fbpx

Trakti Namba 14

TRAKTI NAMBA 14

UTABIRI WA HALI LA VITA

1 (Jalada)

Hati miliki 1943

na, V.T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya kweli aweze kuipata, trakti hii ni, kama huduma ya Kikristo, hu-tumwa bila malipo. Tuma ombi lako. Huweka tu dai moja: wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyajaribu mambo yote na kushika lililo jema. Nyuzi za pekee zinazounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu za Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga. {TN14: 2.1}

Majina na anwani za wa S.D.A. zitakazotumwa kwetu zitathaminiwa.

TRAKTI NAMBA 14

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Imechapishwa Marekani

2

UTABIRI WA HABARI ZA VITA

KUUMENG’ENYA UTABIRI WA NAHUMU

Wakati magari yanafurika njiani, yanaposongana-songana katika njia kuu, yanapokwenda kasi kama umeme, na kuonekana kama mienge, katika siku hiyo yeye asetaye vipande vipande anajiandaa na kuja mbele ya uso wako, Ee mfalme wa Ashuru. Atakufanyaa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana. Kutakuwa na maumivu mengi katika viuno vyako, na nyuso za wote zitakusanya weusi. Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi; mateka hayaondoki. Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka. {TN14: 3.1}

Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali. Maana sasa Bwana ataivunja nira ya Ashuru kutoka shingoni mwako, kuvipasua vifungo vyako, na kukuweka huru. {TN14: 3.2}

Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi. Njia Yake I katika kisulisuli

3

na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu Yake. Yeye ni mwenye wivu na atalipiza kisasi juu ya maadui Zake. Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; Naye huwajua hao wamkimbiliao. Lakini Yeye atawakomesha kabisa waovu, giza litawafuatia adui Zake. Mateso hayatainuka mara ya pili. {TN14: 3.3}

* * *

Nahumu anaziona tawala mbili kuu katika vita vinayoonyeshwa kwa siku ambayo kila kitu juu ya magurudu-mu hukwenda kama “umeme.” Kisha kwa njia tofauti kabisa, hukazia uangalifu kwa mmoja anayetembea dhahiri juu ya milima, si kwa kujificha katika mabonde, na ambaye huchapisha amani badala ya vita. Anamhimiza Yuda kuwa mwaminifu ili kuitekeleza amani hiyo, akimhakikishia kwamba waovu hawatakuwa kati yake tena, na ya kwamba atawekwa huru kutoka kwa nira ya Mwashuru. Kwa wakati uo huo, anauona uwezo mkuu wa Mungu, wivu Wake kwa watu Wake na kisasi Chake kwa adui zao. {TN14: 4.1}

Wakati anatabiri uwezo wa tawala hizi mbili hasimu za kutaka vita, Nahumu kwa wakati uo huo anatabiri ka-nisa kuwekwa huru kutoka kwa nira ya Mwashuru, iliyonakiliwa katika sura ya 1, aya ya 12-15, na katika sura ya 2, aya ya 2; na pia kisasi cha Mungu kilichoandikwa katika sura ya 1, aya ya 1-9. Ili kuwezesha ufahamu wa msomaji wa vipengele hivi jumla vyote vitatu vya utabiri huu, trakti hii inashughulika na kila kimoja mbali mbali. {TN14: 4.2}

4

Sasa basi, nani, hasa, ndio waigizaji katika utabiri huu wa sarakasi? Hasa ni nani, chini ya mpangilio wa sasa au wa baadaye wa mataifa wanaweza kuwa ndio hawa wawili wanaotaka vita? Na je, wamekuja kwa makabili-ano? Ikiwa la, wanakusudia kufanya hivyo lini. {TN14: 5.1}

Iwapo tunataka kujua kwa hakika majibu kwa maswali haya yasiyoweza kuepukika, tutayapata katika

MUHTASARI WA UCHAMBUZI. {TN14: 5.2}

Dola mbili zinaonekana zikiinuka katika uwezo wao kupambana. Kwa hakika, wasiwasi wa kitabu chote cha Nahumu, kwa ujumla sura tatu ndogo tu, ziko na kitovu katika maandalizi ya vita hivi, pambano lenyewe, na majina ya tawala zinazohusika. {TN14: 5.3}

Kidokezi cha kwanza kwa suluhisho hili ni kwamba maandalizi ya vita yanafanyika wakati magari yenye mwako wa mienge “yanafanya mshindo njiani,. . . yanasongana-songana katika njia kuu,” na “yanakwenda kwa kasi kama umeme,” Nah. 2:3, 4. Ni wazi kwamba maandalizi haya yanafanywa wakati barabara za miji na mas-hambani zimesongamana kwa magari. {TN14: 5.4}

Kidokezi cha pili ni kwamba vita vyenyewe vinatukia wakati nguvu za mitambo zimestawi kwa kiwango kwamba magari yanaendeshwa kwa kasi inayoonekana kama umeme.

5

Vita vyenyewe, kwa hivyo, vitapiganwa na majeshi yenye mitambo. {TN14: 5.5}

Kidokezi cha tatu ni kwamba dola moja, inayoitwa “Ashuru,” inalo jina la urithi, ambalo hufichua kwamba ni mwenzi mamboleo wa wakati mmoja ufalme ulioenea sana wa Ashuru ya kale jinsi Babeli mamboleo ya Ufunuo 17, aya ya 5, ni mwenzi wa Babeli ya zamani, na kwa sababu “Misri ya kiroho” ya Ufunuo 11, aya ya 8, ni mwenzi mamboleo wa Misri ya kale. (Tazama Pambano kuu, uk. 269, 270.) Hawa wenzi wote, basi, ni tangazo lingine la Kimaandiko, na thibitisho, la ukweli mkongwe kwamba historia hujirudia tena, na kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko cha asili. {TN14: 6.1}

“Tunasimama kwenye kizingiti cha matukio makuu na mazito. Unabii mwingi unakaribia kutimizwa kwa mfululizo wa haraka. Kila chombo cha nishati karibu kitatumiwa kufanya kazi. Historia iliyopita itarudiwa; mapambano ya kale yatazinduka kwa maisha mapya, na hatari itawazonga-zonga watu wa Mungu kila upande. Ukali unaishikilia familia ya wanadamu. Unaenea kwa kila kitu juu ya nchi.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 116. {TN14: 6.2}

Jambo moja ni kwamba dola nyingine, “Yeye asetaye vipande vipande,” amejipatia jina alilopata kutokana na matendo ya dhuluma zake Dhahiri, kwa hivyo, huashiria taifa linaloongozwa na mtawala

6

asiyekuwa wa nasaba ya kifalme, lakini wa tabia isiyoeleweka na nguvu isiyokuwa na kifani, ambaye ubunifu wake wa kijeshi huwatawanya na kuwaangamiza wote wanaothubutu kumpinga. {TN14: 6.3}

Pasipo kujali endapo huu ufunguo wa njia nne unafichua kambi hizi mbili kuwa “Mhimili” na “Umoja wa Ma-taifa” leo, usalama pekee wa mtu wa kutonaswa na kuharibiwa sasa hivi au baadaye katika mapambano haya yaliyotabiriwa, ni kuifuata kikamilifu njia ambayo Mungu kinabii ameiweka kwenye ramani. Hakika, unabii umepeanwa si kwa sababu nyingine kuliko kuziangazia hatua za msafiri hadi kwa usalama. “. . . Bali wenye haki watapona kwa maarifa.” Mit. 11:9. {TN14: 7.1}

Sasa tukiwa na ufunguo mkononi, tutaweza kuifungua siri, tukianza na

KAKARAKAKARA ZA WANAOTAKA VITA. {TN14: 7.2}

Nahumu, Sura ya Kwanza

Nah. 1:10,11 “Kwa maana wanapopindana kama miiba [wameungana na wengine ili kujilinda], na wakati wamelewa kana kwamba ni walevi [wamejazwa kwa dhana], wataangamizwa kabisa kama mabua makavu [kama wakati moto hupita kati yake]. Ametoka mmoja kwako [taifa linalosifika kama Ashuru ya kale], aniaye mabaya juu ya Bwana, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.” {TN14: 7.3}

Katika nuru ya vifungu hivi, inakuwa wazi tangu mwanzoni kwamba ingawa “Ashuru” amejihami na kuun-gana na mataifa mengine yenye nguvu (“wanapopindana kama miiba”), hata hivyo silaha zake wala

7

muungano wake hautamwokoa. Kwa maana amelewa kama mlevi, akiwa amepokea mashauri maovu ya yule aliyetoka kwake, “wataangamizwa kabisa kama mabua makavu.” “Bwana asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake.” Nah. 1:12, sehemu ya kwanza. {TN14: 7.4}

Sura ya Pili.

