fbpx

Mwajiri wa Nyumba Nyeupe

Asilani hakukuwahi kuwa na mawingu ya vita, ya ajabu na meusi sana yakining’inia kwa ghadhabu ya uzito juu ya ulimwengu, na kamwe ulimwengu haukujiona jinsi ulivyo leo. Kote kote, — serikalini, viwandani, kumbi za kujifunza, makanisa, nyumbani, barabarani — katika nyanja zote za maisha, swali kuu ni, mwanadamu aelekea wapi? {WHR: 3.1}

Kutoka kwa wasemaji wa kisayansi na waandishi mashuhuri wa habari huja maneno yanayo wawakilisha hivi: {WHR: 3.2}

“…Ni nini kisa cha Mwanadamu? Ni kwamba wanadamu hufa, Mtu huishi. Wanadamu sasa wanaonekana karibu sana na hali mbaya zaidi ya zote waliyojifanyia wenyewe katika historia yao ya muda mrefu wa vita. Iwapo upeo waja utabadilisha maisha na dunia. Lakini hauwezi kukomesha maisha, hautaangamiza ulimwengu. Katika upeo wa juu kabisa, au labda katika matarajio yake, wanadamu wanaweza kupata siri ya amani na njia ya kuishi bila uharibifu. Hilo ni tumaini. Hakika ni kwamba Mtu atakuwa duniani, akifanyiza ulimwengu.” — Maisha, Oktoba 3, 1949, uk. 22. {WHR: 3.3}

“…Einstein…hukubali…kwamba mataifa mengine yanaweza kuvumbua upya michakato yetu ya siri wao wenyewe, kwamba hakuna ulinzi wa kijeshi unaoweza kutarajiwa na maandalio ni bure, kwamba kama vita vingine vitalipuka, mabomu ya atomu

4

hakika yataharibu ustaarabu… {WHR:3.4}

“Ni muhimu,” aliendelea kusema, ‘kuangazia maoni ya umma kwa hali halisi kulihusu bomu. Kuzuia vita tu kivitendo kwa kiwango cha kimataifa, ambalo litafanya maandalizi ya vita kutokuwa ya lazima na hata kutowezekana, yaweza kutuokoa kutoka kwa athari zake.'” — Juma ka Habari, Machi 10 1947, uk. 58. {WHR: 4.1}

“…Historia, katika maeneo makubwa ya ulimwengu, imevingirishwa nyuma. Ushupavu umebadili akili; ugaidi, maelewano; chuki, urafiki. Sayansi, elimu, na falsafa, magari ya maendeleo kwa mtu wa Magharibi, yamepotoshwa, kuumbuliwa na kubatilishwa kuwa silaha dhidi ya ustaarabu.” — John Edgar Hoover, katika ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Shirikisho la Upelelezi. {WHR: 4.2}

“Vita vya Kwanza vya Dunia vilikuwa ni mshtuko hakika kwa kipindi cha awali cha matumaini, …Leo hii mshtuko karibu ni ajabu mkubwa zaidi. Ukosefu wa usalama na kushindana ni kawaida kwa sababu mwenendo uliopo ni wasiwasi na wa kutazamia hali mbaya ya kutokuwa na uhakika.” — John Dewey, Ujenzi wa Ufalsafa, uk. 8. {WHR: 4.3}

“Kuna sababu nyingi sana za kutia hofu kwamba ustaarabu wa Magharibi, ikiwa sio ulimwengu wote, yawezekana kwa siku za usoni dunia yote kupitia huzuni kubwa na mateso na maumivu…” — Bertrand Russel juu ya somo hilo, “Ikiwa Tunaokoka Wakati huu wa Giza,” katika gazeti la New York TIMES, Septemba 3,1950. {WHR:4.4}

“Sasa tumefika kwa kituo cha mwisho katika historia. Kile mwishowe kinahitajika kwetu kinahitajika sasa… Tumechelewa sana. Labda hakuna kinachoweza kutuokoa.Lakini

5

ukutani ni dhahiri kabisa. Yanasema kwa watu wa dunia, ‘Muungane au mfe.'” — Dkt Robert M. Hutchins. {WHR: 4.5}

“Kila mtu amekubali kwamba vita vya atomu ni kuinyonga dunia, ambapo hakuna anayeweza kushinda. Hakuna mwana sayansi aliyesifika awe na mashaka kwa ukweli kwamba kila nchi yenye uwezo wa viwanda itakuwa na bomu la atomu ndani ya miaka mitano. Tuna miaka mitano tu ya kujenga kwa ajili ya amani.” — Dkt. Robert M. Hutchins, Kansela wa Chuo Kikuu cha Chicago, katika Jukwaa La Chicago Kila Siku, Machi 26, 1946. {WHR:5.1}

“Hapawezi kuwa na shaka kuhusu mgogoro wa dunia. Tunaishi katika moja ya vituo vinavyopinda vya historia ambavyo hutoa njia mbili, moja ambayo huongoza kwenye kifo na nyingine uzimani. {WHR: 5.2}

“Ukweli ni kwamba, bomu la Hidrojeni linawakilisha ushindi wa mwisho wa watu kujinyonga, kufunguliwa kwa siri za asili kwa madhumuni ya maangamizi ya jumla. Huleta kwenye mtazamo kamili kushindwa kwa ustaarabu wa kidunia ambao umetafuta kupanga maisha yake mbali na Mungu.” — G. Ashton Oldham, aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Episkopali ya Albany, juu ya “Vita vya Dunia na Baadaye,” katika taarifa ya Umoja wa Amani ya Kanisa la Juni. {WHR: 5.3}

“Watu wanagundua kwamba hofu ya kutisha imeingia katika maisha, hata watu wasiokuwa makini wanasaliti, vipindi kwa vipindi, ajabu fulani, hisia ya hali ya kuogopa, na hisia ya mkimbizi kwamba kitu kinatukia ili maisha yasiweze kuwa sawa. {WHR: 5.4 }

“Tandaza na uchunguze mtindo wa matukio na utajikuta uso kwa uso na azimio jipya ambalo

6

hapo kabla halikuwahi kufikiriwa kwa akili ya binadamu…. {WHR: 5.5}

“Waandishi wameshawishika hakuna suluhisho, pande zote au katika mgogoro. Ni mwisho.” — H.G. Wells, Mkaguzi wa Los Angeles, Oktoba 21, 1945. {WHR: 6.1}

Katika maoni yaliyofikiriwa kwa makini ya waangalizi mashuhuri walio kwenye eneo, kizazi hiki kipo kwenye saa sufuri ya ustaarabu. Iwapo tunajua au la, siku ya kiama inafupisha kivuli chake, na tunakabiliwa moja kwa moja na maswala mazito zaidi ambayo daima yatakikabili kizazi cha wanadamu. Vichwa vya atomu, makombora hatari, gesi za sumu, mabomu ya viini, nyambizi bora sana zinazopekecha vilindi virefu, na ndege bora sana zinazochomoza katika anga juu, — ni nini maana ya vyombo hivi na vingine vya kuogofya vya uharibifu? Je, zinamaanisha nini ishara hizi za nyakati zingine kwa Kanisa na kwa ulimwengu wote? Laiti swali lingechipuka kwa kizazi chochote katika siku za manabii wa zamani wa Mungu, basi bila ya shaka wangeweza kujibu: “Kama kanisa liishivyo, na kama hakika kwamba Mungu Yuaishi haiwezekani kuwaacha watu Wake katika giza kwa ishara zinazohusu nyakati zao.” Na jibu lao lazima liwe jibu letu, pia. Aidha ni ukweli wa dhahiri kwamba kama tunataka kujua, Mungu atatuwezesha kujua maana ya kweli ya vitu hivi visivyo kifani vya uharibifu. {WHR: 6.2}

Tangu mwanzoni, yote haya mengi yamedhihirika kabisa: Iwapo mabomu bora, walipuaji bora, na bora yote hayaleti chochote kingine, yote bila shaka hutishia ustaarabu. Wazo hafifu la kutamausha na madhara ya matumizi yake yanapatikana kutoka kwenye eneo la uharibifu wa kutoka angani ulioonyeshwa kwenye ukurasa wa jalada. {WHR: 6.3}

7

Dhahiri, pia, ni uhakika kwamba Mbingu imeruhusu vyombo hivi vya uharibifu kuja ili kuamsha himaya ya Ukristo, ukasisi na waumini vilevile, kwa hatua ya pamoja, yenye nuru, na hatua ya wote kuondoka wakati Bwana anaoongoza mbele kumwokoa mwanadamu dhidi yake na kutoka kwa Ibilisi. Ukristo unashindwa kazi hii, na kuuacha ulimwengu kujiokoa wenyewe iwezekanavyo, Adui kwa muda mfupi ataondoa si tu elimu ya Mungu na ya wokovu bali pia ustaarabu wenyewe. Hakika kila mwangalizi aliye macho anaweza kuona wazi kwamba wakati Mbingu na dunia kwa uchovu zinawangoja Wakristo kuchukua hatua dhidi ya uovu wote, nguvu ya uovu inajitahidi kueneza ushawishi mbaya kabisa ndani ya wanaume na wanawake wasiomcha Kristo kama vile wanaobeba mwenge mwekundu wa Ukomunisti. {WHR: 7.1}

Kwa kweli picha ni ya kuogofya. Na hatari yake kali inarusha changamoto yake kwa jumuiya ya Ukristo kwa ujumla. Tutafanya nini kuihusu? Tuifumbie macho kabisa? au tuamke kuikabili, na kuwa kina Nuhu, Gideoni, Daudi, Eliya, Danieli, Luther, na wale wote walio na imani ya kufanya kitu kuihusu wakati nuru bado inaangaza na wakati fursa ingali yetu? Je! Tutaweka ipasavyo moyoni ukweli wa majonzi kwamba “dhambi ya ukaidi wa dunia i langoni pa kanisa”? — Pambano Kuu uk. 389. Je, sisi sote tutakubali kuitangaza mbiu ya hadhi kubwa, “Utukufu kwa Mungu aliye juu, na duniani amani, mapenzi mema kwa watu wote” (Luka 2:14), kama amana ya hadhi kuu na wajibu wa Kanisa zaidi ya Serikali? Nchi yetu na ulimwengu wote unalihitaji Kanisa, na Mungu anasubiri washirika wake, wote walei na ukasisi, “kuamka, kuangaza.” Isa. 60: 1. {WHR: 7.2}

Kila Mkristo anayefahamu ukweli kwamba injili “ni nguvu ya Mungu kwa wokovu,” anajua kwamba iwapo umati ungeongoka kwa Kristo, haungekuwapo, hakika haungeweza, kuwapo

8

Utawala wa chokochoko wa Kikomunisti au mwingine wa kidikteta duniani, na kwa hivyo hakuna tishio kama Ukomunisti unaotaka vita unaowasilisha kwa ustaarabu. Na kila Mkristo pia anajua kwamba hakuna nguvu duniani, isipokuwa “upanga wa Roho,” ambao unaweza kukikata kichwa cha Goliathi wa leo. Sikitiko lililoje, basi, Ni usaliti ulioje kuuamini, iwapo Kanisa halipaswi kuinua mara moja kutoka kwa mabega ya Serikali sehemu yake iliyopuuzwa, ambayo ni sehemu kubwa zaidi, ya mzigo wa kufanya amani, ila kuendelea kuiacha Serikali kuubeba mzigo wote, na kufanya vizuri iwezavyo bila kuangaziwa nuru ya Mungu na bila nguvu ambayo Kanisa pekee linaweza kupeana. {WHR: 7.3}

Kwa makusudi kulisukuma kanisa nje ya tawala zote za kikomunisti, Adui tayari kwa hila ameiba ushindi muda mrefu juu yake, na sasa anapigana vikali ili kuupanua ushindi wake hadi mwisho akishangilia kwa kulisukuma litoweke haswa kutoka kwa uso wa dunia. Lakini bado hata sasa tumaini iwapo tu katika ujasiri kwa uaminifu litaitikia agizo Takatifu sasa linalopiga kelele mbele ya kila mlinzi wa imani: {WHR: 8.1}

“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu Wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.” Isa. 60: 1-3. {WHR: 8.2}

Katika wazimu wa kutaka mamlaka, kutawala au kuangamiza, kutaka sana vita na kutaka sana kuzimu, mwenendo wa watu kujiangamiza wenyewe, katika mapinduzi ya hasira na majanga, na kufyatuka kwa

9

vitu vya maumbile, na katika kuzidizidi kutimizwa kwa unabii unaokunjua upesi katika Neno la Mungu, ishara za nyakati zangurumisha onyo la rufaa kwamba tuamke katika nuru ya Mungu na kuharakisha kuwaopoa watu Wake kutoka kwa madhara ambayo yanatisha kuiteketeza dunia. Iwapo wa namna hii si utume na wajibu mkuu wa Kanisa wakati huu wa hatari, basi, Bwana na ulimwengu unahitaji gani nalo? Lakini ni nini kanisa laweza kufanya isipokuwa washirika wake,wote, walei na viongozi, waamke kwa pamoja kama mtu mmoja, na wavurumishe vyao vyote katika pambano? {WHR: 8.3}

Kujua vyema tunavyofanya jibu kwa maswali haya ya dharura, tutakuwa na udhuru gani iwapo hatutaamka sasa na watakatifu wote katika himaya ya Ukristo pamoja nasi kufanya lile injili hutuamuru kufanya? Bila kujali jinsi maonyesho ya tamasha na kuvutia ya kanisa linaweza kuvaa, si siri kwamba hata kama halijasukumwa nje ya eneo lolote la nchi, bado katika mwendo wake wa sasa wa kuhubiri Injili ya Ufalme millenia ya muda haitalitosha kuionya dunia, kumaliza kazi, na kuuleta Ufalme ndani. Na kila akili iliyoangazwa nuru inajua huu kwamba ni ukweli usioepukika. {WHR: 9.1}

Angalia tu ya ukatili, majeshi ya uharibifu yanayorandaranda na kuotea kila mahali, na kusababisha dunia nzima kulipuka kwa vurugu, machafuko na hofu. Hakika, yanafanya “watu kuvunjika mioyo [kuzimia] kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu….” Luka 21:26. Je! Wakristo wote kila mahali hawataamka kwa mambo haya na “kuvaa silaha zote za Mungu” na “kuuchukua… upanga wa Roho” (Efe. 6:11, 17) wakimfuata Bwana Akiongoza mbele? Iwapo sivyo, basi

10

hakika ni kwamba Kanisa na Dunia bila tumaini imeangamizwa. Ili kuwa na hakika, hata hivyo, wachache wanaoamka na kujisalimisha kikamilifu inavyohitaji saa, Mungu atawaokoa, dhidi ya moto mkubwa, utakaokuja. {WHR: 9.2}

Vipi, hata hivyo, Yeye atamwokoa yeyote ambaye hawezi kutii ishara za nyakati, na ngurumo za ngoma za kuogofya za Siku ya Maangamizi, ambazo zinamulika machoni na kunguruma masikioni mwetu kwa onyo la kutisha sana kuliko ngurumo za miali ya moto za Sinai? La, Yeye hangeweza tena kuwaokoa kama hawa vipofu kiroho, viziwi, na bubu wasioweza kuponywa kuliko vile Yeye hangeweza kuwaokoa walioishi kabla ya gharika walioshindwa kuingia katika safina ya Nuhu. {WHR: 10.1}

Na sasa sahani za kupaa zinaongezea nini kwa picha ambayo tayari imekuwa mbaya? Iwapo ni mitambo iliyoundwa duniani au ya mbingu, vyombo vya anga vipaavyo kati ya sayari moja hadi nyingine, bado hupaka rangi mbaya zaidi kwa mdhambi. {WHR: 10.2}

Mmoja anaweza kuwa na mshangao, mwingine kushtuka, kwa wazo la Mbingu kuwa na sahani za kupaa. Lakini kwa nini? Ikiwa Mungu amempa mwanadamu maarifa ya kutengeneza vyombo vya angani, hakuna mtu aliye na sababu kudhani kwamba Mbingu haina visivyoweza kulinganishwa kabisa bora zaidi. Hebu tusisahau kilichoufunika mlima wote katika siku ya Elisha (2 Wafalme 6:17). Kwa hakika, Elisha aliviita magari, lakini kama hazikuwa sahani za kupaa za aina fulani, zilikuja vipi duniani? Haijalishi mmoja anaviitaje, ni jinsi vilivyo, na kile vinachofanya, ndilo muhimu. {WHR: 10.3}

Viwe vinavyoweza kuwa, hata hivyo, ishara pande zote kutuzunguka bila kukosea zinaonya kwamba mawingu mazito meusi yanajikusanya juu ya dunia yote ili kumimina kwa dunia isiyokuwa na kinga tufani ya kutisha zaidi tangu majira kuanza.

