30 Jan Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 07, 08
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 7, 8
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
WAKATI WA “WAKATI WA TAABU,” NA THAWABU YA IMANI YA MMOJA KWA MUNGU
UHUISHO NA MATENGENEZO YANATANGULIA SIKU KUU NA YA KUOGOFYA YA BWANA
1
ANDIKO LA SALA
Fundisha Tu Kweli Bayana
Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano, ukurasa wa 43, aya ya kwanza– {2TG7: 2.1}
“Lakini mwalimu wa ukweli mtakatifu anaweza kutoa tu lile ambalo yeye mwenyewe anajua kwa uzoefu. ‘Mpanzi alipanda mbegu yake.’ Kristo alifundisha ukweli kwa sababu Yeye alikuwa kweli… Hivyo na watumwa Wake: Wale ambao wangefundisha neno ni lazima walifanye kuwa uzoefu wao wa kibinafsi…. Katika kuwasi-lisha neno la Mungu kwa wengine, hawapaswi kulifanya liwe la kudhania kuwa hivyo au labda. Wanapaswa kutangaza na mtume Petro. “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu tulipowajulisha nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.” Kila mchungaji wa Kristo na kila mwalimu aweze kusema na mpendwa Yohana, “Uzima huo ulidhihirika, nasi tumeuona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele uliokuwa na Baba, ukadhihirika kwetu.’” {2TG7: 2.2}
Je! Watumwa wa Mungu wanapaswa kufundishaje Kweli? — Wanapaswa kufundisha Ukweli bayana, sio kwa kudhania kuwa hivyo au labda, ila kwa ubayana. Ikiwa hawaneni Ukweli hakika, basi ni mema gani yanayoweza kutokea? Mitume hawakuhubiri kufufuka kwa Kristo na kupaa kwake kama nadharia, bali kama Ukweli hakika. Iwapo mafundisho yetu hujumuisha kudhani na labda basi tutakuwa tunapoteza wakati wetu, nguvu zetu, na wakati wa wale hutusikiliza. Hayatamnufaisha yeyote, na kuwadhuru wote. Tunapaswa sasa kuomba kwa ajili ya uwezo wa kufundisha tu kweli bayana, zile tu ambazo tunazijua kwa uzoefu na nguvu. {2TG7: 2.3}
2
WAKATI WA “WAKATI WA TAABU,” NA THAWABU YA IMANI YA MMOJA KWA MUNGU
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, SEPTEMBA 20, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Mada yetu ya alasiri hii inapatikana katika Danieli, sura ya 11 na 12. Sura ya 12 inasheheni “wakati wa taabu,” lakini wakati wa “wakati wa taabu” unapatikana katika sura ya kumi na moja ya Danieli. Sura ya kumi na mbili ni bila shaka, endelezo la sura ya kumi na moja. Tutaanza uchambuzi wetu na– {2TG7: 3.1}
Dan. 12: 4 — “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukatie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho. Wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”
Danieli aliambiwa kufunga na kukitia muhuri kitabu hata wakati wa mwisho. Kitabu, kwa hivyo, hakikuwa kwa ajili ya ufahamu wa watu kabla ya wakati wa mwisho. Hivyo, basi, wakati kitabu kinafunuliwa na kueleweka tunaweza kujua kwamba wakati wa mwisho umekuja. {2TG7: 3.2}
Licha ya ishara hii, hata hivyo, ipo ishara ya watu kukimbia huko na huko, na ongezeko la maarifa. Ulimwen-gu wote unajua kwamba katika miaka yote ya historia, kabla ya wakati wetu, farasi alikuwa njia ya kasi mno ya usafirishaji na mawasiliano ya wanadamu, na mbinu hii iliendelea katika karne zote. Malaika hata hivyo alimjul-isha Danieli kwamba katika wakati
3
wa mwisho kungekuwa na mabadiliko yaliyokusudiwa, ambayo watu wakati huo wangekimbia huko na huko. Na kuugusa wakati wa mwisho kulingana na unabii wa Nahumu, Uvuvio unatangaza: “Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, yanasongana-songana katika njia kuu: kuonekana kwake ni kama mienge, yanakwenda upesi kama umeme.” Nah . 2: 4. {2TG7: 3.3}
Sasa kwamba maarifa yameongezeka tangu karne iliyopita, au zaidi, na sasa mitambo ya mvuke, mafuta, na umeme imeupindua ulimwengu, na kufanya iwezekane watu kukimbia huko na huko kwa kasi isiyo na kifani, mada inasimama wazi kama kioo kwamba sasa tunaishi katika wakati wa mwisho. Haliwezi kuwapo shaka juu ya hili. Huu ni ukweli yakini, ukweli kwamba huwezi kupingana na bado uiamini Bibilia na historia. {2TG7: 4.1}
Ili kupata mwanzo wa wakati wa mwisho, lazima tusome– {2TG7: 4.2}
Dan. 11:40 — “Na mwanzoni mwa wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.”
