fbpx

Trakti Namba 08

MLIMA ZAYUNI KATIKA “SAA YA KUMI NA MOJA”

1

Hati miliki 1937, 1941

na V. T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

Kwa nia ya kuifikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inalo tumaini la kuepuka njia inayoongoza kwenye maangamizi ya mwili na roho, maadamu toleo hili linadumu, trakti hii itasambazwa bila malipo.

TRAKTI NAMBA 8

TOLEO LILILOREKEBISHWA

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Imechapishwa nchini Marekani

2

MLIMA ZAYUNI KATIKA “SAA YA KUMI NA MOJA”

“Kwa ajili ya Zayuni Sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu Sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.” Isa. 62:1-3. {TN8: 3.1}

Ajabu ya upendo wa Mungu! Tunda la “ahadi ya thamani zaidi” kwamba Mungu ataendelea kuzungumza naye hadi atapokuwa mwenye nguvu kuu na mwanga wa fahari duniani kote na “taji ya utukufu katika mkono wa Bwana” —

Kanisa linaonekana Limesimama Na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni! {TN8: 3.2}

“Ufunuo wa Yesu Kristo, Aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa Wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; Naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa Wake Yohana.” Ufu. 1:1. {TN8: 3.3}

Uthibitisho huu kwamba matukio ya unabii ambayo Yohana alipewa fursa ya kurekodi, yalikuwa “hayana budi kuwako upesi,” si kabla ila “upesi” baada ya kuupokea ufunuo wake, unaonyesha kwamba unabii wa Ufunuo

3

ungetimilika wakati fulani katika kipindi cha Agano Jipya. {TN8: 3.4}

“Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Zayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja Naye, wenye jina Lake na jina la Baba Yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao; na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.” Ufu. 14:1-3. {TN8: 4: 1}

Kabla ya tukio hili la unabii (kusimama watu 144,000 juu ya Mlima Zayuni) “mlango ukafunguka mbinguni: na sauti ile ya kwanza niliyoisikia,” anasema Yohana, “kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, Nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; na Yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu, na mbele ya kile kiti cha enzi

4

kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.” Ufu. 4:1-4,6. {TN8: 4: 2}

“Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.” Ufu. 5:8, 11, 12. {TN8: 5 : 1}

Mwana-Kondoo, anasimama kwanza mbele ya kiti cha enzi mbinguni, anasimama baadaye na watu 144,000 juu ya Mlima Zayuni, juu ya nchi, ingawa Wazee na Wenye Uhai wanaokizunguka kiti cha enzi wanabaki mbinguni. Hivyo, kwa usahihi kuelewa tukio hili la unabii kwa ukamilifu, lazima tutofautishe kwa makini sehemu ambayo inatukia mbinguni kutoka kwa sehemu inayotukia duniani. {TN8: 5: 2}

“Taa saba” (Ufu. 4:5) zikiwa ni sehemu ya vyombo vya hekalu, hutoa ushahidi thabiti kwamba eneo la kiti cha enzi mbinguni linatukia katika hekalu, ilhali eneo linalofuata la Zayuni linatukia juu ya mlima Zayuni, uwanda wa duniani wa kasri la Mfalme, si juu ya mlima Moriah, uwanda wa hekalu,

5

ambapo ingekuwa lazima litukie lingeonyesha kwamba tukio hilo lingefanyika ndani ya hekalu. Maeneo haya kwa hivyo ni ya matukio mawili tofauti, katika maeneo mawili tofauti — mpangilio wa kiti cha enzi mbinguni, na kusimama kwa waliokombolewa na Mwana-Kondoo duniani wakati ambapo shughuli zinazokumbatiwa kwenye mandhari ya kiti cha enzi bado zinaendelea. {TN8: 5: 3}

Zaidi ya hayo, taarifa, “Nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako upesi,” huyaweka hayo matukio katika kipindi cha Ukristo. Na taarifa hiyo, “alisimama Mwana-Kondoo kama aliyechinjwa” (akivuja damu kwa niaba ya mdhambi), huyaweka katika wakati wa muda wa rehema. {TN8: 6: 1}

Kisha kwa kulinganisha Dan. 7:9, 10, 13, na Ufu. 4:2 na 5:1, 11 (tayari imenukuliwa), ukweli ni dhahiri kwamba njozi zote ni za tukio moja — hukumu. Moja inafichua ikitukia katika kipindi cha awamu ya pili cha mnyama dubwana, baada ya pembe yake iliyokuwa na macho ya mwanadamu na kinywa kilichonena mambo makuu kilikuwa kimekufuru (baada ya utawala wa Rumi ya Upapa), na kabla ya yule mnyama kuuawa na mwili wake kutolewa kuteketezwa kwa moto (Dan. 7:11) kabla ya Rumi kuangamizwa. Na ile njozi nyingine inaifichua ikitukia wakati fulani katika kipindi cha Ukristo, na ndani ya muda wa rehema. {TN8: 6: 2}

Danieli aliviona viti vya enzi vikiwekwa, na “Mzee wa siku,” Jaji, akaketi, kuonyesha kwamba Yeye wala viti vya enzi havikuwa hapo kabla. Bila shaka kwenye vile viti

6

vingine vya enzi, “viti,” waliketi wazee ishirini na wanne. Na hatimaye alimwona “Mwana wa Adamu,” Kristo, Wakili, akiletwa mbele ya “Mzee wa siku.” Kwa hivyo, Danieli na Yohana waliona “hukumu. . . ikiwekwa, na vitabu. . . vikafunguliwa.” {TN8: 6: 3}

Na kama vile Yohana aliwaona watu 144,000 wamesimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo baada ya hukumu kuwekwa na kabla ya kufungwa, tukio hilo hivyo halikuji kabla wala baada ya hukumu, ila ndani ya wakati huo. {TN8: 7: 1}

Na sasa kumbuka kwamba maono ya Yohana ya “Mwana-Kondoo kusimama juu ya mlima Zayuni” (Ufu.14:1) humfunua Kristo kama Mwokozi, ilhali maono yake ya “Simba wa kabila la Yuda” akisimama mbele ya hukumu humfunua Yeye kama Mfalme. Yakihusianishwa, yanaonyesha kwamba wakati ambapo Yeye ndiye Mwokozi, kwa wakati uo huo Yeye ni Mfalme wa wafalme. {TN8: 7: 2}

Sasa inakuwa wazi kuhusu ni lini watu 144,000 watatokea, ongezeko la kuchunguza linafuatia kuhusu wao ni nani. Kuona kwamba wao ni wafuasi wa Mwana-Kondoo (Wakristo), pia “wana wa Yakobo,” kwa hivyo wao ni

Waisraeli Kweli Kweli–Si Watu wa Mataifa. {TN8: 7: 3}

Kila mtu aliyeongoka kuwa Mkristo, akimpokea Kristo kama Mwokozi wake kibinafsi, amepata uzoefu ambao umepindua na kubadili kabisa mipango yake ya awali na matumaini, mwenendo wake wote wa maisha. Ameukana ulimwengu na “anasa zake zote za dhambi kwa kitambo” (Ebr. 11:25),

7

na amekuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo, aliyezaliwa upya, mrithi wa ufalme kulingana na ahadi! Hili ndilo Yesu alimaanisha alipomwambia Nikodemo: “Lazima uzaliwe mara ya pili.” Na Paulo, akiwa na ujuzi huu akilini, anasema: “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawasawa na ahadi.” Gal. 3:29. {TN8: 7: 4}

Bila kujali, kwa hivyo, iwapo mmoja ni Myahudi au mtu wa Mataifa, hawezi kuwa na sehemu katika ufalme wa Kristo, isipokuwa kwa kuzaliwa mara ya pili, ambapo anakuwa mmoja wa uzao wa Abrahamu. Badiliko hili la kiroho, hata hivyo, halifanyi kukazia utambulisho wa rangi ya mtu yeyote na nasaba ya kikabila. Haliwezi, kwa maneno mengine, kumfanya mmoja kuwa Myahudi ikiwa yeye si mzawa wa Yuda, au kumfanya Mwefraimu, ikiwa si mzawa wa Efraimu. Vivyo hivyo, watu 144,000, wakiwa wana wa Yakobo, hawawezi kuwa wa nchi za Mataifa. Wao kwa hivyo, kwanza, ni wazawa wa ukoo wa Yakobo, ingawa

Si Lazima wa Kundi la Wayahudi la Sasa Linalofahamika. {TN8: 8: 1}

Makabila kumi (ufalme wa Israeli) walichukuliwa mateka, wakatawanywa katika miji ya Waamedi (2 Wafalme 17:6), na hivyo wakazamishwa kabisa ndani ya bahari ya maisha ya mataifa yaliyowazunguka, na kufyonzwa, hivi kwamba walitoweka kabisa, kijamii, kwa kumbukumbu ya binadamu. {TN8: 8: 2}

Hali kadhalika, kwa vile kabila mbili (ufalme wa Yuda) zilichukuliwa mateka hadi Babeli,

8

na wachache tu walirejea Yerusalemu baada ya miaka sabini ya uhamisho wao kukamilika, umati kati yao pia ulipoteza utambulisho wao. {TN8: 8: 3}

Kisha, pia, kanisa la Kikristo la kwanza liliwajumuisha Wayahudi tu: mitume, watu 120 katika chumba cha juu (Mdo. 1:15), na watu 3,000 ambao waliongoka siku ya Pentekoste (Mdo. 2:41) wote walikuwa Wayahudi, walivyokuwa, hakika, takribani wote “walioongezwa kila siku” kwa miaka mitatu na nusu ya kwanza baada ya kusulubiwa (Dan. 9:26,27; Mdo. 2:47). Na hata baada ya kipindi hiki kupita, na mitume wakaagizwa kuipeleka Injili kwa Mataifa (Mdo. 13:46), Wayahudi wengi zaidi wakawa Wakristo, na baadaye, kama Wakristo badala ya Wayahudi, walitawanyika kati ya mataifa. {TN8: 9: 1}

Dhahiri, kwa hivyo, katika kila tukio wengi wa wana wa Yakobo walipoteza ujamii wao wa taifa. Bwana, hata hivyo, daima amehifadhi nasaba za mataifa yote, hasa za wana wa Yakobo, Yeye, kama alivyoahidi, “Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo. Naam, mintarafu Zayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara. Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo. Sela.” Zab. 87:4-6. {TN8: 9: 2}

Hivyo lilivyo bayana kama ajabu ni ukweli kwamba hakuna yeyote leo ila Myahudi anayefahamika

9

anaweza kuhakiki ukoo wake, na matokeo yake kwamba watu 144,000 wanaweza kukusanywa kutoka karibu kila taifa, jamaa, lugha, na watu, na bado ni wana wa Yakobo! {TN8: 9: 3}

“Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie watu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, Atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, Atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia. Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapiga-piga mlago bahari toka Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.” Isa. 11:11, 12; 27:12. {TN8: 10: 1}

Maadamu, kwa hiyo, historia, mantiki, na maandiko huchanganya ushahidi wavyo kuthibitisha kenyekenye kwamba Mungu amehifadhi nasaba ya tawi lililochaguliwa la jamii ya watu mbele kutoka kwa Adamu hadi kwa Nuhu (Mat. 1:1-17), na nyuma kutoka kwa Yesu hadi Adamu (Luka 3:23-38), Yeye lazima, basi, kwa sababu yenye upatano, pia amehifadhi utambulisho wa wateule leo. Na hili tunaliona, ni haswa ambalo Yeye amelifanya katika kutaja Kwake nasaba ya watu 144,000, kama “kutoka kila kabila ya

10

Waisraeli.” Ufu. 7:4. Na ingawa hatujui tulivyo, na hatuwezi kamwe wenyewe kujijua, Yule anayejua yote kutuhusu, hata kwa unywele wa mwisho wa kila kichwa, anajua ukoo wetu kikamilifu, ingawa wale wenzetu watakaokusanywa kutoka kwa uzao wa Yakobo ni, asema nabii, “kama mchanga wa bahari,” ilhali, kunena kwa kulinganisha, jamii ya Wayahudi wanaofahamika leo, ni wachache tu kwa mataifa, na kwa hivyo hawawezi kuwa wale ambao unahusu

Usemi Israeli, Efraimu, Yusufu. {TN8: 10: 2}

Tukirudi nyuma ki-nukta kwa majilio ya kihistoria kwa somo letu, tunakumbuka kwamba baada ya kifo cha Sulemani, taifa la Israeli (makabila kumi na mawili) liligawanyika katika falme mbili tofauti (1 Wafalme 11:11, 12; 12:19, 27). Ufalme wa kabila kumi, uliomiliki sehemu ya kaskazini ya nchi ya ahadi, uliitwa “Israeli,” pia Efraimu, na mara kwa mara nyumba ya Yusufu: “Israeli,” kwa sababu ya wingi wa makabila yake; Efraimu (Isa. 11:13), kwa sababu wafalme wake walitoka kwa Efraimu; na Yusufu (Ezek. 37:16), kwa sababu alikuwa baba wa Efraimu. Lakini ufalme wa kabila mbili, uliomiliki sehemu ya kusini, uliitwa “Yuda,” kwa sababu wafalme wake walikuwa wa kabila la Yuda, na kwa hivyo wazawa wake wanaitwa “Wayahudi.” Neno “Israeli,” vivyo hivyo, mara nyingi linahusu tu makabila kumi. Kwa hivyo, kuanzia hapa katika kurasa hizi, msomaji akutane na maneno, “Yuda,” “Israeli,” “Efraimu,” na

11

“Yusufu,” ataelewa bayana ni nani ambao yatakuwa yanawakilisha, na hivyo, tunapoendelea, ataelewa vyema mpango wa Mungu wa kuyakusanya makabila kumi na mawili ya Israeli, na kuwaunganisha tena katika

Ufalme Mmoja Mkuu. {TN8: 11: 1}

“Ufalme wa mbinguni” alisema Kristo, “umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.” Mat. 13:31,32. “Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu Wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.” Hos. 1:10. {TN8: 12: 1}

Walipoyasikia mafundisho ya Kristo, kisha wakayakataa na kumsulubisha Yeye, taifa la Wayahudi lilileta juu ya vichwa vyao hasara ambayo Mungu aliitangaza juu yao ambapo kupitia nabii Wake alisema: “Ninyi si watu Wangu, wala Mimi si Mungu wenu,” ingawa kwa wakati uo huo, kwa huruma Yake kuu, Aliruhusu ahadi iandikwe: “Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa [Waisraeli wa kale], ninyi si watu Wangu, hapo wataitwa [Waisraeli wa kale], wana wa Mungu aliye hai.” (Angalia Warumi 9:24-26). {TN8: 12: 2}

12

Hivyo, kwa furaha, watu wale wale, Israeli na Yuda, ambao waliwekwa kando na kutawanywa, “siku hiyo” (wakati wetu) watakubaliwa tena “watajikusanya pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea katika nchi hii.” Hos. 1:11. {TN8: 13: 1}

Baada ya kukaa “siku nyingi bila mfalme” (fungu lao tangu siku za uhamisho wao Babeli mpaka hata leo), “wana wa Israeli . . . kisha “(wakati fulani baadaye), yanasema maandiko,”. . . watarejea, na kumtafuta Bwana Mungu wao, na Daudi mfalme wao; na watamwendea Bwana na wema Wake kwa kicho siku za mwisho.” Hos. 3:4, 5. {TN8: 13: 2}

Lakini kwa sababu Daudi, mfalme wa Israeli wa zamani, alikuwa amekufa miaka mingi wakati unabii huu ulifanywa, na kwa vile haujawahi kutimizwa, alikuwa kivuli cha Daudi atakayekuja. {TN8: 13: 3}

Hivyo, ni wale “wanaomcha Bwana na wema Wake [Waisraeli Wakristo] katika siku za mwisho” (wakati wetu), ambao watamteua mmoja “kichwa” au “mfalme” — Daudi wa uakisi. {TN8: 13: 4}

(Kwa ajili ya somo kamili la Hosea 1 na 2, soma Trakti yetu Namba 4, Habari za Hivi Punde Kwa Mama.) {TN8: 13: 5}

Kutoka kwa ukweli wazi wazi katika aya zilizotangulia, tunaona kwamba wana wa Israeli, waliotawanyika na bila mfalme hizi “siku nyingi,” wata “rejea,” si kama Wayahudi, bali kama Wakristo. Hili shirikisho la

13

falme mbili za zamani, Yuda na Israeli, limewekwa katika nembo,

Vijiti Viwili Vilivyounganishwa. {TN8: 13: 6}

“Na wewe mwanadamu, twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake; ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe kimoja katika mkono wako. {TN8: 14: 1}

“Na wana wa watu Wangu watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonyesha maana ya mambo hayo utendayo? Waambie,

14

Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, Nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi Mwangu. {TN8: 14: 2}

[Picha ya Vijiti Viwili]

[Picha ya Vijiti Viwili Vilivyounganishwa]

“Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake, vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao.

