30 May Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 27, 28
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 27, 28
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
WAGONJWA SUGU KWA MAARIFA MENGI ZAIDI NA UELEWA FINYU SANA
ROHO ILIYOANZISHA UOVU, NA UDHIHIRISHO WAKE LEO
1
ANDIKO LA SALA
Msikilizaji Wa Udongo Mzuri
Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano,” kuanzia ukurasa wa 60, aya ya tatu. {2TG27: 2.1}
“Neno la Mungu mara nyingi hugongana na za mwanadamu tabia na mazoea yake aliyorithi na kukuza ya mai-sha. Lakini msikilizaji wa udongo mzuri, akilipokea neno, huyakubali maagizo na mahitaji yake yote…. {2TG27: 2.2}
“Naye huzaa matunda kwa uvumilivu.’ Hamna wote wanaolipokea neno la Mungu wako huru kutoka kwa ugumu na jaribu; lakini mateso yanapokuja, Mkristo wa kweli hawi asiyetulia, wa kutoamini, au wa kukata ta-maa. Ingawa hatuwezi kuona matokeo hakika ya mambo, au kufahamu kusudi la majaaliwa ya Mungu, hatu-paswi kutupilia mbali imani yetu. Tukizikumbuka fadhila za Bwana, tuweze kumtwika Yeye masumbuko yetu, na kwa uvumilivu tuusubiri wokovu Wake. {2TG27: 2.3}
“Kupitia mapambano maisha ya kiroho huimarishwa. Majaribu yanayohimiliwa vyema yatakuza uthabiti wa tabia, na neema za kiroho za thamani. Tunda kamilifu la imani, unyenyekevu, na upendo mara nyingi hukomaa vyema kati ya mawingu ya dhoruba na giza.” {2TG27: 2.4}
Hebu tuombe kwamba ufahamu wetu wa kiroho uweze kuhuishwa ili kwamba tuweze kuwa tayari kuelewa shughuli za Mungu katika kuyajibu maombi yetu; kwamba kupitia mapambano maisha ya kiroho huimarishwa; kwamba tusiitupilie mbali imani yetu wakati ambapo mateso huinuka, ila kwamba kama Paulo tufurahi kwa ku-wa tumehesabiwa wastahiki kuteseka katika uvumilivu. {2TG27: 2.5}
2
WAGONJWA SUGU KWA MAARIFA MENGI ZAIDI NA UELEWA FINYU SANA
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, FEBRUARI 14, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Ili kuonyesha mada ya uchambuzi wetu alasiri hii, hebu tuchukue kwa mfano kitabu ambacho Dhehebu lime-toa kuhusu Danieli na Ufunuo, vitabu viwili vyenye thamani sana vya Bibilia. Kitabu nilicho nacho mawazoni mwanzoni kiliitwa Mawazo kwa Danieli na Ufunuo. Kimeandikwa katika mtindo wa wasomi, na ya kushawishi ni yaliyomo kwamba maelfu ya nakala zimeuzwa kote duniani katika lugha kadhaa. Yeyote ambaye anaweza kuandika kitabu kama hicho, ni dhahiri anayo maarifa makubwa. Tunapaswa, hata hivyo, kuchunguza ili tuone ni uelewa kiasi gani upo katika vile vitabu vya Danieli na Ufunuo vyenyewe. {2TG27: 3.1}
Chukua kwa mfano Ufunuo sura ya 12, ambapo huzungumza juu ya mwanamke mwenye nyota 12. Dhehebu katika kitabu nilichotaja hufafanua kwamba huyu mwanamke ni nembo ya kanisa la Kikristo, kwamba vazi lake la jua ni Injili ya Kristo, na umma unaonekana kuelewa vizuri sana. {2TG27: 3.2}
Lakini ikiwa wandugu wangaliulizwa swali: “Je! Mwanamke anawezaje kuwa nembo ya kanisa la Kikristo, na wakati uo huo awe mama ya
3
Kristo?” Watajipatia muda kujibu, kwa maana Kristo Mwenyewe alileta kanisa la Kikristo kuwapo miaka the-lathini au zaidi baada Yake kuzaliwa. Kwa sababu hiyo hangaliweza kuwa mama Yake. {2TG27: 3.3}
Na kama wangaliulizwa, “Je! Vazi la jua la mwanamke lingaliwezaje kuwakilisha kanisa la Kikristo lililovikwa Injili ya Kristo, kama unavyobishana?” Wangalikuwa na wakati mgumu kujibu kwa maana yeye alikuwa amevikwa jua kabla ya Kristo kuzaliwa, na kabla Injili hata haijakuwapo. {2TG27: 4.1}