11

Wote walio na sikio la kusikia na jicho la kuona, ishara za nyakati zinaonyesha kwamba kwa upesi tunaenda kukutana uso kwa uso na “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo.” Dan. 12: 1. {WHR:10.4}

Kuelewa vizuri uwezo wa kutisha wa silaha zilizopo sasa, hakuachi shaka la maangamizi ya dunia kwenye picha. Kila mmoja wetu anajua kwamba kama sahani za kupaa ni silaha za siri za jeshi la Marekani, basi mataifa mengine mbali nasi hivi karibuni yatakuwa nazo, pia, iwapo tayari hayana. Ikiwa ndivyo, basi ni nini ambacho vimeundwa kufanya ila kuangamiza uhai, hata yumkini wa walio wateule, ikiwezekana? {WHR: 11.1}

Na kama kweli sahani zinazopaa ni za Bwana, basi ni nini kingine ambacho zimekuja kufanya ila kumwokoa kila mtu ambaye jina lake linapatikana limeandikwa katika Kitabu kile (Dan. 12:1), na kuwaua wale ambao huwadhulumu (Isaya 66:16)? Au ikiwa labda vya Mbinguni havijakuja, bado hakuna kitu kilicho hakika kwamba siku yaharakisha upesi vitakapokuja. La kwanza na muhimu kwa kila mmoja, hata hivyo, ni kujua kwa hakika kwamba jina lake limeandikwa katika kile Kitabu. Ili kuwa na uthibitisho huu mkubwa zaidi, mtu lazima ajue kwanza ni nini kitakacholiondoa jina lake katika Kitabu, na ni nini kitakacholihifadhi humo. {WHR: 11.2}

Mojawapo wa mambo mengi ambayo yataliondoa jina la mtu katika Kitabu cha Mungu, ni mmoja kugeuza sikio lililokufa kwa onyo la Bwana kwamba yeye anayeweka mkono wake kwenye jembe, kisha aangalie nyuma (anayeanza kazi ya injili, kisha arudi nyuma) hafai ‘’kwa Ufalme.” Luka 9:62. Ukweli ni kwamba wote ambao wamehitimu kutoka vyuo vya wajumbe tayari wameweka mikono yao kwenye jembe. Je! Sasa watageuka nyuma? Kwa kumcha Mungu hatutarajii hilo. {WHR: 11.3}

12

Kwetu sisi (Waadventista wa Sabato) haswa, maana ya yale tunayoyaona kutuzunguka yanapaswa kuwa wazi kabisa, yakionyesha dhahiri kwamba wakati umefika kwa kila mshirika wa kanisa kujituma kuutangaza Ujumbe wa Malaika Watatu. Zaidi ya hayo, zipo nafasi maelfu za wachungaji sasa zinazosubiri kujazwa na waliohitimu na wote wanaotarajia kuhitimu wa vyuo vikuu vya ukasisi vya Waadventista wa Sabato. Kwa hivyo asikuwepo yeyote mwenye wasifu huo apatikane tena amesimama pasipo kufanya kazi au akijihusisha na kazi za kidunia ilhali kazi ya Bwana inadhoofika na kukawia. {WHR: 12.1}

Kwa saa hii mamilioni bila tumaini wanasusurika na kupooza, wakiangamia katika nyanda za dhambi, na kwenye viwanja vya vita, kwa sababu hakuna mtu aliyewaongoa kwa Kristo na Injili ya milele. Nani atakayekwenda kwa ajili yao? Ni nani aliye na maono, moyo, na nia ya kwenda kuwaokoa wanadamu kwa ajili ya Kristo? Kwa wote waliohitimu chuoni, wahitimu wa sta-shahada, na watendakazi wa Biblia walio na uwezo na nia ya kujiandaa wenyewe kwa ajili ya kazi, fursa ya huduma na raslimali za kuwastahi na usafiri ziko tayari na zinangoja. Kwa hivyo hakuna sababu za “tafadhali nisamehe.” Luka 14:18. Mwito wa Uvuvio, “Ondoka uangaze,” ni kwa kila nafsi. Je, hamwezi kuitika, Wandugu? Je, hamtajiombea kwa bidii na kwa ajili ya watenda kazi wengine kusaidia kuikusanya ndani nafaka ya dhahabu yenye thamani? Au mtashindwa katika jukumu hili la kutosamehewa, na kukataa upendeleo huu wa upeo wa juu zaidi? {WHR: 12.2}

Swala hilo ni la uvutano mkubwa zaidi. Kristo alijua mbeleni; lingekuwa, na kwa fikira kuu Yeye alilionyesha katika funzo alilolitia taji la mfano Wake wa shamba la mizabibu. Sasa wakati umeifikia saa ya mwisho ya mfano, Ameuwasha huo mfano kwa nuru. Ili kuendelea hatua kwa hatua jinsi Ukweli Wenyewe ulivyo,

13

hebu tuangalie kwa undani zaidi katika mfano huu sasa wakati nuru ya Mungu inaangaza juu yake: {WHR: 12.3}

“Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu; na chochote kilicho sawa, ndicho mtakachopokea.” Mat. 20:1-7. {WHR: 13.1}

Tunawezaje kujua kwa uhakika ni saa ipi ambayo sisi tunajipata ndani, na iwapo mwito wetu wa kuhudumu umekuja? Tunaweza kujua tu kwa kuthibitisha wakati ambapo saa ya mwisho ya mfano unakoma. Na ili kufanya hili tunapaswa kwanza kutia alama kwa wakati wa mwito wa kwanza kwa watumwa, kisha wakati wa kila mwito mfululizo, kuhitimisha na wa mwisho. Kwanza, hata hivyo, kwa mujibu wa umbali huu, lazima tulete kwa mtazamo vipengee muhimu vya mfano: {WHR: 13.2}

(1) “Mwenye nyumba,” jinsi kila mwanafunzi wa Biblia anavyojua, ni Bwana Mwenyewe. (2) Watumwa ni watumishi Wake. (3) Dinari ni malipo yao. (4) Shamba lake la Mizabibu ni mahali ambapo wanapaswa kufanya kazi. (5) Siku ni ya mfano — inawakilisha kipindi cha wakati ambacho kinaangazwa kwa nuru fulani kubwa. (6) Muda wa kazi umetanguliwa mbele na kufuatwa nyuma na usiku

14

— vinginevyo hakungekuwapo “maawio” na “machweo” sehemu za siku. (7) Mwenye nyumba huajiri watumwa kwa nyakati tano tofauti. (8) Vipo vipindi vinne vya muda wa masaa matatu. (9) Miongoni mwa vipindi vitatu vya kwanza, kundi moja tu linaajiriwa. (10) Katika kipindi cha nne na cha mwisho cha masaa matatu, makundi mawili yanaajiriwa. (11) Mapatano ya dinari kwa siku yamefanywa tu na kundi la kwanza. (12) Makundi mengine yatapokea “chochote kilicho sawa.” (13) Mwisho wa siku wote wanapewa malipo sawa — dinari, hata ingawa la mwisho lilifanya kazi saa moja tu. (14) Wa kwanza walilipwa mwisho; wa mwisho, kwanza. {WHR: 13.3}

Sasa ili kuijua saa ambayo tunaambiwa, “Enendeni nanyi,” tunapaswa hapa mwanzoni mwa uchunguzi huu wa somo la kwenda kazini, kuamua ni wapi katika wakati ambapo mfano unaanzia na kufikia kilele. Ili kupata maarifa haya muhimu ni kuzingatia tu kweli zinazopaza sauti zikifuatana kwamba usiku wa mfano uliotangulia kutwa ya mfano lazima uwe kipindi kabla ya “Nuru ya ulimwengu,” Biblia, kuchimbuka — kabla ya nuru ya Maandiko, Neno la Mungu lililoandikwa, kuanza kuangaza hadi ndani ya mioyo ya wanadamu. Kwa maana huko nyuma, ni lazima ikumbukwe, mapenzi ya Mungu yalipitishwa, si kwa Biblia, bali kwa masimulizi kutoka kwa baba hadi kwa mwana, jinsi nuru ya jua usiku hupelekwa kwa dunia kupitia kwa mwezi, badala ya moja kwa moja na jua lenyewe. Kwa sababu hii imekuja kuonekana kwamba ulikuwa wakati wa desturi ya neno lililonenwa kwa mdomo badala ya kuandikwa. {WHR: 14.1}

Lakini kutwa ya kazi inawakilisha kipindi ambapo “Nuru ya ulimwengu,” Biblia Yenyewe, huangaza njia ya mwanadamu. Hivyo ni kwamba katika mfano Wake, Mwalimu, Bwana wa shamba la mizabibu, hutambua Agano la Kale na Jipya kama Siku ya pekee ya wakati wote wa kipindi cha neema, ambamo Yeye huenda sokoni

15

mara tano mfululizo kuajiri watumwa kufanya kazi katika shamba Lake la mizabibu. {WHR: 14.2}

Hatimaye, usiku unaofuata kutwa unaweza tu kuwakilisha kipindi baada ya kazi ya injili kufika mwisho, baada ya rehema kwa wokovu wa mwanadamu kufungwa. Wakati huo, jinsi “Nuru ya ulimwengu” (Neno la Mungu) linazama mbele ya upeo wa kutwa, giza linaifunika “dunia, na giza kuu watu.” Isa. 60:2. Ni wakati ambao unapata hatma ya kila mwanadamu imeamliwa milele. Kisha unafuata mkataa wa mwisho wa Bwana usiotanguka: {WHR: 15.1}

“Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Ufu. 22:11. {WHR: 15.2}

Ndio wakati ambapo “watu watakimbia huko na huko kulitafuta Neno la Bwana, wala hawatalipata” (Amosi 8:12); wakati ambapo wasiojali mwito wa Bwana, na wadhambi sugu kutambua na kulia kwa wazimu na uchungu wa kukata tamaa: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka”! Yer. 8:20. {WHR: 15.3}

Ukweli ni wazi sasa kwamba mfano huo huugawanya wakati wa wokovu katika sehemu mbili sawa za masaa kumi na mbili kila moja — kipindi cha kabla ya Biblia (usiku), na wakati wa Biblia (kutwa). Kutilia nguvu zaidi kwa ukweli kwamba mfano huo hugawanya wakati, Yesu anatangaza: {WHR: 15.4}

“Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.” Yoh. 11:9. {WHR: 15.5}

16

Kuendelea sasa, tunakuja kwenye hatua nyingine ya umuhimu maalum: makundi manne ya kwanza yaliajiriwa kwa muda mfululizo wa hatua mtawalia za masaa matatu matatu ya mfano; Ilhali la tano, kundi la mwisho, lililoajiriwa saa ya kumi na moja, lilikuja masaa mawili tu, badala ya matatu, baada ya kundi la nne, na hivyo saa moja tu ya mfano kabla ya mwisho wa kutwa — muda mfupi kabla muda wa rehema kufunga. {WHR: 16.1}

Kipindi hiki cha masaa mawili, kutoka saa ya tisa hadi saa ya kumi na moja, ni umoja unaokuja kama ubaguzi wa kipekee kwa muundo stadi wa vipindi vinavyofuatana vyenye safu za masaa matatu kati ya mwito. Inaonekana wazi kwamba mwito wa mwisho unakuja bila kutarajiwa na kwa kushangaza ndani ya kipindi cha kundi la saa ya tisa. Kwa hivyo yapo masaa mawili tu ya mfululizo kwa kundi kimoja, na saa moja tu ya mfano kwa kundi lile lingine. {WHR: 16.2}

Kuamua utambulisho wa watendakazi wanaohusika katika kila mojawapo ya wito tofauti mara tano, tunatakiwa kuanza jitihada zetu na WATUMWA WA MWITO WA KWANZA: {WHR: 16.3}

Tumeona tayari kwamba ni Biblia, “Nuru ya ulimwengu,” ambayo hufanya kutwa ya mfano. Sisi sote tunajua, kwamba, Biblia iliwasili na vuguvugu la Kutoka na tangu ilipowasili, Bwana hakujadiliana, kwa mfano na watu wengine, na kwamba ni wao pekee ambao Yeye aliwakabidhi daima maagano ya sherehe na tuzo na ahadi zake zote. Kwa hivyo, bila shaka, kundi la kwanza la mfano, wale ambao walikwenda kufanya kazi “mapema asubuhi,” wakati ilipokuwa ikichomoza nuru ya kiroho, Biblia, na ambao mapatano yalifanywa nao kupata dinari kwa kutwa, walikuwa Waisraeli wa kale walipokuwa wakitoka Misri, wakati uliokuwa

17

mapema asubuhi katika kutwa ya mfano. Katika uiano Roho ya Unabii ainatangaza: {WHR: 16.4}

“Wayahudi walikuwa wa kwanza kuitwa katika shamba la mizabibu la Bwana….” — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 400. {WHR: 17.1}

Wakati huo wa mwanzo, Mungu alipoanza kuyaandika Maandiko (kama Nuru inayoangaza mioyoni mwa watu kuanza kuchomoza), “Yeye…Analikumbuka agano Lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. Agano alilofanya na Abrahamu, Na uapo Wake kwa Isaka. Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele.” Zab. 105:8-10. {WHR: 17.2}

Kuwa hivyo kwa mwito wa kwanza wa watumwa kwa uthabiti kunaweka imara wakati ambapo wito wa kwenda kazini ulianza, sasa tunapaswa kuhaki wakati wa kuitwa kazini kwa WATUMWA WA MWITO WA PILI: {WHR: 17.3}

Kundi la pili, wale waliotumwa saa ya tatu ya mfano, lazima bila kuepuka wawe ni wale walioitwa kwenye kazi ijayo. Nao walikuwa, kwa kweli, Wakristo wa kwanza. Muhimu, pia, Bwana alisulubiwa saa ya tatu mchana (Marko 15:25), na pia Pentekoste alikuja saa ya tatu mchana (Matendo 2:15). {WHR: 17.4}

Hatua nyingine ya umuhimu ambayo tunapaswa kuzingatia ni ukweli kwamba jumbe zilizotangazwa na makundi haya mawili la kwanza, Waisraeli wa kale na Wakristo wa kwanza, hazikuwa za asili ya matengenezo; hazikuwa kweli za kale, zilizokuwa zimesahaulika katika mchakato wa uhuisho na matengenezo; ila kila mmoja ulikuwa ufunuo mpya, “chakula kwa wakati wake” — Ukweli wa sasa mwafaka kikamilifu ili kukidhi mahitaji ya watu katika nyakati zao. Kundi la awali

18

lilivuviwa na kuagizwa kufunza na kutekeleza kweli za wokovu jinsi zilivyokuwa katika mfumo wa sherehe, kundi la mwisho lilivuviwa na kuagizwa kufunza na kutekeleza kweli zilizopo zisizoweza kubadilika katika nuru iliyostawi zaidi – iliyostawi kutoka kwa kawaida za mfano hadi uakisi, kutoka kwa huduma katika hekalu la duniani hadi huduma katika lile la mbinguni; yaani, kutoka kwa dhabihu ya mwana-kondoo wa kundi hadi dhabihu ya Kristo Mwenyewe, Mwana-Kondoo wa Mungu. Hivyo kundi la mwisho lilifundisha ukweli wa zamani katika nuru mpya na ya asili, katika nuru ya Injili — kwamba Kristo alisulubishwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi, akafufuka kwa ushindi kwa dhambi na kifo, na akapaa kufanya upatanisho kwa ajili ya mdhambi anayetubu, si katika hekalu la duniani, bali katika hekalu la mbinguni. {WHR: 17.5}

Kwa sababu jumbe za makundi mawili ya kwanza (mmoja uliopelekwa na Vuguvugu la Kutoka, na mwingine uliopelekwa na Wakristo) zilikuwa kila mmoja katika nyakati zao maalum mpya kutoka kwa utukufu, ukweli huo kwa busara hujisimamisha wenyewe kama kirejelewa na mfumo Mtakatifu kwa jumbe zote za mfano huo. Vivyo hivyo, kila moja ya makundi matatu yaliyosalia lazima vile vile yakabidhiwe ujumbe wa ufunuo mpya na wa aina yake, wa “chakula kwa wakati wake” — ukweli mwafaka haswa na mkamilifu kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu wakati ule uliopo. Kwa hivyo tunahitaji tu kutafuta kwa hatua katika historia ya kanisa chuo kinapokunjua, hadi tutakapoufikia ukweli wa awali na mpya uliotangazwa baada ya ujumbe wa ujio wa kwanza wa Kristo. Ni lazima uonyeshe WATUMWA WA MWITO WA TATU: {WHR: 18.1}

Matengenezo ya Uprotestanti, yakiwa tu jitihada safi za kurejesha kweli za zamani, zilizokuwa zimekanyagiwa chini, na si kufunua mpya, zilizoendelea, hayakuwa na ujumbe mpya wayo yenyewe –

19

hakuna wowote ambao haukuwa umefundishwa katika nyakati zilizopita. Kwa hivyo inafuata kwamba kundi la tatu na ujumbe lazima litafutwe katika miaka inayofuata Matengenezo. {WHR: 18.2}

Ufunuo tu wa ukweli mpya wa kinabii, baada ya Matengenezo, ni tangazo la mwaka ambapo ilianza kazi ya kupatakasa patakatifu, kimsingi kwa ajili ya waliokufa (kwa mujibu wa Danieli 8:14, lakini wakati huo hawakuuelewa kikamilifu). Kwa sababu matangazo yake yalifanywa na Waadventista wa Siku ya Kwanza, lazima inafuata kwamba walikuwa kundi la tatu la watumwa wenye ujumbe mpya na tofauti. Na kama inavyojulikana, walianza kuutangaza katika mwaka 1833, wakitangaza kwamba kutakaswa kwa patakatifu kungeanza mwaka 1844. Hivyo mwaka wa 1833 kidude cha saa ya mfano iligonga saa ya sita. {WHR: 19.1}

