fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 23, 24

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 23, 24

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

HATIMA YA ASHURU NA USHINDI WA KANISA

JE, VITA VYA 2 VYA DUNIA BADO HAVIJAKWISHA, WATAKATIFU BADO HA-WAJAOKOLEWA?

                                    

1

WAZO LA KUTAFAKARI NA SALA

Tutasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 180, aya ya kwanza. Somo limejengwa kwa msingi wa andiko ambao linasema, “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako?” {1TG23: 2.1}

M.B, uk. 180 — “Hata tamko, ‘Wewe unayehukumu hutenda mambo yale yale,’ halifikii ukubwa wa dhambi yake yeye ambaye hutwaa daraka la kumlaumu na kumuhukumu ndugu yake …. Wakati anadhani amegundua kosa katika tabia au maisha, anakuwa wa bidii sana kujaribu kuionyesha wazi; lakini Yesu hutangaza kwamba mwenendo huu wa tabia uliokuzwa kuifanya kazi hii isiyo ya Kristo, ni, kwa ulinganifu na kosa lililoshutumiwa, kama boriti kwa uwiano na kibanzi. Ni ukosefu wa mtu mwenyewe wa roho ya uvumilivu na upendo ambayo humuongoza aifanze dunia kutoka kwa chembe …. Kwa mujibu wa mfano ambao Mwokozi wetu hutumia, yeye ambaye huikuza roho ya ukaguzi anayo hatia ya dhambi kubwa zaidi kuliko yeye anayemuhukumu; kwa maana yeye sio tu huitenda dhambi ile ile, bali huongeza juu yake majivuno na kulaumu.” {1TG23: 2.2}

Shetani anafanya kadiri awezavyo kutufanya tukose katika suala hili ili tuangamie milele. Mungu hajamteua mtu yeyote kuwa polisi wa mwingine. Mungu pekee kupitia kwa manabii Wake ndiye wa kukemea dhambi, lakini kamwe bila kutumia mabavu ya aina yoyote. {1TG23: 2.3}

Tupige magoti sasa, na tuombe kwa ajili ya kutambua kwamba wajibu wetu sio kuwalaumu wengine au kuyazidisha makosa yao, ila kunena na kuutenda Ukweli? Zaidi ya hayo, Ndugu, Dada, hatuhitaji kwenda. Ya-liosalia ni kwa watu na washirika wetu. Waache wajiamulie wenyewe kilicho bora kwa ajili ya roho na mwili. Kweli haipaswi kusukumwa chini ya koo. {1TG23: 2.4}

2

HATMA YA ASHURU NA USHINDI WA KANISA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 11, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Hebu tufungue Zefania 3, na tuanze na aya ya kwanza. {1TG23: 3.1}

Zef. 3: 1 — “Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu!”

Kitangulizi cha kiwakilishi-nomino “yeye” kinapatikana katika aya ya kumi na tatu ya sura iliyopita. Ndani yake inaonekana kwamba “mji” ulioonyeshwa hapa ni Ninawi, mji mkuu wa Ashuru ya kale. Sasa ili kujua kama Ni-nawi huu ni mji mkuu wa Ashuru ya kale au wa Ashuru nyingine fulani, tutasoma aya zilizosalia za sura hii. {1TG23: 3.2}

Aya ya 2 — “Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini Bwana; hakumkaribia Mungu wake.”

Aya hii inaonyesha ukweli kwamba mji na taifa lililotajwa hapa walikuwa na fursa ya kusikia sauti ya Uvuvio, ya kuujua Ukweli wa Mungu, lakini walishindwa kuuzingatia — hawakupokea kurudiwa, hawakumwamini Bwana, hawakumkaribia Mungu. {1TG23: 3.3}

Aya ya 3 — “Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao;

3

makadhi wake ni mbwa-mwitu wa jioni; hawasazi kitu cho chote hata siku ya pili.”

Wakuu wake, wakiwa kama simba wangurumao, lazima wawe watu wa kutia woga ambao kwa udhahiri hufikiri “ubabe hufanya haki.” Waamuzi wake ni, kwa mfano, mbwa mwitu wa jioni; yaani, wako katika shughuli, sio kuitekeleza hukumu, uadilifu, na haki, ila kunasa na kurarua, kuyajaza mapango yao kwa mawindo ingawa wanaweza kuwa na zaidi kuliko wanayojua kutumia. “Hawasazi mifupa hata siku ya pili.” {1TG23: 4.1}

Aya ya 4 — “Manabii wake ni watu hafifu na wadanganyifu; makuhani wake wamepatia unajisi patakati-fu, wameifanyia sheria udhalimu.”

