fbpx

Maalum Kwa Baraza Kuu La 1950

1

1950 Maalum Kwa Baraza Kuu

2

<<<<>>>>

3

MAALUM KWA BARAZA KUU MWAKA ELFU MOJA MIA TISA HAMSINI

Baraza hili maalum la Jumuiya ya Waadventista wa Sabato linafanya maamuzi kuhusu maswali: {GCS: 3.1}

ELIYA WA LEO NI NANI?

ATAREJESHA MAMBO YOTE?

KILE CHA KUWAFANYIA VICHIPUKO

Maswali haya yanashinikizwa miongoni mwetu na jamii ya vichipuko inayozidi kukua, inayojulikana zaidi na inayokera mno ni “Fimbo ya Mchungaji.” Kwa kweli kero zake zimekua hadi kufikia viwango vya kumleta kila Mwadventista wa Sabato wa kweli ana kwa ana nayo. Kwa kweli, Ndugu, uvutano wake unaokua unatupa kila mmoja wetu changamoto kutokwepa swala hili kama walivyofanya Wayahudi katika siku yao, na hivyo kupoteza, bali kukabiliana nalo namna Kristo alivyokabiliana na Sanhedrini na hivyo kushinda kwa utukufu. {GCS: 3.2}

Kongamano hili la Baraza Kuu mwaka huu lazima litatue katika kila ubongo kabisa, maswali kuhusu nani ni nani na nini ni nini. Hata ikiwa wewe mwenyewe haumizwi na Fimbo ya Mchungaji, bado lazima ujihami na ukweli, ili uweze kuwapa marhamu ya uponyaji ya Kweli wale wanaoumia kutokana na maumivu yake. {GCS: 3.3}

Ili kuwaletea uzito

4

wa hali hii ambayo kanisa linajipata saa hii ya mwisho, na tiba ambayo Mungu angependa watu Wake watumie ili kuwaweka huru kutokana na “maudhi” ya vichipuko, kwa hivyo ninafanya jaribio hili la pili kuweka mbele yenu mambo yaliyofunuliwa ili asikuwepo yeyote, iwe mchungaji au mshiriki, atakayetembea tena kwa upofu na katika giza. {GCS: 3.4}

Kwa vile yapo makubaliano ya jumla kwamba Uvuvio wa moja kwa moja kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu ndio nuru pekee ya macho yetu, kwa hivyo yafaa tukubaliane ikiwa tutamruhusu Roho wa Mungu atutawale. Hasa, waamini wapendwa wenzangu, kwa kuwa wakati umewadia kabisa tuweze kuangalia hali hii, kwa sababu watu wa Mungu kila mahali wamezinduliwa na maswali: {GCS: 4.1}

“Je, nabii Eliya amekuja tayari?”

“Nabii wa kale atatokea mwenyewe?”

“Kundi la watu litafanya kazi sawa na ya Eliya wa kale” au nini? {GCS: 4.2}

Kwa vile hakuna yeyote ambaye kwa uaminifu au kutojali atasimama mbali na jibu ambalo linalotoka katika Neno la Mungu lisilokosea, hakika sasa ndugu kupeana kwa uangalifu wa dharura zaidi uzingativu, kutoruhusu chochote kukuondoa katika shughuli hii kwa ajili yako, pamoja nami, lazima tuelewe kwamba linamaanisha maisha na umilele kwetu sisi sote. {GCS: 4.3}

Suala nyeti ambalo maswali haya

5

yanaamsha, yanadai kwamba tukome kujidanganya au kuruhusu wengine kutupumbaza. Iwapo maswali haya hayatajibiwa katika Ukweli chanya, ni heri zaidi basi, yaachwe kwenye rafu hadi chuo kifunuliwe zaidi, kuliko kujibiwa kwa porojo za watu, ambazo zinakanganya na kuchanganya. {GCS: 4.4}

Sasa tunaweza kuhoji, chuo kimekunjua vya kutosha kutatua maswali haya yote? Je, Roho wa Mungu anatusihi kusita, kutazama, na kusikiliza, au bado tungojee? Kwa jibu la Kimbingu hebu tuyafumbue macho yetu kwa busara kwa nuru ya “Neno la unabii lililo imara “ Lenyewe, sasa linalong’aa na kung’aa zaidi kwenye njia yetu: {GCS: 5.1}

“Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” Mal. 4:5, 6. {GCS: 5.2}

Katika nuru ambayo huu unabii unaangazia swala hili, hakuna yeyote atakaye epuka hatima kwamba nabii — mtu — atatumwa “kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya,” na hivyo tu basi kutakapokuwa na kikundi cha watu watakaohusishwa na ujumbe wa Eliya. Maandiko yanaweka wazi na hakika ahadi, wakati na kazi, pia

6

njia ya usalama wetu katika siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya, “ili,” asema Bwana, “nisije nikaipiga dunia kwa laana.” {GCS: 5.3}

Hakuna yeyote atakayeweza kufanya upuzi wa aidha kuchukulia kimzaha au kuwasha cheche zake kwenye mada. Isitoshe, lazima tukumbuke kwamba haiwezekani Mungu atamwacha mmoja wetu gizani iwapo tunataka kujua Kweli, na ikiwa tunajali lile ambalo Mungu angependa sisi tufanye. (“Pambano Kuu,” uk. 560). Kufikia mwisho kwamba hii iwe ni tajriba yetu ya furaha kwetu sote, lazima tuombe kwamba Roho Aongozaye katika Kweli yote aelekeze juhudi hii. {GCS: 6.1}

Hata hivyo, ningewakumbusha, Ndugu, hakuna nabii wa Mungu amewahi kukaribishwa na kanisa. Kinyume chake, kila mmoja kwa wakati wake alikataliwa, akatusiwa, na wengi wao waliuawa na wale wale waliolengwa — wale ambao walifaa kuwa wanamtumikia Mungu! Kwa kweli, Bwana Mwenyewe alilipa bei iyo hiyo. Kwa sababu hii lazima tukumbuke kwamba nabii wa mwisho akija, atakumbana na pingamizi kuu, kwa kuwa Shetani anajua vyema kwamba akipoteza sasa, atapoteza milele. Kile ambacho kinafanya kazi ya Eliya kuwa ngumu hasa ni kwamba kwa muda mrefu Ukristo umeelimishwa kwa dhana kwamba hakuna nabii atakayekuja, pia kuwa hakuna haja ya mmoja, na kwamba, una Ukweli wa kutosha kuupitisha ndani ya Malango ya Lulu. {GCS: 6.2}

7

Kwa hivyo, inatarajiwa tu kwamba Eliya aliyetabiriwa atashtumiwa kuwa nabii wa uongo, labda hata kuwa ni mpinga-Kristo, kichipuko, au yupi siye. {GCS: 6.3}

