fbpx

Kuripoti Shughuli Zisizo Za Uadventista

 

Barua ya Shughuli Zisizo Za Uadventista

[Ikiwa Barua ya ukurasa mmoja iliyoambatanishwa katika Trakti hii]

Mpenzi Mshiriki wa Kanisa:

Wewe bila shaka unajua kwamba katika miaka michache iliyopita makanisa yetu yamevamiwa, kwa mfano, na kikundi kinachojulikana kama Wadaudi Waadventista wa Sabato ambacho vichapisho vyake vinaitwa Fimbo ya Mchungaji. Ingawa sisi kama watu tumefanya kila kitu kwa uwezo wetu kuwaweka chini na nje, lakini licha ya hayo wanaendelea kukua na kukaa katika makanisa yetu. Na kama ilivyoripotiwa kwamba wameenea na bado wanaenea kote katika ulimwengu wa Waadventista hata zaidi ya inavyoonekana, kamati maalum ya uchunguzi iliandaliwa. Kamati hiyo, zaidi ya hayo, iliundwa na watu kutoka majimbo mengi na kutoka nchi za nje, na kwa vile kazi hiyo ilifanywa kwa mawasiliano ya ana kwa ana na mawasiliano ya barua, ilizuru ulimwengu wote wa Waadventista. Kwa hivyo, habari katika ripoti yake sio uvumi wa mtu, lakini habari ya mwanzo iliyokusanywa kutoka kwa watu wengi ulimwenguni. {UAL: 1.1}

Mara tu baada ya kazi yetu kuanza, tuligundua kwamba idadi kubwa zaidi ya Wana-fimbo walikuwa wasomaji wa chini kwa chini na waamini. Na ingawa wale waliojitokeza wazi kwa ajili ya Fimbo na kwa sababu hiyo walitupwa nje ya makanisa, bado wao, pia, wangali makanisani, wakitembea bega kwa bega na washiriki! Mistari hii, kwa hivyo, imeandikwa kwako kwa sababu tunahisi hakika kwamba unaijali sauti ya Mungu na una hamu ya kufanya jambo sahihi kwa wakati unaofaa ili kuja kwa msaada wa Bwana. {UAL: 1.2}

Tulipoiona shida ambayo watu wetu walikuwa ndani, tulifikiri ni busara kufanya uchunguzi wa kina wa shughuli ya Fimbo inayokua kwa haraka kuliko vile ilivyopangwa hapo awali. Kijizuu kilichoambatanaishwa kinasheheni ripoti kamili ya lile kamati ilipata na masadikisho yake ya mwisho na mapendekezo yalivyo. Ripoti hiyo, utaona, inachukua hatua ya kwanza kuelezea ni nini Dhehebu linainuka kupinga, na ijayo kuelezea suluhisho la shughuli zote kama hizi zisizo za Uadventista ambazo ziko kati yetu. Kama wewe, kwa kweli, ungetaka kujua sio tu kupata lakini pia tiba, na jinsi wewe, pia, unavyoweza kujiingiza kwenye vita dhidi ya watenda maovu, tunahisi hakika kuwa utataka kukisoma kijizuu hicho kwa uangalifu. {UAL: 1.3}

Mwaminifu wenu,

KAMATI YA UTAFITI YA SHUGHULI ZISIZO ZA UADVENTISTA

 

Kuripoti Shughuli Zisizo

Za Uadventista

[Picha]

1

RIPOTI YA KWANZA YA SHUGHULI ZISIZO ZA UADVENTISTA KAMATI YA UTAFITI

Huu ni muhtasari kamili wa matokeo yetu wakati tulipokuwa tukichunguza mpenyezo na shughuli za Fimbo ya Mchungaji katika makanisa yetu, pia maoni ya watu ambao hujisomea na kufikiri wenyewe, iwe wamekosea au wako sawa. {RUA: 2.1}

Mara tu baada ya kazi ya kamati yetu kuanza sisi sote tulikuja kusadiki kwamba wapo Wana-fimbo wengi zaidi katika makanisa yetu kuliko ilivyoonekana na ya kwamba wengine wengi kwa njia moja au nyingine wanaweza kuangaliwa angalau wanawaunga mkono. Hili litaonekana kutoka kwa kemeo tulilokumbana nalo kila mahali tulikokwenda. Tulikabiliwa na mazungumzo yaliyoungwa mkono na dondoo kama zifuatazo: {RUA: 2.2}

Wengi wa watu wetu wanaofikiri sana walisema, “Ufanisi wa kupenyeza kwa Fimbo ni kwa sababu ya namna tunavyowashughulikia wafuasi wake.” Walisema, “Ni kwa sababu tumefanya mafundisho yetu kwa upumbavu kuonekana yasiyopatana na shughuli zetu zisizo za haki ili kuzua mashaka kwa unyofu wetu. Tukiwa sikuzote tumeteta dhidi ya wale ambao

2

walifikiri ni hekima kuwatupa nje kutoka kati yao wale waliodhani walikuwa makosani, na sasa sisi wenyewe tunafanya vile vile kama walivyofanya hakuwasaidii watu wetu. Walei,” walisema,”kwa hivyo wanapoteza imani kwa watu wanaoongoza.” {RUA: 2.3}

Wengine walisema, “Ufanisi wa Fimbo ni kwa sababu ya kupuuza sana amri ya Bwana, kuruhusu ngano na magugu kukua pamoja hadi kwa mavuno; ya kwamba kusema kwetu mavuno bado hayajakuja hutufanya kuwa waongo kadiri tunapoendelea kuitupa nje magugu ya Fimbo.” Bado wengine walifikiri kwamba kwetu kuwatupa nje Wana-fimbo sio kitu kipungufu cha kuinyakua nafasi ya malaika, kwamba si dhambi ndogo na tunailipia. Wengi wao walitusomea, na wengine walinukuu yafuatayo: {RUA: 3.1}

