fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 09, 10

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 9, 10

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

UWE CHOMBO KIPYA CHA KUPURA MKONONI MWA MUNGU

MACHIPUKIZI YA SHINA, SIO MACHIPUKO

                                    

 

1

WAZO LA SALA

“Udongo–Kando Ya Njia”

Tutasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, kuanzia ukurasa wa 43, aya ya mwisho: {2TG9: 2.1}

“Hilo ambalo mfano wa mpanzi hushughulikia hasa ni athari inayozalishwa kwa ukuaji wa mbegu katika udongo ambao hutupwa ndani yake. Kwa mfano huu Kristo alikuwa ananena ki-uhalisi kwa wasikilizaji Wake, Sio salama kwenu kusimama kama wakosoaji wa kazi Yangu, au kutojizuia kuvunjika moyo kwa sababu hair-idhishi maoni yenu. Swali la umuhimu mkubwa kwenu ni, Je! Mnautendeaje ujumbe Wangu? Juu ya mapokezi yenu au kuukataa hatima yenu ya milele inategemea. {2TG9: 2.2}

“Mbegu iliyopandwa kando ya njia huwakilisha neno la Mungu wakati linapoanguka kwa moyo wa msikilizaji asiye makini…. Akiwa amezama katika malengo ya ubinafsi na kutojizuia uovu, nafsi ‘huwa ngumu kupitia udanganyifu wa dhambi.’ Nguvu za kiroho hupooza. Watu hulisikia neno, lakini hawaelewi. Hawatambui kuwa linawahusu wao. Hawatambui hitaji lao au hatari yao. Hawauhisi upendo wa Kristo, na hupita kwa ujumbe wa neema Yake kama kitu ambacho hakiwahusu.”{2TG9: 2.3}

Tuombe kwamba tusianguke jinsi ya wale ambao siku zote wako tayari kupata makosa na kulaumu, ila kwam-ba tutoe umakini kamili, tukiweka kando kuchukia bila sababu na mawazo yote yaliyoshikiliwa kimbele, yawe ya kibinafsi au ya Dhehebu; kwamba tunafungue mioyo yetu kwa ukweli, sio kwa sababu ni maarufu, bali kwa sababu Biblia huufundisha, tukigundua kwamba kitu chochote pungufu kwa hili hakika kitatuongoza pale kilipowaongoza Wayahudi wa zamani. {2TG9: 2.4}

2

UWE CHOMBO KIPYA CHA KUPURA MKONONI MWA MUNGU

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, OKTOBA 4, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu alasiri hii inapatikana katika Isaya, sura ya 40 na 41. Tutaanza na aya ya kwanza ya sura ya arobaini: {2TG9: 3.1}

Isa. 40: 1, 2 — “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa ku-wa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.”

Uvuvio, tunaona, hapa unamhimiza mtu fulani awafariji watu wa Mungu. Wataambiwa, sio kwamba vita vyao vitakwisha, lakini kwamba vita vyao vimekwisha; ya kwamba wamesamehewa uovu wao; ya kwamba Yerusal-emu, Kanisa, tayari umepokea maradufu kwa dhambi zake zote. {2TG9: 3.2}

Vita hii, kwa kweli, isingaliweza kukwisha katika wakati wa Isaya, wala katika wakati wa Yohana Mbatizaji, –la, sio hata katika Vizazi vya Kati. Habari hizi za kufariji zinaweza kusemwa kwa Kanisa tu baada ya kuo-kolewa kutoka kwa nira ya Mataifa, katika wakati ambao watu wamelipa maradufu kwa dhambi zao kabla na baada ya kutawanywa. Sura hii, kwa hivyo, kwa ujumla inauhusu wakati wa mwisho, wakati wetu. {2TG9: 3.3}

3

Aya ya 3 — “Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, nyosheni jangwani njia kuu ya Bwana Mungu wetu.”

Hii ndio aya ambayo Yohana Mbatizaji alipata kuwa andiko lake kama mjumbe wa kuiandaa njia ya ujio wa kwanza wa Kristo. Lakini kwa sababu tumeona tayari kwamba sura hii inaanza na ujumbe kwa watu wa Mungu ambao wanaishi katika wakati wa mwisho, wakati ambao wamelipa kwa dhambi zao zote, na maadamu wakati wa ukombozi wao umewasili, bila shaka sura hii ina matumizi ya msingi na vile vile ya mwisho: Inahusu ujio wa kwanza na wa pili wa Kristo. La mwisho kwa matumizi haya ni mfano — sauti iliayo nyikani, sio katika shamba la mizabibu, sio katika nchi ya Yuda (Isa. 5: 7), lakini jangwani, katika nchi za Mataifa. {2TG9: 3.4}

Aya ya 4 — “Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima kitashushwa; palipopotoka patanyoshwa, na palipoparuza patazawazishwa.”

Mzigo wa ujumbe utakaotangazwa ni kuwaandaa watu kukutana na Bwana: kusawazisha maeneo yaliyo-inuka, kuyainua yaliyo chini, kuondoa vizuizi vyote, ili njia kuu ya Bwana, njia ya kuja Kwake, isafishwe. Maneno haya, bila shaka, ki-mfano yanasema: Waliokwezwa watanyenyekezwa; wanyenyekevu na wale wali-otupwa nje watainuliwa; makosa yanapaswa kurekebishwa, maana katika himaya ya Mungu usawa na haki lazi-ma ishinde. {2TG9: 4.1}

“Wakati Roho wa Mungu, na nguvu yake ya uamsho ya ajabu, inapoigusa nafsi, hushusha kiburi cha kibinadamu. Anasa ya kidunia na wadhifa na nguvu zinaonekana kuwa hazina maana. Fikira,

4

na kila kitu kinachojiinua dhidi ya ufahamu wa Mungu, hutupwa chini; kila wazo hutekwa na kuletwa ‘kwa utii wa Kristo.’ Halafu unyenyekevu na upendo wa kujinyima, unaothaminiwa kwa uchache kati ya wanadamu, unakwezwa kama wa pekee wa thamani. Hii ndio kazi ya injili, ambayo ujumbe wa Yohana ulikuwa sehemu yake.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 135. {2TG9: 5.1}

Aya ya 5 — “Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; kwa kuwa kin-ywa cha Bwana kimenena haya.”

