30 Apr Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 21, 22
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 21, 22
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
KANISA LINALOINGIA KWENYE NA NDANI YA KIPINDI CHA MAVUNO
WAYAHUDI WA LEO WANAOCHUKIWA SIO WAYAHUDI WANAOVUTIA WA KESHO
1
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 175, aya ya mwisho. {1TG21: 2.1}
M.B, uk. 175 — “Katika maono ya nabii Ezekieli, lilikuwapo umbo la mkono chini ya mbawa za makerubi. Hili ni kuwafundisha watumwa Wake kwamba ni uwezo wa Mungu unaowapa ufanisi. Wale ambao Mungu huwaajiri kama wajumbe Wake wasijihisi kwamba kazi Yake inawategemea wao. Wanadamu wafaji hawajaachwa kuu-beba mzigo huu wa wajibu. Yeye asiyelala, ambaye daima hufanya kazi kwa ajili ya utimilifu wa mipango Yake, ataiendeleza kazi Yake mwenyewe. Yeye atayazuia madhumuni ya watu waovu, na atayakanganya mashauri ya wale wanaofanya njama ya hila dhidi ya watu Wake. Yeye ambaye ni Mfalme, Bwana wa majeshi, aketiye kati ya makerubi, na katikati ya vita na machafuko ya mataifa Yeye bado anawalinda watoto Wake. Yeye anaye-tawala katika mbingu za mbingu ndiye Mwokozi wetu. Yeye hupima kila jaribio, Yeye hutazama moto wa ta-nuru ambao sharti uipime kila nafsi. Wakati ngome za wafalme zitapinduliwa, wakati mishale ya ghadhabu itakapoichoma mioyo ya adui Zake, watu Wake watakuwa salama mikononi Mwake.” {1TG21: 2.2}
Tutaomba juu ya nini sasa? — Nafikiri tunapaswa kuomba tujue kwamba Mungu, sio mwanadamu, ndiye kiongozi wa kazi; tujue kwamba hakuna mwanadamu kwa nafsi yake anayeweza kuiendeleza au kuizuia kazi ya Mungu; kwamba Mungu Mwenyewe pekee anaweza kuifanya ama; kwamba hatuhitaji kuhisi kwamba kazi ya Mungu inatutegemea sisi; kwamba ikiwa tunakumbuka hili siku zote, tutaweza kutembea karibu Naye. Hili, naamini, ndilo tunapaswa kuomba kwa ajili yake leo. {1TG21: 2.3}
2
KANISA LINALOINGIA KWENYE NA NDANI YA KIPINDI CHA MAVUNO
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, DESEMBA 28, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Haijalishi jinsi gani yalivyo makubwa na yenye kufanikiwa uamsho na matengenezo ambayo hata Mungu mwenyewe anaweza kuyazindua katika kanisa Lake, Maandiko yanaweka wazi kwamba wote wadhambi na wa-takatifu watakuwa kanisani hadi kwa mavuno. Hakuna yeyote anayehitaji kujisifu kwamba washiriki wa kanisa lake ni watakatifu wote, kwamba wote wako na umoja. Ikiwa kwa kweli wanao umoja, basi ni lazima iwe kwamba wote ni magugu, kwamba hakuna mtakatifu kati yao; kanisa hilo kwa hakika sio kanisa ambalo Kristo hunena katika Neno Lake. Iwapo chochote ni wazi katika Biblia ni hili jambo moja. Sasa hebu tufungue sura ya kumi na tatu ya Mathayo. {1TG21: 3.1}
Mat. 13:24, 25 — “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.”
Sababu iliyotolewa kwa ajili ya magugu kuwa miongoni mwa ngano ni kwamba “watu walilala.” Dhahiri basi, kama mtu angaliendelea kuwa macho, Adui asingalikuwa ameyapanda magugu. Sasa, ili kujua ni nini kinacho-maanisha watu kuwa macho, tutasoma kutoka sura ya tatu ya Mathayo. {1TG21: 3.2}
Mat. 3: 5, 6 — “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na
3
Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku waki-ziungama dhambi zao.”
Andiko hili linaweka wazi kwamba Yohana alibatiza wengi, na kwamba wale aliowabatiza walikuwa tu wale walioungama dhambi zao. {1TG21: 4.1}
Aya ya 7, 8 — “Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, ali-waambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba.”
Ingawa hawa walikuwa makundi maarufu ya siku za Yohana, yeye hakukataa tu kuwabatiza, lakini pia waziwa-zi na kwa upole aliwapa kuelewa kwamba ubatizo sio kitu cha kufunikia dhambi, lakini kitu cha kuziosha. Ali-weka wazi kwamba hakuwa katika shughuli ya kuwafanza wanafiki. Yohana hakuacha shaka katika mawazo yao kwamba Mungu hakuwa anawahitaji wao, bali kwamba walikuwa wanamhitaji Yeye. Mafarisayo na Masadukayo kisha wakaenda zao kwa ufahamu kamili kwamba mhubiri mkuu wa siku hiyo aliye kuwa macho hakuchukuliwa na umaarufu wao, sembuse na nasaba yao. Kwa mtazamo wa azimio thabiti la Yohana, na ukw-eli kwamba Bwana alisema hakuna nabii mkuu kuliko yeye aliyekuwa ameinuka, tunajua kwamba Yohana alikuwa macho kabisa, na wahubiri wote wanapaswa kuwa hivyo. {1TG21: 4.2}
Sisi kama washiriki wa kanisa, pia, tunapaswa kuwa macho kama ilivyokuwa Yohana, na imara kama Ayubu, kuweza kusema: “Ingawa Yeye ataniua, bado nitamtegemea ….” Ayubu 13:15. {1TG21: 4.3}
Mat. 22: 9-12 — “Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.