“… Bwana hutukataza kuchukua hatua kwa njia yoyote ya ghasia dhidi ya wale ambao tunafikiri wanakosea, na hatupaswi kutekeleza kuwatenga na kuwashtumu wale ambao ni wenye makosa.’’ — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 47. {RUA: 3.2}

“… Kazi ya utengo imepewa malaika wa Mungu, na haijakabidhiwa mikononi mwa mtu yeyote.” — Kimenukuliwa. {RUA: 3.3}

Naliambiwa mara kwa mara kwamba kutomjali kwetu

3

Bwana ndilo kosa letu kubwa. Kisha wakasoma hii: {RUA: 3.4}

“… Hatupaswi kufikiri, kama walivyofanya Wayahudi, kwamba maandishi na maoni yetu hayana makosa; sio na mapapa, kwamba watu fulani ndio walezi pekee wa ukweli na maarifa, ya kwamba watu hawana haki ya kuyachunguza Maandiko kwa ajili yao wenyewe, lakini lazima wapokee maelezo yaliyotolewa na Mababa wa kanisa….” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 105. {RUA: 4.1}

“Unaweza kuona kutoka kwa vifungu hivi,” walituambia, “isipokuwa tutii maonyo kutoka kwa Mungu tunawajibika kuanguka katika makosa yale yale ambayo wote waliojiona kuwa ni matajiri na wasio na haja ya chochote zaidi, na ambao kama tokeo waliwakataa wajumbe wa Mungu, na wakawaonya kondoo zao dhidi ya jumbe Zake. {RUA: 4.2}

“Tumekwishalipia vibaya tayari,” waliendelea, “lakini ikiwa hatuwezi haswa hivi sasa, na saa hii ya mwisho kubadilisha nia zetu tuhisi kutohitaji chochote, na iwapo hatutambui kwamba hakika tu ‘wenye mashaka, na wanyonge, na maskini, na kipofu, na uchi,’ wanaohitaji kila kitu, jinsi Bwana asemavyo tulivyo, basi hakika jinsi Mungu aishivyo, mwisho wetu utakuwa mbaya mara elfu kuliko mwisho wa yeyote wa watenda maovu waliotutangulia.

4

Fimbo ya Mchungaji inashinda, “walisema,” kwa sababu ya mwenendo wetu wa ‘uvuguvugu’ (kutosheka) — wa kuwa tajiri wa Ukweli na wa kutohitaji kitu zaidi. Hili twajua, bado ni chukizo lingine mbele ya Mungu. Limekatiza mzunguko wetu wa mawasiliano na Mbingu. Ni uharibifu kwa kazi ya Mungu na unyang’anyi kwa nafsi zetu. Kuendelea kufanya yale tunayoyatenda sasa ni kukufuru hakika, haswa baada ya kuambiwa mara kwa mara: {RUA: 4.3}

“Nuru ya thamani itaangaza kutoka kwa Neno la Mungu, na mtu yeyote asithubutu kuamuru ni nini kitakacholetwa au kutoletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangazisha Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yoyote nafasi yake ya mamlaka, hakuna mtu aliye na haki ya kuizimisha nuru kutoka kwa watu. Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu;

5

kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.’” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk 65; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {RUA: 5.1}

“’… Ujumbe huu [Kilio Kikuu] ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao kama vile kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga na ujumbe wa malaika wa pili mwaka wa 1844 ….’” — Maandishi ya Awali, uk. 277. {RUA: 6.1}

“Iwapo ujumbe wa Kilio Kikuu ni nyongeza kwa ujumbe wa Tatu,” walitangaza, “kwa nini sisi hatuutarajii na kuomba kwa ajili yake? Mbona sisi hatuutafuti? Na tutawezaje kuupata ikiwa hata hatutazami katika kazi ya mtu mwingine, haswa wakati inapochipuka kutoka kati yetu, na katika jina la Bwana? Ile ‘Nyongeza,’ tunapaswa kujua, haitatushuka kwetu katika mwavuli wa kurukia, la, sio zaidi ya sehemu ya ujumbe wa malaika wa kwanza ilishuka katika mwavuli. Itakuja kupitia mtu fulani kwa hakika. Mwenendo kama huu wa kutohitaji kitu kama wetu, hukata kabisa njia ya mawasiliano ya Mbingu, na hufanya isiwezekane kabisa

6

jumbe za Mungu kuwahi kutufikia. Omba, omba, lakini fikiri na uchunguze pia.” {RUA: 6.2}

Idadi kubwa ya Waadventista kama hao wanaozungumza kwa sauti kuu walitumia uhuru kusema: “Jinsi mwenendo wa watu wetu sasa unavyosimama wako tayari kukemea na kuzuilia nje kila jambo iwapo mchungaji ataagiza hivyo. Walei wengi kabisa na hata kiroho wanafuatana na elimu kama hiyo ya hila, ingawa kwa ajili yao wenyewe wanaweza kuwa hawana habari ya suala hilo linahusu nini. Tabia hii ya kipumbavu inaendelea siku zote,” walisema, licha ya onyo la Uvuvio: {RUA: 7.1}

“Kemeo la Bwana litatua juu ya wale ambao wataizuia njia, kwamba nuru safi isije kwa watu. Kazi kubwa inapaswa kufanywa, na Mungu huona kwamba viongozi wetu wanahitaji nuru zaidi, ya kwamba waweze kuungana na wajumbe ambao Yeye huwatuma ili kukamilisha kazi Aliyokusudia ifanywe…” — Watendakazi wa Injili, uk. 304 {RUA: 7.2}

Hivyo walisisitiza kwamba Mungu anataka watu wetu wanaoongoza waungane na wajumbe Aliowatuma, sio wale wajumbe kuungana na watu wanaoongoza. {RUA: 7.3}

Kwa kikundi kingine tuliambiwa: “Kilio kwamba tuna Ukweli wote wa kutupeleka hadi kwa Ufalme, msimamo wetu

