fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 42, 43

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 42, 43

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

THAWABU YA ZAYUNI JITIHADA KUBWA ZA MUNGU

MWAKA WA WALIOKOMBOLEWA WAKE — ISHARA YA SIKU YA KISASI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Tumaini Letu Pekee La Kushinda

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa 205, aya ya mwisho: {1TG42: 2.1}

“Tumaini la pekee kwa ajili yetu ikiwa tutaweza kushinda ni kuziunganisha nia zetu kwa mapenzi ya Mungu, na kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja Naye, saa kwa saa, na siku kwa siku. Hatuwezi kuidumisha nafsi, na tena tuingie katika ufalme wa Mungu. Ikiwa tutawahi kuufikia utakatifu, itakuwa kupitia kujikana nafsi, na kuipokea nia ya Kristo. Kiburi na majivuno lazima visulubishwe. Je! Tuko tayari kulipa gharama inayohitajika kutoka kwetu? Je! Tuko tayari kumakinika nia zetu ziletwe katika upatano mkamilifu kwa mapenzi ya Mungu? Mpaka tuwe tayari, neema ya Mungu inayobadilisha haiwezi kudhihirika juu yetu.” {1TG42: 2.2}

Sasa tupige magoti na kuomba kwa ajili ya ufahamu kwamba tumaini letu la kuwa na makao katika Ufalme wa Mungu linategemea kuziunganisha nia zetu na mapenzi Yake, na juu ya kutenda kazi kwa kushirikiana Naye; kwamba utakatifu hutegemea kujikana nafsi na kumpokea Kristo; kwamba kiburi hakina nafasi katika moyo wa Mkristo; kwamba mabadiliko ya neema ya Mungu hupatikana kwa kuishi kwetu kulingana na Neno Lake. {1TG42: 2.3}

2

THAWABU YA ZAYUNI JITIHADA KUBWA ZA MUNGU

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MEI 24, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutaichambua sura ya sitini na mbili ya Isaya. Mambo ya kwanza hasa ambayo tunahitajika kujua kui-husu sura hii ni ikiwa iliandikwa haswa kwa ajili ya watu wa leo au haswa kwa ajili ya watu wa jana, na ikiwa ujumbe wake utaelekezwa kwa kanisa au kwa ulimwengu. Ili kujua tutasoma aya ya kumi na moja: {1TG42: 3.1}

“Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele Yake.” Isa. 62:11. {1TG42: 3.2}

“Tazama,” asema Bwana, “nimetangaza mpaka mwisho wa dunia,” sio kwa wakati mwingine wowote. Utangazaji huu wa Kiungu, kwa hivyo, ni kwa ajili ya wale wanaoishi katika wakati wa mwisho. Kwa wao sura hii sasa imefunuliwa, na utume wao ni kuupeleka kwa binti Zayuni, kwa kanisa. Huwezi kwa hivyo, kumudu kutoa udhuru kutoka kwa mwito huu kwa ajili ya huduma. {1TG42: 3.3}

Aya ya 1 — “Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itaka-potokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.”

3

Hapa tunaambiwa kuwa Bwana ataendelea kusema hivyo, sio kwa ajili ya ulimwengu, bali kwa ajili ya kanisa ili mwishowe lisimame juu ya Mlima Zayuni na Mwana-kondoo; kwamba ataendelea “mpaka haki yake itaka-potokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.” {1TG42: 4.1}

Hii inamaanisha kuwa haki ya watu Wake katika kuitangaza sura hii ni hafifu tu, asaa kwa vyovyote, inaenda mbele, na kwamba “wokovu wake” sasa sio kama taa inayowaka, lakini kama taa ambayo nuru yake imezimimi-ka. Juhudi Yake kubwa hata hivyo ni kuleta badiliko kubwa: Haki ya Kristo itaangaza kwa uangavu kama jua. Hitimisho basi ni kwamba bila ujumbe huu wa ziada kanisa kamwe halitaweza kufikia lengo lake, na mtazamo wa kutojali wa mtu yeyote katika mwito huu wa dharura kwa ajili ya huduma ni hakika utaleta maangamizi yake. Watu wa kweli wa Mungu, hata hivyo, wataamka na kuukumbatia mwito huu. Kwa wao, kama kanisa, asema Bwana: {1TG42: 4.2}

Aya ya 2 — “Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.”

