fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 13, 14

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 13, 14

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

UHUISHO NA MATENGENEZO

ITIKADI, NA TIBA

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma aya ya mwisho kutoka kwa Mlima wa Baraka, uk. 163, baada ya hapo tutashiriki katika msimu wa sa-la. {1TG13: 2.1}

M.B, uk. 163 — “Tunapoomba, ‘Utupe leo mkate wetu wa kila siku,’ tunaomba kwa ajili ya wengine hali kadhali-ka kwa ajili yetu wenyewe. Na tunatambua kwamba kile ambacho Mungu anatupatia sio kwa ajili yetu pekee …. “Yeye apandaye kidogo atavuna pia haba; na yeye apandaye kwa wingi atavuna tele.”…. Kwa kutufundisha kuomba kila siku kwa ajili ya tunayohitaji, — baraka za muda na za kiroho, — Mungu analo kusudi la kuzifaniki-sha kwa ajili ya manufaa yetu.” {1TG13: 2.2}

Uzoefu wa Taasisi ni mfano mzuri wa ukweli kwamba wale ambao huwabariki wengine, wao wenyewe pia wa-tabarikiwa. Mnajua kwamba Taasisi hii ilianza kujengwa mwaka wa 1935, katikati ya unyogovu, na kwamba ka-zi yake ilianza bila kitu chochote zaidi ya ufunuo kutoka kwa Bwana. Katika hali zote mwanzo wake ulikuwa mdogo zaidi ya mdogo na maskini sana wa maskini. Na wakati watu wengi na mashirika ya biashara yalifilisika, ilikua na kufanikiwa. Ilibarikiwa hivyo kwa sababu badala ya kujikusanyia baraka zake ilizopewa na Mungu, ilizitumia kwa ukarimu kuwabariki wengine. Kwa sababu Taasisi hii bila ubinafsi imekuwa ikiwabariki wengine tangu mwanzo wake hadi siku ya leo, hata katika wakati wa unyogovu, umekuwa jinsi ilivyo, basi watu binafsi wanaweza pia kuvuna baraka ikiwa wao, pia, wanafuata kanuni hiyo. {1TG13: 2.3}

Kwa hivyo tunapaswa kuomba kwamba tupewe ufahamu wa maana ya kusema, “Utupe leo mkate wetu wa kila siku;” na kujua kwamba ubinafsi huongoza kweye umasikini na kwamba usimamizi na ukarimu huongoza kwa wingi; kwamba sisi kama Wakristo bila shaka tujue kwamba kulichukua jina la Kristo ni kutenda kile Kristo ali-chofanya — kuwabariki wanadamu, kuruhusu ulimwengu ujue kwamba tuko hapa kuutendea mema, sio kuwa mzigo juu yake. {1TG13: 2.4}

2

UHUISHO NA MATENGENEZO

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 2, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutaanza somo letu pale tulipoachia katika somo letu la awali la unabii wa Hagai na Zekaria. Hebu tufungue {1TG13: 3.1}

Hag. 2: 1-3 — “Katika mwezi wa saba, siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema, Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hayo mabaki ya watu, ukisema, Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu?”

Kama ilivyokuwa katika siku za kulijenga hekalu la mfano hivyo ni lazima iwe hivyo katika siku za kulijenga la uakisi, katika siku zetu. Kutoka kwa mfano huu inaonekana kwamba jinsi Neno la Bwana lilivyopelekwa kwa maliwali, kwa kuhani mkuu, na kwa watu wa kawaida, hivyo Neno la Bwana leo litapelekwa kwa watu wote, bila kujali cheo au nafasi katika maisha. {1TG13: 3.2}

Neno la Bwana kwa watu wote katika siku za Hagai na Zekaria lilikuwa kwamba wajenzi walipaswa kuangalia kwa kuvunjika mioyo yao na kutamaushwa kwamba utukufu wa hekalu walilokuwa wakijenga ulikuwa machoni mwao kama sio kitu cha kulinganisha na utukufu wa

3

hekalu la Sulemani. {1TG13: 3.3}

Aya ya 4, 5 — “Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi; kama neno lile nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope.”

Bwana aliwahakikishia watu Wake kwamba upendo Aliokuwa nao kwa ajili yao haukuwa umepungua, na kwamba uwezo Wake kuokoa na kusaidia ulikuwa bado ule ule kama wakati Yeye alipowaleta baba zao kutoka Misri; kama vile Yeye hakuwaacha kamwe watu Wake katika nyakati hizo basi Yeye hangaliweza kuwaacha aidha, na kwamba roho Yake ilikuwa bado itakaa pamoja nao. {1TG13: 4.1}

Aya ya 6-8 — “Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitaziti-kisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.”

