15 Jun Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 43, 44
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 43, 44
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1950
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
KILELE KILICHOKUFA, KICHIPUKO AU KICHIPUKIZI — KIPI?
ISHARA ZA KUJA KWA YESU MARA YA PILI, AUISHARA ZA UFALME — ZIPI?
1
ANDIKO LA SALA
Uaminifu kwa Kanuni
Kwa wazo letu la sala alasiri hii, nitasoma kutoka Shuhuda, Gombo la 5, ukurasa wa 43, aya ya kwanza: {2TG43: 2.1}
“Tunazo alama za vielelezo vya nguvu imara ya kanuni dhabiti ya kidini …. Pango wazi la simba halingeweza kumzuia Danieli kwa maombi yake ya kila siku, wala lile tanuru la moto halingeweza kumshawishi Shadraki na wenzake wasujudu mbele ya sanamu ambayo Nebukadnezza alisimamisha. Vijana ambao wanazo kanuni imara, watachukia anasa, watayakabili maumivu, na hata wawe jasiri kwa tundu la simba na tanuru iliyowaka moto, badala ya wapatikane si wa kweli kwa Mungu. Angalia tabia ya Yusufu. Wema ulijaribiwa vikali, lakini ushindi wake ulikuwa kamili. Kwa kila hatua kijana mungwana alistahimili jaribio. Kanuni iyo hiyo ya upeo, isiyopinda ilionekana katika kila jaribio. Bwana alikuwa pamoja naye, na neno lake lilikuwa sheria.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 43. {2TG43: 2.2}
Hebu tuombe sasa kwamba tutakuwa na dini ya Daudi, ya Danieli, ya Yusufu. Watu hawa walikuwa tu vijana walipoingia kwa kazi zao, bado walikuwa na msimamo thabiti katika imani yao kama sindano kwa ncha. Ha-wakukengeuka kutoka kwa jukumu au kanuni moja ya haki, bila kujali shinikizo au hali. Uthabiti wao wa tabia na bidii ya kuifanya dunia iwe bora, ilimshawishi Bwana kuwafanya kuwa wafalme. Sasa tunapaswa kuomba kwamba tusiwe wazuifu, ila tuwe wajenzi katika njia kuu ya maendeleo; kwamba badala ya kuchukua nafasi tu, tuwe mizabibu yenye kuzaa matunda katika shamba kubwa la mizabibu la Mungu. {2TG43: 2.3}
2
KILELE KILICHOKUFA, KICHIPUKO AU KICHIPUKIZI — KIPI?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JANUARI 1, 1949
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Watu wote katika vizazi vyote ambao wamewahi kuukumbatia ujumbe mpya kutoka kwa Mungu, walipigwa chapa kama “vichipuko” na kuangaliwa hatari — jambo ambalo mtu lazima ajihadhari asije akapigwa risasi, kwa mfano, kudungwa kisu, kunaswa, au jambo fulani baya, au vigumu kusema ni nini. {2TG43: 3.1}
Kama mnavyojua, sisi pia, tumepigwa chapa hivyo na tunashutumiwa kuliacha Dhehebu hata jinsi ambavyo mitume walishutumiwa kuuacha Uyahudi na kuuchukua Ukristo. Kwa kweli mitume hawakuacha chochote, maana hawakuchukua tu pamoja nao kila ukweli Uyahudi ulikuwa nao, ila waliendelea na Ukweli mpya wa Mungu pia, ilhali Uyahudi ulianguka nyuma. Mitume, isitoshe, wangebaki katika sinagogi iwapo Wayahudi wasingaliwatupa nje. Kwa hili mitume waliitwa “vichipuko,” na kadhalika. {2TG43: 3.2}
Sisi vivyo hivyo hatujajiondoa mbali na Dhehebu, lakini tumetupwa nje kila moja ya makanisa yetu na ku-lazimishwa kwenda kwa jina lingine, Wadaudi Waadventista wa Sabato, — na yote haya bila sababu nyingine isipokuwa kwa
3
kukumbatia Ukweli wa nyongeza uliotoka Mbinguni ambao hutoa nguvu na uwezo kwa ujumbe wa Ujio (Maandishi ya Awali, uk. 277), na ambao hutufanya kuwa Waadventista wa Sabato bora kuliko ambavyo tu-mekuwa au tunavyoweza kuwa. {2TG43: 3.3}
Sasa, ikiwa sisi ni “vichipuko” kwa kutembea katika nuru ambayo mbingu hutuma mara kwa mara kuwaongo-za watu wa Mungu katika njia ya Ukweli na Haki, basi ningependa kujua ndugu zetu wanafikiri wao ni nini, maana kwa ishara iyo hiyo ya busara Dhehebu Mama, Waadventista wa Sabato, lenyewe ni kichipuko kutoka kwa dhehebu lingine. Isitoshe, hii pia ni kweli kuhusu madhehebu yote ya Kiprotestanti, kwa maana nayo ni vi-chipuko vya Katoliki; na la Mitume ni kichipuko cha la Kiyahudi. Je! Nani basi, nje ya Wayahudi si kichipuko? Kwa kweli, iwapo tutarudi mbali nyuma kama wakati wa Abrahamu, tutaona kwamba hata Wayahudi walikuwa kichipuko cha kitu kabla ya wakati wao. Ikiwa vichipuko vinapaswa kuepukwa, kuchukiwa, na kuchukiwa sana, mbona wapo Wakristo wowote? Na iwapo hili ni kifumbua macho kwa wale ambao wanafikiri ni kitu kingine isipokuwa kichipuko, sasa wanapaswa bila kuchelewa waombe usajili kwa Sinagogi, au sivyo waanze kutenda kama watu wa Mungu. {2TG43: 4.1}
Je! Wewe, Ndugu, Dada, unaona kwamba kama visingekuwa “vichipuko,” wale ambao walikuwa na uti wao wa mgongo kusimama kwa Ukweli wa sasa, kwa “chakula kwa wakati wake” (Mat. 24:45), hakuna hata mmoja wetu ambaye angepata nafasi ya kuwa Wakristo — Waprotestanti, Waadventista, au Wadaudi. Sote tungekuwa washiriki wa Sinagogi lililoachwa na Mungu, iwapo wa kitu chochote. Kwa kweli,
4
hatungekuwa na dini ya Bibilia hata kidogo, kwa maana Wayahudi wenyewe wameacha yale machache wali-okuwa wamehifadhi hiyo miaka 2000 iliyopita. Basi, hatupaswi, kushukuru uaminifu wa vichipuko ambao wam-etangulia kabla yetu (iwapo ndivyo walivyo) na kati yao Kristo ni wa kwanza? Mimi, binafsi ninayo fahari kuit-wa kichipuko pamoja na Bwana wangu. Mimi, kwa hivyo, napenda kuwa kichipuko, lakini singependa kuwa kilele kilichokufa. {2TG43: 4.2}
Ndugu zetu wa uhasama, ingawa, kimakosa wanatuita “vichipuko.” Kwa usahihi tunapaswa kuitwa “vichipu-kizi,” kwa maana hivyo ndivyo Ukweli wa nyongeza hufanya kwa Kanisa na kwa kila mtu anayeupokea. Mti ambao hauchipukizi katika msimu unaopaswa, unakufa au umekwisha kufa. Kwa uwazi, basi, bila sisi “vichipu-kizi,” ndugu hawatapata nafasi ya kuustahimili ugonjwa wa Ulaodekia, na wasiwe na nafasi ya kuufikia Ufalme wa utukufu. Wao, wakati wanakufa, watakuwa wakiota daima kwamba ni matajiri na wamejitajirisha, ingawa kwa kweli Bwana Mwenyewe huonyesha kwamba “ni wanyonge, wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi” (Ufu. 3:17), na hawajui. Wanapaswa kuwa na shukrani ilioje kwetu sisi ambao tumehimili mishale yao ya moto kwa ajili ya Ukweli! {2TG43: 5.1}
Katika sura ya ishirini ya Mathayo tunapata vichipukizi kama hivyo vitano. Je! Ungependa kujua hivi vichipu-kizi ni nani? Ili kuwezesha uchambuzi wavyo, nimeiandaa ramani hii, na sasa ni fursa yako kuitazama kwa ukaribu na kwa uaminifu kuizingatia. {2TG43: 5.2}
5
Ramani hii ni nakala ya mfano unaopatikana katika sura ya ishirini ya Mathayo, mfano ambao Bwana huonye-sha kwamba Mwenye Nyumba, Mungu, katika mkondo wa wakati aliwajiri wafanyikazi mara tano tofauti. {2TG43: 6.1}
6
Hebu sasa tusome mfano wenyewe: {2TG43: 7.1}
Mat. 20:1-7 — “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwen-da kuajiri watumwa awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na watumwa ku-wapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mi-zabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba la mizabibu; na iliyo haki nitawapa.”
