fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 11, 12

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 11, 12

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

JENGA MIJI, FARIJI ZAYUNI, CHAGUA YERUSALEMU.

IWAPO 144,000 TU WANAHAMISHWA BILA KUFA, UNAYO NAFASI GANI?

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, uk. 109 hadi 110, kuanzia aya ya kwanza. {1TG11: 2.1}

M.B, uk. 161 — “Mapenzi ya Mungu huonyeshwa katika maagizo ya sheria Yake takatifu, na kanuni za sheria hii ni kanuni za mbinguni …. Lakini mbinguni, huduma haitolewi kwa roho ya kisheria. Wakati Shetani aliasi dhidi ya sheria ya Yehova, wazo la kuwa ilikuwapo sheria liliwajia malaika karibu kama uamsho kwa kitu ambacho hakikufikiriwa. Katika huduma yao malaika sio kama watumwa, bali kama wana. Upo umoja kamili kati yao na Muumba wao. Utiifu kwa wao sio kazi yenye kuchosha. Upendo kwa Mungu huifanya huduma yao kuwa fu-raha. Kwa hivyo ndani ya kila nafsi ambayo Kristo, tumaini la utukufu, hukaa, maneno Yake hutoa mwangwi, ‘Napenda kuyafanya mapenzi Yako, Ee Mungu wangu; Naam, sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” {1TG11: 2.2}

“Ombi, ‘Mapenzi yako yafanyike duniani, kama ilivyo mbinguni,’ ni sala ya kwamba utawala wa uovu hapa du-niani uweze kukomeshwa, ili dhambi iweze kuangamizwa milele, na ufalme wa haki uanzishwe. Kisha duniani kama mbinguni itatimizwa ‘furaha yote ya wema Wake.’ “ {1TG11: 2.3}

Tunapaswa sasa kuomba ili sheria ya Mungu iandikwe mioyoni mwetu; kwamba tunatii sheria kwa sababu tuna-taka, sio kwa sababu ni lazima; ili tutambue kwamba kutii kwetu amri za Mungu ni kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe. Na juu ya yote, hebu tuombe kwaba furaha yetu ya upeo iwe katika kuyatenda mapenzi Yake. Hivyo mapenzi ya Mungu yafanyike duniani kama ilivyo mbinguni. {1TG11: 2.4}

2

JENGA MIJI, FARIJI ZAYUNI, CHAGUA YERUSALEMU.

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, OKTOBA 19, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Katika somo la Sabato iliyopita tulijifunza kwamba unabii wa Zekaria unayahusu makundi mawili ya watu kwa nyakati mbili tofauti: kwanza kwa Wayahudi wakati walipokuwa wakirudi kutoka Babeli kwenda Yerusalemu, na pili kwa wale ambao katika wakati wa mwisho watatoka katika mataifa yote. (Ufu. 7: 9; 18: 4). Tulijifunza pia kkwamba uamsho na matengenezo yaliyotukia siku za Zekaria, ni mfano wa uhuisho na matengenezo am-bayo yatatukia katika siku zetu, na kwamba kurejea kwa watu zamani kutoka Babeli ni mfano wa kurejea kwa watu kutoka katika Babeli ya siku za mwisho (Ufu. 18: 4). {1TG11: 3.1}

Hebu tufungue– {1TG11: 3.2}

Zek. 1: 1 — “Katika mwezi wa nane, mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria ….”

Hapa tunaambiwa kwamba nabii Zekaria aliitwa kwenye ofisi yake ya kinabii katika mwaka wa pili wa Dario, mfalme. Kwa nini aliitwa hasa mwaka huo? — Kwa ajili ya jibu, tutafungua Ezra. “Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu ikakoma; nayo ikakoma hata mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi.” Ezra 4:24. {1TG11: 3.3}

3

Dhahiri kabisa Zekaria aliitwa hasa wakati huo kwa sababu kazi ya hekalu huko Yerusalemu ilikuwa imekatizwa na kuachwa. Bwana, kwa hivyo, kupitia kwa manabii Zekaria na Hagai, alimtuma ujumbe wa kukemea kwa wajenzi na kuwaomba warejee haraka kujenga. {1TG11: 4.1}

Aya ya 2-6 — “Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama ka-ribu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzun-guka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake. Haya! Haya! Ikimbieni nchi ya kaskazini, ase-ma Bwana; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema Bwana.”

Wajenzi walikumbushwa kwanza kwamba walikuwa Babeli kwa sababu baba zao hawakuwa wamelitii Neno la Bwana ambalo liliwajia kupitia kwa manabii Wake; kwamba kwa dhambi zao hekalu na ufalme wao uliangamizwa. Wajenzi waliambiwa wazi kwamba kama mradi wao ungeweza kufanikiwa siku zote, wangepaswa kuepuka mwenendo iliofuatwa na baba zao, na kuwapa utii maalum manabii Zekaria na Hagai. Wajenzi waliahidi kwamba hawataenenda katika njia za baba zao. {1TG11: 4.2}

Ilikuwa katika mwezi wa nane ambapo Zekaria aliwapa ujumbe huu wa matengenezo. Wayahudi kuupokea ujumbe

4

kwa moyo kuliandaa njia kwa ajili ya ujumbe mwingine na ulikuja ndani ya muda wa miezi mitatu. Ndio huu hapa: {1TG11: 4.3}

Aya ya 7, 8 – “Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani, mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, nabii, kus-ema, Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya ki-jivujivu, na weupe.”

Kwa ufafanuzi wa nembo hii tutasoma maswali ya nabii na maelezo ya malaika katika {1TG11: 5.1}

Aya ya 9-11 — “Ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, ni nini hawa? Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Nitakuonyesha ni nini hawa. Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, Hawa ndio Bwana aliowatuma, waende huko na huko duniani. Nao wakamjibu yule malaika wa Bwana aliyesimama kati ya mihadasi, wakasema, Tumekwenda huko na huko duniani, na tazama, dunia yote inatulia, nayo imestarehe.”