Nah. 2:1. “Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.” {TN14: 8.1}

Akija uso kwa uso na uwezo wake “asetaye vipande vipande,” Ashuru anafukuzwa kwa kasi kujiimarisha. Na ingawa kwa kuongezea kujiimarisha kwake, nguvu zake za muungano kwa idadi ni kubwa zaidi kuliko nguvu za muungano wa “yeye asetaye vipande vipande” (ikiwa hakika yeye anaweza kuwa ameungana hata kidogo), hata hivyo jina lake hasa huashiria kwamba dhidi ya uwezo wake ngome zote za Mwashuru “gome zako zote zitaku-wa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye.” Nah. 3:12. {TN14: 8.2}

Nah. 2: 3. “Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yanayo mwako wa nuru siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inati-kiswa kwa namna ya kutisha.” {TN14: 8.3}

Ni dhahiri sana kwamba dola hii ya uchokozi ambayo “huseta vipande vipande,” inajifunga

8

kwa ajili ya vita siku ambayo magari yanayo mwako wa nuru (za umeme taa za mbele za gari) ambazo hufanana na “mienge yenye kuwaka”! Katika siku ya ishara hii, “misunobari [watawala wakuu wa dunia — Ezek. 31:1-14] itatikiswa sana.” {TN14: 8.4}

Nah. 2:4. “Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, Yanasongana-songana katika njia kuu; kuon-ekana kwake ni kama mienge, yanakwenda upesi kama umeme.” {TN14: 9.1}

Tena, hakuna kukwepa hitimisho kwamba dola hizi mbili zinatumbukia vitani moja na nyingine kwa wakati ambapo kila kitu cha magari kinaendeshwa kwa kasi isiyo na kifani, na ya kwamba maandalizi yao ya pupa kwa makabiliano lazima kwa hivyo ni pamoja na utekelezaji wa majeshi yao ya vita ulioimarishwa na “magari” ya-naokwenda kwa kasi. Danieli pia, aliambiwa kwamba katika “wakati wa mwisho; wengi watakaimbia huko na huko, na maarifa yataongezeka.” Dan. 12:4. {TN14: 9.2}

Kwa sababu mpangilio wa vita hivi vikali ni katika siku ya ustawi wa mitambo, havingaliweza kuwa Vita Kuu vya 1 vya Dunia, kwa sababu maandalizi ya moto huo mkubwa yalikuwa kwenye mchakato wakati kizazi cha mitambo kilipokuwa bado kichanga. Hata wakati vita vilipokuwa vinaendelea, magari yalikuwa machache sana, hafifu sana, na ya pole pole sana kusongana-songana kwa namna iliyotabiriwa. Kwa kuutimiza utabiri, hizi dola mbili sharti zijiandae wakati magari ni mengi na yenye nguvu na ya kasi, kama ilivyo leo. {TN14: 9.3}

9

10

11

Hivi si kusema kwamba Vita vya Dunia vya awali vimetengwa kutoka kwa unabii, ila tu kwamba msingi tofauti wa Maandiko umetolewa kwa ajili yake. Mwokozi Mwenyewe alitabiri kwa usahihi kabisa kwamba vita vya kutisha vingefikia upeo karne kumi na tisa za vita na tetesi za vita, aliposema: “Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.” Mat. 24:7, 8. {TN14: 12.1}

Hakika basi (1914-1918), kwa mara ya kwanza tangu maawio ya historia, mataifa na falme ziliinukiana, njaa ilinyemelea nchi zilizoharibiwa kwa vita, kiongozi wa kifo tauni akafuata, na mitetemeko ya ardhi kwa mfululizo wa haraka ilivurumisha uharibifu wake ili kurundika juu ya matatizo ya wanadamu. Majanga haya yote lakini yalielekeza hadi Vita Kuu vya 2, vile vya kutisha sana vya wakati wote. Kweli, hakika majonzi ya Vita Kuu vya 1 vya Dunia viliweka tu saini kwa mwanzo wa huzuni! {TN14: 12.2}

Nah. 2:5-8. “Awakumbuka watu wake wenye heshima; wanajikwaa katika mwendo wao [yaani, ingawa anajiinua ndani yao, hata hivyo, wataanguka]; wanafanya haraka waende ukutani [ngome]; nao ulinzi [na Ashuru] utawekwa tayari. Malango ya mito [hata hivyo] yatafunguka, na jumba la mfalme [wa Ashuru] litayeyushwa. Huzzab naye [wa Ashuru] atachukuliwa mbali mateka, ataletwa, na wajakazi wake [mataifa chini ya utawala wake]

12

watamwongoza kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao. Lakini Ninawi [mji mkuu] tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa [raia wake] wanakimbia; simameni! simameni! watapiga kelele; Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.” {TN14: 12.3}

Tofauti na maji yanayotiririka au yanayoinuka-inuka, maji katika bwawa husimama tulii. Lakini katika hali hii, maji (watu) katika mji mkuu wa “Waashuru,” mamboleo kinyume na matarajio yao yote na desturi yao ya kupi-gana, watakimbia. Na hata wakati watakaposikia amri ya kusimama, watakuwa na wasiwasi sana kumwondokea njiani yeye “asetaye vipande vipande” kwamba hawatathubutu kutazama nyuma. {TN14: 13.1}

Hivyo, kwake yeye “asetaye vipande vipande,” amri ni: “Chukueni nyara za fedha; chukueni nyara za dhaha-bu; kwa maana ni akiba isiyoisha, fahari ya vyombo vipendezavyo.” Nah. 2:9. {TN14: 13.2}

Baada ya kutoa amri hii ya kuiharibu Ashuru, Bwana anaugeukia “mji wa damu” na kutangaza juu yake ad-habu inayosababisha: {TN14: 13.3}

Nah. 2:10-13. “Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yana-gongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu. Kao la simba [makasri ya mfalme] li wapi? Na mahali walishapo wana-simba [utawala wa wakuu wake] pa wapi, mahali alipotembea simba mume na simba mke [mfalme mkuu], na mwana-simba [mwana wa mfalme], wa-la hapana aliyewatia hofu? Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwa-songea wake zake [malkia]

13

nyama, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake [hazina] aliyajaza mawindo [utajiri]. {TN14: 13.4}

“Tazama, Mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi, Nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; Nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.” {TN14: 14.1}

Sura ya Tatu.

Nah. 3:1-19: “Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi; mateka hayaondoki. Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake. {TN14: 14.2}

Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; Nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; Nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako. Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, Nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau. Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikuta-futie wapi wafariji? Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake. Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Putu na

14

Walibia walikuwa wasaidizi wake. Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo. {TN14: 14.3}

“Wewe [Ashuru] utalewa; utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui. Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye. Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako. Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako; Zitie nguvu ngome zako; Ingia katika udongo, yakanyage matope, Itie nguvu tanuru ya kuokea matofali. [sekta ya viwanda]. Huko moto utakuteketeza; Upanga utakukatilia mbali; Utakumeza kama tunutu alavyo; Jifanye kuwa wengi kama tunutu! Jifanye kuwa wengi kama nzige! Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake. Watu wako waliotiwa taji [mabwana wadogo] ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, wa-tuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani. [ni wapenzi wa starehe na anasa]. Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashu-ru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya. Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima?” {TN14: 15.1}

Hata hivyo, “wakati wo wote Nitakapotoa habari

15

za taifa, na habari za ufalme, kuung’oa, na kuuvunja, na kuuangamiza; ikiwa taifa lile Nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake Nitaghairi, Nisitende mabaya yale Niliyoazimia kuwatenda.” Yer. 18:7, 8. {TN14: 15.2}

Kuona kwamba Bwana yu karibu kumshusha “Ashuru” kwa manufaa yake mwenyewe, ila kwamba Yeye an-geghairi kufanya hivyo ikiwa tu angeweza kutubu kama alivyofanya Ninawi wa zamani kwa onyo la Yona, Ni dhahiri kwamba Utabiri huu umechapishwa sio kulifaidisha kanisa pekee bali “ Ashuru” na washirika wake pia, na hata adui wao. {TN14: 16.1}

Hata hivyo, kama hawa wachokozi hawataweza kwa hiari kuamka kwa ukweli kwamba Hatma haipo miko-noni mwao bali katika mikono yenye nguvu ya Mungu aishiye milele na wa Uweza wote, basi Yeye atawaleta bila wao kutaka kuitambua, na kuwaacha tu raia wao wanaomcha Mungu, jinsi Yeye anavyotangaza: {TN14: 16.2}

“Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuru atafika Misri, na Mmis-ri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuru. Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya nchi; kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki, akisema, wa-barikiwe watu Wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono Yangu; na wewe Israeli, urithi Wangu.” Isa. 19:23-25. {TN14: 16.3}

16

Hivyo katika rehema Yake ya milele Bwana angeuinua “mzigo wa Ninawi” leo, kama alivyotenda katika siku ya kale. Hakika, ni kwa ajili ya “baraka kati ya nchi,” hata kwa mataifa yote, kwamba Yeye atasababisha

KANISA KUWEKWA HURU KUTOKA KWA NIRA YA “MWASHURU”. {TN14: 17.1}

Nah. 1:12, 13. “Bwana asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa Nimekutesa, Sitakutesa tena. Na sasa Nitakuvun-jia nira yake kutoka kwako, Nami nitakupasulia mafungo yako.” {TN14: 17.2}

