fbpx

Trakti Namba 10

1

Hati miliki 1940, 1942

Haki zote zimehifadhiwa

V.T. Houteff

Katika nia ya kufikia kila akili inayotafuta ukweli ambayo inatumaini kuiepuka njia inayoongoza kwenye uharibifu wa mwili na roho, trakti hii inasambazwa bila malipo.

TRAKTI NAMBA 10

Toleo Lililosahihishwa

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Imechapishwa Marekani

2

“Ishara ya Yona” NA MAJADILIANO YA MASWALI NA MAJIBU.

MAT. 12:39, 40

Ingawa mara kadhaa tumehitimisha kuyajibu maswali kama (1) iwapo Yesu, ili kutimiza “ishara ya Yona,” alikuwa “siku tatu mchana na usiku” kaburini, au (2) iwapo ishara ilikuwa imetimizwa kwa namna nyingine na (3) ikiwa Yeye alisulubishwa siku ya Ijumaa, ya Alhamisi, au Jumatano, bado inaonekana yangalipo mambo ambayo hayajakuwa wazi kwa wote, la kwanza ni chanzo cha swali:

Je, Kristo Alisulubishwa Siku ile Chachu Ilikuwa Imetolewa nje ya Nyumba — Siku ya Kumi na Nne? {TN10: 3.1}

Marko, ambaye alikuwa shahidi wa tukio hilo anasema, “Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi Wake wakamwambia, Ni wapi utakapo twende tukuandalie uile pasaka? Akatuma wawili katika wanafunzi Wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji. . . Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona

3

kama Alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. Basi ilipokuwa jioni Yuaja pamoja na wale Thenashara. Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, Nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja Nami, atanisaliti.” Marko 14:12, 13, 16-18. {TN10: 3.2}

Kwa sababu kondoo wa Pasaka aliuawa jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza (Kut. 12:6), na kuliwa mwanzoni mwa siku ya kumi na tano (Hes. 28:17), na kwa sababu waandishi wa Injili hutangaza kwamba Yesu aliku-la Pasaka wakati uo huo taifa lote la Wayahudi lilipoila, ukweli umewekwa imara kwamba wakati wa kusulubishwa kwa Kristo haukulingana na wakati wa kumchinja kondoo siku ya kumi na nne kwa ajili ya siku kuu ya kwanza ya sherehe za Pasaka. Ilifanya sanjari, hata hivyo, na kuuawa kwa kondoo kwa ajili ya siku kuu ya pili, kama itakavyoon-ekana kutoka katika aya zifuatazo. {TN10: 4.1}

Hata rekodi za unajimu hukubali kwamba kafara ya siku ya kumi na nne ya chajio cha sikukuu ya Pasaka mwaka huo ilikuja Jumatano, na Biblia husisitiza wazi kwamba sikukuu ya Pasaka ilipaswa kufanyika siku ya kumi na tano (Hes. 28:17), Alhamisi mwaka huo. Yesu, kwa hivyo, haingewezekana kuwa Alisulubishwa kwa aidha moja ya siku hizi mbili. Hili linaelezewa kwa ukweli kwamba, jinsi ilivyoelezwa kabla Yeye alisherehekea sikukuu ya kwanza na wana-funzi. Isitoshe, Mathayo 26:5 hueleza wazi kwamba mkutano wa makuhani na waandishi pamoja na Kayafa katika

4

kiti cha hukumu, waliamua wasimuue Yeye kwa “siku ya karamu” — Alhamisi, siku ya kumi na tano. Hivyo swali: Mbona Biblia husema Yeye alisulubishwa

Siku Ya Maandalio? {TN10: 4.2}

Taarifa ya Marko, “kwa sababu ni Maandalio, ndio siku iliyo kabla ya sabato,” (Marko 15:42), huelezea kwamba siku hii ya maandalio ilikuwa Ijumaa, “siku iliyo kabla ya Sabato.” Na Sabato iyo hiyo, Yohana anaiita “siku kubwa” (Yoh. 19:31), ingeweza kuwa Sabato ya siku ya saba tu katika juma la Pasaka, sabato ndani ya Sabato kwa maana juma la Pasaka lilikuwa hafla ya siku saba (Hes. 28:17), na kwa hivyo kila juma la Pasaka lilikuwa na Sabato ya siku ya saba, na hivyo siku mbili takatifu katika siku moja — siku kubwa. {TN10: 5.1}

Ingawa katika Maandiko kundi la siku za sherehe nyakati zingine huitwa siku za sabato, au sabato. Pasaka ndani yake yenyewe kamwe haijaitwa Sabato. Hii ni kweli hasa katika Agano Jipya. Na yeyote kati ya mitume kuiita siku ya Pasaka, siku ya Sabato, si kwa ajili yao tu kupuuza sababu, ila pia kuikanganya Pasaka na “Sabato ya siku ya saba,” siku ya pekee iliyoitwa “Sabato.” {TN10: 5.2}

Kwa hivyo kutoka kwa pembe hii pia hueleweka kwamba siku ya “maandalio,” siku waliomsulubisha Yesu, ilikuwa Ijumaa — maandalio ya Sabato katika juma la

5

Pasaka; kwamba kondoo wa Pasaka, ambaye aliuawa siku ya Jumatano (siku ya kumi na nne), haikulingana na kusulubishwa; na kwamba Yesu alikula Pasaka siku ya Alhamisi (siku ya kumi na tano), alikamatwa siku hiyo kabla ya kupambazuka, alisulubiwa Ijumaa (siku ya kumi na sita), akazikwa kabla ya Sabato, na kufufuka Jumapili (siku ya kumi na nane). Kweli hizi za Biblia, ambazo huungwa mkono pia na desturi, zinazusha swali:

Je, Yesu Hakuwa Siku Tatu Mchana Na Usiku Kaburini? {TN10: 5.3}

Isisahaulike kwamba Yeye alizikwa siku ile inayoitwa “siku ya maandalio,” Ijumaa, na ya kwamba wakuu wa ma-kuhani na Mafarisayo walienda kwa Pilato “siku iliyofuata ya maandalio” (Mat. 27:62), Sabato, kumsihi aweke ulinzi kwa kaburi. Kwa hivyo ulikuwa usiku wa pili baada ya mazishi Yake kwamba kaburi lilindwa. Na ukweli kwamba huu ulikuwa usiku ambao Yesu alifufuka (Mat. 28:1-5), huthibitisha kwamba Yeye alikuwa kaburini kucha mbili — Ijumaa usiku na Jumamosi usiku. Kwa hivyo, taarifa, “siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi,” lazima inawakilisha kitu zaidi kuliko tu kuwa Kwake kaburini, inavyofasiriwa na wengine. {TN10: 6.1}

Kisha katika Mathayo 28:1, maneno, “ikipambazuka siku ya kwanza ya juma,” hayajanenwa kwa nia ya kusema wa-kati ambapo Yesu alifufuka, ila kuonyesha

6

wakati ambapo wanawake waliwasili penye kaburi, na kwa hivyo hayawezi kuchukuliwa kumaanisha, wanavyofikiri wengine, jioni penye mwisho wa Sabato. Kwa maana wanawake walikuja penye kaburi asubuhi, jinsi kila mwandishi wa injili hushuhudia: {TN10: 6.2}

Luka– “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini.” Luka 24:1. {TN10: 7.1}

Marko– “Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini.” Marko 16:2. {TN10: 7.2}

Yohana– “Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado.” Yohana 20:1. {TN10: 7.3}

Mathayo– “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, [sio ikianza kubadilika kuwa usiku wa kwanza wa juma] Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.” Mat. 28:1. {TN10: 7.4}

Taarifa kwamba Mariamu Magdalene na Maria wa pili walikuja kuliona kaburi “ilipoanza kupambazuka siku ya kwanza ya juma” (Mat. 28:1), imefasiriwa

7

na wengine kuwa na maana ya kwamba walifika kwenye kaburi siku ya Sabato, kabla ya jua kutua, na kisha wakapata kwamba Bwana alikuwa amefufuka tayari. Lakini ikumbukwe kwamba siku ile walipofika, Maria alikutana na Bwana Mwenyewe na akaongea Naye. Iwapo, kwa hivyo malaika walimwambia katika Sabato kwamba Yesu amefufuka kutoka kwa wafu, na yeye mwenyewe basi aliona kaburi likiwa tupu, pia aliongea na Bwana (Mat. 28:1-9), mbona aliweza kufanya upumbavu Jumapili asubuhi kwenda kaburini ili kuuona mwili wa Bwana kana kwamba hakujua chochote kuhusu kufufuka Kwake, wakati badala yake angepaswa kuzingatia maelekezo yake kuwapasha wanafunzi habari, na kukutana Naye huko Galilaya (Mat. 28:1-7; Yoh. 20:1-17)? {TN10: 7.5}

Marko 16:1, 2 na Luka 24:1-10, pia Yohana 20:1, hutoa ushahidi wa mara tatu kwamba kuhusiana na kufufuka kwa Bwana, Mariamu Magdalene hakujua chochote kabla ya Jumapili asubuhi, wakati kwa mshangao wake malaika akasema: “Amefufuka; Hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka Yeye. Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi Wake, na Petro, ya kwamba Awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama Alivyowaambia.” Marko 16:6, 7. {TN10: 8.1}

