fbpx

Mtoa Jibu Kitabu Namba 2

Mtoa Jibu Kitabu Namba 2

1

Hakimiliki 1944, na

V.T. Houteff

Haki Zote Zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kama utumishi wa Ukristo, kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga. {ABN2: 2.1}

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitathaminiwa. {ABN2: 2.2}

“… LAKINI YEYE ATAKAPOKUJA, HUYO ROHO WA KWELI, ATAWAONGOZA AWATIE KWENYE KWELI YOTE; KWA MAANA HATANENA KWA SHAURI LAKE MWENYEWE, LAKINI YOTE ATAKAYOYASIKIA ATAYANENA, NA MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI YAKE.” YOHANA 16:13. {ABN2: 2.3}

2

MTOA JIBU

Kitabu Namba 2

Maswali na Majibu kwa Mada za Ukweli wa Sasa

Katika Masilahi ya Ndugu Waadventista wa Sabato

na Wasomaji

wa

Fimbo ya Mchungaji

Na V.T. Houteff

Huyu “mwandishi,” mwenye elimu

ya ufalme wa

mbinguni, “hutoa

… vitu vipya na vya zamani.”

Mat. 13:52.

Sasa “mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”

1 Pet. 3:15.

3

 

YALIYOMO

 

Mahubiri Ya Stefano Kwa Kanisa Leo ……………………………..5

Je! Tunaweza Kuijua Hiyo Saa? ……………………………………23

Je! Kiti Cha Enzi Kinachokwenda Cha Mungu Ni Gari-Moshi? …24

Je! Ipo Mitende Katika Mikono Ya Baadhi, Au Katika Mikono

Ya Wote? ……………………………………………………………..24

Je! Utaanza Lini Wakati Wa Mwisho? ……………………………..25

Je! Mbona Unabii Katika Nafasi Ya Upendo? …………………….26

Je! Mihuri Ilianza Lini? ……………………………………………….29

Je! Muhuri Ni Nini? …………………………………………………..31

Je! Kutiwa Muhuri Kunafanyika? Ni Nani Wanaotiwa

Muhuri? Yeyote Asiyetenda Dhambi? ……………………………..33

Je! Mavuno Sio Mwisho Wa Dunia? ……………………………….36

Je! Ni Lini Yeye Atayatenga Magugu Kutoka Kwa Ngano? ……..38

Je! Mchinjo Wa Ezekieli Tisa Ni Halisi? ……………………………42

Je! Ni Nani Mwanamke Na Masalia Wake? ……………………….44

Ni Nani Aliyezitambua Sayari Zilizoonekana Katika Maono? ……49

Je! Yote Ya Neno Kwa Kundi Ndogo Ni Sahihi? ………………….51

Je! Umekuwapo Mseto Wa Mwanadamu Na Mnyama? …………52

Mbona Hayafanyiki Maendeleo Bora? ……………………………..53

Je! Mbona Kupekecha Pale Pasipohitajika? ………………………57

Kazi Ndani Au Nje? …………………………………………………..58

Je! Fimbo Bado Hufundisha “Mambo Yale Yale”? ……………….63

Je! Jioni Ni Mwisho Au Mwanzo Wa Siku? ……………………….64

Je! Ni Kweli? ………………………………………………………….65

Katika Muhuri Upi? …………………………………………………..65

Ni Nani Wanakimbilia Milimani? ……………………………………66

Je! Atatoka Lini Hekaluni? …………………………………………..67

Ni Nani Ametanga Mbali Na Mipaka Ya Zamani? ………………..68

Mtazamo Wa Awali Au Wa Mwisho? ………………………………71

Mbona Majina Matatu Kwa Ufalme Uliogawanyika? ……………..73

Je! Ufalme Utasimamishwa Kabla Ya Millenia? ………………….74

Je! Yerusalemu Wa Kale Utajengwa Tena? ………………………86

Karamu Ya Harusi Ya Mwana-Kondoo Mbinguni Au Kwa Nchi?..86

Ufalme wa Mungu Moyoni, Au Kwa Nchi? …………………………89

Je! Pepo Zitaachiliwa Lini? ………………………………………….90

Je! Hasira Ya Mataifa Ni Nini? ………………………………………91

Je! Hatua Yako Inayofuata Itakuwa Nini? …………………………94

Faharisi Ya Maandiko …………………………………………….….95

4

MWITO WA UTANGULIZI WA MTOA JIBU

MAHUBIRI YA STEFANO KWA KANISA LEO

“Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani, akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi Nitakayokuonyesha. “ Matendo 7:2, 3. “Basi Abramu akaondoka, kama Bwana alivyomwamuru” (Mwa. 12:4), akaenda kwa uongozi Wake mpaka Kanaani, ambamo alikaa, ingawa Bwana “hakumpa urithi humo hata kiasi cha kuweka mguu; Akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.” Matendo 7:5. {ABN2: 5.1}

Kisha baada ya muda, Bwana alikusudia kumwongoza Yakobo na familia yake kutoka nchi ya Kanaani, kwenda Misri. Akijua, hata hivyo, kwamba wana wa Yakobo hawataenda kama Abrahamu alivyoenda, kwa kuwaambia tu, Yeye kwa hivyo, kwa majaliwa Yake aliweka ndani ya moyo wa Yakobo upendo mkubwa kwa Yusufu kuliko kwa watoto wake wengine. Hili lilizalisha ndani yao kijicho na wivu, ambayo baadaye ilizaa chuki na tamaa, ikijidhihirisha katika unyanyasaji wao dhalimu na kumuuza Yusufu, ambako kulisababisha achukuliwe kuwa mtumwa Misri. {ABN2: 5.2}

5

Miaka mingi baadaye wakati nduguze Yusufu walipokwenda Misri kununua chakula wakati wa njaa ya miaka saba, Yusufu, akiutambua mpango wa Majaliwa katika sarakasi ya ajabu ya maisha yake kutoka utumwa hadi kuwekwa kwenye kiti cha enzi, aliwaambia nduguze “alipojitambulisha” kwao: “Msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku: maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha … na … kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.” Mwa. 45:1, 5, 7. {ABN2: 6.1}

Hivyo Bwana kwa majaliwa alimkweza Yusufu kushiriki kiti cha enzi cha Misri ili kumwongoza Farao awape Israeli ruhusa ya kuingia katika nchi hiyo. {ABN2: 6.2}

Baadaye, ili kuwavuta huko, Yeye alileta miaka saba ya wingi, ikifuatwa na miaka saba ya njaa. Ambapo, Yeye akatuma neno kwa Yakobo kwamba Yusufu alikuwa bado hai. Kwa ile habari ya kufurahisha, ndani ya baba ikazua hamu isiyozuilika ya kumwona mwanawe. Hili na njaa iliyokuwa ikitishia maisha ya ndugu za Yusufu, liliwalazimisha wahamie katika nchi ya Farao, ambamo waliishi kama wafalme. {ABN2: 6.3}

Pasipo kukusudia, hata hivyo, kuwaacha huko milele, Bwana hakuwacha kuishi kwao kuendelee kupendeza kama hapo mwanzoni, wasije wakakataa kumtii Musa wakati atakapokuja na neno kwamba wakati ulikuwa umewadia wa kurejea nyumbani. Lakini Yeye akaleta majaliwa mengine

6

ya kuokoa, wakati huu akiruhusu ugumu ambao hauwezi kuvumiliwa kuwapata, ili kwamba wakati wangeitwa wangeitikia kwa furaha. Hivyo walipaswa kuwa watumwa: na mbaya zaidi, ilibidi wafilishwe watoto wa kiume, kisha wakiendeshwa bila huruma kwa viboko vikali migongoni mwao ili kutengeneza matofali mengi zaidi. {ABN2: 6.4}

Hivyo nguvu ya Roho mseto na mateso ya kutisha kutoka kwa utumwa wao mgumu wa Misri, ilikuwa nguvu iliyowazidi iliyowalazimisha waiache nchi ya mataifa na kurudi katika nchi yao. {ABN2: 7.1}

Kisha, wakiwa njiani kurejea walikutana na majaliwa mengine — kukaa kwao nyikani kwa muda mrefu, miaka arobaini kwa ujumla — ambayo Mungu aliiruhusu kwa kusudi maalum la kutengwa kati yao wasioamini, umati usio mwaminifu ambao uliambatana na hilo Vuguvugu kutoka Misri. Hawa wakiwa wameangamizwa, walionusurika walivuka Yordani kimuujiza, kama walivyokuwa miaka arobaini awali wamevuka Bahari ya Shamu. Huko wakiondoa kati yao yule mdhambi mmoja, Akani, ambaye wakati huo aliinuka kati yao, wakaingia katika nchi ya ahadi na wakawa ufalme mtukufu zaidi katika siku yao. Watumwa wakawa wafalme — hakika ni muujiza ulioje! {ABN2: 7.2}

Kwa kawaida mtu angefikiri kwamba watu ambao Mungu alikuwa amewaokoa kimuujiza kutoka kwa utumwa, na ambao baadaye Alikuwa amewafanya kuwa ufalme kimuujiza, kamwe hawangeweza kuanguka sasa kwa

7

sababu walikuwa na nguvu. Lakini kwa kukosa kuitazama Nguvu yao walianguka tena utekwani! Kwa udhaifu kama watumwa kwa Farao, Mungu alikuwa amewaleta kwa nguvu juu ya mabwana-kazi wao wa Misri; sasa kwa nguvu zao kama mabwana, wenyewe, Yeye aliwaleta chini ya utumishi kwa mataifa yaliyowazunguka! Muujiza maradufu. {ABN2: 7.3}

Hapa upo uthibitisho mwema kwamba Bwana aliwajenga, na pia akawabomoa (2 Nya. 36:13, 23), “kwamba wao” waweze, kama Yeye asemavyo, “kutoka maawio ya jua na kutoka magharibi kwamba hakuna mwingine isipokuwa Mimi. Mimi ndimi Bwana, na hakuna mwingine. {ABN2: 8.1}

Hatimaye, pamoja na utimilifu wa miaka sabini ambayo Yeremia alitabiri (Yer. 29:10), Mungu kwa mara nyingine aliwarejesha Israeli katika nchi yao. Lakini kadiri miaka ilivyokuwa ikipita, vizazi vipya vikichukua nafasi ya vya zamani, Israeli walikosa kuiona Nguvu yao, wakati huu kabisa hivi kwamba wakati Masihi aliyetarajiwa kwa muda mrefu alikuja mwishowe, walimkataa Yeye na kumsulibisha na kumtemea mate! {ABN2: 8.2}

Kwa kulipiza kisasi, Mungu aliugeuza uso Wake kwa hasira, na akawatia mikononi mwa mdhalimu, ambaye aliliharibu hekalu lao na mji wao, akawafukuza kutoka katika nchi yao, na akawaacha taifa lililoachwa, lililotupwa lisilo na Mungu, bila sarafu, bila nchi, watu waliochukiwa mno na mataifa yote tangu siku hiyo hadi hii ya leo! {ABN2: 8.3}

8

Si wote, hata hivyo, walitupiliwa mbali hivyo. Umati kati yao macho yao yalikuwa yamefumbuliwa kwa ukweli kwamba watu wao wakuu walikuwa wakimshutumu Bwana kwa uongo, wakiupotosha unabii kumhusu Yeye, na kuwadanganya watu. Kupitia wale waliosalia waaminifu, Yeye aliuhifadhi uzao wa Israeli. Walimpokea Kristo na kuwa Wakristo, hawa wana waaminifu wa Yakobo walibadilishwa jina lao kutoka kwa Myahudi kuwa Mkristo, kama ilivyoonyeshwa kimbele Mungu alipobadilisha jina la baba yao kutoka kwa Yakobo kuwa Israeli, na babu yao kutoka kwa Abramu kuwa Abrahamu. {ABN2: 9.1}

Kuanza na wanafunzi 120 waliojazwa Roho, kanisa hili la Kiyahudi-Kikristo liliongoa nafsi 3,000 siku ya Pentekoste kwa hotuba moja rahisi, mahubiri yaliyobuniwa na Roho, na kisha “akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.” Matendo 2:47. {ABN2: 9.2}

Kukusanywa huku kukuu kwa nafsi kulimkasirisha Shetani hivi kwamba kwa kulipiza kisasi “alimtesa yule mwanamke [kanisa la Kiyahudi-Kikristo] ambalo lilimzaa mtoto mwanamume. (Ufu. 12:13), ili kulizuia lisifanze waongofu, na kuwazuia wale ambao liliwafanya kuwa waongofu, wasifanye ushirika nalo. {ABN2: 9.3}

(Kweli za msingi kwamba mtoto wa mwanamke Kristo, ambaye “alinyakuliwa hata kwa Mungu,” Aya ya 5, alizaliwa kwa kanisa la Kiyahudi, na ya kwamba kanisa la Kikristo liliibuka kutoka kwa lile la Kiyahudi, kwa uthabiti humsimamisha mwanamke kuwa mfano wa watumwa waaminifu

9

wa Mungu katika yote makanisa ya Agano la Kale na Jipya.) {ABN2: 9.4}

Kama tokeo la kumtesa mwanamke, Shetani alikuwa, kwa kinyume, akimsaidia tu badala ya kulizuia kusudi la Mungu. Kwa kweli, shamba la kanisa (Mat. 13:38) lilikua tu safi “ngano,” “juya” (Aya ya 47) liliwanasa “samaki” wazuri tu, kwa sababu katika mateso kama hayo, ni waaminifu tu waliothubutu kuchukua msimamo wao kwa Ukweli na kuwa washiriki wa dhehebu lililochukiwa. Hivyo, alipoona matokeo ya udhalimu wake, upesi akabadilisha mbinu zake. {ABN2: 10.1}

“Kwa amri za uvumilivu,” asema Gibbon, “yeye [Konstantino] aliondoa uzuizi wa muda ambao ulikuwa hadi hapo umekwamisha maendeleo ya Ukristo; na wachungaji wake wamilifu wengi walipata idhini ya bure, faraja ya uhuru, kuidhinisha kweli zenye manufaa za ufunuo kwa kila hoja ambayo ingeweza kuathiri fikira au kicho cha wanadamu. Uwiano halisi wa dini mbili [Ukristo na Upagani] uliendelea ila kwa muda …. Miji iliyosainia bidii ya kuendeleza uharibifu wa hiari wa mahekalu yao [ya Wapagani] ilitofautishwa kwa fursa za manispaa, na kutuzwa kwa michango maarufu … Wokovu wa watu wa kawaida ulinunuliwa kwa kiwango cha chini, iwapo ni kweli kwamba, kwa mwaka mmoja, watu kumi na mbili elfu walibatizwa huko Roma, mbali na vipimo vya idadi ya wanawake na watoto, na kwamba

10

vazi jeupe na vipande ishirini vya dhahabu, vilikuwa vimeahidiwa na mfalme kwa kila mwongofu.” Hii ilikuwa “sheria ya Konstantino, ambayo iliwapa uhuru watumwa wote ambao wangeukumbatia Ukristo.” — Rumi ya Gibbon, Gombo la 2, uk. 273, 274 (Toleo la Milman). {ABN2: 10.2}

Mara tu Shetani aliposababisha mawakala wake waache kuwatesa Wakristo, na kuanza kushiriki nao, aliwadanganya wafikiri kwamba yeye ni rafiki yao. Kwa hivyo baada ya kutuliza mateso yake, wakalala kiroho; na walipolala, akapanda magugu. {ABN2: 11.1}

Naam, aligeuka kabisa na hata akawalazimisha wapagani wajiunge na kanisa, na hivyo akatapika kutoka kinywani mwake “maji kama mafuriko nyuma ya huyo mwanamke, amfanye kuchukuliwa na mafuriko.” Ufu 12:15. Kuacha kuwatesa wale ambao wangejiunga na kanisa, aligeuka kuwatesa wale ambao hawakutaka, ili ligharikishwe na wapagani wasiokuwa waongofu na hivyo “kuchukuliwa na mafuriko.” Ufu 12:15. {ABN2: 11.2}

Ili kuudumisha umati gizani katika siku za wana-matengenezo, akawawekelea vibanio vyake, kisha akakifungulia wazi kizima-moto chake dhidi ya nuru iliyokuwa ikiwaka, na kiliposhindwa, aliwaweka “wahubiri wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337. {ABN2: 11.3}

Mwenendo huu wenye mafanikio ya juu sana ameufuata siku zote tangu zamani, hadi kama

11

tokeo kanisa leo karibu linyongwe na magugu. Ni, kama kwa mfano, limepenyezwa ndani kwa safuwima humusi (ya tano). {ABN2: 11.4}

“Usiku huo niliota,” anasema mtumwa wa Bwana kwa mtazamo wa ajabu wa hali hii, “kwamba nalikuwa Battle Creek nikitazama nje kupitia kioo cha kando penye mlango, na nikaliona kundi likitembea kuielekea nyumba, wawili wawili. Walionekana wakali na wenye azimio. Naliwajua vyema, na nikageuka kuufungua mlango wa sebule kuwapokea, lakini nalifikiri nitazame tena. Picha ilikuwa imebadilika. Kundi hilo sasa liliwasilisha muonekano wa maandamano ya Katoliki. Mmoja mkononi mwake alibeba msalaba, mwingine mwanzi. Na walipokaribia, yule aliyebeba mwanzi akafanya mduara kuizunguka nyumba akisema mara tatu, ‘Nyumba hii imepigwa marufuku. Bidhaa lazima zitaifishwe. Wamenena dhidi ya amri yetu takatifu.’ Nilishikwa na hofu, na nikakimbia ndani ya nyumba, hadi nje ya mlango wa kaskazini, na nikajikuta katikati ya kundi, baadhi ambao naliwajua, lakini sikuthubutu kusema neno kwao kwa kuogopa kusalitiwa. Nilijaribu kutafuta mahali pa kupumzikia ambapo ningeweza kulia na kusali bila kukutana na macho yenye ari, ya upekuzi popote nilipogeukia. Nilirudia mara kwa mara Iwapo tu ningaliweza kuelewa hili! Iwapo wataniambia lile nimesema, au lile nimefanya!’ {ABN2: 12.1

“Nalilia na kuomba sana nilipoona bidhaa zetu zimetaifishwa. Nilijaribu kusoma huruma au sikitiko kwa ajili yangu kwenye nyuso za walionizunguka, na nikatambua nyuso za baadhi

