fbpx

Kituo Cha Mafunzo Cha Mlima Karmeli

Kituo cha Mafunzo cha Mlima Karmeli

                                    

ORODHA-MTAALA NA KANUNI YA MAAGIZO

“Na Kwa Maarifa Vyumba Vitajazwa.”

                                    

KITUO CHA MAFUNZO CHA MLIMA KARMELI

—————————————————- ——

ORODHA-MTAALA NA KANUNI YA MAAGIZO

—————————————————- ——

Ilichapishwa, 1942, na

SHIRIKA LA UCHAPISHAJI LA ULIMWENGU .

Kituo cha Mlima Karmeli Waco, Texas

1

LENGO LA MAISHA

“Jicho halijayaona wala sikio halijayasikia, wala hayajaingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Kor. 2:9. {MCTC: 4.1}

“Kukaa milele katika nyumba hii ya wenye heri, kubeba katika nafsi, mwilini na rohoni, sio athari zenye giza za dhambi na laana, lakini sura kamili ya Muumba wetu, na katika vizazi visivyokuwa na mwisho kustawi katika hekima, maarifa na katika utakatifu, daima wakitafiti nyanja mpya za mawazo, daima wakipata maajabu na utukufu mpya, ukiongezeka daima katika uwezo wa kujua na kufurahia na kupenda, na kujua kwamba bado mbele yetu furaha na upendo na hekima isiyokuwa na mwisho, — kama hili ni lengo ambalo tumaini la Mkristo linaelekeza kwalo, ambalo elimu ya Mkristo inatayarisha. Ili kupata elimu hii, na kuwasaidia wengine kuipata, linapaswa kuwa lengo la maisha ya Mkristo.” — Mashauri kwa Walimu, uk. 55. {MCTC: 4.2}

2

YALIYOMO

KITUO CHA MAFUNZO CHA MLIMA KARMELI

Eneo 5

Kusudi 5

Muundo 6

Mazingira 7

Watu wanaokubaliwa 7

Miundo Msingi ya Shule 7

Kozi ya Wachungaji ya Mawasiliano ya Barua 8

Kozi Kabla Uchungaji 8

Mahudhurio 8

Mwenendo 9

MTAALA WA WACHUNGAJI

Elimu ya Kiufundi 10

Roho ya Unabii 11

Unabii wa Mwisho wa Dunia 11

Falsafa Iliyofunuliwa 11

Elimunafsia Iliyofunuliwa 12

Sayasi ya Jamii Iliyofunuliwa 12

Historia Iliyofunuliwa 13

Ushairi na Wimbo Mtakatifu 13

Mahubiri 13

Kiingereza cha Ukristo 14

Ahadi ya Mwanafunzi 14

MAAGIZO NA MIONGOZO YA JUMLA INAYOWAONGOZA WALIMU(VIONGOZI WA IDARA), WANAFUNZI (WAFANYAKAZI), NA WAKAZI WOTE

Wageni na Wapya 16

Vyumba 17

Moto 17

Ibada 18

Fedha 18

Upishi 19

Biashara 19

Ufuaji 20

Kushona 20

Ofisi Kuu 21

Usafirishaji 21

Shule 21

Mambo Mengine 22

Mavazi 24

Afya 25

Matibabu 25

Ajira 26

Vyombo na Vifaa vya Ujenzi 27

Wakuu wa Idara na Wafanyakazi 27

Fomu za Wakati na Wakati wa Ziada 28

Ukaguzi au Kuondoka Kambini 28

Lolote Unalofanya Lifaye Kibiashara 29

3

[Picha ya Jengo la Utawala]

4

Kituo cha Mafunzo cha Mlima Karmeli

Eneo

Kituo cha Mafunzo cha Mlima Karmeli kilianzishwa mwaka 1935, na kinapatikana maili sita kaskazini magharibi mwa Waco, Texas. Ekari zake 375 ni hifadhi ya sylvan, na miinuko yake ya magharibi na kaskazini ikiamuru mandhari ya Ziwa Waco zuri lenye urefu wa futi mia tatu chini, na mandhari maridadi sana ng’ambo, ni furaha kweli kweli kwa hali ya pekee mwituni. {MCTC: 5.1}

Kusudi

Katika mpangilio mzuri mno kama huo, iliinuliwa katika saa hii ya mwisho (ya “kumi na moja” — Mat 20:6) katika historia ya injili, kama msingi wa thibitisho la jeshi hilo la Kikristo (Yoeli 2:2-11; Mika 5:7, 8) ambalo litaurejesha Ufalme unaokuja hivi karibuni wa milele. Kwa hivyo, juu ya wote wanaokuja katika dira ya mvuto wake agizo lake la msingi ni kwamba hiyo kanuni kuu iliyotamkwa na Mwalimu mkuu ulimwengu haujawahi kujua: “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake.” Mat. 6:33. {MCTC: 5.2}

5

Kwa hivyo kimeitwa kutekeleza kazi Takatifu ya kukusanya, kuelimisha, na kuwaadibisha wanaume na wanawake kwa nafasi katika Ufalme uliotumainiwa kwa muda mrefu na, kwa sababu hiyo, kwa ajili ya furaha ya huduma tukufu sasa katika “mavuno” mwanzoni mwa mwisho wa dunia hii, na furaha ya upeo inayofuata ya huduma ya utukufu daima katika ulimwengu ujao. {MCTC: 6.1}

