fbpx

Mtoa Jibu Kitabu Namba 4

Mtoa Jibu Kitabu Namba 4

1

Hakimiliki 1944, na

V.T. Houteff

Haki Zote Zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kama utumishi wa Ukristo, kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga. {ABN4: 2.1}

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitathaminiwa. {ABN4: 2.2}

2

MTOA JIBU

Kitabu Namba 4

Maswali na Majibu kwa Mada za Ukweli wa Sasa

Katika Masilahi ya Ndugu Waadventista wa Sabato

na Wasomaji

wa

Fimbo ya Mchungaji

Na V.T. Houteff

Huyu “mwandishi,” mwenye elimu

ya ufalme wa

mbinguni, “hutoa

… vitu vipya na vya zamani.”

Mat. 13:52.

Sasa “mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”

1 Pet. 3:15.

3

 

YALIYOMO

 

Je! Ni Unabii Wa Yosia Au Wa Yohana Ulitimizwa? ………………………..5

Je! Dhiki Kuu Na Wakati Wa Taabu Ni Sawa? ………………………………6

Ni Lini Walijiita Kwa Jina La Bwana? …………………………………………7

Je! Matengenezo Sio Ukamilifu?………………………………………………10

Kutakaswa Mara Moja, Au Siku Kwa Siku? ……………………….…………12

Kutapikwa Nje, Au Kutupwa Nje? …………………………………………….18

Ni Nini “Fimbo ya Mwanangu?” ……………………………………………….19

Je! Upanga Wa Bwana Ni Nini? ………………………………………………19

Je! “Zayuni” Na “Yerusalemu” Ni Sawa? …………………………………….20

Je! Yeye Amewakanyagia Au Atawakanyagia Chini? ………………………22

Kubatizwa Kwa Ondoleo La Dhambi, Au Kwa Kukaza Mwendo

Na Ukweli? ………………………………………………………………………..23

Ni Nani Mfalme Wa Kituo Cha Mlima Karmeli — Mungu Au Mtu? …………24

Je! Muda Umekwisha Sana Kuingia Katika Juya? ………………………….28

Lipi La Kufanya Unapotengwa Kwa Ushirika? ……………………………….30

Ipo Tofauti Gani Kati ya “Amekuja” Na “Kushuka”?…………………….……33

Iwapo Nusu Na Nusu Wakati Huo, Vipi Sasa ………………………………..34

Je! Ushirika Huchukuwa Nafasi Ya Maarifa Ya Ukweli? ……………………35

Sasa Naamini, Lakini Je! Nina Haki Ya Ushirika? …………………………..36

Vipi Kumhusu Petro Na Funguo? ……………………………………….…….37

Zaka Yangu Inapaswa Kwenda Kwa Nani? …………………………….……41

Je! Nyumba Yangu Haiwezi Kuwa “Ghala” Lake? ……………………….…44

Je! Ni Wajibu Wangu Kurekebisha Hazina Ya Bwana? …………..………..46

Je! Ni Nini Kinachostahili Kuwa Zaka? …………………………………….…47

Vipi Kuhusu Kutoza Zawadi Zaka? ……..…………………………………….48

Je! Ni “Bima” Gani Wakristo Wanapaswa Kuwa Nayo? ………….…….….49

Ni Nani Wanaostahili Sadaka? …………………………………….………….58

Je! Zaka Ya pili Hutumika Kwa Nini? …………………………………………59

Ni Nini Hufanza Umoja? …………………………………………………….….66

Je! Nyumba Inapaswa Kuwa Vipi? ……………………………………………69

Iwapo Wawili Hawapatani Wanawezaje Kutembea Pamoja? ………….….78

Jinsi Ya Kuzuia Kuwalea Wasiofaa? ……………………………………….…81

Hatua Yako Itakayofuata Itakuwa Nini? ………………………………….…..94

4

MASWALI NA MAJIBU

JE! UNABII WA YOSIA AU WA YOHANA ULITIMIZWA?

Swali Namba 77:

Kwa sababu utabiri wake wa anguko la Ufalme wa Uturuki mnamo Agosti 11, 1840, ulitimizwa kwa ajabu, je! Yosia Litch alikuwa sahihi kwa kudai kwamba unabii wa Ufunuo 9:5, 15-20, ulitekelezwa hivyo kikamilifu? {ABN4: 5.1}

Jibu:

Ingawa katika kutukia kwa utabiri wa Litch, kulikuwa na jambo lililoonekana kuwa kitu cha asili kwa tukio la nasibu, tukio linalohojiwa haliwezi kuwa liloelezewa katika unabii wa Yohana, kwani ule wa mwisho hufichua kwamba malaika wanne waliofungwa kwenye Mto Frati wangeua theluthi moja ya watu. Na ni wapi katika Maandiko nchi yoyote ya Mataifa imefananishwa na malaika? Isitoshe, Ufalme wa Uturuki haukuanguka hata kidogo; badala yake, ulijiweka wenyewe “chini ya usimamizi wa mataifa ya Kikristo.” — Pambano Kuu, uk. 335. Zaidi ya hayo, malaika walikuwa na jeshi la wapanda farasi 200,000,000, ilhali Uturuki haukuwahi kuwa na wapanda farasi wengi kama hao katika maisha yake yote! Bado zaidi, unabii wa Ufunuo hudai kuua “theluthi ya wanadamu” (Ufu. 9:15), ilhali katika kutimizwa utabiri wa Litch, hakuna mauaji yaliyofanyika. Kwa mtazamo wa kauli hizi zote, ni uthibitisho wenyewe kwamba ingawa utabiri wa Litch unaweza kuwa

5

umetimia, kwa kweli haukuwa unamaanisha ule wa Waufunuo. {ABN4: 5.2}

Pambano Kuu hunakili tu kwamba utabiri wa Litch mwenyewe, si wa Yohana ulitimizwa. Hivyo, utabiri wa Litch, ukiwa kimakosa umewekwa kwa msingi wa Ufunuo, ulikuwa tukio la nasibu la asili, sio utimizo wa unabii wa Waufunuo. {ABN4: 6.1}

JE! DHIKI KUU NA WAKATI WA TAABU NI SAWA?

Swali Namba 78:

Mtu anawezaje kuthibitisha kwamba “dhiki kuu, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu.…wala haitakuwapo kamwe” (Mat. 24:21), sio “wakati wa taabu mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa”? Dan. 12:1. {ABN4: 6.2}

Jibu:

Kutabiri kuhusu “dhiki kuu,” Kristo alionya kimbele kwamba ungekuwa wakati wa mateso, uhitaji, na kifo kwa watakatifu, na ya kwamba kwa hivyo iliwapasa kukimbilia “milimani” kuokoa maisha yao, isije ikawa “asingeokoka mtu yeyote.” Mat. 24:16, 22. {ABN4: 6.3}

Lakini Danieli hutabiri kwamba katika “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo,” Mikaeli atasimama na kumwokoa kila mmoja wa watakatifu, ili wanusurike kifo. {ABN4: 6.4}

Bila shaka, kwa hivyo, matukio haya mawili yatatukia kwa nyakati tofauti, kila moja lilkiwa maalum

6

na la kipekee, kuu la aina yake. Kwa kweli, unabii hutangaza kwamba haitawahi kuwapo “dhiki” nyingine kama hiyo, na kamwe haitakuwapo “taabu” nyingine kama hiyo. {ABN4: 6.5}

(Tazama Mtoa Jibu, Kitabu Namba 2, Swali Namba 47, kwa maelezo ya kina kuhusumatukio haya mawili.)

NI LINI WALIJIITA KWA JINA LA BWANA?

Swali Namba 79:

Je! Abeli hakuliitia jina la Bwana wakati alitoa dhabihu (Mwa. 4:4)? Iwapo ni hivyo, basi ni kwa nini kitabu cha Mwanzo 4:26 (pambizo) husema kwamba baada ya Sethi kuzaliwa, “ndipo watu walianza kuliitia jina la Bwana”? {ABN4: 7.1}

Jibu:

Ingawa tangu kifo cha Abeli hadi kuzaliwa kwa Sethi (Mwa. 4:25), Kaini alikuwa mwana pekee wa Adamu aliyekuwa anaishi, hata hivyo yeye wala watoto wake hawakuwa wafuasi wa Mungu; kwa hivyo walikuwa “wana wa wanadamu.” Lakini Sethi na wazawa wake, ambao walikuwa na roho ya Abeli, waliliitia jina la Bwana, na walikuwa “wana wa Mungu.” Mwa. 6:2. {ABN4: 7.2}

Hivyo, kwa sababu yalikuwapo makundi mawili tofauti ya waabudu (wa kweli na wa uongo) kwa ukaribu na lingine, ilikuja kuwa lazima wajipatie majina ili kutofautisha kati ya wafuasi wa mwanadamu na wafuasi wa Mungu. Wazawa wa Sethi walikuwa wa kwanza

7

kujiita “kwa jina la Bwana,” kama vile Wayahudi ambao muda mrefu baadaye walimpokea Kristo walikuwa wa kwanza kujiita Wakristo. Na kama vile Wayahudi waliomkataa Kristo waliendelea kujiita Wayahudi, vivyo hivyo wazawa wa Kaini waliendelea kujiita “wana wa wanadamu.” {ABN4: 7.3}

Kutoka kwa andiko hili unakuja ushahidi kwamba mazoea ya kidini ya kutojali na ya ujinga ambayo tunaona leo, na roho yake ya utesi dhidi ya wale wanaomwabudu Mungu kikamilifu jinsi ambavyo Ameamuru, yalianzia kwa Kaini; pia ya kwamba kutoka kwa Abeli huchipuka shina la mvuto wa utiifu, unaofika hata siku ya leo. Kwa hivyo bado wapo ulimwenguni “wana wa wanadamu” na vile vile “wana wa Mungu,” wafuasi wa wanadamu na wafuasi wa Mungu. Na jinsi dini ya “wana wa wanadamu” katika siku hizo ilikuwa kama ile baba yao Kaini alifuata, — sio kulingana na amri ya Mungu, bali kulingana na chaguo lao wenyewe, — ndivyo ilivyo pia dini ya wana wa wanadamu leo. Wengi sana bado huabudu kwa njia ile ile ambayo baba zao waliabudu, bila kuchukua machungu kidogo kujijulia wenyewe tofauti kati ya ile ya uongo na ile ya kweli, lakini kwa kawaida na bila kufikiri wakikimbia kasi kwa maangamizo yao, kama nguruwe wa Wagerazi alikimbia kasi juu ya miamba hadi ndani ya bahari (Mat. 8:32; Marko 5:13). {ABN4: 8.1}

Lakini licha ya jina takatifu ambalo wana wa Sethi walijitwalia katika siku hizo, wengi wao walichangamana na

8

wana wa wanadamu; yaani, “wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” Mwa. 6:2. Mazoea haya maovu kwa haraka yakaubeba uovu wa wana wa wanadamu hadi katika nyumba za wana wa Mungu. “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemuumba mwanadamu duniani, Akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu Niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana Naghairi ya kwamba Nimemuumba.” “Na tazama, Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, Niharibu kila kitu chenye mwili, ambacho ndani yake kuna pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; na kila kilicho ndani ya nchi kitakufa.” Mwa. 6:5-7, 17. {ABN4: 8.2}

Akitazama mbele kwa siku yetu wenyewe, Yesu alitangaza: “Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja Kwake Mwana wa Adamu.” Mat 24:38, 39. Je! Hawapaswi, kwa hivyo, “wana wa Mungu” katika siku hizi watii sana mifano hii na kujitenga mbali na “mabinti za wanadamu”? {ABN4: 9.1}

9

Masomo haya hufundisha kwamba kila mtu mwenyewe, bila ushawishi wa mwingine anapaswa kuamua kujua na kuutekeleza Ukweli iwapo yuataka kuziepuka tando za Adui zisizoonekana alizotandaza kwenye njia ya miguu yake. Sasa anapaswa kujua ubaya zaidi wa kesi yake ikiwa anataka kuihifadhi taji yake ya uzima wa milele, hazina yake ya thamani kubwa. Iwapo hawezi hivyo, ataipoteza. {ABN4: 10.1}

JE! MATENGENEZO SIO UKAMILIFU?

Swali Namba 80:

Ile taarifa katika “Msimbo wa Nembo,” Julai 1935, Gombo la 1, Namba 13, uk. 9, kwamba “ikiwa mtu hawezi kufanya matengenezo wakati ule ule ameshawishika kwa Ukweli, wala hatafanya mageuzi baadaye,” hunitia hofu. Kwa maana iwapo ni hivyo, basi nimetenda mambo ambayo yatasababisha nipotee. Lipo tumaini gani kwa ajili yangu? {ABN4: 10.2}

Jibu:

Msimbo haumaanishi kwa neno “matengenezo” kwamba mtu lazima awe mkamilifu kwa mara moja. Ukamilifu hupatikana kupitia kuendelea katika Kweli na kupanda ngazi ya ukamilifu hatua kwa hatua. (Tazama Shuhuda, Gombo la 1, uk. 187). Mkristo wa kweli huwa hakawii nyuma, lakini kama nafaka kamili ya kondeni hukua hatua kwa hatua hukuwa jani, vivyo hivyo pia yeye hustawi katika nyanja ya Ukristo kadiri Nuru humwongoza mbele. Kwa hivyo iwapo umeanza na

10

bado unapiga mbio katika shindano, hakuna sababu kwa nini upotee, “kwa maana mwenye haki huanguka mara saba, na akainuka tena.” Mit. 24:16. “Na kama mtu akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.” 1 Yohana 2:1. {ABN4: 10.3}

Daraja ambalo haliwezi kufanya matengenezo, kwa mujibu wa Msimbo, ni wale ambao hawawezi kuanza mbio wakati wameshawishwa kwa Ukweli endelevu, lakini ambao, kama Wayahudi wa siku za Kristo au Walaodekia wa leo, husema, “Sisi ni matajiri na tumejitajirisha, wala sina haja ya kitu” (Ufu. 3:17); au ambaye, kama Feliki, hujisalimia, akisema, “Sasa enenda zako; nami nikipata nafasi, nitakuita.” Mdo. 24:25. {ABN4: 11.1}

Ukweli kwamba unajitahidi kushinda dhambi kwa kutembea katika Nuru, ni thibitisho tosha kwamba haujapotea. Na utaendelea hivi, utaokoka, vinginevyo sote tumepotea. {ABN4: 11.2}

Adui angependa kutudanganya kwa njia moja au nyingine, yeye hajali ni ipi, na hatupaswi kumpa fursa yoyote. Ushauri wa Paulo ni: “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.” Ebr. 12:1. {ABN4: 11.3}

11

KUTAKASWA MARA MOJA, AU SIKU KWA SIKU?

Swali Namba 81:

Je! Tunatenda sehemu gani katika mchakato wa utakaso, na mtu hutakaswa wakati gani? {ABN4: 12.1}

Jibu:

“Tunapaswa kuyazingatia maneno ya mtume Paulo, ambayo kwayo huwasihi ndugu zake, kwa rehema za Mungu, waitoe miili yao ‘iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.’… “Utakaso sio tu nadharia, mhemko, au aina ya maneno, bali kanuni iliyo hai, amilifu, inayoingia katika maisha ya kila siku. Huhitaji kwamba tabia zetu za ulaji, kunywa na kuvalia, ziwe za kuhifadhi afya ya kimwili, kiakili na imani, ili tuitoe miili yetu iwe kwa Bwana — si sadaka iliyoharibiwa kwa tabia mbaya, bali- ‘dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.’ Rumi. 12:1” — Mashauri kwa Afya, uk. 67. {ABN4: 12.2}

“Utakaso wa kweli huja kupitia kutekelezwa kwa kanuni ya upendo. ‘Mungu ni upendo naye akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.’ Maisha ya yule ambaye Kristo hukaa moyoni mwake, yatadhihirisha utauwa wa vitendo. Tabia itatakaswa, kuinuliwa, kuadilishwa, na kutukuzwa. Fundisho safi litaunganishwa na matendo ya haki; maagizo ya mbinguni yataungana na mazoea matakatifu. {ABN4: 12.3}

12

“Utakaso…haupatikani kwa hisia ya kupaa kwa furaha, bali ni tokeo la kufia dhambi daima, na siku zote kuishi kwa ajili ya Kristo. Makosa hayawezi kurekebishwa wala matengenezo kutekelezwa katika tabia ya juhudi dhaifu, na za kukatikakatika. Ni kwa juhudi za muda mrefu, za uvumilivu na nidhamu inayohitajika sana, na pambano kali, ya kwamba tunaweza kushinda. Hatujui hata siku moja jinsi pambano letu lijalo litakavyokuwa zito. Kadiri Shetani anapotawala, tutakuwa na unafsi wa kutiisha, kuzishinda dhambi zinazosumbua-sumbua; maadamu maisha yatadumu, hakutakuwa na mahali pa kusimama, hakuna hatua ambayo tunaweza kufikia na kusema, nimefikia ukamilifu. Utakaso ni tokeo la utiifu wa maisha yote.” — Matendo ya Mitume, uk. 560. {ABN4: 13.1}

“Siku kwa siku, saa kwa saa, kazi ya kujikakamua ya kujikana nafsi na ya utakaso lazima iendelee ndani; kisha matendo yatashuhudia kwamba Yesu anakaa moyoni kwa imani. Utakaso hauzifungi njia za nafsi kwa maarifa, lakini hupanua akili, na kuzivuvia kutafuta ukweli kama hazina iliyofichika.” — Ushauri kwa Walimu, uk. 449. {ABN4: 13.2}

“Hakuna utakaso wa Biblia kwa wale wanaotupa sehemu ya ukweli nyuma yao” (Shuhuda, Gombo la 1, uk. 338), kwa maana “kazi hii haiwezi kuendelea ndani ya moyo ilhali nuru kwa sehemu yoyote ya ukweli imekataliwa au kupuuzwa. Nafsi iliyotakaswa haitaridhika kubaki katika upumbavu, bali itatamani kutembea katika nuru na kuitafuta

13

nuru kubwa. Jinsi ambavyo mchimba-mgodi huchimba dhahabu na fedha, vivyo hivyo mfuasi wa Kristo atautafuta ukweli, kama hazina zilizofichika, na atasonga mbele kutoka kwa nuru hadi kwa nuru kubwa, akiongezeka daima katika maarifa. Atakua daima katika neema na maarifa ya ukweli.” — Mapitio na Kutangaza, Juni 17, 1890. {ABN4: 13.3}