Taarifa, “Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile,” akizungumzia kuhusu huo wito maradufu, si mmoja mmoja, kama ilivyo katika wito maradufu uliotangulia, lakini kwa pamoja, inaonyesha kwamba ujumbe na watumwa wa “saa ya sita” walipaswa kufungamana kwa karibu na kushirikishwa na ujumbe na WATUMWA WA MWITO WA NNE: {WHR: 19.2}

Hivyo ilikuwa kwamba kundi la saa ya sita na ujumbe, la Waadventista wa siku ya Kwanza, na kundi la saa ya tisa na ujumbe, lile la Waadventista wa Sabato, yalifungamana kuwa moja kwa sababu ujumbe wa lililotangulia ndani yake ulibuniwa na Mungu ili kuuleta ujumbe wa lililofuata kwa nuru. Isitoshe, mara tu mwisho wa “siku 2300” (Danieli 8:14) za kinabii zilifikiwa Oktoba 1844, pale pale Danieli 8:14; Danieli 7:9, 10; Danieli 12:10-12, pamoja na Ufunuo 14:6,7 (Ujumbe wa malaika wa kwanza

20

katika awamu yake ya msingi), kwa mara ya kwanza ulitangazwa na Waadventista wa Sabato “wakasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja. Msujudieni Yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufu. 14: 7. {WHR: 19.3}

Kwa hivyo Waadventista wa Sabato mwaka wa 1844 walianza kutangaza kile walichokiita “hukumu ya upelelezi kwa wafu,” ambayo kwa istilahi ya Maandiko ni kutupwa nje wale ambao hawajajivika vazi la harusi (Mat. 22:11-13), kufungiwa nje wanawali watano wapumbavu (Mat. 25:10), utengo wa kondoo na mbuzi (Mat. 25:32, 33), kutenganisha “samaki” wabaya kutoka kati ya “samaki” wazuri (Mat. 13:48) — kila moja ya istilahi miongoni mwa wafu. Vile vile, walielewa barabara kuwa ni “siku ya upatanisho ya uakisi” — siku ambayo huondolewa kwenye Vitabu Mbinguni majina ya wale ambao kwa kufunga kazi ya maisha yao walishindwa kupata ustahiki wa kuwa katika ufufuo wa kwanza, ufufuo wa watakatifu (Ufu. 20:5, 6), vipengele hivi vyote vinaeleweka kwa maneno: “Ndipo Patakatifu patakapotakaswa.” Dan. 8:14. {WHR: 20.1}

Kwa sababu kutakaswa kwa Patakatifu kwa niaba ya wafu lazima ni shughuli safi ya kitabu, ndio sababu inafanyika tu katika Hekalu la Mbinguni. Kwa hivyo, majina ya wasiostahiki “ufufuo wa kwanza” yanaondolewa kati ya majina ya wale wanaostahiki. Ya kwamba vitabu vya Mbinguni hushughulikia mambo yote ya maisha ni dhahiri kutoka kwa Zab. 56:8; 69:28; 139:16; Dan. 12:1; Mal. 3:16; Fil. 4: 3; Ufu. 3:5, n.k. Kwa hivyo, unabii unaonyesha kwamba wakati “hukumu ilipoanza, … vitabu vilifunguliwa.” Dan. 7:10. {WHR: 20.2}

21

Kwa sababu ujumbe wa saa ya hukumu ni wa tabia na umuhimu wa kipekee katika historia yote ya kanisa; vile vile ukiwa ni ujumbe pekee wa unabii kusikika ukiufuata ujumbe wa saa ya sita; hakuna kitu kinachoweza kuwa wazi zaidi ya kwamba jinsi ulivyojitokeza mwaka wa 1844 kwa mara ya kwanza, saa ya mfano ya Mungu ikagonga tisa. {WHR: 21.1}

Vivyo hivyo kundi la saa ya tisa katika mfano huo haliwezi kuwa jingine isipokuwa Waadventista wa Sabato, ambao walikuwa kiguu na njia kutangaza kwamba “hukumu imeanza, na vitabu vimefunuliwa” (Dan 7:10), na ya kwamba mtu yeyote ambaye, wakati wa Siku ya Upatanisho ya uakisi kwa wafu, apatikane miongoni mwao pasipo kutubu dhambi zake (pasipo kuitesa nafsi yake, na bila kujivika vazi la harusi) “atakataliwa mbali kutoka kati ya watu wake.” Mat. 22:11-13; Law. 23:29. Kwa ufupi, ujumbe huo ulitangaza kwamba utengo katika kutaniko la wafu ulikuwa umeanza. {WHR: 21.2}

Sasa kwa mara ya kwanza mfano huu umeng’aa kwa nuru isipokuwa tu jicho ambalo kwa kukosa tumaini limeingia katika kifungo cha giza laweza kushindwa kuona wazi kwamba ujumbe ambao sisi Waadventista wa Sabato tulipewa mwaka wa 1844, saa ya tisa, si ujumbe wa saa ya kumi na moja, si ujumbe wa hukumu kwa walio hai, ila tu hukumu kwa wafu. {WHR: 21.3}

Kama watumwa wanaotarajiwa wa Mungu, kila mmoja hapa, katika kitovu hiki cha mfano, tulia kwa muda kaza moyoni kwa makini somo lake lote muhimu jinsi linavyoletwa katika onyesho linalofuata: {WHR: 21.4}

22

Hatua inayofuata ya maamuzi ni kwamba hukumu kwa wafu ilipaswa kutangazwa kwa “watu wengi, na mataifa, na lugha, na wafalme.” Ufu. 10:11. Tia alama neno “wengi.” Kamwe halimaanishi “wote,” na kamwe halimaanishi “kila.” Kwa sababu aya hii ya maandiko hutabiri upanuzi wa kundi la saa ya tisa na ujumbe, itamjazi sana

23

kila mmoja kwa uangalifu kuchunguza lile Ufunuo 10:11 husema kwa jambo hilo. Usithubutu kuongeza kwa Neno wala kuondoa Kwalo. Kisha ulilinganishe na maandiko yanayofuata, yanayotabiri upanuzi wa kundi la saa ya kumi na moja na ujumbe, na utakuwa na ukweli wote kurejelea kwa kukamilisha kazi. {WHR: 22.1}

Sasa ya kwamba wakati umekuja Bwana kuwajiri watumwa Wake wa saa ya kumi na moja, mfano huu wa thamani kubwa umefunuliwa, na kwa mara ya kwanza inaonekana wazi kwamba wakati hukumu kwa wafu ilipaswa kutangazwa kwa mataifa na watu wengi, hukumu kwa walio hai lazima itatangazwa kwa mataifa yote na kwa watu wote duniani. Hapa Uvuvio Wenyewe unasema: {WHR: 23.1}

“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja. Msujudieni Yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufu. 14:6, 7. {WHR: 23.2}

Ya kwamba watumwa wa mwito wa saa kumi na moja — wale ambao “wameokoka,” wale ambao “hawajakataliwa mbali” (Law. 23:29) wakati “nyumba ya Mungu” inahukumiwa (1 Pet. 4:17), tukio ambalo linaashiria mwanzo wa hukumu kwa walio hai, kote duniani — watatumwa kwa mataifa yote, Uvuvio unathibitisha kupitia nabii Isaya: {WHR: 23.3}

“Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

24

Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi…. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:15, 16, 19, 20. {WHR: 23.4}

Kwa maneno haya ya kicho Bwana anaonya kwamba mchinjo (Pasaka ya uakisi — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 505, 211, Shuhuda, Gombo la 1 uk. uk 190, 198) utafanyika kati ya walio katika nyumba ya Mungu, kanisa, kwa maana watakaookoka watatumwa kwa watu ambao hawajawahi kusikia sifa ya Mungu na Utukufu Wake. Ni dhahiri kwamba malaika wanaofanya mauaji hayo watawaondoa wasio waaminifu kanisani — wale ambao wanaonyeshwa kwa mfano mmoja kama “samaki” na katika mfano mwingine kama “wageni” ambao hawakujivika “vazi la harusi.” {WHR: 24.1}

25

Hapa, hebu kila msomaji anayechukua mambo kwa uzito atulie kutafakari lile Uvuvio husema: Isa. 66:19 na 20 hufafanua kwamba wale ambao wanaokoka mchinjo wa Isa. 66:15 na 16, watatumwa kama wamishonari kwa Mataifa, ambao hawamjui Mungu. Kwa hivyo hawa waliookoka (waliosalia) ni masalia wa Mungu, malimbuko Wake, watumwa Wake wasio na uongo, watu 144,000 — wateule. Na ni wao tu, si wengine, Maandiko yanatangaza, watawaleta ndugu zao wote kutoka mataifa yote, katika chombo safi, hadi ndani ya nyumba iliyotakaswa ya Bwana — Nyumba Yake Nyeupe. Zaidi ya hayo, hakuna akili inayofikiria vyema inaweza hata kuanza kuwaza uwezekano kwamba pamoja na chombo chochote kisicho kitakatifu na chenye mapungufu ya kutisha kuliko kama huu ukasisi wenye nguvu — uliookoka kutoka kwa dhambi, na wadhambi, na hukumu — Anaweza na ataweza Bwana wakati wowote “kumaliza kazi, na kuikata katika haki” (Rum. 9:28), na hivyo kuwaokoa watu Wake kutoka kwenye tufani kali ambayo sasa inakaribia kuanguka juu ya dunia na kusambaa kwa urefu na upana wake. {WHR: 24.2}

Shetani kwa huzuni analijua jambo hili. Anajua wakati wake ni mfupi na unakuwa mfupi kwa hofu. Anajua kwamba ukasisi huu mwaminifu kitambo kidogo utafunuliwa uonekane, na kupambana dhidi yake. Anajua huo utakuwa mwisho wa kushindwa kwake kabisa. Hivyo juhudi zake za upeo sasa kuwaangamiza. Hata hivyo mwishowe, akijua kwamba hawezi kufanya hivyo, lengo lake litakalofuata litakuwa ni kuleta wakati wa taabu mfano wake haujawahi kuwapo (Dan. 12:1), kwa tumaini la kuwaangamiza wote. {WHR: 25.1}

Ilikuwa mbinu kama hiyo ya mauaji ya halaiki ambayo alitumia katika siku za Farao, kwa kuwazamisha watoto wa kiume Waebrania (Kut. 1:22), kwa matumaini ya kumwangamiza Musa, na tena katika siku za Herode, kuwaua kikatili watoto wote wachanga “kuanzia miaka miwili kurudi chini” (Mat. 2:16), kwa matumaini ya kumwangamiza Kristo. Lakini jinsi Mungu alivyowahifadhi walio Wake wakati huo, vivyo hivyo atawalinda walio Wake leo: Mikaeli, Mkuu na Mkombozi, atasimama (Dan. 12:1) kwa

26

ajili ya wote wanaosimama kwa ajili Yake, na ambao vile vile majina yao yamehifadhiwa katika Kitabu cha Uzima, na kwa utukufu atawaokoa. Maswala haya mawili ya pambano — Lengo la Shetani kuwangamiza wateule wa Mungu na lengo la Mikaeli kuwaokoa — laleta “Siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” {WHR: 25.2}

Ingawa nuru mpya iliyofunuliwa ya Ukweli ambayo sasa inaangaza kwenye mada ni mpya kwetu sote, si kwa kweli, mpya katika Biblia. Kutuweka macho na chonjo kwa Ukweli unaokunjua kwa uendelevu, Roho wa Mungu kwa miaka mingi alitoa ishara kwa umakini wetu katika taarifa zifuatazo {WHR: 26.1}

“Uwezekano wa maajabu u wazi kwa wale wanaozingatia uhakikisho wa Mungu wa neno Lake. Zipo kweli za utukufu zitakazokuja mbele ya watu wa Mungu. Mapendeleo na majukumu ambayo hata hawadhani yapo katika Biblia yatatandazwa wazi mbele yao. Wanapoendelea kuifuata njia ya utiifu wa unyenyekevu, wakiyatenda mapenzi Yake, watajua zaidi na zaidi maneno ya Mungu.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 322. {WHR: 26.2}

“Sisi hunena kuhusu ujumbe wa malaika wa kwanza na wa malaika wa pili, na hufikiri tunao ufahamu fulani wa ujumbe wa malaika wa tatu. Lakini tukiendelea kuridhika kwa maarifa finyu, tutakoseshwa kupata mitazamo wazi zaidi ya ukweli. ” — Watenda Kazi wa Injili, uk. 251. {WHR: 26.3}

“Bado upo ukweli wa thamani sana ambao utafunuliwa kwa watu katika wakati huu wa hatari na giza, lakini ni kusudi la Shetani aliloazimia kuzuia nuru ya ukweli kuangaza ndani ya mioyo ya wanadamu. Iwapo tungetaka kuwa na nuru ambayo imeandaliwa kwa ajili yetu, tunapaswa kuonyesha tumaini letu kwa ajili yake kwa kulichunguza kwa bidii neno la Mungu. Kweli za thamani ambazo zimekuwa hazijulikani kwa muda mrefu zitafunuliwa kwa nuru ambayo itadhihirisha thamani yake takatifu; kwa maana Mungu atalitukuza neno lake, kwamba liweze kuonekana katika nuru ambayo hatujawahi kuiona hapo awali.” — Shuhuda Kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 62; Mashauri Kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 25. {WHR: 26.4}

“…Kamwe tusitarajie kwamba wakati Bwana anayo nuru kwa watu Wake, Shetani atasimama kwa utulivu karibu, na kutofanya jitihada za kuwazuia kuipokea. Atafanya kazi kwa akili ili kuchochea wivu na kutokuamini. Tujihadhari kwamba tusije tukaikataa nuru ambayo Mungu hutuma, kwa sababu haiji katika njia ya kutupendeza. Tusiache baraka ya Mungu iondolewe kutoka kwetu kwa sababu hatuujui wakati wa kujiliwa kwetu. Iwapo wapo wale wasioiona na kuipokea nuru wenyewe, wasisimame kwenye njia ya wengine. Isinenwe kwa watu hawa waliopendelewa sana, kama vile ilivyonenwa kwa Wayahudi wakati habari njema ya ufalme ilipohubiriwa kwao, ‘Hawakuingia ndani wenyewe, na wale waliokuwa wakiingia waliwazuia.'” — Shuhuda, Gombo la. 5, uk. 728. {WHR: 27.1}

27

Unabii, twajua sote, ni taa ya Mbinguni kwa miguu yetu. Ikiwa tunashindwa kufumbua macho na kufungua mioyo yetu kwa wakati ambao Bwana angetaka tufaidike Chuo kinapoendelea kukunjua, basi tutawezaje kuepuka kuwa kama kipofu anayemwongoza kipofu? {WHR: 27.2}

Wandugu, kwa ajili ya nafsi zenu, msipitie kijuu-juu kwa swala hili la uzima na kifo, maana, jinsi ambavyo mmeona, nuru inayoangaza kwa mada hiyo humulika ukweli kwamba baada ya kundi la saa ya tisa na ujumbe, kwanza ingekuja nyongeza kwa huo ujumbe, kisha watumwa waliotiwa muhuri — ujumbe wote muhimu wa hukumu kwa walio hai, na watumwa wote wenye nguvu, “waliookoka”, ambao watakwenda kwa “mataifa yote,” badala ya kwa “mengi” tu. Hakikisho la awali kwamba ingekuwepo nyongeza kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu, lilitujia zamani sana katika maneno yafuatayo: {WHR: 27.3}

“Naliona malaika wakiharakisha wakiingia na kutoka mbinguni, wakishuka

28

duniani, na tena wakipaa mbinguni, wakifanya tayari kutimizwa kwa tukio lingine muhimu. Kisha nikamuona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake…. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao kama vile kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga na ujumbe wa malaika wa pili mwaka wa 1844.” — Maandishi ya Awali, uk. 277. {WHR: 27.4}

Wazi kabisa, ni watumwa wa saa ya kumi na moja, na ujumbe wa ziada, ujumbe wa hukumu kwa walio hai, watakaowaokoa watu wa Mungu kutoka Babeli. Hakika kamwe haitawezekana mpaka Kanisa lenyewe limewekwa huru dhidi ya wanafiki na machukizo, na hivyo kuwekwa safi na nyeupe, Mungu anaweza kimaadili kumimina Roho Wake katika nguvu ya pentekoste juu ya watu Wake, na kuvumisha kilio: “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4. {WHR: 28.1}

Kumbuka kwamba Sauti ambayo inawaita watu wa Mungu kutoka Babeli, huonyesha wazi kwamba hakuna dhambi mahali ambapo Sauti hiyo inawaitia. Isitoshe, haingekuwepo haki kuwaita watoke Babeli, ili kuwaokoa kutoka kwa mapigo ambayo yatampata kwa sababu ya dhambi zake, iwapo wale walioitwa wangepaswa kuletwa mahali pengine penye dhambi. {WHR: 28.2}

Mshahara wa dhambi hauwezi kuwa wa uharibifu mdogo katika sehemu moja ya dhambi kuliko nyingine. {WHR: 28.3}

