fbpx

Ulawi wa Wadaudi Wadventista wa Sabato

ULAWI WA WADAUDI

WADVENTISTA WA SABATO

Ilichapishwa mara ya kwanza — Februari 12, 1943 (Trakti Namba 13 uk. 46)

na V.T. Houteff

ILICHAPISHWA TENA 1997

1A

DIBAJI

Ya mpito kwa kuanzishwa na vile vile kwa jina, Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato ipo tu kukamilisha kazi iliyowekwa na Mungu ndani ya dhehebu la Waadventista wa Sabato, ambamo kwa hivyo huzuilia shughuli zake kikamilifu. Kadiri kazi yake humo ndani inakaribia kufunga, na “watumwa wa Mungu wetu” (Ufu. 7:3) wanatiwa muhuri, jina lake litabadilishwa (Isa. 56:5; 62:2; 65:15) na kusudi lake na kazi yake itakuwa ya kuikumbatia injili yote (Mat. 17:11; Mdo. 3: 21; Isa. 61:4-7). Wakati huo Katiba yake na Sheria ndogo jinsi zilivyoratibishwa hapa ndani zitaanza kufanya kazi kikamilifu. {LDSDA: 1.1}

1

YALIYOMO

ULAWI

WA

WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

2

KATIBA 3-8
Kipengee cha 1– Jina 3
Kipengee cha 2– Lengo 5
Kipengee cha 3– Ushirika 5
Kipengee cha 4– Maafisa na Kazi zao 5
Kipengee cha 5– Vikao 7
Kipengee cha 6– Sheria ndogo 8
SHERIA NDOGO 9-11
Kipengee cha 1 — Baraza Kuu 9
Kipengee cha 2– Malipo ya Wafanyakazi 10
Kipengee cha 3– Kuwekewa Mikono Wachungaji 10
CHIMBUKO, JINA, UTUME, MUUNDO, SERIKALI 12-20
Ya Musa — Kama hiyo 15
Ya Daudi — Kama hiyo 16
Ya Ezra — Kama hiyo 17
Ya Mitume — Kama hiyo 18
UTARATIBU 21-27
Kanisa la Agano la Kale Kama Hiyo 22
Kanisa la Agano Jipya Kama Hiyo 24
NIDHAMU 28-40
ELIMU 41
Taratibu za Shule na Mtaala 41
Wasifu na Majukumu ya Walimu 51
Ushirikiano wa Wazazi 65
Wasifu kwa Matabibu 67
Wasifu kwa Wauguzi 76
Wasifu kwa Wote 80
Wasifu kwa Washiriki wa Kanisa 87

 

ULAWI

WA

WADAUDI WAADVENTISTA

WA SABATO

KATIBA

KIPENGEE CHA 1– JINA

Sehemu ya 1.

Jumuiya hii itajulikana ki-mpito kama Wadaudi Waadventista wa Sabato mzao wa Waadventista wa Sabato, kanisa la, Laodekia. {LDSDA: 3.1}

Jina, Wadaudi, linapatikana kutoka kwa jina la mfalme wa Israeli ya Zamani, lipo kama dai halali la kutekelezwa na Jumuiya hii kwa sababu ya vipengee vyake vifuatavyo: Kwanza, imetiwa wakfu kwa kazi ya kutangaza na kuleta urejesho (jinsi ulivyotabiriwa katika Hosea 1:11; 3:5) wa Ufalme wa Daudi katika uakisi, kwa kiti cha enzi ambacho Kristo, “mwana wa Daudi,” ataketi. Pili, hudai yenyewe kuwa ni ya kwanza ya malimbuko ya walio hai, watangulizi kutoka kwa wazawa wa siku ya leo wa wale Wayahudi waliofanza Kanisa la Kikristo la Kwanza. Pamoja na kujitokeza kwa watangulizi hawa na jeshi lake, malimbuko, ambamo wamechaguliwa 12,000 kutoka kati ya kila kabila kumi na mbili za Yakobo, “watu 144,000” (Ufu. 14:1; 7:2-8) ambao watasimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo (Ufu. 14:1; 7:2-8), utawala wa Daudi wa uakisi unaanza. {LDSDA: 3.2}

3

Jina Waadventista wa Sabato, ambalo Jumuiya hii hurithi kutoka kwa dhehebu mzazi, ni la mpito (Isa 62:2) na kwa muda pekee wa kazi yake ndani ya dhehebu mzazi. {LDSDA: 4.1}

Sehemu ya 2.

Vitabu vya Jumuiya, Mfululizo wa Fimbo ya Mchungaji, huvuta jina lake kutoka kwa fimbo ya Musa mchungaji wa Midiani. Katika Kutoka kwa siku yake, ilikuwa ni hiyo fimbo iliyowakomboa wana wa Israeli kutoka kwa Wamisri na baadaye ikapiga maji ya Bahari ya Shamu, ikawapa bandari ya kimbilio la wakimbizi na kuweka mtego wa tanzi kwa waliokuwa wakiwasaka. Kwa sababu hii vitabu hivyo hulichukua jina “Fimbo ya Mchungaji” ili kutambulisha na kutofautisha kazi yake maalum, ambayo Isaya aliandika: “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie watu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.” (Isa. 11:11); na kuitisha umakini kwa utimilifu wa kipekee wa unabii wa Mika: “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina Lako: Sikieni hiyo fimbo, na Yeye aliyeiteua.” Mika 6:9. {LDSDA: 4.2}

4

KIPENGEE CHA 2 — LENGO

Sehemu ya 1.

Lengo la Jumuiya hii ni kuleta miongoni mwa watu wa Mungu yale matengenezo yaliyoitishwa katika Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 9, ukurasa wa 126, kama vuguvugu la lazima la kutangaza “Mwito wa saa Kumi na Moja” (Mat. 20:6, 7) wa “Injili ya milele … kwa kila taifa, na jamaa, na lugha, na watu.” Ufu 14:6. Kupitia mwito huu, Kilio Kikuu cha jumbe za malaika watatu, kitawakusanya “watu wa watakatifu wake Aliye Juu” (Dan. 7:27) katika ufalme “ambao hautaangamizwa milele … bali … utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu.” Dan. 2:44. Hivyo utakaribisha utawala wa Kristo kama Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme kwa dunia yote milele na milele. {LDSDA: 5.1}

KIPENGEE CHA 3 — USHIRIKA

Sehemu ya 1.

Ushirika wa Jumuiya hii utajumuishwa tu na watu ambao hukubali imani yote na kuumba katika maisha yao ajenda yote ya Jumuiya iliyotajwa hapo awali. {LDSDA: 5.2}

KIPENGEE CHA 4 — MAAFISA NA KAZI ZAO

Sehemu ya 1.

(a) Maafisa wa kawaida wa Jumuiya hii

5

watakuwa rais, makamu wa rais, katibu, na mtunza hazina. {LDSDA: 5.3}

(b) Rais ataitwa na kuteuliwa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa katika Kutoka, sura ya tatu, aya ya kumi, kumi na tano, na kumi na sita; sura ya nne, aya ya kumi na saba; Ezekieli, sura ya tatu, aya ya kumi na saba; na Luka, sura ya sita, aya ya kumi na tatu. {LDSDA: 6.1}

(c) Maafisa wengine wote wa Jumuiya hii watateuliwa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa katika Hesabu, sura ya kumi na moja, aya kumi na sita, kumi na saba, ishirini na nne, na ishirini na tano, na katika Matendo, sura ya sita, aya yakwanza hadi ya saba; na sura ya kumi na tatu, aya ya kwanza hadi ya tatu. {LDSDA: 6.2}

Sehemu ya 2.

Rais, kama ilivyo kwa mfano katika Kutoka, sura ya nne, na katika Hesabu, sura ya kumi na sita, aya kumi na mbili na ishirini na tano hadi thelathini na mbili, atafanya kazi kama mwenyekiti wa Baraza Kuu kama msimamizi mkuu wa maswala ya Jumuiya, na kama mfanyakazi na mchungaji kwa maslahi ya jumla ya Jumuiya. {LDSDA: 6.3}

Sehemu ya 3.

Naibu Rais, kwa mujibu mfano ulionakiliwa katika Kutoka, sura ya saba, aya ya kwanza na ya pili, atamsaidia rais kusimamia maswala ya Jumuiya. {LDSDA: 6.4}

6

Sehemu ya 4.

Katibu atahifadhi hoja za mikutano yote ya Jumuiya, na kuyatekeleza majukumu mengine kama hayo yanavyolingana na mazingira ya ofisi. {LDSDA: 7.1}

Sehemu ya 5.

Mtunza hazina atapokea fedha zote za Jumuiya na kuzigawa kwa mujibu wa mifano iliyoandikwa katika maandiko yafuatayo: Kutoka, sura ya thelathini na sita, aya ya tatu; Ezra, sura ya nane, aya ishirini na moja, ishirini na nne hadi thelathini; Matendo, sura ya nne, aya thelathini na tano hadi thelathini na saba; na sura ya sita, aya ya tatu. {LDSDA: 7.2}

KIPENGEE CHA 5 — VIKAO

Sehemu ya 1.

Jumuiya hii itafanya vikao vya kawaida kwa wakati na mahali Baraza Kuu itataja katika notisi itakayochapishwa katika Msimbo wa Nembo, chombo rasmi cha jumuiya, katika matoleo mawili mfululizo kabla tarehe ya kufunguliwa kwa kikao. {LDSDA: 7.3}

Sehemu ya 2.

(a) Vikao maalum vinaweza kuitishwa kwa njia ile ile ambayo kikao cha kawaida huitishwa. {LDSDA: 7.4}

(b) Maamuzi katika vikao maalum yatakuwa na nguvu sawa na yale ya vikao vya kawaida. {LDSDA: 7.5}

7

KIPENGEE CHA 6 — SHERIA NDOGO

Sehemu ya 1.

Sheria ndogo zinaweza kukumbatia kifungu chochote kinachopatana na Katiba. {LDSDA: 8.1}

Sehemu ya 2.

Jumuiya, katika kikao chochote, inaweza kutunga, kurekebisha, au kubatilisha sheria ndogo kwa uwakilishi huo na kupiga kura kama ilivyoonyeshwa ki-mfano katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ukurasa wa 195, 196. {LDSDA: 8.2}

8

SHERIA NDOGO

KIPENGEE CHA 1 — BARAZA KUU

Sehemu ya 1.

(a) Baraza Kuu litaundwa kwa kufuata kigezo cha baraza lililofafanuliwa katika Matendo, sura ya sita, aya ya pili hadi ya sita. {LDSDA: 9.1}

(b) Litakuwa na uwezo kamili wa utendaji na uongozi kati ya vikao vya Jumuiya. {LDSDA: 9.2}

(c) Litapewa mamlaka ya kutoa hati ya utambulishi na leseni, na kujaza nafasi ambazo zinaweza kutokea katika ofisi yoyote ya Jumuiya isipokuwa ofisi ya Rais. {LDSDA: 9.3}

Sehemu ya 2.

Sehemu kubwa ya ushirika kamili wa Baraza Kuu, baada ya notisi kwa wanabaraza, watafanyiza jamii ya Baraza Kuu. {LDSDA: 9.4}

Sehemu ya 3.

(a) Mikutano ya Baraza Kuu inaweza kuitishwa na mwenyekiti au na mjumbe yeyote wa Baraza aliyeteuliwa au kutumwa naye. {LDSDA: 9.5}

(b) Mikutano inaweza kuitishwa wakati wowote. {LDSDA: 9.6}

(c) Itafanyika katika makao makuu, isipokuwa vinginevyo itajwe na jamii ya Baraza. {LDSDA: 9.7}

Sehemu ya 4.

Mikutano ya wachache chini ya wanabaraza saba wa Baraza inaweza kufanywa katika Ofisi Kuu ya Uongozi

9

kwa kutekeleza shughuli muhimu au ya kawaida. {LDSDA: 9.8}

KIPENGEE CHA 2 — MALIPO YA WAFANYAKAZI

Sehemu ya 1.

Malipo na gharama za wafanyakazi wote katika ajira ya Jumuiya zitaamuliwa na kurekebishwa na Baraza Kuu. {LDSDA: 10.1}

Sehemu ya 2.

(a) Fedha muhimu za kufanyia kazi za Jumuiya zitajumuisha zaka na sadaka. {LDSDA: 10.2}

(b) Fedha za kigeni zitajumuisha michango, wosia wa kutoa au kuacha urithi, na mapato ya ndani. {LDSDA: 10.3}

KIPENGEE CHA 3 — KUWEKEWA MIKONO WACHUNGAJI

Sehemu ya 1.

(a) Wadaudi Waadventista wa Sabato wataitambua tu sheria ya Maandiko ya kuwekewa mikono, kushuhudia: (1) kwamba mwito kwa ukasisi wa injili lazima umjie mtu kutoka kwa Mungu, na ya kwamba (2) lazima ufuatwe kwa uaminifu kabisa kwa matakwa ya mpangilio wa injili, kama yalivyotajwa katika Luka, sura ya kumi, aya tatu hadi ya tisa; Mathayo, sura ya kumi, aya ya tano hadi ya kumi na moja; na Timotheo wa Kwanza, sura ya tatu, aya ya kwanza hadi ya saba. {LDSDA: 10.4}

(b) Kadiri na wakati ushahidi umesikiwa kwa uthibitisho kamili kwamba utumishi wa mtu unatimiza matakwa haya, Baraza Kuu litaamuru

10

wakati huo atambuliwe kwa mwito wake wa kushiriki katika kazi takatifu ya ukasisi kama inavyofafanuliwa kimsingi katika Mathayo, sura ya kumi, na litamteua au kumsajili (kumpa leseni) jinsi suala hilo litakavyoruhusu. {LDSDA: 10.5}

Sehemu ya 2.

Mchungaji aliyewekewa mikono atakuwa atapewa uwezo wa haki ya kuhubiri na kufundisha kweli, maagizo, na masomo, na kutekeleza majukumu ya ukasisi, huduma, na sherehe, zilizowekwa ndani ya Maandiko. {LDSDA: 11.1}

Sehemu ya 3.

Mchungaji aliyesajiliwa (aliyepewa leseni) atapewa uwezo wa haki ya kuhubiri na kufundisha kweli maagizo, na masomo yaliyowekwa katika Maandiko, lakini hatatekeleza majukumu ya ukasisi, huduma na sherehe zilizowekwa ndani yake, isipokuwa kwa hafla zitakazostahili idhini ya Baraza kuidhinisha haki zilizonenwa. {LDSDA: 11.2}

11

CHIMBUKO, JINA, UTUME, MUUNDO

Wadaudi chipukizi kutoka kwa uliochakaa Uadventista wa Sabato walitabiriwa kinabii katika kitabu cha Ezekieli, sura ya tisa. Washirika wake hasa ni wale ambao wametupwa nje na kunyang’anywa ushirika wa makanisa yao ya Waadventista wa Sabato. Hivyo wakiwa wametengwa na kanisa lao na kunyimwa jina lake kwa sababu wameitii sauti ya Fimbo, sauti ya Mchungaji Mwema, wameitwa kwa jina lililojikita katika kazi ya Fimbo, “Wadaudi Waadventista wa Sabato,” hadi wakati watakapoitwa “kwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.” Isa. 62:2. {LDSDA: 12.1}

Hivi ikiwa imeinuliwa kwa hitaji, si kwa kuchagua, Jumuiya hii ndani ya shirika la Waadventista wa Sabato imewekewa mikono kwa kazi ya mwisho wa pande tatu: (1) Itakwenda kwa nyumba ya “Israeli na Yuda” (Ezek. 9:9), na “kuwaambia wale walioalikwa, njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.” Luka 14:17. Na ingawa wale wa kwanza kuusikia mwito wanaweza kuomba udhuru. (Luka 14:18-20), “maskini, na vilema, na vipofu, na viwete” kutoka kwa “njia kuu na vichochoro vya mji” (Luka 14:21, 22) wataitika. (2) Kwa hivyo, itatekeleza hilo “vuguvugu kubwa la kuleta matengenezo” na utakaso ulioitishwa “miongoni mwa watu wa Mungu.” — Shuhuda Kwa Kanisa, Gombo la 5, ukurasa wa 80;

12

Gombo la 9, ukurasa wa 126. Na matunda yanayofuata kazi hii, malimbuko ya mavuno, yataukaribisha Ufalme (Mika 4:1, 2). (3) Kisha kwa kilio kikuu yatakwenda “barabarani na mipakani” (Luka 14:23), yakitangaza “Injili ya milele … kwa hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa” (Ufu. 14:6), “kuwabatiza … kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: kuwafundisha kuyashika yote” Kristo aliamuru (Mat. 28:19, 20). Pamoja na matunda yanayofuata kazi hii, mavuno ya pili, yataupanua Ufalme hadi uijaze dunia yote (Dan. 2:35). {LDSDA: 12.2}

Hivyo katika kuonyesha “kwa njia ya ishara na maajabu, kwa nguvu za Roho wa Mungu” (Rumi. 15:19), uwezo mkuu wa Ufalme, utatoa ushuhuda kwa ulimwengu kwamba Kristo yu pamoja na kanisa Lake “siku zote, hadi mwisho wa dunia.” Mat. 28:20. {LDSDA: 13.1}

Kinabii walioitwa katika shamba la mizabibu la Bwana mwanzoni mwa “saa ya kumi na moja,” Wadaudi Waadventista wa Sabato wanatangaza Ukweli wa Sasa uliofunuliwa katika kukunjua kwa chuo cha unabii (Shuhuda Kwa Kanisa, Gombo la 6, uk. 17). Kweli zake muhimu “zilizo wazi kwa wale ambao hushikilia ahadi za Neno la Mungu,” “uwezekano wa ajabu” na

13

“fursa na majukumu ambayo hata hawashuku kwamba yamo katika Biblia.” — Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 8, uk. 322. {LDSDA: 13.2}

Kama msingi wa muundo wao wa ufasiri wa Maandiko, Wadaudi hushikilia kwamba “uzoefu wa Israeli uliandikwa kwa ajili ya mafunzo yetu” (Elimu, uk. 50); ya kwamba kwa kweli “basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano: … yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani” (1 Kor. 10:11); ya kwamba, kwa hivyo, pale ambapo hakuna mfano wa msingi, hapawezi kuwa na sio ukweli wa msingi, uakisi; na ya kwamba, kwa sababu hiyo, wale “wasipowasikia… Musa na manabii, hawatashawishiwa, hata mtu akifufuka katika wafu.” Luka 16:31. {LDSDA: 14.1}

Kwa hivyo, jumuiya hii ya matengenezo, utumbo kwa shirika la Waadventista wa Sabato, hukumbatia misingi inayoyajumuisha Maandiko yote. Na kwa sababu hiyo imepewa Katiba na Sheria ndogo zilizo na kanuni za serikali na mfumo mara nne wa kurithi wa vuguvugu la Kutoka, ufalme wa Daudi, Waamuzi, na Mitume, kama inavyoangazwa na Roho ya Unabii katika vifungu vifuatavyo vikifunua kwamba Mungu ndiye kitovu cha mamlaka na ya kwamba watu wa uteuzi Wake ni wasimamizi wa sheria Yake: {LDSDA: 14.2}

14

SERIKALI

YA MUSA — KAMA HIYO

“Serikali ya Israeli ilikuwa na sifa za jumuiya kamili, ya ajabu pia kwa ukamilifu na urahisi wake. Mpangilio ukionyeshwa kwa ubora katika ukamilifu na upangaji wa kazi zote zilizoumbwa na Mungu zilidhihirika katika uchumi wa Waebrania. Mungu alikuwa kitovu cha mamlaka na serikali, Mfalme wa Israeli. Musa alisimama kama kiongozi wao anayeonekana, ambaye aliteuliwa na Mungu, kutekeleza sheria hizo kwa jina Lake. Kutoka kwa wazee wa makabila baraza la sabini baadaye lilichaguliwa kumsaidia Musa katika maswala ya jumla ya taifa. Kisha wakaja makuhani, waliotafuta ushauri kwa Bwana katika patakatifu. Akida, au wakuu, walitawala juu ya makabila. Chini yao walikuwa viongozi wa maelfu, na viongozi wa mamia, na viongozi wa hamsini, na viongozi wa makumi?’ na, mwisho kabisa maafisa ambao wangeweza kuajiriwa kwa kazi maalum.” — Mababu na Manabii, uk. 374. {LDSDA: 15.1}

“Kwa kupatana na mpango huu, ‘Musa alichagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, na kuwafanya wakuu kwa watu, watawala wa maelfu, watawala wa mamia, watawala wa hamsini, na watawala wa makumi. Nao waliwahukumu watu kwa misimu yote. Masuala magumu waliyaleta kwa Musa, lakini kila jambo ndogo waliamua wenyewe. {LDSDA: 15.2}