Katika lugha ya leo aya hii ingalisomwa, “Waalimu wake ni hafifu, sio wa kufikiri na makini; wanacheza; ha-wana simulizi; wao ni wenye hila. Wachungaji wake, badala ya kuwa wameliweka kanisa safi, wamelitia unajisi, na wameivuruga sheria” (wametangaza kuwa Ni bure). {1TG23: 4.2}

Hadi sasa inaonekana kwamba Ashuru wa sura hii anawakilisha kundi la watu ambao wameelimishwa vyema katika mambo ya Mungu, sheria na hekalu. Lakini badala ya kumtii Bwana na kutawala kwa uadilifu na kwa haki, wameasi sana, wameshuka chini katika dhambi kwa kina kama ambacho watu wote wanaweza kwenda. {1TG23: 4.3}

Aya ya 5 — “Bwana kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.”

4

Kwa mtazamo wa ukweli kwamba Mungu yupo kati yao, wao lazima wamefahamishwa barabara mambo ya Mungu, wakijua vizuri kwamba katika majira mwafaka Yeye atawajulisha hukumu Yake. Kwa mtazamo wa haya yote, hitimisho pekee linalowezekana mmoja anaweza kufikia, ni kwamba kanisa la Mungu lazima liko kati yao. {1TG23: 5.1}

Aya ya 6-8 — “Nimekatilia mbali mataifa, buruji zao zina ukiwa; nimeziharibu njia kuu zao, hata hapana mmoja apitaye; miji yao imeangamizwa; hamna mtu hata mmoja, wala hapana akaaye huko. Nalisema, Hakika utaniogopa, utakubali kurudiwa; ili yasikatiliwe mbali makao yake, sawasawa ya yote niliyoagiza katika habari zake; lakini waliondoka mapema na kuyaharibu matendo yao yote. Basi ningojeni, asema Bwana, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili niziku-tanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.”

Bwana mwenyewe anaonya kwamba Yeye amewaangamiza mataifa, kwamba Yeye ameifanya minara yao kuwa ukiwa na njia zao uharibifu, kwamba Yeye ameiharibu miji yao na hajaacha wakazi ndani yake. Yeye anaonye-sha kwamba yote aliyatenda kama somo la kielelezo kwa ajili ya wema wa siku za baadaye, ili kwamba wao ka-ma taifa waweze kumcha Yeye na kuyapokea maagizo, kwamba makao yao yasikatiliwe mbali. Lakini licha ya mifano hii, wao huamka mapema na kuyaharibu matendo yao yote. Hivyo ni kwamba hatimaye Bwana anainuka kwa mawindo, anawakusanya mataifa, anazikutanisha falme, na Ashuru anapata adhabu yake. {1TG23: 5.2}

Kutoka kwa hilo tunaona kwamba Ashuru unaozungumziwa uko ndani ya wakati wa mwisho, wakati ambapo

5

siku kuu na ya kutisha ya Bwana inatukia. Ashuru huu, kwa hivyo, ni uakisi wa Ashuru wa kale kama vile Babeli wa Ufunuo 17 na 18 ni uakisi wa Babeli wa kale. {1TG23: 5.3}

Ashuru, unatuhumu Uvuvio, ni mji ule wa furaha uliokaa pasipo kufikiri, ambao ulisema moyoni mwake, “Mimi niko, wala hapana mwingine ila mimi.” Zef. 2:15. {1TG23: 6.1}

Kwenye hatua hii hebu tutulie kidogo na tufanye muhtasari wa sifa ambazo Ashuru huu mamboleo unavyoweza kutambuliwa. (1) Kama vile mtu anavyoyaangalia mambo, yeye ni mkuu sana kwamba hakuna mwingine ila yeye. Yeye ameelimishwa vizuri katika mambo ya Mungu. (2) Yeye ni mkandamizaji, taifa la utawala wa kunyanyasa. (3) Amelitia unajisi hekalu na ameitangaza sheria ya Mungu kuwa bure. (4) Amerundika utajiri kwa kuutafuta kama mbwa mwitu wa jioni anavyofuata windo lake. (5) Yeye ni kituo cha kanisa la Mungu. (6) Yeye yupo katika wakati ambapo Bwana atazidhihirisha nguvu zake na kuyaangamiza mataifa yote mabaya. (7) Yeye ni kama taifa la Ashuru, lililoenea, taifa la vita. {1TG23: 6.2}

