fbpx

Mtoa Jibu Kitabu Namba 5

Mtoa Jibu Kitabu Namba 5

1

Hakimiliki 1944, na

V.T. Houteff

Haki Zote Zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kama utumishi wa Ukristo, kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga.

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitathaminiwa.

2

MTOA JIBU

Kitabu Namba 5

Maswali na Majibu kwa Mada za Ukweli wa Sasa

Katika Masilahi ya Ndugu Waadventista wa Sabato

na Wasomaji

wa

Fimbo ya Mchungaji

Na V.T. Houteff

Huyu “mwandishi,” mwenye elimu

ya ufalme wa

mbinguni, “hutoa

… vitu vipya na vya zamani.”

Mat. 13:52.

Sasa “mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”

1 Pet. 3:15.

3

 

YALIYOMO

 

Je! Elimu Inadhuru? …………………………………………………………………..5

Dini Ni Nini? …………………………………………………………………………..21

Je! Maono Yanahitajika? ……………………………………………………………27

Je! Mtu Anaweza Kupata Ukweli Bila Kuwa Na Njozi — Maono? ………………28

Mbona Hitaji La Hukumu? ……………………………………………………….….30

Je! “Ndiye,” Au Tumtafute Mwingine? ……………………………………………..31

Tutafute Uchumi Tunapoepukana Na Kiburi? ……………….……………………33

Mfano Nje Ya Ulimwengu Au Katika Ulimwengu Pia? …………………..………34

Je! Nywele Zapaswa Kusukwa? ……………………………………………………35

Suruali Ndefu Au Sketi? …..…………………………………………………………35

Je! Wonyesho Ni Dhambi? ………………………………………………………….37

Je! Mwanamke Asiivue Kofia Yake Mwanamume Anapovua Yake? …………..38

Vipi Kuhusu Ibada Ya Meza ya Bwana? …………………………………………..39

Zawadi Yangu Ni Nini? ………………………………………………………………40

Vipi Kuhusu Kupokea Zawadi? ……………………………………………………..42

Mtu Anawezaje Kusimama Iwapo Anapanga Kuanguka? ……………………….42

Je! Tuombe Jinsi Gani? ……………………………………………………………..43

Tuweze Kuwa Kimbelembele Na Wasiotenda? …………………………………..44

Wakati Wa Kuandika Na Wa Kutoandika? ………………………………………..45

Ni Nani Atatupatia Ujira Wetu? ……………………………………………………..47

Kulisha Kondoo Pekee Au Wana-kondoo Pia? …………………………………..49

Mbona Usifanye Kazi Kwa Ajili Ya Ulimwengu Wakati Wa Nafasi? ……………50

Je! Ni Trakti Zipi Za Watu Wa Nje? ………………………………………………..51

Mambo Ya Kujifunza? ……………………………………………………………….51

Je! Ni Salama Kubishana? ……………………………………………………….…52

Je! Ni Nini Maana Ya “Yale Ambayo Yamechapishwa”? ………………………..55

Jinsi ya Kuthibitisha Kwamba Mchinjo Ni Halisi? …………………………………56

Je! Karama ZOTE Ziko Kati Yetu Sasa? ………………………………………….58

Mtu Mwenye Busara Atafanya Nini? ………………………………………………59

Je! Inatozwa Ushuru? ……………………………………………………………….62

Vipi Kuhusu Fadhili Za Serikali? ……………………………………………………63

Je! Mkristo Anapaswa Kujiunga Na Miungano Ya Wafanyakazi? ……………..64

Je! Ni Makosa Kuchukua Bima Ya Mali? …………………………………………65

Vipi Kuhusu Kununua Hati Akiba Za Dhamana Ya Ulinzi? ……………………..66

Kusalimu Au La? ……………………………………………………….……………67

Je! Uzalendo Ni Ukristo? ……………………………………………………………70

Piga Kura Kwa Au Dhidi Ya Pensheni? …………………………………………..73

Je! Kupiga Kura Ni Sawa Kwa Mkristo? ………………………………………….75

Vipi Kuhusu Kutumia Maziwa Na Mayai? …………………………………………76

Je! Tunapaswa Kufuga Ng’ombe Na Nyuni? ……………………………………..77

Je! Kuna Makosa Gani Kula Nyama SAFI? ………………………………………78

Je! Vikolezi Vyote Ni Hatari Kwa Afya? ……………………………………………81

Nini Humtambulisha Mtu Kama Mdaudi Mwadventista Wa Sabato? .…………82

Je! Lazima Nifikie Ukamilifu Kwanza? ………………………………………….…83

Je! Ubatizo Lazima Utangulie Ushirika? ………………………………………….83

Je! Mtu Ni Mshirika Bila Cheti Cha Ushirika? …………………………………….84

Nani Anaweza Kushikilia Ofisi? ……………………………………………………84

Je! Ni Mpango Wa Nani Kunyakua Fedha? ………………………………………84

Vipi Kama Sina Zaka Za Kulipa? ………………………………………………….85

Kutoza Au Kutotoza Zaka? …………………………………………………………85

Je! Pato Dogo Halitozwi Zaka? …………………………………………………….86

Je! Sesere Ni Sanamu? …………………………………………………………….87

Vipi Kuhusu Kucheza Michezo? ……………………………………………………88

Yeyote Aliyefufuliwa Kati Ya Watu 144,000? …………………………………….89

Je! Watu 144,000 Ni Wayahudi Kwa Kuchukuliwa Tu? …………………………90

Je! “Mlima Mtakatifu” Humaanisha Nini? …………………………………………91

Jinsi Ya Kujisajili Katika Taasisi? ………………………………………………….92

Kusubiri Hadi Baada Ya Kusajiliwa, Au Kujiandikisha Kabla? …………………93

Hatua Yako Itakayofuata Itakuwa Nini? …………………………………………..94

4

MASWALI NA MAJIBU

JE! ELIMU INADHURU?

Swali Namba 108:

Je! Kuna ubaya gani na elimu? Mbona huwafanya wengi kuwa wasiofaa? Je! Sichukui nafasi hatari katika kuwapeleka wanangu shuleni? {ABN5: 5.1}

Jibu:

Elimu yenyewe haina taabu, ila badala yake aina ya elimu ambayo mtu hupokea. Naam, zipo aina mbili za elimu — ya kibinadamu na ya Mungu, ya kawaida na ya kiroho, mbaya na sahihi. Kwa sababu mwanadamu huzaliwa na tamaa ya kupenda ya asili na kuchukia ya kiroho, kwa kawaida, basi, mbinu ya elimu ya mwanadamu imekuzwa sana, na ya Mungu, kupuuzwa sana, ikiwa sio yote kabisa, kupuuzwa. Hivyo ndiyo sababu ya “wasiofaa wengi sana.” {ABN5: 5.2}

Ni ukweli unaotambulika kwamba ya kwanza imekusudiwa kumfunza mwanafunzi, si kuzalisha, bali kutumia — kuwa wa kufumbata na mchoyo; ilhali ya mwisho imekusudiwa kumfunza mwanafunzi kuzalisha zaidi ya ambavyo yeye hutumia — kuwa mkarimu na asiye mchoyo, akiishi kwa ajili ya wengine, sio kwa ubinafsi. {ABN5: 5.3}

Kisha, pia, lazima itambulike kwamba hata ikiwa shule zingalikuwa zinatoa mafunzo ya aina sahihi, yangedhoofishwa na wazazi ambao huwaruhusu watoto wao kupoteza

5

wakati bure, badala ya kuwafunza jinsi ya kuifanya myepesi mizigo ya mtu na kujipatia riziki. Kwa hivyo, iwapo hakuna ushirikiano wa pamoja kati ya shule na nyumba, basi licha ya kuwa na mfumo mzuri wa elimu shuleni, watoto hata hivyo watafunzwa kuwa mzigo kwa wao wenyewe, hasara kwa wazazi wao, na madhara kwa ulimwengu. {ABN5: 5.4}

Badala ya kufanya masomo yao kuwa maandalio ya maisha, wanafunzi wengi huyafanya kuwa likizo kutoka kwa maisha. Kisha siku ya kuhitimu inapowasili kwa tokeo lake hawana wazo la nini wanapaswa kufanya ijayo! Na hata wanapolifanya “wanayo likizo akilini, mara nyingi huwagharimu miaka mingi kujipatia tabia za msingi za kazi inayohitajika katika nafasi zao.” {ABN5: 6.1}

Ni ukweli uliochunguzwa kwamba wakati wa masomo yao, wanafunzi hujifurahisha kupata kwa kuwafyonza wengine, jambo ambalo limekuwa upotovu wa maadili. Na kwa muda mrefu wanapoendelea kwenda shuleni tabia hii ya ubinafsi ndivyo huonekana kuwa. Na ndio maana “waajiri hawashindani tena,” asema Dkt. Henry C. Link, mwanasaikolojia, “katika haraka yao kuajiri mahafali wa vyuo. Isitoshe, katika kufanya uchaguzi wao, mara nyingi hushawishiwa na shughuli za ziada za mwanafunzi kwa mutaala na mafanikio yake katika kushughulika na wanafunzi wenzake, kuliko ufanisi wake na maprofesa wake.” {ABN5: 6.2}

Kile ambacho kizazi cha sasa kinahitaji kujifunza zaidi shuleni ni kuacha kupata

6

kwa kuwafyonza wengine na kuanza kuzalisha, jambo ambalo kinazidi kuhofia. Watoto wanapaswa kufunzwa kwamba, baada ya yote, njia pekee ya mtu kuwa anayestahili maisha ni kimsingi kuwa mzalishaji, akizalisha zaidi ya ambavyo hutumia, na kuwa na hamu, si ya kupokea, bali kutoa, na kutambua kwamba tabia ya ukarimu kama hii isiyo na ubinafsi, ndiyo haswa lango la mafanikio na furaha. {ABN5: 6.3}

Ulikuwa wakati ambapo Abrahamu alionyesha wema wake wa kweli na ukarimu wa upole alipowakaribisha kwa ukunjufu na kisha kuwashawishi wageni hao watatu watulie kwa pumziko na mlo, kwamba ahadi ya mwana iliofanywa miaka kabla, ikatukia. Na Lutu kwa uaminifu kuwashurutisha wawili wa hawa wageni kutulia usiku kucha nyumbani mwake, kulimwokoa kutoka kwa uharibifu wa moto wa Sodoma. {ABN5: 7.1}

Tusisahau kwamba mfano halisi wa kanuni hizi Takatifu ni hatua ya kwanza kuelekea uongofu wa mtu kwa dini ya Kristo. Kupuuza mahitaji haya muhimu wakati unapojaribu kuwa Mkristo kamili, sio upuuzi mdogo kuliko kumwalika mchungaji afanye unganisho la sherehe ya ndoa bila kuwa na mwenzi anayetaka kufunga ndoa. {ABN5: 7.2}

Juu ya mada ya utu, Dkt. Link anaandika: “Nia hazijazaliwa, hupatikana kwa mafunzo. Utu hauzaliwi, hukuzwa kwa mazoea. Lakini hatuna maktaba ya vitabu vya kisayansi kwa mada ya

7

mwisho. Kitabu kikuu cha mwongozo na sahihi zaidi kwa utu bado ni Biblia, na uvumbuzi ambao wanasaikolojia wamefanya kuthibitisha badala ya kupinga tarakimu za utu zinazopatikana humo. Saikolojia hutofautiana na sayansi zingine zote kwa jambo hili muhimu. Ilhali sayansi zingine zimetufundisha kwamba mafundisho na imani zetu za zamani kuhusu maumbile yalikuwa ya uongo, saikolojia inathibitisha kwamba mafundisho na maagizo ya zamani kwa ukuzaji wa tabia njema na utu yalikuwa sawa. {ABN5: 7.3}

“Jambo la msingi ambalo hupitia ndani ya vitu au tabia za utu lililotiwa ndani ya kipimo hiki ni hili: Mtoto hukuza utu mzuri, au angalau misingi ya utu kama huo, kwa kufanya mabo mengi ambayo hafanyi kiasili, na mambo mengi ambayo kwa kweli hapendi. Kula kwa kutumia kisu na uma kwaweza kuwa kawaida kwake katika wakati, na hata kumfurahisha, lakini sio mpaka wazazi wake wametumia bidii ya miaka minne hadi minane kumwezesha avitumie vizuri. Watoto hutofautiana, bila shaka, kwa maumbile na urithi, lakini haijalishi ni wazuri namna gani, tabia za kimsingi lazima zikazwe kikiki kwa mchakato wa nidhamu. Kwa mtazamo wa chuki isiyoweza kuepukika kwa nidhamu ambayo watoto hukuza na ulegevu wao kujipata tabia nyingi zinazohitajika, kila mvuto uliopo, shinikizo, au kifaa ambacho kitawaharakisha kujipata tabia hizi

8

lazima kitumike. Wazazi wengi wanahitaji kila chanzo cha usaidizi au msaada uliopo katika mchakato huu.” — Kurudi kwa Dini. {ABN5: 8.1}

Kwa hitaji, ili kufanikiwa sana maishani, mtu lazima apate kumiliki ustadi, akiwa bora katika mchache, na wa kipekee bora zaidi katika mmoja; pia tumaini kubwa la kuwapendeza na kuwabariki wengine kwanza, na pili kujiridhisha mwenyewe. Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee. Wanadamu kwa hivyo wanapaswa vivyo hivyo kuwa wakarimu kwa kiwango kwamba wao, pia, kwa uhuru watumie wakati na nguvu zao kutumikia masilahi ya wengine. “Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.” Phil. 2:4. Katika mwenendo huo wa furaha watakuwa wakijinufaisha wenyewe hata zaidi ya wengine. “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake,” aamuru Bwana, “na hayo yote mtazidishiwa.” Yule anayeelewa kabisa utendaji wa sheria hii Takatifu, na kuitii bila kusita-sita, ndiye tu anayefanya ufanisi wa kweli wa maisha. Na ukweli kwamba wale ambao hufanya maslahi ya mwajiri wao kuwa shughuli kuu ya maisha yao ndio pekee wanaokwezwa na wanaofaulu kupata nafasi za juu zenye majukumu, huonyesha kwamba sheria hii Takatifu hufanya kazi hata kati ya wasio Wakristo. {ABN5: 9.1}

Mwanafunzi anayeendelea huhitaji kuijaribu nadharia kadiri anavyoendelea na kabla ya kujifunza nadharia mpya. Yaani, badala ya

9

kufuatilia tu katika harakati za kutafuta maarifa, anahitajika kutumia maarifa aliyopata kutafuta riziki. Mbali na hilo, mtu anayekingwa kwa muda mrefu kutoka kwa uhalisi wa maisha ya kufanya kazi, yeye atakuwa na uwezo mdogo kukutana nayo hitaji litakapomkabili. Elimu kama hiyo inaweza kuzalisha wasiofaa — vimelea vya kijamii. Lakini elimu ya kweli “humtayarisha mwanafunzi kwa furaha ya utumishi katika ulimwengu huu, na kwa furaha ya upeo katika utumishi mpana katika ulimwengu ujao.” — Elimu, uk. 13. {ABN5: 9.2}

Kwa hivyo, wazazi watakaowasaidia watoto wao kufanya maisha yawe ya kufaulu na yanayofaa kuishi, hawapaswi kupuuza kuwafunza vijana hivyo. Kisha wataona wazi kwamba aina sahihi ya elimu sio tu kitu kizuri, bali ya kwamba ni kila kitu katika ustawishaji wa tabia njema. Hakuna awezaye kumudu kuwaacha watoto wao bila elimu hii muhimu. Kwa hivyo iwapo watoto wako hawapokei mafunzo kama haya shuleni, basi wanapaswa kuyapokea nyumbani. {ABN5: 10.1}

Na kwa kulichukua jukumu hili, wazazi wanapaswa kukumbuka daima kwamba wanadamu huzaliwa wakiwa wanyonyaji kiasilia. Mtoto hafanyi chochote kujisaidia mwenyewe. Kila kitu muhimu kwa uhai wake hufanywa na wengine. Na njia pekee kabisa ya kumwachisha mtoto kutoka kwa tabia hizi za mkaapweke, ni kuanza kumfunza mapema iwezekanavyo kujisaidia mwenyewe, hadi mwishowe atakapokuwa

10

stadi kwa mahitaji yake yote. Mara tu ndege akitoka nje ya kiota chake, ndege mzazi humfunza kuruka na kujipatia riziki yake. Wazazi ambao hushindwa kutoa mafunzo kwa watoto wao hivyo hawana akili kuliko wanyama bubu, na kwa hakika maadui wabaya zaidi wa watoto wao. {ABN5: 10.2}

Baba fulani alishindwa, kama Eli kuhani wa Israeli ya kale, kulichukua jukumu hili na kwa hivyo alikuwa akipata ugumu mkubwa na mwana wake wa miaka kumi na saba. Kwa Dkt. Link anamjuza hali yake mwenyewe: {ABN5: 11.1}

“Mwanangu, naamini, anazo akili nzuri, lakini katika miaka michache iliyopita kazi yake shuleni imezidi kuwa mbaya. Muhula huu alishindwa katika masomo yake matatu. Hata hivyo, kinachonipa wasiwasi zaidi, hata, kuliko kazi yake ya shule, ni mwenendo wake wa maisha kwa ujumla. Inaonekana anafikiri kwamba ulimwengu na haswa wazazi wake, ni wadeni wa uhai wake. Inatokea kwamba tunaishi katika jamii yenye ustawi. Familia nyingi ni tajiri kuliko sisi, na wakati nimekuwa mkarimu sana kwa mwanangu, nikimpa marupurupu ya ukarimu, mavazi mazuri nikimruhusu kuliendesha gari la familia, n.k., bado haridhiki. Sasa anataka gari lake mwenyewe, na huendelea kuongea kuwahusu wavulana wengi mjini walio na magari yao wenyewe. {ABN5: 11.2}

“Ninapomtaka atunze tanuru au uwanja wa nyasi, au afanye kazi zingine, hunambia kwamba wavulana wengine sio lazima wafanye kitu cha namna hii. Ingawa nyakati zingine mimi humshurutisha afanye kazi, kamwe siwezi kumtegemea aifanye vizuri. Hana hisia kwa jukumu au wajibu, lakini huiangalia familia yake inawajibika kutenda kila kitu chochote ambacho hutaka kifanywe. Kwa kweli wazo lake moja maishani ni burudani, na wazo lake la wakati mzuri, kadiri ninavyoweza

11

kuona, ni kutenda kile anachotaka kufanya, wakati atakapo kukifanya, bila kumjali mtu mwingine yeyote. Nina hofu sana kwamba anaendeleza tabia ambayo itamfanya kuwa asiyefaa kwa ulimwengu; jinsi ambavyo tayari imemfanya kutostahili kwa masomo yake.” {ABN5: 11.3}

Wapo maelfu wa kusikitisha kama huyo wa marika mbalimbali, ambao kutofaulu kwao maishani kunaweza kufuatiliwa kutoka nyuma kwa wazazi wao. Kwa kuwatendea watoto wao kupita kiasi kabisa, waliwanyang’anya fursa yao kujipatia tabia za kujitegemea. Badala yake wamepata wazo kwamba ama wazazi wao au wa mwingine wanawawia riziki, elimu, na anasa ambazo wao huchukulia kwa uzito kama mahitaji. {ABN5: 12.1}

Wakati manufaa ya vitu vya kawaida husaidia kuyafanya maisha ya mtu kuwa rahisi, huifanya tabia yake kuwa dhaifu. Tumaini la wazazi lisiloweza kudhibitiwa la kuwatendea vizuri watoto wao, pamoja na njia za kutends huwaletea madhara yasiyoweza kurekebishwa. Na kwa hivyo dhambi za upumbavu wa baba na maelekezo yake ya ufanisi yasio ya hekima yanajiliwa kwa watoto. Katika muunganisho huu unaonekana zaidi na zaidi, ukweli katika karipio Takatifu: “Tazama uovu wa umbu lako Sodoma, ulikuwa huu, kiburi, na kushiba chakula, na uvivu mwingi ulikuwa ndani yake na kwa binti zake, tena hakuutia nguvu mkono wa maskini na mhitaji.” Ezek. 16:49. {ABN5: 12.2}

Ni ukweli unaojulikana kwamba kama sheria watu waliosoma sana ndio husita-sita sana kuipokea injili ya Kristo, na kati ya wa mwisho kuambatana na Ukweli. Katika

12

hali hii zaidi ya nyingine yoyote hutumika usemi, “heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.” Luka 6:20. {ABN5: 12.3}

Wazazi wanaweza kuwaondolea watoto wao tamaa ya kumiliki utajiri ambao umepatikana na wengine, iwapo tu wao mapema sana katika maisha ya mtoto wataanza kung’oa tabia zake za mkaapweke na kukazia kikiki za utendaji halisi badala yake. Katika pambano la tabia, utu, na umuhimu, watoto wa wazazi maskini wana faida kuliko wale wa wazazi matajiri. {ABN5: 13.1}