15

“Baadaye, wakati wa kuwachagua wazee sabini ili wagawane naye majukumu ya uongozi, Musa alikuwa mwangalifu kuwachagua kama wasaidizi wake, watu wenye heshima, wenye maamuzi mazuri, na uzoefu. Katika agizo lake kwa hao wazee wakati wa kuwekewa mikono, alielezea baadhi ya sifa ambazo humstahilisha mtu kuwa mtawala mwenye busara kanisani. “Sikiza visababishi kati ya ndugu zenu,” alisema Musa, ‘na muamue kwa haki kati ya kila mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. Msiwapendelee watu katika hukumu, lakini mtamsikia mdogo na mkuu, msiogope uso wa mwanadamu, kwa maana hukumu ni ya Mungu.” — Matendo ya Mitume, uk. 93, 94. {LDSDA: 16.1}

“Serikali ya Israeli ilisimamiwa kwa jina na kwa mamlaka ya Mungu. Kazi ya Musa, ya wazee sabini, ya watawala na waamuzi, ilikuwa tu kutekeleza sheria ambazo Mungu alikuwa ametoa; hawakuwa na mamlaka ya kutunga sheria kwa ajili ya taifa. Ilikuwa hivi, na iliendelea kuwa hivyo, hali ya uwepo wa Israeli kama taifa. Tangu kizazi hata kizazi, watu waliovuviwa na Mungu walitumwa kuwapa watu maagizo, na kuelekeza katika utekelezaji wa sheria.” — Mababu na Manabii, uk. 603. {LDSDA: 16.2}

YA DAUDI — KAMA HIYO

“Mfalme Daudi, karibu mwisho wa utawala wake, aliwasilisha agizo zito kwa wale waliobeba mzigo wa kazi ya Mungu katika

16

siku yake. Akawaita Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa makabila, na maakida wa makundi yaliyomtumikia mfalme kwa kweli na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, na wasimamizi kwa vitu na mali yote ya mfalme, na ya wanawe, na maafisa, na mashujaa, na watu wote hodari, mfalme huyo mzee aliwaagiza kwa uzito, machoni pa Israeli wote mkutano wa Bwana, na mbele ya Mungu wetu, ‘kutunza na kutafuta amri zote za Bwana Mungu wako.’ {LDSDA: 16.3}

“Kwa Sulemani, aliyeitwa kuchukua nafasi ya kuongoza, Daudi alimpa agizo maalum: “Wewe, Sulemani mwanangu, umjue Mungu wa baba yako, na umtumikie Yeye kwa moyo safi na wenye nia ya kujitolea: maana Bwana huchunguza mioyo yote, na huelewa mambo yote ya mawazo: ikiwa utamtafuta Yeye, Atapatikana kwako, lakini ukimwacha Yeye, Atakutupa milele. Jihadhari sasa; kwa maana Bwana amekuchagua:…uwe hodari.” — Matendo ya Mitume, uk. 94, 95. {LDSDA: 17.1}

YA EZRA — KAMA HIYO

Tena: “Kama tahadhari maalum kulinda hazina hiyo, Ezra ‘aliwatenga kumi na wawili wa wakuu wa makuhani, — watu ambao uaminifu na uthabiti wao ulikuwa umethibitishwa, — ‘ na wakawapimia fedha,

17

na dhahabu, na vyombo, hata sadaka ya nyumba ya Mungu wetu, ambayo mfalme na washauri wake, na mabwana wake, na Israeli wote waliokuwako, walikuwa wametoa. Watu hawa waliagizwa kwa uzito kutenda kama wasimamizi hodari kwa hazina waliyokabidhiwa kuitunza. ‘Ninyi ni watakatifu kwa Bwana,’ Ezra alisema; vyombo ni vitakatifu pia; na fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana Mungu wa baba zenu. Kesheni ninyi, na kuzihifadhi, mpaka mzipime mbele ya wakuu wa makuhani na Walawi, na wakuu wa baba za Israeli, huko Yerusalemu, katika vyumba vya nyumba ya Bwana.” {LDSDA: 17.2}

“Uangalifu uliotekelezwa na Ezra kwa kutoa usafirishaji na usalama wa hazina ya Bwana, hufundisha somo linalostahili kusomwa kwa makini. Wale tu ambao uaminifu wao ulikuwa umethibitishwa, walichaguliwa; na waliagizwa bayana kwa jukumu lililowekwa juu yao. Katika kuwateua maafisa waaminifu kufanya kama watunza hazina wa bidhaa za Bwana, Ezra alitambua umuhimu na thamani ya mpangilio na jumuiya kuhusiana na kazi ya Mungu.” — Manabii na Wafalme, uk. 616, 617. {LDSDA: 18.1}

YA MITUME — KAMA HIYO

“Kanuni zile zile za kumcha Mungu na haki ambazo zilikuwa za kuwaongoza watawala kati ya watu wa Mungu wakati wa Musa na wa Daudi, pia zingefuatwa na wale waliopewa

18

usimamizi wa kanisa jipya la Mungu katika enzi ya injili. Katika kazi ya kuweka mambo kwa mpangilio katika makanisa yote, na kuwawekea mikono watu wanaofaa kutenda kama maafisa, mitume walishikilia viwango vya juu vya uongozi vilivyoorodheshwa katika Maandiko ya Agano la Kale. Walisisitiza kwamba yeye aliyeitwa kusimama kwa nafasi ya jukumu la uongozi ndani ya kanisa, ‘lazima awe asiyelaumika, kama msimamizi wa Mungu; si wa kujipenda mwenyewe, si wa kukasirika haraka, asyezoelea ulevi, si mpiga watu, asiyependa fedha ya aibu; bali mpenda ukarimu, mpenda watu wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mpole; akishikilia sana neno la uaminifu jinsi alivyofundishwa, ili aweze kuwahimiza na kuwashawishi wakaidi.” — Matendo ya Mitume, uk. 95. {LDSDA: 18.2}

“Wakiitisha mkutano wa waumini, mitume waliongozwa na Roho Mtakatifu kutaja mpango wa mpangilio bora wa nguvu-kazi zote za kanisa. Wakati ulikuwa umekuja, mitume walisema, wakati viongozi wa kiroho wakiwa waangalizi wa kanisa wanapaswa kuachishwa kazi ya kuwasambazia maskini na kutoka kwa mizigo kama hiyo, ili waweze kuwa huru kuendelea na kazi ya kuitangaza injili. “Basi ndugu,” walisema, “chagueni watu saba miongoni mweu walioshuhudiwa kuwa wema wenye kujawa na Roho Mtakatifu na hekima, ili tuwaweke kwa shughuli hili.

19

Na sisi tutadumu katika kuomba, na kulihudumia lile neno.” Ushauri huu ulifuatwa, na kwa sala na kuwekewa mikono, watu saba waliochaguliwa walitengwa kwa majukumu yao kama mashemasi. {LDSDA: 19.1}

“Uteuzi wa wale saba kuchukua usimamizi wa safu maalum za kazi, ulionyesha baraka kubwa kwa kanisa hilo. Maafisa hawa walizingatia kwa uangalifu mahitaji ya mtu mmoja mmoja na vile vile maslahi ya jumla ya kifedha ya kanisa; na kwa usimamizi wao wa busara na mfano wao wa kiungu, walikuwa msaada muhimu kwa maafisa wenzao kufunganisha pamoja masilahi ya kanisa kwa umoja. {LDSDA: 20.1}

“Kwamba hatua hii ilikuwa kwa mpangilio wa Mungu, imefunuliwa katika matokeo ya haraka kwa mema ambayo yalionekana. ‘Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; na jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile imani.’ Kukusanywa huku kwa mioyo kulitokana na uhuru mkubwa uliowekwa na mitume, na kwa bidii na nguvu iliyoonyeshwa na mashemasi hao saba. Ukweli kwamba ndugu hawa walikuwa wamewekewa mkono kwa kazi maalum ya kuchunga mahitaji ya maskini, haikuwatenga wasifundishe imani. Kinyume chake, walikuwa wamehitimu kikamilifu kuwafundisha wengine katika ukweli, na walijihusisha katika kazi hiyo kwa bidii na mafanikio makubwa.” — Kimenukuliwa., uk. 89, 90. {LDSDA: 20.2}

20

UTARATIBU

“Mungu ni Mungu wa utaratibu. Kila kitu kilichounganika na mbingu kiko katika utaratibu kamili; utii na nidhamu kamili hutia alama harakati za jeshi la malaika. Ufanisi unaweza kufuata tu utaratibu na hatua zinazopatana. Mungu huhitaji utaratibu na mfumo katika kazi Yake sasa usiopungua katika siku za Israeli. Wote wanaomtumikia Yeye ni lazima wafanye kazi kwa busara, sio kwa namna ya uzembe, na ya ovyoovvyo. Yeye angetaka kazi Yake ifanywe kwa imani na kwa usahihi, ili Yeye aweke muhuri wa idhini Yake kwayo.” — Mababu na Manabii, uk. 376. {LDSDA: 21.1}

“‘Mungu si mwasisi wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.’ Yeye huhitaji utaratibu na mfumo uzingatiwe katika mwenendo wa masuala ya kanisa leo, sio chini ya siku za zamani. Yeye hutamani kazi Yake iendeshwe mbele kwa ukamilifu na usahihi, ili aweke kwayo muhuri wa idhini yake. Mkristo anapaswa kuunganishwa na Mkristo, kanisa na kanisa, chombo cha kibinadamu kikishirikiana na kitakatifu, kila shirika lililo chini ya Roho Mtakatifu, na yote kwa pamoja kutoa kwa ulimwengu habari njema ya neema ya Mungu.” — Matendo ya Mitume, uk. 96. {LDSDA: 21.2}

“Wakati na nguvu za wale ambao kwa majaliwa ya Mungu wamewekwa katika nafasi za majukumu kuongoza katika kanisa, zinapaswa kutumika kushughulikia masuala mazito yanayodai hekima

21

maalum na moyo mwema. Sio kwa utaratibu wa Mungu kwamba watu kama hao wanapaswa kutafutwa kwa marekebisho ya masuala madogo ambayo wengine wanastahili kuyashughulikia. ‘Kila jambo lililokubwa watakuletea,’ Yethro akapendekeza kwa Musa, ‘lakini kila jambo ndogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. Ikiwa utafanya jambo hili, na Mungu akuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.” — Matendo ya Mitume, uk. 93. {LDSDA : 21.3}

KANISA LA AGANO LA KALE — KAMA HIYO

“Kambi ya Waebrania ilipangwa kwa utaratibu sawa. Iligawanywa katika sehemu kuu tatu, kila moja ikiwa na nafasi yake teule kambini. Katikati lilikuwapo hema ya kukutania, makao ya Mfalme asiyeonekana. Kulizunguka kwa karibu waliwekwa makuhani na Walawi. Mbali kwa hema la kukutania na makuhani na Walawi zilipiga kambi kabila zingine zote. {LDSDA: 22.1}

“Kwa Walawi walipewa jukumu la hema la kukutania, na yote yaliyohusiana nalo, kambini na safarini. Wakati kambi ilisonga mbele, walipaswa kulibomoa hema takatifu; wakati mahali pa kupumzika palifikiwa, walipaswa kulisimamisha. Hakuna mtu wa kabila lingine aliruhusiwa kukaribia, angeuawa. Walawi walitengwa katika migawo mitatu, wazawa wa wana watatu wa Lawi, na kila mmoja alipewa nafasi yake maalum

22

na kazi. Mbele ya hema la kukutania, na karibu kwalo, kulikuwa na mahema ya Musa na Haruni. Upande wa kusini walikuwa Wakohathi, ambao jukumu lao lilikuwa kutunza sanduku na samani zingine; kaskazini Wamerari, ambao waliwekwa juu ya usimamizi wa nguzo, viungio, mbao, nk; nyuma Wagershoni, ambao walikabidhiwa utunzi wa mapazia na vifungo. {LDSDA: 22.2}

Nafasi ya kila kabila pia iliwekwa bayana. Kila mmoja alipaswa kwenda na kupiga kambi kando ya bendera yake, kama BWANA alivyokuwa ameamuru: ‘Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote. Kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao. Umati mseto ambao ulikuwa umeambatana na Israeli kutoka Misri haukuruhusiwa kukaa katika makazi hayo pamoja na makabila lakini ulikaa nje ya marago, na wazawa wao walipaswa kutengwa kutoka kwa jumuiya hadi kizazi cha tatu. {LDSDA: 23.1}

* * *

“Katika safari yote za Israeli, ‘sanduku la agano la Bwana likatangulia,… ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.’ Likichukuliwa na wana wa Kohathi, sanduku takatifu lililokuwa na sheria takatifu ya Mungu lilipaswa kuongoza msafara. Kabla liende Musa na Haruni, na makuhani wakichukua baragumu

23

za fedha, walisimama karibu. Makuhani hawa walipokea maagizo kutoka kwa Musa, ambayo waliwaambia watu kwa baragumu. Lilikuwa jukumu la viongozi wa kila kundi kutoa maelekezo sahihi mintarafu harakati zote zilizopaswa kufanywa, kama yalivyoashiriwa na baragumu. Yeyote aliyepuuza kufuata maagizo yaliyotolewa, aliadhibiwa kwa kifo.” — Mababu na Manabii, uk. 374, 375, 376. {LDSDA: 23.2}

KANISA LA AGANO JIPYA — KAMA HIYO

“Walipokuwa tu wameunganika na Kristo, wanafunzi wangaliweza kutumaini kuwa na nguvu inayoambatana na Roho Mtakatifu, na ushirikiano wa malaika wa mbinguni. Kwa msaada wa mashirika haya matakatifu, wangewasilisha mbele ya ulimwengu kikosi kilichoungana, na wangekuwa washindi katika vita walivyolazimika kuvipiga bila kukoma dhidi ya nguvu za giza. Kadiri ambavyo wangeendelea kufanya kazi kwa umoja, wajumbe wa mbinguni wangetangulia mbele yao, wakifungua njia; mioyo ingetayarishwa kwa mapokezi ya ukweli, na wengi wangevutwa kwa Kristo. Mradi wangedumu kwa umoja, kanisa lingeenda mbele, ‘zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lililo na mabango.’ Hakuna kitu kingeweza kuhimili ustawi wake wa kuendelea. Kanisa lingesonga mbele kwa ushindi likishinda, kwa utukufu likitimiza utume wake mtakatifu wa kutangaza injili kwa ulimwengu. {LDSDA: 24.1}

24

“Mpangilio wa kanisa huko Yerusalemu ulikuwa wa kutumika kama kielelezo kwa mpangilio wa makanisa katika kila sehemu nyingine ambapo wajumbe wa ukweli walipaswa kuwavuta waongofu kwa injili. Wale ambao walipewa jukumu la uangalizi wa jumla kwa kanisa, hawakupaswa kuwa watawala kwa urithi wa Mungu, lakini, kama wachungaji wa busara, walipaswa ‘kulisha kundi la Mungu, … wakiwa vielelezo kwa kundi;’ na mashemasi walipaswa kuwa walioshuhudiwa kuwa wema wenye kujawa na Roho Mtakatifu na hekima.’ Watu hawa walipaswa kuchukua nafasi zao kwa umoja upande wa haki, na kuidumisha kwa uthabiti na uamuzi. Hivyo wangekuwa na mvuto wa kuunganisha kwa kundi lote. {LDSDA: 25.1}

“Baadaye katika historia ya kanisa la awali, wakati katika sehemu mbali mbali za ulimwengu makundi mengi ya waamini yalikuwa yameanzishwa kuwa makanisa, mpangilio wa kanisa uliboreshwa zaidi, ili kwamba utaratibu na utendaji wa ushirikiano uweze kudumishwa. Kila mshiriki alihimizwa kutenda vyema sehemu yake. Kila mmoja alipaswa kutumia kwa hekima talanta aliyokabidhiwa. Wengine walipewa na Roho Mtakatifu vipawa maalum, — ‘wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.’ Lakini madaraja haya yote ya watendakazi yalipaswa kufanya kazi kwa ushirikiano. {LDSDA: 25.2}

“‘Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za

25

huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni Yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho Yeye yule; mwingine imani katika Roho Yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, Yeye yule, akimgawia kila mtu pekee yake kama apendavyo Yeye. Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.’” — Matendo ya Mitume, uk. 90-92. {LDSDA: 25.3}

“Utaratibu uliodumishwa katika kanisa la awali la Kikristo, uliwawezesha kusonga mbele kidete, kama jeshi lililoadibishwa vyema, likiwa limevikwa silaha za Mungu. Makundi ya waamini, ingawa yalitawanyika kwa eneo kubwa, wote walikuwa washiriki wa mwili mmoja, wote walienenda kwa mapatano, na kwa ushirikiano mmoja kwa mwingine. Mzozo ulipozuka katika kanisa la mtaa, jinsi baadaye ulivyotokea Antiokia na mahali pengine, na waamini hawakuweza kuafikiana kati yao, mambo kama haya hayakuruhusiwa

26

kufanya mgawanyiko kanisani lakini yalielekezwa kwa baraza kuu la jamii ya waamini wote, lililoundwa na wajumbe walioteuliwa kutoka kwa makanisa mbali mbali ya eneo, na mitume na wazee katika nafasi za jukumu la kuongoza. Hivyo juhudi za Shetani kulishambulia kanisa katika sehemu za mbali, zilikabiliwa na hatua za pamoja kwa pande zote, na mipango ya adui kuvuruga na kuharibu ilikomeshwa.” — Kimenukuliwa., uk. 95, 96. {LDSDA: 26.1}

“Bibilia kwa njia maalum hutufundisha kuwa waangalifu kwa wepesi kuleta hujuma dhidi ya wale ambao Mungu amewaita kutenda kama mabalozi Wake. Mtume Petro, akielezea daraja ambalo ni wadhambi walioachwa, husema, ‘wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele ya Bwana.’ Na Paulo, katika agizo lake kwa wale waliowekwa kusimamia kanisa, husema, ‘Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.’ Yeye ambaye amewatwika watu jukumu kubwa la viongozi na waalimu wa watu Wake, atawawajibisha watu kwa namna wanavyowatendea watumwa Wake. Tunapaswa kuwaheshimu wale ambao Mungu amewapa heshima.” — Mababu na Manabii, uk. 386. {LDSDA: 27.1}

27

NIDHAMU

“Mungu alikuwa amemchagua Musa, na alikuwa ameiweka Roho Yake juu yake; na Miriamu na Haruni, kwa manung’uniko yao, walikuwa na hatia ya kutokuwa waaminifu, sio tu kwa kiongozi wao aliyeteuliwa, ila kwa Mungu Mwenyewe. Wachochea maasi wanong’onezi hao waliitwa kwa hema, na kuletwa uso kwa uso na Musa. ‘Ndipo Yehova akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama mlangoni pa hema, akawaita Haruni na Miriamu.’ Madai yao kwa karama hiyo ya kinabii hayakukataliwa, Mungu angeweza kusema nao katika maono na ndoto. Lakini kwa Musa, ambaye Bwana Mwenyewe alitangaza ‘mwaminifu katika nyumba Yangu yote,’ mazungumzo ya karibu alikuwa amepewa. Naye Mungu alizungumza mdomo kwa mdomo. ‘Mbona basi hamkuogopa kunena dhidi ya mtumwa Wangu Musa? Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu yao, Naye akaondoka.’ Wingu likatoweka kwenye hema ishara ya kutompendeza Mungu, na Miriamu akapigwa. ‘Akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji.’ Haruni alisazwa, lakini alikaripiwa vikali katika adhabu ya Miriamu. Sasa, majivuno yao yakashushwa mavumbini, Haruni aliungama dhambi yao, na kusihi kwamba dada yake asiachwe aangamie kwa janga hilo baya mno na lenye kuua. Kwa kujibu maombi ya Musa, ukoma ulitakaswa. Miriamu, hata hivyo, alifungiwa nje ya marago kwa siku saba.

28

Ilikuwa ni baada tu ya kuondolewa kwenye marago ndiposa ishara ya neema ya Mungu ilitua juu ya hema? Kwa heshima na nafasi yake ya juu, na huzuni kwa pigo lililomwangukia, kundi lote lilikaa Hazerothi, likingojea kurejea kwake.” — Mababu na Manabii, uk. 384, 385. {LDSDA: 28.1}

Baadaye “njama ya kina iliundwa, tokeo la kusudi lililoazimiwa kupindua mamlaka ya viongozi walioteuliwa na Mungu Mwenyewe. {LDSDA: 29.1}

“Kora, roho iliyoongoza katika harakati hii, alikuwa Mlawi, wa familia ya Kohathi, na binamu wa Musa, alikuwa mtu mwenye uwezo na ushawishi. Ingawa alikuwa ameteuliwa katika huduma ya hema la kukutania, hakuridhika kwa nafasi yake, na akatamani hadhi ya ukuhani. Kipaji kwa Haruni na nyumba yake cha ofisi ya ukuhani, ambayo hapo awali ilimwangukia mwana mzaliwa wa kwanza wa kila familia, ilikuwa amesababisha wivu na kutoridhika, na kwa wakati mwingine Kora alikuwa akipinga kwa siri mamlaka ya Musa na Haruni, ingawa alikuwa hajadiriki kwa tendo lolote la uasi hadharani. Mwishowe alibuni muundo jasiri wa kupindua mamlaka ya kiraia na ya kidini. Hakushindwa kupata wa kumuunga mkono. Karibu kwa mahema ya Kora na Wakohathi, upande wa kusini wa hema la kukutania, palikuwa na kambi ya kabila la Reubeni, hema za Dathani na Abiramu, wakuu wawili wa kabila hili, karibu na lile la Kora.

