fbpx

Trakti Namba 13

1 (Jalada)

Hati miliki 1941, 1944

V. T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

TRAKTI NAMBA 13

TOLEO LA PILI

“Kila zawadi njema, na kila zawadi iliyo kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga; Kwake hakuna ku-badilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.” Yakobo 1:17

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Imechapishwa Marekani

2

ZAWADI

Salamu kwako, rafiki mwaminifu wa Kitabu cha Mungu! — Wewe ambaye unaweza kujitakasa kutoka kwa desturi potovu za watu wa mataifa. Kwako hapa zimemiminwa habari za kutakasa za ukweli wa zawadi! {TN13: 3.1}

Ziweze kufanya nafasi moyoni mwako kwa ajili ya baraka zinazosubiri langoni kuujaza moyo wako, maisha yako, nyumbani mwako, kadiri miaka mipya ikingoja kuchukua nafasi ya ya zamani. {TN13: 3.2}

Hakika, kila siku iweze kuyapata maisha yako na afya tele, furaha, ustawi, na mambo mema kwa ajili yako na vilivyo vyako, wakati kila mmoja wenu akifurahia katika matarajio ya utukufu wa Ufalme unaokuja hivi karibuni, na kujitayarisha kwa ajili ya makao huko. {TN13: 3.3}

Vitabu vingine ni vikubwa sana

Na husema mengi, ni kweli;

Lakini hakuna chochote kingeweza KUKUTAKIA ZAIDI

Kuliko hiki KINAVYOKUTAKIA —

Manyunyu ya baraka

Mara moja na daima,

Kukuhuisha na kukuhifadhi

Mwenye hekima, wa furaha, na mwenye nguvu,

Leo, kesho — milele yote! {TN13: 3.4}

3

 

YALIYOMO

 

Zawadi Kwa Wale Huzawadisha Na Wapokea Zawadi 5

Maadhimisho Ya Krismasi Na Zawadi Za Krismasi 6

Zawadi Za Maadhimisho Ya Miaka 8

Zawadi Ya Upendo 9

Zawadi Ya Ukumusho Ya Pumziko Takatifu Na La Milele 10

Kuiadhimisha Zawadi Ya Sabato Milele 11

Zawadi Kwa “Wote Wenye Mwili” 13

Zawadi Zingine Za Thamani 14

Zawadi Za Andiko Takatifu Kwa Mbao Za Mawe 22,23

Zawadi Za Uhuru Wa Kidini 25

Uache Majivuno, Kujiamini Nafsi, Kiburi Cha Maoni, Kuchukia Bila Sababu 29

Tumia Zawadi Ya Akili Na Kufikiri 31

Zawadi Ya Uongozi 32

Jumla Ya Mambo Yote 36

Sala Yake 38

Faharisi Ya Maandiko 39

         VIELELEZO

Bendera ya Wadaudi 35

Bendera ya Marekani 35

4

Salamu za Kristo

ZAWADI KWA WALE HUZAWADISHA NA WAPOKEA ZAWADI

“Kila zawadi njema, na kila zawadi kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.” Yak. 1:17. {TN13: 5.1}

Kwa zaidi ya karne kumi na tisa, taasisi ya Krismasi, siku maarufu ya kupokezana zawadi, imekuwa mashuhuri katika Kanisa la Kikristo kama mojawapo ya zawadi nzuri na kamilifu za Mungu. Na hisia hii imetukuzwa na kuendelezwa mbele ya uso wa kweli zinazojulikana sana kwamba Krismasi si siku ya kuzaliwa kwa Kristo, kwamba Yeye, kweli, hakuzaliwa mwezi wa Desemba kamwe, kwamba uadhimishaji wa hiyo siku ni desturi tu ya upagani iliyofanywa kuwa ya Kikristo iliyoendelezwa katika haiba ya kisingizio cha Ukristo, na kwamba si zawadi kutoka kwa Mungu. {TN13: 5.2}

“Roho ya Krismasi ilifuatiliwa hadi nyuma katika historia leo,” anasema msafirishaji wa matbaa mwenzi ya Chicago, chini ya tarehe Desemba 23, 1935 “na ikatambuliwa kama ya wakati mmoja ‘adui wa umma.’” {TN13: 5.3}

“Ilipigwa chapa ya uharamia wa kipagani, ikapigwa marufuku Uingereza Mpya na Wapuriti mwaka 1659. {TN13: 5.4}

5

“Uchangamfu wa Krismasi na karamu viliudhi sana zile nguzo takatifu za kanisa, alitangaza Profesa William Warren Sweet, mwana-historia wa kanisa la Chuo Kikuu cha Chicago, kwamba walipitisha sheria katika mahakama kuu ya koloni ya Massachusetts kusema: {TN13: 6.1}

“’Mtu yeyote atakayepatikana akiadhimisha siku yoyote kama Krismasi au kama hiyo, au kwa kutofanya kazi, kula karamu au njia nyingine yoyote, kama tamasha, atafainiwa shilingi tano.’ {TN13: 6.2}

“Katika nusu ya mwisho ya karne iliyopita tu roho ya Krismasi ilipokelewa kwa ujumla nchini Marekani, hata kanisani, Profesa Sweet alisema.” {TN13: 6.3}

Kwa mtazamo wa kweli hizi za kihistoria zinazojulikana sana, awamu hii ya suala haihitaji kushughulikiwa zaidi ya onyo rahisi la Bwana linalohusisha

Maadhimisho Ya Krismasi Na Zawadi Za Krismasi. {TN13: 6.4}

Ilhali kwa umati wa waadhimishaji wa Krismasi, Kristo hamaanishi chochote kupita mtu wa kawaida maarufu, hata kwa umati mkubwa zaidi wa wanaoadhimisha Krismasi “wasiokuwa Wakristo,” Yeye ni kielezo kilichohadithiwa ambacho ni cha ku-wakumbusha karamu za ulafi wakati wa likizo; ingawa hulitaja Jina Lake bure kumkiri katika mikusanyiko ya inayodhaniwa kuwa asili ya hafla ya kidini ya msimu! Hivyo kwa wengi, kama nuru gizani, unasimama ukweli kwamba Krismasi si, kwa uhalisi, huadhimishwa

6

kwa heshima ya Mwokozi, ila kwa kuitukuza desturi ya kipagani na kwa kutosheleza tamaa ya moyo wa kimwili. Kwa sababu hiyo, “Wakristo wote” hawawezi kushiriki kwa hivyo katika kusherehekea hadithi ya Krismasi. Kwa hakika, kufanya hivyo ni wazi kuliweka bure Neno la Mungu, kwa maana “Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo. Maana desturi za watu hao ni ubatili, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka. {TN13: 6.5}

“Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike. Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.” Yer. 10:2-5. {TN13: 7.1}

Na utamaduni wa kupokezana zawadi ambao ni sehemu muhimu ya roho ya kuadhimisha Krismasi, ni desturi ya kuzalisha wivu, mara nyingi ikiharibu tu moyo wa mpokeaji na kukifanya kitupu kipochi cha mnunuzi. Hivyo wakati ambapo huchochea umati mmoja wa watu kufanya wonyesho wa majivuno, hata kuwashawishi kwenye karamu za ulafi, uhawara, na uasherati, huwaendesha wengine, umati wa masikini, ama kwa kijicho au kukata tamaa, au yote, pia si nadra kwa kufa moyo, na nyakati zingine kwa kichaa — hata kufanya mauaji na kujiua. {TN13: 7.2}

7

Taasisi nzima ya Krismasi kwa hiyo ikiwa aina ya ibada ya kipagani ambayo hupotosha mataifa, watumwa wa Bwana siku zote watadinda kupokezana zawadi za Krismasi, watamkataa mtumishi mwovu wa roho ya kisingizio kwa hafla hiyo na msaada wa kibinadamu wa hila. Wakristo hawawezi, hakika, kushiriki katika shughuli yake isiyokuwa takatifu ya kuuza zawadi na kusherehekea, na wakati uo huo kuwa “Wakristo kabisa.” {TN13: 8.1}

“Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa Yako wewe . . . Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu; wakati wa kujiliwa kwao watapotea. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa Bwana; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.” Yer. 10:7, 15, 21. {TN13: 8.2}

Kupokezana zawadi za Krismasi, hata hivyo, si tu desturi inayozalisha uovu: nyingine ambayo ni ya uovu, ni desturi ya kupokezana

