fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 33, 34

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 33, 34

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

KUTAKASWA KWA PATAKATIFU, LINI NA JINSI GANI KUNAVYOFANYWA?

KAMA UNGALIKUWA SI KITU, UNGALICHAGUA KUWA NINI?

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Kua Katika Neema Au Sivyo Ufe

Alasiri hii nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 65, kuanzia aya ya mwisho. {2TG33: 2.1}

“Kuota kwa mbegu huwakilisha mwanzo wa maisha ya kiroho, na ukuaji wa mmea ni mfano mzuri wa ukuaji wa Mkristo. Kama ilivyo kwa maumbile, ndivyo ilivyo katika neema; hayawezi kuwapo maisha bila ukuaji. Mmea lazima ukue au ufe. Kwa sababu ukuaji wake u kimya na usioonekana, bali endelevu, ndivyo ulivyo ukuaji wa maisha ya Mkristo. Katika kila hatua ya ukuaji maisha yetu yanaweza kuwa makamilifu; bali ikiwa kusudi la Mungu kwetu linatimizwa, yatakuwapo maendeleo daima. Utakaso ni kazi ya muda wote wa maisha. Kadiri fursa zetu zinavyoongezeka, uzoefu wetu utapanuka, na ufahamu wetu kuongezeka. Tutakuwa imara kuwajibika, na ukomavu wetu utakuwa kulingana na mapendeleo yetu.” {2TG33: 2.2}

Je! Ni nini hitaji letu la sala alasiri hii? — Hebu tuombe kwamba tukue katika neema kwa maana hayawezi ku-wapo maisha bila ukuaji; tuendelee na ukweli; tutumie manufaa ya fursa zetu zote; tushirikiane na vyombo vya Kiungu; tuwe tayari kubeba majukumu; tutambue kwamba tunapofanya haya yote, basi majukumu yetu yataon-gezeka, na ukomavu wetu utalingana na upendeleo wetu. {2TG33: 2.3}

2

KUTAKASWA KWA PATAKATIFU, LINI NA NI JINSI GANI KUNAVYOFANYWA?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 27, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko letu linapatikana katika Danieli sura ya nane, aya ya 14, nitaanza na aya ya 13. {2TG33: 3.1}

Dan. 8:13,14 — “Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na lile chukizo la uharibifu, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo pa-takatifu patakapotakaswa.”

Kwa swali hili, “Haya maono kwa habari sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na lile chukizo la uharibifu yataendelea hadi lini, kupaganyakisha patakatifu na jeshi?” Jibu likaja, “Hata nyakati za asubuhi na jioni elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Yaani, ndani ya siku 2300 ya kila siku itaondolewa, chukizo la uharibifu kuwekwa, patakatifu na jeshi vitakanyagiwa chini. Baada ya hayo patakatifu patatakaswa. “Kila asubuhi” (pambizo), humaanisha siku za masaa 24 — kipimo kamili cha wakati. Neno “sadaka” sio sehemu ya andiko hilo. {2TG33: 3.2}

3

Aya ya 16, 17 — “Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfaham-ishe mtu huyu maono haya. Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.”

Maelezo ya Gabrieli kwamba maono hayo yatakuwa ya wakati wa mwisho, yanaonyesha kwamba umuhimu mkuu wa maono ni kutakaswa kwa patakatifu, na ya kwamba hakutatukia katika wakati wa Danieli, na sio kabla ya wakati wa mwisho, lakini baada ya mwisho wa siku 2300, katika wakati wa mwisho. {2TG33: 4.1}

Sasa kwa sababu siku 2300 zilianza mahali fulani katika karne ya tano kabla ya Kristo (kama inavyoonekana katika aya zifuatazo), na kwa sababu maono hayo yalikuwa ya siku nyingi, ya wakati wa mwisho, basi bila shaka zile siku 2300 lazima zikadiriwe siku kwa mwaka ilivyo katika Ezekieli 4:6. Siku 2300, kwa hivyo, ni miaka 2300, ambayo mwishoni mwake patakatifu patatakaswa. Je! Ni ishara gani zatia alama wakati wa mwisho? — {2TG33: 4.2}

Dan. 12:4 — “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwi-sho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”

Malaika alifafanua kwamba wakati wa mwisho wengi watakimbia huko na huko, na maarifa yataongezeka. Na ukweli kwamba watu sasa wanakimbia huko na huko na ya kwamba maarifa yameongezeka ndani yake yenyewe yanathibitisha kwamba sasa tunaishi katika wakati wa mwisho, na ya kwamba maono sasa yataeleweka, na ya kwamba patakatifu patatakaswa. {2TG33: 4.3}

4

Dan. 8:18-21 — “Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima. Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa. Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.”

Hapa unaona pale ambapo historia ya kinabii ya maono haya huanzia. Huanza na ufalme wa Wamedi na Waajemi, na hutupeleka katika wakati kupitia ushindi wa Alexander Mkuu. {2TG33: 5.1}

Aya ya 23 — “Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.”