29

Hawa wakuu kwa utayari walijiunga na miradi yake ya tamaa. Wakiwa wazawa kutoka kwa mwana mkubwa wa Yakobo, walidai kwamba mamlaka ya kiraia yalikuwa yao, na waliazimia kugawana na Kora heshima za ukuhani. {LDSDA: 29.2}

“Hali ya hisia kati ya watu ilipendelea mikakati ya Kora. Katika uchungu wa kutamauka kwao, mashaka ya zamani, wivu, na chuki zao zilikuwa zimerejea, na tena malalamishi yao yakaelekezwa dhidi ya kiongozi wao mvumilivu. Waisraeli daima walikuwa wakikosa kuona ukweli kwamba walikuwa chini ya uongozi wa Mungu. Walisahau kwamba Malaika wa agano alikuwa kiongozi wao asiyeonekana, ya kwamba, ukiwa umefunikwa na nguzo ya wingu, uwepo wa Kristo uliwatangulia, na ya kwamba kutoka Kwake Musa alipokea maelekezo yake yote. {LDSDA : 30.1}

“Hawakutaka kunyenyekea kwa hukumu ya kutisha kwamba lazima wote wafe nyikani na kwa hivyo walikuwa tayari kudakia kila kisingizio cha kuamini kwamba si Mungu ila ni Musa ambaye alikuwa akiwaongoza, na ambaye alikuwa ametamka maangamizi yao. Juhudi bora za mtu mpole zaidi juu ya nchi hazingeweza kuzima maasi ya watu hawa, na ingawa alama za kutopendezwa Mungu kwa upotovu wao wa zamani zilikuwa bado mbele yao katika safu zao zilizovunjika na idadi iliyokosekana, hawakuliweka hilo funzo moyoni. Tena walishindwa kwa majaribu. {LDSDA: 30.2}

* * *

30

“Walifanikiwa kuwatenga wakuu mia mbili na hamsini, watu mashuhuri katika kundi. Pamoja na wafuasi hawa hodari na wenye ushawishi walijihisi wajasiri wa kufanya mageuzi makubwa serikalini, na kuboresha sana utawala wa Musa na Haruni. {LDSDA : 31.1}

“Wivu ulikuwa umeiamsha chuki, na chuki uasi. Walikuwa wamejadili hoja ya Musa kuwa na mamlaka makubwa na heshima kama hiyo hadi walipomwona kama mtu anayeshikilia nafasi ya kutamaniwa, ambayo yeyote angeweza kuijaza kama yeye. Na walijidanganya wenyewe na mmoja kwa mwingine kufikiri kwamba Musa na Haruni walikuwa wenyewe wamejitwalia nafasi walizoshikilia. Wasioridhika walisema kwamba viongozi hawa wamejiinua juu ya kundi la Bwana, kwa kujitwalia ukuhani na serikali, lakini nyumba yao haikuwa na haki ya ukuu zaidi ya zingine katika Israeli; hawakuwa watakatifu zaidi ya watu, na imetosha wao wawe kwa kiwango sawa na ndugu zao, ambao kwa usawa walipewa neema kwa uwepo na ulinzi maalum wa Mungu. {LDSDA: 31.2}

“Kazi iliyofuata ya waliokula njama ilikuwa na watu. Kwa wale ambao wamekosea, na kustahili kukaripiwa, hakuna kitu kinachofurahisha zaidi kuliko kupokea huruma na sifa. Na kwa hivyo Kora na washirika wake walipata umakini na kusajili uungwaji mkono wa kundi.

31

Shtaka kwamba manung’uniko ya watu yalikuwa yameleta gadhabu ya Mungu, lilitangazwa kuwa kosa. Walisema kwamba kusanyiko halikuwa na kosa, kwa sababu hawakutaka chochote zaidi ya haki zao, ila kwamba Musa alikuwa mtawala mkandamizaji; ya kwamba alikuwa amewakemea watu kama wenye dhambi, ilhali walikuwa watu watakatifu, na Bwana alikuwa kati yao. {LDSDA: 31.3}

***

“Katika kazi hii ya kufarakana palikuwa na umoja na maelewano makubwa kati ya chembe zisizopatana za kundi kuliko hapo awali. Ufanisi wa Kora na watu uliongeza ujasiri na kumthibitisha katika imani yake kwamba unyakuzi wa mamlaka wa Musa, usipodhibitiwa, utakuwa hatari kwa uhuru wa Israeli; pia alidai kwamba Mungu alikuwa amemfunulia hilo jambo, na alikuwa Amemwamuru kufanya mageuzi serikalini kabla kuchelewa mno. Lakini wengi hawakuwa tayari kuyakubali mashtaka ya Kora dhidi ya Musa. Kumbukumbu ya uvumilivu wake, kazi zake za kujinyima ilikuja mbele yao, na dhamira zikasumbuka. Kwa hivyo ilikuwa ni lazima kupeana hoja fulani ya ubinafsi ya maslahi yake makubwa kwa Israeli, na shtaka la zamani likasisitizwa, kwamba alikuwa amewaongoza waangamie nyikani, ili aweze kunyakua mali yao. {LDSDA: 32.1}

“Kwa muda kazi hii iliendelezwa kwa usiri. Mara tu, hata hivyo, kwa sababu vuguvugu

32

lilikuwa limepata nguvu za kutosha kuidhinisha kipeo cha furaha wazi, Kora alionekana kiongozi wa kikundi hicho, na akawashutumu hadharani Musa na Haruni kunyakua mamlaka ambayo Kora na washirika wake walikuwa na haki ya kugawana. Walishutumu, zaidi, kwamba watu walikuwa wamenyimwa uhuru wao na kujitawala. ‘Ninyi inawatosha,’ walisema wale waliokula njama, ‘kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; ni nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? {LDSDA: 32.2}

“Musa alikuwa hajashuku njama hii ya kina, na maana yake ya kutisha ilipomtokea, akaanguka kifudifudi katika maombi kimya kimya kwa Mungu. Aliinuka kwa huzuni kweli kweli, lakini mtulivu na imara. Alikuwa amepewa mwongozo wa Mungu. ‘Hata kesho’ akasema, ‘Bwana ataonyesha ni nani walio Wake, na ni nani mtakatifu, na atamfanya amkaribie Yeye: hata yeye ambaye Yeye amemchagua atamfanya amkaribie Yeye.’ Mtihani ulipaswa kuahirishwa hadi kesho, ili wote wawe na wakati wa kutafakari. Kisha wale waliotamani ukuhani walipaswa kuja kila mmoja na chetezo, na kutoa uvumba kwenye hema mbele ya mkutano. Sheria ilikuwa wazi kabisa kwamba ni wale tu ambao walikuwa wamewekwa mkono kwa ofisi takatifu ndio waliopaswa kuhudumu katika patakatifu. Na hata makuhani, Nadabu na Abihu, waliangamizwa kwa kujaribu

33

kutoa ‘moto wa kigeni,’ kwa kupuuza amri ya Mungu. Bado Musa aliwasai washtaki wake, ikiwa wangethubutu kukata rufaa hatari, ili kurejeza suala hilo kwa Mungu. {LDSDA: 33.1}

“Akimlenga Kora na Walawi wenzake, Musa akasema, ‘je! Mwaona kuwa ni jambo dogo kwenu, kwamba Mungu wa Israeli amewatenga ninyi na kundi lote la Israeli, ili apate kuwakaribisha Kwake ili mfanye utumishi wa maskani ya Bwana, na kusimama mbele ya mkutano ili kuwatumikia? Tena ya kuwa Yeye amekuleta uwe karibu Naye, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe, nanyi je! mwataka ukuhani pia? Kwa sababu hii wewe na kundi lako lote mmekusanyika kinyume cha Bwana. Na Haruni, je! yeye ni nani hata mkamnung’unikia? {LDSDA: 34.1}

“Dathani na Abiramu walikuwa hawajachukua msimamo wa ujasiri kama wa Kora na Musa, wakitumaini kwamba wangekuwa wamevutwa kwenye njama kabla hawajapotoshwa kabisa, akawaita waje mbele yake, ili asikilize mashtaka yao dhidi yake. Lakini hawakuja, na kwa ujeuri wakakataa kutambua mamlaka yake. Jibu lao, lililonenwa mkutano ukisikia, lilikuwa, ‘Je! ni jambo dogo wewe hukutuleta katika nchi iliyojawa maziwa na asali, ili kutuua nyikani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu kabisa?

34

Isitoshe hukutuleta katika nchi iliyojawa maziwa na asali, wala hukutupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu; Je! unataka kuwafumba macho watu hawa? Hatuji.’ {LDSDA: 34.2}

* * *

“Kesho yake, wale wakuu mia mbili na hamsini, na Kora akiwaongoza, wakajitokeza, na vyetezo vyao. Wakaletwa ndani ya behewa la hema, wakati watu walikusanyika nje, kusubiri tokeo. Hakuwa Musa ambaye aliwakusanya mkutano kutazama kushindwa kwa Kora na kundi lake, bali wale waasi, katika majivuno yao ya upofu walikuwa wamewaita pamoja kushuhudia ushindi wao. Sehemu kubwa ya mkutano huo uliungana na Kora wazi wazi, ambaye matarajio yake yalikuwa kutekeleza hatua yake dhidi ya Haruni. {LDSDA: 35.1}

“Walipokuwa wamekusanyika hivyo mbele ya Mungu, ‘utukufu wa Bwana ukaonekana kwa mkutano wote.’ Onyo la Mungu lilinenwa kwa Musa na Haruni, ‘Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.’ Nao wakaanguka kifudifudi wakasema, ‘Ee Mungu, Mungu wa roho za wote wenye mwili, mtu mmoja atafanya dhambi, Nawe utaukasirikia mkutano wote? {LDSDA: 35.2}

“Kora alikuwa amejitenga na mkutano, kuungana na Dathani na Abiramu, wakati Musa, pamoja na wazee sabini,

35

walienda na onyo la mwisho kwa wale watu waliokuwa wamekataa kuja kwake. Umati ulifuata, na kabla hajauwasilisha ujumbe wake, Musa, kwa mwongozo wa Mungu, aliwaamuru watu, ‘Ondokeni, nawasihi penye hema za watu hawa waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe kwa dhambi zao zote.’ Onyo hilo walitii, kwa wasiwasi wa hukumu iliyowasubiri iliwakalia wote. Waasi wakuu walijiona wameachwa na wale waliokuwa wamewadanganya, lakini ugumu wao haukutikisika. Walisimama na familia zao milangoni mwa hema zao, kana kwamba wanakaidi onyo la Mungu. {LDSDA: 35.3}

“Kwa jina la Mungu wa Israeli, sasa Musa alitangaza, mkutano wakisikia: ‘Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma ili nifanye kazi hizi zote, kwa kuwa mimi sikufanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa watakufa kifo siku zote, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote, hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, washuke shimoni wangali hai, ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana.’ {LDSDA: 36.1}

“Waisraeli wote walimkazia Musa macho walipokuwa wamesimama, kwa hofu na matarajio, wakingojea tukio hilo. Hapo alipokwisha kusema maneno hayo yote, nchi ikafunua kinywa chake, na waasi wakashukia shimoni wali hai.

36

Nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Watu walikimbia wakijihukumu kama washiriki katika dhambi hiyo. {LDSDA: 36.2}

“Lakini hukumu hazikuwa zimekoma. Moto ukimulika kutoka kwenye wingu ukawateketeza wale wakuu mia mbili na hamsini ambao walikuwa wamevukiza uvumba. Watu hawa, hawakuwa wa kwanza katika uasi, hawakuangamizwa pamoja na wala njama wakuu. Waliruhusiwa kuona mwisho wao, na kupata fursa ya kutubu, lakini huruma zao zilikuwa pamoja na waasi, na wakashiriki hatma yao. {LDSDA: 37.1}

“Musa alipokuwa akiwasihi Israeli kukimbia kutoka kwa maangamizi yaliokuwa yakija, hukumu ya Mungu ingeweza kusitishwa wakati huo, ikiwa Kora na kundi lake wangetubu na kutafuta msamaha. Lakini ukaidi wao msumbufu ulitia muhuri maangamizi yao. Kongamano lote lilikuwa washiriki katika hatia yao, maana wote walikuwa, kwa kiasi kikubwa au kidogo wamewaunga mkono. Bado Mungu kwa rehema Yake kubwa alifanya tofauti kati ya viongozi katika uasi na wale waliokuwa wameongozwa. Watu waliokuwa wameruhusu kudanganywa bado walipewa nafasi ya toba. Ushahidi mwingi kupita kiasi walikuwa wamepewa kwamba walikuwa wamekosa, na kwamba Musa alikuwa sawa. Ishara iliyodhihirika ya nguvu za Mungu ilikuwa imeondoa mashaka yote. {LDSDA: 37.2}

* * *

Israeli wote walikuwa wamekimbia kwa mshtuko, kwa kilio cha wadhambi walioangamizwa

37

walioingia shimoni, kwa maana walisema, ‘Nchi isije kutumeza nasisi pia.’ ‘Lakini kesho yake kongamano lote la wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa na Haruni, wakisema, Ninyi mmewaua watu wa Bwana.’ Nao walikuwa karibu kuanza vurugu dhidi ya viongozi wao waaminifu, wa kujidhabihu. {LDSDA: 37.3}

* * *

“Lakini mhudumu wa ghadhabu alikuwa ametokea, pigo lilikuwa linafanya kazi yake ya kifo. Kwa maelekezo ya nduguye, Haruni alichukua chetezo, na akaharakisha kati ya kongamano ili ‘kufanya upatanisho kwa ajili yao.’ ‘Naye akasimama kati ya wafu na walio hai.’ Moshi wa uvumba ulipopanda, sala za Musa kwenye hema zilipanda kwa Mungu; pigo likakoma, lakini baada ya elfu kumi na nne wa Israeli walilala wamekufa, ushahidi wa hatia ya manung’uniko na uasi. {LDSDA: 38.1}

“Lakini ushahidi zaidi ulitolewa kwamba ukuhani ulikuwa umesimamishwa katika familia ya Haruni. Kwa maelekezo ya Mungu kila kabila lilitayarisha fimbo, na kuandika kwayo jina la kabila hilo. Jina la Haruni lilikuwa kwa ile ya Lawi. Hizo fimbo ziliwekwa kwenye hema, ‘mbele ya agano.’ Kuchanua maua kwa fimbo yoyote ilikuwa ishara kwamba Bwana alikuwa amelichagua kabila hilo kwa ukuhani. Siku ya pili yake, ‘tazama, fimbo ya Haruni kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka na imetoa machipukizi, na kuchanua maua na kuza malozi mabivu.

38

Ilionyeshwa kwa watu, na baadaye ikawekwa kwenye hema kama ushahidi kwa vizazi vya siku za baadaye. Muujiza huu ulitatua kwa ufanisi suala la ukuhani. {LDSDA: 38.2}

“Ilikuwa imethibitishwa kikamilifu kwamba Musa na Haruni walikuwa wamenena kwa mamlaka ya Mungu; na watu walilazimika kuamini ukweli ambao haukupendeza kwamba wangekufa nyikani. ‘Tazama,’ walisema, ‘tunakufa, tunaangamia, tunaangamia sisi sote. Walikiri kwamba walikuwa wamefanya dhambi kuasi dhidi ya viongozi wao, na ya kwamba Kora na kundi lake walikuwa wameathirika kutokana na hukumu ya haki ya Mungu.’ — Kimenukuliwa., uk. 395-403. {LDSDA: 39.1}

Katika siku za Ezra, wachache wa wakuu wa Israeli walimwendea na malalamishi mazito. “Baadhi ya ‘watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, walikuwa wamezipuuza amri takatifu za Bwana,’ kwa kuoana na watu waliowazunguka. ‘Wamewatwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao,’ Ezra aliambiwa, ‘basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu’ wa nchi hizi; ‘naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili.’ {LDSDA: 39.2}

* * *

“Wakati wa dhabihu ya jioni, Ezra akainuka, na mara tena akilirarua vazi lake na joho lake akaanguka magotini, akatoa mzigo moyoni mwake akisali kwa Mbingu. Akiikunjua mikono yake kwa

39

Bwana, akasema, ‘Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele yako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni.’ {LDSDA: 39.3}

* * *

“Mmoja wa wale waliokuwepo, Shekania kwa jina, alikubali kwamba ni ukweli maneno yote yaliyosemwa na Ezra. ‘Tumefanya dhambi dhidi ya Mungu wetu,’ alikiri, ‘nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi: lakini kungaliko tumaini kwa Israeli katika jambo hili.’ Shekania alipendekeza kwamba wote ambao wameasi wafanye agano na Mungu kuachana na dhambi zao, na kuhukumiwa ‘kulingana na sheria.’ ‘Inuka,’ akamsihi Ezra, ‘kwa kuwa shughuli hii yakuhusu wewe: na sisi tu pamoja nawe: uwe na moyo mkuu ukaitende.’ Kisha Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Israeli wote, kwamba watatenda kulingana na neno hili. {LDSDA: 40.1}

“Huu ulikuwa mwanzo wa matengenezo ya ajabu. Kwa uvumilivu usio na mwisho na busara, na kwa uangalifu wa kujali haki na maslahi ya kila mtu aliyehusika, Ezra na washirika wake walijitahidi kuwaongoza waliotubu wa Israeli katika njia sahihi. Zaidi ya yote mengine, Ezra alikuwa mwalimu wa sheria; na kadiri alivyokuwa akizingatia umakini kwa kila kesi binafsi, alitafuta kuwavutia watu kwa utakatifu wa sheria hii, na baraka zitakazopatikana kupitia utiifu.” — Manabii na Wafalme, uk. 619-622. {LDSDA: 40.2}

40

ELIMU

TARATIBU ZA SHULE NA MTAALA

Lengo la Kweli la Elimu

“Lengo la kweli la elimu ni kurejesha sura ya Mungu katika nafsi. Hapo mwanzo, Mungu alimuumba mwanadamu kwa sura Yake. Alimpa sifa za ungwana. Akili zake zilizawazika vyema, na nguvu zote za nafsi yake zilikuwa zinapatana. Lakini anguko na athari zake limepotosha zawadi hizi. Dhambi imeharibu na karibu ifute sura ya Mungu ndani ya mwanadamu. Ilikuwa ni kuirejesha ya kwamba mpango wa wokovu ulibuniwa, na maisha ya rehema alipewa mwanadamu. Kumrejesha katika ukamilifu ambao aliumbwa kwa huo kwanza, ndilo lengo la maisha, — lengo ambalo ni msingi wa mengine. Ni kazi ya wazazi na waalimu, katika elimu ya vijana kushirikiana na kusudi la Mungu; na kwa kufanya hivyo wao ni ‘watendakazi pamoja na Mungu.’ {LDSDA: 41.1}

* * *

“‘Kumcha Bwana ni chanzo cha hekima, na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.’ Kazi kuu ya maisha ni kujenga tabia, na maarifa ya Mungu ndio msingi wa elimu yote ya kweli. Kufundisha elimu hii, na kufinyanga tabia kulingana nayo, linapaswa kuwa lengo la kazi ya mwalimu.

