fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 27, 28

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 27, 28

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

FIMBO AMBAYO HUNENA INATAKA MATENGENEZO NA KUSABABISHA VITA KUU

KWENYE UKINGO WA ULIMWENGU MPYA MACHONI PA ULIOCHAKAA

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 184, aya ya mwisho– {1TG27: 2.1}

“Sio mpaka uhisi kwamba unaweza kujinyima hadhi binafsi, na hata kuutoa uhai wako, ili kumwokoa ndugu mkosaji, Umeitoa boriti kutoka kwa jicho lako mwenyewe, ili kwamba uwe tayari kumsaidia ndugu yako. Basi unaweza kumjongea, na kuugusa moyo wake. Hakuna mtu aliyewahi kurejeshwa kutoka kwa msimamo mbaya kwa ukali na kulaumiwa; lakini wengi wamefukuzwa hivyo mbali na Kristo, na kuongozwa kuiziba mioyo yao dhidi ya imani. Roho ya upole, nyororo, na mwenendo wa kuvutia, unaweza kumwokoa mkosaji, na kuficha wingi wa dhambi. Ufunuo wa Kristo ndani ya tabia yako mwenyewe utakuwa na nguvu ya kubadilisha juu ya wote unaokutana nao. Acha Kristo adhihirike kila siku ndani yako, na Yeye atadhihirisha kupitia kwako nguvu ya uumbaji ya neno Lake, — mvuto wa upole, wenye kushawishi, wenye nguvu ya kuziumba upya nafsi zingine katika uzuri wa Bwana Mungu wetu.” {1TG27: 2.2}

Kulingana na macho ya Uvuvio hakuna hata mmoja wetu amehitimu kutafuta kosa kwa mtu yeyote. Je! Umekumbuka tulichosoma? — Kwamba tukifikia tu kwa hatua kwamba tuko tayari kuutoa uhai wetu kwa ajili ya ndugu mkosaji, tutawezeshwa kuhitimu kuwasaidia wengine kuyarekebisha makosa yao. {1TG27: 2.3}

Katika nuru ya hili, hitaji letu ni nini, Ndugu, Dada? Je! Hatupaswi kuomba kwa ajili ya uzoefu ambao Kristo adhihirike ndani yetu; kuomba kwa ajili ya uzoefu ambao utatuandaa kuwasaidia wengine badala ya kuwazuia; kuomba ili tuwe na mvuto wa Ukweli wa upole, wa ushawishi na wenye nguvu juu yao? Ndipo tutaweza ku-wajongea kwa hekima wale wanaokosea, kuigusa mioyo yao, na kuwaonyesha makosa yao. Ni hapo tu watatus-ikiliza kwa hakika lakini sivyo mpaka wakati huo. {1TG27: 2.4}

2

FIMBO AMBAYO HUNENA INATAKA MATENGENEZO NA KUSABABISHA VITA KUU

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 8, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu ya alasiri hii inaanza na– {1TG27: 3.1}

Mika 6: 1, 2 — “Basi sasa, sikieni asemavyo Bwana; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako. Sikieni, enyi milima, mateto ya Bwana, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana Bwana ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli.”

Wa kwanza kukumbukwa ni ukweli kwamba mjoli wa Mungu ameamriwa kushindana mbele ya milima, na kwamba vilima vitaisikia sauti yake. Bila shaka, basi, katika andiko hili kama ilivyo mahali pengine kwenye Bib-lia, milima na vilima lazima iwe mifano ya falme na serikali. {1TG27: 3.2}

Yeye atashindana mbele ya milima sio dhidi yake; yaani, anapaswa kutangaza kwamba Bwana anavyo vita na watu Wake, kwamba Yeye anataka matengenezo kamili kati yao, na kwamba hawataki na hawamuungi mkono. {1TG27: 3.3}

Ilionekana katika masomo yaliyopita kwamba unabii wa Mika 4 na 5 utatimizwa katika siku za mwisho, wakati wetu, katika wakati ambapo Uvuvio kwa ufunuo wa unabii huu unataka matengenezo kati ya watu