Kama maswali haya yangaliulizwa kwa wandugu, nina hakika wangechanganyikiwa sana kwa kujaribu kuji-bu. Lakini ukweli kwamba hakuna yeyote ambaye huuliza maswali haya, huonyesha kwamba upo uelewa finyu sana katika himaya yote ya Ukristo. {2TG27: 4.2}
Tena huwezi kuukana ukweli kwamba Dhehebu limetoa ufafanuzi wa usomi sana kwa Baragumu Saba, wa kulima katika mfano mgumu kama huu, wakitegemeza maelezo yake kwa mafafanuzi na historia na kuwafanya watu wayachukulie vizuri sana kama wanavyofanya. Kwa mbinu zao za usomi, ingawa, wao hubishana kwamba nzige ambao walioachiliwa mara tu Nyota ya Mbinguni ilipolifunua “shimo la kuzimu” ilipovuma baragumu ya tano (Ufu. 9:1-3), ni mfano wa majeshi ya Waturuki. Wao hulifanya hili licha ya ukweli kwamba wale nzige ha-wakufaa kumuua mtu yeyote, ila kuwatesa tu wale ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu kwenye katika vipaji vyao, ilhali Waturuki walimuua kila mtu aliyesimama dhidi yao, haswa Wakristo, wale ambao walikuwa na mu-huri. {2TG27: 4.3}
Zaidi ya hayo, wale wandugu hufafanua kwamba farasi na wapanda farasi 200,000,000 ambao walipaswa kuwaua
4
theluthi moja ya watu (Ufu. 9:18), ni mfano wa askari wapanda farasi wa Uturuki, ingawa Waturuki hawaku-wahi kamwe kuwa na wapanda farasi wengi kama hao katika uwepo wao wote. {2TG27: 4.4}
Isitoshe, Yohana Waufunuo husema wazi wazi kwamba mikia ya farasi ilikuwa kama nyoka, na vichwa vyao vichwa vya simba vilikuwa vikicheua moto, moshi na kiberiti. Kinyume kwa ukweli huu, wale wandugu husema kwamba farasi walikuwa farasi wa kawaida wa Waarabu, kwamba Waturuki wakiwa wamejihami kwa bunduki walikuwa wanawaendesha, kwamba Yohana alishindwa kugundua kwamba moto, moshi na kiberiti vilitoka katika zile bunduki, sio kutoka katika midomo ya farasi. {2TG27: 5.1}
Nasema kwa mtu kuyapotosha hivyo Maandiko na bado kuwafanya watu waamini kwamba yeye hivyo anaukunjua Ukweli, lazima awe na uwezo mkubwa, lakini uelewa finyu sana kuhusu ukweli kwamba iwapo Yo-hana aliachwa kufanya makosa katika sehemu hii ya maono yake, angaliachwa kufanya makosa katika Ufunuo wote, na kwamba kwa mtu yeyote ambaye hutoa sauti ya maoni yake kwa Maandiko hajengi ila anabomoa imani kwa manabii wote, na kusababisha mtu kusema kwamba ikiwa Maandiko sio makamilifu sana jinsi wanavyofan-ya yaonekane kuwa, basi yana uzuri gani? Na tunawezaje kupata ile Kweli na kuokolewa Kwayo, kwa maana iwapo manabii wenyewe hawangeweza kusema ukweli, basi anawezaje yeyote kati yetu kufanya hivyo maelfu ya miaka baada ya wakati wao? {2TG27: 5.2}
Kwa sababu wale wandugu hawajaweza kuona hili, na kwa sababu hakuna yeyote ambaye ameyachambua mafafanuzi yao kulihusu ameweza kuliona ama, basi haionekani kwako kwamba ingawa yapo maarifa mengi ko-te kote, upo uelewa finyu sana mahali popote? {2TG27: 5.3}
5
Kushughulika na hali kama hii, Paulo alitangaza: {2TG27: 5.4}
1 Kor. 3:1 — “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.”
Hapa Paulo aliwakemea wale ambao maarifa yao yalionekana kuwa makubwa, lakini uelewa wao ulio duwaa, wale ambao hawakuwa wamestawi kiroho sambamba na wakati huo, ambao hawakuweza kuambata kikamilifu yale ambayo Neno husema, hawakukua hadi kuwa Wakristo wakomavu. Yeye, kwa hivyo alihimizwa kusema: {2TG27: 6.1}
Aya ya 2 — “Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula kugumu; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi.”