41

Sheria ya Mungu ni uakisi wa tabia Yake. Hivyo mtunga-zaburi husema, ‘Amri Zako zote ni utakatifu;’ na ‘katika maagizo Yako napata ufahamu.’” — Mababu na Manabii, uk. 595, 596. {LDSDA: 41.2}

Mafunzo ya Mapema ya Vijana

“Katika sheria zilizokabidhiwa Israeli, maagizo ya wazi yalipeanwa mintarafu elimu. Kwa Musa hapo Sinai Mungu alikuwa amejionyesha Mwenyewe kama mwingi wa huruma na mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli.’ Hizi kanuni, zilizo katika sheria Yake, kina baba na mama huko Israeli walipaswa kuwafunza watoto wao. Musa kwa mwongozo wa Mungu aliwaambia: ‘Maneno haya, Ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako, nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo na uondokapo.’” — Elimu, uk. 40. {LDSDA: 42.1}

“Bwana Mwenyewe alielekeza elimu ya Israeli. Utunzi Wake haukuzuiliwa tu kwa maslahi yao ya kidini; chochote kilichoathiri akili zao au afya ya mwili pia ilikuwa mada ya majaliwa ya Mungu, na yalikuja katika nyanja ya sheria ya Mungu. {LDSDA: 42.2}

“Mungu alikuwa amewaamuru Waebrania kuwafunza watoto wao matakwa Yake, na kuwafanya wafahamiane na shughuli Zake zote

42

na baba zao. Hili lilikuwa mojawapo ya majukumu maalum ya kila mzazi, — ambayo hayangekabidhiwa mwingine. Badala ya midomo ya wageni, mioyo ya upendo ya baba na mama ilipaswa kutoa maagizo kwa watoto wao. Mawazo ya Mungu yalipaswa kuhusishwa na matukio yote ya maisha ya kila siku. Kazi kuu za Mungu katika ukombozi wa watu Wake, na ahadi za Mkombozi atakayekuja, zilipaswa kusimuliwa mara nyingi katika maskani za Israeli; na utumiaji wa mifano na nembo zilisababisha masomo yaliyotolewa kukazwa kabisa katika kumbukumbu. Kweli kuu za majaliwa ya Mungu na maisha ya baadaye yalipigwa chapa kwa akili changa. Ilifunzwa kumwona Mungu vile vile katika picha za maumbile na maneno ya ufunuo. Nyota za mbinguni, miti na maua ya kondeni, milima mirefu, vijito vya vimawimbi, — yote yalinena kumhusu Muumba. Huduma takatifu ya kutoa dhabihu na ibada hekaluni, na maneno ya manabii, ulikuwa ufunuo wa Mungu. {LDSDA: 42.3}

“Kama hayo yalikuwa mafunzo ya Musa katika nyumba ndogo ya kibanda huko Goshen; ya Samweli, kupitia Hana mwaminifu; ya Daudi, katika makao kilimani Betheli; na Danieli, kabla ya matukio ya utekwa kumtenganisha na nyumba ya baba zake. Kama hayo yalikuwa pia maisha ya Kristo huko Nazareti, mafunzo kama hayo ambayo mtoto Timotheo alijifunza kutoka kwa midomo ya

43

‘bibi yake Loisi, na mama yake Yunike,’ kweli za Maandiko Matakatifu. {LDSDA: 43.1}

Shule za Manabii

“Uandalizi zaidi ulifanywa kwa mafunzo ya vijana, kupitia kuanzishwa kwa shule za manabii. Iwapo kijana alitaka kuchunguza kwa kina ndani ya ukweli wa Neno la Mungu, na kutafuta hekima kutoka juu, ili aweze kuwa mwalimu katika Israeli, shule hizi zilikuwa wazi kwake. Shule za manabii zilianzishwa na Samweli, kutumika kama kizuizi dhidi ya ufisadi ulioenea, kutoa maslahi ya maadili na kiroho ya vijana, na kukuza ustawi wa siku zijazo wa taifa kwa kulipatia watu waliohitimu kutenda kwa kumcha Mungu kama viongozi na washauri. Katika kutimizwa kwa lengo hili, Samweli alikusanya vikundi vya vijana wa kiume ambao walikuwa wenye kicho, werevu na waelekevu. Hao waliitwa wana wa manabii. Walipokuwa wakiwasiliana na Mungu, na kusoma Neno Lake na kazi Zake, hekima kutoka juu iliongezwa kwa vipaji vyao vya asili. Walimu hawakuwa watu walio na ujuzi wa ukweli wa Mungu tu, ila ambao wenyewe walikuwa wamefurahia ushirika na Mungu, na walikuwa wamejaliwa uwezo maalum wa Roho Wake. Walifurahia heshima na imani ya watu wote kwa kujifunza na kwa uchaji. {LDSDA: 44.1}

“Katika siku ya Samweli zilikuwapo tu shule mbili za namna hii, moja huko Rama, nyumbani kwa

44

nabii, na nyingine huko Kirjayearim, pale ambapo sanduku lilikuwa wakati huo. Zingine zilianzishwa katika nyakati za baadaye. {LDSDA: 44.2}

* * *

“Mada kuu za kusoma katika shule hizi zilikuwa sheria ya Mungu, na maagizo aliyopewa Musa, historia takatifu, muziki mtakatifu, na ushairi. Njia ya mafundisho ilikuwa tofauti sana na ile katika shule za kitheolojia za siku ya leo, ambazo kutoka kwazo wanafunzi wengi huhitimu na maarifa duni ya Mungu na ukweli wa kidini kuliko wakati walipoingia. Katika hizo shule za zamani lilikuwa lengo kuu la masomo yote kujifunza mapenzi ya Mungu, na jukumu la mwanadamu Kwake. Katika kumbukumbu za historia takatifu zilitafutwa nyayo za Yehova. Kweli kuu zilizowekwa na mifano zililetwa kwa mtazamo, na imani ilichukua lengo kuu la huo mfumo wote, — Mwana-Kondoo wa Mungu ambaye angeiondoa dhambi ya ulimwengu. {LDSDA: 45.1}

“Roho ya ibada ilikuzwa. Sio tu wanafunzi walifundishwa wajibu wa maombi, bali walifundishwa jinsi ya kuomba, namna ya kumkaribia Muumba wao, jinsi ya kutekeleza imani ndani Yake, na jinsi ya kuelewa na kutii mafundisho ya Roho Wake. Akili zilizotakaswa huleta kutoka kwa hazina ya Mungu, mambo mapya na ya zamani, na Roho wa Mungu alidhihirishwa katika unabii na wimbo mtakatifu. {LDSDA: 45.2}

* * *

“Wanafunzi wa shule hizi walijikimu

45

wenyewe kwa kazi zao kwa kulima ardhi au katika kazi fulani ya kiufundi. Katika Israeli hili halikufikiriwa kuwa la kushangaza au la kudunisha; hakika, ilizingatiwa kuwa ni uhalifu kuruhusu watoto kukua pasipo kujua kazi muhimu. Kwa amri ya Mungu, kila mtoto alifunzwa taaluma fulani, hata ingawa alipaswa kufundishwa kwa ajili ya ofisi takatifu. Walimu wengi wa dini walijiruzuku kwa kazi za mikono. Hata hivi karibuni kama wakati wa mitume, Paulo na Akwila waliheshimiwa sana kwa sababu walipata riziki kwa taaluma yao ya kutengeneza mahema.” — Mababu na Manabii, uk. 592-594. {LDSDA: 45.3}

* * *

“Mafunzo ya kimwili na ya kiroho yaliyotekelezwa katika shule ya Waebrania yanaweza kusomwa kwa faida. Thamani ya mafunzo kama haya haithaminiwi. Upo uhusiano wa karibu kati ya akili na mwili, na ili kufikia kiwango cha juu cha uwezo wa maadili na akili, sheria ambazo hudhibiti uhai wa mwanadamu lazima zizingatiwe. Ili kuhifadhi tabia imara, yenye usawa, nguvu za akili na za mwili lazima zishughulishwe na kustawishwa. Je, ni somo gani linaweza kuwa muhimu zaidi kwa vijana kuliko lile ambalo hushughulikia kiumbe-hai hiki cha ajabu ambacho Mungu ametukabidhi, na sheria ambazo chaweza kuhifadhiwa kiafya? {LDSDA: 46.1}

46

“Na sasa, kama ilivyokuwa katika siku za Israeli, kila kijana anapaswa kuelimishwa katika majukumu ya utendaji katika maisha. Kila mmoja anapaswa kupata ujuzi wa nyanja fulani ya kazi za mikono, ambazo ikiwa zitahitajika, anaweza kujipatia riziki. Hii ni muhimu, sio tu kama ulinzi dhidi ya mabadiliko ya maisha, lakini kutokana na maana yake kwa ukuaji wa mwili, akili, na maadili. Hata ikiwa ilikuwa ni hakika kwamba mtu hangehitaji kamwe kufanya kazi za mikono kujikimu, bado anapaswa kufundishwa kufanya kazi. Bila mazoezi ya mwili, hakuna mtu anayeweza kuwa na mwili mzuri na afya njema; na nidhamu ya kazi iliyotekelezwa vyema ni muhimu sana kwa kuhifadhi akili timamu na timamu na tabia njema. {LDSDA: 47.1}

“Kila mwanafunzi anapaswa kutoa sehemu ya kila siku kwa kufanya kazi amilifu. Hivyo tabia za bidii zingeundwa, na roho ya kujitegemea kuhimizwa, ilhali vijana watalindwa dhidi ya mazoea mengi maovu na mapotovu ambayo mara nyingi huwa ni matokeo ya kutofanya kazi. Na haya yote ni katika kutunza lengo la msingi la elimu; maana katika kuhimiza shughuli, bidii, na usafi, tunakuja kwa upatano na Muumba.” — Mababu na Manabii, uk. 601. {LDSDA: 47.2}

“Kufanya kazi kwa udongo ni moja wapo ya aina bora za ajira, kuita misuli kutenda kazi na kupumzisha akili. Kujifunza katika safu za kilimo kunapaswa kuwa Aa, Ba, na Cha ya elimu inayotolewa katika shule zetu. Hii ndio kazi ya kwanza kabisa ambayo

47

inapaswa kuanzia. Shule zetu hazipaswi kutegemea mazao yaliyaoagizwa kutoka nje, nafaka na mboga, na matunda ambayo ni muhimu sana kwa afya. Vijana wetu wanahitaji elimu katika kukata miti na kulima ardhi na vile vile katika safu za kusoma. Walimu tofauti wanapaswa kuteuliwa kusimamia idadi ya wanafunzi katika kazi zao, na wanapaswa kufanya kazi nao. Hivyo waalimu wenyewe watajifunza kubeba majukumu kama wabeba mzigo. Wanafunzi wanaofaa pia kwa njia hii wanapaswa kuelimishwa kubeba majukumu, na kuwa wafanyakazi pamoja na walimu. Wote wanapaswa kushauriana pamoja kuhusu njia bora zaidi za kuendeleza kazi. {LDSDA: 47.3}

* * *

“Zoezi ambalo hufundisha mkono kuwa wa faida, na kuwafunza watoto kubeba mgawo wao wa mizigo ya maisha, hupeana nguvu ya mwili, na hustawisha kila kiungo. Wote wanapaswa kupata kitu cha kufanya ambacho kitakuwa na faida kwao wenyewe na kuwafaidisha wengine. Mungu aliteua kazi kama baraka, na ni mfanyakazi mwenye bidii tu ndiye hupata utukufu na furaha yakweli ya maisha. {LDSDA: 48.1}

“Ubongo na misuli lazima zikazwe kwa kulinganishwa, iwapo afya na nguvu zitadumishwa. Vijana wanaweza wakati huo kuleta kwa uchunguzi wa Neno la Mungu ufahamu wenye afya na neva zilizosawazishwa vyema. Watakuwa na mawazo safi, na wanaweza kuhifadhi mambo ya thamani ambayo yametolewa kwa Neno. Watazimeng’enya kweli zake,

48

na kama tokeo watakuwa na nguvu ya ubongo kutambua ukweli ni nini. Kisha, kadiri tukio linavyotaka, wao, wanaweza kumjibu kila mtu ambaye anauliza sababu ya tumaini lililo ndani yao kwa unyenyekevu na kutetemeka.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 179, 180. {LDSDA: 48.2}

Bibilia na Maumbile kama Vitabu vya Mafundisho

“Kama nguvu ya kuelimisha, Bibilia haina mpinzani. Katika Neno la Mungu akili hupata mada ya wazo la kina kabisa, matarajio ya upeo zaidi. Bibilia ndio historia inayofundisha zaidi ambayo wanadamu humiliki. Ilikuja ikiwa mpya kutoka kwa chemchemi ya ukweli wa milele, na mkono wa Mungu umeuhifadhi usafi wake katika vizazi vyote. Huangaza mbali sana zamani za kale, ambako utafiti wa wanadamu hutafuta bila kuweza kupenya. Katika Neno la Mungu tunaona nguvu iliyoiweka msingi wa dunia na ambayo iliitandaza mbingu. Hapa ndipo tu tunaweza kupata historia ya jamii yetu ya wanadamu bila kutiwa doa na chuki ya mwanadamu au kiburi chake. Hapa yameandikwa mapambano, kushindwa, na ushindi wa watu wakuu ulimwengu huu haujawahi kamwe kujua. Hapa shida kubwa za wajibu na hatma zimefunuliwa. Pazia linalotenganisha ulimwengu unaoonekana kutoka kwa ule usioonekana limeinuliwa, na tunaona vita vya majeshi kinzani ya wema na uovu, tangu mwanzo wa kuingia kwa dhambi, hadi kwa ushindi wa mwisho wa haki na ukweli, na yote ni ufunuo wa tabia ya Mungu. Katika tafakari ya kicho kwa kweli zilizowasilishwa katika Neno Lake, akili

49

ya mwanafunzi huletwa katika ushirika na akili ya milele. Uchambuzi kama huo hautasafisha tu na kuifanya tabia kuwa adilifu, lakini hauwezi kushindwa kupanua na kusisimua nguvu za akili. {LDSDA: 49.1}

“Mafundisho ya Biblia huchukua umuhimu mkubwa kwa ufanisi wa mwanadamu katika mahusiano yote ya maisha haya. Hufunua kanuni ambazo ni jiwe lapembeni la ustawi wa taifa, — kanuni ambazo ndani yake umefungashwa mustakabali wa jumuiya, na ambazo ni ulinzi wa familia, — pasi na kanuni hizo hakuna mwanadamu anayeweza kupata manufaa, furaha, na heshima katika maisha haya, au kuweza kutumaini kupata maisha ya baadaye, ya kutokufa. Hakuna nafasi katika maisha, hakuna awamu ya uzoefu wa mwanadamu , ambayo mafundisho ya Biblia si maandalizi muhimu. Kujifunza na kutii, Neno la Mungu litaweza kuupatia ulimwengu watu wenye akili amilifu na thabiti zaidi kuliko utumizi wa karibu zaidi wa masomo yote ambayo falsafa ya binadamu hukumbatia. Itaweza kuwapatia watu nguvu na uthabiti wa tabia, wa ufahamu mzuri na uamuzi timamu, — watu ambao watakuwa wa heshima kwa Mungu na baraka kwa dunia. {LDSDA: 50.1}

“Katika kusoma sayansi pia, tunapaswa kupata maarifa kumhusu Muumba. Sayansi yote ya kweli ni ufasiri wa maandishi ya Mungu katika ulimwengu wa maumbile. Sayansi huleta kutoka kwa utafiti wake ushahidi mpya tu wa hekima na nguvu ya Mungu. Vikieleweka vyema, vyote

50

kitabu cha maumbile na neno lililoandikwa hutufanya tumjue Mungu kwa kutufundisha jambo la sheria za hekima na ukarimu ambao Yeye hufanyia kazi. {LDSDA: 50.2}

“Mwanafunzi anapaswa kuongozwa ili amwone Mungu katika kazi zote za uumbaji. Walimu wanapaswa kuiga mfano wa Mwalimu Mkuu, ambaye kutokana na picha za maumbile alivuta mifano iliyorahisisha mafundisho Yake, na kuipiga chapa akilini mwa wasikilizaji Wake. Ndege wakiimba kwenye matawi yenye majani mengi, maua ya bondeni, miti mirefu sana, ardhi zenye mazao, nafaka inayomea, ardhi gumba, jua linalotua likiangazia mbingu mishale yake ya dhahabu, — yote ilitumika kama njia ya mafundisho. Yeye aliunganisha kazi zinazoonekana za Muumba na maneno ya uzima Aliyosema, kwamba kila wakati vitu hivi vitakapowasilishwa kwa macho ya wasikilizaji Wake, mawazo yao yaweze kurejea kwa masomo ya ukweli Aliyounganisha navyo.” — Mababu na Manabii, uk. 596, 599. {LDSDA: 51.1}

“Bwana hutarajia walimu wetu kuondoa katika shule zetu vitabu ambavyo hufundisha hisia ambazo hazipatani na Neno Lake, na kuvipataia nafasi vitabu ambavyo ni vya thamani kubwa zaidi.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 517. {LDSDA: 51.2}

WASIFU NA MAJUKUMU YA WALIMU

“Katika kuchagua walimu tunapaswa kutumia kila tahadhari, tukijua kwamba hili ni

51

suala la zito kama kuchagua watu kwa ukasisi. Watu wenye hekima ambao wanaweza kutambua tabia wanapaswa kufanya huo uteuzi; kwa kipaji bora kabisa inayoweza kupatikana inahitajika kuelimisha na kufinyanga akili za vijana, na kutekeleza kwa mafanikio safu nyingi za kazi ambayo itahitajika kufanywa na mwalimu katika shule zetu za kanisa. Hakuna mtu wa akili duni au finyu anayepaswa kuwekwa kwa usimamizi wa mojawapo wa shule hizi. Usiweke juu ya watoto wadogo na wasio na ujuzi walimu ambao hawana uwezo wa kusimamia; kwa maana juhudi zao zitaelekea kwa mvurugo. Mpangilio ni sheria ya kwanza ya mbinguni, na kila shule inapaswa katika hili kuwa mfano wa mbinguni.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 200, 201. {LDSDA: 51.3}

“Kipaji bora cha uchungaji kinapaswa kuajiriwa kufundisha Biblia katika shule zetu. Wale waliochaguliwa kwa kazi hii wanahitajika kuwa wanafunzi kamili wa Biblia, na kuwa na uzoefu mkubwa wa Ukristo; na mshahara wao unapaswa kulipwa kutoka kwa zaka.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 134, 135. {LDSDA: 52.1}

“Kabla mtu hajajitayarisha kuwa mwalimu wa ukweli kwa wale walio gizani, lazima awe mwanafunzi. Lazima awe tayari kushauriwa. Hawezi kuweka mguu wake kwenye mzunguko wa tatu, wa nne au wa tano wa ngazi ya maendeleo kabla hajaanzia kwa mzunguko wa kwanza. Wengi hujihisi kwamba wanafaa kwa kazi hiyo wakati hawajui chochote kuihusu.

52

Iwapo kama hao wataruhusiwa kuanza kufanya kazi kwa kujiamini, watashindwa kupokea maarifa ambayo ni fursa yao kupata, na watashindwa kupambana na shida nyingi ambazo hawajajiandaa kabisa.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 107. {LDSDA: 52.2}

“Tabia na kanuni za mwalimu zinapaswa kuzingatiwa kuwa za umuhimu zaidi kuliko sifa zake za usomi. Ikiwa ni Mkristo mwaminifu, atahisi umuhimu wa kupendezwa vilevile na elimu ya kimwili, kiakili, kimadili, na ya kiroho ya wanafunzi wake. Ili kudhihirisha mvuto mzuri, anapaswa kujidhibiti kikamilifu, na moyo wake mwenyewe unapaswa kujazwa sana na upendo kwa wanafunzi wake, ambao utaonekana katika uso, maneno na vitendo vyake. Anapaswa kuwa na uthabiti wa tabia na kisha anaweza kufinyanga akili za wanafunzi wake, na pia kuwafundisha katika masomo ya sayansi. Elimu ya mapema ya vijana kwa ujumla hujenga tabia zao za maisha. Wale ambao hushughulika na vijana wanapaswa kuwa waangalifu kutaja sifa za akili, ili waweze kujua jinsi ya kuelekeza vyema nguvu zake ili ziweze kutumiwa kwa rekodi bora kabisa.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 19. {LDSDA: 53.1}

“Mtu anaweza kuwa na elimu na maarifa ya kutosha katika kufunza sayansi; lakini imegundulika kwamba ana busara na hekima ya kushughulika na akili za wanadamu? Iwapo walimu hawana upendo

53

wa Kristo moyoni, hawafai kuletwa kwa uhusiano na watoto, na kubeba majukumu mazito yaliyowekwa juu yao, ya kuwaelimisha watoto na vijana hawa. Wanakosa elimu ya juu na mafunzo ndani yao, na hawajui jinsi ya kushughulika na akili za wanadamu. Ipo roho ya ukaidi wao, mioyo ya asili ambayo inajitahidi kudhibiti, na kuzitiisha akili za plastiki na tabia za watoto kwa nidhamu kama hiyo, ni kuacha makovu na michubuko kwenye akili ambayo haitaweza kufutwa kamwe.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 260, 261. {LDSDA: 53.2}

“Kuweka juu ya watoto wadogo walimu wenye majivuno na wasio na upendo ni uovu. Mwalimu wa chapa hii atafanya madhara makubwa kwa wale ambao wanaendelea kukuza tabia kwa haraka. Iwapo walimu si watiifu kwa Mungu, ikiwa hawana upendo kwa watoto ambao wanasimamia, au iwapo wanaonyesha upendeleo kwa wale wanaoyapendeza matamanio yao, na kuonyesha kutowajali wale ambao hawavutii, au kwa wale ambao hawana utulivu na waoga, hawapaswi kuajiriwa; kwa sababu tokeo la kazi yao itakuwa hasara ya nafsi za Kristo. {LDSDA: 54.1}

“Walimu wanahitajika, haswa kwa aajili ya watoto, ambao ni watulivu na wapole, wanaodhihirisha uvumilivu na upendo kwa wale haswa wanauohitaji sana. Yesu aliwapenda watoto; Yeye aliwatambua kama washiriki wachanga wa familia ya Bwana. Yeye siku zote aliwatendea kwa upole na heshima, na walimu

54

wanapaswa kufuata mfano Wake. Wanapaswa kuwa na roho ya kweli ya umishonari; kwa maana watoto wanapaswa kufunzwa kuwa wamishonari. Wanapaswa kuhisi kwamba Bwana amewakabidhi kama amana takatifu nafsi za watoto na vijana. Shule zetu za kanisa zinahitaji walimu ambao wanazo sifa za maadili ya hali ya juu; wale ambao wanaweza kuaminiwa, wale walio imara katika imani, na wa busara na uvumilivu; wale ambao hutembea na Mungu, na hujitenga na uovu wa kila namna. Katika kazi yao watapata mawingu. Yatakuwapo mawingu na giza, tufani na dhoruba, chuki bila sababu ya kukutana nayo kutoka kwa wazazi walio na dhana zisizo sahihi za tabia ambazo watoto wao wanapaswa kujenga; kwa sababu wapo wengi wanaodai kuamini Biblia, ilhali hushindwa kuleta kanuni zake katika maisha ya nyumbani. Lakini ikiwa walimu ni wanafunzi wa daima katika shule ya Kristo, hali hizi kamwe hazitawashinda.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 200, 201. {LDSDA: 54.2}

“Majukumu ya mwalimu ni mazito na matakatifu, lakini hakuna sehemu ya kazi iliyo muhimu zaidi kuliko kumtunza kijana kwa upole, na upendo wa kubembeleza, ili waweze kuhisi kwamba tunaye rafiki ndani yao. Mara tu ukipata imani yao, na unaweza kuwaongoza, kuwadhibiti, na kuwafunza kwa urahisi. Nia takatifu za kanuni zetu za Ukristo lazima ziletwe maishani mwetu. Wokovu wa wanafunzi wetu ni maslahi ya upeo yaliyokabidhiwa kwa mwalimu anayemcha Mungu.