Kwamba unabii katika aya hizi bado utatimizwa, ni dhahiri kabisa, kwa maana siku ile hekalu hili litajengwa Mungu atazitikisa mbingu, dunia, na mataifa; kwamba matarajio yao yatakuja wakati huo na kwamba hekalu litajazwa na utukufu; kwamba wajenzi wasiwe na wasiwasi juu ya fedha. {1TG13: 4.2}

Ni kweli kwamba watu hudhibiti na kutumia fedha na dhahabu, lakini lazima isisahaulike kwamba zote ni za Mungu, na kwamba kama Yeye anazihitaji, Yeye anaweza kuzichukua na kufanya vile Atakavyo nazo , kwamba wajenzi

4

hawana haja ya kuhofia uhaba wake ikiwa watazitumia kama vile Mungu atakavyotaka wazitumie. {1TG13: 4.3}

Maadamu ni wazi kwamba hekalu la zamani lilikuwa mfano wa hekalu litakalojengwa katika siku ambayo Mun-gu atazitikisa mbingu, dunia, na mataifa, somo hili linakuwa dhahiri kabisa kwamba Uvuvio hapa unazungumza kuhusu hekalu la uakisi. {1TG13: 5.1}

Aya ya 9 — “Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.”

Ahadi ni kwamba utukufu ulioambata hekalu la Sulemani, utazidiwa sana na ule wa hekalu la uakisi, ambalo litajengwa na kanisa lililotakaswa, kanisa katika wakati wa mavuno, wakati ambapo Mungu atazitikisa mbingu, dunia, na mataifa — wakati wa siku kuu na ya kutisha ya Bwana. {1TG13: 5.2}

Kwa sababu ahadi hizi hazikutimizwa katika siku za hekalu la Zerubabeli, somo hili linakuwa wazi kabisa: kwamba sasa zitaweza kutimizwa, na maadamu kweli hizi za siku za mwisho zimefunuliwa kwetu, lazima tuweze kuwa ndio wajenzi wake, utukufu ambao utazidi utukufu wote wa zamani. Zaidi ya hayo, mahali am-bapo hekalu hili la uakisi litasimama patakuwa na amani, na namna ambavyo amani hiyo itakavyopatikana kika-milifu imeelezwa katika– {1TG13: 5.3}

Aya ya 21, 22 — “Sema na Zerubabeli, liwali wa Yuda, ukisema, Nitazitikisa mbingu na dunia; nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao

5

wataanguka chini kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.”

Tena inaonekana kwamba katika siku ambayo Bwana atazitikisa mbingu na nchi, Yeye pia ataziharibu falme za dunia kwa kuwaruhusu kuuana. Sio ajabu basi kwamba mataifa sasa yanahusika katika mashindano ya silaha, na ulimwengu wote u karibu kutumbukia ndani ya vita vya umwagaji damu ambavyo havijawahi kujulikana. Ni vigumu kwa mtu yeyote kufikia hitimisho lingine lolote isipokuwa kwamba siku kuu na ya kutisha ya Bwana imekaribia. {1TG13: 6.1}

Kwa sababu Zerubabeli ni “nembo”, ishara au mfano wa wajenzi katika siku ambayo Bwana atazitikisa mbingu na nchi, basi maelezo ya Ezekieli ya hekalu la kifumbo (sura ya 40-47) ambalo hata hivyo litajengwa, linaweza kuwa ni ramani ya hekalu la uakisi la Zerubabeli. {1TG13: 6.2}

“Lakini,” unaweza kuhoji, “Je, wazo hili sio kinyume na imani yetu ya awali?” — Ninakubali kuwa ni kinyume. Lakini je, Tutaendelea na kile tulichoamini? au kwa kile Neno la Bwana linasema? Na ni wa kusudi gani huo un-abii iwapo hatuwezi kuuzingatia? Na kwa nini sasa unafunuliwa na kuletwa kwa umakini wetu ikiwa huu sio wakati ambapo Mungu atadhihirisha nguvu Zake na kuyatimiza mambo haya yote? Ikumbukwe kwamba sisi sio watu wa kwanza na wa pekee ambao imebidi tubadili namna yetu ya kufikiri; sisi sio watu wa kwanza na wa pekee kugundua kwamba mipango ya Mungu ni kinyume cha mipango yetu. Musa, pia, aligundua kwamba mpango wake wa kuwaokoa wana wa Israeli kutoka katika utumwa wao wa Misri haukuwa mpango wa Mungu. Vivyo hivyo mpango wa Mungu wa njia waliyopaswa kuchukua katika safari yao kwenda nchi ya ahadi hai-kuwa mpango wao. Mitume kwa hakika waliamini kwamba Kristo angalianzisha ufalme Wake wakati wa ujio Wake wa kwanza, lakini wao,

6

pia, ilibidi wabadili imani yao. Zaidi ya hayo, kwa sababu Waebrania, ambao Mungu aliwafanya wafalme kuto-ka kwa watumwa, walikuwa wameahidiwa kwamba ufalme wao ungalisimama milele, kwa hakika walishangaa wakati uliporomoka. Na imekuwapo mishangao mingine siku zote tangu kupambazuka kwa historia. {1TG13: 6.3}

Waasisi wa dhehebu la Waadventista wa Sabato walitarajia Bwana kuja mara tu waongofu 144,000 walijiunga na kanisa, na walitarajia kuishi wamwone Yeye akija. Washiriki wa kanisa ingawa, tayari ni idadi kadhaa za 144,000, waasisi wamelala, na Bwana bado hajaja. Hivyo swali sio endapo tunataka kubadilisha mawazo yetu au la, ila kama tunataka. {1TG13: 7.1}