12

ambao nalifikiri wangesema nami na kunifariji iwapo hawakuogopa kwamba wangetazamwa na wengine. Nilifanya jaribio la kukimbia kutoka kwa umati wa watu, lakini nikaona kwamba nalikuwa nikitazamwa, nikaficha nia yangu. Nikaanza kuomboleza kwa sauti, na kusema, “Iwapo wataniambia lile nimesema, au lile nimefanya!’ Mume wangu, ambaye alikuwa analala kitandani katika chumba kile kile, alinisikia nikiomboleza kwa sauti, na kuniamsha. Mto wangu ulikuwa umelowa kwa machozi, na huzuni ya kufadhaika roho ilikuwa juu yangu.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 578. {ABN2: 12.2}

Ahadi, hata hivyo, ni kwamba mafuriko ya magugu yatasalia ndani tu hadi wakati wa mavuno, wakati wa asili kwa utengo wao — mwisho wa dunia. {ABN2: 13.1}

Alimradi kama Shetani anaweza kuendeleza kazi hii ya mapinduzi kwa kulijaza kanisa mafuriko, yeye kamwe hatasogeza kidole kumtesa yeyote kwa kuungana nalo, asije hivyo basi akauzima ubunifu wake mwovu wa kuweka sega la asali kwa safu zake na mawakala wake — mafuriko, magugu. Ili kuhakikisha mafanikio ya kazi hii kisiri, huwatupa nje wale ambao huthubutu kuishi maisha thabiti ya Ukristo humo kati ya magugu, ilhali akizunguka na kizima-moto chake kikiwa kimewashwa, akijaribu kuzima kila cheche hai ya nuru. {ABN2: 13.2}

Mwishowe, hata hivyo, jinsi unabii hufunua, meza zimepinduliwa, na pambano refu linakoma na Bwana kuwatupa nje na kuwaangamiza (Ufu. 12:16) mawakala wa Shetani, “mafuriko” (magugu, samaki wabaya), na

13

kisha kuingaza nchi kwa utukufu wa malaika Wake (Ufu. 18:1)! {ABN2: 13.3}

Hapa tunaona kwamba kazi inayojongea ya kuondolea mbali mafuriko, na hivyo kuliweka huru kanisa kutoka kwa watu ambao hawajaongoka, ni kazi ya “mavuno” katika “mwisho wa dunia.” Mat. 13:39. Ijayo lazima tuhakiki iwapo “mwisho wa dunia” unaleta enzi ya millenia ya amani au wakati wa taabu ambayo haijawahi kuwapo. Kuamua ni lipi, lazima tuyachunguze matukio yanayofuata. {ABN2: 14.1}

Kwa sababu ni baada ya nchi kuyameza mafuriko, kwamba joka litamkasirikia mwanamke huyo na litaenda zake “kufanya vita juu ya wazao wake waliosalia, hao wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo” (Ufu. 12:16, 17), hakuna kuepuka hitimisho kwamba mavuno, kwa kuondolea mbali kutoka kanisani mafuriko ya Shetani, magugu yake yaliyozidi, hakuleti millenia ya amani. Hakika hapana, lakini badala yake kunaleta gadhabu ya Mungu — wakati wa taabu ambayo haijawahi kuwapo kamwe: wakati ambao watu Wake huko Babeli wanaitwa “watoke kwake” na kuingia katika kanisa Lake lililosafishwa — Ufalme. {ABN2: 14.2}

Mavuno, kwa hivyo, ni kipindi kifupi cha wakati kabla tu, badala ya wakati wa, kuonekana kwa Kristo mawinguni. Ni siku za mwisho za muda wa rehema kwa falme za dunia, — siku na kazi ambazo huuleta mwisho wa dunia. {ABN2: 14.3}

14

Ukweli kwamba wapo masalia (wale ambao wamebaki) wa uzao wa mwanamke, huonyesha kwamba uzao wake umegawanywa katika sehemu mbili, na kwa sababu hiyo nembo huwakilisha makundi matatu ya watu: (1) mwanamke; (2) sehemu ya kwanza ya uzao wake — wale ambao kwa mfano huu sio masalia; (3) sehemu ya pili ya uzao wake — wale ambao ni masalia. {ABN2: 15.1}

Katika nuru ya uwakilishi huu wa nembo, mwanamke mwenyewe, huonekana kuwakilisha sehemu ya mama ya kanisa — wachungaji walioteuliwa na Mungu na kujazwa Roho ambao wanawaleta ndani waongofu waliozaliwa mara ya pili (Yohana 3:3). Sehemu ya kwanza ya uzao wake lazima, basi, iwe malimbuko, watu 144,000, ambao, wametengwa na wadhambi waliokuwa kati yao, wanapelekwa juu ya Mlima Zayuni, hapo kusimama na Mwana-Kondoo (Ufu. 14:1). Kwa hivyo, “wazao wake waliosalia” kwa tukio hili ni wale ambao bado wako duniani wakati Babeli anamwendesha yule mnyama (Ufu. 17). Kwa hivyo ni mavuno ya pili na ya mwisho ambayo yanapaswa kupelekwa katika kanisa lililotakaswa, Ufalme, ambamo hakuna dhambi au hofu kwa mapigo ya Babeli kuwaangukia (Ufu. 18:4). {ABN2: 15.2}

Na sasa, kwa sababu katika ustawi wake wa wakati, mwanamke huwakilisha kila ukasisi unaorithi, kwa hivyo wakati ambao joka linamkasirikia, yeye lazima awakilishe ukasisi wa mwisho uliowekewa mkono, watu 144,000, wale wanaowaleta ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote hadi kwa wa Mungu “mlima mtakatifu Yerusalemu.” Isa. 66:20. {ABN2: 15.3}

15

Pamoja na nuru hii inayoangaza kwenye mada, ukweli unaonekana wazi kwamba baada ya nchi kuyameza mafuriko, baada ya malaika kutenga waovu (“magugu,” samaki “wabaya” kutoka kwa wenye haki (“ngano”) samaki “wazuri” ndani ya kanisa, na kuwapeleka wenye haki hadi Mlima Zayuni (“ghalani,” “vyombo” Mat. 13:30, 48), joka atamkasirikia huyo mwanamke (watumwa wa Mungu), na kama tokeo atafanya vita dhidi ya waliosalia (mavuno ya pili, wale ambao wataitwa kutoka Babeli — Ufu. 18:4). {ABN2: 16.1}

“Katika siku za mwisho,” anasema Mika katika utabiri wake wa wakati ambao malimbuko yatasimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni, na ambapo mavuno ya pili yatatoka Babeli kwenda kwa Mlima Zayuni, “Lakini itakuwa ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. {ABN2: 16.2}

“Na mataifa mengi watakwenda na kusema, njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. {ABN2: 16.3}

“Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, Naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga

Mtoa Jibu Kitabu Namba 2 16

juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivyo.” Mika 4:1-4. {ABN2: 16.4}

Mwisho, kwa hivyo, kanisa la Ufalme lazima “lisimamishwe” kabla Ibilisi awageukie waliosalia, wale ambao wameachwa nyuma na ambao wakati huo wanakusanywa, na dhidi yao anafanya vita kwa sababu wao kukataa kumwabudu yeye katika umbo la mnyama na sanamu yake (Ufu. 13:15). {ABN2: 17.1}

Katika nuru hii iliyoongezeka, mmoja kamwe haoni wazi kabisa kwamba ingawa Bwana ataruhusu mateso yawajie upya watu Wake huko Babeli, Yeye atafanya hivyo tu ili kutimiza mwisho Wake kusababisha watoke katika ufalme wake (kama alivyosababisha watu Wake wa zamani kutoka Misri), na kwenda katika kanisa la Ufalme — mahali pekee kwa dunia ambapo hapatakuwa na dhambi na juu yake uharibifu wa mapigo hautaanguka. (Tazama Ufunuo 18:4). {ABN2: 17.2}

“Hakika hasira ya mwanadamu itakusifu Wewe,” Ee Bwana, na “masalio ya hasira utaizuia.” Zab. 76:10. {ABN2: 17.3}

Utengo wa waovu kutoka kwa wenye haki walipokuwa wakikaa nyikani wakati wa Musa, kabla kuingia katika nchi ya ahadi, haukutekelezwa tu kwa manufaa ya kanisa kwa wakati huo (Israeli wa mfano) bali pia kuwa mfano

17

kwa kanisa la leo (Israeli wa uakisi), ki-mfano ukionyesha utengo ujao wa wabaya kutoka kwa wazuri (Mat. 13:48), kabla ya wazuri kupelekwa kwa Ufalme, nchi yao wenyewe, “ghalani.” Mat. 13:30. “Basi mambo hayo yote,” Kwa hivyo asema Paulo, “yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya ulimwengu.” 1 Kor. 10:11. {ABN2: 17.4}

Kupitia onyo la kimbele, hapa ndani, la majaliwa haya yanayokaribia, Bwana tena anateta na kila mwamini wa Ukweli wa Sasa: {ABN2: 18.1}

“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu Wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; wote wanakusanyana; wanakujia wewe; wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, utajiri wa mataifa utakuwasilia. {ABN2: 18.2}

“Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia vijana wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na uvumba;

18

na kuzitangaza sifa za Bwana. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; watapanda juu ya madhabahu Yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu Wangu. {ABN2: 18.3}

“Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, na merikebu za Tarshishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, kwa ajili Yake Mtakatifu wa Israeli, kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, na wafalme wao watakuhudumu; maana katika ghadhabu Yangu nalikupiga, lakini katika upendeleo Wangu nimekurehemu. {ABN2: 19.1}

“Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.” Isa. 60:1-12. {ABN2: 19.2}

Kwa hivyo, ndugu wapendwa wa Laodekia, ni dhahiri kwamba “wakati hukumu ya upelelezi inaendelea mbinguni, wakati dhambi za waamini waliotubu zinaondolewa kutoka patakatifu, kutakuwa na kazi maalum ya utakaso, ya kuweka mbali dhambi, miongoni mwa watu wa Mungu duniani.” — Pambano Kuu, uk. 425. {ABN2: 19.3}

19

Kisha, “likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ ‘litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. Wakati huo “wale tu ambao wameyastahimili na kuyashindamajaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka kuingia katika Kilio Kikuu.” Mapitio na Kutangaza, Nov. 19, 1908. {ABN2: 20.1}

Kama mwako wa kurunzi katika weusi wa giza la usiku, husimama wazi ukweli kwamba wakati wa taabu mfano wake haujawahi kuwapo, unalipata kanisa huru kwa mafuriko ya magugu, huru kutoka kwa “samaki wabaya,” na kwa hivyo sio tu kumpinga Ibilisi lakini pia likienda mbele likishinda na kushinda katika uwezo mkuu wa Mikaeli, Ambaye kusimama Kwake kunamwokoa “kila mtu atakayepatikana ameandikwa katika kitabu.” Dan. 12:1. {ABN2: 20.2}

Kutoka kwa masimulizi haya ya historia refu ya watu wa Mungu, tunaona kwamba Abrahamu pekee ndiye ambaye Mungu hakumlazimisha, ili kupata matokeo yaliyohitajika, kutumia njia nyingine isipokuwa amri rahisi: “Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi Nitakayokuonyesha.” Mwa. 12:1. {ABN2: 20.3}

Ya Abrahamu imani isiyotiliwa shaka na ya kudumu na utiifu wake usiositasita kwa

20

amri wazi ya Bwana katika kila tukio, ilimfanya kuwa “rafiki wa Mungu,” “baba wa waaminifu,” na nguzo kuu ya ukweli hai, na jina litakalokumbukwa na kuheshimiwa kwa wakati wote na milele. {ABN2: 20.4}

Imani ya Yakobo katika ahadi za Mungu, na hamu yake kubwa zaidi ya kujishughulisha katika mipango ya Bwana na kuitekeleza, ilisababisha yeye kuwa mzazi wa malimbuko au ukasisi wa kanisa la Ufalme — wale wanaosimama na Mwana-Kondoo kwa Mlima Zayuni (Ufu.14:1). {ABN2: 21.1}

Uaminifu wa Yusufu usiobadili msimamo kwa kanuni ulimleta katika hadhi ya upeo, ambayo alikua mtoa-chakula bora zaidi duniani kama mfano wa Kristo, Mtoa-chakula Mkuu wa Kiroho. {ABN2: 21.2}

Musa, katika upole wake (unyenyekevu) na katika azimio lake “afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu, kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda.” (Ebr. 11:25), akainuka kuwa jemedari mkuu zaidi, kiongozi, mkombozi wa nyakati zote, na hata kusimama juu ya mlima wa baraka. {ABN2: 21.3}

Dhabihu ya uhai wa mitume kwa ajili ya Kristo na Ukweli Wake, iliwashindia heshima iliyoinuliwa ya kuwekwa majina yao katika misingi ya Mji Mtakatifu (Ufu. 21:14). {ABN2: 21.4}

Jaribio la bila woga na la uvumilivu la Luther la kuinua Ukweli uliokanyagiwa chini (Dan. 8:11, 12; 11:31),

21

alizalisha Uprotestanti. {ABN2: 21.5}

Bado, Ndugu, Dada, hakuna hata mojawapo ya hadhi hizi za utukufu ni kuu kuliko yako kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. Tunakusihi, kwa hivyo, “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja”! Isa. 60:1. {ABN2: 22.1}

Sasa kwamba kwa upande mmoja Bwana anasihi kwamba uishikilie nuru Yake kuu ya Ukweli na kwa hivyo utengwe na dhambi, ili upate kuokoka kulipiza kisasi Chake, uokolewe kutoka kwa taabu inayokuja, na kuwa na sehemu katika kutangaza Kilio Kikuu cha Jumbe za Malaika Watatu; na ya kwamba kwa upande mwingine Shetani anasihi kwamba ukishikilie kilichochoka sana kizima-moto chake; umeletwa katika bonde la kukata maneno. Sasa imekuja saa Sufuri ya iwapo utamua, ikiwa Bwana ndiye Mungu, ufuate Ukweli Wake wenye nguvu, au ikiwa Baali ndiye Mungu, wafuate watu wake hodari. {ABN2: 22.2}

“Tazama,” asema Mwokozi, “Nasimama mlangoni, Nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, Nitaingia kwake, Nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja Nami.” Ufu. 3:20. {ABN2: 22.3}

Je! Hautafanya, basi, kama walivyofaya watu hawa waaminifu wa zamani, na kuwa watu wakuu wa Mungu leo! O usiruhusu chochote, Ndugu, Dada, kiendelee kuridhia na kukomesha juhudi zako za kuipata ile ahadi sasa — fursa isiyoweza kulinganishwa ya kuwa makuhani na wafalme wa Zayuni! {ABN2: 22.4}

“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anasema …” Ufu 3:22. {ABN2: 22.5}

22

MASWALI NA MAJIBU

TUNAWEZA KUIJUA SAA?

Swali Namba 15:

“Maandishi ya Awali,” uk. 285, husema kwamba Mungu atatangaza siku na saa ya kurudi Kwake. Na “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, uk. 255, huhitimisha kutokana na maelezo yake kuhusu mafuriko kwamba tukio hili la kutia taji la vizazi vyote litakuja Jumatano usiku. Lakini Kristo husema: “… habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hakuna, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba Yangu pekee.” Mat. 24:36. Je! Hizi mbili zawezaje kupatanishwa? {ABN2: 23.1}

Jibu:

Fimbo haiweki kwa vyovyote wakati wa kurudi kwa Kristo. Ijapokuwa huhitimisha kutoka kwa Uchambuzi wa Gharika kwamba Yeye anaweza kuja kwa walio Wake usiku fulani wa katikati ya juma, haisemi hata kwa undani ni usiku wa Jumatano ipi ambao unaweza kuwa. Fimbo haidai kuijua siku hiyo au saa. Na kuhusu taarifa hiyo katika Maandishi ya Awali, maneno ya Kristo katika Mathayo 24:36 hayazuilii kamwe uwezekano Wake kufanya ijulikane siku na saa ya kuja Kwake. Hakika, ingawa Maandiko husema kwamba hata malaika hawaijui saa, bado ikiwa watakuwa tayari kuanza safari na Bwana kwa ujio Wake wa pili, hakika lazima siku moja kimbele wataambiwa kuihusu ili wajiandae na kuanza safari. Na ingawa hakuna mtu sasa anayeijua siku au saa, lakini iwapo Baba anaona inafaa kuitangaza, hatuwezi kukosa kuijua bali tutaijua. {ABN2: 23.2}

23

Isitoshe, huku kuja kwa siri (Mat. 24:36) kunaweza kuwa kwingine kuliko kule kunakojulikana kwa kawaida kama “kuja mara ya pili.” (Kwa uchambuzi zaidi juu ya mada hii, soma Trakti Namba 3, Mavuno, Toleo la 1942, uk. 45-53.) {ABN2: 24.1}

JE! KITI CHA ENZI CHA MUNGU KINACHOKWENDA NI GARI-MOSHI?

Swali Namba 16:

Nimeambiwa kwamba Wadaudi hufundisha kwamba kiti cha enzi cha Isaya 6 ni msafara unaovutwa na gari-moshi linarusha moshi. Je! Wao hufundisha hivyo? {ABN2: 24.2}

Jibu:

Hakuna wazo kama hili popote linapatikana limewekwa katika machapisho ya Fimbo ya Mchungaji, ambamo mafundisho yote ya Wadaudi, yamejikita, kama vile usomaji wa vitabu kwa makini utakavyothibitisha kabisa. {ABN2: 24.3}

Neno “gari moshi” limenukuliwa kutoka kwa Maandiko na humaanisha msafara, “kama lilivyofafanuliwa katika Trakti yetu Namba 1, Ya-Ziada Kabla ya Saa Kumi na Moja, Toleo la 1941, uk. 8. {ABN2: 24.4}

JE! KUNA MITENDE MIKONONI MWA BAADHI, AU MIKONONI MWA WOTE?

Swali Namba 17:

“Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 44, husema kwamba umati mkubwa ukiwa na mitende mikononi mwao ni mavuno ya pili tu ya nchi, ilhali “Pambano Kuu,” uk. 646,

24

ikizungumza juu ya “washindi,” wote husema: “Katika kila mkono unawekwa mtende wa mshindi na kinubi kinachong’aa.” Je! Taarifa hizi zinawezaje kupatanishwa? {ABN2: 24.5}

Jibu:

Umati ambao Fimbo hutolea maelezo na umati ambao Pambano Kuu huzungumzia, ni makundi mawili tofauti, katika maeneo mawili tofauti, na kwa hafla mbili tofauti. La awali, umati wa Ufunuo 7:9, wanayo mitende yao duniani, cha mwisho, umati wa Pambano Kuu, wanapokea mitende yao na vinubi mbinguni. Kweli hizi zinaweza kuonekana wazi kwa kusoma taarifa zinazozungumziwa. {ABN2: 25.1}

NI LINI UTAANZA WAKATI WA MWISHO?

