fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 19, 20

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 19, 20

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

HATIMA YA YERUSALEMU, MWITO WA WAKAZI WAKE WA BAADAYE

UFALME WA YUDA, KUPEPETWA KWA MATAIFA

                                    

1

KAULI YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia aya ya pili ya ukurasa wa 172. {1TG19: 2.1}

M.B, uk. 172 — “Kristo kamwe hataiacha nafsi ambayo Yeye alikufa kwa ajili yake. Nafsi hiyo yaweza kumwa-cha Yeye, na kulemewa na majaribu; lakini Kristo hawezi kamwe kugeuka na kumwacha mtu ambaye kwa ajili yake Yeye amelipia fidia ya maisha Yake …. {1TG19: 2.2}

“Asante Mungu, hatujaachwa peke yetu. Yeye ambaye ‘aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele,’ hatatuacha katika vita na adui wa Mungu na mwa-nadamu. ‘Angalieni,’ Yeye asema, ‘nawapa uwezo wa kuwakanyaga nyoka na nge, na juu ya nguvu zote za adui; na hakuna chochote kitakachowadhuru.” {1TG19: 2.3}

“Ishi katika ushirika na Kristo aliye hai, na Yeye atakushikilia kabisa kwa mkono ambao hautakuacha kamwe. Ujue na uuamini upendo ambao Mungu anao kwetu, na u salama; upendo ni ngome isiyoweza kupenywa kwa uongo na mashambulizi yote ya Shetani. Jina la Bwana ni ngome imara; mwenye haki hukimbilia ndani yake, na kuwa salama.’” {1TG19: 2.4}

Tunapaswa kuomba kwa ajili ya imani ya kutuwezesha kujua kwa hakika kwamba Kristo hatamuacha kamwe yeyote kati yetu, na kwamba ikiwa tutamfuata Yeye hatutashindwa kamwe katika shughuli zetu. Tunapaswa kumsifu Yeye kwa kuifanya iwezekane kwamba ingawa tunaweza, kwa mfano, kukumbana na nyoka na nge, hawawezi kutudhuru. {1TG19: 2.5}

2

HATIMA YA YERUSALEMU, MWITO WA WAKAZI WAKE WA BAADAYE
– Zekaria 14 –

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, DESEMBA 14, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutajifunza Zekaria 14. {1TG19: 3.1}

Zek. 14: 1 — “Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.”

Kama unavyojua, mada ya somo lililosheheni katika sura hii kwa kweli huanzia katika sura kumi na mbili na hu-fululiza kupitia sura ya kumi na nne. Kuhakikisha ni nani anayetajwa kwa kiwakilishi “yako” katika aya hii, shar-ti turudi kwa sura ya kumi na tatu. Humo tunapata kwamba “yako” kinawakilisha Yerusalemu. Ni mateka wa Yerusalemu, basi, ambao watagawanyika kati yake. {1TG19: 3.2}

Aya ya 2 — “Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapig-wa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.”

Kwa mtazamo wa ukweli kwamba Yerusalemu utalindwa kwa ukuta wa moto (Zek. 2: 5) wakati ambapo nyum-ba ya Yuda inatawala huko, ni dhahiri kwamba vita iliyoelezwa hapa lazima vipiganwe kabla ya nyumba ya Yuda kuanzishwa. Katika vita hivyo mataifa yatawashinda watawala wa Nchi ya Ahadi. Kisha inakuwa kwamba

3

nyumba ya Yuda inaanza kusimamishwa. {1TG19: 3.3}

Kwa sababu mataifa yanayopigana yanauzingira mji, na kuzipiga nyumba risasi, pia kuwabaka wanawake, ha-wawezi kwa vyovyote kuwa mataifa ya haki, lakini maadamu sio wakazi wote wanatekwa, na kwa sababu wote hawatakataliwa mbali kutoka kwa mji, lazima iwe kwamba waovu wanachukuliwa na wenye haki kuachwa nda-ni wajiunge na nyumba ya Yuda. {1TG19: 4.1}

Aya ya 3, 4 — “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita. Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusal-emu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.”