Zawadi Za Maadhimisho Ya Miaka. {TN13: 8.3}

Ingawa zawadi za siku ya kuzaliwa kwa heshima ya aliyetoka tu kuzaliwa hupatana na msukumo wa ukarimu na ungwana wa wanadamu, mazoea ya kupeana zawadi kwa mwingine kwenye maadhimisho ya kuzaliwa, ni kama tabia pacha ya kupokezana zawadi za noeli, mkusanyiko ambao huzalisha majivuno, ubadhirifu, shida, kutoridhika, wivu, huzuni, na jeshi la maovu yanayohusiana. Zikiwa ni

8

za lazima, zawadi za siku ya kuzaliwa, kama ilivyo na zawadi za Krismasi, katika uchunguzi wa mwisho si zawadi hata kidogo, ila tu ni biashara halali ambazo, mara nyingi, ovyo tu, za ubadhirifu, na za kuleta madhara. Mfuasi wa Kristo ambaye anayapenda mashuri Yake kwa moyo wote, ataichukia ya uovu desturi hii na tabia, ikiwa ni hafla ya Krismasi, Pasaka, siku za kuzaliwa, au yoyote. Yeye, kwa ufupi, atakataa kuwapa yoyote ila

Zawadi Ya Upendo. {TN13: 8.4}

Iwapo unataka kutoa zawadi ya upendo, isiwe zawadi ya wakati, basi iweze kuwa kitu muhimu, kamwe kisiwe cha anasa au ubatili, na isiokuwa zaidi ya uwezo wako; hebu ichochewe kwa roho safi na ya ukarimu badala ya kulazimishwa kwa majivuno, desturi, au malipo. Hebu, kwa ufupi, iwe zawadi halisi ya upendo kwa heshima ya mpokeaji, si kwa heshima ya wakati ambao sio tu huonyesha tuzo lakini hata kuidai. Wakristo wanapaswa kuwa watoaji, si wachuuzi! {TN13: 9.1}

Hatimaye, roho hiyo isiyokuwa na ubinafsi ambayo ilimsukuma Maria kuivunja “chupa ya alabasta,” na kuyamimina manukato ya thamani kwa heshima ya Yule ambaye damu Yake ya pekee ilimwagwa kuwasafisha wote inapaswa kumchochea mtoaji na mpokeaji na zawadi inapaswa kuwa na athari ile ile sasa yalivyokuwa manukato kabla ya kuzikwa, na ilivyokuwa damu kabla ya kufufuka. {TN13: 9.2}

Wakristo sio tu wanapaswa kuwa wenye hekima na watoaji wasiokuwa na ubinafsi kwa wakati mwafaka, ila pia

9

wapokeaji wa busara na shukrani. Hakika, wanapaswa kufurahi katika zawadi za utukufu za Mungu zaidi kuliko zawadi zinazoharibika za wanadamu. Wakristo kama hao hufurahi katika kutoa zawadi za upendo, lakini furaha yao kuu na baraka itakuwa katika kuiadhimisha

Ya Ukumbusho Zawadi Ya Pumziko Takatifu La Milele. {TN13: 9.3}

Zawadi kubwa zaidi halisi waliyokabidhiwa wanadamu ni dunia nzuri na “vyote viijazavyo,” ikitiwa taji na Siku ya Milele ya Pumziko — Pumziko ambalo humweka mwangalizi wake katika ukweli kwamba Bwana aliumba vitu vyote katika siku sita na “akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Kwa hiyo, kati ya siku zote za juma, hii pekee ndio takatifu. Basi, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Kut. 20:8-11 . {TN13: 10.1}

Kwa ya uaminifu maadhimisho ya Sabato sasa, kila Mkristo wa kweli ataonyesha shukrani yake kwa uandalizi huu wote wa hekima na upendo kwa ustawi wa kimwili, kiakili na wa kiroho wa hali njema ya wanadamu, na kwa hiyo

10

imani yake katika Muumba wake, ili apate kupewa upendeleo wa

Kuiadhimisha Zawadi Ya Sabato Milele. {TN13: 10.2}

“Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, wa-takuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina Langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na ku-cheza-cheza kama ndama wa mazizini. Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile Niifanyayo, asema Bwana wa majeshi.” Mal. 4:1-3. {TN13: 11.1}

“Ikumbukeni [wote watakaoshuhudia kuangamizwa kwa waovu waliotajwa hapo juu] sheria ya Musa, mtumishi Wangu, Niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.” Mal. 4:4. {TN13: 11.2}

Amri hii ya kutunza sheria ambayo Musa alipokea huko Horebu, ni, kwa mujibu wa Maandiko, kwa wote watakaoishi katika siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana — wanaoishi wakati Mungu anapomtuma duniani nabii Wake wa mwisho, Eliya wa uakisi “Angalieni,” Yeye anasema, “Nitawatumia Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.” Mal. 4:5. {TN13: 11.3}

Dhahiri ni kwamba tunapaswa kuikumbuka Zawadi

11

Yake Takatifu, sheria ya Musa, sio tu kabla ya nabii aliyeahidiwa kuwasili na wakati akiitangaza siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana bali hata milele: “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, Nitakazofanya, zitakavyokaa mbele Yangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele Yangu, asema Bwana. Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” Isa. 66:22-24. {TN13: 11.4}

“Omba ninyi,” huagiza Bwana, akitazama mbele kwa wakati wa “dhiki kuu,” “kwamba kukimbia kwako kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.” Mat. 24:20. Kwa hiyo sio tu tuitunze Zawadi ya Sabato, lakini pia tunapaswa kuomba kwa bidii kwamba hali zijielekeze kama kutotuletea tatizo la kuvunja Sabato ambayo kwayo haitawezekana kuokoka. Kwa maana, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya Sabato, dhahiri hiyo ni baraka kwa ajili yake, sio yeye baraka kwa ajili ya hiyo. {TN13: 12.1}

Wakristo wanajua kwa uzoefu kwamba Shetani hujaribu kwa nguvu kuwaibia watu Zawadi ya Sabato kuliko anavyofanya kuwaibia zawadi nyingine yoyote ya Mungu, hata kumvuvia mnyama

12

kunena kwa niaba yake dhidi ya Mungu Aliye Juu Zaidi, na kujaribu kubadili “majira na sheria.” Dan. 7:25. Basi usiwe mfuasi wa mnyama, bali uwe mfuasi wa Kristo, na kwa tabia yako nzuri “kuithibitisha sheria.” Rum. 3:31. Na kumbuka hii Zawadi Takatifu, Sabato, ni Zawadi, sio tu kwa watoto wa Yakobo, ila ni

Zawadi Kwa “Wote Wenye Mwili.” {TN13: 12.2}

“Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote. {TN13: 13.1}

“Wala mgeni [yeye ambaye si Mwisraeli], aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, hakika yake Bwana atanitenga na watu Wake; wala towashi asiseme, mimi ni mti mkavu. {TN13: 13.2}

“Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato Zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo Mimi, na kulishika sana agano Langu; Nitawapa hawa nyumbani Mwangu, na ndani ya kuta Zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; Nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. {TN13: 13.3}

“Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi Wake; kila mmoja aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano Langu; Nitawaleta hao nao hata mlima

13

Wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba Yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu Zangu; kwa maana nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.” Isa. 56:2-7. {TN13: 13.4}

Tathmini sahihi ya Zawadi hii ya Pumziko la Milele itahakikisha tathmini sahihi ya

Zawadi Zingine Za Thamani. {TN13: 14.1}

Mtunza Sabato wa kweli hawezi kuwa asiye na shukrani. Badala yake, atashukuru katika mambo yote, akimshukuru Bwana kwa zawadi ya ujazi na pia kwa zawadi ya uhitaji; na iwe ni kwa nyalio au ole, kutoka moyoni atasema na Paulo: “Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupun-gukiwa.” Fil. 4:11, 12. {TN13: 14.2}

Hivyo kila Mkristo wa kweli, akiwa katika hali mbaya ya hewa au ifaayo, atajifunza kuwaongoza wengine kwa Kristo, akikumbuka kwamba “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; wakati wa

14

kuomboleza, na wakati wa kucheza; wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; wakati wa vita, na wakati wa amani.” Mhu. 3:1-8. {TN13: 14.3}

Mkweli kwa imani yake, mfuasi mwaminifu wa Kristo, kwa uthamini wa utakatifu na shukrani, atashukuru kwa zawadi ya kila wakati na majira na zawadi ya ujazi na zawadi ya uhitaji, pia kwa zawadi ya makao na kwa zawadi ya wapendwa — mume, mke, na watoto; baba na mama; jamaa na marafiki. Naye ataiheshimu kwa shukrani amri ya Bwana: {TN13: 15.1}