Swali Namba 18:

Utaanza lini “wakati wa mwisho,” ambamo kitabu cha Danieli kinafunuliwa? {ABN2: 25.2}

Jibu:

Malaika ambaye alimuagiza Danieli, alitangaza kwamba kitabu hicho kitafungwa na kutiwa muhuri hadi wakati wa mwisho. Kwa hivyo, si kabla au baada, ila katika wakati wa mwisho, kitabu lazima kifunuliwe. {ABN2: 25.3}

Kipindi hiki kinatambulika kwa ongezeko la maarifa na kwa watu kukimbia “huko na huko.” Danieli 12:4, 9. Maadamu sehemu kubwa ya kitabu cha Danieli sasa inaeleweka,

25

na kwa sababu tuko katika kizazi cha magari, kizazi cha maarifa yaliyoongezeka, na watu wanakimbia huko na huko, ni dhahiri kwamba tunaishi katika “wakati wa mwisho.” {ABN2: 25.4}

Danieli 11:40 hufanya wazi kwamba mwanzoni, sio katika, wakati wa mwisho, Mfalme wa Kaskazini angefanya vita dhidi ya Mfalme wa Kusini. Kwa hivyo, “wakati wa mwisho” lazima ulianza mwishoni mwa karne ya kumi na nane na mwanzoni mwa ya kumi na tisa, pamoja na ushindi wa Mfalme wa Kaskazini. (Tazama ramani katika Trakti yetu Namba 12, Dunia Jana, Leo, na Kesho, Toleo la 1941, uk. 97.) {ABN2: 26.1}

JE! MBONA UNABII KATIKA NAFASI YA UPENDO?

Swali Namba 19:

Je! Mbona Wadaudi hawatumii muda mwingi kufundisha upendo wa Yesu — sehemu muhimu zaidi ya Biblia — badala ya kufundisha mafundisho na unabii? {ABN2: 26.2}

Jibu:

Wadaudi hufuata utaratibu huu kwa sababu ya andiko: “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” 2 Pet. 1:19. Unabii, kwa hivyo hujenga upendo kwa Mungu katika moyo wa mwanafunzi kuliko kitu kingine kinavyoweza. {ABN2: 26.3}

26

Ikiwa, zaidi ya hayo, unabii sio muhimu sana kuliko sehemu zingine za Maandiko, kwa nini basi, Bwana aliwafanya watumwa Wake wauandike kwa wingi? Bila shaka, ni muhimu sana. Kitabu cha Ufunuo, ambacho kimeandikiwa moja kwa moja watu ambao watakuwa wanaishi tu kabla ya kuja kwa Bwana, kimefanyizwa na unabii wa mifano, ambao kuihusu Bwana anasema: {ABN2: 27.1}

“Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufu 1:3. “Tazama, Naja upesi. Heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki …. Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Ufu 22:7, 18, 19. {ABN2: 27.2}

Hakika, upendo wa Yesu ndilo hitaji kuu, lakini kuhubiri juu yake kwa kuyatenga mafundisho na unabii, hakutamnufaisha mtu chochote, kwa sababu kupitia unabii na kwa njia ya mafundisho mtu hujifunza sio tu juu ya upendo wa Yesu lakini pia jinsi ya kumtumikia Yeye. “Kila andiko” anasema

27

Paulo, “lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” 2 Tim. 3:16, 17. {ABN2: 27.3}

Laiti kama makanisa leo yangefunza unabii na mafundisho kwa kuutenga upendo wa Yesu, basi bila shaka Wadaudi wangekuwa wakishughulikia sana upendo wa Yesu kuliko unabii. Lakini kwa sababu kinyume ndio hali, upendo wa Yesu ukiwa umeinuliwa kwa kupuuza unabii, basi hitaji letu la kwanza na kuu ni kujifunza upendo wa Yesu kupitia mafundisho; kisha, mzigo wetu mkubwa utakuwa hivyo kuufundisha. {ABN2: 28.1}

Wakati injili ya upendo hutuvuvia kumpenda Bwana, mafundisho hutufunza njia sahihi ya kumpenda Yeye, na nuru ya unabii huongoza miguu yetu katika njia iliyosonga na nyembamba ya kuelekea kwa mji wa Mungu, kama vile usiku taa za gari hutuonyesha njia ya kurudi nyumbani. Bila huo, bila kuepuka tungepoteza njia, kuanguka, na kujirundika gizani — umati wa uharibifu na kifo, labda. Hivyo wakati tunahitaji moja, tunahitaji sana lingine. Kwa hivyo, Wadaudi huchanganya yote mawili, kufundisha upendo wa Yesu kupitia mafundisho, na njia hadi kwa Ufalme kupitia unabii. {ABN2: 28.2}

28

JE! MIHURI ILIANZA LINI?

Swali Namba 20:

Je! Upo uthibitisho gani wa Biblia kuonyesha kwamba matukio ya Mihuri Saba (Ufu. 4-8) huchukua muda wa wote wa historia ya ulimwengu, ambao ni kinyume na mafundisho ya Dhehebu kwamba hufunika kipindi cha kanisa la Kikristo tu? Je! Hamjui kwamba kitabu kilicho na ile mihuri ni mfano wa vitabu vya Danieli na Ufunuo? {ABN2: 29.1}

Jibu:

Msingi ambao hutulia msimamo wa Dhehebu kwamba mihuri ni matukio ya ki-nabii katika kipindi cha Agano Jipya, ni ufasiri wao wa muhuri wa kwanza, mintarafu Yohana anasema: {ABN2: 29.2}

“Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.” Ufu. 6:2. {ABN2: 29.3}

Andiko hili limefasiriwa bila mamlaka kumaanisha kanisa la Kikristo la kwanza. Kweli kwamba farasi katika maono hayo alikuwa mweupe na kanisa hilo changa safi, aliyempanda akishinda na kanisa linalokua ndani yake zenyewe hazifanyi msingi wa mwamba ambao juu yake hujengwa dhana kwamba matukio ya mihuri yalianza na kanisa la Kikristo. {ABN2: 29.4}

Yohana katika maono alionyeshwa mihuri takribani miaka sitini na tano baada ya Pentekoste, katika kipindi ambacho kanisa lilikuwa tayari linaporomoka kutoka kwa kilele chake na usafi na

29

Ukuaji thabiti. Sauti ikamwambia, “Panda hata huku, Nami nitakuonyeshea mambo ambayo hayana budi kuwako hapo baadaye.” Ufu 4:1. Kwa maneno mengine, matukio ambayo alikuwa karibu kuonyeshwa yalikuwa yatukie katika siku za baadaye kutoka wakati alipata maono. Sasa hebu tutilie maanani aliyoyaona: {ABN2: 29.5}

“Nalikuwa katika Roho,” anasema Yohana, “na, tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na Mmoja ameketi juu ya kile kiti cha enzi …. Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba …. Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana, … Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, Yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile mihuri zake saba. Ufu. 4:2; 5:1, 3-5. {ABN2: 30.1}

Weka alama kwamba matukio yaliyoonyeshwa kwa mifano yangetukia wakati fulani baada ya Yohana kuwa na maono, sio kabla. Zaidi ya hayo, ni wapi katika tukio Maandiko yamewahi kulifananisha kanisa na mtu anayempanda farasi? Iwapo farasi huwakilisha kanisa, basi namna gani mtu? {ABN2: 30.2}

Ni dhahiri, kwamba katika maono haya Yohana alikuwa akitazamia mbele mwanzoni mwa hafla fulani muhimu ambayo ingetukia katika siku za baadaye kutoka kwa wakati

30

alipokuwa na maono badala ya nyuma kanisa lilipoanza. Isitoshe, ilikuwa litukie mbinguni, sio duniani. Kwa sababu maelfu kwa maelfu walikizunguka kiti cha enzi ambacho Jaji Mkuu alikuwa ameketi akikishikilia kitabu kilichotiwa mihuri saba, tukio hilo bila shaka ni kama mwanzo wa Hukumu ya Danieli 7:9, 10 kuliko kama mwanzo wa kuhubiri injili. {ABN2: 30.3}

Akinena kuhusu kitabu ambacho kilitiwa muhuri na mihuri saba, Roho wa Kweli anasema: “Hivyo viongozi wa Wayahudi walifanya uchaguzi wao. Uamuzi wao uliandikwa katika kitabu ambacho Yohana alikiona mkononi mwa Yeye aliyeketi juu ya kiti cha enzi, kitabu ambacho hakuna mtu aliyeweza kustahili kukifungua. Katika ulipizi kisasi wake wote uamuzi huu utatokea mbele yao katika siku ambayo kitabu hiki kitafunguliwa na Simba wa kabila la Yuda.” — Mafunzo ya Yesu kwa Mifano, uk. 294. {ABN2: 31.1}

Katika uhusiano huu kila sehemu kijenzi za mfano wote huunganishwa na historia takatifu na najisi, pia na Ujumbe wa Malaika Watatu wenyewe — kwa hivyo kupeana “uwezo na nguvu” kwa wa mwisho. {ABN2: 31.2}

JE! MUHURI NI NINI?

Swali Namba 21:

Je! Ni nini muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso za watu 144,000 (Ufu. 7:3)? Je! Ni muhuri wa Sabato au kitu kingine? {ABN2: 31.3}

31

Jibu:

Kutiwa muhuri katika Kristo “na Roho Mtakatifu yule wa ahadi,” baada ya “kulisikia neno la kweli” (Efe. 1:13; 4:30), watakatifu ndiposa hutiwa muhuri na Ukweli wa Sasa — ukweli uliohubiriwa kwa siku yao hasa. {ABN2: 32.1}

“Muhuri wa Mungu aliye hai,” Ukweli, ambao kwa huo watu 144,000 wanatiwa muhuri (Ufu. 7:2), ni muhuri maalum, ukiwa sawa na “alama” ya Ezekieli 9. (Angalia Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445; Shuhuda, Gombo la 3, uk. 267; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211). Humdai mmoja kuugua na kulia kwa machukizo ambayo humtia unajisi na ambayo huitia unajisi Sabato na nyumba ya Mungu, haswa dhidi ya kuuza vitabu na kuinua malengo wakati wa ibada za Sabato. Kama watakatifu wanao muhuri huu au alama kwenye vipaji vya nyuso zao, malaika watapita juu yao, sio kuwachinja. Ni sawa na damu iliyokuwa kwenye miimo ya mlango usiku wa Pasaka kule Misri. Malaika ataweka alama kwenye vipaji vya nyuso za wote ambao kwa kuugua juu ya dhambi zao wenyewe, na juu ya dhambi katika nyumba ya Mungu, wanaonyesha uaminifu kwa Ukweli. Kisha malaika wa kuangamiza watafuata, kuwaua kabisa wazee na wachanga ambao wameshindwa kuupokea muhuri. (Tazama Shuhuda, Gombo la 5, uk. 505.) {ABN2: 32.2}

Kwa hivyo, muhuri wa awali humwezesha mpokeaji kufufuka kutoka kwa wafu katika siku ya

32

ufufuo wa mwenye haki, ilhali muhuri wa mwisho humwezesha yule anayelia na kuugua kuokoka kifo na milele kuishi kwa Mungu. {ABN2: 32.3}

JE! KUTIWA MUHURI KUNAFANYIKA? NI NANI WANAOTIWA MUHURI? YEYOTE ASIYETENDA DHAMBI?

Swali Namba 22:

Iwapo ujumbe wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000 umekuwa ukienda kwa kanisa tangu mwaka 1929, je! ni sehemu (au wote) wa watu 144,000 tayari wametiwa muhuri? Pia ikiwa hakuna anayeweza kutiwa muhuri isipokuwa awe huru kwa dhambi na iwapo sasa wengine wanatiwa muhuri, je! wamehitimu zaidi ya kutotenda dhambi? {ABN2: 33.1}

Jibu:

Iwapo kutiwa muhuri hakuendelei kwa sasa, basi ujumbe wa kutiwa muhuri ambao tumebeba tangu mwaka 1929 haungekuwa ukweli wa sasa sasa kuliko utangazaji wa Hukumu ya wafu umekuwa ukweli wa sasa kutoka mwaka 1844 hadi 1929, kama wafu hawakuwa wamehukumiwa katika kipindi hicho. Kwa kweli, basi ujumbe wa kutiwa muhuri na kutia muhuri kwenyewe huenda bega kwa bega sawa kama sindano na kipisha uzi wa chini husafiri pamoja mpaka mshono ukamilike. {ABN2: 33.2}

Bwana anamwamuru malaika aliye na kidau cha wino wa mwandishi “kutia alama katika vipaji vya nyuso za watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake” — kanisani — ili wakati watu walio na silaha za kuchinja wakianza kuchinja, wataweza kupita juu ya

33

wale walio na alama. Hivyo, kuugua na kulia tangu 1929 kwa sababu ya machukizo ndani ya kanisa, umekuwa ushahidi mkuu kwamba tunaishi katika kipindi cha kutiwa muhuri. {ABN2: 33.3}

Na kwa sababu matengenezo hayatukii kamwe bila ufunuo wa ukweli mpya, basi hii “kazi ya kufunga kwa kanisa” lazima iambatane na ujumbe (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na lazima utangazwe kwa wote. Na yule ambaye hawezi kufanya matengenezo wakati anaposadikishwa Ukweli, hatafanya mageuzi baadaye. Kwa hivyo, ujumbe wa kutiwa muhuri unapofanza njia yake kanisani, ni wale tu ambao wanaamka na kufanya matengenezo (kuugua) na kujaribu kuwashirikisha wengine (kulia) ile nuru inayoangaza juu yao, wanaupokea muhuri. Wao wakati huo huhesabiwa kwamba hawana dhambi kupitia ukamilifu wa Kristo unaotolewa kwa niaba yao mpaka watakapopewa “moyo mpya” ulioahidiwa katika Ezekieli 36:26, baada ya hapo hawatakuwa na dhambi milele — milele bila sababu ya kutubu. {ABN2: 34.1}

“Nimwambiapo mtu mbaya, hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako.” Ezek. 3:18. {ABN2: 34.2}

Iwapo mtu hawezi kuachana na dhambi zake sasa, wala hataziacha baadaye. Na kwa vile hawezi

34

kumdanganya Mungu, anaachwa bila muhuri, ingawa anaweza kuwa anakiri Ukweli. Mkristo wa kweli, hata hivyo, hajigambi kamwe kuwa ameafikia ukamilifu, kwa maana analo lengo la juu zaidi na zaidi anaposafiri kwenye njia nyembamba. Na anapoendelea kumkaribia Yeye ambaye ukamilifu huanzia na kumalizikia, husema kwa sauti na nabii: “Ole wangu! kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami nakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi.” Isa. 6:5. {ABN2: 34.3}

Kwa hivyo ukweli ni kwamba hakuna mtu aliyeafiki ukamilifu ambao atapata katika hali yake ya baadaye lakini mfuasi wa kweli wa Kristo amepata ukamilifu wa hali ya sasa. Yeye hayuko dakika moja nyuma ya wakati au inchi moja chini ya hatua ya juu zaidi inayoweza kuafikiwa kwa sasa. Yeye hustawi kwa ukamilifu kama jani la mhindi lilivyo kutoka siku unapoota hadi siku unapovunwa. {ABN2: 35.1}

Ikiwa dhambi yoyote itendwe na mtu kama huyo, haitakuwa inayojulikana au ya makusudi. “Basi yeye ajuaye kutenda mema wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.” Yakobo 4:17. Atahukumiwa “kwa sababu ya uovu alioujua.” 1 Sam. 3:13. Kwa hivyo, kwake yeye anayejitolea kwa kila fursa ya kuujua Ukweli na anayezingatia kwa bidii matakwa yake yote, inahesabiwa kwake kuwa haki (Rumi. 4:3) — kuishi bila dhambi. {ABN2: 35.2}

35

JE! MAVUNO SIO MWISHO WA DUNIA?

Swali Namba 23:

Je! Fundisho lako la utengo wa magugu kutoka kwa ngano kanisani linawezaje kupatanishwa na taarifa ambayo husema: “Magugu na ngano vitakua pamoja hadi wakati wa mavuno; na mavuno ni mwisho wa muda wa rehema….Wakati kazi ya injili imekamilika, mara hapo unafuata utengo kati ya wazuri na wabaya, na hatima ya kila daraja inaamuliwa milele”? — “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” uk. 72, 123. {ABN2: 36.1}

Jibu:

Naam, kwa mujibu wa taarifa inayohojiwa “mavuno” ni mwisho wa muda wa rehema unaotukia mwanzoni, sio baada ya kufungwa kwa muda wa rehema. Na ukweli kwamba Hukumu ya Upelelezi hutenda kazi kwa kesi ya mtu baada ya kazi ya maisha yake katika uhusiano na wokovu kukoma na wakati muda wa rehema ungalipo, ni ushahidi mwingine kwamba “mavuno” ni sehemu ya mwisho ya wakati wa rehema. Hii ina umoja na maelezo ya Yeremia, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” Yer. 8:20. Huonyesha kwamba mavuno ni kipindi cha wakati chenye mwanzo na mwisho, na ya kwamba katika wakati wake wanadamu wanaokolewa. Na Maandishi ya Awali, uk. 118, hufichua kwamba Malaika wa Tatu ndiye anayefanya uvunaji, ilhali Mathayo 13:30 huonyesha pia kwamba malaika huyatenga magugu kutoka kwa ngano katika “wakati wa mavuno.” {ABN2: 36.2}

36

Kwa hivyo amri ya Kristo, “Viacheni vyote vikue hadi wakati wa mavuno,” huelekeza hadi kwa siku yetu, “wakati wa mwisho,” kipindi ambamo mavuno yatatekelezwa na “magugu” kutengwa kutoka kwa “ngano.” {ABN2: 37.1}

Hivyo kwa maana zote halisi “mavuno” hakika ni “mwisho wa dunia” — mwisho wa waovu. {ABN2: 37.2}

Njia pekee ambayo mtu anaweza kuelewa vinginevyo Mafunzo ya Kristo kwa Mifano ni kushindwa kutambua kwamba dunia iko hivi sasa haswa “mwishoni mwa wakati.” Kushindwa kuelewa ni nini mwishoni mwa wakati humaanisha hakika, mmoja kwa hivyo anashindwa kwa usahihi kuziunganisha mada zinazohusiana na mavuno. {ABN2: 37.3}

Biblia hufundisha kwamba Bwana “atauchunguza Yerusalemu [kanisa] kwa taa, na kuwaadhibu watu walioganda juu ya sira zao: wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya” (Zef. 1:12); yaani, Yeye atawaadhibu wale ambao kwa matendo yao husema: “Bwana hajishughulishi sana kuhusu yale tuyafanyayo”; ilhali katika ukweli wa onyo zito Mungu anatangaza: “Nitauchunguza Yerusalemu,” sio bila uangalifu na gizani, lakini kwa uangalifu na taa za nuru. {ABN2: 37.4}

“Kwa maana, angalieni, Nitatoa amri, Nami nitaipepeta nyumba ya Israeli katika mataifa yote, kama vile ngano ipepetwavyo katika ungo lakini hata chembe moja iliyo ndogo haitaanguka chini. Wenye dhambi wote katika watu Wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, mabaya hayatatupata wala kutuzuia.” Amosi 9:9, 10. {ABN2: 37.5}

37

“Itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake. Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa Bwana.” Isa. 24:13, 14. {ABN2: 38.1}

Maandiko haya yanaonyesha kwamba baada ya kanisa kutikiswa kwa ujilio wa Bwana, basi washiriki wake waaminifu ambao wameachwa “wataimba kwa utukufu wa Bwana.” Upepeto utakuwa umelifanya kanisa liwe linavyopaswa kuwa. {ABN2: 38.2}

“Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.” Mal. 3:2. {ABN2: 38.3}

“Katika upepeto mkuu utakaotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti [idadi] wa Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha ya kwamba pepeto Lake li mkononi Mwake, Naye atausafisha uwanda Wake kabisa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {ABN2: 38.4}

Kwa hivyo, Maandiko na Roho ya Unabii hutangaza kwamba Yeye Mwenyewe atalitakasa kanisa, na ya kwamba likiwa limetakaswa hivyo “Mataifa wataiona” yake “haki, na wafalme wote” wake “utukufu.” Isa. 62:2. {ABN2: 38.5}

JE! NI LINI YEYE ATAYATENGA MAGUGU KUTOKA KWA NGANO?