Isitoshe, Ibilisi wa zamani tayari ameweka majeshi yake yote kazini, huku akipuliza muziki wake ili kuvutia watafuta Ukweli kupanda gari lake la dhahabu. Puleki yake ya ukweli inayong’aa tayari inawadanganya wengi pamoja na tijara huku nahodha na majemedari wake kwa mayowe wakipaza sauti zao “Halleluyah,” “Roho Mtakatifu,” “karama ya uponyaji,” “zawadi ya lugha,” “karama ya miujiza,” na zingine zote, ingawa wonyesho wa mbwembwe zote hauna hata cheche ya uzima. Kila upepo wa fundisho utakuwa ukivuma, uhuisho na matengenezo ghushi yatakuwa kwenye vilele vyao. Kila kitu kinachoweza kufanywa dhidi ya Kweli kitafanywa ili kupotosha Kweli na hivyo kukengeusha na kuvunja moyo waamini na kuuvuta umakini wao kwa kitu kingine tofauti na ujumbe wa Eliya. {GCS: 7.1}

Hivyo ndivyo itakuwa shughuli ya Ibilisi huku siku ya Bwana ikijongea, na huku Eliya akifanya matangazo ya siku hiyo chuo kinapoendelea kukunjua na unabii unaohusu siku ya Bwana ukiwa unafunuliwa. Kazi na ufasiri wake wa siku kuu utamtambulisha yeye kuwa Eliya nabii. (“Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 475),

8

na hili litamgadhabisha Ibilisi kuliko hapo awali. Walakini, usalama wa yeyote utakuwa katika mafundisho ya Eliya, kwa sababu hakutakuwa na sauti nyingine ya Ukweli mwafaka na mamlaka ambayo yeyote atageukia. Sauti yoyote nyingine itawaongoza wahanga wake kwa kufumbwa macho, hadi kwa uharibifu. {GCS: 7.2}

Kuanzia sasa usiachie mikononi mwa wengine uchunguzi wako wa mada hii. Baada ya kusikiliza ushahidi, wewe pekee katika chumba cha siri cha maombi pamoja na msaada wa Roho unaweza kuamua iwapo Eliya amekuja au bado atakuja. {GCS: 8.1}

Usisahau, hata hivyo, kwamba ujumbe ambao anatangaza utabeba ndani yake wasifu wa Mungu wa Ukweli, na kwamba hakuna kuhani au kuongozi mkuu wa kidini anaweza kukuamulia kwamba Eliya anaweza au hawezi kuwa nani. La, si hata mwonekano kile ujumbe wake unafanya au haufanyi, au ikiwa unafanikiwa au unasambaratika, yanaweza kuchukuliwa kwamba Mungu yu ndani yake. Wala haiwezi idadi ya wafuasi kwa maana hiyo haijawahi kuashiria mkondo sawa kwa wakati wowote ule, Si hata wakati Kristo Mwenyewe alihubiri Injili ya Ufalme. Ujumbe anaouleta ndicho kitu cha pekee cha kufuata. {GCS: 8.2}

Na kwa sababu Adui hawezi kuzingira Ukweli, hufanya lile awezalo kuchafua tabia na kutafuta mapungufu kwa nafsi za watu. Ujumbe wa nabii hata hivyo hauwezi kuamuliwa kutegemea tabia ya waumini wake kwa sababu hata Mitume walijiendesha isivyofaa

9

kabla ya kupaa kwa Kristo. Umati, pia, uliomfuata Musa haukuwa chochote ila mfano tu; kwa hakika, katika hali nyingi walifedhehesha. Na “watu watakatifu wa Mungu” walioandika Maandiko walikuwa wakosefu. Hata Musa mwenyewe hakuwa bila kosa. Bila kujali, hata hivyo, bado alikuwa Musa, na wake ulikuwa ujumbe na vuguvugu la siku hiyo. {GCS: 8.3}

Vivyo hivyo, bila kujali kuzingatia makosa ya kibinafsi, udhaifu, na mapungufu, ujumbe na vuguvugu la Eliya watakuwa wa pekee aliotuma Mungu, wa pekee kuheshimu, kupenda, kutegemea, kuishia au kufia. La, hakutakuwa na kinga nyingine wakati mbingu inafunuka na dhoruba inapasuka kwa kitisho chake cha gadhabu kwa dunia, ili kumimina pasipo kuzuia umeme wake hatari kutoka angani. {GCS: 9.1}

Mwisho, ni kwa lengo gani lingine yeyote mwenye akili iliyo timamu awaze Mungu angemtuma nabii Wake iwapo si wao wamsikilize, kwamba hapo waokoke siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana? Kwa nini kingine, hakika, Bwana angekuwa ameweka kumbukumbu ya Unabii na kuahidi kuhusu nabii Wake wa siku ya mwisho? Fikirini hili, Wandungu, litafakari. {GCS: 9.2}

Basi pia, hata mmoja asisahau kwamba yeyote akijiunga kwa kanisa la Adventista, hufanya hivyo (akiwa katika akili timamu) pasipo idhini ya wachungaji wake wa awali. Wala hajiungi kwa kanisa kwa sababu ya

10

ushirika mkubwa au watu walio na adabu, lakini kwa sababu anajua kwamba amesikia Ukweli ulivyofunuliwa na Roho ya Unabii Yenyewe. Kwa sababu ilikuwa ni kwa kufuata mwenendo huu wa hekima ndipo yeyote miongoni mwetu akaja kumpokea nabii na ujumbe, ndivyo inapaswa kuendelea kuwa iwapo tunataka kumjua na kumpokea Eliya. Kwa hivyo, “kuliko hapo awali, tusiombe tu kwamba watumwa waweze kutumwa katika shamba kubwa la mavuno, ila tuwe na ufahamu safi wa ukweli, ili wajumbe wa kweli watakapokuja, tuweze kuupokea ujumbe na kumheshimu mjumbe. — “Shuhuda,” Gombo la 6, uk. 420. Hakuna njia nyingine ambayo yeyote athubutu kufuata kwa swala hili. Taji ya uzima hudai ulinzi wetu chonjo zaidi, kwa sababu adui mwovu anatafuta kutupokonya. {GCS: 9.3}

Nina imani kwamba ninyi wandugu mmeshawishika kwa ukweli thabiti kufikia hapa. Na sasa kwa kuendelea zaidi, Nina uhakika pia itakubaliwa kwamba iwapo maono yetu ya kiroho ni safi kiasi cha kubainisha wakati ambao Eliya ataonekana, basi tutakuwa na taabu kidogo kugundua majibu kwa maswali yetu mengine. {GCS: 10.1}

Muhimu jinsi ilivyo, hata hivyo kuzingatia wakati wa kumtarajia Eliya ni “kabla haijaja siku ile iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana,” bado hata maarifa haya tu hayatoshi. Ili kujua ni lini na ni nini siku kuu na ya kuogofya

