20 Feb Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 09, 10
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 9,10
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
“NYUMBA YA DAUDI KAMA MALAIKA WA BWANA”
NI NINI HULETA UFANISI KWA UAMSHO NA MATENGENEZO?
1
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, aya mbili za kwanza kwenye ukurasa wa 159. {1TG9: 2.1}
M.B, uk. 159 — “Mungu ni Baba yetu, ambaye anatupenda na kututunza sisi kama watoto Wake; Yeye pia ni Mfalme mkuu wa ulimwengu. Maslahi ya ufalme Wake ni maslahi yetu, na tunapaswa kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wake. {1TG9: 2.2}
“Wanafunzi wa Kristo walikuwa wanatazamia kuja mara moja kwa ufalme wa utukufu Wake; ila kwa kuwapa sala hii Yesu alifundisha kwamba ufalme haungalianzishwa wakati huo. Walipaswa kuomba kwa ajili ya kuja kwake kama tukio bado la baadaye. Lakini ombi hili lilikuwa pia uhakikisho kwao. Ijapo hawangaliuona ufalme ukija katika siku zao, ukweli kwamba Yesu aliwahimiza kuomba kwa ajili yake, ni ushahidi kwamba kwa wakati mwafaka wa Mungu utakuja kwa uhakika.” {1TG9: 2.3}
Je, ni mbegu gani ya wazo ambayo imesheheni katika kusoma hili? Tunapaswa kuomba kuhusu nini? — Ili tuweze kuelewa kwamba sala pekee yake haitatupeleka katika Ufalme; kazi hiyo inahitajika kila sehemu kama ilivyo sala. Naam, maslahi ya Ufalme Wake lazima yawe juu zaidi katika akili zetu. Tunapaswa ‘kufanya kazi’ kwa ajili ya ujenzi wake na pia kuomba kwa ajili yake. {1TG9: 2.4}
2
“NYUMBA YA DAUDI KAMA MALAIKA WA BWANA”
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, OKTOBA 5, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Tutaenda kwa Zekaria, sura ya kumi na mbili. andiko la somo letu linapatikana katika aya ya nane, lakini ili kuu-pata wakati na watu ambao aya hiyo huzugumzia moja kwa moja, lazima tuanze somo letu na aya ya kwanza ya sura hii. {1TG9: 3.1}
Zek. 12: 1 — “Ufunuo wa neno la Bwana juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo Bwana, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.”
Zipo pointi mbili katika aya hii ambazo tunapaswa kuzingatia sana: (1) kwamba mzigo ni wa Bwana, na (2) kwamba mzigo Wake ni kwa ajili ya Israeli, kanisa, sio kwa ulimwengu. {1TG9: 3.2}
Aya ya 2 — “Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa ka-bila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.”
Kutoka kwa aya hii tunajifunza kwamba nchi za Mataifa zitauhusuru sio tu Yerusalemu, lakini dhidi ya Yuda pia — ndiyo, dhidi ya Ufalme wote, kanisa, au watu. Na kwa wakati huo, wakati wa kuuhusuru, Yerusalemu utafanywa kikombe cha kuyumba-yumba
3
kwa watu wote; yaani, watu wote wataogopa Yerusalemu na kutetemeka mbele yake. {1TG9: 3.3}
Aya ya 3 — “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.”
Uzingirwaji huu hautafanywa tu na mataifa yaliyo karibu na Yerusalemu, ila na watu wote wa dunia, jambo am-balo linawezekana tu kwa njia za mawasiliano katika siku zetu. Hivyo Yerusalemu utakuwa jiwe la kuwalemea watu wote wanaouzunguka. Katika jitihada za kukabiliana na hofu yao wanajitwika kwa kuuzingira mji. Kwa kazi hii ya uovu watakatwa-katwa vipande vipande. {1TG9: 4.1}
Aya ya 4 — “Katika siku hiyo, asema Bwana, nitamtia kila farasi ushangao, na yeye ampandaye nitamtia wazimu; nami nitaifunulia nyumba ya Yuda macho yangu, nami nitamtia upofu kila farasi wa hizo kabila za watu.”
Ingawa Bwana atawapiga kwa mshangao, kwa wazimu, na kwa upofu, wale watakaouhusuru mji, hata hivyo Yeye atayafumbua macho Yake juu ya nyumba ya Yuda. {1TG9: 4.2}
Aya ya 5 – “Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu kati-ka Bwana wa majeshi, Mungu wao.”
Baada ya wadhambi kuondolewa kati yake kwa kazi ya Hukumu ya walio hai kisha watawala wa Yuda wa-tafahamu kwamba nguvu zao hutegemea wakaazi watakatifu wa Yerusalemu na kwa Bwana Mungu wao, basi inakuwa kwamba hakika watakuwa wenye nguvu. {1TG9: 4.3}
4
Hebu tuone kile aya inayofuata inasema juu ya hili: {1TG9: 5.1}
Aya ya 6 — “Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kuume na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.”
Haijalishi kile tunachofikiri, Mungu atakuwa na watu wenye nguvu, waaminifu, aina hasa inayoelezwa hapa; na Yerusalemu utakaliwa na watu watakatifu, hakuna mdhambi miongoni mwao. Kwa sababu nabii Eliya wa uaki-si, ambaye anaonekana kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana, tu kabla ya Siku ya Hukumu kwa ajili ya walio hai, analipata kanisa limefurika Ibilisi vibaya mno kama vile lilivyokuwa kanisa la Kiyahudi katika siku ya Kristo, na kama vile watakatifu, malimbuko, yanapaswa kuokolewa mmoja mmoja, Yeye mwanzoni anawatuma wavuvi kuwavua na baadaye wawindaji kuwasaka (Yer. 16:16). Hivyo anawakusanya mmoja mmoja (Isa. 27:12, 13). Na ndivyo ilivyo leo — wanavuliwa kwa vitabu hivi bila kulipia, na sasa wanasakwa na watu nyumba kwa nyumba zao, kama wao wako mjini, kijijini, au mashambani. {1TG9: 5.2}
Aya ya 7 — “Naye Bwana ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili utukufu wa nyumba ya Daudi, na utukufu wa wenyeji wa Yerusalemu, usipate kutukuzwa kuliko Yuda.”
