fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 29, 30

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 29, 30

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

AMRI YA UKWELI DUNIANI NDIO AMRI MBINGUNI

UHUISHO NA MATENGENEZO YATIWA TAJI KWA UTAKASO

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Tegemeo Letu Ni Kwa Mungu

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo katika Mifano,” uk. 63, kuanzia aya ya kwanza: {2TG29: 2.1}

“Mfano wa mbegu hufichua kwamba Mungu yu kazini katika maumbile. Mbegu yenyewe ndani yake ina kanuni ya kuota, kanuni ambayo Mungu Mwenyewe ameiweka; lakini iwapo ikiachwa yenyewe mbegu hiyo haitaweza kuwa na uwezo wa kuota. Mwanadamu anayo sehemu yake ya kutenda katika kuendeleza ukuaji wa ile mbegu. Yeye lazima atayarishe na kuirutubisha ardhi na kupanda ndani yake mbegu. Lazima alilime shamba. Lakini ipo hatua ambayo yeye hawezi kutekeleza chochote. Hakuna nguvu au hekima ya mwanadamu inayowe-za kutokeza kwa mbegu mmea hai. Acha mwanadamu afanye juhudi zake hadi kwa kikomo anachoweza, bado lazima amtegemee Yule ambaye ameunganisha upanzi na uvunaji kwa viunganishi vya ajabu vya uwezo Wake wote.” {2TG29: 2.2}

Tutapiga magoti na kuomba kwa ajili ya hekima, ustadi, na uamuzi mwema katika kupanda mbegu za Ukweli, ili tujue kwamba zaidi ya hili hatuwezi kufanya chochote. Yule Mwenye Uwezo wote ambaye ndani Yake tun-aishi na kwenda na kuwa na uwepo wetu atafanya mengine. {2TG29: 2.3}

2

AMRI YA UKWELI DUNIANI NDIO AMRI MBINGUNI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 28, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko letu liko katika sura ya kumi na sita ya Mathayo. Nitaanza na aya ya 13 na ya 14. {2TG29: 3.1}

Mat. 16:13, 14 — “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi Wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni Nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.”

Hapa Yesu anauliza swali muhimu: Je! Watu wanafikiri Mimi ni nani? Jibu Alilopewa hufunua ujinga wa wa-tu, kwa maana inaonekana kwamba wangalikuwa wamejua kwamba Kristo asingaliweza kuwa Yohana Mbat-izaji; bila shaka wangalikuwa wamejua kwamba Yohana alikuwa Amemubatiza mwanzoni mwa huduma Yake. Isitoshe, Yesu alikuwa akihubiri hata kabla ya Yohana kukatwa kichwa. {2TG29: 3.2}

Aya ya 15, 16 — “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni Nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Aliye Hai.”

Wanafunzi wenyewe walionekana hawakuwa na uhakika Yesu alikuwa ni nani. Petro pekee yake bila kusitasi-ta akajibu, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu Aliye Hai.” {2TG29: 3.3}

3

Aya ya 17 — “Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu haviku-kufunulia hili, bali Baba Yangu aliye mbinguni.”

Petro alipokea baraka kwa sababu yeye ndiye yule ambaye Baba alikuwa amemfunulia Mwanae, kwa sababu alikuwa ameshawishiwa na Roho wa ile Kweli takatifu, na kwa sababu alitamka Ukweli kwa uhuru. Baada ya kujaaliwa zawadi hii kwa sifa yake, Petro aliambiwa: {2TG29: 4.1}

Aya ya 18 — “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu Nitalijenga kanisa Langu; wala malango ya kuzimu haitalishinda.”

Maneno “wewe” na “juu” yanafahamisha vitu viwili — Petro na ukweli alioutamka. Jina “Petro” kwa Kiyunani humaanisha “jiwe.” Na hivyo lile Yesu alikuwa akisema sio kumtaja mtu huyo, ila badala yake kumwambia kwamba alichaguliwa kuwa mmojawapo wa mawe katika jengo la kiroho — kanisa. Lakini “juu ya mwamba huu [sio juu ya jiwe] nitalijenga kanisa Langu,” Yesu alitangaza. Juu ya mwamba gani? — Bila shaka juu ya mwamba thabiti wa Ukweli, ukweli ambao Petro alinena — ukweli kwamba Yesu Kristo ni “Mwana wa Mungu.” {2TG29: 4.2}

Kisha Yesu alifanya ijulikane kwamba malango ya kuzimu hayawezi kuushinda ukweli, kwamba malango hayawezi kuwaweka kuzimu (kaburini) hata wafu katika Kristo, kwamba wao, pia, watakuwa sehemu ya kanisa lililo hai milele. kanisa, kanisa ambalo husimama juu ya Mwamba thabiti wa Ukweli. {2TG29: 4.3}