55

Yeye ni mfanyakazi wa Kristo, na bidii yake maalum na yenye azimio inapaswa kuwa ya kuziokoa nafsi kutoka kwa uharibifu na kuziongoa kwa Yesu Kristo. Mungu atahitaji hili mikononi mwa walimu. Kila mmoja anapaswa kuishi maisha ya uchaji, usafi, juhudi za kuvumilia machungu katika utekelezaji wa kila jukumu. Iwapo moyo unang’aa na upendo wa Mungu, yatakuwapo mapenzi safi, ambayo ni muhimu; sala zitakuwa za bidii, na maonyo ya uaminifu yatatolewa. Puuza haya, na nafsi zilizo chini ya usimamizi wako zitakuwa hatarini. Afadhali tumia muda mchache katika hotuba ndefu, au katika masomo ya kushughulisha sana, na uyahudumie majukumu haya yaliyopuuzwa.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 116, 117. {LDSDA: 55.1}

“Mungu hutaka walimu katika shule zetu wawe wa kufaa. Ikiwa wamestawi katika uelewa wa kiroho, watahisi ni muhimu kwamba wasiwe na upungufu katika maarifa ya sayansi. Kicho na uzoefu wa kidini upo haswa kwenye msingi wa elimu ya kweli. Lakini mtu asijihisi kwamba kuwa na bidii katika masuala ya dini ni yote yaliyo muhimu sana ili kuwa walimu. Wakati hawahitaji uchaji ulio mpungufu, wanahitaji pia maarifa kamili ya sayansi. Haya yatawafanya sio tu Wakristo wazuri, watendaji, bali yatawawezesha kuwaelimisha vijana, na kwa wakati uo huo watakuwa na hekima ya mbinguni kuwaongoza kwenye chemchemi ya maji yaliyo hai. Yeye ni Mkristo ambaye hulenga kupata kufikia upeo zaidi

56

kwa madhumuni ya kuwafanyia wengine mema. Maarifa kwa upatano yakichanganywa na tabia kama ya Kristo yatamfanya mtu kuwa hakika nuru ya ulimwengu.” — Msingi wa Elimu ya Mkristo, uk. 119. {LDSDA: 56.1}

“Wote ambao hufundisha katika shule zetu wanapaswa kuwa na muunganisho wa karibu na Mungu, na ufahamu kamili wa Neno Lake, ili waweze kuleta hekima na maarifa matakatifu katika kazi ya kuwaelimisha vijana kwa manufaa katika maisha haya, na maisha ya baadaye, ya milele. Wapaswa kuwa wanaume na wanawake ambao si walio tu na maarifa ya ukweli, ila ambao ni watendaji wa neno la Mungu. ‘Imeandikwa’ linapaswa kuonyeshwa katika maneno na maisha yao. Kwa mazoea yao wenyewe wanapaswa kufundisha unyenyekevu na tabia sahihi katika kila kitu. Hakuna mwanamme au mwanamke anayepaswa kuunganishwa na shule zetu kama mwalimu, ambaye hajakuwa na uzoefu wa kutii neno la Bwana.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 153. {LDSDA: 57.1}

“Walimu katika shule zetu wanalo jukumu zito la kubeba. Lazima wawe kwa maneno na tabia wanachotaka wanafunzi wao wawe, — wanaume na wanawake wanaomcha Mungu na kutenda haki. Iwapo wanaijua njia wenyewe, wanaweza kuwafundisha vijana kutembea ndani yake. Hawatawaelimisha tu katika sayansi lakini watawafunza kuwa na uhuru wa maadili, kumfanyia Yesu kazi, na kubeba mizigo katika kazi Yake.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 190. {LDSDA: 57.2}

57

“Wale ambao kiasili ni wasumbufu, wanaokasirika kwa urahisi, na ambao wamekuza tabia ya upekuzi, ya kufikiri uovu, wanapaswa kutafuta kazi nyingine ambayo haitazalisha yoyote kati ya tabia zao zisizo za upendo kwa watoto na vijana, kwani zimegharimu sana. Mbingu huona ndani ya mtoto, mwanamme au mwanamke ambaye hajakua, na uwezo na nguvu ambazo, ikiwa zitaongozwa vyema na kukuzwa na hekima ya mbinguni, watakuwa vyombo vya wanadamu ambavyo kupitia kwavyo mivuto mitakatifu inaweza kushirikiana kuwa watendakazi pamoja na Mungu. Maneno makali, na shutuma siku zote humkanganya mtoto, lakini hazimgeuzi. Zuia neno hilo la kuudhi: dumisha roho yako mwenyewe chini ya nidhamu kwa Yesu Kristo, ndipo utajifunza jinsi ya kuwasikitia na kuwahurumia wale walioletwa chini ya mvuto wako. Usionyeshe kukosa subira na ukali, kwa maana iwapo watoto hawa hawakuhitaji kuelimishwa, hawangehitaji manufaa ya shule. Wanahitaji kwa subira, huruma, na kwa upendo kuletwa juu kwa ngazi ya maendeleo, wakipanda hatua kwa hatua katika kupata maarifa.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 263. {LDSDA: 58.1}

“Ipo haja ya kuwa na walimu wangalifu, wanaojali unyonge na udhaifu wao wenyewe na dhambi, na ambao hawatawakandamiza na kuwavunja moyo watoto na vijana. Yanahitajika kuwapo maombi zaidi, imani zaidi, uvumilivu mwingi na ujasiri, ambao Bwana yu tayari kutoa. Kwa maana Mungu huona kila jaribu, na

58

mvuto wa ajabu unaweza kukazwa na walimu, ikiwa watatekeleza mafunzo ambayo Kristo amewapa. Lakini je, walimu hawa watajali mwenendo wao wenyewe wa upotovu, hivi kwamba hufanya juhudi dhaifu sana za kusoma katika shule za Kristo na kutenda kwa upole na unyenyekevu wa moyo kama ule wa Kristo? Walimu wanapaswa kuwa wenyewe katika utiifu kwa Yesu Kristo, na daima wakitenda maneno Yake, ili waweze kuwa mfano katika tabia ya Yesu Kristo kwa wanafunzi. Nuru yenu iangaze katika matendo mema, kuchunga na kutunza kwa uaminifu wana-kondoo wa kundi, kwa subira, kwa wororo, na upendo wa Yesu mioyoni mwenu.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk 269. {LDSDA : 58.2}

“Acha kila mwalimu anayelipokea jukumu la kuwaelimisha watoto na vijana, ajihoji mwenyewe, na asome kwa umakini chanzo na tokeo. Je ukweli wa Mungu unamiliki nafsi yangu? Je, hekima itokayo kwa Yesu Kristo, ambayo kwanza ni ‘safi, ya amani, ya upole, na tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina na bila unafiki’ imeletwa katika tabia yangu? Ninasipomama katika nafasi ya uwajibikaji ya mwalimu, je, ninathamini ile kanuni kwamba ‘tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale wafanyao amani?’ Ukweli haupaswi kuwekwa na kutekelezwa wakati tunajihisi hivyo tu, bali wakati wote na katika maeneo yote. {LDSDA: 59.1}

59

“Akili zenye usawa na tabia za ulinganifu zinahitajika kama walimu katika kila safu. Usipeane kazi hii mikononi mwa wanawake na wanaume vijana ambao hawajui jinsi ya kushughulika na akili za binadamu.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 266. {LDSDA: 59.2}

“Hakuna mwalimu anayeweza kufanya kazi inayokubalika ambaye hakumbuki mapungufu yake mwenyewe na ambaye haondoi katika fikara zake mipango yote ambayo itadhoofisha maisha yake ya kiroho. Walimu wanapokuwa tayari kuondoa katika kazi yao kila kitu kisicho muhimu kwa uzima wa milele, basi wanaweza kunenewa hakika kwamba wanafanya kazi ya wokovu wao kwa hofu na kutetemeka, na ya kwamba wanajenga kwa hekima kwa ajili ya umilele. {LDSDA: 60.1}

“Nimeagizwa kusema kwamba baadhi ya walimu wetu wako nyuma sana katika ufahamu wa aina ya elimu inayohitajika kwa kipindi hiki cha historia ya dunia. Huu sio wakati wa wanafunzi kukusanya rundo kubwa la maarifa ambalo hawawezi kuchukuana nayo hadi kwa shule ya juu. Hebu kwa uangalifu tungoe kwa mwendo wetu wa kujifunza yote ambayo yanaweza kusazwa, ili tuwe na nafasi katika akili za wanafunzi ambayo tutapanda mbegu za haki. Agizo hili litazaa matunda ya uzima wa milele. {LDSDA: 60.2}

“Kila mwalimu anapaswa kuwa mwanafunzi kila siku katika shule ya Kristo, asije akapoteza hisia ya inayofanyiza ubora wa kweli wa mwili, akili na maadili. Hakuna mtu anayepaswa kujiweka mwenyewe kama mwalimu wa wengine

60

ambaye daima hafanyi kazi ya wokovu wake kwa kupokea na kutoa elimu ya pande zote. Mwalimu wa kweli atajielimisha katika ubora wa maadili, kwamba kwa maneno na mfano anaweza kuziongoza nafsi kuelewa masomo ya Mwalimu Mkuu. Hakuna mtu anayepaswa kuhimizwa kufanya kazi ya kufunza ambaye ataridhika kwa kiwango cha chini. Hakuna mtu anayefaa kufundisha siri kuu za uungu mpaka Kristo ameumbwa ndani mwake, tumaini la utukufu. {LDSDA: 60.3}

“Kila mwalimu anahitaji kuupokea ukweli katika upendo wa kanuni zake takatifu; kisha hawezi kushindwa kuweka mvuto ambao unatakasa na kuinua. Mwalimu ambaye roho yake imejikita kwa Kristo atanena na kutenda kama Mkristo. Mtu kama huyo hataridhika mpaka ukweli uyatakase maisha yake kutoka kwa kila kitu kisichokuwa muhimu. Hutaridhika isipokuwa akili zake siku baada ya siku zifinyangwe na mivuto mitakatifu ya Roho wa Mungu. Kisha Kristo anaweza kunena na moyo, na sauti Yake, akisema, ‘Hii ndio njia; tembea ndani yake,’ itasikika na kutiiwa. {LDSDA: 61.1}

“Mwalimu aliye na ufahamu sahihi wa kazi ya elimu ya kweli, hatafikiri inatosha sasa na baadaye kufanya marejeleo ya kawaida kwa Kristo. Kwa moyo wake mwenyewe wenye joto kwa upendo wa Mungu, atamwinua daima Mtu wa Kalvari. Nafsi yake mwenyewe iliyojazwa Roho wa Mungu, atatafuta kukaza umakini wa

61

wanafunzi kwa mfano huo, Kristo Yesu, aliye mkuu kati ya elfu kumi, Ndiye anayependeza kabisa. {LDSDA: 61.2}

* * *

“Kumbuka kwamba Bwana atawakubali tu kama walimu wale ambao watakuwa walimu wa injili. Jukumu kubwa hutua kwa wale wanaojaribu kufundisha ujumbe wa mwisho wa injili. Wanapaswa kuwa watendakazi pamoja na Mungu kuzifunza akili za wanadamu. Mwalimu ambaye hushindwa kudumisha kiwango cha Biblia siku zote mbele yake, hukosa fursa ya kuwa mtendakazi pamoja na Mungu katika kuzipatia akili umbo ambalo ni muhimu kwa nafasi katika nyua za mbinguni.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 525, 526, 527. {LDSDA: 62.1}

“Anayesimama penye uongozi wa shule anapaswa kuweka masilahi yake yasiyo yumbayumba katika kazi ya kuifanya shule iwe jinsi Bwana alikusudia iweze kuwa. Iwapo anatamani kupanda juu na hata juu zaidi, ikiwa atakua juu ya fadhila halisi za kazi yake, na juu ya unyenyekevu wake, na kuzipuuza kanuni takatifu za mbinguni mruhusu ajifunze kutoka kwa uzoefu wa Musa kwamba hakika Bwana ataonyesha kutofurahishwa Kwake kwa sababu ya kushindwa kwake kufikia viwango vilivyowekwa mbele yake. {LDSDA: 62.2}

“Hasa rais wa shule aweze kuziangalia kwa uangalifu fedha za taasisi. Anapaswa kuelewa kanuni za msingi za uhasibu. Anapaswa kwa uaminifu kuripoti matumizi ya fedha zote

62

zinazopitia mkononi mwake kwa matumizi ya shule. Fedha za shule hazipaswi kutolewa kupita kiasi, lakini kila juhudi inapaswa kufanywa ili kuongeza manufaa ya shule. Wale ambao wamekabidhiwa na usimamizi wa kifedha wa taasisi zetu za elimu, lazima wasiruhusu uzembe wowote katika matumizi ya raslimali hiyo. Kila kitu ambacho kimeunganishwa na fedha za shule zetu kinapaswa kuwa kinyoofu kikamilifu. Njia ya Bwana lazima ifuatwe kabisa, ingawa hii inaweza kuwa haipatani na njia za mwanadamu. {LDSDA: 62.3}

“Kwa wale wanaosimamia shule zetu ningesema, Je! mnamfanya Mungu na sheria Yake furaha yenu? Je! kanuni ambazo mnafuata, ni zisizo na kasoro na safi na zisizo na unajisi? Je! mnajitunza, katika mazoea ya maisha, chini ya udhibiti wa Mungu? Je! mnaona umuhimu wa kumtii Yeye katika kila jambo? Ikiwa umejaribiwa kugawa pesa zinazoingia shuleni, kwa njia ambazo hazileti manufaa maalum kwa shule, kiwango chako cha kanuni chahitaji kukosolewa kwa uangalifu, kwamba wakati hautakosa kuja utakapokosolewa na kupatikana umepungukiwa. Karani wako ni nani? Mhasibu wako ni nani? Meneja wako wa biashara ni nani? Je, wao ni makini na stadi? Chunguza hilo. Inawezekana pesa zitumike vibaya bila mtu yeyote kuelewa wazi jinsi ilivyotukia, na inawezekana shule iendelee kupoteza kila wakati kwa sababu ya matumizi yasiyo ya busara

63

wanaosimamia wanaweza kuhisi hasara hii sana, na labda wadhani wamefanya walivyoweza. Lakini mbona wanaruhusu deni kuongezeka? Hebu wale wanaosimamia shule wachunguze kila mwezi hali halisi ya kifedha ya shule.” — Misingi ya Imani ya Mkristo, uk. 510, 511. {LDSDA: 63.1}

“Mungu ametupatia muda wa rehema ambao tunaweza kujiandaa kwa shule ya juu. Kwa ajili ya shule hii vijana wanapaswa kuelimishwa, kuadibishwa, na kufunzwa ili kujenga tabia, kimaadili na kiakili, jinsi Mungu atakavyoidhinisha. Wanapaswa kupokea mafunzo, sio kwa mila na burudani na michezo ya jumuiya hii ya kidunia iliyochafuliwa, ila katika safu za Kristo, mafunzo ambayo yatawafanya wastahili kuwa watendakazi pamoja na wajumbe wa mbinguni. Lakini ni dhihaka ilioje kwamba elimu inayopatikana katika safu za vitabu, ikiwa ni lazima kuvuliwa kwa mwanafunzi akiwa amehesabiwa kustahili kuingia katika maisha ambayo hupimwa na maisha ya Mungu, yeye mwenyewe kuokolewa kama ni kwa moto.” — Misingi ya Elimu ya Mkristo, uk. 397. {LDSDA: 64.1}

“Sifa ya kazi inayofanywa katika shule zetu za kanisa inapaswa kuwa ya hali ya juu sana. Yesu Kristo, Mrejeshi, ndiye suluhisho la pekee kwa elimu mbaya, na masomo yanayofundishwa katika Neno Lake yanapaswa kuwekwa daima mbele ya vijana katika umbo la kuvutia zaidi. Nidhamu ya shule inapaswa kuongezea mafunzo ya nyumbani, kote nyumbani na shuleni unyenyekevu na uungu unapaswa kudumishwa. Wanaume na wanawake watapatikana ambao wana talanta za kufanya kazi katika shule hizi ndogo, lakini ni nani asieweza

64

kufanya kazi kunufaika katika zile kubwa. Wanapojizoesha masomo ya Bibilia, wao wenyewe watapata elimu ya thamani kubwa zaidi.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 200. {LDSDA: 64.2}

USHIRIKIANO WA WAZAZI

“Hebu wazazi wamtafute Bwana kwa bidii, ili wasiweze kuwa mawe ya kujikwaza katika njia ya watoto wao. Ruhusu chuki na wivu ziondolewe kutoka moyoni, na ruhusu amani ya Kristo iingie ndani ili kuwaunganisha washiriki wa kanisa katika ushirika wa kweli wa Ukristo. Ruhusu madirisha ya nafsi yafungwe dhidi ya malaria yenye sumu ya dunia, na yafunguliwe kuelekea mbinguni ili kupokea mionzi ya uponyaji ya jua la haki ya Kristo. Mpaka roho ya kulaumu na tuhuma iondolewe kutoka moyoni, Bwana hawezi kulifanyia kanisa lile ambalo Yeye hutamani kufanya katika kufungua njia ya kuzisimamisha shule; hadi uwepo umoja, Yeye atawaongoza wale ambao Aliwapatia njia na uwezo wa kuiendeleza kazi hii mbele. Wazazi lazima wafikie kiwango cha juu, wakiidumisha njia ya Bwana na kutenda haki, ili wapate kuwa wamulika nuru. Lazima yawepo mabadiliko kamili ya akili na tabia. Roho ya kutengana ikikuzwa mioyoni mwa wachache itajitangaza yenyewe kwa wengine, na kuumbua mvuto wa uzuri ambao ungekazwa na shule. Isipokuwa wazazi wako tayari na

65

shauku ya kushirikiana na mwalimu kwa wokovu wa watoto wao, hawajajiandaa kuwa na shule iliyosimamishwa kati yao.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 202. {LDSDA: 65.1}

“Juu ya kina baba na kina mama hutua jukumu la mafunzo kwa mtoto ya mapema na vile vile ya baadaye, na kwa wazazi wote wawili madai ya uangalifu na maandalizi kamili ni ya hima zaidi. Kabla ya kujichukulia uwezekano wa ubaba na umama, wanaume na wanawake wanapaswa kufahamiana na sheria za ustawi wa mwili, — na fiziolojia (viungo vya mwili) na usafi, na kubeba athari za ujauzito, na sheria za urithi, usafi, mavazi, mazoezi, na tiba za ugonjwa; wanapaswa pia kuelewa sheria za ustawi wa akili na mafunzo ya maadili. {LDSDA: 66.1}