“Wengi…hawaonyeshi ukweli katika maisha yao. Wana mazoezi maalum juu ya utakaso, lakini hulitupa neno la Mungu nyuma yao. Wao huomba utakaso, huimba utakaso, na kupiga mayowe utakaso…Ukweli wa sasa, ambao ndio njia, haujazingatiwa, lakini umekanyagiwa chini ya miguu. Wanadamu wanaweza kupiga kelele, Utakatifu! utakatifu! utakaso! weka wakfu! weka wakfu! na bado hawajui kwa uzoefu yale wanayosema kuliko mdhambi mwenye mielekeo yake potovu. Mungu hivi karibuni atalirarua hili vazi lililopakwa chokaa la utakaso wa kujidai ambalo wengine wenye nia ya mwili wamejivika ili kuuficha upungufu wa nafsi.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 338, 336. {ABN4: 14.1}

“Nabii Danieli alikuwa mfano wa utakaso wa kweli. Maisha yake marefu yalijazwa na huduma bora kwa Bwana wake. Alikuwa mtu ‘aliyependwa sana’ na Mbingu. Bado badala ya kujidai kuwa msafi na mtakatifu, nabii huyu aliyeheshimiwa alijitambulisha na wadhambi sugu wa Israeli, alipomwomba Mungu kwa ajili ya watu wake: {ABN4: 14.2}

14

“Hatuwasilishi maombi yetu mbele Yako kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema Zako nyingi.” “Tumefanya dhambi, tumetenda maovu.’ Yeye atangaza, ‘Nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu.’ Na baadaye Mwana wa Mungu akatokea, kumpa maagizo, Danieli akasema, “uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.” {ABN4: 15.1}

“Ayubu alipoisikia sauti ya Bwana kutoka kwa upepo wa kisulisuli, akasema, “Najichukia nafsi yangu na kutubu katika mavumbi na majivu.” Ilikuwa wakati Isaya alipouona utukufu wa Bwana, na kusikia makerubi wakipiga kelele, ‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi,’ akapiga kelele, “Ole wangu! kwa maana nimepotea.” Paulo baada ya kunyakuliwa mpaka mbingu ya tatu akasikia maneno yasiyotamkika, alijinenea “mimi niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote.’” — Pambano Kuu, uk. 470, 471. {ABN4: 15.2}

“Utakaso wa Paulo ulikuwa tokeo la pambano la daima dhidi ya nafsi. Alisema,” Ninakufa kila siku.” Mapenzi yake na tamaa zake kila siku zilipingana na wajibu na mapenzi ya Mungu. Badala ya kufuata mapendeleo, alitenda mapenzi ya Mungu, ingawa yalikuwa yakiusulubisha utu wake wa kale. {ABN4: 15.3}

“Mungu huwaongoza watu Wake hatua kwa hatua. Maisha ya Mkristo ni pambano na kupiga hatua. Katika pambano hili hakuna kuachiliwa; juhudi lazima ziwe endelevu na za uvumilivu.

15

Ni kwa jitihada zisizokoma kwamba tunadumisha ushindi juu ya majaribu ya Shetani. Uadilifu wa Kikristo lazima utafutwe kwa nguvu imara, na kudumishwa kwa kusudi thabiti la uamuzi. {ABN4: 15.4}

“Hakuna atakayepelekwa juu bila juhudi ka, na za uvumilivu kwa niaba yake. Wote lazima washiriki katika vita hivi kwa ajili yao wenyewe …. Mapambano ya ushindi juu ya nafsi, kwa ajili ya utakatifu na mbingu, ni mapambano ya muda wote wa maisha. Bila juhudi zisizokoma na shughuli za daima, hapawezi kuwapo maendeleo katika maisha ya kiungu, hakuna kupata taji ya mshindi.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 313. {ABN4: 16.1}

“Haya ni mapenzi ya Mungu kwa wanadamu, hata utakaso wao. Katika kuhimiza njia yetu kwenda juu, mbinguni, kila kitivo lazima kiwekwe katika hali ya afya zaidi, kimeandaliwa kutoa ibada ya uaminifu. Nguvu ambazo Mungu amempa mwanadamu zinapaswa kunyooshwa…. Mtu hawawezi kufanya hili yeye mwenyewe; lazima awe na msaada wa Mungu. Je! ni sehemu gani chombo cha mwanadamu kitatenda? — ‘Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi Lake jema.’ Filp. 2:12, 13.” — Kimenukuliwa, uk. 64. {ABN4: 16.2}

Mwishowe, utendaji wa kanuni ya utakaso wa kweli katika moyo wa Mkristo huonyeshwa katika mfano wa Kristo wa mbegu inayokua: “kwanza jani, tena

16

suke, kisha ngano pevu katika suke.” Marko 4:28. {ABN4: 16.3}

Kwa hivyo kutoka kwa neema hadi kwa neema hupanda juu ya utakaso wa kweli, ambao ni mchakato wenye nguvu ya kuzaliwa upya kwa njia ya ushirikisho wa daima kwa haki ya Kristo, “kwa njia ya nguvu ya Roho wa Mungu anayekaa ndani” (Pambano Kuu, uk. 469), kwa maana “kupewa Roho ni kupewa maisha ya Kristo” (Watendakazi wa Injili, uk. 285) — utakaso kamili. {ABN4: 17.1}

Kwa njia ya kulinganisha: “Haki ambayo sisi tumehesabiwa kwayo [awamu ya kwanza ya utakaso] imewekelewa. Haki ambayo tumetakaswa [awamu ya pili] imeshirikishwa. Ya kwanza ni jina letu kwenda mbinguni; ya pili ni kutufanya tustahili kuingia mbinguni.” — Mapitio na Kutangaza, Juni 4, 1895 (Katika Kristo Haki Yetu, uk. 98). {ABN4: 17.2}

“Kuota kwa mbegu huwakilisha mwanzo wa maisha ya kiroho, na ukuaji wa mmea ni mfano mzuri wa ukuaji wa Mkristo. Kama ilivyo kwa maumbile, ndivyo ilivyo katika neema; hayawezi kuwapo maisha bila ukuaji. Mmea lazima ukue au ufe. Kwa sababu ukuaji wake u kimya na usiotambulika , bali endelevu, ndivyo ulivyo ukuaji wa maisha ya Mkristo. Katika kila hatua ya ukuaji maisha yetu yanaweza kuwa makamilifu; bado ikiwa kusudi la Mungu kwetu linatimizwa, yatakuwapo maendeleo daima. Utakaso ni kazi ya muda wote wa maisha. Kadiri fursa zetu

17

zinavyoongezeka, uzoefu wetu utapanuka, na ufahamu wetu kuongezeka. Tutakuwa imara kuwajibika, na ukomavu wetu utakuwa kulingana na mapendeleo yetu.” — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 65, 66. {ABN4: 17.3}

“Hapa ni utakaso wa Biblia. Sio tu maonyesho au matendo ya nje. Ni utakaso unaopatikana kupitia njia ya ukweli. Ni ukweli uliopokelewa moyoni, na kutekelezwa kwa utendaji katika maisha.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 339. {ABN4: 18.1}

“Kristo aliwaombea wanafunzi Wake kwa maneno haya: ‘Uwatakase kwa ile kweli: neno Lako ndiyo kweli.’ Hakuna utakaso wa kweli, isipokuwa kupitia utiifu kwa ukweli.” — Maisha Yaliyotakaswa, uk. 49. {ABN4: 18.2}

KUTAPIKWA NJE, AU KUTUPWA NJE?

Swali Namba 82:

Tafadhali ifafanue taarifa ifuatayo kutoka kwa “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 153: “Sasa kwa watu Wake anawapa mwaka mmoja kufanya vema.” {ABN4: 18.3}

Jibu:

Taarifa iliyotajwa hapo juu humaanisha kwamba Mungu aliwawawekea makataa viongozi wa Laodekia kwa mwaka mmoja ambao walipaswa kuupokea ujumbe wa kutiwa muhuri na kuupeleka kwa makanisa yao mbalimbali. Juu ya kushindwa kwao kufanya hivyo kufikia mwisho wa kipindi hiki cha neema kilichowekewa mpaka, Yeye aliwakataa kama watumwa Wake. Na sasa, ikiwa yeyote kati yao ataupokea ujumbe wa

18

ziada (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106; Watendakazi wa Injili, uk. 304), na ari ya kuupeleka kwa walei, wanaweza kufanya hivyo chini ya maelekezo ya ujumbe wa sasa — ule “mpangilio mpya” ulionenwa katika Kristo Haki Yetu, Toleo la 1941, uk. 121. {ABN4: 18.4}

NI NINI “FIMBO YA MWANANGU”?

Swali Namba 83:

Je! Unaweza kuelezea maana ya “fimbo” kama inavyotumika katika Ezekieli 21:8-15? {ABN4: 19.1}

Jibu:

Kwa kuita Israeli “fimbo” ya mwana Wake (Zab. 74:2; 110:2), Mungu huonyesha kwamba walikuwa fimbo Yake ya kuwaadhibu mataifa, kama vile Ashuru ilivyokuwa fimbo Yake ya kuadhibu Israeli (Isa. 10:5). Kwa hivyo fimbo ni nembo ya utawala au serikali, pia ni chombo cha kuadhibu. {ABN4: 19.2}

JE! UPANGA WA BWANA NI NINI?

Swali Namba 84:

Je! Biblia humaanisha visu, bunduki, au singe wakati inazungumza juu ya “upanga wa Bwana” katika siku za mwisho? {ABN4: 19.3}

Jibu:

Neno hili “upanga,” kama linavyotumiwa katika Maandiko, humaanisha vita, umwagaji wa damu, na kulipiza kisasi. Upanga wa Mungu ni chombo chochote Anachotumia kutekeleza hukumu; sio lazima uwe ubapa wa chuma. Mara nyingi imekuwa

19

tauni, moto, njaa, tetemeko la ardhi, vita, na jeshi la nguvu zingine za waovu kama anavyoshuhudia Daudi kwa kilio: “Kwa upanga Wako, uniokoe nafsi na mtu mbaya.” Zab. 17:13. {ABN4: 19.4}

JE! “ZAYUNI” NA “YERUSALEMU” NI SAWA?

Swali Namba 85:

Tafadhali fafanua tofauti kati ya maneno “Zayuni” na “Yerusalemu” la Isaya 52:1 na la Ufunuo 14:1. {ABN4: 20.1}

Jibu:

“Zayuni” na “Yerusalemu” ya Isaya 52:1 lazima inawakilisha watu, kwa sababu utakuwa ni upumbavu kusema kwa kilima na mji, “Amka, amka, jivike nguvu zako, jivike mavazi yako mazuri.” {ABN4: 20.2}

Kwenye kilima cha kale kilichoinuuliwa cha Zayuni ilisimama ikulu ya mfalme, “wakuu wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale kenda wakae katika miji mingine.” Neh. 11:1. Kwa hivyo familia ya kifalme ilikaa juu ya Mlima Zayuni, na watawala wadogo na wawakilishi wengine wa serikali walikaa katika Yerusalemu wenyewe. {ABN4: 20.3}

Mwito, “Amka, amka jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu,” unalihusu kanisa la Laodekia, la mwisho kati ya makanisa

20

saba, na lile linalokamilisha kipindi cha “ngano” na “magugu” yaliyochangamana, kwa sababu baada ya kujivika mavazi yake mazuri, “aliye najisi hataingia ndani yake tena.” Wale watakaoamka kwa huo mwito wa kuamsha, watajivika nguvu kwa kujitenga na waovu, na kujivika mavazi mazuri kwa kuielekea haki, ni wale ambao, katika “siku za mwisho,” watajumuisha Zayuni na Yerusalemu — wakuu na watawala wa watu katika kanisa la Ufalme uliorejeshwa. {ABN4: 20.4}

Kisha “likiwa limevikwa vazi la silaha za haki ya Kristo, kanisa litaingia kwenye pambano lake la mwisho ‘Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango,’ litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. {ABN4: 21.1}

Kwa hivyo, “ni wale tu ambao wameyastahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu.” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908.” {ABN4: 21.2}

Sasa kuhusu maana ya maneno haya mawili, Zayuni na Yerusalemu kama yanavyotumika katika Ufunuo 14:1, rejeleo la pili linalohojiwa, Waufunuo hufafanua kwamba watu 144,000 wa makabila kumi na mawili ya Israeli ni wale wanaojumuisha Zayuni. Maneno yake ni, “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Zayuni,

21

na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja Naye, wenye jina Lake na jina la Baba Yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 14:1. [ABN4: 21.3}

Hawa wakiwa ni malimbuko (Ufu. 14:4), huonyesha zaidi kwamba wao ni wa kwanza wa mavuno katika “mwisho wa dunia.” Mat. 13:39. Bila shaka, basi, wale ambao walionekana baada yao, “umati mkubwa…wa mataifa yote” (Ufu. 7:9), sio wengine ila mazao ya pili ya mavuno, ambao baadhi yao watakaa Yerusalemu. {ABN4: 22.1}

Hivyo kwa wakati huu wa mavuno, “na itakuwa… kwamba mlima wa nyumba ya Bwana [Mlima Zayuni] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote yatauendea makundi makundi.” Isa. 2:2. {ABN4: 22.2}

JE! YEYE AMEWAKANYAGIA AU ATAWAKANYAGIA CHINI?

Swali Namba 86:

Kupitia Isaya (sura ya 63, aya ya 3) Kristo alitangaza juu Yake Mwenyewe: “Nimelikanyaga shinikizo peke Yangu; wala katika watu hakuwapo mtu pamoja Nami; naam, Nitawakanyaga kwa hasira Yangu, na kuwaponda kwa ghadhabu Yangu; na mavazi yangu yatatiwa madoa kwa damu yao, Nami nitayachafua mavazi Yangu yote.” Je! Andiko hili linahusu kazi ya Kristo wakati wa Ujio Wake wa kwanza au wakati wa Ujio Wake wa pili? {ABN4: 22.3}

Jibu:

Sehemu ya kwanza ya aya hiyo inahusu ujio wa kwanza wa Kristo, na sehemu ya mwisho kwa

22

wakati wa utakaso wa kanisa. Hivyo Kristo kwa kutumia lugha ya kinabii, anaonekana kutazama nyuma kwa wakati wa mateso Yake alipokuwa msalabani, Akisisitiza kwamba hakukuwapo mtu pamoja Naye, na ya kwamba, kwa hivyo, kwa kukata kauli hiyo wale ambao hawakushiriki katika uchungu Wake hawana haki ya kuwatawala wale Aliowaweka huru; na ya kwamba yeyote atakayeendelea kuwashikilia watu Wake utumwani na katika kutoujua Ukweli Wake, Yeye atawakanyaga kwa hasira Yake na kuwaponda kwa ghadhabu Yake na kuinyunyiza damu yao kwa mavazi Yake, na hivyo kutia madoa kwa mavazi Yake yote, na hivyo kuwaweka huru watu Wake. {ABN4: 22.4}

KUBATIZWA KWA ONDOLEO LA DHAMBI, AU KWA KUKAZA MWENDO NA UKWELI?

Swali Namba 87:

Kama tulivyoingizwa katika ushirika wa kanisa la Waadventista wa Sabato kwa Ubatizo wetu wa zamani katika kanisa la Baptisti, je! sasa ni lazima kwetu kubatizwa tena? {ABN4: 23.1}

Jibu:

Maandiko Matakatifu hufundisha hitaji la Ubatizo mmoja tu (Efe. 4:5). Kwa vile ulibatizwa kwa kuzamishwa katika kanisa la Baptisti na baadaye ukajiunga na kanisa la Waadventista wa Sabato bila sababu nyingine isipokuwa kutembea nuru angavu ya Neno, haukuwa na hitaji la kubatizwa tena. Na ikiwa umekuwa mkweli kwa nadhiri zako za Ukristo

23

pia katika kanisa la Waadventista wa Sabato, basi hauhitaji kubatizwa tena. {ABN4: 23.2}

Tuseme ulikuwa umebatizwa na mtume Paulo na kupokelewa katika ushirika wa kanisa, ukaendelea kuishi hadi wakati wa sasa, wakati wote ukitembea katika nuru endelevu ya Bwana, ungalikuwa umemfuata Yeye kupitia katika hatua zote saba mfululizo za Matengenezo — vipindi saba vya kanisa. Katika kipindi cha Uprotestanti, ungalikuwa Mlutheri mwanzoni na Mdaudi mwishoni. Hivyo kuwa kwako katika kuifuata kwa uaminifu nuru ya Ukweli, sio Kimaandiko wala kimantiki kwamba Mungu angalikuhitaji ubatizwe tena kila wakati unapochukua hatua kusonga mbele. {ABN4: 24.1}

NI NANI MFALME WA KITUO CHA MLIMA KARMELI — MUNGU AU MTU?

