fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 41, 42

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 41, 42

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1949

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

MATUKIO YA SASA, HALI YA PALESTINA, NA UTENGO U KARIBU JINSI GANI?

LILE LITAKALOKUWA KATIKA WAKATI WA MWISHO

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Miifano, kuanzia ukurasa wa 130 na aya ya pili: {2TG41: 2.1}

“Uzoefu huu humpa kila mwalimu wa ukweli sifa za ustahili ambazo zitamfanya kuwa mwakilishi wa Kristo. Roho ya fundisho la Kristo itatoa nguvu na uelekevu kwa mawasiliano yake na kwa sala zake. Ushahidi wake kwa Kristo hautakuwa ushuhuda finyu, usiokuwa na uhai. Mchungaji hatahutubu kwa kurudia mahubiri yale yale. Nia yake itakuwa wazi kwa nuru ya daima ya Roho Mtakatifu …. {2TG41: 2.2}

“Tunapoula mwili wa Kristo na kunywa damu Yake, sehemu ya uzima wa milele itapatikana katika ukasisi. Haitakuwapo hazina iliyokauka, ya dhana zinazorudiwa mara kwa mara. Mahubiri laini, butu yatakoma. Kweli za zamani zitawasilishwa, lakini zitaonekana katika nuru mpya. Utakuwapo ufahamu mpya wa ukweli, uangavu na nguvu ambayo wote watatambua. Wale ambao wanayo fursa ya kuketi chini ya ukasisi kama huo, iwapo wanaweza kwa mvuto wa Roho Mtakatifu, watahisi kutiwa nguvu ya uhai mpya. Moto wa upendo wa Mungu utawaka ndani yao. Uwezo wao wa ufahamu utahuishwa kutambua uzuri na utukufu wa ukweli.”{2TG41: 2.3}

Hapa tunaambiwa kwamba kweli za zamani zitawasilishwa katika uhai mpya; pia kwamba mifano katika Bi-bilia itafunuliwa. Hili ndilo haswa jambo ambalo tumeona sasa kwa macho yetu wenyewe. Tunapaswa kuomba ili watu wa Mungu waweze kutambua kwamba ukweli wa zamani sasa umewekwa katika nuru mpya na ya kwamba umepewa uhai mpya. {2TG41: 2.4}

2

MATUKIO YA SASA, HALI YA PALESTINA, NA UTENGO U KARIBU JINSI GANI?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 6, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Nimeombwa kutoa uchambuzi kuhusu matukio ya sasa, kuhusu hali ya Palestina, na kuhusu utengo unaosaba-bishwa na mchinjo ambao umetabiriwa katika maono ya Ezekieli. {2TG41: 3.1}

Natamani ningeweza kuwaambia yote mnayotaka kujua, lakini siwezi kusema ni lini utengo, utakaso wa kani-sa, (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80), utatukia. Mungu pekee ndiye anayejua wakati. Yote ninayojua ni kwamba hauwezi kutukia kabla tuiandae njia, kabla kazi yetu tuliyopewa na Mungu kuhusiana na Ezekieli 9 kutekelezwa. Kisha itakuwa kwamba Bwana atalijia ghafla hekalu Lake (kanisa) na kuwatakasa wana wa Lawi, ukasisi (Mal. 3:1-3). Lakini wale ambao hawataipokea ile alama wataanguka chini kwa silaha za kuchinja za malaika kama walivyofanya “wazaliwa wa kwanza” makafiri usiku wa Pasaka katika nchi ya Misri. {2TG41: 3.2}

Hata hivyo, nina uhakika kwamba Mungu hatatuweka tusiyajue mambo ambayo tunapaswa kujua. Iwapo itakuwa muhimu kwetu kujua mbele ya wakati siku na saa ya utakaso wa kanisa, Pasaka ya uakisi, tutaambiwa. Naam, tutajua angalau mapema jinsi Musa alivyojua kuhusu Pasaka katika siku yake. Hakujua miezi mbele ya siku na saa ya matukio ambayo yangefanyika wakati huo, bali aliamriwa majukumu yake na ya watu na la kuta-rajia siku kwa siku. Wala hakujua mapema kwamba wangelazimika kukumbana na Bahari ya Shamu, lakini kwa sababu wingu liliwaongoza hapo, na maadamu Wamisri waliwaandama nyuma kwa ukaribu, aliambiwa la kufanya wakati

3

huo. Isitoshe, wakati walipoivuka Bahari hakujua ya kwamba wangekaa miaka arobaini jangwani wala kwamba watu wazima kati yao wangeangamia wakiwa kwa safari yao ya kwenda Nchi ya Ahadi. {2TG41: 3.3}

Lazima iwe hivyo leo, kwa sababu “mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu: lakini vitu yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.” Kumb. 29:29. Mungu anajua jinsi ya kuongoza na jinsi ya kuokoa. Siwezi, kwa hivyo, siwezi kuwapa nuru zaidi ya yale uvuvio hufunua. Naweza kusema tu kuhusu mambo ambayo yamefunuliwa. {2TG41: 4.1}

Tukio la kusisimua zaidi sasa ambalo tunajua ni uchaguzi wa rais ambao umesalia siku mbili tu baadaye. Jinsi taifa linavyouona, hili ndilo jambo kubwa zaidi duniani, hata ingawa wengi hawatapata kile wanachotaka, kwa maana kila mojawapo wa vyama tofauti vimetaja mteule wake kwa kura ya urais, lakini ni rais mmoja tu ambaye atachaguliwa. {2TG41: 4.2}

Wote wanaonekana kufikiri kwamba amani na ustawi hutegemea mtu ambaye wao humweka katika Ikulu Nyeupe. Juu ya mamlaka ya Neno, hata hivyo, nasimama kuwaambia kwamba bila kujali ni nani anayewekwa ofisini haitakuwapo amani na ustawi bora wa kudumu, kwa maana Mungu ameachwa nje ya mipango ambayo imebuniwa ingawa Yeye pekee ndiye anayeweza kupeana kile tunachotafuta. Na sasa tunawezaje kujua kwamba Mungu hajashirikishwa? Kidokezo kinachotoa jibu ni hiki: {2TG41: 4.3}

Iwapo washiriki wa kanisa wenyewe hawamjali Mungu na kuwaendea watu kwa ajili ya ushauri badala ya Mungu, basi mtu anawezaje kutarajia ulimwengu kumwendea Yeye? Ninamiliki mamia ya barua kutoka kwa Dhehebu letu ambazo hulithibitisha jambo hili! Wao hunipa habari hii kwa kusema: {2TG41: 4.4}

4

“Kamwe huwa sivisomi vitabu vyako, na kamwe sitavisoma; wachungaji wetu wamechunguza mafundisho yako na wamepata kwamba ni ya uongo. Tuna Ukweli wote; hatuhitaji chochote zaidi. Ondoa jina langu kwenye orodha yako ya barua.” {2TG41: 5.1}

Kwa mazoea ndugu hawa wote ambao wamenaswa kwa Ulaodekia walio na dhana ya “kutohitaji kitu” huja-ribu kukanusha ujumbe wa Ukweli wa sasa kwa kunukuu maandishi ya Dada White, licha ya ukweli kwamba nukuu zao haziihusu mada hiyo na kupotoshwa katika nia zao wenyewe. Wote hunukuu vifungu ambavyo ndugu viongozi wamewapokeza kwa ujanja katika makabrasha yao dhidi yetu, na wote huimba wimbo ule ule wa Ulaodekia ambao wale ndugu viongozi wameuweka vinywani mwao. {2TG41: 5.2}

Mambo haya mara kwa mara yanathibitisha kwamba badala ya kutumia akili zao walizopewa na Mungu, uma-ti wa watu huongozwa na akili za ndugu wachache wenye uadui. Vifungu, hata hivyo, kama ambavyo nakaribia kuvisoma, vimewekwa mbali nao. {2TG41: 5.3}

Hebu sasa nisome hizi rahisi na kwa mada mistari ya Maandishi yaliyovuviwa ambayo hayahitaji maelezo: {2TG41: 5.4}

“Usiwasilishe kitu chochote kitakachozusha mgawanyiko, bila ushahidi wazi kwamba ndani yake Mungu anatoa ujumbe maalum kwa wakati huu.” {2TG41: 5.5}

“Bali jihadharini na kukataa kile ambacho ni kweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na tabia ya kuipekua Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, huwa na imani katika watu wanaoongoza, na huyakubali maamuzi ambayo wao hufanya; na hivyo wengi watazikataa hasa jumbe ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi ha-watazipokea. {2TG41: 5.6}

5

“Hakuna yeyote anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ambayo ipo kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia jambo hili.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {2TG41: 6.1}

