fbpx

Trakti Namba 07

Trakti Namba 7

Pambano Kuu

Juu ya

“Fimbo ya Mchungaji”

Sikiliza na Uhesabu Ushahidi kwa Pande Zote Mbili

Kabla ya Kufyatua kwa Ajili au Dhidi ya

1 Jalada

TRAKTI NAMBA 7

Kilichapishwa tena 1954

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga.

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitathaminiwa.

Kimechapishwa Marekani.

2

PAMBANO KUU

Juu ya

“Fimbo ya Mchungaji”

Na V.T. Houteff

“Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?” Yohana 7:51. Hesabu ushahidi pande zote mbili kabla ya kufyatua kwa ajili ya au dhidi ya.

“Wakajibu,” wakamwambia Wewe pia ni wa Galilaya? “Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.” Yohana 7:52.

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

3

YALIYOMO

 

Mambo Yaliyowekwa Wazi ……….…..…………….…… 5

Hitaji la Uchunguzi wa Kibinafsi ….……………….…… 12

Mapatano ….………..………………………………………..… 14

Wajumbe wa Kamati Walikuwa………………………… 21

Jibu Lililoahidiwa……………….. ……………………………. 22

Nia Iliyoshawishi Dhamiri za Kumi na Wawili….…..25

Kukanusha kwa Uongo ………………………………. …… 29

Ulinganisho Wenye Hila ……………………………..…….. 30

Jicho la Dhehebu ………………………………………….……. 42

Kwa Kamati ya Kumi na Wawili ……………………….…. 48

Neno kwa Waumini ……………………………………………. 51

Ushuhuda wa Binafsi ………………………………………….. 58

Fungu la Kila Mwandishi Anayeleta

Vitu Vipya na vya Zamani ……………………………..….. 61

Nini Kitakachopatikana Au Kupotezwa? …..…………. 66

Kwa Waadventista Wote wa Sabato — Salamu! …. 74

4

PAMBANO KUU

Juu Ya

“Fimbo ya Mchungaji”

Wapenzi Waamini Wenzangu katika Ujumbe wa Malaika wa Tatu:

Kuamini kwamba mungependa kuwa na ufahamu hakika wa mgogoro sasa unaolikumba kanisa letu pendwa S.D.A., sisi kama ndugu wa imani moja ya thamani tunakuja kwenu kwa jina lake Yeye Ambaye, ingawa alikuwa mtakatifu, alikula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, na Ambaye, ingawa Alikuwa mtakatifu, kamwe kwa neno au kwa tendo, hakusema: “Simama peke yako, usinikaribie Mimi, kwa maana Mimi ni mtakatifu kuliko wewe” (Isa. 65:5), ila alisihi: “Haya, kila aonaye kiu, njoni majini.” Isa. 55:1. {TN7: 5.1}

Kuamini kwamba wengi wenu (kabla ya kusaidia upande mmoja au mwingine kufyatua bunduki zao), mtafanya kama Nathanieli (Yohana 1:45-51), mtafuata mfano ambao Bwana ameweka mbele yetu, na kuitikia changamoto ya jukumu la kuchunguza, — “njoo uone” — tunatarajia kwamba, katika kurasa zinazofuata, mtayaangalia bila upendeleo

Mambo Yaliyowekwa Wazi. {TN7: 5.2}

Kwamba ushirika wa S.D.A. umegawanyika kwa swala la machapisho ya Fimbo ya Mchungaji, tunajuta sana, na hivyo zaidi tunapowacha kutambua kwamba kupasuka huku kamwe hakungestahili kutukia, kwa maana Mungu alitumaini sauti Yake, Fimbo, iweze

5

kusikika, jinsi anavyosema Yeye, kupitia kwa nabii Wake: “Sauti ya Bwana inaulilia mji [kanisa], na mtu mwenye akili ataliona jina Lako: Isikieni hiyo fimbo na Yeye aliyeiagiza.” Mika 6:9 {TN7: 5.3}

Kama sababu wewe ni kati ya wengi katika “mji” ambaye sauti ya Bwana inakulilia uisikie Fimbo na kwa vile tunataka kuamini kwamba unayo bidii kwa wokovu wako na kwa wokovu wa ndugu zako, na kwa moyo wote unajitolea kwa ustawi wa dhehebu, lazima tuamini hakika kwamba unahangaika kujua ukweli kuhusu shida hii kubwa ambayo inamkabili sawa sawa kila Mwadventista wa Sabato. {TN7: 6.1}

Katika mwaka wa 1930, wakati Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, lilikuwa bado katika mswada, nakala thelathini na tatu za fotokopi ziliwekwa mikononi mwa baadhi ya ndugu wanaoongoza wa Baraza Kuu. Kwa kujibu ombi la mwandishi kwamba wafanye uchunguzi wa makini kuhusu yaliyomo, wale waliozipokea waliahidi kufanya hivyo na kumjulisha, ama ana kwa ana au kwa barua, matokeo na makusudi yao. Wakati ambapo toleo la kwanza la hii trakti ilipochapishwa, miaka sita ilikuwa imepita, na ndugu wawili tu kati ya thelathini na watatu walikuwa wamejibu (hakuna hata mmoja aliyefanya hivyo hadi sasa). Mmoja, Mzee F.C. Gilbert, kibinafsi aliandika mistari machache, ambayo, kwa sababu tangu wakati huo imezusha maswali ya mara kwa mara kuhusu maandishi yaliyochapishwa ya Fimbo ya Mchungaji, tunaambatisha nakala ya fotokopi kuchunguzwa. {TN7: 6.2}

6

IDARA YA KIYAHUDI Juni 26, 1930

F.C. Gilbert Katibu

Bw. Victor T. Houteff,

Los Angeles, California,

Mpendwa Ndugu:–

Tulipokuwa kwa kongamanao la Baraza Kuu la mwisho lililofanyika huko San Francisco ulinisimamisha siku moja katika ukumbi karibu na mojawapo wa milango ya kuingilia kwenye ukumbi, na kunipa hati kubwa ambayo ulisema ulitaka kuweka mkononi mwangu, na kuniuliza kuisoma, na nikuandikie maoni yangu kuihusu. {TN7: 7.1}

Hati hiyo ilikuwa ni ya namna kubwa ambayo ingeweza kufanya kuwa isiyowezekana kwa mtu wa kawaida kuimaliza katika miezi kadhaa. Natambua kwamba wakati ni wa thamani sana, na bila shaka ninadhani unatumaini kupata aina fulani ya jibu. {TN7: 7.2}

Kwa hivyo nilichukua muda kidogo na kusoma sehemu fulani za waraka huo, na nilidhani nitakupa matokeo yangu. {TN7: 7.3}

Mimi hasa nataka kutambua sehemu yako #3. Sehemu yako #3 hushughulikia kurasa tano. Katika kuchunguza kurasa hizo za sehemu hiyo naona kwamba unazingatia katika kurasa hizo kuwahusu Esau na Yakobo. Unawalinganisha watu hawa wawili kwa mifano. Wao huwakilisha mifano mbalimbali. Katika kurasa hizo tano unafanya maelezo mengi mazito ya matumizi ya watu hao wawili kwa siku yetu ya sasa, lakini haupeani uthibitisho wa Maandiko. Unaelewa, ndugu mpenzi, mtu anapolisema jambo au mtu anamaanisha hivyo na hivyo, lazima awe na uthibitisho wa kiungu kwa dai lake. Ikiwa sivyo, kwa nini mtu aipokee kama mamlaka taarifa yake zaidi kuliko mtu angepaswa kukubali kama mamlaka taarifa ya mtu mwingine yeyote. Katika kulishughulikia na Neno la Mungu, tunapaswa kulindwa kwamba hatupenyezi katika Maandiko kile ambacho hakipaswi kuwa humo. Ikiwa Roho wa Mungu atatatoa maelezo kwa andiko, basi matumizi yamevuviwa. Lakini wakati mtu anafanya madai kuhusu Maandiko na hana mamlaka ya Mungu kuunga mkono madai yake, anaweza kuelekea kulitumia Neno la Mungu kwa hila. Nina hakika hutaki kufanya jambo kama hilo, lakini upo uwezekano hata hivyo. {TN7: 7.4}

Hebu nikuonyeshe ninachomaanisha. Katika Sehemu yako #4, ukurasa #4, unasema:– {TN7: 7.5}

“Mwanzo wa Njaa.”

“Mstari wa kugawa kati ya miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa ni msalaba. Ambapo miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa huanzia. Mwaka wa kwanza wa njaa ni mwanzo wa kanisa la Kristo wakati wa mitume.” {TN7: 7.6}

Sasa, ndugu mpendwa, unapata wapi mamlaka yoyote kutoka kwa Neno la Mungu au kwa Roho ya Unabii kwa madai kama hayo? Unapata wapi katika uvuvio msingi wowote kwa maelezo kama haya? Unafanya tu kauli kwa mamlaka yako mwenyewe, lakini hauna msingi wa Maandiko kufanya taarifa hiyo. {TN7: 7.7}

Itaonekana kwamba kama kulikuwa na wakati ambapo Neno la Mungu lilikuwa kwa wingi ulikuwa wakati ambapo mitume waliondoka kuhubiri Neno la Mungu. Roho Mtakatifu aliwapa wale watu wa Mungu nuru kwa Maandiko ya Agano la Kale hivi kwamba walikuwa na ufahamu wa Neno kwa namna ya wazi sana na imara. Biblia ilikuwa hakika kitabu kipya kwa watu katika siku za hao mitume. Unaposoma Matendo, sura ya pili, tatu, na nne, unapata ufahamu mzuri zaidi katika maana ya baadhi ya Zaburi na maandishi ya Manabii. Yalikuwa ni matumizi ya Maandiko ya Agano la Kale na mitume wale wa Kristo ambao waliwaongoza mamia, naam maelfu kumpokea Mwokozi. Hakika huo haukuwa wakati wa njaa. {TN7: 7.8}

Inaonekana kwangu, ndugu mpendwa, kwamba Mungu ametupatia utajiri katika Neno Lake, katika maandishi ya Roho ya Unabii, na katika vitabu vingi vilivyobarikiwa vilivyoandikwa na watu wa Mungu miongoni mwetu. Inaonekana kwangu kwamba ikiwa kama mtu unataka nuru kwa Maandiko unapaswa kuchukua muda na kusoma maandishi kama hayo, na kisha utapata chakula kingi cha kiroho kwa ajili ya nafsi yako. Iwapo utaendelea kusoma na kujifunza jinsi ambavyo umesimulia katika hati hiyo kubwa, baada ya muda utajikanganya sana. Italeta mchafuko popote utakapopendekeza mambo. {TN7: 7.9}

Niamini, mwaminifu ndugu yako,

F. C. Gilbert.

7

Wachungaji wa Dhehebu, pasipo kutoa kiini cha yaliyomo, walijaribu kuwafanya watu wa Mungu waamini kwamba barua ya Mzee Gilbert iliandikwa kwa niaba ya Kamati ya Baraza Kuu. Kwa mtazamo wa hili, tunawaalika ndugu zetu Waadventista wa Sabato kwa makini kuichunguza barua hiyo, ili kuthibitisha kwa kuridhika kwao kwamba haitoki moja kwa moja kwa Kamati ya Baraza Kuu wala kuiwakilisha, ila kwamba ni kujieleza kwa usadikisho wake binafsi. {TN7: 8.1}

Isitoshe, imetangazwa miongoni mwa Waadventista wa Sabato ya kwamba “Mzee Gilbert hajaona nuru ndani ya huo mswada, na kwa hivyo hawapaswi kupoteza muda kuyachunguza madai yake.” {TN7: 8.2}

Je, watu wa dhehebu lote wanafuata ubongo wa mtu mmoja? Je! Mzee Gilbert atalazimisha tangu sasa na kuendelea kuhusu ni nini kitaletwa na ni nini hakitaletwa mbele ya watu wa Mungu? Iwapo ni hivyo basi fikiri ni katika hatari gani ya kuogofya yatakuwa maslahi yetu ya milele! {TN7: 8.3}

Kumbuka kukiri kwake, katika aya ya kwanza na ya pili ya barua yake, kwamba hajachunguza kwa undani huo mswada uliowasilishwa kwake; lakini alitoa hukumu juu yake! Mswada wenyewe, ingawa, umeonyesha kuthibitisha kwamba Agano la Kale ni ghala kubwa la Neno la Mungu — bohari la ugavi wa chakula cha kiroho kwa watu Wake wakati wa Agano Jipya; lakini Mzee Gilbert anajaribu kupinga ukweli huu wazi kwa taarifa

8

yake “Roho Mtakatifu aliwapa wale watu wa Mungu nuru kwa Maandiko ya Agano la Kale hivi kwamba walikuwa na ufahamu wa Neno kwa namna ya wazi sana na imara. Biblia ilikuwa hakika kitabu kipya kwa watu katika siku za hao mitume.” Lakini akijaribu hivyo kudhoofisha madai ya mswada huo, yeye bila kujua anayathibisha tu. {TN7: 8.4}

Kisha kuhusu somo kutoka kwa uzoefu wa Esau na Yakobo, barua hiyo inasema: “lakini hauna msingi wa Maandiko” kwa “matumizi ya watu hao wawili kwa siku yetu ya sasa.” Mtu yeyote ambaye atavumilia machungu kuichunguza hiyo mada, ambayo sasa imechapishwa katika Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, atapata wingi wa “ushahidi wa Maandiko.” {TN7: 9.1}

Zaidi ya hayo, kama mada ya kitovu cha mswada wote si Agano la Kale na Jipya wala Esau na Yakobo, ila ni cha watu 144,000, wajibu wa Mzee ulikuwa kutupatia maoni yake kuhusu mada hiyo. Kwa hivyo, ubishi wake hafifu kwa mambo ya umuhimu wa pili, ni kando na uhakika halisi katika swala — ukweli kuhusu watu 144,000. {TN7: 9.2}

Katika utofauti maarufu wa wazi kwa barua ya Mzee Gilbert ni barua mbili zinazofuata, moja kutoka kwa mchungaji wa Waadventista wa Sabato awali akishikilia nafasi ya majukumu katika dhehebu, na nyingine kutoka kwa tabibu wa Waadventista wa Sabato, aliyekuwa mwalimu katika mojawapo wa vyuo vikuu vya Dhehebu, na mwanafunzi anayeaminika wa Maandiko. {TN7: 9.3}

9

Charleston, S.C., Desemba 15, 1933.

Mpendwa Ndugu yangu Houteff:

Napenda kukushukuru kwa moyo wote kwa kuita umakini wangu, kama mchungaji wa injili, kwa kweli za thamani za Biblia, na vito vya Roho ya Unabii, ambavyo ni vingi kote kote katika magombo mawili madogo ya “Fimbo ya Mchungaji,” vilivyotumwa kwangu, ama wewe mwenyewe, au kwa ombi lako, sina shaka. {TN7: 10.1}

Kwa miaka mingi nimekuwa na nia ya undani kwa kile Roho ya Unabii hutuambia kinapaswa kufanyika kati yetu kwa njia ya “uamsho na matengenezo,” na kwa hivyo nimetazama kwa shauku kubwa kila jaribio la kuzindua hilo “vuguvugu la matengenezo,” lakini nimekuwa nikikata tamaa kwa yote, kwa sababu hayakutimiza, hivyo wakati vijitabu vyenu vidogo vilikuja vilinipata na njaa sana kwa uamsho huo wa “uungu wa kweli” ndani ya moyo wangu. {TN7: 10.2}

Naweza kusema kwamba nilipotazama kwa mara ya kwanza “Fimbo ya Mchungaji,” jina lenyewe lilionekana kunichukiza, na karibu nikirarue mara kadhaa kabla kukisoma, lakini kila wakati nilipokuwa karibu kukiharibu hicho kitabu, mawazo yangekuja kwangu kwamba hili ni kinyume na kanuni yangu, na ningaliweza kukiweka hicho kitabu tena. Nilipoweza kumaliza kukisoma, Nilishangazwa, na mara nyingi ningelia kwa Mungu anisamehe kwa ajili ya dhambi zangu kama mchungaji, iwapo Yeye alikuwa hakika ananena nami kupitia kigombo hiki kidogo, na nilipokimaliza, nalishawishika kuamini kwamba sikuwa nimesoma kitabu cha kawaida, lakini nikiwa mwangalifu sana kuhusu kulipokea kosa, nalianza kukisoma mara ya pili, nikilinganisha kwa Biblia na Shuhuda kuhakikisha kilikuwa na uwiano na kabla ya kila kusoma, ningemlilia Mungu “kuufunua ukweli na kulifichua kosa,” kulingana na ahadi Yake. Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 107. {TN7: 10.3}

Nilipomaliza kukisoma kitabu hicho mara ya pili, naliogopa kwamba ni ukweli, kwa maana nalijua vyema, iwapo ulikuwa ukweli, mimi, kama mchungaji, ningewajibika kwa Mungu kwa mwenendo wangu kuhusu wingi wa nuru ambayo Yeye aliita usikivu wangu kwayo ambayo kamwe sikuiona awali. Kweli mimi kwa kawaida nalishangaa yalikotoka maarifa hayo, na kuamua kukisoma tena hicho kitabu ili kuhakikisha kwamba sikuwa nimepuuza jambo lolote nilipokuwa nikisoma kushawishi kosa na nilipomaliza mara ya tatu, ingawa sikuelewa kila jambo mle kitabuni, bado nalikuwa na uhakika wa jambo moja, nalo ni, singeweza kukanusha lolote ndani yake, kwa kuwa kiliuwiana na Biblia na Roho ya Unabii. {TN7: 10.4}