Paulo alivunjwa moyo na maendeleo ambayo Wakorintho walikuwa wamefanya: Bado hawakuweza kula chakula kigumu. Kunena kwa uthabiti, alisema — {2TG27: 6.2}
Aya ya 3,4 — “Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmo-ja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wa mwilini?”
Kwa kuunga mmkono upande mmoja, wengine wa Paulo na wengine wa Apollo, kwa kweli walikuwa waki-yapokea yale ambayo Mungu alikuwa ametuma kupitia mjumbe mmoja, na kuyakataa yale Yeye alikuwa ame-tuma kupitia mjumbe yule mwingine. Hili utaliona waziwazi kabisa katika aya zinazofuata: {2TG27: 6.3}
Aya ya 5-7 — “Basi Apollo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama
6
Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.”
Mungu ndiye kila kitu, na watu wa uteuzi Wake ndio vipasa sauti Vyake pekee. {2TG27: 7.1}
Aya ya 8,9 — “Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.”
Huu uchaguzi wa upande mmoja ulikuwa ukiwaharibu Wakristo katika siku za Paulo, na unawaharibu katika siku yetu; yaani, watu huweka upendo wao kwa watu ambao huwaletea maarifa ya Injili badala kwa Yule Am-baye huwatuma na Injili. Na mbaya zaidi ya hili ni ukweli kwamba watu wengi wanaweka upendo wao hata kwa watu ambao hawana hata cheche ya Uvuvio, watu ambao hawajatumwa na Mungu hata kidogo, lakini wanaokimbia kwa ulegevu azimio lao. {2TG27: 7.2}
Aya ya 10 — “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.”
Maisha ya Mkristo ni, kwa mfano, jengo linalojengwa. Mjumbe mmoja wa Mungu huuweka msingi, mwingine hujenga juu yake. Kwa hivyo hakuna mjumbe mmoja anayepewa nyenzo zote za kujengea. {2TG27: 7.3}
Ndiposa, iwapo yeyote achague kumtii huyu au yule mjumbe badala ya
7
Mungu na kwa watumwa Wake wote kama vile Yeye Mwenyewe huwatuma mmoja baada ya mwingine, huyo hakika ataachwa bila nyenzo za kutosha kujenga, na ndiposa bila uwezo ambao anahitaji kuwa nao kwa ajili ya kuja kwa Bwana. {2TG27: 7.4}
Aya ya 11-18 — “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwe-kwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya tha-mani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu ali-yoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto. Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.”
Hapa tunaambiwa kwamba nadharia — kuni, nyasi, makapi — zilizoletwa ndani na watu ambao Mungu haja-watuma, hawajavuviwa, kama wale nilioitia umakini wenu mwanzoni, nadharia ambazo zinaonekana kuchimbu-ka kutoka katika ghala kubwa la maarifa, lakini ambazo hazina Roho, ni kama unavyoona tayari takataka am-bayo moto wa Mungu huvuvumukia na nafsi za wanadamu hufa kwa njaa. {2TG27: 8.1}
Na tena tumeambiwa kwamba hekima ya dunia hii ni upuzi mbele ya Mungu, na ya kwamba ikiwa tunataka jengo letu la Ukweli kustahimili dhoruba, tunahitajika kutupa nje takataka na kuzichukua nyenzo
8
zote zilizotumwa na Mungu tunapoendelea kujenga. {2TG27: 8.2}
Aya ya 19,20 — “Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwam-ba ni ya ubatili.”
Kwa sababu hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu, ingalikuwa bora tusiwe na shughuli nayo, na tuache kuchagua upande mmoja — mmoja wa Luther, mwingine wa Wesley, bado mwingine kwa Campbell, au White — lakini tungalikuwa bora kusimama na Bwana na kuzipokea Kweli zote kutoka kwa watumwa wake wote ambao Yeye huchagua kuwatuma. Vinginevyo tutakapofika mlangoni Yeye atalazimika kutuambia, “On-dokeni kwangu, Sikuwajua ninyi.” {2TG27: 9.1}
Aya ya 21,22 — “Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.”