“Lazima tujifunze wenyewe ukweli. Mtu yeyote asitegemewe kufikiri kwa niaba yetu. Haijalishi yeye ni nani, au ni katika wadhifa gani anaweza kuwekwa, hatupaswi kumtazama mtu yeyote kama kigezo chetu. Tunapaswa kushauriana pamoja, na kujitiisha mmoja kwa mwenziwe; lakini wakati huo huo tunapaswa kutumia uwezo am-bao Mungu ametupatia, ili tujifunze ukweli ni nini. Kila mmoja wetu lazima amtazamie Mungu ili anururishwe Naye. Lazima sisi binafsi tuikuze tabia ambayo itahimili kipimo katika siku ya Mungu. Hatupaswi kujikita kwa dhana zetu, na kufikiri kwamba hakuna yeyote anayepaswa kuingilia maoni yetu.” — Kimenukuliwa, uk. 109, 110. {2TG41: 6.2}

“Mungu anataka tumtegemee Yeye, na si kwa mwanadamu. Hutumaini tuwe na moyo mpya; Yeye ataweza kutupatia mafunuo ya nuru kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu.” — Kimenukuliwa, uk. 111. {2TG41: 6.3}

“… Iwayo yote ile nafasi yake ya mamlaka, hakuna yeyote aliye na haki ya kufungia mbali nuru kutoka kwa watu. Wakati ujumbe unapokuja kwa jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu ataweza kujipatia udhuru wa kutofanya uchunguzi wa madai yake.” — Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {2TG41: 6.4}

Je! Mwenendo wa Dhehebu uliopotoshwa wa kutafuta Ukweli uliofunuliwa na Mbingu hauthibishi kwako kwamba halimjali Mungu, kwamba badala Yake wamewekwa wale ambao wanastahili kuwa watumwa Wake? Inaweza kuwaje iwapo mwanadamu anaulizwa ushauri wakati ambapo Roho wa Mungu anapaswa kutafutwa? Je! Hatujaambiwa na Maandiko kwamba Roho Mwenyewe atatuongoza mmoja mmoja katika Kweli yote? Kwamba tusiufanye mwili kuwa kinga yetu kwa kumruhusu mtu mwingine atuamulie Ukweli ni nini na uongo ni nini? Je! Sisi hatumkani Roho na muunganisho wetu kwa Mbingu tunapochukua mbadala? Na bado iliyo mbaya zaidi ni kutafuta ushauri kwa mtu ambaye tayari yu dhidi ya lile unalotarajia akubali au asikubali. Iwapo Mungu anaweza kumfunza ng’ombe mmoja mmoja kutafuta maji katika nyanda za chini, na sio juu ya milima na vilima, na kutafuta mahali pa joto ambapo upepo hauvumi, basi kwa nini Yeye mwenyewe asiweze kutuonyesha kibinafsi Ukweli ni nini? na uongo ni nini? {2TG41: 6.5}

Je! Wasisi wa kanisa walielekezwa kwenye Ukweli na ushauri wa makasisi na marabi, au na Roho wa Mungu ndani ya mioyo yao? Je! Hatujaambiwa kibinafsi: “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwam-ba zimetokana na Mungu: kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu: Kila Roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwilini yatokana na Mungu.” 1 Yohana 4:1, 2. “Msimzimishe Roho. Msitweze unabii. Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.” 1 The. 5:19-21. {2TG41: 7.1}

Zaidi ya hayo, Amosi kwa jicho la Uvuvio alitazama chini kupitia karne nyingi, hadi ndani ya enzi ya Ukristo, na akatangaza: {2TG41: 7.2}

Amosi 1:2 — “Bwana atanguruma toka Zayuni, atatoa sauti Yake toka Yerusalemu; na malisho ya wa-chungaji yataomboleza, na kilele cha Karmeli kitanyauka.”

Andiko hili, unaona, huakisi janga ambalo lilitukia juu ya Karmeli katika siku za Eliya. Hapa tumepewa kid-okezi kwamba kutakuwa na pambano jingine kati ya nabii wa Mungu na manabii wa Baali. Manabii wa Baali katika siku zetu hata hujigamba kwamba hawajavuviwa, kwamba yale wanayofundisha na kuhubiri ni yale am-bayo wenyewe wamegundua kwa kusoma sana na kuchunguza! Huwadhihaki hata wale wanaodai kuvuviwa na Bwana! Wao huonekana kufikiri kwamba Mungu ameiacha nchi; kwamba Yeye hajali kumtuma Roho Wake kama wakati wa awali; kwamba watu sasa ni werevu sana hivi kwamba lile Roho anaweza kuwafanyia, wao wenyewe wanaweza kufanya

7

vyema zaidi! Ukweli ni, hata hivyo, kwamba iwapo kulipata kuwapo hitaji lolote la wafasiri wa Maandiko waliovuviwa, ni leo wakati pepo nyingi za mafundisho zinavuma kutoka pande zote, zikileta machafuko, miga-wanyiko, na maafa kila mahali. Hakuna wanaoelewana! {2TG41: 7.3}

Kuhusu hali hii ya kusikitisha Roho ya Unabii huonya: {2TG41: 8.1}

“Wale wanaoruhusu chuki izuie nia dhidi ya kuupokea ukweli hawawezi kupokea mnururisho mtakatifu. Hata sasa, wakati wazo la Maandiko linapowasilishwa, wengi hawahoji, Je! Ni kweli, — kwa upatano na neno la Mungu? ila, ni nani anayeliunga mkono? na lisipokuja kupitia njia ambayo haswa huwafurahisha, hawalikubali. Wakiwa wameridhika kabisa na maoni yao wenyewe, kwamba hawatachunguza ushahidi wa Maandiko, na shauku ya kujifunza, bali hukataa kupendezwa, kwa sababu tu ya chuki zao. {2TG41: 8.2}

“Bwana mara nyingi hufanya kazi pale ambapo hatuwezi Kumtarajia; Yeye hutushangaza kwa kuzifunua nguvu Zake kupitia vyombo vya chaguo Lake mwenyewe, ilhali Yeye hupita kwa watu ambao tumewaangalia kama wale ambao nuru inapaswa kupitia ndani yao. Mungu hutaka tuupokee ukweli kwa sifa yake wenyewe, — kwa sababu ni ukweli.”– Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 105, 106. {2TG41: 8.3}

Dunia haijawahi kuliona kundi la wapenda dini sana, wala watu wanaosali na wa kumcha Mungu sana kuliko makuhani, waandishi, na Mafarisayo katika siku ya Kristo. Lakini ni wao haswa walioyapinga mafundisho ya Kristo, ambao walieneza chuki na machafuko kati ya watu na kuwadumisha gizani! Naam, walilidanganya taifa lote. Mwishowe, iwapo Sanhedrini ya Kiyahudi haikuwa ya kuaminika wakati wa ujio wa Kristo wa kwanza, basi tunawezaje kujua kwamba Sanhedrini ya Ukristo katika ujio wa pili wa Kristo itakuwa sadikifu? Zilikuwa Sanhedrini za vizazi vya kati na hadi leo hii ambazo zimepigana dhidi ya Matengenezo yoyote ambayo yameongozwa

8

na Mungu. Hebu niwasomee yale ambayo yalitukia katika siku za uanzilishi wa Dhehebu: {2TG41: 8.4}

“Lakini makanisa kwa ujumla hawakulipokea onyo hilo. Wachungaji wao, ambao kama ‘walinzi kwa nyumba ya Israeli,’ wangekuwa wa kwanza kutambua ishara za kuja kwa Yesu, walikuwa wameshindwa kujifunza ukw-eli, ama kutoka kwa ushuhuda wa manabii au kutoka kwa ishara za nyakati. Kadiri matumaini na matarajio ya ulimwengu yalivyoijaza mioyo, upendo kwa Mungu na imani katika neno Lake ilikuwa imepoa; na fundisho la ujio lilipowasilishwa, liliamsha tu chuki yao na kutoamini. Ukweli kwamba ujumbe huo, kwa kiwango kikubwa, ulitangazwa na walei, ulisisitizwa kama hoja dhidi yake. Kama zamani, ushuhuda wazi wa neno la Mungu ulika-biliwa na kuhoji, “Je! Yupo yeyote kati ya watawala au Mafarisayo aliyeamini?” Na kwa kupata jinsi kazi il-ivyokuwa ngumu ya kupinga hoja zilizotolewa kwa vipindi vya unabii, wengi walipinga kuuchambua unabii huo, wakifundisha kwamba vitabu vya unabii vilitiwa muhuri, na havingeweza kueleweka. Makutano, wakiwaamini kabisa wachungaji wao walikataa kulisikiliza onyo; na wengine, ingawa waliuamini ukweli, hawakuthubutu ku-kiri, wasije wakatupwa nje ya sinagogi.’ Ujumbe ambao Mungu alikuwa ametuma kwa ajili ya kulipima kanisa na kulitakasa, ulifunua kwa hakika umati jinsi ulivyokuwa mkubwa ambao ulikuwa umeweka upendo wao kwa ulimwengu huu badala ya Kristo. Kamba ambazo ziliwafunga duniani zilikuwa na nguvu kuliko vivutio vya kwenda mbinguni. Walichagua kusikiliza sauti ya hekima ya kidunia, na wakakengeuka kwa ujumbe wa kujihoji wa kweli.” — Pambano Kuu, uk. 380. {2TG41: 9.1}