Kutoka kwa maandiko haya yanayokunjua sasa inaonekana wazi pia, kwamba ujumbe wa hukumu kwa walio hai ni toleo la mwisho la Mbingu la habari njema kwa watakatifu, na la habari za kusikitisha kwa wadhambi. Kwa hivyo utangazwa na watumwa wasiokuwa na uongo, watu 144,000 — WATUMWA WA SAA YA KUMI NA MOJA: {WHR: 28.4}

29

Kufikia hapa, ukweli unasimama wazi kwamba mwito huu wa mwisho unakuja saa ya mwisho ya siku ya mfano, kabla tu kazi ya injili kufunga. Ukiwa ni ujumbe wa mwisho wa rehema kwa dunia, na pia mwito wa mwisho kwa watumwa, basi lazima utangazwe na nabii Eliya, naye atakayeonekana tu kabla ya “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” Mal. 4:5; Mat. 17:11. Vivyo hiyo, watumwa wa saa ya kumi na moja lazima waitwe kazini naye anapoitangaza siku ya Bwana, siku ambayo Bwana anachukua pepeto mkononi Mwake (Mat. 3:12; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80; Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 373), na kuusafishauwanda Wake” — kuyapeperusha makapi na kuyachoma magugu. Mara tu anapoiweka ngano katika “ghala” Lake (Mat. 13:30), ndani ya kanisa Lake la Ufalme, linadumu bila magugu, na hivyo “kanisa tukufu, lisilo na waa, kunyanzi, au kitu kingine chochote; … takatifu lisilo na mawaa.” Efe. 5:27. Nyumba Nyeupe ya Mungu kweli kweli! (TazamaIsa. 52: 1, Yoeli 3:17, na Nah. 1:15). {WHR: 29.1}

Katika istlahi zingine za ki-mfano, “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana” ni Yake kuwatupa nje “samaki” wabaya na kuweka “wazuri ndani ya vyombo.” Mat. 13:47, 48. Ni siku ambayo Yeye anaweka “kondoo mkono Wake wa kuume, lakini mbuzi mkono wa kushoto.” Mat. 25:33. Ni siku ya hukumu kwa walio hai, kutakaswa kwa hekalu hapa duniani — kazi ambayo hulitakasa kanisa na kulifanya kuwa “jeupe” (Dan. 12:10, Mal. 3:1-3). {WHR: 29.2}

Kweli, sisi Waadventista wa Sabato, hapo awali hatukuvijua na hatukuvifundisha vipengele hivi vya ziada vya Hukumu, lakini tu kwa sababu Ukweli daima ni wa wakati mwafaka, daima ukikunjua muda unaposonga. Kwa hivyo ni kwamba maarifa yetu ya awamu moja ya ujumbe inafuatwa na Mungu kuifichua awamu ya ufunuo Wake mwingine. Furaha na matarajio yalioje, basi,

30

tunapaswa kuwa wa kushika kasi pamoja na gombo linapokunjua, tukienenda na wakati. Na tunapaswa kuwa wenye furaha ilioje kujua kwamba Mungu hajatuacha, bali “amelijilia kundi Lake la nyumba ya Yuda, na kuwafanya kama farasi Wake mzuri vitani.” Zek. 10:3. {WHR: 29.3}

Sasa kwamba Wakati na Ukweli umeshikana na unaambatana pamoja, lazima upesi tushikilie na kufuata, pia. Hatuwezi kumudu kuyarudia makosa ya Wayahudi na makanisa ya jina tu, na hivyo kuachwa nyuma (Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28-30; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 728). Tusithubutu. Tusijaribu. {WHR: 30.1}

Istlahi hizi kagua, safisha, takasa, kataliwa, tupwa nje, hukumu, vuna, na tenga, nk., sasa zinaonekana kuwa ni visawe vya jumla, zote zaonyesha tukio moja — Bwana kulijia “Hekalu Lake” (kanisa) kuwatakasa watakatifu Wake walio hai. Kazi hii ameionyesha kwa njia mbalimbali: kwanza, kama kutenga magugu kutoka kati ya ngano (Mat. 13:30); ijayo kama kutenga samaki wabaya kutoka kati ya wazuri (Mat. 13:48); hatimaye, kama kutenga kondoo kutoka kati ya mbuzi (Mat. 25:32); tena, kama kuwatupa nje wale wanaoshindwa kuvaa vazi la harusi (Mat. 22:12, 13); na mwisho, kama kutupwa kutoka katika chumba cha wageni (kanisa) wale ambao wanashindwa kuzidisha talanta walizopewa (Mat. 25:28-30). Kazi hii ya hukumu ilioonyeshwa mbali mbali (nembo inayodhibiti katika mifano ya Kristo ya Ufalme), Bwana anaifananisha na “moto wa atakasaye,” kwa “sabuni ya dobi,” na kwa “anayesafisha fedha.” Mal. 3:2, 3. {WHR: 30.2}

Kwa hivyo ni dhahiri kuonekana kwamba “mavuno” ya kiroho ni sawa na mavuno ya asili — yote hutenganisha nafaka zao kutoka kwa magugu na makapi, njema kutoka kwa mbaya. Katika maneno ya Danieli, ni “hukumu,” au

31

wakati ambapo “Patakatifu” patakapo “takaswa” (Danieli 8:14); katika maneno ya Mtume Petro, ni “hukumu….katika nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17); katiaka maneno ya Yohana wa Ufunuo, ni “saa ya hukumu Yake” (Ufu. 14: 7); na kwa maneno ya nabii Malaki, ni “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana” (Mal. 4:5): “Bwana…ghafla kulijia hekalu Lake” (kanisa Lake) ili kulitakasa kama kwa “moto,” kulisafisha kama “sabuni ya dobi,” na “kulitakasa…kama dhahabu na fedha” “wana wa Lawi” (Mal. 3:1-3) — makuhani wa Hekalu wakati wa saa ya kumi na moja. {WHR: 30.3}

Pamoja na zaidi ya wanadamu bilioni mbili waliokomaa na wanaokomaa katika shamba kubwa la mavuno, tunaweza kufikiria ukubwa wa mavuno. Bwana Mwenyewe anathibitisha: “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.” Mat. 9:37. Hata hivyo, hofu ya kuogofya zaidi ni matokeo yake kwa magugu na makapi, wakati utambuzi kwamba wamepotea ukipita juu yao, na kwa kitisho wanalia kwa sauti: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka!” Yer. 8:20. {WHR: 31.1}

Kwa hivyo kuongeza ushahidi kwa ushahidi, Maandiko kwa uzito yanaonyesha wazi mavuno kuwa hukumu kwa walio hai, Bwana kuikusanya “ngano,” walio Wake, kutoka kwa mataifa yote, na Yake kuyaharibu magugu na makapi. Kwa hivyo mavuno, hakika ni “mwisho wa dunia.” Ni wakati ambapo Bwana anaketi “katika kiti cha utukufu Wake; ” (Kanisa lililotakaswa — Mat. 25:31; Isa. 62:1-3; 66:18, 19). Ni Yake kutenganisha kondoo na mbuzi — kazi ambayo inaileta dunia hii ya dhambi mwisho. {WHR: 31.2}

Tusisahau, hata hivyo, kwamba yuko adui ambaye

32

ameamua kuwaweka watu wa Mungu katika giza, kwa kutoujua Ukweli mwafaka. (Tazama Shuhuda, Gombo la 5, uk. 709, 728). Na ni giza lililoje la uharibifu ambalo angetaka kuwaweka ndani yake isipokuwa kutolijua lile Mungu angetaka walijue wakati hukumu yao inangoja kuamuliwa, wakati ambapo wanapimwa kwenye mizani ya Hekalu? Hakuna, hakuna kabisa. {WHR: 31.3}

Ndiposa inatarajiwa kwamba sasa, zaidi ya hapo awali, sisi sote tunapaswa kukabiliwa na upinzani mkali. Wanaoitwa eti watu wakuu, wasio hata na cheche ya nuru Takatifu, watatenda, kama wazimu, kwa haraka kueneza machafuko kila mahali. Hili watalifanya kwa kuanzisha chuki, kwa kuzusha dhana zisizo na msingi, kwa kubuni na kueneza uongo, kwa kurusha dharau na kejeli, kwa kusambaza udaku na uvumi, na kwa kujihusisha katika uhaini wa kuharibu heshima ya mtu. Lakini hakuna lolote kati ya haya litaowaondoa wale ambao ngome yao ni Bwana, na wanaozingatia ushauri Wake, ambao hutii ushauri Wake wa thamani, azizi na wenye kicho katika vifungu vifuatavyo: {WHR: 32.1}

“…Msiwe wasioamini. Kadiri unavyopigwa kikumbo sana, unavyokosa kueleweka, ukinenewa vibaya, ukisingiziwa, ni ushahidi zaidi ulionao kwamba unamfanyia kazi Mwalimu, na kwa karibu zaidi unapaswa kushikamana na Mwokozi wako.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 130. {WHR: 32.2}

“Wote katika siku hiyo ya uovu wataweza kumtumikia Mungu kwa mujibu wa dhamiri zao, watahitaji ujasiri, uimara, na maarifa ya Mungu na neno Lake; maana wale ambao ni wa kweli kwa Mungu watateswa, nia zao zitalalamikiwa, jitihada zao bora zitapotoshwa, na majina yao kutupwa nje kama maovu.” — Watenda Kazi wa Injili, uk. 264. {WHR: 32.3}

“Hasira ya mwanadamu itakusifu Wewe,’ asema mtunga zaburi, ‘masalio ya hasira Utaizuia.’ Mungu humaanisha kwamba ukweli wa uchunguzi utaletwa mbele, na kuwa mada ya uchunguzi na majadiliano, hata kama ni kupitia dharau iliyowekwa juu yake. Mawazo ya watu lazima yachochewe. Kila pambano, kila shutuma, kila singizio, itakuwa ni njia ya Mungu ya kuchochea uchunguzi, na kuziamsha akili ambazo vinginevyo zingesinzia.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 453. {WHR: 33.1}

Kila kitu ambacho kinaweza kufanywa dhidi ya ujumbe wa Mungu wa leo kitafanywa na kisasi kikubwa kuliko kilivyodhihirishwa dhidi ya ujumbe wa Mbingu siku za ujio wa Kristo mara ya kwanza, kwa maana Ibilisi anajua kwamba ikiwa atapoteza sasa, atapoteza milele — kwamba yeye hawezi kupata nafasi nyingine. Usio na kifani, kwa hivyo, ni hima kila mshiriki wa kanisa la saa kumi na moja sasa kwa upesi na kidete ajikaze dhidi ya jitihada za Adui kutoa pigo la mtoano. Lazima tuwe chonjo, pia, kutambua kwamba hilo pigo kwa kushangaza litakuja kutoka kwa adui tusiowatuhumu — kutoka kwa wanaodai kuwa ni marafiki wa injili, ambao ni wacha Mungu zaidi kuliko walivyokuwa makuhani katika siku ya Kristo. Zaidi ya hayo ni kutarajia kwamba Adui atatumia kila chombo iwezekanavyo kumzuia Bwana asiwafunue waonekane Wake sasa wasiojulikana 144,000 watumwa malimbuko, ambao watakwenda kukusanya ndani mavuno ya pili (Ufu. 7:9). Yule Adui atajaribu kila kitu atakachofikiri kukanganya, na kuufunika Ukweli, hasa kwa mada ya watu 144,000. {WHR: 33.2}

33

Hawa 144,000 “watumwa wa Mungu,” wakiwa hatua ya kwanza ya mavuno, wanaitwa “malimbuko.” Na kwa sababu wote ni wa “kabila zote za wana wa Israeli” (Ufu. 7:4), wao kwa hivyo ni lazima wamevunwa kutoka katika Israeli mamboleo — Kanisa Lenyewe. Ilhali

34

umati mkubwa ambao hakuna mtu anayeweza kuuhesabu, wanakusanywa hatimaye kutoka katika “mataifa yote” (Ufu. 7:9) ambao juu yao yule kahaba, Babeli Mkuu, atakuwa anatawala. Kutawala kwake kunaonyeshwa kwa mfano wa kumwendesha (kumtawala) mnyama mwekundu sana — ishara ijayo na ya mwisho ya ulimwengu huu (Ufu. 17; 18:1-4). Hawa walioitwa kutoka bila shaka ni mavuno ya pili: kwa maana sheria ya kuhesabu ni kwamba ikiwapo ya kwanza, lazima ifuate ya pili. {WHR: 33.3}

Hivyo, kupitia kwa watumwa 144,000 malimbuko, ukasisi wa saa kumi na moja, Roho wa Mungu atasababisha Ujumbe wa Malaika Watatu kuumuka hadi Kilio Kikuu wakati wa mavuno, na “utaleta ndani miganda ya wema kutoka katika nyanda za dhambi” mataifa yote — umati mkubwa wa mavuno ya pili ambayo hayajaisikia habari ya Mungu wala kuuona utukufu Wake (Isa. 66:19, 20). Ni upendeleo bora ulioje, Wandugu! Je, haimpasi yeye ambaye angeudharau kwa chochote, astahili kufa fukara kwa bei duni? {WHR: 34.1}

Pamoja na ujumbe kamili wa hukumu katika saa ya kumi na moja, malaika watawatenga watu wa Mungu kutoka kwa watu wa dunia. Na kwa kwa shabaha hili, Uvuvio zamani sana ulitangaza: {WHR: 34.2}

“Kisha nalimwona malaika wa tatu. Akasema malaika aliyeandamana nami, ‘Ya kutisha ni kazi yake. Utume wake ni wa kuogofya. Yeye ndiye malaika atakayeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kufunga, ngano kwa ghala la mbinguni. Mambo haya yanapaswa kuyashughulisha mawazo yote, umakini wote.” — Maandishi ya Awali, uk. 118. {WHR: 34.3}

Ndiposa, wote wanaoitika mwito wa Roho sasa kwa saa hii ya mwisho watatambua sana kwamba

35

hawana muda wa kupoteza kwa kupata na kutumia na kuharibu nguvu zao; hakuna muda wa kupoteza kwa chochote. Lengo lao pekee ni kumaliza kazi waliyopewa na Yeye Ambaye huwaita, kwenda kufanya kazi katika shamba Lake la mizabibu. Wao watafahamu kikamilifu kwamba upo mji ulioandaliwa kwa ajili yao, mji ambao mjenzi na mtengenezaji ni Mungu, na ya kwamba kwa muda mfupi, ndani yake, wote wenye uhai watasisimka kwa vifijo vya ushindi: {WHR: 34.4}

“Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hata machweo yake. Tokea Zayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu amemulika. Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele Yake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu Wake. Nikusanyieni wacha Mungu Wangu Waliofanya agano Nami kwa dhabihu. Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu. Selah.” Zab. 50:1-6. {WHR: 35.1}

“Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima Wake mtakatifu. Kuinuka Kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Zayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. Mungu katika majumba Yake Amejijulisha kuwa ngome. Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia. Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi. Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele. Selah.” Zab. 48:1-8 {WHR: 35.2}

36

“Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu Lako. Kama lilivyo jina Lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa Yako hata miisho ya dunia. Mkono Wako wa kuume umejaa haki; Na ufurahi mlima Zayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu Zako. Tembeeni katika Zayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake, Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja. Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.” Zab. 48:1-14. {WHR: 36.1}

Kwa sababu wakati na injili viko kwa saa yao ya kikomo, na kazi hiyo ndiposa ni ya upeo wa juu sana, upanuzi, na umuhimu, lakiniya kwa muda mfupi sana, Mungu amemwongoza mwanadamu kubuni na kuunda zana na mitambo ya kila aina inayookoa muda, kurahisisha kazi na kuifanya kiajabu sana — maajabu ambayo yangetia kiwewe mawazo na kufukarisha wepesi wa kuamini vizazi vya zamani, licha ya kwamba karne nyingi zilizopita “Yeye Aliye juu, Aliyetukuka, akaaye milele”(Isa. 57:15), alitangaza: “Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.” Dan. 12:4. {WHR: 36.2}

Ukweli kwamba mfano huu wa Ufalme umesimama hivi wazi kabisa utazamwe sasa kwa mara ya kwanza tangu Kristo alipounena, ni ushahidi usiopingwa ndani yake kwamba mpigo wa saa ya kumi na moja karibu utasikika hata kwenye ncha nne za dira. Tukio hili litaashiria ukweli mkuu kwamba kundi Lake la watumwa la mwisho “limefunuliwa lionekane” kwa dunia yote. Kufunuliwa Kutukufu! {WHR: 36.3}

Ukweli huu unawapataje Walaodekia, la mwisho kwa “makanisa saba” ambamo upo mchanganyiko wa ngano

37

na magugu, kondoo na mbuzi, samaki wazuri na wabaya? Ole, katika mwelekeo wa kinaa, wakijidhani kwamba ni matajiri hawahitaji kitu, ilhali katika ukweli wa kusikitisha Bwana kwa mkazo hutangaza kwamba wao ni “wanyonge, wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi” — na wahitaj wa kila kitu: na hata sasa pasipo kujua hatma ya hatari ya umasikini wao (Ufu. 3:14-18). Wao hata ni fukara kwa maarifa ya kwamba hukumu ya walio hai, wala si ya wafu, ni ujumbe wa mwisho, na ya kwamba wale tu wanaosikiza mwito wa saa ya kumi na moja watasazwa katika utengo, na kujumuika kuwa kundi la watumwa la mwisho wakiwa na ujumbe wa mwisho. Vipi mpaka sasa sisi vipofu Walaodekia. Vipi alivyo sahihi Bwana kugundua ugonjwa. Hali mbaya ilioje. Hebu sisi sote bila kukawia, kwa hivyo, tujiulize kwa dhati swali zito: {WHR: 36.4}

