30 Mar Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 15, 16
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 15, 16
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
IMANI YA WAYAHUDI NA WAKRISTO KATIKA MANABII
KUTOKA KWA LEO
1
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Nitasoma kutoka kwa Mlima wa Baraka, uk. 168, kuanzia pale ambapo tuliachia Sabato iliyopita. {1TG15: 2.1}
“Kitu kimoja muhimu kwa ajili yetu ili tuweze kupokea na kutoa upendo wa kusamehe wa Mungu ni kujua na kuamini upendo Yeye alionao kwetu. Shetani anafanya kazi kwa kila hila anayoweza kuamuru, ili kwamba tusi-weze kuutambua upendo huo. Atatuongoza tufikiri kwamba makosa yetu na maovu yetu yamekuwa mabaya sana hivi kwamba Bwana hatayaheheshimu maombi yetu, na hatatubariki na kutuokoa. Ndani yetu hatuwezi kuona chochote ila udhaifu, hakuna chochote cha kutupendekeza kwa Mungu, na Shetani anatuambia kwamba hayana maana; hatuwezi kurekebisha kasoro za tabia zetu. Tunapojaribu kumwendea Mungu, adui atanong’oneza hakuna umuhimu kwako wewe kuomba; Je, hukufanya hilo jambo ovu? Je, haujafanya dhambi dhidi ya Mungu, na kukiuka dhamiri yako mwenyewe? Lakini tunaweza kumwambia adui kwamba “damu ya Yesu Kristo Mwana Wake inatutakasa kutoka kwa dhambi zote.” Tunapohisi kwamba tumetenda dhambi na hatuwezi kuomba, basi huo ndio wakati wa kuomba. Kufedheheka tunavyoweza kuwa, na kwa unyenyekevu sana; lakini tunapaswa kuomba na kuamini ….” {1TG15: 2.2}
Hapa linaonekana kwamba ni kusudi la Shetani alilojifunza kutuvunja myoyo, kutufanya tufikiri kwamba Mun-gu hatupendi, na kwamba Yeye hawezi kutuokoa kutoka kwa dhambi zetu. Kwa hivyo, tuipinge minong’ono ya Adui. Wakati tunapojiona kuwa wadhambi, basi ndio wakati wetu hasa wa kuja kwa Mungu, na kuupokea up-endo Wake na kuamini kikamilifu ndani Yake. {1TG15: 2.3}
Tunapaswa sasa kuomba kwa kutambua kabisa kwamba Mungu yu katika shughuli ya kuwaokoa wadhambi, ambao sisi ni wakuu. Kwamba haijalishi ni katika kina kiasi gani cha dhambi tunachoweza kuwa ndani, iwapo tunaweza kuondoka kwa uovu na kuchagua kutenda mema Yeye kwa furaha atatupatia msamaha. {1TG15: 2.4}
2
IMANI YA WAYAHUDI NA WAKRISTO KATIKA MANABII
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, NOVEMBA 16, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Hebu tuyafungue maandiko ya nabii wa injili ambaye Wayahudi kwa uovu walimpasua vipande viwili kwa msumeno. {1TG15: 3.1}
Isa. 1:18, 19 — “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”
Kwa mapendekezo haya ya Matakatifu kwa watu wanaokiri kuwa wa Mungu, nabii wa injili aliagizwa kukijul-isha kitabu chake. Na sasa kwamba tunaishi katika utumiaji wa siku ya leo wa unabii wake, tusidhubutu kupuuza kuyazingatia mapendekezo mazuri na ya haki ya Uvuvio. Hatua yetu ya kwanza itakuwa kwa uaminifu na bila upendeleo tuangalie mafanikio na kushindwa kwa wale ambao wamesafiri mbele yetu. {1TG15: 3.2}
Hebu kimbele tuyaamshe upya mawazo yetu kwa mwenendo wa Wayahudi dhidi ya manabii: Badala ya kwen-da na kusudi la kujifunza na kufikiria, Wayahudi waliwaendea manabii na nia za ubaguzi, na nia mbaya, na chuki ndani ya mioyo yao, na kwa vyombo vya ukatili . (Hatupaswi.) Roho hii ya uovu ilikuwa imeenea mion-goni mwa Wayahudi katika historia yao yote. Ilidhihirishwa hata dhidi ya Musa ingawa kwa miaka
3
arobaini aliliongoza jeshi la Waebrania kwa ishara na maajabu ya Mungu siku zote kutoka kwenye yadi za ma-tofali za Misri hadi kwenye mipaka ya nchi ya ahadi. {1TG15: 3.3}
Masalia hatimaye walivuka Yordani tu kwa sababu waliamini kwa myoyo yao yote kwamba Musa alikuwa kipa-za sauti cha Mungu, na kwa sababu walikoma kunung’unika, waliyapokea na kuyatii maagizo. Waebrania baadaye daima waliyathamini sana maandishi yake, na heshima kuhususu hii Torati iliendelea miongoni mwa Wayahudi hata kwa siku za Kristo. Kama mtu wa Mungu na kama mkombozi wa taifa na mwasisi wa sherehe zake takatifu, Musa aliheshimiwa sana na wote. {1TG15: 4.1}
Ilishangaza, hata hivyo manabii waliofuata baada ya Musa walikataliwa na taifa la Wayahudi kwa ujumla. Wale waliokoka katika uhamisho wa Babeli waliwapokea manabii Hagai na Zekaria kwa sababu tu walikuwa waasisi wa vuguvugu kwa wakati huo lililokuwa njiani kama alivyokuwa Musa katika siku yake. {1TG15: 4.2}
Wayahudi, kulingana na njia yao ya kufikiri, walikuwa waaminifu, ingawa walikuwa vipofu, kwa kuamua kwamba hawakuwa na hitaji la manabii, kwa sababu walivyoona, maandishi ya Musa yalikuwa kamili, hakuna mapungufu yaliokuwa ndani yake: Yalisheheni sheria zote za kiraia na za kidini. Wao, kwa hivyo, hawakuona hitaji la nuru kubwa na hitaji la nabii mwingine. Kupitia kutokuamini kwao katika manabii, walishindwa kuona kwamba ufalme wao ulikuwa tu mfano wa ule mkuu ambao ungalikuja, walishindwa kuona kwamba Ukweli wa Mungu ni endelevu na daima hukunjua, kwamba kila kizazi lazima kipate nyongeza ya Ukweli hasa mwafaka ili kukidhi mahitaji yao maalum. Upofu wao kwa hili ilikuwa dhambi yao ya msingi iliyowaongoza kwa uharibifu. {1TG15: 4.3}
Wakati ambapo Wayahudi walijisifu kuhusu imani yao katika maandishi,
4
ya Musa, Yesu aliwakemea kwa kusema: “… mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye ali-andika habari zangu.” Yohana 5:46. Alikuwa akirejelea– {1TG15: 4.4}
Kumb. 18:15 — “Bwana, Mungu wako, atakuinulia nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.”
