04 Mar Misingi Ya Imani Na Mipangilio Orodha Ya Wadaudi Waadventista Wa Sabato
Msingi Wa Imani Na Mipangilio Orodha
Ya
Wadaudi Waadventista Wa Sabato
“Pigeni tarumbeta katika Zayuni, Pigeni kelele katika mlima wangu mtakatifu.”
1
MSINGI WA IMANI NA MIPANGILIO ORODHA
Ya
Wadaudi Wadventista Wa Sabato
Kilichapishwa mnamo 1943
Kilichapishwa tena 1997
1
“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia.” {FB: 2.1}
Isa. 60: 1
“Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia.” {FB: 2.2}
Yoeli 2: 1
“Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” {FB: 2.3}
Isa. 58: 12
2
MSINGI WA IMANI
Ukijitokeza mwaka wa 1930 kutoka ndani ya dhehebu la Waadventista wa Sabato (“kanisa la Walaodekia”), Ushirika wa Wanadaudi Waadventista wa Sabato umekabidhiwa kazi ya kiunabii (ilivyotabiriwa katika Isaya 52: 1) ya kuliandaa kanisa la Laodekia, la mwisho na “magugu” kati ya “ngano,” kwa ajili ya kutangaza injili “duniani kote.” Mat. 24:14. {FB: 3.1}
Ushirika huu, kwa pamoja na dhehebu la Waadventista wa Sabato, una ‘imani fulani za msingi, sifa kuu ambazo, pamoja na marejeleo ya Maandiko ambayo juu yake imejengwa,’ mwanzoni imefanywa muhtasari kama ifuatavyo: {FB: 3.2}
“1. Kwamba Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Jipya yalitolewa kwa uvuvio wa Mungu, yanasheheni ufunuo wa kutosha wa mapenzi Yake kwa wanadamu, na ni kanuni isiokosea ya imani na desturi. 2 Tim. 3: 1517. {FB: 3.3}
“2. Kwamba Uungu, au Utatu, huhusisha Baba wa Milele, wa pekee, Kiumbe cha kiroho, Mwenye nguvu, Aliye Mahali Pote, Anayejua yote, asiye na kikomo kwa hekima na upendo, Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Baba wa Milele, ambaye kwa Yeye vitu vyote viliumbwa na kupitia Kwake wokovu wa majeshi ya waliokombolewa utatimizwa;
3
Roho Mtakatifu, kiumbe cha tatu cha Uungu, nguvu kuu ya urejesho katika kazi ya ukombozi. Mat. 28:19. {FB: 3.4}
“3. Kwamba Yesu Kristo ni Mungu hasa, akiwa wa maumbile sawa na asili kama Baba wa Milele. Alipokuwa akihifadhi asili yake ya Uungu Alijitwalia asili ya familia ya kibinadamu, aliishi duniani kama mwanadamu, alionyesha katika maisha Yake kama Mfano wetu kanuni za haki, zilithibitisha uhusiano Wake na Mungu kwa miujiza mingi ya nguvu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu msalabani, akafufuliwa kutoka kwa wafu, na akapaa kwa Baba anakoishi milele ili kutuombea. Yoh. 1: 1, 14; Ebr. 2: 9-18; 8: 1, 2, 4: 14-16; 7:25 {FB: 4.1}
“4. Kwamba kila mtu ili kuupata wokovu lazima apitie uzoefu wa kuzaliwa upya, kwamba huu unajumuisha mabadiliko yote ya maisha na tabia kwa nguvu ya kuumba upya ya Mungu kupitia imani katika Bwana Yesu Kristo Yohana 3:16, Mathayo 18: 3; Matendo 2: 37-39. {FB: 4.2}
“5. Ubatizo ni ibada ya kanisa la Kikristo na unapaswa kufuata toba na msamaha wa dhambi. Katika maadhimisho yake imani inaonyeshwa katika kifo, mazishi, na ufufuo wa Kristo. Kwamba mtindo sahihi wa ubatizo ni kwa kuzamishwa. Warumi 6: 1-6; Matendo 16: 30-33. {FB: 4.3}
“6. Kwamba mapenzi ya Mungu jinsi yanavyohusiana na mienendo ya maadili yanaelezwa katika sheria Yake ya amri kumi, kwamba hizi ni kanuni
4
zisizobadilika, kuu za maadili, zinazowaunganisha wanadamu wote, katika kila kizazi. Kutoka 20: 1-17. {FB: 4.4}
“7. Kwamba amri ya nne ya sheria hii isiyobadilika huhitaji kuadhimisha Sabato ya siku ya saba. Hii taasisi takatifu wakati huo huo ni ukumbusho wa uumbaji na ishara ya utakaso, ishara ya pumziko la anayeamini kutoka kwa kazi zake za dhambi , na kuingia kwake ndani ya pumziko la nafsi ambalo Yesu huahidi kwa wale wanaokuja Kwake (Mwa. 2: 1-3; 1, Kut. 20: 8-11, 31: 12-17; Ebr. 4: 1- 10. {FB: 5.1}
“8. Kwamba sheria ya amri kumi huonyesha wazi dhambi, ambayo adhabu yake ni kifo. Sheria haiwezi kumwokoa mkosaji kutoka kwa dhambi yake, wala kumpa uwezo wa kumzuia kutenda dhambi. Kwa upendo wa milele na rehema, Mungu hutoa njia ambapo hili linaweza kufanywa. Yeye hutoa mbadala, hata Kristo Mwenye Haki, kufa kwa niaba ya mwanadamu, na ‘Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.’ 2 Kor. 5:21. Kwamba mmoja huhesabiwa haki, sio kwa utiifu wa sheria, ila kwa neema iliyo katika Kristo Yesu. Kwa kumkubali Kristo, mwanadamu anapatanishwa na Mungu, anahesabiwa haki kwa damu Yake kwa ajili ya dhambi za zamani, na kuokolewa kutoka kwa nguvu za dhambi kwa maisha yake ya ndani. Hivi injili inakuwa ‘nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila aaminiye.’ Uzoefu huu unafanywa na uwakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humhakikishia habari ya dhambi na kumwongoza hadi kwa Mbeba-Dhambi,