Swali Namba 24:

“Mafunzo ya Kristo kwa Mifano” uk. 123, husema: “Wakati kazi ya injili imekamilika.

38

hapo mara moja hufuata utengo kati ya wema na wabaya.” Je! utengo uliotajwa hapa hautatukia kwa ujio wa pili? {ABN2: 38.6}

Jibu:

Utengo ambao utafanyika wakati Kristo anakuja mara ya pili, ni Wake kuwapeleka watakatifu mbinguni pamoja Naye (Yohana 14:3; 1 Thes. 4:17) na kuwaacha waovu, wamekufa hapa duniani (2 Thes. 2:7, 8). Kwa njia hii kuja Kwake kwa pili kunaleta utengo kimwili. Lakini utengo wa utangulizi ambao utatukia kabla ya ujio wa pili wa Kristo, ni wa wakati wa kuja Kwake kusikoonekana wakati anapowaweka “kondoo” upande Wake wa kulia na “mbuzi” upande Wake wa kushoto (Mat. 25:32, 33, 13:30, Ufu. 18:4; Mat. 13:48). {ABN2: 39.1}

“Naliona watakatifu,” anaandika Dada White, “wakihama mijini na vijijini, na wakiungana pamoja katika makundi, na kuishi katika maeneo ya faragha zaidi. Malaika waliwapatia chakula na maji, ilhali waovu walikuwa wanateseka kwa njaa na kiu. Kisha naliwaona watu wakuu wa dunia wakishauriana, na Shetani na malaika zake wakijishughulisha kuwazunguka. Nikaiona hati, ambayo nakala zake zilitawanywa katika sehemu mbali mbali za nchi, zikitoa amri kwamba isipokuwa watakatifu waisalimishe imani yao ya kipekee, waiache Sabato, na kuiadhimisha siku ya kwanza ya juma, watu walikuwa huru baada ya muda fulani, kuwaua. Lakini katika saa hii ya

39

majaribio watakatifu walikuwa watulivu na makini, walimtegemea Mungu, na kuiegemea ahadi Yake kwamba njia ya kuokoka itafanywa kwa ajili yao. Katika sehemu zingine, kabla ya wakati wa amri hiyo kutekelezwa, waovu waliwavamia watakatifu ili kuwaua; lakini malaika katika umbo la watu wa vita waliwapigania. Shetani alitamani kuwa na fursa ya kuwaangamiza watakatifu wa Aliye Juu; lakini Yesu aliwaagiza malaika Zake kuwalinda. Mungu angeheshimiwa kwa kufanya agano na wale ambao walikuwa wameishika sheria Yake, machoni pa wapagani waliowazunguka; na Yesu angeheshimiwa kwa kuwahamisha bila wao kuonja mauti, wale waaminifu, na waliongojea ambao walikuwa wamemtarajia Yeye kwa muda mrefu. “ Maandishi ya Awali, uk. 282, 283. {ABN2: 39.2}

Ukweli kwamba kinabii watakatifu walionekana katika makundi wao pekee yao kabla ya ujio wa pili wa Kristo, huthibitisha tena kwamba utengo kati ya mtakatifu na mdhambi unafanyika kabla ya kuonekana Kwake. Utengo ambao unasababishwa na kuja kwa Kristo mara ya pili, hata hivyo, bado ni mkubwa zaidi. {ABN2: 40.1}

Kwa hivyo, ingawa ujumbe katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 123, unahusu ule utengo(wenye haki wakiwa wanapelekwa mbinguni na waovu kuachwa kwa dunia) kwa ujio wa pili wa Kristo, bado haupingi kwa vyovyote utengo wa “magugu” kutoka kwa “ngano” (Mat. 13:30),

40

au “kondoo” kutoka kwa “mbuzi” (Mat. 25:32). {ABN2: 40.2}

Na sasa, kwa sababu ukweli wa kipekee wa Hukumu ya Upelelezi mbinguni ni darubini ya Waadventista wa Sabato, hebu tuitumie kwa mada ya utengo. {ABN2: 41.1}

Sehemu hiyo ya Hukumu ya Upelelezi ya walio hai, ambayo kwayo inaamua ni nani ambao dhambi zao zitafutwa na kama tokeo, wapewe uzima wa milele, inaenda sambamba duniani na kazi ya malaika aliye na “kidau cha wino wa mwandishi,” ambaye ameagizwa “kutia alama” (muhuri) kwa kila mmoja ambaye huugua na kulia kwa sababu ya machukizo yote ndani ya Yuda na Israeli — kanisa. Na kazi ya wale wengine watano ambao wanafuata kuwachinja wote ambao hawana “alama” (muhuri), inaenda sambamba mbinguni na kufutwa kwa majina ya wadhambi kutoka katika Kitabu cha Uzima. (Angalia Ezekieli 9; Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211). {ABN2: 41.2}

Hivyo tunaona kwamba kazi hii maradufu ya kinabii ya utengo wa majina ya wadhambi kutoka kwa majina ya wenye haki katika patakatifu, na kuwatenganisha wadhambi kutoka kwa wenye haki kanisani, ni sawa na kazi iliyoamriwa katika mifano: kutenga magugu kutoka kwa ngano (Mat. 13:30); samaki wabaya kutoka kwa wazuri (Mat. 13:48); wale ambao hawana vazi la harusi kutoka kwa wale walio nalo (Mat. 22:1-13);

41

wale ambao hawajazidisha talanta zao kutoka kwa wale ambao wamezidisha (Mat. 25:20-30). {ABN2: 41.3}

Kwa sababu mitengo hii inayolingana inatukia wakati wa Hukumu ya Upelelezi, kabla ya harusi, kutawazwa, mapokezi ya ufalme (Dan. 7:9, 10, 13, 14), ni dhahiri kwamba mavuno na Hukumu ni mapacha, na ya kwamba hufanyika kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema — wakati ambapo Bwana analijia ghafla hekalu Lake ili “kuwatakasa wana wa Lawi.” — Mal. 3:1-3. Na kama Hukumu ya wafu inafuatwa na Hukumu ya walio hai, kwa hivyo Hukumu ya kanisa inafuatwa na Hukumu ya ulimwengu. Na “ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasiotii injili ya Mungu utakuwaje?” (1 Pet. 4:17) — wakati Jaji Mkuu anaketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu Wake, wakati mataifa yote yanakusanyika mbele Yake, wakati kama mchungaji Yeye anawabagua kondoo Wake (Mat. 25:31-46). {ABN2: 42.1}

JE! MCHINJO WA EZEKIELI TISA NI HALISI?

Swali Namba 25:

“Fimbo ya Mchungaji” hufundisha kwamba mchinjo wa Ezekieli 9 ni halisi. Je! hauwezi kuwa uharibifu kama ule unasababishwa na kinachoitwa eti “matendo ya Mungu” — mitetemo ya ardhi, njaa, tauni, mapigo saba ya mwisho, au kama hayo? {ABN2: 42.2}

Jibu:

Wajumbe watano ambao wataangamiza waovu

42

kanisani sio nguvu za maumbile bali watu wenye silaha za kuchinja mikononi mwao. Wao ni viumbe visivyo vya kawaida, sio vitu vya asili. Kwa hivyo hawawezi kuwakilisha mitetemo ya ardhi, njaa, au mengine kama hayo. {ABN2: 42.3}

Wala hawawezi kuwa malaika saba na mapigo saba ya mwisho, kwa maana malaika hawa ni saba kwa idadi, si watano. Isitoshe, hawana “silaha za kuchinjia” mikononi mwao, ila vitasa. Bado zaidi, mapigo yanaanguka Babeli (Ufu. 18:4), ilhali mchinjo wa Ezekieli 9 unatukia ndani ya Yuda na Israeli (Ezek. 9:9). {ABN2: 43.1}

Ezekieli 9, uwe ni halisi au wa mfano, matokeo yake ni utengo kati ya wema na wabaya, magugu na ngano, ndani ya kanisa (Yuda na Israeli), kama vile mapigo mwishowe yanavyofanya Babeli (Ufu. 18:4). Na kwa sababu mapigo ni halisi, basi ni vipi mchinjo usiweze kuwa halisi? {ABN2: 43.2}

Malaika aliye na kidau cha wino wa mwandishi ataweka alama kwenye vipaji vya nyuso za wote ambao huugua na kulia kwa sababu ya machukizo, kisha malaika watawachinja wote wakongwe na wachanga (Ezek. 9:4-6). {ABN2: 43.3}

“Kanisa — hekalu la Bwana,” ndilo “la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao.

43

Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu Wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaza sauti zao kamwe kama tarumbeta kuonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa walio bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {ABN2: 43.4}

Kama ilivyo katika Pambano Kuu, uk. 656, ni ulinganifu tu usio wa moja kwa moja unaweza kuvutwa kati ya mchinjo wa Ezekieli 9 na kuanguka kwa mapigo, kwa sababu mwisho wa kawaida (kifo) unawapata waovu katika kanisa la Laodekia na waovu katika makanisa ya Babeli. Na ni wale tu ambao husema, “hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani,” hufikiri mchinjo si halisi. {ABN2: 44.1}

JE! NI NANI MWANAMKE NA MASALIA WAKE?

Swali Namba 26:

Je! Ufunuo 12:13-17 humaanisha nini? {ABN2: 44.2}

44

Jibu:

“Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 12:13-17. {ABN2: 45.1}

Karibu Wakristo wote hukubali kwamba ufasiri thabiti wa “mwanamke” aliyetajwa hapa, ni kwamba yeye huashiria kanisa. Na ukweli kwamba alimzaa mtoto mwanamume, Kristo, huonyesha kwamba yeye kwa hivyo ni mfano wa kanisa katika angalau kipindi cha Ukristo. {ABN2: 45.2}

Wakati joka lilikuwa likimtesa kupitia kwa makuhani wa Kiyahudi waliodanganywa ambao walimkataa Kristo kama Masiya, “kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria,

45

isipokuwa hao mitume. Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.” Matendo 8:1-4. {ABN2: 45.3}

Kwake yeye, alipewa mabawa ya tai mkubwa — njia yake ya kusafiri hadi nyikani. Na ikiwa kinyume cha shamba la mizabibu (“nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda mche Wake wa kupendeza” — Isa. 5:7), nyikani kwa kawaida huashiria nchi za Mataifa. Mitume, kwa hivyo, katika kutimiza unabii huu waliamriwa, na kupewa mabawa, upesi kwenda kuhubiri kwa mataifa yote. {ABN2: 46.1}

“Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.” Matendo 13:46-49. {ABN2: 46.2}

46

Alipoona haya, yule nyoka akajaribu kuharibu manufaa ya mwanamke huyo kati ya watu wa Mataifa: “akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.” Ufu. 12:15. {ABN2: 47.1}

Mtu yeyote anaweza kuona kwamba “mafuriko” haya yanaweza kuwakilisha tu kanisa linaloingizwa ghafla wapagani ambao hawajaongoka ambao, kama wakati wa Konstantino na kwa miaka mingi baadaye, walichukuliwa hata kwa wingi na kulazimishwa kubatizwa. Katika mifano ya Kristo “mafuriko” haya yameelezwa, lakini chini ya jina tofauti, “magugu.” Na ukweli dhahiri kwamba wangali wengi sana kanisani, hulazimisha utambuzi wa uchungu kwamba nchi bado haijayameza mafuriko. {ABN2: 47.2}

“Mafuriko” na “magugu” ni mifano sawa. Kumezwa kwa mafuriko, kwa hivyo, ni sawa na kuyachoma magugu kama inavyofahamika katika mfano wa mavuno (Mat. 13:30). {ABN2: 47.3}

Mbali na hilo, Waufunuo huonyesha wazi kwamba ni mpaka baada ya mafuriko kumezwa na nchi, baada ya wale hawajaongoka “kuchinjwa” na kuzikwa, na kanisa hivyo kutakaswa, ndipo joka litafanya vita vyake vikali dhidi ya masalia wa uzao wa yule mwanamke. Kwa hivyo, wakati wa mavuno ndani ya kanisa, wakati ambapo nchi inayameza mafuriko, ni kabla ya joka kufanya vita dhidi ya masalia. {ABN2: 47.4}

47

“Mazao” yaliyowekwa ndani ni tokeo la mavuno. Wakati watu 144,000, malimbuko (Ufu. 14:4), wameletwa ndani, na magugu (mafuriko) yanaangamizwa (yanamezwa) kutoka kati yao, watu 144,000 wanapelekwa hadi Mlima Zayuni, ambapo wakati huo wanaunda kanisa Mama, yule mwanamke aliyevikwa taji yenye nyota kumi na mbili, chini ya ulinzi wa Mwana-Kondoo, Yule aliye pamoja nao. Hivi akiwa amelindwa, yu salama kutoka kwa joka kufanya vita dhidi yake. Kwa hivyo yeye anafanya vita dhidi ya “masalia” wake tu, wale ambao bado wataletwa ndani — mavuno ya pili ambao bado wametawanyika ulimwenguni, mbali kutoka kwa Mlima Zayuni. Hiki kilele cha vizazi vyote kilitabiriwa wazi wazi na wote wawili Isaya na Mika: {ABN2: 48.1}

“Lakini katika siku za mwisho,” atangaza Mika, “ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. Mika 4:1, 2. (Tazama pia Isaya 2). {ABN2: 48.2}

Kutoka kwa maandiko haya, inaonekana wazi kwamba Mlima Zayuni unakuwa makao makuu ya kazi ya injili ya mwisho hapa duniani, baada ya wakati watu 144,000 wanawasili huko, na katika

48

wakati ambapo joka anafanya vita dhidi ya masalia, “kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu” — sio tena kutoka kwa Baraza Kuu, au kutoka Kituo cha Mlima Karmeli. {ABN2: 48.3}

Wakati huo mataifa mengi yatasema, “njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake.” Mika 4:2. {ABN2: 49.1}

NI NANI ALIYEZITAMBUA SAYARI ZILIZOONEKANA KATIKA MAONO?

Swali Namba 27:

Katika historia yake ya Vuguvugu la Uadventista, Mzee Loughborough husimulia: “Katika mwezi wa Novemba, 1846, kongamano lilifanyika huko Topsham, Maine, ambapo Mzee Bates alikuwepo. Katika mkutano huo Bi. White…alipokuwa katika maono ambayo yalikuwa sababu ya mzee Bates kuridhika kabisa kuhusu asili yake ya Kiungu….Bi. White, alipokuwa katika maono, alianza kunena kuzihusu nyota, akitoa maelezo ya mikanda ya waridi yenye urangi-rangi iliyokuwa iking’aa ambayo aliiona ikipita kati ya sehemu za baadhi ya sayari, na kuongeza, naona miezi minne.’’ Aa,’ akasema Mzee Bates, ‘anatazama Mshtarii!’ Kisha baada ya kufanya msogeo kana kwamba anasafiri angani, alianza kutoa maelezo ya mikanda na pete kwa uzuri wazo mbalimbali, akasema, ‘Ninaona miezi saba.’ Mzee Bates akasema, ‘Anaelezea Zohali.’ kisha akasema, ‘Naona miezi sita,’ na mara moja akaanza maelezo ya ‘mbingu zilizofunuliwa,’ na utukufu wake…” — “Vuguvugu Kuu La Ujio Wa Pili, uk. 257, 258. {ABN2 : 49.2}

Darubini zenye nguvu zaidi na picha za nyota za leo zimewawezesha wanajimu kugundua kwamba Mshtarii una miezi tisa, na

49

Zohali kumi. Miezi mitano ya nyongeza ya Mshtarii iligunduliwa kati ya mwaka 1892 na 1914. Mwezi wa nane wa Zahali uligunduliwa mwaka 1848, wa tisa mwaka 1899, na wa kumi mwaka 1905. Na baada ya maono yake, imegundulika kwamba Urano ina minne badala ya miezi sita. {ABN2: 49.3}

Katika nuru ya kweli hizi za kinajimu unawezaje kuukabili uvuvio wa maandishi ya Bi. White? {ABN2: 50.1}

Jibu:

Kitabu, Vuguvugu Kuu La Ujio Wa Pili, uk. 257, 258, hakisemi kwamba Dada White alizitaja sayari hizo, lakini kinarudia yale yaliyodaiwa kusemwa na wale waliokuwapo wakati wa tukio la maono ya sayari hizo. Hakithibitishi, isitoshe, hata hakielekei kusema kwamba Dada White alikubaliana na ubunifu mahsusi wa majina ambao Mzee Bates (kwa kuzingatia maarifa ya unajimu ya wakati huo) alipeana kwa sayari ambazo wakati huo yeye alionyeshwa. Ilikuwa kawaida kwake, hata hivyo, kuzitambua kama alivyofanya, kwa maana zote zililingana sawa sawa katika mafundisho ya unajimu ya siku hiyo. Hivyo, kwa sababu tu yeye, katika wakati wa shauku ya bidii isiyo kwa mujibu wa ufunuo wa Mungu, alijitwalia daraka kutambua na kuweka majina kwa yale ambayo Mungu hakutambulisha au kuweka jina, hayatoi hata taswira ya uaminifu kwa mashtaka ambayo swali linapendekeza dhidi yake. {ABN2: 50.2}

Yeye hakika hakujua chochote kuhusu majina ya sayari hizo; Mzee Bates alijua machache, na sisi leo tunajua machache sana ikiwa

50

yapo. Iwapo na lini Mungu ataona inafaa kutangaza majina yazo, utambuzi Wake kuzihusu utakuwa sawa; kwamba sisi tujue. {ABN2: 50.3}

JE, YOTE YA NENO KWA KUNDI NDOGO NI SAHIHI?