Hapa tunaambiwa kwamba wakati “uamsho na matengenezo” haya yanatukia, utukufu wa Bwana utafunu-liwa, na wote wenye mwili watauona pamoja. Hebu basi tugundue kwamba ikiwa tutafanya mambo haya sisi sote tutakuwa watangulizi wa ahadi hizi tukufu, na watumwa wa Mungu kwa wakati huu. {2TG9: 5.2}

Aya ya 6-8 — “Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Hakika watu hawa ni majani. Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.”

Ujumbe wa saa hii ni kuonyesha kwamba wanadamu wote ni wafaji, wasiodumu kuliko nyasi; kwamba hata wema wao sio wa kudumu zaidi kuliko maua ya kondeni; lakini ya kwamba Neno la Mungu ni la milele; kwam-ba wale walio na shauku ya kupata uzima wa milele, kuwa wa milele kama Neno Lenyewe, wasiweke imani kwa mtu yeyote, bali kwa Neno la Mungu tu: kwamba waweze kujiulizia, “Je! Ni Kweli?”

5

na sio, “Inakija kupitia kwa nani?” {2TG9: 5.3}

Aya ya 9 — “Ee Zayuni, uletaye habari njema, panda juu ya mlima mrefu; Ee Yerusalemu, uletaye habari njema, Paza sauti yako kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, tazameni Mungu wenu!”

Wale ambao mwishowe watasimama juu ya Mlima Zayuni, na ambao sasa wanaiandaa njia ya Bwana kwa kuzileta habari hizi njema, wote wanashauriwa kupanda juu ya mlima mrefu, kwa mfano, na kupaza sauti zao pamoja bila kuogopa chochote, kuitangazia miji ya Yuda (kwa makanisa kila mahali) kuiandaa njia ya Bwana na kusema, “Tazameni Mungu wenu.” {2TG9: 6.1}

Aya ya 10 – “Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, na mkono wake ndio utakaomtwalia. Tazameni, thawabu yake I pamoja naye, na ijara Yake I mbele Yake.”

Mkono wa Bwana unaomtawalia lazima uwe mfano wa wale ambao kupitia kwao Yeye hufanya kazi (Isa. 51: 9), wa wale ambao watasimama pamoja Naye juu ya Mlima Zayuni (Ufu. 14: 1), — Kanisa lisilo na doa na wala hila. “Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.” Hos. 3: 4, 5. {2TG9: 6.2}

Wajumbe wa saa hii wanapaswa kutangaza, pia, kwamba thawabu ya Bwana (uzima milele) i pamoja Naye, ila kwamba kazi Yake bado i mbele Yake, bado haijakamilika. {2TG9: 6.3}

6

Aya ya 11 — “Atalilisha kundi lake kama mchungaji. Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake, na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza kwa upole.”

Utunzi huu juu ya watu Wake watauhisi wakati mkono Wake utatawala kwa ajili Yake. Kisha Ataisimamia kazi Yake, na ya watu Wake, kama mchungaji anavyolisimamia kundi. Atatekeleza utunzi wa kibinafsi juu ya wote, wakongwe na wachanga sawa. {2TG9: 7.1}

Aya ya 12 — “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?”

Kwa sababu hakuna mwingine isipokuwa Mungu Mwenyewe anayeweza kuyafanya mambo haya yote, na maadamu Yeye Mwenyewe atalisimamia kundi Lake Mwenyewe, tunajua kwamba utunzi Wake juu yao hautal-inganishwa. Na kwa nini tusiweze kuuharakisha wakati huo? {2TG9: 7.2}

Aya ya 13, 14 — “Ni nani aliyemwongoza Roho wa Bwana, na kuwa mshauri wake aliyemfundisha? Ali-fanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya ufahamu?”

Tunajua ya kwamba Roho Anayeongoza kwenye Kweli yote na maarifa yote hajiongozi Mwenyewe au kufunzwa na mtu yeyote. Hivyo, kwa nini tumtegemee mtu yeyote ambaye hana Uvuvio kupitisha hukumu juu ya Ukweli uliovuviwa? Neno huonyesha kwamba sio wanadamu tu ila hata mataifa ni kama si kitu: {2TG9: 7.3}

Aya ya 15-17 –”Tazama, mataifa ni kama tone la

7

maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; Tazama, yeye hu-vinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana. Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake ha-watoshi kwa kafara. Mataifa yote huwa kama si kitu mbele yake; Huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili. “

Tunapogundua kwamba mataifa duniani kwa kulinganisha na nguvu ya Mungu sio kitu, kwamba mbao wala wanyama wa Lebanoni hawatoshi hata sadaka ya kuteketezwa, kwamba hivi karibuni tutawaona watu wote, pamoja nasi wenyewe, si kitu, na kama wasio na thamani kama mavumbi. Kisha tutaona utegemezi wetu Kwake wa umuhimu na kamili kama utegemezi wa mtoto mchanga kwa wazazi wake. {2TG9: 8.1}

Aya ya 18 — “Basi mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?”

Hili sasa ni swali kwa kila mmoja kujibu katika mawazo yake mwenyewe. {2TG9: 8.2}

Aya ya 19, 20 — “Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii; huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.”

Katika aya hizi zinaonyeshwa jinsi watu walivyo wapumbavu: Hawachii kuzingatia kwamba ingawa kipande cha kuni kinaweza kuwa kizuri kwa kawi, lakini wakati mwanadamu anajaribu kukifanya kuwa mfano wa Mun-gu, ni upumbavu tu na kwamba kukisujudia, ni kupotoka na kukufuru. {2TG9: 8.3}

8

Aya ya 21-27 –”Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia? Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama pan-zi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu. Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakati-fu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake. Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?.”

Kwa sababu Mungu ni mkuu kuliko fikira za wanadamu zinavyoweza kufahamu, kwa nini wanadamu humtegemea Yeye kidogo tu, — na kwa wingi maneno yao wenyewe? Kweli, tunaweza hakika kutoisujudia sanamu, lakini tunaweza kufanya mambo mengine ambayo ni sawa na kuabudu sanamu. Kwa kweli, kama isin-galikuwa hivyo mahimizo haya yasingekuja kwetu kupitia unabii huu uliofunuliwa kwa wakati mwafaka. {2TG9: 9.1}

Aya ya 27-31 — “Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asi-ione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea

9

nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

Haishangazi kwamba Kanisa, kwa kuwa limekuja umbali huu kupitia vizazi vingi, lazima sasa lifundishwe misingi ya kwanza ya imani yake? {2TG9: 10.1}

Isa. 41: 1, 2 — “Nyamazeni mbele yangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu. Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye kati-ka haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake.”