4
Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.
“Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.” {1TG21: 5.1}
Ingawa watumwa wa Mungu wawe macho na kufanya kazi yao sawa sawa, bado baadhi ya washiriki wanaweza kushindwa kujivika vazi la harusi. Vazi, unajua, ni kitu cha kufunika kwa nje ya mwili. Vazi, kwa hivyo, linawakilisha mwenendo wa kila siku kama wa Kristo — haki ya Kristo katika maisha ya kila siku ya mmoja. {1TG21: 5.2}
Ukweli kwamba mtu katika mfano huo alipumbaa alipoulizwa, “Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi?” Unaonyesha kwamba alikuwa na hatia ya kupuuza, sio ya kutojua! Hakuwa na udhuru, na alijua. {1TG21: 5.3}
Hebu kurudi kwa– {1TG21: 5.4}
Matt. 25: 1-5 — “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta kati-ka vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.”
Tena inaonekana wazi kwamba ushirika wa kanisa umegawanyika katika makundi mawili, wenye hekima na wapumbavu. Wenye hekima huwa hawabahatishi; wao huyasaka daima
5
mafuta (Kweli) na wao huvijaza vyombo vyao Nayo kwa fursa ya kwanza. Wapumbavu, hata hivyo, huwa ha-wana haja ya zaidi ya yale yaliyomo katika taa zao; huridhika na yale ambayo tayari wanayo. {1TG21: 5.5}
Mafuta, kitu ambacho huangaza mbele ya njia ya mtu, bila shaka ni mfano wa Ukweli wa kinabii, Ukweli ambao huunurisha moyo kwa kuufunua wakati wa baadaye. Kusema kwa uthabiti, taa iliyojazwa mafuta huashiria hifadhi ya mtu binafsi ya Kweli katika utendaji, Kweli ambayo hukidhi mahitaji yake kwa wakati uliopo tu. Ma-futa ya ziada katika vyombo, kwa hivyo, huwakilisha Ukweli wa ziada, Ukweli ambao huchukulia pale ambapo Ukweli wa zamani huachia. Kwa maneno mengine, mafuta katika taa na mafuta katika vyombo huwakilisha kweli mbili zilizofunuliwa, kwa nyakati mbili tofauti, mmoja ukiufuata mwingine. Kwa mfano, wakati ambapo Hukumu kwa Wafu ni Ukweli katika utendaji, Hukumu kwa Walio Hai ni Ukweli utakaoingia katika utendaji mara tu Hukumu kwa Wafu itakapokuwa imekwisha. {1TG21: 6.1}
Bila shaka, mafuta ambayo yametumika, kama vile mafuta katika taa za wanawali, huwakilisha Kweli iliyopita, Kweli ambayo imekamilisha azimio lake; bali mafuta katika vyombo huwakilisha Kweli iliyo tayari kuamilishwa na kufanywa iangaze mara moja baada ya mafuta katika taa kutumika. Kwa sababu wanawali kumi huwakilisha ushirika wa kanisa wakati wa Hukumu kwa Wafu, mafuta katika taa huwakilisha wazi ukweli wa Hukumu kwa Wafu. Mafuta ya ziada, ambayo yako katika “vyombo” lazima, kwa hivyo, yawakilishe ukweli wa Hukumu kwa Walio Hai, Ukweli wa ziada (M.A. 277). Dhahiri basi, taa zilizoishiwa mafuta huwakilisha Hukumu kwa Wafu inapokwisha, na mafuta katika vyombo huwakilisha Kweli ya Hukumu kwa Walio Hai inapoingia katika utenda-ji. {1TG21: 6.2}
6
Kwa sababu wote kumi walikuwa na mafuta katika taa, lakini nusu yao tu walikuwa na mafuta ndani ya vyom-bo, nembo inaonyesha waziwazi kwamba, kama siku zote, ushirika wote wa kanisa hawakuupokea ujumbe wa Hukumu kwa Walio hai. Wanawali wapumbavu walikuwa wameridhika na Kweli waliyokuwa wamepata wali-pojiunga na kanisa ambalo lilikuwa linatangaza ujumbe wa Hukumu kwa Wafu, lakini walishindwa kujifahamisha na ujumbe wa ziada — ujumbe wa Hukumu kwa Walio Hai. Hatimaye, baada ya hitaji kwa ajili Yake kuwa lazima, wakaanza kuutafuta lakini haukuwatendea mema, walikuwa wamechelewa sana kuupata. {1TG21: 7.1}
Hawa waliachwa nje na magugu tu kwa sababu walimruhusu Ibilisi kupanda mbegu za upumbavu katika mioyo yao, mbegu za kutosheka (uvuguvugu) na ukweli wa kwanza ambao kwa huo walijiunga na kanisa; hivyo kima-kosa walijihisi hawana haja ya nuru ya ziada kutoka kwa Bwana. Lakini wakati unabii ulianza kutimia zaidi ya upeo wao wa maarifa yaliyofunuliwa ya Mungu, na walipoyaona matukio ya Injili yakijiumba yenyewe kinyume na matarajio yao, wakawa na hofu na kuchanganyikiwa, walijiona wenyewe katika giza. {1TG21: 7.2}
Somo hili ni hakika kabisa: Wale ambao daima hujihisi “matajiri, na wamejitajirisha, wala hawana haja ya kitu, hawataufika “mlango” kwa wakati. {1M21: 7.3}
Mbali na magugu kati ya ngano, wapo wasio na kazi, watu wasio waamilifu ambao watatupwa nje na kuharibi-wa pamoja na magugu. Hebu tusome– {1TG21: 7.4}
Mat. 25: 14-30 — “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa
7
mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akas-afiri.”
“Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. {1TG21: 8.1}
“Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. {1TG21: 8.2}
“Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. {1TG21: 8.3}
“Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navu-na nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka
8
fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” {1TG21: 8.4}
Kutoka kwa mfano huu inaonekana kwamba wakati Mkristo analala, Shetani huja na kupanda mbegu za uzembe moyoni mwake ili kumsababisha atupwe nje na magugu. Kwenye mwanzo wa mavuno, kwa hivyo, daraja hili la magugu ni la kwanza kuonekana hivyo. Ni wakati mzuri wa kujifunza kwamba dini sio dawa ya kutia usingizi. {1TG21: 9.1}
Bado liko daraja jingine la washiriki wa kanisa ambao kwa njia tofauti huanguka waathirika pamoja na magugu. Hili tutaliona kutoka– {1TG21: 9.2}
Mat. 25: 31-46 — “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.”
“Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; naliku-wa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni,
9
mkanijia. {1TG21: 9.3}
“Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tu-lipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? {1TG21: 10.1}
“Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. {1TG21: 10.2}
“Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” {1TG21: 10.3}
Dhambi mashuhuri ya daraja la mbuzi wanaodai kuamini ni kwamba wote ni kwa ajili ya ubinafsi wao na hakuna yeyote kwa ajili ya wengine. Daraja la kondoo ni la kinyume kwa tabia. Kwa sababu wale wanaofanya kazi ya upendo hawapaswi kuifanya kuwa wonyesho — sio kuruhusu mkono wa kushoto kujua kile mkono wa kulia un-afanya (Mat. 6: 3) — na maadamu mfumo wa kazi ya ukarimu kama hii imeonyeshwa waziwazi katika Uchumi wa Waebrania, tungefanya vizuri kutazama humo
10
kwa ajili yake: “Kwa kuendeleza kukusanyika kwa watu kwa ajili ya huduma ya kidini, pamoja na kuwakimu maskini, zaka ya pili ya ongezeko lote ilihitajika. Kuhusu zaka ya kwanza, Bwana alitangaza, “Nimewapa wana wa Lawi sehemu ya kumi katika Israeli.” Lakini kuhusiana na ya pili, aliamuru, ‘Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana Mungu wako daima.” Hivyo zaka, au ulingano kifedha, iliwapasa kwa miaka miwili kuileta mahali ambapo hekalu lilikuwa limesimamishwa. Baada ya kuwasilisha sadaka ya shukrani kwa Mungu, na fungu maalum kwa kuhani, walioitoa walipaswa kutumia salio kwa ajili ya karamu ya kidini, ambayo Mlawi, mgeni, yatima, na mjane walipaswa kushiriki. Hivyo maakuli yaliandaliwa kwa ajili ya sadaka za shukrani na karamu katika sherehe za kila mwaka, na watu walikaribishwa kwa jumuiya ya makuhani na Walawi, ili waweze kupokea maagizo na kuhimizwa katika utumishi wa Mungu.” — Mababu na Manabii, uk. 530. Ili kazi hii iendeshwe kwa utaratibu na hazina ya Bwana kwa njia ya zawadi na sadaka za hiari, wakati mwingine huitwa zaka ya pili, hatuwezi ila kufanya vivyo hivyo kama tunahitaji kupata kibali kwa Mungu. Sasa turudi kwa– {1TG21: 10.4}
Mat. 13:44 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoio-na, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.”
Aya ya 45, 46 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.”
11
Mifano hii inaonyesha waziwazi kwamba wale wasiojali kuwekeza kila kitu wanachomiliki, likiwapo hitaji, kuu-pata Ufalme, watatupwa nje na magugu. {1TG21: 12.1}
Aya ya 47, 48 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.”
Juya linalotupwa baharini kwa kawaida huwanasa samaki wazuri na wabaya, samaki wadogo na wakubwa. Lakini samaki, kama viumbe vingine vyote vilivyo hai, huenda katika familia, kila namna na aina yake, na hivyo kila wakati juya linatupwa, hunasa familia za samaki. Kwa hivyo ni kwamba juya la injili katika matukio mengi huwaleta ndani familia na jamaa wote katika mnaso mmoja; yaani, kama wazazi wanapoipokea injili ya Kristo, pamoja nao mara nyingi huletwa watoto, na hata jamaa na marafiki. {1TG21: 12.2}
Samaki wabaya huwakilisha wale ambao, bila maarifa halisi, imani na uongofu wao wenyewe bali kupitia hisia na ushawishi wa wengine hujiunga na kanisa. Kwa hivyo ni kwamba wale ambao hawajajifunza kwa bidii, kwa moyo wote na kwa bidii kuzingatia kanuni za Kristo wanatupwa nje, huko kuangamia pamoja na magugu. Wote ambao ni wavivu sana kujifunza, na ambao humpa Ibilisi nafasi ya kupanda mbegu za ushetani ndani ya mioyo yao, na kuwafanya waamini kwamba mhubiri au mchungaji atawapitisha katika Malango ya Lulu, pasipo kuwa na uzoefu wao wenyewe, wamehadaiwa uzima wa milele; wao badala yake watapata kifo cha milele. {1TG21: 12.3}
Kweli kabisa, Roho wa Mungu husababisha watu kuwa kitu kimoja, na roho wa Shetani huwafanya kuwa kitu kingine, lakini tofauti ni ya kuonekana
12
tu kama wakati wa mavuno unakaribia — wakati Ukweli wa mavuno umefunuliwa. {1TG21: 12.4}
Kutoka kwa mifano hii rahisi unakuja ukweli kwamba Shetani huyainua magugu kanisani na hujaribu daima kwa uwezo wake wote kuyadumisha ndani yake. Kwa nini? — Hebu tupate jibu katika Ufunuo 12 — {1TG21: 13.1}
Ufu. 12:13 — “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mto-to mwanamume.”