15

Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, Nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; Nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele. Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini Nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, Nami nitawatakasa; basi watakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wao. Na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu Zangu, na kuzishika amri Zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi Wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi Wangu, atakuwa mkuu wao milele.” Ezek. 37:16-25. {TN8: 15: 1}

Unabii huu wa mfano hauhitaji kufasiriwa, kwa maana unajifafanua wazi kabisa: kuonyesha kwamba falme mbili za zamani, Yuda na Israeli, bado zitakusanywa kutoka kati ya “watu wa mataifa,” ambao kati yao walikuwa wametawanyika kwa muda mrefu na ya kwamba watakuwa tena taifa moja

16

kubwa — “ufalme, ambao hautaangamizwa milele.” Dan. 2:44. {TN8: 16: 1}

“Zaidi ya hayo,” asema Bwana, “Nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; Nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu Pangu Nitapaweka katikati yao milele. Tena maskani Yangu itakuwa pamoja nao; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Na mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, Mimi niwatakasaye Israeli, patakatifu Pangu patakapokuwa katikati yao milele.” Ezek. 37:26-28. {TN8: 17: 1}

Kwa sababu Mungu husema kwamba Yeye “atawazidisha” wakati watakapokuwa ufalme tena, na ya kwamba “mataifa watajua ya kuwa Ndimi Bwana Mimi niwatakasaye Israeli,” na kwa vile Yeye hawezi “kuzidisha” au “kutakasa” baada ya kufungwa kwa muda wa rehema, falme mbili za zamani lazima kwa uhitaji, hatimaye, zirejeshwe na kuunganishwa wakati wa kipindi cha muda wa rehema —

“Nyakati za Urejesho.” {TN8: 17: 2}

Watu 144,000 wakiwa ni “malimbuko,” lazima kwa hivyo yawepo mavuno ya pili, kwa maana palipo ya kwanza, lazima pia iwepo ya pili. Na kwa vile malimbuko ni “watumwa wa Mungu,” lazima baadaye watumwe kwa mataifa yote kuyakusanya mavuno ya pili (Isa. 66:19, 20) — umati mkubwa (Ufu. 7:9) ambao Yohana aliona baada ya kutazama kutiwa muhuri watu 144,000. (Kwa ajili ya uchunguzi wa kina wa mada hii, — watu 144,000 na

17

umati mkubwa, — tazama Trakti yetu Namba 1, Ya Ziada Kabla Ya Saa Kumi Na Moja!; Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1). {TN8: 17: 3}

Ukweli kwamba “katika vinywa vyao haukuonekana uongo” (Ufu. 14:5), unaenda kuonyesha waziwazi kwamba watatangaza sufuri ila ukweli safi wa injili, na kuyafanya maneno yao yenye mamlaka na lazima kama maneno yaliyoandikwa ya manabii na mitume. Hakika malimbuko hawa wanawekezwa kwa nguvu zaidi na mamlaka: “Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 12:8. {TN8: 18: 1}

Pia “katika siku hiyo,” anaendelea kusema Zekaria, “watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.” Zek. 13:1. {TN8: 18: 2}

Wakati chemchemi hii “kwa dhambi na unajisi” hatimaye inapofunguliwa “kwa watu wa nyumba ya Daudi,” ushahidi wa kutiwa taji utaonekana kwamba kuunganishwa kwa zile falme mbili ni ukweli uliotimizwa, na ya kwamba wakati umefika wa kuitangaza injili katika ulimwenguni wote. {TN8: 18: 3}

“Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena;

18

pia Nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.” Zek. 13: 2. Yaani, wakati ule ambapo ufalme huu wa kutangaza injili utaanzishwa, litakuwa kanisa bila uongo — huru kutoka kwa waabudu sanamu na waalimu wa uongo. Na litalishwa na “mchungaji mmoja. . . naam, mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na Mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; Mimi, Bwana, nimesema haya.” Ezek. 34:23, 24. {TN8: 18: 4}

Wakati Bwana anachukua hivyo “mqmlaka mikononi Mwake mwenyewe” (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300), na kutawala tena kanisa kama serikali ya kitheokrasi (katika siku za mwisho), “Na itakuwa,” anavyosema Isaya, “. . . mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Isa. 2: 2-4. {TN8: 19: 1}

Hivyo katika kuingia kwa ufalme huu wa milele, na hatua ya urejesho wa

19

mambo yote, utakuwapo upande mmoja uamsho mkuu kati ya mataifa; yakikwangua mabohari makubwa ya zana za vita ambazo kwa miaka mingi yamekuwa yakizihifadhi, yatatafuta kukwea na kuwa raia wa ufalme, na kujiunga na majeshi ya Bwana, kumruhusu Yeye awapiganie; ambapo kwa upande mwingine yatakuwapo maandalizi ya haraka ya vita miongoni mwa wale watakaokataa kuamshwa: kuwavurumisha wote katika mpango hodari wa kutengeneza silaha, kugeuza hata zana zao za kilimo kuwa silaha za vita dhidi ya ufalme wa Kristo — kanisa lake (Yoeli 3:9-12; Zek. 12:3). {TN8: 19: 2}

“Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Zayuni wa Mtakatifu wa Israeli.” Isa. 60:11, 14. (Kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu awamu hii ya somo hili, angalia Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, uk. 173-181, ikielezea “Mika Nne.” Na kama mfano wa jinsi vita ni vya Bwana , soma 2 Mambo ya Nyakati 20:15,19, 24-30.) Lakini kwa kuwa mbali, mbali sana, kutoka kwa hadhi hii ya juu na takatifu,

Kanisa Lazima Litakaswe. {TN8: 20: 1}

Hakuna Mkristo wa imani yoyote anayeweza kukataa kwa uaminifu hitaji la kanisa kutakaswa. Na

20

kwa vile Bwana kamwe hafanyi jambo lolote bila umbele kulionya kanisa Lake, sasa Yeye analitumia ujumbe wa utakaso, ili kulipatia mwonjo wa utukufu wa baadaye, ili kwamba kama mwito wazi wa mbinguni kwa matengenezo unapoendelea kuvuma miongoni mwa watu Wake, wanaweza kuwa na furaha ya umakini kwa ukweli Wake, na waweze kujitoa kwa moyo wote kwa kazi ajili ya matengenezo, hivi sasa wakati Yeye anaweka wazi mbele yao mpango Wake wa kuuanzisha ufalme Wake na matokeo ya mwisho kwa wadhambi. Wale ambao wanatii kabisa mwito huu, watakuwa na tumaini lisilozuilika kuja kikamilifu kwenye safu na kumruhusu Bwana awatenganishe kutoka kwa dhambi na wadhambi. Wao tu wataupokea muhuri wa Mungu na kama malimbuko ya ufalme, watu 144,000 wenye nguvu, watasimama na Mwana-Kondoo juu ya “Mlima Zayuni”! {TN8: 20: 2}

Hali kama hii ya utakatifu leo, jinsi ilivyokuwa zamani, itasababisha joka kumkasirikia mwanamke, pia sasa kufanya vita na masalia wake (Ufu. 12:17), pambano ambalo linaelezwa zaidi kwa maneno: {TN8: 21: 1}

“Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, [wakati wa kutiwa muhuri watu 144,000], wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru

21

nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 7:1-3. {TN8: 21: 2}

Hapa yanaletwa kwa mtazamo madhara mawili yaliyo karibu kutukia: moja na pepo, lingine na malaika; na amri mbili kwa malaika: moja ya kwamba wazuie pepo, pepo sizivume “juu ya nchi, wala bahari, wala juu ya mti wowote” (Ufu. 7:1); nyingine kwamba malaika wajizuie kudhuru “juu ya nchi, wala bahari,” na “miti,” mpaka watumwa wa Mungu watiwe muhuri. Ufu. 7:2, 3). Maadamu, kwa hivyo, mara tu watumwa wa Mungu watakapotiwa muhuri upepo na malaika wataanza kudhuru swali linaibuka kuhusu ni nini kazi ya pepo na kazi ya malaika huwakilisha — mzozo wa kisiasa au kitu kingine? Kwa sababu mataifa daima yamekuwa katika vita, kazi hii maradufu ya kudhuru haiwezi kuwakilisha mzozo wa kisiasa. Na kama Yesu anavyosema kwamba wakati wa mwisho “taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;” (Mat. 24:7), ni wazi kwamba kudhuru kwa pepo, pia kudhuru kwa malaika yote mawili yanazuiliwa mpaka watu 144,000 watiwe muhuri, lazima yawe mfano wa kuzuia “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo.” Dan. 12:1. Kwa hivyo, Mungu kuzizuia pepo nne ni kuzuia Kwake shughuli za sanamu ya mnyama (Ufu. 13:15-17) dhidi ya watakatifu, wakati ambapo Kwake kuwazuilia malaika wanne kwamba wasidhuru ni kuzuia Kwake kutekeleza kisasi

22

Chake (Isa. 63:1-4; Yer. 51:18) kwa wadhambi wanaolitaabisha kanisa, mpaka baada ya kutiwa muhuri kwa watu 144,000 kukamilika. Kwa sababu yamefungamana, madhara haya mawili yataleta wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa. {TN8: 22: 1}

Ufunuo 7:1-3, kwa hivyo, hufunua vita maradufu: watu waovu dhidi ya Mungu (kuvuma kwa pepo) na Mungu dhidi yao (malaika wakiwadhuru). Lakini ingawa kuvuma kwa pepo na kudhuru kwa malaika baada ya watumwa wa Mungu kutiwa muhuri, kutaleta “wakati wa taabu,” hata hivyo “ kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile” “ataokolewa.” Dan . 12:1. {TN8: 23: 1}

Kutoka kwa kweli hizi tunaona kwamba wakati huu wa taabu unazuiliwa ili kulinda kutiwa muhuri kwa watumwa 144,000, ili wasije “wateule” wakaletwa chini ili waiabudu sanamu ya mnyama, au kuuawa kwa kukataa. {TN8: 23: 2}

Kwa sababu “katika Ufunuo vitabu vyote vya Biblia hukutana na kwishia” (Matendo ya Mitume, uk. 585), kutiwa muhuri kwa watumwa wa Mungu (Ufu. 7) lazima kwa hitaji kupatikane pia katika unabii. Katika Ezekieli, sura ya tisa, yapo maono ya kumaki wale wanaougua na kulia “kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake” (ndani ya Yuda na Israeli), na mchinjo kwa wale ambao hawaugui hivyo na kulia. Na ukweli kwamba Mungu hajawahi kuwaondoa wadhambi kutoka kati ya wenye haki ndani ya Yuda na Israeli, unaonyesha kwamba unabii huu

23

wa utakaso kwa mchinjo haujawahi kutimizwa. Basi, kwa hivyo, kwa sababu kumaki ni sawa na kutiwa muhuri, malaika kuchinja ni sawa na kudhuru kwa malaika. {TN8: 23: 3}

Huku kudhuru na kutia muhuri alivyoona Yohana, na kuchinja na kumaki alivyoona Ezekieli kumetambuliwa tena kama tukio moja na sawa: “Huu utiwaji muhuri kwa watumwa wa Mungu ni sawa na ule ulioonyeshwa Ezekieli katika maono.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211; Gombo la 3, uk. 267. {TN8: 24: 1}

Ingawa kumaki na mchinjo (Ezek 9) unatimizwa kanisani tu, — Yuda na Israeli, — kudhuru kwa pepo na kudhuru kwa malaika (Ufu. 7) kunatimizwa ulimwenguni kote — “nchi” na “bahari,” ambayo kila moja ni kiashirio cha eneo tofauti: bahari, katika milki ya asili ni ghala (nyumba) la maji, kwa hivyo ni katika milki ya mifano mahali yalipoanzia mataifa — Nchi ya Kale, nchi, kinyume na bahari, vivyo hivyo ni eneo la mbali na Nchi ya Kale. Inatambulishwa kwa Yohana katika nembo ya mnyama wa pembe mbili akiinuka, si kutoka baharini, ila “katika nchi” (Ufu. 13:11), mahali pa pekee ambapo miti hukua. Na kwa mujibu wa Danieli 4:20-22, miti ni mfano wa watawala, kwa hivyo miti katika mfano huu huwakilisha “wazee. . . mbele ya nyumba” (Ezek. 9:6) — ukweli ambao unafichua kwamba katika kipindi hiki, makao makuu ya kanisa yamo katika milki ya mnyama wa pembe mbili — Ulimwengu Mpya, “nchi.” {TN8: 24: 2}

24

Katika nuru ya kweli wazi zilizo mbele yetu, tunaona kwamba lengo kuu la kutia muhuri au kumaki watumwa wa Mungu ni kulisafisha kanisa kutoka kwa dhambi na wadhambi, ili kwamba liweze kusimama imara dhidi ya sanamu ya mnyama katika wakati wa taabu; na ya kwamba wakati kazi hii ya utakaso inapomalizika, “Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.” Isa. 4:3, 4. {TN8: 25: 1}

Wakati hii “kazi maalum ya utakaso, ya kuondoa dhambi kati ya watu wa Mungu,” imetimizwa, wakati huo “kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho. Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango, ‘litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — Pambano Kuu, uk. 425; Manabii na Wafalme, uk. 725. {TN8: 25: 2}

“Tena juu ya makao yote ya mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia

25

na kujificha wakati wa tufani na mvua.” “Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.” Isa. 4:5, 6; 62:12. {TN8: 25: 3}

“Kanisa lote, likitenda kama moja, likichangamana katika umoja mkamilifu, litakuwa hai, chombo kiamilifu cha umishonari, kinachokwenda na kudhibitiwa na Roho Mtakatifu.” “Yote ambayo mitume walifanya, kila mshirika wa kanisa leo anapaswa kufanya.” “Watendakazi Wake hatimaye wataona jicho kwa jicho, na mkono wa Bwana, nguvu ambayo ilionekana katika maisha ya Kristo, itafunuliwa.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 47; Gombo la 7, uk. 33; Gombo la 9, uk. 33. {TN8: 26: 1}

Kisha itakuwa, asema Bwana, “Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana Mungu, Nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. {TN8: 26: 2}

“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu,

26

nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote; Nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena. Nami nitazidisha matunda ya miti, na mazao ya mashamba, msipate tena kutukanwa na mataifa kwa sababu ya njaa. {TN8: 26: 3}

“Ndipo mtazikumbuka njia zenu mbaya, na matendo yenu yasiyokuwa mema, nanyi mtajichukia nafsi zenu kwa macho yenu, kwa sababu ya maovu yenu na machukizo yenu. Ijulikane kwenu ya kuwa Silitendi neno hili kwa ajili yenu, asema Bwana Mungu; tahayarikeni, na kufadhaika, kwa sababu ya njia zenu, Enyi nyumba ya Israeli. Bwana Mungu asema hivi; siku ile Nitakapowatakaseni na maovu yenu yote, Nitaifanya miji ikaliwe na watu, na palipobomolewa pajengwe tena. Ndipo mataifa, waliobaki karibu yenu pande zote, watajua ya kuwa Mimi, Bwana, nimejenga mahali palipoharibika, Nami nimepanda mbegu katika nchi iliyokuwa ukiwa; Mimi, Bwana, nimesema hayo; tena Nitayatenda.” Ezek. 36:23-33, 36. {TN8: 27: 1}

Tena: “Katika kulitakasa hekalu kutoka kwa wanunuzi na wauzaji wa dunia, Yesu aliutangaza utume Wake,” kwanza, “kuusafisha moyo kutoka kwa unajisi wa dhambi, — kutoka kwa tamaa za kidunia, uchu wa ubinafsi, tabia za uovu, ambazo huiharibu nafsi” (Tumaini

27

la Vizazi Vyote, uk.161); na pili, kulitakasa kanisa lote kutoka kwa dhambi na wadhambi. Mara mbili (moja katika kufungwa kwa utangazaji wa Yohana Mbatizaji wa ufalme, na katika ufunguzi wa kipindi cha injili, mwanzoni mwa ukasisi wa Kristo, na mara moja kwa kuifunga kazi Yake na kuifungua ya mitume — Shuhuda Maalum kwa Wachungaji, Namba 7, uk. 54) Yeye alilitakasa hekalu kutoka kwa mazoea maovu ambayo Wayahudi walikuwa wamelitia unajisi (Yoh. 2:15 16, Mat. 21:12, 13), Yeye hivyo basi alipeana onyo mara mbili katika kivuli kwamba pia katika kufungwa kwa kipindi cha Kikristo, Yeye atalitakasa kanisa Lake mara mbili: mara moja wakati wa kutiwa muhuri malimbuko watu 144,000, na tena wakati wa kutiwa muhuri mavuno ya pili, “umati mkubwa.” Ufu. 7:1- 9. {TN8: 27: 2}