Kwa sababu farasi hutumwa na Bwana kutembea huko na huko duniani, na maadamu wanao uwezo wa kunenea, haya yote yanaonyesha bila shaka kwamba farasi ni mfano wa wajumbe wa Bwana, wa wale ambao Yeye huwatuma kwa mataifa. {1TG11: 5.2}

Wekundu, wa kijivujivu, na weupe, aina kadhaa za farasi, huonyesha kundi la watumwa wa jamii na mataifa tofauti. Kwa hivyo, farasi hawawezi kuchukuliwa kuwakilisha ama watumwa wa Waebrania

5

siku za Zekaria, au siku za Kristo kwa sababu watumwa wa Bwana katika siku hizo walikuwa wote wa jamii moja — Wayahudi, sio wa rangi nyekundu, ya kijivujivu, na nyeupe. Baada ya kukamilisha kazi yao, farasi walir-ipoti kwamba “wamekwenda huko na huko duniani” na kwamba hata hivyo dunia imetulia na bado inastarehe — haifanyi chochote juu yake. {1TG11: 5.3}

Kwa kuwa ni ukweli unaojulikana kwamba katika siku za Zekaria wapeleka ujumbe wote walikuwa Wayahudi (watu wa jamii moja na taifa moja), nembo hiyo hakika ni mwafaka kwa siku ambayo Mungu anawateua wain-jilisti wa jamii na mataifa mbalimbali, ambao Yeye anawapeleka hoko na huko duniani — kwa mataifa yote. {1TG11: 6.1}

Vitambulisho hivi vyote hakika vinaonyesha wazi kwamba farasi wanawakilisha Waadventista wa Siku ya Kwanza ambao waliamshwa kati ya miaka ya 1833 na 1844 na ambao wakati huo waliutimiza unabii huu wa mfano kwa kutangaza ujio wa pili wa Kristo kwa kila utume wa Ukristo, duniani kote, lakini wakiwa wamekan-ganya kutakaswa kwa patakatifu (Dan. 8:14) — utakaso wa kanisa, kazi ya Hukumu, mavuno, ya kutenganisha ngano kutoka kwa magugu (Mat. 13:30), samaki wazuri kutoka kwa wabaya (Mat. 13:47, 48), wanawali wenye busara kutoka kwa wapumbavu (Mat. 25: 1-12), kondoo kutoka kwa mbuzi (Mat. 25:32), wageni waliovaa vazi la harusi kutoka kwa wale ambao hawakuwa na hilo vazi (Mat. 22: 2-13). Kazi hii ya Hukumu inaanza kwanza miongoni mwa wafu (kazi ya vitabu tu, bila shaka – Dan. 7:10), kisha miongoni mwa walio hai (utengo halisi wa mwili — kutakasa — Ezek 9). {1TG11: 6.2}

Kwa sababu unabii wa Danieli wa sura ya nane, yaani siku 2300, ulionyesha kwamba kazi ya Hukumu ilikuwa ianze mwaka wa 1844 B.K. lakini kwa kuwa ilivyoeleweka visivyo kwamba dunia ingalifikia mwisho badala yake,

6

walivunjika moyo sana wakati tarehe kamili ilikuja na hakuna kitu kilichotukia. Kwa hivyo ilikuwa kwamba maadamu tarehe kamili ilikaribia walirejea kutoka kwa nyanda za utume wao kwa imani kamili kwamba walikuwa wameikamilisha kazi yao, — kwamba walikuwa “wamekwenda huko na huko duniani “ — na kwamba haukuwapo muda tena, kwamba dunia wakati huo ingefikia kikomo. {1TG11: 6.3}

Kuhusu upeo wa kazi yao Pambano kuu, uk. 368, unayo haya ya kusema: “Maandishi ya Miller na washirika wake yalipelekwa hadi nchi za mbali. Popote wamishonari walikuwa wamepenyeza duniani kote, zilipelekwa habari njema za kurudi haraka kwa Kristo. Kote kote ulienezwa ujumbe wa injili ya milele, “Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” {1TG11: 7.1}

Kwa hiyo ilikuwa ni kwamba farasi (wajumbe) walifikiri kazi yao imekwisha, lakini malaika aliyejua ukweli hakika, na kuwaona watu wa Mungu bado wakiwa mateka, bado wakiwa mbali na nchi yao, wakati ambapo wapagani walikuwa wamestarehe, alisihi kwa ajili ya tendo: {1TG11: 7.2}

Aya ya 12 — “Ndipo yule malaika wa Bwana akajibu, akasema, Ee Bwana wa majeshi, hata lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?”

Utabiri wa nabii Yeremia kwamba Wayahudi wangepaswa kukaa miaka sabini uhamishoni Babeli ulikuwa umekamilika ingawa walikuwa bado Babeli. Lakini kwa vile unabii huu wa mfano unapata utimizo wake katika siku zetu badala ya siku za Zekaria, ombi la malaika “kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda,” kwa hivyo, lin-apata utimizo wake wa moja kwa moja leo. Upo, hata hivyo, huu usambamba: Wakati wa

7

uhamisho wa Babeli ulipishana miaka kadhaa na wakati wa kurudi Yerusalemu, hali kadhalika utabiri wa Yo-hana kwamba kanisa linapaswa kurudi kwenye shamba la mizabibu baada ya kukaa miaka 1260 nyikani (katika nchi za Mataifa) (Ufu. 12: 6), ilikuwa amekwisha na kupishana tangu mwaka wa 1798 na hapakuwa na ishara yake kurejea. Na kwa sababu Dhehebu halikuwa katika hali ya kuupokea Ukweli wa nyongeza, matokeo ni kwamba kanisa bado liko nyikani jambo ambalo Uvuvio ulisema, “Iwapo watu wa Mungu wangekuwa wameenda kufanya kazi kama walivyopaswa kuifanya mara baada ya mkutano wa Minneapolis katika mwaka 1888, dunia ingalikuwa imeonywa kwa miaka miwili na Bwana angalikuwa amekuja.” – Matangazo ya Baraza Kuu, 1892. {1TG11: 7.3}

Ujumbe huu sasa unatangaza kwa hakika kwamba kukaa kwake nyikani kumekaribia kumalizika na kwamba hivi karibuni litasimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo (Ufu. 14: 1). Kutoka kwa mtazamo huu wa uchambuzi inaonekana tena kwamba ombi la malaika kwa ajili ya kuurehemu Yerusalemu na miji ya Yuda li-nahusu moja kwa moja watu katika siku zetu, na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa watu katika siku za Ze-karia. {1TG11: 8.1}

Aya ya 13, 14 — “Naye Bwana akamjibu yule malaika aliyesema nami kwa maneno mazuri, maneno yenye faraja. Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Haya, piga kelele na kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Naona wivu kwa ajili ya Yerusalemu, na kwa ajili ya Sayuni; naona wivu mkuu sana.”

Badala ya kusema, “Zayuni … utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu” — Mika 3:12, Bwana alionyesha wivu Wake mkubwa kwa ajili yao, na akawaamuru watumishi Wake “piga kelele tena” na kusema: {1TG11: 8.2}

Aya ya 16, 17 — “Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi,

8

Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema Bwana wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu. Piga kelele tena, na kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Miji yangu kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko tena; naye Bwana ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena.”