Yeye ataziokoa hema (makao ya unyenyekevu badala ya majumba au makasri) za Yuda kwanza, yaani, Bwana atawaokoa kwanza watu wa kawaida, washiriki ili kwamba ukasisi usiweze kujiinua wenyewe juu ya washiriki, ili wote waweze kujifunza kumpa Mungu utukufu, sio kwa mtu yeyote. {1TG9: 5.3}
Maadamu hakuna kitu kama kile aya hizi za Maandiko hutabiri kimewahi kufanyika huko Yerusalemu au kwa sehemu
5
Nyingine yoyote ya dunia, bila shaka utabiri huu bado haujafikia utimilifu wake. Na sasa tunataka kujua iwapo utatimizwa kwa wakati wetu au baadaye. {1TG9: 5.4}
Kwa sababu kazi tunayoifanya sasa haijafadhiliwa na mtu yeyote, na maadamu Mungu ametuongoza umbali wote kwa uhalisi kama Alivyoongoza vuguvugu la Kutoka, Akiitengeneza njia yetu inchi kwa inchi kama Majaaliwa yanavyoelekeza, na pia kwa kuwa sisi tu ndio watu ambao wanao ujumbe wa kuanzishwa upya kwa Nyumba ya Daudi, na wa kurejesha “mambo yote” (Marko 9:12) na kwa hiyo tumeitwa Wadaudi, hakuna kukwepa hitimisho ila kwamba wakati kwa ajili ya kuutimiza unabii huu umekaribia sana hata mlangoni, sababu ambayo tangazo la matukio haya sasa linapigiwa tarumbeta kote kote katika ulimwengu wa Waadventista. {1TG9: 6.1}
Kwa udhahiri, basi, chochote ambacho Bwana atasema katika sura hii ni kwa ajili yetu kujifunza na kwa ajili ya mahitaji yetu maalum na ya sasa. Ni mawasiliano hasa yanayoelekezwa kwetu na kufunuliwa hasa kwa wa-kati huu ili tuweze kujua ni nini Mungu angependa tufanye na jinsi ya kukifanya hivyo ili kwamba upesi vitu vyote viweze kurejeshwa. {1TG9: 6.2}
Sasa tunasoma andiko la somo letu– {1TG9: 6.3}
Aya ya 8 — “Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.”
Mbali na kutuhakikishia kwamba Bwana atawalinda watu Wake, Uvuvio unawafananisha kwa Daudi kwa Mungu. Hata wale wadhaifu “watakuwa kama Daudi; na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, “ “ kama ma-laika wa Bwana mbele yao.” Ni namna gani
6
Taarifa ya ajabu! Ni ya jinsi gani fursa ya kufananishwa kwa Mungu Mwenyewe! {1TG9: 6.4}
Sasa, ili mmoja ajue maana ya kuwa “kama Daudi,” mmoja lazima ajue ni aina gani ya mtu Daudi wa zamani alikuwa. {1TG9: 7.1}
Mwanzo, alikuwa mchungaji bora, aliyahatarisha maisha yake kwa ajili ya kondoo. Unakumbuka kwamba ili kuwaokoa wana-kondoo yeye kwa ujasiri alimwandama simba na dubu, na akawaua kwa mikono yake mitupu. Na kuuokoa uhuru wa taifa lake na heshima kuu ya Mungu, kwa tukio lingine, tena alihatarisha uhai wake kwa ujasiri alipolikabili jitu Goliathi. Kwa sababu ya uaminifu wa Daudi, Mungu alimwokoa kutoka kwa hayawani na kutoka kwa jitu, na kumfanya kuwa mfalme juu ya watu Wake! {1TG9: 7.2}
Uaminifu wa mtu katika mambo madogo huashiria uaminifu wake katika mambo makubwa pia. Uaminifu daima huleta kukwezwa. Kwa hivyo, ili uwe kama Daudi, mmoja lazima awe mwaminifu, mwenye kutegemewa, na mwenye bidii kwa ajili ya Ufalme wa Mungu alivyokuwa Daudi wa zamani. {1TG9: 7.3}
Sasa, kwamba tuweze kujua maana ya kuwa “kama Mungu,” tunapaswa kujifunza vile Mungu alivyo. Mwanzoni Yeye hakuiumba tu na kuijaza kwa wingi dunia kila kitu chema kwa ajili ya viumbe Wake, lakini pia Yeye alipanda bustani (maskani) kwa ajili ya mtu huyo. Hivyo alifanya makazi ya kielelezo kwa ajili ya wanadamu wote ambao wangeishi baadaye. Yeye alimfundisha Adamu jinsi ya kuyaweka makazi na jinsi ya kuitunza bustani. Yeye alimfundisha kuzungumza na kutambua maumbile kati ya mnyama mmoja na mwingine, kuwaita majina ipasavyo. Mungu alimpa mwanadamu maarifa na maisha ili kumfanya awe na furaha, na wa umuhimu katika kuufanya ulimwengu uwe unavyopaswa kuwa. Hata baada ya jozi takatifu kuanguka dhambini Mungu alikuwa bado
7
anapendezwa ndani yao kama Alivyokuwa awali – kiasi kwamba, kwa kweli, Yeye mara moja alianza kuwafun-disha jinsi ya kujikomboa wenyewe, na kurejea kwa makazi yao ya milele. Tangu siku hiyo hadi hii, Yeye ameendelea kuifunza familia ya wanadamu. {1TG9: 7.4}
Ili kuifanya kazi hii ya kuokoa Mungu alimtuma Roho wa Kweli, Yeye aliwatuma manabii na malaika, pia Mwana Wake pekee — walimu wote wa ukombozi. Yeye mwenyewe alishuka hadi Sinai na hata ingawa wali-waua karibu watumwa Wake wote ikiwa ni pamoja na Mwanawe, bado, kupendezwa Kwake kwa daima katika jamii yaq wanadamu kumeendelea mpaka leo. Bila kuzingatia makosa yetu, ahadi Yake kuturejesha tena Edeni huko ili tuishi pamoja Naye iwapo tutatubu, bado inasimama kwa uhakika kama lifanyavyo jua. {1TG9: 8.1}