Basi, pia, Marko anasema kwamba “Yesu alifufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma,” na pia ya kwamba “siku ya kwanza ya juma [sio siku ya Sabato] Yeye alimtokea kwanza Mariamu Magdalene.” Marko 16:9 . {TN10: 8.2}

Wale, kwa hivyo, ambao hufafanua

8

maneno, “ikipambazuka siku ya kwanza ya juma,” kumaanisha kwamba ilikuwa Sabato alasiri, na ya kwamba Yesu alikuwa amefufuka wakati huo, wako katika makosa makubwa. {TN10: 8.3}

Marko husema, “hata Sabato ilipokwisha kupita,” ilhali Mathayo husema, “hata Sabato ilipokwisha.” Katika tukio lingine, mmoja husema, “hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma”; ilhali mwingine husema, “hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma.” Vishazi hivi vya kulinganisha vyote vina maana sawa. {TN10: 9.1}

Na zaidi ya hayo, ulinganisho wa Mathayo 28:1 na Yohana 20:1 huonyesha kwamba maandiko yote yanarejelea tukio moja na sawa, ingawa wengi hujaribu kuupinga ukweli huo. Yohana husema kwamba wanawake walikuja kwenye ka-buri “siku ya kwanza ya juma. . . kungali giza bado.” Hili haliwezi kumaanisha mwishoni mwa Sabato jua likiwa ka-ribu kutua, kama ungekuwa ni wakati huo, Yohana hangalikuwa amesema,”kungali giza bado,” akionyesha wazi kwamba usiku ulikuwa karibu umetoweka, lakini si kabisa. Na Mathayo, akizungumza kuhusu wakati uo huo, huse-ma: “Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma.” {TN10: 9.2}

Hivyo katika nuru ya injili zote, neno “alfajiri” linaweza kufasiriwa kumaanisha tu kupambazuka kwa siku — asubuhi. Kamusi ya Kiingereza pia huutegemeza ufafanuzi huu. {TN10: 9.3}

Sasa, hata uchunguzi wa kijuujuu wa vifungu hivi vifupi vinne unaweza kusababisha ila tu

9

hitimisho moja kwamba waangalizi wote wanne wanaandika kuhusu tukio moja sawa (ziara ya Mariamu Magdalene na Mariamu yule mwingine kwenda kaburini), kuhusu mahali pale (kaburi la Kristo), na wakati uo huo (mapema alfajiri, siku ya kwanza ya juma), kila mmoja akisimulia jambo hilo kwa maneno yake mwenyewe — hitimisho la mara tatu ambalo linalojitokeza zaidi kwa kulichunguza suala hilo kutoka kwenye pembe ya

Saa Ya Kila Tukio. {TN10: 9.4}

Zamani, saa ilithibitiwa saa kumi na mbili kamili, jua likitua. Usiku wa manane na adhuhuri walikuwa kwa saa sita, na asubuhi kwa saa kumi na mbili. Kutoka kwa mfumo huu asili wa kutunza wakati, rekodi inayohusiana na kuhukumiwa na kusulubiwa imefanywa kama ifuatavyo: {TN10: 10.1}

Kumbukumbu ya Yohana ya hukumu husema kwamba Yesu alikuwa katika ukumbi wa Pilato wa hukumu “karibu saa ya sita” (Yohana 19:14), ilhali rekodi ya Marko ya kusulubishwa husema kwamba Yesu alikuwa akining’inia msal-abani “saa ya sita.” Marko 15:33. Dhahiri, hizi mbili saa “sita” haziwezi kuwa sawa, maana kwa saa sita ya kwanza Yeye alikuwa akihukumiwa katika ukumbi wa Pilato wa hukumu, ilhali ijayo “saa ya sita” (masaa matatu baada ya kusulu-bishwa, na wakati alipokuwa Akining’inia msalabani) jua likatiwa giza: baada ya masaa matatu zaidi, — “saa ya sita” hadi “saa ya tisa,” ambapo jua lilipochomoza tena (Marko 15:33), — Yesu akafa (Marko 15:37). {TN10: 10.2}

10

Lakini yakiwa bado yapo maoni mengine ya apendavyo mtu kwa kauli hii, tutachunguza tokeo la swali,

Wakati Huo Muda Haukuonyeshwa Kwa “Zamu”? {TN10: 11.1}

Kujaribu kupotosha saa kwa kumbukumbu kama “zamu” — vipindi vya masaa manne — badala ya saa halisi za mchana na usiku, ni kuchosha akili hadi kwa hatua ya kuidhoofisha kwa nia ya wazo kwamba yote yanayohusiana na Pasaka, kesi, na kusulubishwa yalifanyika siku moja! {TN10: 11.2}

Kadiri tunavyojua, wanafunzi wote wa Biblia hukubaliana kwamba Yesu alisulubishwa wakati wa mchana na kuzikwa kabla ya jua kutua. Na kama saa za usiku tu ndio siku zote zilihesabiwa kwa “zamu,” vipindi hivyo vya “zamu” hukokotwa kwa upumbavu ndani ya majadiliano. Kwa sababu havina maana kabisa katika muunganisho huu, vyote kwa haki zote haviafiki kuzingatiwa. Kwa ajili, hata hivyo, ya wale ambao wanataka ukweli, lakini wamechang-anyikiwa kwa suala linalojadiliwa, tutalishughulikia kwa ufupi. {TN10: 11.3}

Kwa sababu nadharia ya “zamu” haiwezi kulazimishwa kwa masaa ya wakati wa mchana, hatuna chaguo ila kuhitimisha kwamba Yesu alisulubishwa saa halisi ya tatu (Marko 15:25); kwamba masaa matatu baadaye jua likawa giza kwa saa halisi ya sita (Marko 15:33); na ya kwamba baada ya saa tatu zaidi, Yesu alikufa na jua tena

11

lilichomoza saa halisi ya tisa mchana (Marko 15:34-37), na sio “zamu” fulani ya usiku. {TN10: 11.4}

Na kwa sababu hakuna saa ya sita mbili ila saa ya sita moja tu mchana, kwa hivyo saa ya sita wakati wa kesi katika ukumbi wa Pilato wa hukumu, na saa ya sita wakati wa jua kuwa giza, ambayo ilikuja masaa matatu baada ya Yesu kutundikwa msalabani, sio masaa manne mbalimbali, lakini masaa kumi na mbili au ishirini na nne mbalimbali! Dha-hiri, kwa hivyo, hata kama mmoja atumie mfumo wa kifaa cha “zamu”, mtu hawezi kuhitimisha kwa busara kwamba kesi na jua kutiwa giza, bila kutaja matukio yanayoambatana nayo, yalikuja mchana ule ule. Lazima yalichukua muda mrefu. {TN10: 12.1}

Kisha pia, kwa vile yapo masaa kumi na mbili au “zamu” nne, kati ya kesi hii haswa na jua kuwa giza, na ya kwamba Yeye alisulubishwa saa ya tatu (masaa tisa baada ya kesi, na masaa matatu kabla ya wakati ambapo jua lilikuwa giza), ni upumbavu kujaribu kukusanya kipindi hiki halisi cha masaa kumi na mbili katika kipindi cha masaa manne “zamu”; na bado upumbavu zaidi ni kujaribu kufanya hivyo iwapo kesi ilikuwa alasiri ya Alhamisi. {TN10: 12.2}

Waandishi wa Injili hawamaanishi “zamu” wanaposema “masaa,” maana Yesu hakuwafundisha kusema, Kuna zamu nne kwa mchana; lakini badala yake, saa za mchana si kumi na mbili (Yohana 11:9). Isitoshe, kama ilivyoelezwa awali, kamwe si mchana,

12

ila usiku tu, uligawanywa katika zamu. Na, zaidi ya hayo, geji za vidude vya saa hazikuwahi kutiwa alama kwa zamu, bali kwa saa, na wakati waliposema “saa,” hawakumanisha “zamu.” Ushahidi huu huponda kabisa mpango wa ufafa-nuzi wa “zamu.” {TN10: 12.3}

Usijishikilie kwa dhana za kujitungia zinazoonekana kuyafanya Maandiko yaseme, lakini ukamate kwa dhati lile Ne-no, kwa usahihi, linasema waziwazi. Kufuatilia utaratibu huu, hebu sasa tuipitie tena mada hii katika unaofuata {TN10: 13.1}

Muhtasari.