Wakati hatimaye hukumu ikipita kutoka kwa wafu hadi kwa walio hai, hivyo kuhitimisha awamu ya kwanza ya Ujumbe wa Malaika wa Kwanza (hukumu ya wafu), ni Ukweli upi mwafaka ambao kanisa litakuwa nao kwa ajili yake na kwa ulimwengu? Nini, kwa hakika, ikiwa haliwezi kupokea sasa na kuufanya mazoea haswa Ukweli wa sasa, awamu ya mwisho ya Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, ambao sasa unatangaza kujongea na kunyemelea kwa hukumu juu ya walio hai, na ambayo inabisha penye kila mlango wa moyo? {WHR: 37.1}

Kwa kuhuzunisha, wale ambao sasa wanashindwa kuvijaza vyombo vyao (Mat. 25:1-4) mafuta haya ya ziada (ukweli wa ziada — wa hukumu ya walio hai) yanayomiminika kutoka kwa bakuli la dhahabu (Zek. 4) hatimaye wataziona taa zao zikizima milele kama mshumaa uliokwisha. Lo, katika mshangao ulioje wakati huo watayatafuta mafuta ya dhahabu ya thamani! Na

38

kwa mhangaiko mkubwa kuliko wanavyotafuta sasa dhahabu na fahari! Lakini, ole, basi kama Esau, ingawa watayatafuta “kwa makini na kwa machozi,” hawataipata “nafasi ya kutubu”: wanayanunua mafuta yao wakiwa wamechelewa sana. Mlango umefungwa wanapoufikia. Na kwa kubisha kwao kwa kichaa laja jibu la kutisha, “Sikuwajua ninyi kamwe.” Mat. 7:23. Wakati huo mavuno ya malimbuko yamepita, mazao yamewekwa ndani, na magugu yamefungiwa nje kuangamizwa, huko kwa uchungu kulia na kusaga meno yao: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” Yer. 8:20. {WHR: 37.2}

“Wakati wa Hukumu ni kipindi maalum cha umakini, wakati Bwana anawakusanya walio Wake kutoka kati ya magugu. Wale ambao wamekuwa washirika wa familia moja wanatenganishwa, alama inawekwa kwa mwenye haki.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 234. {WHR: 38.1}

“…Madini safi na taka havitachangamana tena.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 236. {WHR: 38.2}

“…Kanisa litalishwa manna kutoka mbinguni, na kuhifadhiwa chini ya uangalizi wa neema Yake. Likiwa limevikwa silaha kamili za nuru na haki, linaingia kwenye pambano lake la mwisho. Takataka, vifaa visivyofaa, vitateketezwa, na mvuto wa ukweli hushuhudia ulimwengu tabia yake ya kutakasa na kuadilisha….” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 17, 18. {WHR: 38.3}

Ili kulilinda kutoka kwa uharibifu “vito” Vyake (Mal. 3:17) anapovikamilisha, Yeye anaviweka katika Nyumba nyeupe na safi, mbali na wasioamini — wanafiki. Hili Yeye analifanya wakati siku ya mfano inapokaribia kikomo. Vivyo hivyo, watumwa wa saa ya kumi na moja

39

ni wa kwanza kupokea malipo yao — “dinari.” Wanaendelea kuishi hadi watakapokutana na Mungu wao: kumsikia Yeye akiwaambia pongezi ya kusisimua, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu:…ingia katika furaha ya Bwana wako.” Mat. 25:21. “Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu Wake.” Isa. 25:9. Ilhali watumwa wa wito uliotangulia wanasubiri makaburini kutokea wakati wa siku ya ufufuo kujiunga na walio hai katika hii safari wakiimba kwaya ya kuitikiana kuyapokea malipo yao ya dinari — uzima wa milele. Basi “wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.” (Mat. 20:16) — kundi la mwisho, watumwa wa saa ya kumi na moja, wanalipwa kwanza, na watumwa wa wito uliopita wanalipwa mwisho. {WHR: 38.4}

Wote ambao wamesoma kwa uangalifu kurasa hizi hadi hapa, hakika wamejua ukweli kwamba hata uwakilishi huu uliyothibitiwa sana wa “ujumbe wa ziada” — ule wa hukumu ya walio hai — hutoa, wenyewe, nguvu kubwa na uwezo “kwa Ujumbe wa malaika Watatu (Maandishi ya Awali, uk. 277). Lakini ni kwa jinsi gani utatoa kabisa uwezo na nguvu? Kwanza kwa kuleta wazi vipengele vya Hukumu ambavyo hapo awali vilikuwa havijafunuliwa, kisha hatimaye kuwakomboa watu wa Mungu kutoka kwa dhambi na wadhambi, hivyo kusababisha liwepo kanisa lililotazamiwa kwa muda mrefu lililotakaswa “zuri kama mwezi, safi kama jua, la kutisha kama jeshi lenye bendera?” — Wimbo wa Sulemani 6:10; Manabii na Wafalme, uk. 725. Nyumba halisi imara na yenye nguvu kweli kweli! {WHR: 39.1}

Hivyo “likiwa limevikwa silaha za nuru na haki, linaingia katika vita vyake vya mwisho,” “limengarishwa kuangaza

40

kama nembo ya mbinguni, na kuakisi kwa pembe zote mianga mikali, safi ya Jua la Utakatifu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 17. “Huu ndio utukufu wa Mungu, utakaoifunga kazi ya malaika wa tatu.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 19. {WHR: 39.2}

Kweli hizi zenye changamoto ni, bila shaka, kemeo kubwa kwa wale ambao wameweza kupuuza kwa muda mrefu jukumu ambalo wamepewa na Mungu kuelimisha ukasisi na waumini kutarajia, kutazamia, na unapoonekana kwa furaha waupokee “ujumbe wa ziada,” wa saa ya kumi na moja. Wangalikuwa waaminifu kwa imani yao, wangeweza sasa kuutambua ujumbe unaobisha mlangoni pao, kama ni ule ambao umesubiriwa kwa muda mrefu, na wangejua ni ule umetajwa kwa njia mbalimbali: (1) hukumu ya walio hai, (2) mavuno, (3) siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana, (4) kilio kikuu (wakati ujumbe unapoangaza dunia kwa utukufu wa haki ya Kristo inayowavutia kutoka kwa watumwa 144,000 wa Mungu wasiokuwa na uongo). Na, kwa hivyo, wangejua kwamba hivi ndivyo Bwana atakavyoyapepeta mataifa (Isa. 30:28), “kuimaliza kazi, na kuikata katika haki.” Rum. 9:28. {WHR: 40.1}

Lakini licha ya wao kuutelekeza wajibu unaowapasa na matokeo ya upofu, Uvuvio unajitahidi kuwatahadharisha kwa lile ambalo zamani sana uliwaonya kwa uaminifu: {WHR: 40.2}

“…Wakati uliopita umeonyesha kwamba wote walimu na wanafunzi wanajua machache sana kuhusu kweli za kuogofya ambazo ni maswala yaliyo hai ya nyakati hizi. Kama ujumbe wa malaika watatu ungetangazwa katika ukamilifu wake kwa wengi ambao husimama kama walimu, hawangeweza kuuelewa.” — Shuhuda, Gombo la. 6, uk. 165. {WHR: 40.3}

41

“…Vitabu na majarida ambayo hayana ukweli wa sasa yanatukuzwa na watu wameanza kuwa wajanja sana kufuata ‘Bwana asema hivi.’ …walinzi wengi wamelala, wao ni kama kipofu anayemwongoza kipofu. Hata sasa, siku ya Bwana imetufikia. Kama mwizi inanyemelea, na itawachukua pasipo kujua wote ambao hawakeshi. Ni nani kati ya walimu wetu wako macho, na kama mawakili waaminifu wa neema ya Mungu wanaipatia baragumu sauti ya hakika?” — Shuhuda, Gombo la. 6, uk. 166. {WHR: 41.1}

“…Hali ya sasa ya kanisa haimpendezi Mungu. Kumeingia kujiamini nafsi ambapo kumewaongoza kujihisi hawana hitaji la ukweli zaidi na nuru kubwa. Tunaishi kwa wakati ambapo Shetani yu kazini mkono wa kulia na wa kushoto, mbele na nyuma yetu; na bado kama watu tumelala. Mungu anakusudia kwamba sauti itasikika kuwaamsha watu Wake kwa utendaji.” — Shuhuda, Gombo la. 5, uk. 709. {WHR: 41.2}

“Ujumbe ambao utayaamsha makanisa utatangazwa. Kila juhudi ifanywe kupeana nuru, si tu kwa watu wetu, bali kwa ulimwengu. Nimeagizwa kwamba unabii wa Danieli na Ufunuo unapaswa kuchapishwa katika vitabu vidogo, na maelezo muhimu, na vinapaswa kutumwa ulimwenguni kote. Watu wetu wanahitaji kuwa na nuru iliyowekwa mbele yao katika mistari iliyo wazi.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 117. {WHR: 41.3}

“Kemeo la Bwana litatua juu ya wale ambao wataizuia njia, kwamba nuru safi isije kwa watu. Kazi kubwa inapaswa kufanyika, na Mungu anaona kwamba viongozi wetu wanahitaji nuru zaidi, ya kwamba waweze kuungana na wajumbe ambao Yeye anawatuma ili kukamilisha kazi Aliyokusudia ifanywe.” — Watenda kazi wa Injili, uk. 304. {WHR: 41.4}

42

“Naliona malaika wakiharakisha wakiingia na kutoka mbinguni, wakishuka duniani, na tena wakipaa mbinguni, wakifanya tayari kutimizwa kwa tukio lingine muhimu. Kisha nikamuona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake. Uwezo mkuu na utukufu alipewa yule malaika, na aliposhuka, nchi ikaangazwa kwa utukufu wake…. Kazi ya malaika huyu inaingia kwa wakati mzuri kujiunga na kazi kubwa ya mwisho ya ujumbe wa malaika watatu, unapoumuka kuingia kilio kikuu. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao jinsi kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga kwa ujumbe wa malaika wa pili mwaka 1844.” — Maandishi ya Awali, uk. 277. {WHR: 42.1}

“Kwa nafsiambazo zinatafuta nuru kwa bidii, na kupokea kwa furaha kila kianga cha nuru ya Mungu kutoka kwa neno Lake takatifu, — kwa kama hao pekee nuru itapeanwa. Ni kupitia kwa nafsi hizi ya kwamba Mungu ataiufunua hiyo nuru na nguvu ambayo itaangaza nchi yote kwa utukufu wake.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 729. {WHR: 42.2}

“Katika udhihirisho wa nguvu ambayo itaangaza nchi kwa utukufu wake, watakiona tu kitu ambacho katika upofu wao watafikiri ni hatari, kitu ambacho kitaziamsha hofu zao na watajikaza kuupinga. Kwa sababu Bwana hafanyi kazi kulingana na matarajio na mawazo yao, wataipinga kazi. Mbona, wanasema, hatupaswi kumjua Roho wa Mungu, wakati ambapo tumekuwa kazini kwa miaka mingi sana?” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 7, 1918. {WHR: 42.3}

43

“Uangavu, utukufu, na nguvu zitaunganishwa na ujumbe wa malaika wa tatu, na uaminifu utafuata popote ambapo utahubiriwa ukiandamana na Roho. Je! atawezaje yeyote wa ndugu zetu kujua wakati nuru hii itawajia watu wa Mungu? Hata sasa hakika hatujauona nuru ambayo inayajibu maelezo haya. Mungu ana nuru kwa watu Wake, na wote watakaoikubali watauona uovu wa kukaa katika hali ya uvuguvugu.” — Mapitio na Kutangaza, Aprili 1, 1890. {WHR: 43.1}

“…Isipokuwa wale ambao wanaweza kusaidia katika ______ waamshwe kwa hisia ya wajibu wao, hawataitambua kazi ya Mungu wakati kilio kikuu cha malaika wa tatu kitakaposikika. Wakati nuru inakwenda kuiangaza nchi, badala ya kuja kwa msaada wa Bwana, watataka kuifunga kazi Yake ili iafikiane na mawazo yao finyu. Hebu niwaambie kwamba Bwana atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna iliyo kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa wanadamu. Watakuwapo wale kati yetu siku zote watataka kuthibiti kazi ya Mungu, kulazimisha hata hatua gani zitafanyika wakati kazi inakwenda mbele chini ya uongozi wa malaika anayejiunga na malaika wa tatu katika ujumbe utakaopeanwa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua mamlaka mikononi Mwake. Watendakazi watashangazwa kwa njia rahisi ambazo Yeye atatumia kuileta na kuifanya kamilifu kazi Yake ya haki.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 300. {WHR: 43.2}

“Naliuliza maana ya kupepeta nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi Mwaminifu kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo

44

wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu wa moja kwa moja. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” {WHR: 43.3}

“Naliona kwamba ushuhuda mzito wa Shahidi Mwaminifu haujapokelewa hata nusu. Ushuhuda wa kicho ambao juu yake hatima ya kanisa inaning’inia umeheshimiwa kimzaha, ikiwa si kupuuzwa kabisa. Ushuhuda huu sharti ufanye toba ya ndani; wote wanaoupokea kweli kweli watautii, na kutakaswa.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. {WHR: 44.1}

“…Watahoji na kukosoa kila kitu ambacho kinachoinuka katika kukunjua kwa ukweli, watakosoa kazi na msimamo wa wengine, kukosoa kila tawi la kazi ambayo hawana sehemu. Watajilisha makosa na kasoro na mapungufu ya wengine, hadi, akasema malaika, Bwana Yesu atainuka kutoka kwa kazi Yake ya upatanisho katika hekalu la mbinguni, na Kujivika mavazi ya kisasi, na kuwashangaza kwa karamu yao isiyo takatifu; na watajikuta hawajajiandaa kwa karamu ya jioni harusi ya Mwana-Kondoo. Ladha yao imepotoshwa sana hivi kwamba wangeweza kudiriki kuishutumu hata meza ya Bwana katika Ufalme Wake.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690. {WHR: 44.2}

“Kuliko hapo awali, tusiombe tu kwamba watumwa waweze kutumwa katika shamba kubwa la mavuno, ila tuwe na ufahamu safi wa ukweli, ili wajumbe wa kweli watakapokuja, tuweze kuupokea ujumbe na kumheshimu mjumbe.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 420. {WHR:44.3}

“Unabii lazima utimizwe.” Asema Bwana: Angalieni,

45

nitawapelekea nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni hodari sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.'” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 475. {WHR: 44.4}

Kwa ubaya zaidi au uzuri, Wandugu, ninyi sasa, mupo katika nuru inayoangaza ya Neno la Mungu, mmeachwa kufanya uamuzi wenu wenyewe. Iwayo yote, hata hivyo, hamwezi kamwe kuwa na sababu ya haki kumkweza au kumlaumu mwingine; jukumu sasa ni lenu kabisa. Ikiwa uchaguzi wenu utakuwa kwa ubaya zaidi, basi, kuwakumbusha, mara tu mafuta katika taa zenu yatakapokuwa yamekwisha (mara tu ujumbe wa hukumu ya wafu umepita, na hukumu ya walio hai karibu kuanza), mtajipata katika giza kuu la kiroho, na taa zenu zikiwa zimezima, na hamna mafuta ya ziada katika vyombo vyenu — bila maarifa wala maandalizi ya hukumu ya walio hai; kwa hivyo, kutapikwa nje. {WHR: 45.1}

“Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza, Basi ile iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!” Mat. 6:23. {WHR: 45.2}

Ikiwa unashindwa sasa kuyahifadhi mafuta haya ya ziada ya Kweli, kwa muda mfupi utaachwa na hofu kuu tupu na haja ya kuwa nayo. Lakini wakati utambuzi huu wa kutisha utakapokuja juu yenu, itakuwa bure kabisa, maana wakati mnapofanya hatua ya kuyapata mafuta, na kwenda mwendo uliosalia, wakati huo, hakika jinsi muishivyo, Mlango utafunga, na gonga gonga zenu za hodi zitawaletea jibu la kutisha, kutoka ndani: “Amin, nawaambia,

46

Siwajui ninyi.” Mat. 25:12. Na, O, litakuwa janga lisilo na kipimo wala kuelezea, Wandugu. {WHR: 45.3}

Lakini ukifanya uamuzi wako kuwa bora, basi utapata muhuri wa Mungu (Ezek. 9, Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445) kwenye kipaji cha uso wako, uhesabiwe kuwa hauna hatia mbele ya kiti Chake cha hukumu, na uwe na fursa ya kuwa katika ufufuo wa Danieli 12: 2, au kusimama mapema na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni (Ufu. 14:1), kuanzia hapo kuupeleka ujumbe wa Mungu kwa mataifa yote na kuwaleta ndugu zako wote kuwa sadaka katika “nyumba ya Bwana.” Isa. 66:19, 20. Utakuwa sehemu ya malimbuko, kitovu, cha Kanisa la Ufalme, ishara ya mavuno ya pili ya walio hai, wale ambao mtawaleta baadaye. {WHR: 46.1}

