fbpx

Waraka Wa 2 Wa Yezreeli

Barua za Yezreeli, Nos 1-9 / Yezreeli Barua 2

Ndugu Muumini Mpendwa:

Njia pekee ya kuepuka kuchukuliwa na mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo ni kama utaweza kukumbuka ukweli kwamba Ujumbe wa Hukumu, wa mwisho kabla ya Kristo kuja mara ya pili, ndicho kilichotufanya kuwa watu; Yaani, kwa sababu ujumbe ulikuja, na kwa sababu unatakiwa kutangaza, sisi S.D.A. tuliweza kuhusika, na hakika tunataka kukaa hapo mpaka kazi imekamilika. Hatupaswi kuwa idadi ya nyuma kama vile makanisa ya Kiprotestanti tangu wao walikanusha ujumbe mmoja baada ya mwingine. Mungu asiruhusu ya kwamba tuweze “kutapikwa” na kupotea mwishoni mwa siku. Na ukweli wa Hukumu ni nini? – {JL2: 1.1}

Hukumu kama unavyojua iko katika sehemu mbili tofauti i, moja ikifuatia nyingine – Hukumu ya wafu kwanza, na Hukumu ya walio hai mwisho. Hili tunajua ni hivyo na hatupaswi kuruhusu mvuto ulio kinyume, hata kama wao wamejivika katika vazi la Waadventista wa sabato, kutufanya tusiweze kuuona ukweli huu. Sehemu yetu ya Ujumbe wa Hukumu tangu 1844 imekuwa, jinsi unavyojua, kutangaza hukumu ya wafu, si kwa ajili ya waliohai bado. Hukumu ya wafu ni nini?{JL2: 1.2}

Tumefundishwa na Uvuvio kuwa itatenganisha mema na mabaya, si kwa mwili, bali katika vitabu, kwa sababu kabla ya ufufuo, wafu hawajui neno lolote,wala hawana”ijara” tena”katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua.” – Mhu. 9: 5, 6. Kazi hii ya hukumu ni kuwawezesha malaika wajue nani watafufuliwa katika ufufuo wa kwanza, katika ufufuo wa watakatifu (Ufunuo 20: 4, 5, 11-14), na nani watafufuliwa katika ufufuo wa pili, katika ufufuo wa wasio watakatifu. Kwa mwisho huu anasema Danieli “hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” (Dan. 7:10.) {JL2: 1.3}

1

Kwa hivyo ni kwamba Uvuvio unasema kazi ya hukumu, “utakaso au patakatifu” (Dan.

8:14); Yaani, kila profesa wa dini aliyekufa tangu mwanzo wa dhambi, sasa amehukumiwa na kesi ya kila mmoja inaamuliwa kumfufua katika ufufuo wa kwanza au wa pili; Ama kufutwa kutoka kwa rekodi jina la kila mwenye dhambi asiyetubu, au kufuta kabisa kutoka kwa Kitabu dhambi za kila mwenye dhambi anayetubu. Hii imekuwa kazi Mbinguni tangu mwaka

1844, na kila madventista msabato anayesoma anajua. {JL2: 2.1}

Sasa, kwa kuwa ujumbe wa Hukumu kwa waliohai ni muhimu zaidi kuliko ujumbe wa Hukumu kwa Wafu, ni dhahiri inatarajia kwamba Biblia itakuwa na zaidi ya kusema kuhusu hukumu ya waliohai kuliko ya waliokufa. Hii ni kwa sababu Hukumu kwa Waliohai inawahusu Waliohai wao wenyewe, na wajumbe, badala ya kuwa na wafu. Kwa umuhimu, kwa hivyo, hakuna kulinganisha kati ya hizo mbili. Tutawezaje kupata ujumbe wa Hukumu kwa Waliohai? – {JL2: 2.2}