5
kumshawishi aaminiye kuingia agano jipya la uhusiano, ambapo sheria ya Mungu inaandikwa moyoni mwake, na kupitia uwezo unaomwezesha wa Kristo anayekaa ndani, maisha yake yanaletwa kufanana kabisa na maagizo ya Mungu. Heshima na sifa za mabadiliko haya ya ajabu zote ni zake Kristo. 1 Yoh. 3: 4; Rum. 7: 7; Rum. 3:20; Efe. 2: 8-10; 1 Yoh. 2: 1, 2; Rum. 5: 8-10; Gal. 2:20; Efe. 3:17; Ebr. 8: 8-12. {FB: 5.2}
“9. Kwamba Mungu ‘pekee ana hali ya kutokufa.’ 1 Tim. 6:15. Mwanadamu wa uvumbi humiliki asili aliyoridhi ya dhambi na ya kufa. Uzima wa milele ni zawadi ya Mungu kwa njia ya imani ndani ya Kristo. Rum. 6:23. “Yeye aliye na Mwana anao uzima.” 1 Yoh. 5:12. Hali ya kutokufa watapewa waadilifu wakati wa ujio wa pili wa Kristo, wakati watakatifu waliokufa wanafufuliwa kutoka makaburini na wenye haki walio hai wanahamishwa kumlaki Bwana. Kisha inakuwa kwamba wale waliohesabiwa kuwa waaminifu ‘wanavaa kutokufa.’ 1 Kor. 15: 51-55. {FB: 6.1}
“10. Kwamba hali ya mtu katika kifo ni ile ya kukosa fahamu. Kwamba watu wote, wema na wabaya sare, wanasalia kaburini tangu kifo hadi kwa ufufuo. Mhu. 9: 5, 6; Zab. 146: 3, 4; Yoh. 5:28, 29. {FB: 6.2}
“11. Kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote waadilifu na waovu. Ufufuo wa waadilifu utafanyika wakati wa ujio wa pili wa Kristo; ufufuo wa waovu utafanyika miaka
6
elfu baadaye, mwishoni mwa milenia. Yoh. 5:28, 29; 1 Thes. 4: 13-18; Ufu. 20: 5-10. {FB: 6.3}
“12. Kwamba mwishowe wadhambi wasiotubu, Shetani akiwamo, mwasisi wa dhambi, atapunguzwa, kwa moto wa siku ya mwisho hadi kwa hali ya kutokuwa hai na kuwa kana kwamba hakuwa, na hivyo kuusafisha ulimwengu wa dhambi na wadhambi. Rum. 6:23, Mal. 4: 1-3, Ufu. 20: 9, 10; Obadia 16. {FB: 7.1}
“13. Kwamba hakuna kipindi cha unabii [kumaanisha kuweka muda wa kiunabii wa tarehe kamili ya kuja kwa Kristo] kimepeanwa katika Biblia kufikia ujio wa pili, ila kwamba kile kirefu zaidi siku 2300 za Dan. 8:14, kilikoma mwaka wa 1844, na kutuleta kwa tukio linaloitwa kupatakasa patakatifu. {FB: 7.2}
“14. Kwamba hekalu la kweli, ambalo hema ya duniani ilikuwa mfano, ni hekalu la Mungu lililo Mbinguni, ambalo Paulo hulizungumzia katika Waebrania 8 na kuendelea, na ambalo Bwana Yesu kama kuhani wetu mkuu, ni mtumishi; na kazi ya ukuhani ya Bwana wetu ni uakisi wa kazi ya Kuhani wa Kiyahudi wa enzi ya awali; kwamba hili hekalu la mbinguni ndilo la kutakaswa mwishoni mwa siku 2300 za Dan. 8:14; kutakaswa kwalo kukiwa, kama katika mfano, kazi ya hukumu, ikianza na kuingia Kristo kwa awamu ya hukumu ya huduma Yake katika hekalu la mbinguni kivuli chake katika
7
huduma ya la duniani ya kulitakasa hekalu kwa siku ya upatanisho. Kazi hii ya hukumu katika hekalu la mbinguni ilianza maka wa 1844. Kukamilika kwake kutafunga rehema kwa mwanadamu. {FB: 7.3}
“15. Kwamba Mungu, katika wakati wa hukumu na kulingana na kujishughulisha Kwake kwa usawa na jamii ya wanadamu kuwaonya juu ya matukio yanayokuja ya umuhimu yanayoathiri hatima yao (Amosi 3: 6, 7), hutuma umbele utangazaji wa unavyojongea ujio wa pili wa Kristo; kwamba kazi hii inawakilishwa na malaika watatu wa Ufunuo 14, na kwamba ujumbe wao mara tatu huleta kwa mtazamo kazi ya matengenezo ya kuwaandaa watu kukutana Naye wakati wa kuja Kwake. {FB: 8.1}
“16. Kwamba wakati wa kupatakasa patakatifu, unaambatana na kipindi cha kuutangaza ujumbe wa Ufunuo 14, ni wakati wa hukumu ya upelelezi, kwanza kuhusu wafu, na pili, kuhusu walio hai. Hukumu hii ya upelelezi inaamua ni nani kati ya makumi ya maelfu wanaolala katika mavumbi ya dunia wanastahili sehemu katika ufufuo wa kwanza, na ni nani wake walio hai wanastahili kuhamishwa bila kuonja mauti. 1 Pet. 4:17, 18; Dan. 7:9, 10, Ufunuo 14: 6, 7, Luka 20:35. {FB: 8.2}
“17. Kwamba wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa watu wakumcha Mungu, wasioiga misemo ya uovu na maadili yasiyo ya kawaida wala wasiambatane na njia zisizo za haki za dunia, wasiopenda anasa zake za dhambi wala kuupokea upuuzi wake.