Masaa ya Usiku

(Machweo) 1-2-3-4-5-6-7-8-9-10-11-12 {TN10: 13.2}

Masaa ya Mchana

(Maawio) 1-2-3-4-5-6-7-8-9-10-11-12 {TN10: 13.3}

Kutazama, kwa kielezo hapo juu, masaa yaliyotajwa na waandishi wa injili, msomaji ataona kwamba hakuna uwezekano wa kufanya matukio haya yote kuchukua siku moja tu. Kwa kuanza, angalia ya kwanza “saa ya sita” — kesi (Yohana 19:14); kisha tazama “saa ya tatu” — kusulubishwa, (Marko 15:25); ijayo, angalia ya pili “saa ya sita” — jua kuwa giza (Marko 15:33); kisha, “saa ya tisa– kifo” (Marko 15:34-38); na mwisho, “saa ya kumi na mbili”

13

— mazishi (Marko 15:42, 46). {TN10: 13.4}

Kutoka kwa haya itaonekana kwamba matukio haya yote hayakufanyika kutwa moja ya saa kumi na mbili, na ya kwamba lazima, kwa hivyo, Kristo aliletwa mbele ya Pilato aidha usiku wa manane uliotangulia Ijumaa asubuhi au adhuhuri Alhamisi. Kuamua ni ipi, tunahitaji tu kuuliza kumbukumbu ya Yohana ya kesi, ambayo hairuhusu wakati wa adhuhuri wa Alhamisi, maana husema: “Nayo ilikuwa maandalio ya pasaka.” Yohana 19:14. Na kama siku hii ya “maandalio” ilikuwa Ijumaa, tunaweza tu kuhitimisha kwamba Yesu aliletwa mbele ya Pilato karibu usiku wa manane — “saa ya sita” — kile tunachoita Alhamisi usiku, lakini nini, kwa mujibu wa Mwanzo, sura ya 1, na kulingana na Wayahudi kuiadhimisha Sabato, hakika ilikuwa Ijumaa. {TN10: 14.1}

Kwa hivyo, Yesu alikamatwa mapema Alhamisi asubuhi; akahukumiwa mbele ya Anasi wakati bado kungali giza bado (Yohana 18:13); akaletwa mbele ya Kayafa katika baraza la Sanhedrini (kesi Yake kisheria) asubuhi (Mat. 26:57; 27:1); ijayo mbele ya Pilato, Ijumaa, kabla ya pambazuko – karibu saa ya sita (Yohana 19:14); kisha kabla ya Herode (Luka 23: 7); kisha kurudi kwa Pilato (Luka 23:11); na mwishowe alisulubishwa asubuhi ya siku iyo hiyo, saa ya tatu (Mar-ko 15:25) — 9:00 Asubuhi, wakati wa kisasa. {TN10: 14.2}

Hii kumbukumbu ya wakati honyesha kwamba kukamatwa Kwake,

14

kesi Zake, na kusulubishwa Kwake kulipangwa upya kwa umakini na kwa ujanja kufanyike usiku na mapema asubuhi ili kuzuia ghasia yoyote, kwa maana “waliwaogopa watu” Luka 20:19. {TN10: 14.3}

Kwamba Yeye alikuwa kaburini kucha mbili na kufufuka Jumapili; ya kwamba kutwa tatu na kucha tatu ni wakati wa kesi Yake ya kwanza kisheria hadi kwa wakati wa ufufuo Wake; ya kwamba moyo wa dunia umefasiriwa kimakosa kumaanisha kaburi, wakati, badala yake, ni, kama vile uzoefu wa Yona huonyesha, mfano wa kifungo cha Kristo mikononi mwa wadhambi na ndani ya kaburi (Mat. 20:19; Luka 9:22, 24:21, 18:33, 24:7; — “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu” (Luka 24:46), kwamba ishara ya “kutwa tatu na kucha tatu” kihalisi imetimizwa tangu Alhamisi asubuhi, wakati wa kesi Yake kisheria, hadi Jumapili asubuhi Alipofufuka, kwamba kondoo wa pasaka, ambaye alikuwa karibu kuuawa wakati Yesu alipokuwa msalabani, si yule iliyeuawa siku ya kwanza ya juma la Pasaka, siku ya kumi na nne ya mwezi, ila yule iliyeuawa siku ya kumi na sita, siku ya pili ya sherehe; — hizi hitimisho zote zimejengwa kweli imara zilizowekwa hapa ndani za kueleweka kwa urahi-si; si, msomaji mpenzi, kwa hadithi au fasiri usizozijua, au kwa kinachoitwa eti “miswada halisi,” ambayo wewe mwenyewe huwezi kusoma, na ambayo huwezi

15

kuipata, na baadhi yake ambayo haipo hata! {TN10: 15.1}

Sasa kushughulikia maswala mengine katika uhusiano huu tutalitazama swali:

Je, Jioni Ni Mwanzo Au Mwisho Wa Siku? {TN10: 16.1}

Kote kote katika Biblia, kama katika vitabu vilivyoandikwa katika kizazi hiki, neno “jioni” humaanisha alasiri ya siku ile ile. Jumatano jioni kwa hivyo humaanisha mwishoni mwa Jumatano na mwanzoni mwa Alhamisi, si mwishoni mwa Jumanne na mwanzoni mwa Jumatano, ingawa Jumatano usiku hushirikiana na kuwa usiku wa Alhamisi. Ukw-eli huu utaonekana kwa urahisi kutoka kwa maandiko yafuatayo: {TN10: 16.2}

Mapema asubuhi, “Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana,” (Yohana 20:18); “Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma,. . . akaja Yesu, akasimama katikati,” Yohana 20:19. Hivyo katika siku za Yesu, neno “jioni” lilitumika kumaanisha sehemu ya mwisho ya siku. {TN10: 16.3}

Tena: “Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi Wake wakamwambia, Ni wapi Utakapo twende tukuandalie Uile pasaka? Akatuma wawili katika wanafunzi Wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji;

16

mfuateni. . . Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandaliwa tayari; humo tuandalieni. . . Basi ilipokuwa jioni Yuaja pamoja na wale thenashara.” Marko 14:12, 13, 15, 17. {TN10: 16.4}

Hapa Marko anasema kwamba katika siku ya kumi na nne, walipomchinja kondoo wa Pasaka, Yesu aliwatuma wanafunzi Wake wawili, na kwamba baada ya kuandaa mahali, na jioni ya siku iyo hiyo ilipofika, basi Yesu alikuja. Kwa hivyo katika andiko hili pia, tunaona kwamba “jioni” humaanisha, si mwanzo, ila ni mwisho, wa siku. {TN10: 17.1}

Tena: “Ikawa wakati wa jioni, kware wakakaribia” Kut. 16:13. Kama kware hawaruki usiku, kwa hivyo walipaswa kuja kambini kabla ya jua kutua, wakati ambao Musa huita “jioni” — mwisho wa siku, si mwanzo wa usiku. {TN10: 17.2}

Kweli hizi za Biblia huonyesha kwamba amri ya Bwana kwa kondoo wa Pasaka, “Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne. . . na. . . watamchinja jioni” (Kut. 12:6), humaanisha kwamba kondoo angechinjwa jioni ya siku ya kumi na nne. Kwa hivyo, kuita Ijumaa usiku “Sabato jioni,” kama wengine wanavyofanya, si kibiblia na ya kutotegemewa, ka-ma ilivyo

Kauli Inayotegemea Kidokezi, Nyumba Iliyojengwa kwa Msingi wa Mchanga. {TN10: 17.3}

Taarifa, “Usiku ule Yeye alichukuliwa na mikono ya waovu, kusulubishwa na

17

kuuawa” (Pambano Kuu, uk. 399), haimaanishi, kama wengine wanavyofikiri, kwamba Yeye alisulubishwa usiku huo, ila badala yake humaanisha tu, kama inavyosema, kwamba “Alichukuliwa” ili Asulubishwe. Kwa hivyo, ingawa “Ali-chukuliwa usiku ule,” angeweza kuwa Alisulubishwa siku kadhaa baadaye, iwapo ingehitajika, na hivyo hakika ndivyo ilivyokuwa. {TN10: 17.4}

Vivyo hivyo, wala taarifa, “Katika jioni hii ya mwisho na wanafunzi Wake” (Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 643), haimaanishi kwamba ilikuwa jioni ya mwisho kabla ya kusulubishwa, lakini badala yake ilikuwa jioni ya mwisho pamoja na wanafunzi Wake kabla ya kifo Chake. {TN10: 18.1}

Jedwali la wakati katika Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 23-25, halikukusudiwa kuonyesha wakati sahihi wa matukio kama wengine, kwa maslahi yao wenyewe, wanataka kufanya liseme; badala yake lengo lake ni kutoa tu wazo la muda ambao yote yangeweza kuwa yametumika kukamilishwa kwa ajili ya sherehe iwapo kondoo alikuwa ame-chinjwa tu wakati halisi wa machweo: kuonyesha kutowezekana kukamilishwa katika siku moja yote yaliyofanywa kuhusiana na Pasaka, kusalitiwa, kuhukumiwa, kusulubishwa, na kuzikwa. {TN10: 18.2}

Wale ambao wamejaribu kufanya msongano “saa ya sita” iliyoashiria kesi ya Yesu katika chumba cha Pilato cha hukumu, na “saa ya sita” ambayo ilianzisha giza Alipokuwa msalabani, — kipindi cha masaa kumi na mbili, — katika “zamu” Ya masaa manne, hufikiri maandiko hayo mawili huwiana

18

kikamilifu na wazo lao, ambapo kwa ukweli wazi, kama ulivyoonekana hapa, siyo tangamanifu kama usiku na mchana! Bado, hawa hawana mwisho wa kujifurahisha kwa upotovu kwa kutoweza kupatanisha “kukamatwa usiku wa manane” na wakati kama ulivyoonyeshwa katika jedwali lililotajwa mbeleni, ambalo, kulingana na ufahamu wao, huwakilisha utofauti wa masaa matatu au manne! Mbona hawajatumia “mfumo wa zamu” hapa ambapo unaweza kutumika? {TN10: 18.3}

Jedwali la wakati halijaribu kuonyesha “kukamatwa usiku wa manane,” ila tu wakati ambao Wayahudi “walimshikilia Yesu” — Alipoletwa mbele ya makuhani na hasa mbele ya Sanhedrini (Mat. 26:57 ). (Tazama chati, Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 22.) Ilhali Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 699, 760, huzungumza kuhusu wakati Aliposhikwa katika bustani (Mat. 26:50) — “kukamatwa usiku wa manane.” {TN10: 19.1}

