fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 25, 26

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 25, 26

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

TUNDA LA SHULE YA MUNGU NA TUNDA LA SHULE YA MWANADAMU.

USHINTO (IBADA YA SANAMU) NA UKRISTO USIOENDELEA

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Muwe Wasikilizaji Wa Udongo Mzuri

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” kuanzia ukurasa wa 59 aya ya pili: {2TG25: 2.1}

“Msikilizaji wa udongo mzuri hulipokea lile neno, ‘sio kama neno la wanadamu, ila kama lilivyo katika kweli, neno la Mungu.’ Yeye tu ambaye huyapokea Maandiko kama sauti ya Mungu inayozungumza naye ndiye mwa-nafunzi wa kweli. Yeye hutetemeka kwa neno; maana kwake yeye ni uhalisi ulio hai. Yeye huufungua ufahamu wake na moyo wake kulipokea. Wasikilizaji kama hao walikuwa Kornelio na marafiki zake, ambao walimwam-bia mtume Petro, ‘Basi sisi sote tuko hapa mbele ya Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.’ Maarifa ya ukweli hayategemei sana juu ya nguvu ya akili zaidi ya usafi wa kusudi, unyenyekevu wa imani ya dhati…. Wasikilizaji wa udongo mzuri, wakisha lisikia lile neno, hulitunza. Shetani pamoja na mashirika yake yote ya uovu hawezi kulinyakua. Kusikia au kusoma tu neno hakutoshi. Yeye ambaye hutamani kufaidika na Maandiko lazima atafakari juu ya ukweli ambao umewasilishwa kwake. Kwa umakini wa dhati na tafakari ya maombi lazima apate kujifunza maana ya maneno ya ukweli, na kunywa kabisa roho ya maneno matakatifu.” {2TG25: 2.2}

Tunahitaji kuomba kwamba tuwe wasikilizaji wa udongo mzuri na wanafunzi wa kweli; kwamba Neno la Mungu liwe uhalisi ulio hai ndani yetu; kwamba sasa tulisikilize fundisho la Roho Mtakatifu; kwamba tusiwe wasikiaji wa Neno tu, bali pia watendaji. {2TG25: 2.3}

2

TUNDA LA SHULE YA MUNGU NA TUNDA LA SHULE YA MWANADAMU.

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 31, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Zab. 71:17 — “Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.”

Hapa kuna ushuhuda wa Daudi mwenyewe wa ukweli kwamba hakuwa na jambo la kujuta kwa kuwa katika shule ya Mungu maisha yake yote, kwamba alikuwa na hamu ya kutangaza Ukweli wa Mungu. Kisha, pia, tunajua kwamba shule ya Mungu na shule za mwanadamu katika karne nyingi zimekuwa kwa pamoja katika mashindano, na tunapaswa sasa kufanya ulinganisho wa haki wa tunda la moja na tunda la nyingine. {2TG25: 3.1}

Tunajua kwamba shule za wanadamu zimezalisha watu stadi kwa nyanja nyingi. Kwa mfano, watu wamebuni madege makubwa ya kuinua tani nyingi hewani, ndege zinazokwenda upesi sana kama sauti, na kwa kimo cha urefu mkubwa pia. Watu wameunda pia meli kubwa mno zinazobeba maelfu ya tani za shehena na abiria, nazo huvuka bahari nyingi kwa siku chache. Shule za wanadamu pia zimezalisha wasemaji wenye ufasaha na walimu stadi. Wanadamu wamefanya mambo mengi, na tunawapa sifa wanayostahili. Yale ambayo shule za mwana-damu zinafanya , tunayajua vyema, lakini tunajua nini kuzihusu shule za Mungu? Je! Tunajua mengi kuzihusu? Iwapo sivyo, kwa nini sivyo? {2TG25: 3.2}

Hebu sasa tufanye uchunguzi wa haki wa tunda la shule za Mungu. Nitaanza na shule ambayo Henoko, wa saba kutoka kwa Adamu, alihudhuria. Katika shule ya Mungu alijifunza mambo muhimu sana. La kuanzia, Henoko alijifunza kutembea na Mungu (Mwa. 5:22). Mbali na hilo, hadi leo hii anashikilia ubingwa katika safari za angani: Henoko, unajua, aliruka, sio 40, 50, au maili 100 juu, sio kwa maili mia au elfu kwa saa, lakini hadi urefu kwenda juu usioelezeka na kwa kasi isiyoelezeka. Naam, haraka akafika kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Je! Shule za wanadamu zimezalisha stadi mkubwa kama Henoko? {2TG25: 3.3}

Kama Henoko, Nuhu pia, alijifunza kutembea na Bwana wake (Mwa. 6:22). Ustadi wake wa kujenga safina ni sifa kamili kwa shule ya Mungu. Safina ya Nuhu unajua, ilikuwa kubwa kabisa na thabiti kuhifadhi na kubeba jozi moja au nyingi za kila kiumbe hai duniani, pamoja na vyakula vyote muhimu kwa mwanadamu na mnyama kudumu zaidi ya mwaka! Safina yake ilihimili dhoruba mbaya ya mvua na upepo ambao ulimwengu haujawahi kujua. Safina ya Nuhu ilizidi kukaa sio tu kipindi kirefu zaidi cha mvua na upepo uliowahi kujulikana, lakini hata mitetemeko ya ardhi wakati chemchemi za vilindi vilipovunjika vikivurumisha miamba na matope mamia na maelfu ya futikamba angani, ambayo milima mirefu yenye mawe ya dunia ilifanyizwa. Sio tu safina, ila kila kiumbe hai ndani yake kilinusurika! Nuhu bado ni bingwa wa wajenzi wa meli, na bingwa wa manahodha wa baharini, pia. Tunda la shule za Mungu, unaona, ni bora zaidi kuliko kitu chochote ambacho shule za wanadamu zimeweza kuzalisha. {2TG25: 3.4}

Abrahamu, unajua, aliandikishwa katika shule ya Mungu wakati Mungu alimwita aondoke nyumbani kwa ba-ba yake