Katika kikomo cha mwisho wa Wamedi na Wayunani, wakati ambapo wakosaji, Wayahudi, wametimia, mfalme au ufalme mwingine ulikuwa usimame. Bila shaka haukuwa mwingine isipokuwa Rumi, ufalme ambao ulivamia migawanyiko minne ya Uyunani. {2TG33: 5.2}

Aya ya 26, 27 — “Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi. Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna ali-yeyafahamu.”

Danieli hapa hukiri kwamba maelezo machache ambayo Gabrieli alitoa kuhusu maono hayakuwa ya kutosha. Hakuna aliyeweza kuyaelewa.

5

Kwa hivyo, kadiri wakati ulivyoendelea na kwa vile bado hakuweza kuyaelewa maono hayo ingawa wakati uliowekwa wa kuwekwa huru ulikuwa umekuja, alisema kinaganaga: {2TG33: 5.3}

Dan. 9:1-3, 22, 23 — “Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliye-tawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danie-li, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu… Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilit-olewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.”

Kwa sababu Gabrieli alikuwa aanzie pale ambapo aliachia (Dan. 8), alimshauri kwanza Danieli ayafahamu maono hayo. Kisha Gabrieli akasema: {2TG33: 6.1}

Aya ya 24 — “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili ku-komesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta Yeye aliye Mtakatifu.”

Kwa sababu Gabrieli hapa anayafafanua maono ya sura ya 8 — mambo ambayo yangetukia katika siku 2300 — majuma hayo sabini kwa hivyo ni sehemu ya hizo siku 2300. {2TG33: 6.2}

6

7

Hebu sasa tuichambue mada kwa msaada wa chati hii. {2TG33: 8.1}

Majuma sabini kwa kweli ni miaka 490. Weka alama kwamba katika miaka hii 490, watu wa Danieli, Waya-hudi, walipaswa kukomesha dhambi na kufanya upatanisho kwa uovu wao, au sivyo waachwe bila tumaini. Ki-sha Danieli akaambiwa ni wapi ambapo majuma 70 yanaanzia: {2TG33: 8.2}

Aya ya 25 — “Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Ye-rusalemu hata zamani zake Masihi aliye Mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.”

Kutoka kwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hadi kwa Masihi Mkuu, kwa Kristo, yaliku-wa majuma 7 (miaka 49), na majuma 62 (miaka 434) — majuma 69 kwa jumla, au miaka 483. Historia huonyesha kwamba amri ya kuujenga mji wa kale ilitokea mwaka 457 K.K. Kwa hivyo miaka 483 kutoka 457 K.K. hu-tuleta kwa mwaka 27 B.K., ambao Kristo, Masihi alibatizwa. (Tukio hili pia, huthibitisha kwamba siku 2300 hukadiriwa siku kwa mwaka, na ya kwamba majuma sabini ni kipande cha kwanza cha muda kutoka ndani ya siku 2300. Tazama chati.) Tunapaswa sasa kwa hivyo kukumbuka kwamba baada ya kukatwa majuma 69 kutoka kwa majuma 70 bado lipo juma moja lililosalia. Kinachotukia ndani ya juma hili kimesimuliwa katika aya zifu-atazo: {2TG33: 8.3}

Aya ya 26, 27 — “Na baada ya yale majuma sitini na mawili, Masihi atakatiliwa mbali, Naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata

8

mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo Ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuha-ribu.”

Kile tu ambacho kingetukia ndani ya majuma saba ya kwanza au miaka 49 sijajiandaa kusema, lakini katika mwisho wa majuma 62 yajayo, au miaka 434 Masihi angekataliwa mbali, kusulubiwa. Katika juma lililosalia, la 70, Ilikuwa Alithibitishe agano na watu wengi, na katikati ya hilo juma Yeye angekatiliwa mbali, kusulubiwa; yaani, ilikuwapo miaka 3 1/2 kutoka kwa ubatizo Wake hadi kusulubiwa, na miaka 3 1/2 baada ya kusulubiwa ambayo Yeye angelithibitisha agano. Hili hukamilisha majuma 70 na hutuleta kwa wakati ambao mitume waliamriwa kwenda nje kuihubiri Injili kwa Mataifa: Mmoja aliyeitwa Kornelio (Mtu wa Mataifa), na Petro (Myahudi na Mtume) wote walipewa njozi: Kornelio aliamriwa kumwona Petro na Petro aliamriwa kukutana na Kornelio. Tazama Matendo, sura ya 10. Wayahudi kama taifa walishindwa kuikomesha dhambi na kwa hivyo walikataliwa, wakaachwa. {2TG33: 9.1}

Dhabihu yake Kristo mwenyewe mwishoni mwa miaka 3 1/2 ya kwanza ilichukua nafasi ya mfumo wa kafara, na kwa hivyo Yeye alisababisha dhabihu kukoma katikati ya juma. Yote haya, wakati na tukio, unaona, yalitukia haswa jinsi Gabrieli alivyotabiri. {2TG33: 9.2}

Walakini, hata kwa ufafanuzi huu ulioongezwa, Danieli bado hakuweza kuelewa yote

9

ambayo yalikuwa katika maono. Lakini kadiri wakati ulivyoendelea, na kadiri mzigo wake wa ukombozi wa wa-tu wake ulivyoongezeka, akijua ya kwamba wakati umefika, aliomba kwa ajili ya nuru. Sala yake imeandikwa katika sehemu ya kwanza ya sura ya 10, baada ya hapo malaika alionekana na kufafanua tena: {2TG33: 9.3}

Dan. 10:21 — “Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.”