Sio katika, ila mwanzoni mwa wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana na mfalme wa kaskazini. Vi-ta hii ya kinabii, kwa hivyo, inatia alama mwanzo wa wakati wa mwisho. Ili kupata wakati wa vita kati ya wafalme hawa wawili tunahitaji kusom– {2TG7: 4.3}
Aya ya 41-43 — “ Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa:
4
lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni. Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Wamisri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.”
Tia alama kwa uangalifu kwamba mwanzo wa anguko la mfalme wa kusini, mfalme wa kaskazini anapanuka na kuzipindua nchi nyingi; kwamba anaingia katika nchi ya uzuri (Palestina), lakini Edomu, Moabu, na wana wa Amoni wanaokoka kutoka mkononi mwake. Na kumbuka kwamba kazi hii ya kuteka ilikuwa ianze mwanzoni mwa wakati wa mwisho. Hivyo, katika wakati wa mwisho mfalme wa kusini anaporomoka, ilhali mfalme wa kaskazini anapanuka. Na kwa sababu pambano linaanza mwanzoni mwa wakati wa mwisho, kushindwa kwa mmoja na kushinda kwa mwingine kunakamilika ndani ya na katika wakati wa mwisho. {2TG7: 5.1}
Ijayo, ili tujue ni lini miaka ya wakati wa mwisho ilianza, na ni akina nani mfalme wa kusini na mfalme wa kaskazini, yote unahitaji kujua ni lini vita kama hii ilianza, na ni nani katika wakati wa mwisho aliwaachia Wamisri na Palestina kwa dola ya adui, ni dola ipi kama tokeo iliporomoka katika wakati wa mwisho, na ni dola gani imepanuka. Lipo jibu moja tu, na hilo ni: Wakati Ufalme wa Ottoman umekuwa ukididimia tangu 1669 B.K., Ufalme wa Uingereza umekuwa ukipanuka, na leo unatawala Misri na Palestina. Hivyo, leo Uturuki ni mfalme wa kusini, na Uingereza Kuu, mfalme wa kaskazini; na kulingana na vita hii ya kinabii, wakati wa mwi-sho ulianza mwanzoni mwa karne ya kumi na nane. {2TG7: 5.2}
5
Hapa ipo ramani inayoonyesha kuinuka na kuporomoka kwa ufalme wa Ottoman (Uturuki). Iangalie, uicham-bue. Na kwenye ukurasa unaoelekeana ni kupanuka kwa ufalme wa Uingereza katika kipindi sawa cha wakati. {2TG7: 6.1}
6
(Kwa mujibu wa Muujiza wa Uingereza, na Andrew Maurois, Harper & Brothers Publishers.)
7
Huu, unaona, ni ukweli yakini, sio kubahatisha, sio nadharia, sio wazo la kuwaziwa. {2TG7: 8.1}
Ijayo kumbuka kwamba Edomu na Moabu wataokoka kutoka mkononi mwake. Naam, mfalme wa kaskazini atawapoteza. {2TG7: 8.2}
Kama vile vita vya pili vya ulimwengu, hata hivyo, vilileta maporomoko ya kwanza kwa Uingereza Kuu, na jinsi tunavyoiona hapa katika unabii, sehemu yake katika Vita vya 2 vya Dunia lazima pia ipatikane katika Dan-iel 11. Hebu sasa basi tuzichambue aya zilizosalia za sura hiyo. {2TG7: 8.3}
Aya ya 44 — “Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuangamiza, na kuwaondolea mbali watu wengi.”