11

yenyewe, ndio muhimu zaidi. Bila maarifa haya, nani ataweza kutambua Eliya atakapoweza kuonekana? Kwamba ufahamu huu usituponyoke, Uvuvio unajitaabisha tena kuhakiki siku kupitia unabii wa Malaki. {GCS: 10.2}

“Angalieni, namtuma mjumbe Wangu [Eliya Nabii, sura ya 4, aya ya 5], naye ataitengeneza njia mbele Yangu; Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; … Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki.” Mal. 3:1-3. {GCS: 10.3}

Siku ya Bwana, tumeambiwa katika aya hizi ni ya kusafisha, ya kutakasa, ya kupepeta. Zaidi ya hayo, swali, “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake?” linaashiria na msistizo mkali kwamba wengine hawatasimama, kwa wataanguka nje wakati wa kupepetwa (“Maandishi ya Awali,” uk. 270) na hawataustahimili mchakato wa kutakaswa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80; “Shuhuda,” Gombo la 8, uk. 250). {GCS: 10.4}

Utakuwa wewe, nitakuwa mimi kutikiswa nje? Ndilo swali kuu mbele yetu. Haiwezi, hata hivyo, awe mmoja wetu iwapo kwa busara tumeazimia kuruhusu isiwe hivyo. Hakika, Wandugu, asiwepo yeyote

12

katika shaka. Wote kwa hakika wanaweza kujua “siku” pamoja na Eliya anapokuwa akiitangaza, kwa sababu kwa mshangao wetu, ataonyesha kwamba kila nabii wa Biblia anaelezea siku hii na pia kile ambacho Bwana angetaka tufanye siku hiyo inapojongea na halafu tunapopita ndani yake. Wote wataona kwamba si yeyote ila Eliya anaweza kuitangaza hiyo siku. {GCS: 11.1}

Na sasa hebu tutazame tukio hili kupitia macho ya unabii wa Yoeli. Tusingekuwa na maono mengine ya siku hii isipokuwa yake, hayo pekee yangetosha kutupatia picha dhahiri ya ukuu na uogofyo wa siku ile. Yeye anasema: {GCS: 11.2}

“Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Pigeni na kelele katika mlima Wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja.Kwa sababu inakaribia; siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi. {GCS: 11.3}

“Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Adeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao. Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo

13

wanavyopiga mbio. Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. {GCS: 11.4}

“Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu. Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao. {GCS: 13.1}

“Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao. Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwivi. Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza; {GCS: 13.2}

“Naye BWANA anatoa sauti Yake mbele ya jeshi Lake; maana matuo Yake ni makubwa sana; kwa maana Yeye ni hodari atekelezaye neno Lake; kwa kuwa siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili? Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana Yeye

14

ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, Naye hughairi mabaya. Nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma Yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu? {GCS: 13.3}

“Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu Wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi Wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao? {GCS: 14.1}

“Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi Yake, akawahurumia watu Wake. BWANA akajibu, akawaambia watu Wake; Tazameni, Nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala Sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa; {GCS: 14.2}

“Lakini jeshi lililotoka kaskazini Nitaliondolea mbali nanyi, Nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake

15

utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa. {GCS: 14.3}

“Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa BWANA ametenda mambo makuu. Msiogope, enyi wanyama wa kondeni; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. {GCS: 15.1}

“Furahini, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa Yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza. Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. {GCS: 15.2}

“Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu Wangu hawatatahayari kamwe. Nanyi mtajua ya kuwa Mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu Wangu hawatatahayari kamwe. {GCS: 15.3}

“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho Yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, wata

16

tabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, Nitamimina roho Yangu. {GCS: 15.4}

“Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo. {GCS: 16.1}

“Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.” {GCS: 16.2}

“Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, Nitakusanya mataifa yote, Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko Nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi Yangu. Nao wamewapigia kura watu Wangu; na mtoto mwanamume wamemtoa ili kupata kahaba, na mtoto mwanamke wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa. {GCS: 16.3}

“Naam, na ninyi ni kitu gani Kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lo lote? Upesi

17

na kwa haraka Nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. Kwa kuwa mmetwaa fedha Yangu na dhahabu Yangu, nanyi mmevichukua vitu Vyangu vyema vipendezavyo, na kuviingiza katika hekalu zenu; tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao. {GCS: 16.4}

“Tazameni, Nitawaamsha wapatoke mahali mlipowauza, Nami nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. Na Mimi nitawauza wana wenu na binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa Sheba, taifa lililo mbali kabisa; kwa maana BWANA ndiye aliyesema neno hili. {GCS: 17.1}

“Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. {GCS: 17.2}

“Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee BWANA. Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko Nitakakoketi Niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana. {GCS: 17.3}

18

“Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata maneno. Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Naye BWANA atanguruma toka Zayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini BWANA atakuwa kimbilio la watu Wake, na ngome ya wana wa Israeli. {GCS: 18.1}

“Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, Nikaaye Zayuni, mlima Wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe. {GCS: 18.2}

“Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu. Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao. {GCS: 18.3}

“Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Zayuni.” Yoeli 2:1-32; 3:1-21. {GCS: 18.4}

19

Sura mbili za Yoeli zinatupa imara na mtazamo dhahiri sana wa “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” Kutoka kwazo pekee tunaweza kuona wazi itakavyokuwa. Na maadamu Eliya anakuja kabla ya hiyo siku kuanza, lazima yeye kwa hitaji awe ndiye atakayeufasiri unabii huu wa hiyo siku, na ambaye baadaye atatangaza kwamba siku imekaribia. {GCS: 19.1}

Hii hakika linathibitisha hitimisho kwamba kwa sababu Eliya ataitangaza hiyo siku kuu, yeye anaweza kuwa kwa hivyo wa pekee ambaye ataufasiri kwa usahihi unabii wa hiyo siku, ambao bado ni siri kwa Ukristo, na hata kwa Dhehebu letu lenyewe! Kweli, kusisitiza, ni kwa sababu hii haswa ndio maana nabii anatumwa. Yeye atakikunjua chuo ili kufafanua jinsi ilivyo siku ya Bwana, lile ambalo Bwana atafanya wakati huo, na namna tunavyoweza kuziokoka hukumu Zake. Kusisitiza tena ukweli huu, hebu inenwe tena kwamba akiwa wa mwisho wa manabii Eliya ni, kwa hivyo, ndiye pekee atakayeufunulia ufahamu wetu unabii wote wa Maandiko unaiohusu siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana — unabii ambao hadi sasa umekuwa tu siri kwa wote. Kwa hivyo yeye, yasemavyo Maandiko, atapiga tarumbeta katika Zayuni, kupiga kelele katika mlima mtakatifu wa Mungu, kanisani. {GCS: 19.2}