8
Kwamba aaminiye anapaswa kuutambua mwili wake kama hekalu la Roho Mtakatifu, na kwamba kwa hivyo anapaswa kuufunika mwili huo kwa mavazi safi, nadhifu na ya heshima. Zaidi ya hayo, kwamba katika kula na kunywa na katika mkondo wake wote wa mazoea anapaswa kuyageuza maisha yake kama inavyotakiwa kuwa mfuasi wa Mwalimu mpole na mnyenyekevu. Hivi aaminiye ataongozwa kujiepusha na vinywaji vyote vya sumu, tumbaku, na dawa zingine za kulevya, na kujizuia kila tabia na mazoea ya kuutia unajisi mwili na roho. 1 Kor. 3:16, 17; 9:25; 10:31: 1 Tim. 2: 9, 10; 1 Yohana 2: 6. {FB: 8.3}
“18. Kwamba kanuni takatifu ya zaka na sadaka kwa ajili ya kuunga mkono injili ni kuutambua umiliki wa Mungu katika maisha yetu, na kwamba sisi ni wasimamizi ambao wanapaswa kumpa hesabu juu ya yote Ameweka kwa umiliki wetu. Law. 27:30; Mal 3: 8-12; Mat. 23:23; 1 Kor. 9: 9-14, 2 Kor 9: 6-15 {FB: 9.1}
“19. Kwamba Mungu ameweka ndani ya kanisa lake karama za Roho Mtakatifu, kama zilivyoorodheshwa katika 1 Wakorintho 12 na Waefeso 4. Kwamba karama hizi hufanya kazi kwa uwiano na kanuni za Mungu za Biblia, na zimetolewa kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu , kazi ya ukasisi, na kuujenga mwili wa Kristo. Ufu. 12:17, 19:10; 1 Kor 1: 5 {FB: 9.2}
“20. Kwamba ujio wa pili wa Kristo ni tumaini kubwa la kanisa, kilele kikuu cha injili na mpango wa wokovu. Kuja kwake kutakuwa halisi, binafsi,
9
na dhahiri. Matukio mengi muhimu yatahusishwa na kurudi Kwake, kama vile ufufuo wa wafu, kuangamizwa kwa waovu, utakaso wa dunia, tuzo ya wenye haki, kuanzishwa kwa ufalme wake wa milele. Utimilifu karibu wote wa safu mbalimbali za unabii hasa ule uliyomo katika vitabu vya Danieli na Ufunuo, na hali zilizopo katika ulimwengu wa kimwili, kijamii, kiviwanda, kisiasa na kidini, zinaonyesha kwamba kuja kwa Kristo ‘kumekaribia, hata kwenye malangoni. ‘Wakati kamili wa tukio hilo haujatabiriwa. Waumini wanahimizwa kuwa tayari, kwa maana ‘katika saa ile msiyodhani, Mwana wa Adamu’ atafunuliwa. Luka 21: 25-27; 17: 26-30; Yoh. 14: 1-3; Mdo. 1: 9-11; Ufu. 1: 7; Ebr. 9:28; Yak. 5: 1-8; Yoeli 3: 9-16; 2 Tim. 3: 1-5; Dan. 7:27; Mat. 24:36, 44. {FB: 9.3}
“21. Kwamba utawala wa Kristo wa milenia hufunika kipindi kati kati ya ufufuo wa kwanza na wa pili, wakati ambapo watakatifu wa vizazi vyote watakaa pamoja na Mwokozi wao Mbarikiwa Mbinguni. Mwishoni mwa milenia, Mji Mtakatifu na watakatifu wote watashuka kwa dunia. Waovu, waliofufuliwa katika ufufuo wa pili, wataenea juu ya uso wa dunia na Shetani kiongozi wao ili kuizingira kambi ya watakatifu, wakati moto utashuka kutoka kwa Mungu Mbinguni na kuwateketeza. Katika moto mkubwa ambao unamwangamiza Shetani na jeshi lake, dunia yenyewe itaumbwa
10
upya na kutakaswa kutokana na madhara ya laana. Hivi ulimwengu wa Mungu utatakaswa kutoka kwa uchafu wa doa la dhambi. Ufu. 20; Zek. 14: 1-4; 2 Petro 3: 7- 10. {FB: 10.1}
“22. Kwamba Mungu ataumba vitu vyote upya. Dunia, kurejeshwa kwa uzuri wake wa awali, itakuwa milele makao ya watakatifu wa Bwana. Ahadi kwa Abrahamu, kwamba kwa njia ya Kristo yeye na uzao wake wataimiliki dunia katika vizazi visivyokoma vya milele, itatimizwa. Ufalme na utawala na ukuu wa ufalme chini ya mbingu zote utapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu ambaye ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zote zitamtumikia na kumtii Yeye. Kristo, Bwana, atatawala kwa ukuu na kila kiumbe kilicho mbinguni na duniani na chini ya nchi, na vile vilivyo baharini vitatoa baraka na heshima na utukufu na nguvu kwa Yeye anayeketi juu ya kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo milele na milele (Mwa. 13: 14-17, Rum. 4:13, Ebr. 11: 8-16, Mat. 5: 5, Isa. 35, Ufu. 21: 1-7; Dan. 7 : 27; Ufu. 5:13. “ Kitabu cha Mwaka cha Dhehebu la Waadventista wa Sabato, Toleo la 1940, kr. 5-8. {FB: 11.1}
KATIKA NYONGEZA kwa misingi hii ya imani inayoshikiliwa sawa na Waadventista wa Sabato, Ushirika wa Wanadaudi unashikilia: {FB: 11.2}
1. Kwamba karama ya unabii katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (kupitia
11
chombo ambacho kanisa lilianzishwa mwaka wa 1844 na kukuzwa na kudumishwa kwa miongo saba) kilikoma udhihirisho wake mwaka wa 1915 na hakikudhihirishwa tena hadi mwaka wa 1930, na kwamba kikomo hiki na udhihirisho huu ni sambamba na kukoma karama ya unabii katika Agano la Kale na udhihirisho wake katika Agano Jipya. {FB: 11.3}
2. Kwamba ulidhihirisho wa sasa ulipangwa kulingana na unabii wa miaka 430 wa Ezekieli 4, na ya kwamba ndiyo “Nyongeza” iliyotarajiwa katika Maandishi ya Awali, uk. 277. {FB: 12.1}
3. Kwamba kilidhihirishwa upya katika kazi ya kufunga kwa kanisa ili kutekeleza kutiwa muhuri watumwa 144,000 wa Mungu (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), na kupeana nguvu na msukumo (Maandishi ya Awali, uk. 277) kwa Ujumbe wa Malaika Watatu (Ufu. 14: 6-11) ili kwamba watumwa 144,000 wajazwe nguvu waweze kukamilisha kazi ya kufunga kwa dunia, na kuwakusanya ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote (Isaya 66:19, 20; 18: 4). {FB: 12.2}
4. Kwamba kuangamizwa kwa magugu kutoka miongoni mwa malimbuko ya walio hai (Mat. 13:30, 48, 49; Ezek. 9: 6, 7) ni tokeo la utakaso wa kanisa. {FB: 12.3}
5. Kwamba mara muda si muda, malaika wataziachilia pepo nne (Ufu. 7: 1-3), ambapo utaanza wakati wa taabu na Mikaeli kusimama kuwaokoa kutoka
12