Katika wakati wa mwisho, baada ya kufurika katika nchi zilizotajwa hapo awali, mfalme wa kaskazini anaon-ekana tena kwenye vita, lakini sio na mfalme wa kusini. Anavutwa ndani ya pambano hili la mwisho kwa yale yanayoripotiwa kwake kutoka mashariki na kaskazini. Sasa kwamba Vita vya 2 vya Dunia viliota kutoka kwa pande zilizotajwa na Uvuvio, — Ujerumani upande wa kaskazini, na Japani upande wa mashariki, mbali na Urusi katika kaskazini ya pembeni, — kweli mpya kabisa katika mawazo yetu zimefumbuliwa ili kuondoa mashaka yote ila kwamba Vita vya 2 vya Dunia ndivyo ambavyo vimezungumziwa hapa katika unabii. Na tusisahau kwamba Vita vya 2 vya Dunia havijakoma kabisa, kwamba bado havijaisha. Nasema, mbele ya uso wa kweli hizi zinazojulikana kote ulimwenguni, ni vigumu kwa mmoja kukataa yale yaliyoletwa hapa kwa nuru. {2TG7: 8.4}
Dan. 11:45 — “Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa utukufu; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna
8
atakayemsaidia.”
Sasa kwamba muundo wa uchumi wa Uingereza uko katika hatari kubwa ya kuporomoka, na ufalme wake unabomoka haraka, tunahofia kwamba utimilifu wa aya ya 45 labda u karibu zaidi kuliko mtu anavyoweza kung’amua. Iwapo tu wale ambao huongoza ufalme, na pia wakuu wa taifa letu wangalijua na kuelewa unabii, tunaamini Uingereza Kuu ingaliweza kuibuka kwa ushindi kama ulivyofanya Ninawi wa zamani baada ya sim-ulizi kubwa la Yona. {2TG7: 9.1}
Sote tunajua kwamba Uingereza Kuu imesaidiwa na Marekani zaidi ya mara moja. Lakini tukielewa vyema aya hii, matukio ambayo ni endelezo la yale yanayopatikana katika aya ya 44, mfalme hakika ataifikilia ajali yake na hakuna atakayemsaidia. Hili linaweza kutukia kabla ya Vita vya 2 vya Dunia kukoma kabisa, na bado yawezekana visikome. Tunakusanya hili kutoka kwa ukweli kwamba tukio la aya ya 44 linahusiana na tukio la aya ya 45. Uvuvio unaonekana hauruhusu muda kati ya aya ya 44 na 45. Hatujui zamu ambazo vita vitaweza kuchukua, lakini tunajua kwamba unabii wa Bibilia kamwe haushindwi. {2TG7: 9.2}
Kuhusu kuweka hema zake kwenye mlima mtakatifu wa utukufu, haijakuwa wazi kabisa, maana kuweka he-ma za ikulu yake kabla hajaifikilia ajali yake sio lazima kumaanishe kuhamishia kiti chake cha enzi hapo. Kuna-weza kuchukuliwa kumaanisha kuwa na tawi la ikulu yake hapo. Ikiwa ataweka hema zake hapo wakati Mikaeli anasimama, hata hivyo, basi eneo pekee mbali na Nchi Takatifu ambayo tunajua, ni penye Mlima Sinai, kati ya Mediterrania na Bahari ya Shamu. {2TG7: 9.3}
9
Kutoka kwa uchambuzi wa sura ya kumi na moja ya Danieli, tumejifunza kweli kadhaa yakini: 1. Kwamba wakati wa mwisho ulianza katika karne ya kumi na nane; 2. Kwamba mfalme wa kusini ni himaya ya Ottoman; 3. Kwamba mfalme wa kaskazini kwa wakati huu ni Uingereza Kuu haswa; 4. Kwamba Vita vya 2 vya Dunia ni vita katika Danieli kumi na moja. {2TG7: 10.1}
Sasa kwa sababu unabii wa sura ya kumi na moja ya Danieli huendelea hadi kwa ya kumi na mbili, tutafungua aya ya kwanza. {2TG7: 10.2}
Dan. 12: 1 — “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”
Wakati huo (yaani, kwa wakati ambapo mfalme wa kaskazini anaifikilia ajali yake na hakuna mtu wa kumsaidia) Mikaeli atasimama; na kwa wakati uo huo itakuwapo taabu mfano wake haujakuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo. Watu wa Mungu pekee, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu kile, watakaokolewa. Sio wengine. {2TG7: 10.3}
Uchambuzi huu umetuongoza hatua kwa hatua hadi kwa siku yetu. Kupitia uchambuzi huu tunaona kwamba wakati wa taabu ni hatua tu katika siku zijazo, kwamba tukio la pekee ambalo bado linapaswa kutimizwa kabla taabu kuanza ni mfalme wa kaskazini kuufikilia mwisho wake. Kisha inafuata thawabu ya waaminifu. {2TG7: 10.4}
Ni wakati wa uchaji kama nini ambao tumefikia, Ndugu, Dada. Je! Unatambua kwamba iwapo sasa
10
hautafanya bidii kuliweka jina lako kwenye kitabu kile, inawezekana kuwa umechelewa sana milele? Na je! sio bora kuwa na jina lako huko hata kama taabu ingalikuwa miaka mia kadhaa katika siku zijazo? Sasa ndio wakati wa kuchukua hatua. Sasa ni siku ya wokovu imeletwa kwako. Leo Uvuvio unasihi; mnapoisikia sauti Yake msi-ifanye mioyo yenu kuwa migumu. Wale tu ambao hutii Neno la Mungu lililofunuliwa watapata ukombozi na amani, — hakuna weingine watakaoipata. {2TG7: 10.5}
Aya ya 2 — “Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine aibu na kudharauliwa milele.”