Iwapo kukamatwa usiku wa manane, kuhukumiwa mbele ya Pilato, kusulubishwa, na mazishi ya Yesu, yote yalitukia siku moja (Ijumaa), basi Yeye angewezaje kukamatwa katika bustani muda mfupi baada ya usiku wa manane, akaletwa kutoka huko mfululizo hadi kwa Anasi, Kayafa, kwa Sanhedrini, na kwa Pilato, na bado awe katika ukumbi wa Pilato wa hukumu karibu usiku wa manane? Huku kutowezekana kabisa kunapaswa kumshawishi yeyote mwenye akili ya kuelewa kwamba matukio haya lazima hivyo yawe yamegharimu siku mbili na hivyo

19

kauli yoyote inayounga mkono wazo ambalo yaligharimu ila siku moja, si dhidi ya ufasiri wa Fimbo ya Mchungaji, lakini dhidi ya shuhuda za Marko na Yohana, ambao walikuwa mashahidi walioyatazama matukio haya. {TN10: 19.2}

Mengine kama haya maelezo ya kukanganya yamefanywa lakini kwa sababu tulivyozingatia kwa vigezo vipasavyo kwa yote makuu, yale madogo hayastahili maelezo. Yatosha kusema kwamba uzoefu wetu katika kazi ya kuchapisha injili hutufundisha kwamba wengi ambao wametumia karibu masaa yasiohesabika ya muda wa thamani kwa kulikanganya somo la ishara ya Yona, wametumia ila muda mfupi sana kujifunza masomo muhimu zaidi kama vile katazo dhidi ya ufasiri wa apendavyo mtu wa Maandiko (2 Pet. 1:19, 20); Roho ya Unabii (Ufu. 19:10); Sabato (Kut. 20: 8-11); Ubatizo (Mat. 3:15; Mdo. 2:38); Ufalme (Isa. 2:2), Mchinjo wa Ezekieli 9, kulipa Zaka (Mal. 3:10); ingawa masomo haya muhimu hudai utendaji, — wajibu wa kutekeleza kweli ambazo yanafundisha, ilhali ishara ya Yona haidai kitu. {TN10: 20.1}

Baada ya mmoja kuyapata maarifa yote muhimu kuhusiana na ishara ya Yona, yeye si bora wala mbaya zaidi kadiri Ukristo wake unavyohusika, bila kuzingatia muda uliopotea ikiwa mahitimisho yake kwa mada hiyo yawe ya makosa. {TN10: 20.2}

Lakini lililo bado baya zaidi, kikundi cha watu ambao wanatangaza kwa usahihi mafundisho yote yaliyofunuliwa, wa-hitilafiane na hawa

20

wahubiri wenye bidii wa ishara ya Yona, kuhusu ni nini “moyo wa nchi” unaweza kumaanisha, la mwisho katika matukio mengi si tu wataacha ushirika na ndugu zao, na kukoma kusaidia kuyatangaza mafundisho muhimu zaidi, lakini pia watarukwa na akili sana kwa wazo lao kipenzi kwamba akili zao haziwezi kuelewa mengine zaidi. {TN10: 20.3}

Kwa kundi kama hili la watu “Akajibu, akawaambia, kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa isha-ra, ila ishara ya nabii Yona.” (Mat. 12:39), — na hapa wameipata! {TN10: 21.1}

Wayahudi kweli waliona “ishara,” lakini kwa sababu ya kutokuamini kwao, walishindwa kufaidika nayo. Tunatarajia, hata hivyo, ya kwamba kushindwa kwa watafuta ishara siku hizo itakuwa ni onyo kwa watafuta ishara katika siku hizi. {TN10: 21.2}

Sasa, kwa kujifunza chati ya ukurasa wa jalada, msomaji anaweza kulifupisha somo hili lote, na hivyo kupata picha ya kudumu ya ishara imara za Maandiko za kila tukio, na kumalizia kwa kutowezekana kumhukumu Yeye mbele ya mahakama zote za Kiyahudi na za Kirumi, kwa kuongeza kumdhihaki na kumsulubisha Yeye, kwa masaa matatu ma-fupi — tangu maawio (saa ya kumi na mbili) hadi saa ya tatu! Kwa maneno mengine, chati hiyo huonyesha kwamba haiwezekani kabisa katika masaa mafupi matatu kuwa na angalau kesi moja mbele ya Sanhedrini, mbili mbele ya Pila-to, na moja mbele ya Herode, kufanya

21

jumla ya zisizopungua kesi nne, mbali na muda wa kumsulubisha Yeye. Kugawanya jumla ya muda uliotumika (masaa matatu) kwa jumla ya matukio (matano), tunaona kwamba zingekuwapo dakika thelathini na sita tu kwa kila tukio! Lakini kutembea tu kutoka sehemu moja ya hukumu hadi nyingine, pamoja na kupanga kesi, kungekuwa tu ku-megharimu zaidi ya masaa matatu! {TN10: 21.3}

MASWALI NA MAJIBU MAJADILIANO

JE, YESU ALIKULA PASAKA KATIKA SIKU YA PASAKA?

Swali:

Je, Yesu alipaswa kula Pasaka siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu katika juma la Pasaka ya kusulubishwa, au kabla yake? {TN10: 22.1}

Jibu:

Wakati wa kuadhimisha Pasaka likiwa ni takwa la sheria, hakuna yeyote angeweza kuiadhimisha sikukuu yake wakati mwingine na bado apewe thawabu kama mtunza Pasaka. Sembuse, kwa hivyo, Yesu angekuwa ameila hapo awali, kwa sababu Yeye hangekuwa hapo ameweka tu mfano mbaya ila pia Angewapa Wayahudi fursa ya kumshutumu Yeye kwa haki na kusababisha mengi kutoka kwalo, kama lingekuwa kweli lilitukia, mitume kwa kawaida wangekuwa wame-nakili. Ukweli, hata hivyo, kwamba hawakuandika kumbu-

22

kumbu kama hiyo, huonyesha kikamilifu kwamba halikuwapo la kuandikwa. {TN10: 22.2}

Ilikuwa, isitoshe, “siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu,” siku “walipochinja Pasaka” (si kabla), ya kwamba “wanafunzi Wake wakamwambia, Ni wapi Utakapo tuende tukuandalie Uile pasaka? . . . Basi ilipokuwa jioni Yuaja pamoja na wale thenashara. Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja Nami, atanisaliti.” Marko 14:12, 17, 18. {TN10: 23.1}

Hapa Biblia hueleza kwa lugha iliyo wazi iwezekanavyo kwamba Yesu na wale kumi na wawili walikula Pasaka kwa wakati uliowekwa na sheria ya Musa. {TN10: 23.2}

JE, YESU ALIKULA PASAKA SIKU YA KUSULUBISHWA KWAKE?

Swali:

Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 642, husema: “. . . siku ile Pasaka ililiwa, Kristo angetolewa dhabihu.” Iwapo Pasaka ili-liwa Jumatano usiku, angewezaje Yeye kusulubishwa siku ya Ijumaa, na bado taarifa hiyo iwe kweli? {TN10: 23.3}

Jibu:

Ikiwa anayehoji atasoma kwa makini muktadha wote wa taarifa hiyo inayofanyiwa udadisi, ataona haraka kwamba analipotosha neno “dhabihu” jinsi lilivyotumika na mwandishi. Mwandishi mwenyewe hulifasiri

23

kumaanisha “mateso,” Yake, neno ambalo haliwezi kuwekewa mipaka kwa kusulubishwa Kwake, ila hujumuisha, jinsi muktadha wa taarifa inayofanyiwa udadisi inavyoonyesha, kesi Yake, unyanyasaji, na kusulubishwa: {TN10: 23.4}

“Katika chumba cha juu cha maskani huko Yerusalemu, Kristo alikuwa ameketi mezani pamoja na wanafunzi Wake. Walikuwa wamekusanyika kusherehekea Pasaka. Mwokozi alitumaini kuitunza sherehe peke Yake na wale thenashara. Yeye alijua kwamba saa Yake ilikuwa imekuja; Yeye Mwenyewe alikuwa mwana-kondoo wa kweli wa pasaka, na siku ile Pasaka ililiwa, Alipaswa kuwa dhabihu. Alikuwa karibu kunywa kikombe cha ghadhabu; Yeye muda mfupi ujao lazima aupokee ubatizo wa mwisho wa mateso. Lakini masaa kadhaa ya utulivu bado yalisalia Kwake, na yalipaswa kutumika kwa manufaa ya wanafunzi Wake wapendwa.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 642. {TN10: 24.1}

JE, PASAKA ILIKUWA SIKU GANI?