Kujipatia nguvu mpya ni kuweka mbali dhambi, na kumkaribia Mungu, ni kujifunza Kwake. Baada ya kufan-ya haya basi watawaalika wengine kuja hukumuni. Mataifa watanyamaza mpaka wakati huo, kisha watasema, “Njoni, tuende juu mlimani kwa Bwana, na kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Ye-rusalemu.” Mika 4: 2. {2TG9: 10.2}

Kazi yetu kwa hivyo ni kuiandaa njia ya Bwana kwa ajili ya kuwakusanya watu.

Aya ya 3-5 — “Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu Yake.

10

Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye. Visiwa vimeona, vikaogopa; ncha za dunia zilitetemeka; walikaribia, walikuja.”

Aya hizi zinaonyesha wazi kwamba udhihirisho wa nguvu ya Mungu ni lazima utahisiwa kila mahali. {2TG9: 11.1}

Aya ya 6 — “Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake; kila mtu akamwambia ndugu yake, Uwe na moyo mkuu.”

Watu wa Mungu hakika watamsaidia jirani yao. Walakini wapumbavu watafanya upumbavu, na wataendelea katika ibada yao ya sanamu. {2TG9: 11.2}

Aya ya 7-10 — “Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isiti-kisike. Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Abrahamu, rafiki yangu; wewe nili-yekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nime-kuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”

Ahadi za Mungu kwa watumwa Wake ni za hakika. Hebu tuzishikilie sasa. Hatutapata fursa nzuri kama tuliyo nayo leo. Kesho tutakuwa tumechelewa sana; ni bora tuitike wakati ambapo Mungu anatusihi. {2TG9: 11.3}

11

Aya ya 11, 12 — “Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.”

Sasa ni fursa yetu kufanya yote tuwezayo kwa ajili ya wale wanaotupinga, kwa maana hapa tunaambiwa wazi kwamba ikiwa wataendelea katika uhasama wao wataangamia. {2TG9: 12.1}

Aya ya 13 — “Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuam-bia, Usiogope; Nitakusaidia.”

Iwapo sisi kama watu hatuogopi, basi kwa nini rai hizi zote na kutiwa moyo? Kwa nini wito kwamba tutupilie nje hofu yetu? {2TG9: 12.2}

Aya ya 14, 15 — “Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli. Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.”

Kuifikicha milima (falme) ni kuchukua ngano (watakatifu) kutoka kwayo. Watumishi wa Mungu, kwa hivyo, hapa wameahidiwa kifaa kipya, tofauti na chochote kilichowahi kutumika hapo awali; yaani, kukusanywa kwa watakatifu katika wakati wa mavuno kutatekelezwa kwa njia ambayo haikuwaziwa, — kinyume na kila mpango wa mwanadamu. Kifaa hiki kitakuwa na meno; ghafla kitatenganisha ngano kutoka kwa majani na kuyapeperusha makapi. Kristo, “ambaye pepeto lake li mkononi mwake,

12

… atausafisha sana uwanda Wake, na kuikusanya ngano Yake ghalani; bali makapi atayateketeza kwa moto usi-ozimika.” Mat. 3:12. Kwa sababu hii tumeitwa, na kwa kazi hii kuu na kubwa tuitayarishe njia. {2TG9: 12.3}

Aya ya 16, 17 — “Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfu-rahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli. Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.”

Naam, makapi yatapeperushwa nje na upepo wa kisulisuli utayapeperusha mbali yachomwe kwa moto wa ku-teketeza. Lakini watu wa Mungu watafurahi katika Bwana, na masikini wao Yeye atawafariji. {2TG9: 13.1}

Aya ya 18 — “Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemichemi katikati ya mabonde; Nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na nchi kavu kuwa chemichemi ya maji.”

Mvua ya masika, tunaona hapa, itakuwa nyingi. Itafanya mito, chemichemi, na maziwa ambapo hayakutaraj-iwa. Hiya yote ni utabiri wa mavuno makubwa, hata kutoka kwenye maeneo ya jangwa — kutoka kwa nchi za mataifa. “Baada ya hayo nikaona, na tazama, umati mkubwa sana wa watu, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7:9. {2TG9: 13.2}

Aya ya 19 — “Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; Nitatia katika nyika mber-oshi,

13

mtidhari, na mteashuri pamoja.”

Mungu atazirembesha ardhi za Mataifa na watu wenye hulka za Ukristo na neema nzuri kama mhadasi, mbo-no, mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja. Hakuna kitu duniani leo cha kuwapatia wanadamu tumaini na amani ya mawazo ila ahadi hizi za Mungu. {2TG9: 14.1}

Aya ya 20-24 — “Ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa Bwana ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba. Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo. Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yata-kayotokea baadaye. Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja. Tazameni, ninyi si kitu, tena kazi yenu si kitu; awachaguaye ninyi ni chukizo.”

Hapa ni changamoto kwa maadui zetu wote. Ruhusu wawaambie yatakayotokea baadaye iwapo wanaweza, au wacha wawaambie ya kale ikiwa wataweza, Mungu anawapa changamoto. Hivyo waweze sasa kujua kuwa wao ni kama si kitu, na wale ambao huchagua kuwafuata, hata nao watakuwa chukizo Kwake. {2TG9: 14.2}

Aya ya 25 — “Nimemwinua mtu kutoka kaskazini, naye amekuja. Toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina Langu; naye atawajilia maliwali kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi afinyangae udongo.”

14

Huyu ambaye yu katika unabii anatokea mahali fulani kaskazini mwa Nchi ya Ahadi. Yeye anamwita Bwana alfajiri– mapema jua linapochomoza. Yeye huwajilia pia wakuu kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi anayeufinyanga udongo. “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha Ufalme…utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu.” Dan. 2:44. {2TG9: 15.1}

Aya ya 26 — “Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; Naam, hapana hata mmoja aliyetuonye-sha, Naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.”

Je! Yupo mtu yeyote aliyewahi kutangaza mambo haya kwa watu? anauliza Bwana. Kisha analijibu swali Lake Mwenyewe: “Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; Naam, hapana hata mmoja aliyetuonyesha, Naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.” {2TG9: 15.2}

Aya ya 27, 28 — “Mimi kwanza nitauambia Zayuni, Tazama, watazame; nami nitampa Yerusalemu mleta-ji wa habari njema. Maana nilipotazama, hakuwapo mtu; hata katika watu hao, hakuwapo mshauri mmoja, ambaye, nikimuuliza, aweza kunijibu neno.”