Haki ya Zayuni itatamkwa hivyo kwamba Mataifa watavutiwa nayo, na wafalme wao wote kwa utukufu wake. Ni kwa sababu hii haswa kwamba jina la kanisa la sasa halitafaa kwa wakati huo. {1TG42: 4.3}

Kama unavyojua, sasa yapo mamia ya majina ya kanisa duniani, — majina mengi kama zilivyo dhana, zote amba-zo zimetajwa na kinywa cha wanadamu, ingawa Mungu hutambua tu kanisa moja. Mengi ya majina hata hupen-dekeza ushindani wa Kiungu. Kwa mfano, majina kama, “Kanisa la Kristo,” na “Kanisa

4

la Mungu,” hayamfanyi Kristo na Mungu kuwa washindani? {1TG42: 4.4}

Liwalo “jina jipya” lolote, litafaa kanisa kwa haki yake kama linavyoonyeshwa hapa. {1TG42: 5.1}

Sasa tunaishi katika dunia iliyochanganyikiwa. Baadhi ni wa Paulo na baadhi ni wa Apolo, wa Kefa, Petro, Yo-hana, na Yakobo, wengine wa Mungu na wengine wa Kristo. Wakristo wanabishana na kugombana wenyewe kwa wenyewe, mmoja akinena dhidi ya imani ya mwingine, na wakati huo huo wote wanajaribu kuwaongoa kwa Kristo ulimwengu usio wa Ukristo! Giza kama nini! Kwa kanisa, ambalo Mungu analiumba sasa, Yeye husema: {1TG42: 5.2}

Aya ya 3 — “Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.”

Kanisa lililoonyeshwa hapa litafanyizwa tu na watu wema wanaoongozwa na roho, jina lake jipya bila shaka litaonyesha ukweli huu. Ajabu, kweli kweli, kuwa “taji ya utukufu” ya Bwana, na Yake “taji ya kifalme.” Huwe-zi kwa hakika kumudu utukufu huu uponyoke kutoka kwako. Tenda leo. {1TG42: 4

Aya ya 4 — “Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa.”

Kwa sababu Bwana atapendezwa ndani yake, na pia kwa sababu nchi yake itaolewa kwalo, pia litaitwa Hefziba, na nchi yake Beula. Kanisa, nyakati za kale, limeachwa mara kadhaa — mara moja huko Misri, kisha Babeli, kati-ka Rumi, na kadhalika — lakini halitaachwa tena kamwe, na

5

nchi yake haitaachwa tena kamwe kuwa ukiwa. {1TG42: 5.4}

Aya ya 5 — “Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.”

Ndoa huashiria muungano wa milele. Kwa hivyo kanisa lina ahadi kwamba nchi yake sasa itakuwa yake milele, na wanawe (waongofu) hawatatengana nalo. {1TG42: 6.1}

Aya ya 6, 7 — “Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufan-ya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.”

Sio kwamba Ataweka, lakini kwamba tayari Yeye amewaweka walinzi ambao kamwe hawataupuuza wajibu wao usiku au mchana. Na kwa hivyo ninyi mnaomtaja Bwana sasa hampaswi kunyamaza, lakini mumtukuze Yeye na mzungumze juu ya upendo Wake wa ajabu na Ukweli. Sasa ni fursa yako ya kuiendeleza kazi Yake, kuifanya iwe shughuli yako kuu, maslahi yako makuu, furaha yako ya upeo. Sasa ni wakati wa kusema, “Ee Ye-rusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. Ulimi wangu na ugandamane na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.” Zaburi 137: 5, 6. Kufikia hapa omba na ufanye kazi. Usimpe Yeye pumziko mpaka Atakapoufanya Yerusalemu kuwa sifa “duni-ani.” Ruhusu upendezwe na hili jinsi ulivyo upendezi Wake. {1TG42: 6.2}

Aya ya 8, 9 — “Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sita-wapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uli-yoifanyia kazi.