Sasa unaona vile Mungu alivyo, na iwapo tutakuwa “kama Mungu,” basi hivyo ndivyo sisi, pia, tunapaswa ku-wa. Hivyo inamaanasha kwamba lazima tupendezwe mmoja kwa mwingine na katika kuujenga Ufalme Wake kama Yeye anavyopendezwa. Tunapaswa kuwa bila ubinafsi jinsi Yeye alivyo. Lazima tuwafundishe wengine kwa furaha kila kitu ambacho ametufundisha. Tunapaswa kufanya yote tunayoweza ili kuboresha hali ya kuishi ya wengine. Tunapaswa kuifanya dunia kuwa bora zaidi kuliko inavyoweza kuwa kama hatugekuwa ndani yake. Katika juma la uumbaji Mungu alifanya sehemu Yake. Sasa tunapaswa kuifanya sehemu yetu ya uumbaji ikiwa tunapaswa kuwa kama Mungu. {1TG9: 8.2}
Kitu chochote chema ambacho tunaweza kuwa nacho, iwe ni taaluma au zawadi nyingine ambayo ni ya thamani kuwa nayo tunahitajika kuwa waaminifu kwayo na wenye hamu ya kuwafundisha wengine jinsi Yeye alivyo mwaminifu na anayejishughulisha kutufundisha. Ikiwa tunaupuuza wajibu huu, hatuwezi tu kushindwa kuwa kama Mungu, lakini hata tutahitajika kutoa hesabu ya kutokujali kwetu. {1TG9: 8.3}
Katika maisha yangu yote nimewapata watu wanao ubinafsi sana na wanahofia kwamba mtu anaweza kuwapita kwa
8
njia moja au nyingine. {1TG9: 8.4}
Nilipokuwa nikijifunza taaluma yangu, mara nyingi niliona ni muhimu kuuliza maswali, lakini baadhi ya watu ambao nilikuwa nikifanya kazi nao waliyakwepa maswali yangu. Ubinafsi wao, hata hivyo, haukunizuia kujifun-za kile nilitaka kujua. Nilijifunza kwa njia nyingine. Watu hao, hata hivyo, hawakudai kuwa wamestawi katika maisha ya Ukristo kama tunavyodai kuwa, na kwa sababu hii wivu wao na ubinafsi unaweza kuhukumiwa tu kwa kutojua. Lakini sisi ambao tunajua vyema tunapaswa kujaribu kupitisha maarifa yetu kwa wengi iwezeka-navyo, bila kutarajia kupewa chochote ila mafanikio yao katika maisha. Mungu Mwenyewe atatupatia thawabu. Lakini tukijaribu kuyaweka maarifa kwetu wenyewe, sisi kwa hakika zaidi tutapata hasara. Kumbuka, pia, kwamba chochote chema tuchoweza kumiliki ni zawadi kutoka kwa Mungu. Papa hapa msemo wa tangu zamani unafaa vizuri: “Hakuna kikomo kwa mtu mzuri anayeweza kufanya ikiwa hajali ambaye anapata sifa.” {1TG9: 9.1}
Bwana aliwafundisha ndege jinsi ya kuishi na jinsi ya kujenga viota, na jinsi ya kuwalea makinda wao. Basi hatupaswi kuwasaidia wengine kujenga na kuboresha makazi yao na maisha? Unamkumbuka Yesu akisema, “Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.” Mat. 10:42. {1TG9: 9.2}
Mungu asingalikuwa alivyo Yeye, Yeye hangalikuwa Mungu; na iwapo tunaendelea kama tulivyokuwa daima hatuwezi kuwa kamwe “kama Mungu.” {1TG9: 9.3}
Nyumba ya Daudi, zaidi ya hayo, itakuwa “kama malaika wa Bwana mbele yao.” Taarifa hii inamaanisha nini? — Ina maana kwamba ikiwa tunapaswa kuwa washiriki
9
wa nyumba ya Daudi, ni lazima tuwe kama Daudi, kama Mungu, na kama malaika, pia. Malaika ni hodari katika nguvu; hutii amri za Mungu; Wao huisikiliza sauti ya Neno Lake (Zab. 103: 20). Wao kwa ukaribu daima wana-wahudumia watakatifu, na wamewaongoza salama juu kila vita katika vizazi vyote. Mungu anatarajia kanisa Lake na watu kuwa hivyo tu — “kama malaika wa Bwana.” Bila kujali kile sisi kama watu binafsi huchagua ku-wa, Mungu hata hivyo atakuwa na kanisa ambalo litakuwa haya yote. {1TG9: 9.4}
Sasa, ni nini kusudi la jumla la nyumba ya Daudi? — Nyumba ya Daudi, Maandiko yanafunua, inajengwa kwa kusudi la mara tatu: (1) Wakati wa kukusanywa ndani watu, “itajenga mahali pa kale,” ili “kupainua mahali pali-pokuwa ukiwa zamani,” na “kutengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.” Isa. 61: 4. Kazi hii ya kujenga upya na kurejesha inao mfano wake wa kuujenga upya Yerusalemu wa kale na Wayahudi wa kale waliokuwa wakirudi kutoka uhamisho wao Babeli kwenda nchi ya baba zao. Kama vile walivyojenga mahame, uharibifu wa zamani — hekalu la Bwana, mji na kuta — na kurejesha ibada ya Mungu kulingana na mapenzi Matakatifu ya Bwana mwenyewe, hivyo sisi, pia, sasa katika kukusanywa ndani kwa uakisi tunaitwa kufanya kazi sawa na hiyo, ni kubwa zaidi katika upeo na kipimo. Lazima kwa hivyo tufanye kazi hata zaidi bila kukoma kuliko walivyofanya, na kuwa na furaha na shukrani kwa kupewa upendeleo wa kuwa na sehemu katika hii kazi kubwa na yenye utukufu. {1TG9: 10.1}
(2) Zaidi ya hayo kwa kazi hii kuu na kubwa, ambapo katika mkono wa Mungu kama shoka la vita (Yer. 51:20), Yeye kwa hilo ataivunja nira ya Mataifa ambayo sasa iko juu ya mabega ya watu wa Mungu. Kwa hilo Yeye atawakomboa watu Wake kutoka kwa utawala wa Mataifa: “kutoka Ashuru,
10