Miaka iliyopita tuliambiwa kwamba “Watendakazi watashangazwa na njia rahisi ambayo Yeye atatumia kuitimi-za na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki. Wale ambao wanahesabiwa kuwa watendakazi wazuri watahitajika kumkaribia Mungu, watahitaji mguso wa Mungu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {1TG13: 7.2}

Maadamu Uvuvio unakikunjua Chuo, ni kweli, lakini inatarajiwa kwamba utatupata tukishangaza kwamba hatu-jui mambo mengi – ndiyo sababu hasa kwamba Unakunjua. Ikiwa sisi, kwa hivyo, tushindwe kuyabadilisha mawazo yetu kwa ajili ya Bwana basi lipo tumaini gani kwa ajili yetu kufahamishwa na kufaa umilele? Mawazo yetu yaweze kuanguka chini, na unabii wa Bwana uweze kusimama “juu na uinuliwe.” Wajibu wetu ni kuthibit-isha Neno la Mungu sahihi badala ya kushikilia kwa dhati mawazo yetu tuliyoshikilia na dhana potovu mpaka Mungu Mwenyewe aingie na kutuaibisha. {1TG13: 7.3}

Kama Waadventista wa Sabato awali tulijisifu kwamba “tunaifahamu Biblia yetu” lakini tangu kikundi hiki kili-koma kujigamba

7

kiligundua kwamba klijua machache sana kwa kulinganisha na yale kinachojua sasa, na bado siwezi kusema ku-wa ninayo maarifa ya kutosha ya Biblia kunipeleka wazi ndani ya malango ya lulu. Kwa kweli, najua kwamba ninayo mengi zaidi ya kujifunza. {1TG13: 7.4}

Aya ya 10-13 — “Siku ya ishirini na nne, ya mwezi wa kenda, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Waulizeni sasa ma-kuhani katika habari ya sheria, mkisema, Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye akagusa kwa upindo wake mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula cho chote, je! Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La. Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je! Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi.”

Je, mtu anayebeba maneno matakatifu ya Mungu aguse kitu cha kawaida, kitu hicho bado kitakuwa cha kawai-da na kisichofaa kumletea Mungu; lakini mtu ambaye mwili wake umetiwa unajisi aguse kitu kitakatifu, kitu hicho kitakuwa najisi, kisichofaa kutumika kwa ajili ya sadaka ya Bwana. Yaani, mtu aliyetakaswa hapaswi ku-leta kitu najisi kwa Bwana, na mtu najisi asivilete hata vitu visafi Kwake. {1TG13: 8.1}

Aya ya 15-17 — “Na sasa nawaomba, tafakarini; tangu siku hii na siku zilizopita; kabla halijatiwa bado jiwe juu ya jiwe katika nyumba ya Bwana; katika wakati huo wote, mtu alipofikia chungu ya vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia shinikizo apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu. Naliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunielekea mimi, asema Bwana.”

8

Kwa uzoefu huu wa mfano, andiko hili linafundisha kwamba kujaribu kutafuta riziki wakati unapuuza kuifanya kazi ya Bwana, umaskini badala ya mafanikio utakuwa pato la mtu. Kwa hivyo, ni muhimu kabisa kwamba waaminio Ukweli wa sasa watafute kwanza kuujenga Ufalme wa Mungu na haki Yake iwapo watataka kufani-kiwa. (Mat. 6: 28- 34). Hebu tukumbuke daima kwamba ikiwa tuko kabisa kwa upande wa Bwana, nyuma ya ukigo wa Mungu, alivyokuwa Ayubu, hatuhitaji kuogopa chochote, sio hata ibilisi. {1TG13: 9.1}

Aya ya 18, 19 — “Tafakarini, nawaomba; tangu siku hii ya leo na siku zijazo; tangu siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kenda, naam, tangu siku hiyo ulipowekwa msingi wa hekalu la Bwana tafakarini haya. Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.”

Mfano hufundisha kwamba tangu ile siku tunapoanza kuifanya kazi ya Bwana, tangu siku iyo hiyo Bwana ata-tubariki. {1TG13: 9.2}

Aya ya 14 — “… Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema Bwana; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.”

Aya hii inaonyesha kwamba ikiwa tunashindwa kufanya kazi yetu tuliyopewa na Mungu, basi hakuna mbadala kwa ajili yake. {1TG13: 9.3}

Mara tu walipoambiwa kuhusu dhambi za baba zao, na zao wenyewe, mifano wetu kwa furaha walipatana na matakwa ya Bwana. (Angalia Hag. 1: 5-11). Yeye kwa namna hiyo atatubariki kuanzia leo hii kuendelea iwapo sisi, pia, tutayakiri matendo yetu mabaya, na kuyarekebisha. {1TG13: 9.4}

9

Hag. 1: 12-14 — “Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana. Ndipo Hagai mjumbe wa Bwana, katika ujumbe wa Bwana, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema Bwana. Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao.”