3

wa Mungu. Unabii sasa ukiwa umefunuliwa kwa mara ya kwanza tangu ulipoandikwa, na matengenezo tayari yanaendelea, ukweli kwamba badala ya kuupokea kwa furaha ujumbe mpya uliofunuliwa, wanasababisha vita katika makanisa yote ya Waadventista, ni wazi kabisa unaashiria kwamba sasa ni wakati wa kushindana mbele ya milima, sasa ni wakati wao (“milima”) kusikia vita vya Bwana na watu Wake. {1TG27: 3.4}

Maneno, Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako, yanamaanisha kwamba hapo awali sauti yake imesikika tu ndani lakini kwamba sasa lazima akutane na hali hiyo hata kama milima, vilima, na misingi ya dunia iliyo imara isikie kwamba Bwana anavyo vita na watu Wake. {1TG27: 4.1}

Mpaka sasa, tumekuwa tu tukicheza na maadui wa Bwana lakini sasa lazima tuzame katika shughuli pasipo kujali ni nani anayesikia. Watu Wake lazima sasa wageuke milele kutoka kwa maneno ya mwanadamu, yawayo yote, na kuweka imani na tumaini lao katika “Bwana asema hivi,” bila kujali Yeye ananena kupitia kwa nani, au sivyo watapotea. Kama wafuasi wa Bwana, tunapaswa kuusikiliza mwito Wake unaorarua moyo kwa ajili ya uamsho na matengenezo: {1TG27: 4.2}

Aya ya 3 — “Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa habari gani? Shuhudieni juu yangu.”

Fikiria kuhusu hili! Mungu mkuu na wa milele akiwasihi wanadamu wadhaifu na wadhambi kama sisi, akitaka kujua kwa nini wanampinga Yeye. {1TG27: 4.3}

Aya ya 4 — “Kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka

4

Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.”

Mungu anasema nasi ambao ni uzao wa manabii, wa mitume, na wa wanafunzi ambao kupitia miaka ya utumwa kati ya nchi za Mataifa tumepoteza utambulisho wetu wa kitaifa. Ijapokuwa hatuwezi kujiita wenyewe Waisrae-li, Wayakobo, au Wayahudi, Mungu hutuita hivyo. {1TG27: 5.1}

Waaminifu wachache wa Mungu katika vizazi vyote walikuwa tayari na hata wenye furaha kwa ajili ya Ukweli na haki kukabiliana na dharau za ndugu zao vipofu na ambao hawakuwa waaminifu. Je! hatupaswi kufurahi kufanya mengi kama hayo? Walishinda mbio na taji, na hakuna sababu kwa nini tushindwe kufanya hivyo. Kwa kweli hatuwezi kumudu kuipoteza thawabu yetu saa hii ya mwisho. {1TG27: 5.2}

Aya ya 5 — “Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Ba-laamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya Bwa-na.”

Hapa tunaambiwa kwamba kuijua haki ya Bwana ni kukumbuka jinsi Mungu alivyoshughulika na baba zetu, kwa maana upendo Wake kwetu sio mdogo kuliko ulivyokuwa kwao. Yeye anatukumbusha juu ya tukio wakati Balaki aliajiri Balamu kumlaani Israeli, na jinsi alivyomsababisha Balaamu kunena kwa niaba Yake na kuwabari-ki watu Wake, kwamba kwa ajili yao Yeye alileta kusudi la mfalme kuwa bure na kumfanya Balaamu atangaze kwa Balaki: {1TG27 : 5.3}

“Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa wataka-yowatenda watu wako siku za mwisho …. Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israe-li; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia. Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki,

5

waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.” Hes. 24:14, 17, 18. {1TG27: 5.4}

Kwa kweli Balaamu akamwambia mfalme wa Moabu: “Nimejaribu sana kupata kibali chako na laana ya Israeli, lakini Mungu ameshinda. Israeli ameshinda; wewe na mimi tumepoteza. Na zaidi, wacha nikuambie ni nini watu hawa watatenda kwa watu wako katika siku za mwisho: Yeye atakayetawala Israeli atampiga Moabu pande zote, na Israeli atakapotenda kwa ushujaa.” {1TG27: 6.1}

