fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 01, 02

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 1, 2

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1954

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

JIBU LA BWANA KWA MWENYE KUULIZA MUNGU

MCHUNGAJI MMOJA KUYAFANYA YALE UMATI WA WACHUNGAJI WALISHINDWA KUTENDA

                                    

1

WAZO LA SALA

Mfano wa Yesu Katika Kufundisha

Tutasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” aya ya kwanza, ukurasa wa 21: {2TG1: 2.1}

“Tena, Kristo alikuwa na kweli za kuwasilisha ambazo watu walikuwa hawajajiandaa kuzipokea, au hata kuele-wa. Kwa sababu hii Yeye aliwafundisha pia kwa mifano. Kwa kuliunganisha fundisho Lake na matukio ya mai-sha, uzoefu, au maumbile, Alihifadhi usikivu wao na kuigusa mioyo yao. Baadaye, walipovitazama vitu vil-ivyoonyesha mafunzo Yake, waliyakumbuka maneno ya Mwalimu mtakatifu. Kwa akili ambazo zilikuwa wazi kwa Roho Mtakatifu, maana ya mafunzo ya Mwokozi ilifunuliwa zaidi na zaidi. Mafumbo yalikuwa wazi, na lile ambalo lilikuwa gumu kufahamu likawa dhahiri. Yesu alitafuta njia kwa kila moyo. Kwa kutumia aina mbali mbali za vielelezo, Yeye hakuwasilisha tu ukweli katika awamu zake tofauti, lakini aliwavutia wasikilizaji tofauti…. Hakuna ambao walimsikiliza Mwokozi wangaliweza kujihisi kwamba walipuuzwa au walisahaulika. Wanyenyekevu, wadhambi sugu, walisikia katika fundisho Lake sauti iliyozungumza nao kwa huruma na kwa upole.” {2TG1: 2.2}

Kwa sababu watu katika wakati wa Yesu walikuwa kama watu wa leo, wasio na hamu ya kujifunza Ukweli mpya, alitumia Maumbile kunasa umakini wao. Manabii waliongozwa kutumia mbinu iyo hiyo. Sisi, kwa hivyo, tunahitaji kuomba kwa ajili ya shauku inayowaka kuujua Ukweli wa Mungu wa leo. Tunahitaji kuomba kwamba tusije kuwa wa kujiamini, na kuridhika na mafanikio yetu katika Neno la Mungu; kwamba tuweke kando chuki zote na tuwe tayari kujifunza kutoka kwa “mnyenyekevu wa wanyenyekevu.” {2TG1: 2.3}

2

JIBU LA BWANA KWA MWENYE KUULIZA MUNGU

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 9, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu inapatikana katika Ezekieli ishirini. Sura hii, tutapata, inasheheni historia ya unabii ya Kanisa kutoka kwa wakati wa utumwa wake huko Misri hadi kwa wakati wa kutiwa mhuri kwa watu 144,000. {2TG1: 3.1}

Ezekieli 20: 1-8 — “Ikawa katika mwaka wa saba, mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, baadhi ya wazee wa Israeli walikuja ili kuuliza kwa Bwana, wakaketi mbele yangu. Neno la Bwana likanijia, kus-ema, Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja ku-niuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi. Je! Utawahukumu, mwanadamu, utawahukumu? Uwajulishe machukizo ya baba zao; uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile nilipochagua Israeli, na kuwainulia wazao wa nyumba ya Yakobo mkono wangu, na kujidhihirisha kwao katika nchi ya Misri, hapo nilipowainulia mkono wangu, nikisema, Mimi ni Bwana, Mungu wenu; katika siku ile naliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, ijaayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote; nikawaambia, Ki-la mtu kwenu na atupilie mbali machukizo ya macho yake, wala msijitie unajisi kwa vinyago vya Misri,

3

Mimi ni Bwana, Mungu wenu. Lakini waliniasi, wala hawakutaka kunisikiliza; hawakutupilia mbali kila mtu machukizo ya macho yake, wala hawakuviacha vinyago vya Misri; ndipo nikasema kwamba nitam-waga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao, katikati ya nchi ya Misri.”