Kwa sababu huu utakaso maradufu, zaidi ya hayo, ulitukia katika sikukuu ya Pasaka, na maadamu pia, wote ambao “hawakuwa wamejitakasa vya kutosha” (2 Nya. 30:3, Kut. 12:3-6) walikatazwa kushiriki katika Pasaka mwezi wa kwanza, lakini waliruhusiwa kujitayarisha na kuiadhimisha mwezi wa pili (Hes. 9-11; 2 Nya. 30:13), kwa hivyo ni mfano wa utakaso wa kanisa katika sehemu mbili, hivyo kuonyesha tena kwamba upo ukusanywaji maradufu, kutiwa muhuri maradufu, mitengo miwili, makundi mawili — malimbuko na mavuno ya pili. (Kwa ajili ya maelezo zaidi ya kutiwa muhuri mara mbili tazama Trakti yetu Namba 1, Ya Ziada Kabla Ya Saa Kumi Na Moja!, na kwa uakisi wa Pasaka, Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 256). {TN8: 28: 1}

28

“Lazima uwepo,” inasema Roho ya Unabii, “utakaso wa taasisi sawa na ule wa Kristo kulitakasa hekalu la zamani. “Imeandikwa, asema BWANA, ‘Nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala, lakini mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi. Zipo katika taasisi zetu leo shughuli za kibiashara zinazofanana na zile zilizofanyika katika nyua za hekalu Wakati wa Kristo; na mbingu yote inatazama. . . Bwana atafanya kazi kulitakasa kanisa Lake. Nawaambia katika kweli, Bwana yu karibu kupindua na kupindua-pindua katika taasisi zinazoitwa kwa jina Lake. Jinsi gani kwa upesi mchakato huu wa kusafisha utaanza, siwezi kusema, lakini hautakawia kwa muda mrefu. Yeye Ambaye pepeto Lake li mkononi Mwake atalisafisha hekalu Lake dhidi ya unajisi wa maadili yake. Atausafisha uwanda Wake kabisa.” — Ndugu Katika Nyadhifa Za Madaraka, Septemba 1895. {TN8: 29: 1}

Katika kihakiki cha ki-mfano cha utakaso wa kanisa, Kristo alitangaza: “. . . malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki” (Mat.13:49) — kuwaondoa waovu na kuwaacha wema; ilhali katika Ufunuo, akiwatangazia walio Wake Babeli, anasema: “Tokeni kwake, enyi watu Wangu” (Ufu. 18:4) — kuwaita wenye haki watoke na kuwaacha waovu ndani. Wa awali wanatakaswa huku waovu wakitupwa nje kutoka kati yao; wa mwisho, wakiondolewa kutoka kati ya waovu. {TN8: 29: 2}

Pia ipo mifano miwili tofauti ya talanta (Mat. 25:15-30; Luka 19:13-27),

29

yote miwili wazi wazi inaingia kwenye picha katika mazingira yake ya sasa. Katika mmoja, ni watumwa watatu; katika mwingine, watumwa kumi. Tofauti hii muhimu inaonyesha kwamba wa awali una matumizi ya ndani tu, ilhali wa mwisho una matumizi ya ulimwengu wote (hivyo kuonyesha, inavyofanya Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 85, 86, kwamba katika Maandiko, namba “kumi” husimamia ulimwengu wote, na namba “tatu” kwa Utatu ndani ya kanisa). {TN8: 29: 3}

Kweli hizi zisizoweza kutanguliwa za kivuli na mfano na “neno la ushuhuda Wake,” zinatuleta uso kwa uso na uhalisi mzito kwamba tumekuja kwa wakati wa pasaka ya uakisi na utakaso wa hekalu, na kwa mavuno ya dunia, — “Siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” Roho wa Mungu hutuhimiza “kwa kitisho cha kicho, ‘Jitayarishe! jitayarishe! jitayarishe! kwa maana ghadhabu kali ya Bwana itakuja hivi karibuni. Hasira Yake itamiminwa, pasipo kuchanganywa na huruma, na hamjakuwa tayari. Rarueni mioyo, na si mavazi.’” — Maandishi ya Awali, uk. 119. {TN8: 30: 1}

O yeyote asiruhusu kupotoshwa katika kufikiri kwamba baada ya kufungwa kwa muda wa rehema, au baada ya ujio wa pili wa Kristo (baada ya wadhambi ulimwenguni kuangamizwa), kanisa la Mungu litafikia kiwango cha juu cha tabia, na kwa ofisi ya juu, iliyoteuliwa na mbingu, na kutakaswa kutoka kwa dhambi na wadhambi! Kinyume chake, “katika siku hiyo” (kabla ya wadhambi duniani

30

kuangamizwa), asema Bwana, “Tena itakuwa siku hiyo, Nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake. Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao. Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba Nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.” “Siku hiyo katika njuga za farasi yataandikwa maneno haya, WATAKATIFU KWA BWANA; navyo vyombo vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu. Naam, kila chombo katika Yerusalemu, na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa Bwana wa majeshi; nao wote watoao dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya nyumba ya Bwana wa majeshi.” Zek. 12:3, 8, 9; 14:20, 21. {TN8: 30: 2}

Aya hizi zinatangaza wazi wazi kwamba kanisa litakuwa “kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao,” katika wakati wa taabu, wakati ambapo mataifa watakusanyika dhidi yake na Bwana kwa kisasi atawapiga. Muda wa rehema bado unakawia kawia ambapo msururu huu wa matukio unafanyika, “nao wote watoao dhabihu” (tendo linalofanyika kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema) watakuwa kwa hivyo watakatifu, na “hatakuwamo

31

tena mfanya biashara katika nyumba ya Bwana.” {TN8: 31: 1}

Kila mwanafunzi wa kweli wa Biblia anajua kwamba kanisa lazima lifikie usafi huu wa moyo na tabia na nafasi, si baada, ila kabla, kazi ya upatanisho ya Kristo kumalizika na kabla ya “dhabihu” kukoma. Wanafunzi wote wa namna hii wanajua pia kwamba Mungu hawezi kuudhihirisha uwezo Wake mkubwa wa kuwalinda katika wakati ambapo “watu wote wa dunia wanajikusanya pamoja dhidi” yao, wala kuwajazi Roho Wake kama alivyofanya kwa Wakristo wa kwanza siku ya Pentekoste, iwapo wapo wadhambi miongoni mwa watu Wake, na ikiwa kanisa lote haliko “mahali pamoja” (Mdo. 2:1), “likiwa limevaa silaha za haki ya Kristo. . . Zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lililo na mabango’ — kama lilivyokuwa kanisa la mitume, ambalo Roho alishuka kama “upepo wa nguvu ukienda kasi.” Mdo. 2:2. {TN8: 32: 1}

“Wale tu,” inasema Roho ya Unabii, “ambao wameyahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka kuingia katika Kilio Kikuu.” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {TN8: 32: 2}

Na ya kwamba Kilio Kikuu kishindwe kuvuma kwa wakati au kisivume, wale ambao hawawezi kushinda, ambao “waliusaliti uaminifu wao,” — “wazee wa kale, wale ambao Mungu alikuwa amewapatia nuru kubwa, na waliosimama kama walezi wa maslahi ya kiroho ya watu,” — lazima waondolewe. “Hili kwa mkazo limewekwa mbele kwa mfano wa nabii kuhusu kazi ya mwisho chini ya kielelezo cha watu kila mmoja akiwa na chombo cha kufisha mkononi mwake.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266. “Watu, wajakazi, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {TN8: 32: 3}

Tunapokabiliwa na uhakika mkubwa wa utakaso ulio karibu wa kanisa, kutiwa muhuri, na utukufu unaofuata, tunaharakisha kuikabili

Hali ya Kanisa Hasa Kabla ya Utakaso. {TN8: 33: 1}

“Ni udanganyifu mkubwa jinsi gani ulioje unaoweza kuja kwa akili za wanadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui ya kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ilhali wale wanaohutubiwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umaskini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayenena, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {TN8: 33: 2}

“Ni nani anaweza kusema kwa kweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto; mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimwona Mwalimu wetu akiyaonyesha

33

mavazi ya kile kinachoitwa eti utakatifu. Aliyararua, Akaufunua wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha akanambia: ‘Je, huoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia?’ “Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba?” Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu zinakosekana.’” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {TN8: 33: 3}

“Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao . . . Mbwa hawa bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {TN8: 34: 1}

“Ni vigumu kwa wale ambao wanajihisi salama katika ufanisi wao, na wanaojiamini kuwa ni matajiri katika maarifa ya kiroho, kuupokea ujumbe ambao unatangaza kwamba wamedanganywa na wanahitaji kila neema ya kiroho. Moyo ambao haujatakaswa ni ‘mdanganyifu kuliko vitu vyote, na ni mbaya kabisa.’” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253. {TN8: 34: 2}

“Wako wengi ambao hawana busara ya Yoshua, na ambao hawana wajibu maalum kusaka makosa, na kushughulikia haraka dhambi zilizo miongoni mwao. Watu kama hawa wasiwazuie wale walio na

34

mzigo wa kazi hii juu yao; Waache kusimama katika njia ya wale walio na wajibu huu kuufanya. Wengine hufanya kuwa swala la kuhoji, na kuwa na shaka, na kutafuta kosa, kwa sababu wengine wanafanya kazi ambayo Mungu hajaitwika juu yao. Hawa husimama moja kwa moja kwenye njia kuwazuia wale ambao Mungu amewatwika mzigo wa kukemea na kurekebisha dhambi zilizopo, kwamba kununa kwake kuweze kugeuzwa mbali na watu wake. Laiti kesi kama ya Akani ingekuwa kati yetu, wapo wengi ambao wangewashtaki wale ambao wangeweza kutenda sehemu ya Yoshua kusaka makosa, kwamba wanayo roho ya uovu, ya kutafuta makosa. Mungu hapaswi kuchezewa shere, na maonyo Yake kupuuzwa na kudhihakiwa na watu wapotovu. {TN8: 34: 3}

“Ghadhabu ya Mungu iko juu ya watu wake, Yeye hataweza kuzidhihirisha nguvu Zake kati yao wakati dhambi zipo kati yao, na zinakuzwa na wale walio katika nafasi za majukumu. {TN8: 35: 1}

“Wale wanaotenda kazi katika kicho cha Mungu ili kuliondolea kanisa vizuizi, na kurekebisha makosa tele ili watu wa Mungu waweze kuona umuhimu wa kuchukia dhambi, na kufanikiwa katika usafi, na ya kwamba jina la Mungu liweze kutukuzwa, siku zote watakumbana na ushawishi wa kupinga kutoka kwa wasioamini. Hivi Zefania anaelezea hali halisi ya daraja hili, na hukumu za kutisha zitakazowajia:- {TN8: 35: 2}

“Na itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa,

35

Nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko. . .” Zef. 1:12, 14. {TN8: 35: 3}

“Wakati hatari hatimaye inakuja, hakika itakavyokuja, na Mungu kunena kwa niaba ya watu wake, wale ambao wamefanya dhambi, ambao wamekuwa wingu la giza, na ambao wamesimama moja kwa moja njiani dhidi ya Mungu kufanya kazi kwa ajili ya watu wake, wataweza kuhofia umbali ambao wamekwenda kwa kunung’unika na kuleta madhila kwa kazi; na, kama Akani, wakiwa na hofu, watatambua kwamba wamefanya dhambi. Lakini maungamo yao yatakuwa yamechelewa sana, na yasiokuwa ya namna sahihi kuwafaidi, ingawa wataweza kuiondolea huzuni kazi ya Mungu. . . {TN8: 36: 1}

“Wale ambao wamekuwa karibu maisha yao yote wakiongozwa na roho ya kigeni kwa Roho wa Mungu kama ilivyokuwa ya Akani, watakuwa wasiotenda kitu wakati unapokuja kwa ajili ya hatua ya uamuzi kwa sehemu ya wote. Hawatadai kuwa upande wowote.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 270-272. {TN8: 36: 2}

“Tumekuwa na mwelekeo wa kufikiri kwamba pale ambapo hakuna wachungaji waaminifu, hawawezi kuwapo Wakristo wakweli; lakini hii sivyo. Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji si waaminifu Yeye atachukua usimamizi wa kundi mwenyewe. Mungu hajawahi kamwe kulifanya

36

kundi livitegemee kabisa vyombo vya kibinadamu. Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika upepeto mkuu utakaotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha ya kwamba pepeto Lake li mkononi Mwake, Naye atausafisha uwanda Wake kabisa.” {TN8: 36: 3}

“…Wale ambao wameamini katika akili, ustadi, au talanta, hawatasimama baadaye kuwa viongozi wa askari. Hawakufululiza mwendo na nuru. Wale ambao wamejithibitsha kuwa si waaminifu baadaye hawatakabidhiwa kundi. Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa kupepetwa, wa kupimwa watafunuliwa waonekane. Wapo sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu. Lakini, inaweza kuwa chini ya hali ngumu isiyopendeza ya nje ambapo waangavu wa tabia halisi ya Kikristo itafunuliwa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, 81. {TN8: 37: 1}

Mfululizo wa taarifa zilizotangulia zinaonyesha kwamba kanisa lazima litakaswe kabla watu wengine wa Mungu wakusanywe “kutoka katika nchi zote.” Kisha “katika siku zile, na wakati huo, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,” asema Bwana

37

“Nitakusanya mataifa yote, Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko Nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi Yangu.” Yoeli 3:1, 2. {TN8: 37: 2}

Lakini kuokolewa kutoka utekwani, na kumsikia Bwana “akiwahukumu. . . huko” kwa ajili ya watu Wake, mtu hawezi kudharau sasa

Kusihi Kwake. {TN8: 38: 1}

“Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia Mimi? asema Bwana. Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako. Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika. Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, Wewe u Kiongozi wa ujana wangu? {TN8: 38: 2}

“Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana Mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele. Ungama uovu

38

wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti Yangu, asema Bwana. Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana Mimi ni mume wenu; Nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, Nami nitawaleta hata Zayuni; Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo Wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu. Kisha itakuwa, mtakapoongezeka na kuwa wengi katika nchi hiyo, asema Bwana, siku zile hawatasema tena, Sanduku la agano la Bwana; wala halitaingia moyoni; wala hawatalikumbuka, wala hawatalizuru, wala hayatafanyika hayo tena. Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha Bwana; na mataifa yote watakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya. Siku zile nyumba ya Yuda watakwenda pamoja na nyumba ya Israeli, nao watakuja pamoja, kutoka nchi ya kaskazini, mpaka nchi ile niliyowapa baba zenu iwe urithi wao.” Yer. 3:1-4, 12-18. {TN8: 38: 3}

Hata hivyo, asema Bwana: “Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao,

39

na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” Mal. 4:5, 6. {TN8: 39: 1}

“Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula. . . Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele ya Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; Nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi Mimi, asema Bwana wa majeshi. Kwa kuwa Mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.” {TN8: 40: 1}

“Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo Yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni Mimi, Nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? {TN8: 40: 2}

“Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia Mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia

40

kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia Mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba Yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama Sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. {TN8: 40: 3}

“Maneno yenu yamekuwa magumu juu Yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu Yako kwa namna gani? Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo Yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele Ya Bwana wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio wakombolewao. {TN8: 41: 1}

“Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele Yake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina Lake. Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina Yangu hasa; Nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.

