15 May Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 19, 20
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 19, 20
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
UBATIZO NA BWANA HAKI YETU — LANGO LA KUINGIA KANISANI
WALAODEKIA WAANGAMIA BILA “UJUMBE KWA WALAODEKIA”
1
ANDIKO LA SALA
Burudani Huleta Mafuriko Ya Majaribu
Andiko letu leo linaanzia kwenye ukurasa wa 54 wa Mafunzo ya Kristo kwa Mifano. {2TG19: 2.1}
“Hata kanisa, ambalo linapaswa kuwa nguzo na msingi wa ukweli, linapatikana likihimiza ubinafsi wa kupen-da burudani. Wakati fedha zinachangwa kwa madhumuni ya kidini, makanisa mengi hutumia njia zipi? — Mina-da, chakula chajio, maonyesho ya kusisimua, hata bahati nasibu, na mbinu kama hizo. Mara nyingi mahali pali-potengwa kwa ibada ya Mungu huchafuliwa kwa karamu ya kula na kunywa, kununua, kuuza, na kujifurahi-sha…. Kufuatilia anasa na burudani kitovu chake ni mijini. Wazazi wengi ambao huchagua makao ya mijini kwa watoto wao, wakifikiria kuwapa manufaa makubwa, hukumbana na kuvunjika moyo, na huwa wamechelewa sana kutubu makosa yao mabaya. Miji ya leo inaendelea upesi kuwa kama Sodoma na Gomora…. Vijana wanafagiliwa mbali kwa mkondo maarufu. Wale ambao hujifunza kupenda anasa kwa ajili yake, kufungua mlango kwa mafuriko ya majaribu…. Wao huongozwa kutoka kwa aina moja ya udanganyifu hadi mwingine, hadi wapoteze hamu na uwezo wa maisha ya manufaa.” {2TG19: 2.2}
Tuombe sasa kwa ajili ya wazazi na watoto, kwa ajili ya Kanisa lenyewe lilikiwa limedidimia sana linahimiza udunia kwa njia zake potovu za kuchanga pesa; Nyumba ya Mungu imetiwa unajisi, na miji imekuwa kama Sodoma na Gomora. Tuombe kwamba sisi kama wazazi na walezi tuendelee kuwa karibu na Bwana na kutafuta msaada wa Kiungu kwa kuwalea watoto katika mpangilio Mungu mwenyewe, kwa maana wokovu wao u hata-rini. {2TG19: 2.3}
2
UBATIZO NA BWANA HAKI YETU — LANGO LA KUINGIA KANISANI
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, DESEMBA 20, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
“Petro akawaambia, Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Mdo. 2:38. {2TG19: 3.1}
Tikiti kwa ajili ya Ubatizo, tunaona, ni toba. Ubatizo kwa hivyo ndilo lango la kuingia Kanisa. Kisha hufuata zawadi ya Roho Mtakatifu. {2TG19: 3.2}
Sasa basi swali linaibuka, Je! Mtu atatubu kwa nini? — Kwa kusema wazi, jibu litakuwa, Tubu kutoka kwe ye dhambi. Hii ni kweli, lakini tutajuaje dhambi ni nini? Sisi wenyewe hatujui, unatangaza Uvuvio: {2TG19: 3.3}
“Mtu mwovu aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana. Kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji kutoka mbingu-ni, wala hairudi huko, bali huinywesha ardhi, na kuizalisha
3
na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, namtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu litokalo katika kinywa Changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale nililolituma.’’ Isa. 55: 7-11. {2TG19: 3.4}
Uvuvio, zaidi ya hayo, unaonyesha kwamba kwa kuyachunguza Maandiko Yesu Mwenyewe alijifunza tofauti kati ya mema na mabaya: {2TG19: 4.1}
“Kwa hivyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara; Tazama, bikira atachukua mimba atamzaa mtoto mwa-namme, naye atamwita jina Lake Imanueli. Siagi na asali Atakula, ili Ajue kukataa mabaya na kuchagua mema.’’ Isa. 7:14, 15. {2TG19: 4.2}
Kwa kweli aya hizi zinatabiri ujio wa kwanza wa Kristo, lakini maandiko pia husema kwamba Kristo alikula chakula chochote halali kilichoandaliwa mbele yake: “maana Yohana alikuja hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo. Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi. Na hekima imejulikana kuwa na haki kwa kazi yake.” Mat. 11:18, 19. {2TG19: 4.3}
Ile Siagi na asali, basi, lazima viwe vya mfano, na vanaweza kuwa mfano wa nini isipokuwa Neno la Mungu, chanzo ambacho Yesu alijifunza kuchagua mema na kukataa mabaya? Ameweka mfano, na Uvuvio unaonya wazi kwamba “kwa maana kila mtu atakayekula siagi na asali atasalia katika nchi hii.” Isa. 7:22. Bila shaka, wale ambao hawali siagi na asli hii ya kiroho wataondolewa njiani, hawatasalia katika nchi. “Ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.” Isa. 24: 6. {2TG19: 4.4}
4
