fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 36, 37, 38

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 36, 37, 38

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

“WATULIZENI MIOYO, WATULIZENI MIOYO, WATU WANGU”

MWISHO WA WA SAFARI YENU REFU NA YA MAJARIBU

WASIPOAMSHWA SASA, WANAWEZA KULALA MILELE

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Nyembamba, Njia Ya Kwenda Juu

Nitasoma kutoka “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 198 na aya ya pili: {1TG36: 2.1}

“Nyembamba, njia ya kwenda juu inayoelekea nyumbani na kwa pumziko, aliipamba Yesu kwa picha bora ya njia ya Mkristo. Njia ambayo nimeweka mbele yenu, Alisema, ni nyembamba; lango ni vigumu kuingia; kwa maana kanuni ya upendo hutenga kiburi chote na ubinafsi. Ipo, kwa kweli, njia pana; lakini mwisho wake ni uharibifu. Ikiwa ungaliikwea njia ya maisha ya kiroho, lazima daima upande; maana ni njia ya kwenda juu. Lazima uende na wachache; kwa maana umati wa watu wataichagua njia ya kwenda chini. {1TG36: 2.2}

“Katika njia ya kifo jamii yote ya wanadamu inaweza kwenda, pamoja na udunia wao wote, na ubinafsi wao wote, kiburi chao chote, udanganyifu wao, na upotovu wa maadili. Ipo nafasi kwa maoni ya kila mtu na mafun-disho yake, nafasi ya kufuata mielekeo yake, kufanya chochote upendo wake wa ubinafsi unaweza kuamua. Ili kwenda katika njia inayoongoza kwa uharibifu, hakuna hitaji la kuitafuta njia; kwa maana lango ni pana, na njia ni pana, na miguu kwa kawaida huelekea kwenye njia inayoishia katika kifo.” {1TG36: 2.3}

Tunapaswa kuomba kwa ajili ya nguvu ili kutuwezesha kuiepuka njia pana, kuacha kuufuata unafsi — njia am-bayo tunajipata kwayo wenyewe tangu kuzaliwa. Tunapaswa kuomba ili tuichague njia nyembamba pamoja na wachache, kujua kwa hakika kwamba njia nyembamba tu, ya kwenda juu huongoza hadi nyumbani na kwa amani. {1TG36: 2.4}

2

“TULIZENI MIOYO, TULIZENI MIOYO, WATU WANGU”

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, APRILI 12, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Juma lililopita tulimaliza kujifunza sura ya thelathini na tano ya kitabu cha Isaya. Na sasa kwa sababu, kama ina-vyoweza kuonekana kwa utayari, sura ya 36 – 39 kwa ujumla, hukatiza na habari ya kihistoria mada ya unabii wa Isaya, tutaendelea pale ambapo Uvuvio unachukulia uzi wa wazo katika sura ya 40 na rai ya upole kwa watu wanaoutangaza ujumbe wa Mungu: {1TG36: 3.1}

Aya ya 1, 2 — “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.”

Aya ya 2 haiachi shaka kwamba Uvuvio unanena kwa watu katika siku za mwisho, — katika siku ambazo vita, safari ya taabu, na kutekwa kwa watu wa Mungu waliochoka zimekamilika. Baada ya kupokea maradufu kwa dhambi na uasi wao, uovu wao umesamehewa na hivi karibuni watakombolewa. Hauwezi kumudu kuupuuza ujumbe huu wa kufariji. Ni lazima usipuuze kujiandaa, kwa maana hiyo ndio sababu sasa umefunuliwa na kule-twa kwako bila malipo. Jitayarishe kukutana na Mungu wako ndio msingi wake muhimu. {1TG36: 3.2}

Aya ya 3 — “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.”

3

Kweli, aya ya tatu ilitimizwa katika kazi ya Yohana Mbatizaji; ila aya zilizotangulia na pia aya zinazofuata, kwa uwazi zinawahusu watu katika siku za mwisho na kiasi tu kwa watu katika siku ya Yohana. Kwa hivyo ukweli unadhihirika kwa uthabiti kwamba utimilifu wa moja kwa moja wa sura hii unapatikana katika wakati wetu, hivyo kuifanya kazi ya Yohana kuwa mfano wa kazi yetu — kazi ya Yohana mfano, yetu uakisi. {1TG36: 4.1}

“Nyikani” na “jangwa” (Isa. 40: 3) tofauti na “shamba la mizabibu,” nyumba ya Yuda ki-uhalisia na ki-uakisi inasema: “Sauti ya mtu aliaye katika nchi ya Mataifa, inayosema, itengenezeni njia ya Bwana, nyosheni katika ulimwengu wa Mataifa njia kuu kwa Mungu wetu.” {1TG36: 4.2}

Aya ya 4 — “Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pame-nyoka, Na palipoparuza patasawazishwa.”

Ili kuinyosha njia hiyo, “sauti” ni, kama mfano, kuinua mabonde, kukata milima na vilima, na kuyeyusha maeneo yaliyoparuza; yaani, kila kizuizi lazima kiondolewe na kitaondolewa, watakatifu lazima wakusanywe bila kujali wanakoishi. {1TG36: 4.3}

Aya ya 5 — “Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.”

Hili litatimia mara tu njia kuu itakapotengenezwa. {1TG36: 4.4}

Aya ya 6-8 — “Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; Majani yakauka, ua lanyauka;

4

Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Majani yakauka, ua lanyau-ka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.”

“Sauti” inatangaza kwamba wote ni nyasi, kwamba uzuri wote ndani ya wanadamu ni kama maua ya kondeni, lakini Neno la Mungu husimama milele. Lazima iwe, basi, kwamba watu ni vipofu kuuona uhalisi huu, vinginevyo wasingalihitaji kukumbushwa kuuhusu. Lazima iwe ni kwamba wanautegemea mwili, badala ya Ne-no la Mungu na Roho Wake. {1TG36: 5.1}

Aya ya 9-11 – “Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Taza-meni, Mungu wenu. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomta-walia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake. Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wan-yonyeshao atawaongoza polepole.”