Aya hizi zinatuambia kwamba mara tu watu wote walipowatii wajumbe wa Mungu, mara hiyo tu Roho ya Bwa-na alichochea nguvu zao, na kisha mara moja wote wakaenda kufanya kazi. Sisi, pia, tutapata uzoefu kama huo iwapo sasa tunaamua katika mawazo yetu kwamba kutoka sasa hivi kuendelea tutauzingatia kabisa ujumbe wa Mungu na kumtumikia Bwana Mungu wetu kwa moyo na nafsi yote. Hebu tusikawishe baraka za Mungu kuto-ka kwetu. {1TG13: 10.1}

Aya ya 20, 21 — “Kisha neno la Bwana likamjia Hagai mara ya pili, siku ya ishirini na nne ya mwezi, kus-ema, Sema na Zerubabeli, liwali wa Yuda, ukisema, Nitazitikisa mbingu na dunia.”

Kwa mtazamo wa ukweli kwamba Bwana atazitikiza mbingu na dunia, je, sio muhimu kwamba sisi sasa tu-uweke mbali unafiki? Hebu tuache kualika “ukavu,” “mvua ya mawe,” na “ukungu” juu yetu wenyewe. Hebu badala yake tuzisalimishe nafsi zetu kwa Mungu na hivyo kujihakikishia uchangamfu, amani, furaha na uzima wa milele. Tusipofanya hili, hakika tutakung’utwa nje badala ya kuwa mwongofu na kuhuishwa. {1TG13: 10.2}

10

WAZO LA SALA

Nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, uk. 166, kuanzia aya ya kwanza. Somo hili linategemea andiko, “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” {1TG14: 11.1}

M.B. p. 166 — “Yesu hufundisha kwamba tunaweza kupokea msamaha kutoka kwa Mungu tu kama tuna-vyowasamehe wengine. Ni upendo wa Mungu unaotuvuta Kwake, na upendo huo hauwezi kuigusa mioyo yetu pasipo kujenga upendo kwa ajili ya ndugu zetu. {1TG14: 11.2}

“Baada ya kumaliza sala ya Bwana, Yesu aliongeza hivi: ‘Ikiwa mnawasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe pia. Lakini msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu. Yeye asiye samehe, huikatiza njia ile ambayo kwayo pekee anaweza kupokea rehema kutoka kwa Mungu. Hatupaswi kufikiri kwamba isipokuwa wale ambao wametudhuru wayakiri makosa, tunahesabiwa haki kwa ku-wazuilia msamaha wetu. Ni sehemu yao, bila shaka, kuinyenyekeza mioyo yao kwa toba na kukiri; lakini tuna-paswa kuwa na roho ya huruma kwa wale ambao wamekosa dhidi yetu, iwe watakiri makosa yao au la. Hata kama ni vikali wameweza kutuumiza, hatupaswi kuzikuza lawama zetu, na kujihurumia wenyewe juu ya ma-chungu yetu; lakini kwa sababu tunatarajia msamaha kwa ajili ya makosa yetu dhidi ya Mungu, tunapaswa ku-wasamehe wote ambao wametenda maovu kwetu.” {1TG14: 11.3}

Sasa, ni nini mzigo wa maombi yetu alasiri hii? — Kwamba tuweze kuwa na upendo kwa ajili ya ndugu zetu; kwamba tuyasamehe makosa ya wengine iwe wanatusamehe makosa yetu au la, kwamba tukiri dhambi zetu, bila kujali wengine wanaweza kufanya nini. {1TG14: 11.4}

11

ITIKADI, NA TIBA.

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 9, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Hebu niwajulishe somo langu kwa kuwaambia kisa rahisi. {1TG14: 12.1}

Hapo zamani ndugu sita walikuwa wakijenga daraja, inasemekana kwa mungu wa Haki. Madhumuni ya daraja yalikuwa kuunganisha mashariki na magharibi. {1TG14: 12.2}

Hawakuwa na ugumu kujenga misingi na kuweka mihimili. Lakini, lo, walipokuja kuiunganisha sehemu ya mashariki na ile ya magharibi, walijikuta wakikabiliwa na kikwazo cha ajabu: Kile walichokuwa wamejenga wa-kati wa mchana kilibomolewa wakati wa usiku. Muujiza huu uliendelea siku baada ya siku. Hatimaye wandugu waliketi kwenye mkutano wa baraza ili kujadili jinsi wanavyoweza kutatua shida yao iliyowasumbua. Wakihisi kwamba kuiacha kutaweza kuwa upumbavu mkubwa ambao wangeweza kutenda, kwamba kungaliletea majina yao fedheha, walisoma na wakomba. {1TG14: 12.3}