Wanaume na wanawake wa maana wanaoheshimika sana ulimwenguni, ambao wameuachia ulimwengu kitu cha thamani, walitoka katika familia maskini. Kwa njia ya mfano, tutamkumbusha msomaji watu wachache kama hao: {ABN5: 13.2}

Utoto wa Jack London uliteketezwa na umaskini na shida, bado akihangaishwa na matarajio yaliyomwendesha kuwa mwandishi mkuu, akawa mwandishi maarufu wa vitabu hamsini na kimoja, na vile vile hadithi nyingi. Mapato yake ya kila mwaka yakawa maradufu kwa ya Rais wa Marekani. {ABN5: 13.3}

Na Helen Jepson, hapo zamani alikuwa maskini sana hakumudu masomo ya muziki, akawa mmoja wa waimbaji wetu bora. {ABN5: 13.4}

Andrew Carnegie alianza kufanya kazi kwa senti mbili kwa saa, na akatengeneza dola milioni mia nne. {ABN5: 13.5}

13

Marehemu John D. Rockefeller, ambaye alikusanya yaelekea utajiri mkubwa zaidi katika historia yote, alianzia maisha ya uchuuzi wa viazi chini ya jua kali kwa senti nne kwa saa. {ABN5: 14.1}

Thomas A. Edison, ambaye ameitwa raia wa manufaa zaidi wa ulimwengu, alianza kazi yake kama muuza magazeti kwenye Reli ya Grand Trunk. Maabara yake ya kwanza iliwekwa katika gari la kubeba mizigo. {ABN5: 14.2}

Benjamin Franklin alikuwa mtu mashuhuri katika karibu kila uwanja wa shughuli. Mvumbuzi, mwanasayansi, mwandishi, mwanahabari, mwanafalsafa, mchapishaji, mwanadiplomasia, mcheshi — hakika watu wengine wachache waliwahi kujasiri kazi nyingi na kuzitekeleza kwa mafanikio. Walakini alizaliwa katika familia maskini ya mchuuzi wa mafuta, na hakuwa na manufaa maalum kama mtoto. {ABN5: 14.3}

Luther Burbank, aliyeitwa “Mchawi wa Mimea,” hakuweza kwenda mbali zaidi shuleni kuliko shule ya mjini, na akiwa bado mchanga alianza kufanya kazi kiwandani. {ABN5: 14.4}

Maisha na historia ya Dkt. G.W. Carver pia ni mfano wa ukweli kwamba kujenga tabia, kupata elimu, na kufanya mafanikio halisi ya maisha, ni muhimu kwamba mtu aanzie kutoka mwanzo, ajisaidie mwenyewe, na ajilipie njia yake mwenyewe hadi amalize shule. {ABN5: 14.5}

Tunanukuu kutoka kwa ramani ya wasifu wa mwanasayansi huyu mkuu, kama ulivyochapishwa kwenye jarida The Reader’s Digest, Desemba, 1942, kabla ya kifo chake: {ABN5: 14.6}

14

* * *

Alizaliwa Missouri karibu 1864 Dkt. Carver hakuwahi kumjua baba na mama yake — walichukuliwa na wavamizi wa watumwa alipokuwa mtoto. Mkulima mzungu, Moses Carver, alimlea mtoto, akampa jina lake, na kwa sababu ya afya mbaya ya mvulana huyo alimruhusu afanye kazi ya wanawake: kupika, kushona, kufua. {ABN5: 15.1}

Lakini moto wa ajabu ukateketeza. Kitabu pekee ambacho anakumbuka katika nyumba ya Carver kilikuwa Herufi za Webster. Alikikariri. Kwa kuwa waliangukia wakati mgumu wenyewe, Wana-Carver hawakuweza kumpeleka shuleni. Alienda mwenyewe; alilala ndani ya maghala na nyasi kavu; alifanya kazi zozote zilizotokea kwa ajili ya chakula chake, akapata mafunzo yote ambayo shule ya chumba kimoja ilitoa. “Kuwaoshea watu weupe” kulimlipia karo akamaliza shule ya upili. {ABN5: 15.2}

Alisajiliwa kwa barua katika Chuo Kikuu cha Iowa kisha akakataliwa, alipowasili, kwa sababu alikuwa Mnegro. Wakati huo akafungua dobi ndogo na mwisho wa mwaka alilimbikiza fedha za kutosha kupata kiingilio kwa Chuo cha Simpson huko Indianola, Iowa. Aliosha, akapiga deki na kusafisha nyumba zikamwezesha miaka mitatu kwenye shule hiyo na akaendelea kumaliza miaka minne ya masomo ya kilimo katika Chuo cha Jimbo la Iowa. Huko kipaji chake kwa mchanga na mimea kilimshindia, siku ya kuhitimu, nafasi katika kitivo hicho. {ABN5: 15.3}

Ndani ya katikati mwa Alabama, karibu wakati huu Booker T. Washington — mwaasisi na Rais wa Taasisi ya Tuskegee — alikuwa akiotea ukombozi wa kiuchumi kwa mkulima Mnegro. Ndoto zilihitaji mtu. Washington alimchagua Carver mchanga. {ABN5: 15.4}

Carver alipofika Tuskegee, mwaka 1896, ilionekana kuwapo kazi kidogo kwake kufanya na bila kitu cha kutumia kufanya kazi. Washington ilitaka maabara ya kilimo; havikuwapo vifaa wala pesa. Alitaka shamba la shule; udongo ulikuwa mbaya. Alitaka nyasi kwenye behewa la Tuskegee; kulikuwa na mchanga tu. {ABN5: 15.5}

15

Leo, katika kasha la kioo kwenye makavazi ni vifaa ambavyo Carver alitengenezea maabara yake ya kwanza. Kwa joto alitengeneza taa iliyookolewa ghalani. Kinu chake kilikuwa kikombe kizito cha jikoni, alitumia kipande cha chuma kuwa kisagio. Bilauri kubwa za kemia zilitengenezwa kwa kukata vifuniko vya chupa za zamani vilivyookolewa kutoka kwa jaa la shule. Akabadilisha chupa ya wino kuwa taa ya mafuta na kutengeneza utambi wake mwenyewe. {ABN5: 16.1}

Udongo kwa shamba lake la ekari 16 “za utafiti” ulikuwa wa mchanga, uliomomonyoka na duni. Aliwatuma wanafunzi wake kwenye vinamasi na mwituni wakiwa wamejihami kwa vikapu na ndoo. Siku baada ya siku walileta taka na kuvu ya majani na kufunika udongo nayo. Kwenye ekari hizo alionyesha kwamba mchanga mbaya kabisa wa Kusini unaweza kufanywa uzalishe — sio zao moja la viazi vitamu kwa mwaka ila mawili. Humo pia akavuna mojawapo ya robota la kwanza la Alabama kwa ekari ya mimea ya pamba. {ABN5: 16.2}

“Kila mtu alinambia,” anasema, “kwamba udongo haukuwa ukizalisha. Lakini ni udongo ambao niliokuwa nao tu. Haukuwa hauzalishi. Ulikuwa tu hautumiki.” {ABN5: 16.3}

Alipata matumizi mengine kwa ajili yake. Kutoka kwa udongo wenye rangi nyingi wa Kaunti ya Macon alitengeneza vyombo vya ufinyanzi, wino wa bamba ukuta, rangi za kupamba matofali ya saruji. Adui maarufu wa taka, aligeuza vikonyo vya mahindi, pamba na mtama kuwa mbao za kuzuilia joto; alitengeneza karatasi kutoka matawi ya wisteria, alizeti na hibiskasi mwitu; alifuma mikeka yenye mapambo ya mezani kutoka kwa mianzi ya kinamasi; akatengeneza vitambaa virefu vyenye mapambo vya meza, kwa kutumia wino wa udongo unaong’aa kama rangi, kutoka kwa mifuko ya vyakula na mbegu. {ABN5: 16.4}

Ili kupeleka injili yake ya Malisho ya Kijani kwa mkulima alibadilisha rukwama kuukuu kuwa shule tamba ya kilimo, akaipakia maonyesho, akaazima farasi na kufanya ziara za mara kwa mara mashambani. Hii ilikuwa ya kwanza kwa “shule tamba” ambazo leo, zimewekwa kwa lori na trela na kufadhiliwa na Idara ya Kilimo ya Marekani, hutanda Alabama yote. {ABN5: 16.5}

Kaunti ya Macon wakati huo, kama nyingi za Kusini, ilikuza pamba na sio mimea mingine. Ili kuokoa mchanga

16

na kuongeza mapato ya shamba Carver alitetea ukuzaji wa viazi mbatata na njugu. Leo viazi mbatata ni chakula kikuu cha kusini; na wakulima wetu wa njugu wa Kusini mwaka huu watafikia karibu na $ 70,000,000 kwa zao lao. Zaidi ya mtu mwingine yeyote, Dkt. Carver amesaidia kuvunja pamba kukabwa koo kwenye kilimo cha kusini. {ABN5: 16.6}

Katika utangulizi wake wa Kaunti ya Macon, hakupata hata bustani za mboga yoyote, nguruwe, kuku au ng’ombe wachache. Maradhi ya Pellagra — yaliyosababishwa na lishe isiyosawazishwa — yalikuwa yameenea sana. Yeye kwa hivyo alihubiri bustani za jikoni na akafanyiza mwongozo wa mapishi kuonyesha jinsi ya kuandaa na kuhifadhi mboga. Leo, kwa mujibu wa wakala wa kilimo wa kaunti, hakuna shamba la Mnegro katika Kaunti ya Macon bila bustani ya mboga, nguruwe, kuku na angalau ng’ombe mmoja. Pellagra yametoweka kabisa. {ABN5: 17.1}

Dkt. Carver anasisitiza kwamba kanuni ya kuanzia pale ulipo itafanya kazi popote. Miaka kadhaa iliyopita alizungumza mbele ya shirika la Wanegro huko Tulsa, Oklahoma. Kwa vifaa vya kielelezo alikaa mapema asubuhi kwenye Kilima cha Bomba la Mchanga, karibu na Tulsa. Alirudi na mimea 27, yote iliyosheheni uwezo wa dawa. {ABN5: 17.2}

“Kisha,” akasema, “nalikwenda kwa Duka la Dawa la Ferguson na nikanunua dawa saba za haki-miliki zenye vitu fulani vilivyopatikana katika mimea hiyo. Dawa hizo zilikuwa zimesafirishwa kwa meli kutoka New York. Zinapaswa kuwa zilitoka kwa Kilima cha Bomba la Mchanga. ‘pasipo maono watu huangamia.” {ABN5: 17.3}

* * *

Ameitwa — mtu huyu ambaye wazazi wake walikuwa watumwa Wanegro — “mwana-kemia wa malighafi za mimea wa kwanza na mkuu.” Biashara za mamilioni za dola zimejengwa zote au kwa sehemu kutokana na uvumbuzi wake — kubwa kati yazo ikiwa kiwanda cha njugu cha $ 200,000,000 kwa mwaka. Upainia wake wa mazao huweka milioni nyingi kila mwaka katika mifuko ya wakulima wa kusini. {ABN5: 17.4}

17

Amemiminiwa heshima. Thomas Edison alimwalika ajiunge na wafanyakazi wake kwa $ 50,000 kwa mwaka. Henry Ford amempa maabara ya utafiti wa chakula wakati wa vita. Juni iliyopita “Mkulima Mwendelevu” lilimpa tuzo yake ya kila mwaka kwa “utumishi bora kwa kilimo kusini.” Medali ya Theodore Roosevelt ilimwendea mnamo 1939 kama “mkombozi kwa watu wa jamii za weupe na weusi.” {ABN5: 18.1}

“Ni mtu yupi mwingine wa nyakati zetu,” liliuliza gazeti la New York Times “amefanya mengi sana kwa kilimo Kusini?” {ABN5: 18.2}

Ulimwengu ambao unamtafuta Dkt. George Washington Carver bado unampata katika parokia ya kisayansi ambamo ameshafanya kazi kwa miaka 46: Kaunti ya Macon, Alabama, na behewa la Taasisi ya Tuskegee, shule maarufu ya Mnegro. {ABN5: 18.3}

Ni falsafa yake mwenyewe inayomdumisha hapo: imani yake kwamba hakuna malisho ya kijani kuliko yale ya karibu. Kisayansi amepunguza imani hiyo kuwa kanuni: “Anzia pale ulipo, na kile ulicho nacho tengeneza kitu kutoka kwacho usiridhike.” Sasa, akiwa amekaribia 80, bado anaifanya kanuni hiyo itende kazi. {ABN5: 18.4}

Alinipeleka hivi majuzi katika Makavazi ya George Washington Carver huko Tuskegee — yaliyojengwa kutoka kwa akiba yake kuhifadhi matokeo ya uchunguzi na uvumbuzi wake wa karibu. Bado huvalia ile kofia mashuhuri kuukuu na sweta iliyochakaa ya kijivujivu. Sauti yake ni dhaifu na mabega yake yameinama. Lakini hakuna dalili za udhaifu katika akili na roho yake. {ABN5: 18.5}

Kwenye uwanja mdogo nyuma ya makavazi alionyesha kanda nusu ya mia za ubao wa msonobari zilizoanikwa kwa jua. Zilikuwa zimepakwa rangi upya: samawati , manjano, nyekundu, kijani kibichi angavu. {ABN5: 18.6}

“Sababu hapa chini hawapaki rangi nyumba zao,” alisema, “si kwa sababu ni wavivu au hawajali. Ni kwa sababu hawana pesa taslimu za kununua rangi. Rangi zinazofutika kwenye hizi mbao hugharimu karibu na sufuri. Rangi hutoka kwenye udongo papa hapa katika Kaunti ya Macon. Kiungo muhimu ni Mafuta ya gari yaliyotumika.” {ABN5: 18.7}

18

Rangi hii iliyozalishwa nyumbani, iliyotengenezwa na kuthibitishwa na Dkt. Carver huko Tuskegee, sasa inatumiwa na Mamlaka ya Bonde la Tennessee katika maonyesho ya urembeshi wa nyumba za vijijini katika maeneo ya 14 TVA. {ABN5: 19.1}

Dkt. Carver alikuwa wa kwanza na bado ni bingwa mkubwa zaidi wa matumizi ya ardhi tupu ya Kusini na bidhaa taka ili kusawazisha lishe ya kilimo cha kusini. Hii ilihitaji zaidi ya maarifa ya kilimo, kwa hivyo alijifunza kuwa mtaalam wa lishe na upishi. Njia Zake “43 za Kuokoa Mmea wa Mzambarau Mwitu” ni mkusanyiko wa mwongozo wa mapishi yaliyothibitishwa na Carver: jemu ya machungwa, shira, siki, mchuzi, tufe la nyama iliyosagwa, samaki, au mboga zilizofunikwa kwa yai na magombo ya mkate na kutokoswa ndani ya mafuta yanayochemka. {ABN5: 19.2}

Majaribio yake maarufu kwa njugu yalisababisha uzalishaji wa zaidi ya makala muhimu 300. Kati ya yale yanayotengenezwa kibiashara sasa ni siagi yake ya njugu na unga wa njugu, mbali na mafuta na mbolea tofauti tofauti. Kinachotumika sana ni kijitabu kwa mke wa mkulima: “Njia 105 Tofauti za Kuandaa Njugu kwa ajili ya Meza,” pamoja na mwongozo wa mapishi ya mchuzi wa njugu, mkate, biskuti, ganda-kaanga, mandazi, jibini. Kwa matumizi mengi ya aina hiyo mazao ya njugu yaliongezeka kutoka pauni milioni 700 mwaka 1921 hadi milioni 1,400 mwaka 1941. {ABN5: 19.3}

Machi iliyopita Dkt. Carver alichapisha taarifa yake mwenyewe ya Ushindi wa Bustani: “Bustani ya Asili ya Ushindi na Amani.” Jina lake hunukuu kutoka Mwanzo: “Tazama Nimewapa kila mche… vitakuwa ndivyo chakula kwenu.” Ndani yake kuna orodha ya nyasi zaidi ya 100, magugu na maua ya porini ambayo yanaweza kutumika kwa chakula, na mwongozo wa mapishi yanayoonyesha jinsi ya kuyatumia. Ni pamoja na kahawa ya chikori — “wengine wanaipendelea badala ya kahawa halisi” — sambusa “sawa na tofaa au rhubarb” kutoka kwa majani ya uchachu; “matawi machanga ya yungiyungi” kutoka kwa vikonyo vya magugu mbali mbali yanayotoa utomvu wa maziwa, mmea wa porini wenye maua matamu “kwa kachumbari maridadi na za kupendeza”; sandwichi za kachumbari za majani ambazo zina mtindo maarufu kwenye behewa la Tuskegee. {ABN5: 19.4}

* * *

Biblia, Dkt. Carver alinambia, ni muhimu kwa kazi yake kama ilivyo maabara yake. Anazo aya

19

mbili pendwa za Maandiko. Moja ya hizo huiita kifungu chake cha “nuru.” Ni Mithali 3, 6: “Katika njia zako zote mkiri Yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Ile nyingine ni kifungu chake cha “nguvu.” Ni Wafilipi 4, 13: “Nayaweza mambo yote katika Kristo anitiae nguvu.” {ABN5: 19.5}

“Hili ndilo swali la watu weusi lazima wajibu,” nalimsikia akisema kwa kundi la wahubiri Wanegro: “Je! Tunayo ambayo ulimwengu unataka?” Alisimulia kuhusu alivyosikia kikundi cha wazungu wakitafuta mtu ambaye anaweza kupata mafuta. “Walisahau kusema iwapo walimtaka mzungu, mtu mwekundu, mtu manjano au mtu mweusi; walisema tu wanamtaka mtu ambaye anaweza kupata mafuta.” {ABN5: 20.1}

“Usiende kutafuta shamba la mizabibu la Nabothi,” alisema. “Kila mmoja wenu labda analo shamba lote la mizabibu analohitaji.” {ABN5: 20.2}

Wacha wazazi wajibu sasa swali hili muhimu: Je! Ni nini kilichomfanya Dkt. Carver kuwa mwanasayansi mkuu, na mafanikio yake muhimu yawezekane? Je! Hazikuwa hali za ufukara ambazo zilimufunza na ile ari yake ya wakati mwingi mno kuwabariki wanadamu ilimhimiza kufanya? {ABN5: 20.3}

Ni dhahiri kwamba kutoka mwanzoni mwa mafunzo yao, watoto wanapaswa kufunzwa thamani ya wakati na thamani ya dola, na hata kulazimishwa, ikihitajika, kujisaidia wenyewe na kuheshimu haki na mali ya wengine — wawe wajenzi, sio waharibifu, sio wanyonyaji, wa kuleta hasara, au wafujaji. Tabia za kufanya kazi kiholela husababisha utu mbaya. {ABN5: 20.4}

Katika nuru ya amri kumi, kanuni hizi, zaidi kuliko zingine zozote,

20

lazima kila siku zikazwe kikiki ndani ya akili za wachanga. {ABN5: 20.5}

“Kwa hiyo yawekeni maneno Yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana wenu nao, juu ya nchi Bwana aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.” Kumb. 11:18-21. {ABN5: 21.1}

DINI NI NINI?