Swali:

Je, mtu anawezaje kubainisha siku ya juma ambayo iliangukia siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza (mwanzo wa juma la Pasaka ambayo Kristo alisulubishwa)? Je! Mtu anawezaje kuthibitisha kwamba ilikuwa Jumatano? {TN10: 24.2}

Jibu:

Kama kipindi cha siku tatu mchana na usiku kilitumika kumhukumu, kumdhihaki, kumchapa, na, hatimaye, kumsulubisha Kristo, na kisha katika kufa Kwake, akiwa kaburini,

24

na kufufuka (tazama Mathayo 20:19; 16:21; 17:22, 23; 27:63; Luka 9:22; 24:21; 18:33; 24:7, 46), basi kuhesabu kurudi nyuma siku tatu mchana na usiku kutoka Jumapili, siku Aliyofufuka (Marko 16:9), hupeana Jumatano. Hivyo ilikuwa Jumatano usiku ambapo alikula chajio cha Pasaka na wale thenashara. {TN10: 24.3}

JE, SIKU MOJA YAWEZA KUWA NA ASUBUHI MBILI?

Swali:

Kwa kunena kumhusu Yuda hukumuni mbele ya Kayafa, Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 722, husema hivi: “Kwa bidii akilishikashika vazi la Kayafa, alimsihi amwachilie Yesu. . . Baadaye siku iyo hiyo, njiani kutoka kwenye ukumbi wa Pilato kuelekea Kalvari, kulikuwa na mikatizo ya kelele na mizaha ya kundi la waovu waliokuwa wakimwongoza Yesu mahali pa kusulubishwa.” {TN10: 25.1}

Hapa Tumaini la Vizazi Vyote husema kwamba kesi zote mbili mbele ya Kayafa na mbele ya Pilato, pia kusulubishwa, yalitukia siku ile moja, ilhali Fimbo ya Mchungaji huthibitisha wazi kutoka katika Biblia kwamba kesi na kusulubish-wa kuligharimu siku mbili. {TN10: 25.2}

Ni vipi, basi, Tumaini la Vizazi Vyote kinaweza kupatanishwa na Biblia? {TN10: 25.3}

Jibu:

Zingatia ukweli kwamba Kristo alihukumiwa mara saba kwa ujumla: “mara mbili mbele ya

25

makuhani, mara mbili mbele ya Sanhedrini, mara mbili mbele ya Pilato, na mara moja mbele ya Herode” (Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 760). Za kwanza mbili zilikuwa kabla ya pambazuko (Yohana 18:13, 24), na ya tatu ilianza kwa pambazuko (Mat. 26:57; 27: 1). {TN10: 25.4}

Sasa kwa mujibu wa wakati wa siku, kesi mbele ya Pilato ilikuja mapema (kungali bado giza — Yohana 18:28, 29, Yohana 19:14) kuliko ile mbele ya Sanhedrini (asubuhi), ila kwa mpangilio (kwa kweli) ile mbele ya Sanhedrini ilikuja kwanza, na ile mbele ya Pilato baadaye. Kesi hizi mbili, kwa hivyo, hazingeweza kuwa zilifanyika siku ile ile. {TN10: 26.1}

Hivyo taarifa, “siku ile ile,” haiwezi kurejelea siku ambayo Yesu alikamatwa, ila kwa siku baadaye, jinsi Tumaini la Vizazi Vyote chenyewe huweka wazi: {TN10: 26.2}

“Ilipopambazuka, Sanhedrini wakakusanyika tena, na Yesu akaletwa tena ndani ya chumba cha baraza.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 714. {TN10: 26.3}

“Liwali wa Kirumi alikuwa ameitwa kutoka katika chumba chake cha kulala kwa haraka, naye akaazimu kuifanya kazi yake upesi iwezekanavyo. . . yeye akageuka ili kumwona ni mtu wa namna gani alipaswa kumchunguza, kwamba alikuwa ameitwa kutoka kwenye mapumziko yake wakati wa mapema sana hivyo.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 723. {TN10: 26.4}

Kutoka kwa vidokezi hivi inaonekana kwamba Tumaini la Vizazi Vyote hutambua kwamba matukio

26

yalikuwa kwa asubuhi mbili tofauti: lile mbele ya Kayafa, “ilipopambazuka,” na lingine mbele ya Pilato, pia “wakati wa mapema sana hivyo.” {TN10: 26.5}

Kisha, pia, ukweli kwamba “saa baada ya saa ilipita” kabla ya “kesi kukamilika” ya Sanhedrini (Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 721), huonyesha kwamba iliendelea kuchelewa hadi alasiri. {TN10: 27.1}

Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 722, inashughulika na utaratibu wote wa kesi, si katika maeneo ya matukio yake saba, lakini kama mchanganyiko wote — kesi moja isiyobadilika. Kwa maana Yuda akakata tamaa baada ya kuona kwamba Yesu alikuwa katika kila kesi amehukumiwa kusulubishwa, na hivyo alienda na kujinyonga mwenyewe. {TN10: 27.2}

Hiyo, Tumaini la Vizazi Vyote hupatana kikamilifu na Biblia, lakini anayehoji ameshindwa kusoma kwa umakini. {TN10: 27.3}

DHANA YA SHEREHE YA PASAKA IKIJARIBU KUTEGEMEZA KUTUNZA SABATO YA MWEZI

Swali:

Katika jitihada za kujenga dhana yake iliyotungwa, kabrasha inayoitwa Sabato ya Uumbaji hupinga kwamba sherehe ya Pasaka iliadhimishwa mwanzoni mwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, ikikazia kwamba siku ya kumi na tatu ya mwezi uo huo kama maandalio ya kumchinja kondoo wa Pasaka. Je! hili ni sahihi? {TN10: 27.4}

27

Jibu:

“Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni pasaka ya Bwana. Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu.” Law. 23:5, 6. {TN10: 28.1}

Dhahiri kabisa, kwa hivyo, walipaswa kumchinja kondoo wa Pasaka alasiri ya siku ya kumi na nne, na walipaswa kuwa na sikukuu wakati wa usiku au mwanzoni mwa siku ya kumi na tano. {TN10: 28.2}

Hiyo kabrasha pia hupinga kwamba Yesu alikufa siku ya kumi na tatu ya mwezi, ambayo, kwa mujibu wa hesabu zake, kilitukia tu karibu wakati ambapo kondoo wa Pasaka wa siku ya kumi na nne angechinjwa. Ilhali Mathayo, Marko, Luka, na Yohana — wote wanne wa injili — hukubaliana kwamba “hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipochinja pasaka, wanafunzi Wake wakamwambia, Ni wapi Utakapo tuende tukuandalie Uile pasa-ka?” Baada ya kuiandaa,”wakaketi chakulani, wakala.” Marko 14:12, 18; Mat. 26:1-21; Luka 22:1-15; Yohana 13:1, 2. {TN10: 28.3}

Kudhani kwamba Sabato ya siku ya saba huthibitiwa na kalenda ya mwezi, badala ya mzunguko huru wa kila juma,

Kabrasha Husema: {TN10: 28.4}

“Naam, jumuia yote ya Ukristo, isipokuwa baadhi ya watunza Jumamosi, huadhimisha siku ya kipagani ya Jua. Lakini watunza Jumamosi pia huadhimisha, na kuiheshimu siku ya

28

asili ya upagani — siku ya Zohali. Siku hizi zote, na mifumo yao ya majina zilifika kwa Wayunani na Warumi, huko hadi kwa ulimwengu wote kutokea Misri, ambapo Kaisari Juliasi alipata kalenda yake ya siku 365 kwa mwaka, lakini aliongeza robo moja ya siku kila mwaka. Zote mbili ni uongo. {TN10: 28.5}

“Ya Wamisri siku ya kwanza ya juma lao ilikuwa siku ya Zohali (Jumamosi) na siku ya mwezi (Jumatatu) siku yao ya saba. Walikuwa na siku saba kwa juma lao. Lakini Warumi, wakati huo na wakati wa Konstantino, walikuwa na siku nane kwa juma lao. (Angalia Kamusi Elezo Mpya ya Kimataifa, Gombo la 23, uk. 436, kwa uthibitisho.) Kwa hivyo, Jumamosi, kama Jumapili, ni ya chimbuko la kipagani, la kibinadamu, na si la Mungu. Ila wakati Warumi walichukua rasmi juma la siku saba kutoka Misri (ambako Juliasi alikuwa amepata siku 365 kwa mwaka, ingawa aliongeza ya-ziada robo ya siku kila mwaka), tangu siku za Konstantino, 321 B.K. hadi siku za Theodosias Mkuu, karibu miaka 75 baadaye, Warumi walibadilisha jina la Wamisri kwa kuifanya Jumapili (siku ya katikati ya juma la Misri) kuongoza juma la kal-enda yao wenyewe. Hivyo siku ya Jua ilifanywa kuongoza juma, jinsi Kaisari Juliasi alivyofanya Januari (kutoka Janus, mungu wa jua) kuwa baba wa mwaka. Na Jumamosi ikafanywa kuwa siku ya saba ya juma la kalenda yao, na kalenda hii ilifanywa sheria baadaye na kanisa Katoliki na utawala huo kwa ulimwengu wote, na kuzingatiwa na wote

29

Ukristo hadi leo. Ni ukweli huu kwamba umeita kutoka kwa Mungu Ujumbe wa Malaika wa Tatu ili kuwaita watu Wake kutoka kwa ibada hii ya Rumi chini ya adhabu ya kuathirika kwa mapigo saba ya mwisho isipokuwa waiache iba-da ya Kirumi hadi kwa Yake, kwa kuitunza Sabato. . . {TN10: 29.1}