Kwa kufanya haya yote, anaanzisha mwendo

20

wa nguvu itakayorejesha mambo yote. Kwa sababu hiyo tamko bayana la Kristo: “Eliya yuaja kwanza, naye atayarejesha mambo yote.” Mat. 17:11. Bila kuepukika, basi, bila ujumbe wake tutaweza kuangamia katika ujinga wetu na katika dhambi zetu — kutishi kamwe kuona urejesho ukikamilika. {GCS: 19.3}

Hitimisho la unabii wa Yoeli katika sura ya 2 na pia katika sura ya 3, bila shaka hufunua kwamba “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana” ni wakati wa Mungu kuwakomboa watu Wake kutoka kwa mataifa, na Yeye kuitakasa damu yao. Lakini mnasema, hatujawahi kusikia jambo kama hilo? Vyema, iwapo liko katika Neno la Mungu, tunapaswa tulisikie. Na hiyo ndiyo sababu haswa Eliya anatumwa. Kuhusu utakaso, Maandiko husema: {GCS: 20.1}

“Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA… Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Zayuni.” Yoeli 2:32; 3:20, 21. {GCS: 20.2}

Na bado tuweze kuhoji hili litakuwa lini, Yoeli anatupa nuru hata zaidi: {GCS: 20.3}

“Kwa maana, angalieni, katika siku zile, na

21

wakati ule, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, Nitakusanya mataifa yote, Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko Nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi Yangu.” Yoeli 3:1, 2. {GCS: 20.4}

Yoeli anaweka msisitizo mkubwa zaidi kuhusu uogofya wa siku hiyo, kuliko anavyoweka Malaki, kwa maana anasema: {GCS: 21.1}

“…siku ya BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?” Yoeli 2:11. {GCS: 21.2}

Usisitizo mkubwa zaidi wa nabii, unaona, ni kwa uogofya wa siku hiyo kuliko ukuu wake. Tena anaonya: {GCS: 21.3}

“Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.” Yoeli 1:15. {GCS: 21.4}

Bado tena, mara hii kupitia nabii Ezekieli, Uvuvio unanena katika maneno haya: {GCS: 21.5}

“Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli [kanisa], Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina Langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea. Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi

22

kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi BWANA, asema Bwana MUNGU, Nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. {GCS: 21.6}

“Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. {GCS: 22.1}

“Nami Nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. {GCS: 22.2}

“Nanyi mtakaa katika nchi ile Niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu.” Ezek. 36:22-28. {GCS: 22.3}

Kwa sababu Maandiko yanatoa picha ya Eliya na kazi yake wazi, na namna hiyo siku itakavyokuwa, hakuna yeyote atakayeuliza kwa unyenyekevu kumhusu na kazi yake atahitaji kukisia kuwa gizani kuhusu utambulisho au kazi yake, kwa maana ni jukumu lake alilopewa na Mungu kuzichapisha Kweli mwafaka jinzi zinavyofunuliwa kwake kutoka kwa unabii. Na hivyo wote ambao wako radhi na watiifu, hawatakuwa na taabu kumtambua na ujumbe wake (Yohana 7:17). Watajua kwamba yeyote

23

anayekuja na ujumbe tofauti na ujumbe unaopatikana katika unabii kuhusu siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, si Eliya aliyeahidiwa. {GCS: 22.4}

Aidha, iwapo Mungu atamtuma mwingine tofauti na Eliya, yaani, mtu aliye na ujumbe tofauti na ule wa siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, asijidai kwamba ndiye Eliya, hatadanganya. Hivyo, kwa yeyote kudai kuwa ndiye Eliya, lakini atoe ujumbe mwingine tofauti na ule wa siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, ndani yake ni thibitisho bayana kwamba yeye si nabii wa Mungu hata kidogo, bali ni mlaghai wa cheo. Na iwapo yeyote ataweza kukwambia kuwa nabii wa awali ametimiza ahadi hii, ingawa nabii mwenyewe hajanena hivyo, basi pasipokujua kwa hakika kuwa kama hao hawamfanyii kazi Mungu wa Eliya, bali ibilisi, ni Ulaodekia wa aina mbaya sana. {GCS: 23.1}

“…Hebu tutende kama Wakristo, wakweli kama chuma kwa Mungu na kazi Yake takatifu; wepesi kuzitambua hila za Shetani katika uliofichwa, utendakazi wake mdanganyifu kupitia wana wa uasi.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 276. {GCS: 23.2}

Kwa sababu nabii Eliya atakuwa nabii wa mwisho kwa kanisa leo, jinsi Yohana Mbatizaji alivyokuwa nabii wa mwisho kwa kanisa katika katika siku yake, na maadamu kazi ya mwisho duniani ni Hukumu kwa walio Hai, ukweli inasimama wazi kama nuru ya mchana kwamba

24

ujumbe wa Eliya ni ujumbe wa hukumu ka walio Hai, wa mwisho, ambao katika asili ya injili ni wa muhimu na matokeo kuliko ujumbe mwingine ambao umewahi kupelekwa kwa watu. {GCS: 23.3}

Kwa kawaida swali lainuka sasa kwamba asili ya Hukumu kwa walio Hai ni ipi. Kwa sababu sisi sote Waadventista wa Sabato tunafahamu kazi ya Hukumu kwa Wafu, tusiwe na ugumu wowote kutambua asili ya Hukumu kwa walio Hai. Tunajua kwamba ya awali ni kutenganisha, katika vitabu juu, majina ya waliokengeuka na watenda dhambi kutoka kwa majina ya walioungama na waliovumilia ambao ni kati ya wafu. Inaondoa tu majina yao, kwa sababu miili yao si hai. Tunajua, pia, itaamua nani mbingu itawaleta kutoka makaburini mwao katika ufufuo wa kwanza (Ufu. 20:6), na nani aachwe hadi kwa ufufuo wa baada ya miaka elfu (Ufu. 20:5). Kwa hivyo, basi, kwa lipi lingine itakuwa Hukumu kwa walio Hai ila “kutupwa nje” kimwili kwa watenda dhambi ambao bado wako hai miongoni mwa wanaoungama, kama inavyoashiriwa katika mfano wa juya — utengango wa samaki wabaya kutoka kwa wazuri. {GCS: 24.4}

Tukio sawa linaletwa kwa mtazamo wetu katika mfano wa utengo wa ngano kutoka kati ya magugu (Mat. 13:30), pia katika mifano ya vazi la harusi na

25

wa talanta (Mat. 22:1-14; Mat. 25:14-30). Kila moja ya hii hutoa ushahidi zaidi kwamba utengo ni Hukumu, ambapo makapi yanapeperushwa mbali na ngano kuwekwa ghalani. Na kwa sababu kila mmoja hurejelea utengo, Hukumu kwa walio kanisani, katika nyumba ya Mungu, ambamo watatoka malimbuko, watu 144,000, kila mmoja husisitiza ukweli uo huo kama anavyofanya Mtume Petro: {GCS: 24.5}

“Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Pet. 4:17. {GCS: 25.1}

Kwa ushahidi wa ziada, nabii Zefania anena: {GCS: 25.2}

“Kisha itakuwa wakati ule, Nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; Nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake. {GCS: 25.3}

“Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku

26

ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. {GCS: 25.4}

“Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.” Zef. 1:12-18. {GCS: 26.1}

Aya hizi ni wazi kabisa kiasi cha kutohitaji maelezo. {GCS: 26.2}

Mada yetu inaturejesha nyuma kwa unabii wa Yoeli: {GCS: 26.3}

“Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo. Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA. Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, Nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, Nitakusanya mataifa yote,

27

Nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi Yangu.” Yoeli 2:31, 32; 3:1, 2. {GCS: 26.4}

Kutoka katika aya hizi itaonekana kwa kutupia jicho kwanba utengo (Hukumu) utafanyika si tu katika nyumba ya Mungu bali katika dunia yote pia. Kwa usizitizo Bwana anasema, “Nitakusanya mataifa yote, … na huko Nitawahukumu kwa ajili ya watu Wangu, na kwa ajili ya urithi Wangu,…” Yoeli 3:2. {GCS: 27.1}

Tukio hili pia, utengo kanisani, limetabiriwa pia katika Ufunuo: {GCS: 27.2}

“Joka [Ibilisi] akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto [umati ambao haujaongoka], amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake [ikawaangamiza wanafiki, watiliao shaka, na wafuasi wa watu]. Joka akamkasirikia yule mwanamke [kanisa], akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia [na waliookoka] wa uzao wake [wale ambao ni wanawe hakika], wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 12:15-17. {GCS: 27.3}

Kwa hivyo Maandiko na busara vinaweka

28

wazi kwamba hawa waliookoka na kutengwa kwa hakika ni masalia wa Mungu. {GCS: 27.4}

Pindi kanisa limetakaswa, — watenda dhambi wameondolewa kati yake, — wakati huo mwito utafanywa na “masalia” kwamba watu wa Mungu watoke Babeli, utatokea kwa sauti kuu: {GCS: 28.1}

“Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18:4. {GCS: 28.2}

Hawa walioitwa watoke ni, jinsi Maandiko yanavyoweka wazi, wanaitwa mahali (Ezek. 36:24; Isa. 66:20) ambapo hakuna dhambi (Isa. 35:8; 52:1; 62:12) na ambapo hapana hofu ya mapigo kuwaangukia (Isa. 4:5, 6; 32:17-20; Zab. 91:10); yaani, watakusanywa katika kanisa la Mungu likilotakaswa — ufalme wa Malimbuko. {GCS: 28.3}

Utengo huu wa mwisho, ambao unatukia katika milki ya Babeli, unahakikishwa zaidi katika mfano wa Kristo: {GCS: 28.4}

“Na mataifa yote watakusanyika mbele Yake; Naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; Atawaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto.” Mat. 25:32, 33. {GCS: 28.5}

Kuhusu utengo wa awali, ule ambao,

29

unafanyika katika nyumba ya Mungu, inawekwa wazi katika unabii wa Ezekieli na Isaya. {GCS: 28.6}

Ezekieli anatangaza:

“BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine Aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu Pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Ezek. 9:4-6. {GCS: 29.1}

Isaya anatangaza: {GCS: 29.2}

“Maana BWANA atakuja na moto, na magari Yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu Yake kwa moto uwakao, na maonyo Yake kwa miali ya moto. Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi. {GCS: 29.3}

“Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani,

30

visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.” Isa. 66:15, 16, 19, 20. {GCS: 29.4}

Hakuna yeyote isipokuwa Mlaodekia asiye na matumaini, ambaye siku zote hushikilia ndoto yake kwamba hana haja ya kitu zaidi, — hakuna Ukweli au manabii zaidi, — anaweza kukosa kuona kwamba unabii kuhusu siku ya Mungu ni mafumbo kwake, kwamba anahitaji kila kitu badala ya sifuri, na kwamba kazi ya Eliya aliyeahidiwa si kazi ambayo Walaodekia wanafanya. Ujumbe wa Laodekia (Hukumu kwa Wafu) kwa hakika si ujumbe wa Eliya, ingawa wengi wanaweza kufikiri ni huo. Ya kwamba wengi ni vipofu kwa hili, Bwana anaonyesha: “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” {GCS: 30.1}

Isitoshe, sote tunajua kwamba kazi ya Eliya wa asili ilikuwa kuwaondolea mbali manabii na makuhani ambao walimtumikia Baali badala ya Mungu, wale waliowaongoza Waisraeli wa kale

31

katika imani potovu na upumbavu wa siku hiyo. Kwa hivyo, kazi ya Eliya wa uakisi, ikiwa katika roho na nguvu ya Eliya wa asili, kwa hivyo basi lazima iwe sawa na kazi ya Eliya wa asili ya urejesho wa Ukweli na haki na kuleta hukumu juu ya manabii na walimu wa uongo katika siku ya uakisi ambayo yenyewe ni utengo wa makapi kutoka kati ya ngano — kazi ya Hukumu kwa walio Hai. {GCS: 30.2}

Msingi mkubwa wa ushahidi ambao Maandiko haya yameikusanyia mada hii hadi sasa, nina imani tena kwamba yamemuathiri anayetambua kuwa yu ana kwa ana na Ukweli wa Mungu wa kipekee wa masaa haya ya kufunga mlango wa rehema. Wale wote ambao bila ubaguzi wamewazia kwa undani mada hii hadi hapa, kwa hakika wataendelea sasa hadi sehemu inayofuata “jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.” {GCS: 31.1}

Sasa swali: Je, Nabii Eliya wa kale mwenyewe ataonekana tena, au mwingine fulani, akiwa na roho na nguvu ile ile, kuchukua nafasi yake? {GCS: 31.2}

Taarifa yake Yohana Mbatizaji kwamba yeye si Eliya, na taarifa ya Yesu kwamba Yohana alikuwa Eliya wa siku hiyo, si wa siku yetu, hutatua kauli tatu: {GCS: 31.3}

(1) Kwamba Yohana hakuwa akitimiza kwa namna yoyote kazi ya Eliya

32

ambaye alikuwa aje kabla ya siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, ila yeye, nabii wa mwisho kwa kanisa lake la siku hiyo, alikuja tu kwa roho na nguvu ya Eliya, ili kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa kwanza wa Bwana. Ndivyo Eliya wa siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, nabii wa mwisho kwa kanisa hili leo, yuaja katika roho na nguvu ile ile, ili kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa Bwana wa pili. {GCS: 31.4}

(2) Kwamba kama Yohana alikuwa Eliya wa siku yake, wala si Eliya Mtishbi mwenyewe, ndiposa ahadi ya Eliya si lazima itimizwe na nabii mwenyewe binafsi. {GCS: 32.1}

