fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 29, 30

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 29, 30

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

UFALME ULIOKANYAGIWA CHINI UNASIMAMA KWA UMAARUFU NA AMANI

“WANAWAKE SABA WATAMSHIKA MTU MME MMOJA”

                                    

1

WAZO LA SALA

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa 187, aya ya pili. Aya hii imejengwa kwa andiko ambalo husema: “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” {1TG29: 2.1}

M.B., uk. 187 — “Bwana hasemi masharti yoyote isipokuwa kwamba uwe na njaa ya rehema Yake, utumaini ushauri Wake, na uutamani upendo Wake. ‘Omba.’ Kule kuomba hudhihirisha kwamba unatambua uhitaji wako; na ukiomba kwa imani, utapewa … Unapoomba kwa ajili ya baraka unazohitaji, ili uweze kuifanya tabia ifanane kikamilifu na ya Kristo, Bwana anakuhakikishia kwamba unaomba kulingana na ahadi itakayothibitishwa. Kwamba unajihisi na unajua kwamba wewe ni mdhambi, ni msingi thabiti wa kuuliza rehema na huruma Zake. Hali ambayo unaweza kumjia Mungu sio kwamba utakuwa mtakatifu, ila kwamba unamtaka Yeye akusafishe kutoka kwa dhambi yote, na kukutakasa uovu wote. Hoja kwamba tunaweza sasa kumsihi na daima ndilo hitaji letu kubwa, hali yetu ya kutojisaidia kabisa, ambayo humfanya Yeye na nguvu Yake ya ukombozi kuwa jambo la lazima.” {1TG29: 2.2}

Inatuhakikishia tena kama nini sisi wanadamu wadhambi ahadi hii iliyorudiwa mara tatu itakavyokuwa! Bwana huwa haweki masharti ya kutatanisha na magumu kufikia. Yeye husema tu, “Omba.” Kwa kuomba baraka tunazohitaji ili kuzikamilisha tabia zetu ndani ya Kristo, tunaonyesha tumaini letu kwa ushauri Wake na msaada Wake, hivyo huwa tunaonyesha kwamba kweli tunatambua kuwa hoi bila Yeye. Tunapofanya hivi, basi hatuhitaji kuwa na woga kwamba Bwana atatuangusha. Hakika hawezi, kwa maana Yeye ndiye Mtu wa neno Lake. {1TG29: 2.3}

Kwa mtazamo wa hili, sala yetu itakuwa nini alasiri hii? — Kwa ufupi tu kwamba tuweze kugundua mahitaji yetu, kwamba tuweze kuwa na tumaini la kutakaswa kutoka kwa dhambi yote, na kwamba tuweze kwa imani kuomba, tukijua kwa hakika kwamba tutapewa. {1TG29: 2.4}

2

UFALME ULIOKANYAGIWA CHINI UNASIMAMA KWA UMAARUFU NA AMANI

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 22, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Sasa tutajifunza kitabu cha Isaya, kuanzia sura ya kwanza, na kuendelea hadi sura ya pili. Sehemu ya kwanza ya sura ya kwanza, mnajua vizuri, inahusika na dhambi za Israeli wa zamani, ilhali sehemu ya mwisho ya sura hii, pamoja na sura ya pili, hushughulikia kusimamishwa tena kwa Ufalme katika siku za mwisho. Hasa, ni mada hii ya mwisho ambayo tutajifunza leo. {1TG29: 3.1}

Nabii Isaya kuagizwa kwake aandike kile ambacho kingaliwapata watu wa Mungu katika siku za mapema na vile vile katika siku za mwisho za historia yao, haraka kunafichua ukweli kwamba wakati uo huo Bwana hakuwa mawazoni tu na watu Wake katika siku za zamani, lakini pia watu Wake katika wakati wetu. (Desturi hii ya mtazamo maaradufu juu ya mada utaigundua kote kote katika Bibilia.) {1TG29: 3.2}

Katika uhusiano huu tunapaswa kuuliza swali, Je! Kumbukumbu yetu kama watu ni bora au mbaya zaidi kuliko ile ya Wayahudi? Hili linaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kusoma “Shuhuda,” Gombo la 3, Uk. 252, 253. {1TG29: 3.3}

