fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 05, 06

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 5, 6

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

KARAMU AMBAYO HUVINGIRISHA PAZIA, HUFUNGUA MALANGO, NA KUSABABISHA KIFO KUTOWEKA

UZINZI UNATOWEKA KWA LALAMA ZA WATOTO — UAMSHO NA MATENGENEZO YANASHINDA

                                    

1

WAZO LA SALA

Acha Mjadala; Wasilisha Ukweli

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano, kuanzia ukurasa wa 40, aya ya mwisho– {2TG5: 2.1}

“Badala ya kujadili nadharia za uongo, au kutafuta kukabiliana na wapinzani wa injili, fuata mfano wa Kristo. Ruhusu Kweli mpya kutoka kwa hazina ya nyumba ya Mungu zinga’e maishani. ‘’Hubiri Neno.’’ ‘Panda kando ya maji mengi.’ ‘’Uwe mwepesi kwa msimu, na nje ya msimu.’’ ‘Yeye aliye na neno Langu, aseme Neno Langu kwa uaminifu. Je! Makapini nini kwa ngano? asema Bwana.’’ ‘ Kila neno la Mungu ni safi…. Usiongeze kwa maneno Yake, asije Akakukemea, na ukapatikana muongo.’” {2TG5: 2.2}

Tuombe alasiri hii kwa ajili ya uwezo wa kuufuata mfano wa Kristo katika kufundisha. Tuweze pia kusali kwamba tutakumbuka kuwa tumeagizwa tusijihusishe katika mjadala na wale ambao hawakubaliani nasi; ya kwamba Kristo hakufanya mjadala, na lazima tuepuke pia iwapo tutashinda; kwamba Mungu atatupatia kweli mpya za kuleta kwa watu; kwamba ikiwa kweli kama hizo haziwashawishi wapinzani wa “injili ya milele,” haku-na chochote kitakachoweza, hata iwapo wafu wanaweza kufufuka kwa ushahidi dhidi yao; kwamba tuiinue Bi-bilia juu ya vitabu vingine vyote; kwamba tupime vingine vyote kwa kigezo cha Bibilia, na milele kuvivunja vijiti vingine vyote vya kupimia. {2TG5: 2.3}

2

KARAMU AMBAYO HUVINGIRISHA PAZIA, HUFUNGUA MALANGO, NA KUSABABISHA KIFO KUTOWEKA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, SEPTEMBA 6, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko la uchambuzi wetu alasiri hii ni Isaya 25 na 26. Ili kujifahamisha vyema kwenye mada hiyo, tutaanza na aya ya sita ya sura ya ishirini na tano. Baadaye tutazichambua aya tano za kwanza. {2TG5: 3.1}

Aya ya 6 — “Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai ili-yokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.”

Kwanza kabisa tunapaswa kupata ukweli wa mlima huu wa ki-mfano. Kwa habari hii lazima twende kwa aya ya mwisho ya sura ya ishirini na nne, kwa sababu kisa cha sura ya ishirini na tano kinaanza na sura iliyotangulia. Tutasoma aya hizi kwa njia ya kuambatana: {2TG5: 3.2}

Isa. 24:23; 25:6 –”Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Zayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu. Na katika mlima huu [Mlima Zayuni] Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai ili-yokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojoro-jo wake, iliyochujwa sana.”

3

Hapa unaona kwamba”Mlima Zayuni” ni mlima ambao juu yake Bwana ataiandaa karamu kwa watu wote, karamu ya vitu vinavyotamanisha. Hapo watu watakusanyika pamoja. {2TG5: 4.1}

Aya ya 7 — “Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule ulio-tandwa juu ya mataifa yote.”

Wakati kificho ambacho chini yake mataifa sasa yanasimama, kinavingirishwa mbali, ndipo watajikuta palipo wazi — bila ulinzi kwa “upepo” na “dhoruba.” Naam, wakati pazia ambalo sasa huning’inia juu ya watu wote wa dunia, linavingirishwa chini, ndipo watakiona kile wasichoweza kuona sasa. Na nini basi? — {2TG5: 4.2}

Aya ya 8-10 — “Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake. Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa.”

Ili kufanya matukio haya makubwa yawezekane, sio tu wale ambao kwa wakati huo wanaitawala nchi, bali Moabu, pia, tunaona, watakanyagiwa chini. Na Moabu angaliweza kuwa nani kama sio Waarabu ambao sasa wanaweka madai mazito kwa ardhi ya Palestina? Hivi karibuni ulimwengu utagundua kwamba Mungu hajaiacha dunia, na kwamba Mungu ndiye fundi wa hali hiyo. {2TG5: 4.3}

Aya ya 11, 12 — “Naye atanyosha mikono yake

4

katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake. Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini.”