Na sasa baada ya karibu miaka mitatu ya kuangalia tokeo la kusoma “Fimbo ya Mchungaji” juu ya mchungaji na mlei, napata kwamba, karibu wote isipokuwa wachache, wachungaji huukataa ujumbe wa kitabu hicho, ama kwa upofu au kuhofia wakuu wao, na walei, karibu wote isipokuwa wachache, hupokea ujumbe wake wa kemeo na onyo kwa furaha na shangwe, na hutafuta kurekebisha maisha yao vile vile, na hisia za kiroho za watu hao ni za juu zaidi kuliko hapo awali kwa sababu wanaupenda ujumbe wa Malaika Watatu zaidi, na wanawapenda ndugu zaidi kuliko hapo awali. {TN7: 10.5}

Kwa kuhitimisha barua hii napenda kukuambia kwamba ninaamini Bwana amekutumia kuleta kwa watu wetu ujumbe muhimu kama ule aliokuja kwa kanisa la S.D.A. wakati walikuwa wamekongamana huko Minneapolis, na nafikiri nimeelewa vyema, nikiwa mchungaji katika dhehebu hili kwa miaka mingi, na nikiwa nimefanya kazi nchini Marekani na katika nchi za nje. Tumeonekana kuukataa kabisa ujumbe wa matengenezo yaliyowekwa katika “Fimbo ya Mchungaji” kabisa jinsi ndugu zetu walivyoukataa ule wa mwaka 1888. {TN7: 10.6}

Bwana aweze kukubariki sana katika kila kitu unachofanya kwa jina Lake ni sala ya nduguyo katika Kristo. {TN7: 10.7}

E. T. Wilson.

10

KWAKE AMBAYE HILI HUENDA LINAMHUSU:

Kwa kufuata maagizo ya uk. 104-7 wa Shuhuda kwa Wachungaji, “Je! Tuyachunguze Vipi Maandiko,” Nilijitahidi kuwaita pamoja ndugu wachache waliojitoa wakfu Waadventista wa Sabato kukutana na mwandishi wa “Fimbo ya Mchungaji” nyuma ya jengo langu la ofisi huko Chandler, Colorado, — mahali pangu pa zamani pa kufanyia kazi. Hili lilifanyika kwa jukumu langu mwenyewe. Kwa sababu, kupitia kwa ndugu wa karibu sana, ujuzi wa kibinafsi wa pambano huko California kuhusu vitabu vya “Fimbo ya Mchungaji” na udhalimu mkubwa kwa mwandishi, Nilihisi mno kukutana naye uso kwa uso na hivyo kumsikiza kwa makini na kwa uaminifu. Nilijihisi pia ni lazima nialike uwepo wa mchungaji aliyetawazwa kushiriki katika uchunguzi huu. Kwa majaliwa ya Mungu, hali ilionekana kujipanga kwa uwepo wa Mzee E.T. Wilson, rais wa baraza la Carolina. Yeye, pamoja na ndugu na dada H.G. Warden na mzee wa eneo la kanisa la Florence S.D.A. na washirika wake walijumuisha kundi letu kwa uchambuzi. {TN7: 11.1}

MATOKEO

Wale waliohusika katika uchambuzi walisadikishwa sana na ukweli kwamba katika uwezo wa mwanadamu pekee haiwezekani kabisa kutunga, kufanya umbo au kuunganisha pamoja ishara nyingi ngumu za Biblia, mifano, mambo au ukweli, katika uhusiano unaoeleweka wa ufafanuzi ulioonyeshwa ambao unaweza kwa urahisi kufichua uongo, na utata wa kweli mbalimbali zinazohusiana zifanywe kuwa rahisi kwa umbo kama hilo la kueleweka na wale ambao hawajajua kusoma, pamoja na wale wa utamaduni, ambapo wote wanaweza kufanywa kukubali kwamba maneno ya Biblia na yanayopingana wazi yanaweza kupangwa ili yawe rahisi sana kwa ufupi na maana ya umakini. {TN7: 11.2}

Baada ya juma la kujifunza kwa uangalifu vikao vitatu kila siku, vikitangulizwa kwa sala, wote waliohudhuria walishiriki kumsihi Bwana ili kupitia kwa Roho Mtakatifu aweze kuongoza katika ugunduzi wa ukweli, na ya kwamba kosa, iwapo lingekuwapo, lionekane wazi; sote tulikubaliana, kwamba mbali na makosa ya uchapishaji, na katika baadhi ya maswala ya Kiingereza kisicho sahihi, pia baadhi ya taarifa za kihistoria ambazo hatuwezi kuthibitisha au kukataa; na zaidi ya hayo, na kutambua kwamba mwandishi hakuwahi awali kuhusishwa na imani ya mizimu kwa aina yoyote ya mifumo yake, na kama kila uchunguzi ulizidi kupanuka kwa nuru kubwa juu ya “Ujumbe wa Malaika Watatu,” pia mambo mengi muhimu na yanayokinzana ambayo yamekuwa mafumbo ya kutatanisha yalifafanuliwa kikamilifu, halikuachwa swali la shaka katika mawazo yetu kwamba haya magombo yametayarishwa chini ya namna fulani ya nuru ya Mungu; na ya kwamba wakati umewadia kamili kwa ajili ya kuzikunjua kweli hizi kwa ulimwengu unaoangamia. {TN7: 11.3}

Imewasilishwa kwa heshima,

W. G. Butterbaugh M.D.

11

Kwamba Mzee Gilbert, ambaye hajasoma ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, afikiri kwamba anaweza kuitambua kama ni ukweli au uongo, ni ajabu. Lakini kama washiriki wenzake wawili wamekichunguza kikamilifu kitabu hicho, ni busara kabisa kuhitimisha kwamba hukumu yao ni ya kutegemewa. {TN7: 12.1}

Barua hizi kutoka katika faili zetu, ni mbili tu kati ya nyingi, zilizoandikwa na wale ambao wameuchunguza ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, na ambao hukiri kwamba ina mwito wa saa hii. Sasa ruhusu roho ya unabii ibadili zaidi uamuzi wako kuhusu

Hitaji la Uchunguzi wa Kibinafsi. {TN7: 12.2}

“Mungu anayo nuru ya thamani itakayokuja kwa watu Wake…. Wakati nuru mpya inawasilishwa kwa kanisa, ni hatari kujifungia mbali kutoka kwayo…. Kuhukumu lile ambalo hujalisikia na usilolielewa hakutakweza hekima yako machoni pa wale ambao ni waelekevu katika uchunguzi wao wa ukweli. Na kunena kwa kuwadharau wale ambao Mungu amewatuma na ujumbe wa ukweli, ni upumbavu na uwazimu…. Kwa maana Mungu atalitukuza Neno Lake ili liweze kuonekana katika nuru ambayo hatujawahi kuiona hapo awali…. Nuru itakuja kwa kila anayeitafuta kwa bidii, jinsi ilivyokuja kwa Nathanieli…. Lazima uhuru utolewe kwa uchunguzi waziwazi wa ukweli, ili kwamba kila mmoja aweze kujua mwenyewe ni nini ukweli…. {TN7: 12.3}

“Nuru ya thamani itaangaza kutoka kwa Neno la Mungu, na mtu yeyote asithubutu

12

kuamuru ni nini kitakacholetwa au kutoletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangazisha Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yoyote nafasi yake ya mamlaka, hakuna mtu aliye na haki ya kuizimisha nuru kutoka kwa watu. Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 60-65. {TN7: 12.4}

Katika mwaka wa 1933, karibu miaka mitatu baada ya ndugu wa Baraza Kuu kupewa mswada wa Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, na baada ya swala hili kuwa limefika ambapo hawangaliweza kuendelea tena bila kutoa kwa waumini aina fulani ya jibu kwa mtazamo rasmi kuhusu mafundisho ya Fimbo (na kwa nini hawakuwa, kama ndugu, wamewahi kuketi chini na mwandishi na kumsikiza kwa uelekevu), maafisa wa kanisa la Fullerton, California, wakawa chombo kupata Baraza la Muungano wa Pasifiki

13

kumsikiza baada ya kunyimwa kwa muda mrefu. Inayofuata ni taarifa ya neno kwa neno ya

Mapatano: {TN7: 13.1}

Kwa Washiriki wa Kamati ya Mkutano wa Muungano wa Pasifiki:

Wapenzi Ndugu:

Sisi, washiriki wa Kanisa la Tabernacle S.D.A. la Fullerton, Calif., baada ya kushauriana na Victor T. Houteff kuhusu mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji, kwa heshima tuaomba kwamba mteue kamati ya kumi au kumi na wawili “ndugu wa uzoefu” kukutana na Ndugu Houteff wakati akiweka mbele yao ushahidi wa imani yake katika misingi ya ujumbe wake. Mada za kuangaliwa ni — “Mavuno,” “Ezekieli 9,” “Mnyama kama Chui wa Ufunuo 13,” “Hosea sura ya 1-2,” na “Mat. 20.” Katika mada hizo Ndugu Houteff atatumia tu maandishi ya Biblia na Roho ya Unabii. {TN7: 14.1}

Muda wa kutumika haupaswi kuzidi juma moja. {TN7: 14.2}

Baada ya kuitafiti kila mada kamati iliyochaguliwa inaweza kupumzika kushauriana, na kisha inaweza kuwasilisha ushahidi wake kwa ajili ya makosa katika fundisho la Ndugu Houteff, ushahidi huo utolewe katika Biblia na Roho ya Unabii tu. {TN7: 14.3}

Iwapo baada ya somo la kwanza makosa yaweze kuthibitishwa kutoka kwa mamlaka yaliyotajwa hapo juu, masomo zaidi hayapaswi kutolewa. Masharti yale yale yatatawala baada ya kila somo litakalofuata. {TN7: 14.4}

14

Ikiwa kamati itapata makosa katika mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji, na inaweza kuyakanusha kwa mafundisho ya Biblia na Roho ya Unabii Ndugu Houteff anakubali kuacha kuitetea Fimbo ya Mchungaji, na kuyakana hadharani. {TN7: 15.1}

Ndugu Houteff pia anakubali kuacha kueneza Fimbo ya Mchungaji, kwa umbali anaoweza kuthibiti, katika Baraza la Muungano wa Pasifiki, wakati uchunguzi huu unapofanywa. {TN7: 15.2}

Masharti ambayo hapa yeafikiwa ni kwa mapatano ya maagizo katika Shuhuda, Gombo la 5, ukurasa wa 293; Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, ukurasa wa 65-66. {TN7: 15.3}

Yamewasilishwa kwa heshima,

Wawakilishi wa Kanisa la Tabernacle.

J.W. RICH,

L.R. SOMMERVILLE

Kwa niaba ya Fimbo ya Mchungaji,

V.T. HOUTEFF

_____________

Muda mfupi baada ya rufaa iliyotajwa hapo juu, barua inayofuata ilipokelewa: {TN7: 15.4}

Fullerton, Calif.,

Januari 23, 1934.

Victor T. Houteff,

10466 S. Hoover St.

Los Angeles, Calif.

Mpendwa Ndugu Houteff:

Katika mawasiliano ya simu jioni hii kutoka kwa Mzee Prout ananambia kwamba Kamati ya Muungano wa Baraza imekubaliana

15

kutoa kamati iliyoombwa katika mkakati wetu siku ile, na ya kwamba Muungano utajaribu kuwaunganisha wale watu kwa muda usiozidi majuma kadhaa kukusikiza. {TN7: 15.5}

Yeye hakuwajua watu wa kamati hiyo, au angalau hakunijuza majina yao kwa hivyo sijui ni watakuwa nani. Inadhaniwa kwamba mahali na wakati wa mkutano utapangwa hivi karibuni. Hasa jinsi hili litakavyofanywa halikuelezwa, iwapo watawasiliana nawe moja kwa moja, au kututumia maelezo hapa sijui. Angalau tutajua zaidi kuhusu swala hili hivi karibuni. {TN7: 16.1}

Naamini utaratibu mzima utakuwa kwa ajili ya kuinua ukweli wa Mungu na kutusaidia sote katika kujifunza Biblia na Roho ya Unabii, Nasalia,

Wako mwaminifu,

(Sahihi) J.W. RICH {TN7: 16.2}

___________

Majuma manne baada ya kuipokea barua ya Mzee Rich, Mzee Prout na Mzee Rich kibinafsi walitoa uamuzi wa Baraza kufanya mkutano uliopendekezwa Jumatatu iliyofuata. Tulikuwa, hata hivyo, tumepangilia awali shughuli muhimu kwa tarehe hiyo, tuliwajibika kuomba kuahirishwa mkutano huo. {TN7: 16.3}

Hata hivyo, ni wazi kwamba, hali pekee tu iliamua ombi letu, ripoti ilitangazwa kwamba tulijaribu kuepuka kuzingatia mapatano yetu, ingawa kwa miaka

16

mitatu tulikuwa tukiomba, kutumaini, na kujitahidi kupata kikao! Msomaji wa uelekevu, hata hivyo, upesi atajua ukweli wa jambo hili kutoka kwa kweli hizi na kutoka kwa ukweli kwamba masaa machache baada ya Wazee Prout na Rich kuwasilisha ombi letu kwa njia ya mdomo, Mzee Calkins, Rais wa Baraza la Muungano wa Pasifiki, binafsi alituma Barua inayofuata: {TN7: 16.4}

Glendale, California,

Februari 15, 1934.

Victor T. Houteff,

10466 S. Hoover St.,

Los Angeles, California.

Mpendwa Bwana Houteff:

Kwa upatano wa ombi lako kwa maandishi la Januari 18 la kusikizwa mbele yakundi la ndugu viongozi, Kamati ya Baraza la Muungano imeweka Jumatatu, Februari 19, kwa kusudi hili. {TN7: 17.1}

Hii ni kukujulisha kwamba mkutano utafanyika saa 4 asubuhi tarehe hiyo, katika 4800 Barabara ya Hoover Kusini, Los Angeles. {TN7: 17.2}

Hii itathibitisha notisi ya maneno uliyopewa leo asubuhi na Wazee C.S. Prout na J.W. Rich. {TN7: 17.3}

Wako kwa uaminifu sana,

(Sahihi)

GLENN CALKINS.

Wakati barua iliyoonyeshwa hapo juu kutoka kwa Mzee Calkins, kuthibitisha taarifa ya awali ya kamati kwa njia ya maneno ya mdomo, ilikuwa inasafirishwa, tulikuwa, kwa njia ya kuteta rasmi kuhusu kamati ilivyokuwa ikishughulikia swala zima, tuliandika na kumtumia msingi wa

17

ombi la awali la mdomo kwa Wazee Prout na Rich. Maneno ya hiyo barua ni kama ifuatavyo: {TN7: 17.4}

10466 S. Hoover St.,

Los Angeles, Calif.,

Februari 15, 1934.

Mzee Glenn Calkins,

Glendale, Calif.