Mtu huyu (“nimekutesa”) ambaye Bwana amemtia nidhamu, hakika hawezi kuwa mfalme wa Waashuru au taifa lililotajwa awali, kwa sababu Bwana anamkomboa huyu, ilhali anawapiga Waashuru hadi kwa magoti mikononi mwake “asetaye vipande vipande.” Ni nani hasa aliye mtu huyu wa tatu (“nimekutesa”) aliyetajwa hapa anaweza kuwa, anathibitishwa upesi na Isaya katika unabii wake unaouwiana kumhusu Ashuru huyu: {TN14: 17.3}

“Tena itakuwa katika siku hiyo,” asema nabii, “mzigo wake [ya Mwashuru] utaondoka begani mwako [mwa Yuda], na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta.” Isa. 10:27. {TN14: 17.4}

17

Haraka tunaona kwamba katika nuru inayofunuliwa katika maandiko haya, yule mmoja (“nimekutesa”) am-baye, katika matukio yote, anawekwa huru wakati wa kuanguka kwa Ashuru, inathibitisha kwamba ni kanisa (Yuda) anayewekwa huru kutoka kwa utawala wa Mataifa (Mwashuru). Mwisho, kwa hivyo, Isaya anafafanua unabii wa Nahumu akirejelea ukombozi wa kanisa kutoka kwa nira ya Ashuru wa siku ya mwisho. Ukweli, hata hivyo, kwamba kanisa, anavyosema Nahumu, sio tu kuondolewa kwenye mateso na kuwekwa huru kutoka utumwani lakini pia kuhukumiwa kifo (Nah. 1:14), unajenga utatanishi! Uvuvio, hata hivyo, unautatua haraka, tena kupitia Isaya. Akizungumzia kanisa, anatangaza: {TN14: 18.1}

“Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule Wangu. Na Bwana Mungu atakuua; Naye atawaita wa-tumishi Wake kwa jina lingine.” Isa. 65:15. {TN14: 18.2}

Dhahiri, kwa hivyo, katika wakati ambapo Mwashuru anavunjika, Bwana atafanya kazi maradufu kati ya watu Wake wanaomkiri, ambao baadhi yao watawekwa huru kwa sababu ya uaminifu wao, na baadhi yao wa-tachinjwa kwa sababu ya uovu wao. Wale waliookolewa hatimaye wataitwa kwa jina lingine. {TN14: 18.3}

Wakati wa “kazi” hii unaitwa “mavuno.” Mat. 13:30. Kwa hivyo, hadi kwa utengo huu, magugu (wale ambao watachinjwa) na ngano (wale watakaookolewa) pamoja hujumuisha

18

ushirika wa Laodekia (la mwisho kwa makanisa saba — Ufu. 3:14-18), kanisa kabla tu ya “magugu” kutengan-ishwa milele na “ngano” (Mat. 13:30). Dhahiri kabisa, basi, Walaodekia waliotubu wanatengwa kutoka kwa wale ambao hawakutubu wakati wa anguko la Mwashuru, na kisha wanawekwa huru kutoka kwa utawala wake. {TN14: 18.4}

Nah. 1:14. “Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako Nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; Nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.” {TN14: 19.1}

Hivyo, kwa wakati huu, milele anaangamia mwabudu sanamu na sanamu zake. {TN14: 19.2}

Onyesho lenye maelezo la utakaso huu wa kanisa limeonyeshwa katika unabii wa Ezekieli. Humo Bwana anamwamuru yeye ambaye huandika historia ya maisha, malaika mwenye kidau cha mwandishi, kupita kati ya mji na kutia alama (muhuri) kwa wale tu wanaougua na kulia dhidi ya machukizo yaliyo kati yake. Kisha wen-gine watano wanamfuata kuwachinja wote ambao hawana alama. (Tazama Ezekieli 9, Shuhuda kwa Wa-chungaji, uk. 445; Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266, na Gombo la 5, uk. 211.) {TN14: 19.3}

“Mji” ni mfano wa Yuda na Israeli, kanisa ambamo watapatikana watumwa wa Mungu watu 144,000 (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445) wale ambao wataitwa kwa jina lingine baada ya watumwa wasiostahili ku-chinjwa. Na kama

19

watu 144,000 ni malimbuko (Ufu. 14:4) ya mavuno, ndio “waliokoka” wa Isaya 66:19 na Ezekieli 9. Utengo huu wa magugu kutoka kwa ngano kanisani utaashiria mwanzo wa mavuno ya mwisho ya dunia — mwisho wa dunia. Kisha utakuwa umefika wakati wa jina la dhehebu kukoma, kwa sanamu zake zote kukataliwa mbali, na jina ji-pya (Isa. 62:2) kupeanwa kwa wale waliookoka. Ndipo hawa waliookoka watatangaza utukufu wa Mungu na sifa Yake kwa Mataifa, na kuwaleta kutoka kwa mataifa yote ndugu zao wote (wote ambao wataokolewa) hadi katika “nyumba ya Bwana.” Isa. 66:16, 19, 20. {TN14: 19.4}

Ili hukumu kama hiyo iepukwe, kanisa lote lazima liweze kutubu mawazo yake yenye makosa, lianze kujihisi kutokuwa na starehe katika uvuguvugu wake, liweze kuwa baridi au moto (kutotosheka), na kuwa ukiwa kwa ubinafsi na kujazwa na Roho. (Ufu. 3:14-18). {TN14: 20.1}

Nah. 1:15. “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” {TN14: 20.2}

Jina, “Yuda,” huambatishwa kwa kanisa la Kikristo sio tu kwa sababu ya umuhimu wa uakisi lakini pia kwa sababu ya urithi. Hili litaonekana tunapoipitia historia ya Yuda: {TN14: 20.3}

20

Makabila kumi (Ufalme wa Israeli) yalitawanywa na Ashuru ya kale kote kote katika miji ya Wamedi, na ku-fyonzwa na Mataifa ya siku hiyo, ila haikuwa hata miaka kadhaa baadaye ya kwamba makabila mawili (Ufalme wa Yuda) yalichukuliwa Babeli, wakasalia hapo mpaka mwisho wa miaka sabini ya unabii wa Yeremia, kisha wakarudi hadi katika nchi yao. Hivyo ndivyo tu wazawa wa Ufalme wa Yuda ambao hawakuwa waaminifu ya kwamba walimkataa na kumsulubisha Bwana. Lakini waaminifu kati yao walimpokea, na wakawa Wakristo, washiriki waasisi wa kanisa la Agano Jipya. Kanisa lenyewe kwa hivyo, ni binti wa Ufalme wa Yuda. Kwa hivyo bado linaitwa Yuda. {TN14: 21.1}

Wakati likiwa kwa njia ya nasaba, uaminifu, na usafi (bila magugu) kwa uhalali linapaswa kuitwa “Yuda,” bado kwa sababu ya uvuguvugu wao wa siku za mwisho na tokeo la kuingizwa kwa “magugu” ndani ya ushirika wake, ni, kwa hitaji, pia linaitwa “Laodekia.” {TN14: 21.2}

Kwa kujipaka “dawa ya macho” (Ufu. 3:18), watatazama “juu ya milima miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani!” Na wakimwona Yeye, wataupokea ujumbe Wake na wataujua ukweli na ukweli utawaweka

21

huru, na utawaokoa kutokana na kutapikwa nje ya kinywa chake (Ufu. 3:16). {TN14: 21.3}

Kwa hivyo, wanapoamka tu na kuitii sauti ya Shahidi wa Kweli, na kugeuza hatua zao kuelekea malango ya Ufalme, wataweza siku zote kutarajia kushiriki katika tukio la Mungu: “Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” {TN14: 22.1}

Hapa katika usemi wa kinabii sio tu ahadi ya kulitakasa kanisa wakati Ashuru mamboleo anapopondwa, ila pia taarifa ya kupendekeza kuhusu nini kinachojumisha “chakula kwa wakati wake” kwa ajili ya watu leo; na ni vuguvugu gani wanapaswa kujisajili ndani iwapo wangeufanya wa uhakika wokovu. Wanashauriwa kuyakazia maono yao juu ya miguu yake aletaye “habari njema” (ujumbe kutoka kwa Bwana), anayetangaza “amani” (ama-ni ya Ufalme wa Kristo), na ambaye anatangaza kwamba wakati ambapo tawala za dunia zimefunikwa katika vita kubwa, waovu ndani ya kanisa watakatiliwa mbali, hawatapitia kati yake tena. Hasa, nabii anawahimiza wote kwa toba kuigeukia nyumba ya Yuda (Ufalme wa Yuda wa siku za mwisho — Mika 4: Ezek. 37:16-22), kanisa katika utakaso ambamo watatiwa muhuri watu 12,000 kutoka kwa kila kabila 12, kama malimbuko. Na anawahimiza raia wa ufalme kutekeleza kazi zao za kidini na kuziweka