Hivyo divyo Balaam alilazimishwa kutabiri kuzaliwa kwa Kristo na kutawala Kwake, na kusababisha Israeli kutenda kwa ushujaa dhidi ya Moabu na majirani zake katika siku za mwisho. {1TG27: 6.2}

Kujua haya yote ni kumjua Bwana haki yetu; kwamba ikiwa Yeye yuko kwa ajili yetu basi hakuna yeyote anayeweza kushinda chochote dhidi yetu; kwamba vita ni vya Bwana; kwamba hatuna haja ya kuwaogopa adui zetu; kwamba chochote tutakachotenda kitafanikiwa pasipo kujali ni nani aliye kwa ajili au dhidi yetu. {1TG27: 6.3}

Aya ya 6, 7 — “Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?”

Kutoka kwa aya hizi ni dhahiri kwamba kufunuliwa kwa maandiko haya huleta uamsho na matengenezo kati ya watu wa Mungu kama vile ulimwengu haujawahi kuona: Wale wanaoupokea Ukweli katika ujumla Wake, waungame kwa unyenyekevu kwamba wao ni wadhambi na kwamba wanataka kujua ubaya zaidi wa kesi yao. Wanatoa kwa furaha kafara chochote na kila kitu; kwa wao hakuna dhabihu iliyo kubwa mno ambayo inaweza kuwaleta karibu na

6

Bwana. Mara tu majivuno ya maoni yao yanapowaacha, mara tu wanapouliza kwa unyenyekevu jinsi ya kuja na kusujudu mbele ya Bwana, mara hiyo tu jibu linawafikia: {1TG27: 6.4}

Aya ya 8 — “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”

Kutenda haki, kupenda rehema, na kutembea kwa unyenyekevu na Mungu wetu ni zawadi kubwa zaidi ambayo mtu anaweza kuleta kwa Bwana. Ili kujifunza jinsi ya kutenda haki, jinsi ya kupenda rehema, na jinsi ya kutembea kwa unyenyekevu, tunaambiwa kwa mkazo: {1TG27: 7.1}

Aya ya 9 — “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.”

Bwana anatangaza kwamba sauti Yake inaulilia mji (kwa kanisa), na kwamba watu wenye hekima wataliona hilo jina, na wataisikia hiyo Fimbo na Yeye aliyeiteua. {1TG27: 7.2}

Kwa udhahiri, hii fimbo inao uwezo wa kunene na kusikilizwa, kwa hivyo amri “Isikieni Fimbo.” kadri tuna-vyojua, fimbo ya pekee ambayo imewahi kunena ni “FIMBO YA MCHUNGAJI.” Zaidi ya hayo, hayakuwa matokeo ya bidii yoyote ya utafiti wa Bibilia kwamba kitabu hiki kiliitwa hivyo, mwandishi hakuwa amelijua andiko hili, wala hakuwa na ufahamu wowote wa kitabu cha Mika wakati huo jina la heshima “Fimbo ya Mchungaji” lilipopeanwa kwa kitabu hiki. {1TG27: 7.3}

Mimi mmoja wapo siwezi kuusahau, kuupuuza, au kuukataa ushauri wa Bwana katika suala hili. Lazima niisikie Fimbo na Yeye Aliyeiteua ikiwa ninatarajia kuwa na

7

makao katika Ufalme Wake. Siwezi kumudu kufanya kinyume, Mungu akinisaidia, kwa maana Yeye Mwenyewe anatangaza kwamba ikiwa ningalijua jinsi ya kuja mbele Yake, ni dhabihu gani inayokubalika Kwake, jinsi ya kutenda haki, namna ya kupenda rehema na jinsi ya kutembea kwa unyenyekevu mbele Yake. Lazima niisikie Fimbo “inayoulilia mji.” {1TG27: 7.4}