Kujitukuza ndani ya mwanadamu, iwe ni kibinafsi au katika mwingine, ni kujidanganya kwa kila kitu. Chukua kwa mfano Wayahudi: Waliazimia kuwa “wa Musa,” na kama walivyoona, kuwapokea manabii, au hata Kristo, ilimaanisha kumwacha Musa! Kama tokeo, badala ya mambo yote kuwa yao, walipoteza kila kitu, hata Musa, na wako wapi leo? Kuni, nyasi, na makapi ambayo walirundika juu ya jengo la Ukweli baada ya Musa kuwaacha, kwa muda mrefu zimefagiliwa mbali na Moto wa Ukweli, Roho Mtakatifu. {2TG27: 9.2}
Njia pekee salama ya kujenga ni kwa Ukweli uliotumwa kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu. Hivi ndivyo
9
Musa, manabii, na mitume walivyojenga, na hivi ndivyo tunavyopaswa kujenga. Musa, kwa mfano, alianzisha jengo lake la Ukweli kwa mwamba thabiti wa uumbaji, Mwanzo, juu ya kazi yake Yeye Aliyeziumba dunia (Ebr. 1:1). Manabii baada yake, pia mitume, waliendelea kujenga juu ya msingi uo huo, sio kwa nadharia za ma-kuhani na marabi, walioitwa eti waalimu wa kidini wa siku hiyo. Na ndio sababu jengo lao la Ukweli lnasimama kidete zaidi kuliko hapo awali. {2TG27: 9.3}
Maarifa, unaona, bila uelewa wa Kiungu ni maharibifu kwa nafsi kama vile moto ulioachwa ndani ya nyumba iliyojengwa kwa miti na nyasi. Hebu kwa hivyo tusiwe tena wa kuchagua upande mmoja, lakini tuje mezani penye Mungu ameandaa kwa wingi chakula cha kiroho, na bila ubaguzi na huru kutoka kwa chuki isiyo na saba-bu ule ushibe, tuziburudishe nafsi zetu na tuiimarishe migongo yetu kwa uelewa mzuri ili tuwe na uwezo wa kusimama dhidi ya magonjwa sugu ya maarifa ya kidunia; kwamba tuyashinde majaribu kwa nguvu zake Aliye Hodari, na kuruhusiwa kuwa na sehemu katika kuutangaza ujumbe wakati utakapoumuka kuingia Kilio Kikuu. {2TG27: 10.1}
10
Yuaja Hivi Karibuni
Muda mrefu juu ya mlima, wachovu,
Kundi lililotawanyika limeraruliwa;
Giza njia za jangwa, na za kuchosha;
Wamehimili majaribu mazito.
Sasa mwito wa Kukusanywa unavuma,
Ya uchaji sauti yake ya onyo;
Umoja, imani, na upendo, tele,
Himiza kundi ndogo lifurahi.
Sasa nuru ya ukweli wanaitafuta,
Katika njia yake inayoendelea andama;
Ukizishika mri zote kumi,
Ni takatifu, za haki, na za kweli.
Kwa maneno ya uzima wanajilisha,
Ya thamani kwa ladha yao, tamu sana;
Wakiyatii maagizo yote ya Mwalimu wao,
Wakisujudu kwa unyenyekevu miguuni Pake.
Katika ulimwengu huo wa nuru na uzuri,
Katika mji huo wa dhahabu mzuri,
Hivi karibuni malango yake ya lulu wataingia,
Na utukufu wake wote kushiriki.
Huko, kawa utakatifu nafsi kupanuka;
Huru kutoka kwa dhambi, na kifo, na uchungu;
Machozi hayatafifisha kamwe majumba hayo
Ambapo watakatifu wasiokufa hutawala.
Hivi karibuni Yuaja! na mawingu akishuka;
Watakatifu Wake wote, toka kaburini, waamka;
Waliokombolewa, katika nyimbo mseto,
Kelele za ushindi wao kupitia angani.
Ee, tunatamani kuonekana Kwako;
Njoo, Ee Mwokozi, njoo haraka!
Tumaini la baraka! roho zetu zinashangilia,
Chukua waliokombolewa Wako watoto nyumbani.
–Annie R. Smith.