6

Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.”

Watu wa Mungu wamenyang’anywa mara nyingi, na unyang’anyi uliokithiri zaidi na wa udhalimu ambao ume-waathiri umekuwa, na bado unafanywa na ndugu zao katika imani! Vipi? — Kwenye kila hatua ya juu katika Ukweli kote katika historia ya kanisa hadi siku ya leo, wale ambao wamewahi kuzikumbatia kweli mpya, zisizo maarufu, kwa kila tukio wametupwa nje ya kanisa ambalo walisaidia kujenga. Hili limefanywa tu kwa sababu kwa upande mmoja wengi wametawala daima, na kwa upande mwingine ni wachache tu ambao wamewahi ku-wa wepesi kuuona Ukweli wa sasa, kwa “chakula kwa wakati wake.” Wakati umefika, hata hivyo, ambapo kila namna ya unyang’anyi itakoma. Kwa wale ambao wanatupwa nje, shauri hili la kutia moyo na ahadi limetolewa: {1TG42: 7.1}

“Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini wa-tatahayarika.” Isa. 66: 5. {1TG42: 7.2}

Aya ya 10 — “Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.”

Bwana sasa anauliza kwa kurudia-rudia kila mtu ndani ya usikivu wa Sauti Yake apite kwa ujasiri kwenye malango ya Zayuni na kumwambia, “Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele Yake.” {1TG42: 7.3}

7

Sisi kwa hivyo hatuwezi kufanya vinginevyo ila kupita kati, kwa maana ni jukumu letu tulilopewa na Mungu kuiandaa njia kwa ajili ya watu. Lazima tuijenge barabara kuu, njia kwa ajili yao waililie nuru ya Mungu na hivyo kwa Ufalme Wake. Lazima tuondoe kila kizuizi ambacho kimesimama njiani, na lazima tuinue kiwango kwa ajili ya watu, kiwango ambacho wanaweza kuona na kufuata kinapoongoza. Kiwango kinaweza kuwa nini? — Kiwango haswa ambacho watu wanapaswa kukiona na kukifuata ni Yesu katika Kweli Yake. {1TG42: 8.1}

Aya ya 11 — “Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele Yake.”

Aya hii, kama tulivyojifunza mwanzoni mwa uchambuzi wetu, inatatua mambo mawili: Kwanza, kwamba sura hii hakika inasheheni ujumbe kwa kanisa katika mwisho wa dunia; pili, kwamba kwa sababu inathibitisha kwamba sura hii sasa kwa mara ya kwanza inafunuliwa na kuletwa kwa umakini wetu, tumetumwa na ujumbe kwa kanisa, na hakika inaonyesha kwamba tumefika kwa wakati wa mwisho, katika wakati ambapo taasisi zilizoundwa na mwanadamu zitatoweka milele. {1TG42: 8.2}

Neno “tazama” linadokeza kwamba sasa tunapaswa kutambua na kuweza kuona kwamba wokovu wetu unakuja na kwamba wakati thawabu Yake i pamoja Naye, kazi Yake bado i mbele Yake. Malipo yake ni nini? — Je! Ni nini kingine kinachoweza kuwa ila uzima wa milele? Ndivyo itakavyokuwa kwamba malimbuko, watu 144,000, watumwa wa Mungu ambao watasimama hivi karibuni kwenye Mlima Zayuni na Mwana-kondoo ndio wa-takaokuwa wa kwanza kutunukiwa. Kama watumwa wa Mungu wao wataiendeleza kazi iliyo “mbele Yake,” kazi ya kuwakusanya mavuno ya pili. Kama ilivyoelezwa na nabii Isaya: {1TG42: 8.3}

8

“Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utu-kufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli wale-tavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:19, 20. Chaguo sasa ni lako, ama kuambat-ana na Ukweli wa Mungu kwa wakati huu, kuupokea wokovu Wake na kujiandaa kwa kazi iliyo mbele Yake, ya kuwakusanya watakatifu Wake, au kubaki umejitenga na kutapikwa nje. {1TG42: 9.1}

Hebu tufanye chaguo bora sasa tusije tukajikuta katika giza la nje, huko kulia na kusaga meno yetu. {1TG42: 9.2}

Aya ya 12 — “Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa, Aliyetafut-wa, Mji usioachwa.”