Michakato yake ya kielimu kwa hivyo ikiwa inahusiana na mwanadamu mzima kwa wakati wa sasa na umilele, Kusudi la Mlima Karmeli la sikuzote ni kuelimisha mkono, akili, na moyo katika ukuaji sawa wa nguvu za mwili, akili, na kiroho. Kwa elimu hii ya sehemu tatu, hutaka kurejesha ndani ya mwanadamu sura ya Muumba wake — kukuza ustawi wa mwili, akili, na roho, ili ukamilifu wa umilele uliokusudiwa na Mungu katika uumbaji Wake utimilike. {MCTC: 6.2}

Muundo

Kama sharti la kukamilisha kazi hii ya Mungu, shule hii tangu kuanzishwa imebuniwa katika muundo mtakatifu wa shule za manabii za zamani. Ikiwa na mvuto kutoka kwa muundo huu mtakatifu, utaratibu wake wote wa elimu una msingi kwa Neno la Mungu; na kwa masomo yake, lengo kuu la masomo yote: kujifunza mapenzi ya Mungu, maarifa pekee ambayo hufanya kustahili uraia katika “ufalme ulioandaliwa … tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.” Mat. 25:34. {MCTC: 6.3}

6

Mazingira

Ikimilikiwa na urithi huu wa kusudi na muundo mtakatifu, maagizo yamewekezwa kwa mazingira ya maazimio ya upeo. Mwalimu na mwanafunzi wakivuta kabisa pumzi ya uvuvio huu wanachochewa kwa juhudi kubwa kufikia vimo vya upeo ambapo, kati ya wateule, miguuni pa Mwalimu wa walimu, katika Darasa la madarasa, atajifunza Sayansi ya sayansi zote — Ufunguo wa maarifa ambao utamfunulia Ufalme wa Mungu. {MCTC: 7.1}

Watu wanaokubaliwa

Kupatana na muundo huu mtakatifu, Mlima Karmeli huwaandikisha watu kama wale wanaojulikana kukubali kikamilifu imani yake, madhumuni yake, na kanuni zake, na wanaotamani nafasi kwa kazi ya mwisho ya injili — urejesho wa kila taasisi takatifu, na kuingiza duniani amani ya kudumu na mapenzi mema kwa wanadamu. {MCTC: 7.2}

Haki imehifadhiwa kukataa kumwandikisha mtu yeyote anayejitokeza kuingizwa bila kujaza kimbele hati ya maombi na kuirudisha iliyotolewa kwa chuo hicho, na bila kupata arifa ya kukubaliwa. {MCTC: 7.3}

Miundo Msingi ya Shule

Kwa kuzingatia imani yake katika mwisho wa mambo yote ya ulimwengu ulio karibu, na kanuni za unyenyekevu na adabu, taasisi inajenga bila kujionyesha.

7

Miundo msingi yake hadi leo hujumuisha majengo makuu sita na idadi kadhaa ya ziada. Yote isipokuwa moja (ambayo ni ya kigae) ni ya kiunzi (cha mbao) na ujenzi wa mawe. Haya kwa sasa yanatoa kituo cha usimamizi, hekalu, madarasa, mabweni na vyumba vingine vya sebule, jikoni, chumba cha kulia, mahali pa udobi, zahanati, jengo la chekechea, na pa kuhifadhia vifaa, nyumba ya pampu, tangi la kuhifadhi maji, nyumba ya kudhibiti bomba la maji, na ghala la mazao. {MCTC: 7.4}

Kozi ya Wachungaji ya Kuandikiana

Wanafunzi ambao kabla ya kuja hapa wamefanya kazi ya kuridhisha katika kozi yashule ya mawasiliano ya barua wanaruhusiwa ustahilifu wa uchungaji. {MCTC: 8.1}

Kozi Kabla Uchungaji

Kama sehemu muhimu ya muundo wake, mfumo wake wa elimu hutoa maandalio ya jumla ya kabla uchungaji katika kozi endelevu ya vidato kumi na mbili, ikikumbatia matawi ya msingi ya kujifunza, kwa wanafunzi umri wa shule ya msingi, ya kati, na wa shule ya upili. {MCTC: 8.2}

Mahudhurio

1. Kuhudhuria kwa wakati na kwa kawaida katika madarasa yote, mikutano maalum, na ibada za kidini inahitajika kwa wanafunzi. {MCTC: 8.3}

“Kati ya vipengee vyote vya elimu itakayotolewa … mazoea ya kidini ndio ya umuhimu zaidi.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 174. {MCTC: 8.4}

8

2. Orodha za kutokuwepo na kuchelewa zitatangazwa mara moja kwa juma. {MCTC: 9.1}

3. Kutokuwepo kwa jinsi hii, isipokuwa kwa ugonjwa, kama ambavyo kumepangiliwa na taasisi kunaweza kukubalika. {MCTC: 9.2}

4. Sababu za kutokuwepo au kuchelewa lazima ziwasilishwe ndani ya masaa ishirini na nne ya kurudi kwa mwanafunzi katika madarasa yake. {MCTC: 9.3}

5. Mwanafunzi anayepatikana katika darasa moja kutokuwepo jumla ya asilimia 15 ya vikao vyote vya darasa hilo atapata “F” katika somo hilo. {MCTC: 9.4}

