15 Jan Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 36, 37
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 36, 37
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1949
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
UDEMOKRASIA, UKOMUNISTI, UKATOLIKI, AU UPROTESTANTI — NI UPI UNAOFUATA KUTAWALA?
HISTORIA NA UNABII, SHERIA NA MAAGIZO — BIBLIA
1
ANDIKO LA SALA
Kristo Kujitokeza Tena Ndani Ya Watu Wake
Masomo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 69, kuanzia aya ya kwanza: {2TG36: 2.1}
‘’Wakati mazao yanapokomaa, mara moja hutia mundu, kwa maana mavuno yamekuja. ‘Kristo anasubiri kwa shauku sana udhihirisho wake Yeye Mwenyewe katika kanisa Lake. Wakati hulka ya Kristo itakapojitokeza tena kikamilifu ndani ya watu Wake, basi atakuja kuwadai kuwa Wake. Ni upendeleo kwa kila Mkristo, sio kutaza-mia tu, bali kuharakisha kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Laiti wote ambao wanaolikiri jina Lake wanazaa matunda kwa utukufu Wake, ni jinsi gani ulimwengu wote ungepandwa upesi mbegu ya injili. Haraka mavuno mengi ya mwisho yangeweza kukomazwa, na Kristo angeweza kuja kuikusanya nafaka hiyo ya thamani.” {2TG36: 2.2}
Hapa upo ukweli ambao husema ni lini tunaweza kumtarajia Kristo kuja na kuwakusanya walio Wake: “Wa-kati tabia ya Kristo itakapojitokeza tena ndani ya watu Wake.” {2TG36: 2.3}
Tuweze kuomba sasa kwamba tuweke juhudi ya kukua kama Wakristo, kupenda na kutenda kazi kwa ajili ya wengine, tuitokeze tena tabia ya Kristo ndani yetu, kisha dunia hii ya zamani itafikia kikomo, na ulimwengu mpya kwa ajili yetu utaanza. {2TG36: 2.4}
2
UDEMOKRASIA, UKOMUNISTI, UKATOLIKI, AU UPROTESTANTI — NI UPI UNAOFUATA KUTAWALA?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MEI 15, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Je! Mataifa kutoka sasa na kuendelea yataishi katika dunia mbili? Mtu anaweza kudhani, lakini hawezi kutabi-ri. Mungu pekee ndiye anayejua ya siku zijazo. Na iwapo Yeye hatuambii, basi hatutaweza kamwe kujua kabla ya wakati. {2TG36: 3.1}
Danieli 7; Ufunuo 13, 17
3
Kwenye ramani hii yenye mifano unaonekana ulimwengu katika unabii kutoka wakati wa nabii Danieli hadi siku yetu, na kuendelea. Kwa unabii huu wa mifano, kwa hivyo, lazima tuchunguze ili tuone iwapo ipo habari yoyote iliyotolewa kwa jambo linalozungumziwa. {2TG36: 4.1}
Sisi na wengi katika himaya ya Ukristo kwa kawaida tunaamini kwamba simba huwakilisha ufalme wa Babeli wa kale, dubu Umedi na Uajemi, chui Uyunani, na mnyama dubwana katika awamu zake mbili falme za Rumi ya Upagani na ya Upapa. Lakini kwa yule mnyama kama chui, na yule mwekundu sana, hatuwezi kushikilia mitazamo sawa. Na ndio sababu tunahitaji kuchambua sasa kuliko hapo awali iwapo tunataka kuujua Ukweli. {2TG36: 4.2}
Iwapo wanyama wa Danieli, wanyama wanne wa kwanza kwa ramani, huwakilisha vipindi vinne vya wakati, mmoja akimfuata mwingine, kwa nini wale watatu wa mwisho vivyo hivyo wasiweze kuwakilisha vipindi vitatu vya wakati, mmoja akimfuata mwingine? — Kwa akili wanapaswa. Hatuhitaji, hata hivyo, kutegemea kabisa akili, kwa maana zile nembo zenyewe zinapaswa kufafanua wakati na mifumo zinazoonyesha. {2TG36: 4.3}
