fbpx

Msimamo wa Uanajeshi wa Wadaudi Waadventista wa Sabato

Msimamo wa Uanajeshi wa Wadaudi Wadventista wa Sabato

0

MSIMAMO WA UANAJESHI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

Asiye-mpiganaji au Mkataaji Kidhamira — Yupi?

Jibu la Uvuvio Wenyewe kwa Wote Kanisa na Serikali

Katika Vita vya 2 vya Dunia, baadhi ya watu wetu walijisajili kama wasio wapiganaji, na wengine kama wakataaji kidhamira, lakini msimamo wa Jumuiya ulikuwa zaidi kwa upande wa kuwasajili wasio wapiganaji, na ombi maalum kwa makubaliano yaliyowekwa katika chombo kifuatacho, kinachoitwa

AZIMIO LA KANUNI ZA MSINGI WA MSIMAMO KWA UTUMISHI WA KIJESHI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO {MSDSDA: 1.1}

MSINGI: Imani ya msingi kabisa, iliyozalishwa na usadikisho wa nafsi yote ya Uvuvio kamili wa Biblia, kimaadili hutuhimiza, kwa kuangalia pakubwa utumishi wa kijeshi, kwa heshima kuwasilisha msimamo uliowekwa humu kwa makini; kushuhudia: {MSDSDA: 1.2}

KANUNI YA KWANZA: “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu …. si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri …. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.” Rum.13:1, 5, 7. {MSDSDA: 1.3}

Kanuni hii ya jiwe la msingi inashinikizwa zaidi kwa dhamiri zetu katika agizo lililowekwa kwetu na Shuhuda kwa Kanisa (mamlaka yetu ya kufasiri): “Watu wa Mungu watatambua serikali ya mwanadamu kama agizo la

1

uteuzi wa Mungu, na watafundisha utiifu kwayo kama jukumu takatifu katika nyanja yake halali.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 402. {MSDSDA: 1.4}

KANUNI YA PILI: Sheria za kikatiba za Agano la Kale (Law. 20:10-14; Kum. 22:22-30), ikiamuru chini ya kipindi hicho hukumu ya kifo kwa kukiuka utakatifu wa nyumba, humuhimiza Mkristo kwa uwajibikaji kutumia hatua zozote zilizo ndani ya uwezo wake kulinda usalama wa mke na watoto. {MSDSDA: 2.1}

KANUNI YA TATU: Historia ya Agano la Kale huonyesha kwamba wakati kanisa lilikuwa serikali ya kitheokrasia na washirika wake wote katika nchi yao (Palestina), walikuwa na jukumu la kutetea nchi yao wanapovamiwa na maadui, au wakati walipoamriwa na Mungu kufanya kwa hivyo kwa sababu zinazopatana na kusudi Lake la milele katika kipindi hicho. {MSDSDA: 2.2}

Kwa hivyo, tungalikuwa katika hadhi kama hiyo leo (na ndugu zetu wote Wakristo katika nchi moja), hatungeweza kuwa wakataaji kidhamira, lakini tungejukumika, Kibiblia, kuilinda nchi yetu, kama walivyofanya Israeli ya zamani kuilinda yao. Walakini, ndugu zetu Wakristo leo wakiwa wametawanyika katika mataifa mengi, jamaa, lugha, na watu, basi nchi hii ijizamishe vitani na nchi nyingine, sisi kama Wakristo katika nchi hii, ikiwa hatutaepushwa kwa utumishi wa kijeshi wa kupigana vita, tutawekwa kupigana dhidi ya Wakristo katika nchi nyingine. {MSDSDA: 2.3}