Ukitenda yote ambayo Roho wa Mungu hukuamuru kufanya, utakuwa wa “watu watakatifu, waliokombolewa na Bwana,” “waliotafutwa,” “wasioachwa.” {1TG42: 9.3}

Na sasa kufanya muhtasari: Somo hufungua kwa maneno, “Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,’ kwa kanisa la leo. Litakuwa “taji ya utukufu” ya Bwana na Chake “kilemba cha kifalme.” Halitaitwa tena “Ulieachwa,” wala nchi yake haitaitwa “Ukiwa;” kwamba majina haya yatabadilishwa mtawalia kwa Hefzi-ba na

9

Beula, yakimaanisha Mungu atapendezwa na watu Wake na nchi yao; kwamba Mungu atajifurahisha juu ya ka-nisa Lake kama vile bwana arusi anavyomfurahia bibi arusi Wake; kwamba Yeye sasa amewaweka walinzi kwenye kuta za Yerusalemu, ambao hawataupuuza wajibu wao; kwamba hawatanyamaza, ila watamsifu Bwana, na kuwa na bidii ya kufanya kila wawezalo kuuendeleza Ufalme Wake; ya kwamba Yeye ameapa kwa mkono Wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu Zake, kwamba hatawapatia adui chakula cha watoto Wake, kwamba wageni hawatawanyang’anya tena kile ambacho wamekifanyia kazi, kwamba kile watakachozalisha hakika kitakuwa chao wenyewe; kwamba watu Wake wamenyang’anywa mara nyingi nuru yao ya kiroho; kwamba wa-kati nuru ya Mungu ilipowajia, maadui waliizuilia nuru hiyo mbali nao angalau kwa muda; kwamba sasa tume-himizwa “kulisikia Neno la Bwana,” kwa maana ndilo huwasababisha ndugu (washiriki wa kanisa wenzi wetu) kutuchukia ili watutupe nje kutoka kati yao. Wao hufanya hili kwa jina la Bwana, lakini “watatahayarika” wakati Yeye atakapoonekana kwa furaha yetu na kwa aibu yao; kwamba tumeamuriwa kupita kati ya malango ya La-odekia na kuiandaa njia kwa ajili ya watu; kuweka barabara kuu, kuondoa vizuizi, kuinua kiwango kwa ajili ya watu, kuwaonyesha kwamba Bwana “ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,” kumwambia “binti Zayuni” kwamba wokovu wake unakuja, kwamba thawabu Yake i pamoja Naye, na kazi Yake i mbele Yake; kwamba wale watakaokoka mchinjo wa Bwana watatumwa kwa mataifa yote na katika visiwa vya bahari, kwa watu am-bao hawajasikia kumhusu Mwokozi; kwamba watawaleta ndugu zao katika nyumba ya Bwana. {1TG42: 9.4}

Bila shaka sasa unaona thawabu ya Zayuni na jitihada kubwa za Mungu kukujulisha kuhusu Ukweli huu. Wewe hakika utafanya yote uwezavyo kuepuka kisasi cha Mungu na kujiunga na vuguvugu hili la walei kwa ajili ya kuwakusanya watu. {1TG42: 10.1}

10

MWAKA WA WALIOKOMBOLEWA WAKE — ISHARA YA SIKU YA KISASI
Isaya 63

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MEI 31, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Tunaichambua sura ya sitini na tatu ya Isaya. Katika sura hii tunayapata mazungumzo ya kinabii kati ya watu watatu: nabii, Bwana, na mtu anayeishi wakati ambapo unabii wa sura hii unatimizwa. Masomo ya mazungumzo ni Edomu, Israeli ya kale, ukombozi wao kutoka Misri, na ukombozi wa watu katika siku ambayo andiko hili linatimizwa. Sehemu ambayo inapaswa kututia fikira sana ni kuujua wakati. Ili kupata habari hii, nitasoma aya ya 16. “Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.” Isa. 63:16 {1TG43: 11.1}