41

Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.” Mal. 3:1-18. {TN8: 41: 2}

“Kwa ajili ya hayo Bwana, Mungu, asema hivi, Tazama, Naweka jiwe katika Zayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka. Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri. {TN8: 42: 1}

“Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo. Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu. Maana kitanda kile ni kifupi asiweze mtu kujinyosha juu yake, na nguo ile ya kujifunika ni nyembamba asipate mtu kujizingisha. Maana Bwana ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; Apate kufanya kazi Yake, kazi Yake ya ajabu; na kulitimiza tendo Lake, tendo Lake la ajabu. Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, Bwana wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia. {TN8: 42: 2}

42

“Tegeni masikio, sikieni sauti Yangu, sikilizeni mkasikie neno Langu.” Isa. 28:16-23. {TN8: 43: 1}

Kwa sababu “Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji si waaminifu atachukua usimamizi wa kundi Mwenyewe.” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300; Yer. 3:17), na kama wazawa wa Yakobo, kuwa ufalme tena, kujiwekea wenyewe kichwa kimoja (Hos. 1:11), “Daudi mfalme wao” (Hos. 3:5), “na kumtafuta Bwana Mungu wao,” ni wazi ya kwamba kanisa katika wakati wa Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu,

Litakuwa Theokrasia. {TN8: 43: 2}

“Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.” Mwa. 49:10. {TN8: 43: 3}

“Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.” Isa. 32: 1, 2. {TN8: 43: 4}

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi Yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika

43

kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo. Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.” Isa. 9:6-8. {TN8: 43: 5}

“Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono Wake ndio utakaomtawalia Yeye; Tazameni, thawabu Yake i pamoja Naye [wakati huo Yeye atawapatia ufalme] na ijara Yake i mbele Yake [wakati huo atawakusanya watu Wake].” Isa. 40:10. {TN8: 44: 1}

“Basi litatoka chipukizi katika shina la Yesse,” anatabiri Isaya kwa mchoro wa mfano wa ushindi huu wa utukufu wa kusudi la Mungu, “na Tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na Roho ya Bwana atakaa juu yake, Roho ya hekima na ufahamu, Roho ya shauri na uweza, Roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa nchi kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.” Isa. 11:1-5. {TN8: 44: 2}

44

[Picha: Kielezi cha Ufalme]

Katika kielezi hiki wapo watu watatu waliotajwa: Yesse (babaye Daudi), fimbo (Daudi), na Tawi (Kristo). Uhusiano huonyesha kwamba Daudi (fimbo) si Kristo (Tawi), kwa maana “fimbo” imechipuka kutoka kwa shina

45

la Yesse, na Tawi kwa fimbo — ukweli uliojitokeza katika kilio cha umati Kristo alipoingia Yerusalemu. Walipiga kelele: “Hosana kwa mwana wa Daudi.” Mat. 21:15. Dhahiri, kwa hivyo, “fimbo,” inayochipuka kutoka kwa shina la Yesse, ni nembo inayoashiria Daudi; na Tawi, linalochipuka kwa fimbo, ni nembo inayoashiria mwana wa Daudi — Kristo. {TN8: 45: 1}

Juu ya “Ishara” hii (Tawi na fimbo) “Roho wa Bwana atakaa . . . , roho wa hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.” Isa. 11:2-5. {TN8: 46: 1}

Hivyo ingawa “Ishara” ni nembo ya mwunganisho wa watu watatu (Yesse, shina; Daudi fimbo na Kristo, Tawi), lakini uwezo na hekima ya Kristo ni msingi na nguvu yake ya kudhibiti. Kwa hivyo Kristo asema hivi: “Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.” (Ufu. 22:16), akionyesha kwamba Yeye ni yote na katika yote. {TN8: 46: 2}

46

Maana kwa hivyo kutoka kwa “shina” la Yesse ilikuja “fimbo” (Daudi), na kutoka kwa fimbo lilichipuka Tawi (Kristo), Daudi mfalme anayeonekana na Kristo Mfalme wa wafalme asiyeonekana “katika siku hiyo” — wakati wetu — hujumuisha ile “ishara,” na kwayo “ watu wa Mataifa wataitafuta: na tuo lake [au mahali Pake pa kupumzika, — eneo ambalo” fimbo “au ishara inasimama — ufalme] litakuwa na utukufu.” Naam “Nami nitapatukuza mahali pa miguu Yangu” (Isa. 60:13), asema Bwana. {TN8: 47: 1}

“Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi Wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na Mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; Mimi, Bwana, nimesema haya. Nami nitafanya agano la amani nao, Nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni.” Ezek. 34:23-25. {TN8: 47: 2}

Hivyo kanisa Lake, au ufalme, tena linaonyeshwa bila “doa, au kunyanzi, wala lolote kama hayo” (Efe. 5:27), ufalme wa amani, usalama, na kutoshindwa, chini ya utawala wa mchungaji mmoja na mfalme — Daudi, mtumishi Wake. Lakini ukweli kwamba wafalme wengi walitawala juu ya Israeli, ungeweza kuzusha swali katika baadhi ya akili: {TN8: 47: 3}

Mbona Daudi Mfano?

Hapana shaka kwa sababu yeye ndiye pekee anayefaa kikamilifu uakisi — uongozi

47

katika wakati wa Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu. Hili likiwa ni hivyo, basi ni lazima inavyofuata kwamba Sauli, mfalme wa kwanza ambaye alitawala juu ya Israeli, na ambaye aliwajibika pakubwa kwa ujuzi wa mapema wa maisha ya Daudi, ni mfano wa uongozi wa kanisa katika kipindi cha kabla ya Kilio Kikuu — uongozi ambao uliinuliwa mwaka 1844, na kwa madhumuni pekee ya kuwakusanya watu 144,000, malimbuko ya ufalme. Katika kila jambo, mfano hufanana kikamilifu na uakisi. {TN8: 47: 4}

Kwa sbabu ya haiba yake kwa nje ya kifalme, Sauli alichaguliwa na watu, iwapo msomaji atakumbuka, ya kwamba mfalme wao, licha ya kukosa kibali cha Mungu (1 Sam. 8:7). Kisha hatimaye Mungu alipomkataa na kumtia Daudi mafuta ili awe mfalme badala yake, aliazimu kukihifadhi kiti cha enzi akijaribu kumwua Daudi, lakini aliangamia, kabla ya Daudi kukikalia, alipojiua mwenyewe kimakusudi (1 Sam. 31: 4). {TN8: 48: 1}

Wakati umeonyesha tayari kwamba jumuiya ya S.D.A. inatimiza ule mfano. Kwa kuzingatia kuwaingiza, na kuwachagua maofisa kwa kura za watu, kwa hivyo wameonyesha kwamba hawakujali sana kumpendeza Mungu ili waweze kuwa “watu wa milki ya Mungu,” jinsi Yeye angetaka wawe, maadamu wanataka kujifurahisha iwezekanavyo kuwa kama madhehebu mengine — kama wakati wa Sauli watu walitaka kuwa kama mataifa yaliyowazunguka

48

pande zote (1 Sam. 8:5, 7). Na ingawa wamechaguliwa na watu, bado Maofisa wa Baraza Kuu hata hivyo walikubaliwa na Mungu kuwa watawala kwa watu Wake sasa, alivyokuwa Sauli zamani. Jinsi alivyousaliti uaminifu wake, hata hivyo kwa kutolitii Neno la Mungu lilivyonenwa kwake na nabii Samweli, hivyo uongozi wa kanisa wa sasa, “wazee wa kale. . . mbele ya nyumba, “anasema nabii kwa kanisa leo “wameisaliti imani yao.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. (Kwa maelezo mengi zaidi ya mada ya uongozi, tazama wetu Mwongozo wa Jumuiya.) {TN8: 48: 2}

Akinena kwa uongozi wa S.D.A., mtumishi wa Bwana anasema: “Huna haki ya kusimamia, isipokuwa usimamie kwa mpangilio wa Mungu. Je, u chini ya udhibiti wa Mungu? Je, unauona wajibu wako Kwake? . . . Kwamba watu hawa wanapaswa wasimame mahali patakatifu kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, tulivyokuwa tukiamini awali Baraza Kuu kuwa, — ni wakati uliopita. Tunalotaka sasa ni kupangilia upya.” — Taarifa ya Baraza Kuu, kikao cha 34, Gombo la 4, Ziada Namba 1, Aprili 3, 1901, uk. 25, Safuwima 1 na 2. {TN8: 49: 1}

Taarifa hii ya ufunuo huthibitisha hatma kwamba baada ya mkutano wa kihistoria wa Minneapolis mwaka 1888, wakati ambapo viongozi waliukataa ujumbe na ushauri waliopewa (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 468) Bwana hakulitambua tena Baraza Kuu kama

49

watumwa Wake, jinsi hakuweza tena kumtambua Sauli kuwa mfalme juu ya Israeli baada ya kugeuka na kuyaacha maagizo ya Bwana yaliyotumwa kwake. Na sasa, baada ya muda mrefu kupokea takwa maarufu la kulipangilia Baraza Kuu, katika utimizo wa mfano, Mungu anaonya kwamba uvumilivu wake umefikia mwisho leo kama vile ulivyofanya wakati huo. Amin amin kwa uzito inatangaza Roho ya Unabii: {TN8: 49: 2}

“’Mungu huitisha uamsho wa kiroho na matengenezo ya kiroho. Isipokuwa hili litukie, wale ambao ni wavuguvugu wataendelea kuwa wa chukizo zaidi kwa Bwana, mpaka atakataa kuwatambua kama watoto Wake. {TN8: 50: 1}

“’Uamsho na matengenezo lazima yafanyike chini ya msaada wa Roho Mtakatifu. Uamsho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uamsho huashiria upya wa maisha ya kiroho, kuzifanya hai nguvu za akili na moyo, ufufuo kutoka katika kifo cha kiroho. Matengenezo huashiria kuwa na mpangilio mpya badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea. Matengenezo hayawezi kuzaa matunda mazuri ya haki isipokuwa yameunganishwa na uamsho wa Roho. Uamsho na matengenezo lazima yafanye kazi yake iliyowekwa rasmi, na katika kufanya kazi hii ni lazima uchangamane.” — Kristo Haki Yetu, uk. 154. Imechapishwa tena kutoka Mapitio na Kutangaza, Februari 25, 1902. {TN8: 50: 2}

Kama sababu anguko la Sauli lilitokana na kupuuza kutii kikamilifu Neno la Bwana,

50

na kutoka hapo aliruhusu kutotii kwake chini ya udanganyifu kwamba alikuwa amewahifadhi ng’ombe walio bora kwa ajili ya dhabihu ya ibada kwa Mungu, hivyo uongozi wa sasa, ingawa umeagizwa kuepuka miungano yote kwa ulimwengu na mitindo, na kuepuka kila aina ya biashara siku ya Sabato kama kuuza vitabu, kuinua malengo, n.k. hata hivyo, kwa uasi umeshikamana na ulimwengu na kuzifuata njia zilizokatazwa, hata kuigeuza nyumba ya Mungu kuwa nyumba ya biashara (Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250). Kisha ukiendelea kwa mtindo kama wa Sauli, ulisihi udhuru wa kosa hili la kutotii na la kuchukiza kwa msingi kwamba ya namna hii ni kazi nzuri ya kimishonari! Lakini, inasema Roho ya Unabii: {TN8: 50: 3}

“Kosa kubwa limefanywa na baadhi ya watu wanaokiri ukweli wa sasa, kwa kuingiza biashara katika mkondo wa mfululizo wa mikutano, na kwa ulanguzi wao kukengeusha mawazo kutoka kwa kusudi la mikutano. Laiti Kristo angalikuwa sasa duniani, angewafukuza hawa wachuuzi na walanguzi, iwapo ni wachungaji au watu, kwa mijeledi ya kamba ndogo, kama alipoingia hekaluni zamani, ‘na kuwatupa nje wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, na kuzipindua meza za wabadilisha fedha na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa. Akawaambia, Imeandikwa, Nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala, lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wezi.” Wafanyabiashara hawa wangeweza kusihi kama udhuru ya kwamba bidhaa

51

walizoshikilia kuuza zilikuwa kwa ajili ya sadaka za dhabihu. Lakini kusudi lake lilikuwa kupata faida, kupata raslimali, kujilimbikizia. {TN8: 51: 1}

“Nalionyeshwa kwamba iwapo uwezo wa kimaadili na wa kiakili haujafunikwa na mazoea mabaya za kuishi, wachungaji na watu wangekuwa wepesi kuona matokeo maovu ya kuchanganya mambo matakatifu na ya kawaida. Wachungaji wamesimama katika mimbari na kutoa mahubiri ya utakatifu, na kisha kwa kuingiza biashara, na kutenda sehemu ya muuzaji, hata katika nyumba ya Mungu, wamezikengeusha dhamira za wasikilizaji wao kutoka kwa mashauri yaliyopokelewa, na kuharibu matunda ya kazi yao.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 471, 472. {TN8: 52: 1}

Ingawa alimtambua Samweli kuwa nabii wa Mungu, Sauli wakati uo huo kimakusudi hakutii maneno yake; vivyo hivyo, ingawa pia wakimtambua Dada White kama mjoli wa Mungu, Baraza Kuu, kwa huzuni kusema, leo, kwa mkondo wanaoufuata, wanayakana mamlaka yake. Ukweli huu ulio wazi kabisa umefunuliwa mara nyingi katika Roho ya Unabii, taarifa ya uwakilishi ikiwa: {TN8: 52: 2}

“Wale ambao wameamini katika akili, ustadi, au talanta, hawatasimama baadaye kuwa viongozi wa askari. Hawakufululiza mwendo na nuru … Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika

52

wakati wa kupepetwa, wa kupimwa watafunuliwa waonekane.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {TN8: 52: 3}

“Iwapo wanaendelea katika hali hii, Mungu atawakataa.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 427. {TN8: 53: 1}

Kama vile mwonekano wa nje wa Sauli ulisababisha, kwa hiyo, tu yeye kung’olewa na mfalme mwingine, vivyo hivyo watu wakuu wa leo, wale walio katika uongozi wa kazi, na ambao wanaamini “akili, ubunifu, au kipaji,” kubadilishwa na wale ambao, ingawa hawajapakwa rangi kwa mwonekano wa nje, wata “funuliwa waonekane” kwa wakati huu, wakiufunua “wangavu safi wa tabia halisi ya Mkristo.” (Kwa masomo zaidi juu ya mabadiliko ya uongozi, tazama Trakti yetu Namba 2, Utata wa Onyo.) {TN8: 53: 2}

Kwa sababu Sauli, zaidi ya hilo, alimdharau Mungu kwa kukataa kuacha kiti cha enzi, na kwa kutaka kuutoa uhai wa mtiwa-mafuta Wake, mfalme Daudi, kwa hivyo sasa wakati wa kupiga tarumbeta leo, tunaona Baraza Kuu likikataa kumruhusu Mungu achukue mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300), jaribio lao kunyakua kiti Chake cha enzi kwa azimio kwamba watalitawala dhehebu hadi mwisho wa dunia hii, na kujipatia kila fursa ya kutufukuza kati yao, ili kulinda udhibiti wao kwalo. Wale wanaofanya hili ndio ambao nabii Ezekieli alisikika kwa unabii akisema: “Mji huu ni sufuria na sisi ni nyama.” Ezek. 11:3. Wao sasa

53

wanafanya kila kitu iwezekanavyo kujiinua na kujiendeleza wenyewe mamlakani, na kuwaondolea mbali wale ambao katika jina la Bwana “wanatangaza amani,” na kuwaletea “habari njema” kwamba “mwovu hatapita kati yako tena; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. Lakini “mji huu hautakuwa sufuria lenu,” asema Bwana, “wala ninyi hamtakuwa nyama ndani yake; Nitawahukumu katika mpaka wa Israeli.” Ezek. 11:11. {TN8: 53: 3}

Wale walio na hamu kutaka kuujua ukweli kwa ajili yao wenyewe kuhusu namna tumetendewa na viongozi wa kanisa (kama alivyofanywa Daudi mikononi mwa Sauli), anaweza kusoma Trakti yetu Namba 7, Hesabu Ushahidi Pande Zote Mbili Kabla Kufyatua Kwa Ajili au Dhidi Ya. {TN8: 54: 1}

Katika kuukataa ujumbe ambao umewajia kwa maonyo na makemeo, na kwa kuendelea katika njia zao za uovu, ndugu zetu wanamlazimisha Bwana kuwakatakata kwa silaha za mchinjo za Ezekieli 9, isipokuwa mara moja watubu. Ingawa wako njiani kujiua na Sauli, lakini bado wanasema mioyoni mwao: “Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Yeye ni mwenye huruma sana kuwatembelea watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao kamwe hawatapaza tena sauti zao kama tarumbeta kuwaonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa bubu, ambao hawakuweza kubweka, ndio wanaohisi kisasi cha haki ya

54

Mungu aliyekosewa. Wanaume, wasichana, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {TN8: 54: 2}

Kwa sababu Sauli, bado zaidi, aliwajibika kwa kifo si tu cha wanawe, ila pia cha watu (1 Sam. 31:6), hivyo ukasisi utawajibika kwa “wanaume, wasichana, na watoto wadogo” ambao watashindwa kupokea muhuri, na ambao kwa hiyo wataangamia katika mchinjo. {TN8: 55: 1}

Hata hivyo, licha ya dhambi yao kubwa na adhabu iliyo hakika, Daudi, mfano, huonyesha ukweli kwamba, ingawa tunaweza kukata upindo wa mavazi yao wakati wao ni wakali na wenye hasira dhidi yetu, na wanapotufukuza karibu na “mazizi ya kondoo” (1 Sam. 24:3, 4), au ya kwamba tunaweza kuchukua “fumo na gudulia la maji kutoka” kwa mito ya kulazia vichwa vyao “wakati wao” wamelala usingizi mzito kutoka kwa Bwana,” au ya kwamba twaweza, tunapowaona wamelala ndani ya “handaki,” au kuifunika miguu yao katika maeneo yetu ya kujificha (1 Sam. 26:7-12), kuwa nao kwa rehema zetu, na uwezo na fursa ya kuwadhuru sana, lakini hatuwezi kuwaumiza hata kidogo, ila badala yake kuwafanya rafiki. {TN8: 55: 2}

Na wakati wanatutesa, jinsi Sauli alivyomtesa Daudi, kila mmoja aliye katika dhiki, na kila mmoja aliye na deni, na kila mmoja ambaye amefadhaika, atajiunga, jinsi mfano huu unavyoonyesha, nasi (1 Sam. 22:2); ilhali wote ambao “si baridi au moto,. . . vuguvugu” (waliojitajirisha), wako, pamoja na malaika wa kanisa la Laodekia, katika

55

hatari kubwa ya kusalia “wanyonge na wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi,” nawakiwa kama tokeo, “kutapikwa,” kukataliwa — “kukatwa kabisa.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 427; Gombo la 5, uk. 80; Gombo la 1, uk. 190; Gombo la 5, uk. 211. {TN8: 55: 3}