Swali Na. 88:

Wengi wetu tumekuwa na pambano la kujinasua kutoka kwa kamba tulizofungwa nazo na uongozi wa sasa wa kanisa, na inaonekana si zaidi ya haki kwamba tunao uhakika kwamba Bwana anaongoza katika harakati zote hapo Mlima Karmeli. Tungependa tujue ni kiasi gani cha kazi ya Mlima Karmeli kiko chini ya usimamizi wa Bwana? {ABN4: 24.2}

Jibu:

Kufikiria kwa uangalifu juu ya jambo hili kunaweza kwishia tu katika utambuzi kwamba kwa sababu Mungu ameahidi kuchukua hatamu mikononi Mwake, basi hilo ndilo haswa

24

ambalo Yeye lazima yualifanya. Kwa hivyo, machafuko na utata wote unaoambatana na kuhoji na kukosoa, na kutilia shaka juu ya kazi hiyo hakuna maana, wala sababu na kunadhuru. {ABN4: 24.3}

“Shetani,” inasema Roho ya Unabii, “anao uwezo wa kupendekeza mashaka na kubuni pingamizi kwa ushuhuda ulio dhahiri ambao Mungu hutuma, na wengi hufikiri ni fadhila, alama ya ujasusi ndani yao, kuwa wa kutoamini, na kuhoji na kubishana. Wale ambao wanataka kutilia shaka watapata nafasi nyingi. Mungu hapendekezi kuondoa fursa zote kwa kutoamini. Yeye hutoa ushahidi, ambao lazima uchunguzwe kwa uangalifu na akili ya unyenyekevu na roho ya uelekevu, na wote wanapaswa kuamua kutoka kwa uzito wa ushahidi.” — Shuhuda, Gombo la 3 uk. 255. {ABN4: 25.1}

Isitoshe, hakuna mtu anayeweza kuhukumu hiyo kazi kwa hekima yake mwenyewe au kwa hekima ya wanadamu wengine, kwa maana, Roho wa Kweli anasema: “Watendakazi watashangazwa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kuileta na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki….Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna iliyo kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa wanadamu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {ABN4: 25.2}

“Sio kwa ajili yako kutishwa na mionekano ya nje, ijapokuwa ni ya kuzuia

25

inavyoweza kuwa. Ni kwako wewe kuiendeleza kazi jinsi Bwana alivyosema ifanywe.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 141. {ABN4: 25.3}

Ikiwa kila mtu atafanya vema sehemu yake katika kazi aliyopewa kufanya, hivi karibuni ataona kwamba hana haja wala uwezo wa kutunza majukumu ya Bwana, au kufuatilia kazi waliopewa wengine. Atajua kwamba jambo kuu na la pekee sahihi analoweza kufanya ni kwa ujasiri kuipokea changamoto ya upeo ya “malaika wa Bwana” kwa Yoshua: “Kama utatembea katika njia Zangu, na ikiwa utayashika maagizo Yangu, basi nawe utaihukumu pia nyumba Yangu, nawe utazilinda nyua Zangu, Nami nitakupa nafasi ya kutembea kati yao wasimamao karibu.” Zek. 3:7. {ABN4: 26.1}

Kwa waamini wa Ukweli wa hivi Sasa, mojawapo wa shuhuda hakika kwamba Bwana anaongoza katika kazi ya Mlima Karmeli, ni kwamba bila kujali upinzani usiokoma, uhaba wa wafanyakazi, na shida zingine nyingi, kazi inaendelea kusonga mbele daima kwa nguvu isiyozuilika. Ni, hakika, kama mbegu ya haradali. {ABN4: 26.2}

Licha ya mwanzo wake wa umaskini, mdogo, ukosoaji na upinzani dhidi yake, na vipingamizi vya namna nyingi na vikwazo ambavyo umelazimika kuvishinda, unaamsha umati wa watu kote Laodekia. Umeizindua meli ya Matengenezo, na wakati wengi tayari

26

wameipanda, wengine kwa upesi wanakaribia kufanya uamuzi wa kutafuta usalama ambao huwa inaotoa. Wanaichunguza tena Biblia katika Nuru Takatifu ya Fimbo ya Mchungaji. Ujumbe wa Malaika watatu umekuwa kwao wazi na mtamu kama kijito cha mlimani. Na wale ambao hawajawahi kumiliki, na hata wale ambao hawakuyaamini, maandishi ya Roho ya Unabii, sasa wanayanunua magombo yote. {ABN4: 26.3}

Kwa kweli hakuna mtu anayeweza kusema kwa fikra kwamba hiyo ni kazi ya Adui, bila kutoa sifa ya wa Biblia kwa Shetani. Iwapo Biblia ni ya Bwana, ujumbe katika Fimbo hauwezi kuwa wa Ibilisi, kwa maana ni Biblia iliyofunuliwa. Kamwe bila nguvu ya Mungu haungalikuwa umechachisha Dhehebu lote, kwa maana Yeye Mwenye Uwezo wote anatangaza: “Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, asije mtu akaliharibu; usiku na mchana Nitalilinda. Hasira sinayo ndani Yangu; kama mibigili na miiba ingekuwa mbele Yangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.” Isa. 27:3, 4. {ABN4: 27.1}

Wale ambao hudai tu kuwa wanaamini, wanaonywa hapa kwamba Bwana anajua kazi yao, na ya kwamba Yeye hakuwaacha watendakazi Wake gizani kuihusu. Akizifanua siri zao, Anasema: “Nawe, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema,

27

haya! twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa Bwana. Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu Wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi. Na hayo yatakapokuwapo (tazama, yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa nabii amekuwapo kati yao.” Ezek. 33:30-33. {ABN4: 27.2}

JE! MUDA UMEKWISHA SANA KUINGIA KATIKA JUYA?

Swali Namba 89:

Yuko kati yetu mmoja ambaye anafundisha kwamba iwapo juya lilivutwa ufuoni (Mat. 13:47, 48) mwaka 1930, basi wale ambao hawakuwa ndani yake wakati huo (yaani, wale ambao wakati huo hawakuwa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato) hawawezi kutumaini kuwa sehemu ya malimbuko. Iwapo ni kweli, basi mbona mtu ajaribu kuja ndani sasa badala ya kungoja wakati wa mavuno ya pili? Au, iwapo tayari yu katika ujumbe, mbona aendelee kujitahidi kuishi kulingana nao iwapo juhudi zake zimefungwa katika ubatili kwa sababu alikosa tarehe ya mwisho? {ABN4: 28.1}

Jibu:

Tendo la mfano la kulikokota juya ufuoni (Bwana kuingilia kati katika kazi Yake kwa muda ) katika muunganisho

28

halisi, hakumzuii yeyote kuingia ndani yake iwapo wataweka juhudi zinazohitajika. Kwa maana, ingawa samaki, kama samaki, hawawezi kweli kuogelea katika juya baada ya kukokotwa ufuoni, lakini kama watu wanaweza hakika kuingia kanisani hadi mwisho wa muda wa rehema. {ABN4: 28.2}

Kwa kweli iwapo samaki wazuri huweza kuingia katika juya wakati linakokotwa ufuoni, wavuvi hawatawatupa nje na wale wabaya kwa sababu tu juya halikuwanasa. Badala yake watahesabiwa kuwa wa thamani zaidi kwa sababu ya bidii yao ya ziada iliyotumika kuingia ndani, bila yeyote kuwatafuta na lile juya. Iwapo mtu hawezi kuona uwezekano wa yeye mwenyewe kuwa samaki anayeingia katika juya, anaweza kujiona mwenyewe kama kondoo anayeingia katika zizi. {ABN4: 29.1}

Ni wazi, basi, wazo la tarehe ya mwisho ni dhana danganyifu, ambayo yaweza kuvunja moyo maendeleo ya Mkristo, na kusababisha wengine walio tayari katika ujumbe kuhalalisha njia yao kwenda nje kwa sababu ya ubatili wa kukaa ndani, na kuhalalisha wengine kwa kutofanya juhudi zinazohitajika kuingia katika juya la wokovu wakati fursa inapojitokeza. Kwa kweli, hata huwalazimisha kuachana na fursa yao ya sasa na kungojea hiyo ambayo haitakuja kamwe! {ABN4: 29.2}

“Leo,” asema Roho wa Mungu, “kama mtaisikia sauti Yake, msifanye migumu mioyo yenu.” Ebr. 4:7. {ABN4: 29.3}

29

LIPI LA KUFANYA UNAPOTENGWA KWA USHIRIKA?

Swali Namba 90:

Je! Wale kati yetu ambao wametengwa waendelee kuhudhuria ibada za kanisa? Iwapo ni hivyo, na ikiwa fursa hapo itajitokeza kwa ajili yetu kusema neno kwa tukio la Ukweli wa Sasa, tunapaswa? Lakini vipi iwapo tutaulizwa tusiseme jambo linalopendekeza Ukweli wa Sasa — tunapaswa kukubali na kukaa kimya milele? Na tutafanya nini iwapo hawataturuhusu kushiriki katika ibada ya meza ya Bwana? {ABN4: 30.1}

Jibu:

Uhusiano wetu na kanisa ni sawa na ulivyokuwa wa Yohana, Yesu Kristo, na mitume: Tunao ujumbe wa kutangaza kwa kanisa, na ingawa maafisa wa kanisa hutuamuru tutoke ndani, jinsi Sanhedrini ilivyowaamuru mitume watoke “hekaluni,” ni lazima kwa njia ya haki tukatae kuondoka, na lazima tuendelee kurudi kanisani. Kwa maana iwapo tutaondoka na kukaa mbali na kuwa wageni, vipi, basi, tutatangaza ujumbe kwa watu wetu? {ABN4: 30.2}

Wote lazima watambue, hata hivyo, kwamba huwa vibaya Mkristo kusababisha usumbufu wowote wakati wowote, haswa wakati wa ibada za kanisa. Wala haiwezekani kwa yeyote kati yetu kwa mbinu kama hizi kuwasilisha ujumbe kwao, au kuwashawishi kwamba tunanena “maneno ya uzima.” Kwa kushuhudia kimya-kimya, kwa kicho, na kwa busara kanisani na nje ya kanisa, tutaufaya

30

uchokozi kuwa madai yasiyofaa bali mashtaka ya uongo. {ABN4: 30.3}

Katika Shule ya Sabato, ni sawa kabisa na inaruhusiwa kujibu maswali ambayo yanajitokeza kuhusiana na somo. Kwa hili, hawawezi kumshtaki kwa haki mtu yeyote kwa kusababisha usumbufu, kwani kwa kweli sio utangamano wa kusudi lililowekwa na sheria za Shule ya Sabato. Lakini ikiwa mtu yeyote atatakiwa asijibu maswali, basi aache kufanya hivyo badala ya kusababisha ugomvi na lawama. Ni vibaya kuanzisha vita au ubishi kwa hoja zozote ambazo zinaweza kuibuka. Hakuna chochote isipokuwa madhara kwa kazi ya Ukweli wa Sasa yanaweza kutokea kwa mchakato huo. Ruhusu mwenendo wako uivute imani ya watu. {ABN4: 31.1}

Mbili kati ya sababu kuu za kutokaa mbali na Shule ya Sabato na ibada za kanisa ni, (1) ya kwamba tutakuwa tunajinyima fursa ya ibada ya umma katika kanisa ambalo tulisaidia kujenga, na (2) ya kwamba kwa kukosekana wenyewe katika ibada, tutakuwa wageni kwa ndugu zetu na tutalazimika kufahamiana tena nao iwapo tutawahiweza kuwapatia ujumbe. Kwa kuendelea, hata hivyo, kwenda kanisani, basi, baada ya kufumukana, tunapewa nafasi ya kuongea na kina ndugu kwa masilahi ya ujumbe, tukiwasihi wachunguze wenyewe ama kwa kuhudhuria masomo yetu au kwa kusoma machapisho

31

ya Ukweli wa Sasa. Pia, kila wakati zipo fursa za kupata jina moja au mengi mapya na anwani za kutuma kwa orodha yetu ya barua. {ABN4: 31.2}

Kwa hivyo, iwapo tutahiari kukaa mbali na ibada za kanisa, tunajiweka wazi kwa tuhuma ya kuwa vichipuko kutoka kwa kundi, na wakati huo huo tutapoteza fursa ya kukongamana. {ABN4: 32.1}

Isitoshe, ikiwa kwa njia hii tutajitenga wenyewe, basi katika utimizo wa Ezekieli 9, wakati wale ambao hawana “alama” wanatwaliwa, hatutakuwa na haki sawa ya kudai urithi katika Dhehebu. {ABN4: 32.2}

Kwa kuzingatia kushiriki kwetu katika ibada ya Dhehebu kwa meza ya Bwana, tunaamini kwamba maadamu huliadhimisha agizo hili mara kwa mara, tunapaswa kushiriki kadiri inavyowezekana. Kwa maana iwapo tutahiari wenyewe kukaa mbali kwayo, tutawapa mawazo mabaya. Ikiwa kanisa linakataa kututumikia au kuturuhusu kuwatumikia wengine katika agizo la unyenyekevu, hakuna jambo tunaloweza kufanya ila kusubiri hadi ibada ikamilike. Na iwapo watatupuuza wakati wa kupisha mkate na divai, hatupaswi kunung’unika au kusema lolote, bali kustahimili ile dharau kwa upole. Kwa kujishusha hivyo, waaminifu katika kongamano watauona mwenendo usio wa ukristo na upumbavu wa maafisa wa kanisa,

32

na wataanza kuamka na kuchukua hatua kwa hali hiyo. {ABN4: 32.3}

Ingawa tunaweza, dhidi ya mapenzi yetu, kutengwa tusishiriki katika agizo hilo kila mara, sisi pamoja na hayo majina yetu yatakuwa katika Kitabu cha Uzima na kama mwizi msalabani ambaye hakubatizwa, tutaingia Paradiso kwa kuwa tumefanya vema. Kwa hivyo, Wandugu, hebu tuwe waaminifu kuhudhuria ibada za kanisa letu na kwa mwenendo wetu “basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika raha Yake, na tuogope mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.” Ebr. 4:1. {ABN4: 33.1}

IPO TOFAUTI GANI KATI YA “AMEKUJA” NA “KUSHUKA”?

Swali Namba 91:

Katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 20, hoja imefanywa kwamba Yohana alimuona malaika wa Ufunuo 18, si akija, si akiwa ameruka safarini kuja chini, lakini “amekuja” chini, yaani, tayari amewasili. Lakini kwa Kiingereza wazi “kuja chini” humaanisha kushuka. Na Dada White husema: “alipokuwa akishuka.” Vipi, kwa hivyo, “Fimbo” inaweza sawasawa kuweka mkazo kwa wazo kwamba Yohana alimwona akiwa tayari “amekuja” — tayari amewasili? {ABN4: 33.2}

Jibu:

Wakati kitu cha mwendo wa kasi kama risasi au mmweko wa umeme unapokuja, kiwango chake cha juu cha kusafiri hakimpi mtazamaji wakati wa kuona mwendelezo wa kuendelea kwacho mbele — “kuja” kwacho, ana uwezo wa kukiona wakati tu kimewasili mwishowe — “kimekuja.” Kwa hivyo ukweli kwamba malaika

33

wa Ufunuo 18:1 anaonekana, si “akishuka” (kama malaika wa Ufunuo 7:2), lakini “amekuja” humaanisha kwamba anakuja ghafla — kama malaika wa Danieli 9:21. {ABN4: 33.4}

Kwa kulinganisha, kwa kutazama kujongea kwa kitu kama jua, mtazamaji anaweza anaweza kuendelea kutazama “kupanda” kwalo. Kwa hivyo, Fimbo huona kwamba malaika wa Ufunuo 7:2 alionekana akiwa mbali, “akipanda kutoka maawio ya jua,” kwa sababu alikuwa akija polepole kama jua; ilhali malaika wa Ufunuo 18:1 alionekana “amekuja,” ghafla kwa sababu kasi kubwa ya kuruka kwake hadi chini haikuruhusu muda wa kutosha kwa jicho la mwanadamu kumuona “akija.” {ABN4: 34.1}

Upambanuzi huu kati ya kasi ya wale malaika wawili, kwa sababu ya umuhimu tofauti wa kila mmoja, ndiyo hoja ya kusisitiza. {ABN4: 34.2}

IWAPO NUSU NA NUSU WAKATI HUO, VIPI SASA?

Swali Namba 92:

“Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 30, hutoa taarifa kwamba dhehebu la Waadventista wa Sabato lilikuwa na washiriki 300,000 wakati kitabu hicho kilipoandikwa, kauli hii inaonyesha kwamba karibu nusu, 144,000, ni wanawali watano wenye busara na ya kwamba ile nusu nyingine ni wanawali watano wapumbavu. Lakini hii inawezaje kuwa hivyo wakati leo Dhehebu lina Idadi ya washiriki 500,000? {ABN4: 34.3}

Jibu:

Ilipoandika mnamo 1930, Fimbo ilikuwa lazima

34

inanena kwa maneno, sio katika ushirika wa leo ambao haukujulikana wakati huo, bali kwa ushirika uliothibishwa wakati huo. Na ingawa idadi ya wakati huo (300,000) ilipendekeza kwa kawaida mgawanyo sawasawa wa washiriki (madaraja mawili, wazuri na wabaya — “wanawali wenye busara” na “wanawali wapumbavu”), bado kwa kuwa wapo Waisraeli 144,000 tu wa kutiwa muhuri, idadi ya ambao hawangetiwa muhuri ingekuwa hata zaidi ya idadi ya wale wangetiwa muhuri wakati huo. {ABN4: 34.4}

Katika uchanganuzi wa mwisho, hata hivyo, si kusudi la Fimbo wala lengo lake kusema ni wangapi watakuwa wenye busara na wangapi wapumbavu katika mavuno ya malimbuko, kwa maana wakati ukweli wote unapojulikana, mfano wa “wanawali watano wenye busara,” mbali na kuelewa watu 144,000 kutoka katika makabila ya Israeli, wataweza kupatikana wamejumuishwa na idadi kubwa kutoka katika nchi za Mataifa. {ABN4: 35.1}

JE! USHIRIKA HUCHUKUA NAFASI YA MAARIFA YA UKWELI

Swali Namba 93:

Ingawa mimi si mshiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, lakini kwa sababu nina nuru kwa Ezekieli 9 na kwa ukweli wa watu 144,000, je! nitaanguka katika mchinjo wa waovu iwapo sitaipokea nuru kabisa na kuishi kwayo? Na, kwa kinyume, je! nitahusishwa kufurahia haki za watu 144,000 na kuwa mmoja wao ikiwa nitatii nuru yote ya ujumbe huu? {ABN4: 35.2}

35

Jibu:

Hata ingawa wewe si mshiriki wa kanisa, bado utawajibika kwa nuru ambayo unayo kwenye mada hiyo, kwa maana hakuna mtu anayeupata ukweli kimakosa, au kuuona bila msaada wa Roho Mtakatifu. {ABN4: 36.1}

Kwa sheria iyo hiyo ya uwajibikaji au jukumu takatifu, hata ingawa unaweza kuwa umeingia katika ujumbe hivi juzijuzi unaweza kustahiki uteuzi wa watu 144,000 iwapo unaishi kulingana na ujumbe ambao utawatakasa na kuwatia muhuri. Iwe au la, kwa kweli, hata hivyo, utakuwa mmoja wao, hatujui, lakini ikiwa u mwaminifu kwa ujumbe, utakuwa angalau mmoja pamoja nao. {ABN4: 36.2}

SASA NAAMINI, LAKINI JE! NINA HAKI YA USHIRIKA?