Hatimaye walihitimisha kwamba mungu wa Haki alikuwa kwa sababu fulani hajafurahishwa nao na kwamba dhabihu ya mwanadamu ingaliweza kumtuliza. Hivyo ndivyo kwamba waliamua kutoa dhabihu mmoja wa wake zao. Hivyo ilikuwa kwamba waliamua kumtoa kafara bora zaidi kati ya wake zao. Hili hata hivyo halikutakiwa lifichuliwe kwa wanawake hao, ili kufanya chaguo lisilo la upendeleo na ambalo lingekubalika, waliamua zaidi kwamba ile kesho kila mmoja angaliweza kumwagiza mkewe kuandaa iwezekanavyo

12

kifungua kinywa na chakula cha jioni, na kumpelekea chakula kwenye daraja mapema iwezekanavyo. Walipaswa kuwaelezea wake zao kwamba walihitajika kula na kuomba pembezoni mwa daraja kwa ajili ya utu-kufu wa mungu wa Haki, na kwa mafanikio ya mradi wao. Mwanamke wa kwanza kuwasili na chakula ndiye agalikuwa mhanga. {1TG14: 12.4}

Wanaume watano, hata hivyo, hawakuzingatia kiapo chao kizito. Kila mmoja wao mara moja waliwaambia wake zao kile ambacho kingefanyika, na kwamba kwa hivyo hawangeharakisha kwenye daraja na vyakula. {1TG14: 13.1}

Asubuhi, kwa wakati uliowekwa, wanaume walikuwa pembezoni mwa daraja. Muda mfupi baadaye waliona kwa umbali mtu fulani akija kwenye daraja. Kwa nukta kadhaa hakuna mtu aliyejua kwa hakika alikuwa nani, lakini punde yule mtu ambaye alikuwa ametunza sehemu yake ya makubaliano alitambua kuwa ni mkewe. Yeye, bila shaka, mara moja akapasuka kwa machozi, na kwa uchungu akaanguka chini. Kwa kuiona tabia ya ajabu ya mumewe, mkewe akakiangusha kikapu chake cha chakula na akakimbia kwenye eneo ili ajue taabu ilikuwa nini. Lakini alipokuwa akijaribu kumfariji mumewe, wale ndugu wengine watano walimkamata, wakampeleka kwenye pengo katika daraja, na humo wakamfukia akiwa hai. Sasa, ndugu walitarajia kwa imani daraja kudumu, kwa maana walijihisi kwamba wamefanya yote waliyoweza kumridhisha mungu wa Haki. {1TG14: 13.2}

Kwa hivyo ilikuwa ni kwamba wakati wanaume watano wasio waaminifu usiku huo walirejea nyumbani kwa furaha, yule mwaminifu alirudi nyumbani kwake kwa huzuni. {1TG14: 13.3}

Asubuhi iliyofuata, wanaume wote waliharakisha hadi kwenye daraja, wakitarajia kupata limesimama imara. Lakini kwa mshangao wao na fadhaa walipata daraja lote limelala tambarare chini! {1TG14: 13.4}

13

Kwa kawaida, tukio hilo lilivuma kote katika mji huo, na majaji wa mji huo walikwenda kuona msisimko huo mkubwa ulikuwa juu ya nini. Walipowasikia wajenzi wakibishana na kuchanganua kutoka kwa chanzo hadi kwa athari, walijua kwamba mwanamke mhanga hakutolewa kuwa sadaka kwa nafasi ya haki, ila kwa udanganyifu! Hivyo walihukumu kwamba msiba wote ulikuwa kutokana na ukweli kwamba wanadamu wasio wa haki walikuwa wakijaribu kujenga daraja kwa heshima ya mungu wa haki! Swala hilo lililetwa mahakamani na hati-maye majaji waliamua kwamba Haki lazima iridhishwe, ikiwa sivyo sio tu daraja, ila hata mji wao unaweza kuanguka chini. Kwa hivyo, siku iyo hiyo wanaume watano wasio wa haki waliuawa, na yule mwaminifu akafanywa kuwa diwani wa mji. {1TG14: 14.1}

Wakristo wamekuwa wakijenga daraja, kwa mfano, kwa Mungu wa Haki kwa miaka mingi. Lakini hawaonekani kuwa na mafanikio zaidi kuliko walivyokuwa wajenzi sita wa daraja. Na kwa sababu gani? — Kwa sababu ile ile wajenzi sita hawakufanikiwa: Wanadamu wabinafsi wanajishughulisha kwa kazi, na ingawa wanaona hitaji la dhabihu, lakini wao kwa namna fulani daima huweza kuwafanya wengine kutoa kafara. {1TG14: 14.2}

Na mwakumbuka kwamba hata hivyo jengo la mnara wa Babeli lilikuwa likikinzana kwa mapenzi ya Mungu na utaratibu Wake, bado wakati wote wajenzi walifanya kazi kwa maelewano kati yao wenyewe, mradi wao ulifan-ikiwa — mnara wao ulikwenda juu angani. Lakini wakati lugha yao ilipovurugwa na hawangaliweza kuelewana tena, basi maendeleo ya mnara yalikoma. Na kuwaonyesha kwamba Yeye hakufurahishwa na mradi wao na kwamba Yeye Ndiye Aliyekuwa ameivuruga lugha yao, Mungu aliupiga mnara ukaporomoka chini. Kile kili-chotokea kwa daraja kilitukia pia kwa mnara. {1TG14: 14.3}