Swali Namba 28:

“Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, uk. 151, nukuu kutoka katika “Neno kwa Kundi Ndogo,” mintarafu tarakimu ya yule mnyama mwenye pembe mbili. Kwa maana, hata hivyo, kijitabu hicho kimeandikwa kwa sehemu na Mzee James White na kwa sehemu na Dada White, tungependa kujua ni nani aliyeandika taarifa inayohojiwa, maana ikiwa ni kutoka kwa Mzee White, hatuoni jinsi inavyoweza kubeba mamlaka ambayo “Fimbo” huambatanisha kwayo. {ABN2: 51.1}

Jibu:

Ingawa nukuu hiyo kwa uhakika ni kutoka kwa kalamu ya Mzee White, ukweli kwamba Neno kwa Kundi Ndogo kiliandikwa kwa ushirika naye na mkewe, huonyesha kwamba yeye aliidhinisha vifungu vyake katika kijitabu hicho kama vyenye mamlaka sawa na vyake. La sivyo hangaliweza kamwe kuruhusu vya James kuchapishwa kama moja na vyake. Ukweli wowote, zaidi ya hayo, yeye au wale waasisi wengine katika siku hizo walikumbatia, wao waliupokea mwanzoni kupitia kwake. Kwa maneno mengine, katika kuandika kile alichokifanya katika Neno kwa Kundi Ndogo alikuwa akipanga upya tu yale ambayo yalifunuliwa kupitia kwa Dada White. Ukweli wa hili unaonekana upesi kutokana na kauli kwamba taarifa yake juu ya namba ya yule mnyama, ukurasa wa 19, huthibitisha kikamilifu maelezo yake kwenye ukurasa wa 9, sehemu ambayo

51

Fimbo hunukuu. Kupokea, kwa hivyo, mitazamo ya mtu kwa mada hiyo ni kupokea ya yule mwingine. {ABN2: 51.2}

JE! UMEKUWAPO MSETO WA MWANADAMU NA MNYAMA?

Swali Namba 29:

“Tangu kwa gharika,” husema Bi. White, “kumekuwa na mseto wa wanadamu na wanyama, kama inavyoweza kuonekana katika aina zisizokoma za wanyama, na katika jamii fulani za wanadamu.” — “Zawadi za Kiroho,” Gombo la 3, uk. 75 (1864). Je! hili lawezekanaje? {ABN2: 52.1}

Jibu:

Ukweli kwamba ufasiri uliopeanwa kwa taarifa ya Dada White juu ya mseto, husababisha upuuzi wa kibaolojia kama vile tu wajinga na wapumbavu zaidi wanavyoweza kukubali, ni ushahidi bora kwamba maneno yake yamepotoshwa sana. Lolote lile mtu anaweza kusisitiza kwa maana ya kisarufi ya kirai hicho, “mseto wa mwanadamu na mnyama,” ukweli unadumu wazi katika nuru ya lile ameandika kwingine kwa mada hiyo, na kwa msingi wa busara, na vile vile kwa uelewa wake mpana wa Biblia, pamoja na ulimbukeni wake wa mapema kwa maneno, kwamba anajaribu kuonyesha aina mbili za mseto — mmoja kati ya jamii tofauti za wanadamu, ule mwingine kati ya nasaba mbalimbali na aina tofauti za wanyama: kwa mfano, Mwebrania na Mkanaani, na punda na farasi, na kusababisha

52

machotara katika mfano mmoja, na aina ya mseto katika mfano mwingine. Yeye mwenyewe anaelezea: “Kila aina za wanyama ambazo Mungu ameumba zilihifadhiwa ndani ya safina. Aina zilizokanganywa ambazo Mungu hakuumba, ambazo zilisababishwa na mseto, ziliharibiwa kwa gharika.” — Zawadi za Kiroho, Gombo la 3, uk. 75. {ABN2: 52.2}

MBONA HAYAFANYIKI MAENDELEO BORA?

Swali Namba 30:

Kwa mtazamo wa ukuu wa kazi na ufupi wa wakati, mbona ujumbe wa kutia muhuri haufanyi maendeleo bora? {ABN2: 53.1}

Jibu:

Lau kama haungetoka Misri katika wakati wa Musa umati mseto, Vuguvugu la Kutoka lingaliingia ndani ya nchi ya ahadi katika majuma machache. Lakini kwa sababu katika jaribio la Vuguvugu hilo walifuata wengi ambao walikuwa wamepagawa na roho tofauti na ile ya Vuguvugu la Kalebu na Yoshua lilianguka miaka arobaini nyuma ya ratiba ya kuingia katika nchi ya ahadi! {ABN2: 53.2}

Na ingawa kazi ya Yesu wakati wa ujio Wake wa kwanza haikuwa kubwa sana kama kazi yetu sasa, bado ilikuwa ya umuhimu mkubwa zaidi na ya muda mfupi kuliko wetu. Inavyoonekana, hata hivyo, haikufanya maendeleo wakati wowote tunapoangalia kwamba wote walimwacha Yeye katika hukumu Yake, na kwamba Petro, mwenye bidii zaidi

53

kati ya mitume hata alilaani na kuapa kwamba hakuwa mwanafunzi wa Kristo. Lakini, kinyume na matokeo yote ya kuonekana kushindwa, Yesu alitangaza alipokuwa akining’inia msalabani, kwamba kazi Yake ilikuwa imekamilika. {ABN2: 53.3}

Basi, pia, baada ya kufufuka Kwake, Yeye alisafiri kwenda juu, aliacha wafuasi wachache waliokuwa wameongoka nusu ili kuiendeleza hiyo kazi. Kama hayo yalikuwa ndio matokeo ya Yohana Mbatizaji na bidii ya Yesu isiyochoka. Kwa hivyo, kati ya umati uliobatizwa na Yohana na Yesu, walikuwapo, siku ya Pentekoste, wanafunzi mia moja na ishirini katika nia moja kupokea umiminwaji wa Roho wa Mungu. {ABN2: 54.1}

Hakika, sio tu ndogo na duni wakati huo ilivyoonekana kazi hiyo kuwa, lakini pia kutowezekana kuendelea mbele. Walakini, wale waliotilia shaka kati ya umati wa watu walipoona kisababu kilichoonekana kushindwa kabisa katika kusulubishwa kwa Yesu, walijitenga kutoka kati ya waaminifu. Na wakati wale waliosalia wafuasi Wake walipokosa kujiamini wenyewe, wakaukana ubinafsi, na kumtafuta Bwana kwa dhati wakati ambao hapakuwa ndani yao angalau tumaini la kuendeleza kazi, walimpatia Bwana nafasi ya kudhihirisha uwezo Wake mkuu na kuiendeleza kazi Yake kwa haraka sana kwamba kwa hotuba moja ziliongoka nafsi elfu tatu kwa siku moja. Basi kila siku baada ya hapo waliongezwa tu “wale ambao walipaswa kuokolewa” — kama vile

54

waliokuwa wameongoka kabisa. Ndivyo kazi ya injili ilivyoanza kukua haraka, mara Bwana akapata kundi la watu ambalo Yeye angeliamini na kulitumia. {ABN2: 54.2}

Vivyo hivyo, Vuguvugu la Ujio, mara tu baada ya Kongamano la Minneapolis katika mwaka 1888, lingekuwa limeanzisha kazi ya malaika wa Kilio Kikuu, lakini kama tokeo la wengi kutoamini katika Shuhuda za Roho wa Mungu, hicho “kilio” kilizimwa kwa miaka arobaini, wakati Vuguvugu lilikengeuka “kuelekea Misri.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {ABN2: 55.1}

Katika mwaka 1930, Mungu alizungumza tena na watu Wake, kama alivyozungumza na Israeli katika siku za Yoshua, lakini sasa, kama wakati huo, wapo kati yetu wapelelezi kumi, kina Kora, Dathani, na Abiramu, na Akani — wote kama hao wanaopenda kutoa ripoti zenye kuvunja moyo, watafutao wadhifa, ambao hutamani vazi la Babeli, fedha, na kabari ya dhahabu. Na kama tokeo, sisi pia tumezuiwa, na tutaendelea kuzuiwa hadi Bwana adhihirishe uwezo Wake na kuondoa kati yetu wale wanafiki, kutufanya tuwe huru kutoka kwa dhambi na wadhambi, kama katika wakati wa Kora na kama katika wakati wa Akani, na husema kwetu kama alivyomwambia Yoshua “Vuka mto huu Yordani, wewe na watu hawa wote mkaende mpaka nchi Niwapayo, wana wa Israeli.” Yos. 1:2. {ABN2: 55.2}

Ingawa kwa nyakati zingine tunavunjika moyo sana kadiri tunavyoona kati yetu wasio waaminifu,

55

wanaotilia mashaka, watafuta makosa, umati wa wanaojiinua nafsi, pamoja na wale waliomwacha Bwana; na wale ambao wanapowekwa hukumuni kwa sababu ya imani yao hata hulaani na kuapa kwamba wao sio wafuasi wa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji; pamoja na wale ambao huonekana wanaamini na ambao hutangaza kwamba husimama imara kwa ajili ya ujumbe, lakini ambao wanarusha miamba kwetu na kwa kazi yetu — ingawa hakika hatuna shukrani kwa jambo hili, bado kwa vyovyote hatujakata tamaa ila badala yake tumefanywa kufurahi kusimama peke yetu kwa ukweli na haki wakati wengi wanatuacha. {ABN2: 55.3}

Hatuwezi ila kwa unyenyekevu kupaza sauti, Ee Bwana, utusaidie kusimama wakweli Kwako, ingawa ulimwengu wote ukuache Wewe, au hata ingawa lazima tufe kama mitume iwapo ikihitajika. Tuweze kuwa kama Danieli, Shadraki, Meshaki na Abednego — tukisimama wakweli hata kwa hatari ya uhai wetu ili Uweze kuwa na nafasi ya kutukomboa kutoka kwenye tundu la simba, au kutoka kwenye tanuru la moto, inapohitajika, hivyo kufanya Mwenyewe ujulikane kwa ulimwengu wote kupitia uaminifu wetu. Tuweze kuwaka moto kwa bidii ya Nuhu tunaposhiriki katika ujenzi wa safina ya leo, ilhali ndugu wengi wanaoukiri ujumbe wanahoji na kukosoa kazi na msimamo wetu (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690) na kukwamisha maendeleo ya kazi, na ilhali wengine hutushutumu kwa kutawala sana. {ABN2: 56.1}

56

Kamwe tusije tukasema, “Bwana anakawisha kuja Kwake”; au, “Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi”; au “Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona majitu, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao majitu; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.” Hes. 13:31-33. Tusije tukawa wapumbavu na hafifu hivyo. {ABN2: 57.1}

JE! MBONA KUPEKECHA PALE PASIPOHITAJIKA?

Swali Namba 31:

Iwapo Wadaudi hufikiri wanao ujumbe, mbona hawaridhiki kwenda zao na kuwacha wengine waende zao? Je! Mbona waupekeche ujumbe wao kanisani mwetu? {ABN2: 57.2}

Jibu:

Kufuatilia historia ya kanisa katika vizazi vyote, tunapata kwamba iwapo wote wangechukua msimamo sawa kama yule aliyeuliza, Ukweli unaoendelea kamwe usingalikuwa umelifikia kanisa katika kipindi chochote. Kama wajumbe wa Mungu nyakati za zamani wangalishindwa kupekecha ujumbe wao katika makanisa yao wenyewe, vipi, basi, jumbe mbalimbali za matengenezo zingewafikia watu Wake? Je! Yeye hajali maslahi yao zaidi kuliko Alivyo katika mataifa? Yohana Mbatizaji, Yesu, na mitume, wote waliyatoa mhanga

57

maisha yao ili kupeleka ujumbe wao katika makanisa yao. Mbona, basi, Wadaudi wasifanye vivyo hivyo? {ABN2: 57.3}

“Dhidi ya watu hawa [Wycliffe, Huss, Luther, Tyndale, Baxter, Wesley], mateso yaliwaka kwa hasira ya ukatili, bado hawakukoma kutangaza ukweli. Vipindi tofauti katika historia ya kanisa kila kimoja kimetiwa alama kwa ustawi wa ukweli fulani maalum, mwafaka kwa mahitaji ya watu wa Mungu kwa wakati huo. Kila ukweli mpya umefanyiza njia yake dhidi ya chuki na upinzani; wale waliobarikiwa kwa nuru yake walijaribiwa na kuhukumiwa. Bwana hutoa ukweli maalum kwa ajili ya watu katika udharura. Ni nani anayeweza kukataa kuutangaza? Yeye huwaamuru watumwa Wake kutoa mwaliko wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu. Hawawezi kusalia kimya, isipokuwa kwa hatari ya nafsi zao.” — Pambano Kuu, uk. 609. {ABN2: 58.1}

Ndiposa, hatuthubutu kukataa kuuchapisha ukweli maalum wa Wadaudi kwa ajili ya kanisa leo. {ABN2: 58.2}

KAZI NDANI AU NJE?

Swali Namba 32:

Kwa upande mmoja mimi hupata vitabu vyako vikifunza waamini wake wasiache nafasi za kanisa Mama, ilhali kwa upande mwingine huviona vikisababisha taabu isiyokoma kwa kanisa. Je! Unapatanishaje fundisho lako na mfano wako? Mbona usitumie wakati wako kwa juhudi za uinjilisti, ukizileta nafsi zinazokosea kwa maarifa ya Ukweli, na kuachana na kanisa? {ABN2: 58.3}

58

Jibu:

Kwa uhakika tunaamini kwamba huu sio wakati wa kutengana, lakini kwa kweli wa kusonga mbele pamoja. Na ujumbe ambao tunapeleka kwa kanisa, sio tu kwamba hauna fundisho lolote au funzo ambalo laweza kutuamuru tuache nafasi zake na kuwa kijidhehebu tofauti, lakini kinyume na hilo hutukataza kabisa kufanya hivyo. Kwa sababu hizi, tangu mwanzo tumekataa kwa dhati, hata mbele ya kutendewa vibaya, kuacha kanisa Mama. {ABN2: 59.1}

Kwa kadiri tunavyohusika, kwa hivyo, vita na mgawanyiko uliopo ni wajibu wa ndugu viongozi wa Dhehebu, na sio wetu, kwa maana tunatekeleza tu kanuni dhahiri na mfano wa Bwana kamwe kutousalimisha Ukweli. Na wao wenyewe hukiri kwamba tunapaswa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Juu yao, kwa hivyo, hutua hatia nzito ya kurudia upumbavu mbaya wa Wayahudi wakati wa Kristo, kwa kuukataa ujumbe wa ile saa, “wasiingie wenyewe” katika upanuzi wa Ukweli, wakiwazuia wale ambao wangetaka kuingia, na kuwatupa nje wale wanaoingia ndani. {ABN2: 59.2}

Kwa hivyo, kutumia wakati wetu kuuhubiria ulimwengu ilhali tunalipuuza kanisa, litakuwa tendo la jinai, moja la uhaini wa juu kwa wote Mungu na watu Wake. Kanisa lazima liokolewe kwanza kutoka kwa

59

hali yake ya Ulaodekia ya kuwa “nyonge, na lenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Hilo, sio ulimwengu, linakaribia kutapikwa nje. Hilo “ndicho chombo pekee juu ya nchi ambacho Yeye huweka heshima Yake kuu” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 15. {ABN2: 59.3}

Lakini katika hali yake ya kusikitisha ya upofu na ufukara kama ulivyowekwa wazi na Shahidi wa Kweli (Ufu. 3:14-18), halifai kabisa kwa kazi lililopewa, na lazima liokolewe kutoka kwa udanganyifu wake wa kusikitisha kabla liweze kuwa kimbilio salama na mvuto wa kuokoa kwa wale watakaojiunga na nafasi zake. Mungu akiliacha katika hali yake ya Ulaodekia ambamo sasa linadhoofikia, sio tu lenyewe lingepotea lakini, kwa matokeo, ndivyo pia itapotea dunia yote pamoja nalo. Yeye lazima kwa hivyo aliamshe au vinginevyo aliinue lingine lifanye kazi ambayo inangojea kufanywa. {ABN2: 60.1}

Waza, hata hivyo, ni ilioje furaha ya milele ambayo ingekuwa Yeye kuliinua na kulifanya lifae na kulitumia kwa utukufu Wake, badala ya kuachana nalo! Kwa hivyo kabla ya kuliinua lingine kama suluhisho la mwisho, Yeye anajaribu kuliokoa, na Yeye ataliokoa, jinsi Anavyoahidi: {ABN2: 60.2}

“Shetani atafanya miujiza yake kudanganya, ataweka utawala wake kama mkuu. Kanisa linaweza kuonekana kama karibu kuanguka, lakini halianguki. Linadumu, ilhali watenda dhambi katika Zayuni watapepetwa nje.

60

Makapi yanatengwa kutoka kwa ngano ya thamani. Huu ni msiba wa kutisha, lakini ni lazima utukie. Hamna ila wale ambao wamekuwa wakishinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na neno la ushuhuda wao watapatikana na waaminifu na wakweli, bila doa au waa la dhambi, bila hila vinywani mwao. Masalia ambao hutakasa nafsi zao kwa kutii ukweli hukusanya nguvu kutoka kwa mchakato wa kujaribu, wakionyesha uzuri wa utakatifu kati ya mazingira ya uasi…. {ABN2: 60.3}

“Suala kubwa lililo karibu sana litawang’oa wale ambao Mungu hajawateua, Naye atakuwa na ukasisi safi, wa kweli, uliotakaswa kwa ajili ya mvua ya masika.” — B-55-1886. {ABN2: 61.1}

Ikiwa Bwana — ambaye Yeye Mwenyewe alipokuwa duniani alitumia wakati Wake wote katika juhudi ya kipekee ya kuliokoa kanisa Lake lililokuwa limepotea wakati huo — kututuma ulimwenguni badala ya kanisa Lake lililopotea leo, Yeye hangekuwa tu anawaleta ndani wasio na hatia waangamizwe na wenye hatia, lakini pia ingekuwa kupindua kabisa mazoea Yake mwenyewe na kupingana na maagizo Yake mwenyewe kwa mitume Wake kwamba wahubiri ukweli wa sasa kwa kanisa kwanza (Mat. 10:5, 6). {ABN2: 61.2}

Kwa rehema na upatano kwa utaratibu Wake wa milele, kwa hivyo, Alikusudia kwamba “wakati hukumu ya upelelezi inaendelea mbinguni, wakati dhambi za waamini waliotubu zikiwa zinaondolewa katika hekalu, itakuwapo kazi maalum ya utakaso, ya kuondolea mbali dhambi, miongoni mwa watu [Wake] duniani.”