Katika maandishi ya Musa hatuwezi kupata kumbukumbu kuhusu uaminifu wa wana wa Israeli katika nchi ya Misiri. Iwapo walikuwa wema au wabaya, Musa hasemi. Lakini hapa kupitia Ezekieli tunaambiwa walivyokuwa. Sio wote, unakumbuka, walikuwa watu wa kumcha Mungu. Andiko hili linaonyesha wazi kwamba hata wakati Mungu aliwaita waondoke nchi ya Misri, wengi hawakuwa waaminifu katika ibada yao kwa Mungu. {2TG1: 4.1}

Aya ya 9, 10 — “Lakini nalitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nalijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Mis-ri. Basi nikawatoa katika nchi ya Misri, nikawaleta nyikani.”

Sasa tumesoma kumbukumbu ya jeshi la Waebrania, — ya msimamo wao wa kiroho katika nchi ya Misri, na sababu ya Mungu kuwaleta kutoka Misri. Ijayo tutasoma kumbukumbu waliyoifanya nyikani. {2TG1: 4.2}

Aya ya 11-13 — “Nikawapa amri zangu, na kuwaonyesha hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda. Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye. Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda kati-ka amri zangu, wakazikataa hukumu zangu,

4

ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo ni-kasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize.”

Hapa tunaona matendo ya wazawa wa Yakobo hayakuwa ya kupongezwa nyikani kuliko walivyokuwa huko Misri. {2TG1: 5.1}

Aya ya 14- 28 — “Lakini nalitenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi machoni pa mataifa, ambao naliwatoa mbele ya macho yao. Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, ya kwamba sitawaingiza kati-ka nchi ile niliyokuwa nimewapa, ijaayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote; kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao. Walakini jicho langu likawahurumia nisiwaangamize kabisa, wala sikuwakomesha kabisa jangwani. Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda; zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu, wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi sabato zangu, ndipo nikasema, kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao jangwani. Lakini nali-uzuia mkono wangu, nikatenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao mbele ya macho yao naliwatoa. Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya mataifa,

5

na kuwatapanya katika nchi mbalimbali; kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao. Tena naliwapa amri zisizokuwa njema, na hukumu ambazo hawakuweza kuishi kwazo; nami nikawatia unajisi kwa matoleo yao wenyewe, kwa kuwa walipitisha motoni wote waliofungua tumbo; ili kuwafanya kuwa ukiwa, wakapate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wamekosa kosa juu yangu. Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifanya nukato la kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.”

Hawakuwa waaminifu huko Misri, nyikani, na katika nchi ya ahadi. Tutasoma sasa kuhusu matokeo. {2TG1: 6.1}

Aya ya 29-36 — “Ndipo nikawauliza, Nini maana yake mahali palipoinuka mnapopaendea? Basi, jina lake mahali pale ni Bama hata leo. Basi, uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mnajitia unajisi kwa kuzifuata njia za baba zenu? Mnakwenda kufanya uasherati kwa kuyafuata ma-chukizo yao? Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi. Na haya yote yaingiayo katika nia zenu hayatakuwa kamwe;

6

ikiwa mmesema, Sisi tutakuwa sawasawa na mataifa, sawasawa na jamaa za nchi nyingine, kutumikia mi-ti na mawe. Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika, nitakuwa mfalme juu yenu; nami nitawatoa katika ma-taifa, na kuwakusanya, na kuwatoa katika nchi mlizotawanyika ndani yake, kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika; nami nitawaingiza katika jangwa la mataifa, na huko ndiko nitakakoteta nanyi uso kwa uso. Kama nilivyoteta na baba zenu katika jangwa la Misri, ndivyo nitakavyoteta nanyi, asema Bwana MUNGU.”

Kwa upande mmoja tunaona sababu za kuliinua jeshi la Waebrania kutoka kwa watumwa wa Farao hadi kwa makuhani wa Mungu, manabii, na wafalme. Kwa upande mwingine tunaona kutapanywa kwao kote kote katika mataifa yote. Ijayo tunaona ahadi za Mungu za kuwakusanya kutoka katika nchi ambazo wametawanyika. Hili Yeye huahidi kulifanya kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyooshwa. {2TG1: 7.1}

Aya ya 37 — “Nami nitawapitisha chini ya fimbo, nami nitawaingiza katika mafungo ya agano.”