Kama wafuasi wa ukweli wa sasa katika kipindi cha mavuno ya kwanza, Mungu atusaidie sisi sote, Ndugu Dada, kuwa miongoni au pamoja na mavuno ya kwanza, 144,000. Ameachiwa kila mtu kuamua hatima yake mwenyewe. Na juu ya hili kuwa na hakika, kwamba njia pekee ya kutokukosa kupata umilele ni kuisikia na kuifuata sauti ya Mungu; kwa kufanya uamuzi wako katika chumba cha siri cha sala; na kudumu katika uchunguzi kwa unyenyekevu Ukweli uliofunuliwa hasa wakati huu. Ingawa njia ya uhakika ya kupotea na ya kuupoteza ni kuzisikiliza sauti za wanadamu mahali pa sauti ya Mungu. {WHR: 46.2}

Wa umuhimu zaidi bado ni ukweli kwamba mwito wa saa ya kumi na moja unawapata watumwa wake “wanasimama bila kazi” “sokoni” (kanisa), bila kufanya chochote, udhuru wao kwamba, “hakuna mtu ametuajiri.” Kwa mtazamo wa ukweli huu, ni wazi kwamba watuwai wa saa ya kumi na moja hawajumuishi lile la ukasisi, si kati ya wale walio tayari kazini; la, si zaidi walivyokuwa watumwa wa wito uliopita. Historia

47

hutoa ushahidi kwamba karibu wote wale wasio na kazi, walei, siku zote wamewahi kuwa wa kwanza kuitikia mwito wowote wa Mungu! {WHR: 46.3}

“Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa mpepeto, wa kupimwa watafunuliwa waonekane. Wapo sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu….” {WHR: 47.1}

“Wakati miti isiyo na matunda inakatwa kama kwekwe za ardhini, wakati umati wa wandugu wa uongo wanatofautishwa na wa kweli, basi hao waliofichwa watafunuliwa waonekane, pamoja na maneno ya sifa kwa Mungu wanajipanga chini ya bendera ya Kristo. Wale ambao wamekuwa waoga na wasiojiamini, watajitangaza wazi kwa ajili ya Kristo na ukweli wake. Wale dhaifu sana na wa kusitasita kanisani, watakuwa kama Daudi — tayari kutenda na kuthubutu .…” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, 81. {WHR: 47.2}

Taarifa, “watafunuliwa waonekane,” “wa thamani sasa wamefichwa,” na “waliofichwa watafunuliwa waonekane,” wazi wazi yanaufunua ukweli kwamba ingawa watumwa wa saa ya kumi na moja kwa sasa si watu maarufu, si watu wanaojulikana kwa ujumla, wao, hata hivyo, kwa hakika watakuja kwa wakati wao, hatimaye. Kazi hii ya haki ya Kristo, Wandugu, haitaonekana jambo la ajabu sana kwako wakati unapofikiria kwamba kila mwanamme (ila wawili) waliozidi miaka ishirini katika vuguvugu la Kutoka baada ya kuvuka Bahari ya Shamu, waliangamia katika mashaka, au kwa kutafuta makosa dhidi ya Uvuvio, au katika kutafuta ofisi,

48

au kwa uchu wa vyungu vya nyama za Misri, na ya kwamba vijana pekee wa vuguvugu waliishi kuvuka Yordani na kuimiliki Nchi ya Ahadi. Mambo haya, kumbuka, “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Kor. 10:11. {WHR: 47.3}

Kwa wale ambao “wataokoka” na “kufunuliwa waonekane” katika vuguvugu la Kutoka la uakisi, Uvuvio unatagaza kwa shangwe: {WHR: 48.1}

“… maana hao ni watu walio ishara …. na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 3:8; 12:8. {WHR: 48.2}

Ni dhahiri kwamba “watu hawa walio ishara” (“waliokoka” na “kufunuliwa waonekane” saa ya kumi na moja) ni “watumwa” wanaotimiza lililotazamiwa kwa muda mrefu “Vuguvugu la Walei” (Shuhuda, Gombo la 9, uk. 125, 126). Saa ya kumi na moja ni, kwa hivyo, wakati ambao Roho ya unabii huonyesha ikisema: {WHR: 48.3}

“… Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa.… Mungu atafanya kazi katika siku zetu ambayo wachache tu hutarajia. Yeye atawaamsha na kuwainua kati yetu wale ambao wamefundishwa kwa kutiwa mafuta na Roho Wake, kuliko kwa mafunzo ya nje ya taasisi za kisayansi …. Mungu ataonyesha kwamba hawategemei watu wasomi, wabinafsi wanaojiona bora.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, 82. {WHR: 48.4}

Hakika ingewezekanaje kuwa vinginevyo isipokuwa “wasomi,” “watu wakuu” ama kwa unyenyekevu washuke au kamwe wasikipande kiti cha fahari alichokiinua mwanadamu ila alicho kihukumu Mungu ambapo huketi wenye nguvu wasioupokea kamwe Ukweli usiokuwa maarufu,

49

na daima wanaowazuia wengine kuupokea, isipokuwa upate chimbuko ndani mwao? Zaidi ya hayo, ni wapumbavu pekee, wengi wasiokuwa wa kweli na busara, ambao huthubutu kukipanda kiti hicho alichokataza Mungu cha kujiona bora wa nafsi. Wakuu wa kweli wanalijua jambo hili, wanajua pia kwamba Mungu hajawahi hata mara moja kuweza kukitumia kinachojulikana eti mkuu — maarufu — kama vyombo anavyoweza kuvifunulia na kuusambaza Ukweli mpya. Badala yake, tunaambiwa: {WHR: 48.5}

“Lakini Roho Mtakatifu, mara kwa mara, ataufunua ukweli kupitia vyombo vyake alivyovichagua mwenyewe; na hakuna mtu, hata kuhani au mtawala, anayo haki kusema, Huwezi kutangaza maoni yako, kwa sababu MIMI siyaamini. Hiyo ya ajabu “MIMI” yaweza kujaribu kushusha fundisho la Roho Mtakatifu. Watu wanaweza kujaribu kwa muda kulizima na kulikomesha; lakini hilo halitafanya uongo kuwa ukweli, au ukweli kuwa uongo. Akili za ubunifu za wanadamu zimeleta kauli za dhana kwa mambo mbalimbali, na wakati Roho Mtakatifu anawezesha nuru kuangaza ndani ya akili za kibinadamu, haheshimu kila hatua ya mpangilio wa mwanadamu kwa Neno. Mungu aliwapiga chapa watumwa Wake kusema ukweli, bila kujali lile ambalo watu walikuwa wamelichukua kwa dhati kama ukweli. {WHR: 49.1}

“Hata Waadventista wa Sabato wako katika hatari ya kuyafumba macho yao kwa ukweli jinsi ulivyo ndani ya Yesu, kwa sababu hukanusha kitu ambacho wamekichukulia kwa uzito kwamba ni ukweli, lakini ambacho Roho Mtakatifu hufundisha si ukweli.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 70. {WHR: 49.2}

“Lakini jihadharini kukataa lile ambalo ni ukweli. Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika

50

viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali.” {WHR: 49.3}

“Hakuna mtu anayepaswa kudai kwamba anayo nuru yote ilioko kwa ajili ya watu wa Mungu. Bwana hawezi kuvumilia hili, amesema, ‘Nimeweka mbele yako mlango wazi, na hakuna mtu anayeweza kuufunga.’Hata kama viongozi wetu wote wanaweza kukataa nuru na kweli, mlango huo utakuwa bado wazi. Bwana atawainua watu watakaowakabidhi watu ujumbe kwa wakati huu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {WHR: 50.1}

Je, hamwezi sasa, Wandugu, kuamka haraka? au kuyarudia makosa ya siku ya Yoshua, na kuruhusu vijana kuzichukua nafasi zenu? {WHR: 50.2}

“Bwana amewachagua vijana kuwa mkono Wake wa kumsaidia.” — Shuhuda, Gombo la 7, uk. 64. {WHR: 50.3}

“Tunalo jeshi la vijana leo ambao wanaweza kufanya mengi ikiwa wataelekezwa vizuri na kutiwa moyo.” — Taarifa ya Baraza Kuu, Gombo la 5, Namba 2, uk. 24. (Jan. 29, 30, 1893). {WHR: 50.4}

“Kukiwa na jeshi kama hilo la watenda kazi kama vijana wetu, wakifunzwa vyema kwa hakika wataweza kutoa, kwa haraka ujumbe wa aliyesulubishwa, aliyefufuliwa, na Mwokozi atakayekuja hivi karibuni utakavyopelekwa kwa ulimwengu wote!” — Elimu, uk. 271. {WHR: 50.5}

“Vijana wanapaswa wenyewe kuyachunguza Maandiko, hawapaswi kujisikia kwamba yatosha kwa walio wazee katika ujuzi kubainisha ukweli, kwamba wadogo wanaweza kuupokea kutoka kwao kama amri. Wayahudi waliangamia kama taifa kwa sababu walivutwa kutoka kwa ukweli wa Biblia na watawala wao, makuhani, na wazee. Laiti

51

wangeyasikia mafundisho ya Yesu, na kuyachakura Maandiko wenyewe, wasingalipotea.” {WHR: 50.6}

“Vijana katika safu zetu wanatazama kuona roho ambayo wachungaji huja nayo kwa uchunguzi wa Maandiko, iwapo wanayo roho ya kufunzwa, na wanao unyenyekevu wa kutosha kuukubali ushahidi, na kuipokea nuru, kutoka kwa wajumbe ambao Mungu huchagua kuwatuma” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 109. {WHR: 51.1}

Sasa ambapo mwito wa saa ya kumi na moja unavuma, Bwana yu penye mwanzo akiwaita kwenye shamba Lake la mizabibu wagombea wa ukasisi na watenda kazi wa Biblia waliohitimu au bado kuhitimu wa Vyuo vya Waadventista wa Sabato, na wanaosimama bila kazi, wakisubiri “kuajiriwa.” Isitoshe Yeye anatoa mwito kwa ajili ya huduma hii ya mwisho ya utukufu, kwa wote watendakazi watulivu wenye nguvu na afya ya mwili. Je, Wandugu, hamtakuwa na hiari, ninyi nyote, sasa kuitikia huu mwito wa mwisho na wenye utukufu mno? Unaweza kuanza safari ya kwenda shambani baada ya kukamilisha kwa makini warsha ya miezi mitatu ya mafunzo juu ya mafunuo ya Ukweli wa sasa ambao hupeana nguvu na uwezo kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu (Maandishi ya awali, uk. 277), na ambao hufunua hukumu ya walio hai, siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana. {WHR: 51.2}

*Hautahitaji fedha kwa ajili ya mafunzo na chumba cha kukodi wakati unapochukua kozi ya miezi mitatu katika Taasisi ya Walawi wa Wadaudi, Kituo cha Mlima Karmeli, na unapokamilisha masomo yako utapewa nafasi ya kudumu na ujira pamoja na gharama za usafiri kote katika ulimwengu wa Waadventista wa Sabato kwanza, hatimaye kwa kila taifa katika shamba lote la mizabibu la Bwana. Hii ndiyo fursa ya uzima — kupata nafasi “katika kufunga kazi kwa kanisa, wakati wa kutiwa muhuri kwa watu

52

mia na arobaini na nne elfu” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na kupata nafasi kati ya “wale waliookoka,” ambao watakwenda kuwaleta “katika nyumba ya Bwana” ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote, jinsi Isaya anavyotangaza waziwazi: {WHR: 51.3}

“Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:19, 20. {WHR: 52.1}

Hapo nabii anayo maono ya makundi mawili ya watakatifu, — wale wanaokoka, na wale wanaoletwa ndani na waliokoka — na watu 144,000. Kikundi cha kwanza cha watumwa wakiwa malimbuko ya mavuno makubwa, basi haiwezi kuepukika kwa busara kwamba wale ambao wanaletwa kwa Bwana ni mavuno ya pili. Hakika, palipo na ya kwanza, lazima iwepo ya pili. Na makundi ya kwanza na ya pili ni yale ambayo Yohana Waufunuo aliona (Ufu. 7:3-9). Kumbuka kwamba watumwa hawa wa saa ya kumi na moja ambao watakwenda kwa mataifa yote kuwaokoa ndugu zao wote, kuwaleta kama “katika chombo safi hadi ndani ya nyumba ya Bwana” (Isa. 66:20), ndani ya kanisa lililotakaswa, kanisa lisilo na wanafiki wanaoendelea kuyafanya machukizo yao ndani yake — nyumba nyeupe hakika. {WHR: 52.2}

53

Hata hivyo, usimruhusu mtu yeyote akupumbaze uamini kwamba Msajili anakuita utoke katika dhehebu la Waadventista wa Sabato na kuingia kitu kingine. Madai kama hayo na uchongezi hutoka tu kwa wale ambao ni maadui wa ukweli wa Mungu wa saa ya kumi na moja, au Ukweli wa saa ya Hukumu, na ambao si watumishi Wake wala marafiki zenu. Watumwa wa Mungu hupokea maagizo yao kutoka kwa Mungu, na marafiki waangalifu daima huwa hawawashinikizi marafiki zao kuukubali udanganyifu ulioenezwa, hasa wakati Maandiko yanapozingatiwa. Ukweli bayana juu ya Msajili ni kwamba lengo lake ni kuhakikisha unakaa ndani ya Dhehebu, na kukuhifadhi usitupwe nje, si na wanadamu, bali na Bwana wakati anashika njia kuwakagua wageni humo na kuwatupa nje wale ambao wameshindwa kujivika “vazi la harusi” ambalo Msajili huleta. {WHR: 53.1}

Wenye hekima hawatawaruhusu maadui wa Ukweli kuwapumbaza. Badala yake watafanya kadiri wawezavyo kuwaonyesha ukweli hawa marafiki wa hila na kuwahimiza kumruhusu Msajili ayapake macho yao dawa ili waweze kuona kwamba “Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli waliookoka. [Dhehebu la Mungu la leo]. {WHR: 53.2}

“Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni [katika Makao makuu], na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu [kanisani baada ya utakaso], ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.

54

Tena juu ya makao yote ya Mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4:2-6. Kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. {WHR: 53.3}

Sasa ya kwamba “vitu vyote vi tayari.” Ndugu, huu ndio mwito wako wa Utakatifu mwanzo wa saa ya kumi na moja. Mungu anakataza kwamba usiiruhusu fursa hii ya thamani sana ikuponyoke “jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu.” 2 Pet. 1:10. Tenda kwa haraka, kwa maana unabii mpya ambao umefunuliwa unaonyesha kwamba kazi ya hukumu ya wafu karibu inaisha — hii ndio sababu ya mwito huu wa Kiungu uliopangwa na wa haraka kwa huduma sasa wakati Msajili huyu wa Mbinguni anavunja vunja vizuizi vya chuma ambavyo maadui wa Ukweli wamewashikilia mateka wateule wa Mungu katika giza na upofu wa Ulaodekia. {WHR: 54.1}

Akiwa tayari ameingiza polepole ndani ya askari kote kote Laodekia hofu isiyo na kifani na chuki dhidi ya kusoma au kusikiliza kitu chochote isipokuwa kile kinachofurahisha idhini maalum na baraka ya mkuu fulani, wana mapinduzi wa Shetani wamejaribu kuzikata nyaya za mawasiliano kati ya Roho wa Kweli na watu wa Mungu. Kisha kuwashikilia kuwa mateka wao kwa viwango vyao vya kidunia, hutishia kutupwa nje ya sinagogi na kupotea milele yeyote ambaye, anamcha Mungu kuliko mwanadamu, anayekuwa jasiri kudiriki kuujua Ukweli mwenyewe. Na wachache ambao huwa jasiri wa kutekeleza imani zao, mara moja matokeo yake huwa walengwa wa mishale ya Adui mikali zaidi ya upinzani, — machukio bila sababu, kashfa za uongo na kuharibu sifa za tabia njema, dhihaka na dharau

55

na kinyongo, chuki ya kuaibisha na shida. Kwa hiyo wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu” (2 Tim. 3:12) wanajikuta “waliotupwa” (Isaya 66:5; Luka 6:22; Matendo 24:14) mikononi mwa askari watesi wanaoendeleza na hata kuzidi yale mabaya zaidi ambayo yalikuwa yakiendelezwa katika Uyahudi na Urumi. Na lililo baya zaidi, wakati wafuasi hawa wa udhalimu, wakiwa wamejivika mavazi kama ya kitume, hufanikiwa kuikanganya na kuipindua imani ya mchunguzi au mfuasi wa Ukweli wa wakati huu, humlazimisha kutii ili abatizwe tena ndiposa aorodheshwe upya katika ushirika wa kanisa, ingawa amekuwa mwaminifu zaidi kuliko hapo awali! Ni kukufuru kwa ajabu ilioje! {WHR: 54.2}

Ni kwa hiari ya uaminifu watu wa Mungu wataona sasa ya kwamba si umuhimu wowote, iwapo mjumbe wa saa ya kumi na moja — Msajili — anabeba hiki, kile, au kingine ambacho kimepewa kibali cha muhuri wa kibinadamu, lakini kwamba ni muhimu sana Abebe muhuri wa Mungu, na ya kwamba kila “kondoo” wa kundi adai haki yake aliyopewa na Mungu Kumkagua kwa macho yake mwenyewe, na kisha, bila ushawishi wa sauti yoyote ila ile ya Roho wa Kweli anaye kaa ndani, kujiamulia mwenyewe kweli katika kesi hiyo. {WHR: 55.1}

Roho ya sasa ya udikteta na chafu ilianza kujidhihirisha miaka iliyopita, na hata Roho wa Kweli alionya: {WHR: 55.2}

“Lakini jihadharini na kukataa kile ambacho ni ukweli. Hatari kubwa na watu wetu imekuwa ni ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na tabia ya kuipekua Biblia wao wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika watu wanaoongoza, na huyapokea maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa haswa jumbe ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu wanaoongoza hawatazikubali.”