Ikiwa huu ndio umekuwa uzoefu wa zamani, na iwapo sote tungelazimika kufanya uamuzi kwa au dhidi ya ukweli wa Ujio kinyume na maamuzi ya makasisi na wachungaji katika makanisa yetu ya awali, na iwapo hii ilikuwa njia pekee ya kuutafuta Ukweli basi, mbona isiwe hivyo sasa? Je! Sasa tumekosa uwezo kuliko

9

tulivyokuwa kabla ya kuwa Waadventista? Je! Maombi yetu sasa yanashindwa kuleta matokeo? Je! Roho amet-uacha? au tumemwacha Yeye? Lipo tu jibu moja la uaminifu ambalo linaweza kutolewa: {2TG41: 9.2}

Kanisa linatangatanga na ulimwengu nalo, pia, linatarajia watu wakuu wa dunia, sio Roho wa Mungu, kuli-ambia Ukweli ni nini na uongo ni nini, nani ambaye atawekwa ofisini na nani ambaye hastahili. “Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, na kumrudia Bwana tena.” Omb. 3:40. {2TG41: 10.1}

Wazo kwamba sisi, kama Waadventista wa Sabato, tunayo Kweli yote tunayohitaji, ya kwamba sisi ni “tajiri na tumejitajirisha,” wala hatuna haja ya kitu, ni wazo ambalo Sanhedrini katika siku ya Kristo ilitia kasumba ndani ya akili za watu, na hadi leo hii taifa la Wayahudi halijapona kutoka kwa madhara yake. Je! Ndugu zetu Waadventista wa Sabato kwa hivyo hawasimami katika nafasi iyo hiyo isiyofaa ya kukataa nuru yoyote ambayo Mungu anaweza kutuma, iwapo haikubaliani na maoni yao? Na hata ikiwa Kristo Mwenyewe angeileta chini, na iwapo haikubaliani na yao, je! wao kama Wayahudi wa zamani wasingejaribiwa kwa hatari ya kumsulibisha Yeye iwapo wangeweza? O hitaji kubwa la uamsho na matengenezo! Na iwapo hii ndio hali ya watu katika ka-nisa letu, basi ni ipi inaweza kutarajiwa kwingine? Nirudieni, kwa nini muangamie? ni kilio cha Mbingu. {2TG41: 10.2}

Haya ndio baadhi ya matukio ya hivi sasa ambayo yanaonyesha kwamba wanadamu wanatanga mbali zaidi na Mungu na wanajongea zaidi karibu na ubinafsi wa mtu. Iwapo tutamshirikisha Mungu, tutakuwa na amani, usalama, na mafanikio. Lakini jinsi ilivyo sasa, sisi kama taifa na kama watu tunaelekea kwenye taabu na msukosuko nyumbani, na kwa vita nje ya nchi, wakati kanisa linaendelea kulala. {2TG41: 10.3}

Sasa kuhusu lile ninalofikiri juu ya hali ya Palestina yenyewe: Nafikiri Wayahudi wanahitaji kupata mahali pa kwenda,

10

lakini sifikiri Mungu anawaongoza. Iwapo Mungu aliwafukuza Wayahudi kutoka katika nchi Yake kwa sababu ya uovu wao, kwa sababu Yeye hangeendelea kuwavumilia, basi ni hakika kwamba Yeye hawaongozi warejee kwayo sasa ilhali wangali na nia ile ile na wenye uadui dhidi ya Mwanawe wa pekee jinsi walivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita. Wayahudi, kwa hivyo, wanaichukua nchi kwa wajibu wao wenyewe, na zitakapotimia “nya-kati” za Mataifa (Luka 21:24), Taifa jipya la Israeli, jinsi wanavyojiita wenyewe, wakati huo wataondoka katika nchi hiyo upesi sana kuliko sasa wanavyoweza kuichukua, isipokuwa wamtangulize Mungu katika nchi pamoja nao. {2TG41: 10.4}

Mungu hata hivyo atakuwa na watu hapo, lakini watakuwa wa aina Yeye huzungumzia katika Maandiko, ambayo baadhi yake nitasoma sasa: {2TG41: 11.1}

Yer. 30:18-22 — “Bwana asema hivi, Tazama, Nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahu-rumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama il-ivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele Yangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; Nami nitamkari-bisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana. Nanyi mta-kuwa watu Wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

Yer. 31:6-10, 34 — “Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Zayuni, kwa Bwana, Mungu wetu. Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni,

11

mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu Wako, mabaki ya Israeli. Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwa-namke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa. Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni Baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza Wangu. Lisikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kum-linda, kama mchungaji alindavyo kundi lake …. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”

Hos. 3:4, 5 — “Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago.”

Baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema Wake kwa kicho siku za mwisho.” {2TG41: 12.1}

Mungu atakuwa na watu katika nchi sawa, lakini wote watamjua Bwana. Wale, kwa hivyo, ambao sasa wana-jaribu kujiweka wenyewe huko Palestina sio watu hao. Ili kujifunza ni kina nani watu watakaoirithi ile nchi, so-ma Trakti Namba 8, Mlima Zayuni kwa Saa ya Kumi na Moja. {2TG41: 12.2}

Lakini, mwasema, haupo unabii wowote kuhusu yale Wayahudi wanafanya leo ndani ya Palestina? Kwa kweli lazima uwepo unabii. Hebu niwasomee: {2TG41: 12.3}

12

Zef. 2:1-3 — “Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilotakikana; kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapi-ta siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwa-na. Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu Zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.”

Hizi aya za maandiko, mwaona, zitatimizwa kabla tu ya “siku kupita kama makapi,” kabla ya hasira kali ya Bwana kuwajilia taifa lisilotakikana. Na ambapo taifa hili lisilotakikana linajikusanya pamoja, basi inakuwa kwamba wanyenyekevu wote wa nchi, wale ambao wameunga mkono ujumbe wa Bwana “kabla ya siku kuu na ya kuogofya ya Bwana” (kanisa), wanashauriwa waendelee kuutafuta unyenyekevu. Wapo, kwa hivyo, makundi mawili ya watu yalioletwa kwa mtazamo katika aya hizi — taifa ambalo halitakikani na wanyenyekevu wa nchi. {2TG41: 13.1}

Sasa kwa mtazamo wa ukweli kwamba lipo taifa moja tu lisilotakikana, la Kiyahudi, na hakuna lingine, amba-lo linachukiwa na mataifa yote, andiko hili haliwezi kuhusishwa kwa watu wengine. Pia ukweli kwamba sasa wakati tunapoutangaza ujumbe wa siku kuu na ya kuogofya ya Bwana, ile siku kabla ya siku ya hasira ya Bwa-na, Wayahudi wasiotakikana duniani kote wanajikusanya pamoja ndani ya Palestina — Nasema kwa kuzingatia mambo haya yote yanapotukia pamoja sasa, ukweli wa Maandiko unasimama wazi, ukionyesha kwamba hasira ya Bwana itawaangukia Wayahudi isipokuwa wafanye matengenezo, na si wao, ila “wanyenyekevu wa nchi” watairithi hiyo nchi. Na kwa mujibu wa Andiko, Myahudi na Mwarabu sawa sawa watatoka katika Nchi ya Ahadi, na wanyenyekevu wa nchi wataingia ndani yake. {2TG41: 13.2}

Je! Watafikaje huko, na ni nani ataifungua njia? — Jibu la maswali haya tutapata katika: {2TG41: 13.3}

13

Zek. 14:4, 5 — “Na siku hiyo miguu Yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule itaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja Naye.”

Bwana Mwenyewe, unaona, ndiye atakayeifungua njia ya kurudi kwa watu Wake. {2TG41: 14.1}

Isa. 11:11, 12, 16 — “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie wa-tu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia …. Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.”

Isa. 27:12, 13 — “Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapiga-piga mlangobahari toka Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli. Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.”