KANUNI YA NNE: Upo hata hivyo, wajibu wa kuwajali wengine ambao sisi kama Wakristo hatuthubutu kupuuza: jukumu la kujitolea kutoka kwa mfano wa Msamaria mwema (Luka 10:30-37), kuwasaidia waliojeruhiwa ambao huwa nyara za “wanyang’anyi.” Katika nuru ya jukumu hili la upeo la Ukristo, hatungeweza kidhamira “kupitia upande wa pili” wa wenzetu waliojeruhiwa, kama “kuhani” na “Mlawi,” lakini lazima, kama wafuasi wa Bwana, tunakubali kutumika katika nafasi ya wamishonari wa matibabu — wabeba machela, madereva wa ambiulansi, wahudumu, wauguzi, madaktari, au makasisi — kuwahudumia wahitaji, wagonjwa, waliojeruhiwa, na wanaokufa; au kwa njia ya kiroho, kwa wenye afya. {MSDSDA: 2.4}

2

KANUNI YA TANO: Imani yetu, hata hivyo, haikatazi utumishi wetu, isipokuwa kwa siku ya saba ya juma, katika nafasi zingine za asiye-mpiganaji ambazo hazikiuki uadilifu wa kanuni hizo zilizoorodheshwa hapa ndani. {MSDSDA: 3.1}

KANUNI YA SITA: Kama agizo la msingi, kama hiyo nafasi ya siye-mpiganaji, imani yetu, kama ile ya Danieli (Dan. 1:8), huweka juu yetu utaratibu wa kujinyima chakula — ulaji-mboga pekee kamili ambao, kama njia ya kidesturi iliyoanzishwa ya kuishi, itafanya mwili na vile vile kimaadili isiwezekane aidha kwa kuishi kwetu au kujilisha kitoweo chakawaida cha jeshi kwa njia ile ile kama wale ambao hawana majuto ya lishe. {MSDSDA: 3.2}

KANUNI YA SABA: Na tukiwa Wasabato, kuhusika kwetu kwa siku ya saba katika huduma yoyote isiyo ya wapiganaji au mafunzo mengine isipokuwa yale yaliyoorodheshwa chini ya kanuni ya Nne, kunaweza kukiuka hisia zetu za heshima ya kidini katika jambo takatifu la kuitunza Sabato ya kila juma (Jumamosi) (Kutoka 20:8-11). {MSDSDA: 3.3}

TUKATE KAULI: Wakati kanuni ya Kwanza, ya Pili, na ya Tatu zinatuongoza kutia saini Taarifa ya A. Kanuni ya Nne na ya Tano zinazuia upeo wa muunganisho wetu wa asiye-mpiganaji wa kijeshi kwa shughuli zilizoorodheshwa au kuruhusiwa chini ndani yake, kama zinavyostahili kwa kanuni ya Sita na ya Saba. {MSDSDA: 3.4}

HITIMISHO LA KUTEGEMEA: Iwapo mamlaka ya Sheria za Uteuzi wa Utumishi zitaheshimu msimamo uliowekwa mbele hapa ndani — utumishi wa asiye-mpiganaji na lishe ya mboga pekee na haki za Sabato — iliyoamriwa juu yetu kwa imani yetu, sisi basi, kwa dhamiri yote lazima tusaini Taarifa ya A: {MSDSDA: 3.5}

Kwa sababu Mamlaka ya Uteuzi wa Utumishi haikujipata katika nafasi ya kutupatia majibu maradufu (“utumishi wa asiye-mpiganaji na lishe ya mboga pekee na haki za Sabato”) ambayo azimio letu lililotangulia la kanuni zilizowekwa na Maandiko, uamuzi wao ulitufungia kabisa mlango wa uwezekano wa utumishi jeshini katika

3

nafasi yoyote, na kuiacha Jumuiya bila mkondo kimaadili ila ule ambao Maandiko yalifungua kwa mtazamo na ambayo yamewekwa wazi katika aya zifuatazo: {MSDSDA: 3.6}