kwayo, wote ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo (Dan. 12: 1). {FB: 12.4}
6. Kwamba malaika ‘kuziachilia pepo nne kuvuma pembe nne za dunia (Ufu. 7: 1), sio tarajio la vita vya dunia ila badala yake sheria ya kutekelezwa dunia nzima katika Babeli na sanamu ya mnyama, na ya kwamba mtu yeyote asiweze kununua au kuuza isipokuwa yeye anayeiabudu “sanamu.” Ufu. 13: 15-17. {FB: 13.1}
7. Kwamba halafu, wakati wa taabu ya Yakobo (Yer. 30: 7) kwa wale 144,000, wana wa Yakobo, kwa mantiki inatokeza wakiwa safarini kurudi nyumbani (Mwa. 32: 1, 24) kwa nchi ya baba zao (Ezek. 36:28; 37:21, 25). {FB: 13.2}
8. Kwamba tukio la kihistoria ambalo limetajwa hapo juu litasababisha watu 144,000 kupata majina yao yanabadilishwa kama baba yao, Yakobo (Mwa. 32:28), na kama kundi kupokea jina jipya ambalo kinywa cha Bwana kitanena (Isa. 62 : 2). {FB: 13.3}
9. Kwamba haya matukio yatafikia upeo katika kuanzishwa kwa Ufalme (Dan. 2:44; Isa. 2: 1-4; Mika 4; Ezek. 37), ambamo wale 144,000, wamfuatao Mwana-Kondoo “kila aendako” (Ufu. 14: 4), watasimama pamoja naye juu ya Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1), na hapo “kuupokea utajiri wa watu wa mataifa.” Isa. 60: 5, 11. {FB: 13.4}
10. Kwamba pamoja na mfululizo huu wa matukio utahakiki Kilio Kikuu cha Malaika anayeiangaza nchi kwa utukufu wake (Ufu. 18: 1),
13
wakati Sauti nyingine inapiga kelele, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4. {FB: 13.5}
11. Kwamba katika kuitikia mwito huu, mataifa mengi yatasema: “Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika 4: 2. {FB: 14.1}
12. Kwamba Sauti itaacha kupiga kelele wakati watakatifu wote watakakuwa wamekusanywa kutoka katika mataifa yote. Kisha itakuwa “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” Amosi 8:11, 12. {FB: 14.2}
13. Kwamba basi kutafuatia kutenguka kwa muungano wa dunia nzima wa sanamu ya mnyama (Ufu. 19: 1-3), kufungwa kwa hukumu ya upelelezi ya walio hai (Ufu. 15: 5-8), mwisho wa muda wa rehema (Ufu. 22:11), na kumiminwa kwa mapigo saba ya mwisho juu ya waovu (Ufu. 16). {FB: 14.3}
14. Kwamba chini ya pigo la saba, majeshi yaliyojipanga kwa pambano la Har-Magedoni
14
yatapigana na, na yataangamizwa na, majeshi ya Mbinguni (Shuhuda, Gombo la 6, uk. 406), na kwamba Kristo atatokea katika utukufu Wake wote, kuwaangamiza waovu waliosalia, kuwafufua watakatifu waliokufa (1 Thess. 4 : 15-17), na kuikaribisha milenia (Ufu. 20: 5). {FB: 14.4}
15. Kwamba kwa muda mchache (Ufu. 20: 3), miaka mia moja (Isaya 65:20), baada ya milenia, waovu wataishi tena na hatimaye wataangamizwa kwa moto (Ufu. 20: 9), ambapo vitu vyote vitarejeshwa, na mpango halisi wa Mungu utaendelea kufikia utimilifu mkamilifu katika umilele usiokatizwa wa furaha ya mbinguni (Ufu. 21: 4). {FB: 15.1}
15
MIPANGILIO ORODHA
ENEO
AWALI: “Njia na vichochoro vya mji” (Luka 14: 17-21) — kanisa. {FB: 16.1}
MWISHOWE: “Barabara kuu na mipakani” (Luka 14:23, Mat. 24:14) — “kila taifa na jamaa, na lugha, na watu” (Ufu. 14: 6), hata “katika visiwa vya baharini “(Isa. 24:15), — “visiwa vya mbali.” Isa. 66:19. {FB: 16.2}
ANWANI YA OFISI YA NYUMBANI
Simu: Wanadaudi Waadventista wa Sabato, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas.
Kasi na Usafirishaji Mizigo: Shirika la Kimataifa la Biashara., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas.
Posta: Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu. Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas.
MAAFISA WATENDAJI
Rais: V.T. Houteff
Makamu wa Rais: E.T. Wilson
Katibu: Bi F.M. Houteff
Mtunza Hazina: Bi. S. Hermanson
Mkutano wa Ustawi
BARAZA KUU
V.T. Houteff
M.J. Bingham
Bi. S. Hermanson Bi. G.R. Bingham
E.T. Wilson
H.G. Warden
Bi. F.M. Houteff
16
UCHAPISHAJI
Mhariri: V.T. Houteff
Mhariri Msaidizi: M.J. Bingham
Wahariri Washirika: Bi. S. Hermanson
Bi. G.R. Bingham
Meneja wa Kueneza: Bi. L.M. Georgel
MAKATIBU WA IDARA
Elimu: M.J. Bingham
Shule ya Sabato: Bi. G.R. Bingham
Mawasiliano: Binti J.M. Helman
Bi. M.E. Mills
UNUNUZI NA USAMBAZAJI
Binti M.A. Helman
V.V. Smith
MAKATIBU WA KONDENI KWA MAJIMBO YALIYOUNGANA YA AMERIKA
H.G. Warden
Dkt. H.F. Roller
E.T. Wilson
W.J. Banks
WACHUNGAJI
Banks, W. J. | Houteff, V. T. |
Bero, S. | Josselyn, F. H. |
Bingham, M. J. | Knipple, J. |
Boyes, J. H. | Nations, L. W. |
Brewer, B. C. | Richardson, O. O. |
Butterbaugh, Dr. W. S. | Roller, H. F. |
Coffey, W. R. | Rose, A. J. |
Colvin, A. J. | Springer, J. D. |
Deeter, M. L. | Warden, H. G. |
Georgel, R. A. | Wilson, E. T. |
Herrara, L. R. | Wolfe, M. W. |
17
MSAJILI MWANACHUO
Goodman, Milton
Green, G.W.
GreenL.G.
Green R.S.
Helman, C.W.
Hermanson, T.O.
Johnson, M. Mills, H.H.
Saether, G.W.
Sealy, H.C.
Smith, A.G.
Smith, V.V.
Waltin, G.W.
Wilson, J.E.
WATENDAKAZI WA BIBLIA
Achor, Dkt Clara Farr
Aclin, Bi. Emma Bell
Amos Bi. Etta J.
Berolinger, J.B.
Betz, J. H.
Bingham, Bi. Genevieve
Clark, D.D.
Colvin, Bi. Ruth
Conley, Bi. Gay
Davis, Bi. Evelyn
Ferguson, Bi. Evelyn
Fitzsimmons, Bi. Lavada
Gould, Bi. Gladys
Gurney, C.J.
Henderson, T.E.
Hill, Binti Lucy
Hodgen, Bi. Mary L.
Huffaker, L.B.
Kurtz E.E.
Lowe Bi. R.N.
Lyons, Bi. Edna E.
Michael, Bi. Sophrania
Mooney, R.P.
18
Quackenbush, Bi. Louise
Richert, H.
Robles, J.P.
Rogers, Bi. Helen
Rompel, J. B.
Saether, Bi Romana
Schiau, N.
Schleifer, Miss Lillian
Smith, C.T.
Vories, J.R.
Warden, Bi. Vida
Wessel, C.E.
Wilson, C.L.