Ujumbe ambao sura hii inasheheni, tunaona, sio ujumbe wa kuhubiriwa kwa ulimwengu, ila kwa miji ya Yuda wa uakisi, kanisa. Na wale wanaoutangaza ni raia wa Zayuni na Yerusalemu wa uakisi, washiriki wa kanisa. Wanapaswa kwa ujasiri kuzipaaza sauti zao kwa nguvu. {1TG36: 5.2}

Wanapaswa kuelezea kwamba watu ambao Mungu anawatumia kufanya kazi Yake ni “mkono wake”; kwamba watatawala kwa ajili Yake; ya kwamba thawabu Yake iko pamoja Naye, na kazi Yake bado iko mbele Yake; ya kwamba Atalisha kundi Lake, na kwa mkono Wake (na kanisa Lake) atawakusanya wana-kondoo (waongofu wapya) na kuwapeleka kwenye ufalme Wake. {1TG36: 5.3}

5

Aya ya 12-20 — “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani? Ni nani aliyemwongoza roho ya Bwana, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya fahamu? Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana. Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara. Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili. Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani? Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu hui-funika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kuti-kisika.”

Wale wasiomjua Mungu humlinganisha na kitu. Lakini swali kubwa ni, tunamlinganisha Yeye na nini — na kitu ingawa hakuna cha kulinganishwa Kwake? {1TG36: 6.1}

Aya ya 21-26 — “Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia? Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama

6

mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu. Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesa-bu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.”

O, ni mkuu kama nini Mungu Mungu wetu! Na sisi ni wazembe kama nini kuzishika ahadi Zake. Tu wavivu namna gani kumruhusu Yeye achukue usimamizi wetu kamili jinsi anavyoziongoza nyota. {1TG36: 7.1}

Aya ya 27 — “Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?”

Bila shaka watu wa Mungu wamekosea juu ya ufahamu Wake kuzihusu njia zao. {1TG36: 7.2}

Aya ya 28-31 — “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

Aya hizi zinafafanua kwamba watu wa Mungu wanahitaji kujua mambo haya yote kabla waipate haki

7

ya kuingia ndani ya Ufalme Wake Mtakatifu. Na ni pendeleo la ajabu kama nini lililo letu ikiwa sisi tunamngojea Bwana, iwapo tutabaki wakweli na waaminifu kwa Neno Lake. Basi atazihuisha nguvu zetu kama tai; tutakim-bia wala hatutachoka; tutatembea hatutazimia. {1TG36: 7.3}

Maadamu siku kuu na ya kutisha ya Bwana inakaribia kwa haraka, na kwa sababu tumeambiwa tayari cha kufanya ili kujiandaa, hatuhitaji kupatikana tumepungukiwa. “Hakika wokovu wake u karibu na wamchao, Utu-kufu ukae katika nchi yetu …. Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni. Naam, Bwa-na atatoa kilicho chema, Na nchi yetu itatoa mazao yake. Haki itakwenda mbele zake, Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.” Zab. 85: 9-12. {1TG36: 8.1}

Ni wa kufariji kama nini ujumbe huu! Yeyote aone ajabu kwa nini Mwenyezi Mungu anahimiza kwa kuamuru: “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu Wangu.” {1TG36: 8.2}

8

MWISHO WA WA SAFARI YENU REFU NA YA MAJARIBU

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, APRILI 19, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu ya alasiri hii inapatikana katika sura ya hamsini na moja ya Isaya, kuanzia aya ya kwanza. {1TG37: 9.1}

“Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa. Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa ….” Isa. 51: 1, 2. {1TG37: 9.2}

Katika sura hii Mungu ananena kwa uzao wa Abrahamu, kwa kizazi kinachoifuatia haki. Sasa tunahitaji kutafuta katika mkondo wa wakati kizazi haswa ambacho Uvuvio hapa unazungumzia. {1TG37: 9.3}

Je! Ni watu wa wakati wa Musa? wa wakati wa Isaya? wa wakati wa Mitume? wa wakati wetu? au wa wakati mwingine fulani? Ikiwa sura hiyo imeelekezwa kwetu, basi hitaji letu la kujifunza, na shauku yetu ndani yake, itakuwa ya milele kuliko ingalivyokuwa vinginevyo. Habari tunayotafuta inapatikana katika aya ya kumi na saba — {1TG37: 9.4}

“Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea, mkononi mwa Bwana, Kikombe cha hasira yake; Bakuli la kikombe cha kulevya-levya Umelinywea na kulimaliza.” Isa. 51:17. {1TG37: 9.5}

9

Aya hii inafichua kwamba Mungu anena kwa watu ambao wamepitia majaribu yote — ugumu, utumwa, na mate-so waliopewa kwa ajili ya dhambi yao na kutotii — wamekunywa machujo ya kikombe cha kulevya-levya na hata kukimaliza. Mwishowe hakuna machujo yaliosalia ndani ya kikombe. Hili, kwa kweli, halingalinenwa kwa watu katika wakati wa Musa, wala katika wakati wa Isaya, au hata wakati wa Mitume. Halingalinenwa kwa watu wowote wakati wowote ila kwa wale ambao wameufikia wakati wa ukombozi wao kutoka kwa taabu, hofu, na ukosefu wa usalama ambao wameutengeneza kupitia kwa dhambi na uasi wao. Mwito wa Mungu kwa wao kuamka, hata hivyo, unafichua kwamba hata hivyo wakati wa ukombozi umekuja, bado wako kwenye usingizi mzito wa kiroho — hawazijui habari hizi njema. {1TG37: 10.1}

“Bwana, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena.” Isa. 51:22. {1TG37: 10.2}

Mungu, unaona, bila shaka anawahutubia watu ambao tayari wamekwisha kuichukua adhabu yote ambayo wa-listahili, na mwishowe Yeye anawatetea. Hili haliwezi kunenwa wakati wowote kwa watu wowote wa hapo awali. Je! Tunajuaje kwamba wakati umekuja na kwamba Bwana sasa anasema nasi? Tunajua kutoka kwa ukweli kwamba unabii huu fiche juu ya mada hii sasa kwa mara ya kwanza umefunuliwa na kuletwa kwa usikivu. Sasa tuko tayari kujifunza sura hii aya kwa aya. {1TG37: 10.3}

Isa. 51: 1, 2 — “Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa. Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita,

10

nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.”