Aya ya 19 — “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

4

Yesu hapa hutangaza kwamba Petro amekuwa kielelezo, mfano, wa wale wote ambao hutangaza kweli zilizo-funuliwa na Mungu. Kwa hao, kama kwa Petro, wamepewa funguo za Ufalme; yaani, watangazaji wa Ukweli Uliovuviwa wamepewa mamlaka kufunga na kufungua kwa uwezo wa Ukweli. Kile wanachofunga duniani kinatambuliwa hivyo mbinguni. Eliya alifunga kwamba iweze kuwapo njaa kwa miaka mitatu na nusu, na hivyo ikawa. Alisema yeye, “kwa Ahabu… hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.” 1 Wafalme 17: 1. {2TG29: 5.1}

Aya ya 20 — “Ndipo alipowakataza sana wanafunzi Wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba Yeye ndiyeYesu Kristo.”

Kwa sababu watu hawakujua kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliye hai, Yesu alitambua kwamba ku-waambia kiurahisi hivyo, kungaliwafanya wawe na chuki zaidi. Yeye, kwa hivyo, aliwaagiza mitume wafanye kama vile ambayo sisi leo tunaagizwa kufanya. Bila kusema kiurahisi: “Tunayo Kweli, ujumbe wa Saa ya Kumi na Moja.” Badala yake tunapaswa kufundisha kweli za Bibilia zilizofunuliwa na Mungu, na hivyo kuwapa wasikilizaji wetu fursa ya kufanya mahitimisho yao, kufanya maamuzi yao wenyewe. Iwapo wao ni watafuta Ukweli wa kweli, Baba Mwenyewe ataufunua mioyoni mwao kwamba huu ndio ujumbe wa Saa ya Kumi na Moja. {2TG29: 5.2}

Hatupaswi kwa hivyo kusema waziwazi Ukweli wote muhimu wa Mungu. Lazima tutumie uamuzi mzuri na busara. Lazima tupande mbegu katika udongo ulioandaliwa vizuri iwapo tunatarajia baraka ya Mungu, ikiwa tunatarajia mvua Yake na mwangaza wa jua na kusababisha iote na kuzaa matunda. Iwapo ile mbegu haija-pandwa kwa kina kabisa, mmea utanyauka jua linapochomoza; iwapo tutatupa tu mbegu juu ya ardhi, ndege wa-tainyakua. {2TG29: 5.3}

5

Aya ya 21-23 — “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonyesha wanafunzi Wake ya kwamba Imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro Akamchukua, akaanza Kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayataku-pata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma Yangu, Shetani; u kikwazo Kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Hapa umetukuzwa ukweli uliosemwa hapo awali. Kufunga au kufungua kwa Petro duniani kutakubaliwa Mbinguni tu wakati kunafanywa kupitia Ukweli uliofunuliwa na Mungu. Wakati akizungumza kutoka kwa msi-simko na hisia zake mwenyewe, Petro alikemewa vikali, na akaambiwa wazi kwamba mapendekezo yake haya-kuwa Ukweli, lakini yalichochewa na Shetani. Kwa hivyo ni wazi kwamba wafuasi wa Kristo wanaweza tu kufunga au kufungua kwa funguo za Ukweli. Wanapaswa kugundua kwamba Ukweli pekee ndio hufungua wa-zi malango ya Mbinguni. {2TG29: 5.4}

Mwishowe, ikiwa tunao Ukweli wa Mbingu wa saa hii, jinsi Petro alivyokuwa nao katika siku yake, sisi basi tunazo funguo za Mbingu na tunaweza kwazo kufunga au kufungua — Maamuzi ya Ukweli duniani ni maamuzi katika Mbingu. {2TG29: 5.5}

Aya ya 24 — “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, Mtu ye yote akitaka Kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, Anifuate.”

Aya hii inamaanisha kwamba shauku ya Petro ilikuwa zaidi kwa ajili ya maisha yake kuliko maisha ya Yesu, kwa maana Petro alijua kwamba iwapo Yesu angaliuawa, basi maisha yake yangaliweza kuwa hatarini. Kwa hivyo Petro aliambiwa kwamba iwapo mtu yeyote angemfuata Yesu, yeye, pia, angekubali kwa hiari kuubeba msalaba wake ikiwa Ukweli unaamuru hivyo. Wale

6

Mitume, tunaambiwa walifanya jambo lilo hilo, na walikuwa waaminifu hata kufa. {2TG29: 6.1}

Aya ya 25-27 — “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake ataipoteza: na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili Yangu ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba Yake pamoja na malaika Zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.”