7

wa ukaidi eti hatuhitaji kitu zaidi, bila kujali ukweli wa kutisha kwamba hatuwezi kuikabili Fimbo inayokera, na ya kwamba sisi hukimbia mbali kutoka Kwayo ingawa sisi ndio tunaobeba fimbo kubwa mabegani mwetu, ni ungamo bora kwamba tu vibaya sana tunahitaji kitu ambacho hatumiliki kwa sasa; ya wamba ikiwa hatuwezi kukishikilia kitu hicho, hivi karibuni Fimbo itatufanya sote tusujudu Kwayo ilhali tunanena upuzi na kufanya kisirani kwayo mchana na usiku. Katika tukio kama hilo iwapo Fimbo imetoka kwa Ibilisi, basi Ibilisi atakuwa nasi sote kuzimu; na iwapo Fimbo hiyo imetoka kwa Mungu, na iwapo Itatuchukua wakati tunafanya vita dhidi Yake, basi Itatuhukumu na kutupeleka kuzimu sote! Kutoka kwa busara hii isiyoweza kupingwa, ni hakika kwamba tunapigana vita vya kushindwa, iwe Fimbo iko sawa au iwe mbaya.” {RUA: 7.4}

Karibu wote walisisitiza kwamba kuikimbia kwetu mbali kutoka kwa Fimbo na kuonya wengine kujiweka mbali kutoka Kwayo, ni upumbavu. “Mbona tusikabiliane nayo?” Wakauliza, kisha wakaendelea kusema: “Je! Mungu hajatuambia tuzijaribu roho (1 Yohana 4:1)? Na kushika sana lililojema (1 Thes. 5:21) Je! kwa nini hatumjali Yeye? Je! inawezekana kwamba tunajua vyema kuliko Yeye! Ijaribu roho ya Fimbo. Ikiwa ni ya Mungu, ichukue; na iwapo Si Yake, Ithibitishe.

8

Kwa sababu kufumba macho yetu dhidi ya Fimbo hakujafanya Itoweke, au ikome kutuwinda, tunapaswa kujua kufikia sasa kwamba mbinu zetu za kufumba-macho ni zenye akili kama mbuni anayepachika kichwa chake mchangani ili kuepuka mwindaji. Isitoshe, kunena kwetu dhidi ya Fimbo ni kufanya kama upepo unapovuma dhidi ya moto; huuzidisha. Na kuwatupa nje Wana-fimbo ni kuwafanya kuwa wafia imani, sio wazushi. Rumi ilijaribu mbinu hizi zote lakini ilishindwa kuzuia uchochezi wa walioitwa eti waasi. {RUA: 8.1}

Aya hizi zilisomwa kwetu na wengi: {RUA: 9.1}

“Hakuna mtu anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ilioko kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia hili, Yeye amesema, ‘Nimeweka mbele yako mlango ulio wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.’ Hata kama viongozi wetu wote wanaweza kukataa nuru na kweli, mlango huo utakuwa bado wazi. Bwana atawainua watu watakaowakabidhi watu ujumbe kwa wakati huu. {RUA: 9.2}

“Ukweli ni wa milele, na vita na kosa utadhihirisha tu nguvu yake. Hatupaswi kamwe kukataa kuchunguza maandiko na wale ambao, tunayo sababu ya kuamini, wanayo shauku kujua kweli ni nini. Tuseme kaka

9

ashikilia mtazamo ambao ulitofautiana na wako, na aweze kuja kwako, akipendekeza kwamba ukae naye chini na kufanya uchunguzi wa wa jambo hilo katika Maandiko; Je! Utaweza kuinuka, umejawa na chuki bila sababu, na kulaani maoni yake, ilhali ukikataa kumsikiliza kwa uelekevu? Njia sahihi tu itakuwa kukaa chini kama Wakristo, na kuchunguza msimamo uliowasilishwa, katika nuru ya neno la Mungu, ambalo litafunua ukweli na kufichua kosa. Kuyadharau maoni yake hakutaudhoofisha msimamo wake hata kidogo iwapo ni uongo, au kuimarisha msimamo wako ikiwa ni ukweli. Iwapo mihimili ya imani yetu haitastahimili mtihani wa uchunguzi, ni wakati ambapo tunastahili kuijua. Lazima isikuwepo roho ya Ufarisayo inayokuzwa kati yetu “ — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 107 {RUA: 9.3}

Karibu wote waliozungumzia aya hizi walihitimisha na kauli zifuatazo: “Ilikuwa kwa kanuni hii,” walisema, “ambayo tulisimamia wakati tulipokuja kuwa Waadventista. Laiti isingekuwa kwa kufanya hivyo, tungalikuwa bado tulivyokuwa kabla ya nuru kuja kwetu. Na ni nani aliyetushawishi kufuata kanuni hii ya Kiungu? — Sio wachungaji wetu! La, hapana hata kidogo. Walituzuia.

10

Kwa sababu ilikuwa kwa uchunguzi wa kibinafsi, bila kumtegemea kuhani au askofu, kwamba tuliupata ukweli wa Hukumu ya wafu (ujumbe wa malaika wa kwanza, Ufu. 14:7 kwa matumizi yake yasiyokuwa ya moja kwa moja), lazima pia iwe kwa uchunguzi huru wa kibinafsi ambao tutaweza kupata ukweli wa Hukumu ya walio hai (ujumbe wa malaika wa kwanza katika matumizi yake ya moja kwa moja). Kuupokea Ukweli kamwe haijawahi kuwa kazi na jukumu la pamoja, na kamwe haitakuwa. Usijidanganye katika hili, na usiwaruhusu wengine wakudanganye, aidha. Zingatia lile Neno linasema, sio lile mwanadamu anasema au vitu. Ikiwa tutashindwa katika hili, basi hakika kama Mbingu ilivyo, tutapotea. Inawezaje kuwa vinginevyo tunapoendelea kutojali maonyo ya Uvuvio? Mbona usiangalie nyuma na kuweka moyoni kisa cha kusikitisha cha wale ambao wametutangulia? “Hawa walihitimisha kwa kusema, “Ieleweke kwamba juhudi zetu za kujikinga kama za Kirumi zinashindwa na zitashindwa.” {RUA: 10.1}