Tunasoma hivi sasa — {1TG29: 3.4}

“Ujumbe kwa kanisa la Laodekia ni wa kuleta mashitaka na wa kushangaza, na unawahusu watu

3

wa Mungu kwa wakati huu wa sasa. {1TG29: 3.5}

‘”Na kwa malaika wa kanisa la Laodekia andika hivi: “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Na-yajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wase-ma, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.’ {1TG29: 4.1}

“Bwana hapa anaonyesha kwamba ujumbe unaopaswa kupelekwa kwa watu wake na wachungaji ambao ame-waita ili kuwaonya watu, sio ujumbe wa amani na usalama. Sio nadharia tu, lakini wa ki-vitendo katika kila hali. Watu wa Mungu wanawakilishwa katika ujumbe kwa Walaodekia kama walio katika nafasi ya usalama wa mwili. Wako shwari, wanajiamini kuwa katika hali ya juu ya mafanikio ya kiroho. ‘Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.’ {1TG29: 4.2}

“Ni udanganyifu mkubwa jinsi gani unaoweza kuja juu ya akili za wanadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, wakati ambapo wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli unawapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ambapo wale wanaohutubiwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu ya kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umasikini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo

4

na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayesema, na ushuhuda wake lazima uwe sa-hihi.” — “Shuhuda,” Gombo la 3, Uk. 252, 253. {1TG29: 4.3}

“Ni vigumu kwa wale ambao wanajihisi salama katika ufanisi wao, na ambao hujiamini kwamba ni matajiri kati-ka maarifa ya kiroho, kuupokea ujumbe ambao hutangaza kwamba wamedanganywa na wanahitaji kila neema ya kiroho. Moyo ambao haujatakaswa ni ‘mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha nani awezaye kuujua.’ Nalionyeshwa kwamba wengi wanajidanganya kwamba wao ni Wakristo wema ambao hawana mshale wa nuru kutoka kwa Yesu. Hawana uzoefu ulio hai kwa ajili yao wenyewe katika maisha ya utauwa. Wanahitaji uzoefu wa kina na wa kujishusha nafsi mbele ya Mungu, kabla wahisi hitaji lao la kweli la juhudi ya bidii, ya uvumilivu kuihifadhi neema yenye thamani ya Roho.” — “Shuhuda,” Gombo la 3, Uk. 252, 253. {1TG29: 5.1}

Sihitaji kusoma zaidi. Uvuvio unasema wazi kwamba leo upo ujumbe unaopaswa kupelekwa kwa watu wa Mungu; kwamba ujumbe huo hautatangazwa na watu wa kawaida, ila na wachungaji walioitwa hasa kwa ajili ya sababu hiyo; na kwamba sio ujumbe wa amani na usalama kama ambavyo ukasisi kwa ujumla ungalitaka kiuhalisia uweze kuwa. Mwandishi anajaribu kutuonyesha na ukweli kwamba watu wa Mungu wamedanganywa kwa kudhani kuwa wako katika hali nzuri. Naam, watu wa Mungu kwa wakati huu kwa kila jambo wame-danganywa kama Wayahudi katika siku za ujio wa kwanza wa Kristo. Kwa kweli, labda wao ni wabaya zaidi, kwa maana wamekuwa na mifano na vielezo vya zamani vile vile nyongeza ya nuru inayoangaza kwenye njia yao ambayo wa kale hawakuwa nayo. {1TG29: 5.2}

Nabii Isaya alikuwa na habari za kusikitisha kwa watu wa Mungu katika siku zake: Aliwaambia kwamba ikiwa wangaliendelea katika njia zao mbaya, wote, wazuri na mbaya sawa,

5

wangalitawanywa na kufyonzwa na mataifa. Lakini kwa waaminifu wa leo, anayo habari njema: {1TG29: 5.3}

Isa. 1: 24-26 — “Kwa hiyo, asema Bwana, Bwana wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu; nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na ku-kutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote; nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu.”