Sasa ni juu yetu sote mmoja mmoja kuamua ikiwa tutaisikia sauti ya mwanadamu au Sauti ya Fimbo ya Mungu. Huu sasa ni mtihani wa kila mtu, na lazima liwe ni hangaiko la kila mtu, kwa maana mojawapo wa sauti hizi mbi-li — sauti ya wanadamu au Sauti ya Fimbo ya Mungu — itaamua hatima ya kila mtu ama kifo cha milele au uzima wa milele. {1TG27: 8.1}

Kwa sababu ujumbe huu unatangaza kwamba siku kuu na ya kutisha ya Bwana imekaribia — kwamba Hukumu kwa ajili ya Walio hai iko karibu kuanza, na kwa kuwa nabii Isaya alipewa maono ya Bwana kuingia ndani ya hekalu Lake kwa ajili ya kazi hii ya hukumu, Uzoefu wa nabii wakati alipokuwa bado katika maono lazima, kwa hivyo, uwakilishe uzoefu wa watumwa wa Mungu ambao wataitangaza siku ya Bwana. Uzoefu na utume wake lazima uwe uzoefu wetu na utume wetu: {1TG27: 8.2}

“Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi. Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao

8

na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.” Isa. 6: 8-10. {1TG27: 8.3}

“Bwana wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu. Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.” Isa. 8: 13-15. {1TG27: 9.1}

Aya ya 10, 11 — “Je! Hata sasa hazina za uovu zingalimo nyumbani mwa wabaya, na kipimo kilichopun-guka, ambacho ni chukizo? Je! Naweza kuwa safi nami nina mizani ya udhalimu, na mfuko wa mawe ya kupimia ya udanganyifu?”

Hapa inaonyeshwa dhahiri kwamba vitu hivi vya kuchukiza — hazina zilizopatikana kwa vipimo vilivyopungua bado ziko kwenye nyumba ya waovu. Kusudi la kupata utajiri isivyo haki kwa gharama ya jasho la mwingine, limekemewa hapa. Machukizo haya yote, yanayoongozwa na ubinafsi, lazima ziondolewe mbali na wote ambao wanataka kuiokoka siku kuu na ya kutisha ya Bwana. {1TG27: 9.2}

Swali la mwisho la Bwana, “Je! Naweza kuwa safi nami nina mizani ya udhalimu, na mfuko wa mawe ya kupim-ia ya udanganyifu?” Linaashiria kwamba wengine bado wananing’inia kwa mizani zao za udanganyifu, na kima-kosa wanatarajia kuhesabiwa miongoni mwa wasafi. {1TG27: 9.3}

Zipo aina mbili za wezi. Mwizi namba ya kwanza ni mtu ambaye huiba wazi. Mwizi namba mbili ni mtu ambaye katika biashara huweza kupata kidogo zaidi ya kile ambacho ni chake mwenyewe. Hajali ikiwa katika shughuli hiyo mwenzake anapata kidogo au sifuri. Anachojali ni kwamba yeye mwenyewe anaendelea vizuri. Aina hii ya wizi ni mbaya zaidi kwa sababu inatendwa

9

hata na wale wanaoitwa eti Wakristo bora. {1TG27: 9.4}

Aya ya 12 — “Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kinywani mwao.”

Matendo ya dhulma, kusema uwongo na wizi, unatangaza Uvuvio, yapo miongoni mwa watu wa Mungu. {1TG27: 10.1}

Aya ya 13 — “Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako.”

Wakati umekuja, Ndugu, Dada, kusahau ubunafsi na kuwa mwaminifu kwa watu wote, kugundua kwamba ubinafsi ni kama ulivyo mwili wa mtu aliyekufa aliofungwa mgongoni mwa mtu ili kufyonza nguvu na kumfan-ya kuwa mgonjwa kitandani. Kwa kama hawa watu wa uroho, Bwana atangaza: {1TG27: 10.2}

Aya ya 14, 15 — “Utakula, lakini hutashiba; na fedheha yako itakuwa kati yako; nawe utahama, lakini hutachukua kitu salama; na hicho utakachochukua nitakitoa kwa upanga. Utapanda, lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai.”