Mungu huwashauri watu Wake wa leo wamsikilize Yeye. Ni wale ambao wanajitahidi kuipata haki, wanaomta-futa Bwana, na walio na shauku ya kuwa na uamsho na matengenezo kati yao. Sasa wanahimizwa wauangalie mwamba walikochongwa, na kwa tundu la shimo ambalo wametolewa kwa kuchimbuliwa. {1TG37: 11.1}

Hatupaswi kuhitimisha kwamba Wayahudi ndio uzao wa pekee wa Abrahamu. Wale walio na bahati sana kuwa na huu ufunuo kuletwa kwao, ndio watu. Hakuna hitimisho lingine salama ikiwa Mungu husababisha unabii uandikwe, utiwe muhuri, na kisha ufunuliwe kwa mapenzi Yake na kwa wakati ulioamriwa. Wayahudi, kwa hivyo, sio uzao wa pekee wa Abrahamu. Ili kupata haswa ni nani wale wanaotafuta haki, zipo kweli kadhaa za kinasaba kuzingatia: (1) Ni raia wa ufalme wa Yuda tu (ufalme wa makabila mawili, Yuda na Benyamini) ndio waliopokea jina la Wayahudi. (2) Wale wa ufalme wa makabila kumi (ufalme wa Israeli) walitawanywa kati ya mataifa, na huko walipoteza utambulisho wao kabisa. (3) Kanisa la Kikristo lenyewe ni chipukizi la kanisa la Ki-yahudi na taifa — Mitume na wafuasi wake, hadi karibu 35 B.K. wote walikuwa ni Wayahudi. Kisha ilikuwa kwamba tena umati wa Wayahudi walipoteza utambulisho wao kwa kujiita “Wakristo.” Kunena kwa kulingani-sha, ni Wayahudi wachache tu, kutoka kwa Ufalme wa Yuda, ambao wamelihifadhi jina lao la kitaifa, Waya-hudi. {1TG37: 11.2}

Wazawa wa Wayahudi Wakristo wa kwanza na wazawa wa makabila kumi, chini kwa mkondo wa wakati lazi-ma wameongezeka kuwa umati usiohesabika, kwa maana uzao wa Abrahamu ungalikuwa kama mchanga

11

wa bahari kwa umati. Kwa hivyo, ni dhahiri, kwamba Wayahudi wachache waliotambuliwa wa leo sio uzao wa pekee wa Abrahamu, ila kwamba watu wengi wa Mataifa lazima wawe wa Abrahamu. Kwa kuwa hali hii ili-yochanganyika ipo, ni vigumu mtu yeyote aweze kusema kwa hakika kwamba yeye sio mmoja wa watoto wa Abrahamu. Labda nchi nyingi ambazo ulimwengu unawaita Mataifa ni watoto wa Abrahamu. Hatujui kwa haki-ka nani ni nani. Mungu, hata hivyo, ameweka kumbukumbu kamili ya nasaba, kwa kuwa anasema: “Nitataja Ra-habu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo. Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara. Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo. Selah.” Zab. 87: 4-6. {1TG37: 11.3}

Zaidi ya hayo, ingawa mmoja ni wa damu ya Mataifa, iwapo kweli anampokea Kristo yeye kwa kuzaliwa kwake kiroho anakuwa wa uzao wa Abrahamu kwa maana Uvuvio husema, “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawasawa na ahadi.” Gal. 3:29. Watoto wa Abrahamu wanaozungumziwa hapa, kwa hivyo, hawawezi kutafutwa kati ya Wayahudi wakafiri, ila kati ya Wakristo. Wanahimizwa wamwangalie Abrahamu na Sara, na kuzingatia kwamba wakati ambapo Mungu alimwita Abra-hamu, ingawa alikuwa peke yake, alitii hata hivyo na Mungu akambariki; kwamba licha ya kuonekana ku-towezekana kwake yeye na Sara, Yeye alimfanya kuwa wengi. Je! Ikiwa wewe na peke yako ungaliitwa kwa neno Lake, kama alivyokuwa Abrahamu, kusimama peke yako kwa Ukweli na uadilifu, utakuwa shujaa wa Mungu kama alivyokuwa Abrahamu, au utatenda kama Yuda Iskariote aliyekengeuka? {1TG37: 12.1}

Iwapo hatungalikuwa na upendeleo wa kuchagua kama Abrahamu,

12

Mungu asingalikuwa ametukumbusha juu ya uzoefu wa Abrahamu. Tumeambiwa wazi tusiupoteze ujasiri, ila tuwe na imani kwa Mungu, maana Yeye anakusudia kutubariki na kutuzidisha, kama vile Yeye alivyowabariki na kuwazidisha babu zetu, Abrahamu na Sara. Sababu Anayoitoa kwa kutubariki kama vile alivyowabariki, ni hii: {1TG37: 12.2}

Aya ya 3 — “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.”

Kitovu cha Maandiko ni kujenga tena Zayuni, na hilo ndilo agizo letu. {1TG37: 13.1}

Aya ya 4, 5 — “Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa. Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu kabila za watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.”