Katika ufafanuzi ambao umetangulia, tunaona kwamba wale wanaoitikia sauti ya Mchungaji Mwema, ni mfanowe wafuasi wa Daudi, na ya kwamba wale wasioitikia, ni mfanowe Sauli na wafuasi wake. {TN8: 56: 1}

Katika mfano wa Luka wa karamu kuu ya jioni, Kristo tena huleta kwa mtazamo madaraja mawili. Kwa upande mmoja, wanaomuunga mkono Sauli wanawakilishwa katika mfano wale waliotoa udhuru kwa misingi kwamba walikuwa kwa shughuli sana na masumbufu ya maisha haya, na ambao kwa hivyo “wakaanza kutoa wote udhuru kwa nia moja”: Wa kwanza akimwambia Yeye, “Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.” Kwa upande mwingine, wafuasi wa Daudi wanawakilishwa na wale waliopatikana kwenye “njia kuu na vichochoro “vya mji –” maskini, na vilema, na wachechemeao, na vipofu.” Luka 14:17-24. {TN8: 56: 2}

Mara baada ya Sauli kujuzwa na Samweli ya kwamba kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu wake, Mungu alikuwa amemkataa kuwa mtawala kwa watu Wake, Samweli alitumwa kwa siri ili amtie mafuta

56

Daudi kutawala badala ya Sauli. Na ingawa Sauli alikuwa ameambiwa kwamba Bwana amemkataa bado alikataa kujiuzulu, matokeo kwamba Wafilisti walikuwa wakilisumbua jeshi lake, na walikuwa karibu kuuteka ufalme: Jitu Goliathi “Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi. Kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu, na kututumikia. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.” 1 Sam. 17:8-11. {TN8: 56: 3}

Ijapokuwa mtu asiyefaa ila mvulana aliyedharauliwa na nduguze, na lakini mdogo akilinganishwa kwa wengine wote, Daudi alimwambia Sauli, “Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu. Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa mchungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini,

57

akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.” 1 Sam. 17:32, 40, 49-51. {TN8: 57: 1}

Ushindi wa Daudi kwa jitu ambalo hakuna mtu aliyeweza kupigana nalo, ni mfanowe ushindi wa kanisa (nyumba ya Daudi — Zek. 12:8), katika “wakati wa taabu mfano wake haukuwapo,” dhidi ya mnyama na sanamu yake (Goliathi wa uakisi), kuhusu kitisho chake ambacho Waufunuo anahoji: “Ni nani aliye kama mnyama? ni nani anayeweza kupigana naye?” Jitu, Goliathi, kwa hivyo, huwakilisha wale ambao sasa wanawapuuza watumwa wa Mungu, na ambao watajumuisha Sanamu ya Mnyama, huo mfumo wa kidini na kisiasa ambao utayapinga majeshi ya Bwana, na kutoa amri “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. . . na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” Ufu. 13:17, 15. {TN8: 58: 1}

Lakini “katika siku hiyo,” asema Bwana, “Nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote

58

watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake. Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 12: 3, 8. {TN8: 58: 2}

Mawe matano laini katika mkoba wa Daudi, na moja ambalo alitumia kumuua Goliathi, ni nembo ya nguvu mara-tano kwenye mfuko (Biblia) wa mchungaji wa uakisi, na sehemu moja ambayo Mungu atatumia kumpiga mnyama na sanamu yake, mataifa — Goliathi wa uakisi. Na ya kuwa tunajua kwamba ni kwa Neno Lake, katika umbo la ujumbe, kwamba Yeye atayapiga mataifa, basi ni dhahiri kwamba mawe matano laini huwakilisha jumbe tano, wa mwisho ambao utamtia jeraha mnyama, kuiharibu sanamu yake, na kuwaweka huru watu wa Mungu kutoka kwa hofu ya mataifa. {TN8: 59: 1}

Hivyo kwa kuwa mawe matano katika mfuko wa mchungaji ni mfano wa jumbe tano, jumbe hizo kwa hivyo, lazima zimepangwa mahali fulani katika Biblia. Ziko katika mfano wa Kristo wa shamba la mizabibu: wa kwanza, “mapema” alfajiri (mfumo wa sherehe); wa pili, saa “ya tatu” (kusulubishwa na kufufuka kwa Kristo); wa tatu, “saa ya sita” (siku 2300 za Dan. 8:14); wa nne, saa “ya tisa” (hukumu ya wafu); wa tano, na wa mwisho, mwanzoni mwa “saa ya kumi na moja” (hukumu ya walio hai,

59

wakati wa Kilio Kikuu), ambao utamtia jeraha yule mnyama, na kwa upanga wake mwenyewe (pembe kumi za Ufunuo 17:16), utamkata kichwa chake, na kisha kwa moto umwangamize, ili kwamba jeraha lisipone tena. Katika ujumbe wa saa ya sasa kwa hivyo, unapatikana usalama wa watu wa Mungu. (Kwa ajili ya somo kamili la mfano wa Mathayo 20:1-16, na la mnyama wa Ufunuo 17, soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 222-239; 155, 156.) {TN8: 59: 2}

Kutangaza “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana” (Mal. 4:5), “siku ya machinjo” (Isa. 30:25), na “siku ya giza” (Yoeli 2:2), ujumbe huu wa mwisho utatangazwa saa ya kumi na moja — kabla ya wakati ambapo, alivyotabiri Yohana, “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele ya uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” (Ufu. 6:15-17) — hakuna ila wenye haki, viongozi wa baadaye wa kanisa, jinsi utawala wa Daudi ulivyo mfano. {TN8: 60: 1}

“Ni nani aliyemwinua mwenye haki kutoka mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi

60

kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake. Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu yake. Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye atakuja; toka maawio ya jua atakuja anitajaye jina Langu; naye atawajilia maliwali kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi afinyangaye udongo.” Isa. 41:2, 3, 25. {TN8: 60: 2}

“Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana, Mungu wako, na kwa ajili Yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza. {TN8: 61: 1}

“Mtafuteni Bwana, maadamu Anapatikana, Mwiteni, maadamu Yu karibu.” Isa. 55:4-6. {TN8: 61: 2}

Maadamu, kwa ajili ya heshima ya Mungu na kwa ufanisi wa watu Wake, ujumbe wa Eliya na utawala wa Daudi uliyachukua maisha ya wengi (ujumbe wa Eliya, maisha ya walimu waasi katika Israeli — 1 Fal. 18:40; na utawala wa Daudi, maisha ya watu wa mataifa waliomdharau Mungu na majeshi yake — 1 Nya. 22:6-8), basi kazi ya Eliya haswa ni mfanowe siku ya machinjo ndani ya kanisa, na utawala wa Daudi, uangamizaji wa watu wa mataifa na kumiliki nchi (Zek. 12:8, 9; Yer. 30:3, 9). Halafu Kristo (mwana wa Daudi) atatokea dhahiri, autwae Mwenyewe ufalme Wake (Luka 19:15), na kuutukuza kwa

61

amani ya milele (kama mfanowe utawala wa amani wa mwana wa Daudi, Sulemani). Na katika siku hizi za matukio ya uakisi itatimizwa kabisa ahadi: {TN8: 61: 3}

“Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, Nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; Nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, Nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele. Nitakuwa baba yake, naye atakuwa Mwanangu; wala sitamwondolea fadhili Zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako.” 1 Nya. 17:11-13. “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.” Mith. 29:2. {TN8: 62: 1}

Ilhali kwa mwenye haki, Yeye aufanya ufalme mahali Pake na ulinzi, kwa watu wa mataifa,

Mungu Anaufanya Shoka Lake La Vita. {TN8: 62: 2}

“Wewe u shoka Langu na silaha Zangu za vita; kwa wewe Nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe Nitaharibu falme; na kwa wewe Nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe Nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na

62

kwa wewe Nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe Nitawavunja-vunja maliwali na maakida.” Yer. 51:20-23. {TN8: 62: 3}

“Jiwe” (Dan. 2:45, Zek. 3:9), watu 144,000 (Ufu. 14:1), “lililochongwa mlimani [kanisa la Laodekia] bila kazi ya mikono” (bila msaada wa kibinadamu), litavunja-vunja mataifa ambayo yanawakilishwa na “chuma, shaba, udongo, fedha, na dhahabu” ya sanamu kubwa. Na “wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.” Kwa hivyo “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:44. {TN8: 63: 1}

“Bali katika mlima Zayuni utakuwako ukombozi, nao utakuwapo utakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao. Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo. Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau; na watu wa

63

Shefela watawamiliki Wafilisti; nao watalimiliki konde la Efraimu, na konde la Samaria, na Benyamini atamiliki Gileadi. Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli waliotekwa, walio kati ya Wakanaani, watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu. Tena waokozi watakwea juu ya mlima Zayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana.” “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.” Oba. 1:17-21; Yoeli 2:32. {TN8: 63: 2}

“Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo yataharibiwa kabisa.” Isa. 60:12. {TN8: 64: 1}

Kutoka kwa maandiko yaliyotangulia, tunaona kwamba kama tokeo la kuukataa ukweli uliotangazwa na kanisa Lake, waovu wanaenda kwenye uharibifu. Na akitoa mwangwi wa maneno haya ya kinabii ya adhabu yao, Kristo anasema hivi: “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo Yangu hata mwisho, Nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama Mimi nami nilivyopokea kwa Baba Yangu.” Ufu. 2:26, 27. {TN8: 64: 2}

“Na yeye ashindaye” kuwa ndiye atakaye “tawala” “mataifa” “kwa fimbo ya

64

chuma,” na hitaji na kazi ya kushinda ikiwa si Yake bali ya wafuasi Wake”, ukweli ni dhahiri kwamba Bwana atakuwa na taifa lililopata ushindi — ufalme kuwa njia ambayo Yeye atazidhihirishia nguvu Zake kuu, na ambao utakuwa

Ufalme wa Amani. {TN8: 64: 3}

Ya kwamba usalama na amani kama wa mbinguni utaujaza ufalme wakati ambapo Mungu atautumia kama Lake “shoka la vita” ambalo atatumia kuwapiga mataifa, inavyothibitishwa kwa maandiko yafuatayo: {TN8: 65: 1}

“Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima Wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.” Isa. 11:6-9. Wakati ambapo hali hii ya maarifa na amani inaenea katika ufalme, kisha “Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yesse lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye Mataifa watamtafuta: [kwa sababu huo ni wakati wa rehema] na. . . katika siku hiyo,. . . Bwana atapeleka mkono Wake

65

mara ya pili ili ajipatie watu wake watakaosalia.” Isa. 11:10, 11. {TN8: 65: 2}

“Na katika siku hiyo,” asema Bwana kupitia kwa nabii Wake Hosea, akikariri kuhusu agano Lake la amani, “Nami siku hiyo Nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; Nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, Nami nitawalalisha salama salimini.” Hos. 2:18. (Kwa ajili ya ufafanuzi wa kina wa sura ya Hosea moja na mbili soma Trakti yetu Namba 4, Habari Za Hivi Punde Kwa Mama.) {TN8: 66: 1}

Kama ilivyokuwa katika safina ya Nuhu, mfano, hivyo katika safina ya uakisi, ufalme, hakuna kitakachodhuru wala kuharibu: simba, mbwa-mwitu, mwana-kondoo, chui, ndama, na kinono wataishi kwa amani pamoja na, kama ng’ombe, wote watakula “majani.” Kwa hivyo sasa, kama wakati wa Nuhu, Mungu atahifadhi masalia ya mwanadamu na mnyama kutoka kwa uumbaji Wake wote, badala ya kuangamiza kabisa kila kitu kilicho hai, na kisha kuviumba vyote tena. {TN8: 66: 2}

Kuutambua ukweli huu, mtume Paulo anasema: “Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa

66

watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.” Rum. 8:19-23. {TN8: 66: 3}

“Na Yeye katika mlima huu atauharibu [ufalme huu wa amani],” asema Isaya, “uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Yeye atameza mauti kwa ushindi; na Bwana Mungu atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu Wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo.” {TN8: 67: 1}

“Katika siku hiyo watasema [siku ambayo Bwana atafuta machozi kutoka kwa nyuso za watu Wake wote], Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu Wake. Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa.” Isa. 25:7-10. “Wala hapana mwenyeji atakayesema, mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 33:24. {TN8: 67: 2}

“Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,” anashangilia Daudi, “Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina Lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,

67

wala usizisahau fadhili Zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai.” Zab. 103:1-5. (Kwa kujifunza zaidi juu ya somo la uendelezo wa maisha tazama Trakti yetu Namba 5, Onyo la Mwisho, uk. 63-65 Toleo Lililosahihishwa, 1940.) {TN8: 67: 3}

“Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, Nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, Nami nitawarudisha, kwa maana Nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba Sikuwatupa; kwa maana Mimi ni Bwana, Mungu wao, Nami nitawasikia. Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana. Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka. Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi. Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; Nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana. Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka;

68

na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka. Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina Lake, asema Bwana.” (Zek. 10:6-12) — uhakikisho wa kudumu kwamba yetu ni fursa kuu ya

Kumruhusu Mungu Atutawale. {TN8: 68: 1}

Kwa karne nyingi, wafuasi wa Kristo wameomba, “Ufalme Wako uje, mapenzi Yako yafanyike.” Sasa kwa kuwa wakati umewadia wa ombi litimizwe basi tuishi maisha ya maombi yetu, ili asije yeyote kati yetu apatikane miongoni mwa daraja la wasiokuwa waaminifu ambao Kristo anahitimisha kwa mfano unaofuata: {TN8: 69: 1}

“Yeye akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili Ajipatie ufalme na kurudi. Akaita watu kumi katika watumwa Wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata Nitakapokuja. Lakini watu wa mji Wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. Ikawa Aliporudi, ameupata ufalme Wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.” {TN8: 69: 2}

“Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu Lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.” {TN8: 69: 3}

“Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu Lako limeleta mafungu matano faida. Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.” {TN8: 70: 1}

69

“Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu Lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa U mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye Nisichoweka, na kuvuna Nisichopanda; basi, mbona hukuiweka fedha Yangu kwa watoao riba, ili Nijapo niipate pamoja na faida yake? Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. (Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.)” {TN8: 70: 2}

“Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho. Tena, wale adui Zangu, wasiotaka Niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele Yangu.” Luka 19:12-27. {TN8: 70: 3}

“Mtu mmoja kabaila” katika mfano huu ni Kristo, Mwenyewe, Ambaye, baada ya kufufuka Kwake, aliondoka kwenda mbingu za mbingu, “nchi ya mbali,” kuvikwa taji ya Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Watumwa Wake

70

kumi, ambao wangesimamia hata kuja Kwake, wanawakilisha, kwa udhahiri, ukasisi wakati wa kufunga kipindi cha injili. Na watu wa mji wake, kwa hivyo, wanawakilisha wamini — raia wa Ufalme Wake. Pamoja, basi, watumwa Wake na raia Wake hujumuisha ufalme Wake wote — kanisa. {TN8: 70: 4}

Walipotuma “ujumbe baada Yake, wakisema, Hatumtaki mtu huyu atutawale,” hitimisho pekee linalokubalika ni kwamba muda mfupi kabla ya kurudi Kwake, Kristo atawajulisha “raia wa ufalme” Wake kwamba anachukua “mamlaka mikononi Mwake” ili kuusimamisha ufalme Wake, na kwamba wao, wanapolisikia tangazo hilo, watakataa kujisalimisha kwa yule Atakayemtumia kutawala. {TN8: 71: 1}

Angalia kwamba katika ujumbe ambao “walituma kumfuata Yeye,” watumwa Wake hawakusema, “Hatutaki Ututawale,” ila “hatutaki mtu huyu atutawale.” Lile walilokuwa wakipinga ni Kristo kuwatawala kupitia kwa mtu mwingine. Dhahiri, basi, kabla ya kutawazwa, na muda mfupi kabla ya kurudi Kwake kufanya hesabu na watumwa Wake, Anamteua “mtu” kuwatawala kwa niaba Yake. Na hapo wanamwambia Yeye, kwa mwelekeo wao na kusimama dhidi ya ujumbe Wake, “Hatumtaki mtu huyu atutawale,” ingawa “mtu huyu,” jinsi tunavyoona sasa, ni Daudi wa uakisi (“maana rahisi”), mfalme anayeonekana. {TN8: 71: 2}

71

Kwa hivyo, Kristo anaporudi na kufanya hesabu na watumwa Wake, Yeye anawapa thawabu wale waaminifu kwa kadiri walivyozidisha raslimali kwa ile ambayo walianza nayo, lakini anawahukumu wale ambao hawakuwa na mzigo wa kufanya kazi kwa ajili ya roho na kuuendeleza ufalme Wake, na ambao waliridhika kumwacha Yeye atende kazi bila huduma zao. Kwa ukafiri huu, Yeye anachukua kutoka kwao “talanta,” (nuru ya ukweli), ambayo Alikuwa amewapatia, akionyesha hivyo kwamba wote watawajibika “kwa kila mshale wa nuru,” kwa kila wakati uliopotezwa, kwa kila fursa iliyopuuzwa. Na wale ambao hawatamruhusu Yeye kuwatawala hivyo, Atakaporejea, watachinjwa mbele Yake kama wale walioasi dhidi ya serikali ya Mungu katika nyakati za zamani. {TN8: 72: 1}