Hapa tunaambiwa kwamba katika wakati wa taabu hawa wataamka, baadhi waishi milele na baadhi wafe tena. {2TG7: 11.1}
Je! Unajua sasa kwamba sio wakati wa taabu tu u mlangoni, bali hata ufufuo huu maalum? Je! Unaona kweli kuwa katika wakati wa taabu, ambapo watakatifu walio hai wanapokuwa wanaokolewa hawa wafu ambao wa-tafufuka “kwa uzima wa milele,” pia wameokolewa kutoka kwa makaburi yao? Je! Unatambua kwamba wakati huu wa taabu u katika “siku kuu na ya kutisha ya Bwana,” siku ambayo nabii Eliya huitangaza? Je! Unajua kweli ya kuwa ataigeuza mioyo ya baba na watoto kuelekeana? Ili Bwana asije akaipiga “dunia kwa laana.” Mal. 4: 5, 6. Je! Unaona kwamba nabii anaonekana katika siku ambayo anaweza kuyarejesha mambo yote, kila kitu kili-chopotea kupitia dhambi, hata Ufalme? Je! Unajua kwamba ufufuo wa Danieli 12 sio sawa na ufufuo wa 1 Wathesalonike na wa Ufunuo 20: 5? {2TG7: 11.2}
1 Thes. 4:16 — “Kwa sababu Bwana mwenyewe
11
atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: na wafu katika Kristo watafufuliwa kwanza.”
Ufu. 20: 4-6 — “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika.”
Mtume Paulo bila shaka hunena kuhusu ufufuo uleule kama Mtume Yohana kwa sababu ndani yake watakati-fu pekee ndio wanaofufuliwa. Maelezo ya Paulo na ya Yohana yanaonyesha wazi kwamba hawa wanaamka mwanzoni mwa miaka elfu. Hili tunaona kutoka kwa kweli kwamba waliishi na Kristo miaka elfu moja, na kwamba walinyakuliwa kumlaki Bwana angani, kwamba walikuwa safarini kuishi na Kristo wakati wa miaka elfu moja, sio Kristo kuishi pamoja nao. {2TG7: 12.1}
Sasa panga ufufuo wote, lazima tuuzingatie ule wa Ezekieli. {2TG7: 12.2}
Ezek. 37: 1, 11-14 — “Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwa-na, ukaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa …. Kisha Akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote
12
ya Israeli: tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea: Tumekatiliwa mbali kabisa. Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya ku-wa mimi, BWANA, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.”
Katika ufufuo huu ni watu wake Mungu tu, Israeli, wanaamka bila mdhambi kati yao. Hata hivyo, hawa ha-wakutani na Bwana angani; wanapelekwa katika nchi ya Israeli, Palestina. Ufufuo huu, kwa hivyo, sio sawa na ufufuo wa 1 Wathesalonike, wa Ufunuo, au wa Danieli 12. Lazima uwe tofauti. {2TG7: 13.1}
Hebu sasa turejelee– {2TG7: 13.2}
Dan. 12: 1-3 — “Na wakati huo Mikaeli atasimama, jemedari mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo: na wakati huo watu wako wataokolewa; kila kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa an-ga; nao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.”