Aya hizi hushikilia ukweli mbele yetu kwamba haijalishi ni aina gani ya ngome wanadamu wanaweza kubuni, kama hii hata hivyo itaangushwa chini kama majani wakati Bwana atadhihirisha nguvu Yake. Kwa kuwa sasa umeona Ukweli huu wa ajabu wa Bibilia, ruhusu uwe wewe kusema: {2TG5: 5.1}

Isa. 25: 1 — “Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.”

Hapa tunaonyeshwa kwamba kama tokeo la Ukweli huu uliofunuliwa, baadhi kwa kweli watampokea Bwana wa Bibilia kama Mungu wao, na wataahidi kumtukuza Yeye na milele kulisifu jina Lake la ajabu kwa sababu wanaona kwamba Ametenda mambo ya ajabu. Mashauri Yake ya zamani hawatayakataa kwa sababu watajua kutoka kwa uzoefu kwamba mashauri Yake ni uaminifu na Kweli. Kutoka kwa uzoefu wao wa kibinafsi wa-tajua nguvu za Mungu na kusema: {2TG5: 5.2}

Aya ya 2, 3 –”Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wa-geni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele. Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza, Mji wa mataifa watishao utakuogopa.”

Mji wa aya hii lazima uwe ule uliotajwa mwanzo katika Isaya 24: {2TG5: 5.3}

5

“Mji wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote. Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka. Ndani ya mji umebaki ukiwa, na lango lake limepigwa kwa uharibifu. Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake. {2TG5: 6.1}

“Hawa[wale ambao hawajatikiswa wakaanguka] watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga kelele toka baharini. Basi, mtukuzeni Bwana katika mashariki, litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari. Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. [tokeo lake, kutakuwa na waongofu kutoka pembe nne za dunia]. {2TG5: 6.2}

“Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana. Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.” Isa. 24: 10-17. {2TG5: 6.3}

Nukuu ifuatayo kutoka kwa Roho ya Unabii inaongeza nuru kwa aya hizi: {2TG5: 6.4}

“Naliona miale ya nuru iking’aa kutoka mijini na vijijini, na kutoka maeneo ya juu na maeneo ya chini ya dunia. Neno la Mungu lilifuatwa, na kama tokeo kulikuwa na kumbukumbu kwa ajili Yake katika kila mji na kijiji. Kweli Yake ilitangazwa ulimwenguni kote.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 28 na 29. {2TG5: 6.5}

Isa. 26: 1 — “Siku ile wimbo huu utaimbwa

6

katika nchi ya Yuda; Si tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa ukuta na maboma.”

Wimbo wa utukufu wa Bwana kwa hivyo utaimbwa katika Nchi ya Ahadi, na huko watakatifu watakuwa na mji ambao hauwezi kutikiswa ukaanguka, kwa maana utakuwa na wokovu kenye kuta. Kisha itanenwa: {2TG5: 7.1}

Aya ya 2 — “Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.”

Hapa inafundishwa kwamba haya yote yanatukia katika siku ya wokovu, katika siku ambayo malango yana-weza kufunguliwa ili taifa lenye haki liingie ndani. Naam, taifa lote, la kama hao ambao wanapaswa kuokolewa, sio mdhambi kati yao, basi wataitikia mwito, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” {2TG5: 7.2}

Aya ya 3, 4 — “Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anaku-tumaini. Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.”

Ingawa katika miaka yote ya historia mataifa yameendeleza nguvu kubwa, lakini hakuna hata moja ambalo limedumisha nguvu hiyo milele. Lakini hapa tumehakikishiwa tena kwamba wale wanaomtegemea Bwana Yehova watapata amani ya milele na nguvu ya milele. {2TG5: 7.3}

Aya ya 5-10 — “ Kwa kuwa amewashusha Wakaao juu; mji ule ulioinuka, aushusha; Yeye aushusha, aushusha hata nchi; Auleta hata mavumbini. Naam, miguu yao walio maskini,

7

Njia ya mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki. Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki. Mtu mbaya ajapofad-hiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.”

Aya hizi zinatuambia wazi kwamba wakati hukumu za Mungu zitaanguka duniani, wenye akili timamu wa-tajifunza haki; lakini wadhambi wasiotubu hawatajifunza haki bila kujali ni nini kinafanywa kwa ajili yao. Na hii ndio sababu watazuiliwa kutoka kwa mkutano wa wenye haki. Wenye haki, hata hivyo, hata sasa wanahisi mkono wa nguvu wa Bwana na kwa kutangaza kwa machungu: {2TG5: 8.1}

Aya ya 11 — “Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.”

Hakika, wakati mkono wa Mungu umeinuliwa ili kuwakomboa watu Wake, waovu hawatauona. Lakini baada ya wenye haki kuokolewa, waovu watauona wazi na kuwaonea wivu, lakini itakuwa kwa aibu yao na kuwa wamechelewa sana kuwafanyia mema yoyote. Hata sasa wakati “mvua ya masika” inanyesha, wanaojiona kuwa wenye haki ambao hudhani kwamba hawana haja ya kitu, ni ama wanakimbia kutoka kwayo au wanavuta koti la mvua juu ya vichwa vyao. Watafutao haki, hata hivyo, hujitokeza

8

wazi. Hivyo wanajifunza kusema– {2TG5: 8.2}

Aya ya 12 — “Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.”