4

na aende katika nchi ambayo alikuwa hajawahi kuiona. Alichukua mali yoyote aliyokuwa nayo, na pia akamchukua mpwa wake kwa ushirikiano. Tangu mwanzoni walifanikiwa sana, na biashara yao iliongezeka haraka sana hivi kwamba ili kuitunza ilibidi wasambae na kuutenganisha ushirika. {2TG25: 4.1}

Abrahamu alichukua nchi ya vilima baada ya Lutu kuchagua bonde lenye rutuba karibu na masoko ya Sodo-ma na Gomora. Huko familia ya Lutu iliacha shule ya Mungu na kuingia shule ya mwanadamu. Abrahamu hata hivyo na nyumba yake walisalia katika shule ya Mungu, akijifunza jinsi ya kufanya vilima vilipe faida nzuri. Abrahamu akawa “tajiri sana,” lakini Lutu alikuwa maskini sana. Abrahamu unaona, katika shule ya Mungu akawa mfanya biashara mkubwa zaidi ulimwenguni katika siku yake. Alijifunza kufanya kitu kutoka kwa sufuri. Zaidi ya hayo, alikuwa jamadari mkuu wa ulimwengu, maana unakumbuka kwamba akiwa tu na watu wachache aliwashinda wafalme watano, akateka nyara zao na kurudisha mali kwa wamiliki halali. Haya yote aliyafanya bila kupoteza askari mmoja! Bado zaidi alimlea mwana wa pekee aliyejitolea kuchomwa moto juu ya madhabahu ya kafara kwa ajili ya dini ya baba yake. {2TG25: 5.1}

Ijayo tutawaangalia Esau na Yakobo, watoto pacha wa Isaka. Yakobo alihitimu kutoka shule ya Mungu, na Esau kutoka shule ya mwanadamu. Najuaje? Najua hili, kwa sababu kama Esau angalitembea na Mungu asinga-liweza kujifunza kuwinda, kwa maana Mungu sio mwindaji, hapendezwi kuua na kuharibu uhai aliouumba Yeye. Hivyo, badala ya kuchukua mafunzo yake katika shule ya Mungu, Esau alijisomesha katika shule za wanadamu. Hakuona thamani yoyote katika dini, na hakuweka thamani kubwa juu ya haki yake ya kuzaliwa kuliko thamani ya mlo. Yakobo, kwa upande mwingine, alikuwa na hamu ya kutembea na Mungu na kuinunua haki ya kuzaliwa ya Esau

5

kwa gharama yoyote, lakini akaipata kwa mapatano. {2TG25: 5.2}

Je! Najuaje yakini kwamba Yakobo alitembea na Mungu? Najua hili kwa sababu mwishoni mwa siku yake ya kwanza kukimbia kutoka kwa uso wa Esau, Yakobo alipumzika na Mungu, na hapo akawaona malaika wa Mun-gu wakitembea kupanda juu na kuteremka chini kwa ile ngazi ambayo ilikuwa refu umbali kutoka mbinguni hadi duniani. {2TG25: 6.1}

Kisha, baada ya kukaa miaka mingine ishirini katika shule ya Mungu, Yakobo aliondoka Padanaram na kuanza kurudi nyumbani akiwa na utajiri usiojulikana, ingawa alikuwa ametoa miaka kumi na minne ya muda na kazi kutoka kwa miaka ishirini ambayo hakulipwa chochote ila mabinti wawili wa Labani katika ndoa. Yakobo, unaona, katika shule ya Mungu alijifunza jinsi ya kugeuza umasikini kuwa biashara inayolipa vizuri. Isitoshe, hakujitajirisha tu, bali alimfanya baba yake mkwe kuwa tajiri pia. Alijifunza namna ya kufanya kazi na ya kuwe-ka akiba. Lakini hakuacha wakati huo. Aliendelea katika shule ya Mungu, na wakati alipokuwa nchini Misri, mwanawe Yusufu, ambaye wakati huo alikuwa wa pili kwa mfalme, hakuona aibu kumtambulisha baba yake kwa Farao kwenye kiti cha enzi. Yakobo alikuwa mtu mwungwana. {2TG25: 6.2}

Yusufu mwenyewe tangu ujana wake alikuwa mwanafunzi mstahifu katika shule ya Mungu. Mwishowe, ali-chukua kazi yake ya masomo ya juu zaidi huko Misri. Alipopata maarifa ya kutosha akawa mfalme, na Misri yote — kwa kweli ulimwengu wote wa kale — ukamsujudia. {2TG25: 6.3}

Yusufu akawa mwana uchumi mkubwa zaidi wa ulimwengu na mwanabenki pia. Tangu siku yake hakuna mtu aliyefanya mengi kama hayo: aliweza kununua nafaka ya ziada ya nchi yake kwa miaka saba, na katika miaka saba mingine akakusanya fedha zote za watu na ardhi yao — vyote fedha taslimu na amana alizoweka katika benki ya Farao. Mbali na hayo aliukoa ulimwengu kutokana na njaa. Wewe

6

nionyeshe matunda kama haya kutoka kwa shule za mwanadamu, nami nitakuonyesha kwamba mvua haiwezi kunyesha kutoka angani. {2TG25: 6.4}

Kisha akakuwapo Musa. Kuanzia ujana wake hadi miaka yake ya arobaini alienda katika zote shule ya Mungu na shule ya Farao. Na elimu hii maradufu, alijihisi mwenye nguvu na uwezo wa kutosha kuliweka huru taifa la Waebrania kutoka kwa yadi za matofali za Farao. Alianza kwa kumuua Mmisri, na kisha akaikimbia nchi. Mun-gu, hata hivyo, hakuwa amemaliza naye. Alimpeleka mpaka mlima Horebu na huko akamfanya kuwachunga kondoo. Huko alipokuwa akichunga kondoo ili kujikimu maisha na kulipia masomo ya ziada alikuwa anaiacha elimu ya Farao, na huko katika shule ya Mungu, alijifunza jinsi ya kuwa mkombozi-jamadari mkuu wa ulimwen-gu, mwandishi, mtawala, mwalimu, mtunga sheria na nabii. {2TG25: 7.1}