22

nadhiri zao kwa Bwana. Kwa ufupi, anawahimiza kuuzingatia ujumbe wa saa ya sasa — ujumbe unaotangaza ulio karibu sana utakaso wa kanisa, baada yake, ilivyo ahadi, “waovu hawatapita kati yake tena,” kwa maana “wamekwisha kukatiliwa mbali.” (Angalia pia Mat. 13:30, 47-50, Isa. 66:16, 19, 20). {TN14: 22.2}

“Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; na mfalme atamiliki, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina Lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU. Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, aishivyo Bwana, Aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri; lakini, aishivyo Bwana, Aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote Nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.” Yer. 23:5-8. {TN14: 23.1}

Njia pekee ya “malaika” wa Laodekia (ambaye juu yake kemeo la kuwa “mnyonge, mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi,” na bado ameridhika) kuingia katika ufalme huu wa utukufu, ni yeye kwa hiari kuachia mamlaka ya udhibiti wa kanisa, kadiri anavyomuona Bwana

23

Mwenyewe akiyachukua katika mikono Yake Mwenyewe (Shuhuda kwa Waahungaji, uk. 300). Amka, kwa hivyo, Ee “malaika” wa Laodekia, kwa kilio cha mchocheo cha Mbingu: {TN14: 23.2}

“Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa, wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; uondoke, uketi, Ee Yerusalemu; jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa. Sauti ya walinzi wako! Wanapa-za sauti zao, wanaimba pamoja; maana wataona jicho kwa jicho, jinsi Bwana arejeavyo Zayuni.” Isa. 52:1, 2, 8. {TN14: 24.1}

Iwapo Vita vya sasa vya Dunia ndivyo vilivyotabiriwa na Nahumu, na ikiwa kutiwa muhuri au kuwekwa alama kwa “watumwa wa Mungu” kutakamilika bila malaika kukaza tena kuzishikilia pepo (Ufu. 7: 1, Maandishi ya Awali, uk. 38), basi wakati wa kurejesha fahari ya Yakobo na ya Israeli umekaribia. Mwishowe imefika saa ya ukombozi wa Zayuni kutoka kwa utumwa wa Mataifa, na kwa watoto wake kurejea katika nchi ya baba zao (Ezek. 36:23-38), shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi. Kwa hivyo basi asimame tayari na mwenye ari, akisubiri amri ya Bwana Wake kuanza mwendo wa kwenda huko. {TN14: 24.2}

Ni kwa wakati huu ya kwamba Ashuru anaanguka, sababu ikiwa: {TN14: 24.3}

24

Nah. 2:2. “Kwa maana Bwana anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.” {TN14: 25.1}

Akiwa tayari (kupitia kwa watekao nyara) amewaadhibu watu Wake, Bwana hatawaadhibu tena, ila sasa Atawaweka huru. {TN14: 25.2}

Kushiriki pamoja na mataifa hatia ya kuyaharibu matawi ya shamba Lake la mizabibu (Ufalme Wake), huyu Ashuru mamboleo lazima sasa ashiriki katika kisasi cha Mungu wakati Mungu anawarudisha watu Wake katika nchi yao wenyewe. Kwa kufahamu, pamoja na kuanguka kwa “Waashuru” (Mataifa wanaoimiliki Nchi ya Ahadi), “majira ya Mataifa” yatakuwa yametimia (Luka 21:24). {TN14: 25.3}

Kutazama mbele hadi kwa wakati huu wa ukombozi, malaika alimwambia Danieli: “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wa-taokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12:1. {TN14: 25.4}

“Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao

25

watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.” Isa. 27:13. {TN14: 25.5}

Ahadi ya utukufu! Je, moyo wako umejikita kwayo Ndugu, Dada? Basi bila kukawia itikia agizo la Mungu: “Mwelekeeni Yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukim-bia upanga, na vijana wake watashindwa. Naye atapita juu ya ngome yake kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto Wake u katika Zayuni, na tanuru Yake katika Yerusalemu.” Isa. 31:6-9. {TN14: 26.1}

“Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan. 12:10. {TN14: 26.2}

Nahumu huweka wazi kwamba katika vita hivi Mungu anaingilia dhidi ya Ashuru, na ya kwamba kwa tokeo lake hawezi kumkabili yeye “asetaye vipande vipande.” Baada ya Yeye kujiweka kumnyenyekeza, kwa hivyo Yeye anaimarisha mikono ya adui wake. Kwa hivyo, Mwashuru anaanguka, si kwa sababu yeye ni dhaifu na mdogo au kwa sababu yeye amezidiwa kwa idadi

26

na kushindwa, ila kwa sababu kusudi la Mungu linaamua anguko lake. Kwa maneno mengine, muungano ambao unaweza kuwa na rasilimali kubwa na nguvu za wanadamu, na ambao kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu unaweza kuonekana kuwa na uhakika wa kushinda, katika suala hili hakika unapoteza. {TN14: 26.3}

Kama hiki ni kigezo kinyume cha historia. Daima Mungu ameyahukumu mataifa yaliyoelimishwa au watu ambao wamekuwa wenye haki ya ubinafsi na wenye kujitegemea hivi kwamba taa zao zimezimika na kazi zao kuwa za uovu na unafiki. Daima Yeye amewaadhibu kwa upanga wa mbaribari mshenzi na mwovu kabisa. Hili Yeye hufanya kwa sababu mbili: kwanza, ya kwamba waweze kuona upumbavu wa kujidai kuwa watu waadilifu, wakati wao kwa hakika ni wabaya zaidi kuliko washenzi; na pili, ya kwamba wakati hawa wanafiki hapo wanaongozwa kutubu, waliowashinda wanaweza hapo kuongozwa kuona kwamba ushindi wao si kwa nguvu zao wenyewe. Hivyo wote mshindi na mshindwa wanaletwa mahali ambapo wanaweza kujisalimisha kwa Mungu na kumpa Yeye utukufu. {TN14: 27.1}

Baada ya kuishinda Babeli ya zamani, Koreshi, mbaribari, alipata kwamba ushindi wake na hata jina lake lilikuwa limeandikwa katika unabii mtakatifu miaka mingi kabla ya kuzaliwa (Isa. 44:28; 45:1-4). Ambapo “Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu

27

katika ufalme wake wote. . . Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu Wake, Bwana, Mungu Wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (Yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. . . {TN14: 27.2}

“Tena Koreshi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya Bwana, alivyokuwa amevileta Nebukadnezza toka Yerusalemu ,na kuvitia katika nyumba ya miungu yake. Naam, vyombo vile ndivyo alivyovitoa Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwa mkono wa Mithredathi, mtunza hazina; naye akavihesabu mbele ya Sheshbaza, mkuu wa Yuda. Na hii ndiyo hesabu yake; sinia za dhahabu thelathini, sinia za fedha elfu, visu ishirini na kenda. mabakuli ya dhahabu thelathini, mabakuli ya fedha ya namna ya pili mia nne na kumi, na vyombo vingine elfu. Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.” Ezra 1:1-4, 7-11. {TN14: 28.1}

28

Kwa wakati uo huo, wale ambao Koreshi aliwaweka huru kutoka kwa utumwa wa Wakaldayo, walijua kwamba Mungu alikuwa amefanya ukombozi wao. Kwa hivyo, “na wana wa Israeli, na makuhani na Walawi, na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha. Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng’ombe mia, na kondoo waume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli wote, kwa hesabu ya kabila za Israeli. {TN14: 29.1}

“Wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; vile vile kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa. Kisha, wana wa uham-isho wakaifanya Pasaka, mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi. Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja Pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao. Wana wa Israeli wakaila, wale wa-liorudi kuitoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa washenzi wa nchi, ili kumtaka Bwana, Mungu wa Israeli, wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa Bwana amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaelekee, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.” Ezra 6:16-22. {TN14: 29.2}

Kwamba “Ashuru” na washirika wake, wamepindana-pindana pamoja kama miiba, waweze leo kujifunza so-mo lile lile, Mungu huwaruhusu

29

watekwe nyara na kuharibiwa. Kisha, ili kwamba waponywe kwa ugonjwa wao, Bwana kupitia Isaya anatoa

MSINGI WA TATIZO LAO, LISHE YENYE TIBA. {TN14: 29.3}

ISAYA, SURA YA 7, AYA YA 1-16. “Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda. Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo. . . {TN14: 30.1}

“Kwa kuwa Shamu amekusudia mabaya juu yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia, wakisema, haya, na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli. Bwana Mungu asema hivi, Neno hili hal-itasimama wala halitakuwa. Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski [si mbinguni], na kichwa cha Dameski ni Rezini [si Bwana]; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu [ufalme wa kabila kumi] atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena. Tena kichwa cha Efraimu ni Samaria [si mbingu-ni], na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia [si Bwana]. Kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka hamtathibitika. {TN14: 30.2}