na kutoka Misri, na Pathrosi, na Kushi, na Elamu, na Shinari, na Hamathi, na visiwa vya baharini …. “(Isa. 11:11). Kwa hilo Yeye “atawatwekea mataifa bendera,” na “atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, na atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika kutoka ncha nne za dunia.” Isa. 11:12. Ili kazi hii ipate kufanyika mwanzoni tutakuwa “wavuvi wengi,” kisha “wawindaji wengi” (Yer. 16:16). Hivyo ni kwamba malimbuko yatakusanywa “mmoja mmoja.” Isa. 27:12. Tuko sasa katika siku za kuwinda — kutoka mji hadi jiji, kutoka kijiji hadi kijiji, na kutoka kwa mlango hadi kwa mlango, kitu ambacho hakijawahi kufanyika awali. Mbali na kuvua na kuwinda sisi pia tutaitengeneza “njia kuu kwa mabaki ya watu Wake watakaosalia, [baada ya malimbuko ku-kusanywa] watokao Ashuru; kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Mis-ri.” Isa. 11:16. Baada ya uwindaji huu kukamilika na barabara kuu kujengwa, kisha inakuwa kwamba mavuno ya pili yatamiminika kwa mlima wa Bwana. Taifa moja, kama ilivyo, litasema kwa taifa lingine, “Njoni, twende juu ya mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na Neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika. 4: 2. {1TG9: 10.2}
Hivyo kazi yetu pia inao kama mfano wake vuguvugu la Kutoka lilipokuwa likitoka Misri, likijisimamisha katika nchi ya ahadi. Walipowekwa huru kutoka kwa utumwa wao wa Misri, ndivyo tutakavyowekwa huru kutoka kwa nira ya ulimwengu; na kama vile walivyoimiliki nchi hiyo, na kuanzisha ufalme, ndivyo tutakavyofanya ikiwa tutayafanya makosa yao kuwa ngazi yetu kwa ufanisi. {1TG9: 11.1}
(3) Mwishowe, tunapaswa kuharakisha “hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa
11
zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?.” Tunapaswa kuileta “mbingu mpya na nchi mpya, am-bayo haki yakaa ndani yake.” 2 Pet. 3:12, 13. {1TG9: 11.2}
Kwa awamu nyingine ya kazi hii, sisi pia tunayo gharika kama mfano. Maadamu mahubiri ya Nuhu yalileta mwisho wa dunia katika siku yake, hivyo mahubiri yetu yataleta mwisho wa dunia katika siku yetu. Kwa sababu waaminifu wa siku hiyo walipata kimbilio katika safina ya Nuhu, hivyo waaminifu wa leo watapata kimbilio katika Ufalme (kanisa lililotakaswa) ambalo limetabiriwa hapa. {1TG9: 12.1}
Kazi ya mavuguvugu haya matatu – la Zekaria, la Musa, na la Nuhu — kwa hivyo, yanakuwa mifano kwa kila awamu ya kazi yetu. {1TG9: 12.2}
Hapa inaonekana wazi kwamba kazi yetu tuliopewa na Mungu haijumuishi kuhubiri tu, bali pia kazi ya mikono, pia. Wapo maelfu ulimwenguni ambao wanayo hamu kuhubiri kama vile walivyo dubu hujaza matumbo yao baada ya kupisha majira yao ya kipupwe, lakini wapo wachache ambao wataweka mabega yao kwenye gurudu-mu na kuendelea kusukuma. {1TG9: 12.3}
Ulimwengu unachohitaji leo sio wahubiri, ila walimu ambao wanaweza kufundisha kwa mkono mmoja na ku-tumia sululu au koleo kwa mkono mwingine. Wala ulimwengu hauhitaji watu “wanaotaka kupata kwa hila” ofisi ya Musa na ya Haruni, lakini unawahitaji sana watu ambao wanaweza kuzitii amri na kwa ufanisi kuzitekeleza, watu ambao wanadhubutu kukabili jitu, simba, na dubu, — watu wanaodhubutu kuwa mashujaa kwa ajili ya Mungu,” “watu wa kushangaza,” watu wenye imani isiyofifia na uvumilivu usio na kikomo, wanaoamini kwam-ba Mungu Mwenyewe ndiye nahodha wa meli, na kwamba kwa hivyo haiwezekani kushindwa. Kwa kweli ulimwengu unawahitaji watu kama Nuhu, Musa, Daudi, Ezra, Nehemia, na idadi kubwa ya Ayubu. {1TG9: 12.4}
12
Kazi na wajibu wetu sasa umefanywa wazi kama iwezekanavyo hasa kwa wakati huu. Hatuhitaji, kwa hivyo, kukosea. Hatuhitaji kuwa wasiojua kile kinachotakikana kifanyike na jinsi kitakavyofanywa. {1TG9: 13.1}
Wengi huamini kwa kweli kwamba wanafanya kazi ya Mungu, au angalau kuisaidia. Lakini ikiwa watachunguza mafanikio yao ya kila siku, nia zao, malengo na makusudi yao, baadhi wataona kwamba hawafanyi kazi kwa ajili ya Mungu, ila kwamba wao ama wanaupitisha tu wakati, au kufanya kazi kwa ajili ya ubinafsi. Kweli, sasa kama ilivyokuwa wakati wa Musa, zipo nyakati ambapo mtu hupata hasara kujua iwapo watakatifu au mashetani wanajishughulisha kwa kazi kubwa ya Mungu. Tulia, sikiliza, fikiria. Jichunguze wenyewe. Itakuwa vyema kwa muda wako na nguvu zako. Tambua wewe ni nani, nani ulivyo, na wapi ulipo. {1TG9: 13.2}
Ezra na Nehemia walikuwa na wakati mgumu kujenga mahame ya kale. Ninaamini kwamba Mungu angaliweza kuwaweka malaika kuwazuilia mbali maadui wao kutohitilafiana na mradi wao, lakini Yeye alichagua kuwa na wajenzi waaminifu washikilie upanga kwa mkono mmoja na matofali kwa mkono mwingine (Neh. 4:17, 18). Kazi yao ilikuwa ngumu sana, ikiwa haikuwa ngumu kuliko yetu, lakini walikuwa waaminifu kwayo, na hatuwezi kumudu kuwa waaminifu wapungufu kuliko wao. Ndio, walifanya kazi nyingi kama vile walivyokuwa wakifundisha. Hawakufundisha dini tu, bali kujenga, pia. Je, huoni kwamba kama vile mifano inavyoonyesha, mambo tunayoitwa kufanya hayawezi kufanywa kwa kufundisha pekee? Sasa tuko tayari kusoma — {1TG9: 13.3}
Aya ya 9, 10 — “Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu. Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba;
13
nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.”