6. Kutokuwepo mara ya pili bila kuruhusiwa kwa mwaka iwe katika darasa moja au darasa lingine, hubeba faini ya $ .50. (Kutokuwepo kwa ziada bila kuruhusiwa kunakuwa suala la adhabu kali zaidi.) {MCTC: 9.5}

7. Kuchelewa mara mbili ambako hakujaruhusiwa ni sawa na kutokuwepo mara moja bila ruhusa. {MCTC: 9.6}

8. Likizo ya kutokuwepo hairuhusu kutohudhuria madarasa. Sababu ya kila kutokuwepo katika kila darasa lazima iwasilishwe. {MCTC: 9.7}

9. Mwanafunzi yeyote anayejiondoa darasani kwa njia yoyote nyingine isipokuwa njia sahihi, au kuacha kwa sababu ya kazi isiyoridhisha, atapokea “F” katika somo hilo. {MCTC: 9.8}

Mwenendo

Mwanafunzi ambaye mazoea yake, roho yake, au mvuto wake haupatani na viwango na kanuni za taasisi, anaweza kuondolewa wakati wowote hata ingawa hatakuwa amekiuka maagizo yoyote maalum. {MCTC: 9.9}

9

“Mwanafunzi mmoja aliye na mawazo ya ulegevu anaweza kufanya mengi kushusha kiwango, kuliko watu kumi kwa bidii yao yote wanavyoweza kufanya ili kuukabili mvuto wa kupotosha maadili. {MCTC: 10.1}

“Kukosa au kufaulu kutasomwa katika mwenedo ambao wanafunzi hufuata. Iwapo watasimama tayari kuhoji sheria na kanuni na utaratibu, ikiwa watapendelea ubinafsi, na kwa mfano wao wahimize roho ya uasi, usiwape nafasi. Taasisi inaweza kuwa bora ifungwe milango yake kuliko kuruhusu roho hii kuchachisha wasaidizi na kuvunja vizuizi ambavyo imegharimika kupitia, bidii, na maombi ya kuisimamisha.” — Mashauri kwa Walimu, uk. 482. {MCTC: 10.2}

MTAALA WA WACHUNGAJI

Elimu ya Kiufundi

Awamu ya kazi ya mikono ya elimu ya mwanafunzi. Hupatikana kupitia ufuatiaji wa kila siku kwa moja au nyingi za kazi mbali mbali za taasisi. Katika nadharia na utendaji, njia na taratibu zinazofaa hufundishwa daima kwa ajili ya matokeo sahihi. Ufanisi husisitizwa kama tokeo la matumizi ya nguvu na kukazia fikra, uangalifu, ukamilifu, wepesi, na ustadi. Tamaa isiyoweza kuzimwa kwa mema mengine makubwa, nia isiyoshindwa kwa ufanisi, kujitahidi kabisa, uvumilivu usiochoka hukuzwa kama sehemu ya tabia ambayo humfanya mtu kufanikiwa na kuheshimiwa kati ya watu, na ambayo itamshindia kupandishwa vyeo na pongezi zote,

10

“Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, Nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako.” Mat. 25:21. Kazi inaheshimiwa hivyo na kurejeshwa kwa ubora wake wa asili katika michakato ya ukombozi. {MCTC: 10.3}

Kwa hivyo sababu ya msingi na yenye nguvu ya nidhamu na ukuaji katika uzoefu wa mafunzo ya mwanafunzi (pamoja na mapato ya maisha yake), inatumiwa ipasavyo kama chanzo cha uzalishaji na njia ya kustawisha tabia linganifu. {MCTC: 11.1}

Roho ya Unabii

Uchambuzi wa mtazamo wa zawadi ya kinabii, mahali pake muhimu na kusudi lake kanisani, zamani, sasa, na siku zijazo. Umakini maalum umeelekezwa kwa udhihirisho wa mwisho, kazi, na matunda yake. {MCTC: 11.2}

Unabii wa Mwisho wa Dunia

Uchambuzi wa uangalifu wa hali za mwisho na matukio ya mwisho jinsi yanavyofunuliwa katika safu inayolingana na kukaribiana na ushuhuda wa kinabii, mfano, sherehe, na tarakimu. Mkazo mkuu u kwenye ushirikisho wake halisi katika imani ya mwamini. {MCTC: 11.3}

Falsafa Iliyofunuliwa

Swali la kushurutisha utii lisilo la kubahatisha katika mpango wa mambo ya Mungu, katika Ukamilifu na vitengo Vyake. Njia imefanywa kwa lengo katika nuru ya maarifa yaliyofunuliwa. Kusudi ni kuendeleza kuinua na

11

kupanua vipeo vya macho ya roho, na matokeo ya uamilishaji wake kwa upeo mtakatifu wa kuishi, kama maisha mema pekee na tele zaidi — ambayo hupimwa kwa maisha ya Mungu. Vivyo hivyo, kitovu chake cha msingi cha uvumbuzi ni ukubwa na namna mbalimbali ya upendo wa Mungu. {MCTC: 11.4}

Elimunafsia Iliyofunjwa

Uchambuzi wa Maandiko wa sheria kuu za kisaikonafsia zinazotawala usawa wa ukuaji wa kweli wa Mristo kiakili, kimwili na kimaadili. Ustawi huu wa sehemu tatu na ushirikisho wa utu hutazamwa kwa uangalifu katika utimilifu wa kuumbika kwake ndani ymwanadamu, Yesu. Ubora wa utulivu na nguvu ya Kristo hukazwa kwa bidii na kufuatwa. Matumizi hai huorodheshwa. {MCTC: 12.1}