Wafuasi wa Kristo hapa wameambiwa wasiepuke amri ya Ukweli ingawa watahitajika kuyasalimisha maisha yao wenyewe, kwa kuyapoteza hivyo maisha yao hakika watakuwa wanayaokoa kwa ajili ya umilele — wa-taamka katika ufufuo wa wenye haki. Lakini wao kuuacha Ukweli ili kuwapendeza maadui wa Ukweli, na hivyo kuyaokoa maisha yao ya muda hatimaye kungetokeza tokeo la wao kufa kifo ambacho hakuna ufufuo. {2TG29: 7.1}

Inapaswa kuwa shauku kujua iwapo mtume Petro alikuwa wa kwanza kupewa funguo za Mbinguni, au ikiwa wengine walikuwa na Funguo hizo kabla yake. Kwa sababu Ukweli wa Sasa uliokabithiwa mtu binafsi ni Fun-guo za Mbinguni, na maadamu fundisho lake hufunga na kufungua mambo duniani na hivyo kuidhinishwa Mbinguni, basi lazima wengine walikuwa na hizo funguo kabla ya kupitishwa kwa Petro, kwa maana dunia, ka-nisa, na Ukweli uliofunuliwa na Mbingu vilikuwepo kabla ya wakati wa Petro. {2TG29: 7.2}

Chukua kwa mfano Nuhu. Alitangaza kwamba ingaliweza kuwapo gharika, kwamba kila kitu nje ya safina ambayo alikuwa akijenga kingeweza kuangamia, na kwamba kila kitu ambacho kingeiingia ndani kingeweza kuishi. Basi ukweli kwamba Mbingu ilituma gharika mara baada ya Nuhu

7

kuhubiri habari zake ni uthibitisho ndani yake wenyewe kwamba kile ambacho Nuhu alifunga duniani kili-fungwa Mbinguni pia. Petro, wewe, unaona, hakuwa wa kwanza kupewa Funguo za Mbinguni. {2TG29: 7.3}

Baada ya Nuhu, tutaona kwamba Funguo zilipitishwa hadi kwa Abrahamu: kwa sababu kile ambacho kilipaswa kufungwa au kufunguliwa duniani ilibidi kifungwe au kufunguliwa Mbinguni, wajumbe watatu kuto-ka mbinguni walishauriana na Abrahamu kuhusu kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora. Kisha likawekwa agano kwamba iwapo wawepo watu kumi wenye haki katika mji ambao Lutu aliishi wasiuangamize. Na ndivyo ilivyokuwa. Kwa busara, baada ya Abrahamu zile funguo zilipaswa kuwa zilipitishwa hadi kwa Isaka: Isaka ali-amua kwamba Yakobo anapaswa kupokea baraka zilizoahidiwa ingawa kwa haki ya mzaliwa wa kwanza zingekuwa za Esau. Na licha ya ukweli kwamba Yakobo alipata baraka zilizoahidiwa kwa udanganyifu, Mbingu bado iliidhinisha kile ambacho Isaka alifunga duniani — Yakobo akawa babu wa Kristo. {2TG29: 8.1}

Hivyo ni kwamba kupitia uzao wa Yakobo alikuja Bwana, na hivyo ni kwamba wazawa wa Yakobo waliirithi Nchi ya Ahadi. Akiwa mmiliki wa funguo za Ufalme wa Mbinguni, Yakobo kwa saa za mwisho za kufunga maisha yake aliamuru kwamba haki ya mzaliwa wa kwanza Manase ipewe Efraimu; kwa hili Yusufu aliteta kwa kujaribu kumshawishi baba yake aweke mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Manase (Mwa. 48:17-19), lakini kile Yakobo alifunga duniani kilifungwa Mbinguni, kwa miaka baadaye, baada ya kifo cha Sulemani. Ka-bila la Efraimu, sio la Manase, lilitawala ufalme wa Israeli. Tunaona, basi, kwamba kile Yakobo alifunga duniani pia kilifungwa Mbinguni. {2TG29: 8.2}

Sambamba na Yakobo, Yusufu kwa kuifasiri ndoto ya Farao alifunga kwamba

8

itakuwapo miaka saba ya wingi, na miaka saba ya njaa. Hivyo ikawa kwamba amri ya Yusufu ilitekelezwa (ili-fungwa) na Mbingu. {2TG29: 8.3}

Naye Musa akasema, “Kama watu hawa wakifa kifo cha kawaida kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akifanya jambo jipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake, na kuwameza, pamoja na yote walio nayo, nao washuke shimoni wali hai; ndipo mtatambua kwamba watu hawa wamemghadhabisha Bwana.” Hes. 16:29, 30. {2TG29: 9.1}