11
ROHO ILIYOANZISHA UOVU, NA UDHIHIRISHO WAKE LEO
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, FEBRUARI 21, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Andiko letu linapatikana katika Isaya, sura ya 2, aya ya 22. {2TG28: 12.1}
Isa. 2:22 — “Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudha-niwaje kuwa ni kitu?”
Katika aya hii ya Maandiko Mungu hupendekeza kwamba tumwache mwanadamu. Na sababu iliyotolewa ni kwamba pumzi ya mwanadamu i katika mianzi ya pua lake; kwa sababu bila pumzi yeye ni donge la uchafu, na kwa hivyo hana umuhimu. Yeye si Mungu. {2TG28: 12.2}
Kule kusihi hakungalifanywa ikiwa watu hawangaliweka imani yao kwa mwanadamu badala ya Mungu kwa ajili ya wokovu wao; yaani, badala ya kufanya yale waungwana wa Beroya walifanya, kuchunguza ili kujua iwapo “mambo hayo ni hivyo,” watu wa Mungu wanatii yale ambayo wengine hufikiri au kusema. Wanafanya hivi leo yale mamia kwa maelfu walikuwa wakifanya katika siku ya Yesu: wakiyaamini maoni ya wasomi wao makuhani, waandishi, na marabi. Wayahudi kwa kutii uvumi badala ya kujihusisha kwa uchunguzi wa kibinafsi na uzoefu wao wenyewe na chanzo cha ukweli, ni, kwa hivyo,
12
kitu haswa ambacho kilimsulubisha Bwana. {2TG28: 12.3}
Na je! unafikiria imani kama hii kwa mwanadamu ilitokea wapi? — Mara nyingi hufikiria kwamba uovu ulian-zia kwa Hawa wakati alipolifikia tunda lililokatazwa. Lakini ukweli ni kwamba uovu ulikuwepo tayari kabla ya Hawa kukumbana nao. Hebu tulisome hili kutoka kwa nabii Isaya: {2TG28: 13.1}
“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, ewe uliyewaangusha mataifa! Nawa ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu changu juu kuliko nyota za Mungu: nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, pande za mwisho za kaskazini: nitapaa kupita vimo vya mawingu; Nitafanana na Yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu, pande za mwisho za shimo.” — Isa. 14: 12-15. {2TG28: 13.2}
Tunafahamu kwamba jina la Shetani kabla hajatenda dhambi lilikuwa Lusifa, na ya kwamba alitenda dhambi kabla ya Hawa kufanya dhambi, na ya kwamba alijifanya kuwa nyoka aliyemdanganya Hawa. Kwa hivyo tutazingatia dhambi mbinguni kabla ya kuangalia zaidi dhambi hapa duniani. {2TG28: 13.3}
Shetani, Tunaambiwa, hakuwa mdhambi wa pekee Mbinguni, kwa maana pamoja naye walitupwa kutoka Mbinguni theluthi moja ya jeshi la malaika (Ufu. 12:4). Hao walitupwa kutoka Mbinguni kwa sababu walitii maneno ya Lusifa, kwa mwanadamu Mbinguni, badala ya kulitii neno la Mungu. Hili lilikuwa anguko la ma-laika. Lusifa mwenyewe alianguka wakati alitamani kuwa kama Mungu. {2TG28: 13.4}
Dhambi hizi mbili — kumwamini mwanadamu, na tamaa ya kujiinua — bado ni mamnbo ya dhambi ya-nayoongoza
13
sasa hapa duniani. Hili lilikuwa kikwazo cha Hawa na kwa wengi hata leo bado ni kikwazo. La, tamaa ya kula haikuwa sababu ya kuanguka kwa Hawa. Nyoka hakusema, “Unapaswa kula tunda hili kwa sababu ni la kupen-deza, lenye lishe zaidi kuliko tunda lingine lolote katika bustani ya Mungu.” Lakini akasema: “Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwa. 3: 5. {2TG28: 13.5}