Kuhusu kuja kwa Masihi Zekaria pia aliandika: {1TG15: 5.1}
Zek. 9: 9 — “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”
Ingawa walidai kuamini katika wote wawili Musa na Zekaria bado hawakutii lolote kati ya vifungu hivi, na daima tangu wakati huo laana imekuwa juu yao. {1TG15: 5.2}
Kwa kuwakataa manabii Wayahudi walifikiri kwamba hakika walikuwa wakiuzuilia nje udanganyifu, na walif-ikiri kwamba kwa kweli walikuwa waaminifu kwa maandishi ya Musa na pia kwa Mungu. Hili waliliamini sana katika siku za Yesu kama vile Israeli walivyoamini katika siku za Eliya. {1TG15: 5.3}
Hebu sasa tukumbuke kwamba walianguka katika uharibifu tu kwa sababu walikataa kuwatii manabii ambao walipelekwa kuzirekebisha njia zao, kuzirekebisha fasiri zao za uongo za maandishi ya Musa na kuiangaza njia ya miguu miguu yao mwendo wote uliosalia – wazi hadi Paradiso. Baada ya kujinyima wenyewe zawadi ya Roho ya Unabii kwa kuwaangamiza manabii, waliikata kabisa njia ya Mbinguni ya mawasiliano na hivyo wakaachwa katika giza kuu na kuongozwa katika makosa, ushupavu wa kidini, na uhalifu. Walikuwa wenye ku-jitosheleza nafsi, wenye kiburi, wenye majivuno, na wa kujitakia makuu. {1TG15: 5.4}
5
Walijihisi kuwa matajiri na waliojitajirisha, hawakuhitaji kitu chochote zaidi. Hivyo ilikuwa kwamba upotovu wao wa Maandiko kwa fasiri zao ambazo hazikuwa za uvuvio ziliwasababisha kupoteza njia, na hatimaye kumkataa na hata kumsulubisha Mwokozi wao waliyemngoja kwa muda mrefu. {1TG15: 6.1}
Maandiko ya Musa Wayahudi waliyafanya silaha ya nguvu dhidi ya Kristo na manabii wa siku hiyo. Walilaz-imika, hata hivyo, kwa wakati mmoja au mwingine kutambua kwamba baba zao waliokufa walikuwa na hatia ya damu ya manabii. Hilo ni kweli leo. Wengi hukiri kwamba mafarakano yananawiri kwa ufasiri usio na uvuvio wa Maandiko, na bado hawatarajii wafasiri waliovuviwa wa siku hii. Kwa hivyo wanamkataa nabii wa uakisi Eliya hata kabla ya kuonekana kwake ingawa Maandiko yanatabiri dhahiri kuja kwake kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana, kabla ya Hukumu ya Walio Hai. {1TG15: 6.2}
Ikiwa tunalipokea shauri la Uvuvio na kuja na kujadiliana pamoja wakati tunaichunguza misimamo yetu wenyewe na manabii, basi mahali pazuri pa kuanzia ni {1TG15: 6.3}
Mwa. 49:10 — “Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.”
Hapa Musa aliandika kwamba kukusanywa kwa watu kutakuwa katika Yuda, na kwamba wakati Shilo ataka-pokuja, Yuda utakuwa na mfalme na mtoa sheria wake mwenyewe. Je, Sisi kama Waadventista wa Sabato tun-aiamini sehemu hii ya maandishi ya Musa? Ikiwa la, basi hatuwezi kusimama vizuri na Musa kuliko walivyofan-ya Wayahudi. {1TG15: 6.4}
6
Kuutathmini msimamo wetu pamoja na manabii wengine, hatuhitaji kuondoka kwenye suala ambalo Musa ame-lianzisha katika andiko ambalo limenukuliwa. Weka alama kwamba kati ya maandishi ya Musa na ya Isaya, Bib-lia inasheheni kumbukumbu za historia, waamuzi na wafalme. Isaya, basi, ndiye nabii wa pili baada ya Musa tutakayemwendea. {1TG15: 7.1}
Isa. 2: 1, 2 — “Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.”
Sio kwa Bustani ya Takoma, sio kwa Kituo cha Mlima Karmeli, sio kwa sehemu nyingine yoyote, ila kwa nyumba ya Yuda na Yerusalemu ndiko waongofu wa mwisho kutoka katika mataifa yote watauendea. Isaya unaona anathibitisha dhahiri kabisa kwamba kukusanywa kwa watu kutakuwa katika Yuda. Je, wewe? {1TG15: 7.2}
Yeremia akiwa nabii wa pili kwa Isaya, tutasoma {1TG15: 7.3}
Yer. 31: 6 — “Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.”
“Mlima Efraimu,” unajua, ni eneo la ufalme wa kale wa kabila kumi, Israeli. Kwa mujibu wa andiko hili, Ufalme wa Israeli, ambao bado umepotea kati ya mataifa, siku moja utatokea kutoka pembe nne za dunia na kwa furaha kujiunga na ufalme wa Yuda. Hivyo ndivyo kukusanywa kwa watu kutakavyokuwa. {1TG15: 7.4}
Aya ya 7, 8 — “Maana Bwana asema hivi; Mwimbieni
7
kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli. Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.”