Mzee Mpendwa Calkins:

Ninafurahi sana kwa fursa ambayo inanihimiza kukuandikia barua hii. Mzee Prout amenijulisha kwamba umekubali kwa upole kuitikia ombi letu la kukusikiza. {TN7: 18.1}

Nafurahi sana kujua mapatano haya na nitakuwa na furaha sana kuwasilisha kwa kamati jinsi hii nuru ilioongezwa kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu (M.A. 277). Lakini Nafikiri, Mzee Calkins, hakuna jitihada zinazopaswa kuachwa ili kuufanya muda wetu pamoja kuwa mafanikio, maana kusudi la mkutano wetu ama ni wa umuhimu mkubwa sana kwa wote wanaohusika, au labda si wa thamani yoyote. Kwa hivyo, Napenda kupendekeza kwamba upangwe vizuri na ufanywe vyema, bila kuchukua nafasi ya kukiuka mema yoyote ambayo yanaweza kutoka kwa utaratibu huo. {TN7: 18.2}

Wakati rufaa yetu kwa Baraza la Muungano ilifanywa na washiriki wa Kanisa la Tabernacle la Fullerton, California, na mimi mwenyewe, ilikubaliwa kwa maneno kwamba wale ambao wamekuwa katika vita na Fimbo ya Mchungaji waondolewe kwa kamati, lakini orodha ya Mzee Prout ya kamati iliyopendekezwa inaonyesha kwamba

18

karibu kila mtu anayejumuisha wana-kamati tayari anapinga vikali sana. {TN7: 18.3}

Tukitambua kwamba tunashughulikia jambo ambalo linahusisha maslahi yetu ya milele, na hatma ya washiriki wetu wa kanisa, uteuzi hauonekani tu wa hatari lakini pia wenye kasoro kuamini, na ni upumbavu kwangu kuukubali. Kwa maana kadiri Baraza Kuu au kamati za Baraza la Muungano zimetenda kazi kwa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, watu hawa wanajionyesha kuwa hawastahili kwa hafla hiyo, kwa maana hapo awali wamefanya kazi bila kulihusisha baraza — mamlaka ya juu — kwa kunena dhidi ya ujumbe kwenye mimbara na hata wamesababisha baadhi yetu kutupwa kimwili nje ya majengo ya kanisa bila sababu nyingine isipokuwa uwepo wetu — aibu kwa kanisa la Mungu! Wao, kwa hivyo, tayari wamelifanya dhehebu kisheria kuwajibikia uharibifu mkubwa. Je, mtawaacha watu hawa kuendelea zaidi katika hukumu yao dhaifu na ya udikteta? Zaidi ya hayo, wametangaza mbali na kote kwamba nimesikizwa na wawakilishi wa dhehebu ilhali wanajua wazi kwamba hakuna kitu kama hicho kimefanyika wakati wowote! {TN7: 19.1}

Bila kujali namna visa hivyo viwezavyo kuwa si vya maana, hakuna mahakama ya kiraia itakayoweza kuchagua jopo la aina hii. Kwa nini sisi tuweze? Je! Wokovu wetu si muhimu zaidi kuliko faida ya kidunia? {TN7: 19.2}

Hebu nipendekeze, Mzee Calkins, kwamba uwachague watu wa kutegemewa. Watu ambao

19

hawawezi kumhukumu ndugu bila kumsikiza. Watu ambao wanaweza kusimama wakweli kwa agizo hata mbingu zianguke, (si wala watu), na wale tu ambao wanaamini ujumbe wa Malaika wa Tatu kwa mujibu wa Roho ya Unabii. Kisha hebu tukutane kama ndugu kwa maombi na kujifunza katika roho ya Kristo ambapo tunaweza kuwa na uhakika kamili wa uwepo wa Bwana kuufungua ufahamu wetu kwa Neno. Vinginevyo, tutaendelea sana wa kutojua ni nini ukweli ulivyo, na hivyo ingawa wafu waweze kufufuka hatutaamka. {TN7: 19.3}

Nalifahamishwa zaidi kwamba ni lazima Nije pekee yangu mbele ya kamati. Katika hili Sioni hekima hata kidogo. Iwapo kamati itakutana nami kwa kusudi pekee la kumhukumu na kumfukuza mmoja barabarani, kwa mfano, bila kujali haki au ukweli, na kulinyang’anya kanisa la Mungu yamkini baraka iliyo katika ujumbe, basi Nasema, umepangwa kwa ujanja. Lakini sifikirii hii ni nia yako, Mzee Calkins. Nafikiri wewe ni mwaminifu kwako mwenyewe na wa kweli kwa Mungu. Angalau hii ni hisia Niliyokuwa nayo wakati ulikutana na Kamati ya Kanisa la Exposition Park, miaka kadhaa iliyopita, ambalo Nilikuwa mshirika. Ulikuwa ni wakati ulipokuja kutatua shida dhidi ya Mzee Paap. Kwa sababu umewachagua watu wako, je, si sawa na haki kuniruhusu kuwaleta baadhi ya ndugu ambao wanafahamu vyema Fimbo ya Mchungaji? Je! Wanaweza kuleta madhara gani dhidi ya haki? {TN7: 20.1}

Haitawezekana kwangu kukutana nanyi ndugu siku aliyotaarifu Mzee Prout.

Trakiti Namba 7 20

Naomba kwamba mpangilio huo ufanywe juma moja kutoka Jumatatu ijayo — Februari 26. Napenda nisikie kutoka kwenu upesi, ili niweze kupangilia ipasavyo. {TN7: 20.2}

Hebu Bwana mwema akuongoze kwa wakati huu na kukusaidia kwa uaminifu utekeleze wajibu wako kama rais wa Mabaraza, na kwa tatizo hili muhimu la sasa. Mimi

Wako kwa upendo wa undugu,

Roho ya Kikristo,

na kwa wema wa watu Wake,

(Sahihi)

V. T. HOUTEFF {TN7: 20.3}

___________

Kupuuza kabisa maombi yetu kwa maneno ya mdomo na kuteta katika maandishi yetu, wao bila shaka hawakuridhia wakatulazimisha kukutana nao kwa matakwa yao wenyewe. Na kwa hivyo ili kutoiruhusu fursa iponyoke tuliyokuwa tumeitafuta kwa muda mrefu, na ili kutotufanya kuwa kama wakiukaji, kwa hasara ya Ukweli, tulilazimika kunyenyekea kwa furaha yao dhidi ya masumbuko yetu mazito, na pia kwa majaji ambao wengi wao walikuwa tayari maadui sugu wa Fimbo. {TN7: 21.1}

Wajumbe wa Kamati Walikuwa:

A.G. DANIELLS, Mwenyekiti

W.G. WIRTH, Katibu

G.A. ROBERTS

C.S. PROUT

JC. STEVENS

H.M.S. RICHARDS

GLENN CALKINS

C.M. SORENSON

F.C. GILBERT

W.M. ADAMS

J.A. BURDEN

O.J. GRAF

Pendekezo la Fullerton halikuwa na maana kama mapatano ya mwisho, lakini tu kama rufaa. Lakini kwa kupuuza kusudi lake, Baraza la Muungano wa Pasifiki kwa ujeuri, bila hata ushauri kidogo, waliamuru kandarasi ya uchunguzi! {TN7: 21.2}

21

Mada kadhaa ambazo zingezingatiwa ni “Mavuno,” “Ezekieli Tisa,” “Mnyama kama Chui wa Ufunuo 13,” “Hosea, sura ya Kwanza na ya Pili,” na “Mathayo 20.” Wakati haukupaswa kuzidi juma moja kwa idadi nzima. Lakini baada ya somo hasa la kwanza, waliahirisha, na hawakufanya mipangilio ama ya kuwasilisha masomo yaliyokuwa yamesalia yaliyoitishwa au kwa

Jibu Lililoahidiwa. {TN7: 22.1}

Baada ya kupita karibu majuma manne kutoka kwa kikao kilichoahirishwa, tuliambiwa wakati huo kwamba watatoa jibu lao, ambalo walikuwa wamelitayarisha kwa maandishi! Katika mkutano huu, kumi na wawili wafuasi wa Fimbo walikuwepo, hakuna pingamizi ilifanywa kwa kuhudhuria kwao. Mmoja wa wana-kamati aliisoma ripoti iliyocheleweshwa kwa muda mrefu ya uchunguzi wao, ambayo ilionyesha wazi wazi kwamba waraka huo ulijumuishwa na kikomo kilichokusudiwa kwa mtazamo wa kukataa, kwa gharama yoyote, ujumbe wa Fimbo, hata kwa gharama ya kutumia mbinu nyingi zinazotumika dhidi ya ukweli wa Sabato. Ukweli huu utakuwa uchungu ulio wazi kwa wote wanaousoma kwa uaminifu waraka ambao sasa unachapishwa chini ya kichwa, Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji. {TN7: 22.2}

Mara tu baada ya kuusoma kwetu, waliahirisha mkutano, wakitunyima kwa ugumu rai yetu kusisitiza hata wakati wa dakika tatu za kutoa taarifa. Utaratibu wa udikteta na usiojali kama huu, si kitu kwa Ukristo, huashiria kwamba kamati hiyo ilifahamu vyema

22

ripoti yao dhidi ya Fimbo haikuwa imekanusha hata jambo moja. Maana wangalikuwa wameamini vinginevyo, wao papo hapo na wakati huo wangeweza kwa uzito kutuagiza kwa dhati kuheshimu mapatano yetu kukana mafundisho yetu, na kisha wangefungua mkutano wazi kwa shuhuda za kuungama. Lakini hapana, walikataa kusikia neno kutoka kwa yeyote kati yetu! {TN7: 22.3}

Zaidi ya hayo, mapatano hayo yalitaja waziwazi kwamba tunapaswa kwanza kuwapatia somo kuhusu “Mavuno,” na kwa hilo pekee yake walipaswa kujibu. Lakini katika jibu lao lililochelewa, tena wakiyapuuza masharti ya mapatano, walijaribu kwa kipigo kimoja kuukataa ujumbe wote kwa kunukuu kutoka kwa taarifa za magombo ya Fimbo ya Mchungaji taarifa ambazo, zikiwa zimeng’olewa kutoka kwenye muktadha, na ambazo, hivyo zilinyimwa kabisa ushahidi unaozithibitisha, zilionekana kama dhana tupu, zilizoganduliwa mamlaka, na hata kupingana moja kwa nyingine na Roho ya Unabii! {TN7: 23.1}

Hata hivyo, matendo yao yasiyokuwa ya maadili wala kupinga kwao kwa hila, jinsi walivyotumaini kutauzamisha ujumbe huo. Kinyume chake, wametumika tu kuuinua. Wamesababisha, hata hivyo, watepetevu na wa kijuu-juu — kila mmoja ambaye anawategemea wengine kuamua ni nini ukweli na ni nini uongo — kubaki katika hali yao ya Ulaodekia, — wavugu vugu, waliotosheka, wakisubiri “kutapikwa nje.” {TN7: 23.2}

Mzee A.G. Daniells, mwenyekiti wa kamati ya kumi na wawili, alimwahidi Ndugu Houteff nakala ya waraka ambao walitusomea, lakini hadi leo hawajawahi

23

iheshimu ahadi yao. Miezi miwili baada ya mkutano huo, tulipiga simu kwa ofisi ya Baraza la Muungano, kila wakati tu kupokea chenga na ahadi nyingine isiyokuwa na matunda. Hatimaye wakati Baraza la Masika lilikuwa katika kikao huko Washington, D.C., tulimtumia Mzee Daniells telegramu inayofuata: {TN7: 23.3}

Los Angeles, California,

Aprili 28, 1934.

Mzee. A.G. Daniells,

Bustani ya Takoma, Washington, D.C.

Utunzaji wa Baraza la Masika, S.D.A.

“Ingawa uliahidi kututumia nakala ya ripoti kwa somo la Mavuno, baada ya kuihariri, katika muda wa siku chache, majuma sita yamepita, licha ya maombi ya mara kwa mara kwa Baraza la Muungano kuituma kufanywa. Ripoti zinaonyesha, yote, au sehemu, inasambazwa tayari. Piga simu iwapo ni kweli, pia tarehe utaiwasilisha nakala yangu.” {TN7: 24.1}

(Sahihi)

V.T. HOUTEFF

__________

Kwa ombi hili la dharura, vivyo hivyo hakuna jibu liliwahi kufanywa. {TN7: 24.2}

Tunang’gamua kwamba hatua ya kamati ni vigumu kuaminika. Na tunayo majuto sana kwamba wametulazimisha, katika kuulinda Ukweli, hapa ndani kufichua ukweli, ili kila mmoja aweze kujua na kuamua mwenyewe, jinsi ambavyo Roho ya Unabii huagiza: {TN7: 24.3}

“Vile mwanafunzi huutoa kafara uwezo wa kufikiri na kujiamulia mwenyewe, anakuwa mdhaifu wa kutopambanua kati ya ukweli na uongo, na huanguka kuwa windo rahisi kwa udanganyifu.

24

Yeye huongozwa kwa urahisi kufuata utamaduni na desturi …. Akili inayotegemea uamuzi wa wengine ni hakika, punde si punde au baadaye, itapotoshwa.” — Elimu, uk. 230, 231. {TN7: 24.4}

Wakati kama huu wa sasa utaonyesha kwa kila mtu iwapo anamwamini Mungu pekee au pia katika Danieli, Nuhu, au Ayubu. Wale ambao huwaruhusu wengine wafanye kuwawazia na kujifunza kwa niaba yao na kuwaamulia, watavunjika moyo kwa hofu wakati watajikuta hivi karibuni kwa upande mbaya. Kisha “kutakuwa na kilio na kusaga meno.” Hatari hii, kwa hivyo, inatuongoza kuchunguza uhalisi wa lile Jibu, pia kugeji uwezo wa kufasiri wa

Nia Iliyoshawishi Dhamiri za Kumi na Wawili. {TN7: 25.1}

Katika barua kwa Dkt. W.S. Butterbaugh, Profesa Graf anatumia maneno “jopo la kumi na wawili,” kumaanisha kamati ya uchunguzi ya Baraza akurudia vishazi hivyo kwa mara kadhaa, na kufanya wazi kwamba wanapaswa kutambuliwa kama jamii ya mamlaka yenye kuheshimika leo kama Sanhedrini ilivyokuwa wakati wa Kristo. Mmoja wao alikuwa Profesa Graf mwenyewe, ambaye vikabrasha vyake mapema, katika mtungo wa vishazi vyake na mabishano, kwa ulinganisho na yale ya lile Jibu, vyaonyesha kwamba hii “kamati ya kumi na wawili,” kwa mujibu wa mchango wao unavyolihusu lile Jibu, ilikuwa ni kamati ya mtu mmoja tu, na ya kwamba matokeo yao yalikuwa ni zao la mbinu za kufasiri bunifu za yule mmoja. Hivi ndivyo walei wamepunjwa

25

kwa ripoti ya uwakilishi isiokuwa na upendeleo, na kupewa mawazo ya kitheolojia na mtungo wa mawazo ya mmoja, kama matokeo ya kumi na wawili! {TN7: 25.2}

Katika jaribio la kupindua imani ya Daktari katika Fimbo, Profesa katika barua yake anasema: {TN7: 26.1}

“Sasa, ndugu yangu, naamini umekuwa na uzoefu wa kutosha katika uchunguzi na ufasiri wa Maandiko kutambua kwamba ni hatari sana hakika kujaribu kujenga mafundisho muhimu ya Biblia na ufafanuzi kwa msingi wa nembo na mifano.” {TN7: 26.2}

Hapa kwa kweli, ajabu jinsi ilivyo, profesa anasisitiza kwa dhati kwamba kutegemea vivuli, nembo, na mifano ni “hatari sana” kama “msingi” wa kujenga “mafundisho muhimu ya Biblia.” Lakini iwapo madai yake ni sahihi, basi hayashtaki tu mafundisho ya Fimbo, bali pia mafundisho ya S.D.A., maana yamejengwa kwa kiasi kikubwa kwa ufasiri wa mifano! {TN7: 26.3}

Kama ilivyo na wengi wa S.D.A., mwandishi wa trakti hii aliongoka kwa kanisa la Waadventista wa Sabato kupitia mafundisho yake yaliyofunuliwa, hasa yote ambayo yamejengwa kwa nembo na mifano, kama sanamu kubwa ya Danieli 2 na wanyama wa Danieli 7. Hakika, ufasiri wake hutoa ufunguo wa pekee ambao hufunua siku za sasa na za baadaye, kuonyesha kwamba falme za dunia hii zitafikia mwisho wakati utakaposimamishwa ufalme wa Kristo: kwa maana jiwe

26

ambalo “lilichongwa bila kazi ya mikono” (Dan. 2:34), liliipiga hiyo sanamu, na kuivunja vipande vipande, na kuitawanya katika pepo nne. {TN7: 26.4}

Ukweli rahisi ni kwamba ufasiri wa wanyama wa ki-mfano wa Danieli 7 ni uti wa mgongo wa “mafundisho muhimu ya Biblia” ya S.D.A. Ukweli wa “pembe ndogo,” ambayo ilikuwa na “macho kama ya mwanadamu, na kinywa kilichonena maneno makuu” (Dan. 7:8), ndio uliotufanya sisi kujiunga kwa dhehebu la S.D.A.! Kuona, kwa hivyo, kwamba mafundisho muhimu sana ya S.D.A. yamejengwa kwa msingi wa ufafanuzi wa mifano, tulimwuliza Profesa kueleza ni wapi ambapo iko wapi hatari yake. Lakini hadi sasa miaka tisa imepita na bado tunasubiri kwa uvumilivu maelezo yake! {TN7: 27.1}

Tena: iwapo kamati inaamini, jinsi Profesa, anavyofanya kwamba mifano na vivuli si ya kutegemewa, basi dhehebu lazima liwe limebadilisha msimamo wake hivi karibuni, kwa kuwa siku zote, na kwa mkazo sana, limefundisha mifano hii, pia vivuli, kama vile vuguvugu la Kutoka kama vile kivuli cha vuguvugu la 1844. (Tazama Uhakika wa Vuguvugu la Ujio, na kijitabu, Miaka Arobaini Nyikani.) {TN7: 27.2}

Bila shaka, kwa hivyo, kamati inapaswa kukiri makosa yake yasiyo ya kawaida, na kutambua ukweli kwamba mifano si tu muhimu hakika, lakini pia ni salama hakika, kama msingi wa “mafundisho muhimu ya Biblia.” Na haya makosa pekee lazima yatoe kichocheo cha kutosha kwa kila mmoja kufanya kwa uaminifu

Kijitabu Namba 7 27

uchunguzi kamili wa kibinafsi wa Fimbo. {TN7: 27.3}

Sasa tunaweza kuuliza swali, ni nini kilichowachochea kuchukua msimamo huo dhidi ya Fimbo, hata kinyume cha yale wamekuwa wakifundisha? Kwa udhahiri, ni wao kutoweza kukanusha somo la “Mavuno.” Inasema Roho ya Unabii: {TN7: 28.1}

“Mfasiri wa kweli lazima aje. Yule ambaye mifano hii yote iliwakilisha, lazima afasiri maana yake. {TN7: 28.2}

“Kupitia maumbile, kupitia vivuli na mifano, kupitia kwa mababu na manabii Mungu amenena kwa ulimwengu. Mafunzo lazima yapeanwe kwa wanadamu katika lugha ya kibinadamu…. Yeye, mwandishi wa ukweli, lazima autenge ukweli kutoka kwa makapi ya usemi wa mwanadamu, ambao umeuafanya kutokuwa na matokeo. Maagizo ya serikali ya Mungu na mpango wa ukombozi lazima ufafanuliwe wazi. Mafundisho ya Agano la Kale yanapaswa kuwekwa kikamilifu mbele ya wanadamu.” — Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 33, 34. {TN7: 28.3}