Tunda hilo, bila shaka, lilimpendeza, lakini alijaribiwa na wazo la kupata fursa ya kuinuliwa hadi kwa kiti cha enzi cha Mungu, kupandishwa kwa nafasi ile ile ambayo Lusifa mwenyewe alitamani. Lusifa Lazima alikuwa ameamini kwa kweli kwamba angalikuwa kama Mungu iwapo malaika Mbinguni na wanadamu duniani wanga-liweza kupokea amri kutoka kwake. {2TG28: 14.1}
Na hivyo tunaona kwamba Ibilisi alimdanganya Hawa kwa msingi ule ule ambao alijidanganya mwenyewe na malaika zake, tofauti pekee ikiwa kwamba alimfanya Hawa kula tunda ambalo yeye na malaika wake hawanga-liweza kula. Ndiposa, Hawa alifanya dhambi dhidi ya mwili wake wa asili, pia, kwa kuingiza ndani yake kitu ambacho hakikuumbwa kwa ajili ya chakula, na hivyo akafa. Lakini Shetani na malaika zake bado wanaishi. {2TG28: 14.2}
Kizuizi hicho hicho, tamaa ya kujiinua, kimeenea katika vizazi vyote, na huenea leo. La, sifanyi taarifa za haraka na zisizo na maana. Ninazo kweli za kuunga mkono maneno yangu. Kwa mfano, katika siku za Vuguvugu la Kutoka, walikuwapo Kora, Dathani, na Abiramu ambao walitamani ofisi ya Musa na Haruni kama Lusifa alivyokitamani kiti cha enzi cha Mungu, ofisi za juu zaidi ambazo wangaliweza
14
kutamani. Na Lusifa hakuanguka kwa sababu ya kutaka kuwa juu ya wengine wote bila chochote isipokuwa kujiinua nafsi? Na hilo halikuwa kweli sawa kuhusu anguko la Kora, Dathani na Abiramu? {2TG28: 14.3}
Leo huyaona mayowe yale yale kwa ajili ya nafasi hata katika makanisa yetu. Ofisi za Wazee wa Makanisa, Viongozi wa Shule ya Sabato, Makatibu, Wapiga piano, na ofisi zingine za kanisa kama hizo, tukumbuke, hizina malipo ya pesa. Lakini licha ya hilo, kila mwaka katika makanisa mengi, kama vile nimeweza kutazama, yapo makelele na ugomvi wa wanaume na wanawake kwa ajili ya moja au nyingi za ofisi hizi. Kwa sababu hakuna malipo ya kifedha kwa huduma kama hizo, basi fujo hii ni ya nini ikiwa kiuhalisi sio tu kwa kujiinua nafsi, iwapo sio kwa kusudi la kutazamwa kama mtu fulani? {2TG28: 15.1}
Unaona, basi, kwamba kelele zile zile kwa ajili ya kujitukuza ambazo zilikuwepo kwa Lusifa, na Hawa, na wengine katika vizazi vyote, zipo leo. Taarifa yangu, unaona, inaungwa mkono na kweli halisi. Zaidi ya hayo, ikiwa hivi ndivyo hali ilivyo kwa wale ambao hawapokei udhamini wa fedha kwa huduma zao, basi hali itaku-waje kwa wale ambao hulipwa vizuri? Swali hili unaweza kulijibu mwenyewe ili uweze kuridhika. {2TG28: 15.2}
Kwa udhahiri, yeye ambaye hutamani kushika ili kujitukuza tu, haswa wakati ambapo ofisi kama hiyo hushi-kilia majukumu ya kiroho kama ilivyo ofisi ya kanisa, mtu kama huyo hapaswi kuzingatiwa kwa vyovyote. Na iwapo tayari ana kituo chochote cha jukumu, anapaswa kuondolewa, kwa maana viongozi kama hawa wa kujit-akia makuu ni vipofu kiroho, na huwavuta umati kwao binafsi kama alivyofanya Lusifa kuwavuta malaika kwake na kwa angamizo.