Aya hii imehusishwa kwa kiasi fulani na inahitaji kufafanuliwa kwa msaada wa andiko lingine. Hebu tufungue Mambo ya Walawi. {2TG1: 7.2}

“Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakati-fu kwa Bwana.” Law. 27:32. {2TG1: 7.3}

Kubainisha sehemu ya Bwana, zaka, wana-kondoo wa Bwana, mbuzi, au kondoo, walifanywa wapite chini ya fimbo. Kila wa kumi alichukuliwa na kutengwa kwa ajili ya Bwana. Taarifa ya Ezekieli ishirini, aya ya thelathini na saba, “nitawapitisha chini ya fimbo,” kwa hivyo,

7

inamaanisha kuwatenga wateule Wake haswa kutoka kwa umati, kutoka kati ya “magugu,” (Mat. 13:30) au kutoka kati ya “samaki wabaya” (Mat. 13:47, 48). Na baada ya kutengwa hivyo, wanahesabiwa. Hivyo inakuwa kwamba watu 144,000 (Ufu. 7: 3-8; 14: 1) ni kundi lililotengwa na kuhesabiwa. {2TG1: 7.4}

Sasa tunaona kwamba Ezekieli ishirini anasheheni historia ya kinabii kutoka wakati wa kukaa kwao huko Misri hadi kwa wakati wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000, na wa kuwakusanya watu. {2TG1: 8.1}

Wakati Mungu atasababisha watu Wake kupita chini ya fimbo, ndipo Yeye atawaleta kwenye kifungo cha “Agano alilofanya na Abrahamu, Na uapo wake kwa Isaka; Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele. Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa.” 1 Nya. 16: 16-18. {2TG1: 8.2}

Ahadi ambazo walishindwa kuzitambua, Bwana anawahakikishia kwamba sasa Yeye atawaruhusu watu Wake wawe nazo. {2TG1: 8.3}

Aya ya 38 — “Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

Hapa tunaambiwa wazi kwamba wateule tu Yeye atawaleta “katika mafungo ya agano.” Wao tu Yeye atawaleta katika nchi ya Israeli. Wadhambi (magugu, samaki wabaya au mbuzi) ambao sasa wako kati ya watu wa Mungu wataondolewa na hawatakuwapo tena. {2TG1: 8.4}

“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya,” asema Bwana, “lililotupwa baharini, likakusanya samaki

8

wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wa-baya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 13: 47-50. Utengo huu, Hukumu kwa Walio Hai, unakumbuka, unaleta mwisho wa dunia. {2TG1: 8.5}

Aya ya 39 — “Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Enendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago vyenu.”

Mungu sasa ameifanya wazi Yake “kazi safi” ambayo Yeye ataifanya, kwa wote waliotubu na kwa ambao ha-wakutubu. Sasa ni juu yao kuamua iwapo watamtumikia Yeye au kuzitumikia sanamu zao — sasa hawaufanyi uamuzi wao bila kujua. Ikiwa wanataka kuangamia waweze kuendelea kuzitumikia sanamu zao. {2TG1: 9.1}

Aya ya 40, 41 — “Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nita-watakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote. Nitawatakabali kama harufu ipendezayo, nitakapowatoa katika mataifa, na ku-wakusanya toka nchi zile mlizotawanyika; nami nitatakaswa kwenu machoni pa mataifa.”

Mambo haya yote, unaona, yanatukia mbele ya macho ya mataifa. {2TG1: 9.2}

9

Aya ya 42-44 — “Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapowaingiza katika nchi ya Israeli, katika nchi ile ambayo niliuinua mkono wangu kwamba nitawapa baba zenu. Na huko mtazikumbuka njia zenu, na matendo yenu yote, ambayo mmejitia unajisi kwayo; nanyi mtajichukia katika macho yenu wenyewe, kwa sababu ya maovu yenu yote mliyoyatenda. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimetenda nanyi kwa ajili ya jina langu, si sawasawa na njia zenu mbaya, wala si sawa-sawa na matendo yenu maovu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.”

