakati Wake. “Maana Yohana alikuja,” akasema Kristo, “hali wala hanywi, wakasema, Yu na pepo.” Mat. 11:18. Hivyo kwa neno la Bwana Mwenyewe, Yohana hakula kila kitu ambacho Wayahudi walikula. Kama ukweli wa jambo aliishi akila “nzige na asali ya mwitu.” Marko 1:6. Hata hivyo, Wayahudi walitafuta kosa, na wakamshtumu kuwa mwenye msimamo mkali na mwenda wazimu. {TN6: 27.3}

27

Kwa upande mwingine, “Mwana wa Adamu,” asema Bwana kwake Mwenyewe, “alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi.” Mat. 11:19. Katika maneno haya, akionyesha kwamba Yeye alikula chakula chochote halali kilichowekwa mbele Yake, Kristo anaweka dhahiri kwamba Hakuzuilia lishe Yake kwa iliyo halisi

Siagi Na Asali. {TN6: 28.1}

Kama ilivyoelezwa hapo juu hakuna rekodi inayoonyesha kwamba Yesu alikula iliyo halisi; siagi na asali. Lakini kama usemi wa nabii lazima uwe sahihi, hitimisho pekee linalowezekana ni kwamba ile “siagi na asali” ni mfano wa kitu ambacho Kristo alitumia sana, na Kilichomhekimisha na kumwezesha Yeye kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa hivyo, isitoshe, kwa sababu bidhaa hizi mbili halisi za chakula — siagi na asali — ndani yake haziwezi kamwe kumwezesha mtu yeyote kujua tofauti kati ya mema na mabaya, kwa hivyo zinafanywa thabiti maradufu kuwa ni mifano. Na bila shaka uhakika huu unachochea swali:

Ni Mifano Ya Nini? {TN6: 28.2}

Njia pekee ya kugundua nini siagi na asali huwakilisha, ni kubainisha kilichomwezesha Yesu kutofautisha kati ya mema na mabaya, na kulichagua moja na kulikataa lingine — sababu ya Yeye kuvila. {TN6: 28.3}

Mwokozi alizishinda nguvu za uovu kwa kuwa alivuviwa kuyafasiri Maandiko,

28

yaliyomwezesha Yeye kusema: “Imeandikwa.” Hili linafichua kwamba “siagi na asali,” ambayo ilimpa nguvu ya “kuyakataa mabaya” na “kuyachagua mema,” ni mfano wa Maandiko. Hivi alisema, “Mimi nina chakula msichokijua ninyi.” (Yohana 4:32), lazima Alirejelea “siagi na asali” ya Isaya. {TN6: 28.4}

“Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atamlisha ng’ombe mke mchanga na kondoo wake wawili; kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi, atakula siagi; kwa maana kila mtu atakayekula siagi na asali atasalia katika nchi.” Isa. 7:21, 22. {TN6: 29.1}

Kwa sababu “siagi na asali” ya aya ya 15 ni dhahiri imekusudiwa kutoa ufunguo wa kufasiri kwa ajili ya “siagi na asali” ya aya ya 22, wazi wazi, basi, “siagi na asali” ya aya zote inawakilisha Neno la Mungu. Na kwa sababu ya uhusiano mtawalia na mwunganisho wa asili kwa siagi, tunaongozwa kuuliza maana ya

Ng’ombe Mke Mchanga Na Kondoo Wawili. {TN6: 29.2}

Kwa vile siagi hutengenezwa kutoka kwa maziwa, na kwa vile maziwa ambayo “siagi” hii ya kiroho hutengenezwa kwayo, hutoka kwa “kondoo wawili” na “ng’ombe mke mchanga,” ukweli unajitokeza ukitiririka kwamba viumbe hawa watatu wanaozalisha maziwa ni mfano wa vyanzo vitatu tofauti ambavyo Neno la Bwana (siagi) hupatikana. Ng’ombe mke ni mchanga; kondoo hapana. Kwa hivyo, chanzo cha siagi, Neno

29

la Mungu, ambalo huwakilishwa na ng’ombe mke mchanga, ni la chimbuko la baadaye kuliko vyanzo vinavyowakilishwa na kondoo wawili. Kwa hivyo, wawili wa aina moja wanaweza tu kuwakilisha Maandiko ya Agano la Kale na Jipya; ilhali ng’ombe, kwa sababu ni mkubwa na mchanga kuliko kondoo, anawakilisha vivyo hivyo kiasi kikubwa cha chimbuko la baadaye kuliko Biblia. Magombo haya kwa udhahiri ni maandishi ya siku za mwisho ya “Roho ya Unabii” (Ufu. 19:10), ambayo huwawezesha wateja wake “kukataa uovu, na kuchagua wema,” na ambayo huwaletea

Asali. {TN6: 29.3}

Ufunguo wa ufasiri kwa hii “asali” unapatikana katika Ufunuo 10:10. Yohana akasema, “Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.” Huu utamu wa asali (umeelezwa kwa undani katika Trakti yetu Namba 5, Onyo la Mwisho), huwakilisha furaha iliyowajia waamini wakati wa William Miller, kupitia imani yao yote ya dhati kwamba Bwana alikuwa anakuja katika vuli ya 1843 B.K. kuwapeleka hadi nyumbani kwao katika “nchi iliyo mbali sana,” ambapo macho yao “yatamwona Mfalme katika uzuri Wake.” Isa. 33:17. Lakini siku hiyo ilipopita, na tukio lililotarajiwa likakosa kutimizwa, kisha kulemewa kwa kuvunjika moyo, jinsi kulivyoonyeshwa kwa kitabu kidogo kubadilika kuwa “kichungu,” kulimjia kila mtu ambaye, kwa matarajio ya uaminifu, kwa hamu

30

alitazamia hiyo safari iliyongojewa kwa muda mrefu kupitia mbingu zenye nyota hadi kwa mji wa “miraba minne” — Mji Mkuu wa nchi mpya. {TN6: 30.1}

Utamu wa asali ya Ufunuo 10:10 husimamia kama inavyofanya furaha kuu inayosababishwa na kujilisha Neno la Mungu, hupeana moja kwa moja kwa “asali” ya Isaya 7:22 maana ya furaha ambayo itawajia wote wanaojiunga kula ile “siagi” kutoka kwa “ng’ombe” na “kondoo,” ambayo sasa “imeletwa upya.” Wale tu wanaofanya hivyo, “watasalia katika nchi.” {TN6: 31.1}

Mwaliko huu mkunjufu wa kula “siagi na asali” ya kiroho, hata sasa haujawahi kulinganishwa kwa wingi au ubora, umenyooshwa kwa wale ambao hupenda kutilia shaka. Pokea mwaliko huu wa kipekee sana, ndugu zangu, na mtajishawishi kwa uaminifu na uamuzi ambao huchochea ombi letu, na mtafahamu kwa mwonjo wa kwanza kwamba bidhaa kutoka kwa viumbe hivi viungwana ndio zote mnazohitaji kuwahifadhi si tu hai na vyema lakini pia katika furaha na amani “tangu sasa” na milele! Na ingawa upo umati wa kulishwa, hamhitaji kuhofia uhaba wa chakula, kwa maana Duka La Maziwa La Ulimwengu lina

Dunia Ya Maziwa Yanayozalisha Siagi. {TN6: 31.2}

Viumbe hivi viungwana hutoa kiasi kingi cha maziwa hivi kwamba tunalazimika kutenga

31

krimu, na tunaweza kuigawa tu. Maziwa tunahifadhi. Wingi huu huthibitisha kwamba kubarikiwa kwetu kuwa na ukweli mtimilifu (maziwa) kwamba yote tunayoweza kufanya ni kutuma viwango vya juu — siagi au krimu. Ukweli uliofunuliwa awali kamwe haujawahi kujikusanya katika ghala kama hili lisilotindika jinsi ilivyo leo, hukamilisha ushahidi kwamba ufasiri wa huu unabii ni sahihi, na ya kwamba Fimbo ya Mchungaji, ambayo inasheheni ukweli wa wakati huu, imesababisha

Nchi Kufurika “Maziwa Na Asali.” {TN6: 31.3}

Mungu alipoahidi kuwaongoza Waisraeli wa kale katika nchi “inayofurika maziwa na asali,” hali kama hiyo haikutokea kwa kweli katika Kanaani, kwa hivyo maneno hayo yaliweza kuwa mfano tu wakati huo yakipata utimilifu wake kwa ukweli kwamba huko manabii walifanya utabiri na kuandika Maandiko, na hivyo nchi kufurika “maziwa na asali” — ukweli na furaha. {TN6: 32.1}

Mbona kukaa na njaa, ndugu zangu, wakati ambapo upo ugavi usiokuwa na mipaka wa chakula cha kuinawirisha nafsi karibu na mikono yenu? Iwapo hamu yenu haijakuwa hafifu sana, njoo, kisha, mjilishe hii “siagi na asali” mpya. “Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.” Isa. 55:1. Lakini iwapo, kwa sababu, mmepoteza hamu na ladha yenu kwa ukweli, waite basi wawakilishi wetu wa kusambaza. Huduma zao ni za bure na bila mapendeleo, na udhamini wa hakika na matokeo ya

32

kuridhisha. Msiwe kama wale ambao bado wanaendelea kujigamba kwamba wana ukweli wote, na “hawahitaji kitu chochote.” Kwa sababu kwamba Mungu ametuma na bado anatuma ghala kama hili la “chakula kwa wakati wake” ni kuonyesha kwamba badala ya kutokuwa na “hitaji la kitu chochote,” wanahitaji kila kitu, na kwamba ni machukizo yao na ufukara wa kiroho ambao umesababisha Yeye kuliacha

Shamba Lake La Mizabibu Ukiwa. {TN6: 32.2}

“Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu, iliyopata fedha elfu, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu.” Isa. 7:23. {TN6: 33.1}

Ukweli kwamba shamba hili la mizabibu (mfano wa kanisa — Isa. 5:7), ambamo kila mzabibu ulikuwa wa thamani ya “fedha,” limekuwa mahali “pa mbigili na miiba,” unaonyesha kwamba Mkulima wake ameliacha ukiwa, mfano wa hali ambayo Kristo alionyesha kikamilifu katika maneno yafuatayo: {TN6: 33.2}