56

Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {WHR: 55.3} 

“Nuru ya thamani itangaza kutoka katika Neno la Mungu, na mtu yeyote asithubutu kuamuru ni nini kitakacholetwa au kutoletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangazisha Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yoyote nafasi yake ya mamlaka, hakuna mtu aliye na haki ya kuizimisha nuru kutoka kwa watu. Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.” — Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {WHR: 56.1}

“…Nimelazimika kuwasihi watendakazi wetu: Iwayo yote nafasi yako, usiwategemee wanadamu, au kuufanya mwili kuwa kinga yako.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 349, 350. {WHR: 56.2}

Salama kitandani, na bila kujali shauri la Uvuvio, hawa madereva wa dhamiri huchunga waumini kama ng’ombe, kana kwamba Roho wa Kweli huwa hawaongozi wengine isipokuwa wachungaji. Kupitia mstari huu mbaya wa utawala usio halali wa ukasisi, sambamba na masingizio yanayoongezeka, Msajili huyu wa Mbinguni lazima afanye njia yake ili kuwaokoa wote watakaokolewa. {WHR: 56.3}

Mnyanyaso sawa wa utawala wa ukasisi katika siku ya Nikodemo

57

ulimfanya asithubutu kuonekana pamoja na Yesu, bali kwenda kwa siri usiku ili kumwona Yeye. Maana, hata hivyo, hawatakiwi wengi wateule wa Mungu sasa kuja hata usiku ili kuusikia Ukweli wa saa ya kumi na moja, Msajili huyu wa Mbinguni kwa hitaji lao anaenda kwao katika vazi lisilo la kawaida (kama aliyevikwa usiku) — Njia ya pekee Anayoweza kuwafikia na kuwaokoa wote wanaotaka. {WHR: 56.4}

Tena, kwa mlipuko mkubwa wa baragumu ya Israeli, baada ya mzunguko wa saba kimya kimya kwa kuta zisizoweza kupenyeka za Yeriko, lango kubwa la chuma likaanguka ghafla kuta zikiporomoka kwa kishindo ajabu, na Israeli wakaingia ndani — kwa ushindi! Hivyo itakuwa pamoja na kuta kubwa za upinzani ambazo Adui amewaweka Walaodekia katika hali ya uvuguvugu — katika hila kwamba wao ni “matajiri, wamejitajirisha,” na hawahitaji kitu, ilhali wao ni “wanyonge, wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi.” Ufu. 3:17. Kwa hivyo, kwa muda mfupi malango yaliofungwa na kukazwa sasa, kuwekwa vizuizi, na kuwazuia waokozi wa Mbinguni na vyakula vya Ukweli kwa wakati wake, vya kundi la mateka ghafla yataanguka wazi wakati kuta zikiporomoka chini Kiyeriko katika mzunguko wa saba wa Msajili na mlipuko wa baragumu. Kisha wote waliofichika wa Mungu kwa utukufu “watafunuliwa waonekane.” {WHR: 57.1}

“…ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka. Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 33:23, 24. {WHR: 57.2}

“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare;

58

naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.” Zek. 4: 6, 7. {WHR: 57.3}

Kanuni iyo hiyo ya Mungu ilipatikana wakati, wakiwa na tarumbeta na myenge iliyofichwa katika majani ya midumu-mwitu, Gidioni na watu wake 300, chini ya mwongozo na ulinzi wa Mungu, waliihusuru kambi ya adui kimya kama simba marara akinyemelea mawindo yake. Ghafla, mlipuko wa ishara, na kulipuka papo hapo kwa sauti za tarumbeta, wakipigapiga midumu-mwitu, mwanga wa moto, na sauti za kelele walivifanya vikosi vya Wamidiani kuwa na taharuki ya uwazimu, na kuwafanya wasababishe maangamizi na uharibifu juu yao wenyewe. Hivyo, pamoja na mbinu hii iliyozaliswa Mbinguni, Gidioni aliyaokoa majeshi ya Israeli yaliyokuwa hatarini. {WHR: 58.1}

Na sasa, upinzani kama ule uliomlazimisha Gidioni kutumia mbinu iliyofaa kupitia kwa watu wake 300 waliochaguliwa, bila shaka inamlazimu Yezreeli pia kuitumia kama mbinu inayofaa kupitia kwa vitengo vyake vitatu alivyovichagua — (1) Kabari Inayoingia, (2) 1950 Maalum kwa Baraza Kuu, na (3) Msajili wa Nyumba Nyeupe. Kimya kimya vikiwaka kwa nuru ya uzima, vinatengeneza njia yao dhidi ya upinzani na kuifikia mioyo iliyoshikwa mateka. Lakini ni vya kutisha mno vikwazo, kuingiliwa, na hatari za Ushetani ambazo Ukweli lazima uvunje! {WHR: 58.2}

Siku zote imekuwa hivyo. Na hakuna mtu anayeweza kutazama kihalisi kikwazo leo kuwa cha chini ya kile ambacho Kweli katika mwili Mwenyewe, Yesu, alikumbana nacho katika siku Yake. Kwa mfano, wakati “sikukuu ya Wayahudi, Siku kuu ya Vibanda ilikuwa karibu,” “ndugu zake…wakamwambia, Ondoka hapa, uende Yudea, na wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya…. Basi Yesu akawaambia,… Kweeni ninyi kwenda kula siku kuu; Mimi sikwei kwenda,

59

kwa kuwa haujatimia wakati Wangu…. Hata ndugu Zake walipokwisha kukwea kuiendea siku kuu, ndipo Yeye naye alipokwea, si kwa wazi, bali kana kwamba ni kwa siri.” Yoh. 7:2, 3, 6, 8, 10. {WHR: 58.3}

Liwaze hilo, Bwana Mwenyewe katika mwili akipaswa kuegemea kwa aina ya mbinu inayofaa kwa saa ya tatu ya mfano ili kulikamilisha kusudi Lake kwenye sikukuu, jinsi Msajili huyu inavyompasa kuiegemea ili kulitimiza lengo Lake sasa saa ya kumi na moja. Kwa ajili ya umuhimu Aliwaambia wanafunzi Wake kwamba wakati wake ulikuwa haujafika, basi mara tu walipokuwa wamekwenda Yeye aliharakisha Mwenyewe kwa siri! Je jaribio kama hili la tahadhari lilikuwa sababu ya wao kumwita “mdanganyifu”! {WHR: 59.1}

Wakati mtu anajua hatari ya sasa jinsi ilivyo kweli, hakuna tena mshangao wowote kwa nini miaka mingi iliyopita Uvuvio ulifanya ufichuzi ufuatao wa kushtua wa hali ndani ya Laodekia: {WHR: 59.2}

“Ni nani anayeweza kusema kwa ukweli,” Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto, mavazi yetu hayajatiwa mawaa na ulimwengu? Nalimwona Mwalimu wetu akionyesha mavazi yanayoitwa eti utakatifu. Aliyararua, Akatandaza wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha Akaniambia: Je! Huwezi kuona jinsi walivyojifunika kwa ujanja unajisi na uozo wa tabia? Je! Mji mwaminifu umekuwaje kahaba? Nyumba ya Baba yangu imefanywa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu wake umetoka, kwa sababu hii kuna udhaifu, na nguvu zimekosekana.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {WHR: 59.3}

“…mwenendo wetu wenyewe wa kukengeuka daima umetutenganisha na Mungu. Kiburi, kutamani, na kuipenda

60

dunia vimeishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kukatazwa. Dhambi mbaya na za kujitukuza zimekaa miongoni mwetu. Na maoni ya jumla ni ya kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho u katika mipaka yake yote. {WHR: 59.3}

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekuwa ikiangaza kutoka kwa neno Lake na katika Shuhuda, na zote mbili zimedunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {WHR: 60.1}

“Ujumbe kwa kanisa la Walaodekia ni wa kushtua na wa kuleta mashtaka, na unawahusu watu wa Mungu kwa wakati huu. {WHR: 60.2}

“…Watu wa Mungu wamewakilishwa katika ujumbe kwa Walaodekia kama katika nafasi ya usalama wa kimwili. Wako shwari, wanajiamini kuwa katika hali ya upeo wa mafanikio ya Kiroho. Kwa sababu unasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu chochote; wala haujui ya kwamba wewe ni mwenye mashaka, na mnyonge, na maskini, na kipofu, na uchi. {WHR: 60.3}

“Ni udanganyifu mkubwa ulioje unaoweza kuja kwa akili za binadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wao wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi Mwaminifu unawapata watu

61

wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, na hata sasa ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni ya kusikitisha machoni pa Mungu. Wakati wale wanaolengwa wanajidanganya kwamba wako kwenye hali ya juu ya kiroho, Shahidi Mwaminifu huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umaskini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi Mwaminifu anayesema, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {WHR: 60.4}

Ni janga la kutisha kwamba wengi wa wachungaji katika Laodekia, ambao kundi la Mungu limeanguka mikononi mwao, wamedanganywa na Adui bila kujua kujiunga naye kuthubutu kupinga na kujaribu kumshinda hata Mwokozi Mwenye nguvu zote. Je! O, ni vipi wachungaji hawa wenye hatia na kundi lao mateka wanaweza kuokolewa kutoka katika hatari yao? Hapa katika juhudi za karibu mwisho kuwaweka huru si tu waathirika wao kutoka kwao lakini pia wao kutoka kwa wao wenyewe, Roho wa Kweli amkwenda kuwasajili wengi watakaoitikia Mwito wa kuja “Kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu. ” Waamuzi 5:23. {WHR: 61.1}

Sasa mwanzoni mwa saa ya kumi na moja, kwa hivyo, Msajili anapanga majeshi dunia yote kufikia kiwango cha Mfalme Mkuu wa Ukweli, katika maandalizi ya siku ya Maangamizi ya Mbingu iliyo karibu sana ya mashambulio dhidi ya machukizo yanayoendelezwa na wanafiki — na mafuriko ya joka (Ufu. 12:15). Hivi karibuni, hata hivyo, nchi itafunua kinywa chake na kuyameza “mafuriko.” Kisha wale walioachwa, “masalia,” “waliokoka wa Israeli” (Isa. 4:2), kundi la kwanza la makomandoo kwa ajili ya Kristo, “watauweka msimamo na uamuzi katika shuhuda zao kwamba watavunja dhidi ya vizuizi vya Shetani.”

62

Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 413. Wao “watamponda kichwa” atakapofanya vita juu yao (Mwa. 3:15; Ufu. 12:16, 17). {WHR: 61.2}

Umuhimu mzito wa hatua ya uamuzi mara moja katika swala hili, kwa sehemu ya wote, hupata msisitizo wa kutisha katika siku ya Bwana, na ufupi mno wa wakati ulioachwa kwetu ambamo tuweze kupata maandalizi muhimu ya kusimama katika moto wa kuchoma takataka siku hiyo. Kwa mtazamo wa ukweli huu, mistari ifuatayo hakika ni mwafaka zaidi sasa kuliko hapo awali: {WHR: 62.1}

“Sasa wakati karibu uishe, na yale tumekuwa tukijifunza miaka mingi, watahitaji kujifunza katika miezi michache. Wataweza pia kuwa na mengi ya kutangua, na kujifunza mengi tena.” — Maandishi ya Awali, uk. 67. {WHR: 62.2}

“Muda ni mfupi, na unachofanya lazima ukifanye haraka. Azimia kuukomboa wakati. Usizitafute anasa zako mwenyewe. Jiamshe, uishikilie kazi kwa azimio jipya la moyo. Bwana atafungua njia mbele yako. Fanya kila jitihada iwezekanavyo kufanya kazi katika njia ya Kristo, kwa unyenyekevu na kwa upole, ukimtegemea Yeye kwa nguvu. Elewa kazi ambayo Bwana anakupa kufanya, na, kumtegemea Mungu, utawezeshwa kupata nguvu tena na tena, kwa neema hata neema. Utawezeshwa kufanya kazi kwa bidii, uvumilivu, kwa ajili ya watu wako wakati siku ingalipo, kwa maana usiku waja ambapo hakuna mtu atakayefanya kazi.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 200. {WHR: 62.3}

“… harakati za mwisho zitakuwa za haraka.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 11. {WHR: 62.4}

Mwito wa kuorodheshwa chuoni sasa, unahitaji zaidi

63

uamuzi wa haraka kwa sababu shule hiyo inawezeshwa kwa sehemu ya kwanza ya mwaka kuwaandaa kwa ajili ya “shamba la mizabibu” wanafunzi wa ukasisi 60 tu. Maombi ya kuingizwa yatatumwa yatakapohitajika. Elekeza mawasiliano yote kwa *Tume ya Kuwajiri Wajumbe, Kituo cha Mlima Karmeli Waco, Texas. Msiruhusu kuhairishakuwanyang’anye, Wandugu, fursa hii kubwa sana ya maisha. Roho anakusihi kwa jina la yote yaliyo timamu na elekevu. Usipuuze au kuchelewesha maandalio yako ya kazi ya ya maana sana iliyo mbele. Haufai kukosa. Hebu maono ya kusisimua ya Isaya ya matokeo yasio na mfano ya kazi ya saa kumi na moja yakuchochee na kukuongoza papo hapo, kwa hatua kamili: {WHR: 62.4}

“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu Wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. {WHR: 63.1}

“Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia. Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za Bwana. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu. Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu Yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo Wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. {WHR: 63.2}

64

“Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.” Isa. 60:1-12. {WHR: 64.1}

Nabii Hosea, pia, alionyeshwa huu mkusanyo mkuu wa watu wote wa Mungu sasa saa ya kumi na moja: {WHR: 64.2}

Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho. Hos. 3:4, 5. {WHR: 64.3}

Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana. Hos. 1:11. {WHR: 64.4}

Maono ya Hosea yaliyonukuliwa tayari hayaonyeshi tu mpangilio wa Mungu

65

kuubomoa Ufalme Wake wa zamani (wa mfano), na Wake vile vile kuwatawanya watu Wake kote ulimwenguni, na hivyo kuwasababisha, kuupoteza utambulisho wao na kufyonzwa na nchi za Mataifa wakati wa karne nyingi hizi, lakini pia yanaonyesha kuurejesha kwa utukufu Ufalme Wake (wa uakisi), na hatimaye Kuwakusanya ndani Yake watu Wake kutoka katika mataifa yote, wakati Anapoifunga kazi ya Injili. Isitoshe yaliyomo katika maono mwafaka ya Hosea kikamilifu yanaonyesha wazi kwamba kazi hii kubwa dunia yote kuwakusanya haiwezi kuanza mpaka “Yezreeli” aonekane kwenye eneo. Na ni nani mwenye akili timamu anaweza kudhani kwamba Shetani ataruhusu taji hili, la mafanikio ya saa kumi na moja ya injili yafanyike bila kukutana na pambano la kufa au kupona na majeshi ya giza hodari zaidi? Wala mtu yeyote kwa sekunde asidhani kwamba Mwenyezi Mungu hakujua mbeleni hali hii na hakutoa mfumo ambao ungeweza kuikabili, moja ambalo ni jina la maana fiche Yezreeli, jina la uandishi la mshenga Wake wa saa ya kumi na moja. Kwa njia hii rahisi inayofaa (jina lisilojulikana) Mbingu huunyang’anya upinzani silaha, huhifadhi mapokezi kwa Msajili (sauti ya Yezreeli), na hivyo Kumwezesha kuokoka jaa la taka na jiko, na hivyo kuzifikia nia zilizokanganyikiwa kwa uongo, na mioyo iliyofanywa migumu kwa kuchukia bila sababu. {WHR: 64.5}

Shukrani kwa mbinu hii ya ushindi kwa njama ya Shetani, si wateule tu bali hata dunia nzima pia “watamsikia Yezreeli,” na “kuu,” kwa hivyo, “itakuwa siku ya Yezreeli.” Hos. 2:22; 1:11. (Ufafanuzi wa kina wa unabii wote wa Hosea unaweza kupatikana unapoombwa.) {WHR: 65.1}

Ndani ya hizi kurasa, Wandugu, mwito wa Mungu wenye mzigo kwenu unawakilisha tu sehemu ndogo ya ujumbe wa saa ya kumi na moja ambao sasa unavuma kote kote Laodekia kama