Wolfe, Bi. Ethel
MPANGLIO ORODHA WA WAFANYA KAZI
Achor, Dkt. Clara Farr, 402 E. Chandler
Brownwood, Texas
Aclin, Bi. Emma Bell, 72 Mashariki njia ya 6,
San Angelo, Texas
Amos, Bi. Etta J. 4850 Kaskazi Magharibi mwa Ua la 24
Miami, Florida
Banks, W.J., Miji ya Dan, Virginia
Bero, S., Njia ya Chuo Kikuu 9237, Chicago, Illinois.
Berolinger, J.B., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Betz, J.H., Garland, Wyoming
Bingham, Bi. Genevieve, Kituo cha Mlima Karmeli
Waco, Texas
Bingham, M.J., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco,
Texas
Boyes, J.H., Gibbs, Idaho
19
Brewer, B.C, 1699 E. Njia ya 110th, L.A., Cal.
Butterbaugh, Dkt. W.S., Sanduku la Posta 68, Jiji la Canon, Col.
Clark, D.D., 744 E. Njia ya 10 1/2, Houston, Tx.
Coffey, W.R., 926 Mashariki, Njia ya 104th, L.A., Cal.
Colvin, A.J., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Conley, Bi. Gay, Njia ya 1, Springfield, Ohio
Davis, Bi. Evelyn, Rt. 4, Sanduku la Posta 96, Greely, Col.
Deeter, M.L., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Ferguson, Bi. Evelyn, 120 112 Barabara ya S. Giavanola,
San Bernardino, Calif.
Fitzsimmons, Bi. Lavada, 315 Barabara ya Msitu,
San Antonio, Texas
Georgel, R.A., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Gould, Bi. Gladys, Njia ya 3, Sanduku la Posta 9,
Bremerton, Washington
Gurney, C.J., 709 Barabara ya Ukoloni., Norfolk, Vir.
Henderson, T.E., Rt. 4, Cleburne, Texas
Herrera, L.R., Pango la 1925, Mji wa Taifa, Cal.
Hill, Miss Lucy, 1625 Mashariki ya 10, Pueblo, Col.
20
Hodgen, Bi. Mary L., 2831 S. Lincoln, Englewood, Colorado
Houteff, V.T., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Huffaker, L.B., Njia ya 1, Weston, Ohio
Josselyn, F.H., 213 Njia ya Virginia Kaskazi, Clearwater, California
Knipple, L. 308 Barabara ya Mooney, Wilmar, Cal.
Kurtz, E.E., Njia ya 1, Marietta, Georgia
Lowe, Bi. R.N., Darrington, Washington
Lyons, Bi. Edna E., 5905 Barabara ya 21 kusini mashariki, Portland, Oregon
Michael, Bi. Sophrania, Kituo cha Uhuru, Ind.
Mooney, R.P., 680 Barabara ya Kerr, Victoria, B.C., Canada
Nations, L.W., Salem, Carolina Kusini
Quackenbush, Bi. Louise S., 121 Njia ya Mlima wa Vernon,
Bustani ya Ridgefield, N.J.
Richardson, O.O., Njia ya 1, Muncie, Indiana
Richert, H., Rt. 5, Sanduku la Posta 470, Portland, Oregon
Robles, J.P., 711Njia ya Echandia, L.A., Cal.
Rogers, Bi. Helen, 1522 Zuniga Ln., L.A., Cal.
Roller, H.F., 3887 Njia ya 37, San Diego, Cal.
21
Rompel, J.B., Njia ya 2, Sanduku la Posta 72, Chowchilla, California
Rose, A.J., Njia ya 5, Waterford, Pennsylvania
Schiau, N., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Schleifer, Binti Lillian, Njia ya 327 1/2 Delmar Mashariki, Pasadena, California
Smith, C.T., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Smith, V.V., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Springer, J.D., R. 1, Mitchell, Nebraska
Vories, J.R., Rt. 1, Cample Springs Camp, Logansport, Indiana
Warden, H.G., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Warden, Bi. Vida, Kituo cha Mlima Karmeli, Texas
Wessel, C.E., 29 Anwani ya Chestnut, Charleston South Carolina
Wilson, C.L., Njia. 1, n / y J. Ford, Rathdrum, Idaho
Wilson, E.T., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
Wolfe, M.W., Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas
22
AGIZO LA SAA KUMI NA MOJA
“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.” Isa. 60: 1-4. {FB: 23.1}
“Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.” Yoh. 4:35. {FB: 23.2}
“Kweli mavuno ni mazuri. lakini wafanya kazi ni wachache; basi, mwapeni Bwana wa mavuno, atatuma watumishi katika mavuno yake. Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” Mat. 9:37, 38. {FB: 23.3}
“Uhitaji mwingi umefanywa kila mahali kwa ajili ya nuru ambayo Mungu amewapa watu Wake, ila wito huu kwa sehemu kubwa umekuwa bure. Ni nani anahisi uzito wa kujiweka wakfu kwa Mungu na kwa kazi Yake? Wako wapi vijana ambao wanaojipatia uzoefu kujibu wito huu? Maeneo makubwa yamefunguliwa mbele yetu ambapo nuru ya ukweli haijawahi kupenya.