Badala ya kuwaacha wote kama watu kuteseka kwa matokeo ya dhambi, Bwana kwa wakati huu anaahidi kuli-piza kisasi tu kwa maadui Zake, watesi Wake walio ndani ya kanisa Lake. Atalisafisha na kulitakasa kanisa Lake, na kisha kuwarejeza waamuzi na washauri Wake kama hapo kwanza. Basi utaitwa hakika “Mji wa haki, mji mwaminifu.” {1TG29: 6.1}

“Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwa-nadamu na mbegu ya mnyama. Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung’oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema Bwana. {1TG29: 6.2}

“Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi.” Yer. 31: 27-30. {1TG29: 6.3}

Aya ya 27, 28 — “Sayuni utakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki. Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi

6

kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa.”

Katika aya hizi tofauti inafanywa kati ya wakosaji na wadhambi. Hapana shaka kwamba wadhambi ni wale am-bao wanaishi daima katika dhambi, ilhali wakosaji lazima wawe wale ambao hutenda dhambi mara kwa mara. Walakini mwisho wao utakuwa sawa: Wote wadhambi wenye mazoea na wadhambi wa mara kwa mara wa-taangamizwa pamoja. {1TG29: 7.1}

Aya ya 29-31 — “Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua. Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji. Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.”

Hili ndilo tu ambalo waovu wanaweza kutarajia kwa usahihi. Ni bora zaidi ambalo Mungu anaweza kuwapa, kwa maana hawafanyi iwezekane wapate kitu bora. {1TG29: 7.2}

Sasa tutaendelea kwenye sura ya pili ya unabii wa Isaya, kwa maana ni mwendelezo wa ya kwanza. Kwa sababu aya ya kwanza ni utangulizi wa kile nabii atasema, nitaacha kuisoma, na nitaanza na– {1TG29: 7.3}

Sura ya 2, aya ya 2 — “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.”

Kutoka kwa magofu ya Yuda na Israeli, ni unaibuka Ufalme na watu ambao watainuliwa

7

juu ya mataifa. {1TG29: 7.4}

Nabii Danieli, pia, anatangaza waziwazi: “… katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:44. {1TG29: 8.1}

Kumbuka kwamba Ufalme ambao Danieli anazungumza juu yake utasimamishwa “katika siku za wafalme hao,” sio baada ya siku zao. Zaidi ya hayo, kumbuka kwamba ni Ufalme huu (kanisa lililotakaswa) ambao unaivunja sanamu kubwa. Kwa ajili ya Ufalme huu unaokuja (kanisa “lililosafishwa” lililotakaswa) “mkusanyiko wa ma-taifa utakuwa” (Mwa. 49:10). {1TG29: 8.2}

Wakati Makao makuu ya injili yanaposimamishwa hivyo, basi inakuwa hakika kwamba kazi inakamilishwa bila kukawia. Injili ya Kristo wakati huo itavuna mavuno mengi, na umati ulioongoka badala ya kuyafua majembe yao na miundu yao kuwa zana za kuua wanadamu, badala yake wataifua mikuki yao na panga zao kuwa vifaa vya kilimo — badala ya kufanya kazi ya kuua, watalima kulisha. {1TG29: 8.3}

Unabii huu ni rahisi na wenye kufuatana vizuri, wa kuelimisha na kuangaza. Kwa kweli Mungu hawezi kuuokoa ulimwengu akitumia kanisa lililopotea. Wazo hili hasa litaonekana lisilokuwa na busara ikiwa tutajiuliza maswali haya: Je! Ni kwa jinsi gani Yeye kwa kanisa Lake anaweza kuiongoza dunia kutoka kwa dhambi yake ilhali dhambi inastawi kati ya kanisa Lake? Je! Anawezaje kuuongoza ulimwengu katika Kweli yote wakati ambapo wale ambao Yeye anawatumia kufundisha Ukweli unaokua mpaka Aje wanadhani kwamba ni matajiri na ha-wana haja ya kitu zaidi wakati kwa kweli wanahitaji kila kitu? — hata vipofu na uchi, na wao wenyewe karibu