Wayahudi wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo, hawakuelewa utume Wake kwa sababu walikuwa vipofu kuhusu kile ujumbe wao (huduma za sherehe) ulifundisha, na kwa kile ambacho manabii waliandika kumhusu Yeye, walilipotosha fundisho Lake la ufalme. Walitamani sana litimie tumaini lao la muda mrefu la ufalme, walikasirishwa sana na mafundisho ya kigeni ya Kristo, na walikuwa tayari kumpiga Yeye mawe afe badala ya kuruhusu makosa yao yafichuliwe mbele ya umati ambao daima uliwaweka gizani. Hivyo ndivyo ilivyo na kanisa leo. Liko na upofu kwa ujumbe wa saa hii, na kwa ukweli wa ufalme wa Kristo, kama walivyokuwa Wayahudi katika siku yao. Na kama ilivyo ujumbe unapobisha langoni pake na maonyo, jibu lake ni, Nenda zako

72

mbali, Mimi ni “tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu,” ingawa ni lenye “unyonge, na lenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” {TN8: 72: 2}

Kanisa la siku ya Kristo liliazimu ufalme uanzishwe wakati huo, wakati yote yalikuwa bado kuwa tayari kwa ajili yake; kanisa la leo limeazimu usianzishwe sasa, wakati “mwisho wa mambo yote umekaribia” (1 Pet. 4:7) — ambapo wakati umekuja kabisa! Wayahudi waliutaka tena ufalme waliokuwa wameupoteza — ufalme wa dhambi na wadhambi. Walikuwa wenye bidii ya kuwekwa huru kutoka kwa utumwa wa Kirumi tu, badala ya dhambi na wadhambi pia. Kwa hivyo, Kristo aliposema, “Ufalme Wangu si wa ulimwengu huu” (Yoh. 18:36), hawakutaka uwe hivyo; ilhali kanisa leo, kwa upofu likipuuza maandiko ambayo yanatangaza wazi wazi kwamba sasa Mungu anauanzisha ufalme Wake usiokuwa na waa na kuwaweka huru watu Wake, si kutoka kwa utumwa wa Babeli tu, ila kutoka kwa dhambi na wadhambi pia, limeazimu kuuahirisha mpaka baada ya millenia! Hivi ni swala la kejeli la upotovu wa moyo wa utu wa kale — hata usoni pa ukweli kwamba kwa kila hali linaonekana kwenye ukingo hasa wa milele,

Katika Hali Yake Iliyotakaswa. {TN8: 73: 1}

Katika mojawapo wa unabii wake mkuu, Isaya huonyesha katika sura bila kukosea mshirika mkuu pacha wa uakisi wa vuguvugu la Kutoka: “Itakuwako njia kuu kwa masalia ya watu Wake watakaosalia,

73

kutoka Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11:16. Kama “Pasaka” na mchinjo wa “mzaliwa wa kwanza (malimbuko) ambao hawakuwa na damu kwenye” miimo ya milango, “iliwaweka huru watu wa kale wa Mungu kutoka katika utumwa wa Misri, ndivyo pasaka ya uakisi (Ezek. 9:4, Isa. 66:16) itakavyowaweka huru malimbuko, watu 144,000, wazaliwa Wake wa kwanza sasa, kutoka katika utumwa wa dhambi na wadhambi leo. {TN8: 73: 2}

“Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4:3-6. (Kwa maelezo ya kina zaidi ya vuguvugu la kutoka kwa mfano na uakisi, soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, uk. 64-111. {TN8: 74: 1}

Katika nuru ya Ukweli wa Sasa mintarafu ufalme, unabii unaofuata

74

(pamoja na unabii mwingi unaohusiana) unajifasiri wenyewe: {TN8: 74: 2}

“Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi [kwenye kiti chako cha enzi], Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa. Maana Bwana asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha. Maana Bwana Mungu asema hivi, Watu Wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu. Basi sasa, Nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu Wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema Bwana, na jina Langu linatukanwa daima mchana kutwa. Kwa hiyo watu Wangu watalijua jina Langu kwa hivyo watajua siku ile ya kuwa Mimi ndimi Ninenaye; tazama ni Mimi.” {TN8: 75: 1}

“Nu ilioje mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Zayuni, Mungu wako anamiliki! Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Zayuni. {TN8: 75: 2}

75

“Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu Wake, Yeye ameukomboa Yerusalemu. Bwana ameweka wazi mkono Wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu. {TN8: 76: 1}

“Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana. Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde. {TN8: 76: 2}

“Tazama, mtumishi Wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.” Isa. 52:1-15. {TN8: 76: 3}

Tukijiangalia wenyewe kwenye ukingo wa umilele, tunachochewa kujiunga na Mzee James White katika tamko lake la mshangao: “O, Utukufu! Haleluya! moyo wangu maskini umewashwa moto kwa ajili ya ufalme, wakati ninapotulia kwa matarajio haya matamu, mbele ya mwamini wa kweli. Iwapo ‘tunashika sana’ hata hivyo siku chache zaidi, vivuli vyeusi vya usiku vitatoweka

76

mbele ya utukufu wa matukio ya maandalizi ya kuja kwa Mwana wa Adamu.” — Neno kwa Kundi Ndogo, uk. 8. {TN8: 76: 4}

Wale tu walio na sehemu katika vuguvugu hili akisi la kutoka watapewa nafasi ya kuimba “wimbo wa Musa na Mwana-Kondoo,” na kupewa mgawo katika ahadi za

Agano katika Uakisi. {TN8: 77: 1}

“Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile Nililolifanya na baba zao, katika siku ile Nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambao agano Langu hilo walilivunja, ingawa Nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Bali agano hili ndilo Nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria Yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua Mimi wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana Nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.Yer. 31:31-34. {TN8: 77: 2}

“Agano” kuukuu au mapatano kati ya Mungu na watu Wake yalikuwa msingi wa ahadi za pande zote mbili; kushuhudia: “Itakuwa utakaposikia

77

sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo Yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; Naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Bwana atakuweka uwe taifa takatifu Kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia Zake.” {TN8: 77: 3}

“Watu wote wakaitika pamoja wakisema, hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda. Naye Musa akamwambia Bwana maneno ya hao watu.” Kumb. 28:1-9; Kut. 19:8. {TN8: 78: 1}

78

Agano hili la kwanza kutoka kwa wakati lilipoagizwa rasmi hadi kwa kukusanywa kulio karibu na kwa mwisho kwa makabila kumi na mbili kuwa ufalme. Na hata hivyo, ingawa halikubatilishwa kamwe na Mungu, uhalali wake umekuwa ukiendelea kukanushwa na kanisa la Agano Jipya, na utakatifu wake umekiukwa na makanisa ya Agano la Kale na Jipya, hata siku hii ya leo. Kwa hivyo, kama watu, kutozitimiza ahadi zao, wamezivunja amri za Mungu, wao pia wamelivunja “agano la Mungu alilofanya na baba zao.” Bali katika agano jipya, ambalo Bwana yu karibu kulitimiza, amri za Mungu ( Kut. 20:1-17), tofauti na la zamani hazitaandikwa kwa mbao za mawe (Kut. 31:18), ila katika mbao za nyama za mioyo, na kwa wakati huo wote “wamtajua Bwana,. . . tangu mtu aliye mdogo wao hadi mkubwa wao “ (Yer. 31:34) — kuonyesha kanisa bila magugu. {TN8: 79: 1}

Mkataba huu ambao unakaribia kutukia, ni agano la pili, na sheria Yake, ikiwa imeandikwa moyoni, itatunzwa kikamilifu. Wakati huo, na si kabla, baraka ambazo, watu Wake wa kale walishindwa kupokea, zitatekelezwa kikamilifu. {TN8: 79: 2}

Yeremia, pia akishuhudia kwamba ahadi hii iliyoahidiwa bado haijawahi kutimizwa, ila kwamba itaheshimiwa sasa wakati wa kukusanywa, anatangaza: {TN8: 79: 3}

“Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.

79

Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, Nitakapowarejeza watu Wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; Nami nitawarudisha hata nchi Niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.” Yer . 30:2, 3. {TN8: 79: 4}

Aya hizi huonyesha waziwazi kwamba Mungu atalithibitisha agano la pili wakati Yeye anawaleta watu Wake tena kutoka kwa uhamisho wao, wakati aya zinazofuata zinauweka wakati wa uhuru huu au kukusanywa: “Na itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitaivunja nira yake itoke shingoni mwako, Nami nitavipasua vifungo vyako; wala wageni hawatamtumikisha tena; bali watamtumikia Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, Nitakayemwinua kwa ajili yao.” Yer. 30:8, 9. {TN8: 80: 1}

Unabii huu, tunaona, haukupata utimizo wake wakati wa kurejea kwa Wayahudi kutoka kwa uhamisho wao Babeli ya kale, kwa sababu wakati huo Mungu “hakumwinua” Daudi mfalme wao. Wala hawakuwa, na mfalme yeyote wao, lakini walikuwa chini ya utawala wa Wamedi na Waajemi. Unabii, kwa hivyo, hauwezi kutumika kwa wakati mwingine kuliko leo, wakati wote “Israeli na Yuda” wataunganishwa katika ufalme mmoja mkuu, unaosimamishwa katika haki ya milele. Kisha “watanijua Mimi wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao,” asema Bwana. Kwa hivyo, ukweli kwamba hakujawahi kuwa na wakati tangu

80

siku ambayo maandiko haya yaliandikwa hadi siku ya leo, ya kwamba kila mmoja wa watu wa Mungu, kama kanisa au taifa, amemjua Bwana na kuzitunza amri Zake, tena inathibitisha kwamba utimilifu wa agano la pili (ambalo vuguvugu la kutoka lilikuwa mfano), bado ni wa baadaye. {TN8: 80: 2}

“Hata lini,” asema Bwana, “utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamkumbatia mwanamume.” Yer. 31:22. “Mwanamke” huyu lazima awe mfano, maana hakuna mtu mmoja anayeweza kumkumbatia mwingine. Lazima, kwa sababu hii, awe nembo ya kanisa, na “mwanamme” lazima awe Kristo, Ambaye wakati huo “ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni” — amelitakasa kanisa (Isa. 4:4); Shuhuda, Gombo la 5 uk. 80). Ndipo Yeye atakuwa “ukuta wa moto kulizunguka pande zote, na atakuwa huo utukufu ndani yake na . . . atakaa kati yake. Zek. 2:5, 11. {TN8: 81: 1}

Ingawa wengi tofauti-tofauti hupaza sauti zao dhidi ya Mungu kuusimamisha “uzao wa Israeli” kama taifa la haki na takatifu huru kutoka kwa wadhambi, hushindwa kupindua mipango Yake “Awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, Aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi, ndilo jina Lake; Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele Yangu, asema Bwana, ndipo

81

wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele Yangu milele. Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia Nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema Bwana.”Yer. 31:35-37. {TN8: 81: 2}

Kwa sababu ahadi zimefanywa tu kwa Israeli (uzao wa Abrahamu), mzabibu asili, ambao umekanyagiwa chini, mzabibu huu lazima uinuliwe; kisha wadhambi wa Mataifa waliotubu kwa wema wa kukubaliwa kupitia kwa Kristo, watapandikizwa ndani yake, na hivyo tu kuwa pando la Bwana. {TN8: 82: 1}

“Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu Wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Abrahamu, mtu wa kabila ya Benyamini. Mungu hakuwasukumia mbali watu Wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele ya Mungu, Bwana, wamewaua manabii Wako, wamezibomoa madhabahu Zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.” {TN8: 82: 2}

82

“Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito. (Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie,) hata siku hii ya leo Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao; Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.” {TN8: 83: 1}

“Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu, nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa? Tena malimbuko [Myahudi] yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote [Myahudi na mtu wa Mataifa]; na shina [Myahudi] likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika [iwapo ni ya asili au yaliyopandikizwa]. Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu [mti wa Mataifa], ulipandikizwa kati yao,

83

ukawa mshirika wa shina la mzeituni [mzuri] na unono wake, usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe [wa Mataifa] ulichukuaye shina, bali ni shina [Myahudi] likuchukualo wewe. Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi. Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako.” {TN8: 83: 2}

“Usijivune, bali uogope. Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili [Wayahudi wasioamini], wala hatakuachia wewe. Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena. Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe? Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uingie ndani. Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Zayuni; Atatenga Yakobo na maasi yake. Na hili ndilo agano Langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.” {TN8: 84: 1}

84

“Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito Wake. Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili Yeye awarehemu wote.” {TN8: 85: 1}

“Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu Zake hazichunguziki, wala njia Zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri Wake? Au ni nani aliyempa Yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka Kwake, viko kwa uweza Wake, tena vinarejea Kwake. Utukufu una Yeye milele. Amina.” Rum. 11. {TN8: 85: 2}

“Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu Amenitaja jina langu. Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono Wake amenisitiri; Naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo Lake amenificha; akaniambia; Wewe u mtumishi Wangu, Israeli, ambaye katika wewe Nitatukuzwa. Lakini nikasema, nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida;

85

lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.” {TN8: 85: 3}

“Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniita tangu tumboni niwe mtumishi Wake, ili nimletee Yakobo [uzao wake] tena Kwake, ingawa Israeli hawajakusaywa, maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu. [Sisi, pia, twaweza kusema, ingawa ulimwengu wote waweza kumkataa Bwana na ujumbe Wake, “bado nitamwamini Bwana.”] Na akasema, Je, ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi Wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli [pekee yao] waliohifadhiwa: Zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu Wangu hata miisho ya dunia.” Isa. 49:1-6. Kwa maneno mengine, wale (wa Israeli) ambao wanatangaza ujumbe wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000 katika kanisa, watatangaza pia utukufu wa Mungu kati ya Mataifa, hivyo kuwa wokovu Wake hata miisho ya dunia, na “kuwaleta ndugu [zao] wote kuwa sadaka kwa Bwana kutoka katika mataifa yote.” Isa. 66:19, 20. {TN8: 86: 1}

“Bwana asema hivi, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu Wake, kwake yeye anayedharauliwa [yule ambaye walimwita “mtu huyu” (Luka 19:14). Angalia ukurasa wa 71], yeye “anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya Bwana aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua Bwana asema hivi, wakati uliokubalika

86

Nimekujibu, na siku ya wokovu Nimekusaidia; Nami nitakuhifadhi, Nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa; kuwaambia waliofungwa, haya, tokeni; na hao walio katika giza, jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho. Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana Yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji Atawaongoza. Nami nitafanya milima Yangu yote kuwa njia, na njia kuu Zangu zitatukuzwa zote. Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.” {TN8: 86: 2}

“Imbeni, Enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, Enyi milima; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu Wake, Naye atawahurumia watu Wake walioteswa. Bali Zayuni alisema, Bwana ameniacha, Bwana wangu amenisahau.” Isa. 49:7-14. {TN8: 87: 1}

Zayuni, jinsi ambavyo tumeona hapa, likiwa kanisa ambalo watu 144,000 wamo wakati ambapo ujumbe wa kutiwa muhuri unasikika, na likiwa kama mboni ya jicho Lake, Bwana analiuliza: “Je! Mwanamke anaweza kumsahau mtoto wake anayenyonya, kwamba haipaswi huruma mwana wa tumbo lake? Naam, wanaweza kusahau, lakini Mimi sitakusahau. Tazama, Nimekuweka kwenye vitanga vya mikono Yangu; kuta zako zi daima mbele Yangu. Watoto

87

Wako watafanya haraka; waangamizi wako na wale waliokufanya uharibifu watatoka kwako.” Isa. 49:15-17. Yaani, wadhambi wataondolewa kutoka ndani yake, watatupwa “kutoka kati ya wenye haki.” Mat. 13:48, 49. {TN8: 87: 2}

“Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama Niishivyo, asema Bwana, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi. [Angalia Zekaria 8:23; Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 281.] Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali. [Yaani, umati mkubwa utajiunga na kanisa, lakini wenye dhambi watazuiliwa nje yake.] Watoto utakaokuwa nao [wale ambao watakusanywa], baada ya kuwapoteza wengine [wale walioanguka katika mchinjo wa Ezekieli Tisa], watasema masikioni mwako, Mahali hapa ni pembamba, hapanitoshi; nipe nafasi nipate kukaa. Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami ni pekee yangu, nimehamishwa, ninatanga-tanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, naliachwa peke yangu; hawa je! walikuwa wapi? [Swali hili linaonyesha kwamba kanisa halijui umati mkubwa wa Ufunuo 7:9 — mavuno ya pili.] Bwana Mungu asema hivi, Tazama, Nitawainulia mataifa mkono Wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera Yangu;

88

nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao. Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa Mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika.” {TN8: 88: 1}

“Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? Naam, Bwana asema hivi, hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana Nitateta na yeye atetaye nawe, Nami nitawaletea wana wako wokovu. Na hao wanaokuonea Nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa Mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.” Isa. 49:18-26. {TN8: 89: 1}