23
Popote tunapotazama tunaona mavuno mengi yaliyo tayari kukusanywa, lakini hakuna wa kuvuna. Maombi hutolewa kwa ajili ya ukweli kushinda. Je, maombi yenu yanamaanisha nini, ndugu? Mnataka mafanikio ya namna gani? — Mafanikio ya kuufaa utepetevu wenu, tamaa za ubinafsi wenu? — Mafanikio ambayo yatakayojidumisha na kujikimu yenyewe bila jitihada yoyote kwa upande wenu? {FB: 23.4}
“Lazima liwepo badiliko thabiti … ambalo litawasumbua wale wanaolala kwenye masira yao, mbele ya watendakazi ambao wanafaa kwa kazi yao ya kicho kutumwa shambani. Lazima uwepo uamsho, ukarabati wa kiroho. Joto la kicho cha Kikristo linapaswa kuinuliwa. Mipango lazima ibuniwe na kutekelezwa kwa ajili ya kueneza ukweli kwa mataifa yote ya dunia. Shetani anawabembeleza wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo kulala, wakati ambapo roho zinaangamia kuwazunguka pande zote, na ni udhuru gani wanaoweza kumpa Bwana kwa uzembe wao?” {FB: 24.1}
“…’Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?’ Kwa nini hamutendi kazi kwa kadri fulani katika shamba lake la mizabibu “Tena na tena amewaambia, ‘Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na kilicho sahihi nitawapa.’ Lakini mwito huu wa neema kutoka Mbinguni umepuuzwa na wengi kwa upana. Je! Sio wakati mwafaka kwamba muweze kuyatii maagizo ya Mungu? Ipo kazi kwa kila mtu anayejiita kwa jina
24
la Kristo. Sauti kutoka mbinguni inakuita kwa kicho kwa wajibu. Uitii sauti hii, na uende kazini mara moja mahali popote, kwa uwezo wowote. Mbona umesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Kazi ipo kwa ajili yako kufanya, kazi ambayo inadai nguvu zako bora. Kila wakati wa thamani wa maisha unahusiana na wajibu fulani ambao unawiwa na Mungu au kwa wanadamu wenzako, na bado unasimama bila kufanya kazi!” — Shuhuda, Gombo la 5, kr. 203, 204. {FB: 24.2}
“Niruhusu kukuambia,” inaendelea Roho ya Unabii, “iwapo moyo wako uko katika kazi hii, na unayo imani kwa Mungu, hauhitaji idhini ya mchungaji yeyote au mtu yeyote: iwapo unaenda mara kuifanya kazi katika jina la Bwana, kwa njia ya unyenyekevu ukifanya kila unachoweza kufundisha ukweli, Mungu atakutetea. Laiti kazi haingekuwa imezuiliwa na kizuizi hapa, na kizuizi pale, na kwa upande mwingine kizuizi, ingekuwa imeendelea mbele kwa utukufu wake, ingekuwa imeenda katika uanana kwanza, lakini Mungu wa mbinguni anaishi.” — Tathmini na Mapitio, Aprili 16, 1901. (Angalia Pia Shuhuda, Gombo la 7, uk. 25.) {FB: 25.1}
“Kazi kubwa ya kuokoa roho bado inangoja ifanywe. Kila malaika katika utukufu amehusishwa kwa kazi hii, wakati kila pepo wa giza anaipinga. Kristo … anatarajia kujikana nafsi kulingana na kujitolea mhanga kwa upande wa wale ambao yeye alikuja kubariki na kuokoa. Kila mmoja anahitajika
25
kutenda kazi kwa kiwango cha uwezo wake. Kila uzingatifu wa kidunia unapaswa kuwekwa kando kwa ajili ya utukufu wa Mungu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 204. Hili ni msingi wa
Sifa za Watendakazi. {FB: 25.2}
Wale ambao leo wataisikia sauti Yake na kutoifanya mioyo yao migumu kama siku ya kukasirisha, atawafanya watumwa Wake wa baadaye. {FB: 26.1}
“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.” Zek. 4: 6. Watendakazi “watafundishwa zaidi kwa uongozi wa Roho Wake, kuliko kwa mafunzo ya nje ya taasisi za kisayansi … Mungu atadhihirisha kwamba Yeye hawategemei watu wasomi, ambao hujiona ni wa umuhimu kwa ubinafsi.” “Walio dhaifu sana na ambao husita sita kanisani watakuwa kama Daudi — wepesi kutenda na kuthubutu.” — Shuhuda, Gombo la 5. kr. 82, 81. {FB: 26.2}
“Nitawachukua watu wasioweza kusoma au kuandika,” asema Bwana, “watu duni, na kuwaongoza kwa Roho Wangu, kuyatekeleza madhumuni Yangu katika kazi ya kuokoa roho.” Ujumbe wa mwisho wa rehema utatolewa na watu wanaonipenda na kunipa kicho.” — Mapitio na Kuhubiri, Septemba 21, 1904. “Atawatumia watu kwa ajili ya kulifanikisha kusudi Lake ambao baadhi ya ndugu watawakataa kama wasiofaa kushirikishwa katika kazi.” — Mapitio na Kutangaza, Februari 9, 1895. {FB: 26.3}
Katika mwito huu wa mwisho kwa watenda kazi, wote — wadogo au wakuu matajiri au maskini, wasomi au wasio wasomi
26
— wanayo fursa ya juu na iliyoinuliwa ya kuwa wachungaji wa Kristo
Watu wa Kuheshiwa na Majaliwa. {FB: 26.4}
Ukweli wa sasa huongoza kuendelea mbele na kuinuka juu, kuwakusanya ndani wanaohitaji, maskini, waliodhulumiwa, wanaoteseka, na walio hohe hahe. Wote watakaokuja wataingizwa ndani ya zizi. Katika maisha yao yatafanyika matengenezo ambayo yatawajumuisha kuwa wa familia ya kifalme, watoto wa Mfalme wa mbinguni.” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 195, 196. {FB: 27.1}
Kwa watenda kazi hawa, watu 144,000, Bwana anaahidi kwa neema: “Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine [wale wasio miongoni mwa 144,000] watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.” (Isa. 61: 5, 6), iwapo sasa mnaamka na kuharakisha ili kutekeleza
Mpito wa Kazi. {FB: 27.2}
Kama ukasisi huu, ambao “mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.” (Yoeli 2: 2), utakuwa huru kutoka kwa mizigo yote ya kidunia, usimruhusu mtu yeyote tena acheleweshe kuufanikisha mpito ambao hatimaye utamwezesha kujihusisha moyo na nafsi katika “kazi ya kufunga kwa Kanisa” ya Bwana, katika kuwakusanya “malimbuko” ambao watatiwa muhuri
27
kutoka miongoni mwa walio hai Laodekia. Na wakati akijitoa kwa kazi hii, atakuwa wakati uo huo anajiandaa kuutangaza ujumbe wakati wa Kilio Kikuu, ambacho utakaso wa kanisa — ukombozi wa walotiwa muhuri na kuangamizwa kwa wale hawajatiwa muhuri — utakipisha ndani, na ambacho waliotakaswa watatangaza. {FB: 27.3}