Wakati huo Danieli aliahidiwa nuru yote ambayo ingeweza kutolewa, sio tu kwa njozi ya Danieli 8, lakini kwa yote ambayo yameandikwa katika maandiko ya kweli kuhusiana na ile njozi. Yale ambayo malaika alimwonye-sha yameandikwa katika Danieli 11 na 12: {2TG33: 10.1}

Sura ya 11, utaona, huanza na maono ya Danieli 8, na wafalme wa Wamedi-Waajemi na Uyunani kama mfano wa kondoo na beberu katika sura ya 8. Basi Danieli akaambiwa kwamba yale maelezo mwishowe yalitosha, lakini kwamba haingewezekana yeye kuyafahamu yote, kwa maana maono hayo yalitiwa muhuri hadi wakati wa mwisho (sura ya 12, aya ya 8, 9). {2TG33: 10.2}

Kwa historia hii ndefu ya kinabii na jiografia jinsi inavyoonekana katika sura ya 11 na ya 12, malaika anatu-leta hadi wakati wa mwisho, kwa wakati ambapo kutakaswa kutatukia. Na hapa ni asili ya utakaso kwa mujibu wa neno la malaika: {2TG33: 10.3}

Dan. 12:1 — “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa

10

taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”

Kwa kuwaokoa wenye haki, Yeye anawatenga kabisa wenye haki kutoka kati ya waovu — Yeye anawaweka “samaki” wazuri kwenye vyombo na kuwatupa wabaya (Mat. 13:48). Atawatakasa watu Wake kutoka kwa dhambi na wenye dhambi. {2TG33: 11.1}

Aya ya 2, 3 — “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.”

Waovu watakaoamka na wenye haki katika ufufuo huu mseto pia watatengwa na wenye haki. Waovu wa-tapata aibu na kudharauliwa milele, lakini wenye haki watapewa uzima wa milele. {2TG33: 11.2}

Aya ya 10 — “Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.”

Wenye haki walio hai watatakaswa, lakini waovu watakuwa wabaya zaidi. {2TG33: 11.3}

Aya ya 11, 12 — “Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, zitakuwa siku elfu na mia mbili na tisini. Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.”

11

Hapa kipande kingine cha wakati kutoka ndani ya siku 2300 kimeletwa, kuanzia wakati ambapo ya kila siku imeondolewa na lile chukizo kusimamishwa. (Ya kila siku huwakilisha kitu ambacho hakingaliondolewa, na ma-chukizo huwakilisha kitu ambacho hakingewekwa. Neno “sadaka” limeongezwa na halimo kwenye andiko. Kwa ajili ya nuru juu ya hayo soma Trakti Namba 3, Mavuno.) {2TG33: 12.1}

Ikumbukwe, hata hivyo, kwamba baraka iliyoahidiwa (kutakaswa) haianzi hadi baada ya siku 1335, au miaka, kumalizika. {2TG33: 12.2}

Sasa kwa sababu kipindi cha miaka 2300 huanzia 457 K.K., na amri ya kurejesha na kuujenga upya mji wa Yerusalemu, siku 2300 ndiposa hukoma katika mwaka 1844, wakati ambapo siku 1335 hukamilika, kisha siku za baraka zinaanza. Itakumbukwa sasa kwamba huku kutakaswa kwa patakatifu hutia ndani utakaso wa wote wa-takaofufuliwa na wale ambao watakuwa wanaishi katika wakati wa utakaso. Akinene kupitia nabii Ezekieli ku-husu utakaso kati ya walio hai, Bwana husema: {2TG33: 12.3}

Ezek. 36:24-29 — “Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa

12

baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote; Nitaiita ngano, na kuiongeza, wala Sitaweka njaa juu yenu tena.”

Hakuna yeyote wa walio hai kwa kweli anaweza kusafishwa kutokana na alama zote za dhambi wakati am-bapo yu kati ya nchi za Mataifa, unaona. Lazima kwanza watenganishwe kutoka kwa wanafiki na Mataifa, kisha waletwe katika nchi yao, huko watanyunyiziwa maji safi, watakaswe kutoka kwa uchafu wao wote na kutoka kwa sanamu zao zote, watakapofika katika nchi yao, sio kabla. Hata moyo mpya watapewa huko, na roho mpya pia. Hivyo Bwana atawafanya waenende katika kanuni Zake na kuzishika hukumu Zake milele. Hivyo ndivyo watakavyorejea na kukaa katika nchi ya baba zao, Palestina, na hivyo watakuwa watu wa Mungu milele. Mambo haya, unaona, ni ya kabla millenia. {2TG33: 13.1}

Hebu sasa tuangalie kutakaswa kwa mujibu wa nabii Yoeli, Malaki, na Yeremia– {2TG33: 13.2}

Yoeli 3:21 — “Nami nitaitakasa damu yao ambayo Sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye Zayuni.”