Kweli, shule za mwanadamu zimefunza akili kuu, na zimezalisha majemadari wakuu kama vile Eisenhower na McArthur, ambao Marekani na Uingereza Kuu waliwajengea meli kubwa, bunduki kubwa na silaha zingine kubwa, wakasajili majeshi makubwa ya nchi kavu na ya majini. Baada ya miezi mingi ya maandalizi kama haya, ambayo mamilioni ya watu walishiriki, Eisenhower alivuka Mfereji wa Uingereza dhidi ya mtambo-bora wa vita wa Ujerumani na McArthur akarudi Ufilipino na kuimiliki Japani kwa gharama ya mabilioni ya dola na maelfu ya majeruhi. Ufanisi wa kushangaza, hakika! Lakini Musa, bila bunduki, bila ndege, bila meli, na bila mtu yeyote nyumbani kujenga na kutuma vifaa, aliwaweka huru Israeli, akawaongoza salama katika Bahari ya Shamu, na kulizamisha jeshi lote la Wamisri. Aliyatenda haya yote bila bunduki au mshale, bila meli au ndege bila gharama ya mwanadamu wala mnyama. Hakuwa na majeruhi! Ni wapi kati ya matunda ya shule za mwanadamu

7

unapata lililo sawa na hili? {2TG25: 7.2}

Shule za wanadamu zimezalisha wasemaji wakuu, pia, lakini Yohana Mbatizaji alipokuwa bado katika ujana wake, kwa usemaji wake aliivutia miji yote na maeneo ya mashambani ya Yuda, wengi bila kujali kwamba walipaswa kutembea ili kufika huko, na wote, masikini na matajiri sare ilibidi wakae chini kwa ardhi kavu kwa masaa mengi. Umati wa watu walienda nyikani kumsikiza uwanjani. Nao Mitume, ingawa wavuvi wa samaki tu, katika muda usiozidi miaka mitatu katika shule ya Kristo wakawa wahubiri wakuu dunia haijawahi kujua. Ni wao tu kati ya wahubiri wotetangu wakati huo hushikilia rekodi ya kuziongoa nafsi elfu tatu kutoka Uyahudi hadi Ukristo kwa hotuba moja tu! {2TG25: 8.1}

Wakati hautaniruhusu kusema kuwahusu wengine — Yoshua na Kalebu, Danieli na Waebrania watatu, Samsoni, Daudi, manabii, na wengine wengi hata katika siku zetu. Ni ukweli, hata hivyo, kwamba kile shule ya Mungu inaweza kuzalisha, shule ya mwanadamu haiwezi kuwa sawa nacho. {2TG25: 8.2}

Katika shule ya Mungu mwanafunzi amehakikishiwa kuwa bora katika nyanja yoyote anayotumika. Na ushauri wangu kwako ni kwamba iwapo wewe ni nyasi, au mti, kwa mfano, chagua kuwa bora wa aina yake. Unaweza kuwa hivyo ukitaka kufanya hivyo, kwa maana hakuna kushindwa katika shule ya Mungu. Unaweza kuwa mchungaji bora au mfalme bora, mwalimu bora au mhubiri bora, mwanabenki bora, au bora wa chochote kile. {2TG25: 8.3}

Ni la kuvutia, pia, kutambua kwamba zote shule ya Mungu na shule ya mwanadamu zina vitabu vya mwongozo. Moja ina vitabu vya wanadamu, ambavyo likiwapo hitaji hufanywa upya kila mwaka, ile nyingine ina kitabu cha Mungu ambacho hakuna mtu

8

hata sasa ameweza kukiboresha. Cha mwisho ni cha kwanza na bora; hakijawahi kuwapo kama hicho na kamwe haitakuwapo. {2TG25: 8.4}

Shule ya Mungu haifundishi tu kutoka katika kitabu chake, sio tu katika chumba cha shule, fundisha utendaji vile vile na nadharia. Utendaji, kwa kweli, watu wengi hawapendi, na wengine hawawezi kuchukua mafunzo ya vitendo hata kwa zawadi. Hebu tumchukue Yusufu kwa mfano. Alipomaliza kazi ya chumba cha darasa alian-zishwa kwa ile ya utendaji. Mafunzo yake labda yalikuwa ya mtihani sana kwa sababu mwito wake haukuwa mmoja tu mkuu ila wa kipekee pia. Mbali na hilo, mtaala wake ulijumuisha kujifunza lugha ya kigeni na upendo kwa ajili ya maadui zake. Alipaswa kujifunza kwa uzoefu kwamba iwapo mtu humtumikia Mungu kwa uamini-fu, basi chochote kinachompata maishani ajue kwamba ni zawadi kutoka kwa Mungu, na kwamba anapaswa kukitumia inavyofaa. {2TG25: 9.1}

Kwanza kaka zake walimuuza, na akauzwa tena na wafanya biashara wa watumwa. Angaliweza kujifanya mgonjwa kwa majonzi na hofu. Kama angeshindwa kwa hisia zake, wafanya biashara wangalimwacha mahali fulani kwenye njia ya kuelekea Misri, kwa maana wangalikuwa wamejua kwamba mtu mgonjwa angekuwa tu gharama kwao, kwamba hawangaliweza kumuuza kwa ajili ya chochote kwa mtu yeyote. Yusufu, hata hivyo, alijiendesha vyema, akijua kwamba Mungu alifahamu yote kuhusu hali zake. Waishmaeli, pia, waliona kwamba walikuwa hawajawekeza kwa mtumwa wa kawaida. Waligundua kwamba angeuzwa kwa bei kubwa kwa mtu ambaye alikuwa na fedha. Hivyo ikawa kwamba wakampeleka kwa Potifa, mtu tajiri wa Misri. Hapo Yusufu alijifunza jinsi ya kutii maagizo, jinsi ya kutunza mali za watu wengine, na pia jinsi ya kuwaepuka wanawake wazinzi. {2TG25: 9.2}