Kinyume na zile pembe zisizo na vilemba kwa mnyama dubwana (mnyama wa nne wa Danieli) unaona pembe zilizovikwa vilemba kwa mnyama kama chui wa Ufunuo 13. {2TG36: 4.4}
Mbona vipo vilemba kwa mnyama mmoja na hakuna vilemba kwa yule mwingine? — Jibu la kiakili na la kimaandiko linaloweza kutolewa ni hili: Malaika alimfafanulia Danieli kwamba pembe kwa mnyama dubwana huwakilisha wafalme ambao bado hawakuwa na ufalme, kwamba siku moja watasimama, wavitwae vilemba vyao na kutawala. (Danieli 7:24). Na historia inarekodi kwamba
4
hili lilitukia wakati ambapo Rumi ya Upagani ilianguka, na ya kwamba wafalme wakati huo walivitwaa vilemba vyao, falme, ndio wafalme wanaofika hata kwa siku yetu. Wafalme hawa sasa wamepungua karibu wana-toweka, viti vyao vya enzi vinatwaliwa na Ufashisti, Ukomunisti, au na aina fulani ya Ujamhuri. {2TG36: 4.5}
Mnyama kama chui, kwa hivyo, akiwa na pembe zake zenye vilemba, huonyesha wazi kwamba yuajitokeza na kuwapo baada ya kazi ya mnyama dubwana, baada ya anguko la Rumi ya Upagani, na katika wakati hao wafalme wanapokea falme zao, kwa maana pembe zenye vilemba huwakilisha wafalme waliovikwa taji. {2TG36: 5.1}
Isitoshe, mnyama kama chui alimkufuru Mungu na maskani yake miezi arobaini na miwili, ambayo ni sawa na urefu wa wakati ambamo utawala wa pembe ndogo wa mnyama dubwana ungenena dhidi yake Aliye Juu Zaidi na kuwadhoofisha watakatifu. Alipaswa kutenda haya kwa wakati (mwaka mmoja), nyakati (miaka miwili), na nusu wakati (nusu mwaka) sawa na miezi arobaini na miwili (Dan. 7:25). Wote mnyama kama chui na mnyama dubwana katika awamu ya pili, walikuwa dhidi ya Mungu na watu Wake kwa urefu sawa wa wakati — miezi arobaini na miwili ya ki-mfano. {2TG36: 5.2}
Dhahiri, basi, mnyama kama chui hutawala wakati ule ule na awamu ya pili ya mnyama dubwana. {2TG36: 5.3}
Bado zaidi, mnyama kama chui ni mnyama mseto wa wanyama wote waliomtangulia! Kinywa chake cha sim-ba, miguu ya dubu, mwili wa chui, na pembe kumi ni alama zinazomtambulisha kuwa mzawa wa falme nne za dunia za zamani — Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani, na Rumi. Yye kwa hivyo ni mfano wa ulimwengu wa leo, mnyama wa tano ki-mfano. {2TG36: 5.4}
5
Sasa ukweli kwamba kichwa kilichotiwa jeraha cha mnyama kama chui kingeweza kupona jeraha lake, na pia ukweli kwamba mnyama mwekundu sana wa Ufunuo 17 ni mnyama aliye na tabia sawa na za mnyama kama chui, mwenye pembe kumi na vichwa saba ila hana jeraha kwa chochote kwavyo, huthibitisha kwamba mnyama wa mwisho ni mfano wa ule wakati baada ya jeraha la mauti kupona, wa kipindi cha saba cha wakati wa yule mnyama wa pembe mbili kuja kabla ya yule mnyama mwekundu sana, naye ndiye anayeifanya sanamu ya mnyama wa kwanza mbele yake. {2TG36: 6.1}
Sasa tuko tayari kuona kupitia mbinu za huyu mnyama wa ki-mfano, wa saba, aina ya ulimwengu ambao tunaingia, — endapo Udemokrasia, Ukomunisti, Ukatoliki, au Uprotestanti, ndio unafuata kuutawala. Nuru kwa hii mada inaweza kuonekana kutoka kwa zile pembe, na kutoka kwa mwanamke ambaye amempanda, humta-wala, yule mnyama. {2TG36: 6.2}