Kwa wakati Yerusalemu, ambao sasa upo, unaanguka, miguu ya Bwana itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni na huko kufanya bonde kubwa sana; yaani, kuondoa vikwazo na vizuizi, na hivyo kuiandaa nchi kwa ajili ya ku-rejea kwa watu Wake. Kisha inakuwa kwamba unabii wa Zekaria 10: 8 — kwamba Bwana “atapiga kelele” kwa ajili ya watu Wake — utakuwa umetimizwa. {1TG19: 4.2}

Aya ya 5 — “Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima li-taenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.”

Baada ya kufungua hivyo njia kwa ajili ya kusimamishwa tena kwa nyumba ya Yuda, watu Wake, ambao mapema

4

wamefahamishwa kuihusu kupitia kwa Ukweli wa sasa, watakimbilia bondeni, kule ambako miguu ya Bwana imesimama, haraka iwezekanavyo kana kwamba walikuwa wakilikimbia tetemeko la ardhi; na watakatifu wote baada ya hapo kuwafuata. Zipo kweli kadhaa katika andiko hili lenyewe ambazo zinathibitisha kwamba tukio hili ni kabla ya milenia: (1) Kumbuka kwamba miguu ya Bwana inasimama juu ya mlima katika siku ya vita am-bayo Yerusalemu unatekwa na mataifa maovu. (2) Wale ambao wanakimbilia bondeni hawashuki kutoka Mbinguni. (3) Hawawezi kuwa waovu kwa sababu hawakimbii mbali kutoka kwa Bwana, lakini wanakimbia Kwake, hadi ambapo miguu Yake imesimama. (4) Watakatifu wote wanafuata nyuma yao. “Maandishi ya Awali,” uk. 53, hufanya matumizi maradufu ya maandiko haya, lile baada ya milenia. {1TG19: 4.3}

“Katika siku hiyo, asema Bwana, nitamtia kila farasi ushangao, na yeye ampandaye nitamtia wazimu; nami nitaifunulia nyumba ya Yuda macho yangu, nami nitamtia upofu kila farasi wa hizo kabila za watu.” Zek. 12: 4. Yaani, Mungu kwa kushangaza anawakanganya waovu ili waweze kutenda kama watu wenda wazimu. Wakati ambapo Bwana analitimiza hili, Yeye anailinda nyumba ya Yuda. {1TG19: 5.1}

“Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa ku-ume na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusal-emu.” Zek. 12: 6. {1TG19: 5.2}

Wakati Bwana anawapiga majeshi ya mataifa, Yeye pia anawafanya wakuu wa Yuda kama makaa ya moto kati ya kuni. Hivyo wao na “injili ya milele” watawateketeza wapagani pande zote, na hivyo Yerusalemu utakaliwa kwa salama na watu waaminifu wa Mungu. {1TG19: 5.3}

Hivyo inakuwa kwamba “ na katika siku za wafalme hao [sio baada

5

ya siku zao] Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine ha-wataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” Dan. 2:44. {1TG19: 5.4}

Kisha itatukia kwamba “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika. 4: 2. {1TG19: 6.1}

Aya yaa 6, 7 — “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi; lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru.”

Aya hizi zinamaanisha kwamba hapo awali hali mbalimbali, “mwangaza” na “kiwi,” zimedumu, lakini hazitaendelea kuwa hivyo tena. Kwa maana neno “mwangaza,” kwenye pambizo, unakumbuka, linatoa “tha-mani,” na kwa neno “kiwi,” linatoa “unene,” kuonyesha kwamba nuru haitakuwa ikipokezana kwa uhaba na utele, unene na wembamba, mwanga na giza. Badala yake, itakuwa thabiti, ya daima. Andiko, bila shaka, lina-zungumzia nuru ya kiroho — Mwanga wa Kweli, maarifa kutoka kwa Mungu. Kwa mfano, katika siku kabla ya ujio wa kwanza wa Kristo, lilikuwepo giza la kiroho. Kisha uwepo Wake ulitoa nuru kwa muda, baada ya hapo vikafuata Vizazi vya Giza la kidini. Baadaye, kwa njia ya Matengenezo, mwanga tena ulianza kuangaza lakini kwa uhaba sana. Kisha kwa utangazwaji wa Jumbe za Malaika wa Kwanza, wa Pili, na wa Tatu, nuru ikawa an-gavu. Kwa wakati huu, hata hivyo, kupitia kwa nabii Zekaria Bwana anaahidi nuru thabiti na ya kutosha. {1TG19: 6.2}