14

Bwana anaifungua njia, na Bwana anawakusanya watu Wake. {2TG41: 14.2}

Sasa kuhusu vita jinsi vilivyo leo. Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita, ambayo ilitokea miaka kadhaa iliyopita, hunena ukweli kuhusu Vita vya 2 vya Dunia na matokeo yake. Trakti hiyo hupata nuru yake kutoka kwa unabii wa Nahumu. Vita vilivyotabiriwa humo, nabii atangaza, vinapiganwa katika siku ya magari, katika siku ambayo watu “wanaenda mbio huko na huko,” ilhali “magari … yakifanya mshindo njiani, … yakisongana-songana … [yakikwenda upesi] kama umeme,” — katika wakati wetu. Vita hivyo, nyongeza ya trakti — Wakati Na Nafasi Husuluhisha Mafumbo — huthibitisha, ni Vita vya 2 vya Dunia. Nabii alimwona yule asetaye vipande vipande (Hitler) akiwatisha maadui zake kujiandaa dhidi yake. Kisha nabii akawaona wakuu wake yule asetaye vipande vipande (wakuu wa Hitler) wakijikwaa katika mwendo wao (wakianguka kwa kosa katika mwendo wao kupata ushindi). Na hivyo ilikuwa kwamba baada ya Hitler kuzifyatua bunduki zake dhidi ya mataifa yali-yomzunguka, na kuanza kuvunja kila kitu vipande vipande, washirika wakaenda kujiandaa kwa vita. {2TG41: 15.1}

Hitler alisababisha wakuu wake kwa kupigana vita dhidi ya Urusi ilhali alipokuwa vitani na Uingereza Kuu, na kwa kuandama Ugiriki na Misri badala ya kuvuka mlango wa bahari wa Uingereza wakati Uingereza, pasipo yeye kujua, ilikuwa karibu kujisalimisha. Hivyo wakuu wake walijikwaa na kamwe hawakuinuka tena. Mwishowe, Hitler alitoweka na uadui ukakoma. Lakini kwa mujibu wa unabii wa Nahumu, na pia kwa mujibu wa matukio ya sasa yanavyotangazwa na ripoti za habari kila mahali, vita bado vinaendelea; kwa kweli hav-ijakoma, lakini vinachukua mkondo mbaya zaidi, naam, na ni jambo la muda tu kabla ya kuchacha zaidi kuliko vilivyokuwa hapo awali kwa kutoweka kwa Hitler. {2TG41: 15.2}

Isitoshe, halijawahi kuwapo tangazo rasmi kwamba vita vimekwisha. Hamna mapatano kamili na

15

Dola zilizopigana vitani hata sasa yameafikiwa. Mtu yeyote anaweza kuona kwamba dunia inajiandaa upesi ku-rejelea vita kwa nguvu na pigo la mwisho ikiwezekana. Mtu yeyote anaweza kuona, pia, kwamba vita haviku-pata ushindi kwa manufaa ya Uingereza Kuu, ila ya Urusi, na ya kwamba kufuatia kusitishwa kwa hali za uhasama kumesababisha dunia kujiimarisha katika pande mbili kubwa na za uadui, — pande za Magharibi na Mashariki, — bila kutaja vita na tetesi za vita pande zote kutuzunguka. Hili lilitukia kwa sababu Uingereza Kuu ilishirikiana na Urusi isiyoamini, serikali ambayo I dhidi ya Mungu na kanisa Lake. Hivyo Uingereza Kuu ilim-wamini sana adui wa Mungu kuliko Mungu Mwenyewe, na ndio sababu vita bado vitapiganwa. {2TG41: 15.3}

Na sasa ambapo vita baridi kati ya mashariki na magharibi vinaendelea, makanisa, pia, kwa muungano wa Amsterdam, yanaongeza ukubwa wa kila upande. Matangazo ya redio na magazeti hutangaza kwamba makanisa yote isipokuwa halisi ya Kirumi na ya Kirusi yalituma wawakilishi kwenye baraza la Amsterdam. Kanisa halisi la Urusi mnajua, ni kanisa halisi la Ugiriki. Na Je! mbona mnafikiri kanisa lililoko Ugiriki lilijiunga na muungano, ila kanisa lililoko Urusi halikujiunga? Kwa sababu tu ya kuogopa “upande” ambao yapo. Makanisa, pia, yanae-gemea pande zao maalum — Mashariki au Magharibi. (Je! Kanisa la Kirumi litafanya nini? Nalo, pia, kwa lazima baadaye litajiunga na upande wa Magharibi.) {2TG41: 16.1}

Haionekani kwenu kana kwamba dunia inajiandaa kwa serikali ya kidini na kiraia? Nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba ulimwengu bila kujua unafanya juhudi kubwa kumpandisha mnyama mwekundu sana wa Ufunuo 17 na kuketi kwa BABELI MKUU. Tumeelekea kwa serikali ya kidini na kiraia ambayo BABELI MKUU huashiria akiwa amempanda mnyama mwekundu sana, na vita “vinapochacha” tena, Babeli unaweza wakati huo kuchukua nafasi ya Umoja wa

16

Mataifa baadaye. Hivyo inaonekana kwamba ulimwengu katika jaribio lake la kushinda vikwazo ambavyo vinaukabili, ni kwa mfano kuruka kutoka motoni na kuanguka kwa kikaango, kwa sababu tu haumshirikishi Mungu. {2TG41: 16.2}

Ulimwengu unauona ukomunisti kama dubwana mwenye vichwa vingi nyuma ya kichaka, na mataifa tayari, kwa mfano, yanapigapiga magoti yao moja dhidi ya lingine wakati yanapomwangalia. Usalama wao, hata hivyo, hautegemei hofu na silaha, wala kwa mtu ambaye tunamchagua kuwa rais, ila kwa Mungu, kwake Yeye Am-baye huishikilia dunia angani, na Ambaye bado hutawala maswala ya wanadamu. Tangu alfajiri ya historia hadi leo mataifa makuu ambayo yameanguka, yalianguka yalipokuwa yamejihami vyema na yalipokuwa hayamtegemei Mungu. Hili linapaswa kuwa funzo kubwa kwa wote, lakini ni nani anayetambua! {2TG41: 17.1}

Mungu, kwa hivyo, kwa ajili ya mapenzi Yake mwenyewe huweka ndani ya mioyo ya wakomunisti, au dola kama za kikomunisti (pembe kumi za yule mnyama mwekundu sana ambazo humchukia mwanamke, huchukia dini, jinsi ufanyavyo ukomunisti) “kumpa yule mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimizwe.” Ufu. 17:17. {2TG41: 17.2}

Sasa, taarifa “wampa ufalme wao” humaanisha kwamba wana ufalme wa kutoa. Katika aya ya 12, hata hivyo, tunaambiwa kwamba “hawajapokea ufalme bado; lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.” Wakati taarifa zote zinawekwa pamoja basi taarifa hizo husema kwamba ukomunisti unaweza kuwa na ufalme, unaweza kutawala dunia, ila “Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri Lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimizwe.” Wao, kwa hivyo, wanapokea tu nguvu kama wafalme saa moja pamoja na yule mnyama, baada ya hapo wanamwangamiza mwa-namke, mfumo wa serikali ya kanisa na kiraia, na kujitwalia ufalme (Ufu. 17:17). (Kwa maelezo zaidi ya sura ya kumi na saba ya Ufunuo, soma Trakti namba 12,

17

Dunia Jana, Leo, Kesho, uk. 30-33). {2TG41: 17.3}

Namna hili litakavyotukia, sijui; bali najua kwamba vita vikuu zaidi ya vita vyote vitapiganwa juu ya nchi ta-katifu; “Tazama,” asema BWANA, “siku ya Bwana inakuja, ambayo mateka watagawanywa kati yako. Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitapigwa risasi, na wanawake watatendewa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani, ila mabaki ya wa-tu wa mji hawatakatiliwa mbali.” Zekaria 14:1, 2. {2TG41: 18.1}

Taarifa hii ya kinabii, “Mungu ametia mioyoni mwao … kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao,” huthibitisha kweli yale nilijitahidi kusema muda mfupi uliopita: kwamba wakati taifa lolote linapokuwa kuu na kujisimamia, bila Mungu, lijenge mitambo mikubwa ya vita kujikinga na kushambulia, basi ilikuwa kwamba taifa hilo likaishia hapo. Utulivu na ufanisi wa taifa lolote na watu, kwa hivyo, hutegemea msimamo wao na Mungu, sio kwa nguvu zao za kijeshi. {2TG41: 18.2}

Hebu niwakumbushe lile Uvuvio ulisema kuhusu muungano wa mataifa na watu kwa mujibu wa matukio ya sasa. Kwa ajili ya nuru kwa mada hiyo tunaenda katika sura ya nane ya unabii wa Isaya. Wakati hautaniruhusu kuichambua tena nanyi sura yote, na sifikiri ni muhimu, maana tuliichambua si muda mrefu uliopita. Mna-kumbuka kwamba sura hiyo hufunua muungano ambao Israeli ya kale, ufalme wa makabila kumi (kanisa), uli-fanya na Siria ya kale, dola kuu ya dunia, kupigana dhidi ya Yuda, ufalme dada (kanisa). Uvuvio huufanya ku-wa mfano wa muungano wa kanisa na serikali, na kwa huo hakika huonyesha mwenendo ambao makanisa ya jina tu na dola kuu za ulimwengu zitachukua sasa katika uakisi. Unafahamisha, isitoshe, kwamba hawatafaniki-wa ndani yake. {2TG41: 18.3}

18

Nitasoma kwenu sasa lile Mungu Mwenyewe anafikiri kuuhusu: {2TG41: 19.1}

Isa. 8:8-10 — “Naye atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli. Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande. Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.”