Malaki 3:1-3 — “Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anaku-ja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika

13

haki.”

Yer. 31:31-33 — “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile Nililolifanya na baba zao, katika siku ile Nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano Langu hilo walilivunja, ingawa Nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Bali agano hili ndilo Nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria Yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu.”

Agano la kale limekuwa kuzishika amri hizo wakati zimeandikwa, sio katika moyo, lakini kwenye mbao za mawe, dhidi ya mapenzi ya moyo wa jiwe. Lakini agano jipya litawatakasa kutoka kwa mioyo yao ya jiwe, na kuandika sheria kwenye mioyo yao ya nyama. {2TG33: 14.1}

Aya ya 34 — “Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana Watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana Nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao Sitaikumbuka tena.”

Wakati watu wa Mungu wametakaswa hivyo, wote watamjua Bwana. Ndipo watakuwa watu Wake, taifa Lake. Na uhakikisho la Mungu ni huu: {2TG33: 14.2}

Aya ya 35, 36 — “Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku,

14

aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi, ndilo jina Lake; Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele Yangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele Yangu milele.”

Je! Mungu hufanya hivyo kwa sababu watu Wake wamekuwa wazuri au kwa sababu anataka kulitetea jina Lake? Hebu tuone: {2TG33: 15.1}

Ezek. 36:20-24 — “Nao walipoyafikilia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina Langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa Bwana, nao wametoka katika nchi Yake. Lakini, naliwahurumia kwa ajili ya jina Langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli walikuwa wamelitia unajisi katika mataifa waliyoyaendea. Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina Langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mli-yoyaendea. Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, Nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwar-udisha katika nchi yenu wenyewe.”

Kwa udhahiri, Neno hutangaza kwamba patakatifu patatakaswa, kwamba ile nchi pia itakombolewa tena, na Ufalme kurejeshwa, sio kwa sababu ya wema wa watu, bali kwa ajili ya jina la Mungu, kwa ajili ya wema Wake mwenyewe. Mataifa, pia, watajua lile Mungu amewafanyia watu Wake, kwa maana Maandiko yanaonyesha kwamba haya yote yatatukia mbele ya macho yao. Utakaso u huu Kristo anaelezea hivi: {2TG33: 15.2}

15

Mat. 25:32-34 — “Na mataifa yote watakusanyika mbele Yake; Naye atawabagua kama vile mchungaji aba-guavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono Wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu.”

Hapa upo ukweli ambao Dhehebu limepuuza: wao hufikiri kwamba watafanya mstari wa nyuki hadi kwa kiti cha enzi cha Mungu kwa ajili ya Millenia. Lakini kwa mujibu wa maandiko, hapa unaona watu lazima kwanza watengwe kutoka kati ya mataifa, kisha watakaswe kutoka kwa uchafu wao wote, na hivyo kuwezeshwa kusimama mbele ya uwepo wa Mungu msafi na wa milele. Hivi ndivyo patakatifu kati ya walio hai pana-takaswa, na hivyo ndivyo watu watawezeshwa kutawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu. {2TG33: 16.1}

Ndugu, Dada, fanyeni hakika kwamba msipatikane, kati ya mbuzi kushoto Kwake, bali na kondoo kwa kulia Kwake iwapo mtaweza kumsikia Mfalme akisema, “Njoni, mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini ufalme mlio-wekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu.” (Mat. 25:34). {2TG33: 16.2}

Na kumbuka kwamba sasa tumekuwa tukiishi “katika wakati wa mwisho” kwa miaka kadhaa. Isitoshe, nuru hii sasa imekuja kwa sababu kutakaswa kwa washirika walio hai wa kanisa umekaribia. {2TG33: 16.3}

16

KAMA UNGALIKUWA SI KITU, UNGALICHAGUA KUWA NINI?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, APRILI 17, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko letu linapatikana katika: {2TG34: 17.1}

1 Wafalme 3:5 — “Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo Nikupe.”

Sulemani aliomba hekima, na pamoja nayo alipata kila kitu ambacho mwanadamu angependa kuwa nacho. (1 Wafalme 3:10-14.) Iwapo tungepewa kuchagua kama ule Sulemani alipewa, tungeomba nini? — Naogopa wengi wetu hawangeomba kitu kizuri alivyoomba Sulemani. Nafikiri wengi wetu wangeomba pesa kiasi kizuri, na lab-da wengine wetu wangeomba utajiri mkubwa, wengine mke au mume. Na ni nini hunifanya nifikiri haya? — Kwa sababu tu huwaona wengi wakijitahidi kupata mapato na kuwinda, sio kujifunza. {2TG34: 17.2}