“Kazi hii ya elimu Yule wa Milele ameihesabu kuwa ya umuhimu sana hivi kwamba wajumbe kutoka kwenye kiti Chake cha enzi wametumwa kwa mama mtarajiwa, ili kujibu swali, ‘Je! Tutamwamuru vipi mtoto, na tutamleaje?’ na kumwagiza baba mintarafu elimu ya mtoto aliyeahidiwa. {LDSDA: 66.2}

“Kamwe elimu haitatimiza yote ambayo inaweza na inapaswa kufanikisha hadi umuhimu wa kazi ya wazazi utambuliwe kikamilifu, na wapate mafunzo kwa majukumu yake matakatifu.” — Elimu, uk. 276. {LDSDA: 66.3}

66

WASIFU KWA MATABIBU

“Tabibu anayetamani kukubalika kuwa mtendakazi pamoja na Kristo atajitahidi kuwa bora katika kila sehemu ya kazi yake. Atasoma kwa bidii, ili aweze kufuzu vyema kwa majukumu ya taaluma yake, na atajitahidi daima kufikia kiwango cha juu, akitafuta maarifa yaliyoongezeka, ustadi mkubwa, na hekima ya kina. Kila tabibu anapaswa kung’amua kwamba yeye afanyaye kazi dhaifu, isiyofaa sio tu huwaumiza wagonjwa, lakini pia huwatendea isivyo haki matabibu wenzake. Tabibu ambaye ameridhika na kiwango cha chini cha ustadi na maarifa sio tu hudunisha taaluma ya utabibu, lakini humvunjia heshima Kristo, Tabibu mkuu. {LDSDA: 67.1}

“Wale ambao hupata kwamba hawafai kwa kazi ya utabibu wanapaswa kuchagua ajira nyingine. Wale ambao wamezoea vyema kuwatunza wagonjwa, lakini ambao sifa zao za elimu na utabibu ni finyu, watafanya vyema kuchukua sehemu za kazi za unyenyekevu, wakihudumu kwa uaminifu kama wauguzi. Katika huduma ya utulivu chini ya matabibu wenye ustadi, watakuwa wanasoma daima, na kuboresha kila fursa ya kupata maarifa, baada ya muda wanaweza kuwa wenye sifa kamili kwa kazi ya utabibu. Ruhusu matabibu wachanga, ‘kama watendakazi pamoja Naye [Tabibu mkuu]…wasiipokee neema ya Mungu bure,…bila kukosea

67

katika jambo lo lote, ili huduma [ya wagonjwa] isilaumiwe: lakini katika mambo yote tukijithibika wenyewe kuwa watumishi wa Mungu.’ {LDSDA: 67.2}

“Kusudi la Mungu kwetu ni kwamba daima tutaendelea kwenda juu zaidi. Tabibu wa umishonari wa utabibu wa kweli atakuwa mtaalam anayezidi kuwa mwenye ustadi. Matabibu Wakristo wenye vipaji, wakiwa na uwezo mkubwa wa kitaaluma, wanapaswa kutafutwa na kuhimizwa kuingia kwa utumishi wa Mungu katika sehemu ambazo wanaweza kuwaelimisha na kuwafunza wengine kuwa wamishonari wa utabibu. {LDSDA: 68.1}

“Tabibu anapaswa kujikusanyia nafsi yake nuru ya neno la Mungu. Anapaswa kuendelea kukua katika neema kila wakati. Pamoja naye, dini haipaswi kuwa tu mvuto mmoja tu kati ya mingine. Inapaswa kuwa mvuto unaotawala mingine yote. Anapaswa kutenda kutoka kwa nia za upeo, takatifu, — nia ambazo zina nguvu kwa sababu zinatoka kwa Yule aliyeutoa uhai Wake kutupatia nguvu ya kushinda uovu. {LDSDA: 68.2}

“Iwapo tabibu kwa uaminifu na kwa bidii ajitahidi kujifanza kuwa anayefaa katika taaluma yake, ikiwa hujitoa wakfu kwa utumishi wa Kristo, na kuchukua muda kuuchunguza moyo wake mwenyewe, ataelewa jinsi ya kunasa siri za mwito wake mtakatifu. Anaweza kujiadibisha na kujielimisha hivyo kwamba wote walio ndani ya tufe la mvuto wake wataona ubora wa elimu na hekima iliyopatikana na Yule ambaye ameunganishwa na Mungu wa hekima na uwezo. {LDSDA: 68.3}

68

“Msaidizi Mtakatifu katika Chumba cha Wagonjwa”

“Hakuna mahali ambapo upo ushirika unaohitajika wa karibu na Kristo kuliko katika kazi ya tabibu. Yeye anayeweza kutekeleza kazi za utabibu vyema lazima kila siku na kila saa aishi maisha ya Mkristo. Maisha ya mgonjwa yako mikononi mwa tabibu. Uchunguzi mmoja wa kiholela, pendekezo moja lenye makosa, katika hali mahututi, au msogeo mmoja usio stadi wa mkono katika upasuaji, hata ukiwa kwa upana wa unywele, na uhai unaweza kutolewa kafara, nafsi kurushwa katika umilele. Ni zito lililoje wazo! Ni umuhimu ulioje kwamba tabibu awe daima chini ya udhibiti wa Tabibu mtakatifu! {LDSDA: 69.1}

“Mwokozi yu tayari kuwasaidia wote wanaomwita Yeye kwa ajili ya hekima na usafi wa mawazo. Na ni nani anayehitaji hekima na usafi wa mawazo zaidi ya tabibu, ambaye maamuzi yake hutegemewa sana? Hebu yule anayejaribu kuongeza muda wa maisha amtazame Kristo kwa imani ile aelekeze kila msogeo wake. Mwokozi atampa busara na ustadi wa kushughulikia magonjwa magumu. {LDSDA: 69.2}

“Za ajabu ni fursa zinazopeanwa kwa walezi wa wagonjwa. Katika yote ambayo hufanywa kwa urejesho wa wagonjwa, hebu waelewe kwamba tabibu anatafuta kuwasaidia washirikiane na Mungu kupambana na ugonjwa. Waongoze kuhisi kwamba kwa kila hatua inayochukuliwa kwa kuwiana na

69

sheria za Mungu, wanaweza kutarajia msaada wa nguvu ya Mungu. {LDSDA: 69.3}

“Wagonjwa na wanaoathirika watakuwa na imani zaidi kwa tabibu ambaye wanaamini anampenda na kumcha Mungu. Wao hutegemea maneno yake. Wao huhisi hisia ya usalama katika uwepo na usimamizi wa tabibu huyo. {LDSDA: 70.1}

“Kumjua Bwana Yesu, ni majaliwa ya tabibu Mkristo kwa sala kualika uwepo Wake katika chumba cha mgonjwa. Kabla kuufanya upasuaji wenye hatari, hebu tabibu aombe msaada wa Tabibu mkuu. Amhakikishie yule anayeteseka kwamba Mungu anaweza kumleta salama kutoka ndani ya hiyo shida, kwamba katika nyakati zote za dhiki Yeye ni kimbilio la hakika kwa wanaomwamini Yeye. Tabibu ambaye hawezi kufanya hili hupoteza mgonjwa baada ya mgonjwa ambaye labda angeokolewa. Laiti angeweza kunena maneno ambayo yangemvuvia imani ndani ya Mwokozi mwenye huruma, ambaye huhisi kila mpigo wa uchungu, na angeweza kuyawasilisha mahitaji ya ile nafsi Kwake katika sala, hatari hiyo mara nyingi ingepitwa salama. {LDSDA: 70.2}

“Yeye tu anayeusoma moyo anayeweza kujua kulivyo kutetemeka na hofu ambayo wagonjwa wengi huidhinisha kufanyiwa upasuaji chini ya mkono wa tabibu wa upasuaji. Hutambua hatari yake. Ilhali wanaweza kuwa na imani katika ustadi wa tabibu, huwa wanajua kwamba unaweza kukosea. Lakini kadiri wanapomuona tabibu amesujudu katika sala, akiomba msaada kutoka kwa Mungu, wanavuviwa na imani.

70

Shukrani na tumaini hufungua moyo kwa nguvu ya uponyaji ya Mungu, nguvu za mwili wote zinapata uzima, na nguvu za maisha hupata ushindi. {LDSDA: 70.3}

“Kwa tabibu pia uwepo wa Mwokozi ni sehemu ya nguvu. Mara nyingi majukumu na uwezekano wa kazi yake huleta hofu kwa roho. Halijoto ya kutokuwa na uhakika na woga unaweza kuufanya mkono ukose ustadi. Lakini uhakikisho kwamba Mshauri mtakatifu yu kando yake, kumwelekeza na kutegemeza, humpa utulivu na ujasiri. Mguso kwa Kristo kwa mkono wa tabibu huleta nguvu, utulivu, imani, na nguvu. {LDSDA: 71.1}

“Wakati ile hatari imepitwa salama, na ufanisi unaonekana, wacha muda mchache utumike pamoja na mgonjwa katika sala. Toa usemi wa shukrani zako kwa maisha ambayo yamenusurika. Kadiri maneno ya shukrani yanapotiririka kutoka kwa mgonjwa hadi kwa tabibu, ruhusu sifa na shukrani zielekezwe kwa Mungu. Mwambie mgonjwa maisha yake yameokolewa kwa sababu alikuwa chini ya ulinzi wa Tabibu wa mbinguni. {LDSDA: 71.2}

“Tabibu anayeufuata mwenendo kama huu anamwongoza mgonjwa wake kwa Yule ambaye yeye humtegemea kwa uzima, Yeye anayeweza kuwaokoa wote wanaomjia. {LDSDA: 71.3}

“Huduma kwa Roho”

“Katika kazi ya umishonari wa utibabu inapaswa kuletwa na shauku kubwa

71

roho. Kwa tabibu sawa na mchungaji wa injili wamekabidhiwa amana kubwa kuliko yote iliowahi kupewa mwanadamu. Ikiwa huitambua au la, kila tabibu amepewa tiba ya mioyo. {LDSDA: 71.4}

“Katika kazi yao ya kushughulika na ugonjwa na kifo, matabibu mara nyingi hukosa kuona uhalisi mzito wa maisha ya baadaye. Katika juhudi zao za dhati za kuepusha hatari ya mwili, wao husahau hatari ya roho. Yule ambaye wanamuhudumia anaweza kuwa anapoteza uhai wake. Fursa zake za mwisho zinaponyoka kutoka kwa ufahamu wake. Nafsi hii tabibu lazima akutane nayo tena penye kiti cha hukumu cha Kristo. {LDSDA: 72.1}

“Mara nyingi tunakosa baraka za thamani zaidi kwa kupuuza kusema neno kwa msimu. Ikiwa fursa ya dhahabu haitazamiwi, itapotea. Kando ya kitanda cha wagonjwa hakuna neno la itikadi za kidini au ubishi linapaswa kunenwa. Mwelekeze anayeugua kwa Yule ambaye yu tayari kuwaokoa wote wanaokuja Kwake kwa imani. Kwa dhati, kwa upole jitahidi kusaidia nafsi ambayo inaelea kati ya uhai na kifo. {LDSDA: 72.2}

“Tabibu ambaye anajua kwamba Kristo ni Mwokozi wake wa kibinafsi, kwa sababu yeye mwenyewe ameongozwa kwa lile Kimbilio, anajua jinsi ya kushughulikia nafsi zinazotetemeka, zenye hatia, zenye dhambi ambazo humwendea kwa msaada. Anaweza kujibu swali, ‘Nifanye nini ili niokolewe?’ Anaweza kusimulia kisa cha upendo wa Mkombozi. Anaweza kusema kutoka kwa uzoefu wa nguvu ya toba na

72

imani. Kwa maneno rahisi na ya dhati, anaweza kuwasilisha hitaji la hiyo nafsi kwa Mungu katika sala, na anaweza kumtia moyo yule mgonjwa pia kuomba na kupokea rehema za Mwokozi wa huruma. Anapohudumu hivyo kando ya kitanda cha mgonjwa, akijitahidi kusema maneno ambayo yataleta msaada na faraja, Bwana anafanya kazi pamoja naye na kupitia kwake. Kadiri akili za mgonjwa zinavyoelekezwa kwa Mwokozi, amani ya Kristo inaujaza moyo wake, na afya ya kiroho inayomjia inatumika kama mkono wa Mungu unaosaidia kurejesha afya ya mwili. {LDSDA: 72.3}

“Katika kuwahudumia wagonjwa, tabibu mara nyingi atapata fursa ya kuwahudumia marafiki wa mtu aliyeugua. Wanapotazama kando ya kitanda cha anayeugua, wakihisi hawana nguvu ya kuzuia maumivu ya uchungu, mioyo yao inalainika. Mara nyingi huzuni iliyofichwa kwa wengine inafichuliwa wazi kwa tabibu. Wakati huo ni fursa ya kuwaonyesha hao wanaohuzunika kwake Yeye ambaye amewaalika waliochoka na waliolemewa na mizigo kuja Kwake. Mara nyingi sala inaweza kutolewa kwa ajili yao na pamoja nao, ikiwasilisha mahitaji yao kwa Mponyaji wa matatizo yote, Mtulizi wa majonzi yote. {LDSDA: 73.1}

“Ahadi za Mungu”

“Tabibu anazo fursa za thamani za kuwaelekeza wagonjwa wake kwa ahadi za Neno la Mungu. Yeye ataleta kutoka kwa hazina vitu vipya na vya zamani, akinena hapa na pale maneno ya faraja

73

na maelekezo ambayo yanatamaniwa. Hebu tabibu azifanye akili zake kuwa ghala la mawazo safi. Hebu alisome Neno la Mungu kwa bidii, ili apate kujifahamisha ahadi zake. Hebu ajifunze kukariri maneno ya kufariji ambayo Kristo alisema wakati wa ukasisi Wake wa duniani, alipokuwa akitoa masomo Yake na kuwaponya wagonjwa. Anapaswa kuzungumza kuhusu kazi za uponyaji zilizofanywa na Kristo, upole na upendo Wake. Kamwe asipuuze kuzielekeza akili za wagonjwa wake kwa Kristo, Tabibu mkuu. {LDSDA: 73.2}

“Nguvu ileile ambayo Kristo alitumia alipotembea akionekana kati ya wanadamu i katika Neno Lake. Ilikuwa kwa neno Lake Yesu aliponya magonjwa na kufukuza mapepo; kwa neno Lake Yeye aliituliza bahari, na kufufua wafu, na watu wakashuhudia kwamba neno Lake lilikuwa na nguvu. Alinena neno la Mungu, kama alivyokuwa amenena kwa manabii na walimu wote wa Agano la Kale. Bibilia yote ni udhihirisho wa Kristo. {LDSDA: 74.1}

“Maandiko yanapaswa kupokelewa kama Neno la Mungu kwetu, sio yaliyoandikwa tu, bali yaliyonenwa. Wakati wale walioathirika walipokuja kwa Kristo, Yeye hakuona tu wale walioomba usaidizi, lakini wote ambao katika vizazi vyote wataweza kuja Kwake katika hitaji na imani kama hiyo. Alipomwambia yule aliyepooza, ‘Mwanangu, jipe moyo mkuu, umesamehewa dhambi zako.’ Alipomwambia yule mwanamke wa Kapernaumu, ‘Binti, imani yako imekuponya,

74

enenda zako na amani,’ Alisema kwa wengine walioathirika, waliolemewa na mizigo ya dhambi ambao watatafuta msaada Wake. {LDSDA: 74.2}

“Kwa hivyo pamoja na ahadi zote za Neno la Mungu. Ndani yake husema nasi kibinafsi, akizungumza moja kwa moja kana kwamba tunaweza kuisikiliza sauti Yake. Ni katika ahadi hizi ya kwamba Kristo huwasiliana nasi neema Yake na nguvu Zake. Ni majani kutoka kwa ule mti ambao ni kwa ajili ya ‘kuwaponya mataifa.’ Zikipokelewa, kuwekwa akilini, zitakuwa nguvu ya tabia, uvuvio na malisho ya maisha. Hakuna kingine kinachoweza kutoa nguvu na imani, ambayo hutoa nguvu muhimu kwa kiumbe kizima. {LDSDA : 75.1}

“Kwa yule anayesimama akitetemeka kwa hofu kwenye ukingo wa kaburi, kwa nafsi iliochoka na mzigo wa mateso na dhambi, hebu tabibu anapokuwa na fursa kukariri maneno ya Mwokozi — kwa maana maneno yote ya Maandishi Matakatifu ni Yake: {LDSDA: 75.2}

“Usiogope;maana Nimekukomboa; Nimekuita kwa jina lako, wewe u Wangu. Upitapo katika maji mengi Nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana Mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako…. Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni Pangu, na mwenye kuheshimiwa,

75

Nami nimekupenda. ‘Mimi, naam, Mimi, Ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili Yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.’ ‘Usiogope; maana Mimi ni pamoja nawe.’” — Ukasisi wa Uponyaji, uk.116-123. {LDSDA: 75.3}

WASIFU KWA WAUGUZI

“Katika zahanati na hospitali, ambamo wauguzi daima hujihusisha na idadi kubwa ya wagonjwa, huhitaji juhudi yenye uamuzi kupendeza na mchangamufu kila wakati, na kuzingatia uangalifu kwa kila neno na tendo. Katika taasisi hizi ni ya umuhimu mkubwa kwamba wauguzi wajitahidi kufanya kazi yao kwa busara na vyema. Wanahitaji daima kukumbuka kwamba katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, wanamtumikia Bwana Kristo. {LDSDA: 76.1}

“Nia iliyo Tayari”

“Wagonjwa wanahitaji maneno ya busara kunenwa kwao. Wauguzi wanapaswa kusoma Biblia kila siku, ili waweze kusema maneno ambayo yatawaangazia na kuwasaidia wanaougua. Malaika wa Mungu wamo katika vyumba ambavyo hawa wanaougua wanahudumiwa, na mazingira yanayoizunguka nafsi ya yule anayetoa matibabu yanapaswa kuwa safi na ya manukato. Matabibu na wauguzi wanapaswa kukuza kanuni za Kristo. Katika maisha yao fadhila Zake ziweze kuonekana. Kisha, kwa yale wanayotenda na kusema, yatawavuta wagonjwa kwa Mwokozi. {LDSDA: 76.2}

“Muuguzi Mkristo, wakati anapotoa matibabu ya kurejesha afya,

76

kwa kupendeza na kwa ufanisi atavuta akili za mgonjwa kwa Kristo, mponyaji wa roho na mwili pia. Mawazo yaliyowasilishwa, hapa kidogo na pale kidogo, yatakuwa na mvuto wake. Wauguzi wakongwe hawapaswi kupoteza fursa yoyote nzuri ya kuita umakini wa mgonjwa kwa Kristo. Wanapaswa kuwa tayari daima kuchanganya uponyaji wa kiroho na uponyaji wa mwili. {LDSDA: 76.3}

“Kwa mwenendo wa fadhili na upole wauguzi wafundishe kwamba yule ambaye ataweza kuponywa lazima aache kuasi sheria za Mungu. Lazima akome kuchagua maisha ya dhambi. Mungu hawezi kumbariki yule anayeendelea kujiletea ugonjwa na kuteseka kwa ukiukaji wa makusudi wa sheria za mbinguni. Lakini Kristo, kupitia Roho Mtakatifu, huja kama nguvu ya uponyaji kwa wale ambao hukoma kutenda uovu na kujifunza kutenda vyema.” — Ukasisi wa Uponyaji, uk. 222-224. {LDSDA: 77.1}

“Ufanisi Hutegemea Nguvu”

“Ufanisi wa muuguzi hutegemea, kwa kiwango kikubwa, nguvu ya mwili. Afya ikiwa bora, ndivyo bora zaidi ataweza kuvumilia mkazo wa kuwahudumia wagonjwa, na ataweza kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio zaidi. Wale ambao huwatunza wagonjwa wanapaswa kutoa umakini maalum kwa lishe, usafi, hewa safi, na mazoezi. Kama uangalifu kwa upande wa familia utawawezesha pia kuvumilia mizigo ya ziada ambayo huletwa kwao, na

77

itawasaidia wasiambukizwe magonjwa… {LDSDA: 77.2}

“Wauguzi, na wote ambao wanalo la kufanya katika chumba cha wagonjwa, wanapaswa kuwa wangalifu, utulivu, na wenye utaratibu. Papara zote, msisimko, au mchafuko unapaswa kuepukwa. Milango inapaswa kufunguliwa na kufungwa kwa uangalifu, na familia nzima kuwa tulivu. Katika visa vya homa, utunzi maalum unahitajika wakati hatari inakuja na homa inapokuwa ikitoweka. Kisha, kuchunguza mara kwa mara ni muhimu. Kutojua, usahaulifu na uzembe umesababisha vifo vya wengi ambao wangekuwa wanaishi iwapo wangepokea utunzi wa busara, wa makini, wa wauguzi.” — Mashauri kwa Afya, uk. 406, 407. {LDSDA: 78.1}