Naam, hata baada ya wenye dhambi kuondolewa katika nchi, wenye haki katika Bwana, wale ambao wameachwa, wataendelea kusoma Neno la Mungu linalodumu. Kwa udhahiri, basi, kwa yeyote kuhitimisha kwamba anaijua tayari Bibilia, kwamba hakuna lililo zaidi kwake yeye kujifunza, kwa hakika ni kukufuru kadri chuo kinapokunjua. {2TG19: 5.1}
Je! Neno linafafanuaje dhambi? — Tunapata jibu katika maandiko yafuatayo: {2TG19: 5.2}
“Kila atendaye dhambi afanya uasi, kwa maana dhambi ni uasi wa sheria. Nanyi mnajua ya kwamba Yeye alidhihirishwa ili aiondoe dhambi; na dhambi haimo ndani Yake. Kila akaaye ndani Yake hatendi dhambi. Kila atendaye dhambi hakumwona Yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu asiwadanganye. Yeye atendaye haki yu na haki, kama Yeye alivyo na haki. Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezali-wa na Mungu hatendi dhambi; kwa sababu uzao wake wakaa ndani Yake; wala hawezi kutenda dhambi, kwa sababu amezaliwa na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao: mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.” 1 Yoh. 3:4-10. {2TG19: 5.3}
“Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye, ikiwa tunazishika amri Zake. Yeye asemaye, Nimemjua, na hazishiki amri Zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye Neno Lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli; katika hili twajua ya kuwa tumo ndani
5
Yake. Yeye asemaye kuwa anakaa ndani Yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama Yeye alivyoenenda.” Yoh. 2:3-6. {2TG19: 5.4}
“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.” Mat. 5:17-21. {2TG19: 6.1}
“Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” Rum. 8:6, 7. {2TG19: 6.2}
“Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapi-ga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini
6
mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Rum. 7:19-25. {2TG19: 6.3}
Kutoka kwa aya hizi za Maandiko unaona kwamba sheria ya amri kumi, sheria ya milele ambayo daima iliku-wapo na daima itakuwapo, ndiyo sheria ambayo hufafanua dhambi, na ambayo humhukumu mtu kuwa ama sawa au mkosaji. Sasa, kwa sababu wanadamu wote wameivunja sheria hii, wote wamehukumiwa kifo cha milele, lakini tunamshukuru Mungu kwamba Yesu alikufa badala yetu na akafufuka tena, na kutufanya tuwe huru kutoka kwa hukumu ya sheria. Naam, kifo na kufufuka Kwake hutufanya sote tuwe huru kwa kifo am-bacho uvunjaji wa sheria huweka. {2TG19: 7.1}
Wote ambao hutubu kwa kuivunja sheria, na kumpokea Yeye kama Mwokozi wao, huinuka kutembea katika upya wa maisha. Maisha ambayo yanapatana na sheria kwa kweli ni haki ya Kristo. Wao, zaidi ya hayo, ha-waendelei kutenda dhambi, wokovu wao umehifadhiwa kwa sababu, anasema mtume Yohana, “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya, ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi, tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.’’ — 1 Yoh. 2:1. Yeye kwa hivyo yeye hawawezi kutenda dhambi, au kudumu katika dhambi. Yeye ni mtakatifu katika Bwana. {2TG19: 7.2}
Mpaka Bwana atakapoturudisha katika nchi yetu, hata hivyo, huko kuibadilisha mioyo yetu na kuandika juu yake sheria Yake (Ezek. 36:24-28), hadi wakati huo pambano ambalo mtume Paulo alijikuta ndani yake — pam-bano la kutii sheria ya Roho ilhali sheria ya mwili i dhidi yake — litakuwa fungu letu. Lakini tunamshukuru Mungu anayetupa nguvu za kushinda siku kwa siku katika Bwana Mwokozi wetu. {2TG19: 7.3}
7
Ingawa tunaanguka mara saba kwa siku, ingawa tunatenda dhambi bila kukusudia, ikiwa tunainuka na kukimbia mbio tutashinda. Hatuwezi kupoteza, kwa sababu tunaye Mtetezi, hata Yesu Kristo, Mwenye haki. Uhakikisho wa wokovu wetu kwa hivyo umethibitishwa. {2TG19: 8.1}
Tokea sasa, anaonya Yohana Mbatizaji, tusiwe kama waandishi na Mafarisayo: “hata alipoona wengi miongo-ni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi uzao wa nyoka, ni nani ali-yewaonya ninyi kuikimbia hasira inayokuja? Basi, zaeni matunda yapasayo toba. Wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.” Mat. 3: 7-9. {2TG19: 8.2}