Wakati ambapo Mungu anaanza kuyaangamiza mataifa, Yeye atawamwagia watakatifu Wake Roho ya neema, kisha wataomboleza kweli kwa kutenda dhambi dhidi ya Bwana. Ni kwa sababu watu hawana sasa roho hiyo kwamba hisia zao za kibinafsi zinaumizwa kwa urahisi kwa ajili ya kitu chochote kidogo kinachofanyika dhidi yao. Na kwa kuwa Roho ya neema husababisha mtu kuomboleza sio kwa ubinafsi, inaeleweka kwamba kujihu-rumia, na kuumizwa juu ya kile ambacho wengine hufanya au kusema dhidi yake ni ishara ya uhakika kuwa ba-dala ya kujawa na Roho ya neema, yeye anajawa na roho ya Ibilisi, ambaye kila siku anatafuta kukatisha tamaa na kuuvunja moyo kwa kujihurumia. Kumbuka kwamba kujihurumia ni kushindwa nafsi kabisa. Hakuna hata mmoja wetu aliyewahi kuteswa kama alivyokuwa Bwana, na bado “nafsi” ndani yake haikuwahi kuumizwa. {1TG9: 14.1}
Ikiwa tunapaswa kusikitika kwa ajili ya mtu yeyote, hebu tusisikitike kwa ajili ya ubinafsi. Wakati mwingine hufikiri tunasikitikia kutenda kwetu dhambi na kusababisha Bwana ateswe na kusulubishwa, lakini huzuni yetu sio ya kweli; ni ya nadharia tu. Wakati Roho hii ya neema imemwagwa juu yetu, wakati huo tutafahamu kika-milifu kwamba hawakuwa Wayahudi, bali dhambi zetu sote zilizomsulubisha Kristo, na basi tutaweza kuhesabu kuwa ni upendeleo kuteswa kwa ajili ya Kristo. {1TG9: 14.2}
Aya ya 11-14 — “Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao;
14
jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao.”
Siku kuu inakuja, Ndugu, Dada. Iwapo siku hiyo haingalikuwa i karibu, hatungaliweza kuwa tumeangaziwa nuru hii kwenye njia yetu leo. Hebu kwa hivyo tufanye kazi kwa ajili ya kuujenga Ufalme wa Bwana, ili mapen-zi Yake yafanyike ndani yetu, na hivyo mwishowe yafanyike “duniani kama ilivyo mbinguni.” Kama watangu-lizi wa Ufalme Wake, hebu tufanye yote tunayoweza kuthibitisha tunaastahili kusimama pamoja Naye juu ya Mlima Zayuni, kuwa “kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele” ya watakatifu, kuipeleka injili ya milele kwa mataifa yote, na hivyo kuleta dhambi za dunia na mateso kwa kikomo. {1TG9: 15.1}
Usiyakose Manufaa Juu ya Hili
Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG9: 15.2}
15
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, kuanzia aya ya mwisho kwa ukurasa wa 108 hadi 109. {1TG10: 16.1}
MB, uk. 108, 109 — “… ‘Ufalme na mamlaka, na ukuu wa ufalme chini ya mbingu yote,’ utapewa ‘watu wa wa-takatifu wake Aliye Juu.’ Watauridhi ufalme ulioandaliwa kwa ajili yao “tangu mwanzo wa kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Na Kristo atachukua Mwenyewe nguvu Zake kuu na kutawala …. Ni wale tu wanajitolea kwa huduma Yake, wakisema, ‘Mimi hapa; nitume, ‘kuyafumbua macho ya kipofu, kuwageuza watu ‘kutoka gizani hadi kwenye nuru, na kutoka kwa mamlaka ya Shetani hadi kwa ya Mungu, ili wapate kupokea msamaha wa dhambi, na urithi kati ya wale waliotakaswa,’ – wao pekee huomba kwa uaminifu, ‘Ufalme wako uje.’ “ {1TG10: 16.2}
Mistari hii inatuambia kwamba wale ambao kwa uaminifu huomba “Ufalme wako uje,” wale ambao hujitolea kwa utumishi wa Mungu, wale ambao midomo yao huguswa na makaa ya mawe kutoka kwenye madhabahu (ambao hujiona wenyewe kuwa wadhambi), na ambao kisha husema, “Mimi hapa; nitume,” ndio pekee ambao wanastahili kutumwa katika shamba la mizabibu la Mungu leo. {1TG10: 16.3}
Na sasa ombi letu litakuwa nini? — Kwamba tuweze kulingana na dhamiri kusema, “Ufalme wako uje,” tukitam-bua kwamba kwa uhalisi tunasema kwamba tunafanya kila kitu tunachoweza kuufanya uwe hivyo; kwamba tun-afanya kazi kwa ajili yake bila kukoma; kwamba tunayazingatia mapenzi ya Bwana kama walivyo malaika. {1TG10: 16.4}
Inashangaza namna gani mtu kuomba sala ya Bwana wakati anafanya kitu kingine kuliko kufanya kazi kwa ajili ya utimilifu wake! Ni kama mtu anayesema, “Nipe mkono wako,” ilhali wakati huo huo anaupuuzilia mbali. Om-bi kama hilo ni namna moja ya kukufuru. Tunapaswa kuomba ili tuyapatanishe mapenzi yetu kwa mapenzi ya Mungu, kuwa waaminifu katika kazi Yake, na kuwa kwa uaminifu Wake pekee yake. {1TG10: 16.5}
16
NI NINI HULETA UFANISI KWA UAMSHO NA MATENGENEZO?