Swali Namba 94:

Iwapo mtu amesoma mfululizo wa “Fimbo ya Mchungaji” na amejifunza na anaamini yale ujumbe hufundisha, je! unaweza kumshauri kwanza ajiunge, na dhehebu la Waadventista wa Sabato? {ABN4: 36.3}

Jibu:

Iwapo mtu ameipokea Kweli yote kabisa, haki yake na jukumu lake ni kubatizwa aingie katika ushirika wa kanisa. Lakini baada ya kusoma Ujumbe wa Malaika wa Tatu kupitia njia ya Fimbo, ambayo inapingwa na ukasisi wa Waadventista wa Sabato, wao wanaweza pia kumnyimwa ubatizo na ushirika. Walakini, ikiwa amefanya yote awezayo ili kupokea

36

ubatizo na kujiunga na kanisa, na wao wakatae kumusajili, basi jukumu lake ni kupanga na Kituo cha Mlima Karmeli kwa ajili ya ubatizo na ushirika. {ABN4: 36.4}

Ni jina la mtu kuwa vitabuni, sio tu vya kanisa, bali vya mbinguni, yaani tunu ya usalama wa wokovu. Na ni katika kuupokea ujumbe wa saa hii, na juhudi inayolingana na kutii kwa uaminifu mafundisho yake yote, ambayo hushinda cheti cha ushirika wa mtakatifu na kuwa mwana wa mbingu. {ABN4: 37.1}

Kadiri mmoja huushuhudia Ukweli wa Hivi sasa, maadui zake ndani ya Dhehebu watampinga na kumtoa kwa ushirika ikiwa tayari ana ushirika, hapo lakini kunyimwa huko sio lazima kumvunje moyo. “Heri ninyi,” asema Bwana, “watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajali ya Mwana wa Adamu.” Luka 6:22. {ABN4: 37.2}

“Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno Lake; ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isa. 66:5. {ABN4: 37.3}

VIPI KUMHUSU PETRO NA “FUNGUO”?

Swali Namba 95:

Tafadhali fafanua Mathayo 16:15-19. Kwa nini Kristo alimpa Petro funguo? Mbona si kwa mwingine, au kwa wote? {ABN4: 37.4}

37

Jibu:

Petro ndiye pekee aliyetoa jibu sahihi kwa swali, “Nanyi mwaninena Mimi kuwa nani?” Kwa hivyo kwa Petro si kwa mwingine, Yesu alisema, “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni,” baada ya kumhakikishia kwanza kwamba “mwili na damu havikumfunulia” yeye ila Baba Yake aliye mbinguni. {ABN4: 38.1}

Wakati Mungu anamfanya mwanadamu alielewe jambo ambalo ni zaidi ya maarifa ya mfaji, Biblia huliita tendo hilo, Uvuvio. Kwa hivyo, Yesu alitamka kwamba Petro alivuviwa. Uvuvio huu na ushuhuda wa Yesu, kwa hivyo, zilikuwa Funguo za mada kuu ya wokovu wa mwanadamu — maarifa ya Mwana wa Mungu. Huu ndio ukweli, injili, ambayo ilibidi itangazwe. Ilikuwa Ukweli wa Sasa — ujumbe uliovuviwa moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Kwa hivyo alikuwa amepagawa kwa ufunuo ambao kila mtu angehukumiwa ama kwa wokovu au kuhukumiwa kifo, Petro na wenzake wakawa na jukumu la ama kufunga au kufungua wokovu kwa kila nafsi iliyo hai chini ya mbingu. {ABN4: 38.2}

Kwa sababu hiyo, wakati Kristo alimpa Petro funguo, Alimpa injili na agizo takatifu la kuihubiri. Na kwa kadiri Petro na watendakazi wenzake walikuwa wa kweli kwa agizo hili, ndivyo waliendelea kuzimiliki hizo Funguo kuwafungia au kuwafungulia watu ufalme wa Mungu, na kuidhinisha mbinguni lolote walilofunga au kufungua duniani. Vivyo hivyo, pamoja na Uvuvio

38

na ufunuo endelevu, Ukweli wa Sasa, hupokezwa zile Funguo. {ABN4: 38.3}

Bila shaka, kwa hivyo, ujumbe kutoka mbinguni, uliotangazwa na watumwa waliochaguliwa na Mungu, una nguvu zote, na kwa huo hatima ya milele ya mwanadamu huamuliwa. {ABN4: 39.1}

Waziwazi, basi, zile Funguo si kanisa lenyewe, bali ziko katika ujumbe linaloutangaza. Kwa hivyo hakuna mtu au jozi ya wanadamu inazo nguvu za kufunga au kufungua kwa idhinisho la Mbingu isipokuwa kwa ujumbe uliopeanwa moja kwa moja kutoka Mbinguni kwa ajili yao kuutangaza kwa wakati huo uliopo: “Vipindi tofauti katika historia ya kanisa kila kimoja kimetiwa alama na ustawi wa ukweli fulani maalum, kulingana na mahitaji ya watu wa Mungu kwa wakati huo.” — Pambano Kuu, uk. 609. Imekuwa hivyo tangu wakati wa zamani za kale. {ABN4: 39.2}

Nuhu, pia, alikuwa na Funguo, na kwa hivyo aliweza kufunga au kufungua mbinguni na duniani. Ukweli kwamba hata “malango ya kuzimu” hayakuweza kuishinda safina, hushuhudia hili. {ABN4: 39.3}

Na ahadi ya Mungu kwa Abrahamu, “Nami nitawabariki wale wanaokubariki, naye akulaaniye Nitamlaani; na katika wewe familia zote za dunia watabarikiwa” (Mwa. 12:3), huonyesha kwamba yeye pia alikuwa na Funguo za mbinguni. {ABN4: 39.4}

Pia, katika mkono wa Musa uliodhibitiwa na Majaliwa, Fungo zilifungua wazi malango ya ufalme kwa uhuru na

39

wokovu wa wenye haki, na zikawafungia katika maangamizo waovu. Kwa hivyo “Musa akasema, kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washuke shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana. Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.” Hes. 16:28-32. {ABN4: 39.5}

Kupitia kwa Musa Mungu alizikabidhi Funguo kwa jeshi la Waebrania, na kuziondoa katika siku za Kristo Wayahudi walipomkataa Yeye. Kisha Akazihamisha Fungo kwa waasisi wa kanisa la Kikristo. {ABN4: 40.1}

Lakini bila kujali mfano wa zamani wafuasi wa mitume mwishowe pia walirudia makosa ya wafuasi wa Musa. Bado kwa wakati wote wa Vizazi vya Giza, na haswa katika kipindi cha Matengenezo, Mungu aliendelea kumkabidhi mjumbe baada ya mjumbe, na kulikabidhi Vuguvugu baada ya Vuguvugu, urithi wa Kiungu. Lakini tena

40

na tena kupitia Matengenezo hadi kwa mwito wa William Miller, kila kundi mtawalia lilirudia upumbavu wa kuridhika na ujumbe tuli, hadi mwishowe wakati makanisa yote ya Kiprotestanti ya siku ya Miller yaliukataa ujumbe wa kwa wakati huo, wao, pia, bila kujua wakakataa kuwa tena wahifadhi wa Funguo takatifu. {ABN4: 40.2}

Kwa hivyo Miller na washirika wake walizimiliki hadi wakati wa ujumbe wa Mungu uliofuata, hukumu ya wafu, wakati funguo takatifu zilipopita kutoka kwa Vuguvugu la Miller hadi kwa dhehebu la Waadventista wa Sabato. Lakini iwapo sasa litakataa kuteta kwa Mungu la kuyapaka macho yake dawa ya macho ambayo Yeye anatoa kwalo, nalo pia, litaziacha Funguo ziponyoke kwa mkamato wake na kupitishwa hadi mikononi mwa wale watakaoutangaza ujumbe wa ziada, hukumu ya walio hai, ujumbe wa Kilio Kikuu. (Tazama Maandishi ya Awali, uk. 277-279). Na, janga la majanga! jambo hili hili Walaodekia katika upofu wao wanalitenda, na hivyo kurudia historia ya watu wa Mungu kupitia vizazi ote. {ABN4: 41.1}

ZAKA YANGU INAPASWA KWENDA KWA NANI?

Swali Namba 96:

Wakati bado nimeshikilia ushirika katika dhehebu la Waadventista wa Sabato, je! Mtu anapaswa kutoa zaka kwa Wadaudi? {ABN4: 41.2}

Jibu:

Mmoja anaweza kujibu swali hili vyema kwa

41

kujiuliza maswali yafuatayo: {ABN4: 41.3}

Je! Ninaamini kwamba Fimbo ya Mchungaji inasheheni ujumbe wa saa, ujumbe wa kuwatia muhuri watu 144,000? Je! Nimepokea msaada wowote wa kiroho kutoka kwa huo? Je! Umesababisha nitubu dhambi nilizopendelea awali? Je! Mimi sasa ni Mwadventista wa Sabato bora kuliko nilivyokuwa kabla ya kuupokea? Je! Umenifanya niipende Biblia, Roho ya Unabii, na wandugu zaidi kuliko hapo awali? {ABN4: 42.1}

Iwapo jibu la mmoja kwa kila mojawapo wa maswali haya ni “La,” basi anapaswa kulipa zaka yake kwa kanisa ambalo yeye bado ni mshiriki. Ikiwa jibu lake kwayo ni “Naam,” na iwapo bado ana shaka kuhusu ni wapi anapaswa kulipa zaka yake, basi anapaswa kujihoji zaidi: {ABN4: 42.2}

Ningalikuwa nimeendelea katika mwenendo wa Ulaodekia ambao Fimbo ilinipata ndani, ningeokolewa na kuwa tayari kukutana na Bwana wakati wa kuja Kwake? Je! Ndugu zangu Waadventista wa Sabato wanaweza kuokolewa kwa kusalia katika hali yao ya sasa? {ABN4: 42.3}

Iwapo kwa maswali haya jibu la mtu ni “La,” basi majibu yake kwa maswali yafuatayo yatamwelekeza ni wapi atalipa zaka yake. {ABN4: 42.4}

Kwa kuwa mimi ninawajibika kwa nuru ambayo sasa inaangaza njiani mwangu, na kwa sababu lazima nisaidie kuipeana kwa ndugu zangu, ninapaswa kulipa zaka yangu kwa Dhehebu ili ukasisi uwe na fedha

42

zaidi za kutumia kuupiga vita ujumbe na juhudi zangu za kibinafsi kuwafikia watu nao, na hivyo, kufanya kazi kwa makusudi yanayopingana, kuwadumisha tu gizani? Au, niilipe kwa Wadaudi, “ghala” la Ukweli wa Sasa, ambapo kwa kawaida inapaswa kwenda kustawisha maendeleo ya matengenezo ya kuupekua moyo na kuwaokoa ndugu zangu Waadventista wa Sabato kutoka kwa maangamizo ya milele? Na kwa sababu wao wenyewe hawajajiandaa kukutana na Bwana (Shuhuda, Gombo la 6, uk. 371), basi wanawezaje kuwandaa washenzi kikamilifu? Kwa kuzingatia kweli hizi zote, je, zaka yangu itaenda kwa dhehebu la Waadventista wa Sabato kwa niaba ya washenzi au ujumbe wa kutia muhuri kwa niaba ya ndugu? Iwapo sithubutu kuweka zaka yangu kwa udhamini wa lile ninaloamini kuwa ni Ukweli wa Sasa, basi utadhaminiwaje, na ni wapi kwingine naweza kuweka zaka yangu kwa kufuata dhamiri? {ABN4: 42.5}

Isitoshe, iwapo nitaiweka katika Dhehebu itumike kwa kiasi kikubwa kuwahubiria walimwengu, badala ya ghala la Ukweli wa Sasa kutumika kwa manufaa ya ndugu zangu, basi nitakuwa nafanya hivyo kwa kuwapuuza ndugu zangu, na hivyo kukataa kwamba mimi ni mchungaji wa ndugu yangu? {ABN4: 43.1}

Na ninapaswa, zaidi ya hayo, kutii amri ya mchungaji kwenda kuwatafuta kondoo katika nyumba ya Baali, badala ya kutii amri ya Bwana kupeleka dawa iliyotumwa kutoka mbinguni kwa

43

kondoo wagonjwa wadhambi katika nyumba ya Israeli (Mat. 10:6)? Ni ipi kati ya juhudi hizi mbili ambayo itakuwa na uhakika zaidi kunipatia pongezi, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu: ulikuwa mwaminifu kwa machache, Nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya Bwana wako”? Mat. 25:21. {ABN4: 43.2}

“Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye Bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye Bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.” Mat. 24:45, 46. {ABN4: 44.1}

Sasa iwapo baada ya kujibu maswali haya kwa kuridhika kwako, bado hujaamua ni nini unapaswa kufanya na zaka yako, basi soma Trakti Namba 4, Habari za Hivi Punde kwa Mama, Toleo la 1943, uk. 63-70. Kisha “mkumbuke mke wa Lutu,” na utende jinsi Bwana atavyokuamuru. {ABN4: 44.2}

JE! NYUMBA YANGU HAIWEZI KUWA “GHALA” LAKE?

Swali Namba 97:

Je! Ni Kimaandiko kwa mtu kuhifadhi na kutumia kibinafsi zaka na sadaka yake ili kuendeleza kazi ya injili katika jumuiya yake mwenyewe, kwa mujibu wa mipango yake mwenyewe? {ABN4: 44.3}

Jibu:

Hakuna popote katika Maandiko tunapata idhini ya kutumia pesa za Bwana kwa akili

44

zetu wenyewe. Uthibitisho pekee wa kufanya hivyo utakuwa kutokuwa na uwezo kabisa, kwa sababu fulani kuipeleka katika “ghala” la Bwana. Ikiwa mtu kwa hiari, hata hivyo, ajihusishe na mazoea kama hayo basi ataweza kuweka mfano mbaya mbele ya wengine. Na iwapo kwa kufuata mwongozo wake, wengine watachukua haki iyo hiyo, mwenendo wao lazima pasipo kuepukika utasababisha kulemazwa kwa kazi ya Bwana, kuifanya ivuje damu na kuipindua hazina Yake, na hivyo kuvuruga kazi Yake na kulipunguza kanisa kuwa gamba tu, wakati washirika wake wanajiajiri wenyewe kama watendakazi katika shamba la mizabibu la Bwana, wakijisaidia wenyewe kwa pesa za Bwana, na kukimbia bila kutumwa! Ingekuwa Babeli ilioje! {ABN4: 44.4}

Ingawa Bwana huamuru, “Leteni zaka kamili ghalani” (Mal. 3:10), Yeye hasemi leteni sadaka zote. Kwa hivyo, Yeye huonyesha kwamba iwapo tutahusika katika ukarimu wa kibinafsi au shughuli za umishonari, tunapaswa kuzidhamini kutoka kwa sadaka, sio kutoka zaka. {ABN4: 45.1}

“Malaika huhifadhi kumbukumbu ya uaminifu ya kila kazi ya mtu, na wakati hukumu inapita kwa nyumba ya Mungu, kauli ya kila mmoja hunakiliwa kando ya jina lake, na malaika anaagizwa kutowasaza watumwa wasio waaminifu, bali kuwakata kabisa wakati wa mchinjo….Na taji ambazo wangeweza kuvaa, wangalikuwa waaminifu, zinawekwa juu ya vichwa vya wale waliookolewa na watumwa waaminifu ….” Shuhuda, Gombo la 1, uk. 198. {ABN4: 45.2}

45

JE! NI WAJIBU WANGU KUREKEBISHA HAZINA YA BWANA?

Swali Namba 98:

Je! Tunapaswa kulipa zaka yetu kwa “ghala” iwapo tunajua kwamba haitumiwi kwa usahihi? {ABN4: 46.1}

Jibu:

Tukijua kwamba zaka yetu ni mali ya ghala la Mungu, mzigo wetu mkubwa unapaswa kuwa kuona kwamba inalipwa kwa uaminifu pale. Hakuna popote katika Biblia ambapo tunaona kwamba Bwana amemtwika kila mlipa zaka kurekebisha njia ambazo fedha hizi hupitia. {ABN4: 46.2}

Hazina ya Bwana iko chini ya udhibiti Wake, na iwapo Yeye Mwenyewe hataona inafaa kurekebisha dhuluma katika matumizi mabaya ya migawo ya pesa Zake, hakika hatuwezi kuzirekebisha hata kama tutajaribu kwa bidii. Iwapo tutalinda kwa uangalifu ile sehemu ya kazi ambayo Yeye hutupatia, wasiwasi wetu tu utakuwa kujua ni wapi “ghala Lake” lilipo, kisha kwa uaminifu kuweka pesa Zake hapo. Yeye hajatuweka tuwajibike kwa matumizi yake; ya kwamba, Yeye binafsi atachukua hatamu — hata jinsi ambavyo Yeye hivi sasa “anachukua mamlaka mikononi Mwake.” {ABN4: 46.3}

Wakati Nchi ya Ahadi iligawanywa kati ya kabila kumi na mbili za Israeli, kabila la Lawi halikupata ardhi ya urithi, kama zilivyopata kabila kumi na moja. Badala yake, Bwana aliamuru kwamba zaka za kabila zingine zilipaswa kwenda kwa Walawi. Huu ulikuwa urithi wao. Kwa kweli ulikuwa wao wenyewe. Na

46

jinsi wao, kama wapokeaji wa zaka, hawakuwa na haki ya kuwaamuru wengine, walipa kodi wa zaka, yale walipaswa kufanyia kwa ongezeko lao wenyewe baada ya kuondolewa zaka, kwa hivyo walipa zaka hawakuwa na haki ya kuamuru wapokea zaka la kufanyia zaka. Kila kabila lilikuwa lenyewe linamwajibikia Bwana kwa yale Aliyokuwa amelikabidhi. Lazima iwe hivyo leo. {ABN4: 46.4}

JE! NI NINI KINACHOSTAHILI KUWA ZAKA?

Swali Namba 99:

Kumbukumbu la Torati 14:22 husema: “Usiache kutoa zaka katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.” Je! Nitatoa vipi zaka kwa mazao yangu? {ABN4: 47.1}

Jibu:

Ili kuwezesha kulijibu swali hili, hebu tuchunguze kwa mfano kisa cha mkulima wa viazi. Sema kwamba yeye hana gharama ya watu walioajiriwa kazi, unyunyiziaji maji, kodi, n.k. Akiwa huru kwa gharama kama hizo na ikiwa mapato yake ya jumla ni $ 50 kwa ekari, basi kiasi hicho chote kitatozwa zaka, ambayo bila shaka itakuwa $ 5 kwa ekari. Iwapo, hata hivyo, lazima afanye kazi kwa gharama za matumizi ili kuzalisha mazao yake, basi ni dhahiri kwamba gharama hizo zinapaswa kutolewa kwa thamani ya jumla ya mazao, na salio tu kutozwa zaka. Kwa mfano, iwapo jumla ya mazao ni $ 50 kwa ekari, na gharama za kuzalisha ni $ 10 kwa ekari, basi ongezeko la jumla baada ya kutoa gharama, kiasi cha kutozwa zaka,

47

kitakuwa ni $ 40 kwa ekari, na zaka $ 4 tu badala ya $ 5 kwa ekari. {ABN4: 47.2}

Iwapo, kwa upande mwingine, mtu ni mpokeaji wa mshahara, kuruzuku gharama ya usalama wa kijamii, usafiri kwenda na kutoka kazini, n.k., basi atatoa kiasi cha gharama hizo kutoka kwa mshahara wake kabla ya kutoa zaka. Kwa mfano, ikiwa yeye hupokea mshahara wa $ 100 kwa mwezi, na iwapo lazima atumie senti 10 kwa siku, au karibu $ 2.60 kwa mwezi, kwa usafiri, basi atatoa $ 2.60 kutoka kwa $ 100, ambazo zinaacha $ 97.40 za kutozwa zaka. {ABN4: 48.1}

Iwapo mapato ya mtu ni kutoka kwa kodi, basi ataondoa kiasi kinachotumika kwa utunzi wa mali hiyo kutoka kwa mapato yake yote ya jumla ambayo hayajatozwa zaka. Kuhesabu hivyo mapato ya mtu, mtu hutoza zaka ongezeko lake lote. {ABN4: 48.2}

VIPI KUHUSU KUTOZA ZAWADI ZAKA?