Hapa unaona kwamba wale ambao wanataka kubatizwa lazima kwanza wajithibitishe kwamba wametubu, wanastahili. Ni lazima ionekane kwamba wameacha dhambi zao, na wanaishi katika upya wa maisha. Hata hivyo, sio lazima wafikirie kwamba Mungu anawahitaji, kwamba Yeye hawezi kutenda bila wao, bali kwamba wao wanamuhitaji Yeye, maana ikiwa lipo hitaji Anaweza kuwaumba watu kutoka kwa mawe. {2TG19: 8.3}
Kuutafuta ubatizo kama njia ya kuokoka jehanamu, sio kitu kipungufu kuliko kuyarudia matendo ya Mafari-sayo. Ubatizo unapaswa kutafutwa kama njia ya kuwa mwana wa Mungu, kuwa mtu wa milele, na asiyekufa. Ubatizo, unaona, ni kuikana dhambi mbele ya umma, na cheti cha ubatizo; pamoja na zawadi ya haki ya Bwana, unafungua wazi mlango wa Kanisa. {2TG19: 8.4}
Ili kuandaa wanafunzi Wake watarajiwa wa kubatizwa, kwanza Yesu alifundisha mambo yaliyoandikwa
8
katika Mathayo, sura ya 5, 6 na 7, mahubiri juu ya mlima. Hata baada ya ubatizo tunapaswa kufanya vyema kuzisoma sura hizi kila mara, tusije tukasahau. {2TG19: 8.5}
Baada ya kupokea inavyostahili ubatizo wa maji tunahitaji kwa subira na kwa imani kungojea ubatizo wa Roho Mtakatifu na wa moto. Ahadi hii, tutaona sasa, wanafunzi waliipokea katika siku ya Pentekoste. {2TG19: 9.1}
“Hata, alipokuwa amekutana nao, aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, Yeye akasema, ambayo mlisikia habari zake Kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji; bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.” Mdo. 1: 4, 5. {2TG19: 9.2}
“Kisha, wakarudi Yerusalemu kutoka mlima uitwao Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu wapata mwendo wa Sabato. Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo, na Tomasi, Bartholomayo, na Mathayo, Yakobo, mwana wa Alfayo, na Simoni Zelote na Yuda ndugu ya Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.” Mdo. 1: 12-14. {2TG19: 9.3}
“Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana kama ndimi za moto, uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama vile Roho alivyowajaalia kutamka.” Mdo. 2: 3, 4. {2TG19: 9.4}
Tangu siku hiyo watu hawajabatizwa kamwe kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Hakika,
9
wasingaliweza, kwa sababu tangu wakati huo hakuna kundi la Wakristo, kanisa, lililowahi kuja kwa umoja wa imani. Bado ipo hata hivyo ahadi ya ubatizo kama huo baada ya “mvua ya vuli, na mvua ya masika” kunyesha juu ya watu wa Mungu, baada ya watu Wake kuufikia ukomavu kamili wa kiroho. {2TG19: 9.5}
“Furahi, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu, kwa kuwa Yeye amewapa mvua ya vuli kwa kipimo chake, Naye atasababisha mvua, mvua ya vuli na mvua ya masika katika mwezi wa kwanza…. Na itakuwa baadaye, kwamba nitaimimina Roho Yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu na binti zenu watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, vijana wenu wataona maono: na pia juu ya hao watumishi na wajakazi, katika siku zile nitamimina Roho Yangu.” Yoeli 2:23, 28, 29. {2TG19: 10.1}
Taarifa, “juu ya wote wenye mwili,” huonyesha kwamba kama watu, bila kumbagua mmoja, wote tena wa-tapokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. {2TG19: 10.2}
Andiko hili linaonyesha, zaidi ya hayo, kwamba udhihirisho wa Roho, katika Pentekoste ya pili, utakuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa awali, kwamba kwa kulinganisha wa awali ulikuwa tu mfano. {2TG19: 10.3}
Hili litakuwa lini? –Litaweza kuwa mara tu Mungu anapoweza kulipata kundi la watu “kuona jicho kwa jicho” (Isa. 52: 8) kwamba yanayoitwa eti matendo yao mema ni matambara machafu tu, na hivyo kuwa wa moyo mmoja. Kundi la pekee kama hili tu katika unabii, mnajua, ni watu 144,000, malimbuko, watumwa wa Mungu ambao watasimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo bila hila vinywani mwao (Ufu. 14: 1, 4, 5). Ili kufanikisha hali takatifu njema Kanisa lazima lipate uzoefu wa uamsho na
10
matengenezo makubwa, mtikiso, kupepetwa, kama vile halijawahi kuona. Naam, iwapo kila mmoja angaliweza kutupilia mbali maoni na dhana zake za kibinafsi, kwa kweli ungeleta uamsho na matengenezo makubwa tangu siku ya Pentekoste. Hili ndilo lazima sasa lifanyike, na litatukia barabara kama vile andiko lifuatalo linafichua: “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba…. Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, am-baye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’’ Ezek. 9: 1, 2, 4-6. {2TG19: 10.4}