“Bali atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono Yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina Langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli. Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira Yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo Yake imejaa ghadhabu, na ulimi Wake ni moto ulao; na pumzi Yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu

89

ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.” Isa. 29:23; 30:27, 28. {TN8: 89: 2}

“Bali mwungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana. maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda-mwitu, malisho ya makundi ya kondoo; hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu. Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu Wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika. Heri ninyi mpandao mbegu kando ya maji yote, na kuiacha miguu ya ng’ombe na punda waende ko kote.” Isa. 32:8, 14-20. {TN8: 90: 1}

“Sikieni, ninyi mlio mbali, Niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza Wangu. Wenye dhambi walio katika Zayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie

90

habari za damu, afumbaye macho yake asitazame uovu. Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. {TN8: 90: 2}

“Macho yenu yatamwona Mfalme katika uzuri Wake: wataiona nchi ambayo ni mbali sana. Moyo wako utafikiria hofu. Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri Wake, yataona nchi iliyoenea sana. Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu [mwandishi]? wapi wapokeaji [watunza hazina]? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru [katibu wa takwimu] ? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara [marais wa mabaraza]? Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo [utanena na kuelewa lugha zote].” Isa. 33:13-19. {TN8: 91: 1}

“Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi. Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa,

91

njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Zayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.” Isa. 35:3-10. {TN8: 91: 2}

Basi kwa vile “shamba” lina ngano na magugu (Mat. 13:30), na “juya” lina “samaki” wazuri na wabaya (Mat. 13:47, 48), huwakilisha kanisa la injili wakati wa kipindi ambapo watakatifu na wanafiki wamechangamana, basi “vyombo” ambavyo “samaki wazuri” huwekwa baada ya “wabaya” kutupwa “kutoka kati yao”, na “ghala” ambalo “ngano” huwekwa ndani yake baada ya “magugu” kutengwa nayo, ni lazima kwa hivyo huwakilisha kanisa ambalo liko kwa mpito kutoka kwa hali yake iliyo najisi (shamba au juya) hadi nyingine, hali yake iliyotakaswa, ambayo inaashiriwa, si kwa “shamba” au “juya” ila badala yake kwa “ghala” na “vyombo” — eneo jipya salama na safi — ambapo “tokea sasa hataingia . . . asiyetahiriwa wala aliye najisi. “ Isa. 52:1. {TN8: 92: 1}

Basi haijalishi neno ambalo tunaweza kupeana kwa ajili ya eneo hili jipya ambamo watakatifu watakusanywa, eneo, lenyewe, litakuwa

92

huru kabisa kutoka kwa dhambi kwa sababu wadhambi wote kati ya wenye haki watakuwa tayari wameangamizwa. {TN8: 92: 2}

Kwa sababu baada ya utengo wa watu wasio waogofu kutoka kati ya watu wa kweli wa Mungu, kanisa (ambalo linajumuisha watu 144,000, malimbuko ya kabila kumi na mbili za wana wa Israeli) litaibuka kuwa serikali ya kitheokrasia, bila shaka, basi “vyombo” huwakilisha vitengo mseto, makabila, ambamo waliokombolewa wanakusanywa mbalimbali, ilhali “ghala” huwakilisha kitengo mseto, ufalme, ambamo wanakusanywa kwa ujumla. Na mkusanyiko huu mkuu, wa uteuzi, kamili, na wa mwisho, jinsi ulivyo, unaenda tu kuonyesha tena kwamba kuzaliwa kwa ufalme hutegemea kabisa utakaso wa kanisa. {TN8: 93: 1}

“Mimi Yesu nimemtuma malaika Wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye shina na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.” Ufu. 22:16. “Inukeni, twende tukapigane nao; kwa maana tumeiona hiyo nchi nayo ni nchi nzuri sana; nanyi, je! mwanyamaa tu?” (Amu. 18:9.) Msiwe walegevu, tenda upesi, jitayarishe, mfuateni

Mwana-Kondoo hadi kwa Mtawala wa Nchi. {TN8: 93: 2}

“Pelekeni yeye mwana-kondoo, hadi kwa aitawalaye nchi toka Sela kuelekea nyikani, mpaka mlima wa binti Zayuni. Na binti za Moabu watakuwa kama ndege

93

warukao huko na huko, kama kioto cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni. Lete shauri; kata neno; fanya kivuli chako kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche waliofukuzwa; usiwachongee waliopotea. Watu Wangu waliofukuzwa waache wakae pamoja nawe; katika habari za Moabu, uwe sitara kwake mbele ya uso wake anayeharibu; maana yeye atozaye kwa nguvu amekoma; afanyaye ukiwa ametoweka; waliokanyaga watu wametoka katika nchi. Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.” Isa. 16:1-5. {TN8: 93: 3}

Ijapokuwa kifungu hiki kinaonekana kuwa hakina kitu zaidi kuliko lugha ya fumbo ya utaratibu wa usirisiri, bado kina masomo yaliyokusudiwa kumwongoa hata kafiri mgumu kwa ukweli fulani wa Biblia. Hakika, ikiwa watu wa Mungu wangaliweza kwenda zao bila maandiko haya, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye hangechukua aidha wakati wa nabii kuandika au kuweka nafasi katika Biblia yaandikwe. Lingekuwa, kwa ufupi, tu fumbo la shairi la mwimbaji wa kinabii bila matamshi au sababu, basi yangekuwa ni sifuri tu wimbo wa kurudia-rudia bure, dosari — jambo lisilowezekana na Mungu. Ili kutounganisha maana yoyote au umuhimu kwa aya hizo, kungemlaza mmoja chini ya hukumu ya kutisha ya maandiko yafuatayo: {TN8: 94: 1}

“Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na

94

katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Ufu. 22:19. {TN8: 94: 2}

Kwa sababu maneno ya Isaya, kwa hivyo, lazima yasheheni nuru, ikikosa kuwapo, itaiacha gizani njia yetu, kutuweka kwenye hatari ya kutumbukia na kipofu ndani ya shimo, mtafiti mwenye bidii wa ukweli atagundua kwamba ingawa kifungu kinaonekana kimefunikwa na kuhusishwa katika fumbo, ni wazi na rahisi wakati kinapotazamwa katika nuru inayoangaza kutoka juu. {TN8: 95: 1}

“Pelekeni yeye mwana-kondoo, hadi kwa aitawalaye nchi toka Sela kuelekea nyikani, mpaka mlima wa binti Zayuni.” Isa. 16:1. {TN8: 95: 2}

Kibainishi yakini, “yeye,” kinajalia kabisa maana ya nomino, “mwana-kondoo,” kuonyesha kwamba mwana-kondoo, pekee wa aina yake, alikuwa kitu cha amri ya kutuma “mwana-kondoo” kutoka Moabu “mpaka mlima wa binti Zayuni “ — Mlima Zayuni huko Yerusalemu. {TN8: 95: 3}

“Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huko na huko, kama kioto cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.” Yaani, mwana-kondoo alipaswa kuchukuliwa kutoka Moabu kwa sababu Wamoabu “wangetupwa nje” “ kama ndege warukao huku na huko,” “ kwenye vivuko vya Arnoni.” Isa. 16:2. {TN8: 95: 4}

Historia takatifu ina nyaraka kwamba mwana-kondoo mmoja aliyechukuliwa kutoka Moabu kabla ya Wamoabi “kutupwa nje ya kioto [chao],” alikuwa Yule Ambaye Yohana Mbatizaji alisema: “Tazama

95

Mwana-Kondoo wa Mungu” — Kristo. Unabii huonyesha kwamba mwana-kondoo aliharakishwa kutoka Moabu hadi Mlima Zayuni (kasri la Daudi huko Yerusalemu) — tukio lililofanyika wakati Naomi, pamoja na wanawe, walienda Moabu (“nyikani” — taifa lisilo chini ya uangalizi wa moja kwa moja wa Bwana na, wala si shamba la mizabibu) na akamleta Ruthu, Mmoabi, kutoka Moabu hadi Yerusalemu; maana “Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake. . . , naye akamzaa mtoto wa kiume,. . . wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye babaye Yesse, aliye babaye Daudi. . . Na Yesse akamzaa Daudi.” Ruthu 4:13-22. {TN8: 95: 5}

Hivyo, Kristo, Mwana wa Daudi, “alitumwa” kutoka Moabu hadi Mlima Zayuni — kasri la Daudi; na hivyo kuonyesha uungu wa Kristo kama Mwana wa Mungu, na ubinadamu Wake kama Mwana si tu wa Daudi ila pia wa Lutu — Moabu. {TN8: 96: 1}

O ni wa ajabu haswa jinsi gani Mungu wetu: majina, Obedi, Yesse, na Daudi kwa lugha ya Kiebrania humaanisha Kristo — mtumwa (Obedi), ambaye atakuwa uwepo Wangu (Yesse), mpendwa (Daudi). {TN8: 96: 2}

Kristo akiwa katika mwili Mmoabu hali kadhalika Mwisraeli, Mungu anasema: “Watu Wangu waliofukuzwa waache wakae pamoja Nawe; katika habari za Moabu [Kristo]; uwe sitara kwake mbele ya uso wake anayeharibu.” “Na mtu [tena akizungumzia Kristo] atakuwa kama mahali pa kujificha kutoka kwa upepo, na uvuli kutoka kwa dhoruba; kama mito ya maji katika mahali pa kavu, kama kivuli cha mwamba mkuu katika nchi ya uchovu.” Isa. 16:4; {TN8: 96: 3}

96

Pelekeni “Lete shauri; kata neno; fanya kivuli” Chake “kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche waliofukuzwa; usiwachongee waliopotea.” (Isa. 16:3), Kristo, “mahali pa kujificha kutoka kwa upepo, na uvuli kutoka kwa dhoruba” “katika nchi ya uchovu,” ni kivuli kikuu na kikamilifu, hata kama adhuhuri usiku wa manane. Vivyo hivyo pia anasema mtunzi wa Zaburi: “Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili Zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa Zako. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa Zako nitashangilia.” Zab. 36:7; 63:7. {TN8: 97: 1}

Na “kwa hivyo,” apaza sauti nabii wa Injili pia, “walio hodari watakutukuza, Mji wa mataifa watishao utakuogopa. Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao, Kama dhoruba ipigayo ukuta.” Isa. 25:3, 4. {TN8: 97: 2}

“Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na Yeye ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.” Isa. 16:5. {TN8: 97: 3}

Kwa sababu kwa mujibu wa andiko hili kuanzishwa kwa kiti cha enzi cha Kristo bado ni kwa wakati wa baadaye, na kwa kuwa zaidi ya hayo kitasimamishwa katika hema ya Daudi (ambalo halikufanyika wakati wa ujio Wake wa kwanza),

97

Kristo, kwa hivyo, atakapokuja kutawala katika ufalme Wake unaokuja, atakaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi. Na Yeye wakati huo ndiye atakayefanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, na mwepesi wa kutenda haki, utendaji wote unatukia kabla ya kufungwa kwa muda wa rehema — wakati ambapo Yeye anaweza kuharakisha haki. Hivyo, kwa furaha, unabii huu wa ukoo wa Kristo na Wake “kuchukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe,” ulitolewa kwa ajili ya “ushauri na kujifunza” kwa wale ambao watakuwa wanaishi wakati wa mwisho, ambapo “mambo haya yote yatatukia. “Kwa hivyo, la umuhimu wa juu sana, ni hitaji la kukumbuka masomo yake yote muhimu, pamoja na

Kutenda kwa Uaminifu Haraka. {TN8: 97: 4}

Kuona kwamba Lutu pamoja na Abrahamu wanaonekana katika kumbukumbu ya ukoo wa Kristo, swali kwa kawaida linazuka: Kwa nini watu hawa wawili wanaheshimiwa sana? Na jibu linatusubiri: Abrahamu alipata heshima hii kubwa kwa sababu alikuwa mwaminifu kwa Neno la Mungu na kamwe hakulidadisi, ingawa hatma ya vitu vyote ilionekana ikitimia kinyume cha maslahi yake na ahadi za Mungu: Ingawa Mungu aliahidi kumpa nchi hiyo na kwa uzao wake kuwa milki ya milele, Abrahamu, binafsi, kamwe hakuipata hiyo ahadi. Mbali na kustahimili hii mitihani ya kupima imani, alingojea miaka ishirini na mitano mwana wa ahadi, lakini kuamriwa wakati mtoto huyu wa pekee alipokuwa kijana, kumtoa kafara

98

sadaka ya kuteketezwa! Bado, hata hivyo, kupitia kila jaribio, kamwe hakupoteza imani yake kwa Mungu, lakini kikamilifu alimwamini Yeye na kutii amri Zake bila kinyongo. Kwa sababu hii Mungu alimpa heshima kwa ishara. {TN8: 98: 1}

Hata sasa somo kubwa hapa la kujifunza si sana kutoka kwa uzoefu wa Abrahamu, ila kutoka kwa Lutu kwa maana ingawa Lutu hakuwa mkarimu sana kama Abrahamu, na asiye tayari kuishi mbali na ulimwengu, bado imani yake katika ahadi za Mungu kwa Abrahamu ilikuwa kuu kama ilivyokuwa imani ya Abrahamu, mwenyewe, naam, kwa namna fulani, hata kubwa zaidi: kwa maana Mungu alizungumza na Abrahamu moja kwa moja, ilhali alizungumza na Lutu kupitia kwa Abrahamu. Lutu, kwa hivyo, alikuwa na imani kamili kwamba Mungu alikuwa amezungumza naye kupitia kwa Abrahamu. {TN8: 99: 1}

Hivyo katika siku za Abrahamu, zaidi ya hayo, haikuwapo Biblia, kwayo kuthibitisha kwamba kuondoka kwake kutoka nyumba ya baba yake kulikuwa ni kutimiza unabii, na ya kwamba Mungu alikuwa anamwongoza aondoke Ur ya Wakaldayo kwenda nchi ambayo yeye, mwenyewe hakuijua (Ebr. 11:8, 9), tunaona kwamba Lutu hakuwa kama watu wengi leo, ambao huhoji na kulaumu kila kitu katika ukweli unapokunjua. Bila kuhoji hata kidogo au kushuku, aliiweka imani yake kwa Mungu wa Abrahamu, na kwa ujasiri akamfuata katika jitihada za kutafuta nchi iliyoahidiwa. {TN8: 99: 2}

Ni ya namna gani tofauti kati ya tabia ya Lutu na ile ya Wayahudi ambao waliwakataa

99

manabii na hata kuwaua! Kwa sababu hii Mungu alimheshimu Lutu na zawadi kuu ambayo mbingu ingeweza kumpa mwanadamu — kugawana uzazi wa kidunia wa Bwana wa Utukufu, Mfalme wa milele! {TN8: 99: 3}

Ingawa, isitoshe, uzao wa Lutu, Wamoabu na Waamoni, hawakuwa bora zaidi kuliko watu wengine wa mataifa, lakini kwa ajili ya Lutu, Mungu hakuwafanyiza kazi, kama alivyofanya na watu wengine wa mataifa, ila aliamuru Musa “usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.” “Na utakaposongea kuwaelekea wana wa Amoni, usiwasumbue wana wa Amoni, wala usishindane nao; kwa kuwa sitakupa katika nchi ya hao wana wa Amoni kuwa milki yako; kwa sababu nimewapa wana wa Lutu iwe milki yao.” Kumb. 2:9, 19. {TN8: 100: 1}

Na “Mtu akinitumikia,” Yesu akasema, “na anifuate; Nami nilipo, ndipo na mtumishi Wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” Yoh. 12:26. Pia “Ataniita,” anasema mtunga Zaburi, “Nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza.” Zab. 91:15. {TN8: 100: 2}

Mbali na tendo la furaha la kuonyesha ukarimu kwa malaika waliozuru Sodoma (Mwa. 19:1), tendo la kiungwana katika kumbukumbu ya madoadoa ya uhai wa Lutu ni kwamba aliungana na Abrahamu

100

katika dini yake mpya iliyopatikana na ya kigeni na ya kwamba, ili kufanya hivyo, aliondoka nyumbani kwa baba yake na nchi yake bila kujua mahali alipokuwa akienda. Mbali na kupokea, kwa hivyo, baraka ya milele ya kuwa mmoja wa wazazi wa duniani wa Kristo (baraka ambayo ataitambua kupitia kwa Kristo katika siku njema ya ufufuo, na kufurahi kwayo milele na milele), Hakupungukiwa na baraka za maisha ya muda, na wakati akizungukwa na hatari ya kidunia, malaika waliotumwa kutoka mbinguni hata walimwokoa kutoka katika mji ulioangamizwa wa Sodoma kabla ya kupunguzwa kuwa majivu (Mwa. 19:16, 24, 25). {TN8: 100: 3}