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, OKTOBA 12, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Katika Picha za Maisha, uk. 425, tunasoma — “’Nimevutiwa sana na matukio ambayo yamepita hivi karibuni mbele yangu katika msimu wa usiku. Ilionekana kuwapo na vuguvugu kubwa — kazi ya uamsho — ikienda mbele katika maeneo mengi. Watu wetu walikuwa wakiingia kwenye mstari, wakiitikia mwito wa Mungu. Ndugu zangu, Bwana ananena nasi….’” {1TG10: 17.1}
Hapa ni utabiri wa vuguvugu kubwa, vuguvugu ambalo litaendeleza kazi ya uamsho wa mafanikio katika mae-neo mengi. Hapa pia inaonekana kwamba watu wataitikia mwito wa Mungu, na kwamba kazi hii ilioonyeshwa katika maono itaendeshwa na vuguvugu lililopangwa na Mungu, sio na Dhehebu hata hivyo, na sio na mtu hapa na mtu pale. Vuguvugu lenyewe limeundwa na Mungu, sio lililobuniwa na wanadamu. {1TG10: 17.2}
Tumeona katika miaka mingi watu wengi na makundi ya watu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Waadventista ambao kwa wakati mmoja au mwingine walifanya tamasha ya kile walichokiita “uamsho na matengenezo,” lakini hakuna hata mojawapo wayo yamewahi kuweza kufanikisha mengi, ikiwa chochote. Moja baada ya moja yaliishia kwa kujiondoa kwa kuchukiza. Badala ya kuhuishwa na kufanya matengenezo kwa ajili ya kuwa bora, wao baada ya kila jitihada kama hii waliteleza mbali kutoka kwa Mungu na karibu na karibu hadi kwa sakafu ya
17
viwango vya dunia. {1TG10: 17.3}
Ni lazima iwe dhahiri kwa kila mtafuta Ukweli aliye macho kwamba uamsho ambao Picha za Maisha zinatabiri na kuonyesha ni hili vuguvugu la washiriki wa kawaida, maana kando na vuguvugu hili ambalo sasa liko kwa miguu, aste aste lakini kwa uthabiti linafagilia mbali takataka kote kote katika ulimwengu wa Waadventista, hatujawahi kamwe hata sasa ndani ya uwepo wa maandiko ya mwandishi katika Picha za Maisha kuona vuguvugu lililopangwa kama hili likiendesha uamsho kama huu. {1TG10: 18.1}
Biblia inasheheni mpango kamili wa wokovu kwa wanadamu wote. Najuaje hili? — Nalijua kwa sababu kisa Chake huanza na uumbaji na huisha na dunia iliyoumbwa upya. Kati ya ukurasa wa kwanza na wa mwisho wa Biblia, basi, hapo ipo kanuni kamili kwa ajili ya wokovu na ukombozi wa mwanadamu. Na iwapo uhuisho na matengenezo kama haya yaliyotabiriwa yatatukia duniani kati ya matukio hayo mawili (uumbaji na nchi mpya), basi habari na mfano wa kazi hiyo lazima ipatikane mahali fulani katika kurasa za Biblia. {1TG10: 18.2}
Kabla ya kusoma kile ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo, nafikiri tunapaswa kwanza kwa uthabiti tu-fafaue maneno “uamsho” na “matengenezo.” Kwa “uamsho” kamusi inatoa: “Kurejesha; kutia moyo; kufanya upya; kuamsha tena; ili kuanzisha upya.” Na kwa “matengenezo” kamusi inatoa ufafanuzi huu: “kufanya bora kimaadili; mabadiliko kwa ubora.” {1TG10: 18.3}
Kristo Haki Yetu hufafanua maneno haya ya hotuba kama ifuatavyo: “’Uamsho na matengenezo lazima yafanyi-ke chini ya utumishi wa Roho Mtakatifu. Uhuisho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uhuisho huashiria kufanywa upya uhai wa kiroho, kuzifanya
18
kuwa hai nguvu za nia na moyo, ufufuo kutoka katika kifo cha kiroho. Matengenezo huashiria kupanga upya, badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea. Matengenezo hayawezi kuzaa tunda zuri la haki isipoku-wa yameunganishwa na uamsho wa Roho. Uhuisho na matengenezo yanapaswa kufanya kazi yake iliyowekwa rasmi, na kwa kuitenda kazi hii vinapaswa kuchangamana.’” — Uk. 154, toleo la 1926; uk. 121, toleo la 1941. {1TG10: 18.4}
Ipo tofauti gani kati ya “uamsho” na “matengenezo”? — Uhuisho humaanisha kuzirejesha sifa za kiroho kwa uzi-ma; kuifanya hai nia na moyo kwa kuijenga awamu ya kiroho ya maisha; kuianzisha upya, kuirekebisha. Na matengenezo humaanisha kuibadilisha nafsi ya mtu kuwa bora, kuzipanga upya nguvu za maadili chini ya mwongozo wa Mungu. {1TG10: 19.1}
Katika Biblia upo mfano mmoja (kielelezo) wa uamsho na matengenezo kama ule ambao umetabiriwa hapa. Tunaupata umeandikwa katika vitabu vya unabii wa Hagai na Zekaria. {1TG10: 19.2}
Unakumbuka kwamba Wayahudi wa kale waliachiliwa na Koreshi, mfalme wa Uajemi, kutoka kwa uhamisho wao mara tu Babeli ilipoanguka. Alitoa amri ya kwamba warejee katika nchi yao ili kujenga upya mahame na magofu. Mfalme aliamuuru hasa kwamba kulijenga upya hekalu na kuanzisha upya ibada ya Mungu wa Mbinguni kufanyike kwa uaminifu na kwa upesi. Uamsho wa sehemu ya kiroho ya taifa (hekalu na mfumo wake wa ibada) lilikuwa jambo lao kuu. Lakini kwa mujibu wa Ezra 4:24, amri ya Koreshi na nyingine ambayo ilit-olewa miaka michache baadaye, zote zilivurugwa, na katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, Mfalme wa Uajemi, kazi hiyo ilikoma kabisa, na inaonekana
19
hapakuwa na tumaini la kuendelea tena. {1TG10: 19.3}
Kisha ikawa kwamba manabii Hagai na Zekaria waliitwa kwa ofisi yao ya kinabii na wakaamuru kuwahuisha na kuwapanga upya wajenzi kwa ajili ya mradi wa hekalu ulioachwa. Angalia Hagai 1: 1 na Zekaria 1: 1. Matokeo ya kufurahisha na ya kushangaza yalikuwa kwamba ndani ya miaka minne mifupi jengo la kiroho la taifa lilimal-izika haraka, ilhali juhudi zote za awali na za kujikakamua za wafalme na watu, zikifunika kipindi cha zaidi ya miaka thelathini, zilishindwa kabisa. (Angalia Ezra 6:15) {1TG10: 20.1}