“Naliuliza maana ya kupepeta nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi Mwaminifu kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu wa moja kwa moja. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto
12
miongoni mwa watu wa Mungu.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. {2TG19: 11.1}
“Mungu anahitaji uamsho na matengenezo ya kiroho. Isipokuwa haya yafanyike, wale ambao ni vuguvugu wataendelea kukua wa machukizo zaidi kwa Bwana, mpaka Yeye atakataa kuwatambua kama watoto Wake. {2TG19: 12.1}
“Uamsho na matengenezo lazima yafanyike chini ya msaada wa Roho Mtakatifu. Uamsho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uamsho unaashiria upya wa maisha ya kiroho, kuzifanya hai nguvu za akili na moyo, ufufuo kutoka katika kifo cha kiroho. Matengenezo yanaashiria kuwa na mpangilio mpya badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea. Matengenezo hayawezi kuzaa matunda mazuri ya haki isipokuwa ya-meunganishwa na uamsho wa Roho. Uamsho na matengenezo lazima yafanye kazi yake rasmi, na katika kufan-ya kazi hii ni lazima uchangamane.’’’ — Kristo Haki Yetu, uk. 121. {2TG19: 12.2}
Pamoja na kundi kama hili la watendakazi walioletwa nuruni, mada hiyo inakuwa wazi bila shaka. Wanaweza kwa nguvu kuitangaza “Injili ya milele,” injili ya ufalme katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Kati ya wale ambao wanaokoka ule mchinjo (Isa. 66: 16), wale wasio na uongo, asema Bwana: {2TG19: 12.3}
‘’Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu ambao hawajaisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile
12
wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.’’ Isa. 66:19, 20. {2TG19: 12.4}
“Baada ya hayo nikaona, na tazama, umati mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.’’ Ufu. 7: 9. {2TG19: 13.1}
Tusikie sasa jinsi ambavyo Yesu alibatizwa, na lile tunaweza kutarajia baada ya Ubatizo wa maji na kabla ya Ubatizo wa Roho: {2TG19: 13.2}
“Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwa-nangu Mpendwa, Ambaye Ninapendezwa naye.’’ Mat. 3:16, 17. {2TG19: 13.3}
Baada ya kubatizwa kwa kuzamishwa, na mara alipopanda kutoka majini, Yesu aliongozwa mara moja ili kujaribiwa na Ibilisi. {2TG19: 13.4}
“Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha heka-lu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu
13
jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.” Mat. 4: 1-11. {2TG19: 13.5}
Hapa upo mfano wetu. Baada ya ubatizo wa maji, majaribu na ushindi vitakuwa fungu letu, pia. Yesu, unaona, alimkabili Ibilisi na “Bwana asema hivi,” na lile lililoandikwa. Ikiwa hatuwezi kujipendeza na Bibilia kama vile Yeye alivyopendezwa Nayo, iwapo hatuichambui ili kujua lile Yeye angetaka tutende, vipi, basi, tun-aweza kukabiliana na majaribu yetu na kuibuka washindi? Je! Ni ajabu kwamba watu wengi baada ya kubatizwa hupotea kutoka njiani? Jambo hasa ambalo lingewafanya kuwa imara katika imani kadri wanapomwona Mungu akiwapa ushindi mtukufu, wao huogopa, bila kujua kwamba baada ya dhoruba ya mvua na upepo, hapo huja jua na utulivu. Ayubu alijaribiwa mpaka mwisho, lakini alipata ushindi, na baadaye akapokea maradufu kwa ajili ya hasara zake zote. Mbona tusiweze? {2TG19: 14.1}
Baada ya kupata ushindi juu ya jaribu Lake, Yesu hakuwahi tena kutaabishwa na Ibilisi. Na Ayubu na watu wote wakuu wa Mungu kwa ujuzi walipata utulivu kama huo mbali na Shetani. {2TG19: 14.2}
14
Msimamo wetu dhidi ya dhambi, kwa hivyo, lazima uwe dhahiri, bila kuyumbishwa hata kidogo. Sisi, pia, lazima tumwache Ibilisi ajue kwamba hatufanyi mchezo, iwapo tutaweza daima kupata amani. {2TG19: 15.1}
“Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Na hayo tutafanya Mungu akitujalia. Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, hai-wezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.” Ebr. 6: 1-6. Kufanya makusudio ya dhambi, ni kana kwamba mwenyewe ku-lichimba kaburi lako la milele. {2TG19: 15.2}
Sasa, tunataka kujua ni mabatizo mangapi ambayo Biblia hufundisha. “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.” Efe. 4: 4, 5. {2TG19: 15.3}