Swali Namba 109:

Je! Dini hujumuisha kujifunza na kusali, kufunga saumu na kuomboleza, kuhubiri na kufariji, kutubu na kusamehe, kuombaomba na kutoa? Mtu anawezaje kuwa mwamini, na itafanya tofauti gani katika maisha ya mtu? {ABN5: 21.2}

Jibu:

Kama vile Mfano Mkuu wa dini ya Biblia alikuwa Neno (Mwana) wa Mungu katika umbo la mwanadamu (1 Yohana 1:1), vivyo hivyo dini ya Biblia yenyewe ni amri (haki) ya Mungu katika umbo la kibinadamu (2 Kor. 3:3; Kut. 31:18). Lakini kupitia katika chombo ambacho nafsi huja katika uhusiano muhimu na dini ya Biblia, ni Roho Mtakatifu. Na uunganisho huu hai kwa Neno la

21

Mungu ni agizo muhimu sana kwa utendaji wa dini ya Biblia — njia pekee ya ukombozi wa wanadamu, — kurejea kwao kutoka kwa kutangatanga kwao katika pango hadi nyumbani kwao Edeni. Kwa hivyo yeye ambaye atakuwa na dini ya kweli, lazima aombe Roho wa Kweli. Hakuna njia nyingine yoyote anaweza kuwa mwamini kweli kweli — kuwa “mbao za nyama,” amri za Mungu katika umbo la mwanadamu. Kuishi kwake (kutenda) kwazo ndiko kunakomfanya asiabudu miungu ya uongo tu au mfano wowote wa Mungu Mwenyewe lakini pia kuupoteza wakati. Uaminifu kwa amri husababisha afanye kazi zake zote katika siku sita za kufanya kazi kila juma, bila kuacha yoyote kati ya hizo kuendelea kukawia kutoka kwa juma hata kwa juma. Na kupitia katika amri, yeye hukumbushwa kwamba siku ya saba ni Ukumbusho Mtakatifu wa uumbaji (Kut. 20:3-17) na huvutiwa kwamba anapaswa kumpenda jirani yake kama nafsi yake (Marko 12:31). Kwa hivyo tunaona kwamba dini ya kweli hakika hujumuisha kitu zaidi ya kuomba tu, kufunga saumu, kutoa, na kuhubiri; na ya kwamba hakika haijumuishi “kuombaomba.” {ABN5: 21.3}

Washiriki wa kanisa la Ufalme, ni, kwa mujibu wa Isaya, watakuwa na ujuzi katika biashara na taaluma zao. Kama wajenzi, wahandisi, seremala, waashi, fundi wa mitambo, au kitu chochote, wao “watapajenga mahali pa kale palipoharibiwa,…watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, na…kutengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kwa vizazi vingi.” Isa. 61:4. Watakuwa pia wafugaji wa wanyama, wakuza

22

mizabibu, wataalam wa kilimo. Na wakiwa hivyo, wanapaswa kuwa na ujuzi katika sayansi ya usimamizi, na kuajiri maelfu ya wageni, sio tu wayahudumie mahitaji yao na kujenga (Isa. 60:10), bali pia “kusimama na kulisha” makundi yao na kuwa wakulima wao na watunza mizabibu yao (Isa. 61:5). Hivyo ni kwamba “kujifunza katika safu za kilimo kunapaswa kuwa A, Ba, na Cha ya elimu inayotolewa katika shule zetu.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 179. “Dini safi, halisi itadhihirishwa kwa kuishughulikia nchi kama hazina ya Mungu. Kadiri mtu anavyoendelea kuwa na akili zaidi, ndivyo mvuto wa kidini unavyopaswa kung’aa kutoka kwake. Na Bwana angetaka tushughulikie ardhi kama hazina ya thamani tuliyokabidhiwa kwa amana.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 245. {ABN5: 22.1}

Licha ya kuwa wataalam wa kilimo, wasanii, na wafanyabiashara, hawa maliwali wa Ufalme, kama mifano hai ya Ukristo wa kweli, watakuwa wanabenki wataalam wa kimataifa, wanauchumi, wafanyakazi na wahandisi wa trafiki, na watoaji, pamoja wakidhibiti “nguvu” na “utajiri wa Mataifa.” Isa. 6:5, 11; 61:6. Na kwa hivyo wakiwa na uwezo huu mbali mbali wa ustadi bora, wao, zaidi ya yote, watakuwa “Makuhani wa Bwana…wachungaji wa Mungu wetu” — “watu wa kushangaza.” Isa. 61:6; Zek. 3:8. {ABN5: 23.1}

Mchungaji wa injili kwa hivyo anapaswa afahamu vizuri shughuli za utendaji

23

za maisha na kuwa stadi katika kitu kimoja. Kwa kweli mhubiri yeyote anayepata asilimia kumi (zaka) ya mapato ya mkulima, anapaswa kujifunza ili aweze kuwa na uwezo wa kumsaidia kuboresha mbinu zake za kilimo kwa njia ya utendaji wakati wowote iwapo tukio lingetokea. Kwa ufupi, anapaswa kuwa hodari wa kuwasaidia washiriki wa kanisa lake katika kupangilia, kurekebisha, au kuboresha kazi na biashara zao. Yesu aliwafunza wanafunzi Wake sio kuomba tu, kuhubiri na kuitekeleza Kweli, kutoa na kusamehe, lakini pia kutumika, kuvua samaki, kulisha na kuvika, na kulipa bili kibiashara. (Tazama Mathayo 6:5-13; 10:5-7, 27; 5:19, 20; 23:3,4; Yohana 3:20, 21; Matendo 20:20; Mathayo 6:14, 15; 18:21, 22; 20:25-28; Marko 6:35-41; Luka 22:7-13; Yohana 21:3-6; Mathayo 25:31-45; 17:24-27.) {ABN5: 23.2}

Lakini ili kuwa Mkristo kama huyo, mtu mwamini kweli, lazima kwanza kabisa apangilie nafsi yake yote, akiidhibiti kwa usahihi, akisawazisha, na kutumia uwezo wake, nguvu zake, njia zake, na wakati wake. Yeyote anayeshindwa kutekeleza uchumi huu mara nne uliojumuishwa wa nafsi, kamwe hataweza kupata ufanisi wa kweli. Kwa kufanya hivyo, lazima apate “sekunde sitini za umbali wa mwendo aliomaliza kwa kila dakika isiyoweza kusameheka,” dakika sitini za matumizi kamili na mafanikio kwa kila saa ya kufanya kazi au ya kupumzika, na matokeo ya upeo kwa kila msogeo au mpigo. Lazima, kwa ufupi, aondoe kila mwendo uliopotezwa, na vile vile kila misogeo ya kutofikiri,

24

ya mizunguko maradufu na ya kulaliana, ambayo haileti matokeo bali humaliza nguvu yake ya akiba. Kazi ya Mkristo kamili kama huyu haitapatikana kamwe imefanywa kwa mtindo usiofaa au wa ovyo ovyo. {ABN5: 24.1}

Isitoshe, yeye hapatikani anaishi zaidi ya mapato yake, lakini akibajeti kwa umakini fedha zake ili kumwezesha kuishi katika mapato yake na pia mara kwa mara kuweka kando kwenye akiba kidogo kwa ajili ya siku ya mvua. Huepuka kuambukizwa madeni; anajua kwamba tabia ya kukopa siku zote na kutoweza kulipa, ni aina ya unyang’anyi– uongo. {ABN5: 25.1}

Mtu kama huyo, iwe yu maskini au tajiri, haogopi wakati ujao. Yeye bila kimbelembele humtegemea Bwana kwa mahitaji yake ya kila siku; kamwe huwa hana wazo la masumbuko ya “kesho.” Mat. 6:27-34. {ABN5: 25.2}

Kwa ujumla, tunaona kwamba dini ya Biblia, Ukristo, si kitu zaidi au kipungufu kuliko kuacha kumtii Ibilisi, hadi kumtii Bwana, kugeuka kutoka kwa maisha ya kufanya mabaya hadi kwa maisha ya kutenda mema, — kutoka kwa matumizi hadi kwa uzalishaji; kutoka kwa ukopaji hadi kwa kukopesha; kutoka kwa kuombaomba hadi kwa kupeana; kutoka kwa udanganyifu hadi kwa kurejesha na kushughulika kwa uaminifu; kutoka kwa kulipiza hadi kwa kusamehe; na kutoka kwa kutumikiwa hadi kwa utumishi. {ABN5: 25.3}

“Dini ya kweli daima huonekana wazi kabisa katika maneno na mienendo yetu, na katika kila tendo la maisha. Pamoja na wafuasi wa Kristo, dini haipaswi kutengwa kamwe kwa biashara. Vinapaswa kwenda sambamba,

25

na amri za Mungu zinapaswa kuzingatiwa kikamilifu katika shughuli zote za mambo ya kidunia. Maarifa kwamba sisi ni watoto wa Mungu yanapaswa kutoa tabia ya kiwango cha juu hata katika majukumu ya kila siku ya maisha, yakitufanya tusiwe wavivu katika shughuli, lakini wenye bidii katika roho. Dini kama hii hustahimili uchunguzi wa ulimwengu wa kukosoa ulio na ufahamu mkuu wa uadilifu.” — Shuhuda, Gombo la 4, uk. 190, 191. {ABN5: 25.4}

“Ukristo una maana pana zaidi kuliko wengi wameupatia. Sio itikadi. Ni neno lake Yeye aishiye na akaaye milele. Ni kanuni iliyo hai, changamfu, ambayo humiliki akili, moyo, nia, na mtu mzima. Ukristo — Laiti tupate uzoefu wa utendaji kazi wake! Ni uzoefu, muhimu wa kibinafsi, ambao humwinua na kumtia nguvu mtu mzima.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 421, 422. {ABN5: 26.1}

Hayo yote ndio dini ya Kristo ilivyo, na yeye anayeitekeleza, anao upendo wa kweli (1 Kor. 13) — hakika “amezaliwa mara ya pili.” {ABN5: 26.2}

Kusisitiza, kila Mkristo wa kweli kwanza hujipanga mwenyewe, kisha familia yake, na kisha biashara yake. Na zaidi, hujifunza kupitia hayo yote kwamba wengine wanaweza kupangilia, ilhali wengine hawawezi; kwamba wengine hufanya kazi kwa kufanikiwa, ilhali wengine hujitahidi bure; ya kwamba wengine huzalisha, ilhali wengine hutumia tu; ya kwamba wengine hupeana kama mti wa mwaramoni, ilhali wengine hufyonza

26

kila wakati kama sifongo kavu; ya kwamba wengine huubariki ulimwengu kwa mema, ilhali wengine huishi na kaufanyia kazi ubinafsi na hufikiri kwamba wengine wote wanapaswa kuishi na kuwafanyia wao kazi; ya kwamba wengine huitekeleza dini yao kimya kimya, ilhali wengine hufanya onyesho la utakatifu kwa mazungumzo mengi ya kidini na sala, lakini matendo machache yanayolingana nayo, na ya kwamba wengine wanajua wakati wa kuzuru na wa kutozuru, ilhali wengine hawajui aidha wakati wa kuzuru au wa kuondoka, na lazima watenganishwe na kiti kama kombe za bahari ziambatanazo na miamba wakisha kaa! Ni ulioje msitu wa mhubiri! {ABN5: 26.3}

JE! MAONO YANAHITAJIKA?

Swali Namba 110:

Je! Ni muhimu kuwa na picha akilini ya mambo tunayoomba? {ABN5: 27.1}

Jibu:

Iwapo hatuna maono kama hayo, hatutakuwa na jambo halisi na wazi la kuombea na kufanyia kazi. Na kwa kawaida, basi, wala sala au juhudi zetu hazitatimiza chochote. Kila mtu lazima awe na maono yaliyowazi ya mahitaji yake na malengo yake; Akipungukiwa vile, ataenenda kwa upofu, na hatafika popote. Kumbuka kwamba “pale ambapo hakuna maono, watu huangamia.” Mith. 29:18. {ABN5: 27.2}

Wote wanapaswa kujua mapema ni nini watafanya, na watakuwa nini. Wakati huo wanapaswa kuhakikisha kwamba mapenzi yao ni mapenzi ya Mungu, waweke malengo yao juu, na kuona kwamba wanayaafikia. {ABN5: 27.3}

27

JE! MTU ANAWEZA KUPATA UKWELI BILA KUWA NA NJOZI — MAONO?

Swali Namba 111:

Mintarafu yale huandika, Dada White husema, “nalionyeshwa” au “nilichukuliwa katika maono.” Hebu niulize tunaweza kuamini vipi katika vitabu vya “Fimbo ya Mchungaji” iwapo yaliyomo hayakufunuliwa kwa namna kama hiyo — kwa muujiza? {ABN5: 28.1}

Jibu:

Kamwe si salama kwa mtu kuweka msingi wa uamuzi wake kuhusu ujumbe kutoka kwa Bwana namna ambayo hupokelewa. Uzoefu wa nguvu zipitazo za kibinadamu sio ushahidi thabiti wa uhusiano wa mtu na nguvu za Mungu. Kwa kweli, sio lazima thibitisho hata kidogo, kwa maana yapo mafundisho mengi na imani nyingi zilizojengwa kwa muujiza mmoja au mwingine na bado hazina ukweli. Na hakuna mtu anayepaswa kupuuza ukweli kwamba udanganyifu unaokuja ambao utaufagia ulimwengu utawezeshwa kwa miujiza, hata kushusha moto kutoka mbinguni (Ufu. 13:13, 14). Walakini, kwa Neno la Mungu tunaonywa kwamba tusipotoshwe nao. {ABN5: 28.2}

Wala mtu asisahau kwamba si manabii wote wa Biblia walikuwa na njozi. Daudi na Sulemani waliandika, sio yale walipewa katika maono, lakini yale walipokea kupitia njia zingine. Na Yohana Mbatizaji aliitwa zaidi ya nabii, lakini hakuna tamko hata moja la kinabii aliloandika yeye, na wala hakuna kumbukumbu yoyote kwamba aliwahi kupelekwa njozi na kupewa maono. Alikuwa tu

28

Mfasiri wa maandishi ya manabii. Hivyo Mungu alisema zamani katika njia nyingi na manabii Wake (Ebr. 1:1). {ABN5: 28.3}

Ikumbukwe, hata hivyo, kwamba sehemu ndogo tu ya maandishi ya Dada White ilipokelewa kupitia njozi — maono. Na mambo yaliyoonyeshwa katika maono kama hayo ni, kama sheria, ya kinabii — yakitazamia tukio fulani la siku za baadaye — na, zaidi au kidogo, nyongeza kwa unabii, sio kuufasiri. {ABN5: 29.1}

Inaonekana kwamba watu wa Mungu haswa kwa wakati huu hawahitaji maono, lakini badala yake wafasiri wa maono ya manabii wa zamani ambayo bado hayajaeleweka. Na hilo ndilo Yeye ameona linafaa atupatie ili tuweze kuielewa Biblia. Huu ni muujiza mkubwa zaidi uliounganishwa na Fimbo ya Mchungaji, (Tazama kielezo katikaTrakti Namba 6, Kwa Nini Uangamie, toleo la 1944, uk. 18.) {ABN5: 29.2}

Lakini imani yako isiwe katika miujiza au uzoefu wa mwanadamu, bali katika mafunuo ya Neno Lake la kinabii. {ABN5: 29.3}

Na sasa utaratibu pekee salama na timamu ni kusoma kwa ukaribu kila ukurasa wa ujumbe mzito ulio katika machapisho ya Fimbo ya Mchungaji. Usiruhusu mstari uepuke umakini wako. Jifunze kila neno kwa uangalifu na kwa maombi. Uwe hodari na mwenye bidii katika uchunguzi wako wa ukweli, na “thibitisha mambo yote; lishike lililo jema.” 1 Thes. 5:21. {ABN5: 29.4}

29

MBONA HITAJI LA HUKUMU?

Swali Namba 112:

Siwezi kuona hitaji la hukumu. Mbona tuhukumiwe baada ya kuokolewa? {ABN5: 30.1}

Jibu:

Ya kwamba Biblia hufundisha juu ya hukumu inayokuja hakuna anayeweza kukataa. Kwa hivyo tunahitaji tu kutoa sababu kwa ajili yake. Watu wakweli wa Mungu, tunaambiwa, wamechangamana na wasio wakweli, “ngano” pamoja na “magugu.” Hukumu, kwa hivyo, itaamua ni nani “ngano” na ni nani “magugu”, na kutaja mustakabali wa kila mmoja. {ABN5: 30.2}

Kwa mujibu wa mfano wa Yesu, kazi hii itafanyika katika wakati wa mavuno, mwisho wa dunia (Mat. 13:30, 40). Na kwa sababu kongamano la wafu na pia kongamano la walio hai yamechangamana na wazuri na wabaya, hukumu inafanyika kati ya yote mawili, kwanza kati ya wafu, kisha kati ya walio hai. Katika hukumu uamuzi unafanywa ni nani anayeustahili uzima wa milele, na ni nani kifo cha milele (Yohana 5:28, 29); nani ambao watakuja katika ufufuo wa kwanza (Ufu. 20:6), na nani wa pili; pia nani ambao watahamishwa bila mauti wakati Yesu atakapokuja (1 Thes. 4:16, 17), na nani ambao wataangamizwa kwa mwangaza wa kuja Kwake (2 Thes. 2:8). Hii ndio sehemu ya kwanza ya hukumu, na ikiwa ni kazi ya kitabu tu (Dan. 7:10), kazi ambayo haiwasumbui aidha wafu makaburini au walio hai kanisani, hufanyika mbinguni. {ABN5: 30.3}

30

Sehemu ya pili sio kazi ya kitabu lakini utengo halisi wa wafu siku ya ufufuo, na wa walio hai siku ya utakaso — wafu watakatifu wanafufuliwa, na waovu wanaachwa katika makaburi yao, watakatifu walio hai wanatiwa muhuri waishi milele, na waovu waachwe wafe (Ezek. 9:2-7). {ABN5: 31.1}

Ndivyo waliokufa wanaostahili wanahukumiwa waamke katika ufufuo wa kwanza, na wasiostahili katika ufufuo wa pili, ilhali walio hai wanaostahili wanahukumiwa waendelee kuishi, na wasiostahili kuhukumiwa kufa. Na hii ndio sababu rahisi ya hukumu. {ABN5: 31.2}

JE! “NDIYE” AU TUMTAFUTE MWINGINE?

Swali Namba 113:

“Yeye asetaye vipande vipande,” jinsi ninavyoona baada ya kusoma Trakti Namba 14, “Utabiri wa Habari za Vita,” ni Hitler. Lakini hili linawezaje kuwa, wakati sasa anapata mabaya zaidi, na muungano unashinda vita? {ABN5: 31.3}

Jibu:

Trakti hiyo haimtambulishi kwa jina yule “asetaye vipande vipande.” Mahitimisho yoyote, kwa hivyo, ambayo yanaweza kutolewa kwa uchanganuzi wa mmoja kwa yaliyomo, unaweza kuwa tu wa kudhania na kwa hivyo usio hakika. {ABN5: 31.4}

Kutoka kwa maendeleo ya sasa katika ukumbi wa vita vya Ulaya, inaonekana kama Hitler ameangamizwa. Licha ya muonekano huu, hata hivyo unabii wa Nahumu kwa uchanganuzi unamfaa yeye, ingawa inawezekana kwamba mtu mwingine bado anaweza kutokea kuuendeleza

31

utabiri utimizwe. Na iwapo wakati wa vita hivi unabii hautatimizwa kwa ukamilifu wake wote, basi lazima iwe kwamba kutiwa muhuri kwa watakatifu bado hakujakamilika kazi ya ujumbe haijakamilishwa, malimbuko hayako tayari kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. Hili linaonekana kuwa kizuizi cha pekee. {ABN5: 31.5}

Kwa hivyo wakati hatujaona bado njia ambayo utabiri huo utajitimiza, sisi, hata hivyo, tunaambiwa wazi kwamba wakati “Ashuru” ataanguka, Bwana atawaweka huru watu Wake sio tu kutoka kwa wadhambi walio kati yao lakini pia kutoka kwa utawala wa Mataifa. {ABN5: 32.1}

Mwashuri, hata hivyo, “ataanguka kwa upanga, ambao si wa mtu; na upanga usio wa mtu, utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watashindwa.” “Maana kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, naye apigaye kwa bakora.” Isa. 31:8; 30:31. {ABN5: 32.2}

Kwa hivyo, wakati Sauti Takatifu ya unabii inatangaza: “Na sasa Nitakuvunjia nira yake [ya Mwashuri], Nami nitakupasulia mafungo yako,” Inaamuru pia: “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani! … kwa maana mwovu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali. Nah. 1:13, 15. {ABN5: 32.3}

Sasa ni “wakati unaofaa,” mpenzi msomaji, kuchukua msimamo thabiti pamoja naye ambaye analeta habari njema! Usiupuzie mbali. {ABN5: 32.4}

32

TUTAFUTE UCHUMI TUNAPOEPUKANA NA KIBURI?

Swali Namba 114:

Je! Wanawake wanapaswa kuvaa soksi ndefu za hariri au za pamba? {ABN5: 33.1}

Jibu:

Nafasi na hali za wanawake wengine huwafanya iwezekane kuvaa soksi refu za hariri, na wengine, kuvaa soksi refu za pamba. Lakini kuvaa soksi refu za hariri nyembamba, kwa kuwa si nadhifu wala za kufaa kwa njia yoyote ile, ni wazi kwamba ni swala lisilowezekana kwa Wakristo wote. Iwapo, hata hivyo, soksi refu za hariri zenye uzito zithibitike zaidi kwamba zinafaa kutumika na zisizo ghali na vile vile za starehe zaidi kuliko soksi refu za pamba, basi uzani unaowezekana kumudu ndilo chaguo bora. Lakini ikiwa za pamba laini au pamba, zinazowezekana kumudu zaidi na zisizo ghali na vile vile za starehe zaidi, basi ni wazi kwamba zitastahili kuwa afadhali. Hakuna sheria ngumu na ya haraka kwa wote. Hili ni jambo la mazoezi ya uamuzi wa mtu binafsi na dhamiri. {ABN5: 33.1}

“Uchumi katika matumizi ya pesa ni tawi bora la hekima ya Mkristo….Pesa ni zawadi bora ya Mungu. Mikononi mwa watoto Wake ni chakula kwa walio na njaa, kinywaji kwa walio na kiu, na mavazi kwa walio uchi; ni ulinzi kwa waliodhulumiwa, na njia ya kiafya kwa wagonjwa. Fedha hazipaswi kutumika bila hitaji na kwa ubadhirifu kuridhisha majivuno au tamaa.” — Shuhuda, Gombo la 4 uk. 571. {ABN5: 33.2}

“Katika kuanzisha na kuendeleza kazi, uchumi thabiti daima uonyeshwe.” — Mashauri kwa Afya, uk. 319. {ABN5: 33.3}

33

MFANO NJE YA ULIMWENGU, AU KATIKA ULIMWENGU PIA?