Maneno ya mtu anayenena kwa niaba ya watu wanaoletwa uso kwa uso na ufunuo wa sura hii, yanafichua kwamba yeye na watu wake hawajulikani kwa Abrahamu. Kwa kuwa Abrahamu alijua vizuri juu ya kuinuka kwa Israeli ya kale, lakini hakuelewa chochote kwa kweli kuhusu kuinuka kwa Wakristo, basi Wakristo lazima wawe ndio watu ambao yeye hawajui. Ukweli, basi, unadhihirika wazi kuwa sura hiyo inapata utimizo wake katika enzi ya Ukristo. Sasa kupata ikiwa inawahusu Wakristo wa mapema au wa siku za mwisho

11

tutasoma aya ya 18 na 19; pia Isaya 64:10, 11, kwa ajili ya mada ya sura ya 64 ni endelezo la sura ya 63: {1TG43: 11.2}

“Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako. Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.” Isa. 63:18, 19. {1TG43: 12.1}

“Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa. Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika.” Isa. 64:10, 11. {1TG43: 12.2}

Hapa inaonekana kwamba hamu ya watu ni kwa ajili ya urejesho wa hekalu, na kwa ajili ya kumiliki kwao tena nchi ya ahadi. Sasa ukweli kwamba “hekalu” na “nchi” bado ziko mikononi mwa Waarabu na Wayahudi wasi-oamini (wale ambao kamwe hawakuitwa kwa jina Lake, hawaitwi kamwe Wakristo) ni uthibitisho mzuri kwam-ba sura ya 63 na 64 zinatimizwa katika sehemu ya mwisho ya enzi ya Ukristo, katika sehemu ambayo nyakati za Mataifa katika nchi ya ahadi zitakapotimia. Zaidi ya hayo, kwamba sura hizi zimefunuliwa sasa kwetu, na pia ukweli kwamba ujumbe wa leo umesababisha tumlilie Bwana kwa ukombozi kama huo, kweli ni kwamba wakati wa kutimizwa kwa unabii ulio katika sura hizi tayari upo hapa. {1TG43: 12.3}

Kwa sababu sasa unajua wazi kwamba sura hizi zinakuhusu wewe na mimi, tuko tayari kuanza kuzichambua su-ra hizo, aya kwa aya — {1TG43: 12.4}

Isa. 63: 1 — “Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari,

12

Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Mimi ninenaye katika haki, hodari kuokoa”

Katika maono nabii alimwona mtu fulani aliye na mavazi ya kutiwa damu akirudi upesi kutoka Edomu na Bozra. Kwa swali la nabii, “Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra?” Likaja jibu, “Mimi ninenaye katika haki, hodari kuokoa.” {1TG43: 13.1}

Je! Anaweza kuwa nani mwingine ila Bwana Mwenyewe, Mwokozi wa ulimwengu, Mwenye Uwezo wa kuo-koa? {1TG43: 13.2}

Tena nabii akauliza, {1TG43: 13.3}

Aya ya 2 — “Je! Kwa nini mavazi yako yamekuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?”

Jibu kwa maswali haya hujuza mfululizo wa matukio muhimu, matukio yaliyorekodiwa katika {1TG43: 13.4}

Aya ya 3-5 — “Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, Nitawakanyaga kwa hasira Yangu, Nitawaponda kwa ghadhabu Yangu; Na mavazi Yangu yatatiwa madoa kwa damu yao, Nami nitazichafua nguo Zangu zote. Maana siku ya kisasi i moyoni Mwangu, na mwaka wa waliokombolewa Wangu umewadia. Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Ni-kashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.”