Wakati Mungu anawajilia watu Wake na hizi habari njema, hampati mtu yeyote kati ya watumwa Wake kui-fanya kazi hii, na hakuna mshauri kati yao wa kutoa jibu kwa mambo haya! Sisi hata hivyo tunapaswa kufanya yote tuwezayo kuwaamsha. Tunapaswa kuliinua Neno, kuwafariji watu Wake, na kuiandaa njia ili Yeye aweze kutufanya kuwa chombo kipya cha kufikicha. {2TG9: 15.3}

15

Kumwonea Yesu Aibu!

Yesu, na daima itakuwa hivyo,

Mtu mfaji Kukuonea aibu?

Kukuonea aibu, ambaye malaika hukusifu,

Ambaye utukufu huangaza siku zote zisizo na mwisho?

 

Kumwonea Yesu aibu! Mbali upesi

Ruhusu jioni angavu imiliki nyota;

Anaangaza miale ya nuru takatifu

Juu ya nafsi yangu iliomo gizani.

 

Kumuonea Yesu aibu! upesi tu

Acha usiku wa manane uaibikie adhuhuri;

Ulikuwa usiku wa manane kwa nafsi yangu mpaka Yeye,

Nyota Ing’aayo ya Asubuhi, kufukuza giza.

 

Kumuonea Yesu aibu! huyo Rafiki mpendwa

Ambaye Kwake matumaini yangu ya mbinguni hutegemea!

Hapana; Wakati ninaona haya, iwe aibu yangu

Kwamba siliheshimu tena jina Lake.

 

Kumuonea Yesu aibu! naam, naweza

Wakati sina hatia ya kuosha;

Hakuna chozi la kufuta, hakuna zuri la kutamani,

Hakuna hofu ya kuzima, hakuna nafsi ya kuokoa.

 

Mpaka hapo, — au kujisifu kwangu ni bure, —

Mpaka hapo namsifu Mwokozi aliyechinjwa;

Na Ee, huu uweze kuwa wangu utukufu,

Kwamba nisimuaibishe Kristo!

 

—Joseph Grigg

16

MACHIPUKIZI YA SHINA, SIO MACHIPUKO
Kwa Ndugu Walio Ugenini

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Kwa kadri tunavyoulizwa mara nyingi maana ya “D” katika Salamu Mwafaka kuhusiana na jina “Waadvent-ista wa Sabato,” tutajitahidi kuelezea. “D” inasimamia wa-Daudi. Wachapishaji, badala ya kuchapisha jina ka-mili, mara nyingi hutumia ufupisho “D” wakati nafasi ni ndogo. {2TG10: 17.1}

Kimsingi sisi ni Waadventista wa Sabato. Daima tangu wakati ndugu wanaoongoza wa dhehebu la Waadventista wa Sabato waliikataa nyongeza kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu (Maandishi ya Awali, uk. 277) kwa mtindo ule ule kama Wayahudi walivyoikataa injili ya Kristo, na kama vile makanisa maarufu yalivyozikataa jumbe ambazo zilifuata baadaye, Tumesalia kimsingi Waadventista wa Sabato. Tumetengwa na kanisa mama kwa sababu ndugu “wavuguvugu” kwa kura za walio wengi walituondoa kwa ushirika, na kuweka walinzi kwenye milango ya kanisa ili kuhakikisha kwamba tusiingie makanisani siku ya Sabato. Inaonekana kwamba walifanya mambo haya ili kutulazimisha kuukana Ukweli uliofunuliwa wa Bwana, na pia kuwatisha wale ambao walikuwa wakiukumbatia Ukweli wa Sasa na wale ambao wangeweza kujichunguzia wenyewe na kuupokea ujumbe wa saa hii. Haingekuwepo sababu ya kutufukuza. {2TG10: 17.2}

Kwa sababu hatungaliweza kukipa kisogo kilichotumwa na Mungu “chakula kwa msimu unaofaa” bila shaka

17

tulilazimika kuongeza wa-Daudi kwa jina la Waadventista wa Sabato, ili tusije tukashutumiwa kwa kupotosha. Hatujawahi kamwe, hata hivyo, kujitenga kwa dhehebu. Kama watu bado huhudhuria makanisa ya dhehebu wakati wowote tusipozuiliwa kuingia. {2TG10: 17.3}

Kazi yetu kwa uhalisi ni ndani ya dhehebu letu kama ilivyokuwa ya Yohana na ya Kristo ndani ya dhehebu lao. Imani yetu ya msingi kwa hivyo ni sawa na ile ya dhehebu, isipokuwa kweli za mafundisho ya ziada ambazo ujumbe wa ziada unatuletea. Hali, kwa hivyo, zimetuweka katika mahali sawa na pale pa mitume: Imani yao ya kimsingi, pia, ilikuwa imani ya msingi ya Wayahudi, na zaidi ya hizi, walikuwa na Injili ya Kristo. {2TG10: 18.1}

Ili kutupia lawama na kuwafanya watu wawe na chuki dhidi ya ujumbe uliotumwa na Mbingu, upinzani kwa dhihaka hutuita “machipuko.” Usemi wao hasa dhidi yetu, hata hivyo, hututhibitisha kuwa tuko sahihi na wao wabaya. Yasingalikuwa “machipuko,” kanisa la Kikristo lisingaliweza kutokea, — la, sio hata makanisa ya Kiprotestanti, wala Waadventista wa Sabato. {2TG10: 18.2}

Hivyo tunamshukuru Mungu kwamba tumekuwa na uimara wa kutoufanya mwili kuwa kinga yetu (sio ku-lipokea neno la makuhani na marabi, kwa mfano, ila tulichunguze sisi wenyewe, kibinafsi kujua Ukweli ni nini) na kuhimili shutuma kama walivyofanya wale ambao wametutangulia. {2TG10: 18.3}

Hapa ndipo panapofaa na wakati mwafaka kwa taarifa ya nabii Isaya kutumika: “Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye Bwana akaona hayo, akachukizwa