Watumwa wa kwanza, bila shaka, walikuwa Wayahudi katika siku ya Musa. Sasa kwa sababu waliofuata, wale walioajiriwa saa ya tatu walikuwa Wakristo, inafuatia kwamba siku (masaa kumi na mbili ya mfano am-bayo kuajiri kunatekelezwa) ni nembo ya kipindi cha wakati. Ni wakati ambamo Neno lililoandikwa la Mungu, Bibilia, linaonekana na kuangaza moja kwa moja kwa wanadamu — kile kipindi tangu siku ya Musa. {2TG43: 7.2}
Kwa sababu kama watumwa wa kwanza, Wayahudi, ndio walioajiriwa “mapema” katika kutwa, siku ambayo Musa alianza kuandika Bibilia (nuru kutoka kwa Mungu) na kuifanya iangaze kwa ulimwengu, ikaleta kutwa, neno “mapema” kwa hivyo humaanisha kwamba kipindi ambacho kilitangulia
7
kuonekana kwa Bibilia ni usiku wa mfano, wakati hapakuwa na Bibilia duniani. Haikuwapo nuru ya moja kwa moja ya kiroho, bali isiyo ya moja kwa moja — desturi ya mwezi. Mwishowe, basi, kipindi kabla ya Musa na kipindi baada ya Musa (kipindi bila Biblia na kipindi pamoja na Bibilia) hukamilisha mzunguko wa masaa ishirini na nne ya mfano ambayo Bwana aliweka imara mfano Wake, na ambayo ramani hii (ukurasa wa 6) ni uzalishi. {2TG43: 7.3}
Tumeona sasa kwamba kukosekana kwa nuru ya Bibilia kabla ya wakati wa Musa kulisababisha wakati uwakilishwe na usiku, na uwepo wa nuru ya Bibilia tangu wakati wa Musa, ulisababisha kipindi hicho kiitwe kutwa. {2TG43: 8.1}
Kundi la kwanza la watumwa wakiwa ni Wayahudi, na la pili Wakristo, wito mara tatu ujao unaelekeza kwa makundi mengine matatu katika wakati wa Ukristo ambayo yameagizwa kwenda katika shamba la mizabibu. Yatahubiri jambo fulani la asilia kama ulivyokuwa mfumo wa ibada za sherehe ambao Musa alihubiri; na pia asil-ia kama kusulubiwa, kufufuka, na kupaa kwa Kristo ambalo mitume walihubiri, kwa maana ujumbe wa moja lazima ulinganishwe na ujumbe wa lingine; yaani, iwapo jumbe mbili za kwanza zilikuwa za asili, tatu za mwisho lazima ziwe za asili. Ujumbe wa pekee asilia kama huo uliotangazwa baada ya kuhubiri kwa mitume ni siku za kinabii 2300 za Danieli 8:14. Ukihubiriwa kwa mara ya kwanza na Waadventista wa Siku ya Kwanza punde baada ya 1820 B.K. (Pambano Kuu, uk. 331), na ukiwa ni ujumbe wa tatu kwenye mstari wa wito wa mfano kwa watumwa, unaonyesha kwamba katika mkondo wa wakati wa mfano, iligonga saa sita mwaka 1820 B.K. {2TG43: 8.2}
8
Mwito unaofuata wa watumwa kuhubiri jambo jipya na asilia ulikuja mwaka 1844. Ulikuwa kutakaswa kwa Patakatifu baada ya siku za kinabii 2300 kupita, na ulihubiriwa kuhusiana na Sabato ya siku ya saba. Kundi hilo la watumwa walijiita Waadventista wa Sabato. Walitangaza, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imefika. Msujudieni Yeye aliyefanya mbingu, na nchi, na bahari, na chemchemi za maji.” Ufu. 14:7. {2TG43: 9.1}
Saa ya tisa ya mfano, kwa hivyo, iligonga pamoja na kuinuka kwa Waadventista wa Sabato. Lakini ukweli kwamba upo mwito mwingine wa watumwa, ule wa saa ya kumi na moja, wa mwisho, unaonyesha kwamba baada ya ujumbe wa 1844 kutakuwa na ujumbe mwingine kama huo wa asili na pia kundi jipya la watumwa kuutangaza. Ujumbe huu, ujumbe wa saa ya kumi na moja, isitoshe, ni vuguvugu la walei, kwa maana watumwa walipatikana wamesimama na wakitafuta kazi sokoni. {2TG43: 9.2}
“Sokoni” ambapo Mwalimu inasemekana alikuwa ameenda kuwasaka watafuta kazi, ni, bila shaka, kanisa, kwa maana Bwana huwachagua watumwa Wake kutoka kati ya watu Wake walioelimishwa vyema. {2TG43: 9.3}
Je! Tunapaswa kukumbushwa kila mara kwamba katika utangulizi wa kila ujumbe Mwenye nyumba ilimlazi-mu kuwajiri watumwa wapya kutoka kati ya walei? Na je! Siku zote wachungaji hawakujitenga, wakifanya yote walioweza kuwazuia wengine wasikutane na hizo jumbe? Wazo zito lililoje! Jukumu
9
lililoje linakaa juu ya ndugu ambao sasa wanalielekeza kundi! {2TG43: 9.4}
Swali “Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?” linasema kwa udhahiri kwamba wale walioajiriwa si wa wale ambao walikuwa tayari kazini, sio wa ukasisi. Na jibu, “Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri,” lin-afanya dhahiri kwa mkazo kwamba watumwa wa saa ya kumi na moja ni walei waaminifu, wale ambao wanasubiri kwa shauku kumtumikia Bwana, lakini ambao hapo awali hawakupewa nafasi. {2TG43: 10.1}
Kuhusu ujumbe huu wa mwisho Uvuvio ulilionya Dhehebu kwa kuacha kwenye kumbukumbu mistari am-bayo nitasoma sasa: {2TG43: 10.2}
“Naliona,” asema Dada E.G. White, “malaika wakiharakisha kuingia na kutoka mbinguni, wakishuka duniani, na tena wakipaa mbinguni, wakifanya tayari kutimizwa kwa tukio lingine muhimu. Kisha nikamuona malaika mwingine mwenye nguvu ameagizwa kushuka kwa nchi, aiunganishe sauti yake na ya Malaika wa tatu, na kupeana nguvu na uwezo kwa ujumbe wake…. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu, ukiungana nao kama vile kilio cha usiku wa manane kilivyojiunga na ujumbe wa malaika wa pili mwaka wa 1844.” — Maandishi ya Awali, uk. 277. Na ujumbe huo unapaswa kuwa nini iwapo si maandalizi ya dharura kwa hukumu ya walio hai? {2TG43: 10.3}
Tena nalisoma: {2TG43: 10.4}
Ruhusu Mbingu Iongoze
“Unabii lazima utimizwe. Asema Bwana: {2TG43: 10.5}
10
‘Angalieni,nitawapelekea Eliya nabii kabla haijaja siku ile ya Bwana iliyo kuu na ya kuogofya. Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe una bidii sana, hauyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuonyeshe jinsi ya kuufundisha ujumbe wako.’” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475. {2TG43: 11.1}
(Ikiwa unataka kusoma mfano huo katika maelezo yake yote, unaweza kufanya hivyo kwa kusoma Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, Uk. 222-239.) {2TG43: 11.2}
Sasa mnaona ya kwamba wanaoitwa “vichipuko” Kristo Mwenyewe huwaita watumwa wa Mungu. Tunaweza kwa hivyo kuuliza kwa kweli na kwa uaminifu, je! Kanisa na ulimwengu vinaweza kuendelea bila “vichipuko” visivyo maarufu? Jibu ni rahisi: Kama vingeweza kuendelea bila watumwa wa saa ya mapema, na bila watumwa wa saa ya tatu, ya sita na ya tisa, basi kanisa na ulimwengu vingeweza kuendelea bila watumwa wa saa kumi na moja (wanaoitwa eti vichipuko), pia. Lakini katika hali ya kusikitisha kama hii, ulimwengu ungekuwaje? {2TG43: 11.3}
Isitoshe, kwa sababu tangazo la utengo wa watakatifu kutoka kwa wadhambi linatoka kwa watumwa wa saa ya kumi na moja, na maadamu watapiga kelele kwa sauti kubwa na kusema, “Amka, inuka; jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu: kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.” (Isa. 52:1): na pia kusema “Tazama juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani! Ee Yuda,
11
zishike sikukuu zako, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” (Nah. 1:15); inafuata kwamba bila ujumbe wa saa ya kumi na moja na watumwa, Kanisa, Zayuni, lingeachwa kulala milele, kamwe kutoiona miguu yake anayeletea hizi habari njema, ya yeye anayetangaza amani, na kamwe lisijivike mavazi yake mazuri, kamwe kutofanya listahiki Ufalme. {2TG43: 11.4}
Nasema kwamba likiachwa katika hali hii isiyofurahisha na isiyo takatifu yamkini wateule wangebaki najisi na wasiotakaswa milele — waliodanganywa! Na kwa sababu watumwa wa saa ya kumi na moja, Wadaudi, ndio ambao ujumbe wa utakaso huu, “Hukumu ya walio Hai,” wamekabidhiwa, basi wale ambao kwa habari yake ni maadui zetu, wale wanaotenda kila kitu wanachoweza kuwazuia watu wa kawaida wasijue Ukweli na wasiku-tane Nao, ndio wale haswa wanaojaribu kuwadanganya “yamkini wateule,” ikiwezekana. Mshukuru Mungu kwamba haitawezekana. {2TG43: 12.1}