Amri ya Musa ilifungwa Mbinguni, kwa maana”nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao, na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.” Hes. 16:32. {2TG29: 9.2}

Funguo za Ufalme unaona, zilipitishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kwa kingine — kutoka kwa Mababu hadi kwa Manabii, kwa Mitume, na hadi leo. Kwa mfano, takriban miaka sitini iliyopita mwasisi wa Dhehebu la Waadventista wa Sabato alitangaza kwamba Baraza Kuu halikuwa tena mamlaka ya juu zaidi ya Mbingu duni-ani (Matangazo ya Baraza Kuu, Kikao cha 34, Gombo la 4, Ziada # 1, Aprili 3, 1901, uk. 25, Safu wima. 1 & 2). Na hivyo ilikuwa kwamba wakati ulipofika kwa ujumbe wa ziada (ambao unapeana nguvu na msukumo kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu — “Maandishi ya Awali,” uk. 277) kutangazwa kwa kanisa, haukuja kupitia Baraza Kuu ila kupitia kwa walei. Huu ni uthibitisho hakika kwamba funguo ambazo Petro alipewa zinafanya kazi leo. {2TG29: 9.3}

Kwa udhahiri, basi, funguo za Ufalme wa Mbinguni ziko mikononi mwa wale walio na Ukweli wa siku hii. Kwa sababu hiyo ni wazi kama Mbingu inavyoweza kufanya,

9

Ukweli unasimama kwamba Funguo za Ufalme wa Mbinguni leo zimepita kutoka mikononi mwa Baraza Kuu hadi mikononi mwa Jumuiya Kuu ya Wadaudi Waadventista wa Sabato, amini kama zilivyopita kutoka kwa Sanhedrini hadi kwa Petro katika siku za Ujio wa kwanza wa Kristo. Kwa hivyo ni kwamba amri ya Ukweli du-niani leo ndio amri Mbinguni. {2TG29: 9.4}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo ba-dala ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {2TG29: 10.1}

10

UHUISHO NA MATENGENEZO YATIWA TAJI KWA UTAKASO

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 6, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko la mada yetu alasiri hii ni unabii wa Malaki. Hushughulikia uhuisho na matengenezo ambayo ulim-wengu haujawahi kujua. Isitoshe, ukweli kwamba unabii umeandikwa kwa njia kama hiyo kutumika kwa se-hemu kuwahusu Israeli ya kale, na bado haswa kwa watu katika siku za mwisho, kwa ajili ya wale wanaoikaribia siku kuu na ya kuogofya ya Bwana, unathibitisha kwamba matengenezo yaliyohitajika katika siku za Malaki yanahitajika pia katika siku yetu. {2TG30: 11.1}

Hakuna kitu cha mafumbo sana katika maandishi ya Malaki lakini kile mwanafunzi yeyote wa Bibilia anawe-za kuelewa kwa kukichambua kitabu chenyewe. Kwa hivyo nitakichambua pamoja nanyi sura mbili za mwisho. Mbili za kwanza mnaweza kuzichambua katika mapumziko yenu. Tutaanza na– {2TG30: 11.2}

Mal. 3:1,2 — “Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anaku-ja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.”

Watu wawili wamefunuliwa hapa kutazamwa, mjumbe

11

na Bwana. Mjumbe atatangulia kuja kwa Bwana. Yeye ataitayarisha njia, kisha Bwana ataonekana. Na mjumbe huyu anaweza kuwa nani iwapo sio yule ambaye Bwana humtaja? — Yeye anatangaza, “Angalieni, nitawapele-kea Eliya nabii kabla haijaja siku ile ya Bwana iliyo kuu na ya kuogofya.” Mal. 4: 5. {2TG30: 11.3}

Mjumbe huyu wa agano (wa ahadi), Eliya nabii wa uakisi ataiandaa njia; atayarejesha mambo yote. Anapoen-delea kuitengeneza njia, Bwana atakuja ghafla kwa hekalu Lake, kwa kanisa Lake. Na kazi Yake itakuwa nini? Kuwasafisha au kuwatakasa watu Wake kwa kuwang’oa wadhambi ambao hawajatubu kati yao. Swali: “Ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake?” kwa kicho hutangaza kwamba ingekuwa bora sasa tujishughulishe na tu-fanye kile kinachotakikana tuweze kusimama kabla ya utakaso kuanza. {2TG30: 12.1}

Je! Yeye atamtakasa nani haswa? — Hebu tusome– {2TG30: 12.2}

Aya ya 3 — “Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasa-fisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.”