“Vijana wa bidii, waliojitolea wanahitajika kuingia kwa kazi kama wauguzi. Kadiri hawa vijana wanaume na wanawake wakitumia kwa busara maarifa wanayopata, uwezo wao utaongezeka, wakihitimu kwa ubora zaidi na zaidi ili kuwa mkono wa msaada wa Bwana. {LDSDA: 78.2}

“Bwana anataka wanaume na wanawake wa busara, ambao wanaweza kutenda katika viwango vya wauguzi, kuwafariji na kuwasaidia wagonjwa na wanaoteseka. Laiti wote walio wagonjwa waweze kuhudumiwa na matabibu na wauguzi Wakristo ambao wanaweza kuwasaidia kuweka miili yao michovu, yenye maumivu makali katika utunzi wa Mponyaji Mkuu, kwa imani wakimtazama Yeye kwa urejesho! Ikiwa kupitia huduma ya busara mgonjwa ataongozwa kuikabidhi nafsi yake

78

kwa Kristo na kuleta mawazo yake katika utiifu kwa mapenzi ya Mungu, ushindi mkubwa umepatikana… {LDSDA: 78.3}

“Zipo safu nyingi za kazi inayopaswa kuendelezwa mbele na muuguzi wa mmishonari. Zipo fursa kwa wauguzi waliofunzwa vyema kuingia majumbani na humo wanajitahidi kuamsha upendezi kwa ukweli. Katika karibu kila jamii kuna watu wengi ambao hawatasikiliza mafundisho ya Neno la Mungu au kuhudhuria ibada yoyote ya kidini. Ikiwa hawa watafikiwa na injili, lazima ipelekwe manyumbani mwao. Mara nyingi kitulizo cha mahitaji yao ya kimwili ndio njia pekee ambayo wanaweza kufikiwa. {LDSDA: 79.1}

“Wauguzi wamishonari ambao hutunza wagonjwa na kutuliza dhiki za maskini watapata fursa nyingi za kusali pamoja nao, kuwasomea kutoka kwa Neno la Mungu, na kuongea juu ya Mwokozi. Wanaweza kuomba pamoja na kwa ajili ya walio hohe hahe ambao hawana nguvu ya nia kudhibiti hamu ambazo Kutokuwa na nguvu ya utashi kudhibiti hamu ambazo tamaa imedhoofisha. Wanaweza kuleta kianga cha tumaini katika maisha ya walioshindwa na waliovunjika moyo. Ufunuo wa upendo usio na ubinafsi uliodhihirishwa katika matendo safi ya fadhili yatafanya iwe rahisi kwa hawa wanaoteseka kuamini katika upendo wa Kristo.” — Mashauri kwa Afya, uk. 387, 388. {LDSDA: 79.2}

“Mungu anayo kazi kwa kila mwamini anayefanya kazi katika Zahanati. Kila muuguzi anapaswa kuwa njia ya baraka, akipokea nuru

79

kutoka juu, na kuiacha iangaze kwa wengine. Watendakazi hawapaswi kuchukuana na maonyesho ya mitindo ya wale wanaokuja kwenye Zahanati kwa matibabu, lakini wanapaswa kujitoa wenyewe wakfu kwa Mungu. Hewa inayozunguka nafsi zao itakuwa ladha ya uzima hata uzima. Majaribu yatawazonga pande zote, lakini wamwombe Mungu kwa uwepo na uongozi Wake. Bwana alimwambia Musa: ‘Hakika Nitakuwa nawe,’ na kwa kila mtendakazi mwaminifu, aliyejitoa wakfu amepewa uhakikisho huo.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 144. {LDSDA: 79.3}

WASIFU KWA WOTE

“Katika Neno Lake Bwana huorodhesha zawadi na neema ambazo ni muhimu kwa wote wanaounganika na kazi Yake. Yeye hatufunzi kupuuza kujifunza au kudharau elimu; kwa maana inapodhibitiwa na upendo na kumcha Mungu, utamaduni wa utaalamu ni baraka; lakini huu haujawasilishwa kama sifa ya muhimu zaidi kwa utumishi wa Mungu. Yesu aliwapitia wenye hekima wa wakati Wake, watu wa elimu na nyadhifa kwa sababu walikuwa na kiburi sana na kujiridhisha nafsi katika majivuno yao ya ubabe kwamba hawakuweza kuwahurumia wanadamu waliokuwa wakiteseka na kuwa watendakazi pamoja na Mwanadamu wa Nazareti. Katika ushupavu wao walidharau kufunzwa na Kristo. Bwana Yesu angekuwa na watu walioungana na kazi Yake ambao huithamini kazi hiyo kama takatifu; kisha wanaweza kushirikiana na Mungu. Watakuwa njia zisizozibwa

80

ambazo neema Yake inaweza kutiririkia. Sifa za tabia ya Kristo zinaweza kutolewa kwa wale tu wasiojitumaini wenyewe. Elimu ya juu kabisa ya kisayansi ndani yake haiwezi kukuza tabia kama ya Kristo. Matunda ya hekima ya kweli hutoka kwa Kristo tu. {LDSDA: 80.1}

“Kila mtendakazi anapaswa kupima sifa zake mwenyewe kwa Neno la Mungu. Je! watu wanaoshughulikia mambo matakatifu wana ufahamu wazi, utambuzi sahihi, wa mambo ya maslahi ya milele? Je! watakubali kuridhia utendakazi wa Roho Mtakatifu au wataruhusu wenyewe kudhibitiwa na mielekeo yao ya kurithi na waliyoikuza? Inawapasa wote kujichunguza, iwapo wako katika imani. {LDSDA: 81.1}

“Nafasi na Wajibu”

“Wale ambao hushikilia nafasi za uaminifu katika kazi ya Mungu, wanapaswa daima kukumbuka kwamba nafasi hizi hushughulisha wajibu mkubwa. Utendaji sahihi wa kazi takatifu kwa wakati huu, na wokovu wa nafsi zilizounganika nasi kwa njia yoyote ile, hutegemea kwa kiwango kikubwa hali yetu ya kiroho. Wote wanapaswa kukuza hisia safi ya jukumu lao, kwa ustawi wao wa sasa na hatima yao ya milele itaamuliwa na roho wanayothamini. Iwapo ubinafsi umefumwa katika kazi, ni kama sadaka ya moto wa kigeni badala ya mtakatifu. Watendakazi kama hao Bwana hapendezwi nao.

81

Ndugu, ondoa mikono yenu kwa kazi isipokuwa mnaweza kutofautisha moto mtakatifu na wa kawaida. {LDSDA: 81.2}

“Wale ambao wamesimama kama watu wawakilishi wote sio Wakristo waungwana. Ipo roho iliyoenea inayojaribu kutaka kuwadhibiti wengine. Watu hujiona wenyewe kama mamlaka, huonyesha maoni yao na kupitisha maamuzi kwa mambo ambayo hawana maarifa yenye tajiriba. Baadhi ambao wameunganishwa na nyumba ya matbaa huko _______, hupita ofisini, wakizungumza na wengine tofauti, wakitoa maelekezo ambayo wao hudhani ni sahihi kuyatoa, wakati hawaelewi wanayoyazungumzia.” {LDSDA: 82.1}

Haki na Uaminifu

“Dhulma kubwa na hata udanganyifu umetendwa katika mikutano ya halmashauri, kwa kuleta masuala mbele ya wale ambao hawana uzoefu ambao utawawezesha kuwa waamuzi wanaofaa. Miswada imewekwa mikononi mwa watu kwa kukosoa, ilhali macho ya ufahamu wao yalikuwa yamepofushwa kiasi kwamba hawakuweza kutambua umuhimu wa kiroho wa mada ambayo walikuwa wakishughulikia. Zaidi ya hili, hawakuwa na maarifa halisi ya kuchapisha vitabu. Hawakuwa wamesomea wala kufanya kazi katika safu ya uzalishaji wa vitabu. Watu wameketi katika hukumu kwa vitabu na miswada iliyowekwa bila hekima mikononi mwao, wakati wangalikuwa

82

wamekataa kutumika katika nafasi yoyote kama hiyo. Ungekuwa uaminifu tu wao kusema: ‘Sijawahi kuwa na uzoefu katika safu hii ya kazi, na kwa hakika nitafanya dhulma kwangu mwenyewe na kwa wengine, kwa kutoa maoni yangu. Niwie radhi, ndugu: badala ya kuwapa wengine maagizo, nahitaji kwamba mtu fulani anifunze.’ Lakini hili lilikuwa mbali na mawazo yao. Walijieleza kwa uhuru kuhusu mada ya masomo ambayo hawakujua lolote. Mahitimisho yamekubaliwa kama maoni ya watu wa hekima, ilhali yalikuwa tu maoni ya wasio na ujuzi. {LDSDA: 82.2}

“Wakati umekuja ambapo, kwa jina na nguvu za Mungu, kanisa linapaswa kutenda kwa manufaa ya mioyo na kwa heshima ya Mungu. Ukosefu wa imani thabiti na utambuzi wa mambo matakatifu unapaswa kuzingatiwa kama wa kutosha kumzuia mtu yeyote kuunganika na kazi ya Mungu. Hivyo pia kupendelea kukasirika haraka, roho ya ukali, na kukandamiza, hufichua kwamba mmiliki hapaswi kuwekwa pale ambapo ataitwa kuamua maswali mazito ambayo huathiri urithi wa Mungu. Mtu mkali hapaswi kuwa na sehemu ya kutenda kushughulika na akili za wanadamu. Hawezi kuaminiwa kutatua mambo ambayo yana uhusiano na wale ambao Kristo amewanunua kwa bei ya milele. Ikiwa atajitolea kusimamia wanadamu, ataumiza na kuchubua mioyo yao; kwa maana hana mguso laini, utu mwororo, ambao neema ya Kristo hutoa.

83

Moyo wake mwenyewe unahitaji kulainishwa, kutiishwa na Roho wa Mungu; moyo wa jiwe haujakuwa moyo wa nyama.” {LDSDA: 83.1}

“Kumwakilisha Kristo”

“Wale ambao wanamwakilisha Kristo vibaya hivyo, wanaweka ufinyanzi mbaya kwa kazi; kwa maana huwahimiza wote ambao wameunganishwa nao kutenda kama wao. Kwa ajili ya nafsi zao, kwa ajili ya wale ambao wako hatarini kutokana na mvuto wao, wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, kwa maana kumbukumbu itaonekana mbinguni kwamba mtenda mabaya anayo damu ya nafsi nyingi kwenye mavazi yake. Amesababisha wengine kukasirishwa, ndiposa wameacha imani; wengine wamejazwa mioyo yao na tabia zake za kishetani, na uovu uliofanywa hauwezekani kukadiriwa. Wale tu ambao hufanya wazi kwamba mioyo yao inatakaswa kupitia ukweli, wanapaswa kuhifadhiwa katika nafasi za kuaminiwa kwa kazi ya Bwana. {LDSDA: 84.1}

“Wote wafikirie kwamba kazi yao iwayo yote wanapaswa kumwakilisha Kristo. Kwa kusudi thabiti kila mtu atafute kuwa na nia ya Kristo. Haswa wale ambao wameitikia nafasi ya wakurugenzi au washauri wahisi kwamba wanahitajika kuwa katika mambo yote Wakristo waungwana. Wakati, tunaposhughulika na wengine, tunapaswa kuwa waaminifu siku zote, hatupaswi kuwa wajeuri. Nafsi ambazo tunapaswa kufanya nazo ni mali iliyonunuliwa na Bwana,

84

na hatupaswi kuruhusu usemi wa haraka, wa kukandamiza ukwepe midomo yetu. {LDSDA: 84.2}

“Ndugu, watendee watu kama watu, sio kama watumwa, kuamriwa kwa raha zako unavyotaka. Yeye ambaye hupendelea roho ya ukali na ya kukandamiza, itakuwa vyema awe mchungaji wa kondoo, alivyofanya Musa, na hivyo kujifunza maana ya kuwa mchungaji wa kweli. Musa alipata huko Misri ujuzi kama mtawala hodari, na kama kiongozi wa majeshi, lakini huko hakujifunza masomo muhimu kwa ukuu wa kweli. Alihitaji ujuzi katika majukumu ya unyenyekevu zaidi, ili aweze kuwa mtunzi , wa huruma kwa kila kiumbe hai. Katika kutunza kondoo wa Yethro, huruma zake zilielekezwa kwa kondoo na wana-kondoo, na alijifunza kuvilinda viumbe hawa wa Mungu kwa uangalifu mwanana. Ingawa sauti zao hazingeweza kulalamikia unyanyasaji, bado mwenendo wao huonyesha mengi. Mungu hujali hujali viumbe vyote ambavyo Yeye ameumba. Kumtumikia Mungu katika hadhi hii ya chini, Musa alijifunza kuwa mchungaji mpole kwa Israeli. {LDSDA: 85.1}

“Kumtegemea Mungu”

“Bwana angetaka tujifunze somo pia kutoka kwa ujuzi wa Danieli. Wapo wengi ambao wanaweza kuwa mashujaa, ikiwa, kama Mwebrania huyu mwaminifu, watamtegemea Mungu kwa ajili ya neema kuwa washindi, na kwa nguvu na ufanisi katika kazi zao. Danieli alidhihirisha

85

heshima kamilifu kabisa, kuwaelekea wazee na vijana. Alisimama kama shahidi wa Mungu na alitafuta kuchukua mkondo huo ili asiweze kuaibika Mbingu ikisikia maneno au kutazama kazi zake. Danieli alipotakiwa kula unono wa meza ya mfalme, hakupaa kwa tamaa, wala hakuonyesha azimio la kula na kunywa kama alivyopenda. Bila kutamka neno moja la kukaidi, alilipeleka suala hilo kwa Mungu. Yeye na wenzake walitafuta hekima kutoka kwa Bwana, na walipojitokeza kutoka kwa maombi ya dhati, uamuzi wao ulifanywa. Kwa ujasiri wa kweli na heshima ya Kikristo, Danieli aliwasilisha suala hilo kwa afisa aliyekuwa akiwasimamia, akiuliza kwamba wapewe lishe rahisi. Vijana hawa waliona kwamba kanuni zao za kidini zilikuwa hatarini, na walimtegemea Mungu, ambaye walimpenda na kumtumikia. Ombi lao lilikubaliwa, kwa maana walikuwa wamepata kibali kwa Mungu na kwa wanadamu. {LDSDA: 85.2}

“Watu katika kila wadhifa wa uaminifu wanahitaji kuchukua nafasi yao katika shule ya Kristo, na kutii agizo la Mwalimu Mkuu: ‘Mjifunze Kwangu, kwa kuwa Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira Yangu ni laini, na mzigo Wangu ni mwepesi.’ Hatuna udhuru kwa kudhihirisha sifa moja mbaya ya tabia. ‘Si kwa uwezo, wala kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu, asema Bwana wa majeshi.’ Katika kushughulika kwako na wengine, chochote uonacho

86

au usikiacho kinachohitaji kurekebishwa, kwanza umtafute Bwana kwa hekima na neema, ili ukijaribu kuwa mwaminifu, usiweze kuwa mjeuri. Omba Yeye akupe upole wa Kristo: ndipo utakuwa mkweli kwa jukumu lako, mkweli kwa nafasi yako ya kuaminiwa, na mkweli kwa Mungu, msimamizi mwaminifu, anayeshinda mielekeo kwa uovu ya asili na ya mazoea. {LDSDA: 86.1}

“Hakuna isipokuwa Mkristo mwaminifu anaweza kuwa mungwana mkamilifu; lakini ikiwa Kristo anakaa moyoni, roho Wake ataonyeshwa katika adabu, maneno, na vitendo. Upole na upendo uliokuzwa moyoni, utaonekana katika kujikana nafsi, katika heshima ya kweli. Watendakazi kama hao watakuwa nuru ya ulimwengu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 259-264. {LDSDA: 87.1}

WASIFU KWA WASHIRIKI WA KANISA

“Kuongeza washiriki ambao hawajafanywa upya moyoni na kufanya matengenezo maishani ni chanzo cha udhaifu kwa kanisa. Ukweli huu mara nyingi hupuuzwa. Baadhi ya wachungaji na makanisa hupenda sana kuhifadhi ongezeko la idadi hivi kwamba hawatangazi ushuhuda mwaminifu dhidi ya tabia na mazoea yasiyokuwa ya Ukristo. Wale wanaoupokea ukweli hawafunzwi kwamba hawawezi kuwa salama walimwengu katika mwenendo ilhali wao ni Wakristo kwa jina. Hapo awali walikuwa raia wa Shetani, tangu sasa wanapaswa kuwa raia wa Kristo. Maisha lazima yashuhudie

87

badiliko la viongozi. Maoni ya umma hupendelea dai la kuwa Mkristo. Kujikana nafsi kidogo au kujinyima kidogo huhitajika ili kujivika mfano wa utaua, na kuliwezesha jina la mtu liandikwe kwenye kitabu cha kanisa. Hivyo, wengi hujiunga na kanisa bila kwanza kuungana na Kristo. Katika hili Shetani hushinda. Waongofu kama hao ni mawakala wake hodari. Hutumika kama chambo kwa nafsi zingine. Ni taa za uongo, zinazowashawishi wale wasio waangalifu hadi kwa uharibifu. Ni bure kwamba watu wanatafuta kuifanya njia ya Mkristo iwe pana na ya kupendeza kwa walimwengu. Mungu hajalainisha au kupanua njia yenye inayoparuza, nyembamba. Ikiwa tutaingia uzimani, lazima tufuate njia ile ile ambayo Yesu na wanafunzi Wake walikanyaga, — njia ya unyenyekevu, ya kujikana nafsi, na kujitoa mhanga.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 172. {LDSDA: 87.2}

Ukristo — ni wangapi ambao hawaujui ni nini! Si kitu cha kujivika kwa nje. Ni maisha yafanyayo kazi ndani na maisha ya Yesu. Humaanisha kwamba tumevaa vazi la haki ya Kristo. Kuhusiana na ulimwengu, wakristo watasema, hatutajihusisha katika siasa. Watasema bila shaka, sisi ni wasafiri na wageni; uraia wetu uko juu. Hawataonekana wakichagua kundi la burudani. Watasema, tumeacha kupumbazika kimahaba na mambo ya kitoto. Sisi ni wageni na wasafiri, tunatafuta mji ambao una misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. “ — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 131. {LDSDA: 88.1}

88

“Hatua moja isiyo ya busara. hatua moja ya kutojali, inaweza kulitumbukiza kanisa ndani ya magumu na majaribio ambayo haliwezi kupona kwa miaka mingi. Mshiriki mmoja wa kanisa aliyejawa na kutokuamini, anaweza kutoa manufaa kwa adui mkuu ambaye ataathiri mafanikio ya kanisa lote, na nafsi nyingi zinaweza kupotea kama tokeo.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 446. {LDSDA: 89.1}

“Iwapo makanisa yanatarajia nguvu, lazima yaishi kwa ukweli ambao Mungu ameyapatia. Ikiwa washiriki wa makanisa yetu watapuuza nuru kwa mada hii, watavuna matokeo ya uhakika kwa kuzorota kiroho na kimwili. Na mvuto wa hawa washirika wakongwe wa kanisa utachachisha wale wapya waliokuja kwa imani. Bwana hatendi kazi sasa, kuzileta nafsi nyingi katika ukweli, kwa sababu ya washiriki wa kanisa ambao hawajawahi kuongoka, na wale waliokuwa wameongoka lakini wakakengeuka. Ni mvuto gani hawa washiriki wasiomcha mungu watakuwa nao kwa waongofu wapya? Je, hawataufanya usiokuwa na maana ujumbe aliopeana Mungu ambao watu Wake wanapaswa kutangaza?” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 371. {LDSDA: 89.2}

Ubatizo-Ishara

“Maagizo ya Ubatizo na meza ya Bwana ni nguzo mbili za ukumbusho, moja nje na moja ndani ya kanisa. Kwa maagizo haya Kristo ameliandika jina la Mungu wa kweli. {LDSDA: 89.3}

89

“Kristo ameufanya ubatizo kuwa ishara ya kuingia katika ufalme Wake wa kiroho. Amefanya hili liwe kigezo halisi ambacho lazima wote wazingatie wanaotaka watambuliwe kama walio chini ya mamlaka ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Kabla mtu apate makao kanisani, kabla kupita kwa kizingiti cha ufalme wa kiroho wa Mungu, anapaswa kupokea chapa ya jina la Mungu, ‘Bwana haki yetu.’ Yer. 23:6. {LDSDA: 90.1}