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi Nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” (Mat. 23:37, 38) — yaani, imekuwa eneo ambalo uwepo na utukufu wa Mungu umetoweka. {TN6: 33.3}

33

Uaminifu na umilele wa Roho ya Unabii sasa kuwa hauna shaka, kimaadili unatuhimiza kuutambulisha ushuhuda wa Kristo kuihusu hali ya kiroho ya dhehebu la Waadventista wa Sabato kama ilivyoandikwa na Roho ya Unabii: {TN6: 34.1}

“’Je, huoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia?’ Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba? Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu inakosekana.’” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {TN6: 34.2}

Maono ya Isaya huthibitisha kikamilifu ushuhuda ambao umenukuliwa hapo mbele: manabii wote hawangeweza yamkini, isipokuwa kwa Roho mmoja, kuweka wazi hali iyo hiyo kwa uaminifu kama huo kabisa kwa jambo hilo. Hivi kwa Maandiko na kwa busara tunapelekwa hadi kilele cha ushahidi na imani ya kwamba Bi. White alivuviwa na Roho mmoja kama alivyokuwa Isaya. {TN6: 34.3}

Ukweli unaojulikana kwamba manabii wote wawili (Isaya na Bi. White) wako kwa umoja kati yao kuhusu hali halisi ya kanisa ilivyo sasa, unatoa upatano maradufu katika shtaka kwamba “nyumba ya Mungu” haijakuwa nyumba tu ya biashara na pango la wanyang’anyi lakini pia ni

34

Eneo la Kuwatupa Nje Watakatifu. {TN6: 34.4}

“Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mibigili na miiba.” Isa. 7:24. Kwa maneno mengine, shamba la mizabibu limeachwa ukiwa, na hivyo limevamiwa na wanyama wa mwitu (watu ambao hawajaongoka), hivi kwamba iwapo mtakatifu angeingia ndani yake, angelazimika kujihami kwa “mishale” na “uta” (Neno la Mungu) kujilinda (Ebr. 4:12). {TN6: 35.1}

“Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo, (Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli).” Mwa. 49:24. “Uta wako ukafanywa wazi kabisa, … Neno thabiti.” Hab. 3:9. {TN6: 35.2}

Badala yake, kwa hivyo, kanisa kuwa kimbilio, likitoa wokovu kwa watu wa Mungu, limekuwa pango la wezi na eneo la kuwahifadhi wenye dhambi. Kwa maana mara mtu anapoonekana akizingatia kuteta kwa Bwana dhidi ya machukizo, na kujitambulisha kuwa mwana matengenezo, hayawani wa mwituni (wale ambao hawajaongoka kanisani) wako aidha tayari kummeza, jinsi walivyojaribu kumwangamiza Paulo (1 Kor. 15:32), au vinginevyo kumfukuza nje ya mikutano ya makanisa! Hapa mtu yeyote anaweza kuona kwa urahisi mbona wale ambao wanawajibika kwa machukizo wanalipinga fundisho la kanisa safi. {TN6: 35.3}

Hatuhitaji kushangaa kwa upinzani ambao watumwa wa Mungu wanapokea

35

kutoka kwa watu wenye elimu na mamlaka, kwa maana hivi ndivyo imekuwa; na sasa, kama ilivyokuwa katika vizazi vya awali, uwasilishaji wa ukweli unaokemea dhambi na kurekebisha makosa utachochea upinzani. “Maana kila mtu atendaye maovu,” asema Bwana, “huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.” Yohana 3:20. {TN6: 35.4}

Watu wanapoona kwamba hawawezi, kwa Maandiko kudumisha msimamo wao, huamua kuutetea kwa gharama yoyote, na kama kituo chao cha mwisho cha hoja iliyopotezwa hujiingiza katika utu wa watu, wakishambulia tabia na nia za wale wanaokutana nao na ukweli ambao si maarufu. Kujihesabia haki kama huu kwa ubinafsi ni mila ya mfumo ule ule wa ulinzi ambao wameutumia katika vizazi vyote. {TN6: 36.1}

“Eliya alitangazwa kuwa wa kuitaabisha Israeli, Yeremia msaliti, Paulo mchafuzi wa hekalu. Tangu siku hiyo hadi hii, wale ambao watakuwa waaminifu kwa ukweli watahukumiwa kuwa wachochea maasi, wazushi, au waletao mafarakano. Umati ambao ni wa kutoamini sana kupokea neno la unabii lililo imara, watapokea kwa wepesi wa kusadiki bila kuhoji uthibitisho kwa mashtaka dhidi ya wale wanaothubutu kukemea dhambi za mitindo. Roho hii itaongezeka zaidi na zaidi.” — Pambano Kuu, uk. 458, 459. {TN6: 36.2}

“Wale waliotofautiana na mafundisho yaliyowekwa wamefungwa jela, wameteswa na kuuawa, kwa uchochezi wa watu ambao walidai kuwa wanafanya kazi chini ya

36

idhini ya Kristo. Lakini ni roho ya Shetani, si Roho ya Kristo, inayochochea matendo kama hayo. Hii ni mbinu ya Shetani mwenyewe kuuleta ulimwengu chini ya ufalme wake. Mungu amewakilishwa vibaya kupitia kanisa kwa njia hii ya kuwashughulikia wale wanaodhaniwa kwamba ni wazushi.” — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 74. {TN6: 36.3}

“Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno Lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isa. 66:5. {TN6: 37.1}

Na sasa kwa sababu ya hili, je, sisi ambao tuna nuru ya Ukweli tuisaliti imani yetu na kuepuka majukumu yetu? “Kwa mtumwa wa Mungu wakati huu amri imetangazwa kwake, ‘Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu Wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.’ {TN6: 37.2}

“Hadi hapa kadiri fursa zake zinapanuka, kila mmoja ambaye amepokea nuru ya ukweli yu chini ya jukumu lile la uchaji na la kuogofya kama alivyokuwa nabii wa Israeli, ambaye neno la Bwana lilimjia, kusema: ‘Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini

37

damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. {TN6: 37.3}

“Kikwazo kikuu kwa kuupokea na kuutangaza ukweli, ni uhakika kwamba kinahusisha usumbufu na kushutumiwa. Hii ndiyo hoja ya pekee dhidi ya ukweli ambayo watetezi wake hawajaweza kuipinga. Lakini hiki hakiwezi kuwazuia wafuasi wa kweli wa Kristo. Hawa huwa hawasubiri ukweli kuwa maarufu. Kwa sababu wakishawishika kwa jukumu lao, huupokea kwa makusudi msalaba, pamoja na mtume Paulo wakihesabu kwamba ‘mateso yetu madogo, ambayo ni ya muda tu, yanatufanyia uzito mkubwa wa milele na wa utukufu; pamoja na wa zamani, ‘kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri.’” — Pambano Kuu, uk. 459, 460. {TN6: 38.1}

Kwa sababu ya hali hii ya kusikitisha, Mungu sasa anawaagiza wajumbe Wake kwenda na “nyuta” na “mishale” yao na kuchukua kwa uaminifu nafasi zao za wajibu

Hadi Shamba La Mizabibu Lirejeshwe Kikamilifu. {TN6: 38.2}

“Na vilima vyote vilivyolimwa kwa jembe, haitafika huko hofu ya kuiogopa mibigili na miiba.” Isa. 7:25, sehemu ya kwanza. {TN6: 38.3}

Hivi ni kusema, ingawa shamba lote la mizabibu limejaa “mibigili na

38

miiba,” Mungu hajaliacha kabisa, ila atalilima kwa sululu, kung’oa mibigili na miiba, na kulipanda mara tena mizabibu mizuri maana kwalo “Yeye huweka heshima Yake kuu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 15. Na baada ya kutekeleza kazi hii, “hofu ya mibigili na miiba” “haitakuja huko.” Au, kunena kihalisi, katika kulitakasa kanisa, kisasi cha Mungu kitawaondoa waovu miongoni mwa watu Wake! Na kisha kuwaweka nje na kulidumisha kanisa Lake safi milele, bila hofu ya kutiwa unajisi tena. Hivi kwa kung’oa kabisa mibigili na miiba (waovu), Yeye huzuia hata kurudi kwayo. {TN6: 38.4}

Maono ya Isaya huangazia wazi kwa wakati wetu, kwa maana waovu wamekuwa siku zote kanisani na wataendelea kuwa humo hadi utakaso wa mwisho, ambao utatukia hivi karibuni, na ambao, kwa mujibu wa Maandiko, katika mwanzo wake utakuwa

Kama Mbegu Ya Haradali. {TN6: 39.1}

“Haitafika huko hofu ya kuiogopa mibigili na miiba: lakini hapo patakuwa mahali pa kupeleka ng’ombe, mahali pa kukanyagwa na ngombe wadogo.” Isa. 7:25, sehemu ya mwisho. {TN6: 39.2}

Shamba la mizabibu likiwa limelimwa kwa sululu ni ishara kwamba mwanzo wa kazi ya matengenezo itaendelea polepole na ya kwamba itahitaji kazi ngumu, lakini kwamba kila “kilima” au eneo la kanisa

39

likiwa limelimwa litakuwa mahali pa “kupeleka ng’ombe.” Kwa ufupi, kwa wakati huu maalum Yeye atakuwa akiwatuma wamishonari kwenda katika shamba Lake la mizabibu lililopuuzwa (kanisa) badala ya kwenda katika dunia ya watu wa Mataifa. {TN6: 39.3}

Ingawa kazi, zaidi ya hayo itakuwa na mwanzo mdogo mgumu, kama wa kulima na sululu itapata kasi na kuibuka kutoka hatua ya sululu hadi kuingia hatua ya jembe la kukokotwa na ng’ombe — hatua ambayo itawaona waamini wote wa Ukweli wa Sasa (isipokuwa “ng’ombe wadogo”) kwa umoja wakienda kuchimba au kulima” milima “mingine hadi mibigili na miiba yote itakuwa imeng’olewa kote kote kwa ardhi, udongo kuchimbuliwa, na shamba la mizabibu kurejeshwa hata zaidi ya ubora wake wa awali. Hivi likiwa limekombolewa, litakuwa eneo si tu la “kupeleka ng’ombe,” wamishonari, ila pia kwa ajili ya