Hebu sasa tuangalie kwa njia halisi kwa nini jitihada za wajenzi na amri za wafalme mwanzoni zilishindwa, na kwa nini hatimaye walifanikiwa: Kabla Hagai na Zekaria kuitwa kwa ofisi ya kinabii, Wayahudi wengi walirejea kutoka Babeli hadi Yerusalemu, ingawa wengi walibaki huko Babeli; yaani, wajenzi kwa hiari walienda kujenga tu kwa sababu utekwa ulikuwa umeisha, na kwamba mfalme alikuwa ameamuru kwamba hekalu la Mungu lina-paswa kujengwa. Lakini wote wajenzi na jitihada za mfalme walishindwa kabisa — yote yalikuwa sifuri. Kisha ilikuwa kwamba kwa njia ya manabii Wake, Hagai na Zekaria, Mungu aliielekeza kazi hiyo, na kisha ilikuwa kwamba waliikamilisha haraka. Kwa maneno mengine, sio kabla ya Bwana kuyachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe kupitia kwa Roho ya Unabii kazi hiyo ilifanikiwa. Kwa hakika, historia takatifu inathibit-isha kwamba hakuna chochote kilichowahi kufanikiwa katika kazi ya Mungu bila Roho ya Unabii aliye hai ndani yake. {1TG10: 20.2}
Kwa mfano, Musa alielewa tangu utotoni hadi alipokuwa mtu mzima kwamba kura yake ilikuwa ni kuwakom-boa wana wa Israeli kutoka kwa yadi za matofali za Farao. Na alipokua mtu mzima na kuelimishwa vizuri katika nyua za Farao, na kujiona kuwa hodari na mwenye uwezo, yeye
20
haraka alianza kulikomboa jeshi la Waebrania lililofanywa kuwa watumwa: alimuua Mmisri mmoja, akagombana na Mwebrania, kisha akaacha kila kitu, na bila tumaini la kurudi tena aliikimbia nchi kwa kushindwa kabisa. Mi-aka arobaini baadaye, baada ya Mungu kumjaza Roho ya Unabii, alirejea na kwa ushindi aliwaongoza wa-fungwa wa Kiebrania kutoka Misri! {1TG10: 20.3}
Matukio haya maalum hufanya dhahiri kabisa kwamba haijalishi ni jinsi gani watu wataweza kujaribu kuleta uamsho na matengenezo kati ya watu wa Mungu, juhudi zao hazitafanikiwa hata kabla wao hawajaanza iwapo Mungu hawezi Mwenyewe kwa njia ya manabii Wake kuisimamia kazi hiyo. {1TG10: 21.1}
Sasa, kuhusu kile kilichofanyika katika njia ya matengenezo baada ya nyumba ya kale ya Mungu kujengwa, he-bu tusome {1TG10: 21.2}
Ezra 6: 19-21 — “Kisha, wana wa uhamisho wakaifanya Pasaka, mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi. Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja Pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao. Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kuitoka nchi ya uhamisho wao, na wa-tu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka Bwana, Mungu wa Israe-li.”
Hebu sasa tuunganishe rekodi ya Ezra na ile ya Nehemia. {1TG10: 21.3}
Neh. 10: 28-32 — “Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao,
21
na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili; wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za Bwana, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake; wala tusiwaoze watu wa nchi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao; tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula cho chote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai ya kila deni. Tena tukajifanyia maagizo, kujitoza mwaka kwa mwaka theluthi ya shekeli kwa huduma ya nyumba ya Mungu wetu.”
Hapa unaona rekodi kamili ya uhuisho na matengenezo kama vile hayajawahi kuwapo. Mambo yaliyohuishwa ni haya: (1) Nyumba ya Mungu ilijengwa tena na huduma takatifu zikaanzishwa tena; (2) mahame ya zamani yali-jengwa upya, na mji ukakaliwa na watu tena. Matengenezo yaliyotukia yalikuwa: (1) Makuhani na Walawi wote walitakaswa; (2) wana wote wa uhamisho walijitenga na uchafu wa mataifa; (3) wote “waliingia katika laana na kwa kiapo, kutembea katika sheria ya Mungu,” kuzifuata hukumu Zake na sheria Zake, kutowaoza binti zao kwa watu wa nchi, wala kuwatwalia binti zao kuwa wake za wana wao; (4) walifanya utunzaji wa Sabato kuwa she-ria ya kufuatilia sana; na (5) walitoa ahadi kwa ukarimu kuunga mkono kazi ya Mungu kwa raslimali zao. Uams-ho na matengenezo ya kweli kama haya hayakuwa yamewahi kuzinduliwa tangu mwanadamu alipoanguka dhambini. {1TG10: 22.1}
Kwamba uhuisho na matengenezo ya siku hiyo ni mfano wa uamsho na matengenezo yatakayotokea katika siku zetu, yanabainishwa hasa kutoka kwa ukweli kwamba unabii
22
wa Hagai na Zekaria huchanganya matukio maradufu, moja kutukia katika siku yao, na lingine kutukia katika siku zetu. Anasema Bwana: {1TG10: 22.2}
Hag. 2: 21-23 — “Sema na Zerubabeli, liwali wa Yuda, ukisema, Nitazitikisa mbingu na dunia; nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upan-ga wa ndugu yake. Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema Bwana, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi.”
Hapa tunaambiwa kwamba katika siku ambayo Mungu ataharibu nguvu za falme za mataifa, tukio ambalo bado ni la baadaye, Yeye anamfanya Zerubabeli wa kale “ishara” ya Zerubabeli katika siku ile nguvu za falme zinaha-ribiwa. Tena tunasoma: {1TG10: 23.1}
Zek. 2: 5, 11, 13 — “Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake …. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako …. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.”
Ukuta ambao Wayahudi walijenga kuuzunguka Yerusalemu katika siku za Zekaria ulikuwa wa mawe, lakini ule uliotabiriwa hapa utakuwa “wa moto,” bora sana, ukitoa usalama kamili kwa wenyeji walio ndani. Aidha, haku-na watu wengine, hakuna mbali na Wayahudi, waliruhusiwa kujiunga na wajenzi wa Yerusalemu
23
katika siku zake, lakini katika siku zetu mataifa mengi yatajiunga. Zaidi ya hayo, mwanzoni mwa utimilifu wa unabii huu Bwana anasihi kwamba kila mwenye mwili kwa unyenyekevu na kwa ukimya akumbuke kwamba Yeye ameamka na kutoka katika maskani Yake takatifu — kwamba Yeye sasa anaizuru nchi. {1TG10: 23.2}
Zek. 2: 8 — “Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.”