Kwa mujibu wa Mtakatifu Mathayo, sura ya 1, aya ya 23, jina Imanueli ni la Kristo, na kwa ufasiri linamaan-isha “Mungu yu pamoja nasi.” Ni wazi, basi kwamba usemi “Ee Imanueli,” unaonyesha kwamba Uvuvio unanena kwa Kristo. Na kwa sababu hangeweza kuambiwa hivyo kabla Yeye azaliwe na mwanamke na kupokea jina Imanueli, ni dhahiri kwamba muungano huu wa watu unapatikana katika enzi ya Ukristo, katika enzi ambayo Imanueli huishi. {2TG41: 19.2}

Sasa taarifa “Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; semeni neno, lakini halitasimama; kwa maana Mungu yu pamoja nasi,” inasema dhahiri lile nililojitahidi kuwaambia — kwamba mataifa, pamoja na makanisa, yamemwa-cha Imanueli, “Mungu pamoja nasi,” nje ya mipango yao, kwamba yale wanayojaribu kufanya wanatenda kwa ubunifu wao na rasilimali zao wenyewe kwa maana maneno “Mungu yu pamoja nasi” yakitoka kwa mmoja am-baye hayuko pamoja na miungano ya wale watu, bila shaka humaanisha kwamba Imanueli hayuko pamoja nao, na ya kwamba kwa hivyo kazi yao haitasimama. {2TG41: 19.3}

Kutoka kwa maandiko haya inaonekana kwamba matukio ya sasa yaliyoletwa na pande mbili zinazopingana, mashariki na magharibi, hayatatekelezwa kulingana na mipango ya wanadamu, kwamba mipango iliyobuniwa na shirikisho hilo

19

la mataifa na watu litakuwa sifuri isipokuwa wamtafute Mungu kwa ushauri na wamweke Yeye katika ushirikiano. {2TG41: 19.4}

Hebu sasa tusikie lile Bwana angetaka tufanye, msimamo ambao Yeye angetaka watu Wake wachukue: {2TG41: 20.1}

Aya ya 11, 12 — “Maana Bwana aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fiti-na; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.”

Hofu ambayo watu huogopa isiwe hofu yetu; wala mipango yao isiwe mipango yetu. Wajibu wetu ni– {2TG41: 20.2}

Aya ya 13 — “Bwana wa majeshi ndiye Mtakayemtakasa; na awe Yeye hofu yenu, na awe Yeye utisho wenu.”

Kumtakasa Bwana ni kuwa wake Yeye kabisa, pasipo kuwa na yeyote mwingine badala Yake, kuweka tu-maini lako lote ndani Yake, si kuufanya mwili kuwa kinga yako, kwa maana Yeye pekee ndiye anayeweza ku-kuwezesha. Na ingawa unaweza kuwa wa pekee katika ulimwengu wote kuchukua msimamo kama huo, Yeye hatakuangusha. Iwapo kama hii iwe hali yako, basi utakuwa shujaa mkubwa zaidi wa Mbingu. {2TG41: 20.3}

Aya ya 14 — “Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.”

Ukweli huu, unaona, sasa, kama ule ukweli wowote uliofunuliwa na Mungu wakati wowote uliopita, utakuwa mwamba wa kujikwaa na mtego kwa wengi — naam, jinsi Kristo Mwenyewe alivyokuwa kwa Wayahudi — kwa sababu badala ya kuchukua msimamo thabiti kwa ukweli wa Mungu, wanakuwa maadui dhidi yake kama walivyokuwa Wayahudi katika siku ya Kristo. Maadamu unabii huendelea hadi

20

katika sura ya tisa, tutasoma– {2TG41: 20.4}

Isa. 9:20, 21 — “Hupokonya upande wa mkono wa kuume, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe. Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira Yake haikugeukia mbali, lakini mkono Wake umenyoshwa hata sasa.”

Kama haya ytakuwa matokeo ya kumkataa Mungu na ushauri Wake. Wote ambao wanachukua msimamo wao na umati dhidi ya watu wa Mungu watajikuta katika hali ile ile kama Wamidiani walivyojikuta katika wakati wa Gidioni — nuru itakapotokea watauana, lakini waaminifu wataokolewa. Hili, hata hivyo, sio yote: {2TG41: 21.1}

Isa. 8:15 — “Na wengi kati yao watajikwaa, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kutekwa.”

Kwa mujibu wa andiko hili wengi wao watapata “unyakuo” sio kwa upendezi wao na sio kulingana na fun-disho lao. Amri ya Bwana ni: {2TG41: 21.2}

Aya ya 16 — “Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi Wangu.”

“Mwanafunzi” ni yule ambaye humfuata Kristo sikuzote katika Ukweli uliofunuliwa na Mungu ambao huupokea si kwa sababu wengine hufanya hivyo, au la, bali kwa sababu Baba aliye Mbinguni kupitia kwa Roho Wake mwenyewe amemshawishi kibinafsi (Mat. 16:17) — kwa sababu huru kwa yale wengine hufanya au kus-ema yeye kibinafsi ameshawishiwa na Roho. Na “ushuhuda” ni Neno Lake lililo hai lililosambazwa na wajumbe Wake wateule waliojazwa Roho — “Roho ya Unabii” kazini (Ufu. 19:10). Kwa hivyo kufunga ushuhuda kati ya wanafunzi Wake ni kuthibitisha “Roho ya Unabii” kati yao na wao tu. Na kuitia muhuri sheria

21

kati yao ni kuwa na sheria iliyoamriwa na iliyofanywa imara kwa Ukweli, kuwafanya waone umuhimu wa kui-tunza, na kuwawezesha kwa utulivu kusema– {2TG41: 21.3}

Aya ya 17 — “Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso Wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.”

Aya ya 18 — “Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa Bwana wa majeshi, Yeye akaaye katika mlima Zayuni.”

Hivi karibuni itaonekana kwamba wale wanaochukua msimamo thabiti kwa upande wa Ukweli watakuwa kwa ajili ya ishara na maajabu. {2TG41: 22.1}

Aya ya 19 — “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?”

Hapa ulimwengu unaonyeshwa kutoa umakini mkubwa kwa Mizimu kuliko kwa “asema Bwana.” {2TG41: 22.2}

Aya ya 20 — “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.”

Watu wa Mungu watajua kwamba wale ambao huchukua msimamo isipokuwa ule ambao Ukweli umeweka hapa, wanafanya hivyo kwa sababu Roho wa Kweli hakai ndani ya mioyo yao. Na hebu tukumbuke kwamba kuufanya mwili kinga yako, kutafuta ushauri kwa mwanadamu wakati Mungu anapaswa kutafutwa kwa ushau-ri, ni vibaya kabisa kama kutafuta ushauri kwa roho za Giza. {2TG41: 22.3}

“Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu wala si mavazi yenu mkamrudie Bwana Mungu wenu kwa maana Yeye ndiye mwenye neema amejaa huruma, si mwepesi wa hasira,

22

ni Mwingi wa rehema, Naye hughairi mabaya.” Yoeli 2:12, 13. {2TG41: 22.4}

 

MWITO WA MAANDISHI YA DADA WHITE

Maombi ya dharura yamepokelewa kutoka nchi za kigeni ya nakala za Shuhuda kwa Kanisa, Maandishi ya Awali, na maandishi mengine ya Dada E. G. White. Kwa sababu tunayo shauku ya kutosheleza maombi yote kama hiyo ya ndugu na dada ambao hawawezi, ama kwa sababu ya eneo la mashambani au kwa sababu ya ukosefu wa pesa, kujipatia vitabu vya Dada White na Biblia, tunaweza kuthamini sana ukitutumia nakala zozote za ziada ambazo unaweza kuwa nazo. (Tuma kwa: Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas.) {2TG41: 23.1}

23

LILE LITAKALOKUWA KATIKA WAKATI WA MWISHO

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 27, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ili kujua lile litakalotukia katika wakati wa mwisho, lazima kwanza tujue ni wapi wakati wa mwisho huanzia na kwishia. Lazima tujue miisho yote iwapo tunataka kujua yale yanayotukia kati yake. Sasa, ili kujua ni lini “wakati wa mwisho” huanzia, hebu tufungue– {2TG42: 24.1}

Dan. 11:40 — “Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini at-amshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.”