Tunaulizwa kumsikiliza Bwana kwa sababu sheria na hukumu zitakoka Kwake. Hizi zinapaswa kuwa “nuru kwa watu.” Tena, asema Bwana: “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye ata-tufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi,

13

atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa hal-itainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Isa. 2: 2-4. {1TG37: 13.2}

Sheria itatoka wakati ambapo mlima (Ufalme) wa nyumba ya Bwana unasimamishwa juu ya milima (falme), na wakati umeinuliwa juu ya vilima. Wakati huo “nuru” itasababisha mataifa yaliyokaripiwa yamiminike katika mlima wa Bwana. Na, pia, badala ya kufua majembe yao kuwa panga, na miundu yao kuwa mikuki (Yoeli 3: 10), watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Isa. 2: 4. {1TG37: 14.1}

Kusema, “Haki yangu i karibu,” na “Wokovu wangu umekuwa wazi,” ni kusema kwamba wokovu umefika, lakini haki i karibu kuja. Na kweli ilioje! {1TG37: 14.2}

Je! Ni nini “mkono” wa Bwana unaowahukumu watu? Hili tutaona tunaposoma– {1TG37: 14.3}

Aya ya 9-10 — “Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani. Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uli-yeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombole-wa?”

Litakuwa jambo lisiloeleweka Mungu kuwa akijaribu kujiamsha Mwenyewe, kana kwamba Yeye, au mkono Wake, umelala! Aya hii inaonyesha kwamba Yeye anaita Vuguvugu

14

la Kutoka mkono Wake. Sahihi hivyo, kwa sababu Mungu hufanya kazi Yake na watumishi Wake. watumishi Wake, kwa hivyo, ni mkono Wake, nao watahukumu (watawatawala) watu, na watu watawaamini. {1TG37: 14.4}

Aya ya 6 — “Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka.”

Tunakumbushwa hasa kwamba mengine yote yataangamia, lakini wale wanaoupata wokovu wa Mungu na haki Yake watasimama milele. {1TG37: 15.1}

Aya ya 7 — “Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao.”

Wale wanaoijua haki Yake, watu ambao Ukweli huu umefunuliwa kwao, na ambao wanayo sheria Yake mi-oyoni mwao, bila shaka watateswa kwa lawama na matusi ya watu, lakini wamehimizwa wasiogope. Na utaku-wa nini mwisho wa watesi wao? — Hapa lipo jibu: {1TG37: 15.2}

Aya ya 8 — “Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.”

Kwa uchungu tunawasikitikia ndugu zetu Walaodekia ambao wanayo hasira, lakini kwa upofu, dhidi yetu. {1TG37: 15.3}

Aya ya 9, 10 — “Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono

15

wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani. Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?”

Iwapo watu Wake hawangalikuwa wamelala, basi lingalikuwapo hitaji gani la kuwaita waamke? Tunayo furaha kwamba Mungu mwenyewe anatuamsha na kutuambia wazi kwamba kama vile baba zetu walivyotenda mambo makuu, sisi, pia, kama “mkono” wa Bwana, twaweza na tutatenda mambo makuu kuliko wao. {1TG37: 16.1}

Aya ya 11 — “Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.”

Ashukuriwe Mungu kwamba sio tu Atawaamsha watu Wake na kuwafanya waimbe wanapoingia Zayuni, lakini pia anao uwezo wa kuondoa huzuni na maombolezo yao milele. Yeye anao uwezo wa kuiweka shangwe ya milele juu ya vichwa vyao. {1TG37: 16.2}

Aya ya 12 — “Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?”

Katika jaribio la kutuonyesha ulivyo upuuzi kuwaogopa watu ambao watakufa kama vile nyasi chini ya miguu, Uvuvio katika aya hii unasisitiza raha zilizoahidiwa za Isa. 51:11. Lazima iwe kwamba kwa baadhi hofu kwa ajili ya watu ni kubwa. Sasa kwamba tunalo Neno la Mungu na faraja hebu tumwogope Yeye Ambaye tu anayestahili kuogopwa. {1TG37: 16.3}

16

Aya ya 13 — “Ukamsahau Bwana, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo afanya-po tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?”

Tunapoanza kumuogopa mwanadamu, wakati huo huo tunamsahau Mungu. Swali, “Je! i wapi ghadhabu yake aoneaye?” Inamaanisha kwamba kwa kweli hakuna yoyote, kwamba ni udanganyifu tu. {1TG37: 17.1

Aya ya 14, 15 — “Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka. Maana mimi ni Bwana, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. Bwana wa majeshi ndilo jina lake.”

Naam, mateka wanatarajia kuachiliwa, lakini Mungu hatarajii kwamba bahari yenyewe igawanyike, Yeye hui-gawanya apendavyo na kusababisha watu Wake kuivuka kwa nchi kavu. {1TG37: 17.2}

Aya ya 16 — “Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.”

Hapa tunayo taarifa ya Mungu mwenyewe kwamba maneno tunayonena ni maneno ya Ukweli moja kwa moja kutoka Kwake. Zaidi ya hayo, Yeye anatuhakikishia kwamba mkono Wake, utunzi na uhifadhi Wake, umetuzunguka; ili kwa njia hii Aweze kuzipanda mbingu, aiweke misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, “Ninyi ni watu wangu.” {1TG37: 17.3}

Aya ya 17 — “ Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea, mkononi mwa Bwana, kikombe cha hasira yake; Bakuli la kikombe cha

17

kulevya-levya Umelinywea na kulimaliza.”