Kwa sababu nuru juu ya unabii huu sasa inaangaza njiani mwetu kwa mara ya kwanza tangu Zekaria aliuandika, na maadamu ujumbe huu sasa unatangazwa kote kote Laodekia, Ukweli kwamba Bwana, hatimaye, amerejea (amezuru) kwa rehema ni dhahiri sana. {1TG11: 9.1}

Baada ya kuvunjika moyo mwaka wa 1844, wajumbe wa Ukweli katika Kristo waliambiwa “piga kelele tena” (endelea kuhubiri) na kusema “Bwana wa majeshi asema hivi, Miji yangu kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko tena; naye Bwana ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena.” {1TG11: 9.2}

Hivyo ilikuwa kwamba baada tu ya tarehe iliyowekwa mwaka wa 1844 kupita na matumaini ya watu ya-kashindwa, Bwana aliwatia moyo kwa kumpa Dada White maono ya kuwakusanya malimbuko, watu 144,000, wa kwanza kwenda hadi Mlima Zayuni na huko kusimama na Mwana-Kondoo (Ufu. 14: 1), faraja ya Zayuni na Yerusalemu. Kwa hivyo walianza tena kwa lengo la kuwakusanya watumwa wa Mungu ambao hawana uongo watu 144,000, wale ambao watatumika kuwakusanya mavuno ya pili, watu wengi wasiohesabika kutoka katika mataifa yote (Ufu. 7: 9). Lakini kadiri muda ulivyoendelea badala ya kufanya kazi na Mungu Dhehebu lika-kengeuka kwa kutoamini katika Roho ya Unabii (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217) na hivyo kupoteza maono ya ukweli ambao ulikuwa bado ungekunjuliwa, na ambao sasa umeletwa kwenye nuru. {1TG11: 9.3}

9

Hivyo ilikuwa kwamba mara tu kuvunjika moyo kwa 1844 kulipokuja, ambako kunawakilishwa na kitabu kid-ogo kubadilika kuwa uchungu baada ya kukila, malaika alisema: “Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.” Ufu. 10:10, 11. Vuguvugu la ujio wa pili wakati huo lilipangwa upya na jina Waadventista wa Sabato likakabidhiwa kwalo. Hivyo Bwana aliwaagiza wajumbe Wake “piga kelele tena,” wa-tangaze tena, waendelee kuhubiri nuru ya ziada — Hukumu kwa Wafu. Kupatakasa patakatifu (Dan. 8:14), uta-kaso wake kwa kuyaondoa vitabuni (Dan. 7:10) majina ya wale wanaopatikana hawastahili kuamka katika ufufuo wa kwanza, ufufuo wa watakatifu (Ufu. 20: 5, 6). {1TG11: 10.1}

Hapa inaonekana kwamba Uvuvio mara moja hauangazi kwenye njia yetu wazi mpaka mwisho, ila kwamba Un-afanya hivyo hatua kwa hatua; kwamba Ukweli wa Mungu ni endelevu; kwamba hatuwezi kamwe hakika kus-ema sisi tunao Ukweli wote wa kutupeleka wazi kupitia katika Malango ya Lulu. {1TG11: 10.2}

Kuhusu njia ambazo zitawezesha kurejea kwa watu wa Mungu katika nchi yao wenyewe, tutasoma– {1TG11: 10.3}

Aya ya 18, 19 — “Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu.”

Zamani za kale ufalme wa Israeli ulimiliki sehemu ya kaskazini ya nchi ya ahadi, na ufalme wa Yuda ulimiliki sehemu yake ya kusini. Wa awali alikuwa ulitawanywa na wafalme wa Ashuru na wa mwisho na mfalme wa Babeli. Wale ambao walirejea Yerusalemu

10

katika siku za Zekaria walikuwa kutoka ufalme wa Yuda, Wayahudi, lakini kwa sababu ufalme wa Israeli ulikuwa umefyonzwa na mataifa, kwa hivyo ukapoteza utambulisho wake wa jamii na kitaifa. Dola ambzo zili-watawanya Yuda na Israeli, unaona, zinawakilishwa na pembe nne. {1TG11: 10.4}

Aya ya 20, 21 — “Kisha Bwana akanionyesha maseremala wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioin-ua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.”

Hapa dola zile zile zilizowatawanya Yuda na Israeli zinaonekana tena, sio kama pembe, bali kama maseremala; sio kuwatawanya watu wa Mungu, bali kujenga kwa ajili yao, na kuzitupa nje pembe (tawala) za Mataifa — wale wanaoitawala nchi. Kwa uwazi, basi, kwa upande mmoja mataifa ambayo hayamiliki Palestina yatainuka kama “pembe” dhidi ya yale ambayo yanaitawala, na kwa upande mwingine yatainuka kama maseremala kwa ajili ya watu wa Mungu. Hivyo “majira ya Mataifa yatakapotimia” Luka 21:24. Kwa hivyo, wale tu ambao wataokoka hukumu kwa ajili ya Walio Hai, katika nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17), wale ambao majina yao hayajafutwa kutoka Kitabuni (Ufu. 3: 5) watajumuisha kanisa, ambao miongoni mwao watakuwa wana 144,000 wa Yakobo (Ufu. 7: 3-8), na wakati Mikaeli atasimama basi wale majina yao yatakuwa yameachwa katika Kitabu wa-taokolewa kutoka “taabu mfano wake haukuwapo” (Dan. 12: 1). Wao ni “masalia,” wale ambao wanaokoka wakiwa hai kutoka kwa Hukumu kwa ajili ya Walio Hai katika Nyumba ya Mungu. Hivyo hekalu la uakisi litajengwa (Ezekieli sura ya 40-43) na miji itaenea mbali. {1TG11: 11.1}

11

Kisha hawa watumwa wa Mungu ambao hawana uongo, malimbuko, watatumwa kwa mataifa ambayo hayajasikia habari ya Mungu (wasio Wakristo), na watautangaza utukufu Wake kati ya Mataifa na watawaleta ndugu zao wote, mavuno ya pili, wote wanaopaswa kuokolewa, hadi katika nyumba ya Bwana (Isa. 66:16, 19, 20), kwa kanisa la Mungu lililotakaswa, ambamo hamtakuwa na dhambi tena na hakuna kubahatisha kugongwa na mapigo (Ufu. 18: 4). {1TG11: 12.1}

Wapofu kwa Ukweli huu, kwa Hukumu ya Walio Hai, “siku kuu na ya kutisha ya Bwana,” siku ambayo vitu vyote vinapaswa kurejeshwa, Walaodekia wanaonekana wakiwa katika udanganyifu wa kusikitisha. Soma Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253 na Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. Wasipoamka kutoka kwa shida yao wa-tapatikana wamepungua na kutapikwa nje. {1TG11: 12.2}

Wayahudi walipofushwa kwa sababu waliziba masikio yao kwa manabii na hawakuttii yale waliyonena. Malaika wa kanisa la Laodekia leo anasema kwa majivuno, “Sina haja ya ama manabii wala ya Ukweli zaidi” — kukataa unabii na jumbe hata kabla ya kuja, ingawa anajua vyema kwamba ujumbe wa Hukumu kwa ajili ya Wafu sio wa mwisho. Hukumu kwa ajili ya Walio Hai ndio wa mwisho. {1TG11: 12.3}