Katika aya hii ya Maandiko vipo vidokezi vitano ambavyo vinapaswa kuzingatiwa kwa uangalifu: (1) kwam-ba vita vilivyotajwa katika aya hii ni pambano la mwisho kati ya wafalme wawili walionakiliwa katika unabii wa Danieli 11; (2) kwamba ni vita vya kushindwa kwa mfalme wa kusini; (3) kwamba vitapiganwa wakati wa mwi-sho, si kabla, katika, au baadaye; (4) mfalme wa kaskazini anakuwa mkuu ilhali mfalme wa kusini anadhoofika; na (5) ya kwamba taarifa, “wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye,” bila shaka hutia alama mwanzo wa “wakati wa mwisho.” {2TG42: 24.2}

Ikiwa, kwa hivyo, tunapata mwaka ambao vita hii iliyotabiriwa ilianza, tutakuwa tumeanzisha mwanzo wa “wakati wa mwisho.” {2TG42: 24.3}

Kwa sababu mfalme wa kusini anamshaambulia mfalme wa kaskazini, inafuatia kwamba mfalme wa kusini ndiye anayeanzisha vita, anajihisi kuwa mwenye nguvu kushambulia. Hata hivyo anashindwa na mfalme wa kaskazini anaingia kwa nguvu, anakuwa mkuu — anaziteka nchi nyingi, pamoja na zifuatazo: {2TG42: 24.4}

Aya ya 41 — “Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokole-wa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni.”

Hapa imeonekana kwamba mfalme wa kaskazini anakua mkuu sana katika wakati wa mwisho. Yeye anaiteka “nchi ya uzuri” (Palestina), na mbali na kuziteka nchi zingine nyingi, anaziteka pia Edomu na Moabu na Amoni (nchi za Waarabu) ambazo hata hivyo katika wakati “zinaokoka mkononi mwake” — zikajiweka huru. Isitoshe, linasema Andiko: {2TG42: 25.1}

Aya ya 42 — “Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, na nchi ya Misri haitaokoka.”

Hili kwa kweli huonyesha kwamba “katika wakati wa mwisho” dola moja kubwa ambayo imekuwa ikitawala nchi hizi, ambazo kati yazo ni pamoja na Misri na Palestina, inazipoteza na kuwa ndogo, ilhali dola nyingine inaziteka na hata kuwa kubwa . {2TG42: 25.2}

Kwa karne nyingi ufalme wa Uturuki ulizitawala hizi nchi, na historia hunakili kwamba Uturuki kurudi nyuma mara ya kwanza kulitukia karibu mwaka 1699. Tangu wakati huo, Uturuki umekuwa ukidhoofika na mataifa ya Ukristo yakifaidika, lakini ni Uingereza Kuu haswa ambayo imeziteka nchi zilizotajwa na majina katika unabii huu. Ndio ufalme ambao umeziteka nchi zingine nyingi isipokuwa hizi na umekua mkubwa katika wakati wa kudhoofika kwa ufalme wa Uturuki. {2TG42: 25.3}

Bila shaka, kwa hivyo, kweli hizi za kihistoria, mbali

25

na zingine ambazo hatujataja, huthibitisha kwamba ukiinuka kutoka kwenye mapango kusini mwa Palestina, ufalme wa Uturuki, ujao baada ya Waptolemi, hushikilia jina “mfalme wa kusini”; na mataifa kaskazini mwa Pal-estina, mataifa ya Kikristo yaliyoinuka kutoka kwenye ufalme wa Warumi (na sasa Uingereza Kuu haswa) hushikilia jina “mfalme wa kaskazini.” Na kwa sababu kudhoofika kwa ufalme wa Uturuki kulianza mwaka 1699, na ukuaji wa himaya ya Uingereza ulianza katika wakati uo huo, mwanzoni mwa karne ya kumi na nane kwa hivyo ndio mwanzo wa “wakati wa mwisho.” {2TG42: 25.4}

Hatimaye, kwa sababu sasa tunaona kwamba vita vya Waislamu na mataifa ya Kikristo vimetajwa katika un-abii kwa msisitizo maalum kwamba Misri na Palestina, katika wakati wa mwisho, zinaachiwa mfalme wa kaskazini kama sehemu ya mateka yake, hawa wafalme bila shaka wanajulikana. Na anguko la moja na ukuaji wa yule mwingine baada ya Azimio la Corlowitz mwaka 1699 na ambalo “Mustapha wa 2 alikubali kutupilia mbali madai yake kwa Transylvania na sehemu kubwa ya Hungary, kuachilia Marea kwa Venetians kurejesha Polalia na Ukraine kwa Poland, na kuacha Azov kwa Warusi” (Kamusi ya Maelezo ya Karne ya Ishirini, Gombo la 6, uk. 247) hakika huanzisha mwanzo wa wakati wa mwisho. {2TG42: 26.1}

Aya ya 43, 44 — “Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Mis-ri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake. Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi.”

Aya hizi hufichua kwamba baada ya kuteka Misri na Palestina, mfalme wa kaskazini anaingia kwa pambano lingine, si kwa sababu ya mfalme wa kusini, sio na Uturuki, ila badala yake ni kwa sababu ya uvumi kutoka mashariki na kaskazini unaomtaabisha. Huo unamfanya aondoke

26

kwa hasira kubwa kuwaangamiza wengi. Lakini hashindi chochote cha kutajwa, na kwa mujibu wa aya inayofu-ata baadaye anatishwa na kuufikia mwisho wake. Vita hii haswa, kwa hivyo, inaleta maporomoko ya kwanza kwa mfalme wa kaskazini tangu kuporomoka kwa mfalme wa kusini mwaka 1699. {2TG42: 26.2}

Ujerumani na Urusi kutoka kaskazini, pia Japani kutoka mashariki, uvumi ambao uliiweka Uingereza Kuu na washirika wake katika Vita vya 2 vya Dunia, kwa hivyo ni “habari” ambazo zilileta vita na ambazo, ingawa il-ivyoonekana kuwa walishinda vita, viliudhoofisha badala ya kuuimarisha Ufalme wa Uingereza. {2TG42: 27.1}

Aya ya 45 — “Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataif-ikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.”

Sehemu ya pekee ya Danieli 11 ambayo bado haijatimizwa ni aya hii, ya mwisho kwa sura hiyo, namaadamu unabii huu umefanywa ueleweke tu wakati ambapo unatimizwa au baada ya kutimizwa, aya ya 45 haijakuwa wazi jinsi tungependa kuielewa. Ndiposa kuhusu mahali pa hema zake na mwisho wake, na pia iwapo dola nyingine ya Kikristo italirithi jina “mfalme wa kaskazini” kabla ya aya ya 45 kutimizwa, wakati pekee ndio uta-kaonyesha ukweli wote. {2TG42: 27.2}

Jambo ambalo Uvuvio hufanya kuwa wazi kabisa ni ukweli kwamba msimamo ufuatao wa mfalme ndio mwi-sho wake, ilhali wote wanatazama na kusikiliza, lakini hakuna anayekuja kumsaidia. {2TG41: 27.3}

Kwa sababu tumehakiki mwanzo wa “wakati wa mwisho,” hebu sasa tuhakiki mwisho wa “wakati wa mwi-sho.” Kwa ajili ya nuru kwa mada hiyo tufungue– {2TG42: 27.4}

Ufu. 19:19-21 — “Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufan-ya vita Naye

27

aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi Yake. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake Yeye aliyeketi juu ya yule fara-si, upanga utokao katika kinywa Chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”

Yule “Mnyama,” “nabii wa uongo,” na “waliosalia” wametajwa hapa. Wao ni nani? {2TG42: 28.1}

Kwanza yule mnyama na nabii wa uongo halafu waliosalia, wale walioachwa, wanatupwa katika ziwa la mo-to. Kwa sababu “mnyama” na “nabii” ni vitambulisho maalum vya ulimwengu, waliosalia (wale walioachwa) wanawakilisha wa dunia wote ambao hawakutubu waliowaunga mkono yule mnyama na nabii. Kuangamizwa kwa yule nabii, mnyama, na waliosalia, kwa hivyo, ni mwisho wa dunia — mwisho wa wakati wa mwisho. {2TG42: 28.2}

Licha ya aya hizi za Maandiko, sura ya ishirini ya Ufunuo hufichua kwamba pamoja na tukio hili la kabla ya millenia katika sarakasi ya dhambi, Utawala wa millenia wa Kristo na Kanisa unaanza (Ufu. 20:1-3), ambao mwisho wake watafufuka wote ambao hawakuwa na “sehemu katika ufufuo wa kwanza.” Ufu. 20: 5, 6. {2TG42: 28.3}