“Tena Bwana akasema na Ahazi akinena, jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. Lakini Ahazi akasema, sitaitaka,

30

wala sitamjaribu Bwana. Naye akasema, sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; je! ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hivyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina Lake Imanueli. Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, [Resini na Peka] itaachwa ukiwa.” {TN14: 30.3}

ISAYA, SURA YA 8, AYA YA 1-8. “Bwana akaniambia, jipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa kalamu ya binadamu, Kwa Maher-shalal-hash-bazi; Nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia. Nami nikamwendea huyo nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume. Kisha Bwana akaniambia, Mwite jina lake Ma-her-shalal-hash-bazi. Kwa maana kabla mtoto huyo hajapata kujua kusema, Baba Yangu, na mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru. {TN14: 31.1}

“Kisha Bwana akasema nami mara ya pili, akaniambia, Kwa sababu watu hawa [Israeli] wameyakataa maji ya Shiloa [jeshi la ulinzi la mbinguni] yapitayo polepole, kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia, [utukufu wa serikali yao ya taifa]; basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote; naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.” {TN14: 31.2}

31

Yaani, ingawa Yuda wa kale haungeathirika kwa kushindwa na muungano wa Israeli na Shamu, ulikuwa, hata hivyo, pia uletwe chini ya kodi ya Ashuru wa kale. Na, kama tutakavyoona, roho ya muungano huu hai-kukoma na ile ya Israeli na Shamu ya zamani. {TN14: 32.1}

Vipengele vya kilele vya ushirika huu, ambavyo baadhi yavyo bado havijajazwa, huangukia katika mpangilio hivi: {TN14: 32.2}

1. Kupinduliwa kwa zote Israeli ya kale na Shamu na Ashuru ya kale, kama hukumu ya Mungu hasa kwa Is-raeli kwa kuungana dhidi ya ndugu zake, ufalme wa Yuda (Isa. 7:2-9). {TN14: 32.3}

2. Kuzaliwa kwa mwana mwanamume (Imanueli) kwa bikira, kuwa “ishara” kwa “nyumba ya Daudi” (Isa. 7:13, 14). {TN14: 32.4}

3. Kuzaliwa kwa mwana (Maher-shalal-hash-baz) kwa nabii mwenyewe, “kwa ishara na maajabu” katika Is-raeli (Isa. 8:18). {TN14: 32.5}

4. Kupinduliwa kwa Israeli kutukia kabla Imanueli angeweza kujifunza kupambanua maovu kutoka kwa me-ma, na kabla ya Maher-shalal-hash-baz angeweza kusema “baba yangu na mama yangu” (Isa. 7:16, 8:4). {TN14: 32.6}

Katika kukikuza kishada hiki cha matukio, kweli kadhaa zinasimama katika ufafanuzi binafsi wa uhakika: (1) “Imanueli,” kwa msingi wa kuzaliwa kwake kwa bikira na jina lake,

32

“Mungu pamoja nasi” (Mat. 1:23), anaweza tu kuwa Kristo pamoja nasi. (2) Alizaliwa kwa ajili ya ishara kwam-ba muungano usio wa haki kati ya Israeli na Shamu haungefaulu. (3) Nchi, Israeli na Shamu, ambazo Yuda aliz-ichukia, zilipaswa kuachwa na wafalme wao wote — zilitekwa na mfalme wa Ashuru — kabla Imanueli angeweza kukataa uovu na kuchagua wema, na kabla ya Maher-shalal-hash -baz kuwa na uwezo wa kusema “baba yangu na mama yangu.” {TN14: 32.7}

Lakini ukweli rahisi wa kihistoria kwamba falme hizi mbili zilipinduliwa karne nyingi kabla Imanueli hata ku-zaliwa, huleta tofauti ya wakati ambayo inaweza kusuluhishwa tu na hitimisho kwamba mataifa yote manne (Yuda, Israeli, Shamu, na Ashuru) yaliyoshiriki katika tendo hili la kihistoria, yalikuwa mfano wa mengine manne ambayo yangekuja wakati mwingine baada ya kuzaliwa kwa Imanueli; maana baada ya kuzaliwa Kwake, Israeli na Shamu yalipaswa yangepinduliwa na Ashuru. {TN14: 33.1}

Ni lazima, basi, uweze kupatikana katika enzi ya Kikristo utawala wa Kikristo uliokengeuka (Israeli) ulioungana na ule wa kipagani (Shamu), hadi mwisho wa kuwafyonza au kuwaondoa kabisa Wakristo halisi (Yuda). Na muungano wa pekee kama huo katika enzi ya Kikristo ulikuwa umoja wa Kanisa na Serikali ambao ulitawala wakati wa Vizazi vya Giza, na ambao ulitafuta kuwaangamiza wale “waliozaliwa upya,” ambao wali-kataa kuiacha imani ya Mitume

33

na kujitiisha kwa muungano wa Ukristo na Upagani (Israeli na Shamu). {TN14: 33.2}

Kutabiri, kwa Danieli, kazi ya utawala huu mwovu, malaika alitangaza: “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu Wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” Dan. 7:25. Kama tokeo la asili, kwa hivyo, mfano, Ashuru ya kale, hupata “umaradufu” wake katika utawala ambao katika Vizazi vya Kati uliuvunja muungano wa kanisa na serikali. Na kwa sababu umoja huo ulisambaratishwa na mataifa ya sasa ya Waprotes-tanti, hitimisho hakika linafuata kwamba Ashuru mamboleo anafika hadi siku zetu, hivyo kuthibitisha ukweli kwamba unabii wa Isaya ni sawa na wa Nahumu. {TN14: 34.1}

Lakini kwa sababu Ashuru ya kale iliupindua muungano wa Waisraeli na Washami karne nyingi kabla Imanu-eli kuzaliwa, na kwa sababu Ashuru mamboleo aliupindua muungano wa kanisa na serikali wa Vizazi vya Kati karne nyingi baada ya kuzaliwa Kwake, busara inadai kwamba kama Shamu, Yuda, Israeli, na Ashuru ni mifano, hivyo pia Imanueli lazima awe. Kwa hivyo, unabii wa kuzaliwa kwa bikira hakurejelei tu kuzaliwa kwa Kristo, lakini hata zaidi kwa wafuasi Wake — kuzaliwa na ustawi wa himaya ya Ukristo. Vivyo hivyo, Ma-her-shalal-hash-baz lazima awe mfano wa kundi lingine katika enzi

34

Ya Ukristo. Na kwa vile anajua tu kusema “baba yangu, na mama yangu,” wakati Imanueli (Kristo katika umbo la watu Wake) anajua kukataa uovu na kuchagua wema, Maher-shalal-hash-baz kwa udhahiri hawezi kuashiria yeyote aliyeishi kabla ya Imanueli. {TN14: 34.2}

Bado zaidi, ukweli kwamba wote walipaswa kuwa wazaliwe katika Yuda (kanisa), mmoja wa Kiroho na mwingine wa kimwili, ni ushahidi kamili ya uwepo wao, anavyosema nabii, kwa ajili ya “maajabu” na kwa ajili ya “ishara” ya madaraja mawili ya washiriki wa kanisa, wanaoishi kwa wakati mmoja. {TN14: 35.1}

Uwepo Wake na Baba Yake kabla (Ebr. 1:1, 2; Yoh. 1:1, 2), na kisha baada ya kuzaliwa tena katika Bethle-hemu, Imanueli wazi wazi huwakilisha Wakristo “waliozaliwa upya” (Yohana 3:3); ilhali akiwa kamwe hajawahi kuwepo kabla, Maher-shalal-hash-baz anaweza tu kuwakilisha wale ambao “hawajazaliwa upya” — hiyo sehemu ya washiriki wa kanisa ambayo haiwezi kuwakilishwa na Imanueli. Usambamba unapatikana katika mfano wa Ishmaeli na Isaka, ukiwakilisha wale “waliozaliwa kwa mwili” na “waliozaliwa kwa Roho” — Myahudi asiyeku-wa Mkristo na Myahudi Mkristo. (Tazama Wagalatia 4:22-31.) {TN14: 35.2}

Katika mtazamo wazi wa kweli hizi, unakuja nuruni ukweli kwamba Wakristo “waliozaliwa mara ya pili” walioishi wakati Rumi ya Upapa ilipoanguka, na ambao waliwakilishwa na Imanueli, walikuwa kiroho

35

“wachanga” sana, hawakuwa wameenda mbali sana kwa wakati wakilingana na maarifa ya Biblia na ustawi wa kiroho, kupambanua maovu kutoka kwa mema. Kwa hiyo, lazima wayafikie maarifa haya katika kipindi cha Mwashuru (Uprotestanti), kwa maana muungano wa Israeli na Shamu, hebu tukumbuke, ulikuwa uvunjwe na Ashuru baada ya Imanueli kuzaliwa lakini kabla Yeye angeweza “kuukataa uovu na kuuchagua wema”; na sio tu baada ya Maher-shalal-hash-baz kuzaliwa ila pia kabla angeweza kusema “baba yangu na mama yangu.” Na ukweli kwamba kanisa bado si kamilifu, huonyesha kwamba hata Wakristo “waliozaliwa mara ya pili” hadi leo hawawezi kuchagua kwa mfululizo kati ya mema na mabaya, na kwamba wale ambao wamezaliwa tu kwa mwili hawajastawi hata kuwa hawawezi hata kutoa madai halisi ya kumjua baba yao (Mungu) na mama yao (Kanisa). {TN14: 35.3}