Swali Namba 100:

Kwa sababu Biblia hufundisha kwamba mtu anapaswa kutoa zaka kwa ongezeko lake lote, je! mtu hapaswi kutoa zaka kwa zawadi zote? {ABN4: 48.3}

Jibu:

Likitumika kama nomino, neno “ongezeko” humaanisha “ile iliyoongezwa kwa hisa ya asili; faida” — mapato kutoka kwa kazi au urithi wa mtu. Kwa sababu hatujui iwapo inaweza kwa hivyo Kimaandiko kueleweka kuamuru kutoa zaka kwa zawadi ndogo za upendo, uamuzi lazima haswa uwe wa mtu mwenyewe. {ABN4: 48.4}

48

JE! NI “BIMA” GANI WAKRISTO WANAPASWA KUWA NAYO?

Swali Namba 101:

Je! “Bima ya mazishi” huja chini ya mada “bima ya maisha”? {ABN4: 49.1}

Jibu:

Katika asili yake haswa, bima ya mazishi ni aina ya kinachojulikana eti “bima ya maisha.” Kuiweka hivyo, hata hivyo, sio kuihukumu moja kwa moja. Roho ya Unabii hutoa ushuhuda dhidi ya bima ya maisha, si sana kwa sababu ni bima ya maisha, lakini kwa sababu ulimwengu unaiendesha badala ya kanisa. {ABN4: 49.2}

Iwapo uongo na aibu katika shughuli hii sio dhahiri mara moja, huwa dhahiri kwa uchungu wakati mtu akijiuliza mwenyewe maswali: Je! Raia mwaminifu na wa kweli wa Ufalme wa Kristo anapaswa kutafuta msaada au kinga kutoka kwa raia wa ufalme mwingine? Je! Bwana ameuteua ulimwengu au kanisa kuwatunza watu Wake? Je! Yeye huwauliza watoto Wake wakatize mahusiano yote na ulimwengu wakati wako vyema, lakini kuwarudisha wauelekee wanapokuwa kwenye dhiki, ugonjwa, au kifo, ili uwatunze? Je! Wakristo wanapaswa kumtumainia Kristo wakati wako vyema, na kwa Ibilisi wanapokuwa wagonjwa au wanapokufa? Je! Bwana hajalipatia kanisa upendeleo wa kupokea baraka hata kwa kumwesha mmojawapo wa wadogo Wake angaa kikombe cha maji (Mat. 10:42)? {ABN4: 49.3}

49

Majibu yanajithibitisha yenyewe kwa haya na kwa maswali yanayofanana nayo. Yakijumlishwa, yanatoa jibu lote sahihi: Kamwe washiriki wa kanisa hawapaswi kuutegemea ulimwengu. Wanapaswa kulitegemea kanisa tu. Likiwakata manyoya washiriki wake kama mchungaji awakatavyo manyoya kondoo wake kikamilifu wakiwa vyema na wenye “manyoya” ya kutoa, kanisa limefungwa kimaadili kutunza kila mmoja akiwa mgonjwa au kilema na bila kitu chochote cha kutoa, na kisha kumwandalia kila mmoja wao mazishi ya mtakatifu. Kwa hivyo, kanisa linaloruhusu washiriki wake kuchukua sera yoyote ya bima ya kibinafsi isipokuwa na kanisa lenyewe linaudhalilisha Ukristo na hivyo kumdharau Bwana. Na Mkristo ambaye hupuuza kujiweka anayestahili sera ya bima ya kanisa ni kama mtu mpumbavu ambaye huijenga nyumba yake kwa mchanga. Mahitaji ya walei yakiwa karibu yamepuuzwa kabisa, Fimbo sasa inatupigia kelele kwa dharura kwamba sisi, kama waamini wa Ukweli wa Sasa na wana-matengenezo, tuje kwa msaada wa Bwana na mara moja turekebishe maovu haya. {ABN4: 50.1}

Wachungaji wa Mungu hawajaitwa kuwa wauzaji, watangazaji wa biashara, au madalali ili kuchanga fedha za kuiendeleza kazi Yake. Badala yake wameitwa kuwa wahubiri wa Ukweli na wachungaji wadogo wa watu Wake, wakimchunga kila kondoo kwa upole, kwa kuwa wanastahili kutunzwa na kulindwa vema sio tu katika afya bali katika ugonjwa, sio tu maishani bali katika kifo. Ni aibu kwa Kristo wakati

50

watu Wake wameachwa kwa ulezi ama wa kampuni za bima za ulimwengu au kwa rehema za jumuiya za ufadhili za ulimwengu. Kanisa kwa maadili kwa haki lina wajibu kuinyosha mikono yake ya kama mama kwa watoto wake na kuwatunza. {ABN4: 50.2}

Kwa hivyo kama wahifadhi wa kanisa, tunakabiliwa na jukumu hili pia, na tusithubutu kushindwa. Jukumu hili kubwa, pamoja na lile la kuutekeleza mpango wetu wa ukarabati katika Makao makuu ya “kazi ya kufunga kwa kanisa” linahitaji, kwa kweli, kiwango kikubwa zaidi cha fedha kuliko zaka ya kwanza tu, mapato ya ukasisi. Nini basi? {ABN4: 51.1}

Hatuwezi kuiga mazoea ya dhehebu ya kuinua malengo wakati wa ibada za kanisa, kwa maana mazoea kama hayo huondoa fikira kwa kusudi la mikutano, na hunajisi nyumba ya Mungu na Siku Yake Takatifu. Biashara kama hiyo isiyo takatifu kwa ardhi takatifu lazima ikome! Usingoje hadi Bwana adhihirishe uwezo Wake mkubwa, na kuwafukuza nje kondoo na ng’ombe pamoja na wanaobadisha fedha, Akazipindua-pindua meza zao, na kuyatawanya mapato yao haramu! {ABN4: 51.2}

Ujumbe kwa hivyo hutangaza bayana kwamba Wadaudi watakaompendeza Bwana, watachangia kwa uaminifu na kwa kimfumo zaka ya pili ya ongezeko lake kwenye mfuko huu muhimu, na kwa hivyo kusaidia kujenga ukuta wa ulinzi dhidi ya uwezekano wa Adui kuleta biashara ya

51

uovu, inayopoteza wakati na kuua roho ndani ya makongamano yetu ya ibada na elimu. Kwa kufanya hivyo, kila mwamini mwaminifu atakuwa amewekeza moja kwa moja katika sera hii takatifu ya bima ambayo italinda mahitaji yake mwenyewe na ya familia yake sio tu katika maisha haya lakini pia katika maisha ya baadye. {ABN4: 51.3}

Ikiwa mapato ya mmoja ni $ 15 kwa juma, basi zaka yake ya kwanza itakuwa $ 1.50; na zaka yake ya pili kwa salio la $ 13.50 itakuwa $ 1.35. Kwa hivyo, zaka yake ya kwanza na ya pili kutoka kwa ongezeko la $ 15 itakuwa kwa jumla $ 2.85. Je! Hizi ni nyingi sana, Ndugu, Dada, kwa kazi kubwa na kuu kama ile iliyowasilishwa katika ujumbe wa Udaudi, muhimu sana kwa wokovu wako na maslahi yako? {ABN4: 52.1}

Hebu waamini wote wa Ukweli wa sasa walipe kwa uaminifu zaka ya kwanza na ya pili iwezekanavyo, kisha Jumuiya inaweza kudumisha shule yake ya wachungaji, pamoja na shule yake ya mabweni kwa ajili ya watoto wote wahitaji na wanaostahili katika Ukweli wa Sasa ambao ni wa umri wa kwenda shuleni, na kutoa makao kwa walio wakongwe, huduma ya matibabu kwa wagonjwa wastahiki, chakula kwa wenye njaa, na mazishi kwa wale ambao hufa katika zamu zao za kazi. {ABN4: 52.2}

Huu mwito wa dharura na pia wa mtihani, Ndugu na Dada, unatoa changamoto kwa uaminifu wako, utiifu wako, ushirikiano wako, maono yako kamili), kuelewa ujumbe, na upendo wako kwa urithi wa Bwana. Amka, kwa hivyo, uangaze! {ABN4: 52.3}

“ Je! Saumu Niliyoichagua, sio ya namna hii?”

52

anauliza Bwana, “kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? {ABN4: 52.4}

“Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, Naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye Bwana atakuongoza daima, Ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, mwenye kurejeza njia za kukalia.” Isa. 58:6-12. {ABN4: 53.1}

“Michango iliyohitajika kwa Waebrania kwa ajili ya madhumuni kidini na hisani

53

ilifikia jumla ya robo ya mapato yao. Ushuru mzito sana kwa rasilimali za watu unaweza kutarajiwa kuwafanya waweze kuwa maskini; lakini, kinyume chake, kuyazingatia kwa uaminifu maagizo haya ilikuwa mojawapo wa kanuni za ufanisi wao. Kwa sharti la utiifu wao, Mungu aliwaahidi hivi: ‘Nami kwa ajili yenu Nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba….Na mataifa yote watawaiteni wenye heri maana mtakuwa nchi ya kupendeza, asema Bwana wa majeshi.’” — Mababu na Manabii, uk. 527. {ABN4: 53.2}

“Wakati Paulo alimtuma Tito kwenda Korintho ili kuwaimarisha waamini huko, alimwagiza…kwa neema ya kutoa….Ukarimu wao ulishuhudia kwamba hawakuwa wameipokea neema ya Mungu [ujumbe] bure. Ni nini kingeweza kutoa ukarimu kama huu isipokuwa utakaso wa Roho?… {ABN4: 54.1}

“Ufanisi wa kiroho unafungamana kwa karibu na ukarimu wa Mkristo. Wafuasi wa Kristo wanapaswa kufurahi katika fursa ya kufunua katika maisha yao manufaa ya Mkombozi wao. Wanapotoa kwa Bwana, wana uhakikisho kwamba hazina yao inawatangulia hadi kwa nyua za mbinguni….Mpanzi huzidisha mbegu yake kwa kuitupa….Kwa kutoa wao huongeza baraka zao.” — Matendo ya Mitume, uk. 344, 345. {ABN4: 54.2}

Kanisa, kwa hivyo, liko chini ya wajibu

54

mzito wa maadili, na pia halali, wajibu sio tu kuendesha bima kwa wafuasi wake wote wa kweli na waaminifu lakini pia kutunza mahitaji yao yote wakati wowote watakapokuwa hawajiwezi, jinsi ilivyo kwa washiriki wake kuidhamini kazi yake na kutii ujumbe wake mtakatifu. {ABN4: 54.3}

Kuweka jukumu hili lililowekwa na Mungu kwa watu, na mchungaji wao wa Laodekia kutolijali kabisa, pia matokeo ya mwisho ya uzembe wao kwa wajibu, Ezekieli huonya: {ABN4: 55.1}

“Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji … Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; kama Mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, kwa sababu kondoo Zangu walikuwa mateka, kondoo Zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji Wangu hawakutafuta kondoo Zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo Zangu; kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; Bwana Mungu asema hivi; tazama, Mimi ni juu ya wachungaji; Nami nitawataka kondoo Zangu mikononi mwao, Nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; Nami nitawaokoa kondoo Zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. {ABN4: 55.2}

“Maana, Bwana Mungu asema hivi; tazama, Mimi Mwenyewe, naam, Mimi, nitawatafuta kondoo Zangu, na kuwaulizia. Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake

55

waliotawanyika; ndivyo Nitakavyowatafuta kondoo Zangu; Nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza. Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, Nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; Nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu. Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. {ABN4: 55.3}

“Mimi mwenyewe Nitawalisha kondoo Zangu, Nami nitawalaza, asema Bwana Mungu. Nami nitawatafuta waliopotea, Nitawarudisha waliofukuzwa, Nitawafunga waliovunjika, Nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu Nitawaharibu; Nitawalisha hukumu. {ABN4: 56.1}

“Na kwa habari zenu, Enyi kundi Langu, Bwana Mungu asema hivi; Tazama, Nahukumu kati ya ng’ombe na ng’ombe, kondoo waume na beberu pia. Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kula malisho mema, hata mkawa hamna budi kukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyatibua kwa miguu yaliyobaki? Na kwa habari za kondoo Zangu, wao wanakula hayo mliyoyakanyaga kwa miguu yenu, nao wanakunywa maji mliyoyatibua kwa miguu yenu. {ABN4: 56.2}

56

“Kwa sababu hiyo, Bwana Mungu awaambia hivi; Tazama, Mimi, naam, Mimi, Nitahukumu kati ya ng’ombe walionona na ng’ombe waliokonda. Kwa kuwa mmesukuma kwa ubavu, na kwa mabega, na kuwapiga wenye maradhi kwa pembe zenu, hata mkawatawanyia mbali; basi Mimi Nitaliokoa kundi Langu, wala hawatakuwa mateka tena; nami nitahukumu kati ya ng’ombe na ng’ombe. {ABN4: 57.1}

“Nami Nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi Wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Nami, Bwana, Nitakuwa Mungu wao, na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; Mimi, Bwana, Nimesema haya. {ABN4: 57.2}

“Nami Nitafanya agano la amani nao, Nami Nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama nyikani, na kulala misituni. Nami Nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima Wangu, kuwa baraka, Nami Nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka. Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, Nitakapovunja vifungo vya kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha. Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala mnyama

57

wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu. {ABN4: 57.3}

“Nami Nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala hawatachukua tena aibu ya makafiri. Nao watajua ya kuwa Mimi, Bwana, Mungu wao, ni pamoja nao, na ya kuwa wao, nyumba ya Israeli, ni watu Wangu, asema Bwana Mungu. Na ninyi, kondoo Zangu, kondoo za malisho Yangu, ni wanadamu, na Mimi ni Mungu wenu, asema Bwana Mungu.” Ezek. 34:2, 7-31. {ABN4: 58.1}

NI NANI WANAOSTAHILI SADAKA?

Swali Namba 102:

Je! Ni nani “maskini wanaostahili”? {ABN4: 58.2}

Jibu:

“Maskini wanaostahili” ni wale ambao kupitia misiba, sio kwa njia ya matumizi mabaya au uvivu, wamepungukiwa mahitaji ya maisha, na ambao kwa uaminifu wanajitahidi kutembea katika nuru yote ambayo wamepewa. {ABN4: 58.3}

“Kusudi la maneno ya Mwokozi wetu katika Luka 12:33, hayajawasilishwa waziwazi. Naliona kwamba lengo la kuuza sio kuwapa wale ambao wanaweza kufanya kazi na kujisimamia wenyewe, lakini ni kueneza ukweli. Ni dhambi kusaidia na kuwaendeleza katika uvivu wale ambao wanaweza kufanya kazi. Wengine wamekuwa na bidii ya kuhudhuria mikutano yote, sio kwa utukufu wa Mungu,

58

ila kwa “mikate na samaki.” Kama hao ingekuwa bora kwao kuwa nyumbani wakifanya kazi kwa mikono yao, “mambo ambayo ni mazuri,” kukidhi mahitaji ya familia zao, na kuwa na kitu cha kutoa ili kuitegemeza kazi ya thamani. “ — Maandishi ya Awali, uk. 95. {ABN4: 58.4}

Maagizo yaliyovuviwa kwa kanisa (1 Tim. 5:9), hushauri kwamba hakuna mjane aliye na umri chini ya miaka sitini ambaye atalitegemea kanisa kwa mahitaji yake. {ABN4: 59.1}

Kwa jumla, kwa hivyo, tunaona kwamba maskini wanaostahili ni wale washirika waaminifu ambao shida imewapora raslimali za maisha. Na tunahitaji kukumbuka vyema kwamba bahati mbaya hii inaweza kumpata yeyote kati yetu wakati wowote, maana, kama ilivyoandikwa, “wakati na nafasi huwapata wote.” Mhu. 9:11. {ABN4: 59.2}

“Kwa kadiri tupatavyo nafasi,” asema Paulo, “na tuwatendee watu wote mema, na hasa jamii ya waaminio” (Gal. 6:10), kwa wale ambao wanayo Hati ya Ushirika. {ABN4: 59.3}

JE! ZAKA YA PILI HUTUMIKA KWA NINI?

Swali Namba 103:

Je! Zaka ya pili huwekwa kwa madhumuni gani? {ABN4: 59.4}

Jibu:

“Kwa kuendeleza kukusanyika kwa watu kwa ajili ya huduma ya kidini, pamoja na kuwakimu maskini, zaka ya pili ya ongezeko lote ilihitajika.