6

Aya ya 8 — “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu; nusu yake itakwenda upande wa bahari ya mashariki, na nusu yake upande wa bahari ya magharibi; wakati wa hari na wakati wa baridi itakuwa hivi.”

“Maji yaliyo hai” lazima yawakilishe maarifa hai, Ukweli hai — yaani, wale ambao huyanywa, kwa mfano, hayo Maji hawatakufa kamwe. {1TG19: 7.1}

“Mlima” upande wa kaskazini na upande wa kusini husababisha “maji” yatiririke tu mashariki na magharibi kuto-ka Yerusalemu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku zote kwa wakati wa hari na kipupwe — maadamu dunia hii kuukuu na iliyochakaa inaendelea kuwepo. {1TG19: 7.2}

Kwa hivyo Yerusalemu, mahali ambapo miguu ya Bwana itasimama, utakuwa mtenganisho mkuu wa kimataifa na wa kiroho kwa ajili ya injili ya milele. Kutoka Yerusalemu katika bonde la milima malaika atatangaza upya kwa sauti kuu, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya Hukumu Yake [kwa walio hai] imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufu. 14: 7. Kisha kukusanywa kwa watu kunaanza pamoja na rai: {1TG19: 7.3}

“Tokeni kwake [Babeli ambaye ameketi juu ya mnyama — anaitawala dunia], enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4. Hivyo ndivyo nchi “itaangazwa” na utukufu wa malaika, na hivyo ndivyo watakatifu watakavyokusanywa kutoka pembe nne za dunia. {1TG19: 7.4}

Aya ya 9 — “Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.”

7

Bwana anatawala kwanza juu ya Yerusalemu, na hatimaye baada ya watakatifu kukusanywa kutoka pembe nne za dunia Yeye anatawala juu ya dunia yote. {1TG19: 8.1}

Aya ya 10, 11 — “Nchi yote itageuzwa kuwa kama tambarare, toka Geba mpaka Rimoni upande wa kusi-ni wa Yerusalemu; naye atainuliwa juu, atakaa mahali pake mwenyewe, toka lango la Benyamini mpaka mahali pa lango la kwanza, mpaka lango la pembeni; tena toka mnara wa Hananeli mpaka mashinikizo ya mfalme. Na watu watakaa ndani yake, wala hakutakuwako laana tena; lakini Yerusalemu utakaa salama.”

Aya hizi hazihitaji maelezo, isipokuwa wazo maarufu la kale la kusimamishwa kwa Ufalme, kama unavyoona sasa, sio wazo la Mungu. Tungalikuwa afadhali kulichukua wazo Lake, na kuliacha letu. {1TG19: 8.2}

Maadamu wakati hautaturuhusu kuikamilisha sura nzima leo, tutaziacha aya zilizosalia kwa ajili ya juma lijalo, Bwana akipenda. {1TG19: 8.3}

Kabla kufunga, hata hivyo, hebu kwa maneno machache tufanye muhtasari kile tumejifunza alasiri hii. Kabla ya ufalme wa Yuda kuanzishwa huko Yerusalemu, mji huo utazingirwa, nyumba zitapigwa risasi na wanawake wa-tabakwa. Sio wote, hata hivyo, watatekwa. Mabaki hayatakatiliwa mbali kutoka kwa mji, wao bila shaka wa-takuwa sehemu ya nyumba ya Yuda. Kwa wakati huo, ambapo Yerusalemu umeanguka na Bwana ameondoa vizuizi na vikwazo vyote kwa ajili ya kuwakusanya watu Wake, kisha inakuwa kwamba nyumba ya Yuda inasimamishwa tena. Watu wa Mungu watakimbilia “bondeni” upesi kana kwamba walikuwa wanakimbia kuto-ka kwa tetemeko la ardhi. Bwana anawapiga majeshi ya mataifa, ilhali wakati huo huo Yeye anawalinda na ku-wainua watu Wake. {1TG19: 8.4}