15
Zaidi ya hayo, kundi hili la viongozi, wafu kwa Kristo na hai kwa ubinafsi wao, kama sheria hupenda kupiga gwaride, na hata kutilia chumvi matendo yao ya kidini. Kama hao wanapaswa kupigwa chapa kama watafuta-wafuasi waliovuviwa na Shetani. Daraja hili la watu kwa kawaida ni werevu. Huweza kushika imani ya watu kwa mbinu ile ile ambayo makuhani na marabi wakati wa Yesu walilidanganya taifa: waliombea mahali wanga-liweza kuonekana; walivuruga nyuso zao ili waonekane wanafunga; waliifanya kuwa shughuli yao kutangaza kote kote lolote njema walilofanya; walikuwa na weledi wa kujifanya waonekane wa-kidini, wachaji, wafadhili, na wenye haki. {2TG28: 16.1}
Umati mkubwa bado wanapagawa na watu ambao huitwa eti watu wazuri, na watu wengi bila kuhoji huyapokea maamuzi yao kana kwamba yalikuwa maamuzi ya Mungu. Dhidi ya kama hao, kumbuka Uvuvio hu-onya: “Mwacheni mwanadamu, ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” Isa. 2:22. {2TG28: 16.2}
Ili wamba hawa waabudu watu waonekane kwa uhalisi zaidi, hebu nikuambie jambo fulani: Maelfu wame-tushauri tuikane imani iwapo Rais wa Baraza Kuu haioni nuru katika fundisho letu, ikiwa haoni nuru katika uamsho na matengenezo yetu kati ya watu wa Mungu. Wanaonekana kuwa waaminifu katika hili kama vile Wayahudi kwa imani waliunga mkono upande mmoja dhidi ya Yesu kwa kuyafanya maamuzi ya kuhani mkuu kuwa maamuzi yao! {2TG28: 16.3}
Matakwa yao sisi tuikane imani “iwapo rais haoni nuru,” huonyesha kwamba wanawaiga Wayahudi wa za-mani, badala ya kutazama ndani ya jambo wenyewe, kwa imani katika Roho
16
wa Mungu kuwaonyesha kibinafsi Ukweli ni nini; wanayo imani kabisa kwa lile mtu, “rais” huwaambia! {2TG28: 16.4}
Je! Roho hii haswa haikuwa ndani ya mioyo ya watu waliomkataa na kumsulibisha Bwana? Ni wazi daraja hili la watu haliongozwi kwa Ukweli, bali na watu wa nyadhifa. Watu kama hao huwa hawaulizi, “Ni Ukweli?” ila “Ni nani anayeutetea?” Na iwapo hauji kupitia kwa njia ambayo wangetaka upitie, basi, bila shaka Ukweli unakataliwa. {2TG28: 17.1}
Kamwe hawatulii wafikirie kwamba Mungu hapokei maagizo kutoka kwao; kwamba hawachagui watumwa wa Mungu kwa ajili Yake, na kwamba Rais wa Baraza Kuu alichaguliwa na watu, sio kwa sababu ya mamlaka yake juu ya Maandiko, lakini kwa sababu ya uwezo wake wa kuamuru; kwamba Ukweli bado haujawahi ku-chimbuka kupitia kwake, kwamba ukweli wowote wa Bibilia yeye mwenyewe amewahi kujifunza ni ule tu am-bao watu wa Mungu waliovuviwa wamemfundisha. Walei, kwa hivyo, hawajawahi kuwa na hitaji kubwa la ku-waacha wanadamu jinsi walivyo leo. Na iwapo hawatafanya matengenezo, Mungu awahurumie. {2TG28: 17.2}
Itakumbukwa, hata hivyo, kwamba wanafanya jambo hili la kipumbavu kwa sababu tu ukasisi umewafunza hivyo, kwa sababu tu wachungaji wengine wako katika ushirika na roho ambayo ilikuwa ndani ya Kora, Da-thani, na Abiramu wakati walipoitamani nafasi ya Manabii, ingawa Mungu hajawatuma hivyo. {2TG28: 17.3}
Kisha, pia, wakati mhubiri anapoanza kutangaza matendo yake mema na mafanikio yake, pamoja na uzoefu wake wa kidini; pia wakati mhubiri anaposugua macho yake na kupuliza pua yake
17
bila sababu anapohubiri na kujaribu kuwafanya wasikilizaji wake kuanza kulia; — unapoyaona mambo haya nda-ni ya mhubiri, ujue hakika kwamba yeye anavuta pamba kwa macho ya wasikilizaji wake, kwamba kuna kitu kil-icho juu kwa mkono wake. Nasema, unapomwona mhubiri akitenda mambo haya, anakusudia kuandikisha idhini yako kwa jambo lake mwenyewe. Jihadharini! {2TG28: 17.4}