Wakati Ibilisi alipoona kwamba hakuwa tena na kibali cha kuingia Mbinguni, alienda kulitesa kanisa baada ya kumzaa “mtoto mwanamme,” Kristo. Joka, kwa hivyo, atalitesa kanisa katika kipindi chake cha Kikristo. {1TG21: 13.2}
Aya ya 14 — “Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.”
Kwa sababu ya mateso, kanisa lilipewa njia ambazo lingeweza kuruka kutoka nchi ya ahadi (shamba la miza-bibu) hadi katika nchi za Mataifa (nyikani). {1TG21: 13.3}
Aya ya 15 — “Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.”
Mwanzoni, nyoka alilitesa kanisa, lakini alipoona kwamba kanisa bado lilikua na kustawi, alibadilisha mbinu zake, na kuanza badala yake kuwatesa Wapagani ambao hawakutaka kujiunga na kanisa, na kuwainua wa-chungaji ambao angaliwatumia kumletea mafuriko ya wasio
13
waongofu ambao angeweza kuwatumia kulikafirisha kanisa, ili lisiweze kuwafanya kuwa Wakristo. {1TG21: 13.4}
Aya ya 16 — “Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.”
Hivyo ndivyo kanisa linatakaswa na ndivyo magugu yanavyoangamizwa. Kama magugu wanachomwa; kama wafanyakazi wasio na faida wanatupwa katika giza la nje huko kulia na kusaga meno yao; kama wageni wasio-stahili kwa ajili ya harusi wanafungwa mikono na miguu na kutupwa katika giza la nje; kama wanawali wap-umbavu wanazuiliwa kuingia; kama mbuzi wanatumwa kwa adhabu ya milele; kama mafuriko ya joka, wanamezwa na ardhi. Lakini jambo halisi ambalo linafanyika kwa wote pamoja, linaelezewa kikamilifu katika unabii wa Ezekieli, sura ya 9. Hebu tufungue — {1TG21: 14.1}
Ezek. 9: 1-11 — “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
“Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandi-shi kiunoni. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.” {1TG21: 14.2}
14
“Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msim-karibie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee wali-okuwa mbele ya nyumba. Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. {1TG21: 15.1}
“Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? {1TG21: 15.2}
“Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni. Nami, jicho langu hali-taachilia, wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao. Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.” {1TG21: 15.3}
Ahadi ya kuutakasa Yerusalemu, Yuda na Israeli husimama kwa uhakika kama ahadi yoyote katika Neno. Majina, Yerusalemu, Yuda, Israeli unajua, hayawezi kutumika kwa chochote ila kwa kanisa, mahali ambapo kila mtu anapaswa kuomboleza na kulia dhidi ya machukizo. Wale ambao hawaombolezi na kulia wataachwa bila alama, na kisha malaika walio na usimamizi juu ya kanisa watawapiga kila mmoja wao — “wazee na vijana,
15
wajakazi wote na watoto wachanga, na wanawake.” Wale tu walio na alama watasazwa. Wao ni masalia. Ma-laika hivi ndivyo watakavyoshughulikia ngano na magugu. {1TG21: 15.4}
Naam, lazima uwepo uondoaji safi wa kila aina ya gugu kama vile zamani ulikuwepo uondoaji safi wa wazaliwa wote wa kwanza katika nyumba ambazo hazikupaka miimo ya milango kwa damu ya kafara jioni ya Pasaka katika nchi ya Misri. Ndivyo itakavyokuwa mwanzoni mwa mavuno, katika utakaso wa kanisa: Malaika watam-piga kila mmoja anayekuza machukizo “kati yake.” {1TG21: 16.1}
Utakaso huu wa kina utatukia lini? Kwa ajili ya jibu tufungue Zefania, sura ya 1. {1TG21: 16.2}
Zef. 1: 2, 3 — “Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema Bwana. Nitam-komesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo makwazo pamoja na wabaya; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, ase-ma Bwana.”
Hapa ni ahadi kwamba Bwana ataitakasa kabisa nchi, na nina uhakika hakuna hata mmoja wenu atasema kwam-ba unabii huu umewahi kutimizwa. {1TG21: 16.3}
Aya ya 4, 5 — “Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu.”
16
Sio tu nchi bali watu watakaoijumuisha nyumba ya Yuda, watatakaswa: Itakuwapo nchi safi na watu wasafi pia. {1TG21: 17.1}
Aya ya 6 — “Na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata Bwana; na hao wasiomtafuta Bwana, wala kumwulizia.”
Aliyekengeuka na asiye jali, wale wasio na msimamo na wale ambao hawaoni hitaji la Mungu, wataangamia pamoja na magugu. {1TG21: 17.2}
Aya ya 7 — “Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya Bwana i karibu; Kwa kuwa Bwana ameweka tayari dhabihu, Amewatakasa wageni wake.”
Hii ndiyo iliyotarajiwa kwa muda mrefu siku kuu na ya kutisha ya Bwana. {1TG21: 17.3}
Aya ya 8 — “Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya Bwana, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfal-me, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.”
Aya ya 9-11 — “Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu. Na katika siku ile, asema Bwana kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani. Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha wamekatiliwa mbali.”
Kuanguka kwa nguvu kutakuwa kutoka kwa malango yote ya samaki na kutoka vilimani — kutoka ardhini na kutoka baharini. Wote, watumwa ambao huleta uhasama na udanganyifu
17
juu ya nyumba za mabwana wao, na mabwana waovu wenyewe, wataadhibiwa. {1TG21: 17.4}
Aya ya 12-18 — “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu wa-tu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyum-ba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake. Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibi-fu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata wa-takwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.”