Somo la wazi ni kwamba wakati mtu anapoongoka (kuzaliwa upya) kwa Kristo, yeye ni mtoto tu katika mai-sha ya Ukristo, na huhitaji kwa wakati uliopo kulishwa, kama mtoto aliyetoka kuzaliwa, kwa “maziwa ya kweli ya Neno,” ili kwamba “aweze kukua kwayo.” 1 Pet. 2:2. {TN14: 36.1}

Kupitia kwa mtume Paulo, Uvuvio hufasiri haya maziwa kuwa “mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mun-gu.” Ebr. 5:12. Na kupitia Isaya, Unauliza: “Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha

36

nani habari hii?” Kisha, kujibu maswali Yake yenyewe, unatangaza: “Ni wale walioachishwa maziwa, walioon-dolewa matitini.” Isa. 28:9. {TN14: 36.2}

Lakini somo kuu la Isaya, sura ya 7 na 8, hufundisha kwamba kanisa kwa ujumla, lililozaliwa katika karne ya kwanza B.K., leo karibu linapita kutoka katika utoto wake na kulishwa “chakula kigumu” ili kulipatia uwezo wa kuchagua wema na kukataa uovu. “Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa” Uvuvio unatangaza, “hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa ku-tumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.” Ebr. 5:13, 14. Ni dhahiri, kadiri muda unavyoendelea, hivyo Ukweli na Mkristo huendelea kwa kulingana nao. {TN14: 37.1}

Baada ya kulishwa kwa “maziwa” tu — kwa rahisi, mafunuo ya msingi ya Neno — kupitia miaka mingi ya uchanga na utoto, kanisa hatimaye limefikia hatua ambapo linapaswa lichukue “chakula kigumu” pia — yali-yoendelea, mafunuo ya siku za mwisho ya Neno. {TN14: 37.2}

Hili linakuwa dhahiri zaidi tunapoangalia kwamba wakati “Ashuru” katika Vizazi vya Kati ilitekeleza pigo la mauti kwa muungano wa kanisa na serikali ya siku hiyo, wala Maher-shalal-hash-baz, Mkristo aliyezaliwa kwa mwili, wala Imanueli, Mkristo

37

aliyezaliwa kwa Roho, walikuwa hawajakomaa vya kutosha, jinsi tumeona, “kukataa uovu na kuchagua wema.” Sasa, ingawa, wao lazima wanakuja kuwa wakomavu, kwa maana sio tu miaka mingi imepita tangu Mwashuru alitekeleza pigo kwa muungano wa kanisa na serikali, lakini pia umefika wakati wa Ashuru, mwenyewe, kuanguka. Mbali na hilo, “chakula kigumu,” pia, ki hapa. {TN14: 37.3}

Bila shaka wakati umekuja kwa washiriki wote wa kanisa kutambua kwamba sasa wanapita kutoka kwa utoto wa Ukristo kuingia ukomavu wa Ukristo, na wanapaswa, kwa hivyo, kutoendelea kujaribu kufikia kimo cha ukomavu kamili kwa kuendelea kula chakula cha watoto. Hivyo kila mmoja, hata washiriki wachanga (walioza-liwa kwa mwili), wanaweza sasa kuwezeshwa kutambua wazazi wao wa kiroho, hivyo kwa busara kusema, “Baba yangu na Mama yangu”: kwa kumjua Mungu wao ipasavyo kwa njia ya Mwana, na kulijua kanisa lao ipasavyo kupitia Ukweli wa wakati, ndicho kinacholeta uzima wa milele. Na kadiri kila mmoja anavyoki-meng’enya “chakula kigumu,” hapo atakuwa mwenye hekima na imara “kukataa uovu na kuchagua wema.” {TN14: 38.1}

Ya umuhimu, kwa hivyo, “kazi maalum” kwa kanisa, ilivyotabiriwa katika Pambano Kuu, uk. 425, imewekwa rasmi ili kumleta kila mshiriki mwaminifu kwa ukomavu wa Ukristo. {TN14: 38.2}

Kwa hivyo, pia vyakula viwili ambavyo Imanueli alipaswa kula ili “kukataa

38

uovu, na kuchagua wema “lazima viwe mfano; kwa maana siagi na asali ndani yavyo havimiliki fadhila wala uwezo wa kupitisha ufahamu wa maadili, kuihuisha dhamira, na kutakasa moyo. Mbali na hilo, Yeye alikula vyakula vyote safi kwa ujumla (Mat. 11:19). Hizi pointi mbili kwa hivyo hushuhudia kwamba “siagi na asali”, ni nembo ya Maandiko yaliyofunuliwa — “chakula kwa majira yake,” — chakula cha pekee ambacho humpa mtu maarifa na nia ya kutenda haki badala ya makosa. Hivi Kristo alisema: “Ninacho chakula msichokijua ninyi.” Yoh. 4:32. Kwa hivyo, Mkristo ambaye ipasavyo atamjua Mungu wake na kanisa lake ili uovu uondolewe ndani yake na kujazwa wema, lazima sasa ajilishe Ukweli wa Sasa, — Ukweli unaostawi wa Neno lililofunuliwa kupitia Uvuvio. (Kwa ufasiri wa salio la Isaya saba, tazama yetu Trakti Namba 6.) {TN14: 38.3}

Kadiri mtu anavyopenyeza mpini ndani ya mgodi wa Ukweli, hupata kwamba wakati ambapo Uvuvio hufan-ya nyasi kuwa mfano wa watu, basi huifanya “mvua” kuwa mfano wa chakula chao cha kiroho, Ukweli wa wa-kati. Hivyo wakati ambapo maneno nyasi, ngano, au nafaka hutumika kuwataja watu katika siku za mwisho, basi chakula cha kiroho kinachohitajika ili kuwaleta kwenye kimo kamili cha Ukristo kinaitwa kwa kufaa “mvua ya masika” (Zek. 10:1). Na kuonyesha kwamba ni ya kwa ajili ya kuwakuza binadamu, Yoeli huipatia

39

ufananisho katika jina, “mwalimu wa haki” (Yoeli 2:23, pambizo). {TN14: 39.1}

Katika nuru hii iliyostawi, tunaona kwamba mvua ya masika (Yoeli 2:23) na pentekoste ya mwisho (Yoeli 2:28) ni maonyesho mawili tofauti sana na ya mbali mbali lakini yanahusiana kwa undani ya Roho Mtakatifu. {TN14: 40.1}

Zawadi moja ni ukweli maalum, “mwalimu wa haki,” akiliamsha kanisa kutoka kwa Ulaodekia wake na ku-waandaa washiriki wake kwa kazi ya mwisho ya injili ulimwenguni kote. Akiwaona kimbele wakijihusisha ki-amilifu katika kazi hii, Roho wa Kweli anatangaza: “Hofu yote kwa jamaa zao ilikuwa imetoweka, na ukweli pekee uliinuliwa kwa wao. . . Naliuliza kilichokuwa kimefanya badiliko hili kubwa. Malaika akajibu, ‘Ni mvua ya masika, burudiko kutoka kwa uwepo wa Bwana, kilio kikuu cha malaika wa tatu.’” — Maandishi ya Awali, uk. 271. {TN14: 40.2}

Ile zawadi nyingine ni nguvu maalum, ikipeleka kwa kila mpokeaji fadhila yenye nguvu ya mwonaji, iki-wawezesha kuutangaza ukweli maalum kwa ulimwengu wote. “Naliwasikia wale waliovikwa silaha wakinena ukweli kwa nguvu kuu,” inaendelea Roho ya Unabii. “Ulikuwa na athari. Wengi walikuwa wamefungwa; baadhi ya wake kwa waume zao, na baadhi ya watoto kwa wazazi wao. Waaminifu waliokuwa wamezuiliwa kuusikia ukweli sasa kwa hamu waliushikilia.” — Kimenukuliwa. {TN14: 40.3}

40

Ukweli maalum, au maarifa ya Maandiko, hupatikana kama tokeo la kuomba, “kuwa na njaa na kiu,” kwa ajili yake kwa wakati mwafaka (Zek. 10:1). Kisha “mvua ya masika,” au burudiko kutoka kwa uwepo wa Bwana, litakuja, kupeana nguvu kwa sauti kuu ya malaika wa tatu.” — Maandishi ya Awali, uk. 86. Hivyo wakati zawadi ya mvua ya masika — ujumbe wa ziada — unapeana nguvu na msukumo kwa ujumbe kuukuu, zawadi ya pen-tekoste ya mwisho — nyongeza ya nguvu za Roho — kwa mwandamo zinapeana nguvu na msukumo kwa wajumbe wa siku za mwisho. Nguvu hii ya kufanya miujiza, kwa hivyo, haiji kwa sababu ya kuomba kwa ajili yake, ila kwa sababu wajumbe, kupitia kwa mvua ya masika, wametimiza maagizo ya kuipokea. {TN14: 41.1}