13
Katika aya hizi tatu mambo kadhaa yanajitokeza wazi: (1) Wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu wanaokolewa; hawapo kwa hivyo wale “wapumbavu” kati yao; (2) Wale ambao wamefufuliwa, hata hivyo, wamechangamana, wapumbavu na walio na hekima wanafufuka; (3) Taarifa , “na walio na hekima [ikimaanisha kwamba baadhi ni wapumbavu] watang’aa kama mwangaza wa anga” inaashiria kwamba hawa “walio na hekima” ni kutoka miongoni mwa waliofufuliwa; (4) Kwamba ikiwa walio na hekima ni kutoka mion-goni mwa waliofufuliwa na kuwaongoza wengi kutenda haki, basi lazima wafufuliwe katika wakati wa rehema, katika wakati wa wokovu. {2TG7: 14.1}
“Kazi yako, kazi yangu, haitakoma pamoja na maisha haya. Kwa muda mchache tunaweza kupumzika ka-burini, lakini, wakati mwito utakapokuja, katika ufalme wa Mungu, tutachukua kazi yetu tena.”– Shuhuda, Gombo la 7, uk. 17. {2TG7: 14.2}
Aya ya 4, 10 — “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho. Wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Wengi watajitakasa, na kujifan-ya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa. “
Sasa inamaanisha nini kuwa na hekima? — Hebu tufungue– {2TG7: 14.3}
Mat. 25: 1-4 — “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.”
14
Hapa tunaona kwamba wenye busara ni wale ambao huchukua mafuta ya ziada, Ukweli wa ziada ambao huiangaza njia yao yote. Mwishowe, inaonekana wazi kuwa ufufuo huu mseto ni mtihani; yaani, wote wanapewa fursa ya kuwa walio na hekima, kuwaongoza wengi kutenda haki, lakini sehemu yao tu wanafanya hivyo. Baadhi yao wanaanguka tena dhambini, na kwa hivyo wanafufuka kwa aibu na kudharauliwa milele (kutotii milele), lakini wenye busara wanafufuka kwa uzima wa milele, kamwe wasife tena. Hili linaonyesha wa-zi kwamba wale ambao wanajitolea kwa uovu hadi wakati wanapokufa, hawataweza kuwa walio na haki hata kama watapewa nafasi ya pili. Mafuta ya ziada (Ukweli kwa ajili ya wakati huu) ndio huamua hatma ya kila mmoja. Wenye busara wataukumbatia “Ukweli wa ziada,” ilhali hawataweza. Kwa kweli dhambi ni fumbo! {2TG7: 15.1}
15
UHUISHO NA MATENGENEZO YANATANGULIA SIKU KUU NA YA KUOGOFYA YA BWANA
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, SEPTEMBA 27, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Mada yetu alasiri hii inapatikana kwa sehemu katika Danieli 2, Mathayo 4, Yeremia 51, Mika 5, na Malaki 4, lakini haswa katika Yoeli sura ya 2 na ya 3. Kwanza tufungue Malaki: {2TG8: 16.1}
Mal. 4: 5, 6 — “Angalieni, nitawpelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, nisije nikaipiga dunia kwa laana.”
Hapa tunayo ahadi kwamba Mungu atatuma mtu fulani kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana, na ataka-pokuja, ikiwa hatatimiza kitu kingine chochote, ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya wa-toto iwaelekee baba zao. {2TG8: 16.2}
Sasa, inaonekana kushangaza kidogo kwamba mioyo ama ya akina baba au ya watoto inahitaji kugeuzwa kuelekeana. Lakini iwapo tutazingatia kwamba kazi ya Eliya sio ya asili ya kinyumba, bali ya kiroho, basi tutaona kwamba ujumbe wa Eliya utatiliwa mkazo ndani ya mioyo ya wazazi, na vile vile katika mioyo ya wato-to, mzigo kwa ajili ya wokovu wa
16
mwingine. Wazazi wanahangaika kufanya kazi kwa watoto wa watu wengine lakini mara chache kwa watoto wao. Vivyo hivyo watoto wanayo hamu ya kuwahubiria wazazi wengine, lakini hawahangaiki sana kuwahubiria wazazi wao. Ujumbe wa Eliya wa uamsho na matengenezo, hata hivyo, utaweka mzigo wa kuokoa nafsi kimsingi mahali unapofaa. Ujumbe wake utaonekana kuwa wa umuhimu sana badala ya nadharia. Na wafuasi wake watakapotambua kabisa kwamba siku kuu na ya kuogofya ya Bwana i mlangoni, wataonekana wakisihi kwanza kwa ajili ya wale walio karibu sana na mioyo yao. {2TG8: 16.3}
Hebu sasa twende kwa unabii wa Danieli: {2TG8: 17.1}
Dan. 2:44 — “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hau-taangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”
Inaeleweka kwa wanafunzi wengi wa Bibilia kwamba sanamu hii kubwa ya Danieli 2 inawakilisha falme kutoka wakati wa Danieli hadi mwisho. Hapa, unaona, jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono linaipiga sanamu kwa miguu, nalo linaijaza dunia yote. “Katika siku za wafalme hawa,” wakati wetu, unatangaza Uvuvio, Mungu atausimamisha ufalme ambao unawakilishwa na jiwe, na utayapiga mataifa na hapo kuuleta mwisho wao. Je! siku hiyo inaweza kuwa nini ila kuu kwa watu wa Mungu, na ya kuogofya kwa mataifa? Hakika, itakuwa ni siku kuu na ya kuogofya ya Bwana. {2TG8: 17.2}
Aya ya 45 — “Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na
17
ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thab-iti.”