Naam, ipo aina moja tu ya ubatizo, na mtu anahitaji kubatizwa ila mara moja, iwapo mtu amebatizwa ina-vyostahili. Kwa kweli iwapo mtu ataweza kukengeuka kutoka kwa imani, na kuwa kama alivyokuwa kabla ya kubatizwa, — mpagani — anaweza kuruhusiwa kubatizwa tena iwapo mtu huyo atapata kutubu na kuongoka upya. {2TG19: 15.4}
Kubatizwa tena, hata hivyo, hakuhitajiki iwapo mtu anapiga hatua kwa hatua katika Kweli. Kwa mfano,
15
Waza mtume Paulo angalikuwa ameishi tangu siku ile alipobatizwa hadi leo. Yeye kwa sababu hiyo angalikuwa mshiriki wa makanisa katika Matengenezo, — kwanza wa Kiluteri, halafu wa Presbiteri, wa Methodisti, wa Bap-tisti, wa Adventista, n.k, kwa sababu kufunuliwa kwa Ukweli kungalikuwa kumemwongoza kutoka kwa dhehebu moja hadi kwa lingine. Yeye hata hivyo asingelazimika kubatizwa tena kwa kupanda juu kutoka kwa dhehebu moja hadi kwa lingine pamoja na Ukweli unaokunjua daima. {2TG19: 15.5}
Je! Tunapaswa kubatizwa katika nani? — {2TG19: 16.1}
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.” Mat. 28:19. {2TG19: 16.2}
“Huyu Ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye Kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni Umoja.” 1 Yoh. 5: 6, 7. {2TG19: 16.3}
Tunapobatizwa katika jina (umoja, sio “majina”) la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, tunabatizwa katika Muumbaji wetu, damu, na Ukweli, na hawa watatu ni Umoja. Hivyo tumebatizwa katika “jina,” sio majina, kwa sababu hawa watatu ni umoja — Utatu — Uumbaji, Ukombozi, Ukweli. {2TG19: 16.4}
Watu wengi, hata hivyo, hutenda kama wamebatizwa kwa kanisa, kwa jamii, kwa Paulo au Apolo, kwa mfa-no, lakini sisi kama wana matengenezo na waamini wa Ukweli wa Sasa, lazima tuambatane na Ukweli popote unapoongoza, daima tukikumbuka
16
kwamba tumebatizwa kwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. {2TG19: 16.5}
Iwapo hii sio kweli kutuhusu, basi ni hakika kwamba kamwe hatutaendelea mbele zaidi katika maarifa ya Mungu, Kristo, au Kweli Yake, — la, sio zaidi ya vile tulivyokuwa katika siku tulibatizwa. Wale wanaofanya hili huwa mbilikimo badala ya kuwa wakristo wazima, na kamwe hawaufikii ukamilifu wa kimo cha Kristo, kwa maana wameridhika kuwa jinsi walivyo; huhisi hawahitaji chochote zaidi ya kile walichopata kwa ubatizo; wao hawawezi kusonga kama walivyokuwa makuhani, waandishi, na Mafarisayo katika siku ya Yesu. Mungu ana-kataa kwamba yeyote kati yetu aweze kupoteza hivyo. {2TG19: 17.1}
17
WALAODEKIA WAANGAMIA BILA “UJUMBE KWA WALAODEKIA”
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, DESEMBA 27, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Ufu. 3: 15-17 — “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kin-ywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.”
“Ni udanganyifu mkubwa jinsi gani unaoweza kuja juu ya akili za wanadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, wakati ambapo wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli unawapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ambapo wale wanaohutubiwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu ya kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umasikini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayesema, na ushuhuda wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252-253. {2TG20: 18.1}
Wakati watu ni wanyonge, na wenye mashaka, maskini, vipofu, na uchi kama walivyo Walaodekia, na
18
hawajui, basi jina la pekee ambalo wanaweza kupewa ni “Wamedanganywa,” lakini ingawa hivyo Walaodekia ni watu wanaoogopa sana kudanganywa! Hufikiri wao wenyewe hawahitaji chochote, ingawa Bwana Mwenyewe husema kwamba wanahitaji kila kitu. Wao hufikiri ni matajiri wamejitajirisha kwa bidhaa. Bidhaa gani? –Sio pesa, nina uhakika, kwa sababu huwa tunasikia wakiitisha pesa, hata wakiomba-omba. {2TG20: 18.2}
Ni pamoja na kudhani wanayo Kweli ya Bibilia ya kutosha ndiposa wameridhika. Wanayo imani kwamba wanao Ukweli wote uliofunuliwa wanaohitaji kuwapeleka katika Ufalme. Huu ndio udanganyifu wao mkubwa. Hawalijui hitaji lao kubwa la Ukweli wakati Kanisa linakaribia kuingia katika awamu ya mwisho ya kazi yake. Hawatambui kwamba awamu hii ijayo ya kazi ya Kanisa haiwezi kuendelezwa na awamu yake ya zamani ya Ukweli. Kanisa sasa haliwezi kutenda tena bila ujumbe wa ziada (Maandishi ya Awali, uk. 277) kuliko lin-galivyoweza wakati wa kufungwa kwa enzi ya Agano la Kale kuingia kwenye kipindi cha Ukristo na Ukweli mkongwe wa sherehe za Agano la Kale uliotengwa kwa Injili. {2TG20: 19.1}