Wanadamu wasiojua jinsi tulivyo hata hivyo, huamua kupata nguvu maalum badala ya maarifa maalum, am-bayo pekee yatatuwezesha kutumia ile nguvu ipasavyo. Kwa hivyo huwapata watu wakiomba wakati usiofaa, kwa kutojua au kwa kimbelembele, kwa ajili ya kile ambacho hawajaulizwa kukiomba, na hawaombi kwa ajili ya kile kilicho kwa wakati unaofaa, na ambacho wanahimizwa kukiomba! {TN14: 41.2}

“’Nuru hupandwa kwa ajili ya mwenye haki.’ Na hakuna kanisa linaloweza kustawi katika utakatifu isipokuwa washiriki wake wanajitahidi kuitafuta kweli kama hazina iliyofichwa.” — Pambano Kuu, uk. 522. {TN14: 41.3}

41

Ili Mungu kutoa nguvu ya pentekoste kwa mmoja kabla afikie ukomavu kamili wa kiroho, litakuwa lisilofikiriwa kama Halmashauri ya Serikali kutoa leseni ya daktari kwa mwanafunzi wa matibabu kabla hajapata shahada ya udaktari wake! Na Bwana angeweza kuiwekeza ndani mwetu nguvu ya kutenda miujiza, uzoefu ambao tunatamani, kabla Yeye kutupatia maarifa ya miujiza ya Maandiko, ambayo tunahitaji, Yeye atakuwa hatutendei fadhili kuliko ambavyo ingefanya serikali kutoa leseni ya dereva kwa mwombaji yeyote na wote bila kujali sifa zao za kuendesha gari. Yote yakiwa ni matendo yasiyofaa, yangeweza, bila shaka, kusababisha maangamizi ya mtu binafsi na kwa wengine. {TN14: 42.1}

Hii ndio sababu wale ambao hutafuta nguvu ya miujiza ya Roho, ilhali wenyewe si watu wenye maarifa ya miujiza ya Biblia, hawapati ama wowote au hupata hatari wa bandia; Ilhali wale ambao hutafuta kujijua na kuujua Ukweli, hujazwa maarifa zaidi ya matarajio yao. Na baada ya kujifunza hakika wao ni kina nani, na jinsi gani wanapaswa kuwa, wao pia, kama vile Isaya na Paulo (Isa. 6:5; Rumi. 7:22, 23), huwa wanyenyekevu katika tathmini yao wenyewe bali watumwa wenye nguvu na waaminifu katika shamba la mizabibu la Bwana. {TN14: 42.2}

Kwa hiyo, kupitia kukunjua kwa wakati hizi rahisi lakini takwimu za muhimu, hakuna mtu anayepaswa sasa kushindwa kutambua ishara za wakati,

42

na hakuna mtu sasa anayepaswa kujidanganya kuhusu ukweli ambao zinatoa. Kwa maana, huo pekee unaweza kuwafanya watakatifu wastahili nguvu ya pentekoste, kama asemavyo Bwana: “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba Nitamimina Roho Yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.” {TN14: 42.3}

Usiendelee kungoja tena, kwa hivyo, lakini sasa “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, Naye atawapa manyunyu ya mvua, kwa kila unyasi kondeni.” Yoeli 2:28; Zek. 10:1. {TN14: 43.1}

Somo la dharura hapa la kujifunza ni kwamba wale wanaoendelea daima, wakienenda sambamba na hatua za Ukweli, ndio Wakristo pekee wa kweli. Na ingawa hata waliostawi zaidi wa hao bado hawajafikia kiwango cha juu (ukomavu kamili) walichowekewa na Bwana, hata sasa Uvuvio katika karamu ya hivi karibuni ya siagi na asali (mvua ya masika), hutoa nyenzo za kujenga tabia kwa wote. Matokeo yake, maelfu ya waaminifu kwanza (Ufu. 7:3-8, 14:1, 5) na mamilioni mwisho (Ufu. 7:9, Mika 4:1-3, Isa 60:5, 6) watakuwa hatimaye wamekomaa kwa mavuno, kwa kweli kufikia kiwango cha Bwana, na kuufikia “umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” Efe. 4:13. Yalioje

43

mavuno tele ya Wakristo waliokomaa wa kuwekwa ghalani! {TN14: 43.2}

Isa. 8:9,10. “Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, nanyi mtavunjwa vipande vipande; tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande. . . Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; semeni neno, lakini halitasimama; kwa maana Mungu Yu pamoja nasi.” {TN14: 44.1}

Taarifa, “Mungu Yu pamoja nasi,” ina maana kwamba Yeye hayuko pamoja na mataifa ambayo yanashirikiana kwa ajili ya ulinzi wa pamoja, na ya kwamba kwa hivyo yatavunjwa, ilhali wafuasi Wake wakati huo wa-taokolewa. Hata hivyo, ili Mungu kuwa “pamoja nasi” katika ufahamu huu maalum, lazima naam tufanye juhudi spesheli za kuwa na Yeye. Na kwa kufanya hivyo, tunapaswa kwa uaminifu kujifunza njia Yake na kuzifuata kwa furaha hatua Zake nzuri, ambazo hutuongoza kwa maarifa kamili ya siri za kinabii, na kutuwezesha kuepuka mitego, na kusimama ingawa wengine wote huanguka. Hivyo, kwa kuendelea kufuata ili kuijua Njia, Kweli, na Uzima, tunaendelea na uchunguzi wetu ndani ya unabii wa Isaya. {TN14: 44.2}

Isa. 8: 11-22. “Maana Bwana aliniambia hivi, kwa mkono hodari, Akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, msiseme, ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. Bwana wa majeshi Ndiye mtakayemtakasa; na awe Yeye hofu yenu, na awe Yeye utisho wenu. Naye atakuwa ni mahali patakatifu [kwa wafuasi wa ukweli]; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba

44

wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu [kama vile Alivyokuwa kwa ujio Wake wa kwanza]. Na wengi [kwa hivyo] watajikwaa, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kutekwa. {TN14: 44.3}

“Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi Wangu [wafuasi wa ukweli]. Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso Wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. Angalieni [ni wazi sasa kuona], mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa Bwana wa majeshi, Yeye akaaye katika mlima Zayuni. Na wakati watakapokuambia [kwa waliotiwa mu-huri], Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! hai-wapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria [Kut. 20:3-17] na ushuhuda [Ufu. 19:10]; Ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Nao [walio gizani] watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika [kwa njaa] na [baadhi yao] kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na [baadhi yao] kuelekeza nyuso zao juu [na kuongoka]; nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao [walioikataa mvua ya masika] wa-tafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.” katika siku ya

UTAWALA UNAOWAANGAMIZA WAOVU NA KUWAOKOA WENYE HAKI. {TN14: 45.1}

NAHUM, SURA YA 1, AYA YA 1-9: “Ufunuo juu ya Ninawi. Kitabu cha maono aliyoyaona Nahumu, Mwelkoshi. Bwana ni Mungu mwenye wivu, Naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, Naye ni mwingi wa hasira [maana adui Zake wameliharibu shamba Lake la mizabibu]; Bwana hujilipiza kisasi

45

juu ya adui Zake, huwawekea adui Zake akiba ya hasira. Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia Yake katika kisulisuli na tufani, [ilhali ndege za mataifa haziwezi], na mawingu ni mavumbi ya miguu Yake. Yeye huikemea ba-hari na kuikausha, pia huikausha mito yote [ila wanadamu na meli zao huzama ndani wasiamke tena] Ba-shani hulegea, na Karmeli; hulegea nalo ua la Lebanoni. Milima hutetema mbele Yake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele ya uso Wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake. Ni nani awezaye kusimama mbele ya ghadhabu Yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira Yake? Hasira Yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na Yeye. Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; Naye huwajua hao wamkimbiliao. Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui Zake hata gizani. Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili [kwa sababu waovu wamekataliwa mbali, na Ufalme Wake sasa unasimama milele].” {TN14: 45.2}

* * *

Kutoka kwa nyumba ya usambazaji ya utukufu ambayo Imanueli alipokea siagi na asali zamani sana, Roho wa Kweli yu hapa kwa njia hii akionekana akipakua chakula tele cha kuiboresha nafsi kuliko hapo awali. Kila mmo-ja anayeweza kupokea kwa uhuru, sio tu kuuinua moyo wake katika shukrani kwa Mpaji Mkuu wa zawadi zote njema, “Baba wa mianga,” ila pia kwa uhuru kuzitoa juhudi zake bora kushirikiana na Msaidizi Ambaye ameku-ja, kwa hiari