Baada ya kuhitimu kutoka katika nyumba ya Potifa alichukua

9

kozi nyuma ya vyumba vya gereza. Humo miongoni mwa waota ndoto alijifunza kufasiri ndoto. Katika hatua hii ya mafunzo yake alipewa vifaa vya kutawala Misri na kuulisha ulimwengu. {2TG25: 9.3}

Shule za wanadamu hazipeani kozi za namna hii, wala pia huwa hazikuzi wafadhili wa watu, wafalme, wana-benki na wafanya biashara kama Yusufu. {2TG25: 10.1}

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo tunapaswa kujua iwapo sisi wenyewe tutaweza kuhitimu katika shule ya Mungu. Zaidi ya hayo, tunapaswa kujua ni kutoka wapi tunapokea mafunzo yetu, maana inawezekana kwamba tunaweza kuwa katika shule ya ubinafsi wakati tunafikiri kwa kimbelembele kwamba tuko katika shule ya Mun-gu. {2TG25: 10.2}

Je! Tunaweza kujua hakika ni katika shule gani tunapata mafunzo yetu? — Ili kuwa katika shule ya Mungu lazima tutembee na Mungu. Na tunawezaje kujua kwamba tunatembea na Mungu? — Nina hakika kwamba iwapo tutaenda sehemu ambazo Mungu hangeenda, na ikiwa tunafanya kazi mahali ambapo Mungu hangefanya kazi, basi badala ya kutembea na Mungu na kujifunza kutoka Kwake, tutakuwa tunatembea na Ibilisi na kupata mafunzo kutoka kwake. {2TG25: 10.3}

Je! Tunawezaje kujua kwamba kazi tunayofanya ni kazi ambayo Mungu angetaka tufanye? — Ni hakika kwamba Mungu hangeunda zana za kuua bila kujali malipo; ya kwamba Yeye hagaliweza kufanya kazi kwa kitu ambacho Ibilisi hufanyia kazi; wala Yeye hataweza kuingia katika ushirikiano na mtu ambaye hatembei na Mun-gu. {2TG25: 10.4}

Swali kwa kawaida huibuka, tunapaswa kuwafanyia watu kazi au tunapaswa kumfanyia Mungu kazi ili ku-pata riziki? Iwapo Mungu anayo kazi kwa ajili yako kufanya, basi huwezi kwenda kuwafanya wananadamu kazi na utarajie kupokea kibali cha Mungu. Lakini ikiwa Mungu hana kitu kwa ajili yako katika Karakana Yake,

10

kwa mfano, ni wazi kwamba Yeye atakuwa na kitu kwa ajili yako katika duka lisilochukiza la mtu mwingine. {2TG25: 10.5}

Wanafunzi katika shule ya Mungu hujifunza kutoka kwa kanuni na kwa nia moja tu ya lengo la kuuendeleza Ufalme wa Mungu, ilhali wanafunzi katika shule ya mwanadamu hujifunza kutoka kwa mtazamo wa pesa, haswa kutomsaidia mtu yeyote ila wao wenyewe, ambao sisi kama Wakristo hatuwezi kumudu kufanya iwapo tunatarajia kuwa yote Mungu angetaka tuweze kuwa. Mtu yeyote mwenye fikra pevu, ambaye anaangalia mam-bo kutoka kwa mtazamo wa Mungu, hawezi kuwa kitu chochote ila tunda kutoka kwa shule ya Mungu. {2TG25: 11.1}

11

ANDIKO LA SALA

“Zaeni Matunda”

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” uk. 60, aya mbili za kwanza: {2TG26: 12.1}

“Mungu hutusihi tujaze akili na mawazo makuu, mawazo safi. Yeye anayo shauku kwetu tutafakari juu ya up-endo Wake na rehema, tuichambue kazi Yake ya ajabu katika mpango mkubwa wa ukombozi. Basi ulio wazi na wazi zaidi utakuwa ufahamu wetu wa ukweli, wa upeo, mtakatifu, shauku yetu ya usafi wa moyo na uangavu wa mawazo. Nafsi inayokaa katika mazingira safi ya mawazo matakatifu itabadilishwa kwa ushirika pamoja na Mungu kupitia uchambuzi wa Maandiko. {2TG25: 12.2}

“’Na zaeni matunda.’ Wale ambao, baada ya kulisikia lile neno, hulitunza, watazaa matunda katika utiifu. Ne-no la Mungu, likipokelewa ndani ya nafsi, litadhihirika katika matendo mema. Matokeo yake yataonekana katika tabia na maisha kama ya Kristo. Kristo alinena juu Yake, ‘Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu Wangu, ndio furaha yangu; naam, Sheria Yako imo moyoni Mwangu.’ ‘Siyatafuti mapenzi yangu Mimi, bali mapenzi ya Baba Aliyenipeleka.’’ Na Maandiko yanasema, “Yeye asemaye kuwa anakaa ndani Yake imempasa kuenenda kama Yeye alivyoenenda.’” {2TG25: 12.3}

Je! Tutasali kwa ajili ya nini sasa? — Tuombe kwa ajili ya nguvu ili ituwezeshe kutafakari juu ya upendo na hu-ruma Yake na hivyo kusababisha ufahamu wetu wa Ukweli kuwa wa upeo na mtakatifu; tuombe ili tugundue kwamba nafsi ambayo inakaa katika anga la mawazo matakatifu hubadilishwa; tuombe ili tujifunze kwa uzoefu kwamba Neno la Mungu likipokelewa ndani ya nafsi, hujidhihirisha lenyewe katika matendo mema. {2TG25: 12.4}

12

USHINTO (IBADA YA SANAMU) NA UKRISTO USIOENDELEA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 7, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Andiko letu kwa ajili ya uchambuzi wa alasiri hii linapatikana katika– {2TG26: 13.1}

Yer. 10:23 — “Ee Bwana, najua kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.”