Jibu ni wazi kwa wote: Tutalipata kwa njia ile ile tulilolipata mwaka wa 1844. Kwa kuwa lilikuja kwa uvuvio na kupitia chombo cha Mungu alichokiteua, ni hakika kwamba ujumbe huu wa ziada (“Maandishi ya awali,” p. 277), pia, utakuja kwa njia ile ile; Yaani, kwa uvuvio kupitia chombo kiteule cha Mungu . Hakika Ukweli haujafunuliwa kwa njia nyingine yoyote isipokuwa uvuvio. Ona 2 Petro 1:20. {JL2: 2.3}

Jinsi tulipaswa kusikia ujumbe wa zamani mkihubiriwa kabla tuukubali, tutahitaji kusikia ujumbe mpya mkihubiriwa, na tutawezaje “kusikia pasipo mhubiri” (Warumi 10:14)? Na kama vile ujumbe wa zamani haukupendwa mwanzoni , ulidharauliwa, ukachekwa, ulichekwa na kudharauliwa na watu wa cheo na ushawishi, hakika inatarajiwa kuwa ujumbe mpya na wajumbe pia hawatapokewa na hawatatendewa vizuri zaidi bali hata vibaya zaidi . Basi kabisa ilikuwa ni

2

Suala la mtu binafsi, hakuna kuhani au kiongozi angeweza kuingilia dhamiri ya mwingine na hivyo ni lazima iwe hivyo hata sasa. Kila roho ni kufanya uamuzi wake mwenyewe katika chumba chake cha siri kwa msaada wa Roho wa Ukweli. {JL2: 2.4}

Je! Inawezekana mtu kupotea wakati ujumbe wa Hukumu kwa Waliohai umeanza kufanyika, japo hakupotea wakati ujumbe wa Hukumu kwa Wafu ulifanyika? – Roho ya Unabii inajibu hivi: “Hatuna tutakalo liogopa ya kesho isipokuwa tusahau jinsi ambavyo Bwana ametuongoza, na mafundisho Yake katika historia yetu katika miaka ya nyuma “- ‘’ Life sketches ‘p. 196. Ndio, hii na iwe hofu tuliyo nayo pekee. Basi, tukumbuke, na tuhakikishe kabisa kwamba Mungu sasa ndiye anatuongoza kwa njia ile ile alivyofanya mwaka wa 1844 na katika miaka yote. Fanya hakika kabisa kwamba haufuatii aina nyingine yoyote ya uongozi, kwamba usiruhusu mtu yeyote kukugeuza kutoka njia hii sambamba – usiruhusu mtu yeyote akuongoze uamini kwamba Mungu anaongoza sasa kupitia kwa kila [Tom Dick na Harry-mtu]. Hili Hatustahilii kusahau ikiwa tunapaswa kuiga na kufanya kama watakatifu ambao walikuwa mbele yetu, na kama tunatarajia kuokolewa. Ikiwa tutasahau hili, basi hakika tunaposimama, watu watatuongoza mbali na ujumbe wa Mungu na kutugeuza sisi kinyume na wajumbe Wake Kama vile makuhani wale Wayahudi waliwafanya wafuasi wao wapinduke dhidi ya Kristo. Mungu na asiruhusu tufanye dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu kwa kukanusha ujumbe Wake wakati unakuja kwetu. Tu kwa kufuata kikamilifu amri hii ya Mungu tunaweza kuongozwa hakika na kuishi kwenye Hukumu ya Walio hai wakati inapoanza “kuwatenga waovu mbali na wenye haki.” Matt. 13:49. {JL2: 3.1}

Hukumu ya Waliohai Ni nini? Na nini kinachotokea kwa wenye haki, na nini kinachotokea kwa waovu, baada ya kuhukumiwa? – Katika mifano yake Kristo anaonyesha kwamba wenye haki, kama samaki mzuri, hutiwa vyomboni; Kama ngano, huwekwa ghalani; Na kama kondoo, huenda katika uzima wa milele – huwekwa katika usalama dhabiti hutiwa

3

Muhuri kwa umilele. Lakini waovu, kama samaki mbaya, hutupwa nje, kama magugu, huchomwa moto; Na kama mbuzi, wanatumwa katika adhabu ya milele. “Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatega waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; Ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Matt. 13:49, 50. {JL2: 3.2}