Hebu kila mmoja kwa busara autekeleze mpito huu muhimu kwa kupunguza hatua kwa hatua maslahi yake mwenyewe, na kuongeza ufuatiliaji wa maslahi ya Bwana. Kwa njia hii, kila mmoja atapanda hatua kwa hatua kutoka mradi mtupu wa kudharauliwa kwa muda wa ubinafsi, hadi kwa mradi wa Mungu wa utukufu wa baadaye ambao utavuvia “Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki.”Isa. 24:16. {FB: 28.1}
Sasa ni wakati ambapo Mwenye nyumba wa Mbinguni anauliza, “Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?” na anahimiza, “enendeni nanyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki nitawapa.” Mat. 20: 6, 7. {FB: 28.2}
Ndugu zangu, iwapo mnataka sehemu katika kazi hii kamwe ambayo haijakuwa hivyo na utukufu, tendo la kuutia taji kwa ukombozi wa dunia, lazima sasa uharakishe kuwa tayari. Usiruhusu shughuli za maisha haya yakupokonye taji ya uzima wa milele. Usibaki nyuma, kumruhusu Shetani aweke kinywani mwako udhuru: “Nimenunua shamba,
28
sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe:” au, “Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe:” au “Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.” Luka 14: 18-20. “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” 1 Yohana 2:16, 17. {FB: 28.3}
Wakati bado unajihusisha na kazi yako ya sasa, enenda katika shamba la Mizabibu la Bwana, na kadri hamu yako pale inakua, kazi yako mwenyewe itapungua hadi utakapopata kuwa umejitenga kabisa kutoka kwayo na kujishughulisha kwa ya Bwana. {FB: 29.1}
“Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?” ila
“Utafuteni Kwanza Ufalme wa Mungu” — Si Mshahara. {FB: 29.2}
Iwapo mawazo yetu kiwimawima ni kwa ajili ya kuuendeleza Ufalme basi hatungeweza kuwaza kwamba ni nani atakayetupatia malipo, ila tutatulia kwa furaha katika uhakikisho kwamba mahitaji yetu yatashughulikiwa. {FB: 29.3}
Kulingana na mfano huo, watenda kazi ambao Mwalimu huajiri, huenenda kwa imani pasipo
29
Kujua ni nini watapewa mwisho wa kutwa. Iwapo ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji ni wa Mungu, basi watenda kazi wake wangejifunza vyema kwamba utapelekwa nje wote katika njia Yake, sio ya mwanadamu, na kwamba wale wanaotenda kazi kwa ujira kama malipo kwa kazi zao, hawamfanyi kazi kwa ajili ya Kristo, ila badala yake kwa ajili yao wenyewe; pia kwamba ikiwa ofisi inapaswa kutoa usaidizi wa kifedha kwa yeyote anayefanya kazi ambayo si ya wakati wote, yanaweza kufuata mapendezi ya kuwalipa wote ambao walifanya chochote, kiwe kidogo au kikubwa — utangulizi ambao unaweza kuharibu tu kuliko kuwajenga wote mtenda kazi na wale ambao kwa ajili yao angeweza kuwafanyia kazi. {FB: 29.4}
Ndiposa, utaratibu pekee wa haki ni kwamba wote wanaohusika katika kazi hii ya ujumbe wa kutia muhuri, waripoti shughuli zao kwa ofisi hii, ili kwamba waweze kugawiwa matokeo ya kazi zao. Na ikiwa litaweza kuwa ongezeko la mapato ya kutosha kulingana na jitihada hizi ili kuwawezesha kutoa muda wote kamili kwa kufundisha ujumbe, wataweza kupewa hadhi ya muda kamili, kuwapa haki ya matumizi muhimu ya kuishi kutokana na matokeo ya kifedha ya kazi zao. {FB: 30.1}
“Wakati,” yanena Roho ya Unabii, “ni mfupi, na nguvu zetu zinapaswa kupangwa kufanya kazi kubwa. Watenda kazi wanahitajika ambao wanaelewa ukuu wa kazi, na ambao watahusika kwayo, sio kwa mishahara wanayopokea , ila kutoka kwa ufahamu wa kutambua ukaribu wa mwisho. Wakati unadai
30
wepesi mkuu na kujitoa wakfu zaidi” (Shuhuda, Gombo la 9, uk. 27) na
Fadhila Kama Za Kristo. {FB: 30.2}
“Nina ujumbe huu kwa ajili yako kutoka kwa Bwana: Uwe na wema katika hotuba, mpole kwa kutenda Jilinde kwa makini, kwa maana una mwelekeo wa kuwa mkali na dhalimu, na kunena mambo bila kufikiria. Bwana anaongea nawe, akisema, Ukeshe na kuomba, usije ukaingia katika majaribu. Maneno makali humhuzunisha Bwana, maneno yasiyo ya busara hudhuru. Nimeagizwa kukuambia, Uwe mpole katika hotuba yako, angalia vyema maneno yako, usiruhusu ukali uje katika maneno yako au katika ishara zako. Leta ndani ya yote unayofanya na kunena manukato kama ya Kristo. Usiruhusu mienendo ya tabia za asili kudhuru na kuharibu kazi yako. Inakupasa kuwasaidia na kuwaimarisha waliojaribiwa. Usiruhusu ubinafsi uonekane kwa maneno ya papara. Kristo ameutoa uhai wake kwa ajili ya kundi, na kwa ajili ya wote ambao unahudumia. Usiruhusu neno lolote liziweke nafsi juu ya mizani kwa mwelekeo mbaya. Ndani ya mchungaji wa Kristo lazima idhihirishwe tabia kama ya Kristo. {FB: 31.1}
“Hisia za papara, za ujeuri haziuwiani na kazi takatifu ambayo Kristo amewapa wachungaji wake kufanya. Wakati uzoefu wa kila siku ni ule wa kumtazama Yesu na kujifunza Kwake, utaonyesha tabia safi na ya kupatana Naye. Lainisha uwakilishaji wako, na usiruhusu kunena maneno ya kuhukumu. Jifunze
31
kwa Mwalimu mkuu. Maneno ya fadhila na huruma yatafanya vizuri kama dawa, na yataziponya nafsi ambazo zinakata tamaa. Maarifa ya neno la Mungu yakiletwa kivitendo katika maisha yatakuwa na nguvu ya kuponya, ya kutuliza. Ukali wa hotuba kamwe hautaleta baraka kwako au kwa nafsi nyingine yoyote. {FB: 31.2}
“Ndugu yangu, unapaswa kuwa mwakilishi wa upole na uvumilivu na wema wa Kristo. Katika mazungumzo yako mbele ya umma, ruhusu uwakilishi wako uwe wa mfano wa Kristo.”Hekima itokayo juu kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa huruma na matendo mema. Kesha na kuomba, na tiisha ukali ambao mara nyingi hujitokeza ndani yako. Kwa neema ya Kristo inayokaa ndani yako, maneno yako yanaweza kutakaswa. Iwapo ndugu zako hawatendi jinsi unavyofikiri wanapaswa, usiwakabili kwa ukali. Bwana amehuzunishwa nyakati zingine kwa maneno yako makali.” — Watenda kazi wa Injili, kr. 163, 164. {FB: 32.1}
“Sio maneno mengi unayosema,
Kama namna ambayo unayanena.
Sio sana lugha unayotumia,
Kama vile sauti ambazo unatumia kuuwasilisha.