Wakati Biblia haiwaamuru watu wote kila mahali uaminifu na utiifu kwa “mamlaka ambazo zipo” (serikali za kiraia) kama “zilizowekwa na Mungu” (Rumi 13:1), bado wakati uo huo Huwa inawashikilia kujitoa kabisa na uaminifu wa kuridhia Serikali ya Mungu kuliko zingine zote (Rumi. 13:7; Mat. 22:21; Mdo. 4:19, 20), hivyo kutoruhusu yeyote, awe ni mfalme au raia, nabii au kuhani, kamwe kutoziweka kando sheria za Mungu kwa ajili ya sheria za mwanadamu. Na jinsi mambo yanavyosimama sasa, kushiriki kwetu katika utumishi wa jeshi kutatuhusisha kama Azimio letu linavyofichua, katika ukiukaji wa sheria tatu kuu za Mungu: {MSDSDA: 4.1}

1. Ukiukaji wa Amri ya Nne ya Sheria (Kut. 20:8-11) — Ambayo huzuia kuvunja Sabato. — Hakuna mtu mmoja mmoja au taifa linaloweza kumudu kupuuza ukweli kwamba kuvunja Sabato yenyewe ni mojawapo ya dhambi ambazo ziliwaingiza Waisraeli wa zamani katika mazingira yaliyowanasa katika vita hatari, na matokeo ya mwisho viliwagharimu ufalme wao (Ezek. 20). {MSDSDA: 4.2}

2. Ukiukaji wa amri ya Sita (Kut. 20:13) — Ambayo Huzuia Kuua au Kusaidia Kuua Binadamu. — Na kwa sababu, jinsi Azimio letu la Kanuni linavyoweka wazi, washiriki wa kanisa letu ni miongoni mwa raia si wa taifa moja tu bali wa mataifa

4

yote ulimwenguni kote, basi sisi, kama ndugu katika imani, kwa njia yoyote ile tuweze kujiingiza katika vita na taifa lolote, tutakuwa tunajiunga kwenye vita ambavyo vitakuwa ndugu kumwangamiza ndugu katika imani. Na matokeo yake tutakuwa tukijipiga chapa wenyewe kama wauaji wa raia wa Ufalme wa Mungu unaokuja, na kwa hivyo kama maadui wa Ufalme Wenyewe. {MSDSDA: 4.3}

Kurasa za Biblia zimejazwa na hukumu ya Mbingu kwa uhalifu kama huu. Unaojulikana kati ya huo ni muungano usio halali kati ya mfalme wa Israeli na mfalme wa Shamu dhidi ya ufalme wa Yuda (ufalme umbu wa Israeli). Maandiko mintarafu muungano huu, sio tu hukataza ushirika wa kanisa na serikali yoyote ambao unaweza kumhusisha ndugu kumuua ndugu katika imani, lakini pia humuhakikishia mkiukaji anguko ambalo hakuna uwezekano wa kuamka. Hili linaonekana haraka kutokana na ukweli kwamba ushirika huo haukufanikiwa kuubomoa Yuda; lakini badala yake kwamba Mungu alitumia dola ya uwindaji, Ashuru, haraka sana kuubomoa huo ushirika, kuwaangamiza wafalme wote wawili, na kuwatawanya Israeli na Shamu katika miji yote ya Wamedi, hata ingawa ufalme wa Yuda wenyewe haukuwa umejikabidhi kabisa kwa Mungu. (Angalia Isa 7:2, 7, 8; 8:4, 9-14). {MSDSDA: 5.1}

3. Ukiukaji wa Maagizo Matakatifu ya Vyakula (Law. 11:7, 8). — Kwa mujibu wa unabii unaonena katika siku zetu, Mungu hukataza walio na ufahamu kuhusu unabii huu wasile

5

vyakula vyovyote “najisi,” kama nyama ya nguruwe. Hapa lipo tamko la Uvuvio wa kinabii wenyewe dhidi ya ukiukwaji kama huu: {MSDSDA: 5.2}

“Maana kwa moto na kwa upanga Wake Bwana atateta na wote wenye mwili; na watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.” Isa. 66:16, 17. {MSDSDA: 6.1}