Katika aya hii tunaambiwa kwamba njia ambayo mwanadamu anapaswa kuenenda haimo katika nafsi yake, kwamba yeye mwenyewe hajui jinsi ya kuelekeza hatua zake. Mtu fulani mwingine lazima azielekeze ikiwa atakwenda katika mwelekeo sahihi. Kwa sababu hii haswa watu wa Mungu huongozwa na nabii na kuhifadhiwa na nabii. (Hos. 12:13.) Hivyo ilikuwa kwamba kupitia chombo cha manabii Mungu aliliongoza na kulihifadhi Kanisa la Agano la Kale, na kwa Roho yule yule Yeye alilianzisha, ameliongoza, na hadi siku ya leo amelihifad-hi Kanisa la Agano Jipya, ingawa roho ambayo iliasi uongozi wa Mungu zamani, bado i Kanisani leo. {2TG26: 13.2}

Kwa kawaida watu hawafahamu ukweli kwamba hawawezi kuelekeza hatua zao wenyewe hata baada ya Mungu kuwaanzisha kama baba anapoanza kumtembeza mtoto wake mdogo. Tusisahau kamwe kwamba watu wa Mungu wa zamani walipowakataa manabii, hata Yohana Mbatizaji, Yesu Kristo, na Mitume, wakati Hangeweza kuwaongoza tena, miguu yao iliteleza kila mwelekeo,

13

walianguka kutoka kwa neema na wakapoteza kila kitu. Wafuasi wa manabii pekee ndio walisaloia na Mungu na wao pekee ndio walijumuisha kanisa la Kikristo mwanzoni. Hakuna mwingine isipokuwa Mungu aliyezielekeza hatua zao kuingia ndani ya Kanisa. {2TG26: 13.3}

Hebu tuchukue mfano mwingine: Dunia kwa ujumla leo, isipokuwa wachache, ni Wabudha, Waislamu, au Wakristo. Theluthi mbili ya idadi ya watu duniani bado inafuata katika hatua za Buddha, aliyeishi karibu miaka 550 kabla ya Kristo. Fikiria hilo! Theluthi mbili, chini kidogo ya bilioni moja ya wakazi wa dunia bado ni wa-fuasi wa Buddha! {2TG26: 14.1}

Na Buddha alikuwa nani? Alikuwa mtu wa namna gani — mzuri au mbaya? Alikuwa mdanganyifu au alikuwa mwalimu wa haki? {2TG26: 14.2}

Ili kupata jibu, hebu kwanza tuzingatie namna ya watu ambao alikutana nao. Hakukutana na Waebrania, wala na Wakristo, ila tu na watu waliopotoka wa Mashariki. Na wale ambao hawakukutana na mafundisho ya Bud-dha, — wale wa visiwa vya bahari ya kusini haswa — kwa kiwango kikubwa bado ni wala-watu. {2TG26: 14.3}

Kuzingatia kweli hizi kabla ya kupitisha hukumu tunaweza kuhoji, Buddha aliwadanganya wafuasi wake vi-pi? — Hakuna ni jibu la jumla. Na aliwaongoza kuwa nini? Historia hutoa jibu hili; “Lile alilowafunza watu ni kwamba walipaswa kutafuta wokovu sio kwa kuadhimisha ibada na sherehe za kidini, bali kwa uaminifu na usafi wa moyo, kwa upendo na ukarimu na huruma kwa viumbe vyote vilivyo na uhai.” — “Historia ya Jumla,” uk. 66. {2TG26: 14.4}

14

Kwa sababu aina ya mafundisho ya Buddha hakika hayatoki kwa Ibilisi, na kwa sababu aliwaongoza wafuasi wake kutoka kwa ubaya kuwa bora, hangeweza kuwa mdanganyifu. Buddha, zaidi ya hayo, hakufundisha tu maadili mema, lakini, ikiwa historia ni ya kuaminika, yeye mwenyewe aliishi kulingana na yale alifundisha. Mwishowe, kwa kuambatana na mvuto wake mkubwa angaliweza kuwa mtu tajiri, lakini alikufa maskini. Na iwapo viwango vya kuishi vina wema wowote, viwango vya Buddha, iwapo vinazingatiwa, vingaliweza ku-wainua watu wa Mashariki kuliko kiwango cha wengi wanaojiita eti Wakristo katika siku yetu. {2TG26: 15.1}

Buddha kwa hivyo anaonekana alikuwa mhubiri wa haki katika siku yake, kwa maana kiwango chake cha ta-bia kilikuwa kiwango cha zile amri kumi, viwango vya Bibilia. Alipata wapi kiwango kama hicho? Hakika sio kutoka kwa Ibilisi. Tunaweza sasa kuuliza swali, Je! Mungu katika siku ya Buddha alipendezwa tu na taifa la Waebrania? Je! Aliipuuza kabisa sehemu nyingine ya dunia? Na je! Aliruhusu makusudi theluthi ya wakazi wa dunia kuongozwa na Buddha kutoka ubaya hadi ubaya zaidi? au Aliona kwamba waongozwe kutoka ubaya kuwa bora? {2TG26: 15.2}

Lipo tu jibu moja ambalo tunaweza kutoa kwa uaminifu na hekima: Kwamba Mungu kupitia Buddha ali-watendea wapagani yale ambayo yasingaliweza kufanywa kupitia Musa au kupitia manabii wa Kiebrania. {2TG26: 15.3}

Kusema kwa kulinganisha, Mungu kupitia Buddha aliwainua wapagani kutoka kwenye shimo ambamo walikuwa inchi nyingi juu, kama vile Musa alivyowainua Waebrania kutoka shimoni ambamo walikuwa. Wae-brania, bila shaka, waliinuka karibu sana na Mungu kuliko wafuasi wa Buddha kwa sababu shimo ambalo Bud-dha aliwapata wapagani lilikuwa la kina zaidi kuliko shimo ambalo Musa alilipata taifa la Waebrania. {2TG26: 15.4}