Lakini, la kusikitisha kusema, kunena kwa Walaodekia kuhusu Ukweli zaidi kuliko ule walionao tayari ni kujiletea lawama yao kubwa: na wazo kwamba hawahitaji Ukweli zaidi, ya kuwa wanao wote, na ya kwamba mtu fulani anajaribu kuwadanganya, imepekechwa ndani yao kwa undani kama inavyoweza kupekechwa. Hii imewafanya kuwa na chuki na kumtuhumu kila mtu ambaye anathubutu kuwajongea na jambo jipya. Hii ndio huwaweka katika nafasi mbaya kama Wayahudi wa zamani. Dhahiri ni kwamba iwapo Walaodekia wachague hivyo kusalia vuguvugu, wakiwa wameridhika katika udanganyifu wao, watatapikwa nje na milele
19
Kuachwa bila tumaini. {2TG20: 19.2}
Ufu. 3:18 — “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”
Dhahabu iliyojaribiwa kwa moto bila shaka huwakilisha Ukweli uliovuviwa kwa wakati huu, ukweli pekee ambao unaokoa, aina pekee ambayo Mungu angeweza kuuza. Na mavazi meupe yanaweza kuwa nini ambayo Shahidi wa Kweli anawasihi kununua, iwapo si haki ya Kristo? {2TG20: 20.1}
Na mtu lazima afanye nini kuyapata haya? –Tutapata jibu katika– {2TG20: 20.2}
Mika 6: 5 — “Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Ba-laamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya Bwana.”
Hapa tumehimizwa kukumbuka swali la Balaki na jibu la Balaamu iwapo tungetaka kujua haki ya Bwana. Hebu tufungue– {2TG20: 20.3}
Hesabu 24: 17-24 — “Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa Shethi. Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa. Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini. Kisha akamwan-galia Amaleki, akatunga mithali yake,
20
akasema, Makao yako yana nguvu, Na kitundu chako kimewekwa katika jabali. Pamoja na haya Wakeni wa-taangamizwa, Hata Ashuru atakapokuchukua mateka. Akatunga mithali yake akasema, Ole wao! Ni nani ata-kayepona, Mungu atakapofanya haya? Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitam-taabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atafikilia uharibifu.”
Bila shaka huu ni unabii wa Kristo akiwa amechukua “mamlaka mikononi Mwake mwenyewe.” Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. Kama hii ndio Haki Yake ambayo tunahimizwa kuijua. Kunena kwa uthabiti, kuijua haki ya Kristo ni kujua kwa moyo wote kwamba katika siku za mwisho Yeye ataichukua Fimbo ya enzi, ya kwamba Yeye atatawala; kwamba mwanzoni Yeye atazipiga “pembe za Moabu, na kuwaangamiza wana wote wa Shethi’; ya kuwa Edomu na Seiri itakuwa milki ya adui Zake; ya kuwa Israeli watatenda kwa ushujaa; kwamba Yeye atakuwa na ufalme, na kadhalika. Kwa mujibu wa Andiko, hii ndiyo haki yetu ya Kristo iwapo tunaijua. Na yule anayetambua kwamba utawala wa Kristo na ufalme Wake sio kitu kisichoonekana, sio kitu cha kuwaza kinachoelea katika anga, kwa mfano, mahali fulani kuzimuni, bali kitu halisi, halisi kama mmojawapo wa falme za leo, atauliza upesi, kama alivyofanya mtume Paulo, “Unataka nifanye nini Bwana?” Hili tutaliona tena kutoka kwa unabii wa Mika– {2TG20: 21.1}
Mika 6: 6, 7 — “Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na
21
ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?”
Swali hili la watu katika kufunuliwa kwa andiko hili hufichua kile wanachodhani kitampendeza zaidi Bwana. Wanafikiria zawadi ya aina fulani kutoka kwa vitu vya kimwili labda ni zawadi inayokubalika zaidi ambayo wanaweza kutoa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao. Sisi kwa macho yetu kwa kweli huliona jambo hili kote kote makanisani mwetu. Hali hii sawa ilikuwapo katika siku za ujio wa kwanza wa Kristo: Wayahudi walikuwa mahsusi sana kwa kutoa zaka hata kwa kitu kidogo sana cha mapato, kama vile mnanaa, bizari, na jira, lakini waliyaacha “mambo makuu ya sheria, hukumu, rehema, na imani.” Mat. 23:23. Kutoa zaka kwa uaminifu ilikuwa kwa sifa yao, alisema Bwana, lakini kutoa zaka hakufai kuchukua nafasi ya hukumu, rehema, na imani. Jibu hili hili linatujia leo kupitia kwa nabii Mika: {2TG20: 22.1}
Mika 6: 8 — “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako?”