Hapa tunaona kwamba kazi ya hukumu kwa walio hai inaonyeshwa kwa njia mbalimbali, na inaitwa kwa kuambatana: “Hukumu” (Danieli 7:10, Ufunuo 14: 7, 1 Pet 4:17); “Kutakaswa kwa patakatifu “ (Danieli 8:14); “Utakasa Hekalu Lake” (Mal 3: 1-3); “Mavuno” (Mathayo 13:30); “ Mchekecho mkuu,” “utakaso wa kanisa,” (5 T., uk. 80). {JL2: 4.1}

Kuhusu kazi hii ya hukumu, Roho ya Unabii inasema hivi: {JL2: 4.2}

“… Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa kasi .. Mungu atakuwa na watu safi na wa ukweli. Katika mchekecho mkuu ulio karibu kutokea, tutakuwa na uwezo wa kupima nguvu ya Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia wakati Bwana ataonyesha kwambapepeo lake liko mkononi mwake, na atasafisha sakafu yake kabisa …. Hawana mwanga ambao umekuwa mkiangaza kwa nguvu juu yenu. Ila,inawezekana Kuwa chini ya ngozi ngumu isiyopendeza ndio mwangaza safi wa tabia ya mkristo halisi itafunuliwa. “ – “Shuhuda,” Vol. 5, uk. 80, 81. {JL2: 4.3}

Ukweli kwamba ujumbe wa Hukumu ya Waliohai umechambuliwa sana na manabii wote wa Biblia kuliko wa Hukumu ya Wafu, yenyewe ni ushahidi tosha kuwa ni muhimu sana. Hata hivyo, ninaweza kuiongelea kwa ufupi tu katika barua hii – tu kutoa kiini chake: {JL2: 4.4}

Kama inavyoonyeshwa hapo awali, katika Hukumu ya wafu

4

Wenye dhambi hutenganishwa na wenye haki katika vitabu peke yake, lakini katika hukumu ya waliohai wenye dhambi na wenye haki wanatenganishwa kwa mwili mmoja kutoka kwa mwingine kama uvuvio kupitia nabii Ezekieli unavyoeleza: {JL2: 4.5}

“Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi,ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba, akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta,mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.Bwana akamwambia; pita kati ya mji ,kati ya Yerusalemu,ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machmkizo yote yanayofanyika kati yake.Na hao wengine aliwaambia nami nalisikia, piteni kati ya mji nyuma yake,mkapige;jicho lenu lisiachilie ,wala msione huruma;Waueni kabisa,mzee,na kijana,na msichana,na watoto wachanga,na wanawake;lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama;tena anzeni katika patakatifu pangu.Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. “ Eze. 9: 3-6. {JL2: 5.1}

Na kupitia kwa nabii Malaki tunaambiwa kwamba Bwana atamtuma mjumbe mbele, na kwamba baada ya kutayarisha njia, Bwana atajilia hekalu lake ghafla(kanisa) bila sababu yoyote ila kuwatakasa, hasa kuwasafisha Wana wa Lawi, wahudumu. Angalia Malaki 3: 1-3. Kisha, inasema Roho ya Unabii, “Ni wale tu ambao wameshinda majaribu kwa nguvu za Mwenye Nguvu wataruhusiwa kushiriki katika kutangaza [Ujumbe wa Malaika wa Tatu] wakati utakapokuwa umefura katika kilio kikuu.” – “ The Review and Herald,”Novemba 19, 1908. Na kwa “ufunuo huu wa kushangaza” (“Testimonies to Ministers,” uk. 445) nabii Isaya anaongeza: {JL2: 5.2}

“Maana BWANA atakuja na moto,na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli;ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao,na maonyo yake kwa miali

5

ya moto.Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili,kwa moto na kwa upanga wake;nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.Watu wale wajitakasao,na kujisafisha katika bustani,nyuma yake aliye katikati;wakila nyama ya nguruwe, na machmkizo ,na panya;watakoma pamoja,asema BWANA.Nami nayajua matendo yao na mawazo yao;wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote;nao watakuja,nao watauona utukufu wangu.Nami nitaweka ishara kati yao,nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa,Tarshishi,na puli,na Ludi,wavutao upinde,kwa Tubali na Yavani ,visiwa vilivyo mbali;watu wasioisikia habari yangu wala kuuona utukufu wangu;nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote,kuwa sadaka kwa BWANA,juu ya farasi,na katika magari,na katika machela,na juu ya nyumbu na juu ya wanyama wepesi,mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu,asema Bwana;kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi. “ Isa. 66:15-20. {JL2: 5.3}