Tuseme kwamba wewe si kitu, na ulikuwa na hisia za kutosha kuisikia sauti ya Mungu, kama Sulemani, ikise-ma: “Je! Unataka kuwa nini? Omba, na hivyo utakuwa.” Utaweza, bila shaka, kutaka kuwa aliye bora katika uumbaji wa Mungu — mwanadamu. {2TG34: 17.3}

17

Hebu tuwaze kwamba ombi lako umepewa, kwamba sasa umekuwa mwanadamu mzuri, lakini haujaendelea zaidi: Wewe bado sio wa familia yoyote, ujamaa, serikali au watu. Hujui chochote kumhusu Mungu na chochote kuhusu dini. {2TG34: 18.1}

Ijayo katika maendeleo yako kati ya walio hai, ungetaka kuchagua utaifa wako. Je! Ni watu gani kati ya wote duniani ungependa kuchagua kuwa? Ningechagua kuwa Mwebrania, kwa sababu taifa la Waebrania kati ya ma-taifa yote duniani liko na kwa wazazi wake manabii, wafalme, na makuhani. Taifa la Waebrania, bila shaka (simaanishi Wayahudi wasioamini wa sasa), kwa wakati huu wa sasa halina serikali yake lenyewe; limetawanyi-ka kati ya mataifa. Utalazimika kwa hivyo kuchagua serikali ambayo ungependa chini yake kuifanya iwe makao yako. Kwa sababu Marekani ndio taifa lenye ufanisi zaidi, na kwa sababu chini ya utawala wake unaweza kutembea kwa uhuru mkubwa kuliko katika taifa lingine lolote, bila shaka ungechagua kuwa mmoja wa raia wake. {2TG34: 18.2}

Tuseme ijayo umevutiwa sana kujiunganisha na kanisa. Kuna dini tatu tu za kuchagua — Upagani, Ukristo, na Uislamu — ni ipi ungeweza kuchagua iwe yako? Hekima yako uliyopewa na Mungu ingekuambia kwamba itastahili kuwa ile ambayo ina rekodi bora na ndefu zaidi, ile ambayo imethibitisha chimbuko lake na uimara, ambayo imejithibitisha kuwa ina uwezo wa kumwokoa mdhambi, kuwafufua wafu, na kuwahamisha bila kufa walio hai. {2TG34: 18.3}

Kwa sababu dini ya Kristo pekee imejithibitisha yenyewe kwamba ina uwezo wa kutekeleza haya yote na wa kutabiri kuinuka na kuanguka kwa mataifa na watu, zamani, sasa, na siku za baadaye — tangu wakati

18

wa zama za kale hadi wakati wa mwisho. Na kwa sababu mwasisi wake pekee hudai sifa ya kuumba ulimwengu; na ya kuwa Mwana wa Mungu, mwanzo na mwisho, Mwokozi wa wanadamu wote, ungetaka kujiunga nayo. Kwa kweli, iwapo mmoja atapata faida kamili kutoka kwa dini, basi hizi ndizo sifa ambazo dini yake lazima iwe nayo. Na iwapo hizi ndizo sababu kuu za mmoja kuikumbatia dini, basi hakuna zilizo mbadala isipokuwa kuich-agua dini ya Ukristo, kwa sababu ndio ya pekee hutegemezauhakikisho wake kwa ukweli halisi, na utenda kazi halisi. {2TG34: 19.1}

Tuseme sasa umekuwa Mkristo kwa moyo wote, na kabisa, lakini unakabiliwa na tatizo kubwa zaidi; yaani, unapata Ukristo umegawanyika katika madhehebu mengi, moja likitofautiana na yale mengine katika fundisho na mwenendo. Kwa hivyo unalazimika kuchagua dhehebu ambalo ungependa kujiunga kwalo, dhehebu ambalo ungependa kulifanya kuwa lako. {2TG34: 19.2}

Chaguo lako, bila shaka, lingeweza tena kujikita kwa msingi wa ukweli, sio kwa dhana. Na kwa sababu Bibil-ia Yenyewe imekuwa mwongozi wako wa pekee, mwalimu wako wa pekee, itakupasa Kuisoma, na chaguo lako lingefanywa ipasavyo. Na iwapo unaishi sasa katika wakati wa mwisho, wakati ambao Ufunuo wa Yohana hunena hakika na kuangaza kwenye njia ya watakatifu, bila shaka ungeweza kukisoma kitabu cha Ufunuo kwanza na ujiunge na dhehebu ambalo Unapendekeza. Na ni lipi hilo? — Hebu tufungue Ufunuo 12 — {2TG34: 19.3}

Ufu. 12:15 — “Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.”

19

Mwanamke, unajua, ni mfano wa dhehebu hilo, Kanisa. {2TG34: 20.1}

Aya ya 16 — “Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.”

Ni Kanisa hili tu, unaona, limependelewa hata na nchi yenyewe. Dhehebu hili pekee linaokolewa kutoka kwa mafuriko ya Joka, limeokolewa lisichukuliwe na mafuriko ya wanafiki na “magugu” yaliyo kati yake. {2TG34: 20.2}

Aya ya 17 — “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.”