18

kwa kuwa hapana hukumu ya haki.” Isa. 59:15. {2TG10: 18.4}

Ukweli wa suala, hata hivyo, ni kwamba wanaoitwa eti machipuko badala yake ni machipukizi ya shina. Na tukumbuke daima kwamba ikiwa mti hufa unaposhindwa kuchipukiza juu ya shina kila msimu, ndivyo ambavyo hufanya kanisa linaposhindwa kuambatana na Ukweli wa Mbingu unaoendelea. Hata ulimwengu unajua kwam-ba machipukizi ya shina siku zote yamelihifadhi kanisa likiwa hai na huru, na ya kwamba machipukizi ya shina daima yatalihifadhi. Kwa hivyo tunajihisi walioheshimiwa sana kuwa machipukizi ya shina badala ya machipuko bwete. {2TG10: 19.1}

Naam, ni heshima kubwa kuteswa, kudhihakiwa, na kudhulumiwa kwa ajili ya Kristo na Ukweli Wake. Kwa hivyo Yesu anatangaza: “Heri ninyi, watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini siku ile, na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, tha-wabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.” Luka 6:22, 23 {2TG10: 19.2}

“Likieni Neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya Neno Lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, na atukuzwe Bwana, lakini yeye atatokea kwa furaha yako, nao watatahayarika.” Isaya 66: 5. {2TG10: 19.3}

“Na wafalme watakuwa baba zako wa kukulea, na malkia zao mama zako wa kukulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojao ha-watatahayarika. {2TG10: 19.4}

“Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lake waliofungwa halali wataokoka? Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari

19

watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.” Isaya 49: 23-25. {2TG10: 19.5}

Ni wazi kuona kwamba wale ambao huwatupa nje ndugu waamini wa ukweli kutoka kati yao, wanatenda hivyo kwa amri ya Yule Mwovu, kwa maana wale ambao huzingatia amri ya Bwana, huwa hawayatupi nje hata “magugu.” Wanajua kwamba kazi ya kulisafisha kanisa ni ya malaika pekee. {2TG10: 20.1}

“Kisha nalimwona malaika wa tatu. Akasema malaika aliyeandamana nami, ‘Ya kutisha ni kazi yake. Utume wake ni wa kuogofya. Yeye ndiye malaika atakayeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kufunga, ngano kwa ghala la mbinguni. Mambo haya yanapaswa kuyashughulisha mawazo yote, umakini wote.’” — Maandishi ya Awali, uk. 118. {2TG10: 20.2}

“Tena, ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna: hata lilipojaa, walilivuta pwani, wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto: Ndiko kutakuwako na kilio na kusaga meno.” Mat. 13:47-50. {2TG10: 20.3}

Kwa hivyo tuwe sawa au tuwe wakosefu, tunajua kwamba kazi za hao ndugu hazipatani na Bwana. {2TG10: 20.4}

Waasisi wa imani ya Kikristo waliyatoa maisha yao kwa ajili ya Ukweli, kwa nini tusiwe hivyo? {2TG10: 20.5}

Sasa kuhukumu iwapo sisi ni Waadventista wa Sabato au la, ruhusu niweke mbele yako msingi wa

20

imani yetu kutoka katika trakti, “Msingi wa Imani na Faharisi.” Hapa utagundua kwamba orodha yote ya msingi wa imani imenukuliwa kutoka kitabu cha mwaka cha dhehebu la S.D.A. Na kwa nini? — kwa sababu imani yao ni imani yetu, pia. Kisha utagundua kweli za mafundisho ya ziada yanayofuata. {2TG10: 20.6}

 

MISINGI YA IMANI YA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

Ukijitokeza mwaka wa 1930 kutoka ndani ya dhehebu la Waadventista wa Sabato (“kanisa la Walaodekia”), Ushirika wa Wanadaudi Waadventista wa Sabato umekabidhiwa kazi ya kiunabii (ilivyotabiriwa katika Isaya 52: 1) ya kuliandaa kanisa la Laodekia, la mwisho na “magugu” kati ya “ngano,” kwa ajili ya kutangaza injili “duniani kote.” Mat. 24:14. {2TG10: 21.1}

Ushirika huu, kwa pamoja na dhehebu la Waadventista wa Sabato, una ‘imani fulani za msingi, sifa kuu am-bazo, pamoja na marejeleo ya Maandiko ambayo juu yake imejengwa,’ mwanzoni imefanywa muhtasari kama ifuatavyo: {2TG10: 21.2}

“1. Kwamba Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Jipya yalitolewa kwa uvuvio wa Mungu, yanasheheni ufunuo wa kutosha wa mapenzi Yake kwa wanadamu, na ni kanuni isiokosea ya imani na desturi. 2 Tim. 3:15-17. {2TG10: 21.3}

“2. Kwamba Uungu, au Utatu, huhusisha Baba wa Milele, wa pekee, Kiumbe cha kiroho, Mwenye nguvu, Aliye Mahali Pote, Anayejua yote,

21

asiye na kikomo kwa hekima na upendo, Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Baba wa Milele, ambaye kwa Yeye vitu vyote viliumbwa na kupitia Kwake wokovu wa majeshi ya waliokombolewa utatimizwa; Roho Mtakatifu, kiumbe cha tatu cha Uungu, nguvu kuu ya urejesho katika kazi ya ukombozi. Mat. 28:19. {2TG10: 21.4}

“3. Kwamba Yesu Kristo ni Mungu hasa, akiwa wa maumbile sawa na asili kama Baba wa Milele. Alipokuwa aki-hifadhi asili yake ya Uungu Alijitwalia asili ya familia ya kibinadamu, aliishi duniani kama mwanadamu, alionye-sha katika maisha Yake kama Mfano wetu kanuni za haki, zilithibitisha uhusiano Wake na Mungu kwa miujiza mingi ya nguvu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu msalabani, akafufuliwa kutoka kwa wafu, na akapaa kwa Baba anakoishi milele ili kutuombea. Yoh. 1: 1, 14; Ebr. 2: 9-18; 8: 1, 2, 4: 14-16; 7:25 {2TG10: 22.1}

“4. Kwamba kila mtu ili kuupata wokovu lazima apitie uzoefu wa kuzaliwa upya, kwamba huu unajumuisha mabadiliko yote ya maisha na tabia kwa nguvu ya kuumba upya ya Mungu kupitia imani katika Bwana Yesu Kris-to Yohana 3:16, Mathayo 18: 3; Matendo 2: 37-39.{2TG10: 22.2}

“5. Ubatizo ni ibada ya kanisa la Kikristo na unapaswa kufuata toba na msamaha wa dhambi. Katika maadhimi-sho yake imani inaonyeshwa katika kifo, mazishi, na ufufuo wa Kristo. Kwamba mtindo sahihi wa ubatizo ni kwa kuzamishwa. Warumi 6: 1-6; Matendo 16: 30-33.{2TG10: 22.3}