“ENYI WAUME, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi Alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; Apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo Naye Anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili Wake. Kwa sababu hiyo mtu

15

atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Efe. 5:25-31. {TN13: 15.2}

“ENYI WAKE, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo Naye ni kichwa cha Kanisa; Naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” Efe. 5:22-24. “Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.” Rum. 7:2. {TN13: 16.1}

“LAKINI NAWAAMBIA WALE WASIOOA BADO NA WAJANE, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa. {TN13: 16.2}

“NA KWA WALE WALIOKWISHA KUOANA nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe. Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana: {TN13: 16.3}

“YA KWAMBA IWAPO NDUGU MMOJA ANA MKE ASIYEAMINI, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. Kwa

16

maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isin-gekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? {TN13: 16.4}

“KILA MTU NA AKAE KATIKA HALI ILE ILE ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo. Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu. Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele ya Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. {TN13: 17.1}

“KWA HABARI ZA WANAWALI sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. {TN13: 17.2}

“JE! UMEFUNGWA KWA MKE? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu

17

kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo. {TN13: 17.3}

“Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi [ufalme unakuja hivi karibuni]: kwamba wote walio na wake [sasa] na wawe kama hawana; na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu. Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita [na unakuja Ufalme wa Mungu ambamo wote watakuwa sawa]. Lakini nataka msiwe na masumbufu. [msiache vitu vya ulimwengu huu viwafadhaishe; ni vya muda tu; ilhali ufalme ni wa milele]. {TN13: 18.1}

“YEYE AMBAYE HAJAOA HUJISHUGHULISHA na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; bali yeye aliyeoa hu-jishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.” 1 Kor. 7:8-16, 20-34. Wale ambao hawajaoa, kwa hiyo, ha-wakwazwi sana. {TN13: 18.2}

“NI NENO LA KUAMINIWA; MTU AKITAKA KAZI YA ASKOFU, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na

18

busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu ali-yeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. {TN13: 18.3}

“VIVYO HIVYO MASHEMAZI na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu. wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. {TN13: 19.1}

“Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai,

19

nguzo na msingi wa kweli.” 1 Tim. 3:1-15. {TN13: 19.2}

“YEYE ASEMAYE KWAMBA YUMO NURUNI, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho. {TN13: 20.1}

“NAWAANDIKIA NINYI, WATOTO WADOGO, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. {TN13: 20.2}

“NAWAANDIKIA NINYI, AKINA BABA, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. {TN13: 20.3}

“NAWAANDIKIA NINYI, VIJANA, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. {TN13: 20.4}

“NIMEWAANDIKIA NINYI, WATOTO WADOGO, kwa sababu mmemjua Baba. {TN13: 20.5}

“NIMEWAANDIKIA NINYI, AKINA BABA, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. {TN13: 20.6}

“NIMEWAANDIKIA NINYI, VIJANA, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. {TN13: 20.7}

“MTU AKIIPENDA DUNIA, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana

20

kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.” (mwisho wa dunia). 1 Yoh. 2: 9-18. {TN13: 20.8}

“Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.” 1 Yoh. 3: 1-5. {TN13: 21.1}

Hatimaye, wapendwa, “toa tahadhari kubwa sana” kwa

21

ZAWADI YA ANDIKO TAKATIFU KWA MBAO ZA MAWE. {TN13: 21.2}

I

Usiwe na miungu mingine ila mimi. {TN13: 22.1}

II

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; na-wapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. {TN13: 22.2}

III

Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. {TN13: 22.3}

IV

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. {TN13: 22.4}

22

V

Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. {TN13: 23.1}

VI

Usiue. {TN13: 23.2}

VII

Usizini. {TN13: 23.3}

VIII

Usiibe. {TN13: 23.4}

IX

Usimshuhudie jirani yako uongo. {TN13: 23.5}

X

Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.. Kut. 20: 3-17. {TN13: 23.6}

Hizi “Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.” Kut. 31:18 {TN13: 23.7}

23

Sheria hii ya upeo na ya ulimwengu wote, amri kumi, awali zilizoandikwa na Mungu Mwenyewe juu ya mbao mbili za mawe, hutolewa kwa yule anayetaka kwa ajili ya kuzihifadhi zawadi zao za thamani: dini yao, makao yao na hasa maisha yao, makao na maisha ya familia zao, mali zao, miji yao, mataifa yao; na amani na nia njema kwa wanadamu wote. {TN13: 24.1}

Hivyo Yesu aliamuru: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.” Mat. 22: 37-40. {TN13: 24.2}

“Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.” Yak. 2: 10-12. “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.” 1 Yoh. 2: 4. {TN13: 24.3}

Zaidi ya hayo, “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.”

24

Mat. 7: 6. Na ninyi ambao hamna lulu za kutupa, msijaribu kuwasababisha walio nazo, kupoteza zao, ila badala yake wailinde na kuitunza kwa makini

Zawadi Ya Uhuru Wa Kidini. {TN13: 24.4}

“Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.” Rum. 14: 1. Kuwa wenye upendo. {TN13: 25.1}

“Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote,” safi au najisi; “lakini yeye aliye dhaifu hula mboga,” maana ndani yake hupata nguvu kwa ajili ya mwili wake. “Acheni,” kwa hiyo, “yeye alaye,” hata kama ni kwa madhara yake mwenyewe, “asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali. Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.” (Warumi 14: 2-4), lakini hakuna mtu anayeweza kumsimamisha yeyote. {TN13: 25.2}

“Mtu mmoja,” zaidi ya hayo, “ afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe [sio katika akili za mwingine]. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu.” Hiyo ni nini, kwa hivyo, kwako? “tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.”

25

Rum. 14: 5, 6. Usifadhaike tokea sasa na mashaka haya. {TN13: 25.3}

Wote aaminiye na asiyeamini hawapaswi kuhitlafiana na shughuli ya kila mmoja. Wanapaswa kudhibiti vinywa vyao, na wanapaswa kuwa upendo kwa kila mmoja. Acha kila mmoja awe na amani na watu wote. Haswa waumini wanapaswa kufanya hivyo kwa wale ambao ni wa nyumba ya imani. {TN13: 26.1}

Msikataze ndoa, wala usiamuru mtu yeyote “wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.” 1 Tim. 4: 3-5. {TN13: 26.2}

Ninyi mnaojua Ukweli, mnaweza kula kila siku kila kitu ambacho mnaweza na dhamiri iliyoangazishwa kutoa shukrani, kwa kuwa vitu kama hivyo tu “vimetakaswa kwa neno la Mungu na sala.” {TN13: 26.3}

“Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata. Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule

26

utakaokuwapo baadaye. Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa. “1 Tim. 4: 6-9. {TN13: 26.4}

Msiwe kama “Diotrefe, ambaye,” anapenda “kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali, . . . na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.” 3 Yoh. 1: 9, 10. {TN13: 27.1}

Ikiwa unatupwa nje kwa ajili ya Ukweli, usiwe na hasira au kukata tamaa, ila shangilia katika faraja ya Mungu: “Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isa. 66: 5. {TN13: 27.2}

Wala usimlazimishie mmoja kitu chochote ambacho hataki, wala kumnyima chochote ambacho kinaweza kuwa chake. Na kamwe usimame kati yake na Mungu wake, ambaye Kwake pekee anawajibika, na ni Yeye pekee atakayetatua masuala yote: “. . . Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.” Isa. 66: 15-17. {TN13: 27.3}

Usimdhibiti au kumzuia yeyote kwa uchunguzi

27

wa ukweli, bali wasaidie “kuthibitisha mambo yote,” na “kulishika lililo jema.” 1 Thes. 5:21. Usijaribu kuwafanya wasiojiweza au kuwa mpumbavu kwa kuwatarajia kuyapokea maneno yako. Wahimize kujionea na kulibeba jukumu lao wenyewe. {TN13: 27.4}

Kwa maana “nuru ya thamani itangaza kutoka katika Neno la Mungu, na mtu yeyote asidhanie kuamuru ni nini kitakacholetwa au kutoletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangazisha Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yoyote nafasi yake ya mamlaka, hakuna mtu aliye na haki ya kuizimisha nuru kutoka kwa watu. Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndio sababu jumbe za mbinguni hazijawafikia.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {TN13: 28.1}