Sayasi ya Jamii Iliyofunuliwa

Uchunguzi wa muundo wa kweli wa kijamii (mwanadamu wa Edeni, ndani ya makao yake ya Edeni katika shule ya Edeni, katika hali ya Edeni — ufalme wa enzi ya kwanza), sababu za anguko lake, na kanuni za urejesho wake. Utafiti zaidi wa kina umetengwa kwa awamu ya tatu ya kozi hiyo — kwa matengenezo ya kijamii yanayohusika katika kuumbwa upya, na katika mageuzi ya kuingia katika Ufalme wa Mungu, ya mtu binafsi, familia, shule na kanisa kati ya vipengele hivi vya jamii ambavyo huchagua kujitambulisha vyenyewe pamoja na kusudi la Mungu. {MCTC: 12.2}

12

Historia Iliyofunuliwa

Uchunguzi wa historia kutoka kwa mtazamo wa Mungu. Sababu zinazosababisha kuinuka na kuanguka kwa falme na mataifa kutoka kwa uumbaji hadi sasa hufuatiliwa kwa usahihi. Mifano na mizunguko haswa hutambuliwa wazi. Umakini mkuu hukazwa kwenye vyombo vya Majaliwa ya rehema yote kimya kimya, yakitekeleza kwa uvumilivu mashauri ya mapenzi Yake nyuma, juu, na katika sarakasi kubwa na sarakasi pinzani za masilahi na nguvu na tamaa za mwanadamu. Lengo la mwisho ni kwa tukio la mwisho katika tamasha — urejesho wa Ufalme wa Mungu katika nuru ya masomo makuu yanayoletwa kwa mtazamo. {MCTC: 13.1}

Ushairi na Wimbo Mtakatifu

Uchimbaji katika migodi ya ushairi wa ukweli uliofunuliwa. Kozi hiyo hujumuisha mafunzo mafupi yasio ya kiufundi ya mtindo na aina za ushairi katika Biblia, ilhali lengo kuu ni pamoja na ubunifu wa kiroho wa mashairi matakatifu na nyimbo. {MCTC: 13.2}

Mahubiri

Utafiti wa sanaa na sayansi ya utungaji bora na uwasilishaji wa hotuba za Maandiko. Hoja za Uchungaji hufumwa kotekote katika kozi yote. Kipengee cha kiroho hushikiliwa juu kama cha umuhimu zaidi katika hatua zote za mahubiri. Fursa mbalimbali hutolewa kwa kuwasilisha. {MCTC: 13.3}

13

Kiingereza cha Ukristo

Mazoezi ya marekebisho katika misingi ya sarufi, sentensi na muundo wa aya, alama za vituo, na muundo wa insha za mdomo na za uandishi. Mkazo wa daima ni kwa kusoma lugha kutoka kwa mtazamo wa juu, kwamba “iwe na neema siku zote, yaliyokolea munyu,” “udhihirisho wa nje wa neema ya ndani.” {MCTC: 14.1}

Ahadi ya Mwanafunzi

Kama wanafunzi Wakristo Marekani, waliojitolea kwa Mungu, na kwa sababu hiyo ni waaminifu kwa kanuni za serikali hii ya huria iliyo chini ya Mungu, “tunahidi mioyo yetu, akili zetu, mikono yetu, vyetu vyote, kwanza kwa bendera

ya ufalme wa milele wa Mungu, na kwa theokrasia ambayo husimamia, watu wamoja wanaojumuisha mataifa yote, na kufungwa na

14

kamba za upendo wa milele, uhuru, haki, usafi, amani, furaha, nuru na maisha kwa wote, na pili “kwa [bendera]

ya Marekani, na kwa jamhuri ambayo husimamia, taifa moja, lisilogawanyika na uhuru na haki kwa wote.” {MCTC: 14.2}

15

MAAGIZO NA MIONGOZO YA JUMLA INAYOWAONGOZA WALIMU (VIONGOZI WA IDARA), WANAFUNZI (WAFANYAKAZI), NA WAKAZI WOTE

Wageni na Wapya

1. Wageni, wanapofika, waelekezwe kujisajili katika Ofisi Kuu, waeleze kusudi lao la kuja hapa, na wafanye ijulikane wanachokitarajia kutoka kwa taasisi hii. {MCTC: 16.1}

2. Wote wanapaswa kwenda kwa Ofisi Kuu kwa habari. {MCTC: 16.2}

3. Uvutaji sigara ni marufuku kwenye eneo. {MCTC: 16.3}

4. Kuendeleza mazungumzo na wale walio kazini kunashutumiwa kama aina ya wizi, kwa maana huiba wakati na juhudi kutoka kwa kazi hiyo. {MCTC: 16.4}

5. Wageni wanaotaka kusaidia katika kazi, wanapaswa kuripoti kwa Idara ya Ajira, na ikiwa watawekwa kazini, watawasilisha fomu zao za saa. Hawawezi, hata hivyo (isipokuwa chini ya mpango maalum), ili kuingizwa kwenye walipa sajili ya kulipwa. {MCTC: 16.5}