59

Kuhusu zaka ya kwanza, Bwana alitangaza, ‘Nimewapa wana wa Lawi sehemu yote ya kumi katika Israeli.’ Lakini kuhusiana na ya pili, aliamuru, ‘Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana Mungu wako daima.’ Hivyo zaka, au ulingano kifedha, iliwapasa kwa miaka miwili kuileta mahali ambapo hekalu lilikuwa limesimamishwa. Baada ya kuwasilisha sadaka ya shukrani kwa Mungu, na fungu maalum kwa kuhani, walioitoa walipaswa kutumia salio kwa ajili ya karamu ya kidini, ambayo Mlawi, mgeni, yatima, na mjane walipaswa kushiriki. Hivyo maakuli yaliandaliwa kwa ajili ya sadaka za shukrani na karamu katika sherehe za kila mwaka, na watu walikaribishwa kwa jumuiya ya makuhani na Walawi, ili waweze kupokea maagizo na kuhimizwa katika utumishi wa Mungu. {ABN4: 59.5}

“Kila mwaka wa tatu, hata hivyo, zaka hii ya pili ilitumiwa nyumbani, kwa kuwakirimu Walawi na maskini, jinsi Musa alivyosema, ‘Ili waweze kula ndani ya malango yako, na kushiba.’ Hii zaka inaweza kutoa mfuko wa matumizi ya hisani na ukarimu.” {ABN4: 60.1}

“Na matoleo zaidi yalifanywa kwa ajili ya maskini. Hakuna kitu, baada ya wao kutambua madai ya Mungu, ambacho hutofautisha zaidi sheria zilizotolewa na Musa kuliko roho ya ukarimu, ya upole na ya ukaribishaji

60

inayoagizwa kwa ajili ya maskini. Ingawa Mungu alikuwa ameahidi sana kuwabariki watu Wake, haukuwa mpango Wake kwamba umaskini usijulikane kabisa kati yao. Alitangaza kwamba maskini hawatakoma milele katika nchi. Daima watakuwapo miongoni mwa watu Wake wale ambao wataita kwa matumizi huruma zao, upendo mwororo, na ukarimu. Wakati huo, kama sasa, watu walikumbwa na misiba, ugonjwa, na kupoteza mali; Bado mradi waliyafuata maagizo waliyopewa na Mungu, hawakuwapo ombaomba kati yao, wala yeyote aliyeateseka kwa kukosa chakula. {ABN4: 60.2}

“Sheria ya Mungu ilimpa maskini haki kwa sehemu fulani ya mazao ya nchi. Wakati alipokuwa na njaa, mtu alikuwa na uhuru wa kwenda katika konde au shamba shamba la mizabibu la jirani yake, na kula nafaka au matunda ili kuondoa makali ya njaa. Ilikuwa ni kwa mujibu wa idhini hii ya kwamba wanafunzi wa Yesu walichuma na kula ngano iliyokuwa shambani walipokuwa wakipitia humo siku ya Sabato. {ABN4: 61.1}

“Masalio yote ya shamba la mavuno, bustani ya miti, na shamba la mizabibu, yalikuwa mali ya maskini. ‘Uvunapo mavuno yako katika shamba lako,” alisema Musa, ‘ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua…Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili….Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili. Zitakuwa za

61

mgeni, na yatima, na mjane. Nawe utakumbuka ya kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri. {ABN4: 61.2}

“Kila mwaka wa saba, maakuli maalum yalifanywa kwa ajili ya maskini. Mwaka wa Sabato, jinsi ulivyoitwa, ulianza mwishoni mwa mavuno. Wakati wa kupanda mbegu, uliofuatia wakati wa kukusanya, watu hawakupaswa kupanda; kutotilia mbolea shamba la mizabibu wakati wa masika, na kutotarajia kuvuna wala mavuno. Katika yale ambayo nchi ilizalisha yenyewe tu, wangeweza kula yakiwa mapya, lakini hawakupaswa kuweka sehemu yake katika maghala yao. Mazao ya mwaka huo yalipaswa kuwa ya uhuru kwa ajili ya mgeni, na yatima, na mjane, na hata kwa viumbe vya shambani. {ABN4: 62.1}

“Lakini iwapo ardhi ilizalisha kawaida tu kutosheleza mahitaji ya watu, wangewezaje kuishi wakati wa mwaka ambao hakuna mazao yaliyokusanywa? — Kwa ajili ya hili ahadi ya Mungu ilitoa vyakula vya kutosha. ‘Nitawaamuria baraka Yangu iwe juu yenu mwaka wa sita,’ Alisema ‘nao utazaa matunda hesabu ya miaka mitatu. Nanyi mtapanda mbegu mwaka wa nane, na bado mtakula matunda ya zamani hata mwaka wa kenda, hata matunda yake yatakapoletwa ndani mtakula akiba hiyo ya zamani.’” — Mababu na Manabii, uk. 530, 531. {ABN4: 62.2}

Kwa hivyo zaka ya pili, ikiwa kwa msingi wa hiari zaidi kuliko ile ya kwanza, ni muhimu sana, na kwa kweli imewekwa wakfu na Mungu, ni

62

mchango wa masafa marefu kwa maslahi ya mtu mwenyewe. Kwa sasa ni sehemu ya sadaka zetu za jumla. Zamani ilitumika kuendeleza kazi ya Shule yetu na kulipa madeni yake ya zamani. Lakini sasa, kadiri Jumuiya inakua na kupanuka, matumizi ya zaka ya pili pia yanapanuka. {ABN4: 62.3}

Katika nafasi ya kwanza, sasa hukidhi mahitaji ya ile sehemu ya kazi ya Kielimu ambayo zaka ya kwanza haiwezi kutumika kihalali. Na katika nafasi ya pili, hukidhi mahitaji ya maskini anayestahili. Kwa ufupi, ni sera ya bima halisi na ya pekee ya kweli kwa wote, na inapaswa kutekelezwa na Wadaudi wote ambao kwa kuhitimu wanashikilia Hati ya Ushirika. {ABN4: 63.1}

Kwa hivyo wakati ni muhimu kwamba waamini wote wa Ukweli wa Sasa wajipatie hii Hati ya Ushirika, ni kwa dharura zaidi ya kwamba hao wote waweze kuwa walipa zaka ya kwanza na ya pili, kwa sababu ikiwa Cheti cha Ushirika kimepokezwa kwa wale ambao wanaweza kuwa lakini sio walipa zaka, hawatakuwa tu mvuto wa kuharibu kati ya waamini lakini pia viini vya kufisha kati yao. Kwa sababu hii ya wazi Jumuiya kwa hivyo hulazimika kutoa tu Hati ya Ushirika kwa waamini kamili na watendaji wa Neno kwa moyo wa uchangamfu. (Katika hali ambapo haiwezekani kulipa zaka ya pili kamili, basi, kwa kweli, sehemu inakubalika.) {ABN4: 63.2}

Upuuzaji wa Dhehebu kuwatunza washirika wake, ulofa ambao u

63

chini ya hukumu nzito, unapaswa kuwa funzo kali kwetu sisi sote, kwamba sisi kama wana-matengenezo na wachukuzi wa ujumbe tusithubutu kushindwa. Tumebarikiwa kupajenga mahali pa kale palipoharibiwa, kupainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, na kutengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa ukiwa kwa vizazi vingi (Isa. 61:4), lazima ikiwa ni lazima tuukaze kila mshipa na kunyosha kila musuli ili kutii maagizo ya Bwana. Na zaidi katika suala hili kwa sababu ni kwa manufaa ya kimwili na vile vile ya kiroho ya kila mmoja wetu. Ni mpango wa uchumi salama kabisa — sehemu ya mpango uliosawazishwa ambao Musa alipewa na Mungu juu ya Mlima Sinai, na kwa muda mrefu umepuuzwa na kufunikwa. Na hivyo, ni mojawapo wa “taasisi takatifu” (Manabii na Wafalme, uk. 678) ambayo lazima irejeshwe “kabla ije ile siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana.” {ABN4: 63.3}

Kwa hivyo hebu kwa uaminifu na kwa busara tujiulize maswali haya: Iwapo tutaangukia mashirika ya misaada ya ulimwengu au kwa kampuni za bima za ulimwengu, basi sisi Wadaudi tunawezaje kuwa nguzo ya kanisa na kwa hivyo ya ulimwengu? Je! Bwana ameliteua kanisa au ulimwengu kuwatunza watu Wake wa kipekee? Ikiwa sisi, kama waokozi, hatuwezi kutunza mahitaji ya wale walio ulimwenguni, basi kidogo tunachoweza kufanya ni kuwatunza walio wetu wenyewe. {ABN4: 64.1}

“Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa:

64

anyweshwaye atanyweshwa mwenyewe.” Mit. 11:24, 25. {ABN4: 64.2}

“Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.” Mit. 20:4. {ABN4: 65.1}

“Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo Yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. {ABN4: 65.2}

“Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; Naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Bwana atakuweka uwe taifa takatifu Kwake, kama Alivyokuapia;

65

utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia Zake. {ABN4: 65.3}

“Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. Atakufunulia Bwana hazina Yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. {ABN4: 66.1}

“Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya.” Kumb. 28:1-13. {ABN4: 66.2}

NI NINI HUFANZA UMOJA?

Swali Namba 104:

Waamini wanawezaje kupata na kudumisha umoja kati yao wenyewe? {ABN4: 66.3}

Jibu:

Ili kumshinda Adui na kudumisha umoja na maelewano, hebu kila mwamini aache kutafuta makosa kwa ndugu zake; azichunge hatua zake mwenyewe na si zao; atambue kwamba wanayo fursa sawa na aliyo nayo yeye kujua tofauti kati ya haki na

66

makosa; achukue lake mwenyewe na sio jukumu lao; awaone wao kuwa ni bora kuliko yeye mwenyewe; na asitende na asiseme lolote asingependa wamtendee au kumwambia. {ABN4: 66.4}

Wacha kila mmoja atambue, kama vile Paulo alivyofanya, kwamba upendo — uvumilivu kwa njia ya upendo — ndio muhimu zaidi, wa dharura, na wa juu zaidi ya mafanikio yote: {ABN4: 67.1}

“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. {ABN4: 67.2}

“Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. {ABN4: 67.3}

“Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili,

67

iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.” 1 Kor. 13. {ABN4: 67.4}

Tenda hivi, Ndugu, na Ibilisi atakimbia na taabu zenu zitamfuata. {ABN4: 68.1}

Kumbuka kwamba “Shetani anaishi, na yu mwamilifu, na kila siku tunahitaji kumlilia Mungu kwa bidii ili atusaidie na nguvu za kumpinga. Maadamu Shetani anatawala tutakuwa na ubinafsi wa kutiisha, kushinda masumbufu! Na hakuna mahali pa kusimama, hakuna hatua ambayo tunaweza kufikia na kusema tumeshafikia kikamilifu. {ABN4: 68.2}

“Maisha ya Mkristo daima ni kuelekea mbele. Yesu hukaa kama msafishaji na mtakasaji wa watu Wake; na wakati sura Yake inadhihirishwa kikamilifu ndani yao, wao ni wakamilifu na watakatifu, na waliandaliwa kwa kuhamishwa bila kufa.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 340. {ABN4: 68.3}

Iwapo Wakristo hawatiani hatiani kamwe, hawatangazi kamwe makosa, mapungufu, kushindwa, na taabu za wengine, watajikuta wameungana sana hivi kwamba hakuna chochote chaweza kuvunja mshikamano wao wa Ukristo siku zote. Lakini roho kama hiyo ya umoja inaweza kudumishwa

68

tu na watu ambao hukaa chonjo juu yao wenyewe bila kuchoka, siku zote wakiona mamoja na kunena mamoja kwa kuziacha njia na mawazo yao wenyewe kwa kuyabadilisha na ya Bwana. {ABN4: 68.4}

Ni muhimu, kwa hivyo, ya kwamba kila mwamini wa Ukweli wa Sasa afundishe na kutekeleza Ukweli wa Sasa pekee — usifundishe upungufu au zaidi ya ule uliochapishwa, usifume ndani yake ufasiri wa kibinafsi au ujenzi, nadharia na maoni, na usifanye lolote dogo au zaidi kuliko vile ujumbe huhitaji. {ABN4: 69.1}

Hivyo kwa kuweka kando mawazo yenu na njia zenu wenyewe, na kujipatia za Bwana (Isa. 55:8, 9), katika ibada isiyowahusisha wengine kwa Roho wa Kweli, mtaelewana na kunena mambo mamoja. Basi ndivyo tu mtaweza kufukuza roho ya machafuko na kudumisha roho ya upendo na umoja. {ABN4: 69.2}

Na kwa sababu ipo nguvu na maisha ya kiroho pale tu ambapo kuna umoja, hakuna mshirika wa kundi la watu anayeweza kumudu kulipuuza jukumu lake la kudumisha umoja kama huu wa Ukristo. {ABN4: 69.3}

JE! NYUMBA INAPASWA KUWA VIPI?

Swali Namba 105:

Je! Unaweza tafadhali kuelezea Waefeso 5:22-24? {ABN4: 69.4}

Jibu:

“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume

69

ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; Naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” Efe. 5:22-24. {ABN4: 69.5}

Dhahiri, agizo hili takatifu humwagiza mke kumheshimu mumewe kama vile angemheshimu Bwana, mume ikiwa mwokozi wa muda wa familia, kwa maana Bwana ndiye mwokozi wa milele wa kanisa. “…Kristo…alivyolipenda kanisa, akajitoa Mwenyewe kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno.” Efe. 5:25, 26. Wakati anapolipuuza agizo hili takatifu, yeye hukiuka sheria ya Mungu. {ABN4: 70.1}

“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo Naye alivyolipenda kanisa.” Efe. 5:25. {ABN4: 70.2}

Kwa hivyo, jinsi lilivyo la kuunganisha na takatifu ni jukumu la mume kwa mkewe. Anapaswa kumwona kama Kristo anavyoliona kanisa Lake. Wakati wowote anapofanya pungufu kwa hili, yeye hukiuka sheria ya Bwana. {ABN4: 70.3}

Kwa hivyo, wakati kanisa lina jukumu la kumheshimu na kumtii Bwana wake, mke anapaswa kumheshimu na kumtii mumewe; na mume ana wajibu wa kumpenda na kumtunza mke wake jinsi Bwana anavyolipenda na kulitunza kanisa Lake. Kutoka kwa hili inafuata kwamba nyumba ya Bwana inafananishwa na nyumba ya mume. Vivyo hivyo, kwa njia ile ile jinsi Bwana huyadhibiti mambo ya nyumba Yake, kanisa, ndivyo mume anavyopaswa kudhibiti mambo ya nyumbani mwake, familia.

70

Na kwa sababu maslahi ya kanisa lenyewe hutegemea ushirikiano wake na mapenzi ya Bwana, vivyo hivyo maslahi ya familia hutegemea ushirikiano wake na mapenzi ya baba. Waziwazi zaidi, kwa hivyo, ni ukweli kwamba jinsi ambavyo Kristo hushikilia uongozi juu ya kanisa, ndivyo baba hushikilia uongozi juu ya nyumba. Na kama vile kanisa lililoongoka hufurahia kukipendeza Kichwa chake, Kristo, vivyo hivyo mke aliyeongoka hufurahia kukipendeza kichwa chake, mumewe. Katika hali hii ya furaha, mume na mke hugundua kwamba wao, kwa kweli, ni nafsi ya pili ya kila mmoja. {ABN4: 70.4}

“Lakini nataka mjue,” atangaza Paulo, “ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake. Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.” “Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana. Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu.” 1 Kor. 11:3-5, 11, 12. {ABN4: 71.1}

Uhusiano huu mzuri wa nyumba mara nyingi hudhoofishwa na kuharibiwa kwa matumizi mabaya ya pesa au na elimu potovu, au na yote mawili, kwa sababu kielelezo kitakatifu hakifuatwi. Bwana humdhamini mke Wake,

71

kanisa, lakini lenyewe hushughulika na chombo cha ubadilishaji, pesa, kulipia vitu ambavyo hununua; kwa hivyo, ingawa mume hudhamini nyumba, mke anapaswa hushughulika na pesa za vitu vinavyohitajika kuendesha nyumba. Na iwapo mume hupokea mapato ya kujikimu tu, basi zaidi anapaswa kumpa mkewe mshahara wake, ili aweze kufanya bajeti ya kukidhi mahitaji ya nyumbani hadi siku inayofuata ya mshahara. Mke anaposhughulika na pesa, manufaa makubwa yatapatikana, kwa maana, ni yeye pekee anayezitumia, na kwa hivyo ndiye pekee anayejua, vitu ambavyo vinahitajika nyumbani. Kwa hivyo akijua mipaka yake ya kifedha ya kila siku, atajua kwa usahihi kile anachoweza na kile ambacho hawezi kununua ili kuiendesha nyumba. {ABN4: 71.2}

Kwa kawaida, basi, ataona kwa uangalifu kwamba mahitaji muhimu sana tu ya nyumbani yanashughulikiwa kwanza, na hivyo kuzuia ununuzi zaidi wa bidhaa moja kwa upande wake, au kununua chache au bidhaa nyingine na mumewe, au kinyume chake — hali hii ya mwisho itatokea bila kuepukwa iwapo yeye (mume) hushikilia kamba za kipochi cha fedha na kumgawia (mkewe) kwa unyimivu kufanya ununuzi. Ukishughulikiwa jinsi inavyopaswa, mkoba wa fedha hautakosa fedha, na nyumba haitakuwa na upungufu, mafarakano, na kuvunjika. Kwa kweli, mume na mke wanapaswa kushauriana kila wakati kupata idhini ya pamoja kwa kila kitu wanachofanya. {ABN4: 72.1}

72

Iwapo, hata hivyo, mapato ya familia ni zaidi ya riziki tu, basi yeye na mke wanaweza pamoja kwa upana zaidi kupangilia mapato yao, kwanza wakijali gharama zilizopo za matumizi, kisha waweke benkini au kuwekeza yaliyosalia. {ABN4: 73.1}

Kwa hivyo kuelewa kwamba mume sio tu mkoba wa pesa, lakini ni mfalme wa nyumba, “ukanda wa nyumba,” na ya kwamba mke sio mjakazi tu wa kupika milo, kuosha vyombo na nguo, kusafisha sakafu, na kuwatunza na kuwalea watoto, lakini ni malkia wa nyumba, msaidizi, — kuelewa yote haya ni kuthamini kikweli afya ya ndoa iliyovuviwa na Mungu. {ABN4: 73.2}

“Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikebu za biashara; huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla haujaisha usiku; huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; kwa mapato ya mikono yake

73

hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya wema i katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; mumewe naye humsifu, na kusema, binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.” Mit. 31:10-30. {ABN4: 73.3}

Kwa hivyo wakati mke mmalkia huchunga maswala ya ndani ya familia, mume mfalme huchunga maswala ya nje ya familia. {ABN4: 74.1}

Zaidi ya hayo, kwa sababu Bwana Mwenyewe ndiye Mkuu wa kanisa Lake kama shule, na “mke” Wake (kanisa, lakini haswa ukasisi — wale wanaoleta waongofu, watoto, katika imani), mwalimu wa watoto wao (washiriki), kwa hivyo mume ndiye mkuu wa nyumba yake kama shule, na mkewe mwalimu wa watoto wao. {ABN4: 74.2}

74

“Kupata uelewa sahihi juu ya uhusiano wa ndoa,” yanena Roho ya Unabii, “ni kazi ya maisha yote. Wale wanaofunga ndoa huingia shule ambayo kamwe katika maisha haya hawatahitimu. {ABN4: 75.1}