Sasa tumeona kwamba “wakati wa mwisho” hutanda kutoka mwanzoni mwa kudhoofika kwa Dola ya Uturuki, hadi mwisho wa dunia, na ya kwamba mwisho wa dunia ni mwisho wa watu wote isipokuwa Kanisa — “wale walioishi na kutawala pamoja na Kristo miaka elfu.” {2TG42: 28.4}

Hebu sasa tuone lile linalotukia kati ya hizi ishara elekezi mbili. Tutaendelea na unabii wa Danieli kupitia sura ya kumi na mbili. {2TG42: 28.5}

28

Dan. 12:1 — “Na wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”

“Na wakati huo” — yaani, wakati mfalme wa kaskazini atakapoifikia ajali yake (Dan. 11:45) — Mikaeli atasimama na kuwaokoa watu Wake, Kanisa, wote ambao wameandikwa katika Kitabu kile. Lipi lingine litatukia? — {2TG42: 29.1}

Hapa umeonyeshwa ufufuo wa umati mseto, waovu na wenye haki — wapumbavu na wenye busara. Ufufuo huu, basi, si ule “ufufuo wa kwanza” kabla ya millenia, wala ufufuo ule wa waovu baada ya millenia (Ufu. 20:5, 6), ila ni maalum. Iwapo wenye hekima ambao watawaongoza wengi kutenda haki ni kati ya wale waliofufuliwa katika ufufuo huu maalum, na ikiwa wataang’aa kama nyota milele na milele, basi ufufuo huu maalum unatukia katika wakati wa rehema. {2TG42: 29.2}

Aya ya 4 — “Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwi-sho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”

Ufahamu wa hicho kitabu na maneno yake, yalipaswa kutiwa muhuri hadi wakati wa mwisho. Katika wakati wa mwisho, kwa hivyo, kitabu kingefunuliwa. Maarifa pia yangeongezeka. Isitoshe, wengi wangekimbia huko na huko; yaani, mawasiliano yangekuwa ya kasi sana. Hayo yote tayari tumeona yakitukia katika “wakati wa mwisho.” Hivyo hamna nafasi ya kutilia shaka kuhusu wakati tunamoishi — wakati wa mwisho. {2TG42: 29.3}

29

Aya ya 8-10 — “Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje? Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wa-kati wa mwisho. Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.”

Hapa Uvuvio wenyewe hufafanua kwamba hakuna mtu, hata Danieli mwenyewe angeweza kuelewa kitabu hicho kabla ya wakati wa mwisho. Na pia, wakati waovu wangeendelea kutenda mabaya, wengi wangetakaswa, kufanywa weupe na kupimwa; yaani, utakaso wa kanisa, kupatakasa Patakatifu (Dan. 8:14), kungetukia katika wakati wa mwisho. Katika maneno ya nabii Malaki utakaso wa Patakatifu unatanguliwa kwa tangazo hili: {2TG42: 30.1}

Mal. 3:1-3 — “Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anaku-ja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.”

Badala ya kusema “Patakatifu,” Uvuvio katika mfano huu unasema “Hekalu.” Na badala ya kusema “utakaso,” Unatumia maneno kusafisha na kutakasa. Mtume Petro, hata hivyo, huchagua kuuita utakaso wa Patakatifu, “Hukumu” katika “nyumba ya Mungu”: {2TG42: 30.2}

1 Petro 4:17, 18 — “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii

30

Injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?”

Katika mfano, hata hivyo, Yesu huufafanua utakaso wa Patakatifu hivi: {2TG42: 31.1}

Mat. 13:30 — “Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.”

Hapa imewekwa wazi kwamba katika tukio hili waovu miongoni mwa wenye haki wanafananishwa na magugu, na wakati wa utakaso wenyewe, Hukumu, umefananishwa na “mavuno,” ila kwamba utakaso wenyewe unalinganishwa na utengo wa ngano na magugu. {2TG42: 31.2}

Aya ya 2 — “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”

Tena, katika aya ya 47 na ya 48 Kristo huonyesha ulinganifu kati ya Kanisa “juya”; watu Yeye huwalingani-sha kwa “samaki”, na utakaso kwa utengo, ilhali katika Mathayo 25 Yeye huliita Kanisa lililotakaswa Ufalme wa Mungu, na watu Yeye huwalinganisha kwa “wanawali”, na utakaso Yeye huuonyesha kwa mlango ambao hu-waingiza wenye busara lakini huwazuilia nje wapumbavu. Bali mfano Wake wa pili wa Mathayo 25, utengo, tunaambiwa, utakuwa kama bwana anayekuja kufanya hesabu na watumwa wake. Wale ambao hawajafanya chochote chema kuuendeleza ufalme Wake (ambao hawakufanya biashara na kuongeza talanta Zake — Mat. 25:27) wanatupwa nje, huko kusaga meno yao katika “giza la nje.” (Mat. 25:30). Katika mfano Wake wa tatu utengo Yeye huufananisha na mchungaji ambaye huwatenga mbuzi kutoka kwa kondoo (wadhambi kutoka kwa watakatifu); mbuzi wamehukumiwa kufa ila kondoo wanapewa haki ya kuingia Ufalme. {2TG42: 31.3}

Nabii Ezekieli, hata hivyo, anaelezea utakaso wa Patakatifu kutoka upande mwingine: {2TG42: 31.4}

31

Ezek. 9:1, 2, 4-7 — “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba …. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya ma-chukizo yote yanayofanyika kati yake …. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika pa-takatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji.”

Aidha kwa kielelezo hiki kilicho wazi, Uvuvio, kupitia nabii Danieli hufunua kwamba Patakatifu patatakaswa sio tu kutoka kwa wadhambi, bali kutokana na makosa ya mafundisho, pia, maana malaika mmoja aliuliza, — {2TG42: 32.1}

Dan. 8:13, 14, 17 — “… maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo uki-wa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa …. Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.”

Ya daima, kosa lifanyalo ukiwa, pia Patakatifu na jeshi vinahusu mafundisho na watu. Vyote vinapaswa kutakaswa. Na malaika akafafanua kwamba

32

utakaso wa Patakatifu (utakaso kutoka kwa makosa na unafiki) unatukia baada ya siku 2300, katika wakati wa mwisho. {2TG42: 32.2}

Isitoshe, kupitia nabii Zekaria Bwana hufanya mfano mwingine wa kushangaza ambao unaonyesha kwamba watakatifu wenyewe pia wanapaswa kutakaswa: {2TG42: 33.1}

Zek. 3:1-5 — “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na aku-kemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa mo-toni? Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika. Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi. Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa Bwana akasimama karibu.”

Maadamu tumeona tayari kwamba nyumba ya Mungu itatakaswa kutoka kwa makosa na kutoka kwa Wanaf-iki, hapa katika unabii wa Zekaria tunaona kwamba watakatifu wenyewe wanatakaswa kutoka kwa dhambi zao — mavazi yao machafu yanaondolewa, na mavazi safi na mazuri yanatolewa badala yake. Awamu hii ya utakaso imeonyeshwa tena na vazi la harusi. (Mat. 22:11). {2TG42: 33.2}

Na sasa hebu niwakumbushe kwamba baada ya magugu kuondolewa, “ngano” haiachwi katika shamba amba-lo ilikua (yaani, watakatifu hawaachwi pale walipokuwa), lakini inawekwa “ghalani.” {2TG42: 33.3}

Zaidi ya hayo, baada ya “samaki wabaya” (wanafiki)kutupwa nje, “samaki wazuri”(watakatifu) wakati huo wanawekwa “ndani ya vyombo,” hawaachwi ndani ya “juya” (hawaachwi mahali

33

ambapo utakaso ulitukia). Ndiposa kanisa likishatakaswa hivyo, watakatifu wanaondolewa kutoka mahali pao pa awali na kuwekwa mahali salama — mbali na mivuto na mazingira ya kidunia. Baada ya kutakaswa, lazima wanawekwa safi hivyo. Na mahali hapo ni wapi? Wa-Ufunuo analo jibu: {2TG42: 33.4}

Ufu. 14:1, 4, 5 — “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya Mlima Sayuni, na wa-tu mia na arobaini na nne elfu pamoja Naye, wenye jina la Baba Yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao …. Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwa-na-Kondoo. Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.”

Waliotakaswa unaona, ni watu 144,000, nao wanapelekwa juu ya Mlima Sayuni. {2TG42: 34.1}

Kwa udhahiri, basi, utakaso u katika sehemu mbili. Watakatifu 144,000 wasio na hila ambao wametiwa mu-huri kutoka kati ya kabila za Israeli (Ufu. 7:4-7), kanisa, ni malimbuko. Wanapelekwa juu ya Mlima Sayuni. Mwishowe baada ya kusafishwa, au utakaso, wa kanisa kutukia, basi umati mkubwa wa Ufunuo 7:9 wana-kusanywa kutoka mataifa yote. Wao wanajumuisha mavuno ya pili, kwa maana ambapo hakuna ya pili haiwezi kuwapo ya kwanza. {2TG42: 34.2}

Mlima Sayuni uko wapi? Mruhusu nabii Mika atuambie: {2TG42: 34.3}

Mika 3:12; 4: 1, 2 — “Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utaku-wa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni …. Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vili-ma; na watu wa

34

mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.”