Katika siku za Zekaria Bwana hakumtuma mtu yeyote kwa mataifa kutafuta kitu chochote, ila katika siku zetu, Yeye atamtuma Zekaria wa uakisi (mfasiri wa unabii wa Zekaria) kwa mataifa ambayo yanawatawala na ku-wanyanyasa watu Wake, na mataifa hayo yatakuwa nyara na yatajua kwamba Bwana amemtuma. {1TG10: 24.1}
Zek. 2:12 — “Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusale-mu tena.”
Wakati mataifa wanajiunga na Bwana katika Nchi Takatifu, wakati huo inakuwa kwamba atarithi Yuda na kuuchagua Yerusalemu tena. Na, muhimu zaidi ya yote, Anatangaza kwamba Yeye tayari ameamka na kutoka katika maskani yake takatifu ili kuyatimiza mambo haya yote. {1TG10: 24.2}
Zek. 8: 7, 20, 21 — “Bwana wa majeshi asema hivi; Tazama, nitawaokoa watu wangu kutoka nchi ya mashariki, na kutoka nchi ya magharibi; … Bwana wa majeshi asema hivi; Hata hivyo, watu watakuja, na wenyeji wa miji mingi; na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwa mwingine, wakisema, Twende kwa haraka kuomba mbele za Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi: Nitaenda pia.”
24
Umakini wa nabii ulielekezwa kwa wakati ambapo Bwana atawakusanya watu Wake kutoka mashariki na ma-gharibi; kwa wakati ambapo wakaazi wa mji mmoja watawaalika wa mji mwingine kwenda katika Nchi Takati-fu. Unabii huu huonekana katika sura ya pili ya Isaya, na sura ya nne ya Mika. {1TG10: 25.1}
Aya ya 22, 23 — “Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwa-na wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakise-ma, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.”
Kwa hakika, watu kumi ni takwimu ya uwakilishi ya ulimwengu wote mzima kama vile wanawali kumi wa Mathayo 25. Ikiwa ndivyo, basi kanisa kama jamii litanena lugha zote za mataifa. Wao kumshika mmoja ambaye ni Myahudi, na kusema, “Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi” dhahiri inaonyesha kwamba mtu fulani, wa uzao wa Wayahudi Wakristo, atautangaza ujumbe wa Mungu wa kukusanya ndani katika wakati wa mwisho, na kwamba atatambuliwa hivyo. {1TG10: 25.2}
Hebu sasa tufungue — {1TG10: 25.3}
Zek. 9: 9 — “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”
Katika unabii huu unaletwa kwa mtazamo ujio wa kwanza wa Kristo. {1TG10: 25.4}
25
Aya ya 10 – “Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.”
Yaani, Mungu angezikomesha falme za kale, Efraimu na Yerusalemu (Israeli na Yuda), na kisha kuwageukia Mataifa na kunena wokovu kwao. Hivyo ufalme Wake utakuwa juu ya nchi yote. {1TG10: 26.1}
Zek. 12: 3, 8, 9 — “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabi-la zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake. Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu mi-ongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama ma-laika wa Bwana mbele yao. Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.”
Hiyo ni, baada ya kuzisambaratisha falme za kale, Israeli na Yuda, Yeye tena atazianzisha tena na kuziunganisha kama ilivyoonyeshwa katika Ezekieli 36 na katika sehemu zingine za Maandiko. Wakati huo Yerusalemu, mji wa watakatifu, utakuwa jiwe la kuwalemea watu wote wa dunia. Yaani, watauchukia mji na wakaazi wake na wa-tajaribu kuuteka, lakini badala yake watakatwakatwa vipande; kwa maana Bwana atawalinda watu Wake. Kisha inakuwa kwamba hata walio dhaifu zaidi kati ya wakaazi wa Yerusalemu watakuwa tayari, wajasiri, na wenye uwezo alivyokuwa Daudi wa zamani. Na nyumba ya Daudi — Ufalme utakaosimamishwa, ambao ni kanisa lili-lotakaswa, hakuna wadhambi miongoni mwao (Isa. 52: 1), itakuwa kama malaika wa Bwana mbele ya watu. {1TG10: 26.2}
26
Kwa sababu unabii wa Zekaria ulitimizwa kwa sehemu tu katika siku hizo Wayahudi waliporudi kutoka Babeli hadi Yerusalemu, na maadamu maandishi yake yananena kwa kubadilishana na vuguvugu lingine kama hilo, ambalo litakuwa kubwa kuliko la zamani, hakuna shaka, kwa hivyo, ila kwamba la mwisho ni la uakisi kwa la zamani. Kwa hivyo, uamsho na matengenezo ya wakati wa Zekaria yatajirudia katika wakati wetu. Kushindwa kwa wajenzi kuendeleza kazi na kuleta uhuisho na matengenezo kabla ya Hagai na Zekaria kuitwa kwa ofisi ya kinabii, na mafanikio yao baada ya Mungu kupitia kwa manabii kuongoza, kunaonyesha kikamilifu kwamba bila Roho ya Unabii aliye hai kati yao hakuna juhudi za uamsho na matengenezo zinazoweza kufanikiwa, na ndiyo sababu zote hapo awali zilishindwa. Mfano huo pia unaonyesha kikamilifu kwamba maadamu Mungu ameamka sasa kutoka katika maskani yake takatifu, na Ameyachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe, uhuisho na matengenezo ni ya hakika kushinda. Kwa hivyo, hakuna maana ya kuchochea uhuisho na matengenezo iwapo mtu hajui ni nini na ni vipi kuhuishwa au kufanya matengenezo. Ni jambo la kupongezwa kudumisha kiwango lakini hakika sio katika mpangilio wa Mungu kwa mtu “kutengeneza “ kitu na kukiita uhuisho na matengenezo. {1TG10: 27.1}
Kwa kuhitimisha, hebu tufanye muhtasari wa mambo mawili makuu ambayo somo letu la alasiri limebainisha wazi kwetu: (1) Kwamba kazi na vuguvugu sawa na lile la siku za Zekaria kwa mafanikio litaleta uamsho na matengenezo miongoni mwa watu wa Mungu wa leo, kwamba wale ambao wanatarajia baraka zilizoahidiwa lazima waingie kwayo kwa moyo. (2) Kwamba bila Roho ya Unabii aliye hai kati yetu, hayawezi kuwapo mafanikio katika uhuisho na matengenezo yoyote, na kwamba tukijua upesi iwezekanavyo tutafikia lengo letu. {1TG10: 27.2}
27
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 9, 10
Kimechapishwa nchini Marekani
28