Yeremia anafichua kwamnba kukusanywa katika Yuda kutakuwa kutoka pembe nne za dunia. Hakika, Yeremia, Musa na Isaya, wote watatu, wanasema mamoja juu ya suala hili. Swali ni, Je, Unayaamini wanayosema? Ikiwa la, je, wewe ni bora kuliko Wayahudi? {1TG15: 8.1}
Ijayo tunapaswa kuupima msimamo wetu na nabii Ezekieli. {1TG15: 8.2}
Ezek. 36: 17-27 — “Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake. Kwa hiyo nalimwaga hasira yangu juu yao, kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao. Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, naliwahukumu. Nao walipoyaf-ikilia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa Bwana, nao wametoka katika nchi yake. Lakini, naliwahurumia kwa ajili ya jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli walikuwa wamelitia unajisi katika mataifa wali-yoyaendea.
“Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya
8
Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea. Nami nitalita-kasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” {1TG15: 8.3}
Je, ni nini zaidi Uvuvio ungalisema kulifanya suala hilo kuwa dhahiri zaidi? Mungu waziwazi na kwa uzito ali-ahidi kuumba tena na kuujenga upya ufalme wa kale, kuusimamisha katika nchi yake. Hili Yeye atalitenda baada ya Yuda na Israeli kutawanywa kati ya nchi za Mataifa, na kufyonzwa nao — baada ya wao kuupoteza utam-bulisho wao wa kitaifa — hatimaye kama Wakristo, sio kama Wayahudi, Yeye atawakusanya kutoka pembe nne za dunia na kuwaleta katika nchi yao wenyewe. (Na zaidi ya hayo, Maandiko hufundisha kwamba ni kama mchanga wa bahari kwa umati.) Hili Yeye atalitenda, kumbuka, sio kwa sababu wao wanafaa, sio kwa sababu wamekuwa wema kabla au wakati wa kutawanywa kwao kati ya Mataifa, ila kwa sababu Yeye anajishughulisha kulitakasa jina Lake mwenyewe kati ya washenzi. {1TG15: 9.1}
Tena zaidi, baada ya kuwakusanya kutoka nchi zote na kuwaleta katika nchi yao wenyewe, kisha inakuwa kwamba Yeye anaahidi kuwatakasa milele kutoka
9
kwa uchafu wao na kutoka kwa ibada zao za sanamu — kuondoa mapungufu yote ambayo dhambi imefanya ndani yao. Kisha inakuwa kwamba Yeye anawapatia moyo mpya, anaweka Roho Wake juu yao na kuwaweze-sha siku zote kuzishika hukumu Zake. Maki kwa uangalifu kwamba bila kujali mawazo na maoni yetu haya yote yanafanyika baada ya watu wa Mungu kurejea katika nchi ya baba zao. {1TG15: 9.2}
Watu 144,000 wana wa Yakobo, ambao baba zao walifyonzwa na nchi za Mataifa na ambao katika karne nyingi walipoteza utambulisho wa taifa lao, ni malimbuko, wa kwanza kukusanywa katika Yuda. Wao ndio wale wanaosimama juu ya “Mlima Sayuni na Mwana-Kondoo.” Ufu. 14: 1. Wazawa waaminifu wa Wayahudi wali-olijumuisha kanisa la Kikristo la kwanza, na ambao pia walipoteza utambulisho wao wa kitaifa kwa kujiita Wa-kristo (Mdo. 11:26), pia watakusanywa kutoka kila mahali na kuletwa katika Yuda. {1TG15: 10.1}
Mwishowe, kama unabii huu hautatimizwa, iwapo malaika wa kanisa la Laodekia anavyodhani, na ikiwa watu wa Mungu hawatarejea katika nchi yao, basi wataweza kutakaswa vipi kutoka kwa uchafu wao maadamu uta-kaso utafanyika huko tu? Je, watawezaje kubadilishwa myoyo yao? Na ni nini kitakachowafanya wazishike amri na hukumu Zake isipokuwa kama ilivyoahidiwa, kimbele kupokea Roho Wake katika Nchi ya Ahadi? Hakika, iwapo unabii huu unashindwa, basi watu wa Mungu watawezaje kusimama mbele ya Mungu msafi na mtakati-fu? Na watapataje kutokufa na kuwa kwa ratiba ya kuhamishwa bila kufa ikiwa hawawezi kuuzingatia unabii, na mapenzi Yake yaliyofunuliwa na mpango kwa ajili ya watu Wake? Na iwapo wanaupuuza unabii huu, utimi-zo wake ambao ni wakati wa Hukumu kwa Walio Hai, mavuno, wakati wa kukusanywa, ni nafasi gani wanayosimama kuistahimili siku ile kuu na ya kutisha ya Bwana? {1TG15: 10.2}
10
Ili kubainisha zaidi, iwapo dhehebu linashindwa kuzitambua na kuzipokea ahadi hizi, basi ni wapi waumini wa-taelekezwa waende kutoka hapa? Hakika sio kwa Ufalme ikiwa viongozi wao hawaamini ndani Yake. Je, sasa unaamini katika Musa, katika Isaya, na Ezekieli? Au je, bado badala yake unaziamini hadithi zilizotungwa na wanadamu? {1TG15: 11.1}
Karibu na Ezekieli ni nabii Danieli. Lakini, hebu tujikumbushe wenyewe kwamba kwa kuanza, Danieli hakutoa unabii kwa Wayahudi, bali kwa Wakaldayo na kwa Wamedi na Waajemi. Wayahudi walimpokea kama mtumwa wa Mungu tu walipouona unabii wake umetimizwa. Swali kuu mbele yetu, hata hivyo, ni, Je, tunaamini kika-milifu katika maandishi ya nabii Danieli? Hebu tuone. {1TG15: 11.2}
Dan. 2:44, 45 — “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hau-taangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.”
Kwa neno la Danieli mwenyewe, jiwe hilo ni mfano, sio wa kitu kingine, bali wa Ufalme, ambao katika mfano wa ngano na magugu Yesu huuita “ghala,” mahali ambapo Yeye ataweka ngano (watakatifu) baada ya kuten-ganishwa na magugu (Mat. 13:30). Sasa weka alama kwa makini kwamba kulingana na ufasiri wa Danieli jiwe huonyesha Ufalme, ambao Mungu atausimamisha sio baada ya siku za wafalme hawa, ila katika siku zao, na kwamba jiwe Ufalme Wenyewe, sio
11
kitu kingine chochote, utaivunja sanamu kubwa. Iwapo ufasiri wetu wa jiwe unakinzana na ufafanuzi wa Danieli kuuhusu ufalme, basi hatuukatai tu uvuvio wa Danieli, lakini hata kulipotosha Neno la Mungu! Ni bora tuache. Sasa tunakuja kwa nabii Hosea. {1TG15: 11.3}
Hosea 1:11; 3: 5 — “Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana …. Baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.”