8

Kupitia nabii Zekaria, Mungu anawaahidi watu Wake katika siku zetu nuru ya kutosha na thabiti ya kiroho. Kutoka Yerusalemu katika siku hiyo utatokea Ukweli hai. Kisha itakuwa kwamba “mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana.” Ni kama nini matarajio haya! Na ni kama nini msiba iwapo yeyote kati yetu tushindwe kuifanya sehemu yetu ya kuikaribisha siku hiyo ya utukufu. {1TG19: 9.1}

Sheria ya Upendo

Chimba njia kwa mito ya upendo,

Ambapo inaweza kukimbia kwa upana,

Na upendo una mito inayofurika,

Ili kuwajaza kila mmoja.

Lakini ikiwa wakati wowote unashindwa

Njia hizo za kutoa,

Chemchemi ya upendo yenyewe

Hivi karibuni itakuwa kavu na kukauka;

Ni lazima ugawanye iwapo ungependa kuhifadhi

Hiki kitu kizuri kutoka juu.

Kuacha kugawanya, tunakoma kuwa nacho–

Kama hii ndiyo sheria ya Upendo.

–Trench

9

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 174, kuanzia aya ya kwanza. Kichwa cha somo hili ni, “Ufalme ni Wako, na nguvu, na utukufu.” {1TG20: 10.1}

M.B. uk. 174 — “Ya mwisho kama sentensi ya kwanza ya sala ya Bwana, inamwonyesha Baba yetu akiwa juu ya nguvu zote na mamlaka na kila jina ambalo linatajwa … Kati ya vita na uharibifu wa kitaifa, hatua za wanafunzi zingezongwa na hatari, na mara nyingi mioyo yao ingeyanyaswa na hofu. Wangaliuona Yerusalemu kuwa magofu, hekalu limefagiliwa mbali, ibada yake milele imekomeshwa, na Israeli wametawanyika katika nchi zote, kama vile vifusi kwenye pwani ya jangwa. Yesu alisema: ‘Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita.’ ‘Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na mate-temeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. “Hata hivyo wafuasi wa Kristo ha-wakupaswa kuogopa kwamba tumaini lao lilikuwa limepotea, au kwamba Mungu alikuwa ameiacha dunia. Uwezo na utukufu ni Wake ambaye madhumuni Yake makuu yangeendelea bila kuzuiwa hadi kwa utimilifu wake. Katika sala ambayo ina pumzi ya mahitaji yao ya kila siku, wanafunzi wa Kristo walielekezwa kutazama juu zaidi ya nguvu zote na mamlaka ya uovu, katika Bwana Mungu wao, ambaye ufalme Wake unatawala juu ya wote, ambaye ni Baba yao na Rafiki wa milele.” {1TG20 : 10.2}

Wanafunzi waliutarajia Yerusalemu katika wakati wao kuwa mji mkuu wa Ufalme mkuu wa Mungu. Lakini kinyume na matarajio yao, Yesu alitangaza kwamba Yerusalemu ungalikuwa ganjo, na hekalu kuwa magofu! Hivyo, tena na tena tunaongozwa kuona kwamba sisi wanadamu wafaji hatujui kamwe mipango ya Mungu. Hakika, tunahitaji kuomba kwa ajili ya Roho Wake kutuongoza siku zote, na kutuonyesha njia sahihi kwa kila hatua tunapoendelea kusafiri hadi kwa Umilele. Hebu sasa tuombe kwamba maarifa ya kweli hizi yatatufanza tuwe kile tunachopaswa kuwa. {1TG20: 10.3}