Kitabu cha Zekaria kwa ukamilifu wake wote kimekuwa kitabu kilichofungwa, lakini maadamu maana yake ya kiroho ya undani sasa imefunuliwa kwa uwazi na kuletwa kwa usikivu wa kanisa, basi wale wanaoikataa na kufanya kazi dhidi yake wanatenda vibaya zaidi kuliko Wayahudi walivyowaua manabii na Bwana. {1TG11: 12.4}

Sasa inaonekana wazi wazi kwamba Neno la Mungu huishi milele. Mwanadamu anaweza kuwaua wajumbe wa Mungu, lakini

12

hawezi kuliharibu Neno Lake. Kwa hakika ni kama mbegu ya haradali. Ingawa Linaweza kukanyagiwa chini ya mguu ili Lisitafutwe tena kuliko mbegu ya haradali baada ya kutupwa ardhini, lakini mara tu Chuo kin-apokunjua, Linachipuka upya. {1TG11: 12.5}

Wakati ujumbe huu ulianza kukunjua, Walaodekia walijaribu kwa jeuri kuua, lakini bado unaendelea kuwa hai na unakua kwa kasi. Wao bado wanajaribu kuua, lakini kwa vile hawakuweza kufanya hivyo wakati ulikuwa mdogo na dhaifu sana kama vile kijani kidogo cha mbegu ya haradali, wanawezaje kufanya hivyo sasa maadamu umekua na kuzaa matunda? {1TG11: 13.1}

Ssi kwa hivyo hatuna wasiwasi juu ya uwezekano wa mtu yeyote kuidhuru kazi ya Mungu. Wala sisi tusiwe na wasiwasi kuhusu jinsi tunavyoweza kufika Mlima Zayuni, ila tuhakikishe tuwe tayari kupanda gari la Mungu wakati malaika wanapiga kelele, “Nyote ndani!” Hebu tukumbuke daima kwamba wale ambao wakati mmoja waliuharibu ufalme wa zamani na kuwatupa nje watu wake, sasa watakuja kuujenga na kuzitupa nje pembe za Mataifa ambazo sasa zinaitawala nchi, kwa hivyo hata adui zetu wa jana Mungu anawaweka wafanye kazi kwa ajili yetu leo. {1TG11: 13.2}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyo na kifani ya ahadi za Mungu, matarajio ya vizazi vyote, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina lako na anwani kwenye Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG11: 13.3}

13

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Kabla ya kushiriki katika sala, nitasoma kutoka kwa Mlima wa Baraka, uk. 162, 163. Somo lina msingi kwa andiko, “Utupe leo riziki yetu ya kila siku.” {1TG12: 14.1}

M.B., uk. 162, 163 — “Nusu ya kwanza ya sala ambayo Yesu ametufundisha, ni juu ya jina na ufalme na mapen-zi ya Mungu, — kwamba jina lake liheshimiwe, Ufalme Wake uanzishwe, mapenzi Yake yatimizwe. Ukishafanya hivyo huduma ya Mungu kuwa maslahi yako ya kwanza, unaweza kuomba kwa imani kwamba mahitaji yako mwenyewe yanaweza kujazwa …. Usifadhaike ikiwa huna ya kutosha kesho. Unalo hakikisho la ahadi Yake, ‘Utakaa katika nchi, na hakika utashibishwa.’” {1TG12: 14.2}

Yesu hakuchota chochote kutoka ghalani, kwa njia ya mfano. Alipokea siku kwa siku ugavi mpya kwa mahitaji Yake yote, kwa ajili Yake mwenyewe na kwa ajili ya kazi Yake. Naam, kila kitu — mada ya mafundisho Yake, divai kwenye ndoa, chakula cha kulisha umati, na hata sarafu kulipia kodi. Yote haya Yeye aliyapokea kama Alivyoyahitaji. Kamwe Yeye hakupungukiwa chochote. Iwapo tutafanya Ufalme wa Mungu kuwa shughuli yetu kuu Alivyofanya, kufanya kazi kwa ajili Yake kama Alivyotenda, kuomba kama Alivyoomba, kuamini ka-ma Alivyoamini, — basi hatutakuwa na sababu ya kupokea mapungufu kuliko Yeye. Utajiri wa mbinguni utaku-wa mikononi mwetu. Kwa kweli Yeye anatuhakikishia: “Na hayo yote mtazidishiwa.” {1TG12: 14.3}

Sasa tutaomba kwa ajili ya nini? — Tunapaswa kuomba kwamba hangaiko letu la kwanza lisiwe kimsingi la ugavi wetu wenyewe kwa bidhaa za ulimwengu huu, ila, badala yake, litakuwa la kuuendeleza Ufalme wa Mungu; kusali ili tuweze kutambua hakika kwamba ni shughuli Yake na upendezi wake mwema kutumikia mahitaji yetu, na kwamba tufanye kuwa shughuli na furaha yetu kuyatumikia maslahi Yake. {1TG12: 14.4}

14

IWAPO 144,000 TU WANAHAMISHWA BILA KUFA, UNAYO NAFASI GANI?

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, OKTOBA 26, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutaendelea tena na utafiti wetu wa Zekaria mbili. Mambo mengi, hata hivyo, Zekaria mbili ni endele-zo la kisa ambacho huanza katika sura ya kwanza, tutaanza somo letu na hicho. {1TG12: 15.1}

Zek. 1:20, 21 — “Kisha Bwana akanionyesha maseremala wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioin-ua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.”

Awali nabii aliwaona hawa kama pembe nne, kama tawala ambazo ziliwatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu katika nchi zote za Mataifa, lakini kama malaika alivyoonyesha mtazamo wa unabii kwa wakati wa mwisho ali-waona kama maseremala wanne; yaani, kama “pembe” walikuja “kuwatawanya” na “kutupa nje pembe za Ma-taifa” kutoka katika nchi ya Yuda, lakini kama maseremala wao bila shaka wanakuja kujengea Yuda. Inaoneka-na kwamba, basi, wakati pembe (tawala) za Mataifa zinafukuzwa nje ya nchi, na watu wa Mungu kuletwa ndani yake, basi “majira ya Mataifa” yatakuwa yametimizwa. {1TG12: 15.2}

15

Baada ya kuonyeshwa nembo ya pembe nne na maseremala wanne, tahadhari ya nabii iligeuzwa kwa nembo nyingine. Tulisoma kuihusu katika aya nne za kwanza za sura ya pili: {1TG12: 16.1}

Zek. 2: 1-4 — “Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama ka-ribu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake.”