Simulizi la Daniel kuihusu siku hiyo ni fupi sana, lakini Yeremia anaelezea siku hiyo kwa kina: {2TG8: 18.1}
Yer. 51: 21-23 — “Na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwa-namke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwana-mume na kijana mwanamke; na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”
Hapa Uvuvio huelezea kwamba Mungu pamoja na Ufalme Wake atayavunja mataifa, kwamba watu Wake watakuwa shoka Lake la vita. Wote Danieli na Yeremia wako dhahiri kwamba Ufalme huo utaleta mwisho wa falme za dunia. {2TG8: 18.2}
Mika 5: 7 — “Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.”
Mabaki ya Yakobo (wale ambao wamesazwa baada ya magugu kuondolewa), wakati wanasimamishwa kama ufalme, watakuwa kama manyunyu ya baraka kwa wale wanaotafuta wokovu, na kama simba anayerarua vipande-vipande wale wanaoendelea katika dhambi yao. Siku itakuwa kuu kwa kundi moja la watu,
18
na ya kutisha kwa lingine. {2TG8: 18.3}
Sasa twende kwa sura za unabii wa Yoeli ambazo zinatimizwa katika siku za mwisho. {2TG8: 19.1}
Yoeli 2: 1-3 — “Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia; siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi. Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao.”
Hapa unaona kwamba ujumbe unapaswa kutangazwa kwa kanisa, kwa Zayuni, kutangaza kwamba siku kuu na ya kuogofya ya Bwana imekaribia; kwamba itakuwa ya kuteketeza nyuma ya watu Wake, na ya utukufu mbele yao, — kwamba Bwana atauchuja uwanda kabisa, kwamba Ataikusanya kila punje ya “ngano” na kisha kuyachoma magugu. {2TG8: 19.2}
Aya ya 4-6 — “Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopi-ga mbio. Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. Mbele yao watu wana-hangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.”
19
Tunaona kwamba nguvu ambayo iliambatana na Israeli wa zamani wakati walipokuwa wakiichukua Nchi ya Ahadi, pia itaambatana na watumwa wa Mungu wakati huu wa kukusanywa. {2TG8: 20.1}
Aya ya 7, 8 — “Watapiga mbio kama mashujaa; watapanda ukuta kama watu wa vita; nao watatembea kila mtu kwa njia yake, na hawatavunja safu zao: wala mtu hapana mmoja amsukumaye mwenzake; wa-taendelea mbele kila mmoja katika njia yake; na watakapouangukia upanga, hawatajeruhiwa.”
Hakuna kitu kitakachoweza kuwazuia watu wa Mungu. Kila mmoja atahudhuria shughuli yake kikamilifu. Watayakusanya mazao ya nchi na hakuna kitakachowadhuru. Roho ya Unabii inashuhudia: “Watakatifu wali-poondoka mijini na vijijini, waliandamwa na waovu, ambao walitaka kuwachinja. Lakini panga zilizoinuliwa kuwaua watu wa Mungu zilianguka kwa udhaifu kama manyasi” — Maandishi ya Awali, uk. 284-285. {2TG8: 20.2}
Aya ya 9 — “Watakimbia huko na huko mjini; watapiga mbio juu ya ukuta, watapanda juu ya nyumba; wataingia ndani kupitia madirishani kama aingiavyo mwivi.”