Hebu kwanza tubainishe ni nani ambaye yule mwanamke humwakilisha. Kidokezo cha kwanza kipo katika ukweli maarufu sana kwamba Uvuvio kamwe hauzifananishi serikali za kiraia kwa mwanamke, lakini kwa ku-rudia-rudia huifananisha taasisi ya kidini, kanisa, kwa mwanamke, yule ambaye huwaleta waongofu kwa imani yake. Yule mnyama, kama wafanyavyo wanyama wengine wa ki-mfano, tumeona, huwakilisha ulimwengu, il-hali pembe huwakilisha watawala. Pembe, kumi kwa idadi, isitoshe, ni maana ya kuenea ulimwengu wote kama vilivyo vidole kumi kwa sanamu kubwa ya Danieli 2, na wale wanawali kumi wa Mathayo 25. Vichwa, saba kwa idadi, pia vinaashiria ukamilifu, vyote. {2TG36: 6.3}
Sasa ukweli kwamba pembe bado hazijakuwa na ufalme, wakati ambapo mwanamke anamwendesha yule mnyama, pia ukweli kwamba mwanamke ndiye amempanda, anamtawala, ni
6
uthibitisho wa kutosha kwamba ulimwengu u karibu kutawaliwa na kundi la kidini, sio hasa na Udemokrasia au Ukomunisti. {2TG36: 6.4}
Kwamba mwanamke ambaye amempanda mnyama huashiria ulimwengu katika siku hii na kizazi hiki ni dha-hiri kutoka kwa ukweli kwamba zile pembe kumi, zile serikali za kiraia ambazo zitakuwapo wakati wa utawala wa Babeli, zinamchukia mwanamke, Kanisa. Ukomunisti ukiwa utawala ulimwenguni kote tangu dunia ilipoan-za kuchukia dini, Kanisa, wenyewe ni uthibitisho thabiti kwamba hizo pembe ni mfano wa Ukomunisti, na ya kwamba yule mnyama huwakilisha kipindi ambacho Ukomunisti u karibu kutawala kiti cha ulimwengu cha serikali. Mungu hata hivyo atazuia kwa kuweka mioyoni mwao “kumpa yule mnyama mamlaka na nguvu zao,” “na kumpa yule mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimie.” {2TG36: 7.1}
Hivyo wanapokea mamlaka saa moja ya ki-mfano na yule mnyama, wenyewe wakiwa hawana ufalme wao. Na mwisho wa “saa” hiyo “wanamfanya kuwa mkiwa na uchi, na watamla nyama yake na watamteketeza kabisa kwa moto.” Ufu. 17:16. {2TG36: 7.2}
Kwa sababu mwanamke ni “mama wa makahaba” (Ufu. 17:5), ni dhahiri kwamba madhehebu mengine ya-mechipuka kutoka kwake. {2TG36: 7.3}
Tumeona sasa kwamba dinia inakaribia kutawaliwa sio na Udemokrasia, sio na Ukomunisti, sio na Uprotes-tanti, wala Ukatoliki. Utatawaliwa na mfumo wa dini ambamo mabinti zake wote watashiriki — serikali ya kani-sa na nchi, ambayo itakuwa sanamu au mfano wa mnyama kama chui kabla ya kupokea jeraha lake la mauti. {2TG36: 7.4}
7
Hivi karibuni, Ndugu, Dada, tutaingia katika kipindi hiki cha mateso, na tunapaswa kuwa na shukrani jinsi gani kwamba hakuna haja ya kuogopa, hakuna haja ya kupatwa ghafla. Maana pamoja na Nuru inayong’aa sasa kwenye njia yetu tunapaswa kujua nini cha kutarajia na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo. Kwa kweli “nuru hu-wazukia wenye adili gizani.” Zab. 112: 4. {2TG36: 8.1}
MWITO WA MAANDISHI YA DADA WHITE
Maombi ya dharura yamepokelewa kutoka nchi za kigeni ya nakala za Shuhuda kwa Kanisa, Maandishi ya Awali, na maandishi mengine ya Dada E. G. White. Kwa sababu tunayo shauku ya kutosheleza maombi yote kama hiyo ya ndugu na dada ambao hawawezi, ama kwa sababu ya eneo la mashambani au kwa sababu ya ukosefu wa pesa, kujipatia vitabu vya Dada White, tunaweza kuthamini sana ukitutumia nakala zozote za ziada ambazo unaweza kuwa nazo. (Tuma kwa: Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Wa-co, Texas.) {2TG36: 8.2}
8
Bwana Yuaja
Bwana yuaja! bahari, tulia!
Enyi milima, yeyuka kwa moto wa kiowevu.
Enyi bahari, koma kupwa na tiririka!
Hatua Zake za fahari unapaswa kuzijua.
Bwana yuaja! Nani atasimama?