* * *

“Katika muungano wenu wa maisha mapenzi yenu yanapaswa kuingiana na furaha ya kila mmoja….Lakini wakati mnapatana kama mmoja, wala kati yenu mume au mke asiipoteze nafsi yake ndani ya mwingine. Mungu ndiye mmiliki…Mtamuuliza Yeye:… Nitawezaje kutimiza kusudi la uumbaji wangu?…Upendo wenu kwa kile ambacho ni cha mwanadamu ni lazima uwe wa pili kwa upendo wenu kwa Mungu…Je! Mmiminiko wa upendo wako ni mmkubwa Kwake aliyekufilia? Iwapo ni hivyo, mapenzi yenu kwa kila mmoja yatakuwa kwa mpangilio wa Mbingu. {ABN4: 75.2}

* * *

“Mume wala mke asifanye dai la kutawala…Wote ni lazima wakuze roho ya upole, wakiazimia kutomhuzunisha au kumjeruhi mwenzi wake….Msijaribu kulazimishana kutenda jinsi kila mmoja anavyotaka. Hamwezi kufanya hivi, na kudumisha upendo wa kila mmoja. Udhihirisho wa kujitakia makuu utaharibu amani na furaha ya nyumbani. Msiruhusu maisha yenu ya ndoa yawe ya ushindani. Mkifanya hivyo, ninyi wawili hamtakuwa na furaha. Muwe wema katika usemi na wapole katika kutenda, mkiyaacha matakwa yenu wenyewe. Chunga vema maneno yenu, kwa maana yana mvuto wa nguvu kwa mema au mabaya. Msiruhusu ukali wowote kuja ndani ya

75

sauti zenu. Leteni katika maisha yenu ya muungano manukato ya mfano wa Kristo. {ABN4: 75.3}

“Kabla mwanamume kuingia katika muungano wa ukaribu kama uhusiano wa ndoa, anapaswa kujifunza jinsi ya kujidhibiti na namna ya kushughulika na wengine. {ABN4: 76.1}

* * *

“Ndugu yangu, uwe mpole, mwenye subira, na mvumilivu. Kumbuka kwamba mke wako alikukubali kama mume wake, si kwamba uweze kumtawala, bali ya kwamba uweze kuwa msaidizi wake…. {ABN4: 76.2}

“Ushindi mmoja ni muhimu hakika kwa ajili yenu kuupata, — ushindi dhidi ya nia ya ukaidi. Katika pambano hili mwaweza kushinda tu kwa msaada wa Kristo. Mwaweza kujitahidi kwa bidii na kwa muda mrefu kuishinda nafsi, lakini mtashindwa isipokuwa mpokee nguvu kutoka juu. Kwa neema ya Kristo mwaweza kupata ushindi dhidi ya nafsi na ubinafsi. Kadiri mnavyoishi maisha Yake, mkionyesha kujitolea kwa kila hatua. Daima mkionyesha huruma kwa wale wanaohitaji msaada, mtapata ushindi juu ya ushindi. Siku kwa siku mtajifunza vyema jinsi ya kuishinda nafsi na namna ya kuimarisha udhaifu wenu mbalimbali wa tabia. Bwana Yesu atakuwa nuru yenu, nguvu yenu, taji yenu ya kufurahi kwa sababu mmeyatiisha mapenzi yenu kwa mapenzi Yake….Kwa msaada Wake mwaweza kuliharibu kabisa shina la ubinafsi. {ABN4: 76.3}

* * *

“Ustahimilivu na ukarimu hutia alama kwa maneno na matendo ya wale ambao

76

wamezaliwa mara ya pili, kuishi maisha mapya ndani ya Kristo.” — Shuhuda, Gombo la 7, uk. 45-50. {ABN4: 76.4}

“Vuguvugu kubwa la matengenezo lazima lianze katika kuwasilisha kwa kina baba na mama na watoto kanuni za sheria ya Mungu….Onyesha kwamba utiifu kwa neno la Mungu ndio ulinzi wetu pekee dhidi ya maovu ambayo yanaifagilia dunia hadi kwa uharibifu….Kwa mfano na mafundisho yao [ya wazazi], hatima ya milele ya familia zao itaamuliwa kwayo katika hali nyingi…. {ABN4: 77.1}

“Iwapo wazazi wangeweza kuongozwa na kufuatilia matokeo ya hatua yao,…wengi wangevunja mvuto wa mila na desturi…. Kukazia kwa dhamiri ya wazazi usadikisho wa majukumu yao mazito, yaliyopuuzwa kwa muda mrefu. Huu utavunja roho ya Ufarisayo na upinzani kwa ukweli kuliko kitu kingine kinavyoweza. Dini nyumbani ndilo tumaini letu kuu, na hufanya matarajio kuwa maangavu kwa ajili ya uongofu wa familia yote kwa ukweli wa Mungu.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 119. {ABN4: 77.2}

Ni katika tu nyumba ya Kikristo kama hii ndio kielelezo cha Ufalme wa Kristo. Na kwa njia hiyo kuuakisi Ufalme hapa, nyumba zote kama hizi, zinapofungashwa pamoja kwa jumla, zitaunda Ufalme hapo baadaye. Ni umuhimu ulioje, basi, kwamba mama na baba washirikiane kikamilifu kuendesha nyumba katika njia ya Kristo kabisa ili kuhifadhi uwepo wake sasa na milele! {ABN4: 77.3}

77

Kushindwa kwa upande wa mmojawapo, kutekeleza maagizo haya, kutavunja nyumba na kuitawanya familia sio tu sasa lakini pia katika umilele; ilhali kuyatenda kwa uangalifu yatalinda ufanisi na furaha ya familia katika ulimwengu huu, na kuhifadhi mwendelezo wake wa milele katika ulimwengu unaokuja. {ABN4: 78.1}

IWAPO WAWILI HAWAPATANI, WANAWEZAJE KUTEMBEA PAMOJA?

Swali Namba 106:

Je! Mbona Wadaudi Waadventista wa Sabato na Vuguvugu la_______ wasiungane katika moja? {ABN4: 78.2}

Jibu:

Wadaudi Waadventista wa Sabato na Vuguvugu la ________ hawaungani kwa sababu, kwa kusikitisha, hawapatani. Wao wakiwa na tofauti nyingi kwa maswala fulani ya mafundisho, hufanya muungano chini ya hali hizo kuwa ngumu. {ABN4: 78.3}

Tofauti mojawapo ya mafundisho, kwa mfano, ni kwamba Vuguvugu ________ hufundisha kwamba dhambi ndani ya Mama kanisa la Waadventista wa Sababto hulifanya kuwa sehemu ya Babeli, ilhali Wadaudi hufundisha kwamba ingawa liko katika hali ya kusikitisha, bado si, na kwa kweli haliwezi kuwa, Babeli: kwa maana dhambi hazilifanzi jina tena kuliko jina linavyofanya dhambi. Babeli haukuitwa hivyo kwa sababu ya dhambi zake, wala hauhukumiwi kwa sababu ya kuitwa Babeli, bali kwa sababu ya kuwa umeanguka na

78

“umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.” Ufu. 18:2. {ABN4: 78.4}

Kanisa la Waadventista wa Sabato linaweza kuwa katika hali hata mbaya zaidi, — mbaya sana, kwa kweli, hata halijui kwamba lina “unyonge na lenye mashaka, na maskini, na pofu, na uchi’ (Ufu. 3:17); lakini licha ya yote hayo, linaitwa “Laodekia,” si Babeli. Na washiriki wake husimama, si waitwe kutoka ndani yake kama wale walio Babeli, bali waachwe ndani, na “malaika” wake (uongozi) unasimama kutapikwa nje. Wadaudi wanajitahidi kuwaokoa wote kutoka kwa janga hili, kuwafanya upya katika neema ya Mungu na kwa hivyo kuwadumisha ndani ya Mama, ilhali Vuguvugu ______, likiwa halina dawa kwa ugonjwa wa Ulaodekia, linafanya kazi kuwavuta watoke ndani. {ABN4: 79.1}

Kwa kuamini kama linavyofanya na kwa hivyo kuukataa ujumbe wa Wadaudi, dawa, hufanya pande zote kutowezekana kuungana sisi nalo na nalo kuungana nasi. {ABN4: 79.2}

Kama Bwana, zaidi ya hayo, amefunua Ukweli ulio endelevu kupitia kwa Wadaudi, lakini sufuri kupitia kundi _______, ni dhahiri, basi, ungaliweza kuwapo muungano wowote kama huo, wao lazima kwa hitaji warekebishe mitazamo yao kisha wajiunge nasi katika kuupokea ujumbe wa saa kumi na moja, badala ya sisi kutupa baharini vito vyake vya ukweli na kuhifadhi kauli moja au mbili maalum ambazo wao huinua. {ABN4: 79.3}

79

Mbali na hilo, kwa yale wanayofanya sasa, hawadai hata amri ya mamlaka ya Uvuvio. Kwa hivyo bila kuwa na karama ya unabii kati yao, kundi la ________ lazima linakimbia mbio bila kutumwa. {ABN4: 80.1}

“Iwapo umoja,” husema Roho ya Unabii, kwa kuelezea mwenendo wa kanisa la kwanza la Kristo, “unaweza kupatikana tu kwa kuacha msimamo wa ukweli na haki, basi iwepo tofauti, na hata vita.” — Pambano Kuu, uk. 45. {ABN4: 80.2}

“Tunaweza kuungana, lakini si kwa jukwaa la makosa.” — Bi. E. G. White, Mfululizo B:2, uk. 47. {ABN4: 80.3}

Kwa hivyo mtu anaweza kuona kwa urahisi kwamba, ingawa tumaini letu lenye bidii ni kulitimiza ombi la Kristo kwa ajili ya umoja, hatuwezi kuthubutu kujaribu kufanya hivyo kwa kuisaliti Kweli kwa maana wakati huo hatutakuwa wamoja na Kristo, hata kama tungekuwa wamoja na wengine wote. {ABN4: 80.4}

“Kuna hatari ya sisi kuwa na bidii zaidi ya kutengwa na Babeli,” husema mwasisi wa kanisa la Waadventista wa Sabato, “ kwamba tutafanya kosa lake lililojulikana sana — lile la kushikamana na kigingi na kukataa kuking’oa na kusonga mbele. Tunapokoma kujifunza kuacha makosa, tutaanguka kama wale ambao wametangulia. Tumejifunza mengi, na bila shaka yapo mengi zaidi kwa ajili yetu kujifunza….Ni roho ya ‘kufuatilia’ na “kutimiliza” ambayo hatimaye itawaweka masalia ‘bila mawaa’ kwa Mlima Zayuni wa mbinguni. Hitimisho langu ni kwamba hatupaswi kuacha

80

ukweli wa Maandiko, lakini kwamba matumizi yetu na ufasiri wetu wa uongo wa Maandiko, na matokeo ya dhana za uongo za utaratibu na adabu, zinapaswa kuachwa haraka iwezekanavyo.” — Mapitio na Kutangaza, Mei 29, 1860. {ABN4: 80.5}

JINSI YA KUZUIA KUWALEA WASIOFAA?

Swali Namba 107:

Je! Tunawezaje kuwasaidia watoto kati ya umri wa miaka miwili na kumi na miwili, kumiliki wakati wao? {ABN4: 81.1}

Jibu:

Kwa sababu watoto wengi katika enzi hii ya Laodekia kwa namna fulani huruhusiwa kukua kama magugu badala ya kama wanadamu waliofunzwa, swali la wao kutumia vyema wakati wao ni muhimu kweli kweli. {ABN4: 81.2}

Kwanza, wazazi wote wanapaswa kutambua thamani ya kuwa na watoto waliofunzwa kwa uaminifu, kwa ueledi, na kwa ujasiri kubeba majukumu ya maisha na kukutana na matatizo yake, ikiwa hawatakuwa vimelea au wasiofaa kijamii, vigingi vya mraba tu katika mashimo ya mduara. Walakini, wazazi wengi huwatelekeza watoto wao kuelea bila kuwatayarisha kujitunza wenyewe, na kuwa wasiojali changamoto nyingi maishani. Kisha, wanapokuwa watu wazima hizi nafsi zilizojipinda hupata maisha kuwa magumu na ya kuhuzunisha badala ya furaha bora; kwa kila kitu wanachojaribu, kila hatua njiani, wanakutana na kushindwa kuchungu. Nyumba zao zinakuwa chafu na mazingira yasiyo safi, yasiyofaa kuishi ndani; na familia zao, pia, zinapata msongo, ovyo, kundi lisilofaa kwa jumuiya. {ABN4: 81.3}

81

Watoto waliolelewa hivyo, walioachiliwa kwa ubunifu wao wenyewe, ili kupoteza wakati na kutanga-tanga watakavyo, ni kama panzi. Akicheza, akiimba na kuota jua wakati wa msimu wote wa hari, bila kufikiria pumzi baridi ya masika, ambayo mbele yake nyasi za kijani hutoweka mashambani, panzi amepoteza wakati wake bure, na sasa lazima afe njaa kwa kukosa chakula, na kuganda nje uwanjani. Lakini chungu, ambaye amefanya kazi kwa bidii msimu wote wa joto, ana chakula kingi na nyumba nzuri yenye joto kwa msimu wa baridi. Uamuzi duni tu na upendo wa upofu ndio utakaowaachia watoto kukua wenyewe katika tabia za panzi, bila kufunzwa katika hekima ya kufanya kazi zao zote kwa siku sita zilizowekwa ili kustahili pumziko kwa ya saba. Wazazi ambao huruhusu watoto wao wapumbazike kuupoteza wakati, na hivyo kuweka mitego ya mauti mbele yao; wanawafanya wasifae kwa maisha haya na maisha yanayokuja. {ABN4: 82.1}

Katika kuwapatia mafunzo sahihi ya nyumbani, mojawapo wa masomo muhimu zaidi ya kwanza kuwafunza ni siku zote kuwa na mahali pa kawaida pa kuvalia na kuyavua mavazi, na kwa nyakati zote kutundika nguo zao mahali panapo faa, kamwe kutozilaza tu popote. Kwa hivyo kuwa na mahali pa kila kitu na kuweka kila kitu mahali pake, kutoka mwanzo wa familia sio tu kutafanya kazi ya nyumba kuwa nyepesi na kuweka nyumbani mwao safi na nadhifu na kwa mpangilio wakati wa usiku na vile vile wa mchana, na kwa matokeo kuongeza maisha ya

82

nguo na samani zao, lakini pia kwa muda mrefu kukuza usafi na unadhifu wa mtu na maisha yaliyotunzwa vyema na kupangiliwa. {ABN4: 82.2}

Kati ya kazi nyingi muhimu na vile vile za kuwajenga watoto, ni majukumu mbali mbali ya nyumbani kama kuosha vyombo, kutandika vitanda, kufagia, kupanguza vumbi, kuosha madirisha, kusafisha sakafu na kazi za useremala, kuoka, kupika, na hata kutengeneza vyombo rahisi vya mavazi na samani. {ABN4: 83.1}

Kisha zipo kazi za nje kama kuyadumisha majengo yakiwa nadhifu na safi, kutunza bustani, kufuga kuku, n.k., kwa kuongezea kazi zingine za utendaji, pamoja na kufanya ununuzi kiuchumi na kibiashara. {ABN4: 83.2

Na kwanza kabisa, kusoma na kukariri vifungu kutoka kwa Bibilia na Roho ya Unabii kunapaswa kukuzwa kwa uangalifu kama burudani ya kutia taji. {ABN4: 83.3}

Kuwa na utu na tabia nzuri iliyojumuishwa kikamilifu, mtoto lazima astawi vizuri nguvu za kimwili na kiakili na kiroho. Ili kuafiki hayo, mafunzo yake yanapaswa kuanza mapema sana maishani — mara tu anapoweza kutembea na kuongea — kwa sababu ikiwa ataachwa kuupoteza wakati wake hadi akue mtu mzima, atapata maumbile kama ya punda milia — tabia ambayo haiwezekani kubadilisha kutoka kwa kutofanya kitu hadi kufanya kitu. {ABN4: 83.4}

Ili kuepusha ulemavu huu wa tabia na madhara ambayo katika maisha yote hayawezi kurekebishwa

83

yakitokea, mapema mpe mgawo wa majukumu kadhaa ya nyumbani, na anapojua kutenda jambo moja unamkweza kwa lingine. Nyumbani kwapaswa kuwa shule, si uwanja wa kucheza. Wala hafai kuachwa kucheza sana wakati mwingi nje nyumbani ili ajizoeshe tu kwa maisha ya kucheza na ukorofi. {ABN4: 83.5}

Na kwa njia zote kamwe usiwaruhusu watoto wako kuzama katika tabia ya uzembe ya kuacha majukumu ya asubuhi hadi alasiri, au kazi ya siku moja hadi kwa ijayo. Vyombo vinapaswa kuoshwa mara baada ya kila mlo; chakula kamwe kisiachwe kikauke na kuwa kigumu kwavyo. “Siku sita,” asema Bwana, “fanya kazi, utende mambo yako yote.” Kut. 20:9. {ABN4: 84.1}

Pale ambapo kuna watoto kadhaa katika nyumba majukumu ya kila siku nyumbani yanapaswa kugawanywa kati yao, na wazazi wachukue majukumu ya mwalimu. Kwa njia hii kila kijana hatajiepusha tu na ukorofi na kundi baya lakini pia atakuwa wa manufaa na mwenye bidii, wakati huo huo akijenga mwili wenye nguvu, tabia ya ungwana, na utu wenye furaha. Iliyolindwa aina hii ya ukuaji wa utotoni, mmoja itakuwa vigumu sana kuingia katika uhuni wa ukafiri. {ABN4: 84.2}

Lakini, mruhusu mtoto wako aingie katika tabia mbovu ya kufanya kitu baada tu ya kumbembeleza au kumgombeza, na hakika utamfunza kukuchukia wewe mwenyewe na kazi hiyo. Na kwa hivyo, badala ya

84

kumfunza kupenda maisha yenye bidii ambayo yatamfanya kuwa na furaha na kujitegemea, utakuwa unamsukuma kuwa asiyefanya kazi, jambo ambalo unajaribu kumzuia asitende, na hata kusababisha kugombana. Lakini mfahamishe kwamba lile unalosema, unamaanisha, na basi atakuwa na uwezekano mdogo kudhani kwamba umekosea, na kwa upande wake bado atakuwa na uwezekano mdogo kulipinga neno lako na kufikiri kuliasi sio tu halali lakini hata kwa kupongezwa. {ABN4: 84.3}