Tunapaswa, kwa hivyo, kutangaza hizi habari njema za amani hata na bidii zaidi kuliko hapo awali, maana anaamuru Bwana: {2TG43: 12.2}
“Kwa hivyo waambieni nyumba ya Israeli,” kanisa, “Bwana MUNGU asema hivi; … Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, Nitakapotakaswa ndani yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote,
12
na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nita-watakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote, Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu; Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu; nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu.” Ezek. 36:22-28. {2TG43: 12.3}
Hazitatufaa tukipitia juu juu aya hizi za Maandiko jinsi sisi na Dhehebu lote tumekuwa tukifanya hapo awali. Sote tunapaswa kuzingatia kwa uangalifu kwamba Bwana atajitakasa Mwenyewe kwa kuwatoa wateule Wake kutoka kati ya mataifa, na kutoka katika nchi zote, na kuwaleta katika nchi yao, katika nchi ya baba zao. “Wa-kati huo,” watakaporudi katika nchi ya baba zao, yasema maandiko, Yeye atawanyunyizia maji safi, na hivyo watatakaswa uchafu wote na sanamu zao zote. Wakati huo na hapo watapewa moyo mpya, na roho mpya, na wafanywe kuenenda katika sheria za Mungu na kuzishika hukumu Zake. Kwa hili anaongeza Bwana: {2TG43: 13.1}
“Ijulikane kwenu ya kuwa silitendi neno hili kwa ajili yenu, asema Bwana MUNGU: tahayarikeni na kufadhaika kwa sababu ya njia zenu, enyi nyumba ya Israeli. Bwana MUNGU asema hivi; siku ile Nitakayowa-takaseni na maovu yenu yote nitawafanya miji ikaliwe na watu, na palipobomolewa pajengwe tena. Nchi ili-yokuwa ukiwa italimwa,
13
ijapokuwa ilikuwa ukiwa machoni pa wote waliopita.” {2TG43: 13.2}
“Nao watasema, nchi hii iliyokuwa ukiwa imekuwa kama bustani la Edeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa na magofu, sasa ina maboma inakaliwa na watu. Ndipo mataifa yaliyobaki karibu yenu pande zote wa-tajua ya kuwa mimi BWANA namejenga mahali palipoharibika, nami nimepanda mbegu katika nchi iliyokuwa ukiwa; Mimi, Bwana, Nimesema hayo, tena Nitayatenda.” {2TG43: 14.1}
“Bwana MUNGU asema hivi; tena kwa ajili ya jambo hili Nitaulizwa na nyumba ya Israeli, ili Niwatendee; Nami Nitawaongeza kwa watu kama kundi la kondoo. Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu; miji ile iliyokuwa maganjo nao wa-tajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana.” Ezek. 36:32-38. {2TG43: 14.2}
Mtu yeyote asithubutu kusema kwamba ahadi hizi zimetukia, na mtu yeyote asithubutu kusema kwamba ni za baada ya millenia. Fikiri juu yake na uzichambue tena, Ndugu, Dada. Usizipuuzilie mbali, kwa maana ni uzima wako. Zinamaanisha wokovu wako, hatma yako, umilele wako. Hakuna mtu anayestahili kuishi na kutawala na Kristo katika miaka elfu ambaye hashiriki katika utakaso huu. {2TG43: 14.3}
Hatimaye, wale wanaotutupa nje, na wanaonena vibaya dhidi yetu, wale ambao wanapiga vita sana kuzuia ujumbe kwa watu, nina uhakika mnaona wazi, ndio wale ambao haswa hutumiwa na kiongozi wa mwasi ku-wadanganya “yamkini hata walio wateule” (Mat. 24:24). Ni wale waliotutupa nje ya makanisa
14
ambayo tulisaidia kujenga; wale wanaowatisha walei, wakiwakataza kusoma vitabu, na kuwaamuru wavitupe kwenye jiko ili kuwadumisha wasiujue ujumbe wa Mungu wa saa hii. Juhudi zao zote, hata hivyo, zitashindwa kabisa amini amini kama zile juhudi za Wayahudi viongozi dhidi ya ujio wa Kristo wa kwanza. {2TG43: 14.4}
Kwa sababu hii dhahiri kanisa haliwezi kuendelea bila sisi “vichipuko,” kwa usahihi “vichipukizi,” na bado li-okolewe kwa umilele. Hebu sasa nisome ahadi ya Mungu na himizo kwa sisi sote: {2TG43: 15.1}
“Lisikieni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya Neno Lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, na atukuzwe Bwana, lakini Yeye atatokea kwa furaha yenu, nao wataona haya.” (Isa. 66:5) {2TG43: 15.2}
Je! Wadaudi, Ujumbe Wao, Na Mafanikio Yao Yako Katika Unabii ?
Sasa kwa swali hili, nasema kwamba lazima wawepo iwapo Mungu ndiye anayewajibika kwa kuwepo kwao. Tafadhali fungua nami kwa — {2TG43: 15.3}
Hos. 1:10 — “Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usiowe-za kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu Wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai. Na wana wa Yuda na
15
wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kiongozi mmoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.”
Hapa mnaona kwamba Wayahudi wangekataliwa kuwa watu wa Mungu, na mnajua vyema kwamba hili lil-itukia Bwana alipowaambia: “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” Mat. 23:38. {2TG43: 16.1}
Unabii hata hivyo unaendelea na kuonyesha hadi kwa wakati wa kukusanya, wakati ambapo watu wa Mungu waliotubu watajiteulia kiongozi mmoja, mfalme. Hawa, bila shaka, si Wayahudi ambao hawajaongoka wa leo, ila ni wazawa kutoka kati ya wale ambao wamefyonzwa na mataifa na kanisa la Kikristo, kutoka kwa wale ambao wamepoteza utambulisho wao na ambao sasa ni “kama mchanga wa bahari” kwa idadi, lakini sasa kama Mataifa (mataifa kwa ufahamu wao na wa ulimwengu usio wa kuona mbali) wamempokea Kristo. (Wewe ambaye ume-kosa masomo yangu yaliyopita juu ya mada hii, unaweza kusoma Salamu Mwafaka, Gombo la 1, Namba 29 na Trakti Namba 8, Mlima Sayuni katika Saa ya 11, uk. 7-17.) {2TG43: 16.2}
Nani ndiye kiongozi duniani, mfalme, ambaye Maandiko husema watu “watajiwekea” wakati wa ku-kusanywa? — Hebu tusome, {2TG43: 16.3}
Hos. 3: 4, 5 — “Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao,
16
na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema Wake kwa kicho siku za mwisho.”
Katika sehemu hii ya unabii, unaona, tunaambiwa kwamba baada ya kukaa kati ya Mataifa kwa “siku nyingi” bila mfalme, na bila ishara yoyote ya utambulisho (wakiwa wamesahaulika kabisa kama taifa na kama watu), mwishowe watakuwa na wa uakisi Daudi wa kutawala juu yao. Huyu hawezi kuwa Daudi wa zamani kwani alikuwa tayari amekufa wakati unabii huu ulipofanywa. Wala huyu Daudi aliyeahidiwa hawezi kuwa Kristo Mwenyewe, kwa maana Kristo ni mwana wa Daudi (Mat. 22:42), sio Daudi mwenyewe; na ikiwa Yeye, isi-toshe, atakaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi (Luka 1:32), basi lazima Daudi awe na kiti cha enzi cha Yeye kukaa juu yake. {2TG43: 17.1}
Tena, utaona kwamba Hosea 1:11 huahidi kwamba itakuwa kuu siku ya Yezreeli. Na Yezreeli ni nani? — Vyema, katika sura hii unapata kwamba yeye ndiye mzaliwa wa kwanza wa Hosea katika mfano. Katika sehemu hiyo ya mfano ambayo ni ya kipindi cha Uyahudi, na ambayo hupatikana katika sura ya kwanza ya Hosea, majina ya watoto wawili wachanga yamewekwa kiambishi awali “Lo.” Lakini katika sehemu ya mfano ambayo inahusu kipindi cha Ukristo, hadi kwa wakati wa kukusanywa, unavyoonekana katika sura ya 2, herufi “Lo” zimeondolewa, kama vile jina “Wayahudi” tunapata limeachwa na kanisa la Agano Jipya na jina “Wakristo” limechukuliwa badala yake. (Utapata uchambuzi wa kina wa sura hizi kwenye Trakti Namba 4, Habari za hivi Punde kwa “Mama.”) Sura ya pili ya Hosea huanza na amri: {2TG43: 17.2}
17
Hos. 2:1-5 — “Waambieni ndugu zenu wanaume, Ami na ndugu zenu wanawake, Ruhama. Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke Wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake; Nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, Nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame, na kumfisha kwa kiu; naam, Sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi. Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.”