Wakati wa siku ya Bwana unaonyeshwa kwa ongezeko la “ghadhabu,” “taabu,” “dhiki,” “unyaufu,” “uharibifu,” “giza” na “utusitusi” — wakati ambapo hakuna mtu anayejua nini cha kufanya ili kuepusha maafa, wakati wa ho-fu nyingi hata kwa miji yenye ngome. Hadi sasa ninavyojua haijawahi kuwepo kama hii. Hali ya dunia ya leo ndiyo hali ya pekee ambayo inakabiliwa na changamoto ya unabii huu. Maadamu hii ni kweli, basi hii ndiyo siku ambayo
18
Bwana atautafuta Yerusalemu kwa mishumaa. Hii ndiyo siku ambamo Yeye atawatakasa watu Wake kutoka kwa dhambi na wadhambi. Ni “siku kuu na ya kutisha ya Bwana.” {1TG21: 18.1}
Mal. 3: 1-5 — “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani ata-kayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitaku-wa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wam-woneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.”
Je, Hatupaswi kujiangalia kuwa wenye bahati mno duniani kwa kuyajua mambo haya kimbele? Je, tusiweze ku-wa na furaha na wenye kushukuru ya kuwa tumeonywa kimbele kwamba tumefika karibu na wakati wa mavu-no, na kwamba tumepewa fursa ya kujiandaa kwayo? Je, tusiweze kuwa na furaha kwamba hatujaachwa gizani, na kwamba sasa tunaonyeshwa wazi wazi kwamba haya ni masaa ya kufunga kipindi cha kabla ya mavuno, kwamba mavuno yataanza hivi karibuni? {1TG21: 19.1}
19
Ufu. 18: 1 — “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.”
Utimilifu wa andiko hili ni kile kinachoitwa Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu. Lakini kumbuka kwamba dunia yote inaangazwa kwa utukufu wake. Hebu sasa tutilie maanani kile kinachotokea baada ya Ujumbe wa Malaika Watatu kuenea katika nchi, baada ya nchi kuangazwa hivyo na utukufu wa malaika. {1TG21: 20.1}
Aya ya 2 — “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa mas-kani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.”
Kumbe, baada ya dunia kuangazwa, basi inakuwa kwamba Babeli unaanguka. Kwa udhahiri, basi, Babeli bado haujaanguka. Kwa kweli Babeli bado hata sasa haujakuja kuwapo, kwa maana bado hajampanda (kutawala) mnyama (ulimwengu). Angalia Ufunuo 17 na Trakti # 12, “Dunia Jana, Leo, Kesho.” {1TG21: 20.2}
Aya ya 4 — “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”
Hii sauti kutoka mbinguni, unaona, inakuja kwa watu wa Mungu baada ya nchi kuangazwa kwa Kilio Kikuu cha malaika. Mzigo wa Sauti ni kwamba watu wa Mungu wanapaswa kutoka Babeli ili wasishiriki dhambi zake, na wasipokee mapigo yake. Ikiwa kwa simulizi hili lazima wao watoke Babeli, basi ni lazima iwe kwamba mahali ambapo wanaitwa kwenda ni huru kwa dhambi na hivyo kuwa huru kutoka kwa hatari ya
20
mapigo. Na hapo pangaliweza kuwa wapi ila katika nchi iliyotakaswa na kanisa la Mungu, ambapo hakuna tena dhambi na wadhambi kuhatarisha amani ya watu wa Mungu? Bure, hakika, ingalikuwa iwapo watu wangaliitwa kutoka sehemu moja ya dhambi na kuletwa katika sehemu nyingine ya dhambi. Kwa udhahiri kabisa ni kwamba utakaso wa kanisa (“kutakaswa” – Dan. 8:14; Hukumu ya Walio Hai — 1 Pet. 4:17) itatukia kabla ya Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu kuanza ulimwenguni , kabla ya watu wa Mungu kuitwa watoke Babeli. {1TG21: 20.3}
“Ujumbe wa malaika wa tatu utaiangaza nchi kwa utukufu wake; lakini wale tu ambao wameyastahimili majari-bu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza wakati utakapokuwa ume-umuka na kuingia katika kilio kikuu.” — “Mapitio na Kutangaza,” Novemba 19, 1908. {1TG21: 21.1}
Wakristo wengi wanajua kwamba yapo madaraja mawili katika kanisa — ngano na magugu — lakini wachache, ikiwa wapo, wanaonekana kuwa wanaojali. Sisi, kama wana matengenezo hata hivyo, hasa kwa sababu tume-pewa nuru hii kubwa juu ya suala hili, hatuwezi kumudu kuwa wasiojali. Sasa kwa ueledi tunaweza kuchagua kuwa “ngano” au kuchagua kuwa “magugu.” Iwapo baada ya kuujua Ukweli huu, wengine wachague kuwa “magugu,” wao, bila shaka, hawataweza kuwa wamepata kitu na wasistaajabu watakapotua Jahanamu. {1TG21: 21.2}
Kwa wakati wa kazi na mtaji vinagongana, basi inakuwa kwamba Yerusalemu (kanisa) utatafutwa, kwa mfano, na mishumaa. Kisha, watu ambao wametulia ndani ya nyumba zao, wale wanaotenda kana kwamba Bwana ameiacha nchi wataipata adhabu yao. {1TG21: 21.3}