Amka, amka, rafiki yangu kwa ukweli kwamba kutekwa kwetu, huzuni yetu na maombolezo yetu karibu yanakoma; hatutayapitia tena kamwe. Yeye Ambaye huigawanya bahari hakika anaweza kutuweka huru. {1TG37: 18.1}

Aya ya 18 — “Hapana hata mmoja wa kumwongoza Miongoni mwa wana wote aliowazaa, Wala hapana hata mmoja wa kumshika mkono Miongoni mwa wana wote aliowalea.”

Hali ya Zayuni ya zamani na hata ya sasa imeletwa kwa mtazamo kwa ajili yetu kuichunguza. Ni ukiwa kama nini! Ni hali ya kutisha kama nini kwa kanisa kuwa ndani yake baada ya kuwaleta waongofu wengi! Hakuna mmoja wa kulisaidia! {1TG37: 18.2}

Hapa tunaambiwa kwamba walei katika Laodekia sio wa msaada wowote kiroho kwa mama (ukasisi) — la, hakuna hata mmoja anayejaribu kuinua mkono wake kuwasaidia ndugu wachungaji, — wote kwa mengi au machache katika upatano wameamua kukaa “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Ufu 3:17. {1TG37: 18.3}

Aya ya 19 — “Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza?”

Daudi wa zamani alipewa achague moja kati ya mambo matatu: “… Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? … “ 2 Sam. 24: 10-13. Sasa, kwa namna hiyo watu wa Mungu wanaulizwa

18

wachague ama ukiwa na uharibifu, au njaa na upanga. Basi tofauti na siku ya Daudi, Yeye Mwenyewe anatatua shida yetu iwapo tunamruhusu Yeye. {1TG37: 18.4}

Haya ni baadhi ya mambo ambayo watu wa Mungu wamepitia, hata sasa baadhi ya mambo haya bado yanawa-zonga. Tumaini letu, hata hivyo, ni katika ukombozi wa Mungu. {1TG37: 19.1}

Aya ya 20-22 — “Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya Bwana, Lawama ya Mungu wako. Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; Bwana, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena.”

Je! hatupaswi kushukuru kujua kwamba kila mmoja ambaye jina lake linapatikana kwenye kitabu ataokolewa hata kutoka kwa wakati wa taabu ambayo tutaingia hivi karibuni? — Mikaeli atasimama kwa ajili ya watu Wake (Dan. 12: 1)? Mara tu Atakapotukusanya, kamwe hatatutawanya tena. {1TG37: 19.2}

Aya ya 23 — “Nami nitakitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.”

Meza zimepinduliwa: Kile watu wa Mungu walipaswa kupokea kutoka kwa maadui zao, maadui zao lazima wakipokee kutoka kwao hivi karibuni. Kwa hivyo, tusipuuze kuyatumia manufaa ya rai ya Mungu ya ukombozi {1TG37: 19.3}

19

Naam, rafiki zangu, kwa kuwa safari yetu refu na ya majaribu i mwishoni hebu sisi kama “mkono” wa Mungu tutii kwa bidii mwito Wake wa uamsho. Sasa penye mwisho wa safari yetu refu na ya majaribu, tusiruhusu kitu chochote kituzuie kuvipata vitu viwili ambavyo vitatufanya tusimame milele — wokovu wa Mungu na haki Yake. {1TG37: 20.1}

Tunaulizwa sasa kuchagua ama kusimama upande wa Mungu au kwa upande wa maadui Zake (wale ambao tun-awaogopa); wale ambao wanafanya kila kitu kuyafumba macho yetu kwa Ukweli wa Mungu wa wakati huu — ama kumchagua Mungu, Roho Wake na Ukweli Wake uliofunuliwa, au kuchagua watu, ukiwa na uharibifu, njaa na upanga. {1TG37: 20.2}

20

ANDIKO LA SALA

Njia Pana Ni Udanganyifu

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 199, na aya ya kwanza— {1TG38: 21.1}

“Lakini njia ya uzima imesongana; na mlango ni mwembamba. Iwapo unaambata dhambi yoyote inayokuzonga, utaiona njia nyembamba sana kwa ajili yako kuingia. Njia zako mwenyewe, mapenzi yako mwenyewe, tabia za-ko ovu na mazoea, lazima uyaache ikiwa utaweza kuitunza njia ya Bwana …. Siku zote kwenye njia inayoongoza kwenye kifo yapo maumivu na adhabu, ipo huzuni na kuvunjika moyo, yapo maonyo kutoendelea kwayo…. Ni kweli kwamba njia ya Shetani imefanywa ionekane ya kuvutia, lakini yote ni udanganyifu; Katika njia ya uovu yapo majuto machungu na utunzi wa kuharibu. Tunaweza kufikiri inapendeza kufuata majivuno na tamaa ya kidunia; lakini mwisho ni uchungu na huzuni. Mipango ya ubinafsi inaweza kutoa ahadi za kuvutia, na kushikilia tumaini la raha; ila tutaona kwamba furaha yetu imetiwa sumu, na maisha yetu kutiwa uchungu kwa matumaini ambayo yamejikita kwa ubinafsi ….” {1TG38: 21.2}

Tunahitaji kuomba alasiri hii kwa kutambua kwamba pamoja na dhambi zetu hatuwezi kuingia katika Njia Kuu ya Utakatifu (Isa. 35: 8- 10). La, sio na tabia na mazoea yetu ya uovu. Haya lazima yaachwe ikiwa mwisho wetu mkuu utakuwa ni katika Paradiso. Tunastahili kujua kwamba ingawa njia pana huonekana ni ya maua, ni ulaghai tu. Huonekana imetandazwa waridi, lakini chini yake ni miiba — huzuni, machungu na kukata tamaa kwa kila aina. Tuombe kwamba tupate maono ya umuhimu wa kuiacha njia kuu ambayo waliozaliwa kwa mwili husafiri na kuingia kwenye njia kuu ambayo waliozaliwa kwa roho husafiri. {1TG38: 21.3}

21

WASIPOAMSHWA SASA, WANAWEZA KULALA MILELE

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, APRILI 26, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu ya alasiri hii inapatikana katika Isaya, sura ya 52. Tutaanza na aya ya kwanza. {1TG38: 22.1}

Isa. 52: 1 — “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.”