Imekuwa wazi kwamba Mungu anamwagiza Yezreeli, mzaliwa wa kwanza wa watoto hao watatu, anene na kaka yake Ammi na dada yake Ruhama, ambao katika mfano ni nembo ya walei, wote wa kiume na wa kike. Mama ambaye wameamriwa kumrekebisha, ni mfano wa ukasisi, wa wale ambao huzalisha waongofu ndani ya familia ya kanisa. Yule ambaye Mungu hunena naye (Yezreeli), kwa hivyo, ni nembo ya nabii. Hapa unaona wa-zi kwamba “uamsho na matengenezo” hayaji kupitia kwa ukasisi (mama) ila kupitia kwa walei, watoto, na ya kwamba ukasisi (mama) yu katika uhitaji mkubwa zaidi wa matengenezo kuliko walei, kwa maana mama anashtakiwa kwa kutokuwa mwaminifu na kupitia kwa watoto ameshauriwa kufanya matengenezo. Hili hakika ni vuguvugu la walei linaloongozwa na Roho ya Unabii , kwa juhudi na ujumbe wa Yezreeli iliovuviwa na mbingu. {2TG43: 18.1}
Ukweli kwamba siku ya Yezreeli itakuwa kuu, pamoja
18
na ukweli kwamba yeye ni mfano wa nabii, unathibitisha kwamba si tu ujumbe wa Wadaudi wenyewe u katika unabii, lakini kwamba hivyo pia ni mafanikio yake na hitaji la matengenezo lililoandikwa humo. Hapa unaona kwamba juhudi mbovu za Adui kuukomesha ujumbe na kuifanya kazi ya Yezreeli isiwe na matokeo wa-tashindwa, maana “siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana,” asema Yule mwenyezi, wakati Yeye anawaleta watu Wake wote watakwea watoke katika nchi hii. (Hos. 1:11). {2TG43: 18.2}
Ujumbe kwa Walaodekia, pia, umeelekezwa kwa ukasisi, kwa maana asema Bwana: {2TG43: 19.1}
Ufu. 3:14-16 — “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika;… Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, N itakutapika utoke katika kinywa Changu.”
Hapa pia, malaika (ukasisi), ambaye anasimamia kanisa, tena anakemewa na kutakiwa afanye matengenezo. {2TG43: 19.2}
Ezekieli pia ni shahidi wa “ufunuo huu wa kushangaza,” kwa maana anatangaza kwamba utakaso unaanzia “kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba” (Ezek. 9:6). Hebu tufungue unabii wa Ezekieli: {2TG43: 19.3}
Ezek. 9:1-10 — “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. Na huo utukufu wa Bwana wa
19
Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.”
“Na hao wengine Aliwaambia nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige: jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma: Waueni kabisa mzee na kijana, na mjakazi na watoto wachanga, na wanawake: lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu Pangu. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. {2TG43: 20.1}
“Akawaambia, Itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa: haya enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee, Bwana Mungu! utaangamiza mabaki yote ya Israeli wakati wa kumwaga ghadhabu Yako juu ya Yerusalemu? {2TG43: 20.2}
“Ndipo Akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu: maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, Naye Bwana haoni. Nami, jicho Langu halitaachilia, wala Sitaona huruma, lakini Nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao.” {2TG43: 20.3}
Sio ulimwenguni, bali katika Yuda na Israeli,
20
kanisani, uovu ni mwingi, na hapo ndipo mchinjo unafanyika. Isitoshe, umati ambao unaendeleza na kusitawisha machukizo haujui kwamba wanatenda kana kwamba Bwana ameiacha nchi, kana kwamba Amewaachia ili kuiendesha na kuwatenda watu Wake kama watakavyo. {2TG43: 20.4}
Hapa unaona inamaanisha nini kuisikia Fimbo, na inamaanisha nini kuziba masikio yako kwayo. {2TG43: 21.1}
Utakaso wa Kanisa (Hukumu ya walio hai) ni, kupitia nabii Danieli katika sura ya 7, aya ya 10, inaitwa huku-mu, na katika sura ya 8, aya ya 14, inaitwa utakaso wa Patakatifu. Kristo, hata hivyo, katika mmoja wa mifano Yake anafananisha utakaso na mavuno ambayo magugu (wadhambi) huchomwa, na ngano (watakatifu) huwe-kwa ghalani (ndani ya lililotakaswa Kanisa la Ufalme). Ujao Yeye huulinganisha na juya ambalo, baada ya kuvutwa pwani, samaki wabaya (wadhambi) hutupwa nje, na samaki wazuri (watakatifu) hutiwa ndani ya vyombo. {2TG43: 21.2}
Wakati wale ambao hawatapokea alama, na hivyo si muhuri, wataondolewa mbali, kisha kanisa litaonekana “zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha kama jeshi lililo na mabango.” (Manabii na Wafalme, pg. 725), na “wale tu ambao wameyastahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusi-wa kutenda sehemu katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu.” — Mapitio na Kuhubiri, Novemba 19, 1908. {2TG43: 21.3}
21
Hebu sasa tuone lile litakalotukia baada ya umati wenye kupenda machukizo kuanguka chini ya silaha za ku-chinja za malaika; hebu tuone litakalofanywa kwa wale walioachwa. Ili kuona hili tunaenda tena kwa unabii wa Ezekieli: {2TG43: 22.1}
Ezek. 37:16-28 — “Na wewe mwanadamu, twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake:
“Ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja; navyo vitakuwa kijiti kimoja mkononi mwako. Na wana wa watu wako watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonyesha maana ya mambo haya utendayo? {2TG43: 22.2}
“Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, Nami nitawaweka pamoja nacho, yaani pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja, navyo vitakuwa kimoja mkononi Mwangu. {2TG43: 22.3}
“Navyo vijiti ambavyo uliandika juu yake vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao. {2TG43: 22.4}
“Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa wali-kokwenda, Nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe: {2TG43: 22.5}
“Nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya
22
milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena hata milele. {2TG43: 22.6}
“Wala hawatajitia unajisi tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa na kuwatoa katika makao yao yote ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wao. {2TG43: 23.1}
“Na mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao; nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao watae-nenda katika hukumu Zangu, na kuzishika amri Zangu, na kuzitenda. {2TG43: 23.2}
“Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo mtumishi Wangu, ambayo baba zenu wamekaa humo; na wa-takaa wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao milele; na Daudi mtumishi Wangu atakuwa mkuu wao milele. {2TG43: 23.3}
“Tena Nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; Nami Nitawaweka, na ku-wazidisha, Nami nitaweka patakatifu Pangu kati yao milele. {2TG43: 23,4}
“Tena maskani Yangu itakuwa pamoja nao; Nami, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu Wangu. {2TG43: 23.5}
“Na mataifa watajua ya kuwa mimi, Bwana, Mimi niwatakasaye Israeli, patakatifu Pangu patakapokuwa kati yao milele.”{2TG43: 23.6}
23
Hapa unaona kwamba sio tu Mungu atalisafisha kanisa Lake (Yuda na Israeli) kwa kuwaondoa wale wote ambao wanaichafua nyumba Yake ya sala, lakini kwamba baadaye Atawakusanya ndani ya kanisa Lake lili-lotakaswa wote waliotawanyika ambao wamezaliwa kutoka kwa zote Ufalme wa Israeli (makabila kumi) na Ufalme wa Yuda (yale makabila mawili) — wote ambao wako nje sasa kati ya mataifa, sio katika kanisa la Wala-odekia. Atawafanya kuwa taifa moja, ambalo punde kabla ya Millenia, atatawala Daudi wa uakisi, mfalme wao. Hawatakasirishwa tena na wapagani; Hawatakuwa tena kati ya wadhambi; hawatalishwa tena na umati wa wa-chungaji, bali na mmoja tu — na mchungaji aliyeteuliwa na Mungu. Kuu hakika itakuwa siku ya Yezreeli! Juhudi zake na juhudi za watenda kazi wenzake, walei, zitafanikiwa iwapo mama (ukasisi) atasikia au atakataa. {2TG43: 24.1}
Kwa udhahiri, unaona, Wadaudi, ujumbe wao, na mafanikio yao yako katika unabii. {2TG43: 24.2}
Je! Vitabu Vya Fimbo Ya Mchungaji Pia Viko Katika Unabii?
Kwa swali hili nabii Mika anajibu: {2TG43: 24.3}
Mika 6:9 — “Sauti ya Bwana inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na Yeye aliyeiagiza.”
Sasa umesikia Mungu Mwenyewe akipendekeza kwamba uisikie ile Fimbo — naam, Fimbo ya Mchungaji, maana tangu siku ya Mika Fimbo ya Mchungaji ndio fimbo pekee ambayo imenena, fimbo pekee ambayo
24
inaweza kusomwa na kusikilizwa. Wenye hekima wataliona jina lake, na kuisikia sauti yake na pia Yeye Ali-yeiteua. Watavijaza vyombo vyao “mafuta” ya ziada (Mat. 25:4), asema Bwana. {2TG43: 24.4}
Hivyo imeonekana kwamba sio tu vitabu vya Fimbo viko katika unabii, ila kwamba unashauriwa kuisikia. Iwapo utapuuza fursa hii, kwa kawaida utapatikana na wadhambi wanaoendeleza machukizo kanisani. Lakini ikiwa sasa ukitoa umakini kwa Sauti ya Mungu kupitia Fimbo, utapokea muhuri wa idhini ya Mungu. {2TG43: 25.1}
Je! Watakatifu Watafanya Nini Baada Ya Utengo?