Aya ya 16 — “Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.”

Badala ya kutembea katika shauri la Fimbo ya Mungu, waovu hutembea katika mashauri ya waovu. Na washauri wao ni waovu kama nini? — Uvuvio hutangaza kwamba wao ni waovu kama walivyokuwa wale wa nyumba ya

10

Omri na Ahabu. (Soma 1 Wafalme 16:25, 26, 29, 30, 33.) Kwa sababu hiyo hatma yao itakuwa hatma ya nyum-ba ya Ahabu. (Soma 2 Wafalme 10:10, 11.) {1TG27: 10.3}

Hakika Mika 6 haiachi shaka lolote kwamba wakati umefika kabisa kwa watu wa Mungu kuzama katika shughu-li kuliko hapo awali. Ujumbe ambao tumekabidhiwa, Uvuvio unaamuru, unapaswa “kutawanywa kama majani ya vuli.” — “Shuhuda,” Gombo la 9, uk. 231. Na hapa yapo majani. {1TG27: 11.1}

Msaada wa Lazima kwa Ajili ya Mtunzi wa Nyumba

Jumuiya ya K. I. inatangaza kwamba Kitabu chake cha “Kitabu cha Mapishi-sahihi “ sasa kinaweza kutolewa kwa senti 25 kwa sarafu au stampu. Usijaribu kuishi bila kitabu hiki kipya cha kurasa 76 cha mapishi ya mla mboga. Kwa jina lako kamili na anwani pamoja na jina la kanisa lako, andika kwa Jumuia ya K. I. ya Amerika, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani. Na bila shaka hautataka kuwa bila mwenzi wake, “Kabari Inayoingia Kitabu cha Afya,” ambacho unaweza kukipata kwa nyongeza ya senti 15. {1TG27: 11.2}

11

WAZO LA SALA

Ukweli Utakuweka Huru

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 186, aya ya kwanza na ya pili. Aya hizi, utaona, zime-jengwa kwa andiko ambalo husema, “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu.” {1TG28: 12.1}

M.B., uk. 186 — “Yesu hapa anataja daraja ambalo halina hamu ya kuokoka kutoka katika utumwa wa dhambi. Kwa kujifurahisha katika ufisadi na uovu, asili zao zimepotoshwa sana hivi kwamba huambatana na uovu, na hawatatenganishwa nao. Watumwa wa Kristo hawapaswi wajiruhusu kuzuiliwa na wale ambao wataifanya injili iwe suala la ubishi na dhihaka. {1TG28: 12.2}

“Lakini Mwokozi hakuipita kamwe nafsi moja, awayo yote iliyozama katika dhambi, ambayo ilikuwa tayari kupokea kweli za thamani za mbinguni. Kwa watoza ushuru na makahaba maneno Yake yalikuwa mwanzo wa maisha mapya …. Chini ya mandhari ya chuki na dharau, hata chini ya uhalifu na upotovu, inaweza kuwa imefichwa nafsi ambayo neema ya Kristo itaiokoa, kung’aa kama kito kwenye taji ya Mkombozi.” {1TG28: 12.3}

Hapa tunaona kwamba katika taarifa Yake, “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu,” Kristo huwaagiza wafuasi Wake wajiepushe na kujaribu kuushinikiza ukweli wowote wa Bibilia kwa wale ambao hawataki kuwekwa huru kutoka kwa dhambi. Haijalishi ni kimo gani mtu anaweza kuwa ameanguka dhambini, Mungu hataipuuza hata nafsi moja ambayo iko tayari kusaidiwa, na iliyo tayari kuipokea na kuitenda Kweli. Kwa uhakikisho huu, hebu tuombe kwa ajili ya ongezeko la tumaini la kuokoka kutoka katika utumwa wa dhambi. Hakika jambo la muhi-mu sio jinsi wazuri au wabaya ambavyo tulivyo au tumekuwa, lakini ni jinsi tulivyo rahisi na wanyenyekevu kwa Ukweli wa sasa tulio nao wakati Unapokunjua. Mzigo halisi wa ombi letu, unapaswa kuwa kwamba tuyashike maono ya Ukweli ambao huweka huru ikiwa utapokelewa Chuo kinapokunjua. {1TG28: 12.4}