Lipo kundi moja la watu chini ya jua ambalo huitikia maelezo haya yote, na watu hao ni, bila shaka, watu wanaozungumza Kiingereza, ambao kati yao liko kanisa, na kutoka kati yao Injili na Biblia hutiririka kwa ma-taifa yote. Kwa uwazi kama lugha inavyoweza kuonyesha, mzigo wa nabii Zefania ni kwa ulimwengu wa Kikristo unaonena lugha ya Kiingereza. {1TG23: 6.3}

Mungu sasa ananena kwa mji mkuu wa Ashuru, “Hakika, unayatenda machukizo haya yote, lakini huwezi kuen-delea hivyo kwa muda zaidi. Wakati umekaribia.” Weka kikomo kwa upumbavu wako. {1TG23: 6.4}

6

Aya ya 9 — “Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la Bwa-na, wamtumikie kwa nia moja.”

Uvuvio kwa yakini unatangaza kwamba baada ya Ashuru kupokea adhabu yake, na baada ya waovu kuondole-wa ndani ya kanisa lake, basi Injili itatangazwa kwa lugha safi (katika Ukweli wa Injili) kwamba yeyote ataka-yetaka, ataweza kuliita jina la Bwana, “Kumtumikia” kwa moyo na kwa roho. Kisha inakuwa kwamba “wale tu ambao wameyastahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika kilio kikuu.” — “Mapitio na Kutangaza,” Novemba 19, 1908. {1TG23: 7.1}

Aya ya 10, 11 — “Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya Kushi, waniombao dua, yaani, binti za watu wangu waliotawanyika, wataleta matoleo yangu. Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.”

Injili inapotangazwa kwa “lugha safi,” wakati huo hata kutoka miisho ya dunia watu wa Mungu watakuja na sa-daka kwa Bwana. {1TG23: 7.2}

Baada ya kuwaondoa wote wanaofurahi katika kiburi chake kanisa halitakuwa na kiburi tena. {1TG23: 7.3}

Zef. 3:12 — “Lakini nitasaza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la Bwana.”

7

Ukweli kwamba Anawaacha kati yao masikini na watu walioonewa ni ushahidi wa kutosha ndani yake kwamba kutakaswa kwa kanisa kutafanyika kabla ya Milenia, kabla ya Isaya 33:24 kutimizwa na kabla ya Yeye kuusimamisha ufalme uliotajwa humo. {1TG23: 8.1}

Aya ya 13 — “Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaon-ekana kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.”

Mabaki, wale waliosalia baada ya utakaso kufanyika, hawatatenda dhambi tena. Watasimama milele baada ya hapo bila uongo vinywani mwao. {1TG23: 8.2}

Aya ya 14 — “Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.”

Siku kuu inakuja kwa wenye haki, ya kutisha kwa waovu. Sisi, kwa hivyo, kama watoto wa Zayuni, tunatiwa moyo kuimba na kupiga kelele kwa furaha kwa sababu tumefika mwishowe kwa wakati wa ukombozi mkuu wa Mungu. {1TG23: 8.3}

Aya ya 15 — “Bwana ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako; Hutaogopa uovu tena.”

Hakika mafunuo haya ya unabii yanapaswa kumhimiza kila mwamini kupiga kelele kwa furaha anapong’amua kwama siku ambayo ndani yake hatauona tena uovu imekaribia, kwamba Bwana atakuwa mfalme wake pekee yake. {1TG23: 8.4}

Aya ya 16-20 — “Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,

8

Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee. Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuo-koa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba. Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao. Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote. Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nita-wakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema Bwana.”