15

Buddha mwenyewe kamwe hakufikiria kwamba baada ya kifo chake angaliabudiwa kama mungu na wafuasi wake — la, sio zaidi kuliko manabii, mitume, na Mariamu, mama ya Yesu, walifikiri wangaliabudiwa baada ya kifo chao. {2TG26: 16.1}

Sasa unaweza kuona kwamba wakati Buddha alikuwa akielekeza hatua za watu wake, watu waliongozwa ka-ribu na viwango vya Bibilia na kwa maadili ya Kristo kuliko walivyokuwa kabla ya siku yake. Kwa sababu hii ni hivyo, basi Buddha hakuwa mdanganyifu. {2TG26: 16.2}

Mara tu Buddha alipokufa, hata hivyo, wafuasi wake walikimbia dhidi ya ukuta kwa mfano, na maendeleo yao kumwelekea Mungu, Bibilia, na Kristo, yakakoma pale ambapo Buddha aliachia. Kwa kweli wasingaliweza kuendelea zaidi kwa maana walifanya kifo cha Buddha kuwa kizuizi chao dhidi ya kuendelea kumwelekea Mungu. Je! Walifanyaje? — {2TG26: 16.3}

Ni ukweli unaojulikana kwamba wakati watu wanapeana sifa ya tendo la Uungu kwa kiumbe chenye kikomo, basi tumaini lao la mwingine mkuu, au mkuu zaidi kuja kuwasaidia linatoweka milele. Hawaamini kwamba Mungu yu hai, kwamba atamwinua mwingine hata mkuu kuwaongoza mbele, ila huamini kwamba hakuna hitaji la mwingine na hakuna hitaji la ukweli zaidi. Vivyo hivyo maadamu hawamtarajii mwingine, wakati ambapo mwingine anakuja wanamkataa. Hivyo Wabudha waliweka kikomo kwa maendeleo yao ya kiroho. Kwa hivyo unaona kwamba ile nuru iliyo ndani yako ikiwa giza, “Si giza kuu hilo?” Mat. 6:23. {2TG26: 16.4}

Kuhukumu kutoka kwa uzoefu wa zamani, uhuru wa taifa na risasi ya muuaji katili mwaka huu yana uweze-kano wa kuzalisha mungu mwingine — Mohandus K. Gandhi. Yeye inawezekana kuwa Buddha wa leo. Naam, mamilioni ya Wahindu tayari wanampa Bwana Gandhi

16

sifa kwa matendo yake yote mema na ya Kiungu. {2TG26: 16.5}

Yeye, kama Buddha, hakika alikuwa mtu mzuri, kwa viwango vya juu na maadili mema, viwango na maadili ya Bibilia na ya Yesu Kristo. {2TG26: 17.1}

Hili linatuleta kwa swali lingine ngumu la kujibu — Kwa sababu Gandhi aliishi katika enzi ya Ukristo kwa nini hakukuwa Mkristo? — Labda angalikuwa, lakini nadhani alizingatia kwamba kuwa Mkristo na kujiunga na kani-sa la Kikristo kungeshuka badala ya kuinua kiwango chake cha tabia. {2TG26: 17.2}

Alivyoiona, ilionekana kwake kwamba taifa linaloitwa eti la Kikristo lilikuwa linaimwaga damu ya watu wake, kwamba lilikuwa likiwanyanyasa na kuwatendea kama wanadamu duni. Kwa kweli, yeye mwenyewe, kwa msimamo wake juu ya adabu na uhuru wa kitaifa alitumia karibu miaka kumi na miwili gerezani. Haya ni mambo ambayo inawezekana yalimfanya Bwana Gandhi asijiunge na kanisa la Kikristo na watu. Yeye kwa kweli hakuupatia kisogo Ukristo ili aepuke dhabihu yoyote, au kujiingiza katika dhambi yoyote. {2TG26: 17.3}

Nadharia ya Gandhi, zaidi ya hayo, kwa ajili ya uhuru bila vurugu, bila upanga wala bunduki, ilifanikiwa na kuwaweka huru zaidi ya watu 400,000,000 ambao walikuwa watumwa kwa wenye nguvu kwa karibu miaka 200! Hili alifanikiwa wakati ambapo Wakristo walikuwa wakiuana kwa maelfu! Haya ndio baadhi ya mambo ambayo inawezekana yalimzuia Bwana Gandhi kuwa Mkristo. {2TG26: 17.4}

Hebu sasa kwa muda mfupi tumwangalie Mohammed, ambaye kitu kama watu 220,000,000 humsujudu. Alikuwa mtu wa namna gani? Alikuwa mdanganyifu? au alikuwa mwalimu wa haki? — Hebu pia tuangalie

17

watu ambao walifunzwa naye. Walikuwa wazawa wa Lutu na Abrahamu, — Wamoabu, Waesau, na Waishmaeli, nk., wote ni maadui wakali wa Waebrania, na dini yao. {2TG26: 17.5}

Kwa sababu Mohammed aliongoza mamilioni ya Waarabu karibu na dini ya Waebrania-Wakristo kuliko wanaojiita eti Wakristo katika siku yake wangaliweza kuwa wamewaongoza, ni vigumu kuwezekana kwamba alikuwa mdanganyifu. Aliwaongoza wafuasi wake kwa kiwango cha juu cha maisha, unyenyekevu, usafi, uka-waida wa kusali na lishe ya Bibilia kuliko Wakristo wa siku yake wangalivyokuwa wamewaongoza. Nadharia ya Mohammed ya dini kwa mujibu wa historia, na kama Uislamu ulivyo nayo sasa ni hii: {2TG26: 18.1}