Swali Namba 115:

Wengine hufikiri kwamba marinda yaliyochukuliwa na wale wanaoishi Mlima Karmeli, ni marefu sana kwa sisi ambao tunaishi mijini. Je! Ni hivyo? {ABN5: 34.1}

Jibu:

Iwapo rinda fupi halifanyizi “vazi la adabu” kwa mwanamke Mkristo katika eneo tengwa kama Mlima Karmeli, basi litakuwa la fedheha zaidi mjini. {ABN5: 34.2}

Mwanamke yeyote mahali popote ataonekana bora zaidi katika vazi nadhifu la urefu wa adabu na la kupendeza, kuliko atakavyokuwa katika rinda fupi, lisilo na adabu. Kwa hivyo atajistahilisha pongezi kwa wenye uelekevu, na juu ya uchunguzi mwingine wote, atakuwa nguvu ya wema badala ya uovu. {ABN5: 34.3}

Kwa kuanzia, waumbaji wa mitindo waliwaanzisha wanawake wapumbavu kuvaa mavazi mafupi, na watu wengi wa kidunia bila hiari wakafuata kielelezo chao. Na iwapo wana-mitindo wanaweza kuiweka mitindo hiyo kwa mavazi marefu, nadhifu, na ya adabu, umati wa wanawake wa Kikristo wangeweza bila kusita-sita kufuata hatua. {ABN5: 34.4}

Mavazi katikati ya kilegesambwa na kiwiko ni urefu wa adabu, hakika sio mrefu sana kwa mwanamke yeyote Mkristo mahali popote. {ABN5: 34.5}

Mungu hutarajia watu Wake wawe kichwa, kuweka kiwango sahihi. Kwa hivyo, kutoa ushuhuda wa mavazi usio wa kikristo mbali

34

kutoka Mlima Karmeli, ambako mtu hukutana na umati wa ulimwengu, ni mbaya zaidi kuliko kufanya hivyo pale ambapo mvuto wa mtu umefungiwa kabisa kwa waamini. {ABN5: 34.6}

“Hauwajibiki kwa dhambi zozote za ndugu zako isipokuwa mfano wako umesababisha wajikwae, na kusababisha miguu yao kupotoshwa kutoka kwa njia nyembamba.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 256. {ABN5: 35.1}

JE, NYWELE ZAPASWA KUSUKWA?

Swali Namba 116:

Nywele zangu ni bila fahari kabisa hivi kwamba hunifanya nionekane vibaya. Je! Itakuwa vibaya kuzisuka? {ABN5: 35.2}

Jibu:

Kwa sababu mitindo mipotovu imeshutumiwa katika Neno, hatuwezi kukuhimiza ufanye jinsi ulimwengu hufanya. Mkristo hushauriwa ajivike kwa adabu, kwa unadhifu, na kwa ustaarabu. Lakini wakati akiepuka kupita kiasi na upotovu wa ulimwengu, Mkristo anapaswa kuwa mwangalifu asiende kwa upotovu mwingine, asionekane kuwa mchafu. Dumu katikati ya njia; yaani, zinyoshe nywele zako kwa njia ambayo itazuia kuvutia umakini wa jicho la umma kwa sababu ya aidha kupita kiasi. (Soma Isaya 3:16-26). {ABN5: 35.3}

SURUALI NDEFU AU SKETI?

Swali Namba 117:

Je! Ni sawa kwa mwanamke kuvaa suruali ndefu wakati wa kufanya kazi ya ulinzi? Je! Sio mavazi ya wanaume? {ABN5: 35.4}

35

Jibu:

Iwapo kuvaa suruali ndefu kunapaswa kuzuiliwa kwa wanaume tu kwa sababu wanaume leo duniani kote huvaa suruali ndefu, basi sketi za zamani zingalipaswa kunyimwa wanawake kwa sababu vazi hilo wakati huo lilikuwa mavazi ya kawaida ya wanaume. {ABN5: 36.1}

Lakini kwa vile wanaume na wanawake wakati huo walivaa sketi swali halipaswi kuwa kama sketi au suruali ndefu zinapaswa kuvaliwa siku zote au mara kwa mara na wanawake, lakini kuhusu iwapo mavazi ya wanawake yanapaswa kuwa sawa na mavazi ya wanaume. {ABN5: 36.2}

Hebu tukumbuke kwamba hakuna amri ya Biblia kuhusu ikiwa ni namna gani ya vazi walei wanafaa kujivika, isipokuwa amri kwamba linapaswa kuwa la adabu, lisilo ghali (1 Tim. 2:9), na ya kwamba lile la mwanamume linapaswa kutofautishwa kwa lile la mwanamke. “Mwanamke,” asema Bwana, “asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.” Kumb. 22:5. {ABN5: 36.3}

Sasa iwapo suruali ndefu zina haiba ya kipekee ya vazi linalomhusu mwanamke, basi haliwezi kuwekwa katika kundi kama vazi la mwanamume. {ABN5: 36.4}

Iko pia awamu nyingine ya swali la kufikiriwa: Iwapo vazi ni la adabu, sio la kupindukia, lililotengenezwa kukidhi hitaji la anayelivaa, sio tamanio la kuridhisha mitindo ya ulimwengu inayobadilika daima, basi hatuoni uovu kujivika. Tunafikiri kwamba

36

suruali ndefu za adabu ni bora zaidi kuliko magauni mafupi, yasiyo na heshima. Lakini hata suruali ndefu zinazovaliwa mbele ya umma haziwezi kumpa mwanamke ile haiba ya mavazi ya Mkristo. Isipokuwa iwe katika hafla fulani au kwa kazi fulani wakati au mahali gauni ni kizuizi, suruali ndefu hazipaswi kuchukua nafasi ya mavazi nadhifu na ya adabu ambayo humfaa mwanamke Mkristo. {ABN5: 36.5}

Iwapo, hata hivyo, kuvalia suruali ndefu kwahitajika kwa mtu anayefanya kazi kiwandani, basi hatuoni lolote baya kwa kuzivaa wakati wa kufanya kazi. {ABN5: 37.1}

JE! WONYESHO NI DHAMBI?

Swali Namba 118:

Nafikiri ni dhambi kwa binti yangu kuvaa saa ya mkononi. Je! Ni hivyo? {ABN5: 37.2}

Jibu:

Hakuna pingamizi la kubeba saa ya aina yoyote. Lakini wakati mtu anaifanya kuwa wonyesho, iwe ni mkononi au mahali pengine, basi huifanya iwe pambo, na hivyo kudunisha tabia ya yule anayeivaa, humfanya kuwa na majivuno, na wengine kuwa wenye wivu na kijicho. Wakati, zaidi ya hayo, kipande cha mapambo ya vito, huvaliwa kwa wonyesho, yakiwa ni ya muundo na ubora duni, sio tu hudunisha tabia na kupendeza kwa yule anayevaa bali pia humpiga chapa kama mwigaji wa kisingizio. Mkristo ataacha haiba zote za ubatili, na kuwa bila lawama kabisa. Iwapo anahitaji kubeba kidude cha saa, atafanya hivyo kisiri, kama kifaa cha ziada cha lazima, na sio kuivaa sana ili ionekane kuwa mtindo au wonyesho. {ABN5: 37.3}

37

JE! MWANAMKE ASIIVUE KOFIA YAKE MWANAMUME ANAPOVUA YAKE?

Swali Namba 119:

Je! Paulo humaanisha nini katika 1 Wakorintho 11 mintarafu mwanamke kukifunika kichwa chake? Je! Aya ya 15 haionyeshi kwamba nywele ni stara yake? {ABN5: 38.1}

Jibu:

“Lakini nataka,” asema Roho Mtakatifu, “mjue, ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo; na kichwa cha mwanamke ni mwanamume; na kichwa cha Kristo ni Mungu.” 1 Kor. 11:3. {ABN5: 38.2}

Zingatia mpangilio ambao uungu na ubinadamu umeunganishwa: Mungu, Kristo, mwanamume, mwanamke. Hivyo ni kwamba “Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake [Mungu]. Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake [mwanamume]; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa, na akatwe nywele [yaani, ikiwa mwanamke hatavaa kofia basi akate nywele zake]: Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe [basi avae kofia]. Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.” 1 Kor. 11:4-8. {ABN5: 38.3}

Andiko hili lafundisha wazi kwamba mwanaume anapaswa kuvua kofia yake wakati wa kusali au

38

kuhutubu (kufundisha Maandiko), wakati mwanamke anapaswa kwendelea kuvaa yake. {ABN5: 38.3}

Mtu hawezi kwa busara kuhitimisha kutoka 1 Kor. 11:15 kwamba nywele za mwanamke ndio sitara inayotajwa. Iwapo ingalikuwa hivyo, basi kimantiki mwanamume anapaswa kunyoa nywele zake ili kufanya tofauti kati yao wawili. {ABN5: 39.1}

Isitoshe, iwapo nywele za mwanamke ndio stara inayohitajika, basi mbona Maandiko husema anastahili kuvaa wakati “wa kusali au kuhutubu”? Lipi lingine angefanya? Je! Angeweza kuvua nywele zake (stara) wakati hasali, isipokuwa amevaa nywele bandia? {ABN5: 39.2}

Maandiko kwa hivyo huweka wazi kwamba hafla yoyote ya kidini ambayo humhitaji mwanamume kuvua kofia yake, humhitaji mwanamke avae yake. {ABN5: 39.3}

VIPI KUHUSU IBADA YA MEZA YA BWANA?

Swali Namba 120:

Je! Waamini ambao wamekita mizizi katika ujumbe, wapaswa kuiadhimisha ibada ya meza ya Bwana wanapokutana pamoja? {ABN5: 39.4}

Jibu:

Kuhusu kuidhinisha ibada ya meza ya Bwana kati yetu wenyewe, tunaamini kwamba kwa sababu sisi sote, kama Waadventista wa Sabato, tumejitia unajisi jinsi Wayahudi walivyofanya wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo (Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 104) na kwa sababu ibada hii takatifu hufanya hukumu kwa wale ambao huipokea isivyostahili (1 Kor. 11:29), kwa hivyo hatuwezi kuthubutu

39

sasa, kama Wadaudi, kujichukulia manufaa yake matakatifu hadi kama watu maisha yetu yatoe ushahidi wa kusadikisha wa toba kutoka kwa hali ya Ulaodekia. {ABN5: 39.5}

Funzo la kutoidhinisha ibada hii iliyobarikiwa kati yetu wakati huu, kinyume inalinganishwa sana kwa ile ambayo Yohana Mbatizaji alifundisha katika kuweka wakfu na kusisitiza kuhusu ibada ya Ubatizo wakati huo; yaani, Yohana kuianzisha huduma ya Ubatizo wakati huo, ilionyesha kwamba Wayahudi hawakuwa tayari kumlaki Mfalme wao, na Fimbo kutoianzisha ibada ya meza ya Bwana sasa, huonyesha kwamba hatujakuwa tayari kumlaki Mfalme wetu, na ya kwamba kwa hivyo lazima tutubu upesi tutoke katika uvuguvugu wetu, tununue “dawa ya macho”, na tupake macho yetu. Kisha tutaadhimisha ibada ya meza ya Bwana, na aibu ya uchi wetu haitaonekana (Ufu. 3:18). {ABN5: 40.1}

Wale ambao hawahisi hitaji hili kubwa bado ni vipofu kwa hali ya kanisa ambayo haijaimarika, na kwa utakatifu wa Bwana. Imani thabiti ya nje tu katika ujumbe haitoshi; kazi yake ya ndani maishani mwetu ni kazi ya umuhimu wote na ya juu ambayo lazima ifanyike maishani mwetu sote kabla tuweze kuadhimisha kwa dhamiri safi na kwa manufaa meza ya Bwana. Hebu tuharakishe siku hiyo ya furaha. {ABN5: 40.2}

ZAWADI YANGU NI NINI?

Swali Namba 121:

Je! Ni nini maana ya 1 Timotheo 4:14; “Usiache kutumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa

40

kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono na wazee”? {ABN5: 40.3}

Jibu:

Katika andiko linalohojiwa, mtume Paulo anamhimiza Mkristo kuwa mwaminifu na mwenye bidii katika majukumu ambayo Mungu amemtwika, na asipuuze upendeleo na fursa zake, au kupungukiwa na vipaji na uwezo wake kuzidisha “talanta” zake. {ABN5: 41.1}

Jukumu la kwanza la kila Mdaudi ni kuwa mwaminifu katika kutii kanuni za mafundisho, kwa kufanya kazi yoyote anayopewa kufanya, na kwa mafundisho na mfano kuwaowaongoza wengine kufanya vivyo hivyo. {ABN5: 41.2}

Baadhi wanafanya hivyo kwa kujenga Kituo cha Mlima Karmeli, wengine kwa kutoa mafunzo, wengine kwa kuandika barua na kutuma trakti na vitabu kwa jamaa zao, marafiki, na wanaowafahamu, na bado wengine wengi kwa kutuma majina na anwani za Waadventista wa Sabato ambao wanaweza kutumiwa vitabu vya Ukweli wa sasa. {ABN5: 41.3}

Kila mmoja lazima awe mwaminifu katika majukumu yake, kama alivyokuwa Danieli, ili asilete lawama dhidi ya taaluma yake ya kidini, ila badala yake, kwa tabia yake thabiti na utumishi wa uaminifu katika jina la Kristo, awaongoze wengine kwa ujumbe wa saa ya sasa. Leo kuliko hapo awali, Mkristo anapaswa kuwa “si mlegevu katika shughuli,” bali “mwenye juhudi katika roho; akimtumikia Bwana.” Rumi. 12:11. {ABN5: 41.4}

41

VIPI KUHUSU KUPOKEA ZAWADI?

Swali Namba 122:

Kwa mujibu wa Trakti Namba 13, “Salamu za Kristo,” Toleo la 1941, uk. 5, 6, Wakristo hawapaswi kutoa zawadi za “wakati.” Lakini je! ni vibaya kuzipokea? Au je! mtu anapaswa kuzirudisha na hivyo kuhatarisha kumkosea mtoaji? {ABN5: 42.1}

Jibu:

Trakti hiyo haikusudii kuwasilisha wazo kwamba ni makosa kupokea zawadi za “wakati” kutoka kwa wale ambao hawajui kuhusu matokeo mabaya ya mila hiyo, lakini kwamba si sawa kwa wale wanaojua vyema, kuzitoa kwenye hafla za kitamaduni. Iwapo mtu angeikataa zawadi kama hiyo, bila shaka angemkosea mtoaji. {ABN5: 42.2}

MTU ANAWEZAJE KUSIMAMA IWAPO ANAPANGA KUANGUKA?

Swali Namba 123:

Je! Unaweza kufafanua Waebrania 6:4-6? {ABN5: 42.3}

Jibu:

Wale ambao hawaishi kulingana hata na kanuni za kwanza za mafundisho ya Kristo na ambao “hawakazi mwendo kuufikia utimilifu,” lakini ambao huweka “msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai,… ambao hapo zamani walikwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo,” anaonya Paulo, “haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu, kwa kuwa wamsulubisha

42

Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.” Ebr. 6:1, 4-6. {ABN5: 42.4}

Andiko lenyewe huweka wazi kwamba wale ambao wamejaliwa neema kwa njia maalum na nuru kubwa lakini hawaishi kulingana na maagizo yanayovuvia ya mafundisho ya Ukweli wanaweka msingi ambao utawarudisha ulimwenguni, na ikiwa watarudi nyuma hivyo, haitawezekana kwa injili ya Kristo kuufanya upya uongofu wao kwa “msimu unaofaa.” Mifano mizuri ya Mfalme Agrippa na Feliki (Matendo 24, 25, 26) inatia nguvu ushahidi wa hili jambo. {ABN5: 43.1}

JE! TUOMBE JINSI GANI?

Swali Namba 124:

Nimeambiwa kwamba wakati tunaomba kwa Mungu, Baba, tunapaswa kusema siku zote: “Kwa jina la Mwanao mbarikiwa Yesu, Aliyenifilia, naomba kwa unyenyekevu, nk.” Je! Hii ndio njia sahihi ya kusali? {ABN5: 43.2}

Jibu:

Ijapokuwa aina ya maneno yaliyotangulia ya heshima katika maombi yanaweza kuwa mazuri, lakini sala hazihitaji siku zote kuchukua aina hii mahsusi. {ABN5: 43.3}

Katika sala ya kielelezo ya Bwana itapatikana njia kamili. Hicho ni sala nzuri, sala kamili, kila neno lake limejazwa kusudi na maana — “Baba yetu,” si “Baba yangu” (haswa hivyo katika sala ya umma); “tusamehe…kama,” sio tu “tusamehe”; “Ufalme Wako uje, Mapenzi Yako yafanyike duniani” — si mbinguni, bali “kama yalivyo mbinguni.” {ABN5: 43.4}

43

Fupi, bali inahusisha mambo yote na bila marudio, hutufunza kumwita Muumba wetu kwa jina Lake la ubaba Baba yetu, ambalo hutuleta katika kifungo cha karibu cha umoja na Yeye kuliko yanavyoweza majina Yake mengine. Hutufanya tutambue tegemeo letu Kwake kabisa kwa ajili ya mahitaji yetu yote. Huzifunika dhambi zetu na kutupatanisha kwa Baba yetu, na kutufanya marafiki kwa wanadamu wenzetu, hata wale wanaotukosea. Huumba ndani yetu upendo kwa Ufalme Wake, na hutuvuvia bidii ya kufanya kazi kwa ajili ya kuja kwake. Na mwisho, hutuongoza kufanya yote tuwezayo kwa ajili ya kutawazwa mapenzi Yake hapa duniani. {ABN5: 44.1}

Sala ya sala zote, huamuru kusoma kwa kicho na uzingatiaji wa kanuni zake kuu. (Tazama Mlima wa Baraka, uk. 151-176). {ABN5: 44.2}

TUWEZE KUWA KIMBELEMBELE NA WASIOTENDA?

Swali Namba 125:

Je! Haionyeshi ukosefu wa imani kuwaombea wagonjwa na kisha kutafuta kuwaponya? {ABN5: 44.3}

Jibu:

Kuombea tu yule aliye mgonjwa, na bila kumfanyia chochote, kwaweza kumaanisha, katika uchanganuzi wa mwisho, kwamba mwombaji ni mwema sana na mwenye huruma kuliko Mungu, na kwa hivyo anajaribu kumshawishi Bwana kwa jukumu Lake kufanya jambo fulani kwa ajili ya mgonjwa, kana kwamba Yeye tayari hakutaka. {ABN5: 44.4}

Tunapowaombea wengine, hatumjuzi Mungu jambo lolote ambalo

44

Yeye asiye na mwisho tayari amelifahamu vyema zaidi kuliko sisi tunavyojua au tutakavyojua. Kwa sababu Yeye anajua yote kulihusu suala, sababu yetu kusali si kumshawishi Yeye kwamba mtu anahitaji msaada Wake, bali kuomba baraka Zake juu ya lile tunaweza kumfanyia yule mhitaji. Mlawi na kuhani hawakufanya lolote kwa aliyejeruhiwa, na walihukumiwa kwa ukosefu wao wa huruma, ilhali Msamaria alifanya, na akapongezwa kwa ubinadamu wake. {ABN5: 44.5}

Iwe ni, kwa hivyo, tunaomba kwa ajili ya wengine au yetu sisi wenyewe, tunaomba baraka za Bwana kwa juhudi zetu dhaifu. Iwapo Bwana hivyo basi ataona inafaa kutupatia hekima na ustadi wa kuleta majibu kwa maombi yetu wenyewe, je! si uponyaji Wake kwa mgonjwa kupitia juhudi zetu hata wa utukufu zaidi kuliko Yeye kuwaponya bila sisi kuweza kusogeza kidole? {ABN5: 45.1}

WAKATI WA KUANDIKA NA WA KUTOANDIKA?