Kwa kuwa kuchijwa kuliotabiriwa na nabii Isaya kunafanyika kati ya wale wanaodai kuwa wameteuliwa na wametakaswa (kwa uwongowanaamini kuwa hawahitaji kitu chochote zaidi), na kwa kuwa wale waliookoka kati yao wanatumwa kwa mataifa mengine kuhubiri injili, oja tano tofauti na muhimu zaidi zinaonekana waziwazi: (1) Kwa sababu waathirika wa uchijaji ni wale ambao dhidi ya ujuzi wao ambao wamepewa na Mungu hujiunga kwa nyama ya nguruwe na machmkizo mengine, na kwa kuwa wale waliookoka wanajua kazi ya injili ya kutosha ili watumwe Kuhubiri kwa Mataifa,kuchijwa kwa hivyo, kunaonekana kmkifanyika kanisani; (2) wale waliookoka, kulingana na Ezekieli, ni wale wanaoomboleza na kulia juu ya machmkizo, na hivyo kupokea alama ya ukombozi, (3) kwa kuwa wanatumwa kuhubiri Injili kwa Mataifa baada ya wao Kuepuka kuchinjwa, ni “masalio,” wale walioachwa, watumishi wa Mungu wa baadaye; (4)

Tangu wao

6

wanakusanya kutoka kwa Mataifa ndugu zao wote, wote ambao wanaweza kuokoka, wao ndio wanaomaliza kazi ya injili duniani kote, (5) kwa kuwa kuna utenganisho mara mbili – moja kutoka kanisani (Waisraeli), na ingine kutoka kwa Mataifa, – wale waliookoka na wale waliokusanyika – basi wa kwanza ni malimbuko ya kwanza na wa pili ni malimbuko ya pili – yale ya Ufunuo 7: 4, 7-9, moja kutoka kwa makabila ya Israeli , Na moja kutoka kwa makabila ya Mataifa. {JL2: 6.1}

Maandiko haya yote na mengi zaidi, rafiki yangu, kama unavyoona wazi, yanarejelea utakaso wa kanisa, kwa siku kuu na ya kuogofya ya Bwana (Mal 4: 5), kwa Hukumu ya waliohai na Kusanyiko la Watakatifu – “mavuno” ambayo kila nabii ameandika, wengine zaidi na wengine kwa ufupi. Kwa kuwa hii ni hivyo unaona kwamba wazee wetu sasa wanafanya kile ambacho makuhani katika siku ya Kristo walikuwa wakifanya, na pia kile viongozi wa dini chini kupitia matengenezo walikuwa wakifanya, na nia yao haijapungua Ya kuuweka ujumbe huu mbali na waumini, na Na hivyo kuwadanganya hata wateule, wale 144,000, malimbuko ya kwanza ya mavuno, wale watakaookoka hukumu “katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17), watumishi wa Mungu wa baadaye!{JL2: 7.1}

Ikiwa hili sio lengo la adui nyuma ya matendo ya Wazee hawa walio na chmki, na ikiwa Ukweli huu unaweza kukataliwa, hawangefanya kama wendawazimu, hawangezuia majadiliano na sisi, hawangetufukuza nje ya makanisa kwa matumaini kuwa hatutawasiliana na waumini, hawangekushauri usisome lakini ukateketeze vitabu vyetu, hawangekutishia kukufukuza kwa kujifunza ujumbe huu, lakini wangekuwa wanaketi chini na kuukanusha ikiwa sio sahihi wakati wakiketi na wengine wote wasiokubaliana nao. {JL2: 7.2}

Huwezi kuona kwamba roho ambayo sasa inajitokeza kupitia ndugu hawa wanaochmkia Ukweli ni roho iliyojitokeza kupitia