10

UFALME WA YUDA, KUPEPETWA KWA MATAIFA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, DESEMBA 21, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Sabato iliyopita tulihitimisha masomo yetu na aya ya kumi na moja ya Zekaria 14, na sasa ili kuliunganisha somo la leo na la Sabato iliyopita, tutapitia kwa ufupi matukio kuhusu Yerusalemu, kama yalivyotabiriwa katika aya kumi na moja za sura hiyo. {1TG20: 11.1}

Tukio la kwanza lililotabiriwa ni vita dhidi ya Yerusalemu, ambavyo mataifa yote yatashiriki. Katika vita hivyo sehemu ya watu katika Yerusalemu watatekwa, bali wengine wanasalia katika mji. Zaidi ya hayo, siku hiyo mi-guu ya Bwana inasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, na mlima huo unapasuka kuelekea upande wa mashariki na kuelekea magharibi, unafanya bonde kubwa. Kisha kwa bonde hili la milima, mahali ambapo miguu ya Bwa-na imesimama, watu wa Mungu wanakimbilia upesi kana kwamba wanalikimbia tetemeko la ardhi. Hivi ndivyo Yerusalemu utakavyokaliwa tena na watu Wake Mungu. Inaonekana kwamba wale ambao hawajakatiliwa mba-li, wale ambao wameachwa Yerusalemu, ni lazima wawe waaminifu wanaopatikana humo. Lakini wale wanaokimbilia bondeni ambako miguu ya Bwana imesimama — wanakimbilia Kwake, sio mbali kutoka Kwake — lazima wawe waaminifu kutoka mahali pengine. Kwa uwazi, Yerusalemu utakuwa mahali pa kusanyiko kubwa kwa watu wa Mungu. {1TG20: 11.2}

Haya ni baadhi ya mambo ambayo somo la Sabato iliyopita, sehemu ya kwanza ya Zekaria sura ya 14,

11

ilileta kwa mtazamo, na mwanafunzi yeyote wa Biblia anapaswa kuona kwa urahisi kwamba ni ya kabla ya milenia: Watu hawashuki kutoka Mbinguni, ila badala yake wanakimbilia bondeni. Hawakuwa, kwa hivyo, waovu, kwa maana wanakimbilia Kwake, si mbali kutoka Kwake. Sasa hebu tuendelee na aya ya kumi na mbili. {1TG20: 11.3}

Zek. 14:12 — “Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusale-mu; nyama ya miili yao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao.”

Katika moja ya aya zilizotangulia tunaambiwa kwamba Bwana atapigana dhidi ya wote watakaopigana dhidi ya Yerusalemu. Na sasa katika aya hii tunaambiwa kuhusu njia ambazo Bwana atatumia katika vita hivyo. Ha-tazitumia silaha zilizoundwa na mwanadamu, ila pigo. {1TG20: 12.1}

Aya ya 13 — “Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba mashaka makubwa yatokayo kwa Bwana yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake.”

Mbali na pigo, kutakuwa na mchafuko mkubwa — mkanganyiko na msisimko ambao utamgeuza kila mtu dhidi ya jirani yake. Hivyo ndivyo Bwana atawashinda maadui wa watu Wake. {1TG20: 12.2}

Aya ya 14 — “Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote uta-kusanyika, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.”

Katika wakati wa pambano hili la mataifa, Ufalme wa

12

Yuda utarejeshwa. Naye atapigana huko Yerusalemu, naye atajikusanyia mali ya mataifa. {1TG20: 12.3}

Piga linaanguka juu ya watu na wanyama ambao watapatikana katika hema za wasioamini. {1TG20: 13.1}

Aya ya 16 — “Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Ye-rusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, na kuishika sikukuu ya Vibanda.”

Sentensi hii ya Maandiko inamaanisha kwa mkazo kuwa wote ambao wakati huo wa maamuzi watakataa kuongoka kwa Bwana, wataangamia; wale tu watakaomwabudu Bwana huko Yerusalemu kwa sikukuu ya vibanda, wataokolewa. {1TG20: 13.2}

Aya yaa 17 — “Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.”