Bwana anataka tujue kwamba atakapotuondolea uhamisho wetu Yeye atatufanza kuwa jina na sifa kati ya watu wote wa dunia. Ufalme huu wa Yuda (kanisa lililotakaswa na kutengwa), ni kwa hivyo, sio tu kabla ya milenia, ila pia ni wa muda wa kabla ya muda wa rehema kufungwa. Na ni wa furaha kama nini tunapaswa kuwa kwa ajili ya upendeleo wa kuwa kati ya malimbuko. {1TG23: 9.1}

-0-0-0-0-0-0-

Ili kuleta kwa wote furaha hii isiyo na kifani ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi vyote, masomo haya yanachap-ishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina lako na anwani kwa Shiri-ka la Uchapishaji la Ulimwengu, kwa anwani iliyo nyuma ya jalada. {1TG23: 9.2}

9

MAELEZO YA KUFUNGUA NA SALA

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanza na aya ya pili katika ukurasa wa 181. {1TG24: 10.1}

M.B. uk. 181, 182 — “… Yawezekana upo umakini wa ajabu kufahamu kasoro za wengine, lakini kwa kila mmo-ja ambaye hujifurahisha kwa roho hii, Yesu husema, ‘Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.’ Yeye aliye na hatia ya makosa, ndiye wa kwanza kutuhumu. Kwa kumuhukumu mwingine anajaribu kuuficha au kutafuta kisingizio cha uovu wa moyo wake …. {1TG24: 10.2}

“Wakati ambapo watu huifurahisha roho hii ya kuhukumu, huwa hawatosheki na kuonyesha kile wanachodhani kuwa kasoro ndani ya ndugu yao. Ikiwa njia za upole zitashindwa kumfanya atende kile wanachofikiri kina-paswa kufanyika, watageukia kulazimisha. Kwa kadri zitakapoendelea kuwa katika mamlaka yao, watawalazi-misha watu kutii mawazo yao kuhusu kile kilicho sahihi.” {1TG24: 10.3}

Tunahitaji kuomba kwa ajili ya nguvu ili tupinge kuwapekua wengine kuliko sisi wenyewe na hivyo kujongea karibu na karibu kwa Kristo na kupokea kwa wingi neema Yake. Sijawahi kumwona baba au mama akimpekua mwana wao au binti yao. Wakati wazazi wanaposikia wengine wakiwachambua watoto wao, basi wakosoaji ma-ra nyingi huingia katika taabu. Lakini watetezi wale wale wa wana na binti zao, mara nyingi huwapekua wen-gine kwa wazo kwamba wanafanya hivyo kwa wema wa wale wanaowakosoa. Iwapo kwa kweli wao huamini kwamba uchambuzi wao unachochewa na upendo kusaidia badala ya kujeruhi, na sio kuimarisha heshima zao na kufunika dhambi, basi naomba mniambie kwa nini wakosoaji hawawapatii watoto wao baadhi ya ukosoaji wao? {1TG24: 10.4}

Hebu tuombe kwa ajili ya neema ya Kristo ituwezeshe kuwatendea wengine kama vile tungalivyotaka watuten-dee, badala ya kujidumisha katika dhambi kwa kutafuta makosa na utendaji wao wa kidini. Tuzichunguze hatua zetu wenyewe ndiyo yote tunaweza kufanya. {1TG24: 10.5}

10

JE, VITA VYA 2 VYA DUNIA BADO HAVIJAKWISHA, WATAKATIFU BADO HA-WAJAOKOLEWA?
(Na Nahumu)

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 18, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tunajifunza kitabu cha Nahumu. Mzigo wa kitabu hiki chote, sura tatu kwa ujumla, ni kuhusu makun-di mawili tofauti ya watu tofauti. Kuhakiki watu hawa ni nani, tutaanza na– {1TG24: 11.1}

Nah. 1: 1; 3:18 — “Ufunuo juu ya Ninawi. Kitabu cha maono aliyoyaona Nahumu, Mwelkoshi …. Wa-chungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya.”

Kwa udhahiri, Ashuru pamoja na mji wake mkuu, Ninawi, ni kundi moja la watu. {1TG24: 11.2}

Sasa ili kujua ni nani kundi la watu wengine, tutasoma sura ya 1, aya ya 12, 13, na 15 (tukiziacha sehemu za aya zinazohusu Ashuru). {1TG24: 11.3}

Nah. 1:12, 13, 15 — “Bwana asema hivi; … Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena. Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako … Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako;

11

kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.”