66

kelele za king’ora cha moto ziliyochangamana na sauti za nyimbo za kanisa. Je, hautaitika na Isaya kwa “sauti ya Bwana, na kusema kwa uhakika, Mimi hapa, nitumie mimi’? Isa. 6:8. {WHR: 65.2}

Kwa macho yako yakiwa wazi kwa Neno la Mungu, masikio yako yakiwa yamezibwa na kukazwa kwa kutosikia tetesi, na moyo wako ukiwa utupu kwa usafi dhidi ya kuchukia bila sababu na dhana unazoshikilia, ti shauri kwa ajili ya nafsi yako mwito wa tarumbeta inayovuma humu. Tatua mwenyewe mara moja yote kwamba tangu ujumbe wa zamani, hukumu ya wafu, tayari unafunikwa na ujumbe mpya, hukumu ya walio hai, lipo chaguo moja tu la hekima kwa mmoja kutenda kwa ajili yake mwenyewe na kwa kwa ajili ya wengine, nalo ni kujitokeza kikamilifu wazi kama mmoja wa watenda kazi wa saa ya kumi na moja wa Bwana, na hivyo kumwezesha Yeye hivi karibuni kukufunua uonekane mbele ya ulimwengu wote. Vinginevyo itakuwa ni kitambo kidogo tu, hautakuwa na ujumbe hata. Hebu akili zenu zisiwe za kushawishiwa na ripoti na uvumi. Tii ushauri: {WHR: 66.1}

“O kwamba Bwana aweze kukuongoza! Kamwe kwa tukio moja usiruhusu uvumi kukuchochea kutenda.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 299. {WHR: 66.2}

“Kamwe, kamwe usishawishike kwa habari.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 507. {WHR: 66.3}

Huenda umeambiwa kwamba hakuna kitu kizuri kinachoweza kutokea mahali hapa. Ndivyo alivyoambiwa Nathanieli kwamba hakuna kitu kizuri kingetokea Nazareti. Ni busara, hata hivyo, kufanya jinsi alivyofanya — “kuja na kuona,” na hivyo, wewe pia, uwe “Mwisraeli kweli kweli, asiye na hila.” Jiepushe kushawishika kwa taarifa, minong’ono, dharau, na uharibifu wa sifa ya tabia njema. Badala yake, tumia kwa uaminif umacho yako,

67

masikio, na akili. Kisha utakuwa na furaha kama yeye, na alikuwa na furaha ilioje! {WHR: 66.4}

Daima kumbuka, pia, kwamba wapo na siku zote watakuwapo wale wanaotarajia nadharia za kidini za kila aina kupatana na Ukweli wa Mbingu uliofunuliwa. Haiwezekani. Wale watakaokuwa Waadventista wa Sabato waaminifu, kwa hivyo, wataweka moyoni vyema onyo linalofuata na ushauri: {WHR: 67.1}

“…Hawa viongozi…huwa hawaangalii uwezekano kwamba wao wenyewe hawajalielewa vizuri Neno. Hawatafungua macho yao kutambua ukweli kwamba wamefafanua visivyo na kuyatumia vibaya Maandiko, na wamejenga nadharia za uongo, wakiziita mafundisho ya msingi ya imani.… Hata Waadventista wa Sabato wako katika hatari ya kuyafumba macho yao kwa ukweli kama ulivyo katika Yesu, kwa sababu unakanusha kitu ambacho wamekichukulia kwa dhati kwamba ni ukweli, ambacho Roho Mtakatifu hufundisha si ukweli.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 70. {WHR: 67.2}

“…Watu wasijihisi kwamba ni haki yao kuupatia ulimwengu lile wanalodhani kwamba ni ukweli, na kukataa kwamba lolote lisipeanwe kinyume cha mawazo yao. Hii si kazi yao. Mambo mengi yataonekana kwa usahihi kama ukweli, ambayo hayatakubalika kwa wale ambao hufikiri ufasiri wao wa Maandiko siku zote ni sawa. Mabadiliko mengi ya uamuzi yatapaswa kufanywa kuhusiana na mawazo ambayo wengine wameyapokea kama yasiokuwa na makosa.” — Shuhuda Kwa Wachungaji, uk. 76. {WHR: 67.3}

Inatarajiwa, pia, kwamba watakuwapo wale ambao Adui atawabembeleza wasisome wala

68

kujadili mafundisho yasio maarufu. Lakini jinsi Mungu aishivyo hakika, Ibilisi anao wote wa aina hii tayari jahanamu milele kabla moto kuwashwa ndani yake! Tunatarajia watatoka sasa wakati bado wanao uwezo. Wanafunzi wenye hekima hawapimi, kwa nadharia za mtu yeyote, dai lolote kwa ukweli wa Biblia. Hulipima kwa Biblia pekee. {WHR: 67.4}

“Njoo muone” nyinyi wenyewe, Wandugu. Wakati huo, tu, mtatambua mbona Bwana anafanya mashtaka mazito dhidi yetu sisi sote Walaodekia: {WHR: 68.1}

“Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ufu. 3:17-20. {WHR: 68.2}

Iweze kueleweka kikamilifu sasa, Wandugu, kwamba kuufungua mlango wa mmoja kwa Bwana hakumaanishi kuyafungua masikio ya mtu kwa wanaoitwa eti wenye hekima ambao kamwe hawaukumbatii ukweli usiokuwa maarufu, hata hivyo siku zote kwa upesi hukimbia na nadharia zao wenyewe. Wafuasi wa Kristo huchukua muda kuchunguza wao wenyewe lile Neno Lenyewe husema, wala si lile maadui wa Mungu hujaribu kufanya liseme. Wanajua kwamba “si mchanga wala mzee anao uhalali wa kumtegemea mwingine kuwa na ujuzi kwa ajili yake. Malaika akasema, ‘Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yake.’ {WHR: 68.3}

69

“Wanaume, wanawake, na vijana, Mungu huwahitaji mmiliki ushujaa wa kimaadili, uthabiti wa kusudi, ustahimilivu na uvumilivu, akili ambazo haziwezi kuchukua madai ya mwingine, lakini ambazo zitachunguza zenyewe kabla kupokea au kukataa, ambazo zitachambua na kupima ushahidi, na kuupeleka kwa Bwana katika sala.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 130. {WHR: 69.1}

Kwa ufupi, watu wa Mungu ni wenye ujasiri, walio na uwazi, wanafunzi wenye bidii, si kama mashine, si wabaguzi wenye kanuni za wakuu wa makanisa, wala wanaopitia kijuu-juu. {WHR: 69.2}

“Ni watu wangapi katika kizazi hiki cha ulimwengu hushindwa kwenda kina kabisa. Wao huchunguza kijuu-juu tu. Hawatafikiri kwa umakini kabisa waone magumu na kuyakabili, na hawachunguzi kila mada muhimu inayokuja mbele yao kwa uchambuzi makini, na kwa sala, na tahadhari ya kutosha na hamu ya kuona uhakika halisi kwenye swala. Wao huzungumzia mambo ambayo hawajayapima kikamilifu na kwa uangalifu.” — Shuhuda, Gombo la 4, uk. 361. {WHR: 69.3}

Adui hakika atatenda yote katika uwezo wake kuwafanya wote kuamini kwamba maandiko yaliyoshughulikiwa hapa yamefasiriwa kimakosa, na ya kwamba Shuhuda “zimechukuliwa nje ya miktadha yake.” Tayari amepanda imara katika mawazo ya walei na ukasisi uongo kwamba “hakuna hitaji la ukweli zaidi na nuru zaidi” (Watenda Kazi wa Injili, uk. 300), na ya kwamba Roho ya Unabii husema hivyo! Uongo huu wote, bila shaka, aliupanda katika mawazo ya watu miaka mingi mbeleni, kwa jitihada za kuwadanganya wateule wa Mungu kuitupilia mbali “lulu ya thamani kubwa.” Mat. 13:46. Ulinzi na utetezi wa pekee kwa mtu yeyote, kwa hivyo, hautakuwa kumruhusu adhibiti akili: wanadamu si farasi kwa wanaowaendesha kuwadhibiti kwa lijamu katika

70

midomo yao. Hebu kila mmoja kwa nguvu adai haki na wajibu aliopewa na Mungu kuweka kila dai la adui kwa kipimo cha tindi kali, na kwa heshima kudai kwamba maadui wa Msajili waonyeshe jambo bora zaidi, au angalau zuri, mahali pa lile Huleta [Msajili] kutoka kwa Maandiko, au vinginevyo waweze kuwa kimya “cha dhahabu” na kuanza kuyachambua Maandiko kwa bidii. Walazimishe watoe sura na fungu, ukurasa na aya, kuthibitisha uhalali wa dhana nyingi wanazonukuu kila mara, “Tuna ukweli wote kutupeleka hadi mwisho;” “Tuna ukweli wote tunaohitaji.” Bila shaka hakuna uthibitisho kwa hayo utaletwa, kwa sababu taarifa kama hizo hazipatikani ndani ya kurasa za Uvuvio. Badala yake ulio kinyume ni ule ukweli, jinsi unavyothibitishwa katika kemeo la kutisha kwa Laodekia kwa kufikiri kwao kimakosa. (Angalia Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253). {WHR: 69.4}

“Wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama Mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.” Ezek. 14:20. {WHR: 70.1}

“… Vile mwanafunzi hutoa kafara uwezo wa kufikiri na kujiamulia mwenyewe, anakuwa mdhaifu wa kutopambanua kati ya ukweli na uongo, na huanguka kuwa windo rahisi kwa udanganyifu. Yeye huongozwa kwa urahisi kufuata utamaduni na desturi …. Akili inayotegemea uamuzi wa wengine ni hakika, punde si punde au baadaye, itapotoshwa.” — Elimu, uk. 230, 231. {WHR: 70.2}

Hatimaye, Wandugu, ninyi ambao ni wanafunzi wa kufahamu wa Biblia na Roho ya Unabii mtakuwa waelekevu sana kwa ukweli kwamba wengi hawawezi tu kutambua kwamba wa Bwana “wa kushtua na wa kuleta mashtaka” kwa

71

Walaodekia (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252) unawalenga wao. Na iwapo watachagua kuendelea kuwa vipofu, hautakuwa na sababu ya kushangaa kwamba matokeo yake wanaukataa huu wa wazi “Ushuhuda usiopinda uliorejeshwa” wa Shahidi Mwaminifu (Watenda Kazi wa Injili, uk. 307) “ambao juu yake hatima ya kanisa huning’inia.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. Wala hautakuwa na sababu ya kushangazwa kwa ukweli uliounganishwa kwamba mpepeto uliosubiriwa kwa muda mrefu (Maandishi ya Awali, uk. 270) utasababishwa na baadhi kuchukua msimamo, pamoja na mjumbe wa Nuru, upande wa Bwana, na wengine kuchukua msimamo wao, pamoja na wawakilishi wa giza, kwa upande wa Adui. {WHR: 70.3}

Wote ambao wamekuwa na uadilifu wa kusoma hadi hapa, na ufahamu wa kutambua Ukweli unapoonekana, hawataenenda tena pamoja na umati wa Ulaodekia, wakiwa bado wanashikilia dhana wanazozipenda kwamba “hawahitaji kitu” (kwamba wanao Ukweli wote unaohitajika kuwapitisha katika Malango ya Lulu), ingawa msimamo huo unamfanya Bwana kuwa muongo! Basi baada ya kujionea wenyewe, Ndugu zangu, je, mtaweza kutambua jinsi ushuhuda wa Bwana ulivyo wa kweli, na kwa moyo wote kusema: “Nilikuwa kipofu, sasa naona.” Yoh. 9:25. “Bwana, … niko hapa, nitume.” Isa. 6: 8. Hapo basi utaona kwamba awamu ya 1844 ya Ujumbe wa Malaika wa Tatu, hukumu ya wafu, katika awamu yake ya awali, si awamu yake, ya mwisho — si hukumu ya walio hai. {WHR: 71.1}

Kwa sababu katika jukumu la kutosamehe mnawiwa na huu ukweli unaookoa kwenu na kwa ulimwengu, je sasa hamtaamua kuitikia mwito wa rehema wa Mungu, na kuyatumia manufaa ya fursa ya kipekee ambayo inawawezesha kujilisha “chakula kwa wakati wake” mkiwa hapa, na kupata Nchi ya Utukufu ng’ambo, bila kuwekeza au

72

kuhatarisha senti moja? Hamna chochote cha kupoteza ila dhambi zenu, hofu yenu, wasiwasi wenu, kutokuwa na uhakika kwenu, machozi yenu, na kufaidika na kila kitu. {WHR: 71.2}

Kamwe usikose kuonekana, hata hivyo, kwamba kusimama kwa ajili ya Ukweli endelevu ni kanuni na mazoezi ambayo yamewahi kuja kwa gharama ya juu sana — mara nyingi ya juu kama vile kuuawa kwa ajili ya imani, na kamwe si chini ya kundolewa kwa ushirika. {WHR: 72.1}

“Kuwaadhibu wale waliodhaniwa kuwa watenda maovu, kanisa limetafuta nguvu za serikali. Wale waliotofautiana na mafundisho yaliyowekwa wamefungwa jela, wameteswa na kuuawa, kwa uchochezi wa watu ambao walidai kuwa wanafanya kazi chini ya idhini ya Kristo. Lakini ni roho ya Shetani, sio Roho ya Kristo, inayochochea matendo kama hayo. Hii ni mbinu ya Shetani mwenyewe kuuleta ulimwengu chini ya ufalme wake. Mungu amewakilishwa vibaya kupitia kanisa kwa njia hii ya kuwashughulikia wale wanaodhaniwa kwamba ni wazushi.” — Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 74. {WHR: 72.2}

Lakini jinsi kanisa leo karibu kila mahali liko chini ya serikali ya nchi, na kwa hivyo halina kabisa uwezo wa kulazimisha adhabu ya kifungo, mateso, na kifo, kama watangulizi wake walivyofanya mara kwa mara, kwa kuadhibu uliodhaniwa kuwa ni uasi, tisho la kutengwa ni tokeo la bei ghali ambayo Dhehebu linaweza kushinikiza kwa yeyote ambaye ataweza kuthubutu kuwaamsha wake wanaolala. Vivyo hivyo, imekuwa silaha yake yenye nguvu zaidi ya kuwashawishi walioamka kughairi na kurudi tena ndani ya usingizi wa Ulaodekia na kulala. Kwa kweli, hata hivyo, hiki: kitendo cha udhalimu chenyewe sasa kinaongeza kutambua, miongoni mwa wafuasi wa Uvuvio, kwamba mawakala wa Shetani wa kupinga wanalitawala kikamilifu Dhehebu,

73

na wanafanya kila wanaloweza kumtupa nje kila mtu anayethubutu kuitii Sauti ya Mungu Mwenye Nguvu zaidi ya sauti ya kaka-mungu wanaoabudiwa, kinyume cha ukweli kwamba limekuwa siku zote likiyashutumu madhehebu mengine kwa kuwatenga wasiokuwa vibaraka. Hakika tulimsikia kwa sauti akishutumu udikteta kama huu si zamani sana yapata miaka kumi na tano iliyopita, wakati, katika uhariri ufuatao, lilitangaza: {WHR: 72.3}

“Dini maarufu imetanga maili nyingi mbali na mitazamo ambayo waasisi wake walikuwa nayo. Ili kuwa mwasi sasa mmoja anahitaji tu kufuata mafundisho yaliyowekwa awali katika jukwaa la dhehebu lake…. {WHR: 73.1}

“Kutupwa nje ya kanisa kwa sababu mmoja anaamini Biblia! Je, hilo si tangazo la kusikitisha kwa dini ya leo? Haishangazi Yesu alisema, ‘Mwana wa Adamu atakapokuja, atapata imani duniani?” — Alonzo Baker, Ishara za Nyakati, Februari 5, 1935, uk. 11. {WHR: 73.2}

Lakini sasa likiruhusu ndani ya nyumba yake yenyewe uovu ule ambao lilikemea kwa nguvu ndani ya mengine, linaachwa kuwa halifai na lisilo na maana kwa kazi yake Takatifu kama angalivyokuwa mbwa bubu (Isa. 56:10) iwapo angewekwa kuilinda nyumba ya bwana wake. Si tu “halitaweza kubweka” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211) lakini halitaweza kuisikia sauti ya Mungu, ikikemea mazoea yake yasio matakatifu, wakati Yeye anaimarisha imani na uvumilivu wa wake “waliotupwa nje,” jinsi ilivyonenwa kinabii katika aya inayofuata: {WHR: 73.3}

“Lisikieni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa kwa sababu ya neno Lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu;

74

lakini watatahayarika.” Isa. 66: 5. {WHR: 73.4}

“Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.” Luka 6:22, 23. {WHR: 74.1}

Wandugu, hebu mfanye uchaguzi mzuri na wa hekima, hakikisha kusimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo, tayari kupanda sahani ya kupaa ya Mbinguni (Maandishi ya Awali, uk. 287, 288) wakati sauti ya tarumbeta, mlipuko ambao utasikika pande zote duniani Mungu anapoimaliza kazi Yake ya hukumu na watu Wake na ukasisi Wake na makao yake makuu — Baraza Kuu. {WHR: 74.2}

Tume ya

Kuajiri Wajumbe. {WHR: 74.3}

>