6. Wale tu ambao wamesoma na kukubali yote yaliyomo katika mfululizo wote wa vitabu na trakti za Fimbo ya Mchungaji ndio wanaostahili makazi ya kudumu. {MCTC: 16.6}

16

Vyumba

1. Tunza usafi wa vyumba na majengo na kwa mpangilio wakati wote. Uwe mtunza nyumba haswa anayejiheshimu. {MCTC: 17.1}

2. Kupika na kulia katika sehemu za vyumba vilivyojengwa na kuwekwa vifaa kwa ajili ya kulala tu hufanya hali zisizo za kiafya kwa wakaazi, na tisho kwa afya ya taasisi. Katika sehemu kama hizo, kwa hivyo, kuandaa na kula chakula kunapaswa kufanywa tu wakati hakuna njia nyingine ya kupata mulo. Na nyakati kama hizi, chukua tahadhari ili kukiacha chakula kifmefunikwa na hakuna makombo karibu. Isipokuwa wakati haiwezekani kukitunza chumba cha kulia, na kusaidia kukifanya kiweze kuwa kama kinavyopaswa kuwa. {MCTC: 17.2}

Moto

1. Kabla kuondoka kwenye chumba chako wakati wowote, hakikisha kwamba (a) umezima taa zote; (b) funga kabisa viziba jivu vyote vya jiko, (c) zima vifaa vyote vya umeme; (d) hakikisha kwamba nguo zote, kuni, na vitu vinavyoweza kushika moto upesi viko umbali ulio salama kabisa kutoka kwa taa au vifaa vya kupasha joto. {MCTC: 17.3}

2. Usitupe vijiti vya kiberiti vilivyoungua mahali popote bali mahali pavyo sahihi, na hupo tu baada ya kuhakikisha kwamba moto umezimika kabisa. Na uweke vijiti vya kiberiti ambavyo havijatumika mahali pafaapo. {MCTC: 17.4}

17

3. Kwa uangalifu jilinde sana dhidi majiko yanayorusha cheche za moto. {MCTC: 18.1}

4. Moto unapolipuka, arifu Ofisi Kuu mara moja; itisha misaada yote kwa kupiga kengele ya moto haraka na kwa muda mrefu; kisha harakisha na chombo cha maji kwenye eneo la moto. Na mwisho, siku zote uwe mlinzi wa moto anayetegemewa chonjo kulinda maisha na mali. {MCTC: 18.2}

Ibada

Epuka kucheka, kuongea, kunong’oneza kwa kawaida, na kutembea bila kulazimika karibu kabla, wakati, au baada ya ibada. Mwenendo kama huo huitia unajisi nyumba ya Mungu. Kumbuka kwamba Mungu yu katika hekalu Lake na ya kwamba ni nafsi tu isiyokuwa na kicho itahusika katika mwenendo kama huo. {MCTC: 18.3}

Fedha

1. Idara zote zitauza kwa msingi madhubuti wa pesa taslimu tu. {MCTC: 18.4}

2. Isipokuwa katika hitilafu zilizoidhinishwa, sarafu za biashara hazibadilishiwi kwa fedha za kitaifa kwa ununuzi kutoka mahali pengine. {MCTC: 18.5}

3. Fedha za kitaifa hubadilishwa kwa sarafu ya biashara ya Mlima Karmeli katika Ofisi Kuu pekee. {MCTC: 18.6}

4. Ni chini ya uangalizi maalum tu ambapo wageni wanaweza kubadilishana sarafu ya biashara kwa pesa za kitaifa. {MCTC: 18.7}

5. Mtu yeyote anayeweka sarafu atazifunga lakiri kabla kuziweka kwenye sanduku la kuhifadhi. {MCTC: 18.8}

18

Upishi

1. Sahani zote, vifaa vya fedha, na vyombo katika Idara ya Upishi vinapaswa kutumika na kuwekwa ndani tu. Ukiukaji utasababisha faini. {MCTC: 19.1}

2. Mulo hupakuliwa nyakati za kawaida. Usitarajie upakuzi wa mapema au wa kuchelewa. {MCTC: 19.2}

3. Watu walioidhinishwa tu ndio wanafaa kufungua jokofu. {MCTC: 19.3}

4. Wafanyakazi wa Idara ya Upishi pekee walio kazini au wakati wameidhinishwa kwa njia maalum kuwa jikoni au katika kinu cha kuoka mikate. {MCTC: 19.4}

Biashara

1. Uagizaji ujazwe kutoka kwa akiba zaidi ya ile iliopo lazima iwe ndani kabla saa 9:00 alasiri kutangulia siku za ununuzi wa kawaida wa Biashara. {MCTC: 19.5}

2. Ununuzi wa kibinafsi Dukani unaweza kufanywa tu kwa masaa ya kawaida ya kununua. {MCTC: 19.6}

3. Wanunuzi walioidhinishwa tu ndio watakaonunua katika jina la Duka. {MCTC: 19.7}

4. Kufanya maulizo ya biashara yasiyoidhinishwa, miadi, au mikataba aidha na mtu au kwa barua katika jina la Shirika la Duka, kutasababisha mkosaji afutwe kutoka kwa taasisi. {MCTC: 19.8}

5. Mtu yeyote anayefanya ununuzi wa kibinafsi mjini na kumwomba mnunuzi wa taasisi kusafirisha, atatozwa ada ya huduma. {MCTC: 19.9}