Hiya yanaweza kusemwa tu na wale wanaomruhusu Bwana kuitekeleza kazi Yake mioyoni mwao, ili wamsifu Yeye: {2TG5: 9.1}

Aya ya 13-16 — “Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako. Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao. Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii. Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.”

Aya hizi zinatangaza kwamba Israeli ya ahadi, sio Myahudi asiyeamini, wameongezeka kwa idadi tangu wali-poondolewa katika nchi yao, tangu wakati huo wametawanyika hadi miisho ya dunia. Wakati adhabu hii (ya kuwafukuzwa mbali na nchi yao) bado i juu yao, wanamimina maombi na kusema: {2TG5: 9.2}

Aya ya 17, 18 — “Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake; Ndivyo tulivyokuwa sisi mbele yako Ee Bwana. Tu-mekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani; wala hawakuanguka wakaao duniani.”

9

Hapa imeonyeshwa kwamba macho ya waliotubu yatafumbuliwa; watajiona wenyewe kama ambavyo Mungu huwaona, na kukiri kwamba hapo awali wameshindwa katika juhudi zao, kwamba wamekuwa na mimba, wamekuwa na utungu, lakini wamezaa “upepo” tu, kwa mfano, ilhali wasiotubu wanafikiria kwamba wao ni matajiri na wamejitajirisha, wanafanya tendo kubwa, na hawahitaji kitu. {2TG5: 10.1}

Naam, kanisa sasa linaweza kujivunia mafanikio yake, au kinachojulikana kama ushirika mkubwa, lakini sio muda mrefu, nalo pia, litagundua kwamba limeshindwa kumaliza kazi yake, kwamba ulimwengu bado unaharibu nchi, kwamba watu wake hawajaokolewa na kwamba badala ya kuwa limeleta wokovu, halijazaa chochote ila “upepo.” {2TG5: 10.2}

“Katika kupepetwa kukuu kutakakotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zinaonyesha kuwa wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha kwamba pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha uwanda wake kabisa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {2TG5: 10.3}

Aya ya 19 — “Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka. Amkeni kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.”

Sio walio hai tu, lakini wafu pia watakusanywa katika “mji wenye nguvu.” Tunasikia tayari Bwana akiturai sisi sote, akisema: {2TG5: 10.4}

Aya ya 20 — “Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.”

10

Ombi hili linaonyesha kwamba tunakaribia wakati wa taabu na kwamba Mungu anayo hamu ya kutuficha. Wenye busara watamsikia Yeye na kuvipokea vyumba, ulinzi Anaotoa kwa ajili yao. {2TG5: 11.1}

Aya ya 21 — “Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.”

Kweli hizi zote ambazo Mungu analeta kwa usikivu wetu, zinaelekeza kwa jambo moja: Kwamba siku kuu na ya kuogofya ya Bwana imekaribia, kwamba hivi karibuni Yeye atadhihirisha nguvu Yake na kuitikisa dunia ili kila kitu kisichoweza kutikisika kiweze kusimama. Je! Haufurahi, Ndugu, Dada, kwamba Mungu anakupa fursa ya kwanza kujiandaa kwa ajili ya siku ya Mungu, kushika sana Ukweli wake unaoongezeka daima? {2TG5: 11.2}

11

ANDIKO LA SALA

Jinsi Ya Kuhifadhi Maarifa Yasiyoharibika

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano, kuanzia ukurasa wa 41, aya ya tatu– {2TG6: 12.1}

“Kukengeuka kutoka kwa neno la Mungu na kujilisha maandishi ya watu ambao hawajavuviwa, nia hudun-ishwa na kuwa vivi-hivi…. Uelewa hujizoesha wenyewe kwa ufahamu wa mambo ambayo huyajua, na katika ibada hii kwa mambo ya wafaji unadhoofishwa, nguvu yake kuwa finyu, na baada ya muda unashindwa kupanuka. Hii yote ni elimu ya uongo. Kazi ya kila mwalimu inapaswa kuwa ya kukazia akili za vijana juu ya kweli kuu za neno la Uvuvio. Hii ndio elimu muhimu kwa maisha haya na kwa maisha yatakayokuja. Na isi-fikiriwe kwamba hii itazuia masomo ya sayansi, au kusababisha kiwango cha chini katika masomo. Maarifa ya Mungu yako juu sana kama mbingu na mapana kama ulimwengu…. Wacha vijana watafute kuelewa kweli hizi walizopewa na Mungu, na akili zao zitapanuka na kukua imara katika juhudi. Yatamleta kila mwanafunzi am-baye ni mtendaji wa neno katika uwanja mpana wa mawazo, na kumhifadhia utajiri wa maarifa ambao hautaha-ribika…. elimu kama hiyo itarejesha sura ya Mungu ndani ya nafsi.”{2TG6 : 12.2}