61

Hii ndio kazi yake maalum. “Kisha kanisa ambalo … wakati wa kuja Kwake [Yeye] kulipokea Mwenyewe litakuwa kanisa tukufu, lisilo na waa, au kunyanzi, au kitu kingine kama hicho.” — Pambano Kuu, uk. 425. {ABN2: 61.3}

“Bwana hatendi kazi sasa, kuzileta nafsi nyingi katika ukweli, kwa sababu ya washiriki wa kanisa ambao hawajawahi kuongoka, na wale waliokuwa wameongoka lakini wakakengeuka. Ni mvuto gani hawa washiriki wasiomcha mungu watakuwa nao kwa waongofu wapya? Je, hawataufanya usiokuwa na maana ujumbe aliopeana Mungu ambao watu Wake wanapaswa kuutangaza?” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 371. {ABN2: 62.1}

Lakini wakati waliokengeuka na ambao hawajaongoka, magugu, yameondolewa mbali, “kisha litaonekana kama asubuhi, zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango.” — Pambano Kuu, uk. 425. {ABN2: 62.2}

Naam, wa mataifa waaminifu ni lazima na watahubiriwa injili, lakini “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mat. 10:6) lazima watafutwe kwanza. Shukrani ilioje, kwa hivyo, na wanapaswa kuwa na ushirikiano ulioje, na itakuwa, wanapogundua kwamba badala ya kuwa matajiri na waliojitajirisha na hawahitaji chochote, kwa kweli ni “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na

62

vipofu, na uchi” — wahitaji wa kila kitu; na ya kwamba Bwana anawangojea waamke kwa ukweli ili Aweze kuwafanya wawe kama wanavyopaswa kuwa. {ABN2: 62.3}

Kwa sababu hizi, Mungu anasema sasa tufanye kazi ndani ya ushirika wa Walaodekia badala ya nje. Na lile ambalo Yeye husema, ndilo Yeye humaanisha, na tusithubutu kutotii, bila kujali lile watu wanaweza kusema au kufanya. {ABN2: 63.1}

JE! FIMBO BADO HUFUNDISHA “MAMBO YALE YALE”?

Swali Namba 33:

Katika mwanzo wake, “Fimbo ya Mchungaji” ilikubaliana na Roho ya Unabii kwamba “masalia wa uzao wake ni watu 144,000 ambao joka atafanya vita dhidi yao.” — “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, uk. 265. Leo, miaka kumi baadaye, hufundisha kwamba “‘masalia wa uzao wake’ katika hali hii ni wale ambao bado wako ulimwenguni wakati Babeli anamwendesha mnyama (Ufu. 17).” — “Msimbo wa Nembo,” Julai-Desemba, 1941, uk. 9. Lini ilikuwa sawa — wakati huo au sasa? {ABN2: 63.2}

Jibu:

Iwapo mtu hawezi kukataa kwamba watu 144,000, malimbuko, ni washiriki wa kanisa, basi mtu hawezi kukataa kwamba wao ni wa uzao wake. Na wanapoendelea kuwa hai kutoka kwa mchinjo wa wasio waaminifu katikati yao, kwa hivyo wao ni “masalia” — kile ambacho kimesalia. Kwa ishara iyo hiyo ya mantiki, Bila shaka ni sawa kwamba kwa sababu mwanamke wa Ufunuo 12 ni mfano wa kanisa hadi mwisho wa wakati, basi mavuno ya pili ya uzao wake, wale ambao watasalia

63

hai kutoka kwa maangamizo ya waovu ulimwenguni kote, pia ni “masalia.” {ABN2: 63.3}

Dhahiri, kwa hivyo, taarifa zote mbili ni sawa. Jambo pekee la utofauti kati yazo ni kwamba wakati ile iliyo katika Gombo la 2 ilifanywa, Fimbo haikuwa na nuru ya ziada ambayo baadaye iliivuvia ile iliyo katika Msimbo, na ambayo huonyesha kwamba watu 144,000 na umati mkubwa ni masalia: wa awali kwa sababu ya kuokoka kutoka kwa mchinjo wa Bwana kwa wasio waaminifu kanisani (Isa. 66:19), na wa mwisho kwa sababu ya kutoitwa watoke Babeli hadi baada ya wale wa awali wamekwenda katika nchi ya Israeli (Isa. 66:20), pia kwa sababu ya kusalia hai baada ya waovu, ambao wameitwa watoke kati yao, wameangamia. {ABN2: 64.1}

JE! JIONI NI MWISHO AU MWANZO WA SIKU?

Swali Namba 34:

Trakti Namba 10, “Ishara ya Yona,” Toleo la 1942, husema kwamba jioni ndio mwisho, sio mwanzo, wa siku ya masaa ishirini na nne. Lakini Mwanzo 1:5 husema ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya kwanza. Je, Taarifa hii haiweki jioni katika sehemu ya kwanza ya siku? {ABN2: 64.2}

Jibu:

Inakubaliwa kwamba kwa mujibu wa Mwanzo 1:5 jioni hakika ndio sehemu ya kwanza ya siku. Kwa mfano, Ijumaa usiku ni

64

sehemu ya kwanza ya Jumamosi, na Jumamosi usiku ni sehemu ya kwanza ya Jumapili. Ukweli huu wa Biblia ulitambuliwa na watu wa Mungu tangu zamani. Lakini tangu mapema katika wakati wa Biblia hadi leo, neno “jioni” limetumiwa kutaja sehemu ya mwisho ya siku — alasiri (Kut. 12:6; 16:13; Marko 14:12, 13, 15, 17; Yohana 20:19). Kwa hivyo istilahi hii, ingawa hutumika kwa kawaida, haibadilishi kwa vyovyote ukweli kwamba usiku unaofuata “jioni” na kutangulia siku, unapaswa kuhesabiwa kama sehemu ya kwanza ya mzunguko wa masaa ishirini na manne, maana “ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya sita.” Mwa. 1:31. Ni katika nuru hii kwamba taarifa iliyo katika ukurasa wa 17 wa Trakti Namba 10, inapaswa kueleweka. {ABN2: 64.3}

JE! NI KWELI?

Swali Namba 35:

Tungependa kujua iwapo ni kweli jinsi tumesikia kwamba sera ya Mlima Karmeli ni kushughulikia kwa usiri kabisa mawasiliano na maombi yote ya vitabu. {ABN2: 65.1}

Jibu:

Ni mojawapo wa maadili yasiokiukwa ya ofisi ya Mlima Karmeli kwamba hakuna mawasiliano au maombi ya vitabu huwekwa wazi kwa umma isipokuwa kwa tukio au ruhusa ya mwandishi. {ABN2: 65.2}

KATIKA MUHURI UPI?

Swali Namba 36:

Je! Vipi kutiwa muhuri kwa watu 144,000 (malimbuko) na umati mkubwa

65

(mavuno ya pili), yote ifanyike chini ya muhuri wa sita, jinsi Ufunuo 7 huashiria kutoka kwa msimamo wake kati ya matukio ya kufungwa kwa muhuri wa sita na kufunuliwa kwa muhuri wa saba? {ABN2: 65.3}

Jibu:

Ufunuo 7, ukija kama unavyofanya kati ya matukio ya kufunga kwa muhuri wa sita na kufunguliwa kwa wa saba, kwa kawaida huonekana kuweka kutiwa muhuri kwa watu 144,000 na umati mkubwa kati ya matukio ya muhuri wa sita. Lakini uchunguzi wa makini wa mihuri saba, huthibitisha kwamba sura ya sita huunganika na sura ya nane kwa mwendelezo. Kwa hivyo sura ya saba i katika mabano, na haijizuii yenyewe kwa muhuri wa sita au wa saba. {ABN2: 66.1}

Kwa maneno mengine, ingawa sura ya saba hufuata matukio ya muhuri wa sita, na kutangulia matukio ya muhuri wa saba, sura yenyewe haipaswi kuchukuliwa kwa mpangilio wa wakati zaidi ya ilivyo sura ya 12 hadi 22 kuchukuliwa kama sehemu ya muhuri wa saba kwa sababu tu kwamba zimeandikwa baada ya kufuatia matukio yake. Wakati wa matukio ya sura ya saba lazima yathibitishwe kwa kulinganisha, kwa njia ile ile kama vile matukio ya sura ya kumi na mbili hadi ya ishirini na mbili. {ABN2: 66.2}

NI NANI WANAKIMBILIA MILIMANI?

Swali Namba 37:

Iwapo watu wa Mungu wako katika Ufalme wakati wa Kilio Kikuu, vipi wanaweza kuwekwa gerezani

66

au kukimbilia milimani wakati huo, jinsi Roho ya Unabii husisitiza (“Pambano Kuu,” uk. 626)? {ABN2: 66.3}

Jibu:

Wakati inaeleweka kwamba watu 144,000 ni malimbuko tu, watangulizi au walinzi wa mbele wa umati mkubwa wa mavuno ya pili, utata wa swali mara moja unatatuliwa. Malimbuko yanasimama salama na Mwana-kondoo, juu ya Mlima Zayuni (katika Ufalme). Kwa hivyo wale watakaopata kimbilio milimani, na wale watakaowekwa gerezani, wanaweza tu kuwa miongoni mwa mavuno ya pili — wale watakaoupokea ujumbe wakati wa Kilio Kikuu, lakini ambao kwa wakati huo bado hawajafika katika Ufalme. (Tazama Trakti yetu Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho Toleo la 1941, uk. 45-49.) {ABN2: 67.1}

JE! ATATOKA LINI HEKALUNI?

Swali Na. 38:

“Fimbo ya Mchungaji” huonekana kusema kwamba Yesu ataondoka Patakatifu Mno wakati wa utekelezwaji wa mchinjo wa Ezekieli 9, ilhali “Maandishi ya Awali,” uk. 36, huonekana kusema kwamba Ataondoka hapo baada ya kazi Yake katika hekalu kukamilishwa, na kisha yatakuja mapigo saba ya mwisho. Unazipatanishaje hizo mbili? {ABN2: 67.2}

Jibu:

Ingawa mwandishi wa Maandishi ya Awali husema kwamba Kristo hatatoka hekaluni kabla ya Yake “kazi kukamilishwa,” bado kwingine

67

anaandika: “Watajilisha makosa na kasoro na mapungufu ya wengine, ‘hadi,’ akasema malaika, ‘Bwana Yesu atainuka kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, na Kujivika mavazi ya kisasi, na kuwashangaza kwa karamu yao isiyo takatifu; na watajikuta hawajajiandaa kwa karamu ya jioni harusi ya Mwana-Kondoo.’” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690. {ABN2: 67.3}

Kulitazama swali katika nuru ya taarifa zote mbili, tunaona kwamba Kristo anatoka hekaluni kwa wakati fulani katika “kukunjua kwa chuo.” Kulijia kanisa, analipata likiwa na mawaa na pasipo kuwa tayari kumlaki Yeye, ila likiwa limezama dhambini, lakini kwa kinaya likijilisha makosa, kasoro, na mapungufu ya wengine. {ABN2: 68.1}

Sasa shida iliyo mbele yetu sio kupatanisha Fimbo na Maandishi ya Awali, bali Maandishi ya Awali na Shuhuda. Hizi zinapatanishwa moja kwa moja wakati inaeleweka kwamba Kristo hutoka hekaluni zaidi ya wakati mmoja: Mara moja baada ya “kazi ya kufunga kwa kanisa” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na tena baada ya kazi ya kufunga kwa ulimwengu. {ABN2: 68.2}

NI NANI AMETANGA MBALI NA MIPAKA YA ZAMANI?

Swali Namba 39:

Kanisa la Waadventista wa Sabato limefundisha siku zote kwamba namba 666 hutumika kwa mnyama kama chui (Ufu. 13:1-10). Lakini

68

“Fimbo ya Mchungaji” hufundisha kuwa hutumika kwa mnyama mwenye pembe mbili (Ufu. 13:11). Je! Roho ya Unabii haituambii waziwazi kwamba “hakuna mstari wa ukweli ambao umewafanya Waadventista wa Sabato kuwa walivyo, udhoofishwe”? — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 17. Na haitoi onyo zaidi: “Ole wake atakayesogeza jiwe au kuvuruga kigingi cha” jumbe hizo? — “Maandishi ya Awali,” uk. 258. {ABN2: 68.3}

Jibu:

Roho ya Unabii kweli hufundisha hivyo, na kuwa katika upatano wa asilimia mia moja nayo kwa jambo hili kama kwa mengine yote, Fimbo kwa uangalifu inaondoa kwa Ukweli takataka ambazo wanadamu wameufunikia, na kwa hivyo inaurejesha kwa mng’ao wake wa kale. Imefanya hivyo kwa ukweli mintarafu namba 666. {ABN2: 69.1}

Ingawa namba hii ni kweli kwamba imetumika muda mrefu kwa mnyama kama chui, matumizi hayo hayakuanzishwa na waasisi wa dhehebu la Waadventista wa Sabato, wala hawakufunza hivyo katika siku za mwanzo za Vuguvugu. Badala yake, ililetwa ndani kutoka nje na kufumwa katika utando wa mafundisho ya Waadventista wa Sabato licha ya ukweli ya kuwa Roho wa Kweli alitangaza kupitia kwa waasisi wa Dhehebu kwamba ile namba hutumika kwa yule mnyama mwenye pembe mbili: {ABN2: 69.2}

“Mnyama” asema Mzee G.W. Holt, akiandika katika siku za mwanzo za ujumbe, “aliye na vichwa saba na pembe kumi ndiye anayetajwa, na nafikiri ile sanamu, ni mnyama mwenye ‘pembe mbili kama mwana-kondoo,’

69

lakini ‘akanena kama joka.’ Namba yake ni 666.” — Ukweli Wa Sasa, Gombo la 1, Namba 8, Machi, 1850. {ABN2: 69.3}

“Utawala wa mwisho unaowakanyagia chini watakatifu,” asema Mzee White, akiandika karibu wakati uo huo, “unaletwa kwenye mtazamo katika Ufu. 13:11-18. Namba yake ni 666.” — Neno Kwa Kundi Ndogo, uk. 9. {ABN2: 70.1}

Na mwishowe, Dada White katika kuthibitisha msimamo huu, alitangaza: “Naliona wote ambao hawatapokea alama ya Mnyama, na Sanamu yake, kwenye vipaji vya nyuso zao au mikononi mwao, ‘hawataweza kununua au kuuza. Naliona kwamba namba (666) ya Sanamu ya Mnyama ilifanyizwa; na ya kwamba ni mnyama aliyeibadilisha Sabato, na Sanamu ya Mnyama alikuwa amemfuata, na kuitunza ile ya Papa na sio Sabato ya Mungu.” — Neno Kwa Kundi Ndogo, uk. 19. (Kumbuka: Namba 666 iliwekwa kwenye mabano na mhariri wa Neno Kwa Kundi Ndogo.) {ABN2: 70.2}

Hapa tumepata kutoka kwa vinywa vya mashahidi watatu thibitisho kamili kwamba fundisho la sasa la Dhehebu mintarafu namba 666 halikuanzishwa wala kuidhinishwa na baba waasisi; kwamba, kwa kweli, halikuwa mojawapo ya mistari ya ukweli, wala hata mojawapo ya mawe au vigingi vya ujumbe, ambao Mungu aliwapatia watu hawa. Isitoshe, Biblia huiweka namba hiyo kwa yule mnyama mwenye pembe mbili. Kumbuka kwamba sifa zote zinazomhusu yule mnyama mwenye pembe kumi zimeelezwa katika Ufu. 13:1-10, na kwamba zote zinazomhusu

70

mnyama mwenye pembe mbili zimeelezwa katika Ufu.13:11-18. Kwa sababu ile namba hufunga maelezo ya yule mnyama mwenye pembe mbili, haiwezi kwa busara kutumika kwa yule mnyama mwenye pembe kumi. {ABN2: 70.3}

Huu ni mojawapo wa ukengeufu kutoka kwa Ukweli, ambao ulisababisha Dada White mbali sana nyuma (1882) kupiga kelele: “Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekwa ikiangaza kutoka kwa neno Lake na katika Shuhuda, na zote mbili zimedunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {ABN2: 71.1}

“Tumetanga mbali na mipaka ya zamani. Hebu turudi. Ikiwa Bwana ni Mungu, mtumikie: iwapo ni Baali, mtumikie. Unachagua kuwa upande gani?” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 137. {ABN2: 71.2}

MTAZAMO WA AWALI AU WA MWISHO?

Swali Namba 40:

“Maandishi ya Awali,” uk. 75, husema: “Wakati umoja ulikuwapo, kabla ya 1844, karibu wote walikuwa na umoja

71

kwa mtazamo sahihi wa ‘ya kila siku;’ lakini katika mchafuko tangu 1844, mitazamo mingine imekumbatiwa.” Mbona, basi, Trakti Namba 3, “Hukumu na Mavuno,” Toleo la 1942, uk. 31, hutoa mtazamo mwingine ambao haukujulikana hata wakati huo. Je “sadaka ya kila siku” ya Danieli 8:12 haimaanishi “madhabahu ya dhabihu ya Yehova”? {ABN2: 71.3}

Jibu:

Kweli, Maandishi ya Awali husema kwamba kabla ya mwaka 1844 karibu wote walikuwa wameungana kwa mtazamo sahihi, lakini hausemi mtazamo huo ulikuwa nini, na hakuna mtu anayeonekana kujua sasa. Inawezekana ilikuwa kwamba “ya kila siku” haikuwa “swala la jaribio,” au kwamba haikueleweka kabisa, na ya kwamba wote ndiposa walikubaliana kwa usawa kwamba chini ya hali za wakati huo, kimya kilikuwa tunu; hivyo, hilo lingekuwa “mtazamo sahihi” kuchukulia katika hali hiyo. Kwa kweli, upo uwezekano wa mitazamo mingi ambayo kwayo wangeweza kuwa waliungana, lakini ambayo haingekuwa lazima imetegemea ufasiri wazi wa neno “ya kila siku” lenyewe. Jambo moja ni hakika, hata hivyo: kama wangekuwa na ukweli wa “ya kila siku,” mwandishi wa Maandishi ya Awali angaliuchapisha, na wangekuwa wanaufundisha; na sisi sote tungejua leo ni nini. {ABN2: 72.1}

Kwamba ule mtazamo haukuwa hivyo kuifanya “ya kila siku” kuwa “madhabahu ya dhabihu ya Yehova,” imethibitika kimbele kwa ukweli kwamba Maandishi ya Awali, uk. 74, husema kwamba “neno ‘dhabihu’ lilitolewa kwa hekima ya Mwanadamu, na sio la maandiko.” Na bila kuambatanishwa na neno

72

“sadaka,” neno “kila siku” haliwezi lenyewe kuunganishwa na madhabahu yoyote kama hayo. {ABN2: 72.2}

Ufasiri wa ile Trakti wa “ya kila siku” ni ya Kimaandiko na ya kihistoria, na kwa hivyo inaweza kuwa tu “fundisho zuri.” {ABN2: 73.1}

MBONA MAJINA MATATU KWA UFALME ULIOGAWANYIKA?