12

KWENYE UKINGO WA ULIMWENGU MPYA MACHONI PA ULIOCHAKAA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 15, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutajifunza sura ya saba ya Mika. Sura hii inaleta kwa umakini wetu migawanyiko mitatu ya wakati ambayo ndani yake hali tatu tofauti huenea juu ya dunia. Hali ya kwanza imeandikwa katika aya nne za kwanza; ya pili katika aya ya 5-14; na ya tatu, katika aya ya 15 hadi mwisho wa sura hii. {1TG28: 13.1}

Sasa hebu tuanze somo letu na– {1TG28: 13.2}

Mika 7: 1 — “Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa hari, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.”

Kitu kimelinganishwa na mizabibu baada ya matunda yake kukusanywa ndani. Ni nini? Tutapata jibu kwa kusoma— {1TG28: 13.3}

Aya ya 2-6 — “Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu. Mikono yao inayashika mabaya wayatende kwa bidii; mtu mkuu aomba rushwa, kadhi yu tayari kuipokea; mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja. Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama

13

mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya wal-inzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao. Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.”

Wenye haki wakiwa wameondolewa duniani na waovu pekee wameachwa ndani yake, hali yake inawakilishwa na mizabibu ambayo imetwaliwa matunda yake na kuachwa katika hali ya upweke na woga kwa sababu ya uovu kamili. Mchekecho huu unatukia katika siku ambayo Mungu anawazuru walinzi Wake; yaani, katika siku ya Hukumu, siku ambayo Yeye anaitenga “ngano” kutoka kwa magugu (Mat. 13:30), samaki wazuri kutoka kwa samaki wabaya (Mat. 13:47, 48) kondoo kutoka kati ya mbuzi (Mat. 25: 31-46). {1TG28: 14.1}

Aya ya 7-10 — “Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia. Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu. Nitaivumilia ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa nimemwasi; hata atakapo-nitetea teto langu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake. Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi Bwana, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.”

Aya hizi zinawasilisha watu waaminifu wa Mungu, watu ambao unabii huu umefunuliwa kwao wakiwa na adui ambaye analo jina la kike “yeye”. Huyu “yeye” anahoji na kutilia shaka uwepo wa Mungu kati ya watu Wake, anawadhihaki kwa imani yao. {1TG28: 14.2}

14

Kwa sababu unabii huu sasa kwa mara ya kwanza umeletwa kwenye nuru unajumuisha ujumbe wa saa hii; na maadamu juu yetu umetwikwa mzigo wa kuupeleka ujumbe kwa kanisa, na kwa sababu yeye ni adui wetu kama lilivyokuwa kanisa la Kiyahudi kwa Mkristo, Uvuvio unashuhudia hivyo dhidi yake, na kutangaza maangamizi yake. {1TG28: 15.1}

Kisha itakuwa kwamba “Na mataifa wataiona” haki ya watakatifu, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.” Isa. 62: 2. {1TG28: 15.2}

Aya ya 11, 12 — “Ni siku ya kujengwa kuta zako! Siku hiyo mpaka utasongezwa mbali. Siku hiyo wa-takujia kutoka Ashuru na miji ya Misri, na kutoka Misri mpaka huo Mto, na kutoka bahari hii mpaka bahari hii, na kutoka mlima huu mpaka mlima huu.”