“Ng’ombe Wadogo Kukanyaga.” {TN6: 40.1}

Maneno yote “kukanyagwa” na “ng’ombe wadogo” yana maana mbili. “kukanyaga” humaanisha kwenda hatua na kukanyagia kitu chini ya miguu. “Ng’ombe wadogo “ lina maana ng’ombe wachanga na ng’ombe duni. Kwa hivyo kirai “kukanyagwa na ng’ombe wadogo,” kinapochukuliwa katika nuru ya maana ya kwanza, kwa mfululizo huo, wa kila maneno mawili, lazima yatarejelea kwa watoto na wale wapya waliokuja katika ukweli, ambao wataweza kuwa wanakaa, “kwenda hatua,” juu ya milima mipya iliyolimwa. Kinapochukuliwa kwa nuru ya maana ya pili ya kila neno, ni lazima yatarejelea kwa kuwashinikiza au kuwakanyagia-kanyagia, “kwenda hatua”

40

kwa udongo, wote wale wasiokuwa waongofu ambao watatafuta kuingia ndani ya shamba la mizabibu. Kuhusu hili kundi la mwisho, Zekaria anasema: “Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.” Zek. 13:3. {TN6: 40.2}

Utumizi wa moja kwa moja wa maandiko, hata hivyo, ni kwa jozi la mwisho la maana, na wazo la pili tu ni lile linalopatikana kutoka kwa jozi la awali la maana. {TN6: 41.1}

Mtazamo huu wa mwisho wa shamba la mizabibu unawalazimu watu kuchagua utukufu wa baadaye au mwisho usiokuwa na utukufu. Tumaini letu ni kwamba kila mmoja atachagua

Utukufu Wa Wakati Ujao. {TN6: 41.2}

Kwa sababu wakati mwishowe Yeye atakapolirejesha shamba Lake la mizabibu, Bwana hataliacha au kuliruhusu kuchafuliwa na “mbigili na miiba,” furaha ya mwandamu lazima iwe tele, kumfanya amsifu Mungu mchana na usiku kwa upendo Wake usiokoma! Bado linalosisimua zaidi ni wazo kwamba umati sasa upo kwenye hatua hasa ya mpito kutoka hali hii ya kufa kuingia ile ya kutokufa — kamwe kutozoea hali ya kukosa ufahamu ya wafu! Mwito huu uweze kumchochea kila msomaji atoke katika usinziaji wake wa muda mrefu (Mat. 25:5), na kumsihi ajitahidi zaidi ya hapo awali kwa ajili ya “alama” ya Mungu aliye hai (Ezek 9:4). {TN6: 41.3}

41

“Amka, amka”; Usikilize Sauti ya Upendo, “Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” Isa. 52:1. {TN6: 42.1}

Iweni katika kundi la wanawali watano wenye hekima, ndugu zangu, na mjipatie mafuta haya ya ziada sasa kabla ya taa zenu kuzimika na mlango kufungwa milele (Mat. 25:10). “na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Ufu. 3:18. Kuugua na kulia kwa sababu ya machukizo yanayofanyika kanisani (Ezek 9:4), ili mweze kujithibitisha kwamba mnastahili kuupeleka ujumbe kwake. Kisha baada ya kupiga kelele, “Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” (Nah. 1:15, sehemu ya mwisho), itanenwa kuwahusu, “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani.” (Nah. 1:15, sehemu ya kwanza), na

Utanusurika Kupitia “Siagi Na Asali.” {TN6: 42.2}

“Kwa maana siagi na asali atakula kila mtu aliyesalia katika nchi.” Isa. 7:22. {TN6: 42.3}

O ni uhakikisho ulioje wa kuichochea nafsi! Mbona uangamie wakati Baba yako wa Mbinguni anafanya toleo kama hili? Amini kikamilifu katika Roho ya Unabii na uishi milele. “…Waaminini manabii Wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” 2 Nya. 20:20. {TN6: 42.4}

42

Je, bado hamjagundua kwamba, iwe ni katika nyakati za zamani au za mamboleo, kweli zote za Biblia ambazo watu wamewahi kujifunza, zimekuja tu kupitia njia iliyovuviwa — Roho ya Unabii? Vipi, basi, ndugu zangu, Mwaweza kuendelea kuukataa mwaliko huu mkunjufu? Njoo, mle mshibe “siagi na asali,” mwonjo tu ambao utawaanzisha kwenye safari yenu ya uponyaji kutoka katika hali yenu ya kusikitisha ya Ulaodekia. {TN6: 43.1}

Ijapokuwa kanisa sasa ni “vuguvugu” (limeridhika) katika “udanganyifu” wake, hata sasa iwapo litaruhusu fursa hii ya sasa iponyoke kutoka mikononi mwake, siku itakuja ambapo kila mshiriki atasaga meno yake katika mateso ya huzuni yasiyoelezeka. Naam, na wote wanaokana aidha Maandiko ya Agano la kale au Jipya, au Roho ya Unabii, au yote matatu, na ambao, kwa kusalia katika ujinga endelevu, wasiyazingatie matakwa ya Ukweli, “hawatasalia,” ila wataangamia. {TN6: 43.2}

Iwapo Kristo, Muumba wa ulimwengu (Yoh. 1:3, Ebr. 1:2), alijinyenyekeza Mwenyewe kwa kuamini katika maandishi yote ya manabii, basi kwa nini watu wasiyaamini pia? Je, wao ni wakuu zaidi kuliko Yeye? Je, utakuwa miongoni mwa wale ambao Yeye husema, “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii”? Luka 24:25. {TN6: 43.3}

Ikiwa Kristo Mwenyewe alikula “siagi na asali” ili “kukataa uovu, na kuchagua wema,” iweje, basi, unaweza kutarajia kujifunza kilicho chema na kibaya iwapo

43

unayafumba macho yako usije ukaona na kuziba masikio yako usije ukasikia, na hivyo kukaa katika ujinga kabisa wa kutoyajua mapenzi Yake? Pasipo kula “siagi na asali” Yake, haki yako haitakuwa kama “matambara machafu” ya haki ya ubinafsi (Isaya 64:6)? {TN6: 43.4}

Njoo, ndugu zangu, wakati bado upo wingi wa siagi kwa ajili ya utunzi wenu, asali kuwafanya mfurahi, na “bakuli la dhahabu” lililojaa “mafuta” kuwafanya “mwangaze.” Kwa nini mzidi kunyong’onyea gizani, wenye njaa kwa makapi, ilhali Mungu anawapa kibali mpate kuwa marafiki wa “ng’ombe” Wake na “kondoo wawili”? Lakini baada ya yote, mnahitaji kwa ajili yenu wenyewe, si kwa ajili yao, kula siagi yao. Basi njoo muichukue, kwa maana, asema Bwana,

“Mtu Atawalisha.” {TN6: 44.1}

Hapa Bwana anatuambia kwamba kazi ya kuwakamua kondoo wawili na ng’ombe mke mchanga (kuyakunjua magombo yaliyotumwa kutoka mbinguni) haijakabidhiwa wote, ila kwa “mtu” (nabii). Hili linamaanisha kwamba kupitia kwake yule ambaye nuru imefunuliwa, hulisha vyanzo hivi vya usambazaji kwa kuamsha hamu iliyoenea sana kwavyo, na hivyo kuviweka hai vikiendelea kuzalisha. Na kila mmoja ambaye atasalia katika nchi, lazima avipatie mahitaji yake na awe macho, bila shaka, kuichochea hamu ya wengine katika bidhaa zao za kudumu, zanazopeana uzima. {TN6: 44.2}

Akijua kwamba baadhi wangeyakana Maandiko ya Agano la Kale na wengine

44

Agano Jipya, pia kwamba bado wengine wangetilia shaka Roho ya Unabii, Mungu kwa hivyo huitisha umakini kwa yote matatu. Mifano, “ng’ombe mke mchanga na kondoo wawili,” ya kipekee katika uwezo wao wa kuzalisha maziwa, inaweka wazi kwamba bidhaa zao zinaweza kudumisha uzima kwa umilele, na ya kwamba kwa “mtu” ambaye huwalisha watakatifu wanapaswa kumwendea wapate siagi yao. Kisha watajua tofauti kati ya

Roho ya Unabii na Bandia yake. {TN6: 44.3}

Mtu anaweza kusema, “Naam, Naamini katika Roho ya Unabii, lakini si unavyofanya.” Bado ikiwa lile analoamini kuwa Roho ya Unabii halimwongozi “kuzishika amri za Mungu” na kujua kwamba ushuhuda wa Yesu Kristo ni Roho ya Unabii iliyo hai siku zote (Ufu. 12:17; 19:10) ), basi ingekuwa vyema aliache hilo na kulipokea hili, kwa maana “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri Zake, ni muongo, wala kweli haimo ndani yake.” 1 Yoh. 2:4. Vivyo hivyo Bwana asema: “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10. “Heri wazishikao amri Zake, waweze … kuingia mjini kwa malango yake.” Ufu. 22:14. {TN6: 45.1}

Iwapo, zaidi ya hayo, kile mmoja kama huyo huamini kuwa ni Roho ya Unabii ni hicho kweli, basi kingekuwa kimemfunulia kweli zilizokunjuliwa humu ndani. Hivyo kile ambacho hukikubali

45

badala ya kile sisi tunacho kubali kuwa Roho ya Unabii kingekuwa kimethibitishwa na kuinuliwa. {TN6: 45.2}

Si muda mrefu uliopita mchungaji mmoja alisema: “Maoni yangu ya Roho ya Unabii ni tofauti na yako, unabii katika Biblia ndio Roho ya Unabii yangu.” Sasa basi lazima aseme iwapo Roho ya Unabii haikuwa hai wakati wote. Lakini iwapo Roho ya Unabii huanza na kuisha na Biblia, basi Wakristo wote wanayo Roho ya Unabii. Ikiwa hili ni hivyo, hata hivyo, kwa nini Ufunuo hufanya tofauti kati ya Wakristo walio na Roho ya Unabii na wale wasiokuwa nayo? Wazo la mchungaji ni, kusema machache, la uelewa finyu, kwani linaweka Ufunuo 12:17 na 19:10 katika mazingira ya kukosa maana. {TN6: 46.1}