Kwa ajili ya nuru kwa mada hii, tunamwelekea Isaya, nabii– {2TG43: 25.2}
Isa. 66:15, 16, 19, 20 — “Maana Bwana atakuja na moto, na magari Yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu Yake kwa moto uwakao, na maonyo Yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi ….
“Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali, na Yavani, katika visiwa vilivyo mbali, ambao hawajaisikia sifa Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika Mataifa. {2TG43: 25.3}
“Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote kuwa sadaka kwa Bwana juu ya farasi, na katika
25
magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Ye-rusalemu, asema Bwana, kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” {2TG43: 25.4}
Baada ya kuuawa kwa wadhambi ambao wanasema mioyoni mwao kwamba Bwana anakawia kuja Kwake, na wanaokula na kunywa pamoja na walevi (Mat. 24:48, 49), basi inakuwa kwamba Bwana anawatuma wale ambao wataokoka kutoka kwa mchinjo wa Bwana kwa ziara ya umishonari; Yeye anawatuma, unaona, kwa Ma-taifa, kwa nchi ambazo bado hazijamjua Mungu na ujumbe Wake. Waliokoka wanaleta nyumbani kwa Bwana ndugu zao wote, wote watakaookoka. Hivyo ndivyo kazi ya injili inavyokamilishwa, na hivyo watu wa Mungu wanaokolewa na kuitwa watoke Babeli ya uakisi (Ufu. 18:4) hadi mahali safi ambapo hakuna dhambi na hakuna hatari ya mapigo ya Babeli kuwaangukia. {2TG43: 26.1}
Nina uhakika kwamba sasa unaona wazi kwa nini Wadaudi Wadventista wa Sabato si “vichipuko” bali ni “vi-chipukizi,” na inamaanisha nini kuisikia Fimbo na Yeye aliyeiteuwa, na vile vile humaanisha nini kupiga kisogo dhidi Yake. {2TG43: 26.2}
Mnaweza sasa kwa busara kuamua wenyewe ni msimamo gani mtachukua. Mnaweza kuchukua msimamo wenu pamoja na wapinzani dhidi ya Ukweli na matengenezo, au mnaweza kuchukua msimamo wenu kwa Ukw-eli wa Mungu na wajumbe Wake, na kwa kuyageuza maisha yenu wenyewe mnaweza kuwaongoza wengine kufanya vivyo hivyo. Lolote utakaloamua utajua kwamba ni chaguo lako mwenyewe. Mungu, hata hivyo, Am-baye anajua lililo bora kwa maslahi yako mwenyewe hukushauri
26
umfuate Yeye kutenda yale ambayo kweli huamuru. Natumaini hili litakuwa chaguo la moyo wako wote na hivyo furaha ya maisha yako, kwamba hautakubali kamwe kuwa “kilele kilichokufa”, ila kwamba utaamua kwa bidii kuwa “kichipukizi” hai. Natumaini kwamba hamna yeyote kati yenu atawaruhusu maadui wa Mungu wanene utoke kwa kweli hizi zilizofunuliwa kwa Maandiko haya yaliyoachwa na wanadamu, maana unajua tayari kwamba wapinzani wa Ukweli hawana lolote rasmi, hawana la mamlaka, na hawana la busara au la maana kukupatia kwa hizi kweli ambazo hazijafunuliwa zamani. Naam, natumaini kwamba hutaziuza hizi “lulu za tha-mani kubwa” kwa takataka na makapi. {2TG43: 26.3}
27
Kwa Afya Na Starehe I Hapa Nafasi Yako
Ili kudumisha afya ya familia yake na kupata wakati wa kujua ni nini cha kuwapikia, ni lengo la kila mwenye nyumba na shida, siku baada ya siku. Na hivyo, Wenye Nyumba, mbona msiruhusu “Kabari Inayoingia” na “Kitabu cha Mapishi Sahihi” viwasuluhishie hizi shida. Vitabu hivi viwili vinajumuisha kurasa 170, na vi-nasheheni habari muhimu kuhusu afya na upishi, habari ambazo hazipatikani katika vitabu vingine vyovyote. Trakti hizi sio ukumbusho wa jambo fulani, ila ni waalimu wa kila dakika nyumbani, wenye sifa kutoka kwa wenye mamlaka bora. Unaweza kujipatia “Kabari Inayoingia” kwa senti 15 na Kitabu cha “Mapishi Sahihi” kwa senti 25, — vyote vinalipiwa ada ya posta kwa kutuma senti 40 katika sarafu kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. (Ruhusu wiki nne kwa kusafirisha.)
28
ISHARA ZA KUJA KWA YESU MARA YA PILI, AUISHARA ZA UFALME — ZIPI?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JANUARI 22, 1949
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Sisi kama wanafunzi na waalimu wa injili kwa miaka mingi tumekazia fikira sana kwa ishara za kuja mara ya pili kwa Kristo, lakini sivyo kamwe kwa ishara za Ufalme. Kama tokeo la hili, Jumuiya ya Wakristo kinadharia imeziunganisha ishara za Ufalme na ishara za Ujio wa pili. {2TG44: 29.1}
Jambo linalofanana na hili ni lile Wayahudi wa zamani walifanya wakati walipokuwa wakitarajia kuonekana kwa Masihi mara ya kwanza. Kwa mujibu wa uelewa wao walivyopenda walichambua kwa undani ishara za urejesho wa Ufalme, lakini si sana ishara za kuja kwa Masihi. Hivyo ilikuwa kwamba wakati walipoambiwa Masihi alikuwa amekuja lakini si wakati wa kuurejesha Ufalme, viongozi wa Wayahudi, kwa kupuuza kwamba ufasiri wao wapendavyo tu (usio vuviwa) wa Maandiko ulikuwa wa makosa, waliukataa ujumbe wa siku hiyo. Kisha katika jaribio la kulinda ushawishi wao kwa watu wa kawaida na kuwatiisha kwa njia yao ya kufikiri, walimsulibisha Bwana, Mwokozi na Mfalme wao jinsi pia walivyowaua manabii waliomtangulia. Kusisitiza kwao kwamba Ufalme urejeshewe katika siku yao, hata hivyo, hakukuwafaidi chochote. {2TG44: 29.2}
29
Ukweli kwamba Ukristo wenyewe umegawanyika na kukanganyikiwa, moja likiamini jambo moja na jingine jambo lingine, ndani yake wenyewe ni ushahidi wa kutosha kwamba mbali na kuwa katika giza totoro la ishara za Ufalme kwa sababu ya ufasiri wa wapendavyo wa Maandiko, Ukristo lazima uwe gizani kwa mambo men-gine mengi vile vile. Katika kama hiyo iliyovurugwa hali ya imani, Ukristo hakika hauongozwi tena na Roho wa Kweli kuliko walivyokuwa Wayahudi waasi. Uzoefu wa zamani hufundisha, hata hivyo, kwamba kujaribu kushawishi umati kwa ukweli huu itakuwa kazi ngumu kama kuwashawishi Wayahudi hata leo kwamba Kristo ndiye Masihi ambaye angekuja. Ugumu, bila shaka, upo katika ukweli kwamba ni vigumu mwanatheolojia aru-husu uwezekano kwamba uelewa wake wa Bibilia unaweza kuwa angalau kwa kipimo wa makosa, na kwamba Uvuvio unaweza wakati wowote kujidhihirisha Wenyewe upya, ukikunjue chuo na kuleta Ukweli mwafaka, “chakula kwa wakati wake,” na hivyo kufunua dhana zao za kibinafsi za unaoitwa eti ukweli. {2TG44: 30.1}
Sasa kwa heshima na uaminifu wote, kwa mamlaka ya Maandiko na kwa msingi wa kweli zilizo mbele yangu, nasema kwamba itakuwa rahisi kwa kuku kupata kiota chake katika utotoro wa giza kuliko kwa akili ambayo haijavuviwa kuufunua unabii na mifano. Tofauti kati ya hao wawili ni kwamba kuku hutambua ubatili wa kuja-ribu kupata kiota chake baada ya machweo, lakini mtu mkaidi hatambui kwamba hawezi kuufunua Ukweli apendavyo mwenyewe na bila nuru kutoka juu. {2TG43: 30.2}
Sisi kama wakristo tumeshindwa kutambua dhahiri kwamba iwapo mambo ya siri ya Mungu, haijalishi ni rahi-si jinsi gani,
30
yangefunuliwa wakati wowote na mtu yeyote, Uvuvio kamwe usingalikuwa umeyaficha katika nembo na mifano. Jumuiya ya Kikristo bado imepofuka kwa ukweli kwamba kujaribu kuingia ndani ya siri za Mungu itakuwa kujaribu kuyashinda maazimio Yake; naam, kujaribu kuingia katika msimbo wa Mungu, ni kujaribu lisilowezekana. Kwa mfano, hata wakati ulipokuja wa Kitabu kilichofungwa na mihuri saba kufunuliwa (Ufu. 4 na 5), hakuna yeyote mbinguni au duniani aliyeweza kufanya hivyo, ila tu “Simba wa kabila la Yuda” angeweza kuzivunja hizo mihuri na kuyaangalia mambo ambayo baadaye yalionyeshwa kwa Yohana, Waufunuo. Na ingawa Yohana aliyaandika, yeye mwenyewe hangeweza kabla ya wakati kuyafafanua. Basi tunawezaje kufan-ya hivyo kabla ya wakati na bila Uvuvio wa Roho yule yule Ambaye aliyaandikisha? Neno la Mungu linaonya wazi: {2TG43: 30.3}
2 Pet. 1:19-21 — “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo ma-hali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyoto-ka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”
Hakuna yeyote, yasema Maandiko, anaweza apendavyo (bila Uvuvio) kuufunua unabii, kwa maana, anaelezea Mtume, haukuja kwa juhudi za apendavyo mtu — si kwa mapenzi ya wanadamu, ila kupitia kwa watu watakati-fu na Roho — wala hauwezi kwa hivyo kuwa ufasiri wa apendavyo mtu tu, bali kupitia kwa watu watakatifu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Isitoshe, hata
31
baada ya unabii kufasiriwa hivyo, ni kwa wenye haki tu (wanaotubu) ndio hupewa zawadi ya kuelewa (Dan. 12:10). {2TG43: 31.1}
Kwa sababu sisi kama watu tunajua baadhi ya ishara za kuja kwa Kristo mara ya pili, na bila ishara za Ufalme, ingekuwa bora sasa tukazie fikira ishara za Ufalme. {2TG44: 32.1}
Mat. 13:24-30 — “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa Mwenye nyumba wakaenda Wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde Lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa Wakamwambia, Basi, Wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno Nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.”