Walawi, mnajua, walijumuisha kabila ambalo walitoka kwalo ukuhani, wachungaji wa Bwana. Na kwa sababu unabii huu utapata utimilifu wake katika siku yetu, kielezo ki wazi: Walawi, wachungaji wa Bwana katika siku yetu, watatakaswa. Nini basi? {2TG30: 12.3}

Aya ya 4 — “Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele ya Bwana, kama kati-ka

12

siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.”

Aya hii humaanisha kwamba sadaka ambazo tunaleta sasa kwa Bwana hazimpendezi, sio za kupendeza kama zamani. {2TG30: 13.1}

Hapa tunayo ahadi tukufu ya kwamba sio muda mrefu hivyo kutakuwa na ukasisi safi, watu wasafi, — watu wasio na hila katika vinywa vyao, wasio na waa, wala kunyanzi, wala lolote kama hayo. (Efe. 5:27). Wale am-bao hawatafikia kiwango hiki “hawatasimama.” Baada ya hapo hakuna mdhambi atakayesimama kati yao, maa-na “Kwa maana sasa,” asema Bwana, “hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” Isa. 52:1. {2TG30: 13.2}

Utukufu huu wa baadaye ni, zaidi ya hayo, umesisitizwa na Roho ya Unabii katika siku yetu. Hapa ndio huu: {2TG30: 13.3}

“…Wale tu ambao wameyastahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wa-taruhusiwa kutenda sehemu katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka na kuin-gia katika Kilio Kikuu.” — “Mapitio na Kuhubiri,” Novemba 19, 1908. {2TG30: 13.4}

“Tumekuwa na mwelekeo wa kufikiri kwamba pale ambapo hakuna wachungaji waaminifu, hawawezi ku-wapo Wakristo wakweli; lakini hii sivyo. Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji si waaminifu Yeye atachukua usimamizi wa kundi mwenyewe. Mungu hajawahi kamwe kulifanya kundi livitegemee kabisa vyom-bo vya kibinadamu. Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika upepeto mkuu utakaotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha ya kwamba pepeto Lake li mkononi Mwake, naye

13

atausafisha uwanda Wake kabisa.” {2TG30: 13.5}

“Siku zinajongea upesi sana wakati ambapo kutakuwa na kufadhaika sana na machafuko. Shetani, akiwa amevaa mavazi ya malaika, atawadanganya, hata ikiwezekana, wateule. Itakuwapo miungu mingi na mabwana wengi. Kila upepo wa mafundisho utakuwa unavuma. Wale ambao wametoa heshima kubwa kwa ‘sayansi ina-vyoitwa kwa uongo,’ hawatakuwa viongozi baadaye. Wale ambao wameamini katika akili, ustadi, au talanta, hawatasimama baadaye kuwa viongozi wa askari. Hawakufululiza mwendo na nuru. Wale ambao wamejithib-itsha kuwa sio waaminifu baadaye hawatakabidhiwa kundi. Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa kupepetwa, wa mtikiso watafunuliwa waonekane. Wapo sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu.” — “Shuhuda, “ Gombo la 5, uk. 80. {2TG30: 14.1}

Katika wakati wa kupepetwa, wa mtikiso (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80) tutaweza kujua ni wangapi wanaomtumikia Bwana kwa kweli. Wale ambao tunaweza kufikiri wataliongoza kanisa hadi katika Ufalme wanaweza kukosekana, ilhali wengine wasiojulikana kabisa kwetu watazichukua nafasi zao. {2TG30: 14.2}

Zaidi ya hayo, itapatikana kwamba wale ambao daima wanapekecha kwenye akili za walei kwamba ha-watakuwapo wajumbe zaidi watakaotumwa kutoka kwa Mungu, hakuna Ukweli zaidi unaohitajika, na ya kwamba mtu fulani daima anajaribu kuwadanganya; kwamba waweze kujiepusha na kila kitu kisichoafikia idhini ya mchungaji, — wale ambao hufanya hivi ndio wale haswa ambao tayari bila kujua wamewadanganya walei, na wanafanya

14

wawezavyo kuwadumisha wamedanganyika. Ukweli huu, unaona, unasimama juu kama mnara wa taa kwa kili-ma. {2TG30: 14.3}

Jambo la pekee ambalo uangalifu wao wa wasidanganywe utatimiza, isipokuwa waamke, ni kujidumisha wamedanganyika milele na kwa umbali na Ukweli. Hawa hawataweza kusimama Bwana atakapoonekana katika hekalu Lake. Hivyo, uhuisho na matengenezo yaliyoletwa kwa mtazamo katika Malaki ni ya kwanza na ya mwi-sho ya aina yake, na kwa kweli yatatiwa taji kwa utakaso wa Kanisa. Wale ambao hawaamki sasa, kwa hivyo watalala milele. {2TG30: 15.1}