19

6. Ununuzi wa wanafunzi wa shule ni lazima ufanyike kwa hitaji lililosainiwa na mzazi au mlezi na kuidhinishwa na shule. {MCTC: 20.1}

7. Ununuzi wote unapaswa kufanywa kupitia Dukani, kwa sababu kupitia katika ile taasisi Bwana hutoa “mkate wetu wa kila siku.” Wote, kwa hivyo, wanapaswa kutafuta ustawi wake kama hazina iliyofichika. {MCTC: 20.2}

Ufuaji

1. Ufuaji utapokelewa tu siku ya kwanza ya juma hadi saa 4:00 asubuhi. {MCTC: 20.3}

2. Kuosha kutakubaliwa tu na fomu ya kufua iliyotayarishwa vizuri. {MCTC: 20.4}

3. Kupiga pasi kunapaswa kufanywa kwenye eneo la kufulia. Majengo mengine hayajaunganishwa umeme kwa kusudi hili, na kwa hivyo huwa zinaleta hatari ya moto wakati vifaa vinavyohitaji nguvu nyingi za umeme hutumika. {MCTC: 20.5}

4. Watu binafsi ambao wanaopiga pasi nguo zao wenyewe watatozwa ada kwa saa. {MCTC: 20.6}

Kushona

1. Mtu yeyote anayetaka kutumia vifaa vya chumba cha kushonea kwanza lazima afanye mipango na mkuu wa idara hiyo. {MCTC: 20.7}

2. Mitindo, vitabu vya mitindo, nk., vinapaswa kuchukuliwa kutoka kwenye chumba cha kushonea tu kwa idhini kutoka kwa mkuu wa idara. (Idara za Ununuzi, Kufulia, Kilimo, na ya Kushonea

20

ni kwa madhumuni ya kuwahudumia wakazi wa Mlima Karmeli. Kwa hivyo ni jukumu la wote hapa, wageni na wakazi sawa, kuzidumisha huduma hizi kwa kuziendeleza.) {MCTC: 20.8}

Ofisi Kuu

1. Ruhusa ya kuzungumza na wale wanaofanya kazi ofisini ithibitishwe kwenye Meza ya Habari. {MCTC: 21.1}

2. Kuandika, kurudufisha (kutolewa) nakala, au aina yoyote ya kazi inayopaswa kufanywa Ofisini, ni lazima iwasilishwe kwanza kwa meneja wa Ofisi. {MCTC: 21.2}

Usafirishaji

Wale wanaotaka kusafiri kwenda mjini, wanapaswa kufanya mpango na Idara ya Usafirishaji, na kununua tiketi huko. Kukodi magari ya kibinafsi au kulipa watu binafsi kwa ajili ya usafiri kunaruhusiwa tu chini ya maandalizi maalum na usimamizi. {MCTC: 21.3}

Shule

1. Wanafunzi wa shule wanaotaka kuondoka kwenye Chuo cha Shule inavyofaa wanaweza kufanya hivyo tu ikiwa wataambatana na mtu mzima. Makundi mseto hayaruhusiwi. {MCTC: 21.4}

2. Mikopo ya benki hutolewa tu kwa wale wanafunzi ambao mwenendo, udhamini, na kazi yao ni ya ustahili. Maombi ya mikopo kama hiyo lazima iwe

21

iliyosainiwa na shule na mzazi au mlezi, na iliyoidhinishwa na Meneja wa Mikopo. {MCTC: 21.5}

3. Kuwakopesha pesa wanafunzi na kuomba pesa kutoka kwao kunaruhusiwa tu chini ya maandalizi maalum. {MCTC: 22.1}

4. Barua ya mwanafunzi wa chuo, inayoingia na kutoka, ipitie ofisi ya Chuo. {MCTC: 22.2}

5. Kila mmoja alale tu katika chumba chake na katika kitanda chake mwenyewe. {MCTC: 22.3}

6. Redio au simu za rununu haziruhusiwi kwenye mabweni ya wanafunzi. {MCTC: 22.4}

Mambo Mengine

1. Vitu vilivyopotea na vilivyopatikana vinapaswa kupelekwa kwenye meza ya Habari. {MCTC: 22.5}

2. Uharibifu wa mali unapaswa kuripotiwa mara moja kwa Ofisi. {MCTC: 22.6}

3. Kuvunjika-vunjika kwote kunapaswa kuripotiwa mara moja na kutatuliwa kwa yule anayehusika. {MCTC: 22.7}

4. Kukata au kufyeka miti, kuharibu mimea kuchuma maua, au kutupa takataka chuoni, nk., kutatozwa faini. {MCTC: 22.8}

5. Kukosa kufunga shamba lolote, kiunga, bustani ya miti, au lango la ng’ombe vivyo hivyo kutatozw faini. {MCTC: 22.9}

6. Hifadhi maji na umeme kwa kutotumia zaidi ya unavyohitaji. {MCTC: 22.10}

22

7. Epukana na bwawa na maeneo yenye maji. Hutoa maji kwa matumizi ya binadamu na kwa hivyo lazima yahifadhiwe safi kabisa. {MCTC: 23.1}

8. Weka majivu tu kwenye vyombo vya majivu na kuhifadhi bila vioo (glasi). Weka mikebe na glasi katika vyombo tofauti. {MCTC: 23.2}