Lakini lililo baya zaidi, mchungaji yule mmoja baadaye akizungumza na kongamano lake, aliyafanya mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji kuonekana yanapinga maandishi ya Bi. White, ambayo hatimaye aliyaita “Roho ya Unabii”! Naam, ni vigumu kuamini kwamba wachungaji ambao watu wengi huweka imani ndani yao, wanakuwa vigeugeu na kwamba hawa watu wengi ni vipofu mno kuwahusu! {TN6: 46.2}

Kotekote katika kurasa hizi, Roho ya Unabii, katika Neno la kinabii, imejithibitisha Yenyewe kwamba haiwezi kushambuliwa. Imejitetea si kama sauti ilioanza na Musa na kukoma kabla ya Yohana Mbatizaji, ila kwa kuwa ni ushuhuda hai wa daima,

46

kuanzia kwa uumbaji na kuendelea na wazee Henoko, Nuhu, Abrahamu, Isaka, Yakobo; kisha na manabii; ijayo na mitume; na hatimaye, na wajumbe wa Bwana katika siku yetu ya leo na kuendelea. Ikiinuka na kuinuka na kila pambano, jinsi msomaji anavyoweza kuona kwa urahisi, Itainuka juu zaidi wakati ijayo ikizingatiwa kwamba

Shutuma Zinazotupwa Kwa Tabia Za Mtu Haziuathiri Ukweli. {TN6: 46.3}

Kushindwa kutumia njia za haki kufaulu kuipinga kazi ya Dada White, wengine kwa muda mrefu wamekuwa wakiegemea kushambulia tabia yake. Je, mtu yeyote anafikiri kwamba kuhitilafiana na tabia huyafanya maandiko ya mtu kuwa si ukweli? Iwapo ni hivyo, basi watafanya nini na unabii wa Balaamu kumhusu Kristo Mwokozi wetu? Tabia ya nabii huyu asiye na imani ilikuwa duni sana hata wakati alipokuwa akitamani kupata faida kutoka kwa mfalme mwovu wa Moabu, alikuwa katika unafiki mkubwa sana akitoa dhabihu kwa Mungu ili Yeye awalaani Israeli. Bado wakati alipokuwa akijihusisha katika uhaini huu, aliunena unabii mtukufu wa Kristo: {TN6: 47.1}

“… Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia. Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui Zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa. Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo

47

Yeye atakayekuwa na ufalme, atawaangamiza watakaobaki mjini.” Hesabu 24:17-19. {TN6: 47.2}

Athubutu mtu yeyote sasa kumkataa kabisa Kristo kwa sababu tu nabii mwovu aliutabiri ujio Wake? Hapa, kila aaminiye katika Neno la Mungu analazimika kukubali kwamba tabia ya Balaamu ya tamaa haikufanya unabii wake kuwa uongo! Jinsi gani, basi, uzingatiaji wa tabia leo, zaidi ya jana, kumhalalisha yeyote kulikataa Neno la Bwana na hivyo kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu? {TN6: 48.1}

Isitoshe, wale ambao huamua kushambulia utu wa watu, wanapojichunguza wenyewe, hupata tabia zao ni mbovu mara saba zaidi! Hata hivyo wanapokuwa bado wanatumia maelfu ya dola, na miaka ya kazi ngumu kuharibu imani ya watu ndani ya wale ambao dhidi yao hupendelea kubandika mashtaka ya uongo, wao kwa upande mwingine husihi kwamba umati ule ule lazima uyakubali mafundisho yao, ingawa kwa hakika tabia zao chafuchafu hufanya za Bi. White, kwa kulinganisha, nyeupe kama theluji. {TN6: 48.2}

Lakini siri kuu zaidi i katika ukweli kwamba umati hauwezi kutambua upayukaji huu wa milima inayotofautiana! Iwapo tabia ya Bi. White inayodhaniwa kuwa potovu inayafanya maandiko yake kuwa mapotovu, basi ni vipi huzifanya kuwa nyoofu, za ungwana, wanaozishika amri tabia za wale wanaoyapenda? Vile vile, tunawezaje kuyategemea maandishi na hotuba za watu wa namna hii ambao hushuka kwenye vina vya udongo kumhukumu bila kumsikiza,

48

wakati amelala kaburini mwake akiwa hawezi kujitetea mwenyewe? {TN6: 48.3}

Hawajayapinga zaidi maandishi yake kuliko walivyofanya Mafarisayo kuyapinga mafundisho ya Kristo. Na kama maadui wa Kristo hawakuweza kwa ukosoaji wao kubadili tabia Yake kutoka kwa takatifu hadi isiyokuwa takatifu, wala maadui wa Bi. White hawawezi kumfanya mpotovu iwapo ni mnyofu. Kama vile mfuasi wa kweli wa Kristo hawezi, hata hivyo, kuupoteza muda wake katika ama kuwaangusha chini au kuwatetea wanadamu, lengo letu pekee, kwa hivyo, ni kuutetea Ukweli wa Mungu, na kuufunua wazi ukweli kwamba upinzani haujafanya lolote zaidi kuliko onyesho la

Kukanusha Kwa Uongo. {TN6: 49.1}

Kufunua wazi hili, tunahitaji tu kuita umakini wa msomaji kwa jaribio lao thabiti zaidi, ambalo ni kitovu cha utata wote, na ambalo huonyesha mbinu zao na hali kadhalika nembo ya kupinga kwao. Juhudi hii itaweka wazi kosa lolote, ikiwa ni la Bi. White au wapinzani wake. {TN6: 49.2}

Katika kijitabu kilichochapishwa dhidi ya ufasiri wake wa siku 2300 za Danieli 8:14, mwandishi anasema: {TN6: 49.3}

“Hebu tuzilinganishe taarifa hizi za Bi. White na kuona jinsi zinavyojilinganisha na Biblia au maandiko yaliyotajwa hapo juu: Kwanza maandiko hutuambia kwa uhakika kwamba wakati Yesu alienda mbinguni aliingia

49

penye uwepo wa Mungu na akaketi mkono wake wa kuume. Bi. White anakanusha hili na kusema kwamba Yesu alienda mbinguni akaingia ndani ya chumba cha kwanza cha hekalu na kuhudumu mbele ya pazia lililokuwa mbele ya Mungu kwa karne kumi na nane. Yesu angewezaje kuwa mbele ya Mungu na kwa upande wa mkono wake wa kulia na wakati huo huo aweze kuwa akihudumu mbele yake likiwapo pazia likizuia katikati? Je! haitakuwa bora zaidi kukataa lile Bi. White anasema juu ya swala hili na kulikubali Neno la Mungu? Iwapo tunaipokea taarifa ya Bi. White, hatuna budi kuikataa Biblia? {TN6: 49.4}

“Iwapo taarifa ya Bi. White ni ya kweli kwamba Yesu alihudumu mbele ya Mungu jinsi kuhani alikuwa akihudumu kila siku katika chumba cha kwanza cha hekalu la duniani akiwasilisha mbele ya Mungu damu ya sadaka ya dhambi basi Mungu alikuwa wapi? Je, hakuwa katika chumba cha pili? Je, yeyote anaweza kukataa kwamba alikuwa humo kwa mujibu wa mfano wakati Maandiko yanafundisha kwamba alikuwa akikifunika kiti cha rehema wakati ambapo makuhani walikuwa wakihudumu mbele ya pazia kila siku?” — Siku Elfu Mbili Na Mia Tatu Fundisho La 1844 Limepimwa Na Kupatikana Limepungukiwa uk. 44. {TN6: 50.1}

Baada ya kusikia madai ya mshitaki, hebu sasa tulisikie

Jibu La Mshitakiwa. {TN6: 50.2}

Kama mwandishi wa aya mbili za italiki anajihisi vyema kwamba kiti cha enzi cha Mungu siku zote kimekuwa katika hekalu la mbinguni,

50

kwa hivyo anachukua msimamo kwamba wakati Kristo alipaa Juu, Yeye hangeweza kukaa mkono wa kulia wa Mungu mahali pengine popote isipokuwa katika mahali Patakatifu Mno pa hekalu la mbinguni. Msimamo huu unamwongoza haraka kuhitimisha kwamba Kristo, mara baada ya kupaa Kwake, aliingia ndani ya chumba cha Patakatifu Mno na humo akaketi chini kwa mkono wa kuume wa Mungu, badala ya kwamba mara Yeye alipaa mara moja hadi kwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Baba Yake mahali pengine mbinguni, jinsi maandiko ya Bi. White yanavyoelezea. {TN6: 50.3}

Iwapo ni ukweli kwamba kiti cha enzi cha Mungu kimekuwa siku zote katika hekalu, basi, bila shaka, nafasi ya wapinzani wa Bi. White itathibitishwa, na kosa linapaswa kuwekwa wazi. Lakini kabla tuwakubali na kumkataa, hebu kwanza tuhakikishe iwapo au la kiti cha Mungu kilikuwa ndani ya hekalu wakati Kristo alipaa juu. Kwa umbali huu, tunaitisha umakini kwa viti viwili vya enzi kila kimoja mahali tofauti. {TN6: 51.1}

“Baada ya hayo naliona,” asema Yohana, “na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, Nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na Mmoja ameketi juu ya kile kiti.” {TN6:51.2}

“Na Yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana

51

mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. {TN6: 51.3}

“Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikuwa zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. {TN6: 52.1}

“Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote…. Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu.” Ufu. 4:1-6; 5:6, 11. {TN6: 52.2}

Vikiwa ni vya katika Hekalu tu, mwana-kondoo kana kwamba amechinjwa na taa saba kwa hivyo vinaonyesha kwamba Yohana alipewa kimbele tukio la kinabii ambalo lingetukia katika hekalu juu, wakati “mlango” hapo ungejisukuma “kufunguka.” Zaidi ya hayo, kwa kuwa kiti cha enzi kiliwekwa katika patakatifu baada ya mlango kufunguka, hapo hakikuwahi

52

kuwapo kiti chochote kabla. Vivyo hivyo baada ya kupaa Kwake Kristo hakuketi kwa kiti cha enzi kilicho ndani ya hekalu, upande wa mkono wa kuume wa Baba, ila bali kwa kile cha “mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima.” Ufu. 22:1, 2. {TN6: 52.3}