“Ubatizo ni kuukana kabisa ulimwengu rasmi. Wote ambao wamebatizwa kwa jina mara tatu la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, penye haswa mlango wa maisha yao ya Ukristo hutangaza hadharani kwamba wameacha utumishi wa Shetani, na wamekuwa washiriki wa familia ya kifalme, wana wa Mfalme wa mbinguni. Wametii amri, ‘Tokeni kati yao, mkatengwe nao, … msiguse kitu kilicho kichafu.’ Na kwa wao imetimizwa ahadi, ‘Nami nitawakaribisha, Nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa Kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.’ 2 Kor. 6:17, 18. {LDSDA: 90.2}

“Maandalio ya Ubatizo”

“Lipo hitaji la maandalio kamili kwa watahiniwa wa kubatizwa. Wanahitaji zaidi maagizo ya uaminifu kuliko yale wamepewa kwa kawaida. Kanuni za maisha ya Ukristo zinapaswa zifanywe wazi kwa wale wapya ambao wamekuja kwenye kweli. Hakuna anayeweza kutegemea

90

kukiri kwao imani kama thibitisho kwamba wana muunganisho wa kuokoa na Kristo. Hatupaswi kusema tu, ‘naamini,’ ila kuutekeleza ukweli. Ni kwa kufuata mapenzi ya Mungu katika maneno yetu, mwelekeo wetu, tabia yetu, kwamba tunathibitisha uhusiano wetu Naye. Wakati mtu anapoikana dhambi, ambayo ni uasi wa sheria, maisha yake yataletwa kwa kufuata sheria, katika utiifu kamili. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu. Nuru ya Neno inaposomwa kwa uangalifu, sauti ya dhamiri, kujitahidi kwa Roho, huzalisha moyoni upendo wa kweli kwa Kristo, ambaye alijitoa Mwenyewe dhabihu kamili ya kumkomboa mtu mzima, mwili, moyo na roho. Na upendo unadhihirishwa kwa utiifu. Mpaka utakuwa dhahiri na wazi kati ya wale wanaompenda Mungu na kuzishika amri Zake, na wale wasiompenda Yeye na kuyapuuza maagizo Yake. {LDSDA: 90.3}

“Waaminifu Wakristo wanaume na wanawake wanapaswa kupendezwa sana kuileta nafsi iliyosadikishwa kwa maarifa sahihi ya haki katika Kristo Yesu. Iwapo yeyote ameruhusu tamaa ya kupendelea ubinafsi iwe kuu katika maisha yake, waamini waaminifu wazichunge nafsi hizi kama wale wanaopaswa kutoa hesabu. Hawapaswi kupuuza maagizo ya uaminifu, ya upole na upendo yaliyo muhimu sana kwa waongofu wachanga ili isiwepo kazi tepetevu. Uzoefu wa kwanza unapaswa kuwa sahihi. {LDSDA: 91.1}

91

“Shetani hataki mtu yeyote kuona hitaji la kujisalimisha kabisa kwa Mungu. Wakati nafsi inashindwa kujisalimisha, dhambi haijaachwa; hamu na tamaa zinashindana kudhibiti; majaribu huikanganya dhamiri, ili uongofu wa kweli usifanyike. Kama wote wangekuwa na hisia za pambano ambalo kila nafsi lazima ipigane na mashirika ya Shetani ambayo yanatafuta kunasa, kushawishi, na kudanganya, ingewza kuwapo kazi ya bidii zaidi kwa wale ambao ni wachanga katika imani. {LDSDA: 92.1}

“Hizi nafsi, zikiachwa zenyewe, mara nyingi hujaribiwa, na hazitambui uovu wa jaribu. Hebu wajihisi kwamba ni fursa yao kutafuta ushauri. Hebu watafute ushirika wa wale ambao wanaweza kuwasaidia. Kupitia ushirika na wale wanaompenda na kumcha Mungu watapata nguvu.’’ — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 91-93. {LDSDA: 92.2}

“Mtihani wa uanafunzi hauletwi kwa uzito inavyopaswa kuwa kwa wale ambao hujitokeza kubatizwa. Inapaswa kueleweka iwapo wanalichukua tu jina la Waadventista wa Sabato, au ikiwa wanachukua msimamo wao kwa Upande wa Bwana, kutoka kati ya ulimwengu na kutengwa nao, na kutokigusa kitu kichafu. Kabla hawajabatizwa, lazima uwepo uchunguzi kamili kuhusu uzoefu wa watahiniwa. Hebu uchunguzi huu ufanyike, sio kwa njia baridi na ya umbali, lakini kwa fadhili, kwa upole, akiwaonyesha waongofu wapya kwa Mwana-Kondoo wa Mungu

92

aichukuaye dhambi ya ulimwengu. Yalete matakwa ya injili kwa uzito juu ya wagombea wa ubatizo. {LDSDA: 92.3}

“Mojawapo wa hoja ambazo wale wapya wanaokuja kwenye imani watahitaji mafunzo ni mada ya mavazi. Hebu waongofu wapya washughulikiwe kwa uaminifu. Je! wao ni wa ubatili katika mavazi? Je! wanathamini kiburi cha moyo? Ibada ya sanamu kwa mavazi ni ugonjwa wa maadili. Haupaswi kuingizwa katika maisha mapya. Katika masuala mengi, utiifu kwa mahitaji ya injili utadai mabadiliko yenye azimio katika mavazi. {LDSDA: 93.1}

“Maneno ya Maandiko kuhusu mavazi yanapaswa kuzingatiwa kwa uangalifu. Tunahitaji kuelewa kile ambacho Bwana wa mbinguni huthamini katika hata mavazi ya mwili. Wote ambao kwa bidii wanatafuta neema ya Kristo watatii maneno ya thamani ya maagizo yaliyovuviwa na Mungu. Hata mtindo wa mavazi utaonyesha ukweli wa injili.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 95, 96. {LDSDA: 93.2}

“Na jinsi wanafunzi walivyotangaza kwamba hakuna wokovu kwa jina lingine chini ya mbingu, walilopewa wanadamu, vivyo hivyo, pia, watumwa wa Mungu kwa uaminifu na bila woga watawaonya wale ambao wanakumbatia tu sehemu ya kweli zilizounganishwa na ujumbe wa tatu, ya kwamba lazima wapokee kwa furaha jumbe zote kama Mungu alivyowapa, au hawana sehemu katika suala hilo.” — Maandishi ya Awali, uk. 188, 189. {LDSDA: 93.3}

93

“Katika kila kanisa, mavazi ya ubatizo yanapaswa kuandaliwa kwa watahiniwa. Hili halipaswi kuzingatiwa kama matumizi yasiyohitajika ya raslimali. Ni moja ya mambo yanayotakiwa kwa utii wa agizo, ‘Mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.’ 1 Kor. 14:40. {LDSDA: 94.1}

“Si vizuri kwa kanisa moja kutegemea kuazima mavazi kutoka kwa lingine. Mara nyingi wakati mavazi yanahitajika, hayapatikani; baadhi ya walioazimwa wamepuuza kuyarejesha. Kila kanisa linapaswa kujikimu mahitaji yake katika safu hii. Hebu mfuko uanzishwe kwa kusudi hili. Iwapo kanisa lote litaungana katika hili, hautakuwa mzigo mzito. {LDSDA: 94.2}

“Mavazi hayo yanapaswa kufanywa kwa nyenzo kubwa, ya rangi fulani isiyong’aa ambayo maji hayatadhuru, na yanapaswa kuwa na uzito chini. Yawe mavazi masafi, yenye umbo zuri, yaliyotengenezwa kwa mtindo ulioidhinishwa. Lisiwepo jaribio la mapambo, hakuna mikunjo au michoro. Wonyesho wote, uwe wa kuchorwa au mapambo, haustahili kabisa. Wakati watahiniwa wanakuwa na hisia ya maana ya ubatizo, hawatakuwa na ari ya mapambo ya kibinafsi. Bado kisikuwepo chochote kichakavu au kisichofaa, kwa maana hili ni kosa kwa Mungu. Kila kitu kilichounganishwa kwa agizo hili takatifu kinapaswa kuonyesha maandalizi kamili iwezekanavyo.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 97, 98. {LDSDA: 94.3}

94

“Wakati wowote inapowezekana, ubatizo utekelezwe katika ziwa safi au kijito kinachotiririka maji. Na ipatie hafla hiyo umuhimu na uchaji wote ambao unaweza kuletwa ndani yake. Kwenye ibada kama hiyo malaika wa Mungu siku zote huwapo. {LDSDA: 95.1}

“Yeye anayetekeleza agizo la ubatizo anapaswa kutafuta kuufanya hafla ya mvuto wa uchaji, mtakatifu kwa watazamaji wote. Kila agizo la kanisa linapaswa kuendeshwa hivyo ili kuwa la kuinua katika mvuto wake. Chochote kisifanywe kuwa cha kawaida au duni, au kuwekwa kwa usawa na mambo ya kawaida. Makanisa yetu yanahitaji kuelimishwa kwa heshima kubwa na kicho kwa utumishi mtakatifu wa Mungu. Wakati wachungaji wanaendesha huduma zinazohusiana na ibada ya Mungu hivyo wanaelimisha na kuwafunza watu. Matendo madogo yanayoelimisha na kufunza na kuiadibisha nafsi kwa umilele ni ya matokeo makubwa katika kuliinua na kulitakasa kanisa.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 97, 98. {LDSDA: 95.2}

Majukumu baada ya Ubatizo

“Viapo tunavyojichukulia wenyewe katika ubatizo hukumbatia mengi. Kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, tunazikwa kwa mfano wa kifo cha Kristo, na kufufuliwa kwa mfano wa ufufuo Wake, na tunapaswa kuishi maisha mapya. Maisha yetu yanafaa kufungamana na maisha ya Kristo. Tangu sasa mwamini ni lazima akumbuke kwamba ametolewa wakfu kwa Mungu, kwa

95

Kristo na kwa Roho Mtakatifu. Lazima ayafanye mazingatio yote ya ulimwengu kuwa ya pili kwa uhusiano huu mpya. Kwa umma ametangaza kwamba hataendelea kuishi katika majivuno na kuipendelea nafsi. Hataendelea tena kuishi maisha ya utepetevu, na kutojali. Amefanya agano na Mungu. Amekufa kwa ulimwengu. Anapaswa kuishi kwa Bwana, kutumia kwa ajili Yake uwezo wote aliokabidhiwa, kamwe bila kupoteza kutambua kwamba yeye ndiye anayebeba saini ya Mungu, ya kwamba yeye ni raia wa ufalme wa Kristo, mshiriki wa asili ya uungu. Anapaswa kusalimisha kwa Mungu yote alivyo na vyote alivyo navyo, akitumia zawadi zake zote kwa utukufu wa jina Lake. {LDSDA: 95.3}

“Majukumu katika agano la kiroho yaliyofanywa wakati wa ubatizo ni ya wote wawili. Kadiri wanadamu wanatenda sehemu yao kwa utiifu wa moyo wote, wana haki ya kuomba, ‘Ijulikane Bwana, ya kwamba Wewe ndiye Mungu katika Israeli.’ Ukweli kwamba umebatizwa kwa jina la Baba Mwana, na Roho Mtakatifu, ni uhakikisho kwamba ikiwa utadai msaada wao, nguvu hizi zitakusaidia katika kila dharura. Bwana atasikia na kujibu maombi ya wafuasi Wake waaminifu ambao huivaa nira ya Kristo na kujifunza katika shule Yake upole na unyenyekevu Wake. {LDSDA: 96.1}

“‘Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, Ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.’ Kol. 3:1-3. {LDSDA: 96.2}

96

“Jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi fanyeni hivyo. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani…. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.” Kol. 3:12-17. — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 99. {LDSDA: 97.1}

Maisha Yenye Afya

“Elimu ya Waisraeli ilijumuisha tabia zao zote za maisha. Kila kitu ambacho kilihusu hali yao njema kilikuwa mada ya uangalizi wa Mungu, na ilikuja ndani ya mkoa wa sheria za Mungu. Hata katika kutoa chakula chao, Mungu alitafuta manufaa yao ya upeo. Mana ambayo Aliwalisha nyikani ilikuwa ya asili ya kukuza nguvu za mwili, akili na maadili. Ingawa wengi wao waliasi dhidi ya kizuizi cha lishe yao, na wakatamani kurudi kwa siku zile, waliposema, ‘tulikaa kwenye vyungu vya nyama, na tukala chakula tukashiba,’ bado hekima ya chaguo la Mungu kwao ilithibitishwa kwa njia ambayo hawakuweza kupinga. Bila kujali magumu ya maisha yao ya nyikani,

97

hakukuwapo mdhaifu katika makabila yao yote.” — Elimu, uk. 38. {LDSDA: 97.2}

“Wengi wametarajia kwamba Mungu angewazuia dhidi ya magonjwa kwa sababu tu wamemwomba Afanye hivyo. Lakini Mungu hakuzingatia maombi yao, kwa sababu imani yao haikukamilishwa kwa matendo. Mungu hatatenda muujiza kuwazuia wasipatwe na ugonjwa wale ambao hawajitunzi wenyewe, lakini daima wanaendelea kuvunja sheria za afya, na kutofanya juhudi za kuzuia ugonjwa. Wakati tunapofanya yote tunayoweza kwa upande wetu kuwa na afya, basi tunaweza kutarajia kwamba matokeo yaliyobarikiwa yatafuata, na tunaweza kumwomba Mungu kwa imani abariki juhudi zetu kwa ajili ya kuhifadhi afya. Kisha Yeye atajibu ombi letu, iwapo jina Lake linaweza kutukuzwa kwa njia hiyo. Lakini hebu wote waelewe kwamba wanayo kazi ya kufanya. Mungu hatatenda kwa njia ya kimiujiza kuhifadhi afya ya watu ambao kwa uzembe wa kutozijali sheria za afya wanachukua mkondo hakika kujifanya wenyewe wagonjwa.” — Mashauri kwa Afya, uk. 59. {LDSDA: 98.1}

Usafi wa Mazingira

“Katika Israeli ‘sheria kamili endelevu za usafi zilitekelezwa. Hizi ziliamriwa kwa watu, sio tu kama muhimu kwa afya, lakini kama sharti la kudumisha uwepo wa Aliye Mtakatifu kati yao. Kwa mamlaka matakatifu Musa aliwatangazia, ‘Bwana Mungu wako yuatembea katika kituo, ili akuokoe;

98

na iwe takatifu kambi yako.’” — Elimu, uk. 38. {LDSDA: 98.2}

“Usafi kamili na utaratibu wa msimamo mkali kote kote kwenye marago na viunga vyake uliamriwa. Sheria kamili za usafi zilitekelezwa. Kila mtu ambaye alikuwa najisi kutokana na sababu yoyote alikatazwa kuingia kambini. Hatua hizi zilikuwa za muhimu sana katika kuhifadhi afya kati ya umati mkubwa kama huo; na ilihitajika pia kwamba utaratibu kamili na usafi udumishwe, ili Israeli wafurahie uwepo wa Mungu Mtakatifu. Hivyo Yeye alitangaza: ‘Bwana, Mungu wako, yuatembea katika kituo, ili akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako, kwa hivyo iwe takatifu kambi yako.’” — Mababu na Manabii, uk. 375. {LDSDA: 99.1}

“Ugonjwa mbaya unapoingia katika familia, kuna hitaji kubwa la kila mwana-familia kuzingatia kikamilifu usafi wa kibinafsi, na lishe, kujihifadhi mwenyewe katika hali ya kiafya, hivyo kujiimarisha mwenyewe dhidi ya ugonjwa. Pia ni muhimu sana kwamba chumba cha mgonjwa, tangu mwanzo kiweze kuwa, cha kuingiza hewa safi. Hii ni manufaa kwa anayeugua, na ni manufaa sana kuwahifadhi vyema wale wanaolazimika kukaa muda mrefu katika chumba cha mgonjwa. {LDSDA: 99.2}

“Mateso makubwa yanaweza kuepukwa ikiwa wote wangefanya kazi kuzuia magonjwa, kwa kutii kikamilifu sheria za afya. Tabia kamilifu za usafi zinapaswa kuzingatiwa.

99

Wengi, wakiwa na afya, hawatajitaabisha kudumu katika hali yenye afya. Hupuuza usafi wa kibinafsi, na si waangalifu kuweka mavazi yao safi. Uchafu daima na bila kujua hupita kutoka mwilini, kupitia vinyweleo, na iwapo eneo la ngozi halijawekwa katika hali ya kiafya, mwili unalemewa na mzigo wa uchafu. Iwapo mavazi yanayovaliwa hayasafishwi kila mara, na kuanikwa mara kwa mara huchafuka kwa uchafu ambao hutupwa nje ya mwili kwa kupumua kunakofaa na kusikofaa. Na ikiwa nguo zinazovaliwa hazisafishwi mara kwa mara kutoka kwa uchafu huu, vinywelea vya ngozi hufyonza tena uchafu ule ambao ulitupwa nje. Uchafu wa mwili, usiporuhusiwa kutoka, hurudishwa tena ndani ya damu na kushinikizwa kwa viungo vya ndani. Umbile, ili kujiondolea uchafu wenye sumu, hufanya bidii kuuweka mwili huru. Juhudi hii huzalisha homa, na kile kinachoitwa ugonjwa. Lakini hata wakati huo, ikiwa wale ambao wameathirika wangeusaidia Mwili katika juhudi zake, kwa kutumia maji safi, laini, maumivu mengi yangezuiliwa. Lakini wengi, badala ya kufanya hivi, na kutafuta kuondoa uchafu wa sumu mwilini, huongeza zaidi sumu ya kufisha ndani ya mwili, ili kuondoa sumu iliyo ndani tayari. {LDSDA: 99.3}

“Iwapo kila familia ingetambua matokeo yenye manufaa ya usafi kamili, wangefanya juhudi maalum kuondoa kila uchafu kutoka kwa miili yao, na

100

katika nyumba, na wangeeneza juhudi zao kwenye majengo yao. Wengi huruhusu uchafu wa mboga zilizooza kubaki karibu na majengo yao. Hawako macho kwa athari za vitu hivi. Kila wakati kwa vitu hivi vinavyooza hutoka mvuke ambao unatia hewa sumu. Kwa kuvuta pumzi hewa chafu, damu hutiwa sumu, mapafu huathirika, na mwili wote unapata ugonjwa. Ugonjwa wa karibu kila maelezo utasababishwa kwa kuvuta pumzi hewa iliyoathiriwa na vitu hivi vinavyooza. {LDSDA: 100.1}

“Familia zimeathiriwa kwa homa baadhi ya wana-familia wao wamekufa, na sehemu iliyosalia ya mduara wa familia karibu wamemnung’unikia Muumba wao kwa sababu ya fadhaiko la kufiwa kwao, ilhali chanzo pekee cha magonjwa yao yote na kifo kimekuwa tokeo la ulegevu wao. Uchafu karibu na majengo yao umewaletea magonjwa ya kuambukiza, na maradhi ya kusikitisha ambayo wao humushutumu Mungu. Kila familia inayothamini afya inapaswa kusafisha makazi yao vitu vyote vinavyooza. {LDSDA: 101.1}

“Mungu aliamuru kwamba wana wa Israeli asilani wasiruhusu uchafu wa miili yao, au wa mavazi yao. Wale waliokuwa na uchafu wowote wa kibinafsi walifungiwa nje ya marago hadi jioni, kisha walitakiwa waoge na wayasafishe mavazi yao kabla waingie

101

kambini. Pia waliamriwa na Mungu wasiwe na uchafu karibu na majengo yao katika umbali mkubwa wa marago, ili Bwana asije akapita na kuuona uchafu wao. {LDSDA: 101.2}

“Kuhusu usafi, Mungu hahitaji mapungufu kwa watu Wake sasa, kuliko alivyohitaji kwa Israeli wa zamani. Uzembe wa usafi utachochea ugonjwa. Ugonjwa na kifo cha mapema haviji bila chanzo. Homa sugu na ugonjwa wa kusukasuka umekithiri katika vitongoji na miji ambayo zamani ilikuwa ikitambuliwa kuwa yenye afya, na baadhi ya watu wamekufa, ilhali wengine wameachwa na viungo vilivyovunjika, kulemazwa na ugonjwa uhai wao wote. Katika matukio mengi makazi yao wenyewe yalikuwa na wakala wa uharibifu, ambaye alituma sumu mbaya ndani ya anga hewa, ili ivutwe kwa pumzi na familia na mtaani. Kukawia na uzembe unaoshuhudiwa nyakati zingine, ni jambo la kihayawani, na kutokujua matokeo ya mambo kama hayo kwa afya kunashangaza. Maeneo kama hayo yanapaswa kutakaswa hasa katika majira ya hari, kwa chokaa au majivu au kwa kufukia kila siku ardhini.” — Mashauri kwa Afya, uk. 61-63. {LDSDA: 102.1}

————————– 0 ———————— –

“Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu; na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka.” — 2 Petro 2:9, 10.

“Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.” — 1 Kor. 14:40.

102

 

>