Mfano huu wa Ufalme, unaona, una vipindi vitatu vya wakati: Kwanza, kipindi cha kupanda mbegu — wakati wa ukasisi wa Kristo; pili, kipindi cha kukua — wakati kutoka kupaa kwa Kristo hadi kwa mavuno; tatu, wakati wa mavuno — kipindi kifupi cha wakati “mwisho wa dunia” (Mat. 13:49), kipindi ambamo dunia inaangazwa kwa utukufu wa malaika (Ufu. 18:1), na ambamo watu wote wa Mungu wanaitwa watoke Babeli (Ufu. 18:4). Ndipo wale ambao hawakuitikia mwito huu wa kukusanywa watalia: “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatujaokolewa.” Yer. 8:20. “Mavuno,” kwa hivyo, ni “mwisho wa dunia.” Mat. 13:49. Huanzia kanisani na kwishia Babeli. {2TG44: 33.1}
Kazi ya mavuno, kwa udhahiri, ni kisawe na Hukumu ambayo huamua ni nani magugu na ni nani ngano — ni nani watachomwa na kuharibiwa kama magugu sugu, na ni nani kama ngano ya thamani ambao wataingizwa “ghalani,” katika Ufalme. Hivyo ni kwamba Hukumu ni kutakaswa kwa patakatifu (Dan. 8:14), “nyumba ya Mungu,” hekalu ambalo Bwana analijia ghafla na kuwatakasa watumwa Wake, Walawi. Hivi ndivyo andiko la mwisho husoma: {2TG44: 33.2}
Mal. 3:1-3, 5 — “Angalieni, Namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anaku-ja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki …. Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; Nami nitakuwa shahidi mwepesi
33
juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiri-wa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.”
Je! Mazao mangapi ambayo mavuno yatatoa? — Iwapo watu 144,000 ni “malimbuko” (Ufu. 14:4), basi lazima yawepo “mavuno ya pili,” kwa sababu pale ambapo hakuna ya pili hapawezi kuwapo ya kwanza. Neno “malimbuko” hufanya iwe lazima mavuno ya pili. {2TG44: 34.1}
Je! Malimbuko yanatoka wapi, na mavuno ya pili yanatoka wapi? — Tumeambiwa wazi kwamba malimbuko ni Waisraeli — wote kutoka kabila kumi na mbili za Israeli (Ufu. 7:4-8). Israeli hakika huwakilisha ushirika wa kani-sa kwa wakati wametiwa muhuri; jina “Israeli” haliwezi kupotoshwa kumaanisha ulimwengu. Malimbuko, kwa hivyo, yanavunwa kutoka kwa kanisa lenyewe wakati ambapo utengo unaanza. Neno wametiwa “muhuri” hu-maanisha kuwekwa mahali salama — wametiwa muhuri. Hivi hasa ndivyo mtume Petro anasema: {2TG44: 34.2}
1 Pet. 4:17, 18 — “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?”
Sasa, basi, iwapo Hukumu inaanza kwanza katika “nyumba ya Mungu,” kanisani, basi itakwishia duniani, nje ya mizingo ya kanisa. Mfano wa “juya”
34
na Ufunuo wa Yohana kwa ufupi sana na kwa mkato huuonyesha wazi ukweli huu kwa ubora. {2TG44: 34.3}
Mat. 13:47-50 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wa-baya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”
Kwa udhahiri, juya huwakilisha kanisa la injili ambalo huwanasa wote mnafiki na mtakatifu. Kwa hivyo, kati-ka wakati wa mavuno ya malimbuko (Hukumu “katika nyumba ya Mungu”) “mwisho wa dunia” (Mat. 13:49), malaika watawatenga waovu kutoka kati ya wenye haki, sio wenye haki kutoka kati ya waovu. Lakini katika mavuno ya mazao ya pili ya (Hukumu katika ulimwengu) utengo ni kinyume: wenye haki watatolewa kutoka kati ya waovu, sio waovu kutoka kati ya wenye haki, hivyo wasema, Ufunuo: “Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu 18: 4. Kwa udhahiri, Hukumu “katika nyumba ya Mungu” ni mavuno ambayo wanafiki kama “magugu” huchomwa, lakini kama “samaki” wabaya hutupwa nje. Katika Hukumu huko Babeli (ulimwenguni), hata hivyo, sio wabaya, bali wema wanatolewa na kuletwa katika nyumba ya Mungu iliyosafishwa ambamo hakuna dhambi na hamna mdhambi, na mahali ambapo hakuna hatari ya mapigo. Ukweli uu huu kuihusu nyumba ya Mungu tena
35
unatujia kwa maneno haya: {2TG44: 35.1}
Isa. 66:15, 16, 19, 20 — “Maana Bwana atakuja na moto, na magari Yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu Yake kwa moto uwakao, na maonyo Yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi …. Nami nitaweka ishara kati yao, Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.”
Tena tunaona hapa kwamba wale ambao wanaookoka mchinjo wa Bwana “katika nyumba ya Mungu” (bila shaka malimbuko, “watumwa wa Mungu”), wanatumwa kwa mataifa ambayo hayamjui Mungu, na kutoka huko wanawaleta ndugu zao wote (mavuno ya pili) hadi katika nyumba ya Mungu iliyotakaswa ambamo hamna dhambi au mwenye dhambi, na ambamo mapigo ya Babeli hayawezi kuangukia. {2TG44: 36.1}
Tumeona sasa yakini kwamba yapo malimbuko na mavuno ya pili: moja kutoka kwa kanisa — watu 144,000 wana wa Yakobo; na moja kutoka kwa mataifa yote — umati mkubwa ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu (Ufu. 7:9). {2TG44: 36.2}
36
Ni nani anayekusanya malimbuko iwapo malimbuko yanakusanya mavuno ya pili? — Hebu tupate jibu letu kwa kusoma– {2TG44: 37.1}
Ufu. 14:14-19 — “Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa Chake, na katika mkono Wake mundu mkali. Na ma-laika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu Yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu Wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. Na Yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu Wake juu ya nchi, nchi ikavunwa. Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sa-na. Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shin-ikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.”
Hapa tunaambiwa tena kwamba yapo mavuno mawili, moja na Mwana wa Adamu, na lingine na malaika. Uvunaji wa Mwana wa Adamu hutangulia uvunaji wa malaika. “Mwana wa Adamu,” kwa hivyo, hukusanya malimbuko, na malaika hukusanya mavuno ya pili. (Mizabibu, sio zabibu zilizoiva kabisa, yeye anazitupa kwenye kinu cha divai.) Mwana wa Adamu Mwenyewe huvuna malimbuko kwa sababu watumwa Wake (ki-mfano ma-laika wa kanisa la Walaodekia) hawako katika hali ya kufanya kazi kama hiyo, kwa maana wao wenyewe ni “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi,” na hawajui (Ufu. 3:14-18). {2TG44: 37.2}
37
Kutazama chini hadi kwa wakati huu, Roho ya Unabii katika siku za Isaya alisema: {2TG44: 38.1}
Isa. 63:5 — “Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono Wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu Yangu ndiyo iliyonitegemeza.”
Hapa unaona kwamba wakati ulipokuja hapakuwa na hata mmoja kati ya watumwa Wake “kuitegemeza” kazi ya mavuno, na kwa sababu hiyo Bwana Mwenyewe alifanya kazi hiyo bila wao. {2TG44: 38.2}
Kwa uvunaji wa pili, hata hivyo, Yeye hutumia “watumwa” Wake wasio na uongo, “malimbuko,” watu 144,000, kama waliofananishwa kimbele na malaika mwenye mundu mkali (Ufu. 14:17, 18). Na kama vile yapo mavuno mawili na uvunaji mara mbili kutoka sehemu mbili tofauti, kanisa na dunia, kama ilivyoonyeshwa hapo awali, pia njia mbili za kuvuna: mwanzoni wabaya wanaondolewa kutoka kwa wema, na mwishowe wema wanaitwa watoke kati ya wabaya. {2TG44: 38.3}
Hizi ni baadhi ya ishara na matukio ambayo hutangulia Ufalme wa utukufu, kuja mara ya pili kwa Kristo. Ki-sha, pia, zipo ishara zingine, ya kwanza ambayo inaonekana kutoka kwa mfano wa Mathayo 25. {2TG44: 38.4}
Mat. 25:1-12 — “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao,
38
wakatoka kwenda kumlaki Bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walit-waa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata Bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Tazama, Bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao wali-pokuwa wakienda kununua, Bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja Naye arusini; mlan-go ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, Siwajui ninyi.”