Hata idadi kubwa zaidi ya kundi ambalo limetajwa, na kwa mazungumzo ya mkazo zaidi, walitoa maoni: “Kupuuza maonyo ya Uvuvio kanisa halina hata bila kufikiri huwafukuza kwa nguvu wale ambao wangethubutu kusoma

11

vitabu vya Fimbo ya Mchungaji. “Tuliambiwa pia kwamba kanisa” linatenda vibaya zaidi kwa Wana-fimbo kuliko walivyofanya Wayahudi kwa mitume; ya kwamba kwa kuwafukuza kutoka miongoni mwetu kwa mafundisho yao ya utakaso wa kanisa jinsi Roho ya Unabii inavyofundisha, tunajifanya vigeugeu isipokuwa tutupilie mbali roho ya Unabii pia. “Je! hamuoni, tuliulizwa,” jinsi sisi tulivyo vigeugeu, na namna roho zetu zilivyo za ibilisi kwa hali hii? Je! Basi mnamtarajia Mungu mwenye haki ayabariki matendo yetu yasiyofaa? Shuhuda, Vol. 5, uk. 80, husema kwamba utakaso unaharakisha kwa kasi.’ Je! Tunamtazamia Bwana aje hivi karibuni? Basi lazima tuutazamie utakaso wa kanisa kuja karibuni.” {RUA: 11.1}

Wengine walitujia na nukuu na maoni yafuatayo: {RUA: 12.1}

“… Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, angaliwaheshimu kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi…. Hawakwenenda sambamba na nuru…” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 82, 80. {RUA: 12.2}

12

“Iwapo hawakwenda sambamba na nuru, basi watatoaje nuru?” Wakauliza. “Basi, pia, wale ambao hutuambia tusimsikilize yeyote ila wao, wanafanya jambo ambalo Kristo alilaani Aliposema. “Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.”– Luka 11:52. Mungu ametuambia mara kwa mara katika Neno Lake tujichunguze sisi wenyewe.” {RUA: 13.1}

Kundi lingine lilisisitiza kwamba tutulie na tusikilize yafuatayo: {RUA: 13.2}

“… Baadhi ya ndugu zetu viongozi wamekuwa mara kwa mara wakichukua msimamo wao kwa upande mbaya, na iwapo Mungu angetuma ujumbe na kuwasubiri ndugu hawa wazee kufungua njia ya ufanisi wake, hautawafikia watu kamwe ….” — Watendakazi wa Injili, uk. 303. {RUA: 13.3}

“Bwana mara kwa mara hufanya kazi pale ambapo kamwe hatumtaraji Yeye; Yeye hutushangaza kwa kuzifunua nguvu Zake kupitia vyombo vya chaguo Lake mwenyewe, ilhali Yeye hupita kwa watu ambao tumewatazamia kuwa wale ambao nuru inapaswa kupitia ndani yao. Mungu hutaka tuupokee ukweli kwa sifa yake wenyewe, — kwa sababu ni ukweli.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106. {RUA: 13.4}

13

“…Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna iliyo kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa wanadamu. Watakuwapo wale kati yetu siku zote watataka kuthibiti kazi ya Mungu, kulazimisha hata hatua gani zitafanyika wakati kazi inakwenda mbele chini ya uongozi wa malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua mamlaka mikononi Mwake….” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {RUA: 14.1}

“Katika kila kizazi yapo maendeleo mapya ya ukweli, ujumbe wa Mungu kwa watu wa kizazi hicho. Kweli za zamani ni muhimu; ukweli mpya si huru kwa ule wa zamani, bali kukunjuka kwake. Ni pale tu kweli za zamani zinapoeleweka ndiposa tunaweza kufahamu mpya.” — Mafunzo ya Yesu Kwa Mifano, uk. 129. {RUA: 14.2}

“Je! tunaweza kudhani kwa uaminifu,” waliuliza, “kwamba Bwana anaweza kumaliza kazi Yake duniani na sisi Walaodekia tunapoendelea kuwa vipofu? Na ni nani atakayeyafumbua macho yetu ikiwa si Bwana kwa ‘dawa ya macho’ mpya (Ufu. 3:18) Je! Bwana hana ukweli mpya — hakuna chakula kwa wakati wake —

14

kukidhi mahitaji ya watu Wake hasa kwa wakati huu? Je! Ameiacha nchi? Na Yeye atawahukumuje walio hai bila ujumbe kutangaza kwamba kesi zao sasa zitaonekana mbele ya Mungu? Kwa sababu tuna ujumbe wa Hukumu kwa wafu, sio busara na muhimu zaidi ya kwamba tunapaswa kuwa na ujumbe wa Hukumu kwa walio hai? Je! Wa mwisho si muhimu zaidi kuliko ule wa zamani? Na tutajuaje utakapokuja iwapo tutaendelea kufumba macho na kuziba masikio yetu? Ikiwa hatubadilishi mawazo yetu ya sasa yaliyochacha, tutawezaje kuamini hata iwapo tunaweza kusikia bila kukusudia kwamba ujumbe umefika?” {RUA: 14.3}

Bado kikundi kingine kiliuliza maswali haya: “Iwapo Mungu ataliacha kanisa Lake pasipo kujua tukio kubwa zaidi la wakati wote (Hukumu ya walio hai), litatangaza ukweli gani wakati wa saa hiyo ya hitaji? Hukumu ya wafu, hakika mnajua,” walisema, “wakati huo haingekuwa Ukweli wa sasa zaidi tangazo la Nuhu la gharika lingeweza kuwa Ukweli wa sasa sasa. Je! Jaji wa Mbingu angemhukumu mtu bila kesi? Na Yeye atamuhukumu vipi bila notisi?” {RUA: 15.1}