(3) Kwamba kama Eliya wa ujio wa Yesu wa kwanza alikuwa mtu mmoja, na pia kama Eliya wa Mlima Karmeli alivyokuwa mtu mmoja, si umati wa makuhani, basi kwa usawa wa kufikiri, Eliya wa leo lazima pia awe mtu mmoja, si umati wa wachungaji. {GCS: 32.2}

Ahadi hiyo, yenyewe, isitoshe, ni ya mmoja tu, si ya wengi, na, pamoja na isipokuwa mmoja tu, hatujui wakati wowote mwingine ambapo Mungu aliajiri hata manabii wawili (acha hata wengi) kwa wakati mmoja, kupeleka ujumbe mmoja kwa watu wamoja. Yeye sikuzote alimwita mmoja, chini ya uongozi wa Roho, akamtumia kumsaidia kupeleka ujumbe kwa watu. Hivyo ndivyo tu wengine walivyowahi kujitambulisha na yule aliyeitwa. {GCS: 32.3}

33

Wizi ulioje wa kukufuru! — iwapo mtu atajaribu kuficha mbali ukweli kuhusu ofisi ya nabii, ili kupitisha uongo badala yake, — kusema kwamba Eliya si mtu mmoja bali kundi la watu, mbele ya ukweli kwamba mifano, na unabii pia, mbali na sheria na utaratibu wa Mbingu, hauruhusu jambo kama hilo. Hivyo kwenda kinyume cha Maandiko Matakatifu ni jitahada wazi ya kuondolea mbali milele nabii wa Mungu aliyeahidiwa, sawa na Farao alivyoelekea kumuondolea mbali Musa kwa kuwazamisha watoto Waebrania, na vile vile jinsi Herode alivyojaribu kumwondolea mbali Kristo kwa kuwachinja watoto wachanga wa siku yake! Tafakarini hili ki-undani pia, Wandugu. {GCS: 33.1}

Tena, ikiwa mtu yeyote aweze kutumbuiza dhana kwamba ahadi hii ya nabii humaanisha umati wa wahubiri, basi jinsi nafsi yako ishivyo, mtu huyo anajipumbaza vibaya kama wale waliopotoshwa wafuasi wa Kora, Dathani na Abiramu walivyojipumbaza katika mawazo yao ya ukaidi kwamba wale watatu watafuta ofisi ya unabii na wakuza ubinafsi walikuwa pia manabii kama Musa. Wale waghushi watatu, msiwe mmesahau, hata walisema kwamba umati wote ulikuwa mtakatifu (Hes. 16:1-3)! Lakini walikuwa? Hakika kama nchi ilivyowameza wakati huo, hivyo hakika wote kama hao wa siku hizi, pia, watamezwa na nchi wakati itakifunua kinywa chake na kuyaondolea mbali mafuriko (Ufu. 12:16). {GCS: 33.2}

Kwa sikitiko, wale watakaoamini uongo na hivyo kupumbazika, watafanya hivyo; hakuna kitakachowazuia. Inatarajiwa kwa uaminifu, hata hivyo, wandugu, kwamba ninyi ni wafuasi wa Mungu na Roho Wake kwa Kweli; kwamba ninyi si wafuasi wa watu, au wa ubinafsi, kwa maana uzito wa swala unawapa wote changamoto kwa tafakari ya uaminifu zaidi na uamuzi jasiri. Tunapaswa sasa, kwa hivyo, kwa juhudi kuendelea na vigezo hivi vya kuhitimisha: {GCS: 34.1}

Kwa sababu Mungu hafanyi majaribio, na maadamu Yeye humaanisha tu yale Husema, hampaswi kuwa na shaka katika mawazo yenu kwamba Maandiko Matakatifu kumhusu Eliya wa uakisi (yeye ambaye ataliamsha kanisa na kuwaonya Walaodekia kuhusu “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana” hakikisha kwamba yeye ni mtu mmoja. Kwa hakika, yeye atakuwa na wasaidizi waaminifu, lakini kwa mujibu wa nabii Nahumu atatumia sana matbaa na ataeneza ujumbe wake kwa ada ya posta kila mahali, kama majani ya vuli. Hatajali yatakayofanywa kwa vitabu vyake, lakini atahakikisha kwamba vinaingia katika mikono yote, mifuko ya nje na ndani, ua au majaa ya taka kote kote Laodekia. Hapa ni lile Uvuvio Wenyewe una la kusema kuhusu mbinu ya nabii ya kuupeleka ujumbe wake kwa kanisa: {GCS: 34.2}

“Tazama juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani! Zishike sikukuu zako Ee Yuda,

35

ziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukataliwa mbali.” Nah. 1:15. {GCS: 34.3}

Hivyo umelipata kutoka kwa Bwana, kupitia nabii Wake Nahumu, kwamba yeye anayetangaza kwamba wakati umefika wa waovu kukataliwa mbali kutoka kati ya watu wa Mungu, na kwamba hukumu ya walio Hai (ambayo, tumekwisha ona, ni “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana”) karibu inatukia, atafanya matangazo ya matukio haya kwa vitabu vyake. Zaidi kuhusu ukweli huu mwafaka “chakula kwa wakati wake,” Isaya anatangaza kwamba utatolewa kwa wote bila kulipia — “bila fedha na bila thamani.” Anawahimiza pia, kuacha kufuja pesa zao kwa kununua “kile ambacho si chakula” (Isaya 55:1, 2) — ambacho hakijavuviwa na Mungu. {GCS: 35.1}

Nini ushauri wa Bwana kuhusu Sauti ya vitabu vya Eliya? na vimepewa jina gani? {GCS: 35.2}

Jibu linakuja kupitia nabii Mika: {GCS: 35.3}

“Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina Lako; isikieni fimbo, na Yeye aliyeiagiza.” Mika 6:9. {GCS: 35.4}

Hapa ni Fimbo ambayo huzungumza; na sauti yake, andiko huonyesha, ni sauti

36

ya Mungu kwa watu Wake. Na kwa sababu “Fimbo ya Mchungaji,” vitabu vinavyosheheni ujumbe wa “Siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana,” ndio fimbo ya pekee ambayo imewahi kunena, basi ni vitabu vya “Fimbo” ambavyo Bwana hudai wote wavisikie. Wengine wanaweza kuviita hivyo vitabu “vichipuko,” wengine wanaweza kuviita “takataka” (“Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato,” uk. 29), lakini Bwana huviita jina la heshima “Fimbo,” na Ushauri Wake ni kwamba tuisikie sauti Yake. Kwa kweli, kwa sababu Fimbo ni ishara ya mamlaka, kurekebisha, na ukombozi, basi ni jina lipi lingine lingestahili zaidi kuonyesha kwamba Itawakomboa waliotubu na kuwaondolea mbali ambao hawakutubu? Ilikuwa fimbo ya Mchungaji aliyowaokoa Waisraeli wa kale, na Bwana ameichagua “Fimbo ya Mchungaji” kuwakomboa Israeli mamboleo. Ilikuwa ni Fimbo ilioongoza Kutoka kwa kwanza, na sasa inaonekana kwamba Fimbo inafanya utayari kuongoza Kutoka kwa pili (Isa. 11:11, Mika 7:14, 15, Ezek. 20:36, 37). {GCS: 35.5}