Kutoka kwa ukweli kwamba malaika ghafla aliamuru kijana asiupime Yerusalemu, inaonekana wazi kwamba mtu kwa hatua yake mwenyewe alikuwa ameanza kufanya kitu ambacho hakikuwa katika mpango wa Mungu. Kwa hivyo, jitihada zake za kuupima mji (idadi ya wakazi wake) zilikuwa wazo lake la kimakosa au la mwingine fulani ambalo alirekebishwa kwa upesi na kuambiwa dhahiri kuachana na jaribio lake la kuupima mji; kwamba utakuwa kama mji usio na kuta, hakuna mstari wa mipaka uliowekwa, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo; hauwezi, kwa hivyo, “kupimwa” (kuhesabiwa). {1TG12: 16.2}

Kwa kuwa Uvuvio unatazama chini kwa wakati wetu, na kwa kunena katika maneno yetu, “kijana” kwa hivyo anawakilisha watumwa wa Kikristo wa siku za mwisho (vijana, sio wazee) ambao wanajishughulisha na utawala wa wafasiri wa Biblia ambao hawajavuviwa na ambao humwekea Bwana mipaka, hudhani kwamba watakatifu walio hai katika mji watakuwa wachache sana hivi kwamba mtu anaweza kuwahesabu, yaani 144,000, bila kuzingatia kwamba hawa ni “malimbuko” (Ufu. 14: 4) ya “mavuno” makubwa. {1TG12: 16.3}

16

Maelezo ya malaika ya kwamba Yerusalemu utakaliwa na umati wa watu wasioweza kuhesabika na ng’ombe, yanathibitisha kwamba hii ilikuwa habari kwa kijana huyo. Ni lini na jinsi gani katika mzunguko wa wakati am-bapo kijana huyu anarekebishwa? – Hitimisho la kiakili na la haki ambalo mmoja anaweza kufikia, ni kwamba wakati Roho ya Unabii inakunjua chuo, wakati Mungu anapomwinua mfasiri wa Maandiko, basi inakuwa kwamba marekebisho kama hayo ya mafundisho yanaweza kufanywa. {1TG12: 17.1}

Muhimu sana ni Roho ya Unabii aliye hai kanisani, kama uzoefu wa “kijana” unavyothibitisha, kwamba bila kujali bidii ya mmoja, uaminifu na uadilifu, hawezi kumtumikia Mungu ipasavyo bila Hiyo, kwamba hata kazi bora na azimio ni lazima yawe yanayopingana na ya Mungu. Kwa hivyo, ni wakati mzuri kwa kanisa kuanza kuamini yote ambayo manabii wameandika, “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:20, 21. {1TG12: 17.2}

Uvuvio unasisitiza kwamba haiwezekani kabisa kwa mmoja apendavyo (bila Roho wa Kweli) kufasiri maandiko yaliyotiwa muhuri. Na tukumbuke kwamba hakuna Ukweli wowote uliofunuliwa uliwahi kuja, wala utawahi kuja kupitia kwa kumbi za kujifunza. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwamba wewe uwachane na Malaika wa Walaodekia usije, pia, utapikwe nje (Ufu. 3:16). Ikiwa anachagua kulisha kwa hotuba zake tupu, bado akifun-disha kwamba kanisa halihitaji Ukweli zaidi, kwamba anao wa kutosha kumpeleka kupitia katika lango la lulu, kwamba anaweza bila Uvuvio kuyafasiri Maandiko na kujua ni nini Ukweli, basi mwache mwenyewe ale karamu yake isiyotakatifu. Mwambie kwamba unapendelea kuishi kwa “chakula kwa wakati wake” (Mat. 24:45) moja kwa moja kutoka kwa

17

Kiti cha enzi cha Mungu. Sasa sikiliza rai ya Mungu: {1TG12: 17.3}

“Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.” Isa. 3:12. “Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni; nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, wa-takaowalisha kwa maarifa na fahamu.” Yer. 3:14, 15. {1TG12: 18.1}

Daima masikio yako yawe wazi kwa dai lolote la Uvuvio iwapo hutataka kuirudia historia ya Wayahudi. Mungu hatakuacha udanganywe iwapo unayo njaa na kiu cha haki, ikiwa unataka hakika kuijua Kweli, kwa maana Yeye anatazamia kwamba uambatane na Ukweli Wake hatua kwa hatua uliofunuliwa. Kwa hivyo hakuna hatari kwa ajili ya mtu kudanganywa kwa kukutana na uongo, lakini ipo hatari kubwa ya kukaa gizani kwa kutokutana na Ukweli mpya. Ushauri wa Uvuvio ni hivi: {1TG12: 18.2}

“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yoh. 4: 1. Kuishika amri hii ni muhimu sana kama kuishika nyingine yoy-ote. {1TG12: 18.3}

Ili kuwa wazi zaidi, malaika wa Laodekia hudhani kwamba watakuwa tu watakatifu 144,000 walio hai – kundi la kupimwa au la kuhesabiwa — ambao wataujumuisha Ufalme. Pia anaamini kwamba hakuna aina ya ng’ombe watakaopelekwa huko, yote ambayo ni kinyume cha yale malaika wa Mbinguni alifunua: kwamba sio kundi linaloweza kuhesabiwa la watakatifu walio hai ila badala yake umati mkubwa ambao hakuna mtu anayeweza kuuhesabu watakuwa papo hapo wakazi wa Yerusalemu, Ufalme wa milele — kanisa lililotakaswa na kutengwa mbali na ulimwengu ili

18

walioitwa kutoka Babeli waweze kupata kimbilio ndani Yake. Watu 144,000 ni “malimbuko” tu (Ufu. 14: 4) na kundi kubwa la watakatifu wasioweza kuhesabika walioonyeshwa katika Ufunuo 7: 9 ni mavuno ya pili, kwa maana ambapo hakuna la pili hapawezi kuwapo la kwanza. {1TG12: 18.4}

Wazee, ninyi hutuambia kwa kiburi kwamba Dhehebu sasa lina idadi karibu washiriki milioni moja, na kwamba limeweka lengo lake kuwa na washiriki maradufu. Kwa upande mmoja mnajisifu kuhusu ukuaji wake wa haraka, na kwa upande mwingine mnajaribu kulipinga fundisho la “Fimbo ya Mchungaji” kuhusu umati mkubwa wa Ufunuo 7: 9 ambao “Fimbo” huthibitisha kwa Maandiko kwamba ni mazao ya pili ya mavuno. Kwa msimamo wenu kushikilia kuwa idadi ya watakatifu walio hai watakuwa wachache, 144,000 tu, na kujisifu kwenu juu ya ukuaji wa Dhehebu na maelfu mengi ya washiriki walio tayari kanisani, ninyi kwa hivyo mnatengeneza utata kwa ajili ya nafsi zenu na kwa ajili ya wote wanaowaunga mkono. Mbali na hili, mnakubali kwamba sehemu kubwa ya kazi bado itafanyika — kwamba wapo mamilioni juu ya mamilioni hata ndani ya Marekani yenyewe ambao hata sasa hawajapata kusikia sana jina Waadventista wa Sabato, sembuse “Injili ya milele.” Ni dhahiri, kwa hivyo, Wandugu, kwamba kwa kiwango cha sasa cha ukuaji, wakati kazi imekamilika na Yesu anakuja ku-lichukua kanisa Lake hadi kwa nchi ya utukufu, Dhehebu kwa wakati huo litakuwa limeongezeka kwa milioni kadhaa thabiti. {1TG12: 19.1}