Hapa, unaona, masalia — wale ambao wamesalia baada ya wengine kumezwa na nchi, kwa mfano — huzishika amri za Mungu na linao ushuhuda wa Yesu Kristo. Masalia hawa, au dhehebu, ambalo huzishika amri za Mungu, kwa hivyo, ndilo moja tu ambalo Uvuvio hupendekeza, la pekee ambalo linafaa kujiunga nalo, la pekee linaloweza kumfaidi mtu yeyote. Ndilo la pekee humiliki uwezo wa kuokoka lolote na majanga yote ambayo sasa yanatokota duniani kote. Ni dhehebu la pekee ambalo hupata kibali kwa Mungu. Hamna lingine lingeweza, kwa maana hakuna lingine linaweza kukufaidi. {2TG34: 20.3}

Kisha, pia, ni ushuhuda tu wa Yesu Kristo — Roho iliyo hai ya Unabii kati yake (Ufu. 19:10), — Roho Am-baye huongoza katika Kweli yote, Ambaye pekee yake ndiye anayeweza kuyafasiri Maandiko (2 Pet. 1:20, 21). Kwa udhahiri, basi, Uvuvio hautataka ujiunge na dhehebu ila hili “masalia.” {2TG34: 20.4}

20

Kushika amri za Mungu, hata hivyo, huhusisha kuishika kila moja yazo, kwa maana “Mtu awaye yote ataka-yeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10. Na kumbuka pia, kwamba kuzishika zile amri kunaweza kutambuliwa tu kwa kuishika amri ya Sabato, amri ambayo husema: {2TG34: 21.1}

“Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako: Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato. akaitakasa.” Kut. 20:9-11. {2TG34: 21.2}

Siku ya Sabato, unaona, imeumbwa takatifu, lakini siku sita za kwanza zimeumbwa kwa ajili ya kazi. Sabato ya siku ya saba ndio Sabato pekee, na katika Neno lote takatifu la Mungu hakuna amri ya kuitunza siku nyingine badala yake. Utunzaji wa Sabato ya siku ya saba pekee hushuhudia imani ya mtu kwa Muumba, na dhidi ya kupitia mageuzi. Mbadala kwa Sabato, kwa hivyo, haiwezi kukubalika kama amri ya Mungu kuliko ambavyo sadaka ya Kaini isingaliweza kukubaliwa kama dhabihu iliyoagizwa na Mungu. {2TG34: 21.3}

Hapana, usimpinge Bwana kwa kusema kwamba siku ya saba ni ya Wayahudi tu, kwa maana Bwana asema: {2TG34: 21.4}

Isa. 56:2-7 — “Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye Sabato asizivunje, auzuiaye

21

mkono wake usifanye uovu wo wote. Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu Wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. Kwa maana Bwana awaambia hivi ma-towashi, wanaozishika Sabato Zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano Langu; Nitawapa hawa nyumbani Mwangu, na ndani ya kuta Zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi Wake; kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano Langu; Nitawaleta hao nao hata mlima Wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba Yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu Yangu; kwa maana nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”

SABATO ya pekee ambayo Yesu daima aliijua ilikuwa Sabato ya siku ya saba, na akitazama mbele kwa dhiki kuu, katika enzi ya Ukristo, alisema: “Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato; kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.” Mathayo 24:20, 21. Sabato, unaona, ni kwa watu wote, katika nyakati za Agano la Kale na Jipya. Zaidi ya hayo, ukizungumzia tena enzi ya Ukristo, wakati ambapo dunia imeumbwa upya, Uvuvio unatangaza: {2TG34: 22.1}

Isa. 66:23 — “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele

22

Yangu, asema Bwana.”

Kwa sababu “Ufunuo,” kitabu kinachonena kwa watu wa Mungu wakati huu, hupendekeza dhehebu ambalo huzishika amri na ambalo lina karama ya unabii, huwezi kwa busara huwezi kujiunga na dhehebu lingine. Na kwa sababu Mungu hutangaza hivyo, lazima iwe kwamba lipo kundi moja tu la watu haswa ka wakati huu walio na ushuhuda hai wa Yesu Kristo, Zawadi ya Roho ya Unabii. Zaidi ya hayo, kwa Mungu kuiweka hiyo Zawadi kwa kundi la watu zaidi ya moja, ingekuwa kwake Yeye kusababisha mchafuko na msiba kwa kazi Yake, kuli-zuia kusudi Lake mwenyewe. Bado zaidi, iwapo zaidi ya moja yana ile Zawadi, basi lazima yote yangepatana kama moja. Lakini kwa sababu hakuna madhehebu mawili ambayo yanakubaliana, ukweli kwamba lipo dhehebu moja ambalo lina hiyo Zawadi ni uhalisi kamili. Na wakati unaweza kuchagua kuishika amri ya Sabato, huwezi kujivuvia mwenyewe kwa Roho ya Unabii — Zawadi hii imekabidhiwa kwa masalia na Mungu Mwenyewe. {2TG34: 23.1}