Kumbuka, mbele ya kiti cha enzi cha hekalu ipo “bahari ya kioo,” na mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na Mwana-Kondoo upo “mto…wa Uzima.” Sasa, mtu mpumbavu atajaribu kueleza kwamba hivi viti vya enzi viwili (kimoja cha Ufunuo 22:1, 2 na kingine cha Ufunuo 4 na 5) ni kimoja na sawa, au ya kwamba Kristo, baada ya kupaa Kwake, aliketi kwa kiti cha enzi katika hekalu. {TN6: 53.1}

Katika uhusiano na kiti cha mwisho, yanasalia kujibiwa maswali mawili:

Je, Ni Lini Mlango Ulifunguliwa? Je, Ni Lini Viti Vya Enzi Viliwekwa? {TN6: 53.2}

Tumeona tayari kwamba katika wakati wa Yohana mlango ulikuwa bado haujafunguliwa na ya kwamba kiti cha enzi hakikuwa kimewekwa. Ijapokuwa matukio haya hayakufanyika wakati huo, lazima yatukie kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema, kwa maana Mwana-Kondoo “kana kwamba amechinjwa” aliletwa hapo ili afanye upatanisho kwa ajili ya mdhambi — kazi ambayo haiwezi kufanyika baada ya kufungwa kwa muda wa rehema . {TN6: 53.3}

Ni ukweli kwa hivyo kwamba haswa hiki

53

kiti cha enzi kingewekwa baada ya wakati wa Yohana na kabla ya muda wa rehema kufungwa, basi iwapo hakikuwekwa mwaka wa 1844 B.K., jinsi Bi. White alivyotangaza kwamba kiliwekwa, wapinzani wake tafadhali watuambie ni lini kiliwekwa? Wakati tunaposubiri jibu, msomaji anaweza kuangalia

Lengo la Kuweka Kiti Cha Enzi. {TN6: 53.4}

Maelezo ya Yohana ya kiti hiki haswa, ambacho kukizunguka ulikuwa umati wa malaika, Mwana-Kondoo, wazee, wanyama, na kinara cha taa, hukubali tu hitimisho moja kwamba ni kiti cha enzi cha hukumu. Ni mpangilio sawia wa mahakama ambao pia ulionyeshwa kwa Danieli: {TN6: 54.1}

“Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi Yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa Chake kama sufu safi; kiti Chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu Zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa…. Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu mbele Yake.” Dan. 7:9, 10, 13. {TN6: 54.2}

Kwa kusoma aya ya 8, mwanafunzi ataona kwamba kiti cha enzi ambacho Danieli aliona, kiliwekwa baada ya utawala wa pembe ya kutesa

54

(ambayo ilikuwa na “macho kama ya mwanadamu, na kinywa cha kunena makuu” — Dan. 7:8, sehemu ya mwisho) kufanya kazi yake ya uovu. Maneno, “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa” (kuwekwa kwa ajili ya matumizi), huonyesha kwamba viti vya enzi havikuwapo hapo kabla; tena kushinikza hitimisho kwamba karne nyingi baada ya kupaa kwa Kristo, viti hivi vya enzi “viliwekwa,” “hukumu ikaanza, na vitabu vikafunguliwa.” {TN6: 54.3}

Aya ya 13 ya Danieli 7 na aya ya 6 ya Ufunuo 5 huonyesha kwamba “Mmoja kama Mwana wa Adamu” yu mbele ya kiti cha hukumu, kana kwamba mwana-kondoo aliyechinjwa, tayari kufanya upatanisho kwa ajili ya wadhambi. Baada ya kufungwa kwa muda wa rehema, hata hivyo, Yeye hawezi kuwa tena kama Mwokozi wa kusamehe dhambi, ila hatimaye ni kama “MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA, Na upanga mkali hutoka kinywani Mwake ili awapige mataifa kwa huo.” Ufu. 19:16, 15. Na zaidi kupitia Danieli, Roho anaelelezea kwamba wakati, si kabla, ya hukumu, “Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie Yeye: [na kwamba] ufalme Wake ni ufalme wa milele, ambao hautapita kamwe, na ufalme Wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.” Dan. 7:14. {TN6: 55.1}

Maandiko huweka wazi kwamba akiwa bado hekaluni, Kristo anaupokea Ufalme baada ya “viti vya enzi [kuwekwa],” na

55

baada ya hukumu ya upelelezi kukamilika — kabla ya ujio Wake wa pili. Kwamba hivi ndivyo ilivyo, inaonyeshwa zaidi kwa mfano wa Luka 19:15, ambao unasema kwamba Kristo anaupokea ufalme, na kwamba baadaye Yeye nakuja kuwaua adui Zake. {TN6: 55.2}

Danieli 7:22 huonyesha kwamba “hukumu” walipewa watakatifu wake Aliye Juu na kwamba baada ya hukumu, wataumiliki Ufalme. Ambapo hukumu kuu ya waovu wote — ya wale ambao hawakuamka katika “ufufuo wa kwanza” (Ufu. 20:5, 6) — itafanyika baadaye, wakati waovu wamo katika makaburi yao, kwa maana, anasema Yohana: “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufu. 20:12. {TN6: 56.1}

Baada ya hukumu hii, “bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Ufu. 20:13. Na “iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” Ufu. 20:15. “… Hii ndiyo mauti ya pili.” Ufu. 20:14.

56

Kwa sababu zipo hukumu mbili, kila moja kwa wakati tofauti na tabaka, na ufufuo wa aina mbili wa miaka elfu mmoja kutoka kwa mwingine (Ufu. 20:5), kwa hivyo vipo

Viti Vya Enzi Viwili Tofauti — Kimoja Cha Utawala Na Kimoja Cha Hukumu. {TN6: 56.2}

Kiti cha enzi cha utawala kiko penye chanzo cha “mto…wa Uzima” (Ufu. 22:1, 2), katika Paradiso; kiti cha hukumu, penye chanzo cha mto wa moto (Dan. 7:10), “bahari ya kioo” (Ufu. 4:6) “iliyochangamana na moto” (Ufu. 15:2), katika hekalu. Cha mwisho hakikuwa kimewekwa hadi miaka baada ya kupaa kwa Kristo, hupinga uwezekano kwamba ndicho ambacho Yeye aliketi juu yake mkono wa kulia wa Mungu. Vile vile, baada ya kupaa Kwake, Kristo lazima awe Aliketi juu ya kiti cha enzi kilicho penye chanzo cha mto wa uzima — hali ambayo hukipatia hicho kiti jina la heshima, “kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo.” Kutoka kwa hiki kiti cha enzi cha utawala Baba aliinuka, na katika gari la moto (Isaya 6:1) aliingia katika Patakatifu pa Patakatifu ndani ya pazia ambapo mto wa moto, bahari ya kioo, ipo, na hapo akaketi kwa kiti cha enzi (Ufu. 4:2). Baada ya hilo, Kristo pia aliinuka kutoka kwa hicho kiti cha enzi na, katika “gari la mawingu, na magurudumu kama miali ya moto, akizungukwa na malaika,” akaletwa, si kwa mkono wa kuume wa Mungu, ila “karibu mbele Yake” (Dan. 7:13) — kwa

57

kiti cha hukumu pale ambapo Yeye alikuwa ndani ya hekalu. Hivyo ndivyo tukio kuu lilivyoadhimishwa mwaka wa 1844, wakati sherehe ya mahakama ilitukia. (Somo hili limefafanuliwa zaidi katika Trakti yetu Namba 3, Hukumu na Mavuno.) {TN6: 57.1}

Hapa zipo kweli rahisi za matukio haya ya kinabii, na yeye ambaye anashuku ukweli wake dhahiri baadaye ataungama kosa lake, lakini labda bila azma, kwa maana hatimaye litaweza kuwa milele limechelewa sana kumfaidisha, ingawa ataungama “kwa makini na machozi. {TN6: 58.1}

Sasa, sababu kwamba kiti cha enzi cha Mungu hakijakuwa daima katika hekalu la mbinguni na ya kwamba hakitakuwa siku zote humo, ni kwa ufupi kwamba hekalu lilijengwa tu kwa ajili ya kuondoa dhambi, jinsi mmoja anavyoweza kutambua kwa urahisi kupitia huduma za lile la duniani. Akitazama mbele kwa wakati ambapo hakutakuwa na dhambi tena, Yohana anasema: “Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.” Ufu. 21:22, 23. {TN6: 58.2}

Kwa mnyororo wa kweli hapa zilizounganishwa, “fundisho la 1844,” badala ya “kupimwa na kupatikana pungufu,” sasa linasimama zaidi, thabiti, na la uhakika zaidi kuliko wakati wowote, likionyesha

58

kwamba kama mafuta juu ya maji, mafunuo yaliyovuviwa siku zote huinuka juu ya nadharia za kibinafsi, nadharia hizo zikizama na kwa umbali zikiingia kwa usahaulifu. (Kwa kujifunza zaidi Ufunuo 4 na 5, Hukumu, soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 187-201.) {TN6: 58.3}

Ndugu zangu, msiwe kama Wayahudi wa zamani, waliokasirika dhidi ya Ukweli, wakaichukia nuru yake angavu, ila msifu Mungu kwa kuwapa fursa nyingine ya kufanya matengenezo wakati muda wa rehema ungalipo. Na ingawa ungamo la kujihisi moyoni laweza kushusha kiburi cha maoni ya mmoja, bado linaweza kuboresha tabia yake na kumfanya Mungu amukweze “kwa wakati wake” (1 Petro 5:6) kwa uzima wa milele. Ikiwa upinzani wa kibinafsi kwa ujumbe ulitokana tu na kutofahamu maana na kutokuelewa, pasipo kuchangiwa na maslahi ya kibinafsi ila kwa tumaini la dhamira safi tu la kuepuka uongo, hakuna hukumu itakayowekwa kwa shtaka la mtu: ila tu kama mtu kwa ukaidi aendelee kuukataa ushahidi, hukumu itakuwa juu yake. Kukunjua kwa gombo la kinabii kutawafunulia wote ni “roho ya namna gani” (Watendakazi wa Injili, uk. 302) walio nayo — iwapo wako radhi kubadilisha uongo kwa ajili ya ukweli, au iwapo wameazimu kujitambulisha na kundi ambalo litakapatikana milele