Licha ya msingi huu ambao ninyi Wazee mmeujenga wenyewe, lakini kinyume chake, mnafundisha kwamba wakati Yesu anapokuja, watakuwapo watakatifu 144,000 walio hai tu, hakuna zaidi! Je, ninyi Wazee hamja-changanyikiwa na mnakanganya! Iwapo hakika mnaamini katika nadharia yenu ya 144,000, basi mwaweza kati-ka Roho ya Kristo na angalau kwa ajili ya nafsi zenu wenyewe, mchukue karatasi na penseli na ipasavyo mchukue takwimu asilimia

19

ya watakatifu na asilimia ya magugu, mashetani, ambao hata sasa wanajumuisha ushirika wa makanisa yetu? Kwa sababu tayari idadi sio chini ya 800,000, na iwapo watakuwamo watakatifu 144,000 tu ndani yake wakati Yesu anakuja, basi kwa mujibu wa uwiano huu, kwa kuzingatia washiriki wakati huu wa sasa, kutaniko la washiriki 100 hata sasa linaweza kujumuisha watakatifu 18 na mashetani 82! Ikiwa hii ni hivyo, basi unayo nafasi gani? Na maadamu maafisa wanaoendesha makanisa huchaguliwa kwa kura za walio wengi, je, mnaona ni nani aliyewachagua, ni nani aliye katika ofisi, na ni nani anayeyadhibiti makanisa? Je, mwashangaa basi ni kwa nini mambo yanaendeshwa jinsi yalivyo? {1TG12: 19.2}

Ikiwa ni kweli kwamba watakuwapo tu watakatifu 144,000 watakaokuwa hai wakati Yesu atakapokuja, na iwapo ushirika utakuwa maradufu kufikia mwishoni mwa 1953 au 1954 jinsi lengo linavyoonekana kuwa (inga-wa nina shaka), basi kwa kiwango hicho mwaka wa 1955 watakuwapo tu watakatifu 9 kwa mashetani 91 kuto-ka kwa kila washiriki mia moja. Kwa hivyo, ikiwa ushirika utakuwa maradufu mara kadhaa kabla Yesu aje ku-lipokea kanisa Lake, basi hakutakuwa na hata mtakatifu mmoja kati ya washiriki mia! Bado nafasi ndogo zaidi kwako! Ikiwa hili ni hivyo, basi jiulize wenyewe kanisa ni la nani? — la Ibilisi? au la Bwana? na Yeye atalitafuta wapi Atakapokuja? {1TG12: 20.1}

Kweli hizi za kusikitisha zinasimama juu kama milima dhidi ya fasiri zenu za kibinafsi, Wazee, na kama vifum-bua macho kwa makundi yenu. Iwapo kwa hivyo mnaendelea kusema kwamba hamjalala usingizi, kwamba fasiri zenu za Neno haziwezi kutiliwa shaka, kwamba mnao Ukweli wote wa kuwapitisha katika Malango ya Lulu, kwamba hamna haja ya kitu chochote, basi hakuna tumaini; mmeenda mbali sana. {1TG12: 20.2}

Sisi binafsi tunajua, hata hivyo, kwamba wapo wengi ambao hawajapumbazwa sana, ambao hawajamsujudia

20

Baali, ambao hawajajiruhusu wenyewe kufungiwa katika mazizi kwa mfano, kama kondoo na ng’ombe, na walaghai ambao hudhibiti na kulilisha kundi la Mungu huko na maganda ya kiwango cha chini kama haya jinsi somo hili linavyoonyesha. {1TG12: 20.3}

Kujisifu kwenu juu ya mafanikio ya Dhehebu na kwa waongofu wake wengi ulimwenguni kote, iwapo ni kweli, Ukweli sasa unawapatia mtihani kujibu kwa uaminifu maswali ambayo yanajitokeza: Kwa nini mnawapatia ma-tumaini ya makao katika Ufalme iwapo mnajua kwamba hawawezi kuokolewa? Je, huku kuwakusanya ndani sio udanganyifu wa wazi na jaribio kubwa zaidi la kuingiza kanisani magugu ambayo hayajawahi sikika? na huu sio uasherati wa kiroho wa aina mbaya zaidi wa kulijaza kanisa la Mungu na mashetani? {1TG12: 21.1}

Ili kuufunika usingizi mzito unaoonekana kwa takwimu zilizotajwa hapo awali, mchungaji mmoja alielezea: “Wakati kazi inafunga,” alisema, “watakuwa kanisani maelfu wengi zaidi ya watu 144,000 watakatifu wa-takaokuwa hai, bali badala ya kuhamishwa bila kufa, idadi yao kubwa watakufa kutokana na mapigo au kwa tauni kabla ya Yesu kuja, kwa sababu hawatakuwa wazuri ipasavyo kuhamishwa bila kufa ingawa wakamilifu ipasavyo kwa ajili ya ufufuo”! {1TG12: 21.2}

Nini kifumbua jicho cha namna gani kwa waumini haya mafundisho mashuhuri ya uwongo! Na ni nguvu ya namna gani na nafasi nzuri sasa kwa ajili yenu Wazee kukubali shtaka la Kristo kwamba ninyi ni “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi.” Ufu. 3:17. Iwapo Roho wa Kweli hawezi sasa kuwashawishi kwa Ukweli na haki, basi Yeye hataweza kamwe. Kwa hivyo, ni, muhimu kwamba sasa mukiri kwa waumini hatia yenu ya kutoa mafundisho ya uongo, kwamba hamtaendelea kujipumbaza wenyewe au makundi yenu kwa kupoteza wakati na nguvu kujaribu kuupima Yerusalemu. Hekima hupiga

21

kelele kwamba ninyi mara moja muweke moyoni ushauri Wake: {1TG12: 21.3}

“Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, [Ukweli uliovuviwa], upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.” Ufu. 3:18, 19. {1TG12: 22.1}

Kwa ajili yenu mambo haya yamewekwa mbali kwa jicho la umma, lakini kwa sababu mmedharau kabisa kila rai iliyotumwa kutoka Mbinguni kwa miaka ishirini yote, sasa mnavuna mazao. Uchi wenu, mwaona, tayari umean-za kufunuliwa. Na iwapo hamtaitikia Ukweli huu na kugeuka dhidi ya machukizo yaliyofunuliwa hapa, na kwa furaha kuipokea rai hii ya matengenezo, hatimaye kila mmoja atajua kwamba matendo yenu, Wazee, ni majaribio ya makusudi kuwadanganya yamkini “wateule,” watu 144,000, ambao, kwa mujibu wa unabii ambao sasa ume-funuliwa, wote karibu sasa wako ndani ya kanisa. Tutaendelea sasa na unabii wa Zekaria wa sura ya pili: {1TG12: 22.2}

Zek. 2: 5 — “Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.”