Kushindwa kwetu kwa sababu yoyote kutii agizo hili la Mungu dhidi ya utumiaji wa nyama ya nguruwe kunaweza kuwa sawa na sisi wenyewe kujinyonga, maana tungeweza kweli kumlazimisha Bwana kutuua kwa kukiuka kimakusudi Neno Lake la kinabii la leo, baada ya kupokea kutoka Kwalo nuru maalum dhidi ya dhambi kama hiyo. Uasi wetu katika suala hilo kwa hivyo utasababisha kujitumbukiza wenyewe kimakusudi, kwa mfano katika machinjo ya Bwana. {MSDSDA: 6.2}

Wazi wazi, basi, hatupaswi kuridhia katika mafungamano yoyote ambayo katika asili yake lazima yatuhusishe kuvunja Sabato kuua au kusaidia kuua, au katika kula nyama ya nguruwe au vyakula vyovyote ambavyo Mungu hakuviumba kuliwa na wanadamu. Ukiukaji wa yoyote kwa sheria za Mungu utatufanya kuwa laana kwetu wenyewe na hatari kwa mataifa ambayo tunajikuta ndani yake maana “yeye ajuaye kutenda mema wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.” Yakobo 4:17.

6

Na “mshahara wa dhambi ni mauti.” Rumi. 6:23 {MSDSDA 6.3}

Isitoshe, harakati za amani, sio vita, ndilo jukumu letu kuu leo, kwa maana sisi kama watu tumeagizwa kukuza Ufalme wa amani (Mat. 10.12, 13) kwa kulisha ulimwengu chakula cha kiroho na cha mwili — kwa kukazia akili zetu kwa Neno la Mungu, na mikono yetu kwa jembe na kwenye mundu (Mika 4:3). Hili hatuwezi kufanya iwapo tunaweka akili zetu kwa siasa na mikono yetu kwa upanga na mkuki (Yoeli 3:10). {MSDSDA: 7.1}

Kwa hivyo ili sisi tukuze heshima kwa Mungu na baraka kwa mataifa ambayo sisi ni raia, lazima tuwe waaminifu katika Neno la Mungu kama alivyokuwa Danieli na Waebrania watatu katika Babeli ya zamani, na kama alivyokuwa Yusufu huko Misri ya kale, na hivyo kuwa wamishonari wa kitaifa na vile vile wa kimataifa. {MSDSDA: 7.2}

Kujua vyema kama tunavyofanya kwamba usalama na uwepo wa serikali yoyote kimsingi hutegemea, sio nguvu ya kibinadamu na ya kijeshi, bali kwa uvumilivu na ulinzi wa Mungu, kwa sababu hiyo bado tumelazimika zaidi kutoa utiifu kamili kwa kanuni za Mbingu zinazosimamia jukumu letu kwa nchi yetu. Shurutisho hili la upeo hutegemea hata kwa nguvu inayotushurutisha zaidi ambayo tumewekwa kwa Majaliwa hapa Marekani iliyo huru, kwa sababu ya ukweli wa furaha kwamba kwa haya masaa ya

7

mwisho muhimu ya wakati Yeye ameweka makao makuu ya kanisa hapa ambapo litafurahia uhuru wa kidini wa kipekee, kufanya kazi kwa uhuru, na kutekeleza bila kizuizi wajibu wake ulioteuliwa na Mungu ulimwenguni kote. {MSDSDA: 7.3}

Kuipenda nchi yetu hivyo na uzalendo wa kweli wa Ukristo, tunaweza kufanya wema mkubwa, ilhali tuthubutu kujiingiza katika utumishi wa kijeshi, dhamiri zetu zikiwa zimepondeka jinsi ambavyo zingekuwa kama tungekiuka sheria za Mungu, haswa baada ya kuangaziwa kupitia kwa unabii mpya uliofunuliwa, tutakuwa laana na hivyo bila manufaa yoyote kwa jeshi, kuitetea nchi yetu na Ukristo, kuliko mbwa mlinzi bubu kwa bwana wake, au farasi anayechechemea kwa msafara wa farasi, na sio bora kuliko raia msaliti kwa nchi yake. {MSDSDA: 8.1}