Ni funzo gani sio kwa vijana tu ila kwa watu wazima pia! Wacha tuombe kwamba tugundue umuhimu wa kusoma Ukweli uliovuviwa; kwamba tuweze kutambua hauondoshi masomo ya sayansi ya kweli; kwamba kuya-toa maisha yetu kwa Neno la Mungu ni kupata hazina kubwa ya hekima; kwamba hivyo chapa ya Mungu in-arejeshwa ndani ya nafsi. {2TG6: 12.3}

12

UZINZI UNATOWEKA KWA LALAMA ZA WATOTO — UAMSHO NA MATENGENEZO YANASHINDA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, SEPTEMBA 13, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu inapatikana katika sura ya kwanza na ya pili ya Hosea. Tutaanza na– {2TG6: 13.1}

Hos. 1: 2 –”Mwanzo wa neno la Bwana kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda, ukatwae mke wa uzinzi na watoto wa uzinzi: kwa maana nchi hii imefanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.”

Tunaona upesi kwamba mke huyu na watoto hawa wanawakilisha watu wa Mungu wakimwacha Yeye, na kwamba tendo la uovu kama hilo, Yeye huliita uzinzi. {2TG6: 13.2}

Aya ya 3, 4 –”Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Diblaimu; naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamme. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza damu ya Yezreeli kwa nyumba ya Yehu , na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.”

Sababu ya Mungu kumwita hivyo mwana wa maono wa kwanza wa Hosea, ilikuwa kuashiria kwamba kwa muda mchache Angalilipiza kisasi cha damu ya Yezreeli kwa nyumba ya Yehu, ambaye wakati huo alikuwa mfalme wa Israeli. Kisha akatangaza Bwana: {2TG6: 13.3}

13

Aya ya 5 — “Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli, katika bonde la Yezreeli.”

Kuuvunja upinde kungalimaanisha kuivunja nguvu ya jeshi la taifa. Historia ya hili imeandikwa katika 2 Wafalme 10, 11. {2TG6: 14.1}

Aya ya 6 — “Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama: kwa maana sitairehemu tena nyumba ya Israeli; bali nitawaondolea mbali kabisa.”

Jina la mtoto huyu liliashiria uharibifu kamili wa nyumba ya Israeli, ufalme wa kabila kumi. Uharibifu huu, tunajua, ulitekelezwa na mfalme wa Ashuru, aliyewatawanya watu katika miji yote ya Wamedi. Historia ya hili inapatikana katika 2 Wafalme 18:11 — “Na mfalme wa Ashuru akawahamisha Israeli mpakaAshuru, akawaweka katika Hala na katika Habori karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.” {2TG6: 14.2}

Aya ya 7 — “Lakini nitarehemu nyumba ya Yuda, nitawaokoa kwa BWANA Mungu wao, wala sita-waokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.”

Bwana aliahidi kuiokoa nyumba ya Yuda kutokana na uvamizi wa mfalme wa Ashuru. Historia ya tukio hili imeandikwa katika 2 Wafalme 19:35 — “Ikawa usiku uo huo, malaika wa Bwana akatoka, akapiga katika kambi ya Waashuru watu mia na themanini na tano elfu: na watu walipoamka asubuhi na mapema, tazama, wote walikuwa wamekufa.”{2TG6: 14.3}

14

Aya ya 8, 9 — “Basi akishamwachisha Lo-ruhamah, akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamme. Ndipo Mungu akasema, Mwite jina lake Lo-Ammi, kwa kuwa ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa Mungu kwenu.”

Jina la mtoto wa tatu liliashiria kwamba ingawa Israeli na Yuda walikuwa watu wateule wa Mungu, siku ilikuwa inakaribia kwa haraka ambayo hawangeitwa tena watu wa Mungu. Utimilifu wa awamu hii ya unabii unatuleta kwenye enzi ya Ukristo. {2TG6: 15.1}

Hos. 1:10 — “Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itakuwa kama mchanga wa bahari, isiyoweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, baada ya kuambiwa, Ninyi si watu Wangu, wa-taambiwa, Ninyi ni wana wa Mungu aliye hai.”

Licha ya majanga ambayo yangaliwapata wana wa Israeli, walipaswa kuwa wengi sana. Na wanapoongezeka hivyo kwa wingi sana, wataitwa tena wana wa Mungu. Na hivyo hapa tunaona unabii wa uasi wa watu wa Mungu na Mungu kuwakataa, pamoja na toba yao na kukubaliwa tena Naye. {2TG6: 15.2}

Hebu hapa kwa muda tujadiliane majina “Yuda” na “Israeli.” Wakati yanaposomwa kijuujuu majina haya ni kama sheria hupotoshwa na kufanywa yamaanishe Wayahudi waliotambuliwa. Lakini hatupaswi kuwa wasomaji na wawazaji wa kijuujuu. Hebu tuwe wanafunzi wa kina wa Bibilia. Sasa, kila mtu anajua kuwa Wayahudi wal-iotambuliwa wa leo ni wachache tu — hakika sio kama mchanga wa bahari. Wana wa Israeli wasiohesabika, kwa hivyo, hawawezi kuwa Wayahudi wasioamini wa leo. Mbali na hilo,