Sio tu tunaona na kuhisi siku ya Bwana ikijongea ila hata kuisikia Sauti Yake. {1TG21: 21.4}
21
WAZO LA SALA
Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 177. Sasa tunaanza sura mpya, “Sio Kuhukumu bali Kutenda.” Ni kwa msingi wa andiko ambalo linasema, “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.” {1TG22: 22.1}
M.B, uk. 177 — “Jitihada za kupata wokovu kwa matendo ya mtu mwenyewe, bila shaka huwaongoza watu ku-rundika ulipizi wa kibinadamu kama kizuizi dhidi ya dhambi. Maana, kuona kwamba wao wanashindwa kuishi-ka sheria, watatunga sheria na kanuni zao wenyewe kujilazimisha wazitii. Zote hizi huzigeuza nia zao mbali na Mungu hadi kwa ubinafsi. Upendo Wake hufa moyoni, na kwa hivyo huangamiza upendo kwa ajili ya wana-damu wenzake …. Mazingira ya ubinafsi na lawama finyu hukomesha hisia za ungwana na ukarimu, na hu-wasababisha wanadamu kuwa waamuzi wa ubinafsi na wapelelezi wa kudokoadokoa…. {1TG22: 22.2}
“Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo.” Hatuwezi kujua yaliyo moyoni. Sisi wenyewe ni wakosefu, hatuja-hitimu kukaa hukumuni juu ya wengine. Watu wafaji wanaweza kuhukumu tu kwa mtazamo wa nje. Kwake Yeye pekee ajuaye za siri chemchemi za utendaji, na anayejishughulisha kwa upole na kwa huruma, ndiye ali-yepewa kuamua kesi ya kila nafsi….’” {1TG22: 22.3}
Ni kama nini somo la ajabu andiko hili linashikilia kwa ajli ya Wakristo wote, na hasa kwa ajili yetu wenyewe. Na sasa hebu tuombe kwamba Mungu atusaidie kutowahukumu wengine; tusitafute makosa, tusiifanze milima kutoka kwa vilima vya fuko, na tusilaumu; na tusijisimamishe kama vigezo. Hebu tuombe ili tuweze kujua kwamba Mungu ametuita tuufundishe Ukweli, sio kuwasukuma watu ndani Yake. La, sio zaidi ya kuwafukuza watoke ndani Yake. Mungu amemuuliza kila mmoja kuwa mlinzi tu wa matendo yake mwenyewe. Iwapo tuta-fanya hili mikono yetu itajaa kamili. bila nafasi kwa ajili ya mengine. Mlinzi wa pekee juu ya watu Wake Mungu ameweka daima ni manabii Wake, chini ya usimamizi Wake Mwenyewe. {1TG22: 22.4}
22
WAYAHUDI WA LEO WANAOCHUKIWA SIO WAYAHUDI WANAOVUTIA WA KESHO
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JANUARI 4, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Tuko hapa kujifunza Zefania 2, kuanzia aya ya kwanza. {1TG22: 23.1}
Zef. 2: 1, 2 — “Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilotakikana; kabla haijaletwa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwana.”
Kati ya aya zote katika sura hii, hizi mbili ni ngumu zaidi kuhakiki. Miaka michache iliyopita nalimsikia mhubiri akitoa ufafanuzi kwa aya tatu za kwanza, alizitenga kutoka kwa zingine za sura na kuziunganisha na vifungu vingine vya Maandiko. Alitoa hotuba nzuri, na akajaribu kuonyesha kwamba “taifa” lililotajwa katika aya ya 1 ni kanisa la Mungu na kwamba “amri” ni ya mnyama wa pembe mbili wa Ufunuo 13: 15-17. Somo hilo liliwasi-lishwa vyema na mawazo aliyoyatoa yalionekana kuwa ya kuaminika kabisa, lakini sasa kama tunavyojua kwamba Maandiko hayawezi kueleweka kwa usahihi yakiwa yametengwa kutoka kwa mwendelezo wake, tunahitaji kujifunza aya hizi kwanza kwa uhusiano na sura yenyewe. {1TG22: 23.2}
Hebu tukumbuke kwamba taifa linalotajwa hapa litajikusanya
23
lenyewe pamoja; kwamba halitakikani; kwamba gadhabu ya Bwana itaanguka juu yake; na kwamba litajikusanya lenyewe pamoja kabla ya amri kutolewa na kabla ya hasira ya Bwana haijaliangukia. {1TG22: 23.3}
Ni nini kinachofanya taifa hili kujikusanya pamoja? — Hakika sio amri na hasira ya Bwana, kwa maana hii itaku-ja baada ya kujikusanya pamoja. “Amri” hakika haiwezi kuwa amri ya mnyama, kwa maana hakuna hata wazo katika andiko hili ambalo linaonyesha hivyo; lakini hakika linaonyesha kwamba amri sio nyingine isipokuwa amri ya Bwana — hasira kali ya Bwana katika siku ambayo itapita kama makapi. {1TG22: 24.1}
Kwa mujibu wa aya inayofuata, huku kujikusanya pamoja kwa taifa lisilotakikana, ni ishara kwa watu wa Mun-gu, ikiwahimiza waendelee zaidi kuutafuta unyenyekevu: {1TG22: 24.2}
Aya ya 3 — “Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.”