Ni nani atakayepatikana katika mkono Wake wa kuume?–
Yeye amevalia vazi la haki
Ambalo Kristo Mfalme wetu mtukufu alishinda.
Bwana yuaja! Kesha na uombe!
Ili uiharakishe siku hiyo ya furaha;
Hivyo basi utaepuka mtego,
Na utukufu wa milele wa Kristo kushiriki.
–Bila jina.
9
ANDIKO LA SALA
Mbegu Njema Na Mbaya
Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, kuanzia kwa ukurasa wa 70. {2TG37: 10.1}
“‘Ufalme wa mbinguni umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu wali-polala, akaja adui yake akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea, na kuzaa, basi yakaonekana na magugu.’ ‘Shamba,’ Kristo alisema, ‘ni dunia.’ Lakini lazima tuelewe hili kumaan-isha kanisa la Kristo duniani. Mfano huu ni maelezo ya yale ambayo yanauhusu ufalme wa Mungu, kazi Yake kwa wokovu wa wanadamu, na kazi hii inafanikishwa kupitia kanisa…. Mbegu njema huwakilisha wale walioza-liwa kwa neno la Mungu, ukweli. Magugu huwakilisha kundi ambalo ni tunda au mfano halisi wa makosa, la kanuni za uongo. ‘Adui aliyeyapanda ni ibilisi.’ Mungu wala malaika zake hawakuwahi kupanda mbegu ambayo ingezalisha gugu. Magugu siku zote hupandwa na Shetani, adui wa Mungu na mwanadamu.”{2TG37: 10.2}
Kwa mujibu wa andiko hili, sala yetu alasiri hii iwe tutambue kwamba Mungu kupitia katika watumishi wa uteuzi Wake mwenyewe aitimize kazi Yake kwa wokovu wa nafsi, kwamba Yeye wala malaika Zake hawaku-wahi kupanda gugu, ila kwamba Shetani, adui wa Mungu na mwanadamu huyapanda magugu. Hebu tuombe, pia, basi kwamba sisi wenyewe tuwe wa mbegu njema, wale waliozaliwa kwa Ukweli, na sio wa mbegu mbaya, sio wale ambao ni tunda la mwili, bila Roho. {2TG37: 10.3}
10
HISTORIA NA UNABII, SHERIA NA MAAGIZO — BIBLIA
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JULAI 17, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Maisha haya yangalikuwa ya kusikitisha kama nini iwapo isingaliwapo historia — ikiwa haingalikuwapo njia inayowezekana ya kujua ya zamani. Na bado ingalikuwa vibaya zaidi iwapo usingalikuwapo unabii — ikiwa isin-gekuwapo njia ya kupata wazo la yatakavyokuwa siku zijazo. Lakini ingalikuwa vibaya zaidi ya yote iwapo haingalikuwapo nuru kwa ya sasa. {2TG37: 11.1}
Niruhusu nitoe kielezi: Waza unapaswa kutazama nje kupitia madirisha yako kuelekea mashariki na kuelekea magharibi, na upaswe kuiona nchi ikiwa imeangazwa kwa maili nyingi pande zote, hata kwa upeo wa macho, lakini haikuwapo nuru nyumbani mwako mwenyewe! Tena, waza ikiwa ungetamani kuendesha gari kwenda mahali pengine, na hauna wingi wa nuru nyuma na mbele ya gari lako, lakini mtambo hungaliweza kuwaka. Je! Gari lingekuwa uzuri gani kwako? na taa uzuri gani? Hiyo ndio shida halisi ambayo ungekuwa ndani iwapo un-geelewa historia na kuuelewa unabii, lakini hukujua lolote kuhusu hali yako ya kiroho, hukujua kwamba ulikuwa unashindwa kwa mishale mikali ya Ibilisi. Ingalikuwa kama kutembea kulivuka daraja ambalo, bila wewe kujua, lilikuwa likiporomoka. {2TG37: 11.2}
Utakubali, najua, kwamba ni muhimu
11
kabisa kujua historia na unabii, muhimu kabisa kujua ya zamani na ya siku zijazo. Lakini hili lenyewe hal-itakufaidi iwapo nafsi yako inadhoofika gizani, ikiwa umekufa kiroho na hujui; — la, hili halitakufaidi tena kamwe kama lile gari lenye wingi wa nuru mbele na nyuma lakini mtambo uliokufa. Uhai kwa nafsi yako, na ile nuru iliyo karibu kwa nyayo zako ni, kwa hivyo, ya umuhimu wa kwanza. Na hii inawezaje kupatikana? — {2TG37: 11.3}
Biblia, unajua, hujumuisha sehemu tatu: (1) Historia, (2) Amri na Maagizo, (3) Unabii. Zaburi na Mithali, pamoja na Wimbo Ulio Bora, huja chini ya makundi haya matatu. Historia husimulia yaliyopita, na unabii hunena ya wakati ujao, lakini utunzaji wa zile amri na maagizo huleta baraka ambazo zinapaswa kuwa zetu leo, huangazia nafsi, na huulinda mwili. Hakika, Yesu katika amri na maagizo ndiye wokovu wetu pekee. Je! Ni-nanena ukweli? — Hebu tuone lile Yesu Mwenyewe anasema: {2TG37: 12.1}
Ufu 22:16, 13, 14 — “Mimi Yesu nimemtuma malaika Wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika maka-nisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi…. Mimi ni Alfa na Ome-ga, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa malango yake.”