8

kutapikwa nje. Je! Yeye anawezaje kuwaambia watu Wake walio “Babeli,” “Tokeni kwake enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake,” ikiwa Atawaleta kanisani ambamo dhambi imefanywa kuwa mazoea? Kwa mtazamo wa ukweli kwamba kanisa lililo na dhambi na wadhambi kati yake ni la kuathirika kwa mapigo kama ilivyo Babeli, je! watu Wake wangaliweza kuwa wabaya zaidi namna gani iwapo wanga-liachwa mbali Babeli? {1TG29: 8.4}

Jibu la maswali haya yote ni hili tu: Lazima uwepo uamsho kwa umaskini wa kiroho na bidii katika kuutafuta Ukweli. Lazima dhambi ikomeshwe, lazima pawepo mahali ambapo hakuna dhambi na watu wasio na dhambi – safina ya usalama, kwa mfano, ikiwa endapo tutaweza kuokolewa kutoka kwa mapigo. “kina Akani,” pia, lazima waondolewe kabla Israeli aweze kushinda na kuichukua nchi. Mungu kwa hekima Yake anajua kwamba ni bora kuwaangamiza maadui wachache wa Ukweli, kuliko kuupoteza ulimwengu wote. Vizuizi vya kujikwaa vyote lazima viondolewe. {1TG29: 9.1}

Kisha kanisa litakuwa na Pentekoste ya pili. Wakati huo kila mshiriki wa kanisa atajazwa na Roho: “Hata itaku-wa baada ya hayo [baada ya “mvua ya masika”], ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.” Yoeli 2:28, 29. {1TG29: 9.2}

Hebu sasa tutii kwa kicho na kwa bidii mwito wa Bwana kwa watu Wake hasa kwa wakati huu: {1TG29: 9.3}

Aya ya 5 — “Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.”

9

Bila shaka kabisa aya hii inaonyesha kwamba kufikia sasa watu wa Mungu wamekuwa wakitembea katika nuru ya mwanadamu. {1TG29: 10.1}

Aya ya 6 — “Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanajifurahisha wenyewe na wana wa wageni.”

Watu wake kama shirika wamemwacha Yeye, lakini kama watu mmoja mmoja ambao wanakuja kutembea kati-ka nuru Yake kumfuata Yeye katika Kweli na haki wanakubaliwa tena. Wakati vita vya sasa juu ya ujumbe wa sasa hivi vitakapomalizika, basi wale ambao wataokoka mchakato wa utakaso, Hukumu kwa Walio Hai katika nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17), kutakaswa kwa patakatifu (Dan. 8: 14), watakuwa wakazi wa Zayuni na wa Yerusalemu, washiriki wa kanisa, mwili wa Kristo. {1TG29: 10.2}

Aya ya 7 — “Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.”

Kati ya mataifa yote duniani leo, Amerika, taifa ambalo makao makuu ya kanisa yamo ndani yake ndilo tajiri. Hasa ni hivyo kwa wakati huu wakati ambao Ukweli huu unakunjua. Isitoshe, hakuna taifa lingine ambalo lina viongozi wengi wa kanisa (farasi) na makanisa mengi (magari). Hakuna taifa lingine duniani lililo na nafasi kwa ajili ya kila raia wake katika “magari” yake. Hizi ni alama za kutambulisha ambazo Bwana hutumia kuionyesha nchi na watu ambao Yeye ananena nao. {1TG29: 10.3}

Aya ya 8-10 — “Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe. Mtu mnyonge huinama,

10

na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe. Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa Bwana, mbele za utukufu wa enzi yake.”

Taifa hilo, kwa uthibitisho hujisifu sana juu ya mafanikio yake. Wakuu na wadogo wote ni sawa katika suali hili, unasema Uvuvio. Kweli, hakuna chochote kibaya katika maendeleo lakini ustawi haupaswi kamwe kuwa Mungu wetu. Mwishowe wote watafika mwisho wa ibada yao ya sanamu, kwa maana wakati Bwana atakapodhihirisha nguvu Yake, wataziacha sanamu zao na kuikimbilia miamba. {1TG29: 11.1}

Aya ya 11 — “Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitain-amishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.”