“Mfumo wote wa mifano na nembo ulikuwa unabii ulioshindiliwa wa injili, utoaji ambao ulikuwa umefungiwa ahadi za ukombozi.” — Matendo ya Mitume, uk. 14. {TN7: 28.4}

“Hayo yote Yesu aliwaambia makutano katika mifano; wala pasipo mfano Yeye hakuwaambia neno.” Mat. 13:34. {TN7: 28.5}

Profesa kwa udhahiri ni kipofu kwa ukweli kwamba mfumo wa sherehe na ibada zake zote za mifano ni msingi wa mafundisho ya Agano la Kale, na pia, ni pamoja na mifano ya Kristo, vivyo hivyo ni msingi wa mafundisho ya Agano Jipya, na ya kwamba

28

vivuli vya unabii na mifano ya Ezekieli, Danieli, Hosea, Zekaria, Ufunuo, na mingine yote ya Biblia, ikiwa ilipangwa kwa makusudi kuielekeza nuru kwa kazi ya kufunga ya injili, dhahiri ni ya hitaji muhimu na ya usalama wa pekee kama msingi wa “mafundisho muhimu ya Biblia.” Hakika, ingekuwaje tofauti, na bado ingali kama ilivyo — kazi ya msingi ya Maandiko? {TN7: 28.6}

Isitoshe, kwa sababu hizi nembo, vivuli, na mifano haijafafanuliwa katika maandishi ya Dada White (lakini ahadi iliyofanywa humo tu kwamba mtu lazima aje kuifafanua), na kwa vile Profesa hakubali mamlaka mengine ya kufasiri, basi ni dhahiri kwamba yeye na wale wanaoweka imani katika yale anayosema, hawataafikia kamwe kwa ukweli wa mambo haya! Lakini bado lililo baya zaidi, ni wao

Kukanusha kwa Uongo. {TN7: 29.1}

Kwa miaka mingi sisi wa S.D.A. tumekuwa kama watu kwa bidii tukizikabili janja ambazo zimetumika sana dhidi ya kweli za Ujumbe wa Malaika Watatu; kama, kwa mfano, ubishi unaoletwa dhidi ya ukweli wa Sabato, na kama ule ambao huletwa dhidi ya Roho ya Unabii na watetezi wa ufasiri (usiokuwa na uvuvio) wa apendavyo mtu tu, lakini tunashangaa kuona ndugu zetu wa Baraza Kuu wakitumia mbinu zile zile za hila, na baya hata zaidi, wanafanya hivyo dhidi ya ndugu ambaye anajaribu kuuinua Ujumbe wa Malaika wa Tatu na karama ya Roho ya Unabii. {TN7: 29.2}

29

Tunafahamu kikamilifu kwamba mpangilio wa dondoo kutoka kwa Fimbo ya Mchungaji na Roho ya Unabii, kama ilivyowekwa katika kijitabu, Jibu Kwa Fimbo ya Mchungaji, kuzifanya zionekane kuwa zinakinzana moja kwa nyingine. Lakini muonekano huu wa uongo umefanikishwa kwa kutenganisha taarifa kutoka kwa miunganisho yake ya muktadha. Kwa mfano, iwapo tunang’oa kutoka katika Zaburi 53:1, ibara inayosema “hakuna Mungu,” tunamfanya Daudi kunena kama mtu asiyemwamini Mungu, na Biblia kama kazi inayojipinga zaidi katika vitabu vyote. Hii ndio mbinu ya kung’oa taarifa ambayo hujumuisha ufuatao

Ulinganisho Wenye Hila. {TN7: 30.1}

Ulinganisho huu unapatikana katika Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji. {TN7: 30.2}

Fimbo ya Mchungaji

“Uhamisho wa Papa Pius wa 6, mwaka 1798, na kifo chake huko Valence, Ufaransa, Agosti 19, 1799, si [italiki za mwandishi] kutiwa jeraha, si zaidi ya kifo cha papa yeyote kabla au baada yake.” — Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, uk. 215. {TN7: 30.3}

Roho ya Unabii

“Naliona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti; na jeraha lake la mauti likapona; na dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Kutiwa jeraha la mauti huonyesha kuanguka kwa upapa mwaka wa 1798.” — Pambano Kuu, uk. 653 (toleo jipya). {TN7: 30.4}

“Kipindi hiki, kama kilivyoelezwa katika sura zilizotangulia, kilianza na utawala wa upapa, 538 B.K., na kilikoma mwaka 1798. Wakati huo, papa alikamatwa na jeshi la Ufaransa, utawala wa upapa ukapokea jeraha la mauti, na utabiri ukatimizwa “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka.” — Pambano Kuu, uk. 501. {TN7: 30.5}

Taarifa ambazo zimenakiliwa hapo juu zimechapishwa

30

tena neno kwa neno kutoka katika Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji, uk. 42, 38. {TN7: 30.6}

Mbinu ya kijanja ambayo ndugu wametumia katika ulinganisho huu, katika juhudi za kuvunjika moyo za kuthibitisha Fimbo ya Mchungaji ina makosa, inaweza kugeuzwa dhidi ya Biblia na dhidi ya vitabu ya dhehebu lenyewe. Kwa mfano: {TN7: 31.1}

Ishara za Nyakati:

“… Kwa hivyo si sahihi wala kimaandiko kutangaza kwamba Kanisa Katoliki la Rumi ni kichwa cha tano cha joka au mnyama wa Ufunuo 13.” — Ishara za Nyakati, Aprili 12, 1932. {TN7: 31.2}

Fimbo ya Mchungaji:

“Wazo mintarafu matumizi ya nembo ya… mnyama kama chui wa Ufunuo 13, mnyama mwekundu wa Ufunuo 17,… kama nembo za upapa si ya kibiblia na pia ya uelewa finyu.” — Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, uk. 148. {TN7: 31.3}

Kwa mbinu hii ya giza, zaidi ya hayo, mtu anaweza kumpinga kwa urahisi zaidi Paulo akitumia maandishi ya Musa kuliko ambavyo wameipinga Fimbo ya Mchungaji wakitumia Roho ya Unabii, kama inavyoonekana kutoka kwa mifano ifuatayo: {TN7: 31.4}

Anasema Paulo; “Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine?… Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.” Rum. 14:4, 5. {TN7: 31.5}

“Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote.” Kut. 20:10. {TN7: 31.6}

Mbona usimshtaki Paulo kwa kufundisha kwamba mtu anaweza kuitunza siku yoyote almuradi kama “anaitunza kwa Bwana”? {TN7: 31.7}

“Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani.” 1 Tim. 4:4. {TN7: 31.8}

“Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.” Law. 11:4. {TN7: 31.9}

31

Kwa nini hapa pia usimshtaki Paulo kwa kufundisha ya kwamba mtu anaweza kula chochote na kila kitu, ingawa vimekatazwa katika Neno la Mungu? {TN7: 32.1}

“Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu.” Flp. 1:23, 24. {TN7: 32.2}

“Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” Mhu. 9:5. {TN7: 32.3}

Iwapo “kamati ya kumi na wawili” wangalikuwa hai katika siku ambazo Paulo alihubiri, na kama wangeridhia mbinu yao ya sasa ya uchunguzi, basi kwa kushindwa kufikiri jumla ya lile ambalo mtume alikuwa akifundisha katika taarifa zake, wangeweza kumhukumu kama mwalimu wa dhana ya mageuzi ya uumbaji, wa hali ya wafu kufahamu, na wa kutokuwa na kiasi, na chini ya udanganyifu huo wangekuwa miongoni mwa wale wa kwanza kukitaka kichwa chake, vile walivyo sasa katika gari wakilia Fimbo ya Mchungaji ishindwe. {TN7: 32.4}

Wakiwa hafifu kama wangalivyoweza kuwa katika hatia yao iwapo wangaliimwaga damu ya Paulo bado nafasi yao ya kuingia katika uzima wa milele ingalikuwa bora zaidi (kama kutojua kwao kulihusu lile Paulo alikuwa anafundisha kungeweza kuwapa udhuru) kuliko itakavyokuwa iwapo wanaendelea kushughulikia isivyo haki ujumbe wa Fimbo. Kwa maana inaweza kuwa vigumu kuelewa mafundisho haya ya Paulo, lakini hakika si vigumu kuelewa mafundisho ya Fimbo, maana mistari inayofuata upesi ile ambayo kamati hiyo inanukuu, huweka dhahiri kwamba mnyama dubwama na mnyama kama chui huwakilisha upapa. Na isitoshe,

32

ingawa Fimbo husema wazi kwamba pembe yenye kichwa, “iliyo na macho ya mwanadamu, na kinywa kinachonena maneno makuu,” na kichwa kilichotiwa jeraha la mauti, zote huwakilisha upapa, wamezifanya kuonekana kufundisha kinyume. {TN7: 32.5}

Dondoo kutoka kwa Fimbo ya Mchungaji, ilio kwenye ukurasa wa 30 wa trakti hii, huonyesha kwa lile linaloifuata, kwamba Fimbo inajaribu tu kuelezea kuwa ingawa baadhi ya wanyama huwakilisha utawala wa Kirumi, ni yasiokuwa ya Kibiblia na bila busara kudhani kwamba wote huwakilisha mfumo huo, au kwamba mnyama kama chui mzima (vichwa saba na pembe kumi) anaweza kuwa mfano wake peke yake; kwa maana huwakilishwa kwa kichwa kilichotiwa jeraha. Vichwa sita ambavyo havikujeruhiwa na pembe kumi lazima ziwe mifano ya mifumo mingine. Lakini kuzuilia ukweli huu mbali kwa watu, wanaishughulikia isivyo haki Fimbo, na wanawahadaa na kuwakanganya walei. Hakuna udhuru kwa hili, kwa maana kama wao hawana muda wa kusoma, basi kwa kutupia jicho tu kwenye picha kwa ukurasa wa 84 wa Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, wanaweza kutambua kwamba haineni kile wanajaribu kufanya inene. {TN7: 33.1}

Kila hoja nyingine ambayo wameleta dhidi ya Fimbo ili kuwageuza walei kutoka kwayo, inaweza kuzimwa haraka, kwa urahisi, na kabisa kama sampuli ambazo zimetajwa awali. Iwapo mtu yeyote ana shaka, tunaalika maswali yao. Chagua pingamizi thabiti zaidi unayoweza kupata

33

imewekwa na wapinzani wa Fimbo, na tunaahidi kuifyeka. {TN7: 33.2}

Labda kupotosha kwao kukubwa zaidi ni ukweli: “Wakati umakini wa mwandishi wa Fimbo ya Mchungaji uliitwa kwa utata huu wa moja kwa moja, hakuukataa, lakini alidai kwamba ufasiri wake unapaswa kukubaliwa kwa sababu Dada White hakuwa na nuru kamili juu ya mada hiyo.” — Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji, uk. 42. {TN7: 34.1}

Tuhuma hii hushugulika ama katika utungo au makosa yaliyopangwa, kwa maana hakuna wakati tumefanya taarifa kama hiyo, wala hakika hatungeweza kuifanya, jinsi tunavyoiamini Fimbo kuwa katika uwiano kamili na maandiko ya Dada White. Kwa hivyo tunatumaini kwamba kwa ajili yao wenyewe kamati itaheshimiwa sana kurekebisha uongo huu walioueneza. {TN7: 34.2}

Sasa tunaelekeza umakini wa msomaji kwa lile Pambano Kuu hufundisha mintarafu kuanzishwa kwa jeraha, maana lile Jibu hushughulikia Pambano Kuu katika njia sawa ya hiana kama linavyofanya kwa Fimbo ya Mchungaji. Katika hatua hii, linaacha historia yote pana ya kitabu inayoshughulikia mada hiyo, ambayo huonyesha kilichosababisha jeraha kama tokeo, si tendo la nukta tu, bali la mfululizo mrefu wa matukio, kama tunavyoona kifupi tu katika vifungu vifuatavyo: {TN7: 34.3}

“…Pambano kali [alisema Luther] limeanza sasa. Hadi hapa nimekuwa tu nikicheza na papa. Nalianza kazi hii

34

kwa jina la Mungu; itakamilika bila mimi, na kwa uwezo Wake.” {TN7: 34.4}

“’… Naliweka mbele neno la Mungu, Nalihubiri na kuandika — haya yote ndio nilifanya. Na wakati nilipokuwa bado nimelala,… neno ambalo nilikuwa nimehubiri liliupindua upapa, hivi kwamba hakuna hata mkuu wala mfalme ameufanyia madhara kama haya.” {TN7: 35.1}

“… hekima ya mapapa, ya wafalme, na ya makasisi ilifanywa sufuri kwa uwezo wa ukweli. Upapa ulipata pigo ambalo mataifa yote yangeweza kulihisi na katika vizazi vyote.” {TN7: 35.2}

“ … Mapinduzi makubwa yalikuwa yametekelezwa hivyo na Luther kama chombo. Rumi ilikuwa tayari inaporomoka kutoka kwa kiti chake cha enzi, na ilikuwa ni sauti ya mtawa ambayo ilisababisha fedheha hii.” — Pambano Kuu, uk. 142, 190, 162, 155. {TN7: 35.3}

“Nguvu ya utulivu, yenye heshima ya Luther iliwashusha adui zake, na ikafanyiza pigo la kuogofya sana kwa upapa.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 373. {TN7: 35.4}

“Kupitia msaada wa Mungu yeye [Luther] aliwezeshwa kuutikisa utawala mkubwa wa Rumi, hivi kwamba katika kila nchi msingi wa upapa ulitikisika.” — Watendakazi wa Injili, toleo la zamani, uk. 428. {TN7: 35.5}

Pamoja na taarifa hizi mbele yetu, sasa tuko tayari kutathmini vyema kifungu: {TN7: 35.6}

“Wakati huo [1798], papa alikamatwa na jeshi la Ufaransa, utawala wa upapa ulipokea jeraha la mauti, na utabiri ukatimizwa, ‘Mtu

35

akichukua mateka, atachukuliwa mateka.” — Pambano Kuu, uk. 439. {TN7: 35.7}

Taarifa hii husema kwamba aya ya 10 ya Ufunuo 13 (“Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka”), na si aya ya 3 (“kimetiwa jeraha la mauti”), ilitimizwa mwaka 1798! Ufasiri mwingine isipokuwa huu hauwezi kufanywa bila kupuuza dondoo zote zilizonukuliwa tayari kwa suala hilo. Biblia, isitoshe huonyesha wazi kwamba papa kuchukuliwa mateka si kile kilichotia jeraha, maana ilhali papa hakurejea kamwe kutoka kwa kutekwa kwake, ila alikufa ndani yake, “kichwa” kilipona jeraha lake na kikaishi. {TN7: 36.1}

Bado zaidi, Yohana aliona tukio la aya ya 3 (kichwa kutiwa jeraha) likitukia kabla ya lile la aya ya 10 (papa kuchukuliwa mateka). Jeraha kichwani, kwa hivyo, huwakilisha pigo jinsi lilivyosababishwa na Matengenezo ya Uprotestanti. {TN7: 36.2}

Katika usingiziaji mwingine, kamati inasema: “Inadaiwa kwambaLuther wakati huo mwaka (1500 B.K.) alitia jeraha la mauti.” — Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji, uk. 43. Lakini tunawasihi kwa bidii wote wanaopenda Ujumbe wa Malaika wa Tatu, kulichunguza jambo hili muhimu, na waone wenyewe kwamba Fimbo haifundishi kwamba pigo lilitolewa mwaka 1500 kama wanavyojaribu kuwafanya walei waamini kwamba inafundisha hivyo, ila badala yake baada ya mwaka 1500. (Soma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1. uk. 209-222, na Gombo la 2, uk. 85-107.) {TN7: 36.3}

Katika ukurasa wa sita na wa nane, lile Jibu linawasilisha

36

wazo kwamba ni jibu kwa “Somo la Mavuno,” lililowasilishwa kwa “kamati ya kumi na wawili,” na kwamba linatii mapatano ya Fullerton. Ukweli, hata hivyo ni kwamba kamwe kamati haikujibu somo la “Mavuno” (Trakti yetu Namba 3) yenyewe, lakini ilijaribu kuzima kwa namna nyingi za kipigo-bora vitabu vyote vya Fimbo ya Mchungaji. Hakika, jina la kikabrasha hiki huthibitisha kwamba ni “Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji,” na si kwa somo la “Mavuno.” {TN7: 36.4}

Kwa sababu mapatano hayo, isitoshe, yaliitisha masomo matano yawasilishwe katika muda wa juma iwapo la kwanza halingeweza kukanushwa, ilikuwa ni lazima kwamba somo la kwanza lijibiwe ndani ya muda wa masaa ishirini na nne. Lakini licha ya mapatano, masaa zaidi ya mia sita yalipita kabla jibu kutolewa! Na hata wakati huo, kama lilivyoonyeshwa, halikuwa jibu kwa somo lililowasilishwa. {TN7: 37.1}