Maneno yanaweza kuwa ya upole na safi
Na sauti zinaweza kupenyeza kama mshale;
Maneno yanaweza kuwa laini kama hewa ya majira ya joto
Na sauti zinaweza kuupenyeza moyo. “{FB: 32.2}
32
“Ukweli unapaswa kuwasilishwa kwa busara takatifu, upole, na wororo. Ni lazima utoke ndani ya moyo ambao umelainishwa na kufanywa wa huruma. Tunahitaji kuwa na ushirika wa karibu na Mungu,… tunapaswa kukesha kwa sala, na kuwa tayari siku zote kutoa sababu ya tumaini lililo ndani yetu, kwa upole na kwa hofu. Tusije tukavutia isivyopendeza nafsi moja ambayo Kristo alifia, tunapaswa kuidumisha mioyo yetu iliyoinuliwa kwa Mungu ili kwamba wakati fursa itakapojiwasilisha, tutaweza kuwa na neno sahihi la kunena kwa wakati mwafaka.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 400. Hii ni
Sayansi ya Mafanikio. {FB: 33.1}
“Kwa kila mtenda kazi Ningeweza kusema: Enenda kwa imani ya unyenyekevu, na Bwana ataambatana nawe, lakini kesha kwa sala, hii ndiyo sayansi ya kazi yako, uwezo ni wa Mungu.” — Shuhuda, Gombo la 7, uk. 272. {FB: 33.2}
“Nimeagizwa kuwaambia watenda kazi wenzangu, iwapo mngetaka kuwa na hazina ya utajiri wa mbinguni, lazima mshikilie ushirika wa faraghani na Mungu. Msipofanya hili, nafsi zenu zitakuwa hohe hahe kwa Roho Mtakatifu kama vilivyokuwa vilima vya Gilboa kukosa umande na mvua. Wakati unapoharakisha kutoka kwa kitu kimoja hadi kingine, wakati una mengi ya kufanya hivi kwamba huwezi kuchukua muda wa kuzungumza na Mungu, unawezaje kutarajia nguvu katika kazi yako?… {FB: 33.3}
“Zungumza na moyo wako mwenyewe, na kisha zungumza na Mungu. Iwapo hautafanya
33
hili, juhudi zako hazitakuwa na matunda, zitakuwa zimemefanyika hivyo kwa haraka isiyokuwa imetakaswa na kuchanganyikiwa.” — Watenda kazi wa Injili, uku. 272. {FB: 33.4}
“Wale ambao hufundisha na kuhubiri kwa ufanisi zaidi ni wale wanaomngojea Mungu kwa unyenyekevu, na kukesha njaa kwa uongozi Wake na neema Yake. Kesha, omba, fanya kazi — huu ndiyo msemo wa Mkristo. Maisha ya Mkristo wa kweli ni maisha ya sala za daima.” – Watenda kazi wa Injili, uk. 257. {FB: 34.1}
“Mhubiri fulani ambaye mahubiri yake yaliziongoa roho nyingi, alipokea ufunuo kutoka kwa Mungu kwamba hayakuwa mahubiri yake au kazi kwa njia yoyote, ila sala za mlei aliyekuwa hajui kusoma na kuandika ambaye alikuwa ameketi kwenye hatua za mimbari akiomba kwa ajili ya ufanisi wa mahubiri. Itaweza kuwa pamoja nasi katika siku ya ufichuzi wa yote. Tunaweza kuamini, baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kwa uchovu, kwamba heshima zote ni za mjenzi mwingine ambaye maombi yake yalikuwa dhahabu, fedha, na mawe ya thamani, wakati ambapo mahubiri yetu, yalikuwa kando kutoka kwa maombi, ni nyasi na makapi tu.” — C, H. Spurgeon. {FB: 34.2}
“Wajumbe wa Mungu wanapaswa kukaa kwa muda mrefu pamoja Naye, iwapo wangetaka kufanikiwa katika kazi zao.” Hadithi hii imesimuliwa kumhusu mwanamke mzee wa Lancashire aliyekuwa akisikiza sababu ambazo majirani zake walitoa kwa mafanikio ya mchungaji wao. Walizungumzia karama zake, mtindo wake wa kuhutubu, tabia zake. ‘Hapana’, alisema mwanamke mzee, ‘Nitawaambia
34
ni nini. Mtu wenu yu heri sana na Mwenyezi. {FB: 34.3}
“Wakati watu wanajitolea jinsi Eliya alivyokuwa na kuimiliki imani aliyokuwa nayo, Mungu atajidhihirisha Mwenyewe Alivyofanya awali. Wakati watu wanamsihi Bwana jinsi alivyofanya Yakobo, matokeo yaliyoonekana wakati huo tena yataonekana. Nguvu zitakuja kutoka kwa Mungu kujibu ombi la imani.” – Watenda kazi wa Injili, uk. 255. {FB: 35.1}
Kurupukia kazi, wakufunzi wa Ukweli wa Sasa! Fanya kazi zake Yeye aliyewapeleka, “maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.” Yohana 9: 4. “Na iliyo haki nitawapa,” iwapo mtafundisha kwa uaminifu
Kile Tu Ambacho Kinapaswa Kufundishwa. {FB: 35.2}
Biblia na vitabu vya Roho ya Unabii kuwa ni chanzo pekee cha ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, kwa hiyo wakati Fimbo inafundisha, Biblia na Roho ya Unabii zinafundisha. Na kwa kuwa hakuna ila Roho wa Kweli, ambaye alisambaza siri za Uvuvio, anaweza kuzifasiri, basi wale ambao hujaribu kuzifundisha bila Mamlaka hii ya kufasiri iliyovuviwa, bila kuepuka hutumbukia katika zoezi lililopigwa marufuku la ufasiri wa kibinafsi (2 Petro 1:20) — uovu mkuu ambao umeleta himaya ya Kikristo kuwa katika hali ya sasa isiyo na kikomo ya migawanyiko na matokeo ya mchafuko, ugomvi, na ugumba. {FB: 35.3}
35
Tusivyoweza kuthubutu kuifuata njia kama hiyo, kwa hivyo ni lazima, kama wakufunzi wa Fimbo ya Mchungaji (machapisho rasmi ya Ushirika wa Wanadaudi wa S.D.A.), tufundishe tu katika nuru ya Fimbo hivyo vifungu ambavyo kwa njia moja au nyingine vitahitaji kufasiriwa. Hivi tu waaminio wote wa Ukweli wa Sasa watadumu kuwa na nia moja, wakitazama jicho kwa jicho na kunena mamoja (1 Kor. 1:10, 1 Pet. 3: 8, Isa. 52: 8). {FB: 36.1}
Na kama wale wanaochagua kujihusisha katika ufasiri wa kibinafsi wanaulizwa kwa heshima kuacha kufundisha katika jina la Fimbo na kwa gharama zake. Hebu wao, kama watu waaminifu, wafundishe katika majina yao wenyewe na kwa gharama zao wenyewe. {FB: 36.2}
Hatimaye, ndugu zangu, dumisha mawasiliano kwa ofisi kuhusiana na juhudi zako, na kwa upande wake itatoa kila udhamini iwezekanavyo ili kuifanya kazi yako ifanikiwe. Sasa, Mungu akujalie kila la heri! {FB: 36.3}
36
Goodman, Milton | Mills, H. H. |
Green, G.W. | Saether, G.W. |
Green L. G. | Sealy, H. C. |
Green R. S. | Smith, A. G. |
Helman, C. W. | Smith, V. V. |
Hermanson, T. O. | Waltin, G. W. |
Johnson, M. | Wilson, J. E. |