Katika mfano huu imeonekana kwamba kanisa limefananishwa na wanawali kumi, watano ambao hawajajipa-tia mafuta ya ziada — Ukweli maalum kwa wakati huu, yaani, hawa watano hawazingatii ukweli wa Hukumu ya walio hai, utengo au utakaso wa kanisa. Wakati kilio kinapofanywa, “tazama, Bwana arusi; tokeni mwende Kumlaki,” wanawali wote kumi wanaona kwamba nuru ya taa zao inazimika; wanaona kwamba ujumbe wa Hukumu ya wafu inapita. Upesi basi, wanawali watano wenye busara wanazijaza tena taa zao na mafuta ya zi-ada ambayo wamehifadhi katika vyombo vyao, na kuendelea kukutana na Bwana arusi. Lakini wanawali wa-tano wapumbavu, wale waliofikiri haikuwapo haja ya mafuta ya ziada, hakuna haja ya ujumbe wa ziada, ujumbe wa Hukumu
39
ya walio hai, wanajikuta katika giza kuu. Naam, wanajipata hawana nuru ambayo ujumbe wa Hukumu ya walio hai hufunua. Baada ya kugundua kupuuza kwao kwa kipumbavu, wanakimbia kujipatia mafuta, nuru kwa hiyo mada, lakini kwa wakati huo mlango umefungwa (muda wa rehema kwa wanawali, kanisa, umefungwa). Wakati wanaita waingizwe wanaambiwa kwa upole na Bwana Mwenyewe, “Siwajui ninyi.” {2TG44: 39.1}
Ishara ya Ufalme unaokuja ambao mfano huu unaleta, ni bila shaka ujumbe maalum (mafuta ya ziada) ambao hutangaza Hukumu ya walio hai, ujumbe unaowaamsha wenye moyo wa uelekevu wanaoutafuta Ukweli, na ambao huwaangamiza wanaoupinga, wanafiki na wavuguvugu kanisani — wale ambao wametosheka na kujiona matajiri na waliojitajirisha, hawahitaji chochote (hawahitaji Ukweli wa wakati mwafaka), wale ambao kamwe hawawezi kuamka kwa ukweli kwamba wao ni maskini kabisa. Nataka ujue, haya si maneno yangu, soma yale Bwana anasema kwa Laodekia: {2TG44: 40.1}
Ufu. 3: 14-18 — “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika; Haya ndiyo anenayo Yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nime-jitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na
40
mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”
Mtazamo mwingine wa ukweli huu wa kutisha umetolewa katika — {2TG44: 41.1}
Luka 14:16-24 — “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa Wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda ku-wajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. Yule mtumwa akaenda, akampa Bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule Mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa Wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, uka-washurutishe kuingia ndani, nyumba Yangu ipate kujaa. Maana nawaambia ya kwamba katika wale wali-oalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu Yangu.”
Katika mfano huu vimeonekana vipindi viwili vya wakati. Kipindi cha kwanza ni wakati injili “imewaalika wengi” (Luka 14:16) kwa karamu ya arusi, wakati kutoka kwa Mitume hadi wakati wa mtumwa Wake wa mwi-sho na ujumbe wa mwisho
41
Mungu anatuma kwa watu Wake, wakati mambo yote yamekuwa “tayari.” Kipindi kinachofuata ni wakati am-bao mtumwa Wake wa mwisho alihudumu (Luka 14:17). Mtumwa huyu ametumwa, tunaambiwa, kwa “wakati wa chakula cha jioni,” mwishoni mwa siku, akiashiria kwamba amebeba ujumbe wa mwisho. Isitoshe, mwanzoni ametumwa kwa wale ambao hapo awali walikuwa “wamealikwa”; yaani, kwa wale ambao walikuwa tayari kati-ka ukweli wa injili, kanisani. Mwanzoni atawasiliana na kundi la watu walioshughulishwa sana na masumbuko ya maisha haya, na kuwaambia kwamba “mambo yote yako tayari,” kwamba iwapo wanataka wanaweza sasa kujiandaa na kwenda kwenye arusi, huko kufurahia karamu ya Bwana arusi. Huu ndio mwito wa mwisho kwa chakula cha jioni. {2TG44: 41.2}
Lakini nini kinachotukia? — Wanatoa udhuru kwa kutokuwa na chochote cha kufanya na karamu wakati huo. Wengine waliweka lawama kwa taaluma zao, ilhali wengine wanalaumu kwa kuzitafutia familia zao riziki. Kisha yule Mwenye nyumba kwa hasira anamtuma mtumwa Wake kwa maskini na walioteswa, kwa wale walio na njaa na wasiokuwa na shughuli sana kutii, kwa wale ambao hawajazuiwa sana na biashara na nyumba kwamba hata hawawezi kuitikia mwito Wake. Jambo hili haswa hutukia katika “mji” pekee — kanisa. Maskini, wale am-bao wanagundua kwamba wao si “matajiri na waliojitajirisha,” wanaingia, lakini bado ipo nafasi ya zaidi. {2TG44: 42.1}
Kisha ni kwamba Bwana wa mtumwa huyo anaamuru kwamba awaendee wale ambao wako kwenye barabara kuu na mipakani — wale walio nje ya mizingo ya kanisa, hata miisho ya dunia (“mipakani”). Lakini kabla mtum-wa kwenda kwenye barabara kuu na mipakani kwa utume wake
42
wa mwisho, Bwana anamjulisha kwa mkazo kwamba wale waliokuwa wamealikwa na wakatoa udhuru kuto-ingia ndani, watatengwa kabisa kwa karamu; kwamba hakuna yeyote kati yao ambaye ataruhusiwa hata kuonja karamu Yake; kwamba kwa kuziba sikio kwa huo mwito hawa wamejifungia wenyewe wakati wao wa rehema, na ya kwamba sasa hakuna chochote kinachoweza kubadili hali hiyo. Baada ya hili kilio cha kuwachochea cha yule mtumwa kinaenda kwa mataifa na nyumba ya Mwalimu inajaa, arusi inafanyika, na Bwana arusi anawaan-dalia wote walio ndani ya nyumba, lakini si wengine. {2TG44: 42.2}
Tukio hili limepeanwa tena kutoka kwa mtazamo mwingine. Wakati huu na nabii wa injili: {2TG44: 43.1}
Isa. 52:1, 2 — “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Zayuni uliyefungwa.”
Unabii huu hasa hufichua kwamba wakati kanisa, Yerusalemu na Zayuni, limelala na liko uchi pamoja na walio najisi kati yake, na likiwa mateka kati ya Mataifa (mbali na nchi yake), kilio cha kuamsha, ujumbe, unakuja kulihimiza kuamka na kujivika mavazi yake mazuri, kwa maana waovu, hutangaza kilio, hawataingia tena ndani yake, kwa maana watakatiliwa mbali kabisa. {2TG44: 43.2}
43
Ishara za Ufalme, unaona, ni muhimu zaidi kwa mtu kuziangalia kuliko ishara za kuja kwa Kristo. Ikiwa mtu atakosa ishara za Ufalme, basi ufahamu wa ishara za kuja kwa Kristo hautafaidi chochote, kwa maana wote ka-ma hawa wataogopa kwa kuonekana Kwake na kuiambia “milima na miamba. Tuangukieni, tusitirini mbele ya uso Wake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo; kwa maana siku iliyo kuu ya hasira yao imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu. 6:16, 17. {2TG44: 44.1}
Je! Juhudi za kuuanzisha Ufalme wa kabla ya millenia — kanisa lililotakaswa — zinaambatana na ishara na maajabu makubwa, na kelele na mbwembwe? Kwa swali hili Bwana anajibu — {2TG44: 44.2}
Mat. 13:31-33 — “Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake. Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.”
Zek. 4:6 — “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho Yangu, asema Bwana wa majeshi.”