Watu ambao Mungu amewatesa (kwa kutawanyika kwao kati ya mataifa) na ambao Yeye anaahidi kwamba ha-tawatesa tena, na kuwavunjia nira la Ashuru kutoka kwa mabega yao, ndio watu Wake, kanisa Lake –Yuda wa uakisi. Wao ni, kwa hiyo, kundi la watu wengine. {1TG24: 12.1}

Jina la heshima la watu wa Mungu, unaona, ni “Yuda.” Wanashauriwa kumwangalia mjoli wa Mungu ambaye katika utimizo wa unabii huu anawaletea habari njema, habari za amani … ujumbe wa Ufalme wa amani ( Isa. 11: 6-9). Bwana anawashauri kwamba wawe waaminifu Kwake, waaminifu katika madai yao ya imani. Wao, zaidi ya hayo, wanapewa uhakikisho kwamba kwa wakati wa utimizo wa unabii huu malaika wa kuangamiza wa-tawaondoa waovu kati ya wenye haki. Hivi ndivyo waovu “watakavyotwaliwa” mbali na hawatakuwapo tena. {1TG24: 12.2}

Kwa hivyo inakuwa kwamba wakati ambapo Nahumu anatabiri uhuru na amani kwa watu waaminifu wa Mun-gu, anatabiri maafa na fedheha kwa Ashuru ya uakisi (dola inayowatumikisha) na kwa waovu ndani ya kanisa. {1TG24: 12.3}

Aya tatu za sura ya pili zitatosha kuonyesha hatima ya Ashuru: {1TG24: 12.4}

Nah. 2: 6, 10, 13 — “Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa …. Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu …. Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na

12

upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.”

Hapa nabii anatabiri kwamba mji mkuu wa Ashuru utakuwa utupu, na kasri lake kuyeyushwa. Kwa udhahiri, basi, ufalme wa Yuda unasimamishwa katika wakati wa vita na mchafuko. Ni ishara gani zingine zitakazoutam-bulisha wakati huo? — Hebu tusome kutoka katika sura ya pili: {1TG24: 13.1}

Nah. 2: 3, 4 — “Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa taa za umeme siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha. Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, Yanasongana-songana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.”

Kwa sababu unabii huu unapata utimizo wake siku ambapo magari yanazo “taa za umeme”; wakati yanakwenda upesi kama umeme; yakisongana-songana katika barabara kuu, na maadamu trafiki ya magari ya leo kwa utimili-fu na ukamilifu inaitikia maelezo ya nabii kuihusu, basi hakuna hitimisho lingine ila kwamba siku ambamo sasa tunaishi ni siku ambayo unabii wa Nahumu utatimizwa. {1TG24: 13.2}

Sasa, kwa mtazamo wa ukweli kwamba tunaishi katika kipindi kama ilivyoelezwa na Nahumu, pamoja na ukweli kwamba maandalio ya vita vya Nahumu yanafanywa kwa wakati wa usafiri kama umeme, ushahidi unaonekana wazi kwamba unabii wa Nahumu utafikia utimilifu wake katika siku yetu, na ya kwamba “Ashuru” hapa katika unabii, kwa hivyo, sio Ashuru ya zamani, bali ni dola nyingine iliyoenea ambayo ipo “katika wakati wa mwisho” (Dan 12: 9, 10) katika wakati ambao nira yake

13

inaondolewa kutoka kwa watu wa Mungu. {1TG24: 13.3}

Zaidi ya hayo, kwa sababu anguko la Ashuru wa uakisi linawaweka huru watu wa Mungu, na maadamu kuanzia wakati huo na kuendelea waovu hawapitia tena kati yao, wakati na matukio yanashikana kidete: Utabiri huu wote unakuja kutimia katika wakati wa kulitakasa kanisa, katika siku ya Hukumu ya walio hai, katika wakati wa siku kuu na ya kutisha ya Bwana. {1TG24: 14.1}

Nah. 2: 1 — “Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.”

Ni wazi kuona kwamba yule asetaye vipande vipande, na ambaye anakuja mbele ya uso wa Ashuru ndiye anayemlazimisha Ashuru kujiandaa, kujizatiti kwa nguvu za kivita. Maandalizi yake ya kijeshi aliyolazimika kuyafanya, yaliyochochewa na yeye asetaye vipande vipande, yanamwanzisha Ashuru kwa anguko lake. {1TG24: 14.2}

Sasa, ili kujua kitakachotokia kwa yule asetaye vipande vipande — yeye ambaye anamlazimisha Ashuru kujiandaa kwa nguvu, tutasoma– {1TG24: 14.3}

Nah. 2: 5 — “Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.”