Sasa kwamba tumesikia nini Maandiko husema juu ya mada hiyo, hebu tuyasikie yajayo ambayo waasisi wa dhehebu la Waadventista wa Sabato walinena katika siku yao: {GCS: 36.1}

“Je, unabii huo wote ulitimizwa na Yohana Mbatizaji?” Tunajibu, la, kwa maana imeunganishwa kwa undani na siku iliyo kuu ya Bwana kuliko ulivyokuwa utume wa Yohana. Kazi yake ilihusisha ujio wa kwanza lakini unabii lazima

37

uhusiane haswa kwa ujio wa pili, ambao ni tukio la kuweka taji la kuingia katika siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” — “Mapitio na Kutangaza,” Februari 23, 1864. {GCS: 36.2}

“Je! Mwasema unabii lazimwa utimizwe na mtu mmoja?” Tunajibu, Si lazima, kwa sababu utume wa Yohana ilituonyesha kwamba si mtu binafsi bali roho na nguvu hutimiza unabii; na kwa nini isiwezekane hii roho na nguvu iambatane na kundi la watu vile vile na mtu mmoja-mmoja, haswa ikiwa ukubwa na umuhimu wa kazi unahitaji shirika lililoongezeka? “ — “Mapitio na Kutangaza,” Februari 23, 1864. {GCS: 37.1}

“Tuseme, basi, kuwa tunaamini kwamba ujumbe wa malaika wa tatu sasa unakamilisha utimilifu wa Malaki 4:5, 6. Kwa hivyo, basi yeyote asidanganywe kwa dhana kwamba Eliya binafsi ataonekana, lakini wachukue tahadhari kwa kazi ambayo tayari inaendelea mbele ya macho yao.” — “Mapitio na Kutangaza,” Februari 23, 1864. (Italiki ni zetu.) {GCS: 37.2}

Waasisi wa Dhehebu hapa wanaonekana hapa bila shaka kudhoofisha wazo la kuonekana tena binafsi kwa nabii wa zamani. Isitoshe, vifungu hivi husema kwamba ingawa unabii wenyewe unadai nabii binafsi haiweki mipaka kwa mtu binafsi, ila kwa kundi, kwa mwili wa wasaidizi, wakiongozwa na Bwana na kupewa roho

38

na nguvu ya Eliya. {GCS: 37.3}

Nukuu hizi zinafafanuliwa zaidi na “Maandishi ya Awali:” {GCS: 38.1}

“Ya kutisha ni kazi yake. Wa kuogofya ni utume wake. Yeye ndiye malaika atakayeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kuifunga, ngano kwa ghala la mbinguni. Mambo haya yanapaswa kuyashughulisha mawazo yote, umakini wote.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 118. {GCS: 38.2}

Katika nukuu hii tunaambiwa wazi kwamba ujumbe wa malaika wa tatu katika awamu yake ya mwisho ni “mavuno” — Hukumu kwa walio Hai. {GCS: 38.3}

Tena: {GCS: 38.3}

“Wakati wa Hukumu ni kipindi maalum cha kumkumbuka, wakati Bwana anawakusanya walio Wake kutoka miongoni mwa magugu.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 234. {GCS: 38.4}

“Ujumbe wa malaika wa tatu” katika awamu yake ya awali, Hukumu kwa Wafu, ulifunuliwa kwa Dhehebu na mtu mmoja, mwasisi wa Dhehebu, na kwamba yule mmoja aliwaelekeza watenda kazi wenza. Hivyo ni lazima iwe kwa heshima na ujumbe katika awamu yake ya mwisho, Hukumu kwa walio Hai. Isitoshe, kwa vile sehemu ya kwanza ya ujumbe wa malaika wa tatu, Hukumu kwa Wafu, haijumuishi ujumbe

39

wa mwisho wala kukamilisha Hukumu, lakini badala yake hushughulikia awamu yake ya kwanza, basi sehemu ya mwisho ya ujumbe wa malaika wa tatu, Hukumu kwa walio Hai, ni lazima uwe ujumbe wa mwisho na awamu ya mwisho ya Hukumu. Kwa kweli, Ujumbe wa malaika watatu unahusu Hukumu kwa Wafu isivyo moja kwa moja, maana Hukumu kwa walio Hai ni tukio la umuhimu wote; yaani, malaika hajatumwa haswa kufafanua kile hukumu hufanya kwa wafu, ila ni nini hufanya kwa walio hai. {GCS: 38.6}

Hukumu kwa Wafu, zaidi ya hayo, si ujumbe wa “siku iliyo kuu na ya kuogofya.” haugusi hata kwa unabii wa siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana. Na kwa sababu mmoja ambaye ujumbe wa Hukumu kwa Wafu ulifunuliwa tayari alilala miaka hii mingi, na kwa sababu hakuna chochote, bila kutaja “mambo yote,” bado hata sasa kurejeshwa, na pia, tangu hapo mmoja yule hakujidai kuwa ni Eliya, wala kuufunua unabii wa Hukumu kwa walio Hai, hakuna yeyote, kwa hivyo, anaweza kusema kwa uaminifu na bila hatia Eliya amekuja na kwenda. Kwa mtazamo wa kweli hizi, utakuwa ni upumbavu wa kiwango cha chini zaidi, ikiwa si kukufuru, kwa mtu yeyote kumshutumu, au kufikiri kwamba ofisi yake ya kinabii ilitimiza chochote zaidi ya sehemu ya maandalizi ya ujumbe wa Eliya. {GCS: 39.1}

Kwa hivyo tunaona kwamba tunapoiangalia mada

40

zaidi, ndivyo dhahiri zaidi unakuwa ukweli kwamba Ujumbe wa Malaika wa Tatu katika awamu yake ya mwisho ni Hukumu kwa walio Hai, mavuno. Wazi wazi, basi, kazi ya Eliya ni kupeana nuru kuhusu Hukumu kwa walio Hai. Hivyo– {GCS: 39.2}

“… Wale watakaoitayarisha njia ya kuja mara ya pili kwa Kristo, wanawakilishwa na Eliya mwaminifu, kama vile Yohana alivyokuja katika roho ya Eliya ili kutayarisha njia ya ujio wa Kristo wa kwanza ….” — “Shuhuda,” Gombo la 3, uk. 62. {GCS: 40.1}