Swali Namba 126:

Je! Inaruhusiwa siku ya Sabato kuandika barua za kimishonari na kujisajili kwa vitabu vya injili? {ABN5: 45.2}

Jibu:

Maadamu ni vizuri kutenda mema siku ya Sabato, hata hivyo kuna aina fulani za juhudi, kama vile kuandika barua za kimishonari na kuuza au kuchukua maagizo ya vitabu vya injili, ambazo, hata zinapofanywa kwa maslahi ya kazi ya Bwana, haziruhusiwi. (Tazama Shuhuda, Gombo la 1, uk. 471, 472; Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250.) Ni kuibadilisha Sabato kuwa siku

45

ya kazi na biashara, si kuitakasa kama siku ya kupumzika na ibada. Na iwapo inafanywa ndani ya nyumba ya Mungu, biashara kama hiyo ni ya kuitia unajishi. {ABN5: 45.3}

Ingawa kuandika barua za kimishonari kunaonekana afadhali kuliko kuuza vitabu vya injili siku ya Sabato, bado, pia, hubadilisha kusudi halisi la siku ya Sabato kutoka lile la siku ya kupumzika kuwa siku ya kazi. Siku ya Sabato, Mungu alipumzika kutoka kwa “kazi Yake yote.” Mwa. 2:2. Hivyo, kwa siku hiyo Wakristo lazima pia wapumzike kutoka kwa kazi zao zote. {ABN5: 46.1}

Kusaidia mwongozo katika jambo hili, ikumbukwe kama sheria ya jumla kwamba jambo lolote linaloweza kufanywa kwa siku nyingine ni dhambi kulifanya kwa siku takatifu ya Mungu. {ABN5: 46.2}

Jengo la hema ya ibada na dhabihu zilikuwa na umuhimu mkubwa kamili katika ibada ya Mungu (kwa kuiendeleza mbele injili katika kivuli wakati wa Agano la Kale) kama vile uuzaji wa vitabu vya injili na uandishi wa barua za umishonari wakati huu. Walakini wakati Israeli wa zamani walikuwa wanajenga Hema ya ibada kwa utumishi wa Mungu mwenyewe, Yeye hakuwaruhusu kufanya kazi yoyote humo siku ya Sabato. {ABN5: 46.3}

“Maelekezo yalikuwa yametolewa punde,” yasema Roho ya Unabii, “kwa ujenzi bila kukawia wa hema ya ibada kwa huduma ya Mungu; na sasa watu wanaweza kuhitimisha, kwa sababu lengo lililokuwa kwa mtazamo lilikuwa utukufu wa Mungu, na pia kwa sababu ya hitaji lao kubwa la mahali pa ibada, kwamba

46

wangehalalishwa kufanya kazi kwenye jengo hilo siku ya Sabato. Ili kuwalinda kutokana na kosa hili, onyo lilitolewa. [“… yeyote atakayefanya kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.” Kut. 31:14]. Hata utakatifu na uharaka wa kazi hiyo maalum kwa ajili ya Mungu si lazima iwaongoze kuihalifu siku Yake takatifu ya kupumzika.” — Mababu na Manabii, uk. 313, 314. {ABN5: 46.4}

Yesu na mjeledi wa kambaa akawafukuza kutoka hekaluni wale ambao walikuwa wakinunua na kuuza (Yohana 2:15), ingawa wanyama ambao walikuwa wakinuliwa na kuuzwa walipaswa kutumiwa katika huduma ya dhabihu. {ABN5: 47.1}

Kama sheria, wale wanaofikiri inaruhusiwa kuandika barua za kimishonari siku ya Sabato, hufanya machache sana, ikiwa si lolote, kwa ajili ya Mungu wakati wa siku sita za kufanya kazi. Hawako tayari kumpa Yeye wakati wao hata kama unachukua kuandika barua. Kwa hivyo, barua ambazo wao huandika siku ya Sabato, kwa kweli, ni barua ambazo, hazitokani na moyo wa upendo, lakini badala yake kwa ari ya kuokoa wakati kwa ajili ya ubinafsi. Mawasiliano ya kawaida mara nyingi hupakwa dini ili kutuliza dhamiri na kuidhinisha udhuru kama ngao ya kukinga dhambi ya kuyatumia masaa ya Sabato. Shetani huvuvia matendo kama hayo kuifanya dhambi iweze kuwa kubwa kabisa. {ABN5: 47.2}

NI NANI ATATUPATIA UJIRA WETU?

Swali Namba 127:

Watendakazi “wa sehemu ya wakati” ambao wanapata

47

mafanikio kadhaa wanayo haki ya msaada wowote wa kifedha kutoka kwa Jumuiya? {ABN5: 47.3}

Jibu:

Kwa sababu kazi yoyote ya kweli kwa Kristo ni kazi inayotegemea upendo, Wadaudi wote wenye moyo wa kweli daima wanalo jambo kuu moja katika mawazo yao — kuziokoa nafsi. Wao huliacha suala lote la ujira kwa “Mwenye nyumba” katika ufahamu fulani kwamba wakati “jioni itakapokuja” Yeye atawapa “chochote kilicho haki.” Waaminifu ambao Bwana huajiri, huenda kazini bila kujua watapokea nini mwisho wa siku. Kwa hivyo watendakazi Wake ambao Anawatuma katika shamba Lake la mizabibu sasa, saa ya kumi na moja, lazima wajifunze kwamba kazi hiyo inapaswa kufanywa kwa jumla katika njia Yake, sio ya mwanadamu. {ABN5: 48.1}

Iwapo ujumbe ungetoa udhamini wa kifedha kwa wale ambao hufanya kazi ya nyanjani sehemu ya wakati, utakuwa unajifunga kwa kielelezo cha kumuunga mkono mtu yeyote na kila mtu anayefanya chochote, iwe ni kidogo au kikubwa. Kielelezo kama hicho bila shaka hakiwezi kufuatwa. Na hata iwapo kinaweza kuwa hivyo, chaweza kumdhuru mtendakazi na wale ambao anaweza kuwafanyia kazi. {ABN5: 48.2}

Ndiposa, utaratibu sahihi pekee ni kwamba wote wanaohusika katika kazi hii ya ujumbe wa kutiwa muhuri, waripoti shughuli zao kwa Makao Makuu ya kazi, ili Ofisi iweze kuhesabu matokeo ya kazi zao. Na ikiwa kuna faida kutoka kwa juhudi zao fedha za kutosha kuwawezesha kutoa sehemu kamili ya wakati kufundisha ujumbe,

48

basi wanaweza kupewa hadhi ya sehemu yote ya wakati, kuwapa haki ya gharama muhimu ya kuishi kutoka kwa matokeo ya kifedha ya kazi zao. {ABN5: 48.3}

Katika mwito huu wa watendakazi, wote — wadogo au wakubwa, matajiri au maskini, wasomi au wasiojua kusoma wala kuandika — wanao upendeleo wa juu na uliokwezwa wa kuwa wachungaji wa Kristo. {ABN5: 49.1}

“Ukweli wa sasa huongoza kuendelea mbele na kuinuka juu, kuwakusanya ndani wanaohitaji, maskini, waliodhulumiwa, wanaoteseka, na walio hohe hahe. Wote watakaokuja wataingizwa ndani ya zizi. Katika maisha yao yatafanyika matengenezo ambayo yatawajumuisha kuwa wa familia ya kifalme, watoto wa Mfalme wa mbinguni.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 195, 196. {ABN5: 49.2}

Mwisho, walimu wote wa Ukweli wa sasa wanaombwa kudumisha mawasiliano na Ofisi kuhusu jitihada zao, na kwa upande wake itatoa udhamini wowote unaowezekana kufanikisha kazi yao. {ABN5: 49.3}

KULISHA KONDOO PEKEE AU WANA-KONDOO PIA?

Swali Namba 128:

Je! Ni muhimu kuwaendea wapya walioongoka kwa Laodekia kama ilivyo kuwaendea washiriki wakubwa? Mimi nina hisia kwamba wale ambao wamekuwa Waadventista wa Sabato tangu ujumbe wa kutiwa muhuri ulipopeanwa kwanza wanaweza kupata nafasi ya kuja ndani na umati; vinginevyo, kazi inawezaje kukamilishwa, tukizingatia kwamba wapya wanakuja ndani ya Laodekia haraka kuliko tunavyoweza kuwa karibu nao? {ABN5: 49.4}

49

Jibu:

Hatuoni sababu kwa nini wale ambao wameipokea imani ya Uadventista hivi karibuni wapuuzwe. Kwa hakika, itakuwa kazi isiyowezekana kuwabagua. Kwa hivyo si sawa tu lakini muhimu kutumia manufaa ya kila fursa kuwasilisha Ukweli kwa Waadventista wa Sabato, wachanga au wakongwe katika Ujumbe wa Malaika wa Tatu. Zaidi ya hili jukumu liko mikononi mwa Bwana. Yeye ameahidi kuchukua hatamu mikononi Mwake mwenyewe na kuikatiza kazi katika haki. {ABN5: 50.1}

Hata hivyo, katika kuzungumza au kujifunza na mtu unayemjua kuwa mwongofu wa hivi karibuni, unapaswa kutumia uangalifu na uamuzi maalum na busara katika kuwasilisha kweli rahisi za matengenezo kwanza ili usikanganye akili za yule ambaye ni “mtoto” (“Maher-shal-al-hash-bazi”) katika Maandiko. {ABN5: 50.2}

MBONA USIFANYE KAZI KWA AJILI YA ULIMWENGU WAKATI WA NAFASI?

Swali Namba 129:

Wakati hatujafanyi kazi kwa ajili ya wadhambi ndani ya Zayuni basi mbona tusiende kufanya kazi kwa wadhambi ulimwenguni? Je! Bwana ametupatia nuru tiufiche”chini ya pishi,” au kuangaza ulimwengu nayo? {ABN5: 50.3}

Jibu:

Ikiwa hatufanyi kazi kwa ajili ya wadhambi katika Zayuni, basi ingalikuwa bora tungekuwa tunafanya kazi kwa ajili ya wadhambi ulimwenguni. Hata hivyo, iwapo

50

kwa kweli tunaelewa hali ilivyo, na tunaamini katika uaminifu kutekeleza imani yetu, tunapaswa kufanya kazi kwa ajili ya wadhambi ndani ya Zayuni na mzigo unaochukua muda wote ambao kwa sasa hatuna wakati wala nguvu iliyoachwa kufanya kazi kwa ajili ya wadhambi ulimwenguni, ila kwa wale waliowakilishwa na mwanamke “Msirofoinike” (Marko 7:26). Kisha tutakuwa tunafanya sehemu yetu kamili katika mwito wa watu 144,000 kwa kazi yao, na hivyo kuharakisha wakati wa kuukusanya umati mkubwa kutoka ulimwenguni — siku ya Kilio Kikuu. {ABN5: 50.4}

JE! NI TRAKTI ZIPI KWA WATU WA NJE?

Swali Namba 130:

Je! Ni zipi kati ya mfululizo wa trakti za “Fimbo ya Mchungaji” zinafaa kupeanwa kwa wale ambao si washiriki wa dhehebu la Waadventista wa Sabato? {ABN5: 51.1}

Jibu:

Vitabu vya Fimbo ya Mchungaji vimekusudiwa Waadventista wa Sabato, lakini iwapo tukio litadai kuwapatia wengine wasio Waadventista, Trakti Namba 12, 13, na 14 ni bora zaidi. {ABN5: 51.2}

MAMBO YA KUJIFUNZA?

Swali Namba 131:

Je! Masomo yaliyo katika Machapisho ya “Fimbo ya Mchungaji” au yale yaliyo katika kazi zingine, yanapaswa kusomwa katika mikutano yetu ya Sabato? {ABN5: 51.3}

Jibu:

Iwapo Fimbo ya Mchungaji inasheheni ujumbe wa saa ya sasa, basi unachukua kipaumbele

51

kwa kila ukweli mwingine wowote kwa maana Roho ya Unabii husema, “Ni ‘ukweli wa sasa’ ambao kundi linahitaji sasa.” — Maandishi ya Awali, uk. 63. “‘Mambo haya [kutiwa muhuri kwa watakatifu] yanapasa kushughulisha akili yote, umakini wote.’” — Maandishi ya Awali, uk. 118. “Endeleza kanuni mpya, na shindilia ndani ukweli ulio wazi.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 118. {ABN5: 51.4}

JE! NI SALAMA KUBISHANA?

Swali Namba 132:

Iwapo tutaweza “kujaribu mambo yote; na kushika sana lililo jema,” na kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu aulizaye habari za tumaini lililo ndani yetu, basi hatupaswi kuwapa changamoto wale ambao ni maadui wa “Fimbo ya Mchungaji” kuthibitisha kuwa ina makosa? {ABN5: 52.1}

Jibu:

Hata wale ambao wameamua mara moja na kabisa kwamba Fimbo ya Mchungaji inasheheni ujumbe uliotumwa kutoka mbinguni, bila kutaja wale ambao hawawezi kuutetea katika nyanja zake zote, hawana haki yoyote ya kuweka wazi vito vyao vya thamani vya Ukweli kwa Adui, ambaye lengo lake pekee ni kuunyakua kutoka kwao. Haswa hivyo wakati haji na ahadi ya kuwapatia kitu ambacho kitachukua nafasi ya kile walichonacho tayari. Hawawezi kumudu kualika changamoto yake kuthibitisha iwe au la anaweza kuwahadaa hazina yao. Wakati imenyakuliwa, “thibitisho” litakuwa faraja ya kusikitisha! Kujiweka wenyewe hivyo kwa udongo ufaao wa Shetani kutawafanya kuwa na hatia sio tu ya upumbavu wa kimbelembele bali kupoteza wakati na nguvu

52

vile vile. Itakuwa tu kumkaribisha Ibilisi kuwanyang’anya uzima wa milele. {ABN5: 52.2}

Sisi sote lazima tuilinde hazina yetu ya mbinguni kwa uangalifu mkubwa, na tuhifadhi imani yetu kwa kusoma ili kutoa jibu kwa kila mtu aulizaye habari za tumaini lililo ndani yetu, lakini sio kwa kumpa changamoto ya kuendelea kutuuliza maswali ya udanganyifu, na kisha tubishane naye. {ABN5: 53.1}

Iwapo, hata hivyo, kwa sababu yoyote ya kushurutisha ujitwalie hatari ya kukutana na Adui katika vita hii kuu ya kiroho, basi lazima angalau umwajibishe ajibu kwa Ukweli wote; usimruhusu akubadilishe kwa mjadala fulani ambao hakuna mtu, labda, kwa wakati huo angeweza kutatua. Usiruhusu mwenyewe kuingizwa katika nafasi ya kujikinga, lakini badala yake jiweke kwenye ushambulizi, hata hivyo usibishane kamwe. {ABN5: 53.2}

Usisahau kwamba Adui anayetafuta kuchukua taji yako ni hodari kuliko wewe, na ya kwamba kwa hivyo iwapo haujatulia kabisa kwa ujumbe, basi kwa njia zote badala ya kujifunza na maadui wa ujumbe, enenda ujifunze na marafiki za ujumbe. Ni baada tu ya kufanya yote hivyo kuwaruhusu wajumbe wauthibitishe kuwa ni sawa, na bado wameshawishika kwamba si Ukweli wa Sasa, unaweza kujifunza kwa haki na wapinzani wa ujumbe. Fanya yote kuhakikisha kwamba mtu fulani asikudanganye kwa ujumbe kutoka kwa Bwana. Usimruhusu “mtu awaye yote asiitwae taji yako.” Ufu. 3:11. {ABN5: 53.3}

Kumbuka kwamba iwapo kuna mtu aliye tayari kuharibu ukweli mmoja, yupo mwingine

53

tayari kuharibu ukweli mwingine, na kadhalika na kadhalika. Kwa kweli, Adui yu tayari kuharibu kila ukweli uliopo, hata Biblia Yenyewe, ikiwa utampa nafasi. Hakika, hata hivyo, ni ya kwamba Shetani huwa haanzi kuwa na nafasi nyingi za ubishi dhidi ya kweli za Fimbo kama watunza Jumapili wanavyopinga ukweli wa Sabato. {ABN5: 53.4}

Kumbuka daima kwamba “juhudi zinazofanywa kuzuia maendeleo ya ukweli zitasaidia kuuendeleza” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 454), na ya kwamba utakwezwa pamoja nao iwapo utafuliza katikati ya njia, pasipo kukimbia mbele kwa bidii ambayo hailingani na maarifa. {ABN5: 54.1}

“Masadikisho yetu yanahitaji kila siku kutekelezwa tena kwa sala ya unyenyekevu, ya uaminifu na kulisoma neno. Wakati sisi kila mmoja ana nafsi, wakati sisi kila mmoja anapaswa kushikilia masadikisho yetu imara, lazima tuyashike kama ukweli wa Mungu na kwa nguvu ambayo Mungu hutoa. Ikiwa hatutafanya hivyo, yatakamuliwa kutoka kwa ufahamu wetu.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 401. {ABN5: 54.2}

Hivyo, kwa mtu ambaye ametulia katika Ukweli na anayetafuta zaidi, ili kumpinga Adui, ni kama kuweka upanga wa mtu mkononi mwake na kumjasiri kukata kichwa cha mtu. {ABN5: 54.3}

Kamwe usitoe changamoto, kwa hivyo, bali daima uwe tayari kutoa jibu sahihi kwa busara na kwa kumshawishi kila mtu; usibishane kamwe,

54

lakini siku zote fundisha Ukweli; kamwe usiende kwa adui au kwa asiye mwamini wa ujumbe ili kuuthibitisha kwamba ni sawa au si sawa; badala yake, fanya uthibitisho wako wote na marafiki wa ujumbe, na waandishi wake — wale wanaojua yote kuuhusu. {ABN5: 54.4}

JE! NI NINI MAANA YA “LILE AMBALO LIMECHAPISHWA”?

Swali Namba 133:

“Msimbo wa Nembo” husema: “Fundisha tu lile ambalo limechapishwa.” Je! Unaweza kuelezea iwapo kizuio hiki kimekusudiwa kujumuisha Biblia, Roho ya Unabii, na vitabu vya “Fimbo ya Mchungaji,” vyote kwa pamoja, au maandishi ya “Fimbo” tu? {ABN5: 55.1}

Jibu:

Biblia na vitabu vya Roho ya Unabii vikiwa chanzo pekee cha ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, kwa hivyo wakati Fimbo inafundishwa, Biblia na Roho ya Unabii inafundishwa. Na kwa sababu hakuna isipokuwa Roho wa Kweli aliyezipitisha siri za Uvuvio anaweza kuzifasiri, basi wale wanaojaribu kuzifundisha bila mamlaka hii ya ufasiri wa Uvuvio bila shaka hutumbukia katika mazoea yaliyokatazwa ya ufasiri wa apendavyo mtu (2 Pet. 1:20) — uovu mkubwa ambao umeleta himaya ya Ukristo katika hali yake ya sasa isiyokuwa na mipaka ya madhehebu na tokeo la machafuko, mizozo, na udhaifu. {ABN5: 55.2}

Kwa vile hatuthubutu kufuata katika njia hiyo, sisi lazima kwa hivyo, kama walimu wa Fimbo ya Mchungaji (machapisho rasmi ya

55

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato), tufundishe tu katika nuru ya Fimbo vifungu ambavyo kwa njia moja au nyingine vinahitaji kufasiriwa. Hivyo tu waamini wote wa Ukweli wa sasa daima watakuwa na nia moja, wataona jicho kwa jicho na kunena mamoja (1 Kor. 1:10; 1 Pet. 3:8; Isa. 52:8). {ABN5: 55.3}

Na kama wale ambao huchagua kujihusisha na ufasiri apendavyo mtu fulani tu wanaombwa kwa heshima kuacha kufundisha kwa jina la Fimbo na kwa gharama yake. Wao kama watu waaminifu, wafundishe kwa majina yao wenyewe na kwa gharama yao wenyewe. {ABN5: 56.1}

JINSI YA KUTHIBITISHA KWAMBA MCHINJO NI HALISI?