Si mlipuko au ngurumo, na wala si kuponda, lakini Ukweli wazi, mtulivu, Ndugu, Dada, ndio unaowaokoa na kuuleta Ufalme uwepo. {2TG44: 44.3}
44
Ufalme huu wa kabla ya milenia ni kama? Na ni ishara gani zingine zinatangulia kusimaishwa kwake? Jibu kwa swali hili linakuja kupitia Ezekieli — {2TG44: 45.1}
Ezek. 36:23-28 — “Nami Nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, Nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana Nitawatwaa kati ya mataifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nita-watakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”
Hapa zipo ishara za ziada, ishara ambazo zinaonyeshwa ndani na nje ya mtu mwenyewe: makovu na kasoro ambazo dhambi imeandika kwa miili ya watu wa Mungu zinaoshwa; pia moyo mgumu wa dhambi unachongwa kutoka ndani yao na moyo mpya, mpole unaofurahia kushika maagizo na hukumu za Mungu, unawekwa ndani. {2TG44: 45.2}
Je! Hili litatukia lini? — Baada ya Mungu kuwatoa watakatifu Wake “kutoka kati ya mataifa,” “kutoka katika nchi zote,”
45
na kuwaleta katika “nchi yao,” yasema Maandiko. Ndivyo watakavyokaa katika nchi ambayo zamani Mungu aliwapa baba zao, na hivyo watakuwa watu Wake na Yeye Mungu wao. Hapa unaona kwamba hakuna yeyote anayeweza kukutana na Mungu uso kwa uso na kuishi Naye milele bila kwanza kupata uzoefu huu wa utakaso wa mwili na badiliko la moyo. {2TG44: 45.3}
Ni dhahiri kabisa hakuna mtu ambaye anabaki bila kuzijua ishara hizi za Ufalme unaokuja atapata uzoefu huu na kwa sababu hiyo kamwe hataingia ndani yake, kamwe hatastahili kuishi na kutawala na Kristo. {2TG44: 46.1}
Kwa sababu ishara hizi ni muhimu sana kwa wokovu, hazipaswi kuendelea kupuuzwa, bali zinapaswa kuzingatiwa kwanza iwapo tunatarajia kuja kwa Kristo mara ya pili kuwe kwa manufaa yetu, si kwa maangami-zo yetu. Hakika, kwa sababu hii bayana ni kwa saa hii ya mwisho ujumbe huu muhimu umeletwa kwa umakini wetu. {2TG44: 46.2}
Ukweli huu mkuu umetabiriwa tena katika maneno ya Zekaria — {2TG44: 46.3}
Zek. 12:5-14; 13:1-5 — “Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu katika Bwana wa majeshi, Mungu wao. Katika siku hiyo Nitawafanya maliwali wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; na watateketeza watu wa kila kabi-la, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kuume na upande wa mkono wa kushoto; na Yerusalemu utakaliwa tena mahali pake, naam, hapo Yerusalemu. Naye Bwana ataziokoa hema za
46
Yuda kwanza, ili utukufu wa nyumba ya Daudi, na utukufu wa wenyeji wa Yerusalemu, usipate kutukuzwa kuliko Yuda.”
“Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao siku hiyo atakuwa kama Daudi; na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao. Hata itakuwa katika siku hiyo, kwamba Nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupingana na Yerusale-mu. Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba: nao watanitazama Mimi Ambaye walimchoma, nao Watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee, nao wataona uchungu kwa ajili Yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa mzaliwa wake wa kwanza. {2TG44: 47.1}
“Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao; jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao…. {2TG44: 47.2}
“Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi. Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, Nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe
47
tena: pia Nitawafukuza manabii na roho ya uchafu watoke katika nchi. Tena itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii. Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba manabii kila mmoja wao atayaonea haya maono yake, atoapo unabii; wala ha-watavaa joho ya nywele ili kudanganya watu; bali atasema, Mimi si nabii kamwe, mimi ni mkulima; kwa maana mwanadamu alinifundisha kutunza ng’ombe kutoka ujana wangu.” {2TG44: 47.3}
Uamsho na matengenezo yaliyowasilishwa hapa — kuomboleza na kujihoji moyoni kunasababishwa na shukrani kwa rehema kuu na wema wa Mungu — kutakuwa katika siku maliwali wa Yuda watasema, “Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu,” katika siku ambayo Bwana atamfanya aliye mdhaifu sana kati yao kama Daudi, na nyumba ya Daudi kama Mungu, kama malaika wa Bwana. {2TG44: 48.1}
Wakati metengenezo haya kamili yanapotukia basi chemchemi ya utakaso itafunguliwa kwa nyumba yote ya Daudi. Katika siku hiyo waovu watakatiliwa mbali na kuwekwa nje ya nyumba ya Daudi, na walimu wa uongo, “manabii,” wataaibika kwa kuwahi kufundisha mafundisho yao wapendavyo ya Maandiko. Wakati huo watu watatambua kabisa kwamba ingawa wangefunzwa na wanadamu kutunza ng’ombe, bado hakuna mtu angeweza kuwafunza kutoa unabii; kwamba ofisi hii imewekewa mipaka kwa Roho ya Unabii, kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao
48
kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. {2TG44: 48.2}
Je! Utakaso huu, Ufalme kabla ya millenia wa kustahili kuingia mbinguni, kusimamishwa katika wakati wa rehema? — Ili kupata jibu letu tutaelekea kwa unabii wa Mika– {2TG44: 49.1}
Mika 3:12; 4:1, 2 — “Basi, kwa ajili yenu, Zayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utaku-wa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni …. Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vili-ma; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na Neno la Bwana litatoka Ye-rusalemu.”
Hapa tunaambiwa kwamba katika siku za mwisho, katika wakati wetu, Ufalme wa zamani ambao uliharibiwa utasimamishwa tena na kuinuliwa juu ya Falme zingine zote. Wakati huo watu “watauendea” kwa sababu “sheria itatoka Zayuni, na Neno la Bwana kutoka Yerusalemu.” Kazi ya injili, kwa hivyo, itakamilishwa wakati makao yake makuu yanasimama katika Nchi Takatifu. Hivyo Ufalme unasimamishwa katika wakati wa rehema, katika wakati wa wokovu na utakaso wa hukumu, kwa maana baada ya kusimamishwa watu wengine kutoka mataifa mengi wanamiminika ndani. {2TG44: 49.2}
Hili ndilo Biblia husema, na hakika ni kwamba
49
hili ndilo litakalokuwa, kwa maana hata Ibilisi hawezi kushinda mipango ya Mungu au kudanganya watu Wake. Lo, naam, Ibilisi atajaribu kupuuzilia mbali yale Maandiko haya husema, lakini kamwe hawezi kuyafanya yaseme jambo lingine isipokuwa lile yanasema. Mbali na hilo, mtu yeyote anayechukua neno la Ibilisi badala ya la Mungu, anastahili thawabu ya Ibilisi, na nina uhakika hatadanganywa kwayo. {2TG44: 49.3}
Kwa sababu ishara hizi za nyakati, kuongeza kwa zingine, ni za umuhimu mkubwa kuliko “tetemeko la ardhi la Lisbon,” “siku ya giza,” na “nyota zinazoanguka,” ingekuwa bora tuamke kwa madai ambayo zinalazimisha kwetu, na ambayo yatufunga tustahili kwa kuja kwa pili kwa Kristo na kwa makao katika Ufalme Wake ikiwa zitazingatiwa. Lakini iwapo hizi ishara haziwezi kutuamsha, basi ni hakika kwamba zitatufanya tuteleze tu-anguke ndani ya shimo la kuzimu ilhali tukiota kwamba sisi ni matajiri na tumejitajirisha, hatuhitaji chochote, tukidhani kwamba tu njiani kwenda nchi ya utukufu. Kutakuwa kuvunjika moyo na kulia na kusaga meno kuli-oje! {2TG44: 50.1}
Ni nani atakayewafukuza Mataifa kutoka katika ile nchi? — Jibu liko katika {2TG44: 50.2}
Zek. 1:14-17, 20, 21 — “Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Haya, piga kelele na kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Naona wivu kwa ajili ya Yerusalemu, na kwa ajili ya Zayuni; Naona wivu mkuu sana. Nami Ninawakasirikia sana mataifa wanaokaa hali ya raha; kwa maana Mimi sikukasirika ila kidogo tu, na wao waliyahimiza mateso. Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba Yangu itajengwa ndani yake, asema Bwana wa
50
majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu. Piga kelele tena, na kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, Miji Yangu kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko tena; Naye Bwana ataufariji Zayuni tena, ataucha-gua Yerusalemu tena …. Kisha Bwana akanionyesha wafua chuma wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.”
Ni wazi sehemu moja ya nchi za mataifa itakuja dhidi ya sehemu iliyo katika Nchi Takatifu, na kuwafukuza nje ili watoe nafasi kwa watu wa Mungu. Wakati huo miguu ya Bwana itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni na Mlima utapasuka katikati yake na kufanya ndani yake bonde kubwa sana. Ndivyo Bwana atakavyoifungua njia kwa ajili ya watu Wake wakimbilie huko katika “bonde” ambapo miguu ya Bwana itasimama, na watakatifu wote pamoja nao (Zekaria 14:4, 5). {2TG44: 51.1}
Ukweli huu, unaona, unachukua mahali pa kweli zote, kwa maana bila huu kweli zako zingine hazitakufaidi, hazitakupeleka hadi kwa Ufalme. Ni maili ya mwisho kwa maili zote ya imani yetu kupitia maisha ambayo ya-natupeleka Nyumbani. Tumesafiri umbali huu; hebu, kwa hivyo, tuendelee kusafiri moja kwa moja hadi kwa nchi ya utukufu, ambayo haipo zaidi ya upeo wa macho. Maili iliyo mbele hakika ni ya mwisho ambayo itatu-fikisha Nyumbani. {2TG44: 51.2}
51
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 43, 44
Kimechapishwa nchini Marekani
52