Mat. 5:17-22, 27, 28 — “Msidhani ya kuwa Nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta mo-ja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Basi mtu ye yote
12
atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, ham-taingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali Mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanamu ya moto…. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Ni wale tu ambao huzitenda amri za Mungu, unaona, wanaweza kuingia Mji Mtakatifu. Hakuna wengine am-bao wanayo haki hivyo. Hapana, Yesu hakuja kuleta uhalifu na uasi-sheria, ila badala yake kuleta haki na amani kwa kuzifuta dhambi za wote wanaotubu kwa kuvunja sheria. Kuokolewa huhusisha zaidi ya kumwita tu Yeye Bwana na Mwokozi na kupiga kelele halleluia . {2TG37: 13.1}
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba Yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia Siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina Lako? na kwa jina Lako kutoa pepo? Na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo
13
Nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Basi kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” Mat. 7:21-24. {2TG37: 13.2}
Yesu alisema: “Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini Mimi.” Yohana 5:46. Kumwamini Musa ni kuyaamini aliyoyaandika; kumwamini Yesu ni kuamini yale Yeye husema. Ikiwa huwezi kumwamini Musa, basi huwezi kumwamini Yesu. Na tutaamini kiasi gani? — Yesu anajibu: “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii.” Luka 24:25. Iwapo tunatakiwa kuamini yote, basi hebu kwanza tusome— {2TG37: 14.1}
Mal. 4:4, 5 — “Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi Wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israe-li wote, naam, amri na hukumu. Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.”
Unajua kufikia sasa kwamba Malaki, sura ya 3 na ya 4, hunena kinabii kwa watu wa leo, kwa watu kabla ya siku iliyo kuu na ya kutisha, kwa watu ambao nabii Eliya wa uakisi ametumwa kwao. Na ni shauri gani la busara ambalo Bwana hutoa kupitia Malaki? — Yeye husema, “Ikumbukeni Torati ya Musa mtumishi Wangu.” Ni torati gani? — Sheria ya “maagizo na hukumu” ambayo Bwana aliamuru “huko Horebu.” Kwa sababu huu ni ushauri mwaminifu wa Mungu kwa watu Wake wa siku hii, tuweze kufanya vyema kuichambua tena sheria hii ya Musa, na kuikumbuka, kwa maana hatuwezi kuupuuza ushauri Wake na bado tuzitarajie baraka Zake. {2TG37: 14.2}
Ikisemwa kwa mapana, sheria ya Musa
14
hujumuisha sehemu tatu. Ya kwanza ni sheria ya sherehe, sheria ya hekalu — sheria ya kafara. Sheria hii, bila shaka, sisi leo hatupaswi kuizingatia, isipokuwa katika uakisi, kwa maana ilikuwa kivuli cha mambo yatakayoku-ja, haswa ujio wa kwanza wa Kristo. Hivyo ni kwamba iwapo tungaliishi katika nyakati za Agano la Kale na kushindwa kuitii sheria ya kafara na mfumo wa siku hiyo, hivyo tungeonyesha kutomwamini Kristo, Ambaye angekuja. Lakini kwa sababu tunaishi katika enzi ya Ukristo, ikiwa tunapaswa sasa kuzingatia ya mfano sheria na mfumo wa kafara, hivyo basi tutakuwa tumeonyesha kutomwamini Kristo, Ambaye amekuja. {2TG37: 14.3}
Na hivyo, kwa sababu sheria hii iligongomewa msalabani (Kol. 2:14), hatuhitaji, na hatupaswi, kuitekeleza. {2TG37: 15.1}
Sehemu ya pili ya sheria ya Musa, ni sheria ambayo Israeli ilipaswa kuwatawala watu wake, sheria ya kiraia, au sheria ya haki — sheria ambayo hufafanua ni adhabu gani ambayo serikali inapaswa kutoa kwa wale walioka-matwa wakiiba, wakiua, au kama hayo. Sasa, kwa sababu sisi kama Wakristo hatuna serikali yetu wenyewe, lakini bado tuko chini ya serikali za mataifa ya leo, sisi mmoja mmoja, au kama kundi hatuhitajiki kuitekeleza sheria ya Musa ya haki aidha. {2TG37: 15.2}