Ni wazi sana Walaodekia hawawezi kuitayarisha njia ya kuja kwa Kristo mara ya pili bila ujumbe wa Hukumu kwa walio Hai, wa mwisho, na badala yake wao wenyewe, asema Bwana, wako kwenye ukingo wa kutapikwa nje. Lazima Walaodekia wenyewe ikiwezekana waamshwe na nabii Eliya, wasije wanapoota kwamba wao ni tajiri bila ujumbe wake, waangamie katika dhambi zao, na hivyo wasisimame katika hukumu. {GCS: 40.2}

Hapa upo unabii wa Dada White mwenyewe kuhusu kazi wakati wa siku iliyo kuu na ya kuogofya, ambayo, alipoandika, ilikuwa bado ya baadaye: {GCS: 40.3}

“Maneno ya kufunga ya Malaki ni unabii kuhusu kazi ambayo inapaswa kufanywa kwa maandalizi ya ujio wa kwanza na wa pili wa Kristo.” — “Mlinzi wa Kusini,” Machi 21, 1905. {GCS: 40.4}

41

“Kazi ya Yohana Mbatizaji, na kazi ya wale ambao katika siku za mwisho watakwenda katika roho na nguvu ya Eliya kuwaamsha watu kutoka kwa kutojali kwao, ni sawa kwa namna nyingi. Kazi yake ni mfano wa kazi ambayo inapaswa kufanywa katika kizazi hiki. Kristo atakuja mara ya pili kuhukumu ulimwengu kwa haki. Wajumbe wa Mungu ambao wataupeleka ujumbe wa mwisho wa onyo la kutolewa kwa ulimwengu, watajiandaa kwa ajili ya ujio wa pili wa Kristo, jinsi Yohana alivyoitayarisha njia ya ujio Wake wa kwanza.” — “Mlinzi wa Kusini,” Machi 21, 1905. {GCS: 41.1}

“…katika saa ya hatari kuu, Mungu wa Eliya ataviinua vyombo vya kibinadamu kuupeleka ujumbe ambao hautazimwa.” — “Manabii na Wafalme,” uk. 187. {GCS: 41.2}

“Ruhusu Mbingu Iongoze”

“Unabii lazima utimizwe.” Asema Bwana: Angalieni, nitawapelekea nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni hodari sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 475, 476. (Umenukuliwa kutoka “Mapitio na Kutangaza,” Februari 18, 1890.) {GCS: 41.3}

42

Hii ni hatari kubwa kwa zote — hata ya waumini. Hivi wazi ni kweli kwamba “tunayo mengi ya kuhofia kutoka ndani kuliko kutoka nje. Vikwazo kwa nguvu na mafanikio ni vikubwa zaidi kutoka ndani ya kanisa lenyewe kuliko kutoka ulimwenguni.” — “Mapitio na Kutangaza,” Machi 22, 1887. Kusema machache, wale walio ndani wanapaswa kujua vyema kuliko kujijaribu wenyewe kuifanya thabiti safina, kana kwamba Mungu amewateua kuichukua nafasi Yake na kumuelekeza nabii Wake, kuitamani si tu ofisi ya kinabii bali mamlaka ya Mungu pia! Ni tusi lililoje, si kwa akili ya mtu bali pia kwa Mungu Mwenyewe! {GCS: 42.1}

Kutoka kwa nuru inayoangaza sasa kwa mada hii, mwaweza kuona, Wandugu, kuliko hapo awali kwamba tumeifikia saa ya umakini zaidi ya maisha, wakati ambapo hatuwezi tena kulishughulikia tena swala hili kwa wepesi na kwa uzembe, ila ambamo tunapaswa kumwomba Mungu kutuongoza katika Ukweli Wake wa wakati huu, tusije kwa upofu (bila Uvuvio) kuenenda kwenye adhabu. Na kwa bidii mno bado uchaji huu uwekwe moyoni kadiri mtu anavyoyatazama maneno mazito yafuatayo kwa kanisa: {GCS: 42.2}

“…Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa mpepeto, wa kupimwa watafunuliwa waonekane..” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {GCS: 42.3}

43

“…Jumbe kutoka Mbinguni ni za tabia ya kuamsha upinzani. Mashahidi waaminifu kwa ajili ya Kristo na ukweli watakemea dhambi. Maneno yao yatakuwa kama nyundo ya kuuvunja moyo mgumu, kama moto wa kuchoma makapi. Ipo haja daima ya jumbe kali za uamuzi, za onyo. Mungu atakuwa na watu ambao ni wa kweli kwa wajibu. Kwa wakati mwafaka anawatuma wajumbe Wake waaminifu kuifanya kazi kama ile ya Eliya.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 254. {GCS: 43.1}

“Wale tu, ambao wameyahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka kuingia katika Kilio Kikuu.” Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {GCS: 43.2}

Wandugu, lile ambalo kurasa hizi hapa zinawaletea, kuacha mioyoni mwenu kwa maombi kuzingatia kwa bidii, sio nadharia si hekaya tupu ya mtu, bali ni la Uvuvio Wenyewe. Kwa hiyo laweza tu kuwa Ukweli. Hivyo kuzingatia kwako lazima kukufanye uwe na furaha sana. Iwapo kuna shaka lolote, basi Nakuuliza tafadhali uzalishe hoja yako. Tuonyeshe nini kingine ambacho lazima unabii huu na mifano hii humaanisha. Usiupuuzie mbali kwa kusema,

44

“Aa… kichipuko,” au kwa kubandika juu yake jina lingine lisilostahi, maana mkiendelea kufanya hivi, Wandugu, ndivyo mtakavyojiumiza zaidi. Nawasihi kuandika kwa **Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas,** kwa vitabu bila fedha kuhusu ujumbe wa saa ya sasa na kujifunza kabisa — tulia kwa shughuli hii kwa uwazi na umakini mkubwa. Hatimaye hutawahi kutatizwa na vichipuko tena. {GCS: 43.3}

Hivyo, kabla ya kunena mawazo yenu, Wandugu, tafadhali angalia kwa uangalifu ni Ukweli gani mwafaka mtakaokuwa nao kwa ajili yenu wenyewe na kwa ulimwengu baada ya Hukumu kwa Wafu kupita iwapo ajili ya yeyote, ikiwa ni pamoja nanyi wenyewe, wakati “Hukumu kwa walio Hai” itaanza — nini ila taa tupu isipokuwa sasa myapate mafuta ya ziada katika vyombo vyenu? Isipokuwa katika mifano mingine, chuo kikunjue kwa ukweli mwingine uliofunuliwa na Mungu, “chakula kwa wakati wake” (Mat. 24:45), mpewe? Na nini kitatokea iwapo mtaiga makosa ya Wayahudi, Warumi, na Waprotestanti ambao wamezikataa jumbe za Mungu? Mungu akataza isiwe hatma ya kutisha ya mtu yeyote ambaye mwito huu umeelekezwa. {GCS: 44.1}

>