Kutoka 12:1, 2; “Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza (mwezi — sayari) wa mwaka kwenu.” Mwezi (sayari) uliumbwa kupi-ma miezi. Linganisha 1 Samweli 20, aya za 5, 18, 24, 27, 34. Na pia kuashiria majira (Mwa. 1:14 na Zab. 104:19). Mwezi na jua na nyota ni kalenda ya Mungu katika mbingu ambayo watu wote wanaweza kuona na kuashiria nyakati za Mungu pamoja na dunia. . . {TN10: 30.1}

“Sabato ya Biblia, kwa hivyo, ni Sabato ambayo Pasaka huja kwayo kila mwaka. Bwana ameweka makusudi sherehe ya Pasaka kwa Sabato ya pili ya mwezi wa kwanza (Abibu), kila mwaka, kwa ukumbusho wa Sabato kila mwaka (Kut. 20:8). Ni Sabato ya pili ya mwezi wa kwanza, kwa sababu ya Pasaka kuwa siku ya kumi na nne ya mwezi huo, ambayo ndiyo mwezi kamili baada ya mfululizo wa Mlingano wa masika unapoanza.” — Sabato ya Uumbaji, uk. 9, 10, 13, 14, 16. {TN10: 30.2}

Kwa watetezi wa hii hesabu ya Sabato

30

kama ilivyonukuliwa hapo juu, Roho wa Kweli hutoa

Jibu: {TN10: 30.3}

Katika aya za italiki, mwandishi mwenye nia njema lakini ambaye ameelimishwa vibaya anajaribu kuipindua Sabato ya siku ya saba ya kila juma kwa kushambulia mzunguko huru wa kila juma na kuipendelea kalenda ya mwezi. Anaweka siku ya saba, ya kumi na nne, ya ishirini na moja, na ya ishirini na nane ya kila mzunguko wa mwezi (sayari) kama sa-bato za ukumbusho za juma la uumbaji. {TN10: 31.1}

Hatupingi kwamba Warumi wa mwanzo walikuwa na juma la siku nane, na kwamba majina ya miezi na siku za juma ni za chanzo cha kihekaya, lakini tunamuuliza mwandishi wa sabato ya mwezi kwa ushahidi wa msingi wa ukweli, si kwa dhana, kwamba Sabato ya uumbaji iliwahi kuthibitiwa na mzunguko wa mwezi (sayari). Kweli, Bwana akanena na Musa, “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.” Kut. 12:2. Lakini Yeye hakusema, “Ni mwanzo wa majuma kwenu.” Hakika Yeye hakusema, kwa kuwa mwenendo huo ungekuwa

Kinyume Kwa Maumbile Na Mantiki. {TN10: 31.2}

Iwapo mojawapo ya sayari mbili za mwangaza lazima iheshimiwe kuithibiti Sabato takatifu, inapaswa kuwa jua, am-balo hutawala si tu mwezi lakini pia mfumo wote. Mungu angekusudia mwezi

31

kuwa kithibiti cha wakati na kiashirio, mfumo huo ungeitwa mwezi badala jua. Kama Yeye, hata hivyo, alikusudia mwezi uweze kuthibiti wakati wa Sabato takatifu, Angaliweza kuufanya kukamilisha mzunguko wake duniani kote, ikiwa sivyo mara moja katika majuma manne kamili, kisha mara moja kwa juma nzima, au kwa siku moja kamili. Na kama Yeye, zaidi ya hayo, alikusudia jua kuonyesha wakati mtakatifu, dunia lazima, hatimaye, ingekamilisha mzun-guko wake kwa jua katika majuma 52 kamili. {TN10: 31.3}

Sasa tutnapaswa kuleta mbele kwa ufupi kweli zilizopo za jua, mwezi, na za Kibiblia, si maoni, kwamba mzunguko wa kila juma hauwezi kuwa na haujawahi kuthibitiwa na kalenda yoyote ya kila mwezi; kwamba kanisa la Agano la Kale wala Agano Jipya chini ya maongozi ya Mungu kwa wakati wowote limeiadhimisha sabato ya mwezi ya siku ya saba; kwamba kabrasha, Sabato ya Uumbaji, imeitwa hivyo kimakosa, na ya kwamba

Mzunguko Wa Kila Juma Si Wa Jua Wala Wa Mwezi. {TN10: 32.1}

Sabato ambayo Bwana alipumzika ilikuwa siku sita hasa baada ya wakati wa uumbaji kuanza; kisha, siku ya saba Yeye alipumzika (Mwa. 2:2). Kama Yeye, hata hivyo, aliibariki siku inayotawaliwa na mwezi, Angekuwa alipumzika siku ya kumi, kwa maana mwezi haukuumbwa hadi siku ya nne ya uumbaji. (Angalia Mwanzo 1:14-19.) Lakini kuitunza Sabato siku ya saba baada ya kuumbwa kwa mwezi,

32

ungekuwa si ukumbusho wa uumbaji, ila kwa ukumbusho wa mwezi! {TN10: 32.2}

Juma la kwanza la Sabato ya uumbaji likiwa siku tatu kongwe kuliko jua na mwezi, hubainisha waziwazi kwamba hakuna mojawapo wa sayari za mwangaza inayoweza kuthibiti juma la uumbaji. Nguvu ya uthibiti kama hiyo ingekuwa kwa lazima imeunyima Wakati na Uumbaji siku tatu za kwanza, na kuziacha kama mzuka “kipindi kili-chopotea.” {TN10: 33.1}

Aya mbili ambazo zimetangulia hubatilisha kabisa wazo la kwamba juma hutegemea mzunguko wa kila mwezi wa mwezi [sayari], na kufanya yasiyofaa majadiliano yoyote zaidi kwenye mada. Kwa ajili ya, hata hivyo, kutatua kauli zingine zilizokanushwa, pamoja na kujiokolea muda baadaye kuendelea kuyajibu maswali ya kina kwa suala hili, tun-awasilisha uchunguzi ulioambatanishwa. Kutoka kwa huo msomaji anaulizwa kuzingatia kwamba ikiwa sabato ya mwezi ilipewa jina sahihi, haipaswi kuitwa, sabato ya uumbaji, ila badala yake

Sabato ya Sayari Tu? {TN10: 33.2}

Bwana akishapumzika kwa “siku ya saba,” si ya kumi, mzunguko wa kila juma ulianza na siku ya kwanza ya uumbaji, ilhali wakati wa jua na mwezi ulianza siku tatu baadaye. Sabato inayotawaliwa ama na kalenda ya jua au kalenda ya mwezi, hata hivyo, haingeweza kamwe kukumbusha juma

33

la uumbaji, ila badala yake sayari zenyewe tu, na kwa hivyo, iwapo zinapewa jina sahihi, lazima ziitwe “za sayari.” Basi, pia, mzunguko wa kila mwezi wa mwezi [sayari] kwa dunia, si kuratibu na mzunguko wa kila siku wa dunia kwa jua, kama ilivyodokezwa tayari, hufanya

Isiwezekane Kuitunza Sabato Ya Sayari. {TN10: 33.3}

Ukweli kwamba mwezi huchukua muda mrefu zaidi ya siku 28 ili kukamilisha mzunguko wake wote kwa dunia, basi tungesanifisha siku ya saba, ya kumi na nne, ya ishirini na moja, na ya ishirini na nane ya mwezi [sayari], kwa ajili ya kuadhimisha Sabato, jinsi kabrasha ile ilivyoitwa kimakosa hutetea, hatungekuwa tumeambatana na mwezi hata hivyo, kwa maana mwezi wa mwezi [sayari]si siku 28 halisi, ila kwa wastani siku 29-1 / 2. {TN10: 34.1}

Sabato ya mwezi lazima bila shaka lazima iratibu na wakati wa mwezi (sayari) na wa jua. Lakini mwezi wa sabato (siku 28) unapungua siku 1-1 / 2 za mwezi wa sayari [mwezi] (29-1 / 2); na mwaka wa sabato (12 x 4 = majuma 48, 48 x 7 = siku 336) hupungua siku 18 kwa muda wa mwaka wa mwezi (354) na siku 29 pungufu za muda wa mwaka wa jua (365). Kwa hivyo, mwisho wa kila mwaka wa Sabato, mtunza sabato wa mwezi, ili kuenenda kwa wakati wa mzun-guko wa kila juma, pamoja na mzunguko wa dunia na mwezi, ataifanya dunia kutozunguka siku 29 na mwezi siku 18. {TN10: 34.2}

34

Uchanganuzi huu huthibitisha ukweli kwamba mzunguko wa kila juma hauwezi kutawaliwa na mwendo wa aidha mwezi [sayari] au jua, ila tu kwa nguvu za Mungu, ambazo zilileta siku ya kwanza ya uumbaji, siku tatu kabla ya jua au mwezi [sayari]. Na hivyo, jinsi tunavyoonyeshwa tena, Sabato ni ukumbusho, si wa jua au mwezi, ila wa uumbaji. {TN10: 35.1}

Hamna shaka katika mawazo ya yeyote kwamba makanisa ya Wayahudi na Mitume katika wakati wa Kristo walikuwa watunza siku sahihi ya Sabato; na ya kwamba juhudi ambayo Mfalme wa Rumi, Konstantino, alikuwa nayo kwa ima-ni ya Kikristo ingemzuia kabisa kuifuta kalenda ya Kikristo na kuanzisha nyingine ambayo ingeondoa kabisa Sabato ya uumbaji na kumbukumbu yao ya ufufuo. {TN10: 35.2}