Basi, pia, jitahidi kuwaongoza watoto wako kupenda kazi yao kwa kuwaendeleza wavutiwe nayo. Kuwa kama Mungu. Wafunze kwa njia ile ile ambayo Yeye anakufunza. Imeandikwa kwamba “Yeye ambaye Bwana anampenda humrudi.” Ebr. 12:6. Yeye huelezea pande sahihi na mbaya za maisha, na kukuonya waziwazi matokeo ambayo yatafuata kutoka kwa mwenendo wowote ambao unaweza kufuata — baraka kutoka kwa mmoja na laana kutoka kwa mwingine. Fanya vivyo hivyo kwa watoto wako. Lakini uweze kuwa mwangalifu kwamba kwa kufanya hivyo, usiwageuze dhidi ya Mungu kwa kuwatishia kwamba iwapo hawatakuwa wazuri, Yeye atawaadhibu kwa njia hii au kwa njia ile. Badala yake wafundishe kwamba Yeye anawasihi wauepuke mwenendo mbaya kwa sababu, huo, utawaongoza kuvuna laana badala ya baraka. {ABN4: 85.1}

Kuzifanya akili changa zisisahau haya matokeo mawili, tumia vielelezo rahisi. Onyesha kwa mfano, kwamba mtu akishindwa kuondoa vimelea vya chakula kwa meno yake kwa kuyasafisha mara kwa mara baada ya

85

mlo, yataliwa na vimelea, jinsi ambavyo matunda huliwa na chango wakati miti haipuliziwi dawa na kutunzwa, na matokeo mwishowe yatakuwa maumivu, kupoteza meno, ubaya wa umbo, na gharama. Kutoka kwa mlolongo huu maalum wa kisababishi na matokeo, ongoza akili ya mtoto kuona matumizi yake duniani kote — kwamba kukiuka sheria za Mungu kwa hali yoyote kwa kawaida kutasababisha maumivu, huzuni, tabia mbaya , maisha ya fedheha, na kifo cha mapema. {ABN4: 85.2}

Lipaswalo kufikiriwa pia katika jambo hili muhimu na la dharura, ni ukweli wa kushangaza kwamba watoto kimaumbile huwa na mielekeo kwa tabia mbaya badala ya zile nzuri, kama hayawani kiasili hutafuta nyama badala ya mimea. “Ujinga,” tunakumbushwa, “umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.” Mit. 22:15. Lazima afundishwe,aadibishwe, aadhibiwe kwa uvumilivu na kwa busara. “Mlee mtoto katika njia impasayo: naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.” Mit. 22:6. Lakini iwapo atakuwa mugumu na mkaidi, akikataa kufunzwa basi “Mrudi mwanao kama lingaliko tumaini, wala usiizuie nafsi yako kwa kulia kwake.” “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Mit. 19:18; 13:24. Hakika, “Usimnyime mtoto wako mapigo: maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga fimbo na kumwokoa nafsi yake na kuzimu.” Mit. 23:13, 14. {ABN4: 86.1}

86

Hadi umri wa miaka mitano au sita, kulingana na utu wa mtu binafsi, watoto wanaweza kustahili adhabu za viboko wakati hatua zingine za nidhamu na kurekebisha zimekwisha bila mafanikio. Ikiwa kwa hafla kama hizo, kiboko kitatumika vyema, mtoto anaweza kuitikia hivi kwamba hatakihitaji tena. Iwapo, hata hivyo, hitaji laweza kutokea tena, basi kuwa mwangalifu sana kile utakachofanya. Kwa maana watoto kama hao wanaohitaji adhabu kali zaidi kuliko mtoto wa kawaida, wanaweza kuwa wasiotaka kubadilika na hukuza hofu isioeleweka na kuwachukia wanaowaadhibu. Kwa hivyo, wakati adhabu kama hiyo imekusudiwa kuzuia kurudia maovu makubwa ndani yao, upo uwezekano wa kuleta uovu mbaya zaidi, isipokuwa hatua zilizochunguzwa kwa uangalifu zichukuliwe kukinga dhidi ya matokeo yake ya ukatili. Lazima itolewe pamoja na onyesho sawia lenye kushawishi la upendo wa moyoni na wa tumaini kwa yule aliyekosa kwamba hatapoteza upendo wa mzazi na heshima kwa wanaomwadhibu, na maisha yake ya nyumbani huwa ndoto ya kumuwinda kama kumfukuzia mbali wakati fursa itajitokeza. {ABN4: 87.1}

Wazazi “wanapaswa kwanza kujadiliana na watoto wao, waelezewe wazi makosa yao, waonyeshwe dhambi yao, na wasisitiziwe kwamba hawajatenda dhambi dhidi ya wazazi wao, bali dhidi ya Mungu. Kwa moyo wako mwenyewe uliojishusha na mwingi wa sikitiko na huzuni kwa watoto wako wakosaji, omba pamoja nao kabla ya kuwarekebisha.

87

Basi marekebisho yako hayatasababisha watoto wako kukuchukia. Watakupenda. Wataona kwamba hauwaadhibu kwa sababu wamekutaabisha, au kwa sababu unataka kutoa nje kuudhika kwako juu yao; lakini kutokana na hisia ya wajibu, kwa manufaa yao, ya kwamba wasiachwe waendelee kukua katika dhambi.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 398. {ABN4: 87.2}

Kwa gharama zote, lazima siku zote washawishiwe kujihisi kwamba wanaowadhibu ni marafiki wao bora, sio waonevu na maadui. {ABN4: 88.1}

“Mama anaweza kuuliza, ‘Je! Sitawahi kamwe kumwadhibu mtoto wangu?’ Kumcharaza viboko kwaweza kuwa muhimu wakati njia zingine zinaposhindwa, lakini hapaswi kutumia fimbo iwapo inawezekana kuzuia kufanya hivyo. Lakini ikiwa hatua za upole zinathibitika hazitoshi, adhabu ambayo itamleta mtoto kwa akili zake inapaswa kutekelezwa katika upendo. Mara nyingi marekebisho kama hayo mara moja yatakuwa tosha kwa maisha yote, kumwonyesha mtoto kwamba hamiliki kamba za udhibiti.” — Mashauri kwa Walimu, uk. 116. {ABN4: 88.2}

Lakini kuzoea kuwanyaka watoto kwa lolote na kila kero, na kwa hasira kuwatikisa, kuwapiga makonde, kuwapiga makofi, kuwagonga, au kuwacharaza viboko, na kati ya nyakati kukazia juu ya vichwa vyao kitisho cha kuwapiga, ni upumbavu wa kuharibu sana, unaochukiwa sawia na kila uzingativu wa akili, adabu, na ubinadamu. Uendelezaji wake utafanya ugumu na ukatili, uharibifu badala ya kuokoa. Utawafanya wahanga wake kuwa wanyama wadogo wakali badala ya watoto waungwana kama Mungu. {ABN4: 88.3}

88

“Wazazi wengine huwarekebisha watoto wao kwa ukali katika roho ya kutokuwa na uvumilivu, na mara nyingi kwa hasira. Marekebisho kama hayo hayaleti matokeo mazuri. Katika kutafuta kurekebisha uovu mmoja, wao hufanya mawili. Siku zote kuwashutumu na kuwacharaza viboko huwafanya watoto wawe wagumu na kuwatoa kwa wazazi.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 398. {ABN4: 89.1}

Wakati, hata hivyo, unalizimika kutoa adhabu, chukulia hatua hiyo kwa uzito, umaanishe, na ufanye kazi nzuri, ya maana. Uone kwamba unaifanya vyema ili usilazimike kuifanya tena. {ABN4: 89.2}

Leo, kuliko zamani, vijana wanadai kujiamini mapema mno, kwa kiwango kwamba hata wanatishia kuondoka nyumbani iwapo hawatapewa kila wanachokitaka. Lakini usiridhiane nao katika kipindi hiki kigumu, au mwishowe watalazimisha mambo kufikia suala kwamba wataweza kukimbia kutoka nyumbani ili kutumia vyema udanganyifu wao. Usikubali. Wahakikishie kwamba iwapo wanataka kwenda, utawasaidia kuwaanzisha waondoke kwa uwazi na kwa heshima, lakini ya kwamba hawahitaji kukimbia kwa aibu na kunyata kisiri. {ABN4: 89.3}

Mwishowe, usiwafanye wapoteze heshima kwako au kwa dini yako. Hawahitaji sana mafundisho mengi mwanzoni kuliko wanavyohitaji masomo rahisi ya maisha yanayopigwa chapa akilini kidini kila siku. Wafanye waipende dini yako kwa kuwasaidia kuielewa, wauone ukweli na uzuri wake. Kamwe usijaribu kuwalazimisha kuipokea; wataichukia

89

tu. Na kamwe usisahau kwamba iwapo mwenendo wako huwaongoza kukutawala badala yako wewe kuwatawala, au uwatawale kwa mabavu badala ya kwa upendo, utawaangamiza milele na, naam, wewe, pia. Wakati huo Mungu atakapouliza, “Liko wapi kundi ulilopewa, kundi lako zuri?” utatekewa. {ABN4: 89.4}

Wacha kila mzazi au mlezi, kwa neno na kwa kielelezo akazie katika akili za vijana ukweli kwamba

Wakati Ni Wa Thamani 

“Maisha ya Kristo tangu miaka Yake ya kwanza kabisa yalikuwa maisha ya shughuli za bidii.” — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 345. {ABN4: 90.1}

“Wakati wetu ni wa Mungu. Kila dakika ni Yake, na tuko chini ya wajibu mzito wa kuuboresha kwa utukufu Wake. Hakuna talanta yoyote Aliyoitoa atahitaji hesabu kamili kuliko ya wakati wetu. {ABN4: 90.2}

“Thamani ya wakati ni zaidi ya kuweza kuhesabiwa. Kristo aliuona kila wakati kuwa wa thamani, na ndivyo tunavyopaswa kuuona. Maisha ni mafupi sana kuchezewa-chezewa. Tunazo siku chache tu za muda wa rehema ambazo twapaswa kuzitumia kujitayarisha kwa umilele. Hatuna wakati wa kupoteza, hakuna wakati wa kujishughulisha na starehe za ubinafsi, hakuna wakati wa kujifurahisha dhambini. Ni sasa ya kwamba tunapaswa kujenga tabia kwa maisha ya baadaye, ya milele. Ni hivi sasa ya kwamba tunapaswa kujiandaa kwa Hukumu ya upekuzi. {ABN4: 90.3}

“Familia ya wanadamu huwa hata hawajaanza

90

kuishi wakati wanapoanza kufa, na kazi zisizokoma za ulimwengu huishia kwenye ubatili isipokuwa maarifa ya kweli kuhusu uzima wa milele yamepatikana. Mtu ambaye huuthamini wakati kama siku yake ya kufanya kazi atajiwezeshea jumba limfae na kwa maisha ambayo ni ya milele. Ni vema ya kwamba alizaliwa. {ABN4: 90.4}

“Tunahimizwa kuukomboa wakati. Lakini wakati uliopotezwa bure hauwezi kukombolewa kamwe. Hatuwezi kurudisha tena hata dakika moja. Njia pekee ambayo tunaweza kuukomboa wakati wetu ni kutumia vyema ule uliopo, kuwa watendakazi pamoja na Mungu katika mpango Wake mkubwa wa ukombozi. {ABN4: 91.1}

“Katika yeye afanyaye hivi, mabadiliko ya tabia hufanyika. Anakuwa mwana wa Mungu, mshirika wa familia ya kifalme, mtoto wa Mfalme wa mbinguni. Yeye anafanywa afae kuwa mwenzi wa malaika. {ABN4: 91.2}

“Sasa ni wakati wetu kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzetu. Wapo wengine wanaodhani kwamba ikiwa watatoa pesa kwa ajili ya kazi ya Kristo, hii ndio yote wanayohitajika kufanya; wakati wa thamani ambao wanaweza kufanya utumishi wa kibinafsi kwa ajili Yake hupita bila kuboreshwa. Lakini ni fursa na jukumu la wote ambao wanayo afya na nguvu kumpa Mungu huduma amilifu. Wote wanapaswa kufanya kazi kuziongoa nafsi kwa Kristo. Michango ya pesa haiwezi kuchukua nafasi ya hii. {ABN4 : 91.3}

“Kila wakati una kishindo cha matokeo ya milele. Tunapaswa kusimama kama watu halisi, tayari kuhudumu kwa ilani ya nukta moja.

91

Fursa ambayo sasa ni yetu kunena kwa nafsi fulani inayohitaji neno la uzima inaweza kutokuwapo tena kamwe. Mungu anaweza kunena kwa huyo, ‘Usiku huu wa leo wanataka nafsi yako, na kupitia upuuzaji wetu isiwezekane kuwa tayari. Katika siku kuu ya Hukumu, tutatoaje hesabu yetu kwa Mungu? {ABN4: 91.4}

“Maisha ni muhimu sana kuyashughulisha kwa mambo ya muda na ya kidunia, katika shinikizo la mahangaiko na wasiwasi kwa mambo ambayo ni chembe tu yakilinganishwa na mambo ya masilahi ya milele. Bado Mungu ametuita tumtumikie Yeye katika mambo ya maswala ya muda maishani. Bidii katika kazi hii ni sehemu ya dini ya kweli kama ibada. Biblia haipeani idhini kwa uvivu. Ni laana kubwa zaidi ambayo huutesa ulimwengu wetu. Kila mwanaume na mwanamke aliyeongoka kwa kweli atakuwa mtendakazi mwenye bidii. {ABN4: 92.1}

“Kwa uboreshaji sahihi wa wakati wetu hutegemea mafanikio yetu katika kupata maarifa na ukuzaji wa akili. Ukuzaji wa akili hauhitaji kuzuiliwa na umasikini, asili duni, au mazingira yasiyofaa. Acha tu wakati uthaminiwe. Muda mchache hapa na mchache pale, ambao unaweza kupotezwa katika mazungumzo yasiyokuwa na lengo, masaa ya asubuhi ambayo mara nyingi hupotezwa kitandani, wakati unaotumika kusafiri kwa magari au vigari moshi, au kungoja kituoni, wakati wa kungojea vyakula, kuwangojea wale ambao ni walegevu kutunza miadi, — laiti kitabu kingekuwa mkononi, na hivi vipande vya wakati

92

kuboreshwa katika kujifunza, kusoma, au kufikiri kwa uangalifu, lipi ambalo halingeweza kufanikishwa. Kusudi thabiti, bidii isiyokoma, na uchumi makini wa wakati, utawawezesha wanadamu kupata maarifa na nidhamu ya akili ambayo itawastahilisha kwa karibu kila nafasi yoyote ya mvuto na umuhimu. {ABN4: 92.2}

“Ni jukumu la kila Mkristo kujipatia tabia za utaratibu, ukamilifu, na wepesi. Hakuna kisingizio cha tabia yoyote ya kufanya mambo polepole vibaya kazini. Wakati mtu yu daima kazini, na kazi haifanywi kamwe, ni kwa sababu nia na moyo havijawekwa kazini. Yule ambaye ni wa kujikokota, na anayefanya kazi kwa hasara, atambue kwamba haya ni makosa ya kurekebishwa. Anahitaji kuzizoesha akili zake kupanga jinsi ya kutumia wakati ili kuhifadhi matokeo bora. Kwa busara na mbinu, wengine watakamilisha kazi nyingi katika masaa matano ilhali wengine watakamilisha kwa kumi. Wengine ambao wanafanya kazi za nyumbani huwa wakati wote kazini, sio kwa sababu wanazo kazi nyingi za kufanya, ila kwa sababu hawafanyi mpango ili kuokoa wakati. Kwa njia zao za kujikokota na za kukaakaa, wao hufanya kazi chache kuwa nyingi. Lakini wote wanaotaka, wanaweza kuzishinda tabia hizi za kushughulika-shughulika kwa mambo madogo, zenye uvivu. Katika kazi zao hebu waweze kuwa na lengo dhahiri. Waamue ni muda gani unaohitajika kwa kazi iliyopo, na kisha kupinda kila juhudi ili kuikamilisha kazi katika muda unaofaa. Zoezi la nguvu ya nia litafanya mikono isogee kwa wepesi. {ABN4: 93.1}

93

“Kupitia ukosefu wa azimio la kujichukulia mikononi na kufanya matengenezo, watu wanaweza kuwa wasiobadilika katika mwenendo mbaya wa utendaji; au kwa kukuza nguvu zao wanaweza kupata uwezo wa kufanya huduma bora zaidi. Kisha watajikuta wanahitajika mahali popote na kila mahali. Watathaminiwa kwa yote ambayo wanastahili. {ABN4: 94.1}

“Kwa watoto wengi na vijana, wakati hupotezwa ambao unaweza kutumika kubeba mizigo ya nyumbani na hivyo kuonyesha nia ya upendo ndani ya baba na mama. Vijana wanaweza kubeba kwenye mabega yao yaliyo machanga majukumu mengi ambayo mtu fulani lazima abebe.” — Kimenukuliwa, uk. 342-345. {ABN4: 94.2}

“Ni kitovu cha imani kamili kufanya jambo sahihi kwa wakati unaofaa.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 24. {ABN4: 94.3}

(Italiki zote ni zetu)

======

HATUA YAKO ITAKAYOFUATA ITAKUWA NINI?

Sasa ikiwa umefurahia, umethamini, na kufaidika na safari hii ya maswali na majibu kupitia Kitabu Namba 4, na iwapo unatumaini kuendelea, basi tuma ombi kwa Kitabu Namba 5. Kitatumwa kama utumishi wa Kikristo bila malipo au wajibu. {ABN4: 94.4}

94

FAHARISI YA MAANDIKO

95

Mimi sio kazi ya kulazimisha, kubwa —

Maneno yangu yako kwa muhtasari,

Bado ninang’aa sana nyumbani na kanisani

(Katika enzi hii ya kutia muhuri)

Ambamo hukaribishwa na kuthaminiwa,

Kusomwa na kusomwa tena na kutunzwa vyema,

Bila kudharauliwa, kukataliwa, na kushutumiwa na kuchukiwa,

Kulaaniwa, kuraruliwa, na kuchomwa katika roho iliyoanguka. {ABN4: 96.1}

Kwa hivyo ikiwa wewe, mwenyeji mpendwa, wewe si adui kama huyo, bali rafiki,

Basi utavuna kutoka katika kurasa zangu —

Nuru kwa maswali yako kujibu, hofu zako kukoma.

Na taji katika vizazi vyote visivyo na mwisho,

Na utukufu wa wokovu wa milele,

Uamuzi wako wa kuisikia Sauti yangu,

Na uokozi kutoka kati ya kila taifa,

Watakatifu wote nawe kufurahia. {ABN4: 96.2}

96

 

>