15

Wayahudi waliotambuliwa wa leo sio wazawa wa ufalme wa kabila kumi, lakini wa ufalme wa kabila mbili. Je! Ni nani, basi, umati huu wa watu unaorejelewa katika unabii wa Hosea? {2TG6: 15.3}

Tusije tukapuuza ukweli kwamba Injili ya Kristo iligawanya nyumba ya Yuda kwa madhehebu mawili — Uyahudi na Ukristo, kwamba kanisa la Kikristo kwa karibu miaka minne baada ya kufufuka kwa Kristo liliju-muisha Wayahudi tu. Kwa udhahiri, basi, Wakristo wa asili walikuwa Wayahudi damu kamili, — kanisa la Kikristo ni tawi tu la kanisa la Kiyahudi, lakini wao na wazawa wao, katika miaka yote, wamepoteza utam-bulisho wao wa taifa. Basi, pia, wazawa wa zote Israeli na Yuda ambao kupitia miaka ya utumwa walipoteza utambulisho wao kama walivyofanya Wayahudi walioupokea Ukristo, kwa mujibu wa unabii lazima pia waweze kuwa wameongezeka sana. Kwa udhahiri, basi, wengi ambao huchukuliwa kama Mataifa, ni ila wazawa wa-siotambuliwa wa Yuda, Israeli, na Wayahudi Wakristo wa kale. Kanisa la Kikristo lenyewe ni, ambavyo tu-meona, kanisa la Kiyahudi-Kikristo. {2TG6: 16.1}

Hawa wazawa wa Yakobo, ambao walifyonzwa na nchi za mataifa, kwa hivyo, walipaswa kuongezeka kama mchanga wa bahari. Wao ni wale ambao, baada ya kuwa Wakristo, wanaitwa tena wana wa Mungu aliye hai. {2TG6: 16.2}

Kati ya wale wa kwanza kuipokea imani ya Kikristo, mtume Petro anasema hivi: “Ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu: mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.” 1 Pet. 2:10. {2TG6: 16.3}

Na mtume Yohana anasema: “Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kuwa

16

wana wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. ” Yohana 1:12. {2TG6: 16.4}

Sasa tunaona kwamba unabii wa Hosea 1 unaanza na nyumba ya Israeli na Yuda, na unatuleta chini kupitia mkondo wa wakati hadi kwa enzi ya Ukristo. Kwa nuru juu ya kanisa katika kipindi cha Ukristo, tunafungua– {2TG6: 17.1}

Aya ya 11 — “ Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.”

Neno la Mungu, kwa hivyo, linatangaza bayana kwamba raia wa falme zilizobomolewa — Yuda na Israeli — kama Wakristo, pamoja na Mataifa ambao wamejiunga nao, watakusanyika pamoja na kujiteulia mfalme. {2TG6: 17.2}

Kwa nembo kama hiyo, nabii aliambiwa kwamba baada ya siku nyingi za kutojulikana na kutangatanga, “wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana Mungu wao, na Daudi mfalme wao [dhahiri Daudi ndiye “kichwa kimoja” ambaye watamteua] , na watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.” Hos. 3: 5. {2TG6: 17.3}

Kuendelea na mfano uo huo wa familia, na kuelekeza kwa enzi ya Ukristo, Bwana anaamuru: {2TG6: 17.4}

Hos. 2: 1 — “Waambie ndugu zako waume, Ammi; na dada zako, Ruhama.”

Hapa tunaona kwamba majina ya watoto wawili wa sura ya 1 yametajwa tena, lakini herufi mbili za kwanza za kila jina zimeangushwa: {2TG6: 17.5}

17

Lo-ruhamah amekuwa Ruhama, na Lo-Ammi amekuwa Ammi. Sasa ukweli kwamba hawa ni kaka na dada wa Yezreeli, wanaonyesha ukweli kwamba yule ambaye Bwana anaamuru kuongea nao, ni Yezreeli, mzaliwa wa kwanza wa hao watatu. Anapaswa kuupeleka ujumbe kwa ndugu zake, Ammi na Ruhamah. {2TG6: 18.1}

Sasa, haya yote yanahusu nini? — Sio vigumu sana kuona. Yule ambaye Mungu anasema naye, Yezreeli, ana-wakilisha nabii. Ndugu na dada yake, Ammi na Ruhamah, wanaweza tu kuwakilisha ushirika wa kanisa, wote wa kiume na wa kike. Kwa kweli Yezreeli lazima awasilishe ujumbe wa Mungu kwao. Na hapa upo ujumbe: {2TG6: 18.2}

Aya ya 2 — “Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake.”