Likipiga Vita Ukweli Kwa Ujinga. {TN6: 59.1}

Wapinzani wa ukweli, wakipuuza Uvuvio

59

na kushindwa kulipatia swala hilo wazo la uangalifu, kwa kawaida waliongozwa kulikataa fundisho la siku 2300; kwanza, kwa udhuru kwamba William Miller alitangaza ujio wa Bwana duniani badala ya kuja Kwake kwa hukumu; na pili, kwa sababu ya kuwa na chuki dhidi ya Uvuvio wa Dada White. Lakini vile mahusiano ya kidini ya Miller yalikuwa maarufu, Mungu hangeweza kuwa amewaacha watu Wake kupapasa na kujikwaa gizani kuhusu kazi yake. Njema au mbaya, hiyo, pia, kama ya Dada White, sharti ipatikane katika “neno la unabii lililo imara.” 2 Pet. 1:19. Hivyo umakini wetu sasa unaitwa kwa

Zekaria Sura Ya Kwanza. {TN6: 59.2}

“Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe. Ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, ni nini hawa? Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Nitakuonyesha ni nini hawa. Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, Hawa ndio Bwana aliowatuma, waende huko na huko duniani. Nao wakamjibu yule malaika wa Bwana aliyesimama kati ya mihadasi, wakasema, Tumekwenda huko na huko duniani, na tazama, dunia yote inatulia, nayo imestarehe.” Zek. 1:8-11. {TN6: 60.1}

60

[Picha: Zekaria Sura ya 1]

61

“Kondoo wawili” na “ng’ombe mke mchanga” (Isa. 7) ni, kama ilivyoonyeshwa tayari, wanatoa ugavi tele wa maziwa zaidi ya tunavyoweza kusambaza haraka. Hivyo katika somo linalofuata la Zekaria 1, tunalazimika tu kama vile tulipokuwa tunajifunza Isaya 7, pia katika lile la Zekaria 4, kugawa tu “siagi” (krimu) na kuyahifadhi maziwa. {TN6: 62.1}

Katika maono ya Zekaria 1, tunakumbuka kwamba “farasi” “ambao Bwana alikuwa amewatuma kutembea huku na huko duniani,” wanacho kipawa cha kunena, kwa maana “walimjibu malaika wa Bwana…na kusema, Tumekwenda huko na huko duniani.” Umuhimu wazi unaoletwa kwa mfano huu ni kwamba hawa “farasi” wanaweza kuzungumza na ya kwamba wanamtumikia Bwana kwenda kule ambapo Yeye huwatuma. Wao kwa hivyo wanaweza kuwa mfano tu wa watumwa wa Bwana, ukasisi ambao “hutumwa.” {TN6: 62.2}

Bila shaka, basi, huo mfano huonyesha Vuguvugu ambalo hukwenda mbele na ujumbe na, baada ya kumaliza kazi yake ya “kwenda huko na huko duniani,” hurudi. {TN6: 62.3}

Bila kugongana na busara, mtu hawezi kudhani kwamba mfano huu ni maelezo ya kinabii ya watendakazi wa injili ambao wanaonyeshwa kimbele katika unabii wa Kristo kwamba “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Mat. 24:14. Maana baada ya hao farasi

62

kujibu “Tumekwenda huko na huko duniani” — maana yake, “Tumeimaliza kazi yetu,” — Bwana anawaamuru “Kupiga kelele tena;” yaani, tangaza tena! Na amri hii zaidi ya hayo, huonyesha kwamba Bwana alikuwa bado atawapa rehema Yake watu Wake, na bado hajaimaliza kazi Yake ya wokovu, kwa maana husema: “Miji Yangu…itaenezwa huko na huko tena; Naye Bwana ataufariji Zayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena.” Zek. 1:17. {TN6: 62.4}

Lazima, kwa hivyo, wale “farasi” hapa kwa mtazamo huonyesha Vuguvugu njiani, ambalo limeandaliwa kutangaza injili duniani kote. Jibu la farasi, “Tumekwenda huko na huko duniani, na tazama, dunia yote imetulia, nayo imestarehe,” huonyesha kwamba vuguvugu lilifikiri kazi yake imekamilika na upelelezi umefungwa. Kwa maneno mengine, lilidhani kwamba wokovu kupitia injili ulikuwa umefungwa na ya kwamba kuutangaza hakungeweza tena kuifanya dunia kuzalisha waongofu. (Somo la mfano huo kuwa ni uzalishaji wa maisha ya kiroho, ni lazima huita wokovu wa nafsi si kwa ajili ya uzalishaji wa maisha ya maboga au wanyama.) Ilhali, kwa kweli, Bwana aliwaagiza ‘kupiga kelele tena,’ kuwaonyesha kwamba walikuwa wamekosea. {TN6: 63.1}

Kubainisha iwapo unabii huu wa mfano unawalenga watumwa wa Mungu wa zamani, wa sasa, au wa siku zijazo, mtu lazima aichunguze historia ya kanisa. Kurasa zake za kumbukumbu

63

kwamba Vuguvugu la Miller ndilo la pekee ambalo limekwenda na ujumbe kwa kila misheni ya Kikristo duniani (Pambano Kuu, uk. 368), na kufikiri, kimakosa, kwamba kwa kufanya hivyo, mwaliko wa injili wa mwisho ulikuwa umetangazwa kwa kila kiumbe hai chini ya mbingu, na hivyo kuashiria kufungwa kwa upelelezi wa wanadamu. Kinyume chake, mwaliko wa injili kwa wakati huu, badala ya kuwa ulimalizika wakati huo, ulikuwa ndio umeanza tu, na badala ya Bwana kuja duniani wakati huo, Yeye aliingia ndani ya hekalu Lake la mbinguni! {TN6: 63.2}

Mkusanyiko maalum wa hali zilizolizingira Vuguvugu la Miller kabla ya 1844, zinathibitisha kwamba ndilo lililoonyeshwa katika mfano wa Zekaria 1. Na inapaswa ikumbukwe kwamba Bwana kwa upande mmoja hakuambatisha onyo, “Angalia , kwa maana farasi hawa ni manabii wa uongo (wamekosea),” au kwa upande mwingine kuwakemea farasi au kuwaamuru wanyamaze kimya, ila kwamba badala yake Yeye aliwaamuru wapige kelele zaidi. Na malaika wa Bwana, kwa kuthibitisha, anatangaza: “Hawa ndio ambao Bwana ametuma.” {TN6: 64.1}

Yohana Mbatizaji alihubiri kwamba Kristo angeuanzisha ufalme halisi wakati wa ujio Wake wa kwanza, na ingawa Yohana alikuwa amekosea, Bwana alinena kumhusu: “Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.” Mat. 11:11. Na kwa mtazamo wa nuru ambayo sasa inang’aa kutoka kwa Maandiko, mtu yeyote anaweza

64

kutazama kwamba wale ambao wanaendelea kulia “Mbwa mwitu! mbwa mwitu!” katika dhihaka kwa fundisho la siku 2300, ni, kwa kujua au bila kujua, wanafanya kazi dhidi ya Mungu kwa kujaribu kunyamazisha sauti Yake. Wanafanya kaazi yake yeye ambaye anajaribu kuuficha ukweli kwamba ijayo baada ya vuguvugu la Miller lazima litangaze injili

Kwa Wengi Lakini Si Kwa Wote. {TN6: 64.2}

Waufunuo pia alipokuwa amepewa maono ya mavuguvugu haya mawili (yaliyonakiliwa katika sura ya 10 na 11), tunauelekeza umakini wa msomaji kwa “kitabu kidogo” ambacho aliulizwa kukila. Katika “kinywa chake” kilikuwa kitamu kama asali, lakini “tumboni” mwake kilikuwa kichungu sana. Uzoefu huu wa msisimko, katika maono, ya utabiri wa utamu wa kimbele kubadilika kuwa kuvunjika moyo kwa uchungu, hutabiri hasa uzoefu wa mwaka 1844 wa watu wa Mungu. Tumaini lao tamu na lenye kutumia muda wote kabisa katika ahadi ya Bwana, “Nitakuja tena niwakaribishe Kwangu; ili nilipo Mimi, nanyi mwepo.” (Yoh. 14:3), lilikuwa linatarajiwa kuwa uhalisi, ambapo, badala yake, lilibadilika kuwa kuvunjika moyo kwa kuchungu. {TN6: 65.1}

Kufuatia uzoefu huu wa utamu-uchungu, yakaja kutimia maneno ya malaika: “Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.” Ufu. 10:11. {TN6: 65.2}

Hapa, pia, kama vile katika unabii wa Zekaria, Vuguvugu lingetoa “unabii tena” au “kupiga kelele tena”; yaani, kurudia utume wake, kuonyesha kwamba upelelezi haukuwa umefungwa. {TN6: 65.3}

65

Hivyo kwa mamlaka ya maandiko haya, vuguvugu hilo tena, baada ya kuvunjika moyo, litangaze injili, si kwa “wote,” lakini tu kwa “wengi.” Kwa hivyo, dhehebu la Waadventista wa Sabato katika utume wake wa mwaka 1844, ilikuwa litoe “unabii” (kufundisha), si kwa “yote,” ila tu kwa mataifa “mengi.” Kwa hivyo, hatimaye ni lazima, lipokee utume mwingine, ule wa kwenda kwa “mataifa yote.” {TN6: 66.1}

Upo, kwa hivyo, ujumbe mwingine; utajiunga kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu, jinsi ulivyoelezwa na Roho ya Unabii: {TN6: 66.2}

“Kisha nikamuona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake…. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao kama vile kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga na ujumbe wa malaika wa pili mwaka wa 1844.” — Maandishi ya Awali, uk. 277. {TN6: 66.3}

“Wakati nuru inakwenda kuiangaza nchi,” inasema Roho ya Unabii, mintarafu kanisa linavyoupokea ujumbe, na katika njia ambayo Bwana atafanya kazi, “badala ya kuja kwa msaada wa Bwana, watataka kuifunga kazi Yake ili iafikiane na mawazo yao finyu. Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna iliyo kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango

66

wowote wa wanadamu. Watakuwapo wale kati yetu siku zote watakaotaka kuthibiti kazi ya Mungu, kulazimisha hata hatua gani zitafanyika wakati kazi inakwenda mbele chini ya uongozi wa malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua mamlaka mikononi Mwake. Watendakazi watashangazwa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kuileta na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {TN6: 66.4}

Kuligeukia tena “neno la unabii lililo imara,” katika kutafuta agizo kwa mataifa yote, tunapata pia kwamba

Kabla Injili Kwenda Kwa Mataifa Yote, Mchinjo Mkubwa Unatukia. {TN6: 67.1}

“Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.” Isa. 66:16. {TN6: 67.2}

Hapa tunaona haswa jambo hilo — mchinjo mkubwa; ya kwamba na Bwana Mwenyewe. Ila kile ambacho kwa kawaida kinachomhusu msomaji kukijua sana ni wapi na ni lini maangamizi haya yatatukia. Aya ya 19 na 20 zinasema kwamba wale ambao wataokoka mchinjo, Bwana atawatuma kwa mataifa yote ambayo bado hayajawahi kuisikia “habari” Yake, wala kuuona “utukufu” Wake. {TN6: 67.3}

Kutoka kwa utume hadi kwa vuguvugu kuu la umishonari duniani kote ambalo hapa linaletwa kwa mtazamo, na ambalo lazima litukie kabla kufungwa kwa muda wa rehema, mchinjo unaonekana wazi kuwa umetekelezwa kabla “habari njema ya ufalme

67

kuhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo…mwisho kuja.” Mat. 24:14. “Nao [wale waliokoka] watawaleta ndugu zenu wote kuwa sadaka kwa Bwana, kutoka kwa mataifa yote…nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:20. {TN6: 67.4}

Kumbuka kwamba wale ambao wanaokoka mchinjo ni wale wanaozivuna hizi nafsi. Mchinjo, kwa hivyo, ni kuangamizwa kwa “magugu” ambayo yamo miongoni mwa watu wa Mungu — kanisa. Lingepaswa kuwa la wapagani (wale walio nje ya kanisa), basi wale ambao wanaokoka wangepaswa kuwa wapagani wenyewe. Na hivi hawangeweza ama kuutangaza utukufu Wake na habari Yake au kuwaleta ndugu zao wote katika nyumba ya Bwana. Wala halingekuwapo taifa lolote ambalo wale waliookoka wangeweza kwenda! {TN6: 68 .1}

Unganisha pamoja na hili ukweli kwamba wale ambao wanaokoka mchinjo ndio wale wataenda kwa mataifa yote na kuwaleta ndugu zao wote (wote ambao wataokolewa) ndani ya nyumba ya Bwana, na unapata msururu wa ushahidi imara kwamba huu uangamizaji unatukia tu kabla ya injili kuingia katika furiko lake la mwisho duniani kote. {TN6: 68.2}

Ingawa mada hii inayoshughulisha imeangaziwa kwa ufupi hapa ndani, bado kwa ufasaha, uuwiano, na mantiki, ukweli wake unasimama wa kipekee kwa nyingine yoyote. Inatoa muhtasari wa unabii wa historia ya kanisa kutoka wakati wa Miller hadi siku ya sasa, ikionyesha ufunguzi na

68

kufungwa kwa kila Vuguvugu, pia kazi na hatima yake: yaani, kosa lililoathiri Vuguvugu la Miller (kuelewa utakaso wa “hekalu” kuwa lile la duniani); Utume uliowekewa mpaka wa Vuguvugu la Waadventista wa Sabato (kuagizwa kwenda, si kwa mataifa “yote”, ila kwa “mengi”); utakaso wake (kuyaondoa magugu kati yake); kulizindua kama jipya, lililotakaswa, vuguvugu, likiwasilisha kanisa la Kristo linalostahili jina Lake la heri kwa mara ya kwanza tangu siku za mitume. Mwishowe nuru kwa ulimwengu wote, linaitangaza injili kwa kilio kikuu “kuwa ushuhuda kwa mataifa yote:” kisha unakuja ukomo — mwisho usioweza kuepukwa (Mat. 24:14). {TN6: 68.3}

Picha hii ya ufunuo mseto wa kazi ya injili na watendakazi, iliyochangiwa na manabii, inafunua kanisa ambalo huzishika “amri za Mungu” lililo na “ushuhuda wa Yesu Kristo.” Likiwa “limevikwa silaha za haki ya Kristo,… ‘zuri kama mwezi, safi kama jua, la kutisha kama jeshi lenye mabango,… likienda mbele duniani kote, likishinda na kushinda.’ — Manabii na Wafalme, uk. 725. {TN6: 69.1}

Kwa upande mmoja, nuru ya Ukweli wa Sasa inaliwezesha jicho kuona kazi zote ya William Miller na ile ya Dada White zikiwa zimekita mizizi kwa kina katika “neno la unabii lililo imara.” Kwa upande mwingine, umetandazwa wazi umaskini wa kiroho na uchi

69

wa wakosoaji wao. Sauti ya Bwana pia inasikika kunena dhidi yao: “Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; Sikusema nao, lakini walitabiri.” Yer. 23:21. {TN6: 69.2}

Macho ya Bwana, yakichungulia kila mahali duniani kote, hayakushindwa kuwaona kimbele watendakazi hawa ambao hawakuitwa ambao, licha ya onyo Lake zito linalovuma mbali na karibu kwamba “siku iliyo kuu ya kuogofya ya Bwana” i hapa, wamo katika uasi wa upofu kujaribu kuzima sauti ya Ukweli wakiukabili kwa kilio chao cha “amani na usalama.” Basi, ndugu zangu, tugeuze masikio yetu kutoka kwa umati wa sauti zisizo na Roho Mtakatifu, na tutii kwa bidii

Rai Ya Mwisho Ya Bwana. {TN6: 70.1}

“Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana. Daima huwaambia wao wanaonidharau, Bwana amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote. Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la Bwana, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno Langu, na kulisikia?” Yer. 23:16-18. {TN6: 70.2}

“Tazama,” anajibu Bwana Mwenyewe, “tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu Yake, imetokea;

70

hasira ya Bwana haitarudi, hata Atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo Wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa. Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; Sikusema nao, lakini walitabiri. Lakini kama wangalisimama katika baraza Yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu Wangu maneno Yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.” Yer. 23:19-22. {TN6: 70.3}

Dhahiri ni kwamba upinzani umezalishwa na kukuzwa na viongozi waliojiteua ambao hawajaazimu kuweka dai kwa “uvuvio” wako hapo bila kujua wakipiga kelele kwamba Bwana hajawatuma! Hata hivyo wao au wafuasi wao hawatambui aidha kinaya au upumbavu wa nafasi yao! Hivyo basi “wahubiri wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala!” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337. {TN6: 71.1}

Wanapojipata uso kwa uso aidha na “pigo lifurikalo” (Isa. 28:18) la kujiliwa kwa mwisho kwa “ghadhabu ya Mungu” (Ufu. 15:1), watatumbuliwa kwa msiba wa kutambua hawafai kitu . Kile ambacho sasa kwa umbali kinaonekana kwao, kama mazigazi, bahari ya neema, hatimaye bila kuepukwa kitawatumbukiza katika uangamizi wa kina — milele! {TN6: 71.2}

“Maana Bwana atasimama kama vile katika mlima Perazimu, Yeye ataghadhibika kama vile katika bonde

71

la Gibeoni; apate kufanya kazi Yake, kazi Yake ya ajabu; na kulitimiza tendo Lake, tendo Lake la ajabu. {TN6: 71.3}

“Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, Bwana wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia. Tegeni masikio, sikieni sauti Yangu, sikilizeni mkasikie neno Langu.” (Isa 28:21-23), lisije tumaini lako la neema liwe “kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Zayuni.” {TN6: 72.1}

“Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo. Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji. Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri; kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.” Isa. 29:8-12. {TN6: 72.2}

“Wanaume na wanawake wako katika masaa ya mwisho

72

ya muda wa rehema, na bado ni wasiojali na wapumbavu, na wachungaji hawana nguvu ya kuwaamsha; wao wenyewe wamelala. Wahubiri wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala!” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337. {TN6: 72.3}

“Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa…kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {TN6: 73.1}

Ndugu zangu, kwa sababu Bwana anawapenda ninyi, na kwa sababu anachukia kuwafanya chombo cha aibu, Yeye anawaelekezea trakti hii. Sisi, pia, ni wagonjwa wa moyo kwamba, kama Wayahudi wa zamani, mmejihusisha kwa undani katika vita dhidi ya Roho ya Unabii — vita ambavyo hamwezi kushinda. Kwa kukataa jumbe zilizotumwa kutoka mbinguni, kwa kupuuza shauri la hekima la Gamalieli mwalimu (Mdo. 5:34-39), na bila kukoma kujaribu kuunga mkono kwa maandiko ufasiri wenu wa kutiliwa shaka wa Biblia, kama wavunja Sabato katika kuepuka ukweli wa Sabato , mnaufuata mkondo ambao, iwapo mutauendeleza utawaongoza kufanya dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. {TN6: 73.2}

Badala ya kupaza sauti zenu dhidi ya ukweli, zipaze katika sifa za huo na za Bwana, kwa maana Yeye amehesabu makosa yenu kwa kutoujua ukweli. Iwapo mtarejea Kwake kwa onyo hili la mwisho, Atawapokea kwa furaha na kuwaamuru watumwa Wake kuwavika “vazi” Lake bora

73

(Haki ya Kristo — Isa. 52:1), kuweka “pete” kwa kidole chako (ushahidi wa ukuu wako — Esta 3:12; 8:2; Mwa. 41:42, 43), kukuvika “viatu” miguuni mwako (kukuandaa kwa ajili ya kuitangaza Injili — Efe. 6:15) na kisha “kumleta hapa ndama aliyenona” (kuwakaribisha nyumbani katika nyumba Yake — Ufalme — kusherehekea “karamu ya jioni ya harusi ya Mwana-Kondoo” — Luka 15:23; Ufu. 19:9)! {TN6: 73.3}