Kwa kuzingatia ukweli huu ambao unaiweka kamati katika kutofanya kulingana na ahadi yao iliyosainiwa, nafasi yetu ya haki moja kwa moja imethibitishwa, na yao wenyewe kutuhumiwa, ikipunguza hadi sufuri shtaka linalofuata: {TN7: 37.2}

“Tumeikubali changamoto yako kuthibitisha fundisho la Fimbo ya Mchungaji kuwa makosa… Sasa inakuja kwenu changamoto ambayo haijatoka kwetu lakini kwa kanuni rahisi za heshima na uaminifu;… Je! Mwandishi sasa atatumia ‘sera za hila’ na ‘kupinda-pinda na kupotosha na kugeuza-geuza’ kwa ‘makosa’… au atajitokeza kwa uaminifu na heshima na kufanya

37

nzuri ahadi yake:…” — Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji, uk. 37, 49. {TN7: 37.3}

Kwa mbinu ambayo wametumia — kukanusha maandishi ya mtu mmoja kwa kuyalinganisha na ya mwingine — vitabu vyovyote viwili vya Biblia vinaweza kufanywa kupingana. Zaidi ya hayo, mfano unaofuata utaonyesha vya kutosha kwamba si tu maandishi ya watu wawili, ingawa kwa uwiano mkamilifu, yafanywe kupingana, ila pia ya kwamba maandishi ya mtu mmoja yeyote yanaweza kufanywa kuonekana yanapingana. Chukua kwa mfano taarifa mbili zifuatazo kutoka kwa maandishi ya Dada White: {TN7: 38.1}

“Yapo majaribu elfu mafichoni yalioandaliwa kwa wale walio na nuru ya ukweli: na usalama pekee kwa kila mmoja wetu ni katika kutopokea fundisho jipya, wala Maandiko mapya, kabla kwanza kuyawasilisha kwa ndugu wenye ujuzi. Weka mbele yao kwa roho ya unyenyekevu na yenye kufunzwa, kwa sala ya bidii; na iwapo hawaoni nuru ndani yake, ukubaliane na hukumu yao, kwa maana ‘katika wingi wa washauri upo usalama.’” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 293. {TN7: 38.2}

“Kila nafsi inapaswa kumtafuta Mungu kwa toba na unyenyekevu ili Yeye aweze kuelekeza na kuongoza na kubariki. Hatupaswi kuwaamini wengine kuyachunguza Maandiko kwa ajili yetu. Baadhi ya ndugu zetu viongozi wamekuwa mara kwa mara wakichukua msimamo wao kwa upande mbaya, na iwapo Mungu angetuma ujumbe na kuwasubiri ndugu hawa wazee kufungua njia ya ufanisi wake, hautawafikia watu kamwe. {TN7: 38.3}

“Wale ambao hawajakuwa na tabia ya kuipekua Biblia wao wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika watu wanaoongoza, na huyapokea maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa haswa jumbe ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu wanaoongoza hawatazikubali.” — Watendakazi wa Injili, uk. 303; Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {TN7: 38.4}

Kutoka kwa mfano huu, tunaweza kuona haraka sana kwamba ingawa vifungu viwili viwe vimevuviwa

38

kwa Roho mmoja, bado, wakati vinapopotoshwa kwa hila, vinaweza kufanywa kwa urahisi kukinzana. Hata hivyo, wakati lengo la mwandishi anapotoa taarifa linazingatiwa kwanza katika kila suala, kisha basi mmoja anaweza kufasiri sawa sawa wazo lake, na kutopata utata. Katika onyesho maalum la ukweli huu wa jumla, tunaitisha umakini wa msomaji kwa uchambuzi mfupi ufuatao wa taarifa ambayo imefanyiwa kazi kupita kiasi sana na kutumiwa vibaya katika Shuhuda Gombo la 5, uk. 293, kuhusu nuru mpya: {TN7: 38.5}

“Yapo majaribu elfu mafichoni yalioandaliwa kwa wale walio na nuru ya ukweli: na usalama pekee kwa kila mmoja wetu ni katika kutopokea fundisho jipya, wala Maandiko mapya, kabla kwanza kuyawasilisha kwa ndugu wenye ujuzi. Weka mbele yao kwa roho ya unyenyekevu na yenye kufunzwa, kwa sala ya bidii; na iwapo hawaoni nuru ndani yake, ukubaliane na hukumu yao, kwa maana ‘katika wingi wa washauri upo usalama.’” {TN7: 39.1}

Hali ambazo zilichochea taarifa hiyo zilikuwa kwamba Ndugu D_____, kwa kudai alikuwa na nuru, badala yake alikuwa na giza ambalo, kuliko kuangaza, lilitia tu giza ujumbe uliokuja kupitia Roho ya Unabii. Kwa kuzingatia ukweli huu, “ndugu wenye ujuzi” ambao alizungumzia wanaonekana kuwa sio wengine isipokuwa mababa waasisi wa dhehebu la S.D.A., wale ambao walishirikiana na Dada White katika uzoefu wa kipekee wa kuujenga

39

ujumbe hatua kwa hatua, na sio wale ambao walifuata baadaye kuutangaza. {TN7: 39.2}

Dhahiri, basi, njia ya pekee inayowezekana ambayo hawa “ndugu wa ujuzi” wanaweza kutafutwa kwa ushauri wakati huu ni kwa kutii sauti waliyoiacha kwa kumbu kumbu katika shuhuda zao walizoziandika na katika zile haswa za kiongozi wao na hatibu wa Mungu, Dada White. “Malaika” wa Walaodekia, ambaye ni “mwenye mashaka, na huzuni, na maskini, na kipofu, na uchi,” hakika hapaswi kutafutwa kwa ushauri, bali kuhudumiwa kwa mafundisho. {TN7: 40.1}

Vivyo hivyo kamati ya kumi na wawili, na wengine wote ndugu wanaoongoza pia, lazima wakubali kwa unyenyekevu na kenyekenye neno la maandishi yaliyovuviwa kwa kanisa katika mpangilio wake kamili iwapo kila mmoja wao angeweza kutoa mwangwi wa sauti ya ujuzi na ukweli. Laiti wangefanya hivyo, Bwana hangaliweza kutoa taarifa yenye mashtaka: “Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu.” Ufu. 3:16. Kwa maneno mengine, ingawa hawamiliki nafasi sawa kama walivyokuwa “ndugu wenye ujuzi” waliotajwa katika Shuhuda, Gombo la 5, uk. 293, na sasa wako katika hali ya hatari, hata sasa iwapo wangalitekeleza hukumu sawa na roho ile ile kama walivyofanya waasisi, sasa wangekuwa washauri salama, wanaostahiki heshima sawa. {TN7: 40.2}

Ukweli huu unaonyeshwa zaidi na uhakika kwamba iwapo taarifa kutoka kwa Shuhuda, Gombo la 5, inamaanisha kile ndugu

40

wanaoongoza wangetaka sisi kufikiri kinamaanisha, basi Yohana Mbatizaji, Yesu Kristo, Mitume, Luther, Wana Matengenezo, William Miller, na Dada White mwaka wa 1844 na tena mwaka wa 1888, wote, mmoja baada ya mwingine walikufa katika uongo, kwa maana hakuna hata mmoja wao aliheshimu maamuzi ya ndugu zao viongozi ambao kwa nyakati zao zote maalum walisifiwa kwa umaarufu kuwa “ndugu wenye ujuzi,” na ambao kwa kutoiona nuru katika jumbe, walizikataa na wajumbe pia. Na Dada White kamwe hakunyenyekea kwa hukumu yao walipompinga. {TN7: 40.3}

Zaidi ya hayo, angalikusudia taarifa inayozungumziwa kumaanisha kile kamati inasema inamaanisha, kamwe hangaliweza kuandika alivyofanya katika Watendakazi wa Injili, uk. 303 na katika Shuhuda kwa Wachungaji uk. 106, 107, zote mbili ambazo ziko nje ya kifundo na ufasiri wao wapendavyo wa Shuhuda, Gombo la 5, uk. 293. Dhahiri, kwa hivyo, katika kuipiga vita Fimbo kwa msingi mbovu, wao bila kujua wanapoteza shabaha yao, na kuipiga Roho ya Unabii badala yake — na hivyo wanawapofusha, kuwaogofya, na kuwakanganya walei. Ndugu, dada, “Chagua leo hii” yule “mtakayemfuata” — wajumbe wa Mungu au watu wanaoongoza. {TN7: 41.1}

Fimbo haijinyooshi kwa hatua ya kuvunja taarifa yoyote kwa somo liwalo lile, wakati ikipuuza kabisa taarifa zingine zinazolihimili, ila badala yake huzingatia kila taarifa husika. Kwa kanuni hii ambayo kamati ilipuuza kabisa, ufasiri wa pekee unaoweza kuwa wa uwiano ambao

41

wanaweza kuweka kwa Shuhuda, Gombo la 5, uk. 293, ni kwamba wao wenyewe, pamoja na wengine wote ndugu zao, hawapaswi kuingiza ndani ya ujumbe wa mtu yeyote maoni ya kibinafsi hapa na maoni ya kibinafsi pale kabla kwanza kuwasilisha maoni kama hayo kwa mtu ambaye kupitia kwake ujumbe huo ulikuja, jinsi Roho ya Unabii inavyoelekeza: “Iwapo ujumbe unakuja usiouelewa, vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa,” na sio sababu ambazo wachungaji wanaweza kutoa. (Tazama Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65.) {TN7: 41.2}

Kuwa kwa agizo na kwa mfano akisha kuamuru kila mtu aondoe boriti ndani ya jicho lake kabla ya kujaribu “kukitoa kibanzi” ndani ya jicho la ndugu yake (Mat. 7:4), Bwana kwa hivyo ameonyesha kwamba kanisa halipaswi kusema kwa mengine, “Hebu nikingo’oe kibanzi ndani ya jicho lako;” ilhali “tazama, boriti liko ndani ya jicho [lake] lenyewe.” Hivyo basi, tunalo jukumu takatifu kugeuza kurunzi ya upekuzi kwa dhehebu la S.D.A. (sisi wenyewe), si kwa madhehebu mengine (ndugu yetu). Kufuatia maagizo ya Mwalimu, kwa hivyo sasa tunatazama hapa ndani, si kwa jicho la mtu binafsi, bali katika S.D.A. yote kwa ujumla. —

Jicho la Dhehebu. {TN7: 42.1}

Katika ufafanuzi wa Isaya 4:1, chapisho la dhehebu (si tu limechapishwa na kumilikiwa na dhehebu, ila pia limeidhinishwa na kutumika katika Idara ya Shule ya Sabato duniani kote mwaka

42

wa 1928), Isaya, Nabii wa Injili, Gombo la 1, uk. 28, linasema: {TN7: 42.2}

“Wanawake saba, mme mmoja, saba ni tarakimu kamili “Wanawake” huwakilisha kanisa (Ufu. 12:1, 2; 17:3), lakini katika suala hili sio kanisa la kweli au safi kwa sababu ipo fedheha. Ni kweli ilivyo leo kwamba makanisa hayakubali mkate ulioshuka kutoka mbinguni, lakini badala yake yanakula chakula chao yenyewe — mapokeo ya wanadamu. Wanataka jina, lakini wanakataa vazi ambalo Kristo hutoa, na hivyo watapatikana mwishowe bila vazi la harusi.” {TN7: 43.1}

Hata hivyo katika mwaka 1928, kupitia kwa chapisho la Shule ya Sabato, Isaya, Nabii wa Injili, dhehebu lilifundisha rasmi ufasiri uliotangulia wa Isaya 4:1, lakini mwaka wa 1931, kupitia jarida la kanisa la jumla, Mapitio na Kutangaza, lilifundisha rasmi ufasiri tofauti kabisa; yaani: {TN7: 43.2}

“Inaeleweka kwa ujumla kwamba haya ni maelezo ya ki-mfano ya hali ambazo zingeenea Israeli kwa sababu ya vita ambavyo wanaume wengi wangeuawa hivyo kwamba kungechangia kuwapo wanawake wengi. Hatupaswi kutafuta usahihi wa hisabati katika masuala kama haya ya unabii wa Biblia. {TN7: 43.3}

“Hatupaswi kueleweka kama tunataka kutafuta utimilifu wa unabii huu katika Vita vya 1914 – 1918, lakini ni kweli, hata hivyo, kwamba katika nchi kadhaa za Ulaya wanawake ni wengi kwa

43

wanaume, kwa sababu mamilioni ya wanaume walipoteza maisha yao katika mapambano hayo makubwa. Hii ni hali ambayo inaweza kurudiwa katika vita vikubwa ambavyo kwamba hata sasa vinatishia ulimwengu.” — Mapitio na Kutangaza, Juni 11, 1931. {TN7: 43.4}

Hatutajaribu hapa kufafanua Isaya 4:1, lakini tunaliomba Baraza Kuu kutuambia ufasiri gani tunaopaswa kuamini, wa awali au wa mwisho. Maana, kwa kuwa hazipatani, zote haziwezi kuwa sahihi, na hivyo kuidhinisha ama mmoja au zote mbili itakuwa kutoa idhini kwa nadharia, na matokeo kwamba badala ya kuwasaidia ndugu zetu viongozi kuachana na mwenendo huu hatari, tutakuwa tu tunawaunga mkono na kuwastawisha ndani yake. {TN7: 44.1}

Wale ambao huruhusu wengine kufikiri na kuchunguza kwa niaba yao badala ya kufanya uchunguzi wenyewe, na ambao hivyo huyakubali maamuzi ya ndugu viongozi (wanaodai kwamba ni “watu wenye ujuzi”), lazima, iwapo wanaulizwa ni nini wanaamini kwa mada ya Isaya 4:1, kwa uaminifu wote watajibu, hatujui tunachoamini. {TN7: 44.2}

Ufasiri maradufu unaofuata unahusisha kwa [upande mmoja, kijitabu chenye kichwa, Miaka 40 Nyikani, na Taylor G. Bunch, na kwa upande mwingine, Mapitio na Kutangaza, Juni 1, 1930, katika makala yenye kichwa, Ulinganisho wa Miaka Arobaini na Mmoja, na H. E. Rogers, katibu wa takwimu wa dhehebu. Mzee Taylor Bunch, katika kijitrakti chake, hufundisha kwamba tangu mwaka wa 1888 (tangu dhehebu lilipoukataa ujumbe wa “Haki kwa Imani”) hadi mwaka 1928,

44

miaka arobaini, Dhehebu la S.D.A. lilirudia uzoefu wa nyikani wa Israeli ya kale. {TN7: 44.3}

Kwa sababu kitrakti hiki kiliandikwa na mfanyakazi wa Baraza Kuu, na kilisambazwa kote kote kati ya watu, hakuna haja ya kunukuu kutoka kwacho. Kichwa chake, Miaka Arobaini Nyikani, hujieleza chenyewe. {TN7: 45.1}

Sasa tunayageukia makala ya Mzee Rogers, ambayo husema: “Baadhi ya wapinzani wa utume huu hudai kwamba dhehebu tangu kongamano la Minneapolis, mwaka 1888, limekuwa likitanga-tanga nyikani …. {TN7: 45.2}

“Iwapo kutanga-tanga nyikani humaanisha kuzidisha washiriki wa dhehebu kwa zaidi ya kumi, kuongeza idadi ya wafanyakazi zaidi ya mara hamsini,…. dhehebu laweza kukiri makosa kwamba lina hatia kwa shtaka hilo.” {TN7: 45.3}

Hivi kwa msimamo mwingine wa njia mbili, Baraza Kuu tena limetulazimisha kuwapa changamoto kujitokeza na taarifa wazi wazi na ya uhakika kuhusu ni ipi kati ya fasiri hizi mbili kwa mada hiyo ambayo wangependa sisi kuamini, kwa sababu hatuwezi kuamini zote mbili na bado tujue kile tunachoamini. Ikiwa Mzee Taylor G. Bunch, jinsi Mapitio na Kutangaza inavyoshtaki kichini-chini, anafundisha uongo na ni “mpinzani” wa “utume,” kwa nini, basi, Baraza Kuu lilivumilia tu mitazamo yake, lakini hata kumlipa wakati alipokuwa akiwaandikia, na kisha kuidhinisha usambazwaji wake! Kwa upande mwingine, kama Ndugu H.E. Rogers hajaandika ukweli kwa mada hiyo,

45

basi yeye haupotoshi tu Ukweli, bali pia Baraza Kuu na ukasisi wa dhehebu, na hivyo hafai kwa kazi yake na hastahili kuajiriwa. Lakini ukasisi wa S.D.A. unaendelea kuwadumisha wafanyakazi wote wawili kama washiriki katika msimamo unaokubalika. {TN7: 45.4}

Isitoshe, kwa jitihada zao za kuyapinga mafundisho ya Fimbo, kamati kwa dhati inadumisha kwamba pigo ambalo lilisababisha “jeraha la mauti” kwa kimojawapo cha vichwa vya mnyama kama chui (Ufunuo 13) lilitolewa na Berthier, Jemedari wa Ufaransa, mwaka 1798. Na kwa kuunga mkono msimamo huu, wanaomba Pambano Kuu, uk. 439. (Angalia Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji, uk. 42.) Lakini katika kiungo chake rasmi cha kimishonari, Dhehebu hufundisha kwamba “jeraha la mauti” lililotabiriwa hapa lilitimizwa katika Matengenezo ya Uprotestanti, katika Mapinduzi ya Kifaransa, na lilifikia kilele katika kilichoonekana kwamba kipigo kwa moyo wa upapa wakati papa alipong’olewa mamlakani na kufungwa jela na Wafaransa mwaka 1798.” — Ishara za Nyakati, Januari 30, 1934, uk. 6. (Italiki zetu.) {TN7: 46.1}