Wale ambao sasa wanajiinua watainamishwa. {1TG29: 11.2}

Aya ya 12-19 — “Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini. Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; na juu ya milima mirefu yote, na juu ya vilima vyote vilivyoinuka; na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma; na juu ya merikebu zote za Tarshishi, na juu ya kila taswira ipendezayo. Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na ki-buri cha watu kitashushwa; naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Nazo sanamu zitatoweka kabisa. Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.”

11

Ingawa watu sasa wanajiinua wenyewe hata juu ya Mungu, siku i juu yetu ambayo watajiona wenyewe jinsi walivyo. Watajihisi wadogo sana wanapoziona nguvu za Mungu Mkuu. {1TG29: 12.1}

Aya ya 20, 21 — “Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhaha-bu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo; ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.”

Wale ambao sasa hawazitupi sanamu zao kwa fuko na popo, kwa mfano, watalazimika kufanya hivyo baadaye, lakini wakati huo watakuwa wamechelewa sana kufaidika nazo. {1TG29: 12.2}

Aya ya 22 — “Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?”

Hapa lipo suluhisho rahisi la Mungu kwa watu Wake. Wanapaswa kuacha kuwasikiza “waaguzi,” badala yake wanapaswa kusikia kile ambacho Uvuvio unasema. Wanapaswa kujifunza Neno la Mungu wenyewe kwa msaada wa waalimu wakweli wa Mungu waliovuviwa, na kufanya maamuzi yao wenyewe — kamwe, kamwe wasiyategemee maamuzi na hukumu za wengine, bila kujali wao ni nini, au ni nani. {1TG29: 12.3}

Hivi majuzi dada fulani alitoa sababu ya kuacha mafundisho ya mtu mmoja na kukumbatia ya mwingine. Alisema: “Fulani na fulani huomba sana, na anayo Roho zaidi ya fulani na fulani, na ninakusudia kukaa naye. Kamwe sitamtegemea mwanadamu yeyote.” {1TG29: 12.4}

Ni bayana kwamba dada huyu anachagua kukaa kwa mafundisho ya mmoja, sio kwa sababu ya mafundisho yenyewe,

12

lakini kwa sababu ya kuvutia kwa mwanamume huyo. Halafu taarifa yake, “Sitamtegemea mwanadamu tena,” inathibitisha hakika kwamba hajijui mwenyewe, na kwamba hata anajua machache sana kuhusu maana ya “kumtegemea mwanadamu.” {1TG29: 12.5}

Tunaamini katika waandishi wa Bibilia sio jinsi walivyokuwa, bali kwa yale walioandika. Watu wanaodanganya wote ni wanadamu ambao husali, kwa maana Ibilisi anajua kwamba kadiri wanavyojiweka wonyesho na dini yao, watu wengi zaidi watawafuata. Hawana chochote kwa vyovyote. Watu wengi sio waangalifu kwa kile Bib-lia husema hakika na, kwa hivyo, hawajui kwamba Wayahudi waliomsulubisha Bwana walikuwa waki-wadanganya watu wa kawaida kwa kuomba sana mahali wangaliweza kuonekana, hivi kwamba hakuna nabii yeyote alijaribu kujiuza hivyo kwa watu; kwamba kile walichokuwa na hamu kukiuza kwa watu hakikuwa wenyewe, ila Mungu na Ukweli Wake; kwamba wote walikuwa waangalifu sana kutojionyesha. Yesu mwenyewe alithibitisha tena kielelezo hicho: Hakuomba na Nikodemo, au na yule kijana tajiri mtawala, lakini aliwaambia waziwazi Ukweli ni nini. Hakuna kumbukumbu kwamba Yeye aliomba na mtu yeyote. Bali, hata hivyo, namjua mtu akitengeneza chumba cha sala pembezoni mwa choo cha umma! Chochote cha kujiuza kwa watu kwa maana hicho ndicho watu wanatafuta badala ya Ukweli. {1TG29: 13.1}