Wakati ambapo mwito huu wa kuamka unatangazwa kote katika nchi yote, Uvuvio unatangaza kwamba wakati wa mavuno umefika kwa malaika kuwaondoa na kuwaweka nje ya Zayuni na Yerusalemu wasiotahiriwa na walio najisi, kazi ambayo Uvuvio huita kwa njia tofauti-tofauti: kupatakasa patakatifu (Dan. 8:14), (2) ku-watakasa wana wa Lawi (Mal. 3: 1-3), (3) utakaso wa kanisa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80) , (4) Hukumu katika nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17), (5) mavuno (Mat. 13:30), kuwatupa nje samaki wabaya kutoka kwa sa-maki wazuri (Mat. 13: 47, 48), kuwatenga kondoo kutoka kwa mbuzi, — Hukumu ya Walio hai. {1TG38: 22.2}

Wadhambi, tunajua kwamba, wamekuwapo siku zote na bado wapo miongoni mwa watu wa Mungu. Kwamba utimilifu wa Andiko hili, kwa hivyo, u katika hasa siku za hivi karibuni, umeonyeshwa kwa jambo kwamba ukweli wa sura hii sasa umefunuliwa na unapelekwa kanisani, ukijaribu

22

kuwaamsha watu wa Mungu na kuwashawishi kwa ukweli kwamba hivi karibuni mavuno yataanza — mwanzo kutenganisha malimbuko, watu 144,000 kutoka ndani ya “nyumba ya Mungu,” kisha kufuatwa na mavuno ya pili kutoka kwa mataifa yote (Ufu. 7: 9); Andiko pia linaonyesha kwamba wadhambi hawatatembea tena na wa-takatifu na kwamba mavuno yanaleta mwisho wa dunia (Mat. 13:39). Tulia, fikiria, na usome tena Isaya hamsini na moja na hamsini na mbili. Usipite kwa haraka juu ya mada hii ya maisha na kifo. {1TG38: 22.3}

Je! Ni nani ambaye Bwana anamwita kuamka? — Zayuni na Yerusalemu. Kwa nini sio nyumba ya Yuda, nyum-ba ya Israeli, au nyingine yoyote? Zayuni ni nani? na Yerusalemu ni nani? Hapa yapo majibu: Katika wakati wa Isaya Yerusalemu ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Yuda, na Zayuni ilisimama ikulu ya wafalme. Na yanaweza ki-uakisi kuwakilisha nini? – Kunena kwa ulinganisho, “Capital Hill,” jumba kuu la kitaifa la Marekani (“Whitehouse”), tunaweza kuliita Zayuni ya Marekani; na mji mkuu wa taifa, Washington D.C., tunaweza kuuita Yerusalemu ya Marekani. {1TG38: 23.1}

Bwana, hata hivyo, haneni kwa Marekani, na kama Zayuni na Yerusalemu ulivyo kwa tukio hili unafananishwa na mtu, pacha wao kwa hivyo ni kama ifuatavyo: Baraza Kuu, “Ikulu” ya dhehebu lazima iwe Zayuni ya leo; na Mabaraza ya mitaa, watawala wa chini, lazima iwe ni Yerusalemu wa leo. Ni nani, basi, amelala na anaitwa “Amka?” — Baraza Kuu na mabaraza ya mitaa, — matawi ya wasimamizi ya dhehebu! Na iwapo hawajalala, kwa nini Uvuvio ungalikuwa unawaita “waamke?” Zaidi ya hayo sio ukweli kwamba wao hawayaoni maandiko haya? Huyashughulikia kana kwamba hayamo katika Bibilia hata kidogo. Haionekani kwako kwamba mahubiri yao ya kuwa na Ukweli

23

wote, ujumbe wa mwisho, wa kutokuwa na haja ya kitu chochote zaidi, ni udanganyifu wa kibinafsi? Je! Sio ujumbe wa Hukumu kwa Walio hai wa mwisho badala ya Hukumu kwa wafu? Na je wa awali sio wa umuhimu sana kuliko ule wa mwisho? {1TG38: 23.2}

Taarifa hii, “jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu,” inaonyesha wazi kwam-ba Zayuni ni dhaifu, na kwamba Yerusalemu ni ama uchi au umevikwa mavazi machafu, yenye kuchukiza. Sasa kuyahamisha maneno haya kutoka kwa mpangilio wake wa mfano kwenda kwa uhalisi, “nguvu” inaweza kusimamia nini ikiwa sio imani katika utimizo wa unabii huu? Mwalimu alisema kwamba bila imani huwezi kufanya lolote, lakini kwayo unaweza kuihamisha milima. Imani, kwa hivyo, ndio Zayuni na Yerusalemu wanahitaji leo. Imani yenyewe haionekani kama ilivyo hewa, lakini inapowekwa kwa utendaji inaweza kuondoa vizuizi vikubwa zaidi kuliko ambavyo hewa inavyoweza inapowekwa kwa utendaji. Ingawa hatuwezi kuuona upepo, tunaweza kuuhisi na kuyaona matokeo ya nguvu yake. Ndivyo ilivyo na imani. {1TG38: 24.1}

Ijayo kuzingatia ni mavazi. Vazi la mtu ndicho kitu cha kwanza kinachovutia jicho. Lile, “vazi zuri,” kwa hivyo, lazima liwakilishe kitu ambacho hubadilisha muonekano wa yule anayelivaa kutoka kuwa wa kuchukiza kiroho na mchafu hadi kuonekana kuwa mzuri kiroho na wa kuvutia. Ni nini basi, linaweza kuwakilisha kuliko tabia ya Ukristo ya kweli, — wema, upendo, rehema, na haki, — yale ambayo yanaonekana na ambayo humfanya mtu wa kupendeza na Mkristo anayeheshimika kweli. {1TG38: 24.2}

“Nguvu” na “vazi,” pamoja, kwa hivyo, sio kitu kipungufu kuliko haki ya Kristo — tendo la imani na matokeo yake. Hizi ndio kanuni ambazo Zayuni na Yerusalemu ya leo inahitaji.