Ukweli kwamba Mungu mwenyewe anamwita mke wa maono wa nabii Hosea mke Wake mwenyewe, unad-hihirisha kwamba yeye anawakilisha kanisa, kwamba Hosea anamwakilisha Mungu, na kwamba wakati Yezreeli anawakilisha kipaaza sauti cha Mungu, Ammi na Ruhamah wanawakilisha washiriki wa kanisa. Katika utoto (Hosea 1), wanawakilisha kanisa la Agano la Kale, Waebrania, lakini katika ujana wao, wakiwa na majina yali-yobadilishwa, (Hosea 2), wanawakilisha kanisa la Agano Jipya, Wakristo. {2TG6: 18.3}

Sasa kwamba walei, kwa amri ya Mungu ni kupitia kwa nabii watalisihi kanisa, kwa hivyo, matengenezo ya-nayoitishwa hapa yamefadhiliwa na Uvuvio na kutekelezwa na walei. Ni uhuisho na matengenezo yaliyotarajiwa kwa muda mrefu kwa Walaodekia, na kwa hivyo ni vuguvugu la

18

mlei lililoitishwa na Roho ya Unabii iliyoamshwa. {2TG6: 18.4}

Kutoka kwa unabii huu, unaona, Dhehebu linatuhumiwa na Mungu mwenyewe kwa “uasherati,” kuwa na mi-ungano haramu na ulimwengu. Uzinzi huu lazima liachane nao iwapo litapata kibali kwa Mungu. {2TG6: 19.1}

Haya sio maneno ya mwanadamu, unaelewa, ila ni ya Mungu. Na je! Hatupaswi kuwa wa shukurani kwamba Yeye anafanya kila kitu Anachoweza kutuokoa? Kanisa lazima litubu, asema Bwana: {2TG6: 19.2}

Aya ya 3 — “Nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya ku-zaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame, na kumfisha kwa kiu.”

Dhehebu mara nyingi hujivunia kupata faida ya washiriki (watoto), lakini Mungu hushtaki kwamba wale linaowaingiza ni watoto haramu! Na inawezaje kuwa vinginevyo ikiwa kanisa lenyewe limepotoshwa na dunia? Je! Ni nini kingine ambacho waongofu wake watakuwa? Je! Ni nini kitakachowaweka huru kutoka kwa mivuto ya kidunia, iwapo yeye (ukasisi), mwenyewe amechafuliwa na mazoea ya ulimwengu? Hakika waongofu wake hawawezi kuwa watoto halali. {2TG6: 19.3}

Aya ya 5 — “Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.”

Kanisa limeifuata dunia kwa sababu linafikiria kimakosa kwamba msaada wake hutoka kwa walimwengu, kutoka kwa “wapenzi” wake. {2TG6: 19.4}

19

Aya ya 6 — “Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya ukuta juu yake, asipate kuyaona mapito yake.”

Hapa tunaona kwamba kanisa hupendekeza, lakini kwamba Mungu hutoa mwelekeo unaofaa; mipango yake haifanyi kazi kama inavyotarajiwa — hupoteza njia yake kama meli bila ramani au dira ikielea baharini. {2TG6: 20.1}

Aya ya 7 — “Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; naye atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa. “

Tena tunaona kwamba majaribu na hali ngumu ni kwa manufaa yetu, kwa maana ndivyo kanisa linaletwa kwenye hisia zake sahihi. {2TG6: 20.2}

Aya ya 8-12 — “Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye niliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali. Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang’anya sufu yangu na kitani yangu, vya kum-funika uchi wake. Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu ataka-yemwokoa katika mkono wangu. Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa. Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, “Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.”

Kutoka kwa aya hizi tunaona kwamba ilikuwa kumwacha Mungukwa namna hii ambako kulisababisha kanisa katika enzi yake ya kwanza ya Ukristo kupoteza mwelekeo na mali

20

yake yote, pamoja na siku zake za karamu, miezi yake mipya, Sabato zake, na sikukuu zake kuu zote. {2TG6: 20.3}

Hivi ndivyo haswa ilivyotokea wakati “Vizazi vya Giza” la dini vilipoanza. Wapagani ambao katika makucha yao kanisa liliangukia hawakuwa wa kulaumiwa kwa vyovyote kwa ajili ya kanisa kuingia gizani kuliko Wa-kaldayo walivyouangamiza Yuda na hekalu lake. Lawama halisi huanguka juu ya kanisa lenyewe. Na hili lina-paswa kuwa funzo la kudumu kwa kila mmoja wetu, kwamba kamwe tusiwe tena na uhusiano haramu na ulim-wengu, kamwe tusimwache Bwana. {2TG6: 21.1}

Sasa, hebu tusome ni uzoefu upi mwingine ambao kanisa lilikuwa lipitie: {2TG6: 21.2}

Aya ya 13, 14 — “Nami nitawaadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba, hapo ali-pojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito, naye akawafuata wapenzi wake, na kunisahau, ase-ma Bwana. Kwa hivyo, angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo.