Ni kwa sababu washiriki kama sheria ni wepesi kuwasikiliza watu wanaovutia ladha yao, kwamba kwa sababu ya hili maadui wa Ukweli kwa uangalifu na kwa bidii hujaribu kubandika kitu dhidi ya tabia za wale ambao wanautangaza ujumbe wa sasa. Maadui wanajua vizuri kwamba washiriki wanafanya uchaguzi wao kulingana na thamani ya uso wa sifa ya madai ya watu badala ya uzito wa Ukweli. Kwa sababu hii maadui

13

wa Ukweli wanaitumia fursa ya hali hiyo. Na kwa hivyo, kwa sababu hawawezi kuupinga Ukweli, wanalazimika kutumia uongo wa Ufarisayo ambao huutumia kuunguza tabia za wale ambao hawakubaliani nao. {1TG29: 13.2}

Walakini tunayo sababu nzuri kwa ajili ya furaha kuu na kicho kwamba tunalo pendeleo kuishi katika siku am-bayo kutoka kwa magofu ya kale ya Yuda na Israeli, utaibuka Ufalme na watu ambao watainuliwa juu ya falme na mataifa yote ya dunia. Wakati ambapo Makao makuu ya injili yatasimamishwa katika “mlima wa Bwana,” basi kazi itakamilika bila kukawia. Kurudia, mataifa yaliyoongoka yatafua panga zao kuwa vifaa vya kilimo. Wataacha kupigana vita na kuwa wakulima. {1TG29: 14.1}

Baada ya kanisa la Mungu kupita katika mchakato wa utakaso, basi itaonekana wazi kwa wote kwamba kanisa lililopotea halingaliweza kuuokoa ulimwengu uliopotea. Katika wakati wa Pentekoste ya pili kila mshiriki wa kanisa atajazwa Roho, na matokeo yake maelfu bila kusita wataukumbatia Ukweli wa wakati huu. {1TG29: 14.2}

Hakuna wakati wa kupoteza. Siku imekuja ambayo watu watajiona jinsi kwa kweli walivyo. Ukweli, wale am-bao sasa hawazitupi kando sanamu zao, watafanya hivyo baadaye, lakini kama tulivyosema awali, watakuwa wakati huo wamechelewa sana kupata faida yake. Sasa ni wakati wa kuwaacha wanadamu, na kufanya maamuzi yetu wenyewe kulingana na ahadi kwamba kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu na yule anayeutafuta Ukweli Mungu atampa Roho Wake ili amwongoze katika Kweli yote. {1TG29: 14.3}

Hata ingawa maadui wa Ukweli wanaweza kutumia kila ujanja ili kuidhuru kazi, bado Ukweli siku zote hushin-da, na watu wa Mungu pamoja nao. Hakuna kinachoweza kuudhuru

14

Ukweli. Ni kama fuawe: Wakati ambapo nyundo zote za maadui zinachakazwa, Fuawe itaendelea kusimama. {1TG29: 14.4}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji a Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG29: 15.1}

15

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma aya mbili kutoka kwa ukurasa wa 188 wa “Mlima wa Baraka.” Aya ya kwanza inafafanua taarifa, “Ombeni, nanyi mtapewa,” ya pili kwa maneno, “Bisheni, nanyi mtafunguliwa.” {1TG30: 16.1}

“’Ombeni.’ Usitumaini baraka Zake tu, bali Yeye mwenyewe. Jifahamishe sasa Naye, na uwe na amani. ‘Omba, na utapewa. Mungu anakutafuta, na tumaini hilo unalohisi kuja Kwake, ni mvuto wa Roho Wake. Jitiishe kwa mvuto huo. Kristo anasihi kwa ajili ya aliyejaribiwa, mwenye makosa, na asiye na imani. Anatafuta kuwainua katika ushirika Naye mwenyewe. ‘Ikiwa utamtafuta Yeye, Atapatikana kwako.’ {1TG30: 16.2}