7

Wayahudi, na kupitia maadui wa Ukweli wakati wa matengenezo ya Kiprotestanti, na pia mwanzoni mwa harakati ya 1844? Je, huoni kwamba kwa sababu hawawezi kushambulia ujumbe huu juu ya sifa za kibinafsi, uhusisha ubinafsi, kushambulia viongozi na kugemkia kuwachafulia tabia,uvumi na uwongo, kwa kitu chochote katika tumaini la kukugeuza dhidi ya

Ujumbe na mjumbe. Roho ya Unabii ilitabiri uhalifu huu kwa maneno haya: {JL2: 7.3}

“Niliona kuwa roho hiyo ya uwongo, ambayo inaweza kugeuza ukweli kuwa uwongo, nzuri katika baya, na isiyo hatia katika uhalifu, sasa inafanya kazi .. Shetani anafurahi juu ya hali ya watu wanaojiita kwa jina la Mungu ….” – “ Testimonies for the Church, “Vol. 5, uk. 94, 95. {JL2: 8.1}

Kwa Wazee kuwaambia waumini nini cha kusoma na nini sio cha kusoma, ni nani wa kuzungumza naye na ambaye sio wa kuzungumza naye, ni nani atakayekaribishwa nyumbani zao na ambaye wasimkaribishe, ni kufanya wajinga, sanamu, na wagonjwa wa kiroho. Wazee wanapaswa kuambiwa kwamba wanabeba hata mizigo mizito zaidi kuliko walivyofanya Wayahudi au wahudumu katika makanisa yetu ya zamani wakati wengi wetu tulikuwa, tunajifunza ujumbe wa kurejea kwa Yesu kwa mara ya pili. Wanaweza kusaidiwa kama waumini wanawaambia kuwa hili ni suala la kuamuliwa kati ya waumini na Mungu wao; Kwamba ikiwa mtu yeyote ataingia katika Ufalme lazima aende huko kwa uwezo wake mwenyewe aliopewa na Mungu. Waonyeshe kile ambacho Roho wa Mungu anasema kama ifuatavyo: {JL2: 8.2}

“Nuru ya thamani itaangaza kutoka kwa neno la Mungu, mtu yeyote haruhusiwi kusema nini kitaletwa au hakitaletwa mbele ya watu katika ujumbe wa kuangazia watu atakaotuma, na hivyo kumzima Roho wa Mungu Hakuna mtu aliye na haki ya kuzima mwanga kutoka kwa watu, ata iwe nafasi yake ya mamlaka iko vipi.Wakati ujumbe unakuja kwa jina la Bwana kwa watu wake,hakuna mtu anayestahili kujizuia kutokana na uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza Kumudu kusimama

8

Nyuma katika mtazamo wa kutojali na kujiamini, na kusema: ‘Najua ukweli. Ninaridhika na msimamo wangu. Nimeweka vipande vyangu, na sitaondolewa mbali na msimamo wangu, chochote kinachoweza kutokea. Sitausikiza ujumbe wa mjumbe huyu; Kwa maana najua kwamba haiwezi kuwa ukweli. Ilikuwa ni kutokana na kufuata njia hii kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika giza kidogo, na ndio sababu jumbe za mbinguni hazijawafikia. “-” Counsels on Sabbath School Work,”uk. 28. {JL2: 8.3}

Hili ndilo neno “uhuru wa kidini” linamaanisha, rafiki yangu. Je! Hii sio njia sahihi, ya uaminifu na ya kuheshimika ya kukabiliana na hali hiyo? Je! Unapaswa kufuata maneno ya watu, au wewe ufuate Kristo na Ukweli Wake? Waambie Wazee wale wenye uhasama kwamba vita vyao sio kinyume na “Fimbo ya Mchungaji” bali dhidi ya Mungu na dhidi ya nafsi zao wenyewe. {JL2: 9.1}