24

Hizi wanahitaji sasa kwa sababu “tokea sasa….asiyetahiriwa, wala aliye najisi” — wadhambi wasioamini na am-bao hawakusamehewa, wale ambao hawajajivika “mavazi mazuri”, watafungwa katika matita kwa ajili ya moto, hawatapatikana tena kati ya watakatifu. {1TG38: 24.3}

Aya ya 2 — “Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.”

Zayuni na Yerusalemu wa leo hawako tu uchi, lakini ni wachafu: hulala katika mavumbi, kwa mfano, wangali bado mateka na hata hawajui! Na kwa hivyo binti za Sayuni na Yerusalemu, dhehebu lote kwa ujumla, linaulizwa kuamka kutoka mavumbini, na kuketi juu ya kiti chake cha enzi, kujiweka huru kutoka kwa nira ya utumwa wake, vifungo vya shingo lake. Linahitaji kutambua kwamba siku ya ukombozi wake imewadia, na kwamba sasa litafanywa kuwa huru, lisitawaliwe tena na wanadamu. {1TG38: 25.1}

Aya ya 3 — “Maana Bwana asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.”

Kwa vile aya hii haihitaji maelezo, hebu tuendelee na— {1TG38: 25.2}

Aya ya 4, 5 — “Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu. Basi sasa, nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.”

Aya hizi zinamkumbusha Zayuni na Yerusalemu wa leo

25

kwamba wanawakandamiza walei kama vile sayidi wa Wamisri na mabwana wa Mwashuri walivyowadhulumu wana wa Israeli. Wanawafanya watu wa Mungu kulia, na hivyo wanalikufuru jina Lake na kuwazuia watu Wake wasikutane na Ukweli wa Mungu wa wakati huu. {1TG38: 25.3}

Aya ya 6 — “Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.”

Kwa sababu watu wa Mungu wanatawaliwa visivyo, wanapotoshwa, na kunyanyaswa, na jina Lake kutukanwa, Anatangaza kwamba Hatawaacha kwa kutokujua: Anaahidi kwamba hata iwe vigumu jinsi gani watawala wa kimwili wa ambao haujapepetwa Zayuni na Yerusalemu kujaribu kuwadumisha watu katika kutoujua ujumbe huu wa kupepetwa, Yeye, licha ya hayo, atawafanya watu Wake wausikie na kujua kwamba Ndiye anayenena, sio adui jinsi wanavyoambiwa. {1TG38: 26.1}

Je! Mungu anafikiria nini kuhusu ujumbe huu na wajumbe Wake? Hebu tusome– {1TG38: 26.2}

Aya ya 7 — “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako an-amiliki!”

Je! Ni habari gani bora kuliko hizi ambazo watu wangalitaka wakiwa bado uhamishoni? Ikiwa ujumbe huu, Ufalme wa Mungu (kanisa lililosafishwa), sio ujumbe wa amani na usalama, basi tuambie ni nini Uvuvio una-maanisha kwa kusema kwamba mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwa-na-mbuzi, ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, “na mtoto mdogo atawaongoza.” “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 11: 6; 33:24. {1TG38: 26.3}

26

Aya ya 8 — “Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.”

Watumishi wote wa Mungu kwa pamoja, na kwa furaha, watauinua ujumbe Wake (Sauti), kwa sababu wakati Bwana atakapourejesha tena Zayuni wataona jicho kwa jicho. Ni tofauti gani kati ya walinzi wa Zayuni wa kesho, na walinzi wake wa leo ambao kati yao wawili ni vigumu hakika kuona jicho kwa jicho! “wale tu ambao wameyahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu.” — “Mapitio na Kutangaza,” Novemba. 19, 1908. {1TG38: 27.1}

Aya ya 9, 10 — “Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu. Bwana ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.”

Wakati mambo haya yanapotukia, ndipo dunia yote itaona wokovu wa Mungu wetu. Lakini sasa hebu tuusikie ushauri Wake kuhusu kile angalitaka tufanye: {1TG38: 27.2}

Aya ya 11 — “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.”

Wale ambao huupeleka Ukweli wa Mungu lazima wawe safi; lazima wawekwe huru kutoka kwa kila kamba am-bayo huwafunga kwa vitu vya dunia hii. {1TG38: 27.3}

Aya ya 12 — “Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.”

Kuingia kwetu katika nchi ya baba zetu, tunaambiwa hapa, hakutakuwa kwa haraka au kukimbia kwa woga, kwa sababu Bwana Mwenyewe atatutangulia, na Yeye atakuwa nyuma yetu. {1TG38: 28.1}

Aya ya 13, 14 — “Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu).”