Kinyume chake, hata hivyo, kuzingatia kwetu kabisa maagizo ya Mungu, tukifanya lile Yeye angetaka tufanye, ili kutuwezesha kusali “sala ya bidii ya mwenye haki,” ambayo “hufaa sana” (Yakobo 5:16), lazima kwa hitaji itufanye ngome imara dhidi ya uchokozi wowote — dhidi ya maingilio yoyote kwa Demokrasia au kwa Ukristo. Mwanzo 18:23-33 hufichua kwamba kama Mungu angepata watu kumi tu katika Sodoma na Gomora, angaliweza kuiepusha miji hiyo kutoka kwa adhabu ya milele ambayo ilikuwa yao. Yeye hatakosa kufanya hivyo leo. {MSDSDA: 8.2}

8

Labda mfano thabiti zaidi wa Maandiko kwa ubatili wa mmoja kujaribu kukwepa jukumu lake alilopewa na Mungu, ni ile kesi maarufu ya nabii Yona, kwa upande mmoja, alipanda meli kwenda Tarshishi kwa kutamaushwa kukimbia kazi ngumu ambayo Mungu alikuwa amempa — kuonya Ninawi; na Mungu kwa sababu hiyo, kwa upande mwingine, alizidhihirisha nguvu Zake kwa kuvuruga juhudi duni, zenye makosa za nabii, ambazo zilimleta dafrao na janga ambalo, kwa upande wake, lilimshtua atambue uoga mkubwa kwa jukumu lake alilopewa na Mungu, na kuwawezesha mabaharia kutambua sauti ya Mungu ikitamka hukumu ya Yona kupitia kwake mwenyewe, na kudai wamtupe baharini. Laiti Mungu asingeamua kushinda na Yona, na mabaharia, na bahari, kungekuwa na msiba kwa kila nafsi sio tu melini bali pia katika mji mkuu, Ninawi. Lakini mwishowe Yona alipojiona anakuwa hatari kwa wanadamu kwa kuepuka jukumu alilopewa na Mungu, na mabaharia wale walivyoitii kwa uzito Sauti ambayo ilinena kupitia kwake, Mungu aliwaopoa wote kwa taabu hivi kwamba hakuna mtu aliyepatwa na janga. Ungekuwepo kwa hivyo upumbavu wa jinai katika kufuata kwetu mwenendo wowote wa kukwepa wajibu ambao utaweza tu kutuletea adhabu yenye dhiki sana na maafa. {MSDSDA: 9.1}

Kumbukumbu ya historia ya kusikitisha hushuhudia tena na tena kwa ukweli usiopingika kwamba nguvu na usalama wa taifa lolote hutegemea

9

kwanza kwa imani ambayo serikali hupatana na Neno la Mungu huwapa watu Wake haki katika serikali yao, na pili kwa namna ya utendeaji na ulinzi ambao serikali huwapatia. Kwamba ni kwa kanuni hii ya Mungu ambayo serikali yoyote au watu lazima wasimame kwayo, au vinginevyo waanguke, huthibitishwa kidete kwa kesi zifuatazo: {MSDSDA: 9.2}

1. Misri — {MSDSDA: 10.1}

“Farao akawaambia watumwa wake, tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.” Mwa 41:38-41. {MSDSDA: 10.2}

Katika tokeo la kufurahisha la uaminifu wa Yusufu kwa Mungu na jinsi Farao alivyomtendea Yusufu, Mungu hakuuokoa ulimwengu wa siku hiyo kutokana na njaa, lakini pia alikikweza na kukitajirisha kiti cha enzi cha Farao kuliko viti vyote vya enzi vya siku yake. {MSDSDA: 10.3}

2. Amoni na Moabu — {MSDSDA: 10.4}

Kwa sababu Waamoni na Wamoabu walikataa kuwapa watu wa kale wa Mungu

10

usaidizi na kuwalaki walipokuwa wakipitia nchi za Amoni na Moabu, wao kwa tokeo walijiletea wenyewe hukumu kali iliyotabiriwa katika andiko lifuatalo: {MSDSDA: 10.5}

“Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele; kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize. Lakini Bwana, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; Bwana, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda Bwana, Mungu wako. Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele.” Kumb. 23:3-6. {MSDSDA: 11.1}

Kwetu sisi, kwa hivyo, kushindwa kuwa wakweli kwa kanuni na viwango vya Mbingu, vilivyowekwa kwetu haswa, kutatufanya kuwa wajanja zaidi wa mapinduzi, maadui sio tu kwa serikali ya Mungu na kwetu sisi wenyewe binafsi bali pia laana kwa serikali ambazo tunajikuta chini yazo. Hakika, tungalikuwa hivyo kushindwa kutii kwa maarifa yetu ya haki, tungekuwa tunaupotosha Ukristo na Demokrasia, tukizalisha unafiki, na kwa matokeo yake kuhatarisha maisha ya Taifa na Kanisa. {MSDSDA: 11.2}

11

Kwa sababu shauku yetu kuu na kusudi ni kufanya yote kwa nguvu zetu kwa ajili ya ushindi na uhifadhi wa Ukristo na Demokrasia, jukumu letu limefafanuliwa waziwazi na kwa dhati kwetu — kwa uaminifu tusalie kuwa thabiti kwa Nguvu pekee inayoweza kuleta ushindi na ukombozi wa Kanisa na Serikali. Iwapo tu watiifu kwa Mapenzi Yake, na ikiwa Serikali yenyewe wala haihitilafiani nasi kwa zoezi la wajibu wetu kwa Mungu wala vinginevyo kwenda kinyume cha Neno la Mungu, nchi yetu haina haja ya kuogopa chochote. Mungu ataiokoa kwa huruma kama alivyookoa Ninawi, na kuiokoa kwa utukufu kama Alivyookoa, bila majeruhi, majeshi ya Israeli kutoka kwa majeshi ya Farao, kwa Bahari ya Shamu. {MSDSDA: 12.1}

Kwa mtazamo wa vigezo hivi vyote na mifano ya kihistoria, tunaamini kwamba inaweza kueleweka kwamba imani yetu isiyosita-sita kwa Mungu na sala na juhudi zetu kumtumikia Yeye, pia heshima ya Serikali kwa imani yetu kwa Mungu, lazima iwe msaada mkuu wa umilele kwa nchi yetu kuliko chochote kidogo katika utumishi jeshini kwa kukiuka sheria ya Mungu, na kwa kuipuuza kazi Yake, kungeongeza uwezo wa kibinadamu katika nguvu ya jeshi la nchi. (Tazama Isaya 8:9, 10). {MSDSDA: 12.2}

Israeli walitembea kwa unyenyekevu na uadilifu mbele Yake, Mungu alitembea bega kwa bega pamoja nao, na hawakushindwa. Lakini walipomwacha Yeye, Yeye

12

akawaacha, nao wakaanguka windo rahisi kwa mataifa. Vivyo hivyo, taifa lolote ambalo humsahau na kuwadhulumu watu Wake, limeangamia. Shuhudia anguko la falme hizo kuu za ulimwengu — Misri, Ashuru, Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Rumi. Ukuu wa enzi na utukufu wa falme zao za zamani zilizokuwa za majivuno zimetoweka kabisa kutoka kwa nchi, na zote zimesahaulika, na falme zao zilizokuwa zenye nguvu hulala zimevunjika mavumbini kwa sababu tu zilikataa kutembea na Mungu. {MSDSDA: 12.3}

Ni lazima ikumbukwe, pia, kwamba yapo matukio ya mara kwa mara, jinsi Maandiko Matakatifu hufunua, ya kwake Yeye kutumia mataifa yasiyomcha Mungu kuyaadhibu yale yanayodai kumwamini na kumfuata Mungu, lakini ambayo tabia zao za kinafiki zilitia uongo madai yao. (Angalia 2 Mambo ya Nyakati 36:14-21). Hili Yeye hutenda ili kuwaamsha kwa ukweli kwamba wamekuwa wanafiki. Mashuhuri kati ya mataifa kama hayo lilikuwa la Ashuru na Babeli — yale ambayo Mungu alitumia kuadhibu Israeli iliyoasi. (Angalia 2 Wafalme 17; 2 Mambo ya Nyakati 36). {MSDSDA: 13.1}