Lakini ingawa maombi yetu tunayatoa kwa ajili yenu, hayatakuwa na manufaa iwapo mnaendelea kukaidi maagizo ya onyo na kusihi kwa Roho vile vile na uthibitisho wenu wenyewe, na kuzidi kukataa au kupuuza kuyapata maarifa kamili ya kweli za Biblia kwa wakati huu. {TN6: 74.1}

(Wale wanaotaka kujifunza zaidi Ufunuo 11, wanaweza kupata nakala bila malipo za Trakti zetu Namba 5, Onyo la Mwisho, na Namba 2, Utata wa Onyo, ambazo zimerundika ushahidi wa kina kwamba haya Mavuguvugu matatu yanapatikana katika unabii.) {TN6: 74.2}

Ndugu zangu, “amka, uangaze, maana nuru imekuja” Isa. 60:1. “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani!” Anayesema, “Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. Tembea katika nuru, na usiwaruhusu wale ambao daima wanahoji na kukosoa kila kitu ambacho hawana sehemu, kuhatarisha

74

thawabu yako ya milele kwa maswali yao ya ubatili, kama

Vipi Juu Ya Fundisho La Wanawake? {TN6: 74.3}

Wanapoletwa uso kwa uso na ukweli, wengine hutenda kama watu ambao wamepoteza fikra zao. Kama samaki kudakia chambo, wao kwa ujinga huruka kwa hitimisho. Na wakati wanapowekwa huru kutoka kwa ndoano na kupewa fursa ya kuishi, badala ya kuziacha sera zao za uroho, ubinafsi, na kujizuia wasinaswe tena, wanakimbilia chambo kingine, kwa kujipata tu wenyewe wamenaswa tena na tena. Wanapogundua kwamba mara kwa mara wamejiweka katika aibu, wao hata baadaye hawafanyi azimio kupata usahihi na kukaa sahihi. {TN6: 75.1}

Wale ambao hujikuta wamebanwa pembeni na kukatwa kabisa na kila mwanya wa kuukimbia ukweli, badala ya kuzilalimisha dhana zao za uongo, hufanya juhudi za kukwepa kutoka katika tatizo lao, kwa njia ya kubadili-badili na kutenganisha maandiko: “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.” 1 Kor. 14:34. {TN6: 75.2}

Njia hii, hata hivyo, hutoa tu chembe kali zaidi kwa ukweli kwamba kamwe si sawa mtu yeyote kudhania msimamo kwa swala, juu ya uzito wa maoni yaliyotolewa tu kwa aya moja au mbili, bila kwanza kuzingatia aya zote kwa nuru ya sura nzima,

75

naam, hata za Biblia yote; kwa maana kama ufasiri wa mtu kwa Maandiko hautegemezwi na kila sentensi ya Maandiko Matakatifu, ni ufasiri wa udanganyifu, hitimisho la upofu, bila msingi wa Biblia. {TN6: 75.3}

Katika 1 Wakorintho 14, tunapata kwamba wengi wa wanawake walikuwa wenda “wazimu” (aya ya 23) wakinena zaidi kwa lugha zisizojulikana. Hivyo Paulo anajaribu kuondoa mchafuko huo, si kumnyamazisha mtu yeyote aliye na ujumbe uliovuviwa kuuwasilisha. Jaribio la kuwazuia wanawake kuacha kufundisha haliwezi kuuwiana na maandiko yafuatayo: {TN6: 76.1}

“Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue. Waamuzi 4:4, 5. “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya ubikira wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.” Luka 2:36, 37. Pia “Hulda, nabii mke, mkewe Shalumu” alifundisha Israeli (2 Fal. 22:14-16). Na “Filipo, mhubiri … alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri.” Mdo. 21:8, 9. {TN6: 76.2}

Kwa hivyo wale ambao hufikiri kwamba Paulo humkataza mwanamke kufundisha, si hata kidogo

76

wanadharau na kutokuwa na imani kwa ofisi ya Bi. White, ila badala yake bila kufahamu wanatupia shutuma maandishi ya Paulo — wakijaribu kuyaleta katika mgogoro dhahiri na maandishi ya waandishi wenza wa Maandiko. {TN6: 76.3}

Wale ambao hujifunza kwa uangalifu watajifunza kutodakia ndoano zilizo na chambo, ila badala yake kwa unyenyekevu watajiwasilisha kwa mafundisho ya Roho wa Kristo iwapo wanatarajia Yeye awaokoe kutoka kwa laana ya dhambi na ghadhabu ya Mungu. {TN6: 77.1}

(Kuhusu matokeo ya kuwakataa manabii wa Mungu hasa wakati huu, jifunze Trakti yetu Namba 4, Habari Za Hivi Punde kwa Mama, toleo la 1941, uk. 53, 54.) {TN6: 77.2}

Kama vile katika mahubiri siku ya Pentekoste, Roho alihojiana na Wayahudi, kuwaokoa kutoka kwa uharibifu wa milele, vivyo hivyo katika kurasa hizi Yeye anahojiana nanyi, ndugu zangu. Kimsingi Yeye aliwaambia: “Kama vile Daudi alitabiri juu ya Mmoja Ambaye hangeona uharibifu, haingewezekana kwamba unabii wake ulimhusu yeye mwenyewe, mnavyodhani, maana kaburi lake liko kwetu hata leo. Mungu amemfufua Mmoja [Kristo] wala mwili Wake haukuona uharibifu” (Mdo. 2:22-32); kwa hivyo ni lazima Yeye ndiye pekee ambaye unabii wa Daudi unamhusu. {TN6: 77.3}

Hoja za Petro kwamba unabii wa Daudi unahusu ufufuo wa Kristo, hauna ushahidi wowote wazi wa kuutegemeza zaidi kuliko

77

Trakti hii inavyofanya kuonyesha kwamba maandishi ya Bi. White, pamoja na yale yaliyofunuliwa hapa, ni Roho ya Unabii — “ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 19:10. Kwa hivyo iwapo nyinyi pia mtaufuata mwenendo wa aibu ambao hao Wayahudi waovu waliufuata, je! hatia yenu itakuwa ndogo kuliko yao? Mbona, basi, kutenda hivyo sasa ili mshiriki katika hatia hiyo? Mbona badala yake sasa hivi msifanye chaguo bora, na kumruhusu Roho wa Mungu ayaweke maneno sawa vinywani mwenu jinsi Yeye alivyoyaweka vinywani mwa Wayahudi wachache waliotubu, ambao kwa kicho waliuliza, “Tutendeje, ndugu zetu?” Mdo. 2:37. {TN6: 77.4}

Msiwe kama “wadhani kunishawishi” Agrippa. Usiende kinyume cha usadikisho wako, alivyofanya Feliki, kusema: “Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.” (Mdo. 26:28; 24:25), kwa maana Bwana asema: “Leo,kama mtaisikia sauti Yake, Msifanye migumu mioyo yenu.” Ebr. 4:7. {TN6: 78.1}

Sasa, ndugu, mnajua vyema kwamba hamjaweza kupinga sehemu yoyote ya Fimbo ya Mchungaji. Kwa nini, basi, mwendelee kwa ukosoaji wenu katika “kukunjua kwa ukweli,” hadi mwishowe mjikute wenyewe hamwezi kujiondoa kati ya kundi ambalo kazi zao za uovu zilitabiriwa na kunakiliwa na Uvuvio: {TN6: 78.2}

“Watahoji na kukosoa kila kitu ambacho kinainuka katika kukunjua kwa ukweli, watakosoa kazi na msimamo wa wengine, kukosoa kila tawi la kazi ambayo

78

hawana sehemu. Watajilisha makosa na kasoro na mapungufu ya wengine, ‘hadi,’ akasema malaika, ‘Bwana Yesu atainuka kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, na Kujivika mavazi ya kisasi, na kuwashangaza kwa karamu yao isiyo takatifu; na watajikuta hawajajiandaa kwa karamu ya jioni harusi ya Mwana-Kondoo.’ Ladha yao imepotoshwa sana hivi kwamba wangeweza kudiriki kuishutumu hata meza ya Bwana katika Ufalme Wake.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690. {TN6: 78.3}

Hivyo swala lote sasa, hebu watakatifu wasikie na watii

Hitimisho. {TN6: 79.1}

Katika ukamilifu wa nuru ambayo huenea katika kurasa hizi, msomaji anapaswa kuona, kama katika uangavu wa adhuhuri, kwamba Roho ya Unabii iliyo hai siku zote, pekee inaweza kukabiliana na machafuko katika dunia leo, matokeo ya nyingi “pepo za mafundisho.” {TN6: 79.2}

“Angalieni,” lasema Neno, “nitawatumia Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.” Mtamsikiliza yeye. “Na juu ya kila mlima mrefu, na juu ya kila kilima kilichoinuka, itakuwapo mito na vijito vya maji, katika siku ya machinjo makuu itakapoanguka minara.” “Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira Yake, kwa moshi

79

mwingi sana unaopaa juu; midomo Yake imejaa ghadhabu, na ulimi Wake ni moto ulao; na pumzi Yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu,” “kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.” Mal 4:5; Isa. 30:25, 27, 28; 2 Thes. 2:10. {TN6: 79.3}

Hapa umeonekana kwamba unabii na fasiri zake sahihi “wafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu aweze kuwa mkamilifu.” 2 Tim. 3:16, 17. {TN6: 80.1}

Kwa hivyo, wandugu, tatueni mara moja na milele, kwamba kwa msaada wa Bwana hamtachukuliwa tena na pepo za mafundisho ambayo yamebuniwa na kuendeshwa na roho ya uovu, si kwa Roho wa Kweli, ila kwamba mtatafuta daima, na kusimama na, Neno la Mungu Lililovuviwa — “ushuhuda wa Yesu,” ulioletwa kwenu na “Roho ya Unabii” (Ufu. 12:17; 19:10); ya kwamba mta “isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.” Mika 6:9. {TN6: 80.2}

(Italiki Zote Ni Zetu)

80

FAHARISI YA MAANDIKO

FAHARISI YA ROHO YA UNABII

VIELELEZO

“…Roho wa Kweli, amekuja, Yeye atawaongoza awatie kwenye Kweli yote; kwa maana Hatanena kwa shauri Lake Mwenyewe, lakini yote Atakayoyasikia Atayanena, na mambo yajayo Atawapasha habari yake.”

>