Aya hizi, kama unavyojua, zimetumika muda mrefu kwa Bwana. Yeye hata hivyo, hatendi mambo haya binafsi, ila Huyatenda kupitia wajumbe Wake. Sasa kumbuka, katika aya ya 13 tunaambiwa ya kuwa Bwana ameinuliwa juu, ambapo katika aya ya 14 tunaambiwa uso wake uliiharibiwa na umbo lake zaidi ya wanadamu. “Yeye hana umbo wala uzuri;…hana uzuri hata kumtamani.” Isa. 53: 2. Kwa nini? — Jibu la pekee ambalo linaweza kutolewa kwa swali hilo, ni hili: Mungu anajua kwamba asili ya dhambi ya watu huwahimiza kutengeneza sanamu za wanadamu. Wao huanguka ki-urahisi kwa watu ambao wanaweza kuonyesha uso mzuri. Hutenda kana kwamba wamebatizwa kwa majina ya Paulo na Apollo mamboleo. Ni wafuasi wa kiburi na mbwembwe badala ya wa-fuasi wa Mungu na Ukweli Wake unaostawi. Ili kuwatenga na upumbavu huu, Mungu hutuma Ukweli Wake kupitia kwa wale wasiotarajiwa. Hivyo kinyume cha mapendeleo na matarajio yao imeandikwa kwamba Bwana hakuwa na umbo wala uzuri; lakini licha ya hayo, “Atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.” {1TG38: 28.2}

28

Aya ya 15 — “Ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.”

Yeye atayanyunyizia (kuyatakasa — Ezek. 36:25) mataifa mengi. Wale ambao hawataacha kukifuata kiburi cha mwanadamu wataongozwa watumbukie shimoni, kwa mfano. Kila mtu wa ubatili ataanguka nje kupitia “kichu-jio cha ubatili,” lakini wafuasi wa Ukweli na haki wataishi milele. Hakuna lolote la mambo haya limewahi kuambiwa yeyote. Ni, kwa hivyo, muhimu sana kutulia, kutazama, na kusikiliza, kufuata kwa bidii Ukweli Wenyewe. Ujue kwamba wa-ubatili hujifanya wonyesho, kuhusu mafanikio yao, na haswa ya dini yao. Ujue kwamba hufanya hivi ili kuteka mioyo ya wasikilizaji wao kwao wenyewe, ili kupata wafuasi, kuwakazia ushawishi wao, kukiweka kitu fulani. Mafarisayo katika siku za Kristo walikuwa na ujuzi sana katika taaluma hii ya kupora mioyo. Waliomba pembezoni mwa njia ili waonekane na watu, na hivyo waliwahadaa zaidi ya ku-waongoa tena. {1TG38: 29.1}

“Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto ulao; na pumzi yake. [ujumbe Wake leo] ni kijito ki-furikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.” Isa. 30:27, 28. {1TG38: 29.2}

Israeli wa kale walitaka mtu mrefu zaidi katika nchi hiyo awe mfalme wao, na walimpata. Angaliwaongoza kuingia katika maangamizi, hata hivyo, isingalikuwa kwa huyo mwenye afya na wa kutojivuna Daudi ali-yewaokoa kutoka kwa jeshi la Wafilisti na kutoka kwa jitu lao. {1TG38: 29.3}

29

Ni mazoea ya kawaida miongoni mwa Wakristo kutengeneza sanamu za wanadamu. Hili linatambulika hata na ukasisi wa madhehebu mengine. Mchungaji fulani, akizungumza juu ya “Dini katika Maisha,” aliwaambia wasikilizaji wake wa redio kwamba alisimama kwenye kituo cha petroli kulijaza gari lake mafuta siku moja. Ali-pokuwa hapo, mhudumu alifikiria kwamba sauti ya mchungaji ilisikika kuwa anayoijua, na akauliza: “Je! Wewe ndiye mtu ambaye nimekuwa nikimsikiliza kila asubuhi kwenye redio?” Mara tu mhudumu huyo alipomsikia mchungaji huyo akisema naam, alijibu kwa dhati: nimevunjika moyo ndani yako; Nalifikiri nalikuwa nikimsikili-za mhubiri aliye mrefuyapata futi sita, wa uzani usio chini ya pauni mia mbili, lakini sasa naona wewe ni mbilikimo tu.” Zoea hili ni kawaida kati ya Wakristo. {1TG38: 30.1}

27

KWA UFUPI KUFANYA MUHTASARI WA SOMO LETU: Tunaona kwamba wakati wa utakaso wa kanisa umekaribia; kwamba Zayuni (Baraza Kuu) na Yerusalemu (mabaraza ya mitaa) wameitwa “waamke,” ili binti wa Zayuni, kanisa, liweze kuvikwa haki ya Kristo; kwamba yeye ni dhaifu; ya kuwa hana haki ya Kristo; kwamba siku ya ukombozi wake imekaribia; kwamba atawekwa huru kutoka kwa utawala wa mwanadamu na kutoka kwa unafiki; ya kwamba Zayuni na Yerusalemu walivyo leo, wanawakandamiza walei kama vile mabwana wa Mwashuri walivyowadhulumu wana wa Israeli wa kale; kwamba Mungu hatawaacha watu Wake katika kuto-kujua; kwamba watajua kuwa Yeye ndiye anayenena, sio adui jinsi ambavyo wamefanywa kuamini; kwamba ujumbe wa Ufalme wa Mungu ni ujumbe wa faraja; kwamba waaminifu Wake watauinua ujumbe Wake (Sauti); kwamba baada ya Zayuni na Yerusalemu kuamka wataona “jicho kwa jicho,” na ni wale tu ambao wameyahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangazaujumbe huu katika Kilio Kikuu (“Mapitio na Kutangaza,” Nov. 19, 1908); kwamba kisha miisho yote ya dunia watauona wokovu

30

wa Mungu wetu; kwamba Mungu hutuma Ukweli Wake, sio kupitia kwa wale ambao wameinuliwa na kufany-wa sanamu na wanadamu, ila kupitia kwa watumwa wasiotarajiwa; kwamba wale ambao hawatamwacha mwa-nadamu wataanguka, ilhali wafuasi wa Ukweli na haki wataishi milele; hilo ni jukumu takatifu kwa wote wabe-ba-Ukweli kuutangaza ujumbe kwa ndugu wote, kwa maana ikiwa hawataamshwa sasa, wanaweza kulala milele. {1TG38: 30.2}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG38: 31.1}

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG38: 31.2}

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 36, 37, 38

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>