Wakati taifa hili la kuhukumiwa linaanza kujikusanya pamoja kisha inakuwa, zaidi kuliko awali, kwamba wanyenyekevu wa dunia wanahitaji kuutafuta unyenyekevu. {1TG22: 24.3}
Wanyenyekevu wa dunia ni wale ambao wametenda hukumu za Bwana, ambao wameutangaza ujumbe wa siku kuu na ya kutisha ya Bwana. Wao ni watu Wake, kanisa Lake. Taifa lisilotakikana, kwa hivyo, ni kundi moja la watu, na wanyenyekevu wa dunia, kanisa, wale wanaofichwa katika siku ya ghadhabu ya Bwana ni kundi la watu wengine. Moja linajikusanya pamoja, lile lingine linatafuta unyenyekevu. Kwa hivyo, “taifa” la aya ya 1 na 2 sio kanisa
24
Lake, ila watu wa aya ya tatu ndio watu Wake, kanisa Lake. {1TG22: 24.4}
Hebu sasa tusome aya ya 1 na 2 kwa uhusiano
na aya ya 4 na 5, tukiacha aya ya 3, aya inayorejelea kanisa. {1TG22: 25.1}
Aya ya 1, 2, 4, 5 — “Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilotakikana; kabla haijaletwa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwana …. Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ash-dodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang’olewa. Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la Bwana li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.”
Aya ya nne kwa hakika inamaanisha kwamba “taifa” hili litajikusanya pamoja katika miji ya Gaza, Ashkeloni, Ashdodi, na Ekroni, katika nchi ya Wafilisti, katika nchi ya Kanaani – katika Palestina. {1TG22: 25.2}
Kwa mtazamo wa ukweli kwamba maandiko haya sasa yanafunuliwa, na pia ukweli kwamba liko kundi moja la watu tu, taifa moja (wazawa wa waandishi, makuhani, na Mafarisayo wa kale waliomkataa Bwana na ambao hata hadi leo hawajampokea Yeye, ndio ambao hawatakikani bila shaka popote duniani) ambalo sasa linafanya yote liwezalo kujikusanya pamoja huko Palestina — kwa mtazamo wa yote haya, Wayahudi wa leo ndilo taifa lisilotakikana. Juu yake, kwa hivyo, hasira ya Bwana itaanguka iwapo linaendelea kumkana Kristo. Naam, Mya-hudi aliyechukiwa ulimwenguni kote ndilo taifa pekee ambalo limetawanyika katika ulimwengu wa Mataifa, na ndilo la pekee ambalo sasa linajikusanya pamoja ndani ya Palestina. {1TG22: 25.3}
25
Zaidi ya hayo, katika aya hizi, kweli mbili zinaonekana wazi kabisa: (1) kwamba Wayahudi wanajitahidi bure kujisimamisha katika Nchi ya Ahadi; (2) kwamba sisi ambao tunaupeleka ujumbe wa siku kuu na ya kutisha ya Bwana tunashauriwa kuutafuta unyenyekevu na haki, kwa sababu hiyo tu “tutafichwa katika siku ya ghadhabu ya Bwana,” yaani, kuutangaza tu ufahamu wa ujumbe hautatuokoa, inapasa yawepo matendo yanayoambatana nao. {1TG22: 26.1}
Hebu sasa tuunganishe aya ya 3 na aya ya 6 na 7, aya ambazo zinahusishwa kwa watu wa Mungu, wanyenyekevu. {1TG22: 26.2}
Aya ya 3, 6, 7 — “Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana …. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana Bwana, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.”
Sasa, ukweli kwamba Bwana atawaangamiza wakazi wote katika nchi ya Wafilisti (Zef. 2: 5), na kwa wakati uo huo kuifanya nyumba za “wachungaji, na mazizi ya makundi,” unaonyesha kwamba Yeye kwanza atawafukuza waovu wote kutoka katika nchi hiyo, wale wote ambao hawatafuti unyenyekevu, kisha Yeye ataisimamisha “nyumba ya Yuda” ndani yake. {1TG22: 26.3}
Aya ya 8 — “Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao.”
26
Sio tu Wayahudi wasioamini, lakini pia Waarabu wasioamini wanaowapinga wanyenyekevu, watafagiliwa mbali kutoka katika nchi. {1TG22: 27.1}
Aya ya 9 – “Basi kama niishivyo, asema Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi..”
Wakati Moabu na Amoni wanakuwa kama Sodoma na Gomora, wakitoweka, uhamisho wa watu wa Mungu unageuzwa. Wanakuwa taifa huru na kuumiliki utajiri wote wa watu pande zote. {1TG22: 27.2}
Aya ya 10, 11 — “Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa Bwana wa majeshi, na kujitukuza juu yao. Bwana atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.”
Aya ya 12, 13 — “Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu. Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pa-kavu kama jangwa.”
Aya ya 14 — “Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtaku-wa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.”
Nani anayetaka kuupuuza ukweli kwamba hali hizi
27
ni dhahiri kabla ya milenia? Zaidi ya hayo, unabii huu unaonyesha kwamba kufanywa upya kwa ufalme wa kale wa Yuda kitakuwa kitu halisi, sio kitu cha kuwaziwa. Raia wake watakuwa watu halisi, sio mizuka. Sasa tuna-weza kuona kwamba msemo wa kawaida, “kwenda mbinguni,” humaanisha kwanza kwenda katika Nchi ya Ahadi, huko ili tufae jumuiya ya wasafi na wa milele. {1TG22: 27.3}
Aya ya 15 — “Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa pasipo kufikiri, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.”