Udanganyifu wa Ulaodekia kutokea ndani haupaswi kuwa habari kwako, kwa maana unajua vyema kwamba Kanisa halijawahi katika kizazi chochote kudanganywa na yeyote ila na ukasisi wake wenyewe, na wale ambao wamekuwa wakitukuzwa sana kama walivyokuwa wana Sanhedrini, wale waliomsulubisha Bwana, wale wali-olidumisha taifa kwa udanganyifu hadi likawa limechelewa sana kupona. Hivi divyo ilivyokuwa wakati huo, kabla ya wakati huo, na ndivyo ambavyo imekuwa tangu zamani, na ndivyo ilivyo sasa. Tulia na ufikirie hili. {2TG30: 15.2}

Hapana, sikuambii jambo jipya. Unajua hili kuwa hivyo, lakini huwa haulifikirii kamwe, na hiyo ndio taabu kuu kwa Dhehebu lote. {2TG30: 15.3}

Kanisa lililotakaswa hata hivyo litashinda na kwenda hadi kwa ushindi. “’Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango, litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — “Manabii na Wafalme, uk. 725. {2TG30: 15.4}

Hebu mara moja na milele tung’amue kwamba Ibilisi ni mwerevu kuliko vile tunavyoweza kuwaza. Yeye hazingatii haswa kile unachoamini mradi kama anaweza kukuweka usijue Ukweli uliofunuliwa. Hivi ndivyo anavyofanya sasa ndani

15

ya Kanisa, akiwatumia watu wenye ushawishi, watu ambao wanaweza kujionyesha, watu ambao ni wajanja, ambao wanajua jinsi ya kunasa imani ya watu, watu ambao kwa urahisi na kwa utulivu wanaweza kuliongoza Kanisa mbali kutoka kwa jumbe za Mungu za leo, ujumbe wa Hukumu kwa Walio Hai — utakaso wa kanisa, ku-patakasa patakatifu. Shetani anafanya kazi nzuri sasa kama alivyofanya wakati wa Kristo. {2TG30: 15.5}

Je! Sio maarifa ya wa unabii wa Malaki, utakaso wa Kanisa, Hukumu kwa Walio Hai, muhimu zaidi kwa Ka-nisa kuliko Hukumu kwa Wafu? Inaonekana kwako kana kwamba unadanganywa na uchambuzi huu wa Bibilia, au inaonekana kwako kana kwamba unahitaji kufanya matengenezo? {2TG30: 16.1}

Sikia, kwa hivyo, kile ambacho Bwana anakaribia kufanya: {2TG30: 16.2}

Aya ya 5 — “Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.”

Hizi ni baadhi tu ya dhambi ndani ya Kanisa ambazo wanadamu wanapendelea. Kunena kuhusu wale wanaoupeleka ujumbe wa leo na hali ya kanisa Uvuvio unasema zaidi: “…Huugua na kuziteza nafsi zao kwa sababu kiburi, tamaa, ubinafsi, na udanganyifu wa karibu kila aina u kanisani. Roho wa Mungu, ambaye hu-chochea kemeo, anakanyagiwa chini ya miguu, ilhali watumwa wa Shetani hushinda. Mungu amedharauliwa, ukweli umefanywa usiokuwa na maana.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, Uk. 210, 211. {2TG30: 16.3}

16

Utapokea alama ya ukombozi ikiwa tu utaugua na kulia dhidi ya machukizo haya yote. Ezek. 9:4-6. {2TG30: 17.1}

Kwenye orodha hii ya dhambi Bwana huitisha umakini kwa zinazofuata, na hutuuliza kutubu: {2TG30: 17.2}

Aya ya 6-9 — “Kwa kuwa mimi, Bwana, Sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo Yangu, wala hamkuyashika. Niru-dieni Mimi, Nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna ga-ni? Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia Mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mmeniibia Mimi, naam, taifa hili lote.”