Taarifa hizo, “Nalikanyaga shinikizoni peke yangu,” “Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;

13

Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza” (zote katika kitenzi cha wakati uliopita) zinaonyesha bidii na azimio la Mwokozi kuwaokoa watu Wake waliopotoshwa katika ujio Wake wa kwanza, ingawa hakuwapo mtu pamoja Naye kumsaidia; Yaani, makuhani na viongozi wote wa kidini – Baraza Kuu la siku Yake (Sanhed-rini) walikuwa dhidi Yake badala ya kumsaidia katika kazi Yake. Ila taarifa, “Naam, Nitawakanyaga kwa hasira Yangu, Nitawaponda kwa ghadhabu Yangu; Na mavazi Yangu yatatiwa madoa kwa damu yao, Nami nitazi-chafua nguo Zangu zote. Maana siku ya kisasi i moyoni Mwangu, na mwaka wa waliokombolewa Wangu ume-wadia”; na “Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono Wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu Yangu ndiyo iliyonitegemeza” (zote katika kitenzi cha wakati ujao) — zinaonyesha hali ya kanisa la sasa sio tu sawa kama wakati wa ujio Wake mara ya kwanza, ila ni mbaya hata zaidi. Ni kweli namna gani kwamba historia hujirudia! Maadamu siku ya kisasi inajongea, wale wanaotakiwa kutegemeza na kusaidia katika kazi ya ukombozi, wachungaji na viongozi wa dini, Sanhedrini ya leo (Baraza Kuu), wanaonekana wakiizuia, wakisimama katika njia Yake ya kuwafikia watu. Hivyo wanajiletea kutopendezwa Kwake, na kwa lazima anajifunga Mwenyewe ili aweze kuwaokoa watu Wake kutoka mikononi mwa wachungaji wasio waaminifu. Wanamsababisha kuyatia mavazi yake madoa ya damu yao Yeye an-apowakanyaga kwa ghadhabu Yake. {1TG43: 13.5}

Aya ya 6 — “Nitazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, Nitawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nitaimwaga damu yao chini.”

Maelezo mafupi ya Bwana juu ya hali hiyo yanapaazwa-sauti na nabii Ezekieli. Yeye Anasema: {1TG43: 14.1}

“Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na silaha yake ya kufisha

14

mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana silaha yake ya kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka ki-zingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya wa-tu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Ezek. 9: 1-6. {1TG43: 14.2}

Unabii wa Ezekieli unafichua wazi kwamba kazi hii ya utakaso itatukia kanisani (ndani ya Yerusalemu), katika wakati wa kuwatenganisha wasio waaminifu kutoka kwa waaminifu, wakati wa kuyaangamiza “magugu” (Mat. 13:30), kuwatupa nje samaki wabaya (Mat. 13: 47-49), ili kulitakasa kanisa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80), kuutakasa ukasisi (Mal. 3: 1-3); kupatakasa patakatifu (Dan. 8: 14) — kazi ya Hukumu kwa walio Hai. Roho ya Unabii katika siku zetu inayo haya kusema: {1TG43: 15.1}

“… Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa kasi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wa kweli. Kati-ka kupepetwa kukuu kutakakotukia hivi karibuni, tutaweza kuipima nguvu ya Israeli. {1TG43: 15.2}

15

Ishara zinaonyesha kwamba wakati umekaribia ambapo Bwana ataonyesha kuwa pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha uwanda wake kabisa …. {1TG43: 16.1}

“Hapa tunaona kwamba kanisa — patakatifu pa Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapatia nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao. Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wazi wa nguvu ya Mungu kama siku za kale. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwatembelea watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kelele kutoka kwa watu ambao hawatatoa sauti tena kama tarumbeta kuwaonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Hawa mbwa bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi kisasi cha haki cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wasichana, na watoto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80, 211. {1TG43: 16.2}

Na mtume Petro anaongezea: “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?” 1 Pet. 4:17, 18. {1TG43: 16.3}

Kwa sababu watu wa Mungu wa leo hawako katika nchi ya Edomu, kusini mwa Palestina, ila wametawanyika kote duniani, na kwa kuwa Bwana atawaua maadui zao ili awaweke huru, ukweli ni dhahiri: Hizi ni za uakisi Edomu na Bozra. {1TG43: 16.4}