Shida yako inayofuata katika maendeleo yako ya maisha ingekuwa kupata jina maalum la hao watu wanaozishika amri, jina ambalo kwa kweli kwa mazoea litaonyesha kwamba wao ni “masalia,” kwa maana jina lililovuviwa na Mungu lazima kwa uhalisi litambulishe watu ambao Uvuvio hapa huidhinisha. Jina lingine lolote juu yao lingekuwa la kupotosha, na jina lilo hilo kwa watu wengine wowote lingekuwa la kupotosha, pia. {2TG34: 23.2}

Hebu tusipuuze kutambua, pia, kwamba jina la watu sio kwa kweli jina ila mtajo. Na mataji, mnajua, hubadili-ka upesi kadiri Ukweli unavyojikunjua, upesi kadiri Ukweli unavyoendelea kutoka kwa awamu moja ya kazi ya injili hadi kwa nyingine. {2TG34: 23.3}

23

Kwa mfano: Hata majina ya kibinafsi ya mababu, ambayo mavuguvugu mbalimbali ya zamani yalitajwa kwayo, yalibadilishwa kadiri muda ulivyoendelea. Abramu, unakumbuka, katika mchakato wa wakati aliitwa Abrahamu; na Yakobo aliitwa Israeli. Basi, pia, Kanisa la wakati wa Musa liliitwa Waisraeli, wakati wa Kristo liliitwa Yudea, na baada ya hilo la Kikristo. Hatimaye ukafika wakati ambao liliitwa ama Katoliki au la Kiprotestanti. Kisha ama la Walutheri au jingine fulani. Kila mmojawapo la haya lilikuwa uzao wa lile la zamani. Sio wale ambao hubakia nyuma, ila wale ambao huenenda pamoja na jumbe za Mungu, kadiri wakati unavyoen-delea, daima hutambuliwa na Mbingu kama Kanisa. {2TG34: 24.1}

Mwanzoni mwa kila ujumbe watu ambao walienenda mbele na Ukweli walikuwa washiriki mmoja mmoja wa kanisa ambalo lilikuja kuwa kanisa kwa njia ya kuupokea ujumbe, ujumbe ambao mwasisi wake aliuleta. Kwa mfano, kanisa lote la Kiyahudi halikuja kuwa kanisa la Kikristo, lakini kanisa la Kikristo liliwakokota washiriki wake kutoka katika kanisa la Kiyahudi na kuwaleta katika Ukweli ulioendelea, Ukweli mwafaka haswa kwa ajili ya wakati na watu wa wakati huo. {2TG34: 24.2}

Jinsi tunavyoishi sasa katika wakati wa Ufunuo, katika wakati wa kufunuliwa kwa unabii ambao huonyesha kuanzishwa kwa Ufalme na vile vile kwa ujio wa pili wa Kristo, Kanisa wakati huu, kwa hivyo, haliwezi kwa busara kuitwa kwa jina lingine isipokuwa jina ambalo linafaa awamu yake ya sasa (ya juu) ya kazi ya injili. {2TG34: 24.3}

Kwa udhahiri, basi, jina lake lazima lionyeshe kweli ambazo huzitetea: yaani, kuzishika

24

amri, ujio wa pili wa Kristo, na pia urejesho wa Ufalme wa Wadaudi kwa mujibu wa unabii. Kwa hivyo jina la busara ambalo linawakilisha kazi yake kuanzia wakati huu hadi kwa wakati Ufalme unapoanzishwa, litakuwa Wadaudi Waadventista wa Sabato, — jina ambalo hushuhudia ujumbe wa Ufalme, kuzishika amri ambazo ile Sabato ya siku ya saba ni sehemu yazo, na ujio wa pili wa Kristo. {2TG34: 24.4}

Sasa unaona kwamba kila Ukweli wa nyongeza mwafaka huleta jina la nyongeza mwafaka. Na wewe ambaye hujabatizwa katika jina la Kanisa, ila katika jina la Kristo kupitia Ukweli wa Roho, wewe ambaye hujafungwa kwa mtu yeyote, ila kwa Kristo, huwezi kumudu kuendelea na Roho ya Unabii Ambayo huufunua Ukweli na kuwapa jina watu Wake. Hutaweza kwa hivyo, kumudu kusimama kwa utulivu, kuota ndoto ya kwamba u tajiri na umejitajirisha, hauhitaji chochote ilhali kwa kweli wewe ni maskini na uchi kiroho. Na utakaa hivyo iwapo utapuuza kuendelea na Ukweli wa wakati huu. {2TG34: 25.1}

Mwishowe, unahitaji kujua kwa uthabiti ni nini ujumbe wa Ufalme, “ujumbe wa nyongeza” (Maandishi ya Awali, uk. 277), na awamu ya kazi yake ambayo hukweza jina “Waadventista wa Sabato” hadi kwa jina Wadaudi Waadventista wa Sabato. {2TG34: 25.2}

Isa. 11:11, 12, 16 — “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie wa-tu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera,

25

Atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, Atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia. Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyoku-wako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.”