Kumbuka kwamba kila mtu anayo haki

28

kuamini anavyotaka, na kwamba lazima atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Bwana tu, sio kwako. Wapatie wote uhuru wa kidini ambao ungetaka wao kukupatia. Na ingawa Mkristo hawezi kamwe kuusalimisha kanuni, bado daima atakuwa mwangalifu kwa wale wasiokubaliana naye kama vile wale wanaokubaliana naye. {TN13: 28.2}

“Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.” Mat. 7:12. Naam, hivyo ndilo fundisho kwa wote wawili. Na ili kuzipokea zawadi hizi zote takatifu, lazima

Uache Majivuno, Kujiamini Nafsi, Kiburi Cha Maoni, Kuchukia Bila Sababu. {TN13: 29.1}

“Mungu anawaita wale wanaoshikilia nyadhifa katika kazi za shule ya Sabato kuweka mbali majivuno yote, kujiamini nafsi, na kiburi cha maoni; iwapo ujumbe unakuja ambao huuelewi, vumilia ili uweze kusikia sababu ambazo mjumbe ataweza kutoa, ukilinganisha andiko kwa andiko, ili uweze kujua iwapo ndio au la unategemezwa na Neno la Mungu. Ikiwa unaamini kwamba nafasi zilizochukuliwa hazina Neno la Mungu kwa msingi wake, ikiwa nafasi unayoshikilia juu ya suala haiwezi kupingwa, basi zalisha sababu zako thabiti; kwa maana nafasi yako haitatikiswa kwa kukutana na makosa. Hakuna wema wala ubabe kwa kuendeleza vita daima gizani, kufumba macho yako usije ukaona,

29

kuziba masikio yako usije ukasikia, kuufanya moyo wako mgumu kwa ujinga na kutoamini ili usije ukajinyenyekeza na kukiri kwamba umepokea nuru juu ya mambo fulani ya ukweli. {TN13: 29.2}

“Kujitenga mbali na uchunguzi wa ukweli si njia ya kutekeleza agizo la Mwokozi ‘kuyachunguza Maandiko.’ Je, ni kuchimba hazina zilizofichwa kuyaita matokeo ya kazi ya mtu fulani rundo la takataka, na kutofanya uchunguzi wa kina ili kuona iwapo vipo vito vya thamani katika kusanyiko la wazo ambalo unahukumu? Je! Wale wote walio karibu na kila jambo kujifunza kujiweka mbali na kila mkutano ambapo ipo fursa ya kuzichunguza jumbe zinazokuja kwa watu, kwa sababu tu wanadhani maoni yanayoshikiliwa na walimu wa kweli yanaweza kuwa kinyume na lile wamepokea kama ukweli? Hivyo ndivyo kwamba Wayahudi walifanya katika siku za Kristo, na tumeonywa kutotenda walivyofanya na kuongozwa kuchagua giza badala ya nuru kwa sababu ndani yao ulikuwa moyo mwovu wa kutoamini kwa kumwacha Mungu aliye hai. Hakuna hata mmoja kati ya wale wanaofikiri kwamba wanajua yote ni mkongwe sana au wenye akili sana kujifunza kutoka kwa wanyenyekevu wa wajumbe wa Mungu aliye hai.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, kur. 65, 66; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28-30. {TN13: 30.1}

Bwana pekee yake, zaidi ya hayo, aliye na wajibu kwa wokovu wako, na Yeye tu ndiye

30

unayewajibikia dhambi zako. “Mwacheni” baadaye “mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” Isa. 2:22. Usiwe usiyejiweza kwa kuruhusu wengine kukufikiri kwa niaba yako, ila

Tumia Zawadi Ya Akili Na Kufikiri. {TN13: 30.2}

“Wote wanapaswa kuwa makini juu ya kuwasilisha maoni mapya ya Maandiko kabla ya kutoa maelezo haya kupitia kujifunza, na wamejiandaa kikamilifu kuyategemeza kutoka kwa Biblia. Usiwasilishe kitu chochote kitakachozusha mgawanyiko, bila ushahidi wazi kwamba ndani yake Mungu anatoa ujumbe maalum kwa wakati huu. {TN13: 31.1}

“Bali jihadharini na kukataa kile ambacho ni kweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na tabia ya kuipekua Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, huwa na imani katika watu wanaoongoza, na huyakubali maamuzi ambayo wao hufanya; na hivyo wengi watazikataa hasa jumbe ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazipokea. {TN13: 31.2}

“Hakuna yeyote anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ambayo ipo kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia jambo hili. Amesema, “Nimeuweka mbele yako mlango wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.” Hata kama watu wetu viongozi wote wataikataa nuru na kweli, mlango huo utasalia kuwa wazi. Bwana atawainua wanadamu ambao watapeana kwa watu ujumbe

31

wa wakati huu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, kur. 106, 107. Mkristo anayetafuta ukweli hatathamini tu zawadi zote za Mungu zilizotajwa hapo awali lakini pia ataheshimu sawa sawa

Zawadi Ya Uongozi. {TN13: 31.3}

Kwa hiyo “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.” Rum. 13: 1, 2. {TN13: 32.1}

Mamlaka ya Mungu yakuwa ni ya upeo na kamili, “Wakristo kwa ujumla” daima watahiari kumsujudia Mfalme wa mbingu na dunia, ambapo kwa uaminifu wakitafuta kumpa “Kaisari vitu vya Kaisari, na kwa Mungu vitu vilivyo vya Mungu.” Luka 20 : 25. “. . . wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.” Rum. 13: 7. {TN13: 32.2}

Hivi “hawatadaiwa na mtu chochote” maadamu matakwa ya anayedai au mahitaji yake hayahitilafiani na sheria na maagizo ya Mungu. Kama “Wakristo kwa ujumla” watakuwa wa kweli kwa Mungu na kwa wanadamu alivyokuwa Danieli na alivyokuwa Yusufu. {TN13: 32.3}

Wakati “mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; . . . hawakuweza kuona sababu wala kosa. “ Dan. 6: 4. Walipompata hakuwa na hatia, adui zake “walifanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na

32

kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ‘ila kwako,’ Ee mfalme ‘atatupwa katika tundu la simba.’” Aya ya 7. {TN13: 32.4}

Kwa kupata saini ya mfalme juu ya amri, walitaka kubuni hali ambayo lazima kwa uhitaji imuhusishe Danieli katika tendo la uasi dhidi ya mfalme. Walijua kwamba ingawa alikuwa na nia ya kutoa utiifu kwa mfalme, hangeweza kufanya hivyo kwa gharama ya kuonyesha kutomtii Mungu wake. Na kwa vile aliendelea kumwomba Mungu wake kama vile asingeweza kutofanya, alitupwa katika “pango la simba.” Lakini Yule ambaye alikuwa akimwomba aliyaokoa maisha yake kutoka kwa wanyama wa kunyafua. {TN13: 33.1}

Na katikati ya watumwa wa Misri ya kale kinainuka kimo chenye utukufu cha Yusufu, mtoaji mkuu ambaye dunia imewahi kuona. Mtazame kwa uaminifu imara kwa serikali yake, akiinuka kwa heshima mpaka akapewa kushiriki kiti cha enzi hasa cha Farao mwenyewe! {TN13: 33.2}

Kutoka kwa mifano hii na mingineyo ya Biblia, ni dhahiri kwamba uaminifu wa mtu kwa serikali yake ni ahadi yake ya utii kwayo — heshima kwa bendera yake. Kwa jumla, kwa hiyo, tunaona kwamba ambapo kwa upande mmoja mtu kutokuwa mwaminifu kwa serikali ya Mungu ni dhambi dhidi ya Mungu, kwa upande mwingine kutokuwa mwaminifu kwa serikali ya taifa lake ni dhambi dhidi yake, pia isivyo moja kwa moja kwa Mungu, maana kutokuwa mwaminifu kwa serikali ya mmoja ni kutotii amri safi ya Mungu: “Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka

33

na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema.” Tito 3: 1. “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.” 1 Pet. 2:13, 14. {TN13: 33.3}

Kama bendera ya taifa sio sanamu au hirizi ila nembo, kiwango, hivyo kuiheshimu sio ibada ya sanamu, kama wengine wanavyofikiri, ila badala yake kukiri hadharani uaminifu wa mtu kwa serikali ya taifa lake, kama vile tu ubatizo ni ungamo la mtu la uaminifu kwa serikali ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. {TN13: 34.1}