Baada ya Esau wa zamani kuuza haki yake ya kuzaliwa kwa mchuzi wa

16

ndengu aliitwa Edomu; na jina Bozra linamaanisha “zizi la kondoo.” Ni wazi, basi, Waedomu wa Isaya 63: 1 ni wale ambao katika siku yetu wameiuza haki yao ya kuzaliwa, na ambao kwa wakati huo huo wanawatesa (kama alivyofanya Esau kumtesa Yakobo) wale ambao wameinunua, kwa mfano. Kwa hivyo ni kwamba vile watu wa Mungu walipaswa kuokolewa kutoka Sanhedrini katika siku za Kristo, lazima sasa waokolewe kutoka kwa Ba-raza Kuu, wa uakisi ndugu Waedomu, ili waweze kuongozwa katika Kweli yote, na kuingia katika nchi ya baba zao. {1TG43: 16.5}

Maneno, “mwaka wa waliokombolewa Wangu umefika,” na “siku ya kisasi i ndani ya moyo Wangu,” yanasema wazi kwamba kazi ya kushangaza ya Bwana katika Edomu na Bozra ni siku ya kisasi na ishara ya Israeli wa uak-isi (kanisa lililotakaswa) kurejea nchini kwao. {1TG43: 17.1}

Aya ya 7-10 — “Nitautaja wema wa Bwana, sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maa-na alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakom-boa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho wake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.”

Ushuhuda wa mtu huyu unafichua kwamba mabadiliko kamili yamefanyika ndani yake, kwamba amepata maono ya wema wa Bwana, ya uvumilivu Wake na huruma Yake — ameshawishika

17

kwamba Bwana hatamwacha huru mwenye hatia. Kutoka kwa ushuhuda wake inaonekana pia kwamba Bwana sio mtu mkatili, wa unyama, anayetafuta kuua na kuharibu, ila kwamba Yeye ni mkarimu na mwenye rehema, mvumilivu na mwenye haki, kwamba Anastahili kusifiwa. Mtu huyu anajaribu kudhibitisha hili kwa wengine kwa kutaja jinsi Mungu alivyoshughulika na watu Wake wa zamani, kuonyesha kwamba aliwavumilia kwa muda mrefu, kwamba kwa ajili ya faida yao wenyewe Aliwaadhibu — ili awarudishe Kwake, mbali na ibada ya sana-mu na uharibifu wa milele. {1TG43: 17.2}

Zaidi ya hayo, maandiko yanaonyesha wazi kuwa hitaji la ukombozi leo ni sawa na lile la siku ya Musa. {1TG43: 18.1}

Aya ya 11-15 — “Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Ali-yeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasi-jikwae? Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu. Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zime-zuiliwa kwangu.”

Kwa sababu katika unabii kiko kilio cha kuokolewa kama ilivyoonekana katika wakati wa Musa, kweli ziko dhahiri: Kanisa limeelekezwa kuingia utumwani na sasa linahitaji kuokolewa. Miaka iliyopita Uvuvio ulionya umbele: {1TG43: 18.2}

18

“Kanisa limegeuka nyuma na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na aste aste linarudi kuelekea Misri. Hata sasa wachache wameshtuka au kushangaa kwa kutaka nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekuwa ikiangaza kutoka kwa neno lake na katika Shuhuda, na zote mbili zime-dunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 217. {1TG43: 19.1}

Aya ya 16, 17 — “Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. Ee Bwana, mbona umetu-kosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.”

Watu wanaoulilia ukombozi ni wale ambao Abrahamu hakuwajua, na ambao Israeli wa leo (Dhehebu) haliwa-tambui. Yaani, kama ilivyoonyeshwa mwanzoni mwa somo letu, Abrahamu hakuwajua Wakristo, na watu wanaoulilia ukombozi katika utimilifu wa unabii huu hawatambuliwi na Waisraeli wa uakisi (Dhehebu), hivyo. Kwa hivyo ni kwamba ingawa Abrahamu wa zamani hatujui, na ingawa Dhehebu halitutambui, bado tunajua kwamba Mungu ametukabidhi ujumbe, na ya kuwa badiliko limetukia ndani yetu: kwamba hatuendelei kuwa walioridhika, wavuguvugu, na kwamba hatufahamu kuuhusu Ulaodekia wetu, unyonge, mashaka, umasikini,