Idadi kubwa ya watu walijielezea hivi: “Iwapo Hukumu ya

15

Wafu ni kazi ambayo hutenganisha katika vitabu wema kutoka kwa wabaya, — mwenye dhambi kutoka kwa mwenye haki, — na huamuru kwamba mwenye dhambi asifufuke kutoka kwa wafu katika ufufuo wa wenye haki (Ufu. 20:5, 6, 12), na kumhukumu kuathiriwa na kifo cha milele, basi tunadhani kwamba ni nini Hukumu ya walio hai itafanya nini kwa walio hai? Je! Si kuwatenganisha kimwili mmoja kutoka kwa mwingine — kuwaondoa samaki wabaya kutoka kwa wazuri (Mat. 13:48), magugu kutoka kwa ngano (Mat. 13:40), wanawali wapumbavu kutoka kwa wenye busara (Mat. 25: 1012), mbuzi kutoka kati ya kondoo (Mat. 25:33, 46)? Je! Mifano hii hufundisha nini, ikiwa si Ukweli wa Hukumu, “utakaso” wa kanisa? Taarifa ya Uvuvio ifuatayo, pia, walitangaza “huonyesha kwamba kanisa safi ndilo litakalotangaza ujumbe wakati wa Kilio Kikuu. “Kwa hili walinukuu kutoka kwa Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908: {RUA: 15.2}

“Ujumbe wa malaika wa tatu utaiangaza nchi kwa utukufu wake; lakini wale tu ambao wameyastahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika kilio kikuu.” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {RUA: 16.1}

16

Kisha wakafuata na maoni haya: “Kwa sababu hatuwezi kudhamiria kukataa dhamiri yoyote yake, mbona, basi, tunawafukuza waamini wa Fimbo kwa kuitisha umakini wetu kwa mambo haya? Je! Hatufanyi kushindwa kusudi letu wenyewe na kuupinga ujumbe wetu wenyewe? Na je! hatufanyi kuwa vigumu kwetu sisi kufundisha Hukumu ya walio hai? Mungu aturehemu kwa sababu tumeruhusu roho ya Ibilisi kutawala mioyoni mwetu na maishani mwetu. {RUA: 17.1}

“Ndugu,” waliendelea, “sasa ni fursa yetu ya kufikiri zaidi kuliko hapo awali. Tunahitaji kufikiri, tunahitaji kuanza kazi bila mchezo. Tunahitaji kuamka tusije tukalala milele. Tusiendelee kujidanganya tena kwa kushikilia mwenendo wetu wa uvuguvugu kwamba ‘hatuna haja ya kitu.’ Bwana hasemi uongo wala Yeye hajakosea katika onyo Lake kwamba tunahitaji kila kitu, na ya kwamba ikiwa hatutasimama hivi sasa na kuanza kutafuta kitu kingine isipokuwa kile tunacho miliki sasa, tutakua na njaa ya Ukweli baada ya Hukumu ya wafu kupita. Na kwa sababu Yeye hatakuwa na farasi waliokufa ‘ghalani’ Mwake bila shaka Yeye ‘atatutapika’ (atatutupa) nje. Na wakati huo tutakuwa wapi! Kundi hili lilihitimisha na, “O, ni yalioje maelezo ya kusikitisha

17

na kutakuwa kufilisika kiroho kulioje!” {RUA: 17.2}

Bado katika sehemu zingine tuliambiwa: “Ingawa huwa tunapiga kelele kwa kupaza sauti zetu, na ingawa ulimwengu wote hutusikia tukidai kwamba magugu yatakaa makanisani hadi kufungwa kwa muda wa rehema, bado wakati tunapoamka kutoka kwenye ndoto zetu za mchana — wakati huo tutaweza kukiri kwamba utengo wa magugu ni kazi haswa ya Hukumu, kazi ya ujumbe wa malaika wa tatu (Maandishi ya Awali, uk. 118), sio kazi ya mapigo au ya Armagedoni, au mateso ya sheria za jumapili kama tunavyoonekana kutaka sasa. Ibilisi alipanda magugu katika makanisa tulipokuwa tumelala na hakika anapanga wa kuyadumisha humo na kutufanya tuendelee kulala. Ndiye anayetaka yawe kanisani hadi mwisho wa muda wa rehema ili kwamba kanisa kwamwe lisifae kupokea Roho na kamwe lisimalize kazi yake. Upendo wetu wa kudumisha maisha ya magugu, kwa hivyo, si upendo wa kutoka Mbinguni, kuhubiri kwetu kwa hivyo kunampendeza sana Ibilisi. {RUA: 18.1}

Sasa kwa uelekevu na uaminifu ingawa kwa ufupi, tumewasimulia kile sisi kama kamati tulikusanya kutoka kwa umati wa Waadventista wa Sabato,

18

tutaendelea kuwapatia ya hivi punde maoni kamati na ya kibinafsi kwa shida ya Dhehebu na tiba yake. Sisi, kamati, si sisi tu ambao tumeshawishika hivyo, aidha. Maelfu wanajua kwamba sisi kama watu tumelala fofofo, na tumedanganywa vibaya sana; yaani kunatilia shaka kwamba hata bomu haliwezi kutuamsha. Unasema hapana? Wacha tuone: {RUA: 18.2}

Tunashikilia kwamba Dhehebu sasa lina idadi ya karibu washiriki milioni moja, na tumeweka lengo letu kuongeza ushirika maradufu. Tunajivunia mafanikio yetu kwa msisitizo kwamba Mungu anatubariki. Yote husikika vyema na hutufanya kujihisi wenye furaha. Pia, dhehebu lote hukiri kwamba sehemu kubwa ya kazi bado inapaswa kufanywa — ya kwamba wapo mamilioni kwa mamilioni hata katika Marekani yenyewe, ambao bado hawajasikia hata jina Waadventista wa Sabato, achilia mbali “Injili ya milele.” Ni wazi ilivyo, kwa hivyo, ndugu, kwamba kwa kiwango cha sasa cha ukuaji, wakati kazi imekamilishwa na Yesu kuja kulichukua kanisa Lake hadi kwa nchi ya utukufu, Dhehebu kwa wakati huo litakuwa na idadi ya mamilioni kadhaa. {RUA: 19.1}