Ni bayana, basi, kwamba kuadhibu taifa lolote la uasi na lenye unafiki, Mbingu inaweza kutuma juu yake mjeledi mwekundu wa Ukomunisti usioamini (ingawa Maandiko huhakikisha kwamba halitafanikiwa katika mapambano ya ukuu wa ulimwengu kwa sababu kwamba mwisho wake usiomcha Mungu ni kufutilia mbali Ukristo kutoka kwa uso wa dunia). Je! Ulimwengu wa Ukristo ujikute hivyo umenyenyekezwa mikononi mwa watesi wasio mcha Mungu,

13

basi unapaswa kujua kwa hakika kwamba wokovu wake pekee ni kumrudia Mungu kwa toba. Hukumu kamili ambayo Ubolshevisti [Ukomnisti] kafiri ulileta kwa zari [watawala] na kwa raia wao takribani miongo mitatu iliyopita kwa kuharibu dini ya Ukristo hakika haiwezi kusahaulika. {MSDSDA: 13.2}

Mifano ya Maandiko iliyotajwa hapa ndani (mbali na mingine hatutachukua muda wa kutaja) hutoa maagizo na ushauri kwa mataifa na watu wote kwamba “Maana kupata cheo hakuji kutoka mashariki wala magharibi, wala nyikani. Bali Mungu Ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.” Zab. 75:6, 7. {MSDSDA: 14.1}

Mungu atangaza zaidi: “Wakati wo wote Nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuung’oa, na kuuvunja, na kuuangamiza; ikiwa taifa lile Nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake Nitaghairi, Nisitende mabaya yale Niliyoazimia kuwatenda. Na wakati wo wote Nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda, ikiwa watatenda maovu mbele ya macho Yangu, wasiitii sauti Yangu, basi Nitaghairi, Nisitende mema yale Niliyoazimia kuwatendea.” Yer. 18:7-10. {MSDSDA: 14.2}

“… Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni Wake. Yeye hubadili majira na nyakati; Huuzulu wafalme.” Dan. 2:20, 21. {MSDSDA: 14.3}

14

“… Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, Naye humpa amtakaye, tena Humtawaza juu yake aliye mnyonge. “ Dan. 4:17. {MSDSDA: 15.1}

Soma pia Isaya 8:9-14. {MSDSDA: 15.2}

Mwishowe, maadamu katika sababu haswa ya mambo hakuna kitu kinachoweza kuwa matokeo ya bahati, au tukio la bahati nasibu, lakini badala yake kila kitu lazima kiwe ni tokeo la aidha ubunifu wa Majaliwa au itikio la Majaliwa, inafuatia kwamba uwepo wa Muswada wa Haki kikatiba (ambao uliifanya nchi yetu kuwa kuu zaidi kati ya mataifa), na vigezo vilivyoingizwa na mpango ambao sasa hutokea kwavyo hadi kwa “mkataaji kidhamira” mwaminifu, i katika majaliwa ya Mungu. Tunaamini, kwa hivyo, kwamba Bwana amevuvia maandalizi halali ya mpangilo kama huu ili watu Wake waweze kuichagua kulingana na Mapenzi Yake; kwamba Yeye humtarajia kila mwanafunzi anayemwamini Mungu na anayefuata Ukweli kuchukua msimamo wake katika uaminifu kwa usadikisho wa dhamiri aliyopewa na Mungu na yenye kutiwa nuru na Mungu. {MSDSDA: 15.3}

Wazi wazi, basi, kujaribu kwetu kusomea kupigana vita kungeleta tu hasara kabisa si kwetu sisi wenyewe na kwa serikali zetu, haswa, lakini pia kwa Udemokrasia na Ukristo, kwa ujumla. Lililo dhahiri kabisa, basi vigezo vikuu vya utiifu na uaminifu kwa Mungu, mapenzi mema na