Aya hizi haziwalaumu washiriki mmoja mmoja wa kanisa kwa kumwibia Bwana, lakini dhehebu lote, “taifa hili lote.” Zaidi ya hayo, utaona kwamba kisa cha Malaki sura ya tatu kinaanza na sura ya pili. Hapo ndipo uta-gundua ya kwamba Bwana huwaambia ukasasi, sio walei, akisema, “…Enyi makuhani, amri hii yawahusu ninyi.” Mal. 2:1. Ni wazi, basi, shida ipo katika ukweli kwamba ingawa walei kama agizo hulipa zaka na kutoa sadaka za uaminifu Mungu bado anaibiwa kwa sababu Dhehebu linazichukua zaka na wakati uo huo linaupiga vita ba-dala ya kuupokea na kutangaza ujumbe Wake wa leo — Hukumu kwa Walio Hai. Fedha Zake hutumiwa ku-wadanganya watu Wake kutoka kwa ukweli Wake badala ya kuwaangazia Nao — kuwadumisha watu Wake gi-zani na udanganyifu, hata kuwazuia wasiuchunguze ujumbe wa saa hii wao wenyewe. Shtaka lililoje! {2TG30: 17.3}

Hapa lipo ambalo Mungu angependa walei wafanye: {2TG30: 17.4}

17

Aya ya 10 — “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba Yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

Ni wapi mtu atafute ghala la Mungu? — popote pale Ukweli wa Mungu wa leo, kutoka popote “chakula kwa wakati unaofaa” hutolewa. {2TG30: 18.1}

Ile taarifa, “Leteni zaka kamili ghalani,” humaanisha kwamba baadhi tayari wanaleta ndani, lakini sio wote. Hii, pamoja na shtaka kwamba taifa lote linamwibia Mungu, inaonyesha wazi kwamba zaka sasa huletwa, sio kwa ghala la Mungu, lakini kwa nyumba nyingine fulani. Kurudia, ghala la Mungu daima limekuwa na daima litakuwa mahali ambapo “ujumbe wa Saa hii” upo, ambapo “Ukweli wa Sasa” upo, nyumba ambayo kutoka nda-ni yake “chakula kwa wakati unaofaa” kinatolewa wakati zaka zanalipwa. {2TG30: 18.2}

Kwa sababu ujumbe kuukuu, “Hukumu kwa Wafu,” umepitwa na wakati kama ulivyo ujumbe wa gharika ya Nuhu, inaonekana wazi kwamba maadamu Dhehebu lote limeukataa na linaupiga vita ujumbe wa saa hii, lakini bado linakusanya zaka za watu, hakika linamwibia Mungu. {2TG30: 18.3}

Watu Wake, kwa hivyo, wanaombwa kutuma zaka zao “ghalani” ambamo unatolewa Ukweli wa Sasa , kwa sababu ni Ukweli wa Sasa ambao kundi linahitaji sasa. “Zipo kweli nyingi za thamani zilizosheni katika neno la Mungu, ila ni ukweli wa sasa ambao kundi linahitaji sasa.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 63. Wale wanaotii wanayo ahadi hii: {2TG30: 18.4}

18

Aya ya 11-12 — “Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.”

Si chini ya maagizo mengine yoyote Yeye huahidi baraka Zake. Una bahati ngumu? Hauwezi kujipatia riziki? Anza kulipa zaka yako. Kumbuka kwa umakini kwamba Mungu haitaji tu zaka bali zaka kamili; yaani zaka, na sadaka ya hiari. Yeye hataki zitumike kwa kitu cha ubunifu wako mwenyewe. Unapaswa kuzileta “ghalani.” “Kuhusu zaka ya kwanza, Bwana alikuwa ametangaza, ‘Nimewapa wana wa Lawi sehemu yote ya kumi katika Israeli.’ Lakini kuihusu ya pili aliamuru, Nawe utakula mbele ya Bwana, Mungu wako, mahali atakapopachagua kuweka jina lake huko, zaka ya nafaka yako, ya divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa ng’ombe wako na wa kondoo wako; ili ujifunze kumcha Bwana Mungu wako kila wakati.’ Zaka hii, au ulingano katika pesa, walikuwa kwa miaka miwili wailete mahali ambapo patakatifu palijengwa. Baada ya sadaka ya shukrani kwa Mungu, na kubainisha mgawo fulani kwa kuhani, watoaji walipaswa kutumia iliyosalia kwa karamu ya kidini, ambayo Mlawi, mgeni, yatima, na mjane wanapaswa kushiriki. Hivyo maandalizi yalifanywa kwa sadaka za shukrani na karamu katika sherehe za kila mwaka, na watu walikaribishwa katika jumuiya ya ma-kuhani na Walawi, ili wapate maagizo na kutiwa moyo katika huduma ya Mungu. {2TG30: 19.1}

“Kila mwaka wa tatu, hata hivyo, zaka hii ya pili ilitumiwa nyumbani, kwa kuwakirimu Walawi na maskini, jinsi Musa alivyosema, ‘Ili waweze kula ndani

19

milango yako, na kushiba.’ Hii zaka inaweza kutoa mfuko wa matumizi ya hisani na ukarimu.” — “Mababu na Manabii, uk. 530. {2TG30: 19.2}

Amri ni, “… wasitokee mbele ya Bwana mikono mitupu.” Kum. 16:16. {2TG30: 20.1}

Mungu hasemi uongo. Yeye hutimiza ahadi Zake. Yeye kamwe hashindwi. Hakuna kitu kinachomuudhi Yeye zaidi kuliko kutoamini na kutokuwa mwaminifu katika Neno Lake. {2TG30: 20.2}

Aya ya 13-15 — “Maneno yenu yamekuwa magumu juu Yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumes-ema maneno juu Yako kwa namna gani? Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo Yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele ya Bwana wa majeshi? Na sasa twase-ma ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.”