Je, mtu anaweza kumwamini Hosea juu ya somo la Ufalme iwapo haamini katika manabii wa awali ambao wali-fundisha kama yeye? — Bila shaka hapana. {1TG15: 12.1}
Sasa tuko kwa unabii wa Yoeli. {1TG15: 12.2}
Yoeli 3: 1, 2 — “Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nita-wahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.”
Wakati Mungu anawaweka huru watoto wa Yuda na wa Yerusalemu, kanisa la leo, na kuwarejesha tena katika nchi yao wenyewe, kisha inakuwa, unakumbuka, kwamba Yeye anayakusanya mataifa yote katika bonde la Ye-hoshafati. Huko atawahukumu — kuwatenganisha wema kutoka kwa wabaya, (Mat. 13:47, 48), kondoo kutoka kwa mbuzi (Mat. 25:32). Na kazi hii lazima ujue ni kazi ya Hukumu kwa walio hai wote. Je, tutamkataa
12
Yoeli pamoja na manabii waliomtangulia, na kwa hivyo ujumbe wa Hukumu kwa Walio Hai baada ya kuwa zaidi ya karne tumeitangaza hukumu kwa Wafu? Fikiria juu ya yale Maandiko yanasema na hivyo uamue kua-chana na sauti zingine zote. Na iko vipi imani yako kumhusu nabii Amosi? Hebu tusome {1TG15: 12.3}
Amosi 9: 9-15 — “Kwa maana, angalieni, nitatoa amri, nami nitaipepeta nyumba ya Israeli katika mataifa yote, kama vile ngano ipepetwavyo katika ungo lakini hata chembe moja iliyo ndogo haitaanguka chini. Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele. Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobo-moka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale; wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema Bwana, afanyaye hayo. Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka. Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matun-da yake. Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang’olewa tena watoke katika nchi yao nili-yowapa, asema Bwana, Mungu wako.”
Kwa sababu Amosi na msisitizo mkubwa zaidi anatoa ushuhuda uo huo kama manabii wote waliomtangulia, na maadamu usemi juu ya suala hilo ni wazi kabisa kama ulivyo usemi wa manabii wote kabla yake, kiasi kwam-ba hauhitaji maelezo, tutafanya nini naye? Sasa tunasoma {1TG15: 13.1}
13
Obadia. 1: 15-18 — “Kwa maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe. Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kubabaika, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe. Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao. Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo.”
Kwa uwiano na manabii wote kabla yake, na kwa uwazi mkamilifu, Obadia, pia, anasimulia kwamba katika siku ambayo Bwana atawaangamiza washenzi, katika siku ya mavuno, au hukumu, vinginevyo huitwa kulitakasa Hekalu (Dan. 8: 14) na utakaso wa kanisa (Mal. 3: 1-3), na pia siku kuu na ya kutisha ya Bwana, utakuwepo ukombozi juu ya Mlima Sayuni, na nyumba ya Yakobo utaumiliki utajiri wa mataifa. Je, Sasa unaamini katika ushuhuda wa Yesu kupitia katika manabii Wake? Ikiwa la, basi unawezaje kunena kwamba unasema sawa sawa na “sheria na ushuhuda” (Isaya 8:20)? Kumbuka daima kwamba sheria na ushuhuda huenda pamoja. {1TG15: 14.1}
Nabii Yona ndiye anafuata kwa msururu, lakini tutazingatia unabii wake tunapokuja kwa nabii Nahumu. {1TG15: 14.2}
Sasa tutaona ni nini kitakachofanywa na nabii Mika. {1TG15: 14.3}
Mika 3:12; 4: 1, 2 — “Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa
14
kama mahali palipoinuka msituni:… Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyum-ba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauen-dea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwa-na, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.”
Kwa kusisitiza kama manabii wote kabla yake, Mika anatangaza kwamba baada ya uharibifu wa “mlima” wa zamani wa Bwana, (ufalme), unakuja urejesho wake katika siku za mwisho, na kwamba watu na mataifa wa-taingia ndani yake kwa sababu Sheria na Neno la Bwana litatoka Sayuni na Yerusalemu. Je, sasa mtayaziba masikio yenu na kuyafumba macho dhidi ya ahadi hii? au ninyi kama watumwa wa Mungu mnayo azima ya ku-fika pale na malimbuko? Natumaini ni la mwisho. Sasa tunakuja kwa unabii wa Nahumu: {1TG15: 15.1}
Nah. 1:12, 13, 15 — “… Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena. Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako …. Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.”
Mzigo wa Nahumu ni juu ya urejesho, na kuanguka kwa Ashuru, mamlaka ambazo zinawatawala katika siku ambayo Yeye anaurejesha Ufalme wa Yuda wa siku za mwisho; katika siku ambayo Yeye anaipasua nira ya Ashuru, siku ambayo Yeye anayapasua vipande mafungo yanayowafunga watu Wake. Katika
15
siku hiyo Anamtuma mjumbe Wake kuitangaza habari njema kwa watu wake, habari za amani wakati ambaapo dunia inataabishwa na vita. Kupitia kwa Mjumbe Wake anawahimiza watu Wake kuzitimiza ahadi zao, kwa kuwa Yeye atawaondolea mbali waovu kutoka kati yao. Ashuru utaondoka na kuiacha nafasi kwa Yuda. “Maa-na kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, yeye apigaye kwa bakora.” Isa. 30:31. Sasa Yeye anasihi: {1TG15: 15.2}
“Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. Maana katika siku hiyo [katika siku ambayo Ashuru unaanguka] kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi. Na mwamba wake uta-toweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu.” Isa. 31: 6-9.