“Uislamu, jina la kawaida katika nchi za Kikristo kwa dini iliyoanzishwa na Mohammed. Wafuasi wake huita imani yao Uislamu (utiifu kamili kwa amri za Mungu), na kanuni yao ya kawaida ya imani ni, “Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mohammed ndiye nabii wake.” Sehemu ya mafundisho au ya nadharia ya Uislamu hukumbatia kauli zifuatazo: — 1. Imani kwa Mungu, ambaye hana mwanzo au mwisho, Muumba pekee na Bwa-na wa ulimwengu, akiwa na nguvu kamili, maarifa, utukufu na ukamilifu. 2. Imani kwa malaika zake, ambao ni viumbe wanyoofu, walioumbwa kwa nuru. 3. Imani kwa Majini (pepo) wazuri na wabaya, ambao wameumbwa kwa moto usio na moshi, na wanaweza kufa. 4. Imani kwa Maandiko Matakatifu, ambayo ni neno lake lisiloumbwa lililofunuliwa kwa manabii. Kati ya hizi zipo sasa, lakini katika hati iliyopotoshwa sana, Torati, Zaburi, na Injili; na katika hali ambayo haijapotoshwa na isiyoweza kupotoshwa Korani, ambayo hutangua na kushinda mafunuo yote yaliyotangulia. (Angalia Kurani.) 5. Imani kwa manabii na mitume wa Mungu, ambao ni mashuhuri sana ni Adamu, Nuhu, Abrahamu, Musa, Yesu, na Mohammed. Mohammed

18

ndiye mkuu kuliko wote, na wa mwisho kwa manabii na aliye bora zaidi kwa viumbe vya Mungu. 6. Imani kwa ufufuo wa jumla na hukumu ya mwisho, na katika thawabu na adhabu za baadaye, haswa za asili ya mwili. 7. Imani, hata kwa kiwango cha kutisha, ya maarifa kamili ya Mungu ya kujua umbele na kuamua umbele matukio yote mema na mabaya.” — “Kamusi Elezo ya Karne ya Ishirini na Moja,” uk. 507. {2TG26: 18.2}

Kwa mtazamo wa ukweli kwamba Mohammed aliwaongoza watu wake karibu na dini ya biblia kuliko walivyokuwa zamani, je! kweli angeweza kuitwa mdanganyifu? Ikiwa ni hivyo, nambie aliwadanganya kuhusu nini? {2TG26: 19.1}

Kwa sababu Mohammed alikuwa karibu sana kuiamini dini ya Mkristo, tunaweza kuhoji, Je! kwa nini hakuwa Mkristo? — Wacha tuchunguze uwezekano ambao uliweza kumzuia kutofanya hivyo: {2TG26: 19.2}

Mohammed aliishi katika karne ya saba ya enzi ya Ukristo, katikati ya Vizazi vya Giza la dini, wakati ambapo kanisa la Kikristo lilikuwa limezama kabisa katika ibada ya sanamu, ufisadi na uzinzi, mazoea ambayo yameka-tazwa kwa Maandiko. Iwapo hakuna chochote kingine ambacho kingemzuia kujiunga na kanisa la Kikristo, basi ibada ya sanamu pamoja na ulaji ulioenea wa nyama ya nguruwe, zoezi ambalo ni dhidi ya dini yote ya Bibilia, yalitosha kumfanya Mohammed kuupiga Ukristo kisogo. {2TG26: 19.3}

Mohammed, naamini, alifanya vyema kabisa alivyoweza, kwa kuzingatia kwamba katika wakati wake kanisa linaloitwa eti kanisa la Kikristo lilikuwa limedhoofika sana, na ya kwamba maadili na tabia yake ilikuwa juu sana zaidi ya yalivyokuwa maadili na tabia ya wapagani waliofanywa kuwa Wakristo. Kwa kuyatazama haya yote, ni nani anayeweza kusema kwamba Mohammed alikuwa mtu mbaya, kwamba alikuwa mdanganyifu? {2TG26: 19.4}

19

Bado tunauliza kwa nini Mungu alimruhusu Mohammed kufundisha dini yake kwa mamilioni ya wakazi wa dunia? Na bado tunashangaa kwa nini hakuwa Mkristo? — Iwapo ni hivyo, hapa lipo jibu la pili: Mungu alimru-husu kwa sababu Mohammed alikuwa akiwafanya watu kuwa bora zaidi ya walivyokuwa, na kwa sababu Uis-lamu katika siku hiyo ulimleta mtu karibu na dini ya Bibilia kuliko ambavyo ungeweza Ukristo wa upagani. Lakini kwa nini Waislamu bado ni Waislamu? — Waislamu bado ni Waislamu, kwa sababu ile ile kwamba Wab-udha bado ni Wabudha; yaani, kwa sababu baada ya Mohammed kufa, walifanya tu jinsi Wabudha walivyofan-ya: Katika maendeleo ya dini Waislamu walisimama mahali ambapo Mohammed alikoma — kwa kaburi lake. Walisimama hapo ili kuhakikisha kwamba wafuasi wao hawatajiunga na dini nyingine. Waliwafunza watu kwamba hakutakuwa na nabii mwingine, kwamba Mohammed alikuwa wa mwisho, kwamba hakukuwa na hitaji la mwingine, kwamba walikuwa na Ukweli wote wa kuwaongoza kupitia malango ya lulu. Hivyo Uislamu uli-opotoka ulipekecha wazo hili la uongo katika akili za watu wa kawaida wakati huo, na bado Uislamu uliopotoka wa leo, kama madhehebu mengine yote, pamoja na Uadventista uliopotoka, bado hufanya vivyo hivyo. Hivyo ni kwamba hakuna dhehebu kama kundi, ila tu mtu mmoja-mmoja, limewahi kuupokea ujumbe wa ziada na hii ndio sababu ya ulimwengu wa madhehebu mengi. {2TG26: 20.1}

Kwa hivyo kuuliza ni kwa nini Waislamu na Wabudha bado ni Waislamu na Wabudha — kwa nini hawajaen-delea mbele tangu Mohammed na Buddha kufa, ni kama kuuliza kwa nini Wakatoliki bado hawajakuwa Walu-theri, kwa nini Walutheri bado hawajakuwa Waprestiberi, kwa nini Waprestiberi bado hawajakuwa Wameth-odisti?, kwa nini Wamethodisti bado hawajakuwa Wabaptisti, kwa nini Wabaptisti hawajakuwa Waadventista wa Sabato, na kwa nini Waadventista wa Sabato bado hawajakuwa