Tambua kwamba Bwana hulijilia kanisa sio wakati ambapo liko katika msimamo mzuri wa kiroho Naye, ila wakati linapokuwa katika ibada yake kuu ya sanamu. Kwa kweli, hangaliweza kulijilia kwa wakati unaofaa zaidi, kwa sababu wakati tu linapokuwa kwenye giza kuu linaweza kuitambua nuru. Na hali yake, unajua, hai-wezi kuimarika kamwe isipokuwa Yeye aweze kuliita. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika siku ya Yohana Mbatizaji, pia wakati matengenezo ya Kiprotestanti yalipokuja, na ndivyo ilivyo leo. Mungu anajua jinsi ya kuokoa. Kuo-koa ni shughuli Yake kuu. {2TG6: 21.3}

“Mungu hutaka mambo fulani kutoka kwa watu Wake;

21

ikiwa wanasema, Sitaacha kufanya jambo hili, Bwana huwaacha waendelee katika uamuzi wao wanaodhani ni wa busara bila hekima ya mbinguni, mpaka andiko hili [Isa. 28:13] litimie. Usiseme, nitaufuata uongozi wa Bwana hadi kwa hatua fulani ambayo inauwiana na uamuzi wangu, kisha ushike sana maoni yako mwenyewe, ukikataa kufinyangwa katika umbo la Bwana. Ruhusu swali liulizwe, Je! Hiya ni mapenzi ya Bwana? Iwapo sivyo, Je! haya ni maoni au uamuzi wa ________? ” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 419. {2TG6: 21.4}

Na sasa ahadi ya Mungu ni ipi kwa kanisa lake? {2TG6: 22.1}

Aya ya 15 — “Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.”

Kama tokeo la shamba lake la mizabibu kurejeshwa, na pia kwa kupewa bonde la Akori kuwa mlango wa tu-maini, kanisa litaimba kama katika siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri na kuishi katika Nchi ya Ahadi. Je! Shamba lake la mizabibu linaweza kuwa nini isipokuwa nchi yake? Na iwapo bonde la Akori ni mlango wake wa tumaini, linaweza kuwa nini isipokuwa ilivyokuwa wakati wa Yoshua — kuondolewa kwa akina Akani wa leo kutoka kati yake (Hos. 2: 15)? Hakika, hili ni tumaini lake la pekee — kwa kweli, hata zaidi kuliko ilivyokuwa katika siku yakushindwa kwa Israeli huko Ai, lango la kuingia Nchi ya Ahadi. {2TG6: 22.2}

“Daraja ambao hawahisi kuhuzunishwa juu ya kuchakaa kwao kiroho, wala kuomboleza juu ya dhambi za wengine, wataachwa bila muhuri wa Mungu. Bwana huwaamuru malaika zake, watu walio na silaha za

22

kuchinjia mikononi mwao: Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’ {2TG6: 22.3}

“Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao. Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaaza sauti zao tena kama tarumbeta kuonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {2TG6: 23.1}

Aya ya 16 — “Tena siku hiyo itakuwa, asema Bwana, utaniita Ishi; wala hutaniita tena Baali.”

Hivyo inakuwa kwamba baada ya wanafiki na wadhambi kuondolewa, kanisa halitamwita tena Mwokozi Baali (Bwana), lakini litamwita Ishi (Mume). Maana ni kwamba wakati huo Yeye atakuwa kwa kweli mume wake, ilhali sasa Yeye ni kwake kwa mfano kama mtu fulani mkuu tu. {2TG6: 23.2}

23

Aya ya 18 — “Na katika siku hiyo nitawafanya agano na wanyama wa porini kwa ajili yao, na ndege wa angani, na wadudu wa nchi: nami nitavunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nita-wafanya walale salama.”

Hapa kuna amani, amani ya pekee ambayo mtu anaweza kuwa nayo leo iwapo anaitaka. Hii ni amani inayofu-rika kwa usalama. Watakatifu, baada ya wadhambi kuondolewa kutoka miongoni mwao, hawatahitaji ku-waogopa wanyama, ndege au vitu vitambaavyo vya nchi, wala bunduki au upanga; watalala chini kwa imani na uhakikisho kwamba hakuna chochote kitakachowadhuru, kwa maana Yeye “Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, … atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano Yake ghalani; bali makapi atayachoma kwa mo-to usiozimika.” Mat. 3:12. {2TG6: 24.1}

Aya ya 19-21 — “Nami nitakuposa uwe wangu milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa fadhili, na kwa rehema. Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe utamjua Bwana. Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi.”

Kwa kusema kwamba Bwana ataziitikia mbingu, nazo mbingu zitaiitikia nchi, Uvuvio kwa kweli unasema kwamba mambo haya yanapotukia juu ya dunia, Bwana atakuwa kati ya watu Wake, kwamba Yeye atazungumza kutoka duniani na raia Wake mbinguni watamsikia Yeye. {2TG6: 24.2}

Hos. 2:22 — “Nayo nchi itaiitikia nafaka, na

24

divai, na mafuta; nayo yataitikia Yezreeli.”