Kwa sababu amri hii inaondolewa katika siku ambayo Ufalme (kanisa lililotakaswa) umerejeshwa, katika siku ambayo watakatifu wameimarishwa, amri hiyo haina madhara kwao. Katika siku hiyo, unatangaza Uvuvio, kutakuwa na kusanyiko kubwa kutoka Ashuru na kutoka miji yenye maboma, hata kutoka bahari hii mpaka ba-hari hii na mlima huu mpaka mlima huu. Ujumbe huu, kwa hivyo, ndio unaotangulia mavuno ya dunia, siku kuu na ya kutisha ya Bwana, Hukumu kwa ajili ya Walio Hai, siku ambamo mambo yote yatarejeshwa (Marko 9:12). {1TG28: 15.3}

Aya ya 13, 14 — “Hata hivyo nchi itakuwa ukiwa kwa sababu ya hao wakaao ndani yake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao. Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, mwituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.”

15

Kabla ya ahadi hizi kutimizwa, hata hivyo, Uvuvio ulitangaza kwamba ardhi itakuwa ukiwa, kutawanywa kwa watu kungalitukia kwanza. {1TG28: 16.1}

Fimbo hii ya Mungu haineni tu, bali Hulisha pia. Na inaweza kuwa Nini iwapo sio “chakula kwa wakati unaofaa”? ikiwa sio ujumbe wa saa hii? Watu, yanaelezea maandiko, ni wale wakaao peke yao, mwituni katikati ya Karmeli. Unabii, wa ajili ya siku hii na saa hii unapendekeza ujumbe ambao Fimbo inasheheni, na ambao Karmeli hutoa, hakuna mwingine. {1TG28: 16.2}

Aya ya 15 — “Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonyesha mambo ya ajabu.”

Tumepewa ahadi kwamba uzoefu wa watakatifu utakuwa sawa na ule wa vuguvugu la Kutoka; Yaani, kama vile walivyoongozwa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu wa Mungu, na kuletwa salama katika nchi ya ahadi, ndivyo itakavyokuwa sasa. {1TG28: 16.3}

“Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Is-raeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.” Isa. 11:11, 12. {1TG28: 16.4}

Aya ya 16-18 — “Mataifa wataona, na kuzitahayarikia nguvu zao zote; wataweka mikono yao juu ya vinywa vyao, masikio yao yatakuwa na uziwi.”

16

“Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali wali-mojificha, wakitetemeka; watakuja kwa Bwana, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako. Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.” {1TG28: 17.1}

“Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu. Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni wa-tawatii. Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.” Isa. 11: 13-15. {1TG28: 17.2}

Jinsi itakavyokuwa kuu siku ya Bwana kwa waaminifu, itakuwa ya kuogofya hivyo kwa wakafiri. {1TG28: 17.3}

Aya ya 19 — “Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.”

Mungu wetu ni wa ajabu kweli kweli! Yeye hadumishi hasira Yake. Yeye hupenda rehema. Hazikumbuki dhambi za wanaotubu, Yeye huziondolea mbali mahali ambapo haziwezi kupatikana tena. {1TG28: 17.4}

Aya ya 20 — “Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Ibrahimu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.”

Uvuvio unathibitisha tena ahadi zote za Mungu. Hazishindwi

17

kamwe. Unabii Wake ni hakika. Tuko kwenye kizingiti cha ulimwengu mpya machoni pa uliochakaa — hivi ka-ribuni haitakuwapo dhambi tena. “Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.” Ufu 7: 15-17. {1TG28: 17.5}

Hata sasa, asema Bwana, “Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani. {1TG28: 18.1}

“Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. {1TG28: 18.2}

“Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu. Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu. {1TG28: 18.3}

“Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Nao watawaita, Watu wa-takatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe

18

utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.” Isa. 62: 6-12. {1TG28: 18.4}

Tuko hakika kwenye kizingiti cha ulimwengu huu mpya machoni pa uliochakaa. Hebu matendo yetu na imani sasa ijibu maswali ya kushangaza zaidi ya Bwana tangu ulimwengu kuanza: {1TG28: 19.1}

“Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. {1TG28: 19.2}

“Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. {1TG28: 19.3}

“Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi. Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.” Mal. 3: 1-6. {1TG28: 19.4}

19

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 27, 28

Kimechapishwa nchini Marekani

20

>