Ukuta wa mawe tu uliuzunguka Yerusalemu katika wakati wa Zekaria. Bali ukuta wa moto utauzunguka Ye-rusalemu wa wakati wetu, Yerusalemu ambao Zekaria aliagizwa kuandika. Ni kutoka Yerusalemu huu wa mwi-sho ambao Bwana atatufundisha njia Zake, na kutufanya tuenende katika mapito Yake, “kwa maana,” atangaza nabii wa injili “… katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” Isa. 2: 3. Hivyo mwito: {1TG12: 22.3}

22

Aya ya 6 — “Haya, Haya, njooni, Ikimbieni nchi ya kaskazini, asema Bwana; kwa maana mimi nimewa-tawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema Bwana.”

Taarifa “nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni,” haiwezi kuwekewa mpaka kwa Wayahudi huko Babeli. Hukumbatia kutawanywa kimataifa kwa watu wote wa Mungu, Yuda na Israeli, katika nchi zote za Ma-taifa. Kwa sababu unabii huu umeelekezwa kwa wakati wetu, basi mwito wa “njooni” na “ikimbieni nchi ya kaskazini” utatangazwa kwa watu wa Mungu wakati Babeli wa Ufunuo sura ya kumi na saba unatawala. Mwito, “ikimbieni nchi ya kaskazini” ni sawa na mwito, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu.18: 4. Mwito huu hauwezi kuchukuliwa kumaanisha kwamba watu wa Mungu wanapaswa kutokea nje ya jengo moja, au kutoka kwa nchi moja, na kwenda kwa nyingine ambapo, pia, dhambi hufanyika. Mahali ambapo wanaitwa kuja lazima pawe huru kwa dhambi na hivyo huru kwa mapigo. Bila shaka wanaitwa kuja katika Ufalme ambao raia wake papo hapo watakuwa malimbuko, watu 144,000, kanisa lili-lotakaswa na kutengwa na ulimwengu. Kisha litaambiwa, “…maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiye-tahiriwa, wala aliye najisi.” Isa. 52: 1. {1TG12: 23.1}

Aya ya 7 — “Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli.”

Hakika ni kwamba “binti Babeli” hawezi kuwa mama, Babeli wa kale. Badala yake, lazima awe Babeli wa siku za mwisho, Babeli anayemwendesha (mtawala) mnyama mwekundu sana. (Ufu. 17). {1TG12: 23.2}

23

Ni dhahiri, zaidi ya hayo, kwamba watakatifu wote wanaitwa watoke Babeli kabla ya mapigo ya Ufunuo 16 yamwangukia iwapo watataka kuokolewa kutoka kwayo. Lakini Zayuni anaweza kujiokoaje mwenyewe, ikiwa hayasiki maonyo ya Bwana kumwacha Babeli? Kwa hivyo ni ya dharura sana kwamba ujumbe huu uyafikie masikio yake. {1TG12: 24.1}

Aya ya 8 — “Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.”

Mungu aliruhusu watu Wake watawanywe (kuharibiwa) kati ya nchi za Mataifa, lakini sasa Yeye atawatuma wajumbe Wake baada yao kwa sababu wale wanaowagusa, huigusa, kama mfano, mboni ya jicho Lake, kiungo chenye hisia zaidi cha mwili . Kanisa lake, “utukufu,” ndilo Yeye hulijali sana. {1TG12: 24.2}

Aya ya 9 — “Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao walio-watumikia; nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma.”

Watumwa kuwaharibu mabwana zao ni mojawapo wa ishara kwa wakati unabii huu unaletwa nuruni. Na ulim-wengu unajua kwamba kazi na usimamizi sasa umehusishwa katika mapambano yao makubwa, na kwamba kama matokeo ya Ukomunisti unatishia dunia yote. {1TG12: 24.3}

Taarifa, “nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma,” imetumika mara kadhaa katika unabii wa Zekar-ia. Tunaipata mara mbili katika aya ya 9 na 11 mtawalia za sura ya 2, na mara moja katika aya ya 9 ya sura ya 4. Inaashiria nini? — Ni dhahiri inamaanisha kwamba kwa wakati maandiko haya yanafunuliwa, wengi wa watu ni wasiosadiki bali hatimaye watajua kwamba Bwana ameupeleka ujumbe huu kwao. {1TG12: 24.4}

24

Wasiosadiki kama ada husubiri mpaka pawepo ushahidi usio na shaka kabla ya kutambua kwamba ujumbe ni wa kutoka kwa Mungu, lakini huenda usiwatendee mema yoyote saa hiyo ya mwisho. {1TG12: 25.1}

Aya ya 10 — “ Piga na kushangilia, Ee binti Sayuni; maana, tazama, naja, nami nitakaa katikati yako, asema Bwana.”

Kwa hakika huu ujio wa Bwana sio ule watakatifu watakutana Naye katika hewani (1 Thes. 4:16, 17), kwa maana Bwana katika andiko hili hasemi kwamba Anakuja kuwapokea watu Wake ili waweze kukaa na kutawala pamoja Naye miaka elfu (Ufu. 20: 4), ila kwamba baada ya wadhambi kuondolewa mbali kutoka kati yao Anakuja ‘kukaa’ pamoja nao, kuwalinda kutoka kwa hasira ya nchi za Mataifa wakati wa “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa.” Yeye anawalinda kwa “ukuta wa moto kuwazunguka pande zote.” Wakati huo wa taabu u karibu hapa. Dunia inauona ukija. Je, Wewe, Ndugu, Dada? Na unafanya nini kuhusu hilo? {1TG12: 25.2}

“Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka. Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisaf-isha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa

25

sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbil-ia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4: 2-6. {1TG12: 25.3}

Kwa hiyo kuja kwa Bwana katika Zekaria, ni sawa na kusimama kwa Mikaeli kuwaokoa wote ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu. Dan. 12: 1. Kumbuka siku zote kwamba vitabu vimefunguliwa na kuchunguzwa wakati wa Siku ya Hukumu. (Dan. 7:10). Kwamba majina yetu yapatikane katika “Kitabu” hicho inatupasa sasa liwe hangaiko linalomshughulisha sana kila mmoja wetu. {1TG12: 26.1}

Aya ya 11 — “Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako.”