Swali Namba 41:

Tafadhali unaweza kuelezea tofauti katika majina, Yuda, Efraimu, na Israeli? {ABN2: 73.2}

Jibu:

Katika maana yake ya asili na kamili, neno “Israeli” liliwatambulisha wana wa Israeli kutoka siku za Yakobo baba yao, hadi mwisho wa utawala wa Mfalme Sulemani. {ABN2: 73.3}

Itakumbukwa, hata hivyo, kwamba baada ya kifo cha Sulemani, ufalme uligawanyika mara mbili (1 Wafalme 11:11, 12; 12:19, 20, 21). Mgawo mmoja, uliojumuishwa na makabila mawili, ulichukua sehemu ya kusini ya Nchi ya Ahadi, ilhali ule mgawo mwingine, uliojumuisha makabila kumi, ulichukua sehemu ya kaskazini. Wa awali walichukua jina “Yuda” kwa sababu kabila la Yuda liliutawala; wa mwisho walichukua jina “Israeli” kwa sababu lilikuwa linajumuisha makabila mengi. Kwa ufalme huu wa makabila kumi, kwa hivyo, jina “Israeli” huuhusu wakati linapotumiwa katika maana yake ya pili, ukiondoa makabila mawili, Yuda na Benyamini. {ABN2: 73.4}

73

Jina “Efraimu,” kwa maana ya jumla, pia huyatambulisha makabila kumi au ufalme wa kaskazini (Isa. 7:1, 2) kwa sababu kabila la Efraimu liliutawala. Kwa hivyo majina “Israeli” (linapotumiwa tu kwa makabila kumi) na “Efraimu” hutumika kwa mgawo wa kaskazini, na jina la mtu “Yuda” kwa mgawo wa kusini, wa watu wa kale wa Mungu. {ABN2: 74.1}

JE! UFALME UTASIMAMISHWA KABLA YA MILLENIA?

Swali Namba 42:

“Pambano Kuu,” uk. 322, 323, hufundisha kwamba “mpaka kwa ujio wa Kristo binafsi ndipo watu Wake waweze kuupokea ufalme….Lakini Yesu atakapokuja, atawapa kutokufa watu Wake; kisha anawaita waurithi ufalme ambao mpaka sasa wamekuwa warithi tu. Je, Unaweza kusaidia kuoanisha Biblia na “Fimbo ya Mchungaji” na vifungu hivi na vingine katika maandishi ya Dada White kuhusu kuusimamisha Ufalme? {ABN2: 74.2}

Jibu:

Ingawa fundisho la Ufalme haliwezi kuonekana kamili kabisa katika miwani ya maandishi ya Dada White kama lilivyo chini ya miwani ya Fimbo, mmoja hapa asithubutu kukataa kijuujuu mojawapo, lakini lazima alinganishe mitazamo yote miwili ya fundisho hilo chini ya miwani bora ya Biblia. Lazima azingatie kwamba hatujapewa leseni ya kupatanisha Biblia na maandishi mengine yoyote, lakini tumeagizwa kuyapima mengine yote Kwayo. {ABN2: 74.3}

74

Kwanza kabisa, ili kutenda haki kwa Maandiko, kwa maandishi ya Dada White, na kwa Fimbo msimamo wa kila mmoja kwa mada hiyo lazima utazamwe katika nuru ya Maandiko, ambayo bila kupingwa hufundisha kwamba Nchi ya Ahadi itakaliwa tena na watu wa Bwana walioongoka. (Tazama Isaya 2; Mika 4; Ezekieli 36, 37; Yeremia 31-33). {ABN2: 75.1}

Kuhusu taarifa ya Dada White katika Pambano Kuu, yeye hapo anasimulia juu ya Ufalme uliokamilika, baada ya wafu kufufuliwa, wakati watakatifu wanaupokea. Hii ndio ilikuwa awamu pekee ya mada — awamu iliyokamilika — ambayo Majaliwa yalikuwa yamejulisha alipoandika. Sasa wakati chuo cha Ukweli wa kinabii kimekunjua zaidi tangu siku yake, Ufalme kwa uhalisi unaonekana kuwa na ya kati, awamu ya Wadaudi, na vile vile ya mwisho inayojulikana. {ABN2: 75.2}

Mbali na unabii unaohusu Ufalme — halisi — wa Wadaudi, Biblia inayo mafundisho mengine mengi ya unabii ambayo maandishi ya Dada White hayataji hata kidogo, achia mbali kuyashughulikia. Na iwapo sasa Bwana halifunulii kanisa kukidhi hitaji lake leo halitakuwa tayari kwa utimizo wazo bali litaachwa kuangamia katika hali yake ya Ulaodekia. Unabii kwa hivyo lazima ufunuliwe ili kuliimarisha kanisa katika pambano lake la mwisho. Vinginevyo, kwa kusudi gani uliandikwa? {ABN2: 75.3}

75

Hakuna nabii wa Mungu aliyewahi kufua mnyororo kamili wa matukio ya kinabii, bila viunganishi kukosa. Imewachukua waandishi wengi waliovuviwa kukamilisha mnyororo mrefu wa unabii. Nia, kwa hivyo ambayo huchukua msimamo kwamba Dada White alifanya ambayo hakuna nabii ndani au nje ya Biblia amewahi kufanya, hufanya hivyo kwa kupuuza kabisa utaratibu halisi wa Biblia na pia Ukweli uliofunuliwa. {ABN2: 76.1}

Yeye mwenyewe husema kwamba “hakuna mtu, hata hivyo aliyeheshimiwa na Mbingu, amewahi kuafikia ufahamu kamili wa mpango mkuu wa ukombozi, au hata kwa uthamini mkamilifu wa kusudi la Mungu katika kazi ya wakati wake. Watu hawaelewi kabisa lile Mungu angekamilisha kwa kazi ambayo Yeye huwapa wafanye; hawafahamu, katika uchukuzi wake wote, ujumbe ambao wao hutamka kwa jina Lake.” — Pambano Kuu, uk. 343. {ABN2: 76.2}

Watu wengine, wakiwa aina ya kasuku, hutamka taarifa kama kasuku, kamwe bila kukoma wafikiri wanayosema, na inavyoonekana bila kujali iwapo kama taarifa zao husimama au huanguka. Kama hao ndio wale ambao husema kwamba hakuna tukio au matukio mengine yanayoweza kuja kabla, kati, au baada ya yale yaliyowekwa katika maandishi ya Dada White. {ABN2: 76.3}

Ikiwa mtu atasisitiza kwamba mwendelezo wa matukio yaliyoandikwa katika Maandishi ya Awali, uk. 1-16, lazima yachukuliwe kuwa kamili, na ya kwamba hakuna tukio au matukio mengine yanayoweza kupachikwa ndani, basi anajiingiza kabisa katika

76

maji yenye kina kirefu, kwa maana kurasa zilizotajwa kwa kweli hata hazihusiani aidha na mapigo saba ya mwisho au millenia! {ABN2: 76.4}

Tena: Wayahudi walimkataa Bwana kwa sababu sio yote yale ambayo manabii walifundisha na kuandika yalipatikana katika mafundisho ya Musa. “Sisi tunajua,” wakasema, “ya kuwa Mungu alisema na Musa; lakini mtu huyu, hatujui Atokako.” Yohana 9:29. {ABN2: 77.1}

Kwa sababu hakuna maandishi ya nabii yaliwahi kutabiri Ukweli wote unaohitajika na kanisa kulipitisha wazi hadi katika Ufalme, na kama manabii wengine walifuata, aidha wakipanua au kuongeza kwa unabii ambao tayari uliandikwa katika Maandiko, basi mtu yeyote kupuuza habari njema za Ufalme kwa msingi kwamba awamu hii ya Ufalme haipatikani katika maandishi ya Dada White ni kwake yeye kuchukua msimamo ule ule usio na msamaha na mbaya walivyofanya Wayahudi. Ni kusema, “Mimi ni tajiri, na nimejitajirisha, na sina haja ya kitu.” Ufu. 3:17. Ni mwenendo huu ambao unamlazimisha Mungu awatapike kutoka kinywani Mwake Walaodekia, wavuguvugu walioridhika. {ABN2: 77.2}

Ujumbe wa saa kumi na moja umewekewa wakati na kukusudiwa kuufuchua Ufalme wa Wadaudi ukiinuka upya kabla kutokea kwa Kristo mawinguni. Kikiwa hakina nuru ya moja kwa moja, hata hivyo, kwa awamu hii ya Ufalme, Pambano Kuu hakingeweza kujielezea katika maneno dhahiri ambayo ujumbe hutumia leo, kuliko William Miller angeelezea mwenyewe

77

mada ya utakaso wa hekalu, kwa maneno kama hayo tunavyosoma katika Pambano Kuu. {ABN2: 77.3}

Kwa lazima, taarifa zozote zinazohusiana na mada ambayo bado haionekani katika kukunjua kwa Chuo, hufanywa tu kwa maneno ya kushtukia kwa ukweli kama ulivyo wakati unavyoonekana au unavyoeleweka kwa kawaida. Na iwapo ufahamu wa kawaida wa taarifa hizi za kushtukia ni makosa, mwandishi hawezi kuwajibikia lile ambalo ameazima kutoka kwa wengine au kuona isivyo dhahiri na hivyo kuelezea isivyo sahihi. {ABN2: 78.1}

Kwa mfano, katika siku ya Kristo “fundisho la uwepo wa hali ya kujua kati ya kifo na ufufuo ilishikiliwa na wengi wa wale waliokuwa wakiyasikiza maneno ya Kristo. Mwokozi alijua mawazo yao, na akaufanza mfano Wake ili kukazia kweli muhimu kupitia maoni haya yaliyokuwapo. Aliinua mbele ya wasikizaji Wake kioo ili waweze kujiona katika uhusiano wao wa kweli na Mungu. Alitumia maoni yaliyokuwapo ili kulifikisha wazo ambalo alitaka lijulikane kwa wote …. “ — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 263. {ABN2: 78.2}

Hali hii ni ya asili na ya kawaida kwa kila mwandishi anayeshughulikia Ukweli wa Sasa, kuanzia na waandishi wa Agano la Kale, na kuendelea tangu wakati huo, na itakuwa hivyo mpaka kila sehemu kijenzi ya Ukweli itafahamika. Hii imeonyeshwa

78

wazi katika kazi ya Yohana Mbatizaji. Alipaswa kutangaza si kusimamishwa kwa Ufalme, ila kuja kwa Mfalme. Lakini katika kuutangaza mmoja, yeye ghafla alijibu maswali kuhusu ule mwingine. Wakati akinena juu ya Mfalme anayekuja, alieleza katika habari ya Ukweli uliofunuliwa. Lakini kwa uthibitisho akitaja juu ya Ufalme unaokuja, ambao haikuwapo nuru maalum katika siku yake, alielezea katika habari ya mafundisho jinsi yalivyoeleweka kwa kawaida wakati huo. {ABN2: 78.3}

Hata hivyo, wakati kukunjua zaidi kwa chuo kulifunua kwamba Ufalme haungalisimamishwa wakati huo, basi wale waaminifu, watafuta ukweli hawakumshutumu ama Yohana au Kristo, lakini walitazama kwa furaha chuo kikikunjua, na kwa shangwe wakasonga mbele na Ukweli. Ingawa, haikuwa hivyo, na umati mkubwa wa Wayahudi. Kiburi chao cha mawazo, kiliwakataza kuacha makosa yao na kuukumbatia Ukweli unaoendelea, kiliwaongoza kwenye makosa zaidi. {ABN2: 79.1}

“Hivyo ndivyo,” inasema Roho ya Unabii, “kwamba Wayahudi walifanya katika siku za Kristo, na tumeonywa kutotenda walivyofanya na kuongozwa kuchagua giza badala ya nuru kwa sababu ndani yao ulikuwa moyo mwovu wa kutoamini kwa kumwacha Mungu aliye hai. Hakuna hata mmoja kati ya wale wanaofikiri kwamba wanajua yote ni mkongwe sana au mwenye akili sana kujifunza kutoka kwa wanyenyekevu wa wajumbe wa Mungu aliye hai.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65, 66; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28-30. {ABN2: 79.2}

Kwa hivyo Pambano Kuu na Maandishi ya Awali huifanya mada ya Ufalme

79

iwe wazi kabisa kadiri sehemu ya chuo kilichokuwa kikikunjuka ilimruhusu mwandishi kuitazama, katika mojawapo tu ya awamu zake, wakati alipoviandika vitabu vyote viwili. {ABN2: 79.3}

Wakati Pambano Kuu chaweza kuacha kuonyesha kwamba kusimamishwa kwa Ufalme na kuurithi ni matukio mawili tofauti, kwingineko Roho ya Unabii hufanya hivyo: Wakati mitume, inasema, “hawangeuona ujio wa ufalme katika siku yao, ukweli kwamba Yesu aliwaagiza waombe kawa ajili yake, ni ushahidi kwamba katika wakati Mungu ataona umetimia hakika utakuja. {ABN2: 80.1}

“Ufalme wa neema ya Mungu sasa unasimamishwa, kadiri siku kwa siku mioyo ambayo imejaa dhambi na uasi inajitiisha kwa enzi kuu ya upendo Wake. Lakini kusimamishwa kamili kwa ufalme wa utukufu Wake hakutatukia hadi kwa kurudi mara ya pili kwa Kristo kwa dunia hii. ‘Ufalme na enzi, na ukuu wa ufalme chini ya mbingu yote,’ utapewa ‘watu wa watakatifu Wake Aliye juu.’” — Mlima wa Baraka, uk. 159. {ABN2: 80.2}

Kila Mkristo anapaswa kukumbuka kwamba kwa sababu ukweli daima husonga mbele, Hautapatikana leo pale Ulikuwa jana, na ya kuwa kwa hivyo wafuasi wa Kristo lazima wastawi Nao. Hawataifuata mifano ya Wayahudi na Warumi. {ABN2: 80.3}

Wakati Musa aliandika sehemu ya kwanza ya Biblia, hakupewa nuru yote ambayo

80

Mungu alikusudia kufunua kwa watu Wake katika vizazi vyote. Kwa kila saa iliyojongea kwa Ukweli kusonga mbele, akaja kwanza nabii mmoja, kisha mwingine, katika urithi mrefu uliomalizika na Yohana Mbatizaji. Kisha akaja Kristo, mitume, wana-matengenezo, William Miller, na Dada White, kila mmoja kwa zamu akifundisha kweli ambazo hazingetangazwa zote na maandishi ya mtangulizi yeyote. Ili kupata Ukweli wote uliofunuliwa hatua kwa hatua, maandishi ya wote lazima yashirikishwe. {ABN2: 80.4}

Kwa mfano, kwa kuweka sheria ya Pasaka, na katika kuamuru maadhimisho yake, Musa aliandika: “Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.” Kut. 12:5, 6. {ABN2: 81.1}

Sababu ambayo Musa anaagiza uadhimishaji washerehe ya Pasaka ni kwamba ni ukumbusho wa Israeli kutoka Misri (Kumb. 16:1-3). Yohana Mbatizaji, hata hivyo, huiwekea umuhimu wake kwa ujio wa Kristo, “Mwana-Kondoo wa Mungu” (Yohana 1:29), ilhali mitume huiwekea msalabani: “Kwa maana Pasaka wetu,” anasema Paulo, “amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.” 1 Kor. 5:7. Na umuhimu wa kuiadhimisha Pasaka, basi yeye huiambatisha agizo la meza ya Bwana (1 Kor 11:26). {ABN2: 81.2}

81

Vivyo hivyo, Musa hakuelezea kwamba ukuhani wa Walawi katika hekalu la duniani (Kut. 40:15) ulikuwa wa muda tu na kwa hivyo ulikuwa usiodumu, mfano wa ukuhani wa Kristo katika hekalu la mbinguni, jinsi mitume walivyofafanua (Ebr. 6:19, 20; 9:12, 26). {ABN2: 82.1}

Kukosa kusonga mbele na Ukweli unaoendelea, kila kizazi cha Wayahudi kilipata makosa na manabii mmoja mmoja, na kumalizia kwa mitume na Mwana wa Mungu Mwenyewe. Wayahudi walihalalisha matendo yao ya jinai kwa msingi kwamba madai ya manabii wao, ya Kristo, na ya mitume, hayakuwa na msingi kwa maandishi ya Musa. Kwa hivyo wakati walijivunia maandishi ya Musa, waliwakataa na kuwaua manabii waliokuja baada yake — onyo zito kwetu, tusije tukafanya kama walivyofanya, tukutane na hatima yao! {ABN2: 82.2}

Swali kuu kwa hivyo sio kama ni maandishi ya Dada White au ya Musa au ya huyu au ya huyo yanasheheni jumbe zote za siku ya leo, lakini badala yake zinapatikana tu, na kutegemezwa, na Biblia. {ABN2: 82.3}

Fimbo kwa hivyo haidai kwamba ujumbe wake wote unapatikana katika maandishi ya nabii mmoja, lakini badala yake katika maandishi ya manabii wote — “huku kidogo, na huko kidogo.” Isa. 28:13. {ABN2: 82.4}

Yeyote, kwa hivyo, asitumie kwa hila maandishi ya Dada White, kama Wayahudi walivyoyatumia

82

maandishi ya Musa, dhidi ya maendeleo ya Ukweli, na kwa madhara yao milele. Kupitia katika maingilio ya kila pembe, Biblia hutatua mada ya Ufalme, na kufanya isiwezekane mtu kukosea iwapo atafuata kwa usahihi lile Neno husema kuuhusu. {ABN2: 82.5}