Utakaso (Hukumu), hapa unaona, unafanyika kutoka Zayuni na Yerusalemu. Na kupitia Malaki anauliza Roho, “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi [ukasisi], atawasafisha kama dha-habu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3: 2, 3. Je, unampokea Nahumu? Na kwa ku-wa unabii wa Yona ni pacha kwa wa Nahumu, basi ukimkataa Nahumu, moja kwa moja unamkataa Yona pia. {1TG15: 16.1}
Nabii Habakuki aliambiwa “iandike njozi, ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate
16
kukimbia.” {1TG15: 16.2}
Hab. 2: 3 — “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”
Ndipo Habakuki aliomba, akisema, {1TG15: 17.1}
Hab. 3:12, 13 — “Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani. Sela.”
Je, tunaweza kwa imani kuomba kwa ajili ya jambo lile lile aliloomba Habakuki? — Kwamba Bwana atokee kwa ajili ya wokovu wa watu Wake, kwamba njozi itimizwe bila kukawia, na kwamba tukimbie ili kuzitangaza habari njema? Ikiwa sivyo, basi hakika tunamkataa Habakuki pia. {1TG15: 17.2}
Hebu tuone kile Zefania anasema kuihusu nyumba ya Yuda ya siku za mwisho — mlima wa Bwana. {1TG15: 17.3}
Zef. 2: 5-7 — “Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la Bwana li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana Bwana, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wa-fungwa wao.”
17
Maadamu unabii wa Zefania pia ni yakini kwamba Bwana atausimamisha upya ufalme wa Yuda, na kwa vile, pia, hauhitaji maelezo, tutaweza kupita upesi hadi kwa unabii wa Zekaria. {1TG15: 18.1}
Zek. 1:20, 21 — “Kisha Bwana akanionyesha maseremala wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioin-ua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.”
Mara moja Mungu aliziinua “pembe,” mataifa, kuwatawanya watu Wake katika nchi zote za Mataifa, lakini “pembe” hizo katika urejesho wa “mambo yote,” zinaonekana kuwa “maseremala,” ili kwamba zikiwa pembe mwishowe zinayafukuza Mataifa kutoka katika nchi ya ahadi, zinakuwa kama maseremala wa kujenga kwa ajili ya Yuda. Hivyo Zekaria, kama vile manabii wote kabla yake, anatabiri juu ya urejesho wa ufalme wa Yuda. Sasa tutasoma kutoka kwa Malaki, wa mwisho kwa manabii wa Agano la Kale. {1TG15: 18.2}
Mal. 3: 1-3 — “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani ata-kayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.”
18
Iwapo, katika uso wa mafundisho ya wazi na yasiyo na shaka ya manabii wote, sisi kama Waadventista wa Sa-bato tushindwe kuutii ukweli wa Utakaso wa kanisa (Ufalme ulioshughulikiwa hapa), ujumbe wa Hukumu kwa Walio Hai na wa kurejeshwa kwa ufalme wa Yuda — hekalu kwa ajili ya wale waliotakaswa, — basi hakika wen-gine watazichukua nafasi zetu kwa kuutangaza. Kisha pamoja na Wayahudi tutastahili kuichukua hatia ya ku-wakataa manabii wote tangu ulimwengu ulipoanza. Kwa nini? — Kwa sababu isipokuwa tuamini hakika yote ambayo wameandika, unafiki wetu kuamini tu ndani yao kunamaanisha mengi kwa Mbingu kama imani ya Wayahudi katika maandishi ya Musa ilivyomaanisha kwa Bwana. Nini! Kuihubiri Injili ya Ufalme lakini kuukataa Ufalme Wenyewe! {1TG15: 19.1}
Kwa kufunga nitasoma kutoka Maandishi ya Awali, katika sura yenye kichwa “Kilio Kikuu.” {1TG15: 19.2}
“Ujumbe huu [yaani ujumbe unaoanzisha Kilio Kikuu] ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa malaika wa tatu, ukijiunganisha nao kama kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga na ujumbe wa malaika wa pili mwaka wa 1844.” — M.A., uk. 277. Na kwenye ukurasa wa 118 tunasoma: — “Kisha nalimwona malaika wa tatu. Akasema malaika aliyeandamana nami, ‘Ya kutisha ni kazi yake. Wa kuogofya ni utume wake. Yeye ndiye malaika ataka-yeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kuifunga, ngano kwa ghala la mbinguni. Mambo haya yanapaswa kuyashughulisha mawazo yote, umakini wote.’” {1TG15: 19.3}
Mwandishi wa taarifa hizi anaeleza wazi kwamba Kilio Kikuu hakifanyiki kwa kelele nyingi, ila kwa ujumbe wa ziada, na kwamba ujumbe wa malaika wa tatu katika mwisho wa dunia, sio mwisho wenyewe, ataichagua ngano kutoka kwa magugu. Nani kati yenu angekuwa mpumbavu
19
kamili kuyafumba macho na kuyaziba masikio yake kwa ushuhuda wa manabii, na hatimaye katika fadhaa alie, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” Yer. 8:20. {1TG15: 19.4}
Sasa, iwapo sisi kama kanisa hatutarajii hata kidogo ujumbe wa ziada, kando ya kuwakataa manabii wa awali, basi ni bora namna gani mwenendo wetu kwa Mungu na manabii Wake wa leo na wa jana? {1TG15: 20.1}
Wayahudi walitaka ufalme wa wao wenyewe, ufalme wa ulimwengu huu (mtakatifu na mdhambi ndani yake). Naam, walitaka ufalme kwa dunia, lakini sio mbinguni. Zaidi ya hayo, waliutaka miaka elfu mbili kabla ya rati-ba. Sasa, kwa kushangaza, katika wakati wa kurejeshwa kwa Ufalme, Dhehebu linachukua mwenendo tofauti: Linataka ufalme mbinguni, lakini sio kwa dunia. Hakika, linataka kupanda “gari” kutoka kwa Bustani ya Tako-ma. Na kando yake wakati Bwana anasema atayaokoa mataifa, Dhehebu linasema “Yeye atawaokoa tu wana wa Yakobo 144,000,” na kwa hivyo hakuna mwana wa mataifa mengine! {1TG15: 20.2}
Wayahudi hawakutaka chochote ila kile walichotaka, na hawakupata chochote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa Dhehebu ikiwa Ukweli huu wa Biblia wazi kabisa na wa ziada, na mfano wa Wayahudi hauwezi kulisaidia kuona kwamba linaelea “baharini bila ramani au dira.” — Kristo Haki Yetu, uk. 37 (toleo la 1941). Iwapo linaen-delea kutohitaji chochote isipokuwa kile linachotaka, ni hakika kwamba hakuna chochote linaweza kutarajia. {1TG15: 20.3}