Unaweza kupekua Bibilia yote, na ninakuhakikishia kwamba hautaweza kupata mojawapo wa mambo haya yalifanywa na yeyote kati ya manabii. Hawakuwa na lengo la kuwafanya watu wa Mungu kusikitika, ila daima kufurahi katika Bwana. {2TG28: 18.1}
Chukua kwa mfano Yesu Kristo. Kazi Yake, utume Wake, ulikuwa mkubwa na muhimu zaidi kuliko wowote kabla Yake au baada Yake. Alikuwa na uzoefu wa kidini ambao ulikuwa wa kupigiwa mfano, na iwapo utarati-bu kama huo ungalikuwa wa faida katika kazi ya wokovu, Yeye hakika angaliitumia fursa hiyo. Badala ya kuji-hubiri Mwenyewe, hata hivyo, Alihubiri Ukweli. Hakujaribu kamwe kumbembeleza yeyote kwa kunena habari Zake. Alinena tu ukweli wa Bibilia, na alimpa Mungu, sio Yeye Mwenyewe, sifa. Na iwapo yeyote anayeweza kuhubiri toba na upendo, Angaliweza, lakini Yeye kamwe hakujaribu kuchezea hisia za wasikilizaji Wake, kam-we hakujaribu kuwaweka wawe wakilialia juu ya chochote. {2TG28: 18.2}
Hakuna mtu, zaidi ya hayo, pamoja nasi wenyewe, amewahi kuyapokea maandishi ya manabii kwa sifa za wema wao, elimu yao, au uzoefu wao wa kibinafsi wa kidini. Hawakuandika chochote kuwahusu wao wenyewe, na bila chochote cha kuimarisha ofisi yao. Wote ambao wameyapokea, wamefanya hivyo kwa sifa za maandishi yao yenyewe. Ni hilo tu. Hawakujaribu kamwe
18
kuwavuta waongofu kwa kile wao wenyewe walikuwa au hawakuwa. Je! Wao hata sasa hawapati ufanisi? Na je! Sio Ukweli wa Mungu ambao lazima tufuatilie? Wayahudi walitaka ishara, na Wayunani hekima, lakini watu wa Mungu wa leo wanauliza ishara na hekima, badala ya Ukweli. {2TG28: 18.3}
Hebu, kwa hivyo, tusisahau kamwe kwamba roho ya kujiinua nafsi ilianzisha maovu yote ambayo tunaona leo, na ambayo ni ngumu zaidi kazini kuliko hapo zamani. Hatupaswi kumpa Joka nafasi ya kutunasa, na ku-tutupa katika uangamizi pamoja na “theluthi ya malaika” ambao walishikilia mkia wake na hawakuweza kuuachilia. Hebu sote daima tukumbuke kwamba — {2TG28: 19.1}
“Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana yeye peke yake atukuzwa katika siku hiyo.” Isa. 2:11. {2TG28: 19.2}
19
Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutum-wa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchap-ishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG28: 20.1}
20
ZAWADI KWA AJILI YAKO
Je! Unayo nia ya kuchambua zaidi katika kweli muhimu ambazo kwa hitaji zinaguswa tu katika majani haya ya vuli? Iwapo ni hivyo, unaalikwa kutuma ombi la nakala yoyote ya trakti zilizoorodheshwa hapa chini. Zi-natumwa kama huduma ya Kikristo bila bei au sharti, isipokuwa jukumu la nafsi kwayo yenyewe kuyajaribu mambo yote na kulishika lililo jema. {2TG28: 21.1}
Orodha ya Machapisho
Trakti Namba 1, Ya Ziada “Kabla ya Saa ya Kumi na Moja” (Ezekiel 9)
Trakti Namba 2, Utata wa Onyo (Zekaria 6)
Trakti Namba 3, Hukumu na Mavuno
Trakti Namba 4, Habari za Hivi Punde kwa Mama (Hosea 1, 2)
Trakti Namba 5, Onyo La Mwisho (Baragumu Saba)
Trakti Namba 6, Kwa Nini Uangamie? (Isaya 7; Zekaria 4)
Trakti Namba7, Pambano Kuu Juu ya Fimbo ya Mchungaji
Trakti Namba 8, Mlima Zayuni Saa ya Kumi na Moja
Trakti Namba 9, Tazama, Niyafanya Yote Kuwa Mpya
Trakti Namba 10, Ishara ya Yona
Trakti Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho
Trakti Namba 13, Salamu za Kristo
Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita
Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, Toleo la Mfukoni
Kwa Makanisa Saba (Kuifunua Mihuri Saba)
Msururu wa Majibu, Vitabu Namba 1 hadi Namba 5.
21
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 27, 28
Kimechapishwa nchini Marekani
22