46

KUPEANA KWA WOTE WANAOOMBA. {TN14: 46.1}

Hatimaye, kuzua hamu kubwa ya “siagi na asali” zaidi (tusije tukashindwa kuitambua mvua ya masika kadiri inavyonyesha katika matone makubwa pande zote kutuzunguka kwa ajili ya mavuno ya mwisho — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 507), au, kwa maneno mengine, kuutekeleza uchunguzi wa kina wa ufunuo huu wa umuhimu wote, wachapishaji wa kijizuu hiki watawasilisha zawadi seti (* — Tazama uk. 55) ya machapisho ya Ukweli wa Sasa kwa kila mtu ambaye atawasilisha wazo, sahihi au lisilo sahihi, kwamba ni lipi kati ya mataifa ni “Ashuru” wa leo na ni nani “yeye” ambaye “anaseta vipande vipande;” pia kuhusu ni wakati gani vita vya maadui hawa wawili wa kufa litafanyika. Seti hiyo hujumuisha mfululizo wa trakti kumi na tatu, jumla ya kurasa 1000, zinaz-osheheni siri nyingi za kinabii zilizotiwa muhuri kwa muda mrefu ambazo sasa zimefunuliwa — “chakula kigu-mu.” Wale ambao tayari wanayo hii seti ya vijizuu kumi na vitatu, wanaweza kwa kuitisha kupokea bila malipo seti mwenza mpya ya vitabu vitatu maalum vya Ukweli wa Sasa. “. . . kwa maana kila mtu atakayesalia katika nchi hii atakula siagi na asali.” Isa. 7:22. {TN14: 47.1}

* * *

Sasa kwamba mlinzi wa mbinguni ametenda sehemu yake, bado imesalia tu kwa wale waliotumiwa kuifanya yao — watimize madaraka yao ya

JUKUMU LA KIBINAFSI. {TN14: 47.2}

“Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, hapo Nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu

47

wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka awe mlinzi wao; ikiwa, aonapo upanga unakuja juu ya nchi hiyo, apiga tarumbeta na kuwaonya watu; basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake. Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukam-wondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake, lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo. {TN14: 47.3}

“Basi wewe, mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani Mwangu, ukawape maonyo Yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake Nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.” Ezek. 33:2-9. {TN14: 48.1}

“Waambie, kama Mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, Sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake

48

mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? Na wewe, mwanadamu, waambie wana wa watu wako, haki yake mwenye haki haitamwokoa, katika siku ya ku-kosa kwake; na kwa habari ya uovu wake mtu mwovu, hataanguka kwa ajili ya uovu huo, siku ile atakapoghairi na kuuacha uovu wake; wala yeye aliye mwenye haki hataweza kuishi kwa haki yake, siku ile atakapotenda dhambi. Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo. Tena, nimwambiapo mtu mwovu, hakika utakufa; kama akighairi, na kuiacha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki; kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyom-nyang’anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wo wote; hakika ataishi, hatakufa. Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi.” Ezek. 33:11-16. {TN14: 48.2}

Kwako wewe unayelitii onyo hili la wakati, itakuja thawabu hii yenye utukufu: {TN14: 49.1}

“Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa

49

ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni na kuisafisha damu ya Ye-rusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4:3-6. {TN14: 49.2}

Lakini kwako wewe usiyelitii onyo hili, “Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.” Isa. 3:25. {TN14: 50.1}

50

WAKATI NA FURSA HUFUMBUA SIRI

(Mada: Unabii wa Nahumu wa Vita)

Wakati na fursa bado ni mashahidi wa kuaminiwa, vile vile wafichuzi bora wa siri. Sasa wanatoa majibu kwa maswali: Ni lipi kati ya mataifa ni “Ashuru” wa leo? Ni nani “yeye asetaye vipande vipande”? Ni lini vita vya maadui hawa wawili wa kufa litafanyika (uk. 47.)? {TN14: 51.1}

Sasa ya kwamba muda mrefu umepita tangu trakti hii ilitoka kwenye matbaa (miaka 4), na kwa sababu matukio mengi muhimu yamejichonga yenyewe hadi kwa ukomavu tangu wakati huo, wasomaji wetu wa Ukw-eli unaoendelea hawana shaka sasa kwa nafasi nzuri zaidi kuona ukweli kwa udhahiri na kwa uhalisi zaidi kuliko awali. Hivyo, kwa manufaa ya wote, tunaongeza aya hizi. Zinaelezea mtazamo wa Trakti kwenye mada jinsi wakati na matukio yalivyo sasa yanaonyesha. {TN14: 51.2}

Mwelekeo wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia haviachi shaka kwamba ndivyo vilivyotabiriwa na nabii Nahumu. Hili linawekwa dhahiri na kweli

51

kadhaa: {TN14: 51.3}

Uvuvio huonyesha wazi kwamba vita vya Nahumu vinapiganwa wakati magari yanafanya mshindo njiani, ya-kisongana-songana katika njia kuu, yakionekana kama mienge na yakienda kwa kasi kama umeme, katika siku zetu (Nah. 2:4). {TN14: 52.1}

Nabii, isitoshe, anasema kwamba baada ya yule “asetaye vipande vipande” (Nah. 2:1) kuja mbele ya uso wa Ashuru, basi inakuwa kwamba Ashuru anavitia “nguvu viuno vyake,” anaimarisha “uwezo wake sana” (Nah. 2:1) — ambao, jinsi dunia nzima inavyojua, ni tukio lililofanyika wakati Hitler alikuja dhidi ya majeshi ya muungano: Majeshi ya muungano, yakiwa hayajajiandaa kupigana na Hitler alipoanza kuseta vipande vipande, kwa lazima walizimarisha nguvu zao sana baada ya vita kuanza. Kweli hizi zote zinathibitisha kwamba Vita Kuu vya 2 ni vita vilivyotabiriwa na Nahumu, na ya kwamba Hitler ndiye yule “asetaye vipande vipande.” {TN14: 52.2}

Ingawa Nahumu hutabiri “kuanguka kwa Ashuru” kuhusiana na “yeye asetaye vipande vipande,” haumaanishi kwamba yeye asetaye vipande vipande mwenyewe atammaliza

52

Ashuru, kama mmoja kwa kawaida angeweza kuhitimisha. Sasa inaonekana, ingawa, kwamba yeye asetaye vipande vipande, mwenyewe angevunjika au asababishe kuvunjwa vipande vipande sio tu mataifa ya muun-gano, ila taifa lake, pia. Kwa kweli, unabii unasema kwamba “wakuu wake” (wakuu wa yule asetaye vipande vipande), hawangeweza kushinda, lakini kwamba wao “wangejikwaa katika mwendo wao,” wanajikwaa wakiwa kwa mwendo wao wa kushinda (Nah. 2:5) Na ni nini kilichotokea katika majeshi ya Hitler? — Walikosea wali-pokuwa wakijaribu kushinda Urusi. {TN14: 52.3}

Baada ya Nahumu 2:5 hakuna kutajwa tena kwake yeye asetaye vipande vipande, kuonyesha kwamba hayupo tena. Ongeza kwa jambo hili ukweli kwamba vita vimeugawanya ulimwengu wote — kivitendo mataifa yote na watu — katika vipande vya vipimo vyote, na tunazo nanga thabiti kwa ushahidi kwamba Vita Kuu vya 2 ni vita vya Nahumu, na ya kwamba Hitler ndiye yule uvuvio ulimwita “yeye asetaye vipande vipande.” Hakika, aliyagawanya mataifa na watu hivi kwamba hata sasa hakuna yeyote ambaye ameweza kuwaunganisha pamoja. {TN14: 53.1}

53

Zaidi ya hayo, kwa matokeo ya vita, Uingereza kweli haijashinda. Naam, amepoteza zaidi ya kile angepoteza ikiwa angemruhusu Hitler achukue kile alichotaka kwanza — sehemu tu ya Poland. {TN14: 54.1}

Kisha pia, kushindwa kwa Japani na Ujerumani kwa vyovyote hakujamaliza vita. Kumeongeza tu jeraha la mauti la kimataifa. Hivyo uwezekano wa kutimiza kila awamu ya ukweli uliomo katika Trakti Namba 14 sasa ni mwangavu kuliko hapo awali. Kwa mujibu wa Uvuvio, Vita Kuu vya 2 havijaisha. {TN14: 54.2}

Hili ndani yake lenyewe ni ushahidi wa kutosha kwamba ulimwengu sasa, wakati huu wa machafuko ya kimataifa kama haya ambayo haujawahi kuwa nayo — machafuko yanayosababishwa na kila elementi hai — yatazaa kitu fulani. Kadiri tunavyoyaona sasa, mambo yote tunayoyasoma katika Trakti Namba 12 na Namba 14, yanaonekana kuwa yapo njiani kwa utimizo wa haraka. {TN14: 54.3}

54

FAHARISI YA MAANDIKO

55

56

 

>