“Mvua” itazuiliwa kutoka kwa wote ambao wakati huo hawatamwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, ili kwam-ba waweze kutambua kikamilifu kosa lao. Zaidi ya hayo, sio tu wale watakaopigana dhidi ya Yerusalemu, ila hata familia zote za dunia zitapepetwa hivyo. {1TG20: 13.3}

Aya ya 18 — “Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa,

13

wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.”

Ikiwa ukame hautaweza kuwazindua, basi pigo litawachukua hatimaye. Hivyo, wote ambao hawatakuwa wameusikia ujumbe watapewa fursa ya kuusikia. Iwapo hautaweza kuwaokoa mwishowe utawaangamiza. {1TG20: 14.1}

Sasa tunaona kwamba tukio hili (la Bwana kusimama juu ya mlima na watakatifu kukimbilia bondeni) sio tu ka-bla ya milenia, lakini hata kabla ya muda wa rehema kufungwa; kwamba linaanzisha kusimamishwa tena kwa nyumba ya Yuda; kwamba linaandaa njia ya kuiangaza nchi kwa utukufu wa malaika (Ufu. 18: 1); kwamba hatimaye litauleta mwisho wa wadhambi. {1TG20: 14.2}

Aya ya 19 — “Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.”

Tena tunaona umuhimu wa kuyaacha mawazo yetu tuliyoshikilia yasiyofaa kuhusu kazi ya mwisho ya injili. La, Bwana hatadondosha juu ya ulimwengu kama msumari kutoka angani. Yeye atalitukuza kwanza Neno Lake, Uwezo Wake, haki Yake na kanisa Lake au watu. Yeye pia atakuwa ni, kwa mfano, safina ya usalama ambamo atawakusanyia wateule Wake na kuwakinga. Kweli hii yote, unaona, inaonyeshwa wazi wazi katika unabii huu. {1TG20: 14.3}

Aya ya 20 — “Siku hiyo katika njuga za farasi yataandikwa maneno haya, WATAKATIFU KWA Bwa-na; navyo vyombo vilivyomo ndani ya nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyoko mbele ya madhabahu.”

Njuga kwa farasi hazitumiki kwa kusudi lolote isipokuwa kuwasaidia mabwana wao kuwatambua walipo. Hivyo itakuwa kwamba watumwa pekee ambao “njuga” (sauti) husema “Utakatifu kwa Bwana” ndio wale Bwana an-aweza kuwatambua na kuwakusanya kama Wake

14

Mwenyewe. {1TG20: 14.4}

Aya ya 21 — “Naam, kila chombo katika Yerusalemu, na katika Yuda, kitakuwa kitakatifu kwa Bwana wa majeshi; nao wote watoao dhabihu watakuja kuvitwaa vile vyombo, na kutokosa nyama ndani yake; wala siku hiyo hatakuwamo tena mfanya biashara ndani ya nyumba ya Bwana wa majeshi.”

Aya hii inajieleza yenyewe, haina haja ya maelezo. {1TG20: 15.1}

Kwa hivyo inaonekana kwamba pamoja na kuanzishwa kwa Ufalme wa Yuda kunaanza kupepetwa kwa ma-taifa. Ni lazima kwamba tuko kwa ukingo wa kushuhudia utimizo wa unabii huu vinginevyo Chuo hakingaliku-wa kimekunjuliwa hadi sasa kufikia kiwango cha kuufunua kwa wakati huu — hakika haingalikuwa hivyo ikiwa Roho wa Kweli pekee yake huongoza katika Kweli yote, na iwapo Bwana anatoa “chakula kwa wakati wake.” Kwa mtazamo huu, hebu kwa moyo wote tutende anayotaka Mungu na kwa uaminifu tuitekeleze imani yetu katika Neno Lake lisiloshindwa daima. {1TG20: 15.2}

* * *

Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. Iki-wa unataka kupeana yoyote kwa marafiki au jamaa zako Waadvent-ista, unaweza kuagiza nakala za ziada au kutuma majina na anwani zao kwa orodha yetu ya watumiwa. {1TG20: 15.3}

15

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 19, 20

Kimechapishwa nchini Marekani

16

>