Mara tu sisi kama Dhehebu tunapoamka kwa ukweli kwamba “mataifa mengi watajiunga na Bwana,” na kuwa watu Wake, wakati huo tu nadharia ya malimbuko pekee yao itakufa. Na mara tu ujumbe huu unapomfikia kila mshiriki wa kanisa, wakati huo utakaso utatukia. “Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.” Mal. 3: 3, 4. “Yule asiyefaa kitu hatapita tena kamwe” kati yako, “amekwisha kukataliwa mbali.” Nah. 1:15. {1TG12: 26.2}

Sasa yanaonekana wazi jinsi mawazo yetu duni yamekuwa kuhusu kazi kubwa ya Mungu na njia Yake ya kui-kamilisha, bila kujua kwamba wakati kazi inaendelea kukamilika, umati mkubwa, ambao hakuna mtu anayeweza kuuhesabu, kutoka

26

katika mataifa yote (Ufu. 7: 9), watajiunga na “mlima wa nyumba ya Bwana” na watakuwa watu Wake (Isa. 2: 2). Omba, “Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike duniani kama [yalivyo] huko Mbinguni.” Hitaji la uamsho na matengenezo halisi sasa linakuwa dhahiri sana. Je, Uhuisho na matengenezo humaanisha nini? — “Uhuisho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uhuisho huashiria kufanywa upya uhai wa kiroho, kuzifanya kuwa hai nguvu za nia na moyo, ufufuo kutoka katika kifo cha kiroho” na “Matengenezo huashiria kupanga upya, badili-ko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea.” — Kristo Haki Yetu, uk. 121, toleo la 1941. {1TG12: 26.3}

Hatimaye, chunguza kwamba Zekaria 2 inasheheni ukweli ule ule Isaya 2, Mika 4, Yeremia 31, na Ezekieli 36 husheheni. {1TG12: 27.1}

Hebu tuendelee na somo letu na: {1TG12: 27.2}

Aya ya 12 — “Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atauchagua Yerusal-emu tena.”

Hili ndilo Biblia hufundisha, na hakuna yeyote anayeweza kumudu kutoliamini Neno la Mungu. Huu ukiwa ni ujumbe wa sasa, na maadamu wote watahukumiwa kwa Huo, basi ikiwa hatuupokei kikamilifu tutaweza kuwa mbele ya Mungu sifuri ila “kwekwe za ardhi.” Yanayoitwa eti matendo yetu mazuri tu hayatatuongoza kutoka Babeli, ila kufahamu kwetu Ukweli wa wakati huu, na kuutii kikamilifu mwito wa Mungu, mapenzi Yake. {1TG12: 27.3}

Unakumbuka kwamba wakati Nuhu alipokuwa akihubiri kwamba uharibifu ungekuja kutoka kwa Mwenyezi, alikuwa pia akiandaa mahali pa kimbilio — akijenga safina. Wale waliokosa kuliamini tangazo la Nuhu la gharika, na waliodharau wazo kwamba walipaswa kuingia

27

ndani ya safina kwa ajili ya usalama wakati ambapo hapakuwa hata na ishara ya kutisha ya mvua, hawakuen-delea kutoamini tena wakati elementi za asili zilipoachiliwa. Kisha kwa uwazimu wakaikimbilia safina; lakini kwa kufadhaika kwao na kuvunjika moyo kabisa, walipata mlango umefungwa kabisa dhidi yao. Hivyo wote, wema na wabaya waliochagua kubaki nje ya safina, waliangamia. Uzoefu wa walioishi kabla ya gharika una-paswa kutukumbusha kwamba tusiwe wenye kiburi kama walivyokuwa. Tunapaswa badala yake kuliweka moyoni onyo la wazi ambalo linafaa kwa saa hii, maana tumeambiwa kwamba kama ilivyokuwa siku za gharika, ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwa Bwana. {1TG12: 27.4}

Safina ya leo ni “Zayuni na Yerusalemu,” “kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na Neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika. 4: 2. {1TG12: 28.1}

Aya ya 13 — “Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.”

Kumbuka kwa makini kile Neno linasema, “Ameamka,” sio “Ataamka.” Dhahiri, basi, wakati Bwana aliutamka unabii huu, Yeye aliyaonyesha maneno Yake katika siku za baadaye, akizungumza kwa wakati uliopo kana kwamba kwa wakati huo unabii ulikuwa katika mchakato wa kutimizwa. Hivyo taarifa, “kwa maana Ameamka,” inamaanisha kwamba sasa penye ufunuo wa Ukweli huu “Ameamka”; na taarifa, “Bwana atairithi Yuda, iwe se-hemu Yake katika Nchi Takatifu,” inamaanisha kwamba Yeye bado atairithi Yuda, kanisa lililotakaswa. Sasa tunaishi, kwa hivyo, kati ya ncha hizi mbili za wakati — kati ya “Ameamka,” na “ Bwana atairithi.” {1TG12: 28.2}

Azimio letu sasa litakuwa nini? Tutafumba macho yetu kwa mafunuo haya ya kicho na ya utukufu

28

ya matukio ambayo yanafanyika sasa? Tutakosa kuamini na kuendelea kusubiri matokeo? au tutaamka kwa moyo wote na kuyatenda mapenzi ya Mungu? Je, Ufalme Wake au maskani zetu zitafanywa maslahi yetu ya kwanza? Iwapo sasa hatuwezi kurekebisha nia zetu zilizopotoka, basi tunawezaje kusema kwa uaminifu, “Ufal-me wako uje, mapenzi yako yatimizwe”? na tunawezaje kutarajia mambo ya muda kwa maisha “yote tuzidishi-we?” Mat. 6:33. {1TG12: 28.3}

Je, Tumeamua mara moja na milele kumtumikia Mungu, sio ubinafsi, kujifunza zaidi kuliko hapo awali, na kuweka kando kila shaka? Bwana asema hivi, “… Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.” Isa. 49: 6. {1TG12: 29.1}

“… Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.” Zab. 96:13. {1TG12: 29.2}

29

 

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG12: 30.1}

30

Itakuwa Bora Na Wewe

Uwe na utulivu, Ee nafsi yangu,

Tulia kila hofu!

Baba yako anao udhibiti mkuu,

Na Yeye daima yu karibu.

Kamwe ya kura yako usilalame,

Chochote kitakachotokea,

Ugonjwa au huzuni, utunzi au maumivu,

Ni salama hali zote.

Mkono wa adhabu wa Baba

Unaendelea kukuongoza:

Sio mbali ni nchi ya ahadi,

Ambapo unafurika wimbo wa milele.

O, basi, nafsi yangu, tulia!

Ngojea amri kuu ya mbinguni;

Tafuta ila kufanya mapenzi ya Baba yako,

Itakuwa salama nawe.

–Thomas Hastings

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 11, 12

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>