Sheria ya pekee ya Musa, kwa hivyo, ambayo tunaweza kuagizwa kuikumbuka, ni sehemu ya tatu ya sheria yake: sheria ya maadili, ambayo hujumuisha mambo ambayo yanatuhusu sisi kama watu binafsi, mambo ambayo sisi kama watu binafsi lazima tutende, mambo ambayo hufanya iwe kamilifu tabia yetu, mambo ambayo hutu-fanya tuwe watu wa kipekee. Tunahitaji kwa hivyo kuchunguza na kuyatenda mambo yaliyo katika sheria ya Musa ya maadili — “Amri, na maagizo na hukumu.” Kumb. 5:31. {2TG37: 15.3}
15
Na njia hakika ya kuchagua maaadili haya muhimu kutoka kati ya mambo yanayohusiana na mifumo ya kafara na haki, ni kwenda kwa kitabu cha Kumbukumbu la Torati. Kitabu hiki ni muhtasari wa sheria na maagizo yote ambayo Musa alinena kwa Israeli ya kale, maneno yake ya mwisho. {2TG37: 16.1}
Tutaanza na utabiri wake wa hali yetu wenyewe, wa kuishi kwetu katika nchi ya Mataifa, kama ilivyo siku ya leo, uthibitisho wa ukweli kwamba katika mashauri ya maandishi ya Musa sisi, pia, tumejumuishwa. {2TG37: 16.2}
Kumb. 4:26-31 — “Nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa. Na Bwana atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu kidogo hesabu yenu kati ya makabila, mtakako-pelekwa mbali na Bwana. Na huko mtatumikia miungu, kazi za mikono ya watu, miti na mawe, ambao ha-waoni, wala hawasikii, hawali, wala hawanusi. Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu Wako, utam-pata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupat-wa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia Bwana, Mungu Wako, na kuisikiza sauti Yake; kwa kuwa Bwana, Mungu Wako, ni Mungu wa rehema; hatakuacha wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la ba-ba zako Alilowaapia.”
Hapa Musa alitabiri kusambaratika kwa ufalme uliotarajiwa wakati huo, na kutawanywa kwa watu wa Israeli katika mataifa yote,
16
hali halisi ambayo tuko ndani leo. Yeye vile vile humo alitabiri kujiliwa kwetu katika siku za mwisho, wakati wetu — wakati ambao sisi kama Wakristo tunajipata kama wakimbizi na wadhambi kati ya mataifa, wakati am-bao tunajiliwa na Uvuvio na kushauriwa “kumrudia Bwana,” kuwa “watiifu kwa sauti Yake.” Na tukitii, Yeye atatusikia na kutuokoa. {2TG37: 16.3}
Tunapaswa, kwa hivyo, sasa kutega sikio kwa sauti Yake, na lolote Yeye anaamuru lazima tutende iwapo tunataka baraka Zake juu yetu. {2TG37: 17.1}
Kumbuka tuliupoteza Ufalme zamani kwa sababu ya kutozitii amri na maagizo Yake, na ni hakika kwamba hataturudisha huko ndani yake tunapoendelea kupuuza kuitii sauti Yake. Na hapa ipo Sauti ambayo huvuma masikioni mwetu leo kwa sauti kubwa kama ilivyokuwa masikioni mwa watu katika siku ya Musa: {2TG37: 17.2}
Kumb. 5:11-21 — “Usilitaje bure Jina la Bwana, Mungu Wako; maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina Lake bure. Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana Mungu wako alivyokuamuru. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote: lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mun-gu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako; ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe. Nawe utakumbuka ya ku-wa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike siku ya Sa-bato. Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wakoalivyokuamuru,
17
siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Usiue. Wala usizini. Wala usiibe. Wala usimshuhudie jirani yako uongo. Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usi-itamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.”