Kisha, pia, huwa tunafundisha kwamba Yesu atakapokuja, kutakuwa na watakatifu

19

walio hai 144,000 tu, na si zaidi! Je! Wewe basi katika Roho wa Kristo na kwa nafsi yako mwenyewe, chukua karatasi na penseli na uhesabu asilimia ya watakatifu na asilimia ya mashetani, au magugu, ambayo sasa hujumuisha ushirika wa makanisa yetu? Kweli, kwa sababu idadi ya ushirika sasa si chini ya 800,000, na ikiwa wamo watakatifu 144,000 tu ndani yake, basi kulingana na uwiano huu kongamano la washiriki 100 lingejumuisha watakatifu 18 na mashetani 82! Na kwa sababu maafisa wanaoendesha makanisa huchaguliwa na kura ya wengi, unaona, ni nani aliyewachagua, ni nani aliye ofisini, na ni nani anayeyadhibiti makanisa? Je! Unajiuliza mbona mambo yanajiendesha jinsi yalivyo? {RUA: 19.2}

Iwapo ni kweli kwamba watakuwapo watakatifu walio hai 144,000 tu Yesu atakapokuja, na ikiwa tutaongeza ushirika maradufu kufikia mwisho wa 1953 au 1954 jinsi lengo linavyoonekana kuwa, basi kwa kiwango hicho mwaka wa 1955 watakuwapo watakatifu 9 na mashetani 91 kutoka kati ya washiriki mia moja. Na iwapo tunaongeza maradufu ushirika mara kadhaa kabla Yesu kuja kulipokea kanisa Lake, hatakuwapo mtakatifu hata mmoja katika washiriki mia! Kwa hivyo, kanisa ni la nani? la Ibilisi? au

20

la Bwana? Yeye atalitafuta wapi Atakapokuja? Ikiwa, licha ya ukweli huu wa kusikitisha, Ndugu, mnaendelea kusema kwamba hatujalala, kwamba ufasiri wetu wa Neno hauna shaka, kwamba hatuhitaji kitu zaidi, kwamba tunao ukweli wote wa kutupitisha katika Malango ya Lulu, basi hakuna tumaini; mmeenda mbali sana. {RUA: 20.1}

Sisi, kamati, sasa kibinafsi tunajua na tumeona kwa macho yetu, hata hivyo, kwamba wapo wengi ambao hawajapumbazwa vibaya sana, ambao hawajamsujudia Baali, ambao hawajiruhusu kufungiwa ndani ya mazizi kwa mfano kama kondoo na ng’ombe, na walaghai wanaolidhibiti na kulisha kundi la Mungu kwa gredi ya chini kabisa ya makapi wanayoweza kutafuta. Tunatumaini kwamba hawa walisha makapi kwa manufaa yao wataiacha kazi hii ya kishetani hivi karibuni. Wote kama hao ambao wametangulia mbele yao, hawakufaulu; walikufa katika upumbavu wao. {RUA: 21.1}

Je! Ni kwa nini tunawaleta watu zaidi katika makanisa yetu iwapo tunajua kwamba ni watu 144,000 tu kati ya idadi kubwa ya washirika wa kanisa wanaostahili kuhamishwa bila kufa? Mbona tunawaleta kanisani, na kwa nini tunawapatia

21

matumaini ya kuwa katika Ufalme ilhali tunaamini kwamba hawawezi kuokolewa? Je! kukusanya kama huku sio aina ya chini kabisa ya udanganyifu wa makusudi na jaribio kubwa zaidi la kupenyeza kwa kanisa magugu ambayo hayajawahi kusikika? {RUA: 21.2}

Kufunika usingizi mkubwa ambao unaonyeshwa na takwimu zilizotajwa awali, mchungaji alielezea kwamba wakati kazi itakapofunga watakuwapo kanisani zaidi ya watakatifu walio hai 144,000 lakini badala ya kuhamishwa bila kufa, idadi yao kubwa itabidi kufa kutokana na mapigo au kwa tauni kabla Yesu kuja kwa sababu hawatakuwa wema kabisa kuhamishwa bila kufa ingawa wakamilifu kwa ufufuo! {RUA: 22.1}

“Je! fundisho hili limeidhinishwa na Dhehebu, au ni maoni ya kibinafsi ya mtu?” tuliuliza. Basi baada ya kimya cha muda mrefu mmoja mwenye mamlaka akasema: Hakuna lolote kati ya haya ni la dhehebu; mafundisho haya ya ujanja ni maoni ya mtu hapa na ya mtu pale. Mmoja akisema jambo moja na mwingine akisema jambo lingine. Ni vigumu wawili kutoa jibu sawa kwa maswali kuhusu mafundisho haya yote yaliyofunuliwa, lakini wote wana hakika kuwa wanachosema ni ukweli safi! Watu hawa wa anuwai kufikia sasa

22

na maoni yaliyogawanyika hayaruhusiwi kwa uhuru kufundisha mafundisho yao ya kwenda kuzimu, bali hata kulipwa kwa kufanya hivyo! “Bado watu hawa wanapiga kelele dhidi ya makosa na kuwashauri wote walio karibu nao waweze kuwa chonjo kwa Fimbo ya Mchungaji, ya kwamba ina makosa! Ni utata ulioje! {RUA: 22.2}

Kinachoshangaza sana, hata hivyo, ni kwamba kuna wengi, haswa walei, ambao, bila kuhoji na macho yao wakiwa wamefumba macho yao, kama ndege kwenye kiota, humeza chochote wanachokabidhiwa. Wao ni wazembe mno kufikiri, na husinzia sana kufumbua macho yao kujisomea wenyewe. Wao hutarajia mchungaji awabebe mikononi mwake moja kwa moja hadi Mbinguni.” {RUA: 23.1}