Tafadhali eleza, ni nini zaidi ambacho mmoja anaweza kutarajia kupata kutokana na imani pendelevu kwa man-abii, kutoka kwa ufasiri wa mapenzi ya binadamu wa Maandiko, kutoka kwa mfumo
20
wa kuyapotosha Maandiko, wa kuvifanya mafumbo vifungu rahisi kwa kutumia miswada isiyojulikana na mafafanusi ya kidhehebu? Hebu tukishikilie “kitabu cha Bwana” ambacho kinywa Chake kimeamuru, na mi-swada ambayo “….Roho Yake imekusanya.” Isa. 34:16. {1TG15: 20.4}
Sema chochote unachotaka dhidi ya Wayahudi, lakini uchunguzi wangu huniambia kwamba sisi kama Waadventista wa Sabato tunawashinda kwa ukorofi. {1TG15: 21.1}
Zaidi ya hayo, sasa inaonekana kwamba somo letu la alasiri hii ni muhtasari wa ujumbe kwa Walaodekia, ambao hufikiri kwamba ni tajiri na wamejitajirisha kwa bidhaa, na hawana haja ya kitu chochote zaidi, ingawa wanahitaji kila kitu. Ingalikuwa vyema wazinduke kwa umasikini wao. {1TG15: 21.2}
Hakika kweli, hali ya sasa ya mambo yanaonekana kuwa giza. Lakini kwa kuona kwamba siku hii ya giza na ya mawingu inatoa tumaini la siku za baadaye la utukufu usio na kifani, hebu sisi na nabii Habakuki tuseme: “Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.” Hab. 3:17, 18. Hivyo, kama vile mi-tume walivyomshinda adui wa kanisa katika siku zao, vivyo hivyo tutamshinda katika siku zetu. {1TG15: 21.3}
21
KUTOKA KWA LEO
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, NOVEMBA 23, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Alasiri hii tutajifunza Zekaria 8. Kitu cha kwanza tunachohitaji kujua katika kujifunza sura hii ni kama ahadi zake zimefanywa kwa watu wa wakati wa Zekaria au kwa watu wa wakati wetu. Ili kujua jambo hili, ni muhimu kwa ajili yetu kusoma aya chache zilizotawanyika. Tutaanza na {1TG16: 22.1}
Zek. 8: 7, 8 — “Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi; nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.”
Katika aya hizi tunaona kwamba Mungu anaahidi kuwaokoa watu wake sio kutoka katika nchi ya Babeli ya za-mani, ambapo Zekaria alikuwa wakati huo, ila kutoka mashariki na magharibi, na kuwaleta Yerusalemu. Wa-takuwa watu Wake, sio kwa wema wa baba zao, au kwa sababu nyingine, bali katika Kweli na haki. Sasa, maadamu ahadi katika aya hizi haikupata utimizo wake katika siku za Zekaria, wala wakati wowote baada ya hapo, inasimama kufikiri kwamba ni lazima ifikie utimizo wake wakati fulani baadaye. Hebu tusome– {1TG16: 22.2}
Zek. 8:13 — “Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na
22
nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe hodari.”
Mbali na kuahidi kuokoa watu Wake kutoka mashariki na magharibi, Bwana ameahidi kuwaokoa pia nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli, falme zote mbili za kale zilizotawanyika. Mnajua vyema kwamba ufalme wa kabila kumi ulijumuisha nyumba ya Israeli. Na kwa sababu falme hizi mbili bado hazijawahi kuunganishwa na kuletwa tena Yerusalemu, lipo hitimisho moja tu la kuafikia: Ahadi za sura hii zitatimizwa wakati wa “kukusanywa kwa watu” kutoka pembe nne za nchi. Katika mtazamo wa kazi hii kuu na kubwa Bwana anatarajia mikono yetu ku-wa “hodari.” Ijayo tutasoma– {1TG16: 23.1}
Zek. 8: 20-22 — “Bwana wa majeshi asema hivi, Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi; wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi; Mimi nami nitakwenda. Naam, watu wa ka-bila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana.”
Maadamu tunajua kwamba hakuna taifa lolote mbali na taifa la Wayahudi katika siku za Zekaria lilikwenda kumtafuta Bwana na kuomba mbele Yake huko Yerusalemu, hakuna mbadala bali tena kukubali kwamba ahadi za Zekaria 8 ni za watu katika wakati wa mavuno ya mwisho, katika wakati wa kukusanywa. {1TG16: 23.2}
Baada ya kuukamilisha uchunguzi wetu wa wakati ambapo sura hii inapata utimizo wake, tunaweza, ninao uhakika, kujifunza sasa unabii wenyewe kwa upendezi mkubwa zaidi kuliko tungalivyoweza vinginevyo. Hebu tuanze na {1TG16: 23.3}
23
Zek. 8: 1-3 — “Neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu, nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu. Bwana asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa Bwana wa majeshi utaitwa, Mlima mtakatifu.”
Naam, mambo ya ajabu yamenenwa juu ya Zayuni na Yerusalemu. Wakati mmoja Bwana aliuacha mji na ku-watawanya watu. Lakini kwa wakati maandiko haya yanapokuwa yakifunuliwa, Yeye atarudi, kuwakusanya wateule Wake, na kuwaleta Zayuni na Yerusalemu. Wakati kazi hii kubwa itakapokuwa imekamilika Yerusale-mu utaitwa “mji wa Kweli, … mlima mtakatifu” — watu wanaoijua vizuri Kweli yote ya Mungu na bila mdhambi kati yao. Hii ajabu kuu kwa udhahiri inatukia katika wakati wa Hukumu ya Walio Hai, wenye haki wanapele-kwa huko wakati ambapo waovu wanafungwa katika matita kama ilivyopaswa kuharibiwa. Na wakati Bwana anakaa Zayuni, Ukweli Wake basi utatolewa kutoka Zayuni na Yerusalemu. Kisha inakuwa kwamba “watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwa-na.” Sasa ni nafasi yetu kubwa ya kufanya kazi na kuomba “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.” {1TG16: 24.1}
Zek. 8: 4, 5 — “Bwana wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana. Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.”