19

upofu, na uchi. Tunajua kuwa hii ni kazi ya Mungu mioyoni mwetu, kwamba kweli “tunazaliwa mara ya pili,” kuzaliwa kupitia kwa Roho Mtakatifu — kwamba sasa ni Waadventista wa Sabato bora kuliko vile tulivyokuwa awali. Tunaweza, kwa hivyo, kwa ujasiri kusema: Bila shaka Wewe ni Baba yetu, Mkombozi wetu, jina Lako ni la milele, ingawa tunaambiwa na ndugu zetu daima kwa dhihaka, “Hapana, ninyi sio Waadventista wa Sabato.” {1TG43: 19.2}

Aya ya 18, 19 — “Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga pata-katifu pako. Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.”

Kweli, babu zetu walikuwa katika nchi na walifurahia ibada ya patakatifu kwa miaka kadhaa, lakini kwa kuzingatia kwamba wangeimiliki milele, basi taarifa, “Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu,” kwa ujumla ni kweli. Waarabu na Wayahudi ambao hawajaongoka sasa wanaoimiliki nchi sio Wakristo; hawaitwi kwa jina la Kristo, na kamwe hawajawahi kuwa. {1TG43: 20.1}

Aya ya 17 — “Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tus-ikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.”

Hapa yupo mmoja ambaye hutambua kwamba watu wa Mungu wako katika makosa — hawazifuati njia za Mun-gu na kwamba hawamchi Yeye. Rai ya mjumbe ni, kwa hivyo, kwa Mungu awarudie tena, asiwaache milele. {1TG43: 20.2}

Ombi la sura ya sitini na tatu huendelea

20

kote katika sura ya sitini na nne, na hutoa mfano mzuri wa namna maombi yetu yanapaswa kuuhusu wakati huu. Hebu tuisome yote. {1TG43: 20.3}

Isa. 64 — “Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima iteteme mbele zako; kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele yako.”

“Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tutaokolewa. {1TG43: 21.1}

“Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo. Tena hapa-na aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. {1TG43: 21.2}

“Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako. Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa. Nyumba yetu takatifu, nzuri,

21

walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika. Utajizuia usiyaan-galie mambo haya, Ee Bwana? Utanyamaza, na kututesa sana?” {1TG43: 21.3}

Sasa ni fursa yetu; sasa ni haki yetu kufanya maombi haya kibinafsi. Sasa tunaweza kusema kwa busara, Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike duniani kama ilivyo Mbinguni. Sasa tunaweza kusema kwa moyo wote: “Tu-uimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusal-emu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliose-ma, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!” Zab. 137: 4-7. {1TG43: 22.1}

Sasa ya kwamba unaona wazi ishara na wakati wa ukombozi wetu na ya siku ya kisasi cha Mungu dhidi ya wadhambi ambao hawajatubu inakaribia upesi sana, unahimizwa kufanya tayari, kuugua na kulia dhidi ya ma-chukizo, kuipokea alama ya ukombozi, uwe kati ya malimbuko. Sasa unaweza kwa furaha na kwa busara kuuta-futa Ufalme wa Mbinguni na Haki Yake, na kwa uhakiki ujue ya kuwa masumbuko ya maisha hayapaswi kuta-wala juu ya kiroho, kwamba mtazidishiwa (Mat. 6: 25-34). Mbingu, kwa hivyo, inakutazamia bila kukawia kwa dhati na wazi wazi uchukue msimamo wako kwa upande wa Ukweli. Sasa ya kwamba mwaka wa waliokom-bolewa Wake umekuja, kwamba ishara za siku ya kisasi ziko hapa, sasa ni wakati mwafaka kufanya uamuzi wako. Hauwezi kumudu kuchelewesha kwa maana anasema Roho wa Ukweli wote: “Kwa hiyo, (kama anena-vyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasiri-sha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa, Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.

22

kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu; Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.) Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo [sio jana, sio siku ya Miller au ya White]; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote wali-otoka Misri wakiongozwa na Musa? Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.” Ebr. 3: 7-19. {1TG43: 22.2}

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG43: 23.1}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 42, 43

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>