“6. Kwamba mapenzi ya Mungu jinsi yanavyohusiana na mienendo ya maadili yanaelezwa katika sheria

22

Yake ya amri kumi, kwamba hizi ni kanuni zisizobadilika, kuu za maadili, zinazowaunganisha wanadamu wote, katika kila kizazi. Kutoka 20: 1-17.{2TG10: 22.4}

“7. Kwamba amri ya nne ya sheria hii isiyobadilika huhitaji kuadhimisha Sabato ya siku ya saba. Hii taasisi ta-katifu wakati huo huo ni ukumbusho wa uumbaji na ishara ya utakaso, ishara ya pumziko la anayeamini kutoka kwa kazi zake za dhambi , na kuingia kwake ndani ya pumziko la nafsi ambalo Yesu huahidi kwa wale wanaokuja Kwake (Mwa. 2: 1-3; 1, Kut. 20: 8-11, 31: 12-17; Ebr. 4: 1- 10. {2TG10: 23.1}

“8. Kwamba sheria ya amri kumi huonyesha wazi dhambi, ambayo adhabu yake ni kifo. Sheria haiwezi kum-wokoa mkosaji kutoka kwa dhambi yake, wala kumpa uwezo wa kumzuia kutenda dhambi. Kwa upendo wa milele na rehema, Mungu hutoa njia ambapo hili linaweza kufanywa. Yeye hutoa mbadala, hata Kristo Mwenye Haki, kufa kwa niaba ya mwanadamu, na ‘Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.’ 2 Kor. 5:21. Kwamba mmoja huhesabiwa haki, sio kwa utiifu wa sheria, ila kwa neema iliyo katika Kristo Yesu. Kwa kumkubali Kristo, mwanadamu anapatanishwa na Mungu, ana-hesabiwa haki kwa damu Yake kwa ajili ya dhambi za zamani, na kuokolewa kutoka kwa nguvu za dhambi kwa maisha yake ya ndani. Hivi injili inakuwa ‘nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila aaminiye.’ Uzoefu huu unafanywa na uwakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humhakikishia habari ya dhambi na kumwongoza hadi kwa Mbeba-Dhambi, kumshawishi aaminiye kuingia agano jipya la uhusiano, ambapo sheria ya Mungu inaandikwa moyoni mwake, na kupitia uwezo unaomwezesha wa Kristo anayekaa ndani, maisha yake yanaletwa kufanana kabisa na maagizo ya Mungu. Heshima na sifa za

23

mabadiliko haya ya ajabu zote ni zake Kristo. 1 Yoh. 3: 4; Rum. 7: 7; Rum. 3:20; Efe. 2: 8-10; 1 Yoh. 2: 1, 2; Rum. 5: 8-10; Gal. 2:20; Efe. 3:17; Ebr. 8: 8-12. {2TG10: 23.2}

“9. Kwamba Mungu ‘pekee ana hali ya kutokufa.’ 1 Tim. 6:15. Mwanadamu wa uvumbi humiliki asili aliyoridhi ya dhambi na ya kufa. Uzima wa milele ni zawadi ya Mungu kwa njia ya imani ndani ya Kristo. Rum. 6:23. “Yeye aliye na Mwana anao uzima.” 1 Yoh. 5:12. Hali ya kutokufa watapewa waadilifu wakati wa ujio wa pili wa Kristo, wakati watakatifu waliokufa wanafufuliwa kutoka makaburini na wenye haki walio hai wanahamishwa kumlaki Bwana. Kisha inakuwa kwamba wale waliohesabiwa kuwa waaminifu ‘wanavaa kutokufa.’ 1 Kor. 15: 51-55. {2TG10: 24.1}

“10. Kwamba hali ya mtu katika kifo ni ile ya kukosa fahamu. Kwamba watu wote, wema na wabaya sare, wanasalia kaburini tangu kifo hadi kwa ufufuo. Mhu. 9: 5, 6; Zab. 146: 3, 4; Yoh. 5:28, 29. {2TG10: 24.2}

“11. Kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote waadilifu na waovu. Ufufuo wa waadilifu utafanyika wakati wa ujio wa pili wa Kristo; ufufuo wa waovu utafanyika miaka elfu baadaye, mwishoni mwa milenia. Yoh. 5:28, 29; 1 Thes. 4: 13-18; Ufu. 20: 5-10. {2TG10: 24.3}

“12. Kwamba mwishowe wadhambi wasiotubu, Shetani akiwamo, mwasisi wa dhambi, atapunguzwa, kwa moto wa siku ya mwisho hadi kwa hali ya kutokuwa hai na kuwa kana kwamba hakuwa, na hivyo kuusafisha ulimwen-gu wa dhambi na wadhambi. Rum. 6:23, Mal. 4: 1-3, Ufu. 20: 9, 10; Obadia 16. {2TG10: 24.4}

“13. Kwamba hakuna kipindi cha unabii [kumaanisha

24

kuweka muda wa kiunabii wa tarehe kamili ya kuja kwa Kristo] kimepeanwa katika Biblia kufikia ujio wa pili, ila kwamba kile kirefu zaidi siku 2300 za Dan. 8:14, kilikoma mwaka wa 1844, na kutuleta kwa tukio linaloitwa ku-patakasa patakatifu. {2TG10: 24.5}

“14. Kwamba hekalu la kweli, ambalo hema ya duniani ilikuwa mfano, ni hekalu la Mungu lililo Mbinguni, am-balo Paulo hulizungumzia katika Waebrania 8 na kuendelea, na ambalo Bwana Yesu kama kuhani wetu mkuu, ni mtumishi; na kazi ya ukuhani ya Bwana wetu ni uakisi wa kazi ya Kuhani wa Kiyahudi wa enzi ya awali; kwamba hili hekalu la mbinguni ndilo la kutakaswa mwishoni mwa siku 2300 za Dan. 8:14; kutakaswa kwalo kukiwa, ka-ma katika mfano, kazi ya hukumu, ikianza na kuingia Kristo kwa awamu ya hukumu ya huduma Yake katika hekalu la mbinguni kivuli chake katika huduma ya la duniani ya kulitakasa hekalu kwa siku ya upatanisho. Kazi hii ya hukumu katika hekalu la mbinguni ilianza maka wa 1844. Kukamilika kwake kutafunga rehema kwa mwa-nadamu. {2TG10: 25.1}