Yerusalemu utakuwa mji wa furaha, pia. Haitakuwapo
24
hofu au ajali; hata watoto watacheza kwa usalama mitaani. Hakutakuwa na “nyuso za huzuni,” na sura za wasi-wasi. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa wachanga na wazee. {1TG16: 24.2}
Zek. 8: 6 – “Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema Bwana wa majeshi.”
Eti kwa sababu utimizo wa unabii huu unaweza kuwa wa ajabu na usiowezekana, je, lazima kwa hivyo uwe usiowezekana kwa Bwana, pia? — Hakika la. {1TG16: 25.1}
Zek. 8: 7, 8 — “Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi; nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.”
Zekaria anatabiri kukusanywa kwa watakatifu kutoka mataifa yote hadi katika kanisa la Mungu lililotakaswa na kujazwa Kweli, Ufalme, kama vile mfano wa mavuno hufundisha, ngano pekee lazima iwekwe ghalani, kanisa. Hautakuwapo mchanganyiko wa watakatifu na wadhambi katika “mlima mtakatifu wa Bwana.” {1TG16: 25.2}
Zek. 8: 9 – “Bwana wa majeshi asema hivi, Mikono yenu na iwe hodari, ninyi mnaosikia siku hizi maneno haya kwa vinywa vya manabii, waliokuwapo siku hiyo ulipowekwa msingi wa nyumba ya Bwana wa majeshi; yaani, hekalu hilo; ili lijengwe.”
Mungu hapa anatushauri kuiruhusu mikono yetu iwe hodari, na imara. {1TG16: 25.3}
25
Sisi pia tunapaswa kuyasikia maneno ya manabii na ingawa hatujengi hekalu ambalo walikuwa wakijenga, hata sasa hiyo ndiyo njia pekee ambayo kazi yetu inaweza kufanikiwa. Hatuwezi kumudu kuyaziba masikio yetu kwa yale manabii husema, au kukaa chini kwa mwenendo wa kutojali. {1TG16: 26.1}
Zek. 8: 10-12 — “Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake. Lakini sasa sitakuwa kwa mabaki ya watu hawa kama nilivyokuwa siku zile za kwanza, asema Bwana wa majeshi. Kwa maana itakuwako mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na hizo mbingu zitatoa umande wake; nami nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu hivi vyote.”
Twapaswa kuwa wenye shukrani na furaha kama nini kwamba siku za dhiki yetu ziko karibu mwisho, kwamba sasa iwapo tutawasikia manabii Wake, na kujikaza kwa ajili ya kazi hiyo, Bwana anatuhakikishia amani na ufani-si. Hili yawezekana hivi karibuni litakuwa letu ikiwa tu sisi kwa dhati tutauambata Ukweli, na hivyo kwa Bwa-na. {1TG16: 26.2}
Zek. 8:13 — “Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na nyum-ba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe ho-dari.”
Ingawa tumekuwa wadhambi wakuu na laana kubwa kati ya mataifa, hata hivyo zitakuwa kubwa zaidi baraka zetu kama tunamruhusu Yeye atupatie. Mikono yetu, inapaswa kuwa hodari kuiharakisha siku hiyo njema. {1TG16: 26.3}
Zek. 8:14, 15 — “Maana Bwana wa majeshi asema hivi, Kama vile
26
nilivyoazimia kuwatenda ninyi mabaya, baba zenu waliponikasirisha, asema Bwana wa majeshi, wala mimi sikujuta; vivyo hivyo nimeazimia katika siku hizi kuutendea Yerusalemu mema, na nyumba ya Yuda pia; msiogope.”
Tena na tena tumehakikishiwa kwamba kama vile adhabu imekuwa kubwa kwa watu Wake, kwa ukubwa huo tu ndivyo itakavyokuwa furaha na faraja yao sasa katika wakati wa kukusanywa. {1TG16: 27.1}
Zek. 8:16 — “Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu.”
Kila mmoja wetu anahimizwa kuifundisha Kweli kwa jirani yake, kutenda chochote anachopata karibu na mkono wake. Tunahitajika kuitekeleza hukumu ya Kweli badala ya kupoteza pumzi na muda kuzungumza juu ya dhambi za wengine tusije tukashindwa kuiona pingili ya “boriti” katika jicho letu. Hebu, jinsi aya hii inavyoagi-za, tuseme Ukweli, tutekeleze hukumu na amani katika nyumba zetu na miongoni mwetu. Hatupaswi kamwe kujishughulisha na yanayowahusu watu wengine. Tunapaswa kufanya vyema iwapo tutayasimamia yetu wenyewe. {1TG16: 27.2}
Zek. 8:17 — “Wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema Bwana.”
Kwa mambo yote Wakristo wanapaswa kujifunza, jambo moja hili ni la dharura: kwamba wawe waaminifu kwa wao wenyewe na kwa wengine, kwamba siku zote wanene kweli, kwamba wakome kudhani maovu dhidi ya mtu mwingine. Kumbuka, unaporejelea fununu upo uwezekano mkubwa unasema uongo, ama wote au kwa se-hemu. Hilo usimudu kulifanya, kwa maana “hakitaingia kamwe [katika mji] chochote kilicho … afanyaye ma-chukizo na uongo” Ufu. 21:27. Kunena maovu na kukisia uovu
27
ni mambo ambayo Bwana huchukia. {1TG16: 27.3}
Zek. 8:18, 19 — “Tena neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa ku-mi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.”
Saumu hizi za mifano za kale zitakuwa sherehe za uakisi za furaha na furaha. {1TG16: 28.1}
Zek. 8:22 — “Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana.”