Hivi bado tunapelekwa mbali zaidi kwenye bahari ya ukasisi ya theolojia inayopingana, na kuachwa kujiamulia wenyewe ni mashua ipi ambayo itatupeleka kwenye bandari, Ishara za Nyakati, au Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji. {TN7: 46.2}

Kwa sababu lile Jibu tayari limetoboka vibaya sehemu kadhaa, na liko katika hali ya kuzama, na jinsi Ishara za

46

Nyakati katika taarifa yake iliyonukuliwa hapo juu ni ya uwiano mkamilifu na mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji katika mwunganisho huu, mmoja hahitaji kufikiri mara mbili kama kwa ipi ambayo inatoa fursa ya ukombozi kutoka kwa masaibu ambayo Dhehebu limetuweka kuhusu suala hili. Ni wazi kwa yeyote kuona kwamba lile Jibu linavuja sana, na kwamba litawazamisha wote huninginia kwalo. {TN7: 46.3}

Tena: iwapo, jinsi lile Jibu linalishtaki, fundisho la Fimbo ya Mchungaji kuhusu jeraha, ni uzushi, na Dhehebu limeazimu kuliondoa kanisani, basi kwa nini, twawaomba mtuambie, wametumia fedha za Bwana na wakati kufundisha uzushi uo huo katika Ishara za Nyakati! {TN7: 47.1}

Hivi, wakati kwa upande mmoja maelfu za nakala za lile Jibu zinapiga kelele kukanusha, kwa upande mwingine maelfu za nakala za Ishara za Nyakati na Papa Mfalme Tena zinapiga kelele kuthibitisha, kwa swali Je! Matengenezo ya Uprotestanti yalisababisha jeraha la mauti? {TN7: 47.2}

Si ajabu, basi, ya kwamba walei wako katika fadhaa na mkanganyiko kuhusu ni sauti ipi ya kutii, na ni njia gani ya kufuata? Si ajabu kwamba ili kuwaokoa kutoka kwa tatizo lao, “sauti ya Bwana inaulilia mji … isikieni hiyo fimbo, na Yeye aliyeiagiza”? Ni sauti ya Fimbo tu inayoweza kulitatua tatizo hilo. “Mtu mwenye hekima” ataisikia “sauti yake. {TN7: 47.3}

Huu ushahidi wa vinywa vya tarumbeta unapaswa kuwaamsha walei kutoka katika usinziaji wao, hadi kwa uchunguzi wa kina kibinafsi

47

kwa masuala mbalimbali husika. Na uhakika ni kwamba wale ambao hawatazinduka kwa kukosa tumaini ni wasiojali ni kwa mikono ipi ambayo wanakabidhi taji yao ya thamani ya maisha. Hakika, ushahidi huu wa uzoefu unapaswa kuwawezesha wote kutambua kwamba tumaini lao katika Nuhu, Ayubu, au Danieli kuwaongoza hadi katika Kanani ya mbinguni, litaishia kwa uchungu wa kuvunjika moyo badala ya uzima na utukufu wa milele. {TN7: 47.4}

Tunasikitika sana kwamba ndugu zetu wamejihusisha dhidi ya Ukweli hivi kwamba tumelazimika kufunua jitihada zao za ujanja. Lisingekuwa tu lengo letu la kumheshimu Mungu, kwa ajili ya wema wa ndugu hawa na kwa watu Wake wote, hatungeweka ukweli huu kwa umma, lakini wakati rasmi wa, “siku za utakaso” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80), ambao kanisa letu limefikia, unatulazimisha “kupiga kelele, tusiache,” na kutii amri: “paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. {TN7: 48.1}

“Ukweli katika ukali wake wote lazima unenwe. Mashujaa wanahitajika, — watu watakaofanya kazi kwa nguvu ya bidii, isiyochoka kwa ajili ya kulitakasa kanisa na kuuonya ulimwengu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 187. {TN7: 48.2}

Hivyo basi sasa tunaelekeza neno

Kwa Kamati ya Kumi na Wawili. {TN7: 48.3}

Wapendwa Ndugu:

Ingawa mmepinga na kuhoji uadilifu wetu,

48

hatujali kuteta vipengele vya kibinafsi vya kutafakari. Kwa hakika, kweli zilizo hapa ndani zinafichua changamoto yenu na kuiweka wazi kwa tabia yake halisi, hivyo uchi kabisa bila nguvu yoyote ya kuifanya isiokuwa na maana kukutana nayo tena, katika kuutetea Ukweli, kwa kipimo chochote isipokuwa changamoto ya kukabiliana nayo: Kwa uwazi thibitisha makosa yetu kwa unyofu na kwa namna ya ushahidi ambao tumekuwa hapa ndani tukithiubitisha uongo wenu, kisha mujaribu na muone iwapo au la “tutaifanya nzuri” yetu “ahadi.” Au, iwapo mmebanwa kwa wakati na kuhisi kwamba hamwezi kuyachunguza magombo mengine ya Fimbo ya Mchungaji, basi ruhusu kurasa chache za trakti hii zitoshe kama “Ushahidi A” wa kujenga juu yake shtaka lenu. “Tangaza sababu zenu thabiti.” “Njoni sasa, tusemezane.” Lakini sisi, kama ndugu, tunawaonya kwa dhati msiegemee tena mbinu hizo za hila “za kuhepa” ambazo huharibu kabisa lile Jibu kwa Fimbo ya Mchungaji. Tuonyeshe tumekosa, ndugu zetu, na mtastaajabishwa kuona jinsi haraka tutakiri na kuharibu vitabu vyetu vyote, hata ingawa mtaendelea kukuza nadharia zingine zisizopatana. Mnaona, hatuulizi lisilo na maana, ila ni lile ambalo kwa hisia za kawaida mungekuwa na wajibu wa kudai mngalikuwa katika nafasi yetu. {TN7: 48.4}

“Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndio torati na manabii.” Mat. 7:12. {TN7: 49.1}

Sasa, sifikiri kwamba katika kurasa hizi haiji

49

kwenu “changamoto” tu. La hasha; bali rai ya uaminifu inayochochewa na onyo la kimbele la huruma ya Bwana kuhusu mkasa wa kutisha unaolijia kanisa Lake pendwa. Mshangao wa kuogofya! Unatulemea kupiga kelele pamoja naye aliyezipenda nafsi za ndugu zake zaidi yake mwenyewe: “ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili.” Rum. 9:2, 3. {TN7: 49.2}

Tena Inasema Roho ya Unabii: {TN7: 50.1}

“Hata Waadventista wa Sabato wako katika hatari ya kuyafumba macho yao kwa ukweli jinsi ulivyo ndani ya Yesu, kwa sababu hukanusha kitu ambacho wamekichukulia kwa uzito kwamba ni ukweli, lakini ambacho Roho Mtakatifu hufundisha si ukweli…. Lakini jihadhari kukataa lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali.” Shetani husema: “Watu huyakubali mafafanuzi ya wachungaji wao kwa Maandiko, na hawayachunguzi wenyewe. Kwa hivyo kwa kufanya kazi kupitia katika wachungaji, Naweza kuwathibiti watu kulingana na mapenzi yangu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 70, 106, 107, 473. Ushuhuda huu wa onyo unahimiza

50

Neno Kwa Walei: {TN7: 50.2}

Kama waamini imara wa Ujumbe wa Malaika wa Tatu na vuguvugu la mwaka 1844, tunawarai kwa bidii sana, Ndugu, wakati huu mugumu, msiyakubali maamuzi ya wengine au kuidhinisha shutuma zao dhidi yetu bila kufanya uchunguzi makini wa kibinafsi kwa ujumbe katika Fimbo ya Mchungaji, ambao umewajia “katika jina la Bwana.” (Tazama Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65.) {TN7: 51.1}

“Wanaume, wanawake, na vijana, Mungu huwahitaji mmiliki ushujaa wa kimaadili, uthabiti wa kusudi, ustahimilivu na uvumilivu, akili ambazo haziwezi kuchukua madai ya mwingine, lakini ambazo zitachunguza zenyewe kabla kupokea au kukataa, ambazo zitachambua na kupima ushahidi, na kuupeleka kwa Bwana katika sala.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 130. {TN7: 51.2}

Msiyarudie, tunawasihi, makosa ya taifa la Kiyahudi na makanisa ya Kikristo ya jina tu kwa kuhukumu au kukataa bila umakini ulio sawa kwa pande zote mbili. Iwapo ndugu viongozi watakuja kwako na vikwazo kwa uamuzi wako kuufanya uchunguzi wa kibinafsi wa ujumbe, usikubali hadi wakupatie maelezo zaidi ya busara na ya kushawishi kuliko inavyofanya Fimbo, kwa mada husika. {TN7: 51.3}

Uzembe katika suala hili kwa upande wa walei limewatia moyo ndugu wanaoongoza kuzoea katika roho ya ubeberu na yenye ukatili ambayo wametumia kuleta fedheha

51

kwa kanisa la Mungu. Ulisababisha mara moja hata sisi kuitwa mbele ya hakimu wa jiji, na kisha baadaye, kwa sababu mashtaka yaliyotungwa dhidi yetu yalishindwa kusimama, na hivyo kuwanyima washtaki wetu mkono wa sheria kuitumia kututupa nje ya makanisa, uliwaongoza kuchukua mamlaka mikononi mwao, na kwa hafla nne kimwili (mbili kwazo za fujo) kuwanyanyua baadhi yetu nje ya jengo la kanisa. Kwa wakati mwingine, uliwaongoza kumfanya Ndugu Houteff kukamatwa, lakini wakashindwa, maana utawala, baada ya kuzihoji pande zote mbili ulimpata hana hatia, na ukawaamuru maofisa wale waliompeleka kwenye kituo cha polisi kumrudisha tena kanisani ambako walikuwa wamamemtoa, kwa kuwadunisha zaidi na kuwakasirisha washtaki wake. Kisha kwa hafla nyingine, iliwachochea kumpiga kofi usoni; na bado kwa nyingine, bila huruma wakagota kichwa chake na uso hadi kuchubuka. Baada ya shambulio hili la mwisho, la aliyekengeuka wa muda mrefu ambaye walimweka mlangoni kama bawabu kutuzuilia nje, hisia za jumla kwa umati zilikuwa, “Labda sasa atakaa mbali!” {TN7: 51.4}

Kisha bado baadaye, roho iyo hiyo iliwapiga viboko hadi kiwango cha kumfanya afungiwe kwenye chumba cha walio kichaa, na pia kushindwa katika hilo, kisha wakaendelea hata wakajaribu afukuzwe nchini, tena bila kufanikiwa lakini tu aibu kubwa na hasira ya mkizi zaidi kwao wenyewe. {TN7: 52.1}

La aibu sana kwa matendo yao yote, hata hivyo, lilikuwa la mchungaji ambaye, baada ya ibada ya Sabato ambayo Ndugu

52

Houteff alishambuliwa kwa ukatili, alisema, kwa kuhalalisha tendo hili la uhalifu, “Kwa nini msikae mbali ikiwa hawawataki ninyi karibu hapa,” kisha akaendelea kuita kama msingi wa Maandiko kuteta kwake, maneno: “Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. Mat. 10:12, 14. Upotovu usiokuwa na haya kwa maandiko katika utetezi wa aibu wa makosa! {TN7: 52.2}

Katika maneno haya wazi ya Kristo kwa maandiko ambayo yamenukuliwa, Yeye huwaagiza wafuasi Wake, kama msomaji yeyote wa Biblia mwaminifu atakubali, kwenda nje na kukaa huko tu iwapo na wakati hawakaribishwi ndani ya nyumba (nyumbani), lakini si wakati wanatupwa nje ya hekalu (kanisa). Hili linathibitishwa na uzoefu uliofuata: {TN7: 53.1}

Mitume walikuwa “katika ukumbi wa Sulemani.” “Kisha kuhani mkuu akainuka, na wote waliokuwa pamoja naye,… wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu. Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma

53

watu gerezani ili wawalete. Hata watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, wakisema, Gereza tumelikuta limefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu ndani. Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo. Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe. Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” (Mdo. 5:12, 17-29. {TN7: 53.2}

Tofauti na kumbukumbu hii, maeno ya kuruhusu uhasama na vurugu yaliyonenwa na mchungaji ile Sabato yanaonyesha jinsi angemchukulia Petro kama angaliishi wakati wa Petro. Vivyo hivyo na mzee wa kanisa, ambaye alipokuwa kwa mimbari siku hiyo ya Sabato, jinsi tulivyojua baadaye, kama vile Pilato alivyonawa mikono yake asihusike na uajibishwaji wowote wa kile kilichotokea, akadai kwamba tulikuwa tumewaita majina

54

(ambayo ilithibitishwa kuwa uongo kwa ukweli rahisi kwamba wangeweza kuturipoti haraka iwapo ulikuwa ukweli), na ndio sababu iliyomfanya bawabu aliyekuwa ameacha imani kukasirika. Hivi ndivyo hufanya watu wengi leo kama ulivyofanya umati katika wakati wa Kristo, kwa kuwahesabia haki waovu na kuwahukumu waadilifu, wakilia: “Mwondoe mtu huyu, tufungulie Baraba.” {TN7: 54.1}

Muda mfupi baada ya shambulio hilo, hali ya aliyekuwa amejeruhiwa ilidai matibabu, hivyo daktari wa S.D.A., ambaye alikuwa kanisani asubuhi hiyo na aliyeshuhudia majeraha, baadaye aliitwa kwa simu, na baada ya kusita sita sana, alikubali kuja, lakini hakufanya hivyo! {TN7: 55.1}

Hutufanya tuhuzunike kuona katika matendo ya ndugu zetu hasa utimilifu kamili wa mfano (Luka 10:25-37) wa “kuhani” na “Mlawi” ambao walipita kwa ndugu aliyejeruhiwa, aliyejeruhiwa na wapita njia-kuu wenza wa taifa lao, na hivyo kujiletea “laana,” na kusababisha kura ya “baraka” kumwangukia Msamaria mwema — leo hii mwenye moyo wa huruma nje ya dhehebu la S.D.A. {TN7: 55.2}

Kisha wakati mwingine baadaye, ndugu ambaye, alikatazwa kuingia kanisani, alikuwa amesimama kimya kwenye dirisha, akisikiliza somo, alimiminiwa maji kwa bilauri kutoka ndani. Kwenye hafla nyingine, katika kanisa lingine la S.D.A., ndugu huyo, ingawa alikuwa mlemavu, alikuwa, kwa sababu tu ya uwepo wake, kwa ukatili alipigwa mateke

55

(na mmoja wa wazee wa eneo hilo) na kuangushwa kwa mvua na matope kwenye njia ya miguu ya kanisa; bado wakati mwingine katika kanisa dada na kwa sababu iyo hiyo, alishtuliwa (na mchungaji mara hii) kwa ukali kutoka kwa kiti chake, ambapo alikuwa ameketi kwa utulivu kamili, na kimwili akabururwa nje ya kanisa na kutupwa kwenye rundo la taka kwenye njia ya miguu ya nje! Na matendo haya ni sampuli ya mengi kama hayo yanayotekelezwa na kanisa dhidi ya ndugu na dada kwa sababu ya hamu yao ya kuwa wa S.D.A. bora. Naam, hayaaminiki, lakini ni kweli, hata hivyo. {TN7: 55.3}

Si tu yanafunua Roho isiyokuwa ya Kristo, bali pia hujumuisha makosa makuu ya jinai, yanayotendwa dhidi yetu bila sababu yoyote isipokuwa kukataa kwetu kuacha kuhudhuria ibada za Sabato katika makanisa yetu! Ingawa tunachukia kuonewa huruma tunayostahili, tunapiga kelele ya uhitaji kwa haraka kuomba msaada dhidi ya wimbi hili la uovu ambalo, iwapo litaendelezwa, litavunjavunja vipande, iwapo tuko sawa au katika makosa, matumaini ya kimbelembele ya ndugu zetu ambayo yatawasababishia maafa ya kutisha na kufa moyo zaidi kuliko yale yaliyowapata Wayahudi kutokana na matumaini yao ya kujitegemea na kutojali ya kuuendeleza ufalme wao. {TN7: 56.1}

Tena, kujaribu kutufukuza kimabavu kutoka katika makanisa yetu, na kisha kutubandika chapa “vichipukizi,” ni vita vya kustajabisha, haki ambayo hatuwezi kuelewa wala wao kufafanua. {TN7: 56.2}

56

Zaidi ya hayo, wao kuendelea bila kukoma kutushutumu kwamba tunaliita kanisa Babeli, ilhali wao wote wanajua vyema kwamba hatuwezi kufukuzwa tutoke katika dhehebu, na hivyo kuthibitisha kwamba hatuliiti Babeli, bali pia ya kwamba kila chapisho letu huthibitisha haliwezi kuwa Babeli, — hivi wao kuendelea katika shutuma hizi ni kujihusisha wenyewe kutunenea vibaya mbele ya watu na kututia katika majaribu ya kufanya makosa — kuliacha dhehebu. {TN7: 57.1}