Hakika hakuna mtu anayedhani kwamba angekuwa amefanya jambo hilo la uovu, Wakristo wangemheshimu sana hata kumwita mtakatifu na kuiweka siku ya ishirini ya Mei kama sikukuu yake, ambayo baadhi ya watu huiadhimisha mpaka leo. (Tazama Kamusi Elezo ya Karne ya Ishirini, Gombo la 3, uk.13) {TN10: 35.3}

Hakika, Wakristo wangetumia sana ukafiri wake kwamba hakuna hali inayofikiriwa ingeweza kukificha kitendo cha kukufuru kutoka kwa jicho pekuzi la historia. Lakini kiingilio kama hicho hakipatikani katika

35

Kumbukumbu ya Historia. {TN10: 35.4}

“Matumizi ya juma yaliingizwa katika Dola ya Kirumi karibu karne ya 1 au 2 ya enzi ya Kikristo kutoka Misri na yalikuwa yametambuliwa huru kwa Ukristo kabla ya Mfalme Konstantino kuyathibitisha kwa kuagiza utunzaji wa Sabato ya Kikristo. Pamoja na Waislamu juma hilo pia lina tabia ya kidini, Ijumaa ikiadhimishwa na wao kama Saba-to.” — Kamusi Elezo ya Karne ya Ishirini, Gombo la 8, uk. 487. {TN10: 36.1}

“Kipindi cha siku saba. . . kilitumika na Wabrahamini nchini India na majina yale yale yanayotumiwa nasi, na vile vile yalipatikana katika kalenda za Wayahudi, Wamisri, Waarabu na Waashuri.” — Kamusi Sanifu, ufafanuzi “Kalenda.” {TN10: 36.2}

“Juma ni kipindi cha siku saba bila marejezo yoyote kwa misogeo ya kimbingu, — hali ambayo kwayo inawiwa usawa wake thabiti. Kilitumika tangu wakati wa zamani za kale karibu katika nchi zote za mashariki; na, kwa sababu halina umbo la sehemu ya kigawanyo cha mwaka wala mwezi [sayari], wale wanaokataa kumbukumbu ya Musa watapata hasara, kama vile Dalambre anavyosema, kukigawa kwa asili iliyo na sura ya uwezekano kama huo.” — Kamusi Elezi Britannika. {TN10: 36.3}

“Ni furaha yetu (kama vile mtindo wa Kifalme) kwamba mataifa yote, ambayo yanaongozwa na rehema yetu na kiasi,

36

yanapaswa kuzingatia kwa dhati dini iliyofundishwa na Mtakatifu Petro kwa Warumi; ambayo mila ya uaminifu ime-hifadhiwa; na ambayo sasa inadaiwa na Papa Damaso, na kwa Petro, Askofu wa Aleksandria, mtu wa utakatifu wa Mitume. Kwa mujibu wa nidhamu ya Mitume, na fundisho la Injili, hebu tuamini miungu pekee ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu; chini ya utukufu sawa, na Utatu mwaminifu. Tunawaagiza wafuasi wa fundisho hili kuchukua jina la Wakristo Katoliki; na tunapohukumu, kwamba wengine wote ni wanadamu wapotevu wenda wazimu, tuna-wabandika kwa jina lenye sifa mbaya Waasi; na kutangaza kwamba mikusanyiko yao haitachukua tena jina la heshima la makanisa.” — Rumi ya Gibbon, Gombo la 3, uk. 81. (toleo la Milman.) {TN10: 36.4}

Kumbukumbu hii ya kihistoria huonyesha wazi kwamba kipindi cha kila juma cha siku saba kimeendelezwa bila kukatizwa tangu zamani za kale, kwamba Rumi haikuondoa juma la Kikristo ila la Kirumi, na ya kwamba lile ambalo lilichukua nafasi yake lilikuwa sawa na la Wayahudi, au la Ukristo. {TN10: 37.1}

Hata mtetezi wa sabato ya mwezi, mwenyewe, bila kujua anakiri kwamba Konstantino, katika siku za uongofu wake kwa Ukristo, aliacha juma lake la siku nane na akachukua na kuthibitisha juma la siku saba — juma la uumbaji: “Hawa mashahidi watatu [Kamusi Elezi Mpya ya Kimataifa,

37

Kamusi Elezi ya Britannika, na Kamusi Elezi Amerikana],” inasema kabrasha, “hutuambia kwamba Warumi hawakuwa na siku saba kwa juma lao, wala majina yao ya unajimu, hadi siku za Konstantino, ila hadi wakati huo walikuwa na siku nane.” — Sabato ya Uumbaji, uk. 24. {TN10: 37.2}

Ingawa mataifa ya leo hayafuati kalenda ya kila mwezi ya Biblia, ambayo kwa namna iwayo yote haibadili ukweli kwamba mzunguko wa asili wa kila juma haujawahi kubadilishwa. Na jinsi ulivyo huru kabisa kwa kalenda za jua na mwezi [sayari] ambao laiti Mungu hangeuhifadhi katika vizazi vyote kamili, watakatifu, sasa “hata nyakati za kufany-wa upya vitu vyote,” wangekuwa na shida kubwa ya kuurejesha na kuutetea utimilifu wake. Hivyo inavyoonekana kutoka kwa kila mtihani uliowekwa kwayo, kwamba kama hii sabato ya mwezi ni isiyokuwa ya kibiblia na isiyokuwa ya kihistoria na inavyoletwa karibu kwenye nuru, itaonekana dhahiri kuwa

Isiyo Na Maana Hata Zaidi. {TN10: 38.1}

Ni kweli kwamba mfumo wa sherehe (mchanga kuliko taasisi ya Sabato, ulianzishwa kwa sababu dhambi iliingia katika familia ya wanadamu) ulikuwa katika baadhi ya mambo chini ya sheria za mwezi; ila Sabato ya siku ya saba ilianzishwa, si kuhusiana na dhambi, ila tu kuhusiana na kazi kamilifu ya uumbaji, haiwezi kuthibitiwa na sheria ya dhambi kuliko inavyoweza kuthibitiwa kwa sheria ya mwezi. Taasisi ya Sabato ni kuu kwa taasisi ya sherehe na haina kitu

38

cha kufanya na sheria ya dhambi, jinsi lilivyo Hekalu. Sabato, kwa hiyo, haiwezi kusujudu kwa utiifu kwa taasisi am-bayo si tu ndogo kwayo ila pia inayodai uwepo wake tu kwa dhambi! {TN10: 38.2}

Tena tunaona kwamba dhana hii ya mwandishi wa “Sabato ya Sayari” ni ya kukufuru na ya upumbavu na isiyokuwa na maana. {TN10: 39.1}

Mwana-nadharia huyo ametumia maandishi ya wanahistoria fulani, acha mwanafunzi wa Kweli achunguze kwa makini hizo nukuu, na atapata kwamba haziungi mkono dhana hiyo kwa vyovyote kuliko ambavyo Biblia hu-litegemeza, ambayo huongoza kwa

Shida Kuu Ya Mwana-nadharia. {TN10: 39.2}

Kuondoka kwa misharazi kama hii ni kwa sababu ya kusoma kijuu-juu na kufasiri maneno ya wengine bila kuchun-guza kwa kina ili kupata wazo la waandishi halisi. Na sababu kuu ya watetezi wa kosa hudumu katika makosa yao ni kwamba wengi wao wameamua kwa gharama yoyote kusimama na nadharia zao walizojibunia! Na hiyo ndiyo shida yao kuu. Lakini tunatarajia na kuomba kwamba ndugu hawa waliokosea wataukaribisha Ukweli ulivyo wazi katika kauli, yakini, unaong’aa, na wa kimsingi uliowekwa wazi katika kurasa hizi, na kuruhusu Ukweli ukae ndani ya mioyo yao. Hivyo tu wataweza kuongozwa kutembea katika nuru na kupata pumziko ndani Yake Ambaye anayo shauku kutuongoza katika Kweli yote, na Ambaye kwa hiyo, hutuma huu

39

Ushauri Na Mwito. {TN10: 39.3}

Chunga hatua zako, wala usisujudie aidha mwezi au siku ya sabato ya jua. Maana kwa kuiheshimu kwa utakatifu siku kama hiyo ya kawaida, utakuwa unaviabudu vitu ambavyo viliumbwa katika siku tatu za mwisho za juma la uumbaji; yaani, sayari za mbingu na viumbe vya baharini, ndege wa angani na vitambaavyo vya ardhi, wanyama wa kondeni na mwanadamu mfaji wa udongo! {TN10: 40.1}

Fuata uongozi wa Mungu badala ya uongozi wa mwezi. Msiwe waabudu sanamu, maana “. . . siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia Nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.” Zek. 13:2. {TN10: 40.2}

GHARIKA YA VITABU VYA KIDINI

Swali:

Gharika ya vitabu vya kidini mbalimbali na vinavyopingana yananijia, na sijui ni nini la kufanya kwa vyote, kwa saba-bu kimoja kinajaribu kunifunza kwa njia moja, na kingine kinyume, na bado vingine katika njia zingine, na matokeo ya kwamba ni lazima nijaribu wakati uo huo kwenenda katika njia zote zinazotetewa au kuamuriwa, ningependa, kwa mfano, kwamba