Iwapo watu wa Mungu walio Babeli watatoka kwake ili kuokoka mapigo yake (Ufu. 18: 4) na kuziepuka dhambi ambazo ziko Babeli wakati ambapo anamwendesha mnyama huyo na kuutawala ulimwengu (Ufu. 17) lazima kwa hitaji waende mahali pasipo hatarini kwa mapigo yake, na ambapo hamna dhambi. Ni wapi mahali hapo? — Ruhusu Biblia itoe jibu: {2TG34: 26.1}

Ezekieli 37:21-28 — “Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Nitawatwaa wana wa Israeli kuto-ka kati ya mataifa walikokwenda, Nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; Nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele. Wala hawatajitia unajisi tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini Nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, Nami nitawatakasa; basi watakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wao. Na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu Zangu, na kuzishika amri Zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi Wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa

26

humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi Wangu, atakuwa mkuu wao milele. Tena Nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; Nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu Pangu nitapaweka katikati yao milele. Tena maskani Yangu itakuwa pamoja nao; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Na mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwa-na, niwatakasaye Israeli, patakatifu Pangu patakapokuwa katikati yao milele.”

Ezek. 36:22-28 — “Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina Langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaen-dea. Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuziten-da. Nanyi mtakaa katika nchi ile Niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu.”

Sasa unaweza kuliona jina hilo kabisa

27

Wadaudi Waadventista wa Sabato. Na kwa hivyo iwapo ulikuwa si kitu jana, na mwanadamu aliyeangazwa na Mungu leo, mwishowe ungeweza kuwa Mdaudi Mwadventista wa Sabato. {2TG34: 27.1}

Tuseme, hata hivyo, ungetaka kuendelea hadi kwa ukamilifu? Kwa kweli ungeweza bila shaka tena kumlilia Bwana, na kusema: {2TG34: 28.1}

Mika 6:6, 7 — “Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele ya Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sa-daka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?”

Na sasa hili ndilo jibu la Mungu kwa kilio chako: {2TG34: 28.2}

Aya ya 8 — “Ee mwanadamu, Yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.”

Naam, hapa unalo jibu kwa shauku ya moyo wako: Tenda haki, ipende rehema, na uenende kwa unyenyekevu na Mungu wako; usiwe na moyo wa kiburi na wa kujitegemea nafsi. Na nini zaidi, Uvuvio unaendelea: {2TG34: 28.3}

Aya ya 9 — “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na Yeye aliyeiagiza.”

Fimbo ya Mchungaji, vitabu ambavyo Uvuvio uliviita hivyo na kuyavuvia yaliyomo, ikiwa ndio Fimbo ya pekee duniani inayoweza kusikika ikinena, Bwana anaamuru kwamba unapaswa kuisikia, kwamba usiweze kuupoteza wakati wowote kuamua

28

kati ya vitabu vya Fimbo na vingine. Kwa sababu hakuna vingine leo isipokuwa vitabu vya Fimbo ambayo Mungu huidhinisha uvisikie. Na unapoisikia hiyo Fimbo, utajipata umezongwazongwa katika upendo wa Kristo na katika “mikono” ya Mungu. Ijaribu. {2TG34: 28.4}

Sasa sikiliza Neno Lake na umruhusu Yeye katika lugha ya manabii akuambie zaidi kuhusu siku ambayo wewe nami tunaijongea sasa, siku ambayo tumeikaribia uso kwa uso. Pamoja na nuru iliyotolewa tayari, maandi-ko yafuatayo hayahitaji maelezo maalum; yanajifasiri yenyewe. {2TG34: 29.1}

Mika 6:9 — “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na Yeye aliyeiagiza.”

Zek. 13:8, 9 — “Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote, asema Bwana, mafungu mawili ndani yake yata-katiliwa mbali nao watakufa; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, Nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo: wataliitia jina Langu, Nami nitawasikia; Mimi nitasema, Watu hawa ndio Wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.”

Zek. 12:8-10 — “Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwa-na mbele yao. Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba Nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupi-gana na Yerusalemu. Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama Yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea,

29

kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili Yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”

Yer. 30:9 — “Bali watamtumikia Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao.”

Ezek. 37:24-26 — “Na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu Zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi Wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi Wangu, atakuwa mkuu wao milele. Tena Nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; Nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu Pangu nitapaweka katikati yao milele.”

Kwa sababu sasa umefundishwa katika Kweli na haki, na kwa sababu nchi bado haijayameza mafuriko ya Joka, pia kwa sababu ujumbe huu ni tangazo kwamba nchi hivi karibuni itayameza mafuriko, ni kundi lipi la washiriki wa kanisa utapenda zaidi kuhusiana nalo? — Sikiza sasa kundi ambalo Bwana hupendekeza: {2TG34: 30.1}

Mat. 5:3-16 — “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata

30

rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi wa-takapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii wali-okuwa kabla yenu. Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaanga-za wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 33, 34

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>