“15. Kwamba Mungu, katika wakati wa hukumu na kulingana na kujishughulisha Kwake kwa usawa na jamii ya wanadamu kuwaonya juu ya matukio yanayokuja ya umuhimu yanayoathiri hatima yao (Amosi 3: 6, 7), hutuma umbele utangazaji wa unavyojongea ujio wa pili wa Kristo; kwamba kazi hii inawakilishwa na malaika watatu wa Ufunuo 14, na kwamba ujumbe wao mara tatu huleta kwa mtazamo kazi ya matengenezo ya kuwaandaa watu ku-kutana Naye wakati wa kuja Kwake. {2TG10: 25.2}

“16. Kwamba wakati wa kupatakasa patakatifu, unaambatana na kipindi cha

25

kuutangaza ujumbe wa Ufunuo 14, ni wakati wa hukumu ya upelelezi, kwanza kuhusu wafu, na pili, kuhusu walio hai. Hukumu hii ya upelelezi inaamua ni nani kati ya makumi ya maelfu wanaolala katika mavumbi ya dunia wanastahili sehemu katika ufufuo wa kwanza, na ni nani wake walio hai wanastahili kuhamishwa bila kuonja mauti. 1 Pet. 4:17, 18; Dan. 7:9, 10, Ufunuo 14: 6, 7, Luka 20:35. {2TG10: 25.3}

“17. Kwamba wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa watu wakumcha Mungu, wasioiga misemo ya uovu na maa-dili yasiyo ya kawaida wala wasiambatane na njia zisizo za haki za dunia, wasiopenda anasa zake za dhambi wala kuupokea upuuzi wake. Kwamba aaminiye anapaswa kuutambua mwili wake kama hekalu la Roho Mtakatifu, na kwamba kwa hivyo anapaswa kuufunika mwili huo kwa mavazi safi, nadhifu na ya heshima. Zaidi ya hayo, kwamba katika kula na kunywa na katika mkondo wake wote wa mazoea anapaswa kuyageuza maisha yake kama inavyotakiwa kuwa mfuasi wa Mwalimu mpole na mnyenyekevu. Hivi aaminiye ataongozwa kujiepusha na viny-waji vyote vya sumu, tumbaku, na dawa zingine za kulevya, na kujizuia kila tabia na mazoea ya kuutia unajisi mwili na roho. 1 Kor. 3:16, 17; 9:25; 10:31: 1 Tim. 2: 9, 10; 1 Yohana 2: 6. {2TG10: 26.1}

“18. Kwamba kanuni takatifu ya zaka na sadaka kwa ajili ya kuunga mkono injili ni kuutambua umiliki wa Mungu katika maisha yetu, na kwamba sisi ni wasimamizi ambao wanapaswa kumpa hesabu juu ya yote Ameweka kwa umiliki wetu. Law. 27:30; Mal 3: 8-12; Mat. 23:23; 1 Kor. 9: 9-14, 2 Kor 9: 6-15. {2TG10: 26.2}

“19. Kwamba Mungu ameweka ndani ya kanisa lake karama za Roho Mtakatifu, kama zilivyoorodheshwa

26

katika 1 Wakorintho 12 na Waefeso 4. Kwamba karama hizi hufanya kazi kwa uwiano na kanuni za Mungu za Biblia, na zimetolewa kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu , kazi ya ukasisi, na kuujenga mwili wa Kristo. Ufu. 12:17, 19:10; 1 Kor 1: 5 {2TG10: 26.3}

“20. Kwamba ujio wa pili wa Kristo ni tumaini kubwa la kanisa, kilele kikuu cha injili na mpango wa wokovu. Kuja kwake kutakuwa halisi, binafsi, na dhahiri. Matukio mengi muhimu yatahusishwa na kurudi Kwake, kama vile ufufuo wa wafu, kuangamizwa kwa waovu, utakaso wa dunia, tuzo ya wenye haki, kuanzishwa kwa ufalme wake wa milele. Utimilifu karibu wote wa safu mbalimbali za unabii hasa ule uliyomo katika vitabu vya Danieli na Ufunuo, na hali zilizopo katika ulimwengu wa kimwili, kijamii, kiviwanda, kisiasa na kidini, zinaonyesha kwamba kuja kwa Kristo ‘kumekaribia, hata kwenye malangoni. ‘Wakati kamili wa tukio hilo haujatabiriwa. Waumini wanahimizwa kuwa tayari, kwa maana ‘katika saa ile msiyodhani, Mwana wa Adamu’ atafunuliwa. Luka 21: 25-27; 17: 26-30; Yoh. 14: 1-3; Mdo. 1: 9-11; Ufu. 1: 7; Ebr. 9:28; Yak. 5: 1-8; Yoeli 3: 9-16; 2 Tim. 3: 1-5; Dan. 7:27; Mat. 24:36, 44. {2TG10: 27.1}

“21. Kwamba utawala wa Kristo wa milenia hufunika kipindi kati kati ya ufufuo wa kwanza na wa pili, wakati ambapo watakatifu wa vizazi vyote watakaa pamoja na Mwokozi wao Mbarikiwa Mbinguni. Mwishoni mwa mile-nia, Mji Mtakatifu na watakatifu wote watashuka kwa dunia. Waovu, waliofufuliwa katika ufufuo wa pili, watae-nea juu ya uso wa dunia na Shetani kiongozi wao ili

27

kuizingira kambi ya watakatifu, wakati moto utashuka kutoka kwa Mungu Mbinguni na kuwateketeza. Katika moto mkubwa ambao unamwangamiza Shetani na jeshi lake, dunia yenyewe itaumbwa upya na kutakaswa kutokana na madhara ya laana. Hivi ulimwengu wa Mungu utatakaswa kutoka kwa uchafu wa doa la dhambi. Ufu. 20; Zek. 14: 1-4; 2 Petro 3: 7- 10. {2TG10: 27.2}