‘’ … Wale wanaofundisha akili kuchukua kila kitu ambacho wanaweza kutumia kama kigingi cha kushikilia shaka, “inasema Roho ya Unabii,” na kushauri mawazo haya kwa akili zingine, daima watapata nafasi ya shaka. Wao watakuwa na shaka na kukanusha kila kitu kinachotokea katika ufunuo wa ukweli, kukosoa kazi na msimamo wa wengine, kukosoa kila tawi la kazi ambayo hawana sehemu yao wenyewe. Wao watakula juu ya makosa na hatia na dosari za wengine, ‘mpaka,’ alisema malaika, ‘Bwana Yesu atasimama kutoka kazi yake ya upatanishi katika patakatifu, na atavaa mavazi ya kisasi, na kuwashangaza katika sikukuu yao isiyo na utakatifu; Na watajikuta wasio tayari kwa ajili ya arusi ya Mwanakondoo. ‘ Ladha yao imepotoshwa sana kiasi kwamba wangetekeleza hata kulaani meza ya Bwana katika ufalme wake. “-” Testimonies for the Church, “Vol 5, uk. 690. {JL2: 9.2}

“… Kutenganishwa,” anaendelea Roho wa Ukweli, “husababisha maumivu na uchungu kwa pande zote, mbili.

9

Ni utofauti ambao Kristo anatangaza kwamba alikuja kuleta. Lakini waongofu watahisi tamaa ya daima kwamba marafiki wao wataacha yote kwa ajili ya Kristo, wakijua kwamba isipokuwa wafanye hivyo kutakuwa na kutenganishwa kwa mwisho na kwa milele. Mkristo wa ukweli hawezi wakati pamoja na marafiki wasioamini, kuwa mwepesi, na kuongea bila uzito. Thamani ya roho ambayo Kristo aliwafia, ni kubwa mno. “-” Testimonies for the Church, “Vol 5, uk. 83. {JL2: 9.3}

Niamini, rafiki yangu, kwamba ikiwa ujumbe wa Hukumu kwa Waliohai haungekuwa umefunuliwa kwetu kwa nguvu za Mungu, ikiwa haungekuwa na uzito zaidi kuliko ulivyo, ikiwa haungekuwa wazi kama kioo, na kama hatukuamriwa Kuuleta kwako, hatungekuwa tmkiwinda watu wa Mungu waliopotoshwa katika majabali na milimani (Yer 16:16) kama ilivyokuwa – hatungewekwa chini ya Mzigo mzito na gharama kwa kwenda nyumba kwa nyumba katika ulimwengu wa Kiadventista ili kuwaokoa kutoka kwa udanganyifu wa binafsi wa Laodikia; Wala hatungeweza kwa nguvu zetu za binadamu kuchukua matusi ambayo hutupwa kwetu karibu kila saa na wanaume kwa wanawake ambao wanasema kuwa wanamtumikia Mungu! {JL2: 10.1}

“…Katika wakati huu,” asema Roho wa Mungu, “dhahabu itatenganishwa na uchafu katika kanisa. Uungu wa ukweli utafahamika wazi kutoka kwa mwonekano na batili yake. Nyota nyingi ambazo tumezipenda kwa Kung’aa kwake zitaenda nje katika giza. Chafu kama wingu itachukuliwa mbali na upepo, hata kutoka mahali ambapo tunaona tu sakafu ya ngano tajiri. Wote ambao huchukua mapambo ya patakatifu, lakini hawajavikwa utakatifu wa Kristo, wataonekana kwa aibu ya uchi wao wenyewe …. Wale ambao wamekuwa wenye wasiwasi na wasiojiamini watajitangaza kwa uwazi kwa ajili ya Kristo na ukweli wake. Wale dhaifu sana na kusita katika kanisa, watakuwa kama Daudi – tayari kufanya na kuthubutu … Kisha kanisa la Kristo litatokea “sawa kama mwezi, wazi kama jua, na kutisha kama jeshi lenye mabango.” – “ Testimonies for the Church,,” Vol. 5, uk. 81, 82. {JL2: 10.2}

10

Wanadaudi hawa ambao Mungu anawafunua sasa hivi karibuni watakutembelea ili kuweka mipango ya Mungu kwako. Tafadhali wapokee watumishi hawa wa Mungu katika harakati ya Walei mkiwapa heshima sawa na ambayo ungeweza kutarajia wakupokee nayo. {JL2: 11.1}