Kumb. 6:5, 8 — “Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.”
Kumb. 7:6, 12, 15 — “Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu Wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi…. Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako:… Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.”
Kwa mujibu wa aya hizi magonjwa yetu mengi husababishwa kupitia kutotii. Na ukweli haswa kwamba upo ugonjwa mwingi sana katika wakati wetu ni ushahidi ndani yake wenyewe kwamba dunia inavuna kikamilifu kwa kutotii kwake. Hivyo, kadiri tunapoendelea katika dhambi zetu ndivyo tutakavyokuwa vibaya zaidi. {2TG37: 18.1}
Kumb. 10: 12, 13, 19, 20 — “Na sasa, Israeli,
18
Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia Zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za Bwana na sheria Zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?…. Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie Yeye; ambatana Naye, na kuapa kwa jina Lake.”
Kumb. 11:26-28 — “Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; baraka ni hapo mtakapoya-sikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.”
Kumb.12:32 — “Neno niwaagizalo lolote liangalieni kulifanya; usiliongeze wala usilipunguze.”
Kumb. 14:3 — “Usile kitu chochote kichukizacho.”
Kumb. 18:10-12 — “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asion-ekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wa-fu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.”
Kumb. 22: 5-11 — “Mwanamke asivae mavazi
19
yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi. Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko. Usipande shamba lako la mizabibu aina mbili za mbegu; yasije yakaondolewa matunda yote, mbegu ulizopanda na maongeo ya miza-bibu yako. Usilime kwa ng’ombe na punda wakikokota jembe pamoja. Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.”
Katika orodha hii maalum ya sheria na maagizo, unaona kwamba Mungu ni mwangalifu kwa kile watu Wake wanavaa na kile wanachokula. Anawatazamia wawe wema kwa wanyama. Yeye anawataka wawe waangalifu wasiache mitego kwa wasiojua watumbukie ndani au kwa mtu yeyote kuumizwa kwa njia yoyote ile. Kisha, pia, watu wa Mungu wanapaswa kufanya ukulima kulingana na hekima Yake ikiwa wangetaka kuwa na baraka Zake juu ya kazi yao, na kama wangetaka kupata afya kutoka kwa chakula wanachokula. {2TG37: 20.1}
Kumb. 23:19-23 — “Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba; mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi
20
uingiayo kuimiliki.”
“Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa, kwa kuwa Bwana, Mun-gu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako. Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitaku-wa dhambi kwako. Yaliyotoka kinywani mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.” {2TG37: 21.1}
Kumb. 24:6, 10-15 — “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani….
“Ukimkopeshapo jirani yako kitu chochote, usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani yake. Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani. Naye akiwa mtu maskini, usilale na rehani yake; sharti umrudishie rehani lichuapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa haki kwako mbele ya Bwana Mungu wako. Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako ndani ya malango yako: mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wakeameutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako.” {2TG37: 21.2}
Watu wa Mungu hapa wameambiwa wasitoe amana pesa zao au vifaa vyao (sio kutoa nadhiri ya “jiwe la kusagia la juu au la chini”) ambavyo huvitumia kupata mapato. Na hawapaswi kuwa waonevu kwa
21
ndugu zao maskini. Hawafai kuvichukua kwa nguvu, na wasikawie kulipa ujira kwa maskini. {2TG37: 21.3}
Kumb. 25:4, 13-16 — “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa…. Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.”
Kumb. 27:17, 21, 24, 26 — “Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Ami-na…. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina…. Na alaaniwe ampi-gaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina…. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.”
Kumb. 28:1-4, 6, 15-22, 27, 35 — “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo Yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako….
22
“Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo….
“Lakini itakuwa, usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo Yake yote na amri Zake nikuagizazo hivi leo; ndipo zitakapokujia laana hizi zote, na kukupata; utalaaniwa mjini, utalaaniwa mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo. Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi, kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. Bwana atakuam-batanisha na tauni, hata atakapokuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa ku-jikuna, ambayo hupati kupona…. Bwana atakupiga magoti, na miguu, kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.” {2TG37: 23.1}
Aya hizi hazihitaji maelezo. Mahitaji ni wazi kwa wote. {2TG37: 23.2}
Kumb. 30:15 — “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako
23
uzima na mema, na mauti na mabaya.”