Kuitikia nafaka, divai, na mafuta ni kuzisikia zikizungumza, na kwa sababu nafaka halisi, divai, na mafuta haviwezi kunena, lazima viweze kuwa mfano wa chakula na kinywaji cha kiroho — mfano wa ujumbe mkuu katika siku kuu na ya kuogofya ya Bwana. Na kwa ukweli kwamba watu wa dunia watamsikia Yezreeli, kipaaza sauti cha Mungu, imewekwa wazi kwamba mwito, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msiishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake” (Ufu. 18: 4), utakamilisha kazi yake. Wale ambao watatoka kwake, wataingia ma-hali pa usalama ambapo palitajwa hapo awali. Na wale mbao hawatamsikia Yezreeli wataangamia kama Waya-hudi waliowakataa manabii katika siku yao. {2TG6: 25.1}

Hebu sasa tupitie uchambuzi wetu wa leo kwa kufuata mfano huu wa picha {2TG6: 25.2}

25

Hapa tunawaona Yezreeli, Lo-ruhamah, na Lo-ammi kama watoto wadogo kwenye picha wakiwakilisha fal-me za Israeli na Yuda katika misiba yao, kamili ila fupi historia ya kanisa la Agano la Kale na watu wake. {2TG6: 26.1}

Kisha tunaona kwamba herufi “Lo” zimeondolewa kutoka kwa majina Ruhamah na Ammi, kuashiria ku-badilika kwa majina — Wayahudi kuitwa Wakristo, — kumaanisha “rehema” na “watu Wangu” badala ya “sita-warehemu” na “sio watu Wangu.” Jina la Yezreeli, hata hivyo, linasalia sawa, na kwa sababu anawakilisha mana-bii wa Mungu katika nyakati zote, hili linaonyesha kwamba wao ni wazawa wa Yakobo na kwa hivyo lazima tuwasikie na kuwatii. {2TG6: 26.2}

Familia kama watoto wadogo wakiwakilisha watu wa kanisa la Agano la Kale, na kama vijana wanawakilisha kanisa la Agano Jipya, wanaonyesha kwamba ukuaji wa kiroho umefanyika kupitia kwa mkondo wa muda, kwamba sasa wamekua, kuweza kula “chakula kigumu,” na kwa kweli kuwa wana-matengenezo kwa kanisa, na wamishonari kwa ulimwengu. {2TG6: 26.3}

Tunaona pia kwamba mama yule yule na baba yule yule, pamoja na watoto wale wale, wanawakilisha makani-sa ya Agano la Kale na Jipya; kwamba wazawa wa Yakobo kwa kweli ni mzeituni wa zamani (Rumi. 11:24), kwamba njia pekee ambayo Mataifa wanaweza kuingia katika ufalme ni kwa ajili yao kupandikizwa kwenye mzeituni wa zamani. Myahudi au Mtu wa Mataifa, wote lazima wajiunge nao iwapo watakuwa kwenye ufalme. Hili linaweza kufanywa tu kwa idhini na hatua yetu wenyewe sasa wakati Roho anatusihi, na wakati Bwana amesimama tayari kuifanya kazi hiyo. Hakuna mtu anayehitaji kutengwa. Hakuna mtu anayehitaji kubaki Mla-odekia vuguvugu isipokuwa achague hivyo. Tumaini langu ni kwamba wote watachagua maisha

26

badala ya mauti. {2TG6: 26.4}

Ijayo tunaona kwamba kanisa kwa ujumla, kama familia, linajumuishwa na baba, mama, na wana na binti, kwamba baba ni Mungu; kwamba mke ni ukasisi (wale ambao huleta waongofu); kwamba watoto ni walei. Tunaona pia kwamba kanisa (mwanamke) lilikuwa limeolewa kwa Bwana katika ujana wake, katika siku am-bayo lilitoka Misri; kwamba ingawa ukasisi kwa ujumla haukustawi kutoka kwa ukweli mmoja hadi mwingine, kanisa (mke) liliendelea kwa kubadilishwa wachungaji wapya na wanaofuatana mara kwa mara. Na sasa kwa vile limezama katika uzinzi mkubwa, ni wazi kwamba litabadilishwa tena na ukasisi mpya, na hivyo litakuwa aminifu kwa Baba yetu; kwamba hili litatekelezwa kwa kuwaondoa wadhambi kati yake. Kisha litapewa sham-ba lake la mizabibu, na wakati huo kanisa na watoto wake wote wataishi kwa amani na salama. {2TG6: 27.1}

Ni wazi, basi, uzinzi hakika utatoweka, na uhuisho huu na matengenezo yaliyoletwa na vuguvugu hili la mlei yatatimiza kazi yake lililopewa. Na hivyo, unaona kwamba kama tokeo la lalama za watoto, familia yote ya Mungu itaishi kwa furaha kwa amani na usalama milele. {2TG6: 27.2}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 5, 6

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>