“’Ombeni.’ Tunamwendea Mungu kwa mwaliko maalum, na Yeye husubiri kutukaribisha kwenye chumba Chake cha baraza. Wanafunzi wa kwanza waliomfuasa Yesu hawakuridhika na mazungumzo ya haraka Naye njiani; wakasema, ‘Rabi, unakaa wapi? … Wakaja na kuona mahali ambapo Aliishi, wakakaa pamoja Naye siku hiyo.’ Hivyo tunaweza kuingizwa katika uhusiano wa karibu na ushirika na Mungu. ‘Yeye akaaye katika mahali pa siri pa Aliye Juu zaidi atakaa chini ya kivuli cha Mwenyezi.’ Waruhusu wale wanaozitumaini baraka za Mungu, wa-bishe na wasubiri kwenye mlango wa rehema na uhakikisho thabiti, wakisema, Maana Wewe, Bwana Umesema, Kila mtu aombaye hupokea, na yeye atafutaye hupata, na kwake yeye abishaye atafunguliwa.” {1TG30: 16.3}

Sio tu kwamba tunaalikwa kumtafuta Bwana lakini tunahakikishwa kwamba kutafuta kwetu hakutakuwa bure. Tumaini letu la kuja Kwake, ni ushawishi wa Roho Wake. Kwa mvuto huu lazima tuutii. {1TG30: 16.4}

Wacha tuombe kwa imani isiyoyumbayumba katika ahadi Yake kwamba ikiwa tutatafuta, tutapata: tukibisha, tutafunguliwa. {1TG30: 16.5}

16

“WANAWAKE SABA WATAMSHIKA MTU MME MMOJA”

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 1, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Leo tutaendeleza somo letu la kitabu cha Isaya, kuanzia aya ya kwanza ya sura ya nne. {1TG30: 17.1}

Isa. 4: 1 — “Na katika siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.”

Jambo la kwanza tunalohitaji kujua ni wakati ulioonyeshwa kwa neno “katika siku hiyo.” Nomino ya maneno “siku hiyo” inapatikana katika aya 13 na ya 14 ya sura zilizotangulia ambapo sura ya nne ni endelezo. Aya hizi zinabainisha kwamba “siku hiyo” ni siku ya Hukumu, siku ambayo patakatifu (kanisa) patatakaswa — siku ya mavuno. Hivyo, ikionyesha siku ambayo sasa tunaishi, hadi kwa siku ya Hukumu, andiko linafichua katika mfa-no kwamba (maana hivyo ndivyo tarakimu ya biblia “saba” huashiria) makanisa yote yamewasili mahali ambapo kwa matendo yao kwa kweli yanamwambia Bwana: “Hatutaki chochote kutoka kwako ila jina Lako. Wacha tu tuitwe Wakristo ndilo tunalotaka kutoka Kwako. Tunalitaka jina Lako kwa sababu linaondoa aibu yetu; Yaani, ikiwa tutaitwa Wakristo, basi kila tunalofanya laweza kulaumiwa juu Yako; Unapata sifa kwa ajili yake.” {1TG30: 17.2}

17

Kwa hivyo, dunia imefikia siku ambayo Mungu, ili aweze kuliokoa Kanisa, hatimaye amelazimishwa kufanya kitu kikuu na cha mapinduzi kama kilicholetwa na Ujio wa kwanza wa Kristo. Na hicho kinaweza kuwa nini? – Aya zilizosalia za sura hiii zinatoa jibu. {1TG30: 18.1}

Aya ya 2 — “Katika siku hiyo [wakati ambapo wanawake saba wanamshika mtu mme mmoja] chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na ya kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.”

Aya hii inaonyesha kwamba wakati umekuja sasa wa kuleta mapinduzi haya ya utukufu kwa kanisa na kwa ulimwengu. Hebu tukumbuke kwamba historia hujirudia, na kwamba siku ya mawingu yenye giza huwa daima inafuatwa na yenye uangavu. Hivyo uasi huu mkubwa utaandamwa sio kwa machafuko, ila kwa uamsho na matengenezo yenye utukufu, kwa utukufu na ustawi kwa ajili ya watakatifu wote ambao wanaokoka kisasi cha Mungu mkuu. Waaminifu watayavuna mavuno ya mioyo kama walivyofanya Mitume wakati na baada ya Pen-tekoste. {1TG30: 18.2}

“Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU.” Yer. 23: 5, 6. {1TG30: 18.3}

Ujumbe huu, kwa hivyo, ni ujumbe wa “Haki kwa Imani” kwa wale wanaoamini. Katika siku ambayo “chipukizi la haki” litainuliwa, Yuda na Israeli wataokolewa, nao watakaa salama. {1TG30: 18.4}

18

Naam, siku imekuja ambapo kisasi cha Mungu kitaanguka juu ya mahasimu Wake, na falme zilizokanyagiwa chini hapo zamani za Yuda na Israeli zitasimama kwa umaarufu na nguvu. “Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri; lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.” Yer. 23: 7, 8. {1TG30: 19.1}

Kwa udhahiri haya ni mavuno ya mwisho ya dunia, kukusanywa kwa watu kutoka katika nchi zote. Ni siku am-bayo utaimbwa wimbo wa Musa na Mwana-Kondoo. Hili litakuwa Vuguvugu la Kutoka la pili na la mwisho. Hivyo litakuwa kubwa hivi kwamba litazidi kabisa vuguvugu la siku ya Musa. Je! Sisi, basi, tunang’amua kwamba tuko kwenye ukingo wa siku mpya? — siku kuu kwa waaminifu na yenye kuogofya kwa wakafiri? {1TG30: 19.2}

Aya ya 3 — “Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Ye-rusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Ye-rusalemu.”

Aya hii inaonyesha wazi kwamba wakati hakuna mtu muovu katika kanisa ataokoka utakaso, lakini hakuna hata mmoja wa wenye haki ataangamia. Hakika, wote ambao wamesazwa, wataitwa watakatifu, na watafurahia usalama mkubwa zaidi kuliko walivyokuwa watu Wake wa zamani wakati walipoondoka Misri. {1TG30: 19.3}

“Angalieni, … Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfu-rahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake?

19

au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3: 1-3. {1TG30: 19.4}

Aya ya 4-6 — “Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.”

“Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utu-kufu ndani yake.” Zek. 2: 5. {1TG30: 20.1}

Yeyote anayeijua Biblia anaweza kuona kwamba matukio haya yote ni kabla ya milenia. Hivyo ni kwamba uasi huu wa sasa utazalisha “chipukizi lenye matunda la Bwana”; kwamba waovu walio kati ya watu wa Mungu wa-taondolewa, na waaminifu, wale watakaokoka, watakuwa watumwa wa Mungu na wachume mavuno ya nafsi za watu, “za wale watakaoweza kuokolewa,” kwamba siku ya kulipiza kisasi tayari iko kwenye kizingiti cha nyumba; kwamba waaminifu Wake watainuliwa kwa umaarufu na nguvu; kwamba ukuu na utukufu wa vuguvugu hilo utasababisha maajabu ya Vuguvugu la Kutoka na ya kanisa la kwanza la Kikristo kufifia kwa un-yonge. {1TG30: 20.2}

20

Ndugu, Dada, u tayari kuistahimili siku ya kuja Kwake? Je! Itakuwa kwako siku kuu na tukufu? au itakuwa siku ya kuogofya? Je! Utajikuta upande Wake wa kulia, au Wake wa kushoto? Je! Itanenwa kwako “Njoo, uli-yebarikiwa na Baba yangu, urithi Ufalme uliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu?” Au itanenwa kwako, Ondoka kwangu, wewe uliyelaaniwa, uende katika moto wa milele, uliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake”? Je! Mavazi yako yatapita ukaguzi Wake? au utajikuta umetupwa katika giza la nje, huko kulia na kusaga meno yako? {1TG30: 21.1}

Haya ni maswali matakatifu ambayo kila mmoja wetu lazima ayajibu mwenyewe. Iwapo hatuwezi kuyaajibu sasa, basi tutalazimika kuyajibu kwa kusimama tumeduwaa mbele ya Mungu. Hebu kila mmoja wetu aweze kus-ema siku hiyo, “Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuli-yemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” Isa. 25: 9. {1TG30: 21.2}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo bada-la ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {1TG30: 21.3}

21

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 29, 30

Kimechapishwa nchini Marekani

22

>