1 Yohana 1:4-6 — “Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe. Na hii ndiyo habari tuliyoisikia Kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani Yake. Tukisema ya kwamba twashirikiana Naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli.”
Yakobo 2:19, 20 — “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo imekufa?”
Kutii kwako “amri zote, na maagizo, na hukumu” sheria ya Musa ya maadili, unaona, ni ushahidi wako kwamba umezaliwa mara ya pili, kwamba umepewa nguvu kutoka juu, kwamba umewezeshwa kuchagua mema na kukataa maovu, ya kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Ukizishika amri na maagizo katika Bwana, basi ni nuru na ngao ya maisha yako. Ni ishara ya nje kwamba kwa maisha ya Kristo umemshinda Adui wa nafsi na mwili wako. Mfumo huu wa ibada, kwa hivyo, hakika ni Haki kwa imani ambayo huleta haki ya Kristo ndani ya watu wa Mungu. Hebu sasa tukiwa na masikio yalio wazi tusikie kengele ya mpiga-mbiu: {2TG37: 24.1}
Isa. 52:1, 7 — “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi…. Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye
24
Zayuni, Mungu wako anamiliki!”
Nah. 1:15 — “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, ATANGAZAYE amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana MWOVU hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha KUKATALIWA MBALI.”
Hapa Neno la kinabii la Mungu linatangazwa waziwazi na manabii wote wawili Isaya na Nahumu kwamba tunapoziona habari hizi njema zikitangazwa naye ambaye miguu yake inaonekana juu ya milima (na hili linatukia kwa mara ya kwanza tangu hao manabii walipoandika), itakuwa ishara kwamba waovu, wavunjaji wa sheria za Musa, punde watakatiliwa mbali kutoka kati ya watu wa Mungu. {2TG37: 25.1}
Na sasa, kwa sababu umependelewa kuyasikia mambo haya yote, “u heri wewe,” asema Bwana, “ikiwa mna-yatenda.” Ayubu 13:17. {2TG37: 25.2}
Kwa muhtasari wa uchambuzi wetu, ningependa utazame kwa umakini kielezi hiki. Kiangalie, kihifadhi aki-lini mwako, na ukichambue kwa starehe yako. Naam, ushawishike kwa ukweli ambao nimejitahidi kuuwasilisha kwako, kwa maana ni uhai wako, ufanisi wako, afya na furaha yako, umilele wako. {2TG37: 25.3}
25
Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. {2TG37: 26.1}
26
ZAWADI KWA AJILI YAKO
Je! Unayo nia ya kuchambua zaidi katika kweli muhimu ambazo kwa hitaji zinaguswa tu katika majani haya ya vuli? Iwapo ni hivyo, unaalikwa kutuma ombi la nakala yoyote ya trakti zilizoorodheshwa hapa chini. Zi-natumwa kama huduma ya Kikristo bila bei au sharti, isipokuwa jukumu la nafsi kwayo yenyewe kuyajaribu mambo yote na kulishika lililo jema. {2TG37: 26.2}
Orodha ya Machapisho
Trakti Namba 1, Ya Ziada “Kabla ya Saa ya Kumi na Moja” (Ezekiel 9)
Trakti Namba 2, Utata wa Onyo (Zekaria 6)
Trakti Namba 3, Hukumu na Mavuno
Trakti Namba 4, Habari za Hivi Punde kwa Mama (Hosea 1, 2)
Trakti Namba 5, Onyo La Mwisho (Baragumu Saba)
Trakti Namba 6, Kwa Nini Uangamie? (Isaya 7; Zekaria 4)
Trakti Namba7, Pambano Kuu Juu ya Fimbo ya Mchungaji
Trakti Namba 8, Mlima Zayuni Saa ya Kumi na Moja
Trakti Namba 9, Tazama, Niyafanya Yote Kuwa Mpya
Trakti Namba 10, Ishara ya Yona
Trakti Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho
Trakti Namba 13, Salamu za Kristo
Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita
Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, Toleo la Mfukoni
Kwa Makanisa Saba (Kuifunua Mihuri Saba)
27
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 36, 37
Kimechapishwa nchini Marekani
28