Unapojua una uhusiano mwema na Mungu, — unatembea katika nuru, — uwe imara na usiwe wa kuyumbayumba. Usilegeze msimamo kwa Ukweli ili upite juu ya mlima, ila almuradi usimame kidete kwa ajili ya haki na uiache imani yako iuhamishe mlima hadi sehemu zingine. Na iwapo mpinzani wa Ukweli anajaribu kukufunga jela kwa mwenendo fulani, usikubali, kwa maana wake ni udikteta wa moyo wa asili. Pinga na ufanye kinyume, kisha utakuwa salama. Na kwa yote, dumu kanisani mwako, tunza ukweli, na “uugue na kulia dhidi ya machukizo yanayofanyika kati yake,” kwa kuwa hivi ndivyo utakavyotiwa muhuri na kumshinda adui. {TN7: 57.2}

Hivyo kwa ajili ya Ujumbe wa Malaika wa Tatu na wokovu wako mwenyewe, kwa heshima ya Mungu, na kwa maagizo ya uhuru wa kidini, usiuruhusu ukimya wako uweze kukubaliana na matendo ya aibu ya kanisa dhidi ya washirika wake, na hivyo kuleta juu yako “damu ya watakatifu wote iliyomwagwa juu ya nchi, tangu damu ya mwenye haki Abeli “ hadi wakati wa sasa. Tunakuhimiza kwa hivyo

57

utete dhidi ya matendo kama hayo ya Kifarisayo na ya Kirumi. Na hata uweze kuendelea zaidi kuhimizwa unaposoma unaofuata

Ushuhuda wa Binafsi. {TN7: 57.3}

“Mwishoni mwa ibada iliyoendeshwa na katibu wa eneo wa Baraza Kuu la Waadventista wa Sabato katika mojawapo ya makanisa yetu ya mji, Ndugu Houteff alikuwa akimuuliza swali mnenaji wa jioni kuhusu taarifa ambayo alitoa akiwa kwenye mimbari akipinga mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji. Bila onyo au mazungumzo yawayo yote, mwanamume alimkaribia kutoka nyuma, akamnyanyua kwa shingo na mabegani, na kumsukuma nje ya jengo. Na kilichokuwa kibaya mno, mkosaji hakuwa hata Mwadventista; hakika, mama yake alisema hakuwa hata Mkristo! Sasa ni nini kilichomchochea mtu huyo maskini kutenda hivyo pasipo kuchokozwa na kinyume cha sheria? Nini!, isipokuwa shutuma za uongo kutoka kwenye mimbari, zilizofanywa dhidi ya Ndugu Houteff? Kwa maana hadi wakati huo Ndugu Houteff hakuwa amewahi kukutana na mtu huyo au hata kuzungumza naye, na hapakuwa na msisimko wowote, ila tu mahojiano ya kirafiki kwa pande za waliokuwa wakizungumza. {TN7: 58.1}

“Muda mfupi baada ya tukio hili, Ndugu Houteff na Mimi, pamoja na ndugu mwingine, tulihudhuria ibada ya Sabato katika lingine mojawapo ya makanisa yetu, na wakati huu rais wa baraza alinena akipinga Fimbo ya Mchungaji. {TN7: 58.2}

58

“Mwishoni mwa ibada hii, mwanamke mmoja alimwendea Ndugu Houteff na kusema naye akiwa amesimama na wengine mbele ya jengo hilo, na kabla ya kupata muda wa kumjibu, kijana, ambaye pia Ndugu Houteff hakuwa amewahi kumwona awali, akamwendea kwa kasi, akakunja mikono ya shati, na kutishia kuvunja miwani usoni mwake iwapo asingaliacha kuzungumza na mama yake! Lakini mtu fulani akamwongoza kuondoka, na mama yake, pia, alisema hakuwa Mwadventista. Ni nini ambacho kilikuwa kimetia chuki ya namna hiyo ndani ya moyo wa kijana huyo? Ni nini isipokuwa mahubiri aliyosikia kutoka kwenye mimbari? Kwa maana hadi wakati huo hakuna mmoja kati yao alikuwa amemwona au kuzungumza na mwingine! {TN7: 59.1}

“Tukio la tatu lilikuwa sawa na yale yaliyosimuliwa hapo juu lilikuja kwa umakini wangu, yote katika kipindi cha majuma manne. Mara hii rais wa Baraza la Muungano, alikuwa siku ya Sabato ameitisha mkutano mkubwa pamoja, maili nyingi mbali na makanisa yaliyotajwa hapo juu, kumsikia akipinga Fimbo ya Mchungaji. Wakati wa ibada, alijionyesha kwa njia ya kutia ndani ya mioyo ya wasikilizaji wake wote chuki kwa mwandishi wa ujumbe ulio katika mfululizo wa vitabu na trakti za Fimbo ya Mchungaji. Baada ya mkutano kufungwa, kikundi cha vijana kilikusanyika kumzingira Ndugu Houteff nje ya kanisa, karibu na tuta. Ghafula kijana mmoja alienda kasi kwa umati na kujisukuma kwa bidii kadiri alivyoweza kwa mmoja aliyekuwa karibu na Ndugu Houteff kwa jitihada za kumpiga dafrao kwa tuta.

59

Na angeweza hakika kufanikiwa iwapo Ndugu Houteff asingekuwa mwepesi kujimudu kwa wakati kujiepusha kugongana kichwa kwa kichwa! {TN7: 59.2}

“Tena tunaongozwa kuuliza, Ni nini kilichotia chuki ya namna hii ndani ya moyo wa kijana huyu ambaye pia hakuwa amewahi kukutana na Ndugu Houteff? Ni nini, isipokuwa hotuba ambayo alikuwa amesikia? {TN7: 60.1}

“Mashambulizi ya Shetani dhidi ya watetezi wa ukweli yatazidi kuwa makali na yaliyokusudiwa hadi mwisho wa wakati kabisa. Kama katika siku ya Kristo wakuu wa makuhani na watawala waliwachochea watu dhidi Yake, hivyo leo viongozi wa kidini watachochea ukali na chuki dhidi ya ukweli wa wakati huu. Watu wataongozwa kwa vitendo vya uhasama na upinzani ambavyo hawangeweza kufikiri kuvitenda iwapo hawangekuwa wamechochewa na kinyongo cha wanaodai kwamba ni Wakristo dhidi ya ukweli.” — Watendakazi wa Injili, uk. 324. {TN7: 60.2}

“Hakuna mtu anayeweza kumudu kushindwa kufaidika a uzoefu huu au kuhakikisha kwamba hakuna mzizi wa ukali unapata udongo ndani ya moyo wake. Haijalishi wengine wanaweza kufanya nini, yeye ambaye anaugua na kulia dhidi ya ‘machukizo yanayofanyika kati yake,’ lazima adumishe upendo usiokuwa wa unafiki kwa ndugu na hivyo kutembea katika nyayo zake Yeye Ambaye, wakati alitukanwa, hakujibu kwa kutukana tena.” {TN7: 60.3}

— E.T. Wilson.

60

Fungu la Kila Mwandishi Anayeleta Vitu vya Sasa na vya Zamani

Mat. 13:52.

Kukariri huku kufupi kwa dhuluma kupitia ndugu zetu kunatoa tu maelezo machache ya kile wanachofanya katika makanisa yote. Ni vyema, hata hivyo, kuonyesha wazi matokeo maovu ya shughuli zao, si madogo ya kawaida au ya kusikitisha ambayo yanawapa mvuto wengi kuchukua msimamo ambao ni mbaya wa kutoupokea ujumbe iwapo ndugu viongozi wanaupinga! Ingawa hawa hupata udhuru mbali mbali kwa msimamo wao wa kimwili ukweli ni kwamba wakati baadhi yao huhofia kutengwa nje ya sinagogi, wengine huchukia kustahimili kulaumiwa, licha ya agizo la Kristo la kufariji: “Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.” Luka 6:22, 23. {TN7: 61.1}

Kama walivyotenda Wayahudi wa zamani, maelfu leo huamini sana kwamba yapo mazingaombwe fulani ya kuwaokoa wanapokuwa washirika tu kanisani, hivyo kujiachilia kuyathamini na kuyategemea zaidi kuliko ujumbe, ambao hudai kutubu dhambi na kwa malipo humwinua mdhambi aliyetubu kutoka katika shimo la giza na matope, hadi ndani ya nuru ya uponyaji, ya kuokoa ya Ukweli

61

wa Sasa. Laiti hawa waabudu mahekalu yaliyojengwa kwa mikono, wangeishi katika siku za Kristo, wangaliweza kuonyesha ujinga wao kabisa wa kukataa na kupuuza Ukweli, kwa kukataa jumbe hasa za Yohana Mbatizaji, Yesu Kristo, na mitume, ili kudumisha ushirika wao katika “sinagogi” na kuepuka lawama ambazo vinginevyo wangehitajika kuzistahimili. Ilhali watu wa Mungu wa kweli daima wamejifunga wenyewe kwa kweli mpya na zisizo maarufu ambazo, zikiwa bado mpya, watu wa kujigamba kwamba ni “wenye ujuzi” wamezishutumu kuwa uzushi. {TN7: 61.2}

Hebu kila mmoja ajiulize mwenyewe kwa umakini kama angeweza kuyazingatia mafundisho ya Yohana, Kristo, Mitume, Luther, Wanamatengenezo, William Miller, na Dada White, kwa gharama ya kutupwa nje katika kila tukio kwa maana hii kumfuata Mwana-Kondoo popote Yeye aendako, au iwapo angeweza kuulinda ushirika wake kanisani bila kujali matokeo. Kwa kuufuata tu mwenendo wa kale angeweza kutembea na Mungu alivyofanya Henoko wa zamani. Na kwa kuufuata tu mwenendo huo sasa, anaweza kutembea hivyo na Mungu leo. {TN7: 62.1}

Hatari ilivyo siku zote imekuwa kuyakubali kwa upofu maoni ya wengine, zaidi ni hivyo kuegemea kwa ajili ya wokovu maamuzi ambayo hayajavuviwa ya mwanadamu, hasa wakati waandishi wa maamuzi hayo wanakataa kufungua milango ya kanisa kwa ujumbe unaobisha ili uingie. Na ingawa Mungu

62

amewaonya walei mara kwa mara kwamba “kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.” (Isa. 9:16), bado katika kila hatua ya Ukweli, wamerudia makosa haya! {TN7: 62.2}

Tumelemewa sana, kwa hivyo, kwamba sasa, katika mwisho wa dunia, watu wa Mungu, kwa sababu wako na uzoefu wote wa yaliyotukia zamani mbele yao kama ushauri, walitii Neno Lake kwa kulichunguza wenyewe na kufanya maamuzi yao, jinsi wengi wetu tulivyofanya wakati tulipokuwa tukijiunga na vuguvugu la Ujio dhidi ya mapenzi ya wachungaji wa makanisa yetu ya awali. {TN7: 63.1}

Kwa hivyo sala yetu ya dhati na matumaini ni kwamba ndugu zetu hawatarudia historia ya taifa la Kiyahudi, au historia ya kanisa la Kikristo katika siku za Luther, wakati wa Matengenezo, William Miller, na Dada White, katika nyakati zao maalum ambapo watu viongozi katika madhehebu ya wakati huo yalizishutumu kuwa ni uzushi jumbe za Ukweli. Maana leo, tangu wakati ulipoanza, ujumbe kutoka kwa Mungu kwa kanisa lazima pasipo kuepukika uwe wa sauti ya ajabu sana na ya kigeni. Inasema Roho ya Unabii: “Kweli za thamani ambazo zimekuwa hazijulikani kwa muda mrefu zitafunuliwa katika nuru ambayo itadhihirisha thamani yake takatifu, kwa maana Mungu atalitukuza Neno Lake, ili liweze kuonekana katika nuru ambayo hatujawahi kuiona hapo awali.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 62. {TN7: 63.2}

63

Isitoshe, wajumbe Wake wa leo hawatabeba wasifu mkubwa zaidi ya mwito wao kuliko walivyofanya wale wa vizazi vya zamani. Hata Yesu Kristo na kuzaliwa Kwake kwa kiungu, maisha yasiyokuwa ya dhambi, na kazi za miujiza alihukumiwa na watu viongozi wa wakati Wake, waliosema, “Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.” Mat. 12:24. {TN7: 64.1}

Walei wa wakati huo hawakufikiri zaidi ya watu wao wakuu kuliko walei wa leo. Wala viongozi wa Israeli ya kale hawakuwa wacha mungu zaidi ya viongozi wa wakati wetu. Watu wetu viogozi leo tayari wamethibitisha kwamba hawaaminiki kwa tendo lao dhidi ya ujumbe wa 1888, ambalo halikuungwa mkono na “mwenza” ambaye hawakujua ni wapi alikotoka, bali mtumishi wa Mungu ambaye, tangu kuasisi vuguvugu la S.D.A., walikuwa wamemtambua kuwa nabii. Kwa hivyo, kupata kwamba ni rahisi kuamua dhidi yake ambaye alikuwa kwa muda mrefu pamoja nao, basi, waza wewe, ni vipi rahisi sana wao kuamua dhidi ya mjumbe wa leo ambaye hawakumjua awali! {TN7: 64.2}

“Upinzani ni fungu la yote ambayo Mungu hutumia kuwasilisha ukweli maalum mwafaka kwa wakati wao. Ulikuwapo ukweli wa sasa katika siku za Luther, — ukweli kwa wakati huo wa umuhimu maalum; upo ukweli wa sasa kwa kanisa leo.” “Vipindi tofauti katika historia ya kanisa kila kimoja kimetiwa alama kwa ustawi wa ukweli fulani maalum, mwafaka kwa mahitaji ya

64

watu wa Mungu kwa wakati huo. Kila ukweli mpya umefanyiza njia yake dhidi ya chuki na upinzani; wale waliobarikiwa kwa nuru yake walijaribiwa na kuhukumiwa. Bwana hutoa ukweli maalum kwa ajili ya watu katika udharura. Ni nani anayeweza kukataa kuutangaza?” {TN7: 64.3}

“…Wafuasi wakweli wa Kristo…huwa hawasubiri ukweli uwe maarufu. Wakiwa wameshawishiwa kwa wajibu wao, kimakusudi huukubali msalaba.” {TN7: 65.1}

“Watepetevu na wa juu-juu tu hawawezi tena kuegemea kwa imani ya ndugu zao.” {TN7: 65.2}

“Badala ya kuhoji na kupiga chenga kuhusu yale wasiyoyaelewa, hebu waitii nuru ambayo tayari inawaangazia, na watapokea nuru kubwa.” {TN7: 65.3}

“Siku zote limeendelea kuwapo daraja linalojidai kwamba ni la uungu, ambalo, badala ya kufuata kuujua ukweli, hufanya kuwa dini yao kutafuta mapungufu fulani ya tabia au kosa la imani ndani ya wale ambao hawapatani nao. Wa namna hii ni wasaidizi wa mkono wa kuume wa Shetani.” {TN7: 65.4}

“Wote hutafuta kulabu ili kutundika mashaka yao, watazipata. Na wale ambao hukataa kupokea na kutii neno la Mungu mpaka kila kizuizi kiweze kuondolewa, na hamna tena fursa ya shaka, kamwe hawatakuja kwenye nuru.” — Pambano Kuu, uk. 143, 609, 460, 395, 528, 519, 527. Wakiendelea katika mkondo wao wa upofu,

65

na wa mashaka, kwa kawaida hutumbukia katika udanganyifu, ambao wao husingizia kwamba ni ujanja. Kwa hivyo, ndugu, kwa kuhitimisha, waza swali: {TN7: 65.5}

Nini Kitakachopatikana Au Kupotezwa?

Mkondo ambao kanisa linafuata unalipeleka pamoja na kuelea kwa dunia, badala ya kuelekea kwa bandari ya makao yake ya milele. Taasisi zake — shule, hospitali, n.k. — zimepatana na taasisi za ulimwengu, hatari haswa ambayo Roho ya Unabii imeonya tangu zamani sana: {TN7: 66.1}

“Ni udanganyifu mkubwa ulioje unaoweza kuja kwa akili za binadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wao wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi Mwaminifu unawapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, na hata sasa ni waaminifu katika udanganyifu huo.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {TN7: 66.2}

“Nimejaa huzuni wakati ninapowaza hali yetu kama watu. Bwana hajaifunga Mbingu kwetu, lakini mwenendo wetu wa kuendelea kurudi nyuma umetutenga na Mungu. Kiburi, tamaa, na kuipenda dunia vimeiishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kuhukumiwa. Dhambi za kuudhi na za kiburi zimekaa kati yetu. Hata hivyo maoni ya jumla ni kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho upo katika mipaka yake yote.” {TN7: 66.3}

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole .

66

kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {TN7: 66.4}

“Ni nani anaweza kusema kwa kweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto; mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimwona Mwalimu wetu akiyaonyesha mavazi ya kile kinachoitwa eti utakatifu. Aliyararua, Akaufunua wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha akanambia: ‘Je, huoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia?’ “Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba?” Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu zinakosekana.’” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {TN7: 67.1}

“Ukurasa baada ukurasa unaweza kuandikwa kuhusiana na mambo haya. Mabaraza yote yanatiwa chachu kwa kanuni sawa zilizopotoshwa.” Kwa maana matajiri ndani yazo wamejaa uhasama, na wakaaji ndani yake wamenena uongo, na ndimi zao ni za uongo katika vinywa vyao. ‘Bwana atafanya kazi kulitakasa kanisa Lake. Nawaambia katika kweli, Bwana yu karibu kupindua na kupindua-pindua katika taasisi zinazoitwa kwa jina Lake. {TN7: 67.2}

“Jinsi gani kwa upesi mchakato huu wa kusafisha utaanza, siwezi kusema, lakini hautakawia kwa muda mrefu. Yeye Ambaye pepeto Lake li mkononi Mwake atalisafisha hekalu Lake dhidi ya unajisi wa maadili yake. Atausafisha uwanda Wake kabisa.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 372, 373. {TN7: 67.3}

67

Taarifa zilizovuviwa zilizotajwa hapo mibtarafu hali ya kanisa, huonyesha, jinsi unavyofanya ujumbe kwa Walaodekia, kwamba ni mbaya sana, ambayo inafanya hitaji la Bwana kutuma makemeo na maonyo, kuitisha maamuzi ya matengenezo, ambayo yatalisababisha aidha kufanya matengenezo, na hivyo kusababisha Mungu kulikubali, au kulifanya gumu, na hivyo kusababisha Yeye kulitapika “litoke katika kinywa chake.” Ufu. 3:16. “Hebu wachungaji na watu wakumbuke kwamba ukweli wa injili huangamiza iwapo hauwezi kuokoa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 134. Vivyo hivyo, wokovu wetu, kukubaliwa kwetu kwa ufalme Wake wa milele, hutegemea kupokea kwetu ujumbe ambao Bwana hututumia. {TN7: 68.1}

Sisi ambao tumeuchunguza ujumbe ulio sheheni katika Fimbo ya Mchungaji tumeshawishika sana kwamba ni “ujumbe wa Shahidi wa Kweli” “kwa Walaodekia,” ambao unawapata watu wa Mungu katika “udanganyifu wa kusikitisha,” kama ni kwa Sabato au ukweli wowote ambao umewahi kujulikana kwa kanisa. Na hakika tunapaswa kuwa, kwa maana umefungua ufahamu wetu sura baada ya sura ya Maandiko, maana ambazo sisi hapo awali hatukuwa hata na wazo hafifu, lakini ambazo sisi sasa tunaelewa wazi wazi jinsi tunavyofanya kwa ukweli wowote wa Biblia. Kupitia ujumbe huo, sasa tunaona kwamba unabii wa sura hizi (Isaya, Ezekieli, Hosea, Yoeli, Zekaria, Danieli, Ufunuo, n.k.) zinalenga kwa wakati huu, na kuangaza kwa uzuri wa ajabu. Umetuzidishia thibitisho kwamba dhehebu

68

la Waadventista wa Sabato ni kanisa la Mungu, hivyo kuimarisha zaidi kuliko hapo awali, ikiwezekana, nia yetu ya kukaa ndani yake bila kujali hali yake. Na kwa sababu hiyo umetuweka imara zaidi kuliko hapo awali katika Ujumbe wa Malaika wa Tatu, na kutufanya kuwa na upendo wa dhati kwa ndugu. Kisha, hatimaye, umetuwezesha kujifunza Biblia na Roho ya Unabii zaidi ya hapo awali. {TN7: 68.2}

Bila kujisomea mwenyewe machapisho ya Fimbo, mtu hawezi kujua badiliko la ajabu ambalo yanafanya katika maisha ya wote wanaozipokea kweli, wala mtu hawezi kuyafahamu maajabu ya unabii ambao yanafunua, mengi ambayo hapo kabla watu hawajawahi kamwe kujaribu kueleza. Hakuna hekima ya mwanadamu ambayo ingeweza kufungua siri hizi za Mungu ambazo zimefichwa kwa vizazi vingi kutoka kwa wenye hekima na busara. Wale ambao kwa ajili yao wenyewe hawajafanya “uchunguzi wa kina” wa ujumbe ambao Fimbo husheheni, na ambao umekuja “kwa jina la Bwana,” Roho ya Unabii huwashauri wasiseme: “Nimeridhika na msimamo wangu. Nimeweka vigingi vyangu, na Sitaondolewa mbali na nafasi yangu, liwalo liwe. Sitausikiza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65. {TN7: 69.1}

69

Wazi wazi, wale ambao kwa maneno au matendo hushindana kwamba wanajua zaidi kuhusu Fimbo ya Mchungaji kuliko sisi ambao tumejifunza kwa makini, si tu wanazifanya za upumbavu akili zao wenyewe, lakini pia kuzidhulumu zetu. Isitoshe, kwa kuhukumu na kushutumu bila kusikia, wanavunja sheria za haki ya kawaida, na wanalidharau shauri la Bwana na kujiweka juu zaidi ya Kiti Chake cha enzi! {TN7: 70.1}

“Ilikuwa kwa kufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndio sababu ujumbe wa mbinguni haujawafikia…. Hakuna wema au ushujaa kuendeleza vita daima gizani, Kuyafumba macho yako usije ukaona, kufunga masikio yako usije ukasikia, kuufanya mgumu moyo wako kwa ujinga na kutoamini usije ukajishusha na kukubali kwamba umepokea nuru kwa mambo fulani ya ukweli. Kusimama mbali na uchunguzi wa ukweli si njia ya kutekeleza agizo la Mwokozi kuyachunguza Maandiko.’ Je! Ni kuchimba hazina zilizofichwa kuyabandika matokeo ya kazi ya mtu rundo la taka, na usifanye uchunguzi wa makini ili kuona iwapo vipo au la vito vya thamani ya ukweli katika kusanyiko la wazo ambalo unahukumu?” — Shuhuda kwa kazi za Shule ya Sabato, uk. 65, 66. {TN7: 70.2}

Basi, ili kutekeleza kusudi lake la siku zote la kuiweka himaya ya Ukristo kuzongwa-zongwa na waalimu

70

wa uongo, Ibilisi husababisha kila upepo wa mafundisho kuvuma pande zote. Mmoja baada ya mwingine huwafanya waalimu hawa kuchipuka, kama mimea kivulini, kunyauka tu wakati inapowekwa wazi kwa jua. Kwa hivyo kuweka daima mashuhuri mfano wao mbaya na wa wafuasi wao, yeye kwa ustadi huwavunja moyo na kuwatisha wote walio na mazoea ya kuichunguza nuru yoyote inayodaiwa kwenye Maandiko, na hivyo huwaandaa kuukataa ujumbe huo wa Ukweli wakati wowote Mungu atakapoweza kuutuma. {TN7: 70.3}

Wakati, kwa hivyo “ujumbe unakuja kwa jina la Bwana,” iwapo wewe, kwa sababu ya jumbe potovu ambazo adui ameleta katika siku za nyuma, ukatae kufanya uchunguzi mwenyewe, ukisema, “Hakuna maana, ni ‘kichipuko kingine’ tu; najua hauwezi kuwa ukweli;” basi, iwapo ni Fimbo au chapisho lingine lililosheheni ujumbe, hakika ni kwamba punde si punde au baadaye, utaukataa ujumbe unaohitaji hasa kukuokoa kutoka kwa udanganyifu wa kusikitisha wa Ulaodekia. {TN7: 71.1}

Hivyo daima akiweka mbele ya kanisa mwalimu wake mbeba-mkoba, “vichipuko,” Mdanganyifu mzee wa kale anafanikisha mpango wake wa kishetani wa kuwasaliti wengi ili waikatae nuru itakayoiangaza dunia yote. {TN7: 71.2}

Tunajua kwamba Bwana ananena na watu Wake hasa wakati huu kupitia kwa machapisho ya Fimbo ya Mchungaji; kwamba ujumbe yanayosheheni ni ule

71

“utakaosababisha mtikiso miongoni mwa watu wa Mungu” (Maandishi ya Awali, uk. 270); kwamba wale ambao wanaupokea ushauri huu wa Shahidi wa Kweli watapokea muhuri wa Mungu na kuhesabiwa miongoni mwa watu 144,000 (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266); ya kwamba wale wanaoukataa, wataanguka kwa mchinjo wa Ezekieli 9 (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445, Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211) na Isaya 66:16; na ya kwamba wale “watakao okoka,” watu 144,000, malimbuko, watakuwa watumwa wa Mungu wakati wa Kilio Kikuu (Ufu. 14:4, Shuhuda, Gombo la 5 uk. 80, 81) kuyaleta mavuno ya pili kutoka katika “mataifa yote.” Isa. 66:19, 20. {TN7: 71.3}

Kwa hivyo, Wandugu, jinsi tulivyo na “hakikisho kamili la imani” kwamba maarifa yetu, hukumu, na imani katika mafundisho ya S.D.A. ni timamu na yako, na kwa vile hujui msimamo wetu na kwa vile tusivyoujua wako, ipo angalau fursa kubwa ya kuwa sawa kama vile ilivyo yako kuwa sawa. Hivyo kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe, usithubutu kukataa kuchunguza. Iwapo unaziba masikio yako kwa sauti ya Shahidi wa Kweli, itamaanisha maangamizi yako milele! Hii ndio maana mioyo yetu imefadhaika, ndiposa tunahangaika kwamba ninyi mfanye wenyewe uchunguzi wa, ujumbe wa Fimbo. Na iwapo wewe ni “mtu wa hekima” anayetii “sauti ya Bwana…kwa mji,” utaisikia “Fimbo,” na kujua “Yeye aliyeiagiza.” Mika. 6:9. {TN7: 72.1}

Tumelitua jukumu letu. Sasa unapaswa kujitwika lako, na kuushughulisha

72

uwezo uliopewa na Mungu na wajibu wa kuhakiki zawadi yako ya milele. Usiihatarishe taji yako ya uzima pengine, kwa uwezekano wowote wa kupoteza baada ya kuwa kwa miaka katika ujumbe. Ni hasara ilioje, hasara ya kutisha, “dunia isiyokuwa na mwisho” ambayo itakuwa! Pokea ushauri huu na utii madai yake, na utiifu wako utakuhifadhia amani na furaha na uzima wa milele. {TN7: 72.2}

“…Iwapo ujumbe unakuja usiouelewa,” hushauri Roho ya Unabii, “vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa, ukilinganisha andiko kwa andiko, ili uweze kujua iwapo zinaidhinishwa na Neno la Mungu au la. Ikiwa utaamini kwamba msimamo uliochukuliwa hauna msingi katika Neno la Mungu, ikiwa msimamo unaoshikilia juu ya suala hauwezi kupingwa, basi wasilisha sababu zako thabiti, kwa maana msimamo wako hautatikiswa kwa kukutana na makosa.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65, 66. {TN7: 73.1}

“Lakini jihadhari kukataa lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {TN7: 73.2}

73

Kumbuka: Tarakimu za mwongozo zilizotolewa katika makala inayofuata, zinalingana na orodha ya dondoo zilizopeanwa hapa chini. Na ufunguo wa vifupisho ni sawa na mada kwa Maandishi ya Ellen G. White. {TN7: 74.1}

(1) S.W. 468. (2) K.H.Y. 67; Mapitio na Kutangaza, Mei 27, 1890. (3) S.W. 80; S.W. 300. (4) 5 S.G. 209. (5) 6 S.G. 17. (6) S.K.S.S. 65. (7) 9 S.G. 126. (8) S.W. 514, 515; K.H.Y. 154. (9) Isa. 58: 1; S.K.S.S. 56. (10) M.A. 270. (11) S.W. 445, 3 S.G. 266; 5 S.G 211. (12) 5 S.G 136, 81; 3 S.G. 267; 1 S.G. 187. (13) 5 S.G. 80; P.K. 425. (14) M.A. 270; 3 S.G. 252, 253. (15) Ufu. 3: 14-19. (16) M.A. 276, 277; M.W. 725. (17) S.K.S.S. 65. {TN7: 74.2}

Kwa maombi ya dhati kwamba Bwana apate nafasi Yake nasi sote, sisi, tukiwa jamii ya watenda kazi, tunanena

Kwa Waadventista wa Sabato Wote — Salamu! {TN7: 74.3}

Wapenzi Ndugu:

ILHALI, Sisi ambao tunasimama katika nuru inayoendelea ya Ujumbe wa Malaika wa Tatu tumefanya, kama vilejinsi wale walioupokea Ukweli wa Sasa katika vizazi vyote, hatua zetu zimeeleweka visivyo, nia zetu kutiliwa shaka na ujumbe wetu kueleweka vibaya, “kudharauliwa kunenewa kinyume, kudhihakiwa, kukataliwa,” na “kushutumiwa,” kama “unaongoza kwa uzushi na ushupavu uliokithiri” (1); na {TN7: 74.4}

ILHALI, Kwa sababu “nuru ambayo itaangaza dunia kwa utukufu wake” (2),

74

sasa inaitwa “nuru ya uongo” (3), imekuwa lazima kufafanua wazi wazi nafasi yetu katika muunganisho na kufunga kwa kazi ya Ujumbe wa Malaika wa Tatu; na {TN7: 74.5}

ILHALI, Tukiamini kwamba utaratibu na mfumo ni sheria za kwanza za mbinguni, na kutambua kwamba kwa wale ambao “wanasimama katika nuru” (4), limekuja hitaji la lazima la namna fulani la ushauri kuhusu shughuli zao katika kanisa kote ulimwenguni; {TN7: 75.1}

Kwa hivyo, tukiwa jamii yenye umoja ya waamini katika ujumbe wa Ukweli wa Sasa, ulivyosheheni katika machapisho ya Fimbo ya Mchungaji (ambao tunaamini umekuja kwa itikio la kuelimishwa na Mungu, na ni “kukunjua kwa chuo” (5), katika uwiano kamili na Ujumbe wa Malaika wa Tatu jinsi ulivyowekwa katika Biblia na Shuhuda kwa Kanisa, sisi kwa njia hii tunatangaza: {TN7: 75.2}

Iazimiwe, Kwamba tuelekeze uungaji mkono wetu kamili kuutangaza Ukweli wa Sasa, kwa uwiano na mafundisho ya S.D.A. jinsi yalivyotolewa awali kupitia Biblia na Shuhuda; lakini kwamba tutete kwa heshima dhidi ya matendo ya ndugu zetu kuwatupa nje na kuwatenga washirika kutoka kwa makanisa ambayo wamewasaidia kujenga, kwa sababu tu wanaishughulisha haki yao waliopewa na Mungu kwa kufanya uchunguzi kibinafsi wa nuru mpya (6); na {TN7: 75.3}

Iazimiwe zaidi, Kwamba tukiwa katika uwiano na mafundisho ya S.D.A. jinsi yalivyowekwa

75

katika Biblia na Roho ya Unabii, tuna uhakika kwamba haliwezi kuwapo vuguvugu jipya isipokuwa lile lililonenwa kama “Vuguvugu Kuu La Matengenezo Kati Ya Watu Wa Mungu” (7); na {TN7: 75.4}

Bado Iazimiwe zaidi, Kwamba tunakemea shutuma zozote binafsi za ndugu zetu, lakini kutambua, jinsi wao, wenyewe, wanavyofanya, kwamba saa imegonga kwa “uamsho na matengenezo” (8), kama wajumbe wa kweli wa Mungu, “tutapiga kelele tusiachie” (9). {TN7: 76.1}

Azimio lilipitishwa katika kikao cha wazi cha Wadaudi Waadventista wa Sabato waliokongamana siku hii ya kumi na mbili ya Machi, 1934. {TN7: 76.2}

(walitia sahihi ) KAMATI YA USHAURI

Azimio ambalo tumelipitisha hapa laja kwa kuitikia hatua ya kikundi cha wawakilishi wa Waadventista wa Sabato waliokutana huko Los Angeles, California, kutoka majimbo sita yanayoenea kutoka Atlantiki hadi Pasifiki, wote ambao wamefanya uchunguzi wa makini na wa kina wa asili, kazi, na mafundisho ya Fimbo ya Mchungaji. {TN7: 76.3}

“Uamsho na matengenezo” yaliyotajwa katika azimio lililotajwa hapo juu si kingine ila “upepeto” (10), “kutiwa muhuri” (11), “kupimwa” (12), wakati wa “ kutakasa” (13), unaosababishwa na kutangazwa kwa “Ushuhuda usiopinda wa Shahidi wa Kweli kwa Walaodekia” (14), wakati ambapo kanisa litaibuka kutoka katika hali ya “uvuguvugu”

76

wake (15), kwa kupokea vazi la haki ya Kristo, kwa utayari wa kutangaza Kilio Kikuu (16) cha malaika wa tatu. {TN7: 76.4}

Ukweli kwamba haliwezi kuwapo dhehebu jipya unaonyesha wazi kwamba kazi yetu yote lazima ifanyike katika na kwa ajili ya dhehebu letu S.D.A. Tunaamini, kwa hivyo, kwamba tumaini letu la kuabudu katika kanisa la uchaguzi wetu, hata ingawa limetunyang’anya ushirika wetu (na kwamba isipokuwa sababu nyingine ila kuipokea “nuru zaidi” kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu) (17), halitakataliwa, na ya kwamba uwepo wetu hautazuiliwa. {TN7: 77.1}

——–

(Italiki Zetu)

77

(Ukurasa Mtupu)

78

“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndio amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.” Mat. 22:37-40. {TN7: 79.1}

“Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndio torati na manabii.” Mat. 7:12. {TN7: 79.2}

79

>