Kwa amri ya Mungu, Waisraeli walifanya viwango (bendera) kulingana na makabila yao, kwa madhumuni yote ya utambulisho na kuthibitisha uaminifu wao kwa kile ambacho bendera zilisimamia. (Angalia Hesabu 2.) {TN13: 34.2}

Dhahiri, kwa hiyo, kusema kwamba ni ibada ya sanamu kwa mtu kuiheshimu bendera ya taifa lake, itakuwa ni kumshtaki Mungu kwa kulazimisha ibada ya sanamu sio juu ya watu Wake wa kale ila, kwa mfano wao, pia juu ya waaminifu wa wakati wote tangu hapo! {TN13: 34.3}

Hivyo kila Mkristo ambaye angeweza kuzitii amri za Mungu, lazima awe mwaminifu kwa nchi ambamo anaishi. Kwa hiyo kama Wakristo ndani ya Marekani, waliojitolea kwa Mungu, na hivyo waaminifu kwa kanuni za haki za hii huru “serikali chini

34

ya Mungu,” tunatoa mioyo yetu, mawazo yetu, mikono yetu, yetu yote, kwanza kwa bendera

ya Ufalme wa milele wa Mungu, na kwa Serikali inayoongozwa na Mungu ambayo inasimama, watu wamoja wa ma-taifa yote, na waliofungwa kwa kamba za upendo wa milele, uhuru, usafi, haki, amani, furaha, nuru na maisha kwa wote; na pili, kama Wamarekani, kwa bendera

“ya Majimbo ya Marekani Yaliyoungana na Jamhuri ambayo inasimamia, Taifa moja,

35

lisilogawanyika, na uhuru na haki kwa wote.” {TN13: 34.4}

Na maadamu tu Utukufu wa Kale unakunjuka wenyewe kamba nembo ya kanuni safi za Katiba za nchi hii ya watu huru, kwa muda mrefu ni ahadi yetu ya utiifu kwayo jambo lisilovunjwa. {TN13: 36.1}

Na sasa hebu tuisikie

Jumla Ya Mambo Yote. {TN13: 36.2}

Kwa kila mtu ambaye kwa kweli huzithamini zawadi hizi za thamani, ambaye anashika kile alicho nacho kwamba mtu asiichukue taji yake (Ufu. 3:11), inapiga kengele habari njema: “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Ufu. 22:12. {TN13: 36.3}

“Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.” {TN13: 36.4}

“Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. . . Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.” {TN13: 36.5}

“Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.” {TN13: 36.6}

“Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo,

36

kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.” {TN13: 36.7}

“Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.” {TN13: 37.1}

“Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.” {TN13: 37.2}

“Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.” {TN13: 37.3}

“Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” {TN13: 37.4}

“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.” Ufu. 2: 7, 11, 10, 17, 26-28; 3: 5, 12, 21, 20, 22. {TN13: 37.5}

Na hatimaye, ikiwa unajihisi unamhitaji Yeye, na unayo nia ya kupokea zawadi zote kupitia Kwake, hata zawadi ya Roho ili kukuongoza katika Kweli yote (Yohana 14:17; 16:13), basi uweze kwa kutambua kwamba sala ya mwenye haki inayo nguvu sana, kwa kicho sujudu ukiwa

37

unasoma, na umruhusu Mwenye haki Yote akuletee baraka za mbinguni katika

Sala yake. {TN13: 37.6}

“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.” Mat. 6: 9-13. {TN13: 38.1}

MAELEZO KUHUSU BIBLIA

Biblia inasheheni barua 3,566,480, maneno 773,693, aya 31,102, sura 1,189, na vitabu 66. Sura ndefu zaidi ni Zaburi ya 119; sura fupi na ya katikati ni Zaburi ya 117. Aya ya katikati ni 8 ya Zaburi 118. Jina la refu zaidi ni katika sura ya 8 ya Isaya. Neno “na” hutokea mara 46,277; neno “Bwana” mara 7,698. Sura ya 37 ya Isaya na sura ya 19 ya 2 Wafalme ni sawa. Aya ndefu zaidi ni ya 9 sura ya 8 ya Esta, na aya fupi zaidi ni ya 35 sura ya 11 ya Yohana. Kila herufi ya alfabeti isipokuwa “j,” itapatikana katika aya ya 21 ya Ezra 7. “Mungu” hakutajwa katika kitabu cha Esta. {TN13: 38.2}

—– 0-0-0 —–

“Biblia ni fuawe ambayo imechakaza nyundo nyingi.” {TN13: 38.3}

38

MJI WA NEW YORK NA YERUSALEMU MPYA

Tazama kwa muda mfupi Mji wa New York, mwenzi wa miji ya Magharibi! — {TN13: 39.1}

Idadi yake ya watu sasa ni 7,454,995 na eneo la jumla ni maili 327 1/2 mraba, ikiwa ni pamoja na uso wa Maji; wakati uso wa ardhi pekee yake ni maili 285 mraba. {TN13: 39.2}

Jengo lake lililoinuka juu zaidi ni Jumba la Empire State, refu zaidi duniani. Husimama kuwa ajabu kwa mtazamo wa watu, na changamoto kwa hofu yao. Mnara wake wa fahari huinuka katika uzuri rahisi hadi urefu ambao awali haukuwahi kufikiwa na wajenzi wafaji — orofa 103, au futi 1,250, karibu robo ya maili ya umbali wa wima! Hili refu zaidi ya majengo yote ya binadamu tena ni nusu zaidi juu ya Jumba la Woolworth, na zaidi ya kilele cha Jumba la Chrysler kwa futi 204, na kivuli kwa Mnara Eiffel na futi 266! {TN13: 39.3}

Lakini angalia kipeo cha macho kilele cha mji huu mkubwa na fahari ya miundo ya majengo yake ya kujivunia yanakuwa mbilikimo na kutoweka kabisa, maadamu jicho linapotazama Yerusalemu Mpya, mji wa Mungu, ukitanda na kuinuka dhahiri na juu zaidi ya maarifa ya wanadamu, katika hali isiyoelezeka ya kustaajabisha, kubwa sana, yenye fahari, katika utukufu usiotamkika! — {TN13: 39.4}

“Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake: . . . ulikuwa kama maili elfu na mia tano.” Ufu.21:16. {TN13: 39.5}

39

Mji huo ni maili 375 kila upande, na kufanya mraba mkamilifu. Eneo lake, kwa hiyo, ni maili mraba 140,625, au ekari 90,000,000, au futi mraba 3,920,400,000,000 – takribani mara 430 zaidi kuliko eneo la Mji wa New York! Kuruhusu futi 100 mraba kwa kila mtu, au nafasi mraba futi 10, mji huo ungekuwa na watu 39,204,000,000, au ka-ribu mara 20 idadi ya watu duniani. {TN13: 40.1}

Na “marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.” (Ufu. 21:16) – maili 375 kila upande, na maili 375 kimo, utukufu wake wa kuinuka hadi kimo ambacho hakijawahi kuotewa na akili! {TN13: 40.2}

Na kuta zake (“dhiraa mia na arobaini na nne,” au kimo cha futi 216) zimejengwa kwaa yaspi, na “mji” wa “dha-habu safi, mfano wa kioo safi.” Malango yake kumi na mawili ni “lulu kumi na mbili; kila lango. . . lulu moja.” Na juu yake yameandikwa majina ya kabila kumi na mbili za wana wa Israeli. Na njia ya mji ni “dhahabu safi, kama kioo kiangavu.” {TN13: 40.3}

Misingi ya ukuta wa mji “ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna.” {TN13: 40.4}

Hakika lugha ni fukara kuelezea Mji Mtakatifu. Kweli, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuya-sikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Kor. 2: 9. {TN13: 40.5}

40

SHUGHULI WAKILISHI NA MATUKIO KATIKA HISTORIA YA VUGUVUGU LA UJIO

1831

Jumapili ya kwanza Agosti, William Miller alitangaza mahubiri yake ya kwanza juu ya kuja kwa Kristo. {TN13: 41.1}

1840

Machi, William Miller alitoa mhadhara wa kwanza kwa mfululizo wa masoma huko Portland, Maine. Yalihudhuriwa na Ellen G. Harmon, baadaye Bi. E. G. White. {TN13: 41.2}

1844

Sabato ya siku ya Saba kwanza ililetwa kwa uangalifu wa umma wa Waadventista huko Washington, New Hamp-shire, na Bi. Rachel D. Preston, Mbabtisti wa Sabato, kutoka Jimbo la New York. {TN13: 41.3}