Kuchukua kwao kimakusudi mafundisho yasiyokuwa na mamlaka na ufasiri wa apendavyo mtu tu (usiovuviwa) wa Maandiko, kama ule hawa vipofu hufundisha kuwahusu watu 144,000, ni jambo la kushangaza kweli kweli. Wanapaswa kujua kwamba wahalifu wote kama hao ni mawakala wa shughuli zisizo za Uadventista. Watakatifu wanajua kw amba ingawa Yesu anakuja katika wakati wa taabu mfano wake haukuwapo, bado Yeye anamwokoa kila mtu ambaye jina lake limeandikwa katika kitabu kile, na ya kwamba watu wote wa Mungu ambao wako kwa

23

wakati huko Babeli, ulimwengu, na hivyo kuwa chini ya mapigo, wanaitwa watoke, na wote wanapokuwa wakitoka kwake, wote wanaepuka mapigo (Ufu. 18:4); hakuna yeyote atakufa kwa sababu iwayo yote. Wote wanajua kwamba ikiwa ni wema kabisa kuja katika ufufuo wa kwanza, ni wema kabisa kuhamishwa bila kufa. {RUA: 23.2}

Dhihaka ni kusema kwamba kiwango cha wokovu ni cha chini kwa wale waliofufuliwa kuliko kilivyo kwa waliohamishwa bila kufa! Na ni laana ilioje kwa mtu yeyote kuongeza jambo kama hili la kigeni kwa Neno la Mungu! {RUA: 24.1}

Hawa walimu wa uzushi wanapaswa kusaidiwa kwa kuwalazimisha wathibitishe mafundisho yao kwa Bibilia; maana theolojia kama hii ya kigeni, isiyopatana na ya makosa, ni uzushi wa aina duni kabisa. Licha ya kwamba ni kukufuru kwa kupindukia, bado yanaruhusiwa kufundishwa wakati wanapigana na Ukweli ili kuwaweka watu wasiweze Kuujua! {RUA: 24.2}

Sisi kama kamati mwishowe tunajua kwamba lile Fimbo hufundisha, huwa Inalithibitisha. Na hiyo ndio sababu haswa kwamba hawa walimu wa uzushi, ambao wameyapenyeza kanisani leo magugu kwa kiwango kikubwa kuliko walivyofanya walimu wa wa uzushi wakati wa Kristo, wanawaonya wote wasisome Fimbo, bali Waichome, na wakatae Kuichukua. Iwapo

24

kuna hekima yoyote ndani yao wanapaswa kujua kwamba wao kufunika pamba machoni mwa watu kunaweza kudumu kwa muda mchache, lakini sio milele. Hekima huamuru kwamba mtu achunguze katika vita na macho yake mwenyewe na ajue mwenyewe kabla hajatoa maoni yake kwa sauti, na kabla ya kuweka vigingi vyake. {RUA: 24.3}

Shukrani kwa Mungu kwamba watu 144,000 sio watakatifu wote walio hai, bali kwamba wao ni “malimbuko” (Ufu. 14:4) ya mavuno makubwa. Isitoshe, wao hawatoki katika mataifa yote, lakini ni kutoka tu kwa makabila kumi na mbili ya wana wa Israeli (kutoka kanisani mwanzoni mwa mavuno — Hukumu). Umati mkubwa, hata hivyo, ambao Yohana aliuona mara tu baada ya kutiwa muhuri kwa watu 144,000, ni “kutoka katika mataifa yote” (Ufu. 7:9). Wao kwa hivyo ni mavuno ya pili, wale ambao hawajavunwa kutoka kanisani, ila kutoka katika mataifa yote ambayo Babeli inatawala juu yake (Ufu. 17). Hivyo wameitwa watoke kwake (Ufu. 18:4). {RUA: 25.1}

Shukrani kwa Mungu kwamba Yeye atakuwa na kanisa lililojazwa watakatifu, sio na mashetani. Kwamba hakuna anayepaswa afe ili aokolewe lakini wote wataishi waokolewe na Mikaeli atakaposimama (Dan. 12:1). {RUA: 25.2}

“Watu wako pia wote watakuwa wenye haki:

25

Nao watairithi nchi milele; chipukizi nililolipanda Mimi mwenyewe, kazi ya mikono Yangu mwenyewe, ili Mimi nitukuzwe. Mdogo atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, Bwana, nitayahimiza hayo wakati wake.” Isa 60:21, 22. {RUA: 25.3}

Ni jukumu letu kaka, dada, kuwaambia hao walimu wa uzushi kwamba neno “malimbuko” hakika humaanisha kwamba yatakuwapo matunda ya pili, kama vile neno “ufufuo wa kwanza” (Ufu. 20:5) hakika humaanisha kwamba utakuwapo ufufuo wa pili. Waambie kwamba ingalikuwa bora wasingalihitilafiana na Neno la Mungu. Waambie kwa sababu Uvuvio hausemi kwamba umati mkubwa ni wale waliofufuliwa, hawana haki kusema kwamba wao ni wafu. Waambie kwamba wao kuliongeza neno “kufufuliwa,” na kuondoa maneno “matunda ya pili” ambayo yamemaanishwa na neno “malimbuko,” si kitu kipungufu cha kuongeza na kuondoa kimakusudi kwa Neno la Mungu. {RUA: 26.1}

“Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa

26

katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.” Ufu 22:18-20. {RUA: 26.2}

Isitoshe, kila shutuma iliyopigana dhidi ya Fimbo ambayo sisi tulishuhudia kibinafsi iliipiga jeki Fimbo na pigo kwa Dhehebu. Hii ilikuwa hivyo kwa sababu waliishutumu kwa uongo Fimbo kukinzana na maandishi ya Dada White. Mabishano na mbinu zilizotumiwa dhidi ya Fimbo zilikuwa za aina moja na tabia kama zile ambazo watunza Jumapili hutumia dhidi ya Ukweli wa Sabato. Uchunguzi wetu wa kibinafsi wa dondoo zilizowasilishwa hazikuonyesha tofauti kati ya maandishi ya Dada White na Fimbo. Mbali na hilo, hoja ambazo wachinja Fimbo hutumia dhidi ya Fimbo kweli humfanya Dada White kupingana na Bibilia! Wale ambao huihukumu hivyo Fimbo lazima wafanywe kutambua kwamba hakuna mtu isipokuwa roboti itashindwa kutambua ya kuwa wao kuipiga Fimbo vita jinsi hiyo wakitumia