9. Kukaa bila kazi ndani ya magari, kuning’inia kwayo, na kukaa panda zanje likienda, ni marufuku. {MCTC: 23.3}

10. Uzururaji karibu na majengo kabla au baada ya usiku kuingia kutasababisha mkosaji aadhibiwe. {MCTC: 23.4}

11. Ushirika usiozuiliwa wa wanaume na wanawake ambao hawajaingia katika ndoa hauruhusiwi. Wala si kuandikiana, matembezi ya wazi au fiche, kujikalia, au vinginevyo kufanya mwenzi chuoni au mahali pengine, au kukaa pamoja katika makongamano ya umma. Ukiukaji kama huo unasababisha wakosaji kufukuzwa. {MCTC: 23.5}

Mwanafunzi mwanamume ambaye mwenendo wake, usomi, na ukomavu humpa dhamana ya upendeleo huo, anaweza, kwa nyakati ambazo taasisi itaona kuwa za busara, atapata ruhusa ya kumwita mwanafunzi mwanamke katika msimamo kama huo. {MCTC: 23,6}

12. Malalamiko na mapendekezo ya kuboresha yanapaswa kupelekwa tu kwa wale ambao wanawajibika kwa jambo linalohusika. Kuyawasilisha

23

kwa mwingine kunaweza kuchachisha shida na kusababisha huzuni. {MCTC: 23,7}

13. Mtu yeyote ambaye ameidhinishwa au watu watasikiza mashtaka au malalamishi dhidi ya mtu yeyote (wakiwemo vijana na watoto) iwapo tu yameandikwa. {MCTC: 24.1}

14. Maswali yote ya mafundisho na mengineyo yanayohitaji jibu rasmi yanapaswa kuwekwa kwenye sanduku la maswali katika Ofisi Kuu, ili kujibiwa kwa wakati unaofaa, mahali panapofaa. {MCTC: 24.2}

15. Usinene maovu; usisikie maovu; fikiri uzuri na uwe mkarimu na mwenye adabu kwa kila mtu. {MCTC: 24.3}

16. Kamari za aina yoyote, ulevi, kuvuta sigara, lugha chafu, vitabu vichafu au vinavyotiliwa shaka, ni marufuku kabisa. {MCTC: 24.4}

Mavazi

1. Mikono ya mavazi inapaswa kuning’inia chini ya kiwiko. {MCTC: 24.5}

2. Wasichana chini ya umri wa miaka kumi na mbili wanapaswa kuwa na sketi zao theluthi moja urefu kati ya fundo la goti na sakafu. Wanawake wote, na wasichana zaidi ya miaka kumi na mbili, wanapaswa kuwa na yao katikati ya goti na sakafu. {MCTC: 24.6}

3. Kola za shingo zilizo chini zimeshutumiwa. {MCTC: 24.7}

4. Vipini crisping na mapambo ya bandia ni marufuku. {MCTC: 24.8}

24

5. Isipokuwa wanatembea bila vyatu, wanawake na wasichana wanapaswa kuvaa soksi ndefu. {MCTC: 25.1}

6. Soksi nyembamba laini za hariri, soksi zilizovingirishwa chini, manukato, poda, rangi ya mdomo, wanja (rangi ya kupaka kuzunguka macho na nyusi), nk., ni mwiko kabisa. {MCTC: 25.2}

7. Saa za mkononi, vipini vya tai, minyororo ya saa ya wonyesho, wonyesho wa kitambaa cha mkononi, mivalio ya wonyesho ya aina yoyote, na ubatili wowote kama huo, umekataliwa. {MCTC: 25.3}

8. Viatu vyenye visigino virefu si vya kiafya na kwa hivyo vimekataliwa. {MCTC: 25.4}

9. Utaji unapaswa kuvaliwa na wanawake kwa hafla za kidini. {MCTC: 25.5}

Afya

1. Pumzika mapema kitandani, na baada ya hapo dumisha utulivu. {MCTC: 25.6}

2. Jikinge dhidi ya maisha yote yanayohatarisha afya. Afya ikipotezwa mara moja, yawezekana haitarejeshwa tena. “Iweni wenye kiasi katika mambo yote.” {MCTC: 25.7}

Matibabu

1. Katika ishara za kwanza za kuambukizwa ugonjwa unaoambukiza (pamoja na homa, kifaduro, nk.,) ripoti kwa zahanati. {MCTC: 25.8}

2. Gharama za matibabu kwenye zahanati ya mikwaruzo midogo, vidonda, nk., kwa wafanyakazi na wanafunzi wa taasisi, yanapaswa kulipiwa kwa ada ya kila juma kutoka kwa kila mmoja. {MCTC: 25.9}

25

3. Wafanyakazi waaminifu wanaogharimia matibabu katika Zahanati ya Mlima Karmeli, wanaweza kupokea msaada kutoka kwa idara ya Ukarimu. {MCTC: 26.1}

4. Gharama ya hospitali na malipo ya tabibu yanapaswa kulipwa aidha na, au kutozwa, kwa mtu huyo. {MCTC: 26.2}

5. Yeyote anayetaka miadi na daktari anapaswa kufanya hivyo kupitia Ofisi Kuu, na kwa wakati uo huo kufanya mipango humo kwa malipo ya ada. {MCTC: 26.3}