15

amani kwa watu wote, na kujitolea kwetu kwa Udemokrasia na Ukristo, kunaacha bila udhuru sio sisi tu ikiwa tutashindwa kuomba mpango wa mkataaji kidhamira (I-O) lakini pia serikali iwapo itashindwa kutoa uhuru wa kidini na usalama kwa mfuasi yeyote halisi wa Kristo na Bibilia. {MSDSDA: 15.4}

——–O——-

RATIBA YA KAZI KWA I-O

Maelezo ya Mpango wa Kazi ya lazima wa Wakataaji Kidhamira (I-O) yanaweza kupatikana kwa kuiandikia Kamati Kuu ya Wakataaji Kidhamira. Chumba 300, 2006 Barabara ya Walnut, Filadelfia, Pennsylvania. Uliza ripoti ya kina iliyorudufishwa ya kurasa kumi na sita na George Loft kwa umekanika wa mpango wa kazi ya kiraia kama unavyofanya kazi sasa. Nakala moja moja ni bure. {MSDSDA: 16.1}

16

La Hivi Punde la Serikali Jedwali la Mpangilio

I-A Anayepatikana kwa jukumu la jeshi. {MSDSDA: 17.1}

I-A-O Mkataaji Kidhamira anayepatikana kwa jukumu lisilo la Mpiganaji. {MSDSDA: 17.2}

I-O Mkataaji Kidhamira anayepinga yote jukumu la Mpiganaji na asiye mpiganaji na anayepatikana kwa kazi za kiraia. {MSDSDA: 17.3}

I-S Mwanafunzi wa Shule ya Upili, I-S (H), chini ya miaka ishirini; au mwanafunzi wa chuo, 1S (C), ambaye amepokea amri ya kuripoti kwa kusajiliwa na amekawishwa kukamilisha mwaka wake wa shule. {MSDSDA: 17.4}

II-A Aliyekawishwa kwa ajira muhimu isipokuwa kilimo na masomo. {MSDSDA: 17.5}

II-C Aliyekawishwa kwa ajira muhimu ya kilimo. {MSDSDA: 17.6}

II-S Aliyekawishwa kwa masomo. {MSDSDA: 17.7}

I-D Mshirika wa kitengo cha akiba cha vikosi vya jeshi. {MSDSDA: 17.8}

III-A Aliyekawishwa kwa utegemezi IV-A Hati ya jukumu la Vita vya 2 vya Dunia. IV-B Afisa aliyekawishwa na sheria. {MSDSDA: 17.9}

IV-C Wageni fulani. {MSDSDA: 17.10}

IV-D Mchungaji au mwanafunzi wa wakati wote anayejiandaa kwa ukasisi chini ya maelekezo ya kanisa linalotambulika au jumuiya ya kidini. {MSDSDA: 17.11}

IV-F Waliokawishwa kwa wapungufu wa mwili, kiakili, au kiakili. {MSDSDA: 17.12}

V-A Waliozidi umri. {MSDSDA: 17.13}

I-W C.O. waliopewa kazi katika utumishi wa kiraia. Baada ya kumaliza utumishi au kuondolewa mapema, C.O. wameorodheshwa I-W (R) hadi kupitisha umri wa jukumu la usajili wakati wamepangiliwa tena V-A. {MSDSDA: 17.14}

I-C Mwanajeshi. Msajiliwa yeyote aliyetengwa na jeshi na kuhamishiwa kwa wa akiba ameorodheshwa I-C (Mkazi) na wale walioondolewa wameorodheshwa I-C (Huru) hadi wamepitisha umri wa jukumu la usajili wakati watakapopangwa tena V-A. {MSDSDA: 17.15}

Kila msajiliwa anapaswa kupangiliwa katika mpangilio wa chini kabisa ambao anastahiki kulingana na kiwango katika jedwali hapo juu na 1A kikichukuliwa kuwa cha juu zaidi na I-C kikichukuliwa kuwa ya chini zaidi. {MSDSDA: 17.16}

17

 

>