Swali Namba 134:

Nawezaje kuthibitisha kwa Mwaadventista wa Sabato kwamba mchinjo wa Ezekieli 9 ni halisi? {ABN5: 56.2}

Jibu:

Kwanza vuta umakini wake kwa ukweli kwamba Bwana Mwenyewe alikuwa kwenye kizingiti cha nyumba ya kidunia wakati mchinjo ulikuwa ukifanyika ndani yake. Jifunze kwa makini Trakti Namba 1, Viunganishi vya Biblia, ikishughulikia tukio hilo jinsi alivyoliona nabii, na apate ukweli huu pamoja na zinazohusiana zikazwe kikiki akilini. {ABN5: 56.3}

Pili, mfahamishe Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211, ambao husema: “Hapa tunaona ya kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi adhabu ya ghadhabu ya Mungu.” {ABN5: 56.4}

56

Kisha kuijongea mada hiyo kutoka pembe nyingine, ingiza ushahidi wa Roho ya Unabii ambao hufichua kwamba wakati ujumbe wa Ezekieli 9 utatangazwa kwa kanisa, wengine watakanusha utimizo wake halisi, wakisema: “Yeye ni mwenye huruma sana kuwajilia watu Wake kwa hukumu.” — Kimenukuliwa. Na kwa sababu hiyo limeandikwa tamko la kusikitisha: “Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama katika siku za zamani. Nyakati zimebadilika.” — Kimenukuliwa. Kusema kwamba mchinjo wa Ezekieli 9 si halisi, ni kusema, “Kanisa halitahisi kamwe adhabu ya Mungu. Hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama katika siku za zamani.” Wale wanaosema haya, wamehukumiwa kwa kukataa onyo dhahiri la mchinjo halisi, wa kimiujiza, ulioelezwa na Ezekieli. {ABN5: 57.1}

Tatu, kutoka Isaya 66:16, 19, 20 huonyesha kwamba mchinjo uliotajwa katika aya ya 16 utakuwa halisi, kwa maana wale watakaookoka watatumwa kihalisi kwa mataifa yote, kutangaza utukufu Wake na sifa Yake. Isitoshe, kwamba mchinjo huu halisi u kanisani pekee, unaonekana kutoka kwa ukweli kwamba wale ambao “wataokoka” ni watumwa wa Mungu ambao baadaye Yeye anawatuma kwa Mataifa. Iwapo, hata hivyo, mchinjo si halisi, basi utakuwa kwa kusudi gani, na wao “wataokoka” kutoka kwa nini? Ezekieli aliwaona wakiuawa kihalisi (Ezek. 9:8). {ABN5: 57.2}

57

JE! KARAMA ZOTE ZIKO KATI YETU SASA?

Swali Namba 135:

Kutoka kwa mafundisho ya Ndugu ________ ya kwamba karama ya uponyaji bado haijakuwa kati yetu, lakini itarejeshwa baada ya utakaso wa kanisa, je! tunapaswa kuelewa pia kwamba zawadi ya walimu bado haijarejeshwa? Iwapo hili haliwezi kudokeza, basi je, walimu wa “Fimbo ya Mchungaji” wana hiyo zawadi sasa? {ABN5: 58.1}

Jibu:

“Kristo ni yule yule tabibu mwenye huruma sasa,” inatangaza Roho ya Unabii, “ambaye Alikuwa wakati wa ukasisi Wake wa duniani. Ndani Yake kuna uponyaji kwa kila ugonjwa, akirejesha nguvu kwa kila udhaifu. Wanafunzi Wake katika wakati huu wanapaswa kuwaombea wagonjwa jinsi wanafunzi wa zamani walivyoomba. Na uponyaji utafuata, kwa maana ‘sala ya imani itawaokoa wagonjwa.’” — Utumishi wa Uponyaji, uk. 226. {ABN5: 58.2}

Ndugu ______ hakukusudia kuwasilisha hisia kwamba hakuna karama ya uponyaji kati ya watu wa Mungu sasa, ila tu kwamba miujiza mikubwa ya uponyaji, ambayo ile iliyotendwa katika wakati wa kanisa la Kikristo la kwanza ilikuwa kivuli, bado ni ya baadaye. {ABN5: 58.3}

Mintarafu zawadi ya walimu, tunasoma: “Na ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida na maji ya msiba, lakini walimu wako hawatafichwa tena, ila macho yako yatawaona walimu wako.” Isa. 30:20. {ABN5: 58.4}

58

Wakati kanisa limetakaswa, walimu wake watauwa wapokeaji nguvu kubwa ya Pentekoste kuliko hata wanafunzi 120. Hili linaonekana wazi kutoka kwa unabii wa Yoeli wa mvua ya masika, ambayo inakuja kama mwalimu wa haki (Yoeli 2:23 pambizo), na ambayo inawekeza ndani ya wapokeaji wake nguvu (Yoeli 2:28) mwishowe kutangaza haki ulimwenguni kote. (Tazama pia Maandishi ya Awali, uk. 277, 278). {ABN5: 59.1}

MTU MWENYE BUSARA ATAFANYA NINI?

Swali Namba 136:

Je! Ni nini mtu anapaswa kufanya sasa wakati pesa hazipatikani kwa urahisi, lakini wakati bei zimepanda juu sana? Je! Kwa hivyo atumie kila kitu anachopata, au ajinyime ubadhirifu kama huo na aweke akiba iwezekanavyo? Na ataweka wapi mapato yake?

Jibu:

Kutoka kwa uzoefu wa zamani, wenye busara wamejifunza isioepukwa sheria ya maisha ya mfumuko wa bei na mshuko wa kiuchumi. Wanajua kwamba kiwango kisicho cha kawaida cha fedha katika mzunguko hupanua mahitaji ya bidhaa zaidi ya vile ambavyo soko linaweza kusambaza, na kwa hivyo husababisha bei kupanda juu sana. Wao hutambua katika hii ishara ya onyo maafa ya kifedha ambayo yanakaribia. {ABN5: 59.3}

Wenye busara pia hujua kwamba karamu ya ushenzi ya kutumia fedha zote wanazotengeneza lazima hivi karibuni au baadaye imalizikie katika mapinduzi ya uhitaji, huzuni na majuto, — kuvunjika kwa nyumba nyingi. Kwa hivyo wenye busara huchukua hatua mapema ili kujikinga

59

dhidi ya siku isiyoweza kuepukika ya mlipuko wa kiuchumi. Katika wakati wa mfumko wa bei watakana vikali kichaa cha kukifanya anasa kiwango chao cha sasa cha maisha. Na katika wakati huu wa mzunguko wa pesa uliofumuka wataweka, akiba badala ya kutumia. Hawataanguka katika mwenendo huo wa kutojali unaofaa aina duni tu za maisha ya wanyama, — ya “karamu leo na njaa kesho”; wala hawatajiunga na wale ambao husema, “tule, tunywe na tufurahi [tuzitumie pesa zetu haraka kadiri tunavyozipata] maana kesho tutakufa.” {ABN5: 59.4}

Mtu yeyote anayepanda sasa mashua ya anasa kwenye safari yake ya msisimuko wa tafrija kwenye mkondo wa kijito cha upinzani mdogo, ni hakika kuwa atafyonzwa katika mvurugo wa kutosimamia fedha vyema. Amechelewa sana, atajikuta mwenyewe mhanga wa kukosa kulikokithiri kwa maono ya mpangilio wake — cheo cha kudhani. Mfano wa kiakili wa mtu kama huyo unaweza kulinganishwa tu na mruba asiye na hisia (mdudu mfyonza damu) — kiumbe hicho kidogo kijinga cha majini ambacho hujitesa chenyewe kwa njaa wakati hakuna chochote kifaacho kujibandika, kisha hujiua chenyewe kwa kula kupita kiasi wakati kitu mwishowe hukijia. Mtindo huu wa upotevu wa ni aina mbaya zaidi kwa sababu kwa hivyo hakuna “nyumba ya baba” ya kurejea ndani. {ABN5: 60.1}

Iwapo kigezo cha uzoefu kwamba historia hujirudia yenyewe kinapaswa kutambulika, basi kutoka katika vita hivi lazima kije kipindi cha mpito na kushuka kwacho kwa uchumi kusikoweza kuepukika. Dola sasa hupatikana kwa urahisi; na dola

60

iliyowekwa kwa akiba sasa inaweza kuwa na thamani ya dola mbili au tatu baada ya vita, wakati pesa zitakuwa hata adimu kuliko ambavyo zimewahi kuwa. Kwa hivyo sasa ni wakati wa kutumia chache iwezekanavyo na kuweka kando nyingi iwezekanavyo. Sasa ni wakati wa wingi wa kuchuma mavuno na kuyahifadhi hadi kwa wakati wa hitaji ambao uko mbele — sio kutumia kwa “kila kitu ambacho roho inatamani.” {ABN5: 60.2}

Zaidi ya matumizi yoyote muhimu na mapunguzo yanayoongezeka ambayo mtu anaweza kuwa nayo — Ushuru wa Mapato, Ushuru wa Ushindi, Hati Dhamana za Vita, Usalama wa Kijamii, zaka na sadaka — kila mpokea mshahara mwenye hekima kila juma ataweka kando kiasi fulani katika akiba, haijalishi ni kidogo, na kwa dhati aamue kutoruhusu chochote kumgeuza kutoka kwa mpango huu, na bila chochote kuufifisha mfuko huu. Hili, hata hivyo, mtu atapata shida sana kulitenda, kwa sababu ya majaribu ya matumizi, na kwa wafanya-biashara werevu ambao wametumia maisha yote kujifunza jinsi ya kutumia akiba ya mwenzake. Jumuiya kwa hivyo imeandaa Vyeti vya Wosia maalum ambavyo vitamhakikishia mmiliki akiba kwa “siku ya mvua,” au kumlinda dhidi ya janga la kifedha katika siku za ukongwe. {ABN5: 61.1}

Nyuki mwenye shughuli nyingi huhifadhi na kuweka akiba asali yake katika wakati wa miezi ya hari. Kisha msimu wa baridi unapokuja, hana tu ya kutosha kumwezesha kupitia kipindi kigumu lakini pia hata baadhi ya kusaza kwa mlinzi wake. Waamini wa Ukweli wa Sasa hawapaswi kuwa wapungufu wa hekima kuliko nyuki mdogo! Hebu Cheti cha

61

Wosia kiweze kuwa ukumbusho wako kwamba pale ambapo nondo hawawezi kuingia na wezi hawawezi kuvunja, ndio mahali salama kabisa pa kuweka hazina yako. Na machache ya maono kama hayo sasa yatafanya iwe rahisi sana isivyopimika kwa nyumba ya Baba wakati nyakati ngumu zitakapokuja, kwa sababu wakati huo unaweza kutoa kwa mfuko wako wa akiba kwa Cheti chako. Huenda ikawa haiwezekani wakati huo kwa Jumuiya kuwatumikia wale wote walio wahitaji; na wale ambao hawaweki riziki katika wakati huu mchache unaonekana kuwa wa ufanisi, wataweza kuhisi fedheha wakati huo. Bila shaka, hakuna isipokuwa wale ambao wanashikilia Cheti cha Ushirika wanaweza kuwekeza kwenye Cheti cha Wosia — kushiriki katika huu mtakatifu mfumo akiba na usalama wa kijamii uliowekwa wakfu. {ABN5: 61.2}

JE! INATOZWA USHURU?

Swali Namba 137:

Je! changu “Cheti cha Wosia” kinapaswa kutozwa ushuru? {ABN5: 62.1}

Jibu:

Cheti cha Wosia ambacho kimerudufiwa hapa, kinathibitisha wazi kwamba pesa zilizowekwa hivyo kwa Jumuiya Kuu ya Wadaudi Waadventista wa Sabato haziwakilishi arabuni iliyowekwa akiba, lakini wosia, kwa kuzingatia ule ambao Jumuiya hujifungia kwa hiari, kwa maana ya wajibu wa maadili, kuwasaidia washiriki wanaomiliki cheti angalau kwa kiwango wanachokitolea wosia na kuweka. Na arabuni hazitozwi ushuru. {ABN5: 62.2}

62

VIPI KUHUSU FADHILI ZA SERIKALI?

Swali Namba 138:

Je! Ni makosa kwa Mkristo kupokea udhamini kutoka kwa mashirika ya misaada ya serikali? {ABN5: 63.1}

63

Jibu:

Chini ya pensheni ya shirikisho na mipango ya maslahi ya jamii, fedha za serikali za uzeeni na misaada hupatikana kihalali tu kwa raia wake ambao ni washiriki wa kanisa na vile vile kwa raia wake ambao si washiriki wa kanisa. Kwa hivyo Mkristo kama raia anayo haki kamili kimaadili kupokea ufadhili kutoka kwa serikali yake zaidi ya kuwa kama mshiriki wa kanisa anayo haki kupokea ufadhili kutoka kwa kanisa lake. {ABN5: 64.1}

JE! MKRISTO ANAPASWA KUJIUNGA NA MIUNGANO YA WAFANYAKAZI?

Swali Namba 139:

Je! Msimamo wetuunapaswa kuwa upi kuhusu Vyama vya Wafanyakazi? {ABN5: 64.2}

Jibu:

Ingawa katika miaka ya kuundwa kwayo Miungano aidha haikutumia nguvu wala shinikizo ambazo hutumia sasa, lakini hata wakati huo watu walikuwa wakifanya kazi kwa bidii kuifanya iwe ilivyo sasa. Kwa hivyo kumlinda mwamini wa kweli asiafikiane na maamuzi yake na kwa hivyo kuhusika katika migomo na maandamano (sio kumzuia asilipe sehemu ya mshahara wake iwapo watamshurutisha), Shuhuda hukataza kushiriki kwake katika kuendeleza kusudi lao lisilo la Kikristo. (Tazama Shuhuda, Gombo la 7, uk. 84). {ABN5: 64.3}

Kwa kumtesa Yesu na wafuasi Wake, serikali za Kirumi na za Kiyahudi zilikuwa zikifanya jambo lisilo la haki kuliko hata Miungano inavyofanya leo kushinikiza

64

kufanya kazi katika mamlaka yao, lakini Yesu aliwaelekeza wafuasi Wake wakati huo walipe ushuru kwa Kaisari. Kwa hivyo lazima tuhitimishe kwamba iwapo mtu anahitajika kulipa ada wakati anafanya kazi katika kazi ambayo hairuhusu “duka lililo wazi,” kwa hivyo hana njia mbadala ya kukidhi hitaji hili kama mojawapo wa mahitaji ya duka, bila kujali kama Muungano ni shirika zuri au baya. Hivyo, ingawa ili kushikilia kazi yake kujidhamini mwenyewe na familia yake, anaweza kulipa ada ambayo Muungano hutoza kwa ajili ya fursa ya kufanya kazi, lakini hapaswi kushiriki katika shughuli na tamasha zao — kisiasa, kijamii, au vinginevyo. Kwa ufupi, hatakuwa na uhusiano wowote wa undugu nao. {ABN5: 64.4}

Katika hali kama hizi, hakuna tofauti yoyote katika kulipa matozo ya Muungano, ushuru wa serikali, au gharama nyingine muhimu, ada, au gharama ili kudumu kazini. Kwa mtazamo wa hili, wale wanaofuata katika nuru watalipa matozo ya Muungano tu kama inavyopaswa, na wataacha kuilipa haraka iwezekanavyo. {ABN5: 65.1}

JE! NI MAKOSA KUCHUKUA BIMA YA MALI?

Swali Namba 140:

“Shuhuda,” Gombo la 1, uk. 549-551, huzungumza dhidi ya bima. Je! humaanisha kujumuisha bima ya mali? {ABN5: 65.2}

Jibu:

Taarifa hiyo inayohojiwa inahusika tu na bima ya maisha. Kama tunavyojua hakuna

65

kizuio kwa mtu kuchukua bima ya mali, uamuzi lazima usalie na mtu mwenyewe. {ABN5: 65.3}

VIPI KUHUSU KUNUNUA HATI ZA DHAMANA YA ULINZI?

Swali Namba 141:

Je! Ama wafanyakazi wa Mlima Karmeli au taasisi yenyewe inanunua Hati Akiba za Dhamana za Ulinzi za Muungano wa Madola ya Amerika? {ABN5: 66.1}

Jibu:

Kama watendakazi katika taasisi ya kidini ya upendo inayofanya kazi kwa ushirika kwa ujira mdogo wa kujikimu wakazi hapa, kutoka wa chini hadi wa juu, kwa sababu hiyo hawana uwezo wa kununua chochote ila mahitaji muhimu ya maisha. Hakuna yeyote, kwa hivyo, aliye na uwezo wa kutosha kumwezesha kufanya uwekezaji wa aina yoyote wa kifedha. {ABN5: 66.2}

Taasisi yenyewe, ikiwa hasa shirika la ukarimu kwa jumla, liko katika hali kama hiyo. Likiwa chombo kisicho cha faida ambacho kupitia kwacho washirika wake hufanya kazi yao iliyowekwa kwa kuchangia kwacho kutoka kwa mapato yao, ili kiweze kulisha, kuwapa makao, na kuwavika watendakazi wake, kuchapisha vitabu vya dini, na kuvisambaza bila malipo kote ulimwenguni, vile vile hakina fedha zake. Kwa hivyo hakiwezi kimaadili, hata iwapo kingaliweza kifedha, kufanya uwekezaji wowote ambao haujawekwa kwa kusudi hili kikatiba, hata kama uwekezaji huo wenyewe ungaliweza kuwa wa kupendeza. {ABN5: 66.3}

66

Hata hivyo, taasisi hiyo katika kufanya kazi yake ya kawaida kwa manufaa ya wengine, si kwa faida yake, inanunua mamia ya dola za stempu za posta kila mwezi. Hivyo, ingawa haiko katika nafasi ya kusaidia moja kwa moja (kupitia ununuzi wa Hati Akiba za Dhamana za Ulinzi za Muungano wa Madola ya Amerika) katika mpango wa ulinzi, inafanya sehemu yake moja kwa moja (kupitia ununuzi wa stempu za posta za Muungano wa Madola ya Amerika), pesa zake zinaenda tu kwenye sehemu nyingine ya kasha la taifa lile lile, ambalo kutoka kwalo halipokei, bila shaka, riba au akiba. {ABN5: 67.1}

KUSALIMU AU LA?

Swali Namba 142:

Je! Ni makosa kusalimu bendera? {ABN5: 67.2}

Jibu:

“Mlipeni…Kaisari yaliyo ya Kaisari,” “…wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote.” Mat. 22:21; Rumi. 13:7, 8. {ABN5: 67.3}

Wakati “mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu ya kumshtaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; … wala halikuonekana kosa au hatia ndani yake.” Dan. 6:4. Walipokosa kumpata na hatia, maadui zake “walifanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini” isipokuwa kwa mfalme, “atatupwa katika tundu la simba.” Aya ya 7. Kwa

67

kupata saini ya mfalme juu ya amri hiyo, walitaka kusababisha hali ambayo lazima imhusishe Danieli katika tendo la uasi dhidi ya mfalme wake. Walijua kwamba ingawa alikuwa na kusudi la kumtii mfalme kwa bidii, hangaliweza kufanya hivyo kwa gharama ya kutoonyesha utiifu kwa Mungu wake. Danieli kwa hivyo, aliendelea kumwomba Mungu wake kama kawaida, na tokeo kwamba alitupwa katika tundu la simba. Lakini Yule Ambaye aliomba Kwake aliokoa maisha yake kutoka kwa hayawani wenye njaa. {ABN5: 67.4}

Kisha kuna kisa mashuhuri cha Yusufu ambaye kwa uaminifu wake imara kwa serikali ya Misri, aliinuliwa kwa nafasi ya kushiriki kiti cha enzi na Farao. {ABN5: 68.1}

Kutoka kwa haya na matukio mengine ya Biblia, tunagundua kwamba uaminifu wa kila mtu kwa serikali yake ni ahadi yake ya kweli ya utiifu kwayo — salamu kwa bendera yake. {ABN5: 68.2}

Kwa ujumla, kwa hivyo, tunaona kwamba wakati kwa upande mmoja mtu kutokuwa mwaminifu kwa Mungu ni dhambi dhidi Yake, kwa upande mwingine kutokuwa mwaminifu kwa serikali yake ni dhambi dhidi yake, na isivyo moja kwa moja kwa Mungu pia: maana kutokuwa mwaminifu kwa serikali ya mmoja ni kutotii amri iliyo wazi ya Bwana: “Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii mahakimu, na kuwa tayari kwa kila kazi njema.” Tito 3:1. “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa

68

naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. “1 Pet. 2:13, 14. “Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.” Rumi 13:1, 2. {ABN5: 68.3}

Kwa sababu bendera sio sanamu au hirizi ila nembo, kiwango, hivyo kuiheshimu sio ibada ya sanamu, kama wengine wanavyofikiri, ila badala yake kukiri hadharani uaminifu wa mtu kwa serikali ya taifa lake, kama vile tu ubatizo ni ungamo la mtu la uaminifu kwa serikali ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu {ABN5: 69.1}

Kwa amri ya Mungu, Waisraeli walitengeneza viwango (bendera) kulingana na makabila yao, kwa madhumuni ya utambulisho na alama ya uaminifu wao kwa kile ambacho bendera ilisimamia. (Tazama Hesabu 2). {ABN5: 69.2}

Dhahiri, basi, kusema kwamba ni ibada ya sanamu mtu kuiheshimu bendera ya taifa lake, itakuwa ni kumshtaki Mungu kulazimisha ibada ya sanamu si kwa watu Wake wa kale ila, kwa mfano wao, pia kwa waaminifu wa wakati wote tangu hapo! {ABN5: 69.3}

Hivyo kila Mkristo ambaye angeweza kuzitii amri za Mungu, lazima awe mwaminifu kwa nchi ambamo anaishi. Kwa hivyo kama Wakristo ndani ya Marekani, waliojitolea kwa Mungu, na hivyo waaminifu kwa kanuni za haki za hii huru “serikali chini ya Mungu,” tunatoa mioyo yetu, mawazo yetu,

69

mikono yetu, vyetu vyote, kwanza kwa bendera ya Ufalme wa milele wa Mungu, na kwa Serikali inayoongozwa na Mungu ambayo husimamia watu wamoja wa mataifa yote, na waliofungwa kwa kamba za upendo wa milele, uhuru, usafi, haki, amani, furaha, nuru na maisha kwa wote; na pili “tunaahidi utiifu kwa bendera ya Muungano wa Madola ya Amerika, na kwa Jamhuri ambayo husimamia, Taifa moja, lisilogawanyika, na uhuru na haki kwa wote.” Na kwa sababu ya Utukufu wa Kale unaokunjuka wenyewe kama nembo ya kanuni safi za Katiba ya nchi hii ya watu huru kwa muda mrefu ni ahadi yetu ya utiifu kwayo jambo lisilokiukwa. {ABN5: 69.4}

JE! UZALENDO NI UKRISTO?