Inapendeza kuwazia upanuzi wa Ukweli wa Mungu kama ulivyotajwa katika sura hii: Kwanza, mtu mmoja hunena Ukweli kwa mtu mwingine. Kisha mji mmoja huuwasilisha kwa mji mwingine. Hatimaye, taifa moja ho-dari linaalika taifa lingine kujiunga na Bwana. Hivyo ndivyo mavuno yataendelea hadi kazi ya injili imekamilika, mpaka watu wa Mungu waaminifu wasimame upande wa kulia wa Bwana (katika Ufalme), na wanafiki pamoja na washenzi wasimame upande Wake wa kushoto (katika ulimwengu uliohukumiwa wa Wapagani ambao u tayari kuangamia). {1TG16: 28.2}
Zek. 8:23 – “Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nawe, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.”
Ni busara kuhitimisha kwamba watu kumi ambao hushikilia lugha zote za mataifa katika wakati wa huku ku-kusanywa ndani kukuu ni mfano wa kikundi cha watu (kanisa lililowekwa huru kutoka kwa magugu katika wa-kati
28
wa mavuno), kama vile wanawali kumi (Mat. 25: 1) ni mfano wa kanisa wakati magugu bado yamechangamana na ngano. Watumwa kumi (Luka 19:13), na pembe kumi (Ufu. 12: 3; 17: 3) ni tarakimu za ulimwengu wote. Hawa watu kumi watanena lugha zote kama walivyofanya Mitume kwa Pentekoste. {1TG16: 28.3}
Kwa udhahiri, “Myahudi” ambaye nguo yake watu wataishika lazima aweze kuwa ambaye kupitia kwake Bwa-na anatenda kazi ili kujidhihirisha Mwenyewe na Kweli yake kwa watu. Baada ya kuugundua ukweli huu, kwa kawaida watasema, “Tutakwenda pamoja nawe: kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe” Mya-hudi huyu hasa, bila shaka, sio wa Wayahudi wa siku ya leo waliojulikana, ila uwezekano mkubwa ni mzawa wa Wayahudi Wakristo, — labda wa wale ambao katika kizazi cha mitume walipoteza utambulisho wao kwa kujiita Wakristo (Mdo. 11:26). Tena, anaweza kuwa mzao wa mmoja wa Wayahudi ambao walifukuzwa kutoka katika nchi yao, waliotawanyika katika mataifa yote, na kufyonzwa nao, kisha wakaongoka kwa Ukristo. {1TG16: 29.1}
“Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye ma-taifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu. Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya wa-tu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia …. Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake wa-takaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Mis-ri.” Isa. 11: 10-12,16. {1TG16: 29.2}
29
Hivyo ndivyo kukusanywa kwa watu kutakavyokuwa katika kutoka kwa leo kwa mwisho. {1TG16: 30.1}
Hili linatamatisha sura ya nane ya Zekaria, na sasa tutaangalia kwa ufupi baadhi ya mambo ambayo tumejifunza katika somo hili: {1TG16: 30.2}
La kwanza na la muhimu zaidi ya yote, tumejifunza kwamba ahadi zilizosheheni katika unabii wa Zekaria zitat-imizwa katika siku zetu, na kwamba kwa muda mfupi mambo ya ajabu yatatukia; kwamba wakati mmoja Bwana ilimbidi kuuacha Yerusalemu na kuwatawanya watu Wake kote kote duniani, lakini sasa Yeye atarudi na ku-wakusanya wateule Wake kutoka pembe nne za dunia; kwamba Yerusalemu utaitwa mji wa Kweli na wa furaha — hakuna hofu, hakuna ajali, hakuna huzuni huko; kwamba watu wa Mungu watafurahia amani na mafanikio; kwamba wataweza kuzungumza mema kwa kila mtu, hawatapoteza tena pumzi yao au wakati kuzungumza juu ya dhambi za wengine; kwamba kamwe hawatajishughulisha na maswala ya watu wengine; kwamba wataya-simamia yao wenyewe, na kutekeleza hukumu na amani katika maskani zao; kwamba Ukweli wa Mungu uta-panuka haraka: mwanzoni kwa mtu mmoja akinena Ukweli kwa mwingine; kisha mji mmoja unautangaza kwa mji mwingine; mwishowe taifa moja hodari litalialika taifa lingine kujiunga na Bwana. {1TG16: 30.3}
Nakubaliana nawe kwamba ahadi hizi zinaonekana kuwa za kihekaya na hata za kustaajabisha. Lakini zaidi zi-navyoonekana, matarajio maangavu zaidi, kwa maana Mungu huwa hafanyi jambo linalowezekana kwa mwana-damu, lakini Yeye hutenda mambo ambayo huonekana kwa ujumla yasiyowezekana kwa wao. Fikiria juu ya ka-zi ya ajabu ya Mungu katika Vuguvugu la Kutoka: Aliwaongoza kutoka Misri, wakati walitembea kupitia katika Bahari ya Shamu, kupitia jangwani, na kupitia katika Yordani. Alileta chini mana kutoka mbinguni, na akaen-delea kufanya hivyo kwa miaka yote arobaini. Piga picha akilini, kama unaweza,
30
Watumwa wa matofali wa Farao wanakuwa manabii, makuhani, na wafalme! Waebrania watatu kwa starehe wamesimama katikati ya tanuru la moto; ya Danieli katika tundu la simba; ya ushindi wa Mordekai juu ya Hamani; ya ushindi wa Daudi kwa jitu; ya Yusufu kulisha ulimwengu; ya Musa akiokoka mto Nile; ya Samsoni kuliangusha chini hekalu kwa mikono mitupu. Yasiyohesabika ni maajabu ya nguvu kuu za Mungu katika vizazi vyote. Uokoaji huu wote, na mwingine mwingi ulikuwa usiowezekana kabisa kwa wanadamu, lakini unaoweze-kana sana kwa Mungu. Miujiza hii ya uwezo inatuleta uso kwa uso na ukweli kwamba Mungu yu katika shughu-li ya kufanya “yanayowezekana” kutoka kwa isiyopatana “haiwezekani.” Kwa hivyo, “mikono yenu na iwe ho-dari, ninyi mnaosikia siku hizi maneno haya” ya Bwana . {1TG16: 30.4}
—-0—-
Usiyakose Manufaa Juu ya Hili
Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG16: 31.1}
31
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 15, 16
Kimechapishwa nchini Marekani
32