Fimbo haifundishi ama kwamba Yerusalemu utajengwa tena, au kwamba hautajengwa tena, kama mji mkuu wa Ufalme, bali tu kwamba Ufalme huo mwanzoni mwake utasimamishwa katika Nchi ya Ahadi. Na kwa uthibitisho wa ukweli huu, Ezekieli hutabiri

Ugavi Mpya wa Nchi. {ABN2: 83.1}

Nabii huwasilisha ugavi wa nchi tofauti kabisa na ule wa wakati wa Yoshua (Yoshua 17): utakuwa katika mikanda kutoka mashariki hadi magharibi; Dani litakuwa na sehemu ya kwanza kaskazini, na Gadi, sehemu ya mwisho kusini; kati ya mipaka ya haya mawili itakuwa sehemu ya makabila mengine; mji utakuwa katikati ya nchi (Ezek. 48). {ABN2: 83.2}

Ukweli kwamba ugavi kama huo wa Nchi ya Ahadi haujawahi kufanywa, huonyesha kwamba bado ni wa baadaye. Pia ukweli kwamba hekalu litakuwa hapo, ilhali halitakuwapo katika nchi mpya (Ufu. 21:22), tena huthibitisha kwamba mpangilio huu wa kipekee ni wa kabla ya millenia. {ABN2: 83.3}

Kwa kuongezea, ukweli maradufu kwamba jina la mji huo ni “Bwana Yupo Hapa”, na kwamba eneo lake, kwa mujibu wa

83

ugavi wa nchi, kwa hitaji lazima kwa njia fulani uwe tofauti na ule wa Yerusalemu wa kale, huonyesha kwamba Yerusalemu wa leo, mji uliopo, hautaweza kamwe kujengwa tena kama mji mkuu wa Ufalme unaokuja. (Tazama Trakti Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho, Toleo la 1941, uk. 52, 53). {ABN2: 83.4}

Ikiwa Biblia Hujieleza wazi kwa mada yoyote hakika Hufanya hivyo kwa mada ya Ufalme. Na kwa usahihi, kwa maana Ufalme ndio taji ya tumaini la Mkristo,

Lengo la Shetani la Daima, Kikwazo cha Watu Kurudiarudia. {ABN2: 84.1}

Kwamba vita kuu kati ya Kristo na Shetani ni juu ya tumaini hili la taji, Ufalme, vinaonekana kutoka kwa maagizo ya kurudiarudia ya Bwana katika unabii, mifano, na katika mithali; kutoka kwa bidii ya Shetani ya daima kuizuia jamii ya wanadamu nje ya huo; na mwisho, kutoka kwa wanadamu kurudiarudia kushindwa katika vita vyao ili kuwa warithi wa huo. {ABN2: 84.2}

Akifanya kazi kwa kusudi tangu mwanzo ili kuwatumbukiza wanadamu wote kuzimu, Shetani alitunga mkakati wake mkuu wa kuwapotosha mintarafu Ufalme. Alifanikiwa na Wayahudi wengi kwa sababu walitaka Ufalme usimamishwe kabla ya wakati wake uliopangwa au usisimamishwe kabisa. Na anafanikiwa na wengi wa Walaodekia leo kwa sababu sasa, wakati uliopangwa hakika umekuja, wao

84

Wanautaka uje baadaye au usije kabisa! Utata ulioje! Ni kinaya kilioje! Hakika, jinsi historia hujirudia yenyewe, ndivyo pia upumbavu! {ABN2: 84.3}

Bibilia husema: “Na katika siku za wafalme hawa [wafalme wanaowakilishwa na vidole kumi vya ile sanamu] Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa….Bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu.” Dan. 2:44. {ABN2: 85.1}

Tazama kwamba “jiwe” (Ufalme) halikuwi mlima mkubwa hadi baada ya kuipiga sanamu hiyo, likionyesha kwamba Ufalme unaanza katika uchanga wake na malimbuko pekee, ambao hivi karibuni watasimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo, na ambao baadaye, baada ya kuwaleta ndani mavuno ya pili ya walio hai, wanayapiga mataifa mwishowe huko wanatoka kaburini waliookolewa wa vizazi vyote kutengeneza kikamilifu “mlima mkubwa” — Ufalme uliokamilika! {ABN2: 85.2}

Mbele ya uso wa unabii huu wazi na ulioandikwa kwa kurudiarudia, yeyote asiwe mpumbavu kusema, kama walivyofanya Wayahudi kwa kujibu unabii wa Ezekieli, “Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana” (Ezek. 12:27), hivyo kujiletea juu ya kichwa chake maangamizi yale yale ya kutisha. {ABN2: 85.3}

85

JE! YERUSALEMU WA KALE UTAJENGWA TENA?

Swali Namba 43:

Je, Unapatanishaje fundisho la “Fimbo ya Mchungaji” kwamba Ufalme wa Daudi utasimamishwa tena katika Palestina, na “Maandishi ya Awali,” uk. 75, 76: “Yerusalemu wa Kale hautajengwa Kamwe”? {ABN2: 86.1}

Jibu:

Muktadha wa taarifa ya Maandishi ya Awali hufunua kwamba inalihusu Vuguvugu la Kizayuni la Wayahudi, na huonyesha kwamba kusudi waziwazi la hilo Vuguvugu kuisimamisha tena Nchi ya Kitaifa ya Kiyahudi, yenye kitovu katika Yerusalemu wa kale, halitafanikiwa kamwe kwamba Yerusalemu wa Kale hautawahi kujengwa upya kulingana na ufasiri wa Kizayuni, na kamwe Wayahudi wasio Wakristo hawatakuwa raia wa Ufalme. (Angalia Trakti Namba 8, Mlima Zayuni katika Saa ya Kumi na Moja.) {ABN2: 86.2}

KARAMU YA HARUSI YA MWANA-KONDOO MBINGUNI AU KWA NCHI?

Swali Namba 44:

Ni ndoa gani inayozungumziwa katika “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” uk. 307, na katika “Pambano Kuu,” uk. 426, 427? Katika mfano mmoja, husemekana kwamba ni “muungano wa wanadamu na uungu”; katika mwingine “mapokezi ya Kristo kwa ufalme Wake” bado katika mwingine husemekana kwamba ndoa “hufanyika mbinguni, wakati [watakatifu] wako duniani” wakimsubiri “Bwana wao, wakati Atakaporudi kutoka kwenye harusi.” Tafadhali unaweza kulitatua somo hili gumu kwa ajili yangu? {ABN2: 86.3}

86

Jibu:

Hebu tukumbuke kwamba mifano hii ya usemi, pamoja na mingine mingi, ni vielezi vya kweli tu, sio kweli zenyewe. Kwa mfano, kusimamishwa kwa Ufalme kumeelezewa, katika mfano mmoja, na “mavuno;” raia wa Ufalme, na “ngano”; na ufalme wenyewe, na “ghala.” Mat. 13:30. Katika mfano mwingine, kuusimamisha Ufalme na utengo wa wadhambi kutoka kati ya watakatifu, imeelezewa na malaika wanaolikokota “juya” ufukweni kisha wakaketi, kuwabagua samaki wabaya kutoka kwa wazuri, na kuwaweka wazuri ndani “vyombo,” lakini kuwatupa nje wabaya (Mat. 13:48). Katika mfano huu, raia wa Ufalme wanawakilishwa na samaki wazuri; na Ufalme wenyewe, na “vyombo” {ABN2: 87.1}

Kwa hivyo, wakati ni kweli kwamba ndoa ya Kristo ni “muungano wa wanadamu na uungu,” ni kweli pia kwamba ndoa hiyo ni “mapokezi ya ufalme Wake,” kwa sababu wanadamu huufanyiza Ufalme. Kwa hivyo, ndoa ni sawa na kutawazwa; Ufalme wenyewe, kwa mji, au bibi harusi; na wageni, kwa watakatifu au raia wa Ufalme. Kutoka kwa hili tunaona kwamba wakati Kristo anaupokea Ufalme Wake, Yeye hakika ataunganisha wanadamu na uungu. {ABN2: 87.2}

Mapokezi ya Ufalme Wake yanafanyika mbinguni wakati watakatifu bado wangali

87

duniani, jinsi Danieli alivyoonyeshwa: “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa Mwana wa adamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo Mzee wa siku, wakamleta karibu Naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na mataifa yote, na lugha zote, wamtumikie Yeye; mamlaka Yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme Wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.” Dan. 7:13, 14. {ABN2: 87.3}

Kuleta katika mtazamo wa kinabii tukio lile lile Yesu alitangaza kimfano: “Mtu mmoja kabaila alisafiri kwenda nchi ya mbali ili kuupata ufalme, na kurudi.” Luka 19:12. Kumbuka kwamba Yeye anaupokea Ufalme (anapata umiliki wake) wakati Yeye yu mbali, sio wakati Anaporudi. (Tazama Pambano Kuu, uk. 426, 427). {ABN2: 88.1}

Kwa hivyo, ndoa ni kutawazwa kwa Kristo, ambako kunatukia katika hekalu la mbinguni wakati raia Wake wote duniani wametayarishwa, wakati kazi inakaribia kukamilika, na muda wa rehema kufunga. Ni wazi, basi, ndoa inafanyika kabla Yeye aje “kuwapokea” watakatifu Kwake (Yohana 14:3), na kabla wamlaki Yeye “angani.” 1 Thes. 4:16, 17. Baadaye inaandaliwa “karamu.” {ABN2: 88.2}

Kwa hivyo, ingawa harusi inafanyika mbinguni, watakatifu wakiwa duniani ni wageni watarajiwa kwa karamu ya harusi. Kisha, baada ya ndoa

88

kuhalalishwa katika Patakatifu Mno, Yesu anashuka kutoka mbinguni na kuwachukua wageni Kwake, ili alipo Yeye, nao wawepo (Yohana 14:1-3). Hapo wanakula mezani pa “karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo.” — Pambano Kuu, uk. 427; Ufu. 19:9. Katika mfano huu, wakati watakatifu wanasemekana kuwa ni wageni, Mji Mtakatifu unasemekana kuwa ni “bibi harusi.” Ufu. 21:9, 10. {ABN2: 88.3}

Tena: kabla tu ya ndoa, wakati watakatifu wangali duniani, haki yao inasemekana ni ya “kitani nzuri” ya bibi harusi (ya mji). Ufu. 19:8. {ABN2: 89.1}

Masomo ambayo hufundishwa kwa vielezi hivi na vingine yanakuwa vito vya ukweli vyenye thamani kubwa kwa wale wanaoyatii. {ABN2: 89.2}

UFALME WA MUNGU MOYONI, AU KWA NCHI?

Swali Namba 45:

Kwa sababu Yesu husema “ufalme wa Mungu u ndani” yetu (Luka 17:21), vipi, basi, unawezaje kuwa ufalme wa duniani? {ABN2: 89.3}

Jibu:

Ikiwa taarifa inayohojiwa humaanisha kwamba hautakuwepo Ufalme wa Mungu duniani, basi kwa kidokezi hicho hicho cha kufikiri pia lazima imaanishe kwamba wala hautakuwapo ufalme wowote mbinguni. Na iwapo hamna wowote duniani, na wowote mbinguni, basi tumaini letu ni bure. Lakini, kama siku zote, lile ambalo hudhihirika sana, huwa halithibitishi kitu. Ndiposa, kusimama juu ya

89

pendekezo katika lile swali ni kuchukua msimamo kwamba hapawezi kuwapo ufalme halisi ama duniani au mbinguni, bali ufalme wa kiroho tu ndani ya moyo, ambalo litaipunguza mada hiyo kuwa upuuzi. Ni kucheza hadi mikononi mwa Ibilisi, ambaye angependa sana kuuzima ukweli wa Ufalme, na kuusafirisha Ufalme wenyewe usahauliwe kabisa. Lakini katika hili, mshukuru Mungu, Neno hutuhakikishia imekusudiwa atashindwa hakika. {ABN2: 89.4}

Kwa hivyo kabla Ufalme wa Mungu usimamishwe hapa duniani, lazima uwe hakika umesimamishwa kiroho ndani yetu ikiwa tutaweza kuhitimu kuruhusiwa kuingia wakati umeanzishwa kwa uhalisi juu ya “dunia, kama kule mbinguni.” {ABN2: 90.1}

Basi, ufalme wa kiroho wa Mungu ndani, ni ndani ya wale ambao huishi kwa kanuni za utawala wake kabla Ufalme halisi kuanzishwa. Kwa hivyo ufalme wa Mungu “ndani” ndio utaratibu wa maisha ya kiroho; ni kipaumbele kwa urithi katika Ufalme wa nje wa Mungu. {ABN2: 90.2}

JE! PEPO ZITAACHILIWA LINI?

Swali Namba 46:

Iwapo malaika anayewatia muhuri malimbuko, watu 144,000, anaendelea moja kwa moja kuwatia muhuri mavuno ya pili, umati mkubwa (Ufu. 7:9), je, malaika wanne watakuwa wanazishikilia zile pepo nne (Ufu. 7:1) muda wote wa kutiwa muhuri mavuno yote mawili? {ABN2: 90.3}

90

Jibu:

Jinsi Ufunuo 7:14 husema kwamba umati mkubwa (mavuno ya pili) “wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu,” ni hitimisho kwamba pepo nne zitazuiliwa, kama alivyoamuru malaika, “hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu….” Ufu 7:3. Pepo, kwa hivyo, zinaachiliwa na kuvuma baada ya watu 144,000 kutiwa muhuri na wakati umati mkubwa unakusanywa na kutiwa muhuri. Hivi ndivyo tu inavyoweza kunenwa kwamba umati mkubwa ulitoka kwenye “dhiki ile iliyo kuu,” kutoka katika “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo.” Dan. 12:1. {ABN2: 91.1}

JE! HASIRA YA MATAIFA NI NINI?

Swali Namba 47:

“Naliona,” asema Dada White, “ya kwamba hasira ya mataifa, ghadhabu ya Mungu, na wakati wa kuhukumu wafu, yalikuwa mbali mbali na tofauti, moja likifuata lingine, pia kwamba Mikaeli alikuwa hajasimama, na ya kwamba wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo, ulikuwa bado haujaanza.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 36. Je, “Hasira hii ya mataifa” inaweza kuwa “vita vya Armagedoni”? {ABN2: 91.2}

Jibu:

Wakati maono hayo huonyesha wazi kwamba matukio matatu ya kwanza (hukumu ya wafu hasira ya mataifa, na ghadhabu ya Mungu) hufuatana kwa mpangilio mfululizo, yakimiliki vipindi vitatu mbali mbali, tofauti na mfululizo, haionyeshi wazi wakati wa tukio la nne — Mikaeli kusimama. {ABN2: 91.3}

91

Ghadhabu ya Mungu, kama inavyoeleweka kwa kawaida, ni mapigo saba ya mwisho (Ufu. 15:1), na yatakuja katika kipindi kati ya kufungwa kwa muda wa rehema na kuja mara ya pili kwa Kristo. Hukumu ya wafu, kama inavyoeleweka angalau na karibu Waadventista wote, hufunika vipindi viwili: cha kwanza katika wakati wa muda wa rehema, mara moja kabla ya hukumu ya walio hai, na cha pili wakati wa millenia. Kwa hivyo ghadhabu ya Mungu inapokuja katika kipindi kuanzia kufunga kwa muda wa rehema hadi kuja mara ya pili kwa Kristo, hasira ya mataifa inaweza tu kutukia wakati wa hukumu ya walio hai — wakati wa Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu. {ABN2: 92.1}

Hasira ya mataifa haiwezi kwa hivyo kuwa Armagedoni, kwa sababu itatukia wakati wa pigo la sita (Ufu. 16:12-16), katika kipindi cha ghadhabu ya Mungu. Hasira ya mataifa na ghadhabu ya Mungu ni, kama tunavyopaswa daima kukumbuka, matukio mawili “mbali mbali na tofauti,” moja likifuatia lingine.” {ABN2: 92.2}

Kwa hivyo, badala ya kuwa Armagedoni, hasira ya mataifa ni “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo” — wakati ambao Mikaeli, anachukua “mamlaka mikononi Mwake” (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300) , anasimama kumwokoa “kila mtu atakayepatikana ameandikwa katika kile kitabu.” Dan. 12:1. {ABN2: 92.3}

Kwa sababu hasira ya mataifa I katika wakati wa hukumu ya walio hai, —

92

Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu, – “hasira” ni dhahiri imeelekezwa dhidi ya watu wa Mungu, sio dhidi ya mataifa yenyewe. Wazi huu ni ukweli, kwa sababu mataifa kati yao kila mara yamekuwa yakikasirikiana, na yamekasirika hata leo, ingawa bado tuko katika wakati wa hukumu ya wafu. {ABN2: 92.4}

“Hasira ya mataifa” itafuata amri ya mnyama mwenye pembe mbili “kwamba wale wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe” (Ufu. 13:15); wakati huo huo mwanamke maarufu, Babeli Mkuu, atampanda mnyama mwenye rangi nyekundu sana (Ufu. 17) na kuyatawala mataifa. Hii “hatari ile ile itatukia kwa watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 395. {ABN2: 93.1}

Mintarafu hasira hii ya mataifa, muungano wa ulimwengu wote dhidi ya wale ambao watakataa kumsujudia mnyama na sanamu yake, Bwana alitabiri kupitia nabii Zakaria: “Tena itakuwa siku hiyo, Nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watakatwa-katwa vipande; ingawa mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.” Zek. 12:3. {ABN2: 93.2}

“Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 12:8. Kisha “likiwa limevikwa vazi la

93

silaha za haki ya Kristo, “inasema Roho ya Unabii, “kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. {ABN2: 93.3}

“Wale ambao wamekuwa waoga na wasiojiamini, watajitangaza wazi kwa ajili ya Kristo na ukweli Wake. Wale dhaifu sana na wenye kusitasita kanisani watakuwa kama Daudi — tayari kutenda na kuthubutu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 81. {ABN2: 94.1}

“Wale tu ambao wameyastahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {ABN2: 94.2}

(Italiki zote ni zetu.)

======

HATUA YAKO ITAKAYOFUATA ITAKUWA NINI?

Sasa ikiwa umefurahia, umethamini, na kufaidika na safari hii ya maswali na majibu kupitia Kitabu Namba 2, na iwapo unatumaini kuendelea, basi tuma ombi kwa Kitabu Namba 3. Kitatumwa kama utumishi wa Kikristo bila malipo au wajibu. {ABN2: 94.3}

94

FAHARISI YA MAANDIKO

>