Swali Namba 143:

Je! Katika vita hivi tunapaswa kuchukua msimamo wa mkataaji kidhamira au ule wa wazalendo? {ABN5: 70.1}

Jibu:

Mtu yeyote anayechukua msimamo mwingine wowote kuliko ule wa uzalendo hawezi kuwa raia wa kweli wa nchi yake. Mkristo, hata hivyo, lazima daima akumbuke kwamba yuko chini ya serikali mbili, — ya kiroho na ya muda, — na kwa hivyo analazimika kuzihudumia zote mbili, ingawa zaweza kuwapo nyakati ambapo hali zinaweza kutokea kumzuia asizipatie zote mbili kwa usawa “kipimo kamili cha unyenyekevu.” Lakini siku zote atatenda yote awezayo kuzitumikia zote. {ABN5: 70.2}

Biblia hufundisha wazi, na historia mara zisizohesabika imetangaza, kwamba mtu kupuuza maagizo ya Mungu ni hatari

70

kwake mwenyewe na kwa taifa lake. Ukweli huu wa kuhuzunisha, umetekelezwa hivyo bila kikomo katika mvingirisho wa karne nyingi, sio tu kati ya taifa teule la Israeli, lakini pia kati ya mataifa yote ya dunia “kutuonya sisi tuliofikiliwa na mwisho wa dunia.” {ABN5: 70.3}

Kwa hivyo uasi wa mtu kwa amri za Mungu lazima ufanye madhara kwa taifa lake na vile vile kwake mwenyewe, Mkristo hubeba jukumu maradufu la kufanya yote katika uwezo wake kulinda maslahi na kukuza mafanikio ya falme zote mbili wa kiroho na wa muda na kuhakikisha kwamba anajiondolea hatia kabisa juu ya hili zito jukumu maradufu, yeye atatii kabisa amri ya Bwana: “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu.” Marko 12:17. “Nami,” asema Bwana katika ahadi kwa watiifu, “Nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye Nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa.” Mwa. 12:3. {ABN5: 71.1}

Israeli ya kale kama taifa na serikali walilazimika kulinda mali, watu, na familia zao — hata kwa upanga. Lakini hawakupaswa kufanya vita na ndugu zao wenyewe. Wakati ufalme wa makabila kumi, Israeli, uliungana na Shamu kupigana na ufalme wa makabila mawili, Yuda, laana ya Mungu ikatua juu ya Shamu na Israeli, na kila mmoja kwa sababu

71

hiyo ulivunjwa na mfalme wa Ashuru. (Tazama Isaya 7:1-8; 8:4). {ABN5: 71.2}

Lakini wakati waliteswa kwa sababu ya injili, Wakristo waliamriwa wasilipize kisasi: “Lakini Mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.” {ABN5: 72.1}

“ Mmesikia kwamba imenenwa, umpende jirani yako, na, umchukie adui yako; lakini Mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana Yeye huwaangazia jua Lake waovu na wema, Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. “ Mat. 5:39-45. {ABN5: 72.2}

Nuru ambayo inaangaza kutoka kwa Agano la Kale na Jipya, huonyesha kwamba Mkristo, kama raia mwaminifu, katika wakati wa vita atatumika kulinda nchi yake; lakini iwapo vita vitahusisha Wakristo kwa pande zote, jinsi ambavyo vita hufanya leo, yeye, kama raia wa Ufalme wa Kristo, hawezi kwa dhamira kushiriki kuwapiga marisasi raia wenza wa Ufalme huo. Maana “ikiwa ufalme umegawanyika juu yake wenyewe, ufalme

72

huo hauwezi kusimama. Na ikiwa nyumba imegawanyika juu yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.” Marko 3:24, 25. {ABN5: 72.3}

Lakini ingawa katika vita kama hivyo, Wakristo hawapaswi kuchukua silaha ili kuuana, wanafungwa kimaadili kufanya kazi ya kibinadamu kama ile iliyofanywa na Msamaria mwema — kuwahudumia wagonjwa, waliojeruhiwa, na wanaokufa, bila kujali utaifa wao. {ABN5: 73.1}

PIGA KURA KWA AU DHIDI YA MALIPO YA PENSHENI?

Swali Namba 144:

Tafadhali unaweza kuelezea msimamo wako kuhusiana na maswala ya pensheni ambayo sasa yanawasilishwa kwa umma? Je! Unafikiri yanastahili tuyapigie kura? {ABN5: 73.2}

Jibu:

Tumeonywa kwamba kazi ya Mungu “inapaswa kushughulisha akili yote, umakini wote” — Maandishi ya Awali, uk. 118. Hivyo, kwa vile hatuwezi kwa busara kutenga wakati wa kutosha kusoma maswala haya ya kisiasa na kiuchumi na matokeo yake ya mwisho, kutoa uamuzi kwa busara juu yake, hatuwezi kwa makini kupiga kura ama kwa au dhidi yake. Kwa maana upigaji kura wetu usio na ufahamu unaweza kufanya taabu na hasara kwa wengine, ilhali kuwaongoza wengine kwenye njia za kutofanya kazi na ulafi. “Tazama,” asema Bwana “uovu wa umbu lako Sodoma ulikuwa huu, kiburi na kushiba chakula, na uvivu mwingi.” Ezek. 16:49. {ABN5: 73.3}

Katika dunia ya leo, maslahi yake ya kisiasa na kidini hutekelezwa vyema

73

zaidi na wataalamu. Wale tu ambao mioyo na akili zao zote ziko katika mambo ya maisha ya muda, ambao wanaweza kutumia wakati wa kutosha kusoma juu ya maswala ya kiuchumi na kisiasa ya ulimwengu, ndio waliohitimu kushiriki katika maswala kama haya. Wale ambao katika mioyo na nafsi wamejitolea kwa mahitaji ya kiroho ya ulimwengu, ambayo ni ya milele na ya umuhimu mkubwa kuliko mahangaiko ya maisha ya muda ambayo hivi karibuni yataangamia na kusahaulika, hawawezi tena kuutumikia ulimwengu kwa mahitaji yake ya kiuchumi na kisiasa kuliko wanavyoweza wale ambao mioyo na akili zao zimezama katika mambo ya muda, kutumikia mahitaji ya kiroho ya ulimwengu. {ABN5: 73.4}

“Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana! Lakini Yeye naye ana akili, Naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno Yake; bali atainuka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu. Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi wao ni nyama wala si roho; na Bwana atakaponyosha mkono Wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wote pamoja watakoma.” Isa. 31:1-3. “Mwenye haki atamfurahia Bwana, na kumkimbilia; na wote wenye moyo wa adili watajisifu.” Zab. 64:10. {ABN5: 74.1}

74

“Wakati huo mtu atawajibu vipi wajumbe wa taifa? Ya kuwa Bwana ameiweka misingi ya Zayuni, na maskini wa watu Wake wataona kimbilio.” Isa. 14:32. {ABN5: 75.1}

JE! KUPIGA KURA NI SAWA KWA MKRISTO?

Swali Namba 145:

Je! Ni sawa kupiga kura? {ABN5: 75.2}

Jibu:

Kwa kuwa kikatiba ni mojawapo ya haki isiyoweza kutengwa ya watu walio huru, hayawezi kuwapo makosa yoyote kuitekeleza iwapo kwa kufanya hivyo sheria au ofisi za nchi zaweza kutumika vyema. Kupiga kura hata hivyo, ambako kunaweza kutimiza mwisho kama huo, huhitaji kusoma kwa uangalifu; kushindwa hilo, kura ya mtu inaweza kuwa kubahatisha tu kwa upumbavu, na kwa hivyo kuwa mbaya badala ya kufaa kwa serikali nzuri. {ABN5: 75.3}

Wale, kwa hivyo, ambao hawako katika nafasi kutumia wakati na kusoma kwa hitaji la kujifahamisha juu ya maswala ya kisiasa vya kutosha ili kuwastahilisha kupiga kura kwayo kwa busara, hawawezi kupiga kura kama hiyo kwa umakini. {ABN5: 75.4}

Tukiwa wachungaji wa injili, wakati wetu ukiwa wa shughuli nyingi kabisa kwa masilahi ya kiroho ya watu, sisi wenyewe hatuwezi kushughulikia masilahi yao ya kisiasa pia, jinsi tu wawakilishi wa kisiasa wa watu hawawezi kutoa uangalifu unaofaa kwa mahitaji yao ya kiroho pia. Na kwa hivyo nadra, kama inawezekana, tunaona njia yetu wazi kupiga kura. {ABN5: 75.5}

75

VIPI KUHUSU KUTUMIA MAZIWA NA MAYAI?

Swali Namba 146:

Kwa sababu magonjwa kati ya ng’ombe na ndege wanaofugwa yanazidi kuongezeka, makali sana, na ya kuenea kote, je! hatupaswi kuacha kutumia maziwa na mayai katika lishe yetu? {ABN5: 76.1}

Jibu:

Iwapo ipo tauni kati ya ng’ombe na ndege katika mkoa wako au eneo lako, basi lazima utekeleze uangalifu mkubwa wakati unatumia maziwa na mayai, na unapaswa kufanya kazi ya kubadilisha, haraka iwezekanavyo, na vyakula mbadala vinavyofaa. {ABN5: 76.2}

Kwa sasa hatuna maarifa ambayo yanaweza kulazimisha au kuhalalisha taifa lote kutotumia bidhaa kama hizo za kuku na za maziwa, na haswa zaidi iwapo hakuna chakula mbadala kinachopatikana na ikiwa Bwana hajafungua njia ya kuandaa hivyo. Hata hivyo, sisi sote tunapaswa kutafuta kwa bidii kitu bora ili kwamba wakati hali zitakapopevuka kufanya matumizi ya kwendelea kutumia bidhaa hizi kutokuwa salama, hatutapatwa bila chakula mbadala cha kuridhisha. {ABN5: 76.3}

“Ruhusu matengenezo ya lishe yawe endelevu. Hebu watu wafunzwe jinsi ya kuandaa chakula bila kutumia maziwa au siagi. Waambie kwamba wakati utakuja ambapo hautakuwapo usalama katika kutumia mayai, maziwa, krimu au siagi kwa sababu ugonjwa katika wanyama unaongezeka kwa ulinganifu wa uovu kati ya wanadamu. Wakati umekaribia ambapo, kwa sababu ya uovu wa jamii ya wanadamu iliyoanguka, uumbaji wote wa wanyama

76

utaugua chini ya magonjwa ambayo hulaani dunia yetu.” — Shuhuda, Gombo la 7, uk. n135. {ABN5: 76.4}

“Wakati utafika ambapo tutalazimika kuacha baadhi ya bidhaa za lishe tunazotumia sasa, kama maziwa na krimu na mayai; lakini sio lazima kujiletea mfadhaiko kwa vikwazo vya mapema na vya kupita kiasi. Subiri hadi hali itakapodai, na Bwana kuandaa njia yake. {ABN5: 77.1}

* * *

“… Nimeagizwa niwaambie wale chakula ambacho kinaboresha afya zaidi. Siwezi kuwaambia: ‘Lazima msile mayai, au maziwa, au krimu. Lazima msitumie siagi katika matayarisho ya chakula.’ Injili lazima ihubiriwe kwa maskini, lakini wakati bado haujafika ili kuagiza lishe halisi zaidi.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 162, 163. {ABN5: 77.2}

JE! TUNAPASWA KUFUGA NG’OMBE NA NYUNI?

Swali Namba 147:

Je! Inaruhusiwa kufuga ng’ombe na kuku? {ABN5: 77.3}

Jibu:

Iwapo maziwa na mayai bado hujumuisha sehemu ya lishe yetu basi ni bora, ikiwezekana, kuzipata bidha hizo kutoka kwa ng’ombe na kuku wetu. {ABN5: 77.4}

Wale wanaopinga ufugaji wa ng’ombe na kuku, kwa misingi kwamba Roho ya Unabii hukataa, wanachukua msimamo uliojengwa kwa mafafanuzi yaliyokithiri kwa yale yaliyoandikwa. {ABN5: 77.5}

77

Tangu wakati dhehebu la Waadventista wa Sabato lilipangwa ki-usimamizi, hadi sasa, taasisi zake vile vile na washiriki wake wamefuga ng’ombe na nyuni. Kama yangalikuwa makosa kufanya hivyo, Roho ya Unabii ingalikuwa imewapa watu maagizo waziwazi. Kwa sababu, hata hivyo, hakuna kumbukumbu kama hiyo iliyochapishwa, wale ambao huendeleza maoni kama hayo kupita kiasi wanapotosha Roho ya Unabii na kuunga mkono maoni yao wenyewe ya mapinduzi. {ABN5: 78.1}

Dumu “katikati ya njia,” na usiwaruhusu watu wenye msimamo kupita kiasi wakuongoze upande mmoja au mwingine. {ABN5: 78.2}

Tunapaswa kujifunza kuheshimu maandishi ya wengine aidha kusoma ndani yake yale ambayo hayamo au kuacha nje ya yaliyomo yale ambayo mwandishi hajawahi kamwe kukusudia au kuidhinisha. {ABN5: 78.3}

JE! KUNA MAKOSA GANI KULA NYAMA SAFI?

Swali Namba 148:

Katika nuru ya Mat. 15:11 na maandiko mengine, je! si wazi kwamba mfumo ulaji wa mboga ni wa mwanadamu na si wa Mungu? {ABN5: 78.4}

Jibu:

Iwapo maandiko yaliyotajwa yalijumuisha Biblia yote ilivyoishughulikia mada hiyo, basi jibu thabiti la mkazo kwa swali laweza kuhitajika. Lakini hapo mwanzo “Mungu akasema, tazama, Nimewapa kila mche utoao

78

mbegu; ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu.” Mwa. 1:29. Hivi vyote na hapana kingine chochote vingalikuwa “chakula” cha wanadamu. {ABN5: 78.5}

Kwa hivyo hapo mwanzo, lishe ya mwanadamu haikujumuisha chakula cha nyama. Sio mpaka baada ya gharika, wakati kila kitu cha kijani kwa nchi kilikuwa kimeharibiwa, ndipo aliruhusiwa kula nyama. Kisha Mungu akasema: “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani kadhalika nawapeni hivi vyote.” Mwa. 9:3. {ABN5: 79.1}

Baadaye, hata hivyo, wakati wana wa Israeli walikuwa jangwani, Mungu aliwapatia mana. Lakini waliponung’unika dhidi yake, na kuamini kwamba tukio lake lilikuwa kwa hali za kawaida tu, wakidai kwamba ilikuwa haiwezekani kupata vyakula vya nyama jangwani, Yeye kwa makusudi na kwa hasira akawarundikia kware. Kwa gharama gani, hata hivyo! maelfu walikufa ili kutoa funzo kwamba mana haikuwa tu tukio la hali ya kawaida ila badala yake Majaliwa ya kusudi. Kwa maana “hapo nyama ilipokuwa ingali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira ya Bwana ikawaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno.” Hes. 11:33. {ABN5: 79.2}

Kwa sababu vuguvugu la Kutoka lilikuwa la kuwafanya watu wafae kuitwaa nchi ya ahadi na kuusimamisha ufalme wakati huo, jinsi tulivyo sasa, waliagizwa kujiepusha na vyakula vyote vya nyama. Na kwa sababu Yohana Mbatizaji alitangaza ujumbe muhimu katika siku yake (“Tubuni:

79

kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia” — Mat. 3:2) sawa na wetu leo, chakula chake kilikuwa asali na tunda la mti wa nzige. Kwa hivyo, ni muhimu zaidi kama nini, wakati huo, jinsi mifano yetu hufundisha, kwamba sisi ambao tuna ujumbe wa kilele cha injili, na ambao ni watangulizi wa majeshi ya ufalme wa milele, tusiyatie unajisi mahekalu ya nafsi zetu kwa bidhaa ambazo mifano yetu walikatazwa kula. {ABN5: 79.3}

Isitoshe, kama vile Eliya wa Malaki 4:5 na Mathayo 17:11 atarejesha vitu vyote kabla ya siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana, basi lazima atarejesha mfumo ulaji mboga, lishe asili ya mwanadamu. Basi, si mwanadamu tu bali mnyama pia, watakuwa wala mboga kabisa, na wote wataungana tena katika ushirika mpya wa amani ya Edeni. {ABN5: 80.1}

“Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima Wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.” Isa. 11:6-9. {ABN5: 80.2}

80

Bado zaidi, iwapo maneno, “sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani, ndicho kimtiacho mtu unajisi” (Mat. 15:11), yaeleweke kumaanisha kwamba haijalishi tunachokula au tunachokunywa, basi mbona hatupaswi kula nyama ya nguruwe, kunywa chai, kahawa, na hata pombe, na kuvuta sigara, — hakika, kula na kunywa chochote tunachotaka? {ABN5: 81.1}

JE! VIKOLEZI VYOTE NI HATARI KWA AFYA?

Swali Namba 149:

“Shuhuda” hushtumu utumiaji wa vikolezi, lakini hazitoi orodha bayana ya vile ambavyo huitwa havifai kwa matumizi ya binadamu. Je! Vikolezi vyote vinashtumiwa? {ABN5: 81.2}

Jibu:

Ukweli kwamba seji, vitunguu, kitimiri, mnanaa, vitunguu saumu, figili, na mboga zingine kama hizo sio tu zisizo hatari lakini kwa kweli za manufaa kwa mwili, huonyesha wazi kwamba sio kila kikolezi cha mimea chapaswa kuanishwa na viungo visivyofaa. {ABN5: 81.3}

Katika soko la kibiashara, hata hivyo, vitoweo vilivyokolezwa sana na vikolezi, ambavyo, kama ukweli unaojulikana, ni hatari katika matokeo yake kwa mwili. Jinsi tunavyoelewa, hivi ni vikolezi na viungo kama vile ambavyo Dada White hushtumu. {ABN5: 81.4}

Hatujui, hata hivyo, kwamba mdalasini, kungumanga, pimento, majani ya bay, biringanya, vanilla, pilipili kali (nyekundu), karafuu, na tangawizi, iwapo vinatumiwa kwa wastani, husheheni madini

81

ambayo ni hatari kwa afya. Kwa kweli, ugunduzi upo kwamba pilipili nyekundu, zilizokaushwa na kusagwa kuwa unga, hufanya kuzuio kizuri cha mafua. Na pia, vikolezo vilitumiwa katika utumishi wa dhabihu (Kut. 30:23-25, 34). {ABN5: 81.5}

Kwa hivyo, si vikolezi vyote ni vya madhara. Lakini hebu ieleweke kwamba kutumia vikolezi vyovyote kwa kiasi kingi ni hatari, kama ilivyo kwa kiasi kingi chochote. {ABN5: 82.1}

NINI HUMTAMBLISHA MTU KAMA MDAUDI MWADVENTISTA WA SABATO?

Swali Namba 150:

Kwa vile Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato haina ushirika rasmi ni thibitisho gani mtu anaweza kutoa kujitambulisha kama mshiriki wa shirika? Na anawezaje kubainisha muda ambao amekuwa nalo? {ABN5: 82.2}

Jibu:

Udhamini wa mtu kwa ulio mwafaka ujumbe wa Wadaudi, na kuishi kwa kanuni zake (ubatizo, utunzaji wa Sabato pamoja na amri zilizosalia kwa kumi, mfumo ulaji mboga, matengenezo ya mavazi kuepuka kabisa tumbaku na vinywaji vya kulevya, na zingine zote zilizo katika Roho ya Unabii), ni mashahidi wakweli wa ushirika wake, na vithibitisho halisi vinavyoonekana. Hivi ndivyo vithibitisho pekee vya kusadikisha kuhusu ustahiki wa mtu katika ushirika wa Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato. {ABN5: 82.3}

82

Kadiri ni kwa muda gani mtu amekuwa mshirika wa Jumuiya hutegemea ni kwa muda gani mtu amezijua na kuishi kwa mujibu wa kanuni hizi. {ABN5: 83.1}

Kwa wale wanaofanya maombi, Jumuiya itatuma hati tupu ya ombi la Ushirika. Iwapo mwombaji anashindwa kutii kikamilifu mahitaji yote ya ujumbe, basi kwa ombi lake lazima aambatishe taarifa inayoridhisha ya maelezo. Vinginevyo Cheti cha Ushirika hakiwezi kutolewa. {ABN5: 83.2}

JE! LAZIMA NIFIKIE UKAMILIFU KWANZA?