Huu ni ufafanusi wa Uvuvio wenyewe wa mahali ambapo kanisa lililotakaswa litamiliki. Hapa tunaambiwa kwamba ingawa ufalme wa zamani, wa Kiyahudi, ambao mahali pake ulisimama Mlima Zayuni, ungebomolewa kutoka kwa msingi hadi juu, tunaahidiwa hata hivyo wakati huo huo kwamba Ufalme utarejeshwa katika siku za mwisho na ya kwamba utainuliwa juu ya falme zote, juu ya “milima” na “vilima.” vyote. {2TG42: 35.1}

Tena asema Bwana: {2TG42: 35.2}

Ezek. 36:23-25 — “Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nita-watakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.”

Tunaambiwa hapa kwamba utakaso wa mwisho wa watakatifu, utakaso ambao huondoa alama zote za dhambi, unafanywa baada ya Mungu kuwatoa watu Wake kutoka kwa mataifa na kutoka katika nchi zote, na kuwaleta katika nchi yao. {2TG42: 35.3}

Aya ya 26 — “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama.”

35

Watakatifu wanapofika katika Nchi ya Ahadi, basi moyo unaopendelea dhambi, moyo wa jiwe, unaondolewa na moyo wa matumaini matakatifu, moyo wa nyama, wanapewa. Watu wa Mungu hawatapambana tena na majaribu kutoka ndani ili kutenda haki. Wao, katika kipindi cha moyo wa nyama, itakuwa kawaida kutenda haki ilhali sasa katika kipindi cha moyo wa jiwe ni kawaida kufanya uovu. {2TG42: 36.1}

Aya ya 27 — “Nami nitatia roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda.”

Roho wa Mungu, zaidi ya hayo, watakatifu watapewa kwa wingi, na hivyo watakuwa viumbe vikamilifu vya milele, wakamilifu wenye uwezo wa kutembea katika kanuni za Mungu na hukumu Zake. {2TG42: 36.2}

Aya ya 28 — “Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu.”

Hawatakaa, katika nchi nyingine, asema Bwana, bali katika nchi yao, katika nchi Aliyokuwa amepewa baba zao zamani. Watakaa Palestina. {2TG42: 36.3}

Sasa unaona wazi kwamba Wayahudi ambao hawajaoongoka wanaojitahidi kuichukua nchi ya Palestina sio watu ambao vifungu hivi vya Maandiko husema. Sasa unaona kwamba Mwarabu, Myahudi, au mtu wa Mataifa, wote mwishowe itabidi waondoke na kutoa nafasi kwa watu walio wasafi na waliotakaswa wa Mungu. {2TG42: 36.4}

Yoeli 3:1, 2 — “Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Ye-rusalemu, Nitakusanya mataifa yote, Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko Nita-wahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya

36

mataifa, na kuigawanya nchi Yangu.”

Hapa unaipata kwa maelezo wazi kama inavyoweza kwamba wakati Mungu atakapowarejesha watu Wake waliotawanywa, wakati huo Atayakusanya mataifa yote katika bonde la Yehoshafati na kuteta kwa ajili ya watu Wake — kwa ajili ya mavuno Yake ya pili — baada Yeye kuwapeleka malimbuko hadi Mlima Zayuni. {2TG42: 37.1}

Isa. 2:3 — “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Zayuni itatoka sheria, na Neno la Bwana katika Yerusalemu.”

Yoeli 3:20,21 — “Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana Bwana Ndiye akaaye Zayuni.”

Hivyo watakatifu watawezeshwa kuishi milele. {2TG42: 37.2}

Isa. 33:24 — “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.”

Na ni lipi lingine litasemwa baada ya watu kukusanywa na kusafishwa? Hili tu: {2TG42: 37.3}

Ufu. 22:11 — “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.”

Kukamilika kwa utakaso kunaleta kikomo cha wakati wa rehema — mwenye dhambi atadumu milele kuwa mdhambi, na mwenye haki milele mwenye haki. Ndipo wale ambao watajikuta nje ya nchi takatifu watalia na kusaga meno yao. Watasema kwa uchungu: {2TG42: 37.4}

37

Yer. 8:20 — “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.”

Hiyo nchi, isitoshe, itagawanywa kati ya makabila lakini sio jinsi ilivyogawanywa zamani. Wakati hautaniru-husu kusoma maelezo yote ya mgawo, lakini, hapa ninao umetokezwa kwa ramani inayoonyesha kwamba nchi hiyo haijawahi kugawanywa hivyo. Kila kabila litapata ukanda wa urefu kamili kutoka mashariki hadi maghari-bi. Sehemu ya Dani ni ya kwanza kaskazini na sehemu ya Gadi ndio ya mwisho kusini. Katika sura ya 47 na 48 ya Ezekieli utapata maelezo kamili ya mgawo huu wa nchi. {2TG42: 38.1}

38

Zaidi ya hayo, nchi yenyewe itatakaswa; kwa maana asema Bwana: {2TG42: 39.1}

Ezek. 38:14, 16; 39:4, 7, 9-14 — “Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu Wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari? …. Nawe utapanda juu uwajilie watu Wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi Yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao …. Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; Nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa nchi, uliwe na wao …. Na jina Langu takatifu nitalifanya kuwa limejulika kati ya watu Wangu Israeli; wala sitaliacha jina Langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, na Aliye Mtakatifu katika Israeli …. Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba; hata ha-wataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao wa-tawateka nyara watu waliowateka wao, na kunyang’anya vitu vya watu walionyang’anya vitu vyao, asema Bwana MUNGU. Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu. Na kwa muda wa miezi saba nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi. Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU. Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya

39

uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta.”

Bado zaidi, sasa utaona sasa kwamba maajabu haya yote Mungu huwafanyia watu Wake, sio kwa sababu wamekuwa wema, au kwa sababu sasa ni wema, lakini kwa jina kuu la Mungu. Sikiza lile ambalo Bwana Mwenyewe anasema: {2TG42: 40.1}

Ezek. 36:22-24 — “Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina Langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaen-dea. Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.”

Kwa mujibu wa hili, Mungu anarejesha nchi kwa watu wake waliochaguliwa, sio kwa sababu wao kama watu ni wema, lakini kwa sababu anataka kulitetea jina Lake mwenyewe kati ya mataifa. {2TG42: 40.2}

Maadamu wakati unajongea kwa utakaso kutukia mwito wa kuamka kiroho utafanywa: {2TG42: 40.3}

Isa. 52: 1 — “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa, wala aliye najisi.”

Uvuvio hapa hutangaza kwamba baada ya mwito huu wa uamsho na matengenezo, tangu hapo watenda dhambi hawataruhusiwa kuwa na sehemu yoyote kati ya watu waliotakaswa. {2TG42: 40.4}

Nabii Nahumu, pia, ni shahidi wa mwito huu

40

wa Matengenezo. Anaandika: {2TG42: 40.5}

Nah. 1:15 — “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike siku-kuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.”

Hapa unaona kwamba tangazo la hafla hii iliyotarajiwa kwa muda mrefu litafanywa na machapisho ya mtu fu-lani. Isitoshe, yeye huchapisha amani na kwa hivyo atangaza kurejeshwa kwa Ufalme. Hii ndio amani pekee am-bayo ulimwengu unaweza kuwa nayo. Haitakuwapo nyingine. Wale ambao wanazishika “sikukuu” takatifu za Mungu na kuzitimiza nadhiri zao watakuwa na amani hii. Hakuna wengine watakaokuwa nayo. {2TG42: 41.1}

Katika uchambuzi wetu leo tumefanya muhtasari baadhi ya mambo ambayo yatatukia katika wakati wa mwi-sho, lakini jambo la muhimu zaidi, kwa kadiri unavyohusika, ni uamuzi ambao umeachiwa sasa kufanya. {2TG42: 41.2}

41

KWA AJILI YA WAHITAJI NG’AMBO

Simu nyingi kutoka ng’ambo zimepigwa kwetu kwa ajili ya mavazi, lakini hatuwezi kutosheleza mahitaji ya daima. Na kwa hivyo ikiwa una nguo yoyote ya akiba katika hali nzuri ambayo ungependa itumike kwa kazi inayofaa, basi tuma mchango wako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG42: 42.1}

42

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, hizi Salamu Mwafaka zinatumwa bila malipo. Zinaweka tu dai moja — wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyajaribu mambo yote na kulishika lililo je-ma. {2TG42: 43.1}

43

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 41, 42

Kimechapishwa nchini Marekani

44

>