Mambo haya Mungu huwafanyia watu Wake, sio kwa sababu wanastahili, lakini kwa ajili ya jina Lake, kwa sababu ahadi Yake haiwezi kushindwa. Na Ufalme wa Mungu, unaona, hauanzi mbinguni, ila kwa nchi. Na Ufalme, unaona sasa, haujumuishwi na vizuka, lakini wa wanadamu walio hai, wa watakatifu, hamna mdhambi kati yao. {2TG1: 10.1}

Naam, Edeni iliyopotea itarejeshwa. Kwa kweli, Neno hutangaza wazi wazi kwamba Eliya lazima aje kwanza na kuyarejesha mambo yote (Marko 9:12). Jinsi Edeni ilivyokuwa nyumba halisi hapo mwanzo iliyomilikiwa na wanadamu halisi ndivyo itakavyokuwa tena. {2TG1: 10.2}

Aya zilizosalia za Ezekieli ishirini zinachukua mfano mwingine. Ila maadamu wakati hautaturuhusu kuingia ndani, tutahitimisha uchambuzi wetu. Kwanza, hata hivyo, ikumbukwe kwamba aya zilizosalia za sura hii, na pia sura ya 21, pamoja na nuru hii tayari, zinajieleza zenyewe, na unaweza kuzichambua unapopumzika. Aya ya 27 ya sura ya 21 hata hivyo, naweza kuigusia sasa. {2TG1: 10.3}

Aya ya 27 — “Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.”

Katika sura hizi zinaletwa kwa mtazamo zote nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Katika aya hii Mungu ana-tangaza wazi wazi kwamba angalipaswa kufanya upinduzi mara tatu, na kwamba baada ya hapo ufalme haunga-likuwapo tena hadi “atakapokuja yeye ambaye ni haki yake”; yaani, baada ya upinduzi mara tatu, Yeye “ambaye ni haki

10

yake” atakapokuja na Ufalme utarejeshwa. {2TG1: 11.1}

Upinduzi kwa kwanza ulitukia wakati Ashuru iliipindua nyumba ya Israeli, ufalme wa kabila kumi; upinduzi wa pili ulifanyika wakati mfalme wa Babeli aliipindua nyumba ya Yuda, ufalme wa kabila mbili; na upinduzi wa tatu ulitukia wakati Tito mnamo 70 B.K. aliungamiza Yerusalemu. Hivyo inaonekana kwamba sasa tunaishi katika kipindi baada ya upinduzi wa tatu, katika kipindi ambacho “Yeye ambaye ni haki Yake,” atakuja na kuuanzisha Ufalme Wake. {2TG1: 11.2}

Ukweli haswa kwamba Uvuvio sasa umeufunua unabii huu, na umeuleta kwa usikivu wa kanisa, unatuongoza kujua kwa hakika kwamba wakati wa kurejeshwa kwa Ufalme umekaribia; kwamba sasa tuko katika wakati wa kutiwa muhuri kwa watu 144,000; na kwamba iwapo tu waaminifu tutakuwa kati yao, na kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. {2TG1: 11.3}

Hili, Ndugu, Dada, ndilo jibu la Bwana Mwenyewe kwako. {2TG1: 11.4}

Jukumu lako sasa ni kulipokea iwapo unataka maisha ya milele. Usimruhusu adui wa Ukweli alete mashaka kwa mawazo yako, na usimruhusu yeyote anene utoke katika Ukweli huu kwa maana Ibilisi hatasimama karibu bila kufanya kazi. Atatenda yote kukupindua. Kagua tena na tena na uone kwamba Bibilia hufundisha Ukweli huu ili uweze

11

kuushika wako mwenyewe. Hauwezi kumudu kupoteza wakati huu wa machweo. {2TG1: 11.5}

* * *

Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. Iki-wa unataka kupeana yoyote kwa marafiki au jamaa zako Waadventista, unaweza kuagiza nakala za ziada au ku-tuma majina na anwani zao kwa orodha yetu ya watumiwa. {2TG1: 12.1}

Usiyakose Manufaa Juu Ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {2TG1: 12.2}