“Watumwa wa Mungu” hakika watawakusanya ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote (Isa. 66:20). Kwa kweli hivyo, kwa maana miguu ya Injili ni miguu ya watu wanaoitangaza. Bila shaka, ni kwa uratibu kamili na jeshi lenye kinga ya risasi ambapo kazi ya injili inaweza kukamilishwa wakati yule mnyama mwenye pembe mbili atatangaza kwamba “hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” Ufu. 13:15. {2TG8: 20.3}
20
Aya ya 10, 11 — “Nchi itatetemeka mbele yao; mbingu zitatetemeka: jua na mwezi utatiwa giza, na nyota zitaacha kuangaza. Naye Bwana atatoa sauti Yake mbele ya jeshi Lake; kwa maana kambi yake ni kubwa sana: maana ni mkuu atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu na yenye kitisho sana; Naye ni nani awezaye kuistahimili? “
Baada ya kutangaza jinsi siku itakuwa kuu na ya kuogofya, Bwana anatoa ombi hili: {2TG8: 21.1}
Aya ya 12-14 — “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa re-hema, naye hughairi mabaya. Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake; naam, sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu?”
Rai ya Mungu ni kwamba tujiandae kukutana na hiyo siku; kwamba sasa kama Wakristo waaminifu ambao hutambua kuwa kwa saa kama hii ujumbe huu wa rehema umekuja kwetu, kwa kutubu tumwelekee Yeye. {2TG8: 21.2}
Aya ya 15, 16 — “Pigeni tarumbeta katika Zayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu: Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao maziwa: Bwana ha-rusi na atoke chumbani mwake, na bibi harusi katika hema yake.”
Katika aya hizi, kama ilivyo katika Yoeli 2:1, amri imetolewa kupiga tarumbeta katika Zayuni. Hii
21
baragumu ya pili, hata hivyo, sio ya kutangaza siku ya Mungu, bali ni ya kuitakasa saumu na kuwatakasa watu, kuliita kusanyiko takatifu, ambalo hakuna mtu atakayetengwa kutoka kwalo. {2TG8: 21.3}
Aya ya 17 — “Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, waombolee kati ya patakatifu na madhabahu, na waseme, uwaachilie watu wako, Ee Bwana, wala usiutoe urithi wako upate aibu, hata mataifa watawale juu yao: Kwani waseme kati ya watu, yuko wapi Mungu wao?”
Hapa tunaambiwa kwa udhahiri kwamba watu wa Mungu watakabiliwa na mateso na dhiki, na kwamba wasipokuwa karibu na Bwana uwepo wao unaweza kuwa hatarini, jina la Mungu kuvunjiwa heshima, na mataifa kuruhusiwa kuwatawala na kuipinga imani yao kwa Mungu. {2TG8: 22.1}
Aya ya 18, 19 — “Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. Bwana akajibu na kuwaambia watu wake, Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya kuwa aibu tena kati ya mataifa.”
Mungu anapata kimbilio na uhuru kwa ajili yao katika nchi yao ambapo hakuna kitu kitakachokosekana. {2TG8: 22.2}
Aya ya 21-23 — “Usiogope, Ee nchi; furahi na kushangilia; kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu. Msiogope, enyi wanyama wa kondeni, maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. Furahini basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye huwapa ninyi mvua ya vuli, kwa kipimo cha haki, naye huwanye-shea mvua, mvua ya vuli, na mvua ya masika kama kwanza.”
22
Ni wazi kabisa kuona kwamba Mungu ananena kwa watu Wake ambao watapokea zote mvua ya masika na ya vuli katika mwezi wa kwanza. {2TG8: 23.1}
Aya ya 24 — “Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta.”
Uvuvio, bila shaka, hauneni kuhusu mambo ya kiroho tu, bali pia kuhusu mambo ya raslimali. Mvua (Ukweli mpya uliofunuliwa) itazalisha kwa hivyo mavuno mengi ya roho na wingi wa vyakula. {2TG8: 23.2}
Aya ya 25-32 — “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itisha-yo. Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika
23
Mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.”