1845

Ellen G. Harmon alipewa maono yake ya kwanza, juu ya “Safari ya Watu wa Ujio hadi kwa Mji Mtakatifu.” {TN13: 41.4}

1846

James White alimwoa Ellen Gould Harmon, Agosti 30. Kipeperushi cha kurasa mbili na Bi E. G. White, chenye kichwa, “Kwa Masalia Waliotawanyika Mbali,” kilichapishwa. {TN13: 41.5}

1848

Mkutano wa kwanza wa watunza Sabato uliofanyika Rocky Hill, Connecticut, Aprili 20, 21. Bi. E. G. White alikuwa na maono kuhusu mwanzo wa kazi ya uchapishaji. {TN13: 41.6}

1849

Nambari nne za kwanza za chapisho lenye kichwa, Ukweli wa Sasa, lililochapishwa huko Middletown, Connecti-cut. {TN13: 41.7}

41

Ushuhuda wa kwanza kwa Kanisa, ulioelekezwa “Kwa Wale Ambao Wanapokea Muhuri wa Mungu Aliye Hai.” Saini “E. G. White.” {TN13: 41.8}

1852

Namba ya kwanza ya Mapitio ya Ujio na Kutangaza Sabato iliyochapishwa huko Rochester, New York. James White aliiandalia ofisi ya kwanza ya uchapishaji fedha zilizopatikana kwa michango. Michango ilifikia $ 655.84. Gha-rama ya vifaa ilikuwa $ 652.95. Matbaa ya kwanza kununuliwa ilikuwa Washington matbaa ya mkono. Namba ya kwanza ya Mkufunzi wa Vijana ilitokea Agosti. {TN13: 42.1}

1853

Shule ya Sabato ya kwanza ya kawaida ilianzishwa huko Rochester na Buck’s Bridge, New York. {TN13: 42.2}

1854

Mkutano wa kwanza wa kambi ulioongozwa na J. N. Loughborough na M. E. Cornell kwenye Battle Creek, Michigan, Juni 10-12. {TN13: 42.3}

1860

Jina Waadventista wa Sabato lilitoholewa kwa ajili ya dhehebu Oktoba 1. {TN13: 42.4}

1861

Shirika la Uchapishaji la Waadventista wa Sabato (sasa Shirika la Uchapishaji la Mapitio na Kuhubiri) liliingizwa Mei 1. Makanisa kwa mara ya kwanza yakapangwa rasmi. {TN13: 42.5}

1863

Baraza Kuu lilipangwa katika mkutano uliofanyika huko Battle Creek, Michigan, Mei 20-23. John Byington alichaguliwa rais wa kwanza wa Baraka Kuu. {TN13: 42.6}

42

1865

Chapisho la kwanza la afya, “Jinsi ya Kuishi,” kilichapishwa. Kiliandikwa na kuandaliwa na Bi. E. G. White. {TN13: 43.1}

1866

Taasisi ya Matengenezo ya Afya (Zahanati ya Battle Creek) ilifunguliwa kwa wagonjwa, Septemba 5. {TN13: 43.2}

1872

Shule ya kwanza ya dhehebu ilifunguliwa, Juni 3, huko Battle Creek, Michigan. G. H. Bell msimamizi. {TN13: 43.3}

1874

Jumuiya ya Elimu ya Waadventista wa Sabato iliingizwa Machi 11. Namba ya kwanza ya Ishara za Nyakati ilitokea. J. N. Andrews, mmishonari wa kwanza wa kigeni alisafiri baharini kutoka Boston, Septemba 15. {TN13: 43.4}

1881

James White alikufa akiwa Battle Creek Michigan, Agosti 6. (Alizaliwa Agosti 4, 1821.) {TN13: 43.5}

1888

Ujumbe wa “Haki kwa Imani” uliwasilishwa kwenye Mkutano wa Minneapolis na kukataliwa. {TN13: 43.6}

1889

Jumuiya ya Kitaifa ya Uhuru wa Kidini ilianzishwa Julai 21. {TN13: 43.7}

1900

Ujumbe wa “Haki kwa Imani” hatimaye ulikataliwa na wote uongozi na waumini. {TN13: 43.8}

1903

Makao makuu ya Baraza Kuu yalihamishwa hadi Washington, D. C., Agosti 10. {TN13: 43.9}

1915

Bi Ellen G. White alikufa Julai 16, huko St. Helena, California. (Alizaliwa Novemba 26, 1827.) {TN13: 43.10}

43

JEDWALI LA MPANGILIO WA KUINUKA NA USITAWI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

1929

Somo la Kwanza la Ukweli wa Sasa lilitolewa (Isa. 54) Januari 6. {TN13: 44.1}

1930

Ukweli wa watu 144,000 ulifunuliwa Februari 1.

Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, Muswada, nakala 33, ziliwasilishwa kwa ndugu viongozi wa dhehebu la S.D.A., mwezi Juni.

Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, nakala 5,000 zilichapishwa Desemba 4. {TN13: 44.2}

1931

Muambata Fimbo ya Mchungaji wa Kwanza, atengwa kutoka kanisa la S.D.A.

S.D.A. wa kwanza Daktari wa matibabu aliupokea ujumbe mwezi Julai. Zaka ya kwanza kutumwa ilipokelewa Sep-temba 9. {TN13: 44.3}

1932

Safari ya kwanza iliyofanywa kwa aslahi ya ujumbe, Oktoba.

Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, nakala 5,000, zilichapishwa Oktoba 2.

Mkutano wa kwanza ulifanyika katika ukumbi wa umma Novemba 12. {TN13: 44.4}

1933

Mwamini wa kwanza kuuacha ujumbe.

Mtendakazi wa kwanza alitumwa shambani Februari 14.

Trakti Namba 1, Toleo la Kwanza, nakala 3,000, zilichapishwa Agosti 24.

Mchungaji wa kwanza wa S.D.A. aliupokea ujumbe Desemba 15.

44

Trakti Namba 2, Toleo la Kwanza, nakala 3,000 zilichapishwa Desemba 29. {TN13: 44.5}

1934

Kamati ya uchunguzi ya Baraza ilikutana na V.T. Houteff Februari, 25.

Mkutano wa kwanza ulifanyika Februari 25 hadi Machi 12.

Trakti Namba 3, Toleo la Kwanza, nakala 5,000 zilichapishwa Mei 24.

Toleo la Kwanza la Msimbo wa Nembo, ilichapishwa Julai 15.

Trakti Namba 4, Toleo la kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Agosti 28. {TN13: 45.1}

1935

Trakti Namba 5, Toleo la kwanza, nakala 6,000 zilichapishwa Mei 16. Makao makuu yalihamishwa hadi Waco, Texas, Mei 24. {TN13: 45.2}

1936

Kanisa la S.D.A. Waco, Texas, lilifungwa kwa waambata wa Fimbo ya Mchungaji mwezi Machi.

Trakti Namba 6, Toleo la Kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Juni 8.

Trakti Namba 7, Toleo la kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Juni 8. {TN13: 45.3}

1937

Katiba na Kanuni za wa Fimbo ya Mchungaji Waadventista wa Sabato ziliandikwa.

Trakti Namba 8, Toleo la kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Novemba 15. {TN13: 45.4}

1938

Safari ya kwanza ya Ulaya ilifanywa, Mei 21. {TN13: 45.5}

1940

Trakti Namba 9, Toleo la Kwanza, nakala 15,000, zilichapishwa Januari 31.

Trakti Namba 10, Toleo la Kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Agosti 24.

Trakti Namba 11, Toleo la kwanza, nakala 6,000, zilichapishwa Agosti 23. {TN13: 45.6}

45

1941

Masomo ya Kwanza ya Shule ya Sabato kwa watu Wazima yalitumwa.

Bendera ya Ufalme wa Kristo ilibuniwa mwezi Novemba.

Trakti Namba 13, Toleo la Kwanza, nakala 25,000 zilichapishwa Desemba 10. {TN13: 46.1}

1942

Mfululizo wa masomo ya Waalimu wa Biblia (kuandikiana) ulianza.

Mtaala wa Daftari na Mwongozo wa Kanuni, nakala 5,070, zilichapishwa Novemba 28. {TN13: 46.2}

1943

Ushirika uliitwa “Jumuiya ya Jumla ya Wadaudi Waadventista wa Sabato.”