Mara tu baada ya kupata maono ya hitaji kubwa la uamsho na matengenezo, watu wa Mungu wako tayari kufanya karibu kila kitu, hata kuwatoa kafara wazaliwa wao wa kwanza. {2TG20: 22.2}
Kwa habari zaidi Uvuvio unashauri– {2TG20: 22.3}
Aya ya 9 — “… Isikieni hiyo fimbo, na Yeye
22
aliyeiagiza.”
Haya ndio majibu ya Mungu kwa lile swali, “Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele ya Mungu aliye juu?” {2TG20: 23.1}
Kwa sababu tumeulizwa kutenda “kwa haki, na kupenda rehema, na kutembea kwa unyenyekevu na Mungu [wetu],” lazima iwe kwamba sisi kama watu hatuyatekelezi mambo haya, kwamba haupo uaminifu, kutowajali wengine na kiburi. Tunafurahi, hata hivyo, kwamba hatujahukumiwa bila tumaini kwa maovu yetu, lakini kwamba tunaalikwa kuyaacha , kuachana nayo, iwapo tunatarajia kusimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo. {2TG20: 23.2}
Kupitia nabii Ezekieli tunaonyeshwa maeneo tunatumia vibaya zawadi ya rehema na haki: {2TG20: 23.3}
Ezek. 34:21, 22, 31 — “Kwa kuwa mmesukuma kwa ubavu, na kwa mabega, na kuwapiga wenye maradhi kwa pembe zenu, hata mkawatawanyia mbali; basi mimi nitaliokoa kundi langu, wala hawatakuwa mateka tena; nami nitahukumu kati ya mnyama na mnyama….. Na ninyi, kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wana-damu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.”
Wagonjwa, wanyonge, bila shaka ni wale wasio na umaarufu, na kwa sababu moja au nyingine hawawezi kushikilia yaliyo yao. Hawa husukumwa nje kwa pembe na watu wenye nguvu, daraja la wasio haki na wasio na huruma, daraja ambalo hudhibiti kazi. Daraja hili hata hivyo mwishowe litahukumiwa. {2TG20: 23.4}
Ipo njia moja salama tu ya kufuata ikiwa tutaweza kupata kibali kwa Bwana, na njia hiyo imetajwa waziwazi na nabii Isaya: {2TG20: 23.5}
23
Isa. 7:21, 22 — “Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atamlisha ng’ombe mke mchanga na kondoo wawili; kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi atakula siagi: kwa maana kila mtu aliyesalia katika nchi hii atakula siagi na asali.”
Fikiria ng’ombe mmoja na kondoo wawili wakisambaza siagi na asali kwa wote waliosalia katika nchi! Kwa sababu ng’ombe na kondoo wawili halisi hawawezi kufanya hivi, lazima tukubali kwamba ni mfano wa kitu am-bacho sio tu kinaweza kutoa maziwa mengi, lakini pia kinaweza kuhifadhi maisha ya wateja wake. {2TG20: 24.1}
Kuna kitu kimoja ambacho hujumuisha sehemu tatu kama hizi (kondoo wawili na ng’ombe mke mchanga) am-bacho kina uwezo wa kuuweka ulimwengu hai, nacho ni Bibilia — iliyofunuliwa na Roho ya Unabii, Roho ambaye huongoza katika Kweli yote. Kondoo hao wawili, kwa kuwa si wachanga, na wawili wa aina moja, lazima wawe mfano wa Bibilia yenyewe, Maagano yote la Kale na Jipya. Ng’ombe akiwa mchanga na mkubwa kwa ukubwa, bila shaka ni mfano wa kitu cha chimbuko la baadaye, na ni kikubwa kuliko Bibilia yenyewe. Hivyo si kingine isipokuwa kazi zilizochapishwa za Roho ya Unabii inayoishi milele — ufasiri uliovuviwa wa Maandiko. {2TG20: 24.2}
Wale ambao wamesalia katika nchi, kwa hivyo, wakati Kristo anaichukua fimbo Yake kutawala, ni wale ambao huishi kwa siagi na asali ambayo Bibilia na Roho ya Unabii tu inaweza kusambaza. Wengine wote wataangamia pamoja na Waedomu na Wamoabu mamboleo. {2TG20: 24.3}
Katika unabii huo wa mfano tunaonyeshwa
24
kwamba Kristo Mwenyewe alijifunza tofauti kati ya mema na mabaya kwa kuyachambua Maandiko: {2TG20: 24.4}
Isa. 7:14, 15 — “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mto-to mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.”