——0-0-0——

“Bwana huchukia kutojali na kutokuwa mwaminifu wakati wa hatari katika kazi Yake. Ulimwengu wote unaan-galia kwa hamu isiyoelezeka matukio ya kufunga ya pambano kuu kati ya wema na uovu. Watu wa Mungu wanakaribia mipaka ya ulimwengu wa milele; Je, ni nini kinachoweza kuwa cha umuhimu zaidi kwa wao kuliko kwamba waweze kuwa waaminifu kwa Mungu wa mbinguni? Katika vizazi vyote, Mungu amekuwa na mashujaa wenye maadili; na Anao sasa, — wale ambao, kama Yusufu na Eliya na Danieli, hawaoni aibu kujitam-bua kwamba ni watu Wake wateule. Baraka Yake maalum huambatana na kazi za watu wa vitendo; watu ambao hawatayumbishwa kutoka kwa safu sahihi ya wajibu, lakini kwa nguvu takatifu watauliza, “Nani yuko upande wa Bwana?” watu ambao hawatatulia tu kwa kuuliza, lakini watakaoshinikiza kwamba wale wanaochagua kujit-ambulisha na watu wa Mungu watasonga mbele na kuufunua bila kukosea utiifu wao kwa Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Watu kama hao huyafanya mapenzi na mipango yao kuwa chini ya sheria ya Mungu. Kwa ajili ya upendo Kwake, hawayahesabu maisha yao kuwa ya thamani kwao wenyewe. Kazi yao ni kupata nuru kutoka kwa Neno, na kuliangaza kwa dunia katika mianga safi na thabiti. Uaminifu kwa Mungu ndio mwito wao.” – Manabii na Wafalme, uk. 148. {2TG1: 12.3}

12

WAZO LA SALA

Mbona Yesu Alifundisha Katika Mifano

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” uk. 22, aya ya kwanza: {2TG2: 13.1}

“Na Alikuwa na sababu nyingine ya kufundisha katika mifano. Kati ya makutano waliokusanyika Kwake, walikuwapo makuhani na marabi, waandishi na wazee, Waherode na watawala, wapenda dunia, wakaidi, watu wa kujitakia makuu, ambao walitamani zaidi ya vitu vyote kupata mashtaka fulani dhidi Yake. Wapelelezi wao waliziandama hatua Zake siku baada ya siku, ili wapate kutoka kwa kinywa Chake kitu ambacho kingalisaba-bisha hukumu Yake, na kumnyamazisha milele Yule aliyeonekana kuuvuta ulimwengu Umfuate. Mwokozi al-ielewa tabia ya watu hawa, na Aliuwasilisha ukweli kwa njia kwamba wasingaliweza kupata chochote cha kuleta kesi Yake mbele ya Sanhedrini. Katika mifano Alikemea unafiki na matendo mabaya ya wale walioshikilia nafasi za juu, na kwa lugha ya mifano aliuvika ukweli kwa tabia ya kuchonga ambapo ungalikuwa umenenwa kwa shutuma ya moja kwa moja, wasingaliyasikiliza maneno Yake, na wangalikuwa wameikomesha upesi huduma Yake. Lakini Alipokuwa akiwaepuka hao wapelelezi, Alifanya ukweli kuwa wazi kabisa kwamba ma-kosa yalidhihirika, na waaminifu moyoni walifaidika kwa mafunzo Yake ….” {2TG2: 13.2}

Tupige magoti na kuomba kwamba tuweze kuwa macho dhidi ya kuwa wasiouruhusu Ukweli jinsi walivyokuwa Mafarisayo, kwamba tuweze kuwa wenye mioyo ya uaminifu na kufaidika kwa Ukweli unaokuja kwetu. {2TG2: 13.3}

13

MCHUNGAJI MMOJA KUYAFANYA YALE UMATI WA WACHUNGAJI WALISHINDWA KUTENDA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 16, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Hebu tufungue Ezekieli 34, sura tunajifunza leo. {2TG2: 14.1}

Ezek. 34: 1, 2 — “Neno la Bwana likanijia, kusema, Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Is-raeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?”

Ezekieli, tunasoma, alipewa maono ya wachungaji wabinafsi, wachoyo, na wasiofaa. Sasa jambo la kwanza la umuhimu ni kubainisha iwapo wachungaji hawa wabinafsi waliishi katika siku ya Ezekieli, kabla ya siku yake, au baada ya siku yake. Ili kupata habari hii, hebu tusome– {2TG2: 14.2}

Aya ya 23, 24 — “Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, Bwana, nimesema haya.”