Hapa limeonyeshwa hitaji lingine la matengenezo: Sisi kama Dhehebu tunashtakiwa kwa kufikiria kwamba wasiomcha Mungu ni bora kuliko wale humtumikia Mungu. Kabla ya kukata kauli kama hiyo, hebu kila mmoja kwanza ajichunguze na kuona kama anamtumikia Mungu kwa kweli na kwa uaminifu. {2TG30: 20.3}

Aya ya 16, 17 — “Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele Yake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafa-kari jina Lake. Nao watakuwa Wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile Niifanyayo vito Vyangu; nami Nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.”

Iwapo tunapeana kipaumbele kwa Neno la Mungu, ikiwa

20

tunatenda yote Yeye hutuuliza kufanya, tutakuwa watu Wake kweli kweli, “vito” Vyake. Kisha kitabu cha ukumbusho kitaandikwa kutuhusu na matendo yetu mema na ya kishujaa yatasomwa na waliokombolewa milele zote! {2TG30: 20.4}

Aya ya 18 — “Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.”

Sasa hatuwezi kuona tofauti kati yake anayemtumikia Mungu, na yule asiyemtumikia, lakini siku inajongea upesi wakati tofauti hiyo itaonekana kwa wote. {2TG30: 21.1}

Mal. 4:1,4 — “Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi…. Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi Wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.”

Hapa tunaulizwa kuikumbuka sheria ya Musa ambayo Mungu aliamuru kule Horebu — amri kumi, maagizo na hukumu (Kumb. 4:10-14). {2TG30: 21.2}

Aya ya 5,6 — “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuo-gofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili Nisi-je nikaipiga dunia kwa laana.”

Neno “angalieni” huitisha umakini wetu kurejea sura ya 3, aya ya 1, ambapo tunaambiwa kwamba Bwana at-amtuma mjumbe Wake kuitengeneza njia ya Bwana kwa ajili ya Hukumu kwa Walio Hai — kwa utakaso.

21

Bila shaka, mbali na kuitengeneza njia ya Bwana, Eliya, mjumbe wa Bwana, atatangaza kwamba siku kuu na ya kuogofya ya Bwana imekaribia. {2TG30: 21.3}

Kazi ya Eliya wa kale, unajua, ilikuwa kazi ya kufunga kwa ajili ya Israeli ya mfano iliyoasi — Kanisa. Vivyo hivyo kazi ya Eliya wa siku hii lazima iwe kazi ya uakisi ya kufunga kwa hekalu Lake, Kanisa, kabla ya siku kuu na ya kuogofya ya Bwana. (“Shuhuda,” Gombo la 3, uk. 266.) {2TG30: 22.1}

Isitoshe, iwapo Eliya ni mjumbe, atakuwa na ujumbe. Ujumbe wake utakuwa wa kuchunguza moyo, kwa maana ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na mioyo ya watoto iwaelekee baba — kina baba watatamani kuwaona watoto wao wameokolewa, na watoto watatamani kuwaona baba zao wameokolewa. Na uhuisho huu na matengenezo haya kwa kweli yatatiwa taji kwa utakaso wa Kanisa, na Bwana kuwachinja manabii wa uakisi waongo wa leo (Isa. 66:16). “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu: na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Pet. 4:17. “Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake: nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi …. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, kwa Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali, na Yavani, kwa visiwa vilivyo mbali, watu ambao hawajaisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika Mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wotekutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu Mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana, kama wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana

22

katika chombo safi.” Isa. 66:16, 19, 20. {2TG30: 22.2}

Mchinjo huu, unaona, unatukia kabla rehema kufunga kwa sababu waliookoka wanatumwa kwa Mataifa, kukamilisha kazi ya injili — kuwakusanya ndugu zao wote kutoka kati yao. {2TG30: 23.1}

“Kwa hivyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana ikiwa lile neno lili-lonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki; sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii; ambao ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale wali-omsikia Yeye; … Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika raha Yake tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.” Ebr. 2: 1-3; 4: 1. {2TG30: 23.2}

 

Usiyakose Manufaa Juu Ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya suala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {2TG30: 23.3}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 29, 30

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>