Hapa tunaona kwamba wale wanaoliitia jina la Bwana baada ya mvua ya masika kunyesha, watapata uokozi juu ya Mlima Zayuni na katika Yerusalemu, pia katika mabaki ambao Bwana atawaita. {2TG8: 24.1}
Neno la kwanza hasa (“kwa”) la sura inayofuata linaonyesha kwamba unabii wa sura ya pili unaendelea kupitia sura ya tatu yote. {2TG8: 24.2}
Yoeli 3: 1, 2 — “Kwa maana angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nita-wahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.”
Aya hizi huelezea ni kwa nini, ni vipi, na ni lini watu wa Mungu wanaokolewa katika Mlima Zayuni na katika Yerusalemu. Mambo haya, unaona, yatatukia wakati Atakapowarudisha tena mateka wa Yuda na Yerusalemu. Wakati huo atayaleta mataifa yote katika bonde la Yehoshafati na hapo atateta kwa ajili ya watu Wake wote waliotekwa ambao mataifa wametawanya kote duniani. {2TG8: 24.3}
Aya ya 3 — “Nao wamewapigia kura watu wangu; Na mtoto mwanamme wamemtoa ili kupata kahaba, na mtoto mwanamke wamemuuza ili kupata divai, wapate kunywa.”
Aya ya 3 hufichua mazoea ya machukizo ya dunia. {2TG8: 24.4}
Yoeli 3: 4-7 — “Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu,
24
enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lo lote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. Kwa kuwa mmetwaa fedha yangu na dhahabu yangu, nanyi mmevichukua vitu vyangu vyema vipendezavyo, na kuviingiza katika hekalu zenu; tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao.”
Tiro na Zidoni, na pwani ya Palestina, basi, hayo mataifa ambayo yamewatapanya watu wa Mungu, watapata thawabu yao. Malipo yao yatakuwa nini? Hapa lipo jibu: {2TG8: 25.1}
Aya ya 8-10 — “Nami nitawauza wana wenu na binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa Sheba, taifa lililo mbali kabisa; kwa maana Bwana ndiye aliyesema neno hili. Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Ya-fueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.”
Kwa kadri mataifa yatakuwa yanajiandaa kwa vita wakati ambapo unabii huu utakuwa unatimizwa, ni wazi kuona kwamba silaha za atomu hazitaleta amani. {2TG8: 25.2}
Aya ya 11 — “Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelem-she mashujaa wako wote, Ee Bwana.”
Hapa tunaambiwa kwamba mashujaa wa Mungu
25
watakukutana na majeshi ya mataifa. Na Mungu atawahukumu watu wapi? — Aya zinazofuata zinatoa jibu: {2TG8: 25.3}
Aya ya 12-14 — “Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sa-na. Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno.”
Naam, hapa imeelezwa siku ya uamuzi. Umati utalazimika wakati huo kuamua ama kumtumikia Mungu na kuishi au kuendelea kumtumikia Ibilisi na kuangamia pamoja naye. {2TG8: 26.1}
Aya ya 15, 16 — “Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Naye Bwana atanguruma toka Zayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.”
Je! Ni siku kama nini ambayo dunia inaijongea sasa, na ni upofu kama nini kwa ukweli huu ulivyo hata kwa kanisa lenyewe! {2TG8: 26.2}
Aya ya 17-21 — “Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Zayuni, mli-ma wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe. Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea
26
katika nyumba ya Bwana, na kulinywesha bonde la Shitimu. Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao. Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye Zayuni.”
Utakaso wetu wa mwisho utakuwa katika nchi yetu wenyewe. Maandiko, unaona, yanahusiana; ukweli mmo-ja unaelezea mwingine. Aya na sura, kwa hivyo, haziwezi kutengwa kwa muktadha wake iwapo zitaweza kueleweka vyema. Wazo sahihi haliwezi kujengwa juu ya aya yoyote wakati imetengwa na mwendelezo wake. Na ni wakati tu tunapomchukua Mungu kwa neno Lake tunaweza kuyachambua Maandiko katika kweli. Basi tunahitaji tu neno la msingi kuzifunua siri za Mungu. Na hapa tunalo. {2TG8: 27.1}
Uamsho na matengenezo, badiliko la maoni na mazoea, kwa hivyo, ndilo hitaji letu kubwa. Bila hili tuna uhakika wa kupatikana kati ya wale ambao watasema “milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele ya uso wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, yahasira yao imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu 6: 16, 17. {2TG8: 27.2}
27
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 7, 8
Kimechapishwa nchini Marekani
28