40

nakimbia nikijizunguka. Lipo tumaini gani kwa mmoja kuipata njia yake kupitia mzingile kama huu wa mafundisho? Kwa upande mmoja, naogopa kwamba iwapo nitajifunza yote, yataweza kusababisha nikose kuuona hata ukweli nilio nao sasa; na kwa upande mwingine, nahofia kwamba nisipojifunza, naweza kuuacha ukweli fulani wa thamani wa sasa, na hivyo kupoteza umilele. {TN10: 40.3}

Ukweli haswa kwamba zipo pepo nyingi za mafundisho zinazovuma ni, kwa mawazo yangu, zinadhihirisha ushahidi kwamba Bwana lazima Aweze kuwa na ujumbe katika nchi, na ya kwamba mafuriko makubwa ya vitabu vya kidini vinavyofurika ulimwengu wa kidini vinamiminwa katika jaribio la kukata tamaa la kuizamisha sauti ya ujumbe wa Bwana wa leo. {TN10: 41.1}

Hivyo jinsi unavyoonekana kuwa na misingi bora ya Biblia kwa misimamo yako kuliko wengine wanavyofanya kwa yao, na jinsi pia ulivyo na uidhinishaji mmoja wa Maandiko (Mika 6:9) kwa kusikia ujumbe wako, ninao ujasiri ku-kugeukia kwa tumaini kwamba sauti ya Fimbo itaniongoza kutoka katika mchafuko wa sauti zinazolia “lo hapa” na “lo huko”. {TN10: 41.2}

Kwanza unisaidie kuipima dhana ya Uingereza Israeli mintarafu Ufalme? {TN10: 41.3}

Jibu:

Muulizaji ni dhahiri yuko sawa kuhusu pepo nyingi za mafundisho zinazovuma leo. Na kwa mtazamo wa huu mchafuko wa sauti hofu yake kuhusu kuzisikiliza inaeleweka, na

41

kufanya la kupongezwa zaidi azimio lake la kutekeleza wajibu aliopewa na Mungu wa uchunguzi wa kibinafsi: {TN10: 41.4}

“Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, hatutaki kwenda katika njia hiyo.” Yer. 6:16. “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yohana 4:1. {TN10: 42.1}

Kutupa kila kitu ndani ya jaa la takataka hakika sio tu kuutupa nje ukweli huo, ila pia kuipuuza amri ya Bwana kama ambavyo imeonekana katika aya ambazo zimenukuliwa tayari. {TN10: 42.2}

Kwa kila mtafuta ukweli, isitoshe, husimama ahadi ya kwamba Yeye hatamruhusu mmoja wao adanganywe: “Mungu kamwe huwa haheshimu kutokuamini na kuhoji na shaka. Yeye anapozungumza, neno Lake linapaswa kutambuliwa na kutekelezwa katika matendo ya kila siku. Na iwapo moyo wa mwanadamu u katika muunganisho hai na Mungu, sauti inayokuja kutoka juu itatambulika. . . Wale wanaoyafanya mapenzi ya Mungu watalijua fundisho iwapo ni la Mungu kwa maana hakuna udanganyifu wowote utayafunika mawazo yao.” — Shuhuda juu ya Kazi za Shule ya Saba-to, uk. 64, 65. {TN10: 42.3}

Pamoja na ahadi hizi za hakika kusimama kwazo, basi hebu sasa tulichunguze

42

Fundisho La Uingereza-Israeli. {TN10: 42.4}

Jarida linaloitwa, Shule ya Mawasiliano ya Ufalme, uk.18 linaeleza msimamo wa lile vuguvugu: “Sisi Waingereza wa Kale ni watu wale wale walioishi chini ya jina la Israeli katika siku ya Agano la Kale. . . {TN10: 43.1}

“. . . Wafalme kuanzia kwa Sulemani, mfululizo, kwa mstari wa moja kwa moja, usiokatizwa hadi kwa Mfalme wa sasa — George wa 6 — kwa kiti cha enzi nchini Uingereza leo. Tunaamini kwamba Bwana — ambaye ni Mfalme wa wafalme wa kabila la Yuda na wa Nyumba ya Daudi — kwa maana Yeye ni Simba wa kabila la Yuda, (Ufu. 5:5) na ya kwamba hivi karibuni Yeye atarudi na kukichukua kiti cha baba Yake, Daudi.” uk. 1, 8. {TN10: 43.2}

Mwandishi wa taarifa hii hubishana kwamba ingawa watu wa kale wa Mungu walizama kama ufalme wa Israeli, wameibuka leo kama ufalme wa Uingereza. Lakini ikizungumzia Ufalme wa Israeli na watu wake, Roho ya Unabii, wakati wa kale, ilisema: {TN10: 43.3}

“Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu Nitawatawanya kwa pepo zote, kisha Nitafuta upanga nyuma yao. Hivyo ndivyo ghadhabu Yangu itakavyotimia, Nami nitatosheleza hasira Yangu

43

juu yao, Nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeiti-miza ghadhabu yangu juu yao. Tena nitakufanya kuwa ukiwa, na aibu, kati ya mataifa wakuzungukao, machoni pa wa-tu wote wapitao. . . “Basi, Bwana Mungu asema hivi; Angalia, Mimi, naam, Mimi, ni juu yako; Nami nitafanya hukumu kati yako machoni pa mataifa. Nami nitakutenda Nisiyoyatenda zamani, wala Sitafanya tena mambo kama hayo, kwa sababu ya machukizo yako yote. . .” “Nitakipindua, Nitakipindua, Nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja Yeye ambaye ni haki Yake; Nami nitampa.” Ezek. 5:12-14, 8, 9; 21:27. {TN10: 43.4}

“Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena.” Isa. 7:8. {TN10: 44.1}

Jarida lililotajwa hapo awali husisitiza hasa kwamba Uingereza ni kabila la Efraimu, ingawa neno la la unabii lililo imara linaeleza waziwazi kwamba Efraimu “hawatakuwa watu.” Hivyo unabii unatangaza kwamba ufalme wa Israeli ungekoma, na ya kwamba watu wangefukuzwa kati ya mataifa ya dunia. Hata hivyo, ipo ahadi kwamba baada ya mi-aka ya kutapanywa, Bwana “Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, Nami

44

Nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe.” Ezek. 37:21. {TN10: 44.2}

“Naye atawatwekea mataifa bendera, Atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, Atawakusanya watu wa Yuda wali-otawanyika, kutoka ncha nne za dunia.” Isa. 11:12. {TN10: 45.1}

“Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema Wake kwa kicho siku za mwisho.” Hosea 3:4, 5. “Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utaku-wa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena ali-yeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa Bwana Anakufu-rahia, na nchi yako itaolewa. Nao watawaita, watu Watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; nawe utaitwa, Ali-yetafutwa, Mji usioachwa.” Isa. 62:2-4, 12. {TN10: 45.2}

Maandiko haya yanaweka wazi ukweli kwamba Mungu angewatawanya Israeli kila mahali

45

kati ya mataifa, awaache bila mfalme au nchi yao kwa “siku nyingi,” na hatimaye kuwakusanya mmoja mmoja kutoka kwa kila taifa. Wakati huo watamchagua Daudi mfalme wao, na kuwa “watu watakatifu.” Isa. 62:12. {TN10: 45.3}

Kwa ajili ya maelezo ya kina ya Ufalme, soma Trakti zetu Namba 8, Mlima Sayuni Saa ya Kumi na Moja, na Namba 12, Dunia, Jana, Leo na Kesho. {TN10: 46.1}

— 0-0-0 —

Maswali yaliyoshughulikiwa hapa ndani yanafichua kwamba nguvu isiyoonekana ya kishetani ikitenda kazi kupitia wanadamu, inatumia manufaa kwa kila fursa iwezekanavyo kuleta ndani ukengeufu na mchafuko na kuutawanya uwezo wa kufikiri na umakini. Zinaonyesha kwamba wakati mwana-nadharia mmoja anajaribu kuukanganya ukweli mmoja, mwana-nadharia mwingine anajaribu kuukanganya ukweli mwingine. Kwa hivyo ni dhahiri kwamba adui wa Mungu na watu ameamua kwa njia moja au nyingine kuwatumbukiza watu kuzimu. Ili kuepuka janga hili la kutisha, msomaji basi anaonywa kugeuka kuyaacha maandishi ya watu ambao hawajavuviwa na kuzingatia tu wale waliovuviwa na kuchunguza na kujifunza bila kukoma kila kitu kinachokuja kwa jina la Bwana. {TN10: 46.2}

(Italiki zote ni zetu)

Kwa kujifunza zaidi mada ya Ishara ya Yona, soma Gombo la 2 la Fimbo ya

46

Mchungaji, uk. 17-26; Msimbo wa Nembo, Gombo la 1, Namba 6, uk. 5-7 (1934); Gombo la 2, Namba 12, uk. 6 (1936); Gombo la 3, Namba 8-9-10, uk. 10 (1937). {TN10: 46.3}

— 0-0-0 —

Mtu yeyote anayetutumia majina na anwani za Waadventista watunza Sabato, atakuwa na haki ya kupokea, bila malipo, mfululizo wetu wa Ukweli wa Sasa wa trakti kumi na tatu hadi leo, na kiungo chetu rasmi, Msimbo wa Nembo (ambamo maswali yote ya wasomaji yamejibiwa.) {TN10: 46.4}

FAHARISI YA ROHO YA UNABII

47

FAHARISI YA MAANDIKO

>