14

Wakristo wanafanya kazi kwa machafuko kati yao wenyewe. Ndugu mmoja Mkristo anamsaliti mwenziwe. Wa-chungaji wa Kikristo, badala ya kuhubiri Ukweli, wanahubiri mmoja dhidi ya mwingine. Mtu anaenda mbele kujenga, na mwingine njiani nyuma kubomoa. Hawaoni jicho kwa jicho; wala hawaelewani walivyofanya wajenzi wa mnara waliochanganyikiwa. {1TG14: 15.1}

Maadamu tu kama huu ubinafsi na kutokuwa na uaminifu, kuchanganyikiwa na uadui, unakaa kati ya Wakristo, daraja lao na mnara wao, kwa mfano, hautafanikiwa hakika kama vile daraja la wavunja agano sita na kama vile mnara wa wadhihaki wa nabii Nuhu. Hakuna njia ya kuikomesha shida ya itikadi bila kuondoa chanzo — la, sio zaidi kuliko kidonda cha kichane chaweza kuponywa kabla ya kichane hakijaondolewa. {1TG14: 15.2}

Mnaujua ukweli kwamba hapakuwa na shida ya itikadi katika siku za Musa wakati Musa pekee yake alilifasiri Neno la Mungu kwa watu. Lakini mara tu Kora, Dathani, Abiramu na wengine walitaka ofisi ya Musa taabu ilianza. Na tiba ya pekee hata Mungu Mwenyewe angaliweza kupata ilikuwa kuisababisha nchi ikifungue kin-ywa chake na kuumeza umati wa wapumua itikadi, wawakilishi waliochichagua wa Mungu. {1TG14: 15.3}

Katika siku zetu yapo mafuriko makubwa zaidi ya wafasiri binafsi wa Maandiko (chanzo cha itikadi za leo) kul-iko ilivyokuwa katika siku za Musa. Na kwa mujibu wa Ufunuo 12:15, 16, Bwana anaonya kwamba Yeye ata-tumia tiba sawa na ile ya zamani dhidi ya mafuriko yanayozalisha itikadi za leo. Kisha wengine wataweza kuji-funza kuheshimu ofisi ya Roho ya Unabii. Hebu sasa tusome kuhusu hatima ya

15

wale wanaochagua kuendelea kutembea katika cheche za moto waliouwasha wenyewe. {1TG14: 15.4}

Ufu. 12:16 — “… nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.”

Hapa tunaona kwamba tiba ile ambayo ilisababisha itikadi kukoma katika siku za Musa, itatumiwa tena kusaba-bisha itikadi kukoma katika siku zetu, njia ya pekee ambayo maelewano yanaweza kurejeshwa kati ya washirika wenza ndani ya kanisa lenyewe, hali kadhalika miongoni mwa Wakristo kwa ujumla. {1TG14: 16.1}

2 Tim. 3:16, 17 — “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

2 Pet. 1:20, 21 — “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiri-wa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

Yakisemwa kwa uthibitisho, Maandiko yote, sio tu sehemu Yake, yamevuviwa. Yakielezwa kwa kukana, haku-na sehemu Yake inayoweza kufasiriwa apendavyo mtu, kwa sababu kwamba Hayakuja kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu; yaani, jinsi Roho wa Mungu alivyowaongoza watu kuandika Maandiko, hivyo Roho wa Mun-gu lazima afasiri Maandiko kwa wanadamu, kwamba hakuna mtu apendavyo (bila Uvuvio) anayeweza kuufunua unabii uliofunikwa au kufasiri sehemu yake yoyote au hata mwenye uwezo wa kuelewa umuhimu wake baada ya kufasiriwa isipokuwa iwe ni kwa zawadi ya Roho wa Kweli “Wala hataelewa mtu mbaya awaye yote,” kwa hivyo,

16

“bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan. 12:10. {1TG14: 16.2}

Tunapaswa sasa kuwa tumesadiki kabisa kwamba maadamu amri hii ya Mungu na kanuni ya kulifasiri Neno la Mungu imepuuzwa na kuvunjwa, na kama ubinafsi na ushupavu ungalipo kati ya Wakristo kwa ujumla na hasa kati ya wanafunzi wa Biblia, itikadi zitaendelea kuongezeka, na nguvu za watu zitaendelea kupotea kama zil-ivyokuwa nguvu za wajenzi wa daraja na wajenzi wa mnara. Ndio, kwa hakika jisi usiku huufuata mchana, juhudi zao zitakuwa bure, na aibu yao itafunuliwa wazi. {1TG14: 17.1}

Kwamba hatuwezi kuongozwa katika Kweli yote bila zawadi ya Roho ya Unabii, Uvuvio kimfano unaonya kimbele kupitia kwa nabii Zekaria. Hebu tufungue Zekaria 4, na tuanze na aya ya kwanza. {1TG14: 17.2}

Zek. 4: 1-4 — “Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dha-habu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa lile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?”