Angalikuwa amengoja, hata hivyo, kwa ushahidi mkubwa kuhusu iwapo ndio au la Mungu alikuwa anamwongoza katika tukio hili muhimu sana la maisha yake; laiti angesema moyoni mwake, “Sibahatishi, ila nitangoja mpaka mradi huu uwe na mafanikio. Kwanza nitauchunguza na kujua kwa uhakika kwamba hiyo nchi ina rutuba, na hali ya tabia nchi inakubalika kwa familia yangu, jamii, nk.,” hangeweza kuwa na sehemu katika vuguvugu lenyewe, au katika ukoo wa baba wa Bwana wa Utukufu, au katika Ufalme Wake wa milele! {TN8: 101: 1}

O Ndugu, Dada, unayo imani ya Lutu? “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandiikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Kor. 10:11. O hebu, basi, tufuate katika nyayo za watu hawa wa Mungu, tukiliamini Neno Lake

101

lisilobadilika, na kutenda kwalo bila kusita hata kidogo! Usifuate njia ya wale waliokuwa na mashaka, waliohoji, na kulaumu, na ambao, kwa matokeo mabaya, hawakuufikia ujuzi wa kweli. Kama hao ambao waliishi wakati wa Vuguvugu la awali la Ujio, historia ya kanisa inasema: “Umati, waliamini kikamilifu wachungaji wao, walikataa kulisikia onyo; na wengine, ingawa walishawishiwa kwa ukweli, hawakuthubutu kuukiri, ili wasije ‘wakatupwa nje ya sinagogi.’” (TN8: 101: 2}

“Kikwazo kikuu kwa yote mawili kuupokea na kuutangaza ukweli, ni ukweli kwamba kinahusisha usumbufu na kushutumiwa. Hii ndio hoja ya pekee dhidi ya ukweli ambayo watetezi wake hawajawahi kuipinga. Lakini hili huwa haliwazuii wafuasi wa kweli wa Kristo. Hawa huwa hawasubiri ukweli kuwa maarufu. Wakishawishika kwa wajibu wao, huukubali kwa makusudi msalaba, pamoja na mtume Paulo wakihesabu kwamba ‘shida yetu ndogo, ambayo ni ya muda tu, inatufanyia uzito mkubwa zaidi wa utukufu wa milele;’ na mmoja wa zamani, ‘kuheshimu shutuma ya Kristo utajiri zaidi kuliko hazina za Misri.’” — Pambano Kuu, uk. 380, 460. {TN8: 102: 1}

Wote Wamoabu na Waamoni walikuwa wazawa wa Lutu, na Lutu akiwa mmoja na Abrahamu, pia Waedomu kuwa wazao wa Esau, ndugu pacha wa Yakobo, kwa hao wote Mungu alisema, “Na

102

kizazi cha nne kitarudi hapa” (Mwa. 15:13-16), wangekuwa kwa hivyo wamejua kwamba wakati ulikuwa umewadia wa kutimizwa kwa tukio hilo lililokuwa limetarajiwa kwa muda mrefu, na wangekuwa hivyo basi tayari kwalo, au, kama walipoteza macho ya ukweli, basi wangeweza kukumbuka wakati waliona vuguvugu ambalo lilikuwa sasa haswa kwenye mipaka yao. Ikiwa wangekuwa wamemwamini Mungu wa Abrahamu kama Lutu alivyoamini, hawangekuwa wamekataa kuwaruhusu wana wa Israeli, jamaa zao wa damu, kupitia nchi yao kwenda nchi ya ahadi, ila badala yake wangejiunga nao, jinsi Lutu alivyojiunga na Abrahamu, kuwasaidia kuimiliki. {TN8: 102: 2}

Hakika, Wamoabu walikwenda mbali sana katika chuki yao kwa jamaa zao kwamba hata waliajiri Balaamu kuwalaani, licha ya ukweli kwamba Mungu, katika kuwakumbusha Waisraeli katika mawazo ya ahadi Yake kwa Lutu, aliwaamuru kwamba wasiwadhuru ndugu zao (Amu. 11:16-18). {TN8: 103: 1}

Hivyo kwa kukataa kuwakaribisha na kuwapa mwendo salama kwa njia ya nchi, Wamoabu si tu walikataa kutambua majaaliwa ya ajabu ya Mungu, lakini pia wakamkataa Yeye katika umbo la watu Wake ambao walijua vyema kwamba alikuwa Amewaongoza kwa ishara na maajabu, kutoka nchi ya Misri. {TN8: 103: 2}

Hebu somo hili la kuhuzunisha lipenyeze hadi ndani ya mioyo ya wote leo, na kusababisha watambue nguvu za Mwenyezi Mungu

103

kutimiza unabii. Je! Wakristo hawataepuka kasoro na makosa ya siku za zamani na bila kusita, wajiunge na watu wa Mungu kwa pambano lao la kuelekea nchi ya ahadi ya uakisi? Au je, yeyote katika kizazi hiki kilichoelimishwa apuuze kwa ukaidi Neno la Mungu, na kuwapinga watu Wake, walivyofanya Wamoabu na Waamoni, ambao kwa hivyo walipoteza ufalme wao wote na uzima wa milele? Oo, ni janga lililoje, baada ya kuangaziwa hivyo na Neno la kweli, kusikia ikinenwa dhidi ya mmoja binafsi hukumu ili ile ya kutisha ambayo iliwatenga Wamoabu na Waamoni kutoka kwa kutaniko la Bwana! — {TN8: 103: 3}

“Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele; kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize.” Kumb. 23:3, 4. {TN8: 104: 1}

Wamoabu kumwajiri Balaamu kunaitisha umakini kwa ukweli kwamba, katika uakisi, wale ambao wanapaswa kuwakaribisha na kuwabariki watu wa Mungu, badala yake, pamoja na ahadi za fedha na umaarufu, watawaajiri watumwa wa moyo wa uongo kuwalaani. Lakini tunafarijiwa kwa ukweli (katika mfano) kwamba kile ambacho Mungu amebariki, hakuna mtu anayeweza kukilaani. {TN8: 104: 2}

104

“Nimestaajabishwa,” asema mtumwa wa Bwana, “kwamba pamoja na mifano iliyo mbele yetu juu ya kile mwanadamu anaweza kuwa, na kile anachoweza kufanya, hatujachochewa kwa juhudi kubwa ya kuiga matendo mema ya wenye haki. Wote hawawezi kushikilia nafasi ya umaarufu; lakini wote wanaweza kujaza nafasi za utumishi na uaminifu, na wanaweza, kwa uaminifu wao wa uvumilivu, kufanya mema zaidi kuliko wazo lolote walilonalo ambalo wanaweza kufanya. Wale wanaoukumbatia ukweli wanapaswa kutafuta ufahamu safi wa Maandiko, na ufahamu wa uzoefu wa Mwokozi aliye hai. Akili zinapaswa kustawishwa, kikumbuko kukazwa. Uvivu wote wa kiakili ni dhambi, na ulegevu wa kiroho ni kifo.” — Shuhuda, Gombo la 4, uk. 399. {TN8: 105: 1}

“Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.” Ebr. 6:11, 12. {TN8: 105: 2}

Wale wanaomngojea mchungaji aupokee ujumbe kabla, wao wenyewe, kutenda kulingana na imani zao, kamwe hawatafikia kuujua ukweli. Inasema Roho ya Unabii: {TN8: 105: 3}

“Kama nuru na uzima wa wanadamu ulikataliwa na mamlaka ya ukasisi wa kanisa katika siku za Kristo hivyo imekataliwa katika kila kizazi kilichofuata. Tena na tena historia ya Kristo kujiondoa Yudea imejirudia tena. Wakati

105

Wana-matengenezo walihubiri neno la Mungu, hawakuwa na wazo la kujitenga kutoka kwa kanisa lililoanzishwa; lakini viongozi wa kidini hawakuweza kuistahimili nuru, na wale walioitangaza walilazimika kutafuta daraja lingine, ambalo lilikuwa na hamu ya ukweli. Katika siku zetu, wachache kwa wanaodai kuwa wafuasi wa Wana-matengenezo huendeshwa na roho yao. Wachache huisikiliza sauti ya Mungu, na tayari kuupokea ukweli katika umbo lolote ambalo unaweza kuwasilishwa. Mara nyingi wale wanaozifuata hatua za Wana-matengenezo hulazimishwa kuacha makanisa wanayopenda, ili kutangaza mafundisho wazi ya Neno la Mungu. Na mara nyingi wale ambao huitafuta nuru kwa fundisho lile lile huwajibika kuliacha kanisa la baba zao, ili waweze kutoa utii.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 232, aya ya 2. {TN8: 105: 4}

“Katika siku hizo, na wakati huo, asema Bwana, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta Bwana, Mungu wao. Watauliza habari za Zayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na Bwana, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa. Watu Wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika. Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema,

106

sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya Bwana, aliye kao la haki, yaani, Bwana, tumaini la baba zao. Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu [viongozi] mbele ya makundi.” Yer. 50:4-8. {TN8: 106: 1}

“Wakati umekuja kwa matengenezo kamili kutukia. Wakati matengenezo haya yatakapoanza, roho ya sala itamwendesha kila mwamini, na itafukuza kutoka kanisani roho ya chokochoko na mizozo. Wale ambao hawajaishi katika ushirika wa Kikristo watakuja karibu mmoja kwa mwenziwe. Mshiriki mmoja akitenda kazi katika safu sahihi atawaongoza washiriki wengine kuungana pamoja naye kufanya maombezi kwa ajili ya ufunuo wa Roho Mtakatifu. Hakutakuwa na machafuko, kwa sababu wote watakuwa katika umoja na nia ya Roho. Vikwazo vinavyotenganisha mwamini kutoka kwa mwamini vitavunjwa, na watumwa wa Mungu watasema mambo mamoja. Bwana atashirikiana na watumwa Wake. Wote wataomba kwa uelewa sala ambayo Kristo aliwafundisha watumwa Wake: ‘Ufalme Wako uje, Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Mat. 6:10.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 251. {TN8: 107: 1}

“Bwana akasema kwa Bwana wangu, Uketi mkono Wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako. Bwana atainyosha toka Zayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; watu Wako wanajitoa kwa hiari, siku ya

107

uwezo Wako; kwa uzuri wa utakatifu, tokea tumbo la asubuhi, unao umande wa ujana wako. Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. Bwana yu mkono Wako wa kuume; Ataseta wafalme, siku ya ghadhabu Yake. Yeye atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. Atakunywa maji ya mto njiani; kwa hivyo atakiinua kichwa Chake.” Zab. 110:1-7. {TN8: 107: 2}

“Mkumbuke mke wa Lutu.”

“Kimbia kwa ajili ya Maisha Yako.”

Hivyo unajitokeza muundo mbinu wa mnara wa kweli, ukiwatuma ujumbe kwamba ufalme utarejeshwa na nabii Eliya wa uakisi, kabla tu ya kufungwa kwa muda wa rehema, lakini ya kwamba dunia kwa kuwa haifai kwa watakatifu kukaa kwayo milele, basi Yesu kwa hivyo “atakuja tena” na kuwapokea wote waliokombolewa (wote waliofufuliwa kutoka katika makaburi yao na wale ambao watapatikana wakiwa hai wakati wa kuja Kwake — 1 Thes. 4:16, 17), na atawapeleka kwenye majumba ya juu, ambayo Yeye ameenda kuandaa (Yoh. 14:3). Kisha wakati watakatifu wanapanda juu na waovu kufa, dunia itasalia tupu na giza (Yer. 4:23-29) kwa miaka elfu (Ufu. 20:3), baada ya hapo Bwana atashuka pamoja na watakatifu (Ufu. 21:1-3), kuitakasa dunia kwa moto (2 Pet. 3:10-13), na kuifanya upya kwa makaazi ya milele ya watakatifu (Isa. 45:18)! {TN8: 108: 1}

108

Sasa basi iruhusu imani yako katika Neno ifanye upya upendo wako katika ukweli na katika ahadi ya utukufu wa baadaye: {TN8: 109: 1}

“Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana Ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume Wake mwenyewe, mkono Wake mtakatifu umemtendea wokovu. Bwana ameufunua wokovu Wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki Yake. Amezikumbuka rehema Zake, Na uaminifu Wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele ya Mfalme, Bwana. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele ya Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.” Zab. 98:1-9. {TN8: 109: 2}

O ni kama nini matukio ya utukufu wa baadaye! Nani angetaka kuyakosa! Ndugu, Dada, ni lazima uwe hapo. Chochote unachopoteza hapa, uwe na azimio kuhakikisha unayo makao hapo. “. . . Utakuwa ni umilele wa furaha umilele wa heri, ukikunjua utukufu mpya katika vizazi visivyokuwa na mwisho.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 131. {TN8: 109: 3}

109

Tazama “. . . mto wa kioo na mashamba ya kijani, miti inayotikisa-tikisa na chemchemi hai, mji unaong’aa na waimbaji waliovaa mavazi ya rangi nyeupe, wa nyumbani kwetu mbinguni, — ulimwengu huo wa uzuri ambao hakuna msanii anayeweza kuuchora, hakuna lugha ya mwanadamu inayoweza kuusifu. ‘Jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.’” 1 Kor. 2:9. {TN8: 110: 1}

“Kukaa milele ndani katika makao haya ya heri, kuchukua katika nafsi, mwili, na roho, si dalili nyeusi za dhambi na laana, ila mfano kamili wa Muumba wetu, na katika vizazi visivyo na mwisho kuendelea katika hekima, maarifa, na utakatifu, daima kugundua nyanja mpya za kutafakari, siku zote kupata maajabu na utukufu mpya, daima kuongezeka kwa uwezo wa kujua na kufurahia na kupenda, na kujua kwamba bado ipo mbele yetu furaha na upendo na hekima ya milele, — cha namna hii ni kitu ambacho tumaini la Mkristo huelekeza. . .” — Mashauri kwa Walimu, uk. 55. {TN8: 110: 2}

(Aina za Italiki ni Yetu)

110

Faharisi ya Maandiko

Jalada

Hati miliki 1940, 1942

Haki zote zimehifadhiwa

V.T. Houteff

Katika nia ya kufikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inatumaini kuiepuka njia inayoongoza kwenye uharibifu wa mwili na roho, trakti hii inasambazwa bila malipo kadri toleo hili linadumu.

TRAKTI NAMBA 9

TOLEO LA PILI LILILOSAHIHISHWA

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

2

YALIYOMO

“TAZAMA, NAVIFANYA VITU VYOTE KUWA VIPYA”

MILLENIA

Ukiwa Au Inayokaliwa?

Wakati Wa Kuja Kwa Kristo

Wenye Haki Ndio “Walioachwa”

Waliotakaswa-Watasimama Milele

Dunia Kufanywa Upya

Sababu Zaidi

Mbingu Hapo Mwanzo

Kuvunjika Kwa Mfumo-Joto Wa Dunia

Mfumo Wa Jua Na Sayari Zake

Hitaji La Mbingu Ni Mbingu Za Bwana Kufanywa Upya

“Atayarejesha Yote” Mat.17: 11

MATUKIO YA MILLENIA

Kuwachinja Waovu Wote

Watakatifu Wanahamia Eneo Lingine

Shetani Anaachwa Peke yake

Hukumu Wakati Wa Millenia

Baada ya Hukumu

Shetani Afunguliwa Muda Mchache

Mauti Ya Pili

“Imewapasa Ninyi Kuwa Watu Wa Tabia Gani?”

ANAUSIMAMISHA UFALME WAKE

Siku Ambazo Ufalme Utasimamishwa

Ya Ufalme Kazi Ya Kulipiza Kisasi

Amani Kamili Na Usalama Kamili

Kabla Ya Kufungwa Kwa Muda Wa Rehema

Ambapo Ufalme Unasimama; Hapo Dhambi Haipo

Wayahudi Kurejea Yerusalemu

Kuwatambua Watu 144,000

Mazao Ya Kwanza Ya Mavuno

Kundi Ambalo Halijatiwa Unajisi Na Wanawake

Watalikusanya Kundi Lililotiwa Unajisi Na Wanawake, Mavuno Ya Pili

Katika Vinywa vyao Haukuonekana Uongo

Wakati Ambapo Pepo Zinaachiliwa Na Kuvuma

Wale Watakaomwona Mfalme

“Isikieni Hiyo Fimbo Na Yeye Aliyeiagiza.” Mika 6: 9

Kazi Katika Laodekia Huashiria Ile Katika Babeli

Kanisa La Ufalme La Nane, Linasalia Safi

Makundi Matano Ndani Ya Ufalme

Muhtasari Wa Malimbuko Na Mavuno Ya Pili

“Pamoja Na Bwana Milele” 1 Wathesalonike. 4: 16,17

Mbingu Zitatoweka. Waovu Wataililia Milima Iwaangukie

Shetani Anawadanganya Tena

“Mapito Ya Zamani” Yer. 6:16 3,4

4-6

6-11

11-14

14-16

16-19

19-20

20-22

22

24,25

25,26

26-28

28-31

31,32

32,33

33,34

34

34-36

36,37

37,38

37,38

40

40-44

42,43

43,44

44,45

45-47

47-49

49-51

51-54

54,55

55,56

56,57

58

58,59

60,61

61,62

63,64

64,65

65-67

67-71

71,72

72-74

74

74-76

>