Wachungaji wabinafsi ambao dhidi yao nabii ameambiwa aandike, mchungaji mmoja, Daudi atachukua nafasi zao. Wakati hii linatukia watu wa Mungu

14

Wakati huo watakuwa na mchungaji mmoja tu. Hili, kwa kweli, hawezi kuwa Kristo Mwenyewe, kwa maana Uvuvio kamwe haumwiti Yeye Daudi, ila badala yake humwita Mwana wa Daudi. Kwa sababu watu wa Mun-gu siku zote wamekuwa, na bado wanao wachungaji wengi, ukweli unadhihirika wazi kama kioo kwamba Daudi wa aya ya 23 na 24 bado atakuja, na kwamba wachungaji ambao Uvuvio huwalenga ni hasa wale ambao Daudi ataingia mahali pao. {2TG2: 14.3}

Ezekieli, basi, hakupewa maono ya wachungaji katika siku yake, wala ya wale waliokuwa kabla ya siku yake, lakini ya wachungaji baada ya siku yake — siku ambayo Mungu anamwinua huyu Daudi wa uakisi kulilisha kun-di Lake lenye njaa na lililopuuzwa. Watu wa Mungu wakati huo hawatawatumikia wageni tena, “bali wa-tamtumikia Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao.” Yer. 30: 9. Hapa tunaona kwamba sio Ezekieli tu, lakini Yeremia pia alipewa maono ya ukweli huu vile vile. Naam, manabii wote. {2TG2: 15.1}

Ezekieli. 37:24, 25 — “Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao milele.”

Kwa kuwa huu ni nyongeza kwa “Ujumbe wa Malaika wa Tatu” (“Maandishi ya Awali,” uk. 277) na kwa sababu ni ujumbe wa saa ya sasa, kwa hivyo siku ya Ufalme wa Wadaudi imekaribia. hebu tufungue — {2TG2: 15.2}

Hos. 3:4, 5 — “Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi

15

bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.”

Siku nyingi sasa zimekaribia kwisha na wakati wa kuzitimiza ahadi za Mungu bila shaka u hakika kwenye ki-zingiti cha wakati wetu. {2TG2: 16.1}

Ezek. 34:3 — “Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kon-doo.”

Wachungaji katika siku ambayo Ufalme utasimamishwa wanatuhumiwa kwa kuchukua yote wanayoweza kuchukua kutoka kwa kondoo, na kwa kutowajali kondoo. Hili lazima lisije kuwa mazoea yetu. {2TG2: 16.2}

Aya ya 4, 5 — “Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafun-ga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chaku-la cha wanyama-mwitu, wakatawanyika.”

Mwenedo huu wa kutojali kwa upande wa wachungaji unasababisha walei kutanga-tangakutoka kwa dhana mo-ja hadi kwa nyingine kutafuta chakula cha kiroho na utunzi wa mwili. Naam, wanazurura-zurura, kwa mfano, kutoka kwa kilima kimoja hadi kwa kingine, wengi ambao wamekuwa ki-mfano chakula cha hayawani (dhana) kwa sababu hakuna mchungaji wa kuwatunza kondoo, lakini wapo wakata manyoya kuchukua sufu hiyo

16

kutoka migongoni mwao, na mafuta kutoka mbavuni mwao. Wa aibu, kweli! Na ni nani anayethubutu kukataa kutangaza yale Mungu anasema? {2TG2: 16.3}

Aya ya 6-10 — “Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala ku-watafuta. Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wa-chungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu; kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nita-wataka kondoo zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wa-chungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao.”

Tusijipumbaze tena. Mungu hawezi kudhihakiwa. Yeye hatawaacha kondoo Zake milele, Wala Yeye ha-tawaacha milele wachungaji wasio waaminifu kuwachunga kondoo Zake. Yeye hivi karibuni atawaachisha kazi, na Atawataka kwamba watoe hesabu ya kutokuwa waaminifu. Hivyo ni kwamba yale ambayo umati wa wa-chungaji wameshindwa kufanya, mchungaji mmoja, Daudi, ataweza, mikononi mwa Mungu, kufanya. {2TG2: 17.1}

Aya ya 13 — “Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nita-warudisha katika nchi yao wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu.”

Katika siku za huyu wa uakisi Daudi Mungu analikusanya

17

kundi Lake kutoka nchi zote ambapo wametawanyika, na kuwarejesha katika nchi yao wenyewe. Mungu ha-taendelea kuwaacha katika milima na vilima vya Mataifa. “Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana. Baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.” Hos. 1:11; 3: 5. {2TG2: 17.2}

Aya ya 11-16 — “Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nita-watafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapoku-wa kati ya kondoo zake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza. Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; nami nita-walisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu. Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU. Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.”

“… Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji sio wa kweli atalisimamia kundi mwenyewe. Mungu kamwe hajawahi kulifanya kundi litegemee kabisa vyombo vya kibinadamu. Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa

18

na watu wasafi na wakweli. Katika kupepetwa kukuu kutakakotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zinaonyesha kuwa wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha kwamba pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha uwanda wake kabisa.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {2TG2: 18.1}

Aya ya 17 — “Na kwa habari zenu, Enyi kundi langu, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nahukumu kati ya ng’ombe na ng’ombe, kondoo waume na mbuzi waume pia.”

Uvuvio sasa unageuka kutoka kwa wachungaji na kuongea kwa kundi, kwa walei, na kuonya kwamba zipo aina mbili za ng’ombe (matabaka mawili ya washiriki), kondoo waume na mbuzi waume. Hili kwa hivyo ni onyo kwao, na lazima tusishindwe kulitangaza, na lazima wasishindwe kulisikia na kuchukua hatua. Kwa sababu hii haswa ndiposa Salamu Mwafaka zimechapishwa na kutawanywa kama majani ya vuli. {2TG2: 19.1}

Aya ya 18 — “Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kulishwa malisho mema, hata mkawa hamna budi hukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyat-ibua kwa miguu yaliyobaki?”

Baadhi ya ng’ombe wanatuhumiwa kuwa wabaguzi, wanaokula na kunywa tu kile ambacho wanapendelea, na kukanyaga yaliyobaki. Wanaupokea Ukweli wowote wanaokubaliana nao, ila huukataa mwingine. Hapa tutatoa mfano: {2TG2: 19.2}

“ Kazi yangu imekuwa ya kukatisha tamaa sana, kwa kuwa nimeona kwamba lile Mungu alikusudia halijate-kelezwa…. Ndugu hawa waliuchukua msimamo huu: Tunaamini maono, lakini Dada White, kwa kuyaandika, aliweka ndani maneno yake mwenyewe, na tutaamini sehemu ile ambayo tunafikiri

19

ni ya Mungu, na hatutatii ile nyingine.” — “Shuhuda,” Gombo la 1, uk. 234. {2TG2: 19.3}

Kemeo, Enyi “wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!,” ambalo liliwaangukia wanafunzi hao wawili, ni changamoto kwa kila mmoja wetu. Hakuna yeyote kati yetu aliye mkuu kama Bwana, bali Yeye aliyaamini yote ambayo manabii wote waliandika. Imani kamilifu katika manabii ndio huwafanya watu wa Mungu kuwa wakuu. Hapa inaonekana kwamba “kila…ajidhiliye atakwezwa,” na “yeyote ajikwezaye atadhili-wa.” Luka 14:11. {2TG2: 20.1}

Vyema, mimi sihoji chochote ambacho Mungu amenena kupitia kwa manabii Wake. Ninajua kwamba Yeye hasemi uongo; ya kwamba Yeye anao uwezo wa kuyaelekeza maandishi ya manabii Wake; kwamba Yeye huwa hafanyi ahadi za bure; kwamba Anao uwezo wa kuyatimiza yote Asemayo; kwamba unabii Wake kamwe haushindwi. Nachukua ahadi za kemeo kwa utayari kama ahadi za kupongezwa. Huyachambua majukumu yangu jinsi yalivyowekwa Naye kwa fahari kubwa kama vile ambavyo huzisoma ahadi za utukufu. {2TG2: 20.2}

Aya ya 19 — “Na kwa habari za kondoo zangu, wao wanakula hayo mliyoyakanyaga kwa miguu yenu, nao wanakunywa maji mliyoyatibua kwa miguu yenu.”

Watu wa kweli wa Mungu, wakuu kweli kweli, hupokea yale wanaoitwa eti wenye busara hukanyagia chini kwa miguu yao. {2TG2: 20.3}

Aya ya 20, 21 – “Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU awaambia hivi; Tazama, mimi, naam, mimi, nita-hukumu kati ya wanyama walionona na wanyama waliokonda. Kwa kuwa mmesukuma kwa ubavu, na kwa mabega, na kuwapiga wenye maradhi kwa pembe zenu, hata mkawatawanyia mbali.”