Picha ilioonyeshwa hapa, unaona, ni zalisho halisi la mfano wa Zekaria. Ili kwamba utafiti wetu uwe rahisi na wazi, tutajifunza sura hii pamoja na mfano huu. {1TG14: 17.3}

17

Sasa hebu tuisikie maelezo ya malaika kwa mfano huu. {1TG14: 18.1}

Aya ya 5, 6 — “Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.”

Malaika aliyafichua mambo mawili: La kwanza alijulisha kwamba mfano huu unalihusu Neno la Bwana (Biblia) kwa watumwa wa Mungu; la pili, kwamba Neno Lake hufunuliwa, sio kwa nguvu za mwanadamu wala uwezo, bali kwa Roho wa Mungu. {1TG14: 18.2}

Kwa udhahiri mfano huu kwa ujumla huwakilisha mfumo ambao Bwana hueneza Neno Lake lililofunuliwa kwa watu Wake. Ili tuweze kuwa na ufahamu kamili wa mfumo huu uliobuniwa na Mungu, tunahitaji kujua ni nini kila kijenzi cha sehemu ya mfano kinawakilisha. Roho ya Unabii inatoa kidokezi. {1TG14: 18.3}

18

Katika Pambano Kuu, uk. 267 imeelezwa kwamba “miti ya mizeituni” huwakilisha “Agano la Kale na Jipya;” Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 188, husema kwamba mafuta ya dhahabu huwakilisha Roho Mtakatifu; na kwa ukurasa wa 337 wa kitabu hicho, pamoja na Ufunuo 1:20, husema kwamba taa saba huwakilisha kanisa, na kwamba mifereji saba (ukasisi) hupeleka mafuta kwa makanisa. {1TG14: 19.1}

Sasa ujifunze mfano huo wenyewe kama ungalivyojifunza kibonzo chochote. Kwanza kabisa, miti huwakilisha Neno la Mungu (Biblia – Agano la Kale na Jipya — miti miwili). {1TG14: 19.2}

Hapa inaonekana kwamba nembo yote iliyowekwa ni kwa kusudi la kuonyesha mafanikio ya kitu kimoja tu — kuzidumisha taa saba (jumla ya washiriki wa kanisa) zikiwa zimesambaziwa mafuta ya kiroho (Kweli ya Biblia) ili ziweze kutoa nuru ya kiroho pande zote kuzizunguka, kwamba kanisa liweze kuuangazia ulimwengu kwa Ne-no la Mungu lililofunuliwa. Na kwa kuwa jukumu la ukasisi ni kulilisha kanisa kwa chakula cha kiroho, ukweli ni kwamba mifereji saba inawakilisha ukasisi kazini, ikichukua mafuta (Kweli iliyofunuliwa) kutoka kwenye bakuli hadi kwa taa saba, makanisa. Sasa ukweli kwamba katika mfano mifereji (wachungaji) haichukui mafuta moja kwa moja kutoka kwenye mizeituni (Biblia), inaonyesha kwa uhakika kwamba bakuli ambalo mafuta huwekwa huwakilisha chombo au ghala ambamo mkusanyo wa ufasiri wa Biblia Uliovuviwa huhifadhiwa, na kwamba kutoka kwalo, sio kutoka kwa mizeituni, wachungaji hujifaidisha kwa mafuta na kuyapeleka kwenye taa saba (kwa kanisa). {1TG14: 19.3}

Mabomba mawili ya dhahabu, kwa hivyo, yanaweza kuwa tu uwakilishi wa njia zilizovuviwa ambazo zina uwe-zo wa kuyafyonza mafuta (nuru ya Kweli) kutoka kwa

19

miti (kutoka kwa Maagano yote) na kuyahifadhi ndani ya bakuli (vitabu) kwa ajili ya (wachungaji) kuyapitisha hadi kwa kinara cha taa (kwa kanisa). {1TG14: 19.4}

Mfano huu, kwa hivyo, unaonyesha mfumo ambao Mbingu imeuteua kutoa Neno la Bwana kwa kanisa Lake: kwamba Roho ya Unabii kazini ndio tiba ya pekee dhidi ya itikadi ndani ya kanisa na duniani. {1TG14: 20.1}

Wale ambao hawawezi kuyatumia mafuta ya dhahabu, na wale ambao daima wanaendelea kusaka aina fulani ya mafuta, au wanaojaribu kufyonza yao wenyewe, bila shaka, watatumbukia shimoni wakati ambapo nchi itafunua kinywa chake ili kuyameza mafuriko. Kisha inakuwa kwamba wapumua itikadi na watafuta itikadi watapotelea mbali milele. {1TG14: 20.2}

Aya ya 8, 9 — “Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.”