Walawi (Katiba na Kanuni) za Wadaudi Waadventista wa Sabato, nakala 5,075, zilichapishwa Februari 12.

Ya kwanza Masomo ya Shule ya Sabato ya Watoto Wadaudi yalitumwa (Chekechea & Vitengo vya Msingi na vya Kati).

Misingi ya Imani na Mipangilio orodha ya Wadaudi Waadventista wa Sabato, nakala 5,100, zilichapishwa Machi 4.

Trakti Namba 14, Toleo la kwanza, nakala 35,095 zilichapishwa Aprili 30.

Vya kwanza Vyeti vya Ushirika vilitolewa, pamoja na Vyeti vya Wasifu wa Uchungaji, Juni.

46

Vyeti vya Kuachia vilitolewa kwanza, Septemba. {TN13: 46.3}

1944

Cha Kujibu, Kitabu cha Kwanza, nakala 29,760 zilizochapishwa Mei.

Cha Kujibu, Kitabu cha Pili, nakala 29,564 zilichapishwa mwezi Juni.

Cha Kujibu, Kitabu cha Tatu, nakala 29,815, zilichapishwa Julai.

Cha Kujibu, Kitabu Nne, nakala 30,000, zilichapishwa Agosti.

Cha Kujibu, Kitabu cha Tano, nakala 30,000, zilichapishwa Desemba. {TN13: 47.1}

USTAWI WA MLIMA KARMELI

1935

Mahali palinunuliwa, Machi 15.

Uhamisho wa Ofisi kutoka Los Angeles, Mei 17.

Kuwasili kwa wageni wa kwanza, Mei 24.

Jengo la kwanza lilimilikiwa Septemba. Kifo cha kwanza, Desemba 2.

Jengo la Kwanza la Ofisi lilijengwa. Bweni la kwanza lilijengwa (Jengo Namba 4). {TN13: 47.2}

1936

Shirika la Kimataifa la Ki- biashara lilianzishwa, Machi.

Mfumo wa simu uliwekwa Juni.

Shule ya Mlima Karmeli ilifunguliwa, Septemba.

Bwawa Namba 1 lilijengwa. {TN13: 47.3}

1937

Ndoa ya kwanza ilihalalishwa, Januari 1.

Msingi uliwekwa wa bwawa la Ziwa Meribah (Bwawa Namba 2), Aprili 7.

Kiunga cha Pichi Namba 1 kilipandwa, Februari na Machi.

47

Birika la kuhifadhi maji lilikamilika, Novemba.

Pampu ya maji na mtambo wa upepo ulisakinishwa. {TN13: 47.4}

1938

Benki ya Palestina ilianzishwa Januari 1.

Nguvu ya umeme ya mji iliwasilishwa Septemba 10.

Hati ya Mlima Karmeli ilisambazwa, Februari. Ya kwanza sherehe ya harusi maradufu ilifanyika Mei 27.

Njia Kuu ya Mfalme ilipitia kati. {TN13: 48.1}

1939

Uadhimishaji wa kwanza wa mapitio ya historia ya kila mwaka, Oktoba 25 — Siku ya Siku.

Mtoto wa kwanza alizaliwa, Oktoba 26. {TN13: 48.2}

1940

Jengo la usimamizi lilikamika na Ofisi kuhamishiwa humo, Januari 21.

Mfumo wa sauti uliwekwa.

Huduma ya kuandaa chakula kusanyikoni ilizinduliwa, Aprili 10. {TN13: 48.3}

1941

Vyoo vya umma na bafu vilijengwa. {TN13: 48.4}

1942

Njia za kupitia kati ya vilima vya Mlima Karmeli. {TN13: 48.5}

1943

Jina Taasisi ya Wadaudi Walawi lilipitishwa. Jengo la Sayansi ya Nyumbani lilianzishwa. {TN13: 48.6}

1944

Kitengo cha kwanza cha Zahanati kilijengwa. Kituo cha kujaza Mafuta kiliwekwa.

Toleo la kwanza la kiungo cha ndani, Mpiga Panda, lilisambazwa Aprili 7. {TN13: 48.7}

48

KUUTENGENEZA MCHANA KUWA SARAFU ZA DOLA.

Fikiria nini maana ya kuigeuza mikono ya wakati mbele kwa saa moja hadi upande mwingine wa bara zima! Hiyo ndivyo hasa Mjomba Sam alivyofanya saa 8 Alfajiri. Jumatatu ya pili Februari 1942. Na ghafla! Kama kwa mazingaombwe, taifa letu kubwa la watu takribani 132,000,000 lilibadilisha utaratibu wa maisha yao. Labda umepata kuwa vigumu kidogo wakati mwingine kuamka saa moja kabla ya kawaida, lakini fikiria tu kupata idadi kubwa ya watu 132,000,000 nje ya kitanda saa moja mapema, kuanzia siku fulani. Hivi ndivyo tu Serikali yetu ilivyofanya na Sheria yake ya Kuokoa Mchana mwaka wa 1918, na tena mwaka wa 1942. Bila kufungwa, bila mkanganyo hata mdogo au usumbufu, mtambo mzima wa maisha na biashara ulianza kuenenda katika ratiba mpya na halisi, “kuutengeneza mchana kuwa sarafu za dola.” Ilikuwa imepatikana hapo awali kwamba kizuio cha amri ya serikali kwa matumizi ya wonyesho wa ishara kutumia umeme kwa masaa fulani kiliokoa tani 8,000 za makaa ya mawe kwa mwezi, au zaidi ya tani 400,000 kila mwaka. Chini ya Sheria ya Kuokoa Mchana, kupungua kwa ma-tumizi ya mwangaza wa bandia nyumbani na maeneo ya umma yalimaanisha kuokoa kwa mwaka makaa ya mawe pekee tani milioni kadhaa. Ilhali uchumi wa jumla, ikiwa ni pamoja na kuokoa mafuta kutumika katika taa na kutengeneza gesi mwaka 1918, kulikisiwa na Rais wa Chama cha Marekani cha Ustawi wa Sayansi, kwa $ 25,000,000. Sheria ilidumu miezi sita tangu Machi hadi Oktoba. Upinzani wa wakulima ambao waliona kuwa haiwezekani kuhusiana na msaada wa shambani ulisaba-bisha kufutwa kwake mwaka wa 1919. – Imetoholewa kutoka kwa Kitabu Kipya cha Marejeo ya Mwanafunzi. {TN13: 49.1}

49

KUUTENGENEZA MCHANA KUWA SARAFU ZA DOLA.

(Endelezo)

Hapa kinaonekana ni nini shirika kitaifa na uchumi vinaweza kulifanyia taifa kwa ujumla na kwa kila mmoja. Sare kwa umakini shirika la nyumbani na uchumi vitafanya sawa kwa ajili ya nyumba na kwa kila mshirika wake. Panga, na ziba kila tundu! Usizifanyie ubadhirifu zawadi za Mungu — muda wako, nguvu yako, raslimali zako: Ruhusu “kila wakati usio na msamaha” toa “sekunde sitini za thamani ya umbali kukimbia”; kila harakati, ufanisi mkamilifu; na kila senti, kwa uzuri kamili. {TN13: 50.1}

Tumia sana kila haki na fursa yako yote, na ukumbuke kwamba makombo yaliotawanyika yanapokusanywa hufanya “vikapu vilivyojaa”. {TN13: 50.2}

“Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.” Mit. 28:19. {TN13: 50.3}

“Mwendee chungu,. . . zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. . . bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono upate usingizi” (Mit. 6: 6-11), huleta umaskini na hitaji. {TN13: 50.4}

50

MJOMBA SAM NA WAKATI WAKE WA KIWANGO

Picha hii inaonyesha jinsi Serikali inavyowasaidia watu kuweka saa zao na zamu sare kote kote nchini mwetu na kwenye meli baharini. Vidude rasmi vya saa huko Washington hurekebishwa kutokana na uchunguzi unaochukuliwa kila usiku ulio safi wa nafasi za nyota fulani, na kwa siku inayofuata saa sita adhuhuri masaa ya vidude hivi hutumwa. — Kitabu Kipya cha Marejeo ya Mwanafunzi. {TN13: 51.1}