Watu wake wenye heshima (majemadari wake hodari) wanajikwaa katika kutembea kwao; yaani, wanafanya kosa wakati wanaposonga mbele kwa matumaini ya ushindi. Kwa mtazamo wa kosa lao hatari, na kwa taswira ya ukweli kwamba “yeye asetaye vipande vipande” hajatajwa tena katika kitabu cha Nahumu, ni thibitisho kwamba kwa kujikwaa kwake yeye anashindwa vitani. Hata hivyo, kwa mujibu wa aya zinazofuata katika sura za Nahumu, anguko la Ashuru ni hakika {1TG24: 14.4}

14

Swali, basi linatokea, iwapo Ashuru utaanguka, na ikiwa yule anayeanzisha vita, “yeye asetaye vipande vipande,” ndiye wa kwanza kushindwa, basi ni kwa mikono ya nani Ashuru utaanguka? Kwa ajili ya jibu, Hebu tufungue Isaya 31, ambako Ashuru huyu pia analetwa tena kwa mtazamo: {1TG24: 15.1}

Isa. 31: 6-8 — “Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watashindwa.”

Ashuru utaanguka na kuangamizwa, lakini sio kwa upanga wa mtu mnyonge, sio kwa yule asetaye vipande vipande. {1TG24: 15.2}

Sasa ukweli kwamba watu wa Mungu wanahimizwa kumwelekea Yeye ambaye wana wa Israeli wa kale walimwasi, unaonyesha tena kwamba Uvuvio unanena kwa Israeli wa uakisi, kwa watu wa Mungu katika enzi ya Kikristo. {1TG24: 15.3}

Aya ya 7 — “Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhaha-bu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu.”

Bila shaka nabii anatazama chini kwa mkondo wa wakati, kwa wakati wa matengenezo ya kina, katika wakati ambapo wale tu wanaoziacha dhambi zote na kutekeleza Ukweli na haki watasazwa ndani ya kanisa. Hakuna wengine watakaopatikana katika kutaniko la Bwana. Kisha Ashuru utaanguka na hivyo nira yake itaondolewa shingoni mwa watu wa Mungu. {1TG24: 15.4}

15

Mwashuri ataanguka kwa sababu ya uovu wake, na kwa sababu watu wa Mungu wanarudi Kwake, kwa sababu ya uamsho na matengenezo ya kina. {1TG24: 16.1}

Isa. 31: 9 — “Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera ho-fu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu.”

Majanga haya yote yanampata Ashuru mara tu watu wa Mungu wanamwelekea Yeye, mara tu wanapozitupilia mbali sanamu zao. {1TG24: 16.2}

Ni nini moto wa Bwana u Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu? Jibu tutapata katika {1TG24: 16.3}

Mal. 3: 1, 2 — “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani ata-kayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.”

Unabii wa Isaya, pamoja na unabii wa Malaki, unalifanya somo hili kuwa rahisi sana: Kwa mujibu wa unabii huu, wakati wa Hukumu ya Walio Hai na wakati ambapo malimbuko — watumwa wa Mungu, watu 144,000 — watasimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni, makao makuu ya injili yatakuwa katika Zayuni na Ye-rusalemu.” {1TG24: 16.4}

Sasa kabla ya kuamua iwapo Nahumu hutabiri “Vita Kuu vya 2 vya Dunia” itakuwa vyema kuziburudisha nia zetu kwa kufanya muhtasari wa hoja kuu za somo: {1TG24: 16.5}

16

1. Makundi mawili ya watu yanaletwa kwa mtazamo — kanisa, na taifa linalolinganishwa na Ashuru wa zamani, ambalo kanisa limetiishwa chini yake. {1TG24: 17.1}

2. Watu wa Mungu, Yuda, wanaulizwa kumtazama mjoli wa Mungu, ambaye kwa utimizo wa unabii huu na kwa wakati ambao unachemka kwa vita anawaletea habari njema za Ufalme wa amani. {1TG24: 17.2}

3. Unabii huu unatimizwa katika siku ya trafiki ya magari isiyo na kifani, siku ambapo magari (motokaa) yanazo taa za umeme na yanasongana-songana kwenye barabara kuu — bila shaka katika siku yetu. {1TG24: 17.3}

4. Katika siku hii, “yeye asetaye vipande vipande” anafanya vita dhidi ya Ashuru wa uakisi. Anaanzisha anguko lake. {1TG24: 17.4}

5. Ashuru anaimarisha uwezo wake sana baada ya adui yake kuja mbele ya uso wake. {1TG24: 17.5}

6. Katika kusonga mbele kwa ushindi, adui wa Ashuru — “yeye asetaye vipande vipande” — anafanya kosa na hivyo kuanguka, anashindwa vitani. {1TG24: 17.6}