20

Wadaudi Waadventista wa Sabato? Jibu la jumla ni kwamba kila dhehebu lililofuata limeshindwa kuambatana na maendeleo ya Ukweli kwa sababu kila mmoja limeshindwa kupanda juu kuliko kimo cha mwasisi wa kila dhehebu husika angaliweza kuwa amewaongoza katika wakati wake wa maisha. {2TG26: 20.2}

Wayahudi hawakuinuka juu zaidi ya kimo ambacho Musa aliwaongoza. Musa alipokufa, wao kwa mfano walikufa pamoja naye hadi sasa kuhusiana na maendeleo ya kiroho. Hivyo ilikuwa kwamba waliwakataa na ku-waua manabii waliokuja baada ya Musa, bila kumsaza Mwana wa Mungu. {2TG26: 21.1}

Roho iyo hiyo ilishinda katika kanisa la Kikristo. Halikuinuka kamwe zaidi ya kiwango ambacho Mitume waliliacha, na kwa wakati hata lilianguka karibu chini kabisa shimoni. Na lingalianguka kabisa iwapo Mungu asingalikuwa amewajilia watu Wake ndani ya Luther, Knox, Wesley, Campbell na wana matengenezo wengine, ambao kupitia kwao Bwana alileta nuruni sehemu fulani za Ukweli wa Bibilia ambao kwa muda mrefu ulikuwa umekanyagiwa chini. Lakini je! Dunia ya Ukristo kwa ujumla iliiona Nuru? Na je! wote walitembea ndani Yake? La, hakika hapana, sio kama kundi, ila tu kama mtu mmoja-mmoja. Hii ndio sababu ya ulimwengu wa sasa wa madhehebu mengi; yaani, ilipohitajika Kristo kuanzisha kanisa jipya, la Kikristo, lililotengwa na kanisa mama, la Kiyahudi, katika siku Yake, jinsi hiyo wana matengenezo walijikuta wametupwa nje ya makanisa mama, na kwa hitaji walilazimika kuwapangilia wafuasi wa Ukweli unaoendelea kuwa dhehebu jipya, moja baada ya jingine. {2TG26: 21.2}

Katika nuru hii, unaiona roho ambayo huwadumisha Wayahudi kuwa bado Wayahudi, Wabudha kuwa bado Wabudha, Waislamu kuwa bado Waislamu, Wakatoliki kuwa bado Wakatoliki, Walutheri kuwa bado Walutheri.

21

Wamethodisti kuwa bado Wamethodisti, Wabaptisti kuwa bado Wabaptisti — roho iyo hiyo haswa leo inafanya kazi ndani ya dhehebu letu, la Waadventista wa Sabato, kwa kimbelembele wakiamini kwamba wao ni matajiri na wamejitajirisha, na hawana haja ya kitu chochote zaidi. Nalo, pia, linafikiria kwamba mwasisi wake aliyekufa alikuwa wa mwisho katika safu ya manabii, kwamba hakuna hitaji la mwingine. Linajihisi hakika kwamba nuru na kawi katika meli yake, Zayuni, inatosha kulipeleka hadi pwani ya Ufalme, ingawa wanajua vyema kwamba ujumbe wao, Hukumu ya Wafu sio wa mwisho, lakini kwamba Hukumu kwa Walio Hai, ambao bado hawana, ndio wa mwisho! Roho hii ya kukengeuka badala ya kwenda mbele, ya kupinga ukuaji wa kiroho, na kwa wa-kati uo huo kukuza roho ya uvuguvugu, inafanya kazi kwa mafanikio kwa wengi licha ya ukweli kwamba unabii wa Bibilia ambao huelekeza kwa siku yetu, kwa wao bado ni mafumbo. Hawajali kuujua. {2TG26: 21.3}

Ipo kwa hivyo kazi kubwa inayopaswa kufanywa, sio tu kwa mataifa yote, jamaa, lugha, na watu, bali kwa Kanisa lenyewe, iwapo yeyote ataokolewa kutoka kwa maangamizi yanayokuja. Kwa mujibu wa unabii wa Yeremia, Ukristo uliopotoka sio kitu kipungufu kwa mtindo wa Ushinto: {2TG26: 22.1}

Yer. 10:1-5 — “Enyi nyumba ya Israeli, lisikieni neno awaambialo Bwana; Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo. Maana desturi za watu hao ni ubatili, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka. Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike. Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi

22

kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.”

Mti wa Krismasi unaotumiwa sana, tarehe 25 Desemba — mti uliokatwa kutoka kwa chanzo chake cha uzima na kukazwa kwa misumari — hauwakilishi kuzaliwa, ila badala yake kifo cha mmoja na juhudi isiyo na maana ya kumfanya aishi. Kwa kuukata mti, kwa wapagani ulimwakilisha mkuu wao aliyekufa, na kwa kuuegemeza, uli-wakilisha uhai ingawa mtu alikuwa amekufa. Sasa ukweli kwamba mti bandia wa Krismasi husherehekewa sana sio tu na Wakristo, ila pia na wasio Wakristo, ulimwengu kwa tendo hili unawabudu wafu, aina ya Ushinto. Kuabudu manabii waliokufa na kuwaua walio hai, ni juhudi ya kikatili ya kuzuia maendeleo ya Ukweli, kujidanganya mwenyewe na wengine. {2TG26: 23.1}

Mwishowe, laiti usingalikuwa kwa ajili ya ukweli kwamba baadhi fulani walio macho kabisa katika vizazi vyote wamethubutu kuubeba msalaba wao na kumfuata Mungu kupitia kwa manabii Wake ili kuongozwa kuto-ka kwa kimo kimoja cha Ukweli hadi kwa kingine, dunia isingalikuwapo muda huu mrefu. {2TG26: 23.2}

Hamna shaka, Kanisa tangu uumbaji hadi leo limeongozwa na kuhifadhiwa na manabii, na haliwezi kuendelea kwa njia nyingine kutoka hapa kwendelea. {2TG26: 23.3}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutum-wa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchap-ishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG26: 23,4}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 25, 26

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>