51

Kama unavyoona kutoka kwenye mchoro, adhuhuri au saa 6 kamili, ni bila kukawia chini ya Jua, kwa mujibu wa Saa ya Jua, lakini ikiwa ingeachwa kwa maamuzi ya kibinafsi ya watu, mashariki au magharibi ya ncha hizi, kama wakati wa kutwa, ungekuwapo mkanganyiko mwingi, ambao mara nyingi ungeongoza kwenye maafa, kama katika mbio za treni kwa njia ya reli. Kwa hivyo mjomba Sam anaigawanya nchi katika sehemu nne na kwa kujiamulia anaweka kiasi cha umbali kwa pande zote za meridiani zilizotolewa wakati unaoashiriwa na jua kwa hizo meridiani utatanda. Kwa mfano, sehemu ya Pwani ya Magharibi inachukua wakati wake kutoka meridiani ya 120; sehemu ya Majimbo ya Milima ya Rocky kutoka meridiani ya 90; Majimbo ya Mashariki kutoka meridiani ya 75. Huu ndio huitwa Wakati wa Kiwango, na unatofautiana na Nyakati za Jua katika ncha zote mashariki na magharibi ya meridiani hizi zilizowekwa. {TN13: 52.1}

52

UGAVI WA NYAKATI ZA VIWANGO ZA AMERIKA

53

54

MAMBO YA THAMANI KUYAJUA

MTO MREFU SANA duniani, Mississippi-Missouri, ni maili 4,200 kwa urefu. Mto Nile ni wa pili — maili 4,000 kwa urefu. {TN13: 55.1}

Mlima Everest, KIPEO CHA JUU ZAIDI duniani, huinuka kwa kimo cha futi 29,000 juu ya usawa wa bahari, umbali wa takriban maili tano na nusu. Uko katika safu ya Himalaya kwenye mipaka ya Tibet na Nepal, kaskazini mwa India ya Uingereza. {TN13: 55.2}

MWANGA husafiri kwa kiwango cha maili 186,000 kwa sekunde. {TN13: 55.3}

SAUTI hutofautiana, husafiri kwa kasi katika maji kuliko ndani ya gesi, na bado kwa kasi zaidi katika maumbile ya ugumu. Hewa hueneza sauti kwa kiwango cha mita 1,100 kwa sekunde, lakini hutofautiana kidogo na hali ya joto la anga. Sauti iiliyoenezwa kupitia maji ya joto husafiri kati ya futi 4,700 na 4,800 kwa sekunde. Kupitia njia ya kioo, chuma cha pua au chuma, sauti husafiri kwa karibu futi 16,500 kwa sekunde. {TN13: 55.4}

Kwenye ikweta, NUSU KIPENYO ya dunia ni maili 3,963,399; kwenye ncha maili 3949,992, tofauti ya maili 13,407. {TN13: 55.5}

Umbali wastani kutoka kwa dunia hadi kwa JUA ni maili 92,900,000. {TN13: 55.6}

Umbali wastani kutoka kwa dunia hadi kwa MWEZI ni maili 238,854.

55

Mwanzoni mwa Vita Kuu vya 2 vya Dunia, walikuwapo WATAWALA WENYE ENZI 30 waliokuwa wakita-wala katika nchi zao. Mnamo Mei, 1944, 18 tu walisalia kwa hatamu halisi katika nchi zao, sio uhamishoni au katika utiifu kwa taifa lingine. (Tazama Trakti Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho, uk. 66.) {TN13: 55.7}

Vita Kuu vya 1 vya Dunia vilianza mnamo Julai 28, 1914, na kumalizika kwa mkataba Novemba 11, 1918, na kudumu siku 1567. {TN13: 56.1}

Vita vya 2 vya Ulimwenguni, vilianza Septemba 1, 1939, vikavuka siku ya 1567 mnamo Desemba 15, 1943, na vikaingia siku ya 1889 mnamo Novemba 1, 1944. Kwa hiyo Vita Kuu vya 2 vimekuwa vya muda mrefu zaidi katika historia, na tayari vimegharimu zaidi katika damu na taabu za kibinadamu na utajiri wa kitaifa kuliko msiba wa 1914-1918. {TN13: 56.2}

SHERIA ZA BIASHARA

WAKUU wanawajibika kwa vitendo vya mawakala wao. {TN13: 56.3}

MIKATABA ILIYOANDIKWA KUHUSU ARDHI lazima iwe chini ya muhuri. {TN13: 56.4}

VYETI havizalishi RIBA isipokuwa kama imebainishwa hivyo. {TN13: 56.5}

IWAPO CHETI KIMEPOTEA AU KUIBWA, mtengenezaji haachiliwi iwapo nadhiri na kiasi vinaweza kuthibitishwa. {TN13: 56.6}

VYETI VYA MADAI vinapaswa kulipwa wakati vimewasilishwa bila neema, na vinazalisha riba kisheria baada ya dai, ikiwa havijaandikwa hivyo. {TN13: 56.7}

56

MUIDHINISHAJI KWA CHETI CHA DAI anaweza kukamatwa tu kwa muda mdogo, hutofautiana katika Majimbo mbali mbali. {TN13: 57.1}

ILI KIWE CHA KUJADILIWA CHETI lazima ama kulipwe kwa aliyekizalisha au kiidhinishwe vizuri na mtu ambaye amri yake inatekelezwa. {TN13: 57.2}

IWAPO MWIDHINISHAJI anatumaini kuepuka jukumu, anaweza kuidhinisha bila “fursa ya kujitetea.” {TN13: 57.3}

VYETI AMBAVYO WAKATI WAVYO HUTIMIA JUMAPILI au likizo ya kisheria ni, kama sheria, hulipwa siku iliyofuata. {TN13: 57.4}

IWAPO CHETI KIMEVURUGWA kwa njia yoyote na mmiliki kinakuwa kitupu. {TN13: 57.5}

CHETI KILICHOTAYARISHWA NA MTOTO ni kitupu katika baadhi ya Majimbo na ni halali kwa uamuzi wa mahakama katika mengine. {TN13: 57.6}

MKATABA NA MTOTO AU MWENYE KICHAA ni mtupu. {TN13: 57.7}

IKIWA CHETI HAKIJALIPWA WAKATI WAKE UKITIMIA, waidhinishaji, ikiwa yeyote yuko, anapaswa kuarifiwa kisheria kukamatwa. {TN13: 57.8}

CHETI KILICHOPATIKANA KWA UFISADI au kutolewa na mtu mlevi hakiwezi kuchukuliwa. {TN13: 57.9}

NI UFISADI kuuficha ufisadi. {TN13: 57.10}

SAINI KWA KALAMU YA MKAA ni halali kisheria. {TN13: 57.11}

MATENDO YA MWENZI MMOJA huwafunga wengine. {TN13: 57.12}

Kila mtu katika USHIRIKA anawajibika kwa madeni yote ya kampuni isipokuwa katika suala la ushirikiano maalum. {TN13: 57.13}

57

Neno “MPAKA” kuhusiana na majina ya kampuni huashiria kikomo cha jukumu kwa kila mshirika. {TN13: 58.1}

AGANO bila kuzingatia thamani halipo. {TN13: 58.2}

“THAMANI ILIYOPOKELEWA” inapaswa kuandikwa kwenye hati, lakini sio lazima. Isipoandikwa, hutarajiwa na sheria au inaweza kuonyeshwa kwa ajili ya uthibitisho. {TN13: 58.3}

UANGALIFU hautoshi katika sheria iwapo sio halali katika asili yake. {TN13: 58.4}

MWIDHINISHAJI WA HATI ni huru kwa hasara ikiwa hajakabidhiwa ilani ya kutoiheshimu ndani ya masaa 24 ya kutolipa kwake. {TN13: 58.5}

RISITI YA PESA sio kamilifu kisheria. {TN13: 58.6}

YA KWAMBA FURAHA YAKO IJAE

Na sasa, ikiwa umechachawishwa, umethamini, na kufaidika na Zawadi hii, na iwapo unatumaini kwenda sam-bamba na ustawi wa Ukweli, wachapishaji wa kijitabu hiki kama huduma ya Kikristo watakutumia, kwa ombi, *ZAWADI ya ziada — mfululizo wa machapisho ya Ukweli wa Sasa, yenye vijitabu ishirini na moja, na vinavyoju-muisha kurasa 1,682, zilizoelezwa kikamilifu. Kinaweka tu dai moja — wajibu wa nafsi kwa ajili yake yenyewe kuyaja-ribu mambo yote na kulishika lililo jema. {TN13: 58.7}

*Kwa kuwa “ZAWADI ya ziada” tayari ni sehemu ya mkusanyiko huu, haipo. {TN13: 58.8}

58

FAHARISI YA MAANDIKO

59

 

>