Mji mkuu wa Ashuru (dola ambayo huwatawala watu) utakuwa ukiwa. Ninawi huu ni dhahiri uakisi wa Ninawi wa kale, kama vile Babeli wa Ufunuo ni uakisi wa Babeli wa kale. {1TG22: 28.1}
Muhtasari wa sura hii ni huu: Wayahudi waliochukiwa wa leo hawatakuwa Wayahudi wanaovutia wa kesho. Njia ambazo Wayahudi sasa hufuatilia kupata kibali cha kuingia Palestina sio njia ambazo zitawasimamisha huko milele hata kama wataweza kufanikiwa kufika huko. Wayahudi wa pekee na Waarabu ambao wataweza kusalia katika nchi hiyo watakuwa wale wanaomtafuta Bwana, Mungu wa Musa. {1TG22: 28.2}
Na watu wa pekee ambao wataingia huko ni wale ambao watakaa huko. Nchi hiyo imehifadhiwa kwa ajili ya wa uakisi ufalme wa Yuda. Taifa na ufalme ambao hautamtumikia “wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibi-wa kabisa.” Isa. 60:12. {1TG22: 28.3}
Kwa sababu sasa tunashauriwa kwa dhati na moja kwa moja
28
kuutafuta unyenyekevu na haki, tusidhubutu kuipuuza fursa yetu. Zaidi ya hayo, hatujaachwa kukisia juu ya kile kinachohitajika kwetu ili tuweze kujiandaa kwa ajili ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana. Bali tukumbuke kwamba ikiwa tutabuni vikwazo vyetu wenyewe, kanuni ambazo kwazo mara moja tutajilazimishia utiifu kwa Neno kulingana na maoni yetu wenyewe, tutakuwa tunatenda sio kitu kingine isipokuwa haki yetu wenyewe. Hatupaswi kuwa kama Mafarisayo wa zamani, wala tusiwahukumu wengine kwa viwango vyetu vilivyopen-dekezwa na wanadamu. Hatupaswi kuketi juu ya kiti cha hukumu na kutoingilia dhamiri ya mtu mwingine, sio kuwahukumu wengine katika masuala yaliyo kati ya nafsi na Mungu. Yote tunayoitiwa kufanya ni kufundisha na kutekeleza Ukweli wa leo, kuwaruhusu watu kufanya uamuzi wa nia zao wenyewe kwa ajili au dhidi Yake. Hatupaswi kuwalazimisha katika kitu chochote. {1TG22: 28.4}
Hebu tukumbuke kwamba ni kuhusu tu roho kama hii na mazoea kama hayo ya kuziingilia dhamiri za wengine ambapo Yesu alisema, “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi” (Mat. 7: 1). Hatuna haki ya kushinikiza maoni na mitazamo yetu juu ya wengine. Kwa sababu tu wengine hawafikiani matarajio na maadili yetu, hasha sio sababu nzuri ya kuwahukumu ili kuwasaidia. Mbali na hilo. “Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.” 1 Kor. 4: 5. {1TG22: 29.1}
“… Maisha yao yangalikuwa yautukuze uwezo wa Mwokozi ambaye angeweza kuwahesabia haki kwa haki Yake. {1TG22: 29.2}
“Lakini hatua kwa hatua badiliko lilikuja. Waamini walianza kutafuta makosa ndani ya wengine. Walifikiria juu ya makosa, walitoa nafasi kwa lawama za ukatili, walipoteza taswira ya Mwokozi na upendo Wake. Wakawa na juhudi
29
zaidi kuhusiana na sherehe za nje, zaidi hasa juu ya nadharia kuliko utendaji wa imani. Katika bidii yao ya ku-wahukumu wengine, waliyasahau makosa yao wenyewe. Waliupoteza upendo wa undugu ambao Kristo alikuwa amewaamuru, na la kuhuzunisha zaidi ya yote, hawakuwa na ufahamu wa hasara yao. Hawakung’amua kwamba furaha na shangwe zilikuwa zikiondoka katika maisha yao, na kwamba, baada ya kuufunga upendo wa Mungu kutoka mioyoni mwao, wangalitembea muda mfupi baadaye gizani…. {1TG22: 29.3}
“Sio upinzani wa ulimwengu ambao hutisha sana kanisa la Kristo. Ni uovu unaokuzwa mioyoni mwa waamini ambao hutenda kazi ya maafa yao makubwa, na kwa hakika hukwamisha maendeleo ya kazi ya Mungu. Hakuna njia hakika ya kuyadhoofisha maisha ya kiroho kuliko kuukuza wivu, kutuhumu, kutafuta makosa, na kuwaza maovu.” — “Matendo ya Mitume,” uk. 548, 549. {1TG22: 30.1}
Mbali na Ezekieli (kipaza sauti cha Mungu) Mungu huwa hamtumi mwingine kuwa bawabu kwa watu: {1TG22: 30.2}
“Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki
30
aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu aliku-bali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako.” Ezek. 3: 17-21. Kwa ufupi, hatupaswi kukitamani kiti cha enzi “juu ya mlima …., pande za mwisho za kaskazini.” Isa. 14:13. {1TG22: 30.3}
Na daima kumbuka kwamba ikiwa Kweli Yenyewe haiwezi kumbembeleza mdhambi kutubu, mabavu na juhudi za kibinadamu zitafanya mema machache na madhara mengi. Muda wetu ni mfupi sana na kazi yetu pia ni kubwa sana kushiriki katika masuala ya kigeni kwa wajibu wetu. Hatuwezi kumudu kupoteza nguvu zetu tukio-kota makosa ndani ya wengine. Hebu tujiweke tayari kwa ajili ya ufalme, kwa maana lipo kanisa na ulimwengu wa kuokoa, na Mungu anayo hamu sana kwamba tutulie kwa shughuli na upesi sana kama tunataka kuwa mion-goni mwa Wayahudi wanaovutia wa kesho na kuishi katika amani kamilifu chini ya usalama wa milele. {1TG22: 31.1}
-0-0-0-0-0-0-
Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. Iki-wa unataka kupeana yoyote kwa marafiki au jamaa zako Waadventista, unaweza kuagiza nakala za ziada au ku-tuma majina na anwani zao kwa orodha yetu ya watumiwa. {1TG22: 31.2}
31
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 21, 22
Kimechapishwa nchini Marekani
32