Tunakuja kwako kwa Neno safi la Mungu na yote tunayoomba kwako ni kutupa usikilizaji usio na upendeleo na ubaguzi tunapokutembelea nyumbani kwako. Kwa kuwa unaona kwamba barua hii ina ukweli ambao huwazi na haujatambulika, basi mkisikia mtu yeyote akiongea dhidi yake unaweza kumsaidia kwa kumwomba akupe kitu kizuri zaidi kwenye maandiko haya kama anacho, na ikiwa hana, akuache peke yako. {JL2: 11.2}

Ikiwa utawasaidia maadui wa Ukweli, waambie kuchimba kwao waumini kwamba wana ukweli wote, kwamba hawahitaji tena, kwamba wana ujumbe wa mwisho, kwamba Roho ya Unabii inasema hivyo ingawa inasema kinyume chake, Ni uwongo wazi. Waambie, sio hukumu ya wafu mbali ni hukumu ya waliohai ndio ujumbe wa mwisho, na hawana, na badala ya kuutafuta, wanapigana dhidi hivyo, au haithibitishi; Kama haithibitishi, basi uwafanye wakwambie ambapo haifanyi hivyo. {JL2: 11.3}

Alama ya Mungu (Ezekieli 9: 4) na alama ya mnyama (Ufunuo 13:16) hapa zinaonekana kuwa ni vinyume viwili kama vile wanawake wawili wa Ufunuo kumi na mbili na kumi na saba – ukweli na bandia. {JL2: 11.4}

Mnyama tunaambiwa ni mwanadamu (Ufunuo 13:18). Amri ya kuabudu, kutii amri ya mnyama, kwa hivyo, ni amri ya kumwabudu (kumtii) mwanadamu mahali pa Mungu. Alama zote mbili si za madhumuni mengine ila kwa kufafanua nani ni nani – ni nani kwa Mungu na ni nani kwa mnyama. Wale wanaotii ujumbe wa hukumu wa Mungu badala ya amri ya mnyama, watapata alama ya Mungu. Na wale wanaotii amri ya mnyama badala ya ujumbe wa Mungu hupokea alama ya mnyama.

Alama hizi mbili tofauti

11

, unaona, zinawatenganishe waabudu wa Mungu kutoka kwa waabudu wa wanadamu. Na kwa kuwa Yesu anasema kuwa kutenganishwa hufanyika wakati wa mavuno, na kama unavyoona sasa kwamba “mavuno” na “hukumu” kwa waliohai ni maneno sawa, basi hitimisho ni kwamba kama alama ya Mungu inasisitizwa juu ya waumini wa Ujumbe wake wa Hukumu katika kanisa, na kama alama ya mnyama inasisitizwa juu ya waabudu wa mnyama wakati wa Hukumu ulimwenguni, mada hii inakuwa dhahiri: Maadui wa ujumbe wa hukumu katika kanisa, na maadui wa ujumbe wa hukumu ulimwenguni wote wamefungwa na roho ya mnyama – wote wanafanya kazi hiyo hiyo dhidi ya watu wa Mungu, kwanza katika kanisa kisha ulimwenguni. Tofauti pekee kati ya hizi mbili ni kuwa katika ulimwengu alama ya Mnyama inatekelezwa na sheria za kiraia, wakati kanisa sio hivyo, ingawa maadui dhidi ya ujumbe wa hukumu tayari wamefanya kila kitu katika uwezo wao ili kupata mkono wa sheria dhidi yetu. Sasa imebaki kwa kila muumini wa kanisa ili azingatie ujumbe wa hukumu ya Mungu na kupokea alama yake ya ukombozi, au kuzingatia majadiliano ya bure ya watu na kufa chini ya silaha za kuchinjwa za malaika. {JL2: 11.5}

Wako mwaminifu kwa kukusanya

malimnbuko ya kwanza ,

V.H. Yezreeli, H.B.

(Mkurugenzi wa Harakati ya Waleiya S.D.A. Layman)

5 T 80, 81

12

 

>