Maandiko haya yanamaanisha hakika kwamba yapo mashaka katika mawazo ya baadhi ya watu kuona kama Zerubabeli wa uakisi, au mwingine fulani ataikamilisha kazi ambayo Zerubabeli ameianzisha. Zerubabeli anam-wakilisha nani? — {1TG14: 20.3}

Neno la Mungu huelezea kwamba Zerubabeli wa kale ni ishara, mfano, wakati ambapo Mungu anavipindua viti vya enzi vya falme, wakati ambapo majeshi yao yanaangamizwa kwa upanga wa “ndugu” mmoja Mkristo ukim-wua ndugu mwingine Mkristo. (Hagai 2:22, 23). Zerubabeli, kwa hivyo, anamwakilisha mtumishi wa Mungu kwa wakati wafalme wenye taji, “kiti cha enzi cha falme,” kinapinduliwa, na katika wakati ambapo taifa moja la Kikristo

20

linafanya vita na taifa lingine la Kikristo. Kwa kuwa falme zenye taji zinapita kwa haraka, na aina ziingine za serikali zinachukua nafasi zao, yote yanathibitisha kwamba kuonekana kwa Zerubabeli sasa kumewadia. Na jibu la Bwana mwenyewe ni “mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo ita-kayoimaliza.” {1TG14: 20.4}

Aya ya10 — “Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.”

Siku ambayo Andiko hili litatimizwa, ni katika siku ambapo Bwana wa majeshi anaianza kazi ya matengenezo yamkini kwa namna ndogo sana na ya uhafifu, na wale ambao hudharau myanzo midogo na ya udhaifu mwishowe watafurahi kuona kwamba Zerubabeli wa uakisi ndiye atakayeielekeza kazi pamoja na wote (saba) wasaidizi wake. Wao ndio macho ya Bwana. Siku muhimu kama nini! Watu wakuu kama nini! Kwa udhahiri wao wanajumuisha “jiwe” la Zekaria Tatu ambalo tulijifunza majuma kadhaa yaliyopita, na kujua kwamba lina macho saba, maono kamili ya kiroho. Kwa hakika hili ndilo jiwe ambalo litaipiga sanamu kubwa ya Danieli 2:45. {1TG14: 21.1}

Aya ya 11, 12 — “Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao?”

Yote haya yanatukia kwa wakati huu, na unabii sasa umefunuliwa, ni uthibitisho kwamba Zerubabeli wa uakisi lazima awe hapa, na kwamba

21

ameianzisha kazi hiyo, pia lazima aimalize. Ukweli kwamba Uvuvio hujitaabisha kusema ni nani atakayeimaliza kazi ndani yake ni uthibitisho kwamba lazima wapo walaghai wa ofisi yake kama walivyokuwapo wa ofisi ya Musa. {1TG14: 21.2}

Aya ya 13, 14 — “Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.”

Kutoka kwa habari ya malaika sasa inaonekana wazi zaidi kwamba mfano huu unaonyesha mfumo wa kulifasiri Neno la Mungu lililoandikwa, na wa Kulipeleka kwa kanisa. Wakati ambapo ni katika enzi ya Agano Jipya, wa-kati ambapo miti yote miwili ipo. {1TG14: 22.1}

Hebu sasa tufanye muhtasari wa somo kwa msaada wa mfano huo. Hapa tunaona kinara cha taa (kanisa) cha dhahabu tupu, bora zaidi ya vinara vyote (hakuna “magugu” ndani yake). Linajumuisha masalia (wale wali-oachwa baada ya wadhambi kuangamizwa) ambalo kwa kweli huzishika amri za Mungu, na kuwa na Ushuhuda wa Yesu Kristo, Roho ya Unabii (Ufu. 12:17; 19:10). Kinara hiki safi kimejazwa mafuta na kinawaka. Mabomba mawili ya dhahabu (wafasiri wa Mungu waliovuviwa) huyahifadhi mafuta ya dhahabu katika bakuli la dhahabu (vitabu vya Roho ya Unabii). Na mifereji saba (ukuhani wote) hupeleka kutoka katika bakuli la dhahabu mafuta ya dhahabu kwenye taa saba za dhahabu (kwa waumini wote). {1TG14: 22.2}

Chini ya mfumo huu kamili wa kuliandaa, na kulitoa Neno la Mungu, “chakula kwa wakati wake,” kwa watu Wake, hakuna haja ya kuhofia kwamba hifadhi itakosa mafuta, au kwamba taa zitazimika. Huu ndio mfumo wa pekee, zaidi ya hayo, ambao unaweza kulifanya kanisa kuwa kamilifu, bila doa, kunyanzi, au kitu chochote ka-ma hicho — watu ambao hawana uongo katika vinywa vyao, wanaona wote jicho kwa jicho,

22

wote wanena mamoja. Kweli “hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe.” Yoeli 2: 2. Hii bila shaka ndiyo nguvu kuu inayoiangaza nchi, ni Kilio Kikuu. Hakika mfano huu unalifunua kanisa kwa wakati ambapo limejazwa Roho ya Unabii na haki ya Kristo. {1TG14: 22.3}

Kwa uwazi, mfumo wa Ufasiri wa Biblia, ulioelezwa na Zekaria, ni mfumo wa pekee wa Bwana. Ndio tiba ya pekee ya itikadi na kutopatana miongoni mwa Wakristo. Hivyo ni kwamba “Sauti ya walinzi wako! Wanapa-za sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.” Isa. 52: 8. {1TG14: 23.1}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 13, 14

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>