“22. Kwamba Mungu ataumba vitu vyote upya. Dunia, kurejeshwa kwa uzuri wake wa awali, itakuwa milele makao ya watakatifu wa Bwana. Ahadi kwa Abrahamu, kwamba kwa njia ya Kristo yeye na uzao wake wataimili-ki dunia katika vizazi visivyokoma vya milele, itatimizwa. Ufalme na utawala na ukuu wa ufalme chini ya mbingu zote utapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu ambaye ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zote zitamtumikia na kumtii Yeye. Kristo, Bwana, atatawala kwa ukuu na kila kiumbe kilicho mbinguni na duniani na chini ya nchi, na vile vilivyo baharini vitatoa baraka na heshima na utukufu na nguvu kwa Yeye anayeketi juu ya kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo milele na milele (Mwa. 13: 14-17, Rum. 4:13, Ebr. 11: 8-16, Mat. 5: 5, Isa. 35, Ufu. 21: 1-7; Dan. 7 : 27; Ufu. 5:13.) “Kitabu cha Mwaka cha Dhehebu la Waadventista wa Sabato, Toleo la 1940, kr. 5-8.” {2TG10: 28.1}

KATIKA NYONGEZA kwa misingi hii ya imani inayoshikiliwa sawa na Waadventista wa Sabato, Ushirika wa Wadaudi unashikilia: {2TG10: 28.2}

1. Kwamba karama ya unabii katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (kupitia chombo ambacho kanisa lilian-zishwa mwaka wa 1844 na kukuzwa na kudumishwa kwa miongo saba) kilikoma

28

udhihirisho wake mwaka wa 1915 na hakikudhihirishwa tena hadi mwaka wa 1930, na kwamba kikomo hiki na udhihirisho huu ni sambamba na kukoma karama ya unabii katika Agano la Kale na udhihirisho wake katika Agano Jipya. {2TG10: 29.1}

2. Kwamba ulidhihirisho wa sasa ulipangwa kulingana na unabii wa miaka 430 wa Ezekieli 4, na ya kwamba ndiyo “Nyongeza” iliyotarajiwa katika Maandishi ya Awali, uk. 277. {2TG10: 29.2}

3. Kwamba kilidhihirishwa upya katika kazi ya kufunga kwa kanisa ili kutekeleza kutiwa muhuri watumwa 144,000 wa Mungu (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na kupeana nguvu na msukumo (Maandishi ya Awali, uk. 277) kwa Ujumbe wa Malaika Watatu (Ufu. 14: 6-11) ili kwamba watumwa 144,000 wajazwe nguvu waweze kukamilisha kazi ya kufunga kwa dunia, na kuwakusanya ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote (Isaya 66:19, 20; 18: 4). {2TG10: 29.3}

4. Kwamba kuangamizwa kwa magugu kutoka miongoni mwa malimbuko ya walio hai (Mat. 13:30, 48, 49; Ezek. 9: 6, 7) ni tokeo la utakaso wa kanisa. {2TG10: 29.4}

5. Kwamba hapo hapo baada ya hayo, malaika wataziachilia pepo nne (Ufu. 7: 1-3), ambapo utaanza wakati wa taabu na Mikaeli kusimama kuwaokoa kutoka kwayo, wote ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo (Dan. 12: 1). {2TG10: 29.5}

6. Kwamba malaika ‘kuziachilia pepo nne kuvuma pembe nne za dunia (Ufu. 7: 1), sio tarajio la vita vya dunia ila badala yake sheria ya kutekelezwa dunia nzima katika Babeli na sanamu ya mnyama, na ya kwamba mtu yeyote asiweze kununua au kuuza isipokuwa yeye anayeiabudu

29

“sanamu.” Ufu. 13: 15-17. {2TG10: 29.6}

7. Kwamba halafu, wakati wa taabu ya Yakobo (Yer. 30: 7) kwa wale 144,000, wana wa Yakobo, kwa mantiki inatokeza wakiwa safarini kurudi nyumbani (Mwa. 32: 1, 24) kwa nchi ya baba zao (Ezek. 36:28; 37:21, 25). {2TG10: 30.1}

8. Kwamba tukio la kihistoria ambalo limetajwa hapo juu litasababisha watu 144,000 kupata majina yao yanaba-dilishwa kama baba yao, Yakobo (Mwa. 32:28), na kama kundi kupokea jina jipya ambalo kinywa cha Bwana kitanena (Isa. 62 : 2). {2TG10: 30.2}

9. Kwamba haya matukio yatafikia upeo katika kuanzishwa kwa Ufalme (Dan. 2:44; Isa. 2: 1-4; Mika 4; Ezek. 37), ambamo wale 144,000, wamfuatao Mwana-Kondoo “kila aendako” (Ufu. 14: 4), watasimama pamoja naye juu ya Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1), na hapo “kuupokea utajiri wa watu wa mataifa.” Isa. 60: 5, 11. {2TG10: 30.3}

10. Kwamba pamoja na mfululizo huu wa matukio utahakiki Kilio Kikuu cha Malaika anayeiangaza nchi kwa utu-kufu wake (Ufu. 18: 1), wakati Sauti nyingine inapiga kelele, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4. {2TG10: 30.4}

11. Kwamba katika kuitikia mwito huu, mataifa mengi yatasema: “Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika 4: 2. {2TG10: 30.5}

12. Kwamba Sauti itaacha kupiga kelele wakati watakatifu wote watakakuwa wamekusanywa kutoka katika ma-taifa

30

yote. Kisha itakuwa “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” Amosi 8:11, 12. {2TG10: 30,6}

13. Kwamba basi kutafuatia kutenguka kwa muungano wa dunia nzima wa sanamu ya mnyama (Ufu. 19: 1-3), kufungwa kwa hukumu ya upelelezi ya walio hai (Ufu. 15: 5-8), mwisho wa muda wa rehema (Ufu. 22:11), na kumiminwa kwa mapigo saba ya mwisho juu ya waovu (Ufu. 16). {2TG10: 31.1}

14. Kwamba chini ya pigo la saba, majeshi yaliyojipanga kwa pambano la Har-Magedoni yatapigana na, na yataangamizwa na, majeshi ya Mbinguni (Shuhuda, Gombo la 6, uk. 406), na kwamba Kristo atatokea katika utu-kufu Wake wote, kuwaangamiza waovu waliosalia, kuwafufua watakatifu waliokufa (1 Thess. 4:15-17), na kui-karibisha milenia (Ufu. 20: 5). {2TG10: 31.2}

15. Kwamba kwa muda mchache (Ufu. 20: 3), miaka mia moja (Isaya 65:20), baada ya milenia, waovu wataishi tena na hatimaye wataangamizwa kwa moto (Ufu. 20: 9), ambapo vitu vyote vitarejeshwa, na mpango halisi wa Mungu utaendelea kufikia utimilifu mkamilifu katika umilele usiokatizwa wa furaha ya mbinguni (Ufu. 21: 4). {2TG10: 31.3}

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 9, 10

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>