Lipo daraja la washiriki wa kanisa ambalo husukuma

20

kwa ubavu na mabega wale ambao hawawapendi, kawaida wale ambao sio wa aina moja ya kiburi kama wao. Hawa watapata adhabu yao. Na wale wanaotendewa vibaya hivyo hawapaswi kamwe kuhisi wameumizwa, wasije wakakata tamaa, kwa maana Ufalme ni wao, almradi kama “hawatawapiga” na “kuwasukuma” wengine. Wasioamini na “wakutawanya” watapata thawabu yao. {2TG2: 20.4}

Aya ya 22-25 — “Basi mimi nitaliokoa kundi langu, wala hawatakuwa mateka tena; nami nitahukumu kati ya mnyama na mnyama. Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, Bwana, nimesema haya. Nami nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni.”

Hali ya mambo sasa kati ya wote ukasisi na walei itabidi ikome hivi karibuni. Wakosaji hawataendelea tena kuchangamana na watiifu. Mnafiki hataendelea tena kutembea pamoja na mwaminifu. Watu wa Mungu ha-watalazimika tena kusikiliza kila upepo wa fundisho. Hawataendelea kupuuzwa tena, au kuachwa kuathirika na hofu. {2TG2: 21.1}

Maadamu sasa tuko uso kwa uso na Uvuvio, na tunaambiwa tofauti kati ya sahihi na mbaya, tumeachwa bila vazi la kujificha chini yake. Tunaweza sasa kuchagua kwa busara ama kumtumikia Mungu au kuitumikia nafsi na mwanadamu, ama kumtegemea Mungu, kulisoma Neno Lake sisi wenyewe au kuwaamini wanadamu, kuwafan-ya wengine wajifunze kwa niaba yetu na kutuambia Ukweli ni nini na kosa ni nini. Tunaweza sasa kuamua ku-ruhusu chuki kutudhibiti,

21

au kuifungua mioyo yetu ili kwamba Ukweli uweze kupata makao hapo. Tunaweza sasa kuwa kama vyombo visivyoonekana pembeni, au kama nuru angavu juu ya milima. “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Dan. 12: 3. {2TG2: 21.2}

Aya ya 26 — “Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.”

Mara nyingi sisi huimba wimbo, “Yatakuwapo Manyunyu ya baraka,” lakini sasa ni juu yetu — tunaweza kuya-pokea au tunaweza kukimbia kutoka kwayo. Wale ambao hupokea yote ambayo Mungu hutoa, yote manabii wote wameandika, manyunyu yataanguka juu yao. “Wale tu ambao wameyastahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu katika kuutangaza [Ujumbe wa Ma-laika Watatu] utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu.” — “Mapitio na Kuhubiri,” Novemba. 19, 1908. {2TG2: 22.1}

Aya ya 27 — “Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.”

Yatakuwapo manyunyu ya baraka, na yatakuwapo mavuno tele, pia. Hili litakuwa wakati vifungo vya nira yetu vitakapovunjwa, tutakapookolewa kutoka kwa mikono ya wale wanaojilisha badala ya kulilisha kundi. {2TG2: 22.2}

Aya ya 28, 29 — “Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala

22

mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu. Nami nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala ha-watachukua tena aibu ya makafiri.”

Sio tu kwamba Mungu atawaokoa watu Wake kutoka kwa mikono ya ndugu wasio waaminifu na wakatili, lakini pia Yeye atawalinda wasiwe mawindo kwa mataifa, na dhana. {2TG2: 23.1}

Aya ya 30, 31 — “Nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, Mungu wao, ni pamoja nao, na ya kuwa wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana MUNGU. Na ninyi, kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.”

Mungu haliachi kundi Lake. Kwa upole huwaita “kundi Langu,” na huwahakikishia tena kwamba Yeye ndiye Mungu wao. Yeye, atamweka bila kushindwa mchungaji mmoja kuyafanya yale umati wa wachungaji wameshindwa kutenda. Sasa ni fursa yako ya kula “chakula kwa msimu wake,” mkononi mwa mchungaji ali-yechaguliwa na Mungu, au kukaa njaa kwa maganda mkononi mwa umati wa wachungaji. {2TG2: 23.2}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG2: 23.3}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 1, 2

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>