27

maandishi ya White si kuidhuru Fimbo ila, kwa madhara, ni kupinda na kuharibu kabisa Maandiko kwa kutumia maandishi ya Dada White jinsi Wayahudi walivyopinda maandishi ya Musa kwa jaribio la kupinga mafundisho ya Kristo. Hizi ni mbaya zaidi kuliko shughuli zisizo za Uadventista — si kitu kipungufu kuliko makufuru. Kama tulivyo lazima tuthibitishe maandishi ya Dada White sahihi au ya makosa na Bibilia, sio na kitu kingine, vivyo hivyo lazima kwa Bibilia Yenyewe tuthibitishe Fimbo ni au si nini. {RUA: 27.1}

Sisi sote tulihisi hakika kwamba ikiwa walei watawaruhusu hawa watu vipofu na wenye uadui lakini wa kidini kuendelea na upumbavu na makufuru yao, watathibitisha hasara yasiokuwa madogo kwa kanisa wakati huu kuliko walivyofanya makuhani wa kidini wakati wa Kristo kwa upumbavu wao ulithibitisha hasara kwa kanisa la Agano la Kale. Naam, hakika aishivyo Mungu, upumbavu na ubinafsi wa walimu hao wa uzushi utathibitisha hasara makubwa kwa Dhehebu kuliko yale ya ujinga wa Hitler na falsafa yake ya uongo ilithibitisha hasara kwa Ujerumani. {RUA: 28.1}

Ndugu, hili pekee linatosha kumshawishi Mwadventista yeyote aliye na jicho pevu kwamba Dhehebu

28

liko baharini “bila ramani au dira.” Lakini shukrani kwa Mungu kwamba Fimbo imepata zote mbili “ramani na dira” na ya kwamba tunaweza kuwa nazo iwapo tunataka. {RUA: 28.2}

Kwa sababu kanisa kama mwili halijawahi tangu mwanzo wa ulimwengu kuupokea ujumbe mpya, uamuzi, kama kawaida, lazima uwe jambo la mtu binafsi. Lakini kumbuka kwamba uamuzi wako usiwe wa kujiunga na kitu kingine, bali wa kuungana na Kristo na ujumbe Wake wa Hukumu kwa wokovu na ustawi wa Dhehebu. Kaa ndani yake na ulifanyie kazi lirudi kwa Mungu. {RUA: 29.1}

Lile ambalo tumewasilisha katika kurasa hizi ni matokeo aminifu na uamuzi wa wote, wa mwisho na wa sala wa kamati nzima, ambayo uamuzi wake kwa kuchunguza kwa kina na dua nyingi yalikuwa na msingi kwa uchunguzi kimataifa kwa pande zote za pambano, pamoja na uchunguzi wa kina kwa Fimbo ya Mchungaji. Kwa sababu ushirika wa kamati ulijumuisha watu kutoka majimbo mengi na nchi za nje, na kwa sababu kazi yao ilifanywa kwa mawasiliano ya ana kwa ana na ya barua, eneo ambalo tulishughulikia, kwa hivyo, lilikuwa ulimwengu wote halisi wa Waadventista. Iwapo umesadikishwa na ukweli

29

uliowekwa wazi katika kazi hii ya uchunguzi, na ikiwa utaomba msamaha na mwongozo, basi utakuwa mwenye furaha, na tumaini lako halitakuwa bure. Lakini iwapo ripoti hii itashindwa kuyafumbua macho yako, basi unalo tumaini gani ila milele kukaa katika udanganyifu wako wa ubinafsi na kuutumia umilele katika kundi na wale waliomsulubisha Bwana? {RUA: 29.2}

Mapendekezo ya kamati kwa ugonjwa wa Ulaodekia ni, kwa hivyo, haya: {RUA: 30.1}

“Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; “ 1 Thes. 5:17-21. {RUA: 30.2}

Tenda kama Waberoya waungwana ambao “walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” Mdo. 17:11. {RUA: 30.3}

“Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.” 2 Petro 1:20. {RUA: 30.4}

Achana na shughuli zote zisizo za Uadventista; mwelekee Mungu. Epuka ufasiri wa Maandiko ambao haujavuviwa ili usije ukakosa kuongozwa na Roho wa “Kweli yote,” bali na roho ya Ibilisiambayo

30

inafanya kazi kupitia kwa kila mtu ambaye anajihusisha katika ufasiri apendavyo mtu wa Maandiko, uzushi, uongo, na kukashifu tabia — katika kitu chochote ili kujiweka mwenyewe na wengine gizani na mbali na Roho wa Kweli haswa kwa wakati huu. {RUA: 30.5}

“Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua lake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” Isa. 2:22. {RUA: 31.1}

Katika kutafuta ukweli kwa swali hili au lo lote linalobishaniwa, maneno ya Mzee Froom yanasimama kama kielekezi cha hekima: {RUA: 31.2}

“Kuzima majadiliano ni kinyume na ukweli wa uhuru wa kiraia na wa kidini, maana ukweli ni kanuni hai, inayopanuka. Kukandamiza majadiliano siku zote huwa tabia ya udikteta, na kitovu cha nguvu yake hofu ya kuvuruga hali kama ilivyo. Historia huitia alama kama chenye sifa mbaya chombo cha udhalimu na kifaa cha makosa. Pambano lilichukua sehemu kubwa ya malezi ya kanisa la Agano Jipya. Majadiliano huchekecha hoja bandia kutoka kwa uhakika na makosa kutoka kwa ukweli, lakini kudumaa katika uhafidhina pamoja na kununa kwake kunakoambatana kwa majadiliano, huelekea katika wasiwasi mwishowe na msiba; na

31

ukandamizaji wa uchunguzi mara nyingi hukwisha katika machafuko.” — L.E. Froom. {RUA: 31.3}

— Kamati ya Uchunguzi ya Shughuli Zisizo za Uadventista

32

[Picha]

>