Swali Namba 151:

Ili kusaini ombi la “Cheti cha Ushirika,” lazima mtu awe amefikia ukamilifu? {ABN5: 83.3}

Jibu:

Mwombaji lazima aweze kuwa anajitahidi kuwa mshindi — kuwekwa huru kutoka kwa dhambi, kutenda Ukweli na kuendelea mbioni; akijitahidi asianguke bali akiazimia, endapo ataanguka, asimame tena na kukaza mwendo zaidi akiwa mwenye ari kuliko hapo awali ili kufikia lengo. Lazima awe na uwezo hivyo kwa kudhamiria kusaini ombi la ushirika. {ABN5: 83.4}

JE! LAZIMA UBATIZO UTANGULIE USHIRIKA?

Swali Namba 152:

Ingawa sijawahi kubatizwa, lakini naamini kabisa ujumbe wa nyongeza wa “Fimbo ya Mchungaji,” na sasa napenda kujua iwapo ninastahiki kuomba “Cheti cha Ushirika.” {ABN5: 83.5}

83

Jibu:

Ikiwa ndiyo hatua ya kwanza katika kukiri hadharani kwa Mkristo imani yake, ubatizo ni takwa la ushirika. Kwa hivyo kwanza tuma ombi la Ubatizo, na baadaye la cheti. {ABN5: 84.1}

JE! MTU NI MSHIRIKI BILA CHETI CHA USHIRIKA?

Swali Namba 153:

Je! Mtu anaweza kuwa mshiriki wa Jumuiya bila kushikilia “Cheti cha Ushirika?” {ABN5: 84.2}

Jibu:

Naam, mtu anaweza kuwa mshiriki bila kushikilia Cheti cha Ushirika. Lakini kuwa mshiriki aliyeidhinishwa, mwenye haki ya kufurahia kikamilifu manufaa yote ambayo Jumuiya humudu, lazima ashike cheti. {ABN5: 84.3}

NANI ANAWEZA KUSHIKILIA OFISI?

Swali Namba 154:

Je! Wadaudi ambao hawajashika “Cheti cha Ushirika” wanastahili kushikilia wadhifa? {ABN5: 84.4}

Jibu:

Maafisa wote wanaotumikia Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato, pamoja na wakazi wote wa Mlima Karmeli, wanapaswa kushika Cheti cha Ushirika. {ABN5: 84.5}

JE! NI MPANGO WA NANI KUNYAKUA FEDHA?

Swali Namba 155:

Iwapo wale tu ambao hulipa zaka ya pili wanahitimu “Cheti cha Ushirika,” basi je!

84

takwa kama hilo si mpango wa kunyakua pesa tu? {ABN5: 84.6}

Jibu:

Kama ni mmoja anayeweza lakini halipi zaka ya pili ili kupata Cheti cha Ushirika, kwa kweli atakuwa “mnyakuzi wa fedha,” kwa maana atakuwa akivuna mahali ambapo hakupanda — akivuna manufaa kutoka kwa mfuko ambao hakuchangia chochote kuujenga, na ambao alikuwa amekataa kuudhamini. Kwa maneno mengine, wakati anaweka kwa choyo zaka yake ya pili, atakuwa akipata manufaa ya mfuko wa Jumuiya wa zaka ya pili. {ABN5: 85.1}

VIPI KAMA SINA ZAKA ZA KULIPA?

Swali Namba 156:

Je! Mtu anaweza kushikilia “Cheti cha Ushirika” ikiwa hana zaka za kulipa? {ABN5: 85.2}

Jibu:

Naam, iwapo atastahiki vinginevyo. {ABN5: 85.3}

KUTOZA AU KUTOTOZA ZAKA?

Swali Namba 157:

Mume wangu si mwamini na hawezi kuruhusu kulipa kwangu zaka ya kwanza na ya pili kutoka kwa fedha zote ninazoshughulikia. Nifanye nini? {ABN5: 85.4}

Jibu:

Ingawa Bwana ameamuru mwanadamu kutoza zaka kwa faida yake yote, Yeye hatamfanya mwamini awajibike kutoza zaka kwa mapato ya mwenzi asiye mwamini anayepinga kutoa zaka. {ABN5: 85.5}

Yeye amemjalia kila mtu haki isiyoweza kupingwa ya uhuru wa kidini, na hakuna

85

mtu anaweza kwa haki kuichukua kutoka kwa mtu mwingine. Na maradufu ni isiyokiukwa katika familia. Wala mume au mke hawapaswi kuingilia zoezi la kidini la uchaguzi wa mwingine. {ABN5: 85.6}

Mke anayedumisha kwa uaminifu nyumba kwa ajili ya mume na kuitunza familia kwa uaminifu, hafanyi hivyo kama mjakazi au mtumwa: yeye ni mshirika “msaidizi” nyumbani. Na kwa hivyo kwa haki zote za maadili, mapato ya mume ni yake kwa nusu. Wote basi wako chini ya wajibu wa juu kabisa kimaadili kuheshimu haki ya kila mmoja katika suala la zaka. Kwa hivyo, ikiwa mume ataamua kutotoa zaka kwa nusu ya mapato yake ya familia, mke hana haki ya kuhitilafiana naye. {ABN5: 86.1}

JE! PATO DOGO HALITOZWI ZAKA?

Swali Namba 158:

Kwa vile pato langu ni dogo sana, je! mimi naepushwa kutoa zaka? {ABN5: 86.2}

Jibu:

Mungu alibuni mfumo wa ukarimu ili kuufanya uwe sawa kwa maskini na kwa matajiri, hakuna utozaji zaidi kwa senti kuliko kwa milioni. Na hatujui mamlaka yoyote ya Maandiko ya kuepusha kutoa kwa kipato chochote zaka, iwe ni kidogo. Wote, maskini vile vile na tajiri, wamepewa upendeleo wa kurudisha kwa Bwana yaliyo Yake. Wengi walio na mapato ya “senti” wanalipa zaka zote ya kwanza na ya pili, na kwa

86

kurudisha wanapokea baraka nono za ujazi. {ABN5: 86.3}

Kwa hivyo akili hulazimisha hitimisho kwamba iwapo mtu hajalazimika kupokea msaada wa hisani kwa kuongezea mapato yake (iwayo asili yake) kukidhi gharama zake za maisha, basi yeye kutolipa zaka ni kujipunja baraka tele zinazoambatana na uzingativu mwaminifu wa haki ya kifalme kuwa mmoja wa wasimamizi wa Mungu. {ABN5: 87.1}

JE! SESERE NI SANAMU?

Swali Namba 159:

Je! Sesere hazipaswi kutazamwa kama sanamu? Na je! niwaruhusu watoto wangu kucheza nazo? {ABN5: 87.2}

Jibu:

Ijapokuwa sesere hazipaswi kufananishwa na sanamu, na ingawa watu wazima hawawezi kuzifanya kuwa sanamu zao, bado ipo hatari kwamba wale wanaokua wanaweza kuzitumia sana. Hekima hushauri kwamba watoto wafunzwe kupata furaha kwa kufanya mambo madogo nyumbani, ili waweze kuwa wenye manufaa na msaada, badala ya kwamba wasaidiwe kukuza tabia ya kutumia wakati wao kucheza ili waweze kuwa na furaha. Watoto wanaolelewa kucheza hawawezi kuwa wajasiria mali, wala kwa kweli kuwa wenye furaha aidha. Wengi hucheza, kama dawa ya kulevya inayofanyiza uraibu, husababisha hamu inayoongezeka siku zote wakati athari zinapotoweka. Maadamu kama mtoto hashinikizi sesere au vichezeo, ni vyema usiviweke mbele yake. {ABN5: 87.3}

87

VIPI KUHUSU KUCHEZA MICHEZO?

Swali Namba 160:

Je! Ni makosa kwa Wadaudi kucheza karata, sataranji, drafti, tenisi, besiboli, na michezo mingine? {ABN5: 88.1}

Jibu:

“Uchezaji wa karata unapaswa kupigwa marufuku.” “Zipo tafrija, kama minenguo, kucheza karata, sataranji, drafti, n.k., ambazo hatuwezi kuidhinisha, kwa sababu Mbingu huzishtumu.” — Jumbe kwa Vijana, uk. 379, 392. {ABN5: 88.2}

“Taswira ya mambo ilionyeshwa mbele yangu ambayo wanafunzi walikuwa wanacheza michezo ya tenisi na kriketi. Kisha nikapewa maagizo kuhusu tabia ya tafrija hizi. Ziliwasilishwa kwangu kama aina ya ibada ya sanamu, kama sanamu za mataifa.” — Mashauri kwa Walimu, uk. 350. {ABN5: 88.3}

“Hisia ya umma ni kwamba kazi za sulubu ni za udhalilishaji, lakini watu wanaweza kujitahidi kadiri wanavyoweza kuchagua kriketi, besiboli, au kwenye mashindano ya masumbwi, bila kuzingatiwa kama ya udhalilishaji. Shetani hufurahishwa kuona wanadamu wakitumia nguvu zao za mwili na akili kwa kile kisichoelimisha, ambacho si muhimu, ambacho hakiwasaidii na kuwa baraka kwa wale wanaohitaji usaidizi wao. Wakati vijana wanakuwa wataalam katika michezo ambayo haina thamani kwao wenyewe au kwa wengine, Shetani anacheza mchezo wa maisha kwa nafsi zao, akichukua kutoka

88

kwao talanta ambazo Mungu amewapa, na badala yake kuweka tabia zake za uovu…. Anatafuta kushughulisha na kuvutia akili kabisa ili Mungu asipate nafasi katika fikira.” — Mashauri kwa Walimu, uk. 274, 275. {ABN5: 88.4}

YEYOTE ALIYEFUFULIWA KATI YA WATU 144,000?

Swali Namba 161:

Dada White aliambiwa kwamba watu 144,000 pekee ndio wanaoweza kuingia katika hekalu takatifu mbinguni. Kwa sababu, hata hivyo, yeye mwenyewe aliingia ndani (kwa maana anasema, “Mambo ya ajabu ambayo NALIONA huko” — “Maandishi ya Awali,” uk. 19), je! yeye si mmoja wa watu 144,000? {ABN5: 89.1}

Jibu:

Lazima tugundue kwamba Dada White aliingia hekaluni katika maono tu, si katika hali halisi. Watu 144,000 hawakuwa katika mwili hapo, na wala yeye. Alipelekwa huko katika maono bila sababu nyingine isipokuwa kutazama mambo humo, ili aweze kuyaeleza kwetu. Kwa hivyo lazima, bila shaka, ilibidi aingie ndani. Na kwa sababu yeye huthibitisha kwamba watu 144,000 ni “watakatifu walio hai” Maandishi ya Awali, uk. 15) na kwa sababu yeye mwenyewe alikufa, hawezi kuwa mmoja wao, ingawa anaweza kuwa mmoja pamoja nao. {ABN5: 89.2}

Ukweli huu umetolewa wazi katika njozi nyingine ambayo alipelekwa kwa sayari ambayo ilikuwa na miezi saba, pale “alimwona Henoko mzee mwema.” Mahali hapo palikuwa pazuri sana na tumaini lake kubwa la kupendezwa hivi kwamba akamsihi malaika amwache akae

89

huko. “Kisha malaika akasema, ‘Lazima urudi duniani na ikiwa u mwaminifu, wewe, pamoja na watu 144,000 mtakuwa na upendeleo wa kuzuru dunia zote na kutazama kazi za mikono ya Mungu.” — Maandishi ya Awali, uk. 40. {ABN5: 89.3}

Kwa hivyo, ingawa hatakuwa mmoja wao, yeye, kwa furaha, atakuwa pamoja nao. {ABN5: 90.1}

JE! WATU 144,000 NI WAYAHUDI KWA KUCHUKULIWA TU?

Swali Namba 162:

Kwa sababu “majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli” (Ufu. 21:12) yameandikwa kwenye malango kumi na mawili ya Yerusalemu Mpya, je! si lazima watu 144,000 wawe Wayahudi kwa kuchukuliwa tu? {ABN5: 90.2}

Jibu:

Bila ubaguzi, kuchukuliwa kumejaliwa Mataifa tu. Na hakuna popote katika Maandiko hupatikana hata chembe ya pendekezo kwamba watu 144,000 ni watu wa Mataifa. Kinyume chake Ufunuo 7:4-8 hueleza wazi wazi kwamba watu 144,000 wanafanyizwa na elfu kumi na mbili kutoka katika kila kabila la makabila ya “wana wa Israeli.” Kuchukuliwa hakujatajwa tu lakini hata hakujadokezwa. Na Mataifa, ikumbukwe, sio wa makabila kumi na mbili, bali wa mataifa mengi! {ABN5: 90.3}

Iwapo, hata hivyo, bado kuna ubishi kwamba watu 144,000 sio Waisraeli walio hai lakini ni wa Mataifa na kwa hivyo ni Wayahudi kwa kuchukuliwa tu, basi tafadhali tuambieni wao ni kina nani na wale wengine wa Mataifa watakaokombolewa

90

watachukuliwa kwa nani? Iwapo familia ya kweli ya Waisraeli haipo hata leo, basi kuchukuliwa hakuwezekani tena, kwa maana walio hai hawawezi kuchukuliwa kwa wafu! (Tazama Warumi 8, 9.) {ABN5: 90.4}

JE! “MLIMA MTAKATIFU” HUMAANISHA NINI?

Swali Namba 163:

Katika kushughulikia unabii mbalimbali, “Fimbo ya Mchungaji” kwa udumifu hutumia neno, “mlima mtakatifu,” kwa Yerusalemu, kanisa, ilhali hutumia neno, “mlima mtakatifu” wa uzuri (Dan. 11:45), kwa Mlima Sinai. Je! Ni sababu gani unayotoa kwa upotoshaji huu, kwa mfano, kutoka kwa kanuni? {ABN5: 91.1}

Jibu:

Kirai, “mlima mtakatifu wa uzuri,” hauwezi kumaanisha kanisa, kwa maana muktadha wa aya hiyo hauungi mkono dhana hiyo. Kinyume chake, huonyesha wazi kwamba Mfalme wa Kaskazini “atakimbia” kutoka “nchi ya uzuri,” Palestina, na “kupanda” maskani yake katika “mlima mtakatifu wa uzuri,” ilhali maandiko mengine huonyesha kwamba Bwana “atakuja” katika nchi takatifu, na kupanda maskani Yake katika Zayuni “mlima mtakatifu.” Zek. 1:16; 2:10-13; 8:3. Hivyo, kwa sababu maskani zote haziwezi kuwa katika sehemu moja, na kwa sababu ya Bwana itakuwa Yerusalemu, bila shaka, kwa hivyo, “mlima mtakatifu wa uzuri,” ambao Mfalme wa Kaskazini atapanda yake, lazima uwe kwingine. {ABN5: 91.2}

91

JINSI YA KUJISAJILI KATIKA TAASISI?

Swali Namba 164:

Ni nini kinachomfanya mtu kustahili kusajiliwa katika Taasisi ya Ulawi wa Wadaudi? Je! Ni sehemu gani ya matumizi ya mwanafunzi huko Mlima Karmeli ambayo zaka ya pili hutunza, na ni pesa ngapi taslimu lazima mtu alipe? {ABN5: 92.1}

Jibu:

Ni wale tu ambao hushikilia Cheti cha Ushirika cha Jumuiya, wanastahiki kusajiliwa katika Taasisi ya Ulawi wa Wadaudi. Na huhitajika kwamba msajiliwa aweke amana kwa Benki ya Palestina Ada ya Ustahiki ya $ 30. Ada hii itatunza chumba chake, malazi, na kufua nguo katika kipindi cha mwelekezo wake — miezi yake ya kwanza miwili tu. Iwapo atakuwa tayari amejizoesha awamu ya kazi za mikono katika mafunzo yake na, katika kipindi hiki cha miezi miwili ya mwelekezo, atapata ujira wa kutosha kulipia gharama hizi, wakati huo ada ya $ 30 inaweza kuwekwa kwa akaunti yake ya kutoa au kuweka akiba. {ABN5: 92.2}

Kwa kuongezea, anahitajika kuweka fedha za usafiri wa kurudi nyumbani, ili kwamba anapojikuta hafai kuingia katika utaratibu wa shule, au kwa sababu nyingine yoyote aamue kuondoka Mlima Karmeli, yeye na vile vile Taasisi watalindwa dhidi ya kukwama kwake bila pesa za kutosha kuondoka. {ABN5: 92.3}

Zaidi ya hilo, kwa muda wa vita, anahitajika kuleta kitanda chake (cha mtu mmoja), mizani ya kitanda, godoro, na malazi. {ABN5: 92.4}

92

Zaka ya pili hukidhi masomo yake, vitabu, na vifaa vingine, na kwa ujira wa mafunzo ya kazi za mikono anaolipwa zaidi ya ule Idara ambayo imemwajiri inaweza kumlipa — sehemu ambayo hasa hapati ujira kabisa. Kwa ufupi, kuanzia wakati anapowasili Mlima Karmeli, anahitajika kulipa tu kwa kile angelipia akiwa nyumbani — chumba cha malazi, kufua nguo, mavazi, na bidhaa zingine. {ABN5: 93.1}

(Wanaotaka kujisajili, wanaweza kuitisha hati tupu za maombi ya usajili.) {ABN5: 93.2}

KUSUBIRI HADI BAADA YA KUSAJILIWA, AU KUJIANDIKISHA KABLA?

Swali Namba 165:

Inampasa Mdaudi anayepanga kujiandikisha katika Taasisi ya Ulawi wa Wadaudi, na ambaye anakaribia umri wa Usajili kwa Utumishi wa Uteuzi, ajiandikishe baada ya kusajiliwa, au anapaswa kujiunga katika Taasisi kabla kusajiliwa, na kisha ajiandikishe akiwa katika Kituo cha Mlima Karmeli? {ABN5: 93.3}

Jibu:

Mdaudi yeyote ambaye ameitwa na Mungu kusomea ukasisi katika Taasisi ya Ulawi wa Wadaudi, Kituo cha Mlima Karmeli, lakini ambaye anakaribia umri wa Usajili kwa Utumishi wa Uteuzi, inampasa ikiwezekana ajiandikishe katika Taasisi kwa wakati ili asajiliwe kutokea Kituo cha Mlima Karmeli. {ABN5: 93.4}

Ikiwa, hata hivyo, tayari amejisajili kwa Utumishi wa Uteuzi, lakini anapanga kujiandikisha mara moja katika Taasisi hiyo, basi bila kujali kama amerudisha au la

93

Fomu namba 40 ya Utumishi wa Uteuzi kwa Bodi ya alikotoka, inampasa mara moja aombe Bodi hiyo kumhamisha hadi Kaunti ya McLennan, Texas, Bodi ya Mtaa Namba 4, kuwekwa katika kundi. {ABN5: 93.5}

Kushindwa kupata uhamisho huu kabla ya kusafiri kwenda kwa Kituo cha Mlima Karmeli, mtu anaweza kupata amechelewa sana kufanya hivyo anapowasili, na yawezekana asiweze kuzuia matokeo ya matatizo na yasiyoridhisha mara nyingi ambayo huambatana na kuwakilisha habari ya mtu kwa njia ya barua na Bodi yake ya Utumishi wa Uteuzi. {ABN5: 94.1}

Isitoshe, kwa kupuuza kuchukua hatua hizi, ni vigumu mtu kuweza kutarajia Bodi impatie kaawisho la Ukasisi. {ABN5: 94.2}

(Italiki zote ni zetu.)

======

HATUA YAKO ITAKAYOFUATA ITAKUWA NINI?

Sasa ikiwa umefurahia, umethamini, na kufaidika na safari hii ya maswali na majibu kupitia Kitabu Namba 5, na iwapo unatumaini kuendelea, basi tuma ombi kwa Kitabu Namba 6.* Kitatumwa kama utumishi wa Kikristo bila malipo au wajibu. {ABN5: 94.3}

*Mtoa Jibu Kitabu, Namba 6 hakikufanyiwa hatimiliki au kuchapishwa na Ndugu Houteff kabla ya kifo chake katika mwaka 1955; au kuchapishwa na kutumwa nje ya Kituo cha Mlima Karmeli baada ya kifo chake, kwa hivyo si sehemu ya vitabu halisi vya Fimbo ya Mchungaji vilivyochapishwa vinavyopatikana katika muundo uliochapishwa tena leo.

94

FAHARISI YA MAANDIKO

>