Hakuna mtu ambaye angekataa, kama ilivyotajwa katika uchambuzi wetu wa juma lililopita, kwamba huu ni un-abii wa ujio wa kwanza wa Kristo. Na kwa vile tunayo kumbukumbu kwamba Lishe Yake haikuwa siagi ya mazi-wa na asali ya nyuki, hakuzuiliwa kama ilivyokuwa ya Yohana Mbatizaji, pia kwa ukweli kwamba hakuna siagi na asali halisi iliyo na uwezeshaji wa kumlazimisha mtu yeyote kuyachagua mema na kukayataa mabaya, yote ya-nathibitisha kwamba “siagi na asali” ni mfano wa Neno la Mungu, kwamba Kristo Mwenyewe alijifunza kutoka kwa Maandiko kuyachagua mema na kuyakataa mabaya. {2TG20: 25.1}
Hapa unaona kwamba mtu anahitaji ugavi wa kila siku wa siagi na asali ya kiroho iwapo ataweza kuyadumisha maisha yake ya kiroho. Yaani, chakula cha jana hakingeweza kuchukua mahali pa chakula cha leo — la, hapana zaidi ya ujumbe uliovuviwa wa Nuhu kwa siku yake, unaweza kuchukua nafasi ya ujumbe uliovuviwa wa Ufalme leo. {2TG20: 25.2}
Ujumbe pekee wa leo uliotumwa na Mbingu unaweza kuwaokoa watu wa leo. Hii ni halisi na kweli na ya busara kama ilivyo kusema kwamba walio hai hawawezi kuhukumiwa na ujumbe wa hukumu ya Wafu. Naam, “heri mtumwa yule… mwaminifu mwenye akili, ambaye Bwana Wake alimweka juu ya nyumba Yake, awape watu
25
chakula kwa wakati wake.” Mat. 24:45, 46. {2TG20: 25.3}
Ili kujua zaidi kwamba tunahitaji kuchambua ili kutambua machukizo ambayo hutuzunguka, na kujua jinsi ya kuyaepuka, nitasoma kutoka katika Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445: {2TG20: 26.1}
“Huku kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu [watu 144,000] ni sawa na kule ilioonyeshwa Ezekieli katika maono. Yohana pia alikuwa shahidi wa ufunuo huu wa kushangaza.” {2TG20: 26.2}
Ezek. 9: 4-6 — “Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wen-gine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msim-karibie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.”
Wakati siku inakaribia kwa ajili andiko hili litimizwe, basi ukweli wake lazima uwe “chakula kwa wakati wake” kwa ajili ya watu wakati huo. Hakuna kingine kinachoweza kuchukua mahali pake. Na hivyo tunaona kwamba kama Ninawi ulinusurika kwa ujumbe ulioletwa kwake, kwa hivyo Walaodekia wanaweza kuokolewa tu kwa “Ujumbe kwa Walaodekia.” {2TG20: 26.3}
Kutoka kwa yafuatayo tunaona kwamba ujumbe kwa Walaodekia ni utazaa matunda, kwamba wengi watajifun-za kuyachagua mema na kuyakataa mabaya: {2TG20: 26.4}
26
“Katika wakati ambapo ghadhabu yake itatokea kwa hukumu, hawa wanyenyekevu, wafuasi waliojitolea wa Kristo watatofautishwa kutoka kwa wengine wote wa ulimwengu kwa uchungu wa roho yao, ambao unaonye-shwa kwa kuugua na kulia, makemeo na maonyo. Ilhali wengine hujaribu kufunika vazi juu ya uovu uliopo, na kuruhusu uovu mkubwa ulioenea kila mahali, wale walio na bidii kwa heshima ya Mungu na upendo kwa watu, hawatanyamaza ili wapate fadhili za yeyote. Nafsi zao zenye haki zinaudhiwa siku baada ya siku kwa matendo na mazungumzo yasiyo matakatifu ya waovu. Hawana uwezo wa kuuzuia mkondo wa bubujiko la uovu, na hivyo wamejawa na huzuni na kamsa. Wanaugua mbele ya Mungu kuona dini imedharauliwa katika nyumba ha-sa za wale ambao wamepata nuru kubwa. Huomboleza na kuitesa mioyo yao kwa sababu kiburi, tamaa, ubinafsi, na udanganyifu wa karibu kila aina u kanisani.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 210. {2TG20: 27.1}
Kwa sababu sasa tunaona wazi kwamba Walaodekia waangamia bila ujumbe kwa Walaodekia, tunapaswa kuushika sana Ukweli wa wakati huu, na kushinda taji yetu ya uzima, na kwa kuongezea hilo tutasifiwa kwa mavuno maridhawa ya nafsi na na pongezi “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu.” Mat. 25:23. {2TG20: 27.2}
27
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 19, 20
Kimechapishwa nchini Marekani
28