6. Wanafunzi wa chuo wakiripoti kwa Zahanati ya Mlima Karmeli kwa matibabu, au wakitaka kumwona daktari mjini, lazima wawasilishe ombi lililosainiwa na mzazi au mlezi na kuidhinishwa na Ofisi ya Chuo. {MCTC: 26.4}

Ajira

1. Kufanya kazi katika idara yoyote, aidha mgeni au mfanyakazi wa kawaida lazima kwanza apokee mpangilio kutoka kwa Idara ya Ajira. {MCTC: 26.5}

2. Viongozi wa Idara wanaohitaji msaada wanapaswa kuripoti kila jioni kwa Ofisi ya Ajira mahitaji yao kwa siku inayofuata. Kila moja apate msaada wake, apate vifaa vyake, nk., na kuwa tayari kwa kazi asubuhi. Kumbuka kwamba wakati wa ziada ni kwa kazi hii. {MCTC: 26.6}

3. Idara zinaweza kubadilishana usaidizi tu kwa idhini kutoka Idara ya Ajira. {MCTC: 26.7}

26

4. Biashara za kibinafsi za aina yoyote ni marufuku kwa maeneo ya taasisi. {MCTC: 27.1}

5. “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.” 1 Kor. 14:40. {MCTC: 27.2}

Vyombo na Vifaa vya Ujenzi

1. Vifaa vya ujenzi vinaweza kihalali kwa njia tu ya kuhitaji. {MCTC: 27.3}

2. Kupeana au kuazima mtu mmoja au idara vifaa au vyombo kumeshutumiwa. Ikiwa unahitaji kitu, weka oda yako kwa Duka. {MCTC: 27.4}

3. Kila mfanyakazi anawajibika kwa vyombo vyote vilivyoorodheshwa kwake. Baada ya kumaliza kazi, atavirejesha kwa hifadhi yavyo ya kawaida. {MCTC: 27.5}

Wakuu wa Idara na Wafanyakazi

1. Mkuu wa idara mpya aliyeteuliwa ataripoti kwanza Ofisini kwa maagizo kabla ya kuchukua majukumu yake. Mkuu wa idara anayeondoka ataiacha idara hiyo kwa mpangilio unaostahili kumpokeza mrithi wake, na atarejesha kwa Ofisi Kuu vifaa vyote, vitabu, kasha la pesa, nk. {MCTC: 27.6}

2. Mfanyakazi yeyote, mkuu wa idara au mwingine anayetaka habari, ni lazima aende kwa mkuu wake wa karibu. {MCTC: 27.7}

3. Kila mfanyakazi lazima ahudhurie kwa kweli kazi aliyopewa, na asiingilie au kusogea kwa kazi ya mwingine. {MCTC: 27.8}

27

4. Kufanya kazi tu ili kuweka ndani wakati, ni kutokuwa mwaminifu kwa taasisi na hivyo kwa Mungu. {MCTC: 28.1}

5. Jihusishe tu kwa mazungumzo muhimu kazini. {MCTC: 28.2}

6. Hakuna muda wa ziada unaoruhusiwa kwa kazi ya kawaida. {MCTC: 28.3}

7. Iwapo huwezi kuendelea na kazi yako, tafuta kugundua shida. Ikiwa unahitaji msaada zaidi, tuma ombi. Ifanye kazi yako isiendelee kujikokota. {MCTC: 28.4}

8. Kwa uangalifu zuia hasara. {MCTC: 28.5}

Fomu za Wakati na Wakati wa Ziada

1. Fomu za wakati zinapaswa kutayarishwa kwa usahihi na kurejeshwa futwa Ofisini kila jioni. {MCTC: 28.6}

2. Fomu za wakati zilizopitwa na siku moja hadi usiku kuingia masaa yake yatapunguzwa saa moja, ikiwa ni baada kuliko muda huu, hazitaheshimiwa hata kidogo. {MCTC: 28.7}

3. Jumapili yuma ya kila fomu za wakati, andika rekodi ya mahudhurio kwa ibada za kidini kwa juma lililotangulia, na toa sababu ya kuchelewa au kutokuwepo kwokwote. {MCTC: 28.8}

4. Wale tu ambao ni waaminifu na wa kawaida katika kazi zao, ndio watakaopokea muda wa ziada. {MCTC: 28.9}

Kazi au Kuondoka Kambini

1. Mtu yeyote kwa kuamua kukata mafungamano

28

Yake na Mlima Karmeli, atawasilisha kujiuzulu kwake, na kukagua siku moja mbele ya kuondoka kwake. Ikiwa ana watoto ambao watabaki hapa, anapaswa kufanya mipangilio na Ofisi ya Chuo. {MCTC: 28.10}

2. Watu wazima wanaotaka kuondoka kambini wakati wa kazi, ni lazima wapate idhini kutoka kwa idara yao. Wanafunzi wa chuo lazima kwanza wapate kibali kutoka kwa idara yao, kisha kutoka kwa Shule hiyo. {MCTC: 29.1}

3. Nje ya masaa ya kazi, wanafunzi wa Chuo wanapaswa kupata ruhusa kutoka kwa shule. {MCTC: 29.2}

—-O—-

Ukiukaji wowote wa sheria hizi utashughulikiwa kama tendo la adui. {MCTC: 29.3}

—-O—-

Lolote Unalofanya Lifanye Kibiashara

“… utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” Mat. 6:33, 34. “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.” Mat. 7:12. {MCTC: 29.4}

29

>