7. Ashuru, hata hivyo, anaanguka baadaye, pia, lakini sio kwa upanga wa mtu mwenye mnyonge. {1TG24: 17.7}

8. Vita hivyo, magari yapitayo kwa kasi, na uhuisho na matengenezo kama yale ulimwengu haujawahi kuona, ni ishara za utimizo wa unabii wa Nahumu. {1TG24: 17.8}

9. Wakati ambapo watu wa Mungu wanazitupilia mbali sanamu zao zote, kumwelekea Yeye kabisa, kisha ina-kuwa kwamba Ashuru anaanguka. Kisha inakuwa kwamba waovu wanaondolewa kati ya

17

watu wa Mungu, nira ya Ashuru inavunjwa, na watukwa wa Mungu, bila shaka malimbuko, watu 144,000, wanasimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. {1TG24: 17.9}

Hebu sasa tuziangalie kweli ambazo zimekuwa tayari historia: {1TG24: 18.1}

Hitler alifanya maandalizi yake kwa ajili ya vita katika enzi ambapo magari yalikuwa yakifurika njiani, yakienda kasi kama umeme, na yakisongana-songana katika barabara kuu; kwamba baada ya uwezo wa kijeshi wa Hitler ukivunja kila kitu vipande vipande popote alikopeleka bunduki zake kisha ilikuwa kwamba muungano walianza kujenga mitambo mikubwa ya vita; Hitler alijikwaa, kwa mfano, kwa kuanzisha vita dhidi ya Urusi wakati ali-pokuwa bado akipigana na Uingereza Kuu; ingawa Ujerumani ilishindwa vitani, lakini badala ya kukita mizizi kwa kina tangu kuanguka kwa Hitler, Uingereza badala yake inamomonyoka, na sauti za kubomoka kwa ufalme wake zinaendelea kuongezeka kila siku inayopita; Vita vya Hitler vimevunja vipande vipande dunia yote, vipande vyake na nyufa mpya zinasikika na kuonekana kila siku — kwamba zipo siasa mpya za wanamgambo kutoka ndani na kutoka nje katika kila taifa na watu. {1TG24: 18.2}

Kwa sababu maelezo ya Nahumu ya trafiki za mjini na za mashambani kwa wakati ambapo unabii wake wa vita unatimizwa yanalingana kikamilifu na hali za Vita Kuu vya 2 vya Dunia, tunahakikishiwa kwamba vita ambavyo Hitler ilianzisha vitamakoma kwa kweli wakati Ashuru unaanguka, na wakati nira yake inaondolewa kutoka kwenye shingo la watu wa Mungu. Kuanzia wakati huo kuendelea, waovu hawatapatikana tena katika kutaniko la wenye haki. {1TG24: 18.3}

Ni nini kusudi hasa la unabii wa Nahumu? Ni kuwaangazia watu wa Mungu kuhusu ishara za nyakati, kuwafan-ya waweze kujua kwamba “siku kuu na ya kutisha ya Bwana” imekaribia, kwamba kutakaswa

18

kwa kanisa, “Hukumu katika nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17) itatukia hivi karibuni, kwamba waovu ha-wataendelea kuwa kati yao tena, kwamba ukombozi wa wenye haki umekaribia, kwamba lazima wasishindwe kufanya kazi zao walizopewa na Mungu. Hakika, unabii wa Nahumu unawatambulisha waziwazi watu wa Mun-gu wa leo chini ya nira ya Mwashuru, na kuonyesha uhuru wao. {1TG24: 18.4}

La muhimu zaidi kwa yote, hata hivyo, nabii Nahumu anaeleza wazi wazi kwamba mambo haya yote yanatukia katika siku zetu, na kwamba anguko la Ashuru linatukia wakati watu wa Mungu wanamwelekea Yeye, wakati uamsho na matengenezo yanafanyika kwa ufanisi na yeye “anayetangaza amani” (Nah. 1:15). Iwapo sisi, kwa hivyo, tushindwe kuufumbata ujumbe huo, na ikiwa tunashindwa kufanya matengenezo kama unavyopen-dekeza, basi haiwezekani kuokoka siku ya Bwana. {1TG24: 19.1}

(Kwa maelezo ya kina ya kitabu cha Nahumu, jifunze Trakti Namba 14, “Utabiri wa Habari za Vita.”) {